Tafsiri ya Surat Al-Inshiqaq
Tafsiri ya Surat Al-Inshiqaq
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{إِذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ (1) وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ (2) وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ (3) وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ (4) وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ (5) يَاأَيُّهَا الْإِنْسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَى رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ (6) فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ (7) فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا (8) وَيَنْقَلِبُ إِلَى أَهْلِهِ مَسْرُورًا (9) وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ (10) فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا (11) وَيَصْلَى سَعِيرًا (12) إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا (13) إِنَّهُ ظَنَّ أَنْ لَنْ يَحُورَ (14) بَلَى إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا (15)}.
1. Itakapochanika mbingu. 2. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza. 3. Na ardhi itakapotanuliwa. 4. Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake, ikawa tupu. 5. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza. 6. Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. 7. Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia. 8. Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi. 9. Na arudi kwa ahali zake na furaha. 10. Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake. 11. Basi huyo ataomba kuteketea. 12. Na ataingia Motoni. 13. Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. 14. Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. 15. Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
#
{1 - 2} يقول تعالى مبيِّناً لما يكون في يوم القيامة من تغيُّر الأجرام العظام: {إذا السماء انشقَّتْ}؛ أي: انفطرت وتمايز بعضها من بعض، وانتثرت نجومُها، وخسف شمسُها وقمرها، {وأذِنَتْ لربِّها}؛ أي: استمعت لأمره وألقت سمعَها وأصاخت لخطابه، أي: حُقَّ لها ذلك؛ فإنَّها مسخَّرة مدبَّرة تحت مسخِّر ملكٍ عظيمٍ لا يُعصى أمره ولا يخالَف حكمُه.
{1 - 2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema,
akieleza yatakayotokea Siku ya Kiyama kuhusiana na mabadiliko ya miili mikubwa: "Itakapochanika mbingu" na nyota zake zikatawanyika, na jua na mwezi wake vikapatwa. "Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi" ili kusikiliza amri yake, ikatega sikio na kusikiliza kwa makini mazungumzo yake. Yaani, alikuwa na haki kwake kufanya hivyo. Kwani imetiishwa na inaendeshwa na Mfalme Mkuu, ambaye amri yake haiwezi kuasiwa wala hukumu yake haihalifiwi.
#
{3 - 5} {وإذا الأرض مُدَّتْ}؛ أي: رجفت وارتجَّت ونُسِفَتْ عليها جبالُها ودُكَّ ما عليها من بناء ومعلم فسويت، ومدَّها الله مدَّ الأديم، حتى صارت واسعةً جدًّا، تسع أهل الموقف على كثرتهم، فتصير قاعاً صفصفاً، لا ترى فيها عوجاً ولا أمتاً، {وألقتْ ما فيها}: من الأموات والكنوز، {وتخلَّتْ}: منهم؛ فإنَّه ينفخ في الصور، فتخرج الأموات من الأجداث إلى وجه الأرض، وتخرج الأرض كنوزها، حتى تكون كالإسطوان العظيم، يشاهده الخلق ويتحسَّرون على ما هم فيه يتنافسون، {وأذِنَتْ لربِّها وحُقَّتْ}.
{3 - 5} "Na ardhi itakapotanuliwa" na milima yake ikapeperushwa mbali, na majengo na alama zilizo juu yake vikavunjwavunjwa, na Mwenyezi Mungu akaitanua kama kutanuliwa kwa ngozi, mpaka ikawa pana sana, yenye kuwatosha wale watakaosimama mahali pa kisimamo cha Kiyama licha ya wingi wao, na ikawa tambarare uwandachini ya usawa, ambayo hutaona humo mdidimio wala muinuko. "Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake" ya wafu na hazina zake "na ikawa tupu." Kwani itapulizwa katika baragumu, na wafu watatoka makaburini waje juu ya uso wa ardhi, na ardhi itatoa hazina zake mpaka ikawa kama mnara mkubwa, na viumbe vitaitazama na kujuta sana kwa yale waliyokuwa wakishindana juu yake. "Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza."
#
{6} {يا أيُّها الإنسانُ إنَّك كادحٌ إلى ربِّكَ كدحاً فملاقيه}؛ أي: إنك ساعٍ إلى الله وعاملٌ بأوامره ونواهيه ومتقرِّبٌ إليه إمَّا بالخير وإمَّا بالشرِّ، ثم تلاقي الله يوم القيامةِ؛ فلا تعدم منه جزاءً بالفضل أو العدل؛ بالفضل إن كنت سعيداً، وبالعقوبة إن كنت شقيًّا.
{6} "Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi" kwa kutenda amri zake na kujiepusha na makatazo yake, na kujikurubisha kwake ima kwa mema au kwa uovu "basi utamkuta" na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Kwa hivyo, hutakosa kutoka kwake malipo ya fadhila zake au kwa uadilifu wake. Atakulipa kwa fadhila zake ikiwa wewe ni miongoni mwa watu watakaokuwa katika furaha, na kwa adhabu ikiwa utakuwa miongoni mwa watu wa mashakani.
#
{7 - 9} ولهذا ذكر تفصيل الجزاء، فقال: {فأمَّا مَنْ أوتي كتابه بيمينِهِ}: وهم أهل السعادة، {فسوف يحاسَبُ حساباً يسيراً}: وهو العرض اليسير على الله، فيقرِّره الله بذنوبه، حتى إذا ظنَّ العبدُ أنَّه قد هلك؛ قال الله تعالى: إنِّي قد سترتُها عليك في الدُّنيا وأنا أستُرها لك اليوم ، {وينقلبُ إلى أهله}: في الجنة {مسروراً}: لأنَّه قد نجا من العذاب وفاز بالثواب.
{7 - 9} Ndiyo maana akataja malipo hayo kwa undani akisema: "Ama atakayepewa daftari lake kwa mkono wa kulia" na hao ndio watu wa furahani, "Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi." Ambayo ni kuonyeshwa kwepesi mbele ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu amfanye kukubali madhambi yake, mpaka mja atakapodhani kwamba ameangamia,
Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Hakika mimi nimekufichia hayo katika dunia, na tena ninakufichia hayo hivi leo "Na arudi kwa ahali zake" Peponi "kwa furaha" kwa sababu ameepushwa na adhabu na akapata malipo mazuri.
#
{10 - 15} {وأمَّا مَن أوتي كتابَه وراء ظهرِهِ}؛ أي: بشماله من وراء ظهره ، {فسوفَ يدعو ثُبوراً}: من الخزي والفضيحة، وما يجد في كتابه من الأعمال التي قدَّمها ولم يتبْ منها، {ويصلى سعيراً}؛ أي: تحيط به السعير من كلِّ جانب، ويقلَّب على عذابها، وذلك لأنَّه {كان في أهلِهِ مسروراً}: لا يخطُرُ البعث على باله، وقد أساء، ولا يظنُّ أنَّه راجعٌ إلى ربِّه وموقوفٌ بين يديه. {بلى إنَّ ربَّه كان به بصيراً}: فلا يحسُنُ أن يترُكَه سدىً لا يُؤمر ولا يُنهى ولا يُثاب ولا يُعاقب.
{10 - 15} "Na ama atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake." Yaani, kwa mkono wake wa kushoto kwa kupitia nyuma ya mgongo wake. "Basi huyo ataomba kuteketea" kwa sababu ya hizaya na fedheha, na kutokana na yale atakayoyakuta katika kitabu chake, yale aliyoyatanguliza na wala hakutubia. "Na ataingia Motoni" na umzunguke kutokea kila upande, na atapindukapinduka katika adhabu yake, na hilo ni kwa sababu "alikuwa furahani kati ya jamaa zake" na haikuwa ikimjia akilini mwake kwamba atafufuliwa, huku amefanya mabaya, na wala hakudhani kwamba atarejea kwa Mola wake Mlezi na kusimamishwa mbele yake. "Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona sawasawa!" Haikufailia kwamba amuwache bure tu, haamrishwi wala hakatazwi, wala halipwi mazuri wala haadhibiwi.
{فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ (16) وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ (17) وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ (18) لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَنْ طَبَقٍ (19) فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (20) وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ (21) بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ (22) وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ (23) فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (24) إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ (25)}.
16. Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapokuchwa. 17. Na kwa usiku na unavyovikusanya. 18. Na kwa mwezi unapopevuka. 19. Lazima mtapanda tabaka kwa tabaka! 20. Basi wana nini hawaamini? 21. Na wanaposomewa Qur-ani hawasujudu? 22. Bali waliokufuru wanakanusha tu. 23. Na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhamiria. 24. Basi wabashirie adhabu chungu! 25. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usiomalizika.
#
{16 - 19} أقسم في هذا الموضع بآيات الليل، فأقسم بالشَّفق؛ الذي هو بقيَّة نور الشمس الذي هو مفتتح الليل، {والليل وما وَسَقَ}؛ أي: احتوى عليه من حيواناتٍ وغيرها، {والقمرِ إذا اتَّسَقَ}؛ أي: امتلأ نوراً بإبداره، وذلك أحسن ما يكون وأكثر منافع. والمقسَم عليه قوله: {لَتَرْكَبُنَّ}؛ أي: أيُّها الناس {طبقاً}: بعد {طبقٍ}؛ أي: أطواراً متعدِّدة وأحوالاً متباينة من النُّطفة إلى العلقة إلى المضغة إلى نفخ الرُّوح، ثم يكون وليداً وطفلاً ومميزاً ، ثم يجري عليه قَلَمُ التَّكليف والأمر والنَّهي، ثم يموت بعد ذلك، ثم يُبْعَثُ ويجازى بأعماله؛ فهذه الطبقات المختلفة الجارية على العبد دالَّة على أنَّ الله وحده هو المعبودُ الموحَّدُ المدبِّرُ لعباده بحكمته ورحمته، وأنَّ العبد فقيرٌ عاجزٌ تحت تدبير العزيز الرحيم.
{16 - 19} Aliapa mahali hapa kwa ishara za usiku, kama vile jua linapokuchwa. "Na kwa usiku na unavyovikusanya" kama vile wanyama na vitu vingine, "Na kwa mwezi unapopevuka," hapo huwa unakuwa mzuri zaidi na wenye manufaa mengi zaidi. Na kilichokusudiwa na kiapo hiki ni "Lazima mtapanda" enyi watu "tabaka kwa tabaka" na hali tofauti tofauti, kutoka kwa manii hadi pande za damu hadi pande la nyama hadi kupuliziwa roho, kisha anakuwa mtoto mchanga, kisha mtoto mwenye uwezo wa kupambanua mambo, kisha kalamu kujukumishwa inasimama juu yake akawa anaamrishwa na kukatazwa. Kisha anakufa baada ya hayo, kisha atafufuliwa na kulipwa kwa matendo yake. Tabaka hizi tafauti anazozipitia mja zinaashiria kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayepaswa kuabudiwa, anayeendesha waja wake kwa hekima yake na rehema zake, na kwamba mja ni hana uwezo na yuko chini ya uendeshaji wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.
#
{20 - 24} ومع هذا؛ فكثيرٌ من الناس لا يؤمنون، {وإذا قُرِئَ عليهم القرآنُ لا يَسْجُدونَ}؛ أي: لا يخضعون للقرآن ولا ينقادون لأوامره ونواهيه، {بل الذين كفروا يكذِّبون}؛ أي: يعاندون الحقَّ بعدما تبيَّن؛ فلا يُسْتَغْرَبُ عدم إيمانهم وانقيادهم للقرآن؛ فإنَّ المكذِّب بالحقِّ عناداً لا حيلة فيه، {والله أعلم بما يُوعون}؛ أي: بما يعملونه وينوونه سرًّا؛ فالله يعلم سِرَّهم وجهرهم، وسيجازيهم بأعمالهم، ولهذا قال: {فبشِّرْهم بعذابٍ أليم}: وسميت البشارة بشارةً؛ لأنَّها تؤثِّر في البشرة سروراً أو غمًّا.
{20 - 24} Hata hivyo, watu wengi hawaamini, kwa hivyo, "wanaposomewa Qur-ani hawasujudu" wala hawatii amri zake na makatazo yake. "Bali waliokufuru wanakanusha tu." Yaani, wanaipinga haki baada ya kudhihirika kwake. Kwa hivyo, haishangazi kwamba hawaamini na kujisalimisha kwa Qur-ani. Kwani mwenye kukadhibisha haki kwa ukaidi hana njia ya kumsaidia. "Na Mwenyezi Mungu anajua wanayoyadhamiria" kwa maana Mwenyezi Mungu anazijua siri zao na vitendo vyao vilivyo wazi, na atawalipa kwa vitendo vyao,
na ndiyo maana akasema: "Basi wabashirie adhabu chungu!" Na hii imeitwa bishara kwa sababu huathiri kwa njia ya kuleta furaha au huzuni.
#
{25} فهذه حال أكثر الناس؛ التكذيب بالقرآن، وعدم الإيمان به. ومن الناس فريقٌ هداهم الله فآمنوا بالله وقبلوا ما جاءتهم به الرُّسُل، فَـ {آمنوا وعملوا الصالحات}: فهؤلاء {لهم أجرٌ غير ممنونٍ}؛ أي: غير مقطوع، بل هو أجرٌ دائمٌ ممَّا لا عينٌ رأتْ ولا أذنٌ سمعتْ ولا خطرَ على قلبِ بشرٍ. والحمد لله.
{25} Hii ndiyo hali ya watu wengi; kuikadhibisha Qur-ani na kutoiamini. Na katika watu lipo kundi aliloliongoza Mwenyezi Mungu, wakamwamini Mwenyezi Mungu, na wakakubali yale waliyowaletea Mitume, "wale walioamini na wakatenda mema" basi "hao watakuwa na ujira usiomalizika." Bali ni malipo ya kudumu kutokana na yale ambayo jicho halijawahi kuona, sikio halijawahi kusikia, na wala hawajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *