:
Tafsiri ya Surat Ash-Shura
Tafsiri ya Surat Ash-Shura
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 9 #
{حم (1) عسق (2) كَذَلِكَ يُوحِي إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكَ اللَّهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (3) لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ (4) تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْ فَوْقِهِنَّ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَنْ فِي الْأَرْضِ أَلَا إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ (5) وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ اللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَا أَنْتَ عَلَيْهِمْ بِوَكِيلٍ (6) وَكَذَلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِتُنْذِرَ أُمَّ الْقُرَى وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنْذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ فَرِيقٌ فِي الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ (7) وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَكِنْ يُدْخِلُ مَنْ يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُمْ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ (8) أَمِ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ فَاللَّهُ هُوَ الْوَلِيُّ وَهُوَ يُحْيِ الْمَوْتَى وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (9)}.
1. Ha Mim 2. 'Ayn Sin Qaf 3. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hekima anavyokuletea Wahyi wewe na walio kabla yako. 4. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu. 5. Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana. 6. Na wale waliowafanya walinzi wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi bora juu yao. Wala wewe si wakili juu yao. 7. Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi na kundi jengine katika Moto wenye mwako mkali. 8. Na Mwenyezi Mungu angelipenda, angewafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi. 9. Au wamechukua walinzi wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi hasa. Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ndiye Muweza zaidi wa kila kitu.
#
{1 - 5} يخبر تعالى أنَّه أوحى هذا القرآن العظيم على النبيِّ الكريم كما أوحى إلى مَنْ قبلَه من الأنبياء والمرسلين؛ ففيه بيانُ فضلِهِ بإنزال الكتبِ وإرسال الرُّسل سابقاً ولاحقاً، وأنَّ محمداً - صلى الله عليه وسلم - ليس ببدع من الرسل، وأنَّ طريقَته طريقةُ مَنْ قبلَه، وأحوالَه تناسِبُ أحوالَ مَن قبلَه من المرسلين، وما جاء به يشابِهُ ما جاؤوا به؛ لأنَّ الجميع حقٌّ وصدقٌ، وهو تنزيلُ من اتَّصف بالألوهيَّة والعزَّة العظيمة والحكمة البالغةِ، وأنَّ جميع العالم العلويِّ والسفليِّ مُلْكُه وتحت تدبيرِهِ القدريِّ والشرعيِّ، وأنَّه {العليُّ} بذاتِهِ وقدرِهِ وقهرِهِ. {العظيم}: الذي من عظمتِهِ {تكادُ السمواتُ يتفطَّرْنَ من فوقِهِنَّ}: على عظمها وكونها جماداً، {والملائكةُ}: الكرامُ المقرَّبون خاضعون لعظمتِهِ مستكينون لعزَّته مذعنون بربوبِيَّته، {يسبِّحونَ بحمد ربِّهم}: ويعظِّمونه عن كل نقص، ويصِفونه بكل كمال، {ويستغفرونِ لِمَن في الأرض}: عما يصدُرُ منهم مما لا يليقُ بعظمة ربِّهم وكبريائِهِ، مع أنَّه تعالى {الغفورُ الرحيمُ}: الذي لولا مغفرتُه ورحمتُه؛ لعاجَلَ الخلقَ بالعقوبةِ المستأصِلَةِ. وفي وصفِهِ تعالى بهذه الأوصاف بعد أن ذَكَرَ أنَّه أوحى إلى الرسل كلهم عموماً وإلى محمدٍ - صلى الله عليهم وسلم - خصوصاً إشارةٌ إلى أنَّ هذا القرآن الكريم فيه من الأدلةُ والبراهينُ والآياتُ الدالَّةُ على كمال الباري تعالى ووصفِهِ بهذه الأسماء العظيمة الموجبة لامتلاءِ القلوب من معرفتِهِ ومحبتِه وتعظيمِه وإجلالِه وإكرامِه وصرف جميع أنواع العبوديَّة الظاهرة والباطنة له تعالى، وأنَّ من أكبر الظُّلم وأفحش القول اتِّخاذ أندادٍ من دونِهِ، ليس بيدِهِم نفعٌ ولا ضرٌّ ، بل هم مخلوقون مفتقرون إلى الله في جميع أحوالهم.
{1 - 5} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kwamba aliiteremsha Qur-ani hii tukufu kwa Mtume mtukufu, kama alivyoteremsha ufunuo pia kwa Mitume na Mitume wa kabla yake. Ndani yake kuna maelezo ya fadhila zake kwa kuteremsha Vitabu na kutuma Mitume kabla na baada yake, na kwamba Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – si wa mwanzo miongoni mwa Mitume, na kwamba njia yake ni njia ile ile ya wale waliotangulia kabla yake, na hali zake zinawiana na hali za Mitume waliotangulia kabla yake, na yale aliyokuja nayo yanafanana na yale waliyokuja nayo. Kwa sababu yote hayo ni haki na ukweli. Na ni ufunuo wa yule ambaye ana sifa ya uungu, utukufu mkubwa, na hekima kubwa, na kwamba ulimwengu wote wa juu na wa chini ni mali yake, na kiko chini ya uendeshaji wake wa kimungu na wa kisheria, na kwamba Yeye ndiye "Aliye juu zaidi" kwa dhati yake, cheo chake na ushindi wake. "Mkuu" ambaye kwa sababu ya ukuu wake na "ukubwa wake, "Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko" licha ya ukubwa wake na licha ya kuwa kwake mkuu, vitu visivyo na uhai "na Malaika" watukufu, walio karibu na Mwenyezi Mungu, wananyenyekea kwa utukufu wake na wanatii kwa sababu ya utukufu wake, na wanajisalimisha kwa umola wake "wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi," na wanampa taadhima kutokana na kila upungufu na wanamsifu kwa kila ukamilifu, "na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi" kwa sababu ya yale wanayoyafanya miongoni mwa mambo yasiyoufailia ukuu wa Mola wao Mlezi na ukubwa wake, pamoja na kwamba Yeye Mtukufu ni "Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu sana." Ambaye kama si msamaha wake na rehema zake, basi angeharakisha kuwaadhibu viuumbe kwa adhabu ya kuwaangamiza. Na katika kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa hizi baada ya kutaja kuwa aliwateremshia ufunuo Mitume wote kwa ujumla na kwa Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwashukie – hususan, kuna ishara kwamba Qur-ani hii tukufu ina ushahidi, uthibitisho, ishara zinazoonyesha ukamilifu wa Muumba Mtukufu, na kumsifu kwa majina haya makubwa ambayo yanalazimu nyoyo kujaa kumjua, kumpenda, kumpa taadhima, kumtukuza, kumheshimu na kumfanyia aina zote za ibada za dhahiri na zilizofichikana, na kwamba katika dhuluma kubwa zaidi na maneno machafu zaidi ni kumfanyia wenza, ambao hawawezi kufaidi wala kudhuru, bali wameumbwa, na wanamhitaji Mwenyezi Mungu katika hali zao zote.
#
{6} ولهذا عقَّبه بقوله: {والذين اتَّخذوا من دونِهِ أولياءَ}: يتولَّوْنَهم بالعبادة والطاعة؛ كما يعبدون الله ويطيعونَه؛ فإنَّما اتَّخذوا الباطلَ، وليسوا بأولياءٍ على الحقيقة. {اللهُ حفيظٌ عليهم}: يحفظُ عليهم أعمالَهم فيجازيهم بخيرها وشرِّها، {وما أنت عليهم بوكيل}: فتسألُ عن أعمالهم، وإنَّما أنت مبلغٌ أديتَ وظيفتَك.
{6} Ndiyo maana akaifuata kwa kauli yake: "Na wale waliowafanya walinzi wengine badala yake Yeye," ambao wanawafanya kuwa walinzi kwa kuwaabudu na kuwatii kama vile wanavyomwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumtii, basi hakika hao waliowachukua ni batili, wala sio walinzi kiuhakika. "Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi bora juu yao," anawahifadhia matendo yao na atawalipa kwa mema yake na maovu yake. "Wala wewe si wakili juu yao" ndiyo uulizwe juu ya matendo yao. Bali wewe ni mfikishaji tu, na tayari ulishafanya kazi yako.
#
{7} ثم ذكر منَّته على رسوله وعلى الناس حيث أنزل اللهُ {قرآناً عربيًّا} بيِّنَ الألفاظِ والمعاني، {لتنذرَ أمَّ القرى}: وهي مكةُ المكرمةُ، {ومَنْ حولَها}: من قُرى العرب، ثم يسري هذا الإنذارُ إلى سائرِ الخَلْق، {وتنذرَ}: الناس {يوم الجَمْع}: الذي يجمعُ الله به الأوَّلين والآخرين، وتخبِرُهم أنَّه {لا ريبَ فيه}، وأنَّ الخلق ينقسمون فيه فريقينِ: فريقًا {في الجنة}: وهم الذين آمنوا بالله وصدَّقوا المرسلين، وفريقًا {في السعيرِ}: وهم أصنافُ الكفرة المكذِّبين.
{7} Kisha akataja neema yake kwa Mtume wake na kwa watu, ambapo Mwenyezi Mungu aliteremsha "Qur-ani kwa Kiarabu," yenye maneno na maana zilizobainishwa, "ili uwaonye watu wa Mama wa Miji" ambao ni Makka tukufu, "na wale walio pembezoni mwake" miongoni mwa vijiji vya Waarabu. Kisha onyo hili lienee hadi kwenye viumbe vilivyobakia. "Na uhadharishe" watu "Siku ya Mkutano" ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho, na uwaambie kwamba "haina shaka hiyo" na kwamba viumbe watagawanyika siku hiyo makundi mawili: kundi moja "litakuwa Peponi." Hao ndio waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume. Na kundi lingine litakuwa "katika Moto wenye mwako mkali." Na hao ni aina mbalimbali za makafiri wanaokadhibisha.
#
{8} {و} مع هذا فلو شاءَ اللهُ لَجَعَلَ الناس {أمَّةً واحدةً}: على الهدى؛ لأنَّه القادر الذي لا يمتنع عليه شيء، ولكنه أراد أن يُدْخِلَ في رحمتِهِ مَنْ شاء من خواصِّ خلقِهِ، وأمَّا الظالمون الذين لا يَصْلُحون لصالح؛ فإنَّهم محرومون من الرحمة؛ فما لهم من دون الله من وليٍّ يتولاَّهم فيحصِّلُ لهم المحبوب، ولا نصيرٍ يدفعُ عنهم المكروهَ.
{8} "Na" pamoja na haya, lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka, angeliwafanya watu wote "umma mmoja" katika uongofu. Kwa sababu Yeye ndiye Muweza, ambaye hakuna lisilowezekana kwake. Lakini alitaka kumuingiza katika rehema yake amtakaye miongoni mwa viumbe vyake maalumu. Na ama madhalimu ambao hawawezi kutengenea kwa kufanya mambo mema, hao wamenyimwa rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo hawana mlinzi yeyote badala ya Mwenyezi Mungu atakayewalinda ili wapate wanayopenda, wala wa kuwanusuru atakayewaondolea wanayochukia.
#
{9} والذين اتَّخذوا من دونه أولياءَ يتولَّوْنهم بعبادتِهم إيَّاهم؛ فقد غلطوا أقبح غلط؛ {فالله هو الوليُّ} الذي يتولاَّه عبدُه بعبادته وطاعته والتقرُّب إليه بما أمكن من أنواع التقرُّبات، ويتولَّى عباده عموماً بتدبيره ونفوذِ القدر فيهم، ويتولَّى عباده المؤمنين خصوصاً بإخراجهم من الظُّلمات إلى النور، وتربيتهم بلطفه، وإعانتهم في جميع أمورهم. {وهو يُحيي الموتى وهو على كلِّ شيءٍ قديرٌ}؛ أي: هو المتصرِّف بالإحياء والإماتة ونفوذِ المشيئة والقدرةِ؛ فهو الذي يستحقُّ أن يُعْبَدَ وحدَه لا شريك له.
{9} Na wale waliojifanyia walinzi badala yake kwa kuwaabudu, basi walifanya kosa baya zaidi; "Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi hasa" ambaye mja wake anapaswa kumfanya kuwa Mlinzi wake kwa kumwabudu, kumtii Yeye na kujikurubisha kwake kwa namna yoyote ile iwezekanayo ya kujikurubisha. Naye anawasimamia waja wake kwa ujumla kwa uendeshaji wake na kutekeleza mipango yake juu yao, na anawalinda waja wake waumini hasa kwa kuwatoa katika viza na kuwapeleka kwenye nuru, akiwalea kwa upole wake na kuwasaidia katika mambo yao yote. "Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ndiye Mweza zaidi wa kila kitu." Yaani, Yeye ndiye anayehuisha na kufisha, na kutekeleza mapenzi yake na uwezo wake. Basi Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, bila mshirika yeyote.
: 10 - 12 #
{وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِنْ شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ ذَلِكُمُ اللَّهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ (10) فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَعَلَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ (11) لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (12)}.
10. Na mkihitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi ninayemtegemea, na kwake Yeye narejea. 11. Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi. Amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona sana. 12. Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi zaidi wa kila kitu.
#
{10} يقول تعالى: {وما اختلفتُم فيه من شيءٍ}: من أصول دينِكم وفروعِهِ مما لم تتَّفقوا عليه {فحكمُهُ إلى الله}: يُرَدُّ إلى كتابِهِ وإلى سنَّة رسوله؛ فما حكما به؛ فهو الحقُّ، وما خالف ذلك؛ فباطلٌ. {ذلكم الله ربِّي}؛ أي: فكما أنَّه تعالى الربُّ الخالق الرازق المدبِّر؛ فهو تعالى الحاكمُ بين عبادِهِ بشرعِهِ في جميع أمورهم. ومفهومُ الآية الكريمة أنَّ اتِّفاق الأمَّة حجَّةٌ قاطعةٌ؛ لأنَّ الله تعالى لم يأمُرْنا أن نَرُدَّ إليه إلاَّ ما اخْتَلَفْنا فيه؛ فما اتَّفقنا عليه يكفي اتِّفاق الأمة عليه؛ لأنَّها معصومةٌ عن الخطأ، ولا بدَّ أن يكون اتِّفاقها موافقاً لما في كتاب الله وسنَّة رسوله. وقوله: {عليه توكلتُ}؛ أي: اعتمدتُ بقلبي عليه في جَلْب المنافع ودَفْع المضارِّ، واثقاً به تعالى في الإسعاف بذلك، {وإليه أنيبُ}؛ أي: أتوجَّه بقلبي وبدني إليه وإلى طاعته وعبادتِهِ، وهذان الأصلان كثيراً ما يذكُرُهما الله في كتابِهِ؛ لأنَّهما يحصُلُ بمجموعهما كمال العبدِ، ويفوتُهُ الكمال بفَوْتِهِما أو فَوْتِ أحدِهما؛ كقوله تعالى: {إيَّاك نعبدُ وإيَّاكَ نستعينُ}، وقوله: {فاعبُدْه وتوكَّلْ عليه}.
{10} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mkihitalifiana katika jambo lolote" katika misingi ya dini yenu na matawi yake, katika yale msiyokubaliana juu yake, "basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu." Inarejeshwa kwenye Kitabu chake na kwa Sunna za Mtume wake. Kwa hivyo, hukumu watakayotoa, basi hiyo ndiyo kweli. Na chochote kilicho kinyume nayo, basi hicho ni batili. "Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi." Yaani, kama vile Yeye Mtukufu ndiye Mola Mlezi, Muumba, Mwenye kuruzuku, Mwendeshaji mambo, basi Yeye ndiye atakayehukumu kati ya waja wake kwa mujibu wa sheria yake katika mambo yao yote. Maana isiyo ya moja kwa moja ya Aya hii tukufu ni kwamba makubaliano ya umma huu ni hoja ya uhakika. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakutuamrisha kumrudishia isipokuwa yale tuliyohitalifiana juu yake. Kwa hivyo, kile tulichokubaliana juu yake kinautosha umma huu makubaliano yao juu yake. Kwa sababu, umma huu umehifadhiwa kutokana na suala la kukubaliana juu ya kosa, na lazima makubaliano yao yawe kwa mujibu wa yale yaliyomo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake. Na kauli yake: "Kwake ndiye ninayemtegemea," yaani, nilimtegemea kwa moyo wangu katika kuleta manufaa na kuepusha madhara nikiwa na imani naye Mtukufu anisaidie katika hayo. "Na kwake Yeye narejea," yaani, ninauelekeza moyo wangu na mwili wangu kwake, na ninaelekea katika utiifu wake na kumfanyia ibada. Hii miwili ni misingi ambayo mara nyingi Mwenyezi Mungu anaitaja katika Kitabu chake. Kwa sababu,kwa ujumla wake mja hufikia ukamilifu na pia hukosa ukamilifu kwa kukosa mawili hayo au moja yake. Kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wewe tu tunakuabudu na Wewe tu tunakuomba msaada," na kauli yake, "Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye.”
#
{11} {فاطرُ السمواتِ والأرضِ}؛ أي: خالقُهما بقدرتِهِ ومشيئتِهِ وحكمتِهِ. {جَعَلَ لكم من أنفسِكم أزواجاً}: لتَسْكنوا إليها وتنتشرَ منكم الذُّرِّيَّة ويحصُلُ لكم من النفع ما يحصُل، {ومن الأنعام أزواجاً}؛ أي: ومن جميع أصنافِها نوعين ذكراً وأنثى؛ لتبقى وتنمو لمنافعكم الكثيرة، ولهذا عدَّاها باللام الدالَّة على التعليل؛ أي: جعل ذلك لأجلكم ولأجل النِّعمة عليكم، ولهذا قال: {يذرؤُكم فيه}؛ أي: يبثُّكم ويكثركم ويكثر مواشيكم بسبب أن جعل لكم من أنفسكم، وجعل لكم من الأنعام أزواجاً. {ليس كمثلِهِ شيءٌ}: أي: ليس يشبِهُه تعالى ولا يماثِلُه شيء من مخلوقاتِهِ لا في ذاته ولا في أسمائِهِ ولا في صفاتِهِ ولا في أفعالِهِ؛ لأنَّ أسماءه كلَّها حسنى، وصفاتِهِ صفاتُ كمال وعظمة، وأفعالَه تعالى أوجد بها المخلوقاتِ العظيمةَ من غير مشارك؛ فليس كمثله شيءٌ؛ لانفرادِهِ وتوحُّده بالكمال من كلِّ وجه. {وهو السميعُ}: لجميع الأصوات، باختلاف اللغات، على تفنُّن الحاجات. {البصير}: يرى دبيبَ النملة السوداء، في الليلة الظلماء، على الصخرة الصمَّاء، ويرى سَرَيانَ القوتِ في أعضاء الحيوانات الصغيرةِ جدًّا، وسريانَ الماء في الأغصان الدقيقة. وهذه الآية ونحوها دليلٌ لمذهب أهل السنة والجماعة من إثبات الصفاتِ ونفي مماثلة المخلوقات، وفيها ردٌّ على المشبِّهة في قوله: {ليس كمثلِهِ شيءٌ}، وعلى المعطِّلة في قوله: {وهو السميعُ البصيرُ}.
{11} "Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi." Yaani, Muumba wake kwa uwezo wake, mapenzi yake na hekima yake. "Amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu" ili mpate utulivu kwao, na dhuria wenu waenee baina yenu, na muweze kupata manufaa mbalimbali. "Na katika nyama hoa, dume na jike" kutoka katika aina zake zote ili waendelee kubakia na kukua kwa manufaa yenu mengi, na ndiyo maana akasema: "Anakuzidishieni namna hii" nyinyi na mifugo wenu. "Hapana kitu kama mfano wake" katika viumbe vyake, si katika dhati yake, wala katika majina yake, wala katika sifa zake, wala katika vitendo vyake. Kwa sababu majina yake yote ni mazuri zaidi, sifa zake ni sifa za ukamilifu na ukuu, na vitendo vyake Mola Mtukufu ndivyo alivyoumba kwavyo viumbe vikubwa bila ya mshirika yeyote. Basi hapana kitu kama mfano wake kwa sababu ya upekee wake na umoja wake katika ukamilifu kwa namna zote. "Naye ni Mwenye kusikia mno" sauti zote kwa lugha mbali mbali, kwa mahitaji mbalimbali. "Mwenye kuona sana," ambaye anaona kutambaa kwa chungu mweusi katika usiku wa giza zaidi juu ya jiwe gumu. Na anaona mtiririko wa chakula kinapopita katika viungo vya wanyama wadogo sana, na mtiririko wa maji yanapopita katika matawi madogo mno. Aya hii na nyinginezo mfano wake ni ushahidi wa dhehebu la Ahlus-Sunna wal-Jamaa katika kuthibitisha sifa na kukanusha kufanana kwake na viumbe, na pia ina jibu kwa wenye kumfananisha Mwenyezi Mungu na viumbe katika kauli yake: "Hapana kitu kama mfano wake," na pia kuna jibu kwa wale wanaopinga sifa za Mwenyezi Mungu katika kauli yake: "Naye ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona sana."
#
{12} وقوله: {له مقاليدُ السمواتِ والأرضِ}؛ أي: له ملك السماواتِ والأرضِ، وبيدِهِ مفاتيحُ الرحمةِ والأرزاق والنِّعم الظاهرة والباطنة؛ فكلُّ الخلق مفتقرون إلى الله في جَلْب مصالحهم ودَفْع المضارِّ عنهم في كلِّ الأحوال، ليس بيد أحدٍ من الأمر شيء، والله تعالى هو المعطي المانع الضارُّ النافع، الذي ما بالعباد من نعمةٍ إلاَّ منه، ولا يدفع الشرَّ إلاَّ هو، وما يفتح اللهُ للناس من رحمةٍ فلا ممسكَ لها وما يمسك فلا مرسلَ له من بعدِهِ، ولهذا قال هنا: {يبسُطُ الرزقَ لِمَن يشاءُ}؛ أي: يوسِّعه ويعطيه من أصناف الرزقِ ما شاء، {وَيَقْدِرُ}؛ أي: يضيِّق على مَنْ يشاء حتى يكونَ بقدر حاجتِهِ، لا يزيدُ عنها، وكلُّ هذا تابعٌ لعلمه وحكمتِهِ؛ فلهذا قال: {إنَّه بكلِّ شيءٍ عليمٌ}: فيعلم أحوالَ عبادِهِ، فيعطي كلًّا ما يَليقُ بحكمتِهِ، وتقتضيه مشيئتُه.
{12} Na kauli yake: 'Yeye ndiye Mwenye mbingu na ardhi.' Yaani, ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, na mkononi mwake ndio kuna funguo za rehema, riziki na neema za dhahiri na zilizofichikana. Kila kiumbe kinamhitaji Mwenyezi Mungu katika kuleta masilahi yao na kuzuia madhara katika hali zote. Mambo hayo hayako katika mkono wa mwingine yeyote. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye kupeana, Mwenye kuzuia, Mwenye kudhuru, Mwenye kunufaisha, ambaye hakuna neema yoyote waliyonayo waja isipokuwa ni kutoka kwake. Na wala hakuna anayeweza kuzuilia maovu isipokuwa Yeye. Na rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, basi hapana wa kuizuia. Na anayoizuia, hapana wa kuipeleka isipokuwa Yeye. Ndiyo maana akasema, "Humkunjulia riziki amtakaye" akampa katika aina mbalimbali za riziki "na humpimia amtakaye" ikawa inatosha tu haja yake, si zaidi yake. Na yote haya ni kulingana na elimu yake na hekima yake. Ndiyo maana akasema: "Hakika Yeye ni Mjuzi zaidi wa kila kitu" Anazijua hali za waja wake, na anampa kila mmoja wao yale yanayolingana na hekima yake na yanayotaka mapenzi yake.
: 13 #
{شَرَعَ لَكُمْ مِنَ الدِّينِ مَا وَصَّى بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَنْ يُنِيبُ (13)}.
13. Amekuamrisheni Dini ile ile aliyomuusia Nuhu na tuliyokufunulia wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.
#
{13} هذه أكبرُ منَّةٍ أنعم الله بها على عباده أنْ شَرَعَ لهم من الدين خيرَ الأديان وأفضلَها وأزكاها وأطهرَها، دين الإسلام، الذي شَرَعَه الله للمصطَفَيْن المختارين من عباده، بل شَرَعَه الله لخيار الخيار وصفوة الصفوة، وهم أولو العزم من المرسلين، المذكورون في هذه الآية، أعلى الخلق درجة وأكملهم من كلِّ وجه؛ فالدين الذي شرعه الله لهم لا بدَّ أن يكون مناسباً لأحوالهم موافقاً لكمالهم، بل إنَّما كَمَّلَهم الله، واصطفاهم بسبب قيامهم به؛ فلولا الدين الإسلاميُّ؛ ما ارتفع أحدٌ من الخلق؛ فهو روح السعادة وقطبُ رحى الكمال، وهو ما تضمَّنه هذا الكتاب الكريم ودعا إليه من التوحيد والأعمال والأخلاق والآداب. ولهذا قال: {أنْ أقيموا الدِّين}؛ أي: أمركم أن تقيموا جميعَ شرائع الدِّين أصوله وفروعه؛ تقيمونه بأنفسكم، وتجتهدون في إقامته على غيركم، وتعاونون على البرِّ والتَّقوى، ولا تعاونون على الإثم والعدوان، {ولا تتفرَّقوا فيه}؛ أي: ليحصل منكم الاتِّفاق على أصول الدين وفروعه، واحرصوا على أن لا تفرِّقَكم المسائل وتحزِّبَكم أحزاباً، فتكونون شيعاً يعادي بعضُكم بعضاً مع اتِّفاقكم على أصل دينكم. ومن أنواع الاجتماع على الدين وعدم التفرق فيه ما أمر به الشارعُ من الاجتماعات العامَّة؛ كاجتماع الحجِّ والأعياد والجُمَع والصَّلوات الخمس والجهاد وغير ذلك من العبادات التي لا تتمُّ ولا تَكْمُلُ إلاَّ بالاجتماع لها وعدم التفرُّق. {كَبُرَ على المشركين ما تَدْعوهم إليه}؛ أي: شقَّ عليهم غايةَ المشقَّة؛ حيث دعوتَهم إلى الإخلاص لله وحدَه؛ كما قال عنهم: {وإذا ذُكِرَ اللهُ وحدَه اشمأزَّت قلوبُ الذين لا يؤمنون بالآخرة وإذا ذُكِرَ الذين من دونِهِ إذا هم يستبشرونَ}، وقولهم: {أجَعَلَ الآلهةَ إلهاً واحداً إنَّ هذا لشيءٌ عُجابٌ}. {الله يَجْتبي إليه مَن يشاءُ}؛ أي: يختار من خليقتِهِ مَنْ يعلم أنَّه يَصْلُحُ للاجتباء لرسالتِهِ وولايتِهِ، ومنه أنِ اجْتَبى هذه الأمَّة وفضَّلها على سائر الأمم واختارَ لها أفضلَ الأديان وخيرَها. {ويَهْدي إليه من ينيبُ}: هذا السبب الذي من العبد يتوصَّل به إلى هداية الله تعالى، وهو إنابتُه لربِّه، وانجذابُ دواعي قلبِهِ إليه، وكونُه قاصداً وجهه؛ فحسنُ مقصدِ العبد مع اجتهادِهِ في طلب الهدايةِ من أسباب التيسير لها؛ كما قال تعالى: {يَهْدي بهِ الله من اتَّبَعَ رضوانَه سُبُلَ السلام}. وفي هذه الآية أنَّ الله {يَهْدي إليه مَن يُنيبُ}، مع قولِهِ: {واتَّبِعْ سبيلَ من أنابَ إليَّ}، مع العلم بأحوال الصحابة رضي الله عنهم وشدَّة إنابتهم: دليلٌ على أنَّ قولهم حجَّة، خصوصاً الخلفاء الراشدين رضي الله عنهم أجمعين.
{13} Hii ndiyo neema kubwa kabisa aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu waja wake, kwamba amewawekea sheria ya Dini nzuri kabisa, iliyo bora kabisa, iliyotakasika kabisa na iliyo safi kabisa. Dini ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu aliiweka kama sheria kwa ajili ya wateule miongoni mwa waja wake. Bali Mwenyezi Mungu aliiweka kama sheria kwa ajili ya wale walio bora zaidi na walio juu zaidi, ambao ni wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume waliotajwa katika aya hii. Ambao ndio wenye daraja ya juu zaidi ya viumbe wote, na wakamilifu zaidi kati yao kwa njia zote. Kwa hivyo, Dini hii ambayo Mwenyezi Mungu amewawekea kama sheria lazima izifailie hali zao na iendane na ukamilifu wao. Bali Mwenyezi Mungu aliwakamilisha na kuwachagua kwa sababu waliitekeleza. Kama si dini ya Uislamu, basi hakuna yeyote angeinuka juu miongoni mwa viumbe. Hiyo ndiyo roho ya furaha na sehemu ya kati ya jiwe la kusagia la ukamilifu. Hayo ndiyo ambayo Kitabu hiki adhimu kinajumuisha na kuyalingania, kama vile kumpwekesha Mwenyezi Mungu, matendo, maadili na adabu mbalimbali. Ndiyo maana akasema kwamba "shikeni dini sawasawa" kwa kutekeleza sheria zote za dini, misingi yake na matawi yake. Mnaisimamisha juu ya nafsi zenu wenyewe, na mnajitahidi kuisimamisha kwa wengineo, na mnasaidiana katika wema na uchamungu. Wala hamsaidiani katika dhambi na uadui, "wala msifarikiane kwayo." Yaani, fanyeni makubaliano baina yenu juu ya misingi ya dini na matawi yake, na fanyeni bidii kujihadharini mambo yasije yakawafarakanisha masuala mbalimbali na kuwafanya kuwa makundi makundi, mkawa maadui wenyewe kwa wenyewe licha ya kwamba mnaafikiana katika msingi wa dini yenu. Miongoni mwa aina za kukusanyika pamoja juu ya dini na kutogawanyika ndani yake ni mikusanyiko ya hadhara iliyoamrishwa na sheria. Kama vile mkusanyiko wa Hija, Idi, swala ya Ijumaa, swala tano za kila siku, Jihadi na ibada zinginezo ambazo haziwezi kukamilika wala kutimia isipokuwa kwa kukusanyika pamoja, kutotengana. "Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia;" pale ulipowaita kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumkusudia Yeye peke yake. Kama alivyosema kuwahusu: "Na anapotajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasioiamini Akhera huchafuka. Na wanapotajwa wenginewe asiyekuwa Yeye basi wao hufurahi." Na kusema kwao: "Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu." "Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye." Yaani, anawateuwa miongoni mwa viumbe vyake wale anaowajua kuwa wanafaa kuteuliwa kwa ajili ya ujumbe wake na kuwa vipenzi wake. Na miongoni mwa hilo ni kwamba aliuchagua umma huu na akauboresha kuliko umma nyinginezo zote na akauchagulia dini nzuri na bora zaidi, "na humwongoa kwake aelekeaye." Hii, yaani kurudi kwa Mwenyezi Mungu, ndiyo sababu anayofanya mja na ambayo kupatia kwayo anafikia kuongolewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na pia matamanio ya moyo wake kuelekea kwake na kuukusudia uso wake. Kwa hivyo, nia njema ya mja pamoja na bidii yake katika kutafuta uwongofu ni mojawapo ya sababu za kurahisishiwa kuufikia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu huwaongoa wenye kufuata radhi yake katika njia za salama." Katika Aya hii, kuna kwamba Mwenyezi Mungu "humwongoa kwake aelekeaye" kwake, pamoja na kauli yake: "nawe ishike njia ya anayeelekea kwangu." Na pamoja na kujua hali za Maswahaba wa Mtume wake, Mwenyezi Mungu awawiye radhi, na wingi wa kurejea kwao kwake, kuna ushahidi kwamba maneno yao ni ushahidi, hasa Mahalifa waongofu wa Mtume wake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote.
: 14 - 15 #
{وَمَا تَفَرَّقُوا إِلَّا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِنْ رَبِّكَ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّ الَّذِينَ أُورِثُوا الْكِتَابَ مِنْ بَعْدِهِمْ لَفِي شَكٍّ مِنْهُ مُرِيبٍ (14) فَلِذَلِكَ فَادْعُ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَقُلْ آمَنْتُ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنْ كِتَابٍ وَأُمِرْتُ لِأَعْدِلَ بَيْنَكُمُ اللَّهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ لَا حُجَّةَ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ اللَّهُ يَجْمَعُ بَيْنَنَا وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ (15)}.
14. Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia elimu kwa sababu ya husuda iliyokuwa baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya kuahirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka pangelihukumiwa baina yao. Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayowahangaisha. 15. Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyoamrishwa, wala usiyafuate matamanio yao. Na sema: 'Ninaamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu, na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu. Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake.'
#
{14} لما أمَرَ تعالى باجتماع المسلمين على دينِهِم، ونهاهم عن التفرُّق؛ أخبرهم أنَّهم لا يَغْتَرُّوا بما أنزل الله عليهم من الكتاب؛ فإنَّ أهل الكتاب لم يتفرَّقوا حتى أنزل الله عليهم الكتابَ الموجبَ للاجتماع، ففعلوا ضدَّ ما يأمر به كتابُهم، وذلك كلُّه بغياً وعدواناً منهم؛ فإنَّهم تباغضوا، وتحاسدوا، وحصلت بينهم المشاحنةُ والعداوةُ، فوقع الاختلافُ؛ فاحذَروا أيُّها المسلمون أن تكونوا مثلهم. {ولولا كلمةٌ سبقتْ من ربِّك}؛ أي: بتأخير العذاب القاضي إلى أجل مسمًّى، {لَقُضِيَ بينهم}: ولكنَّ حكمتَه وحلمه اقتضى تأخيرَ ذلك عنهم. {وإنَّ الذين أُورِثوا الكتابَ من بعدِهم}؛ أي: الذين ورثوهم، وصاروا خَلَفاً لهم ممَّن ينتسب إلى العلم منهم، {لَفي شكٍّ منهُ مريبٍ}؛ أي: لفي اشتباهٍ كثير يوقعُ في الاختلاف؛ حيث اختلف سَلَفُهم بغياً وعناداً؛ فإنَّ خلفهم اختلفوا شكًّا وارتياباً، والجميعُ مشتركون في الاختلاف المذموم.
{14} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowaamrisha Waislamu kuungana katika dini yao, na akawakataza kutengana, akawaambia wasidanganywe na aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika Kitabu. Kwani, Watu wa Kitabu hawakutawanyika, mpaka Mwenyezi Mungu alipowateremshia Kitabu kinachowataka wakusanyike, lakini wakafanya kinyume na kile kilichoamrishwa na Kitabu chao, na yote hayo ni kwa sababu ya dhuluma na uadui wao. Kwani walichukiana wao kwa wao na wakahusudiana, na ukazuka ugomvi na uadui kati yao, kwa hivyo wakahitilafiana. Basi jihadharini enyi Waislamu msiwe kama wao. "Na lau kuwa haikwishatangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi" ya kuchelewesha adhabu ya kuwaangamiza hadi muda maalumu, "basi bila ya shaka palingelihukumiwa baina yao." Lakini hekima yake na ustahimilivu wake ulihitaji wacheleweshewe hilo. "Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao" wakawa mafuatizi wao miongoni mwao wale ambao wamehusishwa na elimu "wanakitilia shaka inayo wahangaisha." Kwa maana, watangulizi wao walitofautiana kwa sababu ya dhuluma na uadui; kwa hivyo wafuatizi wao nao wakahitalifiana kwa sababu ya shaka na kusitasita. Na hao wote ni sawa katika kuhitilafiana kwao kubaya.
#
{15} {فلذلك فادعُ}؛ أي: فللدين القويم والصراط المستقيم، الذي أنزل الله به كُتُبَه وأرسل رُسُله؛ فادعُ إليه أمَّتك، وحضَّهم عليه، وجاهد عليه مَنْ لم يقبَلْه. {واستَقِمْ}: بنفسك {كما أمرتَ}؛ أي: استقامةً موافقةً لأمر الله؛ لا تفريط ولا إفراط، بل امتثالاً لأوامر الله، واجتناباً لنواهيه، على وجه الاستمرار على ذلك؛ فأمَرَه بتكميل نفسه بلزوم الاستقامة، وبتكميل غيرِهِ بالدَّعوة إلى ذلك. ومن المعلوم أنَّ أمر الرسولِ - صلى الله عليه وسلم - أمرٌ لأمَّته إذا لم يَرِدْ تخصيصٌ له. {ولا تتَّبِعْ أهواءهم}؛ أي: أهواء المنحرفين عن الدِّين من الكفرة والمنافقين، إمَّا باتِّباعهم على بعض دينهم، أو بترك الدَّعوة إلى الله، أو بترك الاستقامة؛ فإنَّك إن اتَّبعت أهواءهم من بعد ما جاءك من العلم إنَّك إذاً لَمِنَ الظالمين، ولم يقل ولا تتَّبِع دينَهم؛ لأنَّ حقيقة دينهم الذي شَرَعَه الله لهم هو دينُ الرسل كلِّهم، ولكنَّهم لم يتَّبِعوه، بل اتَّبعوا أهواءهم واتَّخذوا دينهم لهواً ولعباً، {وقل}: لهم عند جدالهم ومناظرتهم: {آمنتُ بما أنزلَ اللهُ من كتابٍ}؛ أي: لتكنْ مناظرتُك لهم مبنيةً على هذا الأصل العظيم، الدالِّ على شرف الإسلام وجلالته وهيمنتِهِ على سائر الأديان، وأنَّ الدين الذي يزعُمُ أهل الكتاب أنَّهم عليه جزءٌ من الإسلام، وفي هذا إرشادٌ إلى أنَّ أهل الكتاب إن ناظروا مناظرة مبنيَّة على الإيمان ببعض الكتب أو ببعض الرسل دون غيرِهِ؛ فلا يسلمُ لهم ذلك؛ لأنَّ الكتابَ الذي يدعون إليه والرسولَ الذي ينتسبونَ إليه من شرطِهِ أن يكون مصدِّقاً بهذا القرآن وبمن جاء به؛ فكتابُنا ورسولُنا لم يأمرنا إلاَّ بالإيمان بموسى وعيسى والتوراة والإنجيل التي أخبر بها وصدَّق بها وأخبر أنَّها مصدقة له ومقرَّة بصحته، وأما مجرَّدُ التوراة والإنجيل وموسى وعيسى الذين لم يوصفوا لنا ولم يوافِقوا لكتابِنا؛ فلم يأمرْنا بالإيمان بهم. وقوله: {وأمِرْتُ لأعدلَ بينكم}؛ أي: في الحكم فيما اختلفتُم فيه؛ فلا تَمْنَعُني عداوتُكم وبُغضكم يا أهل الكتاب من العدل بينكم، ومن العدل في الحكم بين أهل الأقوال المختلفة من أهل الكتاب وغيرهم أن يُقْبَلَ ما معهم من الحقِّ ويردَّ ما معهم من الباطل. {الله ربُّنا وربُّكم}؛ أي: هو ربُّ الجميع، لستم بأحقَّ به منا، {لنا أعمالُنا ولكُم أعمالُكم}: من خيرٍ وشرٍّ، {لا حجَّةَ بيننا وبينكم}؛ أي: بعدما تبيَّنت الحقائق واتَّضح الحقُّ من الباطل والهدى من الضلال؛ لم يبقَ للجدال والمنازعة محلٌّ؛ لأنَّ المقصود من الجدال إنَّما هو بيانُ الحقِّ من الباطل؛ ليهتدي الراشدُ، ولتقومَ الحجةُ على الغاوي. وليس المرادُ بهذا أنَّ أهلَ الكتاب لا يجادَلون، كيف والله يقولُ: {ولا تجادِلوا أهلَ الكتابِ إلاَّ بالتي هي أحسنُ}؟! وإنَّما المرادُ ما ذكرنا. {الله يجمعُ بينَنا وإليه المصير}: يوم القيامةِ، فيجزي كلاًّ بعملِهِ، ويتبيَّن حينئذٍ الصادق من الكاذب.
{15} "Basi kwa haya waite!" Yaani, kwa ajili ya Dini iliyo madhubuti, na njia iliyonyooka, ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha kwayo vitabu vyake, na akawatuma Mitume wake. Basi waite umma wako kwa hiyo, na wahimize kwayo, na pambana kwa ajili yake wale wasioikubali. "Nawe simama sawa sawa" mwenyewe "kama ulivyoamrishwa" kwa kuafikiana na amri ya Mwenyezi Mungu; si kwa kupitisha kiwango wala kupuuza, bali kwa kutekeleza sawasawa amri za Mwenyezi Mungu na kuepuka makatazo yake kwa kuendelea daima. Hapa, alimuamuru ajikamilishe mwenyewe kwa kushikamana suala la kusimama sawasawa, na pia akamuamrisha kuwakamilisha wengine kwa kuwalingania kwenye hilo. Na inajulikana vyema kwamba anapoamrishwa Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – basi hiyo pia inakuwa ni amri kwa umma wake ikiwa amri hiyo haikukusudiwa yeye hasa. "Wala usiyafuate matamanio yao." Yaani, matamanio ya wale wanaokengeuka mbali na dini, kama vile makafiri na wanafiki. Ima kwa kuwafuata katika baadhi ya mambo ya dini yao, au kwa kuacha kulingania kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuacha kusimama sawasawa. Kwani, kama utayafuata matamanio yao baada ya kukufikia elimu, hakika hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. Hapa, hakusema kwamba usifuate dini yao. Kwa sababu uhakika wa Dini yao aliyowawekea Mwenyezi Mungu ni Dini ya Mitume wote, lakini hawakuifuata. Bali walifuata matamanio yao na wakaifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo. "Na sema" uwaambie unapojadiliana nao "'Ninaamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu;'" na majadiliano yako yajengeke juu ya msingi huu mkubwa unayoashiria heshima ya Uislamu, utukufu wake na ushindi wake dini zote, na kwamba dini wanayodai Watu wa Kitabu kuwa wako ndani yake ni sehemu ya Uislamu. Katika hili kuna maelekezo kwamba ikiwa Watu wa Kitabu watafanya majada kwa hoja ya kuamini baadhi ya vitabu au baadhi ya Mitume peke yao, basi hilo halikubaliwi kutoka kwao. Kwa sababu Kitabu wanachokiitia na Mtume wanayemjinasibisha naye ni sharti kwake kwamba awe anaisadiki Qur-ani hii na yule aliyekuja nayo. Kitabu chetu na Mtume wetu hakutuamrisha isipokuwa kuamini Musa, na Isa, na Taurati, na Injili ambavyo kilituambia juu yake, na kikavisadiki, na kikajulisha kwamba hivyo vinakisadikisha na kukubali usahihi wake. Na ama Taurati tu, na Injili, na Musa na Isa, ambavyo hatukuelezwa sifa zake na wala havikukubaliana na kitabu chetu, hivyo hakutuamrishwa kuviamini. Na kauli yake: "Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu" ninapohukumu katika yale mliyohitalifiana ndani yake. Kwa hivyo, sifai kuzuiwa na uadui wenu na chuki yenu, enyi Watu wa Kitabu, kuwa mwadilifu baina yenu. Na kufanya uadilifu katika kuhukumu baina ya Watu wa Kitabu na watu wengine waliohitilafiana ni kukubali yale waliyo nayo ya haki na kuyakataa waliyo nayo ya batili. "Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi." Yaani, Yeye ndiye Mola Mlezi wetu sote, nanyi hamumstahiki zaidi kutuliko sisi. "Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu," vya heri na vya shari. "Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi." Yaani, baada ya uhakika kubainika na hali kuwa wazi mbali na batili, na uwongofu mbali na upotofu, basi hakuna nafasi yoyote iliyobakia ya mjadala na mabishano. Kwa sababu, makusudio ya mjadala ni kubainisha haki mbali na batili ili mwenye kutaka usawa apate kuongoka, na ili hoja isimame juu ya mpotevu. Lakini, maana yake si kwamba hairuhusiwi kujadiliana na Watu wa Kitabu. Vipi isiruhusiwe ilhali Mwenyezi Mungu anasema: "Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa." Lakini kinachokusudiwa ni kile tulichotaja. "Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake." Siku ya Kiyama, na atamlipa kila mmoja kwa matendo yake, na hapo atabainika mkweli kutokana na mwongo.
: 16 #
{وَالَّذِينَ يُحَاجُّونَ فِي اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مَا اسْتُجِيبَ لَهُ حُجَّتُهُمْ دَاحِضَةٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ (16)}.
16. Na wale wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa, hoja za hawa ni batili mbele ya Mola wao Mlezi, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao adhabu kali.
#
{16} وهذا تقريرٌ لقوله: {لا حجَّة بيننا وبينكم}؛ فأخبر هنا أنَّ {الذين يحاجُّون في الله}: بالحجج الباطلة والشُّبه المتناقضة {من بعد ما استُجيبَ}: للَّه؛ أي: من بعد ما استجاب لله أولو الألباب والعقول لما بيَّن لهم من الآيات القاطعة والبراهين الساطعة؛ فهؤلاء المجادلون للحقِّ من بعدما تبيَّن {حجَّتُهم داحضةٌ}؛ أي: باطلةٌ مدفوعةٌ {عند ربِّهم}؛ لأنَّها مشتملةٌ على ردِّ الحقِّ، وكلُّ ما خالف الحقَّ؛ فهو باطلٌ، {وعَلَيهم غَضَبٌ}: بعصيانهم وإعراضهم عن حجج الله وبيناته وتكذيبها، {ولهم عذابٌ شديدٌ}: هو أثر غضبِ الله عليهم؛ فهذه عقوبة كلِّ مجادل للحقِّ بالباطل.
{16} Huku ni kuthibitisha kauli yake: "Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi." Na hapa akajulisha kwamba, "Na wale wanaohojiana juu ya Mwenyezi Mungu" kwa hoja batili na fikira potofu zenye kupingana "baada ya kukubaliwa," yaani baada ya wale wenye akili na ufahamu mkubwa kumwitikia Mwenyezi Mungu kwa sababu ya yale aliyowabainishia ya Aya za uhakika na hoja zilizo wazi; basi hawa wanaobishana na haki baada ya kudhihirika kwake, "hoja za hawa ni batili mbele ya Mola wao Mlezi." Kwa sababu inajumuisha kuikataa haki, na kila kitu kinachopinga haki ni batili, "na juu yao ipo ghadhabu" kwa sababu ya uasi wao na kuzipa kwao mgongo hoja za Mwenyezi Mungu na ishara zilizo wazi na kuzikadhibisha kwao. "Na itakuwa kwao adhabu kali," kwa sababu ndiyo athari ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu juu yao. Basi hii ni adhabu ya kila anayebishana na haki kwa ajili ya batili.
: 17 - 18 #
{اللَّهُ الَّذِي أَنْزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ قَرِيبٌ (17) يَسْتَعْجِلُ بِهَا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا وَالَّذِينَ آمَنُوا مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا الْحَقُّ أَلَا إِنَّ الَّذِينَ يُمَارُونَ فِي السَّاعَةِ لَفِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ (18)}.
17. Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani. Na ni nini kitakachokujulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu? 18. Wale wasioiamini huihimiza hiyo Saa ifike upesi, lakini wale wanaoamini wanaiogopa na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanaobishana katika habari za hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa.
#
{17} لما ذكر تعالى أنَّ حججه واضحةٌ بينةٌ بحيث استجاب لها كلُّ مَن فيه خيرٌ؛ ذكر أصلَها وقاعدتَها، بل جميع الحجج التي أوصلها إلى العباد ترجِعُ إليه، فقال: {الله الذي أنزل الكتابَ بالحقِّ والميزانِ}: فالكتاب هو هذا القرآنُ العظيم الذي نزل بالحقِّ، واشتمل على الحقِّ والصدق واليقين، وكلُّه آياتٌ بيناتٌ وأدلَّة واضحاتٌ على جميع المطالب الإلهيَّة والعقائد الدينيَّة، فجاء بأحسن المسائل وأوضح الدَّلائل. وأما الميزان؛ فهو العدل والاعتبار بالقياس الصحيح والعقل الرجيح؛ فكلُّ الدلائل العقليَّة من الآيات الأفقيَّة والنفسيَّة والاعتبارات الشرعيَّة والمناسبات والعلل والأحكام والحِكَم داخلةٌ في الميزان الذي أنزله الله تعالى ووضعه بين عبادِهِ لِيَزِنوا به ما أثبته وما نفاه من الأمور، ويعرفوا به صدقَ ما أخبر به وأخبرتْ به رسلُه. فما خرج عن هذين الأمرين ـ عن الكتاب والميزان ـ مما قيل: إنَّه حجةٌ أو برهانٌ أو دليلٌ أو نحو ذلك من العبارات؛ فإنَّه باطلٌ متناقضٌ قد فسدت أصولُه وانهدمت مبانيه وفروعه، يعرِفُ ذلك مَنْ خَبَرَ المسائل ومآخِذَها، وعرف التمييز بين راجح الأدلَّة من مرجوحِها، والفرق بين الحجج والشُّبه. وأما من اغترَّ بالعبارات المزخرفة والألفاظ المموِّهة ولم تنفذْ بصيرتُه إلى المعنى المراد؛ فإنَّه ليس من أهل هذا الشأن، ولا من فرسانِ هذا الميدانِ؛ فوِفاقه وخلافُه سيان. ثم قال تعالى مخوِّفاً للمستعجلين لقيام الساعةِ المنكرينَ لها، فقال: {وما يدريكَ لعلَّ الساعةَ قريبٌ}؛ أي: ليس بمعلوم بُعدها ولا متى تقومُ؛ فهي في كلِّ وقتٍ متوقَّع وقوعُها مخوفٌ وجبتُها.
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa hoja zake ziko wazi na zimeshabainika, kiasi kwamba kila aliye na heri ndani yake aliziitikia, akataja asili yake na msingi wake, bali hoja zote alizozifikisha kwa waja zinarejea kwake. Akasema: "Mwenyezi Mungu ndiye aliyeteremsha Kitabu kwa Haki na Mizani." Kwa hivyo, kitabu ni Qur-ani tukufu ambayo iliteremka kwa haki, na inajumuisha haki, ukweli na yakini. Na yote ni aya zilizo wazi na ushahidi wa wazi wa matakwa ya Mwenyezi Mungu na itikadi zote za kidini. Kwa hivyo, ikawa imekuja na masuala bora zaidi na ushahidi ulio wazi zaidi. Na ama mizani hiyo ni uadilifu na kupima kwa mujibu wa mlinganisho sahihi na akili iliyo sawa. Kwani ushahidi wote wa kiakili, kama vile ishara za kiupeo wa macho na za kinafsi, mazingatio ya kisheria, matukio mbalimbali, sababu mbalimbali, hukumu mbalimbali na hekima, vyote vinajumuishwa katika mizani ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiteremsha na akaiweka miongoni mwa waja wake ili wapime kwayo aliyoyathibitisha na aliyoyakanusha miongoni mwa mambo, na ili kwayo wajue ukweli wa yale aliyojulisha na yale ambayo Mitume wake walijulisha. Kwa hivyo, lolote linalotoka nje ya mawili haya - Kitabu na mizani - miongoni mwa yote yaliyosemwa kwamba ni hoja, au uthibitisho au ushahidi au maneno yanayofanana na hayo, hayo ni batili yanayopingana, ambayo misingi yake ilikwisha haribika na mijengo yake na matawi yake yakabomoka. Hayo anayajua mwenye kuyachunguza vyema masuala mbalimbali na namna yanavyochukuliwa, na akajua kutofautisha kati ya hoja iliyo sahihi zaidi kuliko hoja zinginezo, na tofauti iliyoko kati ya hoja na fikira potofu tu. Na ama yule ambaye amedanganyika na maneno yaliyopambwa na maneno yaliyofichwa ukweli wake na ufahamu wake haukupenya ukafika kwenye maana iliyokusudiwa, basi yeye hakika si katika wanasanaa hii, wala si katika mashujaa wa uwanja huu. Kukubaliana kwake na kutokubali kwake ni sawa. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, akiwatia hofu wale wanaotaka Saa ya Kiyama kufika haraka ambao wanaikataa: "Na ni nini kitakachokujulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu?" Yaani, haujulikani umbali wake wala itatokea lini. Inatarajiwa na kuhofiwa kutokea wakati wowote ule.
#
{18} {يستعجل بها الذين لا يؤمنون بها}: عناداً وتكذيباً وتعجيزاً لربِّهم، {والذين آمنوا مشفِقونَ منها}؛ أي: خائفون؛ لإيمانهم بها، وعلمهم بما تشتمل عليه من الجزاء بالأعمال، وخوفهم لمعرفتهم بربِّهم أنْ لا تكون أعمالُهم منجيةً [لهم] ولا مسعدةً، ولهذا قال: {ويعلمون أنَّها الحقُّ}: الذي لامِرْيَةَ فيه، ولا شكَّ يعتريه. {ألا إنَّ الذين يُمارونَ في الساعةِ}؛ أي: بعدما امتروا فيها، ماروا الرسل وأتباعهم بإثباتها؛ فهم في شقاق {بعيدٍ}؛ أي: معاندةٌ ومخاصمةٌ غير قريبة من الصواب، بل في غاية البعد عن الحق. وأيُّ بعد أبعد ممَّن كذَّب بالدار التي هي الدار على الحقيقة؟ وهي الدار التي خُلِقَتْ للبقاء الدائم والخلود السرمد، وهي دارُ الجزاء التي يُظْهِرُ الله فيها عدلَه وفضلَه، وإنَّما هذه الدار بالنسبة إليها كراكبٍ قال في ظلِّ شجرةٍ ثم رَحَلَ وتركَها، وهي دار عبورٍ وممرٍّ لا محلُّ استقرارٍ، فصدقوا في الدار المضمحلَّة الفانية حيث رأوها وشاهدوها، وكذَّبوا بالدار الآخرة التي تواترت بالأخبار عنها الكتب الإلهية والرسل الكرام وأتباعهم، الذين هم أكمل الخلقِ عقولاً وأغزرُهم علماً وأعظمُهم فطنةً وفهماً.
{18} "Wale wasioiamini hutaka hiyo Saa ifike upesi" kwa sababu ya ukaidi, kuikadhibisha na kutaka kumuonyesha Mola wao Mlezi kwamba hawezi kitu. "Lakini wale wanaoamini wanaiogopa" kwa sababu ya kuiamini kwao na kujua kwao yale yaliyo ndani yake ya malipo kwa matendo, na hofu yao kwa kumjua kwao Mola wao Mlezi, kwamba huenda matendo yao hayatawaokoa wala kuwaletea furaha. Ndiyo maana akasema: "na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli" isiyo na shaka yoyote. "Ama kwa hakika hao wanaobishana katika habari za hiyo Saa." Baada ya kuwa na shaka nayo, wakashindana na Mitume na wafuasi wao. Wao wamo katika upotofu "wa mbali kabisa" ambao hauko karibu na haki. Kwani ni umbali gani ulio mbali zaidi kuliko yule anayeikadhibisha nyumba ambayo ndiyo nyumba kwa hakika? Nayo ndiyo nyumba ambayo aliumbwa kwa ajili ya kuendelea kuwepo na kudumu milele. Nayo ndiyo nyumba ya malipo ambayo Mwenyezi Mungu alitadhihirishia huko uadilifu wake na fadhila yake. Na hakika nyumba hii kwa kulinganishwa na ile ya akhera ni kama mtu aliyepanda kipando, kisha akalala kidogo katika kivuli cha mti, kisha akaondoka na akauacha. Nayo ni nyumba ya kupita, na si nyumba ya kutua humo. Basi wakaisadiki nyumba inayofifia na kuisha kwa kuiona na kuishuhudia, na wakakadhibisha nyumba ya akhera ambayo vilisimulia habari nyingi sana kuhusiana nayo vitabu vya Mwenyezi Mungu, Mitume wake watukufu na wafuasi wao ambao ndio wenye akili kamili zaidi ya viumbe wote, na wenye elimu nyingi zaidi, na wakubwa wao zaidi katika werevu na ufahamu.
: 19 - 20 #
{اللَّهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ (19) مَنْ كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ وَمَنْ كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ نَصِيبٍ (20)}.
19. Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu. 20. Mwenye kutaka mavuno ya Akhera, tutamzidishia katika mavuno yake. Na mwenye kutaka mavuno ya duniani, tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu lolote.
#
{19} يخبر تعالى بلطفه بعبادِهِ: ليعرفوه ويحبُّوه ويتعرَّضوا للطفه وكرمه، واللُّطف من أوصافه تعالى معناه: الذي يدرِكُ الضمائر والسرائر، الذي يوصِلُ عباده ـ وخصوصاً المؤمنين ـ إلى ما فيه الخيرُ لهم من حيثُ لا يعلمون ولا يحتسبون. فمن لطفِهِ بعبدِهِ المؤمن أنْ هداه إلى الخير هدايةً لا تخطُرُ ببالِهِ بما يسَّر له من الأسباب الدَّاعية له إلى ذلك من فطرته على محبَّة الحقِّ والانقياد له وإيزاعه تعالى لملائكتِهِ الكرام أن يُثَبِّتوا عبادَهُ المؤمنين ويحثُّوهم على الخير ويُلْقوا في قلوبهم من تزيين الحقِّ ما يكون داعياً لاتِّباعه. ومن لطفِهِ أن أمر المؤمنين بالعباداتِ الاجتماعية التي بها تقوى عزائِمُهُم وتنبعثُ هِمَمُهم ويحصُلُ منهم التنافس على الخير والرغبة فيه واقتداء بعضهم ببعض. ومن لطفِهِ أن قَيَّضَ كلَّ سبب يعوقُه ويحولُ بينه وبين المعاصي، حتى إنَّه تعالى إذا علم أنَّ الدُّنيا والمال والرياسة ونحوها مما يتنافس فيه أهلُ الدُّنيا تقطعُ عبدَه عن طاعتِهِ أو تحمِلُه على الغفلة عنه أو على معصيتِهِ؛ صرفها عنه، وقَدَرَ عليه رِزْقَه، ولهذا قال هنا: {يرزُقُ مَن يشاءُ}: بحسب اقتضاء حكمته ولطفه، {وهو القويُّ العزيزُ}: الذي له القوَّة كلُّها؛ فلا حول ولا قوة لأحدٍ من المخلوقين إلاَّ به، الذي دانت له جميع الأشياء.
{19} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya upole wake kwa waja wake ili wamjue, wampende na wautafute upole wake huo na ukarimu wake. Na upole ni miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambao maana yake pia ni Mwenye kuzifahamu zaidi dhamira na siri, ambaye huwafikisha waja wake - haswa Waumini - kwenye yale yanayowafaa kwa namna wasiyoijua wala wasiyoitarajia. Basi katika upole wake kwa mja wake muumini ni kwamba alimuongoza kwenye heri kwa njia ambayo hakumtarajia kwa yale aliyomsahilishia ya sababu ambazo zinamhimiza kufanya hivyo kwa kumtia maumbile ya kupenda haki na kuifuata, na Mwenyezi Mungu kuwaamrisha Malaika wake watukufu kuwatia nguvu waja wake waumini, kuwahimiza kutenda mema na kuweka katika nyoyo zao sifa ya kuipamba haki ili kuwahimiza kuifuata. Na katika upole wake ni kwamba aliwaamrisha Waumini kufanya ibada za kimkusanyiko ambazo kwazo azimio zao zinaimarishwa, hima zao zinakakamishwa na wanahimizwa kushindana katika wema, kuutamani, na kuigana wao kwa wao. Na katika upole wake ni kwamba aliondoa kila sababu inayomzuia kutenda maasi, kiasi kwamba Yeye Mtukufu anapojua kwamba dunia, mali, uongozi na mengineyo katika vitu ambavyo watu wa dunia wanashindana juu yake vitamzuia mja wake kumtii au vitamfanya kughafilika au kumuasi, anamuondolea hivyo na kumkunjia riziki yake, na ndiyo maana akasema hapa: "Humruzuku amtakaye" kulingana na hekima yake na upole wake. "Naye ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu." Ambaye ana uwezo wote, na hakuna uwezo wala nguvu kwa yeyote yule miongoni mwa viumbe isipokuwa kwa Yeye, ambaye vitu vyote viko chini yake.
#
{20} ثم قال تعالى: {من كان يريدُ حَرْثَ الآخرةِ}؛ أي: أجرها وثوابَها، فآمن بها وصدَّق وسعى لها سعيها، {نَزِدْ له في حرثِهِ}: بأن نضاعِف عمله وجزاءه أضعافاً كثيرة؛ كما قال تعالى: {ومَنْ أراد الآخرةَ وسعى لها سَعْيَها وهو مؤمنٌ فأولئكَ كان سَعْيُهُمْ مَشْكوراً}، ومع ذلك؛ فنصيبه من الدُّنيا لا بدَّ أن يأتِيَهُ، {ومَن كانَ يريدُ حَرْثَ الدُّنيا}: بأن كانت الدُّنيا هي مقصودَه وغايةَ مطلوبِهِ، فلم يقدِّم لآخرته، ولا رجا ثوابَها، ولم يخشَ عقابَها، {نؤتِهِ منها}: نصيبَه الذي قُسِمَ له، {وما له في الآخرةِ من نصيبٍ}: قد حُرِم الجنَّة ونعيمها، واستحقَّ النار وجحيمها. وهذه الآيةُ شبيهةٌ بقوله تعالى: {مَن كان يريدُ الحياةَ الدُّنيا وزينَتَها نوفِّ إليهم أعمالَهم فيها وهم فيها لا يُبْخَسونَ ... } إلى آخر الآيات.
{20} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Mwenye kutaka mavuno ya Akhera," basi akaimini na akaisadiki, na akaifanyia bidii kwa matendo yanayoifailia, "tutamzidishia katika mavuno yake" kwa kumzidishia matendo yake na malipo yake mazidisho mingi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na anayeitaka Akhera na akazifanyia juhudi amali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa." Na pamoja na hayo, fungu lake la duniani lazima litamjia. "Na mwenye kutaka mavuno ya duniani" kwa kuifanya ikiwa dunia ndio makusudio na lengo lake, na wala hakuitangulizia chochote akhera yake wala hakutarajii malipo yake, wala hakuhofu adhabu yake. Basi "tutampa katika hayo" fungu lake alilowekewa, "lakini katika Akhera hana fungu lolote." Atanyimwa Bustani ya mbinguni na neema zake, na atastahiki Jahannamu na moto wake. Aya hii ni sawa na kauli yake Mola Mtukufu: "Wanaotaka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kamili. Na wao humo hawatopunjwa." Hadi mwisho wa aya hizi.
: 21 - 23 #
{أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُمْ مِنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَنْ بِهِ اللَّهُ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (21) تَرَى الظَّالِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا كَسَبُوا وَهُوَ وَاقِعٌ بِهِمْ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي رَوْضَاتِ الْجَنَّاتِ لَهُمْ مَا يَشَاءُونَ عِنْدَ رَبِّهِمْ ذَلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ (22) ذَلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ قُلْ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَى وَمَنْ يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ شَكُورٌ (23)}.
21. Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu? Na lau lisingekuweko neno la kupambanua, basi wangelikatiwa hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu. 22. Utawaona hao madhalimu wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma, nayo yatawafika tu. Na wale walioamini na wakatenda mema watakuwemo katika mabustani ya Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao Mlezi. Hiyo ndiyo fadhila kubwa. 23. Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema. Sema: 'Sikuombeni malipo yoyote juu yake ila mapenzi katika kujikurubisha. Na anayefanya wema, tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu mno, Mwenye shukrani sana.'
#
{21} يخبر تعالى أنَّ المشركين اتَّخذوا شركاء يوالونهم ويشتركون هم وإيَّاهم في الكفر وأعمالِهِ من شياطين الإنس الدُّعاة إلى الكفر، {شَرَعوا لهم من الدِّينِ ما لمْ يأذَنْ به اللهُ}: من الشِّرك والبدع وتحريم ما أحلَّ اللهُ وتحليل ما حرَّم اللهُ ونحو ذلك ممَّا اقتضته أهواؤُهم، مع أنَّ الدِّين لا يكون إلاَّ ما شَرَعَه الله تعالى لِيَدينَ به العبادُ ويتقرَّبوا به إليه؛ فالأصلُ الحَجْرُ على كلِّ أحدٍ أن يَشْرَعَ شيئاً ما جاء عن اللهِ وعن رسولِهِ؛ فكيف بهؤلاء الفَسَقَةِ المشتركين هم [وآباؤهم] وهم على الكفر. {ولولا كلمةُ الفصل لَقُضِيَ بينَهم}؛ أي: لولا الأجلُ المسمَّى الذي ضَرَبَه الله فاصلاً بين الطوائفِ المختلفة، وأنَّه سيؤخِّرهم إليه؛ لَقُضِي بينهم في الوقت الحاضر بسعادة المحقِّ وإهلاك المبطل؛ لأن المُقتضي للإهلاك موجود، ولكنْ أمامهم العذابُ الأليمُ في الآخرة؛ هؤلاء وكلُّ ظالم.
{21} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa washirikina wamewachukua washirika ambao wanawafanya kuwa vipenzi na ambao wanashirikiana nao katika ukafiri na matendo yake. Nao ni kutoka miongoni mwa mashetani wa kibinadamu wanaolingania katika ukafiri, "waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu?" Kama vile kufanya ushirikina na uzushi, na kuharamisha aliyohalalisha Mwenyezi Mungu, na kuhalalisha aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, na mambo mengineyo yaliyoyatakwa na matamanio yao, licha ya kwamba Dini sahihi si chochote ila yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwawekea waja wake kama sheria ili waifuate na kujiweka kwayo karibu na Yeye. Kanuni ya msingi ni kwamba kila mtu amekatazwa kutungia kitu sheria ambayo haikutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi vipi kuhusu hawa watu waovu, ambao wanashiriki [wao na baba zao] katika ukafiri? "Na lau lisingekuweko neno la kupambanua, basi wangelikatiwa hukumu baina yao." Yaani, lau kuwa si muda maalumu aliouweka Mwenyezi Mungu wa kufarakisha baina ya makundi mbali mbali, na kwamba atawachelewesha hadi waufikie, basi wangelikatiwa hukumu baina yao wakati huu kwa kumfikishia furaha yule aliye katika haki, na kumuangamiza mwana batili, kwa kuwa sababu ya kuwaangamiza tayari imeshapatikana. Lakini mbele yao kuna adhabu chungu katika Akhera, hawa na kila dhalimu.
#
{22} وفي ذلك اليوم {ترى الظالمين}: أنفسَهم بالكفرِ والمعاصي، {مشفقينَ}؛ أي: خائفين وجلين، {مما كَسَبَوا}: أن يعاقَبوا عليه، ولمَّا كان الخائفُ قد يقعُ به ما أشفق منه وخافه وقد لا يقعُ؛ أخبر أنَّه {واقعٌ بهم}: العقابُ الذي خافوه؛ لأنَّهم أتوا بالسبب التامِّ الموجب للعقاب من غير معارض من توبةٍ ولا غيرِها، ووصلوا موضعاً فات فيه الإنظارُ والإمهالُ. {والذين آمنوا} بقلوبهم بالله وبكتبِهِ ورسلِهِ وما جاؤوا به، {وعملوا الصالحات}: يشمَلُ فيه كلَّ عمل صالح من أعمال القلوب وأعمال الجوارح من الواجباتِ والمستحبَّات؛ فهؤلاء {في روضاتِ الجناتِ}؛ أي: الرَّوضات المضافة إلى الجنَّات، والمضاف يكون بحسب المضاف إليه؛ فلا تسألْ عن بهجةِ تلك الرياض المونقةِ، وما فيها من الأنهار المتدفِّقة، والفياض المُعْشِبة، والمناظر الحسنة، والأشجار المثمرة، والطيورِ المغرِّدة، والأصوات الشجيَّة المطرِبة، والاجتماع بكلِّ حبيب، والأخذ من المعاشرةِ والمنادمةِ بأكمل نصيب؛ رياض لا تزداد على طول المدى إلاَّ حسناً وبهاءً، ولا يزدادُ أهلُها إلاَّ اشتياقاً إلى لَذَّاتِها ووداداً. {لهم ما يشاؤونَ}: فيها؛ أي: في الجنات؛ فمهما أرادوا؛ فهو حاصل، ومهما طلبوا؛ حصل، مما لا عينٌ رأتْ، ولا أذنٌ سمعتْ، ولا خطرَ على قلبِ بشرٍ. ذلك {الفضلُ الكبيرُ}: وهل فوز أكبرُ من الفوز برضا الله تعالى والتنعُّم بقربِهِ في دار كرامته؟!
{22} Na siku hiyo "utawaona hao madhalimu" waliojidhulumu wenyewe kwa ukafiri na maasia "wanavyokuwa na hofu kwa sababu ya waliyoyachuma," kwamba wataadhibiwa juu yake. Na kwa vile mwenye hofu huenda yakampata yale anayoyahofu na huenda yasimpate, akajulisha juu ya hilo, akasema: "nayo yatawafika tu" kwa sababu walitenda visababu kamili vinavyolazimu waadhibiwe bila pingamizi lolote, kama vile toba au kitu kingine chochote, na wakafika mahali ambapo haiwezekani kupewa muhula. "Na wale walioamini" kwa nyoyo Mwenyezi Mungu, Vitabu vyake, Mitume wake na yale waliyokuja nayo "na wakatenda mema," ikijumuisha kila kitendo chema miongoni mwa matendo ya nyoyo na matendo ya viungo miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yanayopendekezwa, basi hawa "watakuwemo katika mabustani ya Peponi." Na usiulize juu ya uzuri wa bustani hizo nzuri sana na mito yake inayotiririka, miti mirefu inayofurika, mandhari mazuri, miti yenye matunda, ndege waimbao kwa sauti nzuri za kuimba, kukutana na kila mpendwa na kuchukua sehemu kamili ya urafiki na wendani, bustani ambazo haziongezeki muda huo wote isipokuwa uzuri na urembo, na wakazi wake hawaongezeki isipokuwa hamu kubwa juu ya starehe zake na upendo. "Humo watapata wayatakayo" miongoni mwa mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia, wala hata hayajawahi kufikiriwa na moyo wa mwanadamu yeyote. "Hiyo ndiyo fadhila kubwa." Kwani je, kuna ushindi mkubwa zaidi kuliko kupata radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufurahia kuwa karibu naye katika nyumba ya utukufu wake?
#
{23} {ذلك الذي يبشِّر الله به عبادَه الذين آمنوا وعمِلوا الصالحاتِ}؛ أي: هذه البشارة العظيمة التي هي أكبرُ البشائر على الإطلاق بَشَّرَ بها الرحيم الرحمن على يد أفضل خلقه لأهل الإيمان والعمل الصالح؛ فهي أجلُّ الغايات، والوسيلةُ الموصلةُ إليها أفضلُ الوسائل، {قل لا أسألُكُم عليه}؛ أي: على تبليغي إيَّاكم هذا القرآن ودعوتكم إلى أحكامه {أجراً}؛ فلستُ أريدُ أخذَ أموالكم ولا التولِّي عليكم والترأس ولا غير ذلك من الأغراض {إلاَّ المودَّةَ في القُربى}. يُحتمل أنَّ المراد: لا أسألُكُم عليه أجراً؛ إلاَّ أجراً واحداً، هو لكم، وعائدٌ نفعُه إليكم، وهو أن تَوَدُّوني وتحبُّوني في القرابة؛ أي: لأجل القرابة، ويكون على هذا المودَّة الزائدة على مودَّة الإيمان؛ فإنَّ مودَّة الإيمان بالرسول وتقديم محبَّته على جميع المحابِّ بعد محبَّة الله فرضٌ على كلِّ مسلم، وهؤلاء طَلَبَ منهم زيادةً على ذلك أن يحبُّوه لأجل القرابِةِ؛ لأنَّه - صلى الله عليه وسلم - قد باشر بدعوته أقربَ الناس إليه، حتى إنَّه قيل: إنَّه ليس في بطون قريش أحدٌ إلاَّ ولرسول اللهِ - صلى الله عليه وسلم - فيه قرابةٌ. ويُحتملُ أنَّ المرادَ: إلاَّ مودة الله تعالى المودة الصادقة، وهي التي يصحبُها التقرُّب إلى الله والتوسُّل بطاعته الدالَّة على صحَّتها وصدقها، ولهذا قال: {إلاَّ المودَّة في القربى}؛ أي: في التقرُّب إلى الله. وعلى كلا القولين؛ فهذا الاستثناءُ دليلٌ على أنَّه لا يسألكم عليه أجراً بالكلِّيَّة؛ إلاَّ أن يكون شيئاً يعود نفعُه إليهم؛ فهذا ليس من الأجر في شيء، بل هو من الأجر منه لهم - صلى الله عليه وسلم -؛ كقوله تعالى: {وما نَقَموا منهم إلاَّ أن يؤمِنوا بالله العزيزِ الحميدِ}، وقولهم: ما لفلان عندك ذنبٌ إلاَّ أنَّه محسنٌ إليك. {ومَن يَقْتَرِفْ حسنةً}: من صلاةٍ أو صوم أو حجٍّ أو إحسانٍ إلى الخلق، {نَزِدْ له فيها حُسْناً}: بأن يشرحَ الله صدرَه وييسِّر أمره ويكون سبباً للتوفيق لعمل آخر، ويزدادَ بها عملُ المؤمن ويرتفعَ عند الله وعند خلقِهِ، ويحصُلَ له الثوابُ العاجل والآجل. {إنَّ الله غفورٌ شكورٌ}: يغفر الذنوبَ العظيمةَ، ولو بلغتْ ما بلغتْ عند التوبة منها، ويشكر على العمل القليل بالأجرِ الكثيرِ؛ فبمغفرتِهِ يغفرُ الذنوبَ ويستُر العيوبَ، وبشكرِهِ يتقبَّل الحسناتِ ويضاعِفُها أضعافاً كثيرةً.
{23} "Hayo ndiyo aliyowabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walioamini na wakatenda mema." Bishara hii kubwa ambayo ndiyo bishara kubwa zaidi kuliko zote, aliibashiria Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa rehema, kupitia mikono ya mbora zaidi wa viumbe wake kwa watu wenye imani na matendo mema. Hayo ndiyo malengo makubwa zaidi na njia bora zaidi inayofikisha kwayo. "Sema: 'Siwaombi malipo yoyote juu yake;" yaani, juu ya kuwafikishia hii Qur-ani na kuwaita katika hukumu zake. Sitaki kuchukua mali zenu, wala kuwatawala na kujipa uongozi juu yenu, wala madhumuni mengineyo yoyote, "ila mapenzi katika kujikurubisha." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni: Sikuombeni malipo yoyote juu yake, isipokuwa malipo ya aina moja, ambayo ni yenu na yatakunufaisheni, nayo ni kwamba mnipende mimi kama jamaa wenu. Basi mapenzi haya yanakuwa yameongezeka juu ya yale mapenzi ya kwa ajili ya imani. Kwani mapenzi ya imani kwa Mtume na kutanguliza mapenzi yake juu ya vyote vingine vinavyopendwa baada ya kumpenda Mwenyezi Mungu ni wajibu kwa kila Muislamu, na pamoja na hayo, aliwataka hawa wampende pia kwa ajili ya ujamaa. Kwa sababu yeye Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alilingania katika wito wake watu walio karibu naye zaidi, hadi ikasemwa kwamba hakuna katika makabila ya Maquraish isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ana ujamaa na wao. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni mapenzi ya dhati kwa Mwenyezi Mungu, ambayo yanaambatana na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kumfikia kwa njia ya kuwa mtiifu kwake, ambayo inaashiria usahihi wake na ukweli wake, na ndiyo maana akasema, "ila mapenzi katika kujikurubisha" kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kulingana na kauli zote mbili, jambo hili alilolivua ni ushahidi kwamba yeye hakuombeni kabisa malipo yoyote juu yake, isipokuwa kama ni kitu kinachowanufaisha wao wenyewe; ambacho si malipo hata kidogo kwake, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa," na kama wanavyosema: 'Fulani hana dhambi kwako ila kwa kuwa anakufanyia wema.' "Na anayefanya wema," kama vile Swala, Saumu, Hija, au kuwafanyia viumbe wema, "tutamzidishia wema" kwa namna kwamba Mwenyezi Mungu atakipanua kifua chake na amsahilishie mambo yake, na awe ni sababu ya kumuwezesha matendo mengineyo mema, na kwa sababu ya hayo, yanazidi matendo ya Muumini na ananyanyuka juu kwao mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya viumbe vyake, na anapata malipo ya sasa na ya baadaye. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu mno, Mwenye shukrani sana." Anasamehe madhambi makubwa, hata yakiwa makubwa kiasi gani, pindi mja anapotubia akayaacha. Na anashukuru kwa matendo machache kwa kupeana ujira mwingi. Basi kwa msamaha wake, Yeye husamehe dhambi na hufunika kasoro za waja. Na kwa shukurani Yake, anakubali matendo mema na kuyazidisha mizidisho mingi.
: 24 #
{أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا فَإِنْ يَشَإِ اللَّهُ يَخْتِمْ عَلَى قَلْبِكَ وَيَمْحُ اللَّهُ الْبَاطِلَ وَيُحِقُّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (24)}.
24. Ati wanasema Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda ataziba moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaufuta upotofu na anaithibitisha Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani.
#
{24} يعني: أم يقولُ المكذِّبون للرسول - صلى الله عليه وسلم - جرأة منهم وكذباً: {افْتَرى على اللهِ كَذِباً}: فَرَمَوْكَ بأشنع الأمور وأقبحها، وهو الافتراءُ على الله بادِّعاء النبوَّة والنسبة إلى الله ما هو بريءٌ منه، وهم يعلمونَ صِدْقَكَ وأمانَتَكَ؛ فكيف يتجرؤونَ على هذا الكذبِ الصُّراح؟! بل تجرؤوا بذلك على الله تعالى؛ فإنَّه قدحٌ في الله؛ حيث مكَّنك من هذه الدعوة العظيمة المتضمِّنة ـ على موجب زعمهم ـ أكبر الفسادِ في الأرض؛ حيث مكَّنه الله من التَّصريح بالدَّعوة، ثم بنسبتها إليه، ثم يؤيِّده بالمعجزات الظاهرات والأدلَّة القاهرات والنصر المبين والاستيلاء على مَنْ خالَفَهُ، وهو تعالى قادرٌ على حسم هذه الدَّعوة من أصلها ومادَّتها، وهو أن يختِم على قلب الرسول - صلى الله عليه وسلم -؛ فلا يعي شيئاً، ولا يدخل إليه خيرٌ، وإذا خُتِمَ على قلبه؛ انحَسَم الأمرُ كلُّه وانقطعَ؛ فهذا دليلٌ قاطعٌ على صحَّة ما جاء به الرسولُ، وأقوى شهادة من اللهِ له على ما قال، ولا يوجُد شهادةٌ أعظم منها ولا أكبر، ولهذا من حكمته ورحمته وسنَّته الجارية أنه يمحو الباطل ويزيلُه، وإن كان له صولةٌ في بعض الأوقات؛ فإنَّ عاقبته الاضمحلال، {ويُحِقُّ الحقَّ بكلماتِهِ}: الكونيَّة التي لا تبدَّل ولا تغيَّر ، ووعده الصادق، وكلماته الدينيَّة التي تحقِّق ما شرعه من الحقِّ وتثبِّته في القلوب وتبصِّر أولي الألباب، حتى إنَّ من جملة إحقاقِهِ تعالى الحقَّ أن يقيِّضَ له الباطلَ ليقاوِمَه؛ فإذا قاومه؛ صال عليه الحقُّ ببراهينِهِ وبيِّناتِهِ، فظهر من نوره وهداه ما به يضمحلُّ الباطل وينقمع ويتبيَّن بطلانُه لكلِّ أحدٍ، ويظهر الحقُّ كلَّ الظُّهور لكلِّ أحدٍ. {إنَّه عليمٌ بذات الصُّدور}؛ أي: بما فيها وما اتَّصفت به من خيرٍ وشرٍّ وما أكنَّته ولم تُبْدِهِ.
{24} Maana yake: Au hawa wanaokadhibisha Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – wanasema kwa ujasiri na uwongo, "Ati wanasema Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo?" Hapa, wakawa wamekuzulia mambo mabaya na maovu zaidi, ambayo ni kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo kwa kudai unabii na kumdanganyishia Mwenyezi Mungu mambo ambayo hayakutoka kwake ilhali wanajua vyema ukweli wake na uaminifu wake. Basi vipi wanafanya ujasiri wa kudanganya kwa njia hii iliyowazi mno? Bali na hata walimfanyia ujasiri huu Mwenyezi Mungu pia. Kwani kwa kusema hivyo, ni kumtia dosari Mwenyezi Mungu; kwa alikuwezesha kutekeleza wito huu mkubwa unaojumuisha - kulingana na madai yao - uharibifu mkubwa katika ardhi. Kwani Mwenyezi Mungu alimuwezesha Mtume kusema wazi wazi wito huu na kuunasibisha naye, kisha akamuunga mkono kwa miujiza dhahiri na hoja zenye ushindi, nusura ya wazi na kumshinda yeyote anayemhalifu. Ilhali Yeye Mtukufu anao uwezo wa kuuvunjilia mbali wito huu kwenye mizizi yake na kiini chake. Hilo lingewezekana kwa kuziba moyo wa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, basi asielewe chochote, wala usiweze kuingiwa na heri yoyote. Na anapozibwa moyo, basi jambo hili lote linashindwa na kukatika. Basi hii ni hoja ya uhakika juu ya usahihi wa yale aliyoyaleta Mtume, na ushahidi wenye nguvu zaidi unaomuunga mkono Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya yale aliyoyasema, na hakuna ushahidi mkuu zaidi wala mkubwa zaidi kuliko huo. Ndiyo kwa sababu ya hekima yake, rehema yake na Sunna yake inayoendelea ni kwamba anaifuta batili na kuiondoa, hata kama ina nguvu katika nyakati fulani, mwisho wake utakuwa ni kupotelea mbali. "Na anaithibitisha Haki kwa maneno yake" ya kiulimwengu yasiyobadilika na yasiyogeuka, ahadi yake ya ukweli na maneno yake ya kidini ambayo yanatimiza mambo ya haki aliyoyaweka katika sheria na kuyaimarisha nyoyoni, na kuwafanya wenye ufahamu mkubwa kuona, kiasi kwamba katika jumla ya njia ambazo Yeye Mtukufu anatimiza haki ni kuiwekea batili ili ipingane nayo. Basi inapoipinga, haki inaishambulia batili hiyo kwa hoja zake na ushahidi wake wa wazi, kwa hivyo ikadhihirika kwa nuru yake na uwongofu ambao kwa hayo batili inapotelea mbali na kukatika, na ubatili wake unamdhihirikia kila mtu. Nayo haki pia inamdhihirikia kila mtu wazi wazi. "Hakika Yeye anayajua yaliyomo vifuani," ya heri na mabaya, na yanayoficha bila ya kudhihirishwa.
: 25 - 28 #
{وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ (25) وَيَسْتَجِيبُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَيَزِيدُهُمْ مِنْ فَضْلِهِ وَالْكَافِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ (26) وَلَوْ بَسَطَ اللَّهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَكِنْ يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَا يَشَاءُ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ (27) وَهُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ الْغَيْثَ مِنْ بَعْدِ مَا قَنَطُوا وَيَنْشُرُ رَحْمَتَهُ وَهُوَ الْوَلِيُّ الْحَمِيدُ (28)}.
25. Naye ndiye anayepokea toba kwa waja wake, na anasamehe mabaya, na anayajua mnayoyatenda. 26. Na anawaitikia wanaoamini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na makafiri watakuwa na adhabu chungu. 27. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangelipanda kiburi katika dunia. Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona. 28. Naye ndiye anayeiteremsha mvua baada ya wao kwisha kata tamaa, na hueneza rehema yake. Naye ndiye Mlinzi, Mwenye kusifiwa sana.
#
{25} هذا بيانٌ لكمال كرم الله تعالى وسَعَةِ جودِهِ وتمام لطفِهِ بقبول التوبةَ الصادرة {عن عبادِهِ}: حين يُقْلِعونَ عن ذُنوبهم ويندمون عليها ويعزِمون على أن لا يعاوِدوها إذا قَصَدوا بذلك وجهَ ربِّهم؛ فإنَّ الله يقبلُها بعدما انعقدتْ سبباً للهلاك ووقوع العقوباتِ الدنيويَّة والدينيَّة، فيعفو {عن السَّيِّئاتِ}: ويمحوها، ويمحو أثرها من العيوب، وما اقتضتْه من العقوباتِ، ويعودُ التائبُ عنده كريماً كأنَّه ما عمل سوءاً قطُّ، ويحبُّه ويوفِّقه لما يقرِّبه إليه. ولما كانت التوبةُ من الأعمال العظيمة التي قد تكون كاملةً بسبب تمام الإخلاص والصدق فيها، وقد تكونُ ناقصةً عند نقصِهِما، وقد تكون فاسدةً إذا كان القصدُ منها بلوغَ غَرَضٍ من الأغراض الدنيويَّة، وكان محلُّ ذلك القلبَ الذي لا يعلمه إلاَّ الله؛ ختم هذه الآية بقوله: {ويعلم ما تفعلونَ}.
{25} Haya ni maelezo ya ukamilifu wa ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, upana wa wema wake na ukamilifu wa upole wake katika kukubali toba iliyotoka "kwa waja wake" pindi wanapoacha dhambi zao, wakajuta juu yake na wakaazimia kutozirudia tena, ikiwa wataukusudia uso wa Mola wao Mlezi kwa hayo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anazikubali hata baada ya kupatikana visababu vya kuwaangamiza na kupatwa na adhabu za kidunia na za kidini. Basi anasamehe "mabaya" na anayafuta, na pia anafuta athari zake kama vile kutiwa dosari na kupatwa na adhabu ambayo ilikuwa ni lazima wapatwe nayo, kisha mwenye kutubia anarejea kutoka kwake kwa heshima kana kwamba kamwe hakuwahi kufanya ubaya wowote, na anampenda na kumuwezesha kufikia yale yanayomuweka karibu naye. Kwa kuwa toba ni miongoni mwa matendo makubwa ambayo yanaweza kuwa kamili kutokana na kukamilika ikhlasi ya mtu na ukweli wake, na huenda ikawa pungufu yanapokosekana hayo, na hata inaweza kuwa mbovu ikiwa nia yake ni kufikia moja ya malengo ya kidunia, na inajulikana vyema kwamba mahala pake ni moyoni ambapo hakuna anayeujua zaidi ya Mwenyezi Mungu peke yake, akahitimisha Aya hii kwa kusema, "na anayajua mnayoyatenda."
#
{26} فالله تعالى دعا جميع العباد إلى الإنابة إليه والتوبةِ من التقصيرِ، فانقسموا بحسب الاستجابةِ له إلى قسمين: مستجيبين، وَصَفَهم بقوله: {ويستجيبُ الذين آمنوا وعملوا الصالحاتِ}؛ أي: يستجيبون لربِّهم لما دعاهم إليه، وينقادون له، ويلبُّون دعوته؛ لأنَّ ما معهم من الإيمان والعمل الصالح يحمِلُهم على ذلك؛ فإذا استجابوا له؛ شَكَرَ الله لهم، وهو الغفورُ الشَّكور، وزادهم {من فضلِهِ}: توفيقاً ونشاطاً على العمل، وزادهم مضاعفةً في الأجر زيادةً عن ما تستحقُّه أعمالهم من الثواب والفوز العظيم. وأما غير المستجيبين لله، وهم المعاندون الذين كفروا به وبرسله؛ فلهم عذابٌ شديدٌ في الدُّنيا والآخرة.
{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaita waja wake wote warejee kwake na watubie kutokana na mapungufu yao. Basi wakagawanyika makundi mawili kulingana na mwitikio wao kwake: Wale walioitikia, na akawaelezea kwa kauli yake, "Na anawaitikia wanaoamini na wakatenda mema." Yaani, walimwitikia Mola wao Mlezi kwa yale aliyowaitia na wanafuata maelekezo yake. Kwa sababu yale waliyo nayo ya imani na matendo mema yanawasukuma kufanya hivyo. Kwa hivyo, wanapomwitikia, Yeye Mwenyezi Mungu anawashukuru, naye ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kushukuru, na anawazidishia "katika fadhila zake" mafanikio na nguvu ya kufanya matendo mema, na pia anawazidishia ujira na kufuzu kukubwa maradufu zaidi ya yale ambayo matendo yao yaliyostahiki. Na ama wale wasiomuitikia Mwenyezi Mungu, na hao ndio wakaidi waliomkufuru Yeye na Mitume wake, watapata adhabu kali duniani na Akhera.
#
{27} ثم ذكر أن من لطفِهِ بعبادِهِ أنَّه لا يوسِّع عليهم الدُّنيا سعةً تضرُّ بأديانهم، فقال: {ولو بَسَطَ الله الرزقَ لعبادِهِ لَبَغَوْا في الأرض}؛ أي: لغفلوا عن طاعة الله، وأقبلوا على التمتُّع بشهوات الدُّنيا، فأوجبت لهم الإكباب على ما تشتهيه نفوسُهم، ولو كان معصيةً وظلماً. {ولكن يُنَزِّلُ بَقَدَرٍ ما يشاءُ}: بحسب ما اقتضاه لطفُه وحكمتُه، {إنَّه بعباده خبيرٌ بصيرٌ}: كما في بعض الآثار أنَّ الله تعالى يقول: «إنَّ مِنْ عبادي من لا يُصْلِحُ إيمانَه إلاّ الغنى، ولو أفقرتُه؛ لأفسده ذلك، وإنَّ من عبادي من لا يُصْلِحُ إيمانَه إلاّ الفقرُ، ولو أغنيته؛ لأفسده ذلك، وإنَّ من عبادي من لا يُصْلِحُ إيمانَه إلاَّ الصحةُ، ولو أمرضتُه؛ لأفسده ذلك، وإنَّ من عبادي من لا يُصْلِحُ إيمانَه إلاَّ المرضُ، ولو عافيتُه؛ لأفسده ذلك، إنِّي أدبِّر أمر عبادي بعلمي بما في قلوبهم، إني خبيرٌ بصيرٌ».
{27} Kisha akataja kuwa katika upole wake kwa waja wake ni kutowapanulia mambo ya kidunia ili yasiwadhuru dini zao. Akasema, "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwakunjulia riziki waja wake, basi bila ya shaka wangelipanda kiburi katika dunia." Yaani, wangeghafilika wakaacha kumtii Mwenyezi Mungu na wakaanza kufurahia matamanio ya kidunia tu kulingana na matamanio ya nafsi zao, hata kama ni maasia na dhuluma. "Lakini anaiteremsha kwa kipimo akitakacho" kulingana na unavyotaka upole wake na hekima yake. "Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona." Ilisimuliwa katika baadhi ya riwaya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, 'Hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa mali, na kama ningemfanya masikini, basi hilo lingemharibu. Na hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa umasikini, na kama ningewatajirisha, basi hilo lingewaharibu. Na hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa afya njema, na kama ningewafanya wagonjwa, basi hilo lingewaharibu. Na hakika miongoni mwa waja wangu wapo wale ambao imani yao haiwezi kuwa nzuri isipokuwa kwa maradhi, na kama ningewaponya, basi hilo lingemharibu. Hakika Mimi ninaendesha mambo ya waja wangu kwa kuwa ninajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Hakika Mimi ni Mwenye habari zote, mwenye kuona yote.'
#
{28} {وهو الذي يُنَزِّل الغيثَ}؛ أي: المطر الغزير الذي به يغيثُ البلاد والعباد {من بعدِ ما قَنَطوا}: وانقطع عنهم مُدَّةً ظنُّوا أنه لا يأتيهم، وأيسوا، وعملوا لذلك الجدب أعمالاً، فينزِلُ الله الغيث، {وينشُرُ} به {رحمتَه} من إخراج الأقواتِ للآدميِّين وبهائمهم، فيقع عندهم موقعاً عظيماً، ويستبشرون بذلك ويفرحون. {وهو الوليُّ}: الذي يتولَّى عباده بأنواع التَّدبير، ويتولَّى القيام بمصالح دينهم ودنياهم {الحميد}: في ولايته وتدبيره، الحميد على ما له من الكمال وما أوصله إلى خلقه من أنواع الأفضال.
{28} "Naye ndiye anayeiteremsha mvua" nyingi kwa ajili ya nchi na watu "baada ya wao kwisha kata tamaa" na wakadhani kwamba haitawajia, na wakafanya vitendo mbalimbali kwa sababu ya ukame huo, kisha Mwenyezi Mungu akateremsha mvua, "na akaeneza" kwa hiyo "rehema yake" kwa kuwatolea watu na mifugo vyakula, kwa hivyo likawa jambo la umuhimu mkubwa sana kwao, na wakafurahia hilo furaha kubwa. "Naye ndiye Mlinzi" ambaye huwasimamia waja wake kwa kila aina ya usimamizi, na anasimamia masilahi ya mambo ya Dini yao na dunia yao. katika ulezi wake na usimamizi wake, Mwenye kusifiwa sana" kakatika ulinzi wake na usimamizi, na kwa sababu ukamilifu wake, na kwa sababu ya fadhila alizowafikishia viumbe wake.
: 29 #
{وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِنْ دَابَّةٍ وَهُوَ عَلَى جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ (29)}.
29. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama aliowaeneza ndani yake. Naye ni Mwenye uweza mkubwa wa kuwakusanya apendapo.
#
{29} أي: ومن أدلَّة قدرتِهِ العظيمة وأنَّه سيُحيي الموتى بعد موتهم: {خَلْقُ} هذه {السمواتِ والأرضِ}؛ على عِظَمِهما وسعتهما، الدالُّ على قدرته وسعة سلطانه، وما فيهما من الإتقان والإحكام دالٌّ على حكمته، وما فيهما من المنافع والمصالح دالٌّ على رحمتِهِ، وذلك يدلُّ على أنَّه المستحقُّ لأنواع العبادة كلِّها، وأنَّ إلهيَّة ما سواه باطلةٌ. {وما بثَّ فيهما}؛ أي: نشر في السماواتِ والأرض من أصناف الدوابِّ، التي جعلها الله مصالحَ ومنافعَ لعبادِهِ. {وهو على جمعهم}؛ أي: جمع الخلق بعد موتِهِم لموقفِ القيامةِ {إذا يشاءُ قديرٌ}: فقدرتُه ومشيئتُه صالحان لذلك، ويتوقَّف وقوعُه على وجود الخبر الصادق، وقد عُلم أنَّه قد تواترت أخبار المرسلين وكتبهم بوقوعه.
{29} Yaani, miongoni mwa ushahidi wa uwezo wake mkubwa ni kwamba atawafufua wafu baada ya kufa kwao ni, "kuumba mbingu na ardhi" licha ya ukubwa na upana wake, jambo linaloashiria uwezo wake na upana wa mamlaka yake, na ustadi na usawasawa ulio ndani yake unaashiria hekima yake, na manufaa na masilahi yaliyo ndani yake yanaonyesha rehema yake, na hayo yanaashiria kwamba Yeye ndiye anayestahiki aina zote za ibada, na kwamba uungu wa chochote kisichokuwa Yeye ni batili. "Na wanyama aliowaeneza ndani yake" ambao Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa ni masilahi na manufaa kwa waja wake. "Naye ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo" baada ya kufa kwao ili wasimame katika uwanja wa Kiyama. Kwani, uweza wake na utashi wake unaweza kufanya hivyo. Na kutokea kwake kunategemea kuwepo kwa habari za ukweli, na tayari imeshajulikana kwamba zimekuja habari nyingi sana kutoka kwa Mitume na Vitabu vyao kwamba hilo litatokea.
: 30 - 31 #
{وَمَا أَصَابَكُمْ مِنْ مُصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَنْ كَثِيرٍ (30) وَمَا أَنْتُمْ بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ (31)}.
30. Na misiba inayowasibu ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi. 31. Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu.
#
{30} يخبر تعالى أنَّه ما أصاب العبادَ من مصيبةٍ في أبدانهم وأموالهم وأولادهم وفيما يحبُّون ويكون عزيزاً عليهم إلاَّ بسبب ما قدَّمته أيديهم من السيئاتِ، وأنَّ ما يعفو الله عنه أكثرُ؛ فإنَّ الله لا يظلم العبادَ، ولكن أنفسَهم يظلمونَ، {ولو يؤاخِذُ اللهُ الناس بما كَسَبوا ما تَرَكَ على ظهرها من دابَّةٍ}.
{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba msiba hauwafikii waja wake katika miili yao, mali zao, watoto wao, na katika yale wanayoyapenda na ukawa mkubwa sana kwao isipokuwa kwa sababu ya mabaya waliyoyatanguliza kwa mikono yao, na kwamba yale ambayo Mwenyezi Mungu anayasamehe ni makubwa zaidi. Kwani, hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu waja wake, bali wanajidhulumu wenyewe. "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia ubaya watu kwa waliyoyachuma, basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja."
#
{31} وليس إهمالاً منه تعالى تأخيرُ العقوباتِ ولا عجزاً: فما {أنتُم بمعجزينَ في الأرض}؛ أي: معجزينَ قدرةَ الله عليكم، بل أنتم عاجزون في الأرض، ليس عندكم امتناعٌ عما ينفذه الله فيكم، {وما لكم من دونِ الله من وليٍّ}: يتولاَّكم، فيحصِّل لكم المنافع {ولا نصيرٍ}: يدفع عنكم المضارَّ.
{31} Kuwapa kwake muda Yeye Mtukufu si kuchelewesha adhabu wala kushindwa kuwaadhibu. Kwamba, "nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi" bali nyinyi ndio hamna uwezo katika ardhi, na wala hamuwezi kujizuia kutokana na yale anayoyatekeleza Mwenyezi Mungu juu yenu. "Na wala nyinyi hamna mlinzi" atakayewalinda na kuwafikishia manufaa, "wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu" anayeweza kukukingeni kutokana na madhara.
: 32 - 35 #
{وَمِنْ آيَاتِهِ الْجَوَارِ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ (32) إِنْ يَشَأْ يُسْكِنِ الرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَى ظَهْرِهِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ (33) أَوْ يُوبِقْهُنَّ بِمَا كَسَبُوا وَيَعْفُ عَنْ كَثِيرٍ (34) وَيَعْلَمَ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِنَا مَا لَهُمْ مِنْ مَحِيصٍ (35)}.
32. Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyokwenda na kurejea baharini kama vilima. 33. Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye subira kubwa na akashukuru sana. 34. Au huviangamiza hivyo vyombo kwa sababu ya waliyoyatenda hao watu. Naye husamehe mengi. 35. Na ili wajue wanaojadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahali popote pa kukimbilia.
#
{32} أي: ومن أدلَّة رحمته وعنايته بعباده {الجواري في البحر}: من السُّفن والمراكب الناريَّة والشراعيَّة التي من عظمها {كالأعلامِ}، وهي الجبالُ الكبارُ التي سخَّر لها البحر العجاج، وحفظها من التطام الأمواج، وجعلها تحمِلُكم وتحمِلُ أمتعتَكم الكثيرةَ إلى البلدان والأقطارِ البعيدة، وسخَّر لها من الأسباب ما كان معونةً على ذلك.
{32} Yaani, miongoni mwa ushahidi wa rehema zake na uangalizi wake mzuri kwa waja wake ni "vyombo vinavyokwenda na kurejea baharini," kama vile safina na maboti ambayo kwa sababu ya ukubwa wake ni "kama milima" mikubwa, ambayo Mwenyezi Mungu aliitiishia bahari kuu na akazilinda kutokana na michafuko ya mawimbi, na akazibeba na kuibeba mizigo yenu mingi mpaka nchi na maeneo ya mbali, na akazitiishia njia kuzisaidia kufanya hivyo.
#
{33 - 34} ثم نبَّه على هذه الأسباب بقوله: {إن يشأ يُسْكِنِ الريحَ}: التي جعلها الله سبباً لمشيها، {فيَظْلَلْنَ}؛ أي: الجواري {رواكدَ}: على ظهر البحر لا تتقدَّم ولا تتأخَّر. ولا ينتقض هذا بالمراكب الناريَّة؛ فإنَّ من شرط مشيِها وجودَ الريح، وإنْ شاء الله تعالى؛ أوبق الجواري بما كسب أهلها؛ أي: أغرقها في البحر وأتلفها، ولكنَّه يحلم ويعفو عن كثيرٍ. {إنَّ في ذلك لآياتٍ لكلِّ صبارٍ شكورٍ}؛ أي: كثير الصبر على ما تكرهه نفسه، ويشقُّ عليها فيكرِهها عليه من مشقَّة طاعة أو رَدْع داعٍ إلى معصية أو رَدْع نفسِهِ عند المصائب عن التسخُّط، شكورٍ في الرخاء، وعند النعم يعترفُ بنعمةِ ربِّه، ويخضع له، ويصرِفُها في مرضاتِهِ؛ فهذا الذي ينتفع بآيات الله، وأمَّا الذي لا صبر عنده ولا شكر له عند نعم الله؛ فإنَّه معرضٌ أو معاندٌ لا ينتفع بالآيات.
{33 - 34} Kisha akazibainisha njia hizi kwa kauli yake, "Akitaka, huutuliza upepo" ambao Mwenyezi Mungu aliufanya kuwa sababu ya kwenda kwake, "navyo hivyo vyombo vikasimama tutwe juu ya bahari" bila kusonga mbele wala kurudi nyuma. Hili haliwezi kubatilishwa na motoboti; kwani katika masharti ya kwenda kwake ni uwepo wa upepo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda anavizamisha vyombo hivyo vinavyokwenda na kurejea baharini kwa sababu ya yale waliyoyatenda hao watu wake. Lakini hustahimili na kusamehe mengi. "Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye subira kubwa na akashukuru sana." Yaani, mwenye subira kubwa kwa yale ambayo nafsi yake inayachukia na ni magumu kwake, kwa hivyo akayachukia kwa sababu ya hayo, kama vile ugumu ulioko katika utiifu, au kuzuia hamu ya kuasi, au kujizuia kutoridhika wakati wa msiba. Naye pia ni mwenye kushukuru sana katika hali nzuri nzuri, akakiri neema za Mola wake Mlezi na kumnyenyekea, na anazitumia katika mambo ya kumridhia. Huyu ndiye anayefaidika na Aya za Mwenyezi Mungu. Na ama yule ambaye hana subira na hana shukrani anapopata neema za Mwenyezi Mungu, yeye hupeana mgongo au hukaidi bila ya kufaidika na Aya zake.
#
{35} ثم قال تعالى: {ويعلم الذين يجادلون في آياتنا}: لِيُبْطِلوها بباطلهم، {ما لهم من محيصٍ}؛ أي: لا ينقذهم منقذٌ مما حلَّ بهم من العقوبة.
{35} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Na ili wajue wanaojadiliana katika Ishara zetu" ili wazibatilishe kwa batili zao "hawana pahali popote pa kukimbilia." Yaani, hawatakuwa na mwokozi yeyote atakayewaokoa kutokana na adhabu iliyowapata.
: 36 - 39 #
{فَمَا أُوتِيتُمْ مِنْ شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا عِنْدَ اللَّهِ خَيْرٌ وَأَبْقَى لِلَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ (36) وَالَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُوا هُمْ يَغْفِرُونَ (37) وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَى بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ (38) وَالَّذِينَ إِذَا أَصَابَهُمُ الْبَغْيُ هُمْ يَنْتَصِرُونَ (39)}.
36. Basi vyote mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu zaidi kwa ajili ya walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi. 37. Na wanayoyaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapokasirika wao husamehe. 38.Na wanaomwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao, na kutokana na tulichowaruzuku wakawa wanatoa. 39. Na ambao wanapofanyiwa jeuri hujitetea.
#
{36} هذا تزهيدٌ في الدُّنيا وترغيبٌ في الآخرة وذكرُ الأعمال الموصلةِ إليها؛ فقال: {فما أوتيتم من شيءٍ}: من ملكٍ ورياسةٍ وأموال وبنينَ وصحَّةٍ وعافيةٍ بدنيَّةٍ، {فمتاعُ الحياةِ الدُّنيا}: لذَّةٌ منغصةٌ منقطعةٌ، {وما عندَ اللهِ}: من الثواب الجزيل والأجر الجليل والنعيم المقيم {خيرٌ} من لَذَّات الدُّنيا، خيريَّة لا نسبةَ بينهما {وأبقى}: لأنَّه نعيمٌ لا منغِّص فيه ولا كَدَرَ ولا انتقالَ. ثم ذكر لمن هذا الثواب، فقال: {للذين آمنوا وعلى ربِّهم يتوكَّلونَ}؛ أي: جمعوا بين الإيمان الصحيح المستلزم لأعمال الإيمان الظاهرة والباطنة، وبين التوكُّل الذي هو الآلةُ لكلِّ عمل؛ فكلُّ عمل لا يَصْحَبُه التوكُّل؛ فغير تامٍّ، وهو الاعتماد بالقلب على الله في جَلْب ما يحبُّه العبد ودَفْع ما يكرهُهُ مع الثِّقة به تعالى.
{36} Huku ni kukatisha tamaa na dunia na kuhimiza juu ya Akhera, na kutaja matendo yanayofikisha huko. Akasema, "Basi vyote mlivyopewa" kama vile ufalme, uongozi, mali, watoto, afya nzuri na usalama wa kimwili, "ni starehe ya maisha ya dunia tu," zenye kuisha. "Lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu" ni cha thawabu na ujira mkubwa, na neema ya kudumu. Na hayo "ni bora" kuliko starehe za dunia kwa ubora ambao hakuna ulinganisho kati yake, "na cha kudumu zaidi," kwa sababu ni neema isiyo na usumbufu wowote wala shida, wala haiishi. Kisha akataja yule ambaye malipo haya ni yake, akasema: "kwa ajili ya walioamini na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi. " Yaani, walijumuisha kati ya imani sahihi inayolazimu mtu kutenda matendo ya imani hiyo, ya dhahiri na yaliyofichikana, na kati ya kumtegemea ambako ndio chombo cha kila tendo. Kwani kila tendo ambalo haliambatani na kumtemegea Mwenyezi Mungu, hilo bado halijakamilika. Kwa maana hilo kuteni kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa moyo juu ya kuleta yale anayoyapenda mja na kuzuia anayoyachukia, pamoja na kuwa na imani naye Mtukufu.
#
{37} {والذين يَجتنبونَ كبائرَ الإثم والفواحشَ}: والفرق بين الكبائرِ والفواحشِ ـ مع أنَّ جميعَهما كبائرُ ـ أنَّ الفواحشَ هي الذُّنوب الكبارُ التي في النفوس داعٍ إليها كالزِّنا ونحوه، والكبائرُ ما ليس كذلك، هذا عند الاقتران، وأمَّا مع إفرادِ كلٍّ منهما عن الآخر؛ فإنَّ الآخر يدخُلُ فيه. {وإذا ما غضبوا هم يغفِرونَ}؛ أي: قد تخلَّقوا بمكارم الأخلاق ومحاسن الشِّيم، فصار الحلم لهم سَجِيَّة وحسن الخلق لهم طبيعةً، حتى إذا أغضَبَهم أحدٌ بمقاله أو فعاله؛ كظموا ذلك الغضب، فلم يُنْفِذوه، بل غفروه، ولم يقابِلوا المسيءَ إلاَّ بالإحسان والعفو والصفح، فترتَّب على هذا العفو والصفح من المصالح ودفع المفاسد في أنفسهم وغيرهم شيءٌ كثير؛ كما قال تعالى: {ادفَعْ بالتي هي أحسنُ فإذا الذي بينَكَ وبينَه عدواةٌ كأنَّه وليٌّ حميمٌ. وما يُلَقَّاها إلاَّ الذينَ صَبَروا وما يُلَقَّاها إلاَّ ذو حَظٍّ عظيم}.
{37} "Na wanayoyaepuka madhambi makubwa na mambo machafu." Tofauti iliyoko baina ya madhambi makubwa na machafu, ijapokuwa yote ni madhambi makubwa, ni kwamba machafu ni madhambi makubwa ambayo kuna ya kuitia kuyafanya katika nafsi kama vile uzinifu na mfano wake, na madhambi makubwa ni yale ambayo sivyo. Hili ni pale mawili haya yanapotajwa kwa pamoja. Na ama linapotenganishwa kila moja yake mbali na jingine, basi hilo pia linaingia katika maana ya lenzake. "Na wanapokasirika wao husamehe." Wao wamejipamba kwa tabia njema na maadili ya heshima, basi ustahamilivu ukawa ndio tabia yao isiyoachana nao, na maadili mema yakawa ndiyo umbile lao la asili, hata mtu akiwakasirisha kwa maneno au matendo, wanaizuia ghadhabu yao, na hawaitekelezi. Bali wanasamehe, na hawakabiliani na aliyewatendea mabaya isipokuwa kwa wema na msamaha, na kuachilia mbali. Kwa hivyo, yakatokana na msamaha huu na kuachilia mbali masilahi mengi na kujizuilia maovu wao wenyewe na pia kuwazuilia wengine, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Zuilia mabaya kwa lililojema zaidi. Hapo, yule ambaye baina yako naye pana uadui, atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu."
#
{38} {والذين استجابوا لربِّهم}؛ أي: انقادوا لطاعته، ولبَّوْا دعوته، وصار قصدُهُم رضوانَه وغايتُهُم الفوزَ بقربِهِ، ومن الاستجابة لله إقامُ الصَّلاة وإيتاءُ الزَّكاة؛ فلذلك عطفَهما على ذلك من باب عطف العامِّ على الخاصِّ الدالِّ على شرفه وفضله، فقال: {وأقاموا الصلاةَ}؛ أي: ظاهرها وباطنها فرضها ونفلها، {ومما رَزَقْناهم يُنفِقونَ}: من النفقات الواجبة؛ كالزكاة والنفقة على الأقارب ونحوهم، والمستحبَّة؛ كالصدقات على عموم الخلق. {وأمرُهُم}: الدينيُّ والدنيويُّ، {شورى بينهم}؛ أي: لا يستبدُّ أحدٌ منهم برأيه في أمر من الأمور المشتركة بينهم، وهذا لا يكون إلاَّ فرعاً عن اجتماعهم وتوالُفِهم وتوادُدِهم وتحابُبِهم؛ وكمال عقولهم أنَّهم إذا أرادوا أمراً من الأمور التي تحتاجُ إلى إعمال الفكرِ والرأي فيها؛ اجتمعوا لها وتشاوروا وبحثوا فيها، حتى إذا تبيَّنت لهم المصلحةُ؛ انتهزوها وبادروها، وذلك كالرأي في الغزو والجهاد وتولية الموظَّفين لإمارةٍ أو قضاءٍ أو غيره، وكالبحث في المسائل الدينيَّة عموماً؛ فإنَّها من الأمور المشتركة، والبحثُ فيها لبيان الصَّواب مما يحبُّه الله، وهو داخلٌ في هذه الآية.
{38} "Na wanaomwitikia Mola wao Mlezi" kwa kufuata utiifu wake na wakaitikia wito wake, na makusudio yao yakawa ni radhi zake na lengo lao likawa ni kufikia kuwa karibu naye. Na katika kumuitikia Mwenyezi Mungu ni kusimamisha swala na kutoa zaka. Ndiyo maana akafungamanisha mawili hayo juu yake akitumia mbinu ya kuunganisha kilicho mahsusi kwa cha jumla, kuashiria heshima yake na fadhilla yake. Kwa hivyo akasema: "Na wakashika Sala" kwa dhahiri yake na siri yake, za faradhi na za hiyari, "na kutokana na tulichowaruzuku wakawa wanatoa" miongoni mwa mambo yanayotolewa kwa faradhi, kama vile zaka na kuwapa matumizi jamaa na wengineo, na pia matumizi yanayopendekezwa kama vile kuwapa sadaka watu wote, "na mambo yao" ya kidini na ya kidunia "yakawa ni kwa kushauriana baina yao." Yaani, hakuna hata mmoja wao anayewazuilia wengine kutoa maoni yake juu ya jambo lolote wanaloshirikiana ndani yake, na hili haliwi isipokuwa kutokana na umoja wao, maelewano yao na upendo wao. Na ukamilifu wa akili zao ni kwamba wanapotaka kufanya jambo linalohitaji kutumia fikira na maoni ndani yake, wakakusanyika kwa ajili yake, wakashauriana na kulifanyia utafiti, mpaka masilahi yake yanapowabainikia, wanachukua fursa hiyo na kuianza mara moja, kama vile maoni kuhusu vita vya jihadi, kuwateua wafanyakazi kwa ajili ya uongozi au mahakama, au mambo mengineyo, na kama vile kutafiti masuala ya kidini kwa ujumla. Hayo ni miongoni mwa mambo wanayoshiriki wote ndani yake, na kuyatafiti ili kubainisha yaliyo sahihi ni katika yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu, nayo yanaingia ndani ya aya hii.
#
{39} {والذين إذا أصابَهُمُ البغيُ}؛ أي: وصل إليهم من أعدائهم {هم ينتصرونَ}: لقوَّتهم وعزَّتهم، ولم يكونوا أذلاَّء عاجزين عن الانتصارِ؛ فوصَفَهم بالإيمان، والتوكُّل على الله، واجتنابِ الكبائر والفواحش الذي تُكَفَّرُ به الصغائرُ، والانقياد التامِّ، والاستجابة لربِّهم، وإقامة الصلاة، والإنفاق في وجوه الإحسان، والمشاورة في أمورهم، والقوَّة، والانتصار على أعدائِهِم؛ فهذه خصالُ الكمال قد جَمَعوها، ويلزم من قيامِها فيهم فِعْلُ ما هو دونَها وانتفاءُ ضدِّها.
{39} "Na ambao wanapofanyiwa jeuri" kutoka kwa maadui zao "hujitetea" kwa sababu ya nguvu zao na utukufu wao, na wala hawajidhalilishi wasioweza kujitetea. Basi hapa akawaelezea kwa imani kumtegemea Mwenyezi Mungu, kujiepusha na madhambi makubwa na machafu ambayo kwayo yanafutwa makosa madogo, na pia akawaelezea kwa kufuata kikamilifu kumuitikia Mola wao Mlezi, kusimamisha Swala, kutoa sadaka katika njia za heri, kushauriana katika mambo yao, nguvu na kujitetea dhidi ya maadui zao. Hizi ndizo sifa za ukamilifu ambazo wamezijumuisha. Na inalazimu kutokana na kuwepo kwake ndani yao, kwamba wanafanya yasiyokuwa hayo na kujiepusha kinyume chake.
: 40 - 43 #
{وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِثْلُهَا فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ (40) وَلَمَنِ انْتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَئِكَ مَا عَلَيْهِمْ مِنْ سَبِيلٍ (41) إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (42) وَلَمَنْ صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ (43)}.
40. Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu. 41. Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu. 42. Bali lawama ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu. 43. Na anayekuwa na subira, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.
#
{40} ذكر الله في هذه الآية مراتبَ العقوباتِ، وأنَّها على ثلاث مراتب: عدلٌ، وفضلٌ، وظلمٌ. فمرتبةُ العدل: جزاءُ السيئةِ بسيئةٍ مثِلها؛ لا زيادة ولا نقص؛ فالنفسُ بالنفس، وكلُّ جارحة بالجارحة المماثلة لها، والمال يُضْمَنُ بمثله. ومرتبةُ الفضل: العفو والإصلاحُ عن المسيء، ولهذا قال: {فمَنْ عفا وأصلَحَ فأجرُهُ على الله}؛ يجزيه أجراً عظيماً وثواباً كثيراً، وشَرَطَ الله في العفو الإصلاح فيه ليدلَّ ذلك على أنَّه إذا كان الجاني لا يَليقُ بالعفوِ عنه، وكانت المصلحةُ الشرعيةُ تقتضي عقوبتَه؛ فإنَّه في هذه الحال لا يكون مأموراً به، وفي جعل أجرِ العافي على الله مما يهيجُ على العفوِ وأنْ يعامِلَ العبدُ الخَلْقَ بما يحبُّ أن يعامِلَه الله به؛ فكما يحبُّ أن يعفوَ الله عنه؛ فليعفُ عنهم، وكما يحبُّ أن يسامِحَه الله؛ فليسامِحْهم؛ فإنَّ الجزاء من جنس العمل. وأما مرتبةُ الظُّلم؛ فقد ذَكَرَها بقوله: {إنَّه لا يحبُّ الظالمين}: الذين يجنون على غيرِهِم ابتداءً، أو يقابلون الجاني بأكثر من جنايتِهِ؛ فالزيادة ظلمٌ.
{40} Katika Aya hii, Mwenyezi Mungu ametaja viwango vya adhabu, na kwamba viko katika viwango vitatu: uadilifu, wema na dhuluma. Kiwango cha uadilifu ni kulipa kitendo kibaya kwa kitendo kibaya kama hicho, bila kuongeza wala kupunguza. Nafsi ni kwa nafsi, na kila jeraha kwa jeraha kama hilo, nayo mali inadhaminiwa na kitu mfano wake. Daraja ya wema ni kusamehe na kutengeneza mambo ya aliyetenda mabaya, na ndiyo maana akasema: "Lakini mwenye kusamehe na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu," atamlipa ujira mkubwa na thawabu nyingi. Na Mwenyezi Mungu aliweka sharti la kutengenea katika kusamehe ili kuashiria kwamba ikiwa mkosaji hastahiki kusamehewa, na masilahi ya kisheria yakahitaji kwamba aadhibiwe, basi katika hali hii, haiamrishwi kusamehe. Na katika kuweka malipo ya mwenye kusamehe kwa Mwenyezi Mungu kuna mambo yanayohimiza msamaha, na kwamba mja awatendee viumbe kwa njia ambayo angependa Mwenyezi Mungu aamiliane naye. Kwa hivyo, kama vile anavyopenda Mwenyezi Mungu kumsamehe, basi naye na awasamehe. Na kama vile anavyopenda Mwenyezi Mungu amsamehe, basi naye na awasamehe wengine, kwani malipo ni ya aina sawa na matendo. Na ama kuhusu kiwango cha dhuluma, basi alikitaja katika kauli yake, "Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu." Yaani, wale wanaoanzisha kuwadhulumu wengine, au wale wanaomlipa mkosaji zaidi ya kosa lake, basi ziada hiyo ni dhuluma.
#
{41} {ولَمَنِ انتصر} من {بعد ظلمِهِ}؛ أي: انتصر ممَّن ظَلَمه بعد وقوع الظُّلم عليه {فأولئك ما عليهم من سبيل}؛ أي: لا حرج عليهم في ذلك. ودلَّ قولُه: {والذين إذا أصابَهُمُ البَغْيُ}، وقوله: {ولَمَنِ انتصر بعد ظلمِهِ}: أنَّه لا بدَّ من إصابة البغي والظُّلم ووقوعه، وأما إرادةُ البغي على الغير وإرادةُ ظلمه من غيرِ أن يَقَعَ منه شيءٌ؛ فهذا لا يجازَى بمثله، وإنَّما يؤدَّب تأديباً يردعُه عن قول أو فعل صدر منه.
{41} "Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu." Na iliashiria kauli yake, "Na ambao wanapofanyiwa jeuri," na kauli yake, "Na wanaojitetea baada ya kudhulumiwa," kwamba ni lazima dhuluma hiyo iwe imeshafanyika. Na ama kutaka tu kumdhulumu mwengine bila ya kuifanya dhuluma hiyo, basi huyu hatalipwa kwa njia sawa na alivyofanya. Bali ataadhibiwa kwa namna ambayo itamzuia kutokana na maneno au matendo aliyofanya.
#
{42} {إنَّما السبيلُ}؛ أي: إنَّما تتوجَّه الحجَّة بالعقوبة الشرعيَّة {على الذين يظلِمونَ الناس ويَبْغونَ في الأرض بغير الحقِّ}: وهذا شاملٌ للظُّلم والبغي على الناس في دمائهم وأموالهم وأعراضهم. {أولئك لهم عذابٌ أليمٌ}؛ أي: موجعٌ للقلوب والأبدان بحسب ظلمهم وبغيهم.
{42} "Bali lawama" na adhabu ya kisheria "ipo kwa wale wanaowadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki." Na hili linajumuisha kuwadhulumu watu katika damu zao, mali zao na heshima zao. "Hao watapata adhabu iliyo chungu" juu ya nyoyo zao na miili yao kulingana na dhuluma yao.
#
{43} {وَلَمَن صَبَرَ}: على ما ينالُه من أذى الخلق، {وغَفَرَ}: لهم بأن سمح لهم عمَّا يصدر منهم {إنَّ ذلك لَمِنْ عزم الأمور}؛ أي: لمن الأمور التي حثَّ اللهُ عليها وأكَّدها وأخبر أنَّه لا يُلَقَّاها إلاَّ أهلُ الصبر والحظوظِ العظيمة، ومن الأمور التي لا يوفَّق لها إلاَّ أولو العزائم والهمم وذوو الألباب والبصائر؛ فإنَّ ترك الانتصار للنفس بالقول أو الفعل من أشقِّ شيء عليها، والصبر على الأذى والصفح عنه ومغفرتِهِ ومقابلتِهِ بالإحسان أشقُّ وأشقُّ، ولكنَّه يسيرٌ على من يسَّره الله عليه وجاهد نفسَه على الاتِّصاف به، واستعانَ اللهَ على ذلك، ثم إذا ذاقَ العبدُ حلاوته، ووجد آثارَه؛ تلقَّاه برحب الصدرِ وسعة الخُلُق والتلذُّذ فيه.
{43} "Na anayekuwa na subira" juu ya madhara yanayompata kutoka kwa viumbe, "na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa." Yaani, ni miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyahimiza na akayasisitiza, na akajulisha kwamba hawayafikii isipokuwa watu wenye subira na bahati kubwa, na ni miongoni mwa mambo ambayo hawawezeshwi kuyafikia isipokuwa watu wenye azimio na dhamira kubwa na wale wenye akili nzuri na ufahamu mkubwa. Kwani, kuacha kujitetea kwa maneno au vitendo ni katika mambo magumu zaidi juu ya nafsi. Nako kuwa na subira juu ya maudhi na kuachilia mbali, kusamehe na kumkabili kwa wema, ni vigumu zaidi tena ni vigumu zaidi, lakini ni rahisi kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfanyia kuwa jepesi na akapambana na nafsi yake juu ya kusifika kwayo, na akatafuta msaada wa Mwenyezi Mungu katika hilo. Kisha mja anapoonja utamu wake na akapata athari zake, anayapokea kwa kifua kikunjufu, tabia njema na kuyafurahia.
: 44 - 46 #
{وَمَنْ يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ وَلِيٍّ مِنْ بَعْدِهِ وَتَرَى الظَّالِمِينَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ يَقُولُونَ هَلْ إِلَى مَرَدٍّ مِنْ سَبِيلٍ (44) وَتَرَاهُمْ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا خَاشِعِينَ مِنَ الذُّلِّ يَنْظُرُونَ مِنْ طَرْفٍ خَفِيٍّ وَقَالَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلَا إِنَّ الظَّالِمِينَ فِي عَذَابٍ مُقِيمٍ (45) وَمَا كَانَ لَهُمْ مِنْ أَوْلِيَاءَ يَنْصُرُونَهُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَمَنْ يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ سَبِيلٍ (46)}.
44. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana mlinzi baada yake. Na utawaona wenye kudhulumu watakapoiona adhabu wanasema: 'Je! Ipo njia ya kurudi?' 45. Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na walioamini watasema: 'Hakika wapatao hasara ni hao waliohasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama.' Ama hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya daima. 46. Wala hawatakuwa na walinzi wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana njia yoyote.
#
{44} يخبر تعالى أنَّه المنفرد بالهداية والإضلال، وأنَّه {مَنْ يُضْلِل اللهُ}: بسبب ظلمه {فما له من وليٍّ من بعدِهِ}: يتولَّى أمره ويهديه، {وترى الظالمين لمَّا رأوا العذابَ}: مرأى ومنظراً فظيعاً صعباً شنيعاً يُظْهِرونَ النَّدم العظيم والحزنَ على ما سَلَفَ منهم، و {يقولونَ هل إلى مَرَدٍّ من سبيل}؛ أي: هل لنا طريقٌ أو حيلةٌ إلى رجوعنا إلى الدُّنيا لنعملَ غير الذي كنَّا نعملُ، وهذا طلبٌ للأمر المُحال الذي لا يمكنُ.
{44} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa Yeye ni wa kipekee katika kuongoa na kupotosha, na kwamba "ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea" kwa sababu ya udhalimu wake, "basi hana mlinzi baada yake" atakayemsimamia mambo yake na kumuongoa. "Na utawaona wenye kudhulumu watakapoiona adhabu" ikionekana kwa muonekano wa kutisha sana, mgumu na mbaya zaidi, watadhihirisha majuto makubwa na huzuni juu ya yale yao yaliyopita. Na "Je! Ipo njia ya kurudi" duniani ili tufanye mambo yasiyokuwa yale tuliyokuwa tukifanya? Lakini hili ni kuomba jambo lisilowezekana.
#
{45} {وتراهم يُعْرَضونَ عليها}؛ أي: على النار {خاشعينَ من الذُّلِّ}؛ أي: ترى أجسامَهم خاشعةً للذُّلِّ الذي في قلوبهم، {ينظُرونَ من طرفٍ خفيٍّ}؛ أي: ينظرون إلى النار مسارقةً وشزراً من هيبتها وخوفِها، {وقال الذين آمنوا}: حين ظهرتْ عواقبُ الخلق وتبيَّنَ أهلُ الصدق من غيرِهم: {إنَّ الخاسرينَ}: على الحقيقة، {الذين خَسِروا أنفسَهم وأهليهم يوم القيامةِ}: حيث فوَّتوا أنفسَهم جزيل الثواب وحصلوا على أليم العقاب وفُرِّقَ بينهم وبين أهليهم فلم يجتمعوا بهم آخر ما عليهم. {ألا إنَّ الظالمينَ}: أنفسَهم بالكفر والمعاصي {في عذابٍ مقيم}؛ أي: في سوائه ووسطه منغمِرين لا يخرُجون منه أبداً، ولا يُفَتَّرُ عنهم وهم فيه مُبْلِسونَ.
{45} Yaani, "Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto nao wamenyenyekea kwa unyonge" uliomo ndani ya nyoyo zao, "wanatazama kwa mtazamo wa kificho" kwa sababu ya kutisha kwake na hofu waliyo nayo juu yake. "Na walioamini watasema" wakati wa mwisho wa viumbe ulipodhihirika na wana ukweli wakabainika mbali na wengineo: "Hakika wapatao hasara" kiuhakika "ni hao waliokhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama." Kwa maana walizikosesha nafsi zao ujira mkubwa na wakapata adhabu iumizayo, na wakatenganishwa wao na ahali zao, wala hawakujumuika tena. "Ama hakika wenye kudhulumu" nafsi zao kwa ukafiri na maasia "watakuwa katika adhabu ya daima." Yaani, watatumbukizwa katikati yake na wala hawatatoka humo kamwe, na wala hawatapumzishwa, na humo watakata tamaa.
#
{46} {وما كان لهم من أولياءَ يَنصُرونَهم من دونِ الله}: كما كانوا في الدُّنيا يُمَنُّون أنفسَهم بذلك ؛ ففي القيامةِ يتبيَّن لهم ولغيرِهم أنَّ أسبابهم التي أمَّلوها تقطَّعت، وأنَّه حين جاءهم عذابُ الله لم يُدْفَعْ عنهم، {ومن يُضْلِلِ الله فما له مِن سبيل}: تحصُلُ به هدايتُه؛ فهؤلاء ضلُّوا حين زعموا في شركائِهِم النفعَ ودفعَ الضُّرِّ، فتبيَّن حينئذٍ ضلالُهم.
{46} "Wala hawatakuwa na walinzi wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu," kama walivyokuwa wakijidai hivyo katika dunia. Basi Siku ya Kiyama itawadhihirikia wao na wengineo kwamba njia walizozitarajia zimekatika, na kwamba ilipowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu haikuwezekana kuwaepusha mbali nayo. "Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana njia yoyote" ya kuongoka. Hawa walipotea pindi walipodai kuwa washirika wao watawanufaisha na kuwaepushia madhara, lakini hapo ukabainika upotofu wao huo.
: 47 - 48 #
{اسْتَجِيبُوا لِرَبِّكُمْ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَ يَوْمٌ لَا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّهِ مَا لَكُمْ مِنْ مَلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُمْ مِنْ نَكِيرٍ (47) فَإِنْ أَعْرَضُوا فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا إِنْ عَلَيْكَ إِلَّا الْبَلَاغُ وَإِنَّا إِذَا أَذَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنَّا رَحْمَةً فَرِحَ بِهَا وَإِنْ تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَإِنَّ الْإِنْسَانَ كَفُورٌ (48)}.
47. Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyoepukika, itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukingia. 48. Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu. Na hakika Sisi tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru.
#
{47} يأمر تعالى عبادَه بالاستجابة له بامتثال ما أمَرَ به واجتنابِ ما نهى عنه وبالمبادرةِ بذلك وعدم التَّسويف {مِن قبل أن يأتِيَ}: يوم القيامة، الذي إذا جاء؛ لا يمكنُ ردُّه واستدراكُ الفائتِ، وليس للعبد في ذلك اليوم ملجأ يلجأ إليه فيفوتُ ربَّه ويهربُ منه، بل قد أحاطتِ الملائكةُ بالخليقة من خلفهم، ونودوا: {يا معشرَ الجِنِّ والإنسِ إنِ استَطَعْتُم أن تَنفُذوا من أقطارِ السمواتِ والأرضِ فانفُذوا لا تَنفُذون إلاَّ بسلطانٍ}: وليس للعبد في ذلك اليوم نكيرٌ لما اقترفَه وأجرمَه، بل لو أنكر؛ لشهدتْ عليه جوارحُه. وهذه الآيةُ ونحوُها فيها ذمُّ الأمل والأمرُ بانتهازِ الفرصة في كلِّ عمل يَعْرِضُ للعبد؛ فإنَّ للتأخير آفاتٍ.
{47} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake kumuitikia Yeye kwa kutekeleza aliyowaamrisha na kuyaepuka aliyoyakataza, na kwa kuharakisha kufanya hivyo na kutoahirisha "kabla haijafika siku" ya Siku ya Kiyama, ambayo ikija haiwezekani kuirudisha nyuma ili kufanya mambo ambayo mtu hakuyafanya. Na mja siku hiyo hatakuwa na kimbilio awezalo kukimbilia ili asifikiwe na Mola wake Mlezi na amkimbie. Bali Malaika watawazunguka viumbe kutokea nyuma yao, na wakanadiwa: "Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye pande za mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa uwezo wa kufanya hivyo." Siku hiyo mja hataweza kukataa yale aliyoyafanya. Bali ikiwa atakataa, basi viungo vyake vitashuhudia dhidi yake. Aya hii na nyinginezo mfano wake zinakemea suala la kuwa na matumaini matupu, na kuamrisha mtu kuchukua fursa katika kila tendo linalomtokea mja. Kwani kuchelewa mambo kuna balaa zake.
#
{48} {فإنْ أعْرَضوا}: عمَّا جئتُم به بعد البيانِ التامِّ {فما أرسلناكَ عليهم حفيظاً}: تحفظُ أعمالَهم وتسألُ عنها، {إنْ عليكَ إلاَّ البلاغُ}: فإذا أديتَ ما عليك؛ فقد وجب أجرُكَ على الله، سواء استجابوا أم أعرضوا، وحسابُهم على الله الذي يحفظُ عليهم صغير أعمالِهم وكبيرَها وظاهرَها وباطنها. ثم ذكر تعالى حالةَ الإنسان، وأنَّه إذا أذاقه الله رحمةً من صحَّةِ بدنٍ ورزقٍ رغدٍ وجاه ونحوه؛ {فرِحَ بها}؛ أي: فرح فرحاً مقصوراً عليها لا يتعدَّاها، ويلزم من ذلك طمأنينته بها وإعراضه عن المنعم. {وإن تُصِبْهم سيئةٌ}؛ أي: مرضٌ أو فقرٌ أو نحوهما {بما قدَّمتْ أيديهم فإنَّ الإنسانَ كفورٌ}؛ أي: طبيعته كفرانُ النعمة السابقة والتسخُّط لما أصابه من السيِّئةِ.
{48} "Na wakipuuza" yale uliyowajia nayo baada ya kubainishiwa kikamilifu, "basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao" ili uyalinde matendo yao na uulizwe juu yake. "Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu." Kwa hivyo ukishafanya kile kilicho juu yako, basi tayari malipo yako yatakuwa kwa Mwenyezi Mungu, sawa waitikie au wapuuze, na hesabu yao iko kwa Mwenyezi Mungu ambaye anawahifadhia vitendo vyao, vidogo na vikubwa, vilivyo dhahiri na vilivyofichikana. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hali ya mwanadamu, na kwamba Mwenyezi Mungu anapomuonjesha rehema kama vile afya njema ya kimwili, riziki nyingi, heshima na mfano wa hayo "huifurahia" kwa sababu ya hayo tu, kisha akatulizana kwa ajili yake na akampuuza yule aliyemneemesha. "Na akisibiwa na ovu" kama vile maradhi, ufukara au mengineyo "kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru sana." neema zilizotangulia na akakasirika sana kwa sababu ya mabaya yaliyompata.
: 49 - 50 #
{لِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ يَهَبُ لِمَنْ يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَنْ يَشَاءُ الذُّكُورَ (49) أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا وَيَجْعَلُ مَنْ يَشَاءُ عَقِيمًا إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ (50)}.
49. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume. 50. Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi, Mwenye uweza.
#
{49 - 50} هذه الآية فيها الإخبارُ عن سعةِ ملكِهِ تعالى ونفوذِ تصرُّفه في الملك في الخلق لما يشاء والتدبير لجميع الأمور، حتى إنَّ تدبيره تعالى من عمومِهِ أنَّه يتناول المخلوقة عن الأسباب التي يباشِرُها العباد؛ فإنَّ النِّكاحَ من الأسباب لولادة الأولاد؛ فالله تعالى هو الذي يعطيهم من الأولاد ما يشاءُ؛ فمِنَ الخلق مَن يَهَبُ له إناثاً، ومنهم من يَهَبُ له ذكوراً، ومنهم من يزوِّجُه؛ أي: يجمع له ذكوراً وإناثاً، ومنهم مَنْ يجعلُه عقيماً لا يولَد له. {إنه عليمٌ}: بكلِّ شيءٍ. {قديرٌ}: على كل شيءٍ. فيتصرَّف بعلمه وإتقانه الأشياء وبقدرتِهِ في مخلوقاته.
{49 - 50} Aya hii ina habari kuhusu upana wa ufalme wake Mtukufu na kutekelezeka kwa uendeshaji wake katika ufalme wake, kama vile kuumba atakavyo na kuendesha mambo yote, kwa kiasi kwamba, kwa sababu ya ujumla wa uendeshaji wake Mtukufu unajumuisha visababu vilivyoumbwa anavyofanya mja. Kwa mfano, kuoa ni kisababu cha kuzaa watoto. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayewapa watoto atakavyo. Miongoni mwa viumbe wapo wale anaowatunukia watoto wa kike na miongoni mwao wapo wale anaowatunukia watoto wa kiume, na miongoni mwao wapo wale anaowachanganyia wawili hao: wa kiume na wa kike, na miongoni mwao wapo anaowafanya tasa. "Hakika Yeye ni Mwenye kujua vyema" kila kitu, "Mwenye uwezo mkubwa" juu ya kila kitu. Anawaendesha viumbe wake kwa elimu yake, ustadi wake na uwezo wake.
: 51 - 53 #
{وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَنْ يُكَلِّمَهُ اللَّهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِنْ وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ (51) وَكَذَلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِنْ أَمْرِنَا مَا كُنْتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَكِنْ جَعَلْنَاهُ نُورًا نَهْدِي بِهِ مَنْ نَشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (52) صِرَاطِ اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ أَلَا إِلَى اللَّهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ (53)}.
51. Na haikuwa kwa mwanadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya kizuizi, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hekima. 52. Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunamwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyonyooka. 53. Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu.
#
{51} لما قال المكذِّبون لرسل الله الكافرون بالله: {لولا يكلِّمُنا الله أو تأتينا آيةُ}: من كِبرهم وتجبُّرهم؛ ردَّ الله عليهم بهذه الآية الكريمة، وأنَّ تكليمه تعالى لا يكونُ إلاَّ لخواصِّ خلقه؛ للأنبياء والمرسلين وصفوته من العالمين، وأنَّه يكون على أحد هذه الأوجه: إمَّا أن يكلِّمَه الله وحياً، بأن يُلْقِيَ الوحيَ في قلبِ الرسول من غير إرسال مَلَكٍ ولا مخاطبةٍ منه شفاهاً، {أو} يكلِّمَه منه شفاهاً، لكنه {من وراء حجابٍ}؛ كما حصل لموسى بن عمران كليم الرحمن، {أو} يكلِّمَه الله بواسطة الرسول الملكيِّ؛ فيرسل {رسولاً}؛ كجبريل أو غيره من الملائكة، {فيوحي بإذنه}؛ أي: بإذن ربِّه لا بمجرَّد هواه؛ إنَّه تعالى عليُّ الذات عليُّ الأوصاف، عظيمُها، عليُّ الأفعال، قد قهر كلَّ شيء، ودانت له المخلوقات، {حكيمٌ} في وضعه كلَّ شيء في موضعه من المخلوقات والشرائع.
{51} Wakati wale waliowakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu waliposema: "Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara?" Kwa sababu ya kiburi chao, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa aya hii tukufu, na kwamba Yeye Mtukufu hawaongeleshi isipokuwa viumbe vyake maalumu: Manabii na Mitume, na watukufu wake miongoni mwa walimwengu, na kwamba hilo huwa kwa moja ya njia hizi: Ima Mwenyezi Mungu amzungumzishe kwa kumteremshia ufunuo wake kwa kutia ufunuo ndani ya moyo wa Mtume bila ya kumtumia Malaika au kusema naye moja kwa moja, "au" akazungumza naye kwa maneno moja kwa moja, lakini "kwa nyuma ya kizuizi." Kama ilivyokuwa kwa Musa bin Imran, aliyezungumza moja kwa moja na Mwingi wa rehema. "Au" Mwenyezi Mungu akamzungumzisha kupitia Mtume wa kimalaika, akamtumia "mjumbe" kama vile Jibril au Malaika wengineo. "Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake" Mwenyezi Mungu, na si kwa matamanio yake tu. Yeye Mtukufu ni wa juu zaidi kwa dhati yake, na yuko juu zaidi kwa sifa zake nzuri nzuri, na yuko juu zaidi katika vitendo vyake. Alikishinda kila kitu, na viumbe vyote vinamnyenyekea Yeye. "Mwenye hekima," kwa kuwa anaweka kila kitu mahali pake miongoni mwa viumbe na sheria zake mbalimbali.
#
{52} {وكذلك} حين أوحينا إلى الرسل قبلك، {أوحَيْنا إليك رُوحاً من أمرِنا}: وهو هذا القرآن الكريم، سمَّاه روحاً؛ لأنَّ الروح يحيا به الجسدُ، والقرآن تحيا به القلوبُ والأرواح، وتحيا به مصالحُ الدُّنيا والدين؛ لما فيه من الخير الكثير والعلم الغزير، وهو محضُ منَّة الله على رسولِهِ وعباده المؤمنين من غير سببٍ منهم، ولهذا قال: {ما كنتَ تَدْري}؛ أي: قبل نزوله عليك {ما الكتابُ ولا الإيمانُ}؛ أي: ليس عندك علمٌ بأخبار الكتب السابقة، ولا إيمانٌ وعملٌ بالشرائع الإلهيَّة، بل كنت أميًّا لا تخطُّ ولا تقرأ، فجاءك هذا الكتابُ الذي {جَعَلْناه نوراً نَهدي به من نشاءُ من عبادِنا}: يستضيئون به في ظُلُماتِ الكفر والبدع والأهواء المُرْدِيَة، ويعرِفون به الحقائقَ، ويهتدون به إلى الصراط المستقيم. {وإنَّك لَتَهْدي إلى صراط مستقيم}؛ أي: تبيِّنُه لهم، وتوضِّحه، [وتنيره] وترغِّبهم فيه، وتَنْهاهم عن ضدِّه، وترهِّبهم منه.
{52} "Na namna hivi" tulivyowateremshia ufunuo Mitume wa kabla yako, "tumekufunulia roho (Qur-ani) kwa amri yetu." Mwenyezi Mungu ameiita Qur-ani roho kwa sababu roho huhuisha mwili, nayo Qur-ani inahuisha nyoyo na nafsi, na masilahi ya kidunia na ya kidini yanakuwa sawa kwayo. Kwa sababu ndani yake kuna heri nyingi na elimu tele. Nayo ni neema tupu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake na waja wake waumini bila ya wao kufanya sababu yoyote ya kuipata. Ndiyo maana akasema: "Ulikuwa hujui Kitabu ni nini wala Imani" kabla ya hicho kuteremshwa kwako, na hata hukuwa unajua Vitabu vilivyotangulia. Bali ulikuwa hujui kusoma na kuandika, kisha kikakukujia Kitabu hiki ambacho "tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunamwongoa tumtakaye katika waja wetu," ambacho wanajiangazia kwacho katika viza vya ukafiri, uzushi na matamanio mabaya yaangamizayo, na kwayo wanajua uhakika wa mambo, na wanaongoka kwayo kufikia njia iliyonyooka. "Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyonyooka." Yaani, unawafafanulia njia hiyo, kuwawekea wazi, [kuwaangazia], kuwahimiza juu yake, kuwakataza kinyume chake na unawakatisha moyo juu yake.
#
{53} ثم فسَّر الصراط المستقيم، فقال: {صراطِ الله الذي له ما في السمواتِ وما في الأرضِ}؛ أي: الصراط الذي نَصَبَهُ الله لعبادِهِ وأخبرهم أنَّه موصلٌ إليه وإلى دار كرامتِهِ. {ألا إلى الله تصيرُ الأمورُ}؛ أي: ترجِعُ جميع أمورِ الخير والشرِّ، فيجازي كلاًّ بعملِهِ ؛ إنْ خيراً فخيرٌ وإن شرًّا فشرٌّ.
{53} Kisha akabainisha njia hiyo iliyonyooka, akasema: "Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi," ambayo aliwawekea waja wake na akawajulisha kwamba hiyo ndiyo inayofikisha kwake na kwa nyumba ya utukufu wake. "Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu," ya heri na maovu, kisha atamlipa kila mmoja kwa matendo yake. Ikiwa ni mazuri, basi kwa uzuri. Na ikiwa ni maovu, basi kwa uovu.
Imekamilika tafsiri ya Surat Ash-Shura. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, mwanzo na mwisho, kwa dhahiri na kwa ndani, kwa sababu ya urahisishaji wake.
* * *