:
Tafsiri ya Surat Al-Qital
Tafsiri ya Surat Al-Qital
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ (1) وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَى مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِنْ رَبِّهِمْ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ (2) ذَلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِنْ رَبِّهِمْ كَذَلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ (3)}.
1. Wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao. 2. Na wale walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao. 3. Hayo ni kwa sababu wale waliokufuru wamefuata upotovu, na wale walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.
#
{1} هذه الآياتُ مشتملاتٌ على ذكرِ ثواب المؤمنين، وعقاب العاصين، والسببُ في ذلك، ودعوة الخلق إلى الاعتبار بذلك، فقال: {الذين كفروا وصدُّوا عن سبيل الله}: وهؤلاء رؤساءُ الكفر وأئمَّة الضلال، الذين جمعوا بين الكفر بالله وآياتِهِ والصدِّ لأنفسهم وغيرهم عن سبيل الله، التي هي الإيمانُ بما دعت إليه الرُّسل واتِّباعه؛ فهؤلاء {أضلَّ} الله {أعمالَهم}؛ أي: أبطلها وأشقاهم بسببها، وهذا يشمَلُ أعمالهم التي عملوها لِيَكيدوا بها الحقَّ وأولياء الله، إنَّ الله جَعَلَ كيدَهم في نحورهم، فلم يدرِكوا مما قصدوا شيئاً، وأعمالُهم التي يرجون أن يثابوا عليها؛ إنَّ الله سيُحْبِطُها عليهم، والسبب في ذلك أنَّهم اتَّبعوا الباطل، وهو كلُّ غايةٍ لا يُراد بها وجه الله من عبادة الأصنام والأوثان. والأعمال التي في نصر الباطل لما كانت باطلةً؛ كانت الأعمال لأجلها باطلة.
{1} Aya hizi zinajumuisha kutajwa malipo ya Waumini, adhabu ya wafanyao maasi, sababu ya hayo, na kuwalingania viumbe kuzingatia hayo. Mwenyezi Mungu akasema: "Wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu" Hawa ndio viongozi wa ukafiri na maimamu wa upotofu, ambao walichanganya kati ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na ishara zake na kujizuilia wao wenyewe na wengineo mbali na njia ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni kuamini yale waliyoyalingania Mitume na kuifuata. Basi hawa "Yeye" Mwenyezi Mungu "atavipotoa vitendo vyao" na kuwatia mashakani kwa sababu yake. Na hili linajumuisha matendo yao waliyoyafanya kwa ajili ya kufanya vitimbi dhidi ya haki na vipenzi wa Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu akatia vitimbi vyao hivyo kwenye koo zao, kwa hivyo hawakupata chochote katika yale waliyokusudia, na vitendo vyao wanavyotarajia kulipwa juu yake, Mwenyezi Mungu ataviharibu. Na sababu yake ni kwamba walifuata batili, ambao ni kila lengo ambalo mja hataki kwalo uso wa Mwenyezi Mungu, kama vile kuabudu masanamu na miungu. Na kwa sababu matendo yaliyofanywa kwa ajili ya kuunga mkono batili ni batili pia, basi matendo yanayofanywa kwa ajili yake ni batili pia.
#
{2} وأما {الذين آمنوا} بما أنزل اللهُ على رسلِهِ عموماً وعلى محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - خصوصاً، {وعملوا الصالحات}: بأن قاموا بما عليهم من حقوق الله وحقوق العباد الواجبة والمستحبَّة، {كفَّر الله عنهم سيئاتِهِم}: صغارها وكبارها، وإذا كُفِّرَتْ سيئاتُهم؛ نَجَوْا من عذاب الدُّنيا والآخرة، {وأصلح بالَهم}؛ أي: أصلح دينهم ودنياهم وقلوبهم وأعمالهم، وأصلَحَ ثوابَهم بتنميتِهِ وتزكيتِهِ، وأصلح جميع أحوالهم.
{2} Ama "wale walioamini" katika yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake kwa ujumla na kwa Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - hasa "na wakatenda mema" kwa kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu zilizoko juu yao na haki za waja wake za lazima na zisizokuwa za lazima, "atawafutia makosa yao" madogo na makubwa. Na wakishasamehewa makosa yao, watakuwa wameokoka na adhabu ya duniani na ya Akhera, "na ataitengeneza vizuri hali yao" ya kidini, kidunia, nyoyo zao, na matendo yao, na atazitengeneza thawabu zao kwa kuzikuza na kuzitakasa, na atatengeneza hali zao zote kuwa nzuri.
#
{3} والسبب في ذلك أنهم اتَّبعوا الحقَّ الذي هو الصدق واليقين وما اشتمل عليه هذا القرآن العظيم الصادر من ربهم الذي ربَّاهم بنعمته ودبَّرهم بلطفه، فربَّاهم تعالى بالحقِّ، فاتَّبعوه، فصلحت أمورُهم، فلمَّا كانت الغايةُ المقصودة لهم متعلقةً بالحقِّ المنسوب إلى الله الباقي الحقِّ المبين؛ كانت الوسيلة صالحةً باقيةً، باقٍ ثوابها. {كذلك يضرِبُ الله للناس أمثالَهم}؛ حيث بيَّن لهم تعالى أهل الخير وأهل الشرِّ، وذكر لكلٍّ منهم صفةً يُعرفَون بها ويتميَّزون؛ لِيَهْلِكَ من هَلَكَ عن بيِّنة ويحيا من حَيَّ عن بينةٍ.
{3} Sababu ya hayo ni kwamba waliifuata haki, ambayo ni ukweli na yakini, na yale yaliyomo ndani ya Qur-ani hii tukufu iliyotoka kwa Mola wao Mlezi, ambaye aliwanyanyua kwa fadhila zake na akawalea kwa neema zake, na akawaendesha kwa upole wake. Basi Yeye Mtukufu akawalea kwa haki, hivyo wakaifuata, kwa hivyo mambo yao yakatengenea. Na kwa kuwa lengo lililokusudiwa kwao lilihusiana na haki inayonasibishwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye kubakia, wa Haki, aliye wazi, njia hiyo ikawa nzuri na ya kudumu, na yenye malipo ya kubakia. "Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao." Ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaeleza watu wema na watu waovu, na akawatajia sifa za kila mmoja ambazo kwazo wanajulikana na ni maalumu kwao tu. Ili mwenye kuangamia aangamie kwa hoja iliyo wazi, na mwenye kusalia hai asalie hai kwa hoja iliyo wazi.
: 4 - 6 #
{فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّى إِذَا أَثْخَنْتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّى تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ذَلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللَّهُ لَانْتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَكِنْ لِيَبْلُوَ بَعْضَكُمْ بِبَعْضٍ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَلَنْ يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ (4) سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ (5) وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ (6)}.
4. Basi mnapowakuta wale waliokufuru, wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha, wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndivyo hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu awatie mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, hatayapoteza matendo yao. 5. Atawaongoza na awatengezee hali yao. 6. Na atawaingiza katika Pepo aliyowajuulisha.
#
{4} يقول تعالى مرشداً عباده إلى ما فيه صلاحُهم ونصرُهم على أعدائهم: {فإذا لقيتُم الذين كفروا}: في الحرب والقتال؛ فاصدُقوهم القتال واضرِبوا منهم الأعناق حتى تُثْخِنوهم وتكسروا شوكتهم وتبطلوا شِرَّتهم؛ فإذا فعلتم ذلك ورأيتم الأسر أولى وأصلح؛ {فشدُّوا الوثَاقَ}؛ أي: الرباط، وهذا احتياط لأسرهم لئلاَّ يهربوا؛ فإذا شُدَّ منهم الوَثاق؛ اطمأنَّ المسلمون من حربهم ومن شرِّهم؛ فإذا كانوا تحت أسرِكم؛ فأنتُم بالخيار بين المنِّ عليهم وإطلاقهم بلا مال ولا فداء، وإمّا أن تفدوهم بأن لا تطلقوهم حتى يشتروا أنفسهم، أو يشترِيَهم أصحابُهم بمال أو بأسير مسلم عندهم، وهذا الأمر مستمرٌّ {حتى تَضَعَ الحربُ أوزارها}؛ أي: حتى لا يبقى حربٌ وتبقَون في المسالمة والمهادنة؛ فإنَّ لكلِّ مقام مقالاً، ولكلِّ حال حكماً. فالحال المتقدِّمة إنَّما هي إذا كان قتالٌ وحربٌ؛ فإذا كان في بعض الأوقات لا حرب فيه لسبب من الأسباب؛ فلا قتل ولا أسر. {ذلك}: الحكم المذكور في ابتلاء المؤمنين بالكافرين ومداولة الأيام بينهم وانتصار بعضهم على بعض، {ولو يشاءُ الله لانتصَرَ منهم}: فإنه تعالى على كلِّ شيءٍ قديرٌ، وقادرٌ على أن لا ينتصرَ الكفار في موضع واحدٍ أبداً، حتى يبيدَ المسلمونَ خضراءهم، {ولكن لِيَبْلُوَ بعضَكم ببعض}: ليقوم سوقُ الجهاد، وتتبيَّن بذلك أحوال العباد الصادق من الكاذب، وليؤمن مَنْ آمن إيماناً صحيحاً عن تبصرةٍ لا إيماناً مبنيًّا على متابعة أهل الغلبة؛ فإنَّه إيمانٌ ضعيفٌ جدًّا، لا يكاد يستمرُّ لصاحبه عند المحن والبلايا. {والذين قُتِلوا في سبيل الله}: لهم ثوابٌ جزيلٌ وأجرٌ جميلٌ، وهم الذين قاتلوا مَنْ أمِروا بقتالهم؛ لتكون كلمة الله هي العليا؛ فهؤلاء لن {يضِلَّ} الله {أعمالَهم}؛ أي: لن يحبِطَها ويبطلها، بل يتقبَّلها وينمِّيها لهم ويظهر من أعمالهم نتائجها في الدنيا والآخرة.
{4} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akiwaelekeza waja wake katika yale yaliyo mazuri kwao kuwapa ushindi dhidi ya maadui zao: "Basi mnapowakuta wale waliokufuru" katika vita, basi piganeni nao kweli kweli kwa kupigana shingo zao mpaka muwadhoofishe na mvunje nguvu zao na mbatilishe maovu yao. Mkifanya hivyo na mkaona kwamba kuwashikilia mateka ndilo bora zaidi, "wafungeni pingu sawasawa." Hilo ni ili wasikimbie wakatoroka, na kwa kufanya hivyo, Waislamu wanakuwa na utulivu kutokana na vita vyao na uovu wao. Na hapo mna hiyari baina ya kuwaachilia bure bila ya kulipa mali wala kujikomboa, au mnaweza kuwataka wajikomboe kwa kujinunua wenyewe, au wenzao wawanunue kwa mali au kwa mateka Mwislamu waliye naye. Jambo hili litaendelea hivi "mpaka vita vipoe" kwa kuweka mkataba wa amani. Kwa maana kila nafasi ina maneno yake maalumu, na kila hali ina hukumu yake. Hali iliyotangulia hapo juu ni ikiwa tu kuna vita. Lakini ikiwa katika wakati mwingine hakuna vita kwa sababu yoyote ile, basi hakutakuwa na mauaji wala mateka. "Ndivyo hivyo" ilivyo hukumu iliyotajwa katika kuwajaribu Waumini kwa makafiri na kuhitalifiana kwa siku mbalimbali baina yao na wao kwa wao kushindana. "Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliwashinda mwenyewe." Kwani kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu, na anaweza kuwafanya makafiri wasishinde hata mahali pamoja mpaka Waislamu waangamize vitu vyao vizuri vyote. "Lakini haya ni kwa sababu awatie mitihani nyinyi kwa nyinyi" ili Jihadi iweze kusimama imara, na kwa hilo zibainike hali za waja wa ukweli na waongo, na ili anayeamini aamini imani sahihi kwa elimu ya sawasawa, siyo imani iliyojengeka juu ya kuwafuata wenye ushindi tu. Hiyo hakika ni imani dhaifu sana, ambayo mwenyewe hawezi kudumu juu yake wakati wa majaribio na misiba. "Na wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu" watapata thawabu nyingi na ujira mzuri, na hao ndio wale waliopigana na wale ambao waliamrishwa kupigana nao; ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi. Hao, Mwenyezi Mungu "hatayapoteza matendo yao." Yaani hatayaangusha na kuyabatilisha, bali atayakubali na kuyakuza kwa ajili yao na ataonyesha matokeo ya matendo yao katika dunia hii na akhera.
#
{5} {سيهديهم}: إلى سلوك الطريق الموصلة إلى الجنة، {ويصلِحُ بالَهم}؛ أي: حالهم وأمورهم، وثوابُهم يكون صالحاً كاملاً لا نَكَدَ فيه ولا تنغيصَ بوجه من الوجوه.
{5} "Atawaongoza" wafuate njia yenye kufikisha katika Bustani ya mbinguni, "na awatengezee hali yao kuwa nzuri." Yaani, hali na mambo yao, na malipo yao yatakuwa mazuri na kamili, bila ya ubaya wowote wala dhiki kwa namna yoyote ile.
#
{6} {ويدخِلُهم الجنةَ عرَّفَها لهم}؛ أي: عرَّفها أولاً بأن شوَّقهم إليها، ونعتها لهم، وذكر لهم الأعمال الموصلة إليها، التي من جملتها القتل في سبيل الله، ووفَّقهم للقيام بما أمرهم به ورغَّبهم فيه، ثم إذا دخلوا الجنة؛ عرَّفهم منازلهم وما احتوتْ عليه من النعيم المقيم والعيش السليم.
{6} "Na atawaingiza katika Pepo aliyowajuulisha." Yaani: Kwanza alibainishia kwa kuwafanya kuwa na shauku kubwa nayo, akawaelezea namna ilivyo, na kuwatajia matendo yanayowafikisha huko, ambayo miongoni mwake ni kuuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na akawawezesha kufanya aliyowaamrisha akawahimiza zaidi kufanya hivyo, kisha watakapoingia Peponi, atawajulisha nyumba zao na neema za milele zilizomo humo na maisha ya amani.
: 7 - 9 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ (7) وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ (8) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ (9)}
7. Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye atawanusuruni na ataiimarisha miguu yenu. 8. Na wale waliokufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao. 9. Hayo ni kwa sababu waliyachukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.
#
{7} هذا أمرٌ منه تعالى للمؤمنين أن يَنْصُروا الله بالقيام بدينِهِ والدعوة إليه وجهاد أعدائه، والقصد بذلك وجه الله؛ فإنَّهم إذا فعلوا ذلك؛ نصرهم وثبَّت أقدامهم؛ أي: يربط على قلوبهم بالصبر والطمأنينة والثبات، ويصبِّر أجسادهم على ذلك، ويعينُهم على أعدائهم؛ فهذا وعدٌ من كريم صادق الوعد أنَّ الذي ينصُرُه بالأقوال والأفعال سينصُرُه مولاه، وييسِّر له أسباب النصر من الثبات وغيره.
{7} Hii ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Waumini kumnusuru Mwenyezi Mungu kwa kushikamana sawasawa katika dini yake, kuilingania, na kupigana jihadi dhidi ya maadui zake, na kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu katika hayo. Kwani katika hakika wakifanya hivyo, Yeye atawanusuru na aifanye miguu yao kuwa imara. Yaani, anazifunga nyoyo zao kwa subira, utulivu mkubwa, uthabiti, na ataifanya miili yao kuwa na subira kwa hayo, na kuwasaidia dhidi ya maadui zao. Hii ni ahadi kutoka kwa Mwingi wa Ukarimu ambaye ni mkweli katika ahadi yake kwamba mwenye kumnusuru kwa kauli na matendo, Mola wake atamnusuru na amrahisishie njia za ushindi, kama vile uthabiti na mambo mengineyo.
#
{8} وأمَّا الذين كفروا بربِّهم ونصروا الباطل؛ فإنَّهم في تعس؛ أي: انتكاس من أمرهم وخذلانٍ، {وأضلَّ أعمالَهم}؛ أي: أبطل أعمالهم التي يَكيدونَ بها الحقَّ، فرجع كيدُهم في نحورهم، وبطلت أعمالُهم التي يزعمون أنهم يريدون بها وجه الله.
{8} Ama wale waliomkufuru Mola wao Mlezi na wakainusuru batili, wamo katika mashaka makubwa na kurudi nyuma katika mambo yao na kuachiliwa mbali bila ya kusaidiwa, "na atavipoteza vitendo vyao." Yaani, atavibatilisha vitendo vyao walivyoipangia njama dhidi ya haki, basi vitimbi vyao hivyo vikarejea kooni mwao, na vikabatilika vitendo vyao walivyodai kuwa wanatafuta uso wa Mwenyezi Mungu kwavyo.
#
{9} ذلك الإضلال والتعس للذين كفروا بسبب أنَّهم {كرهوا ما أنزل الله} من القرآن الذي أنزله [اللَّه] صلاحاً للعباد وفلاحاً لهم، فلم يقبلوه، بل أبغضوه وكرهوه، {فأحبط أعمالهم}.
{9} Huko kupotoshwa na kutiwa mashakani kwa wale waliokufuru ni kwa sababu wao "waliyachukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu" katika Qur-ani ambayo [Mwenyezi Mungu] aliiteremsha kwa ajili ya kuwatengeneza waja wake na kwa ajili ya kufaulu kwao, lakini wao hawakuikubali. Bali walikereka nayo na kuichukia, "basi akaviangusha vitendo vyao."
: 10 - 11 #
{أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ دَمَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا (10) ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَى لَهُمْ (11)}
10. Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mifano ya hayo. 11. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Na makafiri hawana mlinzi.
#
{10} أي: أفلا يسير هؤلاء المكذِّبون بالرسول - صلى الله عليه وسلم -، {فينظروا كيف كان عاقبةُ الذين من قبلهم}: فإنَّهم لا يجدون عاقبتهم إلاَّ شرَّ العواقب؛ فإنَّهم لا يلتفتون يمنةً ولا يسرةً إلاَّ وجدوا ما حولهم قد بادوا وهلكوا واستأصلهم التكذيبُ والكفرُ، فخمدوا، ودمَّر الله عليهم أموالهم وديارهم، بل دمَّر أعمالهم ومكرهم، وللكافرين في كلِّ زمان ومكان أمثالُ هذه العواقب الوخيمة والعقوبات الذميمة، وأما المؤمنونَ؛ فإنَّ الله تعالى يُنجيهم من العذاب، ويُجْزِلُ لهم كثير الثواب.
{10} Yaani kwa nini hawa wanaomkadhibisha Mtume – rehema na amani zimshukie – hawatembei "wakaona ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao?" Kwani hawatapata mwisho wao chochote isipokuwa ulikuwa mwisho mbaya zaidi. Kwa maana hawageuki kuliani wala kushotoni ila wataona wameshapotelea mbali na kuangamia, na wakaang'olewa kabisa kabisa na kukadhibisha kwao na ukafiri wao, basi wakazimika. Na Mwenyezi Mungu akaziharibu mali zao na makazi yao, na hata akaviharibu vitendo vyao na njama zao. Basi makafiri katika kila wakati na sehemu wanayo matokeo mabaya sawa na adhabu hizi kubwa na adhabu hizi mbaya zaidi. Ama Waumini, Mwenyezi Mungu Mtukufu huwaepusha adhabu na huwapa malipo mengi.
#
{11} {ذلك بأنَّ الله مولى الذين آمنوا}: فتولاَّهم برحمته، فأخرجهم من الظلمات إلى النور، وتولَّى جزاءهم ونصرهم، {وأنَّ الكافرين}: بالله تعالى؛ حيث قطعوا عنهم ولاية الله، وسدُّوا على أنفسهم رحمته {لا مولى لهم}: يهديهم إلى سبل السلام، ولا يُنجيهم من عذاب الله وعقابه، بل أولياؤُهُم الطاغوتُ؛ يخرِجونَهم من النورِ إلى الظُّلمات، أولئك أصحاب النار هم فيها خالدون.
{11} "Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini." Basi akawachunga kwa rehema yake, na akawatoa katika giza mbalimbali na akawapeleka kwenye nuru, na akasimamia malipo yao na ushindi wao. "Na kwamba makafiri" waliomkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo walikata ulinzi wa Mwenyezi Mungu kutoka kwao, na wakajiweka mbali wenyewe na rehema yake "hawana mlinzi" anayeweza kuongoza kufikia njia za amani, na kuwaokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake. Bali walinzi wao ni Taghut (mashetani na waovu wote), ambao wanawatoa kwenye nuru na kuwaingiza katika giza mbalimbali. Hao ndio wenza wa Moto, humo watadumu milele.
: 12 #
{إِنَّ اللَّهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَهُمْ (12)}
12. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema katika Bustani za mbinguni zipitiwazo na mito kati yake. Na wale waliokufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makazi yao.
#
{12} لما ذكر تعالى أنه وليُّ المؤمنين؛ ذكر ما يفعل بهم في الآخرة من دخول الجناتِ، التي تجري من تحتها الأنهار، التي تسقي تلك البساتين الزاهرة، والأشجار الناضرة المثمرة؛ لكلِّ زوج بَهيج، وكل فاكهة لذيذة. ولمَّا ذَكَرَ أن الكافرين لا مولى لهم؛ ذكر أنَّهم وُكِلوا إلى أنفسهم، فلم يتَّصفوا بصفات المروءة ولا الصفات الإنسانية، بل نزلوا عنها دركاتٍ، وصاروا كالأنعام التي لا عقل لها ولا فضل، بل جلُّ همِّهم ومقصدهم التمتُّع بلذَّات الدُّنيا وشهواتها، فترى حركاتهم الظاهرة والباطنة دائرةً حولها غير متعدِّيةٍ لها إلى ما فيه الخير والسعادة، ولهذا كانت النارُ مثوى لهم؛ أي: منزلاً معدًّا لا يخرجون منها ولا يفتَّر عنهم من عذابها.
{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa Yeye ndiye mlinzi wa Waumini, akataja watakayofanyiwa Akhera ya kuingia katika Bustani zipitazo mito kati yake, zinyweshazo bustani hizo zinazong'aa kwa uzuri, na miti mizuri yenye matunda. Zina kila jozi yenye furaha, na kila tunda lenye ladha. Na alipotaja kwamba makafiri hawana mlinzi, akasema kwamba wameachiwa wenyewe, kwa hivyo hawakusifika kwa sifa za heshima wala sifa za kibinadamu. Bali walishuka kutoka huko matabaka, na wakawa kama wanyama wasio na akili wala heshima. Bali hima yao kuu katika maisha yao na lengo lao ni kufurahia starehe za dunia na matamanio yake. Kwa hivyo utaona harakati zao za nje na za ndani zikizungukia hapo bila kuvuka kwenda kwenye mambo ya heri na furaha, na ndiyo maana Moto utakuwa makazi yao yaliyoandaliwa kwa ajili yao. Hawatatoka humo wala hawatapunguziwa katika adhabu yake.
: 13 #
{وَكَأَيِّنْ مِنْ قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِنْ قَرْيَتِكَ الَّتِي أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ (13)}
13. Na ni miji mingapi iliyokuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu uliokutoa? Tuliwateketeza na wala hawakuwa na yeyote wa kuwanusuru.
#
{13} أي: وكم من قرية من قُرى المكذِّبين هي أشدُّ قوةً من قريتك في الأموال والأولاد والأعوان والأبنية والآلات، أهلكناهم حين كذَّبوا رُسُلنا، ولم تُفِدْ فيهم المواعظُ؛ فلم نجدْ لهم ناصراً، ولم تغنِ عنهم قوتُهم من عذاب الله شيئاً؛ فكيف حال هؤلاء الضعفاء أهل قريتك إذ أخرجوك عن وطنك، وكذَّبوك وعادَوْك، وأنت أفضل المرسلين وخير الأولين والآخرين؟! أليسوا بأحقَّ من غيرهم بالإهلاك والعقوبة، لولا أنَّ الله تعالى بعثَ رسوله بالرحمة والتأنِّي بكل كافرٍ وجاحدٍ.
{13} Yaani, ni miji mingapi miongoni mwa miji ya wale waliokadhibisha ilikuwa ni yenye nguvu zaidi kuliko mji wako kwa mali, watoto, wasaidizi, majengo na ala mbalimbali, tuliwaangamiza walipowakadhibisha Mitume wetu, na wala mawaidha hayakuwafaa kitu. Kwa hivyo hatukuwapata wakiwa na yeyote wa kuwanusuru, na wala nguvu zao hazikuwafaa chochote mbele ya adhabu ya Mwenyezi Mungu. Basi vipi hali ya hawa wanyonge wana kijiji chako walipokufukuza katika mji wako, wakakukadhibisha na wakakufanyia uadui, ilhali wewe ndiye mbora wa Mitume wote na mbora wa wa mwanzo na wa mwisho? Je, wao hawastahiki zaidi kuangamizwa na kuadhibiwa kuliko wengineo, lau kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumtuma Mtume wake kwa rehema na kutokuwa na haraka juu ya kila kafiri na mwenye kukataa?
: 14 #
{أَفَمَنْ كَانَ عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّهِ كَمَنْ زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ (14)}
14. Je, yule aliye kwenye ubainifu kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama yule aliyepambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata matamanio yao?
#
{14} أي: لا يستوي مَنْ هو على بصيرة من أمر دينِهِ علماً وعملاً قد علم الحقَّ واتَّبعه، ورجا ما وعده الله لأهل الحقِّ؛ كمن هو أعمى القلب، قد رَفَضَ الحقَّ وأضلَّه واتَّبع هواه بغير هدى من الله، ومع ذلك يرى أنَّ ما هو عليه هو الحقُّ؛ فما أبعد الفرق بين الفريقين! وما أعظم التفاوت بين الطائفتين! أهل الحقِّ وأهل الغيِّ.
{14} Yaani: Hawi sawa mwenye ufahamu mzuri wa mambo ya dini yake katika elimu na vitendo. Aliijua haki na akaifuata, na akataraji aliyowaahidi Mwenyezi Mungu wana haki. Yeye hawi sawa na mtu ambaye ni kipofu wa moyo, aliyeikataa haki, akaipotosha, na akafuata matamanio yake bila ya uwongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na pamoja na hayo anaona kwamba ayafanyayo hayo ndiyo haki. Basi ni tofauti kubwa iliyoje hii kati ya makundi haya mbili! Wana haki na wana upotovu.
: 15 #
{مَثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ فِيهَا أَنْهَارٌ مِنْ مَاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِنْ لَبَنٍ لَمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِنْ خَمْرٍ لَذَّةٍ لِلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِنْ عَسَلٍ مُصَفًّى وَلَهُمْ فِيهَا مِنْ كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِنْ رَبِّهِمْ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ (15)}
15. Mfano wa Bustani ya mbinguni waliyoahidiwa wachamngu, ina mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa yasiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo wenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakaodumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayochemka ya kuwakatakata matumbo yao?
#
{15} أي: مثل الجنة التي أعدَّها الله لعباده الذين اتَّقوا سَخَطَه، واتَّبعوا رضوانه؛ أي: نعتها وصفتها الجميلة، {فيها أنهارٌ من ماءٍ غير آسنٍ}؛ أي: غير متغيِّر لا بوخم ولا بريح منتنةٍ ولا بمرارة ولا بكدورةٍ، بل هو أعذب المياه وأصفاها وأطيبها ريحاً وألذّها شرباً، {وأنهار من لبنٍ لم يتغيَّر طعمُه}: بحموضة ولا غيرها، {وأنهار من خمرٍ لَذَّةٍ للشاربين}؛ أي: يلتذُّ بها شاربه لذةً عظيمةً، لا كخمر الدنيا الذي يُكره مذاقُه ويُصَدِّع الرأس ويغوِّلُ العقلَ، {وأنهار من عسل مصفًّى}: من شمعه وسائر أوساخه. {ولهم فيها من كلِّ الثمرات}: من نخيل وعنبٍ وتفاح ورمانٍ وأترجٍّ وتينٍ وغير ذلك ممَّا لا نظير له في الدُّنيا؛ فهذا المحبوبُ المطلوبُ قد حَصَلَ لهم. ثم قال: {ومغفرة من ربِّهم}: يزول بها عنهم المرهوبُ؛ فأيُّ هؤلاء خيرٌ أم {من هو خالدٌ في النار}: التي اشتدَّ حرُّها وتضاعف عذابُها، {وسُقوا}: فيها {ماءً حميماً}؛ أي: حارًّا جدًّا، {فقطَّع أمعاءهم}: فسبحان من فاوت بين الدارين والجزاءين والعاملين والعملين.
{15} Yaani mfano wa Bustani ya mbinguni aliyowaandalia Mwenyezi Mungu waja wake walioogopa ghadhabu yake na wakafuata radhi yake, "ina mito ya maji yasiyovunda." Si kwa uvundo wala kwa harufu inayonuka ya kuoza, wala si machungu, wala hayakuchafuliwa. Bali hayo ndiyo maji safi zaidi, yenye harufu nzuri zaidi, na ladha nzuri zaidi ya kunywa. "Na mito ya maziwa yasiyoharibika ladha yake" kwa kuchacha wala kitu kingine chochote. "Na mito ya mvinyo wenye ladha kwa wanywao." Yaani, mnywaji wake atafurahia ladha yake nzuri sana, si kama mvinyo wa dunia hii, ambao ladha yake inachukiwa, unaumiza kichwa, na kuvuruga akili. "Na mito ya asali iliyosafishwa mno" kutokana na nta yake na uchafu wake wote. "Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda" kama vile mitende, mizabibu, tufaha, mikomamanga, mikorogo, tini, na mengineyo miongoni mwa yale yasiyokuwa na mfano wake hapa duniani. Basi kipendwa hiki kinachotafutwa tayari wameshakipata. Kisha akasema: "Na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi" ambayo kwayo yataondoka kila yanayokimbiwa. Basi huyu ndiye aliye bora zaidi au ni wale "watakaodumu Motoni" ambao joto lake ni kali sana, na adhabu yake inazidishwa maradufu "na wakinyweshwa" humo "maji yanayochemka" mno "na yakawakatakata matumbo yao." Basi ametakasika Yule aliyetofautisha baina ya nyumba mbili hizi, malipo mawili haya, watendao wawili hawa na matendo mawili haya.
: 16 - 17 #
{وَمِنْهُمْ مَنْ يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّى إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِنْدِكَ قَالُوا لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا أُولَئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ (16) وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ (17)}
16. Na wapo miongoni mwao wanaokusikiliza, mpaka wakiondoka kwako, huwauliza waliopewa elimu: 'Amesema nini sasa hivi?' Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziba nyoyo zao, na wakafuata matamanio yao. 17. Na wale walioongoka anawazidishia uongofu na anawapa uchamungu wao.
#
{16} يقول تعالى: ومن المنافقين {مَن يستمعُ إليك}: ما تقول؛ استماعاً لا عن قَبول وانقيادٍ، بل معرضةٌ قلوبهم عنه، ولهذا قال: {حتى إذا خرجوا من عندك قالوا للذين أوتوا العلم}: مستفهمينَ عمَّا قلتَ وما سمعوا ممَّا لم يكنْ لهم فيه رغبةٌ: {ماذا قال آنفاً}؛ أي: قريباً! وهذا في غاية الذمِّ لهم؛ فإنَّهم لو كانوا حريصين على الخير؛ لألْقَوْا إليه أسماعهم ووعتْه قلوبُهم وانقادتْ له جوارحهم، ولكنَّهم بعكس هذه الحال، ولهذا قال: {أولئك الذين طَبَعَ الله على قلوبهم}؛ أي: ختم عليها وسدَّ أبواب الخير التي تصل إليها بسبب اتِّباعهم أهواءهم التي لا يهوون فيها إلاَّ الباطل.
{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Na miongoni mwa wanaafiki yupo “wanaokusikiliza,” mnayoyasema; kusikiza si kwa kuridhia na kunyenyekea, bali nyoyo zao zikajiepusha nayo, na kwa ajili hiyo akasema: "mpaka wakiondoka kwako, huwauliza waliopewa elimu" juu ya yale uliyoyasema na yale waliyoyasikia katika yale wasiyokuwa na hamu nayo: "Amesema nini sasa hivi?" Hili ni la kuwakashifu mno, kwa maana ikiwa walikuwa na hamu kubwa ya kufanya mema, wangempa vyema masikio yao, na nyoyo zao zingemuelewa, na viungo vyao vingemfuata. Lakini wao wako kinyume na hali hii, na ndiyo maana akasema: "Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziba nyoyo zao." Yaani, aliwafungia milango ya heri ambayo kupitia hiyo inaifikia nyoyo. Na hilo ni kwa sababu ya kufuata kwao matamanio yao ambayo ndani yake hawatamani ila batili tu.
#
{17} ثم بيَّن حالَ المهتدين، فقال: {والذين اهتدَوْا}: بالإيمان والانقياد واتِّباع ما يرضي الله {زادهم هدىً}: شكراً منه تعالى لهم على ذلك، {وآتاهم تَقْواهم}؛ أي: وفَّقهم للخير، وحفِظَهم من الشرِّ. فذكر للمهتدين جزاءين: العلم النافع، والعمل الصالح.
{17} Kisha akabainisha hali ya walioongoka, na akasema: "Na wale walioongoka" kwa Imani, utiifu, na kuyafuata anayoyaridhia Mwenyezi Mungu "anawazidishia uongofu" iwe ni shukrani yake kwao juu ya hayo, "na anawapa ucha Mungu wao." Yaani, huwaongoza kwenye heri na kuwalinda kutokana na maovu. Basi hapa akataja malipo mawili kwa walioongoka: elimu yenye manufaa na matendo mema.
: 18 #
{فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّى لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ (18)}
18. Kwani wanangojea jengine isipokuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwishakuja. Na itakapowajia, kutawafaa nini kukumbuka kwao?
#
{18} أي: فهل ينظر هؤلاء المكذِّبون أو ينتظرون {إلاَّ الساعة أن تأتِيَهُم بغتةً}؛ أي: فجأة وهم لا يشعرون، {فقد جاء أشراطُها}؛ أي: علاماتها الدالَّة على قربِها {فأنى لهم إذا جاءتهم ذِكْراهم}؛ أي: من أين لهم إذا جاءتْهم الساعةُ وانقطعتْ آجالهم أن يتذكَّروا ويستعتبوا؛ قد فات ذلك وذهب وقتُ التذكُّر؛ فقد عُمِّروا ما يتذكَّر فيه من تذكَّر وجاءهم النذير. ففي هذا الحثُّ على الاستعداد قبل مفاجأة الموت؛ فإنَّ موت الإنسان قيامُ ساعته.
{18} Maana yake ni kwamba hawa wanaokadhibisha wanangoja lingine "isipokuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla" hali ya kuwa hawajui? "Na hakika alama zake zimekwisha kuja." Yaani, ishara zake zinazoashiria ukaribu wake. “Na itakapowajia, kutawafaa nini kukumbuka kwao?" Hayo yatakuwa yameshachelewa na wakati wa kukumbuka umeshapita. Kwani, walipewa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia Mwonyaji? Basi katika haya kuna kutia hamu ya kujiandaa kabla ya kifo kuja ghafla. Kwa sababu, kifo cha mtu ndiyo kusimama kwa Saa yake (ya Kiyama).
: 19 #
{فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنْبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ (19)}
19. Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
#
{19} العلم لا بدَّ فيه من إقرار القلب ومعرفتِهِ بمعنى ما طُلِبَ منه علمه، وتمامه أن يعملَ بمقتضاه. وهذا العلم الذي أمر اللهُ به، وهو العلم بتوحيد الله، فرضُ عينٍ على كلِّ إنسان، لا يسقطُ عن أحدٍ كائناً مَن كان، بل كلٌّ مضطرٌّ إلى ذلك. والطريق إلى العلم بأنَّه لا إله إلاَّ الله أمورٌ: أحدُها ـ بل أعظمها ـ: تدبُّر أسمائه وصفاته وأفعاله الدالَّة على كماله وعظمتِهِ وجلالِهِ؛ فإنَّها توجب بذل الجهد في التألُّه له والتعبُّد للربِّ الكامل الذي له كلُّ حمدٍ ومجدٍ وجلال وجمال. الثاني: العلمُ بأنَّه تعالى المنفردُ بالخلق والتدبير، فيعلم بذلك أنَّه المنفرد بالألوهية. الثالث: العلم بأنَّه المنفرد بالنعم الظاهرة والباطنة الدينيَّة والدنيويَّة؛ فإنَّ ذلك يوجب تعلُّق القلب به ومحبَّته والتألُّه له وحده لا شريك له. الرابع: ما نراه ونسمعه من الثوابِ لأوليائِهِ القائمين بتوحيدِهِ من النصر والنعم العاجلة، ومن عقوبتِهِ لأعدائِهِ المشركين به؛ فإنَّ هذا داعٍ إلى العلم بأنَّه تعالى وحده المستحقُّ للعبادة كلِّها. الخامس: معرفة أوصاف الأوثان والأنداد التي عُبِدَتْ مع الله واتُّخِذت آلهة، وأنَّها ناقصةٌ من جميع الوجوه، فقيرةٌ بالذات، لا تملك لنفسها ولا لعابديها نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، ولا ينصرون مَن عبدهم ولا ينفعونهم بمثقال ذرَّةٍ من جلب خيرٍ أو دفع شرٍّ؛ فإنَّ العلم بذلك يوجب العلم بأنَّه لا إله إلا الله وبطلان إلهيَّة ما سواه. السادس: اتِّفاق كتب الله على ذلك وتواطؤها عليه. السابع: أن خواصَّ الخلق الذين هم أكملُ الخليقة أخلاقاً وعقولاً ورأياً وصواباً وعلماً ـ وهم الرسلُ والأنبياءُ والعلماء الربانيُّون ـ قد شهِدوا لله بذلك. الثامن: ما أقامه الله من الأدلَّة الأفقيَّة والنفسيَّة التي تدلُّ على التوحيد أعظم دلالةٍ وتنادي عليه بلسان حالها بما أوْدَعَها من لطائف صنعتِهِ وبديع حكمتِهِ وغرائب خلقِهِ؛ فهذه الطرق التي أكثر الله من دعوةِ الخلق بها إلى أنَّه لا إله إلاَّ الله، وأبداها في كتابه وأعادها، عند تأمُّل العبد في بعضها؛ لا بدَّ أن يكون عنده يقينٌ وعلمٌ بذلك؛ فكيف إذا اجتمعت وتواطأت واتَّفقت وقامت أدلَّة للتوحيد من كلِّ جانب؟! فهناك يرسخُ الإيمان والعلم بذلك في قلب العبد؛ بحيث يكون كالجبال الرواسي، لا تزلزِلُه الشُّبه والخيالات، ولا يزداد على تكرُّر الباطل والشُّبه إلاَّ نموًّا وكمالاً. هذا، وإن نظرتَ إلى الدليل العظيم والأمر الكبير ـ وهو تدبُّر هذا القرآن العظيم والتأمُّل في آياته؛ فإنَّه البابُ الأعظم إلى العلم بالتوحيد، ويحصُلُ به من تفاصيله وجمله ما لا تحصل في غيره. وقوله: {واستغفر لذنبِك}؛ أي: اطلب من الله المغفرة لذنبك؛ بأنْ تفعلَ أسباب المغفرةِ من التوبة والدُّعاء بالمغفرة والحسنات الماحية وترك الذُّنوب والعفو عن الجرائم، {و} استغفر أيضاً {للمؤمنين والمؤمناتِ}؛ فإنَّهم بسبب إيمانهم كان لهم حقٌّ على كلِّ مسلم ومسلمةٍ، ومن جملة حقوقهم أن يُدعَى لهم ويُسْتَغْفَرَ لذُنوبهم، وإذا كان مأموراً بالاستغفار لهم المتضمِّن لإزالة الذُّنوب وعقوباتها عنهم؛ فإنَّ من لوازم ذلك النُّصح لهم، وأن يحبَّ لهم من الخير ما يحبُّ لنفسه، ويكره لهم من الشرِّ ما يكرهُ لنفسِهِ، ويأمرهم بما فيه الخيرُ لهم، وينهاهم عمَّا فيه ضررُهم، ويعفو عن مساويهم ومعايبهم، ويحرصُ على اجتماعهم اجتماعاً تتألف به قلوبُهم، ويزول ما بينهم من الأحقاد المفضية للمعاداة والشقاق، الذي به تكثُرُ ذنوبهم ومعاصيهم. {واللهُ يعلم مُتَقَلَّبَكُم}؛ أي: تصرُّفاتكم وحركاتكم وذهابكم ومجيئكم، {ومَثْواكم}: الذي به تستقرُّون؛ فهو يعلمكم في الحركات والسَّكَنات، فيجازيكم على ذلك أتمَّ الجزاء وأوفاه.
{19} Kuwa na elimu kunalazimu mtu kukiri kwa moyo na kujua vyema maana ya kile anachotakiwa kukifanya, na utimilifu wake ni mtu kufanya matendo kulingana na matakwa yake. Na kujua huku ambako Mwenyezi Mungu aliamrisha ambako ni kujua upweke wa Mwenyezi Mungu, ni wajibu wa mtu binafsi kwa kila mwanadamu, hautoki wajibu huu kwa yeyote yule, bali kila mtu analazimika kujua hivyo. Na njia ya kujua kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu ni mambo mbalimbali: Moja yake - bali kubwa yake zaidi - ni kuyatafakari majina yake, sifa zake, na vitendo vyake vinavyoashiria ukamilifu wake, ukuu wake, na utukufu wake. Hayo kwa hakika yanalazimu mtu kujitahidi mno kumfanyia Mwenyezi Mungu uungu na kumwabudu Mola Mlezi, Mkamilifu, ambaye ni zake sifa njema zote, taadhima, utukufu na uzuri. La pili ni kujua kwamba Yeye ndiye wa pekee katika kuumba na kuendesha mambo. Kwa hivyo inajulikana kwa hayo kwamba Yeye ndiye wa pekee katika uungu. La tatu ni kujua kwamba Yeye ni wa pekee katika neema za dhahiri na zilizofichika, za kidini na za kidunia. Hayo yanalazimu moyo kufungamana naye, kumpenda na kumfanya uungu Yeye peke yake, bila ya mshirika yeyote. La nne ni yale tunayoyaona na kuyasikia juu ya malipo kwa vipenzi wake wanaompwekesha kwamba atawanusuru na kuwapa neema za sasa hivi, na kuwaadhabu maadui zake wanaomshirikisha. Hayo yanamfanya mtu kujua kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahili ibada zote. La tano ni kujua sifa za masanamu na wale wafanywao kuwa wenza wa Mwenyezi Mungu ambao waliabudiwa pamoja na Mwenyezi Mungu na wakachukuliwa kuwa miungu, na kwamba wana mapungufu kwa namna zote, wao wenyewe ni wahitaji sana, hawajimilikii wenyewe wala hawamilikii wale wanaowaabudu manufaa yoyote, madhara, mauti, uhai wala ufufuo, na hawawezi kuwanusuru wale wanaowaabudu, wala kuwanufaisha kwa uzito wa chembe katika kuwaletea heri au kuwazuilia uovu. Kwani kujua hivyo kunalazimu mtu kujua kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu na ubatili wa uungu wa kitu chochote kisichokuwa Yeye. La sita ni kukubaliana kwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu juu ya hilo. La saba ni kwamba viumbe maalumu ambao ndio viumbe kamili zaidi katika suala la maadili, akili, rai, kuwa katika usahihi na elimu - nao ni Mitume, Manabii wanaomuabudu Mola wao Mlezi tu - walimshuhudilia Mwenyezi Mungu hilo. La nane ni ushahidi mbalimbali wa kiupeo wa macho na wa kibinafsi ambao Mwenyezi Mungu aliusimamisha juu ya upweke wake ni ushahidi mkubwa zaidi, na huo wenyewe tu kwa kuutazama unalingania hilo kwa sababu ya yale aliyoweka Mwenyezi Mungu ndani yake ya maumbile yenye ustadi mkubwa, hekima yake kubwa zaidi na maajabu ya uumbaji wake. Hizi ndizo njia ambazo Mwenyezi Mungu alizitumia zaidi katika kuwalingania viumbe kwa hizo katika kudhibitisha suala kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na akaziweka wazi kabisa katika Kitabu chake na akazirudia, na mja anapozitafakari baadhi yake, lazima atakuwa na yakini na elimu ya hilo. Basi itakuwaje kama utakutana na ushahidi huu, na ukakubaliana na ushahidi wa upweke wake ukasimama kutokea kila upande? Hapo, imani na ujuzi wa jambo hili vitakuwa imara katika moyo wa mja, kiasi kwamba utakuwa kama milima dhabiti isiyotikisika kwa sintowazi na dhana potofu, na wala haiongezeki licha ya kurudiarudia kwa batili na sintowazi isipokuwa kukua sawasawa na kukamilika. Hili ni hivyo, na zaidi ni kwamba ukiangalia ushahidi mkubwa na jambo kubwa - ambao ni kuitafakari Qur-ani hii tukufu na kuzitafakari Aya zake, kwani huo ndilo lango kuu kujua elimu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na elimu hiyo inapatikana humo kwa maelezo ya kina kwa namna ambayo haiwezi kupatikana mahali pengine. Na kauli yake: "Na omba maghufira kwa dhambi zako." Yaani, Mwombe Mwenyezi Mungu msamaha kwa dhambi zako, kwa kufanya visababu vya msamaha, kama vile toba, kuomba dua ya msamaha, kutenda matendo mema yenye kufuta dhambi, na kuacha madhambi, na kusamehe makosa. "na" pia omba msamaha "kwa ajili ya Waumini wanaume na Waumini wanawake." Kwani, sababu ya imani yao wanakuwa na haki juu ya kila Mwislamu mwanamume na mwanamke, na miongoni mwa haki zao ni kuwaombea dua na kuwaombea msamaha kwa madhambi yao. Na ikiwa aliamrishwa kuwaombea msamaha, ambako kunajumuisha kuwafutia madhambi na adhabu yake, basi miongoni mwa mambo yanayofungamana na hilo ni kuwapa ushairi mzuri, na kuwapendea heri anayojipendea mwenyewe, na kuwachukia ubaya anaojichukia mwenyewe, kuwaamrisha kuwafanya yenye heri kwao, na kuwakataza na yale yenye madhara kwao, na kusamehe makosa yao na mapungufu yao, na kufanya hima kubwa ya kuwakusanya kwa njia ya kuziunganisha nyoyo zao, na kuwaondolea yale yenye kinyongo ambayo yanaweza kusababisha uadui na kutengana kwao; mambo ambayo kwa hayo yanazidi madhambi yao na maasia. "Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi" na mkakaa ili kupumzika. Kwa hili anajua harakati zenu na kutulia kwenu, kisha atakulipeni kwa hayo malipo kamili.
: 20 - 23 #
{وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ فَإِذَا أُنْزِلَتْ سُورَةٌ مُحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا الْقِتَالُ رَأَيْتَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ يَنْظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ الْمَغْشِيِّ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ فَأَوْلَى لَهُمْ (20) طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَعْرُوفٌ فَإِذَا عَزَمَ الْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا اللَّهَ لَكَانَ خَيْرًا لَهُمْ (21) فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ (22) أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ (23)}.
20. Na Waumini wanasema: 'Kwa nini haiteremshwi Sura?' Na inapoteremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake habari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa sababu ya mauti. Basi ni bora kwao. 21. Utiifu na kauli njema. Na jambo likishaazimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni heri kwao. 22. Basi mnatarajia kwamba mkigeuka mkaenda zenu kwamba ndio mtafanya uharibifu katika nchi na muwatupe jamaa zenu? 23. Hao ndio aliowalaani Mwenyezi Mungu, na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao.
#
{20} يقول تعالى: {ويقولُ الذين آمنوا}: استعجالاً ومبادرةً للأوامر الشاقَّة: {لولا نُزِّلَتْ سورةٌ}؛ أي: فيها الأمر بالقتال، {فإذا أنزِلَتْ سورةٌ محكمةٌ}؛ أي: ملزم العمل بها، {وذُكِرَ فيها القتالُ}: الذي هو أشقُّ شيء على النفوس؛ لم يثبتْ ضعفاء الإيمان على امتثال هذه الأوامر، ولهذا قال: {رأيتَ الذين في قلوبِهِم مرضٌ ينظُرون إليك نَظَرَ المغشيِّ عليه من الموت}: من كراهتهم لذلك وشدَّته عليهم، وهذا كقوله تعالى: {ألم تَرَ إلى الذين قيل لهم كُفُّوا أيدِيَكم وأقيموا الصلاة وآتوا الزَّكاة فلمَّا كُتِبَ عليهم القتالُ إذا فريقٌ منهم يخشَوْن الناس كخشية الله أو أشدَّ خشيةً}.
{20} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na Waumini wanasema" kwa kuzifanyia haraka amri ngumu: "Kwa nini haiteremshwi Sura?" Yaani, yenye amri ya kupigana vita. "Na inapoteremshwa Sura madhubuti." Yaani, yenye kuwajibisha kuitekeleza, "na ikatajwa ndani yake habari ya vita" jambo ambalo ndilo gumu zaidi kwa nafsi, wale wanyonge wa imani hawawezi kuwa na msimamo imara katika kutekeleza maamrisho haya. Na ndiyo maana akasema: "Utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa sababu ya mauti," kwa sababu ya kuchukia kwao hayo na ugumu wake juu yao, na hili ni kama kauli ya Mwenyezi Mungu: "Je, huwaoni wale walioambiwa: 'Izuieni mikono yenu, na mshike Sala na mtoe Zaka.' Na walipoamrishwa kupigana, mara kundi moja kati yao liliwaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa hofu kubwa zaidi."
#
{20 - 21} ثم ندبهم تعالى إلى ما هو الأليقُ بحالهم، فقال: {فأولى لهم. طاعةٌ وقولٌ معروفٌ}؛ أي: فأولى لهم أن يمتثلوا الأمر الحاضر المحتَّم عليهم، ويَجْمَعوا عليه هِمَمَهم، ولا يطلبوا أن يَشْرَعَ لهم ما هو شاقٌّ عليهم، وليفرَحوا بعافية الله تعالى وعفوِهِ، {فإذا عزم الأمر}؛ أي: جاءهم أمر جدٍّ وأمر محتَّم، ففي هذه الحال، لو {صَدَقوا الله}: بالاستعانة به وبذل الجهد في امتثاله، {لكان خيراً لهم}: من حالهم الأولى، وذلك من وجوه: منها: أنَّ العبد ناقصٌ من كلِّ وجه، لا قدرة له إلاَّ إن أعانه الله؛ فلا يطلب زيادة على ما هو قائم بصدده. ومنها: أنَّه إذا تعلَّقت نفسُه بالمستقبل؛ ضعف عن العمل بوظيفة وقته الحاضر وبوظيفة المستقبل، أما الحال؛ فلأنَّ الهمَّة انتقلت عنه إلى غيره، والعمل تبعٌ للهمَّة. وأما المستقبل؛ فإنَّه لا يجيء حتى تفتُرَ الهمَّة عن نشاطها، فلا يُعان عليه. ومنها: أنَّ العبد المؤمِّل للآمال المستقبلة، مع كسله عن عمل الوقت الحاضر، شبيهٌ بالمتألِّي الذي يجزم بقدرته على ما يستقبل من أموره؛ فأحرى به أن يُخْذَلَ ولا يقوم بما همَّ به و [وطّن] نفسه عليه؛ فالذي ينبغي أن يجمع العبد همَّه وفكرتَه ونشاطَه على وقته الحاضر، ويؤدِّي وظيفته بحسب قدرته، ثم كلَّما جاء وقتٌ؛ استقبله بنشاط وهمَّةٍ عاليةٍ مجتمعةٍ غير متفرِّقة، مستعيناً بربِّه في ذلك؛ فهذا حريٌّ بالتوفيق والتسديد في جميع أموره.
{20 - 21} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawahimiza wafanye yanayoifailia zaidi hali yao, akasema: "Basi ni bora kwao. Utiifu na kauli njema." Yaani, ni bora kwao kutekeleza amri iliyopo sasa juu yao, na kuziunganisha hima zao juu yake, na wasiombe kuwekewa sheria ya yale yatakayowawia magumu, na wafurahie usalama wa Mwenyezi Mungu na msamaha wake, "Na jambo likishaazimiwa." Yaani, jambo zito na lisiloepukika likishawajia katika hali hii, basi lau “wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu” kwa kutafuta msaada wake na kujitahidi kulitekeleza, “bila ya shaka itakuwa ni heri kwao” kuliko hali yao ya awali, na hilo ni kutokana na mambo kadhaa: miongoni mwake ni kwamba mja ni mpungufu katika kila namna, hana uwezo wowote isipokuwa Mwenyezi Mungu akimsaidia; basi na asiombe zaidi ya yale aliyojukumishwa tayari. Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa nafsi yake itafungamana na wakati ujao, basi atadhoofika kufanya matendo ya katika wa sasa na pia wakati ujao. Ama wakati wa sasa, hilo ni kwa sababu hima yake tayari imeshahama hadi kwingine, na matendo hufuatana na hima. Na ama siku zijazo, huo hautakuja isipokuwa itakuwa hima yake juu ya ukakamavu itakuwa tayari imeshapunguka, kwa hivyo hataweza kusaidiwa juu yake. Na miongoni mwake ni kwamba mja anayetarajia matarajio ya wakati ujao, pamoja na kwamba ni mzembe wa kufanya matendo katika wakati uliopo, ni sawa na yule anayejigamba ambaye anajiona kwamba ana uhakika juu ya uwezo wake wa kushughulikia mambo yake ya baadaye. Huyo anafailia zaidi kuachiliwa mbali na asiweze kufanya alichokusudia na akaizoesha nafsi yake juu yake. Kwa hivyo, kinachopaswa kufanywa na mja ni kukusanya hima yake, mawazo yake na ukakamavu wake katika wakati wake wa sasa, na kufanya majukumu yake kulingana na uwezo wake. Kisha wakati wowote unapofika, anaupokea kwa ukakamavu na azimio kubwa, iliyounganishwa na sio iliyotengana, akitafuta msaada wa Mola wake Mlezi katika hilo. Mtu huyu anastahili zaidi kufanikishwa na kuwekwa katika usawa katika mambo yake yote.
#
{22} ثم ذكر تعالى حال المتولِّي عن طاعة ربِّه، وأنَّه لا يتولَّى إلى خيرٍ، بل إلى شرٍّ، فقال: {فهل عسيتُمْ إن تَوَلَّيْتُم أن تفسدوا في الأرض وتقطِّعوا أرحامكم}؛ أي: فهما أمران: إمَّا التزامٌ لطاعة الله وامتثالٌ لأوامره؛ فثَمَّ الخيرُ والرشدُ والفلاح. وإمَّا إعراضٌ عن ذلك وتولي عن طاعةِ الله؛ فما ثَمَّ إلاَّ الفساد في الأرض بالعمل بالمعاصي وقطيعة الأرحام.
{22} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hali ya mwenye kuacha kumtii Mola wake Mlezi, na kwamba hageuki akaenda kwenye heri, bali anageuka kwenda kwenye uovu, akasema: "Basi mnatarajia kwamba mkigeuka mkaenda zenu kwamba ndio mtafanya uharibifu katika nchi na muwatupe jamaa zenu?" Yaani, ni vitu viwili tu: Ima kushikamana na kumtii Mwenyezi Mungu na kufuata amri zake, basi hiyo ndiyo heri na kuwa katika njia ya sawasawa na kufaulu. Au kuyapa mgongo na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu, basi hapo hakuna chochote ila uharibfu katika dunia kwa kufanya maasia na kukata mahusiano ya kifamilia.
#
{23} {أولئك الذين}: أفسدوا في الأرض، وقطَّعوا أرحامهم. {لَعَنَهم الله}: بأن أبعدهم عن رحمته وقربوا من سخط الله {فأصمَّهم وأعمى أبصارَهم}؛ أي: جعلهم لا يسمعون ما ينفَعُهم ولا يبصِرونه؛ فلهم آذانٌ ولكن لا تسمعُ سماع إذعانٍ وقَبولٍ، وإنَّما تسمع سماعاً تقومُ بها حجةُ الله عليها، ولهم أعينٌ ولكن لا يبصِرون بها العبرَ والآيات، ولا يلتفتونَ بها إلى البراهين والبيِّنات.
{23} "Hao ndio" wale waliofanya uharibifu katika ardhi, na wakakata jamaa zao kwa hivyo "aliowalaani Mwenyezi Mungu," kwa kuwaweka mbali na rehema zake na wakawa karibu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu "na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao." Yaani, aliwafanya wasikie yenye kuwafaa wala hata hawayaoni. Kwani wana masikio, lakini hawasikii kwa kusikia kwa kutii na kukubali, bali wanasikia kusikia kwa kuwasimamishia hoja ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na wana macho lakini hawaoni kwayo mazingatio na ishara, na wala hawaangalii kwayo hoja mbalimbali na ushahidi ulio wazi.
: 24 #
{أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَى قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا (24)}
24. Je, hawaizingatii hii Qur-ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli zake?
#
{24} أي: فهلاَّ يتدبَّر هؤلاء المعرضون لكتاب الله ويتأمَّلونه حقَّ التأمُّل؛ فإنهم لو تدبَّروه؛ لدلَّهم على كلِّ خيرٍ، ولحذَّرهم من كلِّ شرٍّ، ولملأ قلوبَهم من الإيمان وأفئدتهم من الإيقان، ولأوصلهم إلى المطالب العالية والمواهبِ الغالية، ولبيَّن لهم الطريقَ الموصلة إلى الله وإلى جنَّته ومكمِّلاتها ومفسداتها، والطريقَ الموصلة إلى العذابِ، وبأيِّ شيء يُحذر ، ولعرَّفهم بربِّهم وأسمائه وصفاته وإحسانه، ولشوَّقهم إلى الثواب الجزيل، ورهَّبهم من العقاب الوبيل، {أم على قلوبٍ أقفالُها}؛ أي: قد أغلق على ما فيها من الإعراض والغفلة والاعتراض ، وأقفِلَت فلا يدخلها خيرٌ أبداً؟! هذا هو الواقع.
{24} Yaani, kwa nini hawa wanaokipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu hawakizingatii na kukitafakari ipasavyo? Kwani ikiwa walikitafakari, kingewaonyesha kila heri, na kingewahadharisha na kila shari, na kingezijaza nyoyo zao imani na sehemu zao za ndani mno kwa yakini, na kingewafikisha kwenye mambo yatafutwayo ya hali ya juu na tunu za thamani kubwa, na kingewabainishia njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na Bustani zake za mbinguni, na vyenye kuikamilisha na vyenye kuiharibu, na njia ifikishayo kwenye adhabu, na kwa kitu kipi inaepukwa, na kingewajulisha Mola wao Mlezi, kwa majina yake, na sifa zake, na wema wake, na kingewapa shauku kubwa ya kufikia thawabu nyingi, na kingewahofisha mno adhabu kali zaidi. "Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli zake?" Yaani, ziliifunga pamoja na yale yaliyomo ya kupeana mgongo, kughafilika na kupinga, kwa hivyo zikafungika kwa hivyo, heri haiwezi kuingia humo kabisa? Hii ndiyo hali halisi.
: 25 - 28 #
{إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَى أَدْبَارِهِمْ مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَى لَهُمْ (25) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللَّهُ سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ (26) فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ (27) ذَلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ (28)}.
25. Kwa hakika wale wanaorudi nyuma baada ya uwongofu kwisha wabainikia, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri. 26. Hayo ni kwa sababu waliwaambia wale waliochukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu: 'Tutakutiini katika baadhi ya mambo.' Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao. 27. Basi itakuwaje Malaika watakapowafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao! 28. Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yale yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.
#
{25} يخبر تعالى عن حالة المرتدِّين عن الهدى والإيمان على أعقابهم إلى الضلال والكفران، ذلك لا عن دليل دلَّهم ولا برهان، وإنَّما هو تسويلٌ من عدوِّهم الشيطان، وتزيينٌ لهم وإملاءٌ منه لهم؛ {يعِدُهم ويمنِّيهم وما يعِدُهُم الشيطانُ إلاَّ غروراً}.
{25} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeleza kuhusu hali ya wale walioritadi wakaacha uwongofu na imani na wakageuka kwenye visigino vyao wakaenda katika upotofu na ukafiri, si kwa sababu ushahidi uliowaelekeza kufanya hivyo wala hoja. Lakini ilikuwa tu kushawishiwa na adui wao, Shetani ambaye aliwapambia na akawatia matarajio marefu. "Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shetani hawaahidi ila udanganyifu."
#
{26} و {ذلك}: أنَّهم قد تبيَّن لهم الهدى، فزهدوا فيه ورفضوه، و {قالوا للذين كرِهوا ما نَزَّلَ الله}: من المبارزين العداوة لله ولرسوله: {سنُطيعكم في بعض الأمرِ}؛ أي: الذي يوافق أهواءهم؛ فلذلك عاقبهم الله بالضلال والإقامة على ما يوصِلُهم إلى الشقاء الأبديِّ والعذاب السرمديِّ، {واللهُ يعلمُ إسرارَهم}: فلذلك فضحهم، وبيَّنها لعباده المؤمنين؛ لئلاَّ يغترُّوا بها.
{26} Na "hayo ni kwa sababu" ya kuwa uwongofu ulikwisha wabainikia, lakini wakakata tamaa nao na wakaukataa. "Wakawaambia wale waliochukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu" miongoni mwa wale wanaosimama kidete katika kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "Tutakutiini katika baadhi ya mambo." Yaani, yale yatakayoafikiana na matamanio yao, basi ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa upotofu na kudumu katika yale yatakayowafikisha kwenye mashaka ya milele na adhabu ya kudumu milele, "na Mwenyezi Mungu anajua siri zao." Kwa hivyo akawafedhehesha kwa hizo, na akawazibainisha kwa waja wake Waumini; wasije wasidanganyike nazo.
#
{27} {فكيف} ترى حالَهم الشنيعة ورؤيتهم الفظيعة، {إذا توفَّتْهم الملائكةُ}: الموكلون بقبض أرواحهم، {يضرِبون وجوهَهم وأدبارَهم}: بالمقامع الشديدة.
{27} "Basi itakuwaje" hali yao mbaya zaidi na mwonekano wao wa kutisha mno "Malaika watakapowafisha," kwa kuchukua roho zao "wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao" kwa marungu makali mno!
#
{28} {ذلك}: العذابُ الذي استحقُّوه ونالوه، بسبب {أنَّهم اتَّبعوا ما أسخَطَ اللهَ}: من كل كفرٍ وفسوقٍ وعصيانٍ، {وكرهوا رِضْوانَه}: فلم يكن لهم رغبةٌ فيما يقرِّبهم إليه ولا يدنيهم منه، {فأحبط أعمالَهم}؛ أي: أبطلها وأذهبها، وهذا بخلاف من اتَّبع ما يُرضي الله وكره سخطه؛ فإنَّه سيكفِّر عنه سيئاتِهِ ويضاعِفُ له أجره وثوابه.
{28} "Hiyo" adhabu waliyostahiki na wakaipata ni kwa sababu "wao waliyafuata yale yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu" miongoni mwa kila ukafiri, kutoka katika mipaka ya Mwenyezi mungu na uasi. "Na wakachukia yanayomridhisha" wakakosa kabisa kutaka yale yenye kuwaweka karibu naye; "basi akaviangusha vitendo vyao." Na hili ni tofauti na yule anayefuata yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na akachukia yanayomkasirisha. Huyu Mwenyezi Mungu atamfutia madhambi yake na amzidishie maradufu malipo yake mazuri.
: 29 - 31 #
{أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ أَنْ لَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ أَضْغَانَهُمْ (29) وَلَوْ نَشَاءُ لَأَرَيْنَاكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُمْ بِسِيمَاهُمْ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ أَعْمَالَكُمْ (30) وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّى نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنْكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ (31)}.
29. Je, wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hatazidhihirisha chuki zao? 30. Na tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao. Lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu. 31. Na bila ya shaka tutawajaribu mpaka tuwajue wapignao Jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazifanyia mtihani habari zenu.
#
{29} يقول تعالى: {أم حَسِبَ الذين في قلوبهم مرضٌ}: من شبهة أو شهوة؛ بحيث تخرِجُ القلب عن حال صحَّته واعتداله، أن الله لا يخرج ما في قلوبهم من الأضغانِ والعداوةِ للإسلام وأهله! هذا ظنٌّ لا يَليقُ بحكمة الله؛ فإنَّه لا بدَّ أن يميِّز الصادق من الكاذب، وذلك بالابتلاء بالمحنِ التي مَن ثَبَتَ عليها ودام إيمانُه فيها؛ فهو المؤمن حقيقةً، ومَن ردَّته على عقبيه، فلم يصبرْ عليها، وحين أتاه الامتحان جَزعَ وضَعُفَ إيمانه وخرج ما في قلبِهِ من الضَّغَن وتبيَّن نفاقُه؛ هذا مقتضى الحكمة الإلهيَّة.
{29} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani" maradhi ya kuwa na shaka au matamanio ya nafsi, kwamba Mwenyezi Mungu hatatoa nje kinyongo na uadui ulio katika nyoyo zao dhidi ya Uislamu na watu wake! Hii ni dhana ambayo haifailii hekima ya Mwenyezi Mungu. Ni lazima kupambanua mkweli na mwongo, na hilo ni kwa kupima kupeana mtihani kwa misukosuko ambayo mwenye kubakia imara ndani yake na imani yake ikadumu humo, basi yeye ndiye Muumini wa kweli. Na mwenye kurudishwa nyuma nayo kwa visigino vyake, akawa hana subira juu yake, na pindi mtihani ulipomjia, alipapatika na imani yake ikadhoofika, na kinyongo kilichokuwa moyoni mwake na unafiki wake ukatoka nje na ukabainika wazi. Hivi ndivyo inavyohitajika katika hekima ya kimungu.
#
{30} مع أنَّه تعالى قال: {لو نشاء لأرَيْناكَهم فلَعَرَفْتَهم بسيماهم}؛ أي: بعلاماتهم التي هي كالرسم في وجوههم، {ولتعرِفَنَّهم في لحنِ القول}؛ أي: لا بدَّ أن يظهرَ ما في قلوبهم ويتبيَّن بفلتاتِ ألسنتهم؛ فإنَّ الألسنَ مغارفُ القلوب، يظهر فيها ما في القلوب من الخير والشرِّ، {والله يعلمُ أعمالَكم}: فيجازيكم عليها.
{30} Ijapokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao" zilizo kama michoro kwenye nyuso zao. "Lakini bila ya shaka, utawajua kwa namna ya msemo wao." Kwani ndimi ndizo zenye kudhihirisha uzuri na uovu ulio katika nyoyo. "Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu" na atawalipa kwa hivyo.
#
{31} ثم ذَكَرَ أعظم امتحانٍ يمتحنُ به عبادَه، وهو الجهادُ في سبيل الله، فقال: {ولَنَبْلُوَنَّكم}؛ أي: نختبر إيمانكم وصبركم، {حتى نعلمَ المجاهدين منكم والصابرين ونبلوَ أخبارَكم}: فمن امتثل أمر الله وجاهدَ في سبيل الله بنصر دينِهِ وإعلاءِ كلمتِهِ؛ فهو المؤمن حقًّا، ومن تكاسل عن ذلك؛ كان ذلك نقصاً في إيمانه.
{31} Kisha akataja mtihani mkubwa zaidi anaowajaribu kwa huo waja wake, ambao ni kipigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, akasema: "Na bila ya shaka, tutawajaribu" imani yenu na subira yenu "mpaka tuwajue wapiganao Jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazifanyia mtihani habari zenu." Basi anayetekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na akapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kunusuru Dini yake na kunyanyua neno lake, basi huyo ndiye Muumini wa kweli. Na mwenye kujitia uvivu katika hilo, huo utakuwa ni upungufu katika imani yake.
: 32 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَشَاقُّوا الرَّسُولَ مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى لَنْ يَضُرُّوا اللَّهَ شَيْئًا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَالَهُمْ (32)}.
32. Kwa hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na Mtume baada ya uwongofu kwishawabainikia, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.
#
{32} هذا وعيدٌ شديدٌ لمن جمع أنواع الشرِّ كلِّها من الكفر بالله وصدِّ الخلق عن سبيل الله الذي نَصَبَه موصلاً إليه، {وشاقُّوا الرسولَ من بعدِ ما تبيَّن لهم الهُدى}؛ أي: عاندوه وخالفوه عن عمدٍ وعنادٍ، لا عن جهل وغيٍّ وضلال؛ فإنَّهم {لن يضرُّوا الله شيئاً}؛ فلا ينقص به ملكه، {وسيُحْبِطُ أعمالَهم}؛ أي: مساعيهم التي بذلوها في نصر الباطل؛ بأنْ لا تثمرَ لهم إلاَّ الخيبة والخسران، وأعمالهم التي يرجون بها الثواب لا تُقبل؛ لعدم وجودِ شرطها.
{32} Hili ni ahadi ya adhabu kali kwa wanaojumuisha kila aina ya uovu, kama vile kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuwazuilia viumbe njia ya Mwenyezi Mungu aliyoiweka iwe ni ya kuwafikisha kwake, "na wakapinzana na Mtume baada ya uwongofu kwisha wabainikia" kwa makusudi na kwa ukaidi, si kwa kutojua, na upotofu. Basi "hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote" na wala ufalme wake hautapungua kwa hayo. "Naye ataviangusha vitendo vyao" walivyovifanyia juhudi katika kubwa katika kuunga mkono batili, kwa namna kwamba havitawazalia chochote isipokuwa kuambulia patupu na kupata hasara, na tena matendo yao wanayoyatarajia hayatakubaliwa; kwa sababu hawakutekeleza sharti lake.
: 33 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ (33)}.
33. Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu.
#
{33} يأمر تعالى المؤمنين بأمرٍ به تتمُّ [أمورُهم] وتحصل سعادتُهم الدينيَّة والدنيويَّة، وهو طاعتُه وطاعة رسولِهِ في أصول الدين وفروعه، والطاعةُ هي امتثال الأمر واجتنابُ النهي على الوجه المأمور به بالإخلاص وتمام المتابعة، وقوله: {ولا تبطلوا أعمالكم}: يشملُ النهي عن إبطالها بعد عملها بما يفسِدُها مِن مَنٍّ بها وإعجابٍ وفخرٍ وسمعةٍ، ومن عملٍ بالمعاصي التي تضمحلُّ معها الأعمال ويحبطُ أجرُها. ويشمل النهي عن إفسادِها حال وقوعها بقطِعها أو الإتيان بمفسدٍ من مفسداتها. فمبطلاتُ الصلاة والصيام والحجِّ ونحوها كلُّها داخلةٌ في هذا ومنهيٌّ عنها. ويستدلُّ الفقهاء بهذه الآية على تحريم قطع الفرض وكراهةِ قطع النفل من غير موجبٍ لذلك، وإذا كان الله قد نهى عن إبطال الأعمال؛ فهو أمرٌ بإصلاحها وإكمالها وإتمامها والإتيان بها على الوجهِ الذي تَصْلُحُ به علماً وعملاً.
{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha Waumini kutekeleza amri ambayo kwayo [mambo yao] yatakamilika na watapata furaha yao ya kidini na ya kidunia, ambayo ni kumtii Yeye na kumtii Mtume wake katika misingi ya dini na matawi yake. Na utiifu ni kutekeleza amri na kujiepusha na makatazo kwa namna ilivyoamrishwa kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake na kumfuta Mtume kikamilifu. Na kauli yake: "Wala msiharibu vitendo vyenu" inajumuisha kuviharibu baada ya kuvifanya; kwa kufanya jambo linaloviharibu, kama vile kujisifia, kujivuna, kujigamba, na kutafuta sifa, na kutenda maasi ambayo yanapunguza matendo na kuharibu thawabu zake. Na inajumuisha kukataza kuviharibu vinapokuwa bado vinafanywa kwa kuvikatisha au kufanya chochote cha kuviharibu. Kwa hivyo, yenye kubatilisha Swala, Saumu, Hija, na mengineyo yote yanaingia katika hili na yamekatazwa. Manazuoni wa elimu ya Fiqh wanaitumia Aya hii kuwa ni ushahidi wa kuharamisha kukatisha Swala za faradhi, na kuchukia kukatisha Swala za hiyari bila ya kuwepo jambo la kuruhusu kufanya hivyo. Ikiwa Mwenyezi Mungu alikataza kubatilisha matendo, basi hiyo ni amri ya kuyafanya kuwa mazuri, makamilifu, na kuyatekeleza kwa namna ambayo ni sahihi kwa elimu na vitendo.
: 34 - 35 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ ثُمَّ مَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَهُمْ (34) فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنْتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَنْ يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ (35)}.
34. Hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao. 35. Basi msilegee na mkataka suluhu, maana nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu.
#
{34} هذه الآية والتي في البقرة قوله: {ومَن يرتَدِدْ منكم عن دينِهِ فيمتْ وهو كافرٌ فأولئك حبطتْ أعمالُهم في الدُّنيا والآخرةِ}: مقيِّدتانِ لكلِّ نصٍّ مطلق فيه إحباط العمل بالكفر؛ فإنَّه مقيدٌ بالموت عليه، فقال هنا: {إنَّ الذين كفروا}: بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر، {وصدُّوا}: الخلق {عن سبيل الله}: بتزهيدهم إيَّاهم بالحقِّ، ودعوتهم إلى الباطل وتزيينه، {ثم ماتوا وهم كفارٌ}: لم يتوبوا منه، {فلن يَغْفِرَ اللهُ لهم}: لا بشفاعة ولا بغيرها؛ لأنَّه قد تحتَّم عليهم العقاب، وفاتهم الثواب، ووجب عليهم الخلود في النار، وسُدَّت عليهم رحمة الرحيم الغفار. ومفهومُ الآية الكريمة أنَّهم إن تابوا من ذلك قبل موتِهِم؛ فإنَّ الله يغفرُ لهم ويرحمهُم ويدخِلُهم الجنَّة، ولو كانوا مفنينَ أعمارَهم في الكفر به والصدِّ عن سبيله والإقدام على معاصيه. فسبحان من فَتَحَ لعبادِهِ أبوابَ الرحمة ولم يغلِقْها عن أحدٍ ما دام حيًّا متمكناً من التوبة. وسبحان الحليم الذي لا يعاجل العاصين بالعقوبة، بل يعافيهم ويرزقُهم كأنَّهم ما عصوه مع قدرته عليهم.
{34} Aya hii, na ile iliyo katika Surat Al-Baqarah, kauli: "Na yeyote katika nyinyi akiacha Dini yake akafa naye ni kafiri, basi hao ndio ambao amali zao zimeharibika duniani na Akhera" zinafungia kila aya ambayo haikufungiwa ambayo ndani yake kuna kuharibu matendo kwa ukafiri, hizo zimefungiwa kwa sharti kwamba afe katika hali hiyo. Na akasema hapa: "Hakika wale waliokufuru" Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, "na wakazuilia" viumbe "njia ya Mwenyezi Mungu" kwa kuwavunja moyo wa kukubali haki na kuwalingania kwenye batili na kuwapambia batili hiyo "kisha wakafa na hali ya kuwa makafiri" bila ya kutubu wakaacha ukafiri huo, "basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao" si kwa uwombezi wala kwa njia nyingine yoyote; kwa sababu imeshahakikika kwamba wataadhibiwa, wakakosa malipo mzuri, ikawa ni lazima watakaa milele katika Jahanamu, na wakafungiwa rehema ya Mwingi wa rehema, Mwingi wa kusamehe. Maana isiyokuwa ya moja kwa moja Aya hii tukufu ni kwamba wakitubia hayo kabla ya kufa kwao, basi Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawarehemu, na atawaingiza katika Bustani za mbinguni, hata kama walimalizia maisha yao katika kumkufuru, na kuzuilia njia yake na kumuasi. Basi ametakasika Yule aliyewafungulia waja wake milango ya rehema na wala hakumfungia yeyote maadamu bado yu hai na anaweza kutubia. Na ametakasika, Mstahamilivu, ambaye hawaharakishii adhabu wale wanaofanya maasi, bali huwaacha salama na kuwaruzuku kana kwamba hawakumuasi, licha ya uwezo wake mkubwa juu yao.
#
{35} ثم قال تعالى: {فلا تَهِنوا}؛ أي: تضعفوا عن قتال عدوِّكم، ويستولي عليكم الخوف، بل اصبروا، واثبتوا، ووطِّنوا أنفسَكم على القتال والجِلادِ طلباً لمرضاة ربِّكم ونصحاً للإسلام وإغضاباً للشيطان، {و} لا {تَدْعوا إلى}: المسالمة والمتاركة بينكم وبين أعدائكم طلباً للراحة، {و} الحال أنَّكم {أنتم الأعْلَوْن واللهُ معكم ولن يَتِرَكُم}؛ أي: ينقصكم {أعمالَكم}: فهذه الأمور الثلاثة كلٌّ منها مقتضٍ للصبر وعدم الوهن كونهم الأعلين؛ أي: قد توفرت لهم أسباب النصر ووعدوا من الله بالوعد الصادق؛ فإنَّ الإنسان لا يهن إلاَّ إذا كان أذلَّ من غيره وأضعف عدداً أو عُدداً وقوةً داخليةً وخارجيةً. الثاني: أنَّ الله معهم؛ فإنَّهم مؤمنون، والله مع المؤمنين بالعون والنصر والتأييد، وذلك موجبٌ لقوَّة قلوبهم وإقدامهم على عدوهم. الثالث: أنَّ الله لا يَنْقُصهم من أعمالهم شيئاً، بل سيوفِّيهم أجورهم ويزيدُهم من فضله، خصوصاً عبادة الجهاد؛ فإنَّ النفقة تضاعَفُ فيه إلى سبعمائة ضعف إلى أضعاف كثيرةٍ، وقال تعالى: {ذلك بأنَّهم لا يصيبُهم ظمأٌ ولا نصبٌ ولا مخمصةٌ في سبيل الله ولا يطؤون موطِئاً يغَيظُ الكفارَ ولا ينالون من عدوٍّ نيلاً إلاَّ كُتِبَ لهم به عملٌ صالحٌ إنَّ الله لا يُضِيعُ أجرَ المحسنين. ولا ينفقونَ نفقةً صغيرةً ولا كبيرةً ولا يقطعونَ وادياً إلاَّ كُتِبَ لهم لِيَجْزِيَهم الله أحسنَ ما كانوا يعملون}. فإذا عرف الإنسان أنَّ الله تعالى لا يُضِيعُ عملَه وجهاده؛ أوجب له ذلك النشاط وبذل الجهد فيما يترتَّب عليه الأجر والثواب؛ فكيف إذا اجتمعتْ هذه الأمور الثلاثة؟! فإنَّ ذلك يوجب النشاط التامَّ. فهذا من ترغيب الله لعباده وتنشيطهم وتقويةِ أنفسهم على ما فيه صلاحُهم وفلاحُهم.
{35} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Basi msilegee" mkaacha kupigana vita na adui zenu, mkashindwa na hofu. Bali subirini, kuweni imara, na zizoesheni nafsi zenu kupigana vita na kukakamia hilo kwa kutafuta radhi za Mola wako Mlezi na kuwa kuwa mwaminifu kwa Uislamu na kumkasirisha Shetani. "Na mkataka suluhu" kati yenu na adui zenu kwa kutaka kupumzika tu. Na hali ni kwamba "nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu." Basi mambo haya matatu, kila kimojawapo kinahitaji subira na kutokadhoofika, na kwamba wao ndio wa juu kabisa; Yaani, tayari wanavyo visababu vya ushindi na waliahidiwa ahadi ya kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwani mtu hadhoofiki isipokuwa ikiwa ni dhalili zaidi kuliko wengineo na dhaifu zaidi kwa idadi au maandalizi, nguvu, ndani na nje. Ya pili ni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja nao. Kwani wao ni Waumini, na Mwenyezi Mungu yu pamoja na Waumini kwa msaada wake, nusura yake na kuwaunga mkono, na hayo yanalazimu wawe na nyoyo imara na kuwa na ujasiri wa kukabiliana na adui yao. La tatu ni kwamba Mwenyezi Mungu hatawapunguzia chochote katika vitendo vyao, bali atawapa ujira wao kikamilifu na kuwazidishia katika fadhila zake, hasa juu ya ibada ya jihadi. Kwani kutoa matumizi kwa sababu yake kunazidishwa mizidisho mara mia saba hadi mizidisho nyingi sana, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kwa sababu ya hayo kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya mema. Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa, wala hawalivuki bonde, ila huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda." Basi mja anapojua kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi matendo na juhudi zake, hilo linamfanya kuwa mkakamavu na kufanya juhudi katika yale ambayo yatamletea malipo mazuri. Kwa hivyo itakuwaje ikiwa vitu hivi vitatu vitakutana? Hayo yanamsababishia kuwa mkakamavu kikamilifu. Kwa hivyo haya ni katika mbinu ambayo Mwenyezi Mungu humtia moyo, na kuwakakamua, na kuzipa nguvu nafsi zao juu ya yale yenye kuwafanya watengenee na kuwafanya wafaulu.
: 36 - 38 #
{إِنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَإِنْ تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْأَلْكُمْ أَمْوَالَكُمْ (36) إِنْ يَسْأَلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا وَيُخْرِجْ أَضْغَانَكُمْ (37) هَاأَنْتُمْ هَؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَمِنْكُمْ مَنْ يَبْخَلُ وَمَنْ يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَنْ نَفْسِهِ وَاللَّهُ الْغَنِيُّ وَأَنْتُمُ الْفُقَرَاءُ وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ (38)}
36. Hakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamcha Mungu, Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hatakutakeni mali zenu. 37. Na akikutakeni hizo na kukushikilieni, mtafanya ubahili, na atatoa undani wa chuki zenu. 38. Angalieni! Nyinyi hawa mnaitwa mtumie mali katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanaofanya ubahili. Na anayefanya ubahili, basi anajifanyia ubahili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka, atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.
#
{36 - 37} هذا تزهيدٌ منه تعالى لعباده في الحياة الدُّنيا؛ بإخبارِهم عن حقيقة أمرِها؛ بأنها لعبٌ ولهوٌ؛ لعبٌ في الأبدان ولهوٌ في القلوب، فلا يزال العبدُ لاهياً في ماله وأولاده وزينتِهِ ولذاتِهِ من النساء والمآكل والمشارب والمساكن والمجالس والمناظر والرياسات، لاعباً في كلِّ عمل لا فائدةَ فيه، بل هو دائرٌ بين البطالة والغفلة والمعاصي، حتى يستكملَ دُنياه ويَحْضُرُه أجلُه؛ فإذا هذه الأمورُ قد ولَّت وفارقتْ ولم يحصُلِ العبدُ منها على طائل، بل قد تبيَّن له خسرانُه وحرمانُه وحضر عذابُه؛ فهذا موجبٌ للعاقل الزهد فيها وعدم الرغبة فيها والاهتمام بشأنها، وإنَّما الذي ينبغي أن يهتمَّ به ما ذكره بقوله: {وإن تؤمنوا وتَتَّقوا}: بأنْ تؤمنوا بالله وملائكتِهِ وكتبِهِ ورسلِهِ واليوم الآخر، وتقوموا بتقواه التي هي من لوازم الإيمان ومقتضياته، وهي العمل بمرضاته على الدوام، مع ترك معاصيه؛ فهذا الذي ينفع العبد، وهو الذي ينبغي أن يُتنافسَ فيه وتُبذل الهمم والأعمالُ في طلبه، وهو مقصودُ الله من عباده؛ رحمةً بهم ولطفاً؛ ليثيبَهم الثوابَ الجزيل، ولهذا قال: {وإن تؤمنوا وتَتَّقوا يؤتِكُم أجورَكم ولا يَسْألْكُم أموالَكم}؛ أي: لا يريدُ تعالى أن يكلفكم ما يشقُّ عليكم ويُعْنِتَكُم من أخذِ أموالكم وبقائكم بلا مال أو يَنْقُصَكم نقصاً يضرُّكم، ولهذا قال: {إن يسألْكُموها فيُحْفِكُم تبخَلوا ويخرِجْ أضغانَكُم}؛ أي: ما في قلوبكم من الضَّغن إذا طُلِبَ منكم ما تكرهون بذلَه.
{36 - 37} Huku ni Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwavunja moyo waja juu ya maisha ya dunia; kwa kuwaambia ukweli kuhusu jambo lake. Kwamba ni mchezo na pumbao. Ni mcheza katika miili na pumbao nyoyoni. Hivyo basi, mja hataacha kuendelea kufanya pumbao katika mali yake, watoto wake, mapambo yake, na starehe zake kama vile wanawake, vyakula, vinywaji, makazi, vikao, mandhari na uongozi, na akaendelea kucheza katika kila matendo yasiyo na faida yoyote. Bali, anazunguka tu kati ya kutofanya chochote, kughafilika, na kufanya maasia, mpaka anapomaliza maisha yake ya kidunia na wakati wake ukamjia; na tazama, mambo hayo yatampa mgongo, na kumuacha, na wala mja hakupata manufaa yoyote kutokana nayo. Bali hasara yake na kunyimwa kwake kukamdhihirikia, na adhabu yake ikamjia. Haya yanamfanya mwenye akili kukata tamaa nayo na kutoyataka na kutoyajali kabisa. Badala yake, anachopaswa kujishughulisha nayo ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: "Na mkiamini na mkamcha Mungu" na kuamini Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kufanya yanayompendeza Yeye daima, pamoja na kuacha kumuasi. Basi hayo ndiyo yanayomnufaisha mja, na ndilo ambalo mtu anapaswa kushindana ndani yake na kujitahidi na kufanya juhudi kubwa katika kuyatafuta, na hayo ndiyo malengo ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake; kwa kuwafanyia rehema na wema; ili awalipe malipo mazuri mengi, na ndiyo maana akasema: "Na mkiamini na mkamcha Mungu, Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hatakutakeni mali zenu." Yaani, Mwenyezi Mungu hataki kuwajukumisha yale yatakayowalemea na kuwadhuru kwa kuchukua mali zenu na kuwaacha bila mali au kuwapunguzia mali hizo kiasi kwamba mtadhurika. Ndiyo maana akasema: "Na akikutakeni hizo na kukushikilieni, mtafanya ubahili, na atatoa undani wa chuki zenu" mtakapoombwa kitu ambacho mnachukia kukitoa.
#
{38} والدليل على أنَّ الله لو طلب منكم أموالكم وأحفاكم بسؤالها أنَّكم تمتنعون منها، أنَّكم {تُدْعَوْنَ لِتُنْفِقوا في سبيل الله}: على هذا الوجه الذي فيه مصلحكتم الدينيَّة والدنيويَّة، {فمنكم من يبخلُ}؛ أي: فكيف لو سألكم وطلب منكم أموالكم في غير أمرٍ تَرَوْنَه مصلحة عاجلة؟! أليس من باب أولى وأحرى امتناعكم من ذلك؟! ثم قال: {ومَن يبخلْ فإنَّما يبخلُ عن نفسِهِ}: لأنَّه حرم نفسه ثوابَ الله تعالى، وفاته خيرٌ كثيرٌ، ولن يضرَّ الله بترك الإنفاق شيئاً، فإن {الله}: هو {الغني وأنتم الفقراءُ}: تحتاجون إليه في جميع أوقاتكم لجميع أموركم، {وإن تَتَوَلَّوا}: عن الإيمان بالله وامتثال ما يأمركم به؛ {يستبدِلْ قوماً غيرَكم ثمَّ لا يكونوا أمثالَكُم}: في التولِّي، بل يطيعونَ الله ورسولَه ويحبُّون الله ورسوله؛ كما قال تعالى: {يا أيُّها الذينَ آمنوا من يَرْتَدَّ منكم عن دينِهِ فسوف يأتي الله بقوم يحبُّهم ويحبُّونَه}.
{38} Ushahidi wa kwamba Mwenyezi Mungu akikutakeni mali zenu na akakushikilieni katika kuziomba kwamba mtazizuia, ni kwamba, nyinyi "mnaitwa mtumie mali katika njia ya Mwenyezi Mungu" kwa njia hii yenye masilahi yenu ya kidini na ya kidunia, "na wapo katika nyinyi wanaofanya ubahili." Basi je, ingekuwaje kama angewaomba mali zenu kwa kitu ambacho hamuoni ndani yake masilahi yenu ya sasa? Je, haitakuwa ni karibu zaidi kwamba mngekataa kufanya hivyo? Kisha akasema: "Na anayefanya ubahili, basi anajifanyia ubahili mwenyewe." Kwa sababu amejizuilia ujira wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akakosa heri nyingi, na wala hatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote kwa kuacha kutoa mali yake. Kwani "Mwenyezi Mungu" ndiye "Asiye mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji" mnaomhitajia katika wakati wenu wote katika mambo yenu yote. "Na mkigeuka" mkaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na kutekeleza yale anayowaamrisha ''atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi" katika kupeana migongo. Bali watakuwa wakimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Enyi mlioamini! Atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anaowapenda nao wanampenda."
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Qital, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe wote.
* * *