Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (1) لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (2) هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (3) هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنْزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنْتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (4) لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ (5) يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (6)}.
1. Kinamsabihi kumtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo ndani ya mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 2. Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye uwezo mno wa kila kitu. 3. Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhahiri na wa Siri, naye ndiye ajuaye zaidi kila kitu. 4. Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akainuka juu ya Kitu cha enzi. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno mnayoyatenda. 5. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake. Na mambo yote yanarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu. 6. Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku. Na Yeye ni Mwenye kuyajua mno yaliyomo vifuani.
#
{1} يخبرُ تعالى عن عظمته وجلاله وسعة سلطانِهِ أنَّ جميع {ما في السمواتِ والأرض} من الحيوانات الناطقة [والصامتة] وغيرها والجوامد تسبِّحُ بحمد ربِّها وتنزِّهه عمَّا لا يليق بجلاله، وأنها قانتةٌ لربِّها، منقادةٌ لعزَّته، قد ظهرت فيها آثار حكمته، ولهذا قال: {وهو العزيز الحكيم}؛ فهذا فيه بيان عموم افتقار المخلوقات العلويَّة والسفليَّة لربِّها في جميع أحوالها، وعموم عزَّته وقهره للأشياء كلِّها، وعموم حكمته في خلقه وأمره.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wake, utukufu wake, na upana wa mamlaka yake, kwamba kila "kilichomo ndani ya mbingu na ardhi" miongoni mwa wanyama wanaozungumza
[na wasiozungumza] na vitu vinginevyo visivyo na uhai vinamtakasa kwa sifa njema za Mola wao Mlezi na vinamuweka mbali na yote yasiyoufailia utukufu wake, na kwamba vyote vinaunyenyekea Mola wao Mlezi na kutii nguvu zake, na zimedhihiri ndani yao athari za hekima yake.
Na ndiyo maana akasema: "Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Haya yanabainisha ujumla wa viumbe vya juu na vya chini kuhitajia zaidi, Mola wao Mlezi katika hali zao zote, na ujumla wa utukufu wake, ushindi wake juu ya kila kitu, na ujumla wa hekima yake katika uumbaji na amri yake.
#
{2} ثم أخبر عن عموم ملكه، فقال: {له ملكُ السمواتِ والأرضِ يحيي ويميتُ}؛ أي: هو الخالق لذلك، الرازق المدبِّر لها بقدرته، {وهو على كلِّ شيءٍ قديرٌ}.
{2} Kisha akajulisha juu ya ujumla wa ufalme wake,
akasema: "Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha." Yaani, Yeye ndiye Muumba wa hayo, Mwenye kuruzuku, Mwenye kuyaendesha kwa uwezo wake, "Na Yeye ni Mwenye uwezo mno wa kila kitu."
#
{3} {هو الأولُ}: الذي ليس قبلَه شيءٌ. {والآخر}: الذي ليس بعدَه شيءٌ. {والظاهر}: الذي ليس فوقَه شيءٌ. {والباطن}: الذي ليس دونَه شيءٌ. {وهو بكلِّ شيءٍ عليمٌ}: قد أحاط علمُه بالظواهر والبواطن والسرائر والخفايا والأمور المتقدِّمة والمتأخِّرة.
{3} "Yeye ndiye wa Mwanzo" ambaye hakuna kitu mbele yake. "Na ndiye wa Mwisho" ambaye hakuna kitu baada yake. "Naye ndiye wa Dhahiri" ambaye juu yake hakuna kitu. "Na wa Siri" ambaye hakuna chini yake. "Naye ndiye ajuaye zaidi kila kitu." Elimu yake imezunguka mambo ya dhahiri na ya nje, siri na mambo yaliyofichikana zaidi, yaliyotangulia na ya baadaye.
#
{4} {هو الذي خلق السمواتِ والأرضَ في ستَّة أيام}: أولُها يومُ الأحد، وآخرُها يومُ الجمعة، {ثم استوى على العرش}: استواءً يَليقُ بجلاله فوق جميع خلقه، {يعلم ما يَلِجُ في الأرض}: من حبٍّ وحيوانٍ ومطرٍ وغير ذلك، {وما يخرج منها}: من نبتٍ وشجرٍ وحيوان وغير ذلك، {وما ينزِلُ من السماء}: من الملائكة والأقدار والأرزاق، {وما يَعْرُجُ فيها}: من الملائكة والأرواح والأدعية والأعمال وغير ذلك، {وهو معكم أينما كُنتم}؛ كقوله: {ما يكون من نجوى ثلاثةٍ إلاَّ هو رابِعُهم ولا خمسةٍ إلاَّ هو سادسُهم ولا أدنى من ذلك ولا أكثر إلاَّ هو معهم أينما كانوا}: وهذه المعيَّة معيَّةُ العلم والاطِّلاع، ولهذا توعَّد ووعد بالمجازاة بالأعمال بقوله: {والله بما تعلمون بصيرٌ}؛ أي: هو تعالى بصيرٌ بما يصدر منكم من الأعمال وما صدرت عنه تلك الأعمال من برٍّ وفجورٍ؛ فمجازيكمعليها وحافظها عليكم.
{4} "Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita." Ya kwanza yake ni Jumapili na ya mwisho yake ni Ijumaa "kisha akainuka juu ya Kitu cha enzi" kuinuka kunakolingana na utukufu wake juu viumbe vyake vyote. "Anayajua yanayoingia katika ardhi" kama vile nafaka, wanyama, mvua na mengineyo. "Na yanayopanda kutoka humo" kama vile mimea, miti, wanyama na mengineyo "na yanayoteremka kutoka mbinguni" kama vile Malaika, mipango yake na riziki. "Na yanayopanda humo" kama vile Malaika, roho, na dua, matendo na vitu vinginevyo. "na Yeye yu pamoja nanyi popote mlipo.
" Kama vile kauli yake: "Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo." Na upamoja wake huu ni kwa elimu yake na kuona kwake. Ndiyo maana akatishia kwa adhabu na akaahidi ahadi ya kulipa kulingana na matendo,
kwa kauli yake: "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno mnayoyatenda." Yaani, Yeye Mtukufu anayaona mno matendo mnayoyafanya na yaliyoyasababisha; ya wema na maovu, kisha atakulipeni kwa hayo na amekulindieni.
#
{5} {له ما في السمواتِ والأرضِ}: ملكاً وخلقاً وعبيداً يتصرَّف فيهم بما شاءه من أوامره القدريَّة والشرعيَّة الجارية على الحكمة الربَّانيَّة، {وإلى الله تُرْجَعُ الأمور}: من الأعمال والعمال، فيعرض عليه العبادُ، فيميز الخبيثُ من الطيِّب، ويجازي المحسن بإحسانه والمسيء بإساءته.
{5} "Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake;" ufalme, uumbaji na waja. Yeye huviendesha anavyotaka kwa amri zake alizozipanga awali, na amri zake za kisheria zinazokwenda kwa hekima ya kimungu. "Na mambo yote yanarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu." Kisha waja watawasilishwa kwake, naye atampambanua muovu mbali na mwema, na amlipe mwema wema wake, na mbaya kwa ubaya wake.
#
{6} {يولِجُ الليل في النَّهار ويولِجُ النهارَ في الليل}؛ أي: يدخِلُ الليل على النهار، فيغشيهم الليل بظلامه، فيسكنون ويهدؤون، ثم يُدْخِلُ النهار على الليل، فيزول ما على الأرض من الظلام، ويضيء الكون، فيتحرَّك العباد، ويقومون إلى مصالحهم ومعايشهم، ولا يزال اللهُ يكوِّر الليلَ على النهار والنهارَ على الليل، ويداول بينهما في الزيادة والنقص والطول والقصر، حتى تقومَ بذلك الفصول وتستقيمَ الأزمنة ويحصلَ من المصالح بذلك ما يحصل ، فتبارك الله ربُّ العالمين، وتعالى الكريم الجواد الذي أنعم على عباده بالنعم الظاهرة والباطنة، {وهو عليمٌ بذات الصُّدور}؛ أي: بما يكون في صدور العالمين، فيوفِّق مَنْ يعلم أنَّه أهلٌ لذلك، ويخذُلُ من يعلم أنَّه لا يَصْلُحُ لهدايتِهِ.
{6} "Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku." Yaani, usiku unaingia katika mchana, kisha unawafunika kwa giza lake, kwa hivyo wanatulia tuli. Kisha mchana unaingilia usiku, na giza lililoko kwenye ardhi linatoweka, na ulimwengu unaangazwa kwa hivyo waja wanatembea huku na kule, wakienda katika masilahi yao na mambo ya maisha yao. Na Mwenyezi Mungu anaendelea kuufunika usiku juu ya mchana, na kuufunika mchana juu ya usiku, na anavizungusha kwa kuongezeka na kupungua, kwa urefu na ufupi, mpaka misimu ipatikane kwa hayo na nyakati zinyooke sawa, ndiyo yapatikane masilahi mbalimbali kwa hayo. Basi ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na ametukuka Mwenye ukarimu, Mwenye kutoa kwa wingi, ambaye amewaneemesha waja wake kwa neema za dhahiri na zilizofichika. "Na Yeye ni Mwenye kuyajua mno yaliyomo vifuani" mwa walimwengu. Kwa hivyo, anamuwezesha anayejua kwamba anafailia hilo, na anamfelisha anayejua kwamba hafailii kuongolewa.
{آمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَأَنْفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُمْ مُسْتَخْلَفِينَ فِيهِ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَأَنْفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ (7) وَمَا لَكُمْ لَا تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ لِتُؤْمِنُوا بِرَبِّكُمْ وَقَدْ أَخَذَ مِيثَاقَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (8) هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَى عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِيُخْرِجَكُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَإِنَّ اللَّهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَحِيمٌ (9) وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلِلَّهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا يَسْتَوِي مِنْكُمْ مَنْ أَنْفَقَ مِنْ قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ أُولَئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِنَ الَّذِينَ أَنْفَقُوا مِنْ بَعْدُ وَقَاتَلُوا وَكُلًّا وَعَدَ اللَّهُ الْحُسْنَى وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (10) مَنْ ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ (11)}.
7. Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na toeni katika alivyokufanyeni nyinyi kuwa ni waangalizi wake. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa. 8. Na mna nini hata hamumuamini Mwenyezi Mungu na hali Mtume anakuiteni mumuamini Mola wenu Mlezi? Naye amekwisha chukua ahadi yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini. 9. Yeye ndiye anayemteremshia mja wake Aya zinazobainisha wazi ili akutoeni gizani hadi kwenye nuru. Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu. 10. Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa miongoni waliotoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walitoa baadaye na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. 11. Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu.
#
{7} يأمر تعالى عبادَه بالإيمان به، وبرسوله وبما جاء به، وبالنفقة في سبيله من الأموال التي جعلها الله في أيديهم واستخْلَفَهم عليها؛ لينظر كيف يعملونَ. ثم لمَّا أمرهم بذلك؛ رغَّبهم وحثَّهم عليه بذكر ما رتَّب عليه من الثواب، فقال: {فالذين آمنوا منكم وأنفقوا لهم أجرٌ كبيرٌ}؛ أي: الذين جمعوا بين الإيمان بالله ورسوله والنفقة في سبيله لهم أجرٌ كبيرٌ، أعظمه وأجلُّه رِضا ربِّهم والفوزُ بدار كرامته وما فيها من النعيم المقيم الذي أعدَّه الله للمؤمنين والمجاهدين.
{7} Mwenyezi Mungu anawaamrisha waja wake kumwamini Yeye na Mtume wake na aliyoyaleta, na watoe mali kwa ajili ya njia Yake kutokana na mali ambazo Mwenyezi Mungu ameweka mikononi mwao na akawafanya kuwa wasimamizi juu wake. Ili aone jinsi wanavyofanya matendo. Kisha alipowaamuru kufanya hivyo, akawatia moyo na akawahimiza kufanya hivyo kwa kutaja malipo aliyowapangia, juu yake,
akasema: "Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, wana malipo makubwa." Yaani, wale waliojumuisha kati ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kutoa mali kwa ajili ya njia yake kwamba watapata malipo makubwa, matukufu ambayo ni kuridhiwa na Mola wao Mlezi na kupata nyumba ya utukufu wake na neema ya milele aliyowaandalia Mwenyezi Mungu Waumini na Mujahidina
(wanaopambana kwa ajili yake).
#
{8} ثم ذكر السَّبب الداعي لهم إلى الإيمان وعدم المانع منه، فقال: {وما لكم لا تؤمنونَ بالله والرسولُ يَدْعوكم لِتُؤْمِنوا بربِّكُم وقد أخذ ميثاقَكُم إن كنتُم مؤمنينَ}؛ أي: وما الذي يمنعكم من الإيمانِ والحالُ أنَّ الرسول محمداً - صلى الله عليه وسلم - أفضلُ الرسل وأكرمُ داعٍ دعا إلى الله يدعوكم؟! فهذا مما يوجِبُ المبادرة إلى إجابة دعوتِهِ والتلبيةِ والإجابةِ للحقِّ الذي جاء به، وقد أخذ عليكم العهدَ والميثاق بالإيمان إن كنتُم مؤمنين.
{8} Kisha akataja sababu itakayowafanya kuamini na kutokuwepo kizuizi cha hilo,
akasema: "Na mna nini hata hamumuamini Mwenyezi Mungu na hali Mtume anakuiteni mumuamini Mola wenu Mlezi? Naye amekwisha chukua ahadi yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini." Yaani, ni nini kinakuzuieni kuamini, na hali Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mbora wa Mitume na mlinganiaji mtukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu anakuiteni? Hili ni katika mambo yanayosababisha kuchukua hatua ya kuitikia wito wake na kuitikia haki aliyokuja nayo, na amechukua ahadi juu yenu na agano madhubuti kwamba mtaamini ikiwa nyinyi ni Waumini.
#
{9} ومع ذلك من لطفه وعنايته بكم أنَّه لم يكتفِ بمجرَّد دعوة الرسول الذي هو أشرف العالَم، بل أيَّده بالمعجزات، ودلَّكم على صدق ما جاء به بالآيات البيِّنات؛ فلهذا قال: {هو الذي يُنَزِّلُ على عبدِهِ آياتٍ بيناتٍ}؛ أي: ظاهرات تدلُّ أهل العقول على صحَّة جميع ما جاء به، وأنَّه الحقُّ اليقين؛ {لِيُخْرِجَكم}: بإرسال الرسول إليكم وما أنزله الله على يده من الكتاب والحكمة {من الظُّلُمات إلى النور}؛ أي: من ظلمات الجهل والكفر إلى نور العلم والإيمان. وهذا من رحمته بكم ورأفته؛ حيث كان أرحم بعباده من الوالدة بولدها، {وإنَّ الله بكم لَرءوفٌ رحيمٌ}.
{9} Pamoja na wema wake huu na kujali kwake, hakutosheka kwa ulinganiaji wa Mtume tu, ambaye ndiye mtukufu zaidi wa walimwengu wote. Bali alimsaidia kwa miujiza na akakuonyesheni ukweli wa yale aliyokuja nayo kwa ishara zilizo wazi.
Ndiyo maana akasema: "Yeye ndiye anayemteremshia mja wake Aya zinazobainisha wazi" zinazowaonyesha wale wenye wenye akili kwamba kila alichokileta ni sahihi, na kwamba ndiyo haki ya yakini. "Akutoeni" kwa kukutumieni Mtume na yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa mkono wake kama vile Kitabu na hekima "kutoka gizani kuingia kwenye nuru." Yaani, kutoka kwenye viza vya ujinga na ukafiri hadi kwenye nuru ya elimu na imani. Haya ni katika rehema na upole wake juu yenu. Ambapo aliwarehemu zaidi waja wake hata kuliko mama kwa mwanawe, "Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu."
#
{10} {وما لكم ألاَّ تُنفِقوا في سبيل اللهِ وللهِ ميراثُ السمواتِ والأرض}؛ أي: وما الذي يمنعكم من النَّفقة في سبيل الله؟ وهي طرق الخير كلُّها، ويوجب لكم أن تبخلوا، {و} الحال أنَّه ليس لكم شيءٌ، بل {لله ميراثُ السمواتِ والأرض}: فجميع الأموال ستنتقلُ من أيديكم أو تنقلون عنها، ثم يعود الملك إلى مالكه تبارك وتعالى؛ فاغتنموا الإنفاق ما دامت الأموال في أيديكم، وانتهِزوا الفرصة. ثم ذَكَرَ تعالى تفاضُلَ الأعمال بحسب الأحوال والحكمة الإلهيَّة، فقال: {لا يستوي منكم من أنفقَ من قبل الفتح وقاتَلَ أولئك أعظمُ درجةً من الذين أنفقوا من بعدُ وقاتَلوا}: المراد بالفتح هنا هو فتحُ الحُدَيْبِيَةِ، حين جرى من الصُّلح بين الرسول وبين قريش، مما هو أعظم الفتوحات التي حصل فيها نشرُ الإسلام واختلاطُ المسلمين بالكافرين والدَّعوة إلى الدين من غير معارض، فدخل الناس من ذلك الوقت في دين الله أفواجاً، واعتزَّ الإسلام عزًّا عظيماً، وكان المسلمون قبل هذا الفتح لا يقدرون على الدَّعوة إلى الدين في غير البقعة التي أسلم أهلُها كالمدينة وتوابعها، وكان مَنْ أسلم من أهل مكَّة وغيرها من ديار المشركين يُؤْذَى ويَخَافُ؛ فلذلك كان مَنْ أسلم قبل الفتح [وأنفق] وقاتل أعظمَ درجةً وأجراً وثواباً ممَّن لم يسلمْ ويقاتِلْ وينفقْ إلاَّ بعد ذلك؛ كما هو مقتضى الحكمة، ولهذا كان السابقون وفضلاء الصحابة غالبهم أسلم قبل الفتح. ولمَّا كان التفضيلُ بين الأمور قد يُتَوَهَّم منه نقصٌ وقدحٌ في المفضول؛ احترز تعالى من هذا بقوله: {وكلًّا وَعَدَ الله الحسنى}؛ أي: الذين أسلموا وقاتلوا وأنفقوا من قبل الفتح وبعده كلُّهم وَعَدَه الله الجنة. وهذا يدلُّ على فضل الصحابة كلِّهم رضي الله عنهم، حيث شهد الله لهم بالإيمان ووعَدَهم الجنة. {والله بما تعملونَ خبيرٌ}: فيجازي كلًّا منكم على ما يعلمه من عمله.
{10} "Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu?" Yaani, ni nini kinachokuzuieni kutumia mali zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu? Nao ni njia za wema zote, na kinawafanya kuwa mabahili. "Na" hali ni kwamba hamna chochote, bali "urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu." Kwani mali zote zitatoka katika mikono yenu au nyinyi wenyewe mtaziacha, kisha umiliki wake utamrudia mmiliki wake hasa, Mwenye baraka nyingi, Mtukufu. Kwa hivyo, tumieni fursa kutoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu madamu bado mna mali mikononi mwenu Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja maelezo ya kina ya matendo kulingana na hali na hekima ya kimwenyezi Mungu,
akasema: "Hawawi sawa miongoni waliotoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walitoa baadaye na wakapigana." Kinachokusudiwa hapa na ushindi ni ule ushindi wa Al-Hudaybiyya, yalipofanyika mapatano ya amani baina ya Mtume na Makureshi, ambao ulikuwa katika ushindi mkubwa zaidi kuliko ambao ndani yake ulienea Uislamu, kuchanganyika Waislamu na makafiri, na kuilingania dini bila upinzani. Basi tangia wakati huo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi, na Uislamu ukapata nguvu kubwa sana, na kabla ya ushindi huu, Waislamu hawakuwa na uwezo wa kuilingania dini katika sehemu nyinginezo isipokuwa katika maeneo ambayo watu wake walikuwa wamesilimu kama vile Madina na viunga vyake. Na watu waliosilimu wa Makka na maeneo mengineyo ya washirikina walikuwa wakiadhibiwa na kuogopa. Kwa hivyo akawa aliyesilimu kabla ya ushindi
[na akatoa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu] na akapigana vita ni mwenye daraja kubwa zaidi na malipo kuliko yule ambaye hakuwa amesilimu, kupigana vita na kutoa mali isipokuwa baada ya hayo, kama inavyotakiwa na hekima, na ndiyo kwa sababu wengi wa waliotangulia na masahaba bora zaidi walisilimu kabla ya ushindi huu. Na kwa kuwa kuboresha kati ya mambo kunaweza kusababisha ifahamike kwamba kuna upungufu na dosari katika kile ambacho hakikuboreshwa,
Mwenyezi Mungu akaondoa hili kwa kauli yake: "Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema." Yaani, wale waliosilimu, wakapigana, na wakatoa mali zao kabla ushindi, na baada yake, wote Mwenyezi Mungu aliwaahidi bustani za mbinguni. Hii inaashiria fadhila za Maswahaba wote, Mungu awe radhi nao, kwani Mwenyezi Mungu alishuhudia imani yao na kuwaahidi Pepo. "Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda." Atamlipa kila mmoja wenu kwa anayoyajua katika matendo yake.
#
{11} ثم حثَّ على النفقة في سبيله؛ لأنَّ الجهاد متوقِّف على النفقة فيه وبذل الأموال في التجهُّز له، فقال: {مَن ذا الذي يُقْرِضُ الله قرضاً حسناً}: وهي النفقة الطيِّبة التي تكون خالصةً لوجه الله موافقةً لمرضاة الله من مال حلال طيبٍ طيبةً به نفسه، وهذا من كرم الله تعالى؛ حيث سمَّاه قرضاً، والمال ماله، والعبيد عبيده ، ووعد بالمضاعفة عليه أضعافاً كثيرةً، وهو الكريم الوهَّابُ، وتلك المضاعفة محلُّها وموضعها يوم القيامةِ، يوم كلٌّ يتبيَّن فقرُه، ويحتاج إلى أقلِّ شيءٍ من الجزاء الحسن، ولهذا قال:
{11} Kisha akawahimiza watu watoe na wapeane katika njia yake; Kwa sababu jihadi inategemea kutoa mali kwa ajili ya kuitayarisha.
Basi akasema: "Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema?" Ambao huwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu na wenye kuafikiana na radhi za Mwenyezi Mungu, kutokana na mali halali, nzuri na aliyotoa kwa moyo safi. Hili ni katika ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; ambapo uliuita mkopo, ilhali mali hiyo ni yake, na waja pia ni waja wake, na akaahidi kuizidisha mali hiyo mizidisho mingi naye ndiye Mkarimu, Mpaji. Na mzidisho huo, mahali pake na siku yake ni siku ya Kiyama. Siku ambayo kila mtu atabainika uhitaji wake, na atahitaji malipo mazuri hata kidogo tu.
Na ndiyo maana akasema:
{يَوْمَ تَرَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ يَسْعَى نُورُهُمْ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (12) يَوْمَ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ لِلَّذِينَ آمَنُوا انْظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِنْ نُورِكُمْ قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُمْ بِسُورٍ لَهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِنْ قِبَلِهِ الْعَذَابُ (13) يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُنْ مَعَكُمْ قَالُوا بَلَى وَلَكِنَّكُمْ فَتَنْتُمْ أَنْفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَارْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ الْأَمَانِيُّ حَتَّى جَاءَ أَمْرُ اللَّهِ وَغَرَّكُمْ بِاللَّهِ الْغَرُورُ (14) فَالْيَوْمَ لَا يُؤْخَذُ مِنْكُمْ فِدْيَةٌ وَلَا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مَأْوَاكُمُ النَّارُ هِيَ مَوْلَاكُمْ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (15)}.
12. Siku utakapowaona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao,
na kuliani kwao: Furaha yenu leo - Bustani zipitazo mito kati yake, mtakaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 13.
Siku wanafiki wanaume na wanafiki wanawake watakapowaambia wale walioamini: 'Tungojeni ili tupate mwangaza katika nuru yenu.
' Waambiwe: 'Rejeeni nyuma yenu mkaitafute nuru!' Kisha itatiwa baina yao ukuta wenye mlango - ndani yake mna rehema, na nje upande wake wa mbele kuna adhabu. 14.
Watawaita wawaambie: 'Kwani hatukuwa pamoja nanyi?' Watawaambia: 'Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya
(Waumini), na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu yule akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu. 15. Basi leo haitachukuliwa kwenu fidia, wala kwa wale waliokufuru. Makazi yenu ni Motoni, ndio bora kwenu; na ni marejeo maovu yalioje!
#
{12} يقول تعالى مبيناً لفضل الإيمان واغتباط أهله به يوم القيامةِ: {يوم تَرى المؤمنينَ والمؤمناتِ يسعى نورُهم بين أيديهم وبأيْمانِهِم}؛ أي: إذا كان يوم القيامةِ، وكوِّرَتِ الشمسُ وخسفَ القمرُ وصار الناس في الظُّلمة، ونُصِبَ الصراط على متن جهنم؛ فحينئذٍ ترى المؤمنين والمؤمنات يسعى نورُهم بين أيديهم وبأيمانهم، فيمشون بنورهم وأيمانهم في ذلك الموقف الهائل الصعب كلٌّ على قَدْرِ إيمانه، ويبشَّرون عند ذلك بأعظم بشارة، فيُقالُ: {بُشراكم اليومَ جناتٌ تجري من تحتِها الأنهارُ خالدين فيها ذلك هو الفوزُ العظيمُ}: فلله ما أحلى هذه البشارة بقلوبهم وألذَّها لنفوسهم؛ حيث حصل لهم كلُّ مطلوب محبوب، ونجوا من كلِّ شرٍّ ومرهوب.
{12} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu,
akieleza fadhila ya Imani na kufurahi kukubwa kwa wana imani Siku ya Kiyama: "Siku utakapowaona Waumini wanaume na Waumini wanawake, nuru yao iko mbele yao, na kuliani kwao." Yaani, ikifika Siku ya Kiyama, na jua likakunjwa na mwezi ukapatwa, na watu wakawa gizani, na ikawekwa Sirat
(njia iliyoko) kwenye mgongo wa Jahannamu; basi hapo utawaona Waumini wanaume na Waumini wanawake wana nuru yao mbele yao na kuliani kwao, kisha watatembea kwa nuru yao katika hali hiyo inayotisha sana na ngumu, kila mmoja kulingana na imani yake, na hapo watapewa bishara njema iliyo kubwa zaidi,
wakiambiwa: "Furaha yenu leo - Bustani zipitazo mito kati yake, mtakaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa." Ee Mwenyezi Mungu, ni bishara njema iliyo nzuri namna gani hii kwenye nyoyo zao, na yenye ladha zaidi kwenye nafsi zao, ambapo walipata kila wanachotafuta, wanachokipenda, na wakaokoka kutokana na kila uovu na kinachohofiwa.
#
{13} فإذا رأى المنافقون المؤمنين يمشون بنورهم ، وهم قد طُفِئَ نورُهم وبقوا في الظُّلمات حائرين؛ قالوا للمؤمنين: {انظُرونا نَقْتَبِسْ من نورِكم}؛ أي: أمهلونا لننال من نوركم ما نمشي به لننجوَ من العذاب، فـ {قيلَ} لهم: {ارجِعوا وراءَكُم فالْتَمِسوا نوراً}؛ أي: إن كان ذلك ممكناً، والحال أنَّ ذلك غير ممكن، بل هو من المحالات، فضُرِبَ بين المؤمنين والمنافقين {بسورٍ}؛ أي: حائط منيع وحصنٍ حصينٍ {له بابٌ باطنُه فيه الرحمةُ}: وهو الذي يلي المؤمنين، {وظاهرُهُ من قِبَلِهِ العذابُ}: وهو الذي يلي المنافقين.
{13} Basi wanaafiki watakapowaona Waumini wanatembea katika nuru yao, ilhali nuru yao imezimwa, na wakabaki gizani wamechanganyikiwa,
watawaambia Waumini: "Tungojeni ili tupate mwangaza katika nuru yenu." Yaani, tungojeni tupate kuweze kutoka katika nuru yenu kitu tutakachoweza kutembea kwacho ili tuepuke na adhabu,
basi wataambiwa: "Rejeeni nyuma yenu mkaitafute nuru." Yaani, ikiwa hilo linawezekana, na hali ni kwamba hilo haliwezekani, bali ni miongoni mwa yasiyowezekana kamwe. Basi "ukuta" wenye kuzuia ulio imara utawekwa baina ya Waumini na wanafiki hao "wenye mlango - ndani yake mna rehema," na huo ni upande wake ulio karibu na Waumini; "na nje upande wake wa mbele kuna adhabu." Nao ni upande wake ulio karibu na wanafiki.
#
{14} فينادي المنافقونَ المؤمنين، فيقولونَ تضرُّعاً وترحُّماً: {ألم نكن معكُمْ}: في الدُّنيا نقول: لا إله إلاَّ الله، ونصلِّي ونصوم ونجاهد ونعمل مثل عملكم؟ {قالوا بلى}: كنتم معنا في الدنيا وعملتُم في الظاهر مثلَ عملنا، ولكنَّ أعمالَكم أعمالُ المنافقين من غيرِ إيمانٍ ولا نيَّةٍ صادقةٍ صالحةٍ، {بل فَتَنتُم أنفسَكم [وتربَّصْتُم] وارْتَبْتُم}؛ أي: شككتم في خبر الله الذي لا يقبل شكًّا، {وغرَّتْكُم الأماني}: الباطلة؛ حيث تمنَّيتم أن تنالوا منالَ المؤمنين وأنتم غير موقنين، {حتى جاء أمرُ الله}؛ أي: حتى جاءكم الموتُ وأنتم بتلك الحالة الذَّميمة، {وغَرَّكم بالله الغَرورُ}: وهو الشيطانُ الذي زين لكم الكفر والريبَ فاطمأننتم به، ووثقتم بوعدِهِ وصدَّقتم خبره.
{14} Kisha wanafiki watawaita Waumini,
na waseme wakiomba kwa njia ya kusihi na kwa huruma kubwa: "Kwani hatukuwa pamoja nanyi" katika dunia,
tukisema: Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, tukiswali, tukifunga, tukifanya jihadi,
na kukifanya matendo kama yenu? "Watawaambia: Ndiyo," mlikuwa pamoja nasi katika dunia na mkatenda matendo kama sisi kwa dhahiri, lakini matendo yenu yalikuwa matendo ya wanafiki wasio na imani wala nia ya ukweli iliyo nzuri. "Lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya
(Waumini), na mkatia shaka" katika habari za Mwenyezi Mungu zisizo na shaka yoyote; "na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni." Ambapo mlikuwa mkitamani kupata yale watakayopata Waumini, na mkawa hata hamna yakini "mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu" ambayo ni mauti nanyi mko katika hali hiyo ya kukashifiwa; "na mdanganyifu yule akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu." Yaani, Shetani ndiye aliyekupambieni ukafiri na shaka, kwa hivyo mkatulia juu yake, na mkawa na imani na ahadi yake na mkasadiki habari zake.
#
{15} {فاليومَ لا يؤخَذُ منكم فديةٌ ولا من الذين كفروا}: ولو افتديتم بملء الأرض ذهباً ومثله معه؛ لما تقبل منكم. {مأواكُمُ النارُ}؛ أي: مستقرُّكم، {هي مولاكم}: التي تتولاَّكم وتضمُّكم إليها، {وبئس المصير}: النار؛ قال تعالى: {وأمَّا مَنْ خَفَّتْ موازينُه. فأمُّه هاويةٌ وما أدراك ما هيه. نارٌ حاميةٌ}.
{15} "Basi leo haitachukuliwa kwenu fidia, wala kwa wale waliokufuru." Na mkijikomboa kwa dhahabu ya ujazo wa ardhi na mfano wake pamoja nayo, hilo halingekubaliwa kutoka kwenu.
"Makazi yenu ni Motoni ndio bora kwenu na ni marejeo maovu yalioje!" Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na yule ambaye mizani yake
(ya mema) itakuwa hafifu. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! Na nini kitakachokujuilisha nini hiyo? Ni Moto mkali!"
{أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ (16) اعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يُحْيِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ (17)}.
16. Je, wakati haujafika bado kwa wale walioamini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyoteremka? Wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao ni wapotovu. 17. Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.
#
{16} لما ذكر حال المؤمنين والمؤمنات والمنافقين والمنافقات في الدار الآخرة؛ كان ذلك مما يدعو القلوب إلى الخشوع لربِّها والاستكانة لعظمته، فعاتب الله المؤمنين على عدم ذلك، فقال: {ألم يأنِ للذين آمنوا أن تَخْشَعَ قلوبُهم لذِكْرِ الله وما نَزَلَ من الحقِّ}؛ أي: ألم يأتِ الوقتُ الذي به تلينُ قلوبهم وتخشعُ لذِكْر الله الذي هو القرآن وتنقادُ لأوامره وزواجره وما نَزَلَ من الحقِّ الذي جاء به محمدٌ - صلى الله عليه وسلم -، وهذا فيه الحثُّ على الاجتهاد على خشوع القلب لله تعالى ولما أنزله من الكتاب والحكمة، وأن يتذكَّر المؤمنون المواعظ الإلهيَّة والأحكام الشرعيَّة كلَّ وقت ويحاسبوا أنفسَهم على ذلك، {ولا يكونوا كالذين أوتوا الكتاب من قَبْلُ فطال عليهم الأمدُ}؛ أي: ولا يكونوا كالذين أنزل الله عليهم الكتابَ الموجبَ لخشوع القلب والانقياد التامِّ، ثم لم يدوموا عليه، ولا ثَبَتوا، بل طال عليهم الزمان، واستمرَّتْ بهم الغفلةُ، فاضمحلَّ إيمانُهم وزال إيقانهم؛ {فقستْ قلوبُهم وكثيرٌ منهم فاسقونَ}: فالقلوب تحتاجُ في كلِّ وقتٍ إلى أن تُذَكَّرَ بما أنزل الله وتناطق بالحكمة، ولا ينبغي الغفلة عن ذلك؛ فإنَّه سببٌ لقسوة القلب وجمود العين.
{16} Alipotaja hali ya Waumini wanaume na Waumini wanawake na wanafiki wanaume na wanafiki wanawake katika Akhera, hayo yakawa katika yale yanayoziitia nyoyo kumnyenyekea Mola wao Mlezi na kuunyenyekea ukuu wake, basi Mwenyezi Mungu akawakemea Waumini kwa kutofanya hivyo,
akasema: "Je, wakati haujafika bado kwa wale walioamini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyoteremka?" Yaani, je, haujafika wakati ambao nyoyo zanafaa kulainika na kuunyenyekea ukumbusho wa Mwenyezi Mungu, nayo ni Qur-ani, na kufuata amri zake na makemeo yake na haki iliyoteremka, ambayo alikuja nayo Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hili ndani yake limo kuwahimiza Waumini kujitahidi kunyenyekea kwa nyoyo zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoyataremsha ya Kitabu na hekima, na kwamba Muumini akumbuke mawaidha ya kimungu na hukumu za kisheria kila wakati, na wajifanyie hesabu juu yake. “Wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu." Yaani, wasiwe kama wale ambao Mwenyezi Mungu aliwateremshia Kitabu kinachohitaji unyenyekevu wa moyo na utiifu kamili, kisha hawakudumu juu yake, wala hawakukaa imara juu yake. Bali muda uliwawia mrefu, wakaendelea kughafilika, na imani yao ikafifia, na yakini yao ikaisha. "Kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao ni wapotovu." Hayo ni kwa sababu, nyoyo zinahitaji kila wakati kukumbushwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kufanywa kutamka hekima yake, na wala mtu hafai kughafilika mbali na hayo. Kwani hiyo ni sababu ya ugumu wa moyo na ukavu wa jicho.
#
{17} {اعلموا أنَّ الله يُحيي الأرض بعد موتِها قد بَيَّنَّا لكم الآياتِ لعلَّكم تَعْقِلونَ}: فإن الآيات تدلُّ العقول على المطالب الإلهيَّة، والذي أحيا الأرض بعد موتها قادرٌ على أن يُحْيِيَ الأموات بعد موتهم فيجازِيَهم بأعمالهم، والذي أحيا الأرض بعد موتها بماء المَطرِ، قادرٌ على أن يُحْيِيَ القلوب الميتة بما أنزله من الحقِّ على رسوله. وهذه الآية تدلُّ على أنه لا عقل لمن لَم يهتدِ بآيات الله ولم ينقدْ لشرائع الله.
{17} "Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia." Kwa kuwa ishara zinaonyesha akili kufikia kwenye matakwa ya Mwenyezi Mungu, na ambaye ndiye aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake ana uwezo wa kuwafufua wafu baada ya kufa kwao na kuwalipa kwa matendo yao. Na aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake kwa maji ya mvua, anaweza kuzifufua nyoyo zilizokufa kwa yale aliyoyateremsha ya haki juu ya Mtume wake. Aya hii inaashiria kwamba hana akili yule ambaye haongokii na ishara
(Aya) za Mwenyezi Mungu na hakufuata sheria za Mwenyezi Mungu.
{إِنَّ الْمُصَّدِّقِينَ وَالْمُصَّدِّقَاتِ وَأَقْرَضُوا اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعَفُ لَهُمْ وَلَهُمْ أَجْرٌ كَرِيمٌ (18) وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ أُولَئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ وَالشُّهَدَاءُ عِنْدَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ (19)}.
18. Kwa hakika wanaume wanaotoa sadaka, na wanawake wanaotoa sadaka, na wakamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, watazidishiwa maradufu na watapata malipo ya ukarimu. 19. Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, hao ndio Masidiqi
(wakweli zaidi) na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ndio wana Motoni.
#
{18} {إنَّ المصَّدِّقينَ والمُصَّدِّقاتِ}: بالتشديد؛ أي: الذين أكثروا من الصدقات الشرعيَّة والنفقات المرضيَّة، {وأقرضوا الله قرضاً حسناً}: بأن قدَّموا من أموالهم في طرق الخيرات ما يكون ذخراً لهم عند ربِّهم، {يضاعَفُ لهم}: الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائة ضعف إلى أضعافٍ كثيرةٍ، {ولهم أجرٌ كريمٌ}: وهو ما أعدَّه الله لهم في الجنة ممَّا لا تعلمُه النفوس.
{18} "Kwa hakika wanaume wanaotoa sadaka, na wanawake wanaotoa sadaka" kwa wingi "na wakamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema" kwa kutoa na kupeana mali zao katika njia za wema ambazo zitakakuwa akiba zao kwa Mola wao Mlezi, "watazidishiwa maradufu" jema moja kwa mara kumi mfano wake, hata mara mia saba, hadi mizidisho mingi, "na watapata malipo ya ukarimu." Nayo ni yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia katika bustani za mbinguni miongoni mwa yale ambayo nafsi haziyajui.
#
{19} {والذين آمنوا باللهِ ورسلِهِ}: والإيمانُ عند أهل السُّنَّة ما دلَّ عليه الكتاب والسنة، هو قول القلب واللسان وعمل القلب واللسان والجوارح، فيشمل ذلك جميع شرائع الدين الظاهرة والباطنة، فالذين جمعوا [بين] هذه الأمور {هم الصدِّيقون}؛ أي: الذين مرتبتهم فوق مرتبة عموم المؤمنين ودون مرتبة الأنبياء. وقوله: {والشهداءُ عند ربِّهم لهم أجرُهم ونورُهم}؛ كما ورد في الحديث الصحيح: «إنَّ في الجنَّة مائةَ درجةٍ، ما بين كلِّ درجتين كما بين السماء والأرض، أعدَّها الله للمجاهدين في سبيله». وهذا يقتضي شدَّة علوِّهم ورفعتهم وقربهم من الله تعالى، {والذين كفروا وكَذَّبوا بآياتِنا أولئك أصحابُ الجحيم}: فهذه الآيات جمعت أصناف الخلق المتصدِّقين والصِّديقين والشهداء وأصحاب الجحيم، فالمتصدِّقون الذين [كان] جُلُّ عملهم الإحسان إلى الخلق وبذلُ النفع لهم بغاية ما يمكنهم، خصوصاً بالنفع بالمال في سبيل الله، والصِّدِّيقون هم الذين كمَّلوا مراتب الإيمان والعمل الصالح والعلم النافع واليقين الصادق، والشهداء هم الذين قاتلوا في سبيل الله لإعلاء كلمة الله، وبَذَلوا أنفسَهم وأموالهم فَقُتِلوا، وأصحاب الجحيم هم الكفار الذين كذَّبوا بآيات الله. وبقي قسمٌ ذكرهم الله في سورة فاطر، وهم المقتصدون الذين أدَّوا الواجبات وتركوا المحرمات؛ إلاَّ أنَّهم حصل منهم بعض التقصير بحقوق الله وحقوق عباده؛ فهؤلاء مآلهم الجنة ، وإن حصل لبعضهم عقوبة ببعض ما فعل.
{19} "Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake" Imani kwa Masunni ni yale yaliyoashiriwa na Kitabu na Sunna, nayo ni maneno ya moyo na ulimi, na matendo ya moyo, ulimi na viungo. Na hayo yanajumuisha sheria zote za Dini zilizo dhahiri na zilizofichikana, kwa hivyo waliounganisha
[baina ya] mambo haya "hao ndio Masidiqi
(wakweli zaidi)" ambao daraja yao iko juu ya daraja za Waumini wote wa kawaida, lakini chini ya daraja za Manabii.
Na kauli yake: "Na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao.
" Kama ilivyokuja katika Hadithi sahihi: “Hakika kuna ngazi mia moja katika bustani za mbinguni, na umbali ulioko kati ya kila daraja mbili ni kama umbali uliopo kati ya mbingu na ardhi. Mwenyezi Mungu amewaandalia wanaofanya jihadi katika njia yake." Haya yanalazimu kwamba wako juu zaidi, na wametukuka zaidi na kwamba wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. "Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ndio wana Motoni." Aya hizi zimejumuisha aina za viumbe wanaotoa sadaka, wakweli zaidi, wale waliokufa katika njia ya Mwenyezi Mungu
(mashahidi), na watu wa Motoni. Wale watoao sadaka, ni wale ambao walikuwa wakitoa na kuwapa viumbe na pia wakiwafanyia yenye kuwanufaisha kiasi wawezavyo, hasa kuwanufaisha kwa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nao wakweli ni wale waliokamilisha viwango vya imani, matendo mema, elimu yenye manufaa na yakini ya kweli. Nao mashahidi ni wale waliopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuinua juu neno la Mwenyezi Mungu, wakajitolea nafsi zao na mali zao na wakauawa. Nao watu wa Motoni ni makafiri waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Na limebakia kundi lingine ambalo Mwenyezi Mungu alilitaja katika Surat Fatir, ambao ni wale wa katikati, ambao walitekeleza mambo ya wajibu na wakaacha yale yaliyoharamishwa. Hata hivyo, hawakufanya sawasawa baadhi ya haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Hao pia marejeo yao yatakuwa katika bustani za mbinguni, hata kama baadhi yao wataadhibiwa kwa yale waliyoyafanya.
{اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانٌ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ (20) سَابِقُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ذَلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ (21)}.
20. Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifahirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu. 21. Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Bustani ya mbinguni ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu.
#
{20} يخبر تعالى عن حقيقة الدُّنيا وما هي عليه، ويبيِّن غايتها وغاية أهلها؛ بأنَّها {لعبٌ ولهوٌ}: تلعب بها الأبدان وتلهو بها القلوب، وهذا مصداقُه ما هو موجودٌ وواقعٌ من أبناء الدُّنيا؛ فإنَّك تجِدُهم قد قطعوا أوقاتَ عُمُرِهِم بلهوِ قلوبهم وغفلتهم عن ذكر الله وعمَّا أمامهم من الوعد والوعيد، وتراهم قد اتَّخذوا دينَهم لعباً ولهواً؛ بخلاف أهل اليقظة وعُمَّال الآخرة؛ فإنَّ قلوبَهم معمورةٌ بذكر الله ومعرفته ومحبَّته، وقد شغلوا أوقاتهم بالأعمال التي تقرِّبهم إلى الله من النفع القاصر والمتعدِّي. وقوله: {وزينةٌ}؛ أي: تزين في اللباس والطعام والشراب والمراكب والدُّور والقصور والجاه وغير ذلك، {وتفاخرٌ بينكم}؛ أي: كلُّ واحدٍ من أهلها يريد مفاخرةَ الآخر، وأن يكونَ هو الغالبَ في أمورها، والذي له الشهرةُ في أحوالها، {وتكاثرٌ في الأموال والأولادِ}؛ أي: كلٌّ يريدُ أن يكون هو الكاثر لغيره في المال والولد، وهذا مصداقُهُ وقوعُهُ من محبِّي الدُّنيا والمطمئنين إليها؛ بخلاف مَنْ عَرَفَ الدُّنيا وحقيقتها، فجعلها معبراً، ولم يجعلها مستقرًّا، فنافس فيما يقرِّبُه إلى الله، واتَّخذ الوسائل التي توصلُه إلى دار كرامته ، وإذا رأى من يكاثُره وينافسه في الأموال والأولاد؛ نافَسَه بالأعمال الصالحة.
ثم ضرب للدُّنيا مثلاً بغيثٍ نزل على الأرض، فاختلط به نباتُ الأرض مما يأكُلُ الناسُ والأنعام، حتى إذا أخذتِ الأرضُ زُخْرُفَها، وأعجب نباتُه الكفارَ الذين قَصَروا نَظَرَهم وهِمَمَهم على الدُّنيا ؛ جاءها من أمرِ الله ما أتلفها، فهاجتْ ويبستْ وعادتْ إلى حالها الأولى ؛ كأنَّه لم ينبتْ فيها خضراءُ ولا رُإِيَ لها مَرْأَى أنيق، كذلك الدُّنيا؛ بينما هي زاهيةٌ لصاحبها زاهرةٌ؛ مهما أراد من مطالبها حصل، ومهما توجَّه لأمر من أمورها؛ وجد أبوابه مفتَّحة؛ إذ أصابها القَدَرُ، فأذهبها من يده، وأزال تسلُّطه عليها، أو ذهب به عنها، فرحل منها صفر اليدين؛ لم يتزَّود منها سوى الكفن، فتبًّا لمن أضحتْ هي غايةَ أمنيَّته ولها عمله وسعيه.
وأما العمل للآخرة؛ فهو الذي ينفع ويُدَّخر لصاحبه ويصحب العبدَ على الأبد، ولهذا قال تعالى: {وفي الآخرة عذابٌ شديدٌ ومغفرةٌ من الله ورضوانٌ}؛ أي: حال الآخرة ما يخلو من هذين الأمرين: إمَّا العذابُ الشديدُ في نار جهنَّم وأغلالها وسلاسلها وأهوالها لمن كانت الدُّنيا هي غايتَهُ ومنتهى مطلبِهِ، فتجرَّأ على معاصي الله، وكذَّب بآيات الله، وكفر بأنعم الله، وإمَّا مغفرةٌ من الله للسيئات، وإزالةُ العقوبات، ورضوانٌ من الله يُحِلُّ من أحَلَّه عليه دارَ الرضوان لمن عرف الدُّنيا وسعى للآخرة سعيها؛ فهذا كلُّه مما يدعو إلى الزهد في الدنيا والرغبة في الآخرة، ولهذا قال: {وما الحياةُ الدُّنيا إلاَّ متاعُ الغُرور}؛ أي: إلاَّ متاعٌ يُتَمَتَّعُ به ويُنْتَفَعُ به ويُسْتَدْفَعُ به الحاجات؛ لا يغترُّ به ويطمئنُّ إليه إلاَّ أهل العقول الضعيفة، الذين يغرُّهم بالله الغرور.
{20} Mwenyezi Mungu anajulisha kuhusu uhalisi wa dunia na jinsi ulivyo, na anaelezea madhumuni yake na madhumuni ya wakazi wake, kwamba ni "mchezo na pumbao." Miili huichezea na nyoyo hujifurahisha kwayo, na hili linathibitishwa na yaliyopo na ni ukweli wa wana dunia. Kwani, utawakuta wanapoteza muda wa maisha yao kwa kufanya pumbao za nyoyo zao na kughafilika mbali na suala la kumkumbuka Mwenyezi Mungu na yale yaliyo mbele yao ya ahadi nzuri na vitisho vya kuadhibiwa. Na utawaona wameifanya dini yao kuwa ni mchezo na pumbao. Tofauti na watu ambao wako macho, na wafanyao matendo sana kwa ajili ya akhera. Mioyo yao imejaa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kumjua vyema na upendo. Wameushughulisha wakati wao kwa matendo yanayowaleta karibu na Mwenyezi Mungu, yenye manufaa yanayowahusu wao tu na manufaa yanayowafikia wengine.
Na kauli yake: "Na pambo;" yaani, kujipamba kwa mavazi, vyakula, vinywaji, vipando, nyumba, makasri na kutafuta heshima na mengineyo. "Na kujifahirisha baina yenu" kila mmoja akitaka kuwa mshindi katika mambo yake, na kwamba awe ndiye mwenye umashuhuri zaidi katika hali zake "na kushindana kwa wingi wa mali na watoto." Na hili linathibitishwa na kutokea kwake katika wale wanaoipenda dunia na kuridhika nayo. Tofauti na yule aliyeijua dunia na uhakika wake, basi akaifanya kuwa ni njia tu ya kupitia, na hakuifanya kuwa ni mahali pa kukaa na kutulia, kwa hivyo akashindana katika yale yatakayomuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na akachukua njia zitakazomfikisha kwenye makazi ya utukufu wake. Na akimuona mwenye kukithirisha mali na watoto na kushindana naye, yeye anashindana naye katika matendo mema. Kisha akaipigia dunia mfano wa mvua iliyoteremka juu ya ardhi, na ikachanganyika nayo mimea ya ardhi wanayokula kwayo watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilika katika pambo lake, na mimea yake ikawafurahisha wakulima, ambao hawakuangalia wala hawakuwa na hima juu ya kitu kingine isipokuwa dunia, amri ya Mwenyezi Mungu ikaijia na kuiharibu. Kwa hivyo ikanyauka na kukauka, na kurudi katika hali yake ya mwanzo. Ni kana kwamba hakuna kijani kibichi kilichowahi kuota juu yake, na wala haikuwahi kuwa na mwonekano mzuri mno. Basi dunia pia iko hivyo. Wakati ilikuwa iking'aa kwa mwenye kuitafuta na ikawa na mwonekana mzuri; chochote alichotaka katika mambo yake yanayotakwa, anakipata. Na chochote alicholenga kufanya katika mambo yake anakuta milango yake imefunguliwa sawasawa. Lakini tazama, ikapatwa na yale aliyoipangia Mwenyezi Mungu, nayo yakaiondoa mikononi mwake, au yakamwondoa yeye akaiacha. Kwa hivyo, akaondoka humo mikono mitupu; hakuchukua humo chochote isipokuwa sanda tu. Basi ole wake mwenye kuifanya kuwa ndiyo lengo kubwa zaidi analilotamani, basi akaifanyia matendo na juhudi kubwa. Na ama kuifanyia akhera matendo, hilo ndilo lenye kunufaisha na kuhifadhiwa mwenye kuyafanya matendo hayo na yatafuatana na mja huyo milele,
na ndiyo maana Mola Mtukufu akasema: "Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi." Yaani,
hali ya Akhera haitoki nje ya mambo mawili: Ima adhabu kali katika moto wa Jahannamu na pingu zake, minyororo yake na vitisho vyake vikubwa kwa yule ambaye dunia ilikuwa ndiyo lengo lake kuu. Kwa hivyo akathubutu kumuasi Mwenyezi Mungu, kukanusha ishara za Mwenyezi Mungu, na kukufuru neema za Mwenyezi Mungu. Au msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa maovu, kuondolewa kwa adhabu mbalimbali, kuridhiwa na Mwenyezi Mungu, na makazi ya kuridhiwa na kuridhia, kwa yule anayemruhusu, ambaye aliijua dunia na akaifanyia Akhera juhudi ipasavyo. Yote hayo ndiyo yanaitia mtu kuipa dunia mgongo na kuitaka sana Akhera,
na ndiyo maana akasema: "Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu." Hadanganyiki nayo isipokuwa watu wenye akili dhaifu tu, ambao yule mdanganyifu anawadanganya wamkatae Mwenyezi Mungu.
#
{21} ثم أمر بالمسابقة إلى مغفرة الله ورضوانه وجنته، وذلك يكون بالسعي بأسباب المغفرةِ من التوبة النَّصوح، والاستغفار النَّافع، والبعد عن الذُّنوب ومظانِّها، والمسابقة إلى رضوان الله بالعمل الصالح، والحرص على ما يُرضي الله على الدَّوام من الإحسان في عبادة الخالق، والإحسان إلى الخلق بجميع وجوه النفع، ولهذا ذكر الله الأعمالَ الموجبةَ لذلك، فقال: {وجنَّةٍ عرضُها السمواتُ والأرضُ أعِدَّتْ للذين آمنوا باللهِ ورسلِهِ}، والإيمانُ بالله ورُسُلِهِ يدخلُ فيه أصولُ الدِّين وفروعها. {ذلك فضلُ الله يؤتيهِ مَن يشاءُ}؛ أي: هذا الذي بيَّنَّاه لكم وذَكَرْنا [لكم فيه] الطُّرُقَ الموصلة إلى الجنة والطُّرُقَ الموصلة إلى النار، وأنَّ ثواب الله بالأجر الجزيل والثواب الجميل من أعظم منَّته على عباده وفضله، {والله ذو الفضل العظيم}: الذي لا يُحصى ثناءٌ عليه، بل هو كما أثنى على نفسه، وفوق ما يُثني عليه أحدٌ من خلقه.
{21} Kisha akatuamrisha tushindanie msamaha wa Mwenyezi Mungu, radhi yake, na bustani zake za mbinguni, na hiyo yanakuwa kwa kujitahidi kutafuta visababu vya msamaha, kama vile toba ya kweli, kuomba msamaha kwenye manufaa, kujiweka mbali na madhambi na sehemu zake, kushindana kufikia radhi za Mwenyezi Mungu kwa kufanya matendo mema, na kufanyia bidii daima yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu kama vile kumuabudu Muumba kwa uzuri, na kuwafanyia ihsani viumbe katika nyanja mbalimbali za manufaa, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja matendo yanayosababisha hayo,
akisema: "Na Bustani ya mbinguni ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake." Kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake kunajumuisha misingi ya dini na matawi yake. "Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye." Yaani, haya tuliyokubainishieni na tukataja njia zinazofikisha katika bustani ya mbinguni na njia zinazofikisha katika Moto, na kwamba malipo ya Mwenyezi Mungu ambayo ni mengi na mazuri ni miongoni mwa neema zake kubwa kwa waja wake na fadhila zake. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu." Ambaye sifa zake hazihesabiki zikadhibitiwa. Bali Yeye ni kama alivyojisifu mwenyewe, na yuko juu zaidi ya namna ambayo yeyote anamsifu miongoni mwa viumbe vyake.
{مَا أَصَابَ مِنْ مُصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنْفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِنْ قَبْلِ أَنْ نَبْرَأَهَا إِنَّ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ (22) لِكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَى مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ (23) الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَمَنْ يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ (24)}.
22. Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 23. Ili msihuzunike kwa kilichokupoteeni, wala msijitape kwa alichokupeni. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna akajifahirisha. 24. Ambao wanafanya ubahili, na wanaamrisha watu wafanye ubahili. Na anayegeuka, basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa mno.
#
{22} يقول تعالى مخبراً عن عموم قضائِهِ وقدرِهِ: {ما أصابَ من مصيبةٍ في الأرض ولا في أنفسِكُم}: وهذا شاملٌ لعموم المصائب التي تُصيبُ الخلق من خيرٍ وشرٍّ؛ فكلُّها قد كُتِبَتْ في اللوح المحفوظ صغيرها وكبيرها، وهذا أمرٌ عظيمٌ لا تحيطُ به العقول، بل تَذْهلُ عنده أفئدةُ أولي الألباب، ولكنَّه على الله يسيرٌ.
{22} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema,
akijulisha kuhusu ujumla wa mipango yake na kupitisha kwake mambo: "Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu." Hili linajumuisha jumla ya misiba inayowasibu viumbe, ikiwa ni nzuri au mbaya. Yote imeandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, kiwe kidogo au kikubwa, na hili ni jambo kubwa lisiloweza kufahamika kikamilifu katika akili za viumbe. Bali nyoyo za wenye akili hustaajabishwa mno nalo, lakini ni rahisi zaidi kwa Mwenyezi Mungu.
#
{23} وأخبر الله عبادَه بذلك لأجل أن تتقرَّرَ هذه القاعدة عندهم، ويبنوا عليها ما أصابهم من الخير والشرِّ؛ فلا يأسَوْا، ويحزنوا على ما فاتهم، مما طَمِحَتْ له أنفسُهم وتشوَّفوا إليه؛ لعلمِهِم أنَّ ذلك مكتوبٌ في اللوح المحفوظ، لا بدَّ من نفوذه ووقوعه؛ فلا سبيل إلى دفعِهِ، ولا يفرحوا بما آتاهم الله فرحَ بَطَرٍ وأشَرٍ؛ لعلمهم أنَّهم ما أدركوه بحولهم وقوَّتهم، وإنَّما أدركوه بفضل الله ومنِّه، فيشتغلوا بشكر مَنْ أولى النِّعم ودفع النِّقم، ولهذا قال: {واللهُ لا يحبُّ كلَّ مختالٍ فخورٍ}؛ أي: متكبِّر فظٍّ غليظٍ معجبٍ بنفسه فخورٍ بنعم الله ينسبها إلى نفسه وتُطغيه وتُلهيه؛ كما قال تعالى: {وإذا أذَقْناه رحمةً منَّا قال إنَّما أوتيتُهُ على علم بَلْ هي فتنةٌ}.
{23} Mwenyezi Mungu aliwajulisha waja wake jambo hili ili kanuni hii ikae imara ndani yao, na wajenge juu yake mema na mabaya yaliyowapata. Basi wasihuzunike kwa yale waliyoyakosa, katika yale ambayo nafsi zao ziliyatamani sana na kuwa na shauku nayo. Kwa sababu wanajua kwamba hilo liliandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, lazima litekelezeke na litokee, na wala hakuna njia ya kulizuia. Na wala wasifurahi kwa aliyowapa Mwenyezi Mungu, kwa furaha ya kiburi na uovu. Kwa sababu wanajua kwamba hawakuipata kwa uwezo wao wala nguvu zao. Bali waliyapata kwa fadhila na neema ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanajishughulisha na kumshukuru yule aliyewapa neema hizo na akawazuilia adhabu,
na ndiyo maana akasema: "Na Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna akajifahirisha" juu ya neema za Mwenyezi Mungu, akawa anajinasibishia neema hizo mwenyewe, na zikampotoa na kumsahaulisha.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na dhara inapomgusa mtu, hutuomba. Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu,
husema: 'Nimepewa haya kwa sababu ya elimu yangu.' Siyo hivyo! Huo ni mtihani!"
#
{24} {الذين يَبْخَلونَ ويأمُرونَ الناس بالبُخْلِ}؛ أي: يجمعون بين الأمرين الذَّميمين اللذين كلٌّ منهما كافٍ في الشرِّ: البخل، وهو منع الحقوق الواجبة، ويأمرون الناس بذلك، فلم يكفِهِم بُخْلُهم، حتى أمروا الناس بذلك، وحثُّوهم [على] هذا الخلق الذميم بقولهم وفعلهم، وهذا من إعراضهم عن طاعة ربِّهم وتولِّيهم عنها، {ومن يَتَوَلَّ}: عن طاعة اللهِ؛ فلا يضرُّ إلاَّ نفسه، ولن يضرَّ الله شيئاً، {فإنَّ الله هو الغنيُّ الحميدُ}: الذي غناه من لوازم ذاته، الذي له مُلْكُ السماواتِ والأرض، وهو الذي أغنى عبادَه وأقْناهم، الحميدُ الذي له كلُّ اسم حسنٍ ووصفٍ كامل وفعل جميل يستحقُّ أن يُحْمَدَ عليه ويُثْنى ويُعَظَّم.
{24} "Ambao wanafanya ubahili, na wanaamrisha watu wafanye ubahili." Yaani, wanaunganisha vitu viwili vya kukashifiwa,
kila kimoja kinatosha kuwa uovu mkubwa: ubakhili ambao ni kutotekeleza haki za faradhi, na tena wanawaamrisha watu kufanya hivyo. Kwa hivyo, ubakhili wao haukuwatosha wao mpaka wakawaamrisha watu pia kufanya hivyo, na kuwahimiza kufanya tabia hii ya kukadshifiwa, kwa maneno yao na vitendo vyao. Na hili ni katika kupeana kwao mgongo mambo ya kumtii Mola wao Mlezi na kugeuka kwao mbali nayo. "Na anayegeuka" akaacha kumtii Mwenyezi Mungu, basi hadhuru yeyote isipokuwa yeye mwenyewe, na wala hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. "Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa mno." Yule ambaye kujitosheleza kwake ni katika sifa zisizoachana na dhati yake, ambaye miliki ya mbingu na ardhi ni yake, na ndiye aliyewatajirisha waja wake na kuwatosheleza. Naye ni msifiwa mno, Mwenye kila jina zuri, sifa kamili, tendo zuri analostahili kusifiwa juu yake na kutukuzwa.
{لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنْزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ وَأَنْزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ (25) وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا وَإِبْرَاهِيمَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ فَمِنْهُمْ مُهْتَدٍ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ (26) ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَى آثَارِهِمْ بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنْجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا فَآتَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ (27)}.
25. Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu na ishara waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda. 26. Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu. Basi wapo miongoni mwao walioongoka, na wengi katika wao ni wavukao mipaka. 27. Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Na tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehema. Na umonaki
(utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyotakiwa kuufuata. Basi wale walioamini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wavukao mipaka.
#
{25} يقول تعالى: {لقد أرْسَلْنا رُسُلَنا بالبيِّناتِ}: وهي الأدلَّة والشواهد والعلامات الدَّالَّة على صدق ما جاؤوا به وحقِّيَّتِهِ، {وأنزلنا معهم الكتابَ}: وهو اسم جنس يَشْمَلُ سائر الكتب التي أنزلها الله لهداية الخلق وإرشادهم ما ينفعهم في دينهم ودنياهم، {والميزانَ}: وهو العدلُ في الأقوال والأفعال، والدين الذي جاءت به الرُّسل كلُّه عدلٌ وقسطٌ في الأوامر والنَّواهي وفي معاملات الخَلْق وفي الجنايات والقِصاص والحدود والمواريث وغير ذلك، وذلك {ليقومَ الناسُ بالقسطِ}: قياماً بدين الله، وتحصيلاً لمصالحهم التي لا يمكنُ حصرُها وعدُّها، وهذا دليلٌ على أنَّ الرسل متَّفقون في قاعدة الشرع، وهو القيامُ بالقسط، وإنِ اختلفتْ صورُ العدل بحسب الأزمنة والأحوال، {وأنزَلْنا الحديدَ فيه بأسٌ شديدٌ}: من آلات الحرب؛ كالسلاح والدُّروع وغير ذلك، {ومنافعُ للناس}: وهو ما يشاهَدُ من نفعه في أنواع الصِّناعات والحرف والأواني وآلات الحَرْثِ، حتى إنَّه قَلَّ أن يوجَدَ شيءٌ إلاَّ وهو يحتاجُ إلى الحديد، {ولِيَعْلَمَ اللهُ مَن يَنصُرُه ورُسُلَه بالغيب}؛ أي: ليقيم تعالى سوقَ الامتحان بما أنزله من الكتاب والحديد، فيتبيَّن من ينصُرُه وينصُرُ رسله في حالة الغيب، التي ينفع فيها الإيمان قبل الشهادة، التي لا فائدة بوجود الإيمان فيها؛ لأنَّه حينئذٍ يكون ضروريًّا. {إنَّ الله لَقَوِيٌّ عزيزٌ}؛ أي: لا يعجِزُه شيءٌ ولا يفوته هاربٌ، ومن قوَّته وعزَّته أن أنزل الحديدَ الذي منه الآلاتُ القويَّة، ومن قوَّته وعزَّته أنه قادرٌ على الانتصار من أعدائه، ولكنَّه يبتلي أولياءه بأعدائه؛ ليعلم من ينصرُهُ بالغيب.
وقَرَنَ تعالى بهذا الموضع بين الكتاب والحديد؛ لأنَّ بهذين الأمرين ينصر الله دينه ويُعلي كلمته: بالكتاب الذي فيه الحجَّة والبرهان، والسيف الناصر بإذن الله، وكلاهما قيامُهُ بالعدل والقِسْط، الذي يستدلُّ به على حكمةِ الباري وكماله وكمال شريعتِهِ التي شرعها على ألسنة رسله.
{25} Anasema Mwenyezi Mungu: "Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu na ishara waziwazi," ambazo ni ushahidi, hoja na ishara zinazoashiria ukweli wa yale waliyokuja nayo na kwamba ni ya haki. "Na tukateremsha Kitabu pamoja nao." Hili linajumuisha vitabu vyote alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwaongoza viumbe na kuwaelekeza katika yale yatakayowafaa katika dini yao na dunia yao. "Na mizani" ambayo ni uadilifu katika kauli na vitendo. Na Dini waliyoileta Mitume yote ni uadilifu na usawa katika maamrisho na makatazo, na katika kuamiliana na viumbe, na katika hukumu za jinai, kulipiza kisasi, adhabu maalumu, mirathi na mambo mengineyo, na hayo ni "ili watu wasimamie uadilifu" ili kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu, na kufikia masilahi yao, ambayo hayawezi kuyadhibiti wala kuyahesabu. Hili linaashiria kwamba Mitume walikubaliana katika kanuni za asasi za kisheria, ambazo ni kufanya uadilifu, hata kama aina za uadilifu huo zitatofautiana kulingana na nyakati na hali mbalimbali "na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi." Iwe ala ya vita, kama vile silaha, deraya na vitu vinginevyo. "Na manufaa kwa watu" ambayo ni kile kinachoonekana kutokana na manufaa yake katika aina mbalimbali za viwanda, ufundi, vyombo, na mashine za kulima, kiasi kwamba ni mara chache hakuna kitu ambacho hakihitaji chuma. "Na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu." Yaani, ili Mwenyezi Mungu Mtukufu aweke mtihani kwa yale aliyoyateremsha katika Kitabu na chuma, ili ibainike ni nani atamnusuru yeye na Mitume wake katika hali ya ghaibu, ambayo imani ina manufaa ndani yake hata kabla ya kuona kwa macho, ambayo yakishapatikana, hapo imani haisaidii kitu. Kwani wakati huo kuamini kunakuwa ni kitu cha lazima. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda." Yaani, hakuna kinachoweza kumshinda, wala mwenye kukimbia hawezi kumponyoka. Na kutokana na nguvu zake na utukufu wake ni kwamba aliteremsha chuma ambacho hutengeneza kutoka humo vyombo vyenye nguvu. Na kutokana na nguvu zake na utukufu wake ni kwamba ana uwezo wa kuwashinda adui zake. Lakini huwajaribu vipenzi wake kwa maadui wake; ili ajue ni nani atamsaidia kwa ghaibu. Hapa, Mwenyezi Mungu ameiunganisha kati ya Kitabu na chuma. Kwa sababu kwa mambo haya mawili, Mwenyezi Mungu huinusuru Dini yake na kuliinua juu na kulitukuza neno lake kwa Kitabu kuna hoja na ushahidi, na kwa upanga kuna ushindi, Mwenyeezi Mungu akipenda. Na vyote viwili ni vinasimamisha uadilifu na usawa, ambavyo vinatumika kama ushahidi wa hekima ya Muumba na ukamilifu wake na ukamilifu wa sheria yake aliyoiweka juu ya ndimi za Mitume wake.
#
{26} ولما ذكر نبوَّة الأنبياء عموماً؛ ذكر من خواصِّهم النَّبِيَّيْنِ الكريميْنِ نوحاً وإبراهيم، اللَّذين جعل الله النبوَّة والكتاب في ذُرِّيَّتهما، فقال: {ولقد أرسَلْنا نوحاً وإبراهيم وجَعَلْنا في ذُرِّيَّتِهِما النبوَّةَ والكتابَ}؛ أي: الأنبياء المتقدِّمين والمتأخِّرين، كلُّهم من ذُرِّيَّة نوح وإبراهيم عليهما السلام، وكذلك الكتب كلُّها نزلت على ذُرِّيَّة هذين النبيَّيْنِ الكريميْنِ. {فمنهم}؛ أي: ممَّن أرسلنا إليهم الرسل {مهتدٍ}: بدعوتهم، منقادٌ لأمرهم، مسترشدٌ بهداهم، {وكثيرٌ منهم فاسقون}؛ أي: خارجون عن طاعة الله وطاعة رسله ؛ كما قال تعالى: {وما أكثر الناس ولو حرصْتَ بمؤمنينَ}.
{26} Na alipotaja unabii wa manabii kwa ujumla wake, akawataja Manabii wawili maalumu watukufu, Nuhu na Ibrahim, ambao Mwenyezi Mungu aliwaweka Unabii na Kitabu katika dhuria zao. "Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu." Yaani, Manabii wa mwanzo na wa baadaye, wote walikuwa kutoka katika kizazi cha Nuhu na Ibrahim, amani iwe juu yao, na vivyo hivyo vitabu vyote vilivyoteremshwa, vyote vilikuwa kutoka katika kizazi cha manabii hawa wawili watukufu. "Basi wapo miongoni mwao." Yaani, miongoni mwa wale tuliowatumia Mitume "walioongoka" kwa wito wao, wakafuata maamrisho yao, na kuongoka kwa uwongofu wao. "Na wengi katika wao ni wavukao mipaka" ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi."
#
{27} {ثم قَفَّيْنا}؛ أي: أتبعنا {على آثارِهم برُسُلِنا وقفَّيْنا بعيسى ابن مريم}: خصَّ الله عيسى عليه السلام؛ لأنَّ السياق مع النصارى، الذين يزعُمون اتِّباع عيسى، {وآتَيْناه الإنجيل}: الذي هو من كتب الله الفاضلة، {وجَعَلْنا في قلوب الذين اتَّبعوه رأفةً ورحمةً}؛ كما قال تعالى: {لَتَجِدَنَّ أشدَّ الناس عداوةً للذين آمنوا اليهودَ والذين أشركوا ولَتَجِدَنَّ أقرَبَهم مودَّةً للذين آمنوا الذين قالوا إنا نصارى ذلك بأنَّ منهم قِسِّيسينَ ورُهْباناً وأنَّهم لا يستكبرونَ ... } الآيات، ولهذا كان النصارى ألين من غيرهم قلوباً حين كانوا على شريعة عيسى عليه السلام، {ورهبانيةً ابْتَدَعوها}: والرهبانيَّة العبادةُ؛ فهم ابتدعوا من عند أنفسهم عبادةً، ووظَّفوها على أنفسهم، والتزموا لوازم ما كتبها الله عليهم ولا فرضها، بل هم الذين التزموا بها من تلقاء أنفسهم؛ قصْدُهم بذلك رضا الله، ومع ذلك؛ {فما رَعَوْها حقَّ رعايتها}؛ أي: ما قاموا بها، ولا أدَّوْا حقوقها، فقصَّروا من وجهين: من جهة ابتداعهم، ومن جهة عدم قيامهم بما فَرَضوه على أنفسهم. فهذه الحالُ هي الغالبُ من أحوالهم، ومنهم من هو مستقيمٌ على أمر الله، ولهذا قال: {فآتَيْنا الذين آمنوا منهم أجْرَهُم}؛ أي: الذين آمنوا بمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم - مع إيمانهم بعيسى؛ كلٌّ أعطاه الله على حسب إيمانِهِ، {وكثيرٌ منهم فاسقونَ}.
{27} "Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu." Mwenyezi Mungu alimtaka hapa kwa jina Isa, amani imshukie, kwa sababu muktadha huu unawahusu Wakristo wanaodai kuwa wanamfuata Yesu
(Isa). "Na tukampa Injili" ambayo ni miongoni mwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyo bora. "Na tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehema.
" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa wale walioamini ni Mayahudi na washirikina.
Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanaosema: 'Sisi ni Manasara.' Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi..." hadi mwisho wa Aya hizi. Basi ndiyo maana Wakristo walikuwa na mioyo laini kuliko wengineo walipofuata sheria ya Isa, amani iwe juu yake. "Na umonaki
(utawa wa mapadri) wameuzua wao" wenyewe tu, na wakajitwikisha ibada hiyo, na wakashikamana na matakwa ambayo Mwenyezi Mungu hakuwaandikia wala kuwawekea wala hakuwalazimisha. Nia yao katika hilo ilikuwa kumridhisha Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, "Hawakuufuata inavyotakiwa kuufuata.
" Hawakuufanya vyema katika njia mbili: ya kwanza ni kwamba waliuzua wenyewe, na ya pili ni kwamba hawakutekeleza yale waliyojiwekea wenyewe. Hali hili ndiyo nyingi zaidi katika hali zao, lakini miongoni mwao wapo wale walio waongofu katika amri ya Mwenyezi Mungu,
ndiyo maana akasema: "Basi wale walioamini katika wao tuliwapa ujira wao." Yaani, wale waliomwamini Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – pamoja na kumwamini Isa. Kila mmoja, alipewa na Mwenyezi Mungu kulingana na imani yake. "Na wengi wao ni wavukao mipaka."
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِنْ رَحْمَتِهِ وَيَجْعَلْ لَكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (28) لِئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَى شَيْءٍ مِنْ فَضْلِ اللَّهِ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ (29)}.
28. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na muaminini Mtume wake, atakupeni sehemu mbili katika rehema yake, na atakufanyieni nuru ya kwenda nayo, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu. 29. Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Na kwamba fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu.
#
{28} وهذا الخطابُ يُحتمل أنه خطابٌ لأهل الكتاب، الذين آمنوا بموسى وعيسى عليهما السلام؛ يأمرهم أن يعملوا بمقتضى إيمانهم؛ بأن يتَّقوا الله فيتركوا معاصِيَه ويؤمنوا برسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، وأنَّهم إن فعلوا ذلك؛ أعطاهم الله {كِفْلَيْنِ من رحمتِهِ}؛ أي: نصيبين من الأجر؛ نصيبٍ على إيمانهم بالأنبياء الأقدمين، ونصيبٍ على إيمانهم بمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم -. ويُحتمل أن يكون الأمرُ عامًّا؛ يدخل فيه أهلُ الكتابِ وغيرُهم، وهذا الظاهر، وأنَّ الله أمرَهَم بالإيمان والتَّقوى، الذي يدخُلُ فيه جميع الدين ظاهره وباطنه أصوله وفروعه، وأنَّهم إن امتثلوا هذا الأمر العظيم؛ أعطاهم [اللَّه] {كِفْلَيْنِ من رحمتِهِ}؛ لا يعلم قدرهما ولا وصفَهما إلاَّ الله تعالى: أجرٌ على الإيمان وأجرٌ على التقوى، أو أجرٌ على امتثال الأوامر وأجرٌ على اجتناب النَّواهي، أو أنَّ التَّثنية المراد بها تكرار الإيتاء مرةً بعد أخرى. {ويَجْعَل لكم نوراً تمشون به}؛ أي: يعطيكم علماً وهدىً ونوراً تمشون به في ظُلُمات الجهل، ويغفر لكم السيئات، {والله ذو الفضل العظيم}: فلا يُسْتَغْرَبُ كثرةُ هذا الثواب على فضل ذي الفضل العظيم، الذي عمَّ فضلُه أهلَ السماواتِ والأرض؛ فلا يخلو مخلوقٌ من فضله طرفةَ عينٍ ولا أقلَّ من ذلك.
{28} Maneno haya inawezekana kuwa wanaambiwa Watu wa Kitabu waliomuamini Musa na Isa, amani iwe juu yao. Anawaamuru kutenda kulingana matakwa ya imani yao. Kwamba wamche Mwenyezi Mungu na waache kumuasi na wamuamini Mtume Wake Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – na kwamba wakifanya hivyo, Mwenyezi Mungu atawapa
“sehemu mbili katika rehema yake.” Yaani, mafungu mawili ya malipo. Fungu moja kwa sababu ya kumuamini kwao kwa Manabii wa zamani, na fungu lingine kwa sababu ya kumuamini kwao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na pia inawezekana kwamba hii ni amri ya jumla, ambayo wanaingia ndani yake Watu wa Kitabu na wengineo, na hili ndiyo maana iliyo dhahiri
(sahihi), na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kuwa na imani na ucha Mungu, jambo ambalo linajumuisha dini yote, ya dhahiri yake na ya ndani yake, misingi yake na matawi yake, na kwamba ikiwa watatekeleza amri hii kubwa,
[Mwenyezi Mungu] atawapa "sehemu mbili katika rehema yake" ambazo hakuna anayejua kiasi chake wala maelezo yake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Malipo hayo ni kwa sababu ya imani yao na malipo mengine kwa sababu ya uchamungu wao. Au malipo kwa sababu ya kutii amri na malipo mengine kwa sababu ya kuepuka makatazo. Au uwili uliotajwa hapa unakusudiwa kwamba watapewa kwa kurudia mara baada ya nyingine. "Na atakufanyieni nuru ya kwenda nayo." Yaani, atakupeni elimu, uwongofu na nuru mtakayotembea kwayo katika viza vya ujinga, na atakusameheni mabaya yenu. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa." Si ajabu kuwa malipo haya ni mengi kama yanatolewa katika fadhila za Mwenye fadhila kubwa, ambaye fadhila zake zimeenea wakazi wa mbinguni na ardhini. Hakuna hata kiumbe mmoja asiye na fadhila zake hata kwa kiasi cha kupepesa jicho, wala kidogo zaidi ya hivyo.
#
{29} وقوله: {لئلاَّ يعلم أهلُ الكتاب ألاَّ يقدِرونَ على شيءٍ من فضل الله}؛ أي: بيَّنا لكم فضلنا وإحساننا لمن آمن إيماناً عامًّا واتَّقى الله وآمن برسوله؛ لأجل أن يكونَ عند أهل الكتاب علمٌ بأنَّهم لا يقدرونَ على شيءٍ من فضل الله؛ أي: لا يحجُرون على الله بحسب أهوائهم وعقولهم الفاسدة، فيقولون: {لن يدخُلَ الجنَّةَ إلاَّ مَن كان هوداً أو نَصارى}، ويَتَمَنَّوْنَ على الله الأمانيَّ الفاسدةَ، فأخبر الله تعالى [أن] المؤمنين برسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، المتَّقين لله أنَّ لهم كِفْلَيْنِ من رحمته ونوراً ومغفرةً؛ رغماً على أنوف أهل الكتاب، وليعلموا {أنَّ الفضلَ بيد الله يؤتيه من يشاءُ}: ممَّنِ اقتضت حكمتُه تعالى أن يؤتِيَه من فضله، {والله ذو الفضل العظيم}: الذي لا يقادَرُ قدرُه.
{29} Na kauli yake: "Ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote juu ya fadhila za Mwenyezi Mungu." Yaani, tulikuelezeni neema zetu na wema wetu kwa wale walioamini imani ya ujumla, na wakamcha Mwenyezi Mungu, na wakamuamini Mtume wake; ili watu wa Kitabu wajue kwamba wao hawana uwezo wowote ju ya fadhila za Mwenyezi Mungu. Yaani, hawawezi kumzuilia yeyote mbali na Mwenyezi Mungu kwa matamanio yao na akili zao mbovu,
kwa kusema kwamba: "Hataingia Peponi ila aliye Myahudi au Mkristo," na wanamtamani kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu] matamanio mabovu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba wale wanaomuani Mtume wake Muhammad – rehema na amani Mwenyezi Mungu zimshukie – wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, kwamba wana dhamana mafungu mawili kutoka kwa rehema yake, nuru na msamaha. Hata wasipopenda hivyo Watu wa Kitabu,
na kwamba wajue kuwa: "Fadhila zote zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa hizo amtakaye" miongoni mwa wale ambao hekima yake inahitaji kwamba wapewe katika fadhila zake. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kuu" ambayo haiwezekani kukadiria kiasi chake.
Imekamilika tafsiri ya [Surat Al-Hadid], na sifa njema na neema ni za Mwenyezi Mungu].
******