Tafsiri ya surat Al-Jathiya
Tafsiri ya surat Al-Jathiya
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{حم (1) تَنْزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ (2) إِنَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِلْمُؤْمِنِينَ (3) وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِنْ دَابَّةٍ آيَاتٌ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ (4) وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنَ السَّمَاءِ مِنْ رِزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ آيَاتٌ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ (5) تِلْكَ آيَاتُ اللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَ اللَّهِ وَآيَاتِهِ يُؤْمِنُونَ (6) وَيْلٌ لِكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ (7) يَسْمَعُ آيَاتِ اللَّهِ تُتْلَى عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَنْ لَمْ يَسْمَعْهَا فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (8) وَإِذَا عَلِمَ مِنْ آيَاتِنَا شَيْئًا اتَّخَذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ (9) مِنْ وَرَائِهِمْ جَهَنَّمُ وَلَا يُغْنِي عَنْهُمْ مَا كَسَبُوا شَيْئًا وَلَا مَا اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ (10) هَذَا هُدًى وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِنْ رِجْزٍ أَلِيمٌ (11)}.
1. Ha, Mim. 2. Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 3. Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini. 4. Na katika umbo lenu na katika wanyama aliowatawanya, zimo Ishara kwa watu wenye yakini. 5. Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili. 6. Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayoiamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? 7. Ole wake kila mzushi mwenye dhambi! 8. Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyokatazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu! 9. Na anapokijua kitu kidogo katika Aya zetu, hukifanyia mzaha. Watu hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha. 10. Na nyuma yao ipo Jahanamu. Na waliyoyachuma hayatawafaa hata kidogo, wala walinzi waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa. 11. Huu ni uwongofu. Na wale wale waliozikataa Ishara za Mola wao Mlezi watapata adhabu inayotokana na ghadhabu, iliyo chungu.
#
{1 - 2} يخبرُ تعالى خبراً يتضمَّن الأمرَ بتعظيم القرآن والاعتناء به؛ أنَّه {تنْزيلٌ من اللهِ}: المألوه المعبود؛ لما اتَّصف به من صفاتِ الكمال، وانفردَ به من النعم، الذي له العزَّة الكاملة والحكمة التَّامَّة.
{1 - 2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu habari inayojumuisha amri ya kuitukuza Qur-ani na kuitunza.
Nayo ni kwamba: "Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu" mwenye kufanyiwa uungu, anayeabudiwa. Kwa sababu ana sifa za ukamilifu, na ndiye mwenye neema peke yake, ambaye ni Mwenye nguvu kamili na hekima timilifu.
#
{3 - 5} ثم أيَّد ذلك بما ذكره من الآيات الأفقيَّة والنفسيَّة؛ من خلق السماوات والأرض، وما بثَّ فيهما من الدوابِّ، وما أودعَ فيهما من المنافع، وما أنزل اللهُ من الماءِ الذي يحيي به اللهُ البلاد والعباد؛ فهذه كلُّها آياتٌ بيناتٌ وأدلة واضحاتٌ على صدقِ هذا القرآن العظيم وصحَّة ما اشتمل عليه من الحكم والأحكام، ودالاَّت أيضاً على ما لله تعالى من الكمال، وعلى البعث والنُّشور.
{3 - 5} Kisha akaunga mkono hili kwa ishara za kwenye upeo wa macho na za kinafsi kama vile kuumba mbingu na ardhi, na aliyoyaeneza miongoni mwa wanyama, na aliyoyaweka ndani yake ya manufaa, na maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu huhuisha ardhi na waja. Zote hizi ni ishara zilizo wazi na ushahidi wa wazi wa ukweli wa Qur-ani hii tukufu na usahihi wa hekima zilizo ndani yake na hukumu zake mbalimbali, ambazo pia zinaashiria ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ufufuo na kuwatawanya viumbe siku ya Kiyama.
#
{6 - 10} ثم قسَّم تعالى الناسَ بالنسبة إلى الانتفاع بآياتِهِ وعدمِهِ إلى قسمين:
قسمٌ يستدلُّون بها، ويتفكَّرون بها، وينتفعون فيرتفعون، وهم المؤمنون باللهِ وملائكتِهِ وكتبِهِ ورسلِهِ واليوم الآخر إيماناً تامًّا، وصل بهم إلى درجة اليقين، فزكَّى منهم العقول، وازدادتْ به معارفُهم وألبابُهم وعلومُهم.
وقسمٌ يسمعُ آيات الله سماعاً تقومُ به الحجةُ عليه، ثم يعرِض عنها ويستكبرُ، كأنه ما سمعها؛ لأنها لم تزكِّ قلبه ولا طهَّرته، بل بسبب استكباره عنها؛ ازداد طغيانُهُ، وأنه إذا علم من آيات الله شيئاً؛ اتَّخذها هزواً، فتوعَّده الله تعالى بالويل، فقال: {ويلٌ لكلِّ أفَّاكٍ أثيم}؛ أي: كذابٍ في مقاله، أثيمٍ في فعاله، وأخبر أن له عذاباً أليماً، وأن {من ورائهم جهنَّم}: تكفي في عقوبتهم البليغة، وأنه {لا يُغني عنهم ما كَسَبوا}: من الأموال {شيئاً ولا ما اتَّخذوا من دون اللهِ أولياءَ}: يستنصرون بهم، فخذلوهم أحوجَ ما كانوا إليهم لو نفعوا.
{6 - 10} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawagawanya watu kulingana na kunufaika na Ishara zake au la katika makundi mawili. Kundi la watu wanaozitumia kama ushahidi na kuzitafakari, na kunufaika nazo na kuinuka juu. Na hawa ni wanaomwamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, vitabu vyake, Mitume wake, na Siku ya Mwisho kwa imani kamili, ambayo iliwafikisha katika kiwango cha yakini. Kwa hivyo imani hiyo ikawatakasa akili, ikawaongeza maarifa na ufahamu wao na elimu zao. Na kuna kundi ambalo linasikia ishara za Mwenyezi Mungu kusikia kwa kuwasimamishia tu hoja, kisha wanazipa mgongo na kufanya kiburi kana kwamba hawakuzisikia. Kwa sababu hazikuutakasa moyo wake wala kuusafisha. Bali kwa sababu ya kuzifanyia kwake kiburi, akazidi kupotoka, na kwamba anapojua chochote katika Ishara za Mwenyezi Mungu, anazifanyia mzaha, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtishia kwa adhabu kali.
Akasema: "'Ole wake kila mzushi mwenye dhambi!'" Yaani, mwongo mkubwa katika anayoyasema, mwenye dhambi sana katika vitendo vyake, na akajulisha kuwa atapata adhabu chungu, na kwamba "nyuma yao ipo Jahannamu," ambayo inatosha kuwaadhibu vikali mno, na kwamba "waliyoyachuma hayatawafaa hata kidogo" miongoni mwa mali "wala walinzi waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, wakawa wamewatupa katika wakati ambao waliwahitaji sana, ikiwa wangeweza kuwanufaisha.
#
{11} فلمَّا بيَّن آياته القرآنيَّة والعيانيَّة، وأن الناس فيها على قسمين؛ أخبر أن القرآن المشتملَ على هذه المطالب العالية؛ أنَّه هدىً، فقال: {هذا هدىً}: وهذا وصفٌ عامٌّ لجميع القرآن؛ فإنَّه يهدي إلى معرفة الله تعالى بصفاته المقدَّسة وأفعاله الحميدة، ويهدي إلى معرفة رسله وأوليائهم وأعدائهم وأوصافهم، ويهدي إلى الأعمال الصالحة، ويدعو إليها، ويبيِّن الأعمال السَّيئة وينهى عنها، ويهدي إلى بيان الجزاء على الأعمال، ويبيِّن الجزاء الدُّنيويَّ والأخرويَّ؛ فالمهتدون اهتَدَوا به فأفلحوا وسعدوا. {والذين كَفَروا بآيات ربِّهم}: الواضحة القاطعة، التي لا يكفرُ بها إلاَّ من اشتدَّ ظلمُه، وتضاعف طغيانه، {لهم عذابٌ من رجزٍ أليم}.
{11} Alipofafanua ishara zake za ki Qur-ani na za kuonekana kwa macho, na kwamba watu katika hizo wamegawanyika makundi mawili, akajulisha kwamba Qur-ani hii inayojumuisha mambo haya makubwa ni uwongofu.
Akasema: "Huu ni uwongofu." Haya ni maelezo ya jumla ya Qur-ani yote. Kwa maana inaongoza kwenye kumjua Mwenyezi Mungu kwa sifa zake takatifu na matendo yake yenye kusifiwa, na inaongoza kwenye kuwajua Mitume wake, vipenzi wao na maadui zao na sifa zao, na inaongoza kwenye matendo mema, na inalingania kwa hayo na kubainisha matendo mabaya na kuyakataza, na inaongoza katika kubainisha malipo ya matendo, na inabainisha malipo ya duniani na akhera. Kwa hivyo, wale walioongoka waliongoka kwayo, nao basi wakafanikiwa na kuwa na furaha. "Na wale wale waliozikataa Ishara za Mola wao Mlezi" zilizo wazi wazi na za uhakika kabisa, ambazo hakuna mwenye kuzikataa isipokuwa mwenye dhuluma kubwa mno na ukazidi upotofu wake, "watapata adhabu inayotokana na ghadhabu, iliyo chungu."
{اللَّهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِنْ فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (12) وَسَخَّرَ لَكُمْ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِنْهُ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ (13)}
12. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite merikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na ili mpate kushukuru. 13. Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.
#
{12} يخبر تعالى عن فضله على عباده وإحسانه إليهم بتسخير البحر لسير المراكب والسُّفن بأمره وتيسيره ، {لتَبْتَغوا من فضله}: بأنواع التجارات والمكاسب، {ولعلَّكم تشكرون}: الله تعالى؛ فإنكم إذا شكرتُموه؛ زادكم من نعمِهِ وأثابكم على شكركم أجراً جزيلاً.
{12} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu fadhila zake juu ya waja wake na wema wake kwao kwa kuitiisha bahari ili vitu vinavyopandwa, kama vile mashua na merikebu, viweze kwenda kwa amri yake na wepesishaji wake, "na ili mtafute fadhila yake" kwa aina mbalimbali za biashara na namna mbalimbali za kuchuma, "na ili mpate kushukuru" Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa maana, ikiwa mtamshukuru, akakuzidishieni neema zake na akakulipeni malipo makubwa kwa kushukuru kwenu.
#
{13} {وسخَّر لكم ما في السمواتِ وما في الأرض جميعاً منه}؛ أي: من فضله وإحسانه، وهذا شامل لأجرام السماواتِ والأرض، ولما أودعَ الله فيهما من الشمس والقمر والكواكب الثَّوابت والسيَّارات وأنواع الحيوانات وأصناف الأشجار والثَّمرات وأجناس المعادن وغير ذلك ممَّا هو معدٌّ لمصالح بني آدم ومصالح ما هو من ضروراتِهِ؛ فهذا يوجب عليهم أن يبذلوا غايةَ جهدِهِم في شكر نعمته، وأن تغلغلَ أفكارهم في تدبُّر آياته وحكمِهِ، ولهذا قال: {إنَّ في ذلك لآياتٍ لقوم يتفكَّرون}. وجملة ذلك أنَّ خلقها وتدبيرها وتسخيرها دالٌّ على نفوذ مشيئة الله وكمال قدرتِهِ.
وما فيها من الإحكام والإتقان وبديع الصنعة وحسن الخِلْقة دالٌّ على كمال حكمته وعلمه.
وما فيها من السعة والعظمة والكثرة دالٌّ على سعة ملكه وسلطانه.
وما فيها من التخصيصات والأشياء المتضادَّات دليلٌ على أنه الفعَّال لما يريد.
وما فيها من المنافع والمصالح الدينيَّة والدنيويَّة دليلٌ على سعة رحمته وشمول فضلِهِ وإحسانِهِ وبديع لطفهِ وبرِّه، وكلُّ ذلك دالٌّ على أنّه وحدَه المألوه المعبودُ الذي لا تنبغي العبادة والذُّلُّ والمحبَّة إلا له، وأنَّ رسله صادقون فيما جاؤوا به. فهذه أدلةٌ عقليةٌ واضحةٌ لا تقبل ريباً ولا شكًّا.
{13} "Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake." Yaani, hayo yote ni kutokana na fadhila zake na wema wake. Hayo yanajumuisha vyombo vilivyo mbinguni na duniani, na vyote alivyoweka humo Mwenyezi Mungu kama vile jua, mwezi, sayari zisizosonga na zenye kusonga, na aina mbalimbali za wanyama, miti, mazao, aina mbalimbali za madini na mambo mengineyo ambayo yametayarishwa kwa ajili ya masilahi ya wanadamu ambayo wanayahitaji sana. Hayo yote yanawalazimu kufanya juhudi kubwa zaidi katika kushukuru neema zake, na kwamba fikira zao zizame katika kuzingatia ishara zake na hekima zake,
na ndiyo maana akasema: "Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri." Kwa ufupi, uumbaji wake, uendeshaji wake na kuvitiisha kwake vyote vinaonyesha kutekelezeka kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa uwezo wake. Na ustadi mkubwa ulio ndani yake, usawasawa wake, ufundi wake wa hali ya juu na maumbile yake mazuri zaidi, yote haya yanaashiria ukamilifu wa hekima yake na elimu yake. Na upana wake, ukubwa wake na wingi wake vinaashiria upana wa ufalme wake na mamlaka yake. Na mambo maalumu yaliyomo, na vitu vilivyo kinyume cha vingine ni ushahidi kwamba Yeye ndiye anafanya kabisa anachotaka. Na manufaa yaliyo ndani yake na masilahi ya kidini na kidunia ni ushahidi wa upana wa rehema yake, ujumla wa fadhila zake na wema wake, na upole wake mkubwa na wema wake, na hayo yote yanaashiria kwamba Yeye peke yake ndiye anayestahiki kufanyiwa uungu na kuabudiwa, ambaye haifai kufanywa ibada wala kujidhalilisha wala kumpenda isipokuwa Yeye, na kwamba Mitume wake ni wakweli katika yale waliyokuja nayo. Huu ni ushahidi wa kiakili ulio wazi, ambao haukubali shaka au kusitasita kokote.
{قُلْ لِلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّهِ لِيَجْزِيَ قَوْمًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (14) مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ثُمَّ إِلَى رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ (15)}.
14. Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma. 15. Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.
#
{14 - 15} يأمر تعالى عبادَه المؤمنين بحسن الخلق والصَّبر على أذيَّة المشركين به الذين {لا يرجون أيام الله}؛ أي: لا يرجون ثوابَه ولا يخافون وقائعَه في العاصين؛ فإنَّه تعالى سيجزي كلَّ قوم {بما كانوا يكسبون}: فأنتم يا معشر المؤمنين يجزيكم على إيمانكم وصفحكم وصبركم ثواباً جزيلاً، وهم إن استمرُّوا على تكذيبهم؛ فلا يحلُّ بكم ما حلَّ بهم من العذاب الشديد والخزي، ولهذا قال: {مَن عَمِلَ صالحاً فلنفسِهِ ومَن أساءَ فعليها ثم إلى ربِّكم تُرْجَعون}.
{14 - 15} Mwenyezi anaamrisha waja wake waumini kuwa na maadili mema na kuwa na subira juu ya udhia wa wale wanaomshirikisha, wale "wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu," yaani malipo yake mazuri, na wala hawaogopi namna anavyowafanyia wale wanaomuasi. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa kila watu "kwa waliyokuwa wakiyachuma." Basi, enyi kundi la Waumini atakulipeni thawabu nyingi kwa Imani yenu, msamaha wenu, na subira yenu, na ikiwa wao wataendelea kukadhibisha kwao huko, basi haitakupateni adhabu kali na hizaya kali itakayowapata wao,
na ndiyo maana akasema: "Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi."
ثم قال تعالى: {وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ (16) وَآتَيْنَاهُمْ بَيِّنَاتٍ مِنَ الْأَمْرِ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ (17)}.
16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu, hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote. 17. Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitilafiana.
#
{16} أي: ولقد أنعمنا على بني إسرائيل نعماً لم تحصُل لغيرهم من الناس، وآتيناهم {الكتاب}؛ أي: التوراة والإنجيل والحكم بين الناس والنبوَّة التي امتازوا بها، وصارت النبوَّة في ذرِّيَّة إبراهيم عليه السلام، أكثرهم من بني إسرائيل، {ورزَقْناهم من الطيِّبات}: من المآكل والمشارب والملابس وإنزال المنِّ والسلوى عليهم، {وفضَّلناهم على العالمين}؛ أي: على الخلق بهذه النعم. ويخرج من هذا العموم اللفظي هذه الأمة؛ فإنهم خير أمة أخرجت للناس، والسياق يدلُّ على أن المراد غير هذه الأمة؛ فإن الله يقصُّ علينا ما امتنَّ به على بني إسرائيل وميَّزهم على غيرهم.
وأيضاً؛ فإن الفضائل التي فاق بها بنو إسرائيل من الكتاب والحكم والنبوة وغيرها من النعوت قد حصلت كلُّها لهذه الأمة، وزادت عليهم هذه الأمة فضائل كثيرة؛ فهذه الشريعة شريعة بني إسرائيل جزء منها؛ فإنَّ هذا الكتاب مهيمنٌ على سائر الكتب السابقة، ومحمدٌ - صلى الله عليه وسلم - مصدِّق لجميع المرسلين.
{16} Yaani, tuliwaneemesha Wana wa Israili neema ambazo hawakuwahi kupewa wasiokuwa wao miongoni mwa watu, na tukawapa "Kitabu;" yaani, Taurati, Injili, kuhukumu baina ya watu, na unabii waliokuwa tofauti sana na watu wengine. Na unabii huo ukawa katika kizazi cha Ibrahim, amani iwe juu yake, ambao wengi wao walikuwa katika Wana wa Israili. "Na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri" kama vile vyakula, vinywaji na mavazi, na tukawateremshia Manna na Salwa. "Na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote." Yaani, juu ya viumbe wengineo kwa neema hizi. Ila umma huu unatoka katika ujumla huu wa kimatamshi, kwani wao ndio umma bora kabisa uliowahi kutolewa kwa ajili ya watu. Na muktadha unaonyesha kwamba kinachokusudiwa ni kingine kisichokuwa umma huu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu anatusimulia yale aliyowaneemesha kwayo Wana wa Israili na akawatofautisha na watu wengine
(wa zama zao). Na pia, fadhila ambazo kwazo Wana wa Israili walifanywa kuwa bora ni kama vile Kitabu, hekima, Unabii na sifa nyinginezo zote zinazopatikana katika umma huu, na umma huu ukawazidi kwa fadhila nyingi sana. Kwa maana, sheria ya Wana wa Israili ni sehemu katika sheria hii. Kwa maana Kitabu hiki ndicho kinachotawala vitabu vyote vilivyotangulia, naye Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – anawasadikisha Mitume wote.
#
{17} {وآتيناهم}؛ أي: آتينا بني إسرائيل {بيناتٍ}؛ أي: دلالاتٍ تبيِّن الحقَّ من الباطل {من الأمر}: القدريّ الذي أوصله الله إليهم، وتلك الآيات هي المعجزاتُ التي رأوها على يد موسى عليه السلام؛ فهذه النعم التي أنعم الله بها على بني إسرائيل تقتضي الحالُ أن يقوموا بها على أكمل الوجوه، وأنْ يجتمعوا على الحقِّ الذي بيَّنه الله لهم، ولكن انعكسَ الأمر، فعاملوها بعكس ما يجبُ، وافترقوا فيما أمروا بالاجتماع به، ولهذا قال: {فما اختلفوا إلاَّ من بعدِ ما جاءهم العلمُ}؛ أي: الموجب لعدم الاختلاف، وإنَّما حملهم على الاختلاف، البغيُ من بعضهم على بعض والظُّلم. {إنَّ ربَّك يقضي بينهم يوم القيامةِ فيما كانوا فيه يختلفون}: فيميِّز المحقَّ من المبطل، والذي حمله على الاختلاف الهوى أو غيره.
{17} "Na tukawapa" Wana wa Israili "maelezo wazi" yanayobainisha haki kutokana na batili "ya amri" inayohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu aliwafikishia. Na maelezo hayo ni miujiza waliyoiona kupitia mkono wa Musa, amani iwe juu yake. Neema hizi alizowapa Mwenyezi Mungu Wana wa Israili zilihitaji wazitekeleze kwa ukamilifu kabisa, na kwamba waungane juu ya haki ambayo Mwenyezi Mungu aliwabainishia. Lakini jambo hilo likawa kinyume, wakayafanyia kinyume na inavyolazimu, na wakahitilafiana katika yale waliyoamrishwa kuungana ndani yake,
na ndiyo maana akasema: "Basi hawakuhitalifiana ila baada ya kuwajia na elimu;" yaani, inayofanya wasitofautiane. Na kilichowafanya kutofautiana ni ukandamizaji na dhuluma ya wenyewe kwa wenyewe. "Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyokuwa wakihitalifiana" ili apambanue aliye kwenye haki na aliye katika batili, na apambanue aliyehitilafiana kwa sababu ya matamanio au kitu chenginecho.
{ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَى شَرِيعَةٍ مِنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ (18) إِنَّهُمْ لَنْ يُغْنُوا عَنْكَ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ (19)}.
18. Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate matamanio ya wasiojua kitu. 19. Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki msaidizi wa wamchao.
#
{18} أي: ثمَّ شرعنا لك شريعةً كاملةً تدعو إلى كلِّ خير، وتنهى عن كل شرٍّ من أمرنا الشرعيِّ، {فاتَّبِعْها}؛ فإنَّ في اتِّباعها السعادة الأبديَّة والصلاح والفلاح، {ولا تتَّبِعْ أهواء الذين لا يعلمونَ}؛ أي: الذين تكون أهويتُهم غيرَ تابعةٍ للعلم ولا ماشيةٍ خلفه، وهم كلُّ من خالف شريعةَ الرسول - صلى الله عليه وسلم - هواه وإرادتُه؛ فإنَّه من أهواء الذين لا يعلمون.
{18} Yaani, kisha tukakuwekeeni sheria kamili inayolingania kwenye kila heri, na inakataza kila ovu. "Basi ifuate," kwani katika kuifuata kuna furaha ya milele, kutengenea na mafanikio. "Wala usifuate matamanio ya wasiojua kitu." Yaani, wale ambao matamanio yao hayafuati elimu. Nao ni kila mwenye kuhalifu sheria ya Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – katika matamanio yake na utashi wake. Hayo ni katika matamanio ya wale wasiojua.
#
{19} {إنَّهم لن يُغنوا عنك من اللهِ شيئاً}؛ أي: لا ينفعونك عند الله، فيحصِّلوا لك الخير، ويدفعوا عنك الشرَّ إنِ اتَّبعتهم على أهوائهم، ولا تصلُحُ أن توافِقَهم وتوالِيَهم؛ فإنَّك وإياهم متباينون، وبعضهم وليٌّ لبعض. {والله وليُّ المتَّقين}: يخرجهم من الظلمات إلى النور بسبب تقواهم وعملهم بطاعته.
{19} "Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu." Yaani, hawatakunufaisha kwa Mwenyezi Mungu, wakakufikishia heri na kukuondolea uovu ikiwa utawafuata katika matamanio yao, na wala hamfai kukubaliana nao na kuwafanya wasaidizi wako. Kwa sababu wewe na wao mnatofautiana sana, na wao wenyewe kwa wenyewe ni vipenzi wanaosaidiana. "Na Mwenyezi Mungu ni rafiki msaidizi wa wamchao." Anawatoa katika giza mbalimbali hadi kwenye nuru kwa sababu ya uchamungu wao na kumtii kwao.
{هَذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ (20)}
20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu na rehema kwa watu wenye yakini.
#
{20} أي: {هذا} القرآن الكريم والذِّكْر الحكيم {بصائرُ للناس}؛ أي: يحصُلُ به التبصرةُ في جميع الأمور للناس، فيحصُلُ به الانتفاع للمؤمنين، {و} الهدى والرحمةُ {لقوم يوقنونَ}: فيهتدون به إلى الصراط المستقيم في أصول الدِّين وفروعه، ويحصُلُ به الخير والسرور والسعادة في الدُّنيا والآخرة، وهي الرحمة، فتزكو به نفوسُهم، وتزدادُ به عقولُهم، ويزيدُ به إيمانُهم ويقينُهم، وتقوم به الحجَّةُ على من أصرَّ وعاند.
{20} Yaani, "hii" Qur-ani Tukufu na Ukumbusho wenye hekima "ni dalili zilizo wazi kwa watu wote." Yaani, kwazo watu wanaweza kuona kwa uwazi kila jambo, na kwa hayo manufaa yanawafikia Waumini, "na" uwongofu na rehema "kwa watu wenye yakini." Basi kwa hizo wanaongoka kwenye njia iliyonyooka katika misingi ya Dini na matawi yake, na wanapata kwayo heri na furaha katika dunia na akhera, nayo ni rehema. Kwa hivyo nafsi zao zinatakasika kwayo, inazitia nguvu akili zao, inawazidishia imani na yakini, na hoja inasimama kwayo mwenye kuendelea kuasi na akafanya ukaidi.
{أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَنْ نَجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ (21)}.
21. Je, wanadhani wale wanaotenda maovu kuwa tutawafanya wawe sawa sawa na wale walioamini, na wakatenda mema, uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya mno wanayoihukumu!
#
{21} أي: أم حسب المسيئون المكثِرون من الذُّنوب المقصِّرون في حقوق ربِّهم، {أن نجعَلَهم كالذين آمنوا وعملوا الصالحات}: بأن قاموا بحقوق ربِّهم، واجتنبوا مساخِطَه، ولم يزالوا مؤثِرين رضاه على هوى أنفسهم؛ أي: أحسبوا أن يكونوا {سواءً} في الدُّنيا والآخرة؟ ساء ما ظنُّوا وحسبوا، وساء ما حكموا به؛ فإنَّه حكمٌ يخالف حكمة أحكم الحاكمين وخير العادلين، ويناقِضُ العقول السليمة والفطر المستقيمة، ويضادُّ ما نزلت به الكتب وأخبرت به الرُّسل، بل الحكم الواقع القطعيُّ أنَّ المؤمنين العاملين الصالحات، لهم النَّصر والفلاح والسعادة والثواب في العاجل والآجل؛ كلٌّ على قدر إحسانه، وأنَّ المسيئين لهم الغضبُ والإهانةُ والعذاب والشقاء في الدُّنيا والآخرة.
{21} Yaani, au je, wale watendao mabaya, madhambi mengi na wakapuuza sana haki za Mola wao Mlezi wanadhani kwamba "tutawafanya kama walioamini na wakatenda mema?" Wale waliotekeleza haki za Mola wao Mlezi, wakajiweka mbali na mambo yanayomkasirisha na wakaendelea kupendelea mambo yanayomridhisha na wakaacha matamanio yao wenyewe. Yaani, je, wanadhani kwamba watakuwa "sawa sawa" na wao hapa duniani na akhera? Ni kibaya muno walichofikiri na kudhani, na ni hukumu mbaya muno hiyo wanayoihukumu! Kwani ni hukumu inayopingana na hekima ya Mbora zaidi wa wanaohukumu na Mbora zaidi wa wafanyao uadilifu, na inapingana na akili timamu na maumbile asili yaliyonyooka, na inapingana na yale yaliyoteremshwa katika vitabu na yakasemwa na Mitume. Bali hukumu iliyoko ya uhakika kabisa ni kwamba waumini wanaotenda mema watapata ushindi, kufaulu, furaha na malipo ya sasa na ya baadaye, kila mmoja kulingana na wema wake. Na kwamba watendao mabaya watapata ghadhabu, fedheha, adhabu na kuwa mashakani duniani na akhera.
{وَخَلَقَ اللَّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَى كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (22)}
22. Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili kila nafsi ilipwe yale iliyoyachuma. Nao hawatadhulumiwa.
#
{22} أي: خلق الله السماواتِ والأرضَ بالحكمة، ولِيُعْبَدَ وحدَه لا شريك له، ثم يجازي بعد ذلك من أمرهم بعبادته، وأنعم عليهم بالنِّعم الظاهرة والباطنة؛ هل شكروا الله تعالى وقاموا بالمأمور؟ أم كفروا فاستحقُّوا جزاء الكَفور؟
{22} Yaani, Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu na ardhi kwa hekima, na ili aabudiwe Yeye peke yake, bila ya mshirika yeyote. Kisha baada ya hayo atawalipa wale walioamrishwa kumwabudu, akawaneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichika. Je, walimshukuru Mungu Mwenyezi Mtukufu na kutekeleza waliyoamrishwa? Au walikufuru na wakastahiki malipo ya mwenye kukufuru?
{أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّهُ عَلَى عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَى سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَى بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَنْ يَهْدِيهِ مِنْ بَعْدِ اللَّهِ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ (23) وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ وَمَا لَهُمْ بِذَلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ (24) وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا أَنْ قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (25) قُلِ اللَّهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (26)}.
23. Je, umemwona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu, na akaziba masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Je, hamkumbuki? 24.
Na walisema: 'Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuangamiza isipokuwa dahari.' Lakini wao hawana elimu ya hayo, ila wao wanadhani tu. 25.
Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: 'Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.' 26.
Sema: 'Mwenyezi Mungu anawahuisha, kisha anawafisha, kisha anawakusanya Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.'
#
{23} يقول تعالى: {أفرأيتَ}: الرجل الضالَّ الذي، {اتَّخذ إلهه هواهُ}: فما هَوِيَهُ سلكه؛ سواء كان يُرْضي الله أم يسخطه، {وأضلَّه الله على علم}: من الله [تعالى] أنَّه لا تَليق به الهداية. ولا يزكو عليها، {وخَتَمَ على سمعِهِ}: فلا يسمع ما ينفعُه، {وقلبِهِ}: فلا يعي الخير، {وجَعَلَ على بصرِهِ غشاوةً}: تمنعُه من نظر الحقِّ. {فمن يهديه من بعد الله}؛ أي: لا أحد يهديه، وقد سدَّ الله عليه أبوابَ الهداية، وفتح له أبواب الغِواية، وما ظلمه الله، ولكن هو الذي ظلم نفسه، وتسبَّب لمنع رحمة الله عليه. {أفلا تذكَّرون}: ما ينفعكم فتسلكونه وما يضرُّكم فتجتنبونه؟!
{23} Mwenyezi Mungu anasema: "Je, umemwona" mtu mpotovu ambaye "aliyafanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake?" Basi kila anachokitamani, anakifanya. Sawa kiwe ni cha kumridhisha Mwenyezi Mungu au ni cha kumchukiza. "Na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu," au Mwenyezi Mungu akampoteza baada ya kujua kwamba hafailii uwongofu, wala hawezi kutakasika kwa huo. "Na akaziba masikio yake," kwa hivyo hawezi kusikia yatakayomnufaisha, "na moyo wake," kwa hivyo hawezi kuelewa mambo ya heri, "na akambandika vitanga machoni mwake" vikamzuilia kuona haki. "Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu?" Ilhali Mwenyezi Mungu ameshamfungia milango ya uwongofu na akamfungulia milango ya upotofu, na wala Mwenyezi Mungu hakumdhulumu, lakini yeye mwenyewe ndiye aliyejidhulumu, na akajisababishia kunyimwa rehema za Mwenyezi Mungu. "Je, hamkumbuki" yenye kuwanufaisha mkayafuata, na yenye kuwadhuru, mkayaepuka?
#
{24} {وقالوا}؛ أي: منكرو البعث: {ما هي إلاَّ حياتُنا الدُّنيا نموت ونحيا وما يُهْلِكُنا إلاَّ الدَّهر}: إن هي إلاَّ عاداتٌ وجريٌ على رسوم الليل والنهار، يموت أناس ويحيا أناس، وما مات؛ فليس براجع إلى الله ولا مجازيه بعمله. وقولهم هذا صادرٌ عن غير علم، {إنْ هم إلاَّ يظنُّون}: فأنكروا المعاد، وكذبوا الرسل الصادقين من غير دليل دلَّهم ولا برهان، إنْ هي إلاَّ ظنون واستبعاداتٌ خالية عن الحقيقة.
{24} "Na walisema" wale waliokanusha kufufuliwa: "Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinachotuangamiza isipokuwa dahari." Yaani, mazoea na mambo kutendeka kulingana na kwenda kwa usiku na mchana, watu wanakufa na wengine wanaishi. Na chenye kufa, hicho hakirudi kwa Mwenyezi Mungu wala hakilipi kwa matendo yake. Lakini kauli yao hii ilitokana na sintojua yao, "ila wao wanadhani tu." Basi wakapinga viumbe kurudishwa Siku ya Kiyama, na wakawakadhibisha Mitume wakweli bila ya ushahidi uliowaonyesha hayo wala hoja. Haya si chochote ila ni dhana tu na kupinga mambo bila ya uhakika wowote.
#
{25} ولهذا قال تعالى: {وإذا تُتلى عليهم آياتُنا بيِّناتٍ ما كان حجَّتَهم إلاَّ أن قالوا ائتوا بآبائنا إن كنتُم صادقين}: وهذا جراءة منهم على الله؛ حيث اقترحوا هذا الاقتراح، وزعموا أنَّ صدق رسل الله متوقِّف على الإتيان بآبائهم، وإنَّهم لو جاؤوهم بكلِّ آيةٍ؛ لم يؤمنوا؛ إلاَّ إن اتَّبعتهم الرسل على ما قالوا، وهم كَذَبَةٌ فيما قالوا، وإنما قصدُهم دفع دعوة الرسل، لا بيانُ الحق.
{25} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: 'Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli." Huku ni kufanya kwao ujasiri dhidi ya Mwenyezi Mungu, kwa kupendekeza pendekezo hili na kudai kwamba ukweli wa Mitume wa Mwenyezi Mungu unategemea kuwaleta baba zao, na kwamba hata ikiwa watawajia na kila ishara, hawataamini, isipokuwa ikiwa Mitume watawafuata katika yale waliyoyasema. Lakini wao ni waongo katika hayo waliyoyasema. Makusudio yao makubwa ni kukataa wito wa Mitume, siyo kueleza haki.
#
{26} قال تعالى: {قلِ اللهُ يحييكم ثم يميتُكم ثم يجمعُكم إلى يوم القيامةِ لا ريبَ فيه ولكنَّ أكثر الناس لا يعلمون}: وإلاَّ؛ فلو وصل العلم باليوم الآخر إلى قلوبهم؛ لعملوا له أعمالاً وتهيؤوا له.
{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Sema: 'Mwenyezi Mungu anawahuisha, kisha anawafisha, kisha anawakusanya Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui." Vinginevyo, ikiwa kujua kwa Siku ya Mwisho kungefika kwenye nyoyo zao, basi wangeufanyia matendo na kujiandaa vyema kwa ajili yake.
{وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ (27) وَتَرَى كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَى إِلَى كِتَابِهَا الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (28) هَذَا كِتَابُنَا يَنْطِقُ عَلَيْكُمْ بِالْحَقِّ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنْسِخُ مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (29) فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِي رَحْمَتِهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ (30) وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا أَفَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَى عَلَيْكُمْ فَاسْتَكْبَرْتُمْ وَكُنْتُمْ قَوْمًا مُجْرِمِينَ (31) وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُمْ مَا نَدْرِي مَا السَّاعَةُ إِنْ نَظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ بِمُسْتَيْقِنِينَ (32) وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِمْ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (33) وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنْسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَذَا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ نَاصِرِينَ (34) ذَلِكُمْ بِأَنَّكُمُ اتَّخَذْتُمْ آيَاتِ اللَّهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فَالْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ (35) فَلِلَّهِ الْحَمْدُ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الْأَرْضِ رَبِّ الْعَالَمِينَ (36) وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (37)}.
27. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu. 28. Na utauona kila umma umepiga magoti,
na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake: Leo mtalipwa mliyokuwa mkiyatenda. 29. Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda. 30. Ama walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kuliko wazi. 31.
Na ama waliokufuru wataambiwa: 'Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi mkapanda kichwa, na mkawa watu wakosefu?' 32.
Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka,
nyinyi mlikuwa mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini. 33. Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara. 34.
Na itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kuwanusuru.' 35. Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao. 36. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote. 37. Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{27} يخبر تعالى عن سعة ملكِهِ وانفرادِهِ بالتصرُّف والتدبير في جميع الأوقات، وأنَّه {يوم تقومُ الساعةُ}؛ ويَجمع الخلائق لموقف القيامة؛ يحصُلُ الخسار على المبطلين، الذين أتوا بالباطل ليدحِضوا به الحقَّ، وكانت أعمالهم باطلةً لأنَّها متعلِّقة بالباطل، فبطلت في يوم القيامة، اليوم الذي تستبين فيه الحقائق واضمحلَّت عنهم، وفاتَهم الثوابُ، وحصلوا على أليم العقاب.
{27} Mwenyezi Mungu anajulisha juu ya upana wa ufalme wake na kwamba Yeye peke yake ndiye anayeendesha na kusimamia mambo yote wakati wote, na kwamba "siku itakaposimama Saa ya Kiyama" na viumbe vikusanywe kwa ajili ya kisimamo cha siku hii, hasara kubwa itawafikia wanabatili. Wale walioleta batii ili kuiangusha kwayo haki, na matendo yao yalikuwa ni batili kwa kuwa yalifungamana na batili. Hiyo ndiyo siku ambayo hakika mbalimbali zitabainika na ipotelee mbali batili, kisha watakosa malipo mazuri na wapate adhabu iumizayo.
#
{28} ثم وصف تعالى شدَّة يوم القيامةِ وهَوْلَهُ ليحذره العباد ويستعدَّ له العُبَّاد، فقال: {وترى}: أيُّها الرائي لذلك اليوم، {كلَّ أمَّةٍ جاثيةً}: على ركبها خوفاً وذعراً وانتظاراً لحكم الملك الرحمن. {كلُّ أمة تُدعى إلى كتابها}؛ أي: إلى شريعة نبيِّهم الذي جاءهم من عند الله، وهل قاموا بها فيحصُلُ [لهم] الثواب والنجاة؟ أم ضيعوها فيحصُلُ لهم الخسران؟ فأمَّة موسى يُدعون إلى شريعة موسى، وأمَّة عيسى كذلك، وأمَّة محمد كذلك، وهكذا غيرهم؛ كلُّ أمة تُدعى إلى شرعها الذي كلفت به، هذا أحد الاحتمالات في الآية، وهو معنى صحيحٌ في نفسه، غير مشكوك فيه.
ويحتمل أن المراد بقوله: {كلُّ أمَّة تُدعى إلى كتابها}؛ أي: إلى كتاب أعمالها وما سطر عليها من خير وشرٍّ، وأنَّ كلَّ أحدٍ يُجازى بما عمله بنفسه؛ كقوله تعالى: {مَنْ عَمِلَ صالحاً فلنفسه ومن أساء فعليها}.
ويحتمل أن المعنيين كليهما مرادٌ من الآية.
{28} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza ukali na mahangaiko ya Siku ya Kiyama ili waja wajihadhari nayo na wajiandae kwa ajili yake.
Akasema: "Na utauona" ewe mwenye kuona siku hiyo, "kila umma umepiga magoti" kwa hofu, kufadhaika na kungojea hukumu ya Mfalme, Mwingi wa rehema. "Kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake." Yaani, kwenye sheria ya Mtume wao aliyewajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na je waliitekeleza; ili wapate malipo mazuri na wokovu? Au waliipoteza; kwa hivyo wapate hasara? Basi umma wa Musa wataitwa kwenye sheria ya Musa, na umma wa Isa utaitwa vivyo hivyo, na umma wa Muhammad utaitwa vivyo hivyo, na wengineo vile vile. Kila umma utaitwa kwenye sheria yake ambayo ulijukumishwa.' Huu ni uwezekano mmoja wa maana za Aya hii, nao ndio wenye maana sahihi yenyewe, usio na shaka yoyote.
Na inawezekana kwamba kile kinachokusudiwa na kauli yake: "Na kila umma utaitwa kwenda kusoma kitabu chake," ni kitabu cha matendo yake waliyoandikiwa; mema na mabaya, na kwamba kila mtu atalipwa kwa aliyoyafanya yeye mwenyewe.
Kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Anayetenda mema, basi anajitendea mwenyewe nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile." Na inawezekana kwamba maana zote mbili zimekusudiwa na Aya hii.
#
{29} ويدل على هذا قولُه: {هذا كتابُنا ينطِقُ عليكم بالحقِّ}؛ أي: هذا كتابنا الذي أنزلنا عليكم يفصِلُ [بينكم] بالحقِّ الذي هو العدل، {إنَّا كنا نَسْتَنسِخُ ما كنتُم تعملون}: فهذا كتابُ الأعمال.
{29} Haya yanaonyeshwa na kauli yake: "Hiki kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki." Yaani, hiki ni Kitabu chetu tulichowateremshia, kinachoamua
[baina yenu] kwa haki, ambayo ni uadilifu. "Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyokuwa mkiyatenda." Basi hiki hapa ni kitabu cha matendo yenu.
#
{30} ولهذا فصَّل ما يفعل الله بالفريقين، فقال: {فأمَّا الذين آمنوا وعملوا الصالحات}: إيماناً صحيحاً، وصدَّقوا إيمانَهم بالأعمال الصالحة من واجبات ومستحبَّات، {فيدخِلُهم ربُّهم في رحمتِهِ}: التي محلُّها الجنة، وما فيها من النعيم المقيم والعيش السليم. {ذلك هو الفوزُ المبينُ}؛ أي: المفاز والنجاة والربح والفلاح الواضح البيِّن، الذي إذا حصل للعبد؛ حصل له كلُّ خير، واندفع عنه كلُّ شرٍّ.
{30} Ndiyo maana akabainisha kwa kina yale ambayo Mwenyezi Mungu atawafanyia makundi mawili hayo akisema: "Ama walioamini na wakatenda mema" kwa Imani ya sahihi, wakasadikisha imani yao kwa matendo mema ya lazima na yasiyokuwa ya lazima, "Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake" ambayo mahali pake ni katika Bustani za mbinguni, na vilivyomo ndani yake vya neema ya kudumu na uhai ulio salama. "Huko ndiko kufuzu kuliko wazi" ambako kunapomtokea mja, basi anakuwa amepata kila heri, na akazuilika na kila ovu.
#
{31} {وأمَّا الذين كفروا}: بالله، فيقال لهم توبيخاً وتقريعاً: {أفلم تكن آياتي تُتْلى عليكم}، وقد دلَّتكم على ما فيه صلاحكم ونهتْكم عما فيه ضررُكم، وهي أكبر نعمة وصلت إليكم لو وفِّقتم لها، ولكن استكبرتُم عنها وأعرضتُم وكفرتُم بها، فجنيتُم أكبر جناية، وأجرمتم أشدَّ الجرم؛ فاليوم تجزون ما كنتم تعملون.
{31} "Na ama waliokufuru" Mwenyezi Mungu wataambiwa kwa kukemewa na kukaripiwa: "Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi," na zikawaonyesha yenye heri kwenu na zikakukatazeni yenye kuwadhuru, na hii ndiyo neema kubwa zaidi iliyowahi kuwafikia lau mngewezeshwa kuzikubali. Lakini mlizifanyia kiburi, mkazipa mgongo na mkazikufuru, basi mkawa mmefanya kosa kubwa zaidi na uhalifu mkubwa zaidi. Kwa hivyo, leo mtalipwa kwa yale mliyokuwa mkitenda.'
#
{32} ويوبَّخون أيضاً بقوله: {وإذا قيل إنَّ وعدَ الله حقٌّ والساعة لا ريبَ فيها قلتم}: منكرين لذلك: {ما ندري ما الساعة إن نظنُّ إلاَّ ظنًّا وما نحن بمستيقنينَ}: فهذه حالهم في الدُّنيا، وحال البعث الإنكار له، وردُّوا قولَ مَنْ جاء به.
{32} Na watakaripiwa pia kwa kauli yake: "Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Saa haina shaka,
nyinyi mlikuwa mkisema" kwa njia ya kukanusha: "Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini." Basi hii ndiyo hali yao katika dunia, na hali ya kufufuliwa ni kukanusha, na wakaikataa kauli ya yule aliyeyaleta.
#
{33} قال تعالى: {وبدا لهم سيئاتُ ما عملوا}؛ أي: وظهر لهم يوم القيامةِ عقوباتُ أعمالهم، {وحاق بهم}؛ أي: نزل {ما كانوا به يستهزِئون}؛ أي: نزل بهم العذابُ الذي كانوا في الدُّنيا يستهزئون بوقوعه وبمن جاء به.
{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia." Yaani, itawadhihirikia adhabu ya vitendo vyao Siku ya Kiyama, "na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara" katika dunia hii. Kwani walikuwa wakifanyia masihara kutokea kwake na pia walikuwa wakimfanyia masihara aliyekuwa na habari hii.
#
{34} {وقيل اليوم ننساكم}؛ أي: نترككم في العذاب {كما نسيتُم لقاء يومكم هذا}؛ فإنَّ الجزاء من جنس العمل، {ومأواكم النارُ}؛ أي: هي مقرُّكم ومصيركم. {وما لكم من ناصرينَ}: ينصرونَكم من عذابِ الله ويدفعون عنكم عقابه.
{34} "Na itasemwa: 'Leo tunawasahau," na tunawaacha katika adhabu "kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii." Kwani, malipo ni ya aina sawa na matendo, "na mahali penu ni Motoni." Yaani, hapo ndipo mahali mtakapokaa na ndiyo maishio yenu, "wala hamna wa kuwanusuru" atakayewanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwakinga adhabu yake.
#
{35} {ذلكم}: الذي حصل لكم من العذاب. بسبب {أنَّكم اتَّخذتم آياتِ الله هزواً}: مع أنها موجبةٌ للجدِّ والاجتهاد وتلقِّيها بالسرور والاستبشار والفرح، {وغرَّتْكُم الحياة الدُّنيا}: بزخارفها ولذَّاتها وشهواتها، فاطمأننتُم إليها، وعملتم لها، وتركتم العمل للدار الباقية. {فاليومَ لا يُخْرَجونَ منها ولا هم يُسْتَعْتَبونَ}؛ أي: ولا يُمْهَلون ولا يردُّون إلى الدُّنيا ليعملوا صالحاً.
{35} "Hayo" yaliyowapata ya adhabu ni kwa sababu "nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu" ingawa zilihitaji kuwa mtu kuzikakamia na kuzifanyia bidii na kuzipokea kwa furaha na bishara njema. "Na maisha ya dunia yakawadanganya" kwa mapambo yake na matamanio yake, basi kila mmoja akatulizana juu yake, na mkayafanyia matendo mbalimbali, na mkaacha kufanyia matendo nyumba ya kubakia milele.' "Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao" na tena hawatarejeshwa duniani ili wafanye mema.
#
{36} {فلله الحمدُ}: كما ينبغي لجلال وجهه وعظيم سلطانه، {ربِّ السمواتِ وربِّ الأرض ربِّ العالمين}؛ أي: له الحمد على ربوبيته لسائر الخلق ؛ حيث خلقهم وربَّاهم، وأنعم عليهم بالنعم الظاهرة والباطنة.
{36} "Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu" kama upasavyo utukufu wa uso wake na ukubwa wa mamlaka yake, "Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote." Yaani, ana sifa njema kwa sababu ya umola wake juu ya viumbe vyote, ambapo aliwaumba, akawalea, akawaneemesha kwa neema za dhahiri na zilizofichika.
#
{37} {وله الكبرياءُ في السمواتِ والأرض}؛ أي: له الجلال والعظمة والمجدُ؛ فالحمد فيه الثناء على الله بصفات الكمال ومحبَّته تعالى وإكرامه، والكبرياء فيها عظمتُه وجلالُه، والعبادة مبنيَّة على ركنين: محبة الله والذُّلُّ له، وهما ناشئان عن العلم بمحامد الله وجلاله وكبريائه، {وهو العزيز}: القاهر لكلِّ شيء. {الحكيم}: الذي يضعُ الأشياء مواضِعَها؛ فلا يشرع ما يشرعُه إلاَّ لحكمة ومصلحة، ولا يخلُقُ ما يخلُقُه إلاَّ لفائدةٍ ومنفعةٍ.
{37} "Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi." Yaani, ni wake utukufu, ukuu na heshima kubwa. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu anasifika kwa sifa njema za ukamilifu, anapendwa na anatukuzwa. Na pia Yeye ni mwenye ukubwa, ukuu na heshima kubwa mno. Kwani,
ibada imejengwa juu ya nguzo mbili: kumpenda Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea. Na mawili hayo yanatokana na kujua sifa njema za Mwenyezi Mungu, utukufu wake na ukubwa wake. "Naye ni Mwenye nguvu," aliyeshinda kila kitu. "Mwenye hekima," anayeweka vitu mahali pake pa sawasawa. Kwa hivyo, hawezi kuweka sheria alizoweka isipokuwa kwa hekima na masilahi, na wala haumbi anachokiumba isipokuwa kwa masilahi na manufaa.
Imekamilika tafsiri ya surat Al-Jathiya, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na neema na fadhila.
* * *