:
Tafsiri ya Surat Nuh, amani iwe juu yake.
Tafsiri ya Surat Nuh, amani iwe juu yake.
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 28 #
{إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ أَنْ أَنْذِرْ قَوْمَكَ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (1) قَالَ يَاقَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُبِينٌ (2) أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ (3) يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى إِنَّ أَجَلَ اللَّهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ لَوْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (4) قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا (5) فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا (6) وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا (7) ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا (8) ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنْتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا (9) فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا (10) يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُمْ مِدْرَارًا (11) وَيُمْدِدْكُمْ بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَلْ لَكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَلْ لَكُمْ أَنْهَارًا (12) مَا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّهِ وَقَارًا (13) وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا (14) أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا (15) وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا (16) وَاللَّهُ أَنْبَتَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا (17) ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا (18) وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا (19) لِتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا (20) قَالَ نُوحٌ رَبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَنْ لَمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا (21) وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا (22) وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا (23) وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا (24) مِمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْصَارًا (25) وَقَالَ نُوحٌ رَبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا (26) إِنَّكَ إِنْ تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا (27) رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَنْ دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا (28)}.
1. Hakika Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake: uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu. 2. Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu. 3. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumtii. 4. Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapofika haucheleweshwi. Laiti mngejua! 5. Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana. 6. Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia. 7. Na hakika mimi kila nilipowaita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno! 8. Tena niliwaita kwa uwazi. 9. Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri. 10. Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. 11. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. 12. Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito. 13. Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu? 14. Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja? 15. Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka? 16. Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa? 17. Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea. 18. Kisha atakurudisheni humo na atakutoeni tena. 19. Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati. 20. Ili mtembee humo katika njia zilizo pana. 21. Nuhu akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara. 22. Na wakapanga vitimbi vikubwa. 23. Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra. 24. Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea. 25. (Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu. 26. Na Nuhu akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri! 27. Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri. 28. Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea.
Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu ametaja hadithi ya Nuhu peke yake. Kwa sababu ya kukaa kwake muda mrefu miongoni mwa watu wake na miito yake ya mara kwa mara ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kukataza kwake ushirikina:
#
{1} فأخبر تعالى أنَّه أرسل نوحاً إلى قومه رحمةً بهم وإنذاراً [لهم] من عذاب أليم؛ خوفاً من استمرارهم على كفرهم، فيهلكهم [اللَّهُ] هلاكاً أبديًّا، ويعذِّبهم عذاباً سرمديًّا.
{1} Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba alimtuma Nuhu kwa watu wake kuwa ni rehema kwao na onyo kutokana na adhabu chungu. Kwa kuogopa wasije wakaendelea katika ukafiri wao, na [Mwenyezi Mungu] akawaangamiza maangamizo ya milele na kuwaadhibu kwa adhabu isiyoisha.
#
{2 - 4} فامتثل نوحٌ عليه السلام لذلك، وابتدر لأمر الله، فقال: {يا قوم إنِّي لكم نذيرٌ مبينٌ}؛ أي: واضح النذارة بينها، وذلك لتوضيحه ما أنذر به وما أنذر عنه، وبأيِّ شيءٍ تحصُلُ النجاة؛ بيَّن ذلك بياناً شافياً، فأخبرهم وأمرهم بأصل ذلك ، فقال: {أنِ اعبُدوا الله واتَّقوه}: وذلك بإفراده تعالى بالعبادة والتوحيد - والبعد عن الشرك وطرقه ووسائله؛ فإنَّهم إذا اتَّقوا الله؛ غَفَرَ ذنوبهم؛ وإذا غفر ذنوبهم، حصل لهم النجاة من العذاب والفوز بالثواب، {ويؤخِّرْكم إلى أجل مسمًّى}؛ أي: يمتِّعكم في هذه الدار ويدفع عنكم الهلاك إلى إجل مسمًّى؛ أي: مقدَّر البقاء في الدنيا بقضاء الله وقدره إلى وقتٍ محدودٍ، وليس المتاع أبداً؛ فإنَّ الموت لا بدَّ منه، ولهذا قال: {إنَّ أجَلَ الله إذا جاء لا يؤخَّرُ لو كنتُم تعلمون}: كما كفرتُم بالله وعاندتُم الحقَّ.
{2 - 4} Basi Nuhu, amani imshukie, akatekeleza hayo, na akaikimbilia amri ya Mwenyezi Mungu, na akasema: "Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu." Hii ni kwa sababu alibainisha alichotahadharisha dhidi yake na kinachotokana nacho, na akabainisha kile ambacho litamwezesha mtu kuokoka. Akawaelezeaa asili ya hayo, akasema: "Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye." Na hayo ni kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada na tauhidi, na kuwa mbali na ushirikina na njia na visababu vyake. Kwani ikiwa watamcha Mwenyezi Mungu, atawasamehe dhambi zao. Na wakisamehewa madhambi yao, wataepushwa na adhabu na kupata malipo mazuri. "Na atakuakhirisheni mpaka muda uliowekwa." Yaani, atakustarehesheni katika nyumba hii na atakukingeni kutokana na maangamizo hadi muda wenu maalumu kwa hukumu na mipango ya Mwenyezi Mungu. Na kamwe si starehe ya kudumu milele. Kwani kifo hakiepukiki, na ndiyo maana akasema: "Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua" kama vile mlivyomkufuru Mwenyezi Mungu na kuasi haki.
#
{5 - 7} فلم يجيبوا لدعوته، ولا انقادوا لأمره، فقال شاكياً لربِّه: {ربِّ إنِّي دعوتُ قومي ليلاً ونهاراً. فلم يزِدْهم دعائي إلاَّ فراراً}؛ أي: نفوراً عن الحقِّ وإعراضاً، فلم يبق لذلك فائدةٌ؛ لأنَّ فائدة الدَّعوة أن يحصل جميع المقصود أو بعضه، {وإنِّي كلَّما دعوتُهم لتغفرَ لهم}؛ أي: لأجل أن يستجيبوا؛ فإذا استجابوا؛ غفرتَ لهم، وهذا محضُ مصلحتهم، ولكن أبوا إلاَّ تمادياً على باطلهم ونفوراً عن الحقِّ، {جعلوا أصابِعَهم في آذانهم}؛ حَذَرَ سماع ما يقول لهم نبيُّهم نوحٌ عليه السلام، {واستَغْشَوا ثيابَهم}؛ أي: تغطوا بها غطاءً يغشاهم بعداً عن الحقِّ وبغضاً له، {وأصرُّوا}: على كفرهم وشرِّهم، {واستَكْبَروا}: على الحقِّ {استِكْباراً}: فشرهم ازداد وخيرهم بعد.
{5 - 7} Lakini hawakuitikia mwito wake, wala hawakufuata amri yake, kwa hivyo akasema akimlalamikia Mola wake Mlezi: "Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana. Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia" kutoka kwa haki na kuipa mgongo. Basi hilo la kuwalingania likawa halina manufaa tena. Kwa sababu manufaa ya kulingania ni kupatikana yote au sehemu ya yale yaliyokusudiwa. "Na hakika mimi kila nilipowaita ili upate kuwaghufiria." Na hili lilikuwa ni kwa ajili ya manufaa yao tu, lakini walikataa ila kung'ang'ania batili yao na kujitenga mbali na haki. "Walijiziba masikio yao kwa vidole vyao" ili wajihadhari na kusikia anayowaambia Nabii wao Nuhu, amani ziwe juu yake, "na wakajigubika nguo zao" ili kujitenga mbali na haki na kuichukia; "na wakakamia" katika ukafiri wao na uovu wao "na wakatakabari" dhidi ya haki. Kwa hivyo, uovu wao ukaongezeka na wema wao ukawa mbali mno.
#
{8 - 9} {ثم إنِّي دعوتُهم جهاراً}؛ أي: بمسمع منهم كلهم، {ثم إنِّي أعلنتُ لهم وأسررتُ لهم إسراراً}: كل هذا حرصٌ ونصحٌ، وإتيانهم بكلِّ طريق يظنُّ به حصول المقصود.
{8 - 9} "Tena niliwaita kwa uwazi" na wote wakasikia wito. "Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri." Yote haya ni kwa sababu ya kulijali sana jambo hili na kuwanasihi, na kuwafuata kwa kila njia inayodhaniwa kwamba yatafikiwa makusudio.
#
{10 - 12} {فقلتُ استَغْفِروا ربَّكم}؛ أي: اتركوا ما أنتم عليه من الذنوب واستغفروا الله منها؛ {إنَّه كان غفاراً}: كثير المغفرة لمن تاب واستغفر، فرغَّبهم بمغفرة الذُّنوب وما يترتب عليها من الثواب واندفاع العقاب، ورغَّبهم أيضاً بخير الدُّنيا العاجل، فقال: {يرسِلِ السماءَ عليكم مِدراراً}؛ أي: مطراً متتابعاً يروي الشعاب والوهاد، ويحيي البلاد والعباد، {ويُمْدِدْكُم بأموال وبنينَ}؛ أي: يكثر أموالكم التي تدركون بها ما تطلبون من الدُّنيا وأولادكم، {ويجعل لكم جناتٍ ويجعل لكم أنهاراً}: وهذا من أبلغ ما يكون من لَذَّاتِ الدُّنيا ومطالبها.
{10 - 12} "Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, acheni madhambi mnayoyafanya na muombe msamaha juu yake kwa Mwenyezi Mungu. "Hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe sana" kwa wanaotubu na wakaomba maghfirah. Basi hapa akawatia moyo kwamba watasamehewa madhambi, na pia yale yanayotokana na hilo ya kupata malipo mazuri na kuepukana na adhabu, na pia akawapa moyo kwa heri ya haraka ya duniani, akasema: "Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo" itakayomwagilia sawasawa milima midogo na mabonde, itapata uhai mzuri ardhi na watu. "Na atakupeni mali na wana" ambavyo kwavyo mtaweza kupata mnavyovitaka katika dunia na pia watoto wenu. "Na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito." Hili ni miongoni mwa starehe kubwa zaidi zinazowezekana katika dunia na yanayotafutwa humo.
#
{13 - 14} {ما لكم لا ترجونَ لله وَقارا}؛ أي: لا تخافون لله عظمةً وليس لله عندكم قَدْرٌ، {وقد خَلَقَكم أطواراً}؛ أي: خلقاً من بعد خلقٍ في بطن الأمِّ ثم في الرَّضاع ثم في سنِّ الطفوليَّة ثم التمييز ثم الشباب ثم إلى آخر ما يصل إليه الخلق؛ فالذي انفردَ بالخَلْق والتَّدبير البديع متعيَّنٌ أن يُفْرَدَ بالعبادة والتوحيد، وفي ذكر ابتداء خلقهم تنبيهٌ لهم على المعاد ، وأنَّ الذي أنشأهم من العدم قادرٌ على أن يعيدَهم بعد موتهم.
{13 - 14} "Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu? Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?" Yaani, alikuumbeni baada ya kuumbwa katika tumbo la uzazi la mama, kisha katika kunyonyesha, kisha katika utoto, kisha umri wa kupambanua mambo, kisha ujana, kisha mpaka umri wa mwisho anaoufikia kiumbe. Aliyekuwa peke yake katika uumbaji na uendeshaji huu wa ajabu anafailia yeye tu kufanyiwa ibada na kupwekeshwa. Na katika kutaja mwanzo wa kuumbwa kwao kuna kuwatanabahisha juu ya kurudishwa kwao (Siku ya Kiyama), na kwamba Yeye aliyewaumba baada ya kutokuwapo kwao, anao uwezo wa kuwarudisha baada ya kufa kwao.
#
{15 - 16} واستدلَّ أيضاً بخلقِ السماواتِ التي هي أكبر من خلق الناس، فقال: {ألم تَرَوْا كيف خَلَقَ الله سبع سمواتٍ طباقاً}؛ أي: كلّ سماءٍ فوق الأخرى، {وجعل القمر فيهنَّ نوراً}: لأهل الأرض، {وجعل الشمسَ سِراجاً}: ففيه تنبيهٌ على عظم خلق هذه الأشياء، وكثرة المنافع في الشمس والقمر، الدالَّة على رحمة الله وسعة إحسانه؛ فالعظيم الرحيم يستحقُّ أن يعظَّم ويُحبَّ - ويُخاف ويُرجى.
{15 - 16} Vile vile akatumia ushahidi wa kuumbwa kwa mbingu ambako ni kukubwa kuliko kuumbwa kwa watu, akasema: "Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?" Yaani, kila mbingu iko juu ya nyingine. "Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru" kwa wakazi wa ardhini, "na akalifanya jua kuwa taa?" Katika haya kuna tanabahisho juu ya ukubwa wa maumbile ya vitu hivi, na wingi wa manufaa katika jua na mwezi, yanayoashiria rehema za Mwenyezi Mungu na upana wa wema wake. Kwa hivyo, Mkuu, Mwingi wa rehema anastahili kutukuzwa, kupendwa, kuogopwa na kutumainiwa.
#
{17 - 18} {والله أنبتَكم من الأرض نباتاً}: حين خلق أباكم آدمَ وأنتم في صلبِهِ، {ثم يعيدُكم فيها}: عند الموت، {ويخرِجُكم إخراجاً}: للبعث والنشور؛ فهو الذي يملك الحياة والموت والنشور.
{17 - 18} "Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea" wakati alipomuumba baba yenu Adam hali nyinyi mkiwa katika kiuno chake, "kisha atakurudisheni humo" wakati wa kufa. "Na atakutoeni tena" kwa ajili ya ufufuo na kutawanywa. Kwani Yeye ndiye anayemiliki uzima, kifo na ufufuo.
#
{19 - 20} {والله جعل لكم الأرض بساطاً}؛ أي: مبسوطةً مهيئة للانتفاع بها، {لِتَسْلُكوا منها سُبُلاً فِجاجاً}: فلولا أنَّه بسطها؛ لما أمكن ذلك، بل ولا أمكنهم حرثها وغرسها وزرعها والبناء والسكون على ظهرها.
{19 - 20} "Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati" iliyoandaliwa ili kunufaika nayo "Ili mtembee humo katika njia zilizo pana." Lau asingeitandaza, hilo lisingewezekana, na hata wasingeweza kulima, kupanda, kujenga na kutulia juu ya mgongo wake.
#
{21 - 24} {قال نوحٌ}: شاكياً لربِّه: إنَّ هذا الكلام والوعظ والتَّذكير ما نَجَعَ فيهم ولا أفاد: {إنَّهم عَصَوْني}: فيما أمرتُهم به، {واتَّبعوا مَنْ لم يَزِده مالُه وولدُه إلاَّ خساراً}؛ أي: عَصَوُا الرسول الناصح الدالَّ على الخير، واتَّبعوا الملأ والأشراف الذين لم تَزِدْهم أموالُهم ولا أولادُهم إلاَّ خساراً؛ أي: هلاكاً وتفويتاً للأرباح؛ فكيف بِمَنِ انقادَ لهم وأطاعهم؟! {ومكروا مَكْراً كُبَّاراً}؛ أي: مكراً كبيراً بليغاً في معاندة الحقِّ. قالوا لهم داعين إلى الشرك مزينين له: {لا تَذَرُنَّ آلهتكم}: فدعوهم إلى التعصُّب على ما هم عليه من الشرك، وأن لا يَدَعوا ما عليه آباؤهم الأقدمون، ثم عيَّنوا آلهتهم، فقالوا: {ولا تَذَرُنَّ ودًّا ولا سُواعاً ولا يَغوثَ ويعوقَ ونَسْراً}: وهذه أسماء رجال صالحين؛ لما ماتوا؛ زيَّن الشيطان لقومهم أن يصوِّروا صورهم؛ لينشطوا بزعمهم على الطاعةِ إذا رأوها، ثم طال الأمدُ، وجاء غير أولئك، فقال لهم الشيطانُ: إنَّ أسلافَكم يعبدونهم ويتوسَّلون بهم، وبهم يُسْقَوْن المطر، فعبدوهم، ولهذا وصَّى رؤساؤهم للتابعين لهم أن لا يَدَعوا عبادة هذه الأصنام ، {وقد أضلُّوا كثيراً}؛ أي: أضلَّ الكبار والرؤساء بدعوتهم كثيراً من الخلق. {ولا تزِدِ الظالمينَ إلاَّ ضلالاً}؛ أي: لو كان ضلالهم عند دعوتي إيَّاهم للحقِّ ؛ لكان مصلحةً، ولكن لا يزيدون بدعوة الرؤساء إلاَّ ضلالاً؛ أي: فلم يبق محلٌّ لنجاحهم وصلاحهم.
{21 - 24} "Nuhu akasema" akimlalamikia Mola wake Mlezi kwamba kauli hii na mawaidha na ukumbusho hayakuwaingia wala hayakuwafaa. "Hakika hao wameniasi" katika niliyowaamrisha. "na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara" Yaani, walimuasi Mtume, mshauri wa kweli, aliyewaongoza watu kwenye heri, lakini wakafuata viongozi na watukufu, ambao mali zao na watoto wao havikuwazidishia ila hasara. Yaani, kuangamia na kukosa faida. Basi vipi wale waliowafuata na kuwatii? "Na wakapanga vitimbi vikubwa" katika kuupinga haki. Wakawaambia wakilingania ushirikina na kuupamba: "Kamwe msiwaache miungu yenu." Hapo, wakawa wamewalingania kushikilia kwa nguvu ushirikina walio juu yake, na kwamba wasiyaache yale waliyo juu yake baba zao wa zamani, kisha wakaainisha miungu yao, wakasema: "wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra." Haya ni majina ya watu wema. Walipokufa, Shetani aliwapambia watu wao kwamba wawatengenezee masanamu ili kwa madai yao waweze kuwa wakakamavu katika kumtii Mwenyezi Mungu wanapoyaona. Kisha ukapita muda mrefu, na wakaja watu wengine, na Shetani akawaambia: 'Hakika wazee wenu walikuwa wakiyaabudu na kupitia kwa katika dua zao, na kupitia kwao wanapata mvua.' Basi wakawaabudu, na ndiyo maana wakuu wao wakausia wafuasi wao kwamba wasiache kuyaabudu masanamu hayo. "Na hao walikwisha wapoteza wengi." Yaani, wakuu hao waliwapoteza watu wengi kwa wito wao huo. "Wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea." Yaani, ikiwa kupotoka kwao kungekuwa wakati wa kuwalingania kwangu kwenye haki, huenda kungekuwa na maana fulani. Lakini wanapotea kwa kulingania kwa viongozi wao tu, na hili linawazidishia upotofu. Kwa maneno mengine, hakuna tena uwezekano wa wokovu wao na kutengenea kwao.
#
{25} ولهذا ذكر الله عذابَهم وعقوبتهم الدنيويَّة والأخرويَّة، فقال: {ممَّا خطيئاتِهِم أغْرِقوا}: في اليمِّ الذي أحاط بهم، {فأدْخِلوا ناراً}: فذهبت أجسادُهم في الغرق وأرواحُهم للنار والحرق. وهذا كلُّه بسبب خطيئاتهم التي أتاهم نبيُّهم [نوح] ينذِرُهم عنها ويخبِرُهم بشؤمها ومغبَّتها، فرفضوا ما قال، حتى حلَّ بهم النَّكال، {فلم يجِدوا لهم من دونِ الله أنصاراً}: ينصُرونهم حين نزل بهم الأمرُ الأمرُّ، ولا أحد يقدر يعارِضُ القضاء والقدر.
{25} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja adhabu yao na mateso yao katika dunia na Akhera, akasema: "(Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa" katika bahari iliyowazunguka pande zote, "na wakaingizwa Motoni." Basi miili yao ikazamishwa kwenye maji, na roho zao zikapelekwa motoni na kuteketezwa. Na hayo yote ni kwa sababu ya madhambi yao aliyowajia Nabii wao (Nuhu) akiwaonya dhidi yake na kuwafahamisha ubaya wake na matokeo yake mabaya. Lakini wakayakataa aliyoyasema mpaka ikawajia adhabu. "Wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu" wenye kuwanusuru wakati amri hiyo ilipowateremkia, na hakuna yeyote awezaye kupinga mapitisho na mipango ya Mwenyezi Mungu.
#
{26 - 27} {وقال نوحٌ ربِّ لا تَذَرْ على الأرضِ من الكافرين ديَّاراً}: يدور على وجه الأرض. وذكر السبب في ذلك، فقال: {إنَّك إن تَذَرْهُم يُضِلُّوا عبادك ولا يَلِدوا إلاَّ فاجراً كفَّاراً}؛ أي: بقاؤهم مفسدةٌ محضةٌ لهم ولغيرهم، وإنَّما قال نوحٌ ذلك؛ لأنَّه مع كثرة مخالطته إيَّاهم ومزاولته لأخلاقهم؛ علم بذلك نتيجة أعمالهم؛ فلهذا استجاب الله له دعوته فأغرقهم أجمعين، ونجَّى نوحاً ومن معه من المؤمنين.
{26 - 27} "Na Nuhu akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri" azunguke juu ya uso wa ardhi. Kisha akataja sababu ya hilo, akasema: "Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri." Yaani, kuendelea kwao kuishi ni uharibifu mtupu kwao na kwa wengine. Na hakika Nuhu alisema haya, kwa sababu licha ya kutangamana kwake nao mara kwa mara na kuamiliana na tabia zao, alijua kutokana na hayo matokeo ya matendo yao. Basi ndiyo maana Mwenyezi Mungu aliitikia wito wake na akawazamisha wote, na akamuokoa Nuhu na waliokuwa pamoja naye miongoni mwa waumini.
#
{28} {ربِّ اغفِرْ لي ولوالديَّ ولِمَنْ دَخَلَ بيتي مؤمناً}: خصَّ المذكورين لتأكُّد حقِّهم وتقديم برِّهم، ثم عمَّم الدُّعاء، فقال: {وللمؤمنين والمؤمنات ولا تزِدِ الظالمينَ إلا تَباراً}؛ أي: خساراً ودماراً وهلاكاً.
{28} "Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini." Aliwataja hawa hasa kwa sababu haki zao ni kubwa zaidi na kutanguliza kuwafanyia wema, kisha akaijumlisha dua yake, akasema "na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie waliodhulumu ila kupotea." Yaani, hasara, uharibifu na kuangamia.
Imekamilika tafasiri ya Surat Nuh, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *