Tafsiri ya Surat Qul uuhiya ilayya (Sema: Imeteremshwa kwangu)
Tafsiri ya Surat Qul uuhiya ilayya
(Sema: Imeteremshwa kwangu)
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا (1) يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا (2)}.
1.
Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza,
na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-ani ya ajabu! 2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
#
{1} أي: {قل}: يا أيُّها الرسول للناس، {أوحِيَ إليَّ أنَّه استمع نفرٌ من الجنِّ}: صرفهم الله إلى رسوله لسماع آياته؛ لتقوم عليهم الحجَّة وتتمَّ عليهم النعمة ويكونوا منذِرين لقومهم، وأمر [اللَّهُ] رسولَه أن يقصَّ نبأهم على الناس، وذلك أنَّهم لما حضروه؛ قالوا: أنصتوا، فلما أنصتوا؛ فهموا معانيه ووصلت حقائقُه إلى قلوبهم. {فقالوا إنَّا سمِعْنا قرآناً عَجَباً}؛ أي: من العجائب الغالية والمطالب العالية.
{1} Yaani, "Sema" ewe Mtume uwaambie watu, "Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza." Mwenyezi Mungu aliwaelekeza kwa Mtume wake ili wazisikie Aya zake; ili hoja ithibitike juu yao, na ili neema itimie juu yao, na ili wawe waonyaji kwa watu wao. Mwenyezi Mungu alimuamrisha Mtume wake kwamba asimulie habari yao hii kwawa watu, kwa sababu, walipoihudhuria,
wakasema: 'Sikilizeni na mnyamaze.' Basi waliponyamaza, walielewa maana zake na uhakika wake ukafikia mioyoni mwao.
'Wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-ani ya ajabu!" Yaani, ni moja ya maajabu ya thamani kubwa sana na mambo ya juu zaidi yatafutwayo.
#
{2} {يهدي إلى الرُّشْدِ}: والرُّشدُ: اسمٌ جامعٌ لكلِّ ما يرشد الناس إلى مصالح دينهم ودنياهم، {فآمنَّا به ولن نُشْرِكَ بربِّنا أحداً}: فجمعوا بين الإيمان الذي يدخُلُ فيه جميع أعمال الخير، وبين التَّقوى المتضمِّنة لترك الشرِّ، وجعلوا السبب الداعي لهم إلى الإيمان وتوابعه ما علموه من إرشادات القرآن، وما اشتمل عليه من المصالح والفوائد واجتناب المضارِّ؛ فإنَّ ذلك آيةٌ عظيمةٌ وحجَّةٌ قاطعةٌ لمن استنار به واهتدى بهديه، وهذا الإيمانُ النافع المثمر لكلِّ خير، المبنيُّ على هداية القرآن؛ بخلاف إيمان العوائد والمَرْبى والإلف ونحو ذلك؛ فإنَّه إيمانُ تقليدٍ تحت خطر الشُّبُهات والعوارض الكثيرة.
"Inaongoza kwenye uwongofu." Na uwongofu ni jina la jumla ambalo linajumuisha kila kitu kinachoongoza binadamu kwenye masilahi ya dini yao na dunia yao. "Kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi." Kwa hivyo, wakaunganisha kati ya imani, ambayo yanaingia ndani yake matendo mema yote, na kati ya ucha Mungu, ambao unaojumuisha kuacha maovu, na wakaifanya sababu ya iliyowasukuma kuingia katika imani na kutimiza mambo yanayofungamana nayo ni yale waliyoyajua ya maelekezo ya Qur-ani Tukufu na yale inayojumuisha ya masilahi na faida mbalimbali, na kujiepusha na mambo yenye madhara. Kwa maana hayo ni ishara kubwa na hoja ya kukata kwa mwenye kutafuta nuru yake na kuongoka kwa mwongozo wake. Na hii ndiyo imani yenye manufaa yenye kuzaa matunda mema yote, iliyojengwa juu ya mwongozo wa Qur-ani. Kinyume na imani ya desturi, malezi, na mazoea ya kila siku; kwa hakika hiyo ni imani ya kuiga iliyo chini ya hatari ya fikira potofu na vikwazo vingi.
[{وَأَنَّهُ تَعَالَى جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا (3) وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّهِ شَطَطًا (4)}].
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana. 4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo uliopindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
#
{3} {وأنَّه تعالى جَدُّ رَبِّنا}؛ أي: تعالت عظمتُه وتقدَّسَتْ أسماؤُه، {ما اتَّخَذَ صاحبةً ولا ولداً}: فعلموا من جَدِّ الله وعظمتِهِ ما دلَّهم على بطلان مَنْ يزعُمُ أنَّ له صاحبةً أو ولداً؛ لأنَّ له العظمة والجلال في كلِّ صفة كمال، واتِّخاذُ الصاحبة والولد ينافي ذلك؛ لأنَّه يضادُّ كمال الغنى.
{3} "Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana." Basi wakajua katika ukubwa wa Mwenyezi Mungu na ukuu wake kitu kilichowaonyesha ubatili wa anayedai kwamba ana mke au mwana. Kwa sababu Yeye ana ukuu na utukufu katika kila sifa ya ukamilifu. Na kuchukua mke na mwana kunapingana na hilo. Kwa sababu vinapingana na ukamilifu wa kujitosheleza.
#
{4} {وأنَّه كان يقولُ سفيهُنا على الله شططاً}؛ أي: قولاً جائراً عن الصواب متعدياً للحدِّ، وما حمله على ذلك إلاَّ سفهُه وضعفُ عقله، وإلاَّ؛ فلو كان رزيناً مطمئناً؛ لعرف كيف يقول.
{4} "Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo uliopindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu." Na hakuna lililomsukuma kufanya hivyo isipokuwa upumbavu wao na udhaifu wa akili yake. Vinginevyo; ikiwa angekuwa wa akili sawasawa iliyotulia, basi angejua namna ya kusema.
{وَأَنَّا ظَنَنَّا أَنْ لَنْ تَقُولَ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا (5)}.
5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uongo Mwenyezi Mungu.
#
{5} أي: كنَّا مغترِّين قبل ذلك، غرَّتنا السادة والرؤساء من الجنِّ والإنس، فأحسنَّا بهم الظنَّ، وحسبناهم لا يتجرؤون على الكذب على الله؛ فلذلك كنَّا قبل ذلك على طريقهم؛ فاليوم إذ بان لنا الحقُّ؛ سلكنا طريقه ، وانقَدْنا له، ولم نبالِ بقول أحدٍ من الخلق يعارض الهدى.
{5} Yaani, sisi tulidanganywa kabla ya hapo. Tulidanganywa na mabwana na viongozi katika majini na wanadamu, kwa hivyo tukawafikiria vyema, na tukadhania kwamba hawatathubutu kumsingizia Mwenyezi Mungu uwongo. Basi sisi ndiyo maana tulikuwa kwenye njia yao kabla ya hayo. Lakini leo, wakati ukweli umeshatudhihirikia; tumeifuata njia yake, tukamtii, wala hatukujali maneno ya yeyote miongoni mwa viumbe anayeupinga uongofu.
{وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِنَ الْإِنْسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا (6)}.
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu waliokuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
#
{6} أي: كان الإنس يعوذون بالجنِّ عند المخاوف والأفزاع ويعبُدونهم، فزاد الإنسُ الجنَّ رهقاً؛ أي: طغياناً وتكبراً، لمَّا رأوا الإنس يعبدونَهم ويستعيذون بهم، ويُحتمل أنَّ الضمير وهي الواو ترجع إلى {الجنِّ}؛ أي: زاد الجنُّ الإنسَ ذُعْراً وتخويفاً لما رأوْهم يستعيذون بهم ليلجِئوهم إلى الاستعاذة بهم والتمسُّك بما هم عليه، فكان الإنسيُّ إذا نزل بوادٍ مخوفٍ؛ قال: أعوذ بسيِّد هذا الوادي من سفهاء قومه.
{6} Yaani, wanadamu walikuwa wakitafuta hifadhi kwa majini wakati wa hofu na mafadhaiko na kuwaabudu, basi wanadamu wakawa wanawaelemea majini, kwa kuwafanya wavuke mipaka na kuwa na kiburi, walipowaona wanadamu wanawaabudu na kutafuta hifadhi kwao. Na inawezekana kwamba maana yake pia ni kwamba "majini" wawalizidisha wanadamu hofu na mafadhaiko kwa walipowaona wakitafuta hifadhi kwao, ili kuwashinikiza wajikinge kwao na washikamane na wanavyofanya wao. Basi wakawa wanadamu wanapoteremka kwenye bonde la kutisha,
wanasema: 'Ninajikinga kwa bwana wa bonde hili kutokana na wapumbavu wa watu wake."
{وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنْتُمْ أَنْ لَنْ يَبْعَثَ اللَّهُ أَحَدًا (7)}.
7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyodhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
#
{7} أي: فلمَّا أنكروا البعث؛ أقدموا على الشرك والطغيان.
{7} Yaani, walipokanusha kufufuliwa, wakaanza kufanya ushirikina na kuvuka mno mipaka.
[{وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا (8) وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ فَمَنْ يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَصَدًا (9)}].
8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo. 9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
#
{8 - 9} {وأنَّا لمسنا السماءَ}؛ أي: أتيناها واختبرناها، {فوجَدْناها مُلِئَتْ حرساً شديداً}: عن الوصول إلى أرجائها والدنوِّ منها، {وشُهُباً}: يرمى بها من استرقَ السمعَ، وهذا مخالفٌ لعادتنا الأولى؛ فإنَّا كنَّا نتمكَّن من الوصول إلى خبر السماء فإنا {كنَّا نقعدُ منها مقاعدَ للسمع}: فنتلقَّف من أخبار السماء ما شاء الله، {فمن يستمِع الآنَ يَجِدْ له شهاباً رصداً}؛ أي: مرصداً له معدًّا لإتلافه وإحراقه؛ أي: وهذا له شأنٌ عظيمٌ ونبأٌ جسيمٌ، وجزموا أنَّ الله تعالى أراد أن يحدِثَ في الأرض حادثاً كبيراً من خيرٍ أو شرٍّ؛ فلهذا قالوا:
{8 - 9} "Nasi tulizigusa mbingu." Yaani, tulizijia na kuzifanyia mtihani, "na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu" wanaozuia kufikia pande zake na hata kuzikaribia. Na vilikuwepo "vimondo" ambavyo hupigwa kwavyo wanaosikiliza kwa siri, na hili ni kinyume na desturi yetu ya hapo mwanzo. Kwani tulikuwa tunaweza kuzifikia habari za mbinguni, basi "tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza" na tungekusanya kutoka katika habari za mbinguni anachotaka Mwenyezi Mungu. "Lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia" na kilichotayarishwa kumharibu na kumteketeza. Na hili lilikuwa kwa sababu ya jambo kubwa na habari kubwa. Basi wakawa na uhakika kwamba Mwenyezi Mungu alitaka kufanya tukio kubwa litokee duniani, la uzuri au ubaya.
Ndiyo maana wakasema:
{وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَنْ فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا (10)}.
10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.
#
{10} أي: لا بدَّ من هذا أو هذا؛ لأنَّهم رأوا الأمر تغيَّر عليهم تغيُّراً أنكروه، فعرفوا بفطنتهم أنَّ هذا الأمر يريده الله ويحدِثُه في الأرض، وفي هذا بيانٌ لأدبهم إذ أضافوا الخير إلى الله تعالى، والشرُّ حذفوا فاعله تأدُّباً [مع اللَّه].
{10} Yaani, ni lazima hiki au kile kitokee. Kwa sababu waliona jambo hilo limewabadilikia kubadilika walikokanusha, kwa hivyo wakajua kwa utambuzi wa akili zao kuwa jambo hili alilitaka Mwenyezi Mungu na atalifanya kutokea duniani, na katika haya kuna maelezo ya adabu zao; kwani walifungamanisha heri tu na Mwenyezi Mungu, nayo shari wakafuta aliyeitenda ili kuonyesha adabu nzuri
[mbele ya Mwenyezi Mungu].
[{وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَلِكَ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا (11)}].
11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.
#
{11} {وأنَّا منَّا الصالحون ومنَّا دون ذلك}؛ أي: فساق وفجار وكفار، {كنَّا طرائِقَ قِدَداً}؛ أي: فرقاً متنوعةً وأهواءً متفرقةً؛ كلُّ حزبٍ بما لديهم فرحون.
{11} "Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo." Yaani, wale wavukao mipaka, waovu na makafiri. "Tumekuwa njia mbali mbali" zenye matamanio tofauti tofauti. Kila kundi kikifurahia kile walicho nacho.
{وَأَنَّا ظَنَنَّا أَنْ لَنْ نُعْجِزَ اللَّهَ فِي الْأَرْضِ وَلَنْ نُعْجِزَهُ هَرَبًا (12)}.
12. Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
#
{12} أي: وأنَّا في وقتنا الآن تبيَّن لنا كمال قدرة الله وكمال عجزنا، وأنَّ نواصينا بيد الله؛ فلن نعجِزَه في الأرض ولن نعجِزَه إن هَرَبْنا وسَعَيْنا بأسباب الفرار والخروج عن قدرته، لا ملجأ منه إلاَّ إليه.
{12} Yaani, katika wakati wetu huu sasa, imetubainikia ukamilifu wa nguvu za Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa kutoweza kwetu, na kwamba nywele za utosini kwetu ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, hatutamshinda duniani, wala hatuwezi kumshinda tukamponyoka kwa kukimbia na kufanya bidii kutafuta njia za kutorokea na kutoka katika uwezo wake. Hatuna kimbilio lolote kutoka kwake isipokuwa kwenda kwake tu.
[{وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَى آمَنَّا بِهِ فَمَنْ يُؤْمِنْ بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا (13) وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا (14)}].
13. Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa. 14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanaoacha haki. Basi waliosilimu, hao ndio waliotafuta uwongofu.
#
{13} {وأنَّا لمَّا سمِعنا الهدى}: وهو القرآن الكريم الهادي إلى الصراط المستقيم، وعرفنا هدايته وإرشاده؛ أثَّر في قلوبنا، فآمنَّا به، ثم ذكروا ما يرغِّب المؤمن، فقالوا: {فمن يؤمِن بربِّه فلا يخافُ بخساً ولا رَهَقاً}؛ أي: من آمن به إيماناً صادقاً؛ فلا عليه نقصٌ ولا أذىً يلحقُه، وإذا سَلِمَ من الشرِّ؛ حصل له الخيرُ؛ فالإيمان سببٌ داعٍ إلى [حصول] كلِّ خيرٍ وانتفاء كلِّ شرٍّ.
{13} "Nasi tulipousikia uwongofu" nayo ni Qur-ani Tukufu inayoongoza kwenye njia iliyonyooka, na tukautambua uwongofu wake na kuelekeza kwake, ikaathiri nyoyo zetu, basi tukaiamini. Kisha wakataja yanayomtamanisha Muumini,
wakasema: "Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa." Na ikiwa atasalimika kutokana na uovu, basi atapata heri. Kwa hivyo, imani ni sababu inayoitia
[kwenye kupata] kila wema na kutokuwepo kwa uovu wote.
#
{14} {وأنَّا منَّا المسلمونَ ومنَّا القاسطونَ}؛ أي: الجائرون العادلون عن الصراط المستقيم، {فَمَنْ أسلم فأولئك تَحَرَّوْا رَشَداً}؛ أي: أصابوا طريق الرشد الموصل لهم إلى الجنة ونعيمها.
{14} "Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanaoacha haki" wanaopotea mbali na njia iliyonyooka. "Basi waliosilimu, hao ndio waliotafuta uwongofu." Yaani, wameifikia njia ya uwongofu itakayowafikisha Peponi na neema zake.
{وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا (15) [وَأَلَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُمْ مَاءً غَدَقًا (16) لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ وَمَنْ يُعْرِضْ عَنْ ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا (17)}].
15. Na ama wanaoacha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu. 16. Na lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia tungeliwanywesha maji kwa wingi. 17. Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anayepuuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.
#
{15 - 17} {وأما القاسطون فكانوا لجهنم حطباً}: وذلك جزاءً على أعمالهم، لا ظلم من الله لهم، فإنَّهم {لو استقاموا على الطريقةِ}: المثلى، {لأسْقَيْناهم ماءً غَدَقاً}؛ أي: هنيئاً مريئاً، ولم يمنعْهم ذلك إلاَّ ظلمهم وعدوانهم، {لِنَفْتِنَهم فيه}؛ أي: لنختبرهم [فيه] ونمتحِنَهم ليظهر الصادق من الكاذب، {ومن يعرِضْ عن ذكر ربِّه يَسْلُكْه عذاباً صَعَداً}؛ أي: من أعرض عن ذكر الله الذي هو كتابه، فلم يتَّبِعْه وينقدْ له، بل لها عنه وغفل ؛ يَسْلُكْه عذاباً صَعَداً؛ أي: بليغاً شديداً.
{15 - 17} "Na ama wanaoacha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu." Hayo ni malipo ya vitendo vyao, si kwamba Mwenyezi Mungu aliwadhulumu. Kwani "lau kama wangelisimama sawasawa juu ya njia" bora zaidi, "tungeliwanywesha maji kwa wingi." Yaani, kwa furaha na starehe, na hakuna kilichowazuilia mbali na hayo isipokuwa dhuluma yao na kuvuka kwao mipaka. "Ili tuwajaribu kwa hayo" ili adhihirike mkweli mbali na mwongo. "Na anayepuuza kumkumbuka Mola wake Mlezi" ambacho ni Kitabu chake, basi akawa hakukifuata na kukitii, bali alikipuuza na kughafilika mbali nacho "atamsukuma kwenye adhabu ngumu."
{وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّهِ أَحَدًا (18) [وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا (19) قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا (20) قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا (21) قُلْ إِنِّي لَنْ يُجِيرَنِي مِنَ اللَّهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِنْ دُونِهِ مُلْتَحَدًا (22) إِلَّا بَلَاغًا مِنَ اللَّهِ وَرِسَالَاتِهِ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا (23) حَتَّى إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا (24) قُلْ إِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ مَا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُ رَبِّي أَمَدًا (25) عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَى غَيْبِهِ أَحَدًا (26) إِلَّا مَنِ ارْتَضَى مِنْ رَسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا (27) لِيَعْلَمَ أَنْ قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَى كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا (28)}].
18. Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu. 19. Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu aliposimama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga! 20.
Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote. 21.
Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni. 22.
Sema: Hakika hapana yeyote awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipokuwa kwake Yeye tu. 23. Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele. 24. Hata watakapo yaona wanayoahidiwa, ndipo watakapojua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi. 25.
Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu. 26. Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake. 27. Isipokuwa Mtume wake aliyemridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake. 28. Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote waliyo nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.
#
{18} {وأنَّ المساجد لله فلا تدعوا مع الله أحداً}؛ أي: لا دعاء عبادةٍ ولا دعاء مسألةٍ؛ فإنَّ المساجد التي هي أعظم محالِّ العبادة مبنيَّةٌ على الإخلاص لله والخضوع لعظمته والاستكانة لعزَّته.
{18} "Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu." Si dua ya ibada wala dua ya kuomba kitu. Kwani misikiti, ambayo ndiyo sehemu kubwa zaidi za ibada, imejengwa juu ya kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, kuunyenyekea ukuu wake, na kutii utukufu wake.
#
{19} {وأنَّه لمَّا قام عبدُ اللهِ يدعوه}؛ أي: يسأله ويتعبَّد له ويقرأ القرآن كاد الجنُّ من تكاثُرِهم عليه، {يكونون عليه لِبَداً}؛ أي: متلبِّدين متراكمين حرصاً على [سماع] ما جاء به من الهدى.
{19} "Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu aliposimama kumwomba" na kumuabudu, na anasoma Qur-ani, majini wakawa karibu zaidi "kumzonga" kwa sababu ya wingi wao, kwa sababu ya shauku yao kubwa ya
[kusikia] uwongofu aliokuja nao.
#
{20} {قل}: لهم يا أيُّها الرسول، مبيِّناً حقيقة ما تدعو إليه: {إنَّما أدعو ربِّي ولا أشرِكُ به أحداً}؛ أي: أوحِّده وحده لا شريك له، وأخلع ما دونَه من الأنداد والأوثان، وكلُّ ما يتَّخذه المشركون من دونه.
{20} "Sema" ewe Mtume,
ukibainisha uhakika wa hayo unayoyalingania: "Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote." Na ninajitenga mbali na vyote visivyokuwa yeye miongoni mwa masanamu na vyote viabudiwavyo na washirikina badala yake.
#
{21 - 22} {قل إنِّي لا أملِكُ لكم ضَرًّا ولا رَشَداً}: فإنِّي عبدٌ ليس لي من الأمر والتصرُّفِ شيءٌ ، {قلْ إنِّي لن يُجيرَني من اللهِ أحدٌ}؛ أي: لا أحدَ أستجير به ينقذني من عذاب الله، وإذا كان الرسولُ الذي هو أكملُ الخلق لا يملكُ ضرًّا ولا رشداً ولا يمنعُ نفسَه من الله شيئاً إن أراده بسوءٍ؛ فغيرُهُ من الخلق من باب أولى وأحرى، {ولن أجدَ من دونِهِ مُلْتَحَداً}؛ أي: ملجأ ومنتصراً.
{21 - 22} "Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni" Kwani mimi ni mja, wala sina chochote katika kuamrisha na kuendesha mambo.
"Sema: Hakika hapana yeyote awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu" ambaye ataweza kuniokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa Mtume, ambaye ni mkamilifu zaidi wa viumbe wote, hawezi kumiliki madhara wala uwongofu, na wala hawezi kujizuia chochote kutokana na Mwenyezi Mungu akimtakia mabaya, basi asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe ndio wanafailia zaidi na kustahili zaidi kutokuwa na uwezo huo, "wala sitapata pa kukimbilia isipokuwa kwake Yeye tu."
#
{23} {إلاَّ بلاغاً من الله ورسالاتِهِ}؛ أي: ليس لي مزيَّةٌ على الناس إلاَّ أنَّ الله خصَّني بإبلاغ رسالاته ودعوة خلقِهِ إليه ، وبذلك تقوم الحجَّةُ على الناس، {ومن يَعْصِ الله ورسولَه فإنَّ له نارَ جهنَّمَ خالدين فيها أبداً}: وهذا المراد به المعصية الكفريَّة كما قيَّدتها النُّصوص الأخر المحكمة، وأمَّا مجرَّد المعصية؛ فإنَّه لا يوجب الخلود في النار؛ كما دلَّت على ذلك آيات القرآن والأحاديث عن النبيِّ - صلى الله عليه وسلم -، وأجمع عليه سَلَفُ الأمَّة وأئمَّة هذه الأمَّة.
{23} "Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na jumbe zake." Yaani, sina sifa mahususi juu ya watu isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu ameniteua mimi kwa ajili ya kufikisha ujumbe wake na kuwalingania viumbe wake, na kwa hayo hoja inasimama juu ya watu. "Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele." Kilichokusudiwa na maasi hapa ni ukafiri, kama vile maandiko mengine yaliyo wazi mno yalivyoizuilia maana hii hivyo. Na ama kuasi tu, huko hakulazimu umilele katika Moto, kama zilivyoashiria hivyo aya za Qur-ani na Hadithi kutoka kwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – na watangulizi wema wa umma huu na maimamu wake wakakubaliana juu yake kwa kauli moja.
#
{24} {حتى إذا رأوا ما يوعدونَ}؛ أي: شاهدوه عياناً وجزموا أنَّه واقعٌ بهم، {فسيعلمون}: في ذلك الوقت حقيقة المعرفة، {مَنْ أضعفُ ناصراً وأقلُّ عدداً}: حين لا ينصرُهُم غيرهم، ولا أنفسهم ينتصِرونَ، وإذْ يُحْشَرون فرادى كما خُلِقوا أوَّلَ مرَّةٍ.
{24} "Hata watakapoyaona wanayoahidiwa" kwa macho yao na wakawa na yakini ya kuwa yameshawafika "ndipo watakapojua" wakati huo uhakika wa kujua "ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi" wakati ambapo wengine hawataweza kuwasaidia, wala wao wenyewe hawatakuwa na uwezo wa kujisaidia, watakapokusanywa mmoja mmoja kama walivyoumbwa mara ya kwanza.
#
{25 - 26} {قل} لهم إنْ سألوك فقالوا: متى هذا الوعد؟: {إنْ أدري أقريبٌ ما توعدونَ أمْ يجعلُ له ربِّي أمداً}؛ أي: غايةً طويلةً؛ فعلمُ ذلك عند الله {عالمُ الغيب فلا يُظْهِرُ على غيبِهِ أحداً}: من الخلق، بل انفرد بعلم الضمائر والأسرار والغيوب.
{25 - 26} "Sema" uwaaambie wakikuuliza na wakasema: Ahadi hii itakuwa lini? "Sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu." Kwa hivyo elimu ya haya yako kwa Mwenyezi Mungu. "Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote ghaibu yake" miongoni mwa viumbe. Bali Yeye tu ndiye ajuaye yaliyo katika dhamiri, siri na ghaibu.
#
{27} {إلاَّ منِ ارتضى من رسول}؛ أي: فإنَّه يخبره بما اقتضت حكمته أن يخبِرَه به، وذلك لأنَّ الرسل ليسوا كغيرهم؛ فإنَّ الله أيَّدهم بتأييدٍ ما أيَّده أحداً من الخلق، وحفظ ما أوحاه إليهم حتى يبلِّغوه على حقيقته؛ من غير أن تَقْرَبَهُ الشياطينُ فيزيدوا فيه أو يَنْقُصوا، ولهذا قال: {فإنَّه يَسْلُكُ من بينِ يديهِ ومن خلفِهِ رَصَداً}؛ أي: يحفظونه بأمر الله.
{27} "Isipokuwa Mtume wake aliyemridhia." Yaani, anamwambia kile ambacho kinaendana na hekima yake amwambie. Na hiyo ni kwa sababu Mitume si kama wengine. Kwani Mwenyezi Mungu aliwaunga mkono kwa njia ambayo hakuwahi kuunga mkono kiumbe chake chochote, na akayahifadhi yale aliyoyateremsha kwao mpaka wayafikishe kama yalivyo kiuhakika. Bila ya mashetani kuyakaribia wakayaongezea au kuyapunguza,
na ndiyo maana akasema: "Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake" ili wamhifadhi kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
#
{28} {ليعلم} بذلك {أن قد أبْلَغوا رسالات ربِّهم}: بما جعله لهم من الأسباب، {وأحاط بما لَدَيْهم}؛ أي: بما عندهم وما أسرُّوه وما أعلنوه، {وأحصى كلَّ شيءٍ عدداً}.
{28} "Ili Yeye ajue" kwa hayo "kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi" na kwa njia ya visababu alivyowawekea. "Na Yeye anayajua vyema yote waliyo nayo" miongoni mwa yale waliyokuwa wakiyaficha na yale waliyoyaweka hadharani. "Na amedhibiti idadi ya kila kitu."
Kuna faida nyingi katika sura hii: Miongoni mwake ni kuwepo kwa majini, na kwamba wamejukumishwa na sheria; waamrishwa na wamekatazwa na watalipwa kwa matendo yao, kama ilivyoelezwa wazi katika Sura hii na nyinginezo. Na miongoni mwake ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alitumwa kwa majini kama vile alivyotumwa kwa wanadamu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alituma kundi la majini kumwendea ili wasikilize yale yanayoteremshwa kwake ili wawafikishie hayo watu wao. Na miongoni mwake ni akili nzuri ya majini na kujua kwao haki, na kwamba kile kilichowapelekea kuamini ni yale waliyokuwa na uhakika nayo ya uwongofu uliopo katika Qur-ani na tabia zao njema katika usemi wao. Na miongoni mwake ni utunzaji wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake na kuhifadhi kwake yale aliyokuja nayo. Kwa maana, zilipoanza dalili za unabii wake, mbingu zikalindwa na vimondo, na mashetani wakakimbia kutoka mahali pao huko, na wakafadhaika wakatoka katika mahali walipokuwa wakiskizia habari za mbinguni, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwarehemu kwaye wakazi wa ardhi kwa rehema isiyo na kipimo, na Mola wao Mlezi akawatakia uwongofu. Kwa hivyo akataka kudhihirisha katika dini yake, sheria yake na elimu yake katika ardhi yale ambayo nyoyo zitapata bashasha, na wafurahi kwayo wenye akili nzuri, na zidhihirike kwayo alama za Kiislamu, na wakomeke kwayo wana masanamu na vyote viabudiwavyo badala ya Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwake ni shauku kubwa ya majini katika kumsikiliza Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na kukusanyika kwao kando yake. Na miongoni mwake ni kwamba Sura hii ilijumuisha amri ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kukataza ushirikina, na ikabainisha hali ya viumbe, na kwamba kila mmoja wao hastahiki uzito wa chembe wa kuabudiwa. Kwa sababu ikiwa Mtume Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - hana uwezo wa kumnufaisha wala kumdhuru yeyote, na hata hana uwezo kwa ajili yake mwenyewe, basi anajulikana kwamba viumbe vyote viko hivi. Kwa hivyo ni makosa na dhuluma kumfanya yule mwenye maelezo haya kuwa mungu mwingine. Na miongoni mwake ni kwamba elimu ya ghaibu anaijua Mwenyezi Mungu tu. Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe anayeijua. Isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemridhia na akamchagua kujua baadhi yake.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *