:
Tafsiri ya Surat Fusswilat
Tafsiri ya Surat Fusswilat
Ilishuka Makka
: 1 - 8 #
{حم (1) تَنْزِيلٌ مِنَ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ (2) كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ (3) بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ (4) وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِنْ بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ (5) قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ يُوحَى إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ وَوَيْلٌ لِلْمُشْرِكِينَ (6) الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ (7) إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ (8)}.
1. Ha Mim 2. Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu. 3. Hiki ni Kitabu kilichopambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanaojua. 4. Kitoacho habari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii. 5. Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi hakika tunatenda. 6. Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanaomshirikisha. 7. Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera. 8. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, watakuwa na ujira usio na ukomo.
#
{2} يخبر تعالى عبادَه أنَّ هذا الكتاب الجليل والقرآن الجميل {تنزيلٌ}: صادر {من الرحمنِ الرحيم}: الذي وسعتْ رحمتُه كلَّ شيء، الذي من أعظم رحمته وأجلِّها إنزال هذا الكتاب، الذي حصل به من العلم والهدى والنور والشفاء والرحمة والخير الكثير ما هو من أجلِّ نعمِهِ على العباد، وهو الطريق للسعادة في الدارين.
{2} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha waja wake kwamba Kitabu hiki kitukufu na Qur-ani yenye heshima kubwa "ni uteremsho uliotoka kwa Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu," ambaye rehema yake imekienea kila kitu, na ambaye katika rehema yake kubwa na tukufu zaidi ni kukiteremsha kitabu hiki ambacho kupitia kwacho ilipatikana elimu, uwongofu, nuru, uponyaji, rehema na heri nyingi ambazo ni katika neema kubwa zaidi juu ya waja wake; nacho ndicho njia ya furaha katika nyumba hizi mbili.
#
{3} ثم أثنى على الكتاب بتمام البيان، فقال: {فُصِّلَتْ آياتُه}؛ أي: فُصِّلَ كلُّ شيء من أنواعه على حِدَتِهِ، وهذا يستلزمُ البيان التامَّ والتفريق بين كلِّ شيء وتمييز الحقائق، {قرآناً عربيًّا}؛ أي: باللغة الفصحى أكمل اللغات، فصلت آياتُهُ وجُعِلَ عربيًّا. {لقوم يَعْلَمونَ}؛ أي: لأجل أن يتبيَّنَ لهم معناه كما يتبيَّن لفظه، ويتَّضحَ لهم الهدى من الضلال والغيُّ من الرشاد، وأمَّا الجاهلون الذين لا يزيدُهم الهدى إلاَّ ضلالاً ولا البيانُ إلا عمىً؛ فهؤلاء لم يَسُقِ الكلامَ لأجلهم، و {سواء عليهم أأنذرتهم أم لم تنذِرْهم لا يؤمنون}.
{3} Kisha akakisifu kitabu hiki kwa maelezo kamili, akasema: "kilipambanuliwa Aya zake," ambapo kila kitu cha aina yake kilifafanuliwa kivyake, jambo ambalo linalazimu kutimia kwa ubainifu kamili na upambanuzi baina ya kila kitu na kuyatenga kando mambo ya uhakika mbali na yasiyokuwa ya uhakika. "Kinachosomwa kwa Kiarabu," chenye ufasaha wa kikale, ambayo ndiyo lugha kamili zaidi "kwa watu wanaojua." Ili maana zake ziwabainikie kama zilivyowabainikia lafudhi zake, na uwawiye wazi uongofu wake mbali na upotofu, na ukengeufu mbali na unyoofu. Na ama wajinga ambao uongofu huu hauwaongezi isipokuwa upotofu, wala ubainisho hauwaongezi isipokuwa upofu, basi hao maneno haya hayakusemwa kwa ajili yao; kwani "ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini."
#
{4} {بشيراً ونذيراً}؛ أي: بشيراً بالثواب العاجل والآجل، ونذيراً بالعقاب العاجل والآجل، وذكر تفصيلَهما، وذكر الأسبابَ والأوصاف التي تحصل بها البشارةُ والنذارةُ، وهذه الأوصاف للكتاب مما يوجب أن يُتَلَقَّى بالقَبول والإذعان والإيمان والعمل به، ولكن أعرض أكثر الخلق عنه إعراض المستكبرين، {فهم لا يسمعون}: له سماع قبول وإجابةٍ، وإن كانوا قد سمِعوه سماعاً تقوُم عليهم به الحجَّة الشرعيَّة.
{4} "Kitoacho habari njema na chenye kuonya." Yaani, kinaleta bishara ya malipo mema ya haraka na ya baadaye, na kinaonya kutokana na adhabu ya haraka na ya baadaye. Kisha akataja maelezo yake ya kina na akataja sababu na sifa ambazo kwazo inapatikana bishara njema na maonyo. Na sifa hizi za kitabu hiki ni katika mambo yanayolazimu kwamba Kitabu hiki kipokelewe kwa kukubaliwa, kujisalimisha kwake, kukiamini na kukifanyia kazi, lakini wengi wa viumbe walikipa mgongo kama wanavyofanya wale wanaotakabari. "Kwa hivyo hawasikii" usikivu wa kukikubali na kukiitikia, ingawa walikisikia kusikia kwa kunakowasimamishia hoja ya kisheria juu yao.
#
{5} {وقالوا}؛ أي: هؤلاء المعرضون عنه مبيِّنين عدم انتفاعهم به بسدِّ الأبواب الموصلة إليه: {قلوبُنا في أكِنَّةٍ}؛ أي: أغطية مغشَّاة، {مما تَدْعونا إليه وفي آذاننا وقرٌ}؛ أي: صمم فلا نسمع لك {ومن بيننا وبينِك حجابٌ}: فلا نراك؛ القصدُ من ذلك أنَّهم أظهروا الإعراض عنه من كلِّ وجه، وأظهروا بُغْضَه والرِّضا بما هم عليه، ولهذا قالوا: {فاعْمَلْ إنَّنا عاملون}؛ أي: كما رضيت بالعمل بدينك؛ فإنَّنا راضون كلَّ الرضا بالعمل في ديننا، وهذا من أعظم الخذلان؛ حيث رضوا بالضَّلال عن الهدى، واستبدلوا الكفرَ بالإيمان، وباعوا الآخرةَ بالدنيا.
{5} "Na wakasema" hao waliokipa mgongo wakibainisha kutokunufaika kwao nacho kwa sababu ya kufungiwa milango ya kukifikia: "Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia, na masikio yetu yana uziwi" basi hatusikii, "na baina yetu na wewe lipo pazia" basi hatuwezi kukuona. Makusudio yao katika hayo ni kuwa walionyesha kujitenga kwao mbali nacho kwa kila namna, na wakaonyesha chuki yao juu yake na kuridhika kwao na yale waliyokuwa nayo,ndiyo maana wakasema: "Basi wewe tenda, nasi hakika tunatenda." Kama ulivyoridhia kufanya kazi kulingana na dini yako, basi pia sisi hakika tumeridhia kabisa kufanya kazi kulingana na dini yetu. Na hili ni katika kuachiliwa mbali na Mwenyezi Mungu kukubwa zaidi. Ambapo waliridhia upotofu mbali na uwongofu, na wakabadilisha imani kwa ukafiri, na wakaiuza akhera kwa dunia.
#
{6 - 7} {قل}: لهم يا أيُّها النبيُّ: {إنَّما أنا بشرٌ مثلُكُم يوحى إليَّ}؛ أي: هذه صفتي ووظيفتي: أني بشرٌ مثلكم، ليس بيدي من الأمر شيء، ولا عندي ما تستعجِلون به، وإنَّما فضَّلني الله عليكم وميَّزني وخصَّني بالوحي الذي أوحاه إليَّ وأمرني باتِّباعه ودعوتِكُم إليه. {فاستَقيموا إليه}؛ أي: اسلكوا الصراط الموصل إلى الله تعالى بتصديقِ الخبر الذي أخبر به واتِّباع الأمر واجتناب النهي، هذا حقيقة الاستقامة، ثم الدوام على ذلك، وفي قوله: {إليه}: تنبيهٌ على الإخلاص، وأنَّ العامل ينبغي له أن يَجْعَلَ مقصودَه وغايتَه التي يعمل لأجلها الوصولَ إلى الله وإلى دار كرامتِهِ؛ فبذلك يكون عملُه خالصاً صالحاً نافعاً، وبفواتِهِ يكون عملُه باطلاً. ولمَّا كان العبدُ ولو حَرَصَ على الاستقامةِ لا بدَّ أن يحصلَ منه خللٌ بتقصير بمأمور أو ارتكاب منهيٍّ؛ أمره بدواء ذلك بالاستغفار المتضمِّن للتوبة، فقال: {واستغفِروه}، ثم توعَّد من ترك الاستقامة فقال: {وويلٌ للمشركينَ. الذين لا يُؤتونَ الزَّكاةَ}؛ أي: الذين عَبَدوا من دونِهِ مَنْ لا يملك نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، ودسُّوا أنفسهم فلم يزكُّوها بتوحيد ربِّهم والإخلاص له، ولم يُصَلُّوا ولا زَكَّوْا؛ فلا إخلاص للخالق بالتوحيد والصلاةِ، ولا نفع للخلق بالزَّكاة وغيرها. {وهم بالآخرةِ هم كافرونَ}؛ أي: لا يؤمنون بالبعث ولا بالجنة والنار؛ فلذلك لما زال الخوفُ من قلوبهم؛ أقدموا على ما أقدموا عليه مما يضرُّهم في الآخرة.
{6 - 7} "Sema" ewe Nabii ukiwaambia: "Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu." Yaani, hii ndiyo sifa yangu na jukumu langu kwamba: Mimi ni binadamu kama nyinyi ambaye sina langu jambo katika suala hili, wala sina hicho mnachokiharakishia. Ni Mwenyezi Mungu tu aliyeniboresha juu yenu kwa wahyi alioniteremshia na akaniamrisha niufuate na nikuiteni katika huo. "Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye" kwa kufuata njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kusadiki habari alizopeana, na kwa kufuata amri zake na kujiepusha na makatazo yake. Huu ndio uhakika wa unyoofu. Kisha dumuni hivyo. Na kuna tanbihi katika kauli yake: "kumwendea Yeye" juu ya kuwa na ikhlas, na kwamba mtendaji matendo anafaa kufanya lengo lake na nia yake anazozifanyia matendo ni kumfikia Mwenyezi Mungu na kwenye makao ya utukufu wake. Kwa hivyo, yanakuwa matendo yake hayo ni ya kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, mema, yenye kunufaisha, na ikiwa hayo yatakosekana, basi matendo yake hayo yanakuwa batili. Kwa kuwa mja, hata ikiwa atafanya bidii kubwa ya kunyooka, ni lazima atapatwa na kasoro kwa kutofanya vyema jambo lililoamrishwa au kutenda lililoharamishwa; akamuamrisha ponya ya hilo ambayo ni kuomba msamaha unaojumuisha toba, akasema: "na mtakeni msamaha." Kisha akawatishia kwa adhabu wale walioacha kunyooka, akasema: "Na ole wao wanaomshirikisha. Ambao hawatoi Zaka," ambao waliabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawamiliki manufaa yoyote, madhara, mauti, uhai wala ufufuo, na wakajichafua nafsi zao na hawakujitakasa kwa kumpwekesha Mola wao Mlezi na kumkusudia Yeye tu, na pia hawakuswali wala hawakumtoa Zaka. Kwa hivyo, hawakumkusudia Muumba kwa kumpwekesha na kuswali, na wala hawakuwanufaisha viumbe kwa kuwapa Zaka na vitu vinginevyo. "Na wanaikataa Akhera." Yaani, hawaamini ufufuo wala Bustani za mbinguni wala Moto. Ndiyo maana hofu ilipoondoka nyoyoni mwao, wakafanya hayo waliyoyafanya, miongoni mwa mambo ya kuwadhuru katika maisha ya akhera.
#
{8} ولما ذَكَرَ الكافرين؛ ذَكَرَ المؤمنين ووَصْفَهم وجزاءهم، فقال: {إن الذين آمنوا}: بهذا الكتاب وما اشتمل عليه ممَّا دعا إليه من الإيمان وصدَّقوا إيمانَهم بالأعمال الصالحة الجامعة للإخلاص والمتابعة، {لهم أجرٌ}؛ أي: عظيم {غيرُ ممنونٍ}؛ أي: غير مقطوع ولا نافذٍ، بل هو مستمرٌّ مدى الأوقات، متزايدٌ على الساعات، مشتملٌ على جميع اللذَّات والمشتَهَيات.
{8} Na alipowataja makafiri, akawataja Waumini, maelezo yao na malipo yao, akasema: "Hakika wale walioamini" kitabu hiki, na yale yaliyomo ndani yake, ambayo kinayalingania ya imani, na wakaisadiki imani yao hiyo kwa matendo mema yanayojumuisha kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake na kumfuata Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, "watakuwa na ujira usio na ukomo." Utaendelea muda wa kuendelea kwa wakati, na utaongezeka katika kila masaa, na utajumuisha raha na matamanio yote.
: 9 - 12 #
{قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَنْدَادًا ذَلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ (9) وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِنْ فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِلسَّائِلِينَ (10) ثُمَّ اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ (11) فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَى فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا وَزَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَحِفْظًا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ (12)}.
9. Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa yule aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote. 10. Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanaouliza. 11. Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu. 12. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hiki ndicho kipimo cha Mwenye Nguvu, ajuaye zaidi.
#
{9 - 10} ينكرُ تعالى ويَعَجّب من كفر الكافرين به، الذين جعلوا معه أنداداً، يُشْرِكونهم معه، ويبذُلون لهم ما يشاؤون من عباداتهم، ويسوُّونهم بالربِّ العظيم الملك الكريم، الذي خلق الأرض الكثيفة العظيمة في يومين، ثم دحاها في يومين؛ بأن جعل فيها رواسيَ من فوقها تُرْسيها عن الزوال والتزلزل وعدم الاستقرارِ؛ فكمَّل خلقها ودحاها وأخرج أقواتها وتوابعَ ذلك {في أربعةِ أيام سواءً للسائلين}: عن ذلك؛ فلا ينبِّئك مثلُ خبير؛ فهذا الخبر الصادق الذي لا زيادة فيه ولا نقص.
{9 - 10} Mola Mtukufu anakanusha na kustaajabia ukafiri wa makafiri waliomkufuru, ambao walimfanyia wenza, wakiwashirikisha pamoja naye na kuwafanyia chochote wanachotaka katika ibada zao, na kuwafanya sawa na Mola Mlezi, Mkuu, Mfalme Mtukufu, ambaye aliumba ardhi kubwa hii katika siku mbili, kisha akaitandaza kwa siku mbili; kwa kuweka humo milima madhubuti kwa juu yake ili iilinde kutokana na kuondoka, kutikisika na kutotulia. Basi akakamilisha uumbaji wake, akaitandaza, na akatia humo vyakula vyake, na yote yanayofuatana na hayo "katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanaouliza" kuhusu hilo. Na hapana atakayekupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari zote. Basi hii ndiyo habari ya ukweli isiyokuwa na nyongeza wala kupunguzwa.
#
{11} {ثم}: بعد أن خَلَقَ الأرض {استوى}؛ أي: قصد {إلى}: خلق {السماء وهي دخانٌ}: قد ثار على وجه الماء، {فقال لها}: ولمَّا كان هذا التخصيصُ يوهِمُ الاختصاص؛ عَطَفَ عليه بقوله: {وللأرض ائْتِيا طوعاً أو كَرْهاً}؛ أي: انقادا لأمري طائعتين أو مُكْرَهَتَيْن؛ فلا بدَّ من نفوذه، {قالتا أتَيْنا طائعينَ}؛ أي: ليس لنا إرادةٌ تخالف إرادتك.
{11} "Kisha" baada ya kuiumba ardhi "akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi" uliokuwa umetanda juu ya uso wa maji, "akaziambia hizo na ardhi: 'Njooni, kwa hiari au kwa nguvu!' Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu." Hatuna utashi unaotofautiana na utashi wako.
#
{12} {فقضاهنَّ سبعَ سمواتٍ في يومين}: فتمَّ خلقُ السماواتِ والأرض في ستة أيام؛ أولها يوم الأحد، وآخرها يوم الجمعة، مع أنَّ قدرةَ الله ومشيئتَه صالحةٌ لخلق الجميع في لحظة واحدة، ولكن مع أنَّه قدير؛ فهو حكيمٌ رفيقٌ؛ فمن حكمته ورفقه أن جعل خَلْقَها في هذه المدة المقدرة. واعلم أنَّ ظاهر هذه الآية مع قوله تعالى في النازعات لما ذَكَرَ خَلْقَ السماواتِ؛ قال: {والأرضَ بعد ذلك دحاها}: يَظْهَرُ منهما التعارضُ! مع أنَّ كتاب الله لا تعارض فيه ولا اختلاف! والجواب عن ذلك ما قاله كثير من السلف: أنَّ خلقَ الأرض وصورتَها متقدِّم على خلق السماواتِ كما هنا. ودَحْيُ الأرض بأن {أخرجَ منها ماءها ومَرْعاها. والجبالَ أرساها}: متأخِّرٌ على خلقِ السماوات؛ كما في سورة النازعات، ولهذا قال [فيها]: {والأرضَ بعد ذلك دَحاها. أخْرَجَ منها ... } إلى آخره، ولم يقلْ: والأرضَ بعد ذلك خَلَقها. وقوله: {وأوحى في كلِّ سماءٍ أمرَها}؛ أي: الأمر والتدبير اللائقَ بها، التي اقتضتْه حكمةُ أحكم الحاكمين، {وزيَّنَّا السماء الدُّنيا بمصابيحَ}: هي النجوم؛ يُستنار بها ويُهتدى، وتكون زينةً وجمالاً للسماء ظاهراً وجمالاً لها باطناً بجعلها رجوماً للشياطين؛ لئلاَّ يسترق السمعَ فيها. {ذلك}: المذكور من الأرض وما فيها والسماء وما فيها {تقديرُ العزيز العليم}: الذي عزَّتُه قَهَرَ بها الأشياء ودبَّرها وخَلَق بها المخلوقات. {العليم} الذي أحاط علمُهُ بالمخلوقات والغائب والشاهد. فترك المشركين الإخلاصَ لهذا الربِّ العظيم الواحد القهَّار، الذي انقادتِ المخلوقاتُ لأمره، ونفذَ فيها قدرُه من أعجب الأشياء، واتِّخاذهم له أنداداً يسوُّونهم به وهم ناقصون في أوصافهم وأفعالهم أعجب وأعجب، ولا دواء لهؤلاء إن استمرَّ إعراضُهم إلاَّ العقوبات الدنيويَّة والأخرويَّة؛ فلهذا خوَّفهم بقوله:
{12} "Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili," kwa hivyo uumbaji wa mbingu na ardhi ukakamilika katika siku sita; ya kwanza yake ikiwa ni siku ya Jumapili na ya mwisho yake ikiwa ni siku ya Ijumaa, ingawa uwezo wa Mwenyezi Mungu na mapenzi yake yanaweza kuumba vyote hivyo katika wakati mmoja. Lakini Yeye ni mwenye uwezo wote, Yeye ni mwenye hekima, mpole. Katika hekima yake na upole wake ni kwamba aliviumba hivi katika kipindi hiki kilichopimwa. Jua kwamba kuna dhana ya kupingana katika maana ya dhahiri ya Aya hii na kauli yake Mtukufu katika Surat Naziat, pale alipotaja kuumbwa kwa mbingu, akasema: "Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi." Ingawa hakuna kupingana au kutofautiana katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu! Jibu la hilo ni kama walivyosema wengi wa wema waliotangulia kwamba: kuumbwa kwa ardhi na kuitia sura kulitangulia kuumbwa mbingu kama ilivyo hapa. Na maana ya kuitandaza ardhi ni kwamba "alitoa ndani yake maji yake na malisho yake. Na milima akaisimamisha" baada ya kuumbwa mbingu. Kama ilivyo katika Surat An-Nazi'at. Ndiyo maana akasema [ndani yake]: "Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. Akatoa ndani yake." Hadi mwisho wa aya hizi. Na wala hakusema: 'Na baada ya hayo,akaiumba ardhi.' Na kauli yake: "na akazipangia kila mbingu mambo yake" yanayolingana nayo, ambayo yalihitajiwa na hekima ya muadilifu kuliko mahakimu wote. "Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa" ambayo ni nyota. Kwazo watu wanapata mwangaza na kuongozwa njia, nazo pia ni pambo na urembo kwa mbingu, na tena zinatumika katika kuwapiga vimondo mashetani; ili wasisikilize kwa siri mambo ya huko. "Hiki" kilichotajwa kuhusiana na ardhi na vilivyomo ndani yake, na mbingu na vilivyomo ndani yake, "ndicho kipimo cha Mwenye Nguvu, ajuaye zaidi." Ambaye nguvu yake ilishinda vitu vyote, ikaviendesha, na kwayo akaumba viumbe vyote. "Ajuaye zaidi," ambaye elimu imewazunguka viumbe, na mambo ya ghaibu na yale yanayoonekana. Basi washirikina kuacha kumkusudia Mola huyu Mlezi, Mkuu, Mmoja, Mshindi, ambaye viumbe vinanyenyekea kwa amri yake, na inatekelezeka kwao mipangilio yake, ni miongoni mwa mambo ya ajabu sana. Na kumfanyia wenza, wakawafanya sawa naye ilhali wenza hao ni wapungufu katika sifa zao na vitendo vyao ni jambo la kushangaza zaidi. Na hakuna dawa kwa watu hawa ikiwa wataendelea kupeana mgongo isipokuwa adhabu za duniani na za akhera; Ndiyo maana akawatia hofu kwa kauli yake:
: 13 - 14 #
{فَإِنْ أَعْرَضُوا فَقُلْ أَنْذَرْتُكُمْ صَاعِقَةً مِثْلَ صَاعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ (13) إِذْ جَاءَتْهُمُ الرُّسُلُ مِنْ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّهَ قَالُوا لَوْ شَاءَ رَبُّنَا لَأَنْزَلَ مَلَائِكَةً فَإِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُمْ بِهِ كَافِرُونَ (14)}.
13. Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya 'Adi na Thamudi. 14. Walipowajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angelitaka Mola wetu Mlezi, bila ya shaka angeliwateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.
#
{13 - 14} أي: فإن أعرض هؤلاء المكذِّبون بعدما بُيِّنَ لهم من أوصافِ القرآن الحميدة ومن صفات الإله العظيم، {فقل أنذرتُكم صاعقةً}؛ أي: عذاباً يستأصِلكم ويجتاحُكم، {مثل صاعقة عادٍ وثمودَ}: القبيلتين المعروفتين؛ حيث اجتاحهم العذابُ، وحلَّ عليهم وَبيل العقاب، وذلك بظلمهم وكفرهم؛ حيث {جاءتهم الرسل من بين أيديهم ومن خلفهم}؛ أي: يَتْبَع بعضهم بعضاً متوالين، ودعوتُهم جميعاً واحدة: {أن لا تَعْبُدوا إلاَّ الله}؛ أي: يأمرون بالإخلاص لله، ويَنْهَوْنَهم عن الشرك به، فردُّوا رسالتهم وكذَّبوهم، و {قالوا لو شاء ربُّنا لأنزل ملائكةً}؛ أي: وأما أنتم؛ فبشرٌ مثلنا، {فإنَّا بما أرْسِلْتم به كافرون}: وهذه الشبهة لم تزل متوارثةً بين المكذِّبين بالأمم، وهي من أوهى الشُّبه؛ فإنَّه ليس من شرط الإرسال أن يكون المرسل ملكاً، وإنَّما شرط الرسالة أن يأتي الرسول بما يدلُّ على صدقه، فليقدحوا إن استطاعوا بصدقِهم بقادح عقليٍّ أو شرعيٍّ، ولن يستطيعوا إلى ذلك سبيلاً.
{13 - 14} Yaani, iwapo hawa wanaokadhibisha watapeana mgongo, baada ya kubainishiwa maelezo ya Qur-ani yenye kusifiwa na baada ya kuelezewa sifa za Mungu Mkuu, "wewe sema: 'Nakuhadharisheni adhabu'" ya kuwang'oeni na kuwafagilieni mbali, "mfano wa adhabu ya 'Adi na Thamudi," ambao ni makabila mawili mashuhuri; ambao adhabu iliwaangamiza wote kwa sababu ya dhuluma yao na ukafiri wao. "Walipowajia Mitume mbele yao na nyuma yao," wakifuatana mmoja baada ya mwingine huku wote wakilingania kwa kitu kimoja, "wakawaambia: 'Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu!'" Yaani, waliwaamrisha wamkusudie Mwenyezi Mungu peke yake na wakawakataza kumshirikisha, lakini wakaukataa ujumbe wao na wakawakadhibisha, na "wakasema: 'Angelitaka Mola wetu Mlezi bila ya shaka angeliwateremsha Malaika." Ama nyinyi, basi ni wanadamu tu kama sisi. "Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyotumwa nayo." Dhana hii potofu ingali inarithiwa baina ya umma miongoni mwa wale wanaokadhibisha, lakini ni miongoni mwa dhana potofu zisizo na nguvu zaidi. Kwani siyo katika masharti ya kutuma kwamba aliyetumwa awe malaika, bali sharti la kutumwa kama mjumbe ni mjumbe huyo kuleta kitu ambacho kinathibitisha ukweli wake. Kwa hivyo, na watie dosari katika ukweli wake kwa dosari ya kiakili au ya kisheria kama wataweza, na kamwe hawataweza kufanya hivyo.
: 15 - 16 #
{فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ (15) فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَحِسَاتٍ لِنُذِيقَهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَى وَهُمْ لَا يُنْصَرُونَ (16)}.
15. Ama kina 'Adi, hao walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Ni nani mwenye nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliyewaumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu! 16. Basi tukawatumia upepo wa kimbunga katika siku za misiba, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.
Haya sasa ndiyo maelezo ya kina ya hadithi ya mataifa haya mawili; 'Adi na Thamudi:
#
{15} فأمَّا عادٌ؛ فكانوا مع كفرهم بالله وجحدهم بآيات الله وكفرهم برسله مستكبرين {في الأرض} قاهرين لمن حولَهم من العباد ظالمين لهم قد أعجبتهم قُوَّتُهم، {وقالوا مَنْ أشدُّ منا قُوَّةً}: قال تعالى ردًّا عليهم بما يعرفه كلُّ أحدٍ: {أولم يَرَوا أنَّ الله الذي خلقهم هو أشدُّ منهم قوةً}: فلولا خلقُه إيَّاهم؛ لم يوجدوا؛ فلو نظروا إلى هذه الحال نظراً صحيحاً؛ لم يغترُّوا بقوَّتِهم.
{15} Ama 'Adi; wao pamoja na kumkufuru kwao Mwenyezi Mungu, na kukataa kwao ishara zake, kuwakufuru kwao Mitume wake, walikuwa "wakijivuna katika nchi" huku wamewashinda wale waliokuwa pembezoni mwao miongoni mwa waja kwa kuwadhulumu kwa sababu ya kujiona na nguvu zao. "Na wakasema: Ni nani aliyekuwa na nguvu kushinda sisi?" Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akiwajibu kwa kile ambacho kila mtu anakijua: "Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliyewaumba ni Mwenye nguvu kushinda wao?" Kwani, kama hangewaumba, basi hawangekuwepo. Basi kama wangeangalia hali hii kwa njia sahihi, hawangedanganyika na nguvu zao hizo.
#
{16} فعاقبهم الله عقوبةً تناسب قوَّتهم التي اغترُّوا بها، {فأرسلنا عليهم ريحاً صرصراً}؛ أي: ريحاً عظيمةً من قوتها وشدَّتها، لها صوتٌ مزعجٌ كالرعد القاصف، فسخَّرها الله {عليهم سبعَ ليالٍ وثمانيةَ أيَّام حسوماً فترى القومَ فيها صرعى كأنَّهم أعجازُ نخل خاويةٍ}، {نحسات}: فدمَّرتهم وأهلكتهم فأصبحوا لا يُرى إلاَّ مساكنُهم، وقال هنا: {لنذيقَهم عذابَ الخِزْي في الحياة الدُّنيا}: الذي اختزوا به وافتُضِحوا بين الخليقة، {ولَعذابُ الآخرة أخزى وهم لا يُنصَرونَ}؛ أي: لا يُمنعون من عذاب الله، ولا يَنْفَعون أنفسَهم.
{16} Basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa adhabu iliyozifailia nguvu zao hizo walizodanganywa nazo; "Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga" wenye sauti ya kusumbua kama vile radi inapopiga, basi Mwenyezi Mungu "akautuma juu yao usiku saba na michana minane mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kana kwamba ni magongo ya mitende yaliyo wazi ndani," nazo siku hizo zilikuwa "za mikosi." Kwa hivyo, ukawaangamiza na ukawafutilia mbali, na wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Na katika aya hii akasema: "na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa," na wala wenyewe hawataweza kujinufaisha.
: 17 - 18 #
{وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَى عَلَى الْهُدَى فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (17) وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ (18)}.
17. Na ama Thamudi, hao tuliwaongoza, lakini walipenda upofu kuliko uwongofu. Basi ukawachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehesha kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma. 18. Na tukawaokoa wale walioamini na wakawa wanamcha Mungu.
#
{17} {وأما ثمودُ}: وهم القبيلة المعروفة، الذين سكنوا الحجرَ وحواليه، الذين أرسل الله إليهم صالحاً عليه السلام يدعوهم إلى توحيدِ ربِّهم وينهاهم عن الشرك، وآتاهم الله الناقةَ آيةً عظيمةً لها شِربٌ ولهم شِربُ يوم معلوم، يشربون لبنَها يوماً ويشربون من الماء يوماً، وليسوا ينفقون عليها، بل تأكل من أرض الله، ولهذا قال هنا: {وأمَّا ثمودُ فهَدَيْناهم}؛ أي: هداية بيان، وإنما نصَّ عليهم، وإن كان جميع الأمم المهلكة قد قامتْ عليهم الحجَّةُ وحصل لهم البيانُ؛ لأن آية ثمودَ آيةٌ باهرةٌ قد رآها صغيرهم وكبيرهم وذكرهم وأنثاهم، وكانت آيةً مبصرةً، فلهذا خصَّهم بزيادة البيان والهدى، ولكنَّهم من ظلمهم وشرِّهم استحبُّوا {العمى} الذي هو الكفر والضلال {على الهدى} الذي هو العلم والإيمان، فأخذهم {العذاب} بما كانوا يكسِبون، لا ظُلماً من الله لهم.
{17} "Na ama Thamudi" nao ni kabila mashuhuri waliokuwa wakiishi Al-Hijr na viunga vyake, ambao Mwenyezi Mungu aliwatumia Nabii Swaleh, amani iwe juu yake, akiwalingania kumpwekesha Mola wao Mlezi na akiwakataza shirki. Mwenyezi Mungu aliwapa ngamia wa kike iwe ni ishara kubwa kwao. Awe akinywa maji siku yake bila ya wao kumtunza. Bali alikuwa akila mwenyewe katika ardhi ya Mwenyezi Mungu. Ndiyo maana akasema hapa: "Na ama Thamudi, tuliwaongoza." Hapa alitaja hasa suala la kuwaongoza pamoja na kwamba umma wote walioangamizwa walisimamishiwa hoja na wakabainishiwa mambo, kwa sababu ishara ya akina Thamud ni ishara inayong’aa sana, waliyoiona wadogo wao na wakubwa wao, wa kiume wao na wa kike wao, nayo ilikuwa ishara ya kuonekana wazi. Ndiyo maana akawataja hasa kwamba aliwabainishia na kuwaongoza zaidi, lakini kwa sababu ya dhuluma yao na uovu wao wakapendelea "upofu" ambao ni ukafiri na upotofu "kuliko uwongofu" ambao ni elimu na imani, basi ikawachukua "adhabu" kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma, na sio kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwadhulumu.
#
{18} {ونجَّيْنا الذين آمنوا وكانوا يتَّقونَ}؛ أي: نجَّى الله صالحاً عليه السلام ومن اتَّبعه من المؤمنين المتَّقين للشرك والمعاصي.
{18} "Na tukawaokoa wale walioamini," yaani Nabii Swaleh na wale waliomfuata miongoni mwa waumini, "na wakawa wanamcha Mungu" kwa kujiepusha na shirki.
: 19 - 24 #
{وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ (19) حَتَّى إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (20) وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدْتُمْ عَلَيْنَا قَالُوا أَنْطَقَنَا اللَّهُ الَّذِي أَنْطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (21) وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَكِنْ ظَنَنْتُمْ أَنَّ اللَّهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِمَّا تَعْمَلُونَ (22) وَذَلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنْتُمْ بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ مِنَ الْخَاسِرِينَ (23) فَإِنْ يَصْبِرُوا فَالنَّارُ مَثْوًى لَهُمْ وَإِنْ يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُمْ مِنَ الْمُعْتَبِينَ (24)}.
19. Na siku watakapokusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao wakigawanywa kwa makundi. 20. Hata watakapoufikia Moto, yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. 21. Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye alitamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa. 22. Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika yale mliyokuwa mkiyatenda. 23. Basi hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi, imekuangamizeni; na mmekuwa miongoni mwa waliohasiri. 24. Basi wakisubiri, Moto ndio maskani yao. Na wakiomba radhi, hawakubaliwi.
#
{19} يخبر تعالى عن أعدائه الذين بارزوه بالكفر به وبآياتِهِ وتكذيب رسلِهِ ومعاداتهم ومحاربتهم وحالِهِم الشنيعةِ حين يُحشرونَ؛ أي: يجمعون {إلى النار فهم يُوزَعونَ}؛ أي: يردُّ أولهم على آخرهم، ويتبعُ آخرُهم أوَّلهم، ويساقون إليها سوقاً عنيفاً، لا يستطيعون امتناعاً ولا يَنصرون أنفسَهم ولا هم يُنصرون.
{19} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu maadui zake waliomuasi kwa kumkufuru Yeye na ishara zake, na kuwakadhibisha Mitume wake, na kuwafanyia uadui, na kupigana nao, na hali yao mbaya watakapokusanywa "kwenye Moto, nao wakigawanywa kwa makundi." Hawataweza kukataa wala kujinusuru, wala hawatanusuriwa.
#
{20} {حتى إذا ما جاؤوها}؛ أي: حتى إذا وردوا على النار وأرادوا الإنكارَ أو أنكروا ما عملوه من المعاصي، {شَهِدَ عليهم سمعُهم وأبصارُهم وجلودُهم}: عمومٌ بعد خصوص، {بما كانوا يعملونَ}؛ أي: شهد عليهم كلُّ عضو من أعضائهم؛ فكل عضو يقول: أنا فعلتُ كذا وكذا يوم كذا وكذا، وخصَّ هذه الأعضاء الثلاثة؛ لأنَّ أكثر الذُّنوب إنما تقع بها أو بسببها.
{20} "Hata watakapoufikia Moto" na wakataka kukataa au kukanusha madhambi waliyoyafanya, "yatawashuhudia masikio yao, macho yao na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda." Kila kiungo kitasema: 'Nilifanya hivi na hivi siku fulani na fulani.' Mwenyezi Mungu alivitaja viungo hivi vitatu hasa kwa sababu dhambi nyingi sana hutokea kwa sababu ya hivyo.
#
{21} فإذا شهدتْ عليهم، عاتبوها {وقالوا لجلودِهِم}: هذا دليلٌ على أنَّ الشهادة تقع من كلِّ عضو كما ذكرنا، {لم شهِدتُم علينا}: ونحن ندافعُ عنكنَّ؟ {قالوا أنطَقَنا اللهُ الذي أنطق كلَّ شيءٍ}: فليس في إمكاننا الامتناعُ عن الشهادة حين أنطقنا الذي لا يَستعصي أحد عن مشيئتِهِ ، {وهو خَلَقَكم أولَ مرةٍ}: فكما خلقكم بذواتكم وأجسامِكم؛ خلق أيضاً صفاتِكم، ومن ذلك الإنطاق. {وإليه تُرْجَعون}: في الآخرة، فيجزيكم بما عملتُم. ويُحتمل أنَّ المراد بذلك الاستدلال على البعثِ بالخَلْقِ الأول كما هو طريقة القرآن.
{21} Vitakaposhuhudia dhidi yao, watavilaumu; "Na wao wataziambia ngozi zao." Huu ni ushahidi kwamba ushahidi utatoka kwa kila kiungo chao. "Kwa nini mmeshuhudia dhidi yetu" ilhali sisi tulikuwa tukiwatetea nyinyi? "Nazo zitasema: 'Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu!'" Kwa hivyo, si katika uwezo wetu kukataa kushuhudia wakati alitutamkisha Yule ambaye hakuna yeyote awezaye kuasi mapenzi yake. "Na Yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza." Kwa hivyo, kama alivyowaumba kwa dhati zenu na miili yenu, pia aliumba sifa zenu, na miongoni mwake ni kutamkisha. "Na kwake Yeye tu mtarejeshwa," huko Akhera, kisha awalipe kwa mliyoyatenda. Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni kutumia uumbaji wa kwanza kama ushahidi juu ya ufufuo, kama ilivyo mbinu ya Qur-ani.
#
{22} {وما كنتُم تستَتِرونَ أن يشهدَ عليكم سمعُكم ولا أبصارُكم ولا جلودُكم}؛ أي: وما كنتُم تختفون عن شهادة أعضائكم عليكم ولا تحاذِرون من ذلك. {ولكن ظننتُم}: بإقدامِكم على المعاصي {أنَّ الله لا يعلمُ كثيراً مما تعمَلونَ}: فلذلك صَدَرَ منكم ما صَدَرَ.
{22} "Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, macho yenu na ngozi zenu zisikushuhudilieni." "Lakini mlidhani" mlipoyaendea madhambi, "kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyokuwa mkiyatenda," ndiyo mkafanya hayo mliyoyafanya.
#
{23} وهذا الظنُّ صار سبب هلاكهم وشقائهم، ولهذا قال: {وذلكم ظنُّكم الذي ظَنَنتُم بربِّكم}: الظنَّ السيِّئَ؛ حيث ظننتُم به ما لا يليقُ بجلاله، {أرداكم}؛ أي: أهلككم، {فأصبحتُم من الخاسرين}: لأنفسهم وأهليهم وأديانهم؛ بسبب الأعمال التي أوجَبَها لكم ظنُّكم القبيح بربِّكم. فحقَّتْ عليكم كلمةُ العقاب والشقاءِ، ووجب عليكم الخلودُ الدائم في العذاب، الذي لا يُفَتَّر عنهم ساعة.
{23} Dhana hii ikawa ndiyo sababu ya maangamizo yao na kuwa kwao mashakani, na ndiyo maana akasema: "Basi hiyo dhana yenu" mbaya "mliyokuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi" pale mlipomdhania jambo lisiloufailia utukufu wake, "imekuangamizeni; na mmekuwa miongoni mwa waliohasiri" nafsi zenu, ahali zenu na Dini yenu kwa sababu ya matendo mliyosababishiwa na dhana yenu hiyo mbaya kwa Mola wako Mlezi. Basi limekwisha thibiti neno la adhabu na kuwa mashakani juu yenu, na imeshaamuliwa kwamba mtabaki milele katika adhabu, ambayo hawatapumzishwa kutokana nayo hata saa moja.
#
{24} {فإن يَصْبِروا فالنارُ مثوىً لهم}: فلا جَلَدَ عليها ولا صبرَ، وكلُّ حالة قُدِّرَ إمكانُ الصبر عليها؛ فالنار لا يمكن الصبرُ عليها، وكيف الصبرُ على نار قد اشتدَّ حرُّها وزادت على نار الدنيا بسبعين ضعفاً وعظم غليانُ حميمها وزاد نَتَنُ صديدها وتضاعف بردُ زمهريرِها، وعظُمَتْ سلاسِلُها وأغلالها، وكَبُرَتْ مقامِعها، وغَلُظَ خُزَّانها، وزال ما في قلوبهم من رحمتهم، وختام ذلك سَخَطُ الجبار، وقوله لهم حين يدعونه ويستغيثون: {اخسؤوا فيها ولا تُكَلِّمونِ}. {وإن يَسْتَعْتِبوا}؛ أي: يطلبوا أن يزال عنهم العتبُ، فيرجعوا إلى الدنيا؛ ليستأنفوا العمل، {فما هم من المُعْتَبين}: لأنَّه ذهب وقته، وعُمِّروا ما يُعَمَّر فيه من تذكَّر، وجاءهم النذير، وانقطعت حجتهم، مع أنَّ استعتابهم كذبٌ منهم، فلو رُدُّوا؛ لَعادوا لما نُهوا عنه وإنَّهم لَكاذبون.
{24} "Kwa hivyo, wakisubiri, basi Moto ndio maskani yao." Hawatakuwa na nguvu dhidi yake wala kuuvumilia. Na watawezaje kuwa na subira juu ya moto wenye joto kali zaidi na ukazidi moto wa dunia kwa mizidisho sabini, na wenye maji ya moto yaliyochemka zaidi, na kukazidi kunuka kwa usaha wake, na ukazidi ubaridi wa baridi yake kali, na ikawa mikubwa zaidi minyororo yake na pingu zake, na zikawa kubwa zaidi nyundo zake, na wakawa wakali zaidi walinzi wake, na yakaisha yale ya kuwahurumia yaliyo katika nyoyo zao, na mwishowe wakakasirikiwa na Mola; afanye atakalo, naye akawaambia watakapomuomba msaada: Na kauli yake kwao walipo muomba na kumuomba msaada: "Tokomeeni humo, wala msinisemeshe." "Na wakiomba radhi" ili waweze kurudi duniani waanze kufanya matendo mema, "hawakubaliwi." Kwa sababu muda wake ulikwisha, na wakapewa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia Mwonyaji, na hoja zao zikakatika, pamoja na kwamba kuomba kwao radhi kulikuwa uwongo mtupu. Kwani kama wangelirudishwa, basi bila ya shaka wangeyarejea yale yale waliyokatazwa. Na hakika hao ni waongo.
: 25 #
{وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَاءَ فَزَيَّنُوا لَهُمْ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِمْ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ (25)}.
25. Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyopita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kuhasirika.
#
{25} أي: {وقيَّضْنا}: لهؤلاء الظالمين الجاحدين للحقِّ {قرناءَ}: من الشياطين؛ كما قال تعالى: {ألم تَرَ أنَّا أرسَلْنا الشياطينَ على الكافرين تَؤُزُّهم أزًّا}؛ أي: تزعِجُهم إلى المعاصي، وتحثُّهم عليها، بسبب ما زيّنوا {لهم ما بين أيديهم وما خلفهم}: فالدنيا زخرفوها بأعينهم ودَعَوْهم إلى لذاتها وشهواتها المحرَّمة، حتى افْتَتَنوا فأقدَموا على معاصي الله وسَلَكوا ما شاؤوا من محاربة الله ورسوله، والآخرة بَعَّدوها عليهم وأنْسَوْهم ذِكْرَها، وربما أوقعوا عليهم الشُّبه بعدم وقوعها، فترحَّلَ خوفُها من قلوبهم، فقادوهم إلى الكفر والبدع والمعاصي. وهذا التسليطُ والتقييضُ من الله للمكذِّبين الشياطين بسبب إعراضِهم عن ذِكْرِ الله وآياته وجحودِهم الحقَّ؛ كما قال تعالى: {ومَنْ يَعْشُ عن ذِكْرِ الرحمن نُقَيِّضْ له شيطاناً فهو له قرينٌ. وإنَّهم لَيَصُدُّونَهم عن السبيل ويَحْسَبونَ أنَّهم مهتدونَ}. {وحقَّ عليهم القولُ}؛ أي: وجب عليهم ونزل القضاءُ والقدرُ بعذابهم {في} جملة {أمم قد خَلَتْ من قبلِهِم من الجنِّ والإنس إنَّهم كانوا خاسرين}: لأديانهم وآخرتهم، ومن خَسِرَ؛ فلا بدَّ أن يَذِلَّ ويشقى ويعذَّبَ.
{25} Yaani, "Na tukawaweke" hawa madhalimu waliokataa haki, "marafiki" miongoni mwa mashetani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashetani kwa makafiri wawachochee kwa uchochezi mkubwa" wa kufanya maasia na kuwahimiza juu yake kwa sababu ya yale waliyoyapambia, "yaliyo mbele yao na nyuma yao." Waliwapambia dunia katika macho yao na wakawaita kwenye starehe zake na matamanio yake yaliyoharamishwa, mpaka wakaingia katika majaribio, wakaingia katika kumuasi Mwenyezi Mungu na wakashika njia ya kupigana vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Akhera wakaiona kuwa ni mbali mno na wakawasahaulisha kuikumbuka. Na huenda waliwatia fikira potofu kwamba haitatokea, kwa hivyo suala la kuihofu likatoka nyoyoni mwao, kwa hivyo wakawapelekea kwenye ukafiri, uzushi na maasia. Na Mwenyezi Mungu kuwapa mamlaka mashetani juu ya wale wanaokadhibisha na kuwafungamanisha nao ni kwa sababu ya kupeana kwao mgongo utajo wa Mwenyezi Mungu na ishara zake, na kukataa kwao haki. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Anayeyafanyia upofu maneno ya Rahmani, tunamwekea shetani kuwa ndiye rafiki yake. Na hakika wao wanawazuilia Njia, na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka." "Basi ikawathibitikia kauli" kutokana na mipango ya Mwenyezi Mungu kwamba wataadhibiwa "pamoja na mataifa yaliyopita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kuhasirika" dini zao na akhera yao. Na mwenye kuhasiri, basi ni lazima atadhalilika, awe mashakani na aadhibiwe.
: 26 - 29 #
{وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ (26) فَلَنُذِيقَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ (27) ذَلِكَ جَزَاءُ أَعْدَاءِ اللَّهِ النَّارُ لَهُمْ فِيهَا دَارُ الْخُلْدِ جَزَاءً بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ (28) وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا رَبَّنَا أَرِنَا اللَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ الْأَسْفَلِينَ (29)}.
26. Na wale waliokufuru walisema: Msiisikilize Qur-ani hii, na timueni zogo ndani yake, huenda mkashinda. 27. Basi hapana shaka tutawaonjesha hao waliokufuru adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo mabaya zaidi kwa yale waliyokuwa wakiyafanya. 28. Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu. 29. Na wale waliokufuru watasema: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe wale waliotupoteza miongoni mwa majini na watu ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni wa walio chini kabisa.
#
{26} يخبر تعالى عن إعراض الكفار عن القرآن وتواصيهم بذلك، فقال: {وقال الذين كَفَروا لا تَسْمَعوا لهذا القرآن}؛ أي: أعرضوا عنه بأسماعكم، وإيَّاكم أن تلتفتوا أو تُصْغوا إليه وإلى مَنْ جاء به؛ فإن اتَّفق أنكم سمعتموه أو سمعتُم الدعوة إلى أحكامه، فالغَوْا فيه؛ أي: تكلَّموا بالكلام الذي لا فائدةَ فيه، بل فيه المضرَّة، ولا تمكِّنوا مع قدرتكم أحداً يملكُ عليكم الكلام به وتلاوةَ ألفاظه ومعانيه، هذا لسانُ حالهم ولسانُ مقالهم في الإعراض عن هذا القرآن. {لعلَّكم}: إن فعلتُم ذلك {تغلِبونَ}: وهذا شهادةٌ من الأعداء، وأوضحُ الحقِّ ما شهدت به الأعداءُ؛ فإنَّهم لم يحكموا بغلبتهم لِمَنْ جاء بالحقِّ إلاَّ في حال الإعراض عنه والتواصي بذلك، ومفهومُ كلامِهم أنَّهم إنْ لم يَلْغَوا فيه، بل استمعوا إليه وألقوا أذهانَهم؛ أنَّهم لا يغلبونَ؛ فإنَّ الحقَّ غالبٌ غير مغلوب، يعرِفُ هذا أصحابُ الحقِّ وأعداؤه.
{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha namna makafiri walivyoipa mgongo Qur-ani na kuhusiana kufanya hivyo. Akasema: "Na wale waliokufuru walisema: 'Msiisikilize Qur-ani hii,'" yaani msiipe masikio yenu, na jihadharini kuisikiliza au kumsikiliza yule aliyekuja nayo. Na ikitokea kwa bahati mbaya kwamba mmeisikia au mmemsikia Muhammad akilingania hukumu zake, semeni kuhusiana nayo maneno yasiyo na manufaa yoyote, na hata yenye madhara, na wala msimuwezeshe mtu yeyote kwa uwezo wenu kuyazungumza maneno yake na kusoma lafudhi zake na maana zake. Hayo ndiyo maneno yao na vitendo vyao vya kuipa mgongo Qur-ani hii. "Huenda" mkifanya hivyo "mtashinda." Huu ni ushahidi kutoka kwa maadui, na haki iliyo wazi kabisa ni kile walichokishuhudia maadui. Kwani hawakuhukumu kuwa walimshinda yule aliyekuja na haki isipokuwa katika hali yao ya kumpa mgongo na kuusiana kufanya hivyo. Na maana yake ya kinyume ni kwamba ikiwa hawataweza kuitimulia zogo, bali waliisikiliza na kuipa akili zao, basi hawataweza kushinda. Kwani haki ni yenye kushinda na wala haishindwi. Hili wanalijua vyema walio kwenye haki na maadui zake.
#
{27} ولمَّا كان هذا ظلماً منهم وعناداً؛ لم يبقَ فيهم مطمعٌ للهداية، فلم يبقَ إلاَّ عذابُهم ونَكالُهم، ولهذا قال: {فَلَنُذيقَنَّ الذين كَفَروا عذاباً شديداً ولَنَجْزِيَنَّهم أسوأ الذي كانوا يعمَلون}: وهو الكفر والمعاصي؛ فإنَّها أسوأ ما كانوا يعملون؛ لكونهم يعملون المعاصي وغيرها؛ فالجزاء بالعقوبة إنَّما هو على عمل الشرك ، ولا يظلمُ ربُّك أحداً.
{27} Na kwa kuwa jambo hili walilifanya kwa njia ya dhuluma na ukaidi, hayakubakia matumaini yoyote ya kuongoka kwao, isipokuwa waadhibiwe na kuteswa. Ndiyo maana akasema: "Basi hapana shaka tutawaonjesha hao waliokufuru adhabu kali, na hapana shaka tutawalipa malipo mabaya zaidi kwa ya yale waliyokuwa wakiyafanya," yaani kufuru na maasia. Hayo kwa hakika ndiyo mabaya zaidi waliyokuwa wakiyafanya. Kwa maana, walitenda madhambi na mambo mengineyo. Nayo malipo ya kuadhibiwa huwa kwa sababu ya kutenda ushirikina, na wala Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.
#
{28} {ذلك جزاءُ أعداءِ الله}: الذين حاربوه وحاربوا أولياءه؛ بالكفر والتكذيب والمجادلة والمجالدةِ. {[النار] لهم فيها دارُ الخلدِ}؛ أي: الخلود الدائم، الذي لا يفتَّر عنهم العذابُ ساعةً ولا هم يُنصرون، وذلك {جزاءً بما كانوا بآياتِنا يجحَدونَ}؛ فإنَّها آياتٌ واضحةٌ وأدلةٌ قاطعةٌ مفيدةٌ لليقين، فأعظم الظُّلم وأكبر العناد جَحْدُها والكفر بها.
{28} "Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu" waliompiga vita Yeye na vipenzi wake, kwa ukafiri na kukadhibisha. "Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu" ambayo hawatapunguziwa adhabu yake hata saa moja wala hawatanusuriwa. Hayo "ndiyo malipo yao, kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu." Kwani ni ishara zilizowazi, na ushahidi wa uhakika wenye yakini. Kwa hivyo, udhalimu mkubwa zaidi na ukaidi mkubwa zaidi ni kuzikataa na kuzikufuru.
#
{29} {وقال الذين كفروا}؛ أي: الأتباع منهم؛ بدليل ما بعدَه على وجه الحنق على مَنْ أضلَّهم: {ربَّنا أرِنا اللَّذَين أضلاَّنا من الجنِّ والإنس}؛ أي: الصنفين اللذين قادانا إلى الضَّلال والعذاب من شياطين الجنِّ وشياطين الإنس الدعاة إلى جهنَّم، {نجعَلْهما تحتَ أقدامِنا ليكونا من الأسفلينَ}؛ أي: الأذلِّين المهانين؛ كما أضلُّونا وفتنونا وصاروا سبباً لنزولنا؛ ففي هذا بيانُ حنقِ بعضهم على بعض، وتبرِّي بعضهم من بعض.
{29} "Na" wafuasi miongoni mwa "wale waliokufuru watasema" kwa njia ya hasira kubwa zaidi juu ya wale waliowapoteza: "'Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe wale waliotupoteza miongoni mwa majini na watu'" waliokuwa wakilingania kwenye Jahanaam, "ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni wa walio chini kabisa.'" Yaani, wadhalilike na wadunishwe pia kama walivyotupotosha, wakatutia katika majaribu na wakawa ndio sababu ya haya tuliyomo. Na haya yanaelezea chuki waliyo nayo wao kwa wao, na kujitenga mbali kwao wenyewe kwa wenyewe.
: 30 - 32 #
{إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ (30) نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنْفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ (31) نُزُلًا مِنْ غَفُورٍ رَحِيمٍ (32)}.
30. Hakika wale waliosema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa. 31. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka. 32. Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
#
{30} يخبر تعالى عن أوليائِهِ، وفي ضمن ذلك تنشيطُهم والحثُّ على الاقتداء بهم، فقال: {إنَّ الذين قالوا ربُّنا الله ثم اسْتَقاموا}؛ أي: اعترفوا ونطقوا ورَضُوا بربوبيَّة الله تعالى واستَسْلَموا لأمره، ثم استقاموا على الصراط المستقيم علماً وعملاً؛ فلهم البُشرى في الحياةِ الدُّنيا وفي الآخرة. {تتنزَّلُ عليهم الملائكةُ}: الكرام؛ أي: يتكرَّر نزولهم عليهم مبشِّرين لهم عند الاحتضار {أن لا تخافوا}: على ما يستقبلُ من أمركم، {ولا تحزَنوا}: على ما مضى، فنفوا عنهم المكروه الماضي والمستقبل. {وأبشِروا بالجنَّة التي كنتُم توعدون}: فإنَّها قد وجبت لكم وثبتت، وكان وعد الله مفعولاً.
{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu vipenzi wake, jambo ambalo linajumuisha kuwaamsha na kuhimiza watu kufuata mfano wao: "Hakika wale waliosema: 'Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu!' Kisha wakanyooka sawa," yaani, walikiri, wakatamka na wakaridhia umola wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakajisalimisha kwa amri yake, kisha wakanyooka sawa katika njia iliyonyooka katika elimu yao na matendo yao, basi wana bishara njema katika maisha ya dunia na akhera. "Hao huwateremkia Malaika" watukufu wakiwapa bishara njema wakati wa kufa kwao: "Msiogope" yatakayokuja katika mambo yenu, "wala msihuzunike" kwa yale yaliyopita. Kwa hivyo wakawa wamewajulisha kutokuwepo mambo ya kuchukiza ya zamani na yajayo. "Nanyi furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa." Kwani imeshaamuliwa kuwa mtaingia humo na hilo limeshathibiti. Na kuwa imefaradhishwa kwenu na imethibiti, na hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu lazima itimizwe!
#
{31} ويقولون لهم أيضاً مثبِّتين لهم ومبشِّرين: {نحنُ أولياؤكم في الحياة الدُّنيا وفي الآخرِة}: يحثُّونهم في الدنيا على الخيرِ ويُزَيِّنونه لهم، ويرهِّبونهم عن الشرِّ ويقبِّحونه في قلوبهم، ويَدْعون الله لهم، ويثبِّتونهم عند المصائبِ والمخاوف، وخصوصاً عند الموت وشدَّته والقبر وظلمته وفي القيامة وأهوالِها، وعلى الصراط وفي الجنَّة؛ يهنُّونهم بكرامة ربِّهم، ويدخُلون عليهم من كلِّ باب، سلامٌ عليكم بما صبرتُم فنعم عُقبى الدار، ويقولون لهم أيضاً: {ولكم فيها}؛ أي: في الجنة، {ما تشتهي أنفسُكم}: قد أُعِدَّ وهُيِّئ، {ولكم فيها ما تَدَّعون}؛ أي: تطلبون من كلِّ ما تتعلَّق به إرادتُكم وتطلُبونه، من أنواع اللَّذَّات والمشتهيات، مما لا عينٌ رأت ولا أذنٌ سمعت ولا خطرَ على قلب بشر.
{31} Na wanawaambia pia kwa kuwaimarisha na kuwapa bishara njema: "Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera." Wanawahimiza kufanya heri katika dunia na wanawapambia heri hiyo, wanawahofisha kutokana na maovu na wanaifanya kuwa mabaya katika nyoyo zao, wanawaombea kwa Mwenyezi Mungu na wanawatia nguvu katika nyakati za misiba na hofu, hasa wakati wa kifo na ukali wake na katika kaburi na giza lake, na katika siku ya Kiyama na vitisho vyake vizito, na katika njia iliyoko juu ya Jahannam, na katika Pepo wanawapongeza kwamba watapata utukufu wa Mola wao Mlezi na wanawaingilia kutokea katika kila mlango wakiwaambia: Amani iwe juu yenu kwa sababu ya mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera. Pia wanawaambia: "Na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu" tayari vimeshaandaliwa na kutayarishwa. "Na humo mtapata mtakavyovitaka" miongoni mwa vitu ambavyo mapenzi yenu yanafungamana navyo na mkaviitisha, kama vile kila aina ya raha na matamanio, ambayo hakuna jicho lililowahi kuyaona wala hakuna sikio lililowahi kuyasikia, na wala hayakuwahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote.
#
{32} {نزلاً من غفورٍ رحيم}؛ أي: هذا الثواب الجزيل والنعيم المقيم نُزُلٌ وضيافةٌ من غفورٍ غفر لكم السيئات، رحيم حيث وفَّقكم لفعل الحسنات ثم قَبِلَها منكم؛ فبمغفِرَتِهِ أزال عنكم المحذورَ، وبرحمتِهِ أنالكم المطلوب.
{32} "Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu," kwa kuwa alikuwezesheni kutenda mazuri kisha akayakubali kutoka kwenu. Kwa hivyo, kwa kukusameheni, akakuondoleeni machukizo, na kwa kukurehemuni, akakupeni mliyokuwa mkitafuta.
: 33 #
{وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ (33)}.
33. Na ni nani mbora zaidi wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?
#
{33} هذا استفهامٌ بمعنى النفي المتقرِّر؛ أي: لا أحد {أحسنُ قولاً}؛ أي: كلاماً وطريقةً وحالة {ممَّن دعا إلى الله}: بتعليم الجاهلين، ووعظ الغافلين والمعرِضين، ومجادلةِ المبطِلين؛ بالأمر بعبادة الله بجميع أنواعها، والحثِّ عليها، وتحسينها مهما أمكن، والزجر عما نهى الله عنه، وتقبيحِهِ بكلِّ طريق يوجب تركَه، خصوصاً من هذه الدعوة إلى أصل دين الإسلام وتحسينه، ومجادلة أعدائِهِ بالتي هي أحسن، والنهي عما يضادُّه من الكفرِ والشرك، والأمر بالمعروف والنهي عن المنكر. ومن الدعوة إلى الله تحبيبُهُ إلى عبادِهِ؛ بذِكْر تفاصيل نِعَمِهِ وسعةِ جودِهِ وكمال رحمتِهِ وذكرِ أوصاف كمالِهِ ونعوت جلاله. ومن الدعوة إلى الله الترغيبُ في اقتباس العلم والهدى من كتاب الله وسنَّة رسوله، والحثُّ على ذلك بكلِّ طريق موصل إليه. ومن ذلك الحثُّ على مكارم الأخلاق، والإحسانُ إلى عموم الخلق، ومقابلةُ المسيء بالإحسان، والأمرُ بصلة الأرحام وبرِّ الوالدين. ومن ذلك الوعظُ لعموم الناس في أوقات المواسم والعوارض والمصائب بما يناسبُ ذلك الحال، إلى غير ذلك ممَّا لا تنحصر أفرادُه بما يشمله الدعوة إلى الخير كله، والترهيبُ من جميع الشرِّ. ثم قال تعالى: {وعمل صالحاً}؛ أي: مع دعوته الخلق إلى الله بادَرَ هو بنفسِهِ إلى امتثال أمرِ الله بالعمل الصالح الذي يُرضي ربَّه، {وقال إنَّني من المسلمين}؛ أي: المنقادين لأمره، السالكين في طريقه، وهذه المرتبةُ تمامها للصدِّيقين الذين عملوا على تكميل أنفسِهم وتكميل غيرِهم وحصلت لهم الوراثةُ التامَّةُ من الرسل؛ كما أنَّ من أشرِّ الناس قولاً من كان من دعاة الضَّلال السالكين لسُبُله، وبين هاتين المرتبتين المتباينتين، التي ارتفعتْ إحداهما إلى أعلى علِّيين، ونزلت الأخرى إلى أسفل سافلين، مراتبُ لا يعلمُها إلاَّ الله، وكلها معمورةٌ بالخلق، ولكلٍّ درجاتٌ مما عملوا، وما ربُّك بغافل عما يعملون.
{33} Hii ni mbinu ya kuuliza swali lenye maana ya kukanusha ambako tayari kunajulikana. Yaani, hakuna "aliyebora zaidi katika usemi," mbinu na hali "kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu" kwa kuwafundisha wasiojua na kuwapa mawaidha walioghafilika na wanaopeana haki mgongo, na kujadiliana na wana batili kwa kuwaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa namna zote, kuhimiza juu ya hilo, na kulifanya kuwa zuri iwezekanavyo, na kukemea yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, na kuyafanya kuwa mabaya kwa kila njia inayolazimu yaachwe, hasa kulingania kwenye msingi wa dini ya Kiislamu na kuifanya kuwa nzuri sana, na kujadiliana na maadui zake kwa njia iliyobora zaidi, na kukataza yale yanayoupinga, kama vile ukafiri na ushirikina, na kuamrisha mema na kukataza maovu. Katika kulingania kwa Mwenyezi Mungu ni kuwafanya waja wake kumpenda kwa kutaja maelezo ya kina ya neema zake, upana wa wema wake, ukamilifu wa rehema yake na kutaja sifa za ukamilifu wake na utukufu wake. Katika kulingania kwa Mwenyezi Mungu ni kuhimiza kutafuta elimu na uwongofu kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake, na kuhimiza kufanya hivyo kwa kila njia inayofikisha kwa hilo. Na katika kufanya hivyo, ni kuhimiza juu ya maadili mema, kuwa mwema kwa viumbe wote, kumlipa mkosaji kwa uzuri na kuamrisha kuunga jamaa za mtu na kuwafanyia wema wazazi. Na katika kufanya hivyo, ni kuwaaidhi watu wote kwa ujumla katika misimu, matukio na misiba mbalimbali kwa njia inayofailia hali hizo, na mambo mengineyo ambayo hayana kikomo, kama vile kulingania kwenye heri yote na kuhofisha dhidi ya maovu yote. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "na akatenda mema." Yaani, pamoja na kulingania kwake viumbe kwa Mwenyezi Mungu, yeye mwenyewe aliharakisha kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu kwa kutenda mema yanayomridhisha Mola wake Mlezi. "Na akasema: 'Hakika mimi ni katika Waislamu.'" Yaani, wale wanaotii amri yake, wanaotembea katika njia yake. Na daraja hii iliyo kamili zaidi ni ya Wakweli waliofanya matendo ya kujikamilisha wenyewe na kuwakamilisha wengine na wakapata urithi kamili kutoka kwa Mitume. Kadhalika, miongoni mwa watu waovu zaidi katika usemi ni wale wanaolingania upotofu na wakafuata njia zake. Baina ya daraja mbili hizi - zinazotofautiana, ambazo moja yake iliinuka juu zaidi ya vyote vilivyo juu, nayo nyingine ikateremka chini zaidi kuliko vyote vilivyo chini - kuna daraja ambazo hakuna azijuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu, na zote zinakaliwa na viumbe, na kila mmoja wao ana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyoyatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika mbali na yale wanayoyatenda.
: 34 - 35 #
{وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ (34) وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ (35)}.
34. Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. 35. Lakini hawapewi wema huu ila wanaosubiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.
#
{34} يقول تعالى: {ولا تَسْتَوي الحسنةُ ولا السيئةُ}؛ أي: لا يستوي فعلُ الحسنات والطاعاتِ لأجل رضا الله تعالى ولا فعل السيئات والمعاصي التي تُسْخِطُه ولا تُرضيه، ولا يستوي الإحسانُ إلى الخلق ولا الإساءة إليهم لا في ذاتها ولا في وصفها ولا في جزائها. {هل جزاءُ الإحسان إلاَّ الإحسانُ}. ثم أمر بإحسان خاصٍّ، له موقعٌ كبيرٌ، وهو الإحسان إلى مَنْ أساء إليك، فقال: {ادفعْ بالتي هي أحسنُ}؛ أي: فإذا أساء إليك مسيءٌ من الخلق، خصوصاً من له حقٌّ كبيرٌ عليك؛ كالأقارب والأصحاب ونحوهم، إساءةً بالقول أو بالفعل؛ فقابِلْه بالإحسان إليه؛ فإنْ قَطَعَكَ؛ فصِلْه، وإنْ ظلمكَ؛ فاعفُ عنه، وإن تكلَّم فيك غائباً أو حاضراً؛ فلا تقابِلْه، بل اعفُ عنه وعامِلْه بالقول الليِّن، وإن هَجَرَكَ وترك خطابك؛ فطيِّبْ له الكلام وابذلْ له السلام؛ فإذا قابلتَ الإساءة بالإحسان؛ حصل فائدةٌ عظيمةٌ. {فإذا الذي بينَك وبينَه عداوةٌ كأنَّه وليٌّ حميمٌ}؛ أي: كأنه قريبٌ شفيقٌ.
{34} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Mema na maovu hayalingani." Yaani, kufanya matendo mema na utiifu kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu hakulingani na kutenda maovu na maasi yanayomchukiza na wala hayamridhishi. Na wala haiwi sawa kuwatendea viumbe wema na kuwafanyia maovu, si katika dhati ya ubaya huo, wala katika sifa zake, wala katika malipo yake. "Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?" Kisha akaamrisha tendo maalumu la ihsani, lenye umuhimu mkubwa, nalo ni kumfanyia wema mtu aliyekufanyia ubaya, akasema: "Pinga uovu kwa lililo jema zaidi." Yaani, Akikuudhi mwenye kukuudhi miongoni mwa viumbe, hasa yule ambaye ana haki kubwa juu yako, kama vile jamaa zako, marafiki, na wengineo, akakufanyia ubaya kwa maneno au kwa vitendo, basi kabilana naye kwa kumfanyia wema. Akikukataa, wewe muunge, na akikudhulumu, wewe msamehe. Na akizungumza juu yako usipokuwepo au ukiwepo, wewe usikabiliane naye kwa njia hiyo, bali msamehe na uamiliane naye kwa maneno ya upole. Na akikupa mgongo na akaacha kusema nawe, wewe msemeshe kwa maneno mazuri na umpe salamu. Ukiukabili ubaya kwa uzuri, kutakuwa na faida kubwa sana. "Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui, atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu."
#
{35} {وما يُلَقَّاها}؛ أي: وما يوفَّق لهذه الخصلة الحميدة {إلاَّ الذين} صَبَّرُوا نفوسَهم على ما تكره، وأجبروها على ما يحبُّه الله؛ فإنَّ النفوس مجبولةٌ على مقابلة المسيء بإساءتِهِ، وعدم العفو عنه؛ فكيف بالإحسان؛ فإذا صبَّر الإنسان نفسَه وامتثل أمر ربِّه وعرف جزيلَ الثواب وعلمَ أنَّ مقابلته للمسيء بجنس عمله لا يفيده شيئاً ولا يزيدُ العداوة إلاَّ شدة، وأنَّ إحسانه إليه ليس بواضع قدرَه، بل مَنْ تواضَعَ لله رَفَعَه؛ هان عليه الأمرُ وفعل ذلك متلذِّذاً مستحلياً له. {وما يُلَقَّاها إلاَّ ذو حظٍّ عظيم}: لكونها من خصال خواصِّ الخلق، التي ينال بها العبد الرفعةَ في الدُّنيا والآخرة، التي هي من أكبرِ خصال مكارم الأخلاق.
{35} "Lakini hawapewi wema huu ila wanaosubiri," wakaacha yale wanayoyachukia na wakajilazimisha kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu anayaridhia. Kwa maana nafsi zimefanywa kupenda kumkabili aliyetenda uovu kwa kumfanyia uovu pia na kutomsamehe. Basi itakuwaje ikiwa nafsi hizo zitafanyiwa hisani? Kwa hivyo, ikiwa mtu ataisubirisha nafsi yake, na akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akajua malipo makubwa ya hilo, na akajua kwamba kukabiliana na mtendaji mabaya kwa aina sawa na mabaya yake hakumfaidi kitu bali kunazidisha uadui kuwa mkubwa, na kwamba akimfanyia ihsani hilo halimpunguzi kitu katika thamani yake, bali anayejinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu, atamwinua. Hayo yanamrahisishia mambo na akalifanya hilo kwa raha na kwa uzuri mkubwa. "Wala hawapewi ila wenye bahati kubwa." Kwa sababu ni miongoni mwa sifa za viumbe maalumu, ambazo kwazo mja anapata kuinuka juu duniani na akhera, ambako ni katika sifa kubwa zaidi za maadili matukufu.
: 36 - 39 #
{وَإِمَّا يَنْزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (36) وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ (37) فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِنْدَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ (38) وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنْزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِ الْمَوْتَى إِنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (39)}.
36. Na Shetani akikuchochea kwa uchochezi, wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, ajuaye zaidi. 37. Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu. 38. Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki. 39. Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapoiteremshia maji, mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka yule aliyeihuisha ardhi ndiye atakayehuisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.
#
{36} لما ذكر تعالى ما يُقَابَلُ به العدوُّ من الإنس، وهو مقابلة إساءته بالإحسان؛ ذكر ما يُدْفَعُ به العدوٌّ الجنيُّ، وهو الاستعاذةُ بالله والاحتماء من شرِّه، فقال: {وإمَّا ينزغَنَّك من الشيطانِ نزعٌ}؛ أي: أي وقت من الأوقات أحسستَ بشيء من نَزَغات الشيطانِ؛ أي: من وساوسه وتزيينه للشرِّ وتكسيله عن الخير وإصابة ببعض الذنوب وإطاعة له ببعض ما يأمر به، {فاستَعِذْ بالله}؛ أي: اسأله مفتقراً إليه أن يعيذَكَ ويعصِمَك منه. {إنَّه هو السميع العليم}: فإنَّه يسمعُ قولك وتضرُّعك، ويعلمُ حالك واضطرارك إلى عصمتِهِ وحمايتِهِ.
{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kile ambacho adui wa kibinadamu anapaswa kujibiwa kwacho, ambacho ni kuukabili ubaya wake kwa wema, akataja yale anayozuiliwa kwayo adui wa kijini, ambacho ni kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu na kujikinga kwake kutokana na shari yake, akasema: "Na Shetani akikuchochea kwa uchochezi" na wasiwasi wake na kuyapamba kwake maovu, kukutia uvivu juu ya kutenda heri, kufanya baadhi ya madhambi na kumtii katika baadhi ya yale anayoamrisha, "wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu" ukimuonyesha hoja yako kubwa ya kutaka akulinde kutoka naye. "Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua vyema." Yeye kwa hakika atasikia maneno yako na kunyenyekea kwako, na anaijua hali yako na haja yako kubwa ya kutafuta ulinzi wake na hifadhi yake.
#
{37} ثم ذكر تعالى أن {من آياتِهِ}: الدالَّة على كمال قدرته ونفوذِ مشيئتِهِ وسعةِ سلطانِهِ ورحمتِهِ بعباده وأنَّه الله وحده لا شريك له، {الليلُ والنهارُ}: هذا بمنفعة ضيائِهِ وتصرُّف العباد فيه، وهذا بمنفعة ظُلَمِهِ وسكون الخلقِ فيه، {والشمسُ والقمرُ}: اللذان لا تستقيم معايِشُ العباد ولا أبدانُهم ولا أبدانُ حيواناتهم إلاَّ بهما، وبهما من المصالح ما لا يُحصى عَدَدُه. {لا تسجُدوا للشمس ولا للقمرِ}: فإنَّهما مدبَّران مسخَّران مخلوقان، {واسجُدوا لله الذي خَلَقَهُنَّ}؛ أي اعبدوه وحدَه؛ لأنَّه الخالق العظيم، ودعوا عبادة ما سواه من المخلوقات، وإن كَبُر جرمه وكثرت مصالحه فإنَّ ذلك ليس منه، وإنَّما هو من خالقه تبارك وتعالى {إن كنتُم إيَّاه تعبُدون}: فخصُّوه بالعبادة وإخلاص الدين له.
{37} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja kwamba: "Na katika Ishara zake" zinazoashiria ukamilifu wa uwezo wake, na utekelezaji wa utashi wake, na upana wa mamlaka yake, na rehema yake kwa waja wake, na kwamba Yeye ndiye Mungu peke yake, hana mshirika, "ni usiku na mchana." Hiki ni kwa ajili ya manufaa ya nuru yake na waja kuweza kufanya mambo yao ndani yake, na hiki ni kwa manufaa ya giza lake na kutulia kwa viumbe humo. "Na jua na mwezi," ambavyo bila ya hivyo hayawezi kunyooka maisha ya waja, wala miili yao, wala miili ya wanyama wao, na pia vinawapa masilahi mengineyo yasiyoweza kudhibitika kwa idadi. "Basi msilisujudie jua wala mwezi," kwani ni viumbe viwili vilivyotiishwa na Mwenyezi Mungu, "bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba" na mumwabudu Yeye peke yake. Kwa sababu Yeye ndiye Muumba Mkuu, na muwache kuviabudu visivyokuwa Yeye miongoni mwa viumbe, hata kama vina miili mikubwa namna gani, na hata kama vina masilahi mengi namna gani. Kwani hayo hayatokani navyo, lakini yanatokana na Muumba wa vitu hivyo, Mwingi wa baraka, Mtukufu. "Ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu," basi mkusudieni Yeye peke yake kwa ibada na dini.
#
{38} {فإن استكْبَروا}: عن عبادة الله تعالى، ولم ينقادوا لها؛ فإنَّهم لن يضرُّوا الله شيئاً، والله غنيٌّ عنهم، وله عبادٌ مكرمون، لا يعصون الله ما أمرهم ويفعلون ما يؤمرونَ، ولهذا قال: {فالذين عند ربِّكَ}؛ يعني: الملائكة المقرَّبين، {يسبِّحون له بالليل والنهارِ وهم لا يسأمونَ}؛ أي: لا يملُّون من عبادته؛ لقوَّتهم وشدَّة الداعي القويِّ منهم إلى ذلك.
{38} "Na ikiwa watajivuna" kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu na wasifuate maamrisho yake, basi wao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu hata kidogo, kwani Mwenyezi Mungu ni Mkwasi asiyewahitaji. Anao waja watukufu ambao hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa. Ndiyo maana akasema: "Basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi," yaani, Malaika waliowekwa karibu naye, "wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki" kumuabudu kwa sababu ya nguvu zao na ukubwa wa kile kilicho ndani yao kinachowasukuma kufanya hivyo.
#
{39} {ومن آياتِهِ}: الدالَّة على كمال قدرته وانفراده بالمُلك والتَّدبير والوحدانيَّة، {أنَّك ترى الأرضَ خاشعةً}؛ [أي]: لا نباتَ فيها، {فإذا أنزلْنا عليها الماءَ}؛ أي: المطر، {اهتزَّتْ}؛ أي: تحرَّكت بالنبات، {وَرَبَتْ}: ثم أنبتت من كلِّ زوج بهيج؛ فحيي بها العبادُ والبلادُ. {إنَّ الذي أحياها}: بعد موتها وهمودها {لَمُحيي الموتى}: من قبورهم إلى يوم بعثِهِم ونشورِهِم. {إنَّه على كلِّ شيءٍ قديرٌ}: فكما لم تعجزْ قدرتُه على إحياءِ الأرض بعد موتِها لا تعجزُ عن إحياء الموتى.
{39} "Na katika Ishara zake" zinazoonyesha ukamilifu wa uwezo wake na upekee wake katika ufalme, uendeshaji na umoja, "ni kwamba unaiona ardhi nyonge," yaani hali ya kuwa haina mimea juu yake. "Lakini tunapoiteremshia maji" ya mvua, "mara husisimka na kututumka" na kumea kila namna ya mimea mizuri. Kwa hivyo, watu na nchi vinakuwa hai. "Bila ya shaka aliyeihuisha ardhi" baada ya kufa kwake na kutulia kwake kimya "ndiye atakayehuisha wafu" kutoka makaburini mwao kwa ajili ya siku ya kufufuliwa kwao na kutolewa kwao humo. "Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu." Kwa sababu kama vile uwezo wake haukushindwa kuifufua ardhi baada ya kufa kwake, basi pia hauwezi kushindwa kuwafufua wafu.
: 40 - 42 #
{إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا أَفَمَنْ يُلْقَى فِي النَّارِ خَيْرٌ أَمْ مَنْ يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (40) إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ (41) لَا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنْزِيلٌ مِنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ (42)}.
40. Hakika wale wanaopindukia mipaka katika Ishara zetu, hawafichikani kwetu. Je, atakayetupwa Motoni ni bora au atakayekuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona vyema mnayoyatenda. 41. Kwa hakika wale walioyakufuru mawaidha haya yanapowajia (wataangamia), na haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu. 42. Haukifikii upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hekima, Msifiwa mno.
#
{40} الإلحادُ في آيات الله: الميلُ بها عن الصواب بأيِّ وجه كان: إمَّا بإنكارها وجحودِها وتكذيبِ مَنْ جاء بها، وإمَّا بتحريفِها وتصريفِها عن معناها الحقيقيِّ وإثباتِ معانٍ ما أرادها الله منها، فتوعَّد تعالى مَنْ ألحد فيها بأنَّه لا يخفى عليه، بل هو مطَّلع على ظاهره وباطنه، وسيجازيه على إلحادِهِ بما كان يعملُ، ولهذا قال: {أفمن يُلْقَى في النار}: مثل الملحدِ بآيات الله {خيرٌ أم من يأتي آمناً يوم القيامةِ}: من عذاب الله، مستحقًّا لثوابه؟ من المعلوم أنَّ هذا خيرٌ. لمَّا تبيَّن الحقُّ من الباطل والطريق المنجي من عذابِهِ من الطريق المهلِكِ؛ قال: {اعملوا ما شِئْتُم}: إن شئتُم؛ فاسلكوا طريق الرُّشدِ الموصلة إلى رضا ربِّكم وجنته، وإن شئتُم؛ فاسْلُكوا طريق الغيِّ المسخطة لربكم الموصلة إلى دار الشقاءِ. {إنَّه بما تعملون بصيرٌ}: يجازيكم بحسب أحوالِكم وأعمالكم؛ كقوله تعالى: {وقُل الحقُّ من ربِّكم فَمَن شاء فليؤمِن ومَن شاء فَلْيَكْفُر}.
{40} Kupindukia mipaka katika ishara za Mwenyezi Mungu ni kuziondoka katika usahihi wake kwa njia yoyote ile: ima kwa kuzikataa, kumkadhibisha aliyekuja nazo au kwa kuzipotosha mbali na maana zake za uhakika na kuthibitisha maana ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuzikusudia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtishia mwenye kupindukia mipaka ndani yake kwamba hafichikani kwake, bali anaijua dhahiri yake na ndani yake, na atamlipa kwa kupindukia kwake huko kwa yale aliyokuwa akiyafanya, na ndiyo maana akasema: "Je, atakayetupwa Motoni" kama vile huyo aliyepindukia katika ishara za Mwenyezi Mungu "ni bora au atakayekuja kwa amani Siku ya Kiyama" mbali na adhabu ya Mwenyezi Mungu, ambaye anastahiki malipo yake mazuri? Inavyojulikana ni kwamba huyu ndiye bora. Haki ilipobainika mbali na batili, na njia kuokoa kutokana na adhabu yake mbali na njia inayoangamiza, akasema: "Tendeni mpendavyo" mkitaka. Ifuateni njia ya unyoofu ifikishayo kwenye radhi ya Mola wenu Mlezi na Pepo yake. Na mkipenda, ifuateni njia ya upotovu inayomkasirisha Mola wenu Mlezi, inayofikisha kwenye nyumba ya mashaka makubwa. "Kwa hakika Yeye anayaona vyema mnayoyatenda" na atakulipeni kulingana na hali zenu na matendo yenu. Kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na sema: 'Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, na aamini. Na atakaye, na akufuru.'"
#
{41 - 42} ثم قال تعالى: {إنَّ الذين كفروا بالذِّكْر}؛ أي: يجحدون القرآن الكريم، المذكِّر للعباد جميع مصالحهم الدينيَّة والدنيويَّة والأخرويَّة، المعلي لِقَدْر من اتَّبعه، {لمَّا جاءهم}: نعمة من ربِّهم على يد أفضل الخلقِ وأكملهم. {و} الحال {إنَّه}: كتابٌ جامعٌ لأوصاف الكمال، {عزيزٌ}؛ أي: منيعٌ مِن كلِّ مَن أراده بتحريف أو سوءٍ، ولهذا قال: {لا يأتيه الباطلُ من بين يديهِ ولا من خلفهِ}؛ أي: لا يَقْرَبُهُ شيطانٌ من شياطين الإنس والجنِّ لا بسرقةٍ ولا بإدخال ما ليس منه به ولا بزيادةٍ ولا نقص؛ فهو محفوظٌ في تنزيله، محفوظةٌ ألفاظهُ ومعانيه، قد تكفَّل مَنْ أنزلَه بحفظِهِ؛ كما قال تعالى: {إنَّا نحنُ نَزَّلْنا الذِّكْر وإنَّا له لحافظونَ}. {تنزيلٌ من حكيم}: في خلقِهِ وأمرِهِ، يضع كلَّ شيء موضِعه وينزلها منازِلَها {حميدٍ}: على ما له من صفات الكمال ونعوت الجلال، وعلى ما له من العدل والإفضال؛ فلهذا كان كتابُهُ مشتملاً على تمام الحكمة وعلى تحصيل المصالح والمنافع ودفع المفاسدِ والمضارِّ التي يُحْمَدُ عليها.
{41 - 42} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Kwa hakika wale waliokufuru mawaidha haya," yaani, kwa kuikataa Qur-ani Tukufu inayowakumbusha waja juu ya masilahi yao yote ya kidini, ya kidunia, na ya kiakhera, na ambayo inainua juu cheo cha mwenye kuifuata, "yanapowajia" kama neema kutoka kwa Mola wao Mlezi kupitia mkono wa kiumbe bora zaidi na mkamilifu wao zaidi, "na haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu" ambacho hakuna anayeweza kukipotosha au kukitakia mabaya, na ndiyo maana akasema: "Hautakifikia upotovu kwa mbele yake wala kwa nyuma yake." Yaani, hakuna shetani miongoni mwa mashetani wa kibinadamu au kijini anayeukaribia, si kwa kuiba wala kwa kuingiza humo yasiyokuwemo, wala kwa kuongezea wala kupunguza. Umehifadhiwa katika kuteremshwa kwake, katika lafudhi zake na maana zake. Yule aliyeuteremsha alichukua dhamana ya kuuhifadhi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda." "Imeteremshwa na Mwenye hekima" katika uumbaji wake na amri yake, ambaye anakiweka kila kitu mahali pake na kukiteremsha katika daraja lake. "Msifiwa mno" juu ya sifa zake za ukamilifu na utukufu, na uadilifu wake na fadhila mbalimbali. Ndiyo maana kitabu chake kinajumuisha hekima kamillifu na kuwafikishia waja masilahi na manufaa, na kuwazuilia maovu na madhara ambayo kwayo anasifiwa.
: 43 #
{مَا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِنْ قَبْلِكَ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ (43)}.
43. Huambiwi ila yale yale waliyoambiwa Mitume wa kabla yako. Hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na ni Mwenye adhabu chungu.
#
{43} أي: {ما يُقالُ لك}: أيُّها الرسول من الأقوال الصادرةِ ممَّن كذَّبك وعاندك {إلاَّ ما قد قيل للرسل من قبلِكَ}؛ أي: من جنسها، بل ربَّما إنهم تكلَّموا بكلام واحدٍ؛ كتعجبِّ جميع الأمم المكذِّبة للرُّسل من دعوتهم إلى الإخلاص لله وعبادتِهِ وحدَه لا شريك له، وردِّهم هذا بكلِّ طريق يقدرون عليه، وقولهم: ما أنتم إلا بشرٌ مثلنا، واقتراحُهم على رسلهم الآياتِ التي لا يلزمُهُم الإتيانُ بها ... ونحو ذلك من أقوال أهل التكذيب؛ لما تشابهت قلوبهم في الكفر؛ تشابهتْ أقوالهم، وصَبَرَ الرسلُ عليهم السلام على أذاهم وتكذيبِهم؛ فاصْبِرْ كما صبر مَنْ قبلك. ثم دعاهم إلى التوبةِ والإتيانِ بأسباب المغفرة، وحذَّرهم من الاستمرار على الغيِّ، فقال: {إنَّ ربَّك لذو مغفرةٍ}؛ أي: عظيمة يمحو بها كلَّ ذنب لمن أقلع وتاب، {وذو عقابٍ أليم}: لمن أصرَّ واستكبر.
{43} Yaani, "Huambiwi" ewe Mtume unayoambiwa miongoni mwa maneno wanayoyasema hao wanaokukadhibisha na kukukaidi "ila yale yale waliyoambiwa Mitume wa kabla yako." Yaani, hayo na yale ni ya aina moja. Bali huenda walisema maneno yale yale kama vile kushangaa kwa umma wote waliowakadhibisha Mitume wao juu ya kulingania kwao kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake na kumuabudu Yeye tu bila mshirika, na kukataa kwao haya kwa kila njia wawezayo, na kusema kwao: 'Nyinyi si kitu ila watu kama sisi', na kuwapendekezea kwao Mitume wao kuleta ishara ambazo hawalazimiki kuzileta. Na kauli nyinginezo kama hizo za wale wanaokadhibisha. Nyoyo zao zilipofanana katika ukafiri, kauli zao pia zikafanana, lakini Mitume, amani iwe juu yao, wakawa na subira juu ya udhia wao na ukadhibishaji wao. Basi subiri kama walivyosubiri wale waliokuwa kabla yako. Kisha akawaita watubu na kufanya visababu vya msamaha, na akawaonya dhidi ya kuendelea kupotea, akasema: "Hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ni Mwenye maghfira" mengi ambayo kwayo anafuta kila dhambi ya mwenye kuachana na dhambi na akatubia, "na ni Mwenye adhabu chungu" kwa mwenye kuendelea na akatakabari.
: 44 #
{وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى أُولَئِكَ يُنَادَوْنَ مِنْ مَكَانٍ بَعِيدٍ (44)}.
44. Na lau tungeliifanya Qur-ani kwa lugha ya kigeni, wangelisema: Kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur-ani ni uwongofu na ponya kwa wenye kuamini. Na wale wasioamini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.
#
{44} يخبر تعالى عن فضله وكرمه؛ حيث أنزل كتابَه عربيًّا على الرسول العربيِّ بلسانِ قومه ليبيِّن لهم، وهذا مما يوجب لهم زيادةَ الاعتناء به والتلقِّي له والتسليم، وأنَّه لو جعله قرآناً أعجميًّا بلغة غير العرب؛ لاعترض المكذِّبون، وقالوا: {لولا فُصِّلَتْ آياتُه}؛ أي: هلاَّ بُيِّنت آياته ووُضِّحت وفُسِّرت، {أأعجميٌّ وعربيٌّ}؛ أي: كيف يكون محمدٌ عربيًّا والكتابُ أعجميًّا؟! هذا لا يكونُ. فنفى الله تعالى كلَّ أمر يكون فيه شبهةٌ لأهل الباطل عن كتابِهِ، ووصَفَه بكلِّ وصفٍ يوجب لهم الانقيادَ، ولكنِ المؤمنون الموفَّقون انتفعوا به وارتفعوا، وغيرُهم بالعكس من أحوالِهِم، ولهذا قال: {قل هو للذين آمنوا هُدىً وشفاءٌ}؛ أي: يهديهم لطريق الرشدِ والصراط المستقيم، ويعلِّمهم من العلوم النافعة ما به تحصُل الهداية التامَّةُ، وشفاءٌ لهم من الأسقام البدنيَّة والأسقام القلبيَّة؛ لأنَّه يزجر عن مساوئ الأخلاق وأقبح الأعمال، ويحث على التوبة النَّصوح التي تغسل الذُّنوب وتشفي القلب. {والذين لا يؤمنونَ}: بالقرآن {في آذانِهِم وقرٌ}؛ أي: صممٌ عن استماعه وإعراضٌ، {وهو عليهم عمىً}؛ أي: لا يبصرون به رشداً، ولا يهتدون به، ولا يزيدهم إلاَّ ضلالاً؛ فإنَّهم إذا ردُّوا الحقَّ؛ ازدادوا عمىً إلى عماهم وغيًّا إلى غيِّهم. {أولئك ينادَوْن من مكانٍ بعيدٍ}؛ أي: ينادون إلى الإيمان ويُدْعَوْن إليه فلا يستجيبون؛ بمنزلة الذي ينادَى وهو في مكان بعيدٍ، لا يسمع داعياً ولا يجيب منادياً. والمقصودُ أنَّ الذين لا يؤمنون بالقرآن لا ينتفعون بهُداه ولا يبصِرون بنورِهِ ولا يستفيدونَ منه خيراً؛ لأنَّهم سدُّوا على أنفسهم أبواب الهدى بإعراضهم وكفرِهم.
{44} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu fadhila zake na ukarimu wake; ambapo alikiteremsha kitabu chake hali ya kuwa ni cha Kiarabu kwa Mtume wa Kiarabu kwa lugha ya watu wake ili awabainishie. Hili ndilo linalowataka waitunze zaidi na kuipokea kwa kujisalimisha kwayo, na kwamba ikiwa angeifanya kuwa Qur-ani ya kigeni kwa lugha isiyokuwa ya Waarabu, basi wanaokadhibisha wangelipinga na kusema: "'Kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa'" na kutafsiriwa wazi? "'Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu?'" Yaani, iweje Muhammad ni Mwarabu ilhali kitabu ni cha kigeni? Hili haliwezekani. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akakanusha kila jambo ambalo wana batili watakuwa na shaka nalo juu ya Kitabu chake, na akakieleza kwa kila sifa itakayowalazimu kukifuata. Lakini Waumini waliowezeshwa walinufaika nacho na wakanyanyuka juu, nao wasiokuwa wao wakawa kinyume na hali yao hiyo. Na ndiyo maana akasema: "Sema: 'Hii Qur-ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini.'" Inawaongoza kwenye njia ya sawa kabisa na iliyonyooka, na inawafunza elimu zenye manufaa ambazo kwazo unapatikana uongofu kamili na poza kutokana na maradhi ya kimwili na maradhi ya kimoyo. Kwa sababu inakemea tabia mbaya na matendo maovu, na inahimiza juu ya toba ya kweli ambayo inaosha madhambi na kuponya moyo. "Na wale wasioamini" Qur-ani "umo uziwi katika masikio yao," na hawawezi kuisikiliza kwa hivyo wanapeana mgongo. "Nayo kwao imezibwa hawaioni" yaliyo ya sawa wala hawaongoki kwayo, na wala haiwazidishii isipokuwa upotofu. Kwa maana wanapoikataa haki, wanaongeza kuwa vipofu juu ya upofu wao na upotofu juu ya upotofu wao. "Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.'" Yaani wanaitwa kwenye imani, lakini hawaitikii, ni kama mtu anayeitwa hali ya kuwa yuko mahali mbali. Hawezi kusikia kitu wala kumjibu huyo anayemuita. Maana yake ni kwamba wale wasioiamini Qur-ani hawafaidiki na uongofu wake, wala hawaoni kwa nuru yake na wala hawapati heri kutokana nayo. Kwa sababu walijifungia wenyewe milango ya uwongofu kwa kupeana kwao migongo na ukafiri wao.
: 45 - 46 #
{وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِنْ رَبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِنْهُ مُرِيبٍ (45) مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِلْعَبِيدِ (46)}.
45. Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea tofauti juu yake. Na lau kuwa halikwishatangulia neno la Mola wako Mlezi, wangelihukumiwa. Na hakika wao wamo katika shaka yenye kuwatia wasiwasi juu yake. 46. Anayetenda mema, basi anajitendea mwenyewe nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.
#
{45} يقول تعالى: {ولقد آتَيْنا موسى الكتابَ}: كما آتَيْناك الكتابَ، فصنع به الناسُ ما صنعوا معك؛ اختلفوا فيه: فمنهم من آمنَ به واهتدى وانتفع، ومنهم من كذَّبه ولم ينتفِعْ به، وإنَّ الله تعالى لولا حِلْمُهُ وكلمتُهُ السابقة بتأخير العذاب إلى أجل مسمّى لا يتقدَّم عليه ولا يتأخر؛ {لَقُضِيَ بينهم}: بمجرَّد ما يتميَّز المؤمنون من الكافرين؛ بإهلاك الكافرين بالحال؛ لأنَّ سبب الهلاك قد وَجَبَ وحقَّ. {وإنَّهم لَفي شكٍّ منه مريبٍ}؛ أي: قد بلغ بهم إلى الريبِ الذي يُقْلِقُهم؛ فلذلك كذَّبوه وجحدوه.
{45} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na hakika tulimpa Musa Kitabu" kama tulivyokupa Kitabu, lakini watu wakakifanyia yale waliyokifanyia; walihitalifiana juu yake. Basi baadhi yao walikiamini, wakaongoka na wakanufaika. Na baadhi yao walikikadhibisha na hawakufaidika nacho. Na lau kuwa si ustahamilivu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na neno lake lililotangulia la kuichelewesha adhabu hadi muda uliowekwa, bila ya haitatanguliza wala kuichelewesha, "wangelihukumiwa" mara tu Waumini wanapobainika kutokana na makafiri kwa kuwaangamiza makafiri papo hapo. Kwa kuwa sababu ya kuwaangamiza ilikwishatokea na wakaistahiki. "Na hakika wao wamo katika shaka yenye kuwatia wasiwasi," ndiyo maana wakaikadhibisha kuikataa.
#
{46} {مَن عَمِلَ صالحاً}: وهو العملُ الذي أمر الله به ورسوله {فَلِنَفْسِهِ}: نفعه وثوابه في الدنيا والآخرة. {ومن أساء فعليها}: ضررُه وعقابُه في الدُّنيا والآخرة، وفي هذا حثٌّ على فعل الخير وترك الشرِّ، وانتفاعُ العاملين بأعمالهم الحسنةِ، وضررُهم بأعمالهم السيئةِ، وأنَّه لا تزِرُ وازرةٌ وِزْرَ أخرى. {وما ربُّك بظلام للعبيدِ}: فيحمِّلُ أحداً فوق سيئاتِهِ.
{46} "Anayetenda mema" ambayo ni matendo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "basi anajitendea mwenyewe, nafsi yake" ndiyo itanufaika na malipo yake mazuri katika dunia na Akhera. "Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile" madhara yake na adhabu yake katika dunia na Akhera. Na katika hayo kuna kuwahimiza watu kutenda mema na kuacha maovu, na watendaji matendo mema kufaidika na matendo yao mema, na kudhurika kwao kwa matendo yao mabaya, na kwamba habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. "Wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja," kwa hivyo hambebeshi yeyote zaidi ya mabaya yake.
: 47 - 48 #
{إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ وَمَا تَخْرُجُ مِنْ ثَمَرَاتٍ مِنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنْثَى وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِنْ شَهِيدٍ (47) وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَدْعُونَ مِنْ قَبْلُ وَظَنُّوا مَا لَهُمْ مِنْ مَحِيصٍ (48)}.
47. Ujuzi wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala cha kike hakichukui mimba, wala hakizai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayowaita, akawaambia: 'Wako wapi washirika wangu?' Hapo watasema: 'Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anayeshuhudia hayo.' 48. Na wakawapotea wale waliokuwa wakiwaomba hapo kwanza, na wakawa na yakini kuwa hawana pa kukimbilia.
#
{47 - 48} هذا إخبارٌ عن سعة علمهِ تعالى واختصاصِهِ بالعلم الذي لا يطَّلع عليه سواه، فقال: {إليه يُرَدُّ علمُ الساعةِ}؛ أي: جميع الخلق يَرُدُّ علمها إلى الله تعالى، ويقرُّون بالعجز عنه؛ الرسلُ والملائكةُ وغيرُهم. {وما تَخْرُجُ من ثمراتٍ من أكمامها}؛ أي: وعائها الذي تخرُجُ منه، وهذا شاملٌ لثمرات جميع الأشجار التي في البلدان والبراري؛ فلا تخرُجُ ثمرةُ شجرةٍ من الأشجار إلاَّ وهو يعلمُها علماً تفصيليًّا. {وما تحمِلُ من أنثى}: من بني آدم وغيرهم من أنواع الحيوانات إلاَّ بعلمه، {ولا تضعُ} [أنثى حملَها] {إلاَّ بعلمِهِ}؛ فكيف سوَّى المشركون به تعالى مَنْ لا علم عنده ولا سمعَ ولا بصرَ؟ {ويوم يناديهم}؛ أي: المشركين به يوم القيامةِ توبيخاً وإظهاراً لكذِبِهم، فيقول لهم: {أين شركائي}: الذين زعمتُم أنَّهم شركائي، فعبدتُموهم وجادلتُم على ذلك وعاديتُم الرسل لأجلهم ؟ {قالوا}: مقرِّين ببطلان إلهيتهم وشركتهم مع الله: {آذَنَّاكَ ما مِنَّا من شهيدٍ}؛ أي: أعلمناك يا ربَّنا واشهدْ علينا أنَّه ما منَّا أحدٌ يشهد بصحة إلهيَّتهم وشركتهم؛ فكلُّنا الآن [قد] رجعنا إلى بطلان عبادتها وتبرَّأنا منها، ولهذا قال: {وضلَّ عنهم ما كانوا يَدْعونَ}: من دون الله؛ أي: ذهبت عقائدُهم وأعمالُهم التي أفَنَوا فيها أعمارهم على عبادة غير الله، وظنُّوا أنها تفيدُهم، وتدفعُ عنهم العذاب، وتشفع لهم عند اللهِ، فخاب سعيُهم، وانتقض ظنُّهم، ولم تُغْنِ عنهم شركاؤهم شيئاً. {وظنُّوا}؛ أي: أيقنوا في تلك الحال {ما لهم من مَحيصٍ}؛ أي: منقذٍ ينقذُهم ولا مغيثٍ ولا ملجأٍ. فهذه عاقبةُ من أشركَ بالله غيرَه، يُبَيِّنُها اللهُ لعباده، ليحذروا الشركَ به.
{47 - 48} Huku ni kujulisha kuhusu upana wa elimu yake Mtukufu na umaalumu wake katika elimu ambayo hapana awezaye kuijua isipokuwa Yeye tu. Alisema: "Ujuzi wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu." Yaani, viumbe wote wanarudisha elimu yao kwa Mwenyezi Mungu, na wanakiri kutoweza kwao kuijua, sawa wawe Mitume, Malaika au wengineo. "Na matunda hayatoki katika mafumba yake." Hili linajumuisha matunda ya miti yote katika miji na jangwani. Kwa hivyo, matunda ya mti wowote hayatoki isipokuwa naye anayajua kwa undani. "Wala cha kike hakichukui mimba" katika wanadamu na wanyama ila kwa kujua kwake, "wala hakizai ila kwa kujua kwake." Basi vipi washirikina walimfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa sawa na visivyokuwa na elimu, wala kusikia, wala kuona? "Na siku atakayowaita" washirikina, Siku ya Kiyama, kwa njia ya kuwakaripia na kuonyesha uwongo wao, atawaambia: "'Wako wapi washirika wangu'" ambao mlikuwa mkidai kuwa ni washirika wangu, na mkawaabudu, mkajadili haki kwa itikadi hiyo na mkawafanyia uadui Mitume kwa ajili yao? "Hapo watasema" wakikiri ubatili wa miungu wao na kuwashirikisha kwao na Mwenyezi Mungu: "'Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anayeshuhudia'" usahihi wa uungu wao na ushirika wao. Sisi sote sasa tumekubali ubatili wa kuwaabudu miungu hao na tumejitenga mbali nao. Ndiyo maana akasema: "Na wakawapotea wale waliokuwa wakiwaomba hapo kwanza" badala ya Mwenyezi Mungu. Yaani, zimepotelea mbali itikadi zao na matendo yao waliyomaliza umri wao katika kuabudu visivyokuwa Mwenyezi Mungu na wakadhani kuwa vitawafaa na kuwaepusha mbali na adhabu, na kuwafanyia uombezi kwa Mwenyezi Mungu. Lakini juhudi zao hizo zikapotelea mbali, na dhana yao hiyo ikaambulia patupu na washirika wao hao hawakuwafaa kitu. "Na wakawa na yakini" katika hali hiyo "kuwa hawana pa kukimbilia." Huu ndio mwisho wa mwenye kumshirikisha yeyote na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anawabainishia waja wake ili wajihadhari na kumshirikisha.
: 49 - 51 #
{لَا يَسْأَمُ الْإِنْسَانُ مِنْ دُعَاءِ الْخَيْرِ وَإِنْ مَسَّهُ الشَّرُّ فَيَئُوسٌ قَنُوطٌ (49) وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِنَّا مِنْ بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِنْ رُجِعْتُ إِلَى رَبِّي إِنَّ لِي عِنْدَهُ لَلْحُسْنَى فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُمْ مِنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ (50) وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنْسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَى بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ (51)}.
49. Mwanadamu hachoki kuomba dua za heri, na inapompata shari, mara huvunjika moyo muno akakata tamaa sana. 50. Na pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya dhara kumgusa, bila ya shaka husema: 'Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nina mema yangu kwake!' Basi kwa yakini tutawaelezea wale waliokufuru hayo waliyoyatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu. 51. Na tukimneemesha mwanadamu, hugeuka na kujitenga upande, na inapomgusa shari, huwa na madua marefu marefu.
#
{49} هذا إخبارٌ عن طبيعة الإنسان من حيثُ هو، وعدم صبرِه وجَلَدِه، لا على الخير ولا على الشرِّ، إلاَّ مَن نقله الله من هذه الحال إلى حال الكمال، فقال: {لا يسأمُ الإنسانُ من دعاءِ الخيرِ}؛ أي: لا يملُّ دائماً من دعاء الله في الغنى والمال والولدِ وغير ذلك من مطالب الدُّنيا، ولا يزال يعملُ على ذلك، ولا يقتنعُ بقليل ولا بكثيرٍ منها؛ فلو حصل له من الدُّنيا ما حصل؛ لم يزل طالباً للزيادة. {وإن مَسَّهُ الشرُّ}؛ أي: المكروه كالمرض والفقر وأنواع البلايا، {فَيؤوسٌ قنوطٌ}؛ أي: ييأس من رحمة الله تعالى، ويظنُّ أن هذا البلاء هو القاضي عليه بالهلاكِ، ويتشوَّشُ من إتيان الأسبابِ على غير ما يحبُّ ويطلبُ؛ إلاَّ الذين آمنوا وعملوا الصالحات؛ فإنَّهم إذا أصابهم الخيرُ والنعمةُ والمحابُّ؛ شكروا الله تعالى، وخافوا أن تكونَ نعمُ الله عليهم استدراجاً وإمهالاً، وإن أصابتْهم مصيبةٌ في أنفسهم وأموالهم وأولادِهم؛ صبروا ورَجَوا فضل ربِّهم فلم ييأسوا.
{49} Hapa Mwenyezi Mungu anaelezea kuhusu maumbile ya asili ya mwanadamu jinsi alivyo, na kutokuwa na subira na ustahimilivu kwake, si juu ya heri wala juu ya shari, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimtoa kutoka katika hali hii na kumpeleka kwenye hali ya ukamilifu. Akasema, "Mwanadamu hachoki kuomba dua za heri" Yaani, hachoki kamwe kuchoki kumuomba Mwenyezi Mungu utajiri, mali, watoto na mahitaji mengineyo ya kidunia, na anaendelea kufanya hivyo tu. Haridhiki na kidogo wala kingi katika hivyo. Lau atapata vile atakavyovipata katika maisha ya kidunia, basi angeendelea tu kutafuta zaidi. "Na inapompata shari" kama vile maradhi, umasikini, na aina mbalimbali za balaa, "mara huvunjika moyo muno akakata tamaa sana" kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anadhani kuwa balaa hii ndiyo itakayompelekea kuangamia, na anachanganyikiwa kwa sababu mambo yamefanyika kwa njia ambayo hapendi. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema. Wao, wanapopatwa na wema, neema, na mambo wanayoyapenda, wanamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wanahofu kwamba neema hiyo ya Mwenyezi Mungu juu yao huenda ni kwa njia ya kuwatwaa polepole na kuwapa muhula. Na wakipatwa na msiba katika nafsi zao, mali zao na watoto wao, wanasubiri na wanatarajia fadhila za Mola wao Mlezi, wala hawakati tamaa.
#
{50} ثم قال تعالى: {ولئِنْ أذَقْناه}؛ أي: الإنسان الذي لا يسأم من دُعاء الخير وإن مسَّه الشرُّ فيؤوسٌ قنوطٌ {رحمةً منَّا}؛ أي: بعد ذلك الشرِّ الذي أصابه؛ بأنْ عافاه الله من مرضِهِ أو أغناه من فقرِهِ؛ فإنَّه لا يشكر الله تعالى؛ بل يبغي ويطغى ويقول: {هذا لي}؛ أي: أتاني لأنِّي له أهلٌ وأنا مستحقٌّ له، {وما أظنُّ الساعةَ قائمةً}، وهذا إنكارٌ منه للبعث، وكفرٌ للنعمة والرحمة التي أذاقها الله له، {ولئن رُجِعْتُ إلى ربِّي إنَّ لي عنده للحُسْنى}؛ أي: على تقدير إتيان الساعة، وأنِّي سأرجع إلى ربي؛ إنَّ لي عنده للحسنى؛ فكما حصلت لي النعمة في الدُّنيا؛ فإنَّها ستحصُلُ لي في الآخرة! وهذا من أعظم الجرأة والقول على الله بلا علم؛ فلهذا توعَّده [اللَّهُ] بقولِهِ: {فَلَنُنَبِّئَنَّ الذين كفروا بما عَمِلوا ولَنُذيقَنَّهم من عذابٍ غليظٍ}؛ أي: شديد جدًّا.
{50} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na pindi tukimwonjesha" mwanadamu huyu ambaye hachoki kuomba heri, lakini inapompata shari, mara huvunjika moyo mno akakata tamaa sana, "rehema itokayo kwetu." Yaani, baada ya shari hiyo iliyompata, kwa njia ya Mwenyezi Mungu kumponya kutokana na ugonjwa wake au kumtajirisha baada ya umaskini wake, yeye hakika hamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu,bali anafanya dhuluma na kutakabari na kusema: "'Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja." Lakini ikichukuliwa kwamba kitakuja na kwamba nitarudi kwa Mola wangu Mlezi, "bila ya shaka nina mema yangu kwake!" Kama vile nilipata neema katika dunia, neema hiyo pia nitaipata huko akhera!' Lakini huu ni katika ujasiri mkubwa zaidi na kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila elimu. Basi ndiyo maana [Mwenyezi Mungu] alimtishia kwa kauli yake: "Basi kwa yakini tutawaelezea wale waliokufuru hayo waliyoyatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu."
#
{51} {وإذا أنْعَمْنا على الإنسان}: بصحَّة أو رزقٍ أو غيرهما {أعرضَ}: عن ربِّه وعن شكرِهِ، {ونأى}؛ أي: ترفَّع {بجانبِهِ}: عجباً وتكبراً، {وإذا مسَّه الشرُّ}: أي: المرضُ أو الفقرُ أو غيرُهما {فذو دعاءٍ عريضٍ}؛ أي: كثير جدًّا؛ لعدم صبره؛ فلا صبر في الضرَّاء ولا شكر في الرَّخاء؛ إلاَّ مَنْ هداه الله ومنَّ عليه.
{51} "Na tukimneemesha mwanadamu" kwa kumpa afya njema, riziki au mambo mengineyo, "hugeuka" mbali na Mola wake Mlezi na hata akaacha kumshukuru, "na kujitenga upande" kwa kujiona na kufanya kiburi. "Na inapomgusa shari," kama vile maradhi au umaskini au mengineyo, "huwa na madua marefu marefu" kwa sababu ya kutokuwa na subira. Basi huwa hana subira katika shida na wala huwa hashukuru katika maisha mepesi, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa na akamneemesha.
: 52 - 54 #
{قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ كَانَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ ثُمَّ كَفَرْتُمْ بِهِ مَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ هُوَ فِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ (52) سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنْفُسِهِمْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ (53) أَلَا إِنَّهُمْ فِي مِرْيَةٍ مِنْ لِقَاءِ رَبِّهِمْ أَلَا إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُحِيطٌ (54)}.
52. Sema: 'Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi ikawa ndio mmeyakataa, ni nani aliyepotea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?' 53. Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je, haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi bora wa kila kitu? 54. Tanabahi, hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Tanabahi, hakika Yeye amekizunguka kila kitu.
#
{52} أي: {قل}: لهؤلاء المكذِّبين بالقرآن المسارعين إلى الكُفران: {أرأيتُم إن كانَ}: هذا القرآنُ {من عندِ الله}: من غير شكٍّ ولا ارتيابٍ، {ثم كفرتُم به مَنْ أضلُّ ممَّنْ هو في شقاقٍ بعيدٍ}؛ أي: معاندة لله ولرسوله؛ لأنَّه تبيَّن لكم الحقُّ والصوابُ، ثم عدلتُم عنه لا إلى حقٍّ، بل إلى باطل وجهل؛ فإذاً تكونون أضلَّ الناس وأظلَمَهم.
{52} Yaani, "sema" ukiwaambia hao wanaoikadhibisha Qur-ani na wanaokimbilia kukufuru: "'Mnaonaje! Ikiwa" Qur-ani hii "inatoka kwa Mwenyezi Mungu" bila ya shaka yoyote wala kusitasita kokote, "nanyi ikawa ndio mmeikataa, ni nani aliyepotea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali,'" ambaye anamkaidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa sababu ilikwisha wabainikia haki na yale yaliyo sahihi, kisha mkayaacha na mkaendea batili na ujinga. Basi nyinyi ndio mnakuwa wapotovu na madhalimu zaidi katika watu wote.
#
{53} فإنْ قلتُم أو شككتُم بصحَّته وحقيقتِهِ؛ فسيقيم الله لكم، ويريكم من آياتِهِ في الآفاق؛ كالآياتِ التي في السماء وفي الأرض وما يُحْدِثُه الله تعالى من الحوادثِ العظيمة الدالَّة للمستبصر على الحقِّ. {وفي أنفسِهِم}: مما اشتملتْ عليه أبدانُهم من بديع آياتِ الله وعجائبِ صنعتِهِ وباهر قدرتِهِ، وفي حلول العقوبات والمَثُلات في المكذِّبين ونصر المؤمنين، {حتى يتبيَّن لهم}: من تلك الآياتِ بياناً لا يقبل الشكَّ، {أنَّه الحقُّ}: وما اشتمل عليه حقٌّ، وقد فعل تعالى؛ فإنَّه أرى عباده من الآيات ما به تبيَّن [لهم] أنه الحقُّ، ولكن الله هو الموفِّق للإيمان مَنْ شاء، والخاذل لمن يشاء. {أو لم يكفِ بربِّك أنَّه على كلِّ شيءٍ شهيدٌ}؛ أي: أولم يكفِهم ـ على أنَّ القرآن حقٌّ، ومن جاء به صادقٌ ـ شهادةُ الله تعالى؛ فإنَّه قد شهد له بالصدق، وهو أصدقُ الشاهدين، وأيَّده ونصره نصراً متضمِّناً لشهادته القوليَّة عند من شكَّ فيها.
{53} Mkisema au mkatilia shaka usahihi wake na uhakika wake, basi Mwenyezi Mungu atawasimamishia na kukuonyesheni baadhi ya Ishara zake katika upeo wa macho, kama vile ishara zilizo mbinguni na ardhini, na yale anayoyaleta Mwenyezi Mungu Mtukufu miongoni mwa matukio makubwa yanayoashiria haki kwa mwenye kutafuta kuiona, "na katika nafsi zao wenyewe" katika yale yaliyomo ndani ya miili yao miongoni mwa Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu ya uumbaji wake na uweza wake unaong'aa, na kutokea kwa adhabu na mifano juu ya wanaokadhibisha na kuwanusuru Waumini, "mpaka iwabainikie" katika ishara hizo kwa ubainifu usio na shaka yoyote "kwamba haya ni kweli" na yaliyomo ndani yake ni kweli. Na tayari Yeye Mtukufu alikwishafanya hivyo, kwani aliwaonyesha waja wake katika Ishara ambazo kwazo ilibainika kwamba haya ndiyo haki. Lakini Mwenyezi Mungu ndiye anayewezesha amtakaye kuamini, naye ndiye anayemuachilia mbali amtakaye. "Je, haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi bora wa kila kitu?" Yaani, je, ushahidi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu hauwatoshi kwamba Qur-ani hii ni ya kweli, na yule aliyekuja nayo ni mkweli? Kwani alimshuhudilia kwamba ni mkweli, na Yeye ndiye mkweli zaidi wa mashahidi wote, na akamuunga mkono na akamnusuru kwa nusura iliyojumuisha ushahidi wake wa kimaneno kwa wale walioutilia shaka.
#
{54} {ألا إنِّهم في مِرْيَةٍ من لقاءِ ربِّهم}؛ أي: في شكٍّ من البعث والقيامةِ، وليس عندَهم دارٌ سوى الدار الدُّنيا؛ فلذلك لم يعملوا للآخرة، ولم يلتفتوا لها. {ألا إنَّه بكلِّ شيءٍ محيطٌ}: علماً وقدرةً وعزةً.
{54} "Tanabahi, hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi!" Yaani, wana shaka juu ya kufufuliwa na Kiyama, na wala hawana nyumba nyingine isiyokuwa nyumba ya duniani. Ndiyo maana hawakuifanyia akhera matendo wala hata hawakuitazama. "Tanabahi, hakika Yeye amekizunguka kila kitu" kwa elimu yake, uwezo wake na utukufu wake.
Imekamilika tafsiri ya Surat As-Sajdah kwa neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
* * *