Tafsiri ya Surat Al-Muzzammil
Tafsiri ya Surat Al-Muzzammil
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{يَاأَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ (1) قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا (2) نِصْفَهُ أَوِ انْقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا (3) أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا (4) إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا (5) إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئًا وَأَقْوَمُ قِيلًا (6) إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا (7) وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا (8) رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا (9) وَاصْبِرْ عَلَى مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا (10) وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا (11)}.
1. Ewe uliyejifunika! 2. Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! 3. Nusu yake, au ipunguze kidogo. 4. Au izidishe - na soma Qur-ani kwa utaratibu na utungo. 5. Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito. 6. Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi. 7. Kwani hakika mchana una shughuli nyingi. 8. Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu. 9. Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipokuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako. 10. Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri. 11. Na niache Mimi na hao wanaokanusha, walioneemeka; na wape muhula kidogo!
#
{1 - 5} المزَّمِّل: المتغطي بثيابه كالمدَّثِّر، وهذا الوصف حصل من رسول الله - صلى الله عليه وسلم - حين أكرمه الله برسالته، وابتدأه بإنزال وحيه بإرسال جبريل إليه ، فرأى أمراً لم يَرَ مثلَه ولا يقدِرُ على الثَّبات عليه إلاَّ المرسلون، فاعتراه عند ذلك - انزعاجٌ، حين رأى جبريلَ عليه السلام، فأتى إلى أهله، فقال: «زمِّلوني زمِّلوني»، وهو ترعَدُ فرائصُه، ثم جاءه جبريلُ، فقال: اقرأ. فقال: «ما أنا بقارئٍ». فغطه حتَّى بلغ منه الجهدَ، وهو يعالجه على القراءة، فقرأ - صلى الله عليه وسلم -.
ثم ألقى الله عليه الثباتَ، وتابع عليه الوحيَ، حتى بَلَغَ مَبْلَغاً ما بَلَغَه أحدٌ من المرسلين؛ فسبحان الله ما أعظم التفاوت بين ابتداء نبوَّته ونهايتها! ولهذا خاطبه الله بهذا الوصف الذي وُجِدَ منه في أول أمره، فأمره هنا بالعباداتِ المتعلِّقة به، ثم أمره بالصبر على أذيَّة قومه ، ثم أمر بالصَّدْع بأمره وإعلان دعوتهم إلى الله، فأمره هنا بأشرف العبادات، وهي الصلاة، وبآكدِ الأوقات وأفضلها، وهو قيامُ الليل. ومن رحمته [تعالى] أنَّه لم يأمرْه بقيام الليل كلِّه، بل قال: {قم الليلَ إلاَّ قليلاً}. ثم قدَّر ذلك فقال: {نصفَه أو انقُصْ منه}؛ أي: من النصف {قليلاً}: بأن يكون الثلث ونحوه، {أو زِدْ عليه}؛ أي: على النصف، فيكون نحو الثلثين ، {ورتِّل القرآن ترتيلاً}؛ فإنَّ ترتيلَ القرآن به يحصُلُ التدبُّر والتفكُّر وتحريك القلوب به والتعبُّد بآياته والتهيُّؤ والاستعداد التامُّ له؛ فإنَّه قال: {إنَّا سنُلقي عليك قولاً ثقيلاً}؛ أي: نوحي إليك هذا القرآن الثقيل؛ أي: العظيمة معانيه، الجليلة أوصافه، وما كان بهذا الوصف حقيقٌ أن يُتَهَيَّأ له ويُرَتَّل ويُتَفَكَّر فيما يشتمل عليه.
{1 - 5} Al-Muzzammil ni mtu aliyejivika nguo yake akajigubika kwayo. Na maelezo haya yalimtokea Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - Mwenyezi Mungu alipomtukuza kwa kumtuma kama mtume, na akaanza kwa kumteremshea ufunuo wake kwa kumpelekea Jibril, na akaona kitu ambacho hakuwahi kukiona mfano wake, na hakuna anayeweza kusimama imara mbele yake isipokuwa Mitume tu. Basi akapatwa na mfadhaiko alipomuona Jibril, amani imshukie, kwa hivyo akaja kwa ahali zake,
akasema: 'Nifunikeni. Nifunikeni' huku akitetemeka viungo vyake.
Kisha Jibril akamjia na kusema: 'Soma.
' Akasema: 'Mimi siwezi kusoma.' Kwa hivyo akamfinya mpaka akamchosha mno, huku akimtaka kusoma. Basi yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akasoma. Kisha Mwenyezi Mungu akampa uthabiti na akaendelea kumteremshia ufunuo, mpaka akafikia kiwango ambacho hakuna hata mmoja katika Mitume aliyewahi kufika. Utakatifu ni wa Mwenyezi Mungu, ni jinsi gani hii ilivyo kubwa tofauti kati ya mwanzo wa unabii wake na mwisho wake! Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwongelesha kwa maelezo haya yaliyopatikana kutoka kwake mwanzoni mwa jambo lake. Basi akamuamuru hapa kufanya ibada zinazohusiana naye, kisha akamuamuru kuwa na subira katika kukabiliana na madhara kutoka kwa watu wake. Kisha akamuamuru kutangaza jambo hili na kulifanya hadharani katika kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu. Basi akamuamrisha hapa ibada yenye heshima kubwa zaidi, ambayo ni swala, na wakati wa uhakika na bora zaidi, ambao ni swala ya usiku. Na kutokana na rehema yake
[Mwenyezi Mungu] ni kwamba hakumuamrisha kuswali usiku mzima,
bali alisema: "Kesha usiku kucha, ila kidogo tu.
" Kisha akalikadiria hilo akasema: “Nusu yake, au ipunguze kidogo" ili iwe theluthi au mfano wake. "Au izidishe " hiyo nusu, ili karibia thuluthi mbili. "Na soma Qur-ani kwa utaratibu na utungo." Kwani kwa kusoma Qur-ani, yanapatikana mazingatio na tafakuri, na nyoyo husukumwa nayo, kufanya ibada kwa aya zake, na kujiandaa kikamilifu na kuwa tayari kwa ajili yake.
Kwani alisema: "Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito." Yaani, tutakuteremshia Qur-ani hii nzito. Yaani, yenye maana kubwa, maelezo matukufu. Na kile chenye maelezo haya kinastahiki zaidi mtu kujitayarisha kwa ajili yake, kusomwa sawasawa na kutafakariwa yale yaliyomo.
#
{6} ثم ذكر الحكمة في أمره بقيام الليل، فقال: {إنَّ ناشئةَ الليل}؛ أي: الصلاة فيه بعد النوم، {هي أشدُّ وطئاً وأقومُ قيلاً}؛ أي: أقرب إلى حصول مقصود القرآن؛ يتواطأ عليه القلب واللسان، وتقلُّ الشواغل، ويفهم ما يقول، ويستقيم له أمره.
{6} Kisha akataja hekima iliyo nyuma ya kumuamrisha kuswali Swala ya usiku,
akasema: "Hakika kuamka usiku;" yaani, kuswali humo baada ya kulala, "kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi." Yaani, ni karibu zaidi kufikia lengo la Qur-ani. Kwani moyo na ulimi vinakubaliana juu yake, wasiwasi hupungua, anaelewa anachosema na mambo yake yananyooka.
#
{7} وهذا بخلاف النهار؛ فإنَّه لا يحصلُ به هذه المقاصد ، ولهذا قال: {إنَّ لك في النهار سبحاً طويلاً}؛ أي: تردُّداً في حوائجك ومعاشك يوجبُ اشتغال القلب وعدم تفرُّغه التفرُّغ التامَّ.
{7} Hili ni tofauti na mchana. Kwani hayafikii humo malengo hayo.
Na ndiyo maana akasema: "Kwani hakika mchana una shughuli nyingi" katika kutafuta mahitaji yako ya maisha, ambayo yanasababisha moyo kujishughulisha sana na kutojitolea kikamilifu.
#
{8} {واذكرِ اسمَ ربِّك}: شاملٌ لأنواع الذِّكْر كلِّها، {وتَبَتَّلْ إليه تَبتيلاً}؛ أي: انقطع إليه ؛ فإنَّ الانقطاع إلى الله والإنابة إليه هو: الانفصالُ بالقلب عن الخلائق، والاتِّصاف بمحبَّة الله وما يقرِّب إليه ويدني من رضاه.
{8} "Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi." Hili linajumuisha kila aina ya utajo, "na ujitolee kwake kwa ukamilifu." Kwani kujitolea kwa Mwenyezi Mungu ni kujitenga kwa moyo mbali na viumbe, na kuwa na sifa ya upendo kwa Mwenyezi Mungu na kile kinachomleta mtu karibu naye na kuwa karibu na radhi zake.
#
{9} {رب المشرق والمغرب}: وهذا اسم جنس؛ يشمل المشارق والمغارب كلَّها؛ فهو تعالى ربُّ المشارق والمغارب، وما يكون فيها من الأنوار، وما هي مصلحةٌ له من العالم العلويِّ والسفليِّ؛ فهو ربُّ كلِّ شيءٍ وخالقُه ومدبِّره. {لا إله إلاَّ هو}؛ أي: لا معبود إلاَّ وجهه الأعلى، الذي يستحقُّ أن يُخَصَّ بالمحبَّة والتعظيم والإجلال والتكريم، ولهذا قال: {فاتَّخِذْه وكيلاً}؛ أي: حافظاً ومدبِّراً لأمورك كلِّها.
{9} "Mola Mlezi wa mashariki na magharibi" Hili linajumuisha Mashariki na Magharibi yote. Yeye, Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, na nuru zilizomo ndani yake, na chenye masilahi kwazo miongoni mwa ulimwengu wa juu na wa chini. Yeye ndiye Bwana, Muumba, na Mwendeshaji wa kila kitu. "Hapana mungu isipokuwa Yeye." Yaani, hapana wa kuabudiwa ila uso wake Yeye wa juu zaidi, anayestahiki kupendwa peke yake na kupewa tadhima, utukufu na heshima. Ndiyo maana akasema, "basi mfanye kuwa Mtegemewa wako" katika mambo yako yote.
#
{10} فلما أمره الله بالصَّلاة خصوصاً وبالذِّكر عموماً، وذلك يحصل للعبد مَلَكَةٌ قويةٌ في تحمُّل الأثقال وفعل المُشِقِّ من الأعمال؛ أمره بالصبر على ما يقوله المعاندون له ويسبُّونه ويسبُّون ما جاء به، وأن يمضِيَ على أمر الله؛ لا يصدُّه عنه صادٌّ ولا يردُّه رادٌّ، وأن يَهْجُرَهُم هجراً جميلاً، وهو الهجر حيث اقتضت المصلحةُ [الهجرَ]، الذي لا أذيَّة فيه، بل يعاملهم بالهجر والإعراض عن أقوالهم التي تؤذيه، وأمره بجدالهم بالتي هي أحسن.
{10} Mwenyezi Mungu alipomuamuru kuswali hasa na kumkumbuka kwa ujumla, na haya yanampa mja jukumu kubwa la kubeba mizigo na kufanya mambo magumu; akamuamuru kuwa na subira kwa yale yanayosemwa na wale wanaompinga na kumtukana yeye na aliyoyaleta, na kwamba aendelee na amri ya Mwenyezi Mungu. Hakuna atakayeweza kumuzuia mbali na hayo, na hakuna atakayeweza kumregesha, na kwamba awahame kwa njia nzuri, ambapo kuna masilahi ya kufanya hivyo ambapo hakuna madhara. Bali aamiliane nao kwa kuwahama kwa kuachana na maneno yao yanayomuudhi, na akamwamrisha kujadiliana nao kwa njia iliyo bora zaidi.
#
{11} {وذرني والمكذِّبينَ}؛ أي: اتركْني وإيَّاهم، فسأنتقم منهم، وإنْ أمْهَلْتُهم؛ فلا أهمِلُهم. وقوله: {أولي النَّعْمةِ}؛ أي: أصحاب النَّعمة والغنى، الذين طَغَوْا حين وسَّع الله عليهم من رزقه وأمدَّهم من فضله؛ كما قال تعالى: {كلاَّ إنَّ الإنسانَ لَيَطْغى. أن رآه استَغْنى}.
{11} "Na niache Mimi na hao wanao kanusha" Kwani nitalipiza kisasi kwao, hata nikiwapa muhula. Sitawapuuzea.
Na kauli yake: "walioneemeka" kwa neema mbalimbali na utajiri. Wale ambao walivuka mipaka pale Mwenyezi Mungu alipowapanulia riziki yake na kuwaruzuku katika fadhila zake.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwani, hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri. Akijiona katajirika."
Kisha akawatishia kwa adhabu yake, akasema:
{إِنَّ لَدَيْنَا أَنْكَالًا وَجَحِيمًا (12) وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا (13) يَوْمَ تَرْجُفُ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبًا مَهِيلًا (14)}.
12. Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unaowaka kwa ukali kabisa! 13. Na chakula kinachokwama kooni, na adhabu inayoumiza. 14. Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga!
#
{12 - 13} أي: إنَّ عندنا {أنكالاً}؛ أي: عذاباً شديداً جعلناه تنكيلاً للذي لا يزال مستمرًّا على ما يغضِبُ الله، {وجحيماً}؛ أي: ناراً حامية، {وطعاماً ذا غُصَّةٍ} وذلك لمرارته وبشاعته وكراهة طعمه وريحه الخبيث المنتن، {وعذاباً أليماً}؛ أي: موجعاً مفظعاً.
{12 - 13} Yaani, tuna "pingu nzito" tulizoziweka ili kumuadhibu yule anayeendelea kufanya yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu. "Na Moto wa Jahannamu" unaowaka kwa ukali kabisa "Na chakula kinachokwama kooni" kwa sababu ya uchungu wake, na uchukizo wake, na ubaya wa ladha yake, na harufu mbaya iliyooza "na adhabu inayoumiza."
#
{14} وذلك {يوم ترجُفُ الأرضُ والجبالُ}: من الهول العظيم، فكانتِ {الجبالُ}: الراسياتُ الصمُّ الصلابُ {كثيباً مَهيلاً}؛ أي: بمنزلة الرمل المنهال المنتثر، ثم إنها تُبَسُّ بعد ذلك فتكون كالهباء المنثور.
{14} Na hiyo ndiyo "Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia" kutokana na mahangaiko makubwa, na "milima" iliyo dhabiti, iliyo ngumu "itakuwa kama tifutifu la mchanga!" Kisha itasagwasagwa iwe mavumbi yaliyotawanyika.
{إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَى فِرْعَوْنَ رَسُولًا (15) فَعَصَى فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا (16)}.
15. Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyomtuma Mtume kwa Firauni. 16. Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso.
#
{15 - 16} يقول تعالى: احْمَدوا ربَّكم على إرسال هذا النبيِّ الأميِّ العربيِّ البشير النذير الشاهد على الأمَّة بأعمالهم، واشكروه، وقوموا بهذه النِّعمة الجليلة، وإيَّاكم أن تَكْفُروا، فتَعْصوا رسولكم، فتكونوا كفرعون حين أرسل الله إليه موسى بن عمران، فدعاه إلى الله، وأمره بالتَّوحيد، فلم يصدِّقْه، بل عصاه، فأخذه الله {أخذاً وبيلاً}؛ أي: شديداً بليغاً.
{15 - 16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mshukuruni Mola wenu Mlezi kwa kumtuma Nabii huyu Mwarabu asiyejua kusoma na kuandika, mleta bishara njema na mwonyaji, shahidi kwa umma huu kwa matendo yao, na mshukuruni, na timizeni neema hii kubwa, na tahadharini na kukufuru na kumuasi Mtume wenu, mkawa kama Firauni pale Mwenyezi Mungu alipomtuma kwake Musa bin Imran, akamlingania kwa Mwenyezi Mungu, na akamuamrisha kumpwekesha, lakini hakumsadiki. Bali akamuasi, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamshika "mshiko wa mateso" makali zaidi.
{فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِنْ كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ الْوِلْدَانَ شِيبًا (17) السَّمَاءُ مُنْفَطِرٌ بِهِ كَانَ وَعْدُهُ مَفْعُولًا (18)}.
17. Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi? 18. Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.
#
{17 - 18} أي: فكيف يحصلُ لكم الفكاكُ والنَّجاة يومَ القيامةِ، اليوم المَهيل أمرُه، العظيمُ خطرُه ، الذي يشيِّبُ الولدان وتذوبُ له الجمادات العظام؛ فتنفطر السماء وتنتثر نجومُها. {كان وعدُه مفعولاً}؛ أي: لا بدَّ من وقوعه ولا حائل دونه.
{17 - 18} Maana yake ni kwamba vipi mtapata kujiepusha na kuokoka Siku ya Kiyama, siku ambayo mambo yake ni ya kutisha, ambayo hatari yake ni kubwa, ambayo itawafanya watoto kuwa na mvi, na kuvifanya vikubwa visivyo na uhai kuyeyuka? Ambapo mbingu zitapasuka na nyota zake kutawanyika. "Ahadi yake itakuwa imetekelezwa" na hakuna kitakachoweza kulizuia hilo.
{إِنَّ هَذِهِ تَذْكِرَةٌ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَى رَبِّهِ سَبِيلًا (19)}.
19. Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi.
#
{19} أي: إنَّ هذه الموعظة التي نبَّأ الله بها من أحوال يوم القيامةِ وأهوالها تذكرةٌ يتذكَّر بها المتَّقون وينزجر بها المؤمنون. {فمن شاءَ اتَّخذ إلى ربِّه سبيلاً}؛ أي: طريقاً موصلاً إليه، وذلك باتِّباع شرعه؛ فإنَّه قد أبانه كلَّ البيان وأوضحه غاية الإيضاح، وفي هذا دليلٌ على أنَّ الله تعالى أقْدَرَ العبادَ على أفعالهم ومكَّنَهم منها، لا كما يقوله الجبريَّةُ: إنَّ أفعالهم تقع بغير مشيئتهم؛ فإنَّ هذا خلاف النقل والعقل.
{19} Yaani, mawaidha haya aliyotoa habari zake Mwenyezi Mungu kuhusu hali na mahangaiko ya Siku ya Kiyama ni ukumbusho ambao kwa huo wacha Mungu watakumbushwa na kwa huo watakemeka waumini. "Basi mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi." Na hilo ni kwa kufuata sheria yake. Kwani ameibainisha sawasawa na kuiweka wazi kabisa, na huu ni ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa uwezo waja wake kufanya vitendo vyao na kuwawezesha kuvifanya, si kama wanavyosema Al-Jabriya kwamba vitendo vyao vinatokea bila ya kutaka kwao. Hili ni kinyume na maandiko na hata akili timamu.
{إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَى مِنْ ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِنَ الَّذِينَ مَعَكَ وَاللَّهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ عَلِمَ أَنْ لَنْ تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ عَلِمَ أَنْ سَيَكُونُ مِنْكُمْ مَرْضَى وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِنْ فَضْلِ اللَّهِ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنْفُسِكُمْ مِنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِنْدَ اللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا وَاسْتَغْفِرُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (20)}.
20. Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur-ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
#
{20} ذكر الله في أول هذه السورة أنَّه أمر رسولَه بقيام نصفِ الليل أو ثلثيه أو ثلثه ، والأصلُ أنَّ أمته أسوةٌ له في الأحكام، وذكر في هذا الموضع أنَّه امتثل ذلك هو وطائفةٌ معه من المؤمنين. ولما كان تحرير الوقت المأمور به مشقَّة على الناس؛ أخبر أنَّه سهَّل عليهم في ذلك غاية التسهيل؛ فقال: {والله يقدِّرُ الليلَ والنهارَ}؛ أي: يعلم مقاديرهما وما يمضي ويبقى منهما ، {علم أن لن تُحصوه}؛ أي: لن تعرِفوا مقداره من غير زيادةٍ ولا نقصٍ؛ لكون ذلك يستدعي انتباهاً وعناءً زائداً؛ أي: فخفَّف عنكم وأمركم بما تيسَّر عليكم سواء زاد على المقدَّر أو نَقَصَ، {فاقرؤوا ما تيسَّرَ من القرآن}؛ أي: ممَّا تعرفون ولا يشقُّ عليكم، ولهذا كان المصلِّي بالليل مأموراً بالصلاة ما دام نشيطاً؛ فإذا فَتَرَ أو كسل أو نعس؛ فليسترحْ ليأتيَ الصلاةَ بطمأنينةٍ وراحةٍ.
ثم ذكر بعضَ الأسباب المناسبة للتخفيف، فقال: {علم أن سيكونُ منكم مرضى}: يشقُّ عليهم صلاة نصف الليل أو ثلثيه أو ثلثه، فليصلِّ المريض ما يسهُلُ عليه، ولا يكون أيضاً مأموراً بالصَّلاة قائماً عند مشَّقة ذلك، بل لو شقَّت عليه الصلاةُ النافلةُ؛ فله تركُها، وله أجرُ ما كان يعمل صحيحاً. {وآخرون يضرِبون في الأرض يبتغونَ من فضل الله}؛ أي: وعلم أنَّ منكم مسافرين يسافرون للتجارة؛ ليستغنوا عن الخلق، ويتكفَّفوا عنهم ؛ أي: فالمسافر حالُهُ تناسِبُ التخفيف، ولهذا خفَّف عنه في صلاة الفرض، فأبيح له جمعُ الصلاتين في وقتٍ واحدٍ وقصرُ الصَّلاة الرُّباعية. وكذلك {آخرون يقاتِلون في سبيل اللهِ فاقرؤوا ما تيسَّرَ منه}: فذكر تعالى تخفيفين؛ تحفيفاً للصحيح المقيم يراعي فيه نشاطه من غير أن يُكَلَّفَ عليه تحرير الوقت، بل يتحرَّى الصلاة الفاضلة، وهي ثلث الليل بعد نصفه الأول، وتخفيفاً للمريض والمسافر، سواء كان سفرُه للتجارة أو لعبادةٍ من جهادٍ أو حجٍّ أو غيره ؛ فإنَّه [أيضاً] يراعي ما لا يكلِّفه؛ فلله الحمد والثناء؛ حيث لم يجعلْ علينا في الدين من حرج، بل سهَّل شرعه، وراعى أحوال عباده ومصالح دينهم وأبدانهم ودنياهم.
ثم أمر العباد بعبادتين هما أمُّ العبادات وعمادُها: إقامة الصلاة التي لا يستقيمُ الدين إلاَّ بها، وإيتاءُ الزَّكاة التي هي برهانُ الإيمان وبها تحصُلُ المواساة للفقراء والمساكين، فقال: {وأقيموا الصلاة}؛ أي: بأركانها وحدودها وشروطها وجميع مكمِّلاتها ، {وأقرِضوا الله قرضاً حسناً}؛ أي: خالصاً لوجه الله بنيَّة صادقةٍ وتثبيتٍ من النفس ومال طيِّبٍ، ويدخُلُ في هذا الصدقة الواجبة والمستحبَّة.
ثم حثَّ على عموم الخير وأفعاله، فقال: {وما تقدِّموا لأنفسكم من خيرٍ تجِدوه عند الله هو خيراً وأعظم أجراً}: الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائةِ ضعفٍ إلى أضعافٍ كثيرة. وليعلمْ أنَّ مثقال ذرَّةٍ في هذه الدار من الخير يقابله أضعافُ أضعافِ الدُّنيا وما عليها في دار النعيم المقيم من اللذَّات والشَّهوات، وأنَّ الخير والبرَّ في هذه الدنيا مادةُ الخير والبرِّ في دار القرار وبذرُه وأصلُه وأساسُه. فوا أسفاه على أوقاتٍ مضت في الغفلات! ووا حسرتاه على أزمانٍ تقضَّت في غير الأعمال الصالحات! ووا غوثاه من قلوبٍ لم يؤثِّرْ فيها وعظُ بارئها ولم ينجَعْ فيها تشويق من هو أرحم بها من نفسها! فلك اللهم الحمدُ وإليك المشتكى وبك المستغاث ولا حول ولا قوَّة إلاَّ بك.
{واستغفروا الله إنَّ الله غفورٌ رحيمٌ}: وفي الأمر بالاستغفار بعد الحثِّ على أفعال الطاعة والخير فائدةٌ كبيرةٌ، وذلك أنَّ العبد لا يخلو من التقصير فيما أُمِرَ به: إما أنْ لا يفعلَه أصلاً، أو يفعله على وجهٍ ناقصٍ، فأُمِرَ بترقيع ذلك بالاستغفار؛ فإنَّ العبد يذنِبُ آناء الليل والنهار؛ فمتى لم يتغمَّدْه الله برحمته ومغفرته؛ فإنَّه هالكٌ.
{20} Mwenyezi Mungu alitaja mwanzoni mwa Sura hii kwamba alimuamuru Mtume wake kuswali usiku wa manane, thuluthi mbili yake, au thuluthi moja yake, na kanuni ya msingi ni kwamba umma wake wanapaswa kumfuata katika hukumu zote. Na alitaja mahali hapa kwamba yeye na kundi la waumini walitekeleza hilo. Na kwa kuwa kuainisha muda unaotakiwa hapa ni taabu kwa watu,
alijulisha kwamba aliwafanyia rahisi sana katika hilo; akasema: "Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana." Yaani, anajua kiasi chake na kinachopita na kinachobakia katika viwili hivyo. "Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu" bila kuongezeka au kupungua. Kwa sababu hilo linahitaji kuwa macho na kufanya jitihada za ziada. Kwa hivyo, akakufanyieni wepesi na akakuamrisheni kufanya yale yaliyo mepesi kwenu, sawa iwe ni zaidi ya yale yaliyoamrishwa au kidogo kuliko yaliyoamrishwa, "basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur-ani" katika yale mnavyojua na ambavyo si vigumu kwenu. Na ndiyo maana akaamrishwa mwenye kuswali usiku kuswali maadamu bado ana ukakamavu. Lakini anapochoka au akaona uvivu au usingizi, basi na apumzike ili aijie swala kwa utulivu huku amepumzika. Kisha akataja baadhi ya sababu zinazofaa kupunguza huko,
akasema: "Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa" ambao itakuwa vigumu kwao kuswali nusu ya usiku, au thuluthi mbili yake au thuluthi moja yake. Basi mgonjwa na aswali lililo jepesi kwake, na pia haamrishwi kuswali hali ya kuwa amesimama pale jambo hili linakuwa gumu kwake. Bali hata ikiwa ni vigumu kwake kuswali swala ya hiyari, basi ana haki ya kuiacha, na atapata thawabu kama alivyokuwa akifanya huku akiwa sahihi. "Na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu." Yaani, alijua kwamba wako wasafiri miongoni mwenu wanaosafiri kwa ajili ya biashara, ili wajitosheleze mbali na viumbe, na kujizuia mbali nao. Kwa hivyo, hali ya msafiri inafailia afanyiwe wepesi, na ndiyo maana amefanyiwa wepesi katika swala ya faradhi kwa ruhusiwa kuunganisha swala mbili kwa wakati mmoja na kufupisha swala za rakaa nne. Vile vile "wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo." Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja wepesishaji mara mbili. Wepesishaji kwa ajili ya mtu aliye sahihi asiyekuwa safarini. Huyo anapaswa kuzingatia ukakamavu wake bila ya kumtwisha mzigo wa kuswali muda mrefu. Bali atajitahidi kuswali swala bora zaidi, ambayo ni thuluthi ya usiku baada ya nusu ya kwanza ya usiku. Na wepesishaji kwa ajili ya mgonjwa na msafiri, iwe safari yake iwe ni kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya ibada, kama vile jihadi, Hija, au kitu kingine. Yeye
[pia] na azingatie kile ambacho hakimpi mzigo mzito. Basi sifa njema ni za Mwenyezi Mungu na kutajwa kwa uzuri. Kwani hakutuwekea ugumu wowote katika dini, bali aliifanya sheria yake kuwa nyepesi, na akazingatia hali za waja wake na masilahi ya dini yao, miili yao na dunia yao. Kisha akawaamrisha waja kufanya ibada mbili,
nazo ndizo mama za ibada zote na nguzo zake: kusimamisha swala ambayo bila ya hiyo dini hainyooki, na kutoa zaka ambayo ni ushahidi wa imani na kwayo faraja inapatikana kwa masikini na mafukara.
Akasema: "na mshike Sala" kwa nguzo zake, na mipaka yake, na masharti yake, na vyote vinavyoikamilisha. "Na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema." Yaani, ambao umekusudiwa kwa huo uso wa Mwenyezi Mungu peke yake, kwa nia ya ukweli, na kuzipa nguvu roho, na mali nzuri, na hili linajumuisha sadaka ya faradhi na ile inayopendekezwa. Kisha akahimiza kufanya heri kwa ujumla na vitendo vyake,
akasema: "Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana," jema moja kwa mara kumi mfano wake hadi mizidisho mia saba, hadi mizidisho mara nyingi. Na ajue kwamba uzito wa chembe wa wema katika makazi haya unalingana mizidisho mara nyingi ya dunia hii na vilivyomo katika nyumba ya neema ya milele miongoni mwa starehe na matamanio, na kwamba heri na wema katika dunia hii ndiyo kiini cha heri na wema katika nyumba ya daima, mbegu yake, asili yake na msingi wake. Basi ninasikitika sana juu ya nyakati zilizopita katika hali ya kughafilika! Na lo, ni majuto yaliyoje kwa nyakati zilizotumiwa katika mambo mengine yasiyo ya matendo mema! Na lo, ni majuto yaliyoje kwa mioyo ambayo mawaidha ya Muumba wao hayakuwa na athari yoyote ndani yake, na ambayo hamu ya Yule aliye na huruma zaidi kwao hata kuliko nafsi zao wenyewe haikuwaingia! Basi ewe Mwenyezi Mungu ni zako sifa njema, na ni kwako ndiko pa kulalamikia, na wewe ndiye unayeombwa msaada, na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwako. "Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu." Kuna faida kubwa katika kuamrisha kuomba msamaha baada ya kuhimiza vitendo vya utiifu na wema,
na hilo ni kuwa mja hakosi kuwa na mapungufu katika yale aliyoamrishwa kuyafanya: Ima kwa kutoyafanya kabisa, au kayafanya kwa njia pungufu. Kwa hivyo akaamrishwa kurekebisha hayo kwa kuomba msamaha. Kwani mja anatenda madhambi nyakati za mchana na usiku. Na Mwenyezi Mungu asipomfunika kwa rehema na msamaha wake, basi atakuwa ameangamia.
Imekamilika tafsiri yake, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *