:
Tafsiri ya Surat Al-Ahqaf
Tafsiri ya Surat Al-Ahqaf
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{حم (1) تَنْزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ (2) مَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُسَمًّى وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنْذِرُوا مُعْرِضُونَ (3)}.
1. Ha, Mim. 2. Uteremsho wa Kitabu uliotoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 3. Hatukuziumba mbingu na ardhi wala yaliyomo baina yake ila kwa haki na kwa muda maalumu. Na wale waliokufuru wanayapuuza yale wanayoonywa.
#
{2} هذا ثناءٌ منه تعالى على كتابه العزيز وتعظيمٌ له، وفي ضمن ذلك إرشادُ العباد إلى الاهتداء بنوره والإقبال على تدبُّر آياته واستخراج كنوزِهِ.
{2} Hii ni sifa itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Kitabu chake kitukufu pamoja na kukipa taadhima. Na ndani ya hayo kuna kuwaongoza waja kwenye kuongoka na nuru yake na kutafakari Aya zake na kutoa hazina zake.
#
{3} ولمَّا بيَّن إنزال كتابه المتضمِّن للأمر والنهي؛ ذكر خلقه السماواتِ والأرض، فجمع بين الخَلْق والأمر، {ألا له الخلقُ والأمر}؛ كما قال تعالى: {الله الذي خَلَقَ سبع سماواتٍ ومن الأرض مِثْلَهُنَّ يتنزَّلُ الأمرُ بينَهُنَّ}، وكما قال تعالى: {ينزِّلُ الملائكة بالرُّوح من أمرِهِ على مَن يشاءُ من عبادِهِ أنْ أنذِروا أنَّه لا إله إلا أنا فاتَّقونِ. خلقَ السمواتِ والأرض بالحقِّ}؛ فالله تعالى هو الذي خَلَقَ المكلَّفين، وخلق مساكِنَهم، وسخَّر لهم ما في السماوات وما في الأرض، ثم أرسل إليهم رسله، وأنزل عليهم كُتُبَه، وأمرهم ونهاهم، وأخبرهم أنَّ هذه الدارَ دارُ أعمال وممرٌّ للعمال، لا دار إقامة لا يرحلُ عنها أهلُها، وهم سينتقلون منها إلى دار الإقامة والقرارة وموطن الخلود والدوام، وإنَّما أعمالُهم التي عملوها في هذه الدار سيجدون ثوابها في تلك الدار كاملاً موفَّراً، وأقام تعالى الأدلَّة الدالَّة على تلك الدار، وأذاق العباد نموذجاً من الثواب والعقاب العاجل؛ ليكون أدعى لهم إلى طلب المحبوب والهرب من المرهوب، ولهذا قال هنا: {ما خَلَقْنا السمواتِ والأرضَ وما بينهما إلاَّ بالحقِّ}؛ أي: لا عبثاً ولا سدىً، بل ليعرف العبادُ عظمة خالقهما، ويستدلُّوا على كماله، ويعلموا أنَّ الذي خلقهما على عظمهما قادرٌ على أن يعيدَ العباد بعد موتِهِم للجزاء، وأنَّ خلقهما وبقاءهما مقدرٌ إلى أجل مسمًّى. فلما أخبر بذلك، وهو أصدق القائلين، وأقام الدليل، وأنار السبيل؛ أخبر مع ذلك أنَّ طائفةً من الخلق قد أبوا إلا إعراضاً عن الحقِّ وصدوفاً عن دعوة الرسل، فقال: {والذين كفروا عمَّا أُنذروا معرضون}. وأمَّا الذين آمنوا؛ فلمَّا علموا حقيقة الحال؛ قبلوا وصايا ربِّهم، وتلقَّوْها بالقبول والتسليم، وقابلوها بالانقياد والتعظيم، ففازوا بكلِّ خير، واندفع عنهم كلُّ شرٍّ.
{3} Na alipoeleza kuteremka kwa Kitabu chake chenye maamrisho na makatazo, akataja kuumba kwake mbingu na ardhi, na akaunganisha kati ya uumbaji na amri, akasema: "Fahamuni! Kuumba ni kwake, na amri." Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu ni yule ambaye aliziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yake." Na kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Huwateremsha Malaika na Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake ili nyinyi muonye kwamba hapana mungu ila Mimi, basi nicheni Mimi. Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki." Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyeumba viumbe wanaojukumishwa kisheria, akaumba maskani zao, na akawatiishia vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, kisha akawatumia Mitume wake, na akawateremshia Vitabu vyake, na akawaamrisha na akawakataza , na akawajulisha kwamba nyumba hii (ya duniani) ni nyumba ya matendo na mapito tu kwa watendao matendo, si nyumba ya kubakia ambayo watu wake hawatatoka wakaiacha, kisha watahama kutoka humo hadi kwenye nyumba ya kubakia na mahali pa makao ya milele na kudumu. Na hakika matendo yao waliyoyafanya katika nyumba hii watapata malipo yake katika nyumba hiyo kwa ukamilifu na kwa wingi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisimamisha sawasawa ushahidi unaoashiria nyumba hiyo, na akawaonjesha waja mfano wa malipo mazuri na adhabu ya sasa; ili iwatie moyo zaidi kutafuta wakipendacho na kukimbia wakiogopacho, na ndiyo maana akasema hapa: "Hatukuziumba mbingu na ardhi wala yaliyomo baina yake ila kwa haki." Yaani: si kwa ajili ya mchezo wala bure tu. Bali ili waja waujue ukuu wa Muumba wa viwili hivyo, na wavitumie kama ushahidi wa ukamilifu wake, na wajue kwamba yule aliyeviumba pamoja na ukubwa wake ana uwezo wa kuwarudisha waja baada ya kufa kwao kwa ajili ya malipo, na kwamba kuumbwa kwake na kusalia kwake kumepangwa vidumu kwa muda maalumu. Aliposema haya, na yeye ndiye mkweli zaidi wa wanaosema, na akasimamisha ushahidi juu yake, na akaiangaza njia, akasema pamoja na hayo kwamba kundi la viumbe walikataa isipokuwa kuipa mgongo haki na kuzuilia wito wa Mitume, akasema: "Na wale waliokufuru wanayapuuza yale wanayoonywa." Ama wale walioamini, walipojua uhakika wa hali hiyo, walikubali wasia wa Mola wao Mlezi, wakazipokea kwa kuzikubaliwa, wakajisalimisha kwazo, wakazifuata na kuzitukuza, basi wakapata kila la heri na wakazuilika na kila uovu.
: 4 - 6 #
{قُلْ أَرَأَيْتُمْ مَا تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِنْ قَبْلِ هَذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِنْ عِلْمٍ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (4) وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللَّهِ مَنْ لَا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَنْ دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ (5) وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ (6)}.
4. Sema: 'Je, mwawaona wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Nionyesheni wameumba nini katika ardhi; au hao wanao ushirika katika mbingu zote? Nileteeni Kitabu kilichokuwa kabla ya hiki, au alama yoyote ya elimu, ikiwa mnasema kweli. 5. Na ni nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama, na wala hata hawatambui maombi yao. 6. Na ambao watu watakapokusanywa watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao.
#
{4} أي: {قل}: لهؤلاء الذين أشركوا بالله أوثاناً وأنداداً لا تملك نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياة ولا نشوراً، قل لهم مبيناً عجز أوثانهم، وأنَّها لا تستحقُّ شيئاً من العبادة: {أروني ماذا خَلَقوا من الأرض أمْ لهم شِرْكٌ في السمواتِ}: هل خلقوا من أجرام السماوات والأرض شيئاً؟ هل خلقوا جبالاً؟ هل أجْرَوْا أنهاراً؟ هل نشروا حيواناً؟ هل أنبتوا أشجاراً؟ هل كان منهم معاونةٌ على خلق شيءٍ من ذلك؟ لا شيء من ذلك بإقرارهم على أنفسهم فضلاً عن غيرهم. فهذا دليلٌ عقليٌّ قاطعٌ على أنَّ كلَّ من سوى الله؛ فعبادتُه باطلةٌ. ثم ذكر انتفاء الدليل النقليِّ، فقال: {ائتوني بكتابٍ من قبل هذا}: الكتاب، يدعو إلى الشرك، {أو أثارةٍ من علم}: موروث عن الرسل يأمر بذلك. من المعلوم أنَّهم عاجزون أن يأتوا عن أحدٍ من الرسل بدليل يدلُّ على ذلك، بل نجزم ونتيقَّن أنَّ جميع الرسل دَعَوْا إلى توحيد ربِّهم ونَهَوْا عن الشرك به، وهي أعظم ما يؤثَر عنهم من العلم؛ قال تعالى: {ولقد بَعَثْنا في كلِّ أمةٍ رسولاً أنِ اعبدوا الله واجتنبوا الطاغوتَ}، وكلُّ رسول قال لقومه: {اعبُدوا الله ما لكم من إلهٍ غيرُه}، فعُلِمَ أنَّ جدال المشركين في شركهم غير مستندين على برهانٍ ولا دليل، وإنَّما اعتمدوا على ظنونٍ كاذبةٍ وآراءٍ كاسدةٍ وعقولٍ فاسدةٍ، يدلك على فسادها استقراء أحوالهم وتتبُّع علومهم وأعمالهم والنظرُ في حال من أفْنَوْا أعمارهم بعبادته؛ هل أفادهم شيئاً في الدُّنيا أو في الآخرة.
{4} Yaani, "Sema" ukiwaambia hao walioshirikisha Mwenyezi Mungu na masanamu na wenza ambavyo havimiliki manufaa wala madhara wala mauti wala uhai wala ufufuo. Waambie ukiwaelezea kutoweza kwa masanamu yao hayo, na kwamba hawastahiki kufanyiwa chochote katika ibada: "Nionyesheni wameumba nini katika ardhi; au hao wanao ushirika katika mbingu zote?" Je, waliumba chochote katika vyombo vya mbinguni na ardhini? Je, waliumba milima? Je, waliitiririsha mito? Je, walieneza mnyama yeyote? Je, waliotesha miti yoyote? Je, walisaidia kuumba chochote katika haya? Hakuna hata moja katika hayo tena kwa kukiri kwao wenyewe, mbali na kukiri kwa wengineo. Huu ni ushahidi kiakili wa uhakika kwamba kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu kuabudiwa kwacho ni batili. Kisha akataja kutokuwepo ushahidi wa kimaandiko, na akasema: "Nileteeni kitabu kabla ya hiki" Kitabu kinacholingania kwenye ushirikina, "au alama yoyote ya elimu" iliyorithiwa kutoka kwa Mitume wanaoamrisha hayo. Lakini kama inavyojulikana ni kuwa hawakuweza kuleta ushahidi wa jambo hilo kutoka kwa yeyote miongoni mwa Mitume unaooyesha hilo. Bali tuna yakini kwamba Mitume wote walilingania upweke Mola wao Mlezi na wakakataza kumshirikisha, na hii ndiyo elimu kubwa zaidi iliyopatwa kutoka kwao. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani." Basi ikajulikana kuwa upinzani wa washirikina kuhusiana na ushirikina wao hautegemei hoja wala ushahidi. Bali unategemea dhana batili na maoni potovu na akili mbovu, ambao unaonekana uovu wake kupitia kuzichunguza vyema hali zao, kufuatilia elimu zao na matendo yao, na kuziangalia hali za wale ambao wao waliharibu umri wao katika kuwaabudu. Je, waliwafaa chochote katika dunia au Akhera?
#
{5 - 6} ولهذا قال تعالى: {ومن أضلُّ ممَّن يدعو من دونِ الله من لا يستجيبُ له إلى يوم القيامةِ}؛ أي: مدة مقامه في الدنيا لا ينتفع به مثقال ذرَّة، {وهم عن دعائهم غافلون}: لا يسمعون منهم دعاءً ولا يجيبون لهم نداءً. هذا حالهم في الدُّنيا، ويوم القيامة يكفرون بشرككم، وإذا حُشِرَ الناس كانوا لهم أعداء يلعن بعضُهم بعضاً، ويتبرأ بعضُهم من بعض وكانوا بعبادتهم كافرين.
{5 - 6} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na ni nani mpotofu mkubwa kuliko hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama." Yaani, kwa muda wa kukaa kwake hapa duniani hata hatamfaa hata kwa uzani wa chembe. "Na wala hata hawatambui maombi yao," hawasikii dua zao wala hawaitikii wito wao. Hii ndiyo hali yao hapa duniani, na Siku ya Kiyama watakufuru shirki yenu hiyo, na watu watakapokusanywa watakuwa maadui kwao, wakilaaniana wao kwa wao, wakikataana wao kwa wao, na watazikufuru ibada zao hizo.
: 7 - 10 #
{وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ هَذَا سِحْرٌ مُبِينٌ (7) أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَلَا تَمْلِكُونَ لِي مِنَ اللَّهِ شَيْئًا هُوَ أَعْلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِ كَفَى بِهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ (8) قُلْ مَا كُنْتُ بِدْعًا مِنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَى إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُبِينٌ (9) قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كَانَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ وَكَفَرْتُمْ بِهِ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَى مِثْلِهِ فَآمَنَ وَاسْتَكْبَرْتُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ (10)}
7. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru husema juu ya haki inapowajia: 'Huu ni uchawi dhahiri.' 8. Au wanasema: 'Ameizua mwenyewe!' Sema: 'Ikiwa nimeizua mimi, basi nyinyi hamwezi kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Yeye anajua zaidi hayo mnayoropokwa; anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Na Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.' 9. Sema: 'Mimi si kitu kigeni miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi. Mimi nafuata niliyofunuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji wa wazi wazi.' 10. Sema: 'Mnaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakufuru, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.'
#
{7} أي: {وإذا تُتْلى}: على المكذِّبين {آياتُنا بيناتٍ}: بحيث تكون على وجهٍ لا يُمترى بها، ولا يشكُّ في وقوعها وحقِّها؛ لم تفِدْهم خيراً، بل قامت عليهم بذلك الحجة، ويقولون من إفكهم وإفترائهم {للحقِّ لمَّا جاءهم هذا سحرٌ مبينٌ}؛ أي: ظاهرٌ لا شكَّ فيه. وهذا من باب قلب الحقائق، الذي لا يروجُ إلاَّ على ضعفاء العقول، وإلاَّ؛ فبين الحقِّ الذي جاء به الرسولُ - صلى الله عليه وسلم - وبين السحر من المنافاة والمخالفة أعظم ممَّا بين السماء والأرض، وكيف يقاسُ الحقُّ ـ الذي علا وارتفع ارتفاعاً علا على الأفلاك، وفاق بضوئه ونوره نور الشمس، وقامت الأدلَّة الأفقيَّة والنفسيَّة عليه، وأقرَّت به، وأذعنت أولو البصائر والعقول الرزينة بالباطل الذي هو السحرُ الذي لا يصدُرُ إلاَّ من ضالٍّ ظالمٍ خبيث النفس خبيث العمل؛ فهو مناسبٌ له وموافقٌ لحاله؟! وهل هذا إلاَّ من البهرجة؟!
{7} Yaani, "Na wanaposomewa" hao wanaokadhibisha "Aya zetu zilizo wazi" kwa njia ambayo haiwezekani kuzitilia shaka, wala haiwezekani kuwa na shaka katika kutokea kwake na uhakika wake, hayo hayawanufaishi kwa chochote. Bali wanasimamishiwa hoja kwa hilo, nao "husema juu ya haki inapowajia: 'Huu ni uchawi dhahiri'" usiokuwa na shaka yoyote. Hii ni katika mbinu za kubadilisha uhakika ambayo haiwezi kuenea isipokuwa kwa watu wenye maono dhaifu. Vinginevyo, kati ya haki aliyoileta Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na uchawi una kupingana na kuhalifiana kukubwa zaidi kuliko kule ambako kuko baina ya mbingu na ardhi. Na vipi inaweza kupimwa haki - iliyotukuka na kunyanyuka juu zaidi ya sayari na mwanga wake na nuru yake vikashinda nuru ya jua, na ukasimama ushahidi wa kiupeo wa macho na wa wa kinafsi juu yake, na wakaikiri na kuinyenyekea wale wenye maovu mazuri mno na akili timamu. Hii inawezaje kuwa sawa na batili ambayo ni uchawi ambao hautokani ispokuwa kwa mpotofu, dhalimu, mwenye roho chafu na matendo machafu. Je, hili linamfailia na kuendana na hali yake? Na je, hili si chochote ila kupamba uovu?
#
{8} {أم يقولون افتراه}؛ أي: افترى محمدٌ هذا القرآن من عند نفسه؛ فليس من عند الله، {قل} لهم: {إن افتريتُهُ}؛ فالله عليَّ قادرٌ وبما تفيضون فيه عالمٌ؛ فكيف لم يعاقبني على افترائي الذي زعمتم؛ فهل {تملِكون لي من الله شيئاً}: إنْ أرادني الله بضرٍّ أو أرادني برحمةٍ؟ {كفى به شهيداً بيني وبينَكم}: فلو كنت متقولاً عليه؛ لأخذ مني باليمين، ولعاقبني عقاباً يراه كلُّ أحدٍ؛ لأنَّ هذا أعظم أنواع الافتراء لو كنت متقوِّلاً. ثم دعاهم إلى التوبة مع ما صدر منهم من معاندة الحقِّ ومخاصمته، فقال: {وهو الغفورُ الرحيم}؛ أي: فتوبوا إليه، وأقلعوا عما أنتم فيه يغفر لكم ذنوبكم، ويرحمكم فيوفقكم للخير، ويثيبكم جزيل الأجر.
{8} ''Au wanasema: 'Ameizua mwenyewe!'" Yaani, je, wanasema kwamba Muhammad ameizua Qur-ani hii yeye mwenyewe, na siyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. "Sema" ukiwaambia: "Ikiwa nimeizua mimi," basi Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kuniadhibu na anajua vyema yote mnayoropokwa. Basi kwa nini hakuniadhibu kwa kusingizia kwangu huku ambako mlidai? Je, "basi nyinyi mnaweza kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu" ikiwa Mwenyezi Mungu atataka kunidhuru au atataka kunirehemu? "Anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi." Kwani, kama ningekuwa ninazungumza uongo juu yake, basi angalinichukua kwa mkono wa kulia, na angeniadhibu adhabu ambayo kila mtu angeiona. Kwa sababu hii ndiyo aina kubwa zaidi ya uzushi ikiwa ningekuwa nimezungumza uongo juu yake. Kisha akawaita watubu pamoja na yale waliyofanya ya kukaidi na kuipinga haki. Akasema: "Na Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu." Yaani, tubieni kwake, na muache hayo mliyo ndani yake, atawasamehe dhambi zenu, na atawahurehemu, na awawezeshe kuifikia heri, kisha atawalipa malipo makubwa.
#
{9} {قلْ ما كنتُ بدعاً من الرُّسل}؛ أي: لست بأول رسول جاءكم حتى تستغربوا رسالتي وتستنكروا دعوتي؛ فقد تقدَّم من الرسل والأنبياء من وافقت دعوتي دعوتهم؛ فلأيِّ شيء تنكرون رسالتي؟! {وما أدري ما يُفْعَلُ بي ولا بكم}؛ أي: لست إلاَّ بشراً، ليس بيدي من الأمر شيء، والله تعالى [هو] المتصرِّفُ بي وبكم، الحاكم عليَّ وعليكم، ولست آتي بالشيء من عندي. {وما أنا إلاَّ نذيرٌ مبينٌ}: فإنْ قبلتُم رسالتي وأجبتُم دعوتي؛ فهو حظُّكم ونصيبُكم في الدُّنيا والآخرة، وإن رددتُم ذلك عليَّ؛ فحسابُكم على الله، وقد أنذرْتكم، ومن أنذر فقد أعذر.
{9} "Sema: 'Mimi si kitu kigeni miongoni mwa Mitume." Yaani, mimi sikuwa mtume wa kwanza kuja ndiyo mnastaajabishwa na ujumbe wangu na kukataa wito wangu. Bali wamekwisha kuja Mitume na Manabii kabla yangu ambao ujumbe wangu unakubaliana na wao. Basi kwa nini mnaukataa ujumbe wangu? "Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi." Yaani, mimi si chochote ila ni mwanadamu tu, sina mamlaka yoyote. Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayeniendesha mimi na nyinyi. Siwezi kuleta chochote mimi mwenyewe, "wala mimi si chochote ila ni mwonyaji wa wazi wazi." Kwa hivyo, ikiwa mtakubali ujumbe wangu na kuuitikia wito wangu, basi hiyo ndiyo bahati yenu na fungu lenu katika dunia na akhera. Na ikiwa mtakataa hayo kutoka kwangu, basi hesabu yenu iko kwa Mwenyezi Mungu, na tayari nimeshawaonya. Na mwenye kuonya, basi amejitoa lawamani.
#
{10} {قل أرأيتُم إن كان من عندِ الله وكفرتُم به وشَهِدَ شاهدٌ من بني إسرائيل على مثلِهِ فآمن واستكبرتُم}؛ أي: أخبروني لو كان هذا القرآن من عند الله، وشهد على صحَّته الموفَّقون من أهل الكتاب، الذين عندهم من الحقِّ ما يعرفون أنَّه الحقُّ، فآمنوا به واهتدَوْا، فتطابقتْ أنباء الأنبياء وأتباعهم النبلاء واستكبرتُم أيُّها الجهلاء الأغبياء؛ فهل هذا إلا أعظم الظلم وأشدُّ الكفر؟! {إنَّ الله لا يهدي القوم الظالمين}: ومن الظُّلم الاستكبار عن الحقِّ بعد التمكُّن منه.
{10} "Sema: 'Mnaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakufuru, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini." Yaani, niambieni ikiwa hii Qur-ani ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wale waliowezeshwa kufikia heri katika Watu wa Kitabu wakashuhudia kwamba ni sahihi, wale ambao wanayo haki wanayojua kwayo kuwa hii ni haki tupu, wakaiamini na kuongoka. Basi habari za Manabii na wafuasi wao wenye maono mazuri zikakubaliana, na nyinyi enyi wajinga wapumbavu mkatakabari, je, hii si dhuluma kubwa zaidi na ukafiri mkubwa mno? "Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu." Na kutoka katika dhuluma ni kutakabaria haki baada ya kuweza kuifuata.
: 11 - 12 #
{وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا لَوْ كَانَ خَيْرًا مَا سَبَقُونَا إِلَيْهِ وَإِذْ لَمْ يَهْتَدُوا بِهِ فَسَيَقُولُونَ هَذَا إِفْكٌ قَدِيمٌ (11) وَمِنْ قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَى إِمَامًا وَرَحْمَةً وَهَذَا كِتَابٌ مُصَدِّقٌ لِسَانًا عَرَبِيًّا لِيُنْذِرَ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَبُشْرَى لِلْمُحْسِنِينَ (12)}.
11. Na wale waliokufuru waliwaambia wale walioamini: 'Lau kuwa hii ni heri, wasingelitutangulia kuifikia.' Na walipokosa kuongoka, wakasema: 'Huu ni uzushi mkubwa wa zamani.' 12. Na kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa, kuwa chenye uwongozi na rehema. Na hiki ni Kitabu cha kusadikisha na kilichokuja kwa lugha ya Kiarabu, ili kiwaonye wale waliodhulumu, na kiwe ni bishara njema kwa watendao mema.
#
{11 - 12} أي: قال الكفار بالحقِّ معاندين له ورادِّين لدعوته: {لو كان خيراً ما سبقونا إليه}؛ أي: ما سَبَقَنا إليه المؤمنون، أي: لكنّا أول مبادرٍ به وسابق إليه! وهذا من البهرجة في مكان؛ فأيُّ دليل يدلُّ على أنَّ علامة الحقِّ سبق المكذبين به للمؤمنين؟! هل هم أزكى نفوساً؟! أم أكمل عقولاً؟! أم الهدى بأيديهم؟! ولكن هذا الكلام الذي صدر منهم يعزُّون به أنفسهم، بمنزلة من لم يقدرْ على الشيء ثم طَفِقَ يذمُّه، ولهذا قال: {وإذْ لم يَهْتَدوا به فسيقولونَ هذا إفكٌ قَديمٌ}؛ أي: هذا السبب الذي دعاهم إليه أنهم لما لم يهتدوا بهذا القرآن، وفاتهم أعظمُ المواهب وأجلُّ الرغائب؛ قدحوا فيه بأنَّه كذبٌ، وهو الحقُّ الذي لا شكَّ فيه ولا امتراء يعتريه، {الذي} قد وافق الكتب السماويَّة، خصوصاً أكملها وأفضلها بعد القرآن، وهي التوراة التي أنزلها الله على {موسى إماماً ورحمة}؛ أي: يقتدي بها بنو إسرائيل ويهتدون بها، ويحصُلُ لهم خير الدنيا والآخرة. {وهذا}: القرآن {كتابٌ مصدقٌ}: للكتب السابقة، شهد بصدِقها وصدَّقها بموافقته لها، وجَعَلَه الله {لساناً عربيًّا}: ليسهل تناوله ويتيسر تذكُّره؛ {لينذر الذين ظلموا}: أنفسهم بالكفر والفسوق والعصيان إن استمرُّوا على ظلمهم بالعذاب الوبيل، ويبشر المحسنين في عبادة الخالق وفي نفع المخلوقين بالثواب الجزيل في الدُّنيا والآخرة، ويذكِّر الأعمال التي ينذر عنها والأعمال التي يبشر بها.
{11 - 12} Yaani, Makafiri walisema juu ya haki wakiifanyia ukaidi na kuikataa wito wake: "Lau kuwa hii ni heri, wasingelitutangulia kuifikia." Yaani, waumini wasingetutangulia kuifikia. bali tungekuwa sisi ndio wa kwanza kuikimbilia na kuifuata! Lakini haya ni hoja isiyo na msingi. Kwani ni ushahidi gani unaonyesha kwamba alama ya haki ni kwamba wanaokadhibisha watangulie waumini kuifuata? Je, wao ndio wana nafsi safi zaidi? Au wao ndio wenye akili kamili zaidi? Au kuongoa kuko mikononi mwao? Lakini maneno haya yanayotoka kwao wanayojifariji kwayo tu ni kama vile mtu asiyeweza kitu kisha akaanza kukikashifu. Ndiyo maana alisema: "Na walipokosa kuongoka, wakasema: "Huu ni uzushi mkubwa wa zamani." Yaani, hii ndiyo sababu iliyowafanya kusema hivyo, nayo ni kwamba waliposhindwa kuongoka kwa Qur-ani hii, na wakakosa tunu kubwa zaidi na mambo makubwa zaidi yanayotamaniwa, wakaikashifu kwamba ni uongo, ilhali hiyo ndiyo haki isiyokuwa na shaka wala utata wowote, "ambayo" inakubaliana na Vitabu vya mbinguni vinginevyo, hasa kitabu kamili na bora zaidi baada ya Qur-ani, yaani Taurati ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa "Musa kuwa chenye uwongozi na rehema." Yaani, ili Wana wa Israili waifuate na waongoke kwayo, na wapate heri ya dunia na akhera. "Na hii" Qur-ani "ni kitabu chenye kuthibitisha" vitabu vya awali, inashuhudia ukweli wake na kuvisadikisha kwa kuafikiana navyo, na Mwenyezi Mungu akaifanya kuwa "kwa lugha ya Kiarabu" ili iwe rahisi kuielewa na kuikumbuka, "ili kiwaonye wale waliodhulumu" nafsi zao kwa ukafiri, kuvuka mipaka na uasi, ikiwa wataendelea na dhuluma yao hiyo adhabu kali, na awabashirie wafanyao vizuri katika kumuabudu Muumba na katika kuwafaidi viumbe kwa thawabu nyingi katika dunia na akhera, na kuwakumbusha matendo ambayo anawaonya dhidi yake na matendo ambayo yanahusiana na bishara njema.
: 13 - 14 #
{إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (13) أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (14)}.
13. Hakika wale waliosema: 'Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu' kisha wakanyooka sawasawa, hawatakuwa na hofu, wala hawatahuzunika. 14. Hao ndio watu wa Bustani za mbinguni, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{13} أي: إنَّ الذين أقرُّوا بربِّهم، وشهدوا له بالوحدانيَّة، والتزموا طاعته، وداموا على ذلك، و {استقاموا} مدَّة حياتهم؛ {فلا خوفٌ عليهم}: من كل شرٍّ أمامهم، {ولا هم يحزنونَ}: على ما خلَّفوا وراءهم.
{13} Yaani, hakika wale waliokubali Mola wao Mlezi, wakashuhudilia upweke, wakashikamana na utiifu na wakaendelea hivyo, na "wakanyooka sawasawa" katika muda wa maisha yao yote "basi hawatakuwa na hofu" kutokana na kila ovu lililo mbele yao," wala hawatahuzunika" juu ya yale waliyoyaacha nyuma yao.
#
{14} {أولئك أصحابُ الجنَّة}؛ أي: أهلها الملازمون لها، الذين لا يبغون عنها حِوَلاً ولا يريدونَ بها بدلاً، {خالدين فيها جزاءً بما كانوا يعملونَ}: من الإيمان بالله، المقتضي للأعمال الصالحة، التي استقاموا عليها.
{14} "Hao ndio watu wa Bustani za mbinguni." Yaani, wakazi wake wa milele, ambao hawatataka kuondoka humo wala hawatataka kupewa chochote badala yake, "watadumu humo, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyatenda," kama vile kumuamini Mwenyezi Mungu ambako kunalazimu kufanya matendo mema, ambayo walinyooka sawasawa juu yake.
: 15 - 16 #
{وَوَصَّيْنَا الْإِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا حَتَّى إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ (15) أُولَئِكَ الَّذِينَ نَتَقَبَّلُ عَنْهُمْ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَنَتَجَاوَزُ عَنْ سَيِّئَاتِهِمْ فِي أَصْحَابِ الْجَنَّةِ وَعْدَ الصِّدْقِ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ (16)}.
15. Na tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thelathini. Hata anapofika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: 'Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayoyapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu.' 16. Hao ndio tunaowapokelea bora ya vitendo vyao walivyovitenda, na tunayasamehe makosa yao. Watakuwa miongoni mwa watu wa Bustani za mbinguni. Miadi ya kweli hiyo waliyokuwa wakiahidiwa.
#
{15} هذا من لطفه تعالى بعباده وشكره للوالدين أن وصَّى الأولاد وعهد إليهم أن يحسنوا إلى والديهم بالقول اللطيف والكلام الليِّن وبَذْل المال والنفقة وغير ذلك من وجوه الإحسان، ثم نبَّه على ذكر السبب الموجب لذلك، فذكر ما تحمَّلته الأمُّ من ولدها، وما قاستْه من المكاره وقت حَمْلِها، ثم مشقَّة ولادتها المشقَّة الكبيرة، ثم مشقَّة الرضاع وخدمة الحضانة، وليست المذكوراتُ مدة يسيرة ساعة أو ساعتين، وإنما ذلك مدة طويلة قدرها {ثلاثون شهراً}: للحمل تسعة أشهر ونحوها، والباقي للرضاع، هذا الغالب. ويستدلُّ بهذه الآية مع قوله: {والوالداتُ يرضِعْن أولادهنَّ حولينِ كاملينِ}: أنَّ أقلَّ مدَّة الحمل ستة أشهر؛ لأنَّ مدَّة الرضاع وهي سنتان إذا سقطت منها السنتان؛ بقي ستة أشهر مدة للحمل، {حتى إذا بلغ أشُدَّه}؛ أي: نهاية قوَّته وشبابه وكمال عقله، {وبَلَغَ أربعين سنةً قال ربِّ أوْزِعْني}؛ أي: ألهمني ووفقني، {أنْ أشكر نعمتَك التي أنعمتَ عليَّ وعلى والديَّ}؛ أي: نعم الدين ونعم الدنيا، وشكره بصرف النعم في طاعة مسديها وموليها ومقابلة منَّته بالاعتراف والعجز عن الشكر والاجتهاد في الثناء بها على الله، والنعم على الوالدين نعم على أولادهم وذُرِّيَّتهم لأنَّهم لا بدَّ أن ينالهم منها ومن أسبابها وآثارها، خصوصاً نعم الدين؛ فإنَّ صلاح الوالدين بالعلم والعمل من أعظم الأسباب لصلاح أولادهم، {وأنْ أعمل صالحاً ترضاه}: بأنْ يكونَ جامعاً لما يصلِحُه سالماً مما يفسِدُه؛ فهذا العمل الذي يرضاه الله ويقبله ويثيبُ عليه، {وأصلحْ لي في ذُرِّيَّتي}: لما دعا لنفسه بالصلاح؛ دعا لذرِّيَّته أن يصلح الله أحوالهم، وذكر أنَّ صلاحهم يعود نفعه على والديهم؛ لقوله: {وأصلِحْ لي}. {إني تبتُ إليك}: من الذَّنوب والمعاصي ورجعت إلى طاعتك، {وإنِّي من المسلمين}.
{15} Hii ni kutokana na huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwashukuru wazazi kwa kuwausia watoto wao na kuwaamuru wawafanyie wema wazazi wao kwa maneno mazuri na laini, na kutumia mali na matumizi mengine mazuri kwa ajili yao. Kisha akaeleza sababu ya jambo hilo, akataja jinsi mama anavyobeba mimba ya mtoto wake, na jinsi alivyoteseka wakati wa ujauzito wake, kisha taabu kubwa zaidi ya kuzaa, kisha taabu ya kunyonyesha na kumlea. Na haya yaliyotajwa si muda mfupi wa saa moja au mbili, bali ni muda mrefu wa "miezi thelathini" kwa ujauzito miezi tisa au karibu na hapo, na muda uliobakia ni wa kunyonyesha katika, hali ya kawaida. Na aya hii pamoja na kauli yake: "Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili," zinatumika kama ushahidi kwamba muda mfupi zaidi wa ujauzito ni miezi sita. Kwa sababu muda wa kunyonyesha ni miaka miwili, nayo ikipunguzwa kutoka kwa muda huo wa miezi thelathini inasalia miezi sita ya ujauzito. "Hata anapofika utu uzima wake;" yaani, hali ya juu zaidi ya nguvu zake na ujana wake na ukamilifu wa akili yake, "na akafikilia miaka arobaini, husema: "Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu." Yaani, neema za dini na za dunia, na kumshukuru kwa kutumia neema zake katika kumtii aliyezineemeesha na kuzitoa, na kuzikubali neema zake kwa kuzitambua na kushindwa kushukuru vilivyo na kujitahidi kumsifu Mwenyezi Mungu kwa neema hizo. Na neema juu ya wazazi ni neema juu ya watoto wao na kizazi chao; kwa sababu ni lazima zitawafikia wao sababu zake na athari zake, hasa neema ya dini; kwa kuwa kutengenea kwa kwa wazazi kwa elimu na matendo mema ni miongoni mwa sababu kubwa za kutengenea kwa watoto wao. "Na nitende mema unayoyaridhia" kwa kujumuisha kati ya yenye kumfanya kutengenea na kumfanya kuwa salama mbali yenye kumharibu. Basi haya ndiyo matendo ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu anayaridhia, kuyakubali na kupeana thawabu juu yake. "Na unitengenezee dhuriya zangu." Baada ya kujiombea mwenyewe wema, akakiombea kizazi chake kwamba Mwenyezi Mungu azifanye hali zao kuwa njema, na akataja kwamba kutengenea kwao inarudi faida yake kwa wazazi wao kwa kauli yake: "Na unitengenezee" kisha akasema: "Hakika mimi nimetubu kwako" kutoka kwa dhambi na maasia na nimerudi katika utiifu wako, "na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu."
#
{16} {أولئك}: الذين ذكرت أوصافهم {الذين نتقبَّلُ عنهم أحسنَ ما عملوا}: وهو الطاعاتُ؛ لأنَّهم يعملون أيضاً غيرها، {ونتجاوزُ عن سيِّئاتِهم في}: جملة {أصحاب الجنة}: فحصل لهم الخيرُ والمحبوبُ، وزال عنهم الشرُّ والمكروه. {وعدَ الصِّدْقِ الذي كانوا يوعدونَ}؛ أي: هذا الوعدُ الذي وعَدْناهم هو وعدٌ صادقٌ من أصدق القائلين الذي لا يُخلف الميعادَ.
{16} "Hao" ambao sifa zao nimetaja "tunaowapokelea bora ya vitendo vyao walivyovitenda" navyo vile vya utiifu; kwa sababu wao pia hufanya mambo mengineyo, "na tunayasamehe makosa yao. Watakuwa miongoni mwa watu wa Bustani za mbinguni" kwa hivyo wakapata heri na wakipendacho, na wakaepushwa na uovu na wakichukiacho. "Miadi ya kweli hiyo waliyokuwa wakiahidiwa" kutoka kwa mkweli zaidi wa wasemao wote ambaye havunji miadi.
: 17 - 19 #
{وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَكُمَا أَتَعِدَانِنِي أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ الْقُرُونُ مِنْ قَبْلِي وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ اللَّهَ وَيْلَكَ آمِنْ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (17) أُولَئِكَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِمْ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ (18) وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِمَّا عَمِلُوا وَلِيُوَفِّيَهُمْ أَعْمَالَهُمْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (19)}.
17. Na yule aliyewafyonya wazazi wake: 'Uff kwenu nyote. Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwishapita kabla yangu!' Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtoto wao): 'Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.' Na yeye husema: 'Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale.' 18. Hao ndio ambao imehakikikishwa hukumu juu yao kama mataifa yaliyokwisha pita kabla yao miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa wenye kuhasiri. 19. Na wote watakuwa na daraja zao mbalimbali kwa waliyoyatenda, na ili awalipe kwa ukamilifu kwa vitendo vyao, na wala hawatadhulumiwa.
#
{17} لما ذكر تعالى حالَ الصالح البارِّ لوالديه؛ ذكر حالة العاقِّ، وأنَّها شرُّ الحالات، فقال: {والذي قال لوالديه}: إذ دعياه إلى الإيمان بالله واليوم الآخر، وخوَّفاه الجزاء، وهذا أعظم إحسان يصدُرُ من الوالدين لولدهما أن يَدْعُواه إلى ما فيه سعادتُه الأبديَّة وفلاحه السرمديُّ، فقابلهما بأقبح مقابلة، فقال: {أفٍّ لكُما}؛ أي: تبًّا لكما، ولما جئتما به. ثم ذكر وجه استبعادِه وإنكاره لذلك، فقال: {أتعدانِني أنْ أُخْرَجَ}: من قبري إلى يوم القيامة {وقد خلتِ القرونُ من قبلي}: على التكذيب، وسلفوا على الكفر، وهم الأئمَّة المقتدى بهم لكلِّ كفورٍ وجهول ومعاندٍ. {وهما}؛ أي: والداه {يستغيثان الله}: عليه ويقولان له: {ويلكَ آمِنْ}؛ أي: يبذلان غاية جهدهما ويسعيان في هدايته أشدَّ السعي، حتى إنَّهما من حرصهما عليه إنهما يستغيثان الله له استغاثةَ الغريق، ويسألانه سؤال الشريق، ويعذلان ولدهما، ويتوجَّعان له، ويبيِّنان له الحقَّ، فيقولان: {إنَّ وعد الله حقٌّ}، ثم يقيمان عليه من الأدلَّة ما أمكنهما، وولدُهما لا يزداد إلا عتوًّا ونفوراً واستكباراً عن الحقِّ وقدحاً فيه، {فيقول ما هذا إلاَّ أساطير الأولينَ}؛ أي: إلا منقولٌ من كتب المتقدِّمين، ليس من عند الله، ولا أوحاه الله إلى رسوله، وكل أحدٍ يعلم أنَّ محمداً - صلى الله عليه وسلم - أميٌّ لا يكتب ولا يقرأ، ولا يتعلَّم من أحد؛ فمن أين يتعلَّمه، وأنَّى للخلق أن يأتوا بمثل هذا القرآن ولو كان بعضُهم لبعضٍ ظهيراً؟!
{17} Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja hali ya mwema na mtiifu kwa wazazi wake, akataja hali ya yule asiye mtiifu kwao, na kwamba ndiyo hali mbaya zaidi. Basi akasema: "Na yule aliyewafyonya wazazi wake" walipomwita kuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakamhofisha kwa malipo mabaya, na huu ndio wema mkubwa zaidi unaoweza kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto wao kwa kumlingania kwenye kile kinachomletea furaha ya milele na mafanikio ya kudumu, lakini yeye akakabiliana nao kwa kukabiliana kuovu zaidi, akasema: 'Uff kwenu nyote' na muangamie na hayo mnayoniambia. Kisha akataja sababu ya kuona kwake kwamba hilo haliwezekani na kulikataa kwake, akasema: "Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa" kutoka kaburini mwangu Siku ya Kiyama "na hali vizazi vingi vimekwisha pita kabla yangu!" Wakikadhibisha haya wakapita hivyo kwa ukafiri ilhali walikuwa viongozi wanaoigwa na kila kafiri, mjinga na mkaidi. "Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu" dhidi yake wakisema: "Na wote wawili;" yaani, wazazi wake "wanamlilia Mwenyezi Mungu;" na wanamwambia: "Ole wako, amini." Yaani, wanajitahidi kwa nguvu zote na wanafanya juhudi kubwa kumwelekeza, hadi wanavyokuwa na wasi wasi naye wanamlilia Mwenyezi Mungu kama vile aliyezama baharini, na wanamuomba kama vile aliye na kiu, wanamnyooshea mkono, na wanateseka kwa ajili yake, wanamueleza ukweli, wakisema: "Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli," kisha wanamsimamishia ushahidi namna wawezavyo, lakini mtoto wao hazidishi ila ukaidi, kujiweka mbali, kuitakabaria haki na kuikashifu. "Naye husema: Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale." Yaani hadithi zilizopokewa kutoka kwa vitabu vya waliotangulia, si kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wala Mwenyezi Mungu hakuyafunulia Mtume wake, ilhali kila mtu anajua kwamba Muhammad - rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - hakuwa anaweza kusoma wala kuandika, na hakuwa akijifunza kutoka kwa yeyote. Basi je, alijifunzia haya wapi? Na viumbe wanawezaje kuleta mfano wa Qur-ani hii hata kama watasaidiana wao kwa wao?
#
{18} {أولئك الذين}: بهذه الحالة الذَّميمة {حقَّ عليهم القولُ}؛ أي: حقَّت عليهم كلمة العذاب {في} جملة {أمم قد خَلَتْ من قبلهم من الجنِّ والإنس}: على الكفر والتكذيب، فسيدخل هؤلاء في غمارهم، ويغرقون في تيَّارهم. {إنَّهم كانوا خاسرينَ}: والخسران فواتُ رأس مال الإنسان، وإذا فقد رأسَ مالِهِ؛ فالأرباح من باب أولى وأحرى؛ فهم قد فاتهم الإيمان، ولم يحصِّلوا شيئاً من النعيم، ولا سلموا من عذاب الجحيم.
{18} "Hao" walio katika hali hii mbaya "ndio ambao imehakikikishwa hukumu juu yao kama mataifa yaliyokwisha pita kabla yao miongoni mwa majini na watu" kwa sababu ya ukafiri wao na kukadhibisha kwao. Kwa hivyo hawa wataingia katika kundi lao, na watazamia katika mawimbi yao. "Hakika hao wamekuwa wenye kuhasiri." Na kama inavyojulikana kwamba hasara ni kupoteza mtaji, basi kupoteza ndilo linawezekana zaidi. Hao walikosa imani, na hawakupata neema yoyote, na wala hawakuepuka mbali na adhabu ya Motoni.
#
{19} {ولكلٍّ}: من أهل الخير وأهل الشرِّ {درجاتٌ مما عملوا}؛ أي: كلٌّ على حسب مرتبته من الخير والشرِّ، ومنازلهم في الدار الآخرة على قدر أعمالهم، ولهذا قال: {ولِيُوَفِّيهم أعمالَهم وهم لا يُظْلَمونَ}: بأن لا يزاد في سيِّئاتهم ولا ينقصَ من حسناتِهِم.
{19} "Na kila mmoja" miongoni mwa watu wema na watu waovu "watakuwa na daraja zao mbalimbali kwa waliyoyatenda" kila mmoja kulingana na kiwango chake katika wema na uovu, na viwango vyao hivi katika maisha ya akhera ni kulingana na matendo yao. Ndiyo sababu akasema: "Na ili awalipe kwa ukamilifu kwa vitendo vyao, na wala hawatadhulumiwa" kwa namna kwamba hawatazidishiwa chochote katika mabaya yao wala hakitapunguzwa kitu katika mema yao.
: 20 #
{وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَاتِكُمْ فِي حَيَاتِكُمُ الدُّنْيَا وَاسْتَمْتَعْتُمْ بِهَا فَالْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنْتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنْتُمْ تَفْسُقُونَ (20)}.
20. Na siku watakapoletwa wale waliokufuru kwenye Moto, wataambiwa: 'Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani, na mkajistarehesha navyo. Basi leo ndio mnalipwa adhabu ya fedheha kwa yale mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa sababu mlikuwa mkivuka mipaka.'
#
{20} يذكر تعالى حال الكفار عند عرضهم على النار حين يُوَبَّخون ويُقَرَّعون، فيقال لهم: {أذهبتم طيباتِكُم في حياتكم الدُّنيا}؛ حيث اطمأننتم إلى الدُّنيا، واغتررتم بلذَّاتها، ورضيتم بشهواتها، وألهتكم طيِّباتُها عن السعي لآخرتكم، وتمتَّعتم تمتُّع الأنعام السارحة؛ فهي حظُّكم من آخرتكم. {فاليوم تُجْزَوْنَ عذاب الهون}؛ أي: العذاب الشديد الذي يهينكم، ويفضحكم [بما كنتُم تقولون على الله غير الحقِّ] ؛ أي: تنسبون الطريق الضالَّة التي أنتم عليها إلى الله وإلى حكمِهِ وأنتم كَذَبة في ذلك، {وبما كنتُم تفسُقونَ}؛ أي: تتكبَّرون عن طاعته، فجمعوا بين قول الباطل والعمل بالباطل والكذب على الله بنسبته إلى رضاه والقدح في الحقِّ والاستكبار عنه، فعوقبوا أشدَّ العقوبة.
{20} Mwenyezi Mungu anataja hali ya makafiri wanapopelekwa kwenye Moto wakati wanapokaripiwa na kukemewa, wanapoambiwa: "Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani" ambapo mlijituliza kwa maisha ya dunia, mkadanganyika na raha zake, mkaridhika na matamanio yake, na raha zake zikawapumbaza mkaacha kutafuta maisha ya akhera yenu, mkifurahia kama vile wanyama walioachiliwa kula huru. Basi hayo ndiyo fungu lenu la akhera. "Basi leo ndiyo mnalipwa adhabu ya fedheha" na kuwadunisha [kwa sababu ya mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki]. Yaani, mnainasibisha njia yenu mbovu kwa Mwenyezi Mungu na hukumu yake ilhali nyinyi ni waongo katika hilo "na kwa sababu mlikuwa mkivuka mipaka." Basi wakajumuisha kati ya batili na kuitendea kazi batili hiyo na kumdanganyishia Mwenyezi Mungu kwa kuunasibisha uwongo huo na radhi zake na kuikashifu haki na kuitakabaria. Basi wakaadhibiwa kwa adhabu kali mno.
: 21 - 26 #
{وَاذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنْذَرَ قَوْمَهُ بِالْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ النُّذُرُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ (21) قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَأْفِكَنَا عَنْ آلِهَتِنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ (22) قَالَ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِنْدَ اللَّهِ وَأُبَلِّغُكُمْ مَا أُرْسِلْتُ بِهِ وَلَكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ (23) فَلَمَّا رَأَوْهُ عَارِضًا مُسْتَقْبِلَ أَوْدِيَتِهِمْ قَالُوا هَذَا عَارِضٌ مُمْطِرُنَا بَلْ هُوَ مَا اسْتَعْجَلْتُمْ بِهِ رِيحٌ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٌ (24) تُدَمِّرُ كُلَّ شَيْءٍ بِأَمْرِ رَبِّهَا فَأَصْبَحُوا لَا يُرَى إِلَّا مَسَاكِنُهُمْ كَذَلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ (25) وَلَقَدْ مَكَّنَّاهُمْ فِيمَا إِنْ مَكَّنَّاكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَارًا وَأَفْئِدَةً فَمَا أَغْنَى عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَا أَبْصَارُهُمْ وَلَا أَفْئِدَتُهُمْ مِنْ شَيْءٍ إِذْ كَانُوا يَجْحَدُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَحَاقَ بِهِمْ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (26)}.
21. Na mtaje ndugu wa kina 'Adi, alipowaonya watu wake kwenye vilima vya mchanga. Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake kuwaambia: 'Msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nawahofia ije kuwapateni adhabu ya siku iliyo kuu.' 22. Wakasema: 'Je, umetujia ili ututenge mbali na miungu yetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.' 23. Akasema: 'Hakika ujua wa hayo uko kwa Mwenyezi Mungu. Mimi nawafikishieni yale niliyotumwa nayo. Lakini nawaona kuwa nyinyi mnafanya ujinga tu.' 24. Basi walipoliona wingu likielekea kwenye mabonde yao, walisema: 'Hili ni wingu la kutunyeshea mvua!' Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyotaka yawajie haraka: upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu! 25. Unaharibu kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi. Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu wahalifu! 26. Na bila ya shaka tuliwaweka vizuri siyo kama tulivyokuwekeni nyinyi, na tuliwapa masikio, na macho, na nyoyo. Na hayakuwafaa kitu masikio yao, wala macho yao, wala nyoyo zao kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara ndiyo yakawafika.
#
{21} أي: {واذكر}: بالثناء الجميل {أخا عادٍ}: وهو هودٌ عليه السلام، حيث كان من الرسل الكرام، الذين فضَّلهم الله تعالى بالدَّعوة إلى دينه وإرشاد الخلق إليه، {إذْ أنذر قومَه}: وهم عادٌ {بالأحقافِ}؛ أي: في منازلهم المعروفة بالأحقاف، وهي الرمال الكثيرة في أرض اليمن، {وقد خَلَتِ النُّذُر من بين يديه ومن خلفِهِ}: فلم يكن بدعاً منهم ولا مخالفاً لهم، قائلاً لهم: {أن لا تعبُدوا إلاَّ الله إنِّي أخافُ عليكم عذابَ يوم عظيم}: فأمرهم بعبادة الله الجامعة لكلِّ قول سديدٍ وعمل حميدٍ، ونهاهم عن الشِّرْكِ والتَّنديد، وخوفهم إنْ لم يطيعوه العذابَ الشَّديد، فلم تُفِدْ فيهم تلك الدعوة.
{21} Yaani: "Na mtaje" kwa sifa nzuri "ndugu wa kina 'Adi" aitwaye Hud amani iwe juu yake, ambaye alikuwa katika Mitume watukufu, ambao Mwenyezi Mungu aliwaboresha kwa kuwatuma kulingania dini yake na kuelekeza watu kwake, "alipowaonya watu wake" 'Adi "kwenye vilima vya mchanga" huko Yemen. "Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake" Kwa hivyo hakuwa wa kwanza wao wala mwenye kuwahalifu, akiwaambia: "Msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nawahofieni ije kuwapata adhabu ya siku iliyo kuu." Basi akawaamuru kumuabudu Mwenyezi Mungu kumuabudu ambako kunajumuisha kila kauli sahihi na tendo la kusifiwa, na akawakataza shirki na kumfanyia Mwenyezi Mungu wenza, na akawahofisha adhabu kali ikiwa hawatamtii, lakini wito huo haukuwafaidi kitu.
#
{22} فَـ {قَالوا أجئتنا لِتأفِكَنا عن آلهتنا}؛ أي: ليس لك من القصد ولا معك من الحقِّ إلاَّ أنك حِدتنا على آلهتنا، فأردتَ أن تصرِفَنا عنها، {فأتِنا بما تَعِدُنا إن كنتَ من الصادقين}: وهذا غاية الجهل والعناد.
{22} Basi "wakasema: Je, umetujia ili ututenge mbali na miungu yetu?" Na wala huna lengo lingine wala hata huko kwenye haki. "Basi tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli." Na huu ndio ujinga na ukaidi mkubwa zaidi.
#
{23} {قال إنَّما العلمُ عند اللهِ}: فهو الذي بيده أزمَّةُ الأمور ومقاليدُها، وهو الذي يأتيكم بالعذاب إن شاء، {وأبَلِّغُكُم ما أرسلتُ به}؛ أي: ليس عليَّ إلاَّ البلاغُ المبين، {ولكني أراكم قوماً تجهلونَ}: فلذلك صدر منكم ما صدر من هذه الجرأة الشديدة.
{23} "Akasema: Maarifa yapo kwa Mungu tu," ndiye mwenye mamlaka juu ya mambo yote na ndiye anayetoa adhabu kama atakavyo, "na nawaambia kile nilichotumwa nacho;" yaani, sina la kufanya isipokuwa kufikisha ujumbe wazi, "lakini naona nyinyi ni watu mnaoishi kwa ujinga." Hivyo ndivyo ilivyowapelekea kuonyesha ujasiri huu mkubwa.
#
{24 - 25} فأرسل اللهُ عليهم العذاب العظيم، وهو الريحُ التي دمَّرتهم وأهلكتهم، ولهذا قال: {فلما رأوْه}؛ أي: العذاب، {عارضاً مستقبلَ أودِيَتِهِم}؛ أي: معترضاً كالسَّحاب، قد أقبل على أوديتهم التي تسيلُ فتسقي نوابتهم ويشربون من آبارها وغدرانها، {قالوا}: مستبشرين: {هذا عارضٌ ممطِرنُا}؛ أي: هذا السحاب سيمطرنا. قال تعالى: {بل هو ما استعجَلْتُم به}؛ أي: هذا الذي جنيتُم به على أنفسِكم حيث قلتُم: {فأتِنا بما تَعِدُنا إن كنتَ من الصادقين}. {ريحٌ فيها عذابٌ أليمٌ. تدمِّرُ كلَّ شيءٍ}: تمرُّ عليه من شدَّتها ونحسها، فسلَّطها الله {عليهم سبع ليالٍ وثمانية أيام حسوماً، فترى القوم فيها صَرْعى كأنَّهم أعجازُ نخل خاويةٍ}، {بأمر ربِّها}؛ أي: بإذنه ومشيئته، {فأصبحوا لا يرى إلاَّ مساكِنُهُم}: قد تلفتْ مواشيهم وأموالُهم وأنفسهم. {كذلك نجزي القوم المجرمين}: بسبب جرمِهِم وظُلمهم.
{24-25} Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawatumia adhabu kubwa, ambayo ilikuwa ni upepo ulioharibu mno na kuangamiza. Ndiyo maana akasema: "Basi walipoliona wingu likielekea kwenye mabonde yao" ambayo yalikuwa yanatiririka maji na kunyunyizia mimea yao na wanakunywa kwenye visima na maziwa yake, "wakasema" wakifurahia: "Hili ni wingu la kutunyeshea mvua!" Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyotaka yawajie haraka." Yaani, hiki ni kile mlichojisababishia wenyewe mliposema: "Basi tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli." Kisha akasema: "upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu! Unaharibu kila kitu" ambao unakipitia kwa sababu ya nguvu yake na uovu wake. Basi Mwenyezi Mungu akaupa mamlaka "juu yao kwa masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Basi utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yaliyo wazi ndani," "kwa amri ya Mola wake Mlezi" na mapenzi yake. "Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu." Mifugo yao, mali zao, na maisha yao vikawa vimeharibiwa. "Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu wahalifu" kwa sababu ya uhalifu wao na dhuluma yao.
#
{26} هذا مع أنَّ الله قد أدرَّ عليهم النِّعم العظيمة فلم يشكُروه ولا ذكَروه، ولهذا قال: {ولقد مكَّنَّاهم فيما إن مَكَّنَّاكم فيه}؛ أي: مكنَّاهم في الأرض يتناولون طيباتها، ويتمتَّعون بشهواتها، وعمَّرناهم عمراً يتذكَّر فيه من تذكَّر ويتَّعظ فيه المهتدي؛ أي: ولقد مكَّنَّا عاداً كما مكَّنَّاكم يا هؤلاء المخاطبون؛ أي: فلا تحسبوا أنَّ ما مَكَّنَّاكم فيه مختصٌّ بكم، وأنَّه سيدفع عنكم من عذاب الله شيئاً، بل غيرُكم أعظمُ منكم تمكيناً، فلم تُغْنِ عنهم أموالُهم ولا أولادُهم ولا جنودُهم من الله شيئاً، {وجَعَلْنا لهم سمعاً وأبصاراً وأفئدةً}؛ أي: لا قصور في أسماعهم ولا أبصارهم ولا أذهانهم حتى يقال: إنَّهم تركوا الحقَّ جهلاً منهم وعدم تمكُّن من العلم به ولا خلل في عقولهم، ولكنَّ التوفيقَ بيدِ الله، {فما أغنى عنهم سمعُهم ولا أبصارُهم ولا أفئدتُهم من شيءٍ}: لا قليل ولا كثير، وذلك بسبب أنهم يجحدون آيات الله الدَّالَّة على توحيدِهِ وإفرادِهِ بالعبادة، {وحاق بهم ما كانوا به يستهزِئون}؛ أي: نزل بهم العذاب الذي يكذِّبون بوقوعه، ويستهزِئون بالرسل الذين حذَّروهم منه.
{26} Hii ni licha ya kwamba Mungu aliwapa neema kubwa sana lakini hawakumshukuru wala kumkumbuka. Hivyo alisema: "Na kwa hakika tumewapa nguvu kama vile tulivyowapa nguvu nyinyi;" yaani: tumewapa nguvu duniani, wakifurahia mema yake, na kuishi kwa muda wa kutosha ambapo wangeweza kukumbuka na kujifunza; yaani: tumeweka nguvu kwa 'Aad kama vile tulivyoweka nguvu kwenu ninyi mnaozungumziwa; yaani: msidhani kuwa yale tuliyowapa ni maalum kwenu, na kwamba yatakuwa kinga dhidi ya adhabu ya Mungu, bali wengine walikuwa na nguvu zaidi kuliko ninyi, hivyo mali zao, watoto wao, na jeshi lao havikuweza kuwalinda dhidi ya Mungu. "Na tukawapa masikio, macho, na mioyo;" yaani, hawakukosa uwezo wa kusikia, kuona, wala kufikiria kwa hivyo wangeweza kuelewa haki na elimu, lakini mafanikio yako mikononi mwa Mungu, "basi masikio yao, macho yao, na mioyo yao hayakuwafaidi chochote;" si kidogo wala kingi, kwa sababu walikataa ishara za Mungu zinazothibitisha umoja wake na kumwabudu peke yake, "na adhabu waliyoikataa ikawajia." Yaani: adhabu walikataa kutokea na kudhihaki mitume waliowaonya kuhusu adhabu hiyo.
: 27 - 28 #
{وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا مَا حَوْلَكُمْ مِنَ الْقُرَى وَصَرَّفْنَا الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (27) فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ قُرْبَانًا آلِهَةً بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ وَذَلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ (28)}
27. Na hakika tuliiangamiza miji iliyo jirani zenu, na tulizitumia Ishara mbalimbali ili wapate kurejea. 28. Basi mbona wale waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu, kuwa ati hao ndio wawakurubishe, hawakuwanusuru? Bali waliwapotea! Na huo ndio uwongo mkubwa waliokuwa wakiuzua.
#
{27 - 28} يحذِّر تعالى مشركي العرب وغيرهم بإهلاك الأمم المكذِّبين الذين هم حول ديارهم، بل كثيرٌ منهم في جزيرة العرب؛ كعادٍ وثمودَ ونحوهم، وأنَّ الله تعالى صَرَّفَ لهم {الآياتِ}؛ أي: نوَّعها من كل وجه، {لعلهم يرجِعونَ}: عمَّا هم عليه من الكفر والتكذيب، فلمَّا لم يؤمنوا؛ أخذهم اللهُ أخذَ عزيزٍ مقتدرٍ، ولم تنفعْهم آلهتُهم التي يَدْعون من دون الله من شيءٍ، ولهذا قال هنا: {فلولا نَصَرَهُم الذين اتَّخذوا من دون الله قُرباناً آلهةً}؛ أي: يتقرَّبون إليهم ويتألَّهونهم لرجاء نفعهم. {بل ضلُّوا عنهم}: فلم يُجيبوهم ولا دَفَعوا عنهم، {وذلك إفْكُهُمْ وما كانوا يفترونَ}: من الكذب الذي يُمَنُّون به أنفسَهم؛ حيث يزعُمون أنَّهم على الحقِّ، وأنَّ أعمالهم ستنفعُهم، فضلَّت وبطلت.
{27 - 28} Mwenyezi Mungu anawatahadharisha washirikina wa Kiarabu na wengine kwa kuangamizwa kwa umma waliokadhibishaa ambao wao wako karibu na makazi yao, bali wengi yake yako katika bara la Arabu, kama vile 'Aad, Thamud, na wengineo kama wao. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapa "ishara mbalimbali" za aina zote, "ili wapate kurejea" kutoka kwa kufuru wao huo na kukadhibisha. Lakini walipokataa kuamini, Mwenyezi Mungu aliwachukua kwa mchukuo wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo, na miungu yao waliyokuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu haikuwasaidia kwa chochote. Ndiyo maana akasema hapa: "Bali waliwapotea!" Hawakuwajibu wala kuwaondolea chochote. "Na huo ndio uongo mkubwa waliokuwa wakiuzua" ya uongo waliojidanganya nayo, ambapo walidai kwamba wako kwenye haki, na kwamba matendo yao yatawanufaisha, lakini yalipotelea mbali na yakabatilika.
: 29 - 32 #
{وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنْصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِمْ مُنْذِرِينَ (29) قَالُوا يَاقَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنْزِلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُسْتَقِيمٍ (30) يَاقَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ (31) وَمَنْ لَا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءُ أُولَئِكَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (32)}.
29. Na wakati tulipowaleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur-ani. Basi walipoihudhuria, walisema: 'Sikilizeni!' Na ilipokwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya. 30. Wakasema: 'Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa, kinachosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na kinachoongoza kwenye Haki na kwenye njia iliyonyooka. 31. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawakinga adhabu chungu. 32. Na wasiomwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhahiri.
#
{29} كان الله تعالى قد أرسل رسولَه محمداً - صلى الله عليه وسلم - إلى الخلق إنسهم وجنهم، وكان لا بدَّ من إبلاغ الجميع لدعوة النبوَّة والرسالة؛ فالإنس يمكنه عليه الصلاة والسلام دعوتُهم وإنذارُهم، وأمَّا الجنُّ؛ فصَرَفَهم الله إليه بقدرته وأرسل إليه {نفراً من الجنِّ يستمعونَ القرآن فلمَّا حَضَروه قالوا أنصِتوا}؛ أي: وصَّى بعضُهم بعضاً بذلك، {فلما قُضِيَ}: وقد وَعَوْه وأثَّر ذلك فيهم، {ولَّوْا إلى قومِهِم منذِرين}: نصحاً منهم لهم، وإقامة لحجَّة الله عليهم، وقيَّضهم الله معونةً لرسوله - صلى الله عليه وسلم - في نشر دعوتِهِ في الجنِّ.
{29} Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa ametuma Mtume wake Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - kwa viumbe wote, wanadamu na majini, na ilikuwa lazima kuwafikishia wote wito wa unabii na utume. Ama watu yeye Mtume - rehema na amani ziwe juu yake - aliweza kuwalingania na kuwaonywa, lakini majini, Mwenyezi Mungu aliwapeleka kwake kwa uwezo wake na kumtumia "kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur-ani. Basi walipoihudhuria, walisema: 'Sikilizeni!' Na ilipokwishasomwa" na wakawa wameshauelewa ujumbe na kuathirika nao, "walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya" kuwapa nasaha, kuwasimamishia hoja ya Mwenyezi Mungu dhidi yao, na Mwenyezi Mungu aliwaleta mwenyewe ili kumsaidia Mtume wake - rehema na amani ziwe juu yake - katika kueneza wito wake kwa majini.
#
{30} {قالوا يا قومَنا إنَّا سَمِعْنا كتاباً أنزِلَ من بعدِ موسى}: لأنَّ كتاب موسى أصلٌ للإنجيل وعمدةٌ لبني إسرائيل في أحكام الشرع، وإنَّما الإنجيل متمِّم ومكمِّل ومغيِّر لبعض الأحكام، {مصدِّقاً لما بين يديه يَهْدي}: هذا الكتاب الذي سَمِعْناه، {إلى الحقِّ}: وهو الصوابُ في كلِّ مطلوبٍ وخبرٍ، {وإلى طريقٍ مستقيمٍ}: موصل إلى الله وإلى جنَّته من العلم بالله وبأحكامه الدينيَّة وأحكام الجزاء.
{30} "Wakasema: 'Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa" kwa sababu Kitabu cha Musa ndio msingi wa Injili na ndicho kiinachotegemewa na Wana wa Israili katika hukumu za kisheria, nayo Injili inakikamilisha tu na kubadilisha baadhi ya hukumu za kisheria, "kinachosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na kinachoongoza" kitabu hiki tulichokisikia, "kwenye Haki" ambayo ni kilicho sahihi miongoni mwa kila kitu kinachotakiwa na habari, "na kwenye njia iliyonyooka" inayofikisha mtu kwa Mwenyezi Mungu na kwenye Bustani zake za mbinguni kutokana na kumjulisha kuhusu Mwenyezi Mungu, hukumu za kidini, na za kimalipo.
#
{31} فلمَّا مَدَحوا القرآن وبيَّنوا محلَّه ومرتبته؛ دَعَوْهم إلى الإيمان به، فقالوا: {يا قومَنا أجيبوا داعيَ اللهِ}؛ أي: الذي لا يدعو إلاَّ إلى ربِّه، لا يدعوكم إلى غرض من أغراضِهِ ولا هوى، وإنَّما يدعوكم إلى ربِّكم لِيُثيبَكم، ويزيلَ عنكم كلَّ شرٍّ ومكروه، ولهذا قالوا: {يغفرْ لكم من ذُنوبِكُم ويُجِرْكُم من عذابٍ أليم}: وإذا أجارهم من العذاب الأليم؛ فما ثمَّ بعد ذلك إلاَّ النعيم؛ فهذا جزاءُ من أجاب داعي الله.
{31} Walipoisifu Qur-ani na kubainisha hadhi yake na nafasi yake, wakawalingania kwenye imani, wakasema: "Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu" yaani: ambaye halinganii isipokuwa kwa Mola wake Mlezi wala hawalinganii kwenye lengo lolote lake la kibinafsi wala matamanio yake, bali anakulinganieni kwa Mola wenu Mlezi ili awalipe mazuri na akuondoleeni kila uovu na mambo yote yanayochukiwa. Ndiyo maana wakasema: "atawasamehe, na atawakinga adhabu chungu." Na ikiwa atawalinda kutokana na adhabu chungu, basi baada ya hapo hakuna kingine isipokuwa furaha tu. Basi haya ndiyo malipo ya mwenye kuitikia yule anayelingania kwa Mwenyezi Mungu.
#
{32} {ومَن لا يُجِبْ داعيَ الله فليس بمعجزٍ في الأرضِ}: فإنَّ الله على كلِّ شيءٍ قديرٌ، فلا يفوته هاربٌ ولا يغالِبُه مغالبٌ، {وليس له من دونِهِ أولياءُ أولئك في ضلالٍ مبينٍ}، وأيُّ ضلال أبلغُ من ضلال مَنْ نادَتْه الرسل، ووصلتْ إليه النُّذُر بالآيات البيِّنات والحجج المتواتراتِ فأعرض واستكبر؟!
{32} "Na wasiomwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatashinda katika ardhi" kwa maana Mwenyezi Mungu ana uwezo mno juu ya kila kitu, kwa hivyo hakuna mwenye kukimbia anayeweza kumkimbia wala hakuna mshindi anayeweza kumshinda. "Wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhahiri." Na ni upotovu gani mbaya zaidi kuliko upotovu wa yule anayelinganiwa na Mitume, na waonyaji wakamfikia kwa ishara mbalimbali zilizo wazi na hoja nyingi sana, lakini akazipa mgongo?
: 33 #
{أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَى بَلَى إِنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (33)}.
33. Je, hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliyeziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.
#
{33} هذا استدلالٌ منه تعالى على الإعادة بعد الموت بما هو أبلغُ منها، وهو {أنَّه الذي خلقَ السماواتِ والأرضَ} على عظمهما وسعتهما وإتقان خلقهما من دون أن يَكْتَرِثَ بذلك، ولم يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ؛ فكيف تعجِزُه إعادتُكم بعد موتكم وهو {على كل شيءٍ قديرٌ}؟!
{33} Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametumia ushahidi juu ya kufufua wafu baada ya kifo kwa kutumia kitu kilicho zaidi ya hicho, ambacho ni kwamba Yeye ndiye "aliyeziumba mbingu na ardhi" pamoja na ukubwa wake na upana wake, na ustadi mkubwa wa kuziumba bila kuchoka kwa sababu ya hilo. Basi vipi atashindwa kuwafufua baada ya kufa kwenu ilhali "Yeye ni Muweza mno wa kila kitu?"
: 34 - 35 #
{وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَلَيْسَ هَذَا بِالْحَقِّ قَالُوا بَلَى وَرَبِّنَا قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنْتُمْ تَكْفُرُونَ (34) فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِلْ لَهُمْ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِنْ نَهَارٍ بَلَاغٌ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ (35)}
34. Na siku watakapoletwa makafiri Motoni, wakaambiwa: 'Je, haya si kweli?' Watasema: 'Ndivyo? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi, ni kweli!' Atasema: 'Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mkikufuru.' 35. Basi subiri, kama walivyosubiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayoyaona hayo waliyoahidiwa, itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipokuwa watu wavukao mipaka tu?
#
{34} يخبر تعالى عن حال الكفار الفظيعة عند عرضِهِم على النار التي كانوا يكذِّبون بها، وأنَّهم يوبَّخون ويُقال لهم: {أليس هذا بالحقِّ}؛ فقد حضرتُموه وشاهدتُموه عياناً، {قالوا بلى وربِّنا}: فاعترفوا بذنوبهم وتبين كذبهم، {قال فَذُوقُوا العَذابَ بما كنتُم تكفُرون}؛ أي: عذاباً لازماً دائماً كما كان كفرُكم صفةً لازمةً.
{34} Mwenyezi Mungu anajulisha kuhusu hali mbaya mno ya makafiri watakaletwa kwenye Moto ambao walikuwa wakiukadhibisha, na kwamba watakaripiwa na kuambiwa: "Je, haya si kweli?" Kwamba mmeshaufikia na mmeuona kwa macho yenu. "Watasema: 'Ndivyo? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi, ni kweli!'" Basi wakakiri dhambi zao na uwongo wao ukadhihirika. "Atasema: 'Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mkikufuru.'" Adhabu hii itakuwa ni ya kudumu kama vile kukufuru kwenu kulikuwa ni sifa mliyodumu nayo.
#
{35} ثم أمر تعالى رسوله أن يصبِرَ على أذيَّة المكذِّبين المعادين له، وأن لا يزال داعياً لهم إلى الله، وأن يقتديَ بصبرِ أولي العزم من المرسَلين سادات الخَلْق أولي العزائم والهِمَم العالية، الذين عَظُم صَبْرُهم وتمَّ يقينُهم؛ فهم أحقُّ الخلق بالأسوة بهم والقفو لآثارهم والاهتداء بمنارِهِم، فامتثل - صلى الله عليه وسلم - لأمر ربِّه، فصبر صبراً لم يصبِرْه نبيٌّ قبله، حتى رماه المعادون له عن قوسٍ واحدةٍ، وقاموا جميعاً بصدِّه عن الدَّعوة إلى الله، وفعلوا ما يمكنهم من المعاداة والمحاربة، وهو - صلى الله عليه وسلم - لم يزل صادعاً بأمر الله، مقيماً على جهاد أعداء الله، صابراً على ما ينالُه من الأذى، حتى مكَّن الله له في الأرض، وأظهر دينَه على سائر الأديان وأمَّته على الأمم، فصلى الله عليه وسلم تسليماً. وقوله: {ولا تستعجل لهم}؛ أي: لهؤلاء المكذِّبين المستعجلين للعذاب؛ فإنَّ هذا من جهلهم وحمقهم؛ فلا يستخفنَّكَ بجهلهم ولا يَحْمِلْك ما ترى من استعجالهم على أنْ تدعُوَ الله عليهم بذلك؛ فإنَّ كلَّ ما هو آتٍ قريبٌ، و {كأنَّهم} حين {يَرَوْنَ ما يوعدونَ لم يَلْبَثوا} في الدُّنيا {إلاَّ ساعةً من نهارٍ}؛ فلا يحزُنْك تمتُّعهم القليل وهم صائرون إلى العذاب الوبيل، {بلاغٌ}؛ أي: هذه الدنيا متاعها وشهواتها ولذَّاتها بلغةٌ منغصةٌ ودفعُ وقتٍ حاضر قليل، أو هذا القرآن العظيم ـ الذي بيَّنَّا لكم فيه البيانَ التامَّ ـ بلاغٌ لكم وزادٌ إلى الدار الآخرة، ونِعْم الزادُ والبلغةُ، زادٌ يوصل إلى دار النعيم، ويعصِمُ من العذابِ الأليم؛ فهو أفضل زاد يتزوَّده الخلائقُ، وأجلُّ نعمة أنعم الله بها عليهم، {فهل يُهْلَكُ}: بالعقوبات {إلاَّ القومُ الفاسقون}؛ أي: الذين لا خير فيهم، وقد خرجوا عن طاعة ربِّهم، ولم يَقْبَلوا الحقَّ الذي جاءتهم به الرسل، وأعذر الله لهم وأنذرهم، فبعد ذلك إذ يستمرُّون على تكذيبهم وكفرهم، نسأل الله العصمة.
{35} Kisha Mwenyezi Mungu akamuamuru Mtume wake kuwa mvumilivu juu ya udhia wa wale wanaomkadhibisha na kumkaidi, na kwamba aendelee kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba awaige Mitume wale waliokuwa na stahamala kubwa, viongozi wa viumbe, wenye azimio na hima kubwa sana, ambao uvumilivu wao ulikuwa mkubwa sana na yakini yao ikakamilika. Basi wao ndio viumbe wenye haki zaidi kuwaiga na kufuata nyayo zao, na kuongoka kwa mwanga wao. Kwa hivyo, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akasubiri subira ambayo Nabii yeyote hakuwahi kusubiri kabla yake, hadi wale wale waliompinga wakamshambulia kwa mpigo mmoja, na wakajitahidi kwa nguvu zao zote kumzuia kulingania kwa Mwenyezi Mungu, na wakafanya kila waliyoweza kuleta kumpinga na kumpiga vita. Hata hivyo, Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliendelea kueneza amri ya Mwenyezi Mungu, akiendelea kupigana vita dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu, na akivumilia yale yaliyompata ya maudhi, hadi Mwenyezi Mungu alipomuimarisha sawasawa katika ardhi, na akaidhihirisha dini yake juu ya dini zingine zote, na umma wake juu ya umma zinginezo. Basi, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na kauli yake: "Wala usiwafanyie haraka" hawa wanaokukadhibisha na wanaotaka adhabu iwajie haraka. Kwani hili ni kwa sababu ya ujinga wao na upumbavu wao. Hivyo basi, usikubali ujinga wao kukuchanganya wala kusikufanye kuharakishwa kwao kumtaka Mwenyezi Mungu kuwaadhibu haraka haraka. Kwa sababu kila kitu kinachokuja kipo karibu, na "itakuwa kama kwamba" wakati "watakayoyaona hayo waliyoahidiwa, hawakukaa" duniani "ila saa moja ya mchana." basi usihuzunishwe na kufurahia kwao kudogo ilhali watakwenda kwenye adhabu kubwa zaidi. "Huu ndio ufikisho!" Maana yake inaweza kuwa ni kwamba starehe, matamanio, na raha za dunia hii ni za muda mfupi na zisizo na faida na za kumaliza muda uliopo ambao ni mchache sana. Au Qur-an hii tukufu — ambayo tumewabainishia ndani yake kwa uwazi kabisa — ni ufikisho kwenu, na chakula cha safarini kwenda katika nyumba ya akhera, na ni chakula bora zaidi na kitu kizuri zaidi cha kumfikisha mtu huko. Ni chakula kinachofikisha kwenye nyumba ya furaha na kinachowakinga kutokana na adhabu kali; kwa hivyo hicho ndicho chakula bora zaidi cha safarini ambacho viumbe wanaweza kuchukua, na ndiyo neema kuu zaidi aliyowapa Mwenyezi Mungu. "Kwani huangamizwa" kwa adhabu mbalimbali "isipokuwa watu wavukao mipaka tu?" Yaani, wasiokuwa na heri ndani yao, ambao walitoka nje ya utiifu kwa Mola wao Mlezi, na hawakukubali haki waliyojiwa nayo na Mitume, na Mwenyezi Mungu akawaonya na kuwatahadharisha. Lakini baada ya yote hayo, tazama, wakaendelea kukadhibisha na kukufuru. Tunamwomba Mwenyezi Mungu kutulinda.
Mwisho wa tafsiri ya Surat Al-Ahqaf, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
* * *