:
Tafsiri ya surat Ad-Dhukhan
Tafsiri ya surat Ad-Dhukhan
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 16 #
{حم (1) وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ (2) إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُبَارَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنْذِرِينَ (3) فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ (4) أَمْرًا مِنْ عِنْدِنَا إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ (5) رَحْمَةً مِنْ رَبِّكَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (6) رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِنْ كُنْتُمْ مُوقِنِينَ (7) لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ (8) بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ (9) فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُبِينٍ (10) يَغْشَى النَّاسَ هَذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ (11) رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ (12) أَنَّى لَهُمُ الذِّكْرَى وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُبِينٌ (13) ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَجْنُونٌ (14) إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا إِنَّكُمْ عَائِدُونَ (15) يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَى إِنَّا مُنْتَقِمُونَ (16)}
1. Ha Mim 2. Ninaapa kwa Kitabu kinachobainisha. 3. Hakika Sisi tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. 4. Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima. 5. Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. 6. Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 7. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. 8. Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. 9 Lakini wao wanacheza katika shaka. 10. Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri. 11. Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu! 12. Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. 13. Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. 14. Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.' 15. Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! 16. Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
#
{1 - 3} هذا قسمٌ بالقرآن على القرآن، فأقسم بالكتاب المبين لكلِّ ما يحتاج إلى بيانه أنَّه أنزله {في ليلةٍ مباركةٍ}؛ أي: كثيرة الخير والبركة، وهي ليلةُ القدرِ، التي هي خيرٌ من ألف شهرٍ، فأنزل أفضلَ الكلام بأفضل الليالي والأيام على أفضل الأنام بلغة العرب الكرام؛ لينذِرَ به قوماً عمَّتهم الجهالةُ وغلبت عليهم الشَّقاوة، فيستضيئوا بنوره، ويقتبِسوا من هُداه، ويسيروا وراءه، فيحصُلُ لهم الخير الدنيويُّ والخير الأخرويُّ، ولهذا قال: {إنَّا كُنَّا منذِرينَ}.
{1 - 3} Hiki ni kiapo kwa Qur-ani juu ya Qur-ani. Kwa hivyo aliapa kwa Kitabu kinachobainisha kila kinachohitaji kuelezwa kwamba alikiteremsha: "katika usiku uliobarikiwa." Yaani: wenye heri na baraka nyingi, nao ni Usiku wa Cheo (Lailatul-Qadr) ambao ni bora kuliko miezi elfu moja. Basi aliteremsha maneno bora zaidi katika usiku na michana bora zaidi kwa kiumbe bora zaidi kwa lugha ya Waarabu watukufu; ili kuwaonya watu waliogubikwa na ujinga na wakasifika mno na hali ya kuwa mashakani, ili waangazwe na nuru yake, wachukue uongofu wake, na watembelee nyuma yake, ili wapate heri ya duniani na akhera, na ndiyo maana akasema: "Hakika Sisi ni Waonyaji."
#
{4} {فيها}؛ أي: في تلك الليلة الفاضلة التي نَزَلَ فيها القرآن، {يُفْرَقُ كلُّ أمرٍ حكيم}؛ أي: يفصل ويميَّز ويُكتب كلُّ أمر قدريٍّ وشرعيٍّ حكم الله به. وهذه الكتابة والفرقان الذي يكون في ليلة القدر إحدى الكتابات التي تُكتب وتميَّز، فتطابق الكتابَ الأوَّلَ الذي كتبَ الله به مقاديرَ الخلائق وآجالهم وأرزاقهم وأعمالهم وأحوالهم. ثم إنَّ الله تعالى قد وَكَلَ ملائكةً تكتب ما سيجري على العبد وهو في بطن أمِّه. ثم وَكَلَهم بعد خروجه إلى الدنيا؛ وَكَلَ به كراماً كاتبين يكتبون ويحفظون عليه أعماله. ثم إنَّه تعالى يقدِّرُ في ليلة القدر ما يكونُ في السنةِ، وكلُّ هذا من تمام علمه وكمال حكمتِهِ وإتقان حفظِهِ واعتنائه تعالى بخلقه.
{4} "Katika usiku huu" mtukufu ambao iliteremka humo Qur-ani, "hubainishwa kila jambo la hekima." Yaani: linapitishwa na kuandikwa kila jambo linalohusiana na mipango ya Mwenyezi Mungu na la kisheria. Uandishi huu na kupambanua huku unaokuwa katika usiku huu wa Cheo ni miongoni mwa uandishi unaoandikwa na kutofautishwa, kwa hivyo ukawiana na uandishi ule wa kwanza ambao Mwenyezi Mungu aliandika kuhusiana na hatima za viumbe, muda wao, riziki zao, matendo yao, na hali zao. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka Malaika kuandika yale yatakayompata mja akiwa ndani ya tumbo la mama yake. Kisha akaweka baada ya kutoka kwake humo na kuja duniani waandishi watukufu ili waandike na kuhifadhi matendo yake. Kisha Yeye Mtukufu katika usiku wa Cheo anapitisha yatakayotokea katika mwaka huo, na yote haya ni katika ukamilifu wa elimu yake, ukamilifu wa hekima yake, kuhifadhi sawasawa kwake, na utunzaji wake Mtukufu wa viumbe vyake.
#
{5} {أمراً من عندنا}؛ أي: هذا الأمر الحكيم أمرٌ صادرٌ من عندنا. {إنَّا كنَّا مرسلينَ}: للرسل ومنزلينَ للكتب، والرسلُ تبلِّغ أوامر المرسَل وتخبِرُ بأقدارِهِ.
{5} "Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma" Mitume na kuteremsha Vitabu. Na Mitume wanafikisha tu amri za aliyewatuma na wanapeana habari za mipango yake.
#
{6} {رحمةً من ربِّك}؛ أي: إن إرسال الرسل وإنزال الكتب التي أفضلُها القرآن رحمةٌ من ربِّ العباد بالعباد؛ فما رحم الله عبادَه برحمةٍ أجلَّ من هدايتهم بالكتب والرسل، وكلُّ خير ينالونه في الدُّنيا والآخرة؛ فإنَّه من أجل ذلك وبسببه. {إنَّه هو السميعُ العليم}؛ أي: يسمع جميع الأصوات، ويعلم جميع الأمور الظاهرة والباطنة، وقد علم تعالى ضرورةَ العباد إلى رسله وكتبه، فرحمهم بذلك ومنَّ عليهم؛ فلله تعالى الحمدُ والمنةُ والإحسان.
{6} "Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi." Yaani: kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu, ambavyo bora zaidi yake ni Qur-ani, ni rehema itokayo kwa Mola Mlezi wa waja kwa waja wake. Na Mwenyezi Mungu hakuwahi kuwarehemu waja wake kwa rehema kubwa kuliko kuwaongoza kwa Vitabu na Mitume, na kila heri wanayoipata duniani na Akhera, basi ni kwa ajili ya hilo na kwa sababu yake. "Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi." Yaani, anasikia vyema sauti zote, na anajua mambo yote ya dhahiri na yaliyofichika. Naye Mtukufu alijua haja kubwa ya waja wake juu ya Mitume wake na Vitabu vyake, basi akawarehemu kwa hivyo na kuvifanya kuwa neema kwao. Kwa hivyo,ni za Mwenyezi Mungu sifa njema, neema na wema.
#
{7 - 8} {ربِّ السموات والأرض وما بينهما}؛ أي: خالق ذلك ومدبِّره والمتصرِّف فيه بما يشاء، {إن كنتُم موقِنين}؛ أي: عالمين بذلك علماً مفيداً لليقين؛ فاعْلموا أنَّ الربَّ للمخلوقات هو إلهها الحقُّ، ولهذا قال: {لا إله إلاَّ هو}؛ أي: لا معبود إلاَّ وجهه، {يحيي ويميتُ}؛ أي: هو المتصرِّف وحده بالإحياء والإماتة، وسيجمعكم بعد موتكم فيَجْزيكم بعَمَلِكم، إن خيراً فخيرٌ، وإن شرًّا فشرٌّ. {ربُّكم وربُّ آبائكم الأوَّلين}؛ أي: ربُّ الأوَّلين والآخرين؛ مربِّيهم بالنعم، الدافع عنهم النقم.
{7 - 8} "Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina ya viwili hivyo." Yaani, Muumba wake, msimamizi wake, na anayeviendesha atakavyo, "ikiwa nyinyi mna yakini." Yaani, ikiwa mnayajua hayo elimu yenye kumfanya mtu kuwa na yakini. Basi jueni kwamba Mola Mlezi wa viumbe ndiye Mungu wavyo wa haki, na ndiyo maana akasema: "Hakuna mungu ila Yeye." Yaani, hakuna anayefaa kuabudiwa kwa haki ila Uso wake. "Anahuisha na anafisha;" yaani, Yeye pekee ndiye mwenye anayeendesha suala la kufufua na kufisha, na atakukusanyeni baada ya kufa kwenu na atakulipeni kwa matendo yenu, ikiwa ni heri, basi kwa heri. Na ikiwa ni shari, basi kwa shari. "Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo." Yaani, Mola Mlezi wa wa mwanzo na wa mwisho. Anayewalea kwa neema zake, anayewazuilia adhabu.
#
{9} فلما قرَّر تعالى ربوبيَّته وألوهيَّته بما يوجب العلم التامَّ ويدفعُ الشكَّ؛ أخبر أنَّ الكافرين مع هذا البيان: {في شكٍّ يلعبونَ}؛ أي: منغمرون في الشُّكوك والشُّبهات، غافلون عمَّا خُلقوا له، قد اشتغلوا باللعب الباطل الذي لا يُجدي عليهم إلاَّ الضَّرر.
{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipothibitisha umola wake na uungu wake kwa njia inalazimu mtu kuwa na elimu kamili na kuondoa shaka, akajulisha kwamba makafiri pamoja na kubainisha huku: "wanacheza katika shaka" na mambo ya kuwatia utata, huku wameghafilika mbali na yale waliyoumbwa kwa ajili yake, na wamejishughulisha na mchezo wa batili ambao hauwaletei isipokuwa madhara tu.
#
{10 - 16} {فارتقِبْ}؛ أي: انتظر فيهم العذابَ؛ فإنَّه قد قربَ وآنَ أوانه، {يومَ تأتي السماءُ بدخانٍ مبينٍ. يغشى الناسَ}؛ أي: يعمُّهم ذلك الدخان، ويقال لهم: {هذا عذابٌ أليمٌ}. واختلف المفسِّرون في المراد بهذا الدُّخان: فقيل: إنَّه الدخان الذي يغشى الناسَ ويعمُّهم حين تقرب النار من المجرمين في يوم القيامة، وأنَّ الله توعَّدهم بعذاب يوم القيامةِ، وأمر نبيَّه أن ينتظر بهم ذلك اليوم. ويؤيد هذا المعنى أنَّ هذه الطريقة هي طريقةُ القرآن في توعُّد الكفَّار والتأنِّي بهم وترهيبهم بذلك اليوم وعذابه وتسلية الرسول والمؤمنين بالانتظار بمن آذاهم. ويؤيِّده أيضاً أنَّه قال في هذه الآية: {أنَّى لهم الذِّكْرى وقد جاءَهُم رسولٌ مبينٌ}، وهذا يُقال يومَ القيامةِ للكفار حين يطلبون الرجوعَ إلى الدُّنيا، فيقال: قد ذهب وقتُ الرجوع. وقيل: إنَّ المراد بذلك ما أصاب كفارَ قريش حين امتنعوا من الإيمان واستَكْبروا على الحقِّ، فدعا عليهم النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -، فقال: «اللهمَّ أعِنِّي عليهم بسنينَ كَسِني يوسُفَ». فأرسل الله عليهم الجوع العظيم، حتى أكلوا الميتات والعظام، وصاروا يَرَوْنَ الذي بين السماء والأرض كهيئة الدخان، وليس به، وذلك من شدَّة الجوع، فيكون على هذا قولُه: {يوم تأتي السماءُ بدخانٍ}: أن ذلك بالنسبة إلى أبصارهم وما يشاهدون، وليس بدخانٍ حقيقةً، ولم يزالوا بهذه الحالة حتى اسْتَرْحموا رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم -، وسألوه أن يَدْعُوَ اللهَ لهم أن يكشِفَه الله عنهم، [فَدَعا رَبَّه]؛ فكشفه الله عنهم، وعلى هذا فيكون قوله: {إنَّا كاشِفو العذابِ قليلاً إنَّكم عائدونَ}: إخبارٌ بأنَّ الله سيصرِفُه عنهم ، وتوعُّدٌ لهم أن يعودوا إلى الاستكبار والتكذيب، وإخبارٌ بوقوعه، فوقع، وأنَّ الله سيعاقِبُهم بالبطشة الكبرى، قالوا: وهي وقعةُ بدرٍ. وفي هذا القول نظرٌ ظاهرٌ. وقيل: إنَّ المراد بذلك أن ذلك من أشراط الساعة، وأنَّه يكون في آخرِ الزَّمان دخانٌ يأخذُ بأنفاس الناس ويصيبُ المؤمنين منه كهيئةِ الدُّخان. والقول هو الأول. وفي الآية احتمالُ أنَّ المراد بقوله: {فارْتَقِبْ يوم تأتي السماءُ بدُخانٍ مبينٍ. يغشى الناسَ هذا عذابٌ أليمٌ. ربَّنا اكشِفْ عنَّا العذابَ إنَّا مؤمنونَ. أنَّى لهم الذِّكرى وقد جاءهُم رسولٌ مبينٌ. ثم تولَّوا عنه وقالوا معلمٌ مجنونٌ}: أنَّ هذا كلَّه [يكون] يوم القيامةِ، وأنَّ قولَه تعالى: {إنَّا كاشفو العذابِ قليلاً إنَّكم عائدونَ. يوم نَبْطِشُ البطشةَ الكُبرى إنَّا منتقمونَ}: أنَّ هذا ما وقع لقريش كما تقدم. وإذا أنزلت هذه الآيات على هذين المعنيين؛ لم تجد في اللفظ ما يمنعُ من ذلك، بل تَجِدُها مطابقةً لهما أتمَّ المطابقة، وهذا الذي يظهر عندي ويترجَّح. والله أعلم.
{10 - 16} "Basi ingoje" adhabu itakayowapata hao. Kwa maana wakati wake umekaribia na umefika. "Siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri. Utakaowafunika watu" na wataambiwa: "Hii ni adhabu chungu!" Wafasiri walitofautiana kuhusu maana ya moshi huu: Ikasemwa kwamba ni moshi utakaowafunika watu na kuwagubika wote Moto utakapowakaribia wahalifu Siku ya Kiyama, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwatishia kwa adhabu Siku ya Kiyama, na akamuamuru Nabii wake awangojee siku hiyo. Maana hii inaungwa mkono na ukweli kwamba njia hii ndiyo njia ya Qur-ani ya kuwatishia makafiri, kutowaharakisha, kuwatia hofu kubwa kwa siku hiyo na adhabu yake, na kumliwaza Mtume na waumini kwamba wawangojee wale waliowatia udhia. Maana hii pia inaungwa mkono na ukweli kwamba alisema katika Aya hii: "Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha." Haya wataambiwa makafiri Siku ya Kiyama watakapoomba kurejea katika dunia, lakini wataambiwa: Tayari wakati wa kurudi umeshapita. Na ikasemwa kwamba maana yake ni yale yaliyowasibu makafiri wa Kiquraishi walipokataa kuamini na wakaifanyia kiburi haki, kwa hivyo Nabii - rehema na amani zimshukie - akawaapiza na akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie dhidi yao kwa miaka (ya ukame) kama miaka (ya ukame) ya Yusuf." Basi Mwenyezi Mungu akawaletea njaa kubwa, hata wakala maiti na mifupa; kiasi kwamba wakaanza kuona kilicho kati ya mbingu na ardhi kama mwonekano wa moshi, lakini haukuwa moshi, na hiyo ilitokana na ukali wa njaa hiyo. Basi inakuwa kauli yake: "siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri" na maana kwamba hayo ni kulingana na macho yao wanavyoona, na wala si moshi kwa uhakika. Basi wakaendelea kuwa katika hali yao hii mpaka wakaomba Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake - rehema na kwamba awaombee kwa Mwenyezi Mungu ili Mwenyezi Mungu awaondolee balaa hiyo, [hivyo akamwomba Mola wake Mlezi]; basi Mwenyezi Mungu akaiondoa kwao. Kwa hivyo kwa msingi huu inakuwa kauli yake: "Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile" ni kujulisha kwamba Mwenyezi Mungu atawaondolea balaa hiyo, ni tishio kwao kwamba wasije rudi kwenye kiburi na kukadhibisha, na kujulisha juu ya kutokea kwake, nayo ikatokea, na kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa mshambulio mkubwa. Walisema kwamba hili lilikuwa vile vita vya Badr, lakini kauli hii ina maana ya mbali iliyo dhahiri. Na ikasemwa kuwa maana yake ni kwamba hii ni moja ya alama za Saa ya Kiyama, na kwamba katika zama za mwisho utatokea moshi utakaochukua pumzi za watu, lakini Waumini watasibiwa na hilo kama mwonekano wa moshi tu. Na kauli sahihi zaidi ni ile ya kwanza. Na katika aya hii kuna uwezekano kwamba kinachomaanishwa na kauli yake: "Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri. Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu! Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu" kwamba haya yote yatatokea Siku ya Kiyama, na kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile. Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa," ni yale yaliyowapata Maquraishi kama ilivyotangulia kutajwa awali. Ikiwa Aya hizi zilieleweka kwamba zina maana hizi mbili, basi hautapata chochote katika maneno yake chenye kuzuilia hilo, badala yake utayapata yanaingiliana nayo kuingiliana kukamilifu, na hili ndilo la sahihi zaidi kulingana na mimi, Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
: 17 - 33 #
{وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ (17) أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّهِ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ (18) وَأَنْ لَا تَعْلُوا عَلَى اللَّهِ إِنِّي آتِيكُمْ بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ (19) وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَنْ تَرْجُمُونِ (20) وَإِنْ لَمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ (21) فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَؤُلَاءِ قَوْمٌ مُجْرِمُونَ (22) فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُمْ مُتَّبَعُونَ (23) وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا إِنَّهُمْ جُنْدٌ مُغْرَقُونَ (24) كَمْ تَرَكُوا مِنْ جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (25) وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ (26) وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ (27) كَذَلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ (28) فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنْظَرِينَ (29) وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ (30) مِنْ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِنَ الْمُسْرِفِينَ (31) وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَى عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ (32) وَآتَيْنَاهُمْ مِنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُبِينٌ (33)}
17 Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. 18. Akasema: 'Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. 19. Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. 20. Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. 21. Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.' 22. Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: 'Hakika watu hawa ni wakosefu.' 23. Mwenyezi Mungu akasema: 'Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. 24. Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.' 25. Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha! 26. Na mimea na vyeo vitukufu! 27. Na neema walizokuwa wakijistareheshea! 28. Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. 29. Basi mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. 30. Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, 31. Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. 32. Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. 33. Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
#
{17} لما ذكر تعالى تكذيبَ من كذَّب الرسول محمداً - صلى الله عليه وسلم -؛ ذكر أن لهم سلفاً من المكذِّبين، فذكر قصَّتهم مع موسى، وما أحلَّ الله بهم؛ ليرتدعَ هؤلاء المكذِّبون عن ما هم عليه، فقال: {ولقد فتنَّا قبلهم قوم فرعون}؛ أي: ابتليناهم واختبرناهم بإرسال رسولنا موسى بن عمران إليهم، الرسول الكريم الذي فيه من الكرم ومكارم الأخلاق ما ليس في غيره.
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kukadhibisha kwa wale waliomkadhibisha Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake, - akataja kuwa wao walikuwa na watangulizi waliokadhibisha, basi akataja kisa chao na Musa, na yale aliyowafikishia Mwenyezi Mungu, ili hawa wanaokadhibisha wakomeke mbali na yale wanayoyafanya, akasema: "Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni" kwa kuwatuma Mtume wetu Musa bin Imran, Mtume mtukufu ambaye alikuwa na utukufu na maadili mema ambayo hayakuwa kwa mwengineye.
#
{18} {أنْ أدُّوا إليَّ عبادَ الله}؛ أي: قال لفرعون وملئهِ: أدُّوا إليَّ عباد الله؛ يعني بهم: بني إسرائيل؛ أي: أرسلوهم وأطلقوهم من عذابكم وسومكم إيَّاهم سوء العذاب؛ فإنَّهم عشيرتي وأفضل العالمين في زمانهم، وأنتم قد ظلمتُموهم واستعبدتُموهم بغير حقٍّ، فأرسلوهم ليعبدوا ربَّهم. {إنِّي لكم رسولٌ أمينٌ}؛ أي: رسول من ربِّ العالمين، أمينٌ على ما أرسلني به، لا أكتُمُكم منه شيئاً، ولا أزيد فيه ولا أنقُصُ، وهذا يوجبُ تمامَ الانقياد له.
{18} Akamwambia Firauni na wakuu wake: "Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu" yaani Wana wa Israili na muwaachilie huru na usiwaadhibu adhabu yako hiyo kali. Kwani wao ni ukoo wangu na bora zaidi wa walimwengu wa zama zao, na nyinyi mmewadhulumu na kuwatumikisha bila haki. Kwa hivyo, waachilieni wamuabudu Mola wao Mlezi. "Kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu." Yaani, Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote, mwaminifu kwa yale aliyonituma nayo, siwafichi chochote katika hayo, wala siongezi, wala sipunguzi. Na hili linalazimu watu kumtii kikamilifu.
#
{19} {وأن لا تَعْلوا على الله}: بالاستكبار عن عبادتِهِ والعلوِّ على عباد الله. {إنِّي آتيكُم بسلطانٍ مبينٍ}؛ أي: بحجَّة بيِّنةٍ ظاهرةٍ، وهو ما أتى به من المعجزات الباهرات والأدلَّة القاهرات.
{19} "Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu" kwa kuacha kumwabudu na kujikweza juu ya waja wa Mwenyezi Mungu. "Hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi." Na huo ni miujiza ya kung'aa na ushahidi wa ushindi alioufanya.
#
{20} فكذَّبوه وهمُّوا بقتله، فلجأ إلى الله من شرِّهم، فقال: {وإنِّي عذتُ بربِّي وربِّكم أن تَرْجُمونِ}؛ أي: تقتلوني أشرَّ القِتلاتِ بالرجم بالحجارة.
{20} Basi wakamkadhibisha na wakataka mno kumuuwa. Kwa hivyo, akakimbilia kwa Mwenyezi Mungu kutokana na uovu wao, na akasema: "Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe" mkaniuwa vibaya zaidi kwa kunipiga mawe.
#
{21} {وإن لم تؤمنوا لي فاْعَتِزلوِن}؛ أي: لكم ثلاث مراتب: الإيماُن بي، وهو مقصودي منكم. فإنْ لم تَحْصُل منكم هذه المرتبة؛ فاعتزلون لا عليَّ ولا لي؛ فاكفوني شرَّكم. فلم تحُصل منهم المرتبة الأولى ولا الثانية، بل لم يزالوا متمرِّدين عاتين على الله محاربين لنبيِّه موسى عليه السلام غير ممكِّنين له من قومه بني إسرائيل.
{21} "Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.'" Yaani, mna viwango vitatu: Kuniamini. Na hilo ndilo ninalokukusudia kwenu. Ikiwa hamtafikia kiwango hiki, basi jitengeni mbali nami, msinidhuru wala nisiwadhuru. Basi nilindeni kutokana na shari yenu. Lakini hakikutokea kwao kiwango hicho cha kwanza wala cha pili. Bali walibakia wakisitasita na wakimfanyia Mwenyezi Mungu ukaidi, wakimpigana vita Nabii wake Musa, amani iwe juu yake, bila ya kumuwezesha kuwatoa watu wake, Wana wa Israili.
#
{22} {فدعا ربَّه أنَّ هؤلاء قومٌ مجرمونَ}؛ أي: قد أجرموا جرماً يوجب تعجيل العقوبةِ، فأخبر عليه السلام بحالهم، وهذا دعاء بالحال التي هي أبلغ من المقال؛ كما قال عن نفسه عليه السلام: {ربِّ إنِّي لما أنزلتَ إليَّ من خيرٍ فقيرٌ}.
{22} "Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: 'Hakika watu hawa ni wahalifu.'" Yaani, wamefanya uhalifu unaolazimu waharakishiwe adhabu. Basi yeye amani iwe juu yake akajulisha juu ya hali yao. Na huku ni kuomba dua kwa kutumia hali, njia ambayo ni bora zaidi hata kuliko kuzungumza. Kama alivyosema kujihusu mwenyewe, yeye amani iwe juu yake: "Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia."
#
{23} فأمره الله أن يسريَ بعباده ليلاً، وأخبره أنَّ فرعون وقومه سيتَّبِعونه.
{23} Basi Mwenyezi Mungu akamwamuru atembee na waja wake usiku, na akamwambia kwamba Firauni na watu wake watamfuata.
#
{24} {واتْرُكِ البحرَ رهواً}؛ [أي: بحاله]، وذلك أنَّه لما سرى موسى ببني إسرائيل كما أمره الله، ثم تبعهم فرعونُ، فأمر الله موسى أن يضرِبَ البحر، فضربه، فصار اثني عشر طريقاً، وصار الماء من بين تلك الطرق كالجبال العظيمةِ، فسلكه موسى وقومُه، فلما خرجوا منه؛ أمره الله أن يترُكَه {رهواً}؛ أي: بحاله؛ ليسلُكَه فرعونُ وجنودُه. {إنَّهم جندٌ مغرَقون}: فلمَّا تكامل قومُ موسى خارجين منه وقومُ فرعونَ داخلينَ فيه؛ أمره الله تعالى أن يَلْتَطِمَ عليهم، فغرقوا عن آخرهم، وتركوا ما مُتِّعوا به من الحياة الدُّنيا، وأورثه الله بني إسرائيل الذين كانوا مستعبَدِين لهم.
{24} "Na iache bahari vivyo hivyo imeachana." Haya ni kwa sababu Musa alipowaongoza Wana wa Israili kama alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, kisha Firauni akawafuata, basi Mwenyezi Mungu akamuamuru Musa aipige bahari, naye akaipiga na ikawa njia kumi na mbili, na maji kati ya njia hizo yakawa kama milima mikubwa. Basi Musa na watu wake wakapitia humo. Walipotoka humo, Mwenyezi Mungu alimwamuru kuiacha vivyo hivyo; ili Firauni na askari wake wapitie humo. "Hakika wao ni jeshi litakalozamishwa majini." Kwa hivyo, walipotoka kaumu ya Musa wote na wakaingia humo watu wa Firauni, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiamrisha kuwafunika, kwa hivyo wakazama wote majini, na wakaacha yale waliyostareheshwa kwayo katika uhai wa duniani, na Mwenyezi Mungu akawarithisha hayo Wana wa Israili, ambao walikuwa watumwa wao.
#
{25 - 28} ولهذا قال: {كم تركوا من جناتٍ وعيونٍ. وزروع ومقام كريم. ونعمةٍ كانوا فيها فاكهينَ. كذلك وأوْرَثْناها}؛ أي: هذه النعمة المذكورة {قوماً آخرينَ}. وفي الآية الأخرى: {كذلك وأوْرَثْناها بني إسرائيلَ}.
{25 - 28} Ndiyo maana akasema: "Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha!. Na mimea na vyeo vitukufu! Na neema walizokuwa wakijistareheshea! Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe." Na katika Aya nyingine alisema: "Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili."
#
{29} {فما بكتْ عليهم السماءُ والأرضُ}؛ أي: لمَّا أتلفهم الله وأهلكهم لم تبكِ عليهم السماء والأرض؛ أي: لم يُحزنْ عليهم ولم يُؤس على فراقهم، بل كلٌّ استبشر بهلاكِهِم وتلفِهِم، حتى السماء والأرض؛ لأنَّهم ما خَلَّفوا من آثارِهم إلاَّ ما يسوِّدُ وجوهَهم ويوجبُ عليهم اللعنةَ والمقتَ من العالمين. {وما كانوا مُنظَرين}؛ أي: ممهَلين عن العقوبة، بل اصطلمتْهم في الحال.
{29} "Basi mbingu wala ardhi havikuwalilia" wala kuwahuzunukia kwa sababu ya kutengana nao Mwenyezi Mungu alipowaharibu na kuwaangamiza. Bali kila moja na hivyo kilifurahia kuangamizwa kwao na kuharibiwa kwao, hata mbingu na ardhi. Kwa sababu hawakuacha ila athari zinazozifanya nyuso zao kuwa nyeusi na kuwasababishia laana na kuchukiwa na walimwengu wote. "Wala hawakupewa muhula" kabla ya kuadhibiwa. Bali waliuawa mara moja.
#
{30 - 31} ثم امتنَّ تعالى على بني إسرائيلَ، فقال: {ولقد نَجَّيْنا بني إسرائيلَ من العذابِ المهينِ}: الذي كانوا فيه {من فرعونَ}: إذ يذبحُ أبناءَهم ويستحيي نساءَهم، {إنَّه كان عالياً}؛ أي: مستكبراً في الأرض بغير الحقِّ، {من المسرفين}: المتجاوزين لحدودِ الله المتجرِّئين على محارمه.
{30 - 31} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia Wana wa Israili juu ya neema yake, akasema: "Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha" ambayo walikuwa ndani yake "Ya Firauni" Kwani alikuwa akiwauwa watoto wao wa kiume na anawaacha hai wanawake wao. "Hakika yeye alikuwa jeuri" na kutakabari katika ardhi bila ya haki, "katika wenye kupindukia mipaka" ya Mwenyezi Mungu kwa kufanyia ujasiri maharamisho yake.
#
{32} {ولقد اختَرْناهم}؛ أي: اصطفيناهم وانتَقَيْناهم {على علم}: منَّا بهم وباستحقاقهم لذلك الفضل {على العالَمين}؛ أي: عالمي زمانهم ومَنْ قبلهم وبعدَهم، حتى أتى اللهُ بأمة محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - ففضَلوا العالمينَ كلَّهم، وجعلهم الله خير أمَّة أخرجت للناس، وامتنَّ عليهم بما لم يمتنَّ به على غيرهم.
{32} "Na tuliwakhiari kwa elimu yetu" kwani tulijua kwamba walistahiki fadhila hiyo "kuliko walimwengu wengineo" wa zama zao, na wale waliokuwa kabla yao na baada yao. Mpaka Mwenyezi Mungu alipowaleta umma wa Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - basi wao wakawa bora kuliko walimwengu wote, na Mwenyezi Mungu akawafanya kuwa umma bora kabisa waliotolewa watu, na akawaneemesha kwa yale ambayo hakuwahi kuwaneemesha wengineo.
#
{33} {وآتَيْناهم}؛ أي: بني إسرائيل {من الآياتِ}: الباهرة والمعجزات الظاهرةِ {ما فيه بلاءٌ مبينٌ}؛ أي: إحسانٌ كثيرٌ ظاهرٌ منَّا عليهم وحجَّة عليهم على صحَّة ما جاءهم به نبيُّهم موسى عليه السلام.
{33} "Na tukawapa" Wana wa Israili "katika ishara" na miujiza inayong'aa na iliyo dhahiri. Ishara hizi ni "zenye majaribio yaliyo wazi." Yaani, tuliwapa wema mwingi ulio dhahiri na ambao ni hoja dhidi yao juu ya usahihi wa yale aliyokuja nayo Nabii wao Musa, amani ziwe juu yake.
: 34 - 37 #
{إِنَّ هَؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ (34) إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَى وَمَا نَحْنُ بِمُنْشَرِينَ (35) فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (36) أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ أَهْلَكْنَاهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ (37)}
34. Hakika hawa wanasema: 35. 'Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. 36. Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.' 37. Je, ni wao bora au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
#
{34 - 35} يخبر تعالى {إنَّ هؤلاء}: المكذِّبين، يقولون: مستبعِدين للبعث والنُّشور: {إنْ هي إلاَّ موتَتُنا الأولى وما نحنُ بمُنشَرينَ}؛ أي: ما هي إلاَّ الحياة الدُّنيا؛ فلا بعثَ ولا نشورَ، ولا جنةَ ولا نارَ.
{34 - 35} Mwenyezi Mungu anajulisha kwamba: "Hakika hawa" wanaokadhibisha wanasema wakikatalia mbali suala la ufufuo na kuwatawanya viumbe: "'Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.'" Yaani, si chochote ila ni maisha ya dunia, na hakutakuwa na ufufuo wala kuwatawanya viumbe huko akhera, wala Bustani za mbinguni wala Moto.
#
{36} ثم قالوا متجرِّئين على ربِّهم معجزين له: {فأتوا بآبائِنا إن كنتُم صادقينَ}: وهذا من اقتراح الجَهَلَةِ المعانِدين في مكان سحيقٍ؛ فأيُّ ملازمة بين صدق الرسول - صلى الله عليه وسلم - وأنَّه متوقِّف على الإتيان بآبائهم؛ فإنَّ الآيات قد قامت على صدِق ما جاءهم به وتواترتْ تواتراً عظيماً من كلِّ وجه؟!
{36} Kisha wakasema kwa kumfanyia ujasiri Mola wao Mlezi na kuona kwamba hawezi kitu: "'Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.'" Haya ni katika mapendekezo ya watu wajinga wakaidi ambayo ni ya mbali mno. Kwani kuna uhusiano gani kati ya ukweli wa Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – na kwamba hawezi kuwa mkweli hadi awaletee baba zao? Kwani ishara zilishasimama juu ya ukweli wa yale aliyowaletea na zikasimuliwa kwa idadi kubwa sana kwa kila namna?
#
{37} قال تعالى: {أهم خيرٌ}؛ أي: هؤلاء المخاطبون، {أم قومُ تُبَّع والذين من قبلِهِم أهْلَكْناهم إنَّهم كانوا مجرمين}؟ فإنَّهم ليسوا خيراً منهم، وقد اشتركوا في الإجرام؛ فليتوقَّعوا من الهلاك ما أصاب إخوانهم المجرمين.
{37} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Je, ni wao bora." Yaani, hawa wanaoongeleshwa "au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wahalifu?" Wao si bora kuliko wale, kwani wameshiriki katika uhalifu. Basi na watarajie maangamizi kama yale yaliyowapata ndugu zao wahalifu.
: 38 - 42 #
{وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ (38) مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (39) إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ (40) يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَنْ مَوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنْصَرُونَ (41) إِلَّا مَنْ رَحِمَ اللَّهُ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (42)}.
38. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. 39. Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. 40. Hakika siku ya Uamuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote. 41. Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. 42. Isipokuwa atakayemrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno.
#
{38 - 39} يخبر تعالى عن كمال قدرتِهِ وتمام حكمتِهِ، وأنَّه ما خَلَقَ السماواتِ والأرض لاعباً، ولا لهواً، وسدىً من غير فائدة، وأنَّه ما خلقهما {إلاَّ بالحقِّ}؛ أي: نفسُ خلقهما بالحقِّ، وخلقُهما مشتملٌ على الحقِّ، وأنه أوجدهما لِيَعبدوه وحدَه لا شريك له، وليأمر العبادَ وينهاهم ويثيبَهم ويعاقِبَهم. {ولكنَّ أكثرَهم لا يعلمونَ}؛ فلذلك لم يتفكَّروا في خَلْقِ السماواتِ والأرض.
{38 - 39} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu wa uwezo wake na ukamilifu wa hekima yake, na kwamba hakuziumba mbingu na ardhi kwa ajili ya mchezo wala kwa pumbao, wala bure bila manufaa, na kwamba hakuziumba "ila kwa Haki." Yaani, kuviumba kwenyewe ni kwa Haki, na uumbaji wake umejumuisha haki, na kwamba aliviumba ili vimuabudu Yeye pekee, bila mshirika, na ili awaamrishe waja wake na awakataze, na awalipe mazuri na awaadhibu; "lakini wengi wao hawajui." Kwa hivyo, hawakutafakari katika kuumbwa mbingu na dunia.
#
{40} {إنَّ يوم الفصل}: وهو يوم القيامة، الذي يفصِلُ الله به بين الأولين والآخرين وبين كل مختلفين، {ميقاتُهم}؛ أي: الخلائق {أجمعين}: كلُّهم سيجمعُهم الله فيه، ويحضِرُهم ويحضِرُ أعمالهم، ويكون الجزاء عليها.
{40} "Hakika siku ya Uamuzi" ambayo ni Siku ya Kiyama, ambayo Mwenyezi Mungu atapambanua baina ya wa mwanzo na wa mwisho na baina ya waliohitilafiana, "ni wakati uliowekwa kwa wao wote." Mwenyezi Mungu atawakusanya wote humo, na atawahudhurisha wao na matendo yao, na atawalipa juu yake.
#
{41} لا ينفع {مولى عن مولى شيئاً}: لا قريب عن قريبه، ولا صديق عن صديقه، {ولا هم يُنصَرونَ}؛ أي: يمنعون من عذاب الله عزَّ وجلَّ؛ لأنَّ أحداً من الخلق لا يملك من الأمر شيئاً.
{41} "Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote" wala jamaa hatamfaa jamaa yake kitu. "Wala hawatanusuriwa" na kuzuiliwa mbali na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mtukufu. Kwa sababu hakuna yeyote miongoni mwa viumbe aliye na mamlaka yoyote juu ya jambo hilo.
#
{42} {إلاَّ مَن رَحِمَ اللهُ إنَّه هو العزيزُ الرحيمُ}: فإنَّه هو الذي ينتفع ويرتفع برحمةِ الله تعالى التي تسبَّب إليها، وسعى لها سعيها في الدنيا. ثم قال تعالى:
{42} "Isipokuwa atakayemrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno." Huyo ndiye atakayenufaika na kuinuka juu kwa sababu ya rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambazo alijisababishia na akazifanyia juhudi namna zinavyostahiki katika dunia hii. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 43 - 50 #
{إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ (43) طَعَامُ الْأَثِيمِ (44) كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ (45) كَغَلْيِ الْحَمِيمِ (46) خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَى سَوَاءِ الْجَحِيمِ (47) ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ (48) ذُقْ إِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ (49) إِنَّ هَذَا مَا كُنْتُمْ بِهِ تَمْتَرُونَ (50)}.
43. Hakika Mti wa Zaqqum 44. Ni chakula cha mwenye dhambi. 45. Kama shaba iliyoyeyushwa, hutokota matumboni. 46. Kama kutokota kwa maji ya moto. 47. (Itasemwa): 'Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! 48. Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayochemka.' 49. Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! 50. Hakika haya ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka.
#
{43 - 50} لما ذَكَرَ يوم القيامة، وأنه يفصِلُ بين عباده فيه؛ ذَكَرَ افتراقهم إلى فريقين: فريقٍ في الجنة، وفريقٍ في السعير، وهم الآثمون بعمل الكفر والمعاصي، وأنَّ طعامهم {شجرة الزَّقُّوم}: شرُّ الأشجار وأفظعُها، وأنَّ طعامها {كالمهل}؛ أي: كالصديد المنتن خبيث الريح والطعم شديد الحرارة، {يَغْلي في} بطونهم {كغَلْي الحميم}، ويُقال للمعذَّب: {ذُقْ}: هذا العذاب الأليم والعقاب الوخيم، {إنَّك أنتَ العزيزُ الكريمُ}؛ أي: بزعمك أنك عزيزٌ ستمتنع من عذاب الله، وأنك كريم على الله لا يصيبُك بعذابٍ؛ فاليوم تبيَّن لك أنَّك أنت الذَّليل المهان الخسيس. {إنَّ هذا} العذاب العظيم، {ما كنتُم به تمترونَ}؛ أي: تشكُّون؛ فالآن صار عندكم حقَّ اليقين.
{43 - 50} Alipotaja Siku ya Kiyama na kwamba atapambanua kati ya waja wake siku hiyo, akataja mgawanyiko wao katika makundi mawili: Kundi la kwenda katika Bustani za mbinguni, na kundi la kwenda Motoni, nao ni wakosefu waliofanya kufuru na maasia, na kwamba chakula chao ni "mti wa Zaqqum." Mti muovu na mbaya zaidi, na kwamba ladha yake ni "kama shaba iliyoyeyushwa" ndani ya matumbo yao. "Kama kutokota kwa maji ya moto." Na mhalifu ataambiwa: "Onja" adhabu hii chungu na kali sana. "Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!" Kwani ulidai kwamba wewe ni mwenye nguvu, kwa hivyo utazuilika na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba wewe ni mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na wala Yeye hawezi kukutia katika adhabu. Basi leo imekudhihirikia kuwa wewe ni mtu dhalili, anayefedheheshwa, aliye duni sana. "Hakika haya" ya adhabu kubwa "ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka." Lakini sasa mmeshajua kwamba ni haki ya yakini.
: 51 - 59 #
{إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ (51) فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (52) يَلْبَسُونَ مِنْ سُنْدُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُتَقَابِلِينَ (53) كَذَلِكَ وَزَوَّجْنَاهُمْ بِحُورٍ عِينٍ (54) يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ (55) لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَى وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ (56) فَضْلًا مِنْ رَبِّكَ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (57) فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ (58) فَارْتَقِبْ إِنَّهُمْ مُرْتَقِبُونَ (59)}
51. Hakika wacha Mungu watakuwa katika mahali pa amani. 52. Katika mabustani na chemchemi. 53. Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana. 54. Hivi ndivyo itakavyokuwa, na tutawaoza mahurilaini. 55. Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. 56. Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu. 57. Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 58. Basi tumeifanya nyepesi hii Qur-ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. 59. Ngoja tu, na wao wangoje pia.
#
{51 - 53} هذا جزاءُ المتَّقين لله، الذي اتَّقوا سَخَطه وعذابه بتركهم المعاصي وفعلهم الطاعات، فلمَّا انتفى السخط عنهم والعذابُ؛ ثبت لهم الرِّضا من الله والثواب العظيم في ظلٍّ ظليل من كثرة الأشجار والفواكه، وعيونٍ سارحةٍ تجري من تحتهم الأنهار يفجِّرونها تفجيراً، في جنات النعيم، فأضاف الجناتِ إلى النعيم؛ لأن كُلَّ ما اشتملت عليه، كله نعيمٌ وسرورٌ كامل من كلِّ وجهٍ، ما فيه منغصٌ ولا مكدرٌ بوجه من الوجوه، ولباسُهم من الحرير الأخضر من السندس والإستبرق؛ أي: غليظ الحرير ورقيقه ممَّا تشتهيهُ أنفسُهم، {متقابلين}: في قلوبهم ووجوههم في كمال الراحة والطمأنينة والمحبَّة والعشرة الحسنة والآداب المستحسنة.
{51 - 53} Haya ni malipo ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, walioogopa ghadhabu yake na adhabu yake kwa kuacha dhambi na kufanya vitendo vya utiifu. Pindi walipoepushwa mbali na ghadhabu na adhabu, wakapata ridhaa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na malipo mazuri makubwa katika kivuli vikubwa mno, katika miti mingi na matunda mengi, na chemchemi zinazotiririka na mito inayopita chini yao, wakiifanya imiminike kwa wingi katika Bustani za mbingu za neema. Mwenyezi Mungu alifungamanisha neema za Bustani hizi kwa sababu kila kitu kilichomo ndani yake ni neema, furaha kamili kwa namna zote, hakuna kitu cha kuhuzunisha wala kuchukiza kwa namna yoyote ile, na nguo zao zitakuwa zimetengenezwa kwa hariri ya kijani iliyotengenezwa kwa hariri laini na hariri nzito ya atilasi miongoni mwa yale yanayotamaniwa na nafsi zao "wakielekeana" nyoyoni mwao na nyuso zao, wakiwa katika raha kamili, utulivu, upendo, kuishi kwa uzuri na tabia njema.
#
{54} {كذلك}: النعيم التام والسرور الكامل، {وزوَّجْناهم بحورٍ} ؛ أي: نساء جميلات من جمالهنَّ وحسنهنَّ أنَّه يَحارُ الطرفُ في حسنهنَّ، وينبهر العقل بجمالهنَّ وينخلبُ اللبُّ لكمالهن، {عينٍ}؛ أي: ضخام الأعين حسانها.
{54} "Hivi ndivyo itakavyokuwa" neema kamili na furaha kamili "na tutawaoza mahurilaini." Nao ni wanawake warembo muno ambao kwa sababu ya urembo wao na uzuri wao huyafanya macho kushangazwa mno, akili kuduwaa na moyo kutekwa na ukamilifu wao. Nao ni wenye macho makubwa, mazuri mno.
#
{55} {يَدْعون فيها}: أي: الجنة {بكلِّ فاكهةٍ}: مما له اسمٌ في الدُّنيا ومما لا يوجدُ له اسمٌ ولا نظير في الدنيا؛ فمهما طلبوه من أنواع الفاكهة وأجناسها؛ أحضر لهم في الحال من غير تعبٍ ولا كلفةٍ، آمنين من انقطاع ذلك، وآمنين من مضرَّته، وآمنين من كلِّ مكدِّر، وآمنين من الخروج منها والموت.
{55} "Humo watataka kila aina ya matunda" miongoni mwa yale yaliyo na jina katika dunia na yasiyo na jina wala mfano wake katika dunia hii. Basi kwa namna yoyote ile watakavyoomba aina yoyote ile ya matunda, wataletewa mara hiyo hiyo bila juhudi yoyote wala kujisumbua, huku wakiwa wamesalimika kutokana na suala la kukatikiwa na hayo, na watakuwa salama kutokana na madhara yake, salama kutokana na kila cha kutia huzuni, na salama kutokana kuondoka humo, na kutokana na kifo.
#
{56} ولهذا قال: {لا يذوقون فيها الموتَ إلاَّ الموتةَ الأولى}؛ أي: ليس فيها موتٌ بالكلِّية، ولو كان فيها موتٌ يُستثنى؛ لم يستثنِ الموتةَ الأولى التي هي الموتة في الدنيا، فتمَّ لهم كلُّ محبوب مطلوب، {ووقاهم عذابَ الجحيم}.
{56} Ndiyo maana akasema: "Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza" ya duniani, na wala humo hakuna mauti yoyote. Kwa hivyo wakapata kwa ukamilifu kila kitu walichokipenda, walichokitafuta "na (Mwenyezi Mungu) atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu."
#
{57} {فضلاً من ربِّك}؛ أي: حصول النعيم واندفاع العذاب عنهم من فضل الله عليهم وكرمِهِ؛ فإنَّه تعالى هو الذي وفَّقهم للأعمال الصالحة، التي بها نالوا خير الآخرة وأعطاهم أيضاً ما لمْ تبلُغْه أعمالُهم. {ذلك هو الفوزُ العظيمُ}: وأيُّ فوزٍ أعظمُ من نيل رضوان الله وجنَّته والسلامة من عذابه وسخطِهِ.
{57} "Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi" kwa kuwapa neema hizo na kuwaondolea adhabu. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye aliyewawezesha kufikia matendo mema, ambayo kwayo walipata heri ya Akhera, na akawapa yale ambayo matendo yao hayakuyafikia. "Huko ndiko kufuzu kukubwa." Na kweli ni kufuzu gani ni kukubwa zaidi kuliko kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, Pepo yake kusalimika kutokana na adhabu yake na ghadhabu yake?
#
{58} {فإنما يَسَّرْناه}؛ أي: القرآن {بلسانِكَ}؛ أي: سهَّلْناه بلسانك الذي هو أفصحُ الألسنةِ على الإطلاق وأجلُّها، فتيسر به لفظه، وتيسر به معناه، {لعلَّهم يتذكَّرون}: ما فيه نفعُهم فيفعلونَه، وما فيه ضررُهم فيترُكونه.
{58} "Basi tumeifanya nyepesi hii Qur-ani kwa ulimi wako" ambao ndio fasaha zaidi kuliko ndimi zote na ambao ndio bora zaidi. Basi kwa huo, maneno yake yakafanywa kuwa wepesi, na maana zake pia zikafanywa kuwa nyepesi "ili wapate kukumbuka" yenye manufaa kwao, wakayafanya. Na yenye madhara kwao, basi wakayaacha.
#
{59} {فارتَقِبْ}؛ أي: انتظرْ ما وعدك ربُّك من الخير والنصر. {إنَّهم مرتقبونَ}: ما يحلُّ بهم من العذاب، وفرقٌ بين الارتقابين: رسول الله وأتباعه يرتقبون الخير في الدُّنيا والآخرة، وضدُّهم يرتقبون الشرَّ في الدُّنيا والآخرة.
{59} "Basi ngoja tu" yale aliyokuahidi Mola wako Mlezi ya heri na ushindi. "Hakika wao pia wanangoja" yale yatakayowapata ya adhabu, lakini kuna tofauti kubwa baina ya kungonja huku kuwili: Mtume wa Mwenyezi Mungu na wafuasi wake wanatazamia heri duniani na Akhera, naye aliye kinyume chao anangojea uovu duniani na Akhera.
Imekamilika tafsiri ya surat Ad-Dukhan, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu na neema.
* * *