:
Tafsiri ya Surat Al-Infitar
Tafsiri ya Surat Al-Infitar
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 5 #
{إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ (1) وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انْتَثَرَتْ (2) وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ (3) وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ (4) عَلِمَتْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ (5)}.
1. Mbingu itakapochanika. 2. Na nyota zitakapotawanyika. 3. Na bahari zitakapopasuliwa. 4. Na makaburi yatakapofukuliwa. 5. Hapo kila nafsi itajua ilichotanguliza, na ilichobakisha nyuma.
#
{1 - 5} أي: إذا انشقَّت السماء، وانفطرت، وتناثرت نجومُها، وزال جمالُها، وفُجِّرت البحار، فصارت بحراً واحداً، وبُعْثِرَتِ القبور بأن أُخْرِج ما فيها من الأموات وحُشِروا للموقف بين يدي الله للجزاء على الأعمال؛ فحينئذٍ ينكشف الغطاء، ويزول ما كان خفيًّا، وتعلم كلُّ نفس ما معها من الأرباح والخسران. هنالك يعضُّ الظالم على يديه إذا رأى ما قدَّمت يداه وأيقن بالشقاء الأبديِّ والعذاب السَّرمديِّ، وهنالك يفوز المتَّقون المقدِّمون لصالح الأعمال بالفوز العظيم والنعيم المقيم والسلامة من عذاب الجحيم.
{1 - 5} Yaani, wakati mbingu zitakapopasuka na kuchanika, nyota zake zikawanyika, uzuri wake ukaondoka, na bahari zikapasuliwa na kuwa bahari moja, na makaburi yakafukuliwa na wafu wakatolewa humo, na wakakusanywa ili kusimama mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya malipo juu ya matendo yao, basi wakati huo kifuniko kitafunuka, na yale yaliyokuwa yamefichika yatawekwa wazi, na kila nafsi itajua ni faida gani na hasara gani iliyo nayo. Hapo, dhalimu atang'ata mikono yake atakapoona yale ambayo mikono yake imefanya na akawa na yakini kwamba atakuwa katika taabu ya milele na adhabu ya kuendelea daima, na huko wacha Mungu, waliotanguliza matendo mema, watapata ushindi mkubwa, neema ya milele, na salama kutoka kwa adhabu ya Jahannamu.
: 6 - 12 #
{يَاأَيُّهَا الْإِنْسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ (6) الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ (7) فِي أَيِّ صُورَةٍ مَا شَاءَ رَكَّبَكَ (8) كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ (9) وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ (10) كِرَامًا كَاتِبِينَ (11) يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ (12)}.
6. Ewe mwanaadamu! Nini kilichokughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? 7. Aliyekuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha. 8. Katika sura yoyote aliyoipenda akakujenga. 9. Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. 10. Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu. 11. Waandishi wenye heshima. 12. Wanayajua mnayoyatenda.
#
{6 - 8} يقول تعالى معاتباً للإنسان المقصِّر في حقِّه المتجرِّئ على معاصيه: {يا أيُّها الإنسان ما غَرَّك بربِّك الكريم}: أتهاوناً منك في حقوقه؟ أم احتقاراً منك لعذابه؟! أم عدم إيمانٍ منك بجزائِهِ؟! أليس هو {الذي خَلَقَكَ فسوَّاك}: في أحسن تقويم، {فعَدَلَك}: وركَّبك تركيباً قويماً معتدلاً في أحسن الأشكال وأجمل الهيئات؟! فهل يَليق بك أن تكفُرَ نعمة المنعِم أو تَجْحَدَ إحسان المحسن؟! إنْ هذا إلاَّ من جهلك وظلمك وعنادك وغشمك؛ فاحمد الله إذْ لم يجعلْ صورتَكَ صورة كلبٍ أو حمارٍ أو نحوهما من الحيوانات، ولهذا قال تعالى: {في أيِّ صورةٍ ما شاء ركَّبَك}.
{6 - 8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akimkemea mtu ambaye amezembe katika haki zake na akathubutu kumuasi: "Ewe mwanaadamu! Nini kilichokughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?" Je, ni kwa sababu umeghafilika mbali na kutekeleza haki zake? Au unaidharau adhabu yake? Au ni kutoamini kwako malipo yake? Je, si Yeye "Aliyekuumba, akakuweka sawa" kwa namna bora zaidi na "akakunyoosha" na akakuweka katika muundo ulionyooka na ulio sawa katika umbo bora na sura nzuri zaidi? Je, inakufailia kukufuru neema za aliyekuneemesha au kukufuru wema wa aliyekufanyia wema? Haya si chochote ila ujinga wako, dhuluma yako, ukaidi wako na udanganyifu wako. Basi msifu Mwenyezi Mungu kwa kuwa hakuifanya sura yako kuwa sura ya mbwa au punda au wanyama wanaofanana na hao, na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga."
#
{9 - 12} وقوله: {كلاَّ بل تكذِّبونَ بالدِّين}؛ أي: مع هذا الوعظ والتَّذكير لا تزالون مستمرِّين على التَّكذيب بالجزاء، وأنتم لا بدَّ أن تُحاسبوا على ما عمِلْتُم، وقد أقام الله عليكم ملائكةً كراماً، يكتُبون أقوالكم وأفعالكم ويَعْلَمونها ، فدخل في هذا أفعالُ القلوبِ وأفعالُ الجوارح؛ فاللائق بكم أن تكرِموهم وتُجِلُّوهم.
{9 - 12} Na kauli yake: "Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo." Yaani, pamoja na mawaidha haya na ukumbusho huu, bado nyinyi mnaendelea kukanusha malipo, na lazima mtaulizwa juu ya matendo yenu mliyoyafanya, na Mwenyezi Mungu amekuteulieni Malaika watukufu wanaoandika maneno yenu na vitendo vyenu na wanavijua. Haya pia yanajumuisha matendo ya nyoyo na matendo ya viungo. Basi linalowafailia ni kuwaheshimu na kuwapa taadhima.
: 13 - 19 #
{إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (13) وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ (14) يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ (15) وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ (16) وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ (17) ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ (18) يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِنَفْسٍ شَيْئًا وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِلَّهِ (19)}.
13. Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema. 14. Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni. 15. Wataingia humo Siku ya Malipo. 16. Na hawatoacha kuwamo humo. 17. Na nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani? 18. Tena nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani? 19. Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.
#
{13 - 19} المراد بالأبرار هم: القائمون بحقوق الله وحقوق عباده، الملازمون للبرِّ في أعمال القلوب وأعمال الجوارح؛ فهؤلاء جزاؤهم النعيم في القلب والرُّوح والبدن في دار الدُّنيا وفي دار البرزخ وفي دار القرار، {وإنَّ الفجَّارَ}: الذين قصَّروا في حقوق الله وحقوق عباده، الذين فَجَرَتْ قلوبُهم ففَجَرَتْ أعمالُهم، {لفي جحيمٍ}؛ أي: عذابٍ أليمٍ في دار الدُّنيا ودار البرزخ وفي دار القرار، {يَصْلَوْنها}: ويعذَّبون بها أشدَّ العذاب {يومَ الدِّينِ}؛ أي: يوم الجزاء على الأعمال، {وما هم عنها بغائبينَ}؛ أي: بل هم ملازمون لها لا يخرُجون منها، {وما أدراك ما يومُ الدِّينِ. ثمَّ ما أدراكَ ما يومُ الدِّينِ}: في هذا تهويلٌ لذلك اليوم الشديد، الذي يحيِّر الأذهان، {يومَ لا تملِكُ نفسٌ لنفسٍ شيئاً}: ولو كانت قريبةً أو حبيبةً مصافيةً ؛ فكلُّ مشتغل بنفسه لا يطلب الفكاك لغيرها. {والأمرُ يومئذٍ لله}: فهو الذي يفصل بين العباد، ويأخُذُ للمظلوم حقَّه من ظالمه. والله أعلم.
{13 - 19} Maana ya watu wema ni wale wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, wanaoshikamana na wema katika matendo ya nyoyo na matendo ya viungo. Hao ujira wao ni furaha katika nyoyo, roho na mwili katika nyumba ya dunia, katika nyumba ya kaburini, na katika makazi ya kubakia milele. "Na hakika waovu" ambao walizembea katika kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, ambao nyoyo zao zilikuwa ovu kwa hivyo vitendo vyao vikawa viovu, "bila ya shaka watakuwa Motoni." Yaani, Adhabu chungu katika nyumba ya dunia, maskani ya kaburini, na katika makazi ya kudumu milele. "Wataingia humo" na waadhibiwe adhabu kali kabisa "Siku ya Malipo" juu ya matendo yao. "Na hawatoacha kuwamo humo" Yaani, bali wao watasalia humo na wala hawatatoka nje yake. "Na nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani? Tena nini kitakachokujulisha Siku ya Malipo ni siku gani?" Huu ni utiaji hofu kuhusiana na siku hiyo kali, ambayo inachanganya. "Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi" hata kama ni jamaa au mpendwa mkubwa mno. Kila mtu atakuwa ameshughulika na nafasi yake mwenyewe, na hatamwombea yeyote ukombozi. "Na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu." Yeye ndiye atakayehukumu baina ya waja, na kumchukulia aliyedhulumiwa haki yake kutoka kwa aliyemdhulumu. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
* * *