Tafsiri ya Surat As-Saffat
Tafsiri ya Surat As-Saffat
[Nayo] ilishuka Makka
{وَالصَّافَّاتِ صَفًّا (1) فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا (2) فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا (3) إِنَّ إِلَهَكُمْ لَوَاحِدٌ (4) رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ (5) إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ (6) وَحِفْظًا مِنْ كُلِّ شَيْطَانٍ مَارِدٍ (7) لَا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَى وَيُقْذَفُونَ مِنْ كُلِّ جَانِبٍ (8) دُحُورًا وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ (9) إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ (10) فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمْ مَنْ خَلَقْنَا إِنَّا خَلَقْنَاهُمْ مِنْ طِينٍ لَازِبٍ (11)}.
1. Ninaapa kwa wanaojipanga kwa safu. 2. Na kwa wenye kukataza mabaya. 3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho. 4. Hakika mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja. 5. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote. 6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. 7. Na kulinda na kila shetani muasi. 8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande. 9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu. 10. Isipokuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinachong'ara. 11.
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tuliowaumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata.
#
{1 - 4} هذا قسمٌ منه تعالى بالملائكة الكرام في حال عباداتها وتدبيرها ما تُدَبِّرُهُ بإذن ربِّها على ألوهيَّتِهِ تعالى وربوبيَّته، فقال: {والصّافاتِ صَفًّا}؛ أي: صفوفاً في خدمة ربِّهم، وهم الملائكة، {فالزاجراتِ زَجْراً}: وهم الملائكة يَزْجُرونَ السحابَ وغيرَه بأمر الله، {فالتَّالِياتِ ذِكْراً}: وهم الملائكة الذين يَتْلون كلامَ الله تعالى، فلمَّا كانوا متألِّهين لربِّهم ومتعبِّدين في خدمتِهِ ولا يعصونَه طرفةَ عين؛ أقسم بهم على ألوهيَّتِهِ، فقال: {إنَّ إلهكم لَواحدٌ}: ليس له شريكٌ في الإلهيَّة؛ فأخلِصوا له الحبَّ والخوفَ والرجاءَ وسائرَ أنواع العبادة.
{1 - 4} Hiki ni kiapo chake Mola Mtukufu kuhusu Malaika watukufu katika hali yao ya ibada na usimamizi wao yale wanavyosimamia, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, kwa mujibu wa uungu wake Mwenyezi Mungu aliyetukuka, na umola wake.
Akasema: "Ninaapa kwa wanaojipanga kwa safu" katika kumtumikia Mola wao Mlezi, na hao ni Malaika. "Na kwa wenye kukataza mabaya," na wale wanaopeperusha mawingu na mengineyo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. "Na kwa wenye kusoma Ukumbusho," nao ni Malaika wale wanaosoma maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwa kuwa wanamfanyia uungu na kumuabudu Mola wao Mlezi, huku wakimtumikia bila ya kumuasi kiasi cha kupepesa jicho. Akaapa kwao kwa uungu wake juu yao,
akasema: "Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja," wala hana mshirika yeyote katika uungu. Kwa hivyo mkusudieni Yeye tu kwa upendo wenu, hofu, matumaini, na aina nyinginezo zote za ibada.
#
{5} {ربُّ السمواتِ والأرضِ وما بينَهما وربُّ المشارقِ}؛ أي: هو الخالق لهذه المخلوقات، الرازقُ لها، الْمدبِّرُ لها؛ فكما أنَّه لا شريك له في ربوبيَّتِهِ إيَّاها؛ فكذلك لا شريك له في ألوهيَّتِهِ. وكثيراً ما يقرِّرُ تعالى توحيد الإلهيَّةِ بتوحيد الربوبيَّةِ؛ لأنَّه دالٌّ عليه. وقد أقرَّ به أيضاً المشركون في العبادة، فيلزمُهم بما أقرُّوا به على ما أنكروه. وخصَّ الله المشارقَ بالذِّكْر؛ لدلالتها على المغارب، أو لأنَّها مشارقُ النجوم التي سيذكرها. فلهذا قال:
{5} "Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote." Yaani, Yeye ndiye Muumba wa viumbe hivi vyote, Mwenye kuviruzuku, na Mwenye kuviendesha. Kwa hivyo, kama vile Yeye hana mshirika yeyote katika umola wake juu yao, basi vile vile hana mshirika yeyote katika uungu wake. Mungu Mwenyezi mara nyingi husimamisha hoja ya upweke wake katika uungu kwa kusimamisha hoja ya upweke wake katika umola; kwa sababu umola unaashiria uungu. Hili ni kwa sababu washirikina pia walikiri hilo katika ibada, kwa hivyo akawafanya kulazimika kukubali kile walichokataa kwa sababu ya kile walichokikiri. Na Mwenyezi Mungu aliyataja Mashariki hapa kwa njia maalumu kwa sababu yanaashiria Magharibi, au kwa sababu ndiyo mashariki ya nyota ambayo ataitaja.
Ndiyo maana akasema:
#
{6 - 9} {إنَّا زَيَّنَّا السماءَ الدُّنيا بزينةٍ الكواكبِ. وحفظاً من كلِّ شيطانٍ ماردٍ. لا يَسَّمَّعونَ إلى الملأ الأعلى}: ذكر الله في الكواكب هاتين الفائدتين العظيمتين: إحداهما: كونُها زينةً للسماء؛ إذ لولاها؛ لكانتِ السماء جرماً مظلماً لا ضوء فيه ، ولكن زيَّنها فيها؛ لتستنيرَ أرجاؤها وتَحْسُنَ صورتُها، ويُهْتَدى بها في ظُلُمات البرِّ والبحر، ويحصُلَ فيها من المصالح ما يحصُلُ. والثانية: حراسةُ السماء عن كلِّ شيطانٍ ماردٍ يصل بتمرُّدِهِ إلى استماع الملأ الأعلى، وهم الملائكة؛ إذا استمعت قذفتها بالشهب الثواقب {من كلِّ جانبٍ}: طَرْداً لهم وإبعاداً عن استماع ما يقولُ الملأُ الأعلى. {ولهم عذابٌ واصِبٌ}؛ أي: دائمٌ معدٌّ لهم لتمرُّدهم عن طاعةِ ربِّهم.
{6 - 9} "Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. Na kulinda na kila shetani muasi. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu.
" Mwenyezi Mungu alizitaja faida kuu mbili hizi kuhusu nyota: Moja yake ni kwamba ni pambo la mbingu. Kwani lau kuwa si hizo, mbingu ingelikuwa na giza bila ya mwangaza wowote. Lakini alizifanya kuwa pambo la mbingu ili pande zake zipate kuangazwa na ziwe na sura nzuri. Pia watu huongozwa kwazo katika viza vya nchi kavu na baharini, na pia kuna manufaa mbalimbali yanayopatikana humo. Ya pili ni kuzilinda mbingu kutokana na kila shetani muasi ambaye uasi wake unafikia kwenda kusikia maneno ya viumbe watukufu wa juu kabisa, ambao ni Malaika. Lakini wakitaka kusikiliza, wanaupiwa vimondo vinavyong'ara "kutokea kila upande" ili kuwafukuza na kuwaweka mbali na suala la kusikiliza kile kinachosemwa na viumbe watukufu wa juu kabisa. "Na wanayo adhabu ya kudumu." kwa sababu waliasi kumtii Mola wao Mlezi.
#
{10} ولولا أنه تعالى استثنى؛ لكان ذلك دليلاً على أنَّهم لا يستمعون شيئاً أصلاً، ولكن قال: {إلاَّ مَنْ خَطِفَ الخَطْفَةَ}؛ أي: إلاَّ مَنْ تَلَقَّفَ من الشياطين المَرَدَةِ الكلمةَ الواحدةَ على وجه الخفيةِ والسرقةِ، {فأتْبَعَهُ شهابٌ ثاقبٌ}: تارة يدرِكُه قبل أن يوصِلَها إلى أوليائِهِ فينقطع خبرُ السماء، وتارةً يُخْبِرُ بها قبل أن يدرِكَه الشهابُ، فيكذِبون معها مائةَ كذبةٍ، يروِّجونها بسبب الكلمةِ التي سُمِعَتْ من السماء.
{10} Na lau kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu asingetenga baadhi ya maneno; basi hii aya ingekuwa ni ushahidi wa kwamba hawasikii kitu chochote,
lakini alisema: "Isipokuwa anayenyakua kitu kidogo" kwa njia ya kisiri, "na mara humfwatia kimondo kinachong'ara." Wakati mwingine kimondo kinamfikia kabla hajakifikisha kitu hicho kwa marafiki wake, basi ikakatika habari hiyo ya mbinguni bila ya kuwafikia. Na wakati mwingine anakifikisha kabla ya kimondo kumfikia, basi marafiki wao hao wakaongeza humo uwongo mia moja, kisha wakaieneza habari hiyo kwa sababu ya neno hilo lililosikiwa kutoka mbinguni.
#
{11} ولَمَّا بيَّن هذه المخلوقاتِ العظيمةَ؛ قال: {فاسْتَفْتِهم}؛ أي: اسأل منكري خَلْقِهِم بعد موتِهِم: {أهم أشدُّ خَلْقاً}؛ أي: إيجادُهم بعد موتهم أشدُّ خَلْقاً وأشقُّ. {أم مَنْ خَلَقْنا}: من هذه المخلوقات؛ فلا بدَّ أن يُقِرُّوا أنَّ خَلْقَ السماواتِ والأرض أكبرُ من خَلْق الناس، فيلزمهم إذاً الإقرار بالبعثِ، بل لو رَجَعوا إلى أنفسهم وفكَّروا فيها؛ لعلموا أنَّ ابتداء خَلْقِهِم من طينٍ لازبٍ أصعب عند الفكر من إنشائهم بعد موتهم، ولهذا قال: {إنَّا خَلَقنَاهُم من طِينٍ لازِب}؛ أي: قويٍّ شديدٍ؛ كقوله تعالى: {ولقد خَلَقْنا الإنسانَ من صَلْصال من حَمَأٍ مسنونٍ}.
{11} Na alipowabainisha viumbe hawa wakubwa,
akasema: "Hebu waulize" hawa wanaokadhibisha uwezekano wa kuumbwa kwao tena baada ya kufa kwao: "Je, wao ndio wenye umbo gumu zaidi?" Yaani, kuwatoa tena baada ya kufa kwao ni kugumu zaidi? "Au hao wengine tuliowaumba," miongoni mwa viumbe hawa? Basi ni lazima watakiri kwamba kuumbwa kwa mbingu na ardhi ndiko kukubwa zaidi kuliko kuumbwa kwa watu. Kwa hilo linawalazimu kukiri kwamba watafufuliwa na kutolewa makaburini. Hata wangerejea nafsini mwao na wakatafakari juu yake, wangetambua kwamba kuanzisha uumbaji wao kutokana na udongo unaonata ni jambo gumu zaidi kulifikiria kuliko kuwaumba tena baada ya kufa kwao.
Na ndiyo maana akasema: "Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata,
" kama vile kauli yake: "Na tulimuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura."
{بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ (12) وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ (13) وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ (14) وَقَالُوا إِنْ هَذَا إِلَّا سِحْرٌ مُبِينٌ (15) أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ (16) أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ (17) قُلْ نَعَمْ وَأَنْتُمْ دَاخِرُونَ (18) فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنْظُرُونَ (19) وَقَالُوا يَاوَيْلَنَا هَذَا يَوْمُ الدِّينِ (20) هَذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ (21)}.
12. Bali unastaajabu, na wao wanafanya masihara. 13. Na wanapokumbushwa, hawakumbuki. 14. Na wanapoona Ishara, wanafanya masihara. 15.
Na husema: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi tu ulio dhahiri. 16. Ati tukishakufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa? 17. Hata baba zetu wa zamani? 18.
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili. 19. Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndipo wataona! 20.
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo. 21. Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyokuwa mkiikadhibisha.
#
{12} {بل عجبتَ}: أيُّها الرسولُ أو أيُّها الإنسانُ من تكذيب مَنْ كَذَّبَ بالبعث بعد أن أرَيْتَهم من الآيات العظيمةِ والأدلَّة المستقيمةِ، وهو حقيقةً محلُّ عجبٍ واستغرابٍ؛ لأنَّه مما لا يَقْبَلُ الإنكارَ. {و} أعجبُ من إنكارِهِم وأبلغُ منه أنَّهم {يسخَرون}: ممَّنْ جاء بالخبر عن البعثِ، فلم يَكْفِهِم مجردُ الإنكار، حتى زادوا السخريةَ بالقول الحقِّ.
{12} "Bali unastaajabu" ewe Mtume au ewe mwanadamu, kutokana na kukadhibisha kwa wale waliokadhibisha kufufuliwa baada ya kuwaonyesha ishara mbalimbali kubwa na hoja zilizonyooka, na hili kweli ndilo jambo la kushangaza. Kwa sababu ni jambo ambalo halifai kukanushwa. "Na" la kustaajabisha zaidi kuliko kukanusha kwao, na kubwa zaidi kuliko hilo ni kwamba "wanafanya masihara" kwa yule aliyekuja na habari za kufufuliwa kwa viumbe. Hakukuwatosha kukanusha tu, mpaka wakazidisha kuifanyia kejeli kauli ya haki.
#
{13} {و} من العجب أيضاً أنَّهم {إذا ذُكِّروا}: ما يعرفون في فِطَرِهِم وعُقولهم وفَطِنوا له ولَفَتَ نَظَرَهم إليه {لا يَذْكرونَ}: ذلك؛ فإنْ كان جهلاً؛ فهو من أدلِّ الدلائل على شِدَّةِ بلادَتِهِم العظيمة؛ حيث ذُكِّروا ما هو مستقرٌّ في الفطر معلومٌ بالعقل لا يقبلُ الإشكالَ، وإن كان تَجاهُلاً وعناداً؛ فهو أعجبُ وأغربُ.
{13} "Na" katika yanayoshangaza pia ni kwamba "wanapokumbushwa" yale wanayoyajua katika maumbile yao ya asili, akili zao, kuyafahamu kwao, na kuyavutia mawazo yao kwayo "hawakumbuki." Ikiwa ni ujinga, basi hilo ni moja ya ushahidi wa wazi zaidi juu ya ukubwa wa ujinga wao. Ambapo walikumbushwa mambo ambayo yalishathibitika katika maumbile yao ya asili, yanajulikana kwa akili na ambayo hayakubali utata wowote. Na ikiwa ni ujinga na ukaidi, basi hilo linakuwa la kushangaza zaidi.
#
{14} ومن العَجَبِ أيضاً أنَّهم إذا أُقيمتْ عليهم الأدلَّةُ، وذُكِّروا الآياتِ التي يخضعُ لها فحولُ الرجال وألبابُ الألِبَّاء، يَسْخَرون منها ويَعْجَبونَ.
{14} Vile vile inastaajabisha kwamba wanaposimamishiwa ushahidi, wakakumbushwa ishara mbalimbali ambazo watu wenye nguvu zaidi na wenye ufahamu mkubwa wanazitii, wao wanazikejeli na kuzistaajabia.
#
{15} ومن العجب أيضاً قولُهُم للحقِّ لما جاءهم: {إنْ هذا إلاَّ سحرٌ مبينٌ}: فجعلوا أعلى الأشياء وأجلَّها ـ وهو الحقُّ ـ في رتبة أخسِّ الأشياء وأحقرِها.
{15} Na pia inastaajabisha kuwa waliiambia haki ilipowajia: "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi tu ulio dhahiri." Basi wakakifanya kitu cha juu zaidi na kilichotukuka zaidi - ambacho ni haki - kwenye daraja ya chini na duni kabisa.
#
{16 - 17} ومن العجب أيضاً قياسُهم قدرةَ ربِّ الأرض والسماواتِ على قدرةِ الآدميِّ الناقص من جميع الوجوه، فقالوا استبعاداً وإنكاراً: {أإذا مِتْنا وكُنَّا تُراباً وعِظاماً أإنَّا لَمَبْعوثونَ. أوَ آباؤنا الأوَّلونَ}.
{16 - 17} Vile vile inastaajabisha kwamba walilinganisha uwezo wa Mola Mlezi wa ardhi na mbingu na uwezo wa mwanadamu mpungufu katika namna zote.
Kwa hivyo wakasema kwa kuona kwamba hilo haliwezekani na kwa njia ya kukanusha: "Ati tukishakufa na tukawa udongo na mifupa ndiyo kweli tutafufuliwa? Hata baba zetu wa zamani?"
#
{18} ولمَّا كانَ هذا منتهى ما عندَهم وغايةَ ما لَدَيْهم؛ أمر الله رسولَه أن يُجيبَهم بجواب مشتمل على ترهيِبِهم ، فقال: {قل نعم}: ستُبْعَثون أنتم وآباؤكم الأولون، {وأنتُم داخِرون}: ذَليلون صاغِرون لا تمتَنعون، ولا تَسْتَعْصون على قدرةِ الله.
{18} Na kwa vile huu ndio mwisho wa kile walicho nacho, Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwajibu kwa jawabu lililojumuisha kuwatia hofu,
akasema: "Sema: Ndiyo!" Nyinyi na baba zenu mtafufuliwa, "Hali nanyi ni madhalili" bila ya kukataa wala kuushinda uwezo wa Mwenyezi Mungu.
#
{19} {فإنَّما هي زجرةٌ واحدةٌ}: يَنْفُخُ إسرافيلُ فيها في الصُّورِ، {فإذا هم} مبعوثونَ من قبورهم {يَنظُرونَ}: كما ابْتُدِئ خَلْقُهم، بُعثِوا بجميع أجزائِهِم حفاةً عراةً غُرلاً.
{19} "Huko utapigwa ukelele mmoja tu," ambao Israfil atapuliza katika baragumu, "na tazama, hapo ndipo wataona!" Kama walivyoanzishwa kuumbwa mara ya kwanza, sasa watafufuliwa kutoka makaburini mwao bila viatu, uchi, na bila ya kutahiriwa.
#
{20} وفي تلك الحال يُظْهِرون الندمَ والخزيَ والخسارَ، ويَدْعونَ بالويل والثُّبور، {وقالوا يا وَيْلَنا هذا يومُ الدينِ}؛ فقد أقرُّوا بما كانوا في الدنيا به يهزؤون!
{20} Katika hali hiyo wataonyesha majuto, hizaya, hasra, na wataomba maangamizo,
"na watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo." Hapo watakiri yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha katika dunia hii!
#
{21} فيُقالُ لهم: {هذا يومُ الفصلِ}: بين العبادِ فيما بينَهم وبين ربِّهم من الحقوق وفيما بينهم وبين غيرِهِم من الخلق.
{21} Kisha wataambiwa: "Hii ndiyo Siku ya Hukumu" baina ya waja, katika mambo yaliyo baina yao na Mola wao Mlezi miongoni mwa haki mbalimbali, na yale yaliyo baina ya viumbe wenyewe kwa wenyewe.
{احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ (22) مِنْ دُونِ اللَّهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَى صِرَاطِ الْجَحِيمِ (23) وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ (24) مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ (25) بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ (26)}.
22. Wakusanyeni wale waliodhulumu, na wake zao, na hao ambao wao waliokuwa wakiwaabudu. 23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! 24. Na wasimamisheni.
Hakika hao wataulizwa: 25. Mna nini? Mbona hamsaidiani? 26. Bali hii leo, watasalimu amri.
#
{22 - 23} أي: إذا حضروا يوم القيامةِ وعاينوا ما به يكذبون ورأوا ما به يستسخرون؛ يُؤْمَرُ بهم إلى النارِ التي بها يكذبون، فيقال: {احشُروا الذين ظلموا}: أنفسَهم بالكفرِ والشركِ والمعاصي {وأزواجَهم}: الذين من جنس عملهم، كلٌّ يُضَمُّ إلى مَنْ يُجانِسُه في العمل، {وما كانوا يَعْبُدون من دونِ الله}: من الأصنام والأندادِ التي زعموها، اجمعوهم جميعاً، واهدوهم {إلى صراطِ الجَحيم}؛ أي: سوقوهم سوقاً عنيفاً إلى جهنم.
{22 - 23} Yaani watakapokuja Siku ya Kiyama na wakaona yale waliyokuwa wakikanusha na wakaona yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara, itaamrishwa waende Motoni waliokuwa wakiukadhibisha.
Itasemwa: "Wakusanyeni waliodhulumu" nafsi zao kwa ukafiri, ushirikina na maasi, "na wake zao" waliofanya matendo aina sawa na wao, "na hao waliokuwa wakiwaabudu adala ya Mwenyezi Mungu" miongoni mwa masanamu, wenza ambao walidai kwamba ni washirika wa Mwenyezi Mungu, kisha waongozeni "kwenda kwenye njia ya Jahannamu" kwa nguvu.
#
{24} {و} بعدما يتعيَّن أمرُهم إلى النار ويَعْرِفون أنَّهم من أهلِ دار البوار؛ يُقالُ: {قِفوهُم}: قبل أن توصِلوهم إلى جهنَّم، {إنَّهم مسؤولونَ}: عمَّا كانوا يفترونَه في الدُّنيا؛ ليظهرَ على رؤوس الأشهادِ كَذِبُهم وفضيحتُهم.
{24} "Na" baada ya kuhukumiwa kwamba watakwenda Jahannamu na wakajua kwamba wao ni miongoni mwa watu wa makaazi ya maangamizo,
itasemwa: "Wasimamisheni" kabla hamjawafikisha katika Jahannamu. "Hakika hao wataulizwa" kuhusu yale waliyokuwa wakiyazua katika dunia hii, ili uongo wao na fedheha yao idhihirike mbele ya viumbe wote
#
{25} فيقال لهم: {ما لكم لا تناصرون}: أي: ما الذي جرى عليكم اليوم، وما الذي طرقكم، لا ينصر بعضكم بعضاً، ولا يغيث بعضُكم بعضاً، بعدما كنتُم تزعُمون في الدُّنيا أنَّ آلهتكم ستدفعُ عنكم العذابَ وتُغيثكم أو تشفعُ لكم عند الله؟!
{25} Kisha wataambiwa: "Mna nini, mbona hamsaidiani," licha ya kwamba mlikuwa mkidai katika dunia kwamba miungu yenu itawaondolea adhabu na kuwanusuru, au kuwafanyia uombezi kwa Mwenyezi Mungu?
#
{26} فكأنهم لا يجيبون هذا السؤال؛ لأنَّهم قد علاهم الذُّلُّ والصَّغارُ، واستسلموا لعذابِ النارِ وخَشَعوا وخَضَعوا وأُبْلِسوا، فلم يَنْطِقوا، ولهذا قال: {بل هُمُ اليومَ مُسْتَسْلِمونَ}.
{26} Ni kana kwamba hawatajibu swali hili, kwa sababu watakuwa wamefedheheka sana na kuwa duni mno. Na wakajisalimisha kwa adhabu ya Moto, wakanyenyekea, wakatii amri, na wakakata tamaa. Kwa hivyo hawakusema kitu,
na ndiyo maana akasema: "Bali hii leo, watasalimu amri."
{وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ (27) قَالُوا إِنَّكُمْ كُنْتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ (28) قَالُوا بَلْ لَمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ (29) وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُمْ مِنْ سُلْطَانٍ بَلْ كُنْتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ (30) فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا إِنَّا لَذَائِقُونَ (31) فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ (32) فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ (33) إِنَّا كَذَلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ (34) إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ (35) وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَجْنُونٍ (36) بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ (37) إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ (38) وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (39)}.
27. Wataelekeana wao kwa wao kuulizana. 28.
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. 29. Watasema
(wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. 30. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. 31. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. 32. Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. 33. Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. 34. Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wahalifu. 35. Wao walipokuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu
(Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu), wanajivuna. 36.
Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? 37. Bali huyu amekuja kwa haki, na amewasadikisha Mitume. 38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. 39. Wala hamlipwi isipokuwa hayo mliyokuwa mkiyafanya.
#
{27 - 28} لما جُمِعوا هم وأزواجهم وآلهتُهم وهُدوا إلى صراط الجحيم ووُقِفوا فسُئِلوا فلم يُجيبوا؛ أقبلوا فيما بينَهم يلومُ بعضُهم بعضاً على إضلالِهِم وضلالِهِم، فقال الأتباعُ للمتبوعينَ الرؤساء: {إنَّكُم كنتُم تأتونَنا عن اليمينِ}؛ أي: بالقوَّة والغلبة فتُضِلُّونا، ولولا أنتُم؛ لكُنَّا مؤمنينَ.
{27 - 28} Walipokusanywa wao, wake zao na miungu yao na kuongozwa kwenye njia ya Jahannamu, na wakasimamishwa na kuulizwa, lakini hawakujibu; wakaanza kulaumiana wao kwa wao kwa sababu ya kupotezana na kupotea kwao.
Basi wafuasi wakawaambia viongozi wao waliokuwa wakiwafuata: "Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia," na mnatupoteza, na lau kuwa si nyinyi, basi tungekuwa waumini.
#
{29 - 32} {قالوا} لهم: {بل لمْ تكونوا مؤمنينَ}؛ أي: ما زلتُم مشرِكين كما نحنُ مشركونَ؛ فأيُّ شيءٍ فضَّلَكم علينا؟! وأيُّ شيء يوجِبُ لومَنا؟! {و} الحالُ أنَّه {ما كان لنا عليكُم من سلطانٍ}؛ أي: قهرٍ لكم على اختيار الكفر، {بل كنتُم قوماً طاغينَ}: متجاوِزين للحدِّ ، {فحقَّ علينا}: نحنُ وإيَّاكُم {قولُ ربِّنا إنَّا لَذائقونَ}: العذاب؛ أي: حقَّ علينا قَدَرُ ربِّنا وقضاؤه أنَّا وإيِّاكم سنذوقُ العذابَ ونشترِكُ في العقاب. {فـ} لذلك {أغْوَيْناكم إنَّا كُنَّا غاوينَ}؛ أي: دَعَوْناكم إلى طريقتِنا التي نحنُ عليها، وهي الغوايةُ، فاستَجَبْتُم لنا؛ فلا تلومونا ولوموا أنفسكم.
{29 - 32} "Wakasema" wakiwaambia: "Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini." Na mliendelea kuwa washirikina, kama sisi pia tulivyokuwa washirikina. Kwa hivyo ni nini kiliwafanya nyinyi kuwa bora kutuliko sisi? Na nini kinalazimu tulaumiwe? "Na" hali ni kwamba "Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu" ya kuwalazimisha kuchagua ukafiri, "bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu" waliokuwa wakivuka mipaka. "Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia" sisi na hata nyinyi. "Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu" na tushiriki sote katika hilo. Basi ndiyo maana "tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu." Tulipowaita kwenye njia tunayoifuata ya upotevu, nanyi mkatuitikia. Kwa hivyo, msitulaumu, lakini jilaumuni wenyewe.
#
{33 - 34} قال تعالى: {فإنَّهم يومئذٍ}؛ أي: يوم القيامةِ {في العذاب مشترِكونَ}: وإن تفاوتتْ مقاديرُ عذابِهِم بحسب جُرمهم؛ كما اشتركوا في الدُّنيا على الكفر اشتركوا في الآخرة بجزائِهِ، ولهذا قال: {إنَّا كذلك نفعلُ بالمجرِمين}.
{33 - 34} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Basi wao kwa hakika siku hiyo" ya Kiyama "watashirikiana katika adhabu pamoja," hata kama kiasi cha adhabu yao kitatofautiana kulingana na makosa yao. Kama walivyoshirikiana katika ukafiri duniani, watashirikiana Akhera katika malipo yake.
Ndiyo maana akasema: "Hakika sisi hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wahalifu."
#
{35 - 36} ثم ذكر أنَّ إجرامَهم قد بَلَغَ الغايةَ وجاوز النهايةَ، فقال: {إنَّهم كانوا إذا قيل لهم لا إله إلاَّ اللهُ}: فدعوا إليها وأمروا بترك إلهيَّة ما سواه {يَسْتَكْبِرونَ}: عنها وعلى مَنْ جاء بها، {ويقولون} معارضةً لها: {أإنَّا لَتارِكو آلهتِنا}: التي لم نزل نعبدُها نحنُ وآباؤنا، لقول {شاعرٍ مجنونٍ}؛ يعنون: محمداً - صلى الله عليه وسلم -، فلم يكفهم قبَّحَهُمُ اللهُ الإعراضُ عنه ولا مجردُ تكذيبِهِ، حتى حكموا عليه بأظلم الأحكام، وجعلوه شاعراً مجنوناً، وهم يعلمون أنَّه لا يعرفُ الشعر والشعراء، ولا وصفُهُ وصفُهم، وأنَّه أعقلُ خَلْقِ اللَّه وأعظمُهم رأياً.
{35 - 36} Kisha akataja kuwa uhalifu wao ulifikia na hata kuvuka kiwango cha mwisho kabisa.
Akasema: "Wao walipokuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu
(Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu)" wakalinganiwa kwake, na wakaamrishwa kuacha kuwafanyia uungu wasiokuwa Yeye, "walijivuna" wakiyakataa hayo na wakimpinga yule aliyewajia nayo.
Na pia walikuwa "wakisema" kwa njia ya kuyapinga: "Hivyo sisi tuiache miungu yetu" ambayo hatujaacha kuiabudu, sisi na baba zetu, "kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?" Wakimaanisha Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hawakutosheka - Mwenyezi Mungu awaangamize - na kumpa mgongo na kumkanusha, lakini pia wakamhukumu kwa hukumu yenye dhuluma kubwa zaidi. Akamfanya kuwa mshairi kichaa, na ilhali wanajua kwamba yeye hayajui mashairi wala washairi, wala hasifiki na sifa zao, bali walijua vyema kwamba yeye ndiye mwenye akili zaidi katika viumbe wa Mwenyezi Mungu na mwenye maoni bora zaidi yao wote.
#
{37} ولهذا قال تعالى ناقضاً لقولهم: {بل جاء}: محمدٌ {بالحقِّ}؛ أي: مجيئه حقًّا، وما جاء به من الشرع والكتاب حقٌّ، {وصدَّقَ المرسلينَ}؛ أي: ومجيئُهُ صَدَّقَ المرسلين؛ فلولا مجيئُهُ وإرسالُهُ؛ لم يكن الرسل صادقين؛ فهو آيةٌ ومعجزةٌ لكلِّ رسول قبله؛ لأنَّهم أخبروا به وبشَّروا، وأخذ الله عليهم العهدَ والميثاق لئن جاءهم ليؤمنُنَّ به ولَيَنْصُرُنَّه، وأخذوا ذلك على أممهم، فلما جاء؛ ظهر صِدْقُ الرسل الذين قبله، وتبيَّن كَذِبُ مَنْ خالفهم، فلو قدر عدم مجيئه، وهم قد أَخْبَروا به؛ لكان ذلك قادحاً في صدقهم. وصَدَّقَ أيضاً المرسلين؛ بأنْ جاء بما جاؤوا به، ودعا إلى ما دَعَوْا إليه، وآمن بهم، وأخبر بصحة رسالتهم ونبوَّتهم وشرعهم.
{37} Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema,
akipinga kauli yao hiyo: "Bali" Muhammad "alikuja kwa haki." Yaani, kuja kwake ni kwa haki, na yale aliyokuja nayo katika sheria na Kitabu ni ya haki. "Na amewasadikisha Mitume," Yaani, kuja kwake kuliwasadikisha Mitume. Kwani lau kuwa si kuja kwake na kutumwa kwake, basi Mitume hawangekuwa wakweli. Kwa hivyo, yeye ni Ishara na muujiza kwa kila Mtume wa kabla yake. Kwa sababu walijulisha juu yake na wakabashiria kuja kwake, na Mwenyezi Mungu akachukua kwao ahadi na agano ya kwamba akiwajia, basi bila shaka watamwamini na kumsaidia, na wakachukua ahadi hiyo pia kwa umma wao. Basi alipokuja, ukweli wa Mitume wa kabla yake ukadhihirika na ukabainika uwongo wa wale waliowapinga. Na ingekuwa kwamba hakuja ilhali walikuwa wamejulisha juu ya kuja kwake, basi hilo lingekuwa la kutia dosari katika ukweli wao. Vile vile aliwasadiki Mitume; ambapo alikuja na yale waliyokuja nayo, na akayalingania yale waliyoyalingania, na akawaamini, na akajulisha juu ya usahihi wa ujumbe wao, unabii wao na sheria yao.
#
{38 - 39} ولما كان قولُهُم السابقُ: {إنَّا لَذائقونَ} قولاً صادراً منهم يحتملُ أنْ يكونَ صدقاً أو غيره؛ أخبر تعالى بالقول الفصل الذي لا يَحْتَمِلُ غيرَ الصدق واليقين، وهو الخبر الصادر منه تعالى، فقال: {إنَّكم لَذائقو العذابِ الأليم}؛ أي: المؤلم الموجع، {وما تُجْزَوْنَ}: في إذاقة العذاب الأليم {إلاَّ ما كُنتُم تعملونَ}: فلم نَظْلِمْكم، وإنَّما عَدَلْنا فيكم.
{38 - 39} Na kwa kuwa kauli yao iliyotangulia ilikuwa kwamba: "Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu." Ni kauli ya kweli, lakini ambayo pia huenda wakawa wakweli katika hilo au la. Yeye Mtukufu akajulisha kuhusu hii ya kukataa ambayo haina uwezekano mwingine isipokuwa ukweli na yakini, ambayo ni habari iliyotoka kwake, Aliyetukuka,
akasema: "Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu, wala hamlipwi ila hayo mliyokuwa mkiyafanya." Na wala hatutawadhulumu, bali tutawafanyia uadilifu.
Kwa kuwa maneno haya ni ya jumla, ingawa waliokusudiwa kwayo ni washirikina hao; Mwenyezi Mungu Mtukufu akawatenga mbali Waumini, akasema:
{إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (40) أُولَئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَعْلُومٌ (41) فَوَاكِهُ وَهُمْ مُكْرَمُونَ (42) فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ (43) عَلَى سُرُرٍ مُتَقَابِلِينَ (44) يُطَافُ عَلَيْهِمْ بِكَأْسٍ مِنْ مَعِينٍ (45) بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِلشَّارِبِينَ (46) لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنْزَفُونَ (47) وَعِنْدَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ (48) كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَكْنُونٌ (49)}.
40. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliohitariwa. 41. Hao ndio watakaopata riziki maalumu. 42. Matunda, nao wataheshimiwa. 43. Katika Bustani za neema. 44. Wako juu ya viti wameelekeana. 45. Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchemi. 46. Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao. 47. Hakina madhara, wala hakiwaleweshi. 48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha, mazuri. 49. Hao wanawake kama mayai yaliyohifadhika.
#
{40} يقول تعالى: {إلاَّ عبادَ الله المُخْلَصينَ}: فإنَّهم غير ذائقي العذاب الأليم؛ لأنهم أخلصوا لله الأعمال، فأخلصهم واختصَّهم برحمتِهِ وجادَ عليهم بلطفِهِ.
{40} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliohitariwa." Wao hawataonja adhabu chungu, kwa sababu walikuwa wakimkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika matendo yao. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaokoa na akawateua kwa rehema yake na akawafanyia upole mkubwa mno.
#
{41 - 42} {أولئك لهم رزقٌ معلومٌ}؛ أي: غير مجهول، وإنَّما هو رزقٌ عظيمٌ جليلٌ لا يُجهلُ أمرُهُ ولا يُبْلَغُ كُنْهُهُ، فسَّره بقوله: {فواكِهُ}: من جميع أنواع الفواكه التي تَتَفَكَّه بها النفس للذَّتِها في لونها وطعمها. {وهم مُكْرَمونَ}: لا مهانون محتَقَرون، بل معظَّمون مبجَّلون موقَّرون، قد أكرم بعضُهم بعضاً، وأكرمَتْهُمُ الملائكةُ الكرامُ، وصاروا يدخُلون عليهم من كلِّ باب، ويهنِّئونهم ببلوغ أهنأ الثواب، وأكرمَهَم أكرمُ الأكرمين وجادَ عليهم بأنواع الكرامات من نعيم القلوب والأرواح والأبدان.
{41 - 42} "Hao ndio watakaopata riziki maalumu." Kwani ni riziki kubwa mno na tukufu, ambayo jambo lake halikosi kujulikana lakini haliwezi kufikiwa uhalisia wake.
Ndiyo maana akalifasiri kwa kauli yake: "Matunda" ya kila aina ambayo nafsi zinayafurahia kwa sababu ya raha yake nzuri, rangi yake na ladha yake. "Nao wataheshimiwa" wala hawatadunishwa na kudharauliwa, bali watapewa taadhima na heshima. Wataheshimiana wao kwa wao, na pia Malaika watukufu watawatukuza, na wakawa wanaingia waliko kupitia kila mlango wakiwapongeza kwa kufikia thawabu nzuri zaidi. Kisha atawakirimu Mkarimu wa wote kwa aina mbalimbali za ukarimu miongoni mwa neema za mioyo, roho na miili.
#
{43} {في جنات النعيم}؛ أي: الجنات التي النعيم وَصْفُها والسرورُ نعمتُها، وذلك لما جَمَعَتْهُ ممَّا لا عينٌ رأتْ، ولا أذنٌ سمعتْ، ولا خَطَرَ على قلب بشر، وسلمتْ من كلِّ مخلٍّ بنعيمها من جميع المكدِّرات والمنغِّصات.
{43} "Katika Bustani za neema." Kwa sababu zimejumuisha mambo ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala hayajawahi kuota katika moyo wa mwanadamu yeyote. Na pia zimesalimika kutokana na kila kitu ambacho huvuruga furaha yake kama vile misukosuko yote.
#
{44} ومن كرامتهم عند ربِّهم وإكرام بعضهم بعضاً أنَّهم على {سُرُرٍ}: وهي المجالس المرتفعةُ المزينة بأنواع الأكسيةِ الفاخرةِ المزخرفة المجملة؛ فهم مُتَّكئونَ عليها على وجهِ الراحةِ والطُّمأنينة والفرح، {متقابلينَ}: فيما بينَهم، قد صَفَتْ قلوبُهم ومحبتُهم فيما بينَهم، ونَعِموا باجتماع بعضهم مع بعض؛ فإنَّ مقابلة وجوههم تدلُّ على تقابل قلوبهم وتأدُّب بعضهم مع بعض، فلم يستدبِرْه أو يجعَلْه إلى جانبه، بل من كمال السرور والأدب ما دلَّ عليه ذلك التقابل.
{44} Na katika utukufu wao kwa Mola wao Mlezi na wao kwa wao kuheshimiana kwamba watakuwa "juu ya viti" vilivyoinuka juu, vilivyopambwa kwa mavazi ya kifahari, mazuri. Watakuwa wameegemea juu yake kwa raha, utulivu, na furaha huku "wameelekeana" kwa maana nyoyo zao zitakuwa safi na watapendana wao kwa wao. Na wakafurahia kukutana wao kwa wao, kwa sababu kuelekeana kwa nyuso zao kunaashiria kuelekeana kwa nyoyo zao, na kupeana adabu wao kwa wao. Kwa hivyo hawatapeana migongo wala kuwa ubavuni mwa wenzao, bali watakuwa katika furaha na adabu kamilifu kama ilivyoashiriwa na kuelekeana huko.
#
{45 - 47} {يُطافُ عليهم بكأسٍ من مَعين}؛ أي: يتردَّدُ الولدان المستعدِّون لخدمتهم عليهم بالأشربةِ اللذَّيذةِ بالكاسات الجميلةِ المنظر المُتْرَعَةِ من الرحيق المختوم بالمسك، وهي كاساتُ الخمر، وتلك الخمرُ تخالِفُ خَمْرَ الدُّنيا من كل وجه؛ فإنَّها في لونها {بيضاء} من أحسن الألوان، وفي طعمها {لَذَّةٍ للشارِبينَ}: يلتذُّ شاربُها بها وقتَ شُربها وبعدَه، وأنَّها سالمةٌ من غول العقل وذهابِهِ ونزفِهِ ونزفِ مال صاحبها، وليس فيها صداعٌ ولا كدرٌ.
{45 - 47} "Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchemi." Watajiwa mara kwa mara na wavulana wa ujana ambao wako tayari kuwahudumia kwa kuwapa vinywaji vya ladha katika vikombe virembo vilivyojaa kinywaji safi kilichofunikwa vyema, chenye miski. Navyo ni vikombe vya pombe tofauti na ile ya duniani kwa kila njia. Kwani rangi yake ni "nyeupe" ambayo ni katika rangi bora zaidi, na katika ladha yake ni "kitamu kwa wanywao." Mwenye kukinywa atakifurahia wakati wa kukinywa na baada yake. Nacho pia ni salama kutokana na kuivuruga akili na kumaliza mali ya mwenye kukinywa, wala hakisababishi kichwa kuuma wala usumbufu.
#
{48 - 49} فلمَّا ذَكَرَ طعامهم وشرابَهم ومجالِسَهم. وعمومُ النعيم وتفاصيلُه داخلٌ في قوله: {جنات النعيم}، لكن فصَّلَ هذه الأشياءَ لِتُعْلَمَ فتشتاقَ النفوس إليها؛ ذَكَرَ أزواجَهم، فقال: {وعندهم قاصراتُ الطَّرْفِ عِينٌ}؛ أي: وعند أهل دار النعيم في محلاَّتهم القريبة حورٌ حسانٌ كاملاتُ الأوصافِ قاصراتُ الطرفِ: إمَّا أنَّها قَصَرَتْ طَرْفَها على زوجِها لعفَّتِها، وعدم مجاوزتِهِ لغيرِهِ، ولجمال زوجِها وكماله؛ بحيث لا تطلبُ في الجنة سواه، ولا ترغبُ إلاَّ به. وإمَّا لأنَّها قَصَرَتْ طَرْفَ زوجها عليها، وذلك يدلُّ على كمالها وجمالها الفائق، الذي أوجب لزوجِها أن يَقْصُرَ طرفَه عليها. وقَصْرُ الطرفِ أيضاً يدلُّ على قَصْرِ النفس والمحبَّة عليها، وكلا المعنيينِ محتملٌ، وكلاهما صحيحٌ.
وكلُّ هذا يدلُّ على جمال الرجال والنساء في الجنَّة ومحبَّة بعضهم بعضاً محبةً لا يَطْمَحُ إلى غيره وشدة عفَّتهم كلِّهم وأنَّه لا حَسَدَ فيها ولا تباغُضَ ولا تشاحُنَ، وذلك لانتفاء أسبابه. {عِيْنٌ}؛ أي: حسانُ الأعين جميلاتُها ملاحُ الحدق. {كأنهنَّ}؛ أي: الحور {بَيْضٌ مكنونٌ}؛ أي: مستورٌ، وذلك من حسنهنَّ وصفائهنَّ، وكون ألوانهنَّ أحسن الألوان وأبهاها، ليس فيه كدرٌ ولا شينٌ.
{48 - 49} Alipotaja vyakula vyao, vinywaji vyao, jinsi watakavyokaa,
na ujumla wa neema na maelezo yake ya kina kama ilivyo katika kauli yake: "Bustani za neema", aliyabainisha mambo haya kwa kina ili yajulikane ili nafsi ziyatamani. Akawataja wake zao,
akasema: "Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha, mazuri." Ima wanawake hawa wana macho ya staha kwa waume zao kwa kuwaelekea wao tu kwa sababu ya usafi wao, na kwa sababu ya uzuri na ukamilifu wa waume wao; kiasi kwamba hawatafuti Peponi yeyote isipokuwa hao, na wala hawatawataka isipokuwa hao tu. Au ni wenye staha kwa sababu waliwafanya waume zao hao kuwaelekea wao tu. Hilo linaonyesha ukamilifu wa uzuri wao mkubwa mno, ambao uliwafanya waume zao kuwatazama wao tu. Kuwatazama kwao waume zao tu pia kunaashiria kwamba wanawapa waume zao hao tu nafsi zao na upendo. Na hizi maana zote mbili zinawezekana, na zote mbili ni sahihi. Yote haya yanaashiria uzuri wa wanaume na wanawake katika Pepo, kupendana kwao wenyewe kwa wenyewe kwa upendo ambao hawawezi kuwatamani wasiokuwa hao, na pia ni ishara ya ukubwa wa ufwasi wao wote, na kwamba humo hakutakuwa na husuda, chuki na kugombana; kwa sababu hakuna sababu za hayo humo. "Wenye macho ya staha mazuri," yenye kufurahisha. "Hao wanawake ni kama mayai yaliyohifadhika" kwa sababu ya uzuri wao, usafi wao, na kwa sababu rangi zao ni rangi bora na nzuri zaidi, ambazo hazina cha kuchukiza wala cha kuwatia dosari.
{فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ (50) قَالَ قَائِلٌ مِنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ (51) يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ (52) أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ (53) قَالَ هَلْ أَنْتُمْ مُطَّلِعُونَ (54) فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ (55) قَالَ تَاللَّهِ إِنْ كِدْتَ لَتُرْدِينِ (56) وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنْتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ (57) أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ (58) إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَى وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ (59) إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (60) لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ (61)}.
50. Basi wakaelekeeana kuulizana wenyewe kwa wenyewe. 51.
Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki. 52.
Aliyekuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanaosadiki. 53. Ati tukishakufa tukawa udongo na mafupa, ndiyo tutalipwa na kufanyiwa hesabu? 54.
Atasema: Je, nyie mnawaona? 55. Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu. 56.
Atasema: Wallahi!
(Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu) Ulikaribia sana kunipoteza. 57. Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa. 58. Je, Sisi hatutakufa? 59. Isipokuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa. 60. Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa. 61. Kwa mfano wa haya na watende watendao.
#
{50 - 59} لمَّا ذَكَرَ تعالى نعيمَهم وتمام سُرورهم بالمآكل والمشارب والأزواج الحسانِ والمجالس الحسنةِ؛ ذَكَرَ تذاكُرَهم فيما بينَهم ومطَارَحَتَهم للأحاديث عن الأمور الماضيةِ وأنَّهم ما زالوا في المحادثة والتساؤل حتى أفضى ذلك بهم إلى أن قال قائلٌ منهم: {إنِّي كان لي قرينٌ}: في الدنيا ينكِرُ البعث ويلومُني على تصديقي به، ويقولُ لي: {أإنَّك لَمِنَ المصدِّقينَ. أإذا مِتْنا وكُنَّا تراباً وعِظاماً أإنَّا لَمَدينونَ}؛ أي: مجازَوْن بأعمالنا؟! أي: كيف تصدِّقُ بهذا الأمر البعيد، الذي في غاية الاستغراب، وهو أنَّنا إذا تَمَزَّقْنا فَصِرْنا تراباً وعظاماً أنَّنا نُبعث ونعادُ ثم نحاسبُ ونُجازى بأعمالنا؛ أي: يقول صاحب الجنة لإخوانه: هذه قصَّتي وهذا خبري أنا وقريني، ما زلتُ أنا مؤمناً مصدِّقاً، وهو ما زال مكذِّباً منكراً للبعث، حتى متنا، ثم بُعِثْنا، فوصلتُ أنا إلى ما تَرَوْن من النعيم الذي أخْبَرَتْنا به الرسل، وهو لا شكَّ أنَّه قد وَصَلَ إلى العذاب. فهل {أنتُم مُطَّلِعونَ}: لننظرَ إليه فنزدادَ غِبْطَةً وسروراً بما نحن فيه، ويكونَ ذلك رأي عين؟! والظاهرُ من حال أهل الجنة وسرورِ بعضِهِم ببعضٍ وموافقة بعضِهِم بعضاً أنَّهم أجابوه لما قال، وذهبوا تبعاً له للاطِّلاع على قرينه. {فاطَّلَع} فرأى قرينَه {في سواء الجحيم}؛ أي: في وسط العذاب وغمراتِهِ. والعذابُ قد أحاطَ به، فقال له لائماً على حالِهِ وشاكراً لله على نعمتِهِ أنْ نجَّاه من كيدِهِ: {تاللهِ إنْ كِدْتَ لَتُرْدينِ}؛ أي: تهلكني بسبب ما أدخلتَ عليَّ من الشُّبه بزعمك، {ولولا نعمةُ ربِّي}: على أن ثبتني على الإسلام {لكنتُ من المُحْضَرينَ}: في العذاب معك. {أفَما نحنُ بِمَيِّتينَ. إلاَّ مَوْتَتَنا الأولى وما نحنُ بِمُعَذَّبينَ}؟ أي: يقوله المؤمن مبتهجاً بنعمة الله على أهل الجنة بالخلودِ الدائم والسلامة من العذاب. استفهامٌ بمعنى الإثبات والتقرير. وقوله: {فأقبل بعضُهُم على بعضٍ يتساءلون}، وحَذَفَ المعمولَ، والمقامُ مقامُ لذَّةٍ وسرور، فدلَّ ذلك على أنهم يتساءلون بكلِّ ما يتلذَّذون بالتحدُّث به والمسائل التي وقع فيها النزاعُ والإشكالُ، ومن المعلوم أنَّ لَذَّةَ أهل العلم بالتساؤل عن العلم والبحث عنه فوق اللَّذَّاتِ الجاريةِ في أحاديث الدُّنيا؛ فلهم من هذا النوع النصيبُ الوافر، ويحصُلُ لهم من انكشافِ الحقائق العلميَّةِ في الجنة ما لا يمكنُ التعبيرُ عنه.
{50 - 59} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja neema yao na furaha yao kamili kwa vyakula, vinywaji, wenza wao wa kindoa wazuri, na vikao vyao vizuri; akataja kukumbuka kwao wao kwa wao na mazungumzo yao kuhusu mambo yaliyopita,
na kwamba waliendelea na mazungumzo hayo na kuulizana mpaka ikapelekea mmoja wao kusema: "Hakika mimi nilikuwa na mwenza katika dunia, na alikuwa akikanusha kufufuliwa na kunilaumu kwamba mimi niliamini hilo,
na akawa ananiambia: 'Hivyo wewe ni katika wanaosadiki?' Ati tukishakufa, tukawa udongo na mafupa, ndiyo tutalipwa na kuhesabiwa juu ya matendo yetu?" 'Vipi unasadiki jambo hili lisilowezekana, ambalo linashangaza sana, ambalo ni kwamba tutakapokatikakatika tukawa udongo na mifupa, kwamba tutafufuliwa na kurudishwa,
kisha tufanyiwe hesabu na kulipwa juu ya matendo yetu?' Basi huyo mmoja wao akawaambia ndugu zake: Hiki ndicho kisa changu kilichotokea kati yangu na mwenzangu huyo. Mimi bado niliendelea kuamini na kusadiki hayo, naye akaendelea kukadhibisha na kupinga kufufuliwa, mpaka tukafa, tukafufuliwa. Kwa hivyo nikafikia mnayoyaona haya ya neema ambayo Mitume waliyotuambia juu yake, na hapana shaka kuwa ameifikia adhabu yake. Basi "je, nyie mnawaona?" Ili tumwangalie kwa macho na tufurahie zaidi na kuridhika na haya tuliyomo. Kilicho dhahiri hapa kulingana na hali ya watu wa Peponi na furaha yao baina yao na mapatano yao baina yao ni kwamba, walimuitikia katika hayo aliyoyasema, na wakamfuata ili waende wamuone huyo mwenziwe. "Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu." Yaani, katikati ya adhabu na vilindi vyake. Na adhabu ilikuwa imemzunguka. Basi akamwambia akimlaumu kwa hali yake,
na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake za kumuokoa kutokana na vitimbi vyake: "Wallahi!
(Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu) Ulikaribia mno kunipoteza," kwa sababu ya utata na fikira potofu ulizoniingiza kwa madai yako yale. "Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi" kwa kunifanya niwe imara katika Uislamu, "bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa" katika adhabu pamoja nawe. "Je, sisi hatutakufa? Isipokuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa?" Haya aliyasema huyo Muumini akifurahia neema za Mwenyezi Mungu juu ya watu wa Peponi kwa kuwapa uzima wa milele na kuwasalimisha kutokana na adhabu. Na pia ni swali linalomaanisha uthibitisho wa mambo hayo.
Na kauli yake: "Wataelekeana kuulizana wenyewe kwa wenyewe," hapa kimefutwa kile watakachoulizana juu yake, ila mambo yanayotajwa hapa ni ya furaha. Basi hilo likaashiria mambo ambayo wanafurahia kuyazungumzia na masuala ambayo yalikuwa ya mgongano na utata. Inajulikana vyema kwamba raha ya watu wenye elimu katika kuulizana juu ya elimu na kuitafuta inazidi raha iliyopo katika mazungumzo ya kidunia. Watakuwa na sehemu kubwa katika aina hii ya mambo, na watafunuliwa mambo mbalimbali ya uhakika ya kielimu huko Peponi ambayo hayawezi kuelezwa.
#
{60} فلما ذكر تعالى نعيمَ الجنَّة ووَصَفَه بهذه الأوصاف الجميلة؛ مَدَحَه وشوَّقَ العاملين وحثَّهم على العمل له، فقال: {إنَّ هذا لهو الفوزُ العظيمُ}: الذي حصلَ لهم به كلُّ خيرٍ وكلُّ ما تهوى النفوس وتشتهي، واندفَعَ عنهم به كلُّ محذورٍ ومكروهٍ؛ فهل فوزٌ يُطْلَبُ فوقَه، أم هو غايةُ الغاياتِ ونهايةُ النهايات؛ حيث حلَّ عليهم رضا ربِّ الأرض والسماواتِ، وفرحوا بقربه، وتنعَّموا بمعرفتِهِ، واسترّوا برؤيتِهِ، وطربوا لكلامه؟!
{60} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja neema ya Pepo na akaielezea kwa maelezo haya mazuri; akaisifu na akawasisimua wafanyaji matendo na akawahimiza kuifanyia matendo.
Akasema: "Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa," ambako kutokana nako walipata kila la heri na kila linalotamaniwa na nafsi zao, na wakazuilika mbali na kila la kuepukwa na la kuchukiza. Basi je, kuna ushindi mwingine zaidi yake unaoweza kutafutwa? Au huu ndio mwisho wa malengo yote, ambapo walipata kuridhiwa na Mola Mlezi wa ardhi na mbingu, na wakafurahia kuwa karibu naye, na wakapata raha katika kumjua, na wakashiba kwa kumuona, na wakafurahia kuyasikiliza maneno yake?
#
{61} {لمثل هذا فليعمل العاملون}: فهو أحقُّ ما أُنْفِقَتْ فيه نفائسُ الأنفاس، وأولى ما شَمَّرَ إليه العارفون الأكياس، والحسرةُ كلُّ الحسرة أن يمضي على الحازم وقتٌ من أوقاته وهو غير مشتغل بالعمل الذي يقرِّبُ لهذه الدار؛ فكيف إذا كان يسير بخطاياه إلى دار البوار؟!
{61} "Kwa mfano wa haya na watende watendao." Kwani ndilo jambo linalostahiki zaidi, vitu vya thamani zaidi kutolewa kwa ajili yake na linalofailia zaidi wajiandae kwa ajili ya watu wajuao, werevu. Na majuto yote kwamba kipite kipindi kwa mtu mwenye azimio kubwa ilhali hajishughulishi na matendo yanayoweza kumleta karibu na nyumba hii. Basi itakuwaje ikiwa anakwenda na dhambi zake kwenye nyumba ya maangamizo?
{أَذَلِكَ خَيْرٌ نُزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ (62) إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِلظَّالِمِينَ (63) إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ (64) طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ (65) فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ (66) ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِنْ حَمِيمٍ (67) ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ (68) إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ (69) فَهُمْ عَلَى آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ (70) وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الْأَوَّلِينَ (71) وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِمْ مُنْذِرِينَ (72) فَانْظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنْذَرِينَ (73) إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (74)}.
62. Je, kukaribishwa hivi si ndiyo bora, au mti wa Zaqqum? 63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa waliodhulumu. 64. Hakika huo ni mti unaotoka katikati ya Jahannamu. 65. Mashada ya matunda yake kama kwamba ni vichwa vya mashetani. 66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo kwayo. 67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyochemka. 68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu. 69. Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. 70. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao. 71. Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani. 72. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji. 73. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walioonywa. 74. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliohitariwa.
#
{62} {أذلك خير}؛ أي: ذلك النعيم الذي وصفناهُ لأهل الجنَّة خيرٌ أم العذابُ الذي يكون في الجحيم من جميع أصنافِ العذاب؛ فأيُّ الطعامين أولى؟ الطعامُ الذي وُصِفَ في الجنة، {أم} طعامُ أهل النار، وهو {شجرةُ الزَّقُّوم}؟
{62} "Je, kukaribishwa hivi si ndiyo bora" kwa wakazi wa Peponi au adhabu ya kila aina iliyomo ndani ya Jahannamu? Ni chakula kipi kinafaa zaidi? Chakula kilichoelezwa Peponi, "au" chakula cha wakazi wa Motoni, ambacho ni "mti wa Zaqqum"?
#
{63 - 66} {إنا جعلناها فتنةً}؛ أي: عذاباً ونكالاً {للظَّالمينَ}: أنفسهم بالكفر والمعاصي. {إنها شجرةٌ تخرجُ في أصل الجحيم}؛ أي: وسطه؛ فهذا مخرجُها ومعدِنُها؛ شرُّ المعادن وأسوؤها، وشرُّ المغرس يدل على شرِّ الغراس وخسَّته، ولهذا نبَّهنا الله على شرِّها بما ذكر أين تنبُت به وبما ذكر من صفة ثمرتها، وأنها كرؤوس الشياطينِ؛ فلا تسألْ بعد هذا عن طعمها وما تفعلُ في أجوافهم وبطونهم. وليس لهم عنها مندوحةٌ ولا مَعْدِلٌ ، ولهذا قال: {فإنَّهم لآكلونَ منها فمالِئونَ منها البطونَ}: فهذا طعامُ أهل النارِ؛ فبئس الطعامُ طعامُهم.
{63 - 66} "Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa waliodhulumu" kwa ukafiri na maasi. "Hakika huo ni mti unaotoka katikati ya Jahannamu," ambapo ndiyo chanzo chake, chanzo kibaya zaidi na kupanda kuovu zaidi kunakoashiria uovu, kilichopandwa na uduni wake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akatutanabahisha uovu wake kwa kutaja mahali unapomea, na kwa kututajia katika maelezo ya matunda yake, kwamba ni kama vichwa vya mashetani. Basi baada ya hayo, usiulize juu ya ladha yake na kile ambacho unafanya ndani ya miili yao na katika matumbo yao. Hawawezi kuuwacha wakaenda kwingine.
Ndiyo maana akasema: "Basi hakika bila ya shaka hao watakula kwayo, na wajaze matumbo." Hiki ndicho chakula cha wakazi wa Motoni; chakula kibovu zaidi ni chakula chao hiki.
#
{67} ثم ذكر شرابهم، فقال: {ثم إنَّ لهم عليها}؛ أي: على أثر هذا الطعام {لَشَوْباً من حَميم}؛ أي: ماءً حارًّا قد تناهى حرُّه؛ كما قال تعالى: {وإن يَسْتَغيثوا يُغاثوا بماءٍ كالمُهْلِ يَشْوي الوجوهَ بئس الشرابُ وساءتْ مُرْتَفَقاً}، وكما قال تعالى: {وسُقوا ماءً حَميماً فقَطَّعَ أمعاءهم}.
{67} Kisha akataja kinywaji chao,
akasema: "Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyochemka.
" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyotibuka, yatakayowababua nyuso zao.
Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!" Na kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wakinyweshwa maji yanayochemka ya kuwakata matumbo yao?"
#
{68} {ثم إنَّ مَرْجِعَهم}؛ أي: مآلهم ومقرّهم ومأواهم {لإلى الجحيم}: ليذوقوا من عذابه الشديد وحرِّه العظيم ما ليس عليه مزيدٌ من الشقاء.
{68} "Kisha,hakika marejeo yao bila ya shaka," ambayo ndiyo makazi yao, "yatakuwa kwenye Jahannamu." Ili waonje adhabu yake kali na joto lake kubwa, ambayo hakuna dhiki zaidi ya hayo.
#
{69 - 73} كأنه قيل: ما الذي أوْصَلَهم إلى هذه الدار؟ فقال: {إنّهم ألْفَوْا}؛ أي: وجدوا {آباءهم ضالِّينَ. فهم على آثارِهِم يُهْرَعونَ}؛ أي: يسرعون في الضلال، فلم يلتفتوا إلى ما دعتهم إليه الرسلُ ولا إلى ما حَذَّرَتْهم عنه الكتبُ ولا إلى أقوال الناصحين، بل عارضوهم بأنْ قالوا: إنَّا وَجَدْنا آباءنا على أمَّةٍ وإنا على آثارهم مقتدونَ. {ولقد ضلَّ قبلَهم}؛ أي: قبل هؤلاء المخاطبينَ {أكثرُ الأولينَ}: وقليلٌ منهم آمن واهتدى، {ولقد أرْسَلْنا فيهم مُنذِرينَ}: ينذِرونَهم عن غيِّهم وضلالهم، {فانظُرْ كيف كان عاقبةُ المنذَرين}: كانت عاقبتهم الهلاك والخزي والفضيحة؛ فليحذرْ هؤلاء أن يستمرُّوا على ضلالهم فيصيبهم مثلُ ما أصابهم.
{69 - 73} Ni kana kwamba ilisemwa: Ni nini kilichowafikisha katika nyumba hii? Akasema: "Hakika waliwakuta baba zao wamepotea. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao." Na hawakuzingatia yale waliyowaitia Mitume, wala yale ambayo vitabu viliwaonya dhidi yake, wala maneno ya washauri.
Bali waliyapinga hayo kwa kusema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao. "Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao" hawa wanaoongeleshwa, "wengi wa watu wa zamani," na ni wachache tu miongoni mwao ndio walioongoka. "Na Sisi hakika tuliwatumia waonyaji" ili wawaonye juu ya kukengeuka kwao na upotovu wao. "Basi, hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wale walioonywa." Mwisho wao ulikuwa maangamio, hizaya na fedheha. Basi na watahadhari watu hawa wasije wakaendelea katika upotofu wao, wakaja kupatwa na yale yale yaliyowapata hao.
#
{74} ولما كان المُنْذَرون ليسوا كلهم ضالِّين، بل منهم مَنْ آمن وأخلصَ الدين لله؛ استثناهُمُ الله من الهلاك، فقال: {إلاَّ عبادَ الله المخلَصين}؛ أي: الذين أخْلَصَهم الله وخَصَّهم برحمتِهِ لإخلاصهم؛ فإنَّ عواقِبَهم صارت حميدةً.
{74} Kwa kuwa wale walioonywa hawakupotea wote, bali miongoni mwao wapo wale walioamini na wakamkusudia Mwenyezi Mungu pekee katika Dini, Mwenyezi Mungu akawatenga mbali na suala la maangamizo,
akasema: "Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliohitariwa." Yaani, wale ambao Mwenyezi Mungu aliwachagua na akawapa rehema yake kwa sababu wao pia walimkusudia Yeye tu, basi hao mwisho wao utakuwa wa kusifiwa.
Kisha akataja mfano wa mwisho wa mataifa waliokadhibisha, akasema:
{وَلَقَدْ نَادَانَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ (75) وَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ (76) وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُ هُمُ الْبَاقِينَ (77) وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ (78) سَلَامٌ عَلَى نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ (79) إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (80) إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ (81) ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ (82)}.
75. Na hakika Nuhu alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji. 76. Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa. 77. Na tuliwajaalia dhuria zake ndio wenye kubakia. 78. Na tukamwachia
(sifa njema) kwa waliokuja baadaye. 79. Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote! 80. Kwa hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema. 81. Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini. 82. Kisha tukawazamisha wale wengine.
#
{75 - 82} يخبر تعالى عن عبدِهِ ورسولِهِ نوح عليه السلام أول الرسل أنَّه لما دعا قومه إلى الله تلك المدةَ الطويلة، فلم يزدهم دعاؤُهُ إلاَّ فراراً؛ أنه نادى ربَّه، فقال: {ربِّ لا تَذَرْ على الأرضِ من الكافرين ديّاراً ... } الآية، وقال: {ربِّ انصُرْني على القوم المُفْسِدينَ}. فاستجاب اللهُ له، ومدح تعالى نفسه، فقال: {فَلَنِعْمَ المجيبونَ}: لدعاء الداعينَ وسماع تَبَتُّلِهِم وتضرُّعهم، أجابه إجابةً طابقتْ ما سأل، نَجَّاه وأهلَه من الكرب العظيم، وأغرقَ جميع الكافرين، وأبقى نسلَه وذُرِّيَّته متسلسلين؛ فجميع الناس من ذُرِّيَّة نوح عليه السلام، وجعل له ثناءً حسناً مستمرًّا إلى وقت الآخرين، وذلك لأنَّه محسنٌ في عبادة الخالق، محسنٌ إلى الخلق، وهذه سنَّته تعالى في المحسنين؛ أنْ يَنْشُرَ لهم من الثناء على حسب إحسانهم، ودلَّ قولُه: {إنَّه من عبادِنا المؤمنينَ}: أنَّ الإيمانَ أرفعُ منازل العباد، وأنَّه مشتملٌ على جميع شرائع الدِّين وأصولِهِ وفروعِهِ؛ لأنَّ الله مَدَحَ به خواصَّ خلقِهِ.
{75 - 82} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu mja wake na Mtume wake, Nuhu, amani iwe juu yake, Mitume wa kwanza, kwamba alipowalingania watu wake kwa Mwenyezi Mungu kwa muda huo mrefu,
lakini wito wake haukuwazidisha isipokuwa kukimbia; kwamba akamwomba Mola wake Mlezi na akasema: "Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkazi wake yeyote katika makafiri..." hadi mwisho wa aya.
Na akasema: "Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru na watu mafisadi hawa!" Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia. Na Mwenyezi Mungu akajisifu,
akasema: "Na Sisi ni bora wa waitikiaji" dua za waombaji na kusikia dua zao na unyenyekevu wao kwetu. Basi Mwenyezi Mungu akamjibu kwa jawabu linalolingana na alivyoomba. Alimuokoa yeye na familia yake kutokana na msiba mkubwa, akawazamisha makafiri wote, na akakibakisha kizazi chake na kizazi kikaendelea kuzaana mfululizo. Basi watu wote ni kizazi cha Nuhu, amani imshukie. Na pia akamjaalia sifa njema zinazoendelea mpaka zama za watu wa mwisho, kwa sababu alikuwa mwema katika kumuabudu Muumba, mwema kwa viumbe. Hii ndiyo desturi yake Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusiana na wanaofanya wema; kuwaenezea sifa njema kulingana na wema wao.
Na kauli yake: "Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini," inaashiria kuwa imani ndiyo daraja ya juu kabisa ya ibada na kwamba inajumuisha sheria zote za Dini, misingi yake na matawi yake,kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwasifu kwayo waja wake maalumu.
{وَإِنَّ مِنْ شِيعَتِهِ لَإِبْرَاهِيمَ (83) إِذْ جَاءَ رَبَّهُ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ (84) إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَاذَا تَعْبُدُونَ (85) أَئِفْكًا آلِهَةً دُونَ اللَّهِ تُرِيدُونَ (86) فَمَا ظَنُّكُمْ بِرَبِّ الْعَالَمِينَ (87) فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ (88) فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ (89) فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ (90) فَرَاغَ إِلَى آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ (91) مَا لَكُمْ لَا تَنْطِقُونَ (92) فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ (93) فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ (94) قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ (95) وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ (96) قَالُوا ابْنُوا لَهُ بُنْيَانًا فَأَلْقُوهُ فِي الْجَحِيمِ (97) فَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَسْفَلِينَ (98) وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَى رَبِّي سَيَهْدِينِ (99) رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ (100) فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ (101) فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَابُنَيَّ إِنِّي أَرَى فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانْظُرْ مَاذَا تَرَى قَالَ يَاأَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ سَتَجِدُنِي إِنْ شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ (102) فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ (103) وَنَادَيْنَاهُ أَنْ يَاإِبْرَاهِيمُ (104) قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (105) إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ (106) وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ (107) وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ (108) سَلَامٌ عَلَى إِبْرَاهِيمَ (109) كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (110) إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ (111) وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِنَ الصَّالِحِينَ (112) وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَى إِسْحَاقَ وَمِنْ ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِنَفْسِهِ مُبِينٌ (113)}.
83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake. 84. Alipomjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima. 85.
Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini? 86. Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu? 87. Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote? 88. Kisha akapiga jicho kutazama nyota. 89.
Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa! 90. Nao wakamwacha, wakampa kisogo. 91. Basi akaiendea miungu yao kwa siri,
akaiambia: Mbona hamli? 92. Mna nini hata hamsemi? 93. Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia. 94. Basi wakamjia upesi upesi. 95.
Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyovichonga wenyewe? 96. Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuumbeni nyinyi na hivyo mnavyovifanya! 97.
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! 98. Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini zaidi. 99.
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa. 100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema. 101. Basi tukambashiria mwana aliye mpole. 102. Basi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye,
alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe,
waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Insha Allah
(Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri. 103. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji. 104.
Tulimwita: Ewe Ibrahim! 105. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaotenda mema. 106. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri. 107. Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu. 108. Na tukamwachia
(sifa njema) kwa watu waliokuja baadaye. 109. Iwe salama kwa Ibrahim! 110. Hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema. 111. Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini. 112. Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. 113. Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuria zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.
#
{83 - 84}؛ أي: وإنَّ من شيعة نوح عليه السلام ومَنْ هو على طريقتِهِ في النبوَّة والرسالة ودعوة الخلقِ إلى اللَّه وإجابةِ الدُّعاء إبراهيم الخليل عليه السلام. {إذْ جاء ربَّه بقلبٍ سليم}: من الشركِ والشُّبَهِ والشَّهَوات المانعة من تصوُّر الحقِّ والعمل به. وإذا كان قلبُ العبدِ سليماً؛ سَلِمَ من كلِّ شرٍّ، وحصل له كلُّ خيرٍ.
{83 - 84}; Yaani, miongoni mwa wale waliokuwa katika kundi la Nuhu, amani iwe juu yake, katika njia ya unabii wake, utume wake na kuwalingania viumbe kwa Mwenyezi Mungu, na kujibiwa dua yake ni Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yake. "Alipomjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima" kutokana na ushirikina, dhana potofu na matamanio ambayo yanamzuilia mtu kuona haki na kuifanyia kazi. Kwani ikiwa moyo wa mja ni mzima, basi anasalimika kutokana na uovu wote na anapata heri yote.
#
{85 - 87} ومن سلامته أنه سليمٌ من غشِّ الخلق وحَسَدِهم وغير ذلك من مساوئ الأخلاق، ولهذا نصح الخلق في الله، وبدأ بأبيه وقومِهِ، فقال: {إذْ قال لأبيه وقومِهِ ماذا تَعْبُدونَ}؟ هذا استفهامٌ على وجه الإنكار وإلزامٌ لهم بالحجة. {أإفكاً آلهةً دون الله تريدونَ}؟ أي: أتعبدون من دون آلهة كذباً ليست بآلهة، ولا تصلُحُ للعبادة؟! {فما ظنُّكم بربِّ العالمين}: أن يفعل بكم وقد عبدتُم معه غيره؟! وهذا ترهيبٌ لهم بالجزاء بالعقابِ على الإقامة على شركهم، وما الذي ظننتُم بربِّ العالمين من النقص حتى جعلتُم له أنداداً وشركاء؟!
{85 - 87} Na katika uzima wake ni kwamba ulikuwa mzima
(salama) kutokana na kuwadanganya viumbe na kuwahusudia, na maovu mengineyo ya kimaadili.
"Alipomwambia baba yake na watu wake: 'Mnaabudu nini?'" Hili ni swali lililokuja kwa mbinu ya kukanusha hayo wanayofanya na kuwafanya wakiri na kuikubali hoja yake. "Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?" Yaani, je, mnaabudu badala ya Mwenyezi Mungu miungu ya uwongo ambayo hata si miungu na isiyofaa kuabudiwa? "Kwani mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?" Kuwa atawafanyia nini nyinyi mnaomuabudu asiyekuwa Yeye? Hili ni tishio kwao kwamba watalipwa adhabu ya kubakia kwa sababu ya kudumu kwao katika ushirikina wao. Na hakika ni upungufu gani mliomdhania Mola Mlezi wa walimwengu ndiyo mkamfanyia wenza na washirika?
#
{88 - 93} فأراد عليه السلام أن يكسِرَ أصنامهم ويتمكَّن من ذلك، فانتهز الفرصةَ في حين غفلةٍ منهم لما ذهبوا إلى عيدٍ من أعيادهم، فخرج معهم، {فَنَظَرَ نظرةً في النجوم. فقال: إني سقيمٌ}: في الحديث الصحيح: «لم يكذبْ إبراهيمُ عليه السلام إلاَّ ثلاثَ كذباتٍ: قولُهُ: إني سقيمٌ، وقوله: بل فعله كبيرُهُم هذا، وقوله عن زوجته: إنها أختي». والقصدُ أنَّه تخلَّف عنهم ليتمَّ له الكيدُ بآلهتهم. ولهذا {تولَّوا عنه مدبِرينَ}، فلما وجد الفرصة؛ {فراغ إلى آلهتهم}؛ أي: أسرع إليها على وجه الخفية والمراوغة، {فقال} متهكِّماً بها: {ألا تأكُلونَ. ما لكم لا تنطقونَ}؛ أي: فكيف يليقُ أن تُعْبَدَ وهي أنقص من الحيوانات التي تأكُلُ و تُكلِّم، وهذه جمادٌ لا تأكل ولا تُكلِّم؟! {فراغَ عليهم ضرباً باليمين}؛ أي: جعل يضربها بقوَّتِهِ ونشاطِهِ حتى جعلها جذاذاً؛ إلاَّ كبيراً لهم لعلَّهم إليه يرجِعون.
{88 - 93} Basi yeye, amani iwe juu yake, akataka kuyavunja masanamu yao na aweze kufanya hivyo. Kwa hivyo, akaichukua fursa hiyo ilhali hawajui walipokuwa wamekwenda kwenye moja ya sikukuu zao, naye pia akatoka pamoja nao. "Kisha akapiga jicho kutazama nyota.
Akasema: 'Hakika mimi ni mgonjwa!'" Imesimuliwa katika hadithi sahihi kuwa: “Ibrahim, amani iwe juu yake,
hakusema uongo ila uongo tatu: kauli yake: 'Mimi ni mgonjwa,
' na kauli yake: 'Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao,
' na kauli yake kuhusu mkewe: 'Yeye ni dada yangu.'" Makusudio ya kufanya hivyo ni ili asalie nyuma yao aweze kukamilisha njama yake dhidi ya miungu yao hiyo. Ndiyo maana "wakamwacha, wakampa kisogo wakienda." Basi alipoipata nafasi hiyo, "akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia" kwa njia ya kejeli "Mbona hamli? Kwa nini hamuongei?" Yaani, vipi inafaa kuabudiwa ilhali ni mipungufu hata kuliko wanyama wanaokula na kuzungumza, na hali hiyo ni vitu visivyo na uhai ambavyo havili wala havisemi? "Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia." Na akaivunja vipande vipande ila kubwa lao, ili wao walirudie.
#
{94 - 96} {فأقبلوا إليه يزِفُّونَ}؛ أي: يسرعون ويُهْرَعون؛ يريدون أن يوقعوا به بعد ما بحثوا و {قالوا: مَنْ فَعَلَ هذا بآلهتنا إنَّه لمن الظالمين}؟ {وقيل لهم: سمِعْنا فتى يذكُرُهم يُقالُ له: إبراهيمُ}، يقول {تالله لأكيدنَّ أصنامَكُم بعدَ أن تُوَلُّوا مدبِرين}. فوبَّخوه ولاموه، فقال: {بل فَعَلَه كبيرُهم هذا فاسألوهم إن كانوا ينطِقون. فرجَعَوا إلى أنفسِهِم فقالوا إنَّكم أنتم الظالمونَ. ثم نُكِسوا على رؤوسِهِم لقد علمتَ ما هؤلاء ينطِقون. قال أفتعبدُونَ من دون اللهِ ما لا ينفعكم شيئاً ولا يضرُّكم ... } الآية، و {قال} هنا: {أتعبدُونَ ما تَنْحِتونَ}؛ أي: تنحِتونه بأيديكم وتصنعونه؛ فكيف تعبُدونهم وأنتم الذين صنعتُموهم، وتتركون الإخلاصَ لله الذي {خَلَقَكُم وما تعمَلون}؟!
{94 - 96} "Basi wakamjia upesi upesi" wakitaka kumuadhibu baada ya kuchunguza na wakasema: "Ni nani aliyeifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni katika waliodhulumu.
" Na wakaambiwa: "Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim,
" na pia alisema: "Na Wallahi!
(Naapa kwa jina la Mweneyzi Mungu) Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya nyinyi mkishageuka kwenda zenu." Basi wakamkemea na kumlaumu,
naye akasema: “Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao." Basi waulizeni ikiwa wanaweza kutamka. Basi wakajirudi nafsi zao,
wakasema: 'Hakika nyinyi mlikuwa madhalimu!' Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: 'Wewe unajua kwamba hawa hawasemi.
' Akasema: 'Basi nyinyi mnawaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, wasiokufaeni kitu wala kukudhuruni...' Hadi mwisho wa aya.
Na hapa akasema: "Hivyo mnaviabudu vitu mnavyovichonga wenyewe" kwa mikono yenu na kuviunda? Vipi mnaviabudu ilhali nyinyi ndio mlioviunda, na mnaacha kumkusudia Mwenyezi Mungu "aliyekuumbeni nyinyi na hivyo mnavyovifanya!"
#
{97 - 98} {قالوا ابنوا له بنياناً}؛ أي: عالياً مرتفعاً وأوقِدوا فيه النارَ، {فألقوه في الجحيم}: جزاءً على ما فعل من تكسير آلهتهم، وأرادوا {به كيداً}: ليقتُلوه أشنعَ قِتْلَةٍ؛ {فجعلناهُمُ الأسفلينَ}: ردَّ الله كيدَهم في نُحورهم، وجَعَلَ النار على إبراهيم برداً وسلاماً.
{97 - 98} "Wakasema: Mjengeeni mjengo" ulioinuka juu kabisa kisha washeni moto ndani yake, "na kisha mtupeni motoni humo!" Yawe malipo yake kwa yale aliyoyafanya ya kuivunja miungu yao. Basi walitaka kumfanyia "vitimbi" ili wamuue vibaya mno "lakini tukawafanya wao ndio wa chini zaidi." Mwenyezi Mungu akawageuzia vitimbi vyao hivyo kooni mwao, na akaufanya Moto kuwa ni baridi na salama kwa Ibrahim.
#
{99} {و} لما فعلوا فيه هذا الفعل، وأقام عليهم الحجة، وأعذر منهم؛ {قال إنِّي ذاهبٌ إلى ربِّي}؛ أي: مهاجر إليه، قاصدٌ إلى الأرض المباركة أرض الشام {سيهدينِ}: يدلُّني على ما فيه الخير لي من أمر ديني ودنياي. وقال في الآية الأخرى: {وأعْتَزِلُكم وما تَدْعونَ من دونِ الله وأدْعو ربِّي عسى ألاَّ أكونَ بِدُعاءِ ربي شَقِيًّا}.
{99} "Na" walipomfanyia kitendo hicho, naye akawasimamishia hoja na akapata udhuru wa kutolaumiwa juu yao.
"Akasema: Hakika mimi ninahama, ninakwenda kwa Mola wangu Mlezi," huko kwenye ardhi iliyobarikiwa, ardhi ya Sham. "Yeye ataniongoa" nifikie yenye heri kwangu katika mambo ya dini yangu na ya dunia yangu.
Na akasema katika Aya nyingine: “Nami ninajitenga mbali nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi, haswa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi."
#
{100} {ربِّ هَبْ لي}: ولداً يكون {من الصالحين}، وذلك عندما أيس من قومه، ولم يَرَ فيهم خيراً؛ دعا الله أن يَهَبَ له غلاماً صالحاً ينفع الله به في حياتِهِ وبعد مماتِهِ.
{100} "Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie" mwana "aliye miongoni mwa watenda mema." Na hapo ni wakati alipokata tamaa na watu wake, wala hakuona heri yoyote kwao. Kwa hivyo, akamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie mtoto mwema ambaye Mwenyezi Mungu atanufaika kwake wakati wa uhai wa Ibrahim na baada ya kifo chake.
#
{101} فاستجابَ اللَّه له وقال: {فبشَّرناه بغلام حَليم}: وهذا إسماعيلُ عليه السلام بلا شكٍّ؛ فإنَّه ذكر بعدَه البشارة بإسحاقَ، ولأنَّ الله تعالى قال في بُشراه بإسحاقَ: {فبشَّرنْاها بإسحاقَ ومِن وراء إسحاقَ يعقوبَ}: فدلَّ على أنَّ إسحاقَ غير الذبيح، ووَصَفَ الله إسماعيلَ عليه السلام بالحلم، وهو يتضمَّنُ الصبرَ وحسنَ الخُلُق وسَعَةَ الصدر والعفو عَمَّنْ جنى.
{101} Mwenyezi Mungu akamuitikia na akasema: "Basi tukambashiria mwana aliye mpole," ambaye ni Ismail, amani iwe juu yake, bila ya shaka yoyote. Kwa sababu alitaja baada yake bishara nyingine ya Is-haq, na kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema katika bishara yake juu ya Is-
haq: "Basi tukambashiria
(kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub." Haya yakaashiria kwamba Is-haq si yule ambaye Ibrahim alitaka kumchinja. Na Mwenyezi Mungu alimuelezea Ismail, amani iwe juu yake, kwamba ni mpole, na hilo linajumuisha subira, maadili mema, ukunjufu wa kifua na kumsamahe anayemkosea.
#
{102} {فلمَّا بَلَغَ الغلامُ معه السعيَ}؛ أي: أدرك أن يسعى معه، وبلغ سنًّا يكون في الغالب أحبَّ ما يكون لوالديه؛ قد ذهبتْ مشقَّتُه وأقبلتْ منفعتُهُ، فقال له إبراهيمُ عليه السلام: {إنِّي أرى في المنام أنِّي أذْبَحُكَ}؛ أي: قد رأيت في النوم والرؤيا أنَّ الله يأمُرُني بِذَبْحِكَ، ورؤيا الأنبياءِ وحيٌ. {فانْظُرْ ماذا ترى}؛ فإنَّ أمر الله تعالى لا بدَّ من تنفيذِهِ، فقال إسماعيلُ صابراً محتسباً مرضياً لربِّه وبارًّا بوالده: {يا أبتِ افْعَلْ ما تُؤْمَرْ}؛ أي: امضِ لما أمَرَكَ الله، {سَتَجِدُني إن شاء الله من الصابرينَ}: أخبر أباه أنَّه موطِّنٌ نفسَه على الصبر، وقَرَنَ ذلك بمشيئة الله تعالى؛ لأنَّه لا يكون شيءٌ بدون مشيئةِ الله.
{102} "Basi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye," katika umri ambao kwa kawaida huwa anapendeza zaidi kwa wazazi wake, ambapo ugumu wa kumlea huwa umepunguka na manufaa yake yakaanza kutokea, basi Ibrahim, amani iwe juu yake,
akamwambia: "Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja," kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na ndoto za Manabii ni ufunuo. Basi angalia wewe, waonaje?" Kwa maana amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni lazima itekelezwe. Kwa hivyo Ismail akasema kwa uvumilivu na kutumaini malipo ya Mwenyezi Mungu,
huku amemridhia Mola wake Mlezi na kumfanyia wema baba yake: "Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Inshallah Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri." Kwa sababu hakuna kinachotokea bila mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
#
{103} {فلمَّا أسْلَما}؛ أي: إبراهيم وابنه إسماعيل: إبراهيم جازماً بقتل ابنه وثمرةِ فؤادِهِ امتثالاً لأمر ربِّه وخوفاً من عقابه، والابن قد وطَّن نفسه على الصبر، وهانتْ عليه في طاعة ربِّه ورضا والده، {وَتَلَّه للجبينِ}؛ أي: تلَّ إبراهيمُ إسماعيلَ على جبينِهِ لِيُضْجِعَه فيذبَحَه، وقد انكبَّ لوجهِهِ؛ لئلاَّ ينظرَ وقت الذبح إلى وجهِهِ.
{103} "Basi wote wawili walipojisalimisha;" yaani, Ibrahim na mwanawe, Ismail huku Ibrahim ameazimia kumuua mwanawe na matunda ya moyo wake kwa kufuata amri ya Mola wake Mlezi na kwa kuhofia kuadhabiwa, naye mwanawe ambaye alikuwa ameshaamua kusubiri, na hilo likawa jepesi kwa ajili ya kumtii Mola wake Mlezi na kumridhisha baba yake. "Na" Ibrahim akamlaza" Ismail "juu ya kipaji" na ili asiuangalie uso wake wakati wa kumchinja.
#
{104 - 105} {وناديناه}: في تلك الحال المزعجة والأمر المدهش: {أن يا إبراهيمُ. قد صَدَّقْتَ الرؤيا}؛ أي: قد فعلتَ ما أُمِرْتَ به؛ فإنَّك وطَّنْتَ نفسك على ذلك، وفعلتَ كلَّ سبب، ولم يبقَ إلاَّ إمرار السكين على حلقه. {إنَّا كذلك نَجْزي المحسنين}: في عبادتنا، المقدِّمين رضانا على شهواتِ أنفسهم.
{104 - 105} "Tulimwita" katika hali hiyo ya kusumbua na katika jambo hilo la kustaajabisha: 'Ewe Ibrahim! Umekwisha itimiliza ndoto." Yaani umeshafanya uliyoagizwa. Kwani tayari ulishaamua kufanya hivyo, na ukaifanya nafsi yako kukubali hilo, na ukafanya visababu vyote, na hakuna kilichobakia isipokuwa kupitisha kisu kwenye koo lake. "Hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaotenda mema" katika ibada zetu, wale ambao wanatanguliza ridha yetu mbele ya matamanio yao.
#
{106} {إنَّ هذا}: الذي امتحنَّا به إبراهيمَ عليه السلام {لهو البَلاءُ المُبينُ}؛ أي: الواضح الذي تَبَيَّنَ به صفاءُ إبراهيم وكمالُ محبَّتِهِ لربِّه وخلَّتِهِ؛ فإن إسماعيلَ عليه الصلاة (والسلام) لما وَهَبَهُ الله لإبراهيم؛ أحبَّه حبًّا شديداً، وهو خليل الرحمن، والخلَّة أعلى أنواع المحبة، وهو منصبٌ لا يقبل المشاركة، ويقتضي أن تكونَ جميعُ أجزاء القلب متعلقةً بالمحبوب، فلما تعلقتْ شعبةٌ من شُعَبِ قلبِهِ بابنه إسماعيلَ؛ أراد الله تعالى أن يُصَفِّي وُدَّه ويختبرَ خُلَّتَهَ، فأمره أن يذبح مَنْ زاحَمَ حبُّه حبَّ ربِّه، فلما قَدَّمَ حبَّ الله وآثره على هواه وعزم على ذبحِهِ وزال ما في القلب من المزاحم، بقي الذبحُ لا فائدة فيه؛ فلهذا قال: {إنَّ هذا لهو البلاءُ المبينُ}.
{106} "Hakika haya" tuliyomtahini kwayo Ibrahim, amani iwe juu yake, "ndiyo majaribio yaliyo dhahiri," ambayo kwayo ulibainika utakaso wa Ibrahim, ukamilifu wa mapenzi yake kwa Mola wake Mlezi na kwamba ni rafiki wake mwandani. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alipomtunuku Ibrahim mwana huyu Ismail, rehema na amani ziwe juu yake, akampenda sana ilhali Ibrahim alikuwa ndiye rafiki mwandani wa Mwingi wa Rehema, ambayo ndiyo daraja ya juu kabisa ya mapenzi na ambayo ni nafasi isiyokubali ushirika kiasi kwamba sehemu zote za moyo zinapaswa kushikamana na mpendwa tu. Basi pindi sehemu moja katika sehemu za moyo wake ziliposhikamana na mwanawe Ismail,Mwenyezi Mungu Mtukufu akataka kuutakasa upendo wake na kuujaribu urafiki wake wa ndani huu. Kwa hivyo akamuamuru amchinje yule ambaye mapenzi yake kwake yalishindana na mapenzi yake kwa Mola wake Mlezi. Na alipoyatanguliza mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuyapendelea kuliko matamanio yake na akaazimia kumchinja, mashindano hayo ya moyoni mwake yakaondoka, basi kukawa kuchinja huko hakuna faida.
Ndiyo maana akasema: "Hakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri."
#
{107} {وفديناه بِذبْحٍ عظيم}؛ أي: صار بَدَلَه ذبحٌ من الغنم عظيمٌ ذبحه إبراهيم، فكان عظيماً: من جهة أنَّه كان فداء لإسماعيلَ، ومن جهة أنَّه من جملة العبادات الجليلة، ومن جهة أنه كان قرباناً وسنةً إلى يوم القيامةِ.
{107} "Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu tukufu," yaani kondoo ambaye Ibrahim alimchinja badala yake. Na akawa dhabihu tukufu kwa kuzingatia kwamba alikuwa fidia ya Ismail, na miongoni mwa ibada kubwa, na kwamba ilikuwa ni sadaka na sunna mpaka Siku ya Kiyama.
#
{108 - 109} {وتركنا عليه في الآخرين. سلام على إبراهيم}؛ أي: وأبقينا عليه ثناءً صادقاً في الآخرين؛ كما كان في الأولين؛ فكل وقت بعد إبراهيم عليه السلام؛ فإنَّه فيه محبوبٌ معظَّم مثنى عليه. {سلامٌ على إبراهيم}؛ أي: تحية عليه؛ كقوله: {قُل الحمدُ لله وسلامٌ على عبادِهِ الذين اصطفى}.
{108 - 109} "Na tukamwachia
(sifa njema) kwa watu waliokuja baadaye. Iwe salama kwa Ibrahim!" Kwani Ibrahim, amani iwe juu yake, anapendwa, anaheshimiwa, na kusifiwa katika zama zote.
"Iwe salama kwa Ibrahim!" Ni kama kauli yake: "Sema: Alhamdu Lillahi!
(Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu) Na amani ishuke juu ya waja wake aliowateua. Je, Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanaowashirikisha naye?"
#
{110} {إنَّا كذلك نجزي المحسنين}: في عبادة الله ومعاملة خلقِهِ أن نُفَرِّجَ عنهم الشدائدَ، ونَجْعَلَ لهم العاقبة والثناء الحسن.
{110} "Hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema" katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na katika kuamiliana na viumbe vyake, kwamba tunawaondolea dhiki na tunawapa mwisho mwema na sifa njema.
#
{111} {إنَّه من عبادِنا المؤمنينَ}: بما أمر الله بالإيمان به، الذين بَلَغَ بهم الإيمانُ إلى درجة اليقين؛ كما قال تعالى: {وكذلك نُري إبراهيمَ مَلَكوتَ السمواتِ والأرضِ وليكون من الموقنين}.
{111} "Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini" yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuyaamini, wale ambao imani yao ilifikia daraja ya yakini.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kadhalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini."
#
{112} {وبَشَّرْناهُ بإسحاقَ نَبِيًّا من الصالحين}: هذه البشارة الثانية بإسحاقَ؛ الذي من ورائِهِ يعقوبَ، فَبُشِّرَ بوجوده وبقائه ووجود ذُرِّيَّتِهِ وكونه نبيًّا من الصالحين؛ فهي بشاراتٌ متعدِّدة.
{112} "Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema." Hii ni bishara ya pili aliyopewa Ibrahim; yaani, kupata mwana aitwaye Is-haq, ambaye nyuma yake atakuja Yakub. Hapo akawa amebashiriwa kuzaliwa kwake, kubakia kwake, kupatikana kwa kizazi chake, na kwamba atakuwa Nabii miongoni mwa watu wema. Hizi ni bishara njema mbalimbali.
#
{113} {وبارَكْنا عليه وعلى إسحاقَ}؛ أي: أنْزَلْنا عليهما البركةَ التي هي النمو والزيادة في علمهما وعملهما وذريتهما، فنشر الله من ذُرِّيَّتِهِما ثلاث أمم عظيمة: أمة العرب من ذُرِّيَّةِ إسماعيلَ، وأمة بني إسرائيل، وأمة الروم من ذُرِّيَّةِ إسحاقَ. {ومن ذُرِّيَّتِهِما محسنٌ وظالمٌ لنفسِهِ مبينٌ}؛ أي: منهم الصالح والطالح، والعادل والظالم، الذي تبيَّن ظلمُهُ بكفرِهِ وشركِهِ، ولعل هذا من باب دفع الإيهام؛ فإنَّه لمَّا قال: {وبارَكْنا عليه وعلى إسحاقَ}؛ اقتضى ذلك البركة في ذُرِّيَّتِهِما، وأنَّ من تمام البركة أن تكون الذُّرِّيَّة كلُّهم محسنين، فأخبر الله تعالى أنَّ منهم محسناً وظالماً. والله أعلم.
{113} "Tukambarikia yeye na Is-haqa" katika elimu yao, matendo yao na vizazi vyao.
Basi Mwenyezi Mungu akaeneza mataifa matatu makubwa kutokana na dhuria zao: Waarabu kutokana na dhuria ya Ismail, Wana wa Israeli na taifa la Kirumi kutokana na kizazi cha Is-haq. "Na miongoni mwa dhuria zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi." Yaani, miongoni mwao wapo wema na wabaya, waadilifu na madhalimu, ambao dhuluma yao imedhihirika kwa ukafiri wao na ushirikina wao.
Na pengine hii ni kwa ajili ya kuondoa dhana mbaya aliposema: "Tukambarikia yeye na Is-haqa." Kwamba hilo linamaanisha kwamba vizazi vyao pia vimebarikiwa na kwamba wao wote ni watu wema. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akatujulisha kwamba miongoni mwao wapo watenda mema na madhalimu. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
{وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَى مُوسَى وَهَارُونَ (114) وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ (115) وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ (116) وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ (117) وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ (118) وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الْآخِرِينَ (119) سَلَامٌ عَلَى مُوسَى وَهَارُونَ (120) إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (121) إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ (122)}.
114. Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni. 115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa. 116. Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda. 117. Na tukawapa wawili hao Kitabu kinachobainisha. 118. Na tukawaongoa kwenye njia iliyonyooka. 119. Na tukawaachia
(sifa njema) katika watu waliokuja baadaye. 120. Iwe salama kwa Musa na Haruni! 121. Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema. 122. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walioamini.
#
{114 - 122} يذكُرُ تعالى منَّته على عبديه ورسوليه موسى وهارون ابني عمران بالنبوَّة والرسالة والدعوة إلى الله تعالى، ونجاتهما وقومهما من عدوِّهما فرعون، ونصرهما عليه، حتى أغرقه الله وهم ينظرون، وإنزال الله عليهما الكتاب المستَبين، وهو التوراة التي فيها الأحكام والمواعظُ وتفصيلُ كلِّ شيء، وأنَّ الله هداهما الصراطَ المستقيم؛ بأنْ شَرَعَ لهما ديناً ذا أحكام وشرائع مستقيمةٍ موصلةٍ إلى الله، ومَنَّ عليهما بسلوكِهِ. {وتَرَكْنا عليهما في الآخرين. سلامٌ على موسى وهارونَ}؛ أي: أبقى عليهما ثناء حسناً وتحيَّةً في الآخرين، ومن باب أولى وأحرى في الأوَّلين. {إنَّا كذلك نَجْزي المحسنين. إنَّهما من عبادِنا المؤمنينَ}.
{114 - 122} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja neema zake kwa waja wake na Mitume wake - Musa na Harun, na wana wa Imran kwa kuwapa Unabii, Utume, kulingania kwa Mwenyezi Mungu, kuwaokoa wao na watu wao kutoka kwa adui yao Firauni na kuwapa ushindi dhidi yao mpaka Mwenyezi Mungu akamzamisha ilhali wanatazama. Pia Mwenyezi Mungu akawateremshia Kitabu kinachobainisha ambacho ni Taurati, ambayo ndani yake kuna hukumu, mawaidha na maelezo ya kina ya kila kitu. Na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaongoa kwenye njia iliyonyooka kwa kuwawekea dini yenye hukumu na sheria zilizonyooka zenye kufikisha kwa Mwenyezi Mungu, na akawawezesha kuifuata. "Na tukawaachia
(sifa njema) katika watu waliokuja baadaye. Iwe salama kwa Musa na Haruni!" Yaani aliwafanya wasifiwe katika watakaokuja baadaye, kwa hivyo kusifiwa kwao katika waliotangulia ni kwingi zaidi. "Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walioamini."
{وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ (123) إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَلَا تَتَّقُونَ (124) أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ (125) اللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ (126) فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ (127) إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (128) وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ (129) سَلَامٌ عَلَى إِلْ يَاسِينَ (130) إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (131) إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ (132)}.
123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume. 124.
Alipowaambia watu wake: Hamumchi Mungu? 125. Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji. 126. Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani? 127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa. 128. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa. 129. Na tumemwachia
(sifa nzuri) kwa waliokuja baadaye. 130. Iwe salama kwa Ilyas. 131. Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema. 132. Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini.
#
{123 - 132} يمدحُ تعالى عبدَه ورسولَه إلياس عليه الصلاةُ والسلام بالنبوَّةِ والرسالة والدَّعوة إلى الله، وأنَّه أمر قومَه بالتَّقوى وعبادة الله وحدَه، ونهاهم عن عبادَتِهِم صنماً لهم يُقالُ له: بعلٌ، وتركِهِم عبادَة الله الذي خَلَقَ الخلقَ، وأحسنَ خَلْقَهم وربَّاهم فأحسنَ تربِيتهم، وأدرَّ عليهم النِّعَمَ الظاهرة والباطنة، وأنَّكم كيف تركتُم عبادةَ مَنْ هذا شأنُه إلى عبادة صنم لا يضرُّ ولا ينفع ولا يخلُق ولا يرزُقُ، بل لا يأكل ولا يتكلَّم، وهل هذا إلاَّ من أعظم الضلال والسَّفه والغيِّ. {فكذَّبوه}: فيما دعاهم إليه، فلم ينقادوا له، قال الله متوعِّداً لهم: {فإنَّهم لَمُحْضَرونَ}؛ أي: يوم القيامةِ في العذاب، ولم يذكرْ لهم عقوبةً دنيويَّةً {إلاَّ عباد الله المُخْلَصينَ}؛ أي: الذين أخلصهم الله ومَنَّ عليهم باتِّباع نبيِّهم؛ فإنَّهم غير محضرين في العذاب، وإنَّما لهم من الله جزيل الثواب. {وتركنا عليه}؛ أي: على إلياس {في الآخِرين}: ثناءً حسناً. {سلامٌ على إل ياسينَ}؛ أي: تحية من الله ومن عبادِهِ عليه. {إنَّا كذلك نَجْزي المُحْسِنينَ. إنَّه من عبادِنا المؤمنينَ}: فأثنى اللهُ عليه كما أثنى على إخوانِهِ صلواتُ الله وسلامُه عليهم أجمعينَ.
{123 - 132} Mwenyezi Mungu anamsifu mja wake na Mtume wake, Ilyas, rehema na amani ziwe juu yake, kwa unabii, utume na kulinganua kwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba aliwaamrisha watu wake kuwa wachamungu na kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na akawakataza kuabudu sanamu lao liitwalo Baa'li. Aliwakemea kutokana na suala lao la kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu aliyewaumba, akawapa neema za dhahiri na zilizofichika kwa wingi,
na akawalaumu: "Vipi mliacha kumuabudu Yule ambaye yuko hivi mkaanza kuabudu sanamu ambalo halidhuru wala halinufaishi, wala haliumbi wala haliruzuku na wala halili chakula wala halizungumzi." Basi je, huu ni nini isipokuwa upotovu mkubwa zaidi, upumbavu na ukengeufu? "Wakamkadhibisha" katika yale aliyowaitia, na wala hawakumtii.
Mwenyezi Mungu alisema akiwaahidi adhabu: "Basi kwa hakika watahudhurishwa" Siku ya Kiyama katika adhabu, lakini hapa hakutaja adhabu yao ya duniani, "Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa" ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa neema ya kumfuata Nabii wao. Hao hawatahudhurishwa katika adhabu na mateso, bali watapata thawabu nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. "Na tulimwachia
(sifa nzuri) kwa waliokuja baadaye." "Iwe salama kwa Ilyas" kutoka kwa Mwenyezi Mungu na waja wake. "Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa waliowema. Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini." Hapa Mwenyezi Mungu akawa amemsifu kama alivyowasifu ndugu zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote.
{وَإِنَّ لُوطًا لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ (133) إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ (134) إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ (135) ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ (136) وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِمْ مُصْبِحِينَ (137) وَبِاللَّيْلِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (138)}.
133. Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume. 134. Tulipomwokoa yeye na ahali zake wote. 135. Isipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma. 136. Kisha tukawaangamiza wale wengineo. 137. Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi. 138. Na usiku. Basi je, hamyatii akilini?
#
{133 - 138} وهذا ثناءٌ منه تعالى على عبدِهِ ورسولِهِ لوطٍ بالنبوَّة والرسالة ودعوتِهِ إلى الله قومَه ونهِيِهم عن الشرك وفعل الفاحشةِ، فلمَّا لم ينتهوا؛ نجَّاه الله وأهلَه أجمعين، فَسَرَوْا ليلاً، فنجَوْا؛ {إلاَّ عجوزاً في الغابرين}؛ أي: الباقين المعذَّبين، وهي زوجة لوطٍ، لم تكن على دينِهِ. {ثم دمَّرْنا الآخرين}: بأن قَلَبْنا عليهم ديارَهم فجَعَلْنا عالِيَها سافِلَها، وأمْطَرْنا عليها حجارةً من سِجِّيل منضودٍ حتى هَمَدوا وخَمَدوا، {وإنَّكُم لتمرُّون عليهم}؛ أي: على ديار قوم لوطٍ {مصبحينَ. وبالليل}؛ أي: في هذه الأوقات يكثُرُ تَرَدُّدُكم إليها ومروركم بها، فلم تقبل الشك والمِرْيَةَ. {أفلا تعقلونَ}: الآياتِ والعِبَرَ وتنزجِرون عمَّا يوجِبُ الهلاكَ؟!
{133 - 138} Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu anamsifu mja wake na Mtume wake Lut'i kwa unabii na utume, kuwalingania watu wake kwa Mwenyezi Mungu na kuwakataza wasishirikiane na kufanya uchafu. Lakini pindi hawakuacha, Mwenyezi Mungu akamuokoa yeye na wana familia yake wote. Walitoka usiku kwa hivyo wakaokolewa, "Isipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma." Na wakaadhibiwa. Naye alikuwa ni mke wa Lut'i ambaye hakuwa katika dini yake. "Kisha tukawaangamiza wale wengine" kwa kuwageuzia majumba yao juu chini, na tukawanyeshea mvua ya changarawe za udongo mgumu uliokamatana wa Motoni, mpaka wakaangamia na kupotelea mbali. "Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi. Na usiku," kwa hivyo hilo si shaka tena wala jambo la kusitasita juu yake. "Basi je, hamyatii akilini" ishara na mafunzo, mkaacha mambo ya kuwaletea maangamizo?
{وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ (139) إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ (140) فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ (141) فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ (142) فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ (143) لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ (144) فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ (145) وَأَنْبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِنْ يَقْطِينٍ (146) وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَى مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ (147) فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَى حِينٍ (148)}.
139. Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume. 140. Alipokimbia akenda katika jahazi lililosheheni. 141. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa. 142. Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa. 143. Na ingelikuwa hakuwa katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu. 144. Bila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa. 145. Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa. 146. Na tukauotesha juu yake mmea wa aina ya mung'unye. 147. Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. 148. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
#
{139} وهذا ثناءٌ منه تعالى على عبدِهِ ورسولِهِ يونسَ بن متَّى؛ كما أثنى على إخوانِهِ المرسَلين بالنبوَّة والرسالة والدَّعوة إلى الله.
{139} Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu anamsifu mja na Mtume wake, Yunus bin Matta, kama alivyowasifu ndugu zake miongoni mwa unabii na mitume na kulingania kwa Mwenyezi Mungu.
#
{140} وذكر تعالى عنه أنَّه عاقَبَه عقوبةً دنيويَّةً أنجاه منها بسبب إيمانِهِ وأعمالِهِ الصالحة، فقال: {إذْ أبَقَ}؛ أي: من ربِّه مغاضِباً له ظانًّا أنه لا يقدِرُ عليه ويحبِسُه في بطن الحوت، ولم يذكُرِ الله ما غاضبَ عليه ولا ذَنْبَهُ الذي ارتكبه؛ لعدم فائِدَتِنا بذكرِهِ، وإنَّما فائدتُنا بما ذكرنا عنه أنه أذنبَ، وعاقبه الله مع كونِهِ من الرُّسل الكرام، وأنَّه نجَّاه بعد ذلك، وأزال عنه الملامَ، وقيَّضَ له ما هو سببُ صلاحِهِ. فلمَّا أبَقَ؛ لجأ {إلى الفلك المشحونِ}: بالركاب والأمتعة.
{140} Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja kwamba alimuadhibu kwa adhabu ya kidunia ambapo baadaye alimuokoa kutokana nayo kwa sababu ya imani yake na matendo yake mema.
Alisema: "Alipokimbia" kutoka kwa Mola wake Mlezi huku amemkasirikia akidhani kwamba Mwenyezi Mungu hangemfikia na kumfungia ndani ya tumbo la nyangumi. Na Mwenyezi Mungu hakutaja kilichomkasirisha Nabii Yunus wala hakutaja dhambi aliyoifanya; kwa sababu kuyataja hayo hakuna faida kwetu. Bali faida tu ni kile alichotaja kwamba alitenda dhambi, na Mwenyezi Mungu akamuadhibu pamoja na kwamba yeye ni miongoni mwa Mitume watukufu, na kwamba alimuokoa baada ya hapo, na akamuondolea lawama, na akampa njia za kumfanya atengee. Alipokimbilia kupanda "katika jahazi lililosheheni" abiria na mizigo.
#
{141} فلما رَكِبَ مع غيره والفلك شاحن؛ ثقلتِ السفينةُ، فاحتاجوا إلى إلقاءِ بعضِ الركبانِ، وكأنَّهم لم يجِدوا لأحدٍ مزيَّةً في ذلك، فاقترعوا على أنَّ مَنْ قُرِعَ وغُلِبَ؛ ألقي في البحر؛ عدلاً من أهل السفينة، وإذا أراد الله أمراً؛ هيَّأ أسبابه، فلما اقترعوا؛ أصابتِ القرعةُ يونسَ. {فكان من المُدْحَضينَ}؛ أي: المغلوبين، فألقي في البحر.
{141} Alipopanda pamoja na wengine huku meli imesheheni, meli hiyo ikawa nzito. Kwa hivyo walihitaji kuwarusha nje baadhi ya abiria, na ni kana kwamba hawakupata mtu yoyote aliyekuwa tofauti na wengine katika hilo. Kwa hivyo wakapiga kura kwamba atakayepigiwa kura na akashinda, basi atatupwa baharini; kama njia ya kuwafanyia uadilifu watu waliokuwa katika meli hiyo. Na Mwenyezi Mungu anapotaka kitu, anakiandalia visababu vyake. Basi walipopiga kura, kura hiyo ikamwendea vibaya Yunus. "Na akawa katika walioshindwa," kwa hivyo akatupwa baharini.
#
{142} {فالْتَقَمَهُ الحوتُ وهو}: وقت التقامِهِ {مُليمٌ}؛ أي: فاعلٌ ما يُلام عليه، وهو مغاضبتُهُ لربِّه.
{142} "Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa" juu ya kumghadhibisha Mola wake Mlezi.
#
{143 - 144} {فلولا أنَّه كان من المسبِّحينَ}؛ أي: في وقتِه السابقِ بكثرةِ عبادته لربِّه وتسبيحِهِ وتحميدِهِ وفي بطن الحوت حيث قال: {لا إله إلا أنت سبحانَكَ إنِّي كُنْتُ من الظالمين}؛ {لَلَبِثَ في بطنِهِ إلى يوم يُبْعَثونَ}؛ أي: لكانتْ مقبرتَهَ، ولكن بسبب تسبيحِهِ وعبادتِهِ لله؛ نجَّاه الله تعالى، وكذلك ينجي الله المؤمنين عند وقوعهم في الشدائد.
{143 - 144} "Na ingelikuwa hakuwa katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu" katika siku zake zilizotangulia,
na kwa kumtakasa Mola wake Mlezi na kumsifu ndani ya tumbo la samaki kwa kusema: "Hapana mungu isipokuwa Wewe Uliyetakasika, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu," basi "bila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa." Na hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowaokoa waumini wanapokuwa katika dhiki.
#
{145} {فَنبَذْناه بالعراءِ}: بأنْ قَذَفَهُ الحوت من بطنِهِ بالعراء، وهي الأرض الخالية العاريةُ من كلِّ أحدٍ، بل ربَّما كانت عارية من الأشجارِ والظِّلال. {وهو سقيمٌ}؛ أي: قد سَقِمَ ومَرِضَ بسبب حبسِهِ في بطن الحوت حتى صار مثل الفرخ الممعوط من البيضة.
{145} "Lakini tulimtupa ufukweni patupu" bila ya watu wala mimea, "hali yu mgonjwa" kutokana na kuzuiliwa ndani ya tumbo la nyangumi huyo hadi akawa kama kifaranga anayetoka kwenye ganda la yai.
#
{146} {وأنبَتْنا عليه شجرةً من يَقْطينٍ}: تُظِلُّه بظلِّها الظليل؛ لأنَّها باردةُ الظِّلال، ولا يسقُطُ عليها ذبابٌ، وهذا من لطفِهِ به وبرِّه.
{146} "Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye" ili umfunike kwa kivuli chake baridi, wala hata haendewi na nzi. Hili ni katika upole wake na wema wake juu yake.
#
{147 - 148} ثم لَطَفَ به لطفاً آخرَ، وامتنَّ عليه مِنَّةً عظمى، وهو أنَّه أرسله {إلى مائةِ ألفٍ}: من الناس {أو يَزيدونَ}: عنها، والمعنى أنَّهم إنْ لم يزيدوا عنها؛ لم ينقُصوا، فدعاهم إلى الله تعالى، {فآمنوا}: فصاروا في موازينِهِ؛ لأنَّه الدَّاعي لهم، {فمتَّعْناهم إلى حينٍ}: بأن صَرَفَ الله عنهم العذابَ بعد ما انعقدتْ أسبابُهُ؛ قال تعالى: {فلولا كانتْ قريةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَها إيمانُها إلاَّ قومَ يونُسَ لما آمنوا كَشَفْنا عنهم عذابَ الخِزْي في الحياة الدُّنيا ومَتَّعْناهم إلى حينٍ}.
{147 - 148} Kisha akamfanyia upole mwingine, na akampa neema kubwa ambayo ni kwamba alimtuma "kwa watu laki moja au zaidi." Kwa hivyo, akawalingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na "wakaamini," naye akalipwa kwa sababu ya hilo kwa kuwa yeye ndiye aliyewalingania. "Na tukawastarehesha kwa muda." Hilo lilikuwa kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaondolea adhabu baada ya sababu zake kutokuwepo.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipokuwa kaumu ya Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia, na tukawastarehesha kwa muda."
{فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ (149) أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ (150) أَلَا إِنَّهُمْ مِنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ (151) وَلَدَ اللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ (152) أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ (153) مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ (154) أَفَلَا تَذَكَّرُونَ (155) أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُبِينٌ (156) فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (157)}.
149.
Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume? 150. Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia? 151. Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema. 152. Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo! 153. Ati amehiari watoto wa kike kuliko wanaume? 154. Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi? 155. Hamkumbuki? 156. Au mnayo hoja iliyo wazi? 157. Basi leteni Kitabu chenu kama nyinyi ni wakweli.
#
{149} يقول تعالى لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم - {فاسْتَفْتِهِمْ}؛ أي: اسأل المشركين باللهِ غيرَه، الذين عبدوا الملائكةَ وزَعَموا أنَّها بناتُ الله، فجمعوا بين الشركِ بالله ووصفِهِ بما لا يَليقُ بجلالِهِ. {ألربِّكَ البناتُ ولهم البنونَ}؛ أي: هذه قسمةٌ ضيزى، وقولٌ جائرٌ من جهة جعلهم الولدَ لله تعالى، ومن جهة جعلِهِم أردأ القسمينِ وأخسَّهما له، وهو البناتُ، التي لا يَرْضَوْنَهُنَّ لأنفسِهِم؛ كما قال في الآية الأخرى: {ويَجْعَلونَ لله البناتِ سبحانَه ولهم ما يَشْتَهونَ}، ومن جهةِ جعلِهِم الملائكةَ بناتٍ لله، وحكمِهِم بذلك.
{149} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake,
rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Basi waulize" wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, waliowaabudu Malaika na wakadai kwamba hao ni mabinti za Mwenyezi Mungu, wakawa wamejumuisha kati ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa yasiyoufailia utukufu wake. "Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?" Huo ni mgawanyo wa dhuluma, kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu mwana, na pia kumfanyia mwana huyo kutoka kwa kiumbe wanachokiona duni zaidi, yaani mwana wa kike, ambaye hata wao wenyewe hawamridhii,
kama alivyosema katika Aya nyingine: "Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu
(Ametakasika)! Na wao wenyewe ati ndio wawe na hayo wanayoyatamani!" Na dhuluma yao kwa upande mwingine kwamba waliwafanya Malaika kuwa binti za Mwenyezi Mungu.
#
{150} قال تعالى في بيان كَذِبِهم: {أمْ خَلَقْنا الملائكةَ إناثاً وهم شاهِدونَ}: خَلْقَهم؛ أي: ليس الأمر كذلك؛ فإنَّهم ما شَهِدوا خلقَهم، فدلَّ على أنَّهم قالوا هذا القول بلا علم، بل افتراءٌ على الله.
{150} Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha uwongo wao: "Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia" wakiumbwa? Wapi! Hawakushuhudia kuumbwa kwao, kwa hivo hilo likaashiria kwamba walisema maneno haya bila ya elimu, bali ni walimzulia uongo Mwenyezi Mungu tu.
#
{151 - 157} ولهذا قال: {ألا إنَّهم من إفْكِهِم}؛ أي: كذبهم الواضح؛ {ليَقولونَ وَلَدَ اللهُ وإنَّهم لَكاذبونَ. أصطفى}؛ أي: اختار {البناتِ على البنينَ. مالَكُم كيفَ تَحْكُمونَ}: هذا الحكمَ الجائرَ. {أفلا تَذَكَّرونَ}: وتميِّزونَ هذا القول الباطل الجائر؟ فإنَّكم لو تَذَكَّرْتُم؛ لم تقولوا هذا القول. {أم لكم سلطانٌ مبينٌ}؛ أي: حجَّة ظاهرةٌ على قولكم من كتابٍ أو رسول، وكلُّ هذا غير واقع، ولهذا قال: {فأتوا بكتابِكُم إن كُنتُم صادقينَ}: فإنَّ مَنْ يقولُ قولاً لا يُقيم عليه حجَّة شرعيَّة؛ فإنَّه كاذبٌ متعمِّدٌ أو قائلٌ على الله بلا علم.
{151 - 157} Ndiyo maana akasema: "Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema: Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo! Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wa kiume? Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi," kwa hukumu hii ya udhalimu? "Basi je, hamkumbuki" mkaipambanua kauli hii batili yenye dhuluma? Kwani kama mngekumbuka, basi hamngesema kauli hii. "Au mnayo hoja iliyo wazi" juu ya kauli yenu hii kutoka kwa kitabu au Mtume? Lakini haya yote hayakuwa,
ndiyo maana akasema: "Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli." Kwa maana, mwenye kusema kauli ambayo hana ushahidi wa kisheria juu yake, basi yeye ni mwongo wa makusudi au anazungumza juu ya Mwenyezi Mungu bila elimu.
{وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ (158) سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ (159) إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (160)}.
158. Na wameweka mahusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa. 159. Ametakasika Mwenyezi Mungu mbali na hayo wanayomsingizia. 160. Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.
#
{158} أي: جعل هؤلاء المشركون باللهِ بين اللهِ وبين الجِنَّةِ نَسَباً؛ حيث زَعَموا أنَّ الملائكةَ بناتُ الله، وأنَّ أمهاتِهِم سَرَواتُ الجنِّ! والحالُ أنَّ الجِنَّةَ قد علمتْ أنَّهم مُحْضَرونَ بين يدي الله لِيُجازِيَهم؛ فهم عبادٌ أذلاَّءٌ؛ فلو كان بينَهم وبينَه نسبٌ؛ لم يكونوا كذلك.
{158} Yaani, hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu waliweka nasaba baina ya Mwenyezi Mungu na majini; ambapo walidai kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu, na kwamba mama zao ni wanawake wa kijini! Hali halisi ni kwamba majini walikwisha jua kwamba watahudhurishwa mbele ya Mwenyezi Mungu ili awalipe, kwani wao pia ni waja wadhalilifu kwake. Kwa hivyo, ikiwa kungekuwa na nasaba baina yao na Yeye, basi hawangekuwa hivyo.
#
{159 - 160} {سبحانَ الله}: الملك العظيم، والكامل الحليم، عما يصِفه به المشركون من كل وصفٍ أوجَبَه كفرُهم وشركُهم. {إلاَّ عبادَ الله المخلَصين}: فإنَّه لم يُنَزِّهْ نفسَه عمَّا وَصَفوه به؛ لأنَّهم لم يَصِفوه إلاَّ بما يليق بجلالِهِ، وبذلك كانوا مخلَصين.
{158} "Ametakasika Mwenyezi Mungu," Mfalme Mkuu, ambaye ndiye mkamilifu, Mstahamilivu mbali na hayo ambayo washirikina wanayomsifu nayo yaliyosababishwa na ukafiri na ushirikina wao. "Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa." Kwa sababu hakujiweka mbali na yale wanayomsifu nayo, kwa kuwa hawakumsifu isipokuwa na yale yanayoufailia utukufu wake, ndiyo maana wakawa katika wale waliosafishwa.
{فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ (161) مَا أَنْتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ (162) إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ (163)}.
161. Basi hakika nyinyi na mnaowaabudu. 162. Hamwezi kuwapoteza. 163. Isipokuwa yule atakayeingia Motoni.
#
{161 - 163} أي: إنَّكم أيُّها المشركون ومَنْ عَبَدْتُموه مع الله لا تقدِرون أن تَفْتِنوا وتُضِلُّوا أحداً إلاَّ مَنْ قضى الله أنَّه من أهل الجحيم، فَنَفَذَ فيه القضاءُ الإلهيُّ. والمقصودُ من هذا بيانُ عجزِهم وعجزِ آلهتهم عن إضلال أحدٍ، وبيانُ كمال قدرةِ الله تعالى؛ أي: فلا تَطْمَعوا بإضلال عبادِ الله المخلَصين وحزبِه المفلحين.
{161 - 163} Yaani, enyi washirikina na wale mnaowaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu, hamwezi kumjaribu wala kumpoteza mtu yeyote, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alipitisha kwamba ni miongoni mwa watu wa Motoni. Kwa hivyo akapotea kwa sababu mipango ya Mwenyezi Mungu ilitekelezeka ndani yake. Kinachokusudiwa na haya ni kueleza kutoweza kwao na kutoweza kwa miungu yao kupotosha mtu yeyote, na kueleza ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wasitamani kuwapoteza waja wa Mwenyezi Mungu wateule na kundi lake lililofaulu.
{وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَعْلُومٌ (164) وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ (165) وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ (166)}.
164. Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu. 165. Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu. 166. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
#
{164 - 166} هذا فيه بيانُ براءة الملائكة عليهم السلام عمَّا قاله فيهم المشركونَ، وأنَّهم عبادُ الله، لا يعصونَه طرفةَ عينٍ؛ فما منهم من أحدٍ إلاَّ وله مقامٌ وتدبيرٌ قد أمره الله به لا يتعدَّاه ولا يتجاوزه، وليس لهم من الأمر شيءٌ، {وإنَّا لنحنُ الصافُّون}: في طاعة الله وخدمتِهِ، {وإنَّا لنحنُ المسبِّحونَ}: لله عما لا يَليقُ به؛ فكيف مع هذا يَصْلُحون أن يكونوا شركاء لله، تعالى الله!
{164 - 166} Haya yana maelezo ya kujitenga kwa Malaika, amani iwe juu yao, mbali na yale ambayo washirikina waliyasema na wakakiri kwamba wao ni waja wa Mwenyezi Mungu, na wala hawamuasi kwa kiasi cha kupepesa jicho. Hakuna hata mmoja wao isipokuwa ana mahali pake na usimamizi ambao Mwenyezi Mungu alimuamrisha asiuvuke, na wao hawana lolote katika jambo hilo. "Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu" katika kumtii Mwenyezi Mungu na kumtumikia. "Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa" Mwenyezi Mungu mbali na yale yasiyomfailia. Basi wanaweza vipi kuwa washirika wa Mungu Mwenyezi pamoja na hayo!
{وَإِنْ كَانُوا لَيَقُولُونَ (167) لَوْ أَنَّ عِنْدَنَا ذِكْرًا مِنَ الْأَوَّلِينَ (168) لَكُنَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (169) فَكَفَرُوا بِهِ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ (170) وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ (171) إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنْصُورُونَ (172) وَإِنَّ جُنْدَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ (173) فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّى حِينٍ (174) وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ (175) أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ (176) فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنْذَرِينَ (177) وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّى حِينٍ (178) وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ (179) سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ (180) وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ (181) وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ (182)}.
167. Na walikuwapo waliokuwa wakisema. 168. Tungelikuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani. 169. Bila ya shaka tungelikuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumkusudia Yeye tu. 170. Lakini waliukufuru. Basi watakuja jua. 171. Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu waliotumwa. 172. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakaonusuriwa. 173. Na kwamba jeshi letu ndilo litakaloshinda. 174. Basi waachilie mbali kwa muda. 175. Na watazame, nao wataona. 176. Je, wanaiharakishia adhabu yetu? 177. Basi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa. 178. Na waache kwa muda. 179. Na tazama, na wao wataona. 180. Ametakasika Mola wako Mlezi Mwenye utukufu mbali na yale wanayomzulia. 181. Na Salamu juu ya Mitume. 182. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
#
{167 - 170} يخبرُ تعالى أنَّ هؤلاء المشركين يُظْهِرونَ التمنِّي ويقولون: لو جاءنا من الذِّكْرِ والكتبِ ما جاء الأولين؛ لأخْلَصْنا لله العبادة، بل لكنَّا المخلِصينَ على الحقيقةِ، وهم كَذَبَةٌ في ذلك؛ فقد جاءهم أفضلُ الكتب فكفروا به، فعُلِمَ أنَّهم متمرِّدونَ على الحقِّ. {فسوف يعلمونَ}: العذابَ حين يقعُ بهم.
{167 - 170} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kuwa washirikina hawa wanadhihirisha matamanio yao na kusema: 'Lau kuwa tungelijiwa na ukumbusho na Kitabu kama walivyojiwa wa mwanzo, basi tungemkusudia Mwenyezi Mungu tu katika ibada zetu.Hata tungelikuwa wanaomkusudia Yeye zaidi kwa uhakika.' Lakini wao ni waongo katika hilo. Kwani walijiwa na Kitabu bora zaidi, lakini wakakikadhibisha. Kwa hivyo ikajulikana kwamba wanaikataa tu haki. "Basi watakuja jua" adhabu itakapowafikia.
#
{171 - 179} ولا يحسبوا أيضاً أنَّهم في الدنيا غالبون، بل قد سَبَقَتْ كلمةُ الله التي لا مردَّ لها ولا مخالفَ لها لعبادِهِ المرسَلين وجندِهِ المفلِحين أنَّهم الغالبونَ لغيرِهِم المنصورون من ربِّهم نصراً عزيزاً يتمكَّنون فيه من إقامة دينهم. وهذه بشارةٌ عظيمةٌ لمن اتَّصف بأنَّه من جندِ الله؛ بأن كانت أحوالُهُ مستقيمةً، وقاتلَ مَنْ أمر بقتالهم أنه غالبٌ منصورٌ. ثم أمر رسولَه بالإعراض عَمَّنْ عاندوا ولم يَقْبَلوا الحقَّ، وأنَّه ما بقي إلاَّ انتظارُ ما يَحِلُّ بهم من العذاب، ولهذا قال: {وأبصرهم فسوفَ يُبْصِرونَ}: مَنْ يَحِلُّ به النَّكالُ؛ فإنَّه سيحلُّ بهم. {فإذا نَزَلَ بساحتِهِم}؛ أي: نزل عليهم وقريباً منهم، {فساء صَباحُ المُنْذَرينَ}؛ لأنَّه صباح الشرِّ والعقوبة والاستئصال. ثم كرَّر الأمر بالتولِّي عنهم وتهديدهم بوقوع العذاب.
{171 - 179} Wala wasifikirie kuwa watakuwa washindi katika dunia hii. Bali tayari lilikwisha pita neno la Mwenyezi Mungu, ambalo haliwezi kupingwa wala hakuna anayeweza kulihalifu kwa waja wake waliotumwa na jeshi lake lililofaulu, kwamba watashinda wengine wote na kwamba wataokolewa na Mola wao Mlezi kwa nusura yenye nguvu ambayo kwayo wataweza kuisimamisha dini yao. Hii ni bishara kubwa kwa wale ambao wanasifika kwamba ni katika jeshi la Mwenyezi Mungu. Nao ni wale ambao hali zao zimenyooka na wakapigana vita dhidi ya wale ambao waliamrishwa kupigana nao, kwamba watashinda na watanusuriwa. Kisha akamwamrisha Mtume wake awaepuke wale waliokaidi na wakakataa kuikubali haki, na kwamba hakikubakia isipokuwa kungojea adhabu itakayowapata.
Ndiyo maana akasema: "Na watazame, nao wataona" yule ambaye atapatwa na adhabu, kwani itawapata hao tu. "Basi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa." Kwa sababu itakuwa asubuhi ya shari, adhabu na kuangamizwa. Kisha akarudia amri ya kwamba aachane nao, na akawatishia kwamba watapatwa na adhabu.
#
{180 - 182} ولما ذكر في هذه السورة كثيراً من أقوالهم الشنيعة التي وَصَفوه بها؛ نزَّهَ نفسَه عنها، فقال: {سبحانَ ربِّك}؛ أي: تنزَّه وتعالى، {ربِّ العزَّةِ}؛ أي: الذي عزَّ فقهر كلَّ شيء، واعتزَّ عن كل سوءٍ يصفونه به، {وسلامٌ على المرسلين}: لسلامتهم من الذُّنوب والآفات، وسلامة ما وصفوا به فاطر الأرض والسماوات. {والحمدُ لله ربِّ العالمين}: الألف واللام للاستغراق؛ فجميعُ أنواع الحمدِ من الصفاتِ الكاملةِ العظيمةِ والأفعالِ التي ربَّى بها العالمينَ وأدَرَّ عليهم فيها النِّعم وصَرَفَ عنهم بها النِّقَمَ ودَبَّرَهم تعالى في حَرَكاتِهِم وسكونِهِم وفي جميع أحوالِهِم كلِّها لله تعالى؛ فهو المقدَّسُ عن النقص، المحمودُ بكلِّ كمال، المحبوبُ المعظَّم، ورسلُهُ سالمون مسلَّم عليهم، ومن اتَّبَعَهم في ذلك له السلامةُ في الدُّنيا والآخرة، وأعداؤُهُ لهم الهلاك والعطبُ في الدُّنيا والآخرة.
{180 - 182} Alipotaja katika Sura hii maneno yao mengi ya kuchukiza waliyomuelezea nayo, akajiweka mbali nayo,
akasema: "Ametakasika Mola wako Mlezi;" yaani Mola Mtukufu "Mola Mwenye enzi" ambaye ni Mwenye nguvu zilizoshinda kila kitu. "Na Salamu juu ya Mitume" kwa sababu wako salama kutokana na madhambi na mapungufu, na pia yako salama yale waliyomsifu nayo Muumba wa ardhi na mbingu. "Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote." Kwa hivyo ni za Mwenyezi Mungu sifa zote njema, kamilifu, zilizo kuu, na vitendo alivyowalea kwavyo walimwengu, akawapa neema nyingi, akawaepusha adhabu mbalimbali, akawaendesha katika harakati zao na utulivu wao na katika hali zao zote. Kwa hivyo Yeye ndiye aliyetakasika mbali na upungufu wowote, anayehimidiwa kwa himidi zote, anayependwa zaidi. Na Mitume wake wako salama na amani iwe juu yao, na yeyote anayewafuata katika hili atapata usalama duniani na akhera, nao maadui zake wataangamia hapa duniani na akhera.
Imekamilika tafsiri ya Surat As-Saffat mnamo Shawwal 6, mwaka wa 1343. Kupitia mikono ya mkusanyaji wake na mwandishi wake, Abdur-Rahman bin Nassir As-Saadi. Na rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wake Muhammad. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye kwa neema zake yanatimia mambo mema.