Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{ن وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ (1) مَا أَنْتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ (2) وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ (3) وَإِنَّكَ لَعَلَى خُلُقٍ عَظِيمٍ (4) فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ (5) بِأَيِّكُمُ الْمَفْتُونُ (6) إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنْ ضَلَّ عَنْ سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ (7)}.
1. Nuun. Ninaapa kwa kalamu na yale wayaandikayo. 2. Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. 3. Na kwa hakika wewe una malipo yasiyokatika. 4. Na hakika wewe una tabia tukufu. 5. Karibu utaona, na wao wataona. 6. Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu. 7. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliyeipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka.
#
{1 - 2} يقسم تعالى بالقلم، وهو اسم جنس شامل للأقلام التي تُكْتَبُ بها أنواع العلوم، ويسطرُ بها المنثور والمنظوم ، وذلك أنَّ القلم وما يسطرُ به من أنواع الكلام من آياته - العظيمة، التي تستحقُّ أن يُقْسِمَ [اللَّهُ] بها على براءة نبيِّه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - مما نسبه إليه أعداؤه من الجنون؛ فنفى عنه ذلك بنعمةِ ربِّه عليه وإحسانه؛ حيث منَّ عليه بالعقل الكامل والرأي الجَزْل والكلام الفَصل، الذي هو أحسن ما جرت به الأقلام وسطره الأنام، وهذا هو السعادة في الدُّنيا.
{1 - 2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa kalamu, nalo ni jina la jenasi linalojumuisha kalamu ambazo aina mbalimbali za elimu zinaandikwa kwazo, na ambazo kwazo nathari na mashairi yanaandikwa. Hilo ni kwa sababu kalamu na vyote vinavyotumika katika kuandika aina mbalimbali za maneno ni miongoni mwa ishara zake kubwa, ambazo kwazo
[Mwenyezi Mungu] anastahiki kuapa kwazo juu kwa kuwa mbali kwa Nabii wake – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani – kutokana na wendawazimu waliomnasibisha nao maadui zake. Basi akamkanushia kwa neema ya Mola wake Mlezi juu yake na wema wake. Ambapo alimneemesha akili kamilifu, maoni ya sawasawa na usemi wenye maamuzi ya kukata, ambao ndicho bora zaidi ambacho kalamu ziliwahi kuandika na kuandikwa na wanadamu, na hili ndilo furaha katika dunia.
#
{3} ثم ذكر سعادته في الآخرة، فقال: {وإنَّ لك لأجرًا غيرَ ممنونٍ}؛ أي: لأجراً عظيماً كما يفيده التنكير، غير مقطوع ، بل هو دائمٌ مستمرٌّ، وذلك لما أسلفه - صلى الله عليه وسلم - من الأعمال الصالحة والأخلاق الكاملة والهداية إلى كلِّ خير.
{3} Kisha akataja furaha yake katika Akhera,
akasema: "Na kwa hakika wewe una malipo yasiyokatika." Yaani, malipo makubwa mno, kama inavyoashiriwa na neno lililotumika hapa, na yasiyo ukomo. Bali ni ya kudumu na yenye kuendelea. Na hiyo ni kwa sababu ya yale aliyotanguliza miongoni mwa matendo mema, maadili kamilifu na kuongoka kufikia kila lililo jema.
#
{4} ولهذا قال: {وإنَّك لَعلى خُلُقٍ عظيم}؛ أي: عليًّا به، مستعلياً بخُلُقك الذي مَنَّ الله عليك به. وحاصل خُلُقِهِ العظيم ما فسَّرته به أمُّ المؤمنين عائشة رضي الله عنها لمن سألها عنه، فقالت: كان خلقه القرآن. وذلك نحو قوله تعالى: {خُذِ العَفْوَ وأْمُرْ بالعُرْفِ وأعرِضْ عن الجاهلينَ}، {فبما رحمةٍ من الله لِنتَ لهم ... } الآية، {لقد جاءكم رسولٌ من أنفسِكُم عزيزٌ عليه ما عَنِتُم ... } الآية، وما أشبه ذلك من الآيات الدالاَّت على اتِّصافه - صلى الله عليه وسلم - بمكارم الأخلاق، والآيات الحاثَّات على كلِّ خُلُقٍ جميل ، فكان له منها أكملها وأجلها، وهو في كلِّ خصلة منها في الذَّروة العليا، فكان [- صلى الله عليه وسلم -] سهلاً ليناً قريباً من الناس، مجيباً لدعوة مَنْ دعاه، قاضياً لحاجة من استقضاه، جابراً لقلب مَنْ سأله لا يحرمه ولا يردُّه خائباً. وإذا أراد أصحابُهُ منه أمراً؛ وافقهم عليه وتابعهم فيه إذا لم يكن فيه محذورٌ، وإن عَزَمَ على أمرٍ؛ لم يستبدَّ به دونهم، بل يشاورهم ويؤامرهم، وكان يقبلُ من محسنهم، ويعفو عن مسيئهم، ولم يكن يعاشِرُ جليساً إلاَّ أتمَّ عشرةٍ وأحسنها، فكان لا يعبسُ في وجهه، ولا يُغْلِظُ عليه في مقاله، ولا يطوي عنه بشره، ولا يمسك عليه فَلَتات لسانِهِ، ولا يؤاخذه بما يصدُرُ منه من جفوةٍ، بل يُحْسِنُ إليه غاية الإحسان، ويحتمله غاية الاحتمال - صلى الله عليه وسلم -.
{4} Ndiyo maana akasema: "Na hakika wewe una tabia tukufu." Yaani, umeinuka juu kwa tabia hizo ambazo Mwenyezi Mungu alikuneemesha kwazo. Na jumla ya tabia zake tukufu ni yale aliyoyafasiri mama wa Waumini, Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alipowambia wale waliomuuliza kumhusu yeye,
akasema: 'Tabia yake ilikuwa ni Qur-ani.
' Haya ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majahili." Na pia akasema, "Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao..." hadi mwisho wa aya hii. Na pia akasema, "Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayokutaabisheni..." hadi mwisho wa Aya hii, na pia Aya zingine mfano wa hizi zinazoashiria kusifika kwake - yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na tabia njema na aya zinazohimiza kila tabia nzuri. Basi yeye akawa anasifika kwa kamilizi zake zaidi na tukufu zake zaidi. Naye katika kila< kipengele katika hizo alikuwa katika kilele cha juu kabisa. Alikuwa mwepesi, laini na karibu sana kwa watu, mwenye kuitikia mwito wa anayemwita, mwenye kutimiza mahitaji ya wale wanaotafuta awakidhie mahitaji yao, mwenye kuliwaza moyo wa anayemwomba, hakuwa akimnyima wala kumrudisha patupu. Na ikiwa maswahaba zake walitaka kitu kutoka kwake; alikuwa akiafikiana nao juu yake na kuwafuata ndani yake ikiwa halina ubaya wowote ndani yake. Na akiazimia kufanya jambo, hakuwapa kisogo bila ya kuwahusisha. Bali alikuwa akishauriana nao na kutaka maoni yao kuhusiana nalo. Na alikuwa akikubali kutoka kwa mtenda mazuri wao, na anamsamehe mtenda mabaya wao, na wala hakuwa akitangamana na anyekaa naye isipokuwa kwa kukaa naye kwa njia kamilifu na nzuri zaidi. Alikuwa hamkunjii uso wake, wala kumfanyia ukali katika kuzungumza naye, wala haachi kumfanyia bashasha kwa sababu ya uovu wake, wala kumshikilia kwa sababu ya kasoro za ulimi wake, wala hamchukulii ubaya kwa sababu ya ugumu anaomfanyia. Bali alikuwa akimtendea wema wa hali ya juu sana, na kumvumilia kwa ustahimilivu wa hali ya juu sana - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
#
{5 - 6} فلمَّا أنزله الله في أعلى المنازل [من جميع الوجوه]، وكان أعداؤه ينسِبون إليه أنَّه مجنونٌ مفتونٌ؛ قال: {فستُبْصِرُ ويُبْصِرونَ. بأيِّكُم المفتونُ}: وقد تبيَّن أنَّه أهدى الناس وأكملهم لنفسه ولغيره، وأنَّ أعداءه أضلُّ الناس وشرُّ الناس للناس ، وأنَّهم هم الذين فتنوا عبادَ الله وأضلُّوهم عن سبيله، وكفى بعلم الله بذلك؛ فإنَّه [هو] المحاسب المجازي.
{5 - 6} Mwenyezi Mungu alipomteremsha kwenye vituo vya juu kabisa
[kwa namna zote], na maadui zake walikuwa wakidai kwamba yeye ni mwendawazimu na amepumbazika,
akasema: “Karibu utaona, na wao wataona. Ni nani kati yenu aliyepandwa na wazimu." Na tayari ilibainika kuwa yeye ndiye mwongofu na mkamilifu zaidi katika watu wote, yeye mwenyewe na kuwafanyia hivyo wengine, na kwamba maadui zake ndio watu wapotovu zaidi na waovu kwa watu, na kwamba wao ndio waliowatia majaribuni waja wa Mwenyezi Mungu na kuwapoteza mbali na njia yake, na elimu ya Mwenyezi Mungu juu ya hilo inatosha kabisa. Kwa maana Yeye ndiye atakayewafanyia hesabu viumbe juu ya matendo yao, Mlipaji.
#
{7} {إنَّ ربَّك هو أعلمُ بمن ضلَّ عن سبيله وهو أعلم بالمهتدينَ}: وهذا فيه تهديدٌ للضَّالِّين، ووعدٌ للمهتدين، وبيانٌ لحكمة الله؛ حيث كان يهدي مَنْ يَصْلُحُ للهداية دون غيره.
{7} "Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliyeipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka." Hili ni lina tishio kwa wale waliopotea, na ni ahadi nzuri kwa wale walioongoka, na lina kubainisha hekima ya Mwenyezi Mungu. Ambapo alimwongoa anayefailia hili uwongofu na kumuacha asiyeufailia.
{فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ (8) وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ (9) وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَهِينٍ (10) هَمَّازٍ مَشَّاءٍ بِنَمِيمٍ (11) مَنَّاعٍ لِلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ (12) عُتُلٍّ بَعْدَ ذَلِكَ زَنِيمٍ (13) أَنْ كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ (14) إِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (15) سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ (16)}.
8. Basi usiwatii wanaokadhibisha. 9. Wanatamani lau ungelainisha ili nao wakulainishie. 10. Wala usimtii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa. 11. Mtapitapi, apitaye akifitini. 12. Mwenye kuzuia mno heri, dhalimu, mwingi wa madhambi. 13. Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. 14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto! 15. Anaposomewa Aya zetu,
husema: Hizi ni simulizi za uongo za watu wa zamani! 16. Tutamtia kovu juu ya pua yake.
#
{8} يقول الله تعالى لنبيِّه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -: {فلا تُطِعِ المكذِّبين}: الذين كذَّبوك وعاندوا الحقَّ؛ فإنَّهم ليسوا أهلاً لأن يُطاعوا؛ لأنَّهم لا يأمرون إلاَّ بما يوافق أهواءهم، وهم لا يريدون إلاَّ الباطل؛ فالمطيع لهم مُقْدِمٌ على ما يضرُّه، وهذا عامٌّ في كلِّ مكذِّب وفي كلِّ طاعةٍ ناشئةٍ عن التكذيب، وإن كان السياقُ في شيءٍ خاصٍّ، وهو أنَّ المشركين طلبوا من النبيِّ - صلى الله عليه وسلم - أن يسكت عن عيب آلهتهم ودينهم ويسكتوا عنه.
{8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad -
rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: - "Basi usiwatii wanaokadhibisha." Wale waliokukadhibisha na wakaipinga haki; kwani hawastahili kutiiwa; kwa sababu hawaamrishi isipokuwa yale yanayoafikiana na matamanio yao tu, nao hawataki isipokuwa batili. Kwa hivyo, mwenye kuwatii, anaendea mambo yenye yatakayomdhuru. Na hili ni la jumla katika kila mwenye kukadhibisha, na katika kila utiifu unaotokana na kukadhibisha, hata kama muktadha huu uko katika jambo maalumu, ambalo ni kwamba washirikina walimuuliza Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anyamaze na aache kuikashifu miungu yao na dini yao.
#
{9} ولهذا قال: {ودُّوا}؛ أي: المشركون، {لو تُدْهِنُ}؛ أي: توافقهم على بعض ما هم عليه: إمَّا بالقول، أو بالفعل، أو بالسكوت عما يتعيَّن الكلام فيه {فَيُدْهِنونَ}، ولكن اصدعْ بأمر الله، وأظهرْ دين الإسلام؛ فإنَّ تمام إظهاره نقضُ ما يضادُّه وعيب ما يناقضه.
{9} Ndiyo maana alisema: "Wanatamani." Yaani, washirikina walitamani kwamba, "lau ungelainisha;" yaani,
uwafikiane nao katika baadhi ya yale waliyo nayo: ima kwa kauli, au kwa vitendo, au kwa kunyamazia yale yapasayo kusemwa "ili nao wakulainishie." Lakini wewe itangaze amri ya Mwenyezi Mungu, na idhihirishe dini ya Uislamu. Kwa maana ukamilifu wa kuidhihiri ni kukanusha yale yanayoipinga na kaonyesha kasoro za yale yanayopingana nayo.
#
{10} {ولا تطِعْ كلَّ حلاَّفٍ}؛ أي: كثير الحلف؛ فإنَّه لا يكون كذلك إلاَّ وهو كذَّابٌ، ولا يكون كذّاباً إلاَّ وهو {مَهينٌ}؛ أي: خسيس النفس، ناقصُ الهمة، ليس له رغبةٌ في الخير، بل إرادتُه في شهوات نفسه الخسيسة.
{10} "Wala usimtii kila mwingi wa kuapa." Kwani hawezi kuwa hivyo isipokuwa awe ni mwongo, na hawezi kuwa mwongo mno isipokuwa ni "wa kudharauliwa" mwenye hima pungufu, asiyekuwa na utashi wa kutenda mema, bali utashi wake ni katika matamanio mabaya ya nafsi yake tu.
#
{11} {همَّازٍ}؛ أي: كثير العيب للناس والطعن فيهم بالغيبة والاستهزاء وغير ذلك، {مشاءٍ بنميمٍ}؛ أي: يمشي بين الناس بالنميمة، وهو نقلُ كلام بعضِ الناس لبعض لقصد الإفسادِ بينهم وإيقاع العداوة والبغضاء.
{11} "Mtapitapi;" yaani, mwingi wa kuwakashifu watu na kuwasengenya, kuwadhihaki, na mambo mengineyo, "apitaye akifitini" na kuharibu mahusiano ya kati yao, na kusababisha uadui na chuki kati yao.
#
{12} {منَّاع للخيرِ}: الذي يلزمه القيام به من النفقات الواجبة والكفارات والزَّكَوات وغير ذلك. {معتدٍ}: على الخلق؛ يظلِمُهم في دمائهم وأموالهم وأعراضهم. {أثيمٍ}؛ أي: كثير الإثم والذُّنوب المتعلِّقة في حقِّ الله [تعالى].
{12} "Mwenye kuzuia mno heri" katika yale yanayomlazimu kuyatekeleza, kama vile kutoa vitolewavyo vya faradhi, kafara, Zaka, na mengineyo. "Dhalimu" anayewadhulumu viumbe katika damu zao, mali zao na heshima zao. "Mwingi wa madhambi" yanayohusiana na haki za Mwenyezi Mungu
[Mtukufu].
#
{13} {عُتُلٍّ بعد ذلك}؛ أي: غليظٍ شرس الخلق، قاسٍ، غير منقادٍ للحقِّ. {زنيمٍ}؛ أي: دعيٍّ ليس له أصلٌ ولا مادةٌ ينتج منها الخير، بل أخلاقه أقبح الأخلاق، ولا يرجى منه فلاحٌ. له زِنْمَةٌ؛ أي: علامةٌ في الشرِّ يعرف بها.
{13} "Mkavu, na juu ya hayo;" yaani, mgumu mno wa tabia, asiyeifuata haki. "Mshari;" yaani, asiyekuwa na kiini kinachoweza kutoa heri. Bali tabia zake ndizo tabia mbaya zaidi, wala hatarajiwi kufaulu, na anayo alama ya uovu anajulikana kwayo.
#
{14} وحاصل هذا أنَّ الله تعالى نهى عن طاعة كلِّ حلافٍ كذابٍ خسيس النفس سيِّئِ الأخلاق، خصوصاً الأخلاق المتضمِّنة للإعجاب بالنفس، والتكبُّر على الحقِّ وعلى الخَلْق، والاحتقار للناس بالغيبة والنَّميمة، والطعن فيهم، وكثرة المعاصي.
{14} Jumla ya haya ni kwamba Mwenyezi Mungu ameharamisha kumtii kila mwingi wa kuapa, mwongo mno, mwenye nafsi duni, mwenye tabia mbaya, hasa tabia za kujiona kwamba yeye ndiye bora tu, kuwafanyia viumbe na haki kiburi, na kuwadharau watu kwa kuwasengenya, kuwafitini, kuwakashifu na kufanya maasia mengi.
#
{15} وهذه الآياتُ وإن كانت نزلتْ في بعض المشركين؛ كالوليد بن المغيرة أو غيره ؛ لقوله عنه: {أن كان ذا مال وبنينَ. إذا تُتْلى عليه آياتُنا قال أساطيرُ الأولينَ}؛ أي: لأجل كثرة ماله وولده طغى واستكبر عن الحقِّ ودَفَعه حين جاءه وجعله من جملة أساطير الأولين التي يمكنُ صدقُها وكذبُها؛ فإنَّها عامةٌ في كلِّ من اتَّصف بهذا الوصف؛ لأنَّ القرآن نزل لهداية الخلق كلِّهم، ويدخل فيه أول الأمة وآخرهم، وربَّما نزل بعض الآياتِ في سببٍ أو [في] شخصٍ من الأشخاص، لتتَّضح به القاعدةُ العامةُ، ويُعْرَفَ به أمثال الجزئيات الداخلة في القضايا العامَّة.
{15} Na Aya hizi hata kama ziliteremshwa kuhusiana na baadhi ya washirikina, kama vile Al-Walid bin Al-Mughirah au wengineo,
kwa sababu ya yale aliyosema juu yake: "Ati kwa kuwa ana mali na watoto! Anaposomewa Aya zetu,
husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!" Yaani, kwa sababu ya mali yake nyingi na watoto wake, alikuvuka mipaka na akaifanyia kiburi haki na akaikataa ilipomjia na akaifanya kuwa miongoni mwa ngano za watu wa kale zinazoweza kuwa za kweli au za uongo, lakini pamoja na hili, aya hii ni ya jumla kwa kila mtu ambaye ana maelezo haya. Kwa sababu Qur-ani imeteremshwa kwa ajili ya kuwaongoa viumbe wote, na inajumuisha wa mwanzo wa Umma huu na wa mwisho wake, na pengine baadhi ya Aya ziliteremshwa kwa sababu ya mtu fulani, ili ibainike vyema kanuni fulani ya jumla, na ili kwa hilo ijulikane mifano ya kina ambayo inajumuishwa katika masuala ya jumla.
#
{16} ثم توعَّد تعالى مَنْ جرى منه ما وَصَفَ الله بأن الله سَيَسِمُهُ {على الخرطوم}: في العذاب، وليعذبه عذاباً ظاهراً يكون عليه سِمَةً وعلامةً في أشقِّ الأشياء عليه وهو وجهه.
{16} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtishia mwenye kufanya aliyoyaelezea Mwenyezi Mungu kwamba Mwenyezi Mungu atamtia kovu "juu ya pua yake" katika adhabu na amwadhibu kwa adhabu iliyo dhahiri, ambayo itakuwa alama na ishara juu yake katika mahali pazito zaidi juu yake, ambapo ni uso wake.
{إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ (17) وَلَا يَسْتَثْنُونَ (18) فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِنْ رَبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ (19) فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ (20) فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ (21) أَنِ اغْدُوا عَلَى حَرْثِكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَارِمِينَ (22) فَانْطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ (23) أَنْ لَا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُمْ مِسْكِينٌ (24) وَغَدَوْا عَلَى حَرْدٍ قَادِرِينَ (25) فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ (26) بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ (27) قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ (28) قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ (29) فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ (30) قَالُوا يَاوَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ (31) عَسَى رَبُّنَا أَنْ يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِنْهَا إِنَّا إِلَى رَبِّنَا رَاغِبُونَ (32) كَذَلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ (33)}.
17. Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyowajaribu wale wenye shamba, walipoapa kwamba watayavuna mazao yake itakapokuwa asubuhi. 18.
Wala hawakusema: Mungu akipenda! 19. Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! 20. Likawa kama usiku wa giza. 21. Asubuhi wakaitana. 22. Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. 23. Basi walikwenda na huku wakinong'onezana. 24. Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. 25. Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. 26. Basi walipoliona,
wakasema: Hakika tumepotea! 27. Bali tumenyimwa! 28.
Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? 29.
Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. 30. Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. 31.
Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! 32. Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lililo bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. 33. Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua!
#
{17 - 18} يقول تعالى: إنَّا بَلَوْنا هؤلاء المكذِّبين بالخير، وأمهلناهم، وأمددناهم بما شئنا من مال وولدٍ وطول عمرٍ ونحو ذلك ممَّا يوافق أهواءهم، لا لكرامتهم علينا، بل ربَّما يكون استدراجاً لهم من حيثُ لا يعلمون، فاغترارهم بذلك نظيرُ اغترار أصحاب الجنَّة الذين هم فيها شركاء، حين أينعت أشجارها، وزهت ثمارها ، وآن وقت صِرامها وجزموا أنَّها في أيديهم وطوع أمرهم، وأنَّه ليس ثَمَّ مانعٌ يمنعهم منها، ولهذا أقسموا وحلفوا من غير استثناءٍ أنَّهم سيصرمونها؛ أي: يجذُّونها مصبحين، ولم يَدْروا أنَّ الله بالمرصادِ، وأنَّ العذاب سيخلفهم عليها ويبادِرُهم إليها.
{17 - 18} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika tuliwatia mtihanini hawa wanaokadhibisha heri, na tukawapa muhula, na tukawaruzuku kila tulichokitaka katika mali watoto, maisha marefu, na mengine mfano wake yaliyoafikiana na matamanio yao si kwa sababu ya heshima yao mbele yetu, lakini pengine hilo lilikuwa ni kuwasongesha polepole na kuwakamatia kutokea mahali ambapo hawakujua. Kwa hivyo kudanganyika kwao na hayo ni kama vile walivyodanganyika nayo watu wa konde lile, ambao walikuwa washirika ndani yake, pale miti yake ilipochanua na matunda yake yakatoka kwa uzuri mno, na wakati wa kuyachuma ukafika, nao wakawa na uhakika kwamba yako mikononi mwao na chini ya amri yao, na kwamba hakuna kizuizi chochote kinachoweza kuwazuia mbali nayo. Na ndiyo maana wakaapa bila kusema "Mwenyezi Mungu akipenda" kwamba lazima watayachuma asubuhi, lakini hwakujua kwamba Mwenyezi Mungu anawatazama kweli kweli, na kwamba adhabu itachukua mahali pa hilo, na itawatangulia kulifikia konde hilo.
#
{19 - 20} {فطاف عليها طائفٌ من ربِّك}؛ أي: عذابٌ نزل عليها ليلاً، {وهم نائمونَ}: فأبادها، وأتلفها، {فأصبحتْ كالصَّريم}؛ أي: كالليل المظلم، وذهبت الأشجار والثمار.
{19 - 20} "Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi." Yaani, Adhabu ililishukia usiku, "nao wamelala!" Kwa hivyo ikaliangamiza na kuliharibu. "Likawa kama usiku wa giza" totoro, na miti na matunda yake yakapotelea mbali.
#
{21 - 22} هذا وهم لا يشعرون بهذا الواقع الملم، ولهذا تنادوا فيما بينهم لما أصبحوا؛ يقول بعضهم لبعض: {اغْدوا على حرثِكم إن كنتُم صارمين}.
{21 - 22} Haya yalitokea nao hawahisi ukweli huu unaohisika,
na ndiyo maana waliitana wao kwa wao walipofika asubuhi; Wakiambiana wenyewe kwa wenyewe: "Nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna."
#
{23 - 24} {فانطلقوا}: قاصدين لها ، {وهم يتخافتونَ}: فيما بينهم بمنع حقِّ الله تعالى، ويقولون: {لا يَدْخُلَنَّها اليومَ عليكم مسكينٌ}؛ أي: بكِّروا قبل انتشار الناس، وتواصوا مع ذلك بمنع الفقراء والمساكين. ومن شدَّة حرصهم وبخلهم أنَّهم يتخافتون بهذا الكلام مخافتةً خوفاً أن يَسْمَعَهم أحدٌ فيخبر الفقراء.
{23 - 24} "Basi walikwenda" wakilikusudia konde hilo "na huku wakinong'onezana" wao kwa wao juu ya kusudio lao la kuzuia haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,
na wakawa wanasema ya kuwa: "Leo hata masikini mmoja asikuingilieni." Yaani, nendeni mapema kabla watu hawajatawanyika na usianeni hilo la kuwazuia mafukara na masikini. Na kwa sababu ya umakini wao na ubakhili wao mkubwa, wakayaficha maneno haya kwa kuhofia kwamba mtu atayasikia na kuwaambia maskini hao.
#
{25} {وغَدَوْا}: في هذه الحالة الشنيعة والقسوة وعدم الرحمة {على حردٍ قادرينَ}؛ أي: على إمساكٍ ومنعٍ لحقِّ الله جازمين بقدرتهم عليها.
{25} "Na walikwenda asubuhi" katika hali hii mbaya mno, ya kikatili, isiyo na huruma "nao wameshikilia azimio hilo" la kuzuia na kushikilia haki ya Mwenyezi Mungu, wakiwa na uhakika kwamba wana uwezo wa kuzitimiza hilo.
#
{26 - 27} {فلمَّا رأوْها}: على الوصف الذي ذَكَرَ الله كالصريم، {قالوا}: من الحيرة والانزعاج، {إنَّا لضالُّون}؛ أي: تائهون عنها، لعلَّها غيرها، فلما تحقَّقوها ورجعت إليهم عقولهم؛ قالوا: {بل نحن محرومون}: منها، فعرفوا حينئذٍ أنَّه عقوبةٌ.
{26 - 27} "Basi walipoliona" kulingana na maelezo aliyoyataja Mwenyezi Mungu kwamba lilikuwa ni kama usiku wa giza, "wakasema" kwa sababu ya kuchanganyikiwa na kukereka, "Hakika tumepotea" mbali na konde letu, na huenda ikawa si hili. Lakini walipopata uhakika na hilo na akili zao zikawarudia,
wakasema: "Bali tumenyimwa" chochote chake. Kwa hivyo wakajua wakati huo kwamba hiyo ni adhabu.
#
{28} فَـ {قَالَ أوسطُهم}؛ أي: أعدلُهم وأحسنُهم طريقةً: {ألم أقل لكم لولا تسبِّحونَ}؛ أي: تنزِّهون الله عما لا يليق به، ومن ذلك ظنُّكم أنَّ قدرتكم مستقلةٌ، فلولا استثنيتم وقلتُم: إنْ شاء الله، وجعلتم مشيئتكم تابعةً لمشيئتِهِ ؛ لما جرى عليكم ما جرى.
{28} Kisha "mbora wao" kwa mwenendo "akasema: 'Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?'" Yaani mumtakase Mwenyezi Mungu kutokana na yale hayamfailii. Na katika hayo ni kuamini kwako kwamba uwezo wao ni wa kujitegemea.
Akawaambia: Lau mngesama kwamba Mwenyezi Mungu akipenda, na mkafanya mapenzi yenu chini ya mapenzi yake, basi kilichokutokeeni hakingekutokeeni.
#
{29} فَـ {قالوا سبحانَ ربِّنا إنَّا كُنَّا ظالمين}؛ أي: استدركوا بعد ذلك، ولكن بعدما وقع العذاب على جنتهم، الذي لا يُرفع، ولكن لعلَّ تسبيحهم هذا وإقرارهم على أنفسهم بالظُّلم ينفعهم في تخفيف الإثم ويكونُ توبةً.
{29} Kwa hivyo,
"wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu." Yaani, waliweza kuirudia njia ya sawa, lakini baada ya adhabu kuliangukia konde lao, ambayo haiwezi kuondolewa. Lakini pengine kumtakasa kwao huku Mwenyezi Mungu na kukiri kwao dhuluma juu ya nafsi zao kutawanufaisha katika kupunguza dhambi na kuwe toba yao.
#
{30 - 32} ولهذا ندموا ندامةً عظيمةً، وأقبل {بعضُهم على بعضٍ يتلاومونَ}: فيما أجروه وفعلوه، {قالوا يا وَيْلَنا إنا كُنَّا طاغينَ}؛ أي: متجاوزين للحدِّ في حقِّ الله وحقِّ عباده، {عسى ربُّنا أن يُبْدِلَنا خيراً منها إنَّا إلى ربِّنا راغبونَ}: فهم رجوا الله أن يبدِّلهم خيراً منها، ووعدوا أن سيرغبون إلى الله ويلحُّون عليه في الدُّنيا؛ فإنْ كانوا كما قالوا؛ فالظاهر أنَّ الله أبدلهم في الدُّنيا خيراً منها؛ لأنَّ من دعا الله صادقاً ورغب إليه ورجاه؛ أعطاه سؤاله.
{30 - 32} Na kwa sababu ya hilo wakajuta sana, na wakageukiana "kulaumiana wao kwa wao" juu ya yale waliyoyafanya.
"Wakasema: 'Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka'" katika haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya waja wake. "Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lililo bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi." Basi wakataraji Mwenyezi Mungu atawapa kilicho bora kuliko hilo, na wakaahidi kwamba watamrudia mno Mwenyezi Mungu na kusisitiza juu ya hilo katika dunia hii. Kwa hivyo, ikiwa wako kama walivyosema, basi linaloonekana ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwabadilishia mahali pake kilicho bora zaidi yake katika dunia hii. Kwa sababu anayemwomba Mwenyezi Mungu kwa ukweli, akamtaka sana na kumtaraji, atampa ombi lake.
#
{33} قال تعالى معظماً ما وقع: {كذلك العذابُ}؛ أي: الدنيويُّ لمن أتى بأسباب العذاب أن يسلبَه الله الشيء الذي طغى به وبغى وآثَرَ الحياةَ الدُّنيا وأن يزيلَه عنه أحوجَ ما يكون إليه، {ولَعذابُ الآخرةِ أكبرُ}: من عذاب الدُّنيا، {لو كانوا يعلمون}: فإنَّ مَنْ عَلِمَ ذلك؛ أوجب له الانزجار عن كلِّ سبب يوجب العقاب ويحرم الثواب.
{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema,
akitukuza yaliyotokea: "Namna hivi yanakuwa mateso" ya kidunia kwa mwenye kufanya visababu vya adhabu ya kidunia, kwamba Mwenyezi Mungu atamnyang'anya jambo alilolivukia mipaka na akapendelea maisha ya dunia, na amtoe kwalo wakati anapolihitaji zaidi. "Na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi" kuliko adhabu ya dunia "laiti wangelijua!" Na anayejua hilo, atalazimika kujiepusha na kila sababu inayoweza kumsababishia adhabu na kumnyima malipo mazuri.
{إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِنْدَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ (34) أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ (35) مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ (36) أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ (37) إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ (38) أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ (39) سَلْهُمْ أَيُّهُمْ بِذَلِكَ زَعِيمٌ (40) أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِنْ كَانُوا صَادِقِينَ (41)}.
34. Hakika wacha Mungu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. 35. Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? 36. Mna nini? Mnahukumu vipi? 37. Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? 38. Kuwa mtapata humo mnayoyapenda? 39. Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayojihukumia? 40.
Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? 41. Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.
#
{34 - 41} يخبر تعالى بما أعدَّه للمتَّقين للكُفْرِ والمعاصي، من أنواع النعيم والعيش السليم في جوار أكرم الأكرمين، وأنَّ حكمته تعالى لا تقتضي أن يجعل المتَّقين القانتين لربِّهم، المنقادين لأوامره، المتَّبِعين مراضِيَه، كالمجرمين الذين أوضَعوا في معاصيه والكفر بآياتِهِ ومعاندةِ رسلِهِ ومحاربة أوليائِهِ، وأنَّ من ظنَّ أنَّه يسوِّيهم في الثواب؛ فإنَّه قد أساء الحكم، وأنَّ حكمه [حكمٌ] باطلٌ ورأيه فاسدٌ، وأن المجرمين إذا ادَّعوا ذلك؛ فليس لهم مستندٌ، لا كتابٌ فيه يدرسون ويتلون أنَّهم من أهل الجنة، وأنَّ لهم ما طلبوا وتخيَّروا، وليس لهم عند الله عهدٌ ويمينٌ بالغةٌ إلى يوم القيامةِ أنَّ لهم ما يحكمون، وليس لهم شركاءُ وأعوانٌ على إدراك ما طلبوا؛ فإنْ كان لهم شركاءُ وأعوانٌ؛ فليأتوا بهم إن كانوا صادقين. ومن المعلوم أنَّ جميع ذلك منتفٍ؛ فليس لهم كتابٌ ولا لهم عهدٌ عند الله في النجاة ولا لهم شركاءُ يعينونَهم، فعُلِمَ أنَّ دعواهم باطلةٌ فاسدةٌ. وقوله: {سَلْهُم أيُّهم بذلك زعيمٌ}؛ أي: أيُّهم الكفيل بهذه الدعوى التي تَبَيَّنَ بطلانها؛ فإنَّه لا يمكن أحداً أن يتصدَّر بها ولا يكون زعيماً فيها.
{34 - 41} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kile alichowaandalia wacha Mungu waliojiepusha na ukafiri na maasi, miongoni mwa aina mbalimbali za furaha na maisha salama mno karibu na Mkarimu zaidi ya wakarimu wote, na kwamba hekima yake Mtukufu haifailii awafanye wacha Mungu, watiifu kwa Mola wao Mlezi, wanaotekeleza amri zake, na wanafuata yale yanayomridhisha, kama wahalifu waliozama katika kumuasi, na kuzikufuru Aya zake, na kuwapinga Mitume wake, na kupigana na vipenzi wake, na kwamba wanaodhani kwamba yeye atawafanya sawa katika malipo, basi hakika amehukumu vibaya, na kwamba hukumu yake hiyo ni
[hukumu] batili na maoni mabovu, na kwamba wahalifu wanapokidai hivyo, wao huwa hawana msingi wowote wa kushikilia, si kitabu ambacho wanakidurusu na kusoma ndani yake kwamba wao ni miongoni mwa watu wa Peponi, na kwamba watapata yale waliyoyaomba na waliyoyachagua, na pia hawana ahadi na kiapo kwa Mwenyezi Mungu vinavyofika Siku ya Kiyama kwamba watapata yale wanayohukumu, na hawana washirika na wasaidizi watakaowasaidia kufikia yale wanayoyataka. Ikiwa wanao washirika na wasaidizi, basi wawalete ikiwa ni wakweli. Lakini kama inavyojulikana kuwa kwamba yote haya hayapo. Hawana kitabu, wala hawana ahadi kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana na kuokoka kwao, wala hawana washirika wa kuwasaidia. Kwa hivyo ikajulikana kwamba madai yao hayo ni batili na mabovu.
Na kauli yake: “Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya" ambayo yameshabainika ubatili wake? Kwani, haiwezekani kwa mtu yeyote kuyaweza wala kuwa mdhamini wake.
{يَوْمَ يُكْشَفُ عَنْ سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ (42) خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ (43)}.
42. Siku utakapowekwa wazi muundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza 43. Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipokuwa wazima.
#
{42 - 43} أي: إذا كان يوم القيامة، وانكشفَ فيه من القلاقل والزلازل والأهوال ما لا يدخُلُ تحت الوهم، وأتى الباري لفصل القضاءِ بين عباده ومجازاتهم، فكشف عن ساقه الكريمة التي لا يشبِهُها شيءٌ، ورأى الخلائقُ من جلال الله وعظمته ما لا يمكن التعبير عنه؛ فحينئذٍ {يُدْعَوْنَ إلى السجود}: لله، فيسجد المؤمنون الذين كانوا يسجُدون لله طوعاً واختياراً، ويذهب الفجَّارُ المنافقون ليسجدوا؛ فلا يقدرون على السجود، وتكون ظهورهم كصياصِي البقرِ؛ لا يستطيعون الانحناء، وهذا الجزاء من جنس عملهم؛ فإنَّهم كانوا يُدْعَوْنَ في الدُّنيا إلى السجود لله وتوحيده وعبادته وهم سالمون لا علَّة فيهم؛ فيستكبرون عن ذلك، ويأبَوْن؛ فلا تسأل يومئذٍ عن حالهم وسوء مآلهم؛ فإنَّ الله قد سَخِطَ عليهم، وحقَّت عليهم كلمة العذاب، وتقطَّعت أسبابهم، ولم تنفعهم الندامة والاعتذار يوم القيامة؛ ففي هذا ما يزعِجُ القلوب عن المقام على المعاصي ويوجب التدارك مدة الإمكان.
{42 - 43} Yaani, itakapofika Siku ya Kiyama, na zikatokea humo wasiwasi, mitetemeko na mahangaiko makubwa yasivyoweza kufikiriwa kwamba si kweli, na akaja Muumba kuhukumu baina ya waja wake na kuwalipa, kisha akaufunua muundi wake mtukufu ambao hakuna kinachofanana nao, na viumbe vikaona katika utukufu na ukuu wa Mwenyezi Mungu usioweza kuelezeka, hapo "na wataitwa kusujudu" kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Waumini waliokuwa wakimsujudia Mwenyezi Mungu kwa hiari yao watasujudu, nao waovu wanafiki watakwenda kusujudu, lakini hawataweza kusujudu. Migongo yao itakuwa kama nundu ya ng'ombe. Hawataweza kuinama, na malipo haya ni ya aina sawa na matendo yao
(ya hapo awali). Kwani walikuwa katika dunia wakiitwa kumsujudia Mwenyezi Mungu, kumpwekesha na kumwabudu, hali wakiwa salama, bila ya kuwa na dosari yoyote, lakini wanalifanyia hilo kiburi na wanakataa. Basi usiulize kuhusu hali yao au hatima mbaya siku hiyo. Kwani Mwenyezi Mungu aliwakasirikia, na neno la adhabu likatimia juu yao, na mahusiano yao yakakatika kabisa, na majuto na kuomba udhuru havitawafaa Siku ya Kiyama. Basi haya ndiyo yanafaa kuisumbua mioyo kujitenga mbali na kutenda maasi na kuitia kufanya mema mapema katika muda wa uwezekano wa kufanya hayo.
{فَذَرْنِي وَمَنْ يُكَذِّبُ بِهَذَا الْحَدِيثِ سَنَسْتَدْرِجُهُمْ مِنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ (44) وَأُمْلِي لَهُمْ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ (45) أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُمْ مِنْ مَغْرَمٍ مُثْقَلُونَ (46) أَمْ عِنْدَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ (47) فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُنْ كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَى وَهُوَ مَكْظُومٌ (48) لَوْلَا أَنْ تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِنْ رَبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ (49) فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ (50) وَإِنْ يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ (51) وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِلْعَالَمِينَ (52)}.
44. Basi niache na wanaokadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kutokea mahali wasipopajua. 45. Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. 46. Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? 47. Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? 48. Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. 49. Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angelitupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. 50. Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. 51. Na waliokufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanaposikia mawaidha,
na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. 52. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
#
{44 - 45} أي: دعني والمكذِّبين بالقرآن العظيم؛ فإنَّ عليَّ جزاءهم، ولا تستعجل لهم؛ فسنستدرِجُهم {من حيث لا يعلمونَ}: فنُمِدُّهم بالأموال والأولاد، ونُمِدُّهم في الأرزاق والأعمال؛ ليغتروا ويستمرُّوا على ما يضرُّهم، وهذا من كيد الله لهم. وكيدُ الله لأعدائه متينٌ قويٌّ، يبلغ من ضررهم وعقوبتهم كلَّ مبلغ.
{44 - 45} Yaani: Niache mimi na hao wanaoikadhibisha Qur-ani Tukufu. Kwani ni juu yangu kuwalipa, wala usiwafanyie haraka. Tutawaleta polepole "kutokea mahali wasipopajua" kwa kuwaruzuku mali na watoto, na riziki nyingi na matendo. Ili wadanganyike na waendelee na yale yatakayowadhuru, na hili ni katika njama za Mwenyezi Mungu juu yao. Njama za Mwenyezi Mungu dhidi ya maadui zake ni madhubuti na zenye nguvu, na madhara yatakayowapata na adhabu yao inafikia kila kiwango.
#
{46} {أم تسألهم أجراً فهم من مَغْرَم مُثْقَلون}؛ أي: ليس لنفورهم عنك وعدم تصديقهم لك سببٌ يوجب لهم ذلك ؛ فإنَّك تعلِّمُهم وتدعوهم إلى الله لمحض مصلحتهم من غير أن تطلبهم من أموالهم مغرماً يَثْقُلُ عليهم.
{46} "Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?" Yaani, kukuchukia kwao na kutokusadiki kwako hakuna sababu ya kuwasababishia kufanya hivyo. Kwani wewe unawafundisha na kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya masilahi yao matupu, bila ya kutaka kutoka katika mali zao mzigo utakaowaelemea.
#
{47} {أم عندَهم الغيبُ فهم يكتُبون}: ما كان عندهم من الغيوب، وقد وجدوا [فيها] أنَّهم على حقٍّ، وأنَّ لهم الثواب عند الله؛ فهذا أمرٌ ما كان، وإنَّما كانت حالهم حال معاندٍ ظالم.
{47} "Au wanazo habari za mambo ya ghaibu, basi wao wanaziandika?" Na wakakuta humo kuwa wako katika haki na kwamba wana malipo mazuri kwa Mwenyezi Mungu. Hili halikuwa jambo lililotokea, bali hali yao ilikuwa ya mtu mkaidi, dhalimu.
#
{48 - 50} فلم يبقَ إلاَّ الصبر لأذاهم والتحمُّل لما يصدُرُ منهم والاستمرار على دعوتهم، ولهذا قال: {فاصبِرْ لحكم ربِّك}؛ أي: لما حكم به شرعاً وقدراً؛ فالحكم القدريُّ يُصْبَرُ على المؤذي منه ولا يُتَلَقَّى بالسخط والجزع، والحكم الشرعيُّ يقابَلُ بالقَبول والتسليم والانقياد [التامِّ] لأمرِهِ. وقوله: {ولا تكن كصاحب الحوتِ}: وهو يونس بن متى عليه الصلاة والسلام؛ أي: ولا تشابِهه في الحال التي أوصلَتْه وأوجبت له الانحباس في بطن الحوت، وهو عدم صبره على قومِهِ الصبرَ المطلوب منه وذَهابُه مغاضباً لربِّه، حتى ركب [في] البحر، فاقترع أهل السفينة حين ثقلت بأهلها أيُّهم يلقون؛ لكي تَخِفَّ بهم، فوقعت القرعةُ عليه، فالتقمه الحوتُ وهو مليمٌ. وقوله: {إذ نادى وهو مكظومٌ}؛ أي: وهو في بطنها قد كظمت عليه، أو: نادى وهو مغتمٌّ مهتمٌّ، فقال: لا إله إلا أنت سبحانك إنِّي كنت من الظالمين، فاستجاب الله له، وقَذَفَتْه الحوتُ من بطنها بالعراء وهو سقيمٌ، وأنبت الله عليه شجرةً من يقطينٍ، ولهذا قال هنا: {لولا أن تدارَكَه نعمةٌ من ربِّه لَنُبِذَ بالعراء}؛ أي: لَطُرِحَ في العراء، وهي الأرض الخالية، {وهو مذمومٌ}: ولكنَّ الله تغمَّده برحمته، فَنُبِذَ وهو ممدوحٌ، وصارت حالُه أحسنَ من حاله الأولى، ولهذا قال: {فاجتباه ربُّه}؛ أي: اختاره واصطفاه ونقَّاه من كلِّ كدرٍ، {فجعله من الصالحين}؛ أي: الذين صَلَحَتْ أعمالهم وأقوالهم ونيَّاتهم وأحوالهم.
{48 - 50} Basi hakikubakia isipokuwa kuwa na subira juu ya maudhi yao, na kustahimili yale yatokayo kwao, na kuendelea katika kuwalingania,
ndiyo maana akasema: "Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi" Yaani, kile alichohukumu kisheria na kulingana na mipango yake. Kwani hukumu inayohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu ni lazima mtu awe mvumilivu juu ya chenye kumdhuru katika hukumu hiyo, wala haikabiliwi kwa ghadhabu na hofu na kutokuwa na subira. Nayo hukumu ya kisharia inakabiliwa kwa kuikubali, kusalimu amri, na kufuata
[kikamilifu].
Na kauli yake: "wala usiwe kama mmezwa na samaki." Naye alikuwa nabii Yunus bin Matta, rehema na amani ziwe juu yake. Yaani, usijifananishe naye katika hali iliyompelekea kunaswa ndani ya tumbo la nyangumi, nayo ni kutokuwa na subira kwa watu wake, subira inayotakiwa kwake, na kwenda kwake kwa hasira akimwacha Mola wake Mlezi. Akapanda baharini, na watu wa merikebu ilipolemewa na watu wake, wakapiga kura ili ijulikane ni nani wao watamtupa ndani ya bahari. Ili merikebu ipate kuwa nyepesi, basi kura ikamwangukia, na nyangumi akammeza huku ni wa kulaumiwa.
Na kauli yake: "aliponadi naye kazongwa." Yaani, alipokuwa tumboni mwake, alikuwa akihuzunika juu yake, au aliita hali ya kuwa amehuzunika na kuzongwa,
na akasema: 'Hapana mungu ila Wewe, umetakasika. Hakika mimi nimekuwa katika madhalimu.' Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia, na nyangumi huyo akamtema nje ya tumbo lake ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. Na Mola wake Mlezi akamuotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. Ndiyo maana akasema hapa, "Kama isingelimfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angelitupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa," lakini Mwenyezi Mungu akamfunika kwa rehema yake, na akatemwa hapo huku anasifiwa kwa uzuri, na hali yake ikawa bora kuliko hali yake ya awali,
ndiyo maana akasema: "Lakini Mola wake Mlezi alimteua" na akamtakasa kutokana na kila uchafu, "na akamfanya miongoni mwa watu wema" katika matendo yao, maneno yao, nia zao na hali zao.
#
{51 - 52} فامتثل نبيُّنا محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - أمر الله ، فصبر لحكم ربِّه صبراً لا يدركه [فيه] أحدٌ من العالمين، فجعل الله له العاقبة، والعاقبةُ للمتقين، ولم يبلغ أعداؤه فيه إلاَّ ما يسوؤهم، حتى إنَّهم حرصوا على أن يُزْلِقوه {بأبصارهم}؛ أي: يصيبوه بأعينهم من حسدهم وحنقهم وغيظهم. هذا منتهى ما قدروا عليه من الأذى الفعليِّ، والله حافظه وناصِرُه. وأمَّا الأذى القوليُّ؛ فيقولون فيه أقوالاً بحسب ما توحي إليهم قلوبهم، فيقولون تارةً: مجنونٌ! وتارةً: شاعرٌ! وتارة: ساحرٌ! قال تعالى: {وما هو إلا ذكرٌ للعالمين}؛ أي: وما هذا القرآن العظيم والذِّكر الحكيم إلاَّ ذكرٌ للعالمين، يتذكَّرون به مصالح دينهم ودنياهم. والحمد لله.
{51 - 52} Basi Mtume wetu Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie - akatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na akavumilia hukumu ya Mola wake Mlezi kwa subira asiyoweza kuifahamu yeyote katika walimwengu. Basi Mwenyezi Mungu akamfanyia mwisho mwema, na hakika mwisho ni kwa wacha Mungu, na maadui zake hawakupata chochote katika hilo ila yale yaliyowawiya mabaya sana, kiasi kwamba wakawa na hamu kubwa ya kumtelezesha "kwa macho yao" kutokana na husuda, chuki na hasira zao. Hiki ndicho kiwango cha mwisho cha madhara halisi waliyoweza kuyafanya, na Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi na msaidizi wake. Ama madhara ya kimaneno, wao walisema mambo juu yake kulingana na yale ambayo nyoyo zao ziliwataka kusema.
Basi mara wakasema: 'Yeye ni kichaa!' mara 'Mshairi!' mara: 'Mchawi!' Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote." Yaani, Qur-ani hii tukufu na Ukumbusho wenye hekima si chochote ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote, ambao kwayo wanakumbuka masilahi ya dini yao na dunia yao, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *