[Nayo] ilishuka Makka
{الْحَمْدُ لِلَّهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَثْنَى وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (1) مَا يَفْتَحِ اللَّهُ لِلنَّاسِ مِنْ رَحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِنْ بَعْدِهِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (2)}.
1. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu. 2. Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, hapana wa kuizuia. Na anayoizuia, hapana wa kuiachilia isipokuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{1} يمدح [اللَّه] تعالى نفسه الكريمة المقدَّسةَ على خلقهِ السماواتِ والأرضَ وما اشتَمَلَتا عليه من المخلوقات؛ لأنَّ ذلك دليلٌ على كمال قدرتِهِ وسَعة ملكِهِ وعموم رحمتِهِ وبديع حكمته وإحاطةِ علمه. ولمَّا ذَكَرَ الخلقَ؛ ذَكَرَ بعده ما يتضمَّنُ الأمر، وهو أنه جعل {الملائكةَ رسلاً}: في تدبيرِ أوامرِهِ القدريَّة ووسائطَ بينَه وبين خلقِهِ في تبليغ أوامره الدينيَّة. وفي ذِكْرِهِ أنَّه جعل الملائكة رسلاً ولم يستثنِ منهم أحداً دليلٌ على كمال طاعتهم لربِّهم وانقيادِهِم لأمرِهِ؛ كما قال تعالى: {لا يعصونَ الله ما أمَرَهم ويفعلون ما يُؤمرون}. ولما كانت الملائكةُ مدبِّراتٍ بإذن الله ما جَعَلَهم الله موكَّلين فيه؛ ذَكَرَ قُوَّتَهم على ذلك وسرعة سيرِهِم؛ بأن جَعَلَهم {أولي أجنحةٍ}: تطير بها فتسرعُ بتنفيذ ما أمرت به، {مثنى وثلاث ورباع}؛ أي: منهم من له جناحان وثلاثة وأربعة بحسب ما اقتضتْه حكمتُه. {يزيدُ في الخَلْقِ ما يشاءُ}؛ أي: يزيد بعضَ مخلوقاتِهِ على بعض في صفة خلقِها وفي القوَّة وفي الحسن وفي زيادة الأعضاء المعهودةِ وفي حسن الأصوات ولذَّةِ النغماتِ. {إنَّ الله على كلِّ شيءٍ قديرٌ}: فقدرتُه تعالى تأتي على ما يشاؤه، ولا يستعصي عليها شيءٌ، ومن ذلك زيادة مخلوقاتِهِ بعضها على بعض.
{1} "Mwenyezi Mungu" Mtukufu anaisifu nafsi yake tukufu na takatifu kwa kuumba mbingu na ardhi na viumbe vilivyomo; kwa sababu huu ni ushahidi wa ukamilifu wa uwezo wake, upana wa ufalme wake, ujumla wa rehema yake, ukubwa wa hekima yake, na elimu yake yenye kudhibiti kila kitu. Alipotaja uumbaji, akataja baada yake mambo yaliyomo katika uumbaji huo. Na hilo ni kwamba amewafanya "kuwa wajumbe" katika kuendesha maamrisho yake ya kimajaliwa, na wapatanishi baina yake na viumbe vyake katika kufikisha amri zake za kidini. Na alipotaja kwamba aliwafanya Malaika kuwa ni wajumbe, na hakumtenga yeyote miongoni mwao nje ya hili, ukawa ushahidi juu ya utiifu wao kamili kwa Mola wao Mlezi, na kufuata kwao amri zake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa." Na kwa kuwa Malaika husimamia mambo ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa kusimamia kwa idhini yake, alitaja nguvu zao katika kufanya hivyo na kasi yao kubwa katika harakati zao kwa kuwafanya wawe "wenye mbawa" ambazo wanaweza kuruka kwazo na kuharakisha kutekeleza waliyoamrishwa, "mbili mbili, na tatu tatu, na nne nne" kulingana na ilivyohitaji hekima yake. "Huzidisha katika kuumba apendavyo" katika namna ya kuviumba, katika nguvu, katika uzuri, katika kuongezewa viungo vya kawaida, na katika uzuri wa sauti. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu." Uweza wake, Mola Mtukufu, unatekelezeka kwa kila alitakalo, na hakuna lisilowezekana kwake, na katika hilo ni kuwaongeza viumbe vyake vingine zaidi ya vingine.
#
{2} ثم ذَكَرَ انفرادَه تعالى بالتدبيرِ والعطاء والمنع، فقال: {ما يَفْتَحِ اللهُ للناس من رحمةٍ فلا مُمْسِكَ لها وما يُمْسِكْ}: من رحمتِهِ عنهم {فلا مرسلَ له من بعدِهِ}: فهذا يوجب التعلُّقَ بالله تعالى والافتقارَ إليه من جميع الوجوه، وأنْ لا يُدعى إلاَّ هو ولا يُخاف ويُرجى إلاَّ هو. {وهو العزيز}: الذي قَهَرَ الأشياءَ كلَّها. {الحكيمُ}: الذي يضع الأشياءَ مواضِعَها، ويُنْزِلُها منازلها.
{2} Kisha akataja kuwa Mwenyezi Mungu ni peke yake katika kuendesha mambo, kupeana, na kuzuia.
Akasema: "Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, hapana wa kuizuia. Na anayoizuia" miongoni mwa rehema yake, "hapana wa kuiachilia isipokuwa Yeye." Hili linalazimu kushikamana na Mwenyezi Mungu na kumhitajia kwa njia zote, na kwamba asiombwe wala kuhofiwa wala kutarajiwa isipokuwa Yeye. "Naye ndiye Mwenye nguvu" ambaye alishinda kila kitu. "Mwenye hekima" anayeweka vitu mahali pake pa sawasawa, na kuvishusha katika vyeo vyake vifaavyo.
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّهِ يَرْزُقُكُمْ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ فَأَنَّى تُؤْفَكُونَ (3) وَإِنْ يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِنْ قَبْلِكَ وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ (4)}.
3. Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayekupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Basi wapi mnakogeuzwa? 4. Na wakikukanusha, basi walikwisha kanushwa Mitume kabla yako. Na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu.
#
{3} يأمرُ تعالى جميع الناس أن يَذْكُروا نعمتَه عليهم، وهذا شاملٌ لِذِكْرِها بالقلب اعترافاً وباللسان ثناءً وبالجوارح انقياداً، فإنَّ ذِكْرَ نعمِهِ تعالى داع لشكرِهِ. ثم نَبَّههم على أصول النِّعم، وهي الخلق والرزق، فقال: {هل من خالق غيرُ الله يرزُقُكم من السماءِ والأرض}: ولما كان من المعلوم أنَّه ليس أحدٌ يَخْلُقُ ويرزقُ إلاَّ الله؛ نتج من ذلك أنْ كان ذلك دليلاً على ألوهيَّته وعبوديَّته، ولهذا قال: {لا إله إلاَّ هو فأنَّى تؤفَكونَ}؛ أي: تُصْرَفون من عبادةِ الخالق الرازق لعبادةِ المخلوق المرزوق.
{3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha watu wote kukumbuka neema zake juu yao, na hili linajumuisha kuzitaja kwa moyo kwa kuzikiri, na kwa ulimi kwa kusifu, na kwa viungo kwa kutii. Kwani kutaja neema zake Mtukufu ni sababu ya kumshukuru. Kisha akawatanabahisha juu ya neema za kimsingi ambazo ni kuwaumba na kuwaruzuku,
na akasema: "Ati yupo muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayekupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi?" Na kwa kuwa inajulikana vyema kuwa hakuna yeyote anayeumba na anayeruzuku isipokuwa Mwenyezi Mungu; ikatokea kutokana na hili kuwa huu ni ushahidi wa uungu wake na umola wake,
na ndiyo maana akasema: "Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Basi wapi mnakogeuzwa?" Yaani, kwa nini mnageuzwa mkaacha kumwabudu Muumba, Mwenye kuruzuku na mkaanza kumuabudu kiumbe anayeruzukiwa.
#
{4} {وإن يُكَذِّبوكَ}: يا أيُّها الرسولُ؛ فلك أسوةٌ بمن قبلَكَ من المرسلين؛ {فقد كُذِّبَتْ رسلٌ من قبلِكَ}: فأُهْلِكَ المكذِّبون، ونَجَّى الله الرسل وأتباعهم. {وإلى اللهِ تُرجع الأمورُ}.
{4} "Na wakikukadhibisha" ewe Mtume, basi unao mfano katika Mitume wa kabla yako; "kwani walikwisha kanushwa Mitume kabla yako" na hapo wakaangamizwa wale waliokadhibisha, na Mwenyezi Mungu akawaokoa Mitume hao na wafuasi wao. "Na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu."
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُمْ بِاللَّهِ الْغَرُورُ (5) إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ (6) الَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ (7)}.
5. Enyi watu! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi kamwe yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala kamwe mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu. 6. Hakika Shetani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Moto wenye mwako mkali. 7. Wale waliokufuru watakuwa na adhabu kali; na wale walioamini na wakatenda mema watapata msamaha na ujira mkubwa.
#
{5 - 6} يقول تعالى: {يا أيُّها الناس إنَّ وعدَ الله}: بالبعث والجزاء على الأعمال {حقٌّ}؛ أي: لا شكَّ فيه ولا مريةَ ولا تردُّد، قد دلَّت على ذلك الأدلة السمعية والبراهين العقلية، فإذا كان وعدُهُ حقًّا؛ فتهيَّؤوا له وبادِروا أوقاتَكم الشريفةَ بالأعمال الصالحة ولا يَقْطَعْكُم عن ذلك قاطعٌ. {فلا تَغُرَّنَّكُمُ الحياةُ الدُّنيا}: بلذَّاتِها وشهواتِها ومطالبِها النفسيَّة، فتُلهيكم عما خُلقتم له، {ولا يَغُرَّنَّكُم بالله الغَرورُ}: الذي هو الشيطانُ، الذي هو عدوُّكم في الحقيقة. {فاتَّخِذوه عَدُوًّا}؛ أي: لتكن منكم عداوته على بالٍ، ولا تُهملوا محاربته كلَّ وقتٍ؛ فإنَّه يراكم وأنتم لا تَرَوْنَه، وهو دائماً لكم بالمرصاد. {إنَّما يَدْعو حِزْبَه ليكونوا من أصحابِ السعيرِ}: هذا غايتُه ومقصودُه مِمَّنْ تَبِعَهُ أن يُهانَ غاية الإهانة بالعذاب الشديد.
{5 - 6} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Enyi watu! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu" ya kuwafufua na kuwalipa juu ya matendo yenu "ni ya kweli" na hakuna shaka yoyote juu yake, ya kusitasita. Kwani kuna ushahidi mwingi wa kusikiwa na wa kiakili ulioashiria hilo. Kwa hivyo, kama ahadi yake hii ni ya kweli, basi jiandaeni kwa ajili yake na harakisheni kuutumia wakati wenu mtukufu katika kufanya matendo mazuri, na kisikuzuieni chochote kufanya hivyo. "Basi kamwe yasikudanganyeni maisha ya dunia" kwa anasa zake, matamanio yake, na matakwa yake ya kinafsi, yaje yakawaghafilisha mbali na yale mliyoumbiwa kwa ajili yake. "Wala kamwe mdanganyifu" ambaye ni Shetani, ambaye ni adui yenu katika hali halisi "asikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu." "Basi mfanyeni kuwa ni adui." Na mkae mkijua hilo, wala msipuuze kupigana naye kila wakati. Yeye anawaona, na nyinyi hamumuoni. Naye daima yuko macho na nyinyi. "Kwani, yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Moto wenye mwako mkali." Haya ndiyo malengo yake na makusudio yake kwa wanaomfuata kwamba wadhalilike kabisa kwa adhabu kali.
#
{7} ثم ذكر أنَّ الناس انقسموا بحسب طاعة الشيطان وعدمِها إلى قسمين، وذَكَرَ جزاءَ كلٍّ منهما، فقال: {الذين كفروا}؛ أي: جحدوا ما جاءتْ به الرسلُ ودلَّت عليه الكتبُ {لهم عذابٌ شديدٌ}: في نار جهنَّم، شديدٌ في ذاتِهِ ووصفِهِ، وأنَّهم خالدون فيها أبداً، {والذين آمنوا}: بقلوبِهِم بما دعا الله إلى الإيمان به، {وعملوا} ـ بمقتضى ذلك الإيمان بجوارِحِهم ـ الأعمالَ الصالحةَ {لهم مغفرةٌ}: لذُنوبهم، يزولُ بها عنهم الشرُّ والمكروه، {وأجرٌ كبيرٌ}: يحصُلُ به المطلوبُ.
{7} Kisha akataja kuwa watu wamegawanyika makundi mawili kulingana na kumtii kwao Shetani na kutomtii, na akataja malipo ya kila moja ya makundi hayo.
Akasema: "Wale waliokufuru" yale waliyoyaleta Mitume na yakaashiriwa na Vitabu "watakuwa na adhabu kali" katika Moto wa Jahannamu, ambao huo wenyewe ni mkali sana na pia ni wenye sifa kali sana, na kwamba watakaa humo milele. "Na wale walioamini " kwa nyoyo zao yale aliyoyalingania Mwenyezi Mungu kwamba wayaamini, "na wakatenda mema" kwa mujibu wa imani hiyo kwa viungo vyao "watapata msamaha" kwa dhambi zao, na kwa hilo wataepushwa na shari na mambo wanayochukia "na" watapata "ujira mkubwa" ambao utawafanya kupata wanachokitaka.
{أَفَمَنْ زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا فَإِنَّ اللَّهَ يُضِلُّ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَاتٍ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِمَا يَصْنَعُونَ (8)}.
8. Je, yule aliyepambiwa matendo yake mabaya na akayaona ni mema - basi hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa amtakaye. Basi, nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia. Hakika Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyafanya.
#
{8} يقولُ تعالى: {أفَمَن زُيِّنَ له}: عملُه السيئ القبيح، زيَّنه له الشيطانُ وحسَّنه في عينِهِ ، {فرآه حسناً}؛ أي: كمن هداه الله إلى الصراطِ المستقيم والدين القويم؛ فهل يستوي هذا وهذا؟! فالأول عمل السيئ، ورأى الحقَّ باطلاً والباطل حقًّا، والثاني عمل الحسنَ ورأى الحقَّ حقًّا والباطل باطلاً، ولكن الهداية والإضلال بيدِ الله تعالى. {فإنَّ الله يُضِلُّ مَن يشاءُ ويَهْدي مَن يشاءُ فلا تَذْهَبْ نفسُك عليهم}؛ أي: على الضالِّين الذين زُيِّنَ لهم سوءُ أعمالِهِم، وصدَّهُم الشيطانُ عن الحقِّ {حسراتٍ}: فليس عليك إلاَّ البلاغُ، وليس عليك مِن هداهم شيءٌ، والله هو الذي يُجازيهم بأعمالهم. {إنَّ الله عليمٌ بما يصنعونَ}.
{8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Je, yule aliyepambiwa" na Shetani matendo yake mabaya, maovu na akamfanya kuyaona kuwa mazuri ni sawa na yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa kwenye njia iliyonyooka na Dini madhubuti. "Je, huyu na huyu ni sawa?" Huyu wa kwanza alitenda mabaya, na akaiona haki kwamba ni batili, nayo batili kuwa ndiyo haki. Naye wa pili alitenda mema na akaiona haki kwamba ni haki, nayo batili kuwa ndiyo batili, lakini uongofu na upotofu uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Basi hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa amtakaye. Basi nafsi yako isijihiliki" juu ya wapotofu hawa ambao wamepambiwa ubaya wa vitendo vyao hivi, na Shetani akawazuia kukubali haki "kwa kuwasikitikia." Kwani si juu yako isipokuwa kufikisha tu, wala si juu yako kuwaongoa. Na Mwenyezi Mungu ndiye atakayewalipa kwa matendo yao. "Hakika Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyafanya."
{وَاللَّهُ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَسُقْنَاهُ إِلَى بَلَدٍ مَيِّتٍ فَأَحْيَيْنَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا كَذَلِكَ النُّشُورُ (9)}.
9. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayezituma Pepo ziyatimue mawingu, nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa, tukaifufua ardhi baada ya kufa kwake. Ndivyo kama hivyo kutakavyokuwa kufufuliwa.
#
{9} يخبر تعالى عن كمال اقتدارِهِ وسَعَة جودِهِ وأنَّه {أرسلَ الرياحَ فتُثير سحاباً فسُقْناه إلى بلدٍ مَيِّتٍ}: فأنزله الله عليها، {فأحْيَيْنا به الأرض بعدَ موتها}: فحييتِ البلادُ والعبادُ، وارتزقت الحيواناتُ، ورَتَعَتْ في تلك الخيرات، {كذلك}: الذي أحيا الأرض بعد موتها ينشر الأمواتَ من قبورهم بعدما مزَّقَهم البلاء، فيسوقُ إليهم مطراً كما ساقه إلى الأرض الميتة، فينزِلُه عليهم، فتحيا الأجساد والأرواح من القبور، فيأتون للقيام بين يدي الله، ليحكم بينهم ويَفْصِلَ بحكمِهِ العدل.
{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha ukamilifu wa uwezo wake na upana wa ukarimu wake, na kwamba yeye "ndiye anayezituma Pepo ziyatimue mawingu" na akaifanya kunyesha huko;"Nasi tukayafikisha kwenye nchi iliyokufa." Kwa hivyo ardhi na waja wakahuishwa, nao wanyama wakaruzukiwa, na wakastarehekea heri hizo. "Ndivyo kama hivyo," yule aliyeihuisha ardhi baada ya kufa kwake, atawafufua wafu kutoka makaburini mwao baada ya kuoza kwao. Atawaletea mvua kama vile alivyoiletea ardhi iliyokufa. Basi itawanyeshea, na miili yao na roho zao zitafufuka kutoka makaburini. Kisha watakuja kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu, ili ahukumu baina yao kwa hukumu yake ya uadilifu.
{مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ وَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَكْرُ أُولَئِكَ هُوَ يَبُورُ (10)}.
10. Mwenye kutaka utukufu, basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye hupanda neno zuri, na tendo jema Yeye hulitukuza. Na wanaopanga vitimbi vya maovu, watapata adhabu kali. Na vitimbi vyao vitaondokea patupu.
#
{10} أي: يا مَن يُريد العزَّةَ! اطْلُبْها ممَّنْ هي بيدِهِ؛ فإنَّ العزَّة بيد اللَّه، ولا تُنال إلاَّ بطاعتِهِ، وقد ذَكَرَها بقولِهِ: {إليه يصعدُ الكلمُ الطيِّبُ}: من قراءة وتسبيح وتحميدٍ وتهليل وكل كلام حسنٍ طيِّبٍ، فيرُفع إلى الله، ويُعرضُ عليه، ويُثني الله على صاحبه بين الملأ الأعلى، {والعملُ الصالح}: من أعمال القلوب وأعمال الجوارح {يرفَعُهُ}: الله تعالى إليه أيضاً كالكلم الطيب. وقيل: والعمل الصالحُ يرفَعُ الكلمَ الطَّيِّبَ؛ فيكون رفع الكلم الطيب بحسب أعمال العبد الصالحة فهي التي ترفع كلمه الطيب، فإذا لم يكنْ له عملٌ صالحٌ؛ لم يُرْفَعْ له قولٌ إلى الله تعالى. فهذه الأعمال التي تُرفع إلى الله تعالى ويَرْفَعُ الله صاحِبَها ويعزُّه، وأمَّا السيئاتُ؛ فإنَّها بالعكس، يريدُ صاحبُها الرفعةَ بها، ويمكرُ ويكيدُ ويعودُ ذلك عليه، ولا يزدادُ إلاَّ هواناً ونزولاً، ولهذا قال: {والعملُ الصالحُ يرفعُهُ والذين يمكرونَ السيئاتِ لهم عذابٌ شديدٌ}: يُهانون فيه غايةَ الإهانة. {ومَكْرُ أولئك هو يبورُ}؛ أي: يهلك ويضمحلُّ ولا يفيدُهم شيئاً؛ لأنَّه مكرٌ بالباطل لأجل الباطل.
{10} Yaani, ewe unayetaka utukufu! Iombe kwa yule ambaye iko mkononi mwake. Utukufu upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na haupatikani isipokuwa kwa kumtii Yeye,
na akataja pale aliposema: "Kwake Yeye maneno mazuri yanapanda" kutoka kwa kisomo, utukufu, sifa, na maneno yote mazuri. Na huinuliwa kwa Mwenyezi Mungu na kuhudhurishwa kwake, na Mwenyezi Mungu humhimidi anayefanya hayo katika mkutano mkuu, "na matendo mema" katika matendo ya nyoyo na viungo "anaiinua." Mwenyezi Mungu pia humnyanyua kwake kama neno zuri.
Ikasemwa: Matendo mema huinua maneno mazuri. Basi maneno mazuri yanainuliwa kwa mujibu wa matendo mema ya mja, kama hayo ndiyo yanayonyanyua maneno yake mazuri ikiwa hana jambo jema. Hakuna neno lililoinuliwa kutoka kwake kwa Mwenyezi Mungu. Haya ni matendo yanayoinuliwa kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu huwatukuza na kuwatukuza watendao maovu. Kinyume chake, mmiliki wake anataka kunyanyuliwa nayo, na anafanya vitimbi na vitimbi, na haya yanamrudia, na yanazidisha unyonge na unyonge.
Na ndiyo maana akasema: "Na mema yanamtukuza, na wala vitimbi viovu vitapata adhabu kali;" watafedheheka kabisa. "Na hila za hao ni uharibifu;" yaani, inaangamia na kutoweka wala haina faida yoyote kwao. Kwa sababu anadanganya kwa uongo kwa ajili ya uongo.
{وَاللَّهُ خَلَقَكُمْ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَاجًا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنْثَى وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ وَمَا يُعَمَّرُ مِنْ مُعَمَّرٍ وَلَا يُنْقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ إِنَّ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ (11)}.
11. Na Mwenyezi Mungu amewaumba kutokana na udongo. Kisha kwa tone la manii. Kisha akawafanya mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote hachukui mimba, wala hazai, isipokuwa kwa elimu yake. Na wala hapewi umri mwenye umri mrefu, wala hapunguziwi katika umri wake, isipokuwa yamo hayo katika Kitabu. Hakika hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
#
{11} يذكر تعالى خلقَه الآدميَّ وتنقُّله في هذه الأطوار من ترابٍ إلى نطفةٍ وما بعدها، {ثم جَعَلَكم أزواجاً}؛ أي: لم يزل ينقُلُكم طوراً بعد طورٍ حتى أوصلكم إلى أنْ كنتُم أزواجاً؛ ذكر يتزوجُ أنثى، ويُرادُ بالزواج الذُّرِّية والأولاد؛ فهو وإنْ كان النكاحُ من الأسبابِ فيه؛ فإنَّه مقترنٌ بقضاء الله وقدره وعلمه. {وما تَحْمِلُ مِن أنثى ولا تضعُ إلاَّ بعلمِهِ}: وكذلك أطوارُ الآدميِّ كلُّها بعلمه وقضائه {وما يُعَمَّرُ من مُعَمَّرٍ ولا يُنقَصُ من عُمُرِهِ}؛ أي: عمر الذي كان معمَّراً عمراً طويلاً، {إلاَّ}: بعلمه تعالى، أو: وما ينقص من عمر الإنسان الذي هو بصدد أن يَصِلَ إليه لولا ما سلكه من أسباب قِصَرِ العمر؛ كالزِّنا وعقوق الوالدين وقطيعة الأرحام ونحو ذلك مما ذُكِرَ أنَّها من أسباب قصر العمر، والمعنى أنَّ طولَ العمر وقِصَرَه بسببٍ وبغير سببٍ كله بعلمه تعالى، وقد أثبت ذلك {في كتابٍ}: حوى ما يجري على العبد في جميع أوقاته وأيام حياته. {إنَّ ذلك على الله يسيرٌ}؛ أي: إحاطة علمه بتلك المعلومات الكثيرة، وإحاطةُ كتابه بها.
فهذه ثلاثةُ أدلَّة من أدلَّة البعث والنشور، كلُّها عقليَّة، نبَّه الله عليها في هذه الآيات: إحياء الأرض بعد موتها، وأنَّ الذي أحياها سيُحيي الموتى. وتَنَقُّل الآدمي في تلك الأطوار، فالذي أوجَدَه ونَقَّلَه طبقاً بعد طبق وحالاً بعد حال حتى بلغ ما قُدِّرَ له؛ فهو على إعادتِهِ وإنشائِهِ النشأةَ الأخرى أقدرُ، وهو أهونُ عليه. وإحاطة علمه بجميع أجزاء العالم العلويِّ والسفليِّ دقيقها وجليلها، الذي في القلوب، والأجنَّة التي في البطون، وزيادة الأعمار ونقصها، وإثباتُ ذلك كلِّه في كتاب؛ فالذي كان هذا يسيراً عليه؛ فإعادتُه للأموات أيسرُ وأيسرُ. فتبارك من كَثُرَ خيرُه، ونبَّه عبادَه على ما فيه صلاحُهم في معاشهم ومعادهم.
{11} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja uumbaji wake wa kibinadamu na harakati zake kupitia hatua hizi kutoka kwenye udongo hadi manii na zaidi. "Kisha akakufanyeni jozi;" yaani, aliendelea kukusongeza hatua baada ya hatua mpaka mkawa wenzi. Mwanamume huoa mwanamke, na kwa ndoa kinachokusudiwa ni uzao na watoto. Hata kama ndoa ni sababu mojawapo; inaunganishwa na agizo la Mwenyezi Mungu, hatima, na ujuzi. "Na mwanamke hachukui mimba wala hazai ila kwa ujuzi wake." Na hali kadhalika hatua zote za wanaadamu ziko kwa elimu Yake na hukumu yake, "wala harefushiwi aliye hai wala hapunguzwi umri wake." Yaani, umri wa mtu aliyeishi maisha marefu, "isipokuwa" kwa ujuzi wake Yeye Mtukufu. Au na yale yanayopungua kutoka kwa umri wa mtu anayekaribia kuufikia lau si kwa sababu za kufupisha maisha yake, bali alichukua kama vile uzinzi, kutotii wazazi, kukata uhusiano wa kifamilia, na mambo mengine ambayo yametajwa kuwa ni miongoni mwa sababu za kufupisha maisha. Na kufupisha maisha kwa sababu au bila sababu, yote ni kwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu; haya yamethibiti "katika kitabu." Kuna yale yanayompata mja katika nyakati zake zote na siku za maisha yake. "Hakika haya kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi." Yaani, kuifunika elimu yake kwa habari nyingi hii, na kuifunika kitabu chake. Hizi ni dalili tatu za kufufuliwa na zote ni za kimantiki,
na Mwenyezi Mungu amezibainisha katika Aya hizi: ufufuo wa ardhi baada ya kufa kwake, na kwamba yule aliyeihuisha atawahuisha wafu. Na mwanadamu akapita katika hatua hizi. Aliyemuumba na akamsogeza tabaka baada ya tabaka na hali baada ya hali mpaka akapata yale aliyoandikiwa. Ana uwezo zaidi wa kuirejesha na kuunda sura nyingine, na ni rahisi kwake. Na kuzunguka elimu yake ya sehemu zote za dunia ya juu na ya chini, dakika yake na tukufu, yaliyomo nyoyoni, na vijusi matumboni, na kuongezeka na kupungua kwa muda wa maisha, na kuyathibitisha yote hayo katika kitabu; Kwa hivyo nini hii ilikuwa rahisi kwa kumrudisha kwa wafu, rahisi na rahisi zaidi. Basi akambariki yule ambaye wema wake ni mwingi, na akawatahadharisha waja wake yale yatakayowanufaisha katika maisha yao na mustakbali wao.
{وَمَا يَسْتَوِي الْبَحْرَانِ هَذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَائِغٌ شَرَابُهُ وَهَذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ وَمِنْ كُلٍّ تَأْكُلُونَ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُونَ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ فِيهِ مَوَاخِرَ لِتَبْتَغُوا مِنْ فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (12) يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُسَمًّى ذَلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِنْ قِطْمِيرٍ (13) إِنْ تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ (14)}.
12. Na bahari mbili haziwi sawa; haya ni matamu yenye ladha, mazuri kunywa. Na haya ni ya chumvi, machungu. Na kutokana na bahari zote mnakula nyama mpya
(isiyochacha). Na mnatoa mapambo mnayoyavaa. Na unaona ndani yake merikebu zinakata maji ili mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru. 13. Anauingiza usiku katika mchana, na anauingiza mchana katika usiku. Na amelifanya jua na mwezi kutumikia, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Na hao mnaowaomba badala yake hawamiliki hata ugozi wa kokwa ya tende. 14. Mkiwaomba hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawawajibu. Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakayekupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari.
#
{12} هذا إخبارٌ عن قدرتِهِ وحكمتِهِ ورحمتِهِ، أنَّه جعل البحرينِ لمصالح العالم الأرضيِّ كلِّهم، وأنَّه لم يسوِّ بينهما؛ لأنَّ المصلحة تقتضي أن تكون الأنهارُ عذبةً فراتاً سائغاً شرابها؛ لينتفعَ بها الشاربون والغارسون والزارعون، وأن يكونَ البحرُ ملحاً أجاجاً؛ لئلاَّ يَفْسُدَ الهواءُ المحيطُ بالأرض بروائح ما يموتُ في البحر من الحيوانات، ولأنَّه ساكنٌ لا يجري؛ فملوحتُه تمنعُه من التغيُّر، ولتكون حيواناتُه أحسنَ وألذَّ، ولهذا قال: {ومن كلٍّ}: من البحر الملح والعذب {تأكلونَ لحماً طريًّا}: وهو السمك المتيسِّرُ صيدُه في البحر، {وتستخرِجون حِلْيَةً تَلْبَسونَها}: من لؤلؤ ومرجانٍ وغيره مما يوجدُ في البحر، فهذه مصالحُ عظيمةٌ للعباد.
ومن المصالح أيضاً والمنافع في البحر أن سَخَّرَه الله تعالى يحملُ الفلكَ من السفن والمراكب، فتراها تمخُرُ البحر وتشقُّه، فتسلكُ من إقليم إلى إقليم آخر ومن محلٍّ إلى محلٍّ، فتحمل السائرين وأثقالَهم وتجاراتِهِم، فيحصُلُ بذلك من فضل الله وإحسانه شيءٌ كثير، ولهذا قال: {ولِتَبْتَغوا من فضلِهِ ولعلَّكم تشكُرون}.
{12} Huku ni kujulisha kuhusu uwezo wake, hekima yake na rehema. Kwamba alizifanya bahari mbili kwa ajili ya masilahi ya ulimwengu wote wa dunia, na kwamba hakuzilinganisha, kwa sababu masilahi yanahitaji kwamba mito iwe na maji matamu yenye ladha, mazuri kunywa; ili wafaidike kwayo wanywaji na wakulima, kwamba pia iwe na maji ya chumvi machungu; ili hewa inayoizunguka ardhi isiharibike kwa harufu za wanyama wanaofia baharini, na kwa sababu imetulia na haitiririki. Hii ni kwa sababu kuwa kwake ni chumvi kunaizuia kubadilika, na ili wanyama wake wawe bora na watamu zaidi.
Ndiyo maana akasema: "Na kutokana na bahari zote mbili" ya maji ya chumvi na ya maji matamu "mnakula nyama mpya
(isiyochacha);" nayo ni samaki anayeweza kuvuliwa katika bahari. Na mnatoa mapambo mnayoyavaa," kama vile lulu na marijani na vitu vinginevyo vinavyopatikana baharini. Haya ni masilahi makubwa kwa watu. Katika masilahi na manufaa mengine katika bahari ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliitiisha ili ibebe merikebu na mashua. Basi utaziona zikiikata na kuipasua bahari zikakwenda kutoka eneo moja kwenda eneo jingine na kutoka sehemu moja hadi nyingine, zikiwabeba wasafiri, mizigo yao na biashara zao. Na kutokana na hayo zinapatikana fadhila za Mwenyezi Mungu na wema wake mwingi sana, na ndiyo maana akasema, "ili mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru."
#
{13} ومن ذلك أيضاً إيلاجُهُ تعالى الليلَ بالنهارِ والنهارَ بالليلِ؛ يُدْخِلُ هذا على هذا وهذا على هذا، كلما أتى أحدُهما؛ ذهب الآخر، ويزيدُ أحدُهما وينقصُ الآخرُ ويتساويان، فيقوم بذلك ما يقومُ من مصالح العبادِ في أبدانهم وحيواناتهم وأشجارِهم وزُروعهم، وكذلك ما جعل الله في تسخير الشمس والقمر من مصالح الضياء والنورِ والحركة والسكون وانتشار العباد في طلب فضله وما فيهما من تنضيج الثمار وتجفيف ما يجفَّف وغير ذلك مما هو من الضَّرورياتِ التي لو فُقِدَتْ؛ لَلَحِقَ الناسَ الضررُ.
وقوله {كلٌّ يجري لأجل مُسَمًّى}؛ أي: كلٌّ من الشمس والقمر يسيران في فلكهما ما شاء الله أن يسيرا؛ فإذا جاء الأجلُ وقَرُبَ انقضاءُ الدُّنيا؛ انقطع سيرُهما، وتعطَّل سلطانُهما، وخسفَ القمرُ، وكُوِّرَتِ الشمسُ، وانتثرتِ النُّجومُ.
فلما بيَّن تعالى ما بيَّن من هذه المخلوقات العظيمة وما فيها من العبرِ الدالَّة على كماله وإحسانِهِ قال: {ذلكُمُ الله ربُّكم له الملكُ}؛ أي: الذي انفرد بخَلْق هذه المذكورات وتسخيرِها هو الربُّ المألوه المعبودُ الذي له الملكُ كلُّه. {والذين تدعونَ من دونِهِ}: من الأوثان والأصنام، لا يملِكونَ {من قِطْميرٍ}؛ أي: لا يملكون شيئاً لا قليلاً ولا كثيراً، حتى ولا القطمير الذي هو أحقر الأشياء، وهذا من تنصيص النفي وعمومه؛ فكيف يُدْعَوْنَ وهم غير مالكينَ لشيء من ملك السماواتِ والأرض؟!
{13} Na katika masilahi hayo ni kuingiza kwake Mtukufu mchana katika usiku, na usiku katika mchana. Kila moja ya hivyo inapokuja, hicho kingine kinatoweka, na pia moja yake inazidi na nyingine inapunguka na pia vinatoshana. Kwa hivyo yakapatikana kwa sababu ya hayo, masilahi ya waja katika miili yao, wanyama wao, miti yao na mazao yao. Na vile vile Mwenyezi Mungu alivyolitiisha jua na mwezi. Hili lina masilahi ya mwangaza, nuru, mwendo, utulivu, na kuenea kwa waja katika kutafuta fadhila zake, na yaliyomo ndani yake kama vile kuivisha matunda na kukausha yale yanayokauka na mambo mengine miongoni mwa mahitaji ambayo yakipotea, basi watu watadhurika.
Na kauli yake: "Kila kimojawapo kinakwenda kwa muda maalumu" anavyotaka Mwenyezi Mungu kikwende. Na muda utakapokuja na mwisho wa dunia ukakaribia, mwendo wake huu utakatika na mamlaka yake yatavurugika, na mwezi utapatwa, na jua litakunjwa, na nyota zitatawanyika. Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoeleza aliyoyaeleza juu ya viumbe hawa wakubwa na mafunzo yaliyomo ndani yao yanayoashiria ukamilifu wake na ukarimu wake,
akasema: "Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi," ambaye aliviumba vitu hivi peke yake na akavitiisha, naye ndiye ni Mola Mlezi anayepasa kuabudiwa ambaye ufalme wote ni wake. "Na hao mnaowaomba badala yake" miongoni mwa vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu na masanamu, havimiliki hata "ugozi wa kokwa ya tende." Yaani, hawamiliki chochote, si kidogo wala kichache, hata ugozi wa kokwa ya tende, ambayo ndiyo kitu kinachodharauliwa zaidi. Na huku ni kukanusha kwa ujumla. Vipi wanaabudiwa ilhali hawamiliki chochote katika ufalme wa mbingu na ardhi?
#
{14} ومع هذا: {إن تَدْعوهم}: لا يسمعوكم؛ لأنهم ما بين جمادٍ وأمواتٍ وملائكةٍ مشغولين بطاعة ربهم، {ولو سمعوا}: على وجه الفرض والتقدير {ما اسْتَجابوا لكم}: لأنَّهم لا يملِكون شيئاً ولا يرضى أكثرُهم بعبادةِ مَنْ عَبَدَه، ولهذا قال: {ويوم القيامةِ يكفُرونَ بشِرْكِكُم}؛ أي: يتبرؤون منكم، ويقولونَ: سبحانك أنتَ ولِيُّنا من دونهم، {ولا ينبِّئُك مثلُ خبيرٍ}؛ أي: لا أحدَ ينبِّئُكَ أصدقُ من الله العليم الخبيرِ؛ فاجْزِمْ بأنَّ هذا الأمر الذي نبأ به كأنه رأيُ عينٍ، فلا تشكَّ فيه ولا تمترِ. فتضمَّنَتْ هذه الآياتُ الأدلَّة والبراهين الساطعةَ الدالَّة على أنَّه تعالى المألوهُ المعبودُ الذي لا يستحقُّ شيئاً من العبادة سواه، وأنَّ عبادةَ ما سواه باطلةٌ متعلقةٌ بباطل لا تفيدُ عابده شيئاً.
{14} Na pamoja na haya: "Ukiwaomba" hawatawasikia; kwa sababu wao wako baina ya vitu visivyo na uhai, wafu. Na Malaika ambao wanajishughulisha na kumtii Mola wao Mlezi, "na hata wakisikia" kama itachukuliwa hivyo "hawakujibuni." Kwa sababu wao hawamiliki chochote na wengi wao hawaridhiki na ibaada za wale wanaowaabudu.
Na ndiyo maana akasema: "Na Siku ya Kiyama watakataa ushirikina wenu." Yaani, watajitenga mbali nanyi,
na watasema: Umetakasika, wewe ndiye mlinzi wetu si wao. "Na hapana atakayekupa habari vilivyo kama Yeye Mwenye habari." Yaani, hakuna anayekupa habari kwa ukweli zaidi kuliko Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa yote, Mwenye habari zote. Basi kuwa na uhakika kwamba jambo hili ni kama kwamba ni jambo linaloonwa kwa jicho, basi huwezi kuwa na shaka nalo na kusitasita. Aya hizi zinajumuisha ushahidi wazi na hoja za kung'aa zinazoonyesha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwenye kufanyiwa uungu na kuabudiwa peke yake. Na ambaye hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, na kwamba kuabudu asiyekuwa Yeye ni batili, na kuabudu huko kunahusiana na batili ambayo haifai kitu mwenye kuiabudu.
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ أَنْتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّهِ وَاللَّهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ (15) إِنْ يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ (16) وَمَا ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ بِعَزِيزٍ (17) وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى وَإِنْ تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَى حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى إِنَّمَا تُنْذِرُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ بِالْغَيْبِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَمَنْ تَزَكَّى فَإِنَّمَا يَتَزَكَّى لِنَفْسِهِ وَإِلَى اللَّهِ الْمَصِيرُ (18)}.
15. Enyi watu, nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa. 16. Akitaka, atawaondoa na alete viumbe vipya. 17. Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu. 18. Na mbebaji hatabeba mzigo wa mwengine. Na aliyetopewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe, hautachukuliwa hata kidogo, hata kama ni jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanaomcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Swala. Na mwenye kujitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
#
{15} يخاطبُ تعالى جميع الناس، ويخبِرُهم بحالِهم ووصفِهم، وأنهم فقراءُ إلى الله من جميع الوجوه: فقراءُ في إيجادِهم؛ فلولا إيجادُه إيَّاهم لم يوجدوا، فقراء في إعدادِهم بالقُوى والأعضاء والجوارح، التي لولا إعدادُه إيَّاهم بها؛ لما استعدُّوا لأيِّ عمل كان، فقراء في إمدادِهم بالأقواتِ والأرزاقِ والنعم الظاهرةِ والباطنة؛ فلولا فضلُه وإحسانُه وتيسيرُه الأمور، لما حصل لهم من الرزقِ والنعم شيءٌ، فقراءُ في صرف النقم عنهم ودفع المكارِهِ وإزالة الكروب والشدائدِ؛ فلولا دفعُه عنهم وتفريجُه لكُرُباتهم وإزالتُهُ لعسرِهِم؛ لاستمرَّتْ عليهم المكارهُ والشدائدُ، فقراءُ إليه في تربيتهم بأنواع التربية وأجناس التدبير، فقراء إليه في تألُّههم له وحُبِّهم له وتعبُّدهم وإخلاص العبادة له تعالى؛ فلو لم يوفِّقْهم لذلك؛ لهلكوا وفسدتْ أرواحُهم وقلوبُهم وأحوالُهم، فقراءُ إليه في تعليمهم ما لا يعلمون وعملهم بما يُصْلِحُهم؛ فلولا تعليمُه؛ لم يتعلَّموا، ولولا توفيقُه؛ لم يَصْلُحوا؛ فهم فقراء بالذات إليه بكلِّ معنى وبكل اعتبارٍ، سواء شعروا ببعض أنواع الفقرِ أم لم يشعُروا، ولكنَّ الموفَّق منهم الذي لا يزال يشاهدُ فَقْرَه في كل حال من أمورِ دينه ودنياه، ويتضرَّعُ له ويسألُه أنْ لا يَكِلَه إلى نفسِهِ طرفةَ عين وأنْ يعينَه على جميع أمورِهِ، ويستصحبُ هذا المعنى في كلِّ وقتٍ؛ فهذا حريٌّ بالإعانة التامَّة من ربِّه وإلهه الذي هو أرحمُ به من الوالدةِ بولدها.
{والله هو الغنيُّ الحميدُ}؛ أي: الذي له الغنى التامُّ من جميع الوجوه؛ فلا يحتاجُ إلى ما يحتاجُ إليه خلقُه، ولا يفتقرُ إلى شيءٍ مما يفتقرُ إليه الخلقُ، وذلك لكمال صفاتِهِ، وكونِها كلها صفاتِ كمال ونعوتَ جلال، ومن غناه تعالى أنَّه أغنى الخلقَ في الدُّنيا والآخرة، الحميدُ في ذاته، وأسمائِهِ؛ لأنَّها حسنى، وأوصافه؛ لكونها عليا، وأفعاله؛ لأنَّها فضلٌ وإحسانٌ وعدلٌ وحكمةٌ ورحمةٌ، وفي أوامره ونواهيه؛ فهو الحميدُ على ما فيه، وعلى ما منّه ، وهو الحميدُ في غناه، الغنيُّ في حمده.
{15} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaongelesha watu wote, na kuwajulisha hali zao na sifa zao.
Na kwamba wao ni masikini mbele ya Mwenyezi Mungu kwa namna zote: Ni wahitaji katika kuwaumba. Kwani, lau asingewaumba, wasingelikuwepo. Nao pia ni wahitaji katika kuwatayarisha na nguvu ambayo lau asingewatayarisha kwa hiyo, wasingejiandaa kwa ajili ya kazi yoyote ile. Nao pia ni wahitaji katika kuwapa kutoa chakula, riziki, neema za dhahiri na zilizofichikana. Na lau kuwa si fadhila zake, wema wake, na kuwasahilishia mambo, basi wasingeliweza kupata riziki wala neema yoyote. Nao pia ni wahitaji katika kuwazuilia adhabu, machukizo, dhiki na magumu. Kwa hivyo, kama hangewazuilia hayo na kuwaondolea dhiki na ugumu wao, machukizo na magumu yangeendelea kuwapata. Nao pia ni wahitaji katika kuwalea kwa aina mbalimbali za malezi na uendeshaji. Na ni wahitaji kwake katika kumfanya kuwa ndiye mungu wao, kumpenda kumuabudu, kumkusudia Yeye tu katika ibada. Na kama hangewawezesha kufanya hivyo, wangeangamia na nafsi zao, mioyo yao, na hali zao zingeharibika. Nao pia ni wahitaji kwake katika kuwafunza yale wasiyoyajua, na kutenda yale ambayo yanawafanya kuwa vizuri. Na kama asingewaliwafunza, basi hawangejifunza. Na kama hangewawezesha, hawangekuwa vizuri. Kwa hivyo, wao ni wahitaji kwake kwa dhati zao kwa kila maana ya uhitaji na kila hali ya mazingatio ya hilo, hata kama watahisi aina fulani za uhitaji au la. Lakini aliyewezeshwa miongoni mwao ni yule anayeendelea kuhusu uhitaji wake katika kila hali miongoni mwa hali zake za kidini yake na dunia, na kumuomba kwa unyenyekevu na kumuomba asimwachie nafsi yale kwa kiasi cha kupepesa jicho, na amsaidie katika mambo yake yote, na aihisi maana hii kila wakati. Mtu kama huyu anastahiki zaidi kusaidiwa kikamilifu kutoka kwa Mola wake Mlezi na Mungu wake, ambaye ni mwingi wa rehema zaidi kwake kuliko mama kwa mtoto wake. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa." Yaani, mwenye ukwasi kamili kwa namna zote. Hahitaji kile ambacho viumbe vyake vinakihitaji, na hapungukiwi na chochote ambacho viumbe vyake vinapungukiwa, na hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wa sifa zake, na ukweli kwamba zote ni sifa za ukamilifu na utukufu. Na katika ukwasi wake Mtukufu ni kwamba Yeye ndiye anayewatosheleza viumbe duniani na akhera. Naye ni Msifiwa katika dhati yake na majina yake. Kwa sababu majina hayo ni mazuri zaidi, na sifa zake ni za juu zaidi, na kwa sababu matendo yake ni fadhila, ihsani, uadilifu, hekima, na rehema, na katika maamrisho yake na makatazo yake. Yeye ndiye Msifiwa kwa yale yaliyomo ndani yake na kwa yale yatokayo kwake, na ni Msifiwa katika ukwasi wake, Mkwasi katika sifa zake.
#
{16} {إن يَشَأْ يُذْهِبْكم ويأتِ بخلقٍ جديدٍ}: يُحتمل أنَّ المرادَ: إنْ يشأ يُذْهِبْكم أيُّها الناس ويأتِ بغيركم من الناس أطوع لله منكم، ويكون في هذا تهديدٌ لهم بالهلاك والإبادة، وأنَّ مشيئتَه غيرُ قاصرة عن ذلك. ويُحتمل أنَّ المرادَ بذلك إثباتُ البعث والنُّشور، وأنَّ مشيئةَ الله تعالى نافذةٌ في كلِّ شيءٍ، وفي إعادتكم بعد موتكم خلقاً جديداً، ولكن لذلك الوقت أجلٌ قدَّره الله لا يتقدَّم عنه ولا يتأخَّر.
{16} "Akitaka, atakuondoeni na alete viumbe vipya.
" Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni kwamba: Akitaka, atawaondoa, enyi watu, na kuwaleta watu wengine watiifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi. Na hili linakuwa ni tishio kwao kwamba wanaweza kuangamizwa na kutokomezwa, na kwamba mapenzi yake hayawezi kushidwa kufanya hilo. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa hapa ni kuthibitisha suala la ufufuo na kutawanyika kwa watu siku ya Kiyama. Na kwamba mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yanatekelezeka katika kila kitu, na katika kuwarudisha baada ya kifo chenu mkawa viumbe vipya. Lakini hilo lina wakati maalumu ambao Mwenyezi Mungu aliuweka na haliwezi kuutangulia wala kuchelewa zaidi yake.
#
{17} {وما ذلك على الله بعزيزٍ}؛ أي: بممتنع ولا معجزٍ له.
{17} "Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, si kitu kisichowezekana wala cha kumshinda.
#
{18} ويدلُّ على المعنى الأخير ما ذكره بعده في قوله: {ولا تزرُ وازرةٌ وِزْرَ أخرى}؛ أي: في يوم القيامةِ كلُّ أحدٍ يُجازى بعمله، ولا يحملُ أحدٌ ذنبَ أحدٍ. {وإن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ}؛ أي: نفسٌ مثقلةٌ بالخطايا والذنوب تستغيثُ بمن يحمل عنها بعضَ أوزارها، {لا يُحْمَلْ منه شيءٌ ولو كان ذا قُربى}: فإنَّه لا يَحْمِلُ عن قريبٍ، فليست حالُ الآخرة بمنزلةِ حال الدُّنيا يساعدُ الحميم حميمَه والصديقُ صديقَه، بل يوم القيامةِ يتمنَّى العبدُ أن يكونَ له حقٌّ على أحدٍ، ولو على والديه وأقاربه. {إنَّما تنذرُ الذين يَخْشَوْنَ ربَّهم بالغيب وأقاموا الصلاة}؛ أي: هؤلاء الذين يقبلون النذارةَ وينتفعون بها، أهلُ الخشية لله بالغيبِ. الذين يخشونَه في حال السرِّ والعلانية والمشهدِ والمغيبِ وأهل إقامةِ الصلاة بحدودِها وشروطِها وأركانها وواجباتها وخُشوعها؛ لأنَّ الخشيةَ لله تستدعي من العبدِ العملَ بما يخشى من تضييعِهِ العقاب والهربَ مما يخشى من ارتكابِهِ العذاب، والصلاة تدعو إلى الخير وتنهى عن الفحشاء والمنكر. {ومن تزكَّى فإنَّما يتزكَّى لنفسِهِ}؛ أي: ومن زكَّى نفسَه بالتنقِّي من العيوب كالرياء والكبر والكذبِ والغشِّ والمكرِ والخداع والنفاقِ ونحو ذلك من الأخلاق الرذيلة، وتحلَّى بالأخلاق الجميلة من الصدقِ والإخلاصِ والتواضُع ولين الجانب والنُّصح للعباد وسلامةِ الصدرِ من الحقدِ والحسدِ وغيرِهما من مساوئ الأخلاق؛ فإنَّ تزكِيَتَه يعود نفعُها إليه ويصلُ مقصودُها إليه، ليس يضيعُ من عملِهِ شيءٌ. {وإلى الله المصيرُ}: فيجازي الخلائقَ على ما أسْلَفوه، ويحاسِبُهم على ما قدَّموه وعَمِلوه، ولا يغادِرُ صغيرةً ولا كبيرةً إلاَّ أحصاها.
{18} Maana ya mwisho inaashiriwa na aliyoyataja baada yake katika kauli yake: "Na mbebaji hatabeba mzigo wa mwengine" Siku ya Kiyama. Kila mmoja atalipwa kwa matendo yake, na hakuna atakayebeba dhambi ya mwengine. "Na aliyetopewa na mzigo wake" yaani, nafsi iliyolemewa na madhambi ikitafuta msaada ili isaidiwe kuibeba baadhi ya mizigo yake "hautachukuliwa hata kidogo, hata kama ni jamaa yake." Kwa sababu hali ya Akhera si kama hali ya dunia ambapo rafiki alikuwa akimsaidia rafiki yake. Bali Siku ya Kiyama mja atatamani lau angekuwa na haki juu ya yeyote, hata kama ni juu ya wazazi wake na jamaa zake. "Hakika wewe unawaonya wale wanaomcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Swala." Yaani, hawa ndio wanaokubali maonyo, na kunufaika nayo, watu wanaomcha Mwenyezi Mungu kwa ghaibu. Wale wanaomuogopa kwa siri na hadharani, wanaosimamisha Swala kwa mipaka yake, masharti yake, nguzo zake, wajibu wake na unyenyekevu wake. Kwa sababu kumhofu Mwenyezi Mungu kunamtaka mja kufanya yale ambayo anayahofia kwamba asipoyafanya ataadhibiwa. Nayo swala inaitia mema na inakataza machafu na maovu. "Na mwenye kujitakasa" kwa kujiweka mbali na kasoro kama vile unafiki, kujionyesha, kiburi, uwongo, udanganyifu, hadaa, njama mbaya na maadili mengine mabaya, na akawa na maadili mazuri kama vile ukweli, ikhlasi, unyenyekevu, ulaini kwa watu
(upole) na nasaha nzuri kwa waja wake, na kifua chake kikawa salama kutokana na chuki, husuda, na maadili mengine maovu; basi manufaa ya kujitakasa kwake huku yanamrudia mwenyewe na madhumuni yake yatamfikia yeye, na hakuna chochote katika matendo yake yatayopotea. "Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu." Naye atawalipa viumbe kwa yale waliyofanya kabla, na atawafanyia hesabu kwa yale waliyoyatanguliza, na wala hataacha kitu chochote kidogo wala kikubwa isipokuwa atakihesabu.
{وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَى وَالْبَصِيرُ (19) وَلَا الظُّلُمَاتُ وَلَا النُّورُ (20) وَلَا الظِّلُّ وَلَا الْحَرُورُ (21) وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَنْ يَشَاءُ وَمَا أَنْتَ بِمُسْمِعٍ مَنْ فِي الْقُبُورِ (22) إِنْ أَنْتَ إِلَّا نَذِيرٌ (23) إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَإِنْ مِنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ (24)}.
19. Na kipofu na mwenye kuona hawalingani. 20. Wala giza na mwangaza. 21. Wala kivuli na joto. 22. Wala hawalingani walio hai na maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini. 23. Hukuwa wewe isipokuwa ni mwonyaji. 24. Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote isipokuwa ulipata mwonyaji kati yao.
#
{19 - 23} يخبر تعالى أنَّه لا يتساوى الأضدادُ في حكمة الله وفيما أوْدَعَه في فِطَرِ عباده، فلا {يستوي الأعمى}: فاقد البصر {والبصيرُ. ولا الظلماتُ ولا النورُ. ولا الظِّلُّ ولا الحَرورُ. وما يستوي الأحياءُ ولا الأمواتُ}؛ فكما أنه من المتقرِّر عندكم الذي لا يَقْبَلُ الشكَّ أنَّ هذه المذكورات لا تتساوى؛ فكذلك فَلْتَعْلَموا أنَّ عدمَ تساوي المتضادَّاتِ المعنويَّةِ أولى وأولى؛ فلا يستوي المؤمنُ والكافرُ، ولا المهتدي والضالُّ، ولا العالم والجاهل، ولا أصحابُ الجنة وأصحابُ النار، ولا أحياءُ القلوبِ وأمواتُها؛ فبين هذه الأشياء من التفاوتِ والفَرْقِ ما لا يعلمُه إلاَّ الله تعالى. فإذا علمتَ المراتبَ وميَّزْتَ الأشياء وبان الذي ينبغي أن يُتَنافَسَ في تحصيله من ضدِّه؛ فليخترِ الحازمُ لنفسه ما هو أولى به وأحقُّ بالإيثار. {إنَّ الله يُسْمِعُ مَن يشاءُ}: سماع فَهْم وقَبول؛ لأنَّه تعالى هو الهادي الموفِّق. {وما أنتَ بمسمعٍ مَن في القبورِ}؛ أي: أمواتُ القلوب، أو: كما أنَّ دعاءَك لا يفيدُ سكانَ القبورِ شيئاً، كذلك لا يفيدُ المعرِضَ المعاندَ شيئاً، ولكنَّ وظيفتَكَ النذارةُ وإبلاغُ ما أرسلتَ به؛ قُبِلَ منك أم لا، ولهذا قال: {إنْ أنتَ إلا نذيرٌ}.
{19 - 23} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuwa vinyume si sawa katika hekima ya Mwenyezi Mungu, na katika yale aliyoyaweka katika maumbile ya waja wake. Kwa hivyo "kipofu halingani" "na anayeona wala giza na nuru, wala kivuli na joto. Wala hawalingani waliohai na maiti." Basi kama vile ilivyokwisha julikana vyema kwenu bila shaka yoyote ya kwamba hivi vilivyotajwa si sawa. Vivyo hivyo, jueni kwamba inafailia zaidi kutolingana vinyume viwili katika vitu visivyo vya kishisia. Kwa hivyo, Muumini na kafiri hawawi sawa, wala aliyeongoka na mpotofu, wala mwanazuoni na mjinga, wala watu wa Peponi na watu wa Motoni, wala waliohai moyoni na waliokufa humo. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mambo haya ambazo hazijui vilivyo isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu. Basi ukishajua viwango na ukapambanua mambo mbalimbali, na kinachopaswa kushindana ili kukipata kikawa wazi mbali na kinyume chake, basi mtu mwenye azimio kubwa na ajichagulie mwenyewe kilicho bora zaidi kwake na kinachostahili zaidi kupendelewa. "Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye" kusikia kwa kufahamu na kukubali. Kwani Yeye Mtukufu ndiye mwenye kuongoa na kuwezesha. "Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini;" yaani, wafu moyoni mwao. Au kama vile dua yako haiwanufaishi walio makaburini, vivyo hivyo haimnufaishi mwenye kupeana mgongo, mkaidi. Bali kazi yako ni kuonya tu na kufikisha uliyotumwa nayo. Sawa yatakubaliwa au yasikubaliwe,
na ndiyo maana akasema: "Hukuwa wewe isipokuwa ni mwonyaji."
#
{24} {إنا أرسلناك بالحقِّ}؛ أي: مجرَّدُ إرسالنا إيَّاك بالحقِّ؛ لأنَّ الله تعالى بَعَثَكَ على حين فترةٍ من الرسل وطموسٍ من السُّبل واندراسٍ من العلم وضرورةٍ عظيمةٍ إلى بعثك، فبعثَكَ اللَّه رحمةً للعالمين، وكذلك ما بَعَثْناك به من الدين القويم والصراطِ المستقيم حقٌّ لا باطل، وكذلك ما أرسلناك به من هذا القرآن العظيم وما اشتملَ عليه من الذِّكْرِ الحكيم حقٌّ وصدقٌ، {بشيراً}: لمن أطاعَكَ بثواب الله العاجل والآجل {ونذيراً}: لمن عصاك بعقاب الله العاجل والآجل، ولست ببدعٍ من الرسل. فما {منْ أمَّةٍ}: من الأمم الماضية والقرون الخالية {إلاَّ خلا فيها نذيرٌ}: يقيمُ عليهم حجَّةَ الله؛ {لِيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عن بَيِّنَةٍ ويَحْيا مَنْ حَيَّ عن بَيِّنَةٍ}.
{24} "Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki." Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alikutuma katika wakati usiokuwa na Mitume, ambapo njia sahihi zilikuwa zimefutika, na elimu ilikuwa imepotea, na kulikuwepo na haja kubwa ya kukutuma kama Mtume. Basi Mwenyezi Mungu akakutuma uwe rehema kwa walimwengu, na vile vile yale tuliyokutuma nayo ya Dini madhubuti na njia iliyonyooka ni haki wala si batili. Na vile vile tuliyokutuma nayo ya Qur-ani hii tukufu na yaliyomo ndani yake ya ukumbusho wenye hekima, ni ya haki na ya ukweli, "kuwa ni mbashiri" kwa mwenye kukutii kwamba atapata malipo mazuri ya Mwenyezi Mungu, ya haraka na ya baadaye. "Na mwonyaji," kwa anayekuasi kwamba atapata adhabu ya Mwenyezi Mungu ya haraka na ya baadaye, nawe si wa kwanza miongoni mwa Mitume. Hakuna "umma" wowote katika umma za zamani na karne zilizopita, "isipokuwa ulipata mwonyaji kati yao" wa kuwasimamishia hoja, "Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio dhahiri, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio dhahiri."
{وَإِنْ يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالزُّبُرِ وَبِالْكِتَابِ الْمُنِيرِ (25) ثُمَّ أَخَذْتُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ (26)}.
25. Na wakikukadhibisha, basi walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa ushahidi wa waziwazi na kwa maandiko na Kitabu chenye nuru. 26. Kisha nikawakamata wale waliokufuru. Basi kuchukia kwangu kulikuwaje?
#
{25} أي: وإنْ يكذِّبْك أيُّها الرسول هؤلاء المشركون؛ فلست أول رسول كُذِّبَ، {فقد كَذَّبَ الذين من قبلهم جاءتْهم رسُلُهم بالبيناتِ}: الدالاَّتِ على الحقِّ وعلى صدقهم فيما أخبروهم به. {والزُّبُرِ}؛ أي: الكتب المكتوبة المجموع فيها كثير من الأحكام. {والكتابِ المنيرِ}؛ أي: المضيء في أخباره الصادقة وأحكامه العادلة، فلم يكن تكذيبُهم إياهم ناشئاً عن اشتباه أو قصورٍ بما جاءتْهم به الرسلُ، بل بسبب ظلمِهِم وعنادِهِم.
{25} Yaani, wakikukadhibisha hawa washirikina, ewe Mtume, basi wewe si Mtume wa kwanza kukadhibishwa. "Wakikukadhibisha, basi walikwisha kanusha wale waliokuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa ushahidi wa waziwazi;" unaoashiria haki na ukweli wao katika yale waliyowajulisha. "Na kwa maandiko" yenye hukumu mbalimbali. "Na Kitabu chenye nuru;" katika habari zake za ukweli na hukumu zake za uadilifu. Na kukadhibisha kwao huko hakukutokana na kuwepo mchanganyiko wowote wala upungufu katika yale waliyowaletea Mitume wao, bali ni kwa sababu ya dhuluma na ukaidi wao.
#
{26} {ثم أخذتُ الذين كفروا}: بأنواع العقوباتِ {فكيف كان نكيرِ}: عليهم؟ كان أشدَّ النكير وأعظمَ التنكيل؛ فإيَّاكم وتكذيبَ هذا الرسول الكريم، فيصيبكم كما أصاب أولئك من العذاب الأليم والخزي الوخيم.
{26} "Kisha nikawakamata wale waliokufuru" kwa namna mbalimbali za adhabu. "Basi kuchukia kwangu kulikuwaje?" Kulikuwa kuchukua kukali na adhabu kubwa zaidi. Basi jihadharini nanyi na kumkadhibisha Mtume huyu mtukufu, mkaja patwa na adhabu chungu na fedheha kubwa kama iliyowapata wale.
{أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ (27) وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالْأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَلِكَ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ (28)}.
27. Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbalimbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana. 28. Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinahitalifiana. Kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja kuumba kwake vitu vilivyo kinyume, ambavyo asili yake ni moja na kiini chake ni kimoja lakini vinatofauti sana kama inavyoonekana na kujulikana, ili awaonyeshe waja wake ukamilifu wa uwezo wake na hekima yake ya ajabu.
#
{27} فمن ذلك أنَّ الله تعالى أنزلَ من السماء ماءً، فأخرج به من الثمراتِ المختلفاتِ والنباتات المتنوعاتِ ما هو مشاهدٌ للناظرين، والماء واحدٌ والأرضُ واحدةٌ. ومن ذلك الجبالُ التي جعلها الله أوتاداً للأرض؛ تجدِها جبالاً مشتبكةً، بل جبلاً واحداً، وفيها ألوان متعددةٌ، فيها {جُدَدٌ بيضٌ}؛ أي: طرائق بيضٌ، وفيها طرائقُ صفرٌ وحمرٌ، وفيها {غرابيبُ سودٌ}؛ أي: شديدة السواد جدًّا.
{27} Na katika hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na akatoa kwayo matunda mbalimbali na mimea mbalimbali inayoonekana kwa wenye kutazama, na maji ni yale mamoja na ardhi ni ile moja. Na miongoni mwa hayo ni milima ambayo Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa vigingi vya ardhi. Utaikuta ni milima iliyofungamana. Bali, hata mlima mmoja tu, ndani yake zimo rangi nyingi. Ndani yake, "imo mistari myeupe." Yaani, zimo njia nyeupe na nyekundu, na pia kuna "myeusi sana."
#
{28} ومن ذلك الناسُ والدوابُّ والأنعام؛ فيها من اختلاف الألوان والأوصافِ والأصواتِ والهيئاتِ ما هو مرئيٌّ بالأبصار مشهودٌ للنُّظَّارِ، والكلُّ من أصل واحدٍ ومادةٍ واحدةٍ، فتفاوتُها دليلٌ عقليٌّ على مشيئةِ الله تعالى التي خَصَّصَتْ ما خَصَّصَتْ منها بلونِهِ ووصفِهِ، وقدرة الله تعالى حيث أوجدها كذلك، وحكمتِهِ ورحمتِهِ حيث كان ذلك الاختلاف وذلك التفاوتُ فيه من المصالح والمنافع ومعرفة الطرق ومعرفة الناس بعضهم بعضاً ما هو معلوم، وذلك أيضاً دليلٌ على سعة علم الله تعالى، وأنه يَبْعَثُ مَنْ في القبور. ولكن الغافل ينظر في هذه الأشياء وغيرها نَظَرَ غفلةٍ لا تحدثُ له تذكُّراً، وإنَّما ينتفع بها من يخشى الله تعالى ويعلم بفكرِهِ الصائب وجهَ الحكمة فيها، ولهذا قال: {إنَّما يخشى اللهَ من عبادِهِ العلماءُ}: فكلُّ من كان بالله أعلم؛ كان أكثرَ له خشيةً، وأوجبتْ له خشيةُ الله الانكفافَ عن المعاصي والاستعدادَ للقاء مَنْ يخشاه، وهذا دليلٌ على فضيلة العلم؛ فإنَّه داع إلى خشية الله، وأهلُ خشيتِهِ هم أهلُ كرامتِهِ؛ كما قال تعالى: {رضي الله عنهم ورَضُوا عنه ذلك لِمَنْ خَشِيَ ربَّه}. {إنَّ الله عزيزٌ}: كامل العزَّة، ومن عزَّته خَلْقُ هذه المخلوقات المتضادَّات. {غفورٌ}: لذنوب التائبين.
28. Na katika hayo ni wamo watu, na wanyama, na mifugo. Ndani yao kuna tofauti katika rangi zao, sifa zao, sauti zao na mionekano yao inayoonekana kwa macho na kushuhudiwa na watazamaji, na vyote hivyo vilitokana na asili moja na kiini kimoja. Kwa hivyo, kutofautiana kwao huku ni ushahidi wa kiakili juu ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ambayo yalivifanya maalumu vitu hivyo kwa kuvipa kila kimoja rangi yake na sifa zake, na pia ni ishara juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu ambapo aliviumba hivyo. Na pia ni ishara juu ya hekima yake na rehema zake ambapo tofauti hizo zina masilahi, manufaa, na kujua njia na watu kujuana wao kwa wao kama inavyojulikana. Haya ni ushahidi juu ya upana wa elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba atawafufua waliomo makaburini. Lakini mtu aliyeghafilika huyatazama mambo haya na mengineyo kwa mtazamo wa kughafilika ambako hakumfanyi kukumbuka. Wale wanaofaidika nayo ni wale wanaomcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na ambao wanajua kwa fikira zao sahihi hekima iliyoko ndani yake,
na ndiyo maana akasema: "Kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni." Kwa hivyo, kila ambaye anamjua vyema Mwenyezi Mungu, anakuwa ni mwenye kumuogopa zaidi, na huku kumhofu Mwenyezi Mungu kunamfanya ajiepushe na dhambi na kujitayarisha kukutana na yule anayemcha.Na huu ni ushahidi wa ubora wa elimu,kwani inaitia kumcha Mwenyezi Mungu. Na wale wanaomcha ndio watakaopata utukufu wake,
kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wako radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi." "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu" kamili. Na katika nguvu zake ni kuumba kwake viumbe hawa walio kinyume. "Mwenye kusamehe" dhambi za waliotubu.
{إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنْفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَنْ تَبُورَ (29) لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ (30)}.
29. Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Swala, na wakatoa kwa siri na kwa dhahiri katika vile tulivyowaruzuku, hao hutaraji biashara isiyobwaga. 30. Ili Yeye awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani kubwa.
#
{29} {إنَّ الذين يتلونَ كتاب الله}؛ أي: يتَّبعونَه في أوامره فيمتَثِلونها وفي نواهيه فيترُكونها وفي أخبارِهِ فيصدِّقونها ويعتَقِدونها ولا يقدِّمون عليه ما خالَفَه من الأقوال، ويتلون أيضاً ألفاظَه بدراستِهِ، ومعانِيه بتتبُّعِها واستخراجِها، ثم خصَّ من التلاوة بعدما عمَّ الصلاةَ ـ التي هي عمادُ الدِّين ونورُ المسلمين وميزانُ الإيمان وعلامةُ صدق الإسلام ـ النفقةَ على الأقارب والمساكين واليتامى وغيرهم من الزكاة والكفارات والنذور والصدقات، {سرًّا وعلانيةً}: في جميع الأوقات؛ {يرجونَ}: بذلك {تجارةً لن تبورَ}؛ أي: لن تكسدَ وتفسدَ، بل تجارة هي أجلُّ التجاراتِ وأعلاها وأفضلُها ألا وهي رضا ربِّهم والفوزُ بجزيل ثوابِهِ والنجاةُ من سخطِهِ وعقابِهِ، وهذا فيه الإخلاصُ بأعمالهم، وأنَّهم لا يرجون بها من المقاصدِ السيئةِ والنيَّاتِ الفاسدةِ شيئاً.
{29} "Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu;" yaani, wanaifuata kwa maamrisho yake, na watatosheka nayo, katika makusudio yake, ili waiache na katika habari zake, waiamini na kuiogopa na wala wasimpe maneno ya utupu wake. Na pia wanasoma maneno yake kwa masomo yake, na maana zake kwa kuifuatilia na kuitoa, kisha ni maalumu kutokana na kisomo baada ya sala ya swala - Kutoa kwa jamaa, masikini, mayatima, na zaka nyingine, kafara,nadhiri na sadaka, kwa siri na hadharani; "Wanatumaini." Kwa hivyo, ni "biashara ambayo haitashindwa;" yaani, haitasimama wala kuharibika. Bali ni biashara iliyo tukufu, ya juu kabisa, na iliyobora kuliko biashara zote, ambayo ni ridhiki ya Mola wao Mlezi, na kupata ujira wake mwingi, na kuepuka ghadhabu na adhabu yake. Hili linahusisha ikhlasi katika matendo yao, na hawana matumaini ya nia yoyote mbaya au nia mbovu kutoka kwayo.
#
{30} ذكر أنَّهم حصل لهم ما رَجَوْه، فقال: {لِيُوَفِّيهم أجورَهم}؛ أي: أجور أعمالهم على حسب قِلَّتِها وكثرتها وحُسنها وعدمِهِ، {ويزيدَهُم من فضلِهِ}: زيادة عن أجورهم. {إنَّه غفورٌ شكورٌ}: غفر لهم السيئاتِ، وقَبِلَ منهم القليل من الحسنات.
{30} Alitaja kuwa walipata yale waliyokuwa wakiyatarajia,
akasema: "Ili Yeye awalipe ujira wao kwa ukamilifu" kulingana na uchache wake, wingi wake, na uzuri wake, na kutokuwepo kwa hayo. "Na awazidishie kutokana na fadhila zake" zaidi ya malipo yao waliyostahiki. "Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani kubwa." Aliwasamehe madhambi yao, na akawakubalia mema machache.
{وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ هُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ إِنَّ اللَّهَ بِعِبَادِهِ لَخَبِيرٌ بَصِيرٌ (31) ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ وَمِنْهُمْ مُقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ (32) جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِنْ ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ (33) وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ (34) الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِنْ فَضْلِهِ لَا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلَا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ (35)}.
31. Na hayo tuliyokufunulia kutoka Kitabuni ni Kweli, yenye kusadikisha yale yaliyokuwa kabla yake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni Mwenye habari na Mwenye kuona. 32. Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateua miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliyejidhulumu, na yupo wa katikati, na yupo aliyetangulia katika mambo ya heri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu. 33. Mabustani ya milele watayaingia. Huko watavikwa vikuku vya dhahabu na lulu, na nguo zao humo ni za hariri. 34.
Na watasema: Alhamdulillahi
(Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu) aliyetuondolea huzuni wote. Hakika Mola wetu Mlezi bila ya shaka ni Mwenye kusamehe, Mwenye shukrani. 35. Ambaye kwa fadhila yake ametuweka makao ya kukaa daima; humu haitugusi taabu wala humu hakutugusi kuchoka.
#
{31} يذكر تعالى أنَّ الكتابَ الذي أوحاه إلى رسوله {هو الحقُّ}: من كثرةِ ما اشتمل عليه من الحقِّ، كأنَّ الحقَّ منحصرٌ فيه؛ فلا يكنْ في قلوبكم حرجٌ منه ولا تتبرَّموا منه ولا تستهينوا به؛ فإذا كان هو الحقَّ؛ لزم أنَّ كلَّ ما دلَّ عليه من المسائل الإلهيَّة والغيبيَّة وغيرها مطابقٌ لما في الواقع؛ فلا يجوز أن يُرادَ به ما يخالفُ ظاهرَه وما دلَّ عليه. {مصدِّقاً لما بينَ يديهِ}: من الكتب والرسل؛ لأنَّها أخبرتْ به، فلما وُجِدَ وظهرَ؛ ظهرَ به صدقُها؛ فهي بشرتْ به وأخبرتْ، وهو صدَّقها، ولهذا لا يمكن أحداً أن يؤمنَ بالكتب السابقة وهو كافرٌ بالقرآن أبداً؛ لأنَّ كفره به ينقضُ إيمانه بها؛ لأنَّ من جملة أخبارِها الخبرَ عن القرآن، ولأنَّ أخبارها مطابقةٌ لأخبار القرآن. {إنَّ الله بعبادِهِ لخبيرٌ بصيرٌ}: فيعطي كلَّ أمةٍ وكلَّ شخص ما هو اللائقُ بحالِهِ، ومن ذلك أنَّ الشرائع السابقة لا تَليق إلاَّ بوقتها وزمانها، ولهذا ما زال الله يرسلُ الرسلَ رسولاً بعد رسول حتى خَتَمَهم بمحمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، فجاء بهذا الشرع الذي يَصْلُحُ لمصالح الخلق إلى يوم القيامةِ، ويتكفَّل بما هو الخير في كل وقت، ولهذا لمَّا كانت هذه الأمةُ أكملَ الأمم عقولاً وأحسنهم أفكاراً وأرقَّهم قلوباً وأزكاهم أنفساً؛ اصطفاهم تعالى واصطفى لهم دينَ الإسلام وأورثهم الكتابَ المهيمنَ على سائر الكتب.
{31} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja kwamba Kitabu alichomteremshia Mtume wake "ni Kweli." Kwa sababu ya haki nyingi iliyo ndani yake, kama kwamba haki iko katika hilo peke yake. Msiwe na haya katika nyoyo zenu, wala msiudhike, wala msidharau. Ikiwa ni ukweli; ni muhimu kwamba kila kitu kinachoonyesha kuhusu mambo ya kimungu, yasiyoonekana na mambo mengine, kiwe sawa na kile ambacho ni halisi. Haijuzu kumaanisha kitu ambacho kinapingana na maana yake dhahiri na kile kinachoashiria, "yenye kuyasadikisha yaliyokuwa kabla yake;" katika vitabu na Mitume. Kwa sababu aliambiwa kuhusu hilo, na lilipopatikana na kuonekana, Unyoofu wake ulionekana. Akampa bishara na akamjulisha, naye akamuamini. Na kwa ajili hiyo haiwezekani kwa yeyote kuamini vitabu vilivyotangulia na hali ya kuwa ni kafiri wa Qur-ani hata kidogo. Kwa sababu kutokuamini kwake kunabatilisha imani yake juu yake. Kwa sababu miongoni mwa habari zake ni habari za Qur-ani, na kwa sababu habari zake zinafanana na habari za Qur-ani. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye kuwaona waja wake." Humpa kila umma na kila mtu inavyomstahiki hali yake.Na kutokana na hayo ni kuwa sheria zilizotangulia hazifai isipokuwa kwa wakati wake na kwa ajili hiyo. Mwenyezi Mungu aliendelea kutuma Mitume, Mtume baada ya Mjumbe, mpaka akawapiga muhuri kwa Muhammad – rehema na Amani zimshukie – basi akaleta sheria ambayo inafaa kwa maslahi ya viumbe mpaka Siku ya Kiyama, na akaichukua kujali yaliyomema kila wakati. Na kwa sababu hii, kwa kuwa taifa hili lina akili kamili zaidi, mawazo bora, mioyo ya upole zaidi, na roho safi kabisa; Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwachagua na akawachagulia Dini ya Kiislamu na akawarithisha Kitabu kinachotawala vitabu vingine vyote.
#
{32} ولهذا قال: {ثم أوْرَثْنا الكتاب الذين اصْطَفَيْنا من عبادِنا}: وهم هذه الأمة. {فمنهم ظالمٌ لنفسِهِ}: بالمعاصي التي هي دون الكفرِ، {ومنهم مقتصدٌ}: مقتصرٌ على ما يجب عليه، تاركٌ للمحرَّم، {ومنهم سابقٌ بالخيرات}؛ أي: سَارَعَ فيها، واجْتَهَدَ فسبق غيره، وهو المؤدي للفرائض، المكثر من النوافل، التارك للمحرم والمكروه؛ فكلهم اصطفاه الله تعالى لوراثة هذا الكتاب، وإن تفاوتتْ مراتِبُهم وتميَّزت أحوالُهم؛ فلكل منهم قسطٌ من وراثتِهِ، حتى الظالم لنفسه؛ فإنَّ ما معه من أصل الإيمان وعلوم الإيمان وأعمال الإيمان من وراثة الكتاب؛ لأنَّ المراد بوراثة الكتاب وراثةُ علمِهِ وعمله ودراسةُ ألفاظِهِ واستخراج معانيه، وقوله: {بإذن الله}: راجعٌ إلى السابق إلى الخيرات ؛ لئلاَّ يغترَّ بعمله، بل ما سَبَقَ إلى الخيرات إلاَّ بتوفيق الله تعالى ومعونته؛ فينبغي له أن يشتغلَ بشكر الله تعالى على ما أنعم به عليه. {ذلك هو الفضلُ الكبيرُ}؛ أي: وراثة الكتاب الجليل لمن اصطفى تعالى من عباده هو الفضلُ الكبيرُ الذي جميع النعم بالنسبة إليه كالعدم، فأجلُّ النعم على الإطلاق وأكبرُ الفضل وراثةُ هذا الكتاب.
{32} Ndiyo maana akasema: "Kisha tukawarithisha Kitabu wale tuliowateua miongoni mwa waja wetu. Na hao ndio Ummah huu. "Na miongoni mwao yuko aliyejidhulumu," kwa madhambi yaliyopungukiwa na ukafiri. "Na na yupo wa katikati," anajiwekea faradhi na kuacha ya haramu. "Na miongoni mwao yuko hutangulia katika mambo mema." Yaani, aliharakisha kufanya hivyo, akafanya kazi kwa bidii, na kuwapita wengine. Yeye ndiye anayetekeleza majukumu ya faradhi, anaswali sana, na anaacha yale yaliyoharamishwa na yasiyopendeza. Wote walichaguliwa na Mwenyezi Mungu kurithi kitabu hiki, hata kama safu zao zilitofautiana na hali zao zilikuwa tofauti. Kila mmoja wao ana sehemu ya urithi wake, hata dhalimu kwake mwenyewe. Kwani yale aliyo nayo ya asili ya imani, elimu ya imani, na matendo ya imani yamerithishwa kutoka katika Kitabu. Kwa sababu kinachokusudiwa kurithi kitabu ni kurithi elimu yake na kazi yake, na kusoma maneno yake, na kutoa maana zake. Na kauli yake Mwenyezi Mungu, "Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu," inarejelea matendo mema yaliyotangulia ili asidanganywe na kazi yake. Bali hatangulii katika mambo mema isipokuwa kwa neema na msaada wa Mwenyezi Mungu. Anapaswa kujishughulisha na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yale aliyomkirimia. "Hiyo ndiyo fadhila ya kuu." Yaani, Kumrithisha Kitabu Kitukufu ambaye Mwenyezi Mungu amemchagua miongoni mwa waja wake ni baraka kubwa ambayo kwake neema zote ni kana kwamba si kitu. Na neema kubwa kuliko zote ni kurithi Kitabu hiki.
#
{33} ثم ذكر جزاء الذين أوْرَثَهم كتابَه، {جناتُ عدنٍ يَدْخُلونها}؛ أي: جناتٌ مشتملاتٌ على الأشجار والظلِّ والظليل والحدائق الحسنة والأنهار المتدفِّقة والقصور العالية والمنازلِ المزخرفةِ في أبدٍ لا يزول وعيش لا يَنْفَدُ. والعَدْنُ: الإقامة؛ فجنات عدنٍ؛ أي: جنات إقامة، أضافها للإقامة لأنَّ الإقامةَ والخلودَ وصفُها ووصفُ أهلها، {يُحَلَّوْنَ فيها من أساورَ من ذهبٍ}: وهو الحُلِيُّ الذي يُجعل في اليدين على ما يحبُّون ويرونَ أنَّه أحسنُ من غيره، الرجال والنساء في الحلية في الجنة سواء. {و} يحلَّوْن فيها {لؤلؤاً}: يُنْظَمُ في ثيابهم وأجسادهم، {ولباسُهُم فيها حريرٌ}: من سندس ومن إستبرقٍ أخضر.
{33} Kisha akataja malipo ya wale aliowaachia kitabu chake: "Wataingia Mabustani ya milele." Yaani, bustani zenye miti, vivuli, bustani nzuri, mito ipitayo, majumba ya kifahari, nyumba zilizopambwa katika umilele usiofifia na uhai usioisha. Kwa hivyo Eden, makazi; Na Bustani za Edeni. Yaani, mabustani ya makazi, iliitwa makazi ya milele watu wake watapambwa humo kwa bangili za dhahabu, ambalo ni pambo linalowekwa kwenye mikono kwa yale wanayoyapenda. Wanaume na wanawake watakuwa sawa katika pambo Peponi. Watapamba humo ndani ya lulu. Imepangwa katika nguo zao na miili yao. Na nguo zao humo ni hariri, za hariri na hariri ya kijani kibichi.
#
{34} {و} لمَّا تمَّ نعيمُهم وكَمُلَتْ لَذَّتُهم؛ {قالوا الحمدُ لله الذي أذْهَبَ عنَّا الحَزَنَ}: وهذا يشملُ كلَّ حزنٍ؛ فلا حزنَ يعرض لهم بسبب نقص في جمالهم ولا في طعامهم وشرابهم ولا في لذَّاتهم ولا في أجسادهم ولا في دوام لَبْثِهم؛ فهم في نعيمٍ ما يرونَ عليه مزيداً، وهو في تزايدٍ أبدَ الآباد. {إنَّ ربَّنا لَغفورٌ}: حيث غَفَرَ لنا الزلاتِ. {شكورٌ}: حيث قَبِلَ منَّا الحسناتِ وضاعَفَها، وأعطانا من فضلِهِ ما لم تَبْلُغْهُ أعمالُنا ولا أمانينا. فبمغفرتِهِ؛ نَجَوْا من كلِّ مكروه ومرهوبٍ، وبشكرِهِ وفضلِهِ؛ حصل لهم كلُّ مرغوبٍ محبوبٍ.
{34} "Na" zilipokamilika neema zao na radhi zao zikakamilika,
"wakasema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametuondolea huzuni." Na haya ni pamoja na huzuni zote. Hakuna huzuni inayowapata kwa sababu ya upungufu wa uzuri wao, wala katika vyakula vyao na vinywaji, wala katika anasa zao, wala katika miili yao, wala katika muda wa kukaa kwao. Wako katika raha ambayo wanaona inaongezeka, na inaongezeka milele. "Hakika Mola wetu Mlezi ni Msamehevu." Ametusamehe madhambi yetu. "Mwenye shukrani," ametukubalia mema yetu na akayazidisha, na akatupa katika fadhila zake ambazo hazikufikiwa na amali na matarajio yetu. Kwa msamaha wake, waliokolewa na madhara na vitisho vyote, na kwa shukrani na neema yake; walipata kila kitu walichotaka na kupenda.
#
{35} {الذي أحَلَّنا}؛ أي: أنزلنا نزول حلول واستقرارٍ، لا نزول معبرٍ واعتبار {دار المُقامةِ}؛ أي: الدار التي تدوم فيها الإقامةُ، والدار التي يُرغب في المقام فيها؛ لكثرة خيراتها وتوالي مسرَّاتها وزوال كدوراتها، وذلك الإحلال بفضلِهِ علينا وكرمِهِ، لا بأعمالنا؛ فلولا فضلُهُ؛ لما وَصَلْنا إلى ما وَصَلْنا إليه، {لا يَمَسُّنا فيها نَصبٌ ولا يَمَسُّنا فيها لُغوبٌ}؛ أي: لا تعبٌ في الأبدان ولا في القلبِ والقُوى ولا في كثرة التمتُّع.
وهذا يدلُّ على أن الله تعالى يَجْعَلُ أبدانَهم في نشأةٍ كاملةٍ ويُهَيِّئُ لهم من أسباب الراحة على الدَّوام ما يكونون بهذه الصفة؛ بحيث لا يمسُّهم نصبٌ ولا لغوبٌ ولا همٌّ ولا حزنٌ.
ويدلُّ على أنهم لا ينامون في الجنة؛ لأنَّ النوم فائدتُه زوالُ التعب وحصولُ الراحة به، وأهل الجنةِ بخلافِ ذلك، ولأنَّه موتٌ أصغر، وأهل الجنة لا يموتون. جعلنا الله منهم بمنِّه وكرمه.
{35} "Ambaye kwa fadhila yake ametuweka," na ambayo watu wanataka kudumu humo; kwa sababu ya heri zake nyingi na furaha zake za kuendelea, na kutoweka huzuni wake. Na kuingizwa huko kunatokana na fadhila na ukarimu wake juu yetu, si kwa matendo yetu. Na lau si kwa neema yake, hatungefikia haya tuliyofikia. "Humu haitugusi taabu wala humu hakutugusi kuchoka." Yaani, hakuna uchovu wowote mwilini, wala moyoni, wala katika wingi wa starehe. Hili linaonyesha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ataiweka miili yao katika ukuaji kamili, na kuwaandalia njia za raha ya daima kiasi kwamba haiwapati tabu, wala uchovu, wala wasiwasi, wala huzuni. Na hilo linaashiria kuwa hawatalala Peponi. Kwa sababu faida ya usingizi ni kumaliza taabu na kupata mapumziko.Na wakazi wa Peponi hawako hivyo, na kwa sababu kulala ni kifo kidogo, na wakazi wa Peponi hawafi. Mwenyezi Mungu alijalie miongoni mwao kwa neema yake na ukarimu wake.
{وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَى عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ مِنْ عَذَابِهَا كَذَلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ (36) وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُمْ مَا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَنْ تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ نَصِيرٍ (37)}.
36. Na wale waliokufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu. Hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri. 37.
Na humo watapiga makelele: 'Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema siyo yale tuliyokuwa tukiyafanya.' Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakukujieni Mwonyaji? Basi onjeni! Kwani wale waliodhulumu hawana wa kuwanusuru.
#
{36} لما ذكر تعالى حال أهل الجنة ونعيمَهم؛ ذكر حالَ أهل النار وعذابَهم، فقال: {والذين كَفَروا}؛ أي: جحدوا ما جاءتْهم به رسُلُهم من الآيات وأنكروا لقاءَ ربِّهم، {لهم نارُ جهنَّم}: يعذَّبون فيها أشدَّ العذاب وأبلغ العقاب، {لا يُقْضى عليهم}: بالموت {فيمَوتوا}: فيستريحوا، {ولا يُخَفَّفُ عنهم من عذابِها}: فشدَّة العذاب وعِظَمُهُ مستمرٌّ عليهم في جميع الآنات واللحظات. {كذلك نجزي كلَّ كفورٍ}.
{36} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja hali ya wakazi wa Peponi na furaha yao, akataja hali ya wakazi wa Motoni na adhabu yao,
akasema: "Na wale waliokufuru" yale waliyowajia nayo Mitume miongoni mwa Ishara walizo nazo na wakapinga kukutana na Mola wao Mlezi, "watakuwa na Moto wa Jahannamu." Wataadhibiwa humo adhabu kali kabisa, "hawahukumiwi" mauti "wakafa" ndiyo wapumzike "wala hawatapunguziwa adhabu yake." Kwa hivyo ukali na ukubwa wa adhabu yao utaendelea juu yao kila wakati. "Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri."
#
{37} {وهم يَصْطَرِخون فيها}؛ أي: يصرخون ويتصايحون ويستغيثون ويقولون: {ربَّنا أخْرِجْنا نَعْمَلْ صالحاً غير الذي كنَّا نعملُ}: فاعترفوا بذنبهم، وعرفوا أنَّ الله عَدَلَ فيهم، ولكنْ سألوا الرجعةَ في غير وقتها، فيُقال لهم ألم: {نُعَمِّرْكُم ما}؛ أي: دهراً وعمراً {يتذكَّرُ فيه مَن تَذَكَّرَ}؛ أي: يتمكَّن فيه من أراد التَذكُّر من العمل، مَتَّعْناكم في الدنيا، وأدررنا عليكم الأرزاق، وقيضْنا لكم أسباب الراحة، ومددْنا لكم في العمر، وتابعْنا عليكم الآياتِ، وواصَلْنا إليكم النُّذُر، وابْتَلَيْناكم بالسراءِ والضراءِ؛ لِتُنيبوا إلينا وترجِعوا إلينا، فلم ينجَعْ فيكم إنذارٌ، ولم تُفِدْ فيكم موعظةٌ، وأخَّرْنا عنكم العقوبةَ، حتى إذا انقضتْ آجالُكم وتمَّتْ أعمارُكم ورحلتُم عن دار الإمكان بأشرِّ الحالات ووصلتُم إلى هذه الدار دار الجزاء على الأعمال؛ سألتُمُ الرجعةَ! هيهات هيهات! فات وقتُ الإمكان، وغضب عليكم الرحيم الرحمن، واشتدَّ عليكم عذاب النار، ونسيَكُم أهلُ الجنة، فامكثوا فيها خالدين مخلَّدين وفي العذاب مُهانين، ولهذا قال: {فذوقوا فما للظالمين من نصيرٍ}: ينصُرُهم فيُخْرِجُهم منها، أو يخفِّفُ عنهم من عذابها.
{37} "Na humo watapiga makelele" wakiomba msaada wakisema: 'Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyokuwa tukiyafanya.'" Basi wakakiri dhambi zao, na wakajua kwamba Mwenyezi Mungu amewafanyia uadilifu, lakini wakaomba kurudi katika wakati usiofaa. Kwa hivyo,
wakaambiwa: "Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka?" Na akaweze kufanya matendo mema; kwani tuliwastarehesha duniani na tukawapa riziki kwa wingi, na tukawaongezea muda wa kuishi, na tukawatumia Ishara kwa kufuatanisha, na pia tukawafikishia waonyaji, na tukawajaribu kwa mema na dhiki, ili mtubu na mrejee kwetu. Lakini maonyo hayo hayakuwaingia, wala mawaidha hayakuwanufaisha, na tukawacheleweshea adhabu itokayo kwenu, mpaka ulipokwisha muda wenu na mkaondoka katika makao ya uwezekano katika hali mbaya zaidi na mkaifikia nyumba hii ya malipo kwa matendo; mkaomba kurudi! Hapana, hapana! Wakati wa kuwezekana umeshapita, na ameshawakasirikia Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa rehema, na adhabu ya Moto imekuwa kali kwenu, na wakazi wa Peponi wameshawasahau. Basi kaeni humo milele na milele katika adhabu mkifedheheshwa.
Na ndiyo maana akasema: "Basi onjeni! Kwani wale waliodhulumu hawana wa kuwanusuru," atakayewanusuru na kuwaondoa humo au atakayewapunguzia adhabu yake.
{إِنَّ اللَّهَ عَالِمُ غَيْبِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (38)}.
38. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbinguni na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliomo vifuani.
#
{38} لمَّا ذكر جزاء أهل الدارين، وذكر أعمال الفريقين؛ أخبر تعالى عن سعةِ علمِهِ تعالى واطِّلاعه على غيب السمواتِ والأرض التي غابت عن أبصارِ الخَلْق وعن علمهم، وأنَّه عالمٌ بالسرائر وما تنطوي عليه الصُّدور من الخير والشرِّ والزكاء وغيره، فيعطي كلاًّ ما يستحقُّه، وينزِلُ كلَّ أحدٍ منزلته.
{38} Alipotaja malipo ya wakazi wa nyumba hizi mbili, na akataja matendo ya makundi mawili haya, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha juu ya upana wa elimu yake na kujua kwake mambo ya ghaibu ya mbingu na ardhi ambayo yamefichikana mbele ya macho ya viumbe na elimu yao. Na kwamba anajua siri na yaliyomo vifuani, ya heri, ya shari, usafi na vitu vingine. Kwa hivyo humpa kila mmoja anachostahiki na humshusha kila mmoja katika daraja lake.
{هُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ فَمَنْ كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ إِلَّا مَقْتًا وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ إِلَّا خَسَارًا (39)}.
39. Yeye ndiye aliyekufanyeni manaibu katika ardhi. Na anayekufuru, basi kufuru yake ni juu yake. Na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao Mlezi ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila hasara.
#
{39} يخبر تعالى عن كمال حكمتِهِ ورحمتِهِ بعبادِهِ أنَّه قَدَّرَ بقضائِهِ السابق أنْ يجعلَ بعضَهم يَخْلُفُ بعضاً في الأرض، ويرسلَ لكلِّ أمَّةٍ من الأمم النُّذُرَ، فينظرَ كيف يعملونَ؛ {فمن كَفَرَ}: بالله وبما جاءتْ به رسلُه؛ فإنَّ كفرَه عليه، وعليه إثمُه وعقوبتُه، ولا يَحْمِلُ عنه أحدٌ، ولا يزداد الكافر بكفرِهِ إلاَّ مقتَ ربِّه له وبغضَه إيَّاه، وأيُّ عقوبة أعظمُ من مقت الربِّ الكريم؟! {ولا يزيد الكافرين كُفْرُهُم إلاَّ خساراً}؛ أي: يخسرون أنفسَهم وأهليهم وأعمالَهم ومنازلَهم في الجنة؛ فالكافر لا يزالُ في زيادةٍ من الشقاء والخسران والخزي عند الله وعند خلقِهِ والحرمان.
{39} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukamilifu wa hekima na rehema zake kwa waja wake kwamba kwa amri yake iliyotangulia, amewajaalia baadhi yao kuwarithi wengineo duniani, na kuwatumia kila umma waonyaji, ili aone jinsi watakavyofanya. "Na anayekufuru" Mwenyezi Mungu na yale waliyoyaleta Mitume wake, basi kufuru yake, dhambi yake na adhabu yake ni juu yake. Na hakuna wa kumbebea hayo, na wala kafiri haongezi kwa ukafiri wake isipokuwa kuchukiwa na Mola wake Mlezi na kumkasirikia. Na ni adhabu gani kubwa zaidi kuliko kuchukiwa na Mola Mlezi, Mkarimu? "Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila hasara" juu ya nafsi zao wenyewe, familia zao, matendo yao na nyumba zao peponi. Kwani kafiri haachi kuwa katika mashaka, hasara, hizaya na kunyimwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya viumbe vyake.
{قُلْ أَرَأَيْتُمْ شُرَكَاءَكُمُ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا فَهُمْ عَلَى بَيِّنَتٍ مِنْهُ بَلْ إِنْ يَعِدُ الظَّالِمُونَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا (40)}.
40.
Sema: Mnawaona hawa miungu wenu wa kishirikina mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu! Nionyesheni wameumba sehemu gani katika ardhi? Au wana ushirika wowote katika mbingu? Au tumewapa Kitabu nao kwa hicho wakawa na hoja zilizo wazi? Lakini madhalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu tu.
#
{40} يقول تعالى معجِّزاً لآلهةِ المشركين ومبيِّناً نقصَها وبطلانَ شِركهم من جميع الوجوه: {قُلْ} يا أيُّها الرسول لهم: {أرأيتُم}؛ أي: أخْبِروني عن شركائكُم {الذين تدعونَ من دونِ الله}: هل هم مستحقُّون للدعاء والعبادةِ؟! فأروني {ماذا خَلَقوا من الأرضِ}: هل خَلَقوا بحراً أم خلقوا جبالاً أو خلقوا حيواناً أو خلقوا جماداً؟! سيقرُّون أنَّ الخالقَ لجميع الأشياء هو الله تعالى. أم لشركائِكُم {شركٌ في السمواتِ}: في خلقها وتدبيرها؟! سيقولون: ليس لهم شركةٌ! فإذا لم يخلقْ شيئاً ولم يَشْركوا الخالقَ في خلقه؛ فلم عبدتُموهم ودعوتُموهم مع إقراركم بعجزهم؟! فانتفى الدليل العقليُّ على صحَّةِ عبادتهم، ودلَّ على بطلانها.
ثم ذكر الدليل السمعيَّ، وأنَّه أيضاً منتفٍ، فلهذا قال: {أم آتَيْناهم كتاباً}: يتكلَّم بما كانوا به يشرِكون؛ يأمُرُهم بالشركِ وعبادةِ الأوثان. {فهم}: في شركهم {على بينةٍ}: من ذلك الكتاب الذي نَزَلَ عليهم في صحة الشرك، ليس الأمر كذلك؛ فإنَّهم ما نزل عليهم كتابٌ قبلَ القرآن، ولا جاءهم نذيرٌ قبل رسول الله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، ولو قُدِّرَ نزولُ كتاب إليهم وإرسالُ رسول إليهم وزعموا أنَّه أمَرَهم بشِرْكِهِم؛ فإنَّا نجزِمُ بكذِبِهم؛ لأنَّ الله قال: {وما أرْسَلْنا من قبلِكَ من رسول إلاَّ نوحي إليه أنَّه لا إله إلاَّ أنا فاعبدونِ}: فالرسلُ والكتبُ كلُّها متفقةٌ على الأمر بإخلاص الدين لله تعالى: {وما أُمِروا إلاَّ لِيَعْبُدوا اللهَ مخلِصينَ له الدينَ حنفاءَ}. فإنْ قيلَ: إذا كان الدليل العقليُّ والنقليُّ قد دلاَّ على بطلان الشرك؛ فما الذي حمل المشركين على الشركِ وفيهم ذوو العقول والذكاء والفطنة؟! أجاب تعالى بقوله: {بل إن يَعِدُ الظالمون بعضُهم بعضاً إلاَّ غروراً}؛ أي: ذلك الذي مَشَوْا عليه ليس لهم فيه حُجَّةٌ، وإنَّما ذلك توصيةُ بعضهم لبعضٍ به، وتزيينُ بعضِهِم لبعضٍ، واقتداءُ المتأخِّر بالمتقدِّم الضالِّ، وأماني منَّاها الشياطين، وزيَّنَ لهم سوءَ أعمالهم ، فنشأت في قلوبهم، وصارتْ صفةً من صفاتها، فعَسُرَ زوالُها وتعسَّرَ انْفِصالها، فحصل ما حَصَلَ من الإقامة على الكفر والشرك الباطل المضمحلِّ.
{40} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema,
akionyesha kutoweza kwa miungu ya washirikina na kuonyesha upungufu wao na ubatili wa ushirikina wao kwa njia zote: "Sema" ewe Mtume ukiwaambia: "Mnawaona," yaani niambieni kuhusu hawa miungu wenu wa kishirikina "mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu!" Je, wanastahiki kuombwa dua na kuabudiwa? Basi nionyesheni "wameumba sehemu gani katika ardhi?" Je, waliumba bahari yoyote, au waliumba mlima wowote, au waliumba wanyama wowote, au waliumba kitu chochote kisichokuwa na uhai? Watakiri kwamba Muumba wa vitu vyote ni Mwenyezi Mungu.
Au washirika wenu hawa wana "ushirika wowote katika mbingu" katika kuziumba na kuziendesha? Watasema: Hawana ushirika wowote. Kwa hivyo, ikiwa hawakuumba chochote na hawakumshiriki Muumba katika kuumba kwake, basi kwa nini mliwaabudu na kuwaomba dua ilhali mnakiri kutokuwa kwao na uwezo? Basi ukaishia hapo ushahidi wa kiakili ulioonyesha ubatili wa kuabudiwa kwao. Kisha akataja ushahidi wa kusikia, na kwamba hilo pia haliko,
na ndiyo maana akasema: "Au tumewapa Kitabu" kinachozungumzia yale waliyokuwa wakiyashirikisha; kikiwaamrisha kufanya ushirikina na kuabudu visivyokuwa Mwenyezi Mungu? "Nao kwa hicho wakawa na hoja zilizowazi katika ushirikina wao huo kupitia kitabu chao hicho kilichowateremkia kikionyesha usahihi wa kufanya ushirikina?" Si hivyo, kwani hawakuteremshiwa Kitabu chochote kabla ya Qur-ani, na wala mwonyaji yeyote hakuwahiwajia kabla ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Lakini hata kama ingechukuliwa kwamba kitabu kiliwashukia na kwamba walitumiwa Mtume, nao wakadai kwamba yeye ndiye aliyeamrisha kufanya ushirikina, basi sisi bila ya shaka tunajua kwamba ni waongo.
Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: "Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu." Basi wameafikiana Mitume wote na Vitabu vyote juu ya suala la kuwaamrisha watu kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika Dini. "Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu.
" Na ikisemwa: Iwapo ushahidi wa kiakili na wa kimaandiko ulionyesha ubatili wa ushirikina wao, basi ni nini kiliwafanya washirikina wafanye ushirikina ilhali miongoni mwao wapo watu wenye akili,
werevu na wenye ufahamu mkubwa? Mwenyezi Mungu Mtukufu akajibu kwa kauli yake: "Lakini madhalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu tu." Yaani, hayo waliyoyafanya hawana hoja yoyote juu yake, bali hayo ni wasia waliousiana wao kwa wao, na wakapambiana wao kwa wao. Na wale waliokuja baadaye kuwaiga waliotangulia ambao walipotea.Na matumaini ambayo mashetani waliwapa na wakawapambia ubaya wa matendo yao, kwa hivyo yakakolea katika nyoyo zao na yakawa ni moja ya sifa zake.Kwa hivyo ikawa vigumu kuyatoa na kutengana nayo, kwa hivyo yakatokea yaliyotokea ya kudumu kwao katika ukafiri na ushirikina wa batili utakaotoweka.
{إِنَّ اللَّهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَنْ تَزُولَا وَلَئِنْ زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِنْ بَعْدِهِ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا (41)}.
41. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayezuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe.
#
{41} يخبر تعالى عن كمال قدرتِهِ وتمام رحمتِهِ وسعةِ حلمِهِ ومغفرتِهِ، وأنَّه تعالى {يمسِكُ السمواتِ والأرضَ}: عن الزوال؛ فإنَّهما لو زالتا؛ ما أمسكهما أحدٌ من الخلق، لعجزتْ قُدَرُهُم وقُواهم عنهما، ولكنَّه تعالى قضى أن يكونا كما وُجِدا؛ ليحصُلَ للخلقِ القرارُ والنفعُ والاعتبارُ، وليعلموا من عظيم سلطانِهِ وقوَّةِ قدرتِهِ ما به تمتلئُ قلوبُهم له إجلالاً وتعظيماً ومحبةً وتكريماً، وليعلموا كمال حِلمِهِ ومغفرتِهِ بإمهال المذنبين وعدم معاجلتِهِ للعاصين، مع أنَّه لو أمر السماء؛ لَحَصَبَتْهم، ولو أذِنَ للأرض؛ لابتلعتْهم، ولكن وَسِعَتْهم مغفرتُه وحلمُه وكرمُه. {إنَّه كان حليماً غفوراً}.
{41} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukamilifu wa uwezo wake, ukamilifu wa rehema yake, upana wa ustahimilivu wake na msamaha wake. Na kwamba Yeye Mtukufu "ndiye anayezuilia mbingu na ardhi" zisiondoke. Kwani, ikiwa zitaondoka basi hakuna kiumbe chochote kingeweza kuzishikilia, kwa sababu uwezo wao na nguvu zao hazingeweza kuzishikilia.Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akafanya zibakie kama zilivyopatikana ili viumbe vipate uthabiti, manufaa, na mazingatio, na ili wapate kujua ukubwa wa mamlaka yake na nguvu za uwezo wake. Mambo ambayo kwa hayo mioyo yao itamheshimu kwa wingi, kumtukuza, kumpenda, na ili wapate kujua ukamilifu wa ustahamilivu wake na msamaha wake kwa kuwapa muhula wafanyao dhambi, na kutowaharakisha waasi. Pamoja na kwamba ikiwa angeziamrisha mbingu, basi ingewapiga kwa mawe, na kama angeipa ardhi ruhusa, basi ingewameza.Lakini wameenewa na msamaha wake, ustahamilivu wake na ukarimu wake. "Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe."
{وَأَقْسَمُوا بِاللَّهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِنْ جَاءَهُمْ نَذِيرٌ لَيَكُونُنَّ أَهْدَى مِنْ إِحْدَى الْأُمَمِ فَلَمَّا جَاءَهُمْ نَذِيرٌ مَا زَادَهُمْ إِلَّا نُفُورًا (42) اسْتِكْبَارًا فِي الْأَرْضِ وَمَكْرَ السَّيِّئِ وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ الْأَوَّلِينَ فَلَنْ تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّهِ تَبْدِيلًا وَلَنْ تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّهِ تَحْوِيلًا (43)}.
42. Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kuapa kwao, kwamba akiwajia mwonyaji, bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote. Lakini alipowajia mwonyaji, hakuwazidishia ila kuikimbia hiyo Haki. 43. Kwa kutakabari kwao katika nchi, na kufanya vitimbi vya uovu. Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliyevifanya. Hebu, hawangojei yale yaliowasibu watu wa kale? Basi hutapata mabadiliko katika mtindo wa Mwenyezi Mungu. Wala hutapata mageuko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu.
#
{42} أي: وأقسم هؤلاء الذين كذَّبوك يا رسول الله قسماً اجتهدوا فيه بالأيمانِ الغليظة: {لَئِن جاءهم نذيرٌ لَيكونُنَّ أهدى من إحدى الأمم}؛ أي: أهدى من اليهودِ والنصارى أهل الكتب، فلم يفوا بتلك الإقسامات والعهود، {فلما جاءهم نذيرٌ}: لم يَهْتَدوا، ولم يَصيروا أهدى من إحدى الأمم، بل لم يَدوموا على ضلالهم الذي كان، بل {ما زادَهم} ذلك {إلاَّ نفوراً}: زيادة ضلال وبغي وعناد.
{42} Yaani, hawa waliokadhibisha, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, waliapa kwa viapo vikali kwamba "akiwajia mwonyaji, bila ya shaka watakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote." Yaani, kuliko watu wa Kitabu kama vile Mayahudi na Wakristo, lakini hawakutimiza viapo hivyo na ahadi zao. "Lakini alipowajia mwonyaji," hawakuongoka wala hawakuwa waongofu zaidi kuliko taifa jingine lolote. Bali waliendelea katika upotofu waliokuwa nao, tena "hakuwazidishia ila kuikimbia hiyo Haki" kwa kuvuka mipaka na kufanya ukaidi.
#
{43} وليس إقسامُهُم المذكورُ لقصدٍ حسنٍ وطلبٍ للحقِّ، وإلاَّ؛ لَوُفِّقوا له، ولكنه صادرٌ عن استكبارٍ في الأرض على الخلق وعلى الحقِّ، وبهرجةٍ في كلامهم هذا؛ يريدون به المكر والخداع، وأنَّهم أهل الحقِّ الحريصون على طلبه، فيغتر بهم المغترُّون، ويمشي خلفهم المقتدون، {ولا يَحيق المكرُ السيِّئُ}: الذي مقصودُهُ مقصودٌ سَيِّئٌ ومآله وما يرمي إليه سَيِّئٌ باطل {إلا بأهلِهِ}: فمكرُهُم إنَّما يعودُ عليهم. وقد أبان الله لعبادِهِ في هذه المقالات وتلك الإقسامات أنَّهم كَذَبَةٌ في ذلك مزوِّرون، فاستبان خِزْيُهُم، وظهرتْ فضيحتُهُم، وتبيَّن قصدُهم السيِّئُ، فعاد مكرُهُم في نحورهم، وردَّ الله كيدَهم في صدورهم، فلم يبقَ لهم إلاَّ انتظارُ ما يَحِلُّ بهم من العذابِ، الذي هو سنَّةُ الله في الأولين، التي لا تُبَدَّلُ ولا تُغَيَّرُ؛ أنَّ كلَّ مَن سار في الظلم والعناد والاستكبار على العباد أنْ تَحِلَّ به نقمتُه وتُسْلَبَ عنه نعمتُه، فليترقَّبْ هؤلاء ما فعل بأولئك.
{43} Kiapo chao kilichotajwa hapo awali hakikuwa kwa nia njema na kutafuta haki. Vinginevyo, wangewezeshwa kufanya hivyo, lakini kulitokana na kutakabari katika ardhi dhidi ya viumbe na dhidi ya haki, na upuuzi wa maneno yao haya ambayo walikusudia tu kupanga vitimbi na kufanya hadaa, na kuonyesha kwamba wao ndio wana haki walio na bidii kubwa ya kuitafuta, ili wadanganyike nao wenye kudanganyika, na ili wenye kuwaiga wawafuate nyuma yao. "Na vitimbi viovu" ambavyo makusudio yake ni mabaya na mwisho wake malengo yake ni batili "havimsibu mwenyewe aliyevifanya." Na Mwenyezi Mungu aliwabainishia waja wake katika maneno haya na viapo hivi kwamba wao ni waongo na wazushi. Basi hizaya yao ikadhihirika na wakafedheheka, na nia zao mbaya zikadhihirika. Kwa hivyo vitimbi vyao hivyo vikawarudi kooni mwao, na Mwenyezi Mungu akawarudishia vitimbi vyao vifuani mwao. Kwa hivyo hakuna kilichowabakia ila kungojea adhabu itakayowapata, ambayo ndiyo desturi ya Mwenyezi Mungu katika wale waliotangulia ambayo haibadiliki wala haigeuki. Nayo ni kwamba kila mtu anayewafanyia waja dhuluma, ukaidi, na kiburi atapata adhabu na kunyang'anywa neema zake. Basi na wangojee watu hawa yale waliyofanyiwa wale.
{أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَكَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُعْجِزَهُ مِنْ شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا (44) وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَى ظَهْرِهَا مِنْ دَابَّةٍ وَلَكِنْ يُؤَخِّرُهُمْ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا (45)}.
44. Je, hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinachoweza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye uweza wote. 45. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa yale waliyoyachuma, basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Na muda wao ukifika, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara.
#
{44} يحضُّ تعالى على السير في الأرض في القلوب والأبدان للاعتبار لا لمجرَّدِ النظر والغفلة، وأن ينظُروا إلى عاقبة الذين من قبلهم ممَّن كذَّبوا الرسلَ وكانوا أكثر منهم أموالاً وأولاداً وأشدَّ قوةً وعمروا الأرض أكثر مما عمرها هؤلاء، فلما جاءهم العذابُ؛ لم تنفعْهم قوتُهم، ولم تغنِ عنهم أموالُهم ولا أولادُهم من الله شيئاً، ونفذتْ فيهم قدرةُ الله ومشيئتُه، {وما كانَ اللهُ لِيُعْجِزَهُ من شيءٍ في السمواتِ ولا في الأرضِ}: لكمال علمه وقدرته. {إنَّه كان عليماً قديراً}.
{44} Mwenyezi Mungu anawahimiza watu watembee katika ardhi kwa nyoyo zao na miili yao kwa ajili ya mazingatio, si kwa ajili ya kutazama tu na kughafilika. Na kwamba waangalie mwisho wa wale waliokuwa kabla yao miongoni mwa wale waliowakadhibisha Mitume na ambao walikuwa na mali nyingi zaidi yao na watoto, na wenye nguvu zaidi kuliko wao, na wakaistaisha ardhi kuliko walivyoistawisha hawa. Lakini adhabu ilipowajia, hazikuwafaa nguvu zao, wala mali zao, wala watoto wao, wala chochote mbele ya Mwenyezi Mungu, bali mapenzi ya Mwenyezi Mungu yalitekelezeka juu yao. "Na hapana kitu kinachoweza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi" kwa sababu ya ukamilifu wa elimu yake na uwezo wake. "Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye uweza wote."
#
{45} ثم ذَكَرَ تعالى كمالَ حلمِهِ وشدَّةَ إمهاله وإنظارِهِ أربابَ الجرائم والذنوب، فقال: {ولو يؤاخِذُ اللهُ الناس بما كَسَبوا}: من الذنوب {ما ترك على ظَهْرِها من دابَّةٍ}؛ أي: لاستوعبت العقوبةُ حتى الحيواناتِ غيرَ المكلَّفةِ. {ولكن}: يُمهلهم تعالى ولا يُهملهم ، {يؤخِّرُهم إلى أجلٍ مسمًّى فإذا جاء أجلُهم فإنَّ الله كانَ بعبادِهِ بصيراً}: فيجازيهم بحسبِ ما عَلِمَهُ منهم من خيرٍ وشرٍّ.
{45} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja ukamilifu wa ustahamilivu wake, na wingi wa kuwapa kwake muhula vigogo wa kufanya uhalifu na madhambi,
akasema: "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa yale waliyoyachuma" miongoni mwa dhambi, "basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja." Yaani, adhabu hiyo ingewajumuisha hata wanyama ambao hawajajukumishwa kisheria. "Lakini" Mwenyezi Mungu huwapa muhula na wala haghafiliki mbali nao "mpaka ufike muda maalumu. Na muda wao ukifika, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara." Na hapo atawalipa kulingana na aliyoyajua kuwahusu,ya heri na maovu.
Imekamilika tafsiri ya Surat Fatir Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *