Tafsiri ya surat Al-Haqqa
Tafsiri ya surat Al-Haqqa
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{الْحَاقَّةُ (1) مَا الْحَاقَّةُ (2) وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ (3) كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ (4) فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ (5) وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ (6) سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَى كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ (7) فَهَلْ تَرَى لَهُمْ مِنْ بَاقِيَةٍ (8)}.
1. Tukio la haki. 2. Nini hilo Tukio la haki? 3. Na nini kitakujulisha nini hilo Tukio la haki? 4. Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unaositusha. 5. Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. 6. Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usiozuilika. 7. Aliowapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yaliyo wazi ndani. 8. Basi je! Unamwona mmoja wao aliyebaki?
#
{1 - 3} {الحاقَّة}: من أسماء يوم القيامة؛ لأنَّها تحقُّ وتنزل بالخلق وتظهر فيها حقائق الأمور ومخبآت الصدور؛ فعظَّم تعالى شأنها وفخَّمه بما كرَّره من قوله: {الحاقَّة. ما الحاقَّة. وما أدراك ما الحاقَّة}؛ فإنَّ لها شأناً عظيماً وهولاً جسيماً.
«ومن عظمتها أن الله أهلك الأمم المكذبة بها بالعذاب العاجل».
{1 - 3} "Tukio la haki" ni katika majina ya Siku ya Kiyama; kwa sababu ni la kweli na litateremka juu ya viumbe, na ndani yake uhakika wa mambo na yale yote yaliyofichika ya vifuani yatadhihirika.
Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaitukuza hadhi yake na kuifanya kuwa kubwa mno kwa kurudia suala hili katika kauli yake: “Tukio la haki. Nini hilo Tukio la haki? Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?” Kwani ni jambo kubwa na lina mahangaiko makubwa.
“Na katika ukuu wake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliangamiza mataifa yaliyoikanusha kwa adhabu ya haraka.”
#
{4} ثم ذكر نموذجاً من أحوالها الموجودة في الدُّنيا المشاهدة فيها، وهو ما أحلَّه من العقوبات البليغة بالأمم العاتية، فقال: {كذَّبتْ ثمودُ}: وهم القبيلةُ المشهورةُ سكان الحِجْر الذين أرسل الله إليهم رسوله صالحاً عليه السلام؛ ينهاهم عمَّا هم عليه من الشِّرك ويأمرهم بالتوحيد، فردُّوا دعوته، وكذَّبوه، وكذَّبوا ما أخبر به من يوم القيامةِ، وهي القارعة التي تقرع الخَلْقَ بأهوالها، وكذلك عادٌ الأولى سكان حضرموت حين بَعَثَ الله إليهم رسوله هوداً عليه الصلاة والسلام، يدعوهم إلى عبادة الله وحده، فكذَّبوه، وأنكروا ما أخبر به من البعث، فأهلك الله الطائفتين بالهلاك العاجل.
{4} Kisha akataja mfano wa hali zao zilizomo duniani na zinazoonekana humo, na hayo ni yale aliyowafikishia ya adhabu kali kwa mataifa walioasi,
na akasema: "Thamudi na A'di waliukadhibisha." Hao ni makabila yanayojulikana, watu waliokuwa wakiishi Al-Hijr, ambao Mwenyezi Mungu aliwatumia Mtume wake, Saleh, amani iwe juu yake, ili awakataze shirki waliyokuwamo na awaamrishe kumpwekesha, lakini waliukataa mwito wake, wakamkadhibisha, na wakakanusha aliyoyasema kuhusu Siku ya Kiyama, ambayo ni tukio kuu litakaliowatisha sana viumbe kwa vitisho vyake. Basi wakakadhibisha A'di wa kwanza, watu waliokuwa wakiishi Hadhramaut, Mwenyezi Mungu alipomtuma kwao Mtume wake Hud, rehema na amani ziwe juu yake, akiwalingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, nao wakamkadhibisha na kuyakanusha yale aliyoyaeleza kuhusu kufufuliwa, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akayaangamiza makundi hayo yote mawili kwa maangamizo ya haraka.
#
{5} {فأمَّا ثمودُ فأهْلِكوا بالطَّاغية}: وهي الصيحة العظيمة الفظيعة، التي قطَّعتْ قلوبهم وزهقتْ لها أرواحهم، فأصبحوا موتى لا يُرى إلاَّ مساكِنُهم وجُثَثُهم.
{5} "Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno." Nao ni ule ukelele mkubwa wa kutisha uliozipasua nyoyo zao na kuzichukua roho zao, na wakawa wafu huku hayaonekani isipokuwa majumba yao na miili yao iliyokufa.
#
{6} {وأمَّا عادٌ فأُهْلِكوا بريح صرصرٍ}؛ أي: قويَّةٍ شديدةِ الهبوب لها صوتٌ أبلغ من صوت الرعد القاصف. {عاتيةٍ}؛ أي: عتت على خزَّانها على قول كثير من المفسرين، أو عتت على عادٍ، وزادت على الحدِّ كما هو الصحيح.
{6} "Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usiozuilika." Yaani, upepo mkali, wenye nguvu ambao una sauti kubwa kuliko radi "usiozuilika." Yaani, haukuzuilika hata kwa walinzi wake kulingana na wasemavyo wafasiri wengi, au haukuweza kuzuilika dhidi ya akina A'di, na ukavuka mipaka, kama ilivyo kauli sahihi.
#
{7} {سخَّرَها عليهم سبعَ ليال وثمانية أيَّام حسوماً}؛ أي: نحساً وشرًّا فظيعاً عليهم فدمَّرتهم وأهلكتهم؛ {فترى القومَ فيها صَرْعى}؛ أي: هَلكى موتى، {كأنَّهم أعجازُ نخلٍ خاويةٍ}؛ أي: كأنهم جذوعُ النخل التي قد قُطِّعت رؤوسها الخاوية الساقط بعضها على بعض.
{7} "Aliowapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita." Yaani, katika muda huu wa balaa mbaya na shari iliyowapata na kuwaangamiza. "Utaona watu wamepinduka" Yaani, wameangamia wamekufa "kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani" yakaangukiana yenyewe kwa yenyewe.
#
{8} {فهل ترى لهم من باقيةٍ}؟: وهذا استفهامٌ بمعنى النفي المتقرِّر.
{8} "Basi je! Unamwona mmoja wao aliyebaki?" Hii ni mbinu ya kuuliza yenye maana ya kukanusha jambo linalojulikana tayari.
{وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَنْ قَبْلَهُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ (9) فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَابِيَةً (10) إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ (11) لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَا أُذُنٌ وَاعِيَةٌ (12)}.
9. Na Firauni na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walileta khatia. 10.Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato uliozidi nguvu. 11. Maji yalipofurika Sisi tulikupandisheni katika safina. 12. Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalosikia liyahifadhi.
#
{9 - 10} أي: وكذلك غير هاتين الأمَّتين الطاغيتين عاد وثمود جاء غيرهم من الطُّغاة العتاة؛ كفرعون مصر الذي أرسل الله إليه عبده ورسوله موسى بن عمران عليه الصلاة والسلام، وأراهم من الآيات البيِّنات ما تيقَّنوا بها الحقَّ، ولكن جحدوا وكفروا ظلماً وعلوًّا، وجاء من قبله من المكذِّبين {والمؤتفكات}؛ أي: قرى قوم لوطٍ؛ الجميع جاؤوا {بالخاطئة}؛ أي: بالفعلة الطاغية، وهو الكفر والتكذيب والظُّلم والمعاندة وما انضمَّ إلى ذلك من أنواع المعاصي والفسوق، {فعصَوْا رسولَ ربِّهم}: وهذا اسم جنس؛ أي: كلٌّ من هؤلاء كذَّبوا الرسول الذي أرسله الله إليهم ؛ فأخذ اللهُ الجميع {أخذةً رابيةً}؛ أي: زائدة على الحدِّ والمقدار الذي يحصُلُ به هلاكهم.
{9 - 10} Yaani, vile vile walikuja madhalimu waasi wakubwa wengine wasiokuwa hawa wawili madhalimu, Adi na Thamud, kama vile Firauni wa Misri ambaye Mwenyezi Mungu alimtumia mja wake na Mtume wake Musa bin Imran, rehema na amani ziwe juu yake, na akawaonyesha ishara zilizo wazi ambazo wangeweza kwazo kuwa na yakini juu ya haki, lakini walikadhibisha, wakakukufuru, wakadhulumu na wakafanya kiburi, na wakaja kabla yake wakadhibishaji "na miji iliyopinduliwa chini juu." Yaani, vijiji vya watu wa Lut'i. Hao wote walikuja "walileta khatia." Yaani, vitendo vilivyopindukia. Navyo ni ukafiri, ukanushaji, dhuluma, ukaidi, na aina zote za dhambi na uchafu uliofungamana na hayo. "Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi" kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakamata "kwa mkamato uliozidi nguvu" na kipimo, ambao ulisababisha kuangamia kwao.
#
{11 - 12} ومن جملة هؤلاء قومُ نوح؛ أغرقهم الله في اليمِّ حين طغى الماءُ على وجه الأرض وعلا على مواضعها الرفيعة، وامتنَّ الله على الخلق الموجودين بعدَهم أن - حملهم {في الجاريةِ}، وهي السفينة؛ في أصلاب آبائهم وأمهاتهم، الذين نجَّاهم الله؛ فاحمدوا الله واشكروا الذي نجَّاكم حين أهلك الطاغين، واعتبروا بآياتِهِ الدالَّة على توحيده، ولهذا قال: {لِنَجْعَلَها}؛ أي: الجارية، والمراد جنسها [لكم] {تذكرةً}: تذكِّركم أول سفينةٍ صُنِعَتْ وما قصَّتها، وكيف نجَّى الله عليها مَنْ آمن به واتَّبع رسوله وأهلك أهل الأرض كلَّهم؛ فإنَّ جنس الشيء مذكِّرٌ بأصله. وقوله: {وتَعِيها أذنٌ واعيةٌ}؛ أي: يعقلها أولو الألباب، ويعرفون المقصود منها ووجه الآية بها. وهذا بخلاف أهل الإعراض والغفلة وأهل البلادة وعدم الفطنة؛ فإنَّهم ليس لهم انتفاعٌ بآيات الله؛ لعدم وعيهم عن الله وتفكُّرهم بآياته.
{11 - 12} Miongoni mwao ni kaumu ya Nuhu; Mwenyezi Mungu aliwazamisha baharini maji yalipoufunika uso wa ardhi na kupanda juu ya sehemu zake zilizoinuka juu, na Mwenyezi Mungu akawaneemesha viumbe waliokuwepo baada yao kwamba - aliwachukua "katika kinachokwenda,", ambacho ni safina, walipokuwa katika viuno vya baba zao na mama zao, ambao Mwenyezi Mungu aliwaokoa. Basi mhimidini Mwenyezi Mungu, na mumshukuru yule aliyekuokoeni alipowaangamiza madhalimu, na zizingatieni Aya zake na ishara zake zinazonyesha upweke wake,
na ndiyo maana akasema: "Ili tuyafanye hayo" Yaani, safina hiyo na mfano huo kuwa ni "waadhi kwenu " atakaokukumbusheni safina ya mwanzo iliyojengwa na kisa chake, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaokolea humo wale waliomuamini na wakamfuata Mtume wake, na akawaangamiza watu wote waliokuwa kwenye ardhi. Kwa maana kitu sawia kinakumbusha asili yake.
Na kauli yake: "Na kila sikio linalosikia liyahifadhi.
" Yaani: wenye akili wayafahamu, na wayajue makusudio yake na vipi ya kuyatumia kuwa ni ishara. Haya ni tofauti na watu wanaopeana mgongo, walioghafilika, watu wagumu wasio na akili ya utambuzi. Kwani wao hawafaidiki na Ishara za Mwenyezi Mungu. Kwa sababu wao hawaelewi kitu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hawazifikirii ishara zake.
{فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَةٌ وَاحِدَةٌ (13) وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً (14) فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ (15) وَانْشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ (16) وَالْمَلَكُ عَلَى أَرْجَائِهَا وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ (17) يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَى مِنْكُمْ خَافِيَةٌ (18)}.
13. Na litapopulizwa barugumu mpulizo mmoja tu. 14. Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja. 15. Siku hiyo ndio Tukio litatukia. 16. Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. 17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. 18. Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.
#
{13 - 18} لمَّا ذكر تعالى ما فعله بالمكذِّبين لرسله، وكيف جازاهم وعجَّل لهم العقوبة في الدُّنيا، وأنَّ الله نجَّى الرسل وأتباعهم؛ كان هذا مقدِّمةً للجزاء الأخرويِّ وتوفيةَ الأعمال كاملةً يوم القيامةِ، فذكر الأمور الهائلة التي تقع أمام يوم القيامةِ، وأنَّ أوَّل ذلك أنَّه ينفخ إسرافيل {في الصور} - إذا تكاملتِ الأجسادُ نابتةً - نفخةً واحدةً؛ فتخرج الأرواح، فتدخلُ كلُّ روح في جسدها؛ فإذا الناس قيامٌ لربِّ العالمين، {وحُمِلَتِ الأرضُ والجبالُ فدُكَّتا دكةً واحدةً}؛ أي: فتِّتت الجبال، واضمحلَّت وخلطت بالأرض، ونُسِفَتْ عليها ، فكان الجميع قاعاً صفصفاً، لا ترى فيها عوجاً ولا أمتاً. هذا ما يُصنع بالأرض وما عليها، وأمَّا ما يُصنع بالسماء؛ فإنَّها تضطرب وتمور وتشقَّق - ويتغيَّر لونُها، وتهي بعد تلك الصلابة والقوة العظيمة، وما ذاك إلا لأمرٍ عظيم أزعجها وكربٍ جسيم هائل أوهاها وأضعفها، {والمَلَكُ}؛ أي: الملائكة الكرام {على أرجائِها}؛ أي: على جوانب السماء وأركانها، خاضعين لربِّهم، مستكينين لعظمته، {ويحمِلُ عرشَ ربِّك فوقَهم يومئذٍ ثمانيةٌ}: أملاكٌ في غاية القوة، إذا أتى للفصل بين العباد والقضاء بينهم بعدله وقسطه وفضله، ولهذا قال: {يومئذٍ تُعْرَضون}: على الله، {لا تَخْفى منكم خافيةٌ}: لا من أجسادكم وذواتكم ، ولا من أعمالكم وصفاتكم؛ فإنَّ الله تعالى عالمُ الغيب والشهادة، ويحشُرُ العباد حفاةً عراةً غُرلاً في أرض مستويةٍ يسمِعُهم الدَّاعي ويَنْفُذُهم البصرُ، فحينئذٍ يجازيهم بما عملوا، ولهذا ذَكَرَ كيفيةَ الجزاءِ، فقال:
{13 - 18} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja aliyowafanyia wale waliokadhibisha Mitume wake, na jinsi alivyowalipa, na akawaharakishia adhabu yao katika dunia, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaokoa Mitume na wafuasi wao, huu ukawa ni utangulizi wa malipo ya kiakhera na utimilifu wa matendo kamili Siku ya Kiyama. "Na litakapopulizwa barugumu mpulizo mmoja tu" - wakati miili itakapokuwa imeota kikamilifu - kwa mpulizo mmoja, hapo roho zitatoka, kisha kila roho itaingia ndani ya mwili wake. Na tazama, watu wote watakuwa tayari wamemsimamia Mola Mlezi wa walimwengu wote. "Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja." Yaani, hivyo vyote vitakuwa tambarare, uwanda. Hutaona humo mdidimio wala muinuko. Hivyo ndivyo itakavyofanywa ardhi na vyote vilivyo juu yake. Na ama mbingu, hizo zitafadhaika, kutikisika na kupasuka - na rangi yake itabadilika, na kuwa dhaifu kabisa baada ya uimara na nguvu zake kubwa, na hayo si kwa sababu ya lolote ila ni kwa sababu ya jambo kubwa lililozisumbua, na balaa kubwa mno iliyozidhoofisha mno. "Na malaika" watukufu "watakuwa pembezoni mwa mbingu" huku wamemnyenyekea Mola wao Mlezi, watiifu kwa ukuu wake; "na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi." Nao ni malaika wenye nguvu kubwa zaidi. Wakati atakapokuja kwa ajili ya kutenganisha kati ya waja na kuhukumu baina yao kwa uadilifu wake na fadhila zake,
na ndiyo maana akasema: "Siku hiyo mtahudhurishwa" kwa Mwenyezi Mungu, "haitafichika siri yoyote yenu." Siyo katika miili yenu na dhati zenu wala katika vitendo vyenu na sifa zenu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua ya ghaibu na yanayoonekana. Na waja watakusanya bila viatu, uchi na bila ya kutahiriwa, kwenye ardhi tambarare ambayo ataweza kuwasikilizisha mwitaji, na ataweza kuwaona mtazamaji, na hapo atawalipa kwa yale waliyofanya, na ndiyo maana akataja namna yatakavyokuwa malipo hayo,
akasema:
{فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ (19) إِنِّي ظَنَنْتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ (20) فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ (21) فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ (22) قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ (23) كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ (24)}.
19. Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia,
atasema: Haya someni kitabu changu! 20. Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. 21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza. 22. Katika Bustani ya juu. 23. Matunda yake ya karibu. 24.
Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita.
#
{19 - 20} وهؤلاء هم أهل السعادة؛ يُعْطَوْن كُتُبهم التي فيها أعمالهم الصالحة بأيمانهم تمييزاً لهم وتنويهاً بشأنهم ورفعاً لمقدارهم، ويقول أحدُهم عند ذلك من الفرح والسرور ومحبَّة أن يطَّلع الخلق على ما منَّ الله عليه به من الكرامة: {هاؤمُ اقرؤوا كتابِيَهْ}؛ أي: دونكم كتابي فاقرؤوه؛ فإنَّه يبشِّر بالجنَّات وأنواع الكرامات ومغفرة الذُّنوب وستر العيوب، والذي أوصلني إلى هذه الحال ما منَّ الله به عليَّ من الإيمان بالبعث والحساب والاستعداد له بالممكن من العمل، ولهذا قال: {إنِّي ظننتُ أنِّي ملاقٍ حسابِيَهْ}؛ أي: أيقنتُ؛ فالظنُّ هنا بمعنى اليقين.
{19 - 20} Na hawa ndio watu watakaopata furaha. Wanapewa vitabu vyao vilivyo na matendo yao mema kwa mikono yao ya kulia, ili kuwapambanua, kuashiria hadhi zao nzuri na kuinua hadhi yao, na hapo mmoja wao atasema kwa sababu ya furaha kubwa na huku wakipenda kwamba viumbe wote wajue ni nini Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwacho cha utukufu. "Haya someni kitabu changu!" Kwani kinanibashiria mabustani ya mbinguni, aina mbalimbali za mambo matukufu, maghufira ya dhambi na kusitiriwa kasoro, na kile kilichonifikisha katika haya ni yale ambayo Mwenyezi Mungu alinineemesha kwayo ya kuamini ufufuo, kuulizwa juu ya matendo, na kujiandaa kwa ajili yake kwa matendo mema yawezekanayo.
Ndiyo maana akasema: "Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu."
#
{21 - 24} {فهو في عيشةٍ راضيةٍ}؛ أي: جامعة لما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعين وقد رضوها ولم يختاروا عليها غيرها، {في جنةٍ عاليةِ}؛ أي: المنازل والقصور عالية المحلِّ، {قطوفُها دانيةٌ}؛ أي: ثمرها وجناها من أنواع الفواكه قريبةٌ سهلة التناول على أهلها، ينالها أهلُها قياماً وقعوداً ومتَّكئين، ويقال لهم إكراماً: {كلوا واشربوا}؛ أي: من كلِّ طعام لذيذٍ وشرابٍ شهيٍّ، {هنيئاً}؛ أي: تامًّا كاملاً من غير مكدِّرٍ ولا منغِّصٍ. وذلك الجزاء حصل لكم {بما أسلفْتُم في الأيَّام الخالية}: من الأعمال الصالحة - وترك الأعمال السيِّئة - من صلاةٍ وصيام وصدقةٍ وحجٍّ وإحسانٍ إلى الخلق وذكر لله وإنابةٍ إليه؛ فالأعمال جعلها الله سبباً لدخول الجنة ومادَّةً لنعيمها وأصلاً لسعادتها.
{21 - 24} "Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza." Yaani, yanayokusanya yale yanayotamaniwa na nafsi na yale ambayo macho yanayafurahia, na tayari waliridhika nayo na wala hawataki kuchagua chochote badala yake.
"Katika Bustani ya juu" Yaani: nyumba na majumba yaliyoinuka juu sana. "Matunda yake yakaribu." Yaani matunda yake ni miongoni mwa aina za matunda yaliyo karibu na yaliyo mepesi sana kwa watu wake kuyachuma huku wakiwa wamesimama, wamekaa, na wameegemea,
na wataambiwa kwa heshima: "Kuleni na mnywe" kutoka katika kila chakula kitamu na kinywaji kitamu, "kwa furaha" kikamilifu bila ya kero wala usumbufu wowote. Na mlipewa malipo hayo "kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita" miongoni mwa matendo mema - na kuacha matendo maovu - kama vile Swala, saumu, sadaka, Hijja, kuwafanyia mema viumbe, kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumgeukia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu aliyafanya matendo kuwa ni sababu ya kuingia katika bustani za mbinguni, na kiini cha furaha yake, na msingi wa furaha yake.
{وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَالَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ (25) وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ (26) يَالَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ (27) مَا أَغْنَى عَنِّي مَالِيَهْ (28) هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ (29) خُذُوهُ فَغُلُّوهُ (30) ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ (31) ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ (32) إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ (33) وَلَا يَحُضُّ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ (34) فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ (35) وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ (36) لَا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ (37)}.
25. Na ama atakayepewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto,
basi yeye atasema: Laiti nisingelipewa kitabu changu! 26. Wala nisingelijua nini hisabu yangu. 27. Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa. 28. Mali yangu hayakunifaa kitu. 29. Madaraka yangu yamenipotea. 30.
(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! 31. Kisha mtupeni Motoni! 32. Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini! 33. Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. 34. Wala hahimizi kulisha masikini. 35. Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu. 36. Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. 37. Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
#
{25 - 29} هؤلاء هم أهل الشقاء؛ يعطَوْن كتبهم المشتملة على أعمالهم السيِّئة بشمالهم؛ تمييزاً لهم وخزياً وعاراً وفضيحةً، فيقول أحدُهم من الهمِّ والغمِّ والحزن: {يا ليتني لم أوتَ كتابِيَهْ}؛ لأنَّه يبشر بدخول النار والخسارة الأبديَّة، {ولم أدرِ ما حسابِيَهْ}؛ أي: ليتني كنت نسياً منسيًّا ولم أُبْعَثْ وأحاسب، ولهذا قال: {يا ليتَها كانتِ القاضيةَ}؛ أي: يا ليت موتتي هي الموتة التي لا بَعْثَ بعدها.
ثم التفت إلى ماله وسلطانه؛ فإذا هو وبالٌ عليه لم يقدِّم منه لآخرته ولا ينفعه لو افتدى به من العذاب شيئاً ، فيقول: {ما أغنى عنِّي مالِيَهْ}؛ أي: ما نفعني لا في الدُّنيا - لم أقدِّم منه شيئاً - ولا في الآخرة؛ قد ذهب وقت نفعه، {هلك عني سُلطانِيَهْ}؛ أي: ذهب واضمحلَّ، فلم تنفع الجنود ولا الكثرة ولا العَدَدُ ولا العُدَدُ ولا الجاه العريض، بل ذهب ذلك كله أدراج الرياح، وفاتت بسببه المتاجر والأرباح، وحضرت بدله الهموم والغموم والأتراح.
{25-29} Hawa ndio watu wa mashakani. Watapewa vitabu vyao vyenye matendo yao maovu kwa mkono wao wa kushoto, ili kuwapambanua, kufedheha, na mmoja wao atasema kwa sababu ya wasiwasi yake kubwa na huzuni, "Laiti nisingeli pewa kitabu changu!" Kwa sababu kinanibashiria kuingia Motoni, na kwamba nitapata hasara ya milele. Natamani "nisingelijua nini hisabu yangu" nikawa nilisahaulika kabisa, na wala hata nisingefufuliwa ndiyo nikaulizwa hivi juu ya matendo yangu. "Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa." Yaani, laiti kifo changu kingekuwa ndicho kifo ambacho hakuna kufufuliwa baada yake. Kisha akageukia mali yake na mamlaka aliyokuwa nayo. Tazama, vyote hivyo vikawa ni msiba juu yake hakujitangulizia katika hivyo kwa ajili ya akhera yake, na wala havitomfaa chochote ikiwa atavitoa kwa ajili ya kukomboa kwavyo kutokana na adhabu.
Hapo atasema: "Mali yangu hayakunifaa kitu" si katika dunia - kwa sababu sikujitangulizia ndani yake kitu - wala katika Akhera, na tayari wakati wa manufaa yake umeshapita. "Madaraka yangu yamenipotea." Yaani, yameondoka na kutoweka, na wala hawakuninufaisha kitu askari wala wingi
(wa mali au wasaidizi) wala maandalizi ya hali ya juu wala heshima kubwa. Bali, yote hayo yalitoweka pamoja na upepo bure kabisa, biashara za faida zikatoweka kwa sababu yake, na badala yake zikaja wasiwasi kubwa, machungu na huzuni.
#
{30 - 37} فحينئذٍ يؤمَر بعذابه، فيقال للزَّبانية الغلاظ الشداد: {خُذوه فغُلُّوه}؛ أي: اجعلوا في عنقه غلًّا يخنقه، {ثم الجَحيم صَلُّوه}؛ أي: قلِّبوه على جمرها ولهبها، {ثم في سلسلةٍ ذَرْعُها سبعون ذراعاً}: من سلاسل الجحيم في غاية الحرارة، {فاسْلُكوه}؛ أي: انظموه فيها بأن تدخل في دبره وتخرج من فمه ويعلَّق فيها فلا يزال يعذَّب هذا العذاب الفظيع؛ فبئس العذاب والعقاب، وواحسرة له من التوبيخ والعتاب؛ فإنَّ السبب الذي أوصله إلى هذا المحلِّ {إنَّه كان لا يؤمن بالله العظيم}: بأن كان كافراً بربِّه معانداً لرسله رادًّا ما جاؤوا به من الحقِّ، {ولا يحضُّ على طعام المسكين}؛ أي: ليس في قلبه رحمةٌ يرحم بها الفقراء والمساكين؛ فلا يطعمهم من ماله ولا يحضُّ غيره على إطعامهم؛ لعدم الوازع في قلبه، وذلك لأنَّ مدار السعادة ومادَّتها أمران: الإخلاص لله الذي أصله الإيمان بالله، والإحسان إلى الخلق بجميع وجوه الإحسان، الذي من أعظمها دفع ضرورة المحتاجين بإطعامهم ما يتقوَّتون به، وهؤلاء لا إخلاص ولا إحسان؛ فلذلك استحقُّوا ما استحقُّوا. {فليس له اليومَ ها هنا}؛ أي: يوم القيامة {حميمٌ}؛ أي: قريب أو صديق يشفع له لينجو من عذاب الله أو يفوز بثوابه. {ولا تنفعُ الشفاعة عندَه إلاَّ لمن أذن له}، {ما للظالمين من حميمٍ ولا شفيع يُطاع}. وليس له {طعامٌ إلاَّ من غِسْلينَ}: وهو صديدُ أهل النار، الذي هو في غاية الحرارة والمرارة ونتن الريح وقبح الطعم ، لا يأكل هذا الطعامَ الذميم {إلاَّ الخاطئونَ}، الذين أخطؤوا الصراط المستقيم، وسلكوا كلَّ طريق يوصِلُهم إلى الجحيم ؛ فلذلك استحقُّوا العذاب الأليم.
{30 - 37} Basi hapo itaamrishwa aadhibiwe,
na wataambiwa Zabaniya wagumu na wakali mno: “Mshikeni! Mtieni pingu! Kisha mtupeni Motoni!" Yaani, mgeuzeni juu ya makaa yake na miale ya moto wake. "Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini" katika minyororo ya ya Motoni ambayo itakuwa moto sana kisha "mtatizeni." Yaani, iingizieni kwenye njia ya haja kubwa na itokee mdomoni mwake, na aning'inizwe humo asalie akiadhibiwa kwa adhabu hii mbaya zaidi. Basi hii ndiyo adhabu na mateso mabaya zaidi, na ni majuto makubwa magani haya, makemeo na lawama! Kwani sababu iliyomfikisha mahali hapa "ni kuwa hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu" kwa maana alikuwa ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi na kuwapinga Mitume wake, akiikataa haki waliyoileta, "wala hahimizi kulisha masikini." Yaani, hakuwa na rehema ndani ya moyo wake ya kuwaonea huruma maskini na wahitaji. Kwa hivyo, hakuwa akiwalisha katika mali zake mwenyewe, wala hakuwa akiwahimiza wengine kuwalisha. Kwa kuwa hakuwa na cha msukumo wa kufanya hivyo moyoni mwake.
Haya ni kwa sababu chanzo cha furaha ni vitu viwili: kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, jambo ambalo msingi wake ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuwafanyia wema viumbe wa aina zote za wema, ambao mkubwa wake zaidi ni kuzuia mahitaji ya masikini kwa kuwalisha vile wanavyoweza kupata nguvu. Nao watu hawa hawamkusudii Mwenyezi Mungu peke yake wala hawafanyi wema, ndiyo maana wakastahili kile walichostahili. "Basi leo" siku ya Kiyama, "hana jamaa wa kumwonea uchungu" na kumfanyia uombezi ili aepuke adhabu ya Mwenyezi Mungu au apate malipo yake mazuri. "Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini" na akasema "Madhalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa." Na wala hatakuwa "na chakula ila usaha wa watu wa Motoni."
Nao utakuwa moto sana, mchungu, wenye harufu mbaya, na wenye ladha mbaya, na hatakila chakula hicho cha kuchukiza mno "ila wakosefu" walioikosa njia iliyonyooka, na wakashika kila njia inayowafikisha kwenye Jahannamu; basi ndiyo wakastahiki adhabu iumizayo.
{فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ (38) وَمَا لَا تُبْصِرُونَ (39) إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ (40) وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ قَلِيلًا مَا تُؤْمِنُونَ (41) وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ (42) تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ (43) وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ (44) لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ (45) ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ (46) فَمَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ (47) وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِلْمُتَّقِينَ (48) وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنْكُمْ مُكَذِّبِينَ (49) وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ (50) وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ (51) فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ (52)}.
38. Basi ninaapa kwa mnavyoviona. 39. Na msivyoviona. 40. Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe mwenye heshima. 41. Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayoyaamini. 42. Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayoyakumbuka. 43. Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 44. Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu. 45. Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. 46. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo! 47. Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia. 48. Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wacha Mungu. 49. Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokadhibisha. 50. Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanaokataa. 51. Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. 52. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.
#
{38 - 43} أقسم تعالى بما يُبْصِرُ الخلقُ من جميع الأشياء وما لا يبصِرونه، فدخل في ذلك كلُّ الخلق، بل دخل في ذلك نفسُه المقدَّسة، على صدق الرسول بما جاء به من هذا القرآن الكريم، وأنَّ الرسول الكريم بلَّغه عن الله تعالى، ونزَّه اللهُ رسولَه عمَّا رماه به أعداؤه من أنَّه شاعرٌ أو ساحرٌ، وأنَّ الذي حملهم على ذلك عدم إيمانهم وتذكُّرهم؛ فلو آمنوا وتذكَّروا ما ينفعهم ويضرُّهم، ومن ذلك أن ينظروا في حال محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - ويرمُقوا أوصافه وأخلاقه ليروا أمراً مثل الشمس يدلُّهم على أنَّه رسول الله حقًّا وأن ما جاء به {تنزيلٌ من ربِّ العالمين}، لا يَليقُ أن يكون قولاً للبشر، بل هو كلامٌ دالٌّ على عظمة من تكلَّم به وجلالة أوصافه وكمال تربيته للخلق وعلوِّه فوق عباده. وأيضاً؛ فإنَّ هذا ظن منهم بما لا يليق بالله وحكمته.
{38 - 43} Mola Mtukufu aliapa kwa vitu vyote vinavyoviona viumbe na visivyoviona, basi viumbe vyote vikajumuishwa katika hilo, na hata nafsi yake tukufu ikajumuishwa katika hilo, kwamba Mtume alikuwa mkweli katika aliyoyaleta katika Qur-ani hii Tukufu, na kwamba Mtukufu Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliifikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mwenyezi Mungu akamtakasa Mtume wake kutokana na yale ambayo maadui zake walimtuhumu kwayo kwamba yeye ni mtunga mashairi au mchawi, na kwamba yale yaliyowachochea kufanya hivyo ilikuwa ni ukosefu wao wa imani na kukumbuka. Lau wangeamini na kukumbuka yale yanayowafaa na yanayowadhuru, na katika hayo ni kuangalia hali ya Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na kuangalia vyema tabia zake na maadili yake ili kuona kitu kama jua ambacho kitawaashiria kwamba hakika yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba aliyoyaleta ni “uteremsho unaotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote" ambao haufailii kuwa kauli kwa wanadamu. Bali ni maneno yanayoashiria ukubwa wa yule ambaye aliyazungumza, utukufu wa sifa zake, ukamilifu wa malezi yake juu ya viumbe, na kuinuka kwake juu ya waja wake. Na pia, haya ni wao kumdhania Mwenyezi Mungu mambo yasiyomfailia Mwenyezi Mungu na hekima yake.
#
{44 - 47} فإنه {لو تقوَّل}: عليه وافترى {بعض الأقاويل}: الكاذبة، {لأخذنا منه باليمين ثم لقطعنا منه الوتينَ}: وهو عرقٌ متصلٌ بالقلب إذا انقطع هلك منه الإنسان؛ فلو قدِّر أنَّ الرسول - حاشا وكلا - تقوَّل على الله؛ لعاجَلَه بالعقوبة وأخذَه أخذَ عزيزٍ مقتدرٍ؛ لأنَّه حكيمٌ قديرٌ على كلِّ شيءٍ ؛ فحكمته تقتضي أن لا يُمْهِلَ الكاذب عليه الذي يزعم أنَّ الله أباح له دماء مَنْ خالفه وأموالهم، وأنَّه هو وأتباعه لهم النجاةُ، ومَنْ خالفَه؛ فله الهلاكُ. فإذا كان الله قد أيَّد رسوله بالمعجزات، وبرهن على صدق ما جاء به بالآيات البيِّنات، ونصره على أعدائه، ومكَّنه من نواصيهم؛ فهو أكبر شهادةٍ منه على رسالته. وقوله: {فما منكم من أحدٍ عنه حاجزينَ}؛ أي: لو أهلكه؛ ما امتنعَ هو بنفسه ولا قَدَرَ أحدٌ أن يمنعه من عذاب الله.
{44 - 47} "Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu. Bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo;" ambao ukikatwa, mtu anaangamia kwa sababu yake. Lau ingechukuliwa kuwa Mtume -Mungu apishe mbali - kasema dhidi ya Mwenyezi Mungu, basi angemharakishia adhabu na kumshika kama anavyoshika mwenye nguvu, mwenye uweza. Kwa sababu Yeye ni Mwenye hekima na Muweza mno wa kila kitu. Hekima yake inamtaka asimpe muda yule anayemsingizia uongo anayedai kuwa Mwenyezi Mungu amemruhusu kumwaga damu na mali za wale wanaompinga, na kwamba yeye na wafuasi wake wataokolewa, na yeyote anayempinga, basi yeye ndiye ataangamia. Kwa hivyo, ikiwa Mwenyezi Mungu alimsaidia Mtume wake kwa miujiza, na akathibitisha ukweli wa yale aliyoyaleta kwa ishara zilizo wazi, na akampa ushindi dhidi ya maadui zake, na akampa nguvu ya kukamata nywele zao za utosini, basi huo ndio ushuhuda mkuu zaidi kutoka kwake juu ya ujumbe wake.
Na kauli yake: "Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia." Yaani, ikiwa atamhiliki, basi; Yeye mwenyewe hakujizuia, na hakuna aliyeweza kumzuia na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
#
{48} {وإنَّه}؛ أي: القرآن الكريم، {لتذكرةٌ للمتَّقين}: يتذكَّرون به مصالح دينهم ودنياهم، فيعرفونها ويعملون عليها، يذكِّرهم العقائد الدينيَّة والأخلاق المرضيَّة والأحكام الشرعيَّة، فيكونون من العلماء الربانيِّين، والعباد العارفين، والأئمَّة المهديِّين.
{48} "Na kwa hakika hii,
" yaani: Qur-ani Tukufu, "ni mawaidha kwa wacha Mungu" kwayo wanakumbuka masilahi ya dini yao na dunia yao, kwa hivyo wanayajua na kuyafanyia kazi. Inawakumbusha itikadi ya dini, maadili yanayoridhiwa, na hukumu za kisheria, kwa hivyo wanakuwa miongoni mwa wanachuoni wanaofanyia matendo Mola wao Mlezi, waja wanaojua na maimamu walioongoka.
#
{49} {وإنَّا لَنَعْلَمُ أنَّ منكم مكذِّبين}: به، وهذا فيه تهديدٌ ووعيدٌ للمكذِّبين، وأنَّه سيعاقِبُهم على تكذيبهم بالعقوبة البليغة.
{49} "Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanaokadhibisha" haya, na haya ndani yake kuna maonyo na ahadi ya adhabu kwa wanaokadhibisha, na kwamba atawaadhibu kwa kukadhibisha kwao adhabu kali mno.
#
{50} {وإنَّه لحسرةٌ على الكافرين}: فإنَّهم لما كفروا به ورأوا ما وَعَدَهم به؛ تحسَّروا إذ لم يهتدوا به ولم ينقادوا لأمره، ففاتهم الثواب، وحصلوا على أشدِّ العذاب، وتقطَّعت بهم الأسباب.
{50} "Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa makafiri." Kwani walipoikufuru na wakayaona yale aliyowaahidi, wakahuzunika sana kwa kuwa hawakuongoka kwayo na hawakufuata amri zake, kwa hivyo wakakosa malipo mazuri, wakapata adhabu kali zaidi, na yakakatika mafungamano yao.
#
{51} {وإنَّه لحقُّ اليقين}؛ أي: أعلى مراتب العلم؛ فإنَّ أعلى مراتب العلم اليقين، وهو العلم الثابت الذي لا يتزلزل ولا يزول. واليقين مراتبه ثلاثةٌ، كلُّ واحدة أعلى مما قبلها: أولُها علم اليقين، وهو العلمُ المستفاد من الخبر. ثم عينُ اليقين، وهو العلم المدرَك بحاسة البصر. ثم حقُّ اليقين، وهو العلم المدرَك بحاسَّة الذوق والمباشرة. وهذا القرآن بهذا الوصف؛ فإنَّ ما فيه من العلوم المؤيَّدة بالبراهين القطعيَّة وما فيه من الحقائق والمعارف الإيمانيَّة يحصُلُ به لمن ذاقه حقُّ اليقين.
{51} "Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini" juu ya viwango vya elimu. Kwani viwango vya juu kabisa vya elimu ni yakini, ambayo ni elimu thabiti isioyumba wala kuondoka. Nayo yakini ina viwango vitatu,
kila kimoja ni cha juu zaidi kuliko cha kabla yake: cha kwanza ni elimu ya yakini, ambayo ni elimu inayopatikana kutokana na habari. Kisha jicho la yakini, ambayo ni elimu inayopatikana kwa kuona kwa macho. Kisha haki ya yakini, ambayo ni elimu inayopatikana kwa hisia ya ladha na kugusana nayo. Na hii Qur-ani ni yenye maelezo haya. Kwa maana elimu iliyomo ndani yake inayoungwa mkono na uthibitisho wa kukata na mambo ya uhakika na elimu ya kiimani iliyo ndani yake anayopata mwenye kuionja ni haki ya yakini.
#
{52} {فسبِّح باسم ربِّك العظيم}؛ أي: نزِّههُ عما لا يَليق بجلاله، وقدِّسْه بذِكْرِ أوصاف جلاله وجماله وكماله.
{52} "Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu" kutokana na yale yasiyoufailia utukufu wake, na mtakase kwa kutaja sifa za utukufu wake, uzuri wake na ukamilifu wake.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Haqqa, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
****