Tafsiri ya Surat Az-Zukhruf
Tafsiri ya Surat Az-Zukhruf
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{حم (1) وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ (2) إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ (3) وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ (4) أَفَنَضْرِبُ عَنْكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَنْ كُنْتُمْ قَوْمًا مُسْرِفِينَ (5)}.
1. Ha Mim 2. Ninaapa kwa Kitabu kinachobainisha. 3. Hakika Sisi tumeifanya Qur-ani kwa Kiarabu ili mfahamu. 4. Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yaliyoko kwetu, ni tukufu na yenye hekima. 5. Je, tuache kuwakumbusha kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mliopita mipaka kwa ukafiri?
#
{1 - 3} هذا قسمٌ بالقرآن على القرآن، فأقسم بالكتاب المبين، وأطلق، ولم يذكُرِ المتعلَّق؛ ليدلَّ على أنه مبينٌ لكل ما يحتاج إليه العباد من أمور الدُّنيا والدِّين والآخرة. {إنَّا جَعَلْناه قرآناً عربيًّا}: هذا المقسَم عليه أنَّه جُعِلَ بأفصح اللغاتِ وأوضحِها وأبينها، وهذا من بيانه. وذكر الحكمةَ في ذلك، فقال: {لعلَّكم تعقلونَ}؛ ألفاظَه ومعانيَه لتيسُّرها وقربها من الأذهان.
{1 - 3} Huku ni kuapa kwa Qur-ani juu ya Qur-ani. Basi akaapa kwa Kitabu kinachobainisha, na akawa ameliachilia hilo bila kulifungia, ili kuashiria kuwa kinabainisha kila wanachohitaji waja katika mambo ya kidunia, kidini na kiakhera. "Hakika Sisi tumeifanya Qur-ani kwa Kiarabu." Haya ndiyo yaliyoapiwa kwamba imefanywa kwa lugha fasaha zaidi, iliyo wazi na bainifu zaidi, na hili ni katika kubainisha kwake. Kisha akataja hekima katika hilo,
akasema: "ili mfahamu" maneno yake na maana zake kwa sababu ya urahisi wake na ukaribu wake na akili.
#
{4} {وإنَّه}؛ أي: هذا الكتاب {لدينا} في الملأ الأعلى في أعلى الرُّتب وأفضلها {لَعَلِيٌّ حكيمٌ}؛ أي: لعليٌّ في قدره وشرفه ومحله، حكيم فيما يشتمل عليه من الأوامر والنواهي والأخبار؛ فليس فيه حكمٌ مخالفٌ للحكمة والعدل والميزان.
{4} "Na hakika hiyo" yaani, Kitabu hiki "kwetu" katika watukufu wa juu kabisa, kiko katika daraja la juu zaidi na bora zaidi "ni tukufu na yenye hekima. "Ni kitukufu katika cheo chake, heshima yake, nafasi yake, na ni chenye hekima katika amri zake, makatazo yake na habari zake. Hakuna hukumu ndani yake ambayo ni kinyume na hekima, uadilifu na usawa.
#
{5} ثم أخبر تعالى أنَّ حكمته وفضلَه يقتضي أنْ لا يتركَ عباده هملاً لا يرسل إليهم رسولاً ولا ينزل عليهم كتاباً ولو كانوا مسرفين ظالمين، فقال: {أفنضرِبُ عنكم الذِّكْرَ صفحاً}؛ أي: أفنعرض عنكم ونترك إنزال الذِّكر إليكم ونضرب عنكم صفحاً لأجل إعراضِكم وعدم انقيادِكم [له]، بل ننزل عليكم الكتابَ، ونوضِّح لكم فيه كلَّ شيءٍ؛ فإنْ آمنتُم به واهتديتُم؛ فهو من توفيقِكم، وإلاَّ؛ قامت عليكم الحجَّة، وكنتُم على بيِّنة من أمركم.
{5} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuambia kwamba hekima yake na fadhila zake zinalataka kwamba asiwaache waja wake wakiwa wameghafilika, bila ya hatawatumia mtume wala kuwateremshia kitabu, hata kama wao ni wapitilizao viwango madhalimu. Akasema, "Je, tuache kuwakumbusha kabisa." Yaani, je, tuwape mgongo na tuache kukuteremshieni ukumbusho kwa sababu ya kupena kwenu migongo na kutokifuata kwenu. Bali tunawateremshia Kitabu na ndani yake tunawabainishia kila kitu. kwa hivyo, mkikiamini na mkaongoka, basi ni kutokana na kuwawezesha kwake. Vinginevyo, tayari hoja ishasimama juu yenu, na tayari mmeshajua vyema jambo lenu hili.
{وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِنْ نَبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ (6) وَمَا يَأْتِيهِمْ مِنْ نَبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (7) فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُمْ بَطْشًا وَمَضَى مَثَلُ الْأَوَّلِينَ (8)}.
6. Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani! 7. Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli. 8. Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita.
#
{6 - 8} يقول تعالى: إنَّ هذه سنَّتُنا في الخلق أن لا نَتْرُكَهم هملاً؛ فكم {أرسَلْنا من نبيٍّ في الأوَّلين}: يأمرونهم بعبادة الله وحده لا شريك له، ولم يزل التكذيبُ موجوداً في الأمم. {وما يأتيهم من نبيٍّ إلاَّ كانوا به يستهزِئونَ}: جَحْداً لما جاء به، وتكبُّراً على الحقِّ، {فأهْلَكْنا أشدَّ} من هؤلاء {بطشاً}؛ أي: قوة وأفعالاً وآثاراً في الأرض، {ومضى مَثَلُ الأوَّلين}؛ أي: مضت أمثالُهم وأخبارُهم وبيَّنَّا لكم منها ما فيه عبرةٌ ومزدجَرٌ عن التكذيب والإنكار.
{6 - 8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Hakik hii ndiyo desturi yetu kuhusu viumbe kwamba hatuwezi kuwaacha bure tu. Kwani ni "Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!" wakawa wanawaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika, lakini umma mbalimbali wakaendelea kukadhibisha. "Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli" na wakikanusha yale aliyokuja nayo, na wakiifanyia jeuri haki. "Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao" katika ardhi. "Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita" na tumekubainishieni hayo ambayo ndani yake yamo mazingatio, makemeo dhidi ya kukadhibisha na kukataa.
{وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ (9) الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ (10) وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنْشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَيْتًا كَذَلِكَ تُخْرَجُونَ (11) وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُمْ مِنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ (12) لِتَسْتَوُوا عَلَى ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ (13) وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ (14)}].
9.
Na ukiwauliza: 'Nani aliyeziumba mbingu na ardhi?' Bila ya shaka watasema: 'Kaziumba Mwenye nguvu, ajuaye zaidi.' 10. Ambaye amewafanyieni ardhi kama tandiko, na akawafanyieni ndani yake njia mpate kuongoka. 11. Na ambaye ndiye aliyeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyokufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa. 12. Na ambaye ndiye aliyeumba katika kila kitu jike na dume, na akawafanyieni merikebu na wanyama mnaowapanda. 13. Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao,
na mseme: 'Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe.' 14. Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.
#
{9} يخبر تعالى عن المشركين أنَّك لو {سألتَهم مَنْ خَلَقَ السمواتِ والأرضَ ليقولنَّ}: الله وحدَه لا شريك له. {العزيز}: الذي دانت لعزَّته جميع المخلوقات. {العليم}: بظواهر الأمور وبواطنها وأوائلها وأواخراها. فإذا كانوا مقرِّين بذلك؛ فكيف يجعلون له الولدَ والصاحبةَ والشريكَ؟! وكيف يشركون به من لا يَخْلُقُ ولا يرزقُ ولا يميتُ ولا يحيي؟!
{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kuhusu washirikina kwamba "ukiwauliza: 'Nani aliyeziumba mbingu na ardhi?' Bila ya shaka watasema" ni Mwenyezi Mungu asiye na mshirika yeyote. "Mwenye nguvu" ambaye viumbe vyote vinanyenyekea kwa sababu ya nguvu zake. "Ajuaye zaidi" mambo ya dhahiri ya vitu na ya ndani yake, ya mwanzo yake na ya mwisho yake. Kwa hivyo, ikiwa wanakiri hivyo, basi vipi wanamfanya kuwa na mtoto, mke na mwenza? Na vipi wanamshirikisha na vitu visivyoumba, wala kuruzuku, wala kufisha wala kuhuisha?
#
{10} ثم ذكر أيضاً من الأدلَّة الدالَّة على كمال نعمته واقتداره بما خَلَقه لعباده من الأرض التي مَهَدها وجعلها قراراً للعباد يتمكَّنون فيها من كلِّ ما يريدون، {وجَعَلَ لكم فيها سُبُلاً}؛ أي: جعل منافذ بين سلاسل الجبال المتَّصلة تنفُذون منها إلى ما ورائها من الأقطار، {لعلَّكم تهتدونَ}: في السير في الطرق ولا تضيعون، ولعلَّكم أيضاً تهتدون في الاعتبار بذلك والادِّكار فيه.
{10} Kisha akataja baadhi ya ushahidi unaoonyesha ukamilifu wa neema zake na uwezo wake kwa sababu ya vile alivyowaumbia waja wake, kama vile ardhi aliyoitandaza na akaifanya kuwa pahala penye utulivu kwa waja wake ambapo wanaweza kufanya humo kila walitakalo. "Na akawafanyieni ndani yake njia mbalimbali" kati ya safu za milima zilizoshikamana, mkawa mnaweza kupita kati yake hadi kwenye pande zilizo ng'ambo yake, "ili mpate kuongoka" katika njia hizo na msipotee, na ili pia mkaongoke kwa kuyazingatia hayo na kukumbuka.
#
{11} {والذي نَزَّلَ من السماءِ ماءً بقدرٍ}: لا يزيدُ ولا ينقُص، ويكون أيضاً بمقدار الحاجةِ؛ لا ينقُصُ بحيث لا يكون فيه نفعٌ، ولا يزيدُ بحيث يضرُّ العباد والبلاد، بل أغاث به العبادَ، وأنقذ به البلادَ من الشدَّة، ولهذا قال: {فأنشَرْنا به بلدةً ميتاً}؛ أي: أحييناها بعد موتها، {كذلك تُخْرَجونَ}؛ أي: فكما أحيا الأرض الميتة الهامدة بالماء؛ كذلك يحييكم بعدما تستكملونَ في البرزخ ليجازِيَكم بأعمالكم.
{11} "Na ambaye ndiye aliyeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi" hayazidi yakawadhuru waja na nchi wala hayapungui yakakosa kuwa na manufaa. Bali yanakuwa kulingana na haja.
Ndiyo maana akasema: "Na kwa hayo tukaifufua nchi iliyokufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyotolewa." Kama vile alivyoihuisha kwa maji ardhi iliyokufa na kutulia, basi vivyo hivyo atakuhuisheni baada ya kumaliza siku zenu za kaburini ili akulipeni kwa matendo yenu.
#
{12} {والذي خَلَقَ الأزواجَ كلَّها}؛ أي: الأصناف جميعها مما تُنْبِتُ الأرض ومن أنفسِهم ومما لا يعلمون؛ من ليل ونهار، وحرٍّ وبرد، وذكر وأنثى ... وغير ذلك، {وجعل لكم من الفُلْكِ}؛ أي: السفن البحريَّة الشراعيَّة والناريَّة ما تركبون، {و} من {الأنعام ما تركبونَ}.
{12} "Na ambaye ndiye aliyeumba katika kila kitu jike na dume" miongoni mwa vile ambavyo vinaoteshwa na ardhi, na katika nafsi zao, na katika wasivyovijua, kama vile usiku na mchana, joto na baridi, dume na jike... na mengineyo. "Na akawafanyia merikebu na wanyama mnaowapanda."
#
{13} {لتستووا على ظهورِهِ}: وهذا شامل لظهورِ الفُلك ولظهور الأنعام؛ أي: لتستقرُّوا عليها. {ثم تذكروا نعمةَ ربِّكم إذا استويتُم عليه}: بالاعتراف بالنعمة لمن سخَّرها والثناء عليه تعالى بذلك، ولهذا قال: {وتقولوا سبحانَ الذي سخَّر لنا هذا وما كُنَّا له مقرِنينَ}؛ أي: لولا تسخيره لنا ما سَخَّر من الفلك والأنعام؛ ما كنا مُطيقينَ لذلك وقادِرين عليه، ولكن من لطفِهِ وكرمِهِ تعالى سخَّرها وذلَّلها ويسَّر أسبابها. والمقصودُ من هذا بيانُ أن الربَّ الموصوفَ بما ذكره من إفاضة النِّعم على العبادِ هو الذي يستحقُّ أن يُعبد، ويصلَّى له ويُسجَد.
{13} "Ili mkae vizuri kwenye migongoni mwao" sawa iwe vyombo vya baharini au wanyama "kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao" kwa kukiri neema zake hizo yule aliyezitiisha na kumsifu.
Ndiyo maana akasema: "Na mseme: 'Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe." Yaani, lau si yeye kututiishia hivyo vyote miongoni mwa merikebu na wanyama, hatukuweza hilo. Lakini kutokana na upole wake na ukarimu wake Mtukufu alivitiisha na akarahisisha sababu zake. Kinachokusudiwa na haya ni kubainisha kuwa Mola Mlezi anayesifika kwa kuwafikishia waja neema mbalimbali, Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, kuswali kwa ajili yake na kumsujudia.
{وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا إِنَّ الْإِنْسَانَ لَكَفُورٌ مُبِينٌ (15) أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُمْ بِالْبَنِينَ (16) وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُمْ بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ (17) أَوَمَنْ يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ (18) وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَنِ إِنَاثًا أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ (19) وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَنُ مَا عَبَدْنَاهُمْ مَا لَهُمْ بِذَلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ (20) أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِنْ قَبْلِهِ فَهُمْ بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ (21) بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِمْ مُهْتَدُونَ (22) وَكَذَلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِنْ نَذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِمْ مُقْتَدُونَ (23) قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُمْ بِأَهْدَى مِمَّا وَجَدْتُمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُمْ بِهِ كَافِرُونَ (24) فَانْتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَانْظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ (25)}.
15. Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhahiri. 16. Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyoviumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume? 17. Na anapobashiriwa mmoja wao kwa yale aliyompigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira. 18. Ati aliyelelewa katika mapambo na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana? 19. Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa! 20.
Nao husema: 'Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu sisi.' Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu! 21. Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, na ikawa wao wanakishikilia hicho. 22.
Bali wanasema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao.' 23.
Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake waliodeka kwa starehe walisema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.' 24. Akasema
(Mwonyaji): 'Hata nikiwaletea yenye uwongofu bora kuliko mliowakuta nao baba zenu?' Wakasema: 'Sisi tunayakataa tu hayo mliyotumwa nayo.' 25. Kwa hivyo, tukawalipizia. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!
#
{15} يخبر تعالى عن شناعةِ قول المشركين الذين جعلوا لله تعالى ولداً، وهو الواحد الأحدُ الفرد الصَّمد، الذي لم يتَّخذ صاحبة ولا ولداً، ولم يكنْ له كفُواً أحدٌ. وأنَّ ذلك باطلٌ من عدة أوجه: منها: أنَّ الخلقَ كلَّهم عباده، والعبوديَّة تنافي الولادة. ومنها: أنَّ الولد جزءٌ من والدِهِ، والله تعالى بائنٌ من خلقِهِ مباينٌ لهم في صفاته ونعوت جلاله، والولدُ جزءٌ من الوالدِ؛ فمحالٌ أن يكون لله تعالى ولدٌ.
{15} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu ubaya mkubwa wa maneno ya washirikina walionasibisha mwana kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ilhali Yeye ndiye Mmoja tu, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakujifanyia mke wala mwana, na hakuna yeyote aliye sawa na Yeye. Hayo wanayoyadai ni batili kwa njia nyingi. Miongoni mwake ni kwamba viumbe vyote ni waja wake, na uja hauwiani na kuwa mwana wa Mwenyezi Mungu. Miongoni mwake ni kwamba mwana ni sehemu ya baba yake, naye Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko tofauti na viumbe vyake katika sifa zake za utukufu, naye mwana ni sehemu ya baba yake. Kwa hivyo, haiwezekani kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana.
#
{16} ومنها: أنَّهم يزعُمون أنَّ الملائكةَ بناتُ الله، ومن المعلوم أنَّ البناتِ أدونُ الصنفينِ؛ فكيف يكون لله البناتُ ويصطفيهم بالبنين ويفضِّلهم بها؟! فإذاً؛ يكونون أفضلَ من الله! تعالى اللهُ عن ذلك علوًّا كبيراً!
{16} Miongoni mwake ni kwamba wanadai kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu, na kama inavyojulikana ni kuwa mabinti huwa chini kuliko wanaume. Basi vipi Mwenyezi Mungu anawezaje kuwa na watoto wa kike na akawapa wao tu watoto wa kiume na kuwaboresha kwa hilo? Kama ni hivyo, basi wao ni bora kuliko Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu yuko juu sana ya hayo!
#
{17}: ومنها: أنَّ الصنف الذي نَسبوه لله ـ وهو البنات ـ أدون الصنفين وأكرههما لهم، حتى إنَّهم من كراهتهم لذلك {إذا بُشِّرَ أحدُهم بما ضَرَبَ للرحمن مثلاً ظلَّ وجهُهُ مسودًّا}؛ من كراهته وشدَّة بغضه؛ فكيف يجعلون لله ما يكرهون؟!
{17}: Miongoni mwake ni kwamba ile aina waliyoinasibisha kwa Mwenyezi Mungu - ambayo ni wasichana - ni ya chini zaidi na inayowachukiza zaidi katika aina mbili hizi, kiasi kwamba kwa sababu ya vile wanavyowachukia "anapobashiriwa mmoja wao kwa yale aliyompigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika" basi wanawezaje kumpa Mwenyezi Mungu kile wanachokichukia?
#
{18} ومنها: أنَّ الأنثى ناقصةٌ في وصفها وفي منطقها وبيانها، ولهذا قال تعالى: {أوَمَن يُنَشَّأ في الحِلْيَةِ}؛ أي: يجمَّل فيها لنقص جمالِهِ، فيجمَّل بأمرٍ خارج منه ، {وهو في الخصام}؛ أي: عند الخصام الموجب لإظهارِ ما عند الشخص من الكلام {غيرُ مبينٍ}؛ أي: غير مبينٍ لحجَّته ولا مفصح عمَّا احتوى عليه ضميرُه؛ فكيف ينسبونهنَّ لله تعالى؟!
{18} Miongoni mwake ni kwamba mwanamke ana mapungufu katika sifa zake, mantiki yake na kubainisha kwake, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Ati aliyelelewa katika mapambo na katika mabishano hawezi kusema" hoja yake "kwa bayana?" Basi je, wanawezaje kuwanasibisha na Mungu Mwenyezi Mtukufu?
#
{19} ومنها: أنَّهم {جعلوا الملائكة الذين هم عبادُ الرحمن إناثاً}: فتجرؤوا على الملائكة العباد المقرَّبين، ورقَّوهم عن مرتبة العبادة والذُّلِّ إلى مرتبة المشاركة لله في شيء من خواصِّه، ثم نزلوا بهم عن مرتبةِ الذُّكوريَّة إلى مرتبة الأنوثيَّة؛ فسبحان من أظهر تناقضَ مَنْ كَذَبَ عليه وعاند رسله! ومنها: أنَّ الله ردَّ عليهم بأنَّهم لم يشهدوا خَلْقَ الله لملائكته؛ فكيف يتكلَّمون بأمرٍ من المعلوم عند كلِّ أحدٍ أنَّه ليس لهم به علمٌ؟! ولكن لا بدَّ أن يُسألوا عن هذه الشهادة، وستُكْتَبُ عليهم ويعاقَبون عليها.
{19}Miongoni mwake ni kwamba "wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake!" Hapo, wakawa wamewafanyia ujasiri Malaika, waja wa karibu na Mwenyezi Mungu, na wakawainua juu kutoka daraja la wao kufanya ibada na kumdhalilikia Mwenyezi Mungu hadi daraja la kumshiriki Mwenyezi Mungu katika baadhi ya mambo yake maalumu. Kisha wakawashusha kutoka kwenye kiwango cha uume hadi kwenye kiwango cha uke. Basi ametakasika Yule aliyedhihirisha kujipinga kwa yule aliyemdanganyishia na akawakaidi Mitume wake! Miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwajibu kwa kusema kwamba hawakushuhudia namna Mwenyezi Mungu alivyoumba Malaika wake. Basi wanawezaje kuzungumza juu ya kitu ambacho kinajulikana kwa kila mtu kwamba hawana elimu nacho? Lakini ni lazima wataulizwa juu ya ushahidi huu, na utaandikwa dhidi yao waadhibiwe kwa sababu yake.
#
{20} وقوله تعالى: {وقالوا لو شاء الرحمنُ ما عَبَدْناهُم}: فاحتجُّوا على عبادتهم الملائكة بالمشيئةِ، وهي حجةٌ لم يزل المشركونَ يطرِقونها، وهي حجةٌ باطلةٌ في نفسها عقلاً وشرعاً؛ فكلُّ عاقل لا يقبلُ الاحتجاج بالقدر، ولو سَلَكَه في حالةٍ من أحواله؛ لم يثبت عليها قدمه، وأمّا شرعاً؛ فإنَّ الله تعالى أبطل الاحتجاج به، ولم يذكُرْه عن غير المشركين به المكذِّبين لرسله؛ فإنَّ الله تعالى قد أقام الحجَّة على العباد؛ فلم يبقَ لأحدٍ عليه حجةٌ أصلاً، ولهذا قال هنا: {ما لهم بذلك من علم إنْ هم إلاَّ يَخْرُصونَ}؛ أي: يتخرَّصون تخرُّصاً لا دليل عليه، ويتخبَّطون خَبْطَ عشواء.
{20} Na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Nao husema: 'Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu sisi.'" Walitumia hoja ya mipango ya Mwenyezi Mungu juu ya kuwaabudu kwao Malaika. Na hii ni hoja ambayo washirikina wameendelea kuitumia, lakini ni hoja batili yenyewe, na hata kiakili na kisheria. Kwani, kila mtu mwenye akili timamu hakubali suala la kutumia hoja ya mipango ya Mwenyezi Mungu, na hata kama angeichukua kuwa hoja katika mojawapo ya hali zake, basi haungetulia juu yake mguu wake. Na ama kisheria, Mwenyezi Mungu alibatilisha kutumia hilo kuwa hoja, na wala hakutaja wanaolitumia isipokuwa wale wanaomshirikisha, wanaowakadhibisha Mitume wake. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alikwisha simamisha hoja dhidi ya waja wake, basi hakuna hata mmoja wao aliyesalia na hoja dhidi yake hata kidogo, na ndiyo maana akasema hapa, "Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uongo tu!" Hawana hoja yoyote na wanazunguka tu ovyo ovyo.
#
{21} ثم قال: {أم آتيناهُم كتاباً من قبلِهِ فهم به مستمسكون}: يخبِرُهم بصحَّة أفعالهم وصدق أقوالهم؟! ليس الأمر كذلك؛ فإنَّ الله أرسل محمداً نذيراً إليهم، وهم لم يأتهم نذيرٌ غيره؛ أي: فلا عقل ولا نقل، وإذا انتفى الأمران؛ فلا ثَمَّ إلاَّ الباطل.
{21} Kisha akasema, "Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, na ikawa wao wanakishikilia hicho" chenye kuwajulisha usahihi wa vitendo vyao na ukweli wa maneno yao? Sivyo hivyo. Kwani Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad kuwa mwonyaji kwao, na hakuwajia mwonyaji mwingine ila yeye. Kwa hivyo, hawana hoja ya kiakili wala ya kimaandiko. Na ikiwa vitu viwili hivi havipo, basi hakuna kinachokuwepo ila batili tu.
#
{22} نعم؛ لهم شبهةٌ من أوهى الشُّبه، وهي تقليد آبائهم الضالِّين، الذين ما زال الكفرة يردُّون بتقليدهم دعوة الرسل، ولهذا قال هنا: {بل قالوا إنَّا وَجَدْنا آباءَنا على أمَّةٍ}؛ أي: على دين وملَّة، {وإنَّا على آثارهم مهتدون}؛ أي: فلا نتَّبع ما جاء به محمدٌ - صلى الله عليه وسلم -.
{22} Ndiyo. Wanayo dhana potofu zaidi, ambayo ni kuwaiga baba zao wapotofu, ambao makafiri hawajaacha kuukataa wito wa Mitume kwa sababu ya kuwaiga hao. Ndiyo maana akasema hapa,
"Bali wanasema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao.'" Kwa hivyo, hatuwezi kufuata yale aliyokuja nayo Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
#
{23} {وكذلك ما أرسلنا من قبلِكَ في قريةٍ من نذيرٍ إلاَّ قال مترفوها}؛ أي: منعَّموها وملؤها الذين أطغَتْهم الدُّنيا وغرَّتهم الأموال واستكبروا على الحقِّ: {إنَّا وجَدْنا آباءنا على أمَّةٍ وإنَّا على آثارهم مقتدون}؛ أي: فهؤلاء ليسوا ببدع منهم، وليسوا بأول من قال هذه المقالة. وهذا الاحتجاج من هؤلاء المشركين الضالِّين بتقليدهم لآبائِهِم الضالِّين ليس المقصودُ به اتباعَ الحقِّ والهدى، وإنَّما هو تعصبٌ محضٌ، يُرادُ به نصرة ما معهم من الباطل.
{23} "Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake waliodeka kwa starehe" ambao ndio wakuu wake waliovushwa mipaka na dunia na mali zikawadanganya na wakaifanyia haki jeuri "walisema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.'" Kwa hivyo, hawa wanaopinga sio wa kwanza katika kusema hivyo. Na hoja hii waliyotumia washirikina hawa wapotofu ya kuwaiga baba zao wapotofu haikukusudiwa kufuata haki na uongofu. Bali ni kutetea kwa njia ya upofu tu, unaokusudiwa kuunga mkono batili yao.
#
{24} ولهذا كلُّ رسول يقول لِمَنْ عارَضَه بهذه الشُّبهة الباطلة: {أولو جئتُكم بأهدى ممَّا وَجَدْتُم عليه آباءَكم}؛ أي: أفتتَّبعوني لأجل الهُدى؟ {قالوا إنَّا بما أرْسِلْتُم به كافرونَ}: فعُلِمَ بهذا أنَّهم ما أرادوا اتِّباعَ الحقِّ والهدى، وإنَّما قصدُهم اتِّباع الباطل والهوى.
24. Ndiyo maana kila Mtume alikuwa akimwambia anayempinga kwa dhana hii batili, "Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mliowakuta nao baba zenu?" Je,
mtanifuata kwa sababu ya uwongofu niliowaletea? "Wakasema: 'Sisi tunayakataa tu hayo mliyotumwa nayo.'" Basi ikajulikana kwa haya ya kwamba hawakukusudia kufuata haki na uwongofu, bali nia yao ni kufuata batili na matamanio.
#
{25} {فانتَقَمْنا منهم}: بتكذيبِهم الحقَّ وردِّهم إيَّاه بهذه الشبهة الباطلة، {فانظُرْ كيف كان عاقبةُ المكذِّبين}: فليحذرْ هؤلاء أن يستمرُّوا على تكذيبهم فيصيبهم ما أصابهم.
{25} "Kwa hivyo, tukawalipizia" kwa sababu ya kukadhibisha kwao haki na kuikataa kwa sababu ya dhana potofu batili. "Basi angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!" Kwa hivyo, na wajihadhari watu hawa wasije wakaendelea kukadhibisha kwao huko wakapatwa na yale yaliyowapata wenzao.
{وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِمَّا تَعْبُدُونَ (26) إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ (27) وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (28) بَلْ مَتَّعْتُ هَؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّى جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُبِينٌ (29) وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ (30) وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَذَا الْقُرْآنُ عَلَى رَجُلٍ مِنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ (31) أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُمْ مَعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا سُخْرِيًّا وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ (32)}.
26.
Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake: 'Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu.' 27. Isipokuwa yule aliyeniumba, kwani Yeye ataniongoa.' 28. Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee. 29. Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliyebainisha. 30.
Na ilipowafikia Haki wakasema: 'Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.' 31.
Na walisema: 'Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?' 32. Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.
#
{26} يخبر تعالى عن ملَّة إبراهيم الخليل عليه السلام، الذي ينتسب إليه أهلُ الكتاب والمشركون، وكلُّهم يزعم أنَّه على طريقته، فأخبر عن دينِهِ الذي ورَّثَه في ذرِّيَّته، فقال: {وإذْ قال إبراهيمُ لأبيه وقومِهِ}: الذين اتَّخذوا من دون الله آلهةً يعبُدونهم ويتقرَّبون إليهم: {إنَّني براءٌ ممَّا تعبدونَ}؛ أي: مبغضٌ له مجتنبٌ معادٍ لأهله.
{26} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu mila ya Ibrahim, mwendani wake, amani iwe juu yake, ambaye wanajinasibisha naye Watu wa Kitabu na washirikina. Na wote wanadai kwamba wako katika njia yake. Kwa hivyo, akaielezea dini yake ambayo aliirithisha dhuria yake,
akasema: "Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake" ambao walichukua miungu badala ya Mwenyezi Mungu wakaiabudu na wakajiweka karibu nayo. "Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu." Yaani, ninayachukia sana, ninajiepusha nayo na ni adui wa wanaoyaabudu.
#
{27} {إلاَّ الذي فَطَرني}؛ فإنِّي أتولاَّه وأرجو أن يَهْدِيَني للعلم بالحقِّ والعمل بالحقِّ؛ فكما فَطَرني ودَبَّرَني بما يُصْلِحُ بدني ودُنياي، فسيهديني لما يُصْلِحُ ديني وآخرتي.
{27} "Isipokuwa yule aliyeniumba." Mimi hakika ninamfanya kuwa kipenzi changu na ninatumaini kwamba ataniongoa kuijua haki na kuifanyia kazi. Kama vile alivyoniumba na akaniendesha kwa yale yanayoutengeneza mwili wangu na dunia yangu, Yeye ataniongoa katika yale yanatengeneza dini yangu na akhera yangu.
#
{28} {وجَعَلَها}؛ أي: هذه الخصلَة الحميدَة التي هي أمُّ الخصال وأساسُها، وهي إخلاصُ العبادة لله وحده، والتبرِّي من عبادة ما سواه {كلمةً باقيةً في عقبِه}؛ أي: في ذرِّيَّتِهِ ، {لعلَّهم}: إليها {يرجِعونَ}: لشهرتها عنه وتوصيته لذُرِّيَّتِهِ وتوصية بعض بنيه كإسحاق ويعقوب لبعض؛ كما قال تعالى: {ومَن يرغَبُ عن مِلَّةِ إبراهيم إلاَّ من سَفِهَ نفسه ... } إلى آخر الآيات.
{28} "Na akalifanya;" yaani, sifa hii yenye kusifiwa, ambayo ndiyo mama wa sifa zote na msingi wake, ambayo ni kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada, na kujitenga na vyote vinavyoabudiwa kisichokuwa Yeye. "Liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee" kwa sababu ya umaarufu wake kuhusiana na Ibrahim, na tena kuusia kwake kizazi chake juu yake, na kuusia kwa baadhi ya wanawe, kama vile Is-haq na Yakub wao kwa wao. Kama alivyosema Mtukufu, "Na ni nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu..." mpaka mwisho wa Aya hizi.
#
{29} فلم تزلْ هذه الكلمة موجودةً في ذرِّيَّته عليه السلام حتى دخلهم التَّرفُ والطغيانُ، فقال تعالى: {بل متَّعْتُ هؤلاء وآباءَهم}: بأنواع الشَّهَوات، حتى صارت هي غايتهم ونهاية مقصودِهم، فلم تزلْ يتربَّى حبُّها في قلوبهم، حتى صارت صفاتٍ راسخةً وعقائدَ متأصلةً. {حتى جاءهم الحقُّ}: الذي لا شكَّ فيه ولا مِرْيَةَ ولا اشتباه، {ورسولٌ مبينٌ}؛ أي: بيِّن الرسالة، قامت أدلَّة رسالته قياماً باهراً بأخلاقه ومعجزاتِهِ، وبما جاء به، وبما صدَّق به المرسلين وبنفس دعوتِهِ - صلى الله عليه وسلم -.
{29} Na neno hili likaendelea kuwepo katika kizazi chake, amani iwe juu yake, mpaka ikawaingia anasa na dhuluma,
basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao" kwa matamanio ya aina mbali mbali mpaka yakawa ndiyo lengo lao na mwisho wa makusudio yao. Basi upendo wake ukiendelea kujistawisha mioyoni mwao, hadi ukawa sifa iliyoimarika ndani yake na itikadi iliyokita mizizi, "mpaka ikawafikia Haki" isipokuwa na shaka yoyote ndani yake wala mchanganyiko, "na Mtume aliyebainisha." Yaani, aliyebainisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, na ambaye ushahidi mbalimbali ulisimama kuthibitisha ujumbe wake kwa njia angavu, kupitia tabia zake nzuri na miujiza yake, na kupitia yale aliyowasadikisha kwayo Mitume, na hata kwa wito wake tu wenyewe, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
#
{30} {ولمَّا جاءهم الحقُّ}: الذي يوجِبُ على من له أدنى دينٍ ومعقول أن يَقْبَلَه وينقادَ له، {قالوا هذا سحرٌ وإنَّا به كافرونَ}: وهذا من أعظم المعاندة والمشاقَّة؛ فإنَّهم لم يكتفوا بمجرَّد الإعراض عنه، بل ولا جحده، فلم يرضَوْا حتى قدحوا به قدحاً شنيعاً، وجعلوه بمنزلة السحر الباطل الذي لا يأتي به إلاَّ أخبثُ الخلق وأعظمُهم افتراءً، والذي حَمَلَهم على ذلك طغيانُهم بما متَّعهم الله به وآباءهم.
{30} "Na ilipowafikia Haki" ambayo inamlazimu kuikubali na kuifuata kila mwenye dini hata kidogo tu na akili timamu "wakasema: 'Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.'" Huu ni katika ukaidi mkubwa zaidi na upinzani. Kwani hawakutosheka na kujiepusha nayo tu, wala hata kuikataa lakini hawakuridhika mpaka wakaikashifu vibaya zaidi, na wakaifanya katika daraja la uchawi wa batili ambao haufanyi isipokuwa na viumbe wabaya zaidi na wakubwa wao zaidi katika kuzua uwongo. Na kilichowapelekea kufanya hivyo ni kupindukia mipaka katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu ya sterehe, wao na baba zao.
#
{31} {وقالوا}: مقترحينَ على الله بعقولهم الفاسدة: {لولا نُزِّلَ هذا القرآنُ على رجل من القريتينِ عظيمٍ}؛ أي: معظَّم عندهم مبجَّل من أهل مكة أو أهل الطائف؛ كالوليد بن المغيرة ونحوه ممَّن هو عندَهم عظيم.
{31} "Na walisema" huku wakimpendekezea Mwenyezi Mungu kwa akili zao mbovu: "'Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?'" Yaani, Makka au Taif. Kama vile Al-Walid bin Al-Mughira na wengineo ambao wao wanamuona kuwa ni mtukufu.
#
{32} قال الله ردًّا لاقتراحهم: {أهم يقسِمونَ رحمةَ ربِّكَ}؛ أي: أهُم الخزَّانُ لرحمة الله، وبيدهم تدبيرُها، فيعطون النبوَّة والرسالة من يشاؤون، ويمنعونها ممَّن يشاؤون؟! {نحن قسَمْنا بينَهم معيشَتَهم في الحياة الدُّنيا ورَفَعْنا بعضَهم فوق بعض درجاتٍ}؛ أي: في الحياة الدُّنيا، {و} الحال أنَّ رحمةَ {ربِّك خيرٌ ممَّا يجمعونَ}: من الدُّنيا؛ فإذا كانت معايشُ العبادِ وأرزاقُهم الدنيويَّة بيد الله تعالى، هو الذي يقسِمُها بين عباده، فيبسِطُ الرزق على من يشاءُ ويضيِّقُه على مَن يشاءُ بحسب حكمته؛ فرحمتُه الدينيَّةُ ـ التي أعلاها النبوَّة والرسالة ـ أولى وأحرى أن تكونَ بيدِ الله تعالى؛ فالله أعلمُ حيثُ يجعلُ رسالَتَه.
فعُلم أنَّ اقتراحهم ساقطٌ لاغٍ، وأنَّ التدبير للأمور كلِّها دينيِّها ودنيويِّها بيد الله وحده، هذا إقناعٌ لهم من جهة غلطهم في الاقتراح الذي ليس في أيديهم منه شيءٌ، إن هو إلاَّ ظلمٌ منهم وردٌّ للحقِّ. وقولهم: {لولا نُزِّلَ هذا القرآنُ على رجل من القريتين عظيم}: لو عرفوا حقائقَ الرجال والصفاتِ التي بها يُعْرَفُ علوُّ قدر الرجل، وعِظَمُ منزلته عند الله وعند خلقِهِ؛ لعلموا أنَّ محمد بن عبد الله بن عبد المطلب هو أعظمُ الرجال قدراً، وأعلاهم فخراً، وأكملُهم عقلاً، وأغزرُهم علماً، وأجلُّهم رأياً وعزماً وحزماً، وأكملُهم خلقاً، وأوسعُهم رحمةً، وأشدُّهم شفقةً، وأهداهم وأتقاهم، وهو قطبُ دائرة الكمال، وإليه المنتهى في أوصاف الرجال، ألا وهو رجلُ العالم على الإطلاق؛ يعرف ذلك أولياؤه وأعداؤه؛ إلاَّ من ضلَّ وكابَرَ؛ فكيف يُفَضِّلُ عليه المشركون مَنْ لم يَشُمَّ مثقال ذرَّةٍ مِنْ كَماله، ومَنْ حَزْمُه ومنتهى عقلِهِ أنْ جعل إلهه الذي يعبُدُه ويدعوه ويتقرَّب إليه صنماً أو شجراً أو حجراً لا يضرُّ ولا ينفع ولا يُعطي ولا يمنعُ، وهو كَلٌّ على مولاه، يحتاجُ لمن يقوم بمصالحه؟! فهل هذا إلا من فعل السُّفهاء والمجانين؟! فكيف يُجعلُ مثلُ هذا عظيماً؟! أم كيف يُفَضَّلُ على خاتم الرسل وسيد ولد آدم - صلى الله عليه وسلم -؟! ولكنَّ الذين كفروا لا يعقلون.
وفي هذه الآية تنبيهٌ على حكمة الله تعالى في تفضيل الله بعضَ العباد على بعض في الدُّنيا؛ {ليتَّخِذَ بعضُهم بعضاً سخريًّا}؛ أي: ليسخِّر بعضُهم بعضاً في الأعمال والحِرَف والصنائع؛ فلو تساوى الناس في الغنى ولم يحتج بعضُهم إلى بعض؛ لتعطَّلَت كثيرٌ من مصالحهم ومنافعهم.
وفيها دليلٌ على أنَّ نعمتَه الدينيَّة خير من النعمة الدنيويَّة؛ كما قال تعالى في الآية الأخرى: {قل بفضل اللهِ وبرحمتِهِ فبذلك فَلْيَفْرَحوا هو خيرٌ ممَّا يجمعونَ}.
{32} Mwenyezi Mungu akasema akipinga pendekezo lao hilo: "Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako Mlezi?" Yaani, kwani wao ndio wanaozihifadhi rehema za Mwenyezi Mungu, na kwamba kuziendesha kwake kuko mikono mwao, ndiyo wakampa unabii na ujumbe wamtakaye, na wakamzuilia wamtakaye? "Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi" Yaani, katika maisha ya dunia, "na" hali ni kwamba rehema "za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya" ya kidunia. Kwa hivyo, ikiwa maisha ya waja na riziki zao za kidunia ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Yeye ndiye anayezigawanya miongoni mwa waja wake, kwa hivyo humkunjulia riziki amtakaye na kumkunjia amtakaye kwa hekima yake. Basi rehema yake ya kidini - ambayo ya juu yake kabisa ni unabii na ujumbe - inafaa zaidi na zaidi kuwa mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi kuliko wote ni wapi anaweka ujumbe wake. Basi ikajulikana kuwa pendekezo lao hilo ni batili, na kwamba uendeshaji wa mambo yote, ya kidini na ya kidunia, uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake. Huku ni kuwashawishi kuhusiana na kukosea kwao katika pendekezo lao hilo ambalo hawana chochote mikononi mwao kuhusiana nalo. Hilo si ila ni dhuluma tu na kukataa haki. Na kauli yao, "Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii" Lau wangelijua uhakika wa watu na sifa zinazojulikana kwazo utukufu wa mtu, na ukubwa wa hadhi yake kwa Mwenyezi Mungu na kwa viumbe vyake, wangejua kwamba Muhammad bin Abdullah bin Abdul-Muttalib ndiye mtu mkubwa zaidi kuliko watu wote kwa hadhi, wa juu wao zaidi kwa fahari, mkamilifu wao zaidi wa akili, mwenye elimu zaidi yao wote, mwenye rai bora zaidi, dhamira na uamuzi mzuri, mkamilifu wao zaidi wa tabia, mpana wao zaidi wa rehema, mwenye huruma zaidi yao wote, mwongofu zaidi yao wote, na mchamungu zaidi yao. Yeye ndiye nguzo ya duara la ukamilifu, na kwake ndiko zinaishia sifa za ukamilifu za wanadamu. Tambueni! Yeye ndiye mwanamume wa ulimwengu wote, ambaye wanajua hilo marafiki zake na maadui zake. Isipokuwa wale waliopotea na wenye kutakabari. Basi vipi washirikina watampendelea zaidi yake mtu ambaye hata hatawahi kunusa chembe ya ukamilifu ya uzito wa chungu, na ambaye dhamiria yake na mwisho wa akili yake ni kumfanya sanamu au mti kuwa ndiye mungu wake ambaye anayemuabudu, kumwomba na kujikurubisha kwake au jiwe lisilomdhuru wala kumnufaisha, wala halipeani wala halinyimi, nalo ni mzigo kwa bwana wake, ambalo linahitaji mtu wa kumfikishia masilahi yake? Je, haya si chochote ila ni matendo ya wapumbavu na wendawazimu? Mtu kama huyu anawezaje kufanywa kuwa mkuu? Au vipi atafanywa kuwa bora kuliko mwisho wa Mitume na bwana wa wana wa Adam – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake? Lakini wale waliokufuru hawatumii vyema akili zao. Katika aya hii, kuna tanabahisho juu ya hekima ya Mwenyezi Mungu katika kuwaboresha baadhi ya waja kuliko wengine katika ulimwengu huu; "ili baadhi yao wawafanye wenginewe wawatumikie" katika kazi, ufundi na sanaa mbalimbali. Lau kuwa watu wote wangekuwa sawa katika utajiri, basi hawangehitajiana, na masilahi na manufaa yao mengi yangevurugika. Aya hii pia ina ushahidi kwamba neema zake za kidini ni bora kuliko neema zake za kidunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya nyingine,
"Sema: 'Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi na wafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.'"
{وَلَوْلَا أَنْ يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَجَعَلْنَا لِمَنْ يَكْفُرُ بِالرَّحْمَنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِنْ فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ (33) وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ (34) وَزُخْرُفًا وَإِنْ كُلُّ ذَلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةُ عِنْدَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ (35)}.
33. Na lau isingekuwa watu watakuwa kundi moja, tungeliwajaalia wanaomkufuru Rahmani nyumba zao kuwa na dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazopandia 34. Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyoegemea juu yake. 35. Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumcha Mungu.
#
{33 - 35} يخبر تعالى بأنَّ الدُّنيا لا تسوى عنده شيئاً، وأنَّه لولا لطفُه ورحمتُه بعباده التي لا يقدم عليها شيئاً؛ لوسَّع الدُّنيا على الذين كفروا توسيعاً عظيماً، ولَجَعَلَ {لبيوتهم سُقُفاً من فضَّة ومعارجَ}؛ أي: درجاً من فضة، {عليها يظهرونَ}: إلى سطوحهم، {ولبيوتِهِم أبواباً وسُرراً عليها يتَّكِئونَ}: من فضَّة، ولجعل لهم {زُخْرفاً}؛ أي: لزخرف لهم دُنياهم بأنواع الزخارف وأعطاهم ما يشتهون، ولكن منعه من ذلك رحمتُه بعباده؛ خوفاً عليهم من التسارع في الكفر وكثرة المعاصي بسبب حبِّ الدُّنيا. ففي هذا دليلٌ على أنَّه يمنع العبادَ بعضَ أمور الدُّنيا منعاً عامًّا أو خاصًّا لمصالحهم، وأنَّ الدُّنيا لا تزن عند الله جناح بعوضة. وأنَّ كلَّ هذه المذكورات متاعُ الحياة الدُّنيا منغصة مكدرة فانية، وأنَّ الآخرة عند الله تعالى خيرٌ للمتَّقين لربِّهم بامتثال أوامره واجتناب نواهيه؛ لأنَّ نعيمَها تامٌّ كاملٌ من كلِّ وجهٍ، وفي الجنة ما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعين، وهم فيها خالدون. فما أشدَّ الفرقَ بين الدارين!
{33 - 35} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba dunia haina thamani yoyote kwake, na kwamba lau si kwa sababu ya upole wake na rehema zake kwa waja wake, ambazo hatangulizi kitu mbele yake, angewapanulia dunia wale waliokufuru kwa upanuzi mkubwa, na angefanya "nyumba zao kuwa na dari ya fedha, na ngazi zao pia" ziwe za fedha, "wanazopandia" wakienda kwenye dari zao. "Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyoegemea juu yake" vya fedha, na angewafanyia "mapambo" mbalimbali katika dunia hii, na akawapa wanachokitamani. Lakini kwa sababu ya rehema yake kwa waja wake hakufanya hivyo kwa kuchelea waje kukimbilia kwenye ukafiri na kufanya maasia mengi kwa kupenda dunia. Katika hili, kuna ushahidi kwamba watu hunyimwa baadhi ya mambo ya kidunia, kwa njia ya ujumla au kwa njia hasa kwa ajili ya masilahi yao wenyewe, na kwamba dunia haina thamani ya uzito wa bawa la mbu kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba mambo yote haya yaliyotajwa ni starehe za maisha ya dunia, yenye usumbufu, dhiki, na yenye kuisha, na kwamba Akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni bora kwa wale wanaomcha Mola wao Mlezi kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha makatazo yake. Kwa sababu neema yake ni kamili kwa namna zote. Na katika Bustani za mbinguni kuna vyote ambavyo nafsi zinavitamani sana na macho yanavifurahia nao watakaa humo milele. Basi ni tofauti gani kubwa hii iliyoko kati ya nyumba hizi mbili!
{وَمَنْ يَعْشُ عَنْ ذِكْرِ الرَّحْمَنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ (36) وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ مُهْتَدُونَ (37) حَتَّى إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَالَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ (38) وَلَنْ يَنْفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذْ ظَلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ (39)}
36. Anayeyafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake. 37. Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka. 38.
Hata atakapotujia atasema: 'Laiti ungelikuweko baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe!' 39. Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.
#
{36} يخبر تعالى عن عقوبَتهِ البليغةِ بمن أعرضَ عن ذكرِهِ، فقال: {ومن يَعْشُ}؛ أي: يعرِضُ ويصدُّ {عن ذِكْرِ الرحمن}: الذي هو القرآنُ العظيمُ، الذي هو أعظم رحمة رحم بها الرحمن عبادَه؛ فمن قَبِلَها؛ فقد قبل خير المواهب، وفاز بأعظم المطالب والرغائب، ومن أعرض عنها وردَّها؛ فقد خاب وخسِرَ خسارةً لا يسعدُ بعدها أبداً، وقيَّض له الرحمن شيطاناً مريداً يقارِنُه ويصاحِبُه ويعِدُه ويمنِّيه ويؤزُّه إلى المعاصي أزًّا.
{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kuhusu adhabu yake kali mno kwa wale wanaoupa mgongo ukumbusho wake, akisema, "anayeyafanyia upofu maneno ya Rahmani" ambao ni Qur-ani tukufu, ambayo ndiyo rehema kubwa zaidi ambayo Mwingi wa rehema amewaneemesha kwayo waja wake. Yeyote anayeikubali, basi atakuwa amekubali tunu bora zaidi, na akafikia makubwa zaidi yanayotafutwa na yanayotakwa. Na yeyote anayejiepusha nayo na kuikataa, basi hakika atakuwa ameambulia patupu na kuhasirika hasara ambayo hatawahi kupata furaha baada yake, na Mwingi wa rehema atamwekea Shetani muasi kuwa ndiye mwenza na sahibu wake, naye atamuahidi na kumtia matumani, na kumchochea kwa uchochezi mkubwa kutenda maasia.
#
{37} {وإنَّهم لَيَصُدُّونهم عن السبيل}؛ أي: الصراط المستقيم والدين القويم، {ويحسَبون أنَّهم مهتدونَ}: بسبب تزيين الشيطانِ للباطل وتحسينِهِ له وإعراضِهِم عن الحقِّ، فاجتمع هذا وهذا. فإن قيل: فهل لهذا من عذرٍ من حيث إنَّه ظنَّ أنَّه مهتدٍ وليس كذلك؟ قيل: لا عذر لهذا وأمثاله الذين مصدرُ جهلهم الإعراضُ عن ذكرِ الله مع تمكُّنهم على الاهتداء، فزهدوا في الهدى مع القدرة عليه، ورغِبوا في الباطل؛ فالذنبُ ذنبُهم والجرم جرمُهم.
{37} "Na hakika wao wanawazuilia Njia" iliyonyooka na Dini iliyo sawa, "na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka" kwa sababu ya kupambiwa na Shetani batili na kuwafanya kuona kwamba ni nzuri, na kuipa kwao mgongo haki, basi hili na lile vikakusanyika pamoja.
Ikisemwa: Je,
kuna udhuru wowote kwa hili kwa kuwa alidhania kwamba ameongoka ilhali hakuwa ameongoka? Itasemwa: Huyu na wengine mfano wake hawana udhuru wowote, ambao chanzo cha ujinga wao ni kuupa mgongo ukumbusho wa Mwenyezi Mungu ijapokuwa walikuwa na uwezo wa kuongoka. Lakini wakakata tamaa ya kuongoka ijapokuwa walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, na wakapenda sana batili. Kwa hivyo, dhambi ni dhambi yao, na kosa ni kosa lao.
#
{38} فهذه حالةُ هذا المعرِض عن ذكرِ الله في الدُّنيا مع قرينه، وهو الضَّلال والغيُّ وانقلاب الحقائق، وأما حاله إذا جاء ربَّه في الآخرة؛ فهو شرُّ الأحوال، وهو الندم والتحسُّر والحزن الذي لا يُجْبَر مصابُه والتبرِّي من قرينه، ولهذا قال تعالى: {حتى إذا جاءنا قال يا ليتَ بيني وبينَكَ بُعْدَ المشرقينِ فبئس القرينُ}؛ كما في قوله تعالى: {ويومَ يَعَضُّ الظالمُ على يديه يقولُ يا ليتني اتَّخذتُ مع الرسولِ سبيلاً. يا ويلتَى ليتني لم أتَّخِذْ فلاناً خليلاً. لقدْ أضَلَّني عن الذِّكْرِ بعد إذ جاءني وكان الشيطانُ للإنسانِ خَذولاً}.
{38} Hii ndiyo hali ya mtu huyu anayeupa mgongo ukumbusho wa Mwenyezi Mungu duniani pamoja na mwenziwe, ambayo ni upotofu, ukengeufu na kupendua uhakika wa mambo. Na ama hali yake atakapomjia Mola wake Mlezi akhera, basi ovu ya hali zote ambayo ni majuto na huzuni kubwa ambayo aliyepatwa nayo haiwezekani kumrekebisha wala hawezi kumkataa mwenzake huyo. Ndiyo maana akasema Mtukufu,
"Hata atakapotujia atasema: 'Laiti ungelikuweko baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi.
Rafiki mwovu mno wewe!'" Kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake,
na huku anasema: 'Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume! Ee, ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani!'"
#
{39} وقوله تعالى: {ولَن يَنفَعَكُم اليومَ إذ ظلمتُم أنَّكم في العذابِ مشترِكونَ}؛ أي: ولا ينفعكم يوم القيامةِ اشتراكُكم في العذاب أنتم وقرناؤكم وأخلاَّؤكم، وذلك لأنكم اشتركتُم في الظُّلم فاشتركتم في عقابه وعذابِهِ، ولن ينفَعَكم أيضاً روح التسلِّي في المصيبة؛ فإنَّ المصيبة إذا وقعت في الدُّنيا واشترك فيها المعاقَبون؛ هان عليهم بعضُ الهون، وتسلَّى بعضُهم ببعضٍ، وأما مصيبةُ الآخرة؛ فإنَّها جَمَعَتْ كلَّ عقابٍ ما فيه أدنى راحةٍ، حتى ولا هذه الراحة. نسألُك يا ربَّنا العافيةَ وأن تُريحنا برحمتِكَ.
{39} Na kauli yake Mtukufu, "Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu." Yaani, Siku ya Kiyama kushiriki kwenu katika adhabu nyinyi na wenzi wenu, na marafiki zenu wendani hakutawanufaisha. Hilo ni kwa sababu mlishiriki nyote katika dhuluma, basi ndiyo mkashiriki nyote katika mateso na adhabu. Na pia roho ya kuliwazika katika msiba haitakunufaisheni. Kwani, msiba unapotokea katika dunia na wale wanaoadhibiwa wakashiriki wote ndani yake, basi msiba huo huwa hafifu kidogo juu yao, na wakaliwazana wenyewe kwa wenyewe. Na ama msiba wa akhera, huo ulikusanya kila adhabu ambayo haina kupumzika hata kidogo. Basi tunakuomba ewe Mola wetu Mlezi salama, na utupumzishe na utufariji kwa rehema zako.
{أَفَأَنْتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَنْ كَانَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (40) فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُمْ مُنْتَقِمُونَ (41) أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِمْ مُقْتَدِرُونَ (42) فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ إِنَّكَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (43) وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَكَ وَلِقَوْمِكَ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ (44) وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ مِنْ رُسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِنْ دُونِ الرَّحْمَنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ (45)}
40. Je, unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi? 41. Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao. 42. Au tutakuonyesha tuliyowaahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao. 43. Basi wewe yashike yaliyofunuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyonyooka. 44. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa. 45.
Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani?'
#
{40} يقولُ تعالى لرسولِهِ - صلى الله عليه وسلم - مسلياً له عن امتناع المكذِّبين عن الاستجابة له وأنَّهم لا خيرَ فيهم ولا فيهم زكاءٌ يدعوهم إلى الهدى: {أفأنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ}؛ أي: الذين لا يسمعون، {أو تَهْدي العُمْيَ}: الذين لا يبصرون أو تهدي مَنْ هو {في ضلال مبين}؛ أي: بيِّن واضح لعلمِهِ بضلالِهِ ورضاه به؛ فكما أنَّ الأصمَّ لا يسمعُ الأصوات، والأعمى لا يبصِر، والضالَّ ضلالاً مبيناً لا يهتدي؛ فهؤلاء قد فسدتْ فِطَرُهم وعقولُهم بإعراضهم عن الذِّكر، واستحدثوا عقائدَ فاسدةً وصفاتٍ خبيثةً تمنعهم وتَحولُ بينَهم وبينَ الهُدى، وتوجِبُ لهم الازديادَ من الرَّدى.
{40} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa njia ya kumliwaza kwa sababu ya kukataa kumuitikia kwa wale wanaomkadhibisha na kwamba hakuna heri ndani yao wala hawana utakaso ndani yao unaowaita kwenye uwongofu. "Je, unaweza kuwasikilizisha viziwi" wasiosikia, "au unaweza kuwaongoa vipofu" wasioona au kuwaongoa wale "waliomo katika upotofu ulio wazi?" Kwa kuwa wanajua vyema upotofu wao na kuridhika kwake mwenyewe. Kama vile viziwi hawasikii sauti, vipofu hawaoni, na yule ambaye amepotea upotevu wa waziwazi haongoki, basi watu hawa yameshaharibika maumbile yao ya asili na akili zao kwa sababu ya kuupa mgongo ukumbusho, na wakazua itikadi potovu na sifa mbovu zilizowazuia kufikia uongofu, na zinawafanya wazidishe kupotea.
#
{41} فهؤلاء لم يبقَ إلاَّ عذابُهم ونَكالُهم إمَّا في الدُّنيا أو في الآخرة، ولهذا قال تعالى: {فإمَّا نَذْهَبَنَّ بك فإنَّا منهم منتَقِمونَ}؛ أي: فإنْ ذهَبْنا بك قبل أن نُرِيَكَ ما نعِدُهم من العذابِ؛ فاعلمْ بخبرنا الصادق أنَّا منهم منتقمون.
{41} Watu hawa hakuna kinachobakia kwao isipokuwa kuwatesa na kuwadhibiwa duniani au Akhera, na ndiyo maana akasema Mtukufu, "Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao." Yaani, tukikuondoa kabla hatujakuonyesha adhabu tunayowaahidi, jua kwa habari zetu za ukweli kwamba Sisi hakika tutawalipiza kisasi.
#
{42} {أو نُرِيَنَّكَ الذي وَعَدْناهم}: من العذاب، {فإنَّا عليهم مقتدرونَ}: ولكن ذلك متوقِّف على اقتضاءِ الحكمة لتعجيلِهِ أو تأخيرِهِ؛ فهذه حالك وحالُ هؤلاء المكذِّبين.
{42} "Au tutakuonyesha tuliyowaahidi" ya adhabu." Lakini hayo inategemea hikmah ya kuihimiza au kuichelewesha. Hii ndiyo hali yako na hali ya waongo hawa.
#
{43} وأمَّا أنت؛ {فاستمسِكْ بالذي أوحِيَ إليك}: فعلاً واتِّصافاً بما يأمر بالاتِّصاف به، ودعوةً إليه، وحرصاً على تنفيذِهِ بنفسك وفي غيرك. {إنَّك على صراطٍ مستقيم}: موصل إلى اللهِ وإلى دارِ كرامتِهِ، وهذا مما يوجِبُ عليك زيادةَ التمسُّك به والاهتداء، إذا علمتَ أنَّه حقٌّ وعدلٌ وصدقٌ تكون بانياً على أصل أصيل، إذا بنى غيرُكَ على الشكوكِ والأوهام والظُّلم والجَوْر.
{43} Na ama wewe, "yashike yaliyofunuliwa kwako" kwa vitendo na kusifika kwa yale aliyoamrisha mtu kusifika kwayo, na kuyalingania, na kufanya bidii ya kuyatekeleza wewe mwenye na kuwafanya wengine pia kuyatekeleza. "Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyonyooka" yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake. Na hayo ndiyo yanayokulazimu kushikamana nayo zaidi na kuongoka. Unapojua kwamba hayo uliyo juu yake ndiyo haki, uadilifu na ukweli, basi utakuwa umejenga juu ya msingi halisi, ilhali wasiokuwa wewe wanajenga juu ya shaka, mambo yasiyokuwa na uhakika, dhuluma na ukandamizaji.
#
{44} {وإنَّه}؛ أي: هذا القرآن الكريم، ذِكْرٌ {لك ولقومِكَ}؛ أي: فخرٌ لكم ومنقبةٌ جليلةٌ ونعمةٌ لا يقادر قدرها ولا يعرف وصفها، ويذكِّرُكم أيضاً ما فيه من الخير الدنيويِّ والأخرويِّ، ويحثُّكم عليه، ويذكِّرُكم الشرَّ ويرهِّبُكم عنه. {وسوف تُسألونَ}: عنه؛ هل قُمتم به فارتفعتُم وانتفعتُم؟ أم لم تقوموا به فيكون حجةً عليكم وكفراً منكم بهذه النعمة؟
{44} "Na hakika haya;" yaani Qur-ani hii Tukufu, ni ukumbusho "kwako na kwa kaumu yako" ambao ni fahari kwenu, heshima kubwa, na neema isiyoweza kukadiriwa kiasi chake wala kuelezewa maelezo yake. Pia inawakumbusha heri ya duniani na akhera iliyo ndani yake, na inawahimiza juu yake, na inawakumbusha maovu na ya kuwahofisha dhidi yake. "Na mtakuja ulizwa" juu yake. Je, mliitekeleza kwa hivyo mkainuka na mkanufaika? Au hamkuifanya; ili iwe ni hoja dhidi yenu na kufuru kwenu juu ya neema hii?
#
{45} {واسأل مَنْ أرْسَلْنا من قبلك من رسُلنا أجعلنا من دونِ الرحمن آلهةً يُعْبَدون}: حتى يكون للمشركين نوعُ حجَّةٍ يتَّبِعون فيها أحداً من الرسل؛ فإنَّك لو سألتهم واستخبرت عن أحوالهم؛ لم تجدْ أحداً منهم يدعو إلى اتِّخاذ إلهٍ آخر مع الله، وأنَّ كلَّ الرُّسل من أوَّلهم إلى آخرِهم يدعون إلى عبادةِ الله وحدَه لا شريك له؛ قال تعالى: {ولقد بَعَثْنا في كلِّ أمَّةٍ رسولاً أنِ اعبُدوا الله واجْتَنِبوا الطاغوتَ}، وكلُّ رسول بعثه الله يقولُ لقومه: {اعبُدوا الله ما لَكُم من إلهٍ غيرُه}، فدلَّ هذا أنَّ المشركين ليس لهم مستندٌ في شركهم لا من عقل صحيح ولا نقل عن الرسل.
{45} "Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani'" ili washirikina wawe na hoja fulani ambayo wanamfuata kwayo yeyote miongoni mwa Mitume. Kwa maana ukiwauliza na kufuatilia hali zao, hutapata yeyote miongoni mwao anayelingania kuchukua mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, na kwamba Mitume wote, kuanzia wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao walilingania kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Twaghut
(Shetani na vyote vinavyoabudiwa visivyokuwa Mwenyezi Mungu)." Na kila Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu alikuwa akiwaambia umma wake, "Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye." Basi hilo likaashiria kwamba washirikina hawana msingi wowote wa kuunga mkono ushirikina wao, si wa aina ya kiakili iliyo sahihi, wala wa kimaandiko kutoka kwa Mitume.
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَى بِآيَاتِنَا إِلَى فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ (46) فَلَمَّا جَاءَهُمْ بِآيَاتِنَا إِذَا هُمْ مِنْهَا يَضْحَكُونَ (47) وَمَا نُرِيهِمْ مِنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا وَأَخَذْنَاهُمْ بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (48) وَقَالُوا يَاأَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِنْدَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ (49) فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنْكُثُونَ (50) وَنَادَى فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَاقَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِنْ تَحْتِي أَفَلَا تُبْصِرُونَ (51) أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِنْ هَذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ (52) فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِنْ ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ (53) فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ (54) فَلَمَّا آسَفُونَا انْتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ (55) فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِلْآخِرِينَ (56)}
46. Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu aende kwa Firauni na waheshimiwa wake,
na akasema: 'Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!' 47. Lakini alipowajia na Ishara zetu, wakaingia kuzicheka. 48. Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingineye. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. 49.
Na wakasema: 'Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyokuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.' 50. Basi tulipowaondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi. 51.
Na Firauni alitangaza kwa watu wake akisema: 'Enyi watu wangu! Kwani mimi si ninao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu. Je, hamwoni? 52. Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi? 53. Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?' 54. Basi aliwachezea watu wake na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu. 55. Walipotukasirisha, tuliwapatiliza tukawazamisha wote! 56. Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.
#
{46} لما قال تعالى: {واسألْ مَنْ أرسلْنا من قبلك من رسلنا أجَعَلْنا من دونِ الرحمن آلهةً يُعْبَدون}؛ بيَّن تعالى حالَ موسى ودعوتَهُ التي هي أشهرُ ما يكونُ من دَعَوات الرسل، ولأنَّ الله تعالى أكثر من ذِكْرِها في كتابه، فذكر حالَه مع فرعون [فقال]: {ولقد أرْسَلْنا موسى بآياتنا}: التي دلَّت دلالةً قاطعةً على صحَّة ما جاء به؛ كالعصا والحية وإرسال الجراد والقمَّل ... إلى آخر الآيات، {إلى فرعون وملئِهِ فقال إنِّي رسولُ ربِّ العالمين}: فدعاهم إلى الإقرار بربِّهم، ونهاهم عن عبادةِ ما سواه.
{46} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema,
"Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani?'" Yeye Mtukufu akabainisha hali na Musa na wito wake ambao ndio mashuhuri zaidi katika miito ya Mitume, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliutaja kwa wingi katika Kitabu chake. Aliitaja hali yake pamoja na Firauni, akasema, "Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu" zilizoashiria kwa ishara ya uhakika mkubwa usahihi wa yale aliyokuja nayo kama vile fimbo, nyoka, na kuwatumia nzige na chawa... hadi mwisho wa ishara hizo. "Aende kwa Firauni na waheshimiwa wake,
na akasema: 'Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!'" Aliwalingania wamkiri Mola wao Mlezi, na akawakataza kuabudu visivyokuwa Yeye.
#
{47 - 48} {فلمَّا جاءهم بآياتِنا إذا هم منها يضحَكونَ}؛ أي: ردُّوها وأنكروها واستهزؤوا بها ظلماً وعلوًّا، فلم يكنْ لقصورٍ بالآيات وعدم وضوح فيها، ولهذا قال: {وما نُريهم من آيةٍ إلاَّ هي أكبرُ من أختِها}؛ أي: الآيةُ المتأخرةُ أعظم من السابقة، {وأخذناهم بالعذاب}: كالجراد والقمل والضفادع والدَّم آياتٍ مفصلاتٍ، {لعلَّهم يرجِعون}: إلى الإسلام ويُذْعِنون له؛ ليزولَ شركهم وشرُّهم.
{47 - 48} "Lakini alipowajia na Ishara zetu, wakaingia kuzicheka." Yaani, walizikataa, wakazikejeli kwa sababu ya dhuluma yao na kiburi, na hilo halikuwa kwa sababu ya upungufu katika ishara hizo wala kutokuwa bainifu. Ndiyo maana akasema, "Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingineye. Na tukawakamata kwa adhabu" kama vile nzige, chawa, vyura na damu kuwa ni ishara mbali mbali, "ili warejee" katika Uislamu na wanyenyekee, ili uishe ushirikina wao na uovu wao.
#
{49} {وقالوا} عندما نزل عليهم العذاب: {يا أيُّها الساحرُ}: يعنون: موسى عليه السلام، وهذا إمَّا من باب التهكُّم به، وإمَّا أن يكون هذا الخطاب عندهم مدحاً، فتضرَّعوا إليه بأن خاطبوه بما يخاطبون به مَنْ يزعُمون أنَّهم علماؤهم، وهم السحرة، فقالوا: {يا أيها الساحرُ ادعُ لنا ربَّك بما عَهِدَ عندك}؛ أي: بما خصَّك الله به وفضَّلك به من الفضائل والمناقب أن يكشفَ عنَّا العذاب، {إنَّنا لمهتدونَ}: إنْ كشف الله عنَّا ذلك.
{49} "Na wakasema" ilipowafikia adhabu, "'Ewe mchawi!" wakimaanisha Musa, amani iwe juu yake. Na hili lilikuwa ima kwa njia ya kumkejeli, au maneno hayo kulingana na wao ni sifa nzuri. Basi wakamsihi kwa kumuongelesha kwa yale wanayowaongelesha wale ambao wao wanadai kuwa ni wanazuoni wao, ambao ni wachawi.
Wakasema: "'Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyokuahidi." Yaani, fadhila na sifa nzuri alizokuwa wewe tu Mwenyezi Mungu na akakuboresha kwazo kwamba atuondolee adhabu "hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka" ikiwa Mwenyezi Mungu atatuondolea adhabu hii.
#
{50} {فلمَّا كَشَفْنا عنهم العذابَ إذا هم ينكُثون}؛ أي: لم يفوا بما قالوا، بل غدروا، واستمرُّوا على كفرهم، وهذا كقولِهِ تعالى: {فأرسَلْنا عليهم الطُّوفان والجرادَ والقمَّلَ والضفادع والدَّم آياتٍ مفصَّلات فاستكبروا وكانوا قوماً مجرِمين}، ولما وقع عليهم الرجزُ؛ قالوا: {يا موسى ادعُ لنا رَبَّكَ بما عهدَ عندك لئنْ كَشَفْتَ عنَّا الرجزَ لنؤمننَّ لك ولنرسلنَّ معك بني إسرائيلَ. فلمَّا كَشَفْنا عنهم الرِّجْزَ إلى أجل هم بالغوه إذا هم ينكُثونَ}.
{50} "Basi tulipowaondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi" na wakaendelea na ukafiri wao. Na hii ni kama kauli yake Mtukufu, "Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbali mbali. Nao wakapanda kiburi, na wakawa watu wahalifu." Na adhabu ilipowafika, wakasema, "Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu hii, hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili waende nawe. Lakini tukiwaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, mara wakivunja ahadi yao."
#
{51} {ونادى فرعونُ في قومه قال}: مستعلياً بباطلِهِ قد غرَّه مُلكه وأطغاه مالُه وجنودُه: {يا قوم أليس لي ملكُ مصرَ}؛ أي: ألست المالك لذلك المتصرف فيه؟ {وهذه الأنهار تجري من تحتي}؛ أي: الأنهار المنسحبة من النيل في وسط القصور والبساتين. {أفلا تبصِرونَ}: هذا الملكَ الطويلَ العريض؟! وهذا من جهله البليغ؛ حيث افتخر بأمرٍ خارج عن ذاته، ولم يفخرْ بأوصافٍ حميدةٍ، ولا أفعال سديدةٍ.
{51} "Na Firauni alitangaza kwa watu wake akisema" kwa sababu ya ukuu wake juu yao na batili yake huku amedanganyika na ufalme wake na akavuka mipaka kwa sababu ya mali yake na wanajeshi wake: "Enyi watu wangu! Kwani mimi si ninao huu ufalme wa Misri" ninauendesha? "Na hii mito inapita chini yangu" kutoka kwenye mto Nile inayopitia katikati ya makasri na mabustani. "Je, hamwoni" ufalme huu mrefu na mpana? Na haya ni katika ujinga wake mkubwa sana, ambapo alijivuna kwa kitu kilicho mbali na dhati yake, wala hakujifahiri kwa mambo ya kusifiwa, wala vitendo vya sawasawa.
#
{52} {أم أنا خيرٌ من هذا الذي هو مَهينٌ}؛ يعني قبَّحه الله بالمَهينِ موسى بن عمران كليم الرحمن الوجيه عند الله؛ أي: أنا العزيز وهو الذَّليل المهان المحتقر؛ فأَيُّنا خيرٌ؟! {و} مع هذا؛ فلا {يكادُ يُبينُ} عما في ضميرِهِ بالكلام؛ لأنَّه ليس بفصيح اللسان، وهذا ليس من العيوب في شيءٍ، إذا كان يُبين ما في قلبِهِ، ولو كان ثقيلاً عليه الكلام.
{52} "Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge" akimaanisha - Mwenyezi Mungu amlaani - Musa bin Imran, aliyezungumza moja kwa moja na Mwingi wa rehema, ambaye ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu. Alimaanisha kwamba yeye ni Mtukufu naye dhalili, duni, wa kudharauliwa. Basi ni nani bora "na" pamoja na hayo "hawezi kusema waziwazi" yale anayodhamiria, kwa sababu si fasaha katika usemi. Lakini hili si kasoro kwa namna yoyote ile, ikiwa ataweza kueleza yaliyomo moyoni mwake, hata ikiwa ni vigumu kwake kuzungumza.
#
{53} ثم قال فرعونُ: {فلولا ألْقِيَ عليه أسورةٌ من ذهبٍ}؛ أي: فهلاَّ كان موسى بهذه الحالة: أن يكون مزيناً مجملاً بالحُلِيِّ والأساور، {أو جاء معه الملائكة مقترنين}: يعاونونه على دعوته ويؤيِّدونه على قوله.
{53} Kisha Firauni akasema, "Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama" ili wamsaidie katika kulingania kwake na wakimuunga mkono katika yale anayoyasema?
#
{54} {فاستخفَّ قومَه فأطاعوه}؛ أي: استخفَّ عقولَهم بما أبدى لهم من هذه الشُّبه، التي لا تسمن ولا تغني من جوع، ولا حقيقة تحتها، وليست دليلاً على حقٍّ ولا على باطل، ولا تروج إلاَّ على ضعفاء العقول؛ فأيُّ دليل يدلُّ على أن فرعون محقٌّ لكون ملك مصرَ له وأنهاره تجري من تحته؟! وأيُّ دليل يدلُّ على بطلان ما جاء به موسى لقلَّة أتباعِهِ وثقل لسانِهِ وعدم تحليةِ الله له؟! ولكنَّه لقي ملأ لا معقول عندَهم؛ فمهما قال؛ اتَّبعوه؛ من حقٍّ وباطل. {إنَّهم كانوا قوماً فاسقينَ}: فبسبب فسقِهِم قيَّض لهم فرعونَ، يزيِّن لهم الشركَ والشرَّ.
{54} "Basi aliwachezea watu wake na wakamtii." Yaani, alizidharau akili zao kwa dhana hizi potovu alizowaonyesha. Nazo hazinenepeshi wala haziondoi njaa wala si za uhakika, na si ushahidi juu ya haki wala batili, wala haziwashawishi isipokuwa watu wenye akili dhaifu. Ni ushahidi gani unaoonyesha kwamba Firauni yuko kwenye haki kwa sababu tu kwamba ufalme wa Misri ni wake na mito yake inapita chini yake? Na ni ushahidi gani unaoonyesha ubatili wa yale aliyokuja nayo Musa kwa sababu tu kwamba ana wafuasi wachache, uzito wa ulimi wake, na Mwenyezi Mungu kutompa mapambo? Lakini alikutana na umati usiokuwa na akili, kiasi kwamba chochote anachosema, wao wanamfuata tu; sawa kiwe cha haki au batili. "Kwa hakika hao walikuwa watu wavukao mipaka." Na kwa sababu ya kuvuka kwao mipaka, wakaekewa Firauni juu yao akawa anawapambia ushirikina na uovu.
#
{55 - 56} {فلمَّا آسفونا}؛ أي: أغضبونا بأفعالهم، {انتَقَمْنا منهم فأغْرَقْناهم أجمعين. فجعلناهم سَلَفاً ومثلاً للآخرين}: ليعتبر بهم المعتبرونَ، ويتَّعِظَ بأحوالهم المتَّعظون.
{55 - 56} "Walipotukasirisha" kwa vitendo vyao, "tuliwapatiliza tukawazamisha wote! Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye" ili wazingatie kwao wenye kuzingatia na wawaidhike kwa hali zao wenye kuwaidhika.
{وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ (57) وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ (58) إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِبَنِي إِسْرَائِيلَ (59) وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنْكُمْ مَلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ (60) وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ هَذَا صِرَاطٌ مُسْتَقِيمٌ (61) وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ (62) وَلَمَّا جَاءَ عِيسَى بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُمْ بِالْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُمْ بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ (63) إِنَّ اللَّهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَذَا صِرَاطٌ مُسْتَقِيمٌ (64) فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِنْ بَيْنِهِمْ فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ (65)}.
57. Na alipopigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele. 58.
Wakasema: 'Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu?' Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi! 59. Hakuwa yeye
(Isa) ila ni Mtumwa tuliyemneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili. 60. Na tungelipenda, tungeliwafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana. 61. Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka. 62. Wala asiwazuilie Shetani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhahiri. 63. Na alipokuja Isa na dalili zilizo wazi,
alisema: 'Nimewajia na hekima na ili niwaeleze baadhi ya yale mliyokhitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii mimi. 64. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka.' 65. Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao waliodhulumu kwa adhabu ya siku chungu.
#
{57} يقول تعالى: {ولما ضُرِبَ ابنُ مريم مثلاً}؛ أي: نُهي عن عبادته وجُعلت عبادتُه بمنزلة عبادة الأصنام والأنداد، {إذا قومُك}: المكذِّبون لك {منه}؛ أي: من أجل هذا المثل المضروب، {يَصِدُّون}؛ أي: يستلجُّون في خصومتهم لك ويصيحون ويزعُمون أنَّهم قد غَلَبوا في حجَّتهم وأفلجوا.
{57} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Na alipopigiwa mfano Mwana wa Mariamu." Yaani, ilikatazwa kumwabudu, na kumuabudu huko kukafanywa kuwa sawa na kuabudu masanamu na vyote vinavyofanywa kuwa wenza wa Mwenyezi Mungu. "Tazama, watu wako" waliokukadhibisha, "waliupigia ukelele" na wanazidisha pingamizi na kudai kuwa wameshinda katika hoja zao na kwamba wamefaulu.
#
{58} {وقالوا أآلهتنُا خيرٌ أم هو}؛ يعني: عيسى؛ حيث نُهي عن عبادة الجميع، وشورك بينهم بالوعيد على من عَبَدهم، ونزل أيضاً قوله تعالى: {إنَّكم وما تَعْبُدونَ من دونِ الله حَصَبُ جهنَّمَ أنتُم لها وارِدونَ}. ووجه حجَّتهم الظالمة أنَّهم قالوا: قد تقرَّر عندنا وعندك يا محمدُ أنَّ عيسى من عبادِ الله المقرَّبين الذين لهم العاقبة الحسنة؛ فَلِمَ سوَّيْت بينه وبينها في النهي عن عبادة الجميع؟! فلولا أن حجَّتك باطلةٌ؛ لم تتناقضْ؟! ولم قلت: {إنَّكم وما تعبُدون من دون الله حَصَبُ جهنَّم أنتم لها وارِدونَ}؟! وهذا اللفظ بزعمهم يعمُّ الأصنام وعيسى؛ فهل هذا إلاَّ تناقضٌ؟ وتناقضُ الحجَّة دليلٌ على بطلانها! هذا أنهى ما يقررون به هذه الشبهة الذين فرحوا بها واستبشروا وجعلوا يصدُّون ويتباشرون. وهي ـ ولله الحمدُ ـ من أضعف الشُّبه وأبطلها؛ فإنَّ تسوية الله بين النهي عن عبادة المسيح وبين النهي عن عبادة الأصنام؛ لأنَّ العبادة حقٌّ لله تعالى، لا يستحقُّها أحدٌ من الخلق لا الملائكة المقرَّبون ولا الأنبياء المرسلون ولا من سواهم من الخلق؛ فأيُّ شبهةٍ في تسوية النهي عن عبادة عيسى وغيره؟!
{58} "Wakasema: 'Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu?'" Yaani, Isa
(Yesu); ambapo ilikuwa imekatazwa kuviabudu vyote, na ikatolewa ahadi ya adhabu kwa anayeviabudu,
na pia ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.
" Msingi wa hoja yao ya dhuluma ni kuwa walisema: 'Imethibiti kwetu na kwenu ewe Muhammad, ya kwamba Isa ni miongoni mwa waja wa karibu muno na Mwenyezi Mungu, ambaye atakuwa na mwisho mwema. Basi kwa nini ulisawazishe baina yake na masanamu katika kukataza kuviabudu vyote? Kama hoja yako haikuwa batili, basi haingepingana hivi.
Na kwa nini ulisema: "'Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu?" Maneno haya, kulingana na madai yao, yanajumuisha masanamu na Isa. "Basi je, huku si chochote ila ni kupingana? Na kupingana kwa hoja ni ushahidi wa ubatili wake!" Hii ndiyo hoja kubwa zaidi wanayothibitisha kwayo fikira hii potofu na ambayo ndiyo batili zaidi ya hoja zote. Basi waliifurahia hoja hii na wakawa kupiga kelele kwa sababu yake na kupokezana habari njema. Lakini hii - sifa njema ni za Mwenyezi Mungu - ni katika fikira potofu, dhaifu na batili zaidi. Kwa maana, kusawazisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kati ya kukataza kumuabudu Masihi na kukataza kuabudu sanamu ni kwa sababu ibada ni haki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hakuna anayeistahiki katika viumbe, si Malaika walio karibu naye, wala Manabii waliotumwa, wala yeyote asiyekuwa wao katika viumbe. Je, kuna suala lolote la utata kwenye kusawazisha kati ya kumwabudu Isa na visivyokuwa yeye?
#
{59} وليس تفضيل عيسى [عليه] السلام وكونِهِ مقرّباً عند ربِّه ما يدلُّ على الفرق بينَه وبينَها في هذا الموضع، وإنَّما هو كما قال تعالى: {إنْ هو إلاَّ عبدٌ أنْعَمْنا عليه}: بالنبوَّة والحكمة والعلم والعمل، {وجَعَلْناه مثلاً لبني إسرائيل}: يعرِفون به قدرةَ الله تعالى على إيجادِهِ من دون أبٍ. وأمَّا قوله تعالى: {إنَّكم وما تعبدونَ من دونِ الله حَصَبُ جهنَّم أنتم لها واردونَ}؛ فالجواب عنها من ثلاثة أوجه: أحدها: أنَّ قوله: {إنَّكم وما تعبُدونَ من دونِ الله} أنَّ {ما} اسمٌ لما لا يعقل لا يدخل فيه المسيح ونحوه. الثاني: أنَّ الخطاب للمشركين الذين بمكَّة وما حولها، وهم إنَّما يعبدون أصناماً وأوثاناً ولا يعبدون المسيح. الثالث: أنَّ الله قال بعد هذه الآية: {إنَّ الذين سبقتْ لهم منَّا الحُسنى أولئك عنها مبعَدونَ}؛ فلا شكَّ أن عيسى وغيره من الأنبياء والأولياء داخلونَ في هذه الآية.
{59} Kumpendelea Isa
[amani iwe juu yake] na uhakika wa kwamba yeye ni katika walio karibu zaidi na Mola wake Mlezi sio jambo linaloonyesha tofauti iliyo baina yake na vyote hivyo katika mahali hapa.
Bali ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuwa yeye
(Isa) ila ni Mtumwa tuliyemneemesha" kwa unabii, na hekima, elimu, na matendo mema, "tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili" ili wapate kujua kupitia kwake uwezo wa Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika kumuumba kwake bila ya baba.
Na ama kauli yake Mtukufu: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu,
" jibu lake ni kwa njia tatu: Moja yake ni kwamba kauli yake: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu," hapa "hao mnaowaabudu" ni nomino inayoweza kutumika kwa vitu visivyokuwa na akili, ambavyo Masihi na wengineo hawajumuishi ndani yake. Ya pili ni kwamba maneno haya wanaambiwa washirikina walioko Makka na wale walioko pembezoni mwake. Nao walikuwa wakiabudu masanamu na miungu tu, na wala hawakuwa wakimuabudu Masihi.
Ya tatu ni kwamba Mwenyezi Mungu alisema baada ya aya hii: "Ama hakika wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa mbali na hayo." Na hakuna shaka yoyote kwamba Isa na manabii wengineo katika vipenzi wa Mwenyezi Mungu wamejumuishwa katika aya hii.
#
{60} ثم قال تعالى: {ولو نشاءُ لَجَعَلْنا منكم ملائكةً في الأرض يخلُفون}؛ أي: لجعلنا بَدَلَكم ملائكةً يخلُفونكم في الأرض، ويكونون في الأرض حتى نرسل إليهم ملائكةً من جنسهم، وأما أنتم يا معشرَ البشر؛ فلا تطيقونَ أن ترسل إليكم الملائكةُ؛ فمن رحمة الله بكم أن أرسلَ إليكم رُسُلاً من جنسكم تتمكَّنون من الأخذ عنهم.
{60} Kisha akasema Mwenyezi Mungu: "Na tungelipenda, tungeliwafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana." Na waendelee kukaa katika ardhi mpaka tuwapelekee mtume wa aina yao kutoka katika Malaika. Na ama nyinyi, enyi wanadamu, hamuwezi kuvumilia kutumiwa malaika kama mtume kwenu. Ni katika rehema ya Mwenyezi Mungu juu yenu kwamba aliwatumia Mitume wa aina yenu ili muweze kujifunza kutoka kwake.
#
{61} {وإنَّه لَعِلْمٌ للساعة}؛ أي: وإنَّ عيسى عليه السلام لدليلٌ على الساعة، وأنَّ القادر على إيجادِهِ من أمٍّ بلا أبٍ قادرٌ على بعثِ الموتى من قبورِهم، أو: وإنَّ عيسى عليه السلام سينزلُ في آخر الزمان ويكونُ نزولُه علامةً من علامات الساعة، {فلا تَمْتَرُنَّ بها}؛ أي: لا تشكُّنَّ في قيام الساعة؛ فإنَّ الشكَّ فيها كفر، {واتَّبعونِ}: بامتثال ما أمرتُكم واجتنابِ ما نهيتُكم، {هذا صراطٌ مستقيمٌ}: موصلٌ إلى الله عزَّ وجلَّ.
{61} "Na kwa hakika yeye," yaani Isa, amani iwe juu yake, "ni alama ya Saa ya Kiyama." Na kwamba Yule aliyeweza kumuumba kutoka kwa mama bila ya baba anaweza kuwafufua wafu kutoka makaburini mwao. Au maana yake ni kwamba Isa, amani iwe juu yake, atashuka katika siku za Mwisho, na kuwe kushuka kwake huko ni ishara katika ishara za Kiyama. "Basi kamwe msiitilie shaka" siku hiyo ya Kiyama, kwani kuwa na shaka nayo ni ukafiri, "na nifuateni" kwa kutekeleza yale niliyokuamrisheni na kuyaepuka yale niliyokukatazeni. "Hii ndiyo Njia Iliyonyooka," inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mtukufu.
#
{62} {ولا يَصُدَّنَّكُمُ الشيطانُ}: عما أمركم الله به؛ فإنَّ الشيطانَ {لكم عدوٌّ مبينٌ}: حريصٌ على إغوائكم، باذلٌ جهدَه في ذلك.
{62} "Wala asiwazuilie Shetani hata kidogo" mkaacha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaamrisha. Kwani, hakika yeye "ni adui yenu wa dhahiri," ambaye anafanya hima ya kuwapoteza, ambaye anafanya juhudi awezavyo kufanya hivyo.
#
{63} {ولمَّا جاء عيسى بالبيِّناتِ}: الدالَّة على صدق نبوَّته وصحَّة ما جاءهم به من إحياء الموتى وإبراء الأكمه والأبرص ونحو ذلك من الآيات، {قال}: لبني إسرائيل: {قد جئتُكم بالحكمةِ}: النبوَّة والعلم بما ينبغي على الوجه الذي ينبغي، {ولأبيِّنَ لكم بعضَ الذي تختلفون فيه}؛ أي: أبين لكم صوابَه وجوابَه، فيزول عنكم بذلك اللبس، فجاء عليه السلام مكمِّلاً ومتمِّماً لشريعة موسى عليه السلام ولأحكام التوراة، وأتى ببعض التسهيلاتِ الموجبة للانقياد له وقَبول ما جاءهم به. {فاتَّقوا الله وأطيعونِ}؛ أي: اعبدوا الله وحدَه لا شريك له، وامتثلوا أمره، واجتنبوا نهيَه، وآمنوا بي، وصدِّقوني، وأطيعون.
{63} "Na alipokuja Isa na hoja zilizowazi" zinazoashiria ukweli wa unabii wake na usahihi wa yale aliyowaletea kama vile kufufua wafu na kuponya vipofu na wakoma na ishara nyinginezo,
"alisema" akiwaambia Wana wa Israili: "'Nimekukujieni na hekima'", yaani unabii na elimu ya yafaayo kwa namna inavyofaa, "na ili nikuelezeni baadhi ya yale mliyokhitalifiana." Yaani, nitakubainishieni usahihi wake na jawabu lake, ili kwa hayo mkanganyiko uondoke. Basi yeye, amani iwe juu yake, akaja katika hali ya kukamilisha na kuitimiza sheria ya Musa, amani iwe juu yake, na hukumu za Taurati, na akaleta baadhi ya wepesishaji uliohitaji kumfuata na kukubali yale aliyokuja nayo. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii mimi." Yaani, mwabuduni Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika, tekelezeni amri zake, jiepusheni na makatazo yake, niaminini mimi, mnisadiki na mnitiini.
#
{64} {إنَّ الله هو ربِّي وربُّكم فاعبُدوه هذا صراطٌ مستقيمٌ}: ففيه الإقرارُ بتوحيدِ الرُّبوبيَّة بأنَّ الله هو المربِّي جميع خلقه بأنواع النِّعم الظاهرة والباطنة، والإقرارُ بتوحيد العبوديَّة بالأمر بعبادة الله وحدَه لا شريك له، وإخبار عيسى عليه السلام أنَّه عبدٌ من عباد الله، ليس كما قال النصارى فيه: إنَّه ابنُ الله أو ثالثُ ثلاثة، والإخبارُ بأنَّ هذا المذكور صراطٌ مستقيمٌ موصلٌ إلى الله وإلى جنَّته.
{64} "Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka." Katika haya kuna kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu katika umola wake kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mlezi wa viumbe vyake vyote kwa kila namna ya neema za dhahiri na siri, na kukiri upweke wake katika kuabudiwa bila ya mshirika, na Isa, amani iwe juu yake, kujulisha kwamba yeye ni mja katika waja wa Mwenyezi Mungu, na siyo kama walivyosema Wakristo juu yake kwamba yeye ni mwana wa Mwenyezi Mungu au wa tatu katika watatu, na kujulisha kwamba hii iliyotajwa ndiyo njia iliyonyooka, inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na Pepo yake.
#
{65} فلما جاءهم عيسى عليه السلام بهذا، {اختلف الأحزابُ}: المتحزِّبون على التكذيب، {من بينِهِم}: كلٌّ قال بعيسى عليه السلام مقالةً باطلةً وردَّ ما جاء به؛ إلاَّ من هدى الله من المؤمنين، الذين شهدوا له بالرسالة، وصدَّقوا بكل ما جاء به، وقالوا: إنَّه عبدُ الله ورسوله. {فويلٌ للذين ظلموا [من عذاب يوم أليم]}؛ أي: ما أشدَّ حزن الظالمين! وما أعظم خسارَهم في ذلك اليوم!
{65} Basi Isa, amani iwe juu yake, alipowajia na haya, "makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao." Kila moja ya makundi hayo likadai madai batili kuhusu Isa, amani iwe juu yake, na likakataa yale aliyoleta; isipokuwa wale aliowaongoza Mwenyezi Mungu miongoni mwa Waumini, ambao walishuhudia kwamba yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. "Basi ole wao wale waliodhulumu kutokana na adhabu ya siku chungu." Watakuwa na huzuni kubwa namna gani, na watakuwa na hasara kubwa namna gani katika siku hiyo!
{هَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ (66) الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ (67) يَاعِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنْتُمْ تَحْزَنُونَ (68) الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ (69) ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنْتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ (70) يُطَافُ عَلَيْهِمْ بِصِحَافٍ مِنْ ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنْفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ وَأَنْتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (71) وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (72) لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِنْهَا تَأْكُلُونَ (73)}
66. Je, nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui? 67. Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui wao kwa wao, isipokuwa wacha Mungu. 68. Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika. 69. Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu. 70. Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo. 71. Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe, na vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele. 72. Na hiyo ni Pepo mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya. 73. Mnayo humo matunda mengi mtakayoyala.
#
{66} يقول تعالى: ما ينتظر المكذِّبون؟! وما يتوقَّعون {إلاَّ الساعة أن تأتِيَهم بغتةً وهم لا يشعرونَ}؛ أي: فإذا جاءت؛ فلا تسألوا عن أحوال من كَذَّب بها واستهزأ بمن جاء بها.
{66} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Makafiri wanangojea nini? Na ni nini wanatarajia "ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?" Na ikishakuja, basi kuhusu hali za wale wanaoikadhibisha na wakamkejeli yule aliyeileta.
#
{67} وإن الأخِلاَّء يومَ القيامةِ، المتخالِّين على الكفر والتكذيب ومعصية الله، {بعضُهم لبعض عدوٌّ}: لأنَّ خُلَّتَهم ومحبَّتهم في الدُّنيا لغير الله، فانقلبت يوم القيامة عداوة {إلاَّ المتَّقين}: للشرك والمعاصي؛ فإنَّ محبَّتهم تدوم وتتَّصل بدوام مَنْ كانت المحبَّة لأجلِهِ.
{67} Na hakika marafiki wendani kwa sababu ya ukafiri, kukadhibisha na kumuasi Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama "watakuwa ni maadui wao kwa wao" kwa sababu mapenzi yao katika dunia yalikuwa ni kwa sababu ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo yakabadilika Siku ya Kiyama yakawa uadui, "isipokuwa wacha Mungu" waliojiepusha ushirikina na maasia. Hao upendo wao hudumu na kuunganishwa na yule ambaye kwa ajili yake walipendana.
#
{68} ثُمَّ ذكر ثواب المتَّقين، وأنَّ الله تعالى يناديهم يوم القيامةِ بما يسرُّ قلوبَهم ويذهب عنهم كلَّ آفةٍ وشرٍّ، فيقول: {يا عبادِ لا خوفٌ عليكُم اليومَ ولا أنتُم تَحْزَنونَ}؛ أي: لا خوفٌ يلحقُكم فيما تستقبِلونه من الأمور، ولا حزنٌ يُصيبُكم فيما مضى منها، وإذا انتفى المكروه من كلِّ وجه؛ ثبت المحبوب المطلوب.
{68} Kisha akataja malipo ya wacha Mungu, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaita Siku ya Kiyama kwa yale yatakayozipendeza nyoyo zao, na atawaondolea kila balaa na uovu,
na atasema: "Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika." Yaani, hawatakuwa na hofu juu yenu katika mambo yajayo, wala haitawasibu huzuni katika mambo yaliyopita. Na hayo yaliyotajwa yakikosekana kwa namna yoyote, basi kinathibiti kile kinachopendwa, kinachotafutwa.
#
{69} {الذين آمنوا بآياتنا وكَانوا مُسلِمِينَ}؛ أي: وصفهم الإيمانُ بآيات الله، وذلك يشمل للتصديق بها، وما لا يتمُّ التصديق إلاَّ به من العلم بمعناها والعمل بمقتضاها، وكانوا مسلمينَ لله منقادينَ له في جميع أحوالِهِم، فجمعوا بين الاتِّصاف بعمل الظاهر والباطن.
{69} "Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu." Yaani, sifa yao ni kuamini Aya za Mwenyezi Mungu, jambo ambalo linajumuisha kuzisadiki, na kisichotimia kuzisadiki isipokuwa kwa hicho, kama vile kujua vyema maana zake na kutenda kulingana na matakwa yake. Nao walikuwa Waislamu kwa Mwenyezi Mungu, wakimtii Yeye katika hali zao zote. Basi wakajumuisha kati ya kusifika kwa kufanya matendo ya nje na ya ndani.
#
{70} {ادخُلوا الجنَّةَ}: التي هي دارُ القرار {أنتُم وأزواجُكم}؛ أي: مَنْ كان على مثل عملِكُم من كلِّ مقارن لكم من زوجةٍ وولدٍ وصاحبٍ وغيرهم، {تُحْبَرونَ}؛ أي: تَنعمون وتُكْرمون، ويأتيكم من فضل ربِّكم من الخيرات والسرور والأفراح واللَّذَّات ما لا تُعَبِّرُ الألسنُ عن وصفه.
{70} "Ingieni Peponi" ambayo ndiyo nyumba ya kutulia daima, "nyinyi na wake zenu." Yaani, wale waliokuwa wakifanya matendo sawa na matendo yenu miongoni mwa wote waliokuwa pamoja nanyi kama vile mke, mtoto, rafiki, na wengineo, "mtafurahishwa humo" kwa kupewa neema na kukirimiwa, na itawajia katika fadhila za Mola wenu Mlezi heri, furaha na starehe ambazo ndimi haziwezi kuzieleza.
#
{71} {يطافُ عليهم بصحافٍ من ذهبٍ وأكوابٍ}؛ أي: تدور عليهم خدَّامهم من الولدانِ المخلَّدين بطعامِهم بأحسنِ الأواني وأفخرِها، وهي صحافُ الذهب، وبشرابهم بألطف الأواني، وهي الأكواب التي لا عرى لها، وهي من أصفى الأواني، من فضة أعظم من صفاءِ القوارير، {وفيها}؛ أي: الجنة {ما تشتهيه الأنفسُ وتلذُّ الأعينُ}: وهذا اللفظ جامعٌ، يأتي على كلِّ نعيم وفرح وقرَّة عين وسرور قلبٍ؛ فكلُّ ما تشتهيه النُّفوس من مطاعم ومشارب وملابس ومناكح، ولذّته العيون من مناظر حسنةٍ وأشجارٍ محدقةٍ ونعم مونقةٍ ومبانٍ مزخرفةٍ؛ فإنَّه حاصلٌ فيها معدٌّ لأهلها على أكمل الوجوه وأفضلها؛ كما قال تعالى: {لهم فيها فاكهةٌ ولهم ما يَدَّعونَ}. {وأنتم فيها خالدونَ}: وهذا هو تمامُ نعيم أهل الجنة، وهو الخُلْدُ الدائمُ فيها، الذي يتضمَّن دوام نعيمِها وزيادتَه وعدم انقطاعه.
{71} "Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe" bora zaidi wakihudumiwa na wavulana wa ujana wa milele. "Na vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia" kama vile vyakula, vinywaji, mavazi, ndoa, na kile kinachopendeza macho kama vile mandhari mazuri, miti ya mabustanini, neema nzuri sana na majengo yaliyopambwa. Hivyo vyote vimeandaliwa humo kwa ajili ya watu wake kwa njia kamili na bora zaidi.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka.
" Na akasema: "Na nyinyi mtakaa humo milele. " Hiki ndicho cha kukamilisha neema ya wale walioko Peponi. Nayo inajumuisha kuendelea daima kwa neema yake, kuongezeka kwake, na kutokatika kwake.
#
{72} {وتلك الجنَّة}: الموصوفة بأكمل الصفات هي {التي أورِثْتُموها بما كُنتُم تعملونَ}؛ أي: أورثكم الله إيَّاها بأعمالكم، وجعلها من فضلِهِ جزاء لها، وأودع فيها من رحمتِهِ ما أودعَ.
{72} "Na hiyo" iliyoelezwa kwa sifa kamilifu zaidi "ndiyo Pepo mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya" na Mwenyezi Mungu, na akaifanya kutoka na fadhila zake kwamba ndiyo malipo yake, na akaweka ndani yake aliyoyaweka katika rehema zake.
#
{73} {لكم فيها فاكهةٌ كثيرةٌ}؛ كما في الآية الأخرى: {فيهما من كلِّ فاكهةٍ زوجانِ}، {منها تأكلونَ}؛ أي: مما تتخيَّرون من تلك الفواكه الشهيَّة والثمار اللذَّيذة تأكلون.
{73} "Mnayo humo matunda mengi" kama alivyosema katika Aya nyingineyo, "Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
" Na hapa akasema: "Mtakayoyala." Yaani, mtachagua katika matunda hayo yenye kumfanya mtu kuyatamani na yenye ladha nzuri.
Alipotaja neema ya Peponi, aliifuatisha na kutaja adhabu ya Jahannam. Akasema:
{إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ (74) لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ (75) وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَكِنْ كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ (76) وَنَادَوْا يَامَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ قَالَ إِنَّكُمْ مَاكِثُونَ (77) لَقَدْ جِئْنَاكُمْ بِالْحَقِّ وَلَكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ (78)}.
74. Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu. 75. Hawatapumzishwa nayo, na humo watakata tamaa. 76. Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu. 77.
Nao watapiga kelele waseme: 'Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi!' Naye aseme: 'Hakika nyinyi mtakaa humo humo!' 78. Kwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.
#
{74} {إنَّ المجرمينَ}: الذين أجرموا بكفرهم وتكذيبهم {في عذاب جهنَّم}؛ أي: منغمرون فيه، محيطٌ بهم العذاب من كلِّ جانب، {خالدونَ}: فيه لا يخرُجونَ منه أبداً.
{74} "Kwa hakika wakosefu" ambao walifanya ukosefu kwa ukafiri wao na kukadhibisha kwao "watakaa daima katika adhabu ya Jahannamu," wazamie humo na adhabu iwazunguke kila upande, na wala hawatatoka humo kamwe.
#
{75} و {لا يُفَتَّرُ عنهم}: العذابُ ساعةً [لا بإزالته] ولا بتهوين عذابه، {وهم فيه مُبْلِسونَ}؛ أي: آيسون من كلِّ خير، غير راجين للفرج، وذلك أنَّهم ينادون ربَّهم، فيقولون: {ربَّنا أخْرِجْنا منها فإنْ عُدْنا فإنَّا ظالمونَ. قال اخسؤوا فيها ولا تُكَلِّمونَ}.
{75} "Hawatapumzishwa kutokana nayo" wala kwa saa moja
[si kwa kuiondoa adhabu hiyo] wala kwa kurahisishiwa adhabu yake. "Na humo watakata tamaa kabisa" kutokana na kila heri bila ya kutaraji nafuu yoyote. Hayo ni kwa sababu watamuita Mola wao Mlezi,
wakisema: "Mola wetu Mlezi, tuondoe humo, basi sisi ni madhalimu.
" Atasema Mwenyezi Mungu: 'Tokomeeni humo, wala msinisemeze.'"
#
{76} وهذا العذابُ العظيم بما قدَّمت أيديهم وبما ظلموا به أنفسَهم، والله لم يظلِمْهم ولم يعاقِبْهم بلا ذنبٍ ولا جرم.
{76} Na hii adhabu kubwa ni kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao na kwa sababu ya yale waliyojidhulumu nayo nafsi zao, na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu na wala hakuwaadhibu bila ya dhambi wala kosa.
#
{77} {ونادوا}: وهم في النار لعلَّهم يحصل لهم استراحةٌ: {يا مالِكُ ليقضِ علينا ربُّك}؛ أي: لِيُمِتْنا فنستريحَ؛ فإنَّنا في غمٍّ شديدٍ وعذابٍ غليظٍ لا صبر لنا عليه ولا جَلَد، فَـ {قال} لهم مالكٌ خازنُ النار حين طلبوا منه أن يَدْعُوَ الله لهم أن يقضي عليهم: {إنَّكم ماكثونَ}؛ أي: مقيمون فيها لا تخرجون عنها أبداً، فلم يحصُلْ لهم ما قصدوه، بل أجابهم بنقيض قصدِهِم، وزادَهم غمًّا إلى غمِّهم.
{77} "Nao watapiga kelele waseme" na hali wamo Motoni wakitaraji kupumzishwa. "'Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi!'" Yaani, basi na tufishe ili tupumzike. Kwani sisi tumo katika huzuni kubwa sana na adhabu kali sana, ambayo hatuwezi kusubiri juu yake wala kustahimili. Basi "aseme" Malik,
mlinzi wa Moto walipomwomba awaombee kwa Mwenyezi Mungu awaangamize: "'Hakika nyinyi mtakaa humo humo!'" Na kamwe hamtatoka. Kwa hivyo hawakuyafikia yale waliyoyakusudia. Bali aliwajibu kwa yaliyo kinyume na makusudio yao, na akawaongezea huzuni kubwa juu ya huzuni yao.
#
{78} ثم وبَّخهم بما فعلوا، فقال: {لقد جئناكم بالحقِّ}: الذي يوجب عليكم أن تتَّبِعوه، فلو تبعْتُموه؛ لفزتُم وسعدتُم، {ولكنَّ أكثركم للحقِّ كارهونَ}: فلذلك شقيتُم شقاوةً لا سعادة بعدها.
{78} Kisha akawakemea kwa yale waliyokuwa wakiyafanya,
na akasema: "Kwa yakini tulikuleteeni Haki" ambayo inawalazimu kuifuata. Na mngeifuata, basi mngefuzu na kupata furaha ,"lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki." Basi ndiyo sababu mmekuwa mashakani na hamtawahi kuwa na furaha yoyote baada yake.
{أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ (79) أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ بَلَى وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ (80)}
79. Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunaopitisha. 80. Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.
#
{79} يقول تعالى: {أم أبرموا}؛ أي: أبرمَ المكذِّبون بالحقِّ المعاندون له {أمراً}؛ أي: كادوا كيداً ومكروا للحقِّ ولمن جاء بالحقِّ ليدحضوه بما موَّهوا من الباطل المزخرف المزوَّق، {فإنَّا مبرِمون}؛ أي: محكمون أمراً ومدبِّرون تدبيراً يعلو تدبيرَهم وينقضُهُ ويبطِلُه. وهو ما قيَّضه الله من الأسباب والأدلَّة لإحقاق الحقِّ وإبطال الباطل؛ كما قال تعالى: {بل نَقْذِفُ بالحقِّ على الباطل فيدمغُهُ}.
{79} Mwenyezi Mungu Mtukufu "Au" hao walioikadhibisha haki na kuipinga "waliweza kupitisha amri yao?" Yaani, walipanga vitimbi na wakapanga njama dhidi ya haki na yule aliyeileta haki hiyo ili waiangushe kwa yale waliyoficha ya batili iliyopambwa. "Bali ni Sisi ndio tunaopitisha." Yaani, tunalifanya jambo letu kuwa sawasawa na kulipanga mpango unaopita mpango wao, na kuupindua na kuubatilisha. Na hayo ni zile sababu na ushahidi ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliviweka kwa ajili ya kuisimamisha haki na kubatilisha batili.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka."
#
{80} {أم يحسبونَ}: بجهلهم وظلمِهِم {أنَّا لا نسمعُ سرَّهم}: الذي لم يتكلَّموا به، بل هو سرٌّ في قلوبهم، {ونجواهم}؛ أي: كلامهم الخفيَّ الذي يتناجَوْن به؛ أي: فلذلك أقدموا على المعاصي، وظنُّوا أنَّها لا تبعةَ لها ولا مجازاة على ما خفي منها، فردَّ الله عليهم بقوله: {بلى}؛ أي: إنا نعلم سرَّهم ونجواهم، {ورسُلُنا}: الملائكة الكرام {لديهم يكتُبونَ}: كلَّ ما عملوه، وسيحفظُ ذلك عليهم حتى يَرِدوا القيامةَ فيجدوا ما عملوا حاضراً، ولا يظلم ربُّك أحداً.
{80} "Au wanadhani" kwa sababu ya ujinga wao na dhuluma yao "kwamba hatusikii siri zao" ambazo hawakuzisema, bali bado ni siri katika nyoyo zao,
"na minong'ono yao" ndiyo maana wakafanya maasia hayo na wakadhani kwamba hawatachukuliwa dhambi kwa hayo wala hawatalipwa kwa yale yaliyofichika hatika hayo? Basi Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kusema: "Wapi!" Yaani: Sisi tunazijua siri zao na minong'ono yao hiyo. "Wajumbe wetu" ambao ni Malaika watukufu "wapo karibu nao, wanayaandika" kila walichokifanya, na watahifadhiwa yote hayo mpaka watakapofika katika Kiyama na wapate waliyokuwa wakiyatenda yakiwa hapo, na Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.
{قُلْ إِنْ كَانَ لِلرَّحْمَنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ (81) سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ (82) فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّى يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ (83)}.
81.
Sema: 'Ingelikuwa Rahmani
(Mwingi wa Rehema) ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu.' 82. Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A'rshi, na hayo wanayomsifia. 83. Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyoahidiwa.
#
{81} أي: قل يا أيُّها الرسول الكريم للذين جعلوا لله ولداً، وهو الواحد الأحد، الفرد الصَّمد، الذي لم يتَّخذ صاحبة ولا ولداً، ولم يكن له كفواً أحدٌ: {قل إن كان للرحمن ولدٌ فأنا أوَّلُ العابدينَ}: لذلك الولد؛ لأنه جزءٌ من والده، وأنا أولى الخلق انقياداً للأوامر المحبوبة لله، ولكنِّي أولُ المنكرين لذلك، وأشدُّهم له نفياً، فعلم بذلك بطلانه؛ فهذا احتجاجٌ عظيم عند من عرفَ أحوال الرسل، وأنَّه إذا علم أنَّهم أكملُ الخلق، وأنَّ كلَّ خير فهم أول الناس سبقاً إليه وتكميلاً له. وكلُّ شرٍّ فهم أولُ الناس تركاً له وإنكاراً له وبعداً منه؛ فلو كان للرحمن ولدٌ، وهو الحقُّ؛ لكان محمدُ بنُ عبد الله أفضلَ الرسل أول مَنْ عَبَدَه، ولم يسبقْه إليه المشركون.
ويُحتمل أنَّ معنى الآية: لو كان للرحمن ولدٌ؛ فأنا أولُ العابدين لله، ومن عبادتي لله إثباتُ ما أثبته ونفيُ ما نفاه؛ فهذا من العبادة القوليَّة الاعتقاديَّة، ويلزم من هذا لو كان حقًّا؛ لكنتُ أول مثبتٍ له، فعلم بذلك بطلانُ دعوى المشركين وفسادها عقلاً ونقلاً.
81 Yaani: Sema, ewe Mtume mtukufu ukiwaambia wale waliomfanyia Mwenyezi Mungu mwana, naye ndiye Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakujifanyia mke wala mwana, wala hana anayelingana naye hata mmoja.
"Sema: 'Ingelikuwa Ar-Rahmani
(Mwingi wa rehema) ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu.'" mwana huyo. Kwa sababu yeye ni sehemu ya baba yake, na mimi ndiye kiumbe anayestahiki zaidi kufuata maamrisho yanayopendwa na Mwenyezi Mungu. Lakini mimi ndiye wa kwanza kulikataa hilo, na mwenye kulikanusha zaidi yao wote, kwa hivyo ubatili wake ukajulikana kwa hilo. Hii ni hoja kubwa sana kwa wale wanaozijua hali za Mitume, na kwamba inapojulikana kuwa wao ndio viumbe kamili zaidi, na kwamba kila heri wao ndio wangekuwa watu wa kwanza kutangulia kuiendea na kuikamilisha, na kwamba kila uovu wao ndio wa kwanza kuuacha, kuukataa na kujiweka mbali nao. Kwa hivyo, kama Mwingi wa Rehema angekuwa na mwana, na hilo likawa ndiyo Haki, basi Muhammad bin Abdullah mbora wa Mitume wote angelikuwa ndiye wa kwanza kumuabudu, na wala washirikina wasingemtangulia katika hilo.
Na inawezekana kwamba maana ya Aya ni kuwa: Lau Mwingi wa Rehema angekuwa na mwana, basi mimi ningekuwa ndiye wa kwanza kumwabudu Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa kumwabudu kwangu Mwenyezi Mungu ni kuthibitisha yale aliyoyathibitisha na kukanusha yale aliyoyakanusha. Hii ni sehemu ya ibada ya kimaneno na kiitikadi, na inalazimu kutokana na haya kwamba ikiwa kweli ni haki, basi ningelikuwa wa kwanza kuyathibitisha. Basi ikajulikana kutokana na hilo ubatili wa madai ya washirikina ni ubovu wake kiakili na kimaandiko.
#
{82} {سبحانَ ربِّ السمواتِ والأرض ربِّ العرش عمَّا يصفونَ}: من الشريك والظَّهير والعوين والولد وغير ذلك مما نسبه إليه المشركون.
{82} "Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa 'Arshi mbali na hayo wanayomsifia" ya mshirika, msaidizi, mwana, mtoto, na mambo mengineyo miongoni mwa yale ambayo washirikina walimnasibisha nayo.
#
{83} {فَذَرْهم يخوضوا ويلعبوا}؛ أي: يخوضوا بالباطل ويلعبوا بالمحال؛ فعلومُهم ضارةٌ غير نافعةٍ، وهي الخوض والبحث بالعلوم التي يعارِضون بها الحقَّ وما جاءت به الرسل، وأعمالهم لعبٌ وسفاهةٌ لا تزكِّي النفوس ولا تثمِرُ المعارفَ، ولهذا توعَّدهم بما أمامهم يوم القيامةِ، فقال: {حتى يلاقوا يومَهم الذي يوعَدونَ}: فسيعلمون فيه ماذا حَصَّلوا، وما حَصَلوا عليه من الشقاءِ الدائم والعذاب المستمرِّ.
{83} "Basi waache wapige porojo wakicheza" Yaani: wapige porojo ya batili na kucheza na yasiyowezekana. Elimu zao hizo ni za kuwadhuru na wala hazina manufaa, nazo ni kuzama na kupekua elimu ambazo kwazo wanaipinga haki na yale waliyokuja nayo Mitume. Na matendo yao hayo ni mchezo na upumbavu usiozitakasa nafsi zao wala haziwapi maarifa, na ndiyo sababu akawaahidi kwa yale yaliyo mbele yao Siku ya Kiyama,
akasema: "Mpaka waikute hiyo siku yao waliyoahidiwa" na hapo ndipo watajua ni nini walichopata cha taabu na adhabu ya kuendelea daima.
{وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَهٌ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ (84) وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِنْدَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (85) وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنْ شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ (86) وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّهُ فَأَنَّى يُؤْفَكُونَ (87) وَقِيلِهِ يَارَبِّ إِنَّ هَؤُلَاءِ قَوْمٌ لَا يُؤْمِنُونَ (88) فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ (89)}.
84. Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye ujuzi. 85. Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa. 86. Wala hao mnaowaomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipokuwa anayeshuhudia kwa haki, na wao wanajua. 87. Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba. Bila ya shaka watasema ni Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanakogeuziwa? 88. Na usemi wake
(Mtume) ni: 'Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasioamini. 89. Basi wasamehe, na uwaambie maneno ya salama. Watakuja jua.'
#
{84} يخبر تعالى أنَّه وحده المألوهُ المعبودُ في السماواتِ والأرض، فأهل السماوات كلُّهم، والمؤمنون من أهل الأرض يعبدُونَه ويعظِّمونه ويخضعون لجلاله ويفتِقرون لكماله، {تسبِّحُ له السمواتُ السبع والأرضُ ومن فيهن}، {وإن من شيءٍ إلاَّ يسبِّحُ بحمدِه}، {ولله يسجُدُ من في السمواتِ والأرض طوعاً وكرهاً}. فهو تعالى المألوه المعبودُ الذي يألهه الخلائق كلُّهم طائعين مختارين وكارهين، وهذه كقولِهِ تعالى: {وهو الله في السماواتِ وفي الأرض}؛ أي: ألوهيَّته ومحبته فيهما وأما هو فإنه فوق عرشه بائن من خلقه متوحدٌ بجلاله متمجدٌ بكماله. {وهو الحكيمُ}: الذي أحكم ما خلقه، وأتقن ما شرعه؛ فما خلق شيئاً إلاَّ لحكمةٍ، ولا شرع شيئاً إلاَّ لحكمةٍ، وحكمهُ القدريُّ والشرعيُّ والجزائيُّ مشتملٌ على الحكمة، {العليم}: بكلِّ شيء، يعلم السِّر وأخفى، ولا يعزُبُ عنه مثقالُ ذرَّة في العالم العلويِّ والسفليِّ ولا أصغر منها ولا أكبر.
{84} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa Yeye peke yake ndiye anayefaa kufanyiwa uungu na kuabidiwa mbinguni na ardhini, kwa hivyo wakaazi wote wa mbinguni, na Waumini miongoni mwa wakazi wa ardhini wanamuabudu Yeye na wanampa taadhima na wananyenyekea chini ya utukufu wake na wanahitaji mno ukamilifu wake. "Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake." "Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake." "Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake." Basi Yeye Mtukufu ndiye anayefanyiwa uungu, anayeabudiwa na viumbe vyote, kwa kutii na kwa kutotaka.
Na hii ni kama kauli yake Mtukufu: "Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini.
" Yaani: Uungu wake na upendo wake vimo ndani ya viwili hivyo, na ama Yeye, ameinuka juu ya kiti chake cha enzi, bali na viumbe vyake, amepwekeka kwa utukufu wake, ametukuka kwa ukamilifu wake. "Naye ndiye Mwenye hekima" ambaye amefanya vilivyo kila alichokiumba, na akafanya sawasawa alichokiweka kuwa sheria. Kwa hivyo, hakuumba chochote ila kwa ajili ya hekima fulani, na hakutunga sheria yoyote isipokuwa kwa hekima fulani. Na hukumu yake ya kimajaaliwa, ya kisheria na ya kimalipo zinajumuisha hekima. "Ajuaye zaidi" kila kitu. Anajua siri na mambo yaliyofichika zaidi, na wala hakifichikani kwake chenye uzito hata wa chembe katika ulimwengu wa juu wala wa chini, wala kidogo zaidi kuliko hicho wala kikubwa zaidi.
#
{85} {وتبارك الذي له ملك السمواتِ والأرض وما بينهما}: {تبارك}؛ بمعنى: تعالى وتعاظم وكثُر خيرُه واتَّسعت صفاتُه وعظُم ملكُه، ولهذا ذكر سَعَةَ ملكِه للسمواتِ والأرض وما بينهما، وسَعَةَ علمِهِ، وأنَّه بكلِّ شيءٍ عليمٌ، حتى إنه تعالى انفردَ بعلم الغيوب ، التي لم يطَّلع عليها أحدٌ من الخلق؛ لا نبيٌّ مرسلٌ ولا ملكٌ مقربٌ، ولهذا قال: {وعنده علمُ الساعةِ}: قدَّم الظرفَ ليفيد الحصر؛ أي: لا يعلم متى تجيء الساعةُ إلاَّ هو. ومن تمام ملكِهِ وسعته أنَّه مالك الدُّنيا والآخرة، ولهذا قال: {وإليه ترجعون}؛ أي: في الآخرة فيحكم بينكم بحكمِهِ العدل.
{85} "Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake" na sifa zake zimepanuka, na ufalme wake ni mkubwa mno, na ndiyo maana akataja upana wa ufalme wake juu ya mbingu na ardhi na vilivyomo baina ya viwili hivyo, na upana wa elimu yake, na kwamba Yeye anajua zaidi kila kitu, kiasi kwamba Yeye pekee ndiye Mwenye elimu ya ghaibu ambayo hakuna hata mmoja katika viumbe aliyewahi kuiona, si Nabii aliyetumwa wala Malaika aliyewekwa karibu na Mwenyezi Mungu,
na ndiyo maana akasema: "Na kwake yeye uko elimu ya Saa.
" Ameleta kielezi ili kutoa kipimo; yaani: hakuna ajuaye Saa itafika lini isipokuwa yeye. Sehemu ya ukamilifu wa ufalme wake na wingi wake ni kuwa Yeye ndiye Mmiliki wa dunia na Akhera.
Na ndiyo maana akasema: "Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama." Yaani, hakuna ajuaye Saa itafika lini isipokuwa Yeye. Na katika sehemu ya ukamilifu wa ufalme wake na upana wake ni kuwa Yeye ndiye Mmiliki wa dunia na Akhera,
na ndiyo maana akasema: "na kwake Yeye" Akhera "mtarudishwa" na ahukumu baina yenu kwa hukumu yake ya uadilifu.
#
{86} ومن تمام ملكِهِ أنَّه لا يملكُ أحدٌ من خلقِهِ من الأمر شيئاً، ولا يقدِم على الشفاعة عنده أحدٌ إلاَّ بإذنه. {ولا يملكُ الذين يدعونَ من دونِهِ الشفاعةَ}؛ أي: كلُّ مَنْ دُعِيَ من دون الله من الأنبياء والملائكة وغيرهم لا يملكونَ الشفاعةَ ولا يشفعونَ إلاَّ بإذن الله ولا يشفعونَ إلاَّ لِمن ارتضى، ولهذا قال: {إلاَّ مَنْ شَهِدَ بالحقِّ}؛ أي: نطق بلسانه مقرًّا بقلبه عالماً بما شهد به، ويشترطُ أن تكونَ شهادته بالحقِّ، وهو الشهادةُ لله تعالى بالوحدانيَّةِ، ولرسله بالنبوَّة والرسالة، وصحَّة ما جاؤوا به من أصول الدين وفروعه وحقائقه وشرائعه؛ فهؤلاء الذين تنفع فيهم شفاعةُ الشافعين، وهؤلاء الناجون من عقاب الله، الحائزون لثوابه.
{86} Na katika utimilifu wa ufalme wake ni kwamba hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyake mwenye mamlaka yoyote juu ya jambo hilo, na hakuna awezaye kumuombea mwingine kwake isipokuwa kwa idhini yake. "Wala hao mnaowaomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu.
" Yaani: kila aombwaye asiyekuwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, Malaika na wengineo hana uwezo wa kuombea, wala hawawezi kuombea wengine isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na wala hawawezi kuombea isipokuwa yule aliyeridhiwa.
Ndiyo akasema: "Isipokuwa anayeshuhudia kwa haki" yaani aliyetamka kwa ulimi wake, akikiri kwa moyo wake, akijua anayoyashuhudia, na ni sharti kuwa ushahidi wake huo uwe kwa haki, ambayo ni kushuhudia upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa Mitume wake kwa unabii na utume, na usahihi wa yale aliyoyaleta miongoni mwa misingi ya dini, matawi yake, hakika zake na sheria zake. Hao ndio ambao uombezi wa waombezi unawafaa, na hao ndio watakaosalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kupata thawabu zake.
#
{87} ثم قال تعالى: {ولئن سألتَهم مَن خَلَقَهُم لَيقولنَّ اللهُ}؛ أي: ولئن سألت المشركين عن توحيد الربوبيَّة ومَن هو الخالق؛ لأقرُّوا أنَّه الله وحدَه لا شريك له، {فأنَّى يُؤْفَكونَ}؛ أي: فكيف يُصْرَفون عن عبادة الله والإخلاص له وحدَه؟! فإقرارهُم بتوحيد الرُّبوبيَّة يلزمهم به الإقرار بتوحيد الألوهية، وهو من أكبر الأدلَّة على بطلان الشرك.
{87} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba.
Bila ya shaka watasema ni Mwenyezi Mungu!" Yaani: Ukiwauliza washirikina kuhusu upweke wa Mwenyezi Mungu katika umola wake na nani Muumba, watakiri kuwa ni Mwenyezi Mungu peke yake,
asiyekuwa na mshirika? "Basi ni wapi wanakogeuziwa?" Yaani: Vipi wanageuzwa mbali wakaacha kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumkusudia Yeye peke yake? Kukiri kwao upweke wake katika umola, kunawalazimu kukiri upweke wake katika uungu, na hilo ni katika ushahidi mkubwa zaidi juu ya ubatili wa ushirikina.
#
{88} {وقيله ياربِّ إنَّ هؤلاء قومٌ لا يؤمنون}: هذا معطوف على قولِهِ: {وعندهُ علمُ الساعةِ}؛ أي: وعنده علم قيلِهِ؛ أي: الرسول - صلى الله عليه وسلم - شاكياً لربِّهِ تكذيب قومِهِ، متحزِّناً على ذلك، متحسِّراً على عدم إيمانهم؛ فالله تعالى عالمٌ بهذه الحال، قادرٌ على معاجلتهم بالعقوبة، ولكنه تعالى حليمٌ، يمهلُ العباد، ويستأني بهم لعلَّهم يتوبون ويرجِعون.
{88} "Na usemi wake
(Mtume) ni: 'Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasioamini.
" hii aya imeambatishwa kwa kauli yake: "Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama" Yaani: Anajua zaidi usemi wake Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akimlalamikia Mola wake Mlezi kwa kukadhibisha kwa watu wake, akihuzunika juu ya hilo, akijutia sana kutoamini kwake. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anaijua hali hii na ana uwezo wa kuwaharakishia adhabu, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mstahamilivu, na anawapa muhula waja wake na kuwafanyia pole pole huenda wakatubu na kurejea kwake.
#
{89} ولهذا قال: {فاصفحْ عنهم وقُلْ سلامٌ}؛ أي: اصفح عنهم ما يأتيك من أذيَّتِهِمْ القوليَّة والفعليَّة، واعفُ عنهم، ولا يبدر منك لهم إلاَّ السلامُ الذي يقابِل به أولو الألباب والبصائر للجاهلين؛ كما قال تعالى عن عباده الصالحين: {وإذا خاطَبَهُمُ الجاهلونَ}؛ أي: خطاباً بمقتضى جهلهم، {قالوا سلاماً}. فامتثل - صلى الله عليه وسلم - لأمر ربِّه، وتلقَّى ما يصدُرُ إليه من قومِهِ وغيرهم من الأذى بالعفو والصفح، ولم يقابِلْهم عليه السلام إلاَّ بالإحسان إليهم والخطاب الجميل؛ فصلوات الله وسلامُه على مَن خصه الله بالخُلُق العظيم الذي فَضَلَ به أهلَ الأرض والسماء، وارتفعَ به أعلى من كواكبِ الجوزاءِ، وقوله: {فسوفَ يَعلمونَ}؛ أي: غِبَّ ذُنوبهم وعاقبةَ جُرمهم.
{89} Ndiyo maana akasema: "Basi wasamehe, na uwaambie maneno ya salama.
" Yaani: Wasamehe kwa udhia wao wa kimaneno na wa kimatendo, wala usiwape chochote isipokuwa salama ambayo wenye akili na maono mazuri wanakutana kwayo wajinga.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu waja wake wema: "na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!" Basi yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alitekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akakutana na udhia uliomfikia kutoka kwa watu wake kwa msamaha na kuachilia mbali, na wala yeye amani iwe juu yake, hakukabiliana nao ila kwa kuwafanyia wema na kuwaongelesha maneno mazuri. Basi rehema na amani ziwe juu ya yule ambaye Mwenyezi Mungu aliyempa yeye tu tabia njema kuu ambayo kwayo alishinda wakazi wa ardhini na mbinguni, na akainuka kwayo juu kuliko nyota za kundinyota Mapacha
(Juaza).
Na kauli yake: "Watakuja jua" ubaya wa dhambi zao na mwisho wa uhalifu wao.
Imekamilika tafsiri ya surat Az-Zukhruf, na sifa njema zote na neema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *