:
Tafsiri ya Surat Saba'
Tafsiri ya Surat Saba'
[Nayo] ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 2 #
{الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي الْآخِرَةِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ (1) يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنْزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ الرَّحِيمُ الْغَفُورُ (2)}
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote vilivyo mbinguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari. 2. Anajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda huko. Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe.
#
{1} {الحمدُ}: الثناء بالصفات الحميدةِ والأفعال الحسنة؛ فلله تعالى الحمدُ؛ لأنَّ جميع صفاته يُحمد عليها لكونها صفاتِ كمال، وأفعالُه يُحمد عليها لأنَّها دائرةٌ بين الفضل الذي يُحمد عليه ويُشكر، والعدل الذي يُحمد عليه ويُعترف بحكمتِهِ فيه. وحَمَدَ نفسَه هنا على أنَّ {له ما في السموات وما في الأرض}: مُلكاً وعبيداً يتصرَّف فيهم بحمده. {وله الحمدُ في الآخرة}: لأنَّ في الآخرة يظهرُ من حمدِهِ والثناء عليه ما لا يكون في الدنيا؛ فإذا قضى الله تعالى بين الخلائق كلِّهم، ورأى الناس والخلق كلُّهم ما حكم به وكمال عدلِهِ وقسطِهِ وحكمته فيه؛ حمدوه كلُّهم على ذلك، حتى أهل العقاب؛ ما دخلوا النار إلاَّ وقلوبُهم ممتلئةٌ من حمده، وأنَّ هذا من جرّاء أعمالهم، وأنَّه عادلٌ في حكمه بعقابهم. وأمَّا ظهورُ حمدِهِ في دار النعيم والثواب؛ فذلك شيء قد تواردتْ به الأخبارُ وتوافقَ عليه الدليلُ السمعيُّ والعقليُّ؛ فإنَّهم في الجنة يرون من توالي نعم الله وإدرارِ خيره وكثرةِ بركاته وسَعَةِ عطاياه التي لم يبقَ في قلوب أهل الجنة أمنيةٌ ولا إرادةٌ إلاَّ وقد أعطي فوق ما تمنَّى وأراد، بل يُعْطَوْنَ من الخير ما لم تتعلَّقْ به أمانيهم ولم يخطُرْ بقلوبِهم؛ فما ظنُّك بحمدِهم لربِّهم في هذه الحال مع أنَّ في الجنة تضمحلُّ العوارض والقواطع التي تقطع عن معرفة الله ومحبَّتِهِ والثناء عليه، ويكون ذلك أحبَّ إلى أهلها من كلِّ نعيم وألذَّ عليهم من كل لَذَّةٍ؟! ولهذا؛ إذا رأوا الله تعالى وسمعوا كلامه عند خطابِهِ لهم؛ أذْهَلَهم ذلك عن كلِّ نعيم، ويكون الذكر لهم في الجنة كالنَفَس متواصلاً في جميع الأوقات، هذا إذا أضفتَ ذلك إلى أنَّه يظهر لأهل الجنة في الجنةِ كلَّ وقتٍ من عظمة ربِّهم وجلالِهِ وجمالِهِ وسعة كمالِهِ ما يوجب لهم كمالَ الحمد والثناء عليه. {وهو الحكيمُ}: في ملكه وتدبيره، الحكيم في أمره ونهيه. {الخبيرُ}: المطَّلعُ على سرائر الأمورِ وخفاياها.
{1} "Alhamdu" inamanisha kusifu kwa sifa njema na matendo mazuri. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, anasifiwa kwa sifa zake zote kwa sababu ni sifa za ukamilifu. Na anasifiwa kwa matendo yake kwa sababu yanazunguka baina ya fadhila anazosifiwa juu yake na kushukuriwa kwazo, na uadilifu anaosifiwa kwa huo na ambao wanakiri hekima yake ndani yake. Alijisifu mwenyewe hapa kwamba, “ni vyake vyote vilivyomo mbinguni na katika ardhi." Vyote ni miliki yake na waja wake, na anaviendesha kwa sifa zake. "Na sifa ni zake Yeye katika Akhera." Kwa sababu huko Akhera zitadhihiri sifa zake ambazo hazipo duniani. Ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu angeamua kati ya viumbe vyote, na watu na viumbe vyote wakaona kile alichotawala na ukamilifu wa uadilifu wake, na hekima ndani yake; wote wakamsifu kwa hilo, hata watu wa adhabu; hawataingia Motoni ila kwa nyoyo zao zikiwa zimemsifu, na kwamba hayo ni matokeo ya matendo yao, na kwamba Yeye ni mwadilifu katika hukumu yake katika kuwaadhibu. Ama kudhihiri kwa sifa zake katika nyumba ya neema na malipo, hili ni jambo ambalo limeripotiwa katika habari nyingi sahihi na ushahidi mbalimbali wa kusikiwa na kiakili ukakubaliana juu yake. Kwani, wao Peponi wataona mfuatano wa neema za Mwenyezi Mungu, wingi wa heri yake, wingi wa baraka zake, na wingi wa vipawa vyake, kiasi kwamba hayabaki matamanio yoyote wala utashi katika nyoyo za wakazi wa Peponi isipokuwa watakuwa wamepewa zaidi ya walivyotamani na kutaka. Bali watapewa hata heri ambayo hawakuitamani na wala hakikupita kwenye nyoyo zao. Basi unamdhaniaje kumsifu kwao Mola wao Mlezi katika hali hii, pamoja na kwamba katika Pepo vitatokewa vizuizi vyote vinavyozuia kumjua Mwenyezi Mungu na kumpenda, na kumsifu. Na hilo ndilo litakuwa pendwa zaidi na wakazi wa humo kuliko neema zote, na ni lenye kufurahisha zaidi kuliko raha zote? Na kwa sababu hii, watakapomuona Mwenyezi Mungu Mtukufu na kusikia maneno yake atakapozungumza nao, hilo litawastaajabisha wasahau neema zote. Na kumtaja Mola wao Mlezi Peponi kutakuwa ni kama pumzi yenye kuendelea katika kila wakati. Yatakuwa hivyo, na zaidi ni kwamba wakazi wa Peponi watadhihirikiwa humo Peponi kila wakati na ukuu wa Mola wao Mlezi, na utukufu wake, na uzuri wake na upana wa ukamilifu wake, jambo lenye kusababisha wamsifu na wamtaje kwa uzuri kikamilifu. "Naye ni Mwenye hekima" katika ufalme wake na usimamizi wake. Mwenye hekima katika amri zake na makatazo yake. "Mwenye habari" ambaye anajua siri za mambo na yale yaliyofichikana zaidi.
#
{2} ولهذا فصَّلَ علمَه بقولِهِ: {يعلم ما يَلِجُ في الأرضِ}؛ أي: من مطر وبذرٍ وحيوان، {وما يخرُجُ منها}: من أنواع النباتاتِ وأصناف الحيواناتِ، {وما ينزِلُ من السماءِ}: من الأملاك والأرزاق والأقدار، {وما يعرُجُ فيها}: من الملائكة والأرواح وغير ذلك. ولمَّا ذَكَرَ مخلوقاتِهِ وحكمتَه فيها وعلمَه بأحوالها؛ ذكر مغفرتَه ورحمتَه لها، فقال: {وهو الرحيمُ الغفورُ}؛ أي: الذي الرحمة والمغفرة وصفُه، ولم تزلْ آثارُهُما تنزِلُ على العباد كلَّ وقتٍ بحسب ما قاموا به من مقتضياتهما.
{2} Na ndiyo maana akabainisha kwa kina kwamba ni mwenye kujua kwa kusema, "Anajua yanayoingia katika ardhi." Yaani, kama vile mvua, mbegu na wanyama, "na yanayotoka humo" miongoni mwa aina mbalimbali za mimea na aina mbalimbali za wanyama, "na yanayoteremka kutoka mbinguni" kama vile mali, riziki na mapitisho yake "na yanayopanda huko" kama vile malaika, roho, na mambo mengine. Na alipotaja viumbe vyake, hekima ya kuhusiana nao, na kujua kwake hali zao; akataja msamaha wake na rehema yake kwao, akasema "Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe." Yaani, yule ambaye sifa yake ni rehema na msamaha. Na athari zake hazijaacha kuendelea kuwashukia waja wakati wote kwa mujibu wa yale waliyoyafanya katika mambo yanayolazimu kushuka kwake.
: 3 - 5 #
{وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ قُلْ بَلَى وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِنْ ذَلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُبِينٍ (3) لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَئِكَ لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ (4) وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مِنْ رِجْزٍ أَلِيمٌ (5)}.
3. Na walisema wale waliokufuru: "Haitatufikia Saa ya Kiyama." Sema: kwani hapana shaka itakufikieni, ninaapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha. 4. Ili awalipe wale walioamini na wakatenda mema. Hao watapata msamaha na riziki ya ukarimu. 5. Na wale waliojitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.
#
{3} لمَّا بيَّن تعالى عظمته بما وصف به نفسه، وكان هذا موجباً لتعظيمه وتقديسه والإيمان به؛ ذكر أنَّ من أصناف الناس طائفةً لم تُقَدِّرْ ربَّها حقَّ قدرِهِ، ولم تعظِّمْه حق عظمته، بل كفروا به وأنكروا قدرتَه على إعادةِ الأموات وقيام الساعة، وعارضوا بذلك رسلَه، فقال: {وقال الذين كفروا}؛ أي: بالله وبرسله وبما جاؤوا به، فقالوا بسبب كفرهم: {لا تَأتينا الساعةُ}؛ أي: ما هي إلاَّ هذه الحياة الدُّنيا نموت ونحيا! فأمر الله رسولَه أنْ يردَّ قولَهم ويُبْطِلَه ويقسِمَ على البعث وأنَّه سيأتيهم، واستدلَّ على ذلك بدليل مَن أقرَّ به؛ لزمه أن يصدِّق بالبعث ضرورةً، وهو علمُه تعالى الواسعُ العامُّ، فقال: {عالم الغيب}؛ أي: الأمور الغائبة عن أبصارنا وعن علمنا؛ فكيف بالشهادة؟! ثم أكَّد علمه فقال: {لا يعزُبُ}؛ أي: لا يغيب عن علمه {مثقالُ ذرَّةٍ في السمواتِ ولا في الأرض}؛ أي: جميع الأشياء بذواتها وأجزائها، حتى أصغر ما يكون من الأجزاء، وهو المثاقيل منها، {ولا أصغر من ذلك ولا أكبر إلاَّ في كتابٍ مبينٍ}؛ أي: قد أحاط به علمُه وجرى به قلمُه وتضمَّنه الكتابُ المبينُ الذي هو اللوحُ المحفوظ. فالذي لا يخفى عن علمِهِ مثقال الذرة فما دونَه في جميع الأوقات، ويعلم ما تَنْقُصُ الأرضُ من الأموات وما يبقى من أجسادهم؛ قادرٌ على بعثهم من باب أولى، وليس بعثُهم بأعجبَ من هذا العلم المحيط.
{3} Mwenyezi Mungu alipobainisha ukuu wake kwa yale aliyojielezea nayo, na hili likawa ni sababu ya kumtukuza, kumtakasa na kumwamini; akataja kuwa miongoni mwa aina za watu, kuna kundi ambalo halikumthamini Mola wao kama anavyostahiki kuthaminiwa, wala halikumtukuza kama anavyostahiki kutukuzwa. Bali walimkufuru na wakakanusha uwezo wake wa kuwafufua wafu, na wakakanusha kusimama kwa Saa ya Kiyama, na wakawapinga Mitume wake kwa hayo. "Na walisema wale waliokufuru" Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na kwa yale waliyoyaleta, kwa hivyo wakasema kwa sababu ya ukafiri wao, "Haitatufikia Saa ya Kiyama." Yaani, si chochote ila huu uhai wetu wa duniani, tunakufa na tunaishi. Basi Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake kuwajibu kauli yao na kuibatilisha, na kuapa kwa kufufuliwa na kwamba siku hiyo itawajia. Na akaliunga mkono hilo kwa ushahidi ambao mwenye kulikiri, inamlazimu kusadiki kufufuliwa kwa njia ya lazima, na huo ni elimu yake Mtukufu, iliyo pana na ya jumla. Akasema, "Mwenye kujua ya ghaibu" ambayo sisi hatuioni wala hatuijui. Basi itakuaje elimu yake kuhusiana na mambo yanayoshuhudiwa? Kisha akasisitiza elimu yake na akasema, "Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi;" kila kitu pamoja na dhati zake, sehemu zake, hata sehemu ndogo kabisa. "Wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha." Yaani, elimu yake iliyadhibiti, na kalamu yake ikayaandika, nayo yako katika kitabu kinachobainisha ambacho ni Ubao Uliohifadhiwa. Basi yule ambaye hakuna kinachoweza kufichika mbali na elimu yake cha uzito wa chembe au kilicho chini ya hivyo katika nyakati zote, na anajua kile ambacho ardhi inapunguza miongoni mwa wale wanaokufa, na kile kinachobakia miongoni mwa miili yao; ana uwezo na anastahili zaidi kuwafufua, na wala kuwafufua si jambo la kushangaza zaidi kuliko elimu hii iliyowazunguka.
#
{4} ثم ذكر المقصودَ من البعث، فقال: {ليجزِيَ الذين آمنوا}: بقلوبهم صدَّقوا الله، وصدَّقوا رسله تصديقاً جازماً، {وعملوا الصالحاتِ}: تصديقاً لإيمانهم. {أولئك لهم مغفرةٌ}: لذنوبهم، بسبب إيمانهم وعملهم يندفعُ بها كلُّ شرٍّ وعقابٍ، {ورزقٌ كريمٌ}: بإحسانهم، يحصلُ لهم به كلُّ مطلوبٍ ومرغوبٍ وأمنيَّة.
{4} Kisha akataja makusudio ya kuwafufua viumbe, akasema, "Ili awalipe wale walioamini" kwa nyoyo zao, ambao walimsadiki Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume wake kwa usadikisho wa uhakika, "wakatenda mema" ili kusadikisha imani yao. "Hao watapata msamaha" wa dhambi zao. Kwa sababu ya imani yao na matendo yao ulizuilika uovu wote na adhabu ikaepukika, "na riziki ya ukarimu" kwa sababu ya wema wao, walifanikiwa kupata kila wanachotafuta na kutamani.
#
{5} {والذين سَعَوْا في آياتنا مُعَاجِزينَ}؛ أي: سعوا فيها كفراً بها وتعجيزاً لمن جاء بها وتعجيزاً لمن أنزلها كما عجَّزوه في الإعادة بعد الموت. {أولئك لهم عذابٌ من رجزٍ أليم}؛ أي: مؤلم لأبدانهم وقلوبهم.
{5} "Na wale waliojitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda" kwa kuzikufuru na kutaka kumshinda yule aliyezileta, na kutaka kumshinda aliyeziteremsha, kama vile walivyoona kwamba hawezi kuwarudisha baada ya kufa. "Hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu" yenye kuumiza miili na nyoyo zao.
: 6 #
{وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنْزِلَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ (6)}.
6. Na wale waliopewa elimu wanaona ya kuwa yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ndiyo haki, nayo huongoa kwendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.
#
{6} لما ذكر تعالى إنكارَ من أنكر البعثَ، وأنَّهم يرونَ ما أنزل على رسوله ليس بحقٍّ؛ ذكر حالة الموفَّقين من العباد، وهم أهل العلم، وأنَّهم يرون ما أنزل الله على رسوله؛ من الكتاب وما اشتملَ عليه من الأخبارِ {هو الحقَّ}؛ أي: الحقُّ منحصرٌ فيه، وما خالفه وناقضه فإنه باطل؛ لأنَّهم وصلوا من العلم إلى درجة اليقين، ويرون أيضاً أنَّه في أوامره ونواهيه؛ {يهدي إلى صراطِ العزيز الحميد}: وذلك لأنَّهم جزموا بصدق ما أخبر بها من وجوهٍ كثيرةٍ: من جهة علمِهم بصدقِ مَنْ أخبر بها، ومن جهةِ موافقتها للأمور الواقعة والكتبِ السابقة، ومن جهةِ ما يشاهِدون من أخبارها التي تقع عياناً، ومن جهة ما يشاهدونَ من الآيات العظيمة الدالَّة عليها في الآفاق وفي أنفسهم، ومن جهةِ موافقتها لما دلَّت عليه أسماؤه تعالى وأوصافُه، ويرون في الأوامر والنواهي أنها تهدي إلى الصراط المستقيم المتضمن للأمور بكل صفةٍ تزكي النفس وتنمي الأجر وتفيد العامل وغيره؛ كالصدق والإخلاص وبر الوالدين وصلة الأرحام والإحسان إلى عموم الخلق ونحو ذلك، وتنهى عن كلِّ صفة قبيحةٍ، تدنِّس النفس، وتحبِطُ الأجر، وتوجِبُ الإثم والوزر من الشرك والزنا والربا والظُّلم في الدماء والأموال والأعراض. وهذه منقبةٌ لأهل العلم وفضيلةٌ وعلامةٌ لهم، وأنَّه كلَّما كان العبد أعظم علماً وتصديقاً بأخبار ما جاء به الرسول وأعظم معرفةً بحكم أوامره ونواهيه؛ كان من أهل العلم الذين جعلهم الله حجةً على ما جاء به الرسول، احتجَّ الله بهم على المكذِّبين المعاندين كما في هذه الآية وغيرها.
{6} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kukanusha kwa wale waliokanusha suala la kufufuliwa, na kwamba wanayaona yale yaliyoteremshwa kwa Mtume wake kuwa si haki, akataja hali ya wale waliofanikishwa miongoni mwa waja wake, ambao ni watu wa elimu, na kwamba wanayaona yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake miongoni mwa kitabu na habari zilizo ndani yake, kwamba "ndiyo haki" na kwamba chochote kinachohalifiana nayo na kupingana nayo ni batili, kwa sababu wamefikia kiwango cha yakini katika elimu, na pia wanaona kwamba katika maamrisho yake na makatazo yake, "huongoa kwendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa." Hayo ni kwa sababu wana yakini juu ya ukweli wa yale aliyosema kwa pande nyingi: kwa upande mmoja ni kuwa wanajua kwamba aliyeyajulisha ni mkweli, na kwa upande mwingine wa pili ambao ni kwamba yanaafikiana na matukio yaliyotokea na vitabu vilivyotangulia, na kwa upande mwingine ambao ni kwamba wanazishuhudia habari zake ambazo zinatokea na kuonwa kwa macho yao wenyewe, na kwa upande wa yale wanayoyashuhudia miongoni mwa Aya kubwa zinazoyaashiria hayo katika upeo wa macho na katika nafsi zao, na kwa upande wa kuafikiana kwake na yale yanayoonyeshwa na majina yake na sifa zake, na wanaona katika maamrisho na makatazo kwamba yanaongoza kwenye njia iliyonyooka inayojumuisha mambo yenye kila sifa inayoitakasa nafsi, inayoongeza malipo, na yanamfaa mtendaji na wengineo; kama vile ukweli, ikhlasi, kuwafanyia wema wazazi, kuwaunga jamaa, na kuwafanyia wema viumbe wote, na mfano wa hayo. Na yanakataza kila tabia mbaya inayoichafua nafsi, na kuharibu malipo, na kusababisha dhambi kutokana na ushirikina, uzinzi, riba, na dhuluma katika damu, mali, na heshima. Hii ni hadhi kubwa kwa watu wenye elimu,fadhila na ishara. Na kwamba kila mja anavyozidi kuwa na elimu na kusadiki habari za yale aliyoyaleta Mtume, na akawa ni mwenye kujua zaidi hukumu za maamrisho yake na makatazo yake; anakuwa miongoni mwa watu wenye elimu ambao Mwenyezi Mungu aliwafanya kuwa ni hoja kwa yale aliyokuja nayo Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ambao Mwenyezi Mungu aliwatumia kama hoja dhidi ya wale wanaokadhibisha, wakaidi, kama ilivyo katika Aya hii na nyinginezo.
: 7 - 9 #
{وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا هَلْ نَدُلُّكُمْ عَلَى رَجُلٍ يُنَبِّئُكُمْ إِذَا مُزِّقْتُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمْ لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ (7) أَفْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَمْ بِهِ جِنَّةٌ بَلِ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ فِي الْعَذَابِ وَالضَّلَالِ الْبَعِيدِ (8) أَفَلَمْ يَرَوْا إِلَى مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنْ نَشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِنَ السَّمَاءِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً لِكُلِّ عَبْدٍ مُنِيبٍ (9)}.
7. Na wale waliokufuru walisema: Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya? 8. Ama amemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au ana wazimu. Bali wale wasioamini Akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali kabisa. 9. Kwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, ya mbingu na ardhi? Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia.
#
{7} أي: {وقال الذين كفروا}: على وجه التكذيب والاستهزاء والاستبعاد، وذِكْر وجه الاستبعاد؛ أي: قال بعضُهم لبعض: {هل ندلُّكم على رَجُل يُنَبِّئُكُم إذا مُزِّقْتُم كلَّ مُمَزَّقٍ إنَّكم لَفي خَلْقٍ جديدٍ}؛ يعنون بذلك الرجل رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم -، وأنَّه رجلٌ أتى بما يُستغرب منه، حتى صار بزعمهم فرجةً يتفرَّجون عليه وأعجوبةً يسخرون منه، وأنَّه كيف يقولُ: إنكم مبعوثون بعد ما مَزَّقَكُمُ البِلى وتفرَّقت أوصالُكم، واضمحلَّتْ أعضاؤكم!
{7} Yaani, "Na wale waliokufuru walisema" kwa njia ya kukadhibisha na masihara na kuona kwamba hilo haliwezekani, na kutaja njia ya kutowezekana kwake; "Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?" Mtu wanayemkusudia hapa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na kwamba ni mtu aliyekuja na jambo la kushangaza kutoka kwa mtu kama yeye, hadi akawa, - kwa mujibu wa madai yao - ni jambo la kutazama kwa furaha tena la ajabu wanalolifanyia masihara. Na kwamba vipi anasema kwamba: Mtafufuliwa baada ya kuchambuliwa mapande mapande na kuishia udongoni, na viungo vyenu vikatawanyika, na viungo vyenu vikapotelea mbali!
#
{8} فهذا الرجلُ الذي يأتي بذلك: هل افْتَرَى {على الله كَذِباً}: فتجرَّأ عليه وقال ما قال، {أم به جِنَّةٌ}: فلا يُستغرب منه؛ فإنَّ الجنون فنونٌ، وكلُّ هذا منهم على وجه العناد والظُّلم، ولقد علموا أنه أصدقُ خلقِ الله وأعقلُهم، ومِنْ علمِهِم أنَّهم أبدووا وأعادوا في معاداتهم، وبذلوا أنفُسَهم وأموالَهم في صدِّ الناس عنه؛ فلو كان كاذباً مجنوناً؛ لم ينبغ لكم يا أهل العقول غير الزاكيةِ أن تُصْغوا لما قال ولا تحتَفِلوا بدعوتِهِ؛ فإنَّ المجنون لا ينبغي للعاقل أن يُلْفِتَ إليه نَظَرَه أو يبلغَ قولُهُ منه كلَّ مبلغ، ولولا عنادُكم وظلمُكم؛ لَبادَرْتُم لإجابته ولَبَّيْتُم دعوتَه، ولكن ما تُغني الآياتُ والنُّذر عن قوم لا يؤمنون، ولهذا قال تعالى: {بل الذين لا يؤمنونَ بالآخرةِ}، ومنهم الذين قالوا تلك المقالَة {في العذابِ والضَّلال البعيدِ}؛ أي: في الشقاء العظيم والضلال البعيدِ الذي ليس بقريبٍ من الصواب، وأيُّ شقاءٍ وضلال أبلغُ من إنكارِهم لقدرةِ الله على البعثِ، وتكذيِبِهم لرسولهم الذي جاء به، واستهزائِهِم به، وجزمِهِم بأنَّ ما جاؤوا به هو الحقُّ فرأوا الحقَّ باطلاً والباطل والضلال حقًّا وهدى؟!
{8} Basi mtu huyu anayefanya hivyo: Je, amemzulia "Mwenyezi Mungu uongo", kwa hivyo akathubutu kusema aliyoyasema, "au ana wazimu" kwani likawa si jambo la kustaajabu. Kwa maana, wazimu ni aina mbalimbali. Na yote haya, wanayafanya kwa njia ya ukaidi na dhuluma, kwani walikwisha jua kwamba yeye ndiye mkweli na mwenye hekima zaidi katika viumbe vya Mwenyezi Mungu. Na katika elimu yao ni kwamba walimwonyesha na kurudia kumfanyia uadui, na wakayatoa maisha yao na mali zao katika kuwazuilia watu mbali naye. Kwa hivyo, ikiwa alikuwa mwongo na wazimu, basi haingewafailia enyi watu wenye akili isiyokuwa safi kusikiliza anachokisema wala kusherehekea wito wake. Kwani haimfailii mwenye akili timamu kujali anachofanya mwendawazimu wala kumwambia maneno magumu. Na lau kuwa si ukaidi wenu na udhalimu wenu, mngefanya haraka kumuitikia na kutii wito wake. Lakini Aya na maonyo hayafai kitu kwa watu wasioamini. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Bali wale wasioiamini Akhera," wakiwa miongoni wale waliosema maneno hayo, "wamo adhabuni na upotofu wa mbali kabisa." Yaani, katika mashaka makubwa na upotofu wa mbali usiokaribia usahihi. Na ni mashaka gani na upotevu gani mkubwa zaidi kuliko kukataa kwao uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, kumkadhibisha kwao Mtume wao aliyeileta habari hiyo, na kumkejeli kwao, na kuwa kwao na uhakika kwamba walichokileta wao ndiyo haki, kwa hivyo, wakaona kwamba haki ndiyo batili, na batili na upotofu ndiyo haki na uwongofu?
#
{9} ثم نبَّههم على الدليل العقلي الدالِّ على عدم استبعاد البعث الذي استبعدوه، وأنَّهم لو نظروا إلى ما بين أيديهم وما خلفهم من السماء والأرض، فرأوا من قدرة الله فيهما ما يُبْهِرُ العقول، ومن عظمتِهِ ما يُذْهِلُ العلماء الفحول، وأنَّ خلقَهما وعظمتَهما وما فيهما من المخلوقات أعظمُ من إعادة الناس بعد موتِهِم من قبورِهم؛ فما الحاملُ لهم على ذلك التكذيب مع التصديق بما هو أكبر منه؟! نعم؛ ذاك خبرٌ غيبيٌّ إلى الآن ما شاهدوه؛ فلذلك كذَّبوا به. قال الله: {إن نَشَأ نَخْسِفْ بِهِمُ الأرضَ أو نُسْقِطْ عليهم كِسَفاً من السماء}؛ أي: من العذاب؛ لأنَّ الأرض والسماء تحت تدبيرنا؛ فإنْ أمرناهما؛ لم يستعصيا؛ فاحذَروا إصرارَكم على تكذيبِكُم فنعاقِبَكُم أشدَّ العقوبة. {إنَّ في ذلك}؛ أي: خلق السماواتِ والأرضِ وما فيهما من المخلوقات {لآيةً لكلِّ عبدٍ منيبٍ}: فكلَّما كان العبدُ أعظم إنابةً إلى الله؛ كان انتفاعُه بالآياتِ أعظم؛ لأنَّ المنيبَ مقبلٌ إلى ربِّه، قد توجَّهت إرادتُه وهمَّاتُه لربِّه، ورجع إليه في كلِّ أمر من أموره، فصار قريباً من ربِّه، ليس له همٌّ إلاَّ الاشتغال بمرضاته، فيكون نظرُهُ للمخلوقات نظرَ فكرةٍ وعبرةٍ لا نظر غفلةٍ غير نافعةٍ.
{9} Kisha akawatanabahisha juu ya hoja ya kiakili yenye kuonyesha kwamba ufufuo si jambo ambalo haliwezi kutokea kama wanavyoona kuwa haliwezi kutokea, na kwamba kama watatazama yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, kama vile mbingu na ardhi, wakaona uwezo wa Mwenyezi Mungu ndani yake wenye kuangaza akili, na ukuu wake wenye kustaajabisha wanazuoni wakubwa, na kwamba kuumbwa kwa viwili hivyo, ukubwa wake, na viumbe walio ndani yake ni mambo makubwa zaidi kuliko kuwarudisha watu kutoka makaburini mwao baada ya kufa kwao. Basi je, ni nini kinachowafanya kukadhibisha licha ya kwamba wanasadiki jambo ambalo ni kubwa zaidi kuliko hili? Ndiyo, hiyo ni habari ya ghaibu ambayo bado hawajaiona hadi sasa; basi ndiyo maana wakaikadhibisha. Mwenyezi Mungu akasema, "Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu." Yaani, adhabu; kwa sababu ardhi na mbingu ziko chini uendeshaji wetu. Tukiviamuru, havitaasi. Basi jihadharini dhidi ya kuendelea kukadhibisha, tukaja kuwaadhibu kwa adhabu kali kabisa. "Hakika katika haya;" yaani, kuziumba mbingu na ardhi na viumbe vyote vilivyomo "zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia." Na kila mja anapokuwa ni wa kurudi kwa Mwenyezi Mungu sana, kunakuwa kufaidika kwake na ishara ni kukubwa zaidi. Kwa sababu mwenye kutubia anaelekea kwa Mola wake Mlezi, tayari utashi wake na hima yake vimeelekea kwa Mola wake Mlezi, na amerejea kwake katika kila jambo miongoni mwa mambo yake, kwa hivyo akawa karibu na Mola wake Mlezi, na akawa hajali kingine isipokuwa kujishughulisha na kumridhisha Yeye, kwa hivyo akawa anawatazama viumbe kwa mtazamo kufikiria na kuzingatia, siyo kutazama kwa kughafilika ambako hakuna faida yoyote.
: 10 - 11 #
{وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا يَاجِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ (10) أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (11)}.
10. Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, tukasema: "Enyi milima, karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia." Na tukamlainishia chuma. 11. Tukamwambia: "Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayoyatenda."
#
{10 - 11} أي: ولقد مَننا على عبدنا ورسولنا داود عليه الصلاة والسلام، وآتيناه فضلاً من العلم النافع والعمل الصالح والنعم الدينيَّة والدنيويَّة: ومن نعمِهِ عليه: ما خصَّه به من أمرِهِ تعالى الجمادات كالجبال والحيوانات من الطيور أن تؤوِّبَ معه وتُرَجِّعَ التسبيحَ بحمدِ ربِّها مجاوبةً له، وفي هذا من النعمة عليه أنْ كان ذلك من خصائصه التي لم تكنْ لأحدٍ قبلَه ولا بعدَه، وأنَّ ذلك يكون منهضاً له ولغيره على التسبيح إذا رأوا هذه الجماداتِ والحيواناتِ تتجاوبُ بتسبيح ربِّها وتمجيدِهِ وتكبيرِهِ وتحميدِهِ؛ كان ذلك مما يُهيج على ذكر الله تعالى. ومنها: أنَّ ذلك كما قال كثيرٌ من العلماء أنَّه طرباً بصوت داودَ؛ فإنَّ الله تعالى قد أعطاه من حُسن الصوت ما فاق به غيرَه، وكان إذا رجَّعَ التسبيحَ والتهليلَ والتمجيدَ بذلك الصوت الرخيم الشَّجِيِّ المطرِب؛ طربَ كلُّ مَنْ سَمِعَهُ من الإنس والجنِّ، حتى الطيور والجبال، وسبَّحت بحمدِ ربِّها. ومنها: أنَّه لعله ليحصل له أجر تسبيحها، لأنه سبب ذلك، وتسبح تبعاً له. ومن فضله عليه أن ألانَ له الحديدَ؛ ليعملَ الدروع السابغاتِ، وعلَّمه تعالى كيفيَّة صنعتِهِ؛ بأن يقدِّرَه في {السردِ}؛ أي: يقدِّره حَلَقاً ويصنعُه كذلك ثم يُدْخِلُ بعضها ببعض، قال تعالى: {وعلَّمْناه صنعةَ لَبوس لكم لِتُحْصِنَكُم من بأسِكُم فهل أنتم شاكرونَ}، ولمَّا ذَكَرَ ما امتنَّ به عليه وعلى آله؛ أمره بشكرِهِ وأن يَعْمَلوا صالحاً، ويراقِبوا الله تعالى فيه بإصلاحه وحفظِهِ من المفسداتِ؛ فإنَّه بصيرٌ بأعمالهم، مطَّلع عليها، لا يخفى عليه منها شيءٌ.
{10 - 11} Yaani, tulimneemesha mja wetu na Mtume wetu Daudi, rehema na amani zimshukie, na tukampa elimu yenye manufaa, matendo mema, na neema za kidini na za kidunia, na miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu yake. Ni yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa yeye tu miongoni mwa vitu visivyo na uhai, kama vile milima na wanyama kama ndege, vije kukariri pamoja naye kumtakasa Mola wao Mlezi na kumsifu na kumwitikia. Hii ni neema kwake kwamba haya alipewa yeye tu, na wala hakuna aliyewahi kupewa kabla yake wala baada yake, na kwamba hilo likawa ni la kumtia moyo yeye na wengine kumtakasa Mwenyezi Mungu watakapoona vitu hivi visivyo na uhai na wanyama wanamuitikia Mola wao Mlezi kwa kumtakasa na kumtukuza, na kusema kwamba yeye ndiye mkubwa na kumsifu. Hili linakuwa ni katika mambo ambayo yanamchochea mtu kumtaja Mwenyezi Mungu. Na Miongoni mwake ni hilo - kama walivyosema wanazuoni wengi - ilikuwa ni furaha ya sauti ya Daudi. Kwani Mwenyezi Mungu alikuwa amempa sauti nzuri iliyozidi ile ya mtu yeyote. Na alikuwa anaporudiarudia kumtakasa Mwenyezi Mungu, na kusema: hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kumtukuza kwa sauti hiyo ya kupendeza, yenye mvuto, yenye kufurahisha; kila aliyemsikia, kuanzia watu hadi majini, hata ndege na milima, walifurahi na wakamtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na miongoni mwake ni labda atapata malipo ya kutakasa kwao huku, kwa sababu yeye ndiye sababu ya wao kufanya hivyo, na walikuwa wakimtakasa Mwenyezi Mungu huku wakimfuata Daudi katika hilo. Na katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yake, ni kwamba alimlainishia chuma ili atengeneze ngao na nguo za chuma pana, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamfundisha jinsi ya kuzitengeneza. Kwamba "na kadiria sawa katika kuunganisha." Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu. Je, mtakuwa wenye kushukuru?" Na alipotaja kile alichomneemesha nacho na juu ya familia yake, akamuamuru kumshukuru, na kwamba wafanye matendo mema na wamchunge Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake kwa kuyatengeneza na kuyahifadhi kutokana na yenye kuyaharibu. Kwani Yeye anayaona vyema matendo yao, anayajua na hakuna chochote katika hayo kinachofichikana kwake.
: 12 - 14 #
{وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ وَأَسَلْنَا لَهُ عَيْنَ الْقِطْرِ وَمِنَ الْجِنِّ مَنْ يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ وَمَنْ يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ (12) يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِنْ مَحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَاسِيَاتٍ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا وَقَلِيلٌ مِنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ (13) فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَى مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنْسَأَتَهُ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَنْ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ (14)}.
12. Naye Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba. Na katika majini, walikuwako waliokuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka. 13. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na vitu vifananavyo vingine, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yaliyo madhubuti. Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru. Na ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru. 14. Na tulipomhukumia kufa, hapana aliyewajulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Na alipoanguka, majini wakatambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha.
#
{12} لمَّا ذَكَرَ فضلَه على داود عليه السلام؛ ذكر فضلَه على ابنه سليمان عليه الصلاة والسلام، وأنَّ الله سخَّر له الريح تجري بأمرِهِ وتحمِلُه وتحمِلُ جميعَ ما معه وتقطعُ المسافة البعيدةَ جدًّا في مدةٍ يسيرةٍ، فتسير في اليوم مسيرة شهرين: {غدوُّها شهرٌ}؛ أي: أول النهار إلى الزوال، {ورواحُها شهرٌ}: من الزَّوال إلى آخر النهار، {وأسَلْنا له عَيْنَ القِطْرِ}؛ أي: سخَّرْنا له عينَ النُّحاس وسهَّلْنا له الأسباب في استخراج ما يُستخرج منها من الأواني وغيرها، وسخَّرَ اللهُ له أيضاً الشياطين والجنَّ لا يقدِرون أن يستعصوا عن أمرِهِ، {ومن يَزِغْ منهم عن أمرِنا نُذِقْه من عذاب السعير}.
{12} Alipotaja fadhila zake juu ya Daudi, amani iwe juu yake, akataja neema yake juu ya mwanawe, Suleiman, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na kwamba Mwenyezi Mungu alimtiishia upepo uendao kwa amri yake na ukawa unambeba yeye na kila kilichokuwa pamoja naye na kukata umbali mrefu sana kwa muda mfupi, ukawa unakwenda katika siku moja umbali wa miezi miwili. "Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba." Yaani, tukamfanyia wepesi njia za kutengeneza vitu vinavyotengenezwa kutoka humo kama vile vyombo na vitu vingine. Na pia, Mwenyezi Mungu alimtiishia mashetani na majini ambao hawakuweza kuasi amri yake. "Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka."
#
{13} وأعمالُهم ؛ كلُّ ما شاء سليمان عَمِلوه؛ {من محاريبَ}: وهو كلُّ بناءٍ يُعقد وتحكم به الأبنية؛ فهذا فيه ذكرُ الأبنية الفخمة. {وتماثيلَ}؛ أي: صور الحيوانات والجمادات من إتقانِ صنعتهم، وقدرتِهِم على ذلك، وعملهم لسليمان. {وجفانٍ كالجوابِ}؛ أي: كالبرك الكبار يعملونها لسليمان للطعام؛ لأنَّه يحتاجُ إلى ما لا يحتاج إليه غيره. {و} يعملونَ له قدوراً {راسياتٍ}: لا تُزالُ عن أماكِنِها من عِظَمِها، فلما ذكر مِنَّتَه عليهم؛ أمَرَهم بشكرها، فقال: {اعْمَلوا آل داودَ}: وهم داودُ وأولادهُ وأهلُه؛ لأنَّ المنَّةَ على الجميع، وكثير من هذه المصالح عائدٌ لكلِّهم {شُكراً}: لله على ما أعطاهم، ومقابلةً لما أولاهم. {وقليلٌ من عبادي الشَّكورُ}: فأكثرُهم لم يشكُروا الله تعالى على ما أوْلاهم من نعمِهِ ودَفَعَ عنهم من النقم. والشكرُ: اعترافُ القلب بمنَّةِ الله تعالى، وتلقِّيها افتقاراً إليها، وصرفُها في طاعة الله تعالى، وصونُها عن صرفها في المعصية.
{13} Na matendo yao yalikuwa kwamba chochote ambacho Suleiman alitaka, walikifanya, kama vile "mihrabu" ambao ni kila mjengo unaojengwa, na ambao kwa huo, mijengo mingine inakuwa na nguvu. Hili linaonyesha kwamba kulikuwepo na majengo ya kifahari. "Na masanamu", yaani picha za wanyama na vitu visivyo na uhai, kwa kuvitengeneza kwa ustadi mkubwa, na kwamba walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, na kumfanyia kazi Suleimani. "Na madeste makubwa kama mahodhi" ambayo walikuwa wamemfanyia Suleiman kwa ajili ya chakula. Kwa sababu alikuwa anahitaji kile ambacho hakuna mtu mwingine alikuwa anakihitaji. "Na" wanamtengenezea masufuria "makubwa" yasiyoondolewa mahala pake kwa sababu ya ukubwa wake. Kwa hivyo, alipotaja neema zake juu yao, akawaamuru wamshukuru kwa hizo. Kwa hivyo akasema, "Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru." Kwa sababu neema hizo ziliwafikia wote, na mengi ya masilahi hayo yalikuwa yanawarudia wote. Kwa hivyo, walipaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa aliyowapa, na pia wamshukuru kwa njia ya kuyakabili yale aliyowaruzuku. "Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru." Kwani, wengi wao hawakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake alizowaneemesha kwazo, na akawaepusha na adhabu. Shukrani ni kukiri kwa moyo neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuipokea kwa sababu mtu anaihitaji, na kuitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuilinda dhidi ya kuitumia katika uasi.
#
{14} فلم يزل الشياطينُ يعملون لسليمانَ عليه الصلاة والسلامُ كلَّ بناءٍ، وكانوا قد موَّهوا على الإنس، وأخبروهم أنهم يعلمون الغيبَ، ويطَّلعون على المكنوناتِ، فأرادَ اللَّه تعالى أن يُرِيَ العبادَ كَذِبَهم في هذه الدعوى، فمكثوا يعملون على عملِهِم، وقضى الله الموتَ على سليمان عليه السلام، واتَّكأ على عصاه، وهي المنسأة، فصاروا إذا مروا به وهو متَّكئٌ عليها؛ ظنُّوه حيًّا وهابوه، فغدوا على عَمَلِهِم كذلك سنةً كاملةً على ما قيل، حتى سُلِّطَتْ دابةُ الأرض على عصاه، فلم تزل ترعاه حتى باد وسقط، فسقط سليمان، وتفرقتِ الشياطينُ وتبينتِ الإنسُ أنَّ الجنَّ {لو كانوا يعلمونَ الغيبَ ما لَبِثوا في العذابِ المُهين}: وهو العملُ الشاقُّ عليهم؛ فلو علموا الغيبَ؛ لعلموا موتَ سليمان الذي هم أحرص شيءٍ عليه ليسلموا ممَّا هم فيه.
{14} Kwa hivyo, mashetani wakaendelea kumfanyia kazi Suleiman, rehema na amani ziwe juu yake. Nao walikuwa wamewapotosha watu na kuwaambia kwamba wanajua mambo ya ghaibu, na kwamba walikuwa na uwezo wa kufikia mambo yaliyofichika. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuwaonyesha waja wake uongo wao katika madai yao haya. Basi wakabakia wakiendelea kufanya kazi yao hiyo. Na Mwenyezi Mungu akapitisha kwamba Suleiman, amani iwe juu yake afe, kwa hivyo akaiegemea fimbo yake. Basi wakawa wanapopita karibu naye hali ya kuwa ameegemea juu yake, wanadhani kwamba yu hai kwa hivyo wanamuogopa. Basi wakawa wanaendelea kufanya kazi zao hivyo hivyo kwa muda wa mwaka mzima, kama ilivyosemwa, mpaka wadudu wa ardhini walipopewa mamlaka kuila fimbo yake. Wakawa wanaila mpaka ikaisha na ikaanguka chini, kwa hivyo Suleiman akaanguka chini pia, nao mashetani wakatawanyika. Kwa hivyo watu wakatambua ya kwamba majini, "lau kuwa wangelijua ya ghaibu, wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha." Yaani, kazi ngumu sana juu yao. Na lau kuwa walikuwa wanaijua ghaibu; basi wangejua kifo cha Suleiman, ambacho ndicho kitu kikubwa zaidi walichotaka kujua ili wasalimike kutokana na kile walichokuwemo.
: 15 - 21 #
{لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِي مَسْكَنِهِمْ آيَةٌ جَنَّتَانِ عَنْ يَمِينٍ وَشِمَالٍ كُلُوا مِنْ رِزْقِ رَبِّكُمْ وَاشْكُرُوا لَهُ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ (15) فَأَعْرَضُوا فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ سَيْلَ الْعَرِمِ وَبَدَّلْنَاهُمْ بِجَنَّتَيْهِمْ جَنَّتَيْنِ ذَوَاتَيْ أُكُلٍ خَمْطٍ وَأَثْلٍ وَشَيْءٍ مِنْ سِدْرٍ قَلِيلٍ (16) ذَلِكَ جَزَيْنَاهُمْ بِمَا كَفَرُوا وَهَلْ نُجَازِي إِلَّا الْكَفُورَ (17) وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ الْقُرَى الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَاهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا السَّيْرَ سِيرُوا فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا آمِنِينَ (18) فَقَالُوا رَبَّنَا بَاعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ فَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَاهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ (19) وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (20) وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِمْ مِنْ سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَنْ يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ وَرَبُّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ (21)}.
15. Hakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu. 16. Lakini wakayapa mgongo. Kwa hivyo, tukawatumia mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda makali, machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi. 17. Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru? 18. Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia, "Nendeni humo usiku na mchana kwa amani." 19. Lakini wakasema, "Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu." Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru mno. 20. Na bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao. Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini. 21. Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, isipokuwa kwa sababu ya kuwajaribu ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.
#
{15 - 19} سبأ قبيلةٌ معروفةٌ في أداني اليمن، ومسكنُهم بلدةٌ يُقالُ لها: مأرِب، ومن نعم الله ولطفِهِ بالناس عموماً وبالعرب خصوصاً أنه قصَّ في القرآن أخبار المهلكين والمعاقَبين ممَّنْ كان يجاوِرُ العرب، ويشاهدُ آثاره، ويتناقلُ الناس أخبارَه؛ ليكونَ ذلك أدعى إلى التصديق وأقربَ للموعظة، فقال: {لقد كان لسبأٍ في مسكنِهِم}؛ أي: محلِّهم الذي يسكنون فيه {آيةٌ}: والآيةُ هنا ما أدرَّ الله عليهم من النعم، وصرف عنهم من النقم، الذي يقتضي ذلك منهم أن يَعْبُدوا الله ويشكُروه. ثم فسَّرَ الآية بقوله: {جنَّتانِ عن يمينٍ وشمال}: وكان لهم وادٍ عظيمٌ تأتيه سيولٌ كثيرةٌ، وكانوا بنوا سدًّا محكماً يكون مجمعاً للماء، فكانت السيول تأتيه، فيجتمع هناك ماءٌ عظيمٌ، فيفرِّقونَه على بساتينهم التي عن يمين ذلك الوادي وشماله، وتُغِلُّ لهم تلك الجنتان العظيمتان من الثمار ما يكفيهم ويَحْصُلُ لهم به الغبطةُ والسرورُ، فأمرهم الله بشكرِ نِعَمِهِ التي أدرَّها عليهم من وجوه كثيرة: منها: هاتان الجنَّتان اللتان غالب أقواتهم منهما. ومنها: أنَّ الله جعل بَلَدَهُم بلدةً طيبةً لحسن هوائها وقلَّة وَخَمِها وحصول الرزق الرغد فيها. ومنها: أنَّ الله تعالى وَعَدَهم إن شكروه أن يغفرَ لهم ويرحَمَهم، ولهذا قال: {بلدةٌ طيبةٌ وربٌّ غفورٌ}. ومنها: أنَّ الله لما علم احتياجَهم في تجاراتِهِم ومكاسِبِهم إلى الأرض المباركة - الظاهرُ أنَّها قُرى صنعاء كما قاله غيرُ واحدٍ من السلف، وقيل: إنَّها الشامُ ـ؛ هيَّأ لهم من الأسباب ما به يتيسَّر وصولُهم إليها بغايةِ السُّهولة من الأمن وعدم الخوف وتواصُل القرى بينهم وبينها؛ بحيثُ لا يكون عليهم مشقَّةٌ بحمل الزاد والمزاد، ولهذا قال: {وجعلنا بينهم وبين القرى التي بارَكْنا فيها قرىً ظاهرةً وقدَّرْنا فيها السيرَ}؛ أي: سيراً مقدراً يعرفونه ويحكمونَ عليه بحيث لا يتيهونَ عنه ليالي وأياماً. {آمنينَ}؛ أي: مطمئنين في السير في تلك الليالي والأيام غير خائفينَ، وهذا من تمام نعمةِ الله عليهم أنْ أمَّنَهم من الخوف. فأعْرَضوا عن المنعِم وعن عبادتِهِ، وبَطِروا النعمةَ وملُّوها، حتى إنَّهم طلبوا وتمنَّوا أن تتباعد أسفارُهم بين تلك القرى التي كان السير فيها متيسراً. {وظلموا أنْفُسَهم}: بكفرِهِم بالله وبنعمتِهِ، فعاقَبَهُمُ الله تعالى بهذه النعمة التي أطْغَتْهم، فأبادها عليهم، فأرسل عليها {سيلَ العَرِم}؛ أي: السيل المتوعِّر الذي خَرَّبَ سدَّهم، وأتلف جناتهم، وخرَّبَ بساتينَهم، فتبدَّلت تلك الجناتُ ذات الحدائق المعجِبَة والأشجار المثمرة، وصار بَدَلَها أشجارٌ لا نفعَ فيها. ولهذا قال: {وبدَّلْناهم بجنَّتَيْهم جنتينِ ذواتي أكُل}؛ أي: شيءٍ قليل من الأكل الذي لا يقع منهم موقعاً، {خَمْطٍ وأثْلٍ وشيءٍ من سدرٍ قليل}: وهذا كله شجرٌ معروفٌ، وهذا من جنس عملهم؛ فكما بدَّلوا الشكر الحسن بالكفر القبيح؛ بُدِّلُوا تلك النعمة بما ذكر. ولهذا قال: {ذلك جَزَيْناهم بما كفروا وهل نُجازي إلاَّ الكفورَ}؛ أي: وهل نُجازي جزاء العقوبة - بدليل السياق - إلاَّ مَنْ كَفَرَ بالله وبَطِرَ النعمة؟! فلمَّا أصابَهم ما أصابَهم؛ تفرَّقوا وتمزَّقوا بعدما كانوا مجتمعينَ، وجَعَلَهُمُ الله أحاديثَ يُتَحَدَّث بهم وأسماراً للناس، وكان يُضْرَبُ بهم المثلُ، فيقالُ: «تفرَّقوا أيدي سبأ»؛ فكلُّ أحدٍ يتحدَّث بما جرى لهم، ولكنْ لا ينتفعُ بالعبرة فيهم إلاَّ مَنْ قال الله: {إنَّ في ذلك لآياتٍ لكلِّ صبارٍ شكورٍ}: صبَّارٍ على المكاره والشدائدِ، يتحمَّلُها لوجه الله، ولا يتسخَّطُها، بل يصبرُ عليها، شكورٍ لنعمة الله تعالى، يُقِرُّ بها، ويعترفُ، ويثني على من أولاها، ويصرِفُها في طاعته. فهذا إذا سمع بقصَّتِهم وما جرى منهم وعليهم؛ عَرَفَ بذلك أنَّ تلك العقوبة جزاءٌ لكفرِهم نعمةَ الله، وأنَّ مَنْ فَعَلَ مثلهم؛ فُعِلَ به كما فُعِلَ بهم، وأنَّ شُكْرَ الله تعالى حافظٌ للنعمة دافعٌ للنقمة، وأنَّ رُسُلَ الله صادقون فيما أخبروا به، وأنَّ الجزاء حقٌّ كما رأى أنموذَجَه في دار الدنيا.
{15 - 19} Sabaa ni kabila mashuhuri katika viunga vya Yemen, na makazi yao yalikuwa katika mji uitwao Ma'rib. Nao ulikuwa ni miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwa watu kwa ujumla na hasa kwa Waarabu, na kwamba aliwasimulia katika Qur-ani habari za wale walioangamizwa na kuadhibiwa miongoni mwa wale waliokuwa majirani na Waarabu. Yanashuhudiwa magofu yao, na watu wananukuu habari zao; ili hili liweze kusaidia kusadiki zaidi na liwe karibu zaidi katika kufikisha mawaidha. Akasema, "Hakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao." Na ishara hapa inamaanisha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha miongoni mwa neema mbalimbali, na akawaepusha kutokana na adhabu, mambo ambayo wanawahitaji kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumshukuru. Kisha akaifafanua ishara hiyo kwa kusema, "bustani mbili, kulia na kushoto." Nao walikuwa na bonde kubwa lenye kujiwa na maji mengi ya mafuriko. Na walikuwa wamejenga bwawa madhubuti lenye kukusanya maji hayo. Kwa hivyo maji hayo ya mafuriko yalikuwa yakija humo, na maji mengi yangekusanyika humo, kisha wanayatawanya katika bustani zao zilizokuwa upande wa kulia na wa kushoto wa bonde hilo. Na zikawa bustani hizo mbili kubwa zinawapa matunda ya kuwatosheleza, na wanafurahia mno. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaamuru kushukuru neema zake alizowapa kwa njia nyingi. Miongoni mwake ni hizi bustani mbili ambazo chakula chao kingi kilikuwa ni kutoka humo. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliifanya nchi yao kuwa nchi nzuri kwa hewa yake nzuri, kutokuwepo na machafuzi yoyote ya hewa, na kuwepo kwa riziki nyingi humo. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi kwamba wakimshukuru, atawasamehe na kuwarehemu. Na ndiyo maana akasema, "Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu." Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu alipojua kwamba wanahitaji ardhi iliyobarikiwa kwa ajili ya biashara zao na mapato yao - na ni dhahiri kwamba huu mji ulikuwa miongoni mwa miji ya Sana’a, kama walivyosema zaidi ya mmoja wa wema waliotangulia. Na ikasemwa kwamba ilikuwa huko Shama, - basi Mwenyezi Mungu akawaandalia njia za kurahisisha kuyafikia hayo kwa kuwapa usalama na kuondoa hofu, na kuifanya miji kuwa na mawasiliano, ili wasipate taabu katika kubeba bidhaa na vyakula. Na ndiyo maana akasema, "Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari." Yaani, safari zilizopangwa wanazozijua na kuzihukumu kwa namna ambayo hawawezi kupotea usiku na mchana. "Kwa amani." Yaani, wakiwa na utulivu katika safari zao, usiku na mchana bila ya hofu yoyote. Na hii ni katika ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu juu yao kwamba aliwapa amani kutokana na hofu. Lakini wakampa mgongo aliyewaneemesha na pia wakakataa kumwabudu. Na wakajivuna na neema hizo na wakachoshwa nazo hadi wakaomba na kutamani kwamba safari zao hizo ziwe mbali kati ya vile miji hiyo ambayo safari ya kati yake ilikuwa rahisi. "Na wakazidhulumu nafsi zao" kwa kumkufuru Mwenyezi Mungu na fadhila zake. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaadhibu kwa neema hizi zilizowapotosha; kwa hivyo akaziangamiza. Aliwatumia, "mafuriko makubwa" ambayo yaliharibu bwawa lao hilo, na yakaharibu bustani zao. Kwa hivyo, bustani hizo zenye mimea ya kupendeza na miti yenye matunda zikabadilishwa na ikawekwa ndani yake miti isiyofaa. Ndiyo maana akasema, "na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda" yanayoweza kuliwa lakini yasiyowasaidia kitu katika kukidhi haja yao ya chakula; "makali, machungu, na mivinje, na kitu kidogo katika miti ya kunazi. Yote hii ni miti mashuhuri, na malipo haya ni ya aina sawa na matendo yao. Kila walivyobadilisha shukrani nzuri kwa ukafiri mbaya; walibadilishiwa neema hizo kwa kile kilichotajwa. Ndiyo maana akasema, "Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru" Mwenyezi Mungu na akajivuna na neema yake? Yalipowapata yaliyowapata, walitengana na kutawanyika baada ya kwamba walikuwa pamoja, na Mwenyezi Mungu akawafanya kuwa ni masimulizi tu ambayo watu wanayazungumzia na ndiyo zikawa ndizo hadithi zao za usiku. Na wakawa wanapigiwa mfano, ikasemwa: 'Walitengana kama walivyotengana watu wa Sabaa.' Kila mtu akawa anazungumza juu ya yale yaliyowasibu, lakini hakuna anayefaidika na kupata mafunzo kutoka kwao isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao: "Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru." Mwenye subira katika machukizo na shida, ambaye anayasubiria kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu, na wala hayachukii, bali anayavumilia, na kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anakiri neema hizo na kuzitambua, na kumsifu aliyemneemesha nazo, na anazitumia katika kumtii. Ndiyo maana, inaposikiwa hadithi yao na kile walichofanya na kile kilichowatokea, inajulikana kwa hayo kwamba adhabu hiyo ni malipo ya kukufuru kwao neema za Mwenyezi Mungu, na kwamba anayefanya mfano wao, atafanyiwa kama walivyofanyiwa wao, na kwamba kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kunahifadhi neema na kuzuia adhabu, na kwamba Mitume wa Mwenyezi Mungu ni wakweli katika yale waliyotuambia, na kwamba malipo ya akhera ni ya kweli, kama ulivyoonekana mfano wake katika dunia hii.
#
{20} ثم ذكر أنَّ قوم سبأ من الذين صَدَّقَ عليهم إبليسُ ظنَّه؛ حيث قال لربِّه: {فبعزَّتِكَ لأُغْوِيَنَّهُمْ أجمعينَ. إلاَّ عبادَكَ منهم المُخْلَصينَ}: وهذا ظنٌّ من إبليس لا يقينٌ؛ لأنَّه لا يعلم الغيبَ ولم يأتِهِ خبرٌ من الله أنَّه سيُغْويهم أجمعين؛ إلاَّ من استثنى؛ فهؤلاء وأمثالهم ممَّنْ صدَّقَ عليه إبليسُ ظنَّه ودعاهم وأغواهم، {فاتَّبَعوه إلاَّ فريقاً من المؤمنين}: ممَّنْ لم يكفرْ بنعمة الله؛ فإنَّه لم يدخُلْ تحتَ ظنِّ إبليس، ويُحتمل أنَّ قصة سبأ انتهت عند قولِهِ: {إنَّ في ذلك لآياتٍ لكلِّ صبارٍ شكورٍ}. ثم ابتدأ فقال: {ولقد صَدَّقَ عليهم}؛ أي: على جنس الناس، فتكون الآيةُ عامةً في كلِّ مَنِ اتَّبَعَهُ.
{20} Kisha akataja kwamba watu wa Sabaa walikuwa miongoni mwa wale ambao Iblisi alihakikisha ile dhana yake juu yao. Alipomwambia Mola wake Mlezi, "Ninaapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote. Isipokuwa waja wako waliosafika miongoni mwao." Hii ilikuwa tu ni dhana ya Iblisi, wala hata hakuwa na yakini juu ya hilo. Kwa sababu yeye hajui ghaibu, wala haikumjia habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba atawapoteza wote. Isipokuwa wale ambao aliwaepusha kutokana na hilo. Hawa na wengine mfano wao ni miongoni mwa wale ambao Iblisi aliwahakikishia ile dhana yake, na akawaita na kuwapoteza. "Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini" katika wale ambao hawakuzikufuru neema za Mwenyezi Mungu; hao hawakuingia katika ile dhana ya Iblisi. Na inawezekana kwamba kisa cha Sabaa kiliishia pale aliposema, “Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru." Kisha akaanza tena na kusema, "Na bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao." Yaani, kwa watu wote, kwa hivyo Aya hii inakuwa ni ya jumla kwa kila aliyemfuata.
#
{21} ثم قال تعالى: {وما كان له}؛ أي: لإبليس {عليهم من سلطانٍ}؛ أي: تسلُّطٍ وقهرٍ وقسرٍ على ما يريده منهم، ولكنَّ حكمةَ الله تعالى اقتضت تسليطَه وتسويلَه لبني آدم؛ {لنعلم من يؤمنُ بالآخرة ممَّنْ هو منها في شكٍّ}؛ أي: ليقوم سوقُ الامتحان، ويُعْلَمَ به الصادقُ من الكاذب، ويُعْرَفَ مَنْ كان إيمانُه صحيحاً يثبتُ عند الامتحان والاختبار وإلقاءِ الشُّبَه الشيطانيَّةِ ممَّنْ إيمانُه غيرُ ثابتٍ يتزلزلُ بأدنى شبهةٍ ويزولُ بأقلِّ داع يدعوه إلى ضدِّه؛ فالله تعالى جعله امتحاناً يمتحن به عبادَه ويُظْهِرُ الخبيثَ من الطيب. {وربُّك على كلِّ شيءٍ حفيظٌ}: يحفظُ العباد ويحفظُ عليهم أعمالهم، ويحفظُ تعالى جزاءَها؛ فيوفِّيهم إيَّاها كاملة موفرةً.
{21} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Na yeye;" yaani, Iblisi, "hakuwa na mamlaka yoyote juu yao." Yaani, kuwatawala, na kuwakandamiza, na kuwalazimisha juu ya kile anachotaka kutoka kwao, lakini hekima ya Mwenyezi Mungu ililazimu kwamba awe na mamlaka na uwezo wa kuwapotosha wanadamu "ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka." Yaani, ili watu waweze kupewa mtihani na kwa huo ijulikane mkweli na mwongo. Na ili ajulikane yule ambaye imani yake ni sahihi, anayekuwa thabiti wakati wa mtihani na majaribu na kutupilia mbali fikira potofu za kishetani na ajulikane yule ambaye imani yake si thabiti, ambaye anajisalimisha anapofikiwa na fikira potovu ndogo zaidi na anakubali kufanya kinyume kunapokuwa na sababu ndogo zaidi inayoliitia hilo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfanya kuwa mtihani na kwake anawafanyia waja wake majaribu ili adhihirike muovu mbali na mwema. "Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu." Anawahifadhi waja wake na anawahifadhia vitendo vyao, na Yeye Mtukufu anahifadhi malipo yao, na atawalipa kwa ukamilifu na ukarimu.
: 22 - 23 #
{قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِنْ شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُمْ مِنْ ظَهِيرٍ (22) وَلَا تَنْفَعُ الشَّفَاعَةُ عِنْدَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ حَتَّى إِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ (23)}.
22. Sema, "Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata uzito wa chembe katika mbingu wala ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao." 23. Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: "Mola wenu Mlezi amesema nini?" Watasema: "Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa."
#
{22 - 23} أي: {قل}: يا أيها الرسولُ للمشركين بالله غيرَهُ من المخلوقاتِ التي لا تنفعُ ولا تضرُّ ملزماً لهم بعجزِها ومبيِّناً بطلان عبادتها: {ادعوا الذينَ زعمتُم من دون الله}؛ أي: زعمتموهم شركاء لله إنْ كان دعاؤكم ينفعُ؛ فإنَّهم قد توفرتْ فيهم أسبابُ العجز وعدم إجابة الدعاء من كلِّ وجه؛ فإنَّهم ليس لهم أدنى ملك، فلا يملكونَ مثقال ذرَّةٍ في السماوات والأرض: على وجه الاستقلال، ولا على وجه الاشتراك، ولهذا قال: {وما لهم}؛ أي: لتلك الآلهة الذين زعمتم {فيهما}؛ أي: في السماواتِ والأرض {من شِرْكٍ}؛ أي: لا شركٌ قليل ولا كثيرٌ؛ فليس لهم ملكٌ ولا شركة ملك. بقي أنْ يُقالَ: ومع ذلك؛ فقد يكونون أعواناً للمالك ووزراء له؛ فدعاؤهم يكون نافعاً؛ لأنَّهم بسبب حاجة الملك إليهم يقضون حوائج مَنْ تعلَّق بهم، فنفى تعالى هذه المرتبةَ، فقال: {وما له}؛ أي: للَّه تعالى الواحد القهار {منهم}؛ أي: من هؤلاء المعبودين {من ظهيرٍ}؛ أي: معاونٍ ووزيرٍ يساعده على الملك والتدبير. فلم يبقَ إلاَّ الشفاعةُ، فنفاها بقوله: {ولا تنفَعُ الشفاعةُ عنده إلا لِمَنْ أذِنَ له}: فهذه أنواع التعلُّقات التي يتعلَّقُ بها المشركون بأندادهم وأوثانهم من البشر والشجر والحجر وغيرهم، قَطَعَها الله وبيَّن بطلانَها تبييناً حاسماً لموادِّ الشرك قاطعاً لأصوله؛ لأنَّ المشرك إنَّما يدعو ويعبدُ غير الله؛ لما يرجو منه من النفع؛ فهذا الرجاء هو الذي أوجبَ له الشركَ؛ فإذا كان من يدعوه غير الله لا مالكاً للنفع والضرِّ ولا شريكاً للمالك ولا عوناً وظهيراً للمالك ولا يقدِرُ أن يَشْفَعَ بدون إذنِ المالك؛ كان هذا الدعاء وهذه العبادة ضلالاً في العقل باطلةً في الشرع، بل ينعكسُ على المشركِ مطلوبُه ومقصودُه؛ فإنَّه يريدُ منها النفع، فبيَّن الله بطلانه وعدمه، وبيَّن في آيات أُخَرَ ضررَها على عابديها ، وأنَّه يوم القيامةِ يكفرُ بعضُهم ببعض ويلعنُ بعضُهم بعضاً ومأواهم النارُ، وإذا حُشِرَ الناس كانوا لهم أعداءً وكانوا بعبادتهم كافرين. والعجب أن المشرك استكبر عن الانقياد للرسل بزعمهم أنهم بشرٌ، ورضي أن يَعْبُدَ ويدعو الشجر والحجر، استكبر عن الإخلاص للملك الرحمن الديان، ورضي بعبادةِ مَنْ ضَرُّهُ أقربُ من نفعِهِ طاعةً لأعدى عدوٍّ له وهو الشيطان! وقوله: {حتى إذا فُزِّعَ عن قلوبِهِم قالوا ماذا قال ربُّكُم قالوا الحقَّ وهو العليُّ الكبيرُ}: يُحتمل أنَّ الضمير في هذا الموضع يعودُ إلى المشركين؛ لأنهم مذكورون في اللفظ، والقاعدة في الضمائرِ أن تعودَ إلى أقرب مذكورٍ، ويكونُ المعنى: إذا كان يوم القيامةِ وفُزِّع عن قلوب المشركين؛ أي: زال الفزع وسُئِلوا حين رجعت إليهم عقولُهم عن حالهم في الدُّنيا وتكذيبهم للحقِّ الذي جاءت به الرسل؛ أنَّهم يقرُّون أنَّ ما هم عليه من الكفر والشرك باطلٌ، وأنَّ ما قال الله وأخبرت به عنه رسلُه هو الحقُّ، فبدا لهم ما كانوا يُخفون من قبلُ، وعلموا أن الحقَّ لله، واعترفوا بذُنوبهم. {وهو العليُّ}: بذاته فوقَ جميع المخلوقاتِ، وقهرُهُ لهم وعلوُّ قدره بما له من الصفات العظيمةِ جليلة المقدار. {الكبيرُ}: في ذاته وصفاته، ومن علوِّه أنَّ حكمه تعالى يعلو، وتُذْعِنُ له النفوسُ، حتى نفوس المتكبرينَ والمشركينَ، وهذا المعنى أظهرُ، وهو الذي يدلُّ عليه السياق. ويُحتمل أنَّ الضمير يعود إلى الملائكة، وذلك أنَّ الله تعالى إذا تكلَّم بالوحي؛ سمعتْه الملائكةُ فصُعِقوا وخرُّوا لله سجداً، فيكون أول من يرفعُ رأسهَ جبريلُ، فيكلِّمه الله من وحيه بما أراد؛ فإذا زال الصعقُ عن قلوب الملائكة وزال الفزعُ، فيسأل بعضُهم بعضاً عن ذلك الكلام الذي صعقوا منه: ماذا قال ربُّكم؟ فيقولُ بعضُهم لبعض: قال الحقَّ: إمَّا إجمالاً لعلمهم أنه لا يقول إلاَّ حقًّا، وإمَّا أن يقولوا: قال كذا وكذا ، للكلام الذي سمعوه منه، وذلك من الحقِّ. فيكون المعنى على هذا أنَّ المشركين الذين عبدوا مع الله تلك الآلهة التي وَصَفْنا لكم عجزها ونقصها وعدم نفعها بوجهٍ من الوجوه كيف صَدَفوا وصَرَفوا عن إخلاص العبادة للربِّ العظيم العليِّ الكبير الذي من عظمته وجلاله أنَّ الملائكة الكرام والمقرَّبين من الخلق يبلغ بهم الخضوعُ والصعقُ عند سماع كلامه هذا المبلغ، ويقرُّون كلُّهم لله أنَّه لا يقول إلاَّ الحقَّ؛ فما بال هؤلاءِ المشركين استكبروا عن عبادةِ مَنْ هذا شأنُه وعظمةُ ملكِهِ وسلطانِهِ؟! فتعالى العليُّ الكبيرُ عن شركِ المشركين وإفكِهِم وكذِبِهم.
{22 - 23} Yaani, "Sema" ewe Mtume, uwaambie wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na viumbe vingine visivyofaa wala kudhuru, ukiwafanya kukubali kwa lazima kwamba hivyo havina uwezo, na ukibainisha ubatili wa kuviabudu, "Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu," mkadai kwamba wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu, ikiwa dua yenu ina manufaa yoyote. Wao kwa hakika tayari wana sababu za kutoweza ndani yao na kushindwa kujibu maombi kwa namna yoyote ile. Kwani wao hawana umiliki hata kidogo, kwa kuwa hawamiliki uzito wa chembe katika mbingu na ardhi, kwa kujitegemea wala kwa njia ya ushirika. Na ndiyo maana akasema, "Wala hawana ushirika wowote humo," si mdogo wala mwingi. Inabakia kusema kwamba: Hata hivyo, wanaweza kuwa wasaidizi na mawaziri wa Mmiliki wa kweli; basi dua yao ikawa ni yenye kunufaisha. Kwa kuwa, kwa sababu Mmiliki wa kweli anawahitaji, wanaweza kutimiza mahitaji ya wale wanaofungamana nao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaikanusha daraja hii, na akasema, "Wala Yeye" Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi, "hana msaidizi yeyote miongoni mwao" anayemsaidia katika kutawala na kuendesha mambo. Basi hakuna kilichobakia isipokuwa uombezi, lakini huo pia akaukanusha kwa kauli yake, "Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini." Hizi ndizo aina za mafungamano wanayofungamana kwayo washirikina na washirika wao na masanamu yao katika wanadamu, miti, mawe na mengineo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akayakata na kubainisha ubatili wao kwa ubainisho wa kukata kiini cha ushirikina, na wa kukata mizizi yake. Kwa sababu mshirikina huomba na kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu akitarajia kunufaika kutoka kwake, na matarajio haya ndiyo yaliyomfanya kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Basi ikiwa huyo ambaye yeye anamuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu hamiliki manufaa yoyote wala madhara, wala hata si mshirika wa Mmiliki wa kweli wala msaidizi wake, wala hawezi kufanyia wengine uombezi bila ya idhini ya Mmiliki wa kweli. Basi inakuwa dua hii na ibada hii ni upotofu katika akili na batili katika Sheria. Bali, mshirikina huyo anajiwa na kinyume cha yale aliyotaka na aliyokusudiwa. Kwa sababu alikuwa anakusudia kunufaika nayo, lakini Mwenyezi Mungu akabainisha ubatili wake na kutokuwepo kwake, na hata akabainisha katika Aya zingine madhara yake kwa wanaowaabudu, na kwamba Siku ya Kiyama wao kwa wao watakufuriana na kulaaniana, na makaazi yao ni Motoni, na ambao watu watakapokusanywa, watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao. Inastaajabisha kwamba mshirikina anatakabari kuwafuata Mitume akidai kuwa wao ni wanadamu, na anaridhia kuabudu na kuomba dua miti na mawe. Alitakabari kumkusudia Mfalme, Mwingi wa rehema, Mlipaji, na akaridhia kuwaabudu wale ambao madhara yao yako karibu zaidi kuliko manufaa yake, kutokana na kumtii adui yake mkubwa zaidi, ambaye ni Shetani! Na kauli yake, "Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: "Mola wenu Mlezi amesema nini?" Watasema: "Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa." Inawezekana kwamba wanaokusudiwa hapa ni washirikina; Kwa sababu hao ndio waliotajwa katika matamshi ya wazi ya aya hii. Na kanuni inasema kwamba kivumishi kinarudia yale yaliyo karibu zaidi nacho, kwa hivyo, maana yake inakuwa ni: Siku ya Kiyama itakapofika na hofu ikaondolewa katika nyoyo za washirikina, na wakaulizwa akili zao zilipowarudia kuhusu hali yao ya hapa duniani na kukadhibisha kwao haki waliyoileta Mitume, watakiri kuwa waliyokuwa wakifanya ya ukafiri na ushirikina ni batili, na kwamba aliyoyasema Mwenyezi Mungu na kuambiwa na Mitume wake ndiyo haki, basi yakawadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha zamani, na wakajua kwamba haki ni ya Mwenyezi Mungu, na waliungama dhambi zao. "Na Yeye ndiye Aliye juu" kwa dhati yake, juu ya viumbe vyote, na kwa kuwashinda, na kwa hadhi yake ya juu kwa sababu ya sifa zake kuu, tukufu zaidi; "Mkubwa" katika dhati yake na sifa zake. Na katika ujuu wake ni kwamba hukumu yake ndiyo yenye kushinda, na nafsi zinanyenyekea kwake kwa ajili yake, hata nafsi za wenye kutakabari na washirikina. Na maana hii ndiyo dhahiri zaidi, nayo ndiyo inayoashiriwa na muktadha huu. Na inawezekana kwamba kilichokusudiwa katika kivumishi kilichotumika ni Malaika, na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anapozungumza kwa ufunuo; Malaika wanamsikia na wanamuangukia chini Mwenyezi Mungu na kumsujudia. Kisha Jibril anakuwa ndiye wa kwanza kuinua kichwa chake, na Mwenyezi Mungu anazungumza naye kutokana na ufunuo wake atakavyo. Kisha kuzimika huko kunapoondoka katika nyoyo za Malaika na hofu pia ikaisha, wanaulizana wao kwa wao juu ya kauli hiyo ambayo kwayo walizimika: 'Amesema nini Mola wenu Mlezi?' Basi huambiana wao kwa wao: 'Amesema kweli', ima kwa ujumla; kwa kuwa wanajua kwamba yeye hasemi isipokuwa kweli tu, au wanasema: 'Amesema hivi na hivi,' wakitaja maneno waliyoyasikia kutoka kwake, na kwamba ni kweli. Basi inakuwa maana kulingana na hivi ni kwamba, washirikina walioabudu pamoja na Mwenyezi Mungu miungu hao ambao tumekuelezeeni upungufu wao, na kutoweza kwao kunufaisha kwa njia yoyote ile, namna walivyogeuka na wakaacha kumkusudia Mola Mlezi, Mkuu, aliye juu, Mkubwa, ambaye katika utukufu wake na ukuu wake ni kwamba Malaika watukufu walio karibu sana naye katika viumbe vyote wananyenyekea namna hii na kuzimika wanaposikia maneno yake, na wote wanakiri kwamba Mwenyezi Mungu hasemi isipokuwa kweli tu. Basi wana nini washirikina hawa waliotakabari kumuabudu yule ambaye hadhi yake ni hii, na ukubwa wa ufalme wake na mamlaka yake? Basi Mwenyezi Mungu yuko juu sana, na ni Mkubwa sana mbali na ushirikina wa washirikina, na uzushi wao na uwongo wao.
: 24 - 27 #
{قُلْ مَنْ يَرْزُقُكُمْ مِنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّهُ وَإِنَّا أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَى هُدًى أَوْ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (24) قُلْ لَا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ (25) قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَهُوَ الْفَتَّاحُ الْعَلِيمُ (26) قُلْ أَرُونِيَ الَّذِينَ أَلْحَقْتُمْ بِهِ شُرَكَاءَ كَلَّا بَلْ هُوَ اللَّهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (27)}.
24. Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi. 25. Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi. 26. Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu, Mwenye kujua vyema. 27. Sema: Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{24} يأمر تعالى نبيَّه محمداً - صلى الله عليه وسلم - أن يقولَ لمن أشركَ بالله ويسألَه عن صحةِ شركِهِ: {من يَرْزُقُكم من السمواتِ والأرضِ}: فإنَّهم لا بدَّ أن يُقرُّوا أنَّه الله، ولئنْ لم يقرُّوا؛ فَـ {قُلِ اللهُ}: فإنَّك لا تجد من يدفعُ هذا القول. فإذا تبيَّن أنَّ الله وحده الذي يرزقُكم من السماواتِ والأرضِ ويُنْزِلُ لكم المطر ويُنْبِتُ لكم النباتَ ويفجِّرُ لكم الأنهارَ ويُطْلِعُ لكم من ثمار الأشجار وجعل لكم الحيواناتِ جميعَها لنفعِكُم ورزقِكُم؛ فلِمَ تعبدون معه من لا يرزُقُكم شيئاً ولا يفيدكم نفعاً؟! وقوله: {وإنا أو إيَّاكم لعلى هدىً أو في ضلال مبينٍ}؛ أي: إحدى الطائفتين منَّا ومنكم على الهدى مستعليةٌ عليه، أو في ضلال بيِّنٍ منغمرةٌ فيه. وهذا الكلام يقولُه من تبيَّن له الحقُّ واتَّضح له الصوابُ وجَزَمَ بالحقِّ الذي هو عليه وبطلانِ ما عليه خصمُه؛ أي: قد شرحنا من الأدلَّة الواضحة عندنا وعندكم ما به يُعْلَم علماً يقينيًّا لا شكَّ فيه مَن المحقُّ منا ومَن المبطلُ ومَن المهتدي ومن الضالُّ، حتى إنَّه يصير التعيينُ بعد ذلك لا فائدة فيه؛ فإنَّك إذا وازنتَ بين من يدعو إلى عبادة الخالقِ لسائر المخلوقات، المتصرِّفِ فيها بجميع أنواع التصرُّفات، المسدي جميع النعم، الذي رزقهم وأوصل إليهم كلَّ نعمة ودفع عنهم كلَّ نقمة، الذي له الحمدُ كلُّه والملكُ كلُّه وكلُّ أحدٍ من الملائكة فَمَنْ دونهم خاضعون لهيبته متذلِّلون لعظمته، وكلُّ الشفعاء تخافه، لا يشفعُ أحدٌ منهم عنده إلاَّ بإذنِهِ، العليُّ الكبيرُ في ذاتِهِ وأوصافِهِ وأفعالِهِ، الذي له كلُّ كمال وكلُّ جلال وكلُّ جمال وكلُّ حمد وثناء ومجدٍ، يدعو إلى التقرُّب لمن هذا شأنه، وإخلاص العمل له، وينهى عن عبادةِ مَنْ سواه، وبين من يتقرَّب إلى أوثان وأصنام وقبور لا تَخْلُقُ ولا ترزقُ ولا تملكُ لأنفسها ولا لِمَنْ عَبَدَها نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً، بل هي جماداتٌ لا تعقل ولا تسمع دعاء عابديها، ولو سمعتْه؛ ما استجابت لهم، ويوم القيامةِ يكفُرون بشِرْكِهم ويتبرؤون منهم ويتلاعنون بينهم، ليس لهم قِسْطٌ من الملك، ولا شركة فيه ولا إعانة فيه، ولا لهم شفاعةٌ يستقلُّون بها دون الله؛ فهو يدعو من هذا وصفُهُ، ويتقرَّبُ إليه مهما أمكَنَه، ويعادي مَنْ أخلصَ الدين لله ويحاربُهُ، ويكذِّبُ رسل الله الذين جاؤوا بالإخلاص لله وحده؛ تبيَّنَ لك أيُّ الفريقين: المهتدي من الضالِّ والشقيِّ من السعيد، ولم يحتج إلى أن يعينَ لك ذلك؛ لأنَّ وصف الحال أوضح من لسان المقال.
{24} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwamrisha Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kumwambia anayemshirikisha Mwenyezi Mungu na kumuuliza juu ya usahihi wa ushirikina wake: "Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi?" Kwani lazima wakiri kwamba huyo ni Mwenyezi Mungu, na ikiwa hawatakiri; basi "Sema: Ni Mwenyezi Mungu!" Hutapata wa kukanusha kauli hii. Basi ikidhihirika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini, na anawateremshia mvua, na anawaoteshia mimea, na anawapitishia mito, na anawaletea matunda ya miti, na amewaumbia wanyama wote kwa manufaa yenu na riziki zenu; basi kwa nini mnamuabudu pamoja naye yule ambaye hawapei chochote na wala hawanufaishi kwa chochote? Na kauli yake, "Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi." Yaani, moja katika makundi mawili haya, miongoni mwetu na miongoni mwenu, liko kwenye uwongofu na kuwa juu yake, au liko katika upotofu ulio wazi tayari limezama humo. Maneno haya yanasemwa na yule ambaye ukweli umemdhihirikia na usawa umemuwia wazi, na ambaye ana yakini juu ya haki aliyo juu yake na ubatili wa kile ambacho mpinzani wake yuko juu yake. Yaani, tumeeleza ushahidi mbalimbali ulio wazi kwetu na kwenu ambao kwa huo inajulikana kwa elimu ya yakini, isiyo na shaka yoyote ni nani miongoni mwetu aliye kwenye haki na ni nani aliye kwenye batili, na ni nani aliyeongoka na ni nani aliyepotea, kiasi kwamba kuashiria mmoja wetu katika hayo hakuna faida yoyote baada ya hilo. Kwani ukilinganisha baina ya yule anayelingania kumuabudu Muumba wa viumbe vyote, ambaye anaviendesha katika njia za kila aina, mpaji wa neema zote, ambaye aliwaruzuku na kuwafikishia kila aina ya neema na akawaepusha kila adhabu, ambaye sifa zote njema ni zake, na ufalme wote ni wake, na vitu vyote kuanzia Malaika na vyote vilivyo chini yao vinaunyenyekea ukubwa wake na kudhalilikia ukuu wake, na waombezi wote wanamuogopea. Na hakuna anayefanya uombezi miongoni mwao kwake isipokuwa kwa idhini yake yeye aliye juu, Mkubwa katika dhati yake, sifa zake, na vitendo vyake, ambaye ni mwenye ukamilifu wote, utukufu wote, uzuri wote, sifa zote na kuhimidiwa na heshima. Anayelingania kumkaribia yule ambaye hadhi yake ni hii na kumkusudia yeye tu katika matendo, na akataza kuabudu asiyekuwa Yeye, ikilinganishwa na anayekurubisha na vinavyoabudiwa visivyo Mwenyezi Mungu, na masanamu, na makaburi, ambavyo haviumbi wala haviruzuku, wala havijimilikii vyenyewe wala wale wanaoviabudu manufaa wala madhara, wala kifo, wala uhai wala ufufuo. Bali hivyo ni vitu visivyo na uhai ambavyo haviwezi kutumia akili wala havisikii maombi ya wale wanavyoviabudu, na hata kama vingewasikia, basi havingewaitikia. Na Siku ya Kiyama watakufuriana wao kwa wao na watajitenga mbali nao, na watalaaniana, na hata hawana fungu lolote katika ufalme wala ushirika ndani yake, wala kumsaidia Mwenyezi Mungu, na wala hawana uombezi ambao wamejitegemea katika kuufanya isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi huyu mshirikina anamuomba yule ambaye hii ndiyo sifa yake, na anajikurubisha kwake bila kujali ni kiasi gani anaweza, na anamfanyia uadui mwenye kumkusudia Mwenyezi Mungu tu katika dini yake na anampiga vita, na anawakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu waliokuja kwa mafundisho ya kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake. Basi kwa haya itakubainikia ni lipi katika makundi mawili haya lililoongoka na ni lipi potovu, na aliye mashakani na mwenye furaha, na hata hakuna haja ya kuonyeshwa ni nani hasa. Kwa sababu maelezo ya hali tu yako wazi zaidi kuliko kusema kwa maneno.
#
{25} {قل} لهم: {لا تُسْألونَ عمَّا أجْرَمْنا ولا نسألُ عما تَعْمَلونَ}؛ أي: كلٌّ منَّا ومنكم له عمله، أنتم لا تُسألون عن إجرامِنا وذنوبِنا لو أذْنَبْنا، ونحنُ لا نُسألُ عن أعمالكم؛ فليكن المقصودُ منَّا ومنكم طَلَبَ الحقائق وسلوكَ طريق الإنصاف، ودَعوا ما كُنَّا نعملُ، ولا يكنْ مانعاً لكم من اتِّباع الحقِّ؛ فإنَّ أحكام الدُّنيا تجري على الظواهر، ويُتَّبَعُ فيها الحقُّ ويُجْتَنَبُ الباطلُ، وأما الأعمال؛ فلها دارٌ أخرى يَحْكُمُ فيها أحكمُ الحاكمين، ويفصِلُ بين المختصمين أعدلُ العادلين.
{25} "Sema" ukiwaambia: "Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi." Yaani, kila mmoja wetu ana matendo yake. Hamtaulizwa juu ya makosa yetu na dhambi zetu ikiwa tutatenda dhambi, nasi hatutaulizwa juu ya matendo yenu. Basi na liwe lengo letu na lenu ni kutafuta ukweli na kufuata njia ya usawa, na tuache yale tuliyokuwa tukiyafanya, wala hicho kisiwe kizuizi cha kuwafanya msifuate haki. Kwani hukumu za dunia zinakwenda kwa sura ya nje, na ukweli ndio unaofuatwa, na uwongo unaepukwa. Ama matendo hayo yana nyumba nyingine ambayo atahukumu huko Mbora wa wanaohukumu na kutenganisha kati ya mahasimu, yule ambaye ni Mwadilifu wa waadilifu wote.
#
{26} ولهذا قال: {قل يَجْمَعُ بينَنا ربُّنا ثم يفتحُ بينَنا}؛ أي: يحكم بينَنا حكماً يتبيَّن به الصادقُ من الكاذب، والمستحقُّ للثواب من المستحقِّ للعقاب وهو خير الفاتحين.
{26} Ndiyo maana akasema: "Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki." Nayo itakuwa hukumu ambayo kwayo atabainika mkweli na mwongo, na anayestahiki malipo mazuri na anayestahiki adhabu, naye ndiye mbora wa wanaohukumu.
#
{27} {قل}: لهم يا أيها الرسولُ، ومَنْ ناب منابك: {أروني الذين ألحقتم به شركاءَ}؛ أي: أين هم؟ وأين السبيل إلى معرفتهم؟ وهل هم في الأرض أم في السماء؟ فإنَّ عالم الغيب والشهادة قد أخبرنا أنَّه ليس في الوجودِ له شريكٌ: {ويعبُدونَ من دون الله ما لا يضرُّهم ولا يَنْفَعُهم ويقولون هؤلاءِ شفعاؤُنا عند اللهِ قل أتنبِّئونَ الله بما لا يعلمُ ... } [الآية]، {وما يتَّبِعُ الذين يدعونَ من دون الله شركاءَ؟ إنْ يتَّبِعونَ إلاَّ الظَّنَّ وإنْ هم إلاَّ يَخْرُصونَ}، وكذلك خواصُّ خلقِهِ من الأنبياء والمرسلين لا يعلَمون له شريكاً؛ فيا أيُّها المشركون! أروني الذين ألحقتم بزعمكم الباطل بالله شركاء! وهذا السؤال لا يمكنهم الإجابةُ عنه، ولهذا قال: {كلا}؛ أي: ليس للَّه شريكٌ ولا ندٌّ ولا ضدٌّ، {بل هو اللهُ}: الذي لا يستحقُّ التألُّه والتعبُّد إلاَّ هو {العزيزُ}: الذي قهر كلَّ شيء؛ فكلُّ ما سواه فهو مقهورٌ مسخَّر مدبَّر. {الحكيمُ}: الذي أتقن ما خَلَقَه، وأحسنَ ما شَرَعَه، ولو لم يكنْ في حكمتِهِ في شرعِهِ إلاَّ أنَّه أمر بتوحيده وإخلاص الدين له، وأحبَّ ذلك وجعله طريقاً للنجاة، ونهى عن الشرك به واتِّخاذ الأندادِ من دونِهِ، وجَعَلَ ذلك طريقاً للشقاء والهلاك؛ لكفى بذلك برهاناً على كمال حكمتِهِ؛ فكيف وجميعُ ما أمر به ونهى عنه مشتملٌ على الحكمة؟!
{27} "Sema, ewe Mtume ukiwaambia wewe na wale watakaochukua nafasi yako. "Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika;" yaani, wako wapi? Na iko wapi njia ya kuwajua? Na Je, wako duniani au mbinguni? Kwani ameshatuambia Mjuzi wa ghaibu na yanayoshuhudiwa kuwa Yeye hana mshirika yeyote. "Nao badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: "Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!" Sema, "Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyoyajua..." hadi mwisho wa Aya. "Wala hawawafuati hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake. Wao hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo." Hali kadhalika wateule miongoni mwa viumbe wake, kama vile Manabii na Mitume, hawajui mshirika yeyote wake. Basi enyi washirikina, nionyesheni wale mliowaunganisha kwa madai yenu batili kuwa washirika wa Mwenyezi Mungu! Swali hili hawawezi kulijibu, na ndiyo maana akasema: "Hasha!" Yaani, Mwenyezi Mungu hana mshirika yeyote, wala mwenza, wala mpinzani, "bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu" ambaye hakuna anayestahiki kufanyiwa uungu wala kuabudiwa isipokuwa Yeye, "Mwenye nguvu" ambaye alishinda kila kitu; kila kitu kisichokuwa Yeye kimeshindwa naye, na kinatiishwa na kuendeshwa. "Mwenye hekima" ambaye aliumba sawasawa vyote alivyoumba, na akafanya kuwa mazuri yale aliyoweka kuwa sheria. Na hata kama haingekuwa katika hekima na sheria yake isipokuwa kwamba aliamrisha kuwa apwekeshwe na akusudiwe Yeye tu katika dini, na akayapenda hayo na akayafanya kuwa ndiyo njia ya wokovu, na akakataza kumshirikisha na kumfanyia wenza wengine badala yake, na akaifanya hiyo kuwa ndiyo njia ya kuwa mashakani na kuangamia, basi hilo lingetosha kuwa uthibitisho tosha wa ukamilifu wa hekima yake. Basi inakuwaje ilhali kila alichoamrisha na kukataza kinajumuisha hekima?
: 28 - 30 #
{وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (28) وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْوَعْدُ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (29) قُلْ لَكُمْ مِيعَادُ يَوْمٍ لَا تَسْتَأْخِرُونَ عَنْهُ سَاعَةً وَلَا تَسْتَقْدِمُونَ (30)}.
28. Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui. 29. Na wanasema: "Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?" 30. Sema: "Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia."
#
{28} يخبر تعالى أنَّه ما أرسل رسولَه - صلى الله عليه وسلم - إلا ليبشِّر جميع الناس بثواب الله، ويخبِرَهم بالأعمال الموجبة لذلك، وينذِرَهم عقاب الله، ويخبِرَهم بالأعمال الموجبة له؛ فليس لك من الأمر شيءٌ، وكلُّ ما اقْتَرَحَ عليك أهلُ التكذيب والعنادِ؛ فليس من وظيفتِكَ، إنَّما ذلك بيد الله تعالى. {ولكنَّ أكثرَ الناس لا يعلمونَ}؛ أي: ليس لهم علمٌ صحيحٌ، بل إمَّا جهالٌ أو معاندونَ لم يعملوا بعلمهم، فكأنَّهم لا علم لهم، ومن عدم علمِهِم جَعْلُهُم عدمَ الإجابة لما اقترحوه على الرسول موجباً لردِّ دعوته.
{28} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kuwa hakumtuma Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – isipokuwa kuwaletea habari njema watu wote kuhusu malipo ya Mwenyezi Mungu, na awajulishe matendo yanayosababisha hilo, na kuwaonya juu ya adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kuwafahamisha matendo yanayosababisha hilo. Nawe huna lako jambo katika suala hilo. Na kila kitu ambacho wale wanaokadhibisha, wakaidi wanakupendekezea sio katika kazi yako. Hilo liko mkononi mwa Mwenyezi Mungu. "Lakini watu wengi hawajui" kwa elimu sahihi. Bali ni wajinga au wakaidi ambao hawakufanyia kazi elimu yao, basi ni kana kwamba hawakuwa na elimu. Na katika yale yanayoonyesha kwamba hawajui ni kufanya kwao kule kutoitikiwa na Mtume juu ya yale waliyopendekeza, kuwa ndiyo sababu ya wao kuukataa wito wake.
#
{29} فممَّا اقترحوه استعجالُهم العذابَ الذي أنْذَرَهم به، فقال: {ويقولونَ متى هذا الوعدُ إن كنتُم صادقينَ}: وهذا ظلمٌ منهم؛ فأيُّ ملازمة بين صدقِهِ وبين الإخبار بوقت وقوعِهِ؟! وهل هذا إلاَّ ردٌّ للحقِّ وسفهٌ في العقل؟! أليس النذير في أمرٍ من أحوال الدُّنيا لو جاء قوماً يعلمون صدقَه ونُصحه ولهم عدوٌّ ينتهزُ الفرصة منهم ويعدُّ لهم، فقال لهم: تركتُ عدوَّكم قد سار يريد اجتِياحَكُم واستئصالَكم؛ فلو قال بعضُهم: إن كنتَ صادقاً؛ فأخبِرْنا بأيَّةِ ساعةٍ يصل إلينا؟ وأين مكانَه الآن؟ فهل يعدُّ هذا القائل عاقلاً أم يُحكم بسفهِهِ وجنونِهِ؟! هذا والمخبر يمكن صدقُهُ وكذبُهُ، والعدوُّ قد يبدو له غيرهم وقد تنحلُّ عزيمته، وهم قد يكون بهم مَنَعَةٌ يدافعون بها عن أنفسهم؛ فكيفَ بمن كذَّبَ أصدقَ الخلقِ المعصوم في خبره، الذي لا ينطِقُ عن الهوى بالعذاب اليقين، الذي لا مَدْفَعَ له ولا ناصر منه، أليس ردُّ خبرِهِ بحجَّة عدم بيان وقت وقوعِهِ من أسفه السفه؟!
{29} Miongoni mwa waliyopendekeza ni kwamba waharakishiwe adhabu aliyowahadharisha nayo. Akasema: "Na wanasema: Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?" Na hii ni dhuluma kutoka kwao. Je, kuna uhusiano gani kati ya ukweli wake na kujulisha kuhusu wakati wa kutokea kwake? Na Je, huku si chochote ila ni kukataa haki na upumbavu katika akili? Je, si kweli kwamba mwonyaji katika mambo ya kidunia ikiwa atawajia watu wanaojua ukweli wake na nasaha zake nzuri, nao wana adui anayetaka kupata fursa kutoka kwao na kujiandaa kwa ajili yao, na mtu huyo akawaambia, 'Nimemwacha adui yenu hali ya kuwa ameshatoka anakuja kuwavamia na kuwatokomeza.' Basi ikiwa baadhi yao watasema, 'Ikiwa wewe ni mkweli, basi tuambie atatufikia saa ngapi? Yuko wapi sasa? Je, huyo mzungumzaji atachukuliwa kuwa na akili timamu au atachukuliwa kwamba ni mpumbavu na kichaa? Huyu mtoa habari anaweza kuwa mkweli au mwongo, na adui anaweza kuonekana kwamba ni adui ya hawa watu lakini si hivyo, na dhamira yake inaweza kudhoofika, na wanaweza kuwa na kizuizi cha kujilinda kwacho. Basi vipi yule ambaye anamkadhibisha mkweli wa viumbe vyote, ambaye amehifadhiwa kusema katika yale anayojulisha, ambaye hasemi kwa matamanio yake kuhusu adhabu yenye yakini, ambayo haiwezi kuzuilika, wala msaidizi kutokana nayo? Je, si kweli kwamba mwenye kukataa habari yake kwa hoja ya kwamba hakusema adhabu hiyo itakuja lini ni katika wapambavu wa wapumbavu wote?
#
{30} {قل} لهم مخبراً بوقت وقوعِهِ الذي لا شكَّ فيه: {لكم ميعادُ يوم لا تستأخِرونَ عنه ساعةً ولا تَسْتَقْدِمونَ}: فاحْذَروا ذلك اليوم وأعدُّوا له عدَّتَه.
{30} "Sema" ukiwajulisha kuhusu wakati wa kutokea kwake ambao hapana shaka yoyote juu yake. "Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia." Basi itahadharini siku hiyo na mjiandae vyema kwa ajili yake.
: 31 - 33 #
{وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَنْ نُؤْمِنَ بِهَذَا الْقُرْآنِ وَلَا بِالَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلَوْ تَرَى إِذِ الظَّالِمُونَ مَوْقُوفُونَ عِنْدَ رَبِّهِمْ يَرْجِعُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ الْقَوْلَ يَقُولُ الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا لَوْلَا أَنْتُمْ لَكُنَّا مُؤْمِنِينَ (31) قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا أَنَحْنُ صَدَدْنَاكُمْ عَنِ الْهُدَى بَعْدَ إِذْ جَاءَكُمْ بَلْ كُنْتُمْ مُجْرِمِينَ (32) وَقَالَ الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا بَلْ مَكْرُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ إِذْ تَأْمُرُونَنَا أَنْ نَكْفُرَ بِاللَّهِ وَنَجْعَلَ لَهُ أَنْدَادًا وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ وَجَعَلْنَا الْأَغْلَالَ فِي أَعْنَاقِ الَّذِينَ كَفَرُوا هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (33)}.
31. Na walisema wale waliokufuru, "Hatutaiamini Qur-ani hii, wala yale yaliyokuwa kabla yake." Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, wakirudishiana maneno wao kwa wao! Wanyonge wakiwaambia wale waliotakabari, "Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi." 32. Na wale waliotakabari watawaambia wanyonge, "Kwani sisi ndio tuliwazuia na uwongofu baada ya huo kukujieni? Bali nyinyi wenyewe ni wahalifu." 33. Na wanyonge wakawaambia wale waliotakabari, "Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika." Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu. Na tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru. Kwani wanalipwa isipokuwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda?
#
{31} لما ذكر تعالى أنَّ ميعادَ المستعجلين بالعذابِ لابدَّ من وقوعه عند حلول أجله؛ ذكر هنا حالَهم في ذلك اليوم، وأنَّك لو رأيتَ حالَهم إذ وُقِفوا عند ربِّهم واجتمع الرؤساءُ والأتباعُ في الكفر والضَّلال؛ لرأيتَ أمراً عظيماً وهولاً جسيماً، ورأيت كيف يتراجع و {يرجِعُ بعضُهم إلى بعضٍ القولَ}، فيقول {الذين استُضْعِفوا}: وهم الأتباعُ، {للذين استَكْبَروا}: وهم القادةُ: {لولا أنتُم لَكُنَّا مؤمنينَ}: ولكنَّكُم حُلْتُم بيننا وبين الإيمان، وزيَّنْتُم لنا الكفرانَ ، فتبعناكم على ذلك، ومقصودُهم بذلك أن يكون العذابُ على الرؤساءِ دونهم.
{31} Mwenyezi Mungu alipotaja kwamba miadi ya wale wanaoharakisha adhabu lazima itokee wakati wake utakapowadia, akataja hapa hali yao siku hiyo, na kwamba lau ungeiona hali yao watakaposimama mbele ya Mola wao Mlezi, na viongozi na wafuasi katika ukafiri na upotofu wakakusanyika pamoja; basi ungeliona jambo kubwa na la kutisha, na ukaona jinsi watakavyogombana, na "wakirudishiana maneno wao kwa wao!" Wakasema, "Wanyonge" nao ndio wafuasi. "Wakiwaambia wale waliotakabari" nao ndio viongozi. "Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi," lakini mlizuia baina yetu na Imani, na mkatupambia ukafiri, basi tukakufuateni katika hayo. Na kusudio lao kwa kusema hivi ni kwamba waadhibiwe viongozi badala ya wao kuadhibiwa.
#
{32} {قال الذين استَكْبَروا للذين استضعفوا}: مستفهمينَ لهم ومخبرينَ أنَّ الجميع مشتركون في الجُرم: {أنحن صَدَدْناكم عن الهُدى بعد إذْ جاءَكُم}؛ أي: بقوَّتنا وقهرِنا لكم، {بل كنتُم مجرمينَ}؛ أي: مختارين للإجرام، لستُم مقهورين عليه، وإن كُنَّا قد زَيَّنَّا لكُم؛ فما كان لنا عليكم من سلطان.
{32} "Na wale waliotakabari watawaambia wanyonge" wakiwauliza na kuwajulisha kwamba wote walishiriki katika uhalifu huo. "Kwani sisi ndio tulikuzuieni na uwongofu baada ya huo kukujieni?" Yaani, kwa nguvu zetu na kuwatiisha kwa nguvu na kuwashinda, "bali nyinyi wenyewe ni wahalifu." Yaani, wenyewe tu mlichagua kufanya uhalifu wala hamkulazimishwa kuufanya, hata kama tuliwapambia uhalifu huo, lakini hatukuwa na mamlaka yoyote juu yenu.
#
{33} فقال {الذين استُضْعِفوا للذينَ استَكْبَروا بلْ مَكْرُ الليل والنهارِ إذْ تأمرونَنا أن نكفُرَ بالله ونجعلَ له أنداداً}؛ أي: بل الذي دهانا منكم ووصل إلينا من إضلالكم ما دبَّرْتُموه من المكر في الليل والنهار؛ إذْ تُحَسِّنون لنا الكفرَ وتدعوننا إليه، وتقولون: إنَّه الحقُّ، وتقدحون في الحقِّ، وتهجِّنونَه وتزعمونَ أنَّه الباطلُ؛ فما زال مكرُكُم بنا وكيدُكُم إيَّانا حتى أغْوَيْتُمونا وفَتَنْتُمونا. فلم تُفِدْ تلك المراجعةُ بينَهم شيئاً إلاَّ تبرِّي بعضِهم من بعضٍ والندامةَ العظيمةَ، ولهذا قال: {وأسرُّوا الندامةَ لما رأوا العذابَ}؛ أي: زال عنهم ذلك الاحتجاج الذي احتجَّ به بعضُهم لينجو من العذاب، وعلم أنَّه ظالمٌ مستحقٌّ له، فندم كلٌّ منهم غاية الندم، وتمنَّى أنْ لو كان على الحقِّ، وأنَّه ترك الباطل الذي أوصله إلى هذا العذاب، سرًّا في أنفسهم؛ لخوفهم من الفضيحة في إقرارهم على أنفسهم! وفي بعض مواقف القيامةِ وعند دخولِهِمُ النارَ يُظْهِرون ذلك الندمَ جهراً: {ويومَ يَعَضُّ الظالمُ على يَدَيْهِ يقولُ يا لَيْتَني اتَّخَذْتُ مع الرسول سَبيلاً. يا وَيْلَتى لَيْتَني لم أتَّخِذْ فُلاناً خليلاً ... } الآيات، {وقالوا لو كُنَّا نَسْمَعُ أو نَعْقِلُ ما كنَّا في أصحابِ السعير. فاعترفوا بذَنْبِهِم فَسُحْقاً لأصحاب السَّعيرِ}. {وجعلنا الأغلال في أعناق الذين كفروا}: يُغَلُّونَ كما يُغَلُّ المسجونُ الذي سيُهانُ في سجنه؛ كما قال تعالى: {إذِ الأغلالُ في أعناقِهِم والسلاسلُ يُسْحَبونَ في الحميم ثم في النارِ يُسْجَرونَ ... } الآيات. {هل يُجْزَوْنَ}: في هذا العذاب والنَّكال وتلك الأغلال الثقال {إلاَّ ما كانوا يَعْمَلونَ}: من الكفر والفسوق والعصيان.
{33} Kisha wakasema, "wanyonge wakawaambia wale waliotakabari, "bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika." Bali kilichotupata na kutufikia kutoka kwenu cha kutupotosha ni vitimbi mlivyotupangia usiku na mchana. Mlipotufanyia ukafiri kuwa mzuri na mkatuita kwa huo na mkasema, 'Hii ndiyo haki', na mkaitia dosari haki yenyewe, na mkaichanganya na mkadai kuwa ni batili. Basi mkaendelea kutufanyia njama na vitimbi mpaka mkatupoteza na kututia majaribuni. Lakini kugombana kwao huku hakukuwafaidi chochote isipokuwa kukataana wao kwa wao, na majuto makubwa. Na ndiyo maana akasema, "Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu." Yaani, ikaisha hoja hiyo waliyoitumia baadhi yao ili kuepuka adhabu, na wakajua kuwa wao ni madhalimu wanaoistahiki, hivyo kila mmoja wao akajuta majuto makubwa mno, na akatamani - kisiri katika nafsi yake mwenyewe, kwa sababu ya hofu ya kufedheheshwa ikiwa watakiri uhalifu huu juu ya nafsi zao - lau kuwa angelikuwa kwenye haki, na lau kuwa aliiacha batili ambayo ilimfikisha kwenye adhabu hii. Katika baadhi ya matukio ya Kiyama na watakapokuwa wanaingia Motoni, watadhihirisha majuto hayo waziwazi. "Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema, 'Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume!' Ee, ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki..." hadi mwisho wa Aya. "Na watasema: Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa na akili, tusingelikuwa katika watu wa Motoni! Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!" "Na tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru." Wakafungwa minyororo kama vile anavyofungwa mfungwa atakayefedheheshwa katika jela. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Zitakapokuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa. Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni..." hadi mwisho wa Aya. "Kwani wanalipwa" katika adhabu hii na mateso, na katika minyororo hii mizito, "isipokuwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda?" Ya kufuru, kuvuka mipaka na kuasi.
: 34 - 39 #
{وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِنْ نَذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُمْ بِهِ كَافِرُونَ (34) وَقَالُوا نَحْنُ أَكْثَرُ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ (35) قُلْ إِنَّ رَبِّي يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (36) وَمَا أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ بِالَّتِي تُقَرِّبُكُمْ عِنْدَنَا زُلْفَى إِلَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَئِكَ لَهُمْ جَزَاءُ الضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا وَهُمْ فِي الْغُرُفَاتِ آمِنُونَ (37) وَالَّذِينَ يَسْعَوْنَ فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ (38) قُلْ إِنَّ رَبِّي يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ وَمَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ (39)}.
34. Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji, isipokuwa walisema wale waliojidekeza kwa starehe zao, wa mji huo, "Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo." 35. Na wakasema, "Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa." 36. Sema, "Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui." 37. Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowasongesha karibu na sisi, muwe karibu sana, isipokuwa yule aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa yale waliyoyafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa. 38. Na wale wanaojitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu. 39. Sema: "Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakachokitoa, Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku."
#
{34} يخبر تعالى عن حالة الأمم الماضية المكذِّبة للرسل أنَّها كحال هؤلاء الحاضرين المكذِّبين لرسولهم محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -، وأنَّ الله إذا أرسل رسولاً في قريةٍ من القرى؛ كفر به مُتْرَفوها، وأبطرتْهم نعمتُهم، وفخروا بها.
{34} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kuhusu hali ya umma waliopita zamani, waliokadhibisha Mitume kwamba ni kama hali ya watu hawa waliopo sasa, wanaomkadhibisha Mtume wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na kwamba Mwenyezi Mungu anapotuma Mtume katika mji miongoni mwa mji, wana starehe yake wanamkadhibisha, wakajivuna kwa neema zao walizopewa na wakajifahirisha kwazo.
#
{35} {وقالوا نحنُ أكثرُ أموالاً وأولاداً}؛ أي: ممَّن اتَّبع الحقَّ، {وما نحن بمعذَّبينَ}؛ أي: أولاً لسنا بمبعوثينَ؛ فإنْ بُعِثْنا؛ فالذي أعطانا الأموال والأولاد في الدنيا؛ سَيُعْطينا أكثر من ذلك في الآخرة، ولا يعذِّبُنا.
{35} "Na wakasema, "Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto,' kuliko wale waliofuata haki. "Wala sisi hatutaadhibiwa." Yaani, kwanza, sisi hatutafufuliwa. Lakini ikiwa tutafufuliwa, basi yule aliyetupa mali hizi na watoto katika dunia, atatupa mengi zaidi ya hayo katika akhera na wala hatatuadhibu.
#
{36} فأجابهم اللهُ تعالى بأنَّ بَسْطَ الرزقِ وتضييقَه ليس دليلاً على ما زعمتُم؛ فإنَّ الرزق تحت مشيئةِ الله؛ إنْ شاءَ؛ بسطه لعبده، وإن شاء؛ ضيَّقَه.
{36} Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akawajibu kwamba kumkujulia mtu riziki na kumkunjia si ushahidi wa hayo mliyodai. Kwani, riziki iko chini ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu; akitaka, anamkunjulia mja wake, na akitaka, anamkunjia.
#
{37} وليست الأموال والأولاد {بالتي} تقرب إلى الله {زُلْفى}: وتُدني إليه، وإنَّما الذي يقرِّبُ منه زلفى الإيمان بما جاء به المرسلونَ والعملُ الصالح الذي هو من لوازم الإيمان؛ فإنَّ أولئك لهم الجزاء عند الله تعالى مضاعفاً الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائةِ ضعفٍ إلى أضعافٍ كثيرة لا يعلمُها إلاَّ الله. {وهم في الغُرُفاتِ آمنونَ}؛ أي: في المنازل العاليات المرتفعات جدًّا، ساكنين فيها مطمئنِّين، آمنون من المكدِّرات والمنغِّصات لما هم فيه من اللذَّات وأنواع المشتَهَياتِ، وآمنون من الخروج منها والحزن فيها.
{37} Na si mali na watoto "ndizo" humkurubisha mtu kwa Mwenyezi Mungu, "akawa karibu sana." Bali kinachomkurubisha zaidi ni kuamini yale yaliyoletwa na Mitume na matendo mema, ambayo ni miongoni mwa matakwa ya imani. Hao, wana malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuzidishiwa jema moja kwa mara kumi mfano wake hadi mara mia saba, hadi mizidisho mingi asiyoijua isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. "Nao watakuwa salama katika maghorofa," mbali na matatizo na masumbuko yenye kuharibu starehe na aina mbalimbali za matamanio wanazozipata, na watakuwa salama kutokana na kuziacha starehe hizi na kuwa na huzuni ndani yake.
#
{38} وأما الذين سعوا في آياتنا على وجه التعجيز لنا ولرسلنا والتكذيب؛ {أولئك في العذاب مُحْضَرونَ}.
{38} Na ama wale wanaojitahidi katika Ishara zetu kwa njia ya kutufanya sisi na Mitume wetu kwamba hatuna uwezo na wakitukadhibisha, "hao watahudhurishwa kwenye adhabu."
#
{39} ثم أعادَ تعالى أنه {يَبْسُطُ الرزقَ لِمَن يشاءُ مِنْ عبادِه ويَقْدِرُ له}: ويَقْدِرُ له ليرتِّبَ عليه قوله: {وما أنفَقْتُم من شيء}: نفقةً واجبةً أو مستحبَّةً على قريب أو جارٍ أو مسكينٍ أو يتيم أو غير ذلك، {فهو} تعالى {يُخْلِفُهُ}: فلا تتوهَّموا أنَّ الإنفاق مما يُنْقِصُ الرزق، بل وعد بالخلف للمنفق الذي يبسط الرزق لمن يشاءُ ويَقْدِرُ. {وهو خيرُ الرازقينَ}: فاطلُبوا الرزقَ منه، واسعَوْا في الأسبابِ التي أمَرَكم بها.
{39} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akarudia kusema: "humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake," ili iwe kwamba "chochote mtakachokitoa" cha matumizi ya faradhi au yale yanayopendekezwa kwa jamaa, jirani, masikini, yatima, au wengineyo. "Yeye" Mtukufu "atakilipa" na usidhani kuwa kutoa matumizi ni katika mambo yanayopunguza riziki. Bali mwenye kutoa mali aliahidiwa na yule ambaye humkunjulia riziki amtakaye na kumkunjia amtakaye. "Naye ni Mbora wa wanaoruzuku," basi tafuteni riziki kutoka kwake, na jitahidini kufanya sababu za riziki alizowamrisha.
: 40 - 42 #
{وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ (40) قَالُوا سُبْحَانَكَ أَنْتَ وَلِيُّنَا مِنْ دُونِهِمْ بَلْ كَانُوا يَعْبُدُونَ الْجِنَّ أَكْثَرُهُمْ بِهِمْ مُؤْمِنُونَ (41) فَالْيَوْمَ لَا يَمْلِكُ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّتِي كُنْتُمْ بِهَا تُكَذِّبُونَ (42)}.
40. Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika, "Je, hawa walikuwa wakikuabuduni?" 41. Waseme, "Subhanak (umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao." 42. Basi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe. Na tutawaambia wale waliodhulumu, "Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha."
#
{40 - 41} {ويوم يحشُرُهم جميعاً}؛ أي: العابدين لغير الله والمعبودين من دونه من الملائكةِ، {ثم يقولُ}: الله {للملائكةِ}: على وجه التوبيخ لِمَنْ عَبَدَهم: {أهؤلاء إيَّاكُم كانوا يعبدونَ}؟ فتبرؤوا من عبادتهم و {قالوا سبحانَكَ}؛ أي: تنزيهاً لك وتقديساً أنْ يكونَ لك شريكٌ أو ندٌّ، {أنت وَلِيُّنا من دونِهِم}: فنحن مفتقِرونَ إلى ولايتك، مضطرُّون إليها؛ فكيف ندعو غيرنا إلى عبادتنا؟ أم كيف نَصْلُحُ لأن نُتَّخَذَ من دونك أولياءَ وشركاءَ، ولكنْ هؤلاء المشركون {كانوا يَعْبُدون الجنَّ}؛ أي: الشياطين، يأمرونَهم بعبادتِنا أو عبادة غيرنا، فيطيعونَهم بذلك، وطاعتُهم هي عبادتُهم؛ لأنَّ العبادة الطاعة؛ كما قال تعالى مخاطباً لكلِّ من اتَّخذ معه آلهة: {ألم أعْهَدْ إليكُم يا بني آدم أنْ لا تَعْبُدوا الشيطانَ إنَّه لكم عدوٌّ مبينٌ. وأنِ أعْبُدوني هذا صراطٌ مستقيمٌ}. {أكْثَرُهم بهم مؤمنونَ}؛ أي: مصدِّقون للجنِّ منقادون لهم؛ لأنَّ الإيمانَ هو التصديقُ الموجِبُ للانقياد.
{40 - 41} "Na siku atakayowakusanya wote;" wale wanaomuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na wale waliokuwa wakiabudiwa kama vile Malaika "Kisha" Mwenyezi Mungu "atawaambia Malaika" kwa njia ya kuwakemea wale waliokuwa wakiwaabudu, "Je, hawa walikuwa wakikuabuduni?" Lakini, wao wakajitenga mbali na ibada yao hiyo na "Waseme, 'Subhanak (umetakasika)," kuwa na mshirika na mwenza. "Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao," Sisi wenyewe tunakuhitajia sana, basi vipi tutawaita wengine kutuabudu sisi? Lakini, wao wakajitenga mbali na ibada yao hiyo na "Waseme, 'Subhanak (umetakasika)" kuwa na mshirika na mwenza. "Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao" Sisi wenyewe tunakuhitajia sana, basi vipi tutawaita wengine kutuabudu sisi? Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo njia iliyonyooka," "wengi wao wakiwaamini hao" na kuwafuata majini. Kwa sababu imani ni kusadiki kunakomlazimu mtu kutii na kufuata.
#
{42} فلما تبرؤوا منهم؛ قال تعالى مخاطباً لهم: {فاليوم لا يملِكُ بعضُكُم لبعضٍ نفعاً ولا ضَرًّا}: تقطَّعت بينكم الأسبابُ، وانقطع بعضُكم من بعض، {ونقولُ للذين ظلموا}: بالكفر والمعاصي بعدما ندخِلُهُمُ النارَ: {ذوقوا عذابَ النارِ التي كنتُم بها تكذِّبون}: فاليوم عايَنْتُموها ودخَلْتُموها جزاءً لتكذيبكم وعقوبةً لما أحدثه ذلك التكذيبُ من عدم الهربِ من أسبابها.
{42} Walipojitenga mbali nao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia, "Basi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe." Kwani, mafungamani ya baina yenu yameshakatika, nanyi kwa nyinyi mkatengana. "Na tutawaambia wale waliodhulumu" kwa kukufuru na kuasi baada ya kuwaingiza Motoni, "Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha." Leo mmeuona na mkaingia humo kuwa ni malipo ya kukadhibisha kwenu na adhabu kwa sababu ya yale yaliyosababishwa na kukadhibisha huko ya kutokimbia sababu zake.
: 43 - 45 #
{وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَذَا إِلَّا رَجُلٌ يُرِيدُ أَنْ يَصُدَّكُمْ عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُكُمْ وَقَالُوا مَا هَذَا إِلَّا إِفْكٌ مُفْتَرًى وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ إِنْ هَذَا إِلَّا سِحْرٌ مُبِينٌ (43) وَمَا آتَيْنَاهُمْ مِنْ كُتُبٍ يَدْرُسُونَهَا وَمَا أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ قَبْلَكَ مِنْ نَذِيرٍ (44) وَكَذَّبَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَمَا بَلَغُوا مِعْشَارَ مَا آتَيْنَاهُمْ فَكَذَّبُوا رُسُلِي فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ (45)}.
43. Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wanasema: "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu." Na wakasema: "Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa." Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri." 44. Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia mwonyaji kabla yako wewe. 45. Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!
#
{43} يخبر تعالى عن حالةِ المشركين عندما تُتلى عليهم آياتُ اللَّه البيناتُ وحججُه الظاهراتُ وبراهينُه القاطعاتُ، الدالةُ على كل خير، الناهيةُ عن كلِّ شرٍّ، التي هي أعظمُ نعمةٍ جاءتهم ومنَّةٍ وصلتْ إليهم، الموجبة لمقابلتها بالإيمان والتصديق والانقياد والتسليم، أنَّهم يقابِلونَها بضدِّ ما ينبغي ويكذِّبونَ مَنْ جاءهم بها ويقولونَ: {ما هذا إلاَّ رجلٌ يريدُ أن يَصُدَّكُم عما كان يعبدُ آباؤُكم}؛ أي: هذا قصدُه حين يأمُرُكم بالإخلاص لله لتتركوا عوائدَ آبائِكُم الذين تعظِّمون وتمشون خلفَهم، فردُّوا الحقَّ بقول الضالِّين، ولم يوردوا برهاناً ولا شبهةً؛ فأيُّ شبهة إذا أمرتِ الرسلُ بعضَ الضالِّين باتِّباع الحقِّ فادَّعَوْا أنَّ إخوانهم الذين على طريقتهم لم يزالوا عليه؟! وهذه السفاهة وردُّ الحقِّ بأقوال الضالين إذا تأملتَ كلَّ حقٍّ رُدَّ؛ فإذا هذا مآلُه، لا يُرَدُّ إلاَّ بأقوال الضالِّين من المشركين والدَّهريين والفلاسفة والصابئين والملحدين في دين الله المارقين؛ فهم أسوةُ كلِّ من رَدَّ الحقَّ إلى يوم القيامةِ. ولمَّا احتجُّوا بفعل آبائِهِم وجعلوها دافعةً لما جاءت به الرسل؛ طعنوا بعد هذا بالحقِّ، {وقالوا ما هذا إلا إفكٌ مفترىً}؛ أي: كذبٌ افتراه هذا الرجلُ الذي جاء به، {وقال الذينَ كفروا للحقِّ لمَّا جاءهم إنْ هذا إلاَّ سحرٌ مبينٌ}؛ أي: سحرٌ ظاهرٌ بيِّنٌ لكلِّ أحدٍ؛ تكذيباً بالحقِّ وترويجاً على السفهاء.
{43} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya washirikina wanaposomewa Aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi, hoja zake zilizo dhahiri na ushahidi wake wa kukata, zinazoashiria kila heri na kukataza kila maovu, ambayo ndiyo neema kubwa zaidi iliyowajia, inayowahitaji kuitikia kwa kuiamini, kuisadiki, kuifuata, na kujisalimisha kwayo, kwamba wao huikabili kwa kuzuia yanayopasa kukubali, na kumkadhibisha yule aliyewaletea hayo. Na wanasema: "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu." Yaani, haya ndiyo makusudio yake anapowaamrisha kumkusudia Mwenyezi Mungu tu, ili muache mila za baba zenu ambao mnawapa taadhima na kutembea nyuma yao. Kwa hivyo, wakaikataa haki kwa sababu ya kauli ya wapotevu, wala hawakutoa ushahidi wowote wala cha kutia shaka. Je, ni shaka gani iliyoko wakati Mitume wanawaamrisha baadhi ya watu wapotofu kufuata haki, nao wakadai kwamba ndugu zao wanaofuata njia yao hawajaacha kuifuata? Huu ndio upumbavu hasa na kuikataa haki kwa sababu ya maneno ya wapotofu. Na ukiitafakari kila haki iliyokataliwa, utakuta kwamba mwisho wake ulikuwa hivi. Haiwezi kukataliwa isipokuwa kwa sababu ya kauli za washirikina wapotofu, wasiomuamini Mwenyezi Mungu, wanafalsafa, Masabii, wale wanaopindukia mipaka katika dini ya Mwenyezi Mungu, waliokengeuka. Hao ndio kiigizo cha kila anayeikadhibisha haki mpaka Siku ya Kiyama. Na walipochukua vitendo vya baba zao kuwa ndivyo hoja, na wakavifanya kuwa ndivyo vya kuyazuia yale ambayo Mitume waliyaleta, wakaitia haki dosari, "Na wakasema: 'Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa" na mwanamume huyu aliyekuja nayo. "Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: 'Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri" kwa kila mtu. Walisema hivi ili kuikadhibisha haki, na kuwachochea wajinga.
#
{44} ولمَّا بيَّن ما ردُّوا به الحقَّ، وأنَّها أقوالٌ دون مرتبة الشُّبهة، فضلاً أن تكون حجَّةً؛ ذكر أنَّهم وإنْ أراد أحدٌ أن يحتجَّ لهم؛ فإنَّهم لا مستند لهم ولا لهم شيءٌ يعتمدونَ عليه أصلاً، فقال: {وما آتَيْناهم من كتبٍ يدرسونَها}: حتى تكون عمدةً لهم، {وما أرسَلْنا إليهم قبلَكَ من نذيرٍ}: حتى يكونَ عندَهم من أقوالِهِ وأحوالِهِ ما يدفعون به ما جئتَهم به؛ فليس عندهم علمٌ ولا أثارَةٌ من علم.
{44} Na alipobainisha yale waliyoikataa haki kwa sababu yake, na kwamba hayo ni kauli ambazo hata haziwezi kumtia mtu shaka, mbali na kwamba zinaweza kufikia kiwango cha kuwa hoja, akasema kwamba ikiwa mtu atataka kuwasimamishia hoja, wao hawana chochote cha kukitegemea kabisa, "Wala hatukuwapa Vitabu wavisome" ili viwe msingi wao, "wala hatukuwatumia mwonyaji kabla yako wewe." Ili kutoka kwa maneno yake na hali zake waweze kupata cha kukanushia yale uliyowaletea. Basi hawana elimu yoyote wala alama ya elimu.
#
{45} ثم خوَّفَهم ما فَعَلَ بالأمم المكذبين قبلَهم، فقال: {وكَذَّبَ الذين من قبلِهِم وما بَلَغوا}؛ أي: ما بلغ هؤلاء المخاطَبون {معشارَ ما آتَيْناهم فكذَّبوا}؛ أي: الأمم الذين من قبلهم {رسلي فكيف كان نكيرِ}؛ أي: إنكاري عليهم وعقوبتي إيَّاهم، قد أَعْلَمَنَا ما فَعَلَ بهم من النَّكال، وأنَّ منهم من أغرقه، ومنهم من أهلكه بالريح العقيم وبالصيحة وبالرجفة وبالخسف بالأرض وبإرسال الحاصِبِ من السماء؛ فاحذَروا يا هؤلاءِ المكذِّبون أن تدوموا على التكذيبِ، فيأخُذَكُم كما أخَذَ مَنْ قبلَكم ويصيبُكم ما أصابَهم.
{45} Kisha akawahofisha kwa yale aliyowafanyia umma waliokadhibisha kabla yao, akasema, "Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikilia" hawa wanaoongeleshwa, "hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha;" yaani, umma wa kabla yao "Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!" Yaani, maonyo yangu na adhabu yangu kwao. Kwani alishatujulisha yale aliyowafanyia ya adhabu, na kwamba miongoni mwao wapo waliowagharikishwa, na wapo aliowaangamiza kwa upepo tasa, na kwa ukelele, na kwa tetemeko la ardhi, na kwa kudidimizwa katika ardhi, na kwa kutumwa tufani la kokoto kutoka mbinguni. Basi jihadharini, enyi mnaokadhibisha msije mkaendelea kukadhibisha hivyo akawaangamiza kama alivyowaangamiza wale waliokuwa kabla yenu, na mkapatwa na yale yaliyowapata.
: 46 - 50 #
{قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُمْ بِوَاحِدَةٍ أَنْ تَقُومُوا لِلَّهِ مَثْنَى وَفُرَادَى ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا مَا بِصَاحِبِكُمْ مِنْ جِنَّةٍ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ لَكُمْ بَيْنَ يَدَيْ عَذَابٍ شَدِيدٍ (46) قُلْ مَا سَأَلْتُكُمْ مِنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّهِ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ (47) قُلْ إِنَّ رَبِّي يَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَّامُ الْغُيُوبِ (48) قُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ (49) قُلْ إِنْ ضَلَلْتُ فَإِنَّمَا أَضِلُّ عَلَى نَفْسِي وَإِنِ اهْتَدَيْتُ فَبِمَا يُوحِي إِلَيَّ رَبِّي إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ (50)}.
46. Sema: "Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote isipokuwa ni mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali." 47. Sema: "Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu." 48. Sema: "Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema ya ghaibu." 49. Sema: "Kweli imefika, na batili haijitokezi, wala hairudi." 50. Sema: "Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kudhuru nafsi yangu mwenyewe. Na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, aliye karibu."
#
{46} أي: {قل}: يا أيُّها الرسولُ لهؤلاء المكذِّبين المعاندين المتصدِّين لردِّ الحقِّ وتكذيبِهِ والقدح بِمَنْ جاء به: {إنَّما أعِظُكم بواحدةٍ}؛ أي: بخصلةٍ واحدةٍ أشيرُ عليكم بها وأنصحُ لكم في سلوكها، وهي طريقٌ نَصَفٌ، لست أدعوكم بها إلى اتِّباع قولي ولا إلى ترك قولِكُم من دون موجبٍ لذلك، وهي: {أن تقوموا للهِ مثنى وفرادى}؛ أي: تنهضوا بهمَّةٍ ونشاطٍ وقصدٍ لاتِّباع الصواب وإخلاصٍ لله مجتمعين ومتباحِثين في ذلك ومتناظرين وفرادى، كلُّ واحدٍ يخاطِبُ نفسَه بذلك؛ فإذا قُمتم لله مثنى وفرادى؛ استعملتُم فِكْرَكُم وأجَلْتُموه وتدبَّرْتُم أحوال رسولِكُم: هل هو مجنونٌ فيه صفاتُ المجانين من كلامِهِ وهيئتِهِ وصفتِهِ؟ أم هو نبيٌّ صادقٌ منذرٌ لكم ما يضرُّكم مما أمامكم من العذاب الشديد؟ فلو قبلوا هذه الموعظةَ واستعملوها؛ لتبيَّن لهم أكثر من غيرهم أنَّ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - ليس بمجنونٍ؛ لأنَّ هيئاته ليست كهيئات المجانين في خنقهم واختلاجهم ونظرهم، بل هيئتُهُ أحسنُ الهيئات، وحركاتُهُ أجلُّ الحركات، وهو أكمل الخلق أدباً وسكينةً وتواضعاً ووقاراً، لا يكون إلاَّ لأرزن الرجال عقلاً. ثم إذا تأمَّلوا كلامَه الفصيحَ ولفظَه المليحَ وكلماتِهِ التي تملأ القلوب أمناً وإيماناً وتزكِّي النفوس وتطهِّرُ القلوب وتبعثُ على مكارم الأخلاق وتحثُّ على محاسن الشِّيَم وترهِّبُ عن مساوئ الأخلاق ورذائِلِها، إذا تكلَّم؛ رَمَقَتْهُ العيونُ هيبةً وإجلالاً وتعظيماً؛ فهل هذا يشبِهُ هَذَيان المجانين وعربَدَتَهم وكلامَهم الذي يشبِهُ أحوالَهم؟! فكلُّ من تدبَّر أحوالَه وقصده استعلام: هل هو رسولُ الله أم لا؟ سواء تفكَّر وحدَه أم معه غيرُهُ؛ جزم بأنه رسولُ الله حقًّا ونبيُّه صدقاً، خصوصاً المخاطبين، الذي هو صاحبُهم، يعرفون أول أمرِهِ وآخرَه.
{46} Yaani, "Sema: "Ewe Mtume ukiwaambia hawa wanaokadhibisha, wakaidi, wanaojitahidi kuikanusha haki na kumkashifu yule aliyeileta: "Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu." Na ninawaita kulifuata, ambalo ndiyo njia ya uadilifu wala siwaiti kufuata maneno yangu wala kuyaacha maneno yenu bila sababu ya kufanya hivyo. Na jambo hili ni "kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja," kwa dhamira ya kufuata yaliyo sawa na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, kwa pamoja, kwa kufanya utafiti na majadiliano, na pia kila mmoja akiwa peke yake, kisha kila mtu ajiongeleshe kuhusiana na hayo. Kwani, mkisimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wawili wawili na mmoja mmoja, mtaweza kutumia fikira zenu vizuri na kuitafakari hali ya Mtume wenu. Je, yeye ni mwendawazimu na ana sifa za wendawazimu katika anayosema na katika mwonekano wake na tabia zake? Au yeye ni Nabii mkweli, anayewaonya kutokana na yatakayowadhuru ya adhabu kali iliyo mbele yenu? Ikiwa wangeyakubali mawaidha haya na kuyatumia, basi ingewabainikia zaidi kuliko wengine kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – si kichaa. Kwa sababu mwonekano wake si kama mwonekano wa vichaa. Bali mwonekano wake ndio mwonekano bora zaidi, na harakati zake ndizo harakati nzuri zaidi, naye ndiye kiumbe mwenye tabia njema zaidi, mtulivu, mnyenyekevu, na mwenye heshima, mambo ambayo hayawi isipokuwa kwa mtu mwenye akili nzuri zaidi ya wote. Kisha, ikiwa wangetafakari mazungumzo yake yenye ufasaha mkubwa, matamshi yake mazuri, na maneno yake ambayo yanaijaza mioyo salama na imani, na yanatakasa nafsi, na yanasafisha mioyo, na yanachochea mtu kuwa na maadili mema, na yanahimiza mtu kuwa na heshima, na yanahofisha dhidi ya tabia mbaya na chafu. Na anapozungumza, macho yalimtazama kwa hofu, heshima na taadhima. Basi je, haya yanafanana na porojo za vichaa na maneno yao yanayofanana na hali zao? Basi kila anayetafakari hali yake na nia yake akiwa na nia ya kuuliza: Je, yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu au la? Sawa atafikiri peke yake au pamoja na mtu mwengine, basi atakuwa na yakini kwamba yeye ni Mtume wa kweli wa Mwenyezi Mungu, na Nabii wake wa kweli. Hasa, watu hawa wanaoongeleshwa, ambao yeye ni mwenzao na wanajua mwanzo na mwisho wa mambo yake.
#
{47} وثَمَّ مانعٌ للنفوس آخرُ عن اتِّباع الداعي إلى الحقِّ، وهو أنه يأخذُ أموال مَن يستجيبُ له ويأخذُ أجرةً على دعوتِهِ، فبيَّن الله تعالى نزاهةَ رسوله عن هذا الأمر، فقال: {قل ما سألتُكُم من أجرٍ}؛ أي: على اتِّباعكم للحقِّ {فهو لكم}؛ أي: فأشهدكم أنَّ ذلك الأجر على التقدير أنَّه لكم. {إنْ أجرِيَ إلاَّ على الله وهو على كلِّ شيءٍ شهيدٌ}؛ أي: محيطٌ علمهُ بما أدعو إليه؛ فلو كنتُ كاذباً؛ لأخذني بعقوبته، وشهيدٌ أيضاً على أعمالِكم، سيحفظُها عليكم ثم يجازيكم بها.
{47} Na kuna kizuizi kingine kinachozuia nafsi kumfuata mlinganiaji kwenye haki, nacho ni kwamba anachukua mali za wale wanaomwitikia na anachukua ujira kwa sababu ya kuwalingania huko. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha kujitakasa kwa Mtume wake mbali na jambo hili, akasema: "Sema: Ujira niliokuombeni," juu ya kufuata kwenu haki "ni wenu nyinyi." "Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu." Yaani, elimu yake imekizunguka kile ninachokilingania. Kama ningekuwa mwongo, basi angenishika kwa adhabu yake. Naye pia ni shahidi juu ya matendo yenu. Atawahifadhia matendo hayo, kisha atawalipa juu yake.
#
{48} ولمَّا بيَّنَ البراهينَ الدالةَ على صحة الحقِّ وبطلان الباطل؛ أخبر تعالى أنَّ هذه سنَّتُه وعادته أن يَقْذِف بالحقِّ على الباطل فيدمَغَهُ فإذا هو زاهقٌ؛ لأنَّه بيَّن من الحقِّ في هذا الموضع وردَّ به أقوالَ المكذِّبين ما كان عبرةً للمعتبرين وآيةً للمتأملين؛ فإنَّك كما ترى كيف اضمحلَّتْ أقوالُ المكذِّبين، وتبيَّن كذِبُهم وعنادُهم، وظهر الحقُّ وسطع، وبطل الباطلُ وانقمعْ، وذلك بسبب بيان {عَلاَّم الغُيوبِ}، الذي يعلم ما تنطوي عليه القلوبُ من الوساوس والشُّبه، ويعلم ما يقابِلُ ذلك ويدفعُه من الحُجج، فيعلِّم بها عبادَه، ويبيِّنُها لهم.
{48} Alipobainisha ushahidi unaoonyesha usahihi wa haki na ubatili wa uongo, Yeye Mtukufu akajulisha kuwa hii ndiyo ada yake na destruri yake, kwamba huitupa haki juu ya batili; na haki hiyo ikaiharibu hiyo batili na kuiondoa. Kwa sababu aliibainisha haki mahali hapa, na akakanusha kwayo kauli za wakadhibishaji, jambo ambalo lilikuwa ni mazingatio kwa wanaozingatia, na ishara kwa wanaotafakari. Kwani, kama unavyoona yametoweka maneno ya wanaokadhibisha, na ukabainika uongo wao na ukaidi wao, nayo haki ikadhihiri na kung'aa, nayo batili ikabatilika na kukomeka kabisa, na hayo ni kwa sababu ya ubainisho wa "Mwenye kujua vyema ya ghaibu," ambaye anajua vilivyomo ndani ya nyoyo kama vile wasiwasi na fikira potofu. Na anajua hoja zinazokabiliana na hayo na kuyazuia. Basi anawafundisha waja wake na kuwabainishia hayo yote.
#
{49} ولهذا قال: {قل جاء الحقُّ}؛ أي: ظهر وبان وصار بمنزلة الشمس وظَهَرَ سلطانُه، {وما يُبدِئُ الباطل وما يعيدُ}؛ أي: اضمحلَّ وبطل أمرُه وذهب سلطانُه؛ فلا يُبدئ ولا يُعيدُ.
{49} Ndiyo maana akasema: "Sema:'Kweli imefika." Yaani, amedhihiri na kubainika mpaka ikawa kama jua, na mamlaka yake yakadhihirika, "na batili haijitokezi, wala hairudi."
#
{50} ولما تبيَّن الحقُّ بما دعا إليه الرسولُ، وكان المكذِّبونَ له يرمونَه بالضَّلال؛ أخبرهم بالحقِّ، ووضَّحه لهم وبيَّن لهم عَجْزَهُم عن مقاومتِهِ، وأخبرَهَم أنَّ رميَهم له بالضلال ليس بضائرٍ الحقَّ شيئاً ولا دافع ما جاء به، وأنَّه إنْ ضلَّ ـ وحاشاه من ذلك، لكن على سبيل التنزُّلِ في المجادلة ـ؛ فإنَّما يَضِلُّ على نفسِهِ؛ أي: ضلالُه قاصرٌ على نفسه، غيرُ متعدٍّ إلى غيرِهِ، {وإنِ اهتديتُ}: فليس ذلك من نفسي وحولي وقوَّتي، وإنَّما هدايتي بما {يوحي إليَّ ربي}: فهو مادة هدايتي؛ كما هو مادةُ هداية غيري؛ إنَّ ربِّي سميعٌ للأقوال والأصواتِ كلِّها، قريبٌ ممَّن دعاه وسأله وعَبَدَهُ.
50. Na haki ilipobainika kwa yale aliyolingania Mtume, na wale walioikadhibisha walikuwa wakiizulia kwamba ni upotofu, yeye akawajulisha haki hiyo na akawawekea wazi, na akawabainishia kutoweza kwao kuipinga. Na akawaambia kwamba kumtuhumu kwao kwamba ni mpotofu hakuidhuru haki kwa vyovyote vile wala kuzuia yale aliyokuja nayo. Na kwamba akipotoka - na hasha litokee hili, lakini ilikuwa tu ni njia ya kujiweka katika kiwango kimoja nao ili aweze kujadili nao - basi yeye mwenyewe tu ndiye anayepotea, na si mwengine. "Na ikiwa nimeongoka," basi si kutokana na nafsi yangu mwenyewe, na uwezo wangu na nguvu zangu. Lakini uwongofu wangu ni kwa sababu ya "kunifunulia Mola wangu Mlezi." Kwani Yeye ndiye kiini cha uwongofu wangu kama vile Yeye ndiye kiini cha uwongofu wa watu wengine. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusikia maneno na sauti zote, yuko karibu na mwenye kumuomba dua na kumuomba kitu na akamuabudu.
: 51 - 54 #
{وَلَوْ تَرَى إِذْ فَزِعُوا فَلَا فَوْتَ وَأُخِذُوا مِنْ مَكَانٍ قَرِيبٍ (51) وَقَالُوا آمَنَّا بِهِ وَأَنَّى لَهُمُ التَّنَاوُشُ مِنْ مَكَانٍ بَعِيدٍ (52) وَقَدْ كَفَرُوا بِهِ مِنْ قَبْلُ وَيَقْذِفُونَ بِالْغَيْبِ مِنْ مَكَانٍ بَعِيدٍ (53) وَحِيلَ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مَا يَشْتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشْيَاعِهِمْ مِنْ قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا فِي شَكٍّ مُرِيبٍ (54)}.
51. Na lau ungeliona watakapobabaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu. 52. Na watasema: "Tunaiamini!" Lakini wataipata wapi kutoka huko mahala mbali? 53. Na hapo kabla yake waliikataa, na wakiyatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali. 54. Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi.
#
{51} يقول تعالى: {ولو ترى}: أيُّها الرسولُ ومَنْ قام مقامَكَ حالَ هؤلاء المكذِّبين {إذْ فَزِعوا}: حين رأوا العذابَ وما أخبرتْهم به الرسلُ وما كذَّبوا به؛ لرأيتَ أمراً هائلاً ومنظراً مفظِعاً وحالةً منكرةً وشدَّةً شديدةً، وذلك حين يحقُّ عليهم العذابُ، وليس لهم عنه مهربٌ ولا فوتٌ، {وأخِذوا من مكانٍ قريبٍ}؛ أي: ليس بعيداً عن محلِّ العذاب، بل يُؤخَذون ثم يُقْذَفون في النار.
{51} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na lau ungeliona," ewe Mtume na yeyote atakayechukua nafasi yako, hali ya hawa waliokadhibisha "watakapobabaika" watakapoiona adhabu na yale ambayo Mitume waliwahadithia, na yale waliyoyakadhibisha, ungeliona manadhari makubwa, jambo la kuogofya, na hali ya kuchukiza, na dhiki kubwa mno. Na hapo ndipo itakapowawajibikia adhabu, na hawatakuwa na pa kukimbilia ili kuiepuka. "Na watakamatwa mahala pa karibu," ambapo si mbali na mahali pa adhabu. Bali watachukuliwa na kutupwa Motoni.
#
{52} {وقالوا}: في تلك الحال: آمنَّا باللهِ، وصدَّقْنا ما به كذَّبْنا، {و} لكنْ {أنَّى لهم التَّناوُشُ}؛ أي: تناولُ الإيمان، {من مكانٍ بعيدٍ}: قد حيل بينَهم وبينَه، وصار من الأمورِ المُحالة في هذه الحالة.
{52} "Na watasema" katika hali hiyo: tulimuamini Mwenyezi Mungu, na tukayasadiki yale tuliyoyakadhibisha. "Lakini wataipata wapi" imani hiyo "kutoka huko mahala mbali?" Kwani tayari imeshazuiliwa baina yao na suala la kuamini, na hilo likawa ni miongoni mwa mambo yasiyowezekana katika hali hii.
#
{53} فلو أنَّهم آمنوا وقتَ الإمكان؛ لكان إيمانُهم مقبولاً، ولكنَّهم {كفروا به من قبلُ ويَقْذِفُونَ}؛ أي: يرمون {بالغيبِ من مكانٍ بعيد}: بقذفهم الباطل لِيُدْحِضوا به الحقَّ، ولكن لا سبيل إلى ذلك؛ كما لا سبيل للرامي من مكانٍ بعيد إلى إصابةِ الغرضِ؛ فكذلك الباطلُ من المُحال أن يغلبَ الحقَّ أو يدفَعَه، وإنَّما يكون له صولةٌ وقتَ غفلةِ الحقِّ عنه، فإذا برزَ الحقُّ وقاوم الباطلَ؛ قمعه.
{53} Lau wangeamini ilipokuwa bado inawezekana, basi imani yao hiyo ingelikubaliwa. Lakini wao "hapo kabla yake waliikataa, na wakayatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali," walipokuwa wanatupa batili kwenye haki ili kuiangamiza, lakini hakuna njia yoyote ya kufanya hivyo sasa. Kama vile hakuna njia yoyote ya kutupa kitu kutokea mahali pa mbali na kugonga shabaha; basi vile vile haiwezekani kwa batili kuishinda haki au kuiondoa. Bali, batili huwa tu na nguvu wakati haki imeighafilikia. Lakini pindi haki inapodhihiri na kuipinga batili, inaitokomeza.
#
{54} {وحِيل بينَهم وبينَ ما يَشْتهونَ}: من الشهواتِ واللَّذَّاتِ والأولاد والأموال والخدم والجنودِ، قد انفردوا بأعمالِهِم، وجاؤوا فرادى كما خُلِقوا وتَركَوا ما خُوِّلوا وراءَ ظهورهم، {كما فعل بأشياعِهِم}: من الأمم السابقين حين جاءهم الهلاك حيل بينَهم وبينَ ما يشتهون. {إنَّهم كانوا في شكٍّ مريبٍ}؛ أي: مُحْدِث الرِّيبة وقلق القلب؛ فلذلك لم يؤمِنوا، ولم يعتَبوا حين استُعْتِبوا.
{54} "Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani" miongoni mwa starehe, watoto, mali, watumishi na majeshi. Watabakia peke yao na matendo yao, na wakaja kila mmoja peke yake kama walivyoumbwa, na wakaacha nyuma ya migongo yao yale waliyopewa, "kama walivyofanyiwa wenzao zamani" katika umma uliotangulia. Wakati walipojiwa na maangamizo, ilizuiliwa kati yao na yale waliyokuwa wanayatamani. "Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi." Na ndiyo maana hawakuamini, na wala hawakutubu walipotakiwa kutubu.
Imekamilika tafsiri ya Surat Sabaa. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na neema na fadhila. Tunaomba msaada kutoka kwake na kwake tunategemea, na tuna imani naye.