:
Tafsiri ya Surat Al-Qiyama
Tafsiri ya Surat Al-Qiyama
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 6 #
{لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ (1) وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ (2) أَيَحْسَبُ الْإِنْسَانُ أَلَّنْ نَجْمَعَ عِظَامَهُ (3) بَلَى قَادِرِينَ عَلَى أَنْ نُسَوِّيَ بَنَانَهُ (4) بَلْ يُرِيدُ الْإِنْسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ (5) يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ (6)}.
1. Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! 2. Na ninaapa kwa nafsi inayojilaumu! 3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? 4. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! 5. Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilizoko mbele yake. 6. Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
#
{1} ليست {لا} ها هنا نافية ولا زائدة، وإنَّما أتي بها للاستفتاح والاهتمام بما بعدها، ولكثرة الإتيان بها مع اليمين لا يستغرب الاستفتاح بها، وإن لم تكن في الأصل موضوعة للاستفتاح؛ فالمقسم به في هذا الموضع هو المقسَم عليه، وهو البعث بعد الموت، وقيام الناس من قبورهم، ثم وقوفهم ينتظرون ما يَحْكُمُ به الربُّ عليهم.
{1} Hapa, neno 'laa' si la kukanusha wala la kusisitiza. Bali lilitumika kama ufunguzi na kuonyesha umuhimu mkubwa wa yale yanayokuja baada yake. Na kutokana na kutokea kwake mara kwa mara katika kiapo, si ajabu kwamba likitumika kama kifunguzi, hata kama katika asili yake halikukusudiwa kama kifunguzi. Kilichotumiwa kuapa hapa ni kile kile kilichoapwa kwa sababu yake, ambacho ni kufufuliwa baada ya kufa, na watu kutoka makaburini mwao, kisha kusimama na kungoja kile atakachowahukumu Mola wao Mlezi kuhusiana nao.
#
{2} {ولا أقسم بالنَّفس اللَّوَّامةِ}: وهي جميع النفوس الخيِّرة والفاجرة، سميِّت لوَّامةً لكثرة تلوُّنها وتردُّدها وعدم ثبوتها على حالةٍ من أحوالها، ولأنَّها عند الموت تلوم صاحبها على ما فعلت ، بل نفسُ المؤمن تلومُ صاحبها في الدُّنيا على ما حصل منه من تفريطٍ أو تقصيرٍ في حقٍّ من الحقوق أو غفلةٍ، فجمع بين الإقسام بالجزاء وعلى الجزاء وبين مستحقِّ الجزاء.
{2} "Na ninaapa kwa nafsi inayojilaumu!" Ni nafsi zote nzuri na zisizo nzuri, iliitwa kwamba ni yenye kujilaumu kwa sababu ya rangi zake nyingi, kusitasita kwake, na kutotulia kwake katika hali yoyote miongoni mwa hali zake, na kwa sababu wakati wa kifo, inamlaumu mwenyewe kwa yale aliyoyafanya. Bali nafsi ya Muumini inamlaumu mwenyewe katika dunia juu ya yale aliyozembea katika haki miongoni mwa haki au kughafilika kwake. Kwa hivyo akaunganisha kati ya kuapa kwa malipo na kati ya yule anayestahili malipo hayo.
#
{3 - 4} ثم أخبر مع هذا أنَّ بعض المعاندين يكذِّبون بيوم القيامة، فقال: {أيحسبُ الإنسانُ أن لن نَجْمَعَ عظامَه}: بعد الموت؛ كما قال [في الآية الأخرى]: {قال مَن يُحيي العظامَ وهي رميمٌ}، فاستبعد من جهله وعدوانه قدرةَ الله على خلق عظامه التي هي عمادُ البدن، فردَّ عليه بقوله: {بلى قادرينَ على أن نُسَوِّيَ بَنانَه}؛ أي: أطراف أصابعه وعظامه، وذلك مستلزمٌ لخلق جميع أجزاء البدن؛ لأنَّها إذا وُجِدت الأنامل والبنان؛ فقد تمَّتْ خلقة الجسد.
{3 - 4} Kisha akajulisha pamoja na haya ya kwamba baadhi ya watu wakaidi wanaikadhibisha Siku ya Kiyama, akasema: "Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake" baada ya kifo? Kama alivyosema [katika Aya nyingine]: "Akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwishamung'unyika?" Basi mtu huyu kutokana na ujinga wake na kuvuka kwake mipaka akaona kwamba hauwezi uwezo wa Mwenyezi Mungu kuumba mifupa yake ambayo ni nguzo za mwili, naye akamjibu kwa kusema: "Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!" Na hilo linalazimu kwamba ataumba viungo vyote vya mwili. Kwa sababu ikiwa vitapatikana vidole na ncha zake, basi umbile la mwili wote litakuwa limeshatimia.
#
{5 - 6} وليس إنكارُه لقدرة الله تعالى قصوراً بالدَّليل الدَّالِّ على ذلك، وإنَّما وقع ذلك منه لأنَّ إرادته وقصده التكذيبُ بما أمامه من البعث. والفجور: الكذب مع التعمُّد.
{5 - 6} Kukanusha kwake uwezo wa Mwenyezi Mungu si kutokana na upungufu ulio katika ushahidi unaoonyesha hilo. Bali jambo hili lilitokea kwa upande wake kwa sababu utashi wake na makusudio yake yalikuwa ni kukadhibisha ufufuo ulio mbele yake.
Kisha akataja hali za Kiyama na akasema:
: 7 - 15 #
{فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ (7) وَخَسَفَ الْقَمَرُ (8) وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ (9) يَقُولُ الْإِنْسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ (10) كَلَّا لَا وَزَرَ (11) إِلَى رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ (12) يُنَبَّأُ الْإِنْسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ (13) بَلِ الْإِنْسَانُ عَلَى نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ (14) وَلَوْ أَلْقَى مَعَاذِيرَهُ (15)}.
7. Basi jicho litakapodawaa, 8. Na mwezi utakapopatwa, 9. Na likakusanywa jua na mwezi, 10. Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? 11. La! Hapana pa kukimbilia! 12. Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. 13. Siku hiyo ataambiwa aliyoyatanguliza na aliyoyaakhirisha. 14. Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. 15. Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
#
{7 - 10} أي: {فإذا} كانت القيامة؛ برقت الأبصار من الهول العظيم وشخصت فلا تطرف؛ كما قال تعالى: {إنَّما يؤخِّرُهم ليومٍ تَشْخَصُ فيه الأبصارُ. مهطِعين مُقْنِعي رؤوسهم لا يرتدُّ إليهم طرفُهم وأفئِدَتُهم هواءٌ}، {وخسف القمر}؛ أي: ذهب نورُه وسُلطانه، {وجُمِعَ الشمسُ والقمرُ}: وهما لم يجتمعا منذ خلقهما الله تعالى، فيجمع الله بينهما يوم القيامةِ، ويُخسف القمر، وتكوَّر الشمس، ثم يقذفان في النار؛ ليرى العباد أنَّهما عبدان مسخَّران، وليرى مَنْ عَبَدَهما أنَّهم كانوا كاذبين، {يقول الإنسانُ}: حين يرى تلك القلاقل المزعجات: {أين المفرُّ}؛ أي: أين الخلاص والفكاك ممَّا طرقنا وألمَّ بنا ؟
{7 - 10} Yaani, "itakapofika siku ya Kiyama" na jicho litakapodawaa kutokana na mahangaiko makubwa na yakakodoka akashindwa hata kupepesa, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapokodoka macho yao. Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu." Kisha akasema "Na mwezi utakapopatwa." Yaani, nuru yake na mamlaka yake yatakapotoweka. "Na likakusanywa jua na mwezi" na viwili hivi havikuwahi kukusanyika pamoja tangu vilipoumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi Mwenyezi Mungu atavikusanya Siku ya Kiyama, na hapo mwezi utapatwa, na jua litakunjwa, kisha vitatupwa Motoni; ili waja waone kuwa viwili hivyo pia ni waja tu waliotiishwa chini ya amri ya Mwenyezi Mungu, na ili wale waliokuwa wakiviabudu waone kuwa walikuwa waongo. "Siku hiyo mtu atasema" atakapoona wasiwasi hizi na masumbuko haya "yako wapi makimbilio" la kuepukana na haya yaliyotufika na kutuzingira?
#
{11 - 13} {كلاَّ لا وَزَرَ}؛ أي: لا ملجأ لأحدٍ دون الله، {إلى ربِّكَ يومئذٍ المستقرُّ}: لسائر العباد، فليس في إمكان أحدٍ أن يستترَ أو يهرب عن ذلك الموضع، بل لا بدَّ من إيقافه؛ ليجزى بعمله، ولهذا قال: {يُنَبَّأ الإنسانُ يومئذٍ بما قَدَّمَ وأخَّرَ}؛ أي: بجميع عمله الحسن والسيئ، في أول وقته وآخره، وينبَّأ بخبرٍ لا ينكِرُه.
{11 - 13} "La! Hapana pa kukimbilia" pasipo kwa Mwenyezi Mungu. "Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu" kwa waja wote, na haitawezekana kwa yeyote kujificha au kutoroka akapakwepa mahali hapo. Bali lazima atasimama hapo ili apate kulipwa kwa matendo yake, na ndiyo maana akasema: “Siku hiyo ataambiwa aliyoyatanguliza na aliyoyaakhirisha." Yaani, ataulizwa juu ya mema yake na mabaya yake yote, mwanzoni mwa zama zake na mwisho wake, na ataambiwa habari ambazo hataweza kuzikanusha.
#
{14 - 15} {بل الإنسانُ على نفسِهِ بصيرةٌ}؛ أي: شاهدٌ ومحاسبٌ، {ولو ألقى معاذيرَةُ}: فإنَّها معاذيرُ لا تُقبل، بل يقرَّر بعمله ، فَيُقِرُّ به؛ كما قال تعالى: {اقرأ كتابَكَ كفى بنفسِكَ اليوم عليك حَسيباً}: فالعبدُ وإن أنكر أو اعتذر عمَّا عمله؛ فإنكارُه واعتذارُه لا يفيدانه شيئاً؛ لأنَّه يشهد عليه سمعُه وبصره وجميعُ جوارحه بما كان يعمل، ولأنَّ استعتابه قد ذهب وقتُه وزال نفعُه، {فيومئذٍ لا ينفعُ الذين ظلموا معذِرَتُهم ولا هم يُسْتَعْتَبونَ}.
{14 - 15} "Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake." Yaani, ni shahidi na ataweza kujifanyia mahesabu ya matendo yake. "Na ingawa atatoa chungu ya udhuru." Kwani ni udhuru usiokubaliwa, bali atafanywa kukiri matendo yake, naye atayakiri. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu." Basi mja hata akikataa au akaleta udhuru juu ya yale aliyoyafanya, kukanusha kwake huko na kuleta kwake udhuru havitamfaa kitu chochote. Kwa sababu kusikia kwake, kuona kwake, na viungo vyake vyote vitashuhudia dhidi yake juu ya yale aliyokuwa akiyafanya, na kwa sababu wakati wake wa kuomba msamaha ulishapita, na hata manufaa yake yakaisha. "Basi Siku hiyo hautawafaa wale waliodhulumu udhuru wao, wala haitatakiwa toba yao."
: 16 - 19 #
{لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ (16) إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ (17) فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ (18) ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ (19)}.
16. Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. 17. Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. 18. Tunapousoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. 19. Kisha ni juu yetu kuubainisha.
#
{16 - 19} كان النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - إذا جاءه جبريلُ بالوحي وشرع في تلاوته [عليه]؛ بادَرَهُ النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - من الحرص قبل أن يفرغ، وتلاه مع تلاوة جبريل إيَّاه ، فنهاه الله عن ذلك، وقال: {ولا تعجل بالقرآن من قبل أن يقضى إليك وحيه}: وقال هنا: {لا تُحرِّكَ به لسَانَكَ لِتَعْجَلَ به}. ثم ضمن له تعالى أنَّه لا بدَّ أن يحفظَه ويقرأه ويجمعه الله في صدره، فقال: {إنَّ علينا جمعَه وقرآنَه}؛ فالحرص الذي في خاطرك إنَّما الداعي له حذر الفوات والنسيان؛ فإذا ضَمِنَه الله لك؛ فلا موجب لذلك، {فإذا قَرَأناه فاتَّبِعْ قرآنه}؛ أي: إذا أكمل جبريلُ ما يوحى إليك ؛ فحينئذٍ اتَّبع ما قرأه فاقرأه ، {ثمَّ إنَّ علينا بيانه}؛ أي: بيان معانيه. فوعده بحفظ لفظه وحفظ معانيه، وهذا أعلى ما يكون، فامتثل - صلى الله عليه وسلم - لأدب ربِّه، فكان إذا تلا عليه جبريلُ القرآن بعد هذا؛ أنصتَ له؛ فإذا فرغ؛ قرأه. وفي هذه الآية أدبٌ لأخذ العلم: أن لا يبادر المتعلِّم للعلم قبل أن يفرغ المعلِّم من المسألة التي شرع فيها؛ فإذا فرغ منها؛ سأله عمَّا أشكل عليه. وكذلك إذا كان في أول الكلام ما يوجب الردَّ أو الاستحسان أن لا يبادِرَ بردِّه أو قَبوله قبل الفراغ من ذلك الكلام؛ ليتبيَّن ما فيه من حقٍّ أو باطل، وليفهمه فهماً يتمكَّن فيه من الكلام فيه على وجه الصواب. وفيها أنَّ النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - كما بيَّن للأمَّة ألفاظ الوحي؛ فإنَّه قد بيَّن لهم معانيه.
{16 - 19} Alikuwa Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - Jibril anapomjia na ufunuo, anaanza kumsomea, Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – anaanza kumfuata haraka katika kisomo kwa sababu ya hamu kubwa juu ya hilo kabla hajaumaliza, na akausoma sawia na kuusoma kwa Jibril. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamkataza kufanya hivyo, na akasema: "Wala usiifanyie haraka hii Qur-ani, kabla haujamalizika ufunuo wake." Na hapa akasema "Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka." Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akamhakikishia kwamba ni lazima ataihifadhi, ataisoma, na Mwenyezi Mungu ataikusanya kifuani mwake, kwa hivyo akasema: "Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha." Basi hamu kubwa iliyoko katika akili yako inasukumwa tu na hofu ya kuikosa na kuisahau. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akikuhakikishia kuwa hautaishau, basi hakuna sababu wewe kufanya hivyo. "Basi tunapousoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake." Yaani, Jibril akikamilisha unayofunuliwa, basi hapo fuata aliyoyasoma na uyasome. "Kisha ni juu yetu kuubainisha." Yaani, kueleza maana zake. Basi akamuahidi kuyahifadhi maneno yake na kuhifadhi maana zake, na hili ndilo jambo la juu kabisa. Kwa hivyo Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie – akatekeleza adabu aliyofunzwa na Mola wake Mlezi, na akawa Jibril anapomsomea Qur-ani, baada ya haya, anamsikiliza kwa utulivu, na anapomaliza, anaisoma. Katika aya hii, kuna adabu za kupata elimu, nazo ni kwamba mwanafunzi asiharakishe kutafuta elimu kabla mwalimu hajamaliza jambo alilolianzisha. Akimaliza, basi mwanafunzi anaruhusiwa kumuuliza shida aliyo nayo. Vile vile, ikiwa kuna jambo mwanzoni mwa maneno ambalo linalazimu jibu, asiharakishe kulijibu au kulikubali kabla ya kumaliza maneno hayo. Ili ibainike haki na batili iliyoko ndani yake, na ili ayaelewe kuelewa kwa njia inayomwezesha kuzungumza juu yake kwa usahihi. Na ndani yake pia kuna kwamba Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kama alivyouelezea umma wake maneno ya ufunuo, pia aliwaeleza maana zake.
: 20 - 25 #
{كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ (20) وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ (21) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَاضِرَةٌ (22) إِلَى رَبِّهَا نَاظِرَةٌ (23) وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ (24) تَظُنُّ أَنْ يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ (25)}
20. Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani. 21. Na mnaacha maisha ya Akhera. 22. Zipo nyuso siku hiyo zitazong'ara. 23. Zinamwangallia Mola wao Mlezi. 24. Na zipo nyuso siku hiyo zitakazokunjana. 25. Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
#
{20 - 21} أي: هذا الذي أوجب لكم الغفلة والإعراض عن وعظ الله وتذكيره أنَّكم {تحبُّونَ العاجلةَ}، وتسعون فيما يحصِّلها وفي لذَّاتها وشهواتها، وتؤثرونها على الآخرة، فتذرون العمل لها؛ لأنَّ الدُّنيا نعيمها ولذاتها عاجلة، والإنسان مولعٌ بحبِّ العاجل، والآخرة متأخِّر ما فيها من النعيم المقيم؛ فلذلك غفلتم عنها وتركتُموها كأنَّكم لم تُخلقوا لها وكأنَّ هذه الدار هي دار القرار التي تُبْذَلُ فيها نفائس الأعمار ويُسعى لها آناء الليل والنهار، وبهذا انقلبت عليكم الحقيقة، وحصل من الخسار ما حصل؛ فلو آثرتُم الآخرة على الدُّنيا ونظرتم العواقب نظر البصير العاقل؛ لأنجحتم وربحتم ربحاً لا خسار معه، وفزتم فوزاً لا شقاء يصحبه.
{20 - 21} Yaani, haya ndiyo yaliwasababishia kughafilika na kujiepusha na mawaidha na ukumbusho wa Mwenyezi Mungu ya kwamba, "nyinyi mnapenda maisha ya duniani" na mnayafanyia bidii ya kutafuta yale yanayopatikana humo na starehe zake na matamanio yake, na kuyapendelea zaidi ya Akhera, na mnaacha kuifanyia Akhera kazi. Kwa sababu neema ya dunia na starehe zake ni za haraka haraka, na mwanadamu anapenda sana vya haraka. Nayo Akhera ni ya baadaye yaliyomo ya neema zake za kudumu. Kwa hivyo, mkaghafilika mbali nayo na mkaiacha kana kwamba hamkuumbwa kwa ajili yake, na kana kwamba nyumba hii ndiyo nyumba ya daima ambayo vitu vya thamani vya maisha vinatolewa kwa ajili yake na kutafutwa katika muda wote wa usiku na mchana, lakini uhakika wa mambo haya ukawabadilikia, na kilichotokea cha hasara kikawatokea. Na kama mngeipendelea akhera kuliko dunia hii, na mkayaangalia matokeo yake kwa macho ya mwenye kuona kuzuri mwenye akili, basi mngefanikiwa na kupata faida bila hasara yoyote pamoja nayo, na mkafuzu kufuzu kusikokuwa na taabu yoyote pamoja nako.
#
{22 - 23} ثم ذكر ما يدعو إلى إيثار الآخرة ببيان حال أهلها وتفاوتهم فيها، فقال في جزاء المؤثرين للآخرة على الدُّنيا: {وجوهٌ يومئذٍ ناضرةٌ}؛ أي: حسنة بهيَّة لها رونقٌ ونورٌ مما هم فيه من نعيم القلوب وبهجة النفوس ولذَّة الأرواح، {إلى ربِّها ناظرةٌ}؛ أي: ينظرون إلى ربِّهم على حسب مراتبهم؛ منهم مَنْ ينظره كلَّ يوم بكرةً وعشيًّا، ومنهم من ينظره كلَّ جمعة مرةً واحدةً، فيتمتَّعون بالنَّظر إلى وجهه الكريم وجماله الباهر الذي ليس كمثله شيءٌ؛ فإذا رأوه؛ نسوا ما هم فيه من النعيم، وحصل لهم من اللَّذَّة والسرور ما لا يمكن التعبير عنه، ونضرت وجوهُهم، فازدادوا جمالاً إلى جمالهم، فنسأل الله الكريم أن يجعَلنَا معهم.
{22 - 23} Kisha akataja kile kinachoitia kuipendelea Akhera kwa kubainisha hali ya watu wake na tafauti zao ndani yake, na akasema kuhusu malipo ya wale wanaoipendelea Akhera kuliko dunia: "Zipo nyuso siku hiyo zitakazong'ara" kwa sababu ya uzuri wake, nuru yake kutokana na yale waliyomo ndani yake ya raha ya nyoyo, furaha ya nafsi na starehe ya roho. "Zinamwangalia Mola wao Mlezi" kulingana na daraja ya kila mmoja wao. Kuna wale watakaoangalia kila siku, asubuhi na jioni, na baadhi yao watamtazama mara moja kila Ijumaa, kwa hivyo wanafurahia kwa sababu ya kuutazama uso wake mtukufu na uzuri wake unaong’aa zaidi, ambao hakuna kitu kingine chochote kama mfano wake. Watakapomwona, watasahau raha waliyokuwa ndani yake, na watapata raha na furaha isiyoweza kuelezeka, na nyuso zao zitang’aa, na hapo zitazidi uzuri juu ya uzuri wao, kwa hivyo tunamwomba Mwenyezi Mungu Mkarimu atufanye miongoni mwao.
#
{24 - 25} وقال في المؤثرين العاجلة على الآجلة، [و] {وجوهٌ يومئذٍ باسرةٌ}؛ أي: معبسةٌ كدرةٌ خاشعةٌ ذليلةٌ، {تظنُّ أن يُفْعَلَ بها فاقرةٌ}؛ أي: عقوبةٌ شديدةٌ وعذابٌ أليمٌ؛ فلذلك تغيَّرت وجوههم وعبست.
{24 - 25} Na akasema kuhusu wale wanaopendelea maisha ya dunia ya haraka kuliko ya baadaye. "Na zipo nyuso siku hiyo zitakazokunjana" kwa sababu ya kukasirika na kudhalilika "Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo" kutokana na mateso makali na adhabu chungu.
: 26 - 40 #
{كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ (26) وَقِيلَ مَنْ رَاقٍ (27) وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ (28) وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ (29) إِلَى رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ (30) فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّى (31) وَلَكِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى (32) ثُمَّ ذَهَبَ إِلَى أَهْلِهِ يَتَمَطَّى (33) أَوْلَى لَكَ فَأَوْلَى (34) ثُمَّ أَوْلَى لَكَ فَأَوْلَى (35) أَيَحْسَبُ الْإِنْسَانُ أَنْ يُتْرَكَ سُدًى (36) أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِنْ مَنِيٍّ يُمْنَى (37) ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّى (38) فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنْثَى (39) أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَى (40)}
26. La, hasha! (Roho) itakapofikia kwenye mafupa ya koo. 27. Na pakasemwa: Nani wa kumganga? 28. Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki. 29. Na utakapoambatishwa muundi kwa muundi. 30. Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! 31. Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali. 32. Bali alikanusha, na akageuka. 33. Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. 34. Ole wako, ole wako! 35. Kisha Ole wako, ole wako! 36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? 37. Kwani hakuwa yeye tone la manii lililoshushwa? 38. Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. 39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. 40. Je, huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?
#
{26 - 30} يَعِظُ تعالى عبادَه بذكر المحتضر حال السياق ، وأنَّه إذا بلغت روحه {التراقي}: وهي العظام المكتنفة لثُغْرَةِ النَّحر؛ فحينئذٍ يشتدُّ الكربُ، ويطلب كلَّ وسيلةٍ وسببٍ يظنُّ أن يحصل به الشفاء والراحة، ولهذا قال: {وقيلَ مَنْ راقٍ}؛ أي: من يرقيه، من الرُّقية؛ لأنَّهم انقطعت آمالهم من الأسباب العاديَّة، فتعلَّقوا بالأسباب الإلهيَّة ، ولكنَّ القضاء والقدر إذا حتم وجاء؛ فلا مردَّ له، {وظنَّ أنَّه الفراقُ}: للدنيا، {والتفَّتِ السَّاقُ بالسَّاق}؛ أي: اجتمعت الشدائد والتفَّت، وعظُم الأمر، وصعُب الكرب، وأريد أن تخرجَ الرُّوح من البدن الذي ألفته ولم تزل معه، فتساق إلى الله تعالى ليجازيها بأعمالها ويقرِّرها بفعالها؛ فهذا الزجر الذي ذكره الله يسوقُ القلوب إلى ما فيه نجاتُها ويزجُرُها عمَّا فيه هلاكها.
{26 - 30} Mwenyezi Mungu anawaaidhi waja wake kwa kumtaja mtu anayekufa katika hali ya kutokwa roho, na kwamba roho yake inapofika "mafupa ya koo" hapo dhiki inazidi mno, na anatafuta kila njia na sababu ambayo kwayo anadhani anaweza kupata uponyaji na faraja. Ndiyo maana akasema: "Na pakasemwa: Nani wa kumganga?" Kwa sababu tayari matumaini yao huwa yamekatikia mbali kuhusiana na sababu za kawaida, kwa hivyo wakajifungamanisha na sababu za kimungu, lakini hukumu na mipango ya Mwenyezi Mungu inapokwisha pitishwa na ikaja, hakuna wa kuirudisha nyuma. "Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki" dunia. "Na utakapoambatishwa muundi kwa muundi" na jambo hilo likamuwia kubwa mno, na dhiki hiyo ikawa ngumu, na ikatakiwa kwamba roho iondoke kwenye mwili ambao imeuzoea na bado iko nao, kisha inaongozwa kwenda kwa Mwenyezi Mungu ili kuilipa kwa matendo yake na kuifanya kukubali vitendo vyake. Karipio hili ambalo Mwenyezi Mungu ametaja linaiongoza mioyo kwa yale ambayo yatakayoiokoa na kuikemea dhidi ya yale ambayo yanaweza kuiangamiza.
#
{31 - 33} ولكنَّ المعاند الذي لا تنفع فيه الآياتُ لا يزال مستمرًّا على غيِّه وكفره وعناده، {فلا صدَّقَ}؛ أي لا آمن بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر والقدر خيره وشرِّه، {ولا صلَّى. ولكن كذَّبَ}: بالحقِّ في مقابلة التصديق، {وتولَّى}: عن الأمر والنَّهي، هذا وهو مطمئنٌّ قلبهُ غير خائفٍ من ربِّه، بل {ذهب إلى أهله يَتَمَطَّى}؛ أي: ليس على بَالِه شيءٌ.
{31 - 33} Lakini mtu mkaidi ambaye Aya hazimnufaishi anaendelea kupotea, kukufuru na ukaidi wake, "hakusadiki" na kuamwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na mipango ya Mwenyezi Mungu mizuri na mibaya. "Wala hakusali. Bali alikanusha" haki "na akageuka" akaipa amri na makatazo mgongo. Anafanya haya hali ya kuwa moyo wake umetulia, wala haumuogopi Mola wake Mlezi. Bali "akaenda kwa ahali zake kwa matao."
#
{34 - 35} ثم توعَّده بقوله: {أولى لك فأولى. ثم أولى لك فأولى}: وهذه كلماتُ وعيدٍ؛ كرَّرها لتكرير وعيدِهِ.
{34 - 35} Kisha akamtishia kwa kusema: "Ole wako, ole wako! Kisha Ole wako, ole wako!" Mwenyezi Mungu aliyarudia haya ili kuirudia tishio lake hili.
#
{36 - 40} ثم ذكَّر الإنسان بخَلْقِهِ الأوَّل، فقال: {أيحسبُ الإنسانُ أن يُتْرَكَ سُدىً}؛ أي: مهملاً لا يؤمر ولا ينهى ولا يُثاب ولا يعاقب؟ هذا حسبانٌ باطلٌ وظنٌّ بالله غير ما يليق بحكمته. {ألم يكُ نطفةً مِن مَنِيٍّ يُمْنى. ثمَّ كان}: بعد المنيِّ {علقةً}؛ أي: دماً، {فَخَلَقَ}: الله منها الحيوان، وسواه؛ أي: أتقنه وأحكمه، {فجعل منه الزوجين الذَّكر والأنثى. أليس ذلك}؛ أي: الذي خلق الإنسان وطوَّره إلى هذه الأطوار المختلفة {بقادرٍ على أن يُحْيِيَ الموتى؟}: بلى إنَّه على كلِّ شيءٍ قديرٌ.
{36 - 40} Kisha akamkumbusha mwanaadamu uumbaji wake wa kwanza, na akasema: "Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?" Yaani, bila ya kuamrishwa na kukatazwa, wala kulipwa mazuri na mabaya? Hii ni dhana batili na kumdhania Mwenyezi Mungu yasiyoingiliana na hekima yake. "Kwani hakuwa yeye tone la manii lililoshushwa? Kisha akawa" baada ya manii "kidonge cha damu tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo" sawasawa. "Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. Je, huyo" aliyemuumba mwanadamu na akampitisha katika awamu hizi tofauti tofauti "hakuwa" ni Muweza wa kufufua wafu?" Kwani? Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Qiyama, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad.
* * *