Tafsiri ya Surat Al-Muddaththir
Tafsiri ya Surat Al-Muddaththir
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{يَاأَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ (1) قُمْ فَأَنْذِرْ (2) وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ (3) وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ (4) وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ (5) وَلَا تَمْنُنْ تَسْتَكْثِرُ (6) وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ (7)}.
1. Ewe uliyejigubika! 2. Simama uonye! 3. Na Mola wako Mlezi mtukuze! 4. Na nguo zako, zisafishe. 5. Na yaliyo machafu yahame! 6. Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa. 7. Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
#
{1 - 2} تقدَّم أنَّ المزَّمِّل والمدَّثر بمعنى واحد، وأنَّ الله أمر رسوله - صلى الله عليه وسلم - بالاجتهاد في عبادات الله القاصرة والمتعدِّية، فتقدَّم هناك الأمر له بالعبادات الفاضلة القاصرة، والصبر على أذى قومه، وأمره هنا بالإعلان بالدَّعوة والصَّدْع بالإنذار، فقال: {قمْ}؛ أي: بجدٍّ ونشاطٍ {فأنذِرْ}: الناس بالأقوال والأفعال التي يحصلُ بها المقصودُ وبيانُ حال المنذَر عنه ليكون ذلك أدعى لتركه.
{1 - 2} Hapo awali ilitajwa kuwa al-Muzzammil na al-Muddaththir ni maneno yenye maana sawa, na kwamba Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - afanye bidii katika ibada zinazomfaa yeye tu na zile za kuwafaa wengine pia. Basi ikatangulia hapo awali kwamba ameamrishwa kufanya ibada bora zaidi zenye kumfaa yeye tu na kuwa na subira na juu ya maudhi ya watu wake, na hapa akamuamuru kutangaza wito wake na kutoa onyo waziwazi.
Kwa hivyo akasema: "Simama" kwa bidii na kwa ukakamavu "uonye" watu kwa kauli na vitendo vinavyofanikisha yaliyokusudiwa na pia kubainisha hali ya kile kinachoonywa juu yake, ili hilo liitie zaidi kuachana nalo.
#
{3} {وربَّك فكبِّرْ}؛ أي: عظِّمه بالتوحيد، واجعل قصدك في إنذارك وجه الله وأن يعظِّمه العباد، ويقوموا بعبادته.
{3} "Na Mola wako Mlezi mtukuze" kwa kumpwekesha, na uyafanye makusudio yako katika maonyo yako kuwa ni uso wa Mwenyezi Mungu na kwamba waja wamtukuze na wamuabudu.
#
{4} {وثيابَكَ فطَهِّرْ}: يُحتمل أنَّ المراد بالثياب أعماله كلها. وبتطهيرها: تخليصها، والنُّصح بها، وإيقاعها على أكمل الوجوه، وتنقيتها عن المبطلات والمفسدات والمنقصات من شركٍ ورياء ونفاق وعُجْبٍ وتكبُّر وغفلةٍ وغير ذلك مما يؤمَرُ العبد باجتنابه في عباداته، ويدخل في ذلك تطهير الثياب من النجاسة؛ فإنَّ ذلك من تمام التطهير للأعمال، خصوصاً في الصلاة، التي قال كثيرٌ من العلماء: إنَّ إزالة النجاسة عنها شرطٌ من شروطها.
ويُحتمل أنَّ المراد بثيابه الثياب المعروفة؛ أنَّه مأمورٌ بتطهيرها عن جميع النجاسات في جميع الأوقات، خصوصاً عند الدُّخول في الصلوات.
{4} "Na nguo zako, zisafishe." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa nguo hapa ni matendo yake yote. Na kwamba kuyasafisha ni kuyatakasa na kumsafia Mwenyezi Mungu ndani yake, na kuyatekeleza kwa namna iliyo kamilifu kabisa, na kuyatakasa kabisa mbali na yale yanayoyabatilisha, ya kuyaharibu na yenye kuyapunguza kama vile ushirikina, kujionyesha, unafiki, kiburi, kughafilika na mengineyo miongoni mwa yale ambayo mja ameamrishwa kuepukana nayo katika ibada yake, na hili linajumuisha kutakasa nguo kutokana na najisi. Kwani hilo ni katika mambo yanayosababisha utakaso kamili wa matendo hasa katika swala ambayo wanavyuoni wengi wamesema kuwa kuondoa najisi ni miongoni mwa masharti yake. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa hapa na nguo zake ni nguo zinazojulikana, kwamba ameamrishwa kuzitakasa mbali na najisi kila wakati, haswa wakati wa kuingia katika swala.
#
{5} وإذا كان مأموراً بطهارة الظَّاهر؛ فإنَّ طهارة الظاهر من تمام طهارة الباطن: {والرُّجْزَ فاهْجُرْ}: يُحتمل أنَّ المراد بالرجز الأصنام والأوثان التي عُبِدَتْ مع الله، فأمره بتركها والبراءة منها ومما نُسِبَ إليها من قول أو عمل، ويُحتمل أنَّ المرادَ بالرُّجز أعمالُ الشرِّ كلُّها وأقوالُه، فيكون أمراً له بترك الذُّنوب صغارها وكبارها ظاهرها وباطنها، فيدخل في هذا الشرك فما دونه.
{5} Ikiwa ameamriwa kuwa safi kwa nje,
basi ni kwa sababu usafi wa nje ni katika utimilifu wa usafi wa ndani: "Na yaliyo machafu yahame!" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa na uchafu ni masanamu na vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo akamuamuru kuyaacha na kujiweka mbali nayo, na yote yaliyonasibishwa nayo kama vile maneno au matendo. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa na uchafu ni matendo na maneno yote maovu, kwa hivyo hii inakuwa amri anayoamrishwa kuacha madhambi, madogo na makubwa, ya dhahiri na yaliyofichikana, kwa hivyo inaingia katika hilo ushirikina na yaliyo chini yake.
#
{6} {ولا تَمْنُنْ تَسْتَكثِرْ}؛ أي: لا تمنُنْ على الناس بما أسديت إليهم من النعم الدينيَّة والدنيويَّة، فتستكثر بتلك المنَّة، وترى لك الفضل عليهم ، بل أحسِنْ إلى الناس مهما أمكنك، وانْسَ عندهم إحسانَك، واطلُبْ أجرك من الله تعالى ، واجعلْ مَن أحسنتَ إليه وغيره على حدٍّ سواء.
وقد قيل: إنَّ معنى هذا ألاَّ تعطي أحداً شيئاً وأنت تريدُ أن يكافِئَك عليه بأكثر منه، فيكون هذا خاصًّا بالنبيِّ صلى الله عليه وسلم .
{6} "Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa." Yaani, usiwape watu neema za kidini na za kidunia ulizowaneemesha kwazo ili uzidishiwe kwa kuneemesha huko. Bali wafanyie wema watu uwezavyo na usahau wema wako kwao, na utafute malipo yako kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wafanye sawa yule uliyemneemesha na yule ambaye hukumneemesha. Na imesemwa kwamba maana yake ni kuwa usimpe mtu kitu ilihali unataka akulipe zaidi ya hicho kitu, basi hili linakuwa ni mahususi kwa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie.
#
{7} {ولربِّكَ فاصْبِرْ}؛ أي: احتسبْ بصبرك واقصدْ به وجهَ الله تعالى.
فامتثل رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - لأمر ربِّه، وبادر فيه ، فأنذر الناس وأوضح لهم بالآياتِ البيناتِ جميع المطالب الإلهيَّة، وعظَّم الله تعالى، ودعا الخلق إلى تعظيمه، وطهَّر أعماله الظاهرة والباطنة من كل سوءٍ، وهجر كلَّ ما يُعْبَدُ من دون الله وما يُعْبَدُ معه من الأصنام وأهلها والشرِّ وأهله، وله المنَّة على الناس بعد منَّة الله، من غير أن يطلبَ عليهم بذلك جزاءً ولا شكوراً، وصبر لربِّه أكمل صبر: فصبر على طاعة الله، وعن معاصيه، وصبر على أقداره المؤلمة، حتى فاق أولي العزم من المرسَلين. صلواتُ الله وسلامُه عليه وعليهم أجمعين.
{7} "Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!" Yaani, tarajia malipo ya Mwenyezi Mungu kwa subira yako na uukusudie kwa hilo uso wa Mwenyezi Mungu. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akachukua hatua ya haraka kufanya hivyo na akawaonya watu wote kwa ishara zilizo wazi juu ya mambo yote ya Mwenyezi Mungu, na akamtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, akavitaka viumbe vimtukuze, akatakasa vitendo vyake vya nje na vilivyofichikana kutokana na ubaya wote, na akaacha kila kitu kilichoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na vile vinavyoabudiwa pamoja naye kama vile masanamu na watu wake, na uovu na watu wake. Basi anafaa kupata fadhila kwa hilo baada ya fadhila za Mwenyezi Mungu, bila ya kuwaomba malipo kwa hilo wala shukurani, na akasubiri kwa ajili ya Mola wake Mlezi subira iliyokamilika zaidi. Alikuwa na subira juu ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kujiepusha mbali na maasi, na akawa na subira juu ya mipango ya michungu ya Mwenyezi Mungu mpaka akawapiku Mitume wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume. Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu yao wote.
{فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ (8) فَذَلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ (9) عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ (10)}.
8. Basi litakapopulizwa barugumu, 9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu. 10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.
#
{8 - 10} أي: فإذا نُفِخَ في الصُّور للقيام من القبور، وجُمِعَ الخلائق للبعث والنشور، {فذلك يومئذٍ يومٌ عسيرٌ}: لكثرة أهواله وشدائده، {على الكافرين غيرُ يسيرٍ}؛ لأنَّهم قد أيِسوا من كلِّ خيرٍ وأيقنوا بالهلاك والبَوار. ومفهومُ ذلك أنَّه على المؤمنين يسيرٌ؛ كما قال تعالى: {يقول الكافرون هذا يومٌ عَسِرٌ}.
{8 - 10} Yaani, linapopulizwa baragumu la kufufuka kutoka makaburini, na viumbe vinakusanywa kwa ajili ya kufufuliwa na kutawanywa. "Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu" kwa sababu ya wingi wa mahangaiko na dhiki zake. "Kwa makafiri haitakuwa nyepesi." Kwa sababu watakata tamaa na wema wote na watakuwa na yakini ya maangamio. Maana yake isiyokuwa na moja kwa moja ni kuwa siku hiyo itakuwa rahisi kwa waumini.
Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu."
{ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا (11) وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَمْدُودًا (12) وَبَنِينَ شُهُودًا (13) وَمَهَّدْتُ لَهُ تَمْهِيدًا (14) ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ (15) كَلَّا إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا (16) سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا (17) إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ (18) فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ (19) ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ (20) ثُمَّ نَظَرَ (21) ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ (22) ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ (23) فَقَالَ إِنْ هَذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ (24) إِنْ هَذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ (25) سَأُصْلِيهِ سَقَرَ (26) وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ (27) لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ (28) لَوَّاحَةٌ لِلْبَشَرِ (29) عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ (30) وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَذَا مَثَلًا كَذَلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَى لِلْبَشَرِ (31)}.
11. Niache peke yangu na niliyemuumba. 12. Na nikamjaalia awe na mali mengi. 13. Na wana wanaoonekana. 14. Na nikamtegenezea mambo vizuri kabisa. 15. Kisha anatumai nimzidishie! 16. Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! 17. Nitamtesa kwa mateso yasiowezekana. 18. Kwani hakika yeye alifikiri na akapima. 19. Basi ameangamia! Vipi alivyopima! 20. Tena ameangamia! Vipi alivyopima! 21. Kisha akatazama. 22. Kisha akakunja kipaji, na akanuna. 23. Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari. 24.
Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. 25. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu. 26. Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. 27. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? 28. Haubakishi wala hausazi. 29. Unababua ngozi iwe nyeusi. 30. Juu yake wapo kumi na tisa. 31. Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru, wapate kuwa na yakini waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini, wala wasiwe na shaka waliopewa Kitabu na Waumini,
na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.
#
{11 - 30} هذه الآيات نزلت في الوليد بن المغيرة ، المعاند للحقِّ، المبارز لله ولرسوله بالمحاربة والمشاقَّة، فذمَّه الله ذمًّا لم يذمَّ به غيره، وهذا جزاءُ كلِّ مَنْ عانَد الحقَّ ونابذه؛ أنَّ له الخزيَ في الدُّنيا ولَعذاب الآخرة أخزى، فقال:
{ذَرْني ومَن خلقتُ وحيداً}؛ أي: خلقته منفرداً بلا مال ولا أهل ولا غيره، فلم أزل أربِّيه وأعطيه، فجعلت {له مالاً ممدوداً}؛ أي: كثيراً، {و} جعلتُ له {بنينَ}؛ أي: ذكوراً، {شهوداً}؛ أي: حاضرين عنده على الدَّوام، يتمتَّع بهم ويقضي بهم حوائِجَه ويستنصِرُ بهم، {ومهَّدْتُ له تمهيداً}؛ أي: مكَّنته من الدُّنيا وأسبابها حتى انقادَتْ له مطالِبُه وحصل له ما يشتهي ويريدُ. {ثم}: مع هذه النعم والإمدادات {يَطْمَعُ أن أزيدَ}؛ أي: يطمع أن ينال نعيم الآخرة كما نال نعيم الدنيا، {كلاَّ}؛ أي: ليس الأمر كما طمع، بل هو بخلاف مقصوده ومطلوبه، وذلك {إنَّه كان لآياتنا عنيداً}: عرفها ثم أنكرها، ودعتْه إلى الحقِّ فلم يَنْقَدْ لها، ولم يكفِهِ أنَّه أعرض عنها وتولَّى ، بل جعل يحاربُها ويسعى في إبطالها، ولهذا قال عنه: {إنَّه فَكَّر}؛ أي: في نفسه. {وقدَّر}: ما فكَّر فيه؛ ليقولَ قولاً يبطِلُ به القرآن، {فقُتِلَ كيف قدَّر. ثم قُتِلَ كيف قدَّر}؛ لأنَّه قدَّر أمراً ليس في طوره، وتسوَّر على ما لا ينالُه هو ولا أمثاله، {ثم نَظَرَ}: ما يقول، {ثم عَبَسَ وبَسَرَ}: في وجهه وظاهره نفرةً عن الحقِّ وبُغضاً له، {ثم أدبر}؛ أي: تولَّى، {واستكبر}: نتيجة سعيه الفكريِّ والعمليِّ والقوليِّ، {فقال إنْ هذا إلاَّ سحرٌ يُؤْثَرُ. إنْ هذا إلاَّ قولُ البشرِ}؛ أي: ما هذا كلام الله، بل كلام البشر، وليس أيضاً كلام البشر الأخيار، بل كلام الأشرار منهم والفجَّار من كل كاذبٍ سحَّارٍ، فتبًّا له! ما أبعده من الصواب! وأحراه بالخسارة والتَّباب! كيف يدور في الأذهان أو يتصوَّره ضميرُ أيِّ إنسان أن يكون أعلى الكلام وأعظمه كلام الربِّ الكريم الماجد العظيم يشبِهُ كلام المخلوقين الفقراء الناقصين؟! أم كيف يتجرَّأ هذا الكاذب العنيد على وصفه بهذا الوصف لكلام الله تعالى ؛ فما حقُّه إلاَّ العذاب الشديد [والنكال]، ولهذا قال تعالى: {سأُصْليه سَقَرَ. وما أدراك ما سَقَرُ. لا تُبْقي ولا تَذَرُ}؛ أي: لا تبقي من الشدَّة ولا على المعذَّب شيئاً إلا وبَلَغَتْه. {لوَّاحةٌ للبشر}؛ أي: تلوحهم وتُصليهم في عذابها وتقلقهم بشدَّة حرِّها وقَرِّها. {عليها تسعةَ عشرَ}: من الملائكة، خزنة لها، غلاظٌ شدادٌ لا يعصون الله ما أمرهم ويفعلون ما يُؤمرون.
{11 - 30} Aya hizi ziliteremshwa kuhusu Al-Walid bin Al-Mughirah, ambaye alikuwa mkaidi dhidi ya haki, na ambaye alisimama kukabiliana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kupigana naye na kumpinga. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamkashifu kwa kashfa ambayo hakuwahi kumkashifu mwingineye. Na haya ndiyo malipo kwa wote wanaoikaidi haki na kupingana nayo; kwamba atapata hizaya katika dunia, na tena adhabu ya Akhera ni ya kufedhehesh zaidi.
Akasema: "Niache peke yangu na niliyemuumba" Yaani: Nilimuumba peke yake, bila ya mali, familia, wala mtu mwingine yeyote. Basi nikaendelea kumlea na kumpa,
na nikamjaalia "awe na mali nyingi na" pia nikamfanyia kuwa na "wana" wa kiume "wanaoonekana" Yaani: waliopo pamoja naye daima, anawafurahia, hutimiza haja zake kupitia kwa hao, na kutafuta msaada kupitia kwao "Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa" katika dunia na sababu zake mpaka yakatekelezeka mambo anayotafuta na kutamani. "Kisha" pamoja na neema hizi na hivi vyote alivyopewa "anatumai nimzidishie!' Yaani anatazamia kupata neema za Akhera kama alivyozipata neema za dunia. "Hasha!" Yaani jambo hili si kama alivyokuwa akitaka, bali ni kinyume na aliyoyakusudia na kuyataka. Na hayo ni "kwa sababu hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!" Alizijua kisha akazikanusha, na zikamwita kwenye haki, lakini hakunyenyekea kwazo, na bado haikumtosha kujiepusha nazo na kuzipa mgongo. Bali alianza kupigana nao vita na kujitahidi kuzibatilisha,
na ndiyo maana akasema juu yake: "Kwani hakika yeye alifikiri" ndani ya nafsi yake "na akapima" kile alichofikiria ili aseme kauli atakayoibatilisha Qur-ani kwayo. "Basi ameangamia! Vipi alivyopima! Tena ameangamia! Vipi alivyopima!" Kwa sababu alipima kitu kisichokuwa ndani ya upeo wake, na akajiingiza katika kile ambacho yeye wala mfano wake hawawezi kukifikia. "Kisha akatazama" cha kusema "kisha akakunja kipaji, na akanuna" ili kuikimbia kuichukia haki. "Kisha akaipa kisogo haki" na akaenda zake "na akatakabari" hili likiwa ni matokeo ya juhudi zake za kiakili, kivitendo na kwa maneno.
"Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. Haya si chochote ila kauli ya binadamu." Yaani, haya si maneno ya Mwenyezi Mungu. Bali ni maneno ya wanadamu, na pia si maneno ya wanadamu wema, bali ni maneno ya waovu miongoni mwao na wasiomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa kila mwongo na mchawi, basi naangamie! Jinsi gani alivyo mbali mno zaidi na usahihi! Na ni mwenye kustahili zaidi vipi hasara na kuangamia! Je, inawezaje kuingia katika akili ya mtu yeyote au kufikiriwa na dhamiri ya mtu yeyote kwamba maneno ya juu kabisa na makuu zaidi, maneno ya Mola Mlezi, Mtukufu, Mwenye heshima, Mkuu kwamba yanafanana na maneno ya viumbe maskini, wapungufu?! Au huyu mwongo mkaidi anathubutu vipi kuelezea maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa maelezo haya? Hastahiki chochote ila adhabu kali
[na mateso mazito],
na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. Na ni nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hausazi" mwenye kuadhibiwa. "Unababua mno ngozi iwe nyeusi." Yaani, unawababua na kuwaingiza mno katika adhabu yake, na unawatia wasiwasi kwa ukali wa joto lake na baridi yake kali. "Juu yake wapo kumi na tisa" miongoni mwa Malaika, wasimamizi wake, wakali na wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu katika anayowaamrisha na wanafanya wanayoamrishwa.
#
{31} {وما جعلنا أصحاب النارِ إلاَّ ملائكةً}: وذلك لشدَّتهم وقوَّتهم، {وما جعلنا عِدَّتهم إلاَّ فتنةً للذين كفروا}: يحتمل أنَّ المراد؛ إلاَّ لعذابهم وعقابهم في الآخرة ولزيادة نَكالهم فيها، والعذاب يسمَّى فتنة؛ كما قال تعالى: {يومَ هم على النَّارِ يُفْتَنونَ}.
ويُحتمل أنَّ المراد أنَّا ما أخبرناكم بعدَّتهم إلاَّ لنعلم من يصدِّق ممَّن يكذِّب. ويدلُّ على هذا ما ذكره بعده في قوله: {ليستيقِنَ الذين أوتوا الكتاب ويزدادَ الذين آمنوا إيماناً}: فإنَّ أهل الكتاب إذا وافق ما عندَهم وطابَقَه؛ ازدادَ يقينُهم بالحقِّ، والمؤمنون كلَّما أنزل الله آيةً، فآمنوا بها وصدَّقوا؛ ازداد إيمانُهم، {ولا يرتابَ الذين أوتوا الكتابَ والمؤمنون}؛ أي: ليزول عنهم الريبُ والشكُّ، وهذه مقاصدُ جليلةٌ يعتني بها أولو الألباب، وهي السعي في اليقين وزيادة الإيمان في كلِّ وقتٍ وكلِّ مسألةٍ من مسائل الدين، ودفع الشكوك والأوهام التي تَعْرِضُ في مقابلة الحقِّ، فجعل ما أنزله على رسولِهِ محصِّلاً لهذه المقاصد الجليلة، ومميزاً للصادقين من الكاذبين ، ولهذا قال: {وليقولَ الذين في قلوبِهِم مرضٌ}؛ أي: شكٌّ وشبهةٌ ونفاقٌ، {والكافرون ماذا أرادَ الله بهذا مثلاً}: وهذا على وجه الحيرة والشكِّ منهم والكفر بآيات الله، وهذا وذاك من هداية الله لمن يهديه وإضلاله لمن يُضِلُّه، ولهذا قال: {كذلك يُضِلُّ الله مَن يشاءُ ويَهْدي مَن يشاءُ}: فمن هداه الله؛ جعل ما أنزل على رسوله رحمةً في حقِّه وزيادةً في إيمانه ودينه، ومن أضلَّه؛ جعل ما أنزله على رسوله زيادةَ شقاءٍ عليه وحيرةً وظلمةً في حقِّه، والواجب أن يُتَلَقى ما أخبر الله به ورسولُه بالتسليم، فإنه {ما يعلمُ جنودَ ربِّك} من الملائكة وغيرهم {إلاَّ هو}: فإذا كنتُم جاهلين بجنوده، وأخبركم بها العليم الخبير؛ فعليكم أن تصدِّقوا خبره من غير شكٍّ ولا ارتياب، {وما هي إلاَّ ذِكْرى للبشرِ}؛ أي: وما هذه الموعظة والتذكار مقصوداً به العبث واللعب، وإنما المقصود به أن يتذكَّر به البشر ما ينفعهم فيفعلونه، وما يضرُّهم فيتركونه.
{31} "Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika" kwa sababu ya ukali wao na nguvu zao. "Wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni 'isipokuwa kwa ajili wawaadhibu huko Akhera humo motoni na kuwazidishia humo adhabu. Adhabu pia inaitwa fitna
(majaribio); kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni." Inawezekana kuwa kinachomaanishwa hapa ni kwamba hatukukuambieni juu ya idadi yao isipokuwa ili tujue ni nani anayesadiki na ni nani anayekadhibisha.
Haya yanaonyeshwa na yale aliyoyataja baada yake katika kauli yake: "wapate kuwa na yakini wale waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini." Kwa maana, Watu wa Kitabu ikiwa haya yataafikiana na yale waliyo nayo na yakalingana, yakini yao juu ya haki inaongezeka. Nao Waumini kila Mwenyezi Mungu anapoteremsha Aya, wakaiamini na kuisadiki, imani yao inaongezeka. "Wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini." Yaani, ili hilo liwaondoshee shaka na kusitasita. Na haya ni malengo makubwa wanayoyachunga mno wenye akili, ambayo ni kujitahidi kuwa na yakini na kuzidisha imani kila wakati na katika kila suala la dini, na kuondosha shaka na fikira potofu zinazojitokeza katika kukabiliana na haki. Basi akayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni yenye kufanikisha malengo haya makubwa, na yenye kupambanua wakweli mbali na waongo,
na ndiyo maana akasema: "Na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao." Yaani, maradhi ya shaka,
dhana na unafiki "na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu?" Haya ni katika njia ya kuchanganyikiwa na shaka kwa upande wao na kukufuru ishara za Mwenyezi Mungu. Na hili na lile ni sehemu katika kuongoa kwa Mwenyezi Mungu yule ambaye amemuongoa na upotoshaji wake kwa yule ambaye anampoteza,
na ndiyo maana akasema: "Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye." Kwa hivyo yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, anayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni rehema kwake na kuzidisha imani yake na dini yake, Na yule ambaye amempotosha, anayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni kuzidisha upotofu juu yake, mkanganyiko na giza kwa upande wake. "Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi" miongoni mwa Malaika na wengineo "ila Yeye tu." Basi ikiwa nyinyi hamjui majeshi yake, na amekujulisheni hayo Mjuzi mno, Mwenye habari zote, basi lazima muamini habari zake bila ya shaka yoyote wala kusitasita. "Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binadamu." Wala hayakukusudiwa mawaidha haya na ukumbusho kuwa ni upumbavu na mchezo. Bali kilichokusudiwa kwayo ni watu kukumbuka yale yanayowanufaisha, wakayafanya, na yale yanayowadhuru, basi wakayaacha.
{كَلَّا وَالْقَمَرِ (32) وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ (33) وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ (34) إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ (35) نَذِيرًا لِلْبَشَرِ (36) لِمَنْ شَاءَ مِنْكُمْ أَنْ يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ (37) كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ (38) إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ (39) فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ (40) عَنِ الْمُجْرِمِينَ (41) مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ (42) قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ (43) وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ (44) وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ (45) وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ (46) حَتَّى أَتَانَا الْيَقِينُ (47) فَمَا تَنْفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ (48) فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ (49) كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُسْتَنْفِرَةٌ (50) فَرَّتْ مِنْ قَسْوَرَةٍ (51) بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِنْهُمْ أَنْ يُؤْتَى صُحُفًا مُنَشَّرَةً (52) كَلَّا بَلْ لَا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ (53) كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ (54) فَمَنْ شَاءَ ذَكَرَهُ (55) وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَى وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ (56)}.
32. Hasha! Naapa kwa mwezi! 33. Na kwa usiku unapokucha! 34. Na kwa asubuhi inapopambazuka! 35. Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa! 36. Ni onyo kwa binaadamu. 37. Kwa anayetaka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa. 38. Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma. 39. Isipokuwa watu wa kuliani. 40. Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana 41.
Habari za wakosefu: 42. Ni nini kilichokupelekeni Motoni? 43.
Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakisali. 44. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. 45. Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu. 46. Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo. 47. Mpaka yakini ilipotufikia. 48. Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi. 49. Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili? 50. Kana kwamba wao ni mapunda waliotimuliwa. 51. Wanaomkimbia simba! 52. Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa. 53. Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera? 54. Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho! 55. Basi anayetaka atakumbuka. 56. Na hawatakumbuka isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.
#
{32 - 34} {كلاَّ}: هنا بمعنى حقًّا، أو بمعنى ألا الاستفتاحية، فأقسم تعالى بالقمر، وبالليل وقتَ إدباره، والنهارِ وقتَ إسفاره؛ لاشتمال المذكورات على آيات الله العظيمة الدالَّة على كمال قدرةِ الله وحكمته وسعة سلطانه وعموم رحمته وإحاطة علمه.
{32 - 34} "Hasha," sivyo hivyo. Kisha Mwenyezi Mungu akaapa kwa mwezi, na kwa usiku wakati wa kucha kwake, na kwa mchana unapopambazuka, kwani hayo yaliyotajwa yanajumuisha ishara kuu za Mwenyezi Mungu zinazoonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu, hekima yake, upana wa mamlaka yake, ujumla wa rehema yake na kujua kwake kila kitu.
#
{35 - 37} والمقسَمُ عليه قوله: {إنَّها لإحدى الكُبَرِ}؛ أي: إنَّ النار لإحدى العظائم الطامَّة والأمور الهامَّة؛ فإذا أعلمناكم بها وكنتُم على بصيرةٍ من أمرها؛ فمن شاء منكم أن يتقدَّم فيعمل بما يقرِّبُه إلى الله ويُدْنيه من رضاه ويُزْلفه من دار كرامته، أو يتأخَّر عمَّا خُلِقَ له وعمَّا يحبُّه الله ويرضاه، فيعمل بالمعاصي، ويتقرَّب إلى جهنَّم؛ كما قال تعالى: {وقلِ الحقُّ من ربِّكم فَمَن شاء فَلْيُؤمِن ومَن شاءَ فَلْيَكْفُرْ ... } الآية.
{35 - 37} Na kile kilichoapiwa ni kauli yake: "Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!" Kwa hivyo, tukikujulisheni juu yake na mkajua vyema jambo lake, basi anayetaka kutangulia miongoni mwenu na kufanya yatakayomweka karibu na Mwenyezi Mungu na kumsogeza karibu mno na radhi zake na nyumba ya utukufu wake, au anayetaka akabaki nyuma katika kile alichoumbwa kwa ajili yake na kile anachokipenda Mwenyezi Mungu na kukiridhia, basi na
afanye maasi na ajiweke karibu na Jahannam.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye aamini..." hadi mwisho wa Aya.
#
{38 - 48} {كلُّ نفس بما كسبتْ}: من أفعال الشرِّ وأعمال السوء {رهينةٌ}: بها موثقةٌ بسعيها، قد أُلْزِمَ عنقها وغُلَّ في رقبتها واستوجبت به العذاب، {إلاَّ أصحابَ اليمين}: فإنَّهم لم يرتهنوا، بل أُطلقوا وفرحوا {في جناتٍ يتساءلونَ. عن المجرمينَ}؛ أي: في جناتٍ قد حصل لهم فيها - جميع مطلوباتهم وتمَّت لهم الراحةُ والطمأنينة، حتى أقبلوا يتساءلون، فأفضتْ بهم المحادثة أن سألوا عن المجرمين؛ أيُّ حال وصلوا إليها؟ وهل وَجَدوا ما وعَدَهم الله [تعالى]؟ فقال بعضهم لبعضٍ هل أنتم مُطَّلعونَ عليهم، فاطَّلعوا عليهم في وسطِ الجحيم يعذَّبون، فقالوا لهم: {ما سَلَككم في سَقَرَ}؛ أي: أيُّ شيءٍ أدخلكم فيها؟ وبأيِّ ذنبٍ اسْتَحَقيْتُموها؟ فقالوا: {لم نَكُ من المصلِّينَ. ولم نكُ نطعِمُ المسكينَ}: فلا إخلاص للمعبودِ ولا إحسانَ ولا نفع للخلق المحتاجين، {وكنَّا نخوضُ مع الخائضينَ}؛ أي: نخوض بالباطل ونجادل به الحقَّ، {وكنَّا نكذِّبُ بيوم الدِّينِ}: هذه آثار الخوض بالباطل، وهو التَّكذيب بالحقِّ، ومن أحقِّ الحقِّ يوم الدين، الذي هو محلُّ الجزاء على الأعمال وظهور مُلك الله وحُكمه العدل لسائر الخلق، فاستمرَّ عَمَلُنا على هذا المذهب الباطل {حتَّى أتانا اليقين}؛ أي: الموت، فلما ماتوا على الكفر؛ تعذَّرت حينئذٍ عليهم الحِيَلُ، وانسدَّ في وجوههم باب الأمل. {فما تَنفَعُهم شفاعةُ الشَّافعين}؛ لأنَّهم لا يشفعون إلاَّ لِمَنِ ارتضى، وهؤلاء لا يرضى الله أعمالهم.
{38 - 48} "Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma" miongoni mwa vitendo viovu na vibaya. Vimefungwa shingoni kwake sawasawa na vikamfanya kustahiki kuadhibiwa kwavyo. "Isipokuwa watu wa kuliani" kwani hawakushikwa rahanini. Bali walifunguliwa huru na wakafurahishwa. "Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana habari za wakosefu." Humo watakuwa wamepewa yote waliyoyataka na itawatimia starehe na utulivu, mpaka wakaelekeana kuulizana maswali, kisha mazungumzo hayo yakawapelekea kuuliza juu ya wahalifu. Walifikia hali gani? Je,
walipata kile ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi? Kisha baadhi yao wakaambiana: 'Je, mnawaona?' Basi wakawatazama na wakawaona katikati ya Jahannamu wakiteswa,
kwa hivyo wakawaambia: “Ni nini kilichokupelekeni Saqr?” Wakasema: "Hatukuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakisali. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini." Kwa hivyo hawakumkusudia mwabudiwa peke yake, wala hawakuwa wakiwafanyia wema na kuwanufaisha viumbe wahitaji. "Na tulikuwa tukizama pamoja na wale waliozama katika maovu" tukiijadili na kuipinga haki kwayo. "Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo." Hizi ndizo athari za kujizamisha katika batili, ambazo ni kukadhibisha haki. Na katika haki kubwa zaidi ni kuamini katika siku ya malipo, ambayo ndiyo siku ya malipo juu ya matendo na kudhihiri ufalme wa Mwenyezi Mungu na hukumu yake ya uadilifu kwa viumbe vyote. Basi sisi tukaendelea kufanya matendo kulingana na dhehebu hili batili. "Mpaka yakini ilipotufikia." Yaani, mauti. Basi walipokufia katika ukafiri, wakakosa hila yoyote, na mlango wa matumaini ukafungika mbele ya nyuso zao. "Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi." Kwa sababu hawamfanyii uombezi yeyote isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemridhia. Na hao, Mwenyezi Mungu hayaridhii matendo yao.
#
{49 - 53} فلمَّا بيَّن الله مآل المخالفين وبيَّن ما يفعل بهم؛ عطف على الموجودين بالعتاب واللوم، فقال: {فما لهم عن التَّذْكِرَةِ معرِضينَ}؛ أي: صادَّين غافلين عنها، {كأنَّهم}: في نفرتِهِم الشديدة منها {حمُرٌ مستنفرةٌ}؛ أي: [كأنّهم] حمُرُ وحشٍ نفرتْ؛ فنفَّر بعضُها بعضاً فزاد عَدْوُها، {فرَّتْ من قَسْوَرَةٍ}؛ أي: من صائدٍ ورامٍ يريدها أو من أسدٍ ونحوه، وهذا من أعظم ما يكون من النُّفور عن الحقِّ، ومع هذا النفور والإعراض يدَّعون الدَّعاوي الكبار؛ فيريد {كلُّ} واحد {منهم أن يُؤْتى صُحُفاً منشَّرةً}: نازلة عليه من السماء؛ يزعم أنَّه لا ينقاد للحقِّ؛ إلاَّ بذلك، وقد كذَّبوا؛ فإنَّهم لو جاءتهم كلُّ آيةٍ؛ لم يؤمنوا حتى يروا العذاب الأليم؛ لأنَّهم جاءتهم الآياتُ البيناتُ، التي تبيِّن الحقَّ وتوضِّحه؛ فلو كان فيهم خيرٌ؛ لآمنوا، ولهذا قال: {كلاَّ}؛ أي: لا نعطيهم ما طلبوا، وهم ما قصدوا بذلك إلاَّ التعجيز، {بل لا يخافونَ الآخرةَ}: فلو كانوا يخافونها؛ لما جرى منهم ما جرى.
{49 - 53} Mwenyezi Mungu alipobainisha hatima ya wale waliohalifu kitambo na akabainisha watakachofanyiwa, akawaelekezea hawa waliopo makaripio na lawama,
akasema: "Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?" Yaani, wanaupinga na na wameghafilika mbali nao. "Kama kwamba wao" katika kuukimbia kwao mno "ni mapunda waliotimuliwa." Basi wakakimbizana wao kwa wao, kwa hivyo wakazidi kukimbia. "Wanaomkimbia simba" au mwindaji na mpiga mishale anayewataka. Na hali hii ndiyo aina mojawapo kubwa zaidi ya kujiweka mbali na haki, lakini pamoja na kujiweka mbali huku na kupeana mgongo, wanadai madai makubwa. "Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa" zimshukie kutoka mbinguni. Anadai kwamba hajisalimishi kwa haki Isipokuwa kwa hilo. Lakini wamesema uwongo. Kwani lau ingewafikia kila ishara, hawangeamini mpaka waione adhabu chungu. Kwa sababu ziliwajia ishara zilizo wazi zinazobainisha na kuiweka wazi haki. Basi ikiwa kulikuwa na wema ndani yao, wangeamini,
na ndiyo maana akasema: "Hasha!" Yaani, hatuwapi kile walichokiomba, kwani hawakukusudia kwa hilo isipokuwa kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ameshindwa. "Kwani wao hawaiogopi Akhera?" Kwa sababu wangekuwa wanaiogopa, hawangefanya hayo waliyoyafanya.
#
{54 - 56} {كلاَّ [إنَّه] تذكرةٌ}: الضمير إمَّا أن يعود على هذه السورة أو على ما اشتملتْ عليه من هذه الموعظة، {فَمَن شاء ذَكَرَهُ}: لأنَّه قد بيَّن له السبيل ووضَح له الدَّليل. {[وما يَذْكُرون] إلاَّ أن يشاءَ اللهُ}: فإنَّ مشيئة اللَّه نافذةٌ عامَّةٌ، لا يخرج عنها حادثٌ قليلٌ ولا كثيرٌ؛ ففيها ردٌّ على القدريَّة، الذين لا يُدْخِلون أفعال العباد تحت مشيئة الله، والجبريَّة، الذين يزعمون أنَّه ليس للعبد مشيئةٌ ولا فعلٌ حقيقةً، وإنَّما هو مجبور على أفعاله، فأثبت تعالى للعباد مشيئةً حقيقةً وفعلاً، وجعل ذلك تابعاً لمشيئته، و {هو أهلُ التَّقوى وأهل المغفرةِ}؛ أي: هو أهل أن يُتَّقى ويُعبد؛ لأنَّه الإله الذي لا تنبغي العبادة إلاَّ له، وأهلٌ أن يَغْفِرَ لمن اتَّقاه واتَّبع رضاه.
{54 - 56} "Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!" Hapa, neno huu linawezekana kwamba linarejelea Sura hii au mawaidha yaliyomo ndani yake. "Basi anayetaka atakumbuka" kwa sababu ameshambainishia njia, na ushahidi ukamuwia wazi. "Na hawatakumbuka isipokuwa Mwenyezi Mungu atake." Kwani utashi wa Mwenyezi Mungu ni wenye kutekelezeka na ni wa jumla, na hakuna tukio dogo wala kubwa linaloweza kutoka nje yake. Katika hili kuna jibu dhidi ya Al-Qadariyya, ambao hawajumuishi vitendo vya waja chini ya utashi wa Mwenyezi Mungu, na pia Al-Jabriya wanaodai kuwa mja hana dhamira ya kweli au kitendo, lakini badala yake analazimishwa kufanya vitendo vyake. Kwa hivyo, hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu amethibitisha kwamba waja wana utashi na wanatenda kiuhakika, lakini akayafanya hayo kuwa chini ya utashi wake, na "Ucha Mungu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye." Yaani, Yeye ndiye anayestahiki kuogopwa na kuabudiwa. Kwa sababu Yeye ndiye Mungu ambaye haipasi kuabudu isipokuwa Yeye, na Yeye ndiye anayestahiki kupeana maghfira kwa wanaomcha na kufuata radhi zake.
Imekamilika (tafsiri yake) na sifa njema na neema ni zake Mwenyezi Mungu.
* * *