:
Tafsiri ya Surat Al-Mutaffifin
Tafsiri ya Surat Al-Mutaffifin
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 6 #
{وَيْلٌ لِلْمُطَفِّفِينَ (1) الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ (2) وَإِذَا كَالُوهُمْ أَوْ وَزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ (3) أَلَا يَظُنُّ أُولَئِكَ أَنَّهُمْ مَبْعُوثُونَ (4) لِيَوْمٍ عَظِيمٍ (5) يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ (6)}.
1. Ole wao hao wapunjao! 2. Ambao wanapojipimia kwa watu hudai watimiziwe. 3. Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. 4. Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa. 5. Katika Siku iliyo kuu. 6. Siku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
#
{1 - 6} {ويلٌ}: كلمة عذابٍ وعقابٍ ، {للمطفِّفين}: وفسر الله المطفِّفين بأنهم {الذين إذا اكتالوا على الناس}؛ أي: أخذوا منهم وفاءً لهم عمَّا قِبَلَهم ، يستوفونه كاملاً من غير نقصٍ، {وإذا كالوهم أو وَزَنوهم}؛ أي: إذا أعطوا الناس حقَّهم الذي لهم عليهم بكيل أو وزن، {يُخْسِرونَ}؛ أي: ينقصِونَهم ذلك إمَّا بمكيال وميزان ناقصين، أو بعدم ملء المِكْيال والميزان، أو بغير ذلك؛ فهذا سرقةٌ لأموال الناس وعدمُ إنصاف لهم منهم. وإذا كان هذا وعيداً على الذين يَبْخَسونَ الناس بالمكيال والميزان؛ فالذي يأخذ أموالهم قهراً وسرقةً أولى بهذا الوعيد من المطفِّفين. ودلَّت الآية الكريمة على أنَّ الإنسان كما يأخذ من الناس الذي له يجب [عليه] أن يعطِيَهم كلَّ ما لهم من الأموال والمعاملات، بل يدخُلُ في عموم هذا الحجج والمقالات؛ فإنَّه كما أنَّ المتناظرين قد جرت العادة أنَّ كل واحدٍ منهما يحرص على ماله من الحجج؛ فيجب عليه أيضاً أن يبيِّن ما لخصمه من الحجَّة التي لا يعلمها، وأن ينظر في أدلَّة خصمه كما ينظر في أدلَّته هو، وفي هذا الموضع يُعْرَفُ إنصاف الإنسان من تعصُّبه واعتسافه وتواضُعُه من كِبْره وعقلُهُ من سَفَهِهِ، نسأل الله التوفيق لكلِّ خير. ثم توعَّد تعالى المطفِّفين، وتعجَّب من حالهم وإقامتهم على ما هم عليه، فقال: {ألا يظنُّ أولئك أنَّهم مبعوثونَ ليومٍ عظيمٍ. يومَ يقومُ الناسُ لربِّ العالمينَ}: فالذي جرَّأهم على التَّطفيف عدمُ إيمانهم باليوم الآخر؛ وإلاَّ؛ فلو آمنوا به وعرفوا أنهم سيقومون بين يدي الله فيحاسبهم على القليل والكثير؛ لأقلعوا عن ذلك وتابوا منه.
{1 - 6} "Ole wao" ni neno la kuashiria adhabu mateso. "Kwa hao wapunjao!" Na Mwenyezi Mungu amewafasiri wapunjao kwamba ni wale "ambao wanapojipimia kwa watu." Yaani, wanachukua kikamilifu kilicho chao bila ya upungufu wowote. "Na wao wanapowapimia watu kwa kipimo au mizani." Yaani, wakiwapa watu haki zao wanazowadai kwa kipimo cha wingi au cha uzito "hupunguza" ima kwa kipimo cha wingi au cha uzito kilichovurugwa au kwa kutojaza kipimo cha wingi au cha uzito au vinginevyo. Huku ni kuiba mali za watu na kuwatendea uadilifu. Na ikiwa hili ni tishio kwa wale wanaopunja watu kwa vipimo vya wingi na vya uzito, basi anayechukua mali zao kwa nguvu na wizi ndiye anayestahili zaidi tishio hili kuliko hao wapunjao. Aya hii tukufu inaashiria kwamba kama vile mtu anavyochukua haki yake kutoka kwa watu, naye pia ni lazima awape mali zao na miamala yao yote. Bali inaingia katika ujumla wa hili hoja mbalimbali na mazungumzo. Kwani, ilivyo kawaida kwa watu wanaojadiliana mada fulani kila mmoja wao anawania kueleza hoja zake, basi pia inamlazimu kumuelezea hasimu wake hoja ambayo haijui, na kwamba aziangalie hoja za mpinzani wake kama anavyoangalia katika hoja zake mwenyewe. Na katika hali hii, uadilifu wa mtu unajulikana kutokana na ushabiki, na unyenyekevu wake kutokana na kiburi chake, na akili yake nzuri kutokana na upumbavu wake. Tunamwomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kila la heri. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaahidi adhabu wale wapunjao, na akastaajabia hali yao na kuendelea kwao kushikilia hali waliyomo. Akasema: “Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa. Katika Siku iliyo kuu. Siku watakapomsimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?" Lililowatia moyo wa kupunja ni kutoiamini kwao Siku ya Mwisho. Vinginevyo, ikiwa wangeiamini na kujua kwamba watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu, naye awaulize juu ya matendo yoa, machache na mengi, basi wangeacha hayo na kutubu kutokana nayo.
: 7 - 17 #
{كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ (7) وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ (8) كِتَابٌ مَرْقُومٌ (9) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (10) الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ (11) وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ (12) إِذَا تُتْلَى عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (13) كَلَّا بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (14) كَلَّا إِنَّهُمْ عَنْ رَبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَمَحْجُوبُونَ (15) ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ (16) ثُمَّ يُقَالُ هَذَا الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ (17)}.
7. Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. 8. Unajua nini Sijjin? 9. Kitabu kilichoandikwa. 10.Ole wao siku hiyo kwa wanaokadhibisha! 11. Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. 12. Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. 13. Anaposomewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! 14. Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao waliokuwa wakiyachuma. 15. Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. 16. Kisha wataingia Motoni! 17. Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyokuwa mkiyakadhabisha.
#
{7 - 9} يقول تعالى: {كلاَّ إنَّ كتاب الفجَّارِ}: وهذا شاملٌ لكلِّ فاجرٍ من أنواع الكفرة والمنافقين والفاسقين، {لفي سِجِّينٍ}. ثم فسَّر ذلك بقوله: {وما أدراكَ ما سِجِّينٌ. كتابٌ مرقومٌ}؛ أي: كتاب مذكور فيه أعمالهم الخبيثة. والسِّجِّينُ: المحلُّ الضيِّق الضَّنك، وسِجِّين ضدّ علِّيين، الذي هو محلُّ كتاب الأبرار كما سيأتي. وقد قيل: إنَّ سجِّين هو أسفل الأرض السابعة مأوى الفجَّار ومستقرُّهم في معادهم.
{7 - 9} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu." Hili linamjumuisha kila mwovu kama vile makafiri, wanafiki na wale wanaovuka mipaka. "Bila ya shaka yamo katika Sijjin" Kisha akaeleza hilo kwa kusema: “Unajua ni nini Sijjin? Kitabu kilichoandikwa." Yaani, ni kitabu ambacho ndani yake yametajwa matendo yao maovu yao. Na Sijjin pia ni mahali pembamba, penye dhiki, napo ni kinyume cha Aliyyin, ambapo ni mahali pa Kitabu cha walio wema, kama itakavyokuja. Pia imesemwa kwamba Sijjin ni chini ya ardhi ya saba, ambapo ni mahali watakapoingia waovu wakae huko milele katika maisha yao ya Akhera.
#
{10 - 13} {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}. ثم بيَّنهم بقوله: {الذين يكذِّبون بيوم الدِّين}؛ أي: يوم الجزاء، يوم يدين الله الناس فيه بأعمالهم. {وما يكذِّبُ به إلاَّ كلُّ معتدٍ}: على محارم الله متعدٍّ من الحلال إلى الحرام. {أثيمٍ}؛ أي: كثير الإثم؛ فهذا يحمله عدوانه على التكذيب، ويوجب له كبره ردَّ الحقِّ ، ولهذا {إذا تُتْلى عليه} آيات الله الدالَّة على الحقِّ وعلى صدق ما جاءت به الرسل؛ كذَّبها وعاندها وقال: هذه {أساطيرُ الأوَّلين}؛ أي: من ترَّهات المتقدِّمين وأخبار الأمم الغابرين، ليس من عند الله؛ تكبُّراً وعناداً.
{10 - 13} "Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!" Kisha akawaelezea kwa kusema: "Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo." Siku ambayo Mwenyezi Mungu atawalipa watu kwa matendo yao. "Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka" ya Mwenyezi Mungu, akavuka mipaka ya halali na akaingia katika haramu, "mwenye dhambi nyingi." Huyu kuvuka kwake mipaka huku ndiko kunamchochea kukanusha, na kiburi chake kinamfanya kukataa haki, ndiyo maana. "Anaposomewa Aya zetu" zinazoonyesha haki na ukweli wa yale waliyoyaleta Mitume, anazikadhibisha na kuzifanyia ukaidi na kusema: Hivi ni "visa vya watu wa kale" wala zivikutoka kwa Mwenyezi Mungu. Anasema hivi kwa jeuri na ukaidi.
#
{14 - 17} وأمَّا مَن أنصف وكان مقصودُه الحقَّ المبين؛ فإنَّه لا يكذِّب بيوم الدين؛ لأنَّ الله قد أقام عليه من الأدلَّة القاطعة والبراهين [الساطعة] ما يجعله حقَّ اليقين ، وصار لبصائرهم بمنزلة الشمس للأبصار؛ بخلاف مَنْ ران على قلبه كسبُه وغطَّتْه معاصيه؛ فإنَّه محجوبٌ عن الحقِّ، ولهذا جوزي على ذلك بأن حُجِبَ عن الله كما حُجِبَ قلبُه [في الدنيا] عن آيات الله. {ثم إنَّهم}: مع هذه العقوبة البليغة، {لصالو الجحيم. ثم يقالُ}: لهم توبيخاً وتقريعاً: {هذا الذي كنتُم به تكذِّبونَ}: فذكر لهم ثلاثة أنواع من العذاب: عذاب الجحيم، وعذاب التوبيخ واللوم، وعذاب الحجاب عن ربِّ العالمين، المتضمِّن لسخطه وغضبه عليهم، وهو أعظم عليهم من عذاب النار. ودلَّ مفهومُ الآية على أنَّ المؤمنين يرون ربَّهم يوم القيامة، وفي الجنة، ويتلذَّذون بالنَّظر إليه أعظم من سائر اللَّذَّات ويبتهجون بخطابه ويفرحون بقربه؛ كما ذكر الله ذلك في عدَّة آيات من القرآن، وتواتر فيه النقل عن رسول الله. وفي هذه الآيات التَّحذير من الذُّنوب؛ فإنَّها ترين على القلب وتغطِّيه شيئاً فشيئاً، حتى ينطمسَ نورُه وتموتَ بصيرتُه، فتنقلب عليه الحقائق، فيرى الباطل حقًّا والحقَّ باطلاً. وهذا من أعظم عقوبات الذُّنوب.
{14 - 17} Ama yule aliyekuwa mwadilifu, na makusudio yake yakawa ni haki iliyo wazi, basi yeye hawezi kuikadhibisha Siku ya Malipo, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemwekea ushahidi wa kukata, na hoja zilizo wazi mno zinazolifanya hilo kuwa haki ya yakini, na likawa kwao kana kwamba ni jua kwa macho. Tofauti na yule ambaye moyo wake una kutu, ambaye amevalia na kufunikwa na maasia yake, basi huyu amezuiliwa mbali na haki, na ndiyo maana akalipwa kwa sababu ya hayo kwa kuzuiwa mbali na Mwenyezi Mungu kama vile moyo wake [katika dunia] ulizuiliwa mbali na ushahidi wa Mwenyezi Mungu. "Kisha" wao pamoja na adhabu hii kali "wataingia Motoni! Kisha waambiwe" kwa njia ya kukemewa na kukaripiwa: “Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha." Basi akawatajia aina tatu za adhabu: adhabu ya Jahannamu, adhabu ya kukemewa na kulaumiwa, na adhabu ya kuzuiliwa mbali na Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambayo inajumuisha ghadhabu yake juu yao, na hili ni kubwa zaidi kwao kuliko adhabu ya Jahannamu. Maana isiyo ya moja kwa moja ya Aya hii inaashiria kwamba Waumini watamuona Mola wao Mlezi Siku ya Kiyama, na katika Peponi, na watafurahia kumtazama Yeye kuliko starehe zote, na watafurahia kuwaongelesha kwake na watafurahia kuwa karibu naye. Mwenyezi Mungu pia alitaja hili katika aya kadhaa za Qur-ani, na pia lilisimuliwa mara kwa mara kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Katika aya hizi kuna onyo dhidi ya madhambi. Kwa maana, hayo hutia kutu kwenye moyo na kuufunika kidogo kidogo, mpaka nuru yake izimike na ufahamu wake ukafa, kisha uhakika ukaubadilikia, ukawa unaona batili kwamba ndiyo haki, nayo haki kwamba ndiyo batili. Hii ndiyo adhabu kubwa zaidi kwa sababu ya madhambi.
: 18 - 28 #
{كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ (18) وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ (19) كِتَابٌ مَرْقُومٌ (20) يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ (21) إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (22) عَلَى الْأَرَائِكِ يَنْظُرُونَ (23) تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ (24) يُسْقَوْنَ مِنْ رَحِيقٍ مَخْتُومٍ (25) خِتَامُهُ مِسْكٌ وَفِي ذَلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ (26) وَمِزَاجُهُ مِنْ تَسْنِيمٍ (27) [عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ] (28)}.
18. Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika Illiyyin. 19. Na nini kitakachokujuvya nini Iliyyin? 20. Kitabu kilichoandikwa. 21. Wanakishuhudia waliokaribishwa. 22. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. 23. Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. 24. Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, 25. Watanyweshwa kinywaji safi kiliyotiwa muhuri. 26. Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. 27. Na mchanganyiko wake ni Tasniim. 28. Chemchemi watakayoinywa waliokurubishwa.
#
{18 - 21} لما ذكر أنَّ كتاب الفجَّار في أسفل الأمكنة وأضيقها؛ ذكر أنَّ كتاب الأبرار في أعلاها وأوسعها وأفسحها، وأنَّ كتابهم المرقوم {يشهدُهُ المقرَّبون}: من الملائكة الكرام وأرواح الأنبياء والصِّدِّيقين والشهداء ، وينوِّه الله بذكرهم في الملأ الأعلى. وعليُّون: اسم لأعلى الجنة.
{18 - 21} Ilipotajwa kwamba kitabu cha waovu kiko katika mahali pa chini kabisa na penye dhiki mno, akataja kwamba Kitabu cha wema kiko mahali pa juu kabisa na papana kabisa, na kwamba Kitabu chao kimeandikwa na "Wanakishuhudia waliowekwa karibu" miongoni mwa Malaika watukufu na roho za Manabii, wakweli mno, wale waliokufa kwa ajili ya dini, na tena Mwenyezi Mungu anaashiria kwamba wao hutajwa mbele ya viumbe watukufu wa juu kabisa. Na Iliyyun na jina la pepo ya juu zaidi.
#
{22 - 28} فلمَّا ذَكَرَ كتابَهم؛ ذَكَرَ أنَّهم في نعيم، وهو اسمٌ جامعٌ لنعيم القلب والرُّوح والبدن. {على الأرائِكِ}؛ أي: على السرر المزيَّنة بالفرش الحسان، {ينظُرونَ}: إلى ما أعدَّ الله لهم من النعيم، وينظرون إلى وجه ربِّهم الكريم، {تعرِفُ}: أيُّها الناظر ، {في وجوههم نَضْرَةَ النَّعيم}؛ أي: بهاءه ونضارته ورونقه؛ فإنَّ توالي اللَّذَّات والمسرَّات والأفراح - يكسب الوجه نوراً وحسناً وبهجةً، {يُسْقَوْنَ من رحيقٍ}: وهو من أطيب ما يكون من الأشربة وألذها، {مختوم} ذلك الشرابُ {ختامُه مسكٌ}: يُحتمل أن المراد مختومٌ عن أن يداخِلَه شيءٌ يُنْقِصُ لذَّته أو يفسِدُ طعمه، وذلك الختام الذي ختم به مسكٌ، ويحتمل أنَّ المراد أنَّه الذي يكون في آخر الإناء الذي يشربون منه الرحيق حثالة، وهي المسك الأذفر؛ فهذا الكدر منه الذي جرت العادة في الدُّنيا أنه يراق يكون في الجنَّة بهذه المثابة. {وفي ذلك}: النعيم المقيم الذي لا يعلم حسنه ومقداره إلاَّ الله، {فَلْيَتَنافَسِ المتنافسونَ}؛ أي: فليتسابقوا في المبادرة إليه والأعمال الموصلة إليه؛ فهذا أولى ما بُذِلَتْ فيه نفائس الأنفاس، وأحرى ما تزاحمت للوصول إليه فحول الرجال. ومزاجُ هذا الشراب {مِنْ تَسْنيم}: وهي عين {يشربُ بها المقرَّبون}: صرفاً، وهي أعلى أشربة الجنة على الإطلاق؛ فلذلك كانت خالصةً للمقرَّبين، الذين هم أعلى الخلق منزلة، وممزوجة لأصحاب اليمين؛ أي: مخلوطة بالرحيق وغيره من الأشربة اللذيذة.
{22 - 28} Alipotaja kitabu chao; akataja kuwa watakuwa katika neema, inayojumuisha neema ya moyo, roho na mwili. "Wakae juu ya viti vya enzi" vilivyopambwa kwa mapambo mazuri, "wakiangalia" yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia ya neema, na pia wanautazama uso mtukufu wa Mola wao Mlezi, "Utatambua" ewe mwenye kutazama "katika nyuso zao mng'aro wa neema." Kwa maana kufuatana mfululizo kwa raha na furaha - huufanya uso kuwa nuru, mzuri na uchangamfu. "Watanyweshwa kinywaji safi" ambacho ndicho kinywaji bora na kitamu zaidi "kilichofunikwa sawasawa" na "kifuniko chake hicho ni miski." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni kwamba kimefunikwa vyema ili kisiingiliwe na kitu ambacho kinaweza kupunguza raha yake au kuharibu ladha yake. Na inawezekana kwamba maana yake ni kuwa ni kile kinachokuwa mwishoni mwa chombo wanachokunywa kutoka humo. Basi uchafu huo kwa kawaida katika dunia ni kwamba huo humwagwa, lakini peponi unakuwa na hadhi hii. "Na katika hayo" ya neema ya milele, ambayo wema wake na kiwango chake hakijui isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. "Washindanie wenye kushindana" kwa kufanya matendo ya kuwafikisha huko. Kwani hayo yanayofailia zaidi kutolewa vitu vya thamani kubwa zaidi kwa ajili yake, na yanayofailia zaidi kusongamana kwa ajili ya kuyawafikia na wanaume mafahali. Na mchanganyiko wa kinywaji hiki "ni Tasniim." Nayo ni chemichemi "watakayoinywa wale waliowekwa karibu" na Mwenyezi Mungu kwa urahisi mno. Nacho nicho kinywaji cha juu kabisa cha Peponi, ndiyo maana kikawa cha wale walio karibu na Mwenyezi Mungu tu. Ambao ndio wenye hadhi ya juu kabisa miongoni mwa viumbe.
: 29 - 36 #
{إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ (29) وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ (30) وَإِذَا انْقَلَبُوا إِلَى أَهْلِهِمُ انْقَلَبُوا فَكِهِينَ (31) وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَؤُلَاءِ لَضَالُّونَ (32) وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ (33) فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ (34) عَلَى الْأَرَائِكِ يَنْظُرُونَ (35) هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ (36)}.
29. Kwa hakika wale waliokuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walioamini. 30. Na wanapopita karibu yao wakikonyezana. 31. Na wanaporudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. 32. Na wanapowaona husema: Hakika hawa ndio hasa waliopotea. 33. Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. 34. Basi leo walioamini ndio watawacheka makafiri. 35. Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. 36. Je, makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda?
#
{29 - 33} لما ذكر تعالى جزاء المجرمينَ وجزاء المحسنين، وذكر ما بينهما من التفاوت العظيم؛ أخبر أنَّ المجرمين كانوا في الدُّنيا يسخرون بالمؤمنين ويستهزِئون بهم و {يضحكون}: منهم، فَـ {يتغامَزون}: بهم عند مرورهم عليهم احتقاراً لهم وازدراءً، ومع هذا تراهم مطمئنِّين لا يخطُر الخوف على بالهم، {وإذا انقلبوا إلى أهِلِهم}: صباحاً أو مساءً، {انقلبوا فَكِهين}؛ أي: مسرورين مغتبطين، وهذا أشدُّ ما يكون من الاغترار؛ أنَّهم جمعوا بين غاية الإساءة مع الأمن في الدُّنيا، حتى كأنَّهم قد جاءهم كتابٌ وعهدٌ من الله - أنَّهم من أهل السعادة، وقد حكموا لأنفسهم أنَّهم أهلُ الهدى، وأنَّ المؤمنين ضالُّون؛ افتراءً على الله، وتجرؤوا على القول عليه بلا علم. قال تعالى: {وما أُرْسِلوا عليهم حافظين}؛ أي: وما أرسلوا وكلاء على المؤمنين، ملزمين بحفظ أعمالهم، حتى يحرصوا على رميهم بالضَّلال، وما هذا منهم إلاَّ تعنُّتٌ وعنادٌ وتلاعبٌ ليس له مستندٌ ولا برهانٌ.
{29 - 33} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja adhabu ya wahalifu na ujira wa wafanyao wema, na akataja ihtilafu kubwa iliyoko baina yao; akajulisha kwamba wahalifu duniani walikuwa wakiwafanyia masihara Waumini, wakiwakejeli, na "wakiwacheka" kisha "wakikonyezana" walipokuwa wakipita karibu nao, ili kuwadharau na kuwadunisha. Na pamoja na hayo unawaona wana utulivu wala haiwafi hofu katika akili zao. "Na wanaporudi kwa watu wao" asubuhi au jioni "hurudi nao wamefurahi." Lakini huku ndiko kudanganyika kubaya zaidi. Kwamba walijumuisha kati ya kufanya ubaya mkubwa zaidi na kujiona kwamba wako katika amani katika dunia hii, kiasi kwamba ni kwamba wamejiwa na kitabu na ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu - kwamba wao watakuwa miongoni mwa watu wa furaha, na tayari wameshajihukumu kwamba wako katika uwongofu, na kwamba Waumini wamepotea; kwa kumzulia tu Mwenyezi Mungu na wakathubutu kusema juu yake bila elimu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wao" wahalifu "hawakutumwa wawe walinzi juu yao." Yaani, juu ya Waumini, wakawa wamebebeshwa kuwahifadhia vitendo vyao, ndiyo wawanie kuwatuhumu kwamba wamepotea. Haya hawakuyafanya isipokuwa kwa sababu ya usugu, ukaidi na kufanya tu mchezo usiokuwa na msingi wala uthibitisho.
#
{34 - 36} ولهذا كان جزاؤهم في الآخرة من جنس عملهم؛ قال تعالى: {فاليوم}؛ أي: يوم القيامة، {الذين آمنوا من الكفَّارِ يضحكون}: حين يرونَهم في غَمَراتِ العذاب يتقلَّبون وقد ذهب عنهم ما كانوا يفترون، والمؤمنون في غاية الراحة والطمأنينة {على الأرائكِ}: وهي السرر المزيَّنة، {ينظُرون}: إلى ما أعدَّ الله لهم من النعيم، وينظرون إلى وجه ربِّهم الكريم. {هل ثُوِّبَ الكفارُ ما كانوا يفعلون}؛ أي: هل جوزوا من جنس عملهم؟ فكما ضحكوا في الدنيا من المؤمنين ورمَوْهم بالضلال؛ ضحك المؤمنون منهم في الآخرة، حين رأوهم في العذاب والنَّكال الذي هو عقوبةُ الغيِّ والضَّلال. نعم؛ ثُوِّبوا ما كانوا يفعلون عدلاً من الله وحكمةً. والله عليمٌ حكيمٌ.
{34 - 36} Ndiyo maana malipo yao katika Akhera ni ya aina sawa na matendo yao. Amesema Mwenyezi Mungu: "Basi leo;" yaani, Siku ya Kiyama "walioamini ndio watawacheka makafiri" watakapowaona katika undani wa adhabu wakipinduka, na yatawatoka yale waliyokuwa wakiyazua, nao Waumini watakuwa katika starehe na utulivu wa hali ya juu, "juu ya viti vya enzi wakiangalia" yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu, na wakiutazama uso wa Mola wao Mlezi Mtukufu. "Je, makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda?" Yaani, je, wamelipwa kwa aina sawa na matendo yao? Kama vile walivyowacheka Waumini katika dunia hii na kuwatuhumu kwamba ni wapotofu, Waumini watawacheka katika Akhera, watakapowaona katika adhabu na mateso, ambayo ndiyo adhabu ya ukengeufu na upotofu. Ndiyo, walilipwa yale waliyokuwa wakiyafanya kwa uadilifu na hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mwenye hekima.
* * *