[Nayo] ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{يس (1) وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ (2) إِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ (3) عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (4) تَنْزِيلَ الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ (5) لِتُنْذِرَ قَوْمًا مَا أُنْذِرَ آبَاؤُهُمْ فَهُمْ غَافِلُونَ (6) لَقَدْ حَقَّ الْقَوْلُ عَلَى أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (7) إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلَالًا فَهِيَ إِلَى الْأَذْقَانِ فَهُمْ مُقْمَحُونَ (8) وَجَعَلْنَا مِنْ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَاهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ (9) وَسَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنْذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنْذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (10) إِنَّمَا تُنْذِرُ مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ وَخَشِيَ الرَّحْمَنَ بِالْغَيْبِ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ (11) إِنَّا نَحْنُ نُحْيِ الْمَوْتَى وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُبِينٍ (12)}.
1. Ya-Sin 2. Kwa Haki ya Qur-ani yenye hekima! 3. Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa. 4. Juu ya njia iliyonyooka. 5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu. 6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika. 7. Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini. 8. Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. 9. Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao. Na tumewafunika macho yao, kwa hivyo hawaoni. 10. Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. 11. Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman
(Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. 12. Hakika Sisi tunawafufua wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza, na wanayoyaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha.
#
{2} هذا قسمٌ من الله تعالى بالقرآن الحكيم الذي وَصْفُهُ الحكمةُ، وهي وضعُ كلِّ شيءٍ موضعَه: وضعُ الأمر والنهي في المحلِّ اللائق بهما، ووضع الجزاء بالخير والشرِّ في محلِّهما اللائق بهما؛ فأحكامُهُ الشرعيَّةُ والجزائيةُ كلُّها مشتملةٌ على غاية الحكمة. ومن حكمة هذا القرآن أنه يجمع بين ذِكْر الحُكْم وحِكْمته، فينبِّه العقول على المناسبات والأوصاف المقتضية لترتيب الحكم عليها.
{2} Hiki ni kiapo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Qur-ani yenye hekima. Ambayo sifa yake ni hekima, ambayo ni kuweka kila kitu mahali pake pafaapo. Kuweka maamrisho na makatazo mahali pake panapofaa, na kuweka malipo ya wema na ya uovu mahali pake panapofaa. Kwa hivyo, hukumu zake za kisheria na za kimalipo zote zina hekima ya hali ya juu. Miongoni mwa hekima za Qur-ani hii ni kwamba inajumuisha kutaja hukumu na hekima yake. Kwa hivyo ikazitanabahisha akili juu ya uwiano na sifa zinazohitaji kuwepo hukumu hiyo juu ya kitu hicho.
#
{3} {إنَّك لَمِنَ المرسلينَ}: هذا المقسَم عليه، وهو رسالةُ محمد - صلى الله عليه وسلم -، وأنَّك يا محمد من جملة المرسلين، فلست ببدع من الرسل. وأيضاً؛ فجئت بما جاء به الرسل من الأصول الدينيَّة. وأيضاً؛ فمن تأمل أحوال المرسلين وأوصافهم وعرف الفرق بينهم وبين غيرهم؛ عرف أنَّك من خيار المرسلين بما فيك من الصفات الكاملة والأخلاق الفاضلة. ولا يخفى ما بين المقسَم به وهو القرآنُ الحكيم وبين المقسَم عليه وهو رسالةُ الرسول محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - من الاتصال، وأنَّه لو لم يكن لرسالتِهِ دليلٌ ولا شاهدٌ إلاَّ هذا القرآن الحكيم؛ لكفى به دليلاً وشاهداً على رسالة محمد [- صلى الله عليه وسلم -]، بل القرآنُ العظيم أقوى الأدلةِ المتصلةِ المستمرةِ على رسالة الرسول، فأدلةُ القرآن كلُّها أدلةٌ لرسالة محمد - صلى الله عليه وسلم -.
{3} "Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa." Na kwamba wewe Muhammad - rehema na amani zimshukie - si wa kwanza miongoni mwa Mitume. Na pia, ulikuwa na misingi ile ile waliyokuja nayo Mitume wa kabla yako. Na pia, Mwenye kutafakari hali na sifa za Mitume na akajua tofauti iliyoko baina yao na watu wengineo, atajua kwamba wewe Muhammad ni miongoni mwa Mitume bora zaidi kwa sababu ya sifa zako kamilifu na maadili bora. Hapa, haufichikani mfungamano ulioko baina ya kile ambacho Mwenyezi Mungu anaapa juu yake ambacho ni Qur-ani yenye hekima, na ujumbe wa Mtume Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake. Na kwamba hata kama utume wake haukuwa na hoja yoyote wala ushahidi isipokuwa Qur-ani hii yenye hekima, basi hilo tu lingetosha kuwa ushahidi juu ya utume wa Muhammad - rehema na amani zimshukie. Bali Qur-ani tukufu ndiyo ushahidi mkubwa zaidi unaoendelea juu ya utume wa Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
#
{4} ثم أخبر بأعظم أوصاف الرسول - صلى الله عليه وسلم -، الدالَّة على رسالته، وهو أنَّه {على صراطٍ مستقيم}: معتدل، موصل إلى الله وإلى دار كرامته، وذلك الصراط المستقيم مشتملٌ على أعمال، وهي الأعمال الصالحة المصلحة للقلب والبدن والدنيا والآخرة، والأخلاق الفاضلة المزكِّية للنفس المطهِّرة للقلب المنمِّية للأجر، فهذا الصراط المستقيم الذي هو وصفُ الرسول - صلى الله عليه وسلم - ووصفُ دينه الذي جاء به.
فتأمَّلْ جلالةَ هذا القرآن الكريم؛ كيف جَمَعَ بين القَسَم بأشرف الأقسام على أجلِّ مُقْسَم عليه، وخبرُ الله وحدَه كافٍ، ولكنَّه تعالى أقام من الأدلَّة الواضحة والبراهين الساطعةِ في هذا الموضع على صحَّة ما أقسم عليه من رسالة رسولِهِ ما نبَّهنا عليه وأشرنا إشارةً لطيفة لسلوك طريقه.
{4} Kisha akajulisha juu ya sifa kubwa zaidi ya Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – ambayo inaonyesha utume wake. Nayo ni kuwa yuko "Juu ya njia iliyonyooka" yenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu na nyumba ya utukufu wake. Na njia hiyo iliyonyooka inajumuisha matendo, ambayo ni matendo mema yenye kutengeneza moyo, mwili, dunia na Akhera, na maadili mema yanayotakasa nafsi, yanayosafisha moyo na kuongeza malipo. Na hii ndiyo njia iliyonyooka ambayo ndiyo sifa ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na ndiyo sifa ya dini yake aliyokuja nayo. Basi tafakari utukufu wa Qur-ani hii Tukufu. Vipi iliunganisha kati ya kuapa kwa viapo vitukufu na elimu ya Mwenyezi Mungu peke yake inatosha. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu aliweka ushahidi ulio wazi na hoja za kung'aa mahali hapa, juu ya usahihi wa yale aliyoapa kwayo ya kwamba Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake. Jambo ambalo kwalo ametutanabahisha na akatuashiria kwa ishara bora zaidi juu ya kufuata njia yake hii.
#
{5} وهذا الصراط المستقيم {تنزيلَ العزيزِ الرَّحيم}؛ فهو الذي أنزلَ به كتابَه وأنزلَه طريقاً لعبادِهِ موصلاً لهم إليه، فحماه بعزَّته عن التغيير والتبديل، ورَحِمَ به عبادَه رحمةً اتَّصلتْ بهم حتى أوصلتْهم إلى دار رحمته، ولهذا ختم الآية بهذين الاسمين الكريمين العزيز الرحيم.
{5} Na njia hii iliyonyooka ni "Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu." Kwani ni katika njia hii ndiyo aliteremsha Kitabu chake na akakiteremsha kuwa ni njia kwa waja wake, inayowafikisha kwake. Na akakilinda kwa nguvu zake kutokana na mageuzi na mabadiliko. Na akawarehemu waja wake kwacho rehema kwa rehema walizoendelea kuwa nazo mpaka zikawafikisha katika nyumba ya rehema zake.
Na ndiyo maana akahitimisha Aya hii kwa majina haya mawili matukufu: Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.
#
{6} فلما أقسم تعالى على رسالته، وأقام الأدلَّةَ عليها؛ ذَكَرَ شدَّةَ الحاجة إليها واقتضاءَ الضَّرورة لها، فقال: {لِتُنذِرَ قوماً ما أُنذِرَ آباؤهم فهم غافلونَ}: وهم العربُ الأميُّون، الذين لم يزالوا خالين من الكتب، عادمين الرسل، قد عَمَّتْهُمُ الجهالة وغمرتْهُمُ الضلالة، وأضْحَكوا عليهم وعلى سَفَهِهِم عقولَ العالمينَ، فأرسل الله إليهم رسولاً من أنفسهم يزكِّيهم، ويعلِّمهم الكتاب والحكمة وإن كانوا من قبل لَفي ضلال مُبين، فينذرُ العربَ الأميِّين ومَنْ لَحِقَ بهم من كلِّ أميٍّ، ويذكِّرُ أهل الكتب بما عندهم من الكتبِ؛ فنعمةُ الله به على العرب خصوصاً وعلى غيرِهم عموماً.
{6} Mwenyezi Mungu alipoapa kwa ujumbe wake, na kuuthibitisha kwa ushahidi mbalimbali, akataja haja kubwa ya viumbe juu yake,
akasema: "Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika." Ambao ni wale Waarabu wasiojua kusoma na kuandika, ambao bado hawakuwa na vitabu na Mitume, ambao walikuwa wamejumuishwa na ujinga na kugubikwa na upotofu, na akili za walimwengu zikawacheka kwa upumbavu wao. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia Mtume kutokana nao wenyewe, ili awatakase na awafundishe Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotofu uliowazi. Alipaswa kuwaonya Waarabu wasiojua kusoma na kuandika na watu wote wanaofanana nao miongoni mwa wale wasiojua kusoma na kuandika, na awakumbushe Watu wa Kitabu vitabu walivyo navyo. Kwa hivyo, Mtume huyu akawa ni neema ya Mwenyezi Mungu juu ya Waarabu hasa na juu ya watu wengine kwa ujumla.
#
{7} ولكن هؤلاء الذين بُعِثْتَ [فيهم] لإنذارِهم بعدما أنذَرْتَهم انقسموا قسمين: قسمٌ ردَّ لما جئتَ به ولم يَقْبَلِ النِّذارة، وهم الذين قال الله فيهم: {لقد حَقَّ القولُ على أكْثَرِهم فهم لا يؤمنونَ}؛ أي: نفذ فيهم القضاءُ والمشيئةُ أنَّهم لا يزالون في كفرهم وشِرْكِهم، وإنَّما حقَّ عليهم القولُ بعد أن عُرِضَ عليهم الحقُّ فرفَضوه؛ فحينئذٍ عوقبوا بالطبع على قلوبهم.
{7} Lakini hawa uliotumwa kwao ili uwaonye, baada ya kuwaonya waligawanyika sehemu mbili; kundi lililokataa yale uliyowajia nayo na wala halikukubali maonyo,
na hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao: "Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini." Hilo liliwafika baada ya kufikishiwa haki lakini wakaikataa. Hapo, wakaadhibiwa kwa kuzibwa nyoyo zao.
#
{8} وذَكَرَ الموانعَ من وصول الإيمان لقلوبهم، فقال: {إنَّا جَعَلْنا في أعناقِهِم أغلالاً}: وهي جمع غِلٍّ، والغلُّ ما يُغَلُّ به العُنُق؛ فهو للعنق بمنزلةِ القيد للرِّجْل. وهذه الأغلالُ التي في [الأذقان] عظيمةٌ قد وصَلَتْ {إلى}: أذقانهم، ورفعت رؤوسهم إلى فوق. {فهم مُقْمَحُونَ}؛ أي: رافعوا رؤوسهم من شدَّةِ الغلِّ الذي في أعناقهم؛ فلا يستطيعون أن يَخْفِضوها.
{8} Akavitaja vizuizi vilivyozuia imani kufika nyoyoni mwao,
akasema: "Hakika sisi tumeweka makongwa shingoni mwao." Pingu hizi zilizo shingoni mwao ni kubwa, kiasi kwamba zimefikia videvu vyao na zikaviinua vichwa vyao juu. "Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu." Kwa sababu ya mvuto mkubwa wa pingu iliyo shingoni mwao, hawawezi kuzipunguza.
#
{9} {وجَعَلْنا مِن بينِ أيْديهم سَدًّا ومن خَلْفِهِم سَدًّا}؛ أي: حاجزاً يحجُزُهم عن الإيمان؛ {فهم لا يُبْصِرونَ}: قد غمرهم الجهلُ والشقاءُ من جميع جوانبهم، فلم تُفِدْ فيهم النِّذارةُ.
{9} "Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao," vilivyowazuia kuamini. "Kwa hivyo hawaoni," kwa maana ujinga wao na uovu wao umewafunika kila upande. Kwa hivyo maonyo hayakuwafaa kitu.
#
{10} {وسواءٌ عليهم أأنذَرْتَهم أم لم تُنذِرْهُم لا يؤمنونَ}: وكيف يؤمِنُ من طبع على قلبه ورأى الحقَّ باطلاً والباطل حَقًّا؟!
{10} "Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini." Na vipi ataamini yule ambaye alizibwa moyo na akaiona haki kuwa ndiyo batili na kwamba batili ndiyo haki?
#
{11} والقسم الثاني الذين قَبِلوا النِّذارَةَ وقد ذَكَرَهُم بقوله: {إنَّما تُنذِرُ}؛ أي: إنَّما تنفعُ نِذارَتُك ويَتَّعِظُ بنُصْحِكَ {مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ}؛ أي: من قصْدُهُ اتِّباع الحقِّ وما ذُكِّر به، {وخَشِيَ الرحمنَ بالغيبِ}؛ أي: مَنِ اتَّصف بهذين الأمرين: القصد الحسن في طلب الحقِّ، وخشية الله تعالى؛ فهم الذين ينتفعونَ برسالتِكَ ويَزْكُون بتعليمِكَ، وهذا الذي وُفِّقَ لهذين الأمرين، بشِّره {بمغفرةٍ}: لذُنوبه {وأجرٍ كريم}: لأعماله الصالحة ونيَّتِهِ الحسنةِ.
{11} Kundi la pili ni wale waliokubali maonyo,
nao aliwataja kwa kauli yake: "Hakika wewe unamwonya." Yaani, maonyo yako na mawaidha yako yanamfaa "mwenye kufuata ukumbusho na akamcha Arrahman
(Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema kwa sababu ya matendo yake mema na nia yake nzuri.
#
{12} {إنَّا نحنُ نُحْيي الموتى}؛ أي: نبعثُهم بعد موتِهِم لِنُجازِيَهم على الأعمال، {ونَكْتُبُ ما قَدَّموا}: من الخير والشرِّ، وهو أعمالُهم التي عملوها وباشَروها في حال حياتِهِم، {وآثارَهُم}: وهي آثار الخير وآثارُ الشرِّ التي كانوا هم السببَ في إيجادها في حال حياتِهِم وبعدَ وفاتِهِم، وتلك الأعمال التي نشأت من أقوالِهِم وأفعالِهِم وأحوالِهِم؛ فكلُّ خيرٍ عمل به أحدٌ من الناس بسبب علم العبد وتعليمِهِ أو نُصحه أو أمرِهِ بالمعروف أو نهيِهِ عن المنكر أو علم أوْدَعَه عند المتعلِّمين أو في كتبٍ يُنْتَفَع بها في حياتِهِ وبعدَ موتِهِ أو عمل خيراً من صلاةٍ أو زكاةٍ أو صدقةٍ أو إحسانٍ فاقتدى به غيرُه، أو عمل مسجداً أو محلاًّ من المحالِّ التي يرتَفِقُ بها الناسُ وما أشبهَ ذلك؛ فإنَّها من آثارِهِ التي تُكْتَبُ له، وكذلك عمل الشرِّ، ولهذا: «من سنَّ سنَّةً حسنةً؛ فله أجْرُها وأجْرُ من عَمِلَ بها إلى يوم القيامةِ، ومن سنَّ سنَّة سيئة، فعليه وزرها ووزر من عمل بها إلى يوم القيامة».
وهذا الموضع يبيِّنُ لك علوَّ مرتبة الدَّعوة إلى الله والهداية إلى سبيله بكلِّ وسيلةٍ وطريق موصل إلى ذلك، ونزول درجة الداعي إلى الشرِّ الإمام فيه، وأنَّه أسفل الخليقة وأشدُّهم جرماً وأعظمُهم إثماً، {وكلَّ شيءٍ}: من الأعمال والنيَّاتِ وغيرها {أحْصَيْناه في إمام مُبينٍ}؛ أي: كتاب هو أمُّ الكتب، وإليه مرجِعُ الكُتُب التي تكون بأيدي الملائكة، وهو اللوحُ المحفوظُ.
{12} "Hakika Sisi tunawafufua wafu" ili tuwalipe kwa matendo yao. Na tunayaandika wanayoyatanguliza miongoni mwa mambo mema na maovu waliyotenda katika uhai wao, "na wanayoyaacha nyuma" ambazo ni athari za heri na athari za shari ambazo walikuwa wao ndio sababu ya kutokea kwake wakati wa uhai wao na baada ya kufa kwao. Na vile vitendo vilivyotokana na maneno yao, vitendo vyao na hali zao. Kila heri aliyofanya mtu kwa sababu ya elimu aliyochukua kwa mtu fulani, au aliyomfundisha, au nasaha, kumuamrisha mema, au kumkataza maovu, au elimu aliyofunza wanafunzi au aliyoandika katika vitabu vyenye kunufaisha wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake. Au akafanya heri kama vile swala, zaka, sadaka, au ihsani, kwa hivyo wengine wakamuiga, au alijenga msikiti au mahali ambapo watu wanakaa na mengineyo; basi hayo yote ni katika athari zake ambazo ameandikiwa, pamoja na matendo yake maovu. Ndiyo maana Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake,
akasema: “Mwenye kuanzisha mwenendo mwema atapata ujira wake na ujira wa mwenye kuutenda mpaka Siku ya Kiyama. Na mwenye kuanzisha mwenendo muovu, basi mzigo wake uko juu yake, na mzigo wa mwenye kuutenda mpaka Siku ya Kiyama." Sehemu hii inakuonyesha kiwango cha juu cha kulingania kwa Mwenyezi Mungu na kuongoka kufikia njia yake kwa kila njia inayofikisha kwenye hilo, na kiwango cha chini cha kiongozi wa kulingania kwenye uovu. Na kwamba yeye ndiye kiumbe wa chini kabisa, na mkubwa wao zaidi katika uhalifu, na mwenye madhambi kubwa zaidi yao wote. "Na kila kitu" miongoni mwa matendo, makusudio na mambo mengineyo "tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha." Yaani, Kitabu ambacho ni mama wa vitabu vyote, na kwake ndiyo marejeo ya vitabu vilivyo mikononi mwa Malaika, nacho ndio Ubao Uliohifadhiwa.
{وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلًا أَصْحَابَ الْقَرْيَةِ إِذْ جَاءَهَا الْمُرْسَلُونَ (13) إِذْ أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمُ اثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوا إِنَّا إِلَيْكُمْ مُرْسَلُونَ (14) قَالُوا مَا أَنْتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُنَا وَمَا أَنْزَلَ الرَّحْمَنُ مِنْ شَيْءٍ إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ (15) قَالُوا رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّا إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ (16) وَمَا عَلَيْنَا إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ (17) قَالُوا إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ لَئِنْ لَمْ تَنْتَهُوا لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُمْ مِنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ (18) قَالُوا طَائِرُكُمْ مَعَكُمْ أَئِنْ ذُكِّرْتُمْ بَلْ أَنْتُمْ قَوْمٌ مُسْرِفُونَ (19) وَجَاءَ مِنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَى قَالَ يَاقَوْمِ اتَّبِعُوا الْمُرْسَلِينَ (20) اتَّبِعُوا مَنْ لَا يَسْأَلُكُمْ أَجْرًا وَهُمْ مُهْتَدُونَ (21) وَمَا لِيَ لَا أَعْبُدُ الَّذِي فَطَرَنِي وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (22) أَأَتَّخِذُ مِنْ دُونِهِ آلِهَةً إِنْ يُرِدْنِ الرَّحْمَنُ بِضُرٍّ لَا تُغْنِ عَنِّي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا وَلَا يُنْقِذُونِ (23) إِنِّي إِذًا لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (24) إِنِّي آمَنْتُ بِرَبِّكُمْ فَاسْمَعُونِ (25) قِيلَ ادْخُلِ الْجَنَّةَ قَالَ يَالَيْتَ قَوْمِي يَعْلَمُونَ (26) بِمَا غَفَرَ لِي رَبِّي وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُكْرَمِينَ (27) وَمَا أَنْزَلْنَا عَلَى قَوْمِهِ مِنْ بَعْدِهِ مِنْ جُنْدٍ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا كُنَّا مُنْزِلِينَ (28) إِنْ كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَامِدُونَ (29) يَاحَسْرَةً عَلَى الْعِبَادِ مَا يَأْتِيهِمْ مِنْ رَسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (30) أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنَ الْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ (31) وَإِنْ كُلٌّ لَمَّا جَمِيعٌ لَدَيْنَا مُحْضَرُونَ (32)}.
13. Na wapigie mfano wa wakazi wa mji walipojiwa na Mitume. 14. Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu.
Wakasema: "Hakika sisi tumetumwa kwenu." 15.
Wakasema: "Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uongo tu." 16.
Wakasema: "Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu." 17. Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi. 18.
Wakasema: "Sisi tumeamua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu." 19.
Wakasema: "Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka." 20. Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini,
akasema: "Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa." 21. Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. 22. Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa? 23. Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani
(Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. 24. Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri. 25. Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni! 26.
Akaambiwa: "Ingia Peponi!" Akasema: "Laiti kuwa watu wangu wangelijua. 27. Jinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe, na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa. 28. Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. 29. Hakukuwa ila ukelele mmoja tu, na mara walizimwa! 30. Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli. 31. Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao. 32. Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.
#
{13} أي: واضرِبْ لهؤلاء المكذِّبين برسالتك الرادِّين لدعوتِكَ مثلاً يعتبرونَ به ويكون لهم موعظةً إن وُفِّقوا للخيرِ، وذلك المثلُ أصحابُ القريةِ وما جرى منهم من التَّكذيب لرسل الله وما جرى عليهم من عقوبتِهِ ونَكاله، وتعيينُ تلك القريةِ لو كان فيه فائدةٌ؛ لعيَّنَها الله، فالتعرُّض لذلك وما أشبهه من باب التكلُّف والتكلُّم بلا علم، ولهذا إذا تكلَّم أحدٌ في مثل هذه الأمور؛ تجدُ عنده من الخَبْطِ والخَلْطِ والاختلاف الذي لا يستقرُّ له قرارٌ ما تعرِفُ به أنَّ طريقَ العلم الصحيح الوقوفُ مع الحقائق وتَرْكُ التعرُّض لما لا فائدة فيه، وبذلك تزكو النفسُ ويزيدُ العلمُ من حيث يظنُّ الجاهل أنَّ زيادتَه بذكر الأقوال التي لا دليلَ عليها ولا حُجَّةَ عليها ولا يَحْصُلُ منها من الفائدة إلاَّ تشويشُ الذهن واعتيادُ الأمور المشكوكِ فيها. والشاهدُ أنَّ هذه القريةَ جَعَلَها الله مثلاً للمخاطَبين. {إذ جاءها المُرْسَلونَ}: من الله تعالى؛ يأمُرونَهم بعبادةِ الله وحدَه وإخلاصِ الدين له، ويَنْهَوْنَهم عن الشرك والمعاصي.
{13} Hii inamaanisha kwamba: Hawa wanaokadhibisha ujumbe wako, wanaokataa wito wako, wapigie mfano watakaouzingatia na ambao utakuwa ni mawaidha kwao ikiwa watawezeshwa kufikia heri. Na mfano huo ni watu wa mji fulani na yale waliyoyafanya ya kuwakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu na adhabu na mateso yaliyowafikia. Na ikiwa kungekuwa na faida katika kujua jina la mji huo hasa, basi Mwenyezi Mungu angelitaja jina lake. Kwa hivyo, kujishughulisha na hilo na jambo lolote linalofanana na hilo ni katika kujisumbua tu na mambo ambayo mtu hana elimu yake. Ndiyo maana, ukimsikia mtu akizungumzia mambo hayo, utakuta ndani yake mchanganyiko na tofauti mbalimbali zisizokuwa na uhakika, jambo linalotufanya kujua kwamba njia sahihi ya elimu ni kusimama pamoja na uhakika wa mambo na kuacha kujisumbua na mambo yasiyokuwa na faida, na kwa hayo nafsi inatakasika na elimu yake inaongezeka. Naye mjinga anadhani lililo sahihi ni kuzidisha kutaja kauli zisizo na ushahidi wala uthibitisho wala zisizo na faida isipokuwa kuchanganya akili na kutegemea juu ya mambo yenye kutiliwa shaka. Na ushahidi ni kwamba Mwenyezi Mungu alikifanya kijiji hiki kuwa mfano kwa wale wanaoongeleshwa. "Walipojiwa na Mitume" kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; wakiwaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake na kumkusudia Yeye tu katika Dini, na wakiwakataza kumshirikisha na kumuasi.
#
{14} {إذ أرْسَلْنا إليهم اثْنَيْنِ فكذَّبوهما فَعَزَّزْنا بثالثٍ}؛ أي: قوَّيْناهما بثالثٍ، فصاروا ثلاثةَ رسل؛ اعتناءً من الله بهم، وإقامةً للحجَّة بتوالي الرسل إليهم، {فقالوا} لهم: {إنَّا إليكُم مُرْسَلونَ}.
{14} "Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwengine wa tatu." Kwa hivyo wakawa Mitume watatu; kutokana na Mwenyezi Mungu kuwajali mno, na kwa sababu ya kuwasimamishia hoja kwa kuwatumia Mitume kwa kufuatanisha.
Wakasema: "Hakika sisi tumetumwa kwenu."
#
{15} فأجابوهم بالجوابِ الذي ما زال مشهوراً عند من ردَّ دعوةَ الرُّسل، فقالوا: {ما أنتُم إلاَّ بشرٌ مثلُنا}؛ أي: فما الذي فضَّلَكم علينا وخصَّكم من دوننا؟!
قالت الرسل لأممهم: إن نحنُ إلاَّ بشرٌ مثلُكم، ولكن [اللَّهَ] يمنُّ على من يشاءُ من عبادِهِ، {وما أنزل الرحمنُ من شيءٍ}؛ أي: أنكروا عمومَ الرسالةِ، ثم أنكروا أيضاً المخاطبين لهم، فقالوا: {إنْ أنتُم إلاَّ تكذِبونَ}.
{15} Lakini wao wakawajibu kwa jawabu ambalo bado ni maarufu miongoni mwa wale waliokanusha wito wa Mitume,
wakasema: "Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi." Yaani,
ni kitu gani kilichokufadhilisheni nyinyi juu yetu na kikawafanya kuwa maalumu zaidi kutuliko sisi? Mitume hao wakawaambia kaumu zao: "Sisi kweli si chochote ila ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake." "Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu." Yaani, walikanusha ujumbe kwa ujumla, kisha wakawapinga hao waliokuwa wanawaongelesha,
wakasema: "Nyinyi mnasema uongo tu."
#
{16} فقالت هؤلاء الرسل الثلاثة: {ربُّنا يعلم إنَّا إليكُم لَمُرْسَلونَ}: فلو كنَّا كاذبينَ؛ لأظهر اللَّهُ خِزْيَنا ولبادَرَنا بالعقوبة.
{16} Kwa hivyo,
Mitume hao watatu wakasema: "Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu." Na lau kuwa tulikuwa waongo, basi Mwenyezi Mungu angedhihirisha hizaya yetu na angetuharakishia adhabu.
#
{17} {وما علينا إلاَّ البلاغُ المُبينُ}؛ أي: البلاغ المبينُ الذي يحصُلُ به توضيحُ الأمور المطلوب بيانها، وما عدا هذا من آيات الاقتراح أو من سرعةِ العذاب؛ فليس إلينا، وإنَّما وظيفتُنا التي هي البلاغُ المبينُ قُمْنا بها وبيَّنَّاها لكم؛ فإنِ اهْتَدَيْتُم؛ فهو حظُّكم وتوفيقُكم، وإن ضَلَلْتُم؛ فليس لنا من الأمر شيءٌ.
{17} "Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe wazi wazi." Ambako kwa huo mambo yanayohitajika kubainishwa yanawekwa wazi. Na zaidi ya haya miongoni mwa ishara wanazopendekeza wao au kuharakishiwa adhabu, siyo juu yetu, bali kazi yetu ambayo ni kufikisha ujumbe wazi wazi, tayari tumeshaifanya. Kwa hivyo, mkiongoka, basi hiyo ni bahati yenu na kuwezeshwa kwenu. Lakini ikiwa mtapotea, basi hatuna chetu kitu katika jambo hilo.
#
{18} فقال أصحاب القرية لرُسُلِهِم: {إنَّا تَطَيَّرْنا بكُم}؛ أي: لم نر على قدومكم علينا واتِّصالكم بنا إلاَّ الشرَّ، وهذا من أعجب العجائب؛ أن يُجْعَلَ من قَدِمَ عليهم بأجَلِّ نعمةٍ يُنْعِمُ اللهُ بها على العبادِ وأجلِّ كرامةٍ يكرِمُهم بها، وضرورتهم إليها فوق كلِّ ضرورةٍ، قد قدم بحالة شَرٍّ زادت على الشرِّ الذي هم عليه واستشأموا بها، ولكنَّ الخِذْلانَ وعدمَ التوفيق يَصْنَعُ بصاحبِهِ أعظمَ مما يَصْنَعُ به عدوُّه، ثم توعَّدوهم فقالوا: {لَئِن لم تَنتَهوا لَنَرْجُمَنَّكُمْ}؛ أي: لَنَقْتُلَنَّكم رجماً بالحجارةِ أشنع القتلات، {ولَيَمَسَّنَّكُم مِنَّا عذابٌ أليمٌ}.
18.
Basi watu wa kijiji hicho wakawaambia Mitume wao: "Sisi tumeamua kuwa nyinyi ni wakorofi." Yaani, hatukuona katika kutujia kwenu na kuingiliana kwenu nasi isipokuwa uovu tu. Lakini hili ni katika maajabu makubwa zaidi ya yote. Kwamba walimfanya yule aliyewajia na neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake, na utukufu mkubwa zaidi aliowakirimu kwa huo, na haja yao juu ya hilo iliyokuwa kubwa zaidi ya mahitaji mengine yote, kwamba alikuja na hali ya uovu ambayo iliwazidishia uovu waliokuwa nao, na wakaona mkosi ndani yake. Lakini huko ni kuachiliwa mbali na Mwenyezi Mungu na kutowezeshwa kunaweza kumfanya mtu huyo mambo makubwa zaidi ya anavyoweza kufanyiwa na adui yake.
Kisha wakawatishia wakisema: "Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe." Yaani, tutawauwa kwa kuwapiga mawe vibaya kabisa. "Na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu."
#
{19} فقالت لهم رسلهم: {طائِرُكُم معكم}: وهو ما معهم من الشركِ والشرِّ المقتضي لوقوع المكروِه والنقمةِ وارتفاع المحبوبِ والنعمةِ. {أإن ذُكِّرْتُم}؛ أي: بسبب أنَّا ذكَّرْناكم ما فيه صلاحُكُم وحظُّكُم قلتُم لنا ما قلتُم، {بل أنتُم قومٌ مسرِفونَ}: متجاوِزونَ للحدِّ مُتَجَرْهِمونَ في قولِكُم. فلم يزِدْهم دعاؤُهم إلاَّ نفوراً واستكباراً.
{19} Basi Mitume wao hao wakawaambia: "Ukorofi wenu mnao wenyewe!" Nao ni ushirikina walionao, na uovu unaopelekea kutokea balaa, adhabu na kuondokewa na mambo wayapendayo na neema. "Je, ni kwa kuwa mnakumbushwa mambo yenye kutengenea kwenu na bahati yenu nzuri, basi ndiyo mkatuambia hayo mliyosema? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka." Basi kuwalingania huko hakukuwazidisha isipokuwa kujitenga na kiburi.
#
{20} {وجاء من أقصى المدينةِ رجلٌ يسعى}: حرصاً على نُصْح قومِهِ حين سمعَ ما دَعَتْ إليه الرسل وآمنَ به وعلم ما ردَّ به قومُه عليهم، فقال لهم: {يا قوم اتَّبِعوا المرسلينَ}: فأمَرَهُم باتِّباعهم، ونَصَحَهم على ذلك، وشهد لهم بالرسالة.
{20} "Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini" akiwa na hima kubwa ya kuwapa nasaha watu wake, aliposikia yale waliyoyalingania Mitume hao. Kwa hivyo akayaamini, na akajua yale waliwajibu nayo watu wake Mitume hao.
Akawaambia: "Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa." Kwa hivyo akawaamuru wawafuate, akawashauri wafanye hivyo, na akawashuhudilia kwamba ni Mitume.
#
{21} ثم ذكر تأييداً لما شهد به ودعا إليه، فقال: {اتَّبِعوا مَن لا يَسْألُكُم أجراً}؛ أي: اتَّبِعوا مَنْ نَصَحَكُم نُصْحاً يعودُ إليكم بالخير، وليس يريدُ منكم أموالَكُم ولا أجراً على نصحِهِ لكم وإرشادِهِ؛ فهذا موجبٌ لاتِّباع مَنْ هذا وصفُهُ. بقي أن يُقالَ: فلعلَّه يَدْعو ولا يأخُذُ أجرةً ولكنَّه ليس على الحقِّ، فدَفَعَ هذا الاحتراز بقوله: {وهم مهتدونَ}: لأنهم لا يَدْعون إلاَّ لما يَشْهَدُ العقلُ الصحيح بحُسْنِهِ، ولا يَنْهَوْنَ إلاَّ بما يشهدُ العقلُ الصحيح بقُبْحِهِ.
{21} Kisha akataja kinachounga mkono yale aliyoyashuhudia na kuyalingania,
akasema: "Wafuateni ambao hawakutakini ujira." Yaani, wafuateni wale waliokunasihini kwa njia ambayo itakuleteeni heri, na wala hawataki mali zenu wala malipo yoyote kwa nasaha yao waliyowapa wala kuwaelekeza kwao walikowaelekeza. Haya yanalazimu kwamba afuatwe mtu ambaye hizi ndizo sifa zake.
Inabakia kusema: Labda analingania bila ya kuomba ujira, lakini hayuko kwenye haki.
Basi akazuia hili kwa kauli yake: "Hali ya kuwa wenyewe wameongoka." Kwa sababu hawalinganii isipokuwa kwenye yale ambayo akili timamu inashuhudia uzuri wake, na wala hawakatazi isipokuwa yale ambayo akili timamu inashuhudia kwamba ni mabaya.
#
{22 - 25} فكأنَّ قومَه لم يَقْبَلوا نُصْحَهُ، بل عادوا لائمين له على اتِّباع الرسل وإخلاص الدين لله وحده، فقال: {وما لي لا أعبُدُ الذي فَطَرَني وإليه تُرْجَعونَ}؛ أي: وما المانعُ لي من عبادةِ مَنْ هو المستحقُّ للعبادة؛ لأنَّه الذي فَطَرني وخَلَقَني ورَزَقَني وإليه مآل جميع الخلق فيجازيهم بأعمالهم؛ فالذي بيدِهِ الخَلْقُ والرزقُ والحكمُ بين العباد في الدُّنيا والآخرة هو الذي يَسْتَحِقُّ أن يُعْبَدَ ويُثْنى عليه ويُمَجَّدَ دون مَنْ لا يملِكُ نفعاً ولا ضرًّا ولا عطاءً ولا منعاً ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، ولهذا قال: {أأتَّخِذُ من دونِهِ آلهةً إن يُرِدْنِ الرحمنُ بِضُرٍّ لا تُغْنِ عنِّي شفاعَتُهُم شيئاً}: لأنَّه لا أحدَ يشفع عند الله إلاَّ بإذنِهِ؛ فلا تُغْني شفاعتُهم عني شيئاً {ولا هم يُنقِذونِ}: من الضُّرِّ الذي أرادَه اللهُ بي. {إنِّي إذاً}؛ أي: إن عبدتُ آلهةً هذا وصفُها {لَفي ضلال مُبينٍ}: فجمع في هذا الكلام بين نُصحهم، والشهادةِ للرسُل بالرسالةِ والاهتداءِ، والإخبار بتعيُّن عبادة الله وحدَه، وذكر الأدلَّة عليها، وأنَّ عبادة غيرِهِ باطلةٌ، وذَكَرَ البراهينَ عليها والأخبارَ بضلال مَنْ عَبَدَها، والإعلان بإيمانِهِ جَهْراً مع خوفِهِ الشديد من قتلهم، فقال: {إنِّي آمنتُ بربِّكُم فاسمعونِ}.
{22 - 25} Ni kana kwamba watu wake hawakukubali nasaha yake, bali walimlaumu kwa kuwafuata Mitume hao na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika Dini.
Basi akasema: "Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa?" Kwani yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, kwa sababu Yeye ndiye aliyeniumba, na akaniruzuku, na kwake Yeye ndiye marejeo ya viumbe vyote. Kwa hivyo Yule ambaye mkononi mwake ndiko kuko kuumba, kuruzuku na kuhukumu baina ya waja duniani na akhera ndiye anayestahiki kuabudiwa, kusifiwa, na kuhimidiwa na si yule ambaye hamiliki manufaa wala madhara wala kupeana wala kuzuia wala mauti wala uhai wala kufufua.
Ndiyo maana akasema: "Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani
(Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu," kwa sababu hapana anayeweza kufanya uombezi kwa Mwenyezi Mungu ila kwa idhini yake. Kwa hivyo, uombezi wa hao hautanifaa kitu "wala hawataniokoa" kutokana na madhara ambayo Mwenyezi Mungu alinitakia. "Basi hakika mimi hapo" ikiwa nikiwaabudu miungu ambao hizi ndizo sifa zao "nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri." Basi akaunganisha katika maneno haya kati ya kuwanasihi na kuwashahidilia Mitume hao kwamba ni Mitume, na kwamba ni waongofu. Na kujulisha kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na akataja ushahidi juu ya hayo, na kwamba kumuabudu asiyekuwa Yeye ni batili, na akataja ushahidi wa hilo, na akajulisha kwamba wenye kuabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu ni wapotofu, na kutangaza imani yake hadharani pamoja na kuhofu sana kwamba wanaweza kumuua.
Alisema: "Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!"
#
{26 - 27} فقتله قومُه لمَّا سَمِعوا منه وراجَعَهم بما راجَعَهم به. {قيل}: له في الحال: {ادْخُلِ الجَنَّةَ}. فقال مخبراً بما وصل إليه من الكرامة على توحيدِهِ وإخلاصِهِ وناصحاً لقومه بعدَ وفاتِهِ كما نَصَحَ لهم في حياته: {يا لَيتَ قَومِي يَعلمُونَ. بمَا غَفَر لي ربِّي}؛ أي: بأي شيءٍ غفر لي فأزال عني أنواع العقوبات، {وجَعَلَني من المُكْرَمينَ}: بأنواع المَثوبات والمسرَّات؛ أي: لو وَصَلَ علمُ ذلك إلى قلوبهم؛ لم يقيموا على شركهم.
{26 - 27} Kwa hivyo, watu wake wakamuua waliposikia kutoka kwake, na akawaambia yale aliyowaambia. "Akaambiwa" papo hapo; "Ingia Peponi!" Basi akasema akijulisha kuhusu yale aliyoyafikia ya utukufu kwa sababu ya kumpwekesha kwake Mwenyezi Mungu na kumkusudia katika dini, na kuwanasihi watu wake,
baada ya kufa kwake kama alivyowanasihi katika uhai wake: "Laiti kuwa watu wangu wangelijua. Jinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe," na akaniondoshea aina zote za adhabu "na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa," kwa kila aina ya malipo na mambo ya kufurahisha. Na lau kuwa nyoyo zao zitapata kujua haya, basi hawangeendelea kushikamana na ushirikina wao.
#
{28} قال الله في عقوبة قومه: {وما أنزَلْنا على قومِهِ من بعدِهِ من جندٍ من السماءِ}؛ أي: ما احْتَجْنا أن نتكَلَّفَ في عقوبتهم فننزلَ جنداً من السماء لإتلافِهِم. {وما كُنَّا منزِلينَ}: لعدم الحاجةِ إلى ذلك، وعظمة اقتدارِ الله تعالى، وشدَّةِ ضعفِ بني آدم، وأنَّهم أدنى شيء يصيبهم من عذاب الله يكفيهم.
{28} Mwenyezi Mungu alisema kuhusu namna walivyoadhibiwa watu wake: "Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni" ili liwaangamize. "Wala si wenye kuteremsha." Kwa sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo, na ukubwa wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ukubwa wa udhaifu wa wanadamu, na kwa sababu kinawatosha hata kitu kidogo tu cha adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
#
{29} {إن كانتْ}؛ أي: ما كانت عقوبتُهم {إلاَّ صيحةً واحدةً}؛ أي: صوتاً واحداً تكلَّم به بعضُ ملائكة الله؛ {فإذا هم خامدونَ}: قد تقطَّعتْ قلوبُهم في أجوافهم وانْزَعَجوا لتلك الصيحةِ فأصبحوا خامدينَ لا صوتَ ولا حركةَ ولا حياةَ بعد ذلك العتوِّ والاستكبار ومقابلة أشرفِ الخَلْقِ بذلك الكلام القبيح وتجبُّرهم عليهم.
{29} "Hakukuwa ila ukelele mmoja tu" waliotoa baadhi ya malaika wa Mwenyezi Mungu. "Na mara walizimwa!" Nyoyo zao zilichanikachanika ndani ya miili yao, na wakafadhaika kwa sababu ya ukelele huo. Kwa hivyo wakazimika, hawakuweza kutoa sauti wala harakati wala uhai baada ya ufidhuli wao ule na kiburi, na kuwakabili viumbe watukufu zaidi kwa maneno hayo machafu na kuwafanyia jeuri.
#
{30} قال الله مترحِماً للعبادِ: {يا حسرةً على العبادِ ما يأتيهم من رسول إلاَّ كانوا به يستهزِئونَ}؛ أي: ما أعظم شقاءَهم وأطولَ عناءَهم وأشدَّ جهلَهم حيث كانوا بهذه الصفةِ القبيحةِ التي هي سببٌ لكلِّ شقاءٍ وعذابٍ ونَكال.
{30} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akiwarehemu waja: "Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli." Yaani, ni upotofu wao upi mkubwa huu, na ukaidi mkubwa huu, na ujinga gani mkubwa huu ambapo waliamua kuwa na sifa hizi mbaya ambazo ndizo sababu ya kuwa mashakani kabisa, na kupata adhabu na mateso.
#
{31 - 32} {ألم يروا كم أهلكنا قبلهم من القرون أنهم إليهم لا يرجعون. وإن كلُّ لمَّا جميعٌ لدينا محضرون}؛ يقول تعالى: ألم يَرَ هؤلاء ويَعْتَبِروا بِمَنْ قبلَهم من القرون المكذِّبة التي أهْلَكَها الله تعالى وأوقَعَ بها عقابَها، وأنَّ جميعَهم قد بادَ وهَلَكَ فلم يرجِعْ إلى الدُّنيا ولنْ يَرْجِعَ إليها، وسيعيدُ الله الجميع خلقاً جديداً، ويبعثُهُم بعد موتِهِم، ويحضُرونَ بين يديهِ تعالى؛ ليحكمَ بينهم بحكمِهِ العدل الذي لا يظلِمُ مثقالَ ذَرَّةٍ وإنْ تَكُ حسنةً يضاعِفْها، ويُؤْتِ من لَدُنْه أجراً عظيماً.
{31 - 32} "Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao." "Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.
" Mwenyezi Mungu anasema: "Je, hawakuona hawa na kuzingatia ni kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, na kwamba kwao hawatarejea katika dunia?" Mwenyezi Mungu atawarudisha wote kwa umbo jipya, na atawafufua baada ya kufa kwao, na watahudhuria mbele yake Mtukufu; ili ahukumu baina yao kwa hukumu yake ya uadilifu, ambaye hadhulumu hata uzito wa chembe. Na ikiwa ni jambo jema, basi Yeye atalizidisha na atapeana malipo makubwa kutoka kwake.
{وَآيَةٌ لَهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ (33) وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّاتٍ مِنْ نَخِيلٍ وَأَعْنَابٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ الْعُيُونِ (34) لِيَأْكُلُوا مِنْ ثَمَرِهِ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ أَفَلَا يَشْكُرُونَ (35) سُبْحَانَ الَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنْبِتُ الْأَرْضُ وَمِنْ أَنْفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ (36)}.
33. Na Ishara hiyo kwao ni ardhi iliyokufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo! 34. Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemichemi ndani yake. 35. Ili wale katika matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru? 36. Ametakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyovijua.
#
{33} أي: {وآيةٌ لهم}: على البعثِ والنُّشور والقيام بين يدي الله تعالى للجزاء على الأعمال هذه {الأرضُ المَيْتَةُ}: أنزل الله عليها المطرَ فأحْياها بعد موتها، {وأخْرَجْنا منها حَبًّا فمنه يأكُلونَ}: من جميع أصناف الزُّروع ومن جميع أصناف النباتِ التي تأكُلُه أنعامُهم.
{33} Yaani, "Na Ishara hiyo kwao" juu ya kufufuliwa na kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa malipo ya vitendo hivyo. Mwenyezi Mungu aliiteremshia mvua na akaihuisha baada ya kufa kwake. "Na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo!" Na kila aina ya mazao na mimea wanayokula wanyama wao.
#
{34} {وجَعَلْنا فيها}؛ أي: في تلك الأرض الميتة {جَنَّاتٍ}؛ أي: بساتين فيها أشجارٌ كثيرةٌ، وخصوصاً النخيل والأعناب، اللذان هما أشرف الأشجار، {وفجَّرْنا فيها}؛ أي: في الأرض {من العيون}: جعلنا في الارض تلكَ الأشجارَ والنخيل والأعناب.
{34} "Na tukafanya ndani yake;" yaani, katika ardhi hiyo iliyokufa "mabustani" yenye miti mingi, hasa mitende na mizabibu, ambayo ndiyo miti bora zaidi. "Na tukatimbua ndani yake;" yaani, katika ardhi "chemchemi." Na tumeifanya katika ardhi hiyo miti na mitende na zabibu.
#
{35} {لِيأكُلوا من ثمرِهِ}: قوتاً وفاكهةً وأدماً ولذَّةً. {و} الحال أنَّ تلك الثمار {ما} عملتها {أيديهم}: وليس لهم فيها صنعٌ ولا عملٌ، إنْ هو إلاَّ صنعةُ أحكم الحاكمين وخيرِ الرازقين، وأيضاً؛ فلم تَعْمَلْهُ أيديهم بطبخ ولا غيرِهِ، بل أوجد اللهُ هذه الثمارَ غير محتاجةٍ لطَبْخ ولا شيءٍ تؤخَذُ من أشجارِها فتُؤكَلُ في الحال. {أفلا يَشْكُرونَ}: مَنْ ساقَ لهم هذه النعم، وأسبغَ عليهم من جُودِهِ وإحسانِهِ ما به تَصْلُحُ أمورُ دينهم ودُنْياهم، أليس الذي أحْيا الأرض بعد موتِها فأنْبَتَ فيها الزُّروعَ والأشجارَ وأوْدَعَ فيها لذيذَ الثمار وأظهر ذلك الجنى من تلك الغصونِ وفَجَّرَ الأرضَ اليابسة الميتة بالعُيونِ بقادرٍ على أن يُحْيِيَ الموتى؟ بلى إنَّه على كل شيء قدير.
{35} "Ili wale katika matunda yake" kama chakula chao kikuu, na matunda ya kawaida, na kitoweo kwa vyakula vingine na wapate kufurahia. "Na" hali ni kwamba matunda haya "hayakufanywa na mikono yao" bali ilikuwa ni kazi ya mikono ya Mwenye hekima zaidi ya wote, na mbora wa wanaoruzuku. Pia si mikono yao iliyoyafanya kwa kuyapika au kitu kingine chochote. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyeyaumba matunda haya bila kuhitaji kupikwa wala chochote. Hayo yanachukuliwa tu kutoka kwenye miti yake na kuliwa moja kwa moja. "Basi je, hawashukuru," yule aliyewapa neema hizi na akawajaalia mengi kwa ukarimu mkubwa mambo ambayo kwayo yanatengenea mambo yao ya kidini na ya kidunia? Je, yule aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake, kisha akaotesha humo mazao, miti, na akatia humo matunda matamu, na akaipasua ardhi kavu iliyokuwa imekufa kwa chemichemi? Kwani huyo hana uwezo wa kuwafufua wafu? Ndiyo, Yeye ni Muweza wa kila kitu.
#
{36} {سبحانَ الذي خَلَقَ الأزواجَ كُلَّها}؛ أي: الأصناف كلَّها {مما تُنْبِتُ الأرضُ}: فَنَوَّعَ فيها من الأصناف ما يعسُرُ تعدادُهُ، {ومن أنفسِهِم}: فنوَّعَهم إلى ذكرٍ وأنثى، وفاوتَ بين خَلْقِهِم وخُلُقِهِم وأوصافهم الظاهرة والباطنة {وممَّا لا يعلمونَ}: من المخلوقات التي قد خُلِقَتْ وغابتْ عن عِلْمِنا، والتي لم تُخْلَقْ بعد؛ فسُبحانه وتعالى أن يكونَ له شريكٌ أو ظهيرٌ أو عوينٌ أو وزيرٌ أو صاحبةٌ أو ولدٌ أو سميٌّ أو شبيهٌ أو مثيلٌ في صفاتِ كماله ونعوتِ جلالِهِ، أو يُعْجِزَه شيءٌ يريدُه.
{36} "Ametakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi." Basi akavifanya kuwa aina mbalimbali ambazo ni vigumu kuvidhibiti. "Na katika nafsi zao" pia akawafanya kuwa wanaume na wanawake, na akatofautisha baina ya maumbile yao, tabia zao, na sifa zao za dhahiri na zilizofichikana. "Na katika wasivyovijua" miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa lakini hatujavijua bado. Na pia viumbe ambavyo bado havijaumbwa. Basi ametakasika na kutukuka kuwa na mshirika, msaidizi, waziri, mwenza, mtoto, mwenye jina kama lake, mwenye kulingana naye, au mfano wake katika sifa za ukamilifu wake na sifa za ukuu wake, au kuwepo kitu kinachoweza kumshinda kufanya atakavyo.
{وَآيَةٌ لَهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ فَإِذَا هُمْ مُظْلِمُونَ (37) وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ (38) وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّى عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ (39) لَا الشَّمْسُ يَنْبَغِي لَهَا أَنْ تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ (40)}.
37. Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. 38. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema. 39. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. 40. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.
#
{37} أي: {وآيةٌ لهم}: على نفوذِ مشيئتِهِ وكمال قدرتِهِ وإحيائِهِ الموتى بعد موتهم {الليلُ نسلخُ منه النهارَ}؛ أي: نزيل الضياءَ العظيمَ الذي طَبَّقَ الأرضَ فنبدِلُه بالظُّلمة ونُحِلُّها محلَّه؛ {فإذا هم مظلِمون}.
{37} Yaani, "Na Ishara kwao" inayoonyesha kutekelezeka kwa mapenzi yake, ukamilifu wa uwezo wake, na kufufua kwake wafu baada ya kufa kwao ni, "usiku ambao tunauvua humo mchana." Yaani, tunauondoa mwangaza mkubwa unaokuwa umetanda kwenye ardhi na tunaubadilisha na giza, "mara wao wanakuwa gizani."
#
{38} وكذلك نزيلُ هذه الظلمةَ التي عَمَّتْهم وشَمِلَتْهم، فنُطْلِعُ الشمسَ، فتضيء الأقطار، وينتشر الخلقُ لمعايشهم ومصالحهم، ولهذا قال: {والشمسُ تجري لِمُسْتَقَرٍّ لها}؛ أي: دائماً تجري لمستقرٍّ لها، قدَّرها الله، لا تتعداه ولا تقصر عنه وليس لها تصرف في نفسها ولا استعصاء على قدرة الله تعالى. {ذلك تقدير العزيزِ}: الذي بعزَّتِهِ دَبَّرَ هذه المخلوقاتِ العظيمةَ بأكمل تدبيرٍ وأحسن نظام. {العليم}: الذي بعِلْمِهِ جَعَلَها مصالح لعبادِهِ ومنافعَ في دينِهِم ودُنياهم.
{38} Na vile vile pia tunaliondoa giza hili lililowafunika na kuwajumuisha wote, na tunalichomoza jua.Nalo likaangaza maeneo, kisha viumbe wakatawanyika sehemu mbalimbali kwa ajili ya kutafuta riziki zao na masilahi yao.
Ndiyo maana akasema: "Na jua linakwenda kwa kiwango chake." Yaani, kwa daima namna alivyolipangia Mwenyezi Mungu, halikwendi zaidi yake wala halipunguki chini yake, na wala halina uwezo wa kujifanyia kitu lenyewe, wala kuuasi uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu" ambaye kwa nguvu zake, anaviendesha viumbe hivi vikubwa kwa mpango ulio kamili zaidi na nidhamu bora kabisa. "Mwenye kujua vyema," ambaye kwa elimu yake amevifanya kuwa masilahi kwa waja wake na manufaa kwao katika Dini yao na dunia yao.
#
{39} {والقَمَرَ قدَّرْناه منازلَ}: ينزِلُها ، كلَّ ليلةٍ ينزِلُ منها واحدةً، {حتى}: يصغُرَ جدًّا فيعود {كالعُرْجونِ القديم}؛ أي: عُرجون النخلةِ الذي من قدمه نَشَّ وصَغُر حجمُهُ وانحنى، ثم بعد ذلك ما زال يزيدُ شيئاً فشيئاً حتى يتمَّ نورُه، وَيَتَّسِقَ ضياؤُه.
{39} "Na mwezi tumeupimia vituo" ambavyo unashukia kila kituo katika usiku mmoja, "mpaka" ukawa mdogo sana, na ukarudi kuwa "kama karara kongwe." Kisha, baada ya hapo ukaendelea kuongezeka kidogo kidogo mpaka nuru yake ikakamilika na mng'aro wake ukawa thabiti.
#
{40} وكلٌّ من الشمس والقمر والليل والنهار قدَّره الله تقديراً لا يتعدَّاه، وكلٌّ له سلطانٌ ووقتٌ، إذا وُجِدَ؛ عُدِمَ الآخرَ، ولهذا قال: {لا الشمسُ ينبغي لها أن تُدْرِكَ القمرَ}؛ أي: في سلطانِهِ الذي هو الليل؛ فلا يمكنُ أن توجدَ الشمسُ في الليل، {ولا الليلُ سابِقُ النهارِ}: فيدخُلُ عليه قبل انقضاءِ سلطانِهِ. {وكلٌّ}: من الشمس والقمر والنجوم {في فَلَكٍ يَسْبِحونَ}؛ أي: يترَّددون على الدوام؛ فكلُّ هذا دليلٌ ظاهرٌ وبرهانٌ باهرٌ على عظمة الخالقِ وعظمةِ أوصافِهِ، خصوصاً وصفَ القدرةِ والحكمةِ والعلم في هذا الموضع.
{40} Na kila moja yake: jua na mwezi, usiku na mchana vimepangwa na Mwenyezi Mungu kwa viwango ambavyo haviwezi kuvizidi, na kila kimoja kina mamlaka yake na wakati wake. Kinapokuwepo, hicho kingine kinakosa kuwepo.
Ndiyo maana akasema: "Haliwi jua kuufikia mwezi." Yaani, katika mamlaka yake ambayo ni usiku. Kwa hivyo, jua haliwezi kupatikana usiku, "wala usiku kuupita mchana" ukatokea kabla ya kumalizika kwa mamlaka yake. "Na vyote," yaani, jua, mwezi, na nyota, "vinaogelea katika njia zao" daima dawamu. Basi yote haya ni ushahidi wa wazi na hoja inayong'aa juu ya ukuu wa Muumba, na ukuu wa sifa zake, hasa sifa ya uwezo, hekima, na elimu katika mahali hapa.
{وَآيَةٌ لَهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ (41) وَخَلَقْنَا لَهُمْ مِنْ مِثْلِهِ مَا يَرْكَبُونَ (42) وَإِنْ نَشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنْقَذُونَ (43) إِلَّا رَحْمَةً مِنَّا وَمَتَاعًا إِلَى حِينٍ (44) وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّقُوا مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (45) وَمَا تَأْتِيهِمْ مِنْ آيَةٍ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ (46) وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنْفِقُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنُطْعِمُ مَنْ لَوْ يَشَاءُ اللَّهُ أَطْعَمَهُ إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (47) وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْوَعْدُ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (48) مَا يَنْظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ (49) فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَا إِلَى أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ (50)}.
41. Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuria zao katika jahazi lililosheheni. 42. Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda. 43. Na tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi. 44. Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda. 45.
Na wanapoambiwa: Jilindeni kutokana na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa... 46. Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa wao huwa ni wenye kuipa mgongo. 47.
Na wanapoambiwa: Toeni katika aliyokupeni Mwenyezi Mungu,
wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi hammo isipokuwa katika upotofu ulio dhahiri. 48.
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli? 49. Hawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana. 50. Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei.
#
{41} أي: ودليلٌ لهم وبرهانٌ على أنَّ اللهَ وحدَه المعبودُ؛ لأنَّه المنعِمُ بالنِّعم الصارف للنِّقم الذي من جملةِ نعمه {أنَّا حَمَلْنا ذُرِّيَّتَهم}: قال كثيرٌ من المفسِّرين: المرادُ بذلك آباؤهم.
{41} Na ushahidi kwao na hoja kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, kwa sababu Yeye ndiye Mneemeshaji wa neema zote, Mwenye kuepusha adhabu zote, ambaye miongoni mwa neema zake ni "kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao." Wengi katika wafasiri walisema kwamba hili linamaanisha baba zao.
#
{42} {وخَلَقْنا لهم}؛ أي: للموجودين من بعدِهم {من مثلِهِ}؛ أي: من مثل ذلك الفلك؛ أي: جنسه {ما يَرْكَبونَ}: به. فذكر نعمتَه على الآباء بِحَمْلِهِم في السفن؛ لأنَّ النعمة عليهم نعمةٌ على الذُّرِّيَّة.
وهذا الموضعُ من أشكل المواضع عليَّ في التفسير؛ فإنَّ ما ذَكَرَه كثيرٌ من المفسِّرين من أنَّ المرادَ بالذُّرِّيَّةِ الآباء مما لا يُعْهَدُ في القرآن إطلاقُ الذُّرِّيَّةِ على الآباء، بل فيه من الإبهام وإخراج الكلام عن موضوعِهِ ما يأباه كلامُ ربِّ العالمين وإرادتُه البيانَ والتوضيحَ لعبادِهِ. وثَمَّ احتمالٌ أحسنُ من هذا، وهو أنَّ المرادَ بالذُّرِّيَّةِ الجنسُ، وأنَّهم هم بأنفسهم؛ لأنَّهم هم من ذُرِّيَّةِ بني آدم، ولكن يَنْقُضُ هذا المعنى قوله: {وخَلَقْنا لهم من مثلِهِ ما يَرْكَبون}: إنْ أريدَ: وخَلَقْنا من مثل ذلك الفُلْك؛ أي: لهؤلاء المخاطبين ما يركبونَ من أنواع الفُلْك، فيكونُ ذلك تكريراً للمعنى تأباه فصاحةُ القرآن. فإنْ أريدَ بقوله: {وخَلَقْنا لهم من مثلِهِ ما يركبونَ}: الإبل التي هي سُفُن البرِّ؛ استقامَ المعنى واتَّضح؛ إلاَّ أنَّه يبقى أيضاً أن يكون الكلامُ فيه تشويشٌ؛ فإنَّه لو أُريد هذا المعنى؛ لقال: وآيةٌ لهم أنَّا حَمَلْناهم في الفُلْكِ المَشْحونِ وخَلَقْنا لهم من مثلِهِ ما يركبونَ، فأمَّا أنْ يُقالَ في الأول: حملنا ذريتهم، وفي الثاني: حملناهم؛ فإنَّه لا يظهرُ المعنى إلاَّ أنْ يقالَ: الضميرُ عائدٌ إلى الذُّرِّيَّةِ. والله أعلم بحقيقةِ الحال.
فلمَّا وصلتُ في الكتابة إلى هذا الموضع؛ ظهر لي معنى ليس ببعيدٍ من مرادِ الله تعالى، وذلك أنَّ مَنْ عَرَفَ جلالة كتابِ الله وبيانَه التامَّ من كلِّ وجهٍ للأمور الحاضرة والماضية والمستقبلةِ، وأنَّه يَذْكُرُ من كلِّ معنى أعلاه وأكمل ما يكون من أحوالِهِ، وكانت الفُلْكُ من آياته تعالى ونعمِهِ على عباده من حين أنعم عليهم بتعلُّمها إلى يوم القيامةِ، ولم تزلْ موجودةً في كلِّ زمان إلى زمانِ المواجَهين بالقرآن، فلمَّا خاطبهم الله تعالى بالقرآن، وذَكَرَ حالةَ الفُلك، وعَلِمَ تَعالى أنَّه سيكونُ أعظمُ آياتِ الفلكِ في غير وقتهم وفي غير زمانهم حين يُعَلِّمُهُم صنعةَ الفُلك البحريَّة الشراعيَّة منها والنّارية والجويَّة السابحة في الجوِّ كالطيور ونحوها والمراكبِ البريَّة ممَّا كانت الآيةُ العظمى فيه لم توجَدُ إلاَّ في الذُّرِّيَّةِ؛ نبَّه في الكتاب على أعلى نوع من أنواع آياتها، فقال: {وآيةٌ لهم أنَّا حَمَلْنا ذُرِّيَّتَهُمْ في الفُلْكِ المشحونِ}؛ أي: المملوء ركباناً وأمتعةً، فحملهم الله تعالى، ونجَّاهم بالأسباب التي علَّمهم اللهُ بها من الغرق.
{42} "Na tukawaumbia" hawa waliokuja baada yao "kutoka mfano wake;" yaani, mfano wa merikebu ile, "wanavyovipanda." Akawa ametaja neema yake juu ya baba zao kwa kuwabeba kwenye merikebu. Kwa sababu neema waliyopewa wao pia ni neema kwa dhuria zao. Mahali hapa ni mojawapo ya mahali pagumu sana kwangu katika kutafsiri. Kwa maana, yale waliyotaja wafasiri wengi kwamba kinachomaanishwa hapa na dhuria ati ni baba zao si jambo la kawaida katika Qur-ani, kutumia neno “dhuriya” kwa mababa. Bali, katika maana hiyo kuna utata, na kuyaondoa maneno kutoka katika mada yake, jambo ambalo linakataliwa na maneno ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, na makusudio yake ya kuwabainishia waja na kuwawekea mambo wazi. Kisha kuna uwezekano mwingine bora zaidi kuliko huu, ambao ni kwamba kinachomaanishwa hapa na dhuria ni jenasi yote, na kwamba walimaanishwa wao wenyewe. Kwa sababu wao ndio kizazi cha kibinadamu.
Lakini maana hii inapingwa na kauli yake: "Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda." Lakini ikiwa maana ya kauli yake, "Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda" ni ngamia ambao ndio merikebu za nchi kavu, basi maana hii ya jenasi inakuwa nyoofu na ya wazi kabisa. Walakini, maneno haya pia yanabaki kuwa ya kutatanisha. Kwani, ikiwa maana hii ingekuwa ndiyo iliyokusudiwa,
basi angesema: 'Na Ishara kwao ni kwamba tuliwabeba katika merikebu iliyosheheni, na tukawaumbia mfano wake wanavyovipanda.' Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi uhakika wa hali hii. Nilipofikia mahali hapa katika kuandika; nikadhihirikiwa na maana ambayo haiko mbali na yale aliyokusudia Mwenyezi Mungu. Nayo ni kwamba yule anayejua utukufu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maelezo yake kamili katika kila njia kinapoeleza mambo ya sasa, yaliyopita na yajayo, na kwamba katika kila maana anataja ile ambayo ni ya juu kabisa na iliyo kamilika kabisa, na pindi zilipokuwa merikebu ni miongoni mwa ishara zake, Mwenyezi Mungu Mtukufu, na neema zake juu ya waja wake tangu alipowaneemesha kwazo, kwa kuzisoma mpaka Siku ya Kiyama, na zimeendelea kuwepo wakati wote mpaka zama za wale walioongeleshwa na Qur-ani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alipozungumza nao kwa Qur-ani, na akataja hali ya merikebu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akajua kwamba hizo zitakuwa ishara kubwa zaidi merikebu zitakuja tokea katika zama zisizokuwa zao, pale atakapowafundisha kutengeneza merikebu mbalimbali zikiwemo zile za matanga, za moto, na za angani zinazokwenda angani kama ndege na vile vile vipando vya nchi kavu, ambazo ni ishara kubwa zaidi ambayo haikuwa isipokuwa wakati wa dhuria zao, akatanabahisha katika Kitabu chake juu ya aina miongoni mwa aina za ishara zake.
Akasema: "Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi iliyosheheni" wapandaji wengi na mizigo. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawabeba na akawaokoa kutokana na kuzama; kwa njia ambazo Mwenyezi Mungu aliwafundisha.
#
{43} ولهذا نبَّههم على نعمتِهِ عليهم حيث أنْجاهم من الغرقِ مع قدرتِهِ على ذلك، فقال: {وإن نشأ نُغْرِقْهم فلا صريخَ لهم}؛ أي: لا أحد يصرُخُ لهم فيعاوِنُهم على الشدَّة ولا يزيلُ عنهم المشقَّة، {ولا هم يُنقَذونَ}: مما هم فيه.
{43} Ndiyo maana aliwatanabahisha juu ya neema yake juu yao, ambapo aliwaokoa kutokana na kuzama majini pamoja na kwamba ana uwezo wa kufanya hivyo.
Akasema: "Na tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia," wala hawaokolewi kutokana na yale waliyomo.
#
{44} {إلاَّ رحمةً مِنَّا ومتاعاً إلى حينٍ}: حيث لم نُغْرِقْهم لطفاً بهم وتمتيعاً لهم إلى حينٍ، لعلَّهم يرجِعونَ، أو يستدرِكون ما فَرَطَ منهم.
{44} "Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda," ambapo hatukuwazamisha kwa sababu ya upole wake na kuwastarehesha tu kwa muda; huenda wakarejea au wakatenda yale waliyopuuza kufanya.
#
{45} {وإذا قيل لهمُ اتَّقوا ما بَيْنَ أيديكم وما خَلْفَكُم}؛ أي: من أحوال البرزخ والقيامةِ وما في الدُّنيا من العقوبات؛ {لعلَّكُم تُرْحَمونَ}: أعرضوا عن ذلك، فلم يرفعوا به رأساً، ولو جاءَتْهم كلُّ آيةٍ.
{45} "Na wanapoambiwa: Jilindeni na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu." Yaani, wajilinde kutokana na hali ya maisha ya kaburini, Kiyama, na adhabu iliyoko duniani; "ili mpate kurehemewa." Wao wanalipa hilo mgongo na kutolijali kabisa, hata kama zitawajia Ishara zote.
#
{46} ولهذا قال: {وما تأتيهم مِن آيةٍ مِن آياتِ ربِّهم إلاَّ كانوا عنها معرضينَ}: وفي إضافة الآياتِ إلى ربِّهم دليلٌ على كمالها ووضوحِها؛ لأنَّه ما أبين من آياتِ اللَّه ولا أعظم بياناً، وإنَّ من جملة تربيةِ الله لعبادِهِ أنْ أوصلَ إليهم الآياتِ التي يستدلُّون بها على ما ينفعُهم في دينهم ودنياهم.
{46} Ndiyo maana akasema: "Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza." Na katika kufungamanisha ishara na Mola wao Mlezi kuna ushahidi juu ya ukamilifu na ubainifu wake. Kwa sababu hakuna ishara zilizo wazi na bainifu zaidi kuliko ishara za Mwenyezi Mungu, na kwamba miongoni mwa jumla ya malezi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kuwa aliwafikishia ishara ambazo kwazo wanaweza kuzitumia kuwa ushahidi juu ya yale yenye kuwafaa katika dini yao na dunia yao.
#
{47} {وإذا قيلَ لهم أنفِقوا ممَّا رَزَقَكُمُ اللهُ}؛ أي: من الرزق الذي مَنَّ به اللهُ عليكم، ولو شاء لَسَلَبَكُم إيَّاه، {قالَ الذين كَفَروا للذين آمنوا}: معارضينَ للحقِّ محتجِّين بالمشيئةِ: {أنُطْعِمُ مَن لو يشاءُ الله أطْعَمَهُ إنْ أنتُم}: أيها المؤمنون، لفي {ضلالٍ مبينٍ}: حيث تأمروننا بذلك، وهذا مما يدلُّ على جهلهم العظيم أو تجاهُلِهِم الوخيم؛ فإنَّ المشيئة ليست حجَّةً لعاصٍ أبداً؛ فإنَّه وإنْ كان ما شاءَ اللهُ كان، وما لم يشأ لم يكنْ؛ فإنَّه تعالى مَكَّنَ العبادَ وأعطاهم من القوَّةِ ما يقدرون على فعل الأمرِ واجتنابِ النَّهْي؛ فإذا تَرَكوا ما أمِروا به؛ كان ذلك اختياراً منهم لا جبراً لهم وقهراً.
{47} "Na wanapoambiwa: Toeni katika vile alivyokupeni Mwenyezi Mungu." kwani angelitaka, angelikunyang'anyeni "wale waliokufuru huwaambia wale walioamini" huku wakiipinga haki na kutumia mipango ya Mwenyezi Mungu kuwa ni ushahidi wa kutofanya hivyo. "Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa, angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi" waumini "hammo ila katika upotofu ulio dhahiri" kwa maana mnaamrisha hilo. Na hili ni katika mambo yanayoonyesha ujinga wao mkubwa na upumbavu. Kwa maana, mipango ya Mwenyezi Mungu kamwe haifai kuwa ndiyo hoja ya mwenye kutenda maasia, kwani hata kile ambacho Mwenyezi Mungu anataka kinakuwa, na asichotaka hakiwi, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwawezesha waja wake na kuwapa nguvu ambazo kwazo wanaweza kufanya maamrisho na kujiepusha na makatazo. Kwa hivyo, wanapoacha yale waliyoamrishwa; hilo linakuwa kwa sababu ya chaguo lao, siyo kwamba walilazimishwa.
#
{48 - 49} {ويقولون}: على وجه التكذيب والاستعجال: {متى هذا الوعدُ إن كُنتُم صادقينَ}. قال الله تعالى: لا يستبعدوا ذلك؛ فإنَّه عن قريبٍ، {ما ينظُرونَ إلاَّ صَيْحَةً واحدةً}: وهي نفخةُ الصور. {تأخُذُهم}؛ أي: تصيبُهم {وهم يَخِصِّمونَ}؛ أي: وهم لاهون عنها، لم تخطُرْ على قلوبِهِم في حال خصومَتِهم وتشاجُرِهم بينَهم، الذي لا يوجد في الغالب إلاَّ وقتَ الغفلة.
{48 - 49} "Na wanasema" kwa njia ya kukadhibisha na pupa: "Ahadi hii itatokea lini,
ikiwa nyinyi ni wakweli?" Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Wasione kwamba hilo haliwezekani; kwani hivi karibuni, "Hawangojei ila ukelele mmoja tu" ambao ni kule kupuliza katika Baragumu "utakaowachukua nao wamo kuzozana" wanafanya mchezo tu, na wala hilo halikupita mioyoni mwao wanapozozana na kubishana.
#
{50} وإذا أخذتُهم وقتَ غفلَتِهِم؛ فإنَّهم لا يُنظرونَ ولا يُمهلون؛ {فلا يستطيعون توصيةً}؛ أي: لا قليلة ولا كثيرة، {ولا إلى أهْلِهِم يَرْجِعونَ}.
{50} Na ukiwakamata wakati wameghafilika, basi hawatapewa muhula "Basi hawataweza kuusia;" yaani, kwa uchache wala kwa wingi, "wala kwa watu wao hawatarejea."
{وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَإِذَا هُمْ مِنَ الْأَجْدَاثِ إِلَى رَبِّهِمْ يَنْسِلُونَ (51) قَالُوا يَاوَيْلَنَا مَنْ بَعَثَنَا مِنْ مَرْقَدِنَا هَذَا مَا وَعَدَ الرَّحْمَنُ وَصَدَقَ الْمُرْسَلُونَ (52) إِنْ كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَدَيْنَا مُحْضَرُونَ (53) فَالْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (54)}.
51. Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. 52.
Watasema: Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume. 53. Haitakuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu. 54. Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
#
{51} النفخة الأولى هي نفخةُ الفزع والموت. وهذه نفخةُ البعثِ والنشور؛ فإذا نُفِخَ في الصور؛ خرجوا {من الأجداث} والقبور {يَنْسِلون} إلى ربِّهم؛ أي: يسرعون للحضور بين يديه، لا يتمكَّنونَ من التأنِّي والتأخُّر.
{51} Kupulizwa kwa kwanza katika baragumu kutakuwa kwa ajili ya kutia mahangaiko kwa viumbe na kuwafisha. Lakini kupuliza huku kwa pili, ni kule kwa kuwafufua na kuwatawanya kutoka makaburini mwao. Basi itakapopulizwa katika baragumu, watatoka "makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi." Na wala hawataweza kungoja wala kuchelewa.
#
{52} وفي تلك الحال يحزنُ المكذِّبون ويُظْهِرونَ الحسرةَ والندم ويقولون: {يا وَيْلَنا مَن بَعَثَنا مِن مَرْقَدِنا}؛ أي: من رقدتنا في القبور؛ لأنه ورد في بعض الأحاديث أنَّ لأهل القبور رقدةٌ قبيل النفخ في الصور. فيُجابون ويُقال لهم: {هذا ما وَعَدَ الرحمنُ وَصَدَقَ المرسلونَ}؛ أي: هذا الذي وعدكم اللَّه به ووعدتْكم به الرسلُ، فظهر صدقُهم رأي عينٍ. ولا تَحْسَبْ أنَّ ذكر الرحمن في هذا الموضع لمجرَّدِ الخبر عن وعدِهِ، وإنَّما ذلك للإخبار بأنَّه في ذلك اليوم العظيم سَيَرَوْنَ من رحمتِهِ ما لا يخطُرُ على الظُّنون ولا حَسَبَ به الحاسبون؛ كقوله: {المُلْكُ يومئذٍ الحقُّ للرحمن}، {وخَشَعَتِ الأصواتُ للرحمنِ}، ونحو ذلك مما يَذْكُرُ اسمَه الرحمن في هذا.
{52} Katika hali hiyo wale waliokadhibisha watahuzunika na kujuta,
na watasema: "Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu?" Yaani, jumo makaburini. Kwa sababu ilisimuliwa katika baadhi ya hadithi kwamba watu wa makaburini watalala kulala fulani muda mfupi tu kabla ya kupulizwa katika baragumu.
Wataitikiwa na waambiwe: "Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume." Na leo yamekuwa kweli mnayaona kwa macho. Wala usidhani kuwa kutajwa kwa Mwingi wa Rehema mahali hapa ni kujulisha tu kuhusu ile ahadi yake. Bali ni kufahamisha kwamba siku hiyo kuu wataona rehema yake kwa namna ambayo haikuwahi kuwapitia akilini mwao wala wenye kutarajia hawakuwahi kutarajia.
Kama vile kauli yake: "Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman
(Mwingi wa Rehema)." Na kauli yake, "Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani Mwingi wa Rahema." Na mfano wa hayo ambapo jina lake 'Arrahmani
(Mwingi wa rehema)' limetajwa.
#
{53} {إن كانت}: البعثة من القبور {إلاَّ صيحةً واحدةً}: يَنْفُخُ فيها إسرافيلُ في الصور، فتحيا الأجساد؛ {فإذا هم جميعٌ لَدَيْنا مُحْضَرونَ}: الأولون والآخرون، والإنس والجن؛ ليحاسبوا على أعمالهم.
{53} "Haitakuwa" kufufuliwa kutoka makaburini "isipokuwa ukelele mmoja tu" alioupuliza Israfil katika baragumu, na miili ikafufuka. "Mara wote watahudhuruishwa mbele yetu;" wa mwanzo na wa mwisho, watu na majini. Kisha watafanyiwa hesabu kwa matendo yao.
#
{54} {فاليومَ لا تُظْلَمُ نفسٌ شيئاً}: لا يُنْقَصُ من حسناتها ولا يُزاد في سيئاتها. {ولا تُجْزَوْنَ إلاَّ ما كنتُم تعملونَ}: من خيرٍ أو شرٍّ؛ فمن وَجَدَ خيراً؛ فليحمد الله، ومن وَجَدَ غير ذلك؛ فلا يلومنَّ إلاَّ نفسه.
{54} "Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu." Mema yake hayatapunguzwa kitu wala maovu yake hayataongezwa chochote. "Wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda" ya heri na maovu. Basi mwenye kupataya ya heri, basi na amsifu Mwenyezi Mungu. Na mwenye kupata yasiyokuwa hayo, basi kamwe asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe tu.
{إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ (55) هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ (56) لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُمْ مَا يَدَّعُونَ (57) سَلَامٌ قَوْلًا مِنْ رَبٍّ رَحِيمٍ (58)}.
55. Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. 56. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya kifahari. 57. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka. 58. "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu.
#
{55 - 56} لما ذكر تعالى أنَّ كلَّ أحدٍ لا يُجْزى إلاَّ ما عَمِلَه؛ ذَكَرَ جزاء الفريقينِ، فبدأ بجزاء أهل الجنة، وأخبر أنَّهم في ذلك اليوم {في شُغُلٍ فاكهونَ}؛ أي: في شُغُل مُفَكِّهٍ للنفس مُلِذٍّ لها من كلِّ ما تهواه النفوس وتَلَذُّه العيون ويتمنَّاه المتمنُّون، ومن ذلك افتضاض العذارى الجميلات؛ كما قال: {هم وأزواجُهُم}: من الحور العين اللاَّتي قد جَمَعْنَ حسنَ الوجوهِ والأبدان وحسنَ الأخلاق {في ظلال على الأرائِكِ}؛ أي: السرر المزيَّنة باللباس المزخْرَفِ الحسن {متَّكِئونَ}: عليها اتِّكاءً دالاً على كمال الراحة والطمأنينة واللذة.
{55 - 56} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba kila mtu hatalipwa ila kwa aliyoyatenda,akataja malipo ya makundi hayo mawili, na akaanza na malipo ya watu wa Peponi. Akajulisha kwamba siku hiyo watakuwa “shughulini, wamefurahi" kwa sababu ya kila kitu ambacho nafsi inakitamani, na macho yanakipenda, na yale yanayotamaniwa na wanaoyatamani, na hayo ni pamoja na kuingiliana na wanawali warembo.
Kama alivyosema: "Wao na wake zao" miongoni mwa hurulaini waliojumuisha kati ya nyuso na miili mizuri na maadili bora "wamo katika vivuli juu ya viti vya fahari" vilivyopambwa kwa mavazi mazuri ya urembo, "wameegemea" juu yake kuegemea kunakoashiria raha kamili, utulivu na ladha.
#
{57} {لهم فيها فاكهةٌ}: كثيرة من جميع أنواع الثمارِ اللذيذة؛ من عنب، وتين، ورمان، وغيرها، {ولهم ما يَدَّعونَ}؛ أي: يطلبون؛ فمهما طلبوه وتمنَّوْه؛ أدْرَكوه.
{57} "Watapata humo kila aina ya matunda" matamu, kama vile zabibu, tini, makomamanga na mengineyo." Na watapata kila watakachokitaka."
#
{58} ولهم أيضاً {سلامٌ} حاصلٌ لهم {من ربٍّ رحيم}: ففي هذا كلام الربِّ تعالى لأهل الجنةِ وسلامُهُ عليهم، وأكَّده بقولِهِ: {قولاً}: وإذا سَلَّم عليهم الربُّ الرحيمُ؛ حَصَلَتْ لهم السلامةُ التامةُ من جميع الوجوه، وحَصَلَتْ لهم التحيةُ التي لا تَحِيَّةَ أعلى منها ولا نعيم مثلها؛ فما ظنُّك بتحيَّة ملك الملوك، الربِّ العظيم، الرءوف الرحيم، لأهل دار كرامته، الذين أحلَّ عليهم رضوانَه؛ فلا يسخط عليهم أبداً؛ فلولا أنَّ الله تعالى قَدَّرَ أنْ لا يموتوا أو تزولَ قلوبُهم عن أماكنها من الفرح والبهجة والسرور؛ لحصل ذلك، فنرجو ربَّنا أن لا يَحْرمَنا ذلك النعيم، وأن يُمَتِّعَنا بالنظر إلى وجهه الكريم.
{58} Na pia humo wakapata "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. Katika hili kuna ushahidi kwamba Mola Mlezi atawaongelesha watu wa Peponi na kuwapa salamu. Na alilisisitiza hilo kwa maneno yake, "kauli." Kwani Mola Mlezi, Mwingi wa Rehema atakapowasalimia, watapata usalama kamili katika nyanja zote na watapata maamkizi ambayo hakuna maamkizi ya juu zaidi yake wala neema mfano wake. Basi unadhania nini salamu ya Mfalme wa wafalme wote, Mola Mlezi Mkuu, Mpole, Mwingi wa kurehemu kwa watu wa makao yake ya heshima, ambao aliwaridhia, na wala kamwe hatawakasirikia. Na lau si kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamuru kwamba hawatakufa wala mioyo yao haitatoka katika nafasi zake za furaha kubwa, basi hilo lingetokea. Basi tunamuomba Mola wetu Mlezi asitunyime neema hiyo, na atufurahishe kwa kuutazama uso wake mtukufu.
{وَامْتَازُوا الْيَوْمَ أَيُّهَا الْمُجْرِمُونَ (59) أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَابَنِي آدَمَ أَنْ لَا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ (60) وَأَنِ اعْبُدُونِي هَذَا صِرَاطٌ مُسْتَقِيمٌ (61) وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنْكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا أَفَلَمْ تَكُونُوا تَعْقِلُونَ (62) هَذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي كُنْتُمْ تُوعَدُونَ (63) اصْلَوْهَا الْيَوْمَ بِمَا كُنْتُمْ تَكْفُرُونَ (64) الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَى أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (65) وَلَوْ نَشَاءُ لَطَمَسْنَا عَلَى أَعْيُنِهِمْ فَاسْتَبَقُوا الصِّرَاطَ فَأَنَّى يُبْصِرُونَ (66) وَلَوْ نَشَاءُ لَمَسَخْنَاهُمْ عَلَى مَكَانَتِهِمْ فَمَا اسْتَطَاعُوا مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ (67)}.
59. Na enyi wakosefu! Jitengeni leo! 60. Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu. 62. Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo njia iliyonyooka. 62. Na bila ya shaka yeye amekwishalipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? 63. Hii basi ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa. 64. Ingieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru. 65. Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma. 66. Na tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje? 67. Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi.
#
{59} لمَّا ذَكَرَ تعالى جزاء المتَّقين؛ ذَكَرَ جزاء المجرمين، {و} أنَّهم يُقال لهم يوم القيامةِ: {امْتازوا اليومَ أيُّها المجرمونَ}؛ أي: تميَّزوا عن المؤمنين، وكونوا على حِدَةٍ؛ ليوبِّخَهم ويُقَرِّعَهم على رؤوس الأشهادِ قبلَ أن يُدْخِلَهُمُ النار، فيقول لهم:
{59} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja malipo ya watu wema, akataja adhabu za wahalifu,
"na" kwamba wataambiwa Siku ya Kiyama: "Enyi wakosefu! Jitengeni leo!" Mbali na Waumini na muwe peke yenu; ili awakemee na kuwakaripia mbele ya viumbe vyote vikiwaona kabla ya kuwaingiza Motoni.
Atawaambia:
#
{60} {ألمْ أعْهَدْ إليكُم}؛ أي: آمرُكُم وأوصيكم على ألسنةِ رُسُلي وأقول لكم: {يا بَني آدمَ أن لا تَعْبُدوا الشيطانَ}؛ أي: لا تطيعوه! وهذا التوبيخ يدخل فيه التوبيخُ عن جميع أنواع الكفرِ والمعاصي؛ لأنَّها كلها طاعةٌ للشيطان وعبادةٌ له، {إنَّه لكم عدوٌّ مُبينٌ}: فحذَّرتكم منه غايةَ التَّحذير، وأنذرتُكم عن طاعتِهِ، وأخبرتُكم بما يدعوكم إليه.
{60} "Je, sikuagana nanyi," Yaani, sikuwaamrisheni na kuwausia kupitia ndimi za Mitume wangu, "na nikakuambieni enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani?" Yaani, msimtii! Karipio hili linajumuisha kukemea aina zote za ukafiri na maasia; kwa sababu yote hayo ni utiifu kwa Shetani na kumuabudu. "Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu," nikawa nimekuhadharisheni juu yake kwa tahadharisho kubwa kabisa, na nikakuonyeni juu ya kumtii, na nikakujulisheni yale anayowaitia.
#
{61} {و} أمرتُكم: أنْ تعبدوني بامتثال أوامري وترك زَواجِري. {هذا}؛ أي: عبادتي وطاعتي ومعصية الشيطان {صراطٌ مستقيمٌ}: فعُلوم الصراط المستقيم وأعمالُهُ ترجعُ إلى هذين الأمرين؛ أي: فلم تَحْفَظوا عهدي ولم تَعْمَلوا بوصِيَّتي، فواليتُم عدوَّكم.
{61} "Na" nikakuamrisheni kwamba mniabudu mimi kwa kutekeleza amri zangu na kuacha makatazo yangu. "Hii;" yaani, kuniabudu huku, kunitii, na kumuasi Shetani "ndiyo njia iliyonyooka." Na mambo yote yanayohusiana na njia iliyonyooka na matendo yake yanarudi kwa mambo mawili haya. Lakini nyinyi hamkushika agano langu wala hamkufanya kulingana na wasia wangu kwenu, bali mlifanya urafiki na adui yenu.
#
{62} فأضلَّ {منكم جِبِلاًّ كثيراً}؛ أي: خلقاً كثيراً. {أفلم تكونوا تعقلونَ}؛ أي: أفلا كان لكم عقلٌ يأمُرُكم بموالاة ربِّكم ووليِّكم الحقِّ، ويزجركم عن اتِّخاذ أعدى الأعداءِ لكم وليًّا؟ فلو كان لكم عقلٌ صحيحٌ؛ لما فعلتُم ذلك.
62. Basi akalipoteza "kundi kubwa miongoni mwenu." "Je, hamkuwa mkifikiri?" Yaani, je, hamkuwa na akili inayokuamrisheni kumfanya Mola wenu Mlezi kuwa kipenzi, na kushikamana na haki, na akili hiyo ikakukemeeni kumfanya adui wenu mkubwa kuwa ndiye kipenzi chenu? Basi, ikiwa mngekuwa na akili timamu; kwa nini mlifanya hivyo?
#
{63} فإذْ أطعتُم الشيطان، وعاديتُم الرحمن، وكذَّبتم بلقائِهِ، ووردتُم القيامةَ دار الجزاء، وحقَّ عليكم القولُ بالعذاب، فَـ {هذه جهنَّمُ التي كنتُم توعَدونَ}: وتكذِّبون بها؛ فانظروا إليها عياناً! فهناك تنزعِجُ منهم القلوبُ، وتزوغُ الأبصارُ، ويحصُلُ الفزعُ الأكبرُ.
{63} Basi mlipomtii Shetani, na mkamfanyia uadui Mwingi wa Rehema, na mkakadhibisha kukutana naye, na mkataka Kiyama ambayo ndiyo nyumba ya malipo, na likawa juu yenu neno la adhabu, basi "hii ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa" nanyi mkaikadhibisha. Basi iangalieni kwa macho yenu wenyewe! Hapo, mioyo yao itafadhaika, nayo macho yao yatakodoka, na watakuwa na hofu kubwa sana.
#
{64} ثم يُكْمِلُ ذلك بأنْ يُؤْمَرَ بهم إلى النار، ويقالَ لهم: {اصْلَوْها اليوم بما كنتُم تكفُرونَ}؛ أي: ادخُلوها على وجه تَصْلاكُم، ويحيطُ بكم حرُّها، ويبلغُ منكم كلَّ مبلغ بسبب كفرِكُم بآيات الله وتكذيبِكُم لرسل الله.
{64} Kisha haya yatakamilishwa kwa kuamrishwa kwamba waingie Motoni.
Wataambiwa: "Ingieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru." Humo, joto lake litawazunguka, na makali yake yatawafikia kila ncha kwa sababu ya kuzikataa kwenu ishara za Mwenyezi Mungu na kukadhibisha kwenu Mitume wa Mwenyezi Mungu.
#
{65} قال تعالى في بيان وَصْفِهم الفظيع في دار الشقاء: {اليوم نَخْتِمُ على أفواهِهِم}: بأن نَجْعَلَهم خُرْساً فلا يتكلمون، فلا يقدِرونَ على إنكارِ ما عَمِلوه من الكُفْرِ والتَّكْذيب. {وتُكَلِّمُنا أيْديهم وتَشْهَدُ أرجُلُهم بما كانوا يَكْسِبونَ}؛ أي: تشهد عليهم أعضاؤُهم بما عملوه، ويُنْطِقُها الذي أنطقَ كلَّ شيءٍ.
{65} Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuelezea hali yao ya kutisha katika nyumba ya dhiki: "Leo tunaviziba vinywa vyao" kwa kuwafanya mabubu wasiweze kusema kitu, ili wasiweze kukataa yale waliyofanya miongoni mwa ukafiri na ukadhibishaji. "Na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyachuma." Hivyo vyote vitatamkishwa na yule aliyevitamkisha vitu vyote.
#
{66} {ولو نشاءُ لَطَمَسْنا على أعيُنِهم}: بأن نُذْهِبَ أبصارَهم كما طَمَسْنا على نُطْقِهِم؛ {فاسْتَبَقوا الصراطَ}؛ أي: فبادروا إليه؛ لأنَّه الطريق إلى الوصول إلى الجنة. {فأنَّى يُبْصِرونَ}: وقد طُمِسَتْ أبصارُهم؟!
{66} "Na tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao," kwa kuwaondolea macho yao kama tulivyoondoa kuongea kwao "wakawa wanaiwania njia" wakiikimbilia; kwa sababu ndiyo njia inayofikisha Peponi. "Lakini wangeionaje" ilhali macho yao yameshaondolewa?
#
{67} {ولو نشاءُ لَمَسَخْناهم على مَكانَتِهِم}؛ أي: لأذْهَبْنا حَرَكَتَهم، {فما استطاعوا مُضِيًّا}: إلى الأمام، {ولا يرجِعونَ}: إلى ورائِهِم، ليبعدُوا عن النار.
والمعنى: أنَّ هؤلاء الكفار حقَّتْ عليهم كلمةُ العذاب، ولم يكن بدٌّ من عقابهم، وفي ذلك الموطن ما ثَمَّ إلاَّ النار قد بُرِّزَتْ، وليس لأحدٍ نجاةٌ إلا بالعبور على الصراط، وهذا لا يستطيعه إلاَّ أهلُ الإيمان الذين يمشونَ في نورِهِم، وأمَّا هؤلاء؛ فليس لهم عند الله عهدٌ في النجاة من النار؛ فإنْ شاء؛ طمس أعْيُنَهم، وأبقى حَرَكَتَهم فلم يَهْتَدوا إلى الصراطِ لو اسْتَبَقوا إليه وبادروه، وإن شاء؛ أذهبَ حِراكهم فلم يَسْتَطيعوا التقدُّم ولا التأخُّر، المقصودُ أنَّهم لا يَعْبُرونه، فلا تحصُلُ لهم النجاةُ.
{67} "Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi" nyuma, ili wawe mbali na Moto. Maana yake ni kwamba hawa makafiri lilikwisha wadhibitikia neno la adhabu, na ikabidi waadhibiwe. Na mahali hapo hapatakuwa isipokuwa Moto uliodhihirishwa, ambao hakuna atakayeweza kuokoa isipokuwa kwa kuvuka kupitia juu Sirat
(njia iliyoko juu ya Moto), jambo ambalo hawaliwezi isipokuwa watu wa imani ambao wanatembelea katika nuru yao. Ama hawa, hawana agano lolote kwa Mwenyezi Mungu kwamba wataokoka kutokana na Moto. Akitaka, atayafutilia mbali macho yao na akaacha watembee, kwa hivyo wasiweze kuifikia Njia iliyonyooka hata kama wataiwania na kuikimbilia. Na akitaka, anaondoa harakati zao, kwa hivyo wasiweze kwenda mbele wala nyuma. Na maana ya haya ni kwamba hawakuweza kuivuka njia hiyo, kwa hivyo, kamwe hawataokoka.
{وَمَنْ نُعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِي الْخَلْقِ أَفَلَا يَعْقِلُونَ (68)}.
68. Na tunayemzeesha, tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii?
#
{68} يقولُ تعالى: {ومَن نُعَمِّرْهُ}: من بني آدم {نُنَكِّسْه في الخَلْقِ}؛ أي: يعود إلى الحالة التي ابتدأ منها؛ حالة الضعف؛ ضعف العقل وضعف القوة. {أفلا يعقلونَ}: أنَّ الآدميَّ ناقصٌ من كلِّ وجه، فيتداركوا قوتهم وعقولَهم، فيستَعْمِلونها في طاعة ربِّهم؟
{68} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tunayemzeesha" miongoni mwa wanadamu "tunamrudisha nyuma katika umbo," akarudi namna alivyoanza katika hali ya udhaifu wa kiakili na udhaifu wa nguvu. "Basi je, hawazingatii" kwamba wanadamu ni wapungufu kwa namna zote, kwa hivyo wakazitumia vyema nguvu zao na akili zao katika kumtii Mola wao Mlezi?
{وَمَا عَلَّمْنَاهُ الشِّعْرَ وَمَا يَنْبَغِي لَهُ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْآنٌ مُبِينٌ (69) لِيُنْذِرَ مَنْ كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ الْقَوْلُ عَلَى الْكَافِرِينَ (70)}.
69. Wala hatukumfundisha
(Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu isipokuwa ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha. 70. Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.
#
{69} ينزِّه تعالى نبيَّه محمداً - صلى الله عليه وسلم - عمَّا رماه به المشركون من أنَّه شاعرٌ، وأنَّ الذي جاء به شعرٌ، فقال: {وما علَّمناه الشعرَ وما يَنبَغي له}: أن يكون شاعراً؛ أي: هذا من جنس المحال أن يكون شاعراً؛ لأنَّه رشيدٌ مهتدٍ، والشعراء غاوون، يتَّبِعُهُم الغاوون، ولأنَّ الله تعالى حَسَمَ جميع الشُّبه التي يتعلَّق بها الضالُّون عن رسوله، فحسم أن يكون يكتبُ أو يقرأ، وأخبر أنَّه ما علَّمه الشعر وما ينبغي له.
{إنْ هو إلاَّ ذِكْرٌ وقرآنٌ مبينٌ}؛ أي: ما هذا الذي جاء به إلاَّ ذكرٌ يتذكَّر به أولو الألباب جميع المطالب الدينيَّة؛ فهو مشتملٌ عليها أتمَّ اشتمال، وهو يذكِّرُ العقولَ ما رَكَزَ اللَّهُ في فِطَرِها من الأمر بكلِّ حسنٍ والنهي عن كلِّ قبيح. {وقرآنٌ مُبينٌ}؛ أي: مبينٌ لما يُطْلَبُ بيانُه، ولهذا حذف المعمولَ؛ ليدلَّ على أنَّه مبينٌ لجميع الحقِّ بأدلَّته التفصيليَّة والإجماليَّة والباطل وأدلَّة بطلانِهِ. أنزله الله كذلك على رسولِهِ.
{69} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamtakasa Nabii wake Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mbali na walivyomsingizia washirikina kuwa yeye ni mtunzi wa mashairi, na kwamba hayo aliyokuja nayo ni mashairi tu.
Akasema: "Wala hatukumfundisha
(Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo," kwamba awe mtunga mashairi. Haiwezekani! Kwa sababu yeye ni mwenye hekima, mwongofu, ilhali washairi wamepotea, na wanawafuata wapotevu.Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alivunjilia mbali kila tuhuma ambazo wanazishikilia wale waliopotea mbali na Mtume wake. Alivunjilia mbali uwezekano kwamba yeye ndiye aliyeiandika au kuisoma kutoka kwingine. Kwa hivyo, akajulisha kwamba hakumfundisha ushairi na wala haimfailii kufanya hivyo. "Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha," ambayo kwayo watu wenye akili watakumbuka matakwa yote ya kidini. Kwani inajumuisha hayo yote kwa njia kamilifu zaidi. Na inazikumbusha akili juu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka katika maumbile yao ya asili ya kuamrisha kila jema, na kukataza kila ovu. "Qur-ani inayobainisha" yale yanayohitajika kubainishwa. Na ndiyo maana akafuta kinachobainishwa ili hilo lionyeshe kwamba inabainisha haki yote kwa ushahidi wake wa kina na wa jumla, na pia inabainisha batili na ushahidi wa ubatilifu wake. Mwenyezi Mungu aliiteremsha hivyo kwa Mtume wake.
#
{70} {لِيُنذِرَ مَن كان حَيًّا}؛ أي: حيَّ القلب واعِيَه؛ فهو الذي يزكو على هذا القرآن، وهو الذي يزداد من العلم منه والعمل، ويكون القرآنُ لقلبِهِ بمنزلة المطرِ للأرض الطيِّبة الزاكية، {ويَحِقَّ القولُ على الكافرينَ}: لأنَّهم قامت عليهم به حُجَّةُ الله وانقطع احتجاجُهم، فلم يبقَ لهم أدنى عذرٍ وشبهةٍ يُدلون بها.
{70} "Ili imwonye aliye hai" moyoni, na anayeifahamu. Huyo ndiye anayetakasika kwa Qur-ani hii, na ndiye anayezidi kuwa na elimu na matendo kutokana nayo. Na Qur-ani kwa moyo wake inakuwa kama ilivyo mvua kwa ardhi nzuri, safi. "Na neno litimie juu ya makafiri," kwa kuwa kwayo hoja ya Mwenyezi Mungu ilisimama juu yao, na upinzani wao ukakatika. Basi hawakubakia na udhuru wowote hata mdogo vipi, wala fikira yenye mchanganyiko wanayoweza kuitumia kama ushahidi.
{أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُمْ مِمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ (71) وَذَلَّلْنَاهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ (72) وَلَهُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَمَشَارِبُ أَفَلَا يَشْكُرُونَ (73)}.
71. Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki. 72. Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala. 73. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
#
{71 - 73} يأمُرُ تعالى العباد بالنظر إلى ما سَخَّر لهم من الأنعام وذلَّلها وجَعَلَهم مالكينَ لها مطاوعةً لهم في كلِّ أمرٍ يريدونَه منها، وأنَّه جعل لهم فيها منافعَ كثيرةً من حَمْلِهم وحَمْل أثقالِهِم ومحامِلِهم وأمْتِعَتِهم من محلٍّ إلى محلٍّ، ومن أكْلِهِم منها، وفيها دفءٌ، ومن أوبارِها وأصوافها وأشعارِها أثاثاً ومتاعاً إلى حينٍ، وفيها زينةٌ وجمالٌ وغيرُ ذلك من المنافع المشاهدة منها. {أفلا يشكرونَ} اللهَ تعالى الذي أنعم بهذه النعم، ويخلِصونَ له العبادةَ، ولا يتمتَّعون بها تمتُّعاً خالياً من العبرة والفكرة؟!
{71 - 73} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake kutazama mifugo aliyowatiishia na kuwadhalilishia, na akawafanya kuwamiliki, wakiwatii katika kila jambo wanalolitaka kutoka kwao. Na kwamba aliweka manufaa mengi ndani yao, kama vile kuwabeba na kuibeba mizigo yao na bidhaa zao kutoka sehemu moja hadi nyingine, na pia kuwala baadhi yao, na pia wanapata joto kutoka kwao. Pia kutokana na sufu zao, manyoya yao, na nywele zao wanapata vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda. "Basi je, hawashukuru" Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyeneemesha kwa neema hizi, na wakamfanyia ibada kwa kumkusudia yeye tu, na wala wasizifurahie tu bila ya kuzingatia na kutafakari?
{وَاتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ آلِهَةً لَعَلَّهُمْ يُنْصَرُونَ (74) لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُنْدٌ مُحْضَرُونَ (75)}.
74. Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa! 75. Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakaohudhurishwa.
#
{74 - 75} هذا بيانٌ لبطلان آلهة المشركين التي اتَّخذوها مع الله تعالى ورَجَوْا نَصْرَها وشَفْعَها؛ فإنها في غاية العجز. {لا يَسْتَطيعون نَصْرَهم}: ولا أنْفُسَهم يَنْصُرونَ: فإذا كانوا لا يستطيعون نَصْرَهم؛ فكيف يَنْصُرونَهم؟! والنصر له شرطانِ: الاستطاعةُ [والقدرةُ] ؛ فإذا استطاع: يبقى: هل يُريدُ نصرةً مِنْ عَبْدِه أم لا؟ فنفي الاستطاعةِ ينفي الأمرين كليهما. {وهم لهم جُندٌ محضَرون}؛ أي: محضَرون هم وهم في العذاب، ومتبرِّئٌ بعضُهم من بعض، أفلا تبرؤوا في الدنيا من عبادة هؤلاء وأخلصوا العبادةَ للذي بيدِهِ الملكُ والنفعُ والضرُّ والعطاءُ والمنعُ وهو الوليُّ النصيرُ؟!
{74 - 75} Huu ni ufafanuzi wa ubatili wa miungu ya washirikina, waliyoichukua kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ambao walikuwa wakitaraji msaada kutoka kwao na uombezi. Hao kwa hakika, hawana uwezo kabisa. "Hawataweza kuwasaidia," wala wenyewe hawawezi kujinusuru. Na ikiwa hawawezi kuwasaidia, basi watawezaje kuwanusuru? Kuna masharti mawili ya kunusuru, nayo ni uwezo
[na nguvu]. Kwa hivyo, ikiwa anaweza,
basi inabakia kwamba: Je, anataka msaada kutoka kwa mja wake au la? Na kukanusha uwezo ni kukanusha mambo yote hayo mawili. "Bali hao ndio watakuwa askari wao watakaohudhurishwa." Yaani, wote wawili watahudhurishwa katika adhabu, na watakimbiana wao kwa wao. Je, kwa nini wasijitenge mbali katika dunia na suala la kuwaabudu hawa, na wakamkusudia kwa ibada Yule ambaye mkononi mwake upo ufalme wote, manufaa yote, madhara yote, kutoa na kunyima, naye ndiye Mlinzi na Msaidizi?
{فَلَا يَحْزُنْكَ قَوْلُهُمْ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ (76)}.
76. Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha.
#
{76} أي: فلا يَحْزُنْكَ يا أيُّها الرسولُ قول المكذِّبين، والمرادُ بالقول ما دلَّ عليه السياقُ، كلُّ قول يَقْدَحون فيه في الرسول أو فيما جاء به؛ أي: فلا تَشْغَلْ قَلْبَكَ بالحزن عليهم. {إنَّا نعلمُ ما يُسِرُّونَ وما يُعْلِنونَ}؛ فنجازِيهم على حسبِ عِلْمِنا بهم، وإلاَّ؛ فقولُهم لا يضرُّك شيئاً.
{76} Yaani, yasikuhuzunishe ewe Mtume yale wanayosema hao wanaokadhibisha; miongoni mwa kila maneno ambayo wanamkashifu kwayo Mtume au wanakashifu kwayo yale aliyokuja nayo. "Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha," na tutawalipa kulingana na jinsi tunavyowajua. Vinginevyo, maneno yao hayo hayatakudhuru hata kidogo.
{أَوَلَمْ يَرَ الْإِنْسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِنْ نُطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُبِينٌ (77) وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ قَالَ مَنْ يُحْيِ الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ (78) قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنْشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ (79) الَّذِي جَعَلَ لَكُمْ مِنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنْتُمْ مِنْهُ تُوقِدُونَ (80) أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ بَلَى وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ (81) إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَنْ يَقُولَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ (82) فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (83)}.
77. Kwani mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiyo amekuwa ndiye mgomvi wa dhahiri! 78. Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake,
akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika? 79.
Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba. 80. Aliyekujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. 81. Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi mno. 82.
Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. 83. Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.
Aya hizi tukufu zinataja tuhuma za wale wanaokanusha ufufuo na kuzijibu kwa jibu kamili, bora na lililo wazi kabisa.
#
{77} فقال تعالى: {أوَلَم يَرَ الإنسانُ}: المنكِرُ للبعث أو الشاكُّ فيه أمراً يفيدُه اليقينَ التامَّ بوقوعه، وهو ابتداءُ خلقِهِ {من نطفةٍ}، ثم تنقُّلُه في الأطوار شيئاً فشيئاً، حتى كبر وشبَّ وتمَّ عقلُه واستتبَّ؛ {فإذا هو خصيمٌ مبينٌ}: بعد أنْ كان ابتداءُ خلقِهِ من نطفةٍ؛ فلينظرِ التفاوتَ بين هاتين الحالتين، ولْيعلمْ أنَّ الذي أنشأه من العدم قادرٌ على أن يعيدَه بعدما تفرَّق وتمزَّق من باب أولى.
{77} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Kwani haoni mwanadamu" anayepinga ufufuo au anayeshuku hili? Haoni kitu ambacho kinamnufaisha yeye kwa yakini kamili juu ya kutokea kwake, ambacho ni mwanzo wa kuumbwa kwake "kutokana na tone la manii?" Kisha kupitia kwake awamu mbalimbali kidogo kidogo, mpaka akawa mkubwa, kisha akawa kijana na akili yake ikakamilika na kuimarika. "Kisha sasa yeye ndiye amekuwa mgomvi wa dhahiri!" Baada ya kwamba mwanzo wa kuumbwa kwake ulikuwa kutokana na tone la manii. Basi na aangalie tofauti iliyopo baina ya hali hizi mbili, na ajue kwamba yule aliyemuumba baada ya kutokuwepo anaweza zaidi kumrejesha baada ya kugawanyika na kumung'unyika.
#
{78} {وضرب لنا مثلاً}: لا ينبغي لأحدٍ أن يضرِبَه، وهو قياسُ قدرةِ الخالق بقدرةِ المخلوق، وأنَّ الأمر المُسْتَبْعَدَ على قدرة المخلوق مُسْتَبْعَدٌ على قدرة الخالق، فَسَّرَ هذا المثل بقوله: {قال}: ذلك الإنسان: {مَن يُحيي العظامَ وهي رميمٌ}؛ أي: هل أحدٌ يحييها؟ استفهام إنكارٍ؛ أي: لا أحَدَ يُحييها بعدما بَلِيَتْ وتلاشَتْ. هذا وجهُ الشبهة والمثل، وهو أنَّ هذا أمرٌ في غاية البعدِ على ما يُعْهَدُ من قدرةِ البشر، وهذا القولُ الذي صَدَرَ من هذا الإنسان غفلةٌ منه ونسيانٌ لابتداء خلقِهِ؛ فلو فَطِنَ لِخَلْقِهِ بعد أن لم يكن شيئاً مذكوراً، فوُجِد عياناً؛ لم يضرِبْ هذا المثل.
{78} "Na akatupigia mfano" ambao haumfailii yeyote kuupiga. Nao ni kuufananisha uwezo wa Muumba na uwezo wa viumbe, na kwamba jambo lisilowezekana kwa uwezo wa viumbe pia haliwezekani kwa uwezo wa Muumba. Basi Mwenyezi Mungu akaufafanua mfano huu kwa kauli yake mwanadamu huyu.
"Akasema:" Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwishamung'unyika?" Huku ni kuuliza kwa njia ya kejeli. Huo ndio mchanganyiko wao na fikira yao potofu, nao huo ndio mfano aliotoa Mwenyezi Mungu. Na hilo ni kwamba jambo hili haliwezekani kabisa kulingana na jinsi wanavyojua wanadamu. Lakini kauli hii aliyosema mwanadamu huyu ni kauli iliyotokana na kughafilika kwake na kusahau mwanzo wa kuumbwa kwake. Lau kuwa angeufahamu vyema uumbaji wake baada ya kwamba hakuwa chochote cha kutajwa, kisha akafanywa kuwepo, akaonekana kwa macho, basi hangepinga mfano huu.
#
{79} فأجاب تعالى عن هذا الاستبعادِ بجوابٍ شافٍ كافٍ، فقال: {قُلْ يُحْييها الذي أنشَأها أوَّلَ مَرَّةٍ}: وهذا بمجرَّدِ تصوُّرِهِ يعلم به علماً يقيناً لا شبهةَ فيه أنَّ الذي أنشأها أوَّلَ مرةٍ قادرٌ على الإعادةِ ثاني مرةٍ، وهو أهونُ على القدرةِ إذا تصوَّره المتصوِّر. {وهو بكلِّ خلقٍ عليمٌ}: هذا أيضاً دليلٌ ثانٍ من صفاتِ الله تعالى، وهو أنَّ علمه تعالى محيطٌ بجميع مخلوقاتِهِ في جميع أحوالِها في جميع الأوقات، ويَعْلَمُ ما تَنْقُصُ الأرضُ من أجسادِ الأمواتِ وما يبقى، ويعلمُ الغيبَ والشهادة؛ فإذا أقرَّ العبدُ بهذا العلم العظيم؛ علم أنَّه أعظمُ وأجلُّ من إحياء اللَّه الموتى من قبورِهم.
{79} Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajibu kuona kwao huku kwamba haliwezekani kwa jawabu la kuponya, la kutosha.
Akasema: "Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo." Na hili, kwa kufikiria tu, anajua kwa yakini na bila ya shaka yoyote kwamba yule aliyeiumba mara ya kwanza ana uwezo wa kuirejesha mara ya pili, na hilo ndilo rahisi zaidi mbele ya uwezo ikiwa atafikiria vyema mwenye kufikiria. "Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba." Huu pia ni ushahidi wa pili juu ya sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nalo ni kwamba elimu yake, Mwenye nguvu, imewazunguka viumbe wake wote katika hali zao zote katika nyakati zote, na anajua ni nini ambacho ardhi inapunguza miongoni mwa miili ya wafu na ile iliyobakia, na anajua ghaibu na mambo ya dhahiri. Kwa hivyo, mja akiikiri elimu hii kubwa,atajua kwamba hilo ni kubwa zaidi na tukufu zaidi hata kuliko Mwenyezi Mungu kuwafufua wafu kutoka kwenye makaburi yao.
#
{80} ثم ذَكَرَ دليلاً ثالثاً، فقال: {الذي جَعَلَ لكم من الشَّجَرِ الأخضرِ ناراً فإذا أنتُم منه توقِدونَ}: فإذا أخرجَ النار اليابسة من الشجر الأخضرِ الذي هو في غاية الرُّطوبة مع تضادِّهما وشدَّة تخالُفِهما؛ فإخْراجُهُ الموتى من قبورِهِم مثلُ ذلك.
80. Kisha akataja ushahidi wa tatu,
akasema: "Aliyekujalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha." Na kama moto mkavu unaweza kutoka katika mti mbichi ambao ni wenye unyevu mkubwa licha ya kuhalifiana kukubwa kwa viwili hivyo, basi kuwatoa wafu makaburini mwao ni mfano tu wa hilo.
#
{81} ثم ذكر دليلاً رابعاً، فقال: {أوَ لَيْسَ الذي خلقَ السمواتِ والأرضَ}: على سعتهما وعظمهما {بقادرٍ على أن يَخْلُقَ مثلَهم}؛ أي: أن يعيدَهم بأعيانهم {بلى}: قادرٌ على ذلك؛ فإنَّ خَلْقَ السماواتِ والأرض أكبرُ من خَلْقِ الناس. {وهو الخلاَّقُ العليمُ}: وهذا دليلٌ خامسٌ؛ فإنَّه تعالى الخلاقُ الذي جميع المخلوقات؛ متقدِّمها ومتأخِّرها، صغيرها وكبيرها؛ كلُّها أثرٌ من آثار خلقِهِ وقدرتِهِ، وأنَّه لا يستعصي عليه مخلوقٌ أراد خَلْقَه؛ فإعادتُهُ للأموات فردٌ من أفراد آثارِ خلقِهِ.
{81} Kisha akataja ushahidi wa nne,
akasema: "Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi" pamoja na upana wake na ukubwa wake "hawezi kuwaumba mfano wao?" Yaani, kuwarudisha vile walivyokuwa, "Kwani!" Yeye anaweza hilo. Kwa maana kuumbwa kwa mbingu na ardhi ni kukubwa kuliko kuumbwa kwa watu. "Naye ndiye Muumbaji Mkuu, ajuaye zaidi." Na huu ndio ushahidi wa tano. Kwani Yeye Mtukufu ndiye Muumbaji wa viumbe vyote vya mwanzo na vya mwisho, vidogo na vikubwa, vyote ni athari miongoni mwa athari za uumbaji wake na uwezo wake, na kwamba hakuna kiumbe kinachoweza kumshinda akitaka kukiumba. Kwa hivyo, kurudisha kwake wafu ni sehemu katika athari za uumbaji wake.
#
{82} ولهذا قال: {إنَّما أمرُهُ إذا أراد شيئاً}: نكرةٌ في سياق الشرط فَتَعُمُّ كلَّ شيءٍ، {أن يقولَ له كُن فيكونُ}؛ أي: في الحال من غير تمانع.
{82} Ndiyo maana akasema: "Hakika amri yake anapotaka kitu" chochote "ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa," bila pingamizi lolote.
#
{83} {فسبحانَ الذي بيدِهِ مَلَكوتُ كُلِّ شيءٍ}: وهذا دليلٌ سادسٌ؛ فإنَّه تعالى هو الملِكُ المالكُ لكلِّ شيءٍ؛ الذي جميعُ ما سكن في العالم العلويِّ والسفليِّ مُلْكٌ له وعبيدٌ مسخَّرون مدبَّرون، يَتَصَرَّفُ فيهم بأقدارِهِ الحكميَّة وأحكامِهِ الشرعيَّة وأحكامِهِ الجزائيَّة؛ فإعادتُه إيَّاهم بعد موتِهِم لينفذَ فيهم حكم الجزاء من تمام ملكِهِ، ولهذا قال: {وإليه تُرْجَعونَ}: من غير امتراءٍ ولا شكٍّ؛ لتواتُرِ البراهين القاطعةِ والأدلَّةِ الساطعةِ على ذلك. فتبارك الذي جَعَلَ في كلامِهِ الهدى والشفاء والنور.
{83} "Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu." Huu ni ushahidi wa sita. Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme anayemiliki kila kitu, ambaye vyote vilivyomo katika ulimwengu wa juu na wa chini ni mali yake na waja waliotiishwa na wanaoendeshwa, anawaendesha kwa mipango yake ya kimajaliwa, hukumu zake za kisheria, na hukumu zake za kimalipo. Basi kuwarudisha baada ya kufa kwao ili awatekelezee malipo ni katika ukamilifu wa ufalme wake.
Na ndiyo maana akasema: "Na kwake Yeye mtarejeshwa." Na hilo halina shaka yoyote, kwa sababu kuna hoja mbalimbali za uhakika na ushahidi unaong'aa juu yake. Basi ametakasika yule ambaye aliweka katika maneno yake mwongozo, uponyaji na nuru.
Imekamilika tafsiri ya Surat Yasin Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kama unavyostahiki utukufu wake, ukamilifu wake, ukuu wake na ukubwa wake. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad.
* * *