Tafsiri ya Surat Al-Hashr
Tafsiri ya Surat Al-Hashr
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (1) هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِنْ دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ مَا ظَنَنْتُمْ أَنْ يَخْرُجُوا وَظَنُّوا أَنَّهُمْ مَانِعَتُهُمْ حُصُونُهُمْ مِنَ اللَّهِ فَأَتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُمْ بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَاأُولِي الْأَبْصَارِ (2) وَلَوْلَا أَنْ كَتَبَ اللَّهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ (3) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَمَنْ يُشَاقِّ اللَّهَ فَإِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ (4) مَا قَطَعْتُمْ مِنْ لِينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَى أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ (5) وَمَا أَفَاءَ اللَّهُ عَلَى رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَكِنَّ اللَّهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَى مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (6) مَا أَفَاءَ اللَّهُ عَلَى رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَى فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ (7) لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا وَيَنْصُرُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُولَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ (8) وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِنْ قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (9) وَالَّذِينَ جَاءُوا مِنْ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ (10) أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نَافَقُوا يَقُولُونَ لِإِخْوَانِهِمُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِنْ قُوتِلْتُمْ لَنَنْصُرَنَّكُمْ وَاللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ (11) لَئِنْ أُخْرِجُوا لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِنْ قُوتِلُوا لَا يَنْصُرُونَهُمْ وَلَئِنْ نَصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ (12) لَأَنْتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِي صُدُورِهِمْ مِنَ اللَّهِ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا يَفْقَهُونَ (13) لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُحَصَّنَةٍ أَوْ مِنْ وَرَاءِ جُدُرٍ بَأْسُهُمْ بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا يَعْقِلُونَ (14) كَمَثَلِ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (15) كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنْسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِنْكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ (16) فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا وَذَلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ (17)}.
1. Vinamtakasa Mwenyezi Mungu vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 2. Yeye ndiye aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wa kwanza. Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda dhidi ya Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu akawafikia kwa mahali ambako hawakutazamia, na akatia uwoga mkubwa katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basi zingatieni enyi wenye macho! 3. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu asingeliwaandikia kutoka, angeliwaadhibu katika dunia. Na katika Akhera watapata adhabu ya Moto. 4. Hayo ni kwa sababu walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 5. Mtende wowote mlioukata au mliouacha umesimama vile vile juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awahizi wavukao mipaka. 6. Na mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao hamkuikimbilia mbio kwa farasi wala ngamia. Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno juu ya kila kitu. 7. Mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili isiwe ikizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anachokupeni Mtume, kichukueni. Na anachokukatazeni, jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 8. Wapewe mafakiri Wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wakweli. 9. Na wale walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda wale waliohamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyopewa
(Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa. 10.
Na wale waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu mno. 11.
Huwaoni wale wanaofanya unafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa, na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamtii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita, lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo. 12. Pindi wakitolewa, hawatatoka pamoja nao. Na wakipigwa vita, hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia, basi watageuza mno migongo; kisha hawatanusuriwa. 13. Hakika nyinyi ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu kitu. 14. Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vilivyoimarishwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotumia akili. 15. Ni kama mfano wa wale waliokuwa kabla yao hivi karibuni, walionja uovu wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu. 16.
Ni kama mfano wa Shetani anapomwambia mtu: 'Kufuru.' Na akikufuru,
humwambia: 'Hakika mimi niko mbali zaidi nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.' 17. Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao ni kuingia Motoni, wadumu humo daima; na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.
Sura hii inaitwa Surat Banu An-Nadhir, nao walikuwa kundi kubwa la Mayahudi karibu na Madina wakati wa utume wa Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Basi Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipotumwa na akahamia Madina, wakamkufuru miongoni mwa Mayahudi waliokufuru, basi Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - akafanya suluhu na makundi ya Mayahudi waliokuwa jirani zake huko Madina. Ilipofika miezi sita hivi baada ya Vita vya Badr, Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akatoka akawaendea na akawaongelesha wamsaidie kulipa mali ya mauaji ya Kilabiyyin waliouawa na Amr bin Umayya Ad-Damri. Wakasema: ‘Ewe babake Al-Qasim, tutafanya hivyo. Keti papa hapa huku tukukidhie haja yako!’ Basi wakabakia peke yao wao kwa wao, na Shet'ani akawashawishi kupitia usugu wao walioandikiwa, kwa hivyo wakafanya njama ya kumuuwa – rehema na amani ziwe juu yake. Wakasema: ‘Ni nani miongoni mwenu atalichukua jiwe hili la kusagia, akapande nalo juu, kisha amtupie kichwani kwake ili ampasue kwalo?’ Basi mwovu wao zaidi, Amr bin Jahash, akasema: ‘Ni mimi’ Kwa hivyo, Salam bin Mishkam akawaambia: ‘Msifanye hivyo. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, bila shaka atapewa habari za mlichokusudia hicho, na hakika litavunjika agano lililo kati yetu na yeye.’ Mara ukamjia ufunuo kutoka kwa Mola wake Mlezi juu ya yale waliyokuwa wameazimia kufanya. Kwa hivyo, akanyanyuka upesi na kuelekea Madina, na maswahaba wake wakamfuata, wakasema: ‘Umenyanyuka na wala hatukukuona!’ Basi akawajulisha yale ambayo Mayahudi walikusudia kufanya. Kwa hiyvo, Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akawatumia ujumbe kwamba: “Ondokeni Madina na wala msiishi humo pamoja nami, na nimekupeni muda wa siku kumi. Kwa hivyo, yeyote yule nitakayempata baada ya hapo, nitalipiga shingo lake.” Naye munafiki, Abdullah bin Ubayy bin Salul akawatumia ujumbe kwamba: Msiondoke katika makazi yenu. Kwani pamoja nami nina watu elfu mbili watakaoingia pamoja nanyi katika ngome yenu, nao wako tayari kufa kwa ajili yenu, tena kabila la Quraydha na washirika wenu kutoka Ghatafan watakuungeni mkono. Basi kiongozi wao, Huyay bin Akhtab, akaingiwa na matumaini kwa yale aliyomwambia, na akamtuma Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie akisema kwamba: ‘Hakika sisi hatutatoka makazini mwetu. Kwa hivyo fanya chochote unachotaka!” Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – na maswahaba wake wakasema “Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa),” kisha wakainuka akawaendea hali ya kuwa Ali bin Abi Twalib amebeba bendera. Kisha wakazingira ngome yao, na wakawa wanarusha mishale na mawe, na hapo Quraydha wakajitenga mbali nao, naye Ibn Ubayy na washirika wao kutoka kabila la Ghatafan wakawasaliti. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawazingira na kuikata mitende yao na akaichoma moto. Basi wakamtumia ujumbe kwamba: ‘Tutatoka Madina.’ Kwa hivyo, akawakubalia hilo kwa sharti kwamba wauache kwa nafsi zao na watoto wao na wala wachukuwe chochote ambacho ngamia wao wataweza kubeba isipokuwa silaha. Kwa hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – akateka mali zao na silaha zao. Na mali walizoacha nyuma Banu An-Nadhir zilikuwa za Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – hasa, kwa ajili ya misiba yake na masilahi ya Waislamu, na wala hakuigawanya sehemu tano kama kawaida. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa bure bila ya Waislamu kuiteka kwa kupanda farasi wala wapanda ngamia, na akawahamisha hadi Khaybar wakiwa pamoja na kiongozi wao Huyay bin Akhtab. Na akateka ardhi na majumba yao, na akateka silaha pia. Basi akapata katika silaha ngao hamsini, helmeti hamsini, na panga mia tatu na arobaini. Hii ndiyo jumla ya kisa chao kama kilivyoelezwa na wanahistoria wa Kiislamu.
#
{1} فافتتح تعالى هذه السورة بالإخبار أنَّ جميع مَن في السماوات والأرض تسبِّح بحمد ربِّها وتنزِّهه عمَّا لا يليق بجلاله وتعبُدُه وتخضعُ لعظمتِهِ ؛ لأنه العزيز الذي قد قهر كلَّ شيء؛ فلا يمتنعُ عليه شيءٌ، ولا يستعصي عليه عسيرٌ ، الحكيم في خلقِه وأمرِه؛ فلا يخلُقُ شيئاً عبثاً، ولا يُشْرِّعُ ما لا مصلحة فيه، ولا يفعل إلا ما هو مقتضى حكمته.
{1} Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifungua Sura hii kwa kutuambia kwamba kila kilicho mbinguni na ardhini kinamtakasa Mola wake Mlezi na kumsifu, na kumuweka mbali na yasiyoufailia utukufu wake, vinamwabudu, na vinanyenyekea kwa ukuu wake. Kwa sababu Yeye ndiye Mwenye nguvu ambaye alishinda kila kitu. Hakuna lisilowezekana kwake, na hakuna jambo gumu kwake. Mwenye hekima katika uumbaji wake. Kwa hivyo, haumbi chochote bure, wala hatungi sheria isiyo na masilahi, na wala hafanyi isipokuwa yale yanayotakiwa na hekima yake.
#
{2} ومن ذلك نصرُه لرسوله - صلى الله عليه وسلم - على الذين كفروا من أهل الكتاب من بني النضير حين غَدَروا برسوله فأخرجهم من ديارهم وأوطانهم التي ألِفوها وأحبوها، وكان إخراجهم منها أولَ حشرٍ وجلاءٍ كتبه الله عليهم على يد رسولِه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، فجلوا إلى خيبر. ودلَّت الآية الكريمة أن لهم حشراً وجلاءً غير هذا؛ فقد وقع حين أجلاهم النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - من خيبر، ثم عمرُ رضي الله عنه أخرج بقيتهم منها. {ما ظننتُم}: أيها المسلمون {أن يخرُجوا}: من ديارهم؛ لحصانتها ومنعتها وعزِّهم فيها، {وظنوا أنهم مانعتُهم حصونُهم من اللهِ}: فأعجبوا بها، وغرَّتْهم، وحسبوا أنهم لا يُنالون بها، ولا يقدِرُ عليها أحدٌ، وقدَرُ الله وراء ذلك كلِّه، لا تغني عنه الحصونُ والقلاعُ ولا تجدي فيه القوةُ والدفاع، ولهذا قال: {فأتاهمُ اللهُ من حيثُ لم يحتسِبوا}؛ أي: من الأمر والباب الذي لم يخطر ببالهم أن يُؤتَوا منه، وهو أنَّه تعالى: {قَذَفَ في قلوبِهِم الرعبَ}: وهو الخوف الشديدُ، الذي هو جند الله الأكبر، الذي لا ينفع معه عددٌ ولا عدةٌ ولا قوةٌ ولا شدةٌ؛ فالأمر الذي يحتسبونه، ويظنُّون أنَّ الخلل يدخل عليهم منه إن دخل، هو الحصون التي تحصَّنوا بها واطمأنتْ نفوسُهم إليها، ومن وَثِقَ بغير الله؛ فهو مخذولٌ، ومن ركن إلى غير الله؛ كان وبالاً عليه ، فأتاهم أمرٌ سماويٌّ نزل على قلوبهم، التي هي محلُّ الثبات والصبر أو الخور والضعف، فأزال قوَّتها وشدَّتها، وأورثها ضعفاً وخوراً وجبناً لا حيلة لهم في دفعه ، فصار ذلك عوناً عليهم، ولهذا قال: {يُخْرِبونَ بيوتَهم بأيديهِم وأيدي المُؤمِنينَ}، وذلك أنَّهم صالحوا النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - على أنَّ لهم ما حملتِ الإبلُ، فنقضوا لذلك كثيراً من سقوفهم التي استحسنوها، وسلَّطوا المؤمنين بسبب بغيهم على إخراب ديارِهِم وهدم حصونِهم، فهم الذين جَنَوا على أنفسهم وصاروا أكبر عونٍ عليها. {فاعْتَبِروا يا أولي الأبصارِ}؛ أي: البصائر النافذة والعقول الكاملة؛ فإنَّ في هذا معتبراً يُعْرَف به صنع الله [تعالى] في المعاندين للحقِّ، المتبعين لأهوائهم، الذين لم تنفعهم عزَّتهم ولا مَنَعَتْهم قوتُهم ولا حصَّنتهم حصونهم، حين جاءهم أمرُ الله؛ وصل إليهم النكال بذنوبهم، والعبرة بعموم المعنى لا بخصوص السبب؛ فإنَّ هذه الآية تدلُّ على الأمر بالاعتبار، وهو اعتبار النظير بنظيره، وقياس الشيء على ما يشابهه ، والتفكُّر فيما تضمَّنته الأحكام من المعاني والحكم التي هي محلُّ العقل والفكرة، وبذلك يكمُلُ العقل، وتتنور البصيرة، ويزداد الإيمان، ويحصل الفهم الحقيقيُّ.
{2} Na katika hayo kuna kumsaidia Mtume wake – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – dhidi ya makafiri miongoni mwa Watu wa Kitabu kutoka kwa kabila la Banu An-Nadhir walipomfanyia hiyana Mtume wake, basi akawatoa majumbani mwao, na makazi yao waliyokuwa wameyazoea na kuyapenda. Kuwafukuza kwao huko kulikuwa kwenda Khaybar ndiko mkusanyiko wa kwanza na kufukuziliwa mbali na Mwenyezi Mungu kupitia mikono ya Mtume wake Muhammad Rehema na Amani zimshukie. Aya hii tukufu iliashiria kuwa watakuwa na mkusanyiko na kufukuziliwa mbali kusiokuwa huku. Hilo lilitokea wakati Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alipowahamisha kutoka Khaybar, na kisha Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, akawafukuza waliosalia humo.
“Hamkudhani” enyi Waislamu
“kuwa watatoka” kutoka katika maskani zao. Kwa sababu ya kutodhurika ugumu wa ngome zao, na ulinzi wake mkali, na nguvu zao ndani yake,
“nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda dhidi ya Mwenyezi Mungu.” Basi wakafurahishwa nazo, na zikawadanganya, na wakadhania kuwa hawataweza kufikiwa humo, wala hakuna anayeziweza. Lakini uweza wa Mwenyezi Mungu uko nyuma ya hayo yote. Ngome na majumba marefu haviwezi kusimama mbele yake wala nguvu na ulinzi havifai chochote.
Ndiyo maana akasema: “Lakini Mwenyezi Mungu akawafikia kwa mahali ambako hawakutazamia.” Na hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Alitia uwoga mkubwa katika nyoyo zao.” Na hilo ndilo jeshi kubwa zaidi la Mwenyezi Mungu, ambalo wala idadi wala vifaa wala nguvu wala ukali havisaidii kitu mbele yake. Na jambo wanalolitarajia, na wanadhania kuwa litawajia kosa ikiwa likiwafikia ni ngome walizojikinga ndani yake, na ambazo nafsi zao zimetulia juu yake. Lakini mwenye kuwa na imani na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi huyo ataachiliwa mbali bila msaada. Na mwenye kutegemea asiyekuwa Mwenyezi Mungu, alilotegemea hilo linakuwa balaa kubwa kwake. Kwa hivyo, wakajiwa na jambo kutoka mbinguni lililoingia katika nyoyo zao, ambazo ndizo mahali pa uthabiti na subira, au udhaifu. Basi akawaondolea nguvu na ukali wao, na akawaacha na udhaifu na woga ambavyo hawakuwa na hila ya kuvizuilia. Na kwa hilo akawa amemsaidia Mtume dhidi yao.
Ndiyo maana akasema: “Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini.” Hayo ni kwa sababu walifanya suluhu na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa sharti ya kwamba wataruhusiwa kuchukua kile ambacho ngamia wataweza kubeba. Kwa hivyo, wakavunja dari zao nyingi walizokuwa wanazipenda mno, na wakawapa mamlaka Waumini kwa sababu ya uasi wao, ili waziharibu nyumba zao na wazibomoe ngome zao. Kwani wao ndio waliojifanyia ubaya wenyewe na wakawa ni msaada mkubwa dhidi yao wenyewe.
“Basi zingatieni enyi wenye macho!” Yaani, wenye macho ya kuona sawasawa na akili kamili. Kwani katika hili kuna mazingatio ambayo kwayo yanajulikana matendo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika wale wanaoipinga haki, wale wanaofuata matamanio yao, ambao kiburi hakikuwafaa kitu, wala nguvu zao hazikuwazuilia kitu, wala ngome zao hazikuwalinda kwa chochote. Wakati jambo la Mwenyezi Mungu lilipowajia mateso yaliwafikia kwa sababu ya dhambi zao, na lililo muhimu ni maana ya jumla, siyo sababu mahususi. Kwa maana, aya hii inaashiria amri ya kuzingatia, ambayo ni kuzingatia kitu sawa na chenzake, kulinganisha kitu na kile kinachofanana nacho, na kutafakari juu ya maana na hekima zilizomo katika hukumu mbalimbali, ambazo ndizo mahali pa akili na kufikiria. Na kwa hayo, akili hukamilika, ufahamu hutiwa nuru, imani huongezeka, na ufahamu wa kweli hupatikana.
#
{3} ثم أخبر تعالى أنَّ هؤلاء اليهود لم يصِبْهم جميع ما يستحقون من العقوبة، وأن الله خفَّف عنهم، فلولا أنه كتبَ عليهم الجلاءَ الذي أصابهم وقضاه عليهم [وقدره] بقدره الذي لا يُبَدَّلُ ولا يُغَيَّرُ؛ لكان لهم شأنٌ آخر من عذاب الدُّنيا ونَكالها، ولكنهم وإن فاتهم العذابُ الشديد الدنيويُّ؛ فإنَّ لهم في الآخرة عذابَ النار الذي لا يمكن أن يعلم شدَّته إلاَّ الله؛ فلا يخطر ببالهم أن عقوبتهم [قد] انقضتْ وفرغتْ ولم يبقَ لهم منها بقيةٌ؛ فما أعدَّ الله لهم من العذابِ في الآخرة أعظم وأطمُّ.
{3} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatujulisha kwamba Mayahudi hawa hawakupatwa na adhabu yote waliyostahiki, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwapunguzia adhabu. Lau asingewaandikia uhamishaji uliowapata na akaupitisha juu yao na akapanga hivyo kwa mipango yake ambayo haiwezi kubadilishwa wala kugeuzwa, basi wangelikuwa na jambo jingine la adhabu na mateso ya duniani. Lakini hata kama walikosa adhabu kali ya duniani, basi hakika huko Akhera watapata adhabu ya Moto wa Jahannam, ambayo ukali wake hakuna awezaye kuujua isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Kwa hivyo, wasifikirie kwamba adhabu yao ilikwisha na kwamba hakuna chochote cha adhabu kilichobakia. Sivyo hivyo! Adhabu ambayo Mwenyezi Mungu aliwaandalia huko Akhera ni kubwa na kali mno.
#
{4} و {ذلك} لأنَّهم {شاقُّوا اللهَ ورسولَه}: وعادَوْهما وحاربوهما وسعوا في معصيتهما، وهذه سنته وعادته فيمن شاقَّه. {ومن يُشاقِّ اللهَ فإنَّ اللهَ شديدُ العقابِ}.
{4} Na
“hayo ni kwa sababu walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake” na wakawafanyia uadui, wakapigana nao na wakafanya bidii katika kuwaasi. Basi hii ndiyo desturi yake katika wale wanaompinga.
“Na mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.”
#
{5} ولما لام بنو النضير رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم - والمسلمين في قطع النخيل والأشجار، وزعموا أن ذلك من الفساد وتوصلوا بذلك إلى الطعن بالمسلمين، أخبر تعالى أنَّ قطع النخيل إن قطعوه أو إبقاءهم إيَّاه إن أبْقَوْه؛ أنه بإذنه [تعالى] وأمره، {ولِيُخْزِيَ الفاسقين}: حيث سلَّطكم على قطع نخلهم وتحريقها؛ ليكون ذلك نكالاً لهم وخزياً في الدُّنيا وذلًّا يُعرف به عجزُهم التامُّ الذي ما قدروا على استنقاذ نخلهم الذي هو مادة قوتهم. واللِّينة تشمل سائرَ النخيل على أصحِّ الاحتمالات وأولاها؛ فهذه حال بني النضير وكيف عاقبهم الله [تعالى] في الدُّنيا.
Na wakati Banu Nadhir walipomlaumu Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na Waislamu kuhusiana na kukata kwao mitende na miti, na wakadai kwamba hilo ni kufanya uharibifu na wakatumia hilo kuwakashifu Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba kukata mitende hiyo ikiwa waliikata au kuiwacha imesimama ikiwa waliiacha, ni kwa idhini yake na amri yake,
“ili awahizi wavukao mipaka,” ambapo aliwawezesha kukata mitende yao na kuichoma; ili hilo liwe ni adhabu kwao na fedheha duniani na udhalilifu utakaoonyesha kutoweza kwao kitu kabisa, kwa kuwa hawakuweza kuokoa mitende yao ambayo ni chanzo cha chakula chao kikuu. Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa hali ya Banu Nadhir na jinsi Mwenyezi Mungu
[Mtukufu] alivyowaadhibu duniani.
#
{6} ثم ذكر مَن انتقلت إليه أموالُهم وأمتعتُهم، فقال: {وما أفاء اللهُ على رسولهِ منهم}؛ أي: من أهل هذه القرية، وهم بنو النضير، {فـ}: إنَّكم يا معشر المسلمين، {ما أوجَفْتُم عليه من خيل ولا ركابٍ}؛ أي: ما أجلبتم وحشدتم ؛ أي: لم تتعبوا بتحصيلها لا بأنفسكم ولا بمواشيكم، بل قذف الله في قلوبهم الرعبَ، فأتتكم صفواً عفواً، ولهذا قال: {ولكنَّ الله يسلِّطُ رسله على من يشاءُ واللهُ على كلِّ شيءٍ قديرٌ}: من تمام قدرته أنَّه لا يمتنع عليه ممتنعٌ ولا يتعزَّز من دونه قويٌّ.
Kisha akataja wale ambao mali na vitu vyao viliwaendea,
akasema: “Na mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao,” yaani kutoka kwa watu wa kijiji hiki, ambao ni Banu Nadhir.
“Basi” enyi kundi la Waislamu, “hamkuikimbilia mbio kwa farasi wala ngamia.” Yaani, hamkuvipata kwa nafsi zenu wenyewe wala kwa wanyama wenu. Bali Mwenyezi Mungu aliwatia hofu kubwa mioyoni mwao, kwa hivyo vikawajia bila juhudi.
Ndiyo maana akasema: “Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno juu ya kila kitu.” Kwa sababu ya utimilifu wa uwezo wake ni kwamba hakuna lisilowezekana linaloweza kukataa atakacho, wala hakuna mtu mwenye nguvu anayeweza kupata nguvu dhidi yake
#
{7} وتعريف الفيء باصطلاح الفقهاء: هو ما أخِذَ من مال الكفار بحقٍّ من غير قتال؛ كهذا المال الذي فرُّوا وتركوه خوفاً من المسلمين، وسُمِّي فيئاً؛ لأنه رجع من الكفار الذين هم غير مستحقِّين له إلى المسلمين الذين لهم الحقُّ الأوفر فيه. وحكمه العامُّ كما ذكره الله بقوله: {ما أفاءَ اللهُ على رسولهِ من أهلِ القُرى}: عموماً، سواء كان في وقت الرسول أو بعده على مَن تَوَلَّى من بعدِهِ من أمَّته، {فللهِ وللرسولِ ولذي القربى واليتامى والمساكينِ وابنِ السبيل}: وهذه الآية نظير الآية التي في سورة الأنفال ، وهي قوله: {واعلموا أنَّما غَنِمْتُم من شيءٍ فأنَّ لله خُمُسَه وللرسول ولذي القُربى واليتامى والمساكينِ وابنِ السبيلِ}؛ فهذا الفيء يُقسم خمسة أقسام: لله ولرسوله يُصْرَفُ في مصالح المسلمين العامة. وخمسٌ لذوي القربى، وهم بنو هاشم وبنو المطلب؛ حيث كانوا، يسوَّى فيه بين ذكورهم وإناثهم، وإنَّما دخل بنو المطَّلب في خمس الخمس مع بني هاشم ولم يدخُلْ بقية بني عبد مناف؛ لأنهم شاركوا بني هاشم في دخولهم الشعبَ حين تعاقدتْ قريشٌ على هجرهم وعداوتهم، فنصروا رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم -؛ بخلاف غيرهم، ولهذا قال النبيُّ صلّى الله عليه وسلّم في بني عبد المطلب: «إنَّهم لم يفارِقوني في جاهليَّة ولا إسلام». وخمسٌ لفقراء اليتامى، وهم من لا أب له ولم يبلغْ. وخمسٌ للمساكين. وخمسٌ لأبناء السبيل، وهم الغرباء المنقطَع بهم في غير أوطانهم.
وإنَّما قدَّر الله هذا التقدير وحصر الفيء في هؤلاء المعيَّنين؛ لكي {لا يكونَ دُولَةً}؛ أي: مداولةً واختصاصاً {بين الأغنياءِ منكم}: فإنَّه لو لم يقدِّره؛ لتداولته الأغنياءُ الأقوياء، ولما حَصَلَ لغيرهم من العاجزين منه شيءٌ، وفي ذلك من الفساد ما لا يعلمه إلا الله؛ كما أنَّ في اتِّباع أمر الله وشرعه من المصالح ما لا يدخل تحت الحصر، ولذلك أمر الله بالقاعدة الكلِّيَّة والأصل العام، فقال: {وما آتاكُمُ الرسولُ فخذوهُ وما نَهاكم عنهُ فانتَهوا}: وهذا شاملٌ لأصول الدين وفروعه ظاهره وباطنه، وأنَّ ما جاء به الرسول يتعيَّن على العباد الأخذ به واتِّباعه، ولا تحلُّ مخالفته، وأنَّ نصَّ الرسول على حكم الشيء كنصِّ الله تعالى؛ لا رخصةَ لأحدٍ ولا عذر له في تركه، ولا يجوز تقديم قول أحدٍ على قوله. ثم أمر بتقواه التي بها عِمارةُ القلوب والأرواح والدُّنيا والآخرة، وبها السعادة الدائمة والفوزُ العظيم، وبإضاعتها الشقاء الأبديُّ والعذاب السرمديُّ، فقال: {واتَّقوا الله إنَّ الله شديدُ العقابِ}: على من ترك التقوى وآثر اتِّباع الهوى.
{7} Al-Fayi ni kulingana na istilahi ya mafaqihi ni kile kilichochukuliwa kutoka kwenye mali za makafiri kwa haki, bila ya kupigana vita. Kama mali hizi walizokimbia na kuziacha kwa kuwaogopa Waislamu. Nazo ziliitwa Al-Fayi kwa sababu ilirejea kutoka kwa makafiri ambao hawakuistahiki na kuwaendea Waislamu ambao wana haki nyingi humo.
Na hukumu yake kwa ujumla ni kama alivyoitaja Mwenyezi Mungu pale aliposema: “Mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji” kwa ujumla, sawa iwe ni katika zama za Mtume au baada yake kwa wale watakaoshika uongozi katika umma wake baada yake,
“ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri.” Na Aya hii inafanana na Aya iliyomo katika Surat Al-Anfal,
nayo ni kauli yake: “Na jueni ya kwamba ngawira mnayoipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri.” Ngawira hii inagawanywa katika sehemu tano: kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo itatumika kwa masilahi ya jumla ya Waislamu. Na humusi kwa ajili ya jamaa zake, yaani Banu Hashim na Banu Al-Muttalib, popote watakapokuwa, wanaume na wanawake wao wako sawa katika hilo. Hao Banu Al-Muttalib walijumuishwa katika humusi hii pamoja na Banu Hashim ilhali haawakuingizwa Banu Abd Manaf wengineo, kwa sababu walishiriki pamoja na Banu Hashim katika kuingia kwao katika bonde wakati Maquraishi walipofanya makubaliano ya kuwatenga na kuwafanyia uadui, kwa hivyo wakamuunga mkono Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – tofauti na wengineo,
na ndiyo maana Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alisema kuhusu Banu Abdul Muttalib: “Hakika, wao hawakujitenga mbali nami wakati wa kabla ya Uislamu wala katika Uislamu.” Na humusi nyingine kwa ajili ya mayatima masikini, ambao ni wale wasio na baba na hawajabaleghe. Na humusi nyingine kwa ajili ya maskini. Na humusi nyingine kwa ajili ya wasafiri, ambao ni wageni waliokwama katika maeneo yaliyo mbali na nchi zao. Mwenyezi Mungu aliweka viwango hivi na akafanya Al-Fayi
(ngawira) kuwa ni ya watu hawa maalumu, ili "isiwe ikizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu” sababu kama Mwenyezi Mungu hakupanga hivyo, basi matajiri wenye nguvu ndio wengeichukua peke yao, na wasio na uwezo hawangepata chochote kwayo, jambo ambalo lingeleta uharibifu mkubwa asioujua isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Kama vile kwa kufuata amri ya Mweneyezi Mungu na sheria yake kuna manufaa mengi yasiyo na mipaka. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaamuru kanuni na msingi wa jumla,
akasema: “Na anachokupeni Mtume, kichukueni. Na anachokukatazeni, jiepusheni nacho.” Hili linajumuisha misingi ya dini na matawi yake, ya dhahiri na ya siri, na kwamba yale aliyokuja nayo Mtume inawalazimu waja kuyachukua na kuyafuata, na si halali kwenda kinyume naye, na kwamba amri ya Mtume juu ya kitu fulani, ni kama amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakuna anayepewa ruhusa wala udhuru wa kuacha amri ya Mtume, na wala hairuhusiwi kutanguliza kauli ya mtu yeyote mbele ya kauli ya Mtume. Kisha Mwenyezi Mungu akaamuru afanyiwe ucha Mungu, ambao kwa huo vinasimama imara mioyo, roho, dunia na akhera, na kwa huo mtu anapata furaha ya kudumu na ushindi mkubwa. Na kwa kuuacha, mtu anaingia katika taabu ya milele na adhabu isiyoisha.
Amesema Mtukufu: “Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu” mwenye kuacha kumcha na akapendelea kufuata matamanio.
#
{8 - 9} ثم ذكر تعالى الحكمة والسبب الموجب لجعله تعالى أموال الفيء لمن قدَّرها له، وأنَّهم حقيقون بالإعانة، مستحقُّون لأن تُجعل لهم، وأنهم ما بين مهاجرين؛ قد هجروا المحبوبات والمألوفات من الديار والأوطان والأحباب والخلان والأموال رغبةً في الله ونصرةً لدين الله ومحبةً لرسول الله؛ فهؤلاء هم الصادقون؛ الذين عملوا بمقتضى إيمانهم، وصدَّقوا إيمانَهم بأعمالهم الصالحة والعبادات الشاقَّة؛ بخلاف مَنِ ادَّعى الإيمان وهو لم يصدِّقْه بالجهاد والهجرة وغيرهما من العبادات، وبين أنصار، وهم الأوس والخزرج، الذين آمنوا بالله ورسوله طوعاً ومحبةً واختياراً، وآووا رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، ومنعوه من الأحمر والأسود، وتبوَّءوا دار الهجرة والإيمان، حتى صارت موئلاً ومرجعاً يرجع إليه المؤمنون، ويلجأ إليه المهاجرون، ويسكن بحماه المسلمون؛ إذ كانت البلدانُ كلُّها بلدانَ حربٍ وشركٍ وشرٍّ، فلم يزل أنصارُ الدين يأوون إلى الأنصار، حتى انتشر الإسلام وقوي وجعل يزداد - شيئاً فشيئاً، [وينمو قليلاً قليلاً] حتى فتحوا القلوبَ بالعلم والإيمان والقرآن، والبلدانَ بالسيف والسنان، الذين من جُملة أوصافهم الجميلة أنهم {يحبُّون مَن هاجَر إليهم}، وهذا لمحبَّتهم لله ورسوله، أحبُّوا أحبابه، وأحبُّوا من نصر دينه. {ولا يجِدونَ في صدورهم حاجةً مما أوتوا}؛ أي: لا يحسُدون المهاجرين على ما آتاهم الله من فضلهِ وخصَّهم به من الفضائل والمناقب الذين هم أهلها.
وهذا يدلُّ على سلامة صدورهم وانتفاء الغلِّ والحقد والحسد عنها، ويدلُّ ذلك على أنَّ المهاجرين أفضل من الأنصار؛ لأنَّ الله قدَّمهم بالذِّكر، وأخبر أنَّ الأنصارَ لا يجدون في صدورهم حاجةً مما أوتوا، فدلَّ على أنَّ الله تعالى آتاهم ما لم يؤتِ الأنصارَ ولا غيرهم، ولأنَّهم جمعوا بين النصرة والهجرة، وقوله: {ويؤثِرونَ على أنفسِهِم ولو كان بهم خَصاصةٌ}؛ أي: ومن أوصاف الأنصار التي فاقوا بها غيرهم وتميَّزوا بها عمَّن سواهم الإيثار، وهو أكمل أنواع الجود، وهو الإيثار بمحابِّ النفس من الأموال وغيرها، وبذلها للغيرِ، مع الحاجة إليها، بل مع الضَّرورة والخَصاصة، وهذا لا يكون إلا من خُلُقٍ زكيٍّ ومحبَّة لله تعالى مقدَّمة على [محبة] شهوات النفس ولذَّاتها. ومن ذلك قصَّة الأنصاريِّ الذي نزلت الآية بسببه حين آثر ضيفَه بطعامه وطعام أهله وأولادِهِ وباتوا جياعاً.
والإيثار عكس الأثَرَةِ؛ فالإيثارُ محمودٌ، والأثَرَةُ مذمومةٌ؛ لأنَّها من خصال البخل والشحِّ، ومن رُزِق الإيثار؛ فقد وُقِيَ شُحَّ نفسِه، {ومَن يوقَ شُحَّ نفسهِ فأولئك همُ المفلحونَ}: ووقايةُ شحِّ النفس يشمل وقايتها الشحَّ في جميع ما أمر به؛ فإنَّه إذا وُقِيَ العبدُ شحَّ نفسه؛ سمحت نفسه بأوامر الله ورسوله، ففعلها طائعاً منقاداً منشرحاً بها صدرُه، وسمحت نفسه بترك ما نهى اللهُ عنه، وإنْ كان محبوباً للنفس؛ تدعو إليه وتطلَّع إليه، وسمحتْ نفسه ببذل الأموال في سبيل الله وابتغاءِ مرضاتِه، وبذلك يحصُلُ الفلاح والفوزُ؛ بخلاف مَنْ لم يوقَ شحَّ نفسه، بل ابْتُلِيَ بالشُّحِّ بالخير الذي هو أصل الشرِّ ومادته.
{8 - 9} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hekima na sababu kwa nini aliwapa hayo makundi ngawira za vita, na kwamba wao wanastahiki kusaidiwa, wanaostahiki kupewa, na kwamba wao ni miongoni mwa wahamiaji; ambao waliziacha nyumba zao wanazozipenda na walizozizoea, nchi zao, wapenzi wao, wendani wao, na mali zao, kwa ajili ya kumtaka Mwenyezi Mungu, na kuunga mkono dini yake, na kumpenda Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hawa ndio wakweli. Wale waliofanya matendo kulingana na Imani yao, na wakaisadikisha Imani yao kwa vitendo vyao vizuri na ibada ngumu; tofauti na wale waliodai kuwa na imani lakini hawakuisadikisha kwa jihadi, kuhama, na ibada nyinginezo, na miongoni mwa Answar, yaani Aws na Khazraj, ambao walimwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kutii, kwa mapenzi na hiari, na wakampa kimbilio Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na wakamzuilia mbali na mwekundu na mweusi, na wakaandaa makazi ya kuhamia na imani, mpaka yakawa ni makazi na marejeo ambayo Waumini hurejea, wahamiaji hutafuta hifadhi huko, na Waislamu wanaishi katika hiyama yake. Kwa vile nchi zote zilikuwa nchi za vita, ushirikina, na uovu, lakini wale wanaoinusuru Dini waliendelea tu kutafuta hifadhi kwa Ansari, mpaka Uislamu ukaenea na kuwa na nguvu na ukaanza kuongezeka - kidogo kidogo,
[na kukua kidogo kidogo] mpaka wakafungua nyoyo kwa elimu, imani, na Qur-ani, na wakfaungua nchi kwa upanga na mikuki, ambayo miongoni mwa maelezo yao ya mazuri ya jumla ni kuwa wao
“wanawapenda wale waliohamia kwao” na hayo ni kwa sababu ya kumpenda kwao Mwenyezi Mungu na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake –
“wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyopewa (Wahajiri)” na Mwenyezi Mungu kutokana na fadhila na sifa maalumu alizowapa wao tu, ambazo wanazistahiki. Hili linaashiria usalama wa nyoyo zao na kwamba hazina chuki wala uhasidi, na hili pia linaashiria kuwa Muhajirina ni bora kuliko Ansari. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwataja kwanza kabla yao, na akajulisha kwamba Ansari hawakuona katika nyoyo zao choyo yoyote ya kile walichopewa. Kwa hivyo hilo likaashiria kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapa kile ambacho hakuwapa Ansari au mtu mwingine yeyote, na kwa sababu walikusanya kati ya usaidizi na kuhama.
Na kauli yake: “Bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.” Yaani, katika Sifa za Ansari ambazo kwazo waliwashinda wengine na ambazo kwazo walijitofautisha na wengine ilikuwa ni kupendelea wengine, jambo ambalo ndilo aina kamili zaidi ya ukarimu wa kutoa, nalo ni kupendelea wengine katika mambo ambayo nafsi inapenda kama vile mali na mengineyo, na kuwapa wengine hivyo, pamoja na kwamba mwenye kutoa anavihitaji. Bali hata anapokuwa na dharura kubwa na hitaji kubwa juu yake. Hili haliwezekani isipokuwa kutokana na tabia safi na kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtanguliza mbele ya kupenda matamanio ya nafsi na ladha zake. Na katika hayo ni kisa cha yule Muanswari ambaye kwa sababu yake aya hii iliteremshwa, pale alipompendelea mgeni wake kwa chakula chake na chakula cha familia yake na watoto wake, na wao wenyewe wakalala njaa. Kupenedelea ni kinyume cha kujipendea. Kwa hivyo, kupendelea ni jambo la kusifiwa, na kujipendea ni jambo la kukashifiwa; kwa sababu ni katika sifa za ubakhili na uchoyo. Mwenye kupewa kupenedelea, basi hakika atakuwa amewekwa mbali na choyo ya nafsi yake.
“Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.” Kuwekwa mbali na choyo ya nafsi kunajumuisha kukingwa mbali na choyo katika yote aliyoyaamrishwa. Kwani ikiwa mja atalindwa mbali na choyo ya nafsi yake, basi nafsi yake itajiruhusu kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atayafanya kwa utiifu, kunyenyekea, na kifua wazi katika kuyafanya, na nafsi yake itamruhusu kuacha yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, hata kama ni mapendwa kwa nafsi yake. Inayaitia na kuyatamani. Na itamruhusu nafsi yake kutoa mali kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, na kwa hilo atapata kufaulu na kushinda. Tofauti na yule ambaye hakuzuiliwa mbali na choyo ya nafsi yake. Bali alipewa mtihani wa choyo wa kufanya heri, jambo ambalo ndilo msingi na kiini cha uovu.
#
{10} فهذان الصنفان الفاضلان الزكيَّان هم الصحابة الكرام والأئمة الأعلام، الذين حازوا من السوابق والفضائل والمناقب ما سَبَقوا به مَن بعدَهم وأدركوا به مَن قبلهم، فصاروا أعيان المؤمنين وسادات المسلمين وقادات المتَّقين، وحسب من بعدهم من الفضل أن يسيرَ خلفَهم ويأتمَّ بهُداهم، ولهذا ذكر الله من اللاحقين مَن هو مؤتمٌّ بهم [وسائر خلفهم]، فقال: {والذين جاؤوا من بعدِهم}؛ أي: من بعد المهاجرين والأنصارِ، {يقولون}: على وجه النُّصح لأنفسهم ولسائر المؤمنين: {ربَّنا اغْفِرْ لنا ولإخوانِنا الذين سَبَقونا بالإيمانِ}: وهذا دعاءٌ شاملٌ لجميع المؤمنين من السابقين من الصحابة ومَن قبلَهم ومَن بعدهم، وهذا من فضائل الإيمان؛ أنَّ المؤمنين ينتفعُ بعضُهم ببعض ويدعو بعضُهم لبعض؛ بسبب المشاركةِ في الإيمان، المقتضي لعقد الأخوَّة بين المؤمنين، التي من فروعها أن يدعوَ بعضُهم لبعض، وأن يحبَّ بعضُهم بعضاً، ولهذا ذكر الله في هذا الدعاء نفي الغلِّ عن القلب، الشامل لقليلِه وكثيرِه، الذي إذا انتفى؛ ثبت ضدُّه، وهو المحبَّة بين المؤمنين والموالاة والنصح ونحو ذلك مما هو من حقوق المؤمنين، فوصفَ الله مَن بعد الصحابة بالإيمان؛ لأنَّ قولهم: {سَبَقونا بالإيمان}: دليلٌ على المشاركة فيه ، وأنَّهم تابعون للصحابة في عقائد الإيمان وأصوله، وهم أهل السنة والجماعة، الذين لا يصدق هذا الوصف التامُّ إلاَّ عليهم، وَوَصَفَهم بالإقرار بالذُّنوب والاستغفار منها واستغفار بعضهم لبعض واجتهادهم في إزالة الغلِّ والحقدِ [عن قلوبهم] لإخوانهم المؤمنين؛ لأنَّ دعاءهم بذلك مستلزمٌ لما ذكرنا ومتضمِّنٌ لمحبَّة بعضهم بعضاً، وأنْ يحبَّ أحدُهم لأخيه ما يحبُّ لنفسه، وأن ينصحَ له حاضراً وغائباً حيًّا وميتاً.
ودلَّت الآية الكريمة على أنَّ هذا من جملة حقوق المؤمنين بعضهم لبعض. ثم ختموا دعاءهم باسمينِ كريمينِ دالَّين على كمال رحمة الله وشدَّة رأفته وإحسانه بهم، الذي من جملته: بل [من] أَجَلِّه توفيقُهم للقيام بحقوقه وحقوق عباده.
فهؤلاء الأصناف الثلاثة هم أصناف هذه الأمة، وهم المستحقُّون للفيء، الذي مصرفه راجعٌ إلى مصالح الإسلام، وهؤلاء أهله الذين هم أهلُه، جعلنا الله منهم بمنِّه وكرمه.
{10} Aina hizi mbili bora safi ni maswahaba watukufu na maimamu wakubwa, waliopata tangulia, fadhila mbalimbali, sifa mbalimbali walizopata walizotangulia kwazo wale waliokuja baada yao na wakawafikia kwazo wale waliokuwa kabla yao, na wakawa waumini wakweli, mabwana wa Waislamu, na viongozi wa wacha Mungu, na inatosha wale waliokuja baada yao kuwa na fadhila ya kutembelea nyuma yao na kuufuata uwongofu wao, na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akataja miongoni mwa watakaofuata wale wanaofuatwa,
[na kutembelea nyuma yao],
akasema: “Na wale waliokuja baada yao.” Yaani, baada ya Muhajirina na Ansari,
“wanasema” kwa njia ya kujinasihi wenyewe na kunasihi Waumini wengine wote: “Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani.” Hii ni dua inayowajumuisha Waumini wote katika wale waliotangulia miongoni mwa masahaba na wale waliokuwa kabla yao na baada yao, na hizi ni miongoni mwa fadhila za imani; kwamba Waumini wananufaika wao kwa wao na wanaombeana wao kwa wao; kwa sababu ya kushirikiana kwao katika imani, jambo linalohitaji kuwepo mafungamano ya udugu baina ya waumini, ambao katika matawi yake ni kuombeana dua wao kwa wao, na kupendana, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja katika dua hii kuondolewa kwa chuki kutoka moyoni, ikijumuisha ndogo na nyingi, ambayo ikiwa haitakuwepo, basi kinyume chake kinathibiti, ambacho ni mapenzi baina ya waumini, kulindana, kushauriana, na mambo mengine ambayo ni miongoni mwa haki za waumini. Basi Mwenyezi Mungu akawasifu wale waliokuwa baada ya maswahaba kwamba wana imani,
kwa sababu kauli yake: “waliotutangulia kwa Imani” ni ishara kwamba wanashirikiana katika hilo, na kwamba wao ni wafuasi wa Maswahaba katika itikadi za imani na misingi yake, na wao ni watu wa Sunna na umoja ambao sifa hii kamili haiwezi kuwa kwa wengine isipokuwa wao tu, na akawaelezea kwamba wanakiri dhambi na kuomba msamaha kwa sababu yake, na kuombeana msamaha, na kujitahidi kuondoa chuki na kinyongo
[katika nyoyo zao] dhidi ya ndugu zao waumini; kwa sababu kuomba kwao haya kunahitajia haya tuliyoyataja na kunajumuisha kupendana wao kwa wao, na kwamba kila mmoja anampendea ndugu yake kile anachojipendea mwenyewe, na kwamba ampe nasaha anapokuwepo na hata kama hayupo, kama yu hai na kama amekufa. Aya hii tukufu inaashiria kwamba hizi ni miongoni mwa haki za waumini wao kwa wao. Kisha wakahitimisha dua yao kwa majina mawili matukufu ya Mwenyezi Mungu yenye kuashiria ukamilifu wa rehema ya Mwenyezi Mungu na ukubwa wa huruma yake na wema wake kwao,
ambayo ni pamoja na: Bali,
[katika] kubwa yake zaidi ni kuwawezesha kutekeleza haki zake na haki za waja wake. Aina hizi tatu ni aina za umma huu, nao wale wanaostahiki ngawira iliyopatikana bila vita, ambayo matumizi yake yanarudi kwenye masilahi ya Uislamu, na hawa ndio watu wake ambao ndio watu wake, Mwenyezi Mungu atufanye miongoni mwao kwa neema yake na ukarimu wake.
#
{11} ثم تعجَّب تعالى من حال المنافقين، الذين طمَّعوا إخوانهم من أهل الكتاب في نصرتهم وموالاتهم على المؤمنين، وأنَّهم يقولون لهم: {لَئنْ أخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ معكم ولا نُطيعُ فيكم أحداً أبداً}؛ أي: لا نطيع في عدم نصرتكم أحداً يعذِلُنا أو يخوَّفنا، {وإن قوتِلْتُم لننصُرَنَّكم واللهُ يشهدُ إنَّهم لَكاذبونَ}: في هذا الوعد الذي غرُّوا به إخوانهم، ولا يستكثرُ هذا عليهم؛ فإنَّ الكذبَ وصفهم، والغرور والخداع مقارنهم، والنفاق والجبن يصحبهم.
{11} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akastaajabia hali ya wanafiki ambao waliwatamanisha ndugu zao katika Watu wa Kitabu kwamba watawasaidia na kuungana nao dhidi ya Waumini,
na wakawaambia: “Mkitolewa, na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamtii yeyote kabisa dhidi yenu.” Yaani, hatutamtii yeyote katika kutowasaidia atakayejaribu kutulaumu au kututia hofu,
“Na mkipigwa vita, lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo” katika ahadi hii ambayo kwayo waliwahadaa ndugu zao. Na hili si kubwa kwao. Kwa maana, kusema uongo ndio sifa yao, na udanganyifu na hadaa haviachani nao, na unafiki na woga huandamana nao daima.
#
{12} ولهذا كذَّبهم الله بقوله الذي وُجِدَ مخبرُه كما أخبر به ووقع طِبْقَ ما قال، فقال: {لَئِنْ أخْرِجوا}؛ أي: من ديارهم جلاءً ونفياً {لا يخرُجون معهم}: لمحبَّتهم للأوطان، وعدم صبرهم على القتال، وعدم وفائهم بالوعد ، {ولَئِن قوتلوا لا يَنصُرونهم}: بل يستولي عليهم الجبنُ ويملكهم الفشل ويَخْذُلون إخوانَهم أحوج ما كانوا إليهم، {ولَئِن نَصَروهم}: على الفرض والتقدير ، {لَيُوَلُّنَّ الأدبارَ ثم لا يُنصرون}؛ أي: سيحصل منهم الإدبار عن القتال والنُّصرة، ولا يحصُل لهم نصرٌ من الله.
{12} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu aliwakanusha kwa kauli yake ambayo alitokea kama alivyosema.
Akasema: “Pindi wakitolewa” kutoka majumbani mwao, kwa kuhamishwa na kufukuzwa
“hawatatoka pamoja nao” kwa sababu wanayapenda sana makazi yao hayo, na kukosa kwao subira ya kupigana vita, na kutotimiza kwao ahadi zao,
“Na wakipigwa vita, hawatawasaidia” bali woga utawakamata sawasawa, na kushindwa kutawamiliki na watawaacha ndugu zao bila ya kuwasaidia wakati watakapokuwa wanawahitaji zaidi,
“Na kama wakiwasaidia” ikichukuliwa kwamba wanaweza kufanya hivyo
“basi watageuza mno migongo; kisha hawatanusuriwa” na Mwenyezi Mungu.
#
{13} والسبب الذي حملهم على ذلك أنَّكم أيُّها المؤمنون {أشدُّ رهبةً في صدورِهِم من اللهِ}: فخافوا منكم أعظم ممَّا يخافون الله، وقدَّموا مخافَة المخلوق الذي لا يملك لنفسه [ولا لغيره] نفعاً ولا ضرًّا على مخافة الخالق الذي بيده الضرُّ والنفع والعطاء والمنع. {ذلك بأنَّهم قومٌ لا يفقهون}: مراتب الأمور، ولا يعرفون حقائق الأشياء، ولا يتصوَّرون العواقب، وإنَّما الفقه كلُّ الفقه أن يكون خوفُ الخالق ورجاؤه ومحبَّتُه مقدمةً على غيرها، وغيرها تبعاً لها.
{13} Na sababu iliyowapelekea kufanya hivyo ni kuwa nyinyi enyi Waumini
“ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu.” Basi wakakuogopeni nyinyi zaidi kuliko wanavyomwogopa Mwenyezi Mungu, na wakatanguliza kumwogopa kiumbe ambaye haimilikii nafsi yake wala nafsi ya mwingine manufaa wala madhara mbele ya kumwogopa Muumba, ambaye mkononi mwake kuna madhara na manufaa, kupeana na kuzuilia.
“Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu kitu” katika daraja za mambo, na wala hawajui uhakika wa mambo, na wala hawafikirii matokeo yake. Na ufahamu wa kweli ni kutanguliza kumhofu Muumba, kumtumaini, kumpenda mbele ya wengineo, na kwamba hao wengineo mambo yao yanakuja nyuma ya mambo ya Mwenyezi Mungu.
#
{14} {لا يقاتِلونَكم جميعاً}؛ أي: في حال الاجتماع {إلاَّ في قرىً محصَّنةٍ أو من وراءِ جُدُرٍ}؛ أي: لا يثبتون على قتالكم ولا يعزِمون عليه إلاَّ إذا كانوا متحصِّنين في القرى أو من وراء الجدر والأسوار؛ فإنهم إذ ذاك ربَّما يحصُل منهم امتناعٌ اعتماداً على حصونهم وجُدُرهم لا شجاعةً بأنفسهم، وهذا من أعظم الذَّمِّ. {بأسُهُم بينَهم شديدٌ}؛ أي: بأسهم فيما بينهم شديدٌ، لا آفة في أبدانهم ولا في قوَّتهم، وإنَّما الآفة في ضعف إيمانهم وعدم اجتماع كَلِمَتهم، ولهذا قال: {تحْسَبُهُم جميعاً}: حين تراهم مجتمعين ومتظاهرين، {و} لكن {قلوبُهم شتًّى}؛ أي: متباغضة متفرِّقة متشتِّتة. {ذلك}: الذي أوجب لهم اتِّصافهم بما ذُكِرَ {بأنَّهم قومٌ لا يعقلونَ}؛ أي: لا عقل عندهم ولا لبَّ؛ فإنَّهم لو كانت لهم عقولٌ؛ لآثروا الفاضل على المفضول، ولَما رضوا لأنفسهم بأبخس الخطَّتين، ولكانت كلمتُهم مجتمعةً وقلوبهم مؤتلفةً؛ فبذلك يتناصرون ويتعاضدون ويتعاونون على مصالحهم [ومنافعهم] الدينيَّة والدنيويَّة؛ مثل هؤلاء المخذولين من أهل الكتاب، الذين انتصر الله لرسوله منهم، وأذاقَهم الخزيَ في الحياة الدنيا، وعدمَ نصرِ مَنْ وعدَهم بالمعاونة.
{14} “Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko.” Yaani, wakiwa wote pamoja,
“isipokuwa katika vijiji vilivyoimarishwa kwa ngome, au nyuma ya kuta.” Yaani, hawatabaki imara katika kupigana nanyi, wala hawawezi kuazimia kufanya hivyo isipokuwa ikiwa watakuwa ndani ya ngome katika vijiji au nyuma ya kuta na ua. Hapo, huenda wanaweza kujizuia kwa kuzitegemea ngome hizo na kuta zao, si kwa sababu ya ushujaa wao wenyewe, na hili ni katika mambo makubwa yanayokashifiwa zaidi.
“Wao kwa wao vita vyao ni vikali.” Yaani, hawana dosari katika miili yao wala nguvu zao, bali dosari yao iko katika udhaifu wa imani yao na ukosefu wa umoja katika neno lao.
Ndiyo maana akasema: “Utawadhania kuwa wako pamoja” wakati unapowaona wakiwa pamoja, wakijionyesha hivyo
“kumbe nyoyo zao ni mbali mbali.” Yaani, zinachukiana, zimetawanyika, na kutengana.
“Hayo” yaliyowasababishia kusifika kwa hayo yaliyotajwa ni “kwa kuwa wao ni watu wasiotumia akili” kwani kama wangekuwa na akili, basi wangependelea kilicho bora kuliko kile ambacho si bora, na wala wasingejiridhia wenyewe kilicho duni kati ya mafungu haypo mawili, na neno lao lingekuwa moja, na nyoyo zao zingeungana. Na kwa hayo, wangeweza kusaidiana wao kwa wao, na wanashirikiana katika masilahi yao
[na manufaa] yao ya kidini na ya kidunia. Basi mfano wa hao ndio wale walioachiliwa mbali katika Watu wa Kitabu, ambao Mwenyezi Mungu alimnusuru Mtume wake dhidi yao, na akawaonjesha hizaya katika maisha ya dunia, na kukosa msaada kutoka kwa wale waliowaahidi kuwasaidia.
#
{15} {كمثل الذين من قبلِهِم قريباً}: وهم كفارُ قريش، الذين {زيَّن لهمُ الشَّيطانُ أعمالهم، وقال: لا غَالِبَ لَكُمُ اليومَ من النَّاس، وإنَّي جَارٌ لكم، فَلَمَّا تَراءتِ الفئتانِ؛ نكص على عقبيهِ ، وقَالَ: إنِّي بَرِيءٌ منكم، إنَّي أرى ما لا ترَوْنَ}! فغرَّتهم أنفسهم، وغرَّهم مَن غرَّهم، الذين لم ينفعوهم ولم يدفعوا عنهم العذاب، حتى أتوا بدراً بفخرهم وخُيَلائِهم، ظانِّين أنهم مدركون برسول الله والمؤمنين أمانيهم، فنصر الله رسوله والمؤمنين عليهم، فقتلوا كبارهم وصناديدهم، وأسروا مَن أسروا منهم، وفرَّ من فرَّ، وذاقوا بذلك وبالَ أمرِهم وعاقبةَ شِركهم وبغيهم. هذا في الدُّنيا، {ولهم} في الآخرة عذابُ النارِ.
{15} “Ni kama mfano wa wale waliokuwa kabla yao hivi karibuni” Hao ni makafiri wa Maquraishi ambao " Shetani alipowapambia vitendo vyao,
na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipoonana majeshi mawili, akarudi nyuma,
na akasema: Hakika mimi si pamoja nanyi. Hakika mimi ninaona msiyoyaona." Basi nafsi zao zikawadanganya, na wale waliowahadaa pia wakawahadaa, ambao hawakuwanufaisha kitu na hawakuwazuilia adhabu, mpaka walipofika Badr kwa kujifahiri kwao na kiburi chao, wakidhania kuwa wao watafikia matajario yao dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini. Basi Mwenyezi Mungu akampa ushindi Mtume wake na Waumini dhidi yao, na wakawaua wakuu wao na vigogo wao, na wakawateka wale waliowateka miongoni mwao, na wakakimbia wale waliokimbia, na wakaonja kwa hilo uovu huo mambo yao na matokeo ya ushirikina wao na kuvuka kwao mipaka. Haya ni katika dunia, na Akhera watapata adhabu ya Moto.
#
{16} ومَثَلُ هؤلاء المنافقين الذين غرُّوا إخوانهم من أهل الكتاب، {كمَثَل الشيطان إذ قال للإنسانِ اكْفُرْ}؛ أي: زيَّن له الكفر وحسَّنه ودعاه إليه، فلما اغتر به وكفر وحصل له الشقاء لم ينفعه الشيطان الذي تولاه ودعاه إلى ما دعاه إليه بل تبرَّأ منه، {وقال إني بريءٌ منك إني أخافُ اللهَ ربَّ العالمين}؛ أي: ليس لي قدرةٌ على دفع العذاب عنك، ولستُ بمغنٍ عنك مثقال ذرَّةٍ من الخير.
{16} Na mfano wa wanafiki waliowahadaa ndugu zao katika Watu wa Kitabu,
"ni kama Shetani anapomwambia mtu: 'Kufuru.'" Yaani, alimpambia ukafiri na akamfanyia kuonekana kuwa mzuri na akamwita kuuendea. Basi alipodanganyika kwa huo na akakufuru na masaibu yatakapompata, Shetani hakumfaa kitu, ambaye alimfanya rafiki na akamwita kwenda katika yale aliyomwita. Bali alijitenga mbali naye.
“Hakika mimi niko mbali zaidi nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.” Yaani, Sina uwezo wa kukuepusha mbali na adhabu, na wala siwezi kukufaa hata uzito wa chembe ya wema.
#
{17} {فكان عاقِبَتَهما}؛ أي: الداعي الذي هو الشيطان والمدعو الذي هو الإنسان حين أطاعه، {أنهما في النار خالدَيْنِ فيها}؛ كما قال تعالى: {إنَّما يدعو حزبَه ليكونوا من أصحابِ السعيرِ}. {وذلك جزاءُ الظالمين}: الذين اشتركوا في الظُّلم والكفر، وإن اختلفوا في شدَّة العذاب وقوته. وهذا دأب الشيطان مع كل أوليائهِ؛ فإنَّه يَدْعوهم ويدلِّيهم بغرور إلى ما يضرُّهم ، حتى إذا وقعوا في الشباك، وحاق بهم أسبابُ الهلاك؛ تبرأ منهم وتخلَّى عنهم، واللَّوم كلُّ اللَّوم على من أطاعه؛ فإنَّ الله قد حذَّر منه وأنذر، وأخبرَ بمقاصده وغايته ونهايته، فالمقدِم على طاعته عاصٍ على بصيرةٍ لا عذر له.
{17} “Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao.” Yaani, mwitaji, ambaye ni Shetani, na anayeitwa, ambaye ni mwanadamu, alipomtii
“ni kuingia Motoni, wadumu humo daima.” Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Moto wenywe mwako mkali.’ Kisha akasema: “Na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.” Wale walioshiriki katika dhuluma na ukafiri, hata wakitofautiana katika ukali na nguvu ya adhabu. Hii ndiyo desturi ya Shetani anavyowafanya marafiki wake wote. Kwani yeye huwaita na kuwabembeleza kwa hadaa hadi katika yale yatakayowadhuru, hata wanapotumbukia kwenye wavu wake na kuzingirwa na visababu vya maangamizo, anajitenga mbali nao na kuwaacha peke yao. Laki lawama zote zinawarudia wale wanaomtii. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ameonya dhidi yake, na akajulisha kuhusu makusudio yake, malengo yake, na mwisho wake. Kwa hivyo mwenye kumtii, anakuwa ameasi baada ya kuwa na ufahamu na hana udhuru wowote.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنْظُرْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ (18) وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّهَ فَأَنْسَاهُمْ أَنْفُسَهُمْ أُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ (19) لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ (20) لَوْ أَنْزَلْنَا هَذَا الْقُرْآنَ عَلَى جَبَلٍ لَرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُتَصَدِّعًا مِنْ خَشْيَةِ اللَّهِ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ (21)}.
18. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari ya mnayoyatenda. 19. Wala msiwe kama wale walio msahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio wavukao mipaka. 20. Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu. 21. Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa hofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri.
#
{18} يأمر تعالى عباده المؤمنين بما يوجبه الإيمان ويقتضيه من لزوم تقواه سرًّا وعلانيةً في جميع الأحوال، وأن يراعوا ما أمرهم الله به من أوامرِهِ وشرائعهِ وحدودِه، وينظُروا ما لهم وما عليهم، وماذا حصلوا عليه من الأعمال التي تنفعهم أو تضرُّهم في يوم القيامةِ؛ فإنَّهم إذا جعلوا الآخرة نصبَ أعينهم وقبلةَ قلوبهم، واهتمُّوا للمقام بها؛ اجتهدوا في كثرة الأعمال الموصلة إليها وتصفيتها من القواطع والعوائق، التي توقِفُهم عن السير أو تَعوقُهم أو تصرِفهم، وإذا علموا أيضاً أنَّ {الله خبيرٌ بما}: يعملون، لا تخفى عليه أعمالُهم، ولا تضيع لديه، ولا يهملها؛ أوجب لهم الجدَّ والاجتهاد.
وهذه الآية الكريمةُ أصلٌ في محاسبة العبد نفسَه، وأنَّه ينبغي له أن يتفقَّدها؛ فإنْ رأى زللاً؛ تداركه بالإقلاع عنه والتوبة النصوح والإعراض عن الأسباب الموصلة إليه، وإن رأى نفسه مقصراً في أمر من أوامر الله؛ بذل جهدَه واستعانَ بربِّه في تتميمه وتكميله وإتقانه، ويقايس بين منن الله عليه وإحسانه وبين تقصيرِهِ؛ فإن ذلك يوجب له الحياء لا محالة.
{18} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake waumini kufanya yale yanayosababishwa na imani na kuhitajiwa nayo, kama vile kushikamana na kumcha Mwenyezi Mungu kwa siri na dhahiri na katika hali zote, na kuzingatia yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa amri zake, sheria zake, na mipaka yake, na waangalie kilicho chao na kilicho juu yao, na yale walichofanya ambayo yatawanufaisha au kuwadhuru Siku ya Kiyama. Kwa kuwa wanapoiweka Akhera mbele ya macho yao na kibla ya mioyo yao na wakajali kwamba watadumu humo milele, hapo watajitahidi kufanya matendo mengi yatayowafikisha huko na kuyaondolea yote vyema kuyasitisha na kuyazuia, ambayo yanawafanya kutoendelea kwenda mbele au kuwazuilia mbali na hilo au hata kuwaondoa kwenye hilo. Na pia wakijua kwamba
“Mwenyezi Mungu anazo habari” za yale anayoyatenda, wala matendo yao hayafichikani kwake, na hayapotelei kwake, wala hayapuuzi, hilo litawafanya kuwa na bidii na jitihada. Aya hii tukufu ndio msingi wa kumfanya mja kujihesabia matendo yake, na kwamba anapaswa kuikagua mara kwa mara. Akiona kosa, analisuluhisha kwa kuliacha, toba ya kweli na kujiweka mbali na visababu vya kufikisha katika kosa hilo. Na akijiona hafanyi kikamilifu katika mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu, anafanya juhudi kubwa na kumuomba msaada Mola wake katika kuikamilisha na kuifanya kwa uzuri mkubwa, na akalinganisha baina ya neema za Mwenyezi Mungu na wema wake juu yake na mapungufu yake. Hilo bila shaka linamfanya kustahi.
#
{19} والحرمانُ كلُّ الحرمان أن يغفل العبد عن هذا الأمر، ويشابه قوماً نسوا الله، وغفلوا عن ذكره والقيام بحقه وأقبلوا على حظوظ أنفسهم وشهواتها فلم ينجحوا ولم يحصلوا على طائل، بل أنساهم الله مصالح أنفسهم، وأغفلهم عن منافعها وفوائدها، فصار أمرهم فُرُطاً، فرجعوا بخسارة الدارين، وغُبِنوا غبناً لا يمكن تداركه ولا يُجبر كسرُه؛ لأنهم {هم الفاسقون} الذين خرجوا عن طاعة ربِّهم، وأوضعوا في معاصيه.
{19} Na kunyimwa kwa hakika ni mja kughafilika mbali na jambo hili, na ajifananishe na watu waliomsahau Mwenyezi Mungu, na wakaghafilika mbali na suala la kumtaja na kutekeleza haki zake, na wakayaendea mambo yenye faida kwao tu na matamanio ya nafsi zao, kwa hivyo hawakufanikiwa wala hawakuwa na manufaa yoyote. Bali Mwenyezi Mungu aliwasahaulisha masilahi ya nafsi zao, na akawaghafilisha mbali na manufaa yao na faida zao, kwa hivyo mambo yao yakawa ni kupita mipaka, kwa hivyo wakarudi na hasara ya nyumba zote mbili, na wakapunjwa kupunjwa ambako hakuwezi kurekebishika na haiwezekani kuunganisha kuvunjika kwake. Kwa sababu
“Hao ndio wavukao mipaka” ambao walitoka nje ya kumtii Mola wao Mlezi, na wakaingia muno katika kumuasi.
#
{20} فهل يستوي مَنْ حافظ على تقوى الله، ونظر لما قدَّم لغده فاستحقَّ جناتِ النعيم والعيش السليم مع الذين أنعم الله عليهم من النبيِّين والصدِّيقين والشُّهداء والصالحين، ومن غَفَل عن ذكره ونسي حقوقَه فشقي في الدُّنيا، واستحقَّ العذاب في الآخرة؛ فالأوَّلون هم الفائزون، والآخرون هم الخاسرون.
{20} Basi je, ni sawa yule anayeshikana na ucha Mungu, na akazingatia yale aliyoyatanguliza kwa ajili ya mustakbali wake, kwa hivyo akastahiki Bustani za mbinguni neema na maisha salama pamoja na wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha miongoni mwa Manabii, wakweli, na Mashahidi na walio wema. Na mwenye kughafilika mbali na kumtaja Mwenyezi Mungu na akasahau haki zake na akawa akawa mpotofu duniani na akastahiki adhabu Akhera? Basi wa mwanzo ndio waliofaulu, na wa mwisho ndio wenye hasara.
#
{21} ولمَّا بيَّن تعالى لعباده ما بيَّن، وأمر عباده ونهاهم في كتابه العزيز؛ كان هذا موجباً لأن يبادروا إلى ما دعاهم إليه وحثَّهم عليه، ولو كانوا في القسوة وصلابة القلوب كالجبال الرواسي؛ فإنَّ هذا القرآن لو أنزله {على جبل؛ لرأيته خاشعاً متصدعاً من خشية الله}؛ أي: لكمال تأثيره في القلوب؛ فإنَّ مواعظَ القرآن أعظمُ المواعظ على الإطلاق، وأوامره ونواهيه محتويةٌ على الحكم والمصالح المقرونة بها وهي من أسهل شيء على النفوس وأيسرها على الأبدان، خاليةٌ من التكلُّف ، لا تناقض فيها ولا اختلاف ولا صعوبة فيها ولا اعتساف، تصلُحُ لكل زمانٍ ومكانٍ، وتليقُ لكلِّ أحدٍ. ثم أخبر تعالى أنه يضرِبُ للناس الأمثال، ويوضِّح لعباده [في كتابه] الحلال والحرام؛ لأجل أن يتفكَّروا في آياته ويتدبَّروها؛ فإنَّ التفكر فيها يفتح للعبد خزائن العلم، ويبيِّن له طرق الخير والشرِّ، ويحثُّه على مكارم الأخلاق ومحاسن الشِّيم، ويزجرُه عن مساوئ الأخلاق؛ فلا أنفع للعبد من التفكُّر في القرآن والتدبُّر لمعانيه.
{21} Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowabainishia waja wake yale aliyoyabainisha, na akawaamrisha na akawakataza waja wake katika Kitabu chake kitukufu, hili lilikuwa ni jambo la kuwafanya kuharakisha kufanya kile alichowaitia na akawahimiza juu yake, hata kama walikuwa wagumu na wenye mioyo migumu kama milima madhubuti. Kwani Qur-ani hii lau ingeteremshwa
“juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu.” Hiyo ni kwa sababu ya athari yake kamili katika mioyo. Kwani mawaidha ya Qur-ani ndiyo mawaidha makubwa zaidi ya zama zote, na maamrisho yake na makatazo yake yana hukumu na masilahi yanayofungamana nayo, na ni miongoni mwa mambo mepesi zaidi kwa nafsi na miili, yasiyo na kujisumbua kukubwa, yasiyo na mgongano, wala kutofautiana, wala ugumu, wala kulazimishwa, ambayo yanafaa kwa kila wakati na mahali, na yanamfailia kila mtu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuambia kuwa anawapigia watu mifano, na anawawekea wazi waja wake
[katika Kitabu chake] halali na haramu; ili wazitafakari Aya zake na kuzizingatia. Kwani kuzitafakari kunamfungulia mja hazina za elimu, na kumbainishia njia za wema na uovu, na kunamhimiza juu ya maadili mema na mambo ya heshima, na kumkemea kutokana na maadili mabaya. Basi hakuna chenye manufaa zaidi kwa mja kuliko kuitafakari Qur-ani na kutafakari maana zake.
{هُوَ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ (22) هُوَ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ (23) هُوَ اللَّهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَى يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (24)}.
22. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyofichikana na yanayoonekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. 23. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anayefanya analolitaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo. 24. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima.
#
{22} هذه الآياتُ الكريماتُ قد اشتملت على كثيرٍ من أسماء الله الحسنى وأوصافه العُلى؛ عظيمة الشأن، وبديعة البرهان. فأخبر أنَّه {الله}: المألوه المعبودُ الذي {لا إله إلاَّ هو}: وذلك لكماله العظيم وإحسانه الشامل وتدبيره العامِّ، وكلُّ إله غيره ؛ فإنَّه باطلٌ لا يستحقُّ من العبادة مثقال ذرَّةٍ؛ لأنه فقيرٌ عاجزٌ ناقصٌ لا يملك لنفسه ولا لغيره شيئاً. ثم وصف نفسه بعموم العلم، الشامل لما غاب عن الخلق وما يشاهدونه. وبعموم رحمته، التي وسعتْ كلَّ شيء، ووصلتْ إلى كلِّ حيٍّ.
{22} Aya hizi tukufu zina majina mengi mazuri ya Mwenyezi Mungu na sifa zake za juu zaidi. Ni yenye cheo kikubwa sana, na ushahidi wa ajabu mno. Akasema kwamba Yeye ni
“Allah (Mwenyezi Mungu)” anayefanyiwa uungu, anayeabudiwa, ambaye
“hapana mungu isipokuwa Yeye tu.” Hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wake mkubwa, wema wake unaojumuisha kila kitu, na uendeshaji mambo wake wa jumla, na kila mungu asiyekuwa Yeye ni batili na hastahiki uzito wa chembe wa kuabudiwa. Kwa sababu yeye ni mhitaji mno, asiye na uwezo, mpungufu, asiyejimilikia mwenye wala wengine chochote. Kisha akajielezea kwamba ana elimu ya jumla, inayojumuisha yote yaliyofichikana kwa viumbe na yale wanayoyaona. Na akajielezea kwa rehema zake za jumla, ambazo zimeenea kila kitu na kukifikia kila kilicho hai.
#
{23} ثم كرَّر ذِكْر عموم إلهيَّته وانفراده بها، وأنَّه المالك لجميع الممالك؛ فالعالَم العلويُّ والسفليُّ وأهله، الجميع مماليكُ لله فقراءُ مدَبَّرون. {القدُّوسُ السلامُ}؛ أي: المقدَّس السالم من كل عيبٍ [وآفة] ونقص المعظَّم الممجَّد؛ لأنَّ القدوس يدلُّ على التنزيه من كل نقص والتعظيم لله في أوصافه وجلاله. {المؤمن}؛ أي: المصدِّق لرسله وأنبيائه بما جاؤوا به بالآيات البيِّنات والبراهين القاطعات والحجج الواضحات. {العزيز}: الذي لا يغالَب ولا يمانَع، بل قد قهر كلَّ شيءٍ، وخضع له كلُّ شيءٍ. {الجبار}: الذي قهر جميع العباد، وأذعن له سائرُ الخلق، الذي يجبرُ الكسيرَ ويغني الفقير. {المتكبِّر}: الذي له الكبرياء والعظمة، المتنزِّه عن جميع العيوب والظُّلم والجور. {سبحان الله عمَّا يشركونَ}: وهذا تنزيهٌ عامٌّ عن كلِّ ما وصفه به من أشرك به وعانده.
{23} Kisha akarudia kutaja jumla ya uungu wake na upekee wake katika hilo, na kwamba yeye ndiye mmiliki wa falme zote. Ulimwengu wa juu na wa chini na wakazi wake wote ni waja wa Mweneyezi Mungu, wahitaji mno, na wanaendeshwa naye.
“Mtakatifu, Mwenye salama.” Yaani, Mtakatifu, aliyesalimika na kila dosari,
[balaa], na mapungufu, anayetukuzwa, anayeheshimiwa. Kwa sababu utakatifu unaonyesha kutakasika kwake kutokana na mapungufu yote na kutukuzwa kwa Mwenyezi Mungu katika sifa na utukufu wake.
“Mtoaji wa amani” na pia ilisemekana kwamba maana yake ni mwenye kuwasadikisha Mitume na Manabii wake katika yale waliyokuja nayo kwa ishara zilizo wazi, na ushahidi wa kukata, na hoja zilizo wazi.
“Mwenye nguvu” ambaye hashindwi wala hazuiliki. Bali Yeye ameshinda kila kitu, na kila kitu kiko chini yake.
“Anayefanya analolitaka” ambaye aliwashinda waja wote, na viumbe vyote vikawa chini yake, ambaye anayewatia nguvu waliovunjika na kuwatajirisha masikini.
“Mkubwa” mwenye ukubwa wote, na ukuu, ambaye ametakasika kutokana na kasoro, dhuluma na ukandamizaji. “Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo.” Huku ni kumtakasa kwa jumla kutokana na kila alichoelezewa kwacho na wale wanaomshirikisha na kumkaidi.
#
{24} {هو اللهُ الخالقُ}: لجميع المخلوقات. {البارئ}: للمبروءات. {المصوِّر}: للمصوَّرات. وهذه الأسماء متعلِّقةٌ بالخلق والتدبير والتقدير، وأنَّ ذلك كله قد انفرد الله به لم يشارِكْه فيه مشاركٌ. {له الأسماءُ الحسنى}؛ أي: له الأسماء الكثيرة جدًّا، التي لا يُحصيها ولا يعلمها أحدٌ إلا هو ، ومع ذلك؛ فكلُّها حسنى؛ أي: صفات كمال، بل تدلُّ على أكمل الصفات وأعظمها، لا نقص في شيء منها بوجهٍ من الوجوه، ومن حسنها أنَّ الله يحبُّها ويحبُّ من يحبُّها ويحبُّ من عباده أن يدعوه ويسألوه بها. ومن كماله وأنَّ له الأسماء الحسنى والصفات العليا أنَّ جميع من في السماوات والأرض مفتقرون إليه على الدَّوام؛ يسبِّحون بحمده، ويسألونه حوائجهم، فيعطيهم من فضله وكرمه ما تقتضيه رحمتُه وحكمتُه. {وهو العزيزُ الحكيم}: الذي لا يريد شيئاً إلاَّ ويكون، ولا يكوِّن شيئاً إلاَّ لحكمةٍ ومصلحةٍ.
{24} “Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji” wa viumbe vyote.
“Mtengenezaji” wa kila kilichotengenezwa.
“Mtia sura” wa vyenye sura. Majina haya yanahusiana na uumbaji, uendeshaji na kupanga mambo, na kwamba yote haya yanafanywa na Mwenyezi Mungu pekee na hakuna anayeshiriki naye katika hayo. “Mwenye majina mazuri kabisa.” Yaani, ana majina mengi sana, ambayo hawezi kuyadhibiti wala kuyajua vyema isipokuwa yeye. Na pamoja na haya yote ni mzuri zaidi. Yaani, ni yenye sifa za ukamilifu, bali yanaashiria sifa kamilifu zaidi na kuu zaidi ambazo hazina upungufu wowote kwa njia yoyote ile. Na katika uzuri wake ni kwamba Mwenyezi Mungu anayapenda na anapenda mwenye kuyapenda, na anapenda kwamba waja wake wamuombe kwayo. Na katika ukamilifu wake na kwamba anayo majina mazuri zaidi na sifa za juu kabisa, ni kwamba kila aliye mbinguni na ardhini anamhitaji Yeye kila wakati. Wanamtakasa kwa sifa zake nzuri, na wanamwomba mahitaji yao, naye anawapa katika fadhila zake na ukarimu wake yale ambayo rehema na hekima yake vinahitaji.
“Naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima.” Ambaye hataki kitu isipokuwa kunakuwa. Na wala hafanyi kitu kuwa isipokuwa kwa hekima na masilahi.
Imekamilika tafsiri ya Sura hii.
***