Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (1) الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ (2) الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا مَا تَرَى فِي خَلْقِ الرَّحْمَنِ مِنْ تَفَاوُتٍ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَى مِنْ فُطُورٍ (3) ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنْقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ حَسِيرٌ (4)}.
1. Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu. 2. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye msamaha mno. 3. Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudia kutazama! Je, unaona kosa lolote? 4. Tena rudia kutazama mara mbili, kutazama kwako kutakurejelea mwenyewe hali ya kuwa kumehizika, kumechoka.
#
{1} {تبارك الذي بيده الملكُ}؛ أي: تعاظم وتعالى وكَثُرَ خيرُه وعمَّ إحسانه، من عظمته أنَّ بيده ملك العالم العلويِّ والسفليِّ، فهو الذي خلقه ويتصرَّف فيه بما شاء من الأحكام القدريَّة والأحكام الدينيَّة التابعة لحكمته. ومن عظمته كمالُ قدرته التي يقدر بها على كلِّ شيءٍ وبها أوجد ما أوجد من المخلوقات العظيمة؛ كالسماوات والأرض.
{1} "Ametukuka ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote." Yaani, ni Mkuu na ametukuka, na heri yake ni nyingi na wema wake umeenea. Katika ukuu wake ni kwamba mkononi mwake kuna ufalme wa ulimwengu wa juu na wa chini. Yeye ndiye aliyeuumba na anauendesha atakavyo kwa hukumu zake za alizozipanga na za kidini zinazofuata hekima yake. Na miongoni mwa ukuu wake ni ukamilifu wa uwezo wake ambao kupitia kwa huo anaweza kila kitu na kupitia kwa huo ameumba viumbe vikubwa alivyoumba kama vile mbingu na ardhi.
#
{2} و {خَلَقَ الموتَ والحياةَ}؛ أي: قدَّر لعباده أن يُحْييَهم ثم يُميتهم؛ {لِيَبْلُوَكم أيُّكم أحسنُ عملاً}؛ أي: أخلصه وأصوبه، وذلك أنَّ الله خلق عباده وأخرجهم لهذه الدار، وأخبرهم أنَّهم سيُنقلون منها، وأمرهم ونهاهم، وابتلاهم بالشهوات المعارضة لأمره؛ فمن انقاد لأمر الله وأحسن العمل؛ أحسن الله له الجزاء في الدارين، ومن مال مع شهوات النفس ونبذ أمر الله؛ فله شرُّ الجزاء. {وهو العزيز}: الذي له العزَّة كلُّها، التي قهر بها جميع الأشياء وانقادتْ له المخلوقاتُ. {الغفور}: عن المسيئين والمقصِّرين والمذنبين، خصوصاً إذا تابوا وأنابوا؛ فإنَّه يغفر ذنوبهم، ولو بلغتْ عنان السماء، ويستُرُ عيوبهم، ولو كانت ملء الدنيا.
{2} Na "ameumba mauti na uhai." Yaani, amewapangia waja wake kuwafanya kuwa hai kisha atawafisha "ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi." Yaani, vilivyokusudiwa Yeye tu, na vilivyo sahihi zaidi. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaumba waja wake na akawaweka kwenye nyumba hii ya duniani, na akawaambia kuwa watahamishwa kutoka humo, na akawaamrisha na kuwakataza, na akawajaribu kwa matamanio ya nafsi yanayowapingana na amri yake. Kwa hivyo, mwenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na akatenda mema, Mwenyezi Mungu atamlipa malipo mema katika nyumba hizi mbili. Na mwenye kufuata matamanio ya nafsi na akatupa amri ya Mwenyezi Mungu, atampata malipo mabaya kabisa. "Na Yeye ni Mwenye nguvu" ambazo kwazo alikishinda kila kitu, na viumbe vyote vikamnyenyekea. "Mwenye msamaha mno" kwa wale waliofanya mabaya, waliopuuza, waliotenda dhambi, hasa wakitubu na wakamrudia. Basi hapo kwa hakika atawasamehe madhambi yao, hata yakifika kwenye sehemu ya juu zaidi ya mbingu, na zitafunikwa kasoro zao, hata kama ni za kujaza dunia.
#
{3} {الذي خلق سبع سمواتٍ طباقاً}؛ أي: كل واحدةٍ فوق الأخرى، ولسن طبقة واحدة، وخلقها في غاية الحسن والإتقان، {ما ترى في خَلْقِ الرحمن من تفاوتٍ}؛ أي: خلل ونقص، وإذا انتفى النقص من كل وجهٍ؛ صارت حسنةً كاملةً متناسبةً من كلِّ وجه في لونها وهيئتها وارتفاعها وما فيها من الشمس [والقمر] والكواكب النيِّرات الثوابت منهنَّ والسيارات، ولمَّا كان كمالُها معلوماً؛ أمر تعالى بتكرار النظر إليها والتأمُّل في أرجائها؛ قال: {فارجِعِ البصرَ}؛ أي: أعده إليها ناظراً معتبراً، {هل ترى من فُطورٍ}؟ أي: نقص واختلال.
{3} "Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka." Yaani, kila moja ikiwa juu ya nyenzake, na wala si tabaka moja tu, na akaziumba kwa uzuri mkubwa mno na ustadi wa hali ya juu. "Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema." Yaani, huwezi kuona kasoro na upungufu. Na ikiwa upungufu haupo kwa namna yoyote ile, basi unakuwa uumbaji huo ni mzuri mkamilifu, unaolingana sawasawa katika kila njia, katika rangi yake, mwonekano wake, kuinuka juu kwake, na vilivyomo kama vile jua
[na mwezi] na sayari zenye mwangaza. Vile visivyosonga miongoni mwake na vile vinavyosonga. Na pindi ukamilifu wake ulipokua jambo linalojulikana, Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuamuru kuziangalia mara kwa mara na kutafakari katika pande zake.
Akasema: "Hebu rudia kutazama!" Yaani, rudia kutazma kwa kuzingatia. "Je, unaona kosa lolote?"
#
{4} {ثم ارجِعِ البصرَ كرَّتيِن}: [و] المراد بذلك كثرة التكرار، {ينقلبْ إليك البصر خاسئاً وهو حسيرٌ}؛ أي: عاجزاً عن أن يرى خللاً أو فطوراً، ولو حرص غاية الحرص.
{4} "Tena rudia kutazama mara mbili, kutazama kwako kutakurejelea mwenyewe hali ya kuwa kumehizika, kumechoka." Yaani, bila ya kuona kasoro yoyote hata kama utakuwa makini namna gani.
Kisha akataja waziwazi uzuri wake, akasema:
{وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِلشَّيَاطِينِ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ (5) وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (6) إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ (7) تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ (8) قَالُوا بَلَى قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّهُ مِنْ شَيْءٍ إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ (9) وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ (10) فَاعْتَرَفُوا بِذَنْبِهِمْ فَسُحْقًا لِأَصْحَابِ السَّعِيرِ (11)}.
5. Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya chini kabisa kwa mataa, na tumeyafanya ili kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto wenye mwako mkali. 6. Na kwa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo! 7. Watakapotupwa humo, watausikia mngurumo wake na huku inafoka. 8. Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo,
walinzi wake huwauliza: 'Kwani hakukujieni mwonyaji?' 9.
Watasema: 'Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha,
na tukasema: 'Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!'' 10.
Na watasema: 'Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa tukitumia akili, tusingelikuwa katika watu wa Moto wenye mwako mkali!' 11. Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Moto wenye mwako mkali!
#
{5} أي: ولقد جمَّلْنا {السماء الدُّنيا}: التي ترونَها وتليكم، {بمصابيحَ}: وهي النجوم على اختلافها في النور والضياء؛ فإنَّه لولا ما فيها من النُّجوم؛ لكانت سقفاً مظلماً لا حسن فيه ولا جمال، ولكن جعل الله هذه النجوم زينةً للسماء، وجمالاً ونوراً وهدايةً يُهتدى بها في ظلمات البرِّ والبحر، ولا ينافي إخباره أنَّه زيَّن السماء الدُّنيا بمصابيح أن يكون كثيرٌ من النجوم فوق السماوات السبع؛ فإنَّ السماواتِ شفافةٌ، وبذلك تحصل الزينة للسماء الدُّنيا وإن لم تكن الكواكب فيها، {وجعلناها}؛ أي: المصابيح {رجوماً للشياطين}: الذين يريدون استراقَ خبر السماء، فجعل الله هذه النجوم حراسةً للسماء عن تلقُّف الشياطين أخبار الأرض؛ فهذه الشهب التي تُرمى من النُّجوم أعدها الله في الدُّنيا للشياطين، {وأعتدنا لهم}: في الآخرة {عذابَ السعير}: لأنَّهم تمرَّدوا على الله، وأضلُّوا عباده.
{5} Yaani, tumeipamba "mbingu ya chini kabisa" mnayoiona na inayofuatana na dunia yenu, "kwa mataa" ambayo ni nyota zinazotofautiana katika nuru na mwangaza wake. Kwa maana lau si nyota zilizomo ndani yake, basi mbingu ingelikuwa ni dari yenye giza isiyo na uzuri wala urembo. Lakini Mwenyezi Mungu alizifanya nyota hizi kuwa pambo la mbingu, uzuri, nuru, na mwongozo wa kutuongoza katika viza vya nchi kavu na baharini. Na kauli yake kwamba ameipamba mbingu iliyo chini kabisa kwa mataa haipingani na ukweli kwamba kuna nyota nyingi juu ya mbingu ya saba. Kwani mbingu ni kitu kinachoweza kuonyesha kilicho nyuma yake, na kwa hilo linapatikana pambo kwa mbingu ya chini kabisa, hata kama sayari hizo hazimo ndani yake. "Na tumeyafanya;" yaani, mataa haya kuwa kitu cha "kuwapigia mashetani" ambao wanataka kusikiliza kwa siri habari za mbinguni. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akazifanya nyota hizi kuwa ni ulinzi wa mbingu kutokana na mashetani kuiba habari za mbinguni na kupeleka dunia. Basi vimondo hivi vya nyota vinavyorushwa vimetayarishwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kwa ajili ya mashetani, "na tumewaandalia" huko Akhera "adhabu ya Moto wenye mwako mkali," kwa sababu walimuasi Mwenyezi Mungu na wakawapoteza waja wake.
#
{6} ولهذا كان أتباعهم من الكفار مثلهم قد أعدَّ الله لهم عذاب السعير؛ فلهذا قال: {وللذين كفروا بربِّهم عذابُ جهنَّم وبئس المصير}: التي يُهان بها أهلُها غايةَ الهوان.
{6} Ndiyo maana wafuasi wao miongoni mwa makafiri ni mfano wao, Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu ya Moto wenye mwako mkali.
Ndiyo maana akasema: "Na kwa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu yalioje hayo," ambayo wakazi wake watadhalilishwa huko kukadhilishwa kukubwa kabisa.
#
{7} {إذا أُلقوا فيها}: على وجه الإهانةِ والذُّلِّ، {سمعوا لها شهيقاً}؛ أي: صوتاً عالياً فظيعاً.
{7} "Watakapotupwa humo" kwa njia ya kudunishwa na kufedheheshwa "watausikia mngurumo wake na huku inafoka."
#
{8} {تكادُ تَمَيَّزُ من الغيظِ}؛ أي: تكاد على اجتماعها أن يفارق بعضها بعضاً وتتقطَّع من شدة غيظها على الكفار؛ فما ظنُّك ما تفعل بهم إذا حُصِّلُوا فيها؟! ثم ذكر توبيخ الخزنة لأهلها، فقال: {كلَّما أُلقي فيها فوجٌ سألهم خَزَنَتُها ألم يأتِكُم نذيرٌ}؛ أي: حالكم هذه واستحقاقكم النار كأنكم لم تخبَّروا عنها ولم تحذِّرْكم النذرُ منها.
{8} "Inakaribia kupasuka kwa hasira" yake juu ya makafiri. Basi unadhani watakapoingia humo itawafanyia nini? Kisha akataja karipio la walinzi wake kwa wale walioingia humo,
akasema: “Kila mara likitupwa kundi humo,
walinzi wake huwauliza: 'Kwani hakukujieni mwonyaji?'" Yaani, hali yenu hii na kustahiki kwenu huku kuingia Motoni ni kana kwamba hamkufahamishwa kuhusu hilo wala waonyaji hawakukutahadharisheni dhidi yake.
#
{9} {قالوا بلى قد جاءنا نذيرٌ فكذَّبنا وقُلْنا ما نَزَّلَ الله من شيءٍ إن أنتُم إلاَّ في ضلالٍ كبيرٍ}: فجمعوا بين تكذيبهم الخاص والتكذيب العامِّ بكلِّ ما أنزل الله، ولم يكفهم ذلك، حتى أعلنوا بضلال الرُّسل المنذرين، وهم الهداة المهتدون، ولم يكتفوا بمجرَّد الضلال، بل جعلوا ضلالهم ضلالاً كبيراً؛ فأيُّ عنادٍ وتكبُّر وظلم يشبه هذا؟!
{9} "Watasema: 'Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha,
na tukasema: 'Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!" Basi wakawa wamejumuisha kati ya kukadhibisha kwao mahususi na kukadhibisha kwao kwa jumla yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, na pia hilo halikuwatosha, mpaka walipotangaza upotovu wa Mitume waonyaji, ilhali wao ndio waongofu wanaoongoza, na tena haikuwatosha kuona kwamba Mitume hao ni wapotofu tu, bali waliona kwamba wako katika upotofu mkubwa. Je, ni ukaidi upi, na kiburi kipi, na dhuluma ipi inayofanana na hayo?
#
{10} {وقالوا}: معترفين بعدم أهليَّتهم للهدى والرشاد: {لو كنَّا نسمعُ أو نعقِلُ ما كنَّا في أصحاب السَّعير}: فنفَوْا عن أنفسهم طرق الهدى، وهي السمع لما أنزل الله وجاءتْ به الرسل، والعقلُ الذي ينفع صاحبَه ويوقفُه على حقائق الأشياء وإيثار الخير والانزجار عن كلِّ ما عاقبته ذميمةٌ، فلا سمعَ لهم ولا عقلَ. وهذا بخلاف أهل اليقين والعرفان وأرباب الصدق والإيمان؛ فإنَّهم أيَّدوا إيمانهم بالأدلَّة السمعيَّة، فسمعوا ما جاء من عند الله وجاء به رسولُ الله علماً ومعرفةً وعملاً، والأدلَّة العقليَّة المعرِّفة للهدى من الضَّلال، والحسن من القبيح، والخير من الشرِّ، وهم في الإيمان بحسب ما منَّ الله عليهم به من الاقتداء بالمعقول والمنقول؛ فسبحان مَن يختصُّ بفضله مَن يشاء، ويمنُّ على مَن يشاء من عباده، ويخذل مَن لا يصلُحُ للخير.
{10} "Na watasema" wakikiri kutostahiki kwao uwongofu na kuelekea kisawasawa, "Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa tukitumia akili, tusingelikuwa katika watu wa Moto wenye mwako mkali!" Basi wakawa wamejikanushia njia za uwongofu, ambazo ni kusikia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na wakaja nayo Mitume, na akili inayomnufaisha mwenyewe na kumfahamisha uhakika wa mambo na kupendelea heri na kukomeka mbali na yote yenye mwisho wa kukashifiwa. Kwa hivyo hawakuweza kusikia wala hawakuweza kutumia akili. Hili ni kinyume na watu wa yakini na elimu na mabwana wa ukweli na imani. Kwani waliiunga mkono imani yao kwa ushahidi wa kusikia, basi wakayasikia yaliyotoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ya elimu, maarifa na matendo, na pia ushahidi wa kiakili unaojulisha na kutofautisha kati ya uongofu na upotofu, uzuri na ubaya, heri na uovu, nao katika imani yao wako kulingana na yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu ya kufuata yale yaliyowafikia kwa njia ya kiakili na kwa njia ya kimaandiko. Basi ametakasika yule anayempa amtakaye tu fadhila zake, na kumneemesha amtakaye katika waja wake, na anawaachilia mbali wasioifailia heri.
#
{11} قال تعالى عن هؤلاء الدَّاخلين للنار المعترفين بظلمهم وعنادهم: {فاعْتَرَفوا بذَنبِهِم فسُحقاً لأصحاب السَّعير}؛ أي: بعداً لهم وخسارةً وشقاءً؛ فما أشقاهم وأرداهم؛ حيث فاتهم ثواب الله، وكانوا ملازمين للسعير التي تستعر في أبدانهم، وتَطَّلِعُ على أفئدتهم.
{11} Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu hao watakaoingia Motoni waliokiri dhuluma yao na ukaidi wao: "Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Moto wenye mwako mkali!" Basi hao ni wenye wana mashakani makubwa yaliyoje na walio katika maangamivu makubwa yaliyoje, ambapo walikosa thawabu za Mwenyezi Mungu, na wakawa katika wale watakaodumu katika moto wenye mwako mkali ambao mwako wake utachoma mno miili yao na kufikia mioyo yao.
{إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ بِالْغَيْبِ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ (12)}.
12. Hakika wale wanaomwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu, watapata maghfira na ujira mkubwa.
#
{12} لما ذكر حالة الأشقياء الفجَّار؛ ذكر وصف الأبرار السعداء ، فقال: {إنَّ الذين يخشَوْنَ ربَّهم بالغيب}؛ أي: في جميع أحوالهم، حتى في الحالة التي لا يطَّلع عليهم فيها إلاَّ الله؛ فلا يقدِمون على معاصيه، ولا يقصِّرون عمَّا أمرهم به. {لهم مغفرةٌ}: لذنوبهم، وإذا غَفَرَ الله ذنوبَهم؛ وقاهم شرَّها ووقاهم عذاب الجحيم. {ولهم أجرٌ كبيرٌ}: وهو ما أعدَّه الله لهم في الجنة من النعيم المقيم والملك الكبير واللذَّاتِ المتواصلات والقصور والمنازل العاليات والحور الحسان والخدم والولدان، وأعظم من ذلك وأكبر، رضا الرحمن الذي يُحِلُّه على ساكني الجنان.
{12} Alipotaja hali ya watu wa mashakani, walio waovu, akataja maelezo ya watu wema wenye furaha,
akasema: "Hakika wale wanaomwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu." Yaani, katika hali zao zote, hata katika hali ambayo hawezi akawaona isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, hawamfanyii maasia, wala hawafanyi chini ya namna alivyowaamrisha. "Watapata maghfira" ya dhambi zao, na ikiwa Mwenyezi Mungu atawasamehe dhambi zao, atawalinda kutokana na uovu wake na atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu "na wana ujira mkubwa." Na hayo ni yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu katika bustani za mbinguni ya neema ya kudumu, na ufalme mkubwa, na starehe zenye kuendelea kuwafikia, na makasri na majumba yaliyoinuka juu, na hurulaini wazuri, na wajakazi na watoto wadogo, na kubwa zaidi kuliko hilo ni radhi za Mwingi wa rehema ambazo atawapa wakazi wa bustani za mbinguni.
{وَأَسِرُّوا قَوْلَكُمْ أَوِ اجْهَرُوا بِهِ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (13) أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ (14)}.
13. Na ficheni kauli zenu, au zidhihirisheni wazi; hakika Yeye anajua mno yaliyomo vifuani. 14. Asijue yule aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?
#
{13} هذا إخبارٌ من الله بسعة علمه وشمول لطفه، فقال: {وأسِرُّوا قولَكم أو اجْهَروا به}؛ أي: كلّها سواءٌ لديه لا يخفى عليه منها خافيةٌ، فَـ {إنَّه عليمٌ بذات الصُّدور}؛ أي: بما فيها من النيَّات والإرادات؛ فكيف بالأقوال والأفعال التي تُسمع وتُرى؟!
{13} Huku ni kujulisha anakojulisha Mwenyezi Mungu juu ya upana wa elimu yake, na ujumuishaji wa upole wake. Akasema, "Na ficheni kauli zenu, au zidhihirisheni wazi." Yaani, yote hayo ni kitu kimoja kwake, hakuna chochote kinachofichikana kwake katika hayo. Kwani, "hakika Yeye anajua mno yaliyomo vifuani." Yaani, yaliyomo ya nia mbalimbali na utashi. Basi vipi kuhusu maneno na vitendo vinavyosikika na kuonekana?
#
{14} ثم قال مستدلًّا بدليل عقليٍّ على علمه: {ألا يعلمُ مَنْ خَلَقَ}؛ فمن خَلَقَ الخلقَ وأتقنه وأحسنه؛ كيف لا يعلمه؟! {وهو اللطيفُ الخبيرُ}: الذي لطف علمه وخبره، حتى أدرك السرائر والضمائر والخبايا والخفايا والغيوب، {وهو الذي يعلمُ السِّرَّ وأخفى}، ومن معاني اللطيف أنَّه الذي يَلْطُفُ بعبدِهِ ووليِّه، فيسوق إليه البِرَّ والإحسان من حيث لا يشعر، ويعصِمُه من الشرِّ من حيث لا يحتسب، ويرقِّيه إلى أعلى المراتب بأسبابٍ لا تكون من العبد على بالٍ، حتى إنَّه يذيقُه المكارِهَ ليوصله بها إلى المحابِّ الجليلة والمطالب النبيلة.
{14} Kisha akasema akibainisha ushahidi wa kiakili juu ya elimu yake: "Asijue yule aliyeumba." Vipi asivijue yule aliyeumba viumbe, akavikamilisha sawasawa na akaviumba kuwa vizuri zaidi, vipi asivijue "naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?" Ambaye ujua wake na kuwa kwake na habari ya kila kitu kunafikia kila kitu, kiasi kwamba anafahamu vyema siri, dhamiri, vilivyofichikana na ghaibu zote. Na Yeye ndiye "anayejua siri na kilicho chini zaidi kuliko siri." Na katika maana za Al-Latwif
(Mpole), ni kwamba Yeye ndiye mwenye kumfanyia upole mja wake na kipenzi chake, kwa hivyo unamfikishia wema na ukarimu kutokea pale asipotambua, na anamkinga mbali na uovu kutokea pale asipotarajia, na anampandisha daraja za juu kwa sababu ambazo hata mja mwenyewe hazijui, kiasi kwamba humwonjesha mambo anayochukia ili amfikishe kwenye mapenzi makubwa na mambo matukufu yanayotafutwa.
{هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِنْ رِزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ (15)}.
15. Yeye ndiye aliyeidhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndiyo kufufuliwa.
#
{15} أي: هو الذي سخَّر لكم الأرضَ وذَلَّلها؛ لتدرِكوا منها كلَّ ما تعلقت به حاجتُكم من غرسٍ وبناءٍ وحرثٍ وطرقٍ يُتَوَصَّلُ بها إلى الأقطار النائية والبلدان الشاسعة، {فامشوا في مناكِبِها}؛ أي: لطلب الرزق والمكاسب، {وكُلوا من رزقِهِ وإليه النشورُ}؛ أي: بعد أن تنتقلوا من هذه الدار التي جَعَلَها الله امتحاناً وبلغةً يُتَبَلَّغُ بها إلى الدار الآخرة؛ تُبعثون بعد موتكم وتُحشرون إلى الله؛ ليجازِيَكم بأعمالكم الحسنة والسيئة.
{15} Yaani, yeye ndiye aliyeitiisha ardhi kwa ajili yenu na akaifanya kuwa dhalili. Ili mpate kutoka kwayo yale yanayofungana na mahitaji yenu kama vile kupanda mimea, kujenga, kulima, na njia ambazo kwazo inawezekana kufika katika pande na nchi za mbali mno. "Basi tembeeni katika pande zake" ili mtafute riziki na kuchuma. "Na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa." Yaani, baada ya kutoka katika nyumba hii ambayo Mwenyezi Mungu ameifanyia mtihani na cha kuwafikishia nyumba ya Akhera, mtafufuliwa baada ya kufa kwenu na mtakusanywa kwa Mwenyezi Mungu; ili awalipe kwa matendo yenu mema na mabaya.
{أَأَمِنْتُمْ مَنْ فِي السَّمَاءِ أَنْ يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ (16) أَمْ أَمِنْتُمْ مَنْ فِي السَّمَاءِ أَنْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ (17) وَلَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ (18)}.
16. Je, mmesalimika kutokana na aliyeko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika! 17. Au mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Basi mtajua vipi maonyo yangu? 18. Na bila ya shaka walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao; basi kulikuwaje kukasirika kwangu?
#
{16} هذا تهديدٌ ووعيدٌ لمن استمرَّ في طغيانه وتعدِّيه وعصيانه الموجب للنَّكال وحلول العقوبة، فقال: {أأمنتُم مَن في السَّماء}: وهو الله تعالى العالي على خلقه، {أن يخسِفَ بكم الأرضَ فإذا هي تمورُ}: بكم وتضطربُ حتى تَهْلِكوا وتَتْلَفوا.
{16} Hili ni tishio na ahadi ya adhabu kwa anayeendelea na kupotoka kwake, kuvuka mipaka na uasi wake, ambao unamsababishia mateso na kufikiwa na adhabu.
Akasema: "Je, mmesalimika kutokana na aliyeko juu" ambaye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliye juu ya viumbe vyake, "kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na tahamaki hiyo inatikisika" pamoja nanyi, na kuyumbayumba ili muangamie na mharibike kabisa?
#
{17 - 18} {أم أمنتُم مَن في السماء أن يرسلَ عليكم حاصباً}؛ أي: عذاباً من السماء يحصِبُكم وينتقمُ الله منكم، {فستعلمون كيف نذيرِ}؛ أي: كيف يأتيكم ما أنذرتْكُم به الرسل والكتب؛ فلا تحسَبوا أنَّ أمنكم من الله أن يعاقِبَكم بعقابٍ من الأرض ومن السماء ينفعُكم، فستجدون عاقبة أمرِكم سواءً طال عليكم الأمدُ أو قَصُرَ؛ فإنَّ مَن قبلكم كذَّبوا كما كذَّبتم، فأهلكهم الله تعالى؛ فانظُروا كيف إنكارُ الله عليهم؛ عاجلهم بالعقوبة الدنيويَّة قبل عقوبة الآخرة؛ فاحذَروا أن يصيبَكم ما أصابَهم.
{17 - 18} "Au mnadhani mko salama kutokana na aliyeko juu ya kuwa Yeye hatakupelekeeni kimbunga chenye changarawe" ili Mwenyezi Mungu akulipizeni kisasi? "Basi mtajua vipi maonyo yangu?" Yaani, mtajua namna yatavyokufikieni yale waliyokuhadharisheni Mitume na Vitabu? Kwa hivyo, msidhani kwamba kutawanufaisha kitu kusalimika kwenu kutokana na Mwenyezi Mungu ni kukuadhibuni kwa adhabu kutoka ardhini na kutoka mbinguni. Kwani mtapata mwisho wa mambo yenu ukiwa mbaya mno sawa muda wenu uwe mrefu au mfupi. Kwa maana wale waliokuwa kabla yenu walikadhibisha kama mlivyokadhibisha, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaangamiza. Basi tazameni jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaonya. Aliwaharakishia adhabu ya duniani kabla ya adhabu ya Akhera. Basi jihadhari yasije yakakupateni yale yaliyowapata.
{أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَنُ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ (19)}.
19. Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyozikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona mno kila kitu.
#
{19} وهذا عتابٌ وحثٌّ على النظر إلى حالة الطير التي سخَّرها الله وسخَّر لها الجوَّ والهواء؛ تصفُّ فيه أجنحتها للطيران وتقبِضُها للوقوع، فتظلُّ سابحةً في الجوِّ متردِّدة فيه بحسب إرادتها وحاجتها، {ما يمسِكُهُنَّ إلاَّ الرحمنُ}: فإنَّه الذي سخَّر لهنَّ الجوَّ وجعل أجسادها وخلقتها في حالة مستعدةٍ للطيران؛ فمن نظر في حالة الطير واعتبر فيها؛ دلَّتْه على قدرة الباري وعنايته الربانيَّة، وأنَّه الواحدُ الأحدُ الذي لا تنبغي العبادة إلاَّ له. {إنَّه بكلِّ شيءٍ بصيرٌ}: فهو المدبِّر لعباده بما يليق بهم وتقتضيه حكمته.
{19} Hii ni lawama na kuhimiza kuangalia hali ya ndege aliowatiisha Mwenyezi Mungu na akawatiishia anga na hewa. Wao hutandaza ndani yake mbawa zao ili waruke na wanazibana ili wasimame, basi hubaki wakipaa angani wakienda huku na kule ndani yake kulingana na mapenzi na mahitaji yao. "Hawashikilii ila Mwingi wa rehema" Yeye ndiye aliyewatiishia anga, na akaifanya miili yao na mbawa zao kuwa tayari kwa ajili ya kupaa. Kwa hivyo, mwenye kutazama hali ya ndege na kuizingatia, hilo litamwelekeza kwenye uwezo wa Muumba na uangalizi wake wa kiungu, na kwamba Yeye ni Mmoja na wa Pekee, ambaye haifai kuabudu isipokuwa Yeye. "Hakika Yeye ni Mwenye kuona mno kila kitu." Yeye ndiye anayewaendesha waja wake kulingana na yale yanayowafailia na kulingana na hekima yake.
{أَمَّنْ هَذَا الَّذِي هُوَ جُنْدٌ لَكُمْ يَنْصُرُكُمْ مِنْ دُونِ الرَّحْمَنِ إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ (20) أَمَّنْ هَذَا الَّذِي يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُ بَلْ لَجُّوا فِي عُتُوٍّ وَنُفُورٍ (21)}.
20. Au ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema? Hakika makafiri hawamo ila katika udanganyifu. 21. Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao wanakakamia tu katika jeuri na kujiweka mbali.
#
{20} يقول تعالى للعتاة النافرين عن أمره، المعرضين عن الحقِّ: {أمّن هذا الذي هو جندٌ لكم ينصُرُكم من دونِ الرحمن}؛ أي: ينصُرُكم إذا أرادَ الرحمن بكم سوءاً فيدفعه عنكم؛ أي: من الذي ينصُرُكم على أعدائكم غير الرحمن؛ فإنَّه تعالى هو الناصر المعزُّ المذلُّ، وغيره من الخلق لو اجتمعوا على نصر عبدٍ لم ينفعوه بمثقال ذرَّةٍ على أيِّ عدوٍّ كان؛ فاستمرارُ الكافرين على كفرهم بعد أن عَلِموا أنَّه لا ينصُرُهم أحدٌ من دون الرحمن غرورٌ وسفهٌ.
{20} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia wale wanaoikataa amri yake na wakaiacha haki: "Au ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema" ikiwa atakutakieni mabaya akawaondoleeni hayo? Yaani, ni nani atakayekusaidieni dhidi ya maadui zenu kando na Mwingi wa Rehema? Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayesaidia, mwenye kutukuza na kufedhehesha. Na wasiokuwa Yeye miongoni mwa viumbe kama wangeungana pamoja ili kumsaidia mja, hawangemnufaisha kwa uzito wa chembe dhidi ya adui yeyote yule. Kwa hivyo, kuendelea kwa makafiri juu ya ukafiri wao baada ya kujua kwamba hakuna wa kuwanusuru isipokuwa Mwingi wa Rehema ni kudanganyika na ni upumbavu.
#
{21} {أمّن هذا الذي يرزقُكُم إن أمسَكَ رزقَه}؛ أي: الرزق كلُّه من الله؛ فلو أمسك عنكم الرزق؛ فمن الذي يرسله لكم؟ فإنَّ الخلق لا يقدرون على رزق أنفسِهِم؛ فكيف بغيرهم؟! فالرازق المنعم الذي لا يصيب العبادَ نعمةٌ إلاَّ منه هو الذي يستحقُّ أن يُفْرَدَ بالعبادة، ولكنْ الكافرون {لَجُّوا}؛ أي: استمروا {في عُتُوٍّ}؛ أي: قسوةٍ وعدم لينٍ للحق، {ونُفورٍ}؛ أي: شرودٍ عن الحقِّ.
{21} "Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake?" Yaani, riziki zote zimetoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kama akikunyimeni riziki, basi ni nani anayeweza kuiachilia ikawafikia? Kwa maana, viumbe hawana uwezo wa kujiruzuku. Basi vipi watawaruzuku wengine? Kwa hivyo, Mwenye kuruzuku, Mwenye kuneemesha, ambaye haiwafikii neema waja isipokuwa huwa imetoka kwake, ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, lakini makafiri "wanakakamia tu katika jeuri" na kutolainika mbele ya haki "na kujieka mbali" na haki hiyo.
{أَفَمَنْ يَمْشِي مُكِبًّا عَلَى وَجْهِهِ أَهْدَى أَمَّنْ يَمْشِي سَوِيًّا عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (22)}.
22. Je, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawasawa katika Njia iliyonyooka?
#
{22} أي: أيُّ الرجلين أهدى؛ من كان تائهاً في الضَّلال غارقاً في الكفر قد انتكس قلبه فصار الحقُّ عنده باطلاً والباطل حقًّا، ومن كان عالماً بالحقِّ، مؤثراً له، عاملاً به، يمشي على الصراط المستقيم في أقواله وأعماله وجميع أحواله؟! فبمجرَّد النظر إلى حال الرجلين؛ يعلم الفرق بينهما والمهتدي من الضالِّ منهما. والأحوالُ أكبرُ شاهدٍ من الأقوال.
{22} Yaani ni yupi kati ya wanaume hawa wawili ndiye aliyeongoka zaidi? Yule ambaye amepotelea katika upotofu na akazama katika ukafiri, moyo wake tayari umeshabadilika, kwa hivyo haki kwake ikawa ndiyo batili, nayo batili ikawa ndiyo haki, ama yule anayeijua haki, akaipendelea, akaifanyia kazi, na akawa anatembelea katika njia iliyonyooka katika maneno yake, matendo yake, na hali zake zote? Kwa kuangalia tu hali ya wanaume hao wawili, inajulikana tafauti baina yao na kujulikana yule aliyeongoka na aliyepotea. Na hali ni ushahidi mkubwa zaidi kuliko maneno.
{قُلْ هُوَ الَّذِي أَنْشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ قَلِيلًا مَا تَشْكُرُونَ (23) قُلْ هُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ (24) وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْوَعْدُ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (25) قُلْ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِنْدَ اللَّهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُبِينٌ (26)}.
23.
Sema: Yeye ndiye aliyekuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu. 24.
Sema: Yeye ndiye aliyekutawanyeni katika ardhi, na kwake mtakusanywa. 25.
Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema ukweli? 26.
Sema: Hakika elimu ya hayo iko kwa Mwenyezi Mungu; na hakika mimi ni mwonyaji wa wazi tu mwenye kubainisha.
#
{23} يقول تعالى مبيِّناً أنَّه المعبودُ وحدَه وداعياً عباده إلى شكره وإفراده بالعبادة: {هو الذي أنشأكم}؛ أي: أوجدكم من العدم؛ من غير معاونٍ له ولا مظاهر، ولما أنشأكم؛ كمَّل لكم الوجود بالسمعِ والأبصارِ والأفئدةِ، وهذه الثلاثة هي أفضل أعضاء البدن وأكمل القوى الجسمانيَّة، ولكنَّكم مع هذا الإنعام {قليلاً ما تشكُرون} الله، قليلٌ منكم الشاكر، وقليلٌ منكم الشكر.
{23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akieleza kuwa Yeye pekee ndiye anayefaa kuabudiwa,
na kuwalingania waja Wake kumshukuru na kumpwekesha katika ibada: "Yeye ndiye aliyekuumbeni" baada ya kutokuwa kwenu kitu; bila ya msaidizi yeyote, na alipokuumbeni, akakukamilishieni kuwepo kwenu kwa kuwapa uwezo wa kusikia, kuona, na mioyo. Na hivi vitatu ndivyo viungo bora kabisa vya mwili na nguvu kamili za mwili, lakini nyinyi pamoja na neema hizi, "Ni kidogo kabisa shukrani zenu."
#
{24} {قل هو الذي ذَرَأكُم في الأرض}؛ أي: بثَّكم في أقطارها، وأسكنَكم في أرجائها، وأمركم ونهاكم، وأسدى عليكم من النِّعم ما به تنتفعون، ثم بعد ذلك يحشُرُكم ليوم القيامةِ، ولكنَّ هذا الوعد بالجزاء ينكِرُه هؤلاء المعاندون.
{24} "Sema: Yeye ndiye aliyekutawanyeni katika ardhi" katika maeneo yake, na akakuwekeni kuishi katika pande zake, na akawaamrisheni na akakukatazeni, na akakumiminieni neema mnazofaidika kwazo, kisha baada ya hayo atakukusanyeni Siku ya Kiyama, lakini ahadi hii ya kuwalipa wanaipinga watu hawa wakaidi.
#
{25} {ويقولون}: تكذيباً: {متى هذا الوعدُ إن كنتُم صادقينَ}؟ جعلوا علامة صدقِهِم أنْ يُخْبِروهم بوقت مجيئِهِ، وهذا ظلمٌ وعنادٌ.
{25} "Na wanasema" kwa njia ya kukadhibisha: "Lini ahadi hii, ikiwa mnasema ukweli?" Walifanya kuwaambia kwao wakati wa kuja kwake ati ndiyo alama ya ukweli wao, na hii ni dhuluma na ukaidi.
#
{26} فإنما {العلم عند الله}: لا عند أحدٍ من الخلق، ولا ملازمة بين هذا الخبر وبين الإخبار بوقته؛ فإنَّ الصدق يُعْرَفُ بأدلَّته، وقد أقام الله من الأدلَّة والبراهين على صحَّته ما لا يبقى معه أدنى شكٍّ لمن ألقى السمع وهو شهيدٌ.
{26} Kwa maana "hakika elimu ya hayo iko kwa Mwenyezi Mungu tu." Si kwa yeyote miongoni mwa viumbe vyote, na hakuna uhusiano wowote baina ya habari hii na kutoa kwao
(Mitume) habari za kuja kwake. Kwa maana ukweli unajulikana kwa ushahidi wake, na tayari Mwenyezi Mungu ameshaweka ushahidi huo na uthibitisho wa usahihi wake ambao haiwezi kubakia shaka yoyote pamoja nao kwa yule anayetega sikio naye yuko anashuhidia sawasawa.
{فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَقِيلَ هَذَا الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تَدَّعُونَ (27) قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِيَ اللَّهُ وَمَنْ مَعِيَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَنْ يُجِيرُ الْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ (28) قُلْ هُوَ الرَّحْمَنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (29) قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَاؤُكُمْ غَوْرًا فَمَنْ يَأْتِيكُمْ بِمَاءٍ مَعِينٍ (30)}.
27. Lakini watakapoiona karibu, nyuso za wale waliokufuru zitahuzunishwa,
na itasemwa: Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba mno. 28.
Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu ataniangamiza mimi na wale walio pamoja nami, au akiturehemu, ni nani atakayewalinda makafiri mbali na adhabu chungu? 29.
Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Basi mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhahiri. 30.
Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, ni nani atakueleteeni maji yanayomiminika?
#
{27} يعني أنَّ محلَّ تكذيب الكفار وغرورهم به حين كانوا في الدُّنيا؛ فإذا كان يوم الجزاء، ورأوا العذاب منهم {زُلْفَةً}؛ أي: قريباً؛ ساءهم ذلك وأفظعهم وأقلقهم ، فتغيَّرت لذلك وجوهُهم، ووُبِّخوا على تكذيبهم، وقيل لهم: {هذا الذي كنتُم به تَدَّعونَ}: فاليوم رأيتموه عياناً، وانْجلى لكم الأمر، وتقطَّعت بكم الأسباب، ولم يبقَ إلاَّ مباشرة العذاب.
{27} Maana yake ni kwamba mahali walipokanushwa makafiri na wakadanganyika napo ni wakati walipokuwa katika dunia hii. Lakini itakapofika Siku ya Malipo, wataiona adhabu "karibu" sana nao, na hilo litawahuzunisha, kuwatisha mno na kuwatia wasiwasi, na nyuso zao zitabadilika kwa sababu yake, na watakemewa kwa sababu ya kukanusha kwao,
na wataambiwa: "Hayo ndiyo mliyokuwa mkiyaomba mno." Leo mmeiona kwa macho yenu, na jambo hilo limekwisha kubainikieni wazi, na njia za mahusiano zenu zimeshakukatikieni, na hakikubakia isipokuwa kuikabili adhabu.
#
{28} ولما كان المكذِّبون للرسول - صلى الله عليه وسلم - الذين يردُّون دعوته ينتظرون هلاكَه ويتربَّصون به ريب المنون؛ أمره الله أن يقولَ لهم: إنَّكم وإن حصلتْ لكم أمنيتُكم و {أهلكني الله ومن معي}: فليس ذلك بنافع لكم شيئاً؛ لأنَّكم كفرتم بآيات الله، واستحققتُم العذاب؛ فمن يجيرُكم {من عذابٍ أليم}: قد تحتَّم وقوعُه بكم؛ فإذاً تعبُكم وحرصُكم على هلاكي غير مفيدٍ ولا مجدٍ لكم شيئاً.
{28} Na kwa vile wale waliomkadhibisha Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - wale walioukataa wito wake wanamngojelea kuangamia, na wanamtarajia kupatilizwa na siku zinaposonga,
Mwenyezi Mungu akamwamrisha kuwaambia: 'Hakika nyinyi hata kama matamanio yenu yatatimia, na "Mwenyezi Mungu akaniangamiza mimi na wale walio pamoja nami" hilo halitakuwa na faida yoyote kwenu. Kwa sababu mlizikufuru Aya za Mwenyezi Mungu, na mkastahiki adhabu. Basi ni nani atakayekuepusheni "mbali na adhabu chungu" ambayo tayari imeshakuwa lazima itakufikieni. Kwa hivyo, juhudi zenu na hamu yenu kubwa ya kuona nikiangamia haina faida yoyote kwenu.
#
{29} ومن قولهم: إنَّهم على هدى والرسول على ضلالٍ؛ أعادوا في ذلك وأبدوا، وجادلوا عليه وقاتلوا، فأمر الله نبيَّه أن يُخْبِرَ عن حاله وحال أتباعه ما به يتبيَّن لكلِّ أحدٍ هداهم وتقواهم، وهو أنْ يقولوا: {آمنَّا به وعليه تَوَكَّلْنا}: والإيمانُ يشملُ التصديق الباطن والأعمال الباطنة والظاهرة، ولمَّا كانت الأعمالُ وجودُها وكمالُها متوقفة على التوكُّل؛ خصَّ الله التوكُّل من بين سائر الأعمال، وإلاَّ؛ فهو داخلٌ في الإيمان، ومن جملة لوازمه؛ كما قال تعالى: {وعلى الله فتوكَّلوا إن كُنتُم مؤمنينَ}؛ فإذا كانت هذه حال الرسول وحال مَن اتَّبعه، وهي الحال التي تتعيَّن للفلاح وتتوقَّف عليها السعادة، وحالة أعدائه بضدِّها؛ فلا إيمان لهم ولا توكُّل؛ عُلِمَ بذلك مَن هو على هدىً ومن هو في ضلال مبينٍ.
{29} Na kutokana na kusema kwao: 'Hakika wao wako kwenye uwongofu, naye Mtume amepotea' na wakairudia na kuiendeleza, na wakajadili juu yake na wakapigana vita. Basi Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwajulisha kuhusu hali yake na hali ya wafuasi wake, ambayo kwayo uwongofu wao na uchamungu wao utadhihirika kwa kila mtu, ambayo ni kwamba waseme, "tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea." Na imani inajumuisha kusadiki kwa ndani na matendo ya ndani na nje. Na kwa kuwa kupatikana kwa matendo na ukamilifu wake kunasimama juu ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akachagua suala la kumtegemea kati ya matendo mengine yote. Vinginevyo, huko pia kunaingia katika imani, na ni miongoni mwa mahitaji yake,
kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini." Kwa hiyo, ikiwa hii ndiyo hali ya Mtume na hali ya waliomfuata, nayo ndiyo hali inayotakiwa ili mtu afaulu na kupata furaha kunategemea juu yake, na hali ya maadui zake ni kinyume chake, kwani wao hawana imani wala kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi kwa hilo inajulikana ni nani yuko kwenye uwongofu na ni nani yuko katika upotofu ulio wazi.
#
{30} ثم أخبر عن انفراده بالنِّعم، خصوصاً الماء الذي جَعَلَ الله منه كلَّ شيءٍ حيٍّ، فقال: {قل أرأيتُم إن أصبحَ ماؤكم غَوْراً}؛ أي: غائراً، {فمن يأتيكم بماءٍ مَعينٍ}: تشربون منه وتسقونَ أنعامكم وأشجارَكم وزُروعكم؟ وهذا استفهامٌ بمعنى النفي؛ أي: لا يقدر أحدٌ على ذلك غير الله تعالى.
{30} Kisha akajulisha kwamba Yeye tu ndiye mwenye neema zote, hasa maji ambayo kwayo Mwenyezi Mungu aliumba kila kiumbe kilicho uhai,
akasema: "Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, ni nani atakueleteeni maji yanayomiminika," ambayo kwayo mtakunywa na kuwanywesha mifugo wenu, miti yenu na mimea yenu? Huku ni kuuliza kwenye maana ya kukanusha. Yaani, hakuna awezaye kufanya hivyo isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu.
Imekamilika tafsiri ya surat Al-Mulk, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.