Tafsiri ya Surat Qad Sami'a Allah (Mwenyezi Mungu amekwisha sikia).
Tafsiri ya Surat Qad Sami'a Allah
(Mwenyezi Mungu amekwisha sikia).
Ilishuka Madina
{قَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّهِ وَاللَّهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ (1) الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنْكُمْ مِنْ نِسَائِهِمْ مَا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنْكَرًا مِنَ الْقَوْلِ وَزُورًا وَإِنَّ اللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ (2) وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنْ نِسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَتَمَاسَّا ذَلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (3) فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَتَمَاسَّا فَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ذَلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ (4)}.
1. Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke anayejadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona zaidi. 2. Wale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa. Na hakika hao wanasema neno ovu mno, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria mno, Mwenye kusamehe zaidi. 3. Na wale wanaojitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyoyasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda. 4. Na asiyepata mtumwa kumkomboa, basi na afunge saumu miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiyeweza hayo, basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na makafiri watapata adhabu chungu.
#
{1} نزلت هذه الآيات الكريماتُ في رجل من الأنصار اشتكتْه زوجته إلى الله وجادلته إلى رسول الله - صلى الله عليه وسلم - لمَّا حرَّمها على نفسه بعد الصُّحبة الطويلة والأولاد، وكان هو رجلاً شيخاً كبيراً، فشكتْ حالَها وحالَه إلى الله وإلى رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، وكرَّرت ذلك، وأبدتْ فيه وأعادتْ، فقال تعالى: {قد سَمِعَ الله قولَ التي تجادِلُك في زوجها وتَشْتَكي إلى الله واللهُ يسمعُ تحاوُرَكما}؛ أي: تخاطُبَكما فيما بينكما. {إنَّ الله سميعٌ}: لجميع الأصوات في جميع الأوقات على تفنُّن الحاجات. {بصيرٌ}: يبصر دبيبَ النملة السوداء، على الصَّخرة الصمَّاء، في الليلة الظلماء.
وهذا إخبارٌ عن كمال سمعه وبصره، وإحاطتهما بالأمور الدَّقيقة والجليلة، وفي ضمن ذلك الإشارة بأنَّ الله [تعالى] سيزيلُ شكواها ويرفع بلواها، ولهذا ذكر حكمها وحكمَ غيرها على وجه العموم، فقال:
{1} Aya hizi tukufu ziliteremshwa kwa sababu ya mwanamume mmoja kutoka kwa answari ambaye mke wake alimlalamikia Mwenyezi Mungu na akamjadili mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, baada ya mume wake kujiharamishia mke huyu baada ya kuishi pamoja naye kwa muda mrefu na kupata watoto. Mume huyo alikuwa ni mzee sana, kwa hivyo mke wake akamlalamikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuhusu hali yake na hali ya mume wake, na akalirudia hilo sana. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke anayejadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno." Anasikia zaidi sauti zote katika nyakati zote, hata pamoja na kutofautiana kwa mahitaji. "Mwenye kuona zaidi." Anamuana sisimizi mweusi, juu ya jiwe jeusi, katika usiku wa giza totoro. Huku ni kupeana habari kuhusu ukamilifu wa kusikia kwake na kuona kwake, na kudhibiti kwake sawasawa mambo ya madogo mno
(ya siri mno) na makubwa pia, na ndani ya hayo kuna ishara kwamba Mwenyezi Mungu
[Mtukufu] atamwondolea malalamiko yake na kutoa balaa yake. Ndiyo maana akataja hukumu yake na hukumu ya wanawake wengineo kwa ujumla,
akasema:
#
{2} {الذين يظاهِرونَ منكم من نسائِهِم ما هنَّ أمَّهاتِهم إن أمَّهاتُهم إلاَّ اللاَّئي وَلَدْنَهم}: المظاهرة من الزوجة أن يقولَ الرجل لزوجته: أنت عليَّ كظهرِ أمِّي، أو غيرها من محارمه، أو أنت عليَّ حرامٌ. وكان المعتاد عندَهم في هذا اللفظ الظهر، ولهذا سماه الله ظِهاراً، فقال: {الذين يظاهِرون منكم من نسائِهِم ما هنَّ أمَّهاتِهم}؛ أي: كيف يتكلَّمون بهذا الكلام الذي يعلمون أنَّه لا حقيقة له، فيشبهون أزواجهم بأمَّهاتِهم اللاَّتي ولدنهم؟! ولهذا عظَّم الله أمره وقبَّحه، فقال: {وإنَّهم لَيقولونَ منكراً من القول وزوراً}؛ أي: قولاً شنيعاً وكذباً ، {وإنَّ الله لَعَفُوٌّ غفورٌ}: عمَّن صَدَرَ منه بعضُ المخالفات فتداركَها بالتَّوْبَةِ النَّصوح.
{2} "Wale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa.
" Na hili ni mwanamume kumwambia mkewe: 'Wewe mgongo wako ni kama mgongo wa mama yangu,' au wanawake wengineo ambao haruhusiwi kuwaoa, au aseme, 'Wewe ni haramu kwangu.' Lakini wao walikuwa wamezoea kutumia neno 'mgongo.
' Basi akasema: "Wale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao." Yaani, vipi wanazungumza maneno haya ambayo wanajua kwamba hayana uhakika, kwa kuwafananisha wake zao na mama zao waliowazaa? Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akachukulia hilo kuwa jambo kubwa mno, na akalifanya kuwa baya sana.
Akasema: "Na hakika hao wanasema neno ovu mno, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria mno, Mwenye kusamehe zaidi" kwa mwenye kufanya baadhi ya makosa kisha akayarekebisha kwa toba ya kweli.
#
{3} {والذين يظاهِرونَ من نسائِهِم ثم يعودونَ لِما قالوا}: اختلف العلماء في معنى العَوْد، فقيل معناه العزمُ على جماع مَنْ ظاهر منها، وأنَّه بمجرَّد عزمِهِ؛ تجب عليه الكفَّارة المذكورة، ويدلُّ على هذا أنَّ الله تعالى ذَكَرَ في الكفَّارة أنَّها تكون قبل المسيس، وذلك إنَّما يكون بمجرَّد العزم، وقيل: معناه حقيقةُ الوطءِ، ويدلُّ على ذلك أنَّ الله قال: {ثم يعودونَ لِما قالوا}، والذي قالوا إنَّما هو الوطءُ، وعلى كلٍّ من القولين؛ فإذا وُجِدَ العَوْدُ؛ صار كفارةُ هذا التحريم {تحرير رقبةٍ}: مؤمنةٍ؛ كما قُيِّدَتْ في آية القتل ؛ ذكرٍ أو أنثى؛ بشرط أن تكون سالمةً من العيوب الضارَّة بالعمل {من قبل أن يَتَماسَّا}؛ أي: يلزم الزوج أن يترك وطء زوجته التي ظاهر منها حتى يكفِّرَ برقبة. {ذلكم}: الحكم الذي ذكرناه لكم {توعظونَ به}؛ أي: يبيِّن لكم حكمه مع الترهيب المقرون به؛ لأن معنى الوعظ ذكر الحكم مع الترغيب والترهيب فالذي يريد أن يظاهر؛ إذا ذَكَرَ أنَّ عليه عتقَ رقبةٍ؛ كفَّ نفسه عنه. {واللهُ بما تعملونَ خبيرٌ}: فيجازي كلَّ عامل بعمله.
{3} “Na wale wanaojitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyoyasema.” Wanachuoni walihitalifiana juu ya maana ya ‘kisha wakarudia’. Basi kuna wale waliosema kuwa ni kuweka azimio ya kumuingilia mke ambaye mtu mwenyewe alikuwa amemfananisha na mama yake, na kwamba kwa kuwa tu na azimio hilo analazimika kutoa kafara iliyotajwa hapo juu, na hili linadhihirishwa na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kwamba kafara iwe kabla ya kujamiiana, na hilo linakuwa kwa kuweka azimio tu. Na ikasemwa kwamba maana yake ni kujamiiana,
na hili linaashiriwa na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu alisema: “Kisha wakarudia katika yale waliyoyasema” Na yale waliyoyasema ni ngono tu. Hata hivyo, kulingana na kauli zote mbili, pindi kurudi kunapopatikana tu, inakuwa kafara ya kujiharamishia huku ni
“kumkomboa mtumwa” Muumini, kama ilivyowekewa sharti hili la imani katika Aya inayohusiana na kuua. Na anaweza kuwa mwanamume au mwanamke, lakini kwa sharti kwamba awe salama kutokana na kasoro zinazoweza kuathiri vibaya utendaji kazi wake,
“kabla hawajagusana. Kwa hayo;” yaani, hukumu tuliyokutajieni
“Mnapewa maonyo” kwa maana akikumbuka kwamba itamlazimu amwachilie huru mtumwa, bila shaka atajizuia kufanya hilo.
“Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda.” Kisha atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake.
#
{4} {فمن لم يجِدْ}: رقبةً يُعْتِقُها؛ بأن لم يجِدْها أو لم يجِدْ ثَمَنَها، {فـ} عليه {صيامُ شهرين متتابعين من قبل أن يَتَماسَّا فمَن لمْ يَسْتَطِعْ}: الصيام، {فإطعامُ ستينَ مسكيناً}: إمَّا أنْ يطعِمَهم من قوت بلده ما يكفيهم؛ كما هو قول كثيرٍ من المفسِّرين، وإمَّا أنْ يطعِمَ كلَّ مسكين مُدَّ بُرٍّ أو نصفَ صاع من غيره مما يُجْزِي في الفطرة؛ كما هو قول طائفة أخرى. {ذلك}: الحكم الذي بيَّنَّاه لكم ووضَّحناه، {لتؤمِنوا بالله ورسولِهِ}: وذلك بالتزام هذا الحكم وغيره من الأحكام والعمل به؛ فإنَّ التزام أحكام الله والعمل بها من الإيمانِ، بل هي المقصودةُ، ويزداد بها الإيمانُ ويكمُلُ وينمو. {وتلك حدودُ اللهِ}: التي تمنع من الوقوع فيها، فيجب أن لا تُتَعَدَّى ولا يُقَصَّرَ عنها. {وللكافرين عذابٌ أليمٌ}.
{4} “Na asiyepata mtumwa kumkomboa” au hakuweza kupata mali ya kumtolea utumwani,
“basi” itamlazimu “afunge saumu miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiyeweza hayo” kufunga saumu,
“basi awalishe masikini sitini.” Ima awalishe kutoka kwa chakula raisi cha nchini kwake kitakachowatosha; kama wanavyosema wafasiri wengi, na ima amlishe kila masikini viganja viwili vya ngano au chakula kinginecho kinachotosheleza katika Zakatul-fitr; kama ilivyo katika kauli ya baadhi ya madhehebu.
“Hayo” ya hukumu tuliyokubainishieni ni “ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Na hilo ni kwa kushikamana na hukumu hii na hukumu nyinginezo na kuzifanyia kazi. Kwani kushikamana na hukumu za Mwenyezi Mungu na kuzifanyia kazi ni katika imani. Bali ndilo hasa linalokusudiwa, na kwa hilo mja anazidisha imani yake na kuikuza na kuikamilisha.
“Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu” ambayo inamzuia mtu kuanguka ndani ya makatazo yake, basi ni lazima isiivuke wala isipunguze chochote kwayo.
“Na makafiri watapata adhabu chungu.”
Kuna hukumu kadhaa katika aya hizi: Miongoni mwake ni upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na utunzaji wake kwao. Ambapo alitaja malalamiko ya mwanamke huyu aliyeteseka, akayaondoa, na akamwondolea balaa. Bali aliiondoa balaa hii kwa hukumu yake ya ujumla kwa kila mtu ambaye atakuwa katika suala kama hili. Na miongoni mwake ni kwamba kumfananisha mke na mama ya mtu ni jambo linalohusiana na mke peke yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: "wake zao." Na ikiwa hilo lingeharamisha kijakazi wake pia, basi hilo halingakuwa dhihar (yaani, kumfananisha mke na mama ya mtu katika uharamu), bali litakuwa ni katika aina moja na kuharamisha vitu vizuri kama vile vyakula na vinywaji, ambalo mtu anapaswa kutoa kafara ya kuapa tu. Na miongoni mwake haiwi sahihi kumfanyia mwanamke dhihar (kumsawazisha na mama ya mtu) kabla ya kumuoa. Kwa sababu bado hajaingia katika wake zake wakati huo, kama vile kumtaliki hakuwi sahihi, sawa alikwisha amua hilo au alilifungamanisha na kitu fulani. Na miongoni mwake ni kwamba dhihar (mtu kumsawazisha mkewe na mama yake) ni haramu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliliita hilo, "neno ovu mno, na la uongo." Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu alitanabahisha juu ya hukumu na hekima yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: “Hao si mama zao." Na miongoni mwake ni kwamba inachukiza kwa mwanaume kumwita mkewe kwa jina la maharimu wake. Kama vile kusema: 'Ewe mama yangu, ewe dada yangu" na mfano wa hayo. Kwa sababu hayo yanafanana na kile kilichoharamishwa. Na miongoni mwake ni kwamba kafara inalazimu anaporudia mwanamume huyo yale aliyojiharamishia, kulingana na kauli mbili tofauti zilizoko, na wala haiwi lazima kwa kujiharamishia huko tu. Na miongoni mwake ni kwamba inatosha katika kafara kutoa huru mtumwa mdogo, au mzee, au mwanamume, au mwanamke. Kwa sababu aya hii haikuwekea hilo kitu mahususi. Na miongoni mwake ni kwamba ni lazima ilipwe kafara hivyo ikiwa ni kumtoa mtumwa utumwani, au kufunga saumu kabla ya kujamiiana. Kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha iwe hivyo. Hii ni tofauti na kafara ya kulisha, ambayo inaruhusika kujamiiana hata kama haijaisha. Na miongoni mwake ni kwamba labda hekima iliyo nyuma ya ufaradhi wa kutoa kafara hii kabla ya kujamiiana ni kwamba hilo linapelekea zaidi kuitoa. Kwa sababu, ikiwa atatamani sana ngono na anajua kuwa hataruhusiwa hilo ila baada ya kutoa kafara, ataharakisha kuitoa. Na miongoni mwake ni kwamba ni lazima kuwalisha watu masikini sitini. Na kama atakusanya chakula cha masikini sitini na akampa mmoja wao au zaidi wanaopungua sitini, hilo halitakubaliwa. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: "Basi awalishe masikini sitini."
{إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ كُبِتُوا كَمَا كُبِتَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَقَدْ أَنْزَلْنَا آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُهِينٌ (5)}.
5. Hakika wanaopinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao. Na tulikwisha teremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha.
#
{5} محادَّة الله ورسوله مخالفتُهما ومعصيتُهما، خصوصاً في الأمور الفظيعة؛ كمحادَّة الله ورسوله بالكفر ومعاداة أولياء الله. وقوله: {كُبِتُوا كما كُبِتَ الذين من قبلهم}؛ أي: أذِلُّوا وأهينوا كما فُعِلَ بمن قبلَهم جزاءً وِفاقاً، وليس لهم حجَّةٌ على الله؛ فإنَّ الله قد قامت حجَّته البالغةُ على الخلق، وقد أنزل من الآيات البيِّناتِ والبراهين ما يبيِّنُ الحقائق ويوضِّحُ المقاصدَ؛ فمن اتَّبعها وعمل عليها، فهو من المهتدين الفائزين. {وللكافرين}: بها {عذابٌ مهينٌ}؛ أي: يهينهم ويُذِلُّهم؛ فكما تكبَّروا عن آيات الله؛ أهانهم وأذلَّهم.
{5} Kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuwaasi, hasa kwa mambo ya kutisha kama vile kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa ukafiri na kuwafanyia uadui vipenzi wa Mwenyezi Mungu.
Na kauli yake: "watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao" ili yawe malipo mwafaka, wala hawatakuwa na hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alikwisha simamisha hoja yake ya kukata juu ya viumbe, na aliteremsha ishara zilizo wazi na hoja zinazobainisha uhakika wa mambo, na kuweka wazi makusudio. Kwa hivyo, mwenye kuzifuata na akazifanyia kazi, basi huyo ni miongoni mwa walioongoka, waliofaulu. "Na makafiri" wanaoyakufuru hayo, "watapata adhabu ya kufedhehesha." Kama vile walivyokuwa wakizidhalilisha ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawadunisha na kuwadhalilisha.
{يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّهُ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُهُمْ بِمَا عَمِلُوا أَحْصَاهُ اللَّهُ وَنَسُوهُ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ (6) أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَا يَكُونُ مِنْ نَجْوَى ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَى مِنْ ذَلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ثُمَّ يُنَبِّئُهُمْ بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (7)}.
6. Siku atakapowafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyoyatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu. 7. Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu.
#
{6} يقول الله تعالى: {يوم يبعثهم اللهُ} الخلقَ جميعاً فيقومون من أجداثهم سريعاً، فيجازيهم بأعمالهم؛ وينبِّئهم بما عملوا من خيرٍ وشرٍّ؛ لأنَّه علم ذلك وكتبه في اللوح المحفوظ، وأمر الملائكة الكرام الحَفَظَة بكتابته، هذا والعاملون قد نسوا ما عملوه والله أحصى ذلك. {والله على كلِّ شيءٍ شهيدٌ}: على الظَّواهر والسَّرائر والخبايا والخفايا.
{6} Anasema Mwenyezi Mungu: "Siku atakapowafufua Mwenyezi Mungu" viumbe vyote, na watasimama kutoka kwenye makaburi yao haraka, kisha atawalipa kwa vitendo vyao, na anawafahamisha mema na mabaya waliyoyafanya. Kwa sababu aliyajua hayo na akayaandika katika Ubao uliohifadhiwa, na akawaamrisha Malaika walinzi wayaandike. Pamoja na haya, wale walioyafanya, waliyasahau waliyoyafanya, lakini Mwenyezi Mungu aliyadhibiti, "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu" cha dhahiri, cha siri na kilichofichikana mno.
#
{7} ولهذا أخبر عن سعةِ علمه وإحاطته بما في السماواتِ والأرض من دقيق وجليل، وأنَّه {ما يكون من نَجْوى ثلاثةٍ إلاَّ هو رابِعُهم ولا خمسةٍ إلاَّ هو سادِسُهم ولا أدنى مِن ذلك ولا أكثر إلاَّ هو مَعَهُم أينما كانوا}: والمراد بهذه المعيَّة معيَّةُ العلم والإحاطة بما تناجَوْا به وأسرُّوه فيما بينَهم، ولهذا قال: {إنَّ الله بكلِّ شيءٍ عليمٌ}.
{7} Ndiyo maana akaeleza upana wa elimu yake na kujua kwake vyema vilivyomo mbinguni na ardhini, vidogo mno na vikubwa, na kwamba "Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo." Kinachokusudiwa na kuwa kwake pamoja nao huku ni kuwa kwake pamoja nao kwa elimu yake na kujua vyema waliyonong'ona na kuyaficha kabisa kati yao,
na ndiyo maana akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu."
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نُهُوا عَنِ النَّجْوَى ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَيَتَنَاجَوْنَ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنْفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّهُ بِمَا نَقُولُ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمَصِيرُ (8) يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَنَاجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَاجَوْا بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَتَنَاجَوْا بِالْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ (9)}.
8. Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong'onezana, kisha wakayarudia yale yale waliyokatazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu.
Na husema katika nafsi zao: 'Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje! 9. Enyi mlioamini! Mnaponong'ona, msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezane kwa kutenda mema na kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote.
#
{8 - 9} النَّجْوى هي التناجي بين اثنين فأكثر، وقد تكون في الخير وتكونُ في الشرِّ، فأمر الله المؤمنين أنْ يَتَناجَوْا بالبرِّ، وهو اسمٌ جامعٌ لكلِّ خيرٍ وطاعةٍ وقيام بحقِّ الله وحقِّ عباده ، والتَّقوى، وهي هنا اسمٌ جامعٌ لترك جميع المحارم والمآثم؛ فالمؤمن يمتثل هذا الأمر الإلهيَّ؛ فلا تجده مناجياً ومتحدثاً إلاَّ بما يقرِّبه إلى الله ويباعده من سخطه، والفاجر يتهاونُ بأمر الله ويناجي بالإثم والعدوان ومعصية الرسول؛ كالمنافقين الذين هذا دأبهم وحالهم مع الرسول - صلى الله عليه وسلم -، قال تعالى: {وإذا جاؤوك حَيَّوْكَ بما لمْ يُحَيِّكَ به الله}؛ أي: يسيئون الأدب في تحيَّتهم لك، {ويقولونَ في أنفُسِهم}؛ أي: يسرُّون فيها - ما ذكره عالم الغيب والشهادة عنهم، وهو قولهم: {لولا يُعَذِّبنا الله بما نقولُ}: ومعنى ذلك أنَّهم يتهاونون بذلك، ويستدلُّون بعدم تعجيل العقوبة عليهم أنَّ ما يقولونه غيرُ محذورٍ، قال تعالى في بيان أنَّه يمهِلُ ولا يهمِلُ: {حَسْبُهُم جهنَّمُ يَصْلَوْنها فبئس المصيرُ}؛ أي: تكفيهم جهنَّم التي جمعت كلَّ عذابٍ وشقاء عليهم، تحيط بهم ويعذَّبون بها؛ فبئس المصير. وهؤلاء المذكورون إما أناس من المنافقين، يظهِرون الإيمان ويخاطبون الرسول - صلى الله عليه وسلم - بهذا الخطاب الذي يوهمون أنَّهم أرادوا به خيراً، وهم كذبةٌ في ذلك، وإما أناسٌ من أهل الكتاب الذين إذا سلَّموا على رسول الله - صلى الله عليه وسلم -؛ قالوا: السام عليك يا محمد. يعنون: الموت.
{8 - 9} Kunong’onezana kunaweza kuwa kwa heri au kwa uovu. Basi Mwenyezi Mungu akawaamrisha Waumini kunong’onezana kwa wema. Nao ni jina linalojumuisha kila heri, utiifu, na kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, na ucha Mungu. Nao hapa ni jina linalijumuisha kuacha vitendo na dhambi yote yaliyoharamishwa. Kwa hivyo, Muumini anatekeleza amri hii ya kimungu. Hutamkuta akinong’ona wala akizungumza ila kwa yale yanayomuweka karibu na Mwenyezi Mungu na yanamweka mbali na ghadhabu yake. Naye mwovu, anazembea katika kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na ananong’ona kwa dhambi, uadui na kumuasi Mtume. Kama wanafiki ambao hii ndiyo ada yao na hali yao wanapoamiliana na Mtume -
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu.” Yaani wanafanya adabu mbaya katika kukuamkua.
“Na husema katika nafsi zao” wakisema: 'Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Maana yake ni kuwa wanaona kwamba hilo ni dogo, na wanalitumia kutoharakishiwa adhabu kuwa ni ushahidi kwamba wanayoyasema si haramu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kwamba Yeye hupeana muda na wala hapuuzi: “Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje!” Yaani, Jahannamu itawatosha, ambayo imewakusanyia adhabu na dhiki zote. Itawazingira na kuwatesa kwayo. Basi hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje! Na hawa waliotajwa ima ni watu kutoka kwa wanafiki wenye kuonesha imani na wanamwongelesha Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa maneno haya ambayo kwayo wanawafanya watu waamini kuwa wana nia njema, lakini ni waongo katika hilo. Au ni watu miongoni mwa Watu wa Kitabu ambao wanapomsalimu Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -
wanasema: ‘Saam alaikum, ewe Muhammad
(yaani, tunakuombea kifo).
{إِنَّمَا النَّجْوَى مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ (10)}.
10. Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe wale walioamini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini.
#
{10} يقول تعالى: {إنَّما النَّجوى}؛ أي: تناجي أعداء المؤمنين بالمؤمنين بالمكرِ والخديعة وطلب السوءِ من الشيطان الذي كيدُهُ ضعيفٌ، [ومكره غير مفيد] {ليحزنَ الذين آمنوا}: هذا غايةُ هذا المكر ومقصوده، {وليس بضارِّهم شيئاً إلاَّ بإذنِ الله}: فإنَّ الله [تعالى] وَعَدَ المؤمنين بالكفاية والنصر على الأعداء، وقال تعالى: {ولا يَحيقُ المكرُ السيِّئُ إلاَّ بأهلِهِ}: فأعداء الله ورسوله والمؤمنين مهما تَناجَوْا ومَكَروا؛ فإنَّ ضَرَرَ ذلك عائدٌ إلى أنفسهم ، ولا يضرُّ المؤمنين إلاَّ شيءٌ قدَّره الله وقضاه. {وعلى الله فَلْيَتَوَكَّلِ المؤمنون}؛ أي: ليعتمدوا عليه ويَثِقوا بوعده؛ فإنَّ مَن تَوَكَّلَ على الله؛ كَفاه وكَفاه أمرَ دينِهِ ودُنياه.
{10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
“Kwa hakika minong'ono;” yaani, minong'ono ya maadui wa Waumini wakiwapangia njama Waumini na kuwahadaa, na kuwatakia uovu ni kutokana na Shetani ambaye njama zake ni dhaifu,
[na hata njama hizo hazifai chochote] “ili awahuzunishe wale walioamini.” Hili ndilo lengo na makusudio ya njama hizi.
“na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.” Kwani hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi Waumini kuwatosheleza na kuwashinda dhidi ya maadui. Na Mwenyezi Mungu,
alisema: “Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliyevifanya.” Kwa hivyo, maadui za Mwenyezi, na Mtume wake, na Waumini, hata wawe wakinong’ona na kupanga njama namna gani, basi hakika madhara ya hayo yanawarudia wao wenyewe, na wala Waumini hawawezi kudhuriwa isipokuwa tu kwa jambo aliloliandikia Mwenyezi Mungu na kulipitisha.
“Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini.” Yaani, wamtegemee na waamini ahadi yake. Kwa maana mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, anamtosheleza yeye na kumtosheleza katika mambo ya dini yake na dunia yake.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّهُ لَكُمْ وَإِذَا قِيلَ انْشُزُوا فَانْشُزُوا يَرْفَعِ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ}.
11.
Enyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi.
Na mkiambiwa: Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
#
{11} هذا أدبٌ من الله لعباده [المؤمنين] إذا اجتمعوا في مجلس من مجالس مجتمعاتهم، واحتاجَ بعضُهم أو بعضُ القادمين [عليهم] للتفسُّح له في المجلس؛ فإنَّ من الأدب أن يَفْسَحوا له؛ تحصيلاً لهذا المقصود، وليس ذلك بضارٍّ للفاسح شيئاً، فيحصلُ مقصود أخيه من غير ضررٍ يلحقه، والجزاء من جنس العمل؛ فإنَّ من فَسَحَ؛ فَسَحَ الله له، ومن وسَّع لأخيه؛ وسَّع الله عليه، {وإذا قيل انشُزوا}؛ أي: ارتفعوا وتَنَحَّوْا عن مجالسكم لحاجةٍ تعرِضُ، {فانشُزوا}؛ أي: فبادروا للقيام لتحصيل تلك المصلحة؛ فإنَّ القيام بمثل هذه الأمور من العلم والإيمان، والله تعالى يرفع أهل العلم والإيمان درجاتٍ بحسب ما خصَّهم [اللَّه] به من العلم والإيمان. {والله بما تعملونَ خبيرٌ}: فيجازي كلَّ عامل بعمله؛ إن خيراً فخيرٌ، وإن شرًّا فشرٌّ. وفي هذه الآية فضيلة العلم، وأنَّ زينته وثمرتَه التأدُّب بآدابه والعمل بمقتضاه.
{11} Hii ni adabu nzuri ambayo Mwenyezi Mungu anawafunza waja wake wanapokuwa wamekusanyika katika mkusanyiko yao, wakati baadhi yao watahitaji kusongewa. Basi ni katika adabu nzuri kwamba afanyiwe nafasi, na hilo halimdhuru mwenye kusonga akatengeneza nafasi kwa chochote, akawa huyo ndugu yake amefikia lengo lake bila ya yeye kufikiwa na madhara yoyote, na malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa sababu, mwenye kusonga akatengeneza nafasi, Mwenyezi Mungu anamfanyia nafasi. Na mwenye kumpanulia ndugu yake, Mwenyezi Mungu anampanulia.
“Na mkiambiwa: Ondokeni” Yaani, simameni na jitengeni na mikusanyiko yenu kwa sababu ya haja fulani inayojitokeza,
“basi ondokeni.” Yaani, harakisheni kunyanyuka ili kufikia masilahi hayo. Kwani, kufanya mambo hayo ni katika elimu na imani, na Mwenyezi Mungu Mtukufu huwanyanyua watu wa elimu na imani kwa daraja mbalimbali kulingana elimu ambayo
[Mwenyezi Mungu] aliwapa.
“Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.” Kisha atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake. Yakiwa ni mazuri, basi kwa uzuri. Na ikiwa ni mabaya, basi kwa ubaya. Katika Aya hii, kuna fadhila ya elimu, na pambo lake na matunda yake ni kuwa na adabu zake na kutenda kulingana na matakwa yake.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ذَلِكَ خَيْرٌ لَكُمْ وَأَطْهَرُ فَإِنْ لَمْ تَجِدُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (12) أَأَشْفَقْتُمْ أَنْ تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَاللَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ (13)}.
12. Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu. Hiyo ni heri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu zaidi. 13. Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu kwa siri? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi shikeni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
#
{12} يأمر تعالى المؤمنين بالصَّدقة أمام مناجاة رسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - تأديباً لهم وتعليماً وتعظيماً للرسول - صلى الله عليه وسلم -؛ فإنَّ هذا التعظيم خيرٌ للمؤمنين وأطهر؛ أي: بذلك يكثر خيركم وأجركم، وتحصُلُ لكم الطهارة من الأدناس، التي من جملتها ترك احترام الرسول - صلى الله عليه وسلم - والأدبِ معه بكثرة المناجاة التي لا ثمرةَ تحتها؛ فإنَّه إذا أمر بالصدقة بين يدي مناجاتِهِ؛ صار هذا ميزاناً لمن كان حريصاً على العلم والخير ؛ فلا يُبالي بالصدقة، ومَنْ لم يكن له حرصٌ ولا رغبةٌ في الخير، وإنَّما مقصودُه مجرَّدُ كثرة الكلام، فينكفُّ بذلك عن الذي يشقُّ على الرسول، هذا في الواجد للصدقة، وأما الذي لا يجد الصدقة؛ فإنَّ الله لم يضيِّقْ عليه الأمر، بل عفا عنه وسامَحَه وأباح له المناجاة بدون تقديم صدقةٍ لا يقدِرُ عليها.
{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha Waumini kutoa sadaka mbele ya mazungumzo yao ya siri na Mtume Wake Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ili kuwaonyesha adabu nzuri, kuwaelimisha na kumheshimu Mtume - rehema na amani ziwe juu yake. Kwa sababu heshima hii ni bora kwa Waumini na safi zaidi. Kwani kwa kufanya hivyo, wema wenu na malipo yenu yanazidi kuwa mengi, na mtapata utakaso kutokana na uchafu, ambao ni pamoja na kuacha kumheshimu Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, – na pia kuacha kuwa na adabu nzuri mbele yake kwa kuzungumza mazungumzo ya mengi ambayo hayana matunda. Iwapo ataamrisha kutoa sadaka kabla ya mtu kumnong’onezea, hilo linakuwa ni mizani inayoonyesha mwenye bidii ya kufatuta elimu na heri, naye hatajali uzito wa kutoa sadaka hiyo, mbali na yule asiyekuwa na bidii wala hamu ya kufanya heri, yule ambaye lengo lake ni kuzungumza mengi tu. Basi huyu atazuilika kwa hilo asifanye kilicho kigumu kwa Mtume. Hilo ni kwa yule ambaye anaweza kupata sadaka. Ama yule asiyeweza kupata sadaka, basi Mwenyezi Mungu hakufanya jambo hili kuwa gumu. Bali alimsamehe na kumruhusu kumnong’onezea bila ya kutoa sadaka ambayo hawawezi kutoa.
#
{13} ثم لما رأى [تبارك و] تعالى شفقةَ المؤمنين ومشقَّةَ الصدقاتِ عليهم عند كلِّ مناجاةٍ؛ سهَّل الأمر عليهم، ولم يؤاخِذْهم بترك الصدقة بين يدي المناجاة، وبقي التعظيم للرسول والاحترام بحاله لم يُنْسَخْ؛ لأنَّ هذا [الحكمَ] من باب المشروع لغيره، ليس مقصوداً لنفسه، وإنَّما المقصود هو الأدب مع الرسول والإكرام له، وأمرهم تعالى أن يقوموا بالمأمورات الكبارِ المقصودةِ بنفسها، فقال: {فإذْ لم تَفْعَلوا}؛ أي: لم يهنْ عليكم تقديم الصدقةِ، ولا يكفي هذا؛ فإنَّه ليس من شرط الأمر أن يكون هيناً على العبد، ولهذا قيَّده بقوله: {وتاب الله عليكم}؛ أي: عفا لكم عن ذلك، {فأقيموا الصلاة}: بأركانها وشروطها وجميع حدودها ولوازمها، {وآتوا الزَّكاةَ}: المفروضة في أموالكم إلى مستحقِّيها.
وهاتان العبادتان هما أمُّ العبادات البدنيَّة والماليَّة؛ فمن قام بهما على الوجه الشرعيِّ؛ فقد قام بحقوق الله وحقوق عباده، ولهذا قال بعده: {وأطيعوا اللهَ ورسولَه}: وهذا أشملُ ما يكون من الأوامر، فيدخُلُ في ذلك طاعة الله وطاعة رسوله بامتثال أوامرِهما واجتنابِ نواهيهما وتصديق ما أخبرا به والوقوفِ عند حدودِ الشرع ، والعبرةُ في ذلك على الإخلاص والإحسان؛ فلهذا قال: {والله خبيرٌ بما تعملون}: فيعلم تعالى أعمالهم، وعلى أيِّ وجه صَدَرَتْ، فيجازيهم على حسب علمه بما في صدورهم.
{13} Basi
[Mwenyezi Mungu, Mwenye baraka nyingi] Mtukufu alipoona huruma kubwa ya Waumini na ugumu wa kuwatolea sadaka wakati wa kumnong’onezea Mtume, akawafanyia jambo hilo kuwa jepesi, na wala hakuwachukulia makosa ya kuacha kutoa sadaka kabla ya kumnong’onezea, kukabakia kumheshimu Mtume na kumpa taadhima kama ilivyo bila ya kufutwa. Kwa sababu
[hukumu] hii katika hukumu zilizowekwa si kwa ajili yake yenyewe. Bali kilichokusudiwa ni kuwa na adabu nzuri mbele ya Mtume na kumheshimu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha kutekeleza maamrisho makubwa yaliyokusudiwa yenyewe.
Akasema: “Ikiwa hamkufanya hayo.” Yaani, ikiwa si rahisi kwenu kutoa sadaka, lakini hili halitoshi. Kwani si sharti la jambo kuwa lazima kwamba liwe jepesi kwa mja,
na ndiyo maana akaliwekea mipaka kwa kusema: “Na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu.” Yaani, akakusameheni hilo, basi shikeni Sala” kwa kutekeleza nguzo zake, masharti yake, na mipaka yake na mambo yote yanayofungamana nayo.
“Na toeni Zaka” ya lazima kutoka katika mali zenu na muwape wale wanaostahiki kupewa. Ibada hizi mbili ndizo mama ya ibada za kimwili na za kimali. Kwa hivyo, mwenye kuzitekeleza ipasavyo kisheria, basi atakuwa ametekeelza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake,
na ndiyo maana akasema baada yake: “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Na hii ndiyo amri inayojumuisha zaidi, kwa hivyo inaingia humo kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake kwa kutekeleza maamrisho yao, kujiepusha na makatazo yao, kusadiki waliyotuambia, kusimamia kwenye mipaka ya Sheria, na kinachozingatiwa zaidi katika hayo ni kumkusudia Mwenyezi Mungu tu na kufanya mambo kwa uzuri zaidi.
Ndiyo maana akasema: “Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.” Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anayajua matendo yenu, na kwa namna gani yalifanyika, kisha atawalipa kulingana na anavyojua yale yaliyomo vifuani mwao.
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مَا هُمْ مِنْكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ (14) أَعَدَّ اللَّهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (15) اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَلَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ (16) لَنْ تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (17) يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَى شَيْءٍ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْكَاذِبُونَ (18) اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنْسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّهِ أُولَئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ (19)}.
14. Huwaoni wale waliofanya urafiki mwendani na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uwongo hali ya kuwa wanajua. 15. Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali. Kwa hakika waliyokuwa wakiyatenda ni maovu kabisa. 16. Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaipinga Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha. 17. Hayatawafaa kitu mali yao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu milele. 18. Siku atakayowafufua Mwenyezi Mungu wote, wamuapie kama wanavyokuapieni nyinyi. Na watadhani kuwa wamepata kitu! Kwa hakika hao ndio waongo. 19. Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Sikilizeni, hakika kundi la Shetani ndilo lenye kuhasirika.
#
{14 - 15} يخبر تعالى عن شناعة حال المنافقين، الذين يَتَوَلَّوْنَ الكافرين من اليهود والنصارى وغيرهم ممَّن غَضِبَ الله عليهم ونالوا من لعنةِ الله أوفى نصيبٍ، وأنَّهم ليسوا من المؤمنين ولا من الكافرين: {مُذَبْذَبين بين ذلك لا إلى هؤلاءِ ولا إلى هؤلاءِ}: فليسوا مؤمنين ظاهراً وباطناً؛ لأنَّ باطنهم مع الكفار، ولا مع الكفار ظاهراً وباطناً؛ لأنَّ ظاهرهم مع المؤمنين، وهذا وصفهم الذي نعتهم الله به، والحالُ أنَّهم يحلفون على ضدِّه الذي هو الكذب، فيحلفون أنَّهم مؤمنون، والحال أنَّهم ليسوا مؤمنين، فجزاءُ هؤلاء الخونة الفجرة الكَذَبة أنَّ الله أعدَّ لهم عذاباً شديداً لا يقادَرُ قدرُه ولا يُعْلَم وصفُه؛ {إنَّهم ساء ما كانوا يعملون}: حيث عملوا بما يُسْخِطُ الله ويوجِبُ عليهم العقوبة واللعنة.
{14 - 15} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ubaya wa hali ya wanafiki, ambao ni washirika wanafanya urafiki wendani na makafiri miongoni mwa Mayahudi, Wakristo, na wengineo ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia na wakapokea fungu kamili katika laana ya Mwenyezi Mungu, na ya kwamba wao si miongoni mwa Waumini wala miongoni mwa makafiri.
“Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako, na huko hawako.” Wao si Waumini kwa dhahiri wala kwa ndani, kwa sababu kwa ndani yao wako pamoja na makafiri, na wala hawako pamoja na makafiri kwa dhahiri na kwa ndani. Kwa sababu kwa dhahiri yao wako pamoja na Waumini. Hii ndiyo sifa yao ambayo Mwenyezi Mungu amewaelezea kwayo, na hali ni kuwa wanaapa kwa kinyume chake, ambacho ni kusema uongo. Wanaapa kwamba wao ni Waumini, na hali ni kwamba wao sio Waumini. Basi malipo ya wahaini hawa,
waovu na waongo ni kwamba Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali ambayo haiwezi kukadiriwa kiasi chake wala hata maelezo yake hayajulikani: “Kwa hakika waliyokuwa wakiyatenda ni maovu kabisa.” Kwa maana walifanya yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu na yanawasababishia kupata adhabu na laana.
#
{16} {اتَّخذوا أيمانَهم جُنَّةً}؛ أي: ترساً ووقايةً يتَّقون بها من لوم الله ورسوله والمؤمنين، فبسبب ذلك صدُّوا أنفسهم وغيرهم عن سبيل الله، وهو الصراط الذي مَن سَلَكَه؛ أفضى به إلى جنات النعيم، ومن صدَّ عنه؛ فليس إلاَّ الصراط الموصل إلى الجحيم، {فلهم عذابٌ مهينٌ}: حيث استَكْبَروا عن الإيمان بالله والانقياد لآياته؛ أهانهم بالعذاب السرمديِّ الذي لا يُفَتَّر عنهم ساعةً ولا هم يُنْظَرونَ.
{16} “Wamefanya viapo vyao ni ngao” wanayojikinga kwayo kutokana na lawama ya Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Waumini. Kwa sababu hiyo, walijizuia mbali na njia ya Mwenyezi Mungu, ambayo ndiyo njia ambayo mwenye kuifuata, inamfikisha katika Bustani za mbinguni za neema. Na mwenye kujizuilia mbali nayo, basi hatakuwa isipokuwa na njia itakayomfikisha katika Jahannamu.
“Basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha” kwani walikuwa wakifanya kiburi wakaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na kunyenyekea Ishara zake, kwa hivyo akawadhalilisha kwa adhabu ya milele ambayo hayatapumzishwa mbali nayo kwa saa moja, wala hawatapewa muda.
#
{17} {لن تُغْنِيَ عنهم أموالُهم ولا أولادُهم من الله شيئاً}؛ أي: لا تَدْفَعُ عنهم شيئاً من العذاب، ولا تحصِّلُ لهم قسطاً من الثواب، {أولئك أصحابُ النار}: الملازمون لها، الذين لا يخرُجون عنها، و {هم فيها خالدون}.
{17} “Hayatawafaa kitu mali yao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu” kutokana na adhabu, wala havitawapa fungu lolote katika malipo mazuri.
“Hao ndio watu wa Motoni” ambao hawatatoka humo,
“na humo watadumu milele.”
#
{18} ومن عاش على شيءٍ؛ مات عليه؛ فكما أنَّ المنافقين في الدُّنيا يموِّهون على المؤمنين ويحلفون لهم أنَّهم مؤمنون، فإذا كان يوم القيامةِ وبعثَهُم الله جميعاً؛ حلفوا لله كما حلفوا للمؤمنين، ويحسبون في حلفهم هذا {أنَّهم على شيءٍ}: لأنَّ كفرهم ونفاقهم وعقائدهم الباطلة لم تَزَلْ تَرْسخُ في أذهانهم شيئاً فشيئاً، حتى غرَّتهم وظنُّوا أنَّهم على شيءٍ يعتدُّ به ويعلَّقُ عليه الثواب، وهم كاذبون في ذلك، ومن المعلوم أن الكذِبَ لا يروجُ على عالم الغيب والشهادة.
{18} Na anayeishi juu ya kitu fulani, atakufia juu yake. Kwa hivyo, kama vile wanafiki katika dunia wanavyowaficha Waumini ukweli wao, na kuwaapia kuwa wao ni Waumini, itakapofika Siku ya Kiyama na Mwenyezi Mungu akawafufua wote, watamuapia Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa wakiwaapia Waumini, na watadhani kwamba katika viapo vyao hivi
“kuwa wamepata kitu!” Kwa sababu ukafiri wao, unafiki wao, na imani zao za batili ziliendelea kukita mizizi katika akili zao kidogo kidogo, mpaka vikawadanganya na kufikiri kwamba wako juu ya kitu chenye kutegemewa na cha kuwaletea malipo mazuri, lakini wao ni waongo katika hilo. Kwa maana, imeshajulikana kwamba uongo hauwezi kumdanganya Mjuzi wa siri na dhahiri.
#
{19} وهذا الذي جرى عليهم من استحواذِ الشيطان الذي استولى عليهم وزَيَّنَ لهم أعمالهم وأنساهم ذِكْرَ الله، وهو العدوُّ المبينُ الذي لا يريدُ بهم إلاَّ الشرَّ، إنَّما يدعو حِزْبَه ليكونوا من أصحاب السعير، {أولئك حزبُ الشيطان ألا إنَّ حزبَ الشيطانِ هم الخاسرون}: الذين خسروا دينَهم ودُنياهم وأنْفُسَهم وأهليهم.
{19} Na haya ndiyo yaliyowapata kutokana na kumilikiwa na kutawaliwa na Shetani, na akawapambia matendo yao na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Naye ndiye adui wa wazi hawatakii isipokuwa mabaya tu. Kwani yeye analiita kundi lake ili liwe katika watu wa Motoni.
“Hao ndio kundi la Shetani. Sikilizeni, hakika kundi la Shetani ndilo lenye kuhasirika.” Wale waliopoteza dini yao, dunia yao, nafsi zao na familia zao.
{إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُولَئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ (20) كَتَبَ اللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ (21)}.
20. Hakika wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho. 21.
Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.
#
{20 - 21} هذا وعدٌ ووعيدٌ، وعيدٌ لمن حادَّ الله ورسوله بالكفر والمعاصي أنَّه مخذولٌ مذلولٌ لا عاقبةَ له حميدةٌ، ولا رايةَ له منصورةٌ، ووعدٌ لمن آمن به وبرسله واتَّبع ما جاء به المرسلون فصار من حزبِ الله المفلحين أنَّ لهم الفتحَ والنصرَ والغلبةَ في الدُّنيا والآخرة، وهذا وعدٌ لا يُخْلَفُ ولا يغيَّر؛ فإنَّه من الصادق القويِّ العزيز الذي لا يعجِزُه شيءٌ يريده.
{20 - 21} Hii ni ahadi ya malipo mazuri na tishio. Ni tishio kwa mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa ukafiri na maasia, kwamba ataachwa bila ya kusaidiwa na atadhalilishwa na kwamba hatakuwa na mwisho wa kusifiwa, na hatakuwa na bendera ya yenye kusaidiwa ikapata ushindi. Na ni ahadi ya malipo mazuri kwa anayemuamini Yeye na Mitume wake, na akafuata waliyokuja nayo Mitume na akawa miongoni mwa kundi la Mwenyezi Mungu lililofaulu, kwamba wao wana ushindi, kusaidiwa katika Dunia na Akhera. Hii ni ahadi isiyoweza kuvunjwa wala kubadilishwa. Kwani hiyo ni kutoka kwa Mkweli, Mwenye nguvu, Mshindi asiyeweza kushindwa na lolote analolitaka.
{لَا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ أُولَئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُمْ بِرُوحٍ مِنْهُ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ أُولَئِكَ حِزْبُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (22)}.
22. Huwakuti watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio
(Hizbullahi) Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.
#
{22} يقول تعالى: {لا تَجِدُ قوماً يؤمنون بالله واليوم الآخرِ يوادُّونَ من حادَّ الله ورسولَه}؛ أي: لا يجتمع هذا وهذا، فلا يكون العبدُ مؤمناً بالله واليوم الآخر حقيقةً إلاَّ كان عاملاً على مقتضى إيمانه ولوازمه من محبَّةِ مَنْ قام بالإيمان وموالاته وبُغْضِ مَنْ لم يَقُمْ به ومعاداتِهِ، ولو كان أقربَ الناس إليه، وهذا هو الإيمان على الحقيقة، الذي وجدت ثمرته والمقصود منه، وأهل هذا الوصف هم الذين {كَتَبَ} الله {في قلوبهم الإيمان}؛ أي: رسمه وثبَّته وغرسه غرساً لا يتزلزلُ ولا تؤثِّر فيه الشُّبه والشُّكوك، وهم الذين قواهم الله {بروح منه}؛ أي: بوحيه ومعونته ومدده الإلهي وإحسانه الرباني وهم الذين لهم الحياة الطيبة في هذه الدار، ولهم جناتُ النعيم في دار القرار، التي فيها كلُّ ما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعين وتختارُ، ولهم أفضل النعيم وأكبره ، وهو أنَّ اللهَ يُحِلُّ عليهم رضوانَه؛ فلا يسخطُ عليهم أبداً، ويرضَوْن عن ربِّهم بما يعطيهم من أنواع الكرامات ووافر المَثوبات وجزيل الهِبات ورفيع الدَّرجات؛ بحيث لا يَرَوْنَ فوق ما أعطاهم مولاهم غايةً ولا وراءه نهايةً، وأما مَنْ يزعُمُ أنَّه يؤمن بالله واليوم الآخر، وهو مع ذلك موادٌّ لأعداء الله محبٌّ لمن نَبَذَ الإيمان وراء ظهرِهِ؛ فإنَّ هذا إيمانٌ زعميٌّ لا حقيقة له؛ فإنَّ كلَّ أمرٍ لا بدَّ له من برهانٍ يصدِّقه؛ فمجرَّدُ الدعوى لا تفيدُ شيئاً ولا يصدَّقُ صاحبها. والحمد لله.
{22} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
“Huwakuti watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Yaani, haya na haya hayajumuiki pamoja. Kwa hivyo mja hawezi kuwa ni mwenye kumuamini kihakika Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho isipokuwa atatenda kulingana na matakwa ya imani yake hiyo na mahitaji yake kama vile kumpenda na kumfanya wendani yule ambaye alimwamini, na kuchukia yule ambaye hakufanya hivyo na kumfanyia uadui, hata kama yeye ndiye mtu wa karibu zaidi naye. Hii ndiyo imani ya kweli, ambayo yamepatikana matunda yake na makusudio wake. Na wanaosifika kwa sifa hizi ndio ambao Mwenyezi Mungu
“ameandika katika nyoyo zao Imani” akaichora humo, akaiimarisha, akaipanda kupanda ambako haitikisiki wala haiathiriwi fikira potofu wala dhana zozote. Nao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa nguvu
“kwa Roho itokayo kwake” yaani kwa wahyi wake, msaada wake wa kimungu, msaada wake, wema wake ya kimungu, nao ndio wenye maisha mema katika nyumba hii, na wana mabustani ya neema katika nyumba ya kubakia, ambayo ndani yake kuna kila kitu ambacho nafsi zinatamani na macho yanafurahia na kuchagua, na wanayo neema iliyo bora zaidi na kubwa zaidi, ambayo ni kwamba Mwenyezi Mungu atawapa radhi yake, na wala hatawakasirikia abadani, nao watamridhia Mola wao Mlezi kwa yale atakayowapa miongoni mwa kila aina ya mambo matukufu, na malipo mazuri mengi, na vipawa teletele, na vyeo vya juu, kiasi kwamba hawataona juu ya yale aliyowapa Mola wao lengo lingine wala mwisho wowote baada yake. Na ama mwenye kudai kwamba anamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, lakini pamoja na hayo, anawapenda maadui wa Mwenyezi Mungu, na kumpenda mwenye kuiacha imani nyuma ya mgongo wake. Hakika hii ni imani ya kujidai tu ambayo haina uhakika wowote. Kwa maana kila jambo ni lazima liwe na ushahidi wa kulisadikisha. Lakini kudai tu hakufai kitu chochote, wala mwenye madai hayo hasadikiwi, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
***