:
Tafsiri ya Surat Al-Ahzab
Tafsiri ya Surat Al-Ahzab
Iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwingi wa kurehemu.
: 1 - 3 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا (1) وَاتَّبِعْ مَا يُوحَى إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا (2) وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ وَكِيلًا (3)}
1. Ewe Nabii, mche Mwenyezi Mungu wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima. 2. Na fuata uliyofunuliwa kwa wahyi kutokana na Mola wako Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari ya mnayoyatenda. 3. Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
#
{1 - 2} أي: يا أيُّها الذي منَّ اللهُ عليه بالنبوَّة واختصَّه بوحيه وفضَّله على سائر الخلق! اشكُرْ نعمة ربِّك عليك باستعمال تَقْواه التي أنت أولى بها من غيرك، والذي يجب عليك منها أعظم من سواك؛ فامتثلْ أوامره ونواهِيَه، وبلِّغْ رسالاته، وأدِّ إلى عبادِهِ وَحْيَهُ، وابذُلِ النصيحةَ للخَلْق، ولا يَصُدَّنَّكَ عن هذا المقصود صادٌّ ولا يردُّك عنه رادٌّ، فلا تُطِع كلَّ كافرٍ قد أظهر العداوة لله ولرسوله ، ولا منافق قد استبطنَ التكذيبَ والكفرَ وأظهر ضدَّه؛ فهؤلاء هم الأعداء على الحقيقة؛ فلا تُطِعْهُم في بعض الأمور التي تنقُضُ التقوى وتناقِضُها، ولا تتَّبِعْ أهواءهم؛ يضلُّوك عن الصواب. {و} لكن {اتَّبِعْ ما يُوحى إليكَ من ربِّكَ}: فإنَّه هو الهدى والرحمة، وارجُ بذلك ثواب ربِّك؛ فإنه {بما تعملون خبيراً}: يجازيكم بحسب ما يَعْلَمُهُ منكم من الخير والشرِّ.
{1 - 2} Yaani, enyi ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha kwa unabii, na akamchagua kwa kumteremshia ufunuo wake na akamfadhilisha juu ya viumbe vingine vyote! Shukuru neema ya Mola wako Mlezi iliyo juu yako kwa kutumia uchamungu wake, ambao wewe unaustahiki zaidi kuliko wengine, na mambo ambayo ni wajibu kwako ndani yake ni mkubwa zaidi kuliko mwingine yeyote. Basi tekeleza maamrisho yake na makatazo yake, fikisha ujumbe wake, na waambie waja wake ufunuo wake, na wape viumbe wake nasaha sana, wala kisikuzuie na kusudio hilo kizuizi chochote wala kisikurudishe chochote chenye kurudisha. Kwa hivyo usimtii kafiri yeyote aliyedhihirisha uadui wake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala mnafiki aliyeficha ukadhibishaji na ukafiri na akadhihirisha kinyume chake. Hawa ndio maadui kwa uhakika. kwa hivyo usiwatii katika baadhi ya mambo yanayopingana na uchamungu, na wala usifuate matamanio yao, watakuja kukupoteza mbali na njia iliyo sahihi. "Na" lakini "fuata uliyofunuliwa kwa wahyi kutokana na Mola wako Mlezi," kwani hayo ndiyo uwongofu na rehema, na tarajia kwa hayo malipo ya Mola wako Mlezi. Kwani Yeye "anazo habari ya mnayoyatenda," na atawalipa kulingana na yale anayoyajua kwenu, ya heri na mabaya.
#
{3} فإنْ وقع في قلبِك أنَّك إن لم تُطِعْهم في أهوائهم المضلَّة؛ حصل عليك منهم ضررٌ، أو حصل نقصٌ في هداية الخلق؛ فادفَعْ ذلك عن نفسك، واستعملْ ما يقاوِمُه ويقاوِمُ غيره، وهو التوكُّل على الله؛ بأن تعتمدَ على ربِّك اعتماد مَنْ لا يملِكُ لنفسه ضرًّا ولا نفعاً ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً في سلامتك من شرِّهم وفي إقامة الدين الذي أمرتَ به، وثِقْ بالله في حُصول ذلك الأمر على أيِّ حال كان. {وكفى بالله وكيلاً}: تُوكلُ إليه الأمور، فيقوم بها وبما هو أصلحُ للعبد، وذلك لعلمِهِ بمصالح عبدِهِ من حيث لا يعلمُ العبدُ، وقدرتِهِ على إيصالها إليه من حيث لا يقدر عليها العبدُ، وأنَّه أرحم بعبده من نفسه ومن والديه وأرأفُ به من كلِّ أحدٍ، خصوصاً خواصَّ عبيده، الذين لم يزل يربِّيهم ببرِّه ويدرُّ عليهم بركاتِهِ الظاهرةَ والباطنةَ، خصوصاً وقد أمَرَهُ بإلقاء أموره إليه، ووعَدَه أن يقوم بها؛ فهناك لا تسأل عن كلِّ أمرٍ يتيسَّر، وصعب يتسهَّل ، وخطوبٍ تهون، وكروبٍ تزول، وأحوال وحوائج تُقضى، وبركاتٍ تنزل، ونِقَم تُدْفَع، وشرورٍ تُرفع. وهناك ترى العبد، الضعيفَ الذي فوَّضَ أمره لسيِّده قد قام بأمورٍ لا تقوم بها أمَّة من الناس، وقد سهَّل الله عليه ما كان يصعُبُ على فحول الرجال. وبالله المستعان.
{3} Na ikiingia moyoni mwako kuwa ikiwa hutawatii katika matamanio yao ya upotofu, yatakukuta madhara kutoka kwao, au kutakuwa na upungufu katika uwongofu wa viumbe, basi jilinde kutokana na hayo, na tumie yenye kuyazuilia ambayo ni kumtegemea Mwenyezi Mungu, kumtegemea kwa yule asiyeimilikia nafsi yake madhara, wala manufaa, wala kifo, wala uhai au ufufuo, ili uwe salama kutokana na maovu yao na katika kuisimamisha Dini uliyoamrishwa. Na kuwa na imani na Mwenyezi Mungu kwamba jambo hilo litatokea hata iweje. "Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa" wa kuachiwa mambo, kwa hivyo akayatekeleza na pia yale ambayo ni bora zaidi kwa mja, kwa sababu ya kujua kwake masilahi ya mja wake ambayo hata mja mwenyewe hayajui. Na anao uwezo wake kuyafikisha masilahi hayo kwake kwa namna ambayo mja mwenyewe hawezi, na kwamba Yeye ni mwingi wa rehema kwa mja wake hata kuliko mja mwenye anavyojirehemu, na wazazi wake, na mwenye huruma zaidi kwake kuliko kila mtu, hasa kwa waja wake maalumu, ambao hajaacha kuendelea kuwalea kwa wema wake na kuwapa baraka nyingi za dhahiri na zilizofichika, ikiongezewa kwamba alimuamrisha kumkabidhi mambo yake, na akamuahidi kuyasimamia. Hapo hata usiulize juu ya kila jambo ambalo litakuwa jepesi, na kila gumu litakalosahilishwa, na kila dhiki itakavyoondolewa, hali kila hali na mahitaji yatakavyotimizwa, na namna baraka zitakavyoshushwa, na namna adhabu zitakavyozuiliwa, na namna maovu yatakavyoondolewa. Hapo utamwona mja dhaifu aliyekabidhi mambo yake kwa bwana wake amefanya mambo ambayo hakuna hata umma wa watu unaweza kulifanya, kwani Mwenyezi Mungu alimfanyia sahali yale ambayo yalikuwa magumu kwa wanaume wenye nguvu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayetakwa msaada.
: 4 - 5 #
{مَا جَعَلَ اللَّهُ لِرَجُلٍ مِنْ قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ وَمَا جَعَلَ أَزْوَاجَكُمُ اللَّائِي تُظَاهِرُونَ مِنْهُنَّ أُمَّهَاتِكُمْ وَمَا جَعَلَ أَدْعِيَاءَكُمْ أَبْنَاءَكُمْ ذَلِكُمْ قَوْلُكُمْ بِأَفْوَاهِكُمْ وَاللَّهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِي السَّبِيلَ (4) ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ فَإِنْ لَمْ تَعْلَمُوا آبَاءَهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ وَمَوَالِيكُمْ وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُمْ بِهِ وَلَكِنْ مَا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا (5)}
4. Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli, naye ndiye anayeongoa Njia. 5. Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na rafiki zenu. Wala si lawama juu yenu kwa mlivyokosea. Lakini ipo lawama katika yale ziliyofanya nyoyo zenu kwa makusudi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
#
{4} يعاتِبُ تعالى عبادَه عن التكلُّم بما لا حقيقةَ له من الأقوال، ولم يجعلْه الله تعالى كما قالوا؛ فإنَّ ذلك القول منكم كذبٌ وزورٌ يترتَّب عليه منكراتٌ من الشرع، وهذه قاعدةٌ عامةٌ في التكلُّم في كلِّ شيء والإخبار بوقوع ووجود ما لَمْ يَجْعَلْه الله تعالى، ولكن خصَّ هذه الأشياء المذكورة لوقوعها وشدة الحاجة إلى بيانها، فقال: {ما جَعَلَ الله لرجل مِن قَلْبَيْنِ في جَوْفِهِ}: هذا لا يوجد؛ فإيَّاكم أن تقولوا عن أحدٍ: إنَّ له قلبينِ في جوفه، فتكونوا كاذبين على الخلقة الإلهية، {وما جعل أزواجَكم اللاَّئي تظاهِرون منهنَّ}: بأن يقولَ أحدكم لزوجتِهِ أنتِ عليَّ كظهر أمي أو كأمي؛ فما جعلهنَّ الله {أمَّهاتِكم}: أمُّك مَنْ وَلَدَتْكَ وصارتْ أعظم النساءِ عليك حرمةً وتحريماً، وزوجتُك أحلُّ النساء لك؛ فكيف تشبِّه أحد المتناقضين بالآخر؟! هذا أمرٌ لا يجوز؛ كما قال تعالى: {الذين يُظاهِرون منكم مِن نسائِهِم ما هنَّ أمَّهاتِهم إنْ أمهاتُهم إلا اللاَّئي وَلَدْنَهُمْ وإنَّهم ليقولون مُنكراً من القول وزوراً}. {وما جَعَلَ أدْعِياءَكم أبناءَكم}: والأدعياء: الولد الذي كان الرجل يدَّعيه وهو ليس له، أو يُدعى إليه بسبب تبنِّيه إيَّاه؛ كما كان الأمر في الجاهلية وأول الإسلام، فأراد الله تعالى أن يُبْطِلَه ويزيلَه، فقدَّم بين يدي ذلك بيانَ قُبحه، وأنَّه باطلٌ وكذبٌ، وكل باطلٍ وكذبٍ لا يوجد في شرع الله ولا يتَّصف به عبادُ الله، يقول تعالى: فالله لم يجعل الأدعياءَ الذين تَدَّعونَهم أو يُدعونَ إليكم أبناءكم؛ فإنَّ أبناءكم في الحقيقة مَنْ وَلَدْتُموهم وكانوا منكم، وأمَّا هؤلاء الأدعياء من غيركم؛ فلا جعل الله هذا كهذا، {ذلكم}: القول الذي تقولون في الدَّعِيِّ: إنَّه ابنُ فلان الذي ادَّعاه، أو والده فلان، {قولُكم بأفواهِكم}؛ أي: قولٌ لا حقيقةَ له ولا معنى له، {واللهُ يقولُ الحقَّ}؛ أي: اليقين والصدق؛ فلذلك أمركم باتِّباعه على قوله وشرعِهِ؛ فقولُه حقٌّ، وشرعُهُ حقٌّ، والأقوال والأفعال الباطلة لا تُنسب إليه بوجه من الوجوه، وليست من هدايته؛ لأنه لا يَهْدي إلاَّ إلى السبيل المستقيمة والطرق الصادقة، وإنْ كان ذلك واقعاً بمشيئتِهِ؛ فمشيئته عامَّةٌ لكلِّ ما وجد من خيرٍ وشرٍّ.
{4} Mwenyezi Mungu anawalaumu waja wake kwa kusema maneno ambayo hayana uhakika, na si Mwenyezi Mungu aliyeyafanya kuwa kama walivyosema. Kwani kauli yako hiyo ni uongo na uzushi na inasababisha mambo maovu katika Sheria. Hii ni kanunu ya jumla kuhusu kuzungumza juu ya kila kitu au kujulisha kuhusu kutokea na kupatikana kwa kitu ambacho Mwenyezi Mungu Mtukufu hakukifanya kuwa hivyo. Lakini ameyataja mambo haya yaliyotajwa hapa hasa kwa sababu ya haja kubwa iliyoko ya kuyabainisha. Kwa hivyo akasema, "Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake." Hili halipo. Basi jihadharini kusema kwamba: fulani anazo nyoyo mbili ndani ya mwili wake, mkawa mmedanganya kuhusu namna alivyoumba Mwenyezi Mungu. "Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu -" mmoja wenu anapowaambia mkewe: Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu kwangu, au ni kama mama yangu. Kwani, Mwenyezi Mungu hukuwafanya wao kuwa ni "mama zenu." Mama yako ni yule aliyekuzaa na akawa ndiye mwanamke haramu zaidi kwako, naye mkeo ndiye mwanamke halali zaidi kwako. Basi unalinganisha vipi kati ya vitu viwili vinavyopingana? Hili ni jambo lisiloruhusika, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Wale miongoni mwenu wanaowatenga wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa. Na hakika hao wanasema neno linalochusha, na la uwongo." "Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu hasa" kama ilivyokuwa katika zama za kabla ya Uislamu na mwanzo wa Uislamu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akataka kulifutilia mbali na kuliondoa. Kwa hivyo akatanguliza mbele yake kubainisha ubaya wake, na kwamba ni batili na uwongo. Na kila batili na uongo havipatikani katika sheria ya Mwenyezi Mungu na wala hawasifiki kwavyo waja wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Mwenyezi Mungu hakuwafanya watoto wenu wa kupanga ambao mnadai kuwa wana wenu au ambao wananasibishwa kwenu kuwa watoto wenu. Kwani watoto wenu kikahikika ni wale mliowazaa, na wakatokana na nyinyi wenyewe. Na ama hawa wa kupanga ambao si kutokana na nyinyi, basi Mwenyezi Mungu hakuwafanya hivi. "Hayo" msemayo kuhusiana na ana hawa wa kupanga kwamba: Yeye ni mtoto wa fulani aliyempanga, au baba yake ni fulani, "ni maneno ya vinywa vyenu tu" na haina uhakika wala maana sahihi. "Na Mwenyezi Mungu ndiye anayesema kweli." Na ndiyo maana akawaamuru kumfuata katika kauli zake na sheria zake. Kwa maana kauli yake ni haki, nasheria yake ni haki, na wala hayanasibishwi kwake maneno na matendo batili kwa njia yoyote ile, na si katika uwongofu wake. Kwa sababu Yeye haongoi isipokuwa kwenye njia iliyonyooka na njia za ukweli. Hata ingawa hilo litatokea kwa mapenzi yake, lakini mapenzi yake ni ya jumla kwa vitu vyote yalivyopo, sawa viwe ni vizuri au vibaya.
#
{5} ثم صرح لهم بترك الحالة الأولى المتضمِّنة للقول الباطل، فقال: {ادْعوهُم}؛ أي: الأدعياء {لآبائِهِم}: الذين ولدوهم {هو أقسطُ عند الله}؛ أي: أعدلُ وأقوم وأهدى، {فإن لم تَعلَموا آباءَهم}: الحقيقيين {فإخوانكم في الدين وَمَواليكُم}؛ أي: إخوتكم في دين الله ومواليكم في ذلك؛ فادْعوهم بالأخوة الإيمانيَّة الصادقة والموالاة على ذلك؛ فترك الدعوة إلى من تبنَّاهم حَتْمٌ لا يجوز فعلها، وأما دعاؤهم لآبائهم؛ فإنْ علموا؛ دعوا إليهم، وإن لم يعلموا؛ اقتُصِر على ما يُعْلَمُ منهم، وهو أخوة الدين والموالاة؛ فلا تظنُّوا أنَّ حالة عدم علمكم بآبائهم عذرٌ في دعوتهم إلى مَن تبنَّاهم؛ لأن المحذور لا يزول بذلك. {وليس عليكم جُناحٌ فيما أخطأتُم به}: بأنْ سَبَقَ على لسان أحدِكم دعوتُهُ إلى مَنْ تبنَّاه؛ فهذا غير مؤاخذٍ به، أو علم أبوه ظاهراً فدعوتُموه إليه، وهو في الباطن غير أبيه ؛ فليس عليكم في ذلك حَرَجٌ إذا كان خطأ. {ولكنْ} يؤاخِذُكُم بما تعمَّدَتْ قلوبُكُم من الكلام بما لا يجوزُ. {وكان الله غفوراً رحيماً}: غفر لكم ورحمكم؛ حيث لم يعاقِبْكم بما سَلَفَ، وسمح لكم بما أخطأتُم به، ورحِمَكُم؛ حيث بين لكم أحكامَه التي تُصْلِحُ دينَكم ودُنياكم؛ فله الحمد تعالى.
{5} Kisha akawaambia wazi wazi kuacha hali yao hiyo ya kwanza lililojumuisha maneno batili, akasema: "Waiteni" wana hawa wa kupanga "kwa baba zao" waliowazaa, "maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu" na la uwongofu zaidi. "Na ikiwa hamuwajui baba zao" wa kweli, "basi ni ndugu zenu katika Dini na marafiki zenu." Kwa hivyo hapo waiteni kwa udugu wa kiimani wa kweli na kusaidiana katika suala hili. Kwa hivyo kuwaita kwa majina ya wale waliowapanga ni suala ambalo haliruhusiwi kabisa kulifanya. Na ama kuwaita kwa baba zao ikiwa wanajulikana, hilo litahitajika liwe hivyo, lakini kama hawajulikanai, basi itatosheleza tu kuwaita kwa kile kinachojulikana kuhusiana nao, ambacho ni udugu wa kidini na kusaidiana. Na msifikirie kuwa kutojua baba zao ni kisingizio cha kuwaita kwa wale waliowapanga; Kwa sababu kilichokatazwa hakiwezi kuondolewa kwa kufanya hivyo. "Wala si lawama juu yenu kwa mlivyokosea" ikiwa mmoja wenu atamuita mwana wake wa kupanga kwa namna iliyokatazwa bila ya kukusudia. Au hata kama mnadhani kwamba fulani ndiye baba yake kwa nje, kwa hivyo mkamkaribisha naye, lakini kwa ndani yeye si baba yake hasa, basi hakuna kosa lolote juu yenu katika hilo kama mlikosea. "Lakini" atawachukulia makosa katika yale ziliyofanya nyoyo zenu kwa makusudi ambapo mlisema yale yasiyoruhusika. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Aliwasamehe na akakurehemuni. Kwa kuwa hakukuadhibuni kwa mliyokuwa mkiyatenda hapo awali, na akawaachilia mbali yale mliyofanya kwa kukosea, na akawarehemu ambapo aliwaelezea hukumu zake ambazo zinatengeneza dini yenu na dunia yenu; basi sifa njema zote ni zake Yeye Mtukufu.
: 6 #
{النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَى بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّهِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ إِلَّا أَنْ تَفْعَلُوا إِلَى أَوْلِيَائِكُمْ مَعْرُوفًا كَانَ ذَلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا (6)}.
6. Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni.
#
{6} يخبر تعالى المؤمنين خبراً يعرِفون به حالة الرسول - صلى الله عليه وسلم - ومرتَبَتَه، فيعامِلونه يمقتضى تلك الحالة، فقال: {النبيُّ أولى بالمؤمنين من أنفُسِهم}: أقرب ما للإنسان وأولى ما له نفسُه؛ فالرسولُ أولى به من نفسِهِ؛ لأنَّه عليه الصلاة والسلام بَذَلَ لهم من النُّصح والشفقة والرأفة ما كان به أرحم الخلق وأرأفهم؛ فرسولُ الله أعظمُ الخلق مِنَّةً عليهم من كلِّ أحدٍ؛ فإنَّه لم يصل إليهم مثقالُ ذرَّةٍ من الخير ولا اندفَعَ عنهم مثقالُ ذرَّةٍ من الشرِّ إلاَّ على يديه وبسببه؛ فلذلك وجب عليهم إذا تعارض مرادُ النفس أو مرادُ أحدٍ من الناس مع مرادِ الرسول أنْ يقدم مراد الرسول، وأنْ لا يعارِضَ قول الرسول بقول أحدٍ كائناً ما كان، وأنْ يَفْدوه بأنفسهم وأموالهم وأولادهم، ويقدِّموا محبَّته على محبة الخلقِ كلِّهم، وألاَّ يقولوا حتى يقولَ، ولا يتقدَّموا بين يديه، وهو - صلى الله عليه وسلم - أبٌ للمؤمنين؛ كما في قراءة بعضِ الصحابة يربِّيهم كما يربِّي الوالدُ أولاده، فترتَّب على هذه الأبوَّة أنْ كان نساؤه أمهاتِهِم؛ أي: في الحرمة والاحترام والإكرام، لا في الخلوة والمحرميَّة، وكأنَّ هذا مقدِّمة لما سيأتي في قصة زيد بن حارثة، الذي كان يُدْعى قبلُ زيد بن محمد، حتى أنزل الله: {ما كانَ محمدٌ أبا أحدٍ من رجالِكم}، فقطع نَسَبَه وانتسابَه منه. فأخبر في هذه الآية أنَّ المؤمنين كلَّهم أولادٌ للرسول؛ فلا مزيَّة لأحدٍ عن أحدٍ، وإن انقطعَ عن أحدِهم انتسابُ الدعوة؛ فإنَّ النسبَ الإيمانيَّ لم ينقطعْ عنه؛ فلا يحزنْ ولا يأسفْ، وترتَّب على أنَّ زوجات الرسول أمهاتُ المؤمنين: أنَّهنَّ لا يحللنَ لأحدٍ من بعده؛ كما سيصرّح بذلك، ولا يحلُّ لكم أن تَنْكِحوا أزواجَه من بعدِهِ أبدا. {وأولو الأرحام}؛ أي: الأقارب قَرُبوا أو بعدوا {بعضُهم أولى ببعضٍ في كتاب الله}؛ أي: في حكمه، فيرثُ بعضُهم بعضاً ويبرُّ بعضُهم بعضاً؛ فهم أولى من الحلف والنصرة، والأدعياءُ الذين كانوا من قبلُ يرثون بهذه الأسباب دون ذوي الأرحام، فقطع تعالى التوارُثَ بذلك، وجعله للأقارب لطفاً منه وحكمةً؛ فإنَّ الأمر لو استمرَّ على العادة السابقة؛ لحصل من الفساد والشرِّ والتحيُّل لحرمان الأقارب من الميراث شيءٌ كثيرٌ، {من المؤمنينَ والمهاجرينَ}؛ أي: سواء كان الأقاربُ مؤمنين مهاجرين أو غيرَ مهاجرين؛ فإنَّ ذوي الأرحام مقدَّمون في ذلك. وهذه الآية حجَّة على ولاية ذوي الأرحام في جميع الولايات؛ كولاية النكاح والمال وغير ذلك، {إلاَّ أن تَفْعَلوا إلى أوليائِكُم معروفاً}؛ أي: ليس لهم حقٌّ مفروضٌ، وإنَّما هو بإرادتِكم، إنْ شئتُم أن تتبرَّعوا لهم تبرُّعاً وتُعطوهم معروفاً منكم، {كان}: ذلك الحكم المذكور {في الكتابِ مسطوراً}؛ أي: قد سُطِرَ وكُتبَ وقدَّره الله؛ فلا بدَّ من نفوذه.
{6} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawajulisha Waumini habari ambazo kwazo watajua hali ya Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na daraja yake, ndiyo waamilaliane naye kulingana na inavyohitaji hadhi hiyo. Akasema, "Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao" kwa sababu yeye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aliwapa nasaha kwa wingi, huruma, upole, mambo ambayo kwayo alikuwa ndiye mwenye huruma na upole zaidi kuliko viumbe wote. Kwa hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu ndiye kiumbe mwenye neema kubwa zaidi juu yao kuliko viumbe vyote. Kwani haikuwafikia chembe ya heri, wala hawakuzuilika na uzito wa chembe ya shari isipokuwa kwa mikono yake na kwa sababu yake. Na ndiyo maana ni wajibu kwao ikiwa yatapingana matamanio ya nafsi zao au kitu anachotaka mtu miongoni mwa watu na anachotaka Mtume, kwamba akitangulize anachotaka Mtume. Na kwamba asiyapinge maneno ya Mtume kwa maneno ya mtu yeyote yule. Na kwamba wamfidie kwa nafsi zao, na mali zao, na watoto wao, na watangulize mapenzi yake mbele ya mapenzi ya viumbe vyote. Na wala wasiseme mpaka yeye aseme. Na wala wasimtangulie, kwa sababu yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni baba wa waumini. Kama ilivyo katika baadhi ya visoma vya baadhi ya Maswahaba: anawalea kama vile baba anavyowalea watoto wake. Kwa hivyo ubaba huu ukasababisha wake zake kuwa mama zao, katika uharamu, heshima, na kukirimu. Si katika kukaa faraghani nao, na kuwa maharimu. Na ni kana kwamba huu ni utangulizi wa yale yatakayokuja katika kisa cha Zaid bin Haritha, aliyekuwa akiitwa Zaid bin Muhammad, hapo kabla, mpaka Mwenyezi Mungu alipoteremsha, "Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu," basi akaacha kujinasibisha na nasaba yake. Hivyo akajulisha katika Aya hii kwamba waumini wote ni watoto wa Mtume, na hakuna ubora wowote kwa yeyote juu ya mwingine, hata kama mmoja wao hataitwa kwa akinasibishwa kwake kwa jina la mwana wa kupanga, basi nasaba yake ya kiimani kwake haikatiki; kwa hivyo asiwe na huzuni au majuto. Na itatokea katika hilo kwamba wake za Mtume ni mama wa Waumini, hawawi halali kwa yeyote kuwaoa baada yake, kama atakavyolisema hilo wazi wazi baadaye. "Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu," yaani katika hukumu yake. Watarithiana wao kwa wao, na kufanyiana wema wao kwa wao. Hao ndio wanaostahikiana zaidi hata kuliko wale waliowekeana kiapo cha kufungamana na kusaidiana, na wana wa kupanga ambao hapo kabla walikuwa wakirithi kwa sababu hizi badala ya jamaa za mtu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akakataza kurithiana kwa sababu hii, na akawafanya jamaa peke yao kurithiana kwa kuwafanyia upole na hekima yake. Kwani, ikiwa suala hili lingeendelea kama lilivyo kuwa, basi uharibifu mwingi ungetokea, na uovu na udanganyifu ili kuwanyima jamaa urithi "kuliko Waumini wengine na Wahamiaji." Yaani, haya ikiwa jamaa hao ni Waumini ambao ni wahajiri au wasiokuwa wahajiri; basi jamaa wanaotokana na tumbo moja la uzazi wanapewa kipaumbele katika suala hili. Aya hii ni ushahidi wa ulezi wa jamaa katika aina zote za ulezi, kama vile usimamizi juu ya ndoa, na mali na vitu vingine. "Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu;" yaani, hawana haki waliyowekewa, lakini hilo ni kwa kupenda kwenu tu, ikiwa mnataka kuwasaidia na kuwapa kwa njia ya kuwafanyia wema. "Haya" ya hukumu zilizotajwa "yamekwisha andikwa Kitabuni," na tayari yameshapitishwa na Mwenyezi Mungu, basi ni lazima yatatekelezeka.
: 7 - 8 #
{وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنْكَ وَمِنْ نُوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَأَخَذْنَا مِنْهُمْ مِيثَاقًا غَلِيظًا (7) لِيَسْأَلَ الصَّادِقِينَ عَنْ صِدْقِهِمْ وَأَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا أَلِيمًا (8)}
7. Na tulipochukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu. 8. Ili Mwenyezi Mungu awaulize wakweli juu ya ukweli wao. Na amewaandalia makafiri adhabu chungu.
#
{7 - 8} يخبر تعالى أنَّه أخذ من النبيِّين عموماً ومن أولي العزم - وهم هؤلاء الخمسة المذكورون خصوصاً - ميثاقَهم الغليظَ وعهدَهم الثقيل المؤكَّد على القيام بدين الله والجهادِ في سبيله، وأنَّ هذا سبيلٌ قد مشى عليه الأنبياءُ المتقدِّمون، حتى خُتموا بسيِّدهم وأفضلهم محمد - صلى الله عليه وسلم -، وأمر الناس بالاقتداء بهم، وسيسأل الله الأنبياء وأتباعهم عن هذا العهد الغليظ؛ هل وَفوا فيه وصدَقوا فيثيبهم جناتِ النعيم، أم كفروا فيعذِّبهم العذاب الأليم؟ قال تعالى: {من المؤمنينَ رجالٌ صَدَقوا ما عاهَدوا الله عليه}.
{7 - 8} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba alichukua kutoka kwa Manabii kwa ujumla na kutoka kwa wale wenye stahamala kubwa - ambao ni wale watano waliotajwa hasa - agano lao lenye nguvu na agano lao zito, lenye mkazo juu ya kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu na kupigana Jihadi katika njia yake. Sababu ni kwamba hii ni njia waliyoipitia Mitume waliotangulia, mpaka walipokamilishwa na bwana wao na mbora wao, Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na akawaamrisha watu kufuata mfano wao. Na Mwenyezi Mungu atawauliza manabii na wafuasi wao kuhusu agano hili zito. Je, walilitimiza na wakawa wakweli, ili awalipe mabustani yenye neema, au walikufuru, ili awaadhibu kwa adhabu iumizayo? Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu."
: 9 - 11 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَمْ تَرَوْهَا وَكَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا (9) إِذْ جَاءُوكُمْ مِنْ فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنْكُمْ وَإِذْ زَاغَتِ الْأَبْصَارُ وَبَلَغَتِ الْقُلُوبُ الْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِاللَّهِ الظُّنُونَا (10) هُنَالِكَ ابْتُلِيَ الْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا زِلْزَالًا شَدِيدًا (11)}
9. Enyi mlioamini, zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu. Pale yalipokufikieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyoaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda. 10. Walipowakujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipokodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbalimbali. 11. Hapo ndipo Waumini walipojaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali.
#
{9 - 11} يذكِّر تعالى عبادَه المؤمنين نعمته عليهم، ويحثُّهم على شكرها حين جاءتهم جنودُ أهل مكَّة والحجاز من فوقهم وأهل نجد من أسفلَ منهم، وتعاقَدوا وتعاهدوا على استئصال الرسول والصحابة، وذلك في وقعة الخندق، ومالأتهم طوائفُ اليهود الذين حوالي المدينة، فجاؤوا بجنودٍ عظيمةٍ وأمم كثيرة، وخندقَ رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - على المدينة، فحصروا المدينة، واشتدَّ الأمر، وبلغتِ القلوب الحناجرَ، حتى بلغ الظنُّ من كثير من الناس كلَّ مبلغ لما رأوا من الأسباب المستحكمة والشدائد الشديدة، فلم يزل الحصارُ على المدينة مدةً طويلة، والأمر كما وصف الله: {وإذْ زاغتِ الأبصارُ وبلغتِ القلوبُ الحناجرَ وتظنُّونَ بالله الظُّنونا}؛ أي: الظنون السيئة أنَّ الله لا ينصر دينَه ولا يتمُّ كلمته، {هنالك ابْتُلي المؤمنون}: بهذه الفتنة العظيمة، {وزُلْزِلوا زلزالاً شديداً}: بالخوف والقلق والجوع؛ ليتبيَّن إيمانهم ويزيد إيقانهم، فظهر ولله الحمد من إيمانهم وشدة يقينهم ما فاقوا فيه الأولين والآخرين. وعندما اشتدَّ الكربُ وتفاقمتِ الشدائدُ؛ صار إيمانُهم عين اليقين، {فلمَّا رأى المؤمنونَ الأحزابَ قالوا هذا ما وَعَدَنا اللهُ ورسولُه وصدق الله ورسوله وما زادَهُم إلاَّ إيماناً وتسليماً}.
{9 - 11} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakumbusha waja wake waumini kuhusu neema yake juu yao, na anawahimiza kushukuru kwa hilo. Walipowajia askari wa watu wa Makkah na Hijazi kutoka juu yao na watu wa Najd kutokea chini yao, na wakaafikiana na wakaahidi kumtokomeza Mtume na Maswahaba, na hayo yalikuwa katika Vita vya Handaki. Na pia makundi ya Mayahudi yaliyokuwa karibu na Madina yakawasaidia maadui katika hilo. Wakaja na askari wengi na watu wengi mno. Naye Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akachimba handaki kandoni mwa mji wa Madina. Kisha maadui wakaizingira Madina, na jambo hilo likazidi kuwa gumu, na nyoyo zikawafikia kooni, mpaka watu wengi wakadhania dhana mbaya mno walipokwa sababu ya yale waliyoyaona ya sababu zenye nguvu na dhiki kubwa mno. Kwa hivyo mzingiro huo juu ya Madina ukuendelea kwa muda mrefu, kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Walipowajia kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipokodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbalimbali." Yaani, dhana mbaya kwamba Mwenyezi Mungu hataiunga mkono Dini yake, wala hayatatimia maneno yake. "Hapo ndipo Waumini walipojaribiwa" kwa mtihani huu mkubwa "na wakatikiswa mtikiso mkali" kwa hofu, na wasiwasi, na njaa ili imani yao ibainike na yakini yao iongezeke. Basi ikadhihirika imani yao na yakini yao kubwa ambayo waliwashinda kwayo wa mwanzo na wa mwisho. Wakati dhiki ilipokuwa kali na ugumu ukazidi, imani yao ikawa ni imani ya jicho la yakini. "Na Waumini walipoyaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na utiifu."
Hapo ukadhihiri unafiki wa wanafiki, na yale waliyokuwa wakiyaficha yakadhihirika. Mwenyezi Mungu amesema:
: 12 #
{وَإِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ مَا وَعَدَنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ إِلَّا غُرُورًا (12)}
12. Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao: "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu."
#
{12} وهذه عادة المنافق عند الشدَّة والمحنة؛ لا يثبتُ إيمانه، وينظُر بعقله القاصر إلى الحالة الحاضرة ، ويصدِّق ظنَّه.
{12} Hii ni tabia ya mnafiki wakati wa dhiki na shida. Hathibitishi imani yake, na anaangalia kwa akili yake finyu katika hali ya sasa, na anaamini mashaka yake.
: 13 - 27 #
{وَإِذْ قَالَتْ طَائِفَةٌ مِنْهُمْ يَاأَهْلَ يَثْرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمْ فَارْجِعُوا وَيَسْتَأْذِنُ فَرِيقٌ مِنْهُمُ النَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوْرَةٌ وَمَا هِيَ بِعَوْرَةٍ إِنْ يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارًا (13) وَلَوْ دُخِلَتْ عَلَيْهِمْ مِنْ أَقْطَارِهَا ثُمَّ سُئِلُوا الْفِتْنَةَ لَآتَوْهَا وَمَا تَلَبَّثُوا بِهَا إِلَّا يَسِيرًا (14) وَلَقَدْ كَانُوا عَاهَدُوا اللَّهَ مِنْ قَبْلُ لَا يُوَلُّونَ الْأَدْبَارَ وَكَانَ عَهْدُ اللَّهِ مَسْئُولًا (15) قُلْ لَنْ يَنْفَعَكُمُ الْفِرَارُ إِنْ فَرَرْتُمْ مِنَ الْمَوْتِ أَوِ الْقَتْلِ وَإِذًا لَا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلًا (16) قُلْ مَنْ ذَا الَّذِي يَعْصِمُكُمْ مِنَ اللَّهِ إِنْ أَرَادَ بِكُمْ سُوءًا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ رَحْمَةً وَلَا يَجِدُونَ لَهُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا (17) قَدْ يَعْلَمُ اللَّهُ الْمُعَوِّقِينَ مِنْكُمْ وَالْقَائِلِينَ لِإِخْوَانِهِمْ هَلُمَّ إِلَيْنَا وَلَا يَأْتُونَ الْبَأْسَ إِلَّا قَلِيلًا (18) أَشِحَّةً عَلَيْكُمْ فَإِذَا جَاءَ الْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنْظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَالَّذِي يُغْشَى عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ فَإِذَا ذَهَبَ الْخَوْفُ سَلَقُوكُمْ بِأَلْسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى الْخَيْرِ أُولَئِكَ لَمْ يُؤْمِنُوا فَأَحْبَطَ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ وَكَانَ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرًا (19) يَحْسَبُونَ الْأَحْزَابَ لَمْ يَذْهَبُوا وَإِنْ يَأْتِ الْأَحْزَابُ يَوَدُّوا لَوْ أَنَّهُمْ بَادُونَ فِي الْأَعْرَابِ يَسْأَلُونَ عَنْ أَنْبَائِكُمْ وَلَوْ كَانُوا فِيكُمْ مَا قَاتَلُوا إِلَّا قَلِيلًا (20) لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيرًا (21) وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَذَا مَا وَعَدَنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا (22) مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا (23) لِيَجْزِيَ اللَّهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ إِنْ شَاءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا (24) وَرَدَّ اللَّهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا وَكَفَى اللَّهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ وَكَانَ اللَّهُ قَوِيًّا عَزِيزًا (25) وَأَنْزَلَ الَّذِينَ ظَاهَرُوهُمْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِنْ صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا (26) وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَمْ تَطَئُوهَا وَكَانَ اللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا (27)}].
13. Na kundi moja katika miongoni mwao liliposema: "Enyi watu wa Yathrib, hapana kukaa nyinyi! Rudini." Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Nabii kwa kusema: "Hakika nyumba zetu ni tupu." Wala hazikuwa tupu; hawakutaka isipokuwa kukimbia tu. 14. Na lau kuwa wangeliingiliwa kwa pande zote, kisha wakatakiwa kufanya hiana, wangelifanya, na wasingelisita isipokuwa kidogo tu. 15. Na hakika walikwishamuahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa. 16. Sema: Kukimbia hakuwafai kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuawa, na hata hivyo hamtastareheshwa isipokuwa kidogo tu. 17. Sema: Ni nani wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu pindi akiwatakia uovu, au akiwatakia rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu. 18. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua hao wanaozuilia, na wanaowaambia ndugu zao: "Njooni kwetu!" Wala hawaingii vitani isipokuwa kidogo tu. 19. Wana choyo juu yenu. Ikifika hofu, utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye alizimia kwa kukaribia mauti. Na hofu ikiondoka, wanawaudhi kwa ndimi kali, nao ni mabahili kwa kila la heri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amevibatilisha vitendo vyao. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 20. Wanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi, watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza habari zenu. Na lau wakiwa pamoja nanyi, hawapigani isipokuwa kidogo tu. 21. Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana. 22. Na Waumini walipoyaona makundi, walisema, "Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli." Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na utiifu. 23. Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha ahadi hata kidogo. 24. Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa sababu ya ukweli wao, na awaadhibu wanafiki pindi akitaka, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 25. Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata heri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza. 26. Na akawateremsha wale waliowasaidia maadui katika Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao, na akatia hofu katika nyoyo zao. Baadhi yao mkawa mnawaua, na wengine mnawateka. 27. Na akawarithisha ardhi zao na nyumba zao na mali zao, na ardhi msiyopata kuikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
#
{13} {وإذ قالت طائفةٌ}: من المنافقين بعد ما جزعوا وقلَّ صبرُهم صاروا أيضاً من المخذِّلين؛ فلا صبروا بأنفسهم، ولا تركوا الناس من شرِّهم، فقالت هذه الطائفة: {يا أهلَ يَثْرِبَ}: يريدون: يا أهل المدينة! فنادَوهْم باسم الوطن المنبئ عن التسمية فيه؛ إشارةً إلى أنَّ الدين والأخوة الإيمانيَّة ليس له في قلوبهم قدرٌ؛ وأنَّ الذي حملهم على ذلك مجردُ الخور الطبيعي. {يا أهلَ يثربَ لا مُقام لكم}؛ أي: في موضعكم الذي خرجتُم إليه خارج المدينة، وكانوا عسكروا دون الخندق وخارج المدينة، {فارجِعوا}: إلى المدينةِ. فهذه الطائفةُ تُخَذِّلُ عن الجهاد وتبيِّن أنَّهم لا قوة لهم بقتال عدوِّهم ويأمرونهم بترك القتال؛ فهذه الطائفةُ أشرُّ الطوائف وأضرُّها، وطائفةٌ أخرى دونهم، أصابهم الجبنُ والجزع، وأحبُّوا أن ينخزلوا عن الصفوف، فجعلوا يعتذرون بالأعذار الباطلة، وهم الذين قال الله فيهم: {ويستأذنُ فريقٌ منهم النبيَّ يقولونَ إنَّ بيوتَنا عورةٌ}؛ أي: عليها الخطر ونخافُ عليها أن يَهْجُمَ عليها الأعداءُ ونحن غيبٌ عنها؛ فأذن لنا؛ نرجع إليها فنحرسها، وهم كذبةٌ في ذلك، {وما هي بعورةٍ إن يريدون}؛ أي: ما قصدُهم {إلاَّ فراراً}: ولكن جعلوا هذا الكلام وسيلةً وعذراً لهم؛ فهؤلاء قلَّ إيمانُهم، وليس له ثبوتٌ عند اشتدادِ المحنِ.
{13} "Na kundi moja katika miongoni mwao liliposema" miongoni mwa wanafiki, baada ya kuwa na hofu na wakawa na subira chache, wakawa miongoni mwa walioachiliwa mbali. Hawakuwa na subira wao wenyewe, wala hawakuwaepusha watu na shari yao. Kundi hili lilisema, "Enyi watu wa Yathrib;" yaani, watu wa Madina! Kwa hivyo wakawaita kwa jina la nchi wanayoishi, na hilo likaashiria kwamba dini na udugu wa kiimani hauna thamani katika nyoyo zao, na kwamba kilichowafanya wafanye hivyo kilikuwa ni udhaifu wa maumbile ya asili tu. "Enyi watu wa Yathrib, hapana kukaa nyinyi!" Yaani, mahali penu mlipokwenda nje ya Madina. Nao walikuwa wamekapiga kambi karibu na handaki nje ya mji wa Madina, "basi rudini" Madina. Kundi hili linaacha jihadi na linaonyesha kuwa halina nguvu za kupigana na adui yao, na pia linawaamuru watu kuacha kupigana vita. Kwa hivyo, kundi hili ndilo kundi baya na lenye madhara makubwa. Na kuna kundi jingine chini yao ambao walipatwa na uoga na hofu, na wakapenda kusalia nyuma wasiende katika safu za vita, kwa hivyo wakaanza kutoa visingizio vya uwongo. Nao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao, "Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Nabii kwa kusema: "Hakika nyumba zetu ni tupu." Yaani, tuko hatarini na tunahofu kwamba maadui watazishambulia hali ya kuwa tuko mbali nazo. Basi tupe ruhusa, ili turejee huko na tuzilinde, lakini walikuwa ni waongo katika hayo. "Wala hazikuwa tupu; hawakutaka isipokuwa kukimbia tu," lakini wakatumia maneno haya kuwa ni njia na kisingizio tu. Kwa hivyo, hawa wana imani chache, ambayo haina uthabiti wakati majaribu yanakuwa makali.
#
{14} {ولو دُخلت عليهم}: المدينةُ {من أقطارِها}؛ أي: لو دخل الكفار إليها من نواحيها واستولوا عليها؛ لا كان ذلك، ثم سُئِلَ هؤلاء {الفتنة}؛ أي: الانقلاب عن دينهم والرجوع إلى دين المستولين المتغلبين، {لأتَوْها}؛ أي: لأعطوها مبادرين، {وما تَلَبَّثوا بها إلاَّ يسيراً}؛ أي: ليس لهم منعة ولا تصلُّب على الدين، بل بمجرَّد ما تكون الدولة للأعداء؛ يعطونهم ما طلبوا، ويوافقونهم على كفرهم.
{14} "Na lau kuwa wangeliingiliwa" mjini Madina na makafiri "kwa pande zote," na wakauteka - na Mwenyezi Mungu apishe mbali hilo - kisha watu hawa wakatakiwa "kufanya hiana." Yaani, kuiacha dini yao na kurejea katika dini ya wale waliowateka "wangelifanya" kwa haraka mno, "na wasingelisita isipokuwa kidogo tu." Yaani, hawana kujizuialia katika kuilinda dini yao wala kuishika kwa nguvu. Bali mara tu nchi inapokuwa ni ya maadui, wanawapa walichotaka kutoka kwao, na wanakubaliana nao katika ukafiri wao.
#
{15} هذه حالهم، والحال أنهم قد {عاهدوا الله من قبلُ لا يولُّونَ الأدبارَ وكانَ عهدُ الله مسؤولاً}: سيسألُهم عن ذلك العهد، فيجِدُهم قد نَقَضوه؛ فما ظنُّهم إذاً بربِّهم؟!
{15} Hii ndiyo hali yao, kwamba “walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa." Atawauliza kuhusu ahadi hiyo, na atakuta kwamba waliivunja. Basi wanamdhnia nini Mola wao Mlezi?
#
{16} {قل}: لهم لائماً على فرارهم ومخبراً أنَّهم لا يفيدُهم ذلك شيئاً: {لن يَنْفَعَكُم الفرارُ إن فَرَرْتُم من الموتِ أو القتل}: فلو كنتُم في بيوتكم؛ لبرزَ الذين كُتِبَ عليهم القتلُ إلى مضاجعهم، والأسبابُ تنفع إذا لم يعارِضْها القضاء والقدر؛ فإذا جاء القضاء والقدر؛ تلاشى كلُّ سبب، وبطلت كل وسيلة ظنها الإنسان تنجيه، {وإذاً}: حين فررتُم؛ لتسلموا من الموت والقتل، لتنعموا في الدنيا؛ فإنَّكم {لا تُمَتَّعون إلاَّ قليلاً}: متاعاً لا يسوى فراركم وترككم أمر الله وتفويتُكم على أنفسِكم التمتُّع الأبديَّ في النعيم السرمديِّ.
{16} "Sema" uwaambie, ukiwalaumu juu ya kukimbia kwao na ukiwajulisha kuwa hilo halitawafaa kitu. "Kukimbia hakuwafai kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuawa" kwa maana, hata kama mlikuwa majumbani mwenu, basi wangelitoka wale walioandikiwa kufa, wakaenda mahali pao pa kuangukia wafe. Kwani, sababu zinafaa tu ikiwa hazipingani na mipango na mapitisho ya Mwenyezi Mungu. Majaliwa yanapokuja, kila sababu inatoweka, na kila njia ambayo mwanadamu alidhani inaweza kumwokoa, inakuwa batili. "Na hata hivyo" mkikimbia ili muwe salama kutokana na kifo na mauaji, ili mfurahie katika dunia, "hamtastareheshwa isipokuwa kidogo tu." Starehe ambayo si sawa na kukimbia kwenu, na kuacha kwenu amri ya Mwenyezi Mungu, na kujinyima kwenu starehe za milele katika neema ya milele.
#
{17} ثم بيَّن أنَّ الأسباب كلَّها لا تغني عن العبد شيئاً إذا أراده الله بسوءٍ، فقال: {قل من ذا الذي يعصِمُكم}؛ أي: يمنَعُكم من {اللهِ إنْ أراد بكم سوءاً}؛ أي: شرًّا، {أو أراد بكم رحمةً}: فإنَّه هو المعطي المانع، الضار النافع، الذي لا يأتي بالخير إلاَّ هو، ولا يدفعُ السوء إلاَّ هو، {ولا يجدونَ لهم من دون الله وليًّا}: يتولاَّهم فيجلب لهم المنافع {ولا نصيراً}: ينصرهم فيدفعُ عنهم المضارَّ؛ فلْيمتثلوا طاعة المنفرد بالأمور كلِّها، الذي نفذت مشيئتُه ومضى قدرُه ولم ينفعْ مع ترك ولايتِهِ ونصرتِهِ وليٌّ ولا ناصرٌ.
{17} Kisha akabainisha kuwa sababu zote hazimfai kitu mja ikiwa Mwenyezi Mungu anamtakia ubaya, Amesema: "Sema: Ni nani wa kuwalinda." Yaani, atakayewazuia kutokana na "Mwenyezi Mungu pindi akiwatakia uovu au akikutakieni rehema?" Kwani, Yeye ndiye mtoaji na mzuiaji, mwenye kudhuru na kunufaisha, ambaye hakuna anayeleta heri isipokuwa Yeye, wala hakuna anayeondoai maovu isipokuwa Yeye. "Wala hawatapata mlinzi isipokuwa Mwenyezi Mungu," atakayewasimamia na kuwaletea manufaa, "wala msaidizi" atakayewanusuru na kuwalinda kutokana na madhara. Basi na wamtii yule ambaye ni wa kipekea katika kila jambo, ambaye mapenzi yake yametekelezwa na mipangilio yake imeshapita, na wala hakuna mlinzi wala msaidizi anayeweza kunufaisha wala kunusuru.
#
{18} ثم توعد تعالى المخذِّلين المعوِّقين وتهدَّدهم فقال: {قد يعلمُ الله المعوِّقينَ منكم}: عن الخروج لمن لم يخرجوا، {والقائلين لإخوانهم}: الذين خرجوا: {هَلُمَّ إلينا}؛ أي: ارجِعوا كما تقدَّم من قولهم: {يا أهل يثربَ لا مُقامَ لكم فارْجِعوا}، وهم مع تعويقِهم وتخذيلِهم {لا يأتون البأسَ}: القتال والجهاد بأنفسهم، {إلاَّ قليلاً}: فهم أشدُّ الناس حرصاً على التخلُّف لعدم الداعي لذلك من الإيمان والصبر، [ووجود] المقتضي للجبن من النفاق وعدم الإيمان.
{18} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaahidi adhabu na kuwatishia wale waliosalia nyuma ya vita na waliozuilia watu kwenda katika vita, akasema: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua hao wanaozuilia miongoni mwenu" watu ili wasitoke katika wale ambao hawakutoka "na wanaowaambia ndugu zao" ambao waliotoka, "Njooni kwetu!" Yaani, rudini, kama ilivyotangulia katika kauli yao, "Enyi watu wa Yathrib, hapana kukaa nyinyi! Rudini." Nao licha ya kuzuilia kwao huku na kusalia kwao nyuma ya vita, "hawaingii vitani" wao wenyewe, "isipokuwa kidogo tu." Kwani wao ndio wanaopenda zaidi kubakia nyuma kuliko watu wote, kwa sababu hawana sababu ya hilo kama vile imani na subira. [Na wakawa] na chenye kuwalazimu wawe na woga kama vile unafiki na ukosefu wa imani.
#
{19} {أشِحَّة عليكم}: بأبدانهم عند القتال، وأموالهم عند النفقة فيه؛ فلا يجاهدون بأموالهم وأنفسهم، {فإذا جاء الخوفُ رأيتَهم ينظُرون إليك}: نظر المَغْشِيِّ {عليه من الموت}: من شدَّة الجبن الذي خلع قلوبَهم والقلقِ الذي أذهلهم وخوفاً من إجبارِهم على ما يكرهون من القتال، {فإذا ذهب الخوفُ}: وصاروا في حال الأمن والطمأنينة؛ {سَلَقوكم بألسنةٍ حدادٍ}؛ أي: خاطبوكم وتكلَّموا معكم بكلام حديدٍ ودعاوٍ غير صحيحة، وحين تسمعُهم تظنُّهم أهلَ الشجاعة والإقدام. {أشحَّة على الخيرِ}: الذي يُراد منهم، وهذا شرُّ ما في الإنسان: أن يكون شحيحاً بما أُمِر به، شحيحاً بماله أن ينفِقَه في وجهه، شحيحاً في بدنِهِ أن يجاهِدَ أعداء الله أو يدعو إلى سبيل الله، شحيحاً بجاهه، شحيحاً بعلمه ونصيحته ورأيه. {أولئك}: الذين بتلك الحالة {لم يُؤْمِنوا}: بسبب عدم إيمانهم؛ أحبط الله أعمالهم. {وكان ذلك على الله يسيراً}: وأما المؤمنون؛ فقد وقاهُم اللهُ شحَّ أنفسهم، ووفَّقهم لبذل ما أُمِروا به من بذل أبدانهم في القتال في سبيله وإعلاء كلمتِهِ، وأموالهم للنفقة في طرق الخير، وجاههم وعلمهم.
{19} "Wana choyo juu yenu" kwa miili yao wakati wa kupigana vita, na mali zao wakati wa kuzitumia. Basi hawapambani kwa mali zao na nafsi zao. "Ikifika hofu, utawaona wanakutazama" mtazamo wa anayezimia "kwa mauti," kutokana na ukali wa woga ulioiondoa mioyo yao, wasiwasi uliowashutua, na hofu ya kwamba watalazimishwa kufanya kile wanachochukia ambacho ni kupigana vita. "Na hofu ikiondoka," wakawa katika hali ya amani na utulivu, "wanakuudhini kwa ndimi kali." Yaani, wanawaongelesha kwa maneno makali, na madai yasiyokuwa sahihi, na unapowasikia, unawadhania kuwa ni watu wa ushujaa na ujasiri. "Nao ni mabahili kwa kila la heri" linalokusudiwa kutoka kwao. Na huu ni uovu mkubwa zaidi unaoweza kuwa kwa mtu kwamba awe bahili kwa alichoamrishwa, bahili kwa mali yake katika kuitumia kwenye njia zake, na bahili katika mwili wake kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu au kulingania kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, bahili katika heshima yake, bahili katika elimu yake, ushauri na maoni yake. "Hao" ambao wana hali hiyo, "hawakuamini" na kwa sababu ya kutoamini kwao, Mwenyezi Mungu akaharibu matendo yao. "Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi." Na ama Waumini, hao Mwenyezi Mungu aliwalinda kutokana na ubahili wa nafsi zao, na akawawezesha kufanya kwa wingi yale waliyoamrishwa, kama vile kutoa miili yao kwa kupigana katika njia yake na kuliinua neno lake, na pia mali zao kwa kuzitumia katika njia za heri, na hadhi yao na elimu yao.
#
{20} {يحسبون الأحزابَ لم يذهبوا}؛ أي: يظنُّون أنَّ هؤلاء الأحزاب الذين تحزَّبوا على حرب رسول الله - صلى الله عليه وسلم - وأصحابِهِ لم يَذْهَبوا حتى يستأصِلوهم، فخاب ظنُّهم، وبطل حسبانهم. {وإن يأتِ الأحزابُ}: مرةً أخرى، {يودُّوا لو أنَّهم بادون في الأعراب يسألونَ عن أنبائِكُم}؛ أي: لو أتى الأحزابُ مرة ثانية مثل هذه المرة؛ ودَّ هؤلاء المنافقون أنهم ليسوا في المدينة، ولا في القربِ منها، وأنهم مع الأعرابِ في البادية، يستخبرون عن أخباركم، ويسألون عن أنبائكم ماذا حَصَلَ عليكم؛ فتبًّا لهم وبعداً؛ فليسوا ممن يُغالى بحضورهم، فلو {كانوا فيكم ما قاتلوا إلاَّ قليلا}: فلا تبالوهم، ولا تأسَوْا عليهم.
{20} "Wanafikiri yale makundi ya maadui" haya yaliyoungana kumpiga vita Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na maswahaba wake hawakwenda mpaka wawaangamize kabisa, lakini matarajio yao yakaambulia patupu, na hesabu zao zikawa batili. "Na yakija hayo makundi" mara nyingine, "watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza habari zenu" Yaani, ikiwa makundi haya yatakuja mara ya pili kama mara hii; hawa wanafiki watatamani wasingekuwamo mjini Madina wala karibu nayo, watatamani kwamba wawe pamoja na Mabedui jangwani wakiuliza kuhusu habari zenu. Je, ni nini kiliwapata? Basi na waangamie na wapotelee mbali. Hao si miongoni mwa wale ambao uwepo wao hauongezi thamani yoyote. Na “Na lau wakiwa pamoja nanyi, hawapigani isipokuwa kidogo tu." Basi msiwajali, wala msiwaonee huruma.
#
{21} {لقد كان لكم في رسول الله أسوةٌ حسنةٌ}: حيث حَضَرَ الهيجاءَ بنفسه الكريمة، وباشرَ موقفَ الحرب وهو الشريفُ الكاملُ والبطل الباسلُ، فكيف تشحُّون بأنفسكم عن أمرٍ جادَ رسولُ الله - صلى الله عليه وسلم - بنفسه فيه، فتأسَّوْا به في هذا الأمر وغيره. واستدَّل الأصوليُّون في هذه الآية على الاحتجاج بأفعال الرسول - صلى الله عليه وسلم -، وأنَّ الأصل أنَّ أمَّتَه أسوتُه في الأحكام؛ إلاَّ ما دلَّ الدليل الشرعيُّ على الاختصاص به؛ فالأسوةُ نوعان: أسوةٌ حسنةٌ وأسوةٌ سيئةٌ، فالأسوةُ الحسنةُ في الرسول - صلى الله عليه وسلم -؛ فإنَّ المتأسِّي به سالكٌ الطريق الموصل إلى كرامة الله، وهو الصراط المستقيم، وأمَّا الأسوة بغيره إذا خالَفَه؛ فهو الأسوة السيئة؛ كقول المشركين حين دعتهم الرسل للتأسِّي بهم: {إنَّا وَجَدْنا آباءنا على أمَّةٍ وإنَّا على آثارِهِم مهتدونَ}: وهذه الأسوةُ الحسنةُ إنَّما يسلُكُها ويوفَّقُ لها مَنْ كان يرجو الله واليوم الآخر؛ فإنَّ ذلك ما معه من الإيمانِ وخوفِ الله ورجاء ثوابِهِ وخوفِ عقابِهِ يحثُّه على التأسِّي بالرسول - صلى الله عليه وسلم -.
{21} "Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu" kwa maana yeye mwenyewe alihudhuria vita pamoja na utukufu wake, na akaingia katika uwanja wa vita, na hali yeye ndiye mtukufu na shujaa jasiri. Basi vipi mnalifalinyia ubahili jambo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – mwenyewe alilifanya mwenyewe vyema sana? Basi fuateni mfano wake katika jambo hili na mengineyo. Wanazuoni wa misingi ya Fiqh waliitumia Aya kuwa ni ushahidi kwamba inaruhusika kutumia matendo ya Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kuwa ndio ushahidi, na kwamba kanuni ya msingi ni kuwa umma wake wanapaswa kumuiga naye katika hukumu zote, isipokuwa katika zile ambazo ushahidi wa kisheria unaonyesha kuwa zinamhusu yeye tu. Na kuna aina mbili za viigizo: kiigizo kizuri na kiigizo kibaya. Kiigizo kizuri kiko ndani ya Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na kumuiga ni kuifuata njia ifikishayo kwenye utukufu wa Mwenyezi Mungu, nayo ndiyo njia iliyonyooka. Na ama kumuiga mwingine katika yale yanayomhalifu, basi hicho ndicho kiigizo kibaya, kama walivyosema washirikina wakati Mitume wao walipowaita ili wawafuate: "Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao." Na mfano huu mzuri unafuatwa tu na anawezeshwa kuufikia yule ambaye anamtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Kwa maana yale aliyo nayo ya imani, kumcha Mwenyezi Mungu, kutaraji malipo Yake, na kuhofu adhabu yake, haya yote yanamhimiza kufuata mfano wa Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
#
{22} لما ذكر حالة المنافقين عند الخوفِ؛ ذكر حالَ المؤمنين فقال: {ولمَّا رأى المؤمنون الأحزابَ}: الذين تحزَّبوا ونزلوا منازِلَهم وانتهى الخوفُ، {قالوا هذا ما وَعَدَنا اللهُ ورسولُه}: في قوله: {أم حسبتُم أن تدخُلوا الجنَّةَ ولما يأتِكُم مَثَلُ الذين خَلَوْا من قبلِكم مسَّتْهم البأساءُ والضَّراءُ وزلزلوا حتى يقولَ الرسول والذين آمنوا معه متى نصرُ الله ألا إنَّ نصر الله قريبٌ}، {وصَدَقَ اللهُ ورسولُه}: فإنا رأينا ما أَخَبَرَنا به، {وما زادَهُم}: ذلك الأمر {إلاَّ إيماناً}: في قلوبهم، {وتسليماً}: في جوارحهم، وانقياداً لأمر الله.
{22} Alipotaja hali ya wanafiki wanapoogopa; akataja hali ya Waumini na akasema: Na Waumini walipoyaona makundi, wale walioungana na wakateremka kwenye vyeo vyao, na hofu ikakoma, wakasema: Haya ndiyo aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika kauli yake: Au mlidhani kuwa mtaingia Peponi ulipowafikia mfano wa waliopita kabla yenu msiba na balaa, wakatikisika mpaka Mtume na walioamini pamoja naye wakasema: "Lini litawafikia? Mwenyezi Mungu atupe ushindi?” Hakika ushindi wa Mwenyezi Mungu u karibu.Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli, maana tumeyaona haya aliyotujulisha, wala hayakuwazidishia mambo hayo isipokuwa imani mioyoni mwao, na utiifu katika viungo vyao, na kutii amri ya Mwenyezi Mungu.
#
{23} ولما ذكر أنَّ المنافقين عاهدوا الله لا يولُّون الأدبار ونقضوا ذلك العهد؛ ذكر وفاء المؤمنين به، فقال: {من المؤمنينَ رجالٌ صَدَقوا ما عاهَدوا الله عليه}؛ أي: وَفَّوْا به وأتموُّه وأكملوه، فبذلوا مُهَجَهُم في مرضاتِهِ، وسبَّلوا نفوسهم في طاعته. {فمنهم من قضى نحبَهُ}؛ أي: إرادته ومطلوبَه وما عليه من الحقِّ، فقُتل في سبيل الله أو مات مؤدياً لحقِّه لم ينقصْه شيئاً، {ومنهم مَن ينتظِرُ}: تكميل ما عليه؛ فهو شارعٌ في قضاء ما عليه ووفاء نحبِهِ ولما يُكْمِلْه، وهو في رجاء تكميله ساعٍ في ذلك مجدٌّ، {وما بَدَّلوا تبديلاً}: كما بدَّل غيرُهم، بل لم يزالوا على العهد، لا يلوون ولا يتغيرون؛ فهؤلاء الرجال على الحقيقة، ومن عداهم فصُورُهم صورُ رجال وأما الصفاتُ؛ فقد قَصُرَتْ عن صفاتِ الرجال.
{23} Na ilipotajwa kuwa wanafiki walimuahidi Mwenyezi Mungu kwamba hawatageuza migongo yao, lakini wakaivunja ahadi hiyo; akataja kwamba Waumini walitimiza ahadi zao, akasema: "Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu" wakajitolea maisha yao katika kumridhisha Yeye, na wakajinyang'anya nafsi zao kuwa ajili ya kumtii Yeye. "Baadhi yao wamekwisha kufa" au inamaanisha kwamba utashi wao na haki aliyo juu yake, basi wakauawa katika njia ya Mwenyezi Mungu au akafa akitimiza haki yake, bila ya kuipunguza kwa chochote. "Na baadhi wanangojea" kukamilisha yale aliyo juu yake. Tayari ameanza kutimiza yale yaliyo juu yake, na kuyakamilisha lakini bado hajayakamilisha, na anataraji kwamba atayakamilisha, na anakimbilia na kujibidiisha katika hilo, "wala hawakubadilisha ahadi hata kidogo." Kama wengineo walivyobadilisha. Bali bado wameishikilia ahadi yao, wala hawapotoshi wala kugeuza kitu. Hawa ndio wanaume wa kweli, na wasiokuwa wao mwonekano wao ni mwonekano wa wanaume, lakini sifa zao, hizo zilipunguka sana kuwa sifa za wanaume.
#
{24} {لِيَجْزِي اللهُ الصادقينَ بصِدْقِهم}؛ أي: بسبب صدقهم في أقوالهم وأحوالهم ومعاملتهم مع الله واستواء ظاهِرِهم وباطِنِهم، قال الله تعالى: {هذا يومُ يَنفَعُ الصادقينَ صدقُهم لهم جناتٌ تجري من تحتها الأنهارُ خالدين فيها أبداً ... } الآية؛ أي: قدَّرنا ما قدَّرنا من هذه الفتن والمحن والزلازل ليتبيَّن الصادق من الكاذب، فيَجِزْيَ الصادقين بصدقهم، {ويعذِّبَ المنافقين}: الذين تغيَّرتْ قلوبُهم وأعمالُهم عند حلول الفتن، ولم يَفوا بما عاهدوا الله عليه، {إن شاءَ}: تعذيبَهم؛ بأنْ لم يشأ هدايتهم، بل علم أنَّهم لا خير فيهم، فلم يوفِّقْهم، {أو يتوبَ عليهم}: بأنْ يوفِّقَهم للتوبة والإنابة، وهذا هو الغالب على كرم الكريم، ولهذا ختم الآية باسمين دالَّيْنِ على المغفرة والفضل والإحسان، فقال: {إنَّ الله كان غفوراً رحيماً}؛ غفوراً لذنوب المسرفين على أنفسهم، ولو أكثروا من العصيان، إذا أتَوْا بالمتاب. {رحيماً}: بهم؛ حيث وفَّقَهم للتوبة، ثم قَبِلها منهم، وستر عليهم ما اجْتَرحوه.
{24} "Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa sababu ya ukweli wao" kwa sababu ya ukweli wao katika maneno yao, hali zao, na muamala wao kwa Mwenyezi Mungu, na usawa wa nafsi zao za nje na za ndani. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Hii ndiyo siku ambayo wakweli watalipwa kwa ukweli wao, watakuwa na Bustani zipitazo mito kati yake, watakaa humo milele... hadi mwisho wa Aya. Yaani, tuliyapitisha yale tuliyoyapitisha miongoni mwa majaribio haya na mitihani hii, na misukosuko, ili mkweli apambanuke mkweli kutokana na mwongo, ili awalipe wakweli kwa ukweli wao. "Na awaadhibu wanafiki" ambao zilibadilika nyoyo zao na vitendo vyao wakati majaribio yalipofika, na wala hawakutimiza yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu, "pindi akitaka" kuwaadhibu. Na hilo ni kwa kutotaka waongoke. Bali alijua ya kwamba hakuna heri ndani yao, kwa hivyo hakuwawezesha, "au apokee toba yao" kwa kuwawezesha kutubu na kurejea kwake. Na haya ndiyo yanayokuwa sana katika ukarimu wa Mwingi wa Ukarimu, na ndiyo maana akahitimisha Aya hiyo kwa majina mawili yanayoonyesha msamaha, fadhila, na ihsani, akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Husamehe dhambi za wavukao mipaka kuhusiana na nafsi zao, hata kama wataasi vipi, ikiwa watatubu. "Mwenye kurehemu" watu hao, ambapo aliwawezesha kutubu, kisha akakubali toba hiyo kutoka kwao, na akawasitiria yale waliyofanya.
#
{25} {وردَّ الله الذين كفروا بغيظِهِم لم ينالوا خيراً}؛ أي: ردَّهم خائبين، لم يحصُل لهم الأمر الذي كانوا حريصين عليه، مغتاظين، قادرين عليه، جازِمين بأنَّ لهم الدائرة، قد غرَّتهم جموعهم وأُعْجبوا بتحزُّبهم وفرِحوا بعددِهم وعددِهم، فأرسل الله عليهم ريحاً عظيمةً، وهي ريح الصَّبا، فزعزعت مراكزَهم، وقوَّضت خيامهم، وكفأت قدورَهم، وأزعجتهم، وضربهم الله بالرعب، فانصرفوا بغيظهم، وهذا من نصر الله لعباده المؤمنين. {وكفى اللهُ المؤمنينَ القتال}: بما صَنَعَ لهم من الأسباب العاديَّة والقدريَّة. {وكان الله قويًّا عزيزاً}: لا يغالِبُه أحدٌ إلاَّ غُلِب، ولا يستنصره أحدٌ إلا غَلَب، ولا يعجِزُه أمرٌ أراده، ولا ينفع أهل القوَّة والعزَّة قوتُهم وعزَّتُهم إن لم يُعِنْهُم بقوَّته وعزَّته.
{25} "Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata heri yoyote." Yaani, aliwarudisha huku wameambulia patupu, bila ya kupata jambo walilokuwa wakilitafuta sana, na huku wakiwa na hasira kubwa, huku wakiona kwamba wana uwezo juu yake, huku wakiwa na uhakika kwamba mambo yatawaendea vyema, huku wamedanganywa na wingi wao na kujiona na makundi yao, na wakafurahia kwa idadi yao. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia upepo mkali, ambao ni ule upepo wa Swabaa, nao ukatikisa mahali pa jeshi lao, ukaharibu mahema yao, ukamwaga vyungu vyao juu chini, na ukawasumbua, na Mwenyezi Mungu akawatia hofu kubwa, kwa hivyo wakaondoka kwa hasira yao, na haya ni katika nusura ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini. "Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita," kwa sababu ya sababu za kawaida na za kimajaliwa alizowafanyia. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza," ambaye hataki kushindana naye mshindani isipokuwa anashindwa, hakuna anayetafuta msaada wa mwingineye isipokuwa anashindwa, wala halimshindi jambo lolote analotaka, wala nguvu na utukufu wa wenye nguvu na utukufu haviwanufaishi kitu kiwa hawasaidii na nguvu zake na utukufu wake.
#
{26} {وأنزلَ الذين ظاهَروهم}؛ أي: عاونوهم {من أهل الكتاب}؛ أي: من اليهود {من صياصِيهم}؛ أي: أنزلهم من حصونهم نزولاً مظفوراً بهم مجعولين تحت حكم الإسلام، {وَقَذَفَ في قلوبِهِمُ الرعبَ}: فلم يقووا على القتال، بل استسلموا وخضعوا وذلُّوا. {فريقاً تقتلون}: وهم الرجال المقاتلون، {وتأسرونَ فريقاً}: من عداهم من النساء والصبيان.
{26} "Na akawateremsha wale waliowasaidia maadui katika Watu wa Kitabu;" kama vile: Mayahudi, "kutoka katika ngome zao" huku wakiwa wameshindwa na wakiwa chini ya hukumu ya Uislamu. "Na akatia hofu katika nyoyo zao" kwa hivyo hawakuweza kupigana, bali walisalimu amri, na wakanyenyekea, na wakafedheheka. "Baadhi yao mkawa mnawaua;" nao walikuwa ni wanaume wapiganaji, "na wengine mnawateka," kama vile wanawake na watoto.
#
{27} {وأورَثَكم}؛ أي: غنمكم {أرضَهم وديارَهم وأموالَهم وأرضاً لم تطؤوها}؛ أي: أرضاً كانت من قبلُ من شرفِها وعزَّتِها عند أهلها لا تتمكَّنون من وطئها، فمكَّنكم الله، وخَذَلَهم، وغَنِمْتُم أموالهم، وقتلتموهم، وأسرْتُموهم، {وكان اللهُ على كلِّ شيءٍ قديراً}: لا يعجِزُه شيء، ومن قدرتِهِ قدَّر لكم ما قدَّر. وكانت هذه الطائفة من أهل الكتاب هم بنو قريظةَ من اليهود في قريةٍ خارج المدينة غير بعيد، وكان النبي - صلى الله عليه وسلم - حين هاجر إلى المدينة وادَعَهم وهادَنَهم فلم يقاتلهم ولم يقاتِلوه، وهم باقون على دينهم، لم يغيِّر عليهم شيئاً، فلما رأوا يوم الخندق الأحزاب الذين تحزَّبوا على رسول الله وكَثْرتَهم وقلَّةَ المسلمين، وظنُّوا أنهم سيستأصلون الرسول والمؤمنين، وساعد على ذلك تدجيلُ بعض رؤسائهم عليهم، فنقضوا العهدَ الذي بينهم وبين رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، ومالؤوا المشركين على قتاله، فلما خَذَلَ الله المشركين؛ تفرَّغ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - لقتالهم، فحاصرهم في حصنهم، فنزلوا على حكم سعد بن معاذ رضي الله عنه، فحكم فيهم أن تُقْتَلَ مقاتِلَتُهُم، وتُسبى ذراريهم وتُغنم أموالهم، فأتمَّ الله لرسوله والمؤمنين المنَّة، وأسبغ عليهم النعمة، وأقر أعينهم بخذلانِ من انخذلَ من أعدائهم، وقتل مَن قَتَلوا، وأسر من أسروا، ولم يزل لطفُ الله بعبادِهِ المؤمنين مستمرًّا.
{27} "Na akawarithisha ardhi zao na nyumba zao na mali zao, na ardhi msiyopata kuikanyaga." Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawawezesha nyinyi, na akawaangusha hao, na mkachukua mali zao, na mkawaua na kuwateka. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu." Hakuna kinachoweza kumshinda. Na kwa sababu ya uwezo wake ndiyo akawaandikia hayo aliyowaandikia. Na kundi hili miongoni mwa Watu wa Kitabu lilikuwa ni Mayahudi wa Banu Quraydha katika kijiji kilicho nje ya Madina, kisichokuwa mbali sana. Na Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alikuwa alipohamia Madina, aliingia nao katika mkataba wa kusitisha vita, kwa hivyo hakupigana nao, wala wao hawakupigana naye, na wakabakia katika Dini yao, na hakuwabadilishia chochote. Basi siku ya handaki walipoona makundi yaliyoshiriki dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wingi wa idadi yao na uchache wa idadi ya Waislamu, na wakadhania kuwa watamuangamiza Mtume na Waumini, na wakasaidiwa katika hilo na baadhi ya viongozi wao. Kwa hivyo, wakaivunja ahadi iliyokuwa baina yao na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na wakaungana na washirikina ili kumpiga vita. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu alipowaangusha washirikina, Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akapata nafasi nzuri ya kupigana nao, basi akawazingira katika ngome yao, nao wakakubali kuhukumiwa kulingana na hukumu ya Sa'd bin Muadh, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Basi Sa'd akahukumu kwamba wauawe wapiganaji, na watoto wao wachukuliwe mateka, na mali zao zichukuliwe kama ngawira. Basi Mwenyezi Mungu akamtimizia neema Mtume wake na waumini, na akawapa neema kwa wingi, na akatuliza macho yao kwa kuwaangusha wale waliosalia nyuma ya vita katika maadui wao, na kuwaua wale waliowaua, na kuwateka wale waliowateka, na fadhila za Mwenyezi Mungu zikaendelea kuwafikia waja wake.
: 28 - 29 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ إِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا (28) وَإِنْ كُنْتُنَّ تُرِدْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنْكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا (29)}
28. Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitawapa kutoka nyumba, na kuwaacha mwachano mzuri. 29. Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.
#
{28} لما اجتمع نساءُ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - عليه في الغيرة، وطلبن منه النفقة والكسوة؛ طلبنَ منه أمراً لا يقدر عليه في كلِّ وقت، ولم يَزَلْنَ في طلبهنَّ متَّفقات وفي مرادهنَّ متعنِّتات، فشقَّ ذلك على الرسول، حتى وصلت به الحالُ إلى أنه آلى منهنَّ شهراً، فأراد الله أن يسهِّلَ الأمرَ على رسولِهِ، وأن يرفع درجةَ زوجاتِهِ، ويُذْهِبَ عنهنَّ كلَّ أمر ينقص أجرهنَّ فأمر رسولَه أن يخيِّرهنَّ ، فقال: {يا أيُّها النبيُّ قلْ لأزواجِك إن كنتنَّ تردنَ الحياةَ الدُّنيا}؛ أي: ليس لَكُنَّ في غيرها مطلبٌ، وصرتنَّ ترضينَ لوجودها وتغضبنَ لِفَقْدِها؛ فليس لي فيكنَّ أربٌ وحاجةٌ وأنتنَّ بهذه الحال، {فتعالَيْن أمتِّعْكُنَّ}: شيئاً مما عندي من الدنيا، {وأسرِّحْكُنَّ}؛ أي: أفارقكن {سراحاً جميلاً}: من دون مغاضبةٍ ولا مشاتمةٍ، بل بسعة صدرٍ وانشراح بال، قبل أن تبلغَ الحالُ إلى ما لا ينبغي.
{28} Pindi wake zake Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - walipokusanyika dhidi ya Nabii kwa husuda na wakamwomba matumizi na mavazi; wakamuomba jambo ambalo haliwezi katika kila wakati, na hawakuacha kumuomba wao wote wakati mmoja lakini waka wanamfanyia ukaidi tu. Kwa hivyo jambo hilo likawa gumu kwa Mtume, mpaka hali ikamfikia kujitenga mbali nao kwa muda wa mwezi mmoja. Basi Mwenyezi Mungu akataka kumsahilishia Mtume wake jambo hili, na kuwanyanyua wake zake vyeo, na kuwaondolea chochote kinachoweza kuwapunguzia malipo yao, na akamuamuru Mtume wake kuwapa hiari. Kwa hivyo akasema, "Ewe Nabii, waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia" na kwamba hamtaki maisha mengine, basi mkawa mnaridhika tu yanapokuwapo, na mnakasirika yanapokosa kuwapo, basi mimi sina haja nanyi mkiwa katika hali hii, "basi njooni, nitawapa kutoka nyumba" mingoni mwa yale niliyo nayo katika vitu vya kidunia, "na kuwaacha mwachano mzuri." Bila ya kuwakasirikia wala kuwatukana, lakini badala yake itakuwa kwa kifua kipana na akili iliyokunjuka, kabla ya hali kufikia kile ambacho hakifai.
#
{29} {وإن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الله ورسولَه والدارَ الآخرة}؛ أي: هذه الأشياء مرادُكُنَّ وغايةُ مقصودِكُنَّ، وإذا حصل لَكُنَّ الله ورسوله والجنة؛ لم تبالينَ بسعة الدنيا وضيقها ويُسرها وعُسرها، وقنعتنَّ من رسول الله بما تيسَّر، ولم تطلبنَ منه ما يشقُّ عليه، {فإنَّ الله أعدَّ للمحسناتِ منكنَّ أجراً عظيماً}: رتَّب الأجر على وصفهنَّ بالإحسان؛ لأنَّه السبب الموجب لذلك، لا لكونهنَّ زوجاتٍ للرسول؛ فإنَّ مجرَد ذلك لا يكفي، بل لا يفيدُ شيئاً مع عدم الإحسان، فخيَّرَهُنَّ رسول الله - صلى الله عليه وسلم - في ذلك، فاخترنَ الله ورسوله والدار الآخرة كلُّهن ، لم يتخلفْ منهنَّ واحدةٌ رضي الله عنهن. وفي هذا التخيير فوائدُ عديدة: منها: الاعتناءُ برسوله والغيرةُ عليه أن يكون بحالة يشقُّ عليه كثرةُ مطالب زوجاته الدنيويَّة. ومنها: سلامتُه - صلى الله عليه وسلم - بهذا التخيير من تَبِعَةِ حقوق الزوجات، وأنَّه يبقى في حرِّية نفسه إن شاء أعطى وإن شاء منع، ما كان على النبيِّ من حرج فيما فرضَ الله له. ومنها: تنزيهُهُ عمَّا لو كان فيهنَّ مَنْ تؤثِرُ الدُّنيا على الله ورسوله والدار الآخرة عنها، وعن مقارنتها. ومنها: سلامةُ زوجاتِهِ رضي الله عنهنَّ عن الإثم والتعرُّض لسخط اللَّه ورسوله، فحسم الله بهذا التخيير عنهنَّ التسخُّط على الرسول الموجب لسَخَطِهِ المُسْخِطِ لربِّه الموجب لعقابه. ومنها: إظهار رفعتهنَّ وعلوِّ درجتهنَّ وبيان علوِّ هممهنَّ أن كان اللهُ ورسولُه والدار الآخرة مرادَهُنَّ ومقصودَهن دون الدُّنيا وحطامها. ومنها: استعدادُهُنَّ بهذا الاختيار للأمر الخيار للوصول إلى خيار درجات الجنة وأنْ يكنَّ زوجاتِهِ في الدُّنيا والآخرة. ومنها: ظهورُ المناسبة بينه وبينهنَّ؛ فإنَّه أكمل الخلق، وأراد الله أن تكون نساؤه كاملاتٍ مكمَّلاتٍ طيباتٍ مطيَّباتٍ، {الطيِّباتُ للطيبين والطيِّبونَ للطيبات}. ومنها: أنَّ هذا التخيير داعٍ وموجب للقناعة التي يطمئنُّ لها القلبُ وينشرحُ لها الصدرُ، ويزول عنهنَّ جشعُ الحرص وعدم الرِّضا الموجب لقلق القلب واضطرابِهِ وهمِّه وغمِّه. ومنها: أن يكون اختيارهنَّ هذا سبباً لزيادة أجرهنَّ ومضاعفتِهِ، وأن يكنَّ بمرتبةٍ ليس فيها أحدٌ من النساء، ولهذا قال:
{29} "Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera," na yakiwatokea kwamba mna Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Pepo, hamuwezi kujali upana wa dunia na dhiki yake, na urahisi wake na ugumu wake, na mkaridhika na kile chepesi anachowapa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wala hamkumuomba yaliyo magumu kwake. "Basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa." Amepanga kuwapa malipo ikiwa watasifika kwa sifa ya ihsani; kwa sababu ndiyo sababu inayosababisha hayo, si kwa kuwa wao ni wake za Mtume. Kwani hilo peke yake halitoshi kitu, bali hata halitoshi kitu ihsani inapokosekana. Kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake - akawapa hiari katika hilo, nao wote wakamchagua Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Nyumba ya akhera, na hakuna hata mmoja wao aliyebakia nyuma katika hilo, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Na hiari hii ina faida nyingi: Miongoni mwake ni Mwenyezi Mungu kumtunza Mtume wake na kumuonea wivu asije akawa katika hali ambayo ni ngumu kwake, kutokana kuombwa kwa wingi na wake zake mambo ya kidunia. Na miongoni mwake ni usalama wake yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kutokana na hiari katika suala la kulaumiwa juu ya haki za wake, na kwamba atabakia katika uhuru wake mwenyewe; akitaka, anatoa, na akitaka, anazuia, na hakuna ugumu wowote kwa nabii katika yale ambayo Mwenyezi Mungu amemuwajibishia. Na miongoni mwake ni kumuweka mbali na yeyote kati yao ambaye anapendelea dunia kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Akhera. Na miongoni mwake ni usalama wa wake zake, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kutokana na dhambi na kupata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akazuia kwa hiari hiyo dhidi ya kumkasirikia Mtume ambako kunasababisha yeye kuwakasirikia, jambo ambalo linamkasirisha Mola wake Mlezi na kulazimu adhabu yake. Miongoni mwake ni kuonyesha utukufu wao na hadhi yao ya juu, na kuonyesha hima yao kubwa mno ambapo alikuwa Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Akhera ndio kitu wanachotaka tu na ndiyo makusudio yao, badala ya dunia na pumbao yake. Na miongoni mwake ni utayari wao, kupitia chaguo hili kuweza kuchagua jambo bora lenye kufikisha kwenye viwango bora kabisa katika Pepo, na kwamba watakuwa wake zake duniani na akhera. Na miongoni mwake ni kudhihirika kuwepo mwingiliano mzuri kati yake na wao; kwani yeye ndiye aliyekamilika zaidi katika viumbe, na Mwenyezi Mungu akataka kwamba wanawake wake wawe wakamilifu, wenye kukamilisha, wazuri na wanaofanya wengine kuwa wazuri. "Wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema." Na miongoni mwake ni kwamba chaguo hili ni sababu yenye kulazimu watosheke, jambo ambalo hutuliza moyo na kufungua kifua, na wanaondokewa na uchu wa kufanya maovu na kutoridhika ambako kunausababishia moyo kuwa na wasiwasi, na kutotulia, na kuwa na huzuni kubwa na dhiki. Na miongoni mwake ilikuwa hivyo ili chaguo lao hili liwe ni sababu ya kuwazidishia malipo yao na ili wawe katika daraja ambalo hakuna mwanamke aliyeko hapo, na ndiyo maana akasema:
: 30 - 31 #
{يَانِسَاءَ النَّبِيِّ مَنْ يَأْتِ مِنْكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ وَكَانَ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرًا (30) وَمَنْ يَقْنُتْ مِنْكُنَّ لِلَّهِ وَرَسُولِهِ وَتَعْمَلْ صَالِحًا نُؤْتِهَا أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا (31)}
30. Enyi wake wa Nabii, atakayefanya uchafu dhahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi. 31. Na miongoni mwenu atakayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu.
#
{30} لما اخترنَ الله ورسولَه والدارَ الآخرة؛ ذَكَرَ مضاعفَة أجرهنَّ ومضاعفةَ وِزْرِهِنَّ وإثمهنَّ لو جرى منهنَّ؛ ليزداد حذرهنَّ وشكرهنَّ الله تعالى، فجعل من أتى منهنَّ بفاحشةٍ ظاهرةٍ لها العذابُ ضعفين.
{30} Wake zake Mtume walipomchagua Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Nyumba ya Akhera; akataja kuzidishiwa kwao ujira na kuzidisha kwao mizigo na dhambi zao ikiwa watafanya; ili tahadhari yao iongezeke, na kumshukuru kwao Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi akamfanya miongoni mwao mwenye kufanya uchafu dhahiri kupata adhabu mara mbili.
#
{31} {ومَن يَقْنُتْ منكنَّ}؛ أي: تطيع اللهَ ورسولَه وتعملْ صالحاً قليلاً أو كثيراً، {نؤتِها أجْرَها مرَّتينِ}؛ أي: مثل ما نعطي غيرها مرَّتين، {وأعْتَدْنا لها رزقاً كريماً}: وهي الجنة، فَقَنَتْنَ للهِ ورسوله وعَمِلْنَ صالحاً، فعلم بذلك أجرهنَّ.
{31} "Na miongoni mwenu atakayemtii Mwenyezi Mungu" na Mtume wake, na akatenda mema, machache au mengi, "tutampa malipo yake mara mbili." Yaani, mara mbili mfano wa vile tutakavyowalipa wengineo. "Na tutamwandalia riziki ya ukarimu," ambayo ni Bustani za mbinguni. Kwa hivyo, wakamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakatenda mema, basi malipo yao yakajulikana kwa sababu ya hayo.
: 32 - 34 #
{يَانِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِنَ النِّسَاءِ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَعْرُوفًا (32) وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَى وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُذْهِبَ عَنْكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا (33) وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَى فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ وَالْحِكْمَةِ إِنَّ اللَّهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا (34)}
32. Enyi wake wa Nabii, nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu, basi msilegeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema. 33. Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kuwasafisheni sawasawa. 34. Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hekima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye habari.
#
{32} يقول تعالى: {يا نساءَ النبيِّ}: خطابٌ لهنَّ كلهنَّ {لستنَّ كأحدٍ من النساء إنِ اتَّقَيْتُنَّ}: الله؛ فإنَّكُنَّ بذلك تفقن النساء ولا يلحقكُنَّ أحدٌ من النساء؛ فكمِّلْنَ التقوى بجميع وسائلها ومقاصدها، فلهذا أرشدهنَّ إلى قطع وسائل المحرم، فقال: {فلا تَخْضَعْنَ بالقول}؛ أي: في مخاطبة الرجال، أو بحيث يسمعون، فَتَلِنَّ في ذلك، وتتكلَّمْنَ بكلام رقيق، يدعو ويطمع {الذي في قلبِهِ مرضٌ}؛ أي: مرض شهوة الزنا فإنه مستعدٌّ ينتظرُ أدنى محركٍ يحرِّكُه لأنَّ قلبه غيرُ صحيح؛ فإنَّ القلب الصحيح ليس فيه شهوةٌ لما حرَّم الله؛ فإنَّ ذلك لا تكاد تُميله ولا تُحركه الأسباب لصحةِ قلبه وسلامتِهِ من المرض؛ بخلاف مريض القلبِ الذي لا يتحمَّلُ ما يتحمَّلُ الصحيح، ولا يصبِرُ على ما يصبِرُ عليه؛ فأدنى سبب يوجَدُ ويدعوه إلى الحرام يُجيب دعوته ولا يتعاصى عليه؛ فهذا دليلٌ على أنَّ الوسائل لها أحكام المقاصد؛ فإنَّ الخضوع بالقول واللين فيه في الأصل مباح، ولكن لمَّا كان وسيلةً إلى المحرَّم؛ منع منه، ولهذا ينبغي للمرأة في مخاطبة الرجال أن لا تُلينَ لهم القول. ولمَّا نهاهنَّ عن الخضوع في القول؛ فربما تُوُهِّم أنهنَّ مأموراتٌ بإغلاظ القول؛ دَفَعَ هذا بقوله: {وقلنَ قولاً معروفاً}؛ أي: غير غليظ ولا جاف؛ كما أنه ليس بليِّنٍ خاضع. وتأمَّلْ كيف قال: {فلا تَخْضَعْنَ بالقول}، ولم يقل: فلا تَلِنَّ بالقول، وذلك لأنَّ المنهيَّ عنه القول الليِّن الذي فيه خضوع المرأة للرجل وانكسارُها عنده، والخاضِعُ هو الذي يُطمع فيه، بخلافِ من تكلَّمَ كلاماً ليِّناً ليس فيه خضوعٌ، بل ربَّما صار فيه ترفُّع وقهرٌ للخصم؛ فإنَّ هذا لا يطمع فيه خصمُه، ولهذا مدح الله رسولَه باللين، فقال: {فبما رحمةٍ من الله لِنتَ لهم}، وقال لموسى وهارون: {اذْهَبا إلى فرعونَ إنَّه طغى. فقولا له قَوْلاً ليِّناً لعله يَتَذَكَّر أو يخشى}. ودل قوله: {فيطمعَ الذي في قلبِهِ مرضٌ}؛ مع أمره بحفظ الفرج وثنائِهِ على الحافظين لفروجهم والحافظات، ونهيه عن قربان الزنا: أنَّه ينبغي للعبد إذا رأى من نفسه هذه الحالة، وأنه يهشُّ لفعل المحرم عندما يرى أو يسمع كلام من يهواه ويجد دواعي طمعِهِ قد انصرفتْ إلى الحرام، فليعرفْ أنَّ ذلك مرض، فليجتهدْ في إضعاف هذا المرض وحسم الخواطر الرديَّة ومجاهدة نفسه على سلامتها من هذا المرض الخطر وسؤال الله العصمة والتوفيق، وأنَّ ذلك من حفظ الفرج المأمور به.
{32} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi wake wa Nabii;" yaani, anawaambia wao wote; "Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha" Mwenyezi Mungu; na kwa kufanya hivyo, mtawapiku wanawake wengineo na hakuna hata mmoja wa wanawake atakayewafikieni. Basi kamilisheni uchamungu kwa kila njia na makusudio yake, na ndiyo maana akawaelekeza kukata njia za mambo haramu. Akasema, "Basi msilegeze sauti zenu mnapozungumza" mnapozungumza na wanaume, au hata wanapokuwa wanasikiliza, basi msiongee kwa ulaini na upole, ikachangia kutamani kwa "mwenye maradhi katika moyo wake." Yaani, mwenye ugonjwa wa matamanio ya uzinzi, kwani yuko tayari na anangoja hatua ndogo tu itakayomsisimua; kwa sababu moyo wake siyo sahihi. Kwa maana moyo ulio sawa hauna matamanio yoyote kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha. Huyo, hata hakaribii kufanywa kuelekea wala hasisimshwi na sababu za matamanio, kwa sababu moyo wake una afya nzuri na uko salama kutokana na ugonjwa. Tofauti na mgonjwa wa moyo ambaye hawezi kustahimili kile ambacho mtu mwenye moyo sahihi anaweza kustahimili, na hana subira juu ya kile anasubiri. Kwa hivyo, sababu ndogo kabisa tu inapopatikana na kumuitia kwenye yale yaliyoharamishwa, inaitikia wito wake na hauasi. Hii ni dalili kwamba njia zina masharti ya malengo. Kwani kunyenyekea kwa maneno na kuwa laini katika hilo ni jambo linaloruhusika, lakini kwa vile ni njia ya kufikia yale yaliyoharamishwa; likaharamishwa. Na kwa sababu hii mwanamke hapaswi kuwa laini anapozungumza na wanaume. Na alipowakataza kunyenyekea wanapozungumza, labda mtu anaweza kufikiria kwamba waliamrishwa kusema kwa ukali, akazuia hilo kwa kusema, "Na semeni maneno mema" yasiyokuwa makali na magumu. Na tazama jinsi alivyosema, "basi msilegeze sauti zenu mnapozungumza," wala hakusema: Msilainishe sauti zenu mnapozungumza. Hilo ni kwa sababu lililokatazwa ni maneno laini ambayo mwanamke anajilegeza kwa mwanamume na kuvunjika mbele yake, kwani aliyejilegeza ndiye anayetamaniwa, tofauti na yule anayezungumza maneno laini ambayo hayana ulegevu, na hata labda anaweza kujiinua ndani yake juu na kumshinda mpinzani wake. Huyu mpinzani wake huwa hana matumaini ya kumshinda. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamsifu Mtume wake kwamba na ulaini, akasema, "Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao." Na akawaambia Musa na Harun, "Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka. Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa." Na iliashiria kauli yake, "akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake" pamoja na amri yake ya kulinda sehemu za siri na kuwasifu kwake wale wanaolinda tupu zao wa kiume na wa kike, na kukataza kwake kuikaribia zinaa kwamba: Ikiwa mja atajiona yuko katika hali hii, na akashawishika kufanya jambo lililoharamishwa, akiona au kusikia maneno ya mtu anayemtamani na akapata kwamba sababu za matamanio yake zimeshageukia yale yaliyoharamishwa, basi na ajue kwamba huu ni ugonjwa, kwa hivyo na ajitahidi kuyadhoofisha maradhi haya, na kukata kabisa mawazo hayo mabaya, na kupambana na nafsi yake ili kuisalimisha kutokana na maradhi haya hatari, na kumuomba Mwenyezi Mungu amlinde na amuwezeshe (kujihifadhi), na kwamba hili ni katika kuhifadhi tupu ambako kuliamrishwa.
#
{33} {وقَرْنَ في بُيوتِكُنَّ}؛ أي: اقْرُرْنَ فيها؛ لأنه أسلمُ وأحفظُ لَكُنَّ، {ولا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الجاهليةِ الأولى}؛ أي: لا تُكْثِرْنَ الخروج متجمِّلات أو متطيِّبات كعادة أهل الجاهلية الأولى، الذين لا علم عندهم ولا دين؛ فكلُّ هذا دفع للشرِّ وأسبابه. ولما أمرهنَّ بالتقوى عموماً وبجزيئات من التقوى نصَّ عليها لحاجة النساء إليها، كذلك أمرهن بالطاعة، خصوصاً الصلاة والزكاة اللتان يحتاجُهما ويضطرُّ إليهما كلُّ أحدٍ، وهما أكبر العبادات وأجلُّ الطاعات، وفي الصلاة الإخلاص للمعبود، وفي الزكاة الإحسان إلى العبيد. ثم أمرهنَّ بالطاعة عموماً، فقال: {وأطِعْنَ الله ورسولَه}: يدخُلُ في طاعة الله ورسوله كلُّ أمرٍ أمرا به أمرَ إيجابٍ أو استحبابٍ، {إنَّما يريدُ الله}: بأمرِكُنَّ بما أمَرَكُنَّ به ونَهْيِكُنَّ عمَّا نهاكنَّ عنه؛ {ليُذْهِبَ عنكم الرجسَ}؛ أي: الأذى والشر والخبث {أهلَ البيتِ ويُطَهِّرَكُم تطهيراً}: حتى تكونوا طاهرينَ مطهَّرين؛ أي: فاحمدوا، ربَّكم واشكُروه على هذه الأوامر والنواهي التي أخبركم بمصلحتها، وأنها محضُ مصلحتِكُم، لم يردِ الله أن يجعلَ عليكم بذلك حرجاً ولا مشقةً، بل لتتزكَّى نفوسُكم، وتتطهَّر أخلاقُكم، وتَحْسُنَ أعمالُكم، ويعظُم بذلك أجركم.
{33} "Na kaeni majumbani kwenu" kwa sababu hilo ni salama zaidi na lenye kuwahifadhi zaidi, "wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani." Yaani, msitoke sana huku mumejipodoa au kujipaka manukato, kama ilivyokuwa desturi ya watu wa zama za ujinga wa zamani, ambao hawakuwa na elimu wala dini. Yote haya ni kwa ajili ya kuzuia uovu na sababu zake. Na alipowaamrisha uchamungu kwa ujumla, na akawaamrisha sehemu ndogo ndogo zinazoingia katika uchamungu alizozitaja hasa kwa sababu wanawake wanazihitaji, pia akawaamrisha kutii, hasa swala na zaka, ambazo kila mtu anazihitajia sana kuzifanya, na hizo ndizo ibada kubwa kabisa. Katika swala kuna ikhlas kwa anayeabudiwa, na katika zaka kuna kufanya wema kwa waja wa Mwenyezi Mungu. Kisha akawaamrisha kutii kwa ujumla, akasema, "Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake". Inaingia katika kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kila amri waliyoamrisha; ya lazima au ya kupendekezwa. "Hakika Mwenyezi Mungu anataka," kwa hayo aliyowaamrisha na akawakataza aliyowakataza, kuwaondolea uchafu enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara. Kwa hivyo, msifuni Mola wenu Mlezi na mumshukuru kwa maamrisho na makatazo haya aliyowaambia manufaa yake, na kwamba ni kwa ajili ya manufaa yenu tu. "Mwenyezi Mungu hakutaka kufanya hili kuwa gumu wala taabu kwenu, bali ni ili kuzitakasa nafsi zenu, na kusafisha tabia zenu, na kufanya matendo yenu kuwa mazuri, na ili malipo yenu yawe mengi.
#
{34} ولمَّا أمرهنَّ بالعمل الذي هو فعلٌ وتركٌ؛ أمرهنَّ بالعلم، وبيَّن لهنَّ طريقه، فقال: {واذْكُرْنَ ما يُتلى في بُيوتِكُنَّ من آياتِ الله والحكمةِ}، والمرادُ بآيات الله القرآن، والحكمةُ أسرارُه أو سنةُ رسوله، وأمْرُهُنَّ بذكره يشمل ذِكْرَ لفظِهِ بتلاوتِهِ وذكر معناه بتدبُّره والتفكُّر فيه واستخراج أحكامه وحِكَمِهِ، وذِكْرَ العمل به وتأويله. {إنَّ الله كان لطيفاً خبيراً}: يدرك سرائر الأمور وخفايا الصدور وخبايا السماواتِ والأرض والأعمال التي تَبين وتُسَرُّ؛ فلطفُه وخبرتُه يقتضي حثُّهنَّ على الإخلاص وإسرار الأعمال ومجازاةِ الله على تلك الأعمال. ومن معاني اللطيف: الذي يسوقُ عبدَه إلى الخير، ويعصِمُه من الشرِّ بطرقٍ خفيةٍ لا يشعر بها، ويسوقُ إليه من الرزق ما لا يدريه، ويريه من الأسباب التي تكرهُها النفوس، ما يكون ذلك طريقاً له إلى أعلى الدرجات وأرفع المنازل.
{34} Na alipowaamrisha kufanya matendo ambayo yanajumuisha kufanya mengine na kuacha mengine, akawaamrisha kuwa na elimu, na akawabainishia njia ya hilo, akasema, "Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hekima." Na maana ya Aya za Mwenyezi Mungu ni Qur-ani, nayo hekima ni siri zake au Sunna za Mtume wake. Na alipowaamrisha kumkumbuka hilo lilijumuisha kutaja maneno yenyewe na kwa kuisoma na kukumbuka maana yake kwa kuizingatia na kuitafakari, na kutoa humo hukumu zake na hekima zake, na kukumbuka kuifanyia kazi na kuitafsiri. "Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye habari." Anayajua mambo ya siri na yaliyofichikana katika vifua, na siri za mbinguni na ardhini, na matendo yaliyo wazi na yaliyofichwa. Kujua kwake huku kwa mambo ya siri na kuwa kwake na habari kunalazimu kuwahimiza wawe na ikhlas, na kuficha matendo yao, na kwamba Mwenyezi Mungu atalipa kwa matendo hayo. Na miongoni mwa maana za Al-Latif (Mpole au Mjuzi wa mambo ya siri) ni yule anayemuongoza mja wake kwenye heri, na akamkinga kutokana na shari kwa njia zilizofichikana ambazo hata yeye mwenyewe hazitambui, na anamletea riziki asiyoijua, na anamuonyesha njia ambazo nafsi zinazichukia, ambazo zinakuwa njia kwake kufikia daraja na vyeo vya juu zaidi.
: 35 #
{إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُمْ مَغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا (35)}
35. Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wanaume watiifu na wanawake watiifu, na wanaume wakweli na wanawake wakweli, na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanyenyekevu na wanawake wanyenyekevu, na wanaume watoao sadaka na wanawake watoao sadaka, na wanaume wanaofunga saumu na wanawake wanaofunga saumu, na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi na wanawake wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.
#
{35} لما ذَكَرَ تعالى ثوابَ زوجاتِ الرسول - صلى الله عليه وسلم - وعقابهنَّ لو قُدِّرَ عدم الامتثال وأنَّه ليس مثلهنَّ أحدٌ من النساء؛ ذكر بقيَّة النساء غيرهنَّ، ولما كان حكمهنَّ والرجال واحداً؛ جعل الحكمَ مشتركاً، فقال: {إنَّ المسلمينَ والمسلماتِ}: وهذا في الشرائع الظاهرة إذا كانوا قائمين بها، {والمؤمنينَ والمؤمناتِ}: وهذا في الأمور الباطنة من عقائد القلب وأعماله، {والقانتينَ}؛ أي: المطيعين لله ولرسوله، {والقانتاتِ والصادقينَ}: في مقالهم وفعالهم، {والصادقاتِ والصابرينَ}: على الشدائد والمصائب، {والصابراتِ والخاشعين}: في جميع أحوالهم خصوصاً في عباداتهم ولا سيما في صلواتهم، {والخاشعاتِ والمتصدِّقين}: فرضاً ونفلاً، {والمتصدقاتِ والصائمينَ والصائماتِ}: شمل ذلك الفرض والنفل، {والحافظينَ فروجَهم}: عن الزنا ومقدِّماته، {والحافظات والذاكرينَ الله كثيراً}؛ أي: في أكثر الأوقات، خصوصاً في أوقات الأوراد المقيَّدة؛ كالصباح والمساء، وأدبار الصلوات المكتوبات، {والذاكرات أعدَّ الله لهم}؛ أي: لهؤلاء الموصوفين بتلك الصفاتِ الجميلةِ والمناقبِ الجليلةِ، التي هي ما بين اعتقاداتٍ وأعمال قلوبٍ وأعمال جوارح وأقوال لسانٍ ونفع متعدٍّ وقاصرٍ وما بين أفعال الخير وترك الشرِّ الذي مَنْ قام بهنَّ فقد قام بالدِّين كلِّه ظاهرِهِ وباطنِهِ بالإسلام والإيمان والإحسان، فجازاهم على عملهم بالمغفرة لذنوبهم؛ لأنَّ الحسنات يُذْهِبْنَ السيئات. {وأجراً عظيماً}: لا يقدرُ قَدْرَهُ إلاَّ الذي أعطاه؛ مما لا عينٌ رأتْ ولا أذنٌ سمعتْ، ولا خطر على قلب بشر. نسألُ الله أن يجعلَنا منهم.
{35} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja malipo ya wake za Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na adhabu yao ikiwa itachukuliwa kwamba hawatofuata sheria na kwamba hakuna mwanamke mwingine mfano wao; akawataja wanawake wengine wasiokuwa wao, na kwa kuwa hukumu yao na ya wanaume ilikuwa sawa; akaifanya hukumu hiyo kuwa ni sawa kati yao, Kwa hivyo akasema, "Hakika waislamu wanaume na Waislamu wanawake." Haya ni katika sheria za dhahiri ikiwa watashikamana nazo, "Na Waumini wanaume na Waumini wanawake." Haya ni katika mambo yaliyofichikana ya itikadi ya moyoni na matendo yake, "na watiifu wanaume" wanaomtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "na watiifu wanawake na wakweli wanaume" katika maneno yao na vitendo vyao, "na wanawake wakweli, na wanaosubiri wanaume" katika dhiki na misiba. "na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanyenyekevu" katika hali zao zote, haswa katika ibada zao na katika Swala zao "na wanawake wanyenyekevu na wanaume watoao sadaka" ya faradhi na ya hiari. "Na wanaofunga wanaume na wanawake." Hili linajumuisha kufunga kwa faradhi na kwa hiari, "na wanaume wanaojihifadhi tupu zao" mbali na zinaa na utangulizi wake, "na wanawake wanaojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi" katika nyakati nyingi, hasa wakati wa nyiradi zilizowekewa muda maalumu; kama vile asubuhi na jioni, na baada ya Swala za faradhi. "Na wanawake wanaomdhukuru Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amewaandalia;" hawa walioelezewa kwa sifa hizo nzuri na fadhila kubwa, ambazo ni baina ya itikadi na matendo ya nyoyo na matendo ya viungo, na maneno ya ulimi, na manufaa yanayowafikia wengine yale yasiyowafikia wengine, na baina ya kutenda heri na kuacha maovu, ambayo mwenye kuyafanya, basi hakika ameitimiza dini nzima, kwa dhahiri na kwa ndani, kwa Uislamu, imani, na ihsan. Kwa hivyo akawalipa kwa matendo yao kwa kuwasamehe madhambi yao; kwa sababu matendo mema huondoa maovu. "Na malipo makubwa" ambayo hawezi kupima wingi wake isipokuwa yule aliyelipa; miongoni mwa mambo ambayo jicho halijapata kuona, wala sikio halijapata kusikia, wala hayajawahi pita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe miongoni mwao.
: 36 #
{وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا (36)}.
36. Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na hiari katika jambo lao, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri katika jambo. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.
#
{36} أي: لا ينبغي ولا يَليقُ بمن اتَّصف بالإيمان إلاَّ الإسراعُ في مرضاة الله ورسولِهِ والهربُ من سَخَطِ الله ورسوله وامتثالُ أمرِهما واجتنابُ نهيِهما؛ فلا يليقُ بمؤمنٍ ولا مؤمنةٍ، {إذا قضى اللهُ ورسولُه أمراً}: من الأمور وحَتَّما به وألزما به {أن يكون لَهُمُ الخِيَرَةُ من أمرِهم}؛ أي: الخيار هل يفعلونَه أم لا؟ بل يعلم المؤمن والمؤمنةُ أنَّ الرسول أولى به من نفسِهِ؛ فلا يجعل بعض أهواء نفسِهِ حجاباً بينَه وبينَ أمر الله ورسوله، {ومَن يعصِ الله ورسولَه فقد ضلَّ ضلالاً مبيناً}؛ أي: بيِّنًا؛ لأنه ترك الصراط المستقيم الموصلة إلى كرامة الله إلى غيرها من الطرق الموصلة للعذاب الأليم، فذكر أولاً السبب الموجب لعدم معارضةِ أمر الله ورسولِهِ، وهو الإيمان، ثم ذَكَرَ المانعَ من ذلك، وهو التخويف بالضَّلال الدالِّ على العقوبة والنكال.
{36} Yaani, haimfalii wala haifai kwa mwenye sifa ya imani isipokuwa kuharakisha kumridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuikimbia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kutii amri zao, na kuepuka makatazo yao. Kwa hivyo, haimfalii Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke, "wakati Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata jambo" miongoni mwa mambo, na wakalipitisha na kuliwajibisha, "kwamba wawe na hiari katika mambo yao." Yaani, wakawa kwamba wana hiari, je walifanye au la? Bali Muumini wa kiume na wa kike anajua kwamba Mtume ana haki zaidi kwake hata kujiliko yeye mwenyewe. Kwa hivyo, hawezi kuweka baadhi ya matamanio yake kuwa ni pazia baina yake na amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika amepotea upotofu ulio wazi." Kwa maana aliiacha njia iliyonyooka inayofikisha kwenye utukufu wa Mwenyezi Mungu na akachukua njia zingine zinazofikisha kwenye adhabu chungu, kwa hivyo akataja kwanza sababu inayolazimu kutoipinga amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo ni imani, kisha akataja kizuizi cha hilo, ambacho ni vitisho juu ya kupotoka kunakoashiria kwamba atapata adhabu na mateso.
: 37 #
{وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّهُ أَحَقُّ أَنْ تَخْشَاهُ فَلَمَّا قَضَى زَيْدٌ مِنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا وَكَانَ أَمْرُ اللَّهِ مَفْعُولًا (37)}
37. Na ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu alimneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea. Basi Zaid alipokwisha haja naye, tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapokuwa wamekwisha timiza nao shuruti za talaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
#
{37} وكان سببُ نزول هذه الآياتِ أنَّ الله تعالى أراد أن يَشْرَعَ شرعاً عامًّا للمؤمنين أنَّ الأدعياء ليسوا في حكم الأبناء حقيقةً من جميع الوجوه، وأنَّ أزواجَهم لا جُناح على مَنْ تَبَنَّاهُم نكاحهنَّ، وكان هذا من الأمور المعتادة التي لا تكاد تزولُ إلا بحادثٍ كبيرٍ، فأرادَ أن يكون هذا الشرع قولاً من رسوله وفعلاً، وإذا أراد الله أمراً؛ جعل له سبباً، فكان زيد بن حارثة يُدعى زيد بن محمد، قد تبنَّاه النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -، فصار يُدعى إليه، حتى نزل {ادْعوهم لآبائِهِم}؛ فقيل له: زيد بن حارثة، وكانت تحته زينب بنت جحش ابنة عمة رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، وكان قد وقع في قلبِ الرسول لو طلَّقها زيدٌ لتزوَّجها، فقدَّر الله أن يكون بينها وبين زيدٍ ما اقتضى أنْ جاء زيد بن حارثة يستأذنُ النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - في فراقها؛ قال الله: {وإذْ تقولُ للذي أنعمَ اللهُ عليه}؛ أي: بالإسلام، {وأنعمتَ عليه}: بالعتق والإرشاد والتعليم حين جاءك مشاوراً في فراقها، فقلتَ له ناصحاً له ومخبراً بمصلحتِهِ مقدِّماً لها على رغبتِك مع وقوعها في قلبك: {أمسِكْ عليك زَوْجَكَ}؛ أي: لا تفارِقْها واصبِرْ على ما جاءك منها. {واتَّقِ الله}: تعالى في أمورك عامَّةً وفي أمر زوجك خاصَّةً؛ فإنَّ التقوى تحثُّ على الصبر وتأمر به، {وتُخفي في نفسِكَ ما الله مُبديه}: والذي أخفاه أنَّه لو طلَّقها زيدٌ؛ لتزوَّجها - صلى الله عليه وسلم -، {وتخشى الناس}: في عدم إبداء ما في نفسك، {والله أحقُّ أن تخشاه}: فإنَّ خشيته جالبةٌ لكلِّ خيرٍ مانعةٌ من كلِّ شرٍّ، {فلما قضى زيدٌ منها وطراً}؛ أي: طابت نفسُه ورغِبَ عنها وفارقها، {زوَّجْناكها}: وإنَّما فَعَلْنا ذلك لفائدةٍ عظيمةٍ، وهي: {لكيلا يكونَ على المؤمنين حرجٌ في أزواج أدعيائِهِم}: حيث رأوك تزوَّجت زوج زيد بن حارثة الذي كان من قَبْلُ يَنْتَسِبُ إليك، ولما كان قولُه: {لِكَيْلا يكونَ على المؤمنين حرجٌ في أزواج أدعيائِهِم}: عامًّا في جميع الأحوال، وكان من الأحوال ما لا يجوز ذلك، وهي قبل انقضاء وطرِهِ منها؛ قيَّد ذلك بقوله: {إذا قَضَوْا منهنَّ وطراً وكان أمرُ الله مفعولاً}؛ أي: لا بدَّ من فعلِهِ ولا عائق له ولا مانع. وفي هذه الآيات المشتملات على هذه القصة فوائد: منها: الثناءُ على زيد بن حارثة، وذلك من وجهين: أحدِهما: أنَّ الله سمَّاه في القرآن ولم يسمِّ من الصحابة باسمه غيره. والثاني: أنَّ الله أخبر أنَّه أنعم عليه؛ أيْ: بنعمة الإسلام والإيمان، وهذه شهادةٌ من الله له أنه مسلم مؤمنٌ ظاهراً وباطناً، وإلاَّ؛ فلا وجه لتخصيصه بالنعمة؛ إلاَّ أنَّ المراد بها النعمة الخاصة. ومنها: أن المُعْتَقَ في نعمة المعتِقِ. ومنها: جواز تزوج زوجة الدَّعي كما صرح به. ومنها: أنَّ التعليم الفعليَّ أبلغُ من القولي، خصوصاً إذا اقترن بالقول؛ فإنَّ ذلك نورٌ على نور. ومنها: أن المحبة التي في قلب العبد لغير زوجته ومملوكته ومحارمه إذا لم يَقْتَرِنْ بها محذورٌ لا يأثم عليها العبد، ولو اقترن بذلك أمنيته أنْ لو طلَّقها زوجُها لتزوَّجها من غير أن يسعى في فرقةٍ بينَهما أو يتسبَّب بأيِّ سبب كان؛ لأنَّ الله أخبر أنَّ الرسول - صلى الله عليه وسلم - أخفى ذلك في نفسه. ومنها: أنَّ الرسول - صلى الله عليه وسلم - قد بلَّغَ البلاغَ المبين، فلم يدعْ شيئاً مما أوحي إليه إلاَّ وبلَّغه، حتى هذا الأمر الذي فيه عتابه، وهذا يدلُّ على أنَّه رسولُ الله، ولا يقول إلاَّ ما أوحي إليه، ولا يريد تعظيمَ نفسِهِ. ومنها: أنَّ المستشارَ مؤتمنٌ، يجبُ عليه ـ إذا استُشير في أمر من الأمور ـ أن يُشير بما يعلمُه أصلَح للمستشيرِ ، ولو كان له حظُّ نفس بتقدُّم مصلحة المستشير على هوى نفسه وغرضه. ومنها: أنَّ من الرأي الحسن لمن استشار في فراق زوجة أن يُؤْمَرَ بإمساكها مهما أمكن صلاحُ الحال؛ فهو أحسن من الفرقة. ومنها: أنَّه يتعيَّن أن يقدِّم العبد خشية الله على خشية الناس، وأنَّها أحقُّ منها وأولى. ومنها: فضيلةُ زينب رضي الله عنها أم المؤمنين؛ حيث تولَّى الله تزويجها من رسوله - صلى الله عليه وسلم - من دون خطبة ولا شهودٍ، ولهذا كانت تفتخرُ بذلك على أزواج رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، وتقول: زوَّجَكُنَّ أهاليكنَّ وزوَّجَني الله من فوق سبع سماواتٍ. ومنها: أنَّ المرأة إذا كانت ذات زوج لا يجوزُ نِكاحها ولا السعيُ فيه وفي أسبابه حتى يقضِيَ زوجُها وَطَرَهُ منها، ولا يقضي وَطَرَهُ حتى تنقضيَ عِدَّتُها؛ لأنَّها قبل انقضاء عدتها وهي في عصمتِهِ أو في حقِّه الذي له وطرٌ إليها ولو من بعض الوجوه.
{37} Sababu ya kuteremshwa aya hizi ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kutunga sheria ya jumla kwa waumini, kwamba wana wa kupanga si wana wa mtu wa kihakika kwa namna yoyote ile, na kwamba hakuna lawama kwa wale waliowapanga kuwaoa wake zao. Na hili lilikuwa ni miongoni mwa mambo ya kawaida ambayo ilikuwa vigumu sana kuliondoa isipokuwa kwa tukio kubwa. Kwa hivyo, akataka kwamba sheria hii isemwe na Mtume wake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu anapotaka jambo, analiwekea sababu zake. Na Zaid bin Haritha alikuwa akiitwa Zaid bin Muhammad, kwani Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa kamchukua kama mwana wa kupanga, kwa hivyo akaanza kunasibishwa naye. Mpaka ikashuka kauli yake, "Waiteni kwa baba zao," basi ndiyo wakaanza kumuita: Zaid bin Haritha. Naye alikuwa amemuoa Zainab bint Jahsh, binti ya ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Naye Mtume alikuwa imemuingia kwenye moyo wake kwamba ikiwa Zaid atamtaliki, basi yeye atamuoa. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akapitisha kwamba yawe baina yake na Zaid yale yaliyomhitaji Zaid bin Haritha aje kumuomba ruhusa Nabii, -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ya kuachana naye. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na ulipomwambia yule Mwenyezi Mungu aliyemneemesha" kwa Uislamu, "nawe ukamneemesha" kwa kumkomboa utumwani, na ukamwongoza na kumuelimisha alipokujia akitafuta nasaha kuhusu kuachana naye, basi ukamwambia ukimnasihi na kumpa habari yenye masilahi kwake, huku ukiyatanguliza hayo mbele ya ulichokuwa unatamani na tayari kilikuwa kimeshaingia moyoni mwako, "Shikamana na mkeo" na usiachane naye, na subiri kwa yale yanayokujia kutoka kwake. "Na mche Mwenyezi Mungu" Mtukufu katika mambo yako kwa ujumla na mambo ya mkeo hasa. Kwani uchamungu unahimiza na unaamrisha kuwa na subira, "Na ukaficha nafsini mwako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyafichua." Na kile alichoficha ni kwamba ikiwa Zaid alimtaliki, basi yeye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, angemuoa. "Nawe ukawachelea watu" kwa kutodhihirisha yaliyomo katika nafsi yako, "hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea." Kwani, kumchelea Yeye kunaleta heri zote na kunazuia maovu yote. "Basi Zaid alipokwisha haja naye" na nafsi yake ikawa nzuri, na akawa hamtaki tena, na akatengana naye; "tulikuoza wewe." Lakini tulifanya hivyo kwa ajili ya manufaa makubwa, nayo ni "ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga;" pale walipokuona umemuoa mke wa Zaid bin Haritha, ambaye hapo zamani alikuwa akinasibishwa nawe. Na pindi ilipokuwa kauli yake, "ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga" ni ya jumla katika hali zote, na ikawa kwamba miongoni mwa hali hizo kuna zile ambazo haziruhusiwi, nayo ni ikiwa kipindi cha eda hakijakamilika, akalizuilia hilo kwa kusema, "watapokuwa wamekwisha timiza nao sharti za talaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa." Yaani, ni lazima ifanyike na hakuna chochote kinachoweza kuizuia. Kuna faida mbalimbali katika aya hizi zenye hadithi hii: Miongoni mwake ni kusifiwa Zaid bin Haritha, na hilo ni kwa njia mbili: Ya kwanza ni kwamba Mwenyezi Mungu alimtaja katika Qur-ani na hakuna Swahaba yeyote asiyekuwa yeye aliyewahi kutajwa kwa jina lake. Ya pili ni kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia kwamba alimneemesha, yaani kwa neema ya Uislamu na imani. Na huu ni ushahidi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwake kwamba yeye ni Mwislamu, Muumini kwa nje na ndani. Vinginevyo, basi hakuna sababu ya kumfanya kuwa maalumu katika neema hii. Hata hivyo, kilimaanishwa na neema hii ni neema maalumu. Na miongoni mwake ni kwamba aliyekombolewa utumwani yuko katika neema ya aliyemkomboa. Na miongoni mwake ni kwamba inaruhusika kumuoa mke wa mwana wa kupanga, kama ilivyokuja hivyo waziwazi katika Qur-ani. Na miongoni mwake ni kwamba kufundisha kwa matendo kunaathiri zaidi kuliko kuzungumza tu, hasa ikiwa matendo hayo yanaambatana na maneno. Hayo ni nuru juu ya nuru. Na miongoni mwake ni kwamba mapenzi yaliyomo moyoni mwa mja kwa asiyekuwa mke wake, wajakazi wake na maharimu wake ikiwa hayaambatani na kitu chochote kilichoharamishwa, basi mja hapati dhambi juu yake, na hata kama yataambatana na matamanio yake kwamba ikiwa mume wake atamtaliki, basi atamuoa bila ya yeye kufanya juhudi ya kuwatenganisha au kusababisha hili kupitia sababu yoyote ile. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alificha hilo ndani ya nafsi yake. Na miongoni mwake ni kwamba Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yakee – alifikisha ujumbe kwa njia iliyo wazi, na hakuacha chochote katika yale aliyoteremshiwa isipokuwa alikifikisha, hata jambo hili ambalo analaumiwa ndani yake. Na hili linaashiria kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na hasemi isipokuwa yale yaliyoteremshwa kwake tu, wala hataki kujitukuza. Na miongoni mwake ni kwamba mshauri anachukuliwa kwamba amechukua amana, na ni wajibu kwake anapotakwa ashauri katika jambo kwamba atoe ushauri ambao ni wenye masilahi zaidi kwa anayeshauriwa, hata kama ana haki yake fulani katika kuyapa kipaumbele masilahi ya mshauriwa juu ya matamanio yake na makusudio yake. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye kuona kwamba ni rai nzuri kwa mtu anayeomba ushauri kuhusu kutengana na mke, kwamba amuamrishe kumshikilia mkewe kwa njia zote zinazowezekana za kusuluhisha hali yao hiyo, basi hilo ni bora kuliko kuachana. Na miongoni mwake ni lazima kwa mja kutanguliza suala la kumhofu Mwenyezi Mungu mbele ya kuwahofu watu, na kwamba kumhofu Mwenyezi Mungu kustahiki zaidi na muhimu zaidi. Na miongoni mwake ni ubora wa Zainab, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, mama wa Waumini. Kwa vile Mwenyezi Mungu mwenyewe alisimamia suala la kumuozesha kwa Mtume wake, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – bila ya posa wala mashahidi, na ndiyo maana alikuwa akijivunia hilo mbele ya wake za Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na anasema, 'Watu wenu waliwaozesha nyinyi, lakini mimi Mwenyezi Mungu ndiye aliyeniozesha kutokea juu ya mbingu saba.' Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa mwanamke ana mume, hairuhusiwi kumuoa, wala kufanya juhudi katika kumfikia wala hata kwa kufanya sababu zake mpaka mumewe ajitimizie matamanio yake kwake, na hilo halitimii pia hadi muda wake wa eda umalizike. Kwa sababu kabla ya kumalizika eda, mke huyu huwa bado yuko chini ya ulinzi wa mumewe au chini ya haki yake hata ikiwa ni kwa njia fulani tu.
: 38 - 39 #
{مَا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّهُ لَهُ سُنَّةَ اللَّهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلُ وَكَانَ أَمْرُ اللَّهِ قَدَرًا مَقْدُورًا (38) الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّهَ وَكَفَى بِاللَّهِ حَسِيبًا (39)}
38. Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyomhalalishia Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa wale waliopita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni mipango iliyokwisha pangwa. 39. Hao wa zamani, waliokuwa wakifikisha jumbe za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.
#
{38} هذا دفعٌ لطعن من طعن في الرسول - صلى الله عليه وسلم - في كثرة أزواجه، وأنَّه طعنٌ بما لا مطعنَ فيه، فقال: {ما كان على النبيِّ من حرجٍ}؛ أي: إثم وذنب {فيما فَرَضَ الله له}؛ أي: قدَّر له من الزوجات؛ فإنَّ هذا قد أباحه الله له كما أباحه للأنبياء قبلَه، ولهذا قال: {سنةَ الله في الذين خَلَوا من قبلُ وكان أمرُ الله قَدَراً مَقْدوراً}؛ أي: لا بدَّ من وقوعِهِ.
{38} Haya ni kuzuia kashfa za wale waliomkashifu Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kuhusu kuoa kwake wake wengi, na kwamba ni kumkashifu kwa kisichofaa kuwa kashfa. Akasema, "Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyomhalalishia Mwenyezi Mungu," kwani aliruhusiwa hili na Mwenyezi Mungu kama vile alivyowaruhusu Manabii waliokuwa kabla yake. Na ndiyo maana akasema, "Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa wale waliopita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni mipango iliyokwisha pangwa;" na ni lazima itokee.
#
{39} ثم ذَكَرَ مَنْ هم الذين من قبلُ قد خلو وهذه سنتهم وعادتهم، وأنهم {الذين يبلِّغونَ رسالاتِ الله}: فيتلون على العباد آياتِ الله وحججه وبراهينه ويدعونَهم إلى الله، {ويَخْشَوْنَه}: وحدَه لا شريك له، {ولا يَخْشَوْنَ أحداً}: إلاَّ الله؛ فإذا كان هذا سنة في الأنبياء المعصومين الذين وظيفتهم قد أدَّوْها وقاموا بها أتم القيام، وهو دعوةُ الخلق إلى الله والخشية منه وحده، التي تقتضي فعل كل مأمور وترك كل محظور، [دلّ ذلك على أنه لا نقص فيه بوجه]. {وكفى بالله حسيباً}: محاسباً عبادَه مراقباً أعمالهم. وعُلِمَ من هذا أنَّ النكاحَ من سنن المرسلين.
{39} Kisha akawataja wale waliokwisha pita, na kwamba hii ndiyo ada yao na desturi yao, na kwamba wao "ndio waliokuwa wakifikisha jumbe za Mwenyezi Mungu," na wanawasomea waja Aya za Mwenyezi Mungu na hoja zake, na wanawalingania kwa Mwenyezi Mungu, “na wanamwogopa Yeye" peke yake bila ya mshirika yeyote; “wala hawamwogopi yeyote” isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi ikiwa hii ndiyo desturi ya Mitume maasumu waliotekeleza majukumu yao kwa ukamilifu zaidi, ambayo ni kuwalingania viumbe kwa Mwenyezi Mungu na kumcha Yeye pekee, jambo ambalo linahitaji kufanya kila lililoamrishwa na kuacha kila jambo lililokatazwa, [hilo linaashiria kwamba hakuna upungufu wowote ndani yake kwa njia yoyote ile]. "Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu." Atawahasibu waja wake na anawaangalia vitendo vyao. Na inafahamika kutokana na hili kwamba kuoa ni miongoni mwa ada za Mitume.
: 40 #
{مَا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِنْ رِجَالِكُمْ وَلَكِنْ رَسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا (40)}
40. Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
#
{40} أي: لم يكن الرسول {محمدٌ}: - صلى الله عليه وسلم - {أبا أحدٍ من رجالِكم}: أيُّها الأمة، فقطع انتساب زيد بن حارثة منه من هذا الباب. ولما كان هذا النفيُ عامًّا في جميع الأحوال إنْ حُمِلَ ظاهر اللفظ على ظاهره؛ أي: لا أبوَّة نسب ولا أبوَّة ادعاء، وكان قد تقرَّر فيما تقدَّم أنَّ الرسول - صلى الله عليه وسلم - أبٌ للمؤمنين كلِّهم، وأزواجَه أمهاتُهم، فاحترز أن يدخُل هذا النوع بعموم النهي المذكور؛ فقال: {ولكن رسولَ الله وخاتَمَ النبيينَ}؛ أي: هذه مرتبته؛ مرتبةُ المطاع المتبوع المهتدَى به الْمُؤْمَنِ له الذي يجبُ تقديم محبته على محبة كلِّ أحدٍ، الناصح، الذي لهم ـ أي: للمؤمنين ـ من بره ونُصحه كأنه أبٌ لهم، {وكان الله بكل شيءٍ عليماً}؛ أي: قد أحاط علمُه بجميع الأشياء، ويعلم حيث يجعل رسالاتِهِ، ومن يَصْلُحُ لفضله ومَنْ لا يَصْلُح.
{40} Yaani, hakuwa Mtume "Muhammad" - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - "baba ya yeyote katika wanaume wenu" enyi umma! Kwa hivyo, hili likakata suala la Zaid bin Haritha kunijasibisha kwake kinasaba kwa mtazamo huu. Kwa kuwa ukanusho huu ni wa jumla katika hali zote, ikiwa maana dhahiri ya neno hilo itachukuliwa jinsi inavyoonekana. Yaani, hakuna ubaba kwa nasaba wala wa kupanga, na tayari ilishathibiti hapo awali kuwa Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ni baba wa Waumini wote, na wake zake ni mama zao, basi akaifanya maana hii kutoingia katika katazo hili la ujumla. Akasema, "bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii." Yaani hiki ndicho cheo chake, cheo cha anayetiiwa, anayefuatwa, anayeigwa katika kuongoka, aliyepewa amana, ambaye ni lazima kutanguliza kumpenda kuliko kumpenda mtu yeyote yule. Naye pia ni mshauri ambaye yeye kwa Waumini ni mwema na mwenye kuwanasihi kama kwamba yeye ni baba yao. "Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu." Ilikwisha zunguka elimu yake kila kitu, na anajua ni wapi anauweka ujumbe wake, na ni nani anayefaa fadhila zake, na ni nani asiyefaa.
: 41 - 44 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْرًا كَثِيرًا (41) وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا (42) هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا (43) تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا (44)}.
41. Enyi mlioamini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru. 42. Na mtakaseni asubuhi na jioni. 43. Yeye ndiye anayekurehemuni na Malaika wake ili akutoeni gizani hadi kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu sana Waumini. 44. Maamkizi yao siku ya kukutana naye yatakuwa Salama! Na amewaandalia malipo ya ukarimu.
#
{41} يأمر تعالى المؤمنين بذكره ذكراً كثيراً؛ من تهليل وتحميد وتسبيح وتكبير وغير ذلك من كل قولٍ فيه قُربة إلى الله، وأقلُّ ذلك أن يلازِمَ الإنسان أوراد الصباح والمساء وأدبار الصلوات الخمس وعند العوارضِ والأسباب، وينبغي مداومة ذلك في جميع الأوقات على جميع الأحوال؛ فإنَّ ذلك عبادةٌ يسبِقُ بها العامل وهو مستريحٌ وداعٍ إلى محبة الله ومعرفتِهِ وعونٌ على الخير وكفٌّ للسان عن الكلام القبيح.
{41} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waumini wamtaje kwa wingi; kama vile kufanya tahlil (kusema: hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu), na kusifu, na kumtakasa, na kusema kwamba Yeye ndiye mkubwa na maneno mengineyo ambayo yanamleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu. Na hali ya chini zaidi katika hayo ni mtu kudumu katika kufanya nyiradi za asubuhi na jioni, na baada ya swala tano za kila siku, na pindi kunapokuwa na haja na sababu za kufanya hivyo. Na inapasa kuyadumisha haya katika nyakati zote na katika hali zote. Kwani, hii ni ibada ambayo mtendaji anatangulia mbele hali ya kuwa amestarehe tu, nayo inaitia kwenye upendo wa Mwenyezi Mungu na kumjua, na pia inasaidi mtu juu ya mambo ya heri, na kuuzuia ulimi usiseme maovu.
#
{42} {وسبِّحوه بكرةً وأصيلاً}؛ أي: أول النهار وآخره؛ لفضلهما وشرفهما وسهولة العمل فيهما.
{42} "Na mtakaseni asubuhi na jioni." Yaani, mwanzo wa siku na mwisho wake, kwa sababu ya ubora wake, utukufu wake, na urahisi wa kufanya matendo mema ndani yake.
#
{43} {هو الذي يصلِّي عليكُم وملائكتُه ليخرِجَكم من الظلماتِ إلى النور وكان بالمؤمنين رحيماً}؛ أي: من رحمته بالمؤمنين ولطفه بهم أنْ جَعَلَ من صلاتِهِ عليهم وثنائِهِ وصلاةِ ملائكته ودعائهم ما يخرِجُهم من ظلمات الذُّنوب والجهل إلى نورِ الإيمان والتوفيق والعلم والعمل؛ فهذه أعظمُ نعمةٍ أنعم بها على العباد الطائعين، تستدعي منهم شكرها والإكثار من ذكر الله الذي لطف بهم ورحمهم وجعل حملةَ عرشهِ أفضل الملائكة ومن حوله يسبِّحون بحمدِ ربِّهم، ويستغفرونَ للذين آمنوا، فيقولون: {ربَّنا وسعتَ كلَّ شيءٍ رحمةً وعلماً فاغفر للذين تابوا واتَّبَعوا سبيلَكَ وقِهِمْ عذابَ الجحيم. ربَّنا وأدْخِلْهم جناتِ عدنٍ التي وَعَدْتَهم ومَن صَلَحَ من آبائهم وأزواجهم وذُرِّيَّاتِهِم إنَّك أنت العزيزُ الحكيم. وقِهِمُ السيئاتِ ومَن تَقِ السيئاتِ يومئذٍ فقد رَحِمْتَه وذلك الفوزُ العظيم}: فهذه رحمتُه ونعمتُه عليهم في الدُّنيا.
{43} "Yeye ndiye anayekurehemuni na Malaika wake ili akutoeni gizani hadi kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu sana Waumini." Yaani, katika rehema zake kwa Waumini na upole wake kwao ni kwamba anawaswalia na kuwasifu, na pia amefanya swala za Malaika wake na dua zao kwao kuwa ni jambo linalowatoa katika giza la madhambi na ujinga hadi kwenye nuru ya imani, mafanikio, maarifa, na matendo mazuri. Hii ndiyo neema kubwa zaidi aliyowapa waja wake watiifu ambayo inawataka kushukuru kwayo na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi, ambaye alifanyia upole na kuwarehemu, na akawafanya wabebaji wa kiti chake cha enzi ambao ndio Malaika bora, na wale walio pembezoni mwake kumtakasa Mola wao Mlezi na kumsifu, na wanawaombea msamaha wale walioamini, na wanasema, "Mola wetu Mlezi, umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe waliotubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu. Mola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi. Na uwape haya pia wale waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuria zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa.
#
{44} وأما رحمتُه بهم في الآخرة؛ فأجلُّ رحمة وأفضلُ ثواب، وهو الفوز برضا ربِّهم وتحيَّته، واستماع كلامه الجليل، ورؤية وجهِهِ الجميل، وحصول الأجر الكبير الذي لا يدريه ولا يعرِفُ كُنْهَهُ إلاَّ من أعطاهم إياه، ولهذا قال: {تحيَّتُهم يوم يَلْقَوْنَه سلامٌ وأعدَّ لهم أجراً كريماً}.
{44} Na ama rehema yake juu yao katika Akhera, hiyo ndiyo rehema kubwa kabisa na malipo bora zaidi, ambayo ni kufuzu kupata ridhaa ya Mola wao Mlezi na maakizi yake, na kusikiliza maneno yake matukufu, na kuuona uso wake mzuri, na kupata malipo makubwa ambayo hapana ajuaye uhalisia wake isipokuwa wale atakayewalipa kwa hayo. Na ndiyo maana akasema: "Maamkizi yao siku ya kukutana naye yatakuwa Salama! Na amewaandalia malipo ya ukarimu."
: 45 - 48 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا (45) وَدَاعِيًا إِلَى اللَّهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُنِيرًا (46) وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُمْ مِنَ اللَّهِ فَضْلًا كَبِيرًا (47) وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ وَكِيلًا (48)}
45. Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji. 46. Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru. 47. Na wabashirie Waumini ya kwamba wana fadhila kubwa inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. 48. Wala usiwatii makafiri na wanafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa.
#
{45} هذه الأشياء التي وصف الله بها رسولَه محمداً - صلى الله عليه وسلم - هي المقصود من رسالتِهِ وزبدتها وأصولها التي اختصَّ بها، وهي خمسةُ أشياء: أحدها: كونُه {شاهداً}؛ أي: شاهداً على أمته بما عملوه من خيرٍ وشرٍّ؛ كما قال تعالى: {لِتكونوا شهداءَ على الناس ويكون الرسولُ عليكم شهيداً}، {فكيف إذا جئنا من كلِّ أمةٍ بشهيدٍ [وجئنا بك على هؤلاء شهيداً]}: فهو - صلى الله عليه وسلم - شاهدُ عدل مقبول. الثاني والثالث: كونه {مبشِّراً ونذيراً}: وهذا يستلزم ذكر المبشَّر والمنذَر وما يبشَّر به ويُنْذَرُ والأعمال الموجبة لذلك: فالمبشَّر هم المؤمنون المتقون، الذين جمعوا بين الإيمان والعمل الصالح وترك المعاصي، لهم البُشرى في الحياة الدنيا بكل ثواب دنيويٍّ ودينيٍّ رُتِّبَ على الإيمان والتقوى، وفي الأخرى بالنعيم المقيم، وذلك كلُّه يستلزم ذكر تفصيل المذكور من تفاصيل الأعمال وخصال التقوى وأنواع الثواب. والمنذَر هم المجرمون الظالمون، أهلُ الظلم والجهل، لهم النذارةُ في الدنيا من العقوبات الدنيويَّة والدينيَّة المرتَّبة على الجهل والظلم، وفي الأخرى بالعقاب الوبيل والعذاب الطويل. وهذه الجملة تفصيلُها ما جاء به - صلى الله عليه وسلم - من الكتاب والسنَّة المشتمل على ذلك.
{45} Mambo haya ambayo Mwenyezi Mungu amemuelezea Mtume wake Muhammad, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ndiyo yaliyokusudiwa katika kutumwa kwake, na ndiyo mambo bora zaidi, na msingi wake ambayo alipewa yeye tu. Nayo ni mambo matano. La kwanza ni kwamba yeye ni "shahidi" atakayeshuhudia kwa umma wake kwa mema na mabaya waliyoyafanya, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu." "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa?" Yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ni shahidi, mwadilifu, anayekubalika. La pili na la tatu ni kwamba yeye ni "mbashiri na mwonyaji." Na hili linalazimu kutajwa mwenye bishara na muonyaji, na kinachobashiriwa na kuonywa dhidi yake, na vitendo vinavyopelekea hayo. Wenye kubashiriwa hapa ni Waumini wachamungu, waliojumuisha kati ya imani na matendo mema na kuacha madhambi. Hao wanayo habari njema katika maisha ya dunia hii kwamba watapata malipo yote ya kidunia na ya kidini ambayo yanatokana na imani na uchamungu, na huko akhera watapata neema ya milele. Na yote hayo yanahitaji kutaja maelezo kina ya vitendo vilivyotajwa, sifa za uchamungu na aina za malipo. Nao wanaoonywa ni wahalifu madhalimu, watu wa dhuluma na ujinga. Wanaonywa katika dunia hii juu ya adhabu za kidunia na za kidini zinazotokana na ujinga na dhuluma, na huko akhera wana adhabu kali na ndefu. Na hili limefafanuliwa kwa kina katika yale aliyoyaleta Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - kutoka katika Qur-ani na Sunna ambayo yamejumuisha haya yote.
#
{46} الرابع: كونُه {داعياً إلى الله}؛ أي: أرسله الله يدعو الخلق إلى ربِّهم ويشوِّقُهم لكرامته ويأمُرُهم بعبادتِهِ التي خُلقوا لها، وذلك يستلزم استقامتَه على ما يدعو إليه وذِكْرَ تفاصيل ما يدعو إليه؛ بتعريفهم لربِّهم بصفاتِهِ المقدَّسة، وتنزيهه عما لا يَليق بجلالِهِ، وذكر أنواع العبوديَّة، والدعوة إلى الله بأقرب طريق موصل إليه، وإعطاء كلِّ ذي حقٍّ حقَّه، وإخلاص الدَّعوة إلى الله لا إلى نفسه وتعظيمها؛ كما قد يعرضُ ذلك لكثير من النفوس في هذا المقام، وذلك كلُّه بإذن ربه له في الدعوة وأمره وإرادتِهِ وقدره. الخامس: كونه {سراجاً منيراً} وذلك يقتضي أنَّ الخلق في ظلمة عظيمة، لا نور يُهتدى به في ظلماتها، ولا علم يُستدلُّ به في جهاتها، حتى جاء الله بهذا النبيِّ الكريم، فأضاء الله به تلك الظلمات، وعلَّم به من الجهالات، وهدى به ضلالاً إلى الصراط المستقيم، فأصبح أهل الاستقامة قد وَضَحَ لهم الطريق، فَمَشَوْا خلف هذا الإمام، وعرفوا به الخير والشرَّ وأهلَ السعادة من أهل الشقاوة، واستناروا به لمعرفةِ معبودِهم، وعرفوه بأوصافِهِ الحميدةِ وأفعالِهِ السَّديدة وأحكامه الرشيدة.
{46} La nne ni kwamba yeye ni "mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu," ili avilinganie viumbe kwa Mola wao Mlezi, na awape shauku juu ya utukufu wake, na awaamrishe kumwabudu Yeye; jambo ambalo waliumbwa kwa ajili yake. Na hili linamlazimu kudumu katika yale anayolingania, na kutaja kwa kina yale anayolingania, kwa kuwajulisha Mola wao Mlezi kwa sifa zake takatifu, na kumtakasa mbali na yasiyoufailia utukufu wake, na kutaja aina za uja, na kulingania kwa Mwenyezi Mungu kwa njia iliyo karibu zaidi katika kufikisha kwake, na kumpa kila mwenye haki haki yake, na kumkusudia Mwenyezi Mungu tu katika kulingania kwake si kujilingania kwake mwenyewe na kujitukuza, kama linavyoweza hili kuzitokea nafsi nyingi katika nafsi hii. Na yote haya ni baada ya kuidhinishwa na Mola wake Mlezi ili alinganie, na ni amri yake, utashi wake, na mipango yake. Ya tano ni kwamba yeye ni "taa yenye kutoa nuru." Na hili linalazimu kwamba viumbe viko katika giza kuu, bila nuru ya kuviongoza katika giza lao, na hakuna elimu ya kuvionyesha kitu katika pande zake, mpaka Mwenyezi Mungu alipomleta Nabii huyu mtukufu. Kwa hivyo, akaangaza giza hilo kupitia kwake, akafundisha yenye kuondoa ujinga kupitia kwake, na akaongoza kwaye hadi kwenye njia iliyonyooka, kwa hivyo njia ikawawia wazi watu wanyoofu, basi wakatembea nyuma ya Imam huyu, na kwaye wakatambua heri na shari , na pia wakajulikana watu wa furahani mbali na watu wa mashakani, na wakajiangaza kwake katika kulijua mwabudiwa wao, na wakamjua kwa sifa zake za kusifiwa, na matendo yake sahihi, na hukumu zake za busara.
#
{47} وقوله: {وبشِّرِ المؤمنين بأنَّ لهم من الله فضلاً كبيراً}: ذكر في هذه الجملة المبشَّر، وهم المؤمنون، وعند ذِكْرِ الإيمان بمفردِهِ تدخُلُ فيه الأعمال الصالحة، وذَكَرَ المبشَّر به، وهو الفضلُ الكبيرُ؛ أي: العظيم الجليل الذي لا يقادَر قَدْرُهُ من النصر في الدنيا وهداية القلوب وغفران الذنوب وكشف الكروب وكثرة الأرزاق الدارَّة وحصول النعم السارَّة والفوز برضا ربِّهم وثوابه والنجاة من سخطه وعقابِهِ، وهذا مما ينشِّطُ العاملين أن يذكُرَ لهم من ثواب الله على أعمالهم ما به يستعينونَ على سلوك الصراط المستقيم، وهذا من جملةِ حِكَم الشرع: كما أنَّ من حِكَمه أن يَذْكُرَ في مقام الترهيب العقوباتِ المرتَّبةَ على ما يُرَهَّبُ منه؛ ليكون عوناً على الكفِّ عما حرم الله.
{47} Na katika kauli yake, "Na wabashirie Waumini ya kwamba wana fadhila kubwa inayotoka kwa Mwenyezi Mungu" akataja wale wanaobashiriwa - nao ni Waumini. Inapotajwa imani peke yake, yanaingia humo matendo mema yote. Na pia akataja kile wanachobashiriwa ambacho ni fadhila kubwa, ambayo haiwezi kupimwa, kama vile kupewa ushindi katika dunia hii, kuziongoa nyoyo, kusamehewa dhambi, kuondolewa dhiki, kuruzukiwa kwa wingi, kupata neema za kufurahisha, kufikia ridhaa ya Mola wao Mlezi, na malipo yake na kuokolewa kutokana na ghadhabu yake na adhabu yake. Na hili ni katika mambo yanayowakakamua watendaji matendo wanapotajiwa malipo ya Mwenyezi Mungu kwa matendo yao, jambo ambalo kwalo wanajisaidia katika kufuata njia iliyonyooka. Na hili ni miongoni mwa hekima za Sheria. Kama vile miongoni mwa hekima zake ni kutaja katika muktadha wa kutishia adhabu zinazompata mtu anapofanya hayo anayotishiwa nayo, ili hilo limsaidie katika kujizuia dhidi ya yale ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha.
#
{48} ولمَّا كان ثَمَّ طائفةٌ من الناس مستعدةٌ للقيام بصدِّ الداعين إلى الله من الرسل وأتباعهم، وهم المنافقون الذين أظهروا الموافقةَ في الإيمان وهم كفرةٌ فجرةٌ في الباطن، والكفار ظاهراً وباطناً؛ نهى الله رسوله عن طاعتهم وحذره ذلك، فقال: {ولا تطع الكافرينَ والمنافقينَ}؛ أي: في كلِّ أمر يصدُّ عن سبيل الله، ولكن لا يقتضي هذا أذاهم، بل لا تُطِعْهُم، {ودَعْ أذاهم}: فإنَّ ذلك جالبٌ لهم وداعٍ إلى قبول الإسلام وإلى كفِّ كثير من أذيَّتِهِم له ولأهله، {وتوكَّلْ على الله}: في إتمام أمرِكَ وخذلانِ عدوِّك، {وكفى بالله وكيلاً}: تُوكَلُ إليه الأمور المهمَّة، فيقوم بها ويسهِّلُها على عبده.
{48} Na kwa kuwa lipo kundi la watu ambalo liko tayari kuwazuilia wale wanaolingania kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na wafuasi wao, nao ni wanafiki waliodhihirisha kwamba wanaafikiana na waumini katika imani, ingawa wao ni makafiri, waovu kwa ndani, na ni makafiri kwa nje na ndani. Mwenyezi Mungu akamkataza Mtume wake kuwatii na akamtahadharisha na hilo akisema, "Wala usiwatii makafiri na wanafiki" katika kila jambo linalomzuilia mtu na njia ya Mwenyezi Mungu, lakini hili halihitaji kuwadhuru, bali usiwatii tu, "na usijali udhia wao;" kwani hili litawafanya na kuwaitia kuukubali Uislamu na kuzuia mengi ya maudhi yao juu yake na juu ya familia yake. "Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu" katika kukamilisha jambo lako, na kumuangusha adui yako; "Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa," ambaye anaachiwa mambo muhimu, kwa hivyo akayasimamia na kumfanyia mja wake kuwa mepesi.
: 49 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِنْ قَبْلِ أَنْ تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا (49)}
49. Enyi mlioamini, mkiwaoa wanawake, Waumini, kisha mkawapa talaka kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayohesabu. Basi wapeni cha kuwaliwaza, na muwaache kwa wema.
#
{49} يخبر تعالى المؤمنين أنَّهم إذا نكحوا المؤمنات ثم طلَّقوهنَّ من قبل أن يَمَسُّوهنَّ؛ فليس عليهنَّ في ذلك عدَّةٌ يعتدُّها أزواجهنَّ عليهن، وأمرهم بتمتيعهنَّ بهذه الحالة بشيء من متاع الدُّنيا الذي يكون فيه جبرٌ لخواطرهنَّ لأجل فراقهنَّ، وأن يفارِقوهنَّ فراقاً جميلاً من غير مخاصمةٍ ولا مشاتمةٍ ولا مطالبةٍ ولا غير ذلك. ويستدلُّ بهذه الآية على أنَّ الطلاق لا يكونُ إلاَّ بعد النكاح، فلو طلَّقها قبل أن ينكحَها أو علَّق طلاقَها على نكاحها؛ لم يقع؛ لقوله: {إذا نَكَحْتُمُ المؤمناتِ ثم طلَّقْتُموهنَّ}، فجعل الطلاق بعد النكاح، فدل على أنَّه قبل ذلك لا محلَّ له. وإذا كان الطلاق الذي هو فرقةٌ تامةٌ وتحريمٌ تامٌّ لا يقع قبل النكاح؛ فالتحريمُ الناقص لظهارٍ أو إيلاءٍ ونحوه من باب أولى وأحرى أن لا يقعَ قبل النكاح؛ كما هو أصحُّ قولي العلماء. و [يدل] على جواز الطلاق لأنَّ الله أخبر به عن المؤمنين على وجهٍ لم يلُمهم عليه، ولم يؤنِّبهم مع تصدير الآية بخطاب المؤمنين. وعلى جوازه قبل المسيس؛ كما قال في الآية الأخرى: {لا جُناحَ عليكم إن طَلَّقْتُمُ النساءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهنَّ}. وعلى أنَّ المطلقة قبل الدخول لا عدَّةَ لها، بل بمجرَّدِ طلاقِها يجوزُ لها التزوجُ حيث لا مانعَ. وعلى أنَّ عليها العدَّة بعد الدُّخول. وهل المراد بالدخول والمسيس الوطءُ كما هو مجمعٌ عليه أو وكذلك الخلوة ولو لم يحصُلْ معها وطءٌ كما أفتى بذلك الخلفاءُ الراشدون، وهو الصحيح؛ فمتى دَخَلَ عليها وطئها أم لا، إذا خلا بها، وجب عليها العِدَّة. وعلى أنَّ المطلقة قبل المسيس تُمتَّع على الموسع قدره وعلى المُقْتِرِ قدرُهُ، ولكن هذا إذا لم يفرض لها مهرٌ؛ فإنْ كان لها مهرٌ مفروضٌ؛ فإنَّه إذا طَلَّقَ قبل الدُّخول؛ تَنَصَّفَ المهر، وكفى عن المتعة. وعلى أنه ينبغي لمن فارق زوجته قبل الدُّخول أو بعده أن يكون الفراقُ جميلاً يَحمدُ فيه كلٌّ منهما الآخر، ولا يكون غيرَ جميل؛ فإنَّ في ذلك من الشرِّ المترتِّب عليه من قدح كلٍّ منهما بالآخر شيء كثير. وعلى أن العدَّة حقٌّ للزوج؛ لقوله: {فما لكم عليهن من عدَّةٍ}: دلَّ مفهومُه أنّه لو طلَّقها بعد المسيس؛ كان له عليها عدة. وعلى أنَّ المفارقة بالوفاة تعتدُّ مطلقاً؛ لقوله: {ثم طلَّقْتُموهنَّ ... } الآية. وعلى أنَّ مَن عدا غير المدخول بها من المفارَقات من الزوجات بموتٍ أو حياةٍ عليهنَّ العدة.
{49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha Waumini kwamba ikiwa watawaoa wanawake Waumini, kisha wakawataliki kabla ya kuwagusa, basi wanawake hao hawatakiwi kukaa eda kwa ajili ya waume zao. Na akawaamrisha kuwafurahisha katika hali hii kwa baadhi ya starehe za kidunia ambazo zinaweza kuwafariji hisia zao kwa sababu ya kutengana kwao, na kwamba watengane nao kwa uzuri bila ugomvi, matusi, wala kudai wala hata kingine chochote. Aya hii inatumika kama ushahidi kwamba talaka haitokei isipokuwa baada ya kuoana. Na kama atamtaliki kabla ya kumuoa au aliifungamanisha talaka yake na siku atakapomuoa, basi talaka hiyo haiwi sahihi, kwa sababu ya kauli yake, "Ikiwa mtawaoa wanawake Waumini kisha mkawataliki," basi akaiweka talaka baada ya kuoana, na hilo likaonyesha kuwa haina nafasi yoyote kabla ya hapo. Na kama talaka, ambayo ni utengano kamili na uharamu kamili, haikutokea kabla ya ndoa, basi uharamu mpungufu kutokana na kufanya dhihaar au ilaa na mfano wa hayo unafaa zaidi kutotokea kabla ya ndoa, kama ilivyo sahihi zaidi kati ya rai mbili za wanachuoni. Inaonyesha pia kwamba talaka ni jambo linaloruhusiwa; kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwajulisha Waumini hilo kwa namna ambayo hakuwalaumu juu yake, wala hakuwakemea, pamoja na kwamba Aya yenyewe ilianza kwa kuwaita, Waumini. Na ni ushahidi kwamba inaruhusiwa kwake kabla ya kumgusa; kama alivyosema katika aya nyingine, “Hapana ubaya kwenu mkiwapa talaka wanawake ambao hamjawagusa." Na kwamba mwanamke aliyepewa talaka kabla ya kumuingilia halazimiki kukaa eda, bali anaruhusiwa kuoleka mara baada ya kutalikiwa, ikiwa hakuna kizuizi. Na kwamba inamlazimu kukaa eda ikiwa alikuwa amemuingilia. Na je, kilichokusudiwa na kuingiliana na kumgusa kama ilivyokubaliwa juu yake au pia kukaa naye faraghani, hata kama hawakuingiliana kama walivyotoa fatwa hivyo Makhalifa waongofu, ambayo ndiyo rai sahihi? Basi pindi atakapokaa naye faraghani sawa waliingiliana au la, basi inamlazimu kukaa eda. Kwa kwamba mwanamke aliyetalikiwa kabla ya kuingiliana anastahiki kupewa cha kumliwaza, mwenye wasaa kwa kiasi cha awezavyo na mwenye dhiki kwa kiasi cha awezavyo, na hili ni kama hakumwekea mahari maalumu. Na ikiwa alimwekea mahari maalumu, akimtaliki kabla ya kuingiliana naye, anapewa nusu ya mahari na hilo linatosheleza suala la kumpa cha kumliwaza. Na kwamba inamlazimu mwenye kutengana na mkewe kabla ya kuingiliana naye au baada yake uwe ni utengano mzuri ambako kila mmoja wao anamsifu mwenzake, na isiwe kwa njia isiyokuwa nzuri. Kwani katika hilo kuna uovu mwingi unaotokana na hilo kama vile kila mmoja wao kumkashifu mwenzake sana. Na kwamba kukaa eda ni haki ya mume, kwa sababu ya kauli yake, "basi hamna eda juu yao mtakayoihesabu." Maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja inaashiria kwamba ikiwa atamtaliki baada ya kujamiiana, basi atalazimika kukaa eda. Na kwamba mwanamke aliyeachwa kwa sababu ya kifo cha mumewe anazingatiwa kuwa katika eda, kwa sababu ya kauli yake, "kisha mkawapa talaka..." hadi mwisho wa Aya. Na kwamba wanawake ambao hawajaingiliwa miongoni mwa wale walioachwa, kwa sababu ya kifo cha waume zao au hata kama bado yuko hai, hao wanalazimika kukaa eda.
: 50 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَحْلَلْنَا لَكَ أَزْوَاجَكَ اللَّاتِي آتَيْتَ أُجُورَهُنَّ وَمَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ مِمَّا أَفَاءَ اللَّهُ عَلَيْكَ وَبَنَاتِ عَمِّكَ وَبَنَاتِ عَمَّاتِكَ وَبَنَاتِ خَالِكَ وَبَنَاتِ خَالَاتِكَ اللَّاتِي هَاجَرْنَ مَعَكَ وَامْرَأَةً مُؤْمِنَةً إِنْ وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلنَّبِيِّ إِنْ أَرَادَ النَّبِيُّ أَنْ يَسْتَنْكِحَهَا خَالِصَةً لَكَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ قَدْ عَلِمْنَا مَا فَرَضْنَا عَلَيْهِمْ فِي أَزْوَاجِهِمْ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ لِكَيْلَا يَكُونَ عَلَيْكَ حَرَجٌ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا (50)}.
50. Ewe Nabii, tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao, na uliowamiliki kwa mkono wako wa kulia katika wale aliokupa Mwenyezi Mungu, na mabinti wa ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako waliohama pamoja nawe; na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumuoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajua tuliyowafaradhishia wao katika wake zao na wanawake iliyowamiliki mikono yao ya kulia, ili isiwe dhiki kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
#
{50} يقول تعالى ممتنًّا على رسولِهِ بإحلاله له ما أحلَّ مما يشترك هو والمؤمنون وما ينفردُ به ويختصُّ: {يا أيُّها النبيُّ إنَّا أحْلَلْنا لك أزواجَكَ اللاَّتي آتيتَ أجورَهُنَّ}؛ أي: أعطيتهنَّ مهورهنَّ من الزوجات، وهذا من الأمور المشتركة بينَه وبين المؤمنين؛ فإنَّ المؤمنين كذلك يباح لهم مَنْ آتَوْهُنَّ أجورَهُنَّ من الأزواج. {و} كذلك أحللنا لك {ما مَلَكَتْ يمينُك}؛ أي: الإماء التي ملكتَ، {ممَّا أفاء الله عليكَ}: من غنيمة الكفار من عبيدِهِم، والأحرار مَنْ لهنَّ زوجٌ منهم ومَنْ لا زوجَ لهن، وهذا أيضاً مشتركٌ، وكذلك من المشترك قوله: {وبناتِ عمِّك وبناتِ عماتِك وبناتِ خالِك وبناتِ خالاتِكَ}: شمل العمَّ والعمة والخال والخالة القريبين والبعيدين، وهذا حصرُ المحللات، يؤخذ من مفهومه أنَّ ما عداهنَّ من الأقارب غير محلَّل؛ كما تقدَّم في سورة النساء؛ فإنَّه لا يُباح من الأقارب من النساء غير هؤلاء الأربع، وما عداهنَّ من الفروع مطلقاً، والأصول مطلقاً، وفروع الأب والأم، وإن نزلوا، وفروع مَنْ فوقَهم لصلبِهِ؛ فإنَّه لا يُباح. وقوله: {اللاَّتي هاجَرْنَ [معك]}: قَيْدٌ لحلِّ هؤلاء للرسول؛ كما هو الصواب من القولين في تفسير هذه الآية، وأما غيره عليه الصلاة والسلام؛ فقد عُلم أنَّ هذا قيد لغير الصحَّةِ. {و} أحللنا لك {امرأةً مؤمنةً إن وهبتْ نفسَها للنبيِّ}: بمجرَّدِ هبتها نفسها، {إنْ أرادَ النبيُّ أن يَسْتَنكِحَها}؛ أي: هذا تحت الإرادة والرغبة، {خالصةً لك من دونِ المؤمنينَ}؛ يعني: إباحة الموهوبة ، وأما المؤمنون؛ فلا يحلُّ لهم أن يتزوَّجوا امرأةً بمجرَّد هبتها نفسها لهم. {قد عَلِمْنا ما فَرَضْنا عليهم في أزواجهم وما ملكتْ أيمانُهم}؛ أي: قد علمنا ما على المؤمنين وما يحلُّ لهم وما لا يحل من الزوجات وملك اليمين، وقد أعْلَمْناهم بذلك، وبيَّنَّا فرائِضَه فما في هذه الآية مما يخالفُ ذلك؛ فإنَّه خاصٌّ لك؛ لكون الله جَعَلَه خطاباً للرسول وحده بقوله: {يا أيُّها النبيُّ إنا أحْلَلْنا لك ... } إلى آخر الآية. وقوله: {خالصةً لك من دونِ المؤمنينَ}: وأبَحْنا لك يا أيُّها النبيُّ ما لم نُبِح لهم، ووسَّعْنا عليك ما لم نوسِّعْ على غيرك؛ {لكيلا يكونَ عليك حرجٌ}: وهذا من زيادة اعتناء الله تعالى برسوله - صلى الله عليه وسلم -، {وكان الله غفوراً رحيماً}؛ أي: لم يزل متصفاً بالمغفرة والرحمة، وينزل على عباده من مغفرته ورحمته وجودِهِ وإحسانِهِ ما اقتضتْه حكمتُه، ووجدت منهم أسبابُه.
{50} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akimkumbusha Mtume wake kwa kumhalalishia yale aliyoyahalalisha miongoni mwa yale anayoshiriki ndani yake yeye na Waumini wote, na yale ambayo ni halali kwake peke yake na ni mahususi kwake tu, "Ewe Nabii, tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao." Hili ni katika mambo ambayo anashiriki yeye na Waumini ndani yake. Kwa maana waumini pia wameruhusiwa kuwaoa wanawake ambao wao waliwapa mahari yao. "Na" vile vile tumekuhalalishia "uliowamiliki kwa mkono wako wa kulia." Yaani wajakazi ambao mnawamiliki "katika wale aliokupa Mwenyezi Mungu" katika ngawira za makafiri, sawa wawe watumwa wao, au walio huru wao, walio na mume miongoni mwao na wasiokuwa na mume. Hili pia ni jambo ambalo waumini wanashiriki na Mtume ndani yake. Na vile vile katika yale anayoshiriki na waumini "na mabinti wa ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako." Hii pia inajumuisha ami, shangazi, mjomba, dada za mama, wa karibu na wa mbali. Na kwa kuwa hii imewataja hawa kwamba ndio wanawake haramu, inafahamika katika maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba wasiokuwa hawa miongoni mwa jamaa wa mtu sio halali, kama ilivyotajwa katika Surat An-Nisaa. Kwani haijuzu kuwaowa jamaa miongoni mwa wanawake isipokuwa hawa wanne. Wengineo ni haramu kama vile kizazi chake chote, wazazi wake wote, na kizazi cha baba yake chote, na kizazi cha mama chote, hata kama watashuka vipi, na kizazi cha walio juu yake katika waliotokana na mgongo wake, hao wote hawaruhusiki. Na kauli yake, "waliohama pamoja nawe" ni sharti la kuwafanya kuwa halali kwa Mtume, kama ilivyo ndiyo kauli sahihi kati ya zile kauli mbili za wanazuoni katika kufasiri Aya hii. Ama asiyekuwa Nabii, rehema na amani ya Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, basi imeshajulikana kuwa hili ni sharti la kufanya kuwaoa kuwa jambo lisilo sahihi. "Na" tumekuhalalishia "na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii" mwanamke aliye Muumini ikiwa atajitoa kwa Mtume kama mwenyewe Nabii akitaka kumuoa." Na hili ameachiwa Nabii mwenyewe kulitaka, "Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine." "Sisi tunajua tuliyowafaradhishia wao katika wake zao na wanawake iliowamiliki mikono yao ya kulia" Yaani, tulikwisha jua yale wasiyoruhusiwa waumini na yale wanayoruhusiwa katika wanawake na wale iliyomiliki mikono yao ya kulia. Na tayari tumeshawabainishia wajibu wake, na chochote kilicho katika Aya hii kinachopingana na hilo, basi hilo ni maalumu kwako tu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuongelesha Mtume peke yake kwa kusema, "Ewe Nabii, tumekuhalalishia... mpaka mwisho wa Aya. Na kauli yake, "Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine." Na tumekufanyia wasaa katika hilo kwa namna ambayo hatukuwafanyia wengineo, "ili isiwe dhiki kwao." Haya ni katika Mwenyezi Mungu Mtukufu kumjali sana Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Yaani, bado hajaacha kusifiwa kwa sifa ya msamaha na rehema, na anawateremshia waja wake msamaha wake, na rehema yake, na ukarimu wake, na ihsani yake kulingana na ambayo hekima yake inahitaji, nao wakawa wametenda sababu za hilo.
: 51 #
{تُرْجِي مَنْ تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَنْ تَشَاءُ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ذَلِكَ أَدْنَى أَنْ تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَا آتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمْ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَلِيمًا (51)}.
51. Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao, na umsogeze umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliyemtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unachowapa wao wote. Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
#
{51} وهذا أيضاً من توسعة الله على رسوله ورحمته به أن أباحَ له تَرْكَ القَسْم بين زوجاتِهِ على وجه الوجوب، وأنَّه إنْ فَعَلَ ذلك؛ فهو تبرعٌ منه، ومع ذلك؛ فقد كان - صلى الله عليه وسلم - يجتهدُ في القَسْم بينهنَّ في كلِّ شيءٍ، ويقول: «اللهم! هذا قَسْمي فيما أملك؛ فلا تَلُمْني فيما لا أملِك» ، فقال هنا: {تُرْجي مَن تشاء منهنَّ}؛ أي: تؤخر من أردتَ من زوجاتك، فلا تؤويها إليك، ولا تبيتُ عندها، {وتُؤوي إليك مَن تشاءُ}؛ أي: تضمُّها وتبيت عندها، {و} مع ذلك؛ لا يتعيَّنُ هذا الأمر. فمن {ابتغيتَ}؛ أي: أن تؤويها، {فلا جُناح عليكَ}: والمعنى أنَّ الخيرة بيدك في ذلك كلِّه. وقال كثيرٌ من المفسِّرين: إنَّ هذا خاصٌّ بالواهبات له أن يُرجي من يشاء ويؤوي من يشاءُ؛ أي: إن شاء؛ قَبِلَ مَنْ وَهَبَتْ نفسها له، وإن شاء؛ لم يقبلها. والله أعلم. ثم بيَّنَ الحكمةَ في ذلك، فقال: {ذلك}؛ أي: التوسعةُ عليك وكونُ الأمر راجعاً إليك وبيدك وكونُ ما جاء منك إليهنَّ تبرعاً منك؛ {أدنى أن تَقَرَّ أعيُنُهُنَّ ولا يحزنَّ ويرضينَ بما آتيتهنَّ كلهنَّ}: لعلمهنَّ أنَّك لم تتركْ واجباً ولم تفرِّطْ في حقٍّ لازم، {والله يعلم ما في قلوبكم}؛ أي: ما يعرض لها عند أداء الحقوق الواجبة والمستحبَّة وعند المزاحمة في الحقوق؛ فلذلك شرع لك التوسعة يا رسول الله؛ لتطمئنَّ قلوبُ زوجاتك، {وكان الله عليماً حليماً}؛ أي: واسع العلم، كثير الحلم، ومِنْ علمِهِ أنْ شَرَعَ لكم ما هو أصلحُ لأموركم وأكثرُ لأجورِكم، ومن حلمِهِ أنْ لم يعاقِبْكُم بما صَدَرَ منكم، وما أصرتْ عليه قلوبُكم من الشرِّ.
{51} Hii pia ni katika Mwenyezi Mungu kumkunjulia Mtume wake na kumrehemu kwamba alimruhusu kuacha kugawanya baina ya wake zake kwa njia ya wajibu, na kwamba akifanya hivyo, basi atakuwa amejitolea tu, lakini pamoja na hilo Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa akijitahidi katika kuwagawanyia katika kila kitu. Na alikuwa akisema, "Ewe Mwenyezi Mungu, huku ndiko kugawanya kwangu katika kile ninachomiliki; basi usinilaumu katika yale ambayo siyamiliki." Akasema hapa, "Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao" na usilale kwake, "na umsogeze umtakaye" na ulale kwake. Na pamoja na haya hili jambo si lazima kwako. Kwa hivyo, "Na kama ukimtaka yule uliyemtenga, basi si vibaya kwako." Hiari iko mkononi mwako katika hayo yote. Wafasiri wengi walisema: Haya ni mahususi kwa wanawake waliojipa kwa Nabii wenyewe kama zawadi, kwamba anaweza kumtenga amtakaye na kumuweka karibu amyakaye. Yaani, akitaka anamkubali yule anayejipa kwake kama zawadi, na akitaka, hamkubali. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi. Kisha akabainisha hekima katika hayo, akasema, "Kufanya hivi;" yaani, kukukunjulia hivi na kwamba wewe ndiye wa kuamua katika hayo, na kwamba jambo lolote unaloona kufanya kuhusiana na hilo ni wewe mwenyewe kujitolea tu, "kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unachowapa wao wote" kwa kuwa wanajua kwamba hukuacha wajibu wowote, wala hukupuuza haki ya wajibu. "Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu;" yaani, kile kinachoingia humo unapokuwa unatekeleza haki za faradhi na zinazopendekezwa na wakati zinapokutana haki mbalimbali mara moja. Na ndiyo maana akakuruhusu kuwa na wasaa katika hilo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili nyoyo za wake wako zipate utulivu. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mstahamilivu." Na katika elimu yake ni kwamba aliwaruhusu yale ambayo ni bora zaidi kwenu na yenye kuwapa malipo mengi zaidi. Na katika ustahamilivu wake ni kwamba hakuwaadhibu kwa mliyofanya, na kwa yale ambayo nyoyo zenu zinaendelea kufanya ya uovu.
: 52 #
{لَا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِنْ بَعْدُ وَلَا أَنْ تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنْ أَزْوَاجٍ وَلَوْ أَعْجَبَكَ حُسْنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ وَكَانَ اللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ رَقِيبًا (52)}.
52. Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine, ingawa uzuri wao ukikupendeza, isipokuwa yule uliyemmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachunga kila kitu.
#
{52} وهذا شكرٌ من الله الذي لم يزل شكوراً لزوجاتِ رسولِهِ رضي الله عنهنَّ، حيث اخترنَ الله ورسولَه والدارَ الآخرة؛ أنْ رَحِمَهُنَّ وقَصَرَ رسولَه عليهنَّ، فقال: {لا يحلُّ لك النساءُ من بعدُ}: زوجاتك الموجودات، {ولا أن تَبَدَّلَ بهنَّ من أزواج}؛ أي: ولا أن تطلِّقَ بعضهنَّ فتأخُذَ بَدَلَها، فحصل بهذا أمنهنَّ من الضرائر ومن الطلاق؛ لأنَّ الله قضى أنهنَّ زوجاتُه في الدنيا والآخرة، لا يكون بينه وبينهنَّ فرقة، {ولو أعجبك حسنهنَّ}؛ أي: حسن غيرهنَّ؛ فلا يَحْلُلْنَ لك، {إلاَّ ما ملكتْ يمينُك}؛ أي: السراري؛ فذلك جائزٌ لك؛ لأنَّ المملوكات في كراهة الزوجات لَسْنَ بمنزلة الزوجات في الإضرار للزوجات. {وكان الله على كل شيءٍ رَقيباً}؛ أي: مراقباً للأمور وعالماً بما إليه تؤول وقائماً بتدبيرها على أكمل نظام وأحسن إحكام.
{52} Hii ni shukurani itokayo kwa Mwenyezi Mungu, ambaye hajaacha kuwa mwenye shukrani sana kwa wake za Mtume wake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, ambapo walimchagua Mwenyezi Mungu, Mtume wake na nyumba ya Akhera ya kwamba aliwarehemu na akamuambia Mtume wake kwamba asiwaoe wengine wasiokuwa hao tu, akasema, "Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine." Yaani, usiwataliki baadhi yao na kuwaoa wengine mahali pao. Kwa hivyo, wakapata amani kwa hilo kutokana na kuwa na wake wenza wengine na kutokana na talaka. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alishapitisha kwamba wao ni wake zake duniani na Akhera, basi haiwezekani kwao kutengana naye. "Ingawa uzuri wao ukikupendeza isipokuwa yule uliyemmiliki kwa mkono wako wa kulia," kwa sababu wanawake wanaomilikiwa katika kuwachukia wake hawako katika nafasi sawa na wake katika kuwadhuru wake. "Na Mwenyezi Mungu anachunga kila kitu." Yaani, ni mwenye kuangalia mambo, na anajua jinsi yatakavyoisha, na anayaendesha kwa nidhamu kamilifu zaidi na kwa ustadi bora zaidi.
: 53 - 54 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَنْ يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَى طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانْتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ إِنَّ ذَلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنْكُمْ وَاللَّهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِنْ وَرَاءِ حِجَابٍ ذَلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ وَمَا كَانَ لَكُمْ أَنْ تُؤْذُوا رَسُولَ اللَّهِ وَلَا أَنْ تَنْكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِنْ بَعْدِهِ أَبَدًا إِنَّ ذَلِكُمْ كَانَ عِنْدَ اللَّهِ عَظِيمًا (53) إِنْ تُبْدُوا شَيْئًا أَوْ تُخْفُوهُ فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا (54)}.
53. Enyi mlioamini, msiingie nyumba za Nabii isipokuwa mpewe ruhusa kwenda kula, siyo kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii, naye anawastahi, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapowauliza wakeze haja, waulizeni kwa nyuma ya mapazia. Hivyo ndivyo usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haiwafaieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. 54. Mkidhihirisha chochote kile, au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
#
{53} يأمر تعالى عبادَه المؤمنين بالتأدُّب مع رسول الله - صلى الله عليه وسلم - في دخول بيوتِهِ، فقال: {يا أيُّها الذين آمنوا لا تدخُلوا بيوت النبيِّ إلاَّ أن يُؤْذَنَ لكم إلى طعام}؛ أي: لا تدخُلوها بغير إذنٍ للدخول فيها لأجل الطعام، وأيضاً لا تكونوا {ناظرينَ إناه}؛ أي: منتظرين ومتأنين لانتظار نضجه أو سعة صدرٍ بعد الفراغ منه. والمعنى: أنكم لا تدخُلوا بيوتَ النبيِّ إلاَّ بشرطين: الإذن لكم بالدخول، وأنْ يكون جلوسُكم بمقدارِ الحاجة، ولهذا قال: {ولكنْ إذا دُعيتُم فادْخُلوا فإذا طَعِمْتُم فانتَشِروا ولا مُسْتَأنِسينَ لحديثٍ}؛ أي: قبل الطعام وبعده. ثم بيَّن حكمةَ النهي وفائدتَه، فقال: {إنَّ ذلكم}؛ أي: انتظاركم الزائد على الحاجة {كان يؤذي النبيَّ}؛ أي: يتكلَّف منه ويشقُّ عليه حبسُكم إيَّاه عن شؤون بيتِهِ وأشغاله فيه، {فيَسْتَحيي منكم}: أن يقولَ لكم: اخرُجوا! كما هو جاري العادة أن الناس ـ خصوصاً أهل الكرم منهم ـ يَسْتَحْيونَ أن يُخْرِجوا الناس من مساكنهم، {و} لكن {الله لا يَسْتَحْيي من الحقِّ}: فالأمر الشرعيُّ، ولو كان يُتَوَهَّم أنَّ في تركِهِ أدباً وحياءً؛ فإنَّ الحزم كلَّ الحزم اتِّباعُ الأمر الشرعيِّ، وأنْ يجزمَ أنَّ ما خالفه ليس من الأدب في شيءٍ، والله تعالى لا يستحيي أنْ يأمُرَكم بما فيه الخيرُ لكم والرفقُ لرسوله كائناً ما كان. فهذا أدبُهم في الدخول في بيوته، وأما أدبُهم معه في خطاب زوجاتِهِ؛ فإنَّه: إمَّا أن يحتاجَ إلى ذلك، أو لا يحتاجُ إليه؛ فإن لم يحتج إليه؛ فلا حاجة إليه، والأدب تركُه، وإن احتيج إليه، كأنْ يسألهنَّ متاعاً أو غيره من أواني البيت أو نحوها؛ فإنَّهنَّ يُسْألْنَ {من وراءِ حجابٍ}؛ أي: يكون بينكم وبينهنَّ سترٌ يستر عن النظر؛ لعدم الحاجة إليه، فصار النظر إليهنَّ ممنوعاً بكلِّ حال، وكلامهنَّ فيه التفصيلُ الذي ذكره الله. ثم ذكر حكمةَ ذلك بقوله: {ذلكُم أطهرُ لقلوبكم وقلوبهنَّ}؛ لأنَّه أبعدُ عن الريبة، وكلَّما بَعُدُ الإنسان عن الأسباب الداعيةِ إلى الشرِّ؛ فإنَّه أسلمُ له وأطهرُ لقلبِهِ؛ فلهذا من الأمور الشرعيَّة التي بيَّن الله كثيراً من تفاصيلها أنَّ جميعَ وسائل الشرِّ وأسبابه ومقدِّماته ممنوعةٌ، وأنه مشروعٌ البعد عنها بكلِّ طريق. ثم قال كلمةً جامعةً وقاعدةً عامةً: {وما كان لكم}: يا معشر المؤمنين؛ أي: غير لائقٍ ولا مستحسنٍ منكم، بل هو أقبحُ شيء، {أن تُؤذوا رسولَ الله}؛ أي: أذيَّة قوليَّة أو فعليَّة بجميع ما يتعلَّق به، {ولا أن تَنكِحوا أزواجَه من بعده أبداً}: هذا من جملة ما يؤذيه؛ فإنَّه - صلى الله عليه وسلم - له مقامُ التعظيم والرفعةِ والإكرام، وتزوُّجُ زوجاتِهِ بعدَه مخلٌّ بهذا المقام، وأيضاً؛ فإنهنَّ زوجاتُه في الدُّنيا والآخرة، والزوجيَّةُ باقيةٌ بعد موته؛ فلذلك لا يحلُّ نكاحُ زوجاتِهِ بعده لأحدٍ من أمته. {إنَّ ذلكم كان عند الله عظيماً}: وقد امتثلتْ هذه الأمة هذا الأمر، واجتنبتْ ما نهى الله عنه منه، ولله الحمد والشكر.
{53} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake waumini kuwa na adabu nzuri mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – wanapoingia majumbani mwake. Kwa hivyo alisema, "Enyi mlio amini, msiingie nyumba za Nabii isipokuwa mpewe ruhusa kwenda kula chakula." Yaani, msiingie humo bila ruhusa ya kuingia humo kwa ajili ya kula chakula, na pia "siyo kungojea kiive," au hata kukaa hapo baada ya kula. Maana yake ni kwamba msiingie katika nyumba za Mtume isipokuwa kwa masharti mawili: ikiwa atawaruhusu kuingia, na kwamba kukaa hapo kwenu kuwe kwa kiasi tu inavyohitajika. Na ndiyo maana akasema, "Lakini mtakapoitwa, basi ingieni, na mkishakula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo" kabla ya kula chakula na baada yake. Kisha akabainisha hekima ya katazo hili na faida yake, akasema, "Hakika hayo," yaani, kungoja kwenu kupita kiasi cha haja "yalikuwa yanamuudhi Nabii;" kwani hilo lilikuwa ni vigumu kwake na lenye kumzuia kuendelea na shughuli zake za kinyumbani; "naye anawastahi" na akaona haya kuwaambia: Ondokeni! Kama ilivyo kawaida, watu - hasa watu wakarimu- wanaona haya kuwatoa watu majumbani mwao. "Na" lakini "Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki." Jambo la kisheria, hata ikidhaniwa kuwa kuna tabia njema na staha katika kuliacha, ila azimio kubwa zaidi katika hali hiyo ni kufuata amri ya kisheria, na kwamba aazimie kwa yakini ya kwamba chochote kinachopingana na hilo si tabia njema hata kidogo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu haoni haya kuwaamrisha kufanya yaliyo mema kwenu na kumhurumia Mtume wake, hata kama ni nani. Hii ndiyo adabu yao wanapoingia majumbani mwake, na adabu zao kwake wanapozungumza na wake zake. Hilo ni ikiwa anaihitaji au haihitaji. Ikiwa haihitaji, basi haihitajiki. Na adabu njema katika hali hii ni kuliacha. Na ikiwa linahitajika, kama vile kuwaomba kitu au vyombo vingine vya nyumbani au mfano wake, basi wataulizwa (Wake zake Nabii) "kwa nyuma ya mapazia" kwa sababu hilo halihitaji kuwatazama. Kwa hivyo ikawa kwamba kuwatazama ni jambo lililokatazwa kwa hali yoyote ile, na pia kuwaongelesha kuna sheria zake kama aliyoyataja Mwenyezi Mungu. Kisha akataja hekima ya hayo kwa kusema, "Hivyo ndivyo usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao;" kwa sababu hilo liko mbali zaidi na dhana mbaya. Na kila mtu anavyokuwa mbali zaidi na sababu zinazompeleka kwenye maovu, basi hilo linakuwa salama zaidi kwake na safi zaidi kwa moyo wake. Na ndiyo maana miongoni mwa mambo ya sheria ya kisheria ambayo Mwenyezi Mungu aliyabainisha kwa kina zaidi ni kwamba, njia zote na sababu za uovu na matangulizi yake yameharamishwa, na kwamba mtu anapaswa kujiepusha mbali nayo kwa kila njia. Kisha akasema neno lenye kukusanya zaidi na kanuni ya jumla, "Wala haikufaieni" enyi kundi la Waumini na ni kitu kibaya zaidi "kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu" kwa maneno au kwa vitendo. "Wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa;" kwani hilo ni katika mambo yanayomuudhi. Kwani yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ana nafasi ya kupewa tadhima, kuinuliwa, na kuheshimiwa. Na kuwaoa wake zake baada yake ni kutia dosari katika nafasi yake hii. Na pia, ni kwa sababu wao ni wake zake duniani na akhera, na ndoa yao itaendelea kubakia hata baada ya kufa kwake. Kwa hivyo, hairuhusiki kwa yeyote katika umma wake kuwaoa wake zake baada yake. "Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu." Na umma huu ulishaitekeleza amri hii na ukaepukana na yale ambayo Mwenyezi Mungu alikataza, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu na shukrani.
#
{54} ثم قال تعالى: {إن تُبْدوا شيئاً}؛ أي: تظهروه، {أوْ تُخفوه فإنَّ الله كان بكلِّ شيءٍ عليماً}: يعلم ما في قلوبكم، وما أظهرتموه؛ فيجازيكم عليه.
{54} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Mkidhihirisha chochote kile;" yaani, kifichueni, "au kificheni au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu." Anayajua yaliyomo nyoyoni mwenu na yale mliyoyadhihirisha, naye atawalipa kwa hayo.
: 55 #
{لَا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِي آبَائِهِنَّ وَلَا أَبْنَائِهِنَّ وَلَا إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ أَخَوَاتِهِنَّ وَلَا نِسَائِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ وَاتَّقِينَ اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا (55)}.
55. Hapana ubaya kwao, wake za Mtume, kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala kaka zao, wala watoto wa kiume wa kaka zao, wala watoto wa kiume wa dada zao, wala wanawake wenzao, wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.
#
{55} لمَّا ذكر أنهنَّ لا يُسألن متاعاً إلاَّ من وراء حجاب، وكان اللفظُ عامًّا لكلِّ أحدٍ؛ احتيجَ أن يُستثنى منه هؤلاء المذكورون من المحارم، وأنَّه {لا جُناحَ عليهنَّ} في عدم الاحتجاب عنهم، ولم يذكر فيها الأعمام والأخوال؛ لأنَّهنَّ إذا لم يَحْتَجِبْنَ عمَّن هنَّ عماته وخالاته من أبناء الإخوة والأخوات مع رفعتهنَّ عليهم؛ فعدم احتجابهنَّ عن عمِّهنَّ وخالهنَّ من باب أولى، ولأنَّ منطوق الآية الأخرى المصرِّحة بذكر العمِّ والخال مقدَّمة على ما يُفهم من هذه الآية، وقوله: {ولا نسائهنَّ}؛ أي: لا جناح عليهن أن لا يحتجبن عن نسائهنَّ؛ أي: اللاتي من جنسهنَّ في الدين، فيكون ذلك مخرجاً لنساء الكفار، ويُحتمل أنَّ المراد جنس النساء؛ فإنَّ المرأة لا تحتجب عن المرأة، {ولا ما مَلَكَتْ أيمانُهُنَّ}: ما دام العبدُ في ملكها جميعه، ولما رفع الجناح عن هؤلاء؛ شَرَطَ فيه وفي غيره لزومَ تقوى الله، وأنْ لا يكون في ذلك محذورٌ شرعيٌّ، فقال: {واتَّقينَ الله}؛ أي: استعملْنَ تقواه في جميع الأحوال. {إن الله كان على كلِّ شيءٍ شهيداً}: يشهد أعمال العباد ظاهرها وباطنها، ويسمعُ أقوالهم، ويرى حركاتِهِم؛ ثم يجازيهم على ذلك أتمَّ الجزاء وأوفاه.
{55} Na ilipotajwa kuwa hawaombwi kitu ila kwa nyuma ya pazia, na maneno haya yakawa ni ya jumla kwa kila mtu, ikahitaji kuwaondoa maharimu hawa waliotajwa katika hilo, na kwamba; "Hapana ubaya kwao" kutojifunika mbele yao. Na wala hawakutajwa ndani yake ami zao na wajomba, kwa sababu ikiwa hawajisitiri mbele ya wale ambao wao ni shangazi zao na halati zao miongoni mwa watoto wa kaka na dada, licha ya kwamba wao wako katika kiwango cha juu zaidi yao; basi inafaa zaidi kwao kutojifunika mbele ya ami zao na wajomba zao, na pia kwa sababu kuna aya nyingine iliyotaja wazi wazi ami na mjomba. Hiyo inatangulia mbele ya kile kinachoeleweka kutoka kwa aya hii. Na kauli yake, "wala wanawake wenzao" lakini si wanawake makafiri. Lakini pia inaweza kueleweka kwamba kinachomaanishwa hapa ni wanawake wote tu; kwa sababu haimpasi mwanamke kujifunika mbele ya mwanamke mwingine, "wala wale waliomilikiwa na mikono yao ya kulia," madamu mtumwa huyo yuko katika miliki yake mzima mzima. Na alipowaondolea ubaya hawa, akaweka sharti katika hilo na katika mambo mengine ambalo ni kushikamana na kumcha Mwenyezi Mungu, na kwamba kusikuwe na katazo la kisheria katika hilo. Kwa hivyo akasema, "Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu" katika hali zote. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu;" katika matendo ya nje na ya ndani ya waja wake, na anayasikia maneno yao, na anaona harakati zao. Kisha atawalipa kwa hayo, malipo kamili zaidi.
: 56 #
{إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا (56)}
56. Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi mlioamini, mswalieni na mumsalimu kwa salamu.
#
{56} وهذا فيه تنبيهٌ على كمال رسول الله - صلى الله عليه وسلم - ورفعةِ درجتِهِ وعلوِّ منزلته عند الله وعند خلقه ورفع ذِكْرِهِ، و {إنَّ الله} تعالى {وملائكتَه يصلُّون} عليه؛ أي: يثني الله عليه بين الملائكةِ وفي الملأ الأعلى لمحبَّته تعالى له، ويُثني عليه الملائكة المقرَّبون، ويدعون له ويتضرَّعون. {يا أيُّها الذين آمنوا صلُّوا عليه وسلِّموا تسليماً}: اقتداءً بالله وملائكته، وجزاءً له على بعض حقوقِهِ عليكم، وتكميلاً لإيمانكم، وتعظيماً له - صلى الله عليه وسلم - ومحبةً وإكراماً، وزيادةً في حسناتكم. وتكفيراً من سيئاتكم، وأفضلُ هيئات الصلاة عليه ـ عليه الصلاة والسلام ـ ما علَّم به أصحابه: «اللهمَّ صلِّ على محمد وعلى آل محمدٍ كما صليت على آل إبراهيم إنك حميد مجيد، وبارك على محمدٍ وعلى آل محمدٍ كما باركت على آل إبراهيم إنَّك حميدٌ مجيدٌ». وهذا الأمر بالصلاة والسلام عليه مشروعٌ في جميع الأوقات، وأوجبَه كثيرٌ من العلماء في الصلاة.
{56} Hili ni tanabahisho juu ya ukamilifu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na kunyanyuliwa kwake cheo na hadhi yake ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu na kwa viumbe vyake na kwamba ana utajo wa juu. "Hakika Mwenyezi Mungu" Mtukufu "na Malaika wake wanamswalia Nabii." Yaani, Mwenyezi Mungu humsifu mbele ya Malaika na mbele ya viumbe wakuu watukufu, kwa sababu Mwenyezi Mungu anampenda, na pia Malaika waliokaribu naye humsifu na kumuombea dua kwa unyenyekevu. "Enyi mlioamini, mswalieni na mumsalimu kwa salamu;" kwa kumuiga Mwenyezi Mungu na Malaika wake, na ili yawe malipo kwake ya baadhi ya haki zake juu yenu, na kwa ajili ya kuikamilisha imani yenu, na kumpa taadhima, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kwa sababu ya kumpenda kumheshimu, na kujizidishia mema, na ili mfutiwe mabaya yenu. Na namna bora zaidi ya kumswalia yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ni yale aliyowafundisha maswahaba wake, “Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyowarehemu jamaa zake Ibrahim. Hakika Wewe ni Mwenye kusifika, Mtukufu. Na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyowabariki jamaa zake Ibrahim. Hakika Wewe ni Mwenye kusifika, Mtukufu.” Na amri hii ya kumuombea na kumtakia amani inaruhusika katika nyakati zote, na hata wengi wa wanachuoni wanaona kwamba ni wajibu katika swala.
: 57 - 58 #
{إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُهِينًا (57) وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُبِينًا (58)}.
57. Hakika wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha. 58. Na wale wanaowaudhi Waumini wanaume na wanawake pasi na wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhuluma kubwa na dhambi iliyodhahiri.
#
{57 - 58} لما أمر تعالى بتعظيم رسوله - صلى الله عليه وسلم - والصلاة والسلام عليه؛ نهى عن أذيَّته، وتوعَّد عليها، فقال: {إنَّ الذين يؤذونَ الله ورسولَه}: وهذا يشملُ كلَّ أذيَّة قوليَّة أو فعليَّة من سبٍّ وشتم أو تنقُّص له أو لدينه أو ما يعود إليه بالأذى، {لَعَنَهُمُ الله في الدُّنيا}؛ أي: أبعدهم وطردهم، ومِنْ لَعْنِهِم في الدُّنيا أنه يتحتَّم قتلُ من شتم الرسول وآذاه، {والآخرةِ وأعدَّ لهم عذاباً [مهيناً]}: جزاءً له على أذاه أن يُؤذى بالعذابِ [الأليم]، فأذيَّة الرسول ليست كأذيَّة غيرِهِ؛ لأنَّه صلى الله عليه وسلم لا يؤمِن العبدُ بالله حتى يؤمنَ برسوله، وله من التعظيم الذي هو من لوازم الإيمانِ ما يقتضي ذلك أنْ لا يكونَ مثلَ غيرِهِ، وإنْ كان أذيَّةُ المؤمنين عظيمةً وإثمهُا عظيماً، ولهذا قال فيها: {والذين يؤذونَ المؤمنين والمؤمناتِ بغير ما اكْتَسَبوا}؛ أي: بغير جناية منهم موجبةٍ للأذى، {فقدِ احْتَمَلوا}: على ظهورِهم {بُهتاناً}: حيث آذَوْهم بغير سببٍ، {وإثماً مبيناً}: حيث تعدَّوْا عليهم وانتهكوا حرمةً أَمرَ اللهُ باحترامِها، ولهذا كان سبُّ آحاد المؤمنين موجباً للتعزير بحسب حالته وعلوِّ مرتبتِهِ؛ فتعزيرُ مَنْ سبَّ الصحابة أبلغُ، وتعزيرُ من سبَّ العلماء وأهل الدين أعظم من غيرهم.
{57 - 58} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamrisha kwamba Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - apewe taadhima, akakataza kumuudhi, na akaahidi adhabu kali juu kufanya hivy. Kwa hivyo akasema, "Hakika wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake" sawa kwa maneno au kwa vitendo, kama vile kutukana, kumtia dosari, kutia dosari dini yake, au chochote kinachoweza kumdhuru, "Mwenyezi Mungu amewalaani duniani;" yaani, aliwaweka mbali na akawafukuzilia mbali. Na katika laana zao duniani ni kwamba anapaswa kuuawa mwenye kumtukana Mtume na kumdhuru "na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha" iwe malipo kwake kwa sababbu ya maudhi yake hayo, na kwamba naye ataudhiwa kwa adhabu [ya kuumiza], kwa maana kumudhi Mtume si kama kumuudhi mtu mwingine. Kwa sababu, yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, hakuna mja anayeweza kumwamini Mwenyezi Mungu mpaka amuamini Mtume wake, na inapasa kumpa taadhima ambayo ni miongoni mwa matakwa ya imani, jambo ambalo linalazimu asiwe kama mtu mwingine yeyote. Ijapokuwa pia kuwaudhi Waumini ni dhambi kubwa, na ndiyo maana akasema kuhusu hilo, "Na wale wanaowaudhi Waumini wanaume na wanawake pasi na wao kufanya kosa lolote;" lenye kulazimu waudhiwe, "bila ya shaka wamebeba" migongoni kwao "dhuluma," ambapo waliwaudhi bila ya sababu "na dhambi iliyodhahiri," ambapo walivuka mipaka yao na wakaivunjia amri ya Mwenyezi Mungu heshima yake iliyohitaji waiheshimu. Ndiyo maana kumtukana mmoja wa waumini kunalazimu mtu kuadhibiwa kulingana na hali yake na kiwango cha cheo chake. Kwa hivo, adhabu ya mwenye kuwatukana Maswahaba ni kubwa zaidi, na adhabu ya mwenye kuwatukana wanazuoni na watu wa dini ni kubwa kuliko watu wengineo.
: 59 - 62 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَنْ يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا (59) لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا (60) مَلْعُونِينَ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا (61) سُنَّةَ اللَّهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلُ وَلَنْ تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّهِ تَبْدِيلًا (62)}.
59. Ewe Nabii, waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana kwa hivyo wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 60. Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitina katika Madina hawataacha, basi kwa yakini tutakupa mamlaka juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako isipokuwa muda mchache tu. 61. Wamelaaniwa! Popote watakapoonekana, watakamatwa na watauliwa kabisa. 62. Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.
#
{59} هذه الآية هي التي تسمَّى آية الحجاب، فأمر الله نبيَّه أن يأمُرَ النساء عموماً، ويبدأ بزوجاتِهِ وبناتِهِ ـ لأنَّهنَّ آكدُ من غيرهنَّ، ولأنَّ الآمر لغيره ينبغي أن يبدأ بأهله قبل غيرهم؛ كما قال تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا قُوا أنفسَكم وأهليكم ناراً}. {يُدْنينَ عليهنَّ من جلابيبِهنَّ}: وهنَّ اللاَّتي يَكُنَّ فوق الثياب من ملحفةٍ وخمارٍ ورداءٍ ونحوه؛ أي: يغطِّين بها وجوهَهن وصدورَهن، ثم ذكر حكمة ذلك، فقال: {ذلك أدنى أن يُعْرَفْنَ فلا يُؤْذَيْنَ}: دلَّ على وجود أذيَّةٍ إن لم يحتَجِبْن، وذلك لأنهنَّ إذا لم يحتجِبْن، ربَّما ظنَّ أنهنَّ غير عفيفاتٍ، فيتعرَّض لَهُنَّ مَنْ في قلبهِ مرضٌ، فيؤذيهنَّ، وربما استُهين بهنَّ، وظُنَّ أنهنَّ إماء، فتهاون بهنَّ من يريدُ الشرَّ؛ فالاحتجابُ حاسمٌ لمطامع الطامعين فيهنَّ. {وكان الله غفوراً رحيماً}: حيث غفر لكم ما سَلَفَ ورَحِمَكُم بأن بيَّن لكم الأحكام وأوضح الحلال والحرام؛ فهذا سدٌّ للباب من جهتهنَّ.
{59} Aya hii ndiyo inayoitwa Aya ya sitara. Basi Mwenyezi Mungu alimwamrisha Nabii wake kuwaamrisha wanawake kwa ujumla, na aanze na wake zake na mabinti zake - kwa sababu wao wana nguvu zaidi kuliko wengine, na kwa sababu mwenye kuamrisha wengine aanze na familia yake kabla ya wengine. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Enyi mlioamini jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto." "Wajiteremshie nguo zao" na haya ni yale mavazi yanayovaliwa juu ya nguo, kama vile shuka, vitambaa vya juu ya kichwa, na mengineyo. Yaani, wafunike kwa hivyo nyuso zao na vifua vyao. Kisha akataja hekima ya hayo, akasema, "Hivyo ni karibu zaidi waweze kutambulikana; kwa hivyo wasiudhiwe" na hili linaashiria kwamba kutakuwa udhia wasipovalia hijabu. Na hilo ni kwa sababu wasipojifunika, huenda wakadhaniwa kuwa wao si wenye kujiweka mbali na machafu, basi mtu mwenye maradhi katika moyo wake akawatakia madhara, kwa hivyo akawaudhi na pengine wanaweza kudunishwa na kuwadhania kuwa wao ni wajakazi, na wale wanaowatakia ubaya wakawafanyia ubaya kwa wepesi. Kwa hivyo, kuvalia hijabu kunakata matamanio ya wale wanaowatamani. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu" ambapo aliwasameheni yaliyokuwa kabla na akawarehemuni kwa kuwabainishieni hukumu na akaweka wazi halali na haramu. Hii ni kufunga mlango kwa upande wa wanawake hao.
#
{60 - 61} وأما من جهة أهل الشرِّ؛ فقد توعَّدهم بقوله: {لئن لم ينتهِ المنافقونَ والذين في قلوبهم مرضٌ}؛ أي: مرض شكٍّ أو شهوةٍ، {والمرجِفون في المدينة}؛ أي: المخوِّفون المرهِبون الأعداء، المتحدِّثون بكثرتِهِم وقوَّتِهِم وضعف المسلمين، ولم يذكرِ المعمولَ الذي ينتهون عنه؛ ليعمَّ ذلك كلَّ ما توحي به أنفسُهم إليهم، وتوسوِسُ به، وتدعو إليه من الشرِّ من التعريض بسبِّ الإسلام وأهله، والإرجاف بالمسلمين، وتوهين قُواهم، والتعرُّض للمؤمنات بالسوء والفاحشة. وغير ذلك من المعاصي الصادرة من أمثال هؤلاء. {لَنُغْرِيَنَّكَ بهم}؛ أي: نأمرك بعقوبتهم وقتالهم ونسلِّطك عليهم، ثم إذا فعلنا ذلك؛ لا طاقةَ لهم بك، وليس لهم قوةٌ ولا امتناعٌ، ولهذا قال: {ثم لا يجاوِرونَكَ فيها إلاَّ قليلاً}؛ أي: لا يجاورونك في المدينة إلاَّ قليلاً؛ بأن تقتُلَهم أو تنفيهم، وهذا فيه دليلٌ لنفي أهل الشرِّ الذين يُتَضَرَّر بإقامتهم بين أظهر المسلمين؛ فإنَّ ذلك أحسم للشرِّ وأبعد منه، ويكونونَ {ملعونينَ أينما ثُقِفوا أُخِذوا وقُتِّلوا تَقْتيلاً}؛ أي: مبعَدين حيثُ وُجِدوا، لا يحصُلُ لهم أمنٌ، ولا يقرُّ - لهم قرارٌ، يخشون أن يُقتلوا أو يُحبسوا أو يعاقَبوا.
{60 - 61} Na ama kwa upande wa watu hao waovu; akawatishia kwa kusema, "Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao." Yaani, maradhi ya shaka au matamanio, "na waenezao fitina katika Madina hawataacha." Yaani, wale wanaowahofisha watu na kuwatishia, na ambao ni maadui, ambao wanazungumzia wingi wao na nguvu zao na udhaifu wa Waislamu, lakini hakutaja matendo wanayokatazwa kuacha; ili lijumuishe kila maovu yote ambayo nafsi zao zinawatia moyoni, na kuwatia wasiwasi kwayo kama vile kuutukana Uislamu na watu wake, na kuwashambulia wanawake Waumini kwa ubaya na usherati. Na dhambi zingine zinazotendwa na watu kama hao. "Basi kwa yakini tutakupa mamlaka juu yao." Yaani, tutakuamrisha kuwaadhibu na kupigana nao, na tutakupa mamlaka juu yao. Kisha tukishfanya hivyo, hawatakuwa na uwezo dhidi yako, wala hawatakuwa na nguvu na kujizuia. Na ndiyo maana akasema, "kisha hawatakaa humo karibu yako isipokuwa muda mchache tu." Yaani, utawaua au kuwafukuza. Na hili lina ushahidi wa kuwafukuza watu waovu ambao watu wanadhurika na kukaa kwao miongoni mwa Waislamu. Kwani, hilo ndilo jambo la kukata zaidi uovu wao na kuwaweka watu mbali zaidi nao, na "Wamelaaniwa! Popote watakapoonekana, watakamatwa na watauliwa kabisa." Hawawezi kupata amani yoyote wala kutulia mahali popote. Wanashinda wakichelea kuuawa, kufungwa gerezani, au kuadhibiwa.
#
{62} {سُنَّةَ الله في الذين خَلَوْا من قبلُ}: أنَّ مَن تمادى في العصيانِ وتجرَّأ على الأذى ولم ينتهِ منه؛ فإنَّه يعاقَب عقوبةً بليغةً، {ولنْ تَجِدَ لسنَّةِ الله تبديلاً}؛ أي: تغييراً، بل سنته تعالى وعادتُه جاريةٌ مع الأسباب المقتضية لأسبابها.
{62} "Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa kwa wale waliopita zamani," kwamba anayeendelea kuasi na akafanya ujasiri wa kuudhi wengine na wala haachi kuufanya hivyo; huyo ataadhibiwa kwa adhabu kali. "Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu," bali desturi yake Mwenyezi Mungu na ada yake inaendelea kuwapo, maadamu zipo sababu zinazolazimu ada hizo kuwapo.
: 63 - 68 #
{يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا (63) إِنَّ اللَّهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا (64) خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا لَا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا (65) يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَالَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا (66) وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا (67) رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا (68)}.
63. Watu wanakuuliza habari ya Saa ya Kiyama. Sema: "Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu." Na nini kitakujulisha, pengine hiyo Saa iko karibu? 64. Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na amewaandalia Moto unaowaka kwa nguvu. 65. Watadumu humo milele. Hawatampata mlinzi wala wa kuwanusuru. 66. Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto, watasema: "Laiti tungelimtii Mwenyezi Mungu, na tungelimtii Mtume!" 67. Na watasema: "Mola wetu Mlezi, hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio waliotupoteza njia." 68. Mola wetu Mlezi, wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa.
#
{63} أي: يستخبرك الناسُ عن الساعة استعجالاً لها، وبعضُهم تكذيباً لوقوعها وتعجيزاً للذي أخبر بها، {قُل} لهم: {إنَّما علمُها عند الله}؛ أي: لا يعلمُها إلاَّ الله؛ فليس لي ولا لغيري بها علمٌ، ومع هذا؛ فلا تستبطئوها، {وما يُدْريكَ لعلَّ الساعةَ تكونُ قريباً}.
{63} Yaani, watu wanakuuliza kuhusu Saa ya Kiyama kwa kuifanyia haraka, na baadhi yao kwa kukadhibisha kutokea kwake, na hata kuona kwamba aliyeahidi kuileta hana uwezo, "Sema" uwaambie, "Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu." Yeye pekee ndiye anayejua hilo. Kwa hivyo, mimi mwenyewe silijui wala hata mwingine yeyote hana elimu yoyote juu yake, na pamoja na hayo, "Na nini kitakujulisha, pengine hiyo Saa iko karibu?"
#
{64 - 66} ومجردُ مجيء الساعة قرباً وبعداً ليس تحته نتيجةٌ ولا فائدةٌ، وإنَّما النتيجة والخسار والربح والشقاوة والسعادة: هل يستحقُّ العبدُ العذاب أو يستحقُّ الثواب؛ فهذه سأخبركم بها وأصفُ لكم مستحقَّها، فوصف مستحقَّ العذاب ووصف العذاب؛ لأنَّ الوصف المذكور منطبقٌ على هؤلاء المكذِّبين بالساعة، فقال: {إنَّ الله لَعَنَ الكافرين}؛ أي: الذين صار الكفر دأبهم وطريقتهم الكفر بالله وبرسُلِهِ وبما جاؤوا به من عند الله، فأبعدهم في الدنيا والآخرة من رحمته، وكفى بذلك عقاباً، {وأعدَّ لهم سعيراً}؛ أي: ناراً موقدةً تُسَعَّرُ في أجسامهم، ويبلغُ العذاب إلى أفئدتهم، ويخلدون في ذلك العذاب الشديد، فلا يخرجونَ منه، ولا يُفَتَّرُ عنهم ساعةً، {ولا يجدون} لهم {وليًّا}: فيعطيهم ما طلبوه {ولا نصيراً}: يدفعُ عنهم العذابَ، بل قد تخلَّى عنهم العلي النصير وأحاطَ بهم عذابُ السعير، وبلغ منهم مبلغاً عظيماً، ولهذا قال: {يوم تُقَلَّبُ وجوهُهم في النارِ}: فيذوقون حرَّها، ويشتدُّ عليهم أمرُها، ويتحسرون على ما أسلفوا. و {يقولونَ يا لَيْتَنا أطَعْنا الله وأطَعْنا الرسولا}: فسلِمْنا من هذا العذاب، واستَحْقَقنا كالمطيعين جزيلَ الثواب، ولكن أمنية فاتَ وقتُها، فلم تفدهم إلا حسرةً وندماً وهمًّا وغمًّا وألماً.
{64 - 66} Na kuja tu kwa Saa, iwe karibu au mbali, hakuna matokeo wala manufaa, bali matokeo, hasara, faida, kuwa mashakani na katika furaha ni je, mja anastahiki adhabu au anastahiki malipo mazuri? Hilo nitakwambieni kulihusu na nitawaelezeni wanaolistahiki. Basi akaelezea anayestahiki adhabu na akaielezea adhabu hiyo, kwa sababu maelezo yaliyotangulia yanaingiliana kabisa na hawa walioikadhibisha Saa ya Kiyama. Basi akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri" ambao mwenendo wao na njia yao ni ukafiri. Wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake na yale waliyoyaleta kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi akawaweka mbali na rehema yake duniani na Akhera, na hilo linatosha kuwa adhabu "na amewaandalia Moto unaowaka kwa nguvu" na wakataa humo milele, wala hawatatoka humo, na wala hawatapumzishwa hata saa moja. "Hawatampata mlinzi" atakayewapa walichoomba, "wala wa kuwanusuru" atakawaepusha na adhabu hiyo. Basi aliye juu zaidi, Mwenye kunusuru aliwaachilia mbali na akawazungushia adhabu ya Moto mkali uliowafikia kiwango kikubwa zaidi. Na ndiyo maana akasema, "Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto" na walionje joto lake, na jambo lake liwawie gumu sana, na wajutie yale waliyotanguliza;" "Watasema: Laiti tungelimtii Mwenyezi Mungu, na tungelimtii Mtume!" Basi tukasalimika kutokana na adhabu hii, na sisi pia tukastahiki malipo makubwa kama wale waliotii. Lakini haya ni matamanio ambayo muda wake ulikwisha pita. Kwa hivyo, hayakuwafaidi ila huzuni, majuto, wasiwasi kubwa, dhiki na maumivu.
#
{67} {وقالوا ربَّنا إنَّا أطَعْنا سادتنا وكبراءنا}: وقلَّدْناهم على ضلالهم، {فأضَلُّونا السبيلا}؛ كقوله تعالى: {ويوم يَعَضُّ الظالمُ على يديهِ يقولُ يا ليتني اتَّخَذْتُ مع الرسولِ سبيلاً. يا وَيْلتى لَيْتَني لم أتَّخِذْ فلاناً خليلاً. لقد أضلَّني عن الذِّكْر [بعد إذ جاءني] ... } الآية.
{67} "Na watasema: "Mola wetu Mlezi, hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu" na tukawaiga katika upotovu wao, "nao ndio waliotupoteza njia." Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume! Ee Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki! Hakika alinipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia... hadi mwisho wa Aya.
#
{68} ولما علموا أنَّهم هم وكبراءهم مستحقُّون للعقاب؛ أرادوا أن يشتفوا ممَّنْ أضلُّوهم، فقالوا: {ربَّنا آتهم ضِعْفَيْنِ من العذاب والْعَنْهم لَعناً كبيراً}: فيقول الله {لكلٍّ ضعف}: فكلُّكم اشتركتُم في الكفر والمعاصي، فتشتركون في العقاب، وإنْ تفاوت عذابُ بعضِكم على بعض بحسب تفواتِ الجرم.
{68} Na walipojua kwamba wao na wakuu wao wanastahiki kuadhibiwa, wakataka kupata ponya kutoka kwa wale waliowapoteza, wakasema: "Mola wetu Mlezi, wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa." Lakini Mwenyezi Mungu atasema "itakuwa kwenu nyote marudufu;" kwani nyote mlishiriki katika ukafiri na uasi, basi mtashiriki katika adhabu, hata kama adhabu ya baadhi yenu itakuwa tofauti kulingana na ukubwa wa utofauti wa uhalifu wake.
: 69 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَى فَبَرَّأَهُ اللَّهُ مِمَّا قَالُوا وَكَانَ عِنْدَ اللَّهِ وَجِيهًا (69)}
69. Enyi mlioamini, msiwe kama wale waliomtaabisha Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na hayo waliyoyasema, naye alikuwa mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.
#
{69} يحذِّر تعالى عبادَه المؤمنين عن أذيَّة رسولهم محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - النبيِّ الكريم الرءوف الرحيم، فيقابلوه بضدِّ ما يجب له من الإكرام والاحترام، وأن لا يتشبَّهوا بحال الذين آذَوْا موسى بن عمران كليم الرحمن، فبرَّأه اللَّه مما قالوا من الأذيَّة؛ أي: أظهر الله لهم براءته، والحالُ أنَّه عليه الصلاة والسلام ليس محلَّ التهمة والأذية؛ فإنَّه كان وجيهاً عند الله، مقرباً لديه، من خواصِّ المرسلين، ومن عباد الله المخلَصين، فلم يزجرهم ما له من الفضائل عن أذيَّته والتعرُّض له بما يكره. فاحذروا أيُّها المؤمنون أن تتشبَّهوا بهم في ذلك، والأذيَّة المشار إليها هي قولُ بني إسرائيل عن موسى لما رأوا شدَّة حيائِهِ وتستُّره عنهم: إنَّه ما يمنعُه من ذلك إلاَّ أنَّه آدرُ؛ أي: كبير الخصيتين، واشتهر ذلك عندهم، فأراد الله أن يبرِّئه منهم، فاغتسل يوماً، ووضع ثوبه على حجر، ففرَّ الحجر بثوبه، فأهوى موسى عليه السلام في طلبه، فمرَّ به على مجالس بني إسرائيل، فرأوه أحسن خلق الله، فزال عنه ما رموه به.
{69} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawatahadharisha waja wake waumi kuhusu kumudhi Mtume wao Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Ambaye ni Nabii mkarimu, mpole, mwenye huruma. Wasije wakaamiliana naye kwa kinyume cha yale wanayolazimika kumfanyia ya kumtukuza na kumheshimu, wala wasijifananishe na hali ya wale waliomuudhi Musa bin Imran aliyezungumza moja kwa moja na Ar-Rahman. Basi Mwenyezi Mungu akamuondoshea udhia waliosema juu yake, kwani uhakika wa wa mambo ulikuwa kwamba hakustahiki hata kidogo kukashifiwa na kuudhiwa. Kwani alikuwa mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, aliye karibu naye, miongoni mwa Mitume maalumu, na miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu wanaomkusudia yeye tu. Na hawa hawakuzuiliwa na fadhila alizo nazo kuacha kumuudhi na kusema juu yake yale anayochukia. Basi, enyi Waumini, jihadharini msiwaige katika hili. Na udhia unaoashiriwa hapa ni namna walivyosema Wana wa Israili kuhusu Musa walipoona staha yake kubwa sana na kujisitiri kwake mno mbali nao, wakasema: Hakuna kinachomzuilia kufanya hayo isipokuwa kwamba ana korodani kubwa. Na hilo likajulikana sana miongoni mwao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akataka kumwondolea tuhuma hii. Basi siku moja akaoga, na akawa ameweka vazi lake juu ya jiwe, na jiwe hilo likatoroka na vazi lake. Musa, amani iwe juu yake, akaanza kulifuata mbio, mpaka akapita akilikimbiza mbele ya Wana wa Israili waliokuwa wamekaa barazani, nao wakamuona hali ya kuwa ni mwenye umbile bora zaidi kuliko viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo yakamuondokea yale waliyomzuilia.
: 70 - 71 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا (70) يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا (71)}.
70. Enyi mlioamini, mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa. 71. Atawatengenezea vitendo vyenu na awasamehe madhambi yenu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefuzu kufuzu kukubwa.
#
{70} يأمر تعالى المؤمنين بتقواه في جميع أحوالِهِم في السرِّ والعلانية، ويخصُّ منها ويندب للقول السديد، وهو القول الموافق للصواب أو المقارب له عند تعذُّر اليقين من قراءةٍ وذكرٍ وأمرٍ بمعروف ونهي عن منكر وتعلُّم علم وتعليمه والحرص على إصابة الصواب في المسائل العلميَّة وسلوك كلِّ طريق موصِل لذلك وكل وسيلةٍ تُعين عليه. ومن القول السديد لينُ الكلام ولطفُه في مخاطبة الأنام والقول المتضمِّن للنُّصح والإشارة بما هو الأصلح.
{70} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha Waumini wamche katika hali zao zote, kwa siri na hadharani, na anahimiza hasa na kupendekeza maneno ya sawasawa, ambayo ni maneno yanayoafikiana na kilicho sahihi au kilicho karibu na usahihi wakati hakuna yakini, kuhusiana na mambo kama vile kusoma, kumtaja Mwenyezi Mungu, kuamrisha mema na kukataza maovu, kujifunza elimu na kuifundisha, na kufanya bidii kufikia yaliyo sawa katika masuala ya kielimu, na kufuata kila njia yenye kufikisha katika hayo, na kila chenye kusaidia katika kuyafanikisha hayo. Na katika maneno yaliyo sawasawa ni kulainisha maneno na kuwa na upole katika kuzungumza na watu, na pia ni maneno yanayojumuisha nasaha na kuelekeza kwa kilicho bora zaidi.
#
{71} ثم ذَكَرَ ما يترتَّب على تقواه وقول القول السديدِ، فقال: {يُصْلِحْ لكم أعمالَكم}؛ أي: يكون ذلك سبباً لصلاحها وطريقاً لقَبولها؛ لأنَّ استعمال التقوى تُتَقَبَّلُ به الأعمال؛ كما قال تعالى: {إنَّما يتقبَّلُ الله من المتَّقينَ}: ويوفَّق فيه الإنسان للعمل الصالح، ويُصْلِحُ الله الأعمال أيضاً بحفظها عما يُفْسِدُها وحفظِ ثوابها ومضاعفتِهِ؛ كما أنَّ الإخلال بالتقوى والقول السديد سببٌ لفسادِ الأعمال وعدم قَبولها وعدم ترتب آثارِها عليها، {ويَغْفِرْ لكم}: أيضاً {ذنوبكم}: التي هي السببُ في هلاكِكُم؛ فالتَّقْوى تستقيمُ بها الأمور، ويندفعُ بها كلُّ محذور، ولهذا قال: {ومَن يُطِع اللهَ ورسولَه فقد فاز فوزاً عظيماً}.
{71} Kisha akataja yanayotokaa na kumcha Mungu na kusema maneno yaliyo sawa, akasema, "Atawatengenezea vitendo vyenu." Yaani, hiyo itakuwa sababu ya kuyafanya yatengenee na njia ya kuyafanya yakubaliwe. Kwa sababu kwa kutumia uchamungu, matendo yanakubaliwa, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu tu." Na kwa sababu yake anamuwezesha mwandamu kutenda mema. Na pia Mwenyezi Mungu hufanya matendo kutengenea kwa kuyalinda kutokana na yale yanayoyaharibia, na kuhifadhi malipo yake na kuyazidisha. Kadhalika, kuuvunja uchamungu na maneno yaliyo sawa ni sababu ya kuharibika kwa vitendo, na kutokubalika kwake, na kutofungamana na athari zake. "Na awasamehe madhambi yenu" ambayo ndiyo sababu ya kuangamia kwenu. Kwani, kwa uchamungu mambo yananyooka, na yanazuilika kwa huo yote yanayotahadhariwa. Na ndiyo maana akasema, "Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefuzu kufuzu kukubwa."
: 72 - 73 #
{إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَنْ يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنْسَانُ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا (72) لِيُعَذِّبَ اللَّهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ وَيَتُوبَ اللَّهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا (73)}
72. Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima, na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhalimu, mjinga. 73. Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake. Na awapokelee toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
#
{72} يعظِّم تعالى شأنَ الأمانةَ التي ائتمنَ اللَّه عليها المكلَّفين، التي هي امتثال الأوامر واجتناب المحارم في حال السرِّ والخفية كحال العلانية، وأنَّه تعالى عَرَضَها على المخلوقات العظيمة السماواتِ والأرض والجبال عرضَ تخييرٍ لا تحتيم، وأنَّكِ إن قمتِ بها وأدَّيْتِيها على وجهها؛ فلكِ الثوابُ، وإنْ لم تَقومي بها ولم تؤدِّيها؛ فعليكِ العقاب، {فأبَيْنَ أن يَحْمِلْنَها وأشفَقْنَ منها}؛ أي: خوفاً أن لا يقمنَ بما حملن، لا عصياناً لربِّهن ولا زهداً في ثوابه، وعرضها الله على الإنسان على ذلك الشرط المذكور، فقَبِلَها وحملها مع ظلمِهِ وجهلِهِ، وحمل هذا الحمل الثقيل.
{72} Mwenyezi Mungu ametukuza hadhi ya amana ambayo aliwakabidhi viumbe wanaojukumishwa na sheria, ambayo ni kufuata maamrisho na kuepukana na mambo ya haramu katika hali ya siri na ya kufichika kama tu katika hali ya hadharani. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliipa kwa viumbe vikubwa: mbingu, ardhi na milima, kwa njia ya hiari isiyo ya lazima, na kwamba ukiitekeleza na ukaifanya kwa namna yake ya sawasawa, basi utapata thawabu. Na ikiwa hutaifanya na kuitekeleza, utapata adhabu. "Na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa" kwamba havitaitekeleza amana hiyo ambayo vilibebeshwa, na havikukataa kwa njia ya kumuasi Mola wao Mlezi wala kutotaka thawabu zake. Kisha Mwenyezi Mungu akaipa kwa mwanadamu kwa sharti hilo lililotajwa, naye akaikubali na akaibeba pamoja na dhuluma yake na ujinga wake, na akaubeba mzigo huu mzito.
#
{73} فانقسم الناس بحسب قيامهم بها وعدمِهِ إلى ثلاثة أقسام: منافقون [أظهروا أنهم] قاموا بها ظاهراً لا باطناً، ومشركون تركوها ظاهراً وباطناً، ومؤمنون قائمون بها ظاهراً وباطناً. فذكرَ الله تعالى أعمالَ هذه الأقسام الثلاثة وما لهم من الثوابِ والعقابِ، فقال: {ليعذِّبَ الله المنافقينَ والمنافقاتِ والمشركينَ والمشركاتِ ويتوبَ الله على المؤمنين والمؤمنات وكان الله غفوراً رحيماً}: فله تعالى الحمدُ حيث خَتَمَ هذه الآية بهذين الاسمين الكريمين الدالَّيْن على تمام مغفرةِ الله وسعة رحمتِهِ وعموم جوده، مع أنَّ المحكوم عليهم كثيرٌ، منهم لم يستحقَّ المغفرة والرحمة، لنفاقِهِ وشركِهِ.
{73} Kwa hivyo, watu wakagawanyika kulingana na wanavyoitekeleza na kutoitekeleza katika makundi matatu: wanafiki, ambao walidhihirisha kwamba waliitekeleza kwa nje na si kwa ndani, na washirikina, ambao waliiacha kwa nje na ndani, na Waumini, ambao waliitekeleza kwa nje na ndani. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja vitendo vya makundi hayo matatu na malipo na adhabu yao, akasema, "ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake. Na awapokelee toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Basi ni zake yeye Mtukufu sifa njema ambapo alihitimisha Aya hii kwa majina haya mawili matukufu yanayoashiria msamaha kamili wa Mwenyezi Mungu na upana wa rehema yake, na ujumla wa ukarimu wake, licha ya kuwa wanaokirimiwa ni wengi, ambao baadhi yao hawakustahiki msamaha na rehema kutokana na unafiki wao na ushirikina wao.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Ahzab, kwa sifa ya Mwenyezi Mungu na msaada wake.
* * *