:
Tafsiri ya Suratul-Baqarah
Tafsiri ya Suratul-Baqarah
Nayo iliteremka Madinah
: 1 - 5 #
{الم (1) ذَلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِلْمُتَّقِينَ (2) الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ (3) وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ (4) أُولَئِكَ عَلَى هُدًى مِنْ رَبِّهِمْ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (5)}.
1. Alif Lam Mim (1) (2). 2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu. 3. Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika (1) tuliyowapa (tuliyowaruzuku). 4. Na ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako, na yaliyoteremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo. 5. Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofaulu.
Mazungumzo kuhusu Al-Basmalah (yaani, Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema mwenye kurehemu) yalikwisha tangulia.
#
{1} وأما الحروف المقطَّعة في أوائل السورة ؛ فالأسلم فيها السكوت عن التعرُّض لمعناها من غير مستند شرعي، مع الجزم بأن الله تعالى لم ينزلها عبثاً، بل لحكمة لا نعلمها.
(1) Na ama herufi za mkato mwanzoni mwa sura mbalimbali. Lililo salama zaidi kuhusiana nazo ni kukaa kimya na kutoziingilia maana zake bila ya dalili ya Kisheria; pamoja na kuwa na yakini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuziteremsha bure, bali kwa hekima tusiyoijua.
#
{2} وقوله: {ذلك الكتاب}؛ أي: هذا الكتاب العظيم، الذي هو الكتاب على الحقيقة، المشتمل على ما لم تشتمل عليه كتب المتقدمين والمتأخرين من العلم العظيم والحقِّ المبين؛ {لا ريب فيه} فلا ريب فيه ولا شكَّ بوجه من الوجوه، ونفي الرَّيب عنه يستلزم ضده إذ ضد الريب والشك اليقين، فهذا الكتاب مشتمل على علم اليقين المزيل للشك والريب. وهذه قاعدة مفيدة أن النفي المقصود به المدح لا بد أن يكون متضمناً لضده وهو الكمال؛ لأن النفي عدم، والعدم المحض لا مدح فيه، فلما اشتمل على اليقين وكانت الهداية لا تحصل إلا باليقين؛ قال: {هدىً للمتقين}، والهدى ما تحصل به الهداية من الضلالة والشُّبَه، وما به الهداية إلى سلوك الطرق النافعة. وقال: {هدى} وحذف المعمولَ، فلم يقل: هدى للمصلحة الفلانية ولا للشيء الفلاني؛ لإرادة العموم وأنه هدى لجميع مصالح الدارين، فهو مرشدٌ للعباد في المسائل الأصولية والفروعية، ومبين للحق من الباطل والصحيح من الضعيف، ومبين لهم كيف يسلكون الطرق النافعة لهم في دنياهم وأخراهم. وقال في موضع آخر: {هدى للناس} فعمَّم، وفي هذا الموضع وغيره: {هدى للمتقين} لأنه في نفسه هدى لجميع الناس ، فالأشقياء لم يرفعوا به رأساً ولم يقبلوا هدى الله، فقامت عليهم به الحجة، ولم ينتفعوا به لشقائهم. وأما المتقون الذين أتوا بالسبب الأكبر لحصول الهداية وهو التقوى التي حقيقتها: اتخاذ ما يقي سخط الله وعذابه بامتثال أوامره، واجتناب النواهي، فاهتدوا به، وانتفعوا غاية الانتفاع، قال تعالى: {يا أيها الذين آمنوا إن تتقوا الله يجعل لكم فرقاناً} فالمتقون هم المنتفعون بالآيات القرآنية والآيات الكونية. ولأن الهداية نوعان: هداية البيان، وهداية التوفيق، فالمتقون حصلت لهم الهدايتان وغيرهم لم تحصل لهم هداية التوفيق، وهداية البيان بدون توفيق للعمل بها ليست هداية حقيقية تامة.
(2) Na kauli yake “Hiki ni Kitabu” yaani, kitabu hiki kitukufu ambacho ni kitabu kiuhakika, ambacho kinajumuisha yale ambayo vitabu vya watu wa mwanzo na wa mwisho havikujumuisha katika elimu kubwa na haki iliyo wazi. "Kisichokuwa na shaka ndani yake” basi hakina kusitasita wala shaka kwa namna yoyote ile. Na kukanusha shaka kuhusiana nacho kunalazimisha (kuwepo) kinyume chake, kwa sababu kinyume cha kusitasita na shaka ni yakini. Kwa hivyo, kitabu hiki kinajumuisha elimu ya yakini inayoondosha shaka na kusitasita. Na huu ni msingi unaomaanisha kwamba kukanusha kunakokusudiwa kusifu ni lazima kujumuishe kinyume chake, ambacho ni ukamilifu; kwa sababu ukanushaji unamaanisha kutokuwepo kwa kitu. Na kutokuwepo kwa kitu peke yake tu (bila ya kuthibitisha kinyume chake) hakuna kusifu kokote. Na pindi (kitabu hiki) kilipojumuisha yakini, na kukawa kuongoza hakupatikani ila kwa yakini; (Mwenyezi Mungu) akasema “ni uwongofu kwa wachamungu.” Nao uwongofu ndio unaoleta kuongoka kutoka kwa upotovu na mambo yasiyo ya wazi (shubuhaat), na kwa uwongofu mtu huongozwa kushika njia za manufaa. Na (Mwenyezi Mungu) alisema “uwongofu” na akafuta (yaani hakutaja) ma’amuul (yani ni uwongofu kwa nyanja gani za wachamungu). Ndiyo maana hakusema: Ni uwongofu kwa masilahi fulani, wala kwa kitu fulani; kwa sababu alikusudia kujumuisha, na kwamba ni uwongofu kwa masilahi yote ya Nyumba mbili (dunia na akhera). Kwa hivyo, kinawaongoza waja katika masuala ya kimsingi na ya tanzu, na kinabainisha haki kutoka kwa batili, na kilicho sahihi kutoka kwa kilicho dhaifu, na kinawabainishia jinsi ya kufuata njia zenye manufaa kwao katika dunia yao na akhera yao. Na alisema katika mahali pengine “ni uwongofu kwa watu” basi akawa amejumuisha (watu wote). Lakini hapa mahali na penginepo, akasema “ni uwongofu kwa wachamungu” kwa sababu (hiki kitabu) chenyewe ni uwongofu kwa watu wote. Ama wale waovu, wao hawakukinyanyulia kichwa juu (yaani hawakukijali), na hawakukubali uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo hoja ikasimama juu yao kwacho, na hawakufaidika kwacho kwa sababu ya uovu wao. Na ama wachamungu ambao walifanya sababu kubwa ya kupata uwongofu ambayo ni uchamungu ambao uhakika wake ni kufanya yanayozuia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake, kwa kufanya maamrisho yake na kuacha makatazo yake. Kwa hivyo, wakaongoka kwacho, na wakanufaika kunufaika kukubwa mno. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: “Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atakupeni kipambanuo.” Kwa hivyo, wachamungu ndio wanaofaidika na aya za Qur-aani na aya (ishara) za kiulimwengu. Na kwa sababu kuongoza ni kwa aina mbili: kuongoza kwa kueleza, na kuongoza kwa kuwezesha. Kwa wachamungu, wao walipata miongozo hii miwili. Na ama wasiokuwa wao, hawakupata mwongozo wa kuwezeshwa. Na mwongozo wa kueleza bila ya kuwezeshwa kuufanyia matendo (mema) sio mwongozo kamili kihakika.
Kisha akawaeleza wachamungu kwa itikadi na vitendo vya ndani (vilivyofichika) na vitendo vya dhahiri, kwa sababu uchamungu unajumuisha hayo, akasema:
#
{3} {الذين يؤمنون بالغيب} حقيقة الإيمان هو التصديق التام بما أخبرت به الرسل، المتضمن لانقياد الجوارح، وليس الشأن في الإيمان بالأشياء المشاهدة بالحسِّ، فإنه لا يتميز بها المسلم من الكافر، إنما الشأنُ في الإيمان بالغيب الذي لم نره ولم نشاهده، وإنما نؤمن به لخبر الله وخبر رسوله. فهذا الإيمان الذي يميز به المسلم من الكافر؛ لأنه تصديق مجرد لله ورسله، فالمؤمن يؤمن بكل ما أخبر الله به، أو أخبر به رسوله سواء شاهده أو لم يشاهده، وسواء فهمه وعقله، أو لم يهتدِ إليه عقله وفهمه، بخلاف الزنادقة المكذبين بالأمور الغيبية لأن عقولهم القاصرة المقصرة لم تهتدِ إليها فكذبوا بما لم يحيطوا بعلمه؛ ففسدت عقولهم، ومرجت أحلامهم؛ وزكت عقول المؤمنين المصدقين المهتدين بهدى الله. ويدخل في الإيمان بالغيب الإيمان بجميع ما أخبر الله به من الغيوب الماضية والمستقبلة وأحوال الآخرة وحقائق أوصاف الله وكيفيتها وما أخبرت به الرسل من ذلك، فيؤمنون بصفات الله ووجودها، ويتيقنونها وإن لم يفهموا كيفيتها. ثم قال: {ويقيمون الصلاة} لم يقل: يفعلون الصلاة؛ أو يأتون بالصلاة لأنه لا يكفي فيها مجرد الإتيان بصورتها الظاهرة، فإقامة الصلاة، إقامتها ظاهراً، بإتمام أركانها وواجباتها وشروطها، وإقامتها باطناً ، بإقامة روحها وهو حضور القلب فيها وتدبر ما يقول ويفعله منها، فهذه الصلاة هي التي قال الله فيها: {إن الصلاة تنهى عن الفحشاء والمنكر} وهي التي يترتب عليها الثواب، فلا ثواب للعبد من صلاته إلا ما عقل منها، ويدخل في الصلاة فرائضها ونوافلها. ثم قال: {ومما رزقناهم ينفقون} يدخل فيه النفقات الواجبة؛ كالزكاة، والنفقة على الزوجات والأقارب والمماليك ونحو ذلك، والنفقات المستحبة بجميع طرق الخير، ولم يذكر المنفَق عليه لكثرة أسبابه وتنوع أهله، ولأن النفقة من حيث هي قربة إلى الله، وأتى «بِمِن» الدالة على التبعيض؛ لينبههم أنه لم يرد منهم إلا جزءاً يسيراً من أموالهم غير ضار لهم، ولا مثقل بل ينتفعون هم بإنفاقه، وينتفع به إخوانهم، وفي قوله: {رزقناهم} إشارة إلى أن هذه الأموال التي بين أيديكم ليست حاصلة بقوتكم وملككم، وإنما هي رزق الله الذي خوّلكم وأنعم به عليكم، فكما أنعم عليكم وفضلكم على كثير من عباده فاشكروه بإخراج بعض ما أنعم به عليكم، وواسوا إخوانكم المعدمين. وكثيراً ما يجمع تعالى بين الصلاة والزكاة في القرآن؛ لأن الصلاة متضمنة للإخلاص للمعبود، والزكاة والنفقة متضمنة للإحسان على عبيده؛ فعنوان سعادة العبد إخلاصه للمعبود وسعيه في نفع الخلق، كما أن عنوان شقاوة العبد عدم هذين الأمرين منه فلا إخلاص ولا إحسان.
(3) “Ambao huyaamini ya ghaibu” kiuhakika. Na imani ni kusadiki kukamilifu kwa yale waliyojulisha Mitume, ambayo inajumuisha kunyenyekea kwa viungo. Na hili jambo halihusu kuamini katika mambo yanayoshuhudiwa kwa hisia. Kwa sababu, Muislamu na kafiri hawawezi kutofautishwa kwa hilo. Hakika, jambo hili linahusu kuyaamini ya ghaibu ambayo hatujawahi kuyaona wala kuyashuhudia, bali tunayaamini kwa sababu ya habari itokayo kwa Mwenyezi Mungu na habari itokayo kwa Mtume wake. Hii ndiyo imani ambayo anatofautishwa kwayo Muislamu na kafiri; kwa sababu ni kumsadiki tu Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hivyo basi, Muumini anaamini kila alichojulisha Mwenyezi Mungu, au alichojulisha Mtume wake, sawa awe amekiona au hakukiona, na sawa alikifahamu na akakielewa, au akili yake na ufahamu wake haukuongoka kuyaelewa. Tofauti na Az-Zanaadiqa (waasi wakubwa) wanaokanusha mambo ya ghaibu, kwa sababu akili zao pungufu zenye kupuuza hazikuongoka kwayo; basi wakayakanusha wasiyoyaelewa elimu yake. Kwa hivyo, akili zao zikaharibika na fikra zao zikakorogeka. Na zikatakasika akili za Waumini wanaosadiki, walioongoka kwa uwongofu wa Mwenyezi Mungu. Na inaingia katika kuamini (mambo) ya ghaibu, kuamini yote aliyoeleza Mwenyezi Mungu ya ghaibu yaliyopita na yajayo, na hali ya Akhera, na uhakika wa sifa za Mwenyezi Mungu na jinsi zilivyo, na yale waliyosema Mitume kuhusu hayo. Kwa hivyo, wanaamini katika sifa za Mwenyezi Mungu na kuwepo kwazo, na wana yakini nazo, hata kama hawaelewi jinsi zilivyo. Kisha akasema “na hushika Swala,” na hakusema; hufanya swala, wala huleta swala, kwa sababu haitoshi katika hilo kufanya sura yake ya nje tu. Kwa maana, kushika swala, ni kuishika kwa nje kwa kukamilisha nguzo zake, wajibu wake, na masharti yake. Na kuishika kwa ndani kwa kushika roho yake, ambayo ni kuhudhuria moyo ndani yake, na kutafakari anachokisema na kutenda ndani yake. Na swala hii ndiyo aliyosema Mwenyezi Mungu kuihusu. “Hakika swala inazuilia (mambo) machafu na maovu,” na hii (swala) ndiyo ambayo ina malipo. Kwa maana hakuna malipo mazuri kwa mja katika swala yake isipokuwa kwa kile alichokielewa ndani yake. Na zinaingia katika swala, swala za faradhi na za sunnah. Kisha akasema “na hutoa katika tuliyowapa.” Inaingia ndani yake kutoa kwa lazima kama vile zaka, na kumpa matumizi mke, jamaa, watumwa na mfano wao, na pia kutoa kunakopendekezwa katika njia zote za heri. Na (Mwenyezi Mungu) hakutaja yule anayepewa (hapa) kwa sababu ya wingi wa sababu zake na aina mbali mbali za wastahiki wake, na kwa sababu kutoa kama kulivyo ni jambo la kujiweka kwalo karibu na Mwenyezi Mungu. Na alitumia neno “min (katika) linalomaanisha baadhi (ya kitu), ili awatanabahishe kuwa yeye kwa hakika hakutaka kutoka kwao isipokuwa sehemu ndogo kutoka kwa mali zao, ambayo haina madhara kwao wala uzito wowote, bali wao wanafaidika kwa kuitoa, na pia ndugu zao wanafaidika kwayo. Na katika kauli yake “tuliyowapa.” Kuna ishara ya kwamba hizi mali ambazo zimo mikononi mwenu hazipatikani kwa nguvu zenu na uwezo wenu, bali ni riziki ya Mwenyezi Mungu ndiye aliyewapa na akawaneemesha kwacho. Na namna alivyowaneemesha na akawaboresha juu ya wengi katika waja wake, basi mshukuruni kwa kutoa baadhi ya kile alichowaneemesha kwacho, na wafarijini ndugu zenu wasiokuwa nacho (mafukara). Na Mwenyezi Mungu Mtukufu mara nyingi hukusanya kati ya swala na zaka katika Qur-ani, kwa sababu swala inajumuisha kumpwekesha mwabudiwa, nayo zaka na kutoa kwa ajili ya matumizi inajumuisha kuwafanyia ihsani (wema) waja wake. Kwa hivyo, anuani ya kufanikiwa kwa mja ni kumkusudia muabudiwa wake peke yake, na kufanya juhudi kwake katika kuwanufaisha viumbe. Kama vile anuani ya upotovu wa mja ni kutokuwa na mambo mawili haya, kwa hivyo akawa hamkusudii peke yake wala hafanyi ihsani.
#
{4} ثم قال: {والذين يؤمنون بما أنزل إليك} وهو: القرآن والسنة، قال تعالى: {وأنزل الله عليك الكتاب والحكمة} فالمتقون يؤمنون بجميع ما جاء به الرسول ولا يفرقون بين بعض ما أنزل إليه، فيؤمنون ببعضه، ولا يؤمنون ببعضه، إما بجحده، أو تأويله على غير مراد الله ورسوله، كما يفعل ذلك من يفعله من المبتدعة الذين يؤولون النصوص الدالة على خلاف قولهم بما حاصله عدم التصديق بمعناها وإن صدقوا بلفظها، فلم يؤمنوا بها إيماناً حقيقيًّا. وقوله: {وما أنزل من قبلك} يشمل الإيمان بجميع الكتب السابقة، ويتضمن الإيمانُ بالكتب الإيمان بالرسل وبما اشتملت عليه خصوصاً التوراة والإنجيل والزبور، وهذه خاصية المؤمنين يؤمنون بالكتب السماوية كلها وبجميع الرسل فلا يفرقون بين أحد منهم. ثم قال: {وبالآخرة هم يوقنون} والآخرة: اسم لما يكون بعد الموت، وخصه بالذكر بعد العموم؛ لأن الإيمان باليوم الآخر أحد أركان الإيمان؛ ولأنه أعظم باعث على الرغبة والرهبة والعمل، واليقين هو: العلم التام، الذي ليس فيه أدنى شك، الموجب للعمل.
(4) Kisha akasema “Na ambao wanayaamini yaliyoteremshwa kwako” nayo ni Qur-ani na Sunnah. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima.” Kwa hivyo, wachamungu huyaamini yote waliyokuja nayo Mitume, na wala hawatofautishi kati ya baadhi ya yale yaliyoteremshwa juu yake. Wakawa wanaamini baadhi yake na hawaamini baadhi yake, ima kwa kuyakanusha au kwa kuyafasiri kinyume na alivyokusudia Mwenyezi Mungu na Mtume wake; kama anavyofanywa hivyo mwenye kufanya miongoni mwa wazushi wanaoyafasiri maandiko yanayoashiria kinyume na kauli yao kwa ufasiri ambao, matokeo yake ni kutosadiki maana yake hata kama wanasadiki matamshi yake, basi hawakuamini kwayo imani ya kweli. Na kauli yake “na yaliyoteremshwa kabla yako” inakusanya kuamini katika vitabu vyote vilivyotangulia. Na kuamini katika vitabu kunajumuisha kuwaamini Mitume na yale yaliyomo (katika Vitabu hivyo) hasa Taurati, Injili na Zaburi. Na hii ni sifa maalumu ya Waumini, kuwa wanaamini katika vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka mbinguni, na katika Mitume wote, na hawatofautishi baina ya yeyote miongoni mwao. Kisha akasema “na Akhera wana yakini nayo.” Nayo “Akhera” ni jina la yatakayotokea baada ya kufa, na aliitaja hususan baada ya ujumla, kwa sababu kuamini katika Siku ya Mwisho ni moja katika nguzo za imani na kwa sababu ndicho chanzo kikuu zaidi cha kumfanya mtu kuwa na tamaa, hofu, na kutenda vitendo (vyema). Na "yakini" ni kuwa na elimu kamili ambayo haina shaka hata kidogo ndani yake, na ambayo inamlazimu mtu kutenda (matendo mema).
#
{5} {أولئك}؛ أي: الموصوفون بتلك الصفات الحميدة {على هدى من ربهم}؛ أي: على هدى عظيم؛ لأن التنكير للتعظيم، وأيُّ هداية أعظم من تلك الصفات المذكورة المتضمنة للعقيدة الصحيحة والأعمال المستقيمة؟! وهل الهداية في الحقيقة إلا هدايتهم وما سواها مما خالفها فهي ضلالة؟! وأتى بعلى في هذا الموضع الدالة على الاستعلاء، وفي الضلالة يأتي بفي كما في قوله: {وإنا أو إياكم لعلى هدى أو في ضلال مبين}؛ لأن صاحب الهدى مستعلٍ بالهدى مرتفع به، وصاحب الضلال منغمس فيه محتقر. ثم قال: {وأولئك هم المفلحون} والفلاح هو الفوز بالمطلوب والنجاة من المرهوب، حصر الفلاح فيهم؛ لأنه لا سبيل إلى الفلاح إلا بسلوك سبيلهم، وما عدا تلك السبيل فهي سبل الشقاء والهلاك والخسار التي تفضي بسالكها إلى الهلاك؛ فلهذا لما ذكر صفات المؤمنين حقًّا ذكر صفات الكفار المظهرين لكفرهم المعاندين للرسول فقال:
(5) “Hao” yani wale walioelezwa kwa sifa njema hizi “wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi;” yaani, juu ya uwongofu mkubwa, kwa sababu ukawaida (yaani siyo jina maalum) uliopo ndani yake (yaani neno uwongofu) umekusudiwa kutukuza. Na uwongofu upi ambao ni mkubwa kuliko zile sifa zilizotajwa ambazo zinajumuisha itikadi (Imani) sahihi na matendo yaliyonyooka? Na je, sivyo kuwa uwongofu wa hakika siyo isipokuwa uwongofu wao, na kishichokuwa hilo katika yale yanayoupinga basi ni upotovu? Na alitumia neno "’alaa" (juu ya) mahali hapa kuashiria (hali ya) kuwa juu. Na katika upotovu hutumia neno “fii (katika).” Kama katika kauli yake, “Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko juu ya uwongofu au katika upotovu ulio wazi;” kwa sababu mwenye uwongofu yuko juu (ametukuka) kwa sababu ya uwongofu, na yuko juu na ameinuka kwa sababu yake; naye mwenye upotovu amedidimia ndani yake, na anadharauliwa. Kisha akasema “na hao ndio waliofaulu;” na kufaulu ni kufikia mahitaji na kuokoka kutokana na chenye kuhofisha. Na amethibiti kufaulu katika hao peke yao kwa sababu hakuna njia ya kufaulu isipokuwa kwa kufuata njia yao. Na zisizokuwa njia hiyo ni njia za upotovu, maangamio na hasara ambazo humpeleka mwenye kuzifuata katika maangamio. Kwa sababu hiyo, alipotaja sifa za Waumini wa kweli, alitaja sifa za makafiri wanaodhihirisha ukafiri wao, wanaompinga Mtume, akasema:
: 6 - 7 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنْذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنْذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (6) خَتَمَ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ وَعَلَى سَمْعِهِمْ وَعَلَى أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ (7)}.
6. Hakika, wale waliokufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini. (1) 7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana pazia. Nao wana adhabu kubwa.
#
{6} يخبر تعالى {إن الذين كفروا}، أي: اتصفوا بالكفر وانصبغوا به، وصار وصفاً لهم لازماً لا يردعهم عنه رادع، ولا ينجع فيهم وعظ أنهم مستمرون على كفرهم، فسواء عليهم {أأنذرتهم أم لم تنذرهم لا يؤمنون}. وحقيقة الكفر هو الجحود لما جاء به الرسول أو جحد بعضه، فهؤلاء الكفار لا تفيدهم الدعوة إلا إقامة الحجة عليهم، وكأن في هذا قطعاً لطمع الرسول - صلى الله عليه وسلم - في إيمانهم وأنك لا تأس عليهم، ولا تذهب نفسك عليهم حسرات.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba, “Hakika wale waliokufuru", yani wanaosifika kwa ukafiri, na wakajipaka ukafiri, na ukawa sifa ya lazima kwao, na hakuna kemeo lolote linaloweza kuwazuia kutokana nao, na wala mawaidha hayawezi kuwaingia; na kwamba wao wanaendelea katika ukafiri wao. Kwa hivyo, ni sawa kwao "ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini." Na uhakika wa ukafiri ni kukataa aliyokuja nayo Mtume au kukataa baadhi yake. Kwa hivyo, makafiri hao hauwafaidi ulinganizi (kwa Mwenyezi Mungu) isipokuwa tu kwa ajili ya kusimamishia hoja juu yao. Na ni kana kwamba katika hili kuna kukata matumaini ya Mtume - rehema na amani ziwe juu yake - katika kuamini kwao. Kwa hivyo, usiwe na huzuni juu yao, wala nafsi yako isijihiliki kwa kuwasikitikia.
Kisha akataja vizuizi vinavyowazuia kuamini, akasema:
#
{7} {ختم الله على قلوبهم وعلى سمعهم}؛ أي: طبع عليها بطابع لا يدخلها الإيمان ولا ينفذ فيها؛ فلا يعون ما ينفعهم ولا يسمعون ما يفيدهم {وعلى أبصارهم غشاوة}؛ أي: غشاءً وغطاءً وأكنَّة تمنعها عن النظر الذي ينفعهم، وهذه طرق العلم والخير قد سدت عليهم، فلا مطمع فيهم ولا خير يرجى عندهم، وإنما منعوا ذلك وسدت عنهم أبواب الإيمان بسبب كفرهم وجحودهم ومعاندتهم بعد ما تبين لهم الحق، كما قال تعالى: {ونقلب أفئدتهم وأبصارهم كما لم يؤمنوا به أول مرة} وهذا عقاب عاجل، ثم ذكر العقاب الآجل فقال: {ولهم عذابٌ عظيم} وهو عذاب النار، وسخط الجبار المستمر الدائم.
(7) “Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao.” Yaani, amepiga juu yake kwa chapa ambazo imani haiwezi kuingia ndani yake, wala haiwezi kupita ndani yake. Kwa hivyo, hawaelewi kuelewa kwa kuwanufaisha, na wala hawasikii kusikia kwa kuwafaidi. “Na juu ya macho yao pana pazia,” yaani pazia, kifuniko, na kizuizi, ambavyo vinayazuia (macho) wasione kuona kwa kuwanufaisha. Na hizi ndizo njia za elimu na heri ambazo wameshafungiwa, kwa hivyo hakuna matumaini yoyote juu yao, wala haitarajiwi heri yoyote kwao. Na kwa hakika, walizuiwa hayo, na wakafungiwa milango ya imani kwa sababu ya ukafiri wao, na kukataa kwao, na upinzani wao baada ya haki kuwabainikia, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao kama walivyokuwa hawakuamini mara ya kwanza;” na hii ni adhabu ya haraka. Kisha akataja adhabu ya baadaye, akasema: “Basi watapata adhabu kubwa.” Nayo ni adhabu ya Motoni, na ghadhabu ya Al-Jabbar (afanyaye atakalo) yenye kuendelea, yenye kudumu.
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika kuwaeleza wanafiki ambao sura yao ya nje ni Uislamu, lakini ndani yao ni ukafiri:
: 8 - 10 #
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُمْ بِمُؤْمِنِينَ (8) يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ (9) فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّهُ مَرَضًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ (10)}.
8. Na katika watu, wapo wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini. 9. Wanamhadaa Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawahadai ila nafsi zao; nao hawatambui. 10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uongo. (1)
#
{8 - 9} واعلم أن النفاق هو إظهار الخير وإبطان الشر، ويدخل في هذا التعريف النفاق الاعتقادي والنفاق العملي؛ فالنفاق العملي؛ كالذي ذكر النبي - صلى الله عليه وسلم - في قوله: «آية المنافق ثلاث: إذا حدث كذب، وإذا وعد أخلف، وإذا ائتمن خان»؛ وفي رواية «وإذا خاصم فجر». وأما النفاق الاعتقادي المخرج عن دائرة الإسلام؛ فهو الذي وصف الله به المنافقين في هذه السورة وغيرها، ولم يكن النفاق موجوداً قبل هجرة النبي - صلى الله عليه وسلم - من مكة إلى المدينة ولا بعد الهجرة، حتى كانت وقعة بدر وأظهر الله المؤمنين وأعزهم؛ فذل - من في المدينة ممن لم يسلم، فأظهر الإسلامَ بعضُهم خوفاً ومخادعة؛ ولتحقن دماؤهم وتسلم أموالهم، فكانوا بين أظهر المسلمين في الظاهر أنهم منهم، وفي الحقيقة ليسوا منهم. فمن لطف الله بالمؤمنين أن جَلا أحوالهم، ووصفهم بأوصاف يتميزون بها لئلا يغتر بهم المؤمنون، ولينقمعوا أيضاً عن كثير من فجورهم، قال تعالى: {يحذر المنافقون أن تنزل عليهم سورة تنبئهم بما في قلوبهم}؛ فوصفهم الله بأصل النفاق فقال: {وَمِنَ النَّاسِ مَن يقُولُ آمنَّا باللَّهِ وبِاليومِ الآخِرِ وَمَا هُم بمؤمنين}؛ فإنهم يقولون بألسنتهم ما ليس في قلوبهم فأكذبهم الله بقوله: {وما هُم بمؤمنين}؛ لأن الإيمان الحقيقي ما تواطأ عليه القلب واللسان، وإنما هذا مخادعة لله ولعباده المؤمنين، والمخادعة: أن يظهر المخادع لمن يخادعه شيئاً، ويبطن خلافه لكي يتمكن من مقصوده ممن يخادع، فهؤلاء المنافقون سلكوا مع الله وعباده هذا المسلك؛ فعاد خداعهم على أنفسهم، وهذا من العجائب ؛ لأن المخادع إما أن ينتج خداعه ويحصل له مقصوده أو يسلم لا له ولا عليه، وهؤلاء عاد خداعهم على أنفسهم ، فكأنهم يعملون ما يعملون من المكر لإهلاك أنفسهم وإضرارها وكيدها؛ لأن الله لا يتضرر بخداعهم شيئاً، وعباده المؤمنين لا يضرهم كيدهم شيئاً، فلا يضر المؤمنين أن أظهر المنافقون الإيمان؛ فسلمت بذلك أموالهم، وحقنت دماؤهم، وصار كيدهم في نحورهم، وحصل لهم بذلك الخزي والفضيحة في الدنيا، والحزن المستمر بسبب ما يحصل للمؤمنين من القوة والنصرة، ثم في الآخرة لهم العذاب الأليم الموجع المفجع بسبب كذبهم وكفرهم وفجورهم، والحال أنهم من جهلهم وحماقتهم لا يشعرون بذلك.
(8-9) Na jua ya kuwa unafiki ni kuonyesha heri na kuficha shari (maovu). Na unaingia katika huu ufafanuzi unafiki wa kiitikadi (kiimani) na unafiki wa kivitendo. Na unafiki wa kivitendo ni kama ule alioutaja Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - katika kauli yake. "Alama za mnafiki ni tatu: Anapozungumza, husema uongo. Na anapoahidi, huvunja ahadi. Na anapoaminiwa, hufanya hiyana.” Na katika riwaya, “Na anapogombana, hupita mipaka (anaacha haki)." Na ama unafiki wa kiitikadi unaomtaoa (mtu) nje ya duara ya Uislamu; ni ule aliowaeleza nao Mwenyezi Mungu wanafiki katika Sura hii na (sura) nyinginezo. Na unafiki haukuwepo kabla ya kuhama kwa Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - kutoka Makka kwenda Madina, wala baada ya Hijra, mpaka vilipotokea vita vya Badr, na Mwenyezi Mungu akawapa Waumini ushindi na nguvu, na kadhalilika wale waliokuwa Madina miongoni mwa wale ambao hawakusilimu. Kwa hivyo, baadhi yao wakaudhihirisha Uislamu kwa hofu na kuhadaa, na kwa minajili ya kuhifadhi damu zao, na kufanya mali zao ziwe salama. Basi wakawa miongoni mwa Waislamu walioonekana kwa nje zaidi kuwa wao ni miongoni mwao, lakini kwa hakika wao hawakuwa miongoni mwao. Na kutokana na upole wa Mwenyezi Mungu kwa Waumini ni kwamba aliweka wazi hali zao (yaani wanafiki), na akawaeleza kwa maelezo ambayo wanapambanuka kwayo, ili Waumini wasidanganyike nao, na ili waweze kudidimiza (kuzuia) mengi katika maovu yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Wanafiki wanaogopa isije ikateremshwa Sura itakayowatajia yaliyomo katika nyoyo zao.” Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaeleza kuwa wana unafiki asili, akasema: “Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.” Kwa maana, wao kwa hakika husema kwa ndimi zao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Basi Mwenyezi Mungu akawakadhibisha kwa kauli yake “wala wao si wenye kuamini.” Kwa sababu, imani ya kweli ni ile ambayo moyo na ulimi vimekubaliana juu yake. Ama huu mwingine, ni kumhadaa tu Mwenyezi Mungu na waja wake Waumini. Na kuhadaa ni mwenye kuhadaa kumdhihirishia kitu yule anayehadaa na anaficha kinyume chake ili aweze kufikia makusudio yake kutoka kwa anayehadaa. Na hawa wanafiki walimchukulia Mwenyezi Mungu na waja wake njia hii, lakini kuhadaa kwao kukawarudia wao wenywe. Na hili kwa hakika ni katika maajabu. Kwa maana, mwenye kuhadaa ima afanikiwe katika kuhadaa kwake na apate kile anachotaka, au asalimike kwa namna ya kwamba si kwa faida yake wala hasara yake. Lakini hawa kuhadaa kwao kuliwarudia wao wenyewe, kama kwamba wanafanya yale wanayofanya katika vitimbi (hila) ili kujiangamiza nafsi zao, na kuzidhuru, na kuzifanyia vitimbi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu hadhuriki kitu na kuhadaa kwao. Nao waja wake Waumini haviwadhuru kitu vitimbi vyao. Kwa hivyo, haiwadhuru Waumini ikiwa wanafiki watadhihirisha imani. Kwa hivyo mali zao zikasalimika kwa hilo, nazo damu zao zikahifadhika, lakini vitimbi vyao vikawafika kwenye koo zao. Na wakapata kudhalilishwa na fedheha kwa sababu ya hilo katika dunia hii, na huzuni yenye kuendelea kwa sababu ya yale wanayopata Waumini ya kuwa na nguvu na ushindi. Kisha huko Akhera watapata adhabu chungu, yenye kuumiza na kuhuzunisha kwa sababu ya uongo wao, ukafiri wao, na uovu wao. Na hali ni kwamba kwa sababu ya ujinga wao na upumbavu wao, hawalitambui hilo.
#
{10} وقوله: {في قلوبهم مرض}؛ المراد بالمرض هنا: مرض الشك، والشبهات، والنفاق، وذلك أن القلب يعرض له مرضان يخرجانه عن صحته واعتداله: مرض الشبهات الباطلة، ومرض الشهوات المُرْدِيَة. فالكفر والنفاق والشكوك والبِدَع كلها من مرض الشبهات، والزِنا ومحبة الفواحش والمعاصي وفعلها من مرض الشهوات؛ كما قال تعالى: {فيطمع الذي في قلبه مرض}؛ وهو شهوة الزنا، والمعافى من عوفي من هذين المرضين، فحصل له اليقين والإيمان والصبر عن كل معصية، فرفل في أثواب العافية. وفي قوله عن المنافقين: {في قلوبهم مرض فزادهم الله مرضاً}؛ بيان لحكمته تعالى في تقدير المعاصي، على العاصين وأنه بسبب ذنوبهم السابقة؛ يبتليهم بالمعاصي اللاحقة الموجبة لعقوباتها، كما قال تعالى: {ونقلب أفئدتهم وأبصارهم كما لم يؤمنوا به أول مرة}، وقال تعالى: {فلما زاغوا أزاغ الله قلوبهم}، وقال تعالى: {وأما الذين في قلوبهم مرضٌ فزادتهم رجساً إلى رجسهم} فعقوبة المعصية المعصية بعدها، كما أن من ثواب الحسنة الحسنة بعدها؛ قال تعالى: {ويزيد الله الذين اهتدوا هدى}.
(10) Na kauli yake: “Nyoyoni mwao mna maradhi” kilichokusudiwa na maradhi hapa ni maradhi ya shaka, dhana potovu na unafiki. Kwa sababu, moyo hupatwa na maradhi mawili ambayo yanautoa katika afya yake na wastani wake: Maradhi ya dhana potovu, na maradhi ya matamanio mabaya. Kwa hivyo, ukafiri, unafiki, shaka na uzushi, vyote ni katika maradhi ya dhana potovu. Nao uzinzi, na kupenda machafu na maasia na kuyafanya ni katika maradhi ya matamanio, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake” nayo ni matamanio ya zinaa. Naye aliyeepushwa ni yule aliyeepushwa na haya maradhi mawili, kwa hivyo akapata yakini na imani, na subira kutokana na kila maasia, kwa hivyo akajifahiri katika nguo ndefu za usalama. Na katika kauli yake kuhusu wanafiki: “Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi." Inabainisha hekima yake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwaandikia waasi maasia, na kwamba kwa sababu ya madhambi yao yaliyotangulia; anawapa mtihani wa maasia yajayo ambayo yanalazimu adhabu zake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao kama walivyokuwa hawakuamini kwayo mara ya kwanza.” Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Walipopotoka, Mwenyezi Mungu aliziachia nyoyo zao zipotoke.” Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Na ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi yanawazidishia uovu juu ya uovu wao.” Kwa hivyo, adhabu ya maasia ni maasia baada yake, kama vile malipo ya wema ni wema baada yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wale walioongoka.”
: 11 - 12 #
{وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ (11) أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَكِنْ لَا يَشْعُرُونَ (12)}.
11. Na wanapoambiwa: Msifanye uharibifu katika ardhi. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. 12. Tambueni! Kwa hakika, wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.
#
{11} أي: إذا نُهِيَ هؤلاء المنافقون عن الإفساد في الأرض، وهو العمل بالكفر والمعاصي، ومنه إظهار سرائر المؤمنين لعدوهم وموالاتهم للكافرين: {قالوا إنما نحن مصلحون}؛ فجمعوا بين العمل بالفساد في الأرض وإظهار أنه ليس بإفساد، بل هو إصلاح قلباً للحقائق، وجمعاً بين فعل الباطل واعتقاده حقًّا، وهؤلاء أعظم جناية ممن يعمل بالمعاصي مع اعتقاد تحريمها ، فهذا أقرب للسلامة وأرجى لرجوعه، ولما كان في قولهم: {إنما نحن مصلحون}؛ حصر للإصلاح في جانبهم ـ وفي ضمنه أن المؤمنين ليسوا من أهل الإصلاح ـ قلب الله عليهم دعواهم بقوله:
(11) Yaani, wanapokatazwa hawa wanafiki kufanya uharibifu katika ardhi, nao ni kufanya ukafiri na maasia, miongoni mwake ni kufichua siri za Waumini kwa adui wao na kuwategemea makafiri, “wanasema: Bali sisi ni watengenezaji;” basi wakachanganya baina ya kufanya ufisadi katika ardhi na kuonyesha kwamba huo sio ufisadi, bali ni utengenezaji ili kugeuza uhakika. Na kuchanganya kati ya kufanya batili na kuitakidi kuwa ndio haki; na hao wanafanya dhambi kubwa mno kuliko anayetenda maasia pamoja na kuitakidi uharamu wake. Huyu yuko karibu zaidi na usalama, na anatarajiwa zaidi kwamba atarudi. Na pindi ilipokuwa katika kusema kwao “Bali sisi ni watengenezaji," kuzuilia utengenezaji upande wao tu – ambako (huko kuzuilia) kunamaanisha kuwa Waumini sio miongoni mwa watu wanaotengeneza - Mwenyezi Mungu aliwageuzia madai yao hayo kwa kauli yake:
#
{12} {ألا إنهم هم المفسدون} فإنه لا أعظم إفساداً ممن كفر بآيات الله، وصد عن سبيل الله، وخادع الله وأولياءه، ووالى المحاربين لله ورسوله، وزعم مع هذا أن هذا إصلاح، فهل بعد هذا الفساد فساد؟! ولكن لا يعلمون علماً ينفعهم وإن كانوا قد علموا بذلك علماً تقوم به عليهم حجة الله، وإنما كان العمل [بالمعاصي] في الأرض إفساداً؛ لأنه سبب لفساد ما على وجه الأرض من الحبوب والثمار والأشجار والنبات لما يحصل فيها من الآفات التي سببها المعاصي، ولأن الإصلاح في الأرض أن تُعمَر بطاعة الله والإيمان به، لهذا خلق الله الخلق وأسكنهم [في] الأرض وأدرَّ عليهم الأرزاق؛ ليستعينوا بها على طاعته وعبادته، فإذا عُمِل فيها بضده كان سعياً فيها بالفساد وإخراباً لها عمَّا خُلِقت له.
(12) “Hakika wao ndio waharibifu." Kwa maana, hakuna mharibifu mkubwa zaidi kuliko mwenye kukufuru (kukataa) aya (ishara) za Mwenyezi Mungu, na akazuia njia ya Mwenyezi Mungu. Na akamhadaa Mwenyezi Mungu na vipenzi wake, na akawategemea wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na akadai pamoja na hayo kuwa huko ni kutengeneza. Basi je, baada ya uharibifu huu kuna uharibifu mwingine? Lakini wao hawajui elimu ya kuwanufaisha, ingawa walikwisha jua elimu ambayo kwayo hoja ya Mwenyezi Mungu ilisimama juu yao. Na kulikuwa kutenda [maasia] katika ardhi uharibifu kwa kuwa ndiyo sababu ya kuharibika kwa yale yaliyopo juu ya uso wa ardhi kama vile nafaka, matunda, miti, na mimea, kwa sababu ya ule uharibifu unaovipata kwa sababu ya maasia. Na kwa sababu kutengeneza mambo katika ardhi ni kuiimarisha kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumwamini. Hii ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliwaumba viumbe na akawafanya kuishi katika ardhi, na akawapa riziki ili wajisaidie kwayo katika kumtii na kumuabudu. Kwa hivyo, yakifanyika humo kinyume chake, basi hilo litakuwa kuwania kufanya uharibifu (ufisadi) ndani yake na kuibomoa, tofauti na ilichoumbwa (ardhi) kwa ajili yake.
: 13 #
{وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَكِنْ لَا يَعْلَمُونَ (13)}.
13. Na wanapoambiwa: Aminini kama walivyoamini watu. Husema: Tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui tu.
#
{13} أي: إذا قيل للمنافقين آمنوا كما آمن الناس، أي: كإيمان الصحابة رضي الله عنهم وهو: الإيمان بالقلب واللسان، قالوا بزعمهم الباطل: أنؤمن كما آمن السفهاء؟ يعنون ـ قبحهم الله ـ الصحابة رضي الله عنهم؛ لزعمهم أن سفههم أوجب لهم الإيمان، وترك الأوطان، ومعاداة الكفار، والعقل عندهم يقتضي ضد ذلك، فنسبوهم إلى السَفَه، وفي ضمن ذلك أنهم هم العقلاء أرباب الحجى والنُهى؛ فرد الله ذلك عليهم وأخبر أنهم هم السفهاء على الحقيقة؛ لأن حقيقة السفه جهل الإنسان بمصالح نفسه، وسعيه فيما يضرها، وهذه الصفة منطبقة عليهم، [وصادقة عليهم] كما أن العقل والحجى معرفة الإنسان بمصالح نفسه والسعي فيما ينفعه وفي دفع ما يضره، وهذه الصفة منطبقة على الصحابة والمؤمنين؛ فالعبرة بالأوصاف والبرهان، لا بالدعاوي المجردة والأقوال الفارغة.
(13) Yaani wanapoambiwa wanafiki “Aminini kama walivyoamini watu,” yaani, kama imani ya maswahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ambayo ni imani kwa moyo na ulimi. Wanasema kwa madai yao ya uwongo, "tuamini kama walivyoamini wapumbavu?" Wakimaanisha - Mwenyezi Mungu awalaani - maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao; wakidai kwamba upumbavu wao (maswahaba) uliwafanya kuamini, na kuondoka katika nchi zao, na kuwafanyia uadui makafiri. Lakini akili zao (wanafiki) zikaona kwamba kinyume cha hayo ndicho kilifaa, hivyo basi wakawanasibisha (maswahaba) na upumbavu. Na ndani ya hilo ni kwamba wao ndio wenye hekima zaidi, wababe wa ufahamu na akili. Lakini Mwenyezi Mungu akawajibu hilo, na akasema kwamba wao ndio wapumbavu kwa hakika. Kwa sababu uhakika wa upumbavu ni mtu kutojua masilahi ya nafsi yake, na akawania katika yale yenye kuidhuru, na sifa hii inawafaa zaidi, [na ni ya ukweli juu yao]. Kama vile akili na ujuzi ni mtu kujua masilahi ya nafsi yake na akawania katika yale yenye kumnufaisha, na katika kuzuia yale yenye kumdhuru. Na sifa hii inawafaa maswahaba na Waumini. Kwa hivyo, la kuzingatiwa ni sifa (maelezo) na dalili, siyo madai tu na maneno matupu.
: 14 - 15 #
{وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَى شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ (14) اللَّهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ (15)}.
14. Na wanapokutana na walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao na mashet'ani wao, husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi tunawadhihaki tu. 15. Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawaacha katika upotovu wao wakitangatanga ovyo.
#
{14} هذا من قولهم بألسنتهم ما ليس في قلوبهم، وذلك أنهم إذا اجتمعوا بالمؤمنين أظهروا أنهم على طريقتهم، وأنهم معهم، فإذا خلوا إلى شياطينهم ـ أي كبرائهم ورؤسائهم بالشر ـ قالوا: إنا معكم في الحقيقة وإنما نحن مستهزئون بالمؤمنين بإظهارنا لهم أننا على طريقتهم، فهذه حالهم الباطنة والظاهرة، ولا يحيق المكر السيئ إلا بأهله.
(14) Haya ni kutokana na kusema kwao kwa ndimi zao yale yasiyokuwa kakika nyoyo zao. Na hilo ni kwamba wanapokutana na Waumini, wanadhihirisha kuwa wako katika njia yao (njia ya waumini), na kwamba wako pamoja nao. Na wanapobaki peke yao na mashetani wao – yaani viongozi wao na wakuu wao katika shari – wanasema: Sisi tu pamoja nanyi kwa hakika, lakini sisi tunawakejeli tu Waumini kwa kuwadhihirishia kwamba sisi tuko kwenye njia yao. Na hii ndiyo hali yao ya ndani na ya nje; na vitimbi viovu havimpati isipokuwa mwenyewe aliyevifanya.
#
{15} قال تعالى: {الله يستهزئُ بهم ويمدهم في طغيانهم يعمهون}؛ وهذا جزاء لهم على استهزائهم بعباده، فمن استهزائه بهم أن زين لهم ما كانوا فيه من الشقاء، والأحوال الخبيثة حتى ظنوا أنهم مع المؤمنين لَمَّا لم يسلطْ الله المؤمنين عليهم، ومن استهزائه بهم يوم القيامة: أنه يعطيهم مع المؤمنين نوراً ظاهراً، فإذا مشى المؤمنون بنورهم طفئ نور المنافقين وبقُوا في الظلمة بعد النور متحيرين، فما أعظم اليأس بعد الطمع {ينادونهم ألم نكن معكم، قالوا بلى ولكنكم فتنتم أنفسكم وتربصتم وارتبتم ... } الآية. قوله: {ويمدهم}؛ أي: يزيدهم {في طغيانهم}؛ أي: فجورهم وكفرهم {يعمهون}؛ أي: حائرون مترددون، وهذا من استهزائه تعالى بهم.
(15) Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawaacha katika upotovu wao wakitangatanga ovyo." Na haya ni malipo yao kwa kukejeli kwao waja wake. Na katika kejeli yake (Mwenyezi Mungu) kwao ni kwamba aliwapambia maovu ambayo wamo ndani yake na hali zao mbaya, mpaka wakadhani kuwa wako pamoja na Waumini pindi Mwenyezi Mungu alipoacha kuwapa Waumini mamlaka juu yao. Na katika kejeli yake kwao Siku ya Kiyama ni kwamba atawapa nuru iliyo dhahiri pamoja na Waumini. Na Waumini watakapokwenda na nuru yao, nuru ya wanafiki itazimika, na watabaki wamechanganyikiwa gizani baada ya kuwa na nuru. Basi ni kukata tamaa kulikoje huku baada ya kuwa na matumaini. "Watawaita (wawaambie): Kwani hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkangoja, na mkatia shaka..." hadi mwisho wa aya. Kauli yake "na atawaacha;" yaani, atawazidishia muhula "katika upotovu wao" yani uovu wao na ukafiri wao; "wakitangatanga ovyo" yaani, huku wamechanganyikiwa na kusitasita. Na hii ni katika kejeli yake (Mwenyezi Mungu) Mtukufu kwao.
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akifichua uhakika wa hali yao:
: 16 #
{أُولَئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَى فَمَا رَبِحَتْ تِجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ (16)}
16. Hao ndio walioununua upotovu kwa uwongofu; lakini biashara yao haikupata faida, wala hawakuwa wenye kuongoka.
#
{16} أولئك؛ أي: المنافقون الموصوفون بتلك الصفات {الذين اشتروا الضلالة بالهدى}؛ أي: رغبوا في الضلالة رغبة المشتري في السلعة ، التي ـ من رغبته فيها ـ يبذل فيها الأموال النفيسة، وهذا من أحسن الأمثلة، فإنه جعل الضلالة التي هي غاية الشر كالسلعة، وجعل الهدى الذي هو غاية الصلاح بمنزلة الثمن، فبذلوا الهدى رغبة عنه في الضلالة رغبة فيها، فهذه تجارتهم؛ فبئس التجارة، وهذه صفقتهم؛ فبئست الصفقة. وإذا كان من يبذل ديناراً في مقابلة درهم خاسراً فكيف من بذل جوهرة وأخذ عنها درهماً، فكيف من بذل الهدى في مقابلة الضلالة، واختار الشقاء على السعادة، ورغب في سافل الأمور وترك عاليها ، فما ربحت تجارته بل خسر فيها أعظم خسارة، أولئك الذين خسروا أنفسهم وأهليهم يوم القيامة ألا ذلك هو الخسران المبين. وقوله: {وما كانوا مهتدين}؛ تحقيق لضلالهم وأنهم لم يحصل لهم من الهداية شيء، فهذه أوصافهم القبيحة، ثم ذكر مثلهم [الكاشف لها غاية الكشف]، فقال:
(16) "Hao", yaani wanafiki wanaosifika kwa sifa hizi "ndio walionunua upotovu kwa uwongofu." Yaani, walitaka sana upotovu kama vile mnunuzi anavyotaka sana bidhaa, ambayo - kwa sababu ya kuitaka (kuipenda) - anaitolea mali yenye thamani kubwa. Na huu ni katika mifano mizuri kabisa, kwani (mnafiki) aliufanya upotovu ambao ndiyo shari kubwa zaidi kuwa bidhaa. Na akaufanya uwongofu ambao ndio kutengenea kukubwa zaidi pahali pa bei, kwa hivyo wakautoa uwongofu kwa kuukataa katika kuutaka upotovu. Basi hii ndiyo biashara yao; nayo ndiyo biashara mbaya mno. Na haya ndiyo mapatano yao; nayo ndiyo mapatano mabaya mno. Na ikiwa mwenye kutoa dinari moja na kuchukua dirhamu moja ni mwenye hasara, basi atakuwaje mwenye kutoa johari na kuchukua dirhamu moja badala yake? Na vipi mwenye kutoa uwongofu badala ya upotofu, na akachagua uovu badala ya kufaulu (furaha), na akapenda mambo duni na akayaacha ya juu? Basi biashara yake haikupata faida, bali alipata hasara kubwa sana ndani yake. Hao ndio waliozihasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri. Na kauli yake "wala hawakuwa wenye kuongoka" ni kusisitiza upotofu wao, na kwamba hawakupata chochote katika uwongofu. Na hizi ndizo sifa zao mbaya. Kisha akataja mfano wao [unaoziweka wazi (hizi sifa) uwazi wa juu zaidi], akasema:
: 17 - 20 #
{مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَا يُبْصِرُونَ (17) صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ (18) أَوْ كَصَيِّبٍ مِنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ مِنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ وَاللَّهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ (19) يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُمْ مَشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (20)}.
(17) Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, na ulipoangaza vile vilivyoko kandokando yake, Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawaacha katika viza mbalimbali, hawaoni. (18) Ni viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea. (19) Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni, ina viza mbalimbali, na radi, na umeme; wakawa wanatia vidole vyao katika masikio yao kwa sababu ya mapigo ya radi, kwa kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri. (20) Unakaribia umeme kunyakua macho yao. Kila ukiwatolea mwangaza, wanatembea ndani yake. Na linapowawia giza, wanasimama. Na angelitaka Mwenyezi Mungu angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
#
{17} أي: مثلهم المطابق لما كانوا عليه كمثل الذي استوقد ناراً أي: كان في ظلمة عظيمة، وحاجة إلى النار شديدة فاستوقدها من غيره، ولم تكن عنده معدة بل هي خارجة عنه، فلما أضاءت النار ما حوله، ونظر المحل الذي هو فيه وما فيه من المخاوف، وأمنها وانتفع بتلك النار، وقرت بها عينه، وظن أنه قادر عليها، فبينما هو كذلك، إذ ذهب الله بنوره؛ فزال عنه النور وذهب معه السرور، وبقي في الظلمة العظيمة والنار المحرقة؛ فذهب ما فيها من الإشراق وبقي ما فيها من الإحراق، فبقي في ظلمات متعددة: ظلمة الليل، وظلمة السحاب، وظلمة المطر، والظلمة الحاصلة بعد النور، فكيف يكون حال هذا الموصوف؟ فكذلك هؤلاء المنافقون استوقدوا نار الإيمان من المؤمنين ولم تكن صفة لهم، فاستضاؤوا بها مؤقتاً وانتفعوا؛ فحقنت بذلك دماؤهم، وسلمت أموالهم، وحصل لهم نوع من الأمن في الدنيا، فبينما هم كذلك إذ هجم عليهم الموت؛ فسلبهم الانتفاع بذلك النور، وحصل لهم كل هم وغم وعذاب، وحصل لهم ظلمة القبر، وظلمة الكفر، وظلمة النفاق، وظلمة المعاصي على اختلاف أنواعها، وبعد ذلك ظلمة النار وبئس القرار؛ فلهذا قال تعالى عنهم:
(17) Yani mfano wao unaoingiana na walivyo ni mfano wa yule aliyewasha moto, yani alikuwa katika giza kubwa na akihitaji moto vikubwa. Basi akauwasha kutoka kwa mtu mwingine, na haukuwa tayari pamoja naye, bali alichukua kutoka kwa mwingineye. Pindi moto ulipoangaza vilivyokuwa kandokando yake, na akatazama mahali ambapo yeye yupo na hofu iliyopo hapo, na amani yake (moto huo), na akanufaika na moto huo, na macho yake yakaburudika kwa moto huo; na akadhani kuwa ana uwezo juu yake. Basi, alipokuwa hivyo, hapo Mwenyezi Mungu akaiondoa nuru yake, kwa hivyo, nuru hiyo ikamtoka na furaha ikaondoka pamoja nao, na akabaki ndani ya giza totoro na moto wenye kuchoma. Kwa hivyo, kule kuangaza kulikokuwa ndani yake kukaondoka, na kukabaki kule kuchoma kuliomo ndani yake, basi akabaki katika giza mbalimbali: giza la usiku, giza la mawingu, giza la mvua na giza lilichotokea baada ya nuru hiyo. Basi inakuaje hali ya huyu anayeelezwa? Kadhalika, wanaafiki hawa waliwasha moto wa imani kutoka kwa Waumini, na haikuwa sifa yao. Basi wakapata mwangaza wake kwa muda, na wakanufaika. Kwa hivyo, damu zao zikahifadhika kwa hilo, na mali zao zikasalia salama, na wakapata usalama fulani katika dunia hii. Na walipokuwa hivyo, mauti yakawashambulia ghafla na yakawanyang'anya kunufaika na nuru hiyo, na wakapatwa na kila wasiwasi na dhiki na adhabu. Na wakapatwa na giza la kaburini, na giza la ukafiri, na giza la unafiki, na giza la maasia kwa aina zake mbalimbali. Na baada ya hayo, giza la Moto, na ni makazi mabaya mno. Ndio maana Mwenyezi Mungu alisema kuwahusu:
#
{18} {صمٌّ}؛ أي: عن سماع الخير {بكمٌ}، أي: عن النطق به {عميٌ} عن رؤية الحق {فهم لا يرجعون}؛ لأنهم تركوا الحق بعد أن عرفوه؛ فلا يرجعون إليه، بخلاف من ترك الحق عن جهل وضلال؛ فإنه لا يعقل، وهو أقرب رجوعاً منهم.
(18) "Ni viziwi" yani wasiosikia heri "mabubu" yani wasioweza kuitamka heri, "vipofu" yani wasioweza kuiona haki. "Kwa hivyo hawatarejea" kwa sababu wao waliiacha haki baada ya kuijua; basi hawairudii. Tofauti na mwenye kuiacha haki kwa ujinga na upotofu; kwa sababu hakuielewa, basi yeye yuko karibu zaidi na kurudi katika haki.
#
{19} ثم قال تعالى: {أو كصيب من السماء}؛ أي: كصاحب صيب وهو: المطر الذي يصوب؛ أي: ينزل بكثرة {فيه ظلمات}؛ ظلمة الليل، وظلمة السحاب، وظلمة المطر، وفيه {رعد}؛ وهو: الصوت الذي يسمع من السحاب وفيه {برق}؛ وهو الضوء اللامع المشاهد من السحاب.
(19) Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema "Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni" yani kama yule wa mvua. Nayo ni mvua inayonyesha kwa wingi. "Ina giza mbalimbali"; giza la usiku, na giza la mawingu, na giza la mvua, na pia ina "radi". Nayo ni ile sauti ya mngurumo inayosikia kutoka kwenye mawingu. Na ina "umeme", nao ni mwangaza unaong'aa na kuonekana kutoka kwenye mawingu.
#
{20} {كلما أضاء لهم}؛ البرق في تلك الظلمات {مشوا فيه وإذا أظلم عليهم قاموا}؛ أي: وقفوا، فهكذا حالة المنافقين إذا سمعوا القرآن، وأوامره ونواهيه، ووعده ووعيده؛ جعلوا أصابعهم في آذانهم، وأعرضوا عن أمره ونهيه، ووعده ووعيده؛ فيروعهم وعيده، وتزعجهم وعوده، فهم يعرضون عنها غاية ما يمكنهم ويكرهونها كراهة صاحب الصيب الذي يسمع الرعد فيجعل أصابعه في أذنيه خشية الموت، فهذا ربما حصلت له السلامة ، وأما المنافقون فأنى لهم السلامة وهو تعالى محيط بهم قدرة وعلماً فلا يفوتونه ولا يعجزونه، بل يحفظ عليهم أعمالهم ويجازيهم عليها أتم الجزاء. ولما كانوا مبتلين بالصمم والبكم والعمى المعنوي ومسدودة عليهم طُرُقُ الإيمان قال تعالى: {ولو شاء الله لذهب بسمعهم وأبصارهم}؛ أي الحسية، ففيه تخويف لهم وتحذير من العقوبة الدنيوية؛ ليحذروا فيرتدعوا عن بعض شرهم ونفاقهم {إن الله على كل شيء قدير}؛ فلا يعجزه شيء، ومن قدرته أنه إذا شاء شيئاً فعله من غير ممانع ولا معارض. وفي هذه الآية وما أشبهها ردٌّ على القدرية القائلين بأن أفعالَهم غير داخلة في قدرة الله تعالى؛ لأن أفعالهم من جملة الأشياء الداخلة في قوله: {إن الله على كل شيء قدير}.
(20) "Kila ukiwatolea mwangaza" yani umeme huo katika giza hizo. "Wanatembea ndani yake. Na linapowawia giza, wanasimama." Yani wanaacha kutembea. Na hivi ndivyo ilivyo hali ya wanafiki wanapoisikia Qur-ani na maamrisho yake na makatazo yake, na ahadi zake na vitisho vyake, wanatia vidole vyao katika masiki yao. Na wanayapa mgongo maamrisho yake na makatazo yake, na ahadi zake, na vitisho vyake. Kwa hivyo, vitisho hivyo vyake vinawatia hofu, na ahadi zake zinawasumbua. Kwa hivyo, wanajiepusha nazo kadiri wawezavyo, na wanazichukia kama vile yule wa mvua anayesikia radi; kwa hivyo akatia vidole vyake katika masikio yake mawili kwa kuogopa kifo. Na huyu (wa mvua) huenda akapata usalama. Ama wanafiki, itakuwaje wapate usalama, ilhali Yeye Mtukufu amewazunguka kwa uwezo na elimu? Basi hawawezi kumkwepa, na wala hawawezi kumshinda. Bali anawahifadhia matendo yao, na atawalipa malipo kamili zaidi. Na pindi walipojaribiwa na uziwi, ububu, na upofu (visivyo vya hisia), na wakafungiwa njia za imani, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema "Na angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao," yani kihisia. Basi ndani yake kuna kuwahofisha, na kuwatahadharisha dhidi ya adhabu ya duniani, ili wajihadhari, na wakomeke kutokana na baadhi ya maovu yao na unafiki wao. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." Hakimshindi chochote. Na katika uwezo wake ni kwamba akitaka kitu, anakifanya bila ya kizuizi wala mpinzani. Na katika aya hii na mfano wake, kuna majibu kwa Al-Qadariyya wanaosema kuwa vitendo vyao haviingii katika uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu vitendo vyao ni miongoni mwa mambo yanayoingia katika kauli yake "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu."
: 21 - 22 #
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ (21) الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَكُمْ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّهِ أَنْدَادًا وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ (22)}.
(21) Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate Kumcha Mwenyezi Mungu. (22) (Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni ardhi hii kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa. Na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa mazao yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua. (1)
#
{21} هذا أمر عام لجميع الناس بأمر عام وهو العبادة الجامعة لامتثال أوامر الله واجتناب نواهيه وتصديق خبره، فأمرهم تعالى بما خلقهم له، قال تعالى: {وما خلقت الجن والإنس إلا ليعبدون}؛ ثم استدل على وجوب عبادته وحده بأنه ربكم الذي رباكم بأصناف النعم، فخلقكم بعد العدم، وخلق الذين من قبلكم.
(21) Hii ni amri ya jumla kwa watu wote wenye amri ya jumla, ambayo ni ibada inayojumuisha kufuata amri za Mwenyezi Mungu, na kuwacha makatazo yake, na kusadiki habari zake. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha lile alilowaumbia kwa ajili yake. Mwenyezi Mungu alisema: "Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi". Kisha akaleta dalili ya ulazima wa kumuabudu Yeye peke yake, kwamba Yeye ndiye Mola wenu Mlezi ambaye amekuleeni kwa aina mbalimbali za neema. Alikuumbeni baada ya kutokuwepo, na akawaumba wale wa kabla yenu.
#
{22} وأنعم عليكم بالنعم الظاهرة والباطنة، فجعل لكم الأرض فراشاً تستقرون عليها، وتنتفعون بالأبنية والزراعة والحراثة والسلوك من محل إلى محل، وغير ذلك من وجوه الانتفاع بها، وجعل السماء بناء لمسكنكم وأودع فيها من المنافع ما هو من ضروراتكم وحاجاتكم كالشمس والقمر والنجوم {وأنزل من السماء ماء}؛ والسماء هو: كل ما علا فوقك فهو سماء، ولهذا قال المفسرون: المراد بالسماء ههنا السحاب، فأنزل منه تعالى ماء {فأخرج به من الثمرات}؛ كالحبوب والثمار من نخيل وفواكه وزروع وغيرها {رزقاً لكم}؛ به ترتزقون وتتقوتون وتعيشون وتفكهون ، {فلا تجعلوا لله أنداداً}؛ أي: أشباهاً ونظراء من المخلوقين؛ فتعبدونهم كما تعبدون الله، وتحبونهم كما تحبونه ، وهم مِثْلكم مخلوقون مرزوقون مُدبَّرون، لا يملكون مثقال ذرة في الأرض، ولا في السماء ، ولا ينفعونكم ولا يضرون {وأنتم تعلمون}؛ أن الله ليس له شريك، ولا نظير لا في الخلق والرزق والتدبير، ولا في الألوهية والكمال ، فكيف تعبدون معه آلهة أخرى مع علمكم بذلك؟ هذا من أعجب العجب وأسفه السفه. وهذه الآية جمعت بين الأمر بعبادة الله وحده، والنهي عن عبادة ما سواه، وبيان الدليل الباهر على وجوب عبادته وبطلان عبادة ما سواه، وهو ذكر توحيد الربوبية المتضمن انفراده بالخلق والرزق والتدبير، فإذا كان كل أحد مقرًّا بأنه ليس له شريك بذلك فكذلك؛ فليكن الإقرار بأن الله ليس له شريك في عبادته ، وهذا أوضح دليل عقلي على وحدانية الباري تعالى وبطلان الشرك. وقوله: {لعلكم تتقون}؛ يحتمل أن المعنى أنكم إذا عبدتم الله وحده اتقيتم بذلك سخطه وعذابه؛ لأنكم أتيتم بالسبب الدافع لذلك، ويحتمل أن يكون المعنى أنكم إذا عبدتم الله صرتم من المتقين الموصوفين بالتقوى، وكلا المعنيين صحيح، وهما متلازمان، فمن أتى بالعبادة كاملة؛ كان من المتقين، ومن كان من المتقين؛ حصلت له النجاة من عذاب الله، وسخطه.
(22) Na akakuneemesheni kwa neema zilizo dhahiri na zilizofichika. Amekufanyieni ardhi kuwa ni tandiko. Mnakaa sawasawa juu yake, na mnanufaika kwa majengo, kilimo, kulima, na kutembea kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine; na visivyo hivyo miongoni mwa aina za kunufaika nayo. Na akaifanya mbingu kuwa kama mjengo (paa) kwa sababu ya maisha yenu, na akaweka humo manufaa ambayo ni katika mahitaji yenu kama vile jua, mwezi na nyota. "Na akateremsha maji kutoka mbinguni". Na mbingu ni kila kilichoko juu yako, basi hilo ni mbingu. Na kwa sababu hii wafasiri walisema: Kinachokusudiwa hapa na "mbingu" ni mawingu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha maji kutoka humo "na kwayo akatoa mazao" kama vile, nafaka na matunda mfano mitende, mimea na vinginevyo "yawe riziki zenu." Kwavyo mnapata riziki, chakula kikuu, na mnaishi na mnakula matunda. "Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika." Yani wa kumfanana na wenza miongoni mwa viumbe; hivyo mkawaabudu kama mnavyomuabudu Mwenyezi Mungu, na mnawapenda kama mnavyompenda Mwenyezi Mungu, ilhali wao ni kama nyinyi, wameumbwa, wanaruzukiwa na wanaendeshwa. Wao hawamiliki uzito wa chembe katika ardhi wala katika mbingu, wala hawawanufaishi wala hawawadhuru. "Na hali nyinyi mnajua" kwamba Mwenyezi Mungu hana mshirika, wala aliye sawa naye siyo katika kuumba, kuruzuku, na kuendesha mambo, wala katika ibada na ukamilifu. Basi vipi mnaabudu miungu wengine pamoja naye na hali mnajua hilo? Hili ni katika maajabu ya maajabu, na upumbavu wa upumbavu. Na aya hii inajumuisha kati ya amri ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kukataza kumwabudu asiyekuwa Yeye. Na kubainisha dalili wazi ya ulazima wa kumuabudu Yeye, na ubatili wa kumuabudu asiyekuwa Yeye. Nako ni kutaja Tauhid Ar-rububiyya ambayo inajumuisha kumpwekesha katika uumbaji, kuruzuku na kuendesha mambo. Basi ikiwa kila mtu anakiri kwamba yeye (Mwenyezi Mungu) hana mshirika katika hayo, basi vivyo hivyo naakiri kwamba (Mwenyezi Mungu) hana mshirika katika ibada yake. Na hii ndiyo dalili ya kiakili ya wazi mno juu ya upweke wa Muumba, Mtukufu, na ubatili wa ushirikina. Na kauli yake (Mwenyezi Mungu) "ili mpate kuokoka" inawezekana kuwa maana yake ni kwamba, mkimuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, mtaokoka kwa hilo ghadhabu yake na adhabu yake; kwa sababu mmefanya sababu inayozuia hilo. Na inawezekana kuwa maana yake ni kwamba mkimuabudu Mwenyezi Mungu, mtakuwa miongoni mwa wachamungu ambao wanasifika kwa uchamungu. Na kila ya maana mbili hizi ni sahihi. Nazo (maana mbili hizi) zinaenda sambamba. Kwa sababu, mwenye kufanya ibada kamili; atakuwa miongoni mwa wachamungu. Na atakayekuwa miongoni mwa wachamungu, atapata kuokoka na adhabu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.
: 23 - 24 #
{وَإِنْ كُنْتُمْ فِي رَيْبٍ مِمَّا نَزَّلْنَا عَلَى عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِنْ مِثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (23) فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا وَلَنْ تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ (24)}.
(23) Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mja wetu, basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. (24) Na ikiwa hamtofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa makafiri.
#
{23} وهذا دليل عقلي على صدق رسول الله - صلى الله عليه وسلم - وصحة ما جاء به فقال: وإن كنتم ـ يا معشر المعاندين للرسول الرادين دعوته الزاعمين كذبه ـ في شك، واشتباه مما نزلنا على عبدنا، هل هو حق أو غيره؟ فههنا أمر نَصَفٌ فيه الفيصلة بينكم وبينه، وهو: أنه بشر مثلكم ليس من جنس آخر ، وأنتم تعرفونه منذ نشأ بينكم لا يكتب ولا يقرأ، فأتاكم بكتاب زعم أنه من عند الله، وقلتم أنتم إنه تقوَّله وافتراه، فإن كان الأمر كما تقولون؛ فأتوا بسورة من مثله، واستعينوا بمن تقدرون عليه من أعوانكم وشهدائكم، فإن هذا أمر يسير عليكم، خصوصاً وأنتم أهل الفصاحة والخطابة والعداوة العظيمة للرسول، فإن جئتم بسورة من مثله؛ فهو كما زعمتم، وإن لم تأتوا بسورة من مثله وعجزتم غاية العجز [ولن تأتوا بسورة من مثله، ولكنّ هذا التقييم على وجه الإنصاف والتنزل معكم]؛ فهذا آية كبيرة ودليل واضح جلي على صدقه وصدق ما جاء به؛ فيتعين عليكم اتباعه، واتقاء النار التي بلغت في الحرارة العظيمة والشدة، أن كان وقودها الناس والحجارة، ليست كنار الدنيا التي إنما تُتَّقَد بالحطب، وهذه النار الموصوفة مُعَدة ومُهَيأة للكافرين بالله ورسله؛ فاحذروا الكفر برسوله بعدما تبين لكم أنه رسول الله.
(23) Na hii ni dalili ya kiakili juu ya ukweli wa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake na usahihi wa yale aliyoyaleta. Akasema: “Na ikiwa - enyi kundi la wale wanaompinga Mtume, wanaokataa ulinganizi wake, wanaodai kuwa ni mwongo - mna shaka, mchanganyiko juu ya hayo tuliyomteremshia mja wetu; je, ni kweli au ni linginelo? Basi hapa kuna jambo la uadilifu lenye upambanuzi baina yenu na yeye, nalo ni kuwa yeye ni binadamu kama nyinyi, sio wa jamii nyingine. Nanyi mnamjua tangu alipoinukia kati yenu, hawezi kuandika wala kusoma. Kisha akawajia na kitabu anachodai kuwa kimetoka kwa Mwenyezi Mungu. Nanyi mkasema: Hakika yeye amekitunga na akakizua. Kwa hivyo, ikiwa mambo ni kama mnavyosema, basi leteni sura moja ya mfano wake. Na tafuteni msaada kutoka kwa yeyote mnayeweza katika wasaidizi wenu na mashahidi wenu, kwani hili ni jambo jepesi kwenu. Hasa kwamba nyinyi ni watu wa ufasaha na usemi, na uadui mkubwa kwa Mtume. Hivyo, mkija na sura mfano wake, basi ni kama mlivyodai. Na msipoleta sura mfano wake, na mkashindwa kabisa [na wala hamtaleta sura mfano wake. Lakini tathmini hii ni katika mlango wa kufanya uadilifu tu na kuendelea kwenda ni nyinyi.] Basi hii ni ishara kubwa, na dalili ya wazi na ya peupe juu ya ukweli wake (Mtume), na ukweli wa aliyokuja nayo. Basi ni wajibu juu yenu kumfuata, na kuepukana na Moto ambao ulifika katika ukubwa na ukali wa joto lake kiwango kwamba kuni zake ni watu na mawe, siyo kama moto wa duniani ambao unawashwa tu kwa kuni. Na moto huu ulioelezwa umetengenezwa na kutayarishwa kwa ajili ya wanaomkufuru Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Hivyo, jihadharini na kumkufuru Mtume wake baada ya kukubainikieni kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
#
{24} وهذه الآية ونحوها يسمونها: آية التحدي، وهو: تعجيز الخلق عن أن يأتوا بمثل هذا القرآن أو يعارضوه بوجه، قال تعالى: {قل لئن اجتمعت الإنس والجن على أن يأتوا بمثل هذا القرآن لا يأتون بمثله ولو كان بعضهم لبعض ظهيراً}؛ وكيف يقدر المخلوق من تراب أن يكون كلامه ككلام رب الأرباب، أم كيف يقدر الفقير الناقص من جميع الوجوه أن يأتي بكلام ككلام الكامل، الذي له الكمال المطلق، والغنى الواسع من جميع الوجوه ؟ هذا ليس في الإمكان ولا في قدرة الإنسان، وكل من له أدنى ذوق ومعرفة بأنواع الكلام ، إذا وزن هذا القرآن [العظيم] بغيره من كلام البلغاء، ظهر له الفرق العظيم. وفي قوله: {وإن كنتم في ريب}؛ إلى آخره، دليل على أن الذي يرجى له الهداية من الضلالة هو الشاك الحائر، الذي لم يعرف الحق من الضلالة، فهذا الذي إذا بين له الحق حري باتباعه إن كان صادقاً في طلب الحق، وأما المعاند الذي يعرف الحق ويتركه، فهذا لا يمكن رجوعه؛ لأنه ترك الحق بعد ما تبين له، لم يتركه عن جهل فلا حيلة فيه، وكذلك الشاكُّ الذي ليس بصادق في طلب الحق بل هو معرض غير مجتهد بطلبه؛ فهذا في الغالب لا يوفق. وفي وصف الرسول بالعبودية في هذا المقام العظيم دليل على أن أعظم أوصافه - صلى الله عليه وسلم - قيامه بالعبودية التي لا يلحقه فيها أحد من الأولين والآخرين، كما وصفه بالعبودية في مقام الإسراء فقال: {سبحان الذي أسرى بعبده ليلاً}؛ وفي مقام الإنزال فقال: {تبارك الذي نزل الفرقان على عبده ليكون للعالمين نذيراً}. وفي قوله: {أعدت للكافرين}؛ ونحوها من الآيات دليل لمذهب أهل السنة والجماعة أن الجنة والنار مخلوقتان، خلافاً للمعتزلة. وفيها أيضاً: أن الموحدين وإن ارتكبوا بعض الكبائر لا يخلدون في النار لأنه قال: {أعدت للكافرين}؛ فلو كان عصاة الموحدين يخلدون فيها لم تكن معدة للكافرين وحدهم، خلافاً للخوارج والمعتزلة وفيها: دلالة على أن العذاب مُستَحَق بأسبابه وهو الكفر وأنواع المعاصي على اختلافها.
(24) Na aya hii na mfano wake wanaziita Aya za changamoto. Nayo ni kuwashinda viumbe kuleta mfano wa hii Qur-ani au kuipinga kwa namna yoyote. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema "Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa Qur-ani hii, basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao." Hivyo basi, vipi kitaweza kiumbe kilichoumbwa kwa udongo (kusema) kwamba maneno yake ni kama maneno ya Mola Mlezi wa mabwana? Au atawezaje fakiri mwenye upungufu wa namna zote kuleta maneno kama maneno ya yule Mkamilifu ambaye ana ukamilifu wote, na maana pana kwa namna zote? Hili haliko katika uwezekano, wala katika uwezo wa mwanadamu. Na kila mwenye ladha na ujuzi mdogo mno wa aina za maneno, ikiwa ataipima Qur-ani hii [Tukufu] dhidi ya maneno mengineyo ya watu wenye ufasaha, basi tofauti hii kubwa itamdhihirikia. Na katika kauli yake: "Na ikiwa mna shaka" hadi mwisho wake, ipo dalili ya kwamba anayetarajiwa kuongoka kutokana na upotovu ni yule mwenye shaka, aliyechanganyikiwa, ambaye hakuijua haki kutokana na upotovu. Na huyo ndiye yule ambaye akifafanuliwa ukweli, basi atafanya uchu kuufuata ikiwa ni mkweli katika kutafuta haki. Ama mkaidi ambaye anajua haki lakini anaiacha, huyo kurudi kwake hakuwezekani. Kwa sababu, aliiacha haki baada ya kumpambanukia. Hakuiacha kwa ujinga, kwa hivyo hakuna hila katika hilo. Na vile vile mwenye shaka ambaye si mkweli katika kutafuta haki, bali yeye alikengeuka na wala hajitahidi katika kuitafuta; basi na huyu mara nyingi hafanikiwi. Na katika kumuelezea Mtume kuwa ni mja katika huu muktadha mkubwa, kuna dalili ya kwamba sifa yake - rehema na amani ziwe juu yake - kubwa zaidi ni kufanya kwake ibada ambayo hawezi kumfikia katika hilo yeyote miongoni mwa wale wa mwanzo na wa mwisho. Vile vile alimsifu kwa sifa ya uja katika muktadha wa Isra, akasema: "Ametakasika aliyemchukua mja wake usiku"; na katika muktadha wa kuteremsha Ufunuo (wahyi), akasema: "Ni mwenye baraka nyingi aliyeteremsha Al-Furqani (upambanuo) kwa mja wake ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote". Na katika kauli yake "umeandaliwa makafiri" na mfano wake miongoni mwa aya, kuna dalili ya dhehebu la Ahlus-sunna waljama'a kwamba Pepo na Moto vimeshaumbwa, kinyume na Al-Muutazilah. Na ndani yake pia ni kwamba, wanaomwabudu Mwenyezi Mungu peke yake hata wakifanya madhambi makubwa, wao hawatakaa milele Motoni. Kwa sababu alisema, "umeandaliwa makafiri." Na ingekuwa kwamba Waumini wanaofanya maasia watakaa humo milele, basi haungekuwa umeandaliwa makafiri peke yao, tofauti na Al-Khawarij na Al-Mu'utazila. Na ndani yake kuna dalili ya kwamba adhabu inastahiki kutokana na sababu zake, ambazo ni ukafiri, na aina mbalimbali za dhambi.
: 25 #
{وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِنْ ثَمَرَةٍ رِزْقًا قَالُوا هَذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِنْ قَبْلُ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُطَهَّرَةٌ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (25)}.
(25) Na wabashirie walioamini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watakapopewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyopewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyofanana; na humo watakuwa na wake waliotakasika; na wao humo watadumu.
#
{25} لمَّا ذكر جزاء الكافرين ذكر جزاء المؤمنين أهل الأعمال الصالحات كما هي طريقته تعالى في كتابه يجمع بين الترغيب والترهيب؛ ليكون العبد راغباً راهباً خائفاً راجياً فقال: {وبشّر}؛ أي: أيها الرسول ، ومن قام مقامك {الذين آمنوا}؛ بقلوبهم {وعملوا الصالحات}؛ بجوارحهم؛ فصدقوا إيمانهم بأعمالهم الصالحة، ووُصِفت أعمال الخير بالصالحات؛ لأن بها تصلح أحوال العبد، وأمور دينه ودنياه، وحياته الدنيوية والأخروية، ويزول بها عنه فساد الأحوال؛ فيكون بذلك من الصالحين الذين يصلحون لمجاورة الرحمن في جنته فبشرهم {أن لهم جنات}؛ أي: بساتين جامعة للأشجار العجيبة والثمار الأنيقة والظل المديد والأغصان والأفنان، وبذلك صارت جنة يجتن بها داخلها وينعم فيها ساكنها {تجري من تحتها الأنهار}؛ أي: أنهار الماء واللبن والعسل والخمر يفجرونها كيف شاؤوا، ويصرفونها أين أرادوا، وتُسقَى منها تلك الأشجار؛ فتنبت أصناف الثمار {كلما رزقوا منها من ثمرة رزقاً قالوا هذا الذي رزقنا من قبل}؛ أي: هذا من جنسه وعلى وصفه، كلها متشابهة في الحسن واللذة ليس فيها ثمرة خاسَّةٌ، وليس لهم وقت خالٍ من اللَّذة؛ فهم دائماً متلذذون بأُكُلِها، وقوله: {وأتوا به متشابهاً}؛ قيل: متشابهاً في الاسم مختلفاً في الطعم ، وقيل: متشابهاً في اللون مختلف في الاسم، وقيل: يشبه بعضه بعضاً في الحسن واللذة والفكاهة، ولعل هذا أحسن. ثم لما ذكر مسكنهم، وأقواتهم من الطعام والشراب، وفواكههم ذكر أزواجهم؛ فوصفهنَّ بأكمل وصف وأوجزه وأوضحه؛ فقال: {ولهُم فيها أزواجٌ مُطهرةٌ}؛ فلم يقل مطهرةٌ من العيب الفلاني؛ ليشمل جميع أنواع التطهير، فهنَّ مطهرات الأخلاق، مطهرات الخلق، مطهرات اللسان، مطهرات الأبصار، فأخلاقهن أنهن عُرُبٌ متحببات إلى أزواجهن بالخلق الحسن وحسن التبعل والأدب القولي والفعلي، ومطهرٌ خَلْقُهن من الحيض والنفاس والمني والبول والغائط والمخاط والبصاق والرائحة الكريهة، ومُطَهرات الخَلْق أيضاً بكمال الجمال؛ فليس فيهن عيب ولا دمامة خَلْق، بل هن خيرات حسان، مطهرات اللسان والطرف، قاصرات طرفهن على أزواجهن، وقاصرات ألسنتهن عن كل كلام قبيح. ففي هذه الآية الكريمة ذكر المبشِّر والمُبشَّر والمُبَشَّر به والسبب الموصل لهذه البشارة؛ فالمبشر هو: الرسول - صلى الله عليه وسلم - ومن قام مقامه من أمته، والمبشَّر هم: المؤمنون العاملون الصالحات، والمبشر به هي: الجنات الموصوفات بتلك الصفات، والسبب الموصل لذلك، هو: الإيمان والعمل الصالح، فلا سبيل إلى الوصول إلى هذه البشارة إلا بهما، وهذا أعظم بشارة حاصلة على يد أفضل الخلق بأفضل الأسباب، وفيه استحباب بشارة المؤمنين وتنشيطهم على الأعمال بذكر جزائها وثمراتها؛ فإنها بذلك تخف وتسهل، وأعظم بشرى حاصلة للإنسان توفيقه للإيمان والعمل الصالح، فذلك أول البشارة وأصلها، ومن بعده البشرى عند الموت، ومن بعده الوصول إلى هذا النعيم المقيم. نسأل الله من فضله.
(25) Alipotaja malipo ya makafiri, akataja malipo ya Waumini, watu wa matendo mema, kama ilivyo njia yake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake; Yeye hujumuisha kati ya kupeana matumani na kuhofisha; ili mja awe na matumaini (shauku), mwenye kutishika na kuhofu, mwenye matarajio, basi akasema: "Na wabashirie" yani ewe Mtume, na atakayesimama mahali pako "walioamini" kwa nyoyo zao "na wakatenda mema"; kwa viungo vyao. Basi wakawa wamesadikisha imani yao kwa matendo yao mema. Na matendo ya heri yamesifiwa kuwa ni mema; kwa sababu kwayo, hali ya mja hutengenea, na mambo ya dini yake na dunia yake, na maisha yake ya kidunia na ya kiakhera, na kunamwondokea kwayo kuharibikiwa hali. Basi akawa kwa hayo miongoni mwa wema wanaostahiki kuwa karibu na Ar-rahman (Mwingi wa Rehema) katika Pepo yake, basi akawabashiria "kwamba watapata mabustani" yani mabustani yaliyokusanya miti ya ajabu, na matunda ya kifahari, na vivuli virefu, na matawi ya kawaida na matawi yaliyotanda. Na kwa sababu ya hilo, ikawa pepo ambayo ndani yake anasitirika kwayo aingiaye humo, na ananeemeshwa ndani yake mkazi wake "yapitayo mito chini yake." Yani mito ya maji, na maziwa, na asali na pombe, wakivifanya vimiminike kwa wingi wapendavyo, na wanavipeleka popote wapendapo, na miti hiyo hunyweshwa kutoka humo; basi ikaotesha aina mbalimbali za matunda "kila watakapopewa matunda kutoka humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele." Yani hii ni ya aina yake na yenye sifa zake, yote yanafanana katika uzuri na ladha, hakuna humo matunda mabaya, na hawana wakati usiokuwa na ladha; hivyo basi wao daima wanapata ladha ya matunda yake. Na kauli yake: "Na wataletewa matunda yaliyofanana" ilisemwa kuwa ni yenye kufanana katika jina tu, lakini ni tofauti katika ladha. Na ilisemwa kuwa ni yenye kufanana katika rangi lakini ni tofauti katika majina. Na ilisemwa kuwa yanafanana yenyewe kwa yenyewe katika uzuri na ladha na katika kufurahisha. Na huenda hii ndiyo bora zaidi. Kisha alipoyataja makazi yao, na vyakula vyao, na vinywaji vyao, na matunda yao, akawataja wake zao, na akawaeleza kwa sifa kamilifu zaidi, na fupi zaidi, na bainifu zaidi. Akasema, “na humo watakuwa na wake waliotakasika” na hakusema kuwa ni safi kutokana na dosari fulani, ili ziweze kuingia humo aina zote za usafi. Wao ni safi wa tabia, safi wa mwenendo, safi wa ulimi, safi wa macho. Hivyo, tabia zao ni kwamba wanapendana na waume wao kwa tabia nzuri. Na watiifu kwa waume wao, wenye adabu za usemi na vitendo, waliosafika katika uumbaji wao kutokana na hedhi, na nifasi, na manii, na mkojo, na kinyesi, na kamasi, na mate, na harufu mbaya. Na wamesafika maumbile yao pia kwa ukamilifu wa uzuri, kwa hivyo wao hawana kasoro, wala maumbile mabaya, bali wao ni wema wazuri, waliosafika ndimi na macho, wenye kuwatulizia waume zao macho yao, wenye kuwatulizia waume zao ndimi zao kutokana na kila maneno maovu. Katika hii aya tukufu, amemtaja anayeleta bishara na anayepewa bishara na kinachobashiriwa kupatwa, na sababu inayopelekea hii bishara. Basi anayeleta bishara ni Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na anayesimama mahali pake katika umma wake. Naye anayepewa bishara ni Waumini wanaotenda mema. Nacho kinachobashiriwa kupatwa ni Pepo zilizoelezwa kwa sifa hizo. Nayo sababu inayopelekea bishara hii ni kuwa na imani na kutenda mema. Na hakuna njia yenye kufikisha kwenye bishara hii isipokuwa kwa mawili haya. Na hii ndiyo bishara kubwa mno iliyoletwa kwenye mikono ya mbora zaidi wa viumbe wote, kwa sababu bora zaidi. Na ndani yake kuna pendekezo la kuwapa Waumini bishara na kuwafanya wawe wakakamavu juu ya matendo kwa kutaja malipo yake na matunda yake. Kwa sababu, kwa hili (matendo) yanakuwa hafifu na sahali. Na bishara kubwa mno inayopata mtu ni kumwezesha kuamini na kutenda mema. Na hii ndiyo bishara ya kwanza na asili yake, na baada yake ni bishara ile wakati wa kufa, na baada yake ni kuifikia neema hii ya kudumu. Tunamwomba Mwenyezi Mungu katika fadhila zake.
: 26 - 27 #
{إِنَّ اللَّهَ لَا يَسْتَحْيِي أَنْ يَضْرِبَ مَثَلًا مَا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّهِمْ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَذَا مَثَلًا يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ (26) الَّذِينَ يَنْقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَنْ يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ (27)}
(26) Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walioamini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale waliokufuru husema: Ni nini analokusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapotezi ila wale wapotovu. (27) Wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye hasara.
#
{26} يقول تعالى: {إن الله لا يستحيي أن يضرب مثلاً ما}؛ أيْ: أيُّ مثل كان {بعوضة فما فوقها}؛ لاشتمال الأمثال على الحكمة وإيضاح الحق، والله لا يستحيي من الحق، وكأنّ في هذا جواباً لمن أنكر ضرب الأمثال في الأشياء الحقيرة، واعترض على الله في ذلك؛ فليس في ذلك محل اعتراض، بل هو من تعليم الله لعباده ورحمته بهم، فيجب أن تتلقى بالقبول والشكر، ولهذا قال: {فأما الذين آمنوا فيعلمون أنه الحق من ربهم}؛ فيفهمونها ويتفكرون فيها، فإن علموا ما اشتملت عليه على وجه التفصيل ازداد بذلك علمهم وإيمانهم، وإلا علموا أنها حق، وما اشتملت عليه حق، وإن خفي عليهم وجه الحق فيها، لعلمهم بأن الله لم يضربها عبثاً بل لحكمة بالغة ونعمة سابغة، {وأما الذين كفروا فيقولون ماذا أراد الله بهذا مثلاً}؛ فيعترضون ويتحيرون فيزدادون كفراً إلى كفرهم كما ازداد المؤمنون إيماناً على إيمانهم؛ ولهذا قال: {يضل به كثيراً ويهدي به كثيراً}؛ فهذه حال المؤمنين والكافرين عند نزول الآيات القرآنية، قال تعالى: {وإذا ما أنزلت سورة فمنهم من يقول أيكم زادته هذه إيماناً، فأما الذين آمنوا فزادتهم إيماناً وهم يستبشرون. وأما الذين في قلوبهم مرض فزادتهم رجساً إلى رجسهم وماتوا وهم كافرون}؛ فلا أعظم نعمة على العباد من نزول الآيات القرآنية، ومع هذا تكون لقوم محنة وحيرة وضلالة وزيادة شر إلى شرهم، ولقوم منحة ورحمة وزيادة خير إلى خيرهم، فسبحان من فاوت بين عباده، وانفرد بالهداية والإضلال. ثم ذكر حكمته وعدله في إضلاله من يضل ؛ فقال: {وما يضل به إلا الفاسقين}؛ أي: الخارجين عن طاعة الله المعاندين لرسل الله الذين صار الفسق وصفهم؛ فلا يبغون به بدلاً، فاقتضت حكمته تعالى إضلالهم؛ لعدم صلاحيتهم للهدى، كما اقتضى فضله وحكمته هداية من اتصف بالإيمان وتحلى بالأعمال الصالحة. والفسق نوعان: نوع مخرج من الدين وهو الفسق المقتضي للخروج من الإيمان كالمذكور في هذه الآية ونحوها، ونوع غير مخرج من الإيمان كما في قوله تعالى: {يا أيها الذين آمنوا إن جاءكم فاسق بنبأ فتبينوا ... }؛ الآية.
(26) Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema “Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano.” Yani mfano wowote ule “wa mbu na ulio wa zaidi yake.” Kwa sababu mifano ina hekima, na kubainisha ukweli, na Mwenyezi Mungu haoni haya juu ya haki. Na ni kana kwamba katika hili kuna jibu kwa wale waliopinga kupiga mfano katika vitu duni, na wakampinga Mwenyezi Mungu katika hilo. Lakini hakuna upingamizi wowote katika hilo. Bali ni mafundisho ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na rehema yake juu yao. Basi ni lazima ipokewe (mifano hiyo) kwa kuikubali na kushukuru. Ndio maana akasema: “Ama wale walioamini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi,“ wao wanatafuta kuifahamu na wanaitafakari. Hivyo, wakijua kilichomo ndani yake kwa undani, basi elimu yao na imani yao vinaongezeka. Vinginevyo, wanajua kwamba ni kweli, na kile kilichomo ni kweli, hata ikiwa namna wa ukweli humo ndani yake itafichika kwao. Kwa sababu wajua kwamba Mwenyezi Mungu hakuipiga (mifano hiyo) bure, bali kwa hekima kubwa na neema nyingi. “Lakini wale waliokufuru husema: Ni nini analokusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” Basi wao wanapinga na wanatahayari, hivyo wanazidisha ukafiri juu ya ukafiri wao, kama vile Waumini walivyozidisha imani juu ya imani yao. Ndio maana alisema “Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi.” Na hii ndiyo hali ya Waumini na makafiri wakati wa kuteremka kwa aya za Qur-ani. Mwenyezi Mungu amesema: “Na inapoteremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walioamini inawazidishia Imani, nao wanafurahi. Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ni makafiri.“ Kwa hivyo, hakuna neema kubwa kwa waja kuliko kuteremka kwa aya za Qur-ani. Na pamoja na hayo zinakuwa kwa watu wengine mtihani na tahayari, na upotovu, na kuongezeka kwa uovu juu ya uovu wao. Na kwa watu wengine ni hiba na rehema na kuzidishiwa heri juu ya heri yao. Basi ametakasika yule aliyetofautisha kati ya waja wake, na akapwekeka katika kuongoza na kupoteza. Kisha akataja hekima yake na uadilifu wake katika kuwapoteza yeye wale anaowapoteza, akasema: “Lakini hawapotezi ila wale wanaopindukia mipaka.” Yani wale wanaotoka katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu, wanaowapinga Mitume wa Mwenyezi Mungu, ambao hupindukia mipaka imekuwa sifa yao, hivyo hawatafuti badala ya hilo. Kwa hivyo, hekima yake Mtukufu ikahitaji wapotezwe, kwa sababu hawakuufalia uongofu, kama ilivyohitaji hekima yake na neema yake kumwongoza yule ambaye anasifika kwa sifa ya imani na akajipamba kwa matendo mema. Na kupindukia mipaka ni aina mbili: Aina ya kumtoa mtu katika dini. Nako ni kupindukia mipaka kunakomlazimu (mtu) kutoka katika imani; kama kule kulikotajwa katika aya hii na mfano wake. Na aina nyingine siyo ya kumtoa mtu katika imani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Enyi mlioamini, akikujieni mpotofu na habari yoyote, chunguzeni...” hadi mwisho wa aya.
Kisha akawaeleza wanaopindukia mipaka, akasema:
#
{27} {الذين ينقضون عهد الله من بعد ميثاقه}؛ وهذا يعم العهد الذي بينهم وبين ربهم ، والذي بينهم وبين الخلق ، الذي أكده عليهم بالمواثيق الثقيلة والإلزامات، فلا يبالون بتلك المواثيق، بل ينقضونها، ويتركون أوامره، ويرتكبون نواهيه، وينقضون العهود التي بينهم وبين الخلق {ويقطعون ما أمر الله به أن يوصل}؛ وهذا يدخل فيه أشياء كثيرة، فإن الله أمرنا أن نصل ما بيننا وبينه بالإيمان به والقيام بعبوديته، وما بيننا وبين رسوله بالإيمان به ومحبته وتعزيره والقيام بحقوقه، وما بيننا وبين الوالدين والأقارب والأصحاب وسائر الخلق بالقيام بحقوقهم التي أمر الله أن نصلها، فأما المؤمنون فوصلوا ما أمر الله به أن يوصل من هذه الحقوق، وقاموا بها أتم القيام؛ وأما الفاسقون فقطعوها ونبذوها وراء ظهورهم معتاضين عنها بالفسق والقطيعة والعمل بالمعاصي وهو الإفساد في الأرض، {فأولئك}؛ أي: من هذه صفته {هم الخاسرون}؛ في الدنيا والآخرة، فحصر الخسارة فيهم؛ لأن خسرانهم عام في كل أحوالهم ليس لهم نوع من الربح، لأن كل عمل صالح شرطه الإيمان، فمن لا إيمان له؛ لا عمل له، وهذا الخسار هو: خسار الكفر، وأما الخسار الذي قد يكون كفراً وقد يكون معصية وقد يكون تفريطاً في ترك مستحب، المذكور في قوله تعالى: {إن الإنسان لفي خسر}؛ فهذا عام لكل مخلوق إلا من اتصف بالإيمان والعمل الصالح والتواصي بالحق والتواصي بالصبر، وحقيقته فوات الخير الذي كان العبد بصدد تحصيله وهو تحت إمكانه.
(27) “Wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga.” Na hili linajumuisha ahadi iliyopo baina yao na Mola wao Mlezi, na ile iliyopo baina yao na viumbe, ambayo aliisisitiza juu yao kwa maagano mazito na wajibu mbalimbali, kisha hawajali hayo maagano; bali wanayavunja na wanaacha amri zake na wanafanya makatazo yake. Na wanavunja ahadi ambazo zipo baina yao na viumbe wengine. “Na wakayakata aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa.” Na hili, yanaingia mambo mengi ndani. Kwa maana Mwenyezi Mungu alituamrisha kuunga yaliyopo kati yetu na Yeye, na kumwamini, na kumuabudu. Na yale yaliyopo kati yetu na Mtume wake, kwa kumwamini, na kumpenda, na kumsaidia, na kumtekelezea haki zake. Na yale yaliyopo kati yetu na wazazi wawili, jamaa, marafiki na viumbe wote kwa kuwatekelezea haki zao ambazo Mwenyezi Mungu aliamrisha kwamba tuziunge. Ama Waumini, wao waliunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kwamba yaungwe katika haki hizi, na wakayatimiza kikamilifu. Na ama wapotovu, wao waliyakata, na wakayatupa nyuma ya migongo yao, wakayabadilisha na upindukiaji mipaka, na kuyakata na kufanya maasia, nayo ni kufanya uharibifu katika ardhi. Basi “hao” ambao hizi ndizo sifa zao “ndio wenye hasara” katika dunia na Akhera. Na akawa amefungamanisha hasara na wao peke yao. Kwa maana, hasara yao inaingia katika kila hali zao; hawana aina yoyote ya faida. Kwa sababu, kila tendo jema sharti lake ni imani. Naye asiyekuwa na imani, hana matendo. Na hasara hii ndiyo hasara ya ukafiri. Na ama hasara ambayo inaweza kuwa ukafiri na inaweza kuwa maasia, na inaweza kuwa kupuuza kwa kuacha yale yanayopendekezwa, ambayo yametajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika mwanadamu bila ya shaka yumo katika hasara”, hii ni jumla katika kila kiumbe; isipokuwa mwenye kusifika na imani na matendo mema; na kuusiana kwa haki na kuusiana subira. Na uhakika wake ni kupoteza heri ambayo mja alikuwa karibu mno kuifanya hali ya kuwa ipo katika uwezo wake.
Kisha (Mwenyezi Mungu) Mtukufu akasema:
: 28 #
{كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّهِ وَكُنْتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (28)}.
(28) Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu, akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake mtarejeshwa?
#
{28} هذا استفهام بمعنى التعجب والتوبيخ والإنكار؛ أي: كيف يحصل منكم الكفر بالله الذي خلقكم من العدم، وأنعم عليكم بأصناف النعم، ثم يميتكم عند استكمال آجالكم، ويجازيكم في القبور، ثم يحييكم بعد البعث والنشور، ثم إليه ترجعون فيجازيكم الجزاء الأوفى، فإذا كنتم في تصرفه وتدبيره وبره وتحت أوامره الدينية، وبعد ذلك تحت دينه الجزائي أَفَيَليق بكم أن تكفروا به؟ وهل هذا إلا جهل عظيم وسفه كبير ؟ بل الذي يليق بكم أن تتقوه وتشكروه، وتؤمنوا به ، وتخافوا عذابه، وترجوا ثوابه.
(28) Hili ni swali lenye maana ya mshangao, kukemea, na kukataza. Yani kumkufuru Mwenyezi Mungu kunatokea kwenu; ambaye amekuumbeni siyo kutokana na kitu. Na akakuneemesheni kwa aina mbalimbali za neema; kisha atakufisheni itakapokamilika mida yenu; na atakulipeni katika makaburi. Kisha akakufufueni baada ufufuo; kisha kwake mtarejeshwa; kisha atakulipeni malipo kamili. Na ikiwa mpo chini ya usimamizi wake, na uendeshaji wake, na wema wake, na chini ya amri zake za kidini; na baada ya hayo chini ya hukumu yake ya malipo; je, inawafalia kumkufuru? Na je, huu si isipokuwa ujinga mkubwa, na upumbavu mkubwa? Bali kinachokufalieni ni kumcha, kumshukuru, na kumuamini, kuogopa adhabu yake, na mtarajie malipo yake mazuri.
#
{29} أي: خلق لكم برًّا بكم ورحمة جميع ما على الأرض للانتفاع والاستمتاع والاعتبار. وفي هذه الآية الكريمة دليل على أن الأصل في الأشياء الإباحة والطهارة؛ لأنها سيقت في معرض الامتنان، يخرج بذلك الخبائث فإن تحريمها أيضاً يؤخذ من فحوى الآية، وبيان المقصود منها، وأنه خلقها لنفعنا، فما فيه ضرر؛ فهو خارج من ذلك، ومن تمام نعمته منعنا من الخبائث تنزيهاً لنا؛ وقوله: {ثُمَّ اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (29)}. «استوى»: ترد في القرآن على ثلاثة معانٍ: فتارة لا تُعدَّى بالحرف فيكون معناها: الكمال والتمام، كما في قوله عن موسى: {ولما بلغ أشده واستوى}؛ وتارة تكون بمعنى علا وارتفع، وذلك إذا عديت «بعلى» كقوله تعالى: {الرحمن على العرش استوى} ؛ {لتستووا على ظهوره}؛ وتارة تكون بمعنى قصد كما إذا عُدِيت «بإلى» كما في هذه الآية، أي: لما خلق تعالى الأرض قصد إلى خلق السماوات فسواهن سبع سماوات فخلقها وأحكمها وأتقنها وهو بكل شيء عليم، فيعلم ما يلج في الأرض وما يخرج منها، وما ينزل من السماء وما يعرج فيها، ويعلم ما تسرون وما تعلنون، يعلم السر وأخفى. وكثيراً ما يقرن بين خلقه وإثبات علمه كما في هذه الآية وكما في قوله تعالى: {ألا يعلم من خلق وهو اللطيف الخبير}؛ لأن خلقه للمخلوقات أدل دليل على علمه وحكمته وقدرته.
(29) Yani amekuumbieni katika hali ya kuwafanyia wema na rehema vyote vilivyomo katika ardhi kwa manufaa yenu, na starehe na mazingatio. Na katika aya hii tukufu kuna dalili kwamba hali ya asili (kanuni ya msingi) katika vitu ni kwamba vinaruhusiwa na ni safi. Kwa sababu (aya hii) ilisimuliwa katika muktadha wa kuonyesha neema; hivyo machafu yanatoka kwa hili. Kwa sababu uharamu wake unachukuliwa kutokana na maana ya aya hii, na kujua makusudio yake, na kwamba aliviumba kwa manufaa yetu; hivyo lenye madhara lipo nje ya hilo. Na katika ukamilifu wa neema yake ni kwamba alitukataza machafu ili kutusafisha. Na kauli yake: (29) Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. (Neno) “Istawa” linatokea katika Qur-ani kwa maana tatu: Mara huivuki kwa msaada wa herufi (harf); hivyo linamaanisha “ukamilifu na utimilifu”, kama katika kauli yake kuhusu Musa: “Na Musa alipofika utu-uzima baraabara” Na mara nyingine linakuwa na maana ya “kuwa juu” na “kuinuka” na hilo ni ikiwa litavukishwa na “alaa (juu) kama katika kauli Yake Mtukufu “Ar-Rahman (Mwingi wa Rehema) aliyetawala juu ya Kiti cha Enzi” “Ili make vizuri juu ya migongo yao”. Na wakati mwingine linakuwa na maana ya “kukusudia” kama vile linapovukishwa na “ilaa (kuelekea) kama ilivyo katika aya hii. Yani yeye Mtukufu alipoumba ardhi, akaelekea kuziumba mbingu “na akazifanya mbingu saba.” Basi akaziumba na akaziimarisha na akazifanya vilivyo Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. Kwa hivyo, anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Na anajua mnayoyaficha na mnayoyatangaza. Anajua siri na kilichofichika zaidi (kuliko siri). Na mara nyingi anaunganisha baina ya uumbaji wake na kuthibitisha elimu yake, kama ilivyo katika aya hii, na kama katika kauli yake: “Asijue aliyeumba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?” Kwa kuwa, uumbaji wake wa viumbe ni dalili ya kutosha juu ya elimu yake, hekima yake, na uwezo wake.
: 30 - 34 #
{وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَنْ يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ (30) وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنْبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَؤُلَاءِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (31) قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنْتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ (32) قَالَ يَاآدَمُ أَنْبِئْهُمْ بِأَسْمَائِهِمْ فَلَمَّا أَنْبَأَهُمْ بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنْتُمْ تَكْتُمُونَ (33) وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَى وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ (34)}.
(30) Na pale Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyoyajua. (31) Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. (32) Wakasema: Subhanaka (Wewe umetakasika!) Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyotufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hekima. (33) Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipowaambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mnayaficha? (34) Na tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipokuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.
#
{30} هذا شروع في ابتداء خلق آدم عليه السلام أبي البشر وفضلهِ، وأن الله تعالى حين أراد خلقه أخبر الملائكة بذلك، وأن الله مستخلفه في الأرض، فقالت الملائكة عليهم السلام: أتجعل فيها من يفسد فيها بالمعاصي ويسفك الدماء، وهذا تخصيص بعد تعميم؛ لبيان شدة مفسدة القتل، وهذا بحسب ظنهم أن الخليفةَ المَجْعُول في الأرض سيحْدُثُ منه ذلك، فنزهوا الباري عن ذلك وعظموه، وأخبروا أنهم قائمون بعبادة الله على وجه خالٍ من المفسدة فقالوا: {ونحن نسبح بحمدك}؛ أي: ننزهك التنزيه اللائق بحمدك وجلالك {ونقدس لك}؛ يحتمل أن معناها ونقدسك؛ فتكون اللام مفيدة للتخصيص والإخلاص، ويحتمل أن يكون: ونقدس لك أنفسنا؛ أي: نطهرها بالأخلاق الجميلة؛ كمحبة الله، وخشيته، وتعظيمه، ونطهرها من الأخلاق الرذيلة {قال}؛ الله للملائكة: {إني أعلم}؛ من هذا الخليفة {ما لا تعلمون}؛ لأن كلامكم بحسب ما ظننتم، وأنا عالم بالظواهر والسرائر، وأعلم أن الخير الحاصل بخلق هذا الخليفة أضعاف أضعاف ما في ضمن ذلك من الشر، فلو لم يكن في ذلك، إلا أن الله تعالى أراد أن يجتبي منهم الأنبياء والصديقين والشهداء والصالحين، ولتظهر آياته للخلق ، ويحصل من العبوديات التي لم تكن تحصل بدون خلق هذا الخليفة كالجهاد وغيره، وليظهر ما كمن في غرائز المكلفين من الخير والشر بالامتحان، وليتبين عدوه من وليه وحزبه من حربه، وليظهر ما كَمُن في نفس إبليس من الشر الذي انطوى عليه واتصف به، فهذه حكم عظيمة يكفي بعضها في ذلك.
(30) Huu ni mwanzo wa kutaja uumbaji wa Adam, amani iwe juu yake, baba wa wanadamu na fadhila zake, na kwamba Mwenyezi Mungu alipotaka kumuumba; aliwaambia Malaika hayo, na kwamba Mwenyezi Mungu atamfamya kuwa Khalifa (mfwatizi) katika dunia. Malaika amani iwe juu yao wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo kwa maasia na kumwaga damu. Na huku ni kutaja kilicho maalum baada kutaja cha jumla, ili kubainisha ukubwa wa uharibifu wa kuua. Na hii ni kwa mujibu wa dhana (fikra) zao kwamba huyo Khalifa atakayewekwa katika ardhi atayafanya hayo. Kwa hivyo wakamtakasa Al-Bari (Mola Muumbaji) kutokana na hilo, na wakamtukuza, na wakamwambia kwamba wao kwa hakika wanamuabudu Mwenyezi Mungu kwa njia ambayo haina uharibifu, wakasema: “Hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako.” Yani tunakutakasa utakaso unaolingana na sifa zako na utukufu wako, “na tunakutaja kwa utakatifu wako?” Maana yake inaweza kuwa: Tunakutakasa Wewe. Basi inakuwa herufi Laam hapo ni yenye maana ya kumteua na kumpwekesha Mwenyezi Mungu peke yake katika hilo. Na inaweza kuwa na maana; “na tunakutakasia Wewe nafsi zetu.” Yani tunazisafisha kwa tabia nzuri kama vile kumpenda Mwenyezi Mungu, na kumnyenyekea, na kumtukuza. Na tunazitakasa kutokana na maadili maovu. “Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kuwaambia Malaika: “Hakika Mimi nayajua” kuhusu huyu khalifa “msiyoyajua” Kwa sababu maneno yenu ni kulingana na dhana (fikira) yenu, nami ninajua (mambo) ya siri na ya dhahiri. Na ninajua kwamba heri itakayotokea kwa kumuumba huyu khalifa inazidi kwa mizidisho mingi kilichomo ndani yake cha uovu. Na kama haingekuwa katika hili isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu alitaka kuteua kati yao Manabii, Masidiqi (wakweli), Mashahidi, na watu wema, na ili awadhihirishie vuimbe ishara zake. Na ili zifanyike ibada ambazo hazingefanyika bila ya kumuumba huyu khalifa, kama vile jihadi na mengineyo. Na ili afichue yaliyofichika katika silika ya wanadamu ya kheri na shari kwa kuwafanyia mtihani, na ili adhihirike adui wake na rafiki wake, na kikundi chake kutokana na wanaompiga vita, na ili yadhihirike yaliyofichika katika nafsi ya Iblisi ya shari iliyomfunika, na akasifika kwayo, basi hizi ni hekima kubwa, baadhi yake inatosha katika hilo.
Kisha, pale kauli ya Malaika, amani iwe juu yao, ilipokuwa inaashiria ubora wao juu ya huyo khalifa ambaye Mwenyezi Mungu atamweka katika ardhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuwabainishia katika ubora wa Adam. Ambao kwa ubora huo watajua ubora wake, na ukamilifu wa hekima na elimu ya Mwenyezi Mungu.
#
{31} فَعَلَّمَ {آدم الأسماء كلَّها}؛ أي: أسماء الأشياء ومن هو مسمى بها، فعلمه الاسم والمُسمَّى؛ أي: الألفاظ والمعاني حتى المصغر من الأسماء والمكبر؛ كالقصعة والقُصيْعَة {ثم عرضهم}؛ أي: عرض المسمَّيَات {على الملائكة}؛ امتحاناً لهم هل يعرفونها أم لا {فقال أنبئوني بأسماء هؤلاء إن كنتم صادقين}؛ في قولكم وظنكم أنكم أفضل من هذا الخليفة.
(31) Hivyo, “akamfundisha Adam majina yote.” Yani ya vitu vyote, yani namna vinavyoitwa, na akamfunza jina na maana yake, yani matamshi na maana, hata ukubwa wa neno kama vile ‘hili bakuli’, na udogo kama vile ‘kijibakuli’. “Kisha akaviweka,” yani aliweka hivyo vilivyotajwa “mbele ya Malaika” ili kuwajaribu, je wanavijua au la?" Na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli,” katika ile kauli yenu na dhana (firika) yenu kuwa nyinyi ni bora kuliko khalifa huyu.
#
{32} {قالوا سبحانك}؛ أي ننزهك من الاعتراض منَّا عليك، ومخالفة أمرك {لا علم لنا}؛ بوجه من الوجوه، {إلا ما علمتنا}؛ إياه فضلاً منك وجوداً {إنك أنت العليم الحكيم}؛ العليم الذي أحاط علماً بكل شيء، فلا يغيب عنه ولا يعزب مثقال ذرة في السماوات والأرض ولا أصغر من ذلك ولا أكبر، الحكيم: من له الحكمة التامة التي لا يخرج عنها مخلوق ولا يشذ عنها مأمور، فما خلق شيئاً إلا لحكمة، ولا أمر بشيء إلا لحكمة، والحكمة وضع الشيء في موضعه اللائق به. فأقروا واعترفوا بعلم الله وحكمته وقصورهم عن معرفة أدنى شيء، واعترافهم بفضل الله عليهم وتعليمه إياهم ما لا يعلمون.
(32) “Wakasema: Subhanaka (Wewe umetakasika!) Yani: Tunakutakasa kutokana na pingamizi kutoka kwetu dhidi yako, na kuhalifu amri yako. “Hatuna elimu (ujuzi) kwa njia yoyote ile “isipokuwa kwa uliyotufunza Wewe” kutokana na fadhila na ukarimu wako. “Hakika Wewe ndiye Mwenye elimu (Mjuzi), Mwenye hekima.” Al-‘Alim (Mwenye elimu) ni yule anayejua kila kitu, na kitu chochote hakikosekani kuwepo kwake. Na wala hakuna kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, sio katika mbingu wala ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi. Al-Hakim (Mwenye hekima) ni yule mwenye hekima kamili ambayo hakuna kiumbe anayeweza kutoka ndani yake. Na wala hakuna aliyeamrishwa anayeweza kujitenga nayo. Kwa hivyo, hakuumba chochote isipokuwa kwa hekima, na wala hakuamrisha kitu ila kwa hekima. Na hekima ni kukiweka kitu katika mahali pake panapostahiki. Hivyo basi, wao (Malaika) wakakiri na kukubali elimu ya Mwenyezi Mungu na hekima yake, na kushindwa kwao kujua hata kitu kidogo zaidi, na wakakubali fadhila za Mwenyezi Mungu juu yao, na yeye kuwafunza wao wasiyoyajua.
#
{33} فحينئذ قال الله: {يا آدم أنبئهم بأسمائهم}؛ أي: أسماء المسميات التي عرضها الله على الملائكة؛ فعجزوا عنها {فلما أنبأهم بأسمائهم}؛ تبين للملائكة فضل آدم عليهم، وحكمة الباري وعلمه في استخلاف هذا الخليفة {قال ألم أقل لكم إني أعلم غيب السموات والأرض} وهو ما غاب عنا فلم نشاهده، فإذا كان عالماً بالغيب، فالشهادة من باب أولى {وأعلم ما تبدون}؛ أي: تظهرون {وما كنتم تكتمون}.
(33) Na hapo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema “Ewe Adam! Waambie majina yavyo.” Yani majina ya vile vilivyotajwa, ambavyo Mwenyezi Mungu aliviweka mbele ya Malaika; nao wakashindwa kuvitaja majina. “Basi alipowaambia majina yake,” ukawabainikia Malaika ubora wa Adam juu yao, na hekima na elimu ya Al-Bari (Muumbaji) katika kumteua huyu khalifa. “Alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani.” Nayo (ghaibu) ni kila kilichofichikana kwetu; tukawa hatukioni. Na ikiwa (Yeye Mwenyezi Mungu) anajua ghaibu; basi ya dhahiri yanastahiki zaidi (yeye kuyajua). “Na ninayajua mnayoyadhihirisha,” yani mnayoweka wazi; “na mliyokuwa mnayaficha.”
#
{34} ثم أمرهم تعالى بالسجود لآدم إكراماً له وتعظيماً وعبودية لله تعالى؛ فامتثلوا أمر الله، وبادروا كلهم بالسجود، {إلا إبليس أبى} امتنع عن السجود، واستكبر عن أمر الله، وعلى آدم قال: {أأسجد لمن خلقت طيناً} وهذا الإباء منه، والاستكبار نتيجة الكفر الذي هو منطوٍ عليه، فتبينت حينئذ عداوته لله ولآدم وكفره واستكباره. وفي هذه الآيات من العِبَر والآيات إثبات الكلام لله تعالى، وأنه لم يزل متكلماً يقول ما شاء، ويتكلم بما شاء وأنه عليم حكيم، وفيه أن العبد إذا خفيت عليه حكمة الله في بعض المخلوقات، والمأمورات؛ فالواجب عليه التسليم واتهامُ عقله والإقرار لله بالحكمة؛ وفيه اعتناء الله بشأن الملائكة وإحسانه بهم بتعليمهم ما جهلوا، وتنبيههم على ما لم يعلموه. وفيه فضيلة العلم من وجوه: منها: أن الله تعرف لملائكته بعلمه وحكمته. ومنها: أن الله عرفهم فضل آدم بالعلم، وأنه أفضل صفة تكون في العبد. ومنها: أن الله أمرهم بالسجود لآدم إكراماً له لمَّا بانَ فضل علمه. ومنها: أن الامتحان للغير إذا عجزوا عما امتحنوا به ثم عرفه صاحب الفضيلة فهو أكمل مما عرفه ابتداء. ومنها: الاعتبار بحال أبوي الإنس والجن وبيان فضل آدم وأفضال الله عليه وعداوة إبليس له، إلى غير ذلك من العبر.
(34) Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha wamsujudie Adam; kama ishara ya heshima na kumtukuza; na kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, wakatii amri ya Mwenyezi Mungu, na wote wakafanya haraka kusujudu “isipokuwa Iblis, alikataa” kusujudu; na akajivuna juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, na juu ya Adam, akasema: “Je, nimsujudie uliyemuumba kwa udongo?” Na huku kukataa kwake na kiburi chake ni kutokana na ukafiri uliomfunika. Hapo, ukadhihirika uadui wake kwa Mwenyezi Mungu na Adam na ukafiri wake na kiburi chake. Na katika aya hizi kuna mazingatio na ishara kama vile kuthibitisha usemi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; na kwamba hajaacha kuzungumza; anasema chochote anachotaka; na anazungumza kwa chochote anachotaka, na kwamba Yeye ni mwenye elimu na hekima. Pia zina mazingatio kwamba ikiwa hekima ya Mwenyezi Mungu itafichikana kwa mja katika baadhi ya viumbe na maamrisho, basi la wajibu juu yake ni kusalimu amri, na kuishutumu akili yake, na kumkiria Mwenyezi Mungu hekima. Na ndani pia kuna utunzaji wa Mwenyezi Mungu wa mambo ya Malaika, na wema wake kwao; kwa kuwafundisha yale wasiyoyajua, na kuwatanabahisha juu ya yale ambayo hakuwafundisha. Na pia kuna fadhila ya elimu kwa namna mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu anawajua Malaika wake; kwa elimu na hekima yake. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwafahamisha ubora wa Adam kwa sababu ya elimu, na kwamba hiyo ndiyo sifa bora zaidi inayokuwa katika mja. Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamrisha wamsujudie Adam ili kumheshimu ilipobainika fadhila ya elimu yake. Na miongoni mwake ni kwamba katika kuwatahini wengine, ni bora zaidi kuwatahini (kwa kuwauliza maswali kwanza, kabla ya kuwapa jawabu), na akishindwa alichotahiniwa, anaambiwa na yule aliye bora (anayejua), na hivi ni bora zaidi badala ya kumwambia (jibu) mwanzoni. Na miongoni mwake ni kuzingatia hali ya wazazi wawili wa watu na majini, na kubanisha ubora wa Adam na fadhila za Mwenyezi Mungu juu yake, na uadui wa Iblisi kwake; na yasiyokuwa hayo miongoni mwa mazingatio.
: 35 - 36 #
{وَقُلْنَا يَاآدَمُ اسْكُنْ أَنْتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ (35) فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَى حِينٍ (36)}.
(35) Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale waliodhulumu. (36) Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyokuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda.
#
{35} لما خلق الله آدم وفضَّله، أتمَّ نعمته عليه بأن خلق منه زوجة؛ ليسكن إليها ويستأنس بها، وأمرهما بسكنى الجنة والأكل منها رغداً؛ أي: واسعاً هنيئاً {حيث شئتما}؛ أي: من أصناف الثمار والفواكه، وقال الله له: {إن لك أن لا تجوع فيها ولا تعرى، وأنك لا تظمأ فيها ولا تضحى}، {ولا تقربا هذه الشجرة}؛ نوع من أنواع شجر الجنة الله أعلم بها، وإنما نهاهما عنها امتحاناً وابتلاء أو لحكمة غير معلومة لنا، {فتكونا من الظالمين}؛ دل على أن النهي للتحريم؛ لأنه رتب الظلم عليه ؛ فلم يزل عدوهما يوسوس لهما ويزين لهما تناول ما نُهيا عنه حتى أزلهما أي حملهما على الزلل بتزيينه {وقاسمهما}؛ بالله {إني لكما لمن الناصحين}.
(35) Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na akamfanya kuwa bora, akakamilisha neema zake juu yake; kwamba alimuumba kutokana naye mke; ili akae naye kwa utulivu na usuhuba. Akawaamrisha waishi Peponi, na wale humo raghadan (yani kwa upana maridhawa) “popote mpendapo” yani katika aina mbalimbali za thimaar (mazao) na matunda. Na Mwenyezi Mungu akamwambia: “Hakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa uchi. Na hakika, hutapata kiu humo wala hutapata joto.” “Lakini msiukaribie mti huu tu;” aina moja katika aina za miti ya Peponi. Mwenyezi Mungu ndiye anayeujua zaidi. Lakini aliwakataza mti huo ili kuwapa mtihani na majaribio au kwa sababu ya hekima tusiyoijua. “Mkawa katika wale waliodhulumu.” Inaonyesha kwamba huko kukataza kulikuwa kwa kuharamisha, kwa sababu alikufungamanisha na dhuluma. Basi adui yao hakuacha kuwashawishi, na kuwapambia kula kile walichokatazwa, mpaka akawatelezesha kwa kuwapambia. “Naye akawaapia” kwa jina la Mwenyezi Mungu. “Kwa yakini, mimi ni miongoni mwa wanaokusihini.”
#
{36} فاغترا به وأطاعاه؛ فأخرجهما مما كانا فيه من النعيم، والرغد، وأُهْبِطوا إلى دار التعب والنصب والمجاهدة {بعضكم لبعض عدو}؛ أي: آدم وذريته أعداء لإبليس وذريته. ومن المعلوم أن العدو يَجِدُّ ويجتهد في ضرر عدوه وإيصال الشر إليه بكل طريق وحرمانه الخير بكل طريق، ففي ضمن هذا تحذير بني آدم من الشيطان كما قال تعالى: {إنّ الشيطان لكم عدو فاتخذوه عدواً إنما يدعو حزبه ليكونوا من أصحاب السعير} {أفتتخذونه وذريته أولياء من دوني وهم لكم عدو بئس للظالمين بدلاً} ثم ذكر منتهى الإهباط فقال: {ولكم في الأرض مستقر}؛ أي: مسكن وقرار {ومتاعٌ إلى حين}؛ انقضاء آجالكم ثم تنتقلون منها للدار التي خُلقتم لها وخلقت لكم، ففيها أن مدة هذه الحياة مؤقتة عارضة ليست مسكناً حقيقياً، وإنما هي معبر يُتزوَّد منها لتلك الدار، ولا تُعمَّر للاستقرار.
(36) Basi wakadanganyika naye na wakamtii. Hivyo basi, akawatoa katika yale waliyokuwamo katika neema na ukunjufu; na wakashukishwa kwenda katika nyumba ya taabu, uchovu na kupambana. “Nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi.” Yani Adam na kizazi chake ni maadui wa Iblis na kizazi chake. Na kama inavyojulikana, adui hukakamia na kujitahidi katika kumdhuru adui yake na kumfikishia shari kwa kila njia, na kumnyima heri kwa kila njia. Hivyo basi, ndani ya haya kuna tahadharisho kwa wanaadamu dhidi ya Shetani, kama alivyosema (Mwenyezi Mungu) Mtukufu: “Hakika Shet'ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni.” “Je, Mnamfanya yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.” Kisha akataja mwisho wa kuteremka katika ardhi, akasema: “Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu,” yani maskani na mahali pa kutua “na starehe kwa muda.” Wa kwisha kwa muda wenu, kisha mtatoka humo kwenda kwenye nyumba ambayo mliumbwa kwa ajili yake, nayo ikaumbwa kwa ajili yenu. Na katika aya hii kuna kwamba muda wa maisha haya (ya duniani) ni ya muda mfupi na wa kupita, siyo maskani ya kweli. Lakini, ni njia ya mapito ambayo mtu anapaswa kuchukua chakula kutoka humo kwa ajili ya nyumba ile nyingine, na wala haifai kuyaimarisha kwa ajili ya kukaa humo milele.
: 37 #
[{فَتَلَقَّى آدَمُ مِنْ رَبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (37)}].
(37) Kisha Adam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.
#
{37} {فتلقّى آدم}؛ أي: تلقف وتلقن وألهمه الله {من ربه كلمات}؛ وهي قوله: {ربنا ظلمنا أنفسنا ... }؛ الآية؛ فاعترف بذنبه، وسأل الله مغفرته {فتاب}؛ الله، {عليه}؛ ورحمه {إنه هو التواب}؛ لمن تاب إليه وأناب. وتوبته نوعان: توفيقه أولاً. ثم قبوله للتوبة إذا اجتمعت شروطها ثانياً. {الرحيم}؛ بعباده، ومن رحمته بهم أن وفقهم للتوبة وعفا عنهم وصفح.
(37) “Kisha Adam akapokea,” yani Mwenyezi Mungu alimfunulia “maneno kutoka kwa Mola wake Mlezi;” nayo ni kauli yake: “Mola wetu Mlezi, Tumezidhulumu nafsi zetu” hadi mwisho wa aya. Kwa hivyo, akakiri dhambi zake, na akamuomba Mwenyezi Mungu msamaha juu yake. “Na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake” na akamrehemu “hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba;” kwa mwenye kutubia kwake na akarejea kwake. Na toba yake ni ya aina mbili: Kumwezesha kwanza, kisha pili kukubali kwake (Mwenyezi Mungu) toba hiyo ikiwa itajumuisha masharti yake. “Na Mwenye kurehemu,” kwa waja wake. Na katika rehema yake juu yao ni kuwawezesha kutubu, na akawasamehe, na akaachilia.
: 38 - 39 #
{قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنْ تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (38) وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (39)}.
(38) Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakaofuata uwongofu wangu huo, haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. (39) Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio wenza wa Moto, wao watadumu humo.
#
{38} كرر الإهباط؛ ليرتب عليه ما ذكر، وهو قوله: {فإما يأتينكم مني هدى}؛ أي: أيُّ وقت وزمان جاءكم مني يا معشرَ الثقلين هدى؛ أي: رسول وكتاب يهديكم لما يقربكم مني، ويدنيكم من رضائي فمن تبع هداي منكم، بأن آمن برسلي، وكتبي واهتدى بهم، وذلك بتصديق جميع أخبار الرسل والكتب والامتثال للأمر والاجتناب للنهي، {فلا خوف عليهم ولا هم يحزنون}؛ وفي الآية الأخرى، {فمن اتبع هداي فلا يضل ولا يشقى}. فرتب على اتباع هداه أربعة أشياء: نفي الخوف والحزن والفرق بينهما: أن المكروه إن كان قد مضى أحدث الحزن وإن كان منتظراً أحدث الخوف، فنفاهما عمن اتبع الهدى وإذا انتفيا حصل ضدهما وهو الأمن التام.
(38) Alirudia kuteremka, ili yapatikane yale yaliyotajwa, nayo ni kauli yake “na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu.” Yani wakati utakapowajia kutoka kwangu - Enyi kundi la wazito wawili - uwongofu, yani Mtume na Kitabu kinachowaongoza kwenye yale yenye kuwaweka karibu na Mimi, na yenye kuwaweka karibu na radhi zangu. Basi watakaofuata uwongofu wangu huo miongoni mwenu, kwa kuwaamini Mitume wangu na Vitabu vyangu, na akaongoka nao. Na hilo ni kwa kusadiki habari zote za Mitume na Vitabu, na kutekeleza amri, na kujiepusha na makatazo. “Basi haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.” Na katika aya nyingine “basi atakayeufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” Kwa hivyo, akafungamanisha mambo manne na kufuata mwongozo wake: Kukanusha hofu na huzuni. Na tofauti iliyopo kati ya hayo ni kuwa chenye kuchukiza ikiwa kilikuwa kimeshapita, huwa kinaleta huzuni. Na ikiwa bado kinangonjewa, huwa kinaleta hofu. Basi akayakanusha haya mawili kwa mwenye kufuata uwongofu wake. Na mawili haya yasipokuwa, basi kinyume chake kinatokea, nacho ni amani kamili.
#
{39} وكذلك: نفي الضلال والشقاء عمن اتبع هداه، وإذا انتفيا ثبت ضدهما، وهو الهدى والسعادة، فمن اتبع هداه حصل له الأمن والسعادة الدنيوية والأخروية والهدى وانتفى عنه كل مكروه من الخوف والحزن والضلال والشقاء؛ فحصل له المرغوب واندفع عنه المرهوب، وهذا عكس من لم يتبع هداه فكفر به وكذب بآياته؛ فأولئك أصحاب النار، أي: الملازمون لها ملازمة الصاحب لصاحبه، والغريم لغريمه {هم فيها خالدون} لا يخرجون منها ولا يفتر عنهم العذاب ولا هم ينصرون. وفي هذه الآيات، وما أشبهها انقسام الخلق من الجن والإنس إلى أهل السعادة، وأهل الشقاوة، وفيها صفات الفريقين والأعمال الموجبة لذلك، وأن الجن كالإنس في الثواب والعقاب، كما أنهم مثلهم في الأمر والنهي.
(39) Na vile vile, kukanusha upotovu na uovu juu ya mwenye kufuata uwongofu wake. Na viwili hivi visipokuwepo, basi kinyume chake kinathibiti, nao ni uwongofu na kufaulu. Hivyo basi, mwenye kufuata uwongofu wake, atapata amani na kufaulu duniani na akhera, na uwongofu, na akaepuka kila yanayochukiza kama hofu, huzuni, upotovu, uovu, basi akapata kinachopendeza, na akaepuka kinachohofiwa. Na huyu ni kinyume cha mwenye kutofuata uongofu wake, akaukufuru na akakadhibisha aya zake. Basi hao ndio watakaokuwa wenza wa Moto. Yani watakaokaa pamoja nao kama vile mwenza anavyokaa pamoja na mwenza wake, na mdaiwa na mdai wake “humo watadumu.” Hawatatoka nje yake wala adhabu haitawaisha, na wala hawatasaidiwa. Na katika aya hizi na mfano wake, kuna kugawanyika kwa viumbe: Majini na wanadamu katika wale kufaulu na wale wa kuhasiri. Na ndani yake kuna sifa za makundi haya mawili na matendo yanayosababisha hayo. Na kwamba majini ni kama wanadamu katika malipo na adhabu, kama walivyo sawa katika amri na makatazo.
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaanza kuwakumbusha Wana wa Israili neema zake juu yao na ihsani yake, akasema:
: 40 - 43 #
{يَابَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ (40) وَآمِنُوا بِمَا أَنْزَلْتُ مُصَدِّقًا لِمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ (41) وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ (42) وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ (43)}.
(40) Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni, na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu. (41) Na aminini niliyoyateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo. Na niogopeni Mimi tu. (42) Wala msichanganye kweli na uwongo, na mkaificha kweli nanyi mnajua. (43) Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanaoinama.
#
{40} {يا بني إسرائيل}؛ المراد بإسرائيل: يعقوب عليه السلام، والخطاب مع فِرَق بني إسرائيل، الذين بالمدينة وما حولها ويدخل فيهم من أتى بعدهم، فأمرهم بأمر عام فقال: {اذكروا نعمتي التي أنعمت عليكم}؛ وهو يشمل سائر النعم التي سيذكر في هذه السورة بعضها، والمراد بذكرها بالقلب اعترافاً، وباللسان ثناءً، وبالجوارح باستعمالها فيما يحبه ويرضيه {وأوفوا بعهدي}؛ وهو ما عهده إليهم من الإيمان به، وبرسله، وإقامة شرعه {أوف بعهدكم}؛ وهو المجازاة على ذلك، والمراد بذلك ما ذكره الله في قوله: {ولقد أخذ الله ميثاق بني إسرائيل وبعثنا منهم اثني عشر نقيباً وقال الله إني معكم لئن أقمتم الصلاة وآتيتم الزكاة وآمنتم برسلي}؛ إلى قوله: {فقد ضل سواء السبيل}؛ ثم أمرهم بالسبب الحامل لهم على الوفاء بعهده، وهو الرهبة منه تعالى، وخشيته وحده، فإن من خشيه أوجبت له خشيته امتثال أمره، واجتناب نهيه، ثم أمرهم بالأمر الخاص الذي لا يتم إيمانهم ولا يصح إلا به فقال:
(40) “Enyi Wana wa Israili!” Anayekusudiwa na Israili ni Yaaqub, amani iwe juu yake. Na haya maneno ni kwa makundi ya Wana wa Israili waliokuweko huko Madina na pembezoni mwake. Na wanaingia ndani yao waliokuja baada yao. Basi akawaamrisha amri ya jumla, akasema: “Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni.” Nayo inajumuisha neema zote ambazo baadhi yake zitatajwa katika sura hii. Na kinachokusudiwa ni kuzitaja kwa moyo ili kuzikubali, na kwa ulimi ili kuzisifu, na kwa viungo kwa kuzitumia katika yale anayoyapenda na kuyaridhia. “Na timizeni ahadi yangu,” nayo ni yale aliyowaagiza kama vile kumuamini Yeye na Mitume wake na kusimamisha Sheria yake. “Na Mimi nitatimiza ahadi yenu,” nayo ni malipo kwa hayo. Na makusudio ya hilo ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika kauli yake: “Na Mwenyezi Mungu alichukua agano la Wana wa Israili. Na tukawateulia kutokana nao wakuu kumi na wawili. Na Mwenyezi Mungu akasema: Kwa yakini Mimi ni pamoja nanyi. Mkisali, na mkatoa Zaka, na mkawaamini Mitume wangu;” hadi kauli yake “bila ya shaka atakuwa amepotea njia iliyo sawa.” Kisha akawaamrisha sababu itakayowafanya kutimiza agano lake, nayo ni kumhofu yeye Mtukufu, na kumnyenyekea yeye peke yake. Kwa sababu mwenye kumnyenyekea, huko kunyenyekea kwake kutamfanya kutekeleza amri yake na kuepukana na makatazo yake. Kisha akawaamrisha amri maalumu, ambayo haitimii imani yao wala haikubaliki isipokuwa kwayo, akasema:
#
{41} {وآمنوا بما أنزلت}؛ وهو: القرآن الذي أنزله على عبده ورسوله محمد - صلى الله عليه وسلم -، فأمرهم بالإيمان به واتباعه، ويستلزم ذلك، الإيمان بمن أنزل عليه، وذكر الداعي لإيمانهم، فقال: {مصدقاً لما معكم}؛ أي: موافقاً له لا مخالفاً ولا مناقضاً، فإذا كان موافقاً لما معكم من الكتب غير مخالف لها فلا مانع لكم من الإيمان به؛ لأنه جاء بما جاءت به المرسلون، فأنتم أولى من آمن به وصدق به؛ لكونكم أهل الكتب والعلم. وأيضاً فإن في قوله: {مصدقاً لما معكم}؛ إشارة إلى أنكم إن لم تؤمنوا به عاد ذلك عليكم بتكذيب ما معكم؛ لأن ما جاء به هو الذي جاء به موسى وعيسى وغيرهما من الأنبياء، فتكذيبكم له تكذيب لما معكم. وأيضاً فإن في الكتب التي بأيديكم صفة هذا النبي الذي جاء بهذا القرآن، والبشارة به، فإن لم تؤمنوا به؛ كذبتم ببعض ما أنزل إليكم، ومن كذب ببعض ما أنزل إليه؛ فقد كذب بجميعه، كما أن من كفر برسولٍ؛ فقد كذب الرسل جميعهم، فلما أمرهم بالإيمان به نهاهم، وحذرهم عن ضده وهو الكفر به فقال: {ولا تكونوا أول كافر به}؛ أي: بالرسول والقرآن، وفي قوله: {أول كافر به}؛ أبلغ من قوله ولا تكفروا به؛ لأنهم إذا كانوا أول كافر به كان فيه مبادرتهم إلى الكفر [به] عكس ما ينبغي منهم، وصار عليهم إثمهم وإثم من اقتدى بهم من بعدهم. ثم ذكر المانع لهم من الإيمان وهو اختيار العرض الأدنى على السعادة الأبدية فقال: {ولا تشتروا بآياتي ثمناً قليلاً}؛ وهو ما يحصل لهم من المناصب والمآكل التي يتوهمون انقطاعها إن آمنوا بالله ورسوله، فاشتروها بآيات الله واستحبوها وآثروها {وإياي}؛ أي: لا غيري، {فاتقون}؛ فإنكم إذا اتقيتم الله وحده أوجبت لكم تقواه تقديم الإيمان بآياته على الثمن القليل، كما أنكم إذا اخترتم الثمن القليل؛ فهو دليل على ترحل التقوى من قلوبكم، ثم قال:
(41) “Na aminini niliyoyateremsha,” nayo ni Qur-ani ambayo aliiteremsha kwa mja wake na Mtume wake Muhammad rehema ana amani ziwe juu yake. Basi akawaamrisha kuiamini, na kuifuata. Na hilo linalazimisha kumwamini yule aliyeteremshiwa juu yake. Na akataja sababu ya kuwafanya waamini. Akasema: “ambayo yanasadikisha mliyo nayo.” Yani yanayokubaliana nayo, na hayatofautiani nayo; hivyo basi hamna kizuizi cha kutomuamini, kwa sababu kilikuja na waliyokuja nayo Mitume. Basi nyinyi ndio mnastahiki zaidi kukiamini na kukisadiki, kwa sababu nyinyi ni watu wa vitabu na elimu. Pia katika kauli yake: “ambayo yanasadikisha mliyo nayo,” kuna ishara kwamba msipokiamini, hilo litawarudia wenyewe kwa kumaanisha mnayakanusha yale mliyo nayo. Kwa maana yale ambayo kilikuja nayo ndiyo Musa alikuja nayo, na Isa na wengineo miongoni mwa Manabii. Hivyo basi, kukikanusha kwenu ni kukataa yale mliyo nayo. Pia, katika vitabu vilivyo mikononi mwenu kuna sifa za Nabii huyu ambaye alikuja na Qur-ani hii, na bishara yake. Kwa hivyo, msipoiamini, mtakuwa mmekadhibisha baadhi ya yale yaliyoteremshwa juu yenu. Na mwenye kukadhibisha baadhi ya yale yaliyoteremshwa juu yake, basi kwa hakika atakuwa amekadhibisha yote. Kama vile mwenye kumkufuru Mtume mmoja, basi kwa hakika atakuwa amewakufuru Mitume wote. Alipowaamrisha kumwamini, akawakataza na akawaonya kinyume chake, nacho ni kuikufuru. Akasema: “Wala msiwe wa kwanza kuyakufuru.” Yani Mtume na Qur-ani. Na katika kauli yake: “Wa kwanza kuyakufuru” ina ufasaha zaidi kuliko kauli yake, “wala msikikufuru” kwa sababu, ikiwa watakuwa wa kwanza kukikufuru, basi itakuwa katika hili kukimbilia kwao kukikufuru, kinyume cha kinachowapasa, na dhambi zao zikawa juu yao na dhambi za mwenye kuwafuata baada yao. Kisha akataja kinachowazuia kuamini, ambacho ni kuchagua anasa ya chini kuliko furaha ya milele. Akasema, "Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo." Ambayo ni kile wanachopata miongoni mwa vyeo na vyakula ambavyo wanadhani kuwa vitakatika ikiwa watamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi wakavinunua kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakavipenda na kuvipendelea. "Na Mimi tu." Yani siyo mwingine, "nicheni;" kwa sababu ikiwa mtamcha Mwenyezi Mungu peke yake, basi huko kumcha kutawalazimu kutanguliza mbele kuziamini Ishara zake badala ya thamani ndogo. Kama vile ikiwa mtachagua thamani hiyo ndogo; basi hiyo ni dalili ya kuondoka kwa uchamungu kutoka katika nyoyo zenu. Kisha akasema:
#
{42} {ولا تلبسوا}؛ أي: تخلطوا {الحق بالباطل وتكتموا الحق}؛ فنهاهم عن شيئين، عن خلط الحق بالباطل وكتمان الحق؛ لأن المقصود من أهل الكتب والعلم تمييز الحق [من الباطل] وإظهار الحق، ليهتدي بذلك المهتدون، ويرجع الضالون وتقوم الحجة على المعاندين؛ لأن الله فصل آياته وأوضح بيناته؛ ليميز الحق من الباطل، ولتستبين سبيل المهتدين من سبيل المجرمين، فمن عمل بهذا من أهل العلم؛ فهو من خلفاء الرسل وهداة الأمم، ومن لَبَّس الحق بالباطل فلم يميز هذا من هذا مع علمه بذلك، وكتم الحق الذي يعلمه وأُمِرَ بإظهاره؛ فهو من دعاة جهنم؛ لأن الناس لا يقتدون في أمر دينهم بغير علمائهم، فاختاروا لأنفسكم إحدى الحالتين.
(42) "Wala msichanganye kweli na uongo na mkaificha kweli," basi akawakataza mambo mawili: Kuchanganya haki (kweli) na batili (uwongo), na kuificha haki. Kwa sababu, kilichokusudiwa na "watu wa vitabu na elimu” ni kupambanua haki [kutoka kwa batili], na kudhihirisha haki, ili waongofu waongoke kwa hilo, na warejee waliopotea; na hoja isimame juu ya wakaidi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alizipambanua ishara (aya) zake na akazibainisha hoja zake zilizo wazi; ili haki ipambanuke kutoka kwa batili, na ili ibainike njia ya walioongoka kutokana na njia ya wakosefu. Basi mwenye kufanya hivi katika watu wa elimu; basi yeye ni katika washikilizi wa Mitume na viongozi wa umma. Na mwenye kuchanganya haki na batili, na hakutofautisha hili kutoka kwa lile pamoja na kujua kwake hilo, na akaficha haki anayoijua, na akaamrishwa kuidhihirisha, basi yeye ni miongoni mwa walinganiaji wa Jahannam (motoni); kwa sababu, watu katika mambo ya dini yao, hawafuati wasiokuwa wanachuoni wao. Basi zichagulieni nafsi zenu moja ya hizo hali mbili.
#
{43} ثم قال: {وأقيموا الصلاة}؛ أي: ظاهراً وباطناً {وآتوا الزكاة}؛ مستحقيها، {واركعوا مع الراكعين}؛ أي: صلوا مع المصلين، فإنكم إذا فعلتم ذلك مع الإيمان برسل الله وآيات الله، فقد جمعتم بين الأعمال الظاهرة والباطنة، وبين الإخلاص للمعبود والإحسان إلى عبيده، وبين العبادات القلبية والبدنية والمالية، وقوله: {واركعوا مع الراكعين}؛ أي: صلوا مع المصلين، ففيه، الأمر بالجماعة للصلاة، ووجوبها، وفيه، أن الركوع ركن من أركان الصلاة، لأنه عبر عن الصلاة بالركوع، والتعبير عن العبادة بجزئها يدل على فرضيته فيها.
(43) Kisha akasema "Na shikeni Sala," yani kwa nje na kwa ndani "na toeni Zaka" muwape wanaoistahiki "na inameni (rukuuni) pamoja na wanaoinama." Yani swalini pamoja na wanaoswali. Kwa sababu, mkifanya hivyo kwa kuwaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu na Ishara (aya) za Mwenyezi Mungu, basi mtakuwa mmekusanya kati ya matendo ya nje na ya ndani (yaliyofichika), na kati ya kumpwekesha muabudiwa (yani Mwenyezi Mungu), na kuwafanyia wema waja wake. Na kati ya ibada za moyoni, kiwiliwili, na kimali. Na kauli yake, "na inameni (rukuuni) pamoja na wanaoinama." Maana yake ni swalini pamoja na wanaoswali. Basi ndani yake imo amri ya kuswali katika Jamaa (mkusanyiko) na ulazima wake. Na ndani yake kuna kwamba rukuu ni katika nguzo za swala; kwa sababu yeye alizungumzia swala kwa kutaja rukuu. Na kuzungumzia ibada kwa kutaja sehemu yake kunaonyesha ulazima wake ndani yake.
: 44 #
[{أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنْسَوْنَ أَنْفُسَكُمْ وَأَنْتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (44)}].
(44) Je, mnawaamrisha watu mema na mnazisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii?
#
{44} {أتأمرون الناس بالبر}؛ أي: بالإيمان والخير، {وتنسون أنفسكم}؛ أي: تتركونها عن أمرها بذلك والحال، {وأنتم تتلون الكتاب أفلا تعقلون}؛ وسُمِّي العقل عقلاً؛ لأنه يعقل به ما ينفعه من الخير، وينعقل به عما يضره، وذلك أن العقل يحث صاحبه أن يكون أول فاعل لما يأمر به، وأول تارك لما ينهى عنه، فمن أمر غيره بالخير ولم يفعله أو نهاه عن الشر فلم يتركه دل على عدم عقله وجهله، خصوصاً إذا كان عالماً بذلك، قد قامت عليه الحجة، وهذه الآية وإن كانت نزلت في سبب بني إسرائيل، فهي عامة لكل أحد لقوله تعالى: {يا أيها الذين آمنوا لم تقولون ما لا تفعلون كبر مقتاً عند الله أن تقولوا ما لا تفعلون}؛ وليس في الآية أن الإنسان إذا لم يقم بما أُمِر به أنه يترك الأمر بالمعروف، والنهي عن المنكر؛ لأنها دلت على التوبيخ بالنسبة إلى الواجبَيْنِ، وإلا فمن المعلوم أن على الإنسان واجبين: أمر غيره ونهيه، وأمر نفسه ونهيها، فترك أحدهما لا يكون رخصة في ترك الآخر، فإن الكمال أن يقوم الإنسان بالواجبَيْنِ، والنقص الكامل أن يتركهما، وأما قيامه بأحدهما دون الآخر فليس في رتبة الأول وهو دون الأخير، وأيضاً فإن النفوس مجبولة على عدم الانقياد لمن يخالف قولَه فعلُه، فاقتداؤهم بالأفعال أبلغ من اقتدائهم بالأقوال المجردة.
(44) "Je, mnawaamrisha watu mema" yani imani na heri, wema "na mnazisahau nafsi zenu." Yani mnaziacha bila ya kuziamrisha kufanya hivyo, na hali ni kuwa "nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii." Na akili iliitwa akili kwa sababu anatambua kwayo yale yenye kumnufaisha katika heri, na anajizuia kwayo kutokana na yenye kumdhuru. Na hilo ni kwamba akili inamhimiza aliye nayo kuwa wa kwanza kufanya anachoamrisha, na wa kwanza kuacha anachokataza. Basi mwenye kumwamrisha mwengine kufanya heri; na asifanye yeye, au akamkataza maovu, na asiyaache yeye. Basi hilo linaashiria kutokuwa kwake na akili, na ujinga wake, hasa akiwa analijua hilo, basi hoja imekwishathibiti juu yake. Na aya hii ijapokuwa iliteremka kuhusu Wana wa Israili, ni ya jumla kwa kila mtu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?" Na hakuna katika aya hii kuwa ikiwa mtu hafanyi analoamrishwa, aache kuamrisha mema na kukataza maovu. Kwa sababu inaashiria kukemea kuhusiana na haya majukumu mawili, vinginevyo inajulikana kuwa mtu ana kazi mbili: Kuamrisha wengine na kumkataza, na kuiamrisha nafsi yake na kuikataza. Na kuacha moja ya hayo, sio ruhusa ya kuacha hilo lingine. Kwa sababu ukamilifu ni kwamba mwanadamu afanye hizi wajibu mbili. Nao upungufu kamili ni kuyaacha yote mawili. Na ama yeye kufanya moja yake bila ya hilo lingine, siyo katika daraja ya ile hali (kamilifu) ya kwanza, lakini iko kabla ya ile ya mwisho. Na pia, nafsi zimeumbika kutomfuata yule ambaye maneno yake yanapingana na vitendo vyake. Kwa hivyo, kufuata kwao matendo kuko juu zaidi kuliko kuyafuata maneno bure.
: 45 - 48 #
{وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ (45) الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُمْ مُلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ (46) يَابَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ (47) وَاتَّقُوا يَوْمًا لَا تَجْزِي نَفْسٌ عَنْ نَفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنْصَرُونَ (48)}.
(45) Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu. (46) Ambao wana yakini kuwa hakika watakutana na Mola wao Mlezi na ya kuwa hakika watarejea kwake. (47) Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizokuneemesheni, na nikakuteueni kuliko wote wengineo. (48) Na icheni Siku ambayo mtu hatomfaa mtu kwa lolote, wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake; wala hawatanusuriwa.
#
{45} أمرهم الله أن يستعينوا في أمورهم كلها بالصبر بجميع أنواعه، وهو الصبر على طاعة الله حتى يؤديها، والصبر عن معصية الله حتى يتركها، والصبر على أقدار الله المؤلمة فلا يتسخطها، فبالصبر وحبس النفس على ما أمر الله بالصبر عليه معونة عظيمة على كل أمر من الأمور، ومن يتصبر يصبره الله، وكذلك الصلاة التي هي ميزان الإيمان، وتنهى عن الفحشاء والمنكر يستعان بها على كل أمر من الأمور، {وإنها}؛ أي: الصلاة، {لكبيرة}؛ أي: شاقة {إلا على الخاشعين}؛ فإنها سهلة عليهم خفيفة؛ لأن الخشوع وخشيةَ الله ورجاءَ ما عنده يوجب له فعلها منشرحاً صدره لترقبه للثواب وخشيته من العقاب، بخلاف من لم يكن كذلك، فإنه لا داعي له يدعوه إليها، وإذا فعلها صارت من أثقل الأشياء عليه. والخشوع: هو خضوع القلب وطمأنينته وسكونه لله تعالى وانكساره بين يديه ذلًّا وافتقاراً وإيماناً به وبلقائه، ولهذا قال:
(45) Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kutafuta msaada katika mambo yao yote kwa subira ya kila aina, nayo ni kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu mpaka alifanye (jambo hilo). Na kusubiri juu ya kumuasi Mwenyezi Mungu mpaka aliache (jambo hilo). Na kusubiri juu ya makadirio machungu ya Mwenyezi Mungu; na asiyachukie. Hivyo basi, kwa subira na kujizuia nafsi juu ya yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kusubiri juu yake ni msaada mkubwa katika kila jambo miongoni mwa mambo. Na mwenye kujisubirisha, basi Mwenyezi Mungu atampa subira. Kadhalika swala ambayo ni mizani ya imani, na inakataza mtu machafu na maovu, inatafutwa kwayo msaada juu ya kila jambo miongoni mwa mambo. "Na kwa hakika, jambo hilo," yani swala, "ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu" kwani ni rahisi na hafifu kwao. Kwa sababu, kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, na kutaraji yaliyoko kwake, yanamletea kuifanya kwa kifua kikunjufu akitafuta (kutaraji) malipo mazuri na akihofu adhabu. Tofauti na asiyekuwa hivyo. Yeye hana haja inayomwita kuiendea. Na anapoifanya, inakuwa katika mambo mazito zaidi kwake. Na khushuu' ni kunyenyekea kwa moyo na kutua kwake, na kutulia kwake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuvunjika kwake mbele yake kwa unyonge na kuonyesha haja kubwa, na kumwamini, na kukutana naye. Ndio maana akasema:
#
{46} {الذين يظنون}؛ أي يستيقنون {أنهم ملاقو ربهم}؛ فيجازيهم بأعمالهم، {وأنهم إليه راجعون}؛ فهذا الذي خفف عليهم العبادات وأوجب لهم التسلي في المصيبات ونفس عنهم الكربات وزجرهم عن فعل السيئات، فهؤلاء لهم النعيمُ المقيمُ في الغرفاتِ العالياتِ، وأما من لم يؤمن بلقاء ربه كانت الصلاة وغيرها من العبادات من أشق شيء عليه.
(46) "Ambao wana yakini kuwa hakika watakutana na Mola wao Mlezi" na awalipe kwa vitendo vyao, "na ya kuwa hakika watarejea kwake." Haya ndiyo yaliyowafanyia ibada kuwa nyepesi, na kuwaletea faraja katika misiba, na kuwaondoshea shida, na kuwakemea kufanya maovu. Basi hao wana neema ya kudumu ndani ya vyumba vya juu. Na ama yule ambaye hakuamini katika kukutana na Mola wake Mlezi, swala na mengineyo miongoni mwa ibada vikawa miongoni mwa vitu vigumu zaidi kwake.
#
{47} ثم: كرر على بني إسرائيل التذكير بنعمته وعظاً لهم وتحذيراً وحثًّا.
(47) Kisha akarudia kuwakumbusha Wana wa Israili neema zake akiwapa mawaidha, na kuwatahadharisha, na kuwahimiza.
#
{48} وخوفهم بيوم القيامة الذي: {لا تجزي}؛ فيه أي لا تغني {نفس}؛ ولو كانت من الأنفس الكريمة كالأنبياء والصالحين، {عن نفس}؛ ولو كانت من العشيرة الأقربين، {شيئاً}؛ لا كبيراً ولا صغيراً وإنما ينفع الإنسانَ عملُه الذي قدمه {ولا يقبل منها}؛ أي: النفس، {شفاعة}؛ لأحد بدون إذن الله ورضاه عن المشفوع له، ولا يرضى من العمل إلا ما أُريد به وجهه وكان على السبيل والسنة، {ولا يؤخذ منها عدل}؛ أي فداء ولو أن لكل نفس ظلمت ما في الأرض جميعاً ومثله معه لافتدوا به من عذاب الله ولا يقبل منهم ذلك، {ولا هم ينصرون}؛ أي: يدفع عنهم المكروه، فنفى الانتفاعَ من الخلق بوجه من الوجوه، فقوله: {لا تَجْزِي نفس عن نفس شيئاً} هذا في تحصيل المنافع، {ولا هم ينصرون} هذا في دفع المضار، فهذا النفي للأمر المستقبل به النافع، {ولا يقبل منها شفاعة ولا يؤخذ منها عدل} هذا نفي للنفع الذي يطلب ممن يملكه بعوض، كالعدل أو بغيره كالشفاعة؛ فهذا يوجب للعبد أن ينقطع قلبه من التعلق بالمخلوقين لعلمه أنهم لا يملكون له مثقال ذرة من النفع، وأن يعلقه بالله الذي يجلب المنافع ويدفع المضار فيعبده وحده لا شريك له، ويستعينه على عبادته.
(48) Na akawahofisha na Siku ya Kiyama ambayo, "hatomfaa mtu" hata ikiwa ni katika nafsi tukufu zaidi kama vile Manabii na watu wema. "Mtu" hata kama ni wa ukoo wa karibu zaidi "chochote" siyo kikubwa wala kidogo. Lakini binadamu yatamnufaisha tu matendo yake ambayo alitanguliza mbele. "Wala hayatakubaliwa kwake maombezi" kwa yeyote bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu na kumridhia kwake yule anayeombewa. Na wala haridhii katika matendo isipokuwa yale yaliyokusudiwa kwayo uso wake, na yalikuwa kwenye Njia na Sunnah. "Na wala hakitapokewa kikomboleo kutoka kwake" na lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilimo katika ardhi pamoja na mfano wake; bila shaka ingelitoa fidia vyote kujikomboa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wala halitakubaliwa hilo kutoka kwao. "Wala hawatanusuriwa" yani hawataondolewa machukizo hayo. Basi akakanusha kunufaika kutoka kwa viumbe kwa namna yoyote ile. Hivyo, kauli yake "mtu hatomfaa mtu kwa chochote,” ni katika kutafuta manufaa, "wala hawatanusuriwa" hili ni katika kuzuia madhara. Na huku ni kukanusha jambo ambalo mwenye kunufaisha anajiwa nalo. "Wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake." Na huku ni kukanusha (kupata) manufaa yanayoombwa kutoka kwa anayeyamiliki kwa kubadilishana, kama vile uadilifu, au kwa kitu kingine, kama vile uombezi. Kwa hivyo, hili linamlazimu mja kuukata moyo wake kutokana na kufungamana na viumbe akishajua kuwa wao hawatamanufaisha uzito wa chembe, na kwamba aufungamanishe na Mwenyezi Mungu ambaye analeta manufaa, na anazuia madhara. Basi amuabudu Yeye peke yake, hana mshirika yeyote, na amtake msaada katika kumuabudu.
: 49 - 57 #
{وَإِذْ نَجَّيْنَاكُمْ مِنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ وَفِي ذَلِكُمْ بَلَاءٌ مِنْ رَبِّكُمْ عَظِيمٌ (49) وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنْجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنْتُمْ تَنْظُرُونَ (50) وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَى أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِنْ بَعْدِهِ وَأَنْتُمْ ظَالِمُونَ (51) ثُمَّ عَفَوْنَا عَنْكُمْ مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (52) وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ (53) وَإِذْ قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ يَاقَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنْفُسَكُمْ بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَى بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنْفُسَكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ عِنْدَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (54) وَإِذْ قُلْتُمْ يَامُوسَى لَنْ نُؤْمِنَ لَكَ حَتَّى نَرَى اللَّهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنْتُمْ تَنْظُرُونَ (55) ثُمَّ بَعَثْنَاكُمْ مِنْ بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (56) وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنْزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَى كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَكِنْ كَانُوا أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ (57)}.
(49) Na (kumbukeni) tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni, waliokuwa wakiwapa adhabu mbaya, wakiwachinja wana wenu wa kiume, na wakiwawacha hai wanawake wenu. Na katika hayo kulikuwa na mtihani mkubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi. (50) Na tulipoipasua bahari kwa ajili yenu na tukakuokoeni, tukawazamisha watu wa Firauni, na huku mnatazama. (51) Na tulipomuahidi Musa masiku arubaini, kisha mkamchukua ndama (mkamuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu. (52) Kisha tukakusameheni baada ya hayo, ili mpate kushukuru. (53) Na tulipompa Musa Kitabu na pambanuo ili mpate kuongoka. (54) Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kuchukua kwenu ndama (kumuabudu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na ziueni nafsi zenu. Haya ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Naye akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba na Mwenye kurehemu. (55) Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi. Ukakunyakueni mpigo wa radi nanyi mnaangalia. (56) Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru. (57) Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna na Salwa; tukakwambieni: Kuleni vitu vizuri hivi tulivyokuruzukuni. Nao hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wanazidhulumu nafsi zao.
#
{49 - 54} هذا: شروع في تعداد نعمه على بني إسرائيل على وجه التفصيل فقال: {وإذ نجيناكم من آل فرعون}؛ أي: من فرعون وملئه وجنوده وكانوا قبل ذلك، {يسومونكم}؛ أي: يولونهم ويستعملونهم {سوء العذاب}؛ أي: أشده بأن كانوا، {يذبحون أبناءكم}؛ خشية نموكم، {ويستحيون نساءكم}؛ أي: فلا يقتلونهن فأنتم بين قتيل ومُذلَّل بالأعمال الشاقة مستحيَى على وجه المنة عليه والاستعلاء عليه فهذا غاية الإهانة، فَمَنَّ الله عليهم بالنجاة التامة، وإغراق عدوهم، وهم ينظرون لتَقَرَّ أعينهم {وفي ذلكم}؛ أي: الإنجاء {بلاء}؛ أي: إحسان {من ربكم عظيم}؛ فهذا مما يوجب عليكم الشكر والقيام بأوامره. ثم ذكر منته عليهم بوعده لموسى أربعين ليلة؛ لينزل عليهم التوراة المتضمنة للنعم العظيمة والمصالح العميمة، ثم إنهم لم يصبروا قبل استكمال الميعاد حتى عبدوا العجل من بعده؛ أي ذهابه {وأنتم ظالمون}؛ عالمون بظلمكم، قد قامت عليكم الحجة، فهو أعظم جرماً، وأكبر إثماً. ثم إنه أمركم بالتوبة على لسان نبيه موسى بأن يقتل بعضكم بعضاً؛ فعفا الله عنكم بسبب ذلك {لعلكم تشكرون}؛ الله.
(49-54) Huu ndio mwanzo wa kubainisha neema zake (Mwenyezi Mungu) juu ya Wana wa Israili kwa undani. Akasema: "Na vile tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Firauni." Yani kutoka kwa Firauni na wakuu wake na majeshi yake. Na walikuwa kabla ya hapo "waliokupeni" yani kuwatumia na kuwapa "adhabu mbaya" yani kali sana. "Wakiwachinja wana wenu wa kiume" kwa kuogopa kuongezeka kwenu. "Na wakawawacha hai wanawake" yani hawakuwa wakiwaua. Basi mkawa kati ya wanaouawa na wale wanaodhalilishwa kwa kazi ngumu, wanaoachwa kuishi kwa njia ya hisani na kutawaliwa. Basi huku ndiko kudhalilishwa kwa juu mno. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa uokozi kamili, na kumzamisha adui yao hali ya kuwa wanatazama ili macho yao yafurahike "katika hayo" yani kuwaokoa "ulikuwa (uokozi huo) ni ihsani kubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Kwa hivyo, hayo ndiyo yanayowalazimu nyinyi kushukuru na kutekeleza maamrisho yake. Kisha akawatajia neema yake juu yao ya kumwahidi Musa usiku arubaini; ili awateremshie Taurati iliyojumuisha neema kubwa na masilahi ya jumla. Kisha wao hawakungoja mpaka kukamilika kwa miadi hiyo mpaka wakamwabudu ndama nyuma ya kuondoka kwake (Musa). "Na mkawa wenye kudhulumu" huku mkijua dhuluma yenu, na hoja imekwishathibitika juu yenu. Hilo ni kosa kubwa mno na dhambi kubwa sana. Kisha akakuamrisheni kutubu juu ya ulimi wa Nabii wake Musa kwa kuuana nyinyi kwa nyinyi, basi Mwenyezi Mungu akakusameheni kwa sababu ya hayo "ili mpate kushukuru" Mwenyezi Mungu.
#
{55} {وإذ قلتم يا موسى لن نؤمن لك حتى نرى الله جهرة}؛ وهذا غاية الجرأة على الله وعلى رسوله، {فأخذتكم الصاعقة}؛ إما الموت أو الغشية العظيمة {وأنتم تنظرون}؛ وقوع ذلك كل ينظر إلى صاحبه.
(55) "Na mliposema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi." Na huu ndio ujasiri mkubwa zaidi juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake "Ukakunyakueni mpigo wa radi" ima kwa kifo au kuzimia kukubwa. "Nanyi mnaangalia" kutokea kwa hayo. Kila mmoja akimtazama mwenzake.
#
{56} {ثم بعثناكم من بعد موتكم لعلكم تشكرون}؛ ثم ذكر نعمته عليهم في التِيه والبرية الخالية من الظلال وسعة الأرزاق فقال:
(56) "Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru." Kisha akataja neema yake ya (kuwapa) vivuli na wasaa wa riziki katika jangwa na nchi kavu. Akasema:
#
{57} {وظللنا عليكم الغمام وأنزلنا عليكم المنّ}؛ وهو: اسم جامع لكل رزق [حسن] يحصل بلا تعب، ومنه الزنجبيل والكمأة، والخبز، وغير ذلك، {والسلوى}؛ طائر صغير يقال له: السماني طيب اللحم؛ فكان ينزل عليهم من المنِّ والسلوى ما يكفيهم ويقيتهم {كلوا من طيبات ما رزقناكم}؛ أي: رزقاً لا يحصل نظيره لأهل المدن المترفهين، فلم يشكروا هذه النعمة ، واستمروا على قساوة القلوب وكثرة الذنوب {وما ظلمونا}؛ يعني بتلك الأفعال المخالفة لأوامرنا، لأن الله لا تضره معصية العاصين كما لا تنفعه طاعات الطائعين {ولكن كانوا أنفسهم يظلمون}؛ فيعود ضرره عليهم.
(57) "Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna" nalo ni jina linalojumuisha kila riziki [njema] inayopatikana bila ya taabu. Na miongoni mwake ni tangawizi, uyoga, mkate, na mengineyo. "Na Salwa" Naye ni ndege mdogo anayeitwa kware, mwenye nyama nzuri. Na alikuwa akiwateremshia Manna na Salwa (kware) vinavyowatosha na kama riziki ya kuwatunza. "Kuleni vitu vizuri hivi tulivyokuruzukuni." Yani riziki ambayo hawapewi mfano wake watu wa miji mingine waliostareheshwa. Lakini hawakushukuru neema hii, na wakaendelea na ugumu wa nyoyo na wingi wa dhambi. "Nao hawakutudhulumu Sisi." Yani kwa hayo matendo yaliyohalifu maamrisho yetu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hadhuriwi na uasi wa waasi. Kama vile hakumnufaishi kumtii kwa wenye kutii. "Lakini walikuwa wanazidhulumu nafsi zao." Hivyo madhara yake yakawarudia wao.
: 58 - 59 #
{وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ (58) فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنْزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ (59)}.
(58) Na tuliposema: Ingieni mji huu, na humo mle mpendapo maridhawa, na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, na semeni: Tusamehe! Tutakusameheni makosa yenu, na tutawazidishia wema wafanyao wema. (59) Lakini waliodhulumu waliibadili kauli isiyo kuwa waliyoambiwa. Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya walivyokuwa wamepotoka.
#
{58} وهذا أيضاً من نعمته عليهم بعد معصيتهم إياه، فأمرهم بدخول قرية تكون لهم عزًّا ووطناً ومسكناً، ويحصل لهم فيها الرزقُ الرغدُ، وأن يكون دخولهم على وجه خاضعين لله فيه بالفعل، وهو دخول الباب سجداً، أي: خاضعين ذليلين، وبالقول وهو أن يقولوا: {حطة}؛ أي: أن يحط عنهم خطاياهم بسؤالهم إياه مغفرته، {نغفر لكم خطاياكم}؛ بسؤالكم المغفرة {وسنزيد المحسنين}؛ بأعمالهم أي: جزاء عاجلاً وآجلاً.
(58) Na hii pia ni katika neema zake juu yao baada ya kumuasi Yeye. Basi akawaamrisha waingie katika mji ambao humo watakuwa na utukufu, na nchi na makazi. Na watapata humo riziki nyingi. Na kwamba kuingia kwao kuwe kwa namna ambayo kwayo watamnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa vitendo, nako ni kuingia mlangoni kwa kusujudu, yani kwa unyenyekevu na udhalilifu. Na kwa kauli, ambayo ni kusema: "Tusamehe!" Yani kuwasamehe dhambi zao kwa wao kumuomba Yeye msamaha. "Tutakusameheni makosa yenu" kwa kuomba kwenu msamaha, "na tutawazidishia wema wafanyao wema." Kwa vitendo vyao, yani kuwalipa malipo ya haraka na ya baadaye.
#
{59} {فبدل الذين ظلموا}؛ منهم، ولم يقل فبدلوا؛ لأنهم لم يكونوا كلهم بدلوا {قولاً غير الذي قيل لهم}؛ فقالوا: بدل حطة، حبة في حنطة، استهانة بأمر الله، واستهزاء وإذا بدلوا القول مع خفته فتبديلهم للفعل من باب أولى وأحرى، ولهذا دخلوا يزحفون على أدبارهم، ولما كان هذا الطغيان أكبر سببٍ لوقوع عقوبة الله بهم قال: {فأنزلنا على الذين ظلموا}؛ منهم {رجزاً}؛ أي: عذاباً {من السماء}؛ بسبب فسقهم وبغيهم.
(59) "Lakini waliodhulumu waliibadili" miongoni mwao. Na wala hakusema "lakini walibadili." Kwa kuwa siyo wote walikuwa wamebadili "kauli isiyo kuwa waliyoambiwa." Na badala ya "Tusamehe" wakasema "punje katika ngano," huku wakipuuza amri ya Mwenyezi Mungu, na kwa kejeli. Na ikiwa waliibadilisha kauli hiyo pamoja na wepesi wake, basi kubadilisha kwao kitendo ni katika mlango wa uwezekano mkubwa na ufaao zaidi. Na kwa sababu ya hilo, wakaingia wakitambaa juu ya makalio yao. Na kulipokuwa huku kupindukia ndiyo iliyokuwa sababu kubwa ya kuwashukia adhabu ya Mwenyezi Mungu, akasema: "Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni." Kwa sababu ya kupindukia kwao mipaka na kufanya kwao jeuri.
: 60 #
{وَإِذِ اسْتَسْقَى مُوسَى لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْحَجَرَ فَانْفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَشْرَبَهُمْ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِنْ رِزْقِ اللَّهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ (60)}.
(60) Na Musa alipoomba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemichemi kumi na mbili; kila kabila likajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.
#
{60} {استسقى}؛ أي: طلب لهم ماء يشربون منه {فقلنا اضرب بعصاك الحجر}؛ إما حجر مخصوص معلوم عنده، وإما اسم جنس؛ {فانفجرت منه اثنتا عشرة عيناً}؛ وقبائل بني إسرائيل اثنتا عشرة قبيلة، {قد علم كل أناس}؛ منهم {مشربهم}؛ أي: محلهم الذي يشربون عليه من هذه الأعين، فلا يزاحم بعضهم بعضاً بل يشربونه متهنئين لا متكدرين، ولهذا قال: {كلوا واشربوا من رزق الله}؛ أي: الذي آتاكم من غير سعي ولا تعب {ولا تعثوا في الأرض}؛ أي: تخربوا على وجه الإفساد.
(60) "Istasqaa" yani (Musa) alipoomba maji ili wanywe kwayo "tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako." Ima jiwe mahususi analolijua, au jiwe lolote lile "Mara zikatimbuka chemichemi kumi na mbili." Na makabila ya Wana wa Israili yalikuwa kumi na mawili. "Kila kabila" miongoni "likajua mahali pake pa kunywea," katika hizo chemichemi. Kwa hivyo, hawasongamani wao kwa wao, bali wanakunywa kwa furaha siyo kwa kukasirikiana. Na ndio kwa maana akasema: "Kuleni na mnywe katika riziki ya Mwenyezi Mungu." Yani ambayo amekupeni bila ya juhudi wala kutaabika "wala msiende katika ardhi," yani mkifanya uharibifu.
: 61 #
{وَإِذْ قُلْتُمْ يَامُوسَى لَنْ نَصْبِرَ عَلَى طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنْبِتُ الْأَرْضُ مِنْ بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَى بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُمْ مَا سَأَلْتُمْ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِنَ اللَّهِ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ (61)}.
(61) Na mliposema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyomea katika Ardhi, kama mboga zake, na matango yake, na thom zake, na adesi zake, na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko mtapata mlivyoviomba. Na wakapigwa na unyonge,na umasikini, na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasipo haki. Hayo ni kwa walivyoasi na wakapindukia mipaka.
#
{61} أي: واذكروا {إذ قلتم} لموسى على وجه التملل لنعم الله، والاحتقار لها {لن نصبر على طعام واحد}؛ أي: جنس من الطعام وإن كان كما تقدم أنواعاً لكنها لا تتغير {فادع لنا ربك يخرج لنا مما تنبت الأرض من بقلها}؛ أي: نباتها الذي ليس بشجر يقوم على ساقه {وقثائها}؛ وهو الخيار {وفومها}؛ أي: ثومها والعدس والبصل معروف، قال لهم موسى: {أتستبدلون الذي هو أدنى}؛ وهو الأطعمة المذكورة {بالذي هو خير}؛ وهو المن والسلوى، فهذا غير لائق بكم، فإن هذه الأطعمة التي طلبتم، أي مِصْرٍ هبطتموه وجدتموها، وأما طعامكم الذي منَّ الله به عليكم فهو خير الأطعمة وأشرفها فكيف تطلبون به بدلاً؟ ولما كان الذي جرى منهم فيه أكبر دليل على قلة صبرهم، واحتقارهم لأوامر الله ونعمه جازاهم من جنس عملهم فقال: {وضربت عليهم الذلة}؛ التي تُشاهدَ على ظاهر أبدانهم {والمسكنة}؛ بقلوبهم فلم تكن أنفسهم عزيزة، ولا لهم همم عالية بل أنفسهم أنفس مهينة، وهممهم أردأ الهمم {وباؤوا بغضب من الله}؛ أي: لم تكن غنيمتهم التي رجعوا بها، وفازوا إلا أن رجعوا بسخطه عليهم؛ فبئس الغنيمة غنيمتهم، وبئس الحالة حالتهم {ذلك}؛ الذي استحقوا به غضبه {بأنهم كانوا يكفرون بآيات الله}؛ الدالات على الحق الموضحة لهم، فلما كفروا بها عاقبهم بغضبه عليهم وبما كانوا {يقتلون النبيين بغير الحق}؛ وقوله: {بغير الحق} زيادة شناعة، وإلا فمن المعلوم أن قتل النبيين لا يكون بحق، لكن لئلا يظن جهلهم وعدم علمهم {ذلك بما عصوا}؛ بأن ارتكبوا معاصي الله {وكانوا يعتدون}؛ على عباد الله؛ فإن المعاصي يجر بعضها بعضاً، فالغفلة ينشأ عنها الذنب الصغير، ثم ينشأ عنه الذنب الكبير، ثم ينشأ عنها أنواع البدع والكفر وغير ذلك، فنسأل الله العافية من كل بلاء. واعلم أن الخطاب في هذه الآيات لأمة بني إسرائيل الذين كانوا موجودين وقت نزول القرآن، وهذه الأفعال المذكورة خوطبوا بها وهي فعل أسلافهم، ونسبت لهم لفوائد عديدة. منها: أنهم كانوا يتمدحون، ويزكون أنفسهم، ويزعمون فضلهم على محمد ومن آمن به؛ فبين الله من أحوال سلفهم التي قد تقررت عندهم ما يبين به لكل واحد منهم أنهم ليسوا من أهل الصبر، ومكارم الأخلاق، ومعالي الأعمال، فإذا كانت هذه حالة سلفهم ـ مع أن المظنة أنهم أولى وأرفع حالة ممن بعدهم ـ فكيف الظن بالمخاطبين! ومنها: أن نعمة الله على المتقدمين منهم نعمة واصلة إلى المتأخرين، والنعمة على الآباء نعمة على الأبناء، فخوطبوا بها، لأنها نعم تشملهم وتعمهم. ومنها: أن الخطاب لهم بأفعال غيرهم مما يدل على أن الأمة المجتمعة على دين تتكافل وتتساعد على مصالحها، حتى كأنَّ متقدمهم ومتأخرهم في وقت واحد، وكأن الحادثَ من بعضهم حادثٌ من الجميع؛ لأن ما يعمله بعضهم من الخير يعود بمصلحة الجميع، وما يعمله من الشر يعود بضرر الجميع. ومنها: أن أفعالهم أكثرها لم ينكروها، والراضي بالمعصية شريك للعاصي، إلى غير ذلك من الحكم التي لا يعلمها إلا الله.
(61) Yani kumbukeni "mliposema" kumwambia Musa kwa namna ya kuchoshwa na kudharau neema za Mwenyezi Mungu. "Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu" yani aina moja ya chakula, ingawa kama ilivyotangulia, kulikuwa na aina mbalimbali, lakini havikuwa vinabadilika. "Basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyomea katika ardhi, kama mboga zake." Yani mimea yake isiyokuwa miti inayosimama juu ya shina lake, "na matango yake, na thom zake, na adesi zake," ambavyo ni vyakula maarufu. Musa akawaambia "Mnabadili kilicho duni" ambavyo ni hivyo vyakula vilivyotajwa, "kwa kile kilicho bora?" Nazo ni Manna na Salwa. Hili haliwafailii. Kwa sababu, vyakula hivi mlivyoviomba, mji wowote mnaotua, humo mtavipata. Na ama chakula chenu ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa hicho ndicho chakula bora na cha heshima. Basi vipi mnaomba badala yake? Na kwa kuwa yale waliyofanya yalikuwa ni dalili kubwa ya subira yao chache, na kudharau kwao maamrisho ya Mwenyezi Mungu na neema zake, akawalipa na malipo kama matendo yao. Akasema: "Na wakapigwa na unyonge" unaoonekana juu ya miili yao "na umasikini" ndani ya nyoyo zao. Kwa hivyo, roho zao hazikuwa za kuheshimika, wala hawakuwa na hima kubwa, bali nafsi zao zilikuwa duni, na azma zao zilikuwa mbaya zaidi "na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu." Yani haikuwa ngawira yao waliorudi nayo na wakafaulu isipokuwa kwamba walirudi na ghadhabu yake juu yao. Basi ngawira mbaya mno ni ngawira yao. Na hali mbaya mno ni hali yao mbaya. "Na hayo" ambayo kwayo walistahiki ghadhabu yake, "ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu," yanayoashiria haki waliyobainishiwa. Basi walipozikataa, akawaadhibu kwa hasira yake juu yao, na kwa yale waliyokuwa "wakiwauwa Manabii pasipo haki." Na kauli yake "pasipo haki." Ni ziada ya kuonyesha ubaya wa hilo. Vinginevyo inajulikana kuwa siyo haki kumuua Nabii, lakini (hili neno liliongezwa) ili usije ukafikiriwa ujinga wao na kutojua kwao. "Hayo ni kwa walivyoasi" kwa kuwa walimuasi Mwenyezi Mungu "na wakapindukia mipaka." dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu maasia yanaitana yenyewe kwa yenyewe. Na kughafilika kunasababisha dhambi ndogo, kisha yanatokana na hilo madhambi makubwa, kisha zinatokana na hilo aina mbali mbali za uzushi, ukafiri na mengineyo. Hivyo basi, tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde kutokana na kila balaa. Na jua ya kwamba maneno katika Aya hizi yamekusudiwa umma wa Wana wa Israili waliokuwepo wakati wa kuteremka kwa Qur-ani. Na hivi vitendo vilivyotajwa waliongeleshwa wao kwavyo, ingawa ni vitendo vya mababu zao. Na walinasibishwa navyo kwa faida mbalimbali. Miongoni mwake ni kwamba walikuwa wakijisifu na wakizitakasa nafsi zao, na wanadai kuwa wao ni bora kumliko Muhammad na wale waliomwamini. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akabainisha katika hali za watangulizi (mababu) zao ambazo walikwisha jua vizuri kile kinachomwekea wazi kila mmoja wao kwamba wao si miongoni mwa watu wenye subira, na maadili mema, na matendo ya juu. Basi ikiwa hii ndiyo hali ya watangulizi wao - pamoja na kwamba dhana kubwa ni kuwa wao (watangulizi) wanastahili na ni wa hali ya juu zaidi kuliko wale wa baada yao – basi itakuwa vipi dhana juu ya wale wanaoongeleshwa. Na miongoni mwake ni kwamba neema ya Mwenyezi Mungu juu ya waliotangulia miongoni mwao ni neema ya kuendelea hadi kwa waliokuja baadaye. Na neema juu ya mababa ni neema juu ya watoto. Kwa hivyo, wakaongeleshwa kwazo (hizo neema), kwa sababu ni neema zinazowaenea na kuwajumuisha. Na miongoni mwake ni kwamba kuwaongelesha kwa vitendo vya wengine, ni katika yale yanayoashiria kuwa umma uliokusanyika juu ya dini moja, unategemeana na kusaidiana kwa masilahi yake, kiasi kwamba ni kama kwamba wa kwanza na wa mwisho wao wako katika wakati mmoja. Na ni kama kwamba tukio la baadhi yao ni tukio kutoka kwa wote. Kwa sababu anachoyafanya mmoja wao katika kwa heri, inaleta masilahi ya wote. Na anachoyafanya katika maovu, madhara yake yanawarudia wote. Na miongoni mwake ni kwamba wao hawakupinga mengi ya matendo yao (yani ya mababu zao). Na mwenye kuridhia uasi, basi yeye ni mshiriki wa huyo muasi, na mengineyo miongoni mwa hekima ambazo hazijui isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akihukumu kati ya makundi ya waliopewa kitabu:
: 62 #
{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَى وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (62)}.
(62) Hakika Walioamini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika.
#
{62} وهذا الحكم على أهل الكتاب خاصة، لأن الصابئين الصحيح: أنهم من جملة فرق النصارى، فأخبر الله أن المؤمنين من هذه الأمة واليهود والنصارى والصابئين من آمن بالله [منهم] واليوم الآخر وصدقوا رسلهم، فإن لهم الأجر العظيم، والأمن، ولا خوف عليهم ولا هم يحزنون، وأما من كفر منهم بالله ورسله واليوم الآخر، فهو بضد هذه الحال؛ فعليه الخوف والحزن. والصحيح: أن هذا الحكم بين هذه الطوائف من حيث هم لا بالنسبة إلى الإيمان بمحمد، فإن هذا إخبار عنهم قبل بعثة محمد، وإن هذا مضمون أحوالهم، وهذه طريقة القرآن إذا وقع في بعض النفوس ـ عند سياق الآيات ـ بعض الأوهام، فلا بد أن تجد ما يزيل ذلك الوهم؛ لأنه تنزيل من يعلم الأشياء قبل وجودها، ومن رحمته وسعت كل شيء، وذلك ـ والله أعلم ـ أنه لما ذكر بني إسرائيل وذمهم وذكر معاصيَهم وقبائحهم ربما وقع في بعض النفوس أنهم كلهم يشملهم الذم، فأراد الباري تعالى أن يبين من لا يلحقه الذم منهم بوصفه، ولما كان أيضاً ذكر بني إسرائيل خاصة يوهم الاختصاص بهم، ذكر تعالى حكماً عامًّا يشمل الطوائف كلها؛ ليتضح الحق ويزول التوهم والإشكال، فسبحان من أودع في كتابه ما يبهر عقول العالمين.
(62) Na hukumu hii ni ya Watu wa Kitabu hususan, kwa sababu Wasabai wapo sahihi ya kwamba wao ni miongoni mwa makundi ya Kikristo. Basi Mwenyezi Mungu akatoa habari kuwa Waumini wa huu Ummah, na Mayahudi, na Wakristo na Wasabai, mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu [miongoni mwao] na Siku ya Mwisho na wakawasadiki Mitume wao. Basi watapata malipo makubwa na amani, wala haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika. Na ama mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu miongoni mwao, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, basi yeye yuko kinyume na hali hii; hivyo, hofu na huzuni vitakuwa juu yake. Na sahihi ni kwamba hukumu hii baina ya haya makundi ni kuhusiana na jinsi walivyo, sio kuhusiana na kumuamini Muhammad. Kwa sababu, huku ni kuwazungumzia kabla ya utume wa Muhammad. Na hivi ndivyo zilivyo hali zao. Na hii ndiyo njia ya Qur-ani inapoingia katika baadhi ya nafsi – wakati wa kusimulia Aya – baadhi ya fikira potofu, basi huwa hakuna budi kwamba utapata kinachoondoa fikira hiyo potofu. Kwa sababu (Qur-ani hii) ni uteremsho kutoka kwa yule anayeyajua mambo kabla hayajatokea, na yule ambaye rehema zake zimeenea kila kitu. Na hilo - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - ni kwamba, alipowataja Wana wa Israili na kuwakashifu, na akataja dhambi zao na maovu yao, huenda ikaingia katika baadhi ya nafsi kwamba wote pia wanaingia katika kashfa hiyo. Kwa hivyo, Muumba Mtukufu alitaka kubainisha wale ambao hawaingii katika kashfa hiyo miongoni mwao kwa kueleza sifa zake. Na pindi alipowataja Wana wa Israili hasa, ikaleta fikira kuwa hilo ni mahususi kwao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hukumu ya jumla inayojumuisha makundi yote. Ili ukweli ubainike na fikira upotovu na mkanganyiko viondoke. Basi ametakasika yule ambaye ameweka katika Kitabu chake yale yanayoangaza akili za wenye elimu.
Kisha (Mwenyezi Mungu) Mwenye baraka na Mtukufu akarudia kuwakemea Wana wa Israili kwa yale waliyofanya watangulizi wao.
: 63 - 64 #
{وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُمْ بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ (63) ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنْتُمْ مِنَ الْخَاسِرِينَ (64)}
(63) Na tulipochukua ahadi yenu, na tukaunyanyua mlima juu yenu (tukakwambieni): Shikeni kwa nguvu haya tuliyokupeni, na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mpate kuokoka. (64) Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema zake, mngelikuwa miongoni mwa wenye kupata hasara.
#
{63} أي: واذكروا، {إذ أخذنا ميثاقكم}؛ وهو العهد الثقيل المؤكد بالتخويف لهم برفع الطور فوقهم وقيل لهم، {خذوا ما آتيناكم}؛ من التوراة {بقوة}؛ أي بجد واجتهاد، وصبر على أوامر الله {واذكروا ما فيه}؛ أي: ما في كتابكم بأن تتلوه وتتعلموه {لعلكم تتقون}؛ عذاب الله وسخطه، أو لتكونوا من أهل التقوى.
(63) Yani kumbukeni "tulipochukua ahadi yenu" nayo ni ahadi nzito iliyosisitizwa kwa kuwatishia kwa kunyanyua mlima juu yao, na wakaambiwa "Shikeni haya tuliyokupeni" katika Taurati "kwa nguvu" yani bidii na jitihada, na kuwa na subira juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu, "na yakumbukeni yaliyomo ndani yake" yani yaliyomo katika kitabu chenu, kwamba myasome na mjifunze "ili mpate kuwa kuokoka." na adhabu ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu yake, au ili muwe miongoni mwa wachamungu.
#
{64} فبعد هذا التأكيد البليغ {توليتم}؛ وأعرضتم وكان ذلك موجباً لأن يحل بكم أعظم العقوبات ولكن {لولا فضل الله عليكم ورحمته لكنتم من الخاسرين}.
(64) Na baada ya huku kusisitiza kukubwa "mligeuka" na mkapeana mgongo. Na hilo lililazimu ikupateni adhabu kubwa zaidi, lakini "na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema zake, mngelikuwa miongoni mwa wenye kukhasirika."
: 65 - 66 #
{وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنْكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ (65) فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِلْمُتَّقِينَ (66)}.
(65) Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu waliopindukia mipaka kuhusu Sabato, (siku ya mapumziko, Jumamosi) na tukawaambia: Kuweni manyani mliodhalilika. (66) Kwa hivyo tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale waliokuwa katika zama zao na waliokuja baada yao, na mawaidha kwa wachamungu.
#
{65} أي: ولقد تقرر عندكم حالةُ، {الذين اعتدوا منكم في السبت}؛ وهم الذين ذكر الله قصتهم مبسوطة في سورة الأعراف في قوله: {واسألهم عن القرية التي كانت حاضرة البحر إذ يعدون في السبت ... } الآيات؛ فأوجب لهم هذا الذنب العظيم أن غضب الله عليهم، وجعلهم {قردة خاسئين}؛ حقيرين ذليلين، وجعل الله هذه العقوبة:
(65) Yani mlikwisha jua hali ya "wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato (siku ya mapumziko, Jumamosi)." Nao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu alitaja kisa chao katika Suratul-A’raf kwa upana, katika kauli yake. "Na waulize khabari za mji uliokuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato..." hadi mwisho wa hizi Aya. Basi hii dhambi kubwa ikafanya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwajibike juu yao, na akawafanya kuwa "manyani wadhalilifu"; wanaodharauliwa, na wanaodhalilishwa. Na Mungu akaifanya hii adhabu:
#
{66} {نكالاً لما بين يديها}؛ أي: لمن حضرها من الأمم، وبلغه خبرها ممن هو في وقتهم {وما خلفها}؛ أي: من بعدها فتقوم على العباد حجة الله، وليرتدعوا عن معاصيه، ولكنها لا تكون موعظة نافعة إلا للمتقين، وأما من عداهم فلا ينتفعون بالآيات.
(66) "Kuwa onyo kwa wale walio kuwa katika zama zao." Yani kwa waliohudhuria hilo tukio miongoni mwa mataifa, na zikamfikia habari zake kwa waliokuwa katika zama zao, "na waliokuja baada yao" ili hoja ya Mwenyezi Mungu isimame juu ya waja, na wakomeke kumuasi. Lakini halitakuwa ni mawaidha yenye manufaa isipokuwa kwa wachamungu. Na ama wengineo, wao hawanufaiki kwa Aya.
: 67 - 74 #
{وَإِذْ قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تَذْبَحُوا بَقَرَةً قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا قَالَ أَعُوذُ بِاللَّهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ (67) قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّنْ لَنَا مَا هِيَ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَلِكَ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ (68) قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّنْ لَنَا مَا لَوْنُهَا قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ (69) قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّنْ لَنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ لَمُهْتَدُونَ (70) قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَا شِيَةَ فِيهَا قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ (71) وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا وَاللَّهُ مُخْرِجٌ مَا كُنْتُمْ تَكْتُمُونَ (72) فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا كَذَلِكَ يُحْيِ اللَّهُ الْمَوْتَى وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ (73) ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُمْ مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّهِ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ (74)}.
(67) Na Musa alipowaambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje Ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: "Audhu billahi!" Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga. (68) Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni Ng'ombe gani? Akasema: Hakika Yeye anasema kwamba Ng'ombe huyo si mpevu, wala si kinda, bali ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyoamrishwa. (69) Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ipi rangi yake? Akasema: Yeye anasema, kuwa Ng'ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imekoza, huwapendeza wanaomtazama. (70) Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi? Hakika tunaona ng'ombe wamefanana. Na kwa yakini, Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, tutaongoka. (71) Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni Ng'ombe asiyetiwa kazini kulima Ardhi wala kumwagia maji mimea, mzima, hana baka. Wakasema: Sasa umeleta (jambo la) haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo. (72) Na mlipo muua mtu, kisha mkakhitalifiana kwayo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyokuwa mkiyaficha. (73) Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo Ng'ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate kufahamu. (74) Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayotimbuka mito, na kuna mengine yanayopasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumhofu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyafanya.
#
{67} أي: واذكروا ما جرى لكم مع موسى حين قتلتم قتيلاً؛ فادّارَأْتم فيه، أي: تدافعتم واختلفتم في قاتله حتى تفاقم الأمر بينكم، وكاد ـ لولا تبيين الله لكم ـ يحدث بينكم شر كبير، فقال لكم موسى في تبيين القاتل: اذبحوا بقرة، وكان من الواجب المبادرة إلى امتثال أمره وعدم الاعتراض عليه، ولكنهم أبوا إلا الاعتراض فقالوا: {أتتخذنا هزواً}؛ فقال نبي الله: {أعوذ بالله أن أكون من الجاهلين}؛ فإن الجاهل هو الذي يتكلم بالكلام الذي لا فائدة فيه وهو الذي يستهزئ بالناس، وأما العاقل فيرى أن من أكبر العيوب المزرية بالدين والعقل استهزاءه بمن هو آدمي مثله. وإن كان قد فضل عليه فتفضيله يقتضي منه الشكر لربه والرحمة لعباده: فلما قال لهم موسى ذلك علموا أن ذلك صدق، فقالوا:
(67) Yani: Na kumbukeni yale yaliyowapata pamoja na Musa wakati mlipomuua mtu; hivyo mkahitilafiana kwa hilo juu ya muuaji wake mpaka jambo hilo likawa kubwa baina yenu, na ikakaribia sana - lau kuwa si Mwenyezi Mungu kuwabainishia -, kutokea uovu mkubwa baina yenu. Basi Musa akawaambia katika kubainisha muuaji: Mchinjeni ng'ombe (wa kike). Na ilikuwa wajibu kuharakisha kutekeleza amri yake na kutoipinga. Lakini wao wakakataa isipokuwa kuipinga, na wakasema: "Je, unatufanyia mzaha?" Nabii wa Mwenyezi Mungu akasema: "Audhu billahi (Najikinga kwa Mwenyezi Mungu) nisiwe miongoni mwa wajinga." Kwa maana, mjinga ni yule anayesema maneno yasiyokuwa na faida. Naye ndiye huwafanyia watu mzaha. Na ama mwenye akili timamu, yeye anaona kuwa moja ya makosa makubwa ya kidini na kiakili ni kumfanyia mzaha yule ambaye ni mwanadamu kama yeye. Na ikiwa ameboreshwa juu yake, basi kuboreshwa kwake huko kunamlazimu amshukuru Mola wake Mlezi, na awarehemu waja wake. Na Musa alipowaambia hayo, wakajua kwamba hilo ni kweli, hivyo wakasema:
#
{68} {ادع لنا ربك يبين لنا ما هي}؛ أي ما سنُّها {قال إنه يقول إنها بقرة لا فارض}؛ أي: كبيرة، {ولا بكر}؛ أي: صغيرة، {عوان بين ذلك فافعلوا ما تؤمرون}؛ واتركوا التشديد والتعنت.
(68) "Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni ng'ombe gani?" yani umri wake ni upi? "Akasema: Hakika Yeye anasema kwamba ng'ombe huyo si mpevu" yani mzee, "wala si kinda" yani mchanga, "bali ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyoamrishwa." na muache kujifanyia ugumu, na ukaidi.
#
{69} {قالوا ادع لنا ربك يبين لنا ما لونها قال إنه يقول إنها بقرة صفراء فاقع لونها}؛ أي: شديد، {تسر الناظرين}؛ من حسنها.
(69) "Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ipi rangi yake? Akasema: Yeye anasema, kuwa ng'ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imekoza huwapendeza wana mtazama." kwa sababu ya uzuri wake.
#
{70} {قالوا ادع لنا ربك يبين لنا ما هي إن البقر تشابه علينا}؛ فلم نهتد إلى ما تريد، {وإنا إن شاء الله لمهتدون}.
(70) "Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi? Hakika, tunaona ng'ombe wamefanana." hivyo, hatukuongoka kumpata yule unayemtaka, "Na kwa yakini, Inshaallah (Mwenyezi Mungu akipenda), tutaongoka."
#
{71} {قال إنه يقول إنها بقرة لا ذلول}؛ أي: مذللة بالعمل {تثير الأرض}؛ بالحراثة {ولا تسقي الحرث}؛ أي: ليست بسانية، {مسلمة}؛ من العيوب أو من العمل {لا شية فيها}؛ أي: لا لون فيها غير لونها الموصوف المتقدم، {قالوا الآن جئت بالحق}؛ أي: بالبيان الواضح، وهذا من جهلهم، وإلا فقد جاءهم بالحق أول مرة، فلو أنهم اعترضوا أيَّ بقرة لحصل المقصود، ولكنهم شددوا بكثرة الأسئلة؛ فشدد الله عليهم، ولو لم يقولوا إن شاء الله لم يهتدوا أيضاً إليها، {فذبحوها}؛ أي: البقرة التي وصفت بتلك الصفات، {وما كادوا يفعلون}؛ بسبب التعنت الذي جرى منهم.
(71) "Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni ng'ombe asiyetiwa kazini" yani aliyedunishwa kwa kazi "kulima ardhi wala kumwagia maji mimea, yu salama," hana kasoro zozote au ni salama kutokana na kulima "hana baka." Yani hakuna rangi ndani yake zaidi ya rangi iliyoelezwa hapo juu "Wakasema: Sasa umeleta (jambo la) haki." Yani ubainisho wa wazi. Na hili ni kutokana na ujinga wao. Vinginevyo, bila shaka alikwishawajia na haki mara ya kwanza. Lau kuwa walimleta ng'ombe yeyote, basi kile kilichokusudiwa kingetokea. Lakini walijifanyia ugumu kwa maswali mengi. Basi Mwenyezi Mungu akawafanyia ugumu. Na lau kuwa hawawakusema, "In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akipenda)", pia wasingeliongoka kwa hilo. "Basi wakamchinja" yani yule ng'ombe aliyeelezwa kwa sifa hizo. "Na walikaribia mno kuwa wasifanye hayo." Kwa sababu ya ukaidi uliotokea kutoka kwao.
#
{72 - 73} فلما ذبحوها قلنا لهم اضربوا القتيل ببعضها، أي: بعضو منها إما بعضو معين أو أي عضو منها فليس في تعيينه فائدة؛ فضربوه ببعضها؛ فأحياه الله، وأخرج ما كانوا يكتمون؛ فأخبر بقاتله، وكان في إحيائه - وهم يشاهدون - ما يدل على إحياء الله الموتى، لعلكم تعقلون؛ فتنزجرون عن ما يضركم.
(72-73) Walipomchinja tuliwaambia: Mpigeni huyo aliyeuawa kwa kipande chake, ima kwa kiungo maalumu au kiungo chake chochote, lakini hakuna faida yoyote katika kukiainisha. Basi wakampiga kwa kipande chake, na Mwenyezi Mungu akamfufua, na akatoa yale waliyokuwa wakiyaficha. Basi akatoa habari kuhusu yule aliyemuua. Na katika kufufuliwa kwake - hali ya kuwa wanatazama -, kulikuwa na dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu hufufua wafu, ili mpate kufahamu; hivyo mtakatazika kutokana na yenye kuwadhuru.
#
{74} {ثم قست قلوبكم}؛ أي: اشتدت وغلظت فلم تؤثر فيها الموعظة {من بعد ذلك}؛ أي: من بعد ما أنعم الله عليكم بالنعم العظيمة وأراكم الآيات، ولم يكن ينبغي أن تقسو قلوبكم لأن ما شاهدتم مما يوجب رقة القلب وانقياده، ثم وصف قسوتها بأنها {كالحجارة} التي هي أشد قسوة من الحديد، لأن الحديد؛ والرصاص إذا أذيب في النار ذاب بخلاف الأحجار، وقوله: {أو أشد قسوة}؛ أي: أنها لا تقصر عن قساوة الأحجار، وليست «أو» بمعنى بل. ثم ذكر فضيلة الأحجار على قلوبهم فقال: {وإن من الحجارة لما يتفجر منه الأنهار وإن منها لما يشقق فيخرج منه الماء وإن منها لما يهبط من خشية الله}، فبهذه الأمور فَضَلَتْ قلوبَكم. ثم توعدهم تعالى أشد الوعيد فقال: {وما الله بغافل عمَّا تعملون}، بل هو عالم بها حافظ لصغيرها وكبيرها، وسيجازيكم على ذلك أتم الجزاء وأوفاه. واعلم أن كثيراً من المفسرين رحمهم الله قد أكثروا في حشو تفاسيرهم من قصص بني إسرائيل، ونزَّلوا عليها الآيات القرآنية، وجعلوها تفسيراً لكتاب الله، محتجين بقوله - صلى الله عليه وسلم -: «حدثوا عن بني إسرائيل ولا حرج». والذي أرى أنه وإن جاز نقل أحاديثهم على وجه تكون مفردة غير مقرونة ولا منزلة على كتاب الله، فإنه لا يجوز جعلها تفسيراً لكتاب الله قطعاً إذا لم تصح عن رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، وذلك أن مرتبتها كما قال - صلى الله عليه وسلم -: «لا تصدقوا أهل الكتاب ولا تكذبوهم» ، فإذا كانت مرتبتها أن تكون مشكوكاً فيها، وكان من المعلوم بالضرورة من دين الإسلام أن القرآن يجب الإيمان به والقطع بألفاظه ومعانيه، فلا يجوز أن تجعل تلك القصص المنقولة بالروايات المجهولة التي يغلب على الظن كذبها، أو كذب أكثرها معاني لكتاب الله مقطوعاً بها، ولا يستريب بهذا أحد، ولكن بسبب الغفلة عن هذا حصل ما حصل، والله الموفق.
(74) "Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu" yani zikawa ngumu na sugu ambazo haziathiriwi na mawaidha "baada ya hayo" yani baada ya Mwenyezi Mungu kuwapa neema kubwa na akawaonyesha ishara. Na wala nyoyo zenu hazikufaa kuwa ngumu, kwa sababu mliyoyaona ni katika yale yanayolazimu upole wa nyoyo na kufuata kwake amri. Kisha akaueleza ugumu wake kuwa ni "kama mawe" ambayo huwa magumu zaidi kuliko chuma. Kwa sababu, chuma na risasi vikiyeyuka katika moto, vinayeyuka, kinyume na mawe. Na kauli yake "au ngumu zaidi" yani hazipunguki chini ya ugumu wa mawe. Na "au" hapa haimaanishi "bali" Kisha akataja ubora wa mawe juu ya nyoyo zao. Akasema "kwani kuna mawe yanayotimbuka mito, na kuna mengine yanayopasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya kumhofu Mwenyezi Mungu." Na kwa sababu ya mambo haya, mawe ni bora zaidi kuliko nyoyo zenu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawatishia kwa tishio kali kabisa, akasema "Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyafanya." Bali Yeye anayajua na anayahifadhi, madogo yake na makubwa yake, na atawalipa kwa hayo, malipo kamili na timilifu. Na jua ya kwamba wengi katika wafasiri - Mwenyezi Mungu awarehemu - wamezijaza kwa wingi tafsiri zao kwa visa vya Wana wa Israili, na wakaviteremshia Aya za Qur-ani, na wakavifanya kuwa tafsiri ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, huku wakiichukua kama hoja kauli yake (Mtume) rehema na amani ziwe juu yake. "Simulieni kutoka kwa Wana wa Israili, wala hakuna ubaya." Na ninachokiona mimi ni kuwa, hata ikiruhusika kuzisimulia hadithi zao kwa namna ambayo zinakuwa pekee yake bila ya kuziunganisha wala kuziteremsha juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi hairuhusiki kabisa kuzifanya kuwa tafsiri ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu; ikiwa hazikupokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake. Na hilo ni kwa sababu daraja yake ni kama alivyosema (Mtume) rehema na amani ziwe juu yake. "Msiwasadiki watu wa Kitabu wala msiwakadhibishe.” Hivyo basi, ikiwa daraja yake ni kwamba zina shaka ndani yake, na jambo linalojulikana kwa lazima katika dini ya Uislamu ni kwamba ni lazima kuiamini Qur-ani. Na kuwa na uhakika na maneno na maana zake, basi hairuhusiki kuzifanya hadithi hizo - zinazosimuliwa kwa riwaya zisizojulikana (ambazo zinadhaniwa sana kwamba ni za uongo), au zenye uongo katika nyingi zake - kuwa maana ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa hakika. Na wala hakuna yeyote mwenye shaka juu ya hili. Lakini kwa sababu ya kughafilika katika haya, yaliyotokea yalitokea, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwezesha.
: 75 - 78 #
{أَفَتَطْمَعُونَ أَنْ يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِنْ بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ (75) وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُمْ بِمَا فَتَحَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُمْ بِهِ عِنْدَ رَبِّكُمْ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (76) أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ (77) وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ (78)}.
(75) Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wanayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua? (76) Na wanapokutana na wale walioamini, husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyokufunulieni Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojieni mbele ya Mola wenu Mlezi? Basi hamfahamu nyinyi? (77) Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza? (78) Na wamo miongoni mwao wasiojua kusoma; hawakijui Kitabu isipokuwa uongo wanaoutamani, nao hawana ila ni kudhania tu.
#
{75} هذا قطع لأطماع المؤمنين من إيمان أهل الكتاب؛ أي فلا تطمعوا في إيمانهم، وأخلاقهم لا تقتضي الطمع فيهم؛ فإنهم كانوا يحرفون كلام الله من بعد ما عقلوه وعلموه، فيضعون له معانيَ ما أرادها الله؛ ليوهموا الناس أنها من عند الله، وما هي من عند الله، فإذا كانت حالهم في كتابهم الذي يرونه شرفهم ودينهم يصدون به الناس عن سبيل الله، فكيف يرجى منهم إيمان لكم؟! فهذا من أبعد الأشياء.
(75) Huku ni kukata matumaini ya Waumini katika kuamini kwa Watu wa Kitabu. Yani msitumai kuwa wataamini, hali ya kuwa maadili yao hayaambatani na kuwa na matumaini juu yao. Kwa maana, walikuwa wakiyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu baada ya kuyafahamu na kuyajua. Wakawa wanayawekea maana ambazo Mwenyezi Mungu hakuzitaka, ili wawafanye watu kufikiria kwamba yametoka kwa Mwenyezi Mungu, na wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi ikiwa hali yao katika Kitabu chao ambacho wanakiona kuwa ndiyo heshima yao na dini yao, wanachozuia kwacho watu njia ya Mwenyezi Mungu, basi inawezekanaje kutarajiwa kutoka kwao kwamba watawaamini nyinyi? Basi hiki ni katika vitu vya mbali zaidi.
#
{76} ثم ذكر حال منافقي أهل الكتاب، فقال: {وإذا لقوا الذين آمنوا قالوا آمنا}، فأظهروا لهم الإيمان قولاً بألسنتهم ما ليس في قلوبهم، {وإذا خلا بعضهم إلى بعض}؛ فلم يكن عندهم أحد من غير أهل دينهم قال بعضهم لبعض: {أتحدثونهم بما فتح الله عليكم}؛ أي: أتظهرون لهم الإيمان وتخبرونهم أنكم مثلهم؟ فيكون ذلك حجة لهم عليكم، يقولون إنهم قد أقروا بأن ما نحن عليه حق وما هم عليه باطل، فيحتجون عليكم بذلك عند ربكم {أفلا تعقلون}؛ أي: أفلا يكون لكم عقل فتتركون ما هو حجة عليكم؟
(76) Kisha akataja hali ya wanafiki katika Watu wa Kitabu, akasema "Na wanapokutana na wale walioamini, husema: Tumeamini." Basi wakawadhihirishia imani kwa kusema kwa ndimi zao yasiyokuwa katika nyoyo zao. "Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao" bila ya kuwepo pamoja nao yeyote asiyekuwa wa dini yao, wanaambiana wao kwa wao, "Mnawaambia (mambo) aliyokufunulieni Mwenyezi Mungu." Yani mnawadhihirishia imani na kuwaambia kuwa nyinyi ni kama wao? Basi hilo likawa ni hoja yao juu yenu, wakisema kuwa: Hakika wao (Watu wa Kitabu) wamekiri kwamba tuliyo juu yake ni ya haki, na waliyo juu yake ni ya uongo. Basi wakawahoji kwa hilo kwa Mola wenu Mlezi. "Basi hamfahamu nyinyi?" Yani hamna akili, mkaacha lile ambalo ni hoja juu yenu?
#
{77} هذا يقوله بعضهم لبعض: {أو لا يعلمون أن الله يعلم ما يسرون وما يعلنون}، فهم وإن أسروا ما يعتقدونه فيما بينهم، وزعموا أنهم بإسرارهم لا يتطرق عليهم حجة للمؤمنين؛ فإن هذا غلط منهم وجهل كبير؛ فإن الله يعلم سرهم وعلنهم؛ فيظهر لعباده ما هم عليه.
(77) Haya ndiyo wanayoambiana wao kwa wao "Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?" Na wao hata ikiwa wataficha wanayoamini kati yao, na wakadai kuwa kwa kuficha kwao, hoja ya Waumini haisimami juu yao. Hili kwa hakika ni kosa kwa upande wao na ni ujinga mkubwa. Kwani, Mwenyezi Mungu anaijua siri yao na dhahiri yao; na atawadhihirishia waja wake jinsi walivyo.
#
{78} {ومنهم}؛ أي: من أهل الكتاب {أميون}؛ أي: عوام، وليسوا من أهل العلم {لا يعلمون الكتاب إلا أماني}؛ أي: ليس لهم حظ من كتاب الله إلا التلاوة فقط، وليس عندهم خبر بما عند الأولين الذين يعلمون حق المعرفة حالهم، وهؤلاء إنما معهم ظنون وتقاليد لأهل العلم منهم. فذكر في هذه الآيات علماءهم وعوامهم ومنافقيهم ومن لم ينافق منهم، فالعلماء منهم متمسكون بما هم عليه من الضلال، والعوام مقلدون لهم، لا بصيرة عندهم؛ فلا مطمع لكم في الطائفتين.
(78) "Na wamo miongoni mwao" yani miongoni hawa watu wa Kitabu "wasiojua kusoma" yani watu wa kawaida wasiokuwa miongoni mwa wenye elimu. "Hawakijui Kitabu isipokuwa uongo wanaoutamani," yani wao hawana fungu katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu isipokuwa kusoma tu. Na hawana habari kwa yale waliyokuwa nayo watu wa mwanzo ambao wanazijua hali zao haki ya kuzijua. Na hawa (watu) wana dhana tu, na mila za watu wa elimu miongoni mwao. Basi akawataja katika hizi Aya wanachuoni wao, watu wao wa kawaida, wanafiki wao, na wale ambao sio wanafiki miongoni mwao. Basi, wanachuoni miongoni mwao, wao wanashikamana na upotovu walio nao. Nao watu wa kawaida, wanawaiga wao, na hawana ufahamu. Hivyo basi, nyinyi hamna matumaini yoyote katika makundi haya mawili.
: 79 #
{فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَذَا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَوَيْلٌ لَهُمْ مِمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَهُمْ مِمَّا يَكْسِبُونَ (79)}.
(79) Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wanunue kwacho thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma.
#
{79} توعد تعالى المحرفين للكتاب الذين يقولون لتحريفهم وما يكتبون {هذا من عند الله}، وهذا فيه إظهار الباطل وكتم الحق، وإنما فعلوا ذلك مع علمهم، {ليشتروا به ثمناً قليلاً}، والدنيا كلها من أولها إلى آخرها ثمن قليل، فجعلوا باطلهم شَرَكاً يصطادون به ما في أيدي الناس. فظلموهم من وجهين: من جهة تلبيس دينهم عليهم، ومن جهة أخذ أموالهم بغير حق بل بأبطل الباطل، [وذلك] أعظم ممن يأخذها غصباً وسرقة ونحوهما، ولهذا توعدهم بهذين الأمرين، فقال: {فويل لهم مما كتبت أيديهم}؛ أي من التحريف والباطل {وويل لهم مما يكسبون}؛ من الأموال، والويل شدة العذاب والحسرة، وفي ضمنها الوعيد الشديد. قال شيخ الإسلام لما ذكر هذه الآيات من قوله: أفتطمعون إلى يكسبون: «فإن الله ذم الذين يحرفون الكلم عن مواضعه، وهو متناول لمن حمل الكتاب والسنة على ما أصَّلَه من البدع الباطلة، وذم الذين لا يعلمون الكتاب إلا أماني وهو متناول لمن ترك تدبر القرآن ولم يعلم إلا مجرد تلاوة حروفه، ومتناول لمن كتب كتاباً بيده مخالفاً لكتاب الله لينال به دنيا وقال: إنه من عند الله، مثل أن يقول: هذا هو الشرع والدين، وهذا معنى الكتاب والسنة، وهذا [معقول] السلف والأئمة، وهذا هو أصول الدين الذي يجب اعتقاده على الأعيان أو الكفاية، ومتناول لمن كتم ما عنده من الكتاب والسنة، لئلا يَحْتَجَّ به مخالفه في الحق الذي يقوله، وهذه الأمور كثيرة جداً في أهل الأهواء جملة، كالرافضة [والجهمية ونحوهم من أهل الأهواء والكلام، وفي أهل الأهواء] وتفصيلاً مثل كثير من المنتسبين إلى الفقهاء ... » انتهى.
(79) Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi adhabu wale wanaopotosha Kitabu, ambao wanasema kuhusu kuwapotosha kwao na uongo wao. "Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu," na hili ndani yake lina kudhihirisha uongo na kuficha haki. Na walifanya hivyo pamoja na kujua kwao "ili wanunue kwacho thamani ndogo." Na dunia nzima tangu mwanzo wake hadi mwisho wake ni thamani ndogo. Hivyo basi, wakaufanya uongo wao kuwa mtego ambao kwa (mtego) huo, wanawinda vilivyo mikononi mwa watu. Basi wakawadhulumu (watu) kwa namna mbili: kwa upande wa kuwachanganyia dini yao, na kwa upande wa kuwachukulia mali zao bila ya haki, bali kwa batili ya batili zote. Na [hilo] ni kubwa zaidi kuliko mwenye kuzichukua kwa nguvu, wizi na mfano wake. Kwa sababu ya hayo, (Mwenyezi Mungu) aliwaahidi adhabu kwa mambo haya mawili akasema, "Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao." Yani kwa sababu ya kukibadilisha na (kwa sababu ya) uongo. "Na ole wao kwa yale wanayoyachuma." katika mali. Na "wayl" ni adhabu kali na majuto, ambayo miongoni mwake ni ahadi ya adhabu kubwa. Alisema Sheikhul-Islaam alipozitaja Aya hizi kuanzia kauli yake "Je, mnatumai?" hadi (kauli yake) "wanayoyachuma": Hakika Mwenyezi Mungu amewakashifu wale wanaobadilisha maneno (ya Mwenyezi Mungu) kutoka mahali pake. Na hilo anaingia ndani yake yule anayebebesha Kitabu na Sunnah yale aliyoanzisha miongoni mwa uzushi na batili. Na akamkashifu yule asiyejua Kitabu isipokuwa uongo anaoutamani. Na hilo anaingia ndani yake yule aliyeacha kuizingatia Qur-ani, na hakuijua isipokuwa kuzisoma herufi zake tu. Na anaingia ndani yake mwenye kuandika kitabu kwa mkono wake, kinachohalifu Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili apate kwacho dunia. Na akasema: Hakika, hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, kama vile aseme: Hii ndiyo Sheria na Dini. Na hii ndiyo maana ya Kitabu na Sunnah. Na huku ndiko kufahamu kwa watangulizi wema na maimamu. Na hii ndiyo misingi ya Dini ambayo ni lazima iaminiwe na kila kibinafsi na kijumla. Na anaingia ndani yake mwenye kuficha alichonacho katika Kitabu na Sunnah, ili asije mwenye kumpinga kuichukua kuwa hoja dhidi yake katika haki ambayo anaisema. Na mambo haya ni mengi sana katika watu wa matamanio kijumla, kama vile Ar-rafidhwa [na Al-Jahmiyya na mfano wao miongoni mwa watu wa matamanio na Kalaam (yani wanaotegemea akili zao katika kuthibitisha imani), na katika watu wa matamanio] kila mmoja wao kivyake, kama vile wengi wa wanaojinasibisha na mafaqihi (wanachuoni) ... » mwisho.
: 80 - 82 #
{وَقَالُوا لَنْ تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَعْدُودَةً قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِنْدَ اللَّهِ عَهْدًا فَلَنْ يُخْلِفَ اللَّهُ عَهْدَهُ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ (80) بَلَى مَنْ كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (81) وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (82)}.
(80) Na walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema: Mmechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu? Kweli Mwenyezi Mungu hatokwenda kinyume na ahadi yake. Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua? (81) Ndiyo, anayechuma ubaya - na makosa yake yakamzunguka, hao ndio wenzi wa Moto; humo watadumu. (82) Na wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio wenzi wa Pepo, humo watadumu.
#
{80} ذكر أفعالهم القبيحة، ثم ذكر ـ مع هذا ـ أنهم يزكون أنفسهم، ويشهدون لها بالنجاة من عذاب الله والفوز بثوابه، وأنهم لن تمسهم النار إلا أياماً معدودة؛ أي قليلة تعد بالأصابع، فجمعوا بين الإساءة والأمن، ولما كان هذا مجرد دعوى رد تعالى عليهم؛ فقال: {قل}؛ لهم يا أيها الرسول، {أتخذتم عند الله عهداً}؛ أي: بالإيمان به وبرسله وبطاعته، فهذا الوعد الموجب لنجاة صاحبه الذي لا يتغير ولا يتبدل {أم تقولون على الله مالا تعلمون}؛ فأخبر تعالى أن صدق دعواهم متوقفة على أحد هذين الأمرين اللذين لا ثالث لهما. إما أن يكونوا قد اتخذوا عند الله عهداً؛ فتكون دعواهم صحيحة. وإما أن يكونوا متقولين عليه؛ فتكون كاذبة فيكون أبلغ لخزيهم وعذابهم، وقد عُلِم من حالهم أنهم لم يتخذوا عند الله عهداً لتكذيبهم كثيراً من الأنبياء حتى وصلت بهم الحال إلى أن قتلوا طائفة منهم، ولنكولهم عن طاعة الله ونقضهم المواثيق، فتعين بذلك أنهم متقولون مختلقون قائلون عليه ما لا يعلمون، والقول عليه بلا علم من أعظم المحرمات وأشنع القبيحات.
(80) Alitaja matendo yao maovu, kisha akataja - pamoja na hayo - kwamba wao wanazitakasa nafsi zao, na kwamba wanajishuhudia kwamba wataepukana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na watapata malipo yake mazuri. Na kwamba hawataguswa na Moto ila siku chache zinazohesabika kwa vidole. Kwa hivyo, wakawa wamekusanya kati ya kuasi na amani. Na pindi yalipokuwa haya ni madai tu, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwajibu, akasema "Sema" uwaambie ewe Mtume "Je, mmechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu?” Yani kwa kumuamini Yeye na Mitume wake na kumtii. Na hii ndiyo ahadi yenye kumwokoa mtu wake (mwenye kuchukua ahadi), ambayo haibadiliki wala haigeuki. "Au mnasema juu ya Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua?" Basi (Mwenyezi Mungu) Mtukufu akatoa habari kwamba ukweli wa madai yao unategemea moja ya mambo haya mawili, ambayo hayana la tatu. Ima wawe walichukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu; kwa hivyo madai yao yakawa ni sahihi. Na ima wawe wanamsingizia; basi yakawa ya uongo, kwa hivyo ikawa inafaa zaidi kuwapa hizaya na kuwaadhibu. Na imekwisha julikana katika hali yao kwamba, hawakuchukua ahadi na Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kukadhibisha kwao wengi wa Manabii, mpaka hali ikawafikia kiwango kwamba waliua kundi miongoni mwao, na kwa kukataa kwao kumtii Mwenyezi Mungu na kuvunja kwao maagano. Basi ikawa wazi kwa hilo kwamba wanamsingizia na kumzulia tu yale wasiyoyajua? Na kumzungumizia (Mwenyezi Mungu) bila ya elimu ni katika haramu kubwa mno na mambo mabaya ya kuchukiza zaidi.
Kisha (Mwenyezi Mungu) Mtukufu akataja hukumu ya jumla kwa kila mtu, wanaingia humo Wana wa Israili na wasiokuwa wao. Nayo ni hukumu ambayo hakuna hukumu ngingine isiyokuwa hiyo, na sio uongo wanaoutamani na madai yao kuhusu walioangamia, na waliofaulu. Hivyo basi akasema "Ndiyo" yani hili jambo sio kama mlivyotaja. Kwani ni kauli tu isiyokuwa na uhakika wowote. Lakini:
#
{81} {من كسب سيئة}؛ وهو نكرة في سياق الشرط؛ فيعم الشرك فما دونه، والمراد به الشرك، هنا بدليل قوله: {وأحاطت به خطيئته}؛ أي: أحاطت بعاملها فلم تدع له منفذاً، وهذا لا يكون إلا الشرك، فإن من معه الإيمان لا تحيط به خطيئته، {فأولئك أصحاب النار هم فيها خالدون}؛ وقد احتج بها الخوارج على كفر صاحب المعصية، وهي حجة عليهم كما ترى، فإنها ظاهرة في الشرك، وهكذا كل مُبْطِل يحتَجُّ بآية أو حديث صحيح على قوله الباطل؛ فلا بد أن يكون فيما احتج به حجة عليه.
(81) "anaye chuma ubaya" Nalo hili neno ni nakira (yani halimaanishi kosa maalum) katika muktadha wa sharti, kwa hivyo linajumuisha shirki na kilicho chini yake, na hapa limekusudiwa shirki kwa dalili ya kauli yake "- na makosa yake yakamzunguka" yani yakamzunguka mwenye kuyatenda, na hayakumwachia njia ya kutokea. Na hili haliwi isipokuwa shirki tu. Kwa maana, yule ambaye ana imani, makosa yake hayamzunguki." Na Al-khawarij waliitumia aya hii kama hoja kwamba mwenye kutenda dhambi ni kafiri. Lakini hiyo ni hoja juu yao kama unavyoona, kwa sababu, inadhihirika waziwazi katika shirki tu. Na vivyo hivyo, mwenye batili anayetumia aya fulani au hadithi sahihi kama hoja yake katika kusema batili (uongo); ni lazima kuna hoja juu yake katika hicho alichotumia kama hoja yake.
#
{82} {والذين آمنوا}؛ بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر {وعملوا الصالحات}؛ ولا تكون الأعمال صالحة إلا بشرطين: أن تكون خالصة لوجه الله، متبعاً بها سنة رسوله. فحاصل هاتين الآيتين أن أهل النجاة والفوز أهل الإيمان والعمل الصالح، والهالكون أهل النار المشركون بالله الكافرون به.
(82) "Na wale walioamini" Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho "na wakatenda mema", na matendo hayawi mema isipokuwa kwa masharti mawili: Yawe kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu tu, na yenye kufuatwa kwayo Sunnah za Mtume Wake. Hivyo basi, jumla ya Aya hizi mbili ni kwamba wale watakaookoka na kufaulu ni watu wa imani na matendo mema. Nao walioangamia, ni watu wa Motoni wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaomkufuru.
: 83 #
{وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِنْكُمْ وَأَنْتُمْ مُعْرِضُونَ (83)}.
(83) Na tulipofunga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na semeni na watu kwa wema, na shikeni Swala, na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipokuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza (1).
#
{83} فهذه الشرائع من أصول الدين التي أمر الله بها في كل شريعة لاشتمالها على المصالح العامة في كل زمان ومكان؛ فلا يدخلها نسخ، كأصل الدين، ولهذا أمرنا الله بها في قوله: {واعبدوا الله ولا تشركوا به شيئاً}؛ إلى آخر الآية. فقوله: {وإذ أخذنا ميثاق بني إسرائيل}؛ هذا من قسوتهم أن كل أمر أمروا به استعصوا، فلا يقبلونه إلا بالأيمان الغليظة والعهود الموَثَّقة {لا تعبدون إلا الله}؛ هذا أمر بعبادة الله وحده ونهي عن الشرك به، وهذا أصل الدين فلا تقبل الأعمال كلها إن لم يكن هذا أساسها، فهذا حق الله تعالى على عباده، ثم قال: {وبالوالدين إحساناً}؛ أي أحسنوا بالوالدين إحساناً، وهذا يعم كل إحسان قولي وفعلي مما هو إحسان إليهم، وفيه النهي عن الإساءة إلى الوالدين أو عدم الإحسان والإساءة؛ لأن الواجب الإحسان، والأمر بالشيء نهي عن ضده، وللإحسان ضدان: الإساءة وهي أعظم جرماً، وترك الإحسان بدون إساءة وهذا محرم لكن لا يجب أن يلحق بالأول. وكذا يقال في صلة الأقارب واليتامى والمساكين، وتفاصيل الإحسان لا تنحصر بالعد بل تكون بالحد كما تقدم. ثم أمر بالإحسان إلى الناس عموماً فقال: {وقولوا للناس حسناً}؛ ومن القول الحسن أمرهم بالمعروف ونهيهم عن المنكر وتعليمهم العلم وبذل السلام والبشاشة وغير ذلك من كل كلام طيب، ولما كان الإنسان لا يسع الناس بماله أُمر بأمر يقدر به على الإحسان إلى كل مخلوق وهو الإحسان بالقول، فيكون في ضمن ذلك النهي عن الكلام القبيح للناس حتى للكفار، ولهذا قال تعالى: {ولا تجادلوا أهل الكتاب إلا بالتي هي أحسن}؛ ومن أدب الإنسان الذي أدب الله به عباده أن يكون الإنسان نزيهاً في أقواله وأفعاله، غير فاحش ولا بذيء ولا شاتم ولا مخاصم، بل يكون حسن الخلق واسع الحلم، مجاملاً لكلِّ أحد، صبوراً على ما يناله من أذى الخلق امتثالاً لأمر الله ورجاءً لثوابه. ثم أمرهم بإقامة الصلاة وإيتاء الزكاة لما تقدم أن الصلاة متضمنة للإخلاص للمعبود، والزكاة متضمنة للإحسان إلى العبيد، ثم بعد هذا الأمر لكم بهذه الأوامر الحسنة التي إذا نظر إليها البصير العاقل، عرف أن من إحسان الله على عباده أن أمرهم بها وتفضل بها، عليهم وأخذ المواثيق عليكم {توليتم}؛ على وجه الإعراض؛ لأن المتولي قد يتولى وله نية رجوع إلى ما تولى عنه، وهؤلاء ليس لهم رغبة ولا رجوع في هذه الأوامر، فنعوذ بالله من الخذلان. وقوله: {إلا قليلاً منكم}؛ هذا استثناء؛ لئلا يوهم أنهم تولوا كلهم، فأخبر أن قليلاً منهم عصمهم الله وثبتهم.
(83) Sheria hizi ni miongoni mwa misingi ya dini ambayo Mwenyezi Mungu aliiamrisha katika kila sheria kwa sababu zinajumuisha masilahi ya jumla katika kila zama na mahali. Basi hayaingiwi na ufutaji wowote kama asili ya dini. Ndio maana, Mwenyezi Mungu alituamrisha kwayo katika kauli yake "Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote," hadi mwisho wa aya. Basi kauli yake "Na tulipofunga agano na Wana wa Israili" haya ni kutokana na ugumu wao, na kwamba kila amri waliyoamrishwa waliiasi, na wala hawaikubali ila kwa viapo vikali na ahadi zilizofungwa imara. "Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu." Hii ni amri ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kukataza kumshirikisha. Na huu ndio msingi wa dini, kwa hivyo matendo yote hayakubaliki ikiwa huu sio msingi wake, kwani hii ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake. Kisha akasema, "na muwafanyie wema wazazi" yani wafanyieni wazazi wema kikamilifu. Na hili linajumuisha kila wema wa kimaneno na kimatendo ambao ni wema kwao. Na ndani yake kuna makatazo ya kuwafanyia wazazi ubaya, au kutowafanyia wema na kuwafanyia ubaya. Kwa sababu lililo la wajibu ni kufanya wema. Na kuamrisha kitu ni kukataza kinyume chake. Nao wema una vinyume viwili: kufanya ubaya, nalo ni kosa kubwa zaidi. Na kuacha kuwafanyia wema bila ya kuwafanyia ubaya. Na hili ni haramu, lakini sio lazima kutoshana na (ile aina) ya kwanza. Na vile vile inasemwa kuhusiana na kuwaunga jamaa, na mayatima, na masikini. Na maelezo ya ndani ya wema hayakomei kwa kuhesabu, bali kwa kuyafafanua kama ilivyotangulia hapo awali. Kisha akaamrisha kuwafanyia wema watu wote, akasema: "Na semeni na watu kwa wema" Na miongoni mwa maneno mema ni kuwaamrisha kufanya mema na kuwakataza maovu, na kuwafunza elimu, kuwapa salamu, na bashasha na yasiyokuwa hayo katika kila maneno mazuri. Na kwa kuwa mtu hawezi kumudu kuwapa watu wote mali zake, aliamrishwa kitu ambacho anaweza kwacho kuwafanyia wema kila kiumbe ambacho ni kusema (maneno) mema . Basi inakuwa ndani ya hayo katazo la kuwaambia watu maneno mabaya, hata makafiri. Na kwa sababu hii (Mwenyezi Mungu) Mtukufu alisema: "Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa." Na miongoni mwa adabu za mtu ambazo Mwenyezi Mungu amewafunza waja wake ni kwamba mtu awe safi katika maneno yake na matendo yake. Asifanye yasiyofaa, wala machafu, wala mwenye matusi, wala mgomvi. Bali awe na tabia njema, mwingi wa upole, anayeamiliana na watu wote kwa urahisi, mvumilivu kwa yale yanayompata miongoni mwa maudhi ya viumbe, kwa ajili ya kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kutarajia malipo yake mazuri. Kisha akawaamrisha kusimamisha swala na kutoa zaka kama ilivyotangulia ya kwamba swala inajumuisha kumpwekesha anayeabudiwa, nayo zaka inajumuisha kuwafanyia wema waja. Kisha baada ya amri hii kwenu kwa haya maamrisho mazuri - ambayo ikiwa mwenye busara na akili atayatazama, ataajua kwamba katika ihsani ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake ni kwamba, aliwaamrisha hayo (swala na zaka) na akawapa kama neema juu yao, na akachukua ahadi juu yenu -"mkageuka" kwa kuyapa mgongo. Kwa sababu mwenye kugeuka, huenda akageuka huku ana nia ya kurejea katika yale aliyoyageuka. Lakini hawa, hawana hamu wala kurejea katika maamrisho haya. Basi tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kutosaidiwa na Mwenyezi Mungu. Na kauli yake "isipokuwa wachache tu katika nyinyi" huku ni kuondoa baadhi; ili isifikiriwe kwamba wote waligeuka. Basi akatoa habari kwamba, wachache miongoni mwao walilindwa na Mwenyezi Mungu na akawaimarisha.
: 84 - 86 #
{وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنْفُسَكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنْتُمْ تَشْهَدُونَ (84) ثُمَّ أَنْتُمْ هَؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنْفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِنْكُمْ مِنْ دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِمْ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِنْ يَأْتُوكُمْ أُسَارَى تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ فَمَا جَزَاءُ مَنْ يَفْعَلُ ذَلِكَ مِنْكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَى أَشَدِّ الْعَذَابِ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ (85) أُولَئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنْصَرُونَ (86)}.
(84) Na tulipochukua agano lenu kuwa hamtamwaga damu zenu, wala hamtatoana majumbani mwenu; nanyi mkakubali, nanyi mnashuhudia. (85) Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani mwao, mkisaidiana (na adui zao) dhidi yao kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka, mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi ni yapi malipo ya mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila aibu katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda. (86) Hao ndio walionunua uhai wa dunia kwa (uhai wa) Akhera. Kwa hivyo, hawatapunguziwa adhabu, wala hawatanusuriwa.
#
{84 - 85} وهذا الفعل المذكور في هذه الآية فعل للذين كانوا في زمن الوحي بالمدينة، وذلك أن الأوس والخزرج - وهم الأنصار - كانوا قبل مبعث النبي - صلى الله عليه وسلم - مشركين، وكانوا يقتتلون على عادة الجاهلية، فنزلت عليهم الفرق الثلاث من فرق اليهود: بنو قريظة، وبنو النضير، وبنو قينقاع، فكل فرقة منهم حالفت فرقة من أهل المدينة، فكانوا إذا اقتتلوا أعان اليهودي حليفه على مقاتليه الذين يُعِينونهم الفرقة الأخرى من اليهود، فيقتل اليهوديُ اليهوديَ، ويخرجه من دياره إذا حصل جلاء ونهب، ثم إذا وضعت الحرب أوزارها، وكان قد حصل أسارى بين الطائفتين فدى بعضهم بعضاً، والأمور الثلاثة كلها قد فرضت عليهم: ففرض عليهم أن لا يسفك بعضهم دم بعض، ولا يخرج بعضهم بعضاً، وإذا وجدوا أسيراً منهم وجب عليهم فداؤه، فعملوا بالأخير وتركوا الأولين، فأنكر الله عليهم ذلك فقال: {أفتؤمنون ببعض الكتاب}؛ وهو فداء الأسير {وتكفرون ببعض}؛ وهو القتل والإخراج، وفيها دليل على أن الإيمان يقتضي فعل الأوامر واجتناب النواهي، وأن المأمورات من الإيمان. قال تعالى: {فما جزاء من يفعل ذلك منكم إلا خزي في الحياة الدنيا}؛ وقد وقع ذلك فأخزاهم الله، وسلط رسوله عليهم فقتل من قتل، وسبى من سبى منهم، وأجلى من أجلى، {ويوم القيامة يردون إلى أشد العذاب}؛ أي: أعظمه، {وما الله بغافل عما تعملون}؛ ثم أخبر تعالى عن السبب الذي أوجب لهم الكفر ببعض الكتاب والإيمان ببعضه، فقال:
(84-85) Na kitendo hiki kilichotajwa katika Aya hii ni kitendo cha wale waliokuwa katika wakati wa kuteremka kwa wahyi (ufunuo) huko Madina. Na hilo ni kwa sababu Aws na Khazraj - ambao ni Ansari - walikuwa washirikina kabla ya kitumilizwa kwa Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - na walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe kwa desturi ya Jahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu). Kwa hivyo, walishukiwa na makundi matatu ya Kiyahudi: Banu Quraydha, na Banu Nadhir, na Banu Qaynuqa'. Kwa hivyo, kila mojawapo ya makundi hayo likainigia katika mkataba na watu wa Madina. Basi wakawa wanapopigana vita, Mayahudi wanamsaidia yule waliyeingia naye katika mkataba dhidi ya wale wanaopigana nao, ambao wanasaidiwa na yale makundi mengine ya Mayahudi. Hivyo basi, Myahudi akawa anamuua Myahudi mwenzake, na anamtoa katika makazi yake kunapokuwa na kutolewa na uporaji. Kisha vita vinapopoa, na ikawa kulikuwa na mateka kati ya pande mbili, wanakomboana wenyewe kwa wenyewe. Na mambo hayo matatu yote walikuwa wamefaradhishiwa. Walifaradhishiwa kwamba wasimwage damu zao wenyewe kwa wenyewe, wala wasitoane wenyewe kwa wenyewe, na wakimkuta mateka miongoni mwao, lazima wamkomboe. Basi wakalifanyia kazi hilo la mwisho, na wakayaacha yale mawili ya kwanza. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakosoa katika hilo. "Je, mnaamini baadhi ya Kitabu" nalo ni kumfidia mateka "na mnakataa baadhi yake?" nalo ni kuua na kutoa nje. Na ndani yake kuna dalili ya kwamba imani inahitaji kufanya maamrisho na kuacha makatazo. Na kwamba maamrisho ni katika imani. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Basi ni nini malipo ya mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila aibu katika maisha ya duniani" Na hilo lilikwishafanyika, na Mwenyezi Mungu akawafedhehesha, na akampa nguvu Mtume wake dhidi yao, hivyo, (Mtume) akawauwa aliouwaua. Na akawateka aliowateka miongoni mwao, na akawafukuzilia mbali wale aliofukuzilia mbali. "Na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda." Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza sababu iliyowalazimu kukufuru baadhi ya Kitabu na kuamini baadhi yake, akasema:
#
{86} {أولئك الذين اشتروا الحياة الدنيا بالآخرة}؛ توهموا أنهم إن لم يعينوا حلفاءهم حصل لهم عار فاختاروا النار على العار، فلهذا قال: {فلا يخفف عنهم العذاب}؛ بل هو باقٍ على شدته، ولا يحصل لهم راحة بوقت من الأوقات {ولا هم ينصرون}؛ أي: يدفع عنهم مكروه.
(86) "Hao ndio walionunua uhai wa dunia kwa (uhai wa) Akhera" Walidhani kuwa wasipowasaidia washirika wao, basi watapatwa na aibu, basi wakachagua moto kuliko aibu. Ndio maana alisema, "kwa hivyo hawatapunguziwa adhabu" bali utabakia na ukali wake, na hawatapata kupumzika wakati wowote ule "wala hawatanusuriwa" kwa kuwaondoshea hayo machukizo.
: 87 #
{وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِنْ بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَى أَنْفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ (87)}.
(87) Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume wengine. Na tukampa Isa, mwana wa Mariamu hoja waziwazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Basi kila walipokufikieni Mitume kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna; wengine mkawakanusha, na wengine mkawauwa.
#
{87} يمتنُّ تعالى على بني إسرائيل أن أرسل إليهم كليمه موسى وآتاه التوراة، ثم تابع من بعده بالرسل الذين يحكمون بالتوراة، إلى أن ختم أنبياءهم بعيسى [بن مريم] عليه السلام وآتاه من الآيات البينات ما يؤمن على مثله البشر {وأيدناه بروح القدس}؛ أي: قواه الله بروح القدس، قال أكثر المفسرين إنه جبريل عليه السلام، وقيل إنه الإيمان الذي يؤيد الله به عباده، ثم مع هذه النعم التي لا يُقدَر قدرُها لمَّا أتوكم {بما لا تهوى أنفسكم استكبرتم}؛ عن الإيمان بهم، {ففريقاً}؛ منهم، {كذبتم وفريقاً تقتلون}؛ فقدمتم الهوى على الهدى وآثرتم الدنيا على الآخرة، وفيها من التوبيخ والتشديد ما لا يخفى.
(87) Mwenyezi Mungu Mtukufu anasimulia hisani yake juu ya Wana wa Israili kwamba aliwatumia Musa ambaye alizungumza naye (moja kwa moja), na akampa Taurati. Kisha akafuatisha baada yake Mitume wanaohukumu kwa Taurati, mpaka alipowahitimisha Manabii wao kwa Isa [Ibn Maryam] amani iwe juu yake. Na akampa katika ishara zilizo wazi wanazoamini wanadamu mfano wake. "Na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu." Wafasiri wengi walisema kuwa yeye ni Jibril, amani iwe juu yake, na ikasemwa kuwa ni imani ambayo Mwenyezi Mungu anawaunga nayo mkono waja wake. Kisha pamoja na hizi neema ambazo thamani yake haikadiriki walipowajia "kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna" mkaacha kuwaamini, "hivyo basi, kundi" miongoni mwao "mkawakanusha, na kundi lingine mkawauwa." Basi mkatanguliza matamanio yenu juu ya uongofu, na mkaipendelea dunia juu ya Akhera. Na ndani yake kuna makemeo na kuwafanyia ukali kwa namna isiyofichika.
: 88 #
{وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ بَلْ لَعَنَهُمُ اللَّهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَا يُؤْمِنُونَ (88)}.
(88) Na walisema: Nyoyo zetu zimefunikwa. Bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao; kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini.
#
{88} أي: اعتذروا عن الإيمان لما دعوتهم إليه يا أيها الرسول بأن قلوبهم غلف أي عليها غلاف وأغطية فلا تفقه ما تقول، يعني فيكون لهم ـ بزعمهم ـ عذر لعدم العلم، وهذا كذب منهم، فلهذا قال تعالى: {بل لعنهم الله بكفرهم}؛ أي: أنهم مطرودون ملعونون بسبب كفرهم؛ فقليلاً المؤمن منهم، أو قليلاً إيمانهم، وكفرهم هو الكثير.
(88) Yani walitoa udhuru wa kutoamini kile unachowalingania ewe Mtume, kwamba nyoyo zao zimefunikwa, yani zina vifuniko na vizibo, hivyo basi hazifahamu yale unayosema. Ikimaanisha ili wapate udhuru - kama wanavyodai - kwa sababu hawana elimu. Na huu ni uongo kutoka kwao. Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema "Bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao" yani walifukuzwa, wamelaaniwa kwa sababu ya ukafiri wao; basi Waumini ni wachache tu miongoni mwao, au imani yao ni chache na ukafiri wao ndio mwingi.
: 89 - 90 #
{وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ مُصَدِّقٌ لِمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِنْ قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُمْ مَا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ فَلَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الْكَافِرِينَ (89) بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنْفُسَهُمْ أَنْ يَكْفُرُوا بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ بَغْيًا أَنْ يُنَزِّلَ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ عَلَى مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَى غَضَبٍ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُهِينٌ (90)}.
(89) Na kilipowajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipowajia yale waliyokuwa wakiyajua, waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao! (90) Kiovu kweli walichoziuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kuona haya kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa waja wake. Basi wamejiletea wenyewe ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata mateso ya kudhalilisha.
#
{89 - 90} أي: {ولما جاءهم [كتابٌ]} من عند الله على يد أفضل الخلق وخاتم الأنبياء، المشتمل على تصديق ما معهم من التوراة، وقد علموا به، وتيقنوه على أنهم إذا كان وقع بينهم وبين المشركين في الجاهلية حروب استنصروا بهذا النبي وتوعدوهم بخروجه، وأنهم يقاتلون المشركين معه، فلما جاءهم هذا الكتاب والنبي الذي عرفوا؛ كفروا به بغياً وحسداً أن ينزل الله من فضله على من يشاء من عباده، فلعنهم الله وغضب عليهم غضباً بعد غضب؛ لكثرة كفرهم وتوالي شكهم وشركهم، ولهم في الآخرة عذاب مهين أي مؤلم موجع، وهو صلْيُ الجحيم وفوت النعيم المقيم، فبئس الحال حالهم، وبئس ما استعاضوا واستبدلوا من الإيمان بالله وكتبه ورسله، الكفر به وبكتبه وبرسله مع علمهم وتيقنهم، فيكون أعظمَ لعذابهم.
(89-90) Yani "Na kilipowajia [Kitabu]" kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mikono ya mbora wa viumbe na mwisho wa Manabii, kinachojumuisha kusadikisha yale waliyo nayo katika Taurati. Na walikwishamjua, na wakawa na yakini juu yake kiasi kwamba vita vilipokuwa vinatokea baina yao na washirikina katika zama za kabla ya Uislamu, wangetafuta msaada kupitia Nabii huyu. Na wangewaonya kuwa atatokea, na kwamba watapigana na washirikina pamoja naye. Basi kilipowajia kitabu hiki na Nabii huyo ambaye walimjua; walimkufuru kwa dhuluma na husuda kwa kuwa Mwenyezi Mungu humteremshia katika fadhila zake amtakaye katika waja wake. Basi Mwenyezi Mungu akawalaani na akawakasirikia ghadhabu baada ya ghadhabu, kwa sababu ya ukafiri wao mwingi na mfuatano wa shaka yao na ushirikina wao. Na huko Akhera wana adhabu idhalilishayo, yani adhabu chungu yenye kuumiza. Nayo ni kuingia Jahiim na kukosa neema ya milele. Basi hali mbaya mno ni hali yao. Na ni kibaya mno walichobadilishana na kubadilisha badala ya kumwamini Mwenyezi Mungu, na Vitabu vyake na Mitume Wake, wakakumkufuru Yeye na Vitabu vyake na Mitume wake pamoja na kujua kwao na yakini yao. Basi likawa ni kubwa mno la kuwaadhibu kwa sababu yake.
: 91 - 93 #
{وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنْزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِمَا مَعَهُمْ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنْبِيَاءَ اللَّهِ مِنْ قَبْلُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (91) وَلَقَدْ جَاءَكُمْ مُوسَى بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِنْ بَعْدِهِ وَأَنْتُمْ ظَالِمُونَ (92) وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُمْ بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُمْ بِهِ إِيمَانُكُمْ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (93)}.
(91) Na wanapoambiwa: Yaaminini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Wao husema: Tunaamini tuliyoteremshiwa sisi. Na huyakataa yasiyokuwa hayo. Na hali ya kuwa hii ndiyo haki inayothibitisha yale waliyo nayo wao. Sema: Mbona mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu hapo zamani ikiwa kweli mlikuwa Waumini? (92) Na alikujieni Musa na hoja zilizo wazi, kisha mkamchukua ndama (kumuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu. (93) Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya tuliyokupeni na sikieni. Wakasema: Tumesikia na tumekataa! Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa kufuru yao. Sema: Ni uovu mno iliyokuamrisheni imani yenu ikiwa ni wenye kuamini.
#
{91} أي: وإذا أُمِر اليهود بالإيمان بما أنزل الله على رسوله وهو القرآن استكبروا وعتوا و {قالوا نؤمن بما أنزل علينا ويكفرون بما وراءه}؛ أي: بما سواه من الكتب، مع أن الواجب أن يؤمنوا بما أنزل الله مطلقاً سواء أنزل عليهم أو على غيرهم، وهذا هو الإيمان النافع، الإيمان بما أنزل الله على جميع رسل [الله]، وأما التفريق بين الرسل والكتب وزعم الإيمان ببعضها دون بعض فهذا ليس بإيمان بل هو الكفر بعينه، ولهذا قال تعالى: {إن الذين يكفرون بالله ورسله ويريدون أن يفرقوا بين الله ورسله ويقولون نؤمن ببعض ونكفر ببعض ويريدون أن يتخذوا بين ذلك سبيلا أولئك هم الكافرون حقًّا}؛ ولهذا رد عليهم تبارك وتعالى هنا ردًّا شافياً وألزمهم إلزاماً لا محيد لهم عنه فرد عليهم بكفرهم بالقرآن بأمرين فقال: {وهو الحق}؛ فإذا كان هو الحق في جميع ما اشتمل عليه من الإخبارات والأوامر والنواهي وهو من عند ربهم؛ فالكفر به بعد ذلك كفر بالله وكفر بالحق الذي أنزله. ثم قال: {مصدقاً لما معهم}؛ أي: موافقاً له في كلِّ ما دل عليه من الحق ومهيمناً عليه، فَلِمَ تؤمنون بما أنزل عليكم وتكفرون بنظيره، هل هذا إلا تعصب واتباع للهوى لا للهدى؟ وأيضاً فإن كون القرآن مصدقاً لما معهم يقتضي أنه حجة لهم على صدق ما في أيديهم من الكتب، فلا سبيل لهم إلى إثباتها إلا به، فإذا كفروا به وجحدوه صاروا بمنزلة من ادعى دعوى بحجة وبينة ليس له غيرها، ولا تتم دعواه إلا بسلامة بينته، ثم يأتي هو لبينته وحجته فيقدح فيها ويكذب بها، أليس هذا من الحماقة والجنون؟ فكان كفرهم بالقرآن كفراً بما في أيديهم ونقضاً له. ثم نقض عليهم تعالى دعواهم الإيمان بما أنزل إليهم بقوله: {قل}؛ لهم {فَلِمَ تقتلون أنبياء الله من قبل إن كنتم مؤمنين}.
(91) Yani Mayahudi wanapoamrishwa kuamini aliyoteremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake, nayo ni Qur-ani, wanajivuna na kufanya jeuri, na "Wao husema: Tunaamini tuliyo teremshiwa sisi. Na huyakataa yasiyokuwa hayo." Katika vitabu vinginevyo, pamoja na kwamba wajibu ni kwamba waamini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu yote, sawa yawe yaliteremshwa kwao au kwa wasiokuwa wao. Na hii ndiyo imani yenye manufaa. Kuamini aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wote [wa Mwenyezi Mungu]. Na ama kutofautisha baina ya Mitume na Vitabu, na kudai kuamini baadhi yake na sio baadhi yake, hili sio imani, bali ndio ukafiri wenyewe. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema "Hakika wale wanaomkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo katikati ya haya, hao ndio makafiri kweli." Ndio maana Mwenyezi Mungu Mwenye baraka, Mtukufu aliwajibu hapa kwa jawabu la kutosheleza, na akalazimisha kulazimisha ambako hawana njia ya kutokea. Akajibu kukufuru kwao Qur-ani kwa mambo mawili, akasema: "Na hali ya kuwa hii ndiyo haki." Basi ikiwa ni haki katika yote iliyojumuisha katika habari, na maamrisho, na makatazo, nayo inatoka kwa Mola wao Mlezi; basi kuikufuru baada ya hilo ni kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuikufuru haki ambayo aliteremsha. Kisha akasema "inayothibitisha yale waliyo nayo wao" yani inayoafikiana nayo katika kila iliyoashiria katika haki, na yenye kuyalinda. Basi kwa nini mnaamini yaliyoteremshwa juu yenu na mnakikataa kilicho sawa nayo? Je, huu sio tu ushabiki na kufuata matamanio, badala ya uwongofu? Vilevile, kwa kuwa Qur-ani inasadikisha yale waliyo nayo inalazimu kuwa ni hoja kwao juu ya usahihi wa yale yaliyomo mikononi mwao miongoni mwa vitabu, kwa hivyo hawana njia ya kuyathibitisha isipokuwa kwa hiyo (Qur-ani). Na wakiikufuru na kuikanusha, wanakuwa katika nafasi ya yule aliyedai madai kwa hoja na ushahidi, ambavyo hana vingine visivyokuwa hivyo, na wala madai yake hayawezi kutimia isipokuwa kwa ushahidi wake kusalimika. Kisha akaujia huo ushahidi wake na hoja yake na akavikashifu na akavikadhibisha. Je, huu si upumbavu na wazimu tu? Basi ukawa kuikufuru kwao Qur-ani ni kukufuru yale waliyo nayo mikononi mwao, na kuyapinga. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawapinga juu ya hayo madai yao kwamba wanaamini yaliyoteremshwa kwao kwa kauli yake. "Sema," uwaambie: "Mbona mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu hapo zamani ikiwa kweli mlikuwa Waumini?"
#
{92} {ولقد جاءكم موسى بالبينات}؛ أي: بالأدلة الواضحات المبينة للحق {ثم اتخذتم العجل من بعده}؛ أي: بعد مجيئه {وأنتم ظالمون}؛ في ذلك ليس لكم عذر.
(92) "Na alikujieni Musa na hoja zilizo wazi" yani dalili zilizo wazi zenye kubainisha haki. "Kisha mkamchukua ndama (kumuabudu) baada yake" yani baada ya kuja kwake "na mkawa wenye kudhulumu." Katika hilo na hamkuwa na udhuru wowote.
#
{93} {وإذ أخذنا ميثاقكم ورفعنا فوقكم الطور خذوا ما آتيناكم بقوة واسمعوا}؛ أي: سماع قبول وطاعة واستجابة، {قالوا سمعنا وعصينا}؛ أي: صارت هذه حالتهم {وأشربوا في قلوبهم العجل}؛ أي: صُبِغ حب العجل وحب عبادته في قلوبهم وشربها بسبب كفرهم {قل بئسما يأمركم به إيمانكم إن كنتم مؤمنين}؛ أي: أنتم تدعون الإيمان وتتمدحون بالدين الحق وأنتم قتلتم أنبياء الله واتخذتم العجل إلهاً من دون الله لمَّا غاب عنكم موسى نبي الله، ولم تقبلوا أوامره ونواهيه إلا بعد التهديد وَرَفْعِ الطور فوقكم، فالتزمتم بالقول ونقضتم بالفعل، فما هذا الإيمان الذي ادعيتم؟ وما هذا الدين؟ فإن كان هذا إيماناً على زعمكم، فبئس الإيمان الداعي صاحبه إلى الطغيان والكفر برسل الله وكثرة العصيان، وقد عُهِد أن الإيمان الصحيح يأمر صاحبه بكل خير وينهاه عن كل شرٍّ، فوضح بهذا كذبهم وتبين تناقضهم.
(93) "Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya tuliyokupeni na sikieni." yani kusikia kwa kukubali, kutii, na kuitikia. "Wakasema: Tumesikia na tumekataa!" Yani ikawa hii ndiyo hali yao. "Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya kumwabudu) ndama." Yani wakapakwa ndani ya nyoyo zao kupenda ndama, na kupenda kumuabudu. Na huko kunyweshwa kwao ni kwa sababu ya kukufuru kwao. "Sema: Ni uovu mno iliyokuamrisheni imani yenu ikiwa ni wenye kuamini". Yani nyinyi mnadai kuwa mnaamini na mnajisifu kuwa mna dini ya haki. Hali ya kuwa nyinyi mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu na mkamchukua ndama kuwa mungu badala ya Mwenyezi Mungu; wakati Musa Nabii wa Mwenyezi Mungu alipokwenda mbali na nyinyi. Na hamkuyakubali maamrisho yake na makatazo yake isipokuwa baada ya vitisho na kuinua mlima juu yenu. Basi mkashikamana na kauli, na mkavunja hilo kwa matendo yenu. Basi imani gani hii mliyodai? Na hii ni dini gani? Na ikiwa hii ni imani kama mnavyodai, basi ni mbaya mno. Imani inayomwita anayeiamini katika upotovu na kuwakufuru Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuasi kwa wingi. Na ilikwisha julikana kuwa imani sahihi inamuamrisha mwenyewe (mwenye imani) kila jema na inamkataza kila ovu. Kwa hivyo, ikabainika kwa hilo uongo wao na mgongano wao.
: 94 - 96 #
{قُلْ إِنْ كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِنْدَ اللَّهِ خَالِصَةً مِنْ دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (94) وَلَنْ يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ (95) وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَى حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَنْ يُعَمَّرَ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ (96)}.
(94) Sema: Ikiwa ile nyumba ya Akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti kama nyinyi mnasema kweli. (95) Wala hawatayatamani kamwe; kwa sababu ya yale mikono yao ilitanguliza. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwajua vyema wanaodhulumu. (96) Na hakika utawapata ni wenye pupa ya kuishi kuwashinda watu wote, na kuliko washirikina. Mmoja wao anatamani lau angelipewa umri wa miaka elfu. Wala hilo (la kuzidishiwa umri) haliwezi kumweka mbali na adhabu, ili apewe umri mrefu. Na Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda.
#
{94} أي: {قل}؛ لهم على وجه تصحيح دعواهم، {إن كانت لكم الدار الآخرة}؛ يعني الجنة، {خالصة من دون الناس}؛ كما زعمتم أنه لن يدخل الجنة إلا من كان هوداً أو نصارى، وأن النار لن تمسهم إلا أياماً معدودة فإن كنتم صادقين بهذه الدعوى، {فتمنوا الموت}؛ وهذا نوع مباهلة بينهم وبين رسول الله - صلى الله عليه وسلم - وليس بعد هذا الإلجاء والمضايقة لهم بعد العناد منهم إلا أحد أمرين: إما أن يؤمنوا بالله ورسوله، وإما أن يباهلوا على ما هم عليه بأمر يسير عليهم وهو تمني الموت الذي يوصلهم إلى الدار التي هي خالصة لهم، فامتنعوا عن ذلك؛ فعلم كل أحد أنهم في غاية المعاندة والمحادّة لله ورسوله مع علمهم بذلك، ولهذا قال تعالى:
(94) Yani "Sema" uwaambie katika hali ya kusahihisha madai yao "Ikiwa nyumba ya Akhera ni yenu tu " yani Pepo " bila ya watu wengine" kama mlivyodai kuwa hataingia Peponi ila aliyekuwa Myahudi au Mkristo; na kwamba Moto hautawagusa ila kwa siku chache tu. Basi ikiwa nyinyi ni wakweli katika madai haya, "basi tamanini mauti." Hii ni aina ya mubahala (kulaaniana) baina yao na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake. – Na hakuna baada ya huku kuwalazimisha na kuwafanyia ugumu baada ya ukaidi kutoka kwao ila moja ya mambo mawili: Ima wamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na ima wafanye mubahala (kulaaniana) kwa yale waliyo juu yake kwa kitu chepesi kwao, ambacho ni kutamani mauti ambayo yatawafikisha kwenye nyumba ambayo ni mahsusi kwao tu. Lakini wakakataa kufanya hivyo, kwa hivyo, kila mtu akajua kwamba wao wanafanya ukaidi mkubwa mno, na kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, licha ya kujua kwao hilo. Na kwa sababu ya hilo, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema:
#
{95} {ولن يتمنوه أبداً بما قدمت أيديهم}؛ من الكفر والمعاصي؛ لأنهم يعلمون أنه طريق لهم إلى المجازاة بأعمالهم الخبيثة، فالموت أكره شيء إليهم، وهم أحرص على الحياة من كل أحد من الناس حتى من المشركين الذين لا يؤمنون بأحد من الرسل والكتب. ثم ذكر شدة محبتهم الدنيا فقال:
(95) "Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale mikono yao iliyatanguliza" kama ukafiri na maasia. Kwa sababu wanajua kuwa ni njia yao ya kuwapelekea kuwalipa kwa matendo yao maovu. Basi kifo ndicho kitu kinawachochukiza zaidi, na wana pupa kubwa juu ya kuishi kuliko kila mtu katika watu, hata kuliko washirikina ambao hamwamini yeyote katika Mitume na Vitabu. Kisha akataja ukubwa wa mapenzi yao juu ya dunia, akasema:
#
{96} {يود أحدهم لو يعمر ألف سنة}؛ وهذا: أبلغ ما يكون من الحرص تمنوا حالة هي من المحالات، والحال أنهم لو عُمِّروا العمر المذكور لم يغن عنهم شيئاً، ولا دفع عنهم من العذاب شيئاً، {والله بصير بما يعملون}؛ تهديد لهم على المجازاة بأعمالهم.
(96) "Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale mikono yao ilitanguliza" kama ukafiri na maasia. Kwa sababu wanajua kuwa ni njia yao ya kuwapelekea kuwalipa kwa matendo yao maovu. Basi kifo kikawa ndicho kitu kinawachochukiza zaidi, na wana pupa kubwa juu ya kuishi kuliko kila mtu katika watu, hata kuliko washirikina ambao hamwamini yeyote katika Mitume na Vitabu. Kisha akataja ukubwa wa mapenzi yao juu ya dunia, akasema:
: 97 - 98 #
{قُلْ مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَى قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّهِ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ (97) مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِلَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّهَ عَدُوٌّ لِلْكَافِرِينَ (98)}.
(97) Sema: Aliyekuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliyeiteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayothibitisha yaliyokuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini. (98) Aliyekuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.
#
{97 - 98} أي: قل لهؤلاء اليهود الذين زعموا أن الذي منعهم من الإيمان أن وليك جبريل عليه السلام ولو كان غيره من ملائكة الله لآمنوا بك وصدقوا: إن هذا الزعم منكم تناقض وتهافت وتكبر على الله، فإن جبريل عليه السلام هو الذي نزل بالقرآن من عند الله على قلبك، وهو الذي ينزل على الأنبياء قبلك، والله هو الذي أمره وأرسله بذلك، فهو رسول محض، مع أن هذا الكتاب الذي نزل به جبريل مصدقاً لما تقدمه من الكتب غير مخالف لها ولا مناقض، وفيه الهداية التامة من أنواع الضلالات، والبشارة بالخير الدنيوي والأخروي لمن آمن به، فالعداوة لجبريل الموصوف بذلك كفر بالله وآياته وعداوة لله ولرسله وملائكته، فإن عداوتهم لجبريل لا لذاته، بل لما ينزل به من عند الله من الحق على رسل الله، فيتضمن الكفر والعداوة للذي أنزله وأرسله والذي أرسل به والذي أرسل إليه، فهذا وجه ذلك.
(97-98) Yani waambie hawa Mayahudi ambao walidai kuwa kilichowazuia kuamini ni kwamba rafiki yako ni Jibril amani iwe juu yake, na lau kuwa angelikuwa asiyekuwa yeye miongoni mwa Malaika wa Mwenyezi Mungu, basi wangekuamini na kukusadiki. Hakika, madai yenu haya ni mgongano haya ni yenye kupingana, na kuanguka chini, kumfanyia Mwenyezi Mungu kiburi. Kwani Jibril, amani iwe juu yake, ndiye aliyeiteremsha Qur-ani kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndani ya moyo wako. Naye ndiye aliyeteremsha kwa Manabii wa kabla yako, na Mwenyezi Mungu ndiye aliyemuamrisha na kumtuma na hayo. Basi, yeye ni Mtume tu, pamoja na kwamba kitabu hiki alichoteremka nacho Jibril kinasadikisha vilivyokitangulia miongoni mwa vitabu bila ya kutofautiana navyo wala kuvipinga. Na ndani yake mna uwongofu mkamilifu kutokana na kila aina ya upotovu, na bishara ya heri ya kidunia na kiakhera kwa mwenye kuiamini. Basi uadui juu ya Jibril anayeelezwa kwa hayo ni kumkufuru Mwenyezi Mungu na Aya zake, na uadui kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake na Malaika wake. Kwa maana, uadui wao juu ya Jibril sio kwa ajili yake mwenyewe, bali ni kwa sababu ya haki aliyoteremka nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu. Basi inajumuisha kufuru na uadui kwa yule aliyeiteremsha na kuituma, na yule ambaye alitumwa nayo, na yule aliyetumiwa. Na hii ndiyo sababu ya hilo.
: 99 #
{وَلَقَدْ أَنْزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ (99)}.
(99) Hakika tumekuteremshia Ishara zilizo wazi na hapana anayezikufuru isipokuwa wenye kupindukia mipaka (wapotovu).
#
{99} يقول لنبيه - صلى الله عليه وسلم -: {ولقد أنزلنا إليك آيات بينات}؛ تحصل بها الهداية لمن استهدى وإقامة الحجة على من عاند، وهي في الوضوح والدلالة على الحق قد بلغت مبلغاً عظيماً، ووصلت إلى حالة لا يمتنع من قبولها إلا من فسق عن أمر الله وخرج عن طاعة الله، واستكبر غاية التكبر.
(99) Anamwambia Nabii wake - rehema na amani ziwe juu yake - "Hakika tumekuteremshia Ishara zilizo wazi" ambazo kwazo unapatikana uwongofu kwa anayetaka uwongofu, na kusimamisha hoja dhidi ya mwenye kukaidi. Nazo katika ubainifu na ushahidi juu ya ukweli zimefikia kiwango kikubwa mno. Na zimefikia hali ambayo haachi kuikubali isipokuwa aliyepindukia amri ya Mwenyezi Mungu, na akatoka katika utiifu wa Mwenyezi Mungu, na wakafanya kiburi cha kiwango cha juu mno.
: 100 #
{أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَبَذَهُ فَرِيقٌ مِنْهُمْ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (100)}.
(100) Je, ati ndio kila wanapofunga ahadi, huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini.
#
{100} وهذا فيه التعجب من كثرة معاهداتهم وعدم صبرهم على الوفاء بها فكلما تفيد التكرار، فكلما وجد العهد ترتب عليه النقض، ما السبب في ذلك؟ السبب أن أكثرهم لا يؤمنون، فعدم إيمانهم هو الذي أوجب لهم نقض العهود، ولو صدق إيمانهم لكانوا مثل من قال الله فيهم: {من المؤمنين رجال صدقوا ما عاهدوا الله عليه}.
(100) Na haya ndani yake kuna kustaajabu, kwa sababu ya wingi wa mikataba yao na kutokuwa kwao na subira katika kuitimiza. Na "kila" inamaanisha kurudia. Hivyo basi, kila ahadi ilipopatikana, matokeo yake yalikuwa kwamba inavunjwa. Ni nini sababu ya hilo? Sababu ni kuwa wengi wao hawaamini. Na kutokuamini kwao ndiko kunawaletea kuvunja ahadi. Na lau kuwa imani yao ingekuwa kweli, wangekuwa kama wale aliosema Mwenyezi Mungu kuwahusu. "Miongoni mwa Waumini, wapo watu wakweli kwa yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu."
: 101 - 103 #
{وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ مُصَدِّقٌ لِمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (101) وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَى مُلْكِ سُلَيْمَانَ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنْزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّى يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ وَمَا هُمْ بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنْفَعُهُمْ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنْفُسَهُمْ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ (102) [وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ خَيْرٌ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ (103)]}.
(101) Na alipowajia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kuthibitisha yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu hicho nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui. (102) Na wakafuata yale waliyosoma mashetani katika ufalme wa Suleiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyoteremshwa kwa wale Malaika wawili, Haarut na Maarut huko Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka kwa Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yenye kuwadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika, walikwishajua kwamba mwenye kuununua (uchawi), hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walichouza kwacho nafsi zao, laiti wangelikuwa wanajua (1). (103) Na lau kuwa wangeamini na wakamcha Mungu, bila ya shaka malipo yatokayo kwa Mwenyezi Mungu yangekuwa bora. Laiti wangelikuwa wanajua!
#
{101} أي: ولما جاءهم هذا الرسول الكريم بالكتاب العظيم بالحق الموافق لما معهم وكانوا يزعمون أنهم متمسكون بكتابهم، فلما كفروا بهذا الرسول وبما جاء به {نبذ فريق من الذين أوتوا الكتاب كتاب الله}؛ الذي أنزل إليهم أي طرحوه رغبة عنه {وراء ظهورهم}؛ وهذا أبلغ في الإعراض كأنهم في فعلهم هذا من الجاهلين وهم يعلمون صدقه وحقيقة ما جاء به، تبين بهذا أن هذا الفريق من أهل الكتاب لم يبق في أيديهم شيء حيث لم يؤمنوا بهذا الرسول، فصار كفرهم به كفراً بكتابهم من حيث لا يشعرون. ولما كان من العوائد القدرية والحكمة الإلهية أن من ترك ما ينفعه وأمكنه الانتفاع به ولم ينتفع؛ ابتلي بالاشتغال بما يضره، فمن ترك عبادة الرحمن؛ ابتليَ بعبادة الأوثان، ومن ترك محبة الله وخوفه ورجاءه؛ ابتليَ بمحبة غير الله وخوفه ورجائه، ومن لم ينفق ماله في طاعة الله أنفقه في طاعة الشيطان، ومن ترك الذلَّ لربه؛ ابتليَ بالذل للعبيد، ومن ترك الحق؛ ابتليَ بالباطل.
(101) Yani alipowajia Mtume huyu mtukufu na Kitabu kitukufu kwa haki inayokubaliana na waliyo nayo. Na walikuwa wakidai kuwa wao wameshikamana na Kitabu chao. Na walipomkufuru Mtume huyu na yale aliyokuja nayo, "kundi moja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu lilitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu hicho" ambacho kiliteremshwa juu yao. Yani walikitupa kwa kukikataa "nyuma ya migongo yao." Na huku ndiko kupeana mgongo kwa juu mno, kana kwamba wao katika kitendo chao hiki ni wajinga, hali ya kuwa wanajua ukweli wake na uhakika wa yale aliyokuja nayo. Inabainika kwa hili kwamba kundi hili la Watu wa Kitabu halikubaki na chochote katika mikono yao, kwa vile hawakumuamini Mtume huyu. Basi, kukawa kumkufuru kwao ni kukikufuru kitabu chao bila ya kutambua. Na pindi ilipokuwa miongoni mwa marejeo ya majaaliwa na hekima ya Mwenyezi Mungu ni kwamba, mwenye kuacha yale yanayomnufaisha hali ya kuwa anaweza kunufaika nayo, na asifaidike nayo; anapewa mtihani wa kujishughulisha na yenye kumdhuru. Kwa hivyo, mwenye kuacha kumuabudu Arrahman (Mwingi wa Rehema); anapewa mtihani wa kuabudu masanamu. Na mwenye kuacha kumpenda Mwenyezi Mungu, kumhofu na kumtumaini; anapewa mtihani wa kupenda asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kumhofu, na kumtumaini. Na yule asiyetumia mali yake katika kumtii Mwenyezi Mungu, ataitumia katika kumtii Shetani. Na mwenye kuacha kumdhalilikia Mola wake Mlezi; anapewa mtihani wa kuwadhalilikia waja. Na mwenye kuiacha haki; anajaribiwa na batili (uongo).
#
{102 - 103} كذلك: هؤلاء اليهود لما نبذوا كتاب الله اتبعوا ما تتلوا الشياطين، وتختلق من السحر على ملك سليمان حيث أخرجت الشياطين للناس السحر، وزعموا أن سليمان عليه السلام كان يستعمله وبه حصل له الملك العظيم، وهم كذبة في ذلك فلم يستعمله سليمان بل نزهه الصادق في قيله: {وما كفر سليمان}؛ أي: بتعلم السحر فلم يتعلمه، {ولكن الشياطين كفروا}؛ في ذلك {يعلمون الناس السحر}؛ من إضلالهم وحرصهم على إغواء بني آدم وكذلك اتبع اليهود السحر الذي أُنْزِلَ على الملكين الكائنين بأرض بابل من أرض العراق، أنزل عليهما السحر امتحاناً وابتلاءً من الله لعباده فيعلمانهم السحر، {وما يعلمان من أحد حتى}؛ ينصحاه و {يقولا إنما نحن فتنة فلا تكفر}؛ أي: لا تتعلم السحر؛ فإنه كفر، فينهيانه عن السحر ويخبرانه عن مرتبته، فتعليم الشياطين للسحر على وجه التدليس والإضلال، ونسبته وترويجه إلى من برأه الله منه وهو سليمان عليه السلام، وتعليم الملكين امتحاناً مع نصحمها لئلا يكون لهم حجة، فهؤلاء اليهود يتبعون السحر الذي تعلمه الشياطين والسحر الذي يعلمه الملكان، فتركوا علم الأنبياء والمرسلين وأقبلوا على علم الشياطين، وكلٌّ يصبو إلى ما يناسبه. ثم ذكر مفاسد السحر فقال: {فيتعلمون منهما ما يفرقون به بين المرء وزوجه}؛ مع أن محبة الزوجين لا تقاس بمحبة غيرهما، لأن الله قال في حقهما: {وجعل بينكم مودة ورحمة}؛ وفي هذا دليل على أن السحر له حقيقة، وأنه يضر بإذن الله؛ أي: بإرادة الله، والإذن نوعان: إذن قدري: وهو المتعلق بمشيئة الله كما في هذه الآية، وإذن شرعي كما في قوله تعالى في الآية السابقة: {فإنه نزله على قلبك بإذن الله}؛ وفي هذه الآية وما أشبهها أن الأسباب مهما بلغت في قوة التأثير فإنها تابعة للقضاء والقدر ليست مستقلة في التأثير، ولم يخالف في هذا الأصل أحد من فرق الأمة غير القدرية في أفعال العباد زعموا: أنها مستقلة غير تابعة للمشيئة، فأخرجوها عن قدرة الله، فخالفوا كتاب الله وسنة رسوله وإجماع الصحابة والتابعين. ثم ذكر أن علم السحر مضرة محضة، ليس فيه منفعة لا دينية ولا دنيوية، كما يوجد بعض المنافع الدنيوية في بعض المعاصي كما قال تعالى في الخمر والميسر: {قل فيهما إثم كبير ومنافع للناس وإثمهما أكبر من نفعهما}؛ فهذا السحر مضرة محضة فليس له داعٍ أصلاً، فالمنهيات كلها إما مضرة محضة أو شرها أكبر من خيرها، كما أن المأمورات إما مصلحة محضة أو خيرها أكثر من شرها. {ولقد علموا}؛ أي: اليهود، {لمن اشتراه}؛ أي: رغب في السحر رغبة المشتري في السلعة، {ما له في الآخرة من خلاق}؛ أي: نصيب بل هو موجب للعقوبة، فلم يكن فعلهم إياه جهلاً ولكنهم استحبوا الحياة الدنيا على الآخرة فلبئس {ما شروا به أنفسهم لو كانوا يعلمون}؛ علماً يثمر العمل ما فعلوه.
(102-103) Vile vile, Mayahudi hawa walipokitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakawafuata mashetani wale; na walikuwa wakisoma na kuzua uchawi katika ufalme wa Sulaiman, wakati mashetani walipowatolea watu uchawi. Na wakadai kuwa Sulaiman, amani iwe juu yake alikuwa akiutumia, na kwa sababu yake alipata ufalme mkubwa. Nao ni waongo katika hilo. Sulaiman hakuutumia, bali Mkweli alimtakasa katika kauli yake: "Na wala Suleiman hakukufuru" yani kwa kujifunza uchawi, wala hakuifunza, "bali mashetani ndio waliokufuru" katika hilo "wakiwafundisha watu uchawi"; kutokana na kupotosha kwao na pupa yao ya kuwapoteza wanadamu. Na hali kadhalika, Mayahudi waliufuata uchawi ulioteremshwa kwa Malaika wawili waliokuwa katika mji wa Babeli katika nchi ya Iraqi. Waliteremshiwa uchawi kama mtihani na majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake. Basi wakawa wanawafundisha uchawi, "Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka" wamnasihi na "wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru." yani usijifunze uchawi; kwa maana ni ukafiri. Kwa hivyo, wanamkataza uchawi na kumpa habari juu ya daraja yake. Hivyo, mashetani kufundisha (watu) uchawi ni kwa njia ya ulaghai na kupotosha, na kuunasibisha na kuueneza kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimtakasa kutokana na hilo, naye ni Sulaiman amani iwe juu yake. Na kufundisha kwa wale Malaika wawili kulikuwa mtihani pamoja na kumpa nasaha ili wasiwe na hoja. Basi hawa Mayahudi wanafuata uchawi ambao mashetani waliusoma, na uchawi ambao wale Malaika wawili waliufundisha. Hivyo basi, wakaacha elimu ya Manabii na Mitume, na wakaielekea elimu ya mashetani. Na kila mmoja anamili kwa yale yanayomfaa. Kisha akataja maovu ya uchawi, akasema "Wakajifunza kwa hao wawili (Malaika wa Babeli) yale ya kumfarikisha mtu na mkewe." Pamoja na kwamba mapenzi ya wanandoa wawili hayawezi kulinganishwa na mapenzi ya wasio kuwa wao. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema juu yao "Na akaweka baina yenu mapenzi na huruma” Na katika hilo kuna dalili ya kwamba uchawi una uhakika, na kwamba unadhuru kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, yani kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Na idhini ni aina mbili: idhini iliyokwisha pangwa, ambayo inahusiana na matakwa ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyo katika Aya hii. Na idhini ya kisheria, kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya iliyotangulia "basi huyo ndiye aliyeiteremsha (Qur-ani) moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu". Na katika Aya hii na mfano wake kuna kwamba mwanadamu hata akifika nguvu kiasi gani katika kuathiri, basi (hizo nguvu) zinafuata makadirio na amri ya Mwenyezi Mungu, hazijitegemei katika kuathiri. Na hakuna yeyote katika madhehebu ya umma aliyehalifu msingi huu isipokuwa Al-Qadariyya kuhusiana na vitendo vya Mwenyezi Mungu. Wao walidai kwamba vinajitegemea wala havifuati mapenzi ya Mwenyezi Mungu; kwa hivyo wakavitoa nje ya uwezo wa Mwenyezi Mungu. Basi wakawa wamehalifu kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake na Ijmaa (makubaliano) ya Maswahaba na wafuatilizi wao. Kisha akataja kuwa elimu ya uchawi ni yenye madhara matupu, na hakuna manufaa yoyote ndani yake, sio ya kidini wala ya kidunia, kama vile yanavyopatikana baadhi ya manufaa ya kidunia katika baadhi ya madhambi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu pombe na kamari; "Sema: Katika hivyo (pombe na kamari) zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake." Na uchawi huu ni wenye madhara matupu, na wala hauhitajiki hata kidogo. Kwani makatazo yote ima yana madhara matupu au ubaya wake ni mkubwa kuliko heri yake. Kama vile maamrisho pia ima yana faida tupu au heri yake ni nyingi zaidi ya ubaya wake. "Na hakika walikwisha jua" yani Mayahudi "kwamba mwenye kuununua " yani kuutaka uchawi kama vile mnunuzi anavyotaka bidhaa "hatakuwa na fungu lolote katika Akhera." Yani mgao, bali inalazimu aadhibiwe. Kwa sababu, kitendo hicho chao sio kwamba walifanya hivyo kwa kutojua, lakini walipendelea maisha ya dunia kuliko ya Akhera. Basi ni kiovu mno "walichouza kwacho nafsi zao, laiti wangelikuwa wanajua" elimu yenye kuzaa matendo, basi hawangeufanya.
: 104 - 105 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انْظُرْنَا وَاسْمَعُوا وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ (104) مَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَنْ يُنَزَّلَ عَلَيْكُمْ مِنْ خَيْرٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَاللَّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ (105)}
(104) Enyi mlioamini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu. (105) Waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe heri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.
#
{104} كان المسلمون يقولون حين خطابهم للرسول عند تعلمهم أمر الدين: {راعنا}؛ أي: راع أحوالنا فيقصدون بها معنى صحيحاً، وكان اليهود يريدون بها معنى فاسداً، فانتهزوا الفرصة فصاروا يخاطبون الرسول بذلك ويقصدون المعنى الفاسد، فنهى الله المؤمنين عن هذه الكلمة سَدًّا لهذا الباب، ففيه النهي عن الجائز إذا كان وسيلة إلى محرم، وفيه الأدب واستعمال الألفاظ التي لا تحتمل إلا الحسن وعدم الفحش وترك الألفاظ القبيحة أو التي فيها نوع تشويش واحتمال لأمر غير لائق، فأمرهم بلفظة لا تحتمل إلا الحسن فقال: {وقولوا انظرنا}؛ فإنها كافية يحصل بها المقصود من غير محذور، {واسمعوا}؛ لم يذكر المسموع ليعم ما أمر باستماعه فيدخل فيه سماع القرآن وسماع السنة التي هي الحكمة لفظاً ومعنى واستجابة ففيه الأدب والطاعة، ثم توعد الكافرين بالعذاب المؤلم الموجع.
(104) Waislamu walikuwa wakisema wanapomwongelesha Mtume wakati wanaposoma jambo la dini "Raa'inaa", yani tuchunge hali zetu. Nao walikuwa wakikusudia kwa hayo maana yake sahihi. Nao Mayahudi walikuwa wakitaka kwayo maana potovu. Kwa hivyo, wakaichukua fursa hiyo na wakaanza kumsemesha Mtume kwa hayo na wakakusudia maana potofu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawakataza Waumini kutokana na hili neno, ili kuufunga mlango huu. Ndani yake kuna katazo la linaloruhusika ikiwa ni njia ya kufikisha kwa la haramu. Na ndani yake kuna adabu na matumizi ya maneno ambayo hayamaanishi isipokuwa uzuri, na kutokuwa na maneno machafu. Pia kuacha maneno mabaya au yenye aina fulani ya mkanganyiko na yenye uwezekano wa kumaanisha jambo lisilofaa. Kwa hivyo, akawaamrisha neno lisiloweza kumaanisha isipokuwa uzuri, akasema "na semeni: "Ndhurna (Tuangalieni)” kwa maana linatosha kufikia yaliyokusudiwa bila ya linalotahadharishwa. ”Na sikieni!" Na hapa hakutaja kinachosikilizwa, ili lijumuishe aliyoamrishwa asikilize, ndio iingie ndani yake kusikiliza Qur-ani na kusikiliza Sunnah, ambayo ndiyo hekima kimatamshi na kimaana, na kuitikia. Kwa hivyo, ndani yake kuna adabu na utiifu. Kisha akawatishia makafiri adhabu chungu iumizayo.
#
{105} وأخبر عن عداوة اليهود والمشركين للمؤمنين أنهم ما يودون، {أن ينزل عليكم من خير}؛ أي: لا قليلاً ولا كثيرًا، {من ربكم}؛ حسدًا منهم وبغضاً لكم أن يختصكم بفضله فإنه، {ذو الفضل العظيم} ومن فضله عليكم؛ إنزال الكتاب على رسولكم ليزكيكم ويعلمكم الكتاب والحكمة ويعلمكم ما لم تكونوا تعلمون، فله الحمد والمنة.
(105) Na akapeana habari kuhusu uadui wa Mayahudi na washirikina kwa Waumini kwamba, wao hawapendi kwamba "mteremshiwe kheri yoyote" yani sio kidogo wala nyingi "kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Kwa husuda kutoka kwao na kwa kuwachukia kwamba anakupeni nyinyi tu fadhila zake. Lakini yeye "ni mwenye fadhila kubwa." Na katika fadhila yake juu yenu ni kuteremsha Kitabu juu ya Mtume wenu ili awatakase na awafundishe Kitabu na hekima, na awafundishe ambayo hamkuwa mnayajua. Basi sifa njema zote na shukrani ni zake.
: 106 - 107 #
{مَا نَنْسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنْسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِنْهَا أَوْ مِثْلِهَا أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (106) أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ (107)}.
(106) Ishara yoyote tunayoifuta au tunayoisahaulisha, tunaileta iliyo bora kuliko hiyo, au iliyo mfano wake. Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu? (107) Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa Mbingu na Ardhi? Nanyi hamna mlinzi wala msaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu.
#
{106} النسخ هو النقل، فحقيقة النسخ نقل المكلفين من حكم مشروع إلى حكم آخر أو إلى إسقاطه، وكان اليهود ينكرون النسخ ويزعمون أنه لا يجوز، وهو مذكور عندهم في التوراة، فإنكارهم له كفر وهوى محض، فأخبر الله تعالى عن حكمته في النسخ، وأنه ما ينسخ {من آية أو ننسها}؛ أي: ننسها العباد فنزيلها من قلوبهم، {نأت بخير منها}؛ وأنفع لكم، {أو مثلها}؛ فدل على أن النسخ لا يكون لأقل مصلحة لكم من الأول لأن فضله تعالى يزداد خصوصاً على هذه الأمة التي سهل عليها دينها غاية التسهيل، وأخبر أن من قدح في النسخ [فقد] قدح في ملكه وقدرته فقال: {ألم تعلم أن الله على كل شيء قدير}.
(106) (An-Naskh) Ufutaji ni uhamisho. Na uhakika wa ufutaji ni kuwahamisha Mukallafin (yani anayewajibika kutekeleza sheria) kutoka hukumu ya kisheria moja kwenda kwa hukumu nyingine, au kuifutilia mbali. Na Mayahudi walikuwa wakiukanusha ufutaji na kudai kuwa hauruhusiki. Nao (ufutaji) umetajwa kwao katika Taurati. Kwa hivyo, kuukanusha kwao ni kufuru na matamanio matupu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akafahamisha kuhusu hekima yake katika ufutaji, na kwamba hafuti "ishara (aya) au tunayoisahaulisha" yani tunawasahaulisha waja, na tunaiondoa kutoka kwa nyoyo zao "tunaileta iliyo bora kuliko hiyo" na yenye manufaa zaidi kwenu; "au iliyo mfano wake." Basi ikaashiria kuwa ufutaji hauwi kwa lenye manufaa kidogo kwenu kuliko (ishara) ya kwanza. Kwa sababu, fadhila zake Mwenyezi Mungu Mtukufu huongezeka, hasa juu ya umma huu ambao amewarahisishia mno dini yao. Na akasema kwamba mwenye kuukashifu ufutaji [basi kwa hakika] ameukashifu ufalme wake na uwezo wake. Akasema :"Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu?"
#
{107} {ألم تعلم أن الله له ملك السموات والأرض}؛ فإذا كان مالكاً لكم متصرفاً فيكم تصرف المالك البر الرحيم في أقداره وأوامره ونواهيه، فكما أنه لا حجر عليه في تقدير ما يقدره على عباده من أنواع التقادير، كذلك لا يعترض عليه فيما يشرعه لعباده من الأحكام، فالعبد مدبر مسخر تحت أوامر ربه الدينية والقدرية فما له والاعتراض، وهو أيضاً ولي عباده ونصيرهم، فيتولاهم في تحصيل منافعهم، وينصرهم في دفع مضارهم، فمن ولايته لهم، أن يشرع لهم من الأحكام ما تقتضيه حكمته ورحمته بهم. ومن تأمل ما وقع في القرآن والسنة من النسخ، عرف بذلك حكمة الله، ورحمته عباده، وإيصالهم إلى مصالحهم من حيث لا يشعرون بلطفه.
(107) "Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa Mbingu na Ardhi?" Basi ikiwa yeye ni mmiliki wenu, anayewaendesha kuendesha kwa mmiliki mwema, mwenye huruma katika makadirio yake, na maamrisho yake, na makatazo yake. Na kama vile hakuna kizuizi chochote juu yake katika kukadiria anayoyakadiria juu ya waja wake miongoni mwa aina za makadirio, basi kadhalika asimpinge katika yale anayowawekea waja wake miongoni mwa hukumu. Hivyo basi, mja anatawaliwa, amefanywa kuwa chini ya amri za kidini na za kimakadirio za Mola wake Mlezi. Vipi sasa atapinga? Naye pia ni mlinzi wa waja wake na msaidizi wao. Anawachunga katika kupata manufaa yao, na anawasaidia katika kuwaondolea madhara yao. Na katika kuwachunga ni kwamba awaekee hukumu kulingana na inavyohitajiwa na hekima yake na rehema yake kwao. Na anayetafakari yaliyotokea katika Qur-ani na Sunna ya ufutaji, atajua kwa hilo, hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa waja wake. Na kuwafikisha kwenye masilahi yao kutoka pale wasipotambua kwa sababu ya upole wake.
: 108 - 110 #
{أَمْ تُرِيدُونَ أَنْ تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَى مِنْ قَبْلُ وَمَنْ يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ (108) وَدَّ كَثِيرٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُمْ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِنْ عِنْدِ أَنْفُسِهِمْ مِنْ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّى يَأْتِيَ اللَّهُ بِأَمْرِهِ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (109) وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنْفُسِكُمْ مِنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِنْدَ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (110)}.
(108) Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Musa zamani? Na anayebadilisha Imani kwa ukafiri bila ya shaka, huyo ameipotea njia iliyo sawa. (109) Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wangekurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia haki. Basi sameheni na tupilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atakapoleta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. (110) Na simamisheni Swala na toeni Zaka; na heri mtakazozitangulizia nafsi zenu, mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyafanya.
#
{108} ينهى الله المؤمنين أو اليهود بأن يسألوا رسولهم، {كما سئل موسى من قبل}؛ والمراد بذلك أسئلة التعنت والاعتراض، كما قال تعالى: {يسألك أهل الكتاب أن تنزل عليهم كتاباً من السماء فقد سألوا موسى أكبر من ذلك فقالوا أرنا الله جهرة}؛ وقال تعالى: {يا أيها الذين آمنوا لا تسألوا عن أشياء إن تبد لكم تسؤكم}؛ فهذه ونحوها هي المنهي عنها. وأما سؤال الاسترشاد والتعلم فهذا محمود قد أمر الله به كما قال تعالى: {فاسألوا أهل الذكر إن كنتم لا تعلمون}؛ ويقرهم عليه كما في قوله: {يسألونك عن الخمر والميسر}؛ و {يسألونك عن اليتامى}؛ ونحو ذلك. ولما كانت المسائل المنهي عنها مذمومة قد تصل بصاحبها إلى الكفر قال: {ومن يتبدل الكفر بالإيمان فقد ضل سواء السبيل}.
(108) Mwenyezi Mungu anawakataza Waumini au Mayahudi kumuuliza Mtume wao "kama alivyoulizwa Musa zamani."Na maana yake ni maswali ya ukaidi na upinzani, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha muuliza Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi." Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni." Haya na mfano wake ndiyo yaliyokatazwa. Na ama swali la kutafuta mwongozo na kujifunza, basi hili ni jambo la kusifiwa, Mwenyezi Mungu ameamrisha hilo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu; "Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui." Na anawakubalia kwa hayo kama katika kauli yake: "Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari" na "Na wanakuuliza juu ya mayatima." na mfano wa hayo. Na kwa kuwa maswali yaliyokatazwa ni yenye kukashifiwa, ambayo huenda yakampelekea mwenyewe katika ukafiri, akasema: "Na anayebadilisha Imani kwa ukafiri, bila ya shaka huyo ameipotea njia iliyo sawa."
#
{109} ثم أخبر عن حسد كثير من أهل الكتاب وأنهم بلغت بهم الحال أنهم ودوا {لو يردونكم من بعد إيمانكم كفاراً}؛ وسعوا في ذلك، وعملوا المكايد، وكيدهم راجع عليهم كما قال تعالى: {وقالت طائفة من أهل الكتاب آمنوا بالذي أنزل على الذين آمنوا وجه النهار واكفروا آخره لعلهم يرجعون}؛ وهذا من حسدهم الصادر من عند أنفسهم، فأمرهم الله بمقابلة من أساء إليهم [غاية الإساءة] بالعفو عنهم والصفح حتى يأتي الله بأمره، ثم بعد ذلك أتى الله بأمره إياهم بالجهاد، فشفى الله أنفس المؤمنين منهم، فقتلوا من قتلوا واسترقوا من استرقوا، وأجلوا من أجلوا، {إن الله على كل شيء قدير}.
(109) Kisha akajulisha kuhusu husuda ya wengi katika Watu wa Kitabu, na ya kwamba wamefikia hali ya kuwa wanatamani, "lau wangekurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu." Na wakafanya juhudi katika hilo, na wakafanya hila mbalimbali, lakini hila zao zinawarudia kama alivyosema Mtukufu. "Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyoteremshiwa wenye kuamini mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea." Na hii ni kutokana na husuda yao itokayo katika nafsi zao. Lakini Mwenyezi Mungu akawaamrisha wakabiliane na wale waliowaudhi [vibaya mno] kwa kuwasamehe na kuwatupilia mbali mpaka Mwenyezi Mungu atakapoleta amri yake. Kisha baada ya hayo, Mwenyezi Mungu akawaletea amri yake kwamba wafanye jihadi. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu akaziponya nafsi za Waumini kutokana nao, na wakawauwa waliowauwa, na wakawafanya watumwa, na wakawatoa wale waliowatoa. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu."
#
{110} ثم أمرهم الله بالاشتغال بالوقت الحاضر بإقامة الصلاة وإيتاء الزكاة وفعل كل القربات، ووعدهم أنهم مهما فعلوا من خير فإنه لا يضيع عند الله بل يجدونه عنده وافراً موفراً قد حفظه {إن الله بما تعملون بصير}.
(110) Kisha Mwenyezi Mungu akawaamrisha washughulikie wakati wa sasa kwa kushika Sala, na kutoa Zaka, na kufanya ibada zote. Na akawaahidi kuwa wema wowote watakaoufanya, haupotezwi kwa Mwenyezi Mungu, bali wataupata kwake ukiwa mwingi uliozidishwa, tayari ameshauhifadhi. "Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyafanya."
: 111 - 112 #
{وَقَالُوا لَنْ يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَى تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (111) بَلَى مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِنْدَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (112)}.
(111) Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Myahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli. (112) Sivyo hivyo! Yeyote anayeelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.
#
{111} أي: قال اليهود: لن يدخل الجنة إلا من كان هوداً، وقالت النصارى: لن يدخل الجنة إلا من كان نصارى، فحكموا لأنفسهم بالجنة وحدهم، وهذا مجرد أماني غير مقبولة إلا بحجة وبرهان فأتوا بها إن كنتم صادقين، وهكذا كل من ادعى دعوى لا بد أن يقيم البرهان على صِحة دعواه، وإلا فلو قلبت عليه دعواه وادعى مدع عكس ما ادعى بلا برهان لكان لا فرق بينهما، فالبرهان هو الذي يصدق الدعاوي أو يكذبها، ولما لم يكن بأيديهم برهان علم كذبهم بتلك الدعوى.
(111) Yani Mayahudi walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Myahudi. Nao Wakristo wakasema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Mkristo. Basi wakajihukumia kwamba wao peke yao ndio watakaoingia Peponi. Na haya ni matamanio tu ambayo hayakubaliwi isipokuwa kwa hoja na dalili. Basi ileteni (hoja) ikiwa nyinyi ni wakweli. Na vivyo hivyo, kila mwenye kudai madai, ni lazima ayaletee ushahidi (dalili) juu ya usahihi wa madai yake. Vinginevyo, ikiwa madai yake yatageuzwa dhidi yake, na mwenye kudai mwingine akadai kinyume cha alichodai bila ushahidi, itakuwa hakuna tofauti yoyote kati yao. Kwa hivyo, ushahidi ndio unaosadikisha madai au uyakadhibishe. Na kwa vile hakukuwa na ushahidi mikononi mwao, ulijulikana uongo wao kwa (kudai) madai hayo.
#
{112} ثم ذكر تعالى البرهان الجلي العام لكل أحد فقال: {بلى}؛ أي: ليس بأمانيكم ودعاويكم ولكن، {من أسلم وجهه لله}؛ أي: أخلص لله أعماله متوجهاً إليه بقلبه، {وهو}؛ مع إخلاصه {محسن}؛ في عبادة ربه بأن عبده بشرعه فأولئك هم أهل الجنة وحدهم، فلهم أجرهم عند ربهم؛ وهو الجنة بما اشتملت عليه من النعيم، {ولا خوف عليهم ولا هم يحزنون}؛ فحصل لهم المرغوب ونجوا من المرهوب، ويفهم منها أن من ليس كذلك فهو من أهل النار الهالكين، فلا نجاة إلا لأهل الإخلاص للمعبود والمتابعة للرسول.
(112) Kisha Mwenyezi Mungu akataja dalili zilizo wazi, zenye kujumuisha kila mtu, akasema: "Sivyo hivyo!" yani sio kwa matamanio yenu wala madai yenu. Lakini "yeyote anayeelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu;" yani anayemfanyia Mwenyezi Mungu peke yake matendo yake, huku amemwelekea kwa moyo wake "naye ni mtenda mema" katika kumwabudu Mola wake Mlezi, kwa kumwabudu kwa sheria yake, basi hao ndio watu wa Peponi peke yao. Nao wana malipo yao kwa Mola wao Mlezi. Nayo ni Pepo iliyomo pamoja na ilivyojumuisha ndani yake miongoni mwa neema "wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika." Basi wakapata yanayotamaniwa, na wakaokoka kutokana na yanayohofisha. Na inafahamika kutoka humo kwamba asiyekuwa hivyo, basi huyo ni katika watu wa Motoni walioangamia. Hivyo, hakuna wokovu wowote ila kwa watu wenye ikhlasi (wanomfanyia matendo Mwenyezi Mungu peke yake) kwa mwabudiwa wao na kumfuata Mtume (wa Mwenyezi Mungu).
: 113 #
{وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَى عَلَى شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَى لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَى شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ كَذَلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ فَاللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ (113)}.
(113) Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo (wanalolifuata). Na Wakristo husema: Mayahudi hawana lao jambo (wanalolifuata). Na ilhali wote wanasoma Kitabu kicho hicho (Biblia). Na kadhaalika walisema wale wasiojua kitu mfano wa kauli yao hii. Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.
#
{113} وذلك أنه بلغ بأهل الكتاب الهوى والحسد إلى أن بعضهم ضلل بعضاً، وكفر بعضهم بعضاً كما فعل الأميون من مشركي العرب وغيرهم، فكل فرقة تضلل [الفرقةَ] الأخرى، ويحكم الله في الآخرة بين المختلفين بحكمه العدل الذي أخبر به عباده، فإنه لا فوز ولا نجاة إلا لمن صدَّق جميع الأنبياء والمرسلين، وامتثل أوامر ربه، واجتنب نواهيه، ومن عداهم فهو هالك.
(113) Na hayo ni kuwa matamanio na husuda yaliwafikisha Watu wa Kitabu kiwango kwamba wenyewe kwa wenyewe wanaonana kuwa wapotofu, na wanakufurishana wao kwa wao, kama walivyofanya wasiojua kusoma katika washirikina wa Waarabu na wengineo. Kila kundi linaona lingine kuwa ni potofu. Na Mwenyezi Mungu atahukumu Akhera baina ya wale waliotofautiana kwa hukumu yake ya uadilifu aliyowaambia waja wake. Kwani hakuna kufaulu wala kuokoka ila kwa yule aliyewaamini Manabii na Mitume wote, akatekeleza maamrisho ya Mola wake Mlezi, na akajiepusha na makatazo yake. Na asiyekuwa hao, basi yeye ni mwangamivu.
: 114 #
{وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ مَنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَنْ يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَى فِي خَرَابِهَا أُولَئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَنْ يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ (114)}.
(114) Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake, na akajitahidi kuiharibu? (Watu) hao haitawafalia kuingia humo isipokuwa kwa hofu. Duniani watapata hizaya (aibu kubwa maishani), na Akhera watapata adhabu kubwa.
#
{114} أي: لا أحد أظلم وأشد جرماً ممن منع مساجد الله عن ذكر الله فيها وإقامة الصلاة وغيرها من [أنواع] الطاعات، {وسعى}؛ أي: اجتهد وبذل وسعه، {في خرابها}؛ الحسي والمعنوي، فالخراب الحسي هدمها وتخريبها وتقذيرها، والخراب المعنوي منع الذاكرين لاسم الله فيها، وهذا عام لكل من اتصف بهذه الصفة فيدخل في ذلك أصحاب الفيل وقريش حين صدوا رسول الله عنها عام الحديبية، والنصارى حين أخربوا بيت المقدس، وغيرهم من أنواع الظلمة الساعين في خرابها محادّة لله ومشاقة، فجازاهم الله بأن منعهم دخولها شرعاً وقدراً إلا خائفين ذليلين، فلما أخافوا عباد الله أخافهم الله، فالمشركون الذين صدوا رسوله لم يلبث رسول الله - صلى الله عليه وسلم - إلا يسيراً حتى أذن الله له في فتح مكة ومنع المشركين من قربان بيته فقال تعالى: {يا أيها الذين آمنوا إنما المشركون نجس فلا يقربوا المسجد الحرام بعد عامهم هذا}؛ وأصحاب الفيل قد ذكر الله ما جرى عليهم، والنصارى سلط الله عليهم المؤمنين فأجلوهم [عنه]، وهكذا كل من اتصف بوصفهم فلا بد أن يناله قسطه، وهذا من الآيات العظيمة أخبر بها الباري قبل وقوعها فوقعت كما أخبر، واستدل العلماء بالآية الكريمة على أنه لا يجوز تمكين الكفار من دخول المساجد {لهم في الدنيا خزي}؛ [أي]: فضيحة؛ كما تقدم {ولهم في الآخرة عذاب عظيم}؛ وإذا كان لا أظلم ممن منع مساجد الله أن يذكر فيها اسمه، فلا أعظم إيماناً ممن سعى في عمارة المساجد بالعمارة الحسية والمعنوية؛ كما قال تعالى: {إنما يعمر مساجد الله من آمن بالله واليوم الآخر}؛ بل قد أمر الله تعالى برفع بيوته وتعظيمها وتكريمها فقال تعالى: {في بيوت أذن الله أن ترفع ويذكر فيها اسمه}. وللمساجد أحكام كثيرة يرجع حاصلها إلى مضمون هذه الآيات الكريمة.
(114) Yani hakuna yeyote dhalimu mkubwa na mwenye makosa makubwa zaidi kuliko yule anayeizuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na kusimamisha Swala na mengineyo katika [aina za] utiifu. "Na akajitahidi" yani akafanya jitihada kadiri awezavyo "katika kuiharibu." Kihisia na kimaana. Nako kuharibu kwa kihisia ni kuibomoa, kuiharibu, na kuichafua. Nako kuharibu kwa kimaana ni kuzuia wale wanaolitaja jina la Mwenyezi Mungu ndani yake. Na hili ni la jumla kwa kila anayesifika kwa hizo sifa. Kwa hivyo, wanaingia humo wale wenye tembo, na Maquraishi walipomzuia Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mwaka wa Hudaybiya. Na Wakristo walipoiharibu Baitul-Maqdis na aina nyinginezo za madhalimu wanaojitahidi katika kuiharibu, wakimpinga Mwenyezi Mungu na kumuasi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawalipa kwamba aliwazuia kuingia humo kisheria na kimakadirio isipokuww kwa hofu, wadhalilifu. Basi walipowaogopesha waja wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akawatia hofu. Hivyo, wale washirikina waliomzuia Mtume wake, hakukaa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kwa muda mfupi tu na Mwenyezi Mungu akamruhusu kuiteka Makka na kuwazuia washirikina kuikaribia nyumba yake. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu "Enyi mlioamini! hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtukufu baada ya mwaka wao huu." Na wale wenye tembo, Mwenyezi Mungu amekwisha taja yaliyowasibu. Nao Wakristo, Mwenyezi Mungu aliwatia nguvu Waumini juu yao, basi wakawatoa [huko]. Na vivyo hivyo kila anayesifika kwa sifa zao, basi ni lazima apatwe na fungu lake. Na hii ni miongoni mwa Aya (Ishara) kubwa alizozieleza Muumba kabla ya kutokea kwake, hivyo zikatokea kama alivyosema. Na wanachuoni walitumia aya hii tukufu kama hoja kuwa hairuhusiki kuwawezesha makafiri kuingia misikitini. "Duniani watapata hizaya" [yani] yenye fedheha kama ilivyotangulia "na Akhera watapata adhabu kubwa." Na ikiwa hakuna dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake, basi hakuna mwenye imani kubwa kuliko yule anayejitahidi katika kuiimarisha misikiti; kuimarisha kwa kihisia na kwa kimaana, kama alivyosema Mtukufu. "Anayestawisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni yeye tu amwaminiye Mwenyezi Mungu na Siku ya mwisho." Bali Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamrisha nyumba zake zinyanyuliwe, zitukuzwe na ziheshimiwe. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu zinyanyuliwe, na humo litajwe jina lake" Na misikiti ina hukumu nyingi jumla yake inarudi kwa yaliyomo katika Aya hizi tukufu.
: 115 #
{وَلِلَّهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ (115)}.
(115) Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Basi kokote mnakoelekea, huko Mwenyezi Mungu yupo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye elimu.
#
{115} أي: {ولله المشرق والمغرب}؛ خصهما بالذكر لأنهما محل الآيات العظيمة [فهما] مطالع الأنوار ومغاربها، فإذا كان مالكاً لها كان مالكاً لكل الجهات {فأينما تولوا}؛ وجوهكم من الجهات إذا كان توليكم إياها بأمره، إما أن يأمركم باستقبال الكعبة بعد أن كنتم مأمورين باستقبال بيت المقدس، أو تؤمرون بالصلاة في السفر على الراحلة ونحوها، فإن القبلة حيثما توجه العبد، أو تشتبه القبلة فيتحرى الصلاة إليها، ثم يتبين له الخطأ أو يكون معذوراً بصلب أو مرض ونحو ذلك، فهذه الأمور إما أن يكون العبد فيها معذوراً أو مأموراً. وبكل حال فما استقبل جهة من الجهات خارجة عن ملك ربه {فثم وجه الله إن الله واسع عليم}؛ فيه إثبات الوجه لله تعالى على الوجه اللائق به تعالى، وإن لله وجهاً لا تشبهه الوجوه، وهو تعالى واسع الفضل والصفات عظيمها عليم بسرائركم ونياتكم، فمن سعته وعلمه، وسع لكم الأمر، وقبل منكم المأمور، فله الحمد والشكر.
(115) Yani "Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu." na alizitaja hususan kwa sababu hizo ndizo mahali pa ishara kubwa [kwani mbili hizo ndizo] mapambazuko ya mianga na magharibi yake. Basi ikiwa yeye ndiye mmiliki wake, yeye ndiye mmiliki wa pande zote. "Basi kokote mnakoelekea," nyuso zenu miongoni mwa pande, ikiwa kuzielekea kwenu ni kwa amri yake; ima anakuamrisheni kuielekea Al-Kaaba baada ya kuamrishwa kuielekea Al-Bait Al-Maqdis, au mmeamrishwa kuswali katika safiri juu ya ngamia na mfano wake; basi Qibla ni popote anapoelekeza mja. Au ikiwa Qibla kinakuwa na mashaka, basi atajaribu kuswali kwa kukielekea, kisha hilo kosa likimdhihirikia au awe ni mwenye udhuru kwa sababu ya kusulubiwa au maradhi na mfano wake, basi katika haya mambo, mja huwa amepewa udhuru au ameamrishwa. Vyovyote iwavyo, kuelekea upande miongoni mwa pande hakutoki nje ya milki ya Mola wake Mlezi, "uso wa Mwenyezi Mungu upo (upande huo). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkunjufu) na Mwenye elimu." Ndani yake kuna kumthibitishia Mwenyezi Mungu uso kwa namna inayomfaa Yeye Mtukufu. Na kwamba Mwenyezi Mungu ana uso usiofanana na nyuso zingine. Naye Mtukufu (Mwenyezi Mungu) ni mkunjufu (mpana) wa fadhila, na sifa nyingi kuu, Mjuzi wa siri na makusudio yenu. Na katika wasaa wake na elimu yake, ni kwamba aliwafanyia ukunjufu katika jambo hili, na akakubali kutoka kwenu alilowaamrisha. Basi ni zake sifa njema na shukrani.
: 116 - 117 #
{وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا سُبْحَانَهُ بَلْ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَهُ قَانِتُونَ (116) بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِذَا قَضَى أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ (117)}.
(116) Na ati wanasema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu (ametakasika na hayo!) Bali vyote vilivyomo mbinguni na duniani ni vyake. Vyote vinamdhalilikia Yeye kwa hofu (1). (117) Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina mfano wa awali; na anapotaka jambo, basi Yeye kwa hakika huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa.
#
{116} {وقالوا}؛ أي: اليهود والنصارى والمشركون وكل من قال ذلك، {اتخذ الله ولداً}؛ فنسبوه إلى ما لا يليق بجلاله وأساءوا كل الإساءة وظلموا أنفسهم وهو تعالى صابر على ذلك منهم، قد حلم عليهم، وعافاهم، ورزقهم مع تنقصهم إياه {سبحانه}؛ أي: تنزه وتقدس عن كل ما وصفه به المشركون والظالمون مما لا يليق بجلاله، فسبحان من له الكمال المطلق من جميع الوجوه الذي لا يعتريه نقصٌ بوجه من الوجوه، ومع رده لقولهم أقام الحجة والبرهان على تنزيهه عن ذلك فقال: {بل له ما في السموات والأرض}؛ أي: جميعهم ملكه وعبيده يتصرف فيهم تصرف المالك بالمماليك وهم قانتون له مسخرون تحت تدبيره، فإذا كانوا كلهم عبيده مفتقرين إليه، وهو غني عنهم فكيف يكون منهم أحد يكون له ولداً، والولد لا بد أن يكون من جنس والده لأنه جزء منه، والله تعالى المالك القاهر وأنتم المملوكون المقهورون وهو الغني وأنتم الفقراء، فكيف مع هذا يكون له ولد؟ هذا من أبطل الباطل وأسمجه. والقنوت نوعان: قنوت عام وهو قنوت الخلق كلهم تحت تدبير الخالق، وخاص وهو قنوت العبادة. فالنوع الأول كما في هذه الآية، والنوع الثاني كما في قوله تعالى: {وقوموا لله قانتين}. ثم قال:
(116) "Na ati wanasema," yani Mayahudi, Wakristo, washirikina, na kila aliyesema hayo. "Mwenyezi Mungu ana mwana" Basi wakamhusisha na yale yasiyoufalia utukufu wake, na wakafanya kila ubaya, na wakazidhulumu nafsi zao. Na Yeye Mtukufu ana subira kwa hayo kutoka kwao, na akawafanya kuwa salama, na akawaruzuku pamoja na kumpunguzia kwao hadhi. "Ametakasika na hayo" yani yuko mbali na hayo, na ametakasika kutokana na kila waliyomueleza nayo washirikina na madhalimu, miongoni mwa yale yasiyofailia utukufu Wake. Basi ametakasika Yule ambaye ni Wake ukamilifu wote kwa namna yote, asiyepungukiwa hadhi kwa namna yoyote. Na pamoja na kujibu hiyo kauli yao, alisimamisha hoja na ushahidi juu ya kutakasika kwake na hilo, akasema: "Bali vyote vilivyomo mbinguni na duniani ni vyake" yani hivyo vyote ni miliki yake na watumwa wake. Anawaendesha kama anavyoendesha mmiliki wale anaowamiliki. Nao ni watiifu kwake, wamefanywa kuwa chini ya uendeshaji wake. Basi ikiwa wote ni waja wake wanaomhitaji, ilhali Yeye ni mwenye kujitosheleza hawahitaji wao, basi vipi atakuwapo yeyote miongoni mwao ambaye ni mtoto wake? Na mtoto ni lazima awe kutoka kwa sura ya baba yake, kwa sababu yeye ni sehemu yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mmiliki, Mwenye nguvu, nanyi ndio wamilikiwa wanaotawaliwa. Naye hamhitaji yeyote, nanyi ni wahitaji. Basi vipi pamoja na haya atakuwa na mwana? Hii ndiyo batili ya batili zote na yenye kuchukiza mno. Na Qunuut ni ya aina mbili: qunuut ya jumla, ambayo ni qunuut ya viumbe vyote chini ya kuendesha kwa Muumba, na qunuut maalumu, ambayo ni qunuut ya ibada. Na aina ya kwanza ni kama ilivyo katika Aya hii, nayo aina ya pili ni kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye Qunuut (wanyenyekevu). Kisha akasema:
#
{117} {بديع السموات والأرض}؛ أي: خالقهما على وجه قد أتقنهما وأحسنهما على غير مثال سبق، {وإذا قضى أمراً فإنما يقول له كن فيكون}؛ فلا يستعصي عليه ولا يمتنع منه.
(117) "Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza." Yani aliviumba kwa namna ya ukamilifu na uzuri sana bila ya mifano uliotangulia. "Na anapotaka jambo, basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa." na wala haliwi gumu kwake na wala halikatai.
: 118 - 119 #
{وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ كَذَلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ مِثْلَ قَوْلِهِمْ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ (118) إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ (119)}.
(118) Na walisema wale wasiojua kitu: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi au zikatufikia Ishara. Kama hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hii. Nyoyo zao zimefanana. Hakika Sisi tumeziweka wazi Ishara kwa watu wenye yakini. (119) Hakika Sisi tumekutuma kwa haki uwe mbashiri, na mwonyaji. Na wala hutaulizwa juu ya watu wa Motoni.
#
{118} أي: قال الجهلة من أهل الكتاب وغيرهم هلا يكلمنا الله كما كلم الرسل، {أو تأتينا آية}؛ يعنون آيات الاقتراح التي يقترحونها بعقولهم الفاسدة وآرائهم الكاسدة التي تجرؤوا بها على الخالق واستكبروا على رسله كقولهم: {لن نؤمن لك حتى نرى الله جهرة}؛ {يسألك أهل الكتاب أن تنزل عليهم كتاباً من السماء فقد سألوا موسى أكبر من ذلك ... }؛ الآية. {وقالوا مالِ هذا الرسول يأكل الطعام ويمشي في الأسواق لولا أنزل إليه ملك فيكون معه نذيراً أو يلقى إليه كنز أو تكون له جنة يأكل منها ... }؛ الآيات، وقوله: {وقالوا لن نؤمن لك حتى تفجر لنا من الأرض ينبوعاً ... }؛ الآيات. فهذا دأبهم مع رسلهم يطلبون آيات التعنت لا آيات الاسترشاد، ولم يكن قصدهم تبيين الحق فإن الرسل قد جاؤوا من الآيات بما يؤمن على مثله البشر، ولهذا قال تعالى: {قد بينا الآيات لقوم يوقنون}؛ فكل موقن فقد عرف من آيات الله الباهرة وبراهينه الظاهرة ما حصل له به اليقين، واندفع عنه كل شك وريب.
(118) Yani: Walisema wajinga miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi nasi kama alivyowasemesha Mitume "au zikatufikia Ishara." Wanamaanisha Aya za mapendekezo ambayo wanapendekeza kwa akili zao mbovu na rai zao potovu, ambazo walifanya ujasiri kwazo dhidi ya Muumba na wakawafanyia kiburi Mitume wake. Kama kauli yao, "hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi" (na) "Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo" hadi mwisho wa Aya. "Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula, na anatembea masokoni! Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye? Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale kutoka humo?" Hadi mwisho wa Aya hizi. Na kauli yake. "Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemichemi katika ardhi hii." Hadi mwisho wa Aya hizi. Basi haya ndiyo mazoea yao kwa Mitume wao, kutaka dalili za uasi, na sio dalili za uwongofu; na hayakuwa makusudio yao kubainishiwa haki. Kwani Mitume walikuja na Ishara ambazo mfano wake watu waliziamini. Na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Hakika sisi, tumeshazibainisha Ishara kwa watu wenye yakini." Hivyo basi, kila mwenye yakini alikwishajua kutokana na aya (ishara) za Mwenyezi Mungu zinazong'aa na dalili zilizo dhahiri, kilichomfanya kuwa na yakini; na inamwondokea kila shaka na kusitasita.
Kisha Mtukufu akataja baadhi ya Aya zilizofupishwa, zenye kujumuisha aya ambazo zinaonyesha ukweli wake - rehema na amani ziwe juu yake - na usahihi wa kile alichokuja nacho, akasema:
#
{119} {إنا أرسلناك بالحق بشيراً ونذيراً}؛ فهذا مشتمل على الآيات التي جاء بها، وهي ترجع إلى ثلاثة أمور: الأول في نفس إرساله، والثاني في سيرته وهديه ودِلِّه، والثالث في معرفة ما جاء به من القرآن والسنة. فالأول والثاني قد دخلا في قوله: {إنا أرسلناك}؛ والثالث [دخل] في قوله: {بالحق}. وبيان الأمر الأول: وهو ـ نفس إرساله ـ أنه قد علم حالة أهل الأرض قبل بعثته - صلى الله عليه وسلم - وما كانوا عليه من عبادة الأوثان والنيران والصلبان وتبديلهم للأديان حتى كانوا في ظلمة من الكفر قد عمتهم وشملتهم، إلا بقايا من أهل الكتاب قد انقرضوا قبيل البعثة، وقد علم أن الله تعالى لم يخلق خلقه سدى ولم يتركهم هملاً، لأنه حكيم عليم قدير رحيم، فمن حكمته ورحمته بعباده أن أرسل إليهم هذا الرسول العظيم يأمرهم بعبادة الرحمن وحده لا شريك له، فبمجرد رسالته يعرف العاقل صدقه، وهو آية كبيرة على أنه رسول الله. وأما الثاني فمن عرف النبي - صلى الله عليه وسلم - معرفة تامة، وعرف سيرته وهديه قبل البعثة ونشوءه على أكمل الخصال، ثم من بعد ذلك قد ازدادت مكارمه وأخلاقه العظيمة الباهرة للناظرين، فمن عرفها وسبر أحواله عرف أنها لا تكون إلا أخلاق الأنبياء الكاملين؛ لأنه تعالى جعل الأوصاف أكبر دليل على معرفة أصحابها وصدقهم وكذبهم. وأما الثالث: فهو معرفة ما جاء به - صلى الله عليه وسلم - من الشرع العظيم والقرآن الكريم المشتمل على الإخبارات الصادقة والأوامر الحسنة والنهي عن كل قبيح، والمعجزات الباهرة، فجميع الآيات تدخل في هذه الثلاثة. قوله: {بشيراً}؛ أي: لمن أطاعك بالسعادة الدنيوية والأخروية، {نذيراً}؛ لمن عصاك بالشقاوة والهلاك الدنيوي والأخروي، {ولا تسأل عن أصحاب الجحيم}؛ أي: لست مسؤولاً عنهم، إنما عليك البلاغ وعلينا الحساب.
(119) "Hakika Sisi tumekutuma kwa haki uwe mbashiri, na mwonyaji." Na hii (Aya) imejumuisha ishara alizokuja nazo. Nazo zinarudi kwa mambo matatu: La kwanza ni kumtuma kwenyewe. Nalo la pili ni katika siira (maisha) yake, muongozo wake, na welekezi wake. Na la tatu ni katika kujua yale aliyoleta katika Qur-ani na Sunnah. Hivyo, la kwanza na la pili yanaingia katika kauli yake: "Hakika Sisi tumekutuma". Nalo la tatu [linaingia] katika kauli yake: "Kwa haki". Na kubainisha jambo hilo la kwanza - ambalo ni kutumwa kwake kwenyewe - ni kwamba Yeye alishajua hali ya watu wa ardhini kabla ya kumtuma kwake - rehema na amani ziwe juu yake.- Na yale waliyokuwa juu yake ya kuabudu masanamu, moto na misalaba, na kubadilisha dini zao mpaka wakawa katika giza la ukafiri lililowajumuisha na kuwaenea, isipokuwa mabaki ya Watu wa Kitabu waliokuwa wametoweka kabla ya utume wake. Na ilikwisha julikana kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaumba viumbe wake bure, na wala hakutelekeza. Kwa sababu, Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye elimu, Mwenye uwezo, Mwenye kurehemu. Kwa hivyo, katika hekima yake na rehema zake kwa waja wake, ni kuwa aliwatumia huyu Mtume mtukufu akiwaamrisha kumwabudu Mwingi wa Rehema peke yake, asiyekuwa na mshirika. Basi kwa kumtuma tu, mwenye akili timamu anaujua ukweli wake, nao ni dalili kubwa ya kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ama la pili, mwenye kumjua Nabii – rehema na amani ziwe juu yake – kumjua kukamilifu, na akajua siira (maisha) yake na mwenendo wake kabla ya utume na kuinukia kwake juu ya sifa kamilifu zaidi. Kisha baada ya hapo heshima yake kubwa na maadili yake yanayoshangaza watazamaji yakaongezeka. Kwa hivyo, mwenye kujua hayo na kukusanya vyema hali zake, atajua kwamba sio chochote ila ni maadili ya Manabii wakamilifu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alizifanya sifa za mtu (kitu) kuwa ushahidi mkubwa zaidi ya kuwajua wenyewe, na ukweli wao na uongo wao. Na ama la tatu ni kujua aliyoyaleta - rehema na amani ziwe juu yake.- Yale ya sheria kuu na Qur-ani Tukufu, inayojumuisha habari za kweli, maamrisho mazuri, kukataza maovu yote, na miujiza ya kuvutia. Hivyo basi, ishara zote zinaingia katika haya matatu. Kauli yake "uwe mbashiri," yani kwa mwenye kukutii kuwa atapata furaha ya duniani na ya Akhera. "Mwonyaji" kwa mwenye kukuasi kuwa atapata taabu na maangamivu ya duniani na ya Akhera. "Na wala hutaulizwa juu ya wenzi wa Moto." Yani wewe hutaulizwa juu yao. Juu yako wewe ni kufikisha (ujumbe), na juu yetu ni hisabu.
: 120 #
{وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ (120)}.
(120) Na Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya yaliyokujia katika elimu, hutapata mlinzi wala msaidizi kando na Mwenyezi Mungu.
#
{120} يخبر تعالى رسوله أنه لا يرضى منه اليهود ولا النصارى إلا باتباعه دينهم؛ لأنهم دعاة إلى الدين الذي هم عليه يزعمون أنه الهدى، فقل لهم: {إن هدى الله}؛ الذي أرسلت به {هو الهدى}؛ وأما ما أنتم عليه فهو الهوى بدليل قوله: {ولئن اتبعت أهواءهم بعد الذي جاءك من العلم ما لك من الله من ولي ولا نصير}؛ فهذا فيه النهي العظيم عن اتباع أهواء اليهود والنصارى والتشبه بهم بما يختص به دينهم. والخطاب وإن كان لرسول الله - صلى الله عليه وسلم -، فإن أمته داخلة في ذلك؛ لأن الاعتبار بعموم المعنى لا بخصوص المخاطب، كما أن العبرة بعموم اللفظ لا بخصوص السبب.
(120) Mwenyezi Mungu anamfahamisha Mtume wake kwamba Mayahudi wala Manaswara hawawi radhi naye isipokuwa kwa kufuata yeye dini yao. Kwa sababu, wao ni walinganizi kwa dini waliyo nayo, wakidai kuwa ndiyo uwongofu. Basi waambie "Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu" ambao nimetumwa nao "ndio uwongofu." Na ama yale mliyo nayo, hayo ni matamanio tu, kwa dalili ya kauli yake: "Na kama ukifuata matamanio yao baada ya yale yaliyokujia katika elimu, hutapata mlinzi wala msaidizi kando na Mwenyezi Mungu." Na hili lina katazo kubwa la kufuata matamanio ya Mayahudi na Wakristo, na kuwaiga katika yale ambayo ni mahususi kwa dini yao. Na ijapokuwa kauli (hii) ni ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake, - umma wake unaingia katika hayo. Kwa sababu, mazingatio ni katika ujumla wa maana, na sio katika umaalumu wa anayeambiwa. Kama vile mazingatio ni katika ujumla wa tamko, na sio katika umahususi wa sababu.
Kisha akasema:
: 121 - 123 #
{الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ وَمَنْ يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ (121) يَابَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ (122) وَاتَّقُوا يَوْمًا لَا تَجْزِي نَفْسٌ عَنْ نَفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنْفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنْصَرُونَ (123)}.
(121) Wale tuliowapa Kitabu, wanakisoma kama ipasavyo kusomwa. Hao ndio kweli wanakiamini. Na wanaokikataa, basi hao ndio wenye kukhasiri. (122) Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni, na hakika Mimi nikakufadhilisheni kuliko wengineo wote. (123) Na icheni siku ambayo hatamfaa mtu mwenziwe kwa lolote, wala hakitakubaliwa kwake kikomboleo, wala maombezi hayatamfaa, wala hawatanusuriwa.
#
{121} يخبر تعالى أن الذين آتاهم الكتاب ومنَّ عليهم به منِّة مطلقة أنهم {يتلونه حق تلاوته}؛ أي: يتبعونه حق اتباعه، والتلاوة الاتِّباع، فيحلون حلاله، ويحرمون حرامه، ويعملون بمحكمه، ويؤمنون بمتشابهه، وهؤلاء هم السعداء من أهل الكتاب الذين عرفوا نعمة الله وشكروها، وآمنوا بكل الرسل ولم يفرقوا بين أحد منهم، فهؤلاء هم المؤمنون حقًّا لا من قال منهم نؤمن بما أنزل علينا ويكفرون بما وراءه، ولهذا توعدهم بقوله: {ومن يكفر به فأولئك هم الخاسرون}.
(121) Mwenyezi Mungu anafahamisha ya kwamba, wale waliojiwa na Kitabu na akawaneemesha kwacho neema isiyo na kifani, kwamba "wanakisoma kama ipasavyo kusomwa." Yani wanakifuata kwa haki ya kukifuata. Na kisomo ni kufuata. Kwa hivyo, wanahalalisha halali yake, na wanaharamisha haramu yake, na wanatenda kwa muhkam yake (Aya zenye maana wazi); na wanaamini katika Mutashabih yake (aya zisizo na maana wazi). Na hawa ndio wenye furaha miongoni mwa Watu wa Kitabu ambao walizijua neema za Mwenyezi Mungu na wakazishukuru, na wakamwamini kila Mtume, na wala hawakutofautisha baina ya yeyote miongoni mwao. Na hawa ndio Waumini wa kweli. Sio yule aliyesema miongoni mwao: Tunaamini tuliyoteremshiwa sisi, na wanayakataa yasiyokuwa hayo. Na kwa sababu ya hili, akawatishia kwa kusema: "Na wanao kikataa, basi hao ndio wenye kukhasiri."
#
{122 - 123} وقد تقدم تفسير الآية التي بعدها.
(122-123) Tafsiri ya Aya za baada yake ilikwisha tangulia mwanzo.
: 124 - 125 #
{وَإِذِ ابْتَلَى إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا قَالَ وَمِنْ ذُرِّيَّتِي قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ (124) وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى وَعَهِدْنَا إِلَى إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَنْ طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ (125)}.
(124) Na Mola wake Mlezi alipomjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza. Akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika kizazi changu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. (125) Na kumbukeni tulipoifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahali pa kukusanyikia watu na pahali pa amani. Na alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na wanaojitenga huko kwa ibada, na wanaoinama na kusujudu.
#
{124} يخبر تعالى عن عبده وخليله إبراهيم عليه السلام المتفق على إمامته وجلالته الذي كل من طوائف أهل الكتاب تدعيه، بل وكذلك المشركون أن الله ابتلاه وامتحنه بكلمات أي بأوامر ونواهٍ كما هي عادة الله في ابتلائه لعباده ليتبين الكاذب الذي لا يثبت عند الابتلاء والامتحان من الصادق، الذي ترتفع درجته، ويزيد قدره، ويزكو عمله ويخلص ذهبه، وكان من أجلِّهم في هذا المقام الخليل عليه السلام، فأتم ما ابتلاه الله به وأكمله ووفاه، فشكر الله له ذلك، ولم يزل الله شكوراً فقال: {إني جاعلك للناس إماماً}؛ أي: يقتدون بك في الهدي ويمشون خلفك إلى سعادتهم الأبدية، ويحصل لك الثناء الدائم والأجر الجزيل والتعظيم من كل أحد. وهذه ـ لعمر الله ـ أفضل درجة تنافس فيها المتنافسون، وأعلى مقام شمر إليه العاملون، وأكمل حالة حصلها أولو العزم من المرسلين وأتباعهم من كل صِدِّيق متبع لهم داعٍ إلى الله وإلى سبيله، فلما اغتبط إبراهيم بهذا المقام، وأدرك هذا، طلب ذلك لذريته لتعلو درجته ودرجة ذريته، وهذا أيضاً من إمامته ونصحه لعباد الله ومحبته أن يكثر فيهم المرشدون، فلله عظمة هذه الهمم العالية والمقامات السامية. فأجابه الرحيم اللطيف وأخبر بالمانع من نيل هذا المقام فقال: {لا ينال عهدي الظالمين}؛ أي: لا ينال الإمامة في الدين من ظلم نفسه وضرها وحطَّ قدرها لمنافاة الظلم لهذا المقام، فإنه مقام آلته الصبر واليقين، ونتيجته أن يكون صاحبه على جانب عظيم من الإيمان والأعمال الصالحة والأخلاق الجميلة والشمائل السديدة والمحبة التامة والخشية والإنابة، فأين الظلم وهذا المقام؟ ودلَّ مفهوم الآية أن غير الظالم سينال الإمامة، ولكن مع إتيانه بأسبابها.
(124) Mwenyezi Mungu anafahamisha kuhusu mja wake na rafiki mwendani wake Ibrahim, amani iwe juu yake, ambaye imekubaliwa juu ya Uimamu wake na utukufu wake; ambaye kila moja ya makundi ya Watu wa Kitabu wanadai, bali hata washirikina; kwamba Mwenyezi Mungu alimjaribu na akampa mtihani kwa maneno. Yani kwa maamrisho na makatazo, kama ilivyo ada ya Mwenyezi Mungu katika kuwajaribu waja wake, ili ibainike mwongo ambaye haimariki wakati wa majaribio na mtihani kutokana na mkweli ambaye cheo chake kinapanda, heshima yake inaongezeka na matendo yake yanatakasika; na ubongo wake wake unakuwa safi. Na aliyekuwa mtukufu wao zaidi katika nafasi hii ni Al-Khalil (rafiki mwendani wa Mwenyezi Mungu), amani iwe juu yake. Yeye alitimiza yale ambayo Mwenyezi Mungu alimjaribu kwayo, akayakamilisha na kuyatimiza, kwa hivyo akamshukuru kwa hilo. Na Mwenyezi Mungu hakuacha kumshukuru, na akasema: "Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu." Yani watakufuata katika uwongofu, na watatembea nyuma yako kwenda kwa furaha yao ya milele, na unapata sifa ya kudumu; malipo makubwa na kutukuzwa na kila mtu. Na hii - ninaapa kwa umri wa Mwenyezi Mungu - ndiyo daraja bora zaidi ambayo washindani walishindania, na kituo cha juu kabisa ambacho wenye kutenda matendo walijiandaa kwa ajili yake. Na hali kamili zaidi iliyofikiwa na wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume na wafuasi wao miongoni mwa kila mkweli anayewafuata; anayelingalia kwa Mwenyezi Mungu, na kwa njia yake. Ibrahim alipokifurahia cheo hiki, na akakipata , aliomba hilo kwa ajili ya kizazi chake, ili cheo chake na cheo cha kizazi chake kiinuke. Na hili pia ni kutokana na uongozi wake na nasaha zake kwa waja wa Mwenyezi Mungu na mapenzi yake kwamba waongofu wazidi kati yao. Basi utukufu ni kwa Mwenyezi Mungu kwa hima hizi za juu, na vyeo vya hali ya juu. Kwa hivyo, Mwenye huruma, Mpole akajibu na akafahamisha juu ya kizuizi cha kupata hiki cheo, akasema: "Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu." Yani uongozi katika dini hatapewa mwenye kuidhulumu nafsi yake, akaidhuru, na akaishushia hadhi, kwa sababu, dhuluma inapingana na cheo hiki. Kwa kuwa ni cheo ambacho chombo chake ni subira na yakini. Na matokeo yake ni kwamba mwenyewe awe upande mkubwa wa imani, matendo mema, tabia nzuri, maadili sahihi, upendo kamili, hofu, na toba. Basi iko wapi dhuluma na cheo hiki? Na ufahamu wa Aya uliashiria kwamba asiyedhulumu atapata uongozi, lakini kwa kufanya sababu zake.
#
{125} ثم ذكر تعالى أنموذجاً باقياً دالاًّ على إمامة إبراهيم وهو: هذا البيت الحرام الذي جعل قصده ركناً من أركان الإسلام حاطاًّ للذنوب والآثام، وفيه من آثار الخليل وذريته ما عرف به إمامته وتُذُكِّرت به حالته فقال: {وإذ جعلنا البيت مثابة للناس}؛ أي: مرجعاً يثوبون إليه بحصول منافعهم الدينية والدنيوية، يترددون إليه ولا يقضون منه وطراً، وجعله {أمناً}؛ يأمن به كلُّ أحد حتى الوحش وحتى الجمادات كالأشجار، ولهذا كانوا في الجاهلية ـ على شركهم ـ يحترمونه أشد الاحترام ويجد أحدهم قاتل أبيه في الحرم فلا يهيجه، فلما جاء الإسلام زاده حرمة وتعظيماً وتشريفاً وتكريماً، {واتخذوا من مقام إبراهيم مصلى}؛ يحتمل أن يكون المراد بذلك المقام المعروف الذي قد جعل الآن مقابل باب الكعبة، وأن المراد بهذا ركعتا الطواف يستحب أن تكونا خلف مقام إبراهيم وعليه جمهور المفسرين ويحتمل أن يكون المقام مفرداً مضافاً فيعم جميع مقامات إبراهيم في الحج، وهي المشاعر كلها من الطواف والسعي والوقوف بعرفة ومزدلفة ورمي الجمار والنحر وغير ذلك من أفعال الحج، فيكون معنى قوله: {مصلى}؛ أي: معبداً، أي اقتدوا به في شعائر الحج، ولعل هذا المعنى أولى لدخول المعنى الأول فيه واحتمال اللفظ له. {وعهدنا إلى إبراهيم وإسماعيل}؛ أي: أوحينا إليهما وأمرناهما بتطهير بيت الله من الشرك والكفر والمعاصي ومن الرجس والنجاسات والأقذار ليكون {للطائفين}؛ فيه {والعاكفين والركع السجود}؛ أي: المصلين، قدّم الطواف لاختصاصه بالمسجد الحرام، ثم الاعتكاف لأن من شرطه المسجد مطلقاً، ثم الصلاة مع أنها أفضل لهذا المعنى، وأضاف الباري البيت إليه لفوائد: منها: أن ذلك يقتضي شدة اهتمام إبراهيم وإسماعيل بتطهيره لكونه بيت الله فيبذلان جهدهما، ويستفرغان وسعهما في ذلك. ومنها: أن الإضافة تقتضي التشريف والإكرام ففي ضمنها أمر عباده بتعظيمه وتكريمه. ومنها: أن هذه الإضافة هي السبب الجالب للقلوب إليه.
(125) Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akautaja mfano wa kudumu unaoonyesha uongozi wa Ibrahim. Nao ni Nyumba hii tukufu, ambayo amefanya kuikusudia kuwa nguzo ya Uislamu inayofuta madhambi na makosa. Na ndani yake zimo athari za Al-Khalil (Ibrahim) na kizazi chake, ambazo kwazo ulijulikana uongozi wake, na kukumbushwa kwazo hali yake, hivyo akasema: "Na kumbukeni tulipoifanya Nyumba ile (ya Alkaaba) iwe pahali pa kukusanyikia watu." Yani marejeo ambayo wanarejea huko ili kupata manufaa yao ya kidini na ya kidunia. Na wanarudirudi huko na wala hawamalizi huko haja zao. Na aliifanya "pahali pa amani." Kila mtu anapata amani ndani yake, hata mnyama mwitu, na hata vitu visivyo kuwa hai kama miti. Na ndiyo maana walikuwa - katika Jahiliyyah yao – pamoja na ushirikina wao – wakiiheshimu kwa heshima kubwa. Na mmoja wao akamkuta muuaji wa baba yake kwenye pahali patakatifu (Al-Haram) lakini hamsumbui. Na Uislamu ulipokuja, uliizidisha utakatifu, utukufu, cheo, na heshima. "Na alipokuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kusalia." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapo ni sehemu inayojulikana sana ambayo sasa imetengenezwa mbele ya mlango wa Al-Kaaba, na kwamba kinachokusudiwa hapa ni zile rakaa mbili za baada ya kuzunguka Al-Kaba ambazo inapendekezwa kwamba ziwe nyuma ya Maqam Ibrahim (alipo kuwa akisimama Ibrahim). Na haya ndiyo maoni ya wengi wa wafasiri. Na inawezekana kwamba maqam ni ya (neno la) umoja lililounganishwa (na neno Ibrahim) basi likawa linajumuisha maeneo yote aliyosimama Ibrahim katika Hijja. Nayo ni Masha'ir (mambo takatifu) yote kama vile kuzunguka kando ya Al-Kaba, kufanya Sa'yi kati ya vilima vya Swafa na Marwa, na kusimama 'Arafa na Muzdalifah; na kurusha vijiwe kwenye Jamarat, na kuchinja na vitendo vinginevyo vya Hijja. Hivyo, inakuwa maana ya kauli yake "pawe pa kuswalia" yani mahali pa ibada. Yani mfuateni (Ibrahim) katika matendo takatifu ya Hijja. Na huenda maana hii ndiyo inayofaa zaidi kwa sababu maana ya kwanza inaigia humo, na kwa sababu neno hili linaweza kuwa na maana hii. "Na tulimwagiza Ibrahim na Ismail." yani tuliwateremshia wahyi na tukawaamrisha kuisafisha Nyumba ya Mwenyezi Mungu kutokana na ushirikina, ukafiri, maasia, na uchafu, najisi, na yasiyokuwa safi; ili iwe "kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kut'ufu" humo "na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanaoinama na kusujudu." Yani wanaoswali. Na alitaja Twawaf (kuzunguka kando ya Al-Kaba) kwanza kwa sababu ni mahsusi kwa Msikiti Mtakatifu. Kisha Itikafu kwa kuwa miongoni mwa masharti yake ni kwamba iwe msikitini tu. Kisha akataja swala ingawa ndiyo bora zaidi kwa hii maana (yani sio mahususi na Nyumba hii). Na Al-Bari (Muumbaji) aliiungaanisha Nyumba na nafsi yake kwa manufaa mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba, hilo linalazimu kujali kukubwa kwa Ibrahimu na Ismaili katika kuitakasa, kwa sababu ni nyumba ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo wanafanya wawezavyo, na wanajitolea nguvu zao katika hilo. Miongoni mwake ni kwamba, huko kuunganisha kunalazimu heshima na kutukuza. Kwa hivyo, ndani yake kuna kuwaamrisha waja wake kuitukuza na kuiheshimu. Miongoni mwake ni kwamba, huku kuunganisha ndiyo sababu inayoleta nyoyo kwake.
: 126 #
{وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُمْ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ قَالَ وَمَنْ كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَى عَذَابِ النَّارِ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (126)}.
(126) "Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo, kisha nitamsukumiza kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahali pabaya mno pa kurejea.
#
{126} أي: وإذ دعا إبراهيم لهذا البيت أن يجعله الله بلداً آمناً ويرزق أهله من أنواع الثمرات، ثم قيد عليه السلام هذا الدعاء للمؤمنين تأدباً مع الله إذ كان دعاؤه الأول فيه الإطلاق، فجاء الجواب فيه مقيداً بغير الظالم، فلما دعا لهم بالرزق وقيده بالمؤمن وكان رزق الله شاملاً للمؤمن والكافر والعاصي والطائع قال تعالى: {ومن كفر}؛ أي: أرزقهم كلهم مسلمهم وكافرهم، أما المسلم فيستعين بالرزق على عبادة الله ثم ينتقل منه إلى نعيم الجنة، وأما الكافر فيتمتع فيها قليلاً، {ثم أضطره}؛ أي: ألجئه وأخرجه مكرهاً {إلى عذاب النار وبئس المصير}.
(126) Yani Ibrahim alipoiombea Nyumba hii kwamba Mwenyezi Mungu aifanye kuwa nchi yenye amani, na awaruzuku watu wake kutokana na aina za matunda. Kisha yeye, amani iwe juu yake, aliwekea hii dua kwa Waumini peke yao kwa sababu ya kuwa na adabu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa dua yake ya kwanza ilikuwa ya jumla kabisa. Basi jawabu likaja huku limewabania nje wenye kudhulumu. Kwa hivyo, alipowaombea riziki na akawikewa kwa ajili ya Muumini peke yake, na ikawa riziki ya Mwenyezi Mungu inamfikia Muumini, kafiri, muasi, na mtiifu, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na mwenye kukufuru pia" yani nitawaruzuku wote, Muislamu wao na kafiri wao. Ama Muislamu, yeye atatumia hiyo riziki katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, kisha atatoka humo kwenda kwenye neema ya Peponi. Na ama kafiri, yeye atastarehe humo kidogo "kisha nitamsukumiza," yani nitamtoa kwa lazima na kwa nguvu kwenda "kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahali pabaya mno pa kurejea."
: 127 - 129 #
{وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنْتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (127) رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِنْ ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُسْلِمَةً لَكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (128) رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ إِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (129)}
(127) Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tukubalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mwenye elimu. (128) Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma uliosilimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. (129) Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anayetokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hekima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{127} أي: واذكر إبراهيم وإسماعيل في حالة رفعهما القواعد من البيت الأساس واستمرارهما على هذا العمل العظيم، وكيف كانت حالهما من الخوف والرجاء حتى إنهما مع هذا العمل دعوا الله أن يتقبل منهما عملهما حتى يجعل فيه النفع العميم.
(127) Yani mkumbuke Ibrahim na Ismail katika hali ya kunyanyua kwao misingi ya asasi ya Nyumba, na kuendelea kwao katika kazi hizi kubwa. Na jinsi hali yao ilivyokuwa ya hofu na matumaini mpaka wao pamoja na matendo haya, walimwomba Mwenyezi Mungu kwamba ayakubali matendo yao ili afanye ndani yake manufaa ya jumla.
#
{128} ودعوا لأنفسهما وذريتهما بالإسلام الذي حقيقته خضوع القلب وانقياده لربه المتضمن لانقياد الجوارح {وأرنا مناسكنا}؛ أي: علمناها على وجه الإراءة والمشاهدة ليكون أبلغ، يحتمل أن يكون المراد بالمناسك أعمال الحج كلها كما يدل عليه السياق والمقام ويحتمل أن يكون المراد ما هو أعم من ذلك وهو الدين كله والعبادات كلها كما يدل عليه عموم اللفظ، لأن النسك التعبد، ولكن غلب على متعبدات الحج تغليباً عرفياً، فيكون حاصل دعائهما يرجع إلى التوفيق للعلم النافع والعمل الصالح. ولما كان العبد مهما كان لا بد أن يعتريه التقصير ويحتاج إلى التوبة قالا: {وتب علينا إنك أنت التواب الرحيم}.
(128) Na walijiombea nafsi zao na vizazi vyao kwamba wawe Waislamu. Ambao uhakika wake ni kunyenyekea moyo na kufuata kwake Mola wake Mlezi, ambako kunajumuisha kufuata kwa viungo. "Na utuonyeshe njia za ibada yetu," yani tufundishe hayo kwa njia ya kuonyesha na kushuhudia, ili iwe yenye kuathiri zaidi. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa na manasik ni matendo yote ya Hijja, kama inavyoashiriwa na muktadha na mahali. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni cha jumla zaidi ya hilo, nacho ni dini yote na ibada zote mbalimbali; kama inavyoashiriwa na ujumla wa neno hili. Kwa sababu, nusuk ni kuabudu, lakini limetumika sana kidesturi katika ibada mbalimbali za Hijja. Kwa hivyo, yanakuwa matokeo ya dua yao ni yenye kurudi kwa kuwezeshwa kuwa na elimu yenye manufaa na matendo mema. Na kwa vile mja, hata aweje, ni lazima apatwe na mapungufu na ahitaji kutubia, akasema, "na utusamehe. Bila shaka, Wewe ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."
#
{129} {ربنا وابعث فيهم}؛ أي: في ذريتنا {رسولاً منهم}؛ ليكون أرفع لدرجتهما ولينقادوا له وليعرفوه حقيقة المعرفة {يتلو عليهم آياتك}؛ لفظاً وحفظاً وتحفيظاً، {ويعلمهم الكتاب والحكمة}؛ معنى {ويزكيهم}؛ بالتربية على الأعمال الصالحة والتبري من الأعمال الردية التي لا تزكو النفس معها، {إنك أنت العزيز}؛ أي: القاهر لكلِّ شيء الذي لا يمتنع على قوته شيء {الحكيم}؛ الذي يضع الأشياء مواضعها، فبعزتك وحكمتك ابعث فيهم هذا الرسول. فاستجاب اللهُ لهما؛ فبعث الله هذا الرسول الكريم الذي رحم الله به ذريتهما خاصة وسائر الخلق عامة، ولهذا قال عليه الصلاة والسلام: «أنا دعوة أبي إبراهيم».
(129) "Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee kati yao," yani katika kizazi chetu "Mtume anaye tokana na wao" ili liwe la kuinua zaidi daraja zao; na ili waweze kumfuata, na ili wamjue hakika ya kumjua. "Awasomee Aya zako" kwa maneno, kuhifadhi, na kuhifadhisha "na awafundishe Kitabu na hekima" kimaana "na awatakase." Kwa kuwalea juu ya matendo mema, na kuwa mbali na matendo maovu ambayo nafsi hazitakasiki pamoja nayo. "Hakika Wewe, ndiye Mwenye nguvu," yani mwenye nguvu za kushinda kila kitu, ambaye hakiizuii nguvu zake chochote "Mwenye hekima." Ambaye huweka vitu pahali pake. Basi kwa Nguvu zako na hekima yako, mtume huyu mtume kati yao. Mwenyezi Mungu akawaitikia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamtuma Mtume huyu mtukufu ambaye kupitia kwake Mwenyezi Mungu aliirehemu dhuria yao wawili hasa, na viumbe vingine vyote kwa ujumla. Na kwa sababu hiyo, akasema, rehema na amani ziwe juu yake, “Mimi ni dua ya baba yangu Ibrahim."
Na Ibrahim alipomtukuza Mwenyezi Mungu, huku kumtukuza, na akaeleza sifa zake kamilifu, Yeye Mtukufu akasema:
: 130 - 134 #
{وَمَنْ يَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَنْ سَفِهَ نَفْسَهُ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ (130) إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ (131) وَوَصَّى بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَابَنِيَّ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ (132) أَمْ كُنْتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِنْ بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَهَكَ وَإِلَهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ (133) تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُمْ مَا كَسَبْتُمْ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ (134)}
(130) Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini, Sisi tulimteua yeye katika dunia. Na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema. (131) Na Mola wake Mlezi alipomwambia: Silimu! Alinena: Nimesilimu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. (132) Na Ibrahim akawausia wanawe hilo, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii. Basi msife ila nanyi ni Waislamu. (133) Je! Mlikuwapo yalipomfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-hak, Mungu Mmoja tu. Na sisi tunasilimu kwake. (134) Hao ni watu waliokwisha pita. Watapata waliyoyachuma, nanyi mtapata mtakayoyachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyokuwa wakiyafanya wao.
#
{130} أي: ما يرغب {عن ملة إبراهيم}؛ بعد ما عرف من فضله، {إلا من سفه نفسه}؛ أي: جهلها وامتهنها ورضي لها بالدون وباعها بصفقة المغبون كما أنه لا أرشد وأكمل ممَّن رغب في ملة إبراهيم، ثم أخبر عن حالته في الدنيا والآخرة فقال: {ولقد اصطفيناه في الدنيا}؛ أي: اخترناه ووفقناه للأعمال التي صار بها من المصطفين الأخيار، {وإنه في الآخرة لمن الصالحين}؛ الذين لهم أعلى الدرجات.
(130) Yani hajitengi "na mila ya Ibrahim" baada ya kujua katika fadhila zake, "isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu?" Yani aliipuuza, akaidhalilisha, akaikubalia kuwa duni, na akaiuza kwa mapatano ya waliopunjwa. Kama vile hakuna mwongofu na mkamilifu zaidi kuliko mwenye kuitaka mila ya Ibrahim. Kisha akaeleza kuhusu hali yake katika dunia na Akhera, akasema: "Na kwa yakini, Sisi tulimteua yeye katika dunia." Yani tulimchagua na tukamwezesha kufanya matendo ambayo kwayo aliweza kuwa miongoni mwa wateule walio bora. "Na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema." ambao wana daraja za juu zaidi.
#
{131} {إذ قال له ربُّه أسلم قال}؛ امتثالاً لربه {أسلمتُ لربِّ العالمين}؛ إخلاصاً وتوحيداً ومحبة وإنابة فكان التوحيدُ للهِ نعته، ثم ورَّثه في ذريته ووصاهم به، وجعلها كلمة باقية في عقبه، وتوارثت فيهم حتى وصلت ليعقوبَ فوصى بها بنيه.
(131) "Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu! Alinena" kwa kumfuata Mola wake Mlezi "Nimesilimu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote." kwa Ikhlasi, Tauhidi, mapenzi, na toba. Hivyo basi, ikawa kumpwekesha Mwenyezi Mungu ni sifa yake. Kisha akairithisha katika dhuria yake na akawausia hiyo (Tauhid), na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika dhuria yake, na ikarithishwa baina yao mpaka ikamfikia Yaaqub, naye (pia) akawausia wanawe hiyo.
Basi nyinyi - enyi wana wa Yaaqub - mmeusiwa nyinyi hasa na baba yenu. Kwa hivyo, inawalazimu mtii kikamilifu, na mumfuate mwisho wa Manabii. Alisema:
#
{132} {يا بني إن الله اصطفى لكم الدين}؛ أي: اختاره، وتخيره لكم رحمة بكم وإحساناً إليكم، فقوموا به، واتصفوا بشرائعه، وانصبغوا بأخلاقه حتى تستمروا على ذلك فلا يأتيكم الموت إلا وأنتم عليه، لأن من عاش على شيء مات عليه، ومن مات على شيء بعث عليه.
(132) "Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii." Yani aliichagua na akawateulia kama rehema na wema kwenu. Basi simameni kwayo, na sifikeni kwa sheria zake, na jipakeni maadili yake mpaka mdumu namna hiyo; na yasikufikieni mauti isipokuwa nyinyi mko juu yake. Kwa sababu, mwenye kuishi juu ya kitu, atakufa juu yake. Na mwenye kufa juu ya kitu, atafufuliwa juu yake.
#
{133} ولما كان اليهود يزعمون أنهم على ملة إبراهيم ومن بعده يعقوب قال تعالى منكراً عليهم: {أم كنتم شهداء}؛ أي: حضوراً {إذ حضر يعقوب الموت}؛ أي: مقدماته وأسبابه فقال لبنيه على وجه الاختبار ولتقرَّ عينُه في حياته بامتثالهم ما وصاهم به: {ما تعبدون من بعدي}؛ فأجابوه بما قرت به عينُه فقالوا: {نعبد إلهك وإله آبائك إبراهيم وإسماعيل وإسحاق إلهاً واحداً}؛ فلا نشرك به شيئاً ولا نعدل به {ونحن له مسلمون}؛ فجمعوا بين التوحيد والعمل، ومن المعلوم أنهم لم يحضروا يعقوب، لأنهم لم يوجدوا بعد، فإذا لم يحضروا، فقد أخبر الله عنه أنه وصى بنيه بالحنيفية لا باليهودية، ثم قال تعالى:
(133) Na Mayahudi walipokuwa wakidai kuwa wao wako katika mila ya Ibrahim na baada yake Yaaqub, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema huku akiwakanusha. "Je! Mlikuwapo" yani mlihudhuria "yalipomfikia Yaaqub mauti" yani vitangulizi vyake, na sababu zake. Hivyo, akawaambia wanawe katika hali ya kuwapa mtihani, na ili lifurahie jicho lake katika uhai wake kwa kufuata kwao yale aliyowausia. "Mtamuabudu nani baada yangu?" Basi wakamjibu kwa yale yaliofurahisha jicho lake, wakasema "Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-hak, Mungu Mmoja tu." Na wala hatumshirikishi na chochote, wala hatumsawazishi na chochote "na sisi tunasilimu kwake". Basi wakajumuisha baina ya Tauhid na vitendo. Na linalojulikana ni kwamba wao hawakumhudhuria Yaaqub, kwa sababu hawakuwa wemeumbwa bado. Na ikiwa hawakuhudhuria, basi Mwenyezi Mungu alikwisha waambia kuwa aliwausia watoto wake kwa Hanifiyya (kuelekea kwa Mwenyezi Mungu peke yake na kujiepusha na vinginevyo), na sio kwa Uyahudi. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
#
{134} {تلك أمة قد خلت}؛ أي: مضت {لها ما كسبت ولكم ما كسبتم}؛ أي: كلٌّ له عمله، وكلٌّ سيجازى بما فعله، لا يُؤَاخذ أحد بذنب أحد، ولا ينفع أحداً إلا إيمانه وتقواه، فاشتغالكم بهم وادعاؤكم أنكم على ملتهم والرضا بمجرد القول أمر فارغ لا حقيقة له، بل الواجب عليكم أن تنظروا حالتكم التي أنتم عليها هل تصلح للنجاة أم لا؟
(134) "Hao ni watu waliokwisha pita." Yani walikwishaondoka, "Watapata waliyoyachuma, nanyi mtapata mtakayoyachuma," yani kila mmoja wao ana matendo yake, na kila mmoja atalipwa kwa aliyoyafanya, na wala hatalipwa yeyoye kwa dhambi za yeyote, na wala haitamfaidi yeyote isipokuwa imani yake na uchamungu wake. Basi kujishughulisha kwenu nao na kudai kwenu ya kuwa nyinyi mko kwenye mila yao na kuridhia kwa maneno tu ni jambo tupu lisilo na uhakika. Bali, la wajibu kwenu ni kuangalia hali yenu mliyomo, je, inafaa kwa wokovu au hapana?
: 135 #
{وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَى تَهْتَدُوا قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ (135)}
(135) Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.
#
{135} أي: دعا كل من اليهود والنصارى المسلمين إلى الدخول في دينهم زاعمين أنهم هم المهتدون وغيرهم ضال، [قل] له مجيباً جواباً شافياً {بل}؛ نتبع {ملة إبراهيم حنيفاً}؛ أي: مقبلاً على الله معرضاً عما سواه قائماً بالتوحيد تاركاً للشرك والتنديد، فهذا الذي في اتباعه الهداية وفي الإعراض عن ملته الكفر والغواية.
(135) Yani Mayahudi na Manasara kila mmoja wao aliwalingania Waislamu kuingia katika Dini yao wakidai kuwa wao ndio walioongoka, na asiyekuwa wao ni mpotevu. "Sema" umwambie ukimjibu jibu la kutosha: "Bali" tunashika "mila ya Ibrahim mwongofu," yani aliyeelekea kwa Mwenyezi Mungu, na kumpa mgongo asiyekuwa Yeye, akisimamisha Tauhid (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), akiacha shirki na kumfanyia wenza. Basi huyu ndiye ambaye katika kumfuata kuna uwongofu, na katika kuipa mgongo dini yake ni ukafiri na kupotea.
: 136 #
{قُولُوا آمَنَّا بِاللَّهِ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنْزِلَ إِلَى إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَى وَعِيسَى وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِنْ رَبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ (136)}
(136) Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na watoto wake, na waliyopewa Musa na Isa, na pia waliyopewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi kwake tumesilimu.
#
{136} هذه الآية الكريمة قد اشتملت على جميع ما يجب الإيمان به. واعلم أن الإيمان الذي هو تصديق القلب التام بهذه الأصول، وإقراره المتضمن لأعمال القلوب والجوارح، وهو ـ بهذا الاعتبار ـ يدخل فيه الإسلام وتدخل فيه الأعمال الصالحة كلها، فهي من الإيمان وأثر من آثاره، فحيث أطلق الإيمان دخل فيه ما ذكر، وكذلك الإسلام إذا أطلق دخل فيه الإيمان، فإذا قرن بينهما كان الإيمان اسماً لما في القلب من الإقرار والتصديق، والإسلام اسماً للأعمال الظاهرة. وكذلك إذا جمع بين الإيمان والأعمال الصالحة. فقوله تعالى: {قولوا}؛ أي: بألسنتكم متواطئة عليها قلوبكم، وهذا هو القول التام المترتب عليه الثواب والجزاء، فكما أن النطق باللسان بدون اعتقاد القلب نفاق وكفر، فالقول الخالي من العمل عمل القلب عديم التأثير قليل الفائدة، وإن كان العبد يؤجر عليه إذا كان خيراً ومعه أصل الإيمان، لكن فرق بين القول المجرد والمقترن به عمل القلب. وفي قوله {قولوا}؛ إشارة إلى الإعلان بالعقيدة والصدع بها والدعوة لها، إذ هي أصل الدين وأساسه، وفي قوله {آمنا}؛ ونحوه مما فيه صدور الفعل منسوباً إلى جميع الأمة إشارة إلى أنه يجب على الأمة الاعتصام بحبل الله جميعاً والحث على الائتلاف حتى يكون داعيهم واحداً وعملهم متحداً، وفي ضمنه النهي عن الافتراق. وفيه أن المؤمنين كالجسد الواحد. وفي قوله: {قولوا آمنا بالله ... } الخ؛ دلالة على جواز إضافة الإنسان إلى نفسه الإيمان على وجه التقييد، بل على وجوب ذلك، بخلاف قوله أنا مؤمن ونحوه فإنه لا يقال إلا مقروناً بالاستثناء بالمشيئة لما فيه من تزكية النفس والشهادة على نفسه بالإيمان، فقوله: {آمنا بالله}؛ أي: بأنه واجب الوجود واحد أحد متصف بكل صفة كمال، منزه عن كل نقص وعيب، مستحق لإفراده بالعبادة كلها وعدم الإشراك به في شيء منها بوجه من الوجوه. {وما أنزل إلينا}؛ يشمل القرآن والسنة لقوله تعالى: {وأنزل الله عليك الكتاب والحكمة}؛ فيدخل فيه الإيمان بما تضمنه كتاب الله وسنة رسوله من صفات الباري وصفات رسله واليوم الآخر والغيوب الماضية والمستقبلة، والإيمان بما تضمنه ذلك من الأحكام الشرعية الأمرية وأحكام الجزاء وغير ذلك {وما أنزل إلى إبراهيم ... }؛ إلى آخر الآية، فيه الإيمان بجميع الكتب المنزلة على جميع الأنبياء، والإيمان بالأنبياء عموماً وخصوصاً ما نص عليه في الآية لشرفهم ولإتيانهم بالشرائع الكبار، فالواجب في الإيمان بالأنبياء والكتب أن يؤمن بهم على وجه العموم والشمول، ثم ما عرف منهم بالتفصيل وجب الإيمان به مفصلاً. وقوله: {لا نفرق بين أحد منهم}؛ أي: بل نؤمن بهم كلهم، هذه خاصية المسلمين التي انفردوا بها عن كلِّ من يدعي أنه على دين، فاليهود والنصارى والصابئون وغيرهم وإن زعموا أنهم يؤمنون بما يؤمنون به من الرسل والكتب فإنهم يكفرون بغيره فيفرقون بين الرسل والكتب، بعضها يؤمنون به وبعضها يكفرون به، وينقض تكذيبهم تصديقهم، فإن الرسول الذي زعموا أنهم قد آمنوا به قد صدق سائر الرسل وخصوصاً محمداً - صلى الله عليه وسلم -، فإذا كذبوا محمداً فقد كذبوا رسولهم فيما أخبرهم به فيكون كفراً برسولهم، وفي قوله: {وما أوتي النبيون من ربهم}؛ دلالة على أن عطية الدين هي العطية الحقيقية المتصلة بالسعادة الدنيوية والأخروية، لم يأمرنا أن نؤمن بما أوتي الأنبياء من الملك والمال ونحو ذلك، بل أمرنا أن نؤمن بما أعطوا من الكتب والشرائع، وفيه أن الأنبياء مبلغون عن الله ووسائط بين الله وبين خلقه في تبليغ دينه، ليس لهم من الأمر شيء. وفي قوله: {من ربهم}؛ إشارة إلى أنه من كمال ربوبيته لعباده أن ينزل عليهم الكتب ويرسل إليهم الرسل، فلا تقتضي ربوبيته تركهم سدى ولا هملاً، وإذا كان ما أوتي النبيون إنما هو من ربهم ففيه الفرق بين الأنبياء وبين من يدعي النبوة، وأنه يحصل الفرق بينهم بمجرد معرفة ما يدعون إليه، فالرسل لا يدعون إلا لخير ولا ينهون إلا عن كل شر، وكل واحد منهم يصدق الآخر ويشهد له بالحق من غير تخالف ولا تناقض لكونه من عند ربهم، {فلو كان من عند غير الله لوجدوا فيه اختلافاً كثيراً}؛ وهذا بخلاف من ادعى النبوة فلا بد أن يتناقضوا في أخبارهم وأوامرهم ونواهيهم كما يعلم ذلك من سبر أحوال الجميع وعرف ما يدعون إليه، فلما بين تعالى جميع ما يؤمن به عموماً وخصوصاً وكان القول لا يغني عن العمل قال: {ونحن له مسلمون}؛ أي: خاضعون لعظمته منقادون لعبادته بباطننا وظاهرنا مخلصون له العبادة، بدليل تقديم المعمول وهو {له}؛ على العامل وهو، {مسلمون}. فقد اشتملت هذه الآية الكريمة على إيجازها واختصارها على أنواع التوحيد الثلاثة: توحيد الربوبية، وتوحيد الألوهية، وتوحيد الأسماء والصفات. واشتملت على الإيمان بجميع الرسل وجميع الكتب، وعلى التخصيص الدال على الفضل بعد التعميم، وعلى التصديق بالقلب واللسان والجوارح والإخلاص لله في ذلك، وعلى الفرق بين الرسل الصادقين ومن ادعى النبوة من الكاذبين، وعلى تعليم الباري عباده كيف يقولون، ورحمته وإحسانه عليهم بالنعم الدينية المتصلة بسعادة الدنيا والآخرة. فسبحان من جعل كتابه تبياناً لكل شيء وهدى ورحمة لقوم يؤمنون.
(136) Hii aya tukufu inajumuisha kila kitu ambacho ni lazima kiaminewe. Na jua ya kwamba imani ambayo ni kusadiki kikamilifu kwa moyo kwa hii misingi na kukiri kwake kunakojumuisha matendo ya nyoyo na viungo, ambako - Kwa huu mtazamo - Uislamu unaingia ndani yake; na matendo mema yote yanaingia ndani yake pia. Hivyo basi, hayo ni sehemu ya imani na athari katika athari zake. Na imani (neno) inapotajwa peke yake, yale yaliyotajwa huingia ndani yake. Na vile vile Uislamu unapoatajwa peke yake, imani huingia ndani yake. Na vinapotajwa kwa pamoja, imani huwa jina kwa yale yaliyomo ndani ya moyo kama vile kukiri na kusadiki. Nao Uislamu huwa jina kwa matendo ya nje, na kadhalika ikiwa imani na matendo mema vitatajwa kwa pamoja. Basi, kauli yake Mtukufu "Semeni nyinyi," yani kwa ndimi zenu nyoyo zikiwa zinaafikiana na ndimi juu ya hayo. Na hii ndiyo kauli kamili inayosababisha thawabu na malipo. Na kama vile kutamka kwa ulimi bila ya moyo kuamini ni unafiki na ukafiri. Basi vile vile kauli isiyokuwa na vitendo, vitendo vya moyo, hayana athari, na yana manufaa faida ndogo, ingawa mja hulipwa kwa hilo ikiwa ni la heri na yeye kimsingi anaamini. Lakini tofautisha kati ya kauli tupu, na ile (kauli) iliyofungamana na matendo ya moyo. Na katika kauli yake "Semeni nyinyi" kuna ishara ya kuiweka wazi na kuitangaza itikadi (imani), na kulingania kwayo, kwani ndiyo msingi wa dini na asasi yake. Na katika kauli yake, "Tumemuamini" na mfano wake, ambayo ndani yake kuna kitendo kinachotoka kwa umma wote kuna ishara kuwa ni lazima juu ya umma kushikamana wote na kamba ya Mwenyezi Mungu, na kuuhimiza muungano ili kulingania kwao kuwe kumoja, na matendo yao yake yameungana. Na ndani yake kuna katazo la kutengana. Na ndani yake kuna kwamba Waumini ni kama mwili mmoja. Na katika kauli yake "Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu" hadi mwisho, kuna dalili ya kuruhusiwa mtu kujinasibishia nafsi yake imani kwa namna ya kubana. Bali ni lazima kufanya hivyo, kinyume na kauli yake "Mimi ni Muumini” na mfano wake. Kwa maana, haisemwi hivi isipokuwa kwa kuifungamanisha na mapenzi ya Mwenyezi Mungu (yani kusema in shaa Allah). Kwa sababu, ndani yake kuna kujitakasa nafsi na kujishuhudia mwenyewe kuwa na imani. Kwa hivyo, kauli yake;"tumemuamini Mwenyezi Mungu," yani kwamba Yeye yupo, Mmoja, Mpweke, mwenye kusifika kwa sifa zote za ukamilifu, aliyetakasika kutokana na kila upungufu na kasoro, anayestahiki kupwekeshwa na ibada zote, na kutomshirikisha na chochote katika hayo kwa njia yoyote ile. "Na yale tuliyoteremshiwa sisi" yanajumuisha Qur-ani na Sunnah kwa kauli yake Mtukufu. "Na Mwenyezi Mungu alikuteremshia Kitabu na hekima." Kwa hivyo, ikaingia ndani yake kuamini yale yaliyomo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake, miongoni mwa sifa za Muumba, sifa za Mitume wake, Siku ya Mwisho na ghaibu zilizopita na zijazo. Na kuamini yaliyomo ndani ya hayo miognoni mwa hukumu za kisheria za lazima, hukumu za adhabu na kadhalika. "Na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim" hadi mwisho wa Aya hii, ndani yake kuna imani katika vitabu vyote vilivyoteremshwa kwa Manabii wote, na kuwaamini Manabii kwa ujumla. Na pia kindani, hasa wale waliotajwa katika Aya hii kwa sababu ya heshima yao, na kwa sababu ya kuleta kwao sheria kubwa. Hivyo basi, la wajibu katika kuamini katika Manabii na Vitabu ni kuwaamini kwa namna ya ujumla, na ya kuwaingiza wote. Kisha kile kinachojulikana kuwahusu kwa undani, ni lazima kukiamini kwa undani. Na kauli yake, "hatutofautishi baina ya yeyote katika hao," yani bali sisi tunawaamini wote. Hii ni sifa ya kipekee ya Waislamu ambayo wanasifika kwayo wao tu kando na kila anayedai kuwa kwenye dini fulani. Kwa hivyo, Mayahudi, Wakristo, Masabii na wengineo, hata kama wanadai kuwa wanaamini wanayoyaamini miongoni mwa Mitume na Vitabu, wao kwa hakika wanaamini baadhi yake; na wakakufuru baadhi yake. Kwa hivyo, kukadhibisha kwao kunabatilisha kusadiki kwao. Kwa maana, Mtume ambaye walidai kuwa walimwamini, yeye aliwasadiki Mitume wote hasa Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake. Kwa hivyo, wakimkadhibisha Muhammad, basi watakuwa wamemkadhibisha Mtume wao katika yale aliyowaambia, na hilo linakuwa kumkufuru Mtume wao. Na katika kauli yake, "na pia waliyopewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi." Kuna dalili ya kuwa kipawa cha dini ndicho kipawa cha uhakika, kinachohusiana na furaha ya kidunia na ya kiakhera. Hakutuamrisha tuyaamini waliyopewa Manabii katika ufalme na mali na mfano wa hayo. Bali alituamrisha tuyaamini waliyopewa katika Vitabu na sheria. Na ndani yake kuna kwamba Manabii ni wafikishaji tu kwa niaba ya Mwenyezi Mungu, na wapatanishi baina ya Mwenyezi Mungu na viumbe vyake katika kuifikisha dini yake. Hawana lao katika hili jambo. Na katika kauli yake, "kutoka kwa Mola wao Mlezi" kuna ishara kwamba kwa sababu ya ukamilifu wa uungu wake kwa waja wake, ni kwamba awateremshie Vitabu na kuwatumia Mitume. Kwa hivyo, haifailii uungu wake kuwaacha bure au kuwapuuza. Na ikiwa walichopewa Manabii ni kutoka kwa Mola wao Mlezi, basi ndani yake kuna tafauti baina ya Manabii na wale wanaodai unabii. Na kwamba tofauti kati yao hutokea mara tu unapojua wanachokilingania. Mitume hawalinganii ila kwa heri, na wala hawakatazi isipokuwa kila shari. Na kila mmoja wao anamsadikisha mwenzake, na kumshuhudia haki bila ya kupingana wala kutenguana kwa sababu imetoka kwa Mola wao Mlezi. "Na lau kuwa imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi." Na hii ni tofauti na wale waliodai unabii. Hakuna budi watenguane katika habari zao, amri zao, na makatazo yao, kama linavyojulikana hilo kutokana na kuzichunguza hali zao wote, kikajulikana wanachokilingania. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipobainisha kila kitu ambacho mtu anapaswa kukiamini kwa ujumla na kwa namna maalumu, na ikawa kauli haitoshi bila ya vitendo, akasema, "na sisi kwake tumesilimu." Yani tunaunyenyekea ukuu wake, tunatekeleza ibada zake kwa ndani yetu na kwa nje yetu, tunamkusudia yeye tu kwa ibada zetu, kwa dalili ya kutanguliza mwathiriwa ambaye ni "kwake" kabla ya mtendaji ambaye ni, "tumesilimu". Aya hii tukufu pamoja na ufupi wake na mukhtasari wake, ilijumuisha aina tatu za Tauhidi: Tauhid Rububiyya (uungu), na Tauhid Uluhiyya (Ibada) na Tauhid Al-Asmaa was-Swifaat (majina na sifa). Na ilijumuisha kuwaamini Mitume wote na Vitabu vyote. Na inajumuisha mbinu ya kutaja cha mahususi baada ya cha jumla ili kuonyesha ubora wake (yani kile mahususi). Na inajumuisha kusadiki kwa moyo, ulimi, na viungo, na kumkusudia Mwenyezi Mungu katika hayo. Na inajumuisha kutofautisha kati ya Mitume wa kweli na wenye kudai unabii miongoni mwa waongo. Na inajumuisha ufundishaji wa Muumba kwa waja wake jinsi ya kusema, na rehema zake na wema wake juu yao kwa neema za kidini ambazo zinaungana na furaha ya duniani na ya Akhera. Hivyo, ametakasika aliyekifanya Kitabu chake kuwa cha kubainisha kila kitu, na uwongofu na rehema kwa watu wanaoamini.
: 137 #
{فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنْتُمْ بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوْا وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّهُ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (137)}
(137) Basi wakiamini kama mnavyoamini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka, basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mwenye elimu.
#
{137} أي: فإن آمن أهل الكتاب بمثل ما آمنتم به يا معشر المؤمنين من جميع الرسل، وجميع الكتب، الذين أول من دخل فيهم وأولى خاتمهم وأفضلهم محمد - صلى الله عليه وسلم -، والقرآن، وأسلموا لله وحده ولم يفرقوا بين أحد من الرسل ، {فقد اهتدوا}؛ للصراط المستقيم الموصل لجنات النعيم؛ أي فلا سبيل لهم إلى الهداية إلا بهذا الإيمان، لا كما زعموا بقولهم كونوا هوداً أو نصارى تهتدوا فزعموا أن الهداية خاصة بما كانوا عليه. والهدى: هو العلم بالحق والعمل به، وضده الضلال عن العلم، والضلال عن العمل بعد العلم وهو الشقاق الذي كانوا عليه لما تولوا وأعرضوا، فالمشاق هو الذي يكون في شقٍّ والله ورسوله في شقٍّ، ويلزم من المشاقة المحادَّة والعداوة البليغة التي من لوازمها بذل ما يقدرون عليه من أذية الرسول، فلهذا وعد الله رسوله أن يكفيه إياهم لأنه {السميع} لجميع الأصوات باختلاف اللغات على تفنن الحاجات. {العليم} بما بين أيديهم وما خلفهم بالغيب والشهادة بالظواهر والبواطن، فإذا كان كذلك كفاك الله شرهم، وقد أنجز الله لرسوله وعده، وسلطه عليهم حتى قتل بعضهم، وسبى بعضهم، وأجلى بعضهم، وشردهم كل مشرد، ففيه معجزة من معجزات القرآن وهو الإخبار بالشيء قبل وقوعه فوقع طبق ما أخبر.
(137) Yani ikiwa Watu wa Kitabu wataamini kama mnavyoamini nyinyi, enyi kundi la Waumini, katika Mitume wote na Vitabu vyote. Ambao wa kwanza kuingia miongoni mwao na anayefaa zaidi kuwa wa mwisho wao, na mbora wao ni Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - na Qur-ani, na wajisalimishe kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Wala wasitofautishe yeyote kati ya Mitume "itakuwa kweli wameongoka" kwenye njia iliyonyooka inayofikisha kwenye Pepo zenye neema. Yani hawana njia yoyote ya kuongoka isipokuwa kwa imani hii. Sio kama walivyodai kwa kauli yao: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Basi wakadai kuwa uwongofu ni mahususi katika yale waliyoko juu yake. Na uongofu ni kujua haki na kuitendea matendo mema. Na kinyume chake ni kupotea mbali na elimu, na kupotea mbali na matendo (mema) baada ya kuyajua. Nako ndiko kupinga walikokuwa nako walipogeuka na kukengeuka. hivyo, mpinzani ni yule ambaye anakuwa upande mmoja, naye Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika upande mwingine. Na inalazimu kutokana na upinzani, kuwepo uadui mkubwa ambao unalazimu kufanya iwezekanavyo kumuudhi Mtume. Kwa sababu ya hilo, Mwenyezi Mungu alimwahidi Mtume wake kwamba atamtosheleza kutokana nao, kwa maana, Yeye ndiye "Msikizi" wa sauti zote katika lugha mbalimbali kwa mahitaji tofauti tofauti. "Mwenye elimu (Mjuzi)" wa yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao katika yaliyofichika na yale yanayoonekana, ya dhahiri na ya ndani (yaliyofichika). Na ikiwa hivyo, basi Mwenyezi Mungu atakulinda na shari yao. Na Mwenyezi Mungu alimtimizia Mtume wake ahadi yake, na akampa nguvu juu yao mpaka akawauwa baadhi yao, na akawateka baadhi yao, na akawatoa baadhi yao, na akawakimbiza kila pande zote. Basi ndani yake kuna muujiza miongoni mwa miujiza ya Qur-ani, ambao ni kupeana habari ya jambo kabla halijatokea, kisha likatokea kwa mujibu wa ilivyosema.
: 138 #
{صِبْغَةَ اللَّهِ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ صِبْغَةً وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ (138)}
(138) Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu. Na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.
#
{138} أي: الزموا صبغة الله وهو دينه، وقوموا به قياماً تامًّا بجميع أعماله الظاهرة والباطنة وجميع عقائده في جميع الأوقات حتى يكون لكم صبغة وصفة من صفاتكم، فإذا كان صفة من صفاتكم أوجب ذلك لكم الانقياد لأوامره طوعاً واختياراً ومحبة، وصار الدين طبيعة لكم بمنزلة الصبغ التام للثوب الذي صار له صفة، فحصلت لكم السعادة الدنيوية والأخروية لحثِّ الدين على مكارم الأخلاق ومحاسن الأعمال ومعالي الأمور. فلهذا قال على سبيل التعجب المتقرر للعقول الزكية؛ {ومن أحسن من الله صبغة}؛ أي: لا أحسن صبغة من صبغته ، وإذا أردت أن تعرف نموذجاً يبين لك الفرق بين صبغة الله وبين غيرها من الصبغ فقس الشيء بضده، فكيف ترى في عبد آمن بربه إيماناً صحيحاً أثر معه خضوع القلب وانقياد الجوارح، فلم يزل يتحلى بكل وصف حسن وفعل جميل وخلق كامل ونعت جليل، ويتخلى من كل وصف قبيح ورذيلة وعيب فَوَصْفُهُ الصدق في قوله وفعله والصبر والحلم والعفة والشجاعة والإحسان القولي والفعلي ومحبة الله وخشيته وخوفه ورجاؤه، فحاله الإخلاص للمعبود والإحسان لعبيده، فقسه بعبد كفر بربه وشرد عنه وأقبل على غيره من المخلوقين فاتصف بالصفات القبيحة من الكفر والشرك والكذب والخيانة والمكر والخداع وعدم العفة والإساءة إلى الخلق في أقواله وأفعاله فلا إخلاص للمعبود ولا إحسان إلى عبيده؛ فإنه يظهر لك الفرق العظيم بينهما، ويتبين لك أنه لا أحسن [صبغة] من صبغة الله، وفي ضمنه أنه لا أقبح صبغة ممن انصبغ بغير دينه. وفي قوله: {ونحن له عابدون}؛ بيان لهذه الصبغة وهي القيام بهذين الأصلين الإخلاص والمتابعة؛ لأن العبادة: اسم جامع لكل ما يحبه الله ويرضاه من الأعمال والأقوال الظاهرة والباطنة، ولا تكون كذلك حتى يشرعها الله على لسان رسوله. والإخلاص أن يقصد العبد وجه الله وحده في تلك الأعمال، فتقديم المعمول يؤذن بالحصر، وقال: {ونحن له عابدون}؛ فوصفهم باسم الفاعل الدال على الثبوت والاستقرار؛ ليدلَّ على اتصافهم بذلك [وكونه صار صبغةً لهم ملازماً].
(138) Yani shikamaneni na upakaji rangi wa Mwenyezi Mungu ambao ni Dini Yake, na isimamisheni kusimama kukamilifu kwa matendo yake yote ya dhahiri na ya yaliyofichika, na itikadi zake zote katika nyakati zote ili muwe na upakaji rangi na sifa moja katika sifa zenu. Na ikiwa ni sifa katika sifa zenu, hilo litawaletea kufuata amri zake kwa hiari, na mapenzi, na dini inakuwa asili yenu kama kupaka rangi nguo kamili ambako kumekuwa sifa yake, basi mkapata furaha ya kidunia na ya kiakhera kwa sababu Dini inahimiza maadili mema, matendo mazuri, na mambo ya juu. Ndio maana akasema kwa njia ya mshangao unaofanya akili safi kufikiria. "Na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu?" yani hakuna aliye bora wa kupaka rangi kuliko kupaka rangi kwake. Na ukitaka kujua mfano unaokubainishia tofauti iliyopo kati ya upakaji rangi wa Mwenyezi Mungu, na upakaji rangi usiokuwa huo miongoni mwa upakaji rangi, basi kipime kitu na kinyume chake. Unaonaje katika mja aliyemuamini Mola wake Mlezi imani sahihi iliyomtia unyenyekevu wa moyo na utiifu wa viungo. Basi hajaacha kujipamba kwa kila sifa nzuri na vitendo vizuri, na tabia kamili, na maelezo matukufu. Na anaacha kila sifa mbaya na mbovu, na upungufu. Basi sifa yake ni ukweli katika kauli yake, na kitendo chake na subira, na ustahimilivu, na usafi, na ujasiri, na ukarimu wa kauli na matendo, na kumpenda Mwenyezi Mungu, na kumnyenyekea, na kumhofu na kumtumaini. Basi, hali yake ni ikhlasi kwa mwabudiwa wake, na wema kwa waja wake. Na mpime yeye na mja aliyemkufuru Mola wake Mlezi, na akamkimbia, na akamwelekea asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe na akasifika kwa sifa mbaya mbaya kama vile: Ukafiri, ushirikina, uwongo, khiyana, kupanga vitimbi, kuhadaa, kutokuwa safi, na kuwaudhi viumbe katika kauli yake na vitendo vyake, hivyo akawa hana ikhlasi kwa mwabudiwa wake, wala wema kwa waja wake. Basi itakudhihirikia tofauti kubwa baina yao, na ikubainikie kwamba hakuna [mwenye kupaka rangi] mbora zaidi kuliko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu. Na ndani yake ni kwamba hakuna aliye mbaya zaidi wa kupaka rangi kuliko yule aliyejipaka rangi siyo kwa dini yake. Na katika kauli yake: "Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu." Kuna kubainisha kwa huku kupaka rangi. Nako ni kutekeleza misingi hii miwili: Ikhlasi na kumfuata (Mtume). Kwa sababu, ibada ni jina linalojumuisha kila akipendacho Mwenyezi Mungu na anakiridhia katika vitendo na maneno, ya dhahiri na ya ndani (yaliyofichika). Na haiwi hivyo mpaka Mwenyezi Mungu aiweke kuwa sheria kwa ulimi wa Mtume wake. Na ikhlasi ni mja aukusudie uso wa Mwenyezi Mungu peke yake katika matendo hayo. Kwa hivyo, kumtaja kwanza mwathiriwa, inamanisha kuthibiti (kufungia sifa hizo kwake tu), na akasema "Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu." Kwa hivyo, akawaelezea kwa ismul-fail. {Yani nomino itokanayo na kitenzi, na hapa ni neno 'aabiduun (wenye kumuabudu)} inayoashiria kuimarika na kutulia, ili ionyeshe kuwa wanasifika kwa hilo (la kumwabudu) [na kwamba imekuwa upakaji rangi usiofutika kwao].
: 139 #
{قُلْ أَتُحَاجُّونَنَا فِي اللَّهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُخْلِصُونَ (139)}
(139) Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.
#
{139} المحاجة: هي المجادلة بين اثنين فأكثر تتعلق في المسائل الخلافية حتى يكون كل من الخصمين يريد نصرة قوله وإبطال قول خصمه، فكل واحد منهما يجتهد في إقامة الحجة على ذلك، والمطلوب منها أن تكون بالتي هي أحسن بأقرب طريق يرد الضال إلى الحق، ويقيم الحجة على المعاند، ويوضح الحق، ويبين الباطل، فإن خرجت عن هذه الأمور كانت مماراة ومخاصمة لا خير فيها، وأحدثت من الشرِّ ما أحدثت، فكان أهل الكتاب يزعمون أنهم أولى بالله من المسلمين، وهذا مجرد دعوى تفتقر إلى برهان ودليل، فإذا كان رب الجميع واحداً ليس ربًّا لكم دوننا، وكلٌّ منا ومنكم له عمله، فاستوينا نحن وأنتم بذلك، فهذا لا يوجب أن يكون أحد الفريقين أولى بالله من غيره؛ لأن التفريق مع الاشتراك في الشيء من غير فرق مؤثر دعوى باطلة، وتفريق بين متماثلين ومكابرة ظاهرة، وإنما يحصل التفضيل بإخلاص الأعمال الصالحة لله وحده، وهذه الحالة وصف المؤمنين وحدهم فتعين أنهم أولى بالله من غيرهم لأن الإخلاص هو الطريق إلى الخلاص. فهذا هو الفرق بين أولياء الرحمن وأولياء الشيطان بالأوصاف الحقيقية التي يسلمها أهل العقول ولا ينازع فيها إلا كل مكابر جهول، ففي هذه الآية إرشاد لطيف لطريق المحاجة، وأن الأمور مبنية على الجمع بين المتماثلين، والفرق بين المختلفين.
(139) Kuhojiana ni majadiliano baina ya watu wawili au zaidi kunakohusiana na masuala yenye utata, kiasi kwamba, kila mmoja wa wapinzani hao wawili anataka kuunga mkono kauli yake na kubatilisha kauli ya mpinzani wake. Hivyo basi, kila mmoja wao anajitahidi katika kusimamisha hoja juu ya hilo. Na linalotakiwa katika kuhojiana ni kwamba kuwe kwa yaliyo mema kwa njia ya karibu zaidi ambayo mpotevu anaweza kurudishwa katika haki. Na inasimamisha hoja juu ya mkaidi, na inaweka wazi haki na inabainisha batili. Na majadiliano yakitoka nje ya mambo haya, basi yanakuwa kubishana na kugombana kusikokuwa na heri ndani yake, na kunakoleta uovu kiasi kunavyoleta. Na watu wa kitabu walikuwa wanadai kwamba wao ndio wanaomstahiki zaidi Mwenyezi Mungu kuliko Waislamu. Na haya ni madai tu ambayo hayana dalili na ushahidi. Ikiwa Mola Mlezi wa watu wote ni mmoja, basi (yeye) siyo Mola Mlezi wenu tu na siyo sisi, na kila mmoja kati yetu na nyinyi ana matendo yake, basi sisi na nyinyi tunakuwa sawa katika hilo. Na hilo halilazimu kwamba moja ya makundi haya mawili limstahiki zaidi Mwenyezi Mungu kuliko lingine. Kwa sababu, kutenganisha katika vitu vinavyoshirikina katika jambo bila ya tofauti yenye kuathiri ni madai ya uwongo, na kutenganisha baina ya vitu vinavyofanana na kiburi cha dhahiri. Lakini ubora hupatikana kwa kumsafishia Mwenyezi Mungu matendo mema. Na hali ni sifa ya waumini peke yao. Kwa hivyo, ikabakia tu kwamba wao ndio wanaomstahili zaidi Mwenyezi Mungu kuliko wengine, kwa sababu kumsafishia Mwenyezi Mungu matendo ndiyo njia ya wokovu. Hii ndiyo tofauti baina ya marafiki wa Ar-rahman (Mwingi wa Rehema) na marafiki wa Shetani kwa sifa za kweli, ambazo watu wenye akili wanazikubali na wala hapingani katika hilo isipokuwa kila mwenye jeuri, mjinga. Kwa hivyo, katika aya hii, upo mwongozo mzuri mno wa njia ya kuhojiana, na kwamba mambo yamejengeka juu ya kuleta pamoja yale yanayofanana, na kutenganisha baina yale yaliyo tofauti.
: 140 #
{أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطَ كَانُوا هُودًا أَوْ نَصَارَى قُلْ أَأَنْتُمْ أَعْلَمُ أَمِ اللَّهُ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ كَتَمَ شَهَادَةً عِنْدَهُ مِنَ اللَّهِ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ (140)}
(140) Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na watoto wake walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.
#
{140} وهذه دعوى أخرى منهم ومحاجة في رسل الله زعموا أنهم أولى بهؤلاء الرسل المذكورين من المسلمين؛ فردَّ الله عليهم بقوله: {أأنتم أعلم أم الله}؛ فالله يقول: {ما كان إبراهيم يهودياً ولا نصرانياً ولكن كان حنيفاً مسلماً وما كان من المشركين}؛ وهم يقولون بل كان يهودياً أو نصرانياً، فإما أن يكونوا هم الصادقين العالمين أو يكون الله تعالى هو الصادق العالم بذلك، فأحد الأمرين متعين لا محالة، وصورة الجواب مبهم وهو في غاية الوضوح والبيان، حتى أنه من وضوحه لم يحتج أن يقول بل الله أعلم وهو أصدق، ونحو ذلك لانجلائه لكل أحد، كما إذا قيل الليل أنور أم النهار؟ والنار أحر أم الماء؟ والشرك أحسن أم التوحيد؟ ونحو ذلك، وهذا يعرفه كل من له أدنى عقل حتى أنهم بأنفسهم يعرفون ذلك ويعرفون أن إبراهيم وغيره من الأنبياء لم يكونوا هوداً ولا نصارى، فكتموا هذا العلم وهذه الشهادة، فلهذا كان ظلمهم أعظم الظلم، ولهذا قال تعالى: {ومن أظلم ممن كتم شهادة عنده من الله}؛ فهي شهادة عندهم مودعة من الله لا من الخلق فيقتضي الاهتمام بإقامتها، فكتموها وأظهروا ضدها، جمعوا بين كتم الحق وعدم النطق به وإظهار الباطل والدعوة إليه، أليس هذا أعظم الظلم؟ بلى والله وسيعاقبهم عليه أشد العقوبة، فلهذا قال: {وما الله بغافل عما تعملون}؛ بل قد أحصى أعمالهم وعدها وادَّخر لهم جزاءها، فبئس الجزاءُ جزاؤهم، وبئست النار مثوى للظالمين. وهذه طريقة القرآن في ذكر العلم والقدرة عقب الآيات المتضمنة للأعمال التي يجازى عليها، فيفيد ذلك الوعد والوعيد والترغيب والترهيب، ويفيد أيضاً ذكر الأسماء الحسنى بعد الأحكام أن الأمر الديني والجزائي أثرٌ من آثارها وموجب من موجباتها وهي مقتضية له. ثم قال تعالى:
(140) Na haya ni madai mengine kutoka kwao, na kuhojiana katika Mitume wa Mwenyezi Mungu. Walidai kuwa wao wanawastahiki zaidi Mitume hawa waliotajwa kuliko Waislamu. Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kusema: "Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu?" Mwenyezi Mungu anasema, "Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina." Nao wanasema, bali yeye alikuwa ni Myahudi au Mkristo. Basi ima hao ndio wakweli na wenye elimu (la hilo), au Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mkweli na mwenye elimu ya hilo. Kwa maana, moja ya hayo mambo mawili ni hakika na hakuna njia nyingine. Na sura ya jibu siyo bayana. Lakini liko wazi na bainifu kabisa, kiasi kwamba kutokana na uwazi wake hakuhitaji kusema kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ajuae zaidi, naye ndiye mkweli zaidi, na mfano wake, kwa sababu liko wazi kwa kila mtu. Ni kama ingesemwa: Usiku ndio unaangaza zaidi au mchana? Na mchana ndio moto zaidi au maji? Na je , ushirikina ndio bora au Tauhid? na mfano wa hayo. Na haya anayajua kila mwenye akili hata kidogo kiasi kwamba wao wenyewe wanalijua hilo, na wanajua kwamba Ibrahim na Mitume wengine hawakuwa Mayahudi wala Wakristo, kwa hivyo wakaificha elimu hii na ushahidi huu. Na kwa sababu ya hayo, dhuluma yao ilikuwa kubwa zaidi. Na kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu?" Na ni ushahidi walio nao uliowekwa kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu, siyo kutoka kwa viumbe. Kwa hivyo, inahitaji kufanya hima kuisimamisha, lakini wao wakaificha na wakadhihirisha kinyume chake. Wakakusanya kati ya kuficha haki na kutoitamka, na kuonyesha uwongo na kuulingania. Je, hii si dhuluma kubwa zaidi? Ndiyo. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, na atawaadhibu juu yake kwa adhabu kali kabisa. Ndio maana akasema: "Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo." Bali alikwishathibiti vitendo vyao na akavihisabu, na akawahifadhia ujira wake. Basi malipo mabaya zaidi ni malipo yao, na Moto ndio makazi maovu mno ya madhalimu. Na hii ndiyo njia ya Qur-ani katika kutaja elimu na uwezo (wa Mwenyezi Mungu) nyuma ya Aya zilizomo matendo ambayo yanaadhibiwa juu yake. Basi hilo linamaanisha ahadi, maonyo, vitisho na kuhofisha. Na pia kutaja Majina mazuri (ya Mwenyezi Mungu) baada ya hukumu inamaanisha kwamba, amri ya kidini na ya kiadhabu ni athari katika athari zake, na yenye kuleta miongoni mwa vyenye kuleta vyake; na kwamba yanalazimu hivyo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 141 #
{تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُمْ مَا كَسَبْتُمْ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ (141)}.
(141) Hao ni watu waliokwisha pita. Wao watapata waliyoyachuma, na nyinyi mtapata mliyoyachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyokuwa wakiyafanya wao.
#
{141} تقدم تفسيرها وكررها لقطع التعلق بالمخلوقين، وإن المعول عليه ما اتصف به الإنسان لا عمل أسلافه وآبائه، فالنفع الحقيقي بالأعمال لا بالانتساب المجرد للرجال.
(141) Ilikwisha tangulia tafsiri yake, na aliirudia (hapa) ili kukata kujifungamanisha na viumbe. Na kwamba kinachotegemewa ni kile ambacho mwanadamu anasifika kwacho, siyo matendo ya watangulizi wake na baba zake. Kwa hivyo, faida halisi ni kwa matendo, siyo katika mahusiano ya kinasaba tu na watu.
#
{142} قد اشتملت الآية الأولى على معجزة وتسلية وتطمين قلوب المؤمنين واعتراض، وجوابه من ثلاثة أوجه وصفة المعترض وصفة المُسلِّم لحكم الله دينه، فأخبر تعالى أنه سيعترض السفهاء من الناس وهم الذين لا يعرفون مصالح أنفسهم بل يضيعونها ويبيعونها بأبخس ثمن وهم اليهود والنصارى ومن أشبههم من المعترضين على أحكام الله وشرائعه، وذلك أن المسلمين كانوا مأمورين باستقبال بيت المقدس مدة مقامهم بمكة ثم بعد الهجرة إلى المدينة نحو سنة ونصف لما لله [تعالى] في ذلك من الحكم التي سيشير إلى بعضها، وكانت حكمته تقتضي أمرهم باستقبال الكعبة فأخبرهم أنه لا بد أن يقول السفهاء من الناس: {ما ولاَّهم عن قبلتهم التي كانوا عليها}؛ وهي استقبال بيت المقدس أيْ: أيُّ شيء صرفهم عنه؟ وفي ذلك الاعتراض على حكم الله وشرعه وفضله وإحسانه، فسَّلاهم وأخبر بوقوعه وأنه إنما يقع ممن اتصف بالسفه قليل العقل والحلم والديانة، فلا تبالوا بهم إذ قد عُلِم مصدر هذا الكلام، فالعاقل لا يبالي باعتراض السفيه ولا يلقي له ذهنه. ودلت الآية على أنه لا يعترض على أحكام الله إلا سفيه جاهل معاند، وأما الرشيد المؤمن العاقل فيتلقى أحكام ربه بالقبول والانقياد والتسليم كما قال تعالى: {وما كان لمؤمن ولا مؤمنة إذا قضى الله ورسوله أمراً أن يكون لهم الخيرة من أمرهم}؛ {فلا وربك لا يؤمنون حتى يحكموك فيما شجر بينهم}؛ الآية {إنما كان قول المؤمنين إذا دعوا إلى الله ورسوله ليحكم بينهم أن يقولوا سمعنا وأطعنا}؛ وقد كان في قوله السفهاء ما يغني عن رد قولهم وعدم المبالاة به، ولكنه تعالى مع هذا لم يترك هذه الشبهة حتى أزالها وكشفها مما سيعرض لبعض القلوب من الاعتراض فقال تعالى: {قل}؛ لهم مجيباً: {لله المشرق والمغرب يهدي من يشاء إلى صراط مستقيم}؛ أي: فإذا كان المشرق والمغرب ملكاً لله ليس جهة من الجهات خارجة عن ملكه ومع هذا يهدي من يشاء إلى صراط مستقيم ومنه هدايتكم إلى هذه القبلة التي هي ملة أبيكم إبراهيم فلأي شيء يعترض المعترض بتوليتكم قبلة داخلة تحت ملك الله؟ لم تستقبلوا جهة ليست ملكاً له فهذا يوجب التسليم لأمره بمجرد ذلك، فكيف وهو من فضل الله عليكم وهدايته وإحسانه أن هداكم لذلك، فالمعترض عليكم معترض على فضل الله حسداً لكم وبغياً. ولما كان قوله: {يهدي من يشاء إلى صراط مستقيم}؛ مطلقاً والمطلق يُحمَل على المقيد فإن الهداية والضلال لهما أسباب أوجبتها حكمة الله وعدله وقد أخبر في غير موضع من كتابه بأسباب الهداية التي إذا أتى بها العبد حصل له الهدى كما قال تعالى: {يهدي به الله من اتبع رضوانه سبل السلام}؛ ذكر في هذه الآية السبب الموجب لهداية هذه الأمة مطلقاً بجميع أنواع الهداية ومنَّة الله عليها فقال:
Aya ya kwanza inajumuisha muujiza, na kufariji, na kutuliza nyoyo za Waumini. Na (pia ina) pingamizi na jawabu lake kwa namna tatu, na sifa za mwenye kupinga, na sifa za anayeisalimisha dini yake kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu. Basi, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa wajinga miongoni mwa watu watapinga. Nao ni wale wasioyajua masilahi ya nafsi zao. Bali wanayapoteza na wanayauza kwa thamani ya chini kabisa. Nao ni Mayahudi na Manasara na wale wanaofanana nao miongoni mwa wanaopinga hukumu za Mwenyezi Mungu na sheria zake. Na hilo ni kwa sababu Waislamu walikuwa wameamrishwa kuielekea Baitul-Maqdis (katika) muda waliokuwa wamekaa huko Makka. Kisha baada ya kuhamia Madina - takriban mwaka mmoja na nusu - kwa sababu ya hekima za Mwenyezi Mungu katika hilo, ambazo ataashiria baadhi yake, na hekima yake ilikuwa inalazimu kuwaamrisha kuielekee Al-Kaaba. Kwa hivyo, akawajulisha kuwa hakuna budi kwamba wapumbavu katika watu watasema, "Nini kilichowageuza kutoka kibla chao walichokuwa wakikielekea?" Nako ni kuelekea Baitul-Maqdis. Yani ni kitu gani kilichowageuza kutoielekea? Na katika hilo, kuna upingamizi dhidi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na sheria yake, na fadhila yake na wema wake. Kwa hivyo, akawafariji, na akajulisha kutokea kwake. Na kwamba hilo linatokea tu kutoka kwa anayesifika kwa upumbavu, mchache wa akili, kutofahamu na dini. Basi msiwajali, kwa sababu chanzo cha hayo maneno tayari kilikwishajulikana. Kwa maana, mwenye akili timamu hajali pingamizi la mpumbavu, na wala hana wasiwasi nalo. Na Aya hii ilionyesha kuwa hazipingi hukumu za Mwenyezi Mungu isipokuwa mpumbavu, mjinga, na mkaidi. Ama Muumini mwenye busara na akili timamu, yeye huzipokea hukumu za Mola wake Mlezi kwa kuzikubali, kuzifuata, na kusalimu amri, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na hiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri katika jambo lao.” “Hapana! Ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayohitalifiana” hadi mwisho wa Aya. “Haiwi kauli ya Waumini wanapoitwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, isipokuwa ni kusema: Tumesikia, na tumetii!” Na kulikuwa katika kauli yake “wapumbavu” kinachotosheleza kuijibu kauli yao, na kutoijali. Hata hivyo, Yeye Mtukufu pamoja na hili, hakuiacha dhana hii potofu mpaka alipoiondoa na kuiweka wazi kwa sababu ya ule upinzani ambao huenda ukaingia katika baadhi ya nyoyo. Kwa hivyo, Yeye Mtukufu akasema, “Sema” ukiwajibu. “Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyonyooka.” Yani ikiwa Mashariki na Magharibi ni miliki ya Mwenyezi Mungu, na wala hakuna upande wowote katika pande zote unaotoka nje ya miliki yake .Na pamoja na hilo, Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyonyooka. Na katika hilo ni kuwaongoa nyinyi kwenye Kibla hiki ambacho ni katika mila ya baba yenu Ibrahim. Basi ni kwa kitu gani mpingani anafanya upinzani kwa sababu ya kuwaelekeza nyinyi kwenye Kibla kilichomo ndani ya miliki ya Mwenyezi Mungu? Nyinyi hamkuelekea upande usiokuwa miliki yake? Na hili, linalazimu kusalimu amri yake kwa hilo tu? Basi, itakuwa vipi ilhali katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu, na kuongoa kwake na wema wake ni kwamba aliwaongoa kwa hilo. Kwa hivyo, mwenye kuwapinga (katika hilo), basi anapinga fadhila za Mwenyezi Mungu kwa kuwahusudu na dhuluma. Na ilipokuwa kauli yake, “humwongoa amtakaye kwenye njia iliyonyooka.” Ni ya jumla (Al-Mutlaq), na cha jumla kinapaswa kueleweka kwa mujibu wa kile ambacho ni mahususi (Al-Muqayyad), basi uongofu na upotovu vina sababu ambazo ziliwekwa kwa hekima na uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Na (Mwenyezi Mungu) ameeleza katika sehemu zaidi ya moja katika Kitabu chake sababu za uwongofu. Ambazo mja akizitekeleza, basi atapata uwongofu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu. “Mwenyezi Mungu huwaongoa kwacho wenye kufuata radhi yake katika njia za salama.” Katika Aya hii, (Mwenyezi Mungu) alitaja sababu za jumla ambazo zinauletea umma huu uwongofu katika aina zote za uwongofu. Na pia wema wa Mwenyezi Mungu juu yake. Akasema:
“Na vivyo hivyo, tumewafanya muwe Umma wa wastani.” Yani waadilifu na bora. Na kitu chochote kisichokuwa cha wastani, basi hicho ni cha kando kando, na ambacho kinaingia katika hatari. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akaufanya Umma huu kuwa wastani katika mambo yote ya dini: Wastani katika Manabii - baina ya waliowainua juu kupindukia kiasi, kama vile Wakristo, na baina ya wale waliowadunisha, kama vile Mayahudi - kwa kuwaamini wote kwa namna inayostahiki. Na wastani katika Sheria, siyo kama kujifanyia ugumu kwa Mayahudi na mizigo yao, wala ulegevu wa Wakristo. Na katika mlango wa usafi na kula, wao siyo kama Mayahudi ambao haziwi swala zao sahihi isipokuwa wakiswalia katika masinagogi yao, na makanisa yao, na kwamba maji hayawasafishi kutokana na najisi. Nao pia wameharamishiwa vitu vizuri ili kuwaadhibu. Na pia siyo kama Wakristo ambao hawaoni unajisi wa chochote, na wala hawaharamishi chochote. Bali wameruhusu (kuwa chakula) chochote kinachotembea na kutambaa juu ya uso wa ardhi. Bali (Waislamu), usafi wao ndio usafi kamili zaidi na timilifu zaidi. Na Mwenyezi Mungu amewaruhusu vitu vizuri katika vyakula, vinywaji, mavazi na ndoa. Na akawaharimishia machafu katika hayo. Kwa hivyo, Umma huu una dini kamilifu zaidi, na maadili ya juu zaidi, na matendo bora zaidi. Na Mwenyezi Mungu aliwapa elimu, ustahimilivu, uadilifu, na wema ambao hakuwahi kuupa umma mwingineo. Ndio maana wakawa “Umma wa wastani,” wakamilifu wa kati na kati ili wawe “mashahidi juu ya watu”; kwa sababu ya uadilifu wao, na kuhukumu kwao kwa uadilifu. Nao watawahukumu watu wote miongoni mwa watu wa dini zote, na wala hawatahukumiwa wao na mwingine yule. Kwa hivyo, chochote ambacho Umma huu utashuhudia juu yake kuwa kinakubalika, basi hicho kitakubaliwa. Na chochote ambacho utashuhudia kuwa kinakatalika, basi hicho kitakataliwa. Na ikisemwa: Vipi itakubaliwa hukumu yao juu ya wengine, na hali ni kwamba kila mmoja wa wapinzani wawili haikubaliki kauli ya kila mmoja wao juu ya mwenziwe? Itasemwa: Kauli ya mmoja wa hao wapinzani wawili haikukubaliwa kwa sababu ya kuwepo kwa tuhuma. Ama iwapo tuhuma hiyo haipo, na uadilifu kamili ukapatikana, kama ilivyo katika umma huu, basi kinachokusudiwa ni kuhukumu kwa uadilifu na haki. Na sharti ya hayo ni kuwa na elimu na uadilifu. Na viwili hivyo vinapatikana katika umma huu. Basi ndiyo kauli yake ikakubaliwa. Na mwenye kushuku yeyote akishuku fadhila zake (umma huu), na akataka mwenye kuutakasa, basi ni yule mkamilifu zaidi wa viumbe, Nabii wao, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, “na Mtume awe shahidi juu yenu.” Na miongoni mwa ushahidi wa umma huu juu ya watu wengine ni kwamba, itakapokuwa Siku ya Kiyama, na Mwenyezi Mungu akawauliza Mitume kuhusu kufikisha kwao ujumbe, na akawauliza umma wanaowakadhibisha kuhusu hilo. Nao wakakataa kuwa Mitume waliwafikishia, basi, hao Manabii watatafuta ushahidi wa umma huu, naye Nabii wao (umma huu) atawatakasa. Na katika Aya hii, kuna ushahidi wa kwamba Ijmaa ya umma huu ni hoja ya uhakika, na kwamba wao wamehifadhiwa kutokana na kukosea kwa sababu ya ujumla wa kauli yake “wastani”. Na kama ingewezekana kuwa wanaweza kukubaliana kukosea (kupotoka), basi hawangekuwa wastani isipokuwa katika baadhi ya mambo tu. Na kauli yake “ili muwe mashahidi juu ya watu” inalazimu kwamba, wakishuhudia juu ya hukumu ya kwamba Mwenyezi Mungu aliihalalalisha au aliiharamisha, au aliifanya kuwa lazima, basi umehifadhiwa (umma huu) katika hilo. Na ndani yake kuna kwamba uadilifu ni sharti katika kuhukumu, kushuhudia, kutoa fatwa, na mfano wa hayo.
: 143 #
{وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنْتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَنْ يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّنْ يَنْقَلِبُ عَلَى عَقِبَيْهِ وَإِنْ كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّهُ وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ إِنَّ اللَّهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَحِيمٌ (143)}.
(143) Na vivyo hivyo tumewafanya muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulichokuwa juu yake isipokuwa ili tupate kumjua yule anayemfuata Mtume, na yule anayegeuka akarejea kwa visigino vyake. Na kwa yakini, hilo lilikuwa jambo kubwa isipokuwa kwa wale aliowaongoa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu kwa watu ni Mpole, Mwenye kuwarehemu.
#
{143} يقول تعالى: {وما جعلنا القبلة التي كنت عليها}؛ وهي: استقبال بيت المقدس أولاً، {إلا لنعلم}؛ أي: علماً يتعلق به الثواب والعقاب، وإلا فهو تعالى عالم بكل الأمور قبل وجودها، ولكن هذا العلم لا يعلق عليه ثواباً ولا عقاباً لتمام عدله وإقامة الحجة على عباده، بل إذا وجدت أعمالهم ترتب عليها الثواب والعقاب، أي شرعنا تلك القبلة لنعلم ونمتحن {من يتبع الرسول}؛ ويؤمن به فيتبعه على كل حال لأنه عبد مأمور مدبر، ولأنه قد أخبرت الكتب المتقدمة أنه يستقبل الكعبة فالمنصف الذي مقصوده الحق مما يزيده ذلك إيماناً وطاعة للرسول، وأما من انقلب على عقبيه وأعرض عن الحق واتبع هواه فإنه يزداد كفراً إلى كفره وحيرة إلى حيرته ويدلي بالحجة الباطلة المبنية على شبهة لا حقيقة لها {وإن كانت}؛ أي: صرفك عنها {لكبيرة}؛ أي: شاقة {إلا على الذين هدى الله}؛ فعرفوا بذلك نعمة الله عليهم وشكروا وأقروا له بالإحسان حيث وجههم إلى هذا البيت العظيم الذي فضله على سائر بقاع الأرض وجعل قصده ركناً من أركان الإسلام وهادماً للذنوب والآثام، فلهذا خفَّ عليهم ذلك وشقَّ على من سواهم. ثم قال تعالى: {وما كان الله ليضيع إيمانكم}؛ أي: ما ينبغي له ولا يليق به تعالى بل هي من الممتنعات عليه، فأخبر أنه ممتنع عليه ومستحيل أن يضيع إيمانكم، وفي هذا بشارة عظيمة لمن منَّ الله عليهم بالإسلام والإيمان بأن الله سيحفظ عليهم إيمانهم فلا يضيعه، وحفظه نوعان: حفظ عن الضياع والبطلان بعصمته لهم عن كل مفسد ومزيل له ومنقص من المحن المقلقة والأهواء الصادة، وحفظ بتنميته لهم وتوفيقهم لما يزداد به إيمانهم ويتم به إيقانهم، فكما ابتدأكم بأن هداكم للإيمان فسيحفظه لكم ويتم نعمته بتنميته وتنمية أجره وثوابه وحفظه من كل مكدر، بل إذا وجدت المحن التي المقصود منها تبيين المؤمن الصادق من الكاذب فإنها تمحص المؤمنين وتظهر صدقهم، وكأن في هذا احترازاً عما قد يقال أن قوله: {وما جعلنا القبلة التي كنت عليها إلا لنعلم من يتبع الرسول ممن ينقلب على عقبيه}؛ قد يكون سبباً لترك بعض المؤمنين إيمانهم فدفع هذا الوهم بقوله: {وما كان الله ليضيع إيمانكم}؛ بتقديره لهذه المحنة أو غيرها، ودخل في ذلك من مات من المؤمنين قبل تحويل الكعبة فإن الله لا يضيع إيمانهم لكونهم امتثلوا أمر الله وطاعة رسوله في وقتها، وطاعة الله امتثال أمره في كل وقت بحسب ذلك. وفي هذه الآية دليل لمذهب أهل السنة والجماعة أن الإيمان تدخل فيه أعمال الجوارح. وقوله: {إن الله بالنَّاسِ لرءوفٌ رحيمٌ}؛ أي: شديد الرحمة بهم عظيمها، فمن رأفته ورحمته بهم أن يُتِمَّ عليهم نعمته التي ابتدأهم بها، وأن ميز عنهم من دخل في الإيمان بلسانه دون قلبه، وأن امتحنهم امتحاناً زاد به إيمانهم وارتفعت به درجتهم، وأن وجههم إلى أشرف البيوت وأجلها.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Na hatukukifanya kibla ulichokuwa juu yake” ambacho ni kuelekea Bait Al-Maqdis mwanzoni “isipokuwa ili tupate kujua.” Yani elimu ambayo malipo na adhabu vinahusiana nayo. Vinginevyo, Yeye Mwenye Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua mambo yote kabla ya kupatikana kwake. Lakini elimu hii (ya azali) haihusiani nayo malipo wala adhabu, kwa sababu ya ukamilifu wa uadilifu wake, na kusimamisha hoja juu ya waja wake. Bali matendo yao yanapopatikana, ndio yanatokea hapo malipo na adhabu. Yani tumeiweka sheria ya kuelekea Kibla hicho ili tumjue na kumtahini “yule anayemfuata Mtume” na kumwamini. Basi akawa anamfuata katika kila hali. Kwa sababu, yeye (Mtume) ni mja tu anayeamrishwa, anayeendeshwa. Na kwa sababu vitabu vilivyotangulia vilikwishasema kuwa ataelekea Al-Ka'ba. Kwa hivyo, muadilifu ni yule ambaye lengo lake ni haki, ambayo inazidishia imani yake na kumtii Mtume. Na ama mwenye kugeukia kwa visigino vyake, akaipa mgongo haki, na akafuata matamanio yake, basi yeye atazidisha ukafiri juu ya ukafiri wake, na kuchanganyikiwa juu ya kuchanganyikiwa kwake, na ataleta hoja batili iliyojengeka juu ya dhana potofu isiyokuwa na hakika. “Na kwa yakini, hilo lilikuwa” yani kukugeuza kutoielekea “jambo kubwa” yani gumu “isipokuwa kwa wale aliowaongoa Mwenyezi Mungu.” Basi wakatambua kwa hilo neema ya Mwenyezi Mungu juu yao, na wakashukuru, na wakakiria wema wake. Kwa maana aliwaelekeza kwenye nyumba hii tukufu, ambayo aliiboresha juu ya sehemu nyinginezo za ardhi, na akafanya kuikusudia kuwa nguzo katika nguzo za Uislamu, na yenye kuyabomoa dhambi na makosa. Na kwa sababu hii, (jambo hili) liliwawia rahisi, na likawa gumu kwa wasiokuwa wao. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu.” Yani haimfailii wala haiendani na Yeye Mtukufu. Bali hilo ni miongoni mwa yasiyowezekana kwake. Kwa hivyo, akajulisha kwamba hilo haliwezekani kwake, na ni mustahili kwake kuipoteza imani yenu. Na katika hili kuna bishara njema kubwa kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwapa neema ya Uislamu na imani kwamba Mwenyezi Mungu atawahifadhia imani yao, na wala hataipoteza. Na kuihifadhi kwake ni kwa aina mbili: Kuihifadhi kutokana na kupotea na kubatilishwa, kwa kuwahifadhi kutokana na kila chenye kuiondoa, na kuipunguza miongoni mwa mitihani inayoleta wasiwasi, na matamanio yenye kuzuia. Na (pili) kuihifadhi kwa kuwakuzia imani hiyo na kuwawezesha yale ambayo imani yao itaongezeka kwayo, na kutimia kwayo yakini yao. Kama vile alivyowaanzisha kwa kuwaongoa kwenye imani, hivyo basi atawahifadhia na kuwatimizia neema yake kwa kuikuza na kukuza malipo yake na thawabu zake, na kuilinda kutokana na kila chenye kuichafua. Bali, ikipatikana mitihani ambayo imekusudiwa kubainisha Muumini wa kweli kutokana na mwongo, basi hiyo huwasafisha Waumini na kudhihirisha ukweli wao. Na ni kana kwamba katika hili kuna kuondoa kile ambacho kingesemwa kwamba kauli yake; “na hatukukifanya kibla ulichokuwa juu yake isipokuwa ili tupate kumjua yule anayemfuata Mtume na yule anayegeukia kwenye visigino vyake.” Huenda ikawa ni sababu ya baadhi ya Waumini kuacha imani yao. Kwa hivyo, akaizuia fikira hii potovu kwa kauli yake; “na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza Imani yenu,” kwa kuweka kwake mtihani huu au (mitihani) isiyokuwa huu. Na waliingia katika hilo, wale waliokufa miongoni mwa Waumini kabla ya kugeuza kwa Al-Kaaba. Kwa maana, Mwenyezi Mungu hapotezi imani yao, kwa sababu walitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na wakamtii Mtume wake katika wakati wake. Na kumtii Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza amri yake katika kila wakati ni kama hivyo. Na katika aya hii, kuna ushahidi wa dhehebu la Ahlul-Sunnah wal-Jama'a kwamba imani inajumuisha matendo ya viungo. Na kauli yake; “kwa hakika, Mwenyezi Mungu kwa watu ni Mpole, Mwenye kuwarehemu.” Yani Yeye ni mwingi wa rehema kwao. Na katika upole wake na rehema yake kwao ni kwamba aliwakamilishia neema zake juu yao ambazo aliwaanzisha nazo. Na kwamba aliwapambanua na yule aliyeingia katika Imani kwa ulimi wake tu bila ya moyo wake. Na kwamba aliwajaribu kujaribu ambako kwa sababu yake imani yao iliongezeka, na daraja zao zikapanda kwa sababu yake. Na kwamba aliwaelekeza kwenye Nyumba ya heshima kubwa zaidi na tukufu zaidi ya (nyumba) zote.
: 144 #
{قَدْ نَرَى تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنْتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِنْ رَبِّهِمْ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ (144)}
(144) Kwa yakini, tuliona unavyougeuza geuza uso wako mbinguni. Basi, tutakuelekeza kwenye Kibla unachokiridhia. Basi, elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu. Na popote mnapokuwa, zielekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika, wale waliopewa Kitabu wanajua sana kwamba hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda.
#
{144} يقول الله لنبيه: {قد نرى تقلب وجهك في السماء}؛ أي كثرة تردده في جميع جهاته شوقاً وانتظاراً لنزول الوحي باستقبال الكعبة، وقال: {وجهك}؛ ولم يقل بصرك لزيادة اهتمامه، ولأن تقليب الوجه مستلزم لتقليب البصر، {فلنُوَلِّيَنَّكَ}؛ أي: نوجهك لولايتنا إياك، {قبلة ترضاها}؛ أي: تحبها، وهي الكعبة، وفي هذا بيان لفضله وشرفه - صلى الله عليه وسلم -، حيث أن الله تعالى يسارع في رضاه. ثم صرح له باستقبالها فقال: {فولِّ وجهك شطر المسجد الحرام}؛ والوجه: ما أقبل من بدن الإنسان {وحيث ما كنتم}؛ أي: من بر وبحر شرق وغرب جنوب وشمال، {فولوا وجوهكم شطره}؛ أي: جهته، ففيها اشتراط استقبال الكعبة للصلوات كلها فرضها ونفلها، وأنه إن أمكن استقبال عينها وإلا فيكفي شطرها وجهتها، وأن الالتفات بالبدن مبطل للصلاة؛ لأن الأمر بالشيء نهي عن ضده. ولما ذكر تعالى ـ فيما تقدم ـ المعترضين على ذلك من أهل الكتاب وغيرهم وذكر جوابهم، ذكر هنا أن أهل الكتاب والعلمِ منهم يعلمون أنك في ذلك على حقٍّ واضحٍ لما يجدونه في كتبهم فيعترضون عناداً وبغياً، فإذا كانوا يعلمون بخطئهم فلا تبالوا بذلك، فإن الإنسان إنما يغمه اعتراض من اعترض عليه إذا كان الأمر مشتبهاً وكان ممكناً أن يكون معه صواب، فأما إذا تيقن أن الصواب والحق مع المعترض عليه وأن المعترض معاند عارف ببطلان قوله فإنه لا محل للمبالاة، بل يُنتظَر بالمعترض العقوبة الدنيوية والأخروية فلهذا قال تعالى: {وما الله بغافل عمَّا يعملُون}؛ بل يحفظ عليهم أعمالهم ويجازيهم عليها، وفيها وعيد للمعترضين وتسلية للمؤمنين.
(144) Mwenyezi Mungu anamwambia Nabii wake: ”Kwa yakini, tuliona unavyougeuza geuza uso wako mbinguni.” Yani kuangalia katika pande zote kwa wingi akiwa na shauku na kungojea wahyi uteremke wenye kuamrisha kuielekea Al-Ka'aba. Na alisema “uso wako”, wala hakusema ‘macho yako’, kwa sababu ya hamu yake kubwa, na kwa sababu kugeuza uso kunalazimu kugeuza macho. “Basi tutakuelekeza kwenye Kibla unachokiridhia” yani ukipendacho, nayo ni Al-Ka'aba. Na katika hili, kuna kubainisha fadhila yake na heshima yake (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaharakisha kumridhisha. Kisha akamwambia waziwazi kuielekea, akasema: “Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu.” Na Al-Wajh ni upande wa mbele wa mwili wa mwanadamu. “Na popote mnapokuwa,” yani kwenye nchi kavu na baharini, mashariki na magharibi, kusini na kaskazini, “zielekezeni nyuso zenu upande wake” yani huo mwelekeo wake. Na ndani yake, kuna sharti la kuielekea Al-Ka'aba katika swala zote za faradhi na za sunna. Na kwamba ikiwezekana kuielekea yenyewe, ni sawa, vinginevyo, inatosheleza kuelekea upande wake na mwelekeo wake. Na kwamba kugeuka kwa mwili wote kunabatilisha swala. Kwa sababu, kuamrisha jambo fulani, ni kukataza kinyume chake. Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja - katika yaliyotangulia - wale waliopinga hilo miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo, na akataja jibu alilowajibu kwalo, alitaja hapa kwamba Watu wa Kitabu na wenye elimu miongoni mwao wanajua kwamba wewe katika hilo upo kwenye haki iliyo wazi, kwa sababu ya yale wanayoyakuta katika vitabu vyao. Kwa hivyo, wanapinga kwa ukaidi na kwa dhuluma tu. Basi ikiwa wanajua kosa lao, wewe usilijali hilo. Kwani, mwanadamu huwa na dhiki kwa sababu ya upinzani wa mwenye kumpinga ikiwa jambo hilo silo lenye uwazi, na ikawa inawezekana kwamba (mpinzani) yuko sahihi. Lakini ikiwa ana yakini kwamba usahihi na ukweli uko pamoja na anayepingwa, na kwamba mwenye kupinga ni mkaidi tu na anaujua ubatilifu wa kauli yake, basi hilo si mahali pa kujali. Bali anangojewa mwenye kupinga kupata adhabu ya kidunia na ya Akhera. Kwa hivyo, ndio maana Mola Mtukufu akasema: “Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda”. Bali anawahifadhia matendo yao, na atawalipa juu yake. Na ndani yake kuna onyo la adhabu kwa wanaopinga, na kupeana faraja kwa Waumini.
: 145 #
{وَلَئِنْ أَتَيْتَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ بِكُلِّ آيَةٍ مَا تَبِعُوا قِبْلَتَكَ وَمَا أَنْتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ وَمَا بَعْضُهُمْ بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُمْ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ إِنَّكَ إِذًا لَمِنَ الظَّالِمِينَ (145)}
(145) Na hata ukiwaletea hao waliopewa Kitabu hoja za kila namna, hawatafuata Kibla chako. Wala wewe hutafuata kibla chao. Wala baadhi yao hawatafuata kibla cha wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kile kilichokufikia katika elimu, wewe kwa hakika hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
#
{145} كان النبي - صلى الله عليه وسلم - من كمال حرصه على هداية الخلق يبذل [لهم] غاية ما يقدر عليه من النصيحة ويتلطف بهدايتهم، ويحزن إذا لم ينقادوا لأمر الله، فكان من الكفار من تمرَّد عن أمر الله واستكبر على رسل الله وترك الهدى عمداً وعدواناً فمنهم اليهود والنصارى أهل الكتاب الأول الذين كفروا بمحمد عن يقين لا عن جهل؛ فلهذا أخبره الله تعالى أنك لو {أتيت الذين أتُوا الكتاب بكل آيةٍ}؛ أي: بكلِّ برهان ودليل يوضح قولك ويبين ما تدعو إليه، {ما تبعوا قبلتك}؛ أي: ما تبعوك؛ لأن اتباع القبلة دليل على اتباعه، ولأن السبب هو شأن القبلة، وإنما كان الأمر كذلك لأنهم معاندون عرفوا الحقَّ وتركوه، فالآياتُ إنما [تفيد و] ينتفع بها من يتطلب الحق وهو مشتبه عليه؛ فتوضح له الآيات البينات، وأما من جزم بعدم اتباع الحق فلا حيلة فيه، وأيضاً فإن اختلافهم فيما بينهم حاصل، وبعضهم غير تابع قبلة بعض، فليس بغريب منهم مع ذلك أن لا يتبعوا قبلتك يا محمد وهم الأعداء حقيقة الحسدة. وقوله: {وما أنت بتابع قبلتهُم}؛ أبلغ من قوله ولا تتبع؛ لأن ذلك يتضمن أنه - صلى الله عليه وسلم -، اتصف بمخالفتهم، فلا يمكن وقوع ذلك منه، ولم يقل ولو أُتُوا بكل آية؛ لأنهم لا دليل لهم على قولهم، وكذلك إذا تبين الحق بأدلته اليقينية لم يلزم الإتيان بأجوبة الشُبَه الواردة عليه؛ لأنه لا حد لها، ولأنه يعلم بطلانها للعلم بأن كلَّ ما نافى الحق الواضح فهو باطل، فيكون حل الشبه من باب التبرع. {ولئن اتَّبعت أهواءهُم}؛ إنما قال: أهواءهم ولم يقل دينهم؛ لأن ما هم عليه مجرد أهوية نفس، حتى هم في قلوبهم يعلمون أنه ليس بدين، ومن ترك الدين اتبع الهوى ولا محالة، قال تعالى: {أفرأيت من اتخذ إلهه هواه}، {من بعد ما جاءك من العلم}؛ بأنك على الحق وهم على الباطل، {إنَّك إذاً}؛ أي: إن اتبعتهم، فهذا احتراز لئلا تنفصل هذه الجملة عما قبلها ولو في الأفهام {لمن الظالمين}؛ أي: داخل فيهم ومندرج في جملتهم، وأي ظلم أعظم من ظلم من علم الحق والباطل؟ فآثر الباطل على الحق، وهذا وإن كان الخطاب له - صلى الله عليه وسلم -، فإن أمته داخلة في ذلك؛ وأيضاً فإذا كان هو - صلى الله عليه وسلم -، لو فعل ذلك ـ وحاشاه ـ صار ظالماً مع علو مرتبته وكثرة إحسانه فغيره من باب أولى وأحرى. ثم قال تعالى:
(145) Alikuwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kutokana na ukamilifu wa pupa yake ya kuwaongoza viumbe, akiwapa [wao] nasaha nyingi namna awezavyo. Na anafanya upole katika kuwaongoza, na anahuzunika wasipoifuata amri ya Mwenyezi Mungu. Basi miongoni mwa makafiri kulikuwa yule aliyeasi amri ya Mwenyezi Mungu na akawafanyia kiburi Mitume wa Mwenyezi Mungu, na akaacha uwongofu kwa makusudi na kwa uadui. Na miongoni mwao ni Mayahudi na Wakristo, watu wa Kitabu cha kwanza ambao walimkufuru Muhammad baada ya kuwa na yakini, na si kwa ujinga. Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwambia kwamba, wewe “hata ukiwaletea hao waliopewa Kitabu hoja za kila namna.” Yani kwa kila ushahidi na dalili inayobainisha kauli yako na inayobainisha unayolingania; “hawatafuata Kibla chako,” yani hawatakufuata. Kwa sababu, kufuata kibla ni dalili ya kumfuata (Mtume), na kwa kuwa sababu ni suala la kibla. Na jambo hili lilikuwa hivyo kwa sababu wao ni wakaidi walioijua haki na wakaiacha. Hivyo basi, aya (hoja) [zinamfaidisha na] ananufaika nazo anayeifuata haki hali ya kuwa haiko wazi kwake; kwa hivyo, zinambainishia Aya hizo wazi. Na ama mwenye kuweka azma ya kutofuata haki, basi huyo hana hila. Na pia imeshatokea hitilafu baina yao, na baadhi yao hawafuati kibla ya wengine. Kwa hivyo, hilo si ajabu kwao, pamoja na hayo wao kutofuata kibla chako, ewe Muhammad, na wao ndio maadui wa kweli, wenye husuda. Na kauli yake: “Wala wewe hutafuata kibla chao,” ni yenye ufasaha kuliko kauli yake ‘wala usifuate.’ Kwa sababu, hiyo ina maana kwamba yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa na sifa ya kuwapinga, hivyo basi haiwezekani kutokea hilo kutoka kwake. Na wala hakusema kwamba ‘hata wakipewa kila Aya’ kwa sababu hawana ushahidi kwa kauli yao. Na pia ikiwa ukweli utabainika kwa dalili zake za yakini, si lazima kuleta majibu ya fikira potofu zinazozijia, kwa sababu hazina kikomo. Na kwa sababu unajulikana ubatili wake kuwa inajulikana kwamba chochote chenye kupingana na ukweli ulio wazi, hicho ni batili. Kwa hivyo, linakuwa suluhisho la hizo fikira potofu ni katika mlango wa kujitolea. “Na kama ukiyafuata matamanio yao,” Yeye alisema tu ‘matamanio yao’ na wala hakusema ‘dini yao’. Kwa sababu yale waliyoko juu yake ni matamanio ya nafsi tu, hata wao wanajua nyoyoni mwao kuwa hiyo si dini. Na mwenye kuacha dini yake, atafuata matamanio, na hakuna shaka. Mola Mtukufu alisema: “Je, umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake?” (Na akasema,) “baada ya kile kilichokufikia katika elimu,” kwamba wewe uko katika haki, nao wako katika batili; “wewe kwa hakika hapo,” yani ukiwafuata. Na huku ni kuondoa ili sentensi hii isije ikatengana na ile ya kabla yake hata ikiwa ni katika ufahamu, “utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.” Yani ndani yao na kujumuishwa katika hukumu yao. Na ni dhuluma gani kubwa kuliko dhuluma ya aliyeijua haki na batili? Kisha akaipendelea batili juu ya haki. Na hili hata kama anaambiwa yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – maneno haya, umma wake umejumuishwa katika hayo. Na pia lau kuwa yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - angefanya hivyo - Mwenyezi Mungu amwepushie hilo, - utakuwa udhalimu licha ya cheo chake cha juu na wingi wa wema wake. Basi asiyekuwa yeye ndiye anayefaa zaidi (kutofuata). Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 146 - 147 #
{الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ وَإِنَّ فَرِيقًا مِنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ (146) الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ (147)}
(146) Wale tuliowapa Kitabu, wanayajua haya kama wanavyowajua watoto wao. Na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua. (147) Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka.
#
{146} يخبر تعالى أن أهل الكتاب قد تقرر عندهم وعرفوا أن محمداً رسول الله وأن ما جاء به حق وصدق، وتيقنوا ذلك كما تيقنوا أبناءهم بحيث لا يشتبهون [عليهم] بغيرهم، فمعرفتهم بمحمد - صلى الله عليه وسلم -، وصلت إلى حد لا يشكون فيه ولا يمترون. لكن فريقاً منهم وهم أكثرهم الذين كفروا به كتموا هذه الشهادة مع تيقنها وهم يعلمون، ومن أظلم ممن كتم شهادة عنده من الله وفي ضمن ذلك تسلية للرسول والمؤمنين وتحذير لهم من شرهم وشبههم، وفريق منهم لم يكتموا الحق وهم يعلمون، فمنهم من آمن به، ومنهم من كفر به جهلاً. فالعالم عليه إظهار الحق وتبيينه وتزيينه بكلِّ ما يقدر عليه من عبارة وبرهان ومثال وغير ذلك، وإبطال الباطل وتمييزه عن الحق وتشيينه وتقبيحه للنفوس بكل طريق مؤدٍّ لذلك، فهؤلاء الكاتمون عكسوا الأمر فانعكست أحوالهم.
(146) Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha ya kwamba Watu wa Kitabu imekwisha thibiti kwao na wakajua ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwamba aliyokuja nayo ni haki na ukweli. Na wakawa na yakini na hilo kama walivyo na yakini juu ya watoto wao kwa namna kwamba, hawawafananii kama watoto wengine. Basi elimu yao juu ya Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ilifikia kiwango ambacho hawana shaka ndani yake, wala hawana wasiwasi wowote. Lakini, kundi miongoni mwao, nao ndio wengi wao, ambao walimkufuru, waliuficha ushuhuda huu pamoja na kuwa na yakini juu yake hali ya kuwa wanajua. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayeficha ushahidi alionao kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Na ndani ya hayo, kuna kumfariji Mtume na Waumini, na ni kuwatahadharisha kutokana na maovu yao na fikira zao potofu. Na kundi miongoni mwao halikuificha haki hali ya kuwa wanajua. Basi, wapo miongoni mwao walioiamini, na miongoni mwao wapo walioikufuru kwa kutojua. Hivyo basi, mwanachuoni hana budi kuidhihirisha haki, kuibainisha, na kuipamba kwa kila neno awezalo, dalili, mfano, na yasiyokuwa hayo. Na kuibatilisha batili (uwongo), kuipambanua kutokana na haki, kuidhalilisha, na kuifanya kuwa mbaya katika nafsi kwa kila njia ifikishayo kwa hilo. Basi, hawa wafichaji waligeuza jambo hili, basi hali zao zikawa kinyume.
#
{147} {الحق من ربك}؛ أي: هذا الحق الذي هو أحق أن يسمى حقًّا من كلِّ شيء لما اشتمل عليه من المطالب العالية والأوامر الحسنة وتزكية النفوس وحثها على تحصيل مصالحها ودفع مفاسدها لصدوره من ربك الذي من جملة تربيته لك أن أنزل عليك هذا القرآن الذي فيه تربية العقول والنفوس وجميع المصالح، {فلا تكونن من الممترين}؛ أي: فلا يحصل لك أدنى شك وريبة فيه، بل تفكر فيه وتأمل حتى تصل بذلك إلى اليقين، لأن التفكر فيه لا محالة دافع للشك موصل لليقين.
(147) “Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi.” Yani haki hii ambayo inastahiki zaidi kuitwa haki kuliko kila kitu, kwa sababu ya kile kinachojumuisha cha mahitaji makubwa, maamrisho mazuri, utakaso wa nafsi na kuzihimiza kutafuta masilahi yake. Na kuzuia yenye kuziharibu kwa sababu, imetoka kwa Mola wako Mlezi ambaye katika jumla ya malezi yake kwako ni kwamba alikuteremshia Qur-ani hii juu yako. Ambayo ndani yake kuna malezi ya akili na nafsi, na masilahi yote. “Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka.” Yani isikupate hata chembe ndogo mno ya shaka na kusitasita juu yake. Bali tafakari juu yake na uangalie kwa makini mpaka upate yakini kwa hayo. Kwa sababu, kutafakari juu yake, bila shaka kunazuia shaka na kunafikisha kwenye yakini.
: 148 #
{وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّهُ جَمِيعًا إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (148)}
(148) Na kila mmoja anao mwelekeo anaoelekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
#
{148} أي: كل أهل دين وملة له وجهة يتوجه إليها في عبادته، وليس الشأن في استقبال القبلة فإنه من الشرائع التي تتغير بها الأزمنة والأحوال ويدخلها النسخ والنقل من جهة إلى جهة، ولكن الشأن كل الشأن في امتثال طاعة الله والتقرب إليه وطلب الزلفى عنده، فهذا هو عنوان السعادة ومنشور الولاية، وهو الذي إذا لم تتصف به النفوس حصلت لها خسارة الدنيا والآخرة، كما أنها إذا اتصفت به فهي الرابحة على الحقيقة، وهذا أمر متفق عليه في جميع الشرائع، وهو الذي خلق الله له الخلق وأمرهم به، والأمر بالاستباق إلى الخيرات قدر زائد على الأمر بفعل الخيرات، فإن الاستباق إليها يتضمن فعلها وتكميلها وإيقاعها على أكمل الأحوال والمبادرة إليها، ومن سبق في الدنيا إلى الخيرات فهو السابق في الآخرة إلى الجنات، فالسابقون أعلى الخلق درجة، والخيرات تشمل جميع الفرائض والنوافل من صلاة وصيام وزكاة وحج وعمرة وجهاد ونفع متعدٍّ وقاصر، ولما كان أقوى ما يحث النفوس على المسارعة إلى الخير وينشطها ما رتب الله عليها من الثواب قال: {أينما تكونوا يأت بكم الله جميعاً إن الله على كلِّ شيء قدير}؛ فيجمعكم ليوم القيامة بقدرته، فيجازي كل عامل بعمله؛ {ليجزي الذين أساءوا بما عملوا ويجزي الذين أحسنوا بالحسنى}. ويستدل بهذه الآية الشريفة على الإتيان بكل فضيلة يتصف بها العمل، كالصلاة في أول وقتها، والمبادرة إلى إبراء الذمة من الصيام والحجِّ والعمرة وإخراج الزكاة، والإتيان بسنن العبادات وآدابها، فلله ما أجمعها وأنفعها من آية.
(148) Yani kila watu wa dini fulani na mila fulani wana mwelekeo wanaouelekea katika ibada zao. Na jambo la muhimu si katika kukielekea kibla. Kwa sababu, ni miongoni mwa sheria ambazo hubadilishwa na nyakati na hali, na zinaingiwa na ufutaji na kugeuzwa kutoka upande mmoja hadi upande mwingine. Lakini, jambo lote kabisa ni katika kutekeleza utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwake na kutafuta ukaribu mno naye. Hiki ndicho kichwa cha furaha na hati ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Nacho ndicho ikiwa nafsi hazitasifika kwacho, basi zitapata hasara ya duniani na Akhera. Kama vile ikiwa (nafsi) zitasifika kwacho, basi hizo ndizo zenye faida kwa hakika. Na hili ni jambo lililokubaliwa katika sheria zote. Nalo ndilo ambalo Mwenyezi Mungu aliumba viumbe kwa ajili yake, na akawaamrisha kulifanya. Na amri ya kushindana kuendea mema ni kiwango cha ziada juu ya amri ya kutenda mema tu. Kwani, kushindana kuyaendea (mema), kunajumuisha kuyafanya, kuyakamilisha, na kuyatekeleza katika hali bora zaidi, na kuyakimbilia. Na mwenye kushindana katika heri duniani, basi yeye ndiye wa kwanza Akhera kwenda Peponi. Kwa hivyo, wanaoshindana ndio wa daraja la juu kabisa miongoni mwa viumbe. Nazo heri zinajumuisha mambo ya faradhi yote na ya sunna kama vile Swala, Swaumu, Zaka, Hija, 'Umra, Jihad, na manufaa yanayowafikia wengine; na yale yasiyowafikia wengine. Na kwa kuwa jambo lenye nguvu zaidi linalozihimiza nafsi kukimbilia heri na kuzitia nguvu ni yale aliyoyawekea Mwenyezi Mungu ya malipo, akasema: “Popote mlipo, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” Atawakusanya Siku ya Kiyama kwa uwezo wake, na atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake, “ili awalipe waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda, na awalipe waliotenda mema kwa wema.” Na Aya hii tukufu inatumiwa kama ushahidi wa kufanya kila jema ambalo matendo yanasifika kwalo, kama vile kuswali mwanzoni mwa wakati wake, kuharakisha kutekeleza faradhi za kufunga, Hija na 'Umra, na kutoa Zaka, na kutekeleza sunna za ibada na adabu zake. Basi ee Mwenyezi Mungu! Ni ya kujumuisha na kunufaisha kulikoje huku kwa Aya hii!
: 149 - 150 #
{وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ (149) وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنْتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ (150)}
(149) Na kokote uendako, uelekeze uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo kwa hakika ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyatenda. (150) Na kokote uendako, uelekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo, zielekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi, msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi. Na ili niwatimizie neema yangu, na ili mpate kuongoka
#
{149} أي: {ومن حيث خرجت}؛ في أسفارك وغيرها وهذا للعموم، {فولِّ وجهك شطر المسجد الحرام}؛ أي: جهته. ثم خاطب الأمة عموماً فقال:
(149) Yani, “na kokote uendako” katika safari zako na mengineyo. Na hili ni la watu wote; “uelekeze uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu.” Yani upande wake. Kisha akawaongelesha umma kwa ujumla, akasema:
#
{150} {وحيث ما كنتم فولوا وجوهكم شطره}؛ وقال: {وإنه للحق من ربك}؛ أكده بأن، واللام لئلا يقع لأحد فيه أدنى شبهة، ولئلا يظن أنه على سبيل التشهي لا الامتثال، {وما الله بغافل عما تعملون}؛ بل هو مطلع عليكم في جميع أحوالكم فتأدبوا معه وراقبوه بامتثال أوامره واجتناب نواهيه، فإن أعمالكم غير مغفول عنها بل مجازون عليها أتم الجزاء إن خيراً فخير وإن شرًّا فشر، وقال هنا: {لئلا يكون للناس عليكم حجة}؛ أي: شرعنا لكم استقبال الكعبة المشرفة لينقطع عنكم احتجاج الناس من أهل الكتاب والمشركين، فإنه لو بقي مستقبلاً لبيت المقدس لتوجهت عليه الحجة، فإن أهل الكتاب يجدون في كتابهم أن قبلته المستقرة هي الكعبة البيت الحرام، والمشركين يرون أن من مفاخرهم هذا البيت العظيم، وأنه من ملة إبراهيم، وأنه إذا لم يستقبله محمد - صلى الله عليه وسلم -، توجهت نحوه حججهم، وقالوا كيف يدَّعي أنه على ملة إبراهيم وهو من ذريته وقد ترك استقبال قبلته، فباستقبال القبلة قامت الحجة على أهل الكتاب والمشركين وانقطعت حججهم عليه، إلا من ظلم منهم؛ أي: من احتج منهم بحجة هو ظالم فيها وليس لها مستند إلا اتباع الهوى والظلم؛ فهذا لا سبيل إلى إقناعه والاحتجاج عليه، وكذلك لا معنى لجعل الشبهة التي يوردونها على سبيل الاحتجاج محلا يؤبه لها ولا يلقى لها بال، فلهذا قال تعالى: {فلا تخشوهم}؛ لأن حجتهم باطلة، والباطل كاسمه مخذول، مخذول صاحبه، وهذا بخلاف صاحب الحقِّ فإن للحق صولة وعزًّا يوجب خشية من هو معه، وأمر تعالى بخشيته التي هي رأس كل خير، فمن لم يخشَ الله؛ لم ينكف عن معصيته، ولم يمتثل أمره. وكان صرف المسلمين إلى الكعبة مما حصلت فيها فتنة كبيرة أشاعها أهل الكتاب والمنافقون والمشركون وأكثروا فيها من الكلام والشبه، فلهذا بسطها الله تعالى، وبينها أكمل بيان، وأكدها بأنواع من التأكيدات التي تضمنتها هذه الآيات. منها: الأمر بها ثلاث مرات مع كفاية المرة الواحدة. ومنها: أن المعهود أن الأمر إما أن يكون للرسول فتدخل فيه الأمة [تبعاً] أو للأمة عموماً، وفي هذه الآية أمر فيها الرسول بالخصوص في قوله: {فول وجهك}؛ والأمة عموماً في قوله: {فولوا وجوهكم}. ومنها: أنه ردَّ فيه جميع الاحتجاجات الباطلة التي أوردها أهل العناد وأبطلها شبهة شبهة كما تقدم توضيحها. ومنها: أنه قطع الأطماع من اتباع الرسول قبلة أهل الكتاب. ومنها: قوله: {وإنه للحق من ربك}؛ فمجرد إخبار الصادق العظيم كافٍ شافٍ، ولكن مع هذا قال: {وإنه للحق من ربك}. ومنها: أنه أخبر وهو العالم بالخفيات أن أهل الكتاب متقرر عندهم صحة هذا الأمر، ولكنهم يكتمون هذه الشهادة مع العلم. ولما كان توليته لنا إلى استقبال القبلة نعمة عظيمة وكان لطفه بهذه الأمة ورحمته لم يزل يتزايد وكلما شرع لهم شريعة فهي نعمة عظيمة قال: {ولأتم نعمتي عليكم}؛ فأصل النعمة الهداية لدينه بإرسال رسوله وإنزال كتابه، ثم بعد ذلك النعم المتممات لهذا الأصل لا تعد كثرة ولا تحصر منذ بعث الله رسوله إلى أن قرب رحيله من الدنيا وقد أعطاه الله من الأحوال والنعم وأعطى أمته ما أتم به نعمته عليه وعليهم وأنزل الله عليه {اليوم أكملت لكم دينكم وأتممت عليكم نعمتي ورضيت لكم الإسلام ديناً}؛ فلله الحمد على فضله الذي لا نبلغ له عدًّا فضلاً عن القيام بشكره، {ولعلكم تهتدون}؛ أي: تعلمون الحق وتعملون به، فالله تبارك وتعالى من رحمته بالعباد قد يسَّر لهم أسباب الهداية غاية التيسير ونبههم على سلوك طرقها وبينها لهم أتم تبيين حتى أن من جملة ذلك أنه يقيض للحق المعاندين له فيجادلون فيه فيتضح بذلك الحق وتظهر آياته وأعلامه، ويتضح بطلان الباطل وأنه لا حقيقة له، ولولا قيامه في مقابلة الحق لربما لم يتبين حاله لأكثر الخلق وبضدها تتبين الأشياء، فلولا الليل ما عرف فضل النهار، ولولا القبيح ما عرف فضل الحسن، ولولا الظلمة ما عرف منفعة النور، ولولا الباطل ما اتضح الحق اتضاحاً ظاهراً. فلله الحمد على ذلك.
(150) “Na popote mlipo, zielekezeni nyuso zenu upande wake.” Na akasema: “Na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi.” Alisisitiza (hilo) kwa "anna" (hakika)’ na "Laam" (hakika)’ ili isije ikaingia fikira potofu hata kidogo kwa yeyote katika hilo. Na ili isije ikadhaniwa kuwa ni kwa njia ya mwenye kutaka (tu ndiyo afanye), na sio kwa njia ya kutekeleza (amri). “Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyatenda.” Bali Yeye anawaona katika hali zenu zote. Basi kueni na adabu mbele yake, na mchungeni kwa kutekeleza maamrisho Yake na kuacha makatazo Yake. Kwani, matendo yenu hayakughafilikiwa, bali mtalipwa juu yake malipo kamilifu. Ikiwa ni ya heri, basi kwa heri. Na ikiwa ni ya shari, basi kwa shari. Na hapa alisema, “ili watu wasiwe na hoja juu yenu”. Yani tuliwawekea sheria ya kuielekea Al-Ka'aba tukufu, ili hoja za watu wa Kitabu na washirikina zisisimame juu yenu. Kwa sababu, angebakia (Mtume) akielekea Baitul-Maqdis, basi hoja ingemwelekea. Kwa sababu, watu wa Kitabu wanapata katika kitabu chao kwamba kibla chake (Mtume) kilicho imara ni Al-Ka'aba, Nyumba tukufu. Nao washirikina wanaona kwamba katika yale wanayojifakhirisha nayo ni Nyumba hii tukufu. Na kwamba ni katika mila ya Ibrahim, na kwamba ikiwa Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – hataielekea, basi hoja zao zitamwelekea, na waseme: Vipi anadai kuwa yeye yuko katika mila ya Ibrahim, naye ni katika kizazi chake, na ameacha kukielekea kibla chake? Kwa hivyo, kwa kukielekea kibla, hoja ikasimama juu ya watu wa Kitabu na washirikina, na hoja zao zikakatika juu yake; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Yani yule miongoni mwao aliyetumia hoja ambayo yeye ni dhalimu ndani yake, na wala haina msingi wowote isipokuwa kufuata matamanio na dhuluma. Basi, huyo hakuna njia ya kumshawishi na kuweka hoja dhidi yake. Na vile vile hakuna maana ya kuzifanya fikira potofu wanazozitaja kwa njia ya kuweka hoja kuwa ni mahali pa kuzingatia, wala kuzijali. Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Basi msiwaogope wao”. Kwa sababu, hoja yao ni batili. Na batili (uwongo) kama jina lake, inaachwa, na mwenyewe pia huachwa. Hili ni tofauti na mwenye haki, kwani haki ina nguvu na heshima inayomlazimu yule aliye pamoja nayo kunyenyekea. Ambako ndiko kichwa cha kila heri. Hivyo basi, asiyemnyenyekea Mwenyezi Mungu, hawezi kuacha kumuasi, na hawezi kufanya amri yake. Na kulikuwa kuwaelekeza Waislamu kwenye Al-Ka'aba miongoni mwa yale ambayo fitina kubwa ilitokea. Ambayo ilienezwa na watu wa Kitabu, wanafiki, na washirikina, na wakazidisha mazungumzo na fikira potofu katika hilo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akalipanua na akalifafanua ufafanuzi kamili kabisa. Na akalisisitiza kwa aina mbalimbali za kusisitiza ambazo Aya hizi zinajumuisha. Miongoni mwake ikiwa kuamrisha hilo mara tatu, licha ya kwamba mara moja tu ingetosha. Miongoni mwake ni kwamba inajulikana kuwa amri ima ni kwa Mtume, kisha umma uingie humo [kwa kumfuata yeye]. Au iwe kwa umma kwa ujumla. Na katika Aya hii, Mtume aliamrishwa yeye hasa katika kauli yake. "Uelekeze uso wako,” nao umma kwa ujumla katika kauli yake; “zielekezeni nyuso zenu”. Na miongoni mwake ni kwamba alijibu katika Aya hii hoja zote batili ambazo wakaidi walizileta, na akazibatilisha fikira potofu baada ya fikira potofu kama ilivyoelezwa hapo mwanzo. Na miongoni mwake ni kwamba alikata matumaini yao juu ya Mtume kukifuata kibla cha Watu wa Kitabu. Na miongoni mwake ni kauli yake: “Na hiyo kwa hakika ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi.” Basi kwa kusema tu kwa aliye Mkweli Mkuu, hilo linatosha na linaponya. Lakini pamoja na haya, akasema, “na hiyo kwa hakika ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi.” Na miongoni mwake ni kwamba alijulisha, na hali Yeye ndiye mwenye elimu ya siri zote kwamba Watu wa Kitabu walikwisha jua usahihi wa jambo hili, lakini wao wanauficha ushuhuda huu kwa kujua. Na pindi kulipokuwa kutugeuza kwake kuelekea kibla ni neema kubwa, na ukawa upole wake kwa umma huu na rehema yake haujaacha kuendelea kuongezeka. Na kila anapowawekea sheria, inakuwa neema ni kubwa. Akasema, “ili niwatimizie neema yangu.” Na asili ya neema ni uwongofu kwa dini yake kwa kumtuma Mtume wake na kuteremsha Kitabu chake. Kisha baada ya hayo, neema zinazokamilisha asili hii, ambazo hazihesabiki kwa sababu ya wingi wake. Na wala haziwekewi mipaka tangu Mwenyezi Mungu alipomtuma Mtume wake mpaka ilipokaribia kuondoka kwake duniani, na tayari Mwenyezi Mungu alikuwa ameshampa katika hali mbalimbali na neema. Na akawapa umma wake aliokamilisha kwacho neema yake juu yake na juu yao, na Mwenyezi Mungu akamteremshia,. “Leo nimewakamilishia Dini yenu, na nimewatimizia neema yangu, na nimewapendelea Uislamu uwe ndiyo Dini.” Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake, ambazo hatuzifikii kwa kuzihesabu, mbali na kuzishukuru; “ili mpate kuongoka.” Yani mnajua haki na mnaifanyia kazi. Kwani, Mwenyezi Mungu, mwingi wa baraka, Mtukufu kutokana na rehema zake kwa waja; amewafanyia wepesi sana sababu za uwongofu. Na amewatanabahisha wafuate njia zake, na akawafafanulia (hizo njia) kwa ukamilifu kabisa, kiasi kwamba miongoni mwa hayo ni kwamba anaiwekea haki wale wanaoipinga. Basi wakaijadili, kwa hivyo haki ikabainika kwa hilo, na Aya zake na ishara zake zikaonekana. Na ukabainika ubatili wa batili, na kwamba haina uhakika, na lau kuwa si kusimama kwake mbale ya haki, pengine hali yake isingebainika kwa viumbe wengi. Na kwa kinyume cha kitu, kitu hicho hubainika. Na lau kuwa siyo usiku, basi fadhila ya mchana isingejulikana. Na lau kuwa sio ubaya, basi fadhila ya wema isingejulikana. Na lau kuwa sio giza, basi faida ya nuru isingejulikana. Na lau kuwa sio batili (uwongo), basi haki isingebainika kubainika kuliko dhahiri. Basi, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa hilo.
: 151 - 152 #
{كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِنْكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُمْ مَا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ (151) فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ (152)}
(151) Kama tulivyomtuma Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anawasomea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima, na anawafundisha ambayo hamkuwa mnayajua. Basi nikumbukeni, nitawakumbuka. Na nishukuruni, wala msinikufuru.
#
{151} يقول تعالى: إن إنعامنا عليكم باستقبال الكعبة وإتمامها بالشرائع والنعم المتممة ليس ذلك ببدع من إحساننا ولا بأوله بل أنعمنا عليكم بأصول النعم ومتمماتها فأبلغها إرسالنا إليكم هذا الرسول الكريم منكم تعرفون نسبه وصدقه وأمانته وكماله ونصحه {يتلو عليكم آياتنا}؛ وهذا يعم الآيات القرآنية وغيرها، فهو يتلو عليكم الآيات المبينة للحق من الباطل والهدى من الضلال التي دلتكم أولاً على توحيد الله وكماله ثم على صدق رسوله ووجوب الإيمان به ثم على جميع ما أخبر به من المعاد والغيوب، حتى حصل لكم الهداية التامة والعلم اليقيني {ويزكيكم}؛ أي: يطهر أخلاقكم ونفوسكم بتربيتها على الأخلاق الجميلة، وتنزيهها عن الأخلاق الرذيلة، وذلك كتزكيتهم من الشرك إلى التوحيد ومن الرياء إلى الإخلاص، ومن الكذب إلى الصدق، ومن الخيانة إلى الأمانة، ومن الكبر إلى التواضع، ومن سوء الخلق، إلى حسن الخلق ومن التباغض والتهاجر والتقاطع إلى التحاب والتواصل والتوادد وغير ذلك من أنواع التزكية {ويعلمكم الكتاب}؛ أي: القرآن ألفاظه ومعانيه {والحكمة}؛ قيل هي السنة، وقيل: الحكمة معرفة أسرار الشريعة والفقه فيها وتنزيل الأمور منازلها، فيكون على هذا تعليم السنة داخلاً في تعليم الكتاب؛ لأن السنة تبين القرآن وتفسره وتعبر عنه {ويعلمكم ما لم تكونوا تعلمون}؛ لأنهم كانوا قبل بعثته في ضلال مبين لا علم ولا عمل، فكل علم أو عمل نالته هذه الأمة فعلى يده - صلى الله عليه وسلم -، وبسببه كان. فهذه النعم هي أصول النعم على الإطلاق، وهي أكبر نعم ينعم بها على عباده؛ فوظيفتهم شكر الله عليها والقيام بها، فلهذا قال تعالى:
(151) Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hakika neema yetu juu yenu kwa kuwaelekeza Al-Ka'aba na kuikamilisha kwa sheria na neema zinazokamilisha. Hilo siyo uvumbuzi mpya wa hisani yetu, wala la kwanza lake. Bali tumewaneemesha kwa misingi ya neema na yenye kuikamilisha, na ya juu yake zaidi ni kwamba, sisi tumekutumia huyu Mtume mtukufu kutoka miongoni mwenu. Mnaijua nasaba yake, ukweli wake, uaminifu wake, na ukamilifu wa nasaha yake, “anakusomeeni Aya zetu.” Na hili linajumuisha Aya za Qur-ani na mengineyo. Kwani, yeye anakusomeeni Aya zinazobainisha haki kutokana na batili, na uongofu kutokana na upotofu ambao zilikuonyesheni hapo mwanzo upweke wa Mwenyezi Mungu na ukamilifu wake. Kisha kwenye ukweli wa Mtume wake na ulazima wa kumuamini. Kisha kwenye yote aliyoyaeleza ya kufufuliwa na ghaibu, mpaka mkapata uwongofu kamili, na elimu ya yakini, “zetu na kuwatakasa.” Yani azitakase tabia zenu na nafsi zenu kwa kuzilea juu ya tabia nzuri, na kuzitakasa kutokana na maadili machafu. Na hilo ni kama kuwatakasa kutoka katika shirki hadi kwa Tauhid, na kutoka katika kujionyesha (riyaa) hadi katika ikhlas (kumwelekea Mwenyezi Mungu peke yake). Na pia kutoka kwa uongo hadi kwa ukweli, na kutoka katika khiyana hadi katika uaminifu. Na kutoka katika kiburi hadi katika unyenyekevu, na kutoka katika tabia mbaya hadi katika tabia njema, na kutoka katika chuki na kuhamana na kukatana hadi katika mapenzi, kuwasiliana, kupendana na yasiyokuwa hayo miongoni mwa aina utakaso. “Na kuwafundisha Kitabu,” yani Qur-ani, maneno yake na maana zake, “na hekima” ilisemwa kuwa ni Sunna. Na ikasemwa kuwa hekima ni kujua siri za Sheria na ufahamu wake, na kuteremsha mambo katika viwango vyake. Kwa hivyo kwa mujibu wa haya, inakuwa kufundishwa Sunna kumejumuishwa katika kufundishwa Kitabu. Kwa sababu Sunna inabainisha, inafasiri na inaieleza Qur-ani, “na kukufundisheni mliyokuwa hamyajui.” Kwa sababu kabla ya utume wake walikuwa katika upotofu ulio wazi, bila ya elimu wala vitendo. Basi kila elimu au kitendo walichopata umma huu kilikuwa kwa mikono yake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na kwa sababu yake ilikuwa hivyo. Kwa hivyo, neema hizi ndizo misingi ya neema zote. Nazo ndizo neema kubwa zaidi anazowapa waja wake. Basi kazi yao ni kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, na kuzitekeleza. Ndio maana, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
#
{152} {فاذكروني أذكركم}؛ فأمر تعالى بذكره، ووعد عليه أفضل جزاء وهو ذكره؛ لمن ذكره كما قال تعالى على لسان رسوله: «من ذكرني في نفسه ذكرته في نفسي، ومن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم» ، وذكر الله تعالى أفضله ما تواطأ عليه القلب واللسان وهو [الذكرُ] الذي يثمر معرفة الله ومحبته وكثرة ثوابه، والذكر هو رأس الشكر فلهذا أمر به خصوصاً ثم من بعده أمر بالشكر عموماً فقال: {واشكروا لي}؛ أي: على ما أنعمت عليكم بهذه النعم ودفعت عنكم صنوف النقم، والشكر يكون بالقلب إقراراً بالنعم واعترافاً، وباللسان ذكراً وثناءً، وبالجوارح طاعةً لله وانقياداً لأمره واجتناباً لنهيه، فالشكر فيه بقاء النعمة الموجودة وزيادة في النعم المفقودة، قال تعالى: {لئن شكرتم لأزيدنكم}. وفي الإتيان بالأمر بالشكر بعد النعم الدينية من العلم وتزكية الأخلاق والتوفيق للأعمال بيان أنها أكبر النعم، بل هي النعم الحقيقية التي تدوم إذا زال غيرها، وإنه ينبغي لمن وفقوا لعلم أو عمل أن يشكروا الله على ذلك ليزيدهم من فضله وليندفع عنهم الإعجاب فيشتغلوا بالشكر، ولما كان الشكر ضده الكفر نهى عن ضده فقال: {ولا تكفرون}؛ المراد بالكفر ههنا ما يقابل الشكر، فهو كفر النعم وجحدها وعدم القيام بها. ويحتمل أن يكون المعنى عامًّا فيكون الكفر أنواعاً كثيرة أعظمه الكفر بالله، ثم أنواع المعاصي على اختلاف أنواعها وأجناسها من الشرك فما دونه.
(152) “Basi nikumbukeni nitakukumbukeni.” Basi Mola Mtukufu akaamrisha kumkumbuka, na akaahidi malipo bora zaidi juu yake, ambayo ni kukumbuka kwake mwenye kumkumbuka. Kama alivyosema Mtukufu juu ya ulimi wa Mtume wake. “Mwenye kunikumbuka katika nafsi yake, basi mimi natamkumbuka katika nafsi yangu. Na mwenye kunikumbuka katika mkusanyiko, nitamkumbuka katika mkusanyiko bora kuliko wao.” Na kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko bora zaidi ni kule ambako moyo na ulimi vimekubaliana ju yake. Nako ndiko [kukumbuka] ambako kunaoleta kumjua Mwenyezi Mungu, kumpenda, na wingi wa malipo yake. Na kukumbuka ndiko kichwa cha shukurani. Ndio maana akaliamrisha hilo hasa, kisha baada yake akaamrisha kushukuru kwa ujumla, akasema, “na nishukuruni”. Yani kwa yale niliyokuneemesheni kwa neema hizi, na nikawaondolea kila aina ya maovu. Na kushukuru kunakuwa pia kwa moyo kwa kukiri na kutambua neema. Na kwa ulimi kwa kutaja na kusifu. Na kwa viungo kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kutekeleza amri zake na kuacha makatazo yake. Na katika kushukuru kuna kuendelea kubakia kwa neema iliyopo, na kuongezwa neema zisizokuwepo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “mkishukuru, nitakuzidishieni.” Na katika kuweka amri ya kushukuru baada ya neema za kidini kama vile elimu, utakaso wa maadili, na na kuwezeshwa katika matendo; kuna kubainisha kuwa hizo ndizo neema kubwa zaidi. Bali ndizo neema za kihakika ambazo zinadumu zinapotoweka neema zinginezo. Na kwamba inampasa mwenye kuwezeshwa elimu au tendo fulani kwamba, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo ili awazidishie katika fadhila zake na ili kujisifu kujiepushe nao. Na pia wajishughulishe na kushukuru. Na kilipokuwa kinyume cha kushukuru ni kukufuru, akasema, “wala msinikufuru.” Na kilichokusudiwa na kukufuru hapa ni kinyume cha kushukuru, nako ni kukufuru neema na kuzikanusha na kutozitekeleza. Na inawezekana kuwa maana yake ni ya jumla, kwa hivyo kukawa kukufuru kuna aina nyingi, kubwa zaidi ikiwa ni kumkufuru Mwenyezi Mungu. Kisha aina za maasia mbalimbali na jinsi zake kama shirki na kilichoko chini yake.
: 153 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ (153)}
(153) Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swala. Hakika, Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri.
#
{153} أمر الله تعالى المؤمنين بالاستعانة على أمورهم الدينية والدنيوية {بالصبر والصلاة}؛ فالصبر هو حبس النفس وكفها على ما تكره، فهو ثلاثة أقسام: صبرها على طاعة الله حتى تؤديها، وعن معصية الله حتى تتركها، وعلى أقدار الله المؤلمة فلا تتسخطها. فالصبر هو المعونة العظيمة على كل أمر، فلا سبيل لغير الصابر أن يدرك مطلوبه، خصوصاً الطاعات الشاقة المستمرة فإنها مفتقرة أشد الافتقار إلى تحمل الصبر وتجرع المرارة الشاقة، فإذا لازم صاحبها الصبر فاز بالنجاح، وإن رده المكروه والمشقة عن الصبر والملازمة عليها لم يدرك شيئاً وحصل على الحرمان، وكذلك المعصية التي تشتد دواعي النفس ونوازعها إليها وهي في محل قدرة العبد، فهذه لا يمكن تركها إلا بصبر عظيم وكف لدواعي قلبه ونوازعها لله تعالى واستعانة بالله على العصمة منها فإنها من الفتن الكبار، وكذلك البلاء الشاق خصوصاً إن استمر، فهذا تضعف معه القوى النفسانية والجسدية ويوجد مقتضاها وهو التسخط إن لم يقاومها صاحبها بالصبر لله والتوكل عليه واللجْأ إليه والافتقار على الدوام، فعلمت أن الصبر محتاج إليه العبد، بل مضطر في كل حالة من أحواله، فلهذا أمر الله تعالى به وأخبر أنه {مع الصابرين}؛ أي: مع من كان الصبر لهم خلقاً وصفة وملكة بمعونته وتوفيقه وتسديده فهانت عليهم بذلك المشاق والمكاره وسهل عليهم كل عظيم وزالت عنهم كل صعوبة، وهذه معية خاصة تقتضي محبته ومعونته ونصره وقربه وهذه منقبة عظيمة للصابرين فلو لم يكن للصابرين فضيلة إلا أنهم فازوا بهذه المعية من الله لكفى بها فضلاً وشرفاً، وأما المعية العامة فهي معية العلم والقدرة كما في قوله تعالى: {وهو معكم أينما كنتم} وهذه عامة للخلق. وأمر تعالى بالاستعانة بالصلاة لأن الصلاة هي عماد الدين ونور المؤمنين، وهي الصلة بين العبد وبين ربه، فإذا كانت صلاة العبد صلاة كاملة مجتمعاً فيها ما يلزم فيها وما يسن، وحصل فيها حضور القلب الذي هو لبها فصار العبد إذا دخل فيها استشعر دخوله على ربه ووقوفه بين يديه موقف العبد الخادم المتأدب مستحضراً لكل ما يقوله وما يفعله مستغرقاً بمناجاة ربه ودعائه، لا جرم أن هذه الصلاة من أكبر المعونة على جميع الأمور، فإن الصلاة تنهى عن الفحشاء والمنكر، ولأن هذا الحضور الذي يكون في الصلاة يوجب للعبد في قلبه وصفاً وداعياً يدعوه إلى امتثال أوامر ربه واجتناب نواهيه، هذه هي الصلاة التي أمر الله أن نستعين بها على كل شيء.
(153) Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamrisha Waumini kutafuta msaada katika mambo yao ya kidini na ya kidunia, “kwa subira na swala.” Subira ni kuishikilia nafsi na kuizuilia yale inayoyachukia. Nayo (subira) ni aina tatu: subira yake katika kumtii Mwenyezi Mungu mpaka uutekeleze (utiifu). Na (pili) kutokana na kumuasi Mwenyezi Mungu mpaka uache (kumuasi). Na (tatu) katika majaliwa ya Mwenyezi Mungu machungu mpaka usiwe na hasira nayo. Hivyo basi, subira ndio msaada mkubwa katika kila jambo. Na hakuna njia ya kupata mahitaji kwa asiyekuwa na subira; hususan mambo ya utiifu (ibada) ngumu yenye kuendelea. Kwani, hizo zinahitaji vikubwa mtu kuwa na subira na kumeza uchungu mgumu. Na ikiwa mwenyewe atashikamana na subira, atapata mafanikio. Na ikiwa atazuiwa na yenye kuchukiza na ugumu kutokuwa na subira na kushikamana nayo, hatapata chochote; na atanyimwa. Na vivyo hivyo maasia ambayo ni migumu mno misukumo ya nafsi na ni mikali mno mielekeo ya nafsi kwayo, nayo iko ndani ya uwezo wa mja. Basi hili haliwezi kuachwa isipokuwa kwa subira kubwa, na kuzuia misukumo na mwelekeo wa moyo wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; na kutafuta msaada wa Mwenyezi Mungu ili amkinge kutokana nayo. Kwani, ni katika fitina kubwa. Na vivyo hivyo majaribu magumu, haswa ikiwa inaendelea. Hapo, inadhoofika nayo nguvu za kisaikolojia na za kimwili, na yanapatikana yale yanayoletwa na hayo. Ambayo ni kughadhabika, ikiwa mwenyewe hatakabiliana nazo kwa kuwa na subira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kumtegemea, kumkimbilia, na kumhitaji daima. Kwa hivyo, umeshajua kuwa mja anahitaji subira, bali analazimika kuwa nayo kwa kila hali katika hali zake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu alimuamrisha subira, na akajulisha kuwa: “Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” Yani kwa wale ambao subira kwao ni tabia, na sifa, uwezo kwa kumsaidia, kumwezesha, na kumwongoa. Basi magumu na machukizo yakawawia rahisi kwa hayo, na kila jambo kubwa linakuwa jepesi kwao, na kila ugumu unawaondokea. Na huu ni upamoja maalumu unaolazimu mapenzi yake, msaada wake, ushindi wake, na ukaribu wake. Na haya ni malipo makubwa kwa mwenye subira. Na kama wenye subira hawangekuwa na fadhila isipokuwa kwamba waliyapata huu upamoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi ingetosha kuwa fadhila na heshima. Na ama upamoja wa jumla, huo ni upamoja wa elimu na uwezo, kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Yeye yu pamoja nanyi popote mlipo.” Na hii ni kwa viumbe vyote kwa ujumla. Na Mola Mtukufu aliamrisha kutafuta usaidizi katika swala, kwa sababu swala ndiyo nguzo ya dini, na nuru ya Waumini. Nayo ndicho kiunganishi baina ya mja na Mola wake Mlezi. Kwa hivyo ikiwa swala ya mja ni swala kamili, yenye kile kinachohitajika na kile ambacho ni Sunna, na moyo ambao ndio kiini chake ukawa umehudhuria ndani yake. Basi akawa mja anapoingia humo (katika swala), anahisi kuingia kwake kwa Mola wake Mlezi na kusimama kwake mbele yake kisimamo cha mja, mtumishi, mwenye adabu. Huku akikumbuka kila kitu anachosema na anachofanya. Huku amezama katika kuzungumza kwa faragha na Mola wake Mlezi na kumuomba, basi hapana shaka kwamba swala hii ni moja ya misaada mikubwa katika mambo yote. Kwa sababu, swala inakataza machafu na maovu. Na kwa sababu huku kuwepo ndani ya swala kunalazimu kwa mja moyoni mwake kuwa na sifa, na sababu inayomwita kutekeleza amri za Mola wake Mlezi. Na (pia) kuachana na makatazo yake. Hii ndiyo swala ambayo Mwenyezi Mungu alituamrisha tuombe msaada kwayo katika kila kitu.
: 154 #
{وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتٌ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَكِنْ لَا تَشْعُرُونَ (154)}
(154) Wala msiseme kuwa wale waliouwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti. Bali hao ni hai. Lakini nyinyi hamtambui.
#
{154} لما ذكر تبارك وتعالى الأمر بالاستعانة بالصبر على جميع الأحوال ذكر نموذجاً مما يستعان بالصبر عليه وهو الجهاد في سبيله وهو أفضل الطاعات البدنية وأشقها على النفوس لمشقته في نفسه ولكونه مؤدياً للقتل وعدم الحياة التي إنما يرغب الراغبون في هذه الدنيا لحصول الحياة ولوازمها، فكل ما يتصرفون به فإنه سعيٌ لها ودفع لما يضادها. ومن المعلوم أن المحبوب لا يتركه العاقل إلا لمحبوب أعلى منه وأعظم، فأخبر تعالى أن من قتل في سبيله بأن قاتل في سبيل الله لتكون كلمة الله هي العليا ودينه الظاهر لا لغير ذلك من الأغراض فإنه لم تفته الحياة المحبوبة بل حصل له حياة أعظم وأكمل مما تظنون وتحسبون، فالشهداء {أحياء عند ربهم يرزقون. فرحين بما آتاهم الله من فضله ويستبشرون بالذين لم يلحقوا بهم من خلفهم ألاَّ خوف عليهم ولا هم يحزنون. يستبشرون بنعمة من الله وفضل وأن الله لا يضيع أجر المؤمنين}؛ فهل أعظم من هذه الحياة المتضمنة للقرب من الله تعالى وتمتعهم برزقه البدني في المأكولات والمشروبات اللذيذة والرزق الروحي وهو الفرح وهو الاستبشار وزوال كل خوف وحزن وهذه حياة برزخية أكمل من الحياة الدنيا، بل قد أخبر النبي - صلى الله عليه وسلم - أن أرواح الشهداء في أجواف طير خضر ترد أنهار الجنة، وتأكل من ثمارها وتأوي إلى قناديل معلقة بالعرش. وفي هذه الآية أعظم حث على الجهاد في سبيل الله وملازمة الصبر عليه، فلو شعر العباد بما للمقتولين في سبيل الله من الثواب لم يتخلف عنه أحد، ولكن عدم العلم اليقيني التام هو الذي فتر العزائم وزاد نوم النائم وأفات الأجور العظيمة والغنائم، لم لا يكون كذلك والله تعالى قد {اشترى من المؤمنين أنفسهم وأموالهم بأن لهم الجنة يقاتلون في سبيل الله فيقتلون ويقتلون}؛ فوالله لو كان للإنسان ألف نفس تذهب نفساً فنفساً في سبيل الله لم يكن عظيماً في جانب هذا الأجر العظيم. ولهذا لا يتمنى الشهداء بعدما عاينوا من ثواب الله وحسن جزائه إلا أن يُرَدُّوا إلى الدنيا؛ حتى يقتلوا في سبيله مرة بعد مرة. وفي الآية دليل على نعيم البرزخ وعذابه كما تكاثرت بذلك النصوص.
(154) Alipotaja Mwingi wa baraka, Mtukufu amri ya kutafuta msaada kwa subira katika hali zote, akataja mfano wa yale ambayo msaada wa subira unatumika ndani yake. Ambayo ni jihadi katika njia yake. Nayo ndiyo matendo ya utiifu ya kimwili bora zaidi, na lililo gumu zaidi kwa nafsi kwa sababu ya ugumu wake yenyewe. Na kwa sababu inapelekea kuua na kukosa uhai ambao wale wanaoitaka hii dunia wanautaka ili kupata maisha na mahitaji yake. Hivyo basi, chochote wanachokitenda ni kukifanyia juhudi na kukizuilia yenye kuipinga. Na inajulikana kuwa kipenzi hakiachiwi na wenye akili timamu isipokuwa kwa ajili ya kipenzi kilicho juu na kikubwa kukiliko. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuuawa katika njia yake, kwamba alipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi. Na dini yake iliyo dhahiri, na si kwa lisilokuwa hayo miongoni mwa malengo. Basi yeye kwa hakika hajakosa uhai mpendwa, lakini alipata uhai mkubwa na kamili zaidi kuliko mnavyofikiria na kuchukulia. Basi Mashahidi, “169. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. 170. Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. 171. Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini”. Basi je, kuna kubwa zaidi kuliko huu uhai ambao unajumuisha ukaribu na Mwenyezi Mungu Mtukufu? Na kufurahia kwao riziki yake ya kimwili katika vyakula na vinywaji vyenye ladha nzuri? Na riziki ya kiroho, ambayo ni furaha, ambayo ni bishara njema na kuondolewa kwa kila hofu na huzuni? Na huu uhai wa Barzakh (kaburini) ni makamilifu zaidi kuliko uhai wa duniani. Bali Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alijulisha kuwa roho za mashahidi ziko ndani ya ndege wa kijani kibichi, wanaokwenda kunywa kwenye mito ya Peponi. Na wanakula katika matunda yake, na wanarudi kukaa kwenye taa zinazoning'inia kwenye Kiti cha Enzi. Na katika Aya hii kuna himizo kubwa zaidi juu ya kufanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kushikamana na subira juu yake. Na lau kuwa waja wangehisi malipo ya waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakuna ambaye angebaki nyuma katika hilo. Lakini ukosefu elimu ya yakini kamili ndiyo iliyotuliza hima, na ikamzidishia usingizi mwenye kulala; na ikapoteza malipo makubwa na ngawira. Kwa nini isiwe hivyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “hakika Mwenyezi Mungu amenunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa.” Wallahi (Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu,) lau kuwa mtu angekuwa na nafsi elfu moja zikawa zinakwenda nafsi baada ya nafsi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, halingekuwa kubwa zaidi kuliko haya malipo makubwa. Ndio maana mashahidi, baada ya kushuhudia katika thawabu za Mwenyezi Mungu na malipo yake mazuri, hawatamani isipokuwa kurejeshwa hapa duniani ili wauawe katika njia yake mara baada ya mara. Na katika Aya hii, kuna dalili ya furaha ya Barzakh na adhabu yake, kama maandiko mengi yalivyosimulia hilo.
: 155 - 157 #
{وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ (155) الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ (156) أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ (157)}
(155) Hapana shaka, tutakujaribuni kwa chembe ya hofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na mazao. Na wabashirie wanaosubiri.. (156) Wale ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. (157) Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Na hao ndio walioongoka.
#
{155} أخبر تعالى أنه لا بد أن يبتليَ عباده بالمحن ليتبين الصادق من الكاذب والجازع من الصابر، وهذه سنته تعالى في عباده، لأن السراء لو استمرت لأهل الإيمان ولم يحصل معها محنة لحصل الاختلاط الذي هو فساد، وحكمة الله تقتضي تمييز أهل الخير من أهل الشر، هذه فائدة المحن لا إزالة ما مع المؤمنين من الإيمان ولا ردهم عن دينهم، فما كان الله ليضيع إيمان المؤمنين. فأخبر في هذه الآية أنه سيبتلي عباده، {بشيء من الخوف}؛ من الأعداء، {والجوع}؛ أي: بشيء يسير منهما لأنه لو ابتلاهم بالخوف كله أو الجوع لهلكوا، والمحن تمحص لا تهلك، {ونقص من الأموال}؛ وهذا يشمل جميع النقص المعتري للأموال من جوائح سماوية وغرق وضياع وأخذ الظلمة للأموال من الملوك الظلمة وقطاع الطريق وغير ذلك {والأنفس}؛ أي: ذهاب الأحباب من الأولاد والأقارب والأصحاب، ومن أنواع الأمراض في بدن العبد أو بدن من يحبه، {والثمرات}؛ أي: الحبوب وثمار النخيل والأشجار كلها والخضر ببرد أو برَد أو حرق أو آفة سماوية من جراد ونحوه، فهذه الأمور لا بد أن تقع لأن العليم الخبير أخبر بها فوقعت كما أخبر، فإذا وقعت انقسم الناس قسمين: جازعين وصابرين. فالجازع حصلت له المصيبتان، فوات المحبوب وهو وجود هذه المصيبة وفوات ما هو أعظم منها وهو الأجر بامتثال أمر الله بالصبر ففاز بالخسارة والحرمان ونقص ما معه من الإيمان، وفاته الصبر والرضا والشكران وحصل له السخط الدال على شدة النقصان. وأما من وفقه الله للصبر عند وجود هذه المصائب فحبس نفسه عن التسخط قولاً وفعلاً واحتسب أجرها عند الله وعلم أن ما يدركه من الأجر بصبره أعظم من المصيبة التي حصلت له، بل المصيبة تكون نعمة في حقه لأنها صارت طريقاً لحصول ما هو خير له وأنفع منها، فقد امتثل أمر الله وفاز بالثواب، فلهذا قال تعالى: {وبشر الصابرين}؛ أي: بشرهم بأنهم يوفون أجرهم بغير حساب، فالصابرون هم الذين فازوا بالبشارة العظيمة والمنحة الجسيمة، ثم وصفهم بقوله:
(155) Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba ni lazima atawatia waja wake mitihani, ili apambanuke mkweli na mwongo, na asiyeridhia na mwenye subira. Na huu ndio mwendo wake Mtukufu katika waja wake. Kwa sababu, ikiwa raha itaendelea kwa watu wa imani, na matatizo yasiwepo pamoja nayo (hiyo raha), basi mchanganyiko ungetokea, ambao ni ufisadi. Na hekima ya Mwenyezi Mungu inahitaji kuwapambanua watu wema kutokana na watu waovu. Hii ndiyo faida ya matatizo, na sio kuondoa yale waliyo nayo Waumini ya imani, wala kuwatoa katika dini yao; kwani Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza imani ya Waumini. Basi akajulisha katika Aya hii kuwa atawajaribu waja wake, “kwa chembe ya hofu” kutoka kwa madui, “na njaa.” Yaani kitu kichache katika mawili hayo. Kwa sababu, lau kuwa angewatia hofu au njaa yote, basi wangeangamia. Na matatizo yanatakasa, wala hayaangamizi. “Na upungufu wa mali.” Na hili linajumuisha upungufu wote unaoipata mali kama vile majanga ya mbinguni, na kuzama, na kupotea. Na mali kuchukuliwa na madhalimu kama vile wafalme madhalimu na majambazi wa barabarani na mengineyo. “Na watu,” yani kuondoka kwa wapendwa miongoni mwa watoto, na jamaa, na marafiki, na aina za magonjwa katika mwili wa mja au mwili wa ampendaye. “Na mazao” yani nafaka, matunda ya mitende, na miti yote, na mboga kwa mvua ya mawe, au moto, au janga kutoka mbinguni kama vile nzige na mfano wake. Kwa hivyo, haya mambo ni lazima yatokee, kwa sababu Mwenye elimu, Mwenye habari, alijulisha kuyahusu, na yakatokea kama alivyojulisha. Basi yanapotokea, watu hugawanyika katika makundi mawili: wenye huzuni na wenye subira. Basi mwenye kuhuzunika, anapata misiba miwili: kupoteza akipendacho, ambacho ni kuwepo kwa huu msiba, na kupoteza kilicho kikubwa kuliko hicho. Ambacho ni malipo ya kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu ya kuwa na subira, kwa hivyo akapata hasara na kunyimwa, na kupunguka kwa kile alichokuwa nacho katika imani. Na akapoteza subira, kuridhia, na shukrani, na akapata kukasirika kunakoashiria ukubwa wa huo upungufu. Ama yule ambaye Mwenyezi Mungu amemwezesha kuwa na subira misiba hii inapotokea, hivyo akajizuia kutoridhika katika kauli na vitendo. Na akatarajia malipo yake kwa Mwenyezi Mungu, na akajua kwamba atakayoyapata miongoni mwa malipo kwa subira yake ni makubwa kuliko msiba uliompata. Bali msiba huo unakuwa neema kwake kwa sababu unakuwa njia ya kupata kilicho bora zaidi kwake na chenye manufaa zaidi kuliko msiba huo. Kwa kuwa ameshatekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na akapata malipo mazuri. Ndio maana Mwenyezi Mungu akasema: “Na wabashirie wanaosubiri,” yaani wape habari njema ya kwamba watalipwa ujira wao kamili bila ya hisabu. Hivyo basi, wenye subira ndio waliopata bishara kubwa, na kipawa kikubwa. Kisha akawaeleza kwa kauli yake:
#
{156} {الذين إذا أصابتهم مصيبة}؛ وهي كل ما يؤلم القلب أو البدن أو كليهما مما تقدم ذكره، {قالوا إنا لله}؛ أي: مملوكون لله مدبرون تحت أمره وتصريفه فليس لنا من أنفسنا وأموالنا شيء، فإذا ابتلانا بشيء منها فقد تصرف أرحم الراحمين بمماليكه وأموالهم فلا اعتراض عليه، بل من كمال عبودية العبد علمه بأن وقوع البلية من المالك الحكيم الذي هو أرحم بعبده من نفسه، فيوجب له ذلك الرِّضا عن الله والشكر له على تدبيره لما هو خير لعبده وإن لم يشعر بذلك، ومع أننا مملوكون لله فإنا إليه راجعون يوم المعاد، فمجازٍ كل عامل بعمله، فإن صبرنا واحتسبنا وجدنا أجرنا موفراً عنده، وإن جزعنا وسخطنا لم يكن حظنا إلا السخط وفوات الأجر، فكون العبد لله وراجعاً إليه من أقوى أسباب الصبر.
(156) “Wale ambao ukiwapata msiba.” Nao (msiba) ni kila kinachoumiza moyo au mwili au vyote viwili katika yale yaliyotangulia kutajwa. “Husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu.” Yani tunamilikiwa na Mwenyezi Mungu, tunasimamiwa, chini ya amri yake na uendeshaji wake. Kwa hivyo, hatuna chochote katika nafsi zetu wala mali zetu. Basi ikitujaribu na kitu katika hayo, basi Yeye Mwingi wa Rehema atakuwa amewaendesha wamilikiwa wake na mali zake. Kwa hivyo hakuna pingamizi dhidi yake. Bali katika ukamilifu wa utumwa wa mja, ni kujua kwake kwamba kutokea kwa msiba ni kutoka kwa Mmiliki mwenye hekima. Ambaye ana huruma zaidi kwa mja wake kwa nafsi yake mwenyewe, hivyo hilo likawa linamfanya kumridhia Mwenyezi Mungu na kumshukuru juu ya usimamizi kwa lile ambalo ni bora kwa mja wake, hata kama haoni hivyo. Na sisi ni wamilikiwa wa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo tutarejea kwake Siku ya Kiyama, na kila mtendaji atalipwa kwa matendo yake. Kwa hivyo, tukiwa na subira na kutarajia malipo, tutapata malipo yetu ni mengi kwake. Na ikiwa tutalalamika na kutoridhika, basi bahati yetu haitakuwa ila kutoridhika na kupoteza malipo. Kwa hivyo kuwa mja wa Mungu na kurejea kwake ni katika sababu zenye nguvu zaidi za kuwa na subira.
#
{157} {أولئك}؛ الموصوفون بالصبر المذكور {عليهم صلوات من ربهم}؛ أي: ثناء وتنويه بحالهم، {ورحمة}؛ عظيمة، ومن رحمته إياهم أن وفقهم للصبر الذي ينالون به كمال الأجر {وأولئك هم المهتدون}؛ الذين عرفوا الحق، وهو في هذا الموضع علمهم بأنهم لله وأنهم إليه راجعون وعملوا به وهو هنا صبرهم لله، ودلت هذه الآية على أن من لم يصبر فله ضد ما لهم فحصل له الذم من الله والعقوبة والضلال والخسار، فما أعظم الفرق بين الفريقين وما أقل تعب الصابرين وأعظم عناء الجازعين. فقد اشتملت هاتان الآيتان على توطين النفوس على المصائب قبل وقوعها لتخف وتسهل إذا وقعت، وبيان ما تقابل به إذا وقعت وهو الصبر، وبيان ما يعين على الصبر وما للصابرين من الأجر. ويعلم حال غير الصابر بضد حالة الصابر وأن هذا الابتلاء والامتحان سنة الله التي قد خلت ولن تجد لسنة الله تبديلاً وبيان أنواع المصائب.
157) “Hao” waliosifika kwa subira iliyotajwa, “juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi.” Yani sifa na utajo wa hali zao, “na rehema” kubwa. Na katika rehema yake juu yao ni kuwa aliwawezesha kuwa na subira ambayo kwayo wakapata malipo kamilifu, “na hao ndio walioongoka.” Ambao waliijua haki. Nayo mahali hapa ni kujua kwao kwamba wao ni wa Mwenyezi Mungu na kwamba kwake Yeye watarejea. Na wakaifanyia kazi. Nako huko wakaifanyia kazi kwao hapa ni ile subira yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na Aya hii inaashiria kwamba asiyekuwa na subira, atakuwa na kinyume cha walichonacho. Basi atapata kashfa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na adhabu, na upotofu na hasara. Basi ni kubwa vipi tofauti iliyopo kati ya haya makundi mawili! Na ni machovu machache yaliyoje ya wenye subira, na shida kubwa iliyoje ya wanaohuzunika. Aya hizi mbili zinajumuisha kutuliza nafsi kabla ya misimba kutokea ili iwe (misiba) rahisi na mepesi inapotekea. Na kubainisha yale inayokabiliwa (misiba) kwayo inapotokea, nayo ni subira. Na kubainisha yale yanayosaidia katika subira kile walichonacho wenye subira katika malipo. Na inajulikana hali ya asiyekuwa na subira kwa kinyume cha hali ya mwenye subira. Na kwamba majaribio na mitihani ni mwendo wa Mwenyezi Mungu ambao ulikwisha pita, na hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu. Na pia kuna kubainisha aina za misiba.
: 158 #
{إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا وَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ (158)}
(158) Hakika, vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi, anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri. Basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mwenye elimu.
#
{158} يخبر تعالى: {إن الصفا والمروة}؛ وهما معروفان {من شعائر الله}؛ أي: أعلام دينه الظاهرة التي تعبَّد الله بها عباده، وإذا كانا من شعائر الله فقد أمر الله بتعظيم شعائره فقال: {ومن يعظم شعائر الله فإنها من تقوى القلوب}؛ فدل مجموع النصين أنهما من شعائر الله، وأن تعظيم شعائره من تقوى القلوب، والتقوى واجبة على كل مكلف، وذلك يدل على أن السعي بهما فرض لازم للحج والعمرة كما عليه الجمهور، ودلت عليه الأحاديث النبوية، وفعله النبي - صلى الله عليه وسلم -، وقال: «خذوا عني مناسككم». {فمن حج البيت أو اعتمر فلا جناح عليه أن يطوف بهما}؛ هذا دفع لوهم من توهم وتحرج من المسلمين عن الطواف بينهما لكونهما في الجاهلية تعبد عندهما الأصنام، فنفى تعالى الجناح لدفع هذا الوهم لا لأنه غير لازم، ودل تقييد نفي الجناح فيمن تطوف بهما في الحج والعمرة أنه لا يتطوع بالسعي مفرداً إلا مع انضمامه لحج أو عمرة، بخلاف الطواف بالبيت فإنه يشرع مع العمرة والحج وهو عبادة مفردة. فأما السعي والوقوف بعرفة ومزدلفة ورمي الجمار فإنها تتبع النسك، فلو فعلت غير تابعة للنسك كانت بدعة، لأن البدعة نوعان: نوع يتعبد لله بعبادة لم يشرعها أصلاً، ونوع يتعبد له بعبادة قد شرعها على صفة مخصوصة فتفعل على غير تلك الصفة وهذا منه. وقوله: {ومن تطوع}؛ أي: فعل طاعة مخلصاً بها لله تعالى {خيراً}؛ من حج وعمرة وطواف وصلاة وصوم وغير ذلك، فهو خير له؛ فدل هذا على أنه كلما ازداد العبد من طاعة الله ازداد خيره وكماله ودرجته عند الله لزيادة إيمانه، ودل تقييد التطوع بالخير أن من تطوع بالبدع التي لم يشرعها الله ولا رسوله أنه لا يحصل له إلا العناء، وليس بخير له، بل قد يكون شرًّا له إن كان متعمداً عالماً لعدم مشروعية العمل. {فإن الله شاكر عليم}؛ الشاكر والشكور من أسماء الله تعالى الذي يقبل من عباده اليسير من العمل، ويجازيهم عليه العظيم من الأجر الذي إذا قام عبده بأوامره وامتثل طاعته أعانه على ذلك وأثنى عليه ومدحه وجازاه في قلبه نوراً وإيماناً وسعة وفي بدنه قوة ونشاطاً وفي جميع أحواله زيادة بركة ونماء وفي أعماله زيادة توفيق، ثم بعد ذلك يقدم على الثواب الآجل عند ربه كاملاً موفراً لم تنقصه هذه الأمور، ومن شكره لعبده أن من ترك شيئاً لله أعاضه الله خيراً منه، ومن تقرب منه شبراً تقرب منه ذراعاً، ومن تقرب منه ذراعاً تقرب منه باعاً، ومن أتاه يمشي أتاه هرولة، ومن عامله ربح عليه أضعافاً مضاعفة، ومع أنه شاكر فهو عليم بمن يستحق الثواب الكامل بحسب نيته وإيمانه وتقواه ممن ليس كذلك، عليم بأعمال العباد فلا يضيعها بل يجدونها أوفر ما كانت على حسب نياتهم التي اطلع عليها العليم الحكيم.
(158) Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuwa, “hakika, vilima vya Safaa na Marwa” navyo ni vilima vinavyojulikana. “Ni katika alama za Mwenyezi Mungu,” yani alama za dhahiri za dini yake ambazo Mwenyezi Mungu amewafanya waja wake kumuabudu kwazo. Na ikiwa (vilima hivyo) ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu aliamrisha ziheshimiwe alama zake. Akasema, “na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” Kwa hivyo, jumla ya maandiko haya mawili yanaonyesha kuwa ni miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, na kwamba kuziheshimu alama zake ni katika uchamungu wa nyoyo. Nao uchamungu ni wajibu kwa kila aliyeamrishwa. Na hilo linaashiria kuwa kwenda kati ya viwili hivyo, (Sa’ayi) ni faradhi ya lazima katika Hijja na Umra kama wengi wa wanazuoni wanavyoona. Na hadithi za Nabii ziliashiria hivyo. Na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – aliifanya (hiyo Sa’ayi), na akasema: “Chukueni ibada zenu kutoka kwangu”. “Basi, anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka.” Hili ni ili kuondoa dhana potofu ya yule aliyedhani vibaya na akaona ubaya miongoni mwa Waislamu kuzunguka baina yake kwa sababu, walikuwa katika siku za ujinga masanamu yalikuwa yakiabudiwa hapo. Basi Mwenyezi Mungu akakanusha ubaya ili kuzuia dhana hiyo potofu, siyo kwa sababu siyo lazima. Na kuzuilia huo ubaya kwa mwenye kuvizunguka katika Hijja au Umra kunaashiria kuwa mtu hawezi kujitolea kuvizunguka hivyo peke yake isipokuwa kwa kuunganisha hilo na Hijja au Umra. Tofauti na kuizunguka Nyumba, imeekwa kama sheria pamoja na Umra na Hija, nayo pia ibada kivyake. Ama kufanya Sa’ayi, kusimama Arafa na Muzdalifah, na kuipiga Jamarat kwa vijiwe, hayo yanafuata matendo ya Hijja. Na lau kuwa yatafanywa bila ya kuyaunga na matendo ya Hijja, basi yanakuwa uzushi (Bid'a). Kwa sababu, uzushi ni aina mbili: Aina ya kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa ibada ambayo hakuiweka katika sharia kabisa. Na aina nyingine ni kumuabudu Yeye kwa ibada aliyoiweka katika sheria kwa njia maalumu, lakini ikafanywa kwa njia isiyokuwa hiyo. Na hii ni katika aina hii. Na kauli yake, "na anayejitendea mwenyewe." Mwenye kutenda kitendo cha utiifu akikusudia kwayo Mwenyezi Mungu Mtukufu, "heri" kama vile hijja, umra, kuizunguka Al-Kaba, swala, saumu na mengineyo, basi hilo ni bora kwake. Na hili linaashiria kwamba kila mja anavyoongeza kumtii Mwenyezi Mungu, ndivyo heri yake inavyoongezeka. Na ukamilifu wake, na daraja yake kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kuongezeka kwa imani yake. Na aliiashiria kuzuilia kujitolea katika heri kuwa mwenye kujitolea kwa kufanya uzushi ambao Mwenyezi Mungu hakuuweka kama sheria wala Mtume wake. Kwamba hilo hatapata isipokuwa taabu tu, na wala siyo heri kwake. Bali huenda ikawa shari kwake ikiwa anaifanya kuwa ibada pamoja na kujua kuwa siyo katika sheria kuifanya, "basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mwenye elimu." Ash-Shakir na Ash-Shakur ni katika majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye anakubali kutoka kwa waja wake matendo madogo. Na anawalipa kwayo malipo makubwa, ambaye mja wake anapofanya maamrisho yake na akatekeleza ya kumtii, yeye humsaidia katika hilo. Na anamsifu, na kumlipa nuru moyo wake, na imani, na wasaa, na katika mwili wake nguvu na nashati, na katika hali zake zote kuongezeka kwa baraka na kukua. Na katika matendo yake kuongezeka kuwezeshwa, kisha baada ya hayo atayaendea malipo ya baadaye kwa Mola wake Mlezi kwa ukamilifu, nyingi hali ya kuwa havipungukiwi vitu hivyo. Na katika kumshukuru kwake mja wake ni kwamba mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atampa kilicho bora kuliko hicho. Na mwenye kumkaribia kwa shubiri moja, basi yeye atamkaribia dhiraa moja. Na wenye kumkaribia kwa dhiraa moja, yeye atamkaribia kwa mkono mmoja. Na mwenye kumjia kwa kutembea, yeye atamjia kwa hatua za haraka. Na mwenye kuamiliana naye, atapata faida mizidisho mingi. Na pamoja na kwamba yeye ni mwenye kushukuru, lakini anajua ni nani anayestahiki ujira kamili kulingana na nia yake, imani, na uchamungu wake, kutokana na yule asiyekuwa hivyo. Anayajua matendo ya waja, basi Yeye hayapotezi, bali wanayakuta ni mengi zaidi kuliko yalivyokuwa kulingana na nia zao ambazo alizijua Mwenye elimu. Mwenye hekima.
: 159 - 162 #
{إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنْزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَى مِنْ بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ أُولَئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ (159) إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (160) إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ (161) خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنْظَرُونَ (162)}
(159) Hakika, wale wanaoficha tuliyoyateremsha, nazo ni hoja zilizo wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni. Hao anawalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani. (160) Isipokuwa wale waliotubu, wakatengeneza na wakabainisha. Basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu. (161) Hakika, waliokufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote. (162) Watadumu humo. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa kupumzika.
#
{159} هذه الآية وإن كانت نازلة في أهل الكتاب وما كتموا من شأن الرسول - صلى الله عليه وسلم -، وصفاته فإن حكمها عامٌّ لكل من اتصف بكتمان ما أنزل الله {من البينات}؛ الدالات على الحق المظهرات له {والهدى}؛ وهو العلم الذي تحصل به الهداية إلى الصراط المستقيم، ويتبين به طريق أهل النعيم من طريق أهل الجحيم، فإن الله أخذ الميثاق على أهل العلم بأن يبينوا للناس ما منَّ الله به عليهم من علم الكتاب ولا يكتموه، فمن نبذ ذلك وجمع بين المفسدتين: كتم ما أنزل الله والغش لعباد الله فأولئك {يلعنهم الله}؛ أي: يبعدهم ويطردهم عن قربه ورحمته {ويلعنهم اللاعنون}؛ وهم جميع الخليقة، فتقع عليهم اللعنة من جميع الخليقة لسعيهم في غش الخلق وفساد أديانهم وإبعادهم من رحمة الله، فجوزوا من جنس عملهم، كما أن معلم الناس الخير يصلي الله عليه وملائكته حتى الحوت في جوف الماء لسعيه في مصلحة الخلق وإصلاح أديانهم، وقربهم من رحمة الله، فجوزي من جنس عمله. فالكاتم لما أنزله الله مضاد لأمر الله مشاق لله، يبين الله الآيات للناس ويوضحها، وهذا يسعى في طمسها وإخفائها ، فهذا عليه هذا الوعيد الشديد.
Aya hii ijapokuwa iliteremshwa kuhusiana na watu wa Kitabu, na walichoficha katika hali ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na sifa zake. Ila hukumu yake ni ya jumla kwa kila mwenye sifa ya kuficha yale Mwenyezi Mungu aliteremsha, “katika hoja yaliyo wazi” zenye kuelekeza kwenye haki. Zenye kuidhihirisha, “na uwongofu” nayo ni elimu ambayo kwayo kunapatikana kuongoka kwenye njia iliyonyooka, na inabainisha kwayo njia ya watu wa neema kutokana na njia ya watu wa Motoni. Kwani, Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kutoka kwa watu wa elimu kwamba wawaelezee watu kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa katika elimu ya Kitabu, na wala wasiifiche. Kwa hivyo, mwenye kulitupa hilo, na akajumuisha kati ya maovu mawili, yani kuficha aliyoteremsha Mwenyezi Mungu na kuwapunja waja wa Mwenyezi Mungu, basi hao, “Mwenyezi Mungu anawalaani.” Yani anawaweka mbali na anawafukuza kutokuwa karibu naye, na rehema zake. “Na wanawalaani kila wenye kulaani.” Nao ni viumbe wote. Basi laana inawafikia kutoka kwa viumbe vyote, kwa sababu ya kufanya kwao juhudi katika kuwapunja viumbe na kuharibu dini zao, na kuwaweka mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, wakalipwa aina sawa na matendo yao. Sawa na vile mwenye kuwafundisha watu heri, anaswaliwa na Mwenyezi Mungu, na malaika wake, hata nyangumi ndani ya maji. Kwa sababu ya kufanya kwake juhudi katika masilahi ya viumbe, na kurekebisha dini zao, na kuwaleta karibu na rehema za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, akalipwa aina sawa na matendo yake. Kwa maana, mwenye kuficha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha anakwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, na anampinga Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anawabainishia watu Aya na anaziweka wazi, ilhali huyu anazifutilia mbali. Ndiyo maana, kuna tishio hili kali juu yake.
#
{160} {إلا الذين تابوا}؛ أي: رجعوا عما هم عليه من الذنوب ندماً وإقلاعاً وعزماً على عدم المعاودة {وأصلحوا}؛ ما فسد من أعمالهم؛ فلا يكفي ترك القبيح حتى يحصل فعل الحسن، ولا يكفي ذلك في الكاتم أيضاً حتى يبين ما كتمه ويبدي ضد ما أخفى فهذا يتوب الله عليه لأن توبة الله غير محجوب عنها، فمن أتى بسبب التوبة تاب الله عليه لأنه {التواب}؛ أي: الرجاع على عباده بالعفو والصفح بعد الذنب إذا تابوا وبالإحسان والنعم بعد المنع إذا رجعوا {الرحيم}؛ الذي اتصف بالرحمة العظيمة التي وسعت كل شيء، ومن رحمته أن وفقهم للتوبة والإنابة فتابوا وأنابوا ثم رحمهم بأن قبل ذلك منهم لطفاً وكرماً، هذا حكم التائب من الذنب.
“Isipokuwa wale waliotubu,” yani waliyaacha madhambi yao na wakajuta na kuwachana nayo kabisa, na wakaazimia kutorejea. “Wakatengeneza” yale waliyoharibika katika matendo yao. Na haitoshi kuacha ubaya tu mpaka kupatikane kufanya mema. Na hilo pia halitoshi kwa mwenye kuficha mpaka abainishe yale aliyoyaficha, na aonyeshe kinyume cha aliyoyaficha. Basi huyu, Mwenyezi Mungu atamkubalia toba yake, kwa sababu toba ya Mwenyezi Mungu haizuiliwi. Basi, atakayefanya sababu ya toba, Mwenyezi Mungu atamkubalia toba yake, kwa sababu yeye ndiye, “Mwenye kupokea toba.” Yani kuwarudia waja wake kwa kuwasamehe na kuwachilia baada ya dhambi wakitubu, wanapotubu. Na kwa wema na neema baada ya kuzuia wakirejea, “Mwenye kurehemu.” Ambaye anasifika kwa rehema kubwa ambayo inaenea kila kitu. Na katika rehema yake ni kuwa aliwawezesha kutubu na kurudi kwake, kwa hivyo wakatubu na wakarudi kwake. Kisha akawarehemu kwa kukubali hayo kutoka kwao, kwa upole na ukarimu. Na hii ndiyo hukumu ya mwenye kutubia dhambi.
#
{161} وأما من كفر واستمر على كفره حتى مات لم يرجع إلى ربه ولم ينب إليه ولم يتب عن قريب فأولئك {عليهم لعنة الله والملائكة والناس أجمعين}؛ لأنه لما صار كفرهم وصفاً ثابتاً صارت اللعنة عليهم وصفاً ثابتاً لا تزول، لأن الحكم يدور مع علته وجوداً وعدماً.
Na ama mwenye kufuru na akaendelea na ukafiri wake mpaka akafa na asirejee kwa Mola wake Mlezi, wala asitubie kwa haraka. Basi hao, “hao laana ya Mwenyezi Mungu iko juu yao na ya Malaika na ya watu wote”. Kwa sababu, ukafiri wao ulipokuwa ni sifa madhubuti, lana juu yao ikawa ni sifa madhubuti isiyoondoka. Kwa sababu, hukumu inazunguka pamoja na sababu yake, kuwepo na kutokuwepo kwake.
#
{162} {خالدين فيها}؛ أي: في اللعنة أو في العذاب وهما متلازمان {لا يخفف عنهم العذاب}؛ بل عذابهم دائم شديد مستمر {ولا هم ينظرون}؛ أي: يمهلون لأن وقت الإمهال وهو الدنيا قد مضى، ولم يبق لهم عذر فيعتذرون.
Na, “watadumu humo.” Yani katika laana, au katika adhabu au hizo maana mbili. “Hawatapunguziwa adhabu” bali, adhabu yao ni ya kudumu, kali na yenye kuendelea. “Wala hawatapumzishwa,” yani kupewa muhula, kwa sababu wakati wa muhula ambao ni duniani ulikwisha pita. Na hawakubaki na udhuru wowote ili watoe udhuru.
: 163 #
{وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ (163)}
(163) Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
#
{163} يخبر تعالى وهو أصدق القائلين أنه {إله واحد}؛ أي: متوحد منفرد في ذاته وأسمائه وصفاته وأفعاله فليس له شريك في ذاته ولا سمي له ولا كفو له ولا مثل ولا نظير ولا خالق ولا مدبر غيره، فإذا كان كذلك فهو المستحق لأن يؤله ويعبد بجميع أنواع العبادة ولا يشرك به أحد من خلقه لأنه {الرحمن الرحيم}؛ المتصف بالرحمة العظيمة التي لا يماثلها رحمة أحد فقد وسعت كل شيء وعمت كل حي، فبرحمته وجدت المخلوقات وبرحمته حصلت لها أنواع الكمالات، وبرحمته اندفع عنها كل نقمة، وبرحمته عرَّف عباده نفسه بصفاته وآلائه وبين لهم كل ما يحتاجون إليه من مصالح دينهم ودنياهم بإرسال الرسل وإنزال الكتب، فإذا علم أن ما بالعباد من نعمة فمن الله وأن أحداً من المخلوقين لا ينفع أحداً عُلِمَ أن الله هو المستحق لجميع أنواع العبادة وأن يفرد بالمحبة والخوف والرجاء والتعظيم والتوكل وغير ذلك من أنواع الطاعات وأن من أظلم الظلم وأقبح القبيح أن يعدل عن عبادته إلى عبادة العبيد وأن يشرك المخلوقين من تراب برب الأرباب أو يعبد المخلوق المدبر العاجز من جميع الوجوه مع الخالق المدبر القادر القوي الذي [قد] قهر كل شيء، ودان له كل شيء. ففي هذه الآية إثبات وحدانية الباري وإلهيته وتقريرها بنفيها عن غيره من المخلوقين وبيان أصل الدليل على ذلك وهو إثبات رحمته التي من آثارها وجود جميع النعم واندفاع جميع النقم، فهذا دليل إجمالي على وحدانيته تعالى. ثم ذكر الأدلة التفصيلية فقال:
Mwenyezi Mungu Mtukufu anatoa habari - na Yeye ndiye mkweli zaidi wa wasemao – kwamba Yeye, “ni Mungu mmoja tu.” Yani Mpweke, Mmoja tu dhati yake, majina yake, sifa zake, na vitendo vyake. Hana mshirika yeyote katika dhati yake, wala mwenye jina kama lake, wala anayelingana naye, wala mfano wake, wala aliye sawa naye, wala Muumba, wala Mwendeshaji isipokuwa Yeye. Na ikiwa ni hivyo, basi Yeye ndiye anayestahiki kufanyiwa uungu na kuabudiwa kwa kila aina za ibada. Na asishirikishwe yeyote pamoja naye katika viumbe vyake, kwa sababu Yeye ni, “Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.” Anayesifika kwa rehema kubwa ambayo haifanani nayo rehema ya yeyote yule. Kwa maana, (rehema zake) zimeenea na kujumuisha kila kilicho hai. Na kwa rehema yake, viumbe vilipatikana, na kwa rehema yake vilipata aina za vyakula. Na kwa rehema yake kila mateso, na kwa rehema zake aliwajulisha waja wake nafsi yake kwa sifa zake na neema zake. Na akawabainishia kila wanalohitaji katika masilahi ya dini yao na dunia yao kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu. Na ikishajulikana kuwa chochote walichonacho waja katika neema ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba hakuna mmoja katika viumbe hawezi kumfaidi mwingine, basi anajulikana kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayestahiki ibada za aina zote. Na kwamba Yeye peke yake apendwe, ahofiwe, atumainiwe, atukuzwe, ategemewe, na aina nyingine za utiifu. Na kwamba dhuluma ya dhuluma zote na ubaya wa ubaya wote ni kuacha kumuabudu na kwenda kuwaabudu waja. Na kumshirikisha Mola Mlezi wa mabwana wote na viumbe walioumbwa kutokana na udongo, au kumwabudu kiumbe anayeendeshwa. Asiyekuwa na uwezo kwa namna zote pamoja na Muumba, mwenye kuendesha kila kitu, mwenye uwezo, mwenye nguvu, ambaye [tayari] alikwishashinda kila kitu; na kila kitu kikawa chini ya hukumu yake. Na katika Aya hii, kuna uthibitisho wa upweke wa Muumba mwanzilishi na Uungu wake. Na kutia hilo mkazo kwa kukanusha hilo kutoka kwa asiyekuwa yeye katika viumbe. Na kubainisha asili ya dalili ya hilo, ambayo ni kuthibitisha rehema yake ambayo miongoni mwa athari zake, ni kuwepo kwa neema zote na kuzuilika kwa mateso zote. Basi hii ni dalili ya ujumla juu ya upweke wake Mtukufu. Kisha akataja dalili za kina, akasema:
: 164 #
{إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنْفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنَ السَّمَاءِ مِنْ مَاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِنْ كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ (164)}
Hakika, katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana. Na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni Na kwa hayo, akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo. Na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanaozingatia.
#
{164} أخبر تعالى أن في هذه المخلوقات العظيمة آيات؛ أي: أدلة على وحدانية الباري وإلهيته وعظيم سلطانه ورحمته وسائر صفاته، ولكنها {لقوم يعقلون}؛ أي: لمن لهم عقول يعملونها فيما خلقت له، فعلى حسب ما منَّ الله على عبده من العقل ينتفع بالآيات ويعرفها بعقله وفكره وتدبره، ففي {خلق السموات}؛ في ارتفاعها واتساعها وإحكامها وإتقانها وما جعل الله فيها من الشمس والقمر والنجوم وتنظيمها لمصالح العباد وفي خلق {الأرض}؛ مهاداً للخلق يمكنهم القرار عليها والانتفاع بما عليها والاعتبار، ما يدل ذلك على انفراد الله تعالى بالخلق والتدبير وبيان قدرته العظيمة التي بها خلقها، وحكمته التي بها أتقنها وأحسنها ونظمها، وعلمه ورحمته التي بها أودع ما أودع من منافع الخلق ومصالحهم وضروراتهم وحاجاتهم، وفي ذلك أبلغ الدليل على كماله واستحقاقه أن يفرد بالعبادة لانفراده بالخلق والتدبير والقيام بشؤون عباده. وفي {اختلاف الليل والنهار}؛ وهو تعاقبهما على الدوام إذا ذهب أحدهما خلفه الآخر، وفي اختلافهما في الحر والبرد والتوسط، وفي الطول والقصر والتوسط، وما ينشأ عن ذلك من الفصول التي بها انتظام مصالح بني آدم وحيواناتهم، وجميع ما على وجه الأرض من أشجار ونوابت، كل ذلك بانتظام وتدبير وتسخير تنبهر له العقول، وتعجز عن إدراكه من الرجال الفحول ما يدل ذلك على قدرة مصرفها وعلمه وحكمته ورحمته الواسعة ولطفه الشامل وتصريفه وتدبيره الذي تفرد به وعظمته وعظمة ملكه وسلطانه ممّا يوجب أن يؤله ويعبد ويفرد بالمحبة والتعظيم والخوف والرجاء وبذل الجهد في محابه ومراضيه. وفي {الفلك التي تجري في البحر} وهي السفن والمراكب ونحوها مما ألهم الله عباده صنعتها وخلق لهم من الآلات الداخلية والخارجية ما أقدرهم عليها ثم سخر لها هذا البحر العظيم والرياح التي تحملها بما فيها من الركاب والأموال والبضائع التي هي من منافع الناس وبما تقوم مصالحهم وتنتظم معايشهم، فمن الذي ألهمهم صنعتها وأقدرهم عليها وخلق لهم من الآلات ما به يعملونها، أم من الذي سخر لها البحر تجري فيه بإذنه وتسخيره والرياح، أم من الذي خلق للمراكب البرية والبحرية النار والمعادن المعينة على حملها وحمل ما فيها من الأموال، فهل هذه الأمور حصلت اتفاقاً أم استقل بعملها هذا المخلوق الضعيف العاجز الذي خرج من بطن أمه لا علم له ولا قدرة، ثم خلق له ربه القدرة وعلمه ما يشاء تعليمه، أم المسخر لذلك رب واحد حكيم عليم لا يعجزه شيء ولا يمتنع عليه شيء. بل الأشياء قد دانت لربوبيته، واستكانت لعظمته، وخضعت لجبروته. وغاية العبد الضعيف أن جعله الله جزءاً من أجزاء الأسباب التي بها وجدت هذه الأمور العظام، فهذا يدل على رحمة الله وعنايته بخلقه، وذلك يوجب أن تكون المحبة كلها له والخوف والرجاء وجميع الطاعة والذل والتعظيم {وما أنزل الله من السماء من ماء}؛ وهو المطر النازل من السحاب {فأحيا به الأرض بعد موتها}؛ فأظهرت من أنواع الأقوات وأصناف النبات ما هو من ضرورات الخلائق التي لا يعيشون بدونها، أليس ذلك دليلاً على قدرة من أنزله وأخرج به ما أخرج ورحمته ولطفه بعباده وقيامه بمصالحهم وشدة افتقارهم وضرورتهم إليه من كل وجه؟ أَما يوجب ذلك أن يكون هو معبودهم وإلههم؟ أليس ذلك دليلاً على إحياء الموتى ومجازاتهم بأعمالهم؟ {وبث فيها}؛ أي في الأرض {من كلِّ دابة}؛ أي: نشر في أقطار الأرض من الدواب المتنوعة ما هو دليل على قدرته وعظمته ووحدانيته وسلطانه العظيم، وسخرها للناس ينتفعون بها بجميع وجوه الانتفاع: فمنها ما يأكلون من لحمه ويشربون من دره، ومنها ما يركبون، ومنها ما هو ساعٍ في مصالحهم وحراستهم، ومنها ما يعتبر به، ومنها أنه بث فيها من كل دابة فإنه سبحانه هو القائم بأرزاقهم المتكفل بأقواتهم، فما من دابة في الأرض إلا على الله رزقها ويعلم مستقرها ومستودعها. وفي {تصريف الرياح}؛ باردة وحارة وجنوباً وشمالاً وشرقاً ودبوراً وبين ذلك، وتارة تثير السحاب، وتارة تؤلف بينه، وتارة تلقحه، وتارة تدره، وتارة تمزقه، وتزيل ضرره، وتارة تكون رحمة، وتارة ترسل بالعذاب، فمن الذي صرفها هذا التصريف وأودع فيها من منافع العباد ما لا يستغنون عنه، وسخرها ليعيش فيها جميع الحيوانات وتصلح الأبدان والأشجار والحبوب والنوابت إلا العزيز الحكيم الرحيم اللطيف بعباده المستحق لكل ذلٍّ وخضوع ومحبةٍ وإنابة وعبادة، وفي تسخير السحاب بين السماء والأرض على خفته ولطافته يحمل الماء الكثير فيسوقه الله إلى حيث شاء فيحيي به البلاد والعباد ويروي التلول والوهاد وينزله على الخلق وقت حاجتهم إليه، فإذا كان يضرهم كثرته أمسكه عنهم فينزله رحمة ولطفاً ويصرفه عناية وعطفاً، فما أعظم سلطانه وأغزر إحسانه وألطف امتنانه، أليس من القبيح بالعباد أن يتمتعوا برزقه ويعيشوا ببره وهم يستعينون بذلك على مساخطه ومعاصيه، أليس ذلك دليلاً على حلمه وصبره وعفوه وصفحه وعظيم لطفه، فله الحمد أولاً وآخراً وباطناً وظاهراً. والحاصل أنه كلما تدبر العاقل في هذه المخلوقات، وتغلغل فكره في بدائع المبتدعات، وازداد تأمله للصنعة وما أودع فيها من لطائف البر والحكمة علم بذلك أنها خلقت للحق وبالحق، وأنها صحائف آيات وكتب دلالات على ما أخبر به الله عن نفسه ووحدانيته وما أخبرت به الرسل من اليوم الآخر، وأنها مسخرات ليس لها تدبير ولا استعصاء على مدبرها ومصرفها، فتعرف أن العالم العلوي والسفلي كلهم إليه مفتقرون وإليه صامدون، وأنه الغني بالذات عن جميع المخلوقات فلا إله إلا الله، ولا رب سواه.
(164) Mwenyezi Mungu Mtukufu anatoa habari kwamba katika hivi viumbe vikubwa kuna ishara; yani dalili za upweke wa Muumba mwanzilishi, Uungu wake, Ukubwa wa mamlaka yake, Rehema zake, na Sifa zake zinginezo. Lakini ni, “kwa watu wanaozingatia” yani kwa wale wenye akili wanaozitumia katika yale zilizoumbiwa kwa ajili yake. Basi kwa kadiri Mwenyezi Mungu alivyompa mja wake katika akili, ananufaika kwa hizi Aya na anazijua kwa akili yake, na fikira yake na kuzingatia kwake. Na katika, “hakika, katika kuumbwa kwa mbingu” katika kuinuka kwake, upana wake, kuimarika kwake, na kutengenezeka kwake vizuri. Na kile Mwenyezi Mungu alichoweka ndani yake kama jua, na mwezi, na nyota, na mpangilio wake wa masilahi ya waja. Na katika uumbaji wa, “ardhi” kama tandiko kwa viumbe, wanaweza kutulia juu yake na kunufaika na vile vilivyo juu yake na kuzingatia. Hayo yanaonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji, uendeshaji wa mambo, na kubainisha uwezo wake mkubwa ambao kwao aliiumba. Na hekima yake ambayo kwayo aliitengeneza sawasawa, na akaifanya kuwa vizuri, na akaipanga. Na elimu yake na rehema zake ambazo kwazo aliweka ndani yake kile alichoweka miongoni mwa manufaa ya viumbe, masilahi yao, mahitaji yao ya lazima na mahitaji yao ya kawaida. Na katika hilo, kuna dalili kubwa mno ya ukamilifu wake na kustahiki kwake kupwekeshwa katika ibada kwa sababu ya upweke wake katika kuumba, kuendesha na kusimamia mambo ya waja wake. Na katika, “kukhitalifiana usiku na mchana.” Nako ni kufuatana kwake kwa kuendelea, moja yake inapoondoka, nyingine huifuata. Na katika kutofautiana kwake katika joto, baridi, wastani, urefu, ufupi, na kuwa kati na kati na majira yanayotokea kutokana na hayo. Ambayo kwayo masilahi ya wanadamu na wanyama wao yanapangika vizuri. Na kila kilichoko juu ya uso wa ardhi, kama vile miti na mimea, vyote hivyo ni kwa mpangilio, uendeshaji, na kuvifanya kutii, hayo yote akili zinashangazwa kwayo. Na haziwezi kueleweka na wanaume wenye nguvu, ambayo yanaonyesha uwezo wa mwendeshaji wake, na elimu yake, na hekima yake, na rehema yake pana. Na upole wake wenye kujumuisha, na utendaji wake na utendeshaji wake ambao yu pekee katika hilo. Na ukuu wake, na ukuu wa ufalme wake na mamlaka yake, ambayo inamlazimu kwamba afanyiwe yeye uungu na aabudiwe. Na apwekeshwe katika upendo na utukufu, na khofu na matumaini, na kufanya juhudi katika anayopenda na kuridhia. Na katika, “marikebu ambazo hupita baharini.” Nazo ni safina na majahazi na mfano wake, ambayo Mwenyezi Mungu aliwafunulia waja wake namna ya kuyatengeneza. Na akawaumbia ala za ndani na nje zilizowawezesha kufanya hivyo. Kisha akaitiisha bahari hii kuu na pepo ambavyo vinazibeba (marikebu) pamoja na vilivyomo kama vile abiria, mali, na bidhaa ambazo ni miongoni mwa manufaa ya watu; na zinazowahudumia masilahi yao na yanapangika maisha yao. Basi ni nani aliyewafunulia namna ya kuzitengeneza, na akawawezesha kufanya hivyo, na akawaumbia ala ambazo kwazo wanaweza kuziunda? Au ni nani aliyeitiisha bahari kwa ajili yake, zinapita humo kwa idhini yake, na kutiisha kwake, na pepo? Au ni nani aliyeumbia vyombo vya nchi kavu na vya baharini moto na madini vinavyosaidia kuvibeba (vyombo) na kubeba mali zilizomo ndani yake? Basi je, mambo haya yalitokea tu kwa sadfa, au vilitengenezwa na huyu kiumbe dhaifu peke yake asiyekuwa na uwezo. Ambaye alitoka katika tumbo la mama yake bila ya kuwa na elimu wala uwezo, kisha Mola wake Mlezi akamuumbia uwezo. Na akamfundisha alichotaka kumfunza, au aliyevitiisha hivi ni Mola Mlezi Mmoja, Mwenye hekima na elimu, asiyeshindwa na chochote, na wala hakizuiki chochote kwake? Bali mambo yote yako chini ya uungu wake, na yameutii ukuu wake, na yameunyenyekea uwezo wake. Na mwisho wa mja huyu dhaifu ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfanya kuwa sehemu katika sehemu za sababu ambazo kwazo mambo haya makubwa yanapatikana. Na hili linaashiria rehema ya Mwenyezi Mungu na kuwatunza kwake viumbe wake. Na hilo linalazimu kwamba mapenzi yote yawe kwake, na hofu, na matumaini, na utiifu wote, unyenyekevu na utukufu. "Na maji anayoteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni," nayo ni mvua ishukayo kutoka katika mawingu. "Na kwayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake." Kwa hivyo ikadhirisha aina za vyakula na sampuli za mimea ambavyo ni katika mahitaji ya lazima ya viumbe ambavyo hawawezi kuishi bila hivyo. Je, huo sio ushahidi wa uwezo wa yule aliyeyateremsha na akatoa kwayo alichokitoa? Na rehema zake na upole wake kwa waja wake, na kuwatimizia maslahi yao, na ukubwa wa kumhitaji kwao, na udharura wao kwake kwa njia zote? Je, hilo halihitaji kwamba awe mwabudiwa wao na Mungu wao? Je, huo sio ushahidi wa kuwafufua wafu na kuwalipa kwa matendo yao? “Na akaeneza humo,” yani katika ardhi “katika kila aina ya wanyama.” Yani alieneza katika maeneo ya ardhi wanyama mbalimbali ambayo ni dalili juu ya uwezo wake, utukufu wake, upweke wake, na mamlaka yake makubwa. Na aliwatiisha (viumbe hao) kwa watu ili wanufaike kwayo kwa njia zote za kunufaika. Miongoni mwake kuna wale wanaokula katika nyama yake, na wanakunywa katika maziwa yake. Na miongoni mwake kuna wale wanaowapanda. Na miongoni mwake kuna wale wanaotumika katika masilahi yao na ulinzi wao. Na miongoni mwake kuna wale ambao ni mazingatio. Na miongoni mwake ni kuwa ameeneza humo katika kila mnyama, kwani Yeye, aliyetakasika ndiye anayesimamia riziki zao, na anajua makao yake na mapitio yake. “Na katika mabadiliko ya pepo” (ambazo huwa) baridi na moto, kusini na kaskazini, mashariki na magharibi, na kati ya hayo. Na wakati mwingine huyatimua mawingu, na wakati mwingine huambatanisha kati yake. Na wakati mwingine huichavusha, na wakati mwingine husababisha mvua, na wakati mwingine huipasua na huondoa madhara yake. Na wakati mwingine huwa ni rehema, na wakati mwingine hutumwa ili kuadhibu. Basi ni nani aliyezibadilisha huku kubadilika. Na akaweka ndani yake katika manufaa ya waja ambayo hawawezi kufanya bila hayo? Na akazitiisha ili wanyama wote waishi humo, na ili miili, miti, nafaka na mimea viwe bora isipokuwa kwa Mwenye nguvu, Mwenye hekima, Mwingi wa huruma, Mpole kwa waja wake. Ambaye anastahiki kudhalilikiwa kwote, kunyenyekewa, upendo, kurudi kwake (toba), na kuabudiwa? Na katika kuyatiisha mawingu baina ya mbingu na ardhi, licha ya wepesi na wembamba wake, hubeba maji mengi. Basi Mwenyezi Mungu huyapeleka popote apendapo, na kuihuisha nchi na watu kwayo. Na anamwagilia milima na mabonde, na kuiteremsha kwa watu wakati wanayahitaji. Basi ikiwa wingi wake unawadhuru, yeye huishikilia isiwanyee, kisha huiteremsha kwa rehema na upole, na huiondoa kwa kuwajali na kuwahurumia. Basi ni ukubwa ulioje wa Mamlaka yake, na wema (ukarimu) mwingi ulioje, na upole zaidi wa neema. Je, siyo jambo baya mno kwa waja wake kufurahia riziki yake na kuishi kwa wema wake, huku wakijiasaidia na hayo katika kumkasirisha na kumuasi? Je, hiyo siyo dalili ya stahamala yake na subira yake? Na msamaha wake na kuachilia kwake mbali (makosa) na ukubwa wa upole wake? Basi ni zake sifa njema mwanzo na mwisho, ndani na dhahiri. Na jumla ya hayo ni kwamba kila mtu mwenye akili timamu anavyotafakari katika hawa viumbe. Na mawazo yake yakapenya ndani ya maajabu ya uumbaji. Na kila anavyozidi kutafakari katika ufundi na kile alichowekwa ndani yake katika wema na hekima zinazopendeza, atajua kwa hayo kwamba, viliumbwa kwa ajili ya haki na kwa haki. Na kwamba ni karatasi za Aya (ishara) na vitabu vya dalili za yale aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu juu ya nafsi yake na upweke wake. Na yale waliyosimulia Mitume kuhusu Siku ya Mwisho. Na kwamba vimetiishwa na wala havina utendaji wala ugumu wowote kwa mpangaji wake na mwendeshaji wake. Basi utajua kwamba ulimwengu wa juu na wa chini wote ni wenye kumuhitajia Yeye, na kwake wanakusudia. Na kwamba Yeye ndiye Aliyejitosheleza kwa dhati yake kutokana na viumbe vyote, hapana mungu ila Mwenyezi Mungu. Basi hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hapana mola mlezi isipokuwa Yeye.
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 165 - 167 #
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِلَّهِ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ (165) إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ (166) وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ (167)}.
(165) Na katika watu wapo wanaojifanyia waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana. Na laiti waliodhulumu wakajua watakapoiona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu, na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu! (1660 Waliofuatwa watakapo wakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. (167) Na watasema wale waliofuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyotukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.
#
{165 - 166 - 167} ما أحسن اتصال هذه الآية بالتي قبلها، فإنه تعالى لما بين وحدانيته وأدلتها القاطعة وبراهينها الساطعة الموصلة إل علم اليقين المزيلة لكل شك ذكر هنا أن {من الناس}، مع هذا البيان التام {من يتخذ} من المخلوقين {أنداداً} لله؛ أي: نظراء ومثلاء يساويهم في الله بالعبادة والمحبة والتعظيم والطاعة، ومن كان بهذه الحالة - بعد إقامة الحجة وبيان التوحيد - علم أنه معاند لله، مشاق له، أو معرض عن تدبر آياته، والتفكر في مخلوقاته فليس له أدنى عذر في ذلك، بل قد حقت عليه كلمة العذاب، وهؤلاء الذين يتخذون الأنداد مع الله لا يسوونهم بالله في الخلق والرزق والتدبير، وإنما يسوونهم به في العبادة فيعبدونهم ليقربوهم إليه، وفي قوله اتخذوا دليل على أنه ليس لله ندٌّ وإنما المشركون جعلوا بعض المخلوقات أنداداً له تسمية مجردة ولفظاً فارغاً من المعنى؛ كما قال تعالى: {وجعلوا لله شركاء قل سموهم أم تنبئونه بما لا يعلم في الأرض أم بظاهر من القول}؛ {إن هي إلاَّ أسماء سميتموها أنتم وآباؤكم ما أنزل الله بها من سلطان إن يتبعون إلاَّ الظن}. فالمخلوق ليس ندًّا لله لأن الله هو الخالق وغيره مخلوق والرب الرازق ومن عداه مرزوق، والله هو الغني وأنتم الفقراء وهو الكامل من كل الوجوه، والعبيد ناقصون من جميع الوجوه، والله هو النافع الضار، والمخلوق ليس له من النفع والضر والأمر شيء، فعلم علماً يقيناً بطلان قول من اتخذ من دون الله آلهة وأنداداً سواء كان ملكاً أو نبيًّا أو صالحاً أو صنماً أو غير ذلك وإن الله هو المستحق للمحبة الكاملة والذل التام، فلهذا مدح الله المؤمنين بقوله: {والذين آمنوا أشد حبًّا لله}؛ أي: من أهل الأنداد لأندادهم لأنهم أخلصوا محبتهم له وهؤلاء أشركوا بها، ولأنهم أحبوا من يستحق المحبة على الحقيقة الذي محبته هي عين صلاح العبد وسعادته وفوزه. والمشركون أحبوا من لا يستحق من الحب شيئاً ومحبته عين شقاء العبد وفساده وتشتت أمره. فلهذا توعدهم الله بقوله: {ولو يرى الذين ظلموا}؛ باتخاذ الأنداد والانقياد لغير رب العباد وظلموا الخلق بصدهم عن سبيل الله وسعيهم فيما يضرهم {إذ يرون العذاب}؛ أي: يوم القيامة عياناً بأبصارهم {أن القوة لله جميعاً وأن الله شديد العذاب}؛ أي: لعلموا علماً جازماً أن القوة والقدرة لله كلها وأن أندادهم ليس فيها من القوة شيء، فتبين لهم في ذلك اليوم ضعفها وعجزها لا كما اشتبه عليهم في الدنيا، وظنوا أن لها من الأمر شيئاً وأنها تقربهم إليه وتوصلهم إليه فخاب ظنهم، وبطل سعيهم، وحق عليهم شدة العذاب ولم تدفع عنهم أندادهم شيئاً، ولم تغن عنهم مثقال ذرة من النفع، بل يحصل لهم الضرر منها من حيث ظنوا نفعها. وتبرأ المتبعون من التابعين، وتقطعت بينهم الوصل التي كانت في الدنيا لأنها كانت لغير الله وعلى غير أمر الله، ومتعلقة بالباطل الذي لا حقيقة له فاضمحلت أعمالهم، وتلاشت أحوالهم، وتبين لهم أنهم كانوا كاذبين وأن أعمالهم التي يؤملون نفعها وحصول نتيجتها انقلبت عليهم حسرة وندامة وأنهم خالدون في النار لا يخرجون منها أبداً، فهل بعد هذا الخسران خسران؟ ذلك بأنهم اتبعوا الباطل فعملوا العمل الباطل ورجوا غير مرجوٍ وتعلقوا بغير متعلق فبطلت الأعمال ببطلان متعلقها ولما بطلت وقعت الحسرة بما فاتهم من الأمل فيها فضرتهم غاية الضرر، وهذا بخلاف من تعلق بالله الملك الحق المبين، وأخلص العمل لوجهه، ورجا نفعه فهذا قد وضع الحق في موضعه، فكانت أعماله حقًّا لتعلقها بالحق ففاز بنتيجة عمله ووجد جزاءه عند ربه غير منقطع كما قال تعالى: {الذين كفروا وصدوا عن سبيل الله أضل أعمالهم، والذين آمنوا وعملوا الصالحات وآمنوا بما نزل على محمد وهو الحق من ربهم كفر عنهم سيئاتهم وأصلح بالهم، ذلك بأن الذين كفروا اتبعوا الباطل وأن الذين آمنوا اتبعوا الحق من ربهم كذلك يضرب الله للناس أمثالهم}. وحينئذ يتمنى التابعون أن يردوا إلى الدنيا فيتبرؤوا من متبوعهم بأن يتركوا الشرك بالله ويقبلوا على إخلاص العمل لله، وهيهات فات الأمر وليس الوقت وقت إمهال وإنظار، ومع هذا فهم كذبة فلو ردوا لعادوا لما نهوا عنه وإنما هو قول يقولونه وأماني يتمنونها حنقاً وغيظاً على المتبوعين لما تبرؤوا منهم والذنب ذنبهم فرأس المتبوعين على الشر إبليس ومع هذا يقول لأتباعه: {لما قضي الأمر إن الله وعدكم وعد الحق ووعدتكم فأخلفتكم، وما كان لي عليكم من سلطان إلا أن دعوتكم فاستجبتم لي فلا تلوموني ولوموا أنفسكم}.
(165, 166, 167) Ni uzuri ulioje wa kuiunganisha Aya hii na ile ya kabla yake. Kwani Yeye Aliyetukuka alipobainisha upweke wake na dalili zake wa zisizokuwa na shaka. Na hoja zake zenye kung'aa na zilizounganishwa na elimu yenye yakini, yenye kuondoa kila shaka. Akataja hapa kwamba “na katika watu” pamoja na huku kubainisha kukamilifu kuna wale wanaomfanyia Mwenyezi Mungu waungu kutoka kwa viumbe. Yani wanamfanyia visawe, na mifano wakiwafanya sawa Mwenyezi Mungu katika ibada, upendo, utukufu na utiifu. Na yule ambaye yuko katika hali hii - baada ya kusimamishiwa hoja na kubainishiwa Tauhidi, - atajulikana kwamba yeye ni mkaidi na mpinzani kwa Mwenyezi Mungu. Au anayekupa mgongo kutafakari Aya zake na kufikiria katika viumbe vyake. Basi yeye hana udhuru hata kidogo katika hilo, bali neno la adhabu limekwisha thibiti juu yake.Na hao ambao wanachukua wenza pamoja na Mwenyezi Mungu hawawafanyi kuwa sawa na Mwenyezi Mungu katika uumbaji, riziki na kupanga mambo. Bali wanawafanya kuwa sawa naye katika ibada, na wanawaabudu ili wawaweke karibu naye. Na katika kauli yake “walijifanyia (waungu) ni dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu hana mwenza, lakini washirikina ndio waliowafanya baadhi ya viumbe kuwa wenza wake. Jina la dhahania tu, na neno lisilokuwa na maana, kama alivyosema Mtukufu: “Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika! Sema: Watajeni. Au ndio mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu?” [Na kauli yake:] “Hayo hayakuwa isipokuwa ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati isipokuwa dhana tu.” Kwa hivyo, kiumbe hakilingani na Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye Muumba, na visivyokuwa yeye vimeumbwa. Na Mola Mlezi ndiye Mwenye kuruzuku, nao wasiokuwa yeye wanaruzukiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejitosheleza, nanyi ndio masikini. Naye ndiye mkamilifu kwa namna zote, nao waja ni wapungufu kwa namna zote. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kunufaisha, mwenye kudhuru, nao viumbe hawana chochote katika kunufaisha na kudhuru na amri. Basi akajulikana elimu ya yakini ubatili wa kauli ya aliyejichukulia miungu na wenza badala ya Mwenyezi Mungu. Sawa awe mfalme au nabii, au mwema, au sanamu, au visivyokuwa hivyo. Na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayestahili upendo kamili na unyenyekevu kamili. Ndio maana Mwenyezi Mungu akawasifu Waumini kwa kauli yake: “Lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana.” Yani kushinda (upendo wa) hao wafanyao wenza kwa wenza wao. Kwa kuwa wao (Waumini) walimfanyia yeye tu mapenzi yao, nao hao waliwashirikisha hao wenza. Na kwa sababu (Waumini) walimpenda yule anayestahiki kupendwa kwa hakika. Ambaye kumpenda ndio kutengenea hasa kwa mja na furaha yake na kufaulu kwake. Nao washirikina waliwapenda wasiostahiki chochote katika mapenzi. Na kuwapenda ndio upotofu wenyewe na uharibifu wake, na kutawanyika kwa mambo yake. Ndio maana Mwenyezi Mungu akawatishia kwa kauli yake: “Na lau waliodhulumu wakajua,” kwa kumchukulia (Mwenyezi Mungu) wenza na kumfuata asiyekuwa Mola Mlezi wa waja. Na wakawadhulumu viumbe kwa kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, na kujitahidi kwao katika yale yanayowadhuru. “Watakapoiona adhabu,” yani Siku ya Kiyama kwa macho yao waziwazi, “kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu!” Yani wangelijua kujua kwa uthabiti kwamba nguvu na uwezo wote ni wa Mwenyezi Mungu. Na kwamba hao wenza wao hawana nguvu yoyote. Basi ikawabainikia katika siku hiyo udhaifu wao (hao wenza) na upungufu wao. Kama walivyowachanganya katika dunia na wakadhania kuwa wana kitu katika hilo jambo, na kwamba wanawaweka karibu kwake (Mwenyezi Mungu) na wanawafikisha kwake. Lakini, ikahasirika dhana yao, na juhudi zao zikawa bure, na ukali wa adhabu ukastahiki juu yao; na wenza wao hawakuzuilia chochote. Na hawakuwafaa hata chembe ya sisimizi ya manufaa, bali wanapata madhara kutoka kwao, ilhali walidhani kuwa watawanufaisha. Na wanaofuatwa wakawatenga wafuasi wao, na mafungamano ambayo yalikuwa kati yao duniani yatakatika. Kwa sababu yalikuwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na juu ya isiyokuwa amri ya Mwenyezi Mungu, na wanayohusiana na batili ambayo haina uhakika wowote. Basi matendo yao yakapotelea mbali, na hali zao zikaangamia, na ikawadhihirikia kuwa wao walikuwa ni waongo.Na kwamba matendo yao waliyoyatarajia yawanufaishe na wapate matokeo yake yaliwabadilikia kuwa masikitiko na majuto. Na kwamba watadumu ndani ya Moto milele wala hawatatoka humo abadani. Basi je baada ya hasara hii kuna hasara nyingine? Hilo ni kwa sababu walifuata batili, hivyo wakafanya matendo batili, na wakataraji jambo lisilotarajiwa. Na wakashikamana na lisiloshikamanwa nalo, basi matendo yao yakabatilika kwa sababu ya kubatilika kwa kile yaliyoshikamana nacho. Na (matendo yao) yalipobatilika, wakapata kusikitika juu ya matumaini waliyokosa ndani yake, kwa hivyo yakawadhuru kudhuru kukubwa mno. Hili ni tofauti na aliyeshikamana na Mwenyezi Mungu, Mfalme wa haki iliyo wazi. Na akaufanyia uso wake tu matendo, na akatarajia manufaa yake. Basi huyu bila shaka aliiweka haki mahali pake. Kwa hivyo matendo yake yakawa haki, kwa sababu ya kushikamana kwake na haki, basi akafaulu kupata matokeo ya matendo yake. Na akakuta malipo yake yasiyokatika kwa Mola wake Mlezi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu “1. Waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao. 2. Na walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi -, atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao. 3. Hayo ni kwa sababu, waliokufuru wamefuata upotovu, na walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.” Na wakati huo, wafuasi watatamani kwamba warudishwe duniani, ili wajitenge na wale ambao wao waliwafuata kwa kuacha kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Na waelekee kwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu tu matendo. Lakini, ni mbali mno vipi hilo! Jambo hilo (wanalotaka) limeshapita, na huu wakati siyo wakati wa kupewa muhula. Na pamoja na hayo, wao ni waongo, kwa maana wangelirudishwa bila ya shaka wangeyarejea yale waliyokatazwa. Lakini hiyo ni kauli wanayosema tu, na matamanio tu wanayotamani, kwa sababu ya ghadhabu kubwa juu ya wale ambao wao waliwafuata walipojitenga nao, ijapokuwa lawama ni zao. Na kichwa cha wale wanaofuatwa katika uovu ni Shetani, na licha ya hayo, anawaambia wafuasi wake wakati itakapokatwa hukumu. “Hakika, Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nilikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipokuwa kwamba nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe.”
: 168 - 170 #
{يَاأَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ (168) إِنَّمَا يَأْمُرُكُمْ بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَنْ تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ (169) وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ (170)}
(168) Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhahiri. (169) Yeye anakuamrisheni maovu na machafu, na mumsingizie Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua. (170) Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?
#
{168} هذا خطاب للناس كلهم مؤمنهم وكافرهم، فامتن عليهم بأن أمرهم أن يأكلوا من جميع ما في الأرض من حبوب وثمار وفواكه وحيوانات حالة كونها {حلالاً}؛ أي: محللاً لكم تناوله ليس بغصب ولا سرقة ولا محصلاً بمعاملة محرمة أو على وجه محرم أو معيناً على محرم {طيباً}؛ أي: ليس بخبيث كالميتة والدم ولحم الخنزير والخبائث كلها. ففي هذه الآية دليل على أن الأصل في الأعيان الإباحة أكلاً وانتفاعاً وأن المحرم نوعان: إما محرم لذاته وهو الخبيث الذي هو ضد الطيب، وإما محرم لما عرض له وهو المحرم لتعلق حق الله أو حق عباده به، وهو ضد الحلال. وفيه دليل على أن الأكل بقدر ما يقيم البنية واجب يأثم تاركه لظاهر الأمر، ولما أمرهم باتباع ما أمرهم به إذ هو عين صلاحهم نهاهم عن اتباع {خطوات الشيطان}؛ أي: طرقه التي يأمر بها، وهي جميع المعاصي من كفر وفسوق وظلم، ويدخل في ذلك تحريم السوائب والحام ونحو ذلك، ويدخل فيه [أيضاً] تناول المأكولات المحرمة. {إنه لكم عدو مبين}؛ أي: ظاهر العداوة فلا يريد بأمركم إلا غشكم وأن تكونوا من أصحاب السعير، فلم يكتف ربنا بنهينا عن اتباع خطواته حتى أخبرنا وهو أصدق القائلين بعداوته الداعية للحذر منه، ثم لم يكتف بذلك حتى أخبرنا بتفصيل ما يأمر به، وأنه أقبح الأشياء، وأعظمها مفسدة، فقال:
(168) Haya ni maneno kwa watu wote, Waumini wao na makafiri wao. Basi akawaonyesha ihisani kwamba aliwaamrisha wale kila kilichomo ardhini, kama nafaka, mazao, matunda na wanyama hali ya kuwa ni “halali.” Yani kwa namna inaruhusika kwenu kuvitumia, sio kwa nguvu wala kwa wizi, wala kuvipata kwa mapatano ya haramu au kwa namna iliyo haramu; au kwa kusaidia juu ya kilicho haramu. “Na vizuri,” yani sio vibaya kama vile nyamafu, damu, nyama ya nguruwe na machafu yote. Na katika Aya hii, kuna dalili ya kwamba hali ya asili katika vitu ni kuruhusiwa: Kula na kunufaika. Na kwamba kilichoharamishwa ni aina mbili: Ima kimeharamishwa chenyewe, nacho ndicho kichafu ambacho ni kinyume cha kizuri. Na ima ni haramu kwa sababu ya kilichokifikia, hivyo ni haramu kwa sababu kinaambatana na haki ya Mwenyezi Mungu, au haki ya waja wake, na hiki ni kinyume cha halali. Na kuna dalili ya kwamba ni lazima kula kadri inavyoweka muundo sawa. Na mwenye kuacha anapata dhambi kwa sababu ya inavyoonekana katika udhahiri wa amri hii. Na alipowaamrisha kuyafuata yale aliyowaamrisha, - kwa kuwa huko ndiko kutengea kwao kwenyewe, - akawakataza kufuata “nyayo za Shet'ani.” Yani njia zake ambazo yeye huziamrisha. Nazo ni madhambi yote kama vile kufuru, kupindukia mipaka, dhuluma, na inaingia ndani ya hilo kuharamisha Assawaib. (Nao ni ngamia walioachiliwa huru kwa sababu ya masanamu yao.) Na Haam (yani ngamia wa kiume anayezalisha wanangamia kumi, hivyo akaachiliwa huru) na mfano wa hayo. Na yanaingia katika hilo pia kula vyakula vilivyoharamishwa. “Hakika yeye ni adui yenu aliye dhahiri.” Yani mwenye uadui wa dhahiri, hivyo hataki katika kuuamrisheni isipokuwa kuwapunja, na kwamba muwe miongoni mwa wa wenza wa Moto mkali. Na Mola wetu Mlezi hakutoshea katika kutukaza tu kufuata nyayo zake. Mpaka alipotuambia – naye ndiye mkweli zaidi wa wale wanaosema - juu ya uadui wake unaotaka mtu kujitahadharisha naye. Kisha hakutoshea kwa hilo mpaka akatujulisha yale anayoamrisha kwa kina, na kwamba ndivyo vitu viovu zaidi, na vyenye uharibifu mkubwa zaidi, akasema:
#
{169} {إنما يأمركم بالسوء}؛ أي: الشر الذي يسوء صاحبه، فيدخل في ذلك جميع المعاصي فيكون قوله، {والفحشاء}؛ من باب عطف الخاص على العام لأن الفحشاء من المعاصي ما تناهى قبحه كالزنا وشرب الخمر والقتل والقذف والبخل ونحو ذلك مما يستفحشه من له عقل {وأن تقولوا على الله مالا تعلمون}؛ فيدخل في ذلك القول على الله بلا علم في شرعه وقدره، فمن وصف الله بغير ما وصف به نفسه، أو وصفه به رسوله، أو نفى عنه ما أثبته لنفسه، أو أثبت له ما نفاه عن نفسه؛ فقد قال على الله بلا علم، ومن زعم أن لله ندًّا وأوثاناً تقرب مَنْ عَبَدَها من الله فقد قال على الله تعالى بلا علم، ومن قال: إن الله أحل كذا، أو حرم كذا، أو أمر بكذا، أو نهى عن كذا بغير بصيرة، فقد قال على الله بلا علم، ومن قال: إنَّ الله خلق هذا الصنف من المخلوقات للعلة الفلانية بلا برهان له بذلك؛ فقد قال على الله بلا علم. ومن أعظم القول على الله بلا علم أن يتأول المتأول كلامه أو كلام رسوله على معاني اصطلح عليها طائفة من طوائف الضلال ثم يقول إن الله أرادها، فالقول على الله بلا علم من أكبر المحرمات وأشملها وأكبر طرق الشيطان التي يدعو إليها، فهذه طرق الشيطان التي يدعو إليها هو وجنوده، ويبذلون مكرهم وخداعهم على إغواء الخلق بما يقدرون عليه، وأما الله تعالى فإنه يأمر بالعدل والإحسان وإيتاء ذي القربى وينهى عن الفحشاء والمنكر والبغي. فلينظر العبد نفسه مع أي الداعيَيْنِ [هو] ومن أي الحِزْبَيْنِ؟ أتتبع داعي الله الذي يريد لك الخير والسعادة الدنيوية والأخروية الذي كل الفلاح بطاعته وكل الفوز في خدمته وجميع الأرباح في معاملة المنعم بالنعم الظاهرة والباطنة، الذي لا يأمر إلا بالخير ولا ينهى إلا عن الشرِّ، أم تتبع داعي الشيطان الذي هو عدو الإنسان الذي يريد لك الشرَّ ويسعى بجهده على إهلاكك في الدنيا والآخرة؟ الذي كل الشرِّ في طاعته وكل الخسران في ولايته، الذي لا يأمر إلا بشرٍّ ولا ينهى إلا عن خير.
“Yeye anakuamrisheni maovu,” yani shari ambayo ni mbaya kwa mwenyewe. Kwa hivyo, yanaingia katika hilo maasia yote, na inakuwa kauli yake, “na machafu;" katika mlango wa kutaja kilicho maalumu baada ya kilicho cha ujumla. Kwa sababu machafu katika dhambi ni yale ambayo ubaya ni mkubwa mno, kama vile uzinzi, unywaji pombe, uuaji, kukashifa mtu na machafu, ubakhili, na mfano wa hayo. Ambayo anayaona kuwa ni machafu hata yule asiyekuwa na akili timamu. “Na mumsingizie Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua.” Kwa hivyo, inaingia katika hilo kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, katika sheria yake na majaliwa yake. Hivyo basi, mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu kwa kitu ambacho hakujisifu kwacho nafsi yake, au Mtume wake hakumsifu kwacho. Au akanushe juu ya nafsi yake kile alichojithibitishia, au amthibitishie nafsi yake kile alichokikanusha juu ya nafsi yake. Basi atakuwa amesema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu. Na mwenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana mwenza na masanamu; wanaomweka mwenye kuyaabudu karibu na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amesema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu. Na mwenye kusema: Hakika, Mwenyezi Mungu ameruhusu hivi na hivi, au aliharamisha hivi na hivi, au aliamrisha hivi na hivi, au alikataza hivi na hivi bila ya elimu. Basi huyo atakuwa amesema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu. Na mwenye kusema: Mwenyezi Mungu aliumba aina hii ya viumbe kwa sababu fulani bila ya kuwa na dalili kwa hilo, basi atakuwa amesema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu. Na katika kusema kubwa juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, ni mwenye kufasiri anayafasiri maneno yake au maneno ya Mtume wake juu ya maana ambazo, kundi la watu wapotevu wameafikiana juu yake. Kisha akasema: Hakika Mwenyezi Mungu aliitaka (maana hii). Hivyo basi, kumsema juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu ni miongoni mwa haramu kubwa mno na yenye kujumuisha zaidi. Na njia kubwa kabisa za Shetani ambazo analingania kwake. Na hizi ndizo njia za Shetani ambazo yeye na jeshi lake wanaita kwake, na wanatumia hila zao na hadaa zao katika kuwapoteza viumbe kwa kile wanachoweza kufanya. Na ama Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye kwa hakika anaamrisha uadilifu na ihsani, na kuwapa jamaa, na anakataza machafu, na maovu, na dhuluma. Basi mja ajifikirie kuwa yuko pamoja na yupi kati ya hao walinganiaji wawili na katika kundi lipi? Je, utamfuata mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu ambaye anakutakia kheri na furaha ya duniani na Akhera? Ambaye kila mafanikio ni kwa kumtii? Na kila kufaulu ni katika kumtumikia yeye? Na faida zote ni katika kuamiliana na yule anayeneemesha neema za dhahiri na za ndani (zilizojificha)? Ambaye haamrishi isipokuwa kheri na hakatazi isipokuwa shari (maovu)? Au utamfuata mlinganiaji wa Shetani ambaye ni adui wa mtu ambaye anakutakia shari (maovu), na anajitahidi kukuangamiza duniani na Akhera? Ambaye kila shari (maovu) iko katika kumtii yeye? Na kila hasara iko katika kufanya kuwa msaidizi? Na ambaye haamrishi isipokuwa shari (maovu), na hakatazi isipokuwa ya heri?
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatoa habari kuhusu hali ya washirikina wanapoamrishwa kufuata yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake – katika yale yaliyoelezwa hapo awali, - wanajitenga nayo, na wanasema:
#
{170} {بل نتبع ما ألفينا عليه آباءنا} فاكتفوا بتقليد الآباء، وزهدوا في الإيمان بالأنبياء، ومع هذا فآباؤهم أجهل الناس وأشدهم ضلالاً. وهذه شبهة لرد الحق واهية، فهذا دليل على إعراضهم عن الحق ورغبتهم عنه وعدم إنصافهم، فلو هدوا لرشدهم وحسن قصدهم لكان الحق هو القصد، ومن جعل الحق قصده، ووازن بينه وبين غيره، تبين له الحق قطعاً واتبعه إن كان منصفاً. ثم قال تعالى:
“Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.” Basi wakatosheka tu na kuwafuata baba zao, na wakaacha kuwafuata Manabii, pamoja na kwamba ndio wajinga kuliko watu wote, na wapotofu wao zaidi. Na hii dhana potofu inayotumika kuikataa haki ni dhaifu mno. Na hii ni dalili juu ya kukengeuka kwao kutoka kwenye haki, na kutoitaka kwao, na kutokuwa kwao na uadilifu. Na lau kuwa wangeongoka kwenye uwongofu wao, na nia yao ikawa nzuri, basi kwa hakika ingelikuwa haki ndiyo makusudio yao. Na mwenye kuifanya haki kuwa ndiyo lengo lake, na akapima baina yake na vinginevyo, kwa hakika haki itambainikia bila shaka yoyote, na ataifuata ikiwa yeye ni mwadilifu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema,
: 171 #
{وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ (171)}
“Na mfano wa waliokufuru ni kama mfano wa anayempigia kelele asiyesikia isipokuwa wito na sauti tu. Ni viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo hawaelewi”.
#
{171} لما بين تعالى عدم انقيادهم لما جاءت به الرسل وردهم لذلك بالتقليد علم من ذلك أنهم غير قابلين للحق ولا مستجيبين له، بل كان معلوماً لكل أحد أنهم لن يزولوا عن عنادهم، أخبر تعالى أن مثلهم عند دعاء الداعي لهم إلى الإيمان كمثل البهائم التي ينعق لها راعيها وليس لها علم بما يقول داعيها ومناديها، فهم يسمعون مجرد الصوت الذي تقوم به عليهم الحجة، ولكنهم لا يفقهونه فقهاً ينفعهم، فلهذا كانوا صمًّاً لا يسمعون الحق سماع فهم وقبول، عمياً لا ينظرون نظر اعتبار، بُكماً فلا ينطقون بما فيه خير لهم، والسبب الموجب لذلك كله أنه ليس لهم عقل صحيح بل هم أسفه السفهاء وأجهل الجهلاء. فهل يستريب العاقل أن من دُعِيَ إلى الرشاد وذيد عن الفساد، ونُهِيَ عن اقتحام العذاب، وأُمِرَ بما فيه صلاحه وفلاحه وفوزه ونعيمه، فعصى الناصح، وتولى عن أمر ربه، واقتحم النار على بصيرة واتبع الباطل ونبذ الحق أن هذا ليس له مسكة من عقل، وأنه لو اتصف بالمكر والخديعة والدهاء فإنه من أسفه السفهاء.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipobainisha kutofuata kwao yale waliyoyaleta Mitume, na kukataa kwao hayo kwa kuwaiga baba zao; ikajulikana kwa hilo kwamba wao hawataikubali haki, wala hawatamuitikia. Bali ilikuwa ishajulikana kwa kila mtu kwamba hawataacha kuendelea na ukaidi wao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akapeana habari kwamba mfano wao anapowalingania mlinganiaji kwenye imani, ni kama mfano wa wanyama ambao mchungaji wao huwaongelesha kwa sauti kubwa. Ilhali wao hawafahamu kile anachokisema mchungaji huyo wao na mwitaji wao. Wao (washirikina) wanasikia sauti tu, ambayo kwayo hoja inasimama juu yao, lakini hawaielewi kuelewa kwa kuwanufaisha. Ndio maana, wakawa viziwi wasioisikia haki; kusikia kwa kuelewa na kuikubali. Vipofu wasioona kuona kwa kuzingatia, mabubu wasioweza kutamka yale yenye kheri kwao. Na sababu yenye kuleta haya yote ni kwamba hawana akili timamu, bali wao ndio wajinga wa wajinga wote, na wapumbavu wa wapumbavu wote. Basi je, mwenye akili timamu anaweza kuwa na shaka kuwa mwenye kuitwa kwenye uwongofu, na akatenganishwa na ufisadi, na akakatazwa kuingia ndani ya adhabu? Na akaamrishwa yale yenye kutengenea kwake, kufaulu kwake, mafanikio yake, na neema yake, kisha akamuasi huyo mwenye kumshauri na akajitenga na amri ya Mola wake Mlezi? Na akaingia Motoni kwa kujua, na akafuata batili (uongo), na akatupa haki, - ya kuwa huyu hana akili yoyote? - Na kwamba ikiwa pia anasifika kwa hila, na hadaa, na ujanja, basi huyo ndiye mjinga wa wajinga wote.
: 172 - 173 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ (172) إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنْزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (173)}
(172) Enyi mlio amini! Kuleni katika vizuri tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu. (173) Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
#
{172} هذا أمر للمؤمنين خاصة بعد الأمر العام، وذلك أنهم هم المنتفعون على الحقيقة بالأوامر والنواهي بسبب إيمانهم، فأمرهم بأكل الطيبات من الرزق والشكر لله على إنعامه باستعمالها بطاعته والتقوي بها على ما يوصل إليه، فأمرهم بما أمر به المرسلين في قوله: {يا أيها الرسل كلوا من الطيبات واعملوا صالحاً}؛ فالشكر في هذه الآية هو العمل الصالح، وهنا لم يقل حلالاً لأن المؤمن أباح الله له الطيبات من الرزق خالصة من التبعة، ولأن إيمانه يحجزه عن تناول ما ليس له. وقوله: {إن كنتم إياه تعبدون}؛ أي: فاشكروه فدل على أن من لم يشكر الله لم يعبده وحده، كما أن من شكره فقد عبده وأتى بما أمر به، ويدل أيضاً على أن أكل الطيب سبب للعمل الصالح وقبوله. والأمر بالشكر عقيب النعم، لأن الشكر يحفظ النعم الموجودة، ويجلب النعم المفقودة، كما أن الكفر ينفر النعم المفقودة، ويزيل النعم الموجودة.
Hii ni amri kwa Waumini hasa, baada ya amri ya jumla. Na hilo ni kwa sababu wao ndio wanaonufaika kwa hakika na maamrisho na makatazo, kwa sababu ya imani yao. Kwa hivyo, akawaamrisha kula vitu vizuri katika riziki, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake, kwa kuzitumia katika kumtii; na kupata nguvu kwavyo kwa yale yanayofikisha kwake. Hivyo, akawaamrisha yale aliyowaamrisha Mitume katika kauli yake. “Enyi Mitume, kuleni katika vizuri na tendeni mema.” Basi kushukuru katika Aya hii ni matendo mema. Na hapa hakusema “halali” kwa sababu, Mwenyezi Mungu alimruhusu Muumini kula vitu vizuri kutoka katika riziki ilimradi visiwe na matokeo yoyote mabaya. Na kwa sababu imani yake inamzuia kula kisichokuwa chake. Na kauli yake “ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu,” yani mshukuruni. Kwa hivyo, inaashiria kwamba yule asiyemshukuru Mwenyezi Mungu, basi hajamuabudu Yeye peke yake. Kama vile mwenye kumshukuru atakuwa amemuabudu, na amefanya yale aliyoamrishwa. Na pia inaashiria kwamba kula vilivyo vizuri ni sababu ya kutenda mema na kukubaliwa kwake. Na amri ya kushukuru baada ya kuneemeshwa ni kwa sababu shukrani huhifadhi neema zilizopo, na huleta neema zisizokuwepo. Kama vile kufuru hufukuza neema zisizokuwepo na huondoa neema zilizopo.
#
{173} ولما ذكر تعالى إباحة الطيبات ذكر تحريم الخبائث فقال: {إنما حرم عليكم الميتة}؛ وهي: ما مات بغير تذكية شرعية؛ لأن الميتة خبيثة مضرة لرداءتها في نفسها ولأن الأغلب أن تكون عن مرض فيكون زيادة مرض ، واستثنى الشارع من هذا العموم ميتة الجراد وسمك البحر فإنه حلال طيب {والدم}؛ أي: المسفوح كما قيد في الآية الأخرى {وما أهل به لغير الله}؛ أي ذبح لغير الله كالذي يذبح للأصنام والأوثان من الأحجار والقبور ونحوها، وهذا المذكور غير حاصر للمحرمات، وجيء به لبيان أجناس الخبائث المدلول عليه بمفهوم قوله: {طيبات}؛ فعموم المحرمات تستفاد من الآية السابقة من قوله: {حلالاً طيباً}؛ كما تقدم وإنما حرم علينا هذه الخبائث ونحوها لطفاً بنا وتنزيهاً عن المضر، ومع هذا {فمن اضطر}؛ أي ألجئ إلى المحرم بجوع وعدم أو إكراه {غير باغ}؛ أي: غير طالب للمحرم مع قدرته على الحلال أو مع عدم جوعه {ولا عاد}؛ أي: متجاوز الحد في تناول ما أبيح له اضطراراً فمن اضطر وهو غير قادر على الحلال، وأكل بقدر الضرورة فلا يزيد عليها {فلا إثم}؛ أي: جناح {عليه}؛ وإذا ارتفع الإثم رجع الأمر إلى ما كان عليه، والإنسان بهذه الحالة مأمور بالأكل بل منهيٌّ أن يلقي بيده إلى التهلكة وأن يقتل نفسه، فيجب إذاً عليه الأكل ويأثم إن ترك الأكل حتى مات فيكون قاتلاً لنفسه، وهذه الإباحة والتوسعة من رحمته تعالى بعباده، فلهذا ختمها بهذين الاسمين الكريمين المناسبين غاية المناسبة فقال: {إن الله غفورٌ رحيم}. ولما كان الحل مشروطاً بهذين الشرطين، وكان الإنسان في هذه الحالة ربما لا يستقصي تمام الاستقصاء في تحقيقها، أخبر [تعالى] أنه غفور، فيغفر [له] ما أخطأ فيه في هذه الحال خصوصاً، وقد غلبته الضرورة، وأذهبت حواسه المشقة. وفي هذه الآية دليل على القاعدة المشهورة «الضرورات تبيح المحظورات»، فكل محظور اضطر له الإنسان فقد أباحه له الملك الرحمن، فله الحمد والشكر أولاً وآخراً وظاهراً وباطناً.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuruhusiwa kwa vilivyo vizuri, akataja uharamu wa vilivyo vichafu, akasema: “Yeye amekuharimishieni mzoga tu.” Nao ni kilichokufa bila ya kuchinjwa kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Kwa sababu, mzoga ni mchafu na una madhara, kutokana na ubaya wake wenyewe na kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kuwa; kufa kwake kulitokana na maradhi, hivyo ukaongeza madhara. Na Mwenye Sheria ya Kiislamu aliwatenga kutoka kwa ujumla huu nzige waliokufa na samaki wa baharini, kwa kuwa ni halali na wazuri. “Na damu” yani Al-Masfuuh (inayotoka kwa wingi), kama ilivyozuiliwa hivi katika Aya zinginezo. “Na kilichotajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika kuchinjwa kwake.” Yani kilichinjwa kwa sababu ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kama vile wale wanaochinjwa kwa sababu ya masanamu na Awthaan (chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu, kinachoabudiwa huku kimeridhia). Kama vile mawe, makaburi na mfano wake. Na haya yaliyotajwa hapa hayafungii vilivyo haramu katika hivi tu, lakini vilitajwa ili kubainisha aina za machafu yaliyoashiriwa katika maana ya kauli yake “vizuri”. Kwa hivyo, jumla ya vile vilivyoharamishwa inapatikana kutoka katika Aya iliyotangulia kutoka kwa kauli yake, “halali na vizuri,” kama ilivyotangulia. Na alituharamishia vitu hivi vichafu na mfano wake kwa kutufanyia upole, na kutuepusha na madhara. Na pamoja na hili; “lakini aliyefikiwa na dharura.” Yani aliyelazimika kutumia kilicho haramu kwa sababu ya njaa na ukosefu, au kulazimishwa “bila ya kutamani.” Yani bila kuitafuta hiyo haramu huku anao uwezo wa kutumia kilicho halali, au bila yeye kuwa na njaa. "Wala kupita kiasi,” yani kupita mpaka katika kula kile alichoruhusiwa kwa sababu ya dharura. Basi mwenye kulazimishwa na hali hawezi kupata kilicho halali, na akala kadiri ya dharura hiyo, basi asizidishe juu yake. “Basi yeye hana dhambi” [yani ubaya] juu yake. Na ikiwa ubaya na dhambi vitakwisha, bali hilo jambo (la uharamu) litarejea jinsi lilivyokuwa. Na mtu aliye katika hali hii ameamrishwa ale, bali ni amekatazwa kujitupa kwa mkono wake katika maangamizo, na kuiua nafsi yake. Kwa hivyo, inalazimu ale, na anapata dhambi ikiwa ataacha kula mpaka akafa; ambapo atakuwa ameiua nafsi yake. Na ruhusa hii na ukunjufu ni kunatokana na rehema yake, Aliyetukuka kwa waja wake. Na ndiyo maana akaihitimisha (Aya hii) kwa majina haya yake mawili matukufu, yanayofaa kufaa kukubwa zaidi, akasema: “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”. Na kwa vile uhalali uliwekewa masharti haya mawili, na akawa mtu aliye katika hali hii kuenda asichunguze kwa ukamilifu; - Mola Mtukufu akasema kuwa Yeye ni Mwenye kusamehe.- Hivyo husamehe alichokosea katika hali hii, hasa kwa sababu alishindwa na dharura hiyo, na ugumu ukaondoka hisia zake. Na katika Aya hii, kuna dalili ya kanuni inayojulikana sana ambayo ni, “dharura (mahitaji) hufanya yaliyokatazwa kuruhusika.” Hivyo, kila jambo lililokatazwa ambalo mtu analazimishwa juu yake, basi amekwisharuhusiwa na Mfalme, Mwingi wa Rehema. [Basi ni zake sifa njema zote na shukrani, mwanzo na mwisho, kwa dhahiri na ndani].
: 174 - 176 #
{إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (174) أُولَئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَى وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ (175) ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ (176)}.
(174) Hakika, wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu. Na wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali katika tumbo zao isipokuwa moto. Wala Mwenyezi Mungu hatawaongelesha Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao wana adhabu chungu. (175) Hao ndio walionunua upotofu kwa uwongofu, na adhabu kwa maghfira (msamaha). Ama wavumilivu wa Moto watu hawa! (176) Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki. Na hakika wale waliohitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki.
#
{174 - 175} هذا وعيد شديد لمن كتم ما أنزل الله على رسله من العلم الذي أخذ الله الميثاق على أهله أن يبينوه للناس ولا يكتموه، فمن تعوض عنه بالحطام الدنيوي ونبذ أمر الله فأولئك {ما يأكلون في بطونهم إلا النار}؛ لأن هذا الثمن الذي اكتسبوه إنما حصل لهم بأقبح المكاسب وأعظم المحرمات، فكان جزاؤهم من جنس عملهم، {ولا يكلمهم الله يوم القيامة}؛ بل قد سخط عليهم وأعرض عنهم، فهذا أعظم عليهم من عذاب النار، {ولا يزكيهم}؛ أي: لا يطهرهم من الأخلاق الرذيلة، وليس لهم أعمال تصلح للمدح والرضا والجزاء عليها، وإنما لم يزكهم لأنهم فعلوا أسباب عدم التزكية التي أعظم أسبابها العمل بكتاب الله والاهتداء به والدعوة إليه، فهؤلاء نبذوا كتاب الله وأعرضوا عنه واختاروا الضلالة على الهدى والعذاب على المغفرة فهؤلاء لا يصلح لهم إلا النار، فكيف يصبرون عليها؟ وأنَّى لهم الجلد عليها؟
(174 - 175) Hili ni tishio kali kwa wale wanaoficha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake katika elimu, ambayo Mwenyezi Mungu alichukua agano juu ya watu wake. Kwamba waibainishe kwa watu na wala wasiifiche. Basi mwenye kuibadilisha kwa takataka za kidunia, na akaficha amri ya Mwenyezi Mungu, basi hao “hawali katika tumbo zao isipokuwa moto.” Kwa sababu hiyo ndiyo thamani waliyoichuma, lakini iliwafikia kwa mapato mabaya mno, haramu iliyo kubwa zaidi. Kwa hivyo malipo yao yakawa ya aina sawa na matendo yao, “wala Mwenyezi Mungu hatawaongelesha Siku ya Kiyama.” Bali alikwisha wakasirikia na akawapa mgongo. “Wala hatawatakasa,” yani hatawatakasa kutokana na tabia chafu. Na wala hawana matendo yanayostahiki sifa, kuridhiwa, na malipo juu yake. Na hakuwatakasa kwa sababu, walifanya sababu za kutowatakasa ambako (huko kutakaswa) sababu zake kubwa ni kufanya matendo kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kuongoka kukielekea, na kukilingania. Lakini hawa walikitupa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakakipa mgongo, na wakachagua upotovu badala ya uwongofu, na adhabu badala ya msamaha. Kwa hivyo hawa (watu) hakiwafai kitu isipokuwa moto, basi vipi watakuwa na subira juu yake (moto), na ni vipi watakuwa na stahmala juu yake?
#
{176} {ذلك}؛ المذكور وهو مجازاته بالعدل ومنعه أسباب الهداية ممن أباها واختار سواها {بأن الله نزل الكتاب بالحق}؛ ومن الحق مجازاة المحسن بإحسانه والمسيء بإساءته، وأيضاً ففي قوله: {نزل الكتاب بالحق}؛ ما يدل على أن الله أنزله لهداية خلقه وتبيين الحق من الباطل والهدى من الضلال، فمن صرفه عن مقصوده فهو حقيق بأن يجازَى بأعظم العقوبة، {وإن الذين اختلفوا في الكتاب لفي شقاق بعيد}؛ أي: وإن الذين اختلفوا في الكتاب فآمنوا ببعضه وكفروا ببعضه والذين حرفوه وصرفوه على أهوائهم ومراداتهم {لفي شقاق}؛ أي: محادة {بعيد}؛ من الحق، لأنهم قد خالفوا الكتاب الذي جاء بالحق الموجب للاتفاق وعدم التناقض، فمرج أمرهم، وكثر شقاقهم، وترتب على ذلك افتراقهم، بخلاف أهل الكتاب الذين آمنوا به، وحكموه في كل شيء، فإنهم اتفقوا، وارتفقوا بالمحبة والاجتماع عليه. وقد تضمنت هذه الآيات الوعيد للكاتمين لما أنزل الله المؤثرين عليه عرض الدنيا بالعذاب والسخط، وأن الله لا يطهرهم بالتوفيق ولا بالمغفرة. وذكر السبب في ذلك بإيثارهم الضلالة على الهدى، فترتب على ذلك اختيار العذاب على المغفرة ثم توجع لهم بشدة صبرهم على النار لعملهم بالأسباب التي يعلمون أنها موصلة لها، وأن الكتاب مشتمل على الحق الموجب للاتفاق عليه وعدم الافتراق، وأن كل من خالفه فهو في غاية البعد عن الحق والمنازعة والمخاصمة. والله أعلم.
(176) “Hayo,” yaliyotajwa ambayo ni malipo yake kwa uadilifu, na kuzuia kwake sababu za uwongofu kwa yule aliyezikataa na akachagua zisizokuwa hizo. “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki.” Na katika haki ni kumlipa mwema kwa wema wake, na mwovu kwa wovu wake. Na pia katika kauli yake, “ameteremsha Kitabu kwa haki;” kuna dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu alikiteremsha ili kuwaongoa viumbe wake, na kubainisha haki kutokana na batili. Kwa hivyo, mwenye kukigeuza kutoka kwa makusudio yake, basi yeye anastahiki kulipwa kwa adhabu kubwa kabisa. “Na hakika, wale waliohitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki.” Yani kwa hakika wale waliohitalifiana katika Kitabu, na wakaamini baadhi yake na baadhi yake wakaikataa, na wale waliokibadilisha na wakakigeuza kwa matamanio yao na malengo yao. “Wamo katika upinzani ulio mbali na haki” kwa sababu walikihalifu Kitabu kilicholeta haki yenye kuleta kuafikiana na kutopingana. Basi mambo yao yakachafuka, na upinzani wao ukawa mwingi, na hilo likasababisha kujitenga kwao, kinyume na Ahlul-Kitab (watu wa Kitabu). Ambao walikiamini na wakahukumu kwacho katika kila jambo, hao walikubaliana na wakafanya urafiki kwa mapenzi na umoja juu yake. Aya hizi zilijumuisha tishio kwa wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Wanaopendelea badala yake mapambo ya dunia kwa adhabu na ghadhabu, na kwamba Mwenyezi Mungu hatawatakasa kwa kuwawezesha wala kwa msamaha. Na akataja sababu ya hayo, kwamba ni kupendelea kwao upotovu kuliko uwongofu, na hilo likapelekea kuchagua adhabu kuliko msamaha. Kisha akawaonea uchungu katika ukubwa wa subira yao juu ya moto, kwa sababu ya kutenda kwao sababu ambazo wanajua kuwa zinafikisha huko. Na kwamba Kitabu hiki kinajumuisha haki inayolazimu mapatano juu yake, na kutotengana. Na kwamba kila anayekipinga yuko mbali sana na haki, na kwamba yuko katika mzozo na ugomvi, na Mwenyzi Mungu anajua zaidi.
: 177 #
{لَيْسَ الْبِرَّ أَنْ تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَى حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ أُولَئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ (177)}
177. Siyo wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii. Na anawapa mali, licha ya kuipenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ukombozi. Na akawa anashika Swala, na akatoa Zaka, na wanaotimiza ahadi yao wanapoahidi, na wanaovumilia katika shida na dhara na wakati wa vita. Hao ndio walio sadikisha, na hao ndio wachamungu.
#
{177} يقول تعالى: {ليس البر أن تولوا وجوهكم قبل المشرق والمغرب}؛ أي: ليس هذا هو البر المقصود من العباد فيكون كثرة البحث فيه والجدال من العناء الذي ليس تحته إلا الشقاق والخلاف، وهذا نظير قوله - صلى الله عليه وسلم -: «ليس الشديد بالصرعة إنما الشديد الذي يملك نفسه عند الغضب» ، ونحو ذلك، {ولكن البر من آمن بالله}؛ أي: بأنه إله واحد موصوف بكل صفة كمال منزَّه عن كلِّ نقص {واليوم الآخر}؛ وهو كل ما أخبر الله به في كتابه أو أخبر به الرسول مما يكون بعد الموت {والملائكة}؛ الذين وصفهم الله لنا في كتابه ووصفهم رسوله - صلى الله عليه وسلم -، {والكتاب}؛ أي: جنس الكتب التي أنزلها الله على رسله وأعظمها القرآن فيؤمن بما تضمنه من الأخبار والأحكام. {والنبيين}؛ عموماً، خصوصاً خاتمهم وأفضلهم محمد - صلى الله عليه وسلم - {وآتى المال}؛ وهو كل ما يتمول الإنسان من مال قليلاً كان أو كثيراً أي أعطى المال {على حبه}؛ أي: حب المال بين به أن المال محبوب للنفوس فلا يكاد يخرجه العبد، فمن أخرجه مع حبه له تقرباً إلى الله تعالى كان هذا برهاناً لإيمانه، ومن إيتاء المال على حبه أن يتصدق وهو صحيح شحيح يأمل الغنى ويخشى الفقر، وكذلك إذا كانت الصدقة عن قلة كان أفضل لأنه في هذه الحال يحب إمساكه لما يتوهمه من العُدْم والفقر، وكذلك إخراج النفيس من المال وما يحبه من ماله كما قال تعالى: {لن تنالوا البر حتى تنفقوا مما تحبون}؛ فكل هؤلاء ممن آتى المال على حبه. ثم ذكر المنفق عليه وهم أولى الناس ببرِّك وإحسانك من الأقارب؛ الذين تتوجع لمصابهم وتفرح بسرورهم الذين يتناصرون ويتعاقلون، فمن أحسن البر وأوفقه تعاهد الأقارب بالإحسان المالي والقولي على حسب قربهم وحاجتهم، ومن {اليتامى}؛ الذين لا كاسب لهم وليس لهم قوة يستغنون بها، وهذا من رحمته تعالى بالعباد الدالة على أنه تعالى أرحم بهم من الوالد بولده، فالله قد أوصى العباد وفرض عليهم في أموالهم الإحسان إلى من فقد آباؤهم ليصيروا كمن لم يفقد والديه، ولأن الجزاء من جنس العمل فمن رحم يتيمَ غيره رُحِم يتيمه. {والمساكين}؛ وهم الذين أسكنتهم الحاجة وأذلهم الفقر فلهم حق على الأغنياء بما يدفع مسكنتهم أو يخففها بما يقدرون عليه وبما يتيسر. {وابن السبيل}؛ وهو الغريب المنقطع به في غير بلده. فحث الله عباده على إعطائه من المال ما يعينه على سفره لكونه مظنة الحاجة وكثرة المصارف، فعلى من أنعم الله عليه بوطنه وراحته وخوَّله من نعمته أن يرحم أخاه الغريب الذي بهذه الصفة على حسب استطاعته ولو بتزويده أو إعطائه آلة لسفره أو دفع ما ينوبه من المظالم وغيرها. {والسائلين}؛ أي: الذين تعرض لهم حاجة من الحوائج توجب السؤال، كمن ابتلي بأرش جناية أو ضريبة عليه من ولاة الأمور أو يسأل الناس لتعمير المصالح العامة كالمساجد والمدارس والقناطر ونحو ذلك فهذا له الحق وإن كان غنياً. {وفي الرقاب}؛ فيدخل فيه العتق والإعانة عليه وبذل مال للمكاتَب ليوفي سيده وفداء الأسراء عند الكفار أو عند الظلمة. {وأقام الصلاة وآتى الزكاة}؛ قد تقدم مراراً أن الله تعالى يقرن بين الصلاة والزكاة لكونهما أفضل العبادات، وأكمل القربات عبادات قلبية وبدنية ومالية، وبهما يوزن الإيمان ويعرف ما مع صاحبه من الإيقان، {والموفون بعهدهم إذا عاهدوا}؛ والعهد هو الالتزام بإلزام الله أو إلزام العبد لنفسه فدخل في ذلك حقوق الله كلها، لكون الله ألزم بها عباده والتزموها، ودخلوا تحت عهدتها ووجب عليهم أداؤها، وحقوق العباد التي أوجبها الله عليهم والحقوق التي التزمها العبد كالأيمان والنذور ونحو ذلك. {والصابرين في البأساء}؛ أي: الفقر لأن الفقير يحتاج إلى الصبر من وجوه كثيرة لكونه يحصل له من الآلام القلبية والبدنية المستمرة ما لا يحصل لغيره، فإن تنعم الأغنياء بما لا يقدر عليه تألم وإن جاع أو جاعت عياله تألم، وإن أكل طعاماً غير موافق لهواه تألم، وإن عري أو كاد تألم، وإن نظر إلى ما بين يديه وما يتوهمه من المستقبل الذي يستعد له تألم، وإن أصابه البرد الذي لا يقدر على دفعه تألم، فكل هذه ونحوها مصائب يؤمر بالصبر عليها والاحتساب ورجاء الثواب من الله عليها {والضراء}؛ أي: المرض على اختلاف أنواعه من حمى وقروح ورياح ووجع عضو حتى الضرس والإصبع ونحو ذلك فإنه يحتاج إلى الصبر على ذلك، لأن النفس تضعف والبدنَ يألم وذلك في غاية المشقة على النفوس، خصوصاً مع تطاول ذلك، فإنه يؤمر بالصبر احتساباً لثواب الله تعالى {وحين البأس}؛ أي: وقت القتال للأعداء المأمور بقتالهم، لأن الجلاد يشق غاية المشقة على النفس ويجزع الإنسان من القتل أو الجراح أو الأسر، فاحتيج إلى الصبر في ذلك احتساباً ورجاء لثواب الله تعالى الذي منه النصر والمعونة التي وعدها الصابرين. {أولئك}؛ أي: المتصفون بما ذكر من العقائد الحسنة والأعمال التي هي آثار الإيمان وبرهانه ونوره والأخلاق التي هي جمال الإنسان وحقيقة الإنسانية فأولئك {الذين صدقوا}؛ في إيمانهم لأن أعمالهم صدقت إيمانهم {وأولئك هم المتقون}؛ لأنهم تركوا المحظور وفعلوا المأمور، لأن هذه الأمور مشتملة على كل خصال الخير تضمناً ولزوماً لأن الوفاء بالعهد يدخل فيه الدين كله، ولأن العبادات المنصوص عليها في هذه الآية أكبر العبادات، ومن قام بها كان بما سواها أقوم، فهؤلاء [هم] الأبرار الصادقون المتقون. وقد علم ما رتب الله على هذه الأمور الثلاثة من الثواب الدنيوي والأخروي مما لا يمكن تفصيله في مثل هذا الموضع.
(177) Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema: “Siyo wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi.” Yani huu siyo wema uliokusudiwa kutoka kwa waja. Ndiyo inakuwa kufanya utafiti mwingi na mjadala juu yake ni katika kusumbukana ambako, hakuna kitu chini yake isipokuwa upinzani na hitilafu tu. Na hili ni sawa na kauli yake, (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. “Mwenye nguvu siyo mwenye kuwapiga watu miereka. Lakini mwenye nguvu ni yule anayejidhibiti nafsi yake anapokasirika,” na mfano wake. “Bali wema ni wa anayemuamini Mwenyezi Mungu” yani kwamba yeye ndiye Mungu mmoja. Anayesifika kwa kila sifa ya ukamilifu, aliyetakasika na kila upungufu. “Na Siku ya Mwisho” nayo ni kila aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake. Au aliyoyaeleza Mtume wake kuhusu yatakayotokea baada ya kufa. “Na Malaika” ambao Mwenyezi Mungu aliotueleza katika Kitabu chake na aliowaeleza Mtume wake rehema na amani zimshukie. “Na Kitabu,” yani vitabu vyote ambavyo Mwenyezi Mungu alivyoteremsha kwa Mtume wake. Na kitukufu zaidi kati yake ni Qur-ani. Basi ayaamini yaliyomo katika habari zake na hukumu zake, “na Manabii” kwa ujumla. Hususan wa mwisho wao na mbora wao wote, Muhammad rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie. “Na akawapa mali.” Nayo ni kila anachokichuma mtu katika mali, sawa iwe kidogo au nyingi. Yani akatoa mali “licha ya kuipenda kwake,” yani kuipenda mali. Hivyo akabainisha hapa kwamba mali inapendwa na nafsi, na hakaribii mja kuitoa. Kwa hivyo, mwenye kuitoa licha ya kuipenda ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi huu ni uthibitisho wa imani yake. Na katika kutoa mali licha ya kuipenda ni kwamba atoe sadaka hali ya kuwa ni mwenye afya nzuri, bahili mwenye utu nayo; hali ya kuwa anatarajia utajiri, anachelea umasikini. Kadhalika, ikiwa atatoa sadaka katika hali ya upungufu, inakuwa bora zaidi, kwa sababu katika hii hali, anapenda kuizuilia, kwa kile anachofikiri kuhusiana na kuikosa na ufukara. Na vivyo hivyo katika kutoa chenye thamani katika mali, na anachokipenda katika mali yake, kama alivyosema Aliyetukua. “Kamwe hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda.” Na hawa wote ni katika wale waliotoa mali pamoja na kuipenda. Kisha akataja wanaopewa. Nao ni wale watu wanaostahiki zaidi wema wako na ihsani yako, miongoni mwa jamaa ambao inakuumiza misiba yao, na unafurahia kwa furaha yao. Ambao wanasaidiana na wanasaidiana kutoa fidia ya mauaji. Basi katika wema ulio bora zaidi na kamilifu ni kuwahudumia jamaa kwa ihsani ya kimali na kikauli, kulingana na ukaribu wao na haja yao. Na pia mayatima ambao hawana mwenye kuwachumia. Na wala hawana uwezo wa kujitosheleza kwao. Na hii ni kutokana na rehema yake [Mwenyezi Mungu Mtukufu] kwa waja wake, ambayo inaonyesha kuwa Yeye ni mwenye rehema (huruma) zaidi kwao kuliko baba kwa mtoto wake. Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake, na akawafaradhishia katika mali zao kuwafanyia wema waliofiwa na wazazi wao, ili wawe kama wale ambao hawakupoteza wazazi wao. Na kwa sababu malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa hivyo, mwenye kumrehemu yatima wa asiyekuwa yeye, yatima wake atarehemewa. “Na masikini,” nao ndio wale ambao haja imewatuliza, na ufukara ukawadhalilisha. Basi wanayo haki juu ya matajiri kwa kile chenye kuondosha umasikini wao au kuupunguza. Kwa kile wanachoweza, na kwa kile kilicho chepesi. “Na wasafiri,” naye ni mgeni aliyekatikiwa katika nchi isiyokuwa ya nchi yake. Basi Mwenyezi Mungu akawahimiza waja wake wampe katika mali kile chenye kumsaidia katika safari yake, kwa sababu yeye kwa kawaida huwa na mahitaji, na mwenye gharama nyingi. Kwa hivyo, ni juu ya yule ambaye Mwenyezi Mungu amempa neema ya kuwa katika nchi yake na raha yake. Na akampa katika neema zake amrehemu ndugu yake mgeni, ambaye yuko katika sifa hizi kulingana na uwezo wake. Hata kama ni kwa kumpatia chakula cha njiani au kumpa chombo kwa ajili ya safari yake, au kumzuilia kinachompa katika dhuluma na mengineyo. “Na waombao,” yani wale wanaopatwa na haja miongoni mwa haja ambazo zinawalazimu kuomba. Kama vile yule aliyepewa mtihani wa kulipa fidia ya kufanya kosa la jinai au kodi anayolazimika kuwalipa viongozi. Au anayewaomba watu ili kuimarisha masilahi ya umma kama vile misikiti, shule, madaraja na mfano wake. Basi huyu ana haki (ya kupewa) hata kama ni tajiri. “Na katika ukombozi,” basi anaingia humo kumweka huru mtumwa na kumsaidia. Na kumpa mali Al-mukaatab (yule aliyeandikiana na bwana wake kujilipia pole pole mali ya kujikomboa) ili amtimizie bwana wake. Na kuwakomboa mateka wa vita kutoka kwa makafiri au kutoka kwa madhalimu. “Na akashika Swala na akatoa Zaka.” Na haya yalikwisha tangulia mara nyingi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweka pamoja swala na zaka. Kwa sababu hizo ndizo ibada bora zaidi. Na mambo ya kujiweka karibu kwa Mwenyezi Mungu kwayo yaliyo kamili zaidi ni ibada za moyoni, kimwili, na kimali. Na kwazo inapimwa imani, na inajulikana kwazo yakini ya mwenye hivyo. “Na wanaotimiza ahadi yao wanapoahidi.” Na ahadi ni kutekeleza alichowajibisha Mwenyezi Mungu au alichojiwajibishia mja mwenyewe. Basi akaingia katika hilo haki zote za Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewawajibishia hizo waja wake. Nao wakaziitikia basi wanalazimika kuzitimiza, na wakaingia chini ya ahadi yake, na ikawa ni wajibu kwao kuzitekeleza. Na haki za waja ambazo Mwenyezi Mungu aliziwajibisha juu yao. Na haki ambazo mja alijilazimishia mwenyewe kama vile viapo na nadhiri, na mfano wake. “Na wanaovumilia katika shida.” Yani ufukara, kwa sababu fukara anahitaji subira katika njia nyingi. Kwa sababu anapatwa na maumivu yenye kuendelea ya kimoyo na kimwili ambayo hayamfikii asiyekuwa yeye. Kwa maana, matajiri wakifurahia kwa kile asichoweza kukipata, anaumia. Na akipata njaa au watoto wake wakipatwa na njaa, anaumia. Na akila chakula kisichoendana na matamanio yake, anaumia. Na akiwa uchi au akakaribia kuwa uchi, anaumia. Na akitazama kilichoko mbele yake (cha sasa) na kile anachofikiria kukipata wakati ujao anaojitayarisha kwa ajili yake, anaumia. Na akipatwa na baridi ambayo hawezi kuizuia, anaumia. Basi haya yote na mfano wake ni taabu anazoamrishwa kuwa na subira juu yake. Kutumaini na kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili yake. “Na dhara,” yani maradhi kwa aina zake tofauti tofauti. Kuanzia homa, vidonda, upepo, na maumivu ya viungo, hata jino na kidole, na mfano wake. Yeye kwa hakika anahitaji subira kwa hayo. Kwa sababu, nafsi inadhoofika, na mwili unauma, na hilo ni gumu mno kwa nafsi, hasa ikiwa ni kwa muda mrefu. Hivyo basi ameamrishwa kuwa na subira, kwa kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu [Mtukufu]. “Na wakati wa vita,” yani wakati wa kupigana na maadui walioamrishwa kupigana nao. Kwa sababu, kusimama imara ni kugumu sana juu ya nafsi. Na mtu anahuzunika kwa sababu ya kuuawa, au kujeruhiwa, au kushikwa mateka. Kwa hivyo, anahitaji subira katika hayo akitarajia na kutumaini malipo ya Mwenyezi Mungu [Mtukufu]. Ambaye ushindi na usaidizi ni kutoka kwake, ambao aliwaahidi wenye subira. “Hao,” yani wale wanaosifika kwa yale yaliyotajwa ya imani njema, na matendo ambayo ni athari ya imani, na uthibitisho wake, na nuru yake. Na maadili ambayo ni uzuri wa mwanadamu na uhakika wa ubinadamu, basi hao “ndio waliosadikisha” katika imani yao. Kwa sababu matendo yao yalisadikisha imani yao, “na hao ndio wachamungu” kwa sababu waliacha makatazo, na wakafanya maamrisho. Kwa sababu mambo haya yanajumuisha sifa zote za heri kwa ndani yake na kwa kile zinazolazimu. Kwa sababu kutimiza ahadi kunajumuisha dini nzima, na kwa sababu ibada zilizotajwa katika Aya hii ndizo ibada kubwa kabisa. Na atakayezifanya, atasimama bora zaidi kwa zinginezo. Basi hao ndio watu wema, wakweli, wachamungu. Na imekwisha julikana kile alichoyawekea Mwenyezi Mungu mambo haya matatu ya malipo ya kidunia na ya kiakhera. Ambayo haiwezekani kuyabainisha kwa kina katika [mfano wa] mahali hapa.
: 178 - 179 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنْثَى بِالْأُنْثَى فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ذَلِكَ تَخْفِيفٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ فَمَنِ اعْتَدَى بَعْدَ ذَلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ (178) وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَاأُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ (179)}.
(178) Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika waliouawa - muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko ni kupunguziwa kulikotokana na Mola wenu Mlezi, na ni rehema. Na atakayevuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu chungu. (179) Mtakuwa na uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili mpate kuwa wachamungu.
#
{178} يَمْتَنُّ تعالى على عباده المؤمنين بأنه فرض عليهم {القصاص في القتلى}؛ أي: المساواة فيه، وأن يقتل القاتل على الصفة التي قتل عليها المقتول، إقامة للعدل والقسط بين العباد، وتوجيه الخطاب لعموم المؤمنين فيه دليل على أنه يجب عليهم كلهم حتى أولياء القاتل حتى القاتل بنفسه إعانة ولي المقتول إذا طلب القصاص، ويمكنه من القاتل، وأنه لا يجوز لهم أن يحولوا بين هذا الحد، ويمنعوا الولي من الاقتصاص كما عليه عادة الجاهلية ومن أشبههم من إيواء المحدِثين. ثم بين تفصيل ذلك فقال: {الحر بالحر}؛ يدخل بمنطوقها الذكر بالذكر، والأنثى بالأنثى؛ والأنثى بالذكر والذكر بالأنثى، فيكون منطوقها مقدماً على مفهوم قوله الأنثى بالأنثى مع دلالة السنة على أن الذكر يقتل بالأنثى، وخرج من عموم هذا الأبوان وإن علوا فلا يقتلان بالولد لورود السنة بذلك مع أن في قوله: {القصاص}؛ ما يدل على أنه ليس من العدل أن يقتل الوالد بولده ولأن ما في قلب الوالد من الشفقة والرحمة ما يمنعه من القتل لولده إلا بسبب اختلال في عقله أو أذية شديدة جدًّا من الولد له، وخرج من العموم أيضاً الكافر بالسنة مع أن الآية في خطاب المؤمنين خاصة، وأيضاً فليس من العدل أن يقتل ولي الله بعدوه، {والعبد بالعبد}؛ ذكراً كان أو أنثى تساوت قيمهما أو اختلفت، ودل بمفهومها على أن الحر لا يقتل بالعبد لكونه غير مساوٍ له، {والأنثى بالأنثى}؛ أخذ بمفهومها بعض أهل العلم فلم يجز قتل الرجل بالمرأة، وتقدم وجه ذلك. وفي هذه الآية دليل على أن الأصل وجوب القود في القتل وأن الدية بدل عنه، فلهذا قال: {فمن عفي له من أخيه شيء}؛ أي: عفا ولي المقتول عن القاتل إلى الدية أو عفا بعض الأولياء فإنه يسقط القصاص وتجب الدية وتكون الخيرة في القود واختيار الدية إلى الولي، فإذا عفا عنه، وجب على الولي؛ أي ولي المقتول أن يتبع القاتل، {بالمعروف}؛ من غير أن يشق عليه ولا يحمله ما لا يطيق، بل يحسن الاقتضاء والطلب ولا يحرجه. وعلى القاتل {أداء إليه بإحسان}؛ من غير مطلٍ ولا نقص ولا إساءة فعلية أو قولية، فهل جزاء الإحسان إليه بالعفو إلا الإحسان بحسن القضاء، وهذا مأمور به في كل ما ثبت في ذمم الناس للإنسان مأمور من له الحق بالاتباع بالمعروف ومن عليه الحق بالأداء بالإحسان ، وفي قوله: {فمن عفي له من أخيه}؛ ترقيق وحث على العفو إلى الدية وأحسن من ذلك العفو مجاناً. وفي قوله: {أخيه}؛ دليل على أن القاتل لا يكفر لأن المراد بالأخوة هنا أخوة الإيمان فلم يخرج بالقتل منها ومن باب أولى أن سائر المعاصي التي هي دون الكفر لا يكفر بها فاعلها وإنما ينقص بذلك إيمانه، وإذا عفا أولياء المقتول أو عفا بعضهم احتقن دم القاتل وصار معصوماً منهم ومن غيرهم، ولهذا قال: {فمن اعتدى بعد ذلك}؛ أي: بعد العفو، {فله عذاب أليم}؛ أي في الآخرة، وأما قتله وعدمه فيؤخذ مما تقدم لأنه قتل مكافئاً له فيجب قتله بذلك، وأما من فسر العذاب الأليم بالقتل، وأن الآية تدل على أنه يتعين قتله ولا يجوز العفو عنه، وبذلك قال بعض العلماء، والصحيح الأول لأن جنايته لا تزيد على جناية غيره.
{178} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakumbusha waja wake Waumini neema yake juu yao kwamba aliwafaradhishia “kisasi katika waliouawa.” Yani kufanya usawa katika hilo, na kwamba muuaji auawe kwa namna ambayo alimuulia aliyeuawa, ili kusimamisha uadilifu na haki kati ya waja. Na kuyaelekeza maneno haya kwa Waumini, kwa ujumla ndani yake kuna dalili kwamba ni wajibu kwao wote. Hata jamaa wa muuaji, hata muuaji mwenyewe, kumsaidia jamaa wa aliyeuawa; ikiwa ataitisha malipo na kuwezeshwa juu ya muuaji. Na kwamba hairuhusiki kwao kuzuia hadd hii (adhabu maalumu), na kumzuia jamaa huyo kufanya kisasi. Kama ilivyokuwa tabia ya Jahiliyya, na mwenye kufanana nao miongoni mwa wanaowapa wakosefu ulinzi. Kisha akabainisha undani wa hayo, akasema: “Muungwana kwa muungwana” anaingia katika tamko lake mwanamume kwa mwanamume, “na mwanamke kwa mwanamke” na mwanamke kwa mwanamume, na mwanamume kwa mwanamke. Na inakuwa kwamba, tamko lake lilitangulizwa mbele ya yanayofahamika katika kauli yake. “Mwanamke kwa mwanamke” pamoja na dalili ya Sunnah kwamba mwanamume huuawa kwa mwanamke. Na walitoka katika ujumla wa hili wazazi wawili hata kama watakwenda juu vipi. Hao hawauawi kwa mtoto wao, kwa sababu ya Sunnah inayoonyesha hilo. Pamoja na kwamba katika kauli yake “kulipiza kisasi,” kuna kinachoashiria kuwa siyo katika uadilifu kumuua baba kwa sababu ya kumuua mtoto wake. Na kwa sababu katika moyo wa baba wa huruma na rehema, kile kinachomzuia kumuua mtoto wake isipokuwa kwa sababu ya kasoro katika akili yake. Au madhara makubwa sana kutoka kwa mtoto wake. Pia ametoka katika ujumla huo ni kafiri kulingana na Sunnah, ingawa Aya inawazungumzia hasa Waumini. Pia, siyo katika haki kumuua rafiki ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya adui yake. Na mtumwa kwa mtumwa, awe mwanamume au mwanamke, thamani yao iwe sawa au tofauti. Na (aya) inaonyesha kwa maana yake isiyo ya moja kwa moja kwamba mtu huru hauawi kwa ajili ya mtumwa. Kwa sababu yeye (huru) sio sawa naye. Na katika “mwanamke kwa mwanamke,” na baadhi ya wanachuoni walizingatia maana yake isiyo ya moja kwa moja. Kwa hivyo hawakuruhusu kumuua mwanamume kwa ajili ya mwanamke, lakini kuruhusika kwa hilo kulikwisha tangulia. Na katika Aya hii, kuna dalili kwamba kanuni ya msingi ni ulazima wa kulipiza kisasi katika kuua. Na kwamba diya (fidia ya mauaji) ni badala yake. Ndiyo maana akasema: “Na anayesamehewa na ndugu yake chochote.” Yani jamaa ya aliyeuawa akamsamehe muuaji, na akakubali kuchukua diya (fidia ya mauaji) au baadhi ya jamaa wakasamehe. Basi hapo kisasi hakitakuwepo, na diya inakuwa lazima. Na hiari kati ya kisasi na kuchukua diya ni juu ya jamaa ya aliyeuawa. Ikiwa atamsamehe, basi itamlazimu jamaa [yani ya aliyeuawa] kumfuata muuaji [kwa wema] bila ya kumfanyia ugumu. Na wala kumbebesha kile asichoweza kustahimili. Bali afanye wema katika kudai na kuitisha, na wala asimfadhaishe. Na ni juu ya muuaji, “alipe kwa ihsani” bila ya kuchelewesha, wala kupunguza, wala kufanya ubaya kimatendo wala kimaneno. Je, malipo ya kumfanyia wema wa kumsamehe siyo isipokuwa (yeye) kufanya wema kwa kulipa vyema? Na haya yameamrishwa katika kila kilichothibitika dhima za watu miongoni mwa haki za wengine. Na ameamrishwa mwenye haki juu ya kuifuata kwa wema, ambaye haki iko juu yake kuilipa kwa wema. Na katika kauli yake,“ na anayesamehewa na ndugu yake chochote.” Kuna kufanya upole na kuhimiza kusamehe na kuchukua mali ya damu, na bora zaidi kuliko hilo ni kusamehe bure. Na katika kauli yake, “ndugu yake” kuna dalili ya kwamba muuaji hawi kafiri. Kwa sababu hapa kinachokusudiwa na udugu ni udugu wa imani. Basi hakutoka humo kwa kuua. Na katika mlango wa yale yanayofaa zaidi kuwa hivyo ni dhambi zinginezo zote zilizoko chini ya ukafiri; kwamba hawi kafiri kwazo mwenye kuzitenda. Bali hayo yanapunguza tu imani yake. Na ikiwa jamaa za aliyeuawa watasamehe, au baadhi yao wakasamehe, basi damu ya muuaji itahifadhika. Na atakuwa amehifadhika kutokana nao na kutokana na wengineo, na kwa ajili hiyo akasema: “Na atakayevuka mipaka baada ya haya.” Yani baada ya kusamehe, “basi yeye ana adhabu chungu,” yani katika Akhera. Na ama kuhusu kuua kwake na kutoua kwake, basi hayo yanachukuliwa kutoka kwa yale yaliyotangulia. Kwa sababu atakuwa amemuua aliye sawa naye, basi inalazima auawe kwa hilo. Ama yule aliyefasiri adhabu chungu kuwa ni kuua (muuaji baada ya kumsamehe), basi Aya hii inaashiria kuwa ni lazima auawe; na wala hairuhusiki kumsamehe. Na hilo ndilo walilosema baadhi ya wanachuoni, lakini lile la kwanza ndilo sahihi. Kwa sababu kosa lake la jinai halizidi kosa la jinai la wengine.
Kisha Mola Mtukufu akabainisha hekima yake kubwa katika kuweka sheria ya kulipiza kisasi, akasema:
#
{179} {ولكم في القصاص حياة}؛ أي: تنحقن بذلك الدماء وتنقمع به الأشقياء، لأن من عرف أنه مقتول إذا قتل لا يكاد يصدر منه القتل، وإذا رُئيَ القاتل مقتولاً انذعر بذلك غيره وانزجر، فلو كانت عقوبة القاتل غير القتل لم يحصل انكفاف الشر الذي يحصل بالقتل، وهكذا سائر الحدود الشرعية فيها من النكاية والانزجار ما يدل على حكمة الحكيم الغفار. ونكر الحياة لإفادة التعظيم والتكثير، ولما كان هذا الحكم لا يعرف حقيقته إلا أهل العقول الكاملة والألباب الثقيلة خصهم بالخطاب دون غيرهم، وهذا يدل على أن الله تعالى يحب من عباده أن يعملوا أفكارهم وعقولهم في تدبر ما في أحكامه من الحكم والمصالح الدالة على كماله وكمال حكمته وحمده وعدله ورحمته الواسعة، وأن من كان بهذه المثابة فقد استحقَّ المدح بأنه من ذوي الألباب الذين وجه إليهم الخطاب وناداهم رب الأرباب، وكفى بذلك فضلاً وشرفاً لقوم يعقلون. وقوله: {لعلكم تتقون}؛ وذلك أن من عرف ربه، وعرف ما في دينه وشرعه من الأسرار العظيمة والحكم البديعة والآيات الرفيعة أوجب له ذلك أن ينقاد لأمر الله، ويعظم معاصيه فيتركها؛ فيستحق بذلك أن يكون من المتقين.
“Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi” yani damu zitahifadhika kwa hilo, na watazuilika waovu kwa hilo. Kwa sababu anayejua kwamba yeye atauawa akiua, basi haitakaribia kuua kutokea kwake. Na muuaji anapoonekana ameuawa, basi asiyekuwa yeye ataogopa na kukomeka. Na lau kuwa adhabu ya muuaji haingekuwa siyo kuua, basi haingezuilika shari (uovu) kama kule kuzuilika kunakotokana (kutekeleza adhabu ya) na kuua. Na vivyo hivyo adhabu za kisheria zote zenye kinaya na kukomeka kuna kile kinachoonyesha hekima ya Mwenye hekima, Mwenye kusamehe. Na neno “uhai” limeachwa katika hali ya nomino ya kawaida ili iwe na maana ya utukufu na wingi. Na kwa vile hukumu hii haijui uhalisia wake isipokuwa wenye akili timilifu na wenye ufahamu mkubwa, amewahusisha na usemi huu na siyo wasiokuwa wao. Na hili linaashiria kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kwa waja wake kwamba, wazitumie fikira zao na akili zao katika kutafakari zile hekima zilizoko katika hukumu zake na masilahi yanayoashiria ukamilifu wake, na ukamilifu wa hekima yake, na sifa zake na uadilifu, wake na rehema yake pana. Na kwamba yeyote aliye katika daraja hii, basi anastahiki kusifiwa katika wenye akili ambao usemi huu ulielekezwa kwao, na akawaita Mola Mlezi wa mabwana wote. Na hiyo inatosha kuwa fadhila na heshima kwa watu wanaotumia akili zao. Na kauli yake, “ili mpate kuwa wachamungu.” Na hilo ni kwamba anayemjua Mola wake Mlezi na anayajua yaliyomo katika dini yake, na sheria miongoni mwa siri kubwa na hekima ya ajabu na Aya (ishara) tukufu. Hayo yatamlazimu kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, na kuyaona maasia yake kuwa jambo kubwa, ili ayaache. Kwa hivyo akastahiki kwa hayo kuwa miongoni mwa wachamungu.
: 180 - 182 #
{كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِنْ تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ (180) فَمَنْ بَدَّلَهُ بَعْدَ مَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (181) فَمَنْ خَافَ مِنْ مُوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (182)}
(180) Mmeandikiwa mmoja wenu anapofikwa na mauti, kama ataacha heri (yani mali), afanye wasia kwa wazazi wake wawili, na jamaa zake kwa wema. Ni haki juu ya wachamungu. (181) Na atakayeibadilisha (wasia) baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoibadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. (182) Na mwenye kumhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi, na akasuluhisha baina yao, basi hakuna dhambi yoyote juu yake. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.
#
{180} أي: فرض الله عليكم يا معشر المؤمنين {إذا حضر أحدكم الموت}؛ أي: أسبابه كالمرض المشرف على الهلاك وحضور أسباب المهالك وكان قد {ترك خيراً }؛ وهو المال الكثير عرفاً فعليه أن يوصي لوالديه وأقرب الناس إليه بالمعروف على قدر حاله من غير سرف ولا اقتصار على الأبعد دون الأقرب، بل يرتبهم على القرب والحاجة ولهذا أتى فيه بأفعل التفضيل، وقوله: {حقًّا على المتقين}؛ دل على وجوب ذلك، لأن الحق هو الثابت، وقد جعله الله من موجبات التقوى. واعلم أن جمهور المفسرين يرون أن هذه الآية منسوخة بآية المواريث، وبعضهم يرى أنها في الوالدين والأقربين غير الوارثين، مع أنه لم يدل على التخصيص بذلك دليل، والأحسن في هذا أن يقال إن هذه الوصية للوالدين والأقربين مجملة ردها الله تعالى إلى العرف الجاري، ثم إن الله تعالى قدر للوالدين الوارثين وغيرهما من الأقارب الوارثين هذا المعروف في آيات المواريث بعد أن كان مجملاً، وبقي الحكم فيمن لم يرثوا من الوالدين الممنوعين من الإرث وغيرهما ممن حُجِب بشخص أو وصف، فإن الإنسان مأمور بالوصية لهؤلاء وهم أحق الناس ببره، وهذا القول تتفق عليه الأمة، ويحصل به الجمع بين القولَيْنِ المتقدِمَيْنِ، لأن كلاًّ من القائلَيْنِ بهما كلٌّ منهم لَحظَ مَلْحَظاً واختلف المورد، فبهذا الجمع يحصل الاتفاق والجمع بين الآيات، فإنه مهما أمكن الجمع كان أحسن من ادعاء النسخ الذي لم يدل عليه دليل صحيح.
Yani Mwenyezi Mungu aliwafaradhishieni nyinyi, enyi kundi la Waumini, “mmoja wenu anapofikwa na mauti.” Yani sababu zake kama vile maradhi yanayokaribia kuangamiza, na kuwepo kwa sababu za maangamizo. Na alikuwa “ataacha heri” [yani mali] ambayo ni mali nyingi kwa mujibu wa desturi. Basi inamlazimu awausie wazazi wake wawili na jamaa wa karibu kwake kwa wema, kwa kadiri ya hali yake bila ya uharibifu. Na wala kumpa wa mbali zaidi peke yake na siyo wa karibu zaidi, bali awapange kulingana na ukaribu wao na haja zao. Na kwa sababu hii ndiyo alitumia ndani yake vitendo vya kuboresha. Na kauli yake, “ni haki juu ya wachamungu” inaonyesha ulazima wa hilo. Kwa sababu, haki ni kile kilichothubutu. Na Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni miongoni mwa yale yenye kuleta uchamungu. Na jua ya kwamba wengi wa wafasiri wanaona kuwa Aya hii ilifutwa na Aya ya mirathi. Na baadhi yao wanaona kuwa inahusiana na wazazi wawili na jamaa ambao si warithi; ingawa hakuna dalili inayobainisha umahsusi huo. Katika suala hili, ni bora zaidi kusema: Hakika wasia hii ni kwa wazazi wawili na jamaa kwa ujumla, ila Mwenyezi Mungu Mtukufu alirudisha (maelezo yake yaamuliwe) kwa desturi ya sasa (ya watu). Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawawekea viwango wazazi wawili wanaorithi na jamaa wengine wanaorithi wema huo katika Aya za mirathi. Baada ya kwamba (wema huo) ulikuwa kiujumla, na ikabaki hukumu kuhusu wale ambao hawakurithi miongoni mwa wazazi waliozuiliwa kurithi na wengineo ambao walizuiwa kwa sababu ya mtu au sifa fulani. Basi mtu ameamrishwa kuwafanyia wasia watu hawa, na wao ndio wanaostahiki zaidi wema wake. Na kauli hii umma umekubaliana juu yake, na kwayo kunapatikana kupatanisha kati ya zile kauli mbili zilizotangulia. Kwa sababu, kila mmoja ya wale wanaozisema kila mmoja wao aliona kitu, lakini mitazamo ikatofautiana. Na kwa huku kupatanisha, kunakuwa na kuafikiana na kupatanisha kati ya Aya hizi. Kwa sababu, kila inapowezekana kupatanisha inakuwa bora zaidi kuliko kudai kuwepo ufutaji ambao hauungwi mkono na dalili yoyote sahihi.
Na kwa kuwa mwenye kuusia anaweza kukataa kuusia, kwa sababu ya anachodhania kwamba wale wa baada yake anaweza badili aliyoyausia, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
#
{181 - 182} {فمن بدله}؛ أي: الإيصاء للمذكورين أو غيرهم {بعدما سمعه}؛ أي: بعد ما عقله وعرف طرقه وتنفيذه {فإنما إثمه على الذين يبدلونه}؛ وإلا فالموصي وقع أجره على الله، وإنما الإثم على المبدل المغير {إن الله سميع}؛ يسمع سائر الأصوات ومنه سماعه لمقالة الموصي ووصيته فينبغي له أن يراقب من يسمعه ويراه وأن لا يجور في وصيته، {عليم}؛ بنيته وعليم بعمل الموصَى إليه، فإذا اجتهد الموصي، وعلم الله من نيته ذلك أثابه ولو أخطأ، وفيه التحذير للموصَى إليه من التبديل، فإن الله عليم به مطلع على [ما] فعله فليحذر من الله، هذا حكم الوصية العادلة وأما الوصية التي فيها حيف وجنف وإثم فينبغي لمن حضر الموصي وقت الوصية بها أن ينصحه بما هو الأحسن والأعدل، وأن ينهاه عن الجور والجنف وهو الميل بها عن خطأ من غير تعمد، والإثم وهو التعمد لذلك، فإن لم يفعل ذلك فينبغي له أن يصلح بين الموصَى إليهم ويتوصل إلى العدل بينهم على وجه التراضي والمصالحة ووعظهم بتبرئة ذمة ميتهم، فهذا قد فعل معروفاً عظيماً، وليس عليه إثم كما على مبدل الوصية الجائزة ولهذا قال: {إن الله غفور}؛ أي: يغفر جميع الزلات ويصفح عن التبعات لمن تاب إليه، ومنه مغفرته لمن غض من نفسه وترك بعض حقه لأخيه لأن من سامح سامحه الله، غفور لميتهم الجائر في وصيته إذا احتسبوا بمسامحة بعضهم بعضاً لأجل براءة ذمته، {رحيم}؛ بعباده حيث شرع لهم كل أمر به يتراحمون ويتعاطفون. فدلت هذه الآيات على الحث على الوصية وعلى بيان من هي له وعلى وعيد المبدل للوصية العادلة والترغيب في الإصلاح في الوصية الجائرة.
{181 - 182} “Na atakayeibadilisha,” yani wasia kwa waliotajwa au wengineo “baada ya kuusikia” [yani] baada ya kuufahamu. Na akazijua njia zake na kuutekeleza kwake, "basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoibadilisha." Vinginevyo, aliyeusia malipo yake tayari yamekwisha fika kwa Mwenyezi Mungu, lakini dhambi ni juu ya mwenye kubadilisha, mwenye kughairi. “Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia.” Yeye husikia sauti zote, pamoja na kusikia kwake maneno ya mwenye kuusia na wasia wake. Kwa hivyo, inampasa amchunge yule anayemsikia na kumuona, na wala asifanye dhuluma katika wasia wake. “Mwenye kujua” nia yake na anayajua matendo ya aliyeusiwa. Basi mwenye kuusia akijitahidi, na Mwenyezi Mungu akajua hilo katika nia yake, atamlipa hata ikiwa atakosea. Na ndani yake kuna onyo kwa yule anayeusiwa dhidi ya kubadilisha. Kwani Mwenyezi Mungu anamjua (alieyusiwa), na anaona anayofanya, basi na amtahadhari Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo hukumu ya wasia yenye uadilifu. Na ama wasia ambayo ina dhuluma ndani yake na kwenda kombo, na dhambi, basi inampasa anayemhudhuria mwenye kuusia wakati wa wasia kumshauri kwa lililo bora zaidi na lenye uadilifu; na kwamba amkataze dhidi ya dhuluma na kwenda kombo. Nako ni kule kwenda kombo katika wasia bila ya kukusudia. Nalo dhambi ni kukusudia kufanya hivyo.Na asipofanya hivyo, basi inampasa (mwenye kusuluhisha) kusuluhisha baina ya waliousiwa, na afikie uadilifu baina yao kwa msingi wa kuridhiana na kusuluhishana, na kuwausia kuiondolea dhima (lawama) maiti wao. Basi mwenye kufanya hivyo, atakuwa amefanya wema mkubwa, na hakuna dhambi juu yao, kama ilivyo dhambi juu ya aliyebadilisha wasia. Na ndio maana akasema: “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu.” Yani Yeye husamehe makosa yote, na hutupilia mbali yale yanayotokana na hayo kwa mwenye kutubu kwake. Na pia inaingia hapo msamaha wake kwa mwenye kujikasirikia na kumwachia ndugu yake baadhi ya haki zake. Kwa sababu anayesamehe, Mwenyezi Mungu humsamehe, na ni Msamehevu kwa maiti wao aliyefanya dhuluma katika wasia wake; ikiwa watatarajia malipo (kwa Mwenyezi Mungu) kwa kusameheana wao kwa wao kwa ajili kuitoa dhima yake (maiti) katika lawama. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema kwa waja wake, ambapo aliwawekea sheria ya kila amri ambayo kwayo wanarehemeana na kuhurumiana. Basi aya hizi zikaonyesha kuhimizwa kufanya wasia, na kubainisha ni kwa nani, na tishio la adhabu kwa mwenye kuibadilisha wasia yenye uadilifu, na kuhimiza kusuluhisha wasia yenye dhuluma.
: 183 - 185 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ (183) أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ فَمَنْ تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ وَأَنْ تَصُومُوا خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (184) شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (185)}
(183) Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Saumu, kama walivyoandikiwa (watu) waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. (184) (Mfunge) siku zenye kuhesabika. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini, basi atimize hesabu katika siku nyingine. Na wale wasioweza, watoe fidia kwa kumlisha masikini. Na atakayefanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ndiyo bora kwenu, ikiwa mnajua. (185) Mwezi wa Ramadhani ndio ambao imeteremshwa Qur-ani ndani yake kuwa uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Kwa hivyo, atakayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hesabu katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anawatakia yaliyo mepesi, wala hawatakii yaliyo mazito, na ili mkamilishe hesabu hiyo, na ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa yale aliyowaongoa ili mpate kushukuru.
#
{183} يخبر تعالى بما منَّ الله به على عباده بأنه فرض عليهم الصيام كما فرضه على الأمم السابقة لأنه من الشرائع والأوامر التي هي مصلحة للخلق في كل زمان، وفيه تنشيط لهذه الأمة بأنه ينبغي لكم أن تنافسوا غيركم في تكميل الأعمال والمسارعة إلى صالح الخصال، وأنه ليس من الأمور الثقيلة التي اختصَّيتم بها. ثم ذكر تعالى حكمته في مشروعية الصيام فقال: {لعلكم تتقون}؛ فإن الصيام من أكبر أسباب التقوى لأن فيه امتثال أمر الله واجتناب نهيه، فممِّا اشتمل عليه من التقوى أن الصائم يترك ما حرم الله عليه من الأكل والشرب والجماع ونحوها التي تميل إليها نفسه متقرباً بذلك إلى الله راجياً بتركها ثوابه، فهذا من التقوى، ومنها: أن الصائم يدرب نفسه على مراقبة الله تعالى فيترك ما تهوى نفسه مع قدرته عليه لعلمه باطلاع الله عليه، ومنها: أنَّ الصيام يضيق مجاري الشيطان فإنه يجري من ابن ادم مجرى الدم فبالصيام يضعف نفوذه وتقل منه المعاصي، ومنها: أن الصائم في الغالب تكثر طاعته والطاعات من خصال التقوى، ومنها: أن الغني إذا ذاق ألم الجوع أوجب له ذلك مواساة الفقراء المعدمين. وهذا من خصال التقوى.
({83} Mola Mtukufu anatoa habari yale aliyowaneemesha kwayo waja wake kwamba aliwafaradhishia kufunga Saumu kama alivyoifaradhisha kwa umma zilizopita. Kwa sababu ni miongoni mwa sheria na maamrisho ambayo ni masilahi ya viumbe katika nyakati zote. Na ndani yake kuna kuuhimiza umma huu kwamba mnapaswa mshindane na wengineo katika kukamilisha matendo, na kuharakisha kuziendea sifa zilizo njema; na kwamba siyo katika mambo mazito ambayo ni mahususi kwenu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hekima yake katika kuweka sheria ya kufunga Saumu akasema, “ili mpate kumcha Mungu.” Kwa sababu kufunga saumu ni miongoni mwa sababu kubwa za uchamungu. Kwa sababu ndani yake kuna kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake. Na katika yale inayojumuisha ya uchamungu ni kuwa mtu mwenye Saumu anaacha yale ambayo Mwenyezi Mungu amemharamishia katika kula, kunywa, kujamiiana na mfano wake, ambayo nafsi yake huyaelekea. Akifanya hivyo ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu, akitaraji malipo yake kwa kuyaacha, na hilo ni katika uchamungu. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye Saumu anaizoesha nafsi yake juu ya kumchunga Mwenyezi Mungu Mtukufu. Basi anaacha kile kinachotamaniwa na nafsi yake ijapokuwa ana uwezo juu yake, kwa sababu anajua kwamba Mwenyezi Mungu anamwona. Na miongoni mwake ni kwamba Saumu hupunguza njia za Shetani. Kwa maana, yeye (Shetani) hupita katika mwanadamu kama kupita kwa damu, kwa hivyo kwa kufunga Saumu, athari zake hudhoofika, na dhambi zinapungua kutoka kwake. Na miongoni mwake ni kwamba mwenye kufunga Saumu mara nyingi utiifu wake huwa mwingi. Na mambo ya utiifu ni miongoni mwa sifa za uchamungu. Na miongoni mwake ni kwamba, tajiri anapoonja uchungu wa njaa, hilo linamlazimu kuwafariji mafukara wasiokuwa na kitu. Na hilo ni katika sifa za uchamungu.
#
{184} ولما ذكر أنه فرض عليهم الصيام أخبر أنه أيام معدودات أي قليلة في غاية السهولة ثم سهل تسهيلاً آخر فقال: {فمن كان منكم مريضاً أو على سفر فعدة من أيام أخر}؛ وذلك للمشقة في الغالب رخص الله لهما في الفطر، ولما كان لا بد من حصول مصلحة الصيام لكل مؤمن أمرهما أن يقضياه في أيام أخر إذا زال المرض وانقضى السفر وحصلت الراحة، وفي قوله: {فعدة من أيام}؛ فيه دليل على أنه يقضي عدد أيام رمضان كاملاً كان أو ناقصاً وعلى أنه يجوز أن يقضي أياماً قصيرة باردة عن أيام طويلة حارة كالعكس، وقوله: {وعلى الذين يطيقونه}؛ أي: يطيقون الصيام {فدية}؛ عن كل يوم يفطرونه {طعام مسكين}؛ وهذا في ابتداء فرض الصيام لما كانوا غير معتادين للصيام وكان فرضه حتماً فيه مشقة عليهم دَرَّجَهم الربُّ الحكيم بأسهل طريق، وخَيَّرَ المطيق للصوم بين أن يصوم وهو أفضل أو يطعم ولهذا قال: {وأن تصوموا خير لكم}؛ ثم بعد ذلك جعل الصيام حتماً على المطيق، وغير المطيق يفطر ويقضيه في أيام أُخَر، وقيل: وعلى الذين يطيقون؛ أي يتكلفونه، ويشق عليهم مشقة غير محتملة كالشيخ الكبير، فدية عن كل يوم مسكين، وهذا هو الصحيح.
{184} Na alipotaja kuwa aliwafaradhishia kufunga Saumu, alitoa habari kuwa ni siku zenye kuhesabika, yani chache na rahisi sana. Kisha akafanya urahisi mwingine. Akasema “Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini, basi atimize hesabu katika siku nyingine.” Na hayo ni kwa sababu ya ugumu (dhiki) mara nyingi, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaruhusu wafungue. Na kwa kuwa ilikuwa ni lazima kila Muumini kupata faida ya kufunga Saumu, akawaamrisha walipe katika siku nyingine ugonjwa unapoisha, na safari ikaisha, na raha (kupumzika) ikapatikana. Na katika kauli yake, “basi atimize hesabu katika siku nyingine.” Kuna dalili ya kwamba analipa kwa idadi ya siku za Ramadhani, sawa (mwezi) ulikuwa kamili au mpungufu. Na kwamba inaruhusika kulipa siku zilizokuwa fupi zenye baridi katika siku ndefu zenye joto, na kinyume chake. Na kauli yake “Na wale wanaoweza kufunga” yani wanaoweza kufunga Saumu, “watoe fidia” kwa kila siku wanayofungua ndani yake “kwa kumlisha masikini”. Na hii (hukumu) ilikuwa mwanzoni mwa kufaradhishwa kufunga Saumu, walipokuwa hawajazoea kufunga saumu. Na pindi kuifanya kuwa faradhi juu yao kungekuwa bila shaka na ugumu juu yao, ndio maana Mola Mlezi, Mwenye hekima akawawazoesha kwa njia nyepesi. Na akampa hiari mwenye uwezo wa kufunga Saumu kati ya kufunga Saumu, nalo ndilo bora, au kulisha (masikini). Ndiyo akasema: “Na mkifunga ndiyo bora kwenu.” Kisha baada ya hayo akafanya kufunga Saumu kuwa lazima kwa wale wenye uwezo. Nao wasioweza, wanafuturu na wanazilipa katika siku nyingine. [Na ilisemwa maana yake ni “wale wanaoweza kufunga,” yani wanoweza kwa shida, na kufunga kunawawia kugumu; ugumu ambao haustahimiliki. Kama vile mzee sana, basi atalipa fidia kwa kila siku masikini, na hii ndiyo kauli sahihi].
#
{185} {شهر رمضان الذي أنزل فيه القرآن}؛ أي: الصوم المفروض عليكم هو شهر رمضان الشهر العظيم الذي قد حصل لكم فيه من الله الفضل العظيم، وهو القرآن الكريم المشتمل على الهداية لمصالحكم الدينية والدنيوية وتبيين الحق بأوضح بيان، والفرقان بين الحق والباطل والهدى والضلال وأهل السعادة وأهل الشقاوة، فحقيق بشهر هذا فضله، وهذا إحسان الله عليكم فيه، أن يكون موسماً للعباد مفروضاً فيه الصيام، فلما قرره وبين فضيلته وحكمة الله تعالى في تخصيصه قال: {فمن شهد منكم الشهر فليصمه}؛ هذا فيه تعيين الصيام على القادر الصحيح الحاضر، ولما كان النسخ للتخيير بين الصيام والفداء خاصة، أعاد الرخصة للمريض والمسافر لئلا يتوهم أن الرخصة أيضاً منسوخة فقال: {يريد الله بكم اليسر ولا يريد بكم العسر}؛ أي: يريد الله تعالى أن ييسر عليكم الطرق الموصلة إلى رضوانه أعظم تيسير ويسهلها أبلغ تسهيل، ولهذا كان جميع ما أمر الله به عباده في غاية السهولة في أصله، وإذا حصلت بعض العوارض الموجبة لثقله؛ سهله تسهيلاً آخر إما بإسقاطه أو تخفيفه بأنواع التخفيفات، وهذه جملة لا يمكن تفصيلها، لأن تفاصيلها جميع الشرعيات، ويدخل فيها جميع الرخص والتخفيفات. {ولتكملوا العدة}؛ وهذا والله أعلم لئلا يتوهم متوهم أن صيام رمضان يحصل المقصود منه ببعضه، دفع هذا الوهم بالأمر بتكميل عدته، ويشكر الله تعالى عند إتمامه على توفيقه وتسهيله وتبيينه لعباده وبالتكبير عند انقضائه، ويدخل في ذلك التكبير عند رؤية هلال شوال إلى فراغ خطبة العيد.
{185} “Mwezi wa Ramadhani ndio ambao imeteremshwa Qur-ani ndani yake.” Yani maana Saumu iliyofaradhishwa juu yenu ni ya mwezi wa Ramadhani. Mwezi mtukufu ambao ndani yake mlipata fadhila kubwa sana kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nayo ni Qur-ani Tukufu, ambayo inajumuisha uwongofu kwa masilahi yenu ya kidini na kidunia, na kubainisha haki kwa njia iliyo wazi zaidi. Na upambanuzi kati ya haki na batili, uwongofu na upotofu, na watu wa furaha (waliobahatika) na watu wa mashakani (waliohasirika). Kwa hivyo, haishangazi kwamba mwezi ambao hizi ndizo fadhila zake, na hii ihsani ya Mwenyezi Mungu juu yenu ndani yake, uwe ndio msimu wa ibada; ambao kufunga Saumu kumefaradhishwa ndani yake. Na alipothibitisha hilo, na akabainisha fadhila zake, na hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuuteua, akasema: “Kwa hivyo, atakayeushuhudia mwezi miongoni mwenu, basi na afunge”. Na aya hii ndani yake kuna kuifanya kufunga Saumu kuwa jambo mahususi kwa mwenye uwezo, aliye sahihi, ambaye si msafiri. Na kwa vile sheria ya hiari ya kati ya kufunga kufidia ilipofutwa hasa, alirudia ruhusa ile ya mgonjwa na msafiri kutofunga, ili asifikiriwe kwamba ruhusa hiyo pia ilifutwa. [Akasema]: “Mwenyezi Mungu anawatakia yaliyo mepesi, wala hawatakii yaliyo mazito.” Yani Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka kuwasahilishieni njia zifikishazo kwenye radhi zake kwa wepesi mkubwa zaidi, na azifanye kuwa nyepesi mno. Ndiyo maana yote ambayo Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake yalikuwa rahisi mno katika asili yake. Na ikiwa kutatokea baadhi ya vizuizi vyenye kusababisha uzito ndani yake, basi Yeye huzirahisisha ibada kurahisisha kwingine. Ima kwa kuitupilia mbali, au kuipunguza kwa aina za kupunguza. Hii ni sentensi haiwezi kufafanuliwa ikaisha, kwa sababu maelezo yake yote ndiyo sheria zote, na zinaingia humo ruhusa zote, na upunguzaji wote. “Na ili mkamilishe hesabu hiyo.” Na hili, - na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi – ili mwenye kufikiria fikira potovu asije akafirikia kwamba kufunga Saumu ya Ramadhani yanatimia makusudio yake kwa kufunga baadhi yake tu. Akazuia fikra hiyo potovu kwa kumwamrisha akamilishe hesabu ya siku zake. Na amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya kukamilika kwake kwa ajili ya kumwezesha kwake, na kusahilisha kwake, na kubainisha kwake kwa waja wake; na kwa kufanya takbira mwisho wake. Na inaingia katika hilo kufanya takbira wakati wa kuuona mwezi mwandamo wa Shawwal hadi mwisho wa khutba ya Idi.
: 186 #
{وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ (186)}
(186) Na waja wangu watakapokuuliza kunihusu Mimi, basi Mimi kwa hakika nipo karibu. Ninaitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.
#
{186} هذا جواب سؤال. سأل النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - بعضُ أصحابه فقالوا: يا رسول الله، أقريب ربنا فنناجيه، أم بعيد فنناديه؟ فنزل {وإذا سألك عبادي عني فإني قريب}؛ لأنه تعالى الرقيب الشهيد المطلع على السر وأخفى يعلم خائنةَ الأعين وما تخفي الصدور فهو قريب أيضاً من داعيه بالإجابة، ولهذا قال: {أجيب دعوة الداع إذا دعان}؛ والدعاء نوعان: دعاء عبادة، ودعاء مسألة. والقرب نوعان: قرب بعلمه من كل خلقه، وقرب من عابديه وداعيه بالإجابة والمعونة والتوفيق. فمن دعا ربه بقلب حاضر ودعاء مشروع ولم يمنع مانع من إجابة الدعاء كأكل الحرام ونحوه فإن الله قد وعده بالإجابة، وخصوصاً إذا أتى بأسباب إجابة الدعاء وهي الاستجابة لله تعالى بالانقياد لأوامره ونواهيه القولية والفعلية والإيمان به الموجب للاستجابة، فلهذا قال: {فليستجيبوا لي وليؤمنوا بي لعلهم يرشدون}؛ أي: يحصل لهم الرشد الذي هو الهداية للإيمان والأعمال الصالحة ويزول عنهم الغي المنافي للإيمان والأعمال الصالحة، ولأن الإيمان بالله والاستجابة لأمره سبب لحصول العلم كما قال تعالى: {يا أيها الذين آمنوا إن تتقوا الله يجعل لكم فرقاناً}. ثم قال تعالى:
Hili ni jibu la swali ambalo baadhi ya maswahaba zake walimuuliza Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, Mola wetu Mlezi yuko karibu, ili tunong’one naye, au yuko mbali ili tumwite kwa sauti kubwa? Basi ikateremka, “na waja wangu watakapokuuliza habari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu.” Kwa sababu yeye Mtukufu ndiye Mwangalizi, Shahidi, mwenye kujua siri na kilichofichika zaidi, anayejua khiyana ya macho na yale ambayo vifua vinaficha. Basi yeye pia yuko karibu na mwenye kumuomba kwa kuitikia, na ndiyo maana akasema: “Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.” Na dua (kuita) ni aina mbili: Kuita kwa ibada na kuita kwa kuomba jambo. Na ukaribu ni aina mbili: Ukaribu kwa elimu yake juu ya kila kiumbe chake, na ukaribu kwa waja wake na wenye kumuomba kwa kujibu, kusaidia, na kuwezesha. Basi, mwenye kumuomba Mola wake Mlezi kwa moyo uliopo, na dua ya halali, na hakuna kizuizi chochote kinachozuia kuitikia dua hiyo, kama vile kula haramu na mengineyo. Basi Mwenyezi Mungu amemuahidi kumuitikia, na hasa akifanya sababu za kuitikiwa dua. Ambazo ni kumuitikia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufuata maamrisho yake na kuepuka makatazo yake ya kikauli na kivitendo, na kumuamini, yenye kusababisha aitikiwe. Ndiyo maana akasema: “Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.” Yani watapata kuongoka ambako ndio uwongofu kwenye imani na matendo mema, na wataondolewa upotovu unaopingana na imani na matendo mema. Na kwa sababu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuitikia amri yake ni sababu ya kupata elimu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu. “Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atakupeni kipambanuzi.” Kisha Mtukufu akasema:
: 187 #
{أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَى نِسَائِكُمْ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنْتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ (187)}
(187) Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu alikwisha jua kwamba mlikuwa mkizihini nafsi zenu. Kwa hivyo amewakubalia toba yenu na amewasamehe. Basi sasa changanyikeni nao na tafuteni kile alichowaandikia Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa alfajiri kutokana na weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao hali ya kuwa mmekaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya (Ishara) zake watu ili wapate kumcha.
#
{187} كان في أول فرض الصيام يحرم على المسلمين الأكل والشرب والجماع في الليل بعد النوم ، فحصلت المشقة لبعضهم، فخفف الله تعالى عنهم ذلك وأباح في ليالي الصيام كلها الأكل والشرب والجماع، سواء نام أو لم ينم، لكونهم يختانون أنفسهم بترك بعض ما أمروا به، {فتاب}؛ الله {عليكم}؛ بأن وسع لكم أمراً كان لولا توسعته موجباً للإثم، {وعفا عنكم}؛ ما سلف من التخون {فالآن}؛ بعد هذه الرخصة والسعة من الله {باشروهن}؛ وطئاً وقبلة ولمساً وغير ذلك {وابتغوا ما كتب الله لكم}؛ أي: انووا في مباشرتكم لزوجاتكم التقرب إلى الله تعالى، والمقصود الأعظم من الوطء، وهو حصول الذرية وإعفاف فرجه وفرج زوجته، وحصول مقاصد النكاح، ومما كتب الله لكم ليلة القدر الموافقة لليالي صيام رمضان، فلا ينبغي لكم أن تشتغلوا بهذه اللذة عنها وتضيعوها، فاللذة مدركة وليلة القدر إذا فاتت لم تدرك. {وكلوا واشربوا حتى يتبين لكم الخيط الأبيض من الخيط الأسود من الفجر}؛ هذا غاية للأكل والشرب والجماع، وفيه أنه إذا أكل ونحوه شاكًّا في طلوع الفجر فلا بأس عليه، وفيه دليل على استحباب السحور للأمر، وأنه يستحب تأخيره، أخذاً من معنى رخصة الله وتسهيله على العباد، وفيه أيضاً دليل على أنه يجوز أن يدركه الفجر وهو جنب من الجماع قبل أن يغتسل، ويصح صيامه لأن لازم إباحة الجماع إلى طلوع الفجر، أن يدركه الفجر وهو جنب، ولازم الحق حق {ثم}؛ إذا طلع الفجر {أتموا الصيام}؛ أي: الإمساك عن المفطرات {إلى الليل}؛ وهو غروب الشمس، ولما كان إباحة الوطء في ليالي الصيام ليست إباحة عامة لكل أحد، فإن المعتكف لا يحل له ذلك استثناه بقوله: {ولا تباشروهن وأنتم عاكفون في المساجد}؛ أي: وأنتم متصفون بذلك. ودلت الآية على مشروعية الاعتكاف وهو لزوم المسجد لطاعة الله تعالى وانقطاعاً إليه، وأن الاعتكاف لا يصح إلا في مسجدٍ، ويستفاد من تعريف المساجد أنها المساجد المعروفة عندهم، وهي التي تقام فيها الصلوات الخمس، وفيه أن الوطء من مفسدات الاعتكاف. تلك المذكورات وهو تحريم الأكل والشرب والجماع، ونحوه من المفطرات في الصيام، وتحريم الفطر على غير المعذور، وتحريم الوطء على المعتكف، ونحو ذلك من المحرمات {حدود الله}؛ التي حدها لعباده ونهاهم عنها فقال: {فلا تقربوها}؛ أبلغ من قوله فلا تفعلوها؛ لأن القربان يشمل النهي عن فعل المحرم بنفسه، والنهي عن وسائله الموصلة إليه. والعبد مأمور بترك المحرمات والبعد منها غاية ما يمكنه، وترك كل سبب يدعو إليها، وأما الأوامر فيقول الله فيها تلك حدود الله فلا تعتدوها فينهى عن مجاوزتها {كذلك}؛ أي: بيَّن الله لعباده الأحكام السابقة أتم تبيين وأوضحها لهم أكمل إيضاح {يبين الله آياته للناس لعلهم يتقون}؛ فإنهم إذا بان لهم الحق اتبعوه، وإذا تبين لهم الباطل اجتنبوه، فإن الإنسان قد يفعل المحرم، على وجه الجهل بأنه محرم ولو علم تحريمه لم يفعله، فإذا بين الله للناس آياته؛ لم يبق لهم عذر ولا حجة، فكان ذلك سبباً للتقوى.
{187} Mwanzoni mwa kulazimishwa kwa Saumu ilikuwa ni haramu kwa Waislamu usiku baada ya kulala kula, kunywa na kujamiiana. Kwa hivyo, dhiki ikawapata baadhi yao, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafanyia wepesi katika hilo, na akaruhusu kula, kunywa, na kujamiiana. Sawa mtu awe alilala au hakulala, kwa sababu walikuwa wanajihini nafsi zao kwa kuacha baadhi ya waliyoamrishwa. “Kwa hivyo amewakubalia toba yenu” kwa kuwakunjulia jambo ambalo - lau si kulikunjua kwake -, basi lingelesababisha dhambi “na akawasamehe” ile hiana iliyotangulia. “Basi sasa,” baada ya ruhusa hii na ukunjufu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, “changanyikeni nao” kwa kufanya jimai, kubusu, kugusana, na kadhalika. “Na tafuteni kile alichowaandikia Mwenyezi Mungu.” Yani kusudieni katika kuchanganyika kwenu na wake zenu kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lakini makusudio makubwa zaidi ya kujamiiana tu, nako ni kupata watoto, na kutunza tupu yake na tupu ya mkewe, na kufikia malengo ya ndoa. Na katika yale aliyowaandikia Mwenyezi Mungu ni Lailatul-Qadr (usiku wa cheo) inayoafikiana na usiku za kufunga kwa Ramadhani. Hampaswi kujishughulisha na raha hii mkaiacha na mkaipoteza. Kwa kuwa, raha inaweza kufikiwa baadaye, lakini Usiku wa cheo ukipita, hauwezi kufikiwa tena. “Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa alfajiri kutokana na weusi wa usiku.” Na huu ndio mwisho wa kula, kunywa, na kujamiiana. Na ndani yake kuna kwamba akila, na mfano wake huku ana shaka kuhusu kupambazuka kwa alfajiri, basi hakuna ubaya juu yake. Na ndani yake kuna ushahidi wa kupendekezwa kula daku (suhuur) kwa sababu ya amri hii. Na kuwa inapendekezwa kuichelewesha kwa kuchukua hilo kutoka katika maana ya ruhusa ya Mwenyezi Mungu, na usahilishaji wake kwa waja wake. Na ndani yake pia kuna dalili kwamba inaruhusika apatwe na alfajiri hali ya kuwa ana janaba kutokana na kujamiiana kabla ya kuoga na ikakubalika saumu yake. Kwa sababu, ni lazima kwamba kuruhusu kujamiiana mpaka alfajiri, atapatwa na alfajiri hali ya kuwa ana janaba. Na chenye kulazimu haki ni haki. “Kisha” inapoingia alfajiri, “timizeni saumu.” Yani kujizuia na mambo yenye kufuturisha “mpaka usiku,” nao ni wakati wa kuzama kwa jua. Na kwa kuwa kuruhusiwa jimai katika usiku za Saumu si ruhusa ya ujumla kwa kila mtu, kwani mtu anayefanya Itikafu haruhusiwi hilo. Mwenyezi Mungu alimtoa katika hukumu hiyo. Akasema: “Wala msichanganyike nao hali ya kuwa mmekaa Itikafu Msikitini”. Yani, hali ya kuwa nyinyi mnasifika kwa hilo. Na hii Aya inaashiria sheria ya kufanya itikafu, ambayo ni kukaa msikitini kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu [Mtukufu], na kujitoa kukwendea yeye. Na kwamba itikafu haikubaliki isipokuwa msikitini tu. Na faida ya kuitaja misikiti kwa nomino ya pekee katika hii Aya ni kuonyesha kuwa ni ile ile misikiti wanayoijua, ambamo husimamishwa swala tano za kila siku. Na ndani yake pia kuna kwamba kujamiiana ni miongoni mwa yale yenye kuharibu Itikafu. “Hayo” iliyotajwa - ambayo ni kuharamisha kula, kunywa, kujamiiana, na mfano wake miongoni wa yenye kuharibu funga ya Saumu.Na kumharamishia mtu asiyekuwa na udhuru katika kutofunga, na kuharamisha jimai kwa aliye katika itikafu. Na sawa na hayo miongoni mwa yale yaliyoharamishwa ni “mipaka ya Mwenyezi Mungu” ambayo aliwawekea waja wake. Na akawakataza, na akasema: “Basi msiikaribie” nayo ni yenye ufasaha zaidi kuliko kauli yake "Msiifanye." Kwa sababu, kukaribia kunajumuisha kukataza kufanya yaliyoharamishwa yenyewe, na kukataza njia zake zenye kuifikia mipaka hiyo. Na mja ameamrishwa kuacha yaliyo haramu, na kujiweka mbali nayo kabisa kadiri awezavyo, na kuacha kila sababu inayoitaka kuyaendea (yaliyo haramu). Na ama maamrisho, Mwenyezi Mungu anasema kuyahusu “Hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiivunje,” kwa hivyo akakataza kuivuka. “Hivyo ndivyo” yani [Mwenyezi Mungu] alivyowabainishia waja wake hukumu hizo zilizotangulia kwa ubainisho mkamilifu kabisa, na akaziweka wazi kwao kwa uwazi mkamilifu kabisa. “Anavyowabainishia Aya (Ishara) zake watu ili wapate kumcha.” Kwani ikiwa watabainikiwa na haki, wataifuata. Na ikiwa watabainikiwa na batili, watajiepusha nayo. Kwa sababu, mtu anaweza kufanya yale yaliyoharamishwa kwa kutojua kwamba ni haramu, na lau kuwa angejua uharamu wake, basi asingefanya. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anawabainishia watu ishara zake, hawatabaki na udhuru wowote wala hoja. Basi hilo linakuwa ni sababu ya uchamungu.
: 188 #
{وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَيْنَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ (188)}
(188) Wala msiliane mali zenu kwa batili, na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua.
#
{188} أي: ولا تأخذوا أموالكم أي أموال غيركم، أضافه إليهم لأنه ينبغي للمسلم أن يحب لأخيه ما يحب لنفسه، ويحترم ماله كما يحترم ماله، ولأن أكله لمال غيره يجرئ غيره على أكل ماله عند القدرة، ولما كان أكلها نوعين: نوعاً بحقٍّ ونوعاً بباطل، وكان المحرم إنما هو أكلها بالباطل قيده تعالى بذلك، ويدخل بذلك أكلها على وجه الغصب والسرقة والخيانة في وديعة أو عارية أو نحو ذلك، ويدخل فيه أيضاً أخذها على وجه المعاوضة بمعاوضة محرمة، كعقود الربا والقمار كلها فإنها من أكل المال بالباطل، لأنه ليس في مقابلة عوض مباح، ويدخل في ذلك أخذها بسبب غش في البيع والشراء والإجارة ونحوها، ويدخل في ذلك استعمال الأجراء وأكل أجرتهم، وكذلك أخذهم أجرة على عمل لم يقوموا بواجبه، ويدخل في ذلك أخذ الأجرة على العبادات والقربات التي لا تصح حتى يقصد بها وجه الله تعالى، ويدخل في ذلك الأخذ من الزكوات والصدقات والأوقاف والوصايا، لمن ليس له حق منها أو فوق حقه، فكل هذا ونحوه من أكل المال بالباطل، فلا يحل ذلك بوجه من الوجوه حتى ولو حصل فيه النزاع والارتفاع إلى حاكم الشرع، وأدلى من يريد أكلها بالباطل بحجة غلبت حجة المحق، وحكم له الحاكم بذلك، فإن حكم الحاكم لا يبيح محرماً ولا يحلل حراماً، إنما يحكم على نحو مما يسمع، وإلا فحقائق الأمور باقية، فليس في حكم الحاكم للمبطل راحة ولا شبهة ولا استراحة، فمن أدلى إلى الحاكم بحجة باطلة، وحكم له بذلك فإنه لا يحل له، ويكون آكلاً لمال غيره بالباطل والإثم، وهو عالم بذلك فيكون أبلغ في عقوبته وأشد في نكاله. وعلى هذا؛ فالوكيل إذا علم أن موكله مبطل في دعواه لم يحل له أن يخاصم عن الخائن كما قال تعالى: {ولا تكن للخائنين خصيماً}.
{188} Yani msichukue mali za wengine. Na alizinasibisha nao kwa sababu Muislamu anapaswa kumpendea ndugu yake kile anachokipendea nafsi yake. Na aiheshimu mali yake kwa vile anavyoiheshimu mali yake (mwenyewe). Na kwa sababu ulaji wake wa mali ya wengine kunampa huyo mwingine ujasiri wa kula mali yake pia anapokuwa na uwezo. Na kwa vile kula kwake ni kwa aina mbili: Aina moja kwa haki, na aina nyingine kwa batili. Na kwamba iliyoharamishwa ni kuila kwa batili, Mwenyezi Mungu akazuia uharamu katika hiyo aina (ya batili). Na inaingia katika hilo kula kwa njia ya unyang'anyi, wizi, kufanya hiana katika amana au kile ulichosaidia kutumia au mfano wa hayo. Na inaingia katika hilo pia kuichukua kwa namna ya kubadilishana kubadilishana kwa haramu kama vile mapatano ya riba, na kamari zote. Hiyo yote ni katika kula mali kwa batili, kwa sababu sio kubadilishana kwa badala inaoruhusika. Na inaingia ndani yake pia kuichukua kwa sababu ya ulaghai katika kuuza, kununua, kukodisha na mfano wa hayo. Na inaingia ndani yake kuwatumia wafanyakazi na kula ujira wao. Na vile vile kuchukua ujira kwa kazi ambayo hawakuitimiza wajibu wake. Na inaingia katika hilo kuchukua ujira kwa ibada na mambo ya kujikurubisha nayo kwa Mwenyezi Mungu ambayo hayawi sahihi mpaka ukusudiwe kwazo uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na inaingia katika hilo kuchukua kutoka katika zaka, sadaka, waqfu, na wasia kwa yule ambaye hana haki humo, au kuchukua zaidi ya haki yake. Haya yote na mfano wake ni katika kula mali kwa batili, kwa hivyo hayo hayaruhusiki kwa hali yoyote ile, hata ikiwa kutakuwa na mzozo ndani yake. Na hilo likapelekwa kwa hakimu wa kisheria, na anayetaka kuila kwa dhuluma akaleta hoja yenye kushinda hoja ya yule anayestahiki, na hakimu akahukumu akampa yeye kwa hilo. Kwa sababu, hukumu ya hakimu hairuhusu kilichoharamishwa, wala haihalalishi kilichoharamishwa, bali anahukumu kulingana na anavyosikia, vinginevyo uhakika wa mambo unabaki. Kwa hivyo, hakuna raha, wala shaka, wala utulivu kwa mwenye batili katika hukumu ya hakimu. Kwa hivyo, mwenye atawasilisha hoja batili kwa hakimu, naye akahukumu kwamba yeye ndiye mshindi kwa hilo. Basi mali hiyo haiwi halali kwake, na anakuwa mwenye kula mali ya wengine kwa batili na dhambi hali ya kuwa anajua hilo. Basi adhabu yake ikawa ni kubwa zaidi, na onyo lake likawa ni kali zaidi. Na kwa kuzingatia hayo, ikiwa wakili atajua kuwa mteja wake ni batili katika madai yake, basi haitaruhusika kwake kumtetea mhaini. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala usiwe mtetezi wa wahaini”.
: 189 #
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَنْ تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ ظُهُورِهَا وَلَكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَى وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (189)}.
(189) Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na Hija. Wala sio wema kwamba mziingie nyumba kwa nyuma yake. Bali mwema ni mwenye kumcha Mungu. Na ingieni majumbani kupitia milangoni mwake. Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.
#
{189} فقوله تعالى: {يسألونك عن الأهلة}؛ ـ جمع هلال ـ ما فائدتها وحكمتها أو عن ذاتها {قل هي مواقيت للناس}؛ أي: جعلها الله تعالى بلطفه ورحمته على هذا التدبير، يبدو الهلال ضعيفاً في أول الشهر، ثم يتزايد إلى نصفه، ثم يشرع في النقص إلى كماله، وهكذا ليعرف الناس بذلك مواقيت عباداتهم؛ من الصيام وأوقات الزكاة والكفارات وأوقات الحج، ولما كان الحج يقع في أشهر معلومات، ويستغرق أوقاتاً كثيرة قال: {والحج}؛ وكذلك تعرف بذلك أوقات الديون المؤجلات، ومدة الإجارات ومدة العدد والحمل، وغير ذلك مما هو من حاجات الخلق، فجعله تعالى حساباً يعرفه كل أحد من صغير وكبير وعالم وجاهل، فلو كان الحساب بالسنة الشمسية لم يعرفه إلا النادر من الناس. {وليس البر بأن تأتوا البيوت من ظهورها}؛ وهذا كما كان الأنصار وغيرهم من العرب إذا أحرموا لم يدخلوا البيوت من أبوابها؛ تعبداً بذلك وظنًّا أنه برٌّ، فأخبر تعالى أنه ليس من البرِّ ؛ لأن الله تعالى لم يشرعه لهم، وكل من تعبد بعبادة لم يشرعها الله ولا رسوله فهو متعبد ببدعة، وأمرهم أن يأتوا البيوت من أبوابها؛ لما فيه من السهولة عليهم التي هي قاعدة من قواعد الشرع. ويستفاد من إشارة الآية أنه ينبغي في كل أمر من الأمور أن يأتيه الإنسان من الطريق السهل القريب الذي قد جعل له موصلاً، فالآمر بالمعروف والناهي عن المنكر، ينبغي أن ينظر في حالة المأمور، ويستعمل معه الرفق والسياسة التي بها يحصل المقصود أو بعضه، والمتعلم والمعلم ينبغي أن يسلك أقرب طريق وأسهله يحصل به مقصوده، وهكذا كل من حاول أمراً من الأمور، وأتاه من أبوابه، وثابر عليه فلا بد أن يحصل له المقصود بعون الملك المعبود. {واتقوا الله}؛ هذا هو البرُّ الذي أمر الله به، وهو لزوم تقواه على الدوام بامتثال أوامره واجتناب نواهيه، فإنه سبب للفلاح الذي هو الفوز بالمطلوب والنجاة من المرهوب، فمن لم يتق الله تعالى لم يكن له سبيل إلى الفلاح، ومن اتقاه فاز بالفلاح والنجاح.
{189} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Wanakuuliza kuhusu miandamo ya mwezi.” Ahilla ni wingi wa hilaal (miezi miandamo). Ni nini faida yake na hekima yake? Au yenyewe ni nini? “Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu“. Yani Mwenyezi Mungu Mtukufu aliifanya kutokana na wema wake na rehema juu yake kwa huu mpangilio. Miezi miandamo inazunguka ikiwa dhaifu katika mwanzo wa mwezi, kisha inongezeka hadi nusu yake, kisha inaanza kupunguka mpaka iishe. Na vivyo hivyo, ili watu wajue kwa hilo nyakati za ibada zao kama vile kufunga Saumu, na nyakati za Zaka, na kafara mbalimbali, na nyakati za Hija. Na kwa kuwa Hija hufanyika katika miezi inayojulikana, na inachukua muda mwingi, akasema: “Na Hija.” Na pia hujulikana kwayo madeni yaliyoahirishwa, na muda wa kodi, na muda wa eda na mimba, na yasiyokuwa hayo katika yale ambayo ni katika mahitaji ya viumbe. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifanya kuwa ni hesabu ambayo kila mtu anaijua, kuanzia mdogo na mkubwa, wenye elimu na wasiokuwa na elimu (wajinga). Na ikiwa hesabu ingekuwa kwa mwaka wa jua, basi hawangeijua isipokuwa wachache tu miongoni mwa watu. “Wala sio wema kwamba mziingie nyumba kwa nyuma yake.” Hili ni kama vile walivyokuwa Ansari na Waarabu wengine walipokuwa wanaingia kwenye Ihram. Hawakuwa wanaziingia nyumba kupitia milangoni mwake wakiifanya hiyo kuwa ibada, na wakidhani kuwa ni wema. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akatoa habari kwamba sio wema, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwawekea sheria hiyo. Na kila mwenye kuabudu kwa ibada ambayo Mwenyezi Mungu hakuifanya kuwa sheria wala Mtume wake, basi yeye anafanya bidaa kuwa ibada. Na Mwenyezi Mungu akawaamrisha kwamba waingie majumbani kupitia milangoni mwake, kwa sababu ya urahisi uliopo katika hilo kwao; ambao (huo urahisi) ni mojawapo ya misingi ya sheria. Na inafahamika kutokana na dalili ya Aya hii kuwa katika kila jambo miongoni mwa mambo, mtu anafaa kulijia kwa upande wake mwepesi ulio karibu. Ambao Mwenyezi Mungu ameufanya kuwa njia ya kulifikia. Kwa hivyo, mwenye kuamrisha mema na kukataza maovu, anafaa kuangalia katika hali ya yule aliyeamrishwa. Na atumie upole na sera nzuri pamoja naye, ambazo kwazo yote au baadhi ya makusudio yanafikiwa. Na mwanafunzi na mwalimu wanafaa kuchukua njia ya karibu na nyepesi zaidi ambayo lengo lake linafikiwa kwayo. Na vivyo hivyo, kila anayejaribu jambo miongoni mwa mambo, na akalijia kutoka kwenye milango yake, na akavumilia juu yake, basi hakuna budi atapata makusudio yake kwa msaada wa Mfalme Anayeabudiwa. “Na mcheni Mwenyezi Mungu.” Huu ndio wema ambao Mwenyezi Mungu aliamrisha, ambao ni kushikana na kumcha Yeye daima, kwa kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake. Kwani hilo ndiyo sababu ya kufaulu, ambako ndiko kupata yale yanayotafutwa, na kuokoka kutokana na yanayohofiwa. Kwa hivyo, mwenye kutomcha Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hatakuwa na njia ya kufaulu. Na mwenye kumcha, atapata kufaulu na kupita.
: 190 - 193 #
{وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ (190) وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِنْدَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّى يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ فَإِنْ قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ كَذَلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ (191) فَإِنِ انْتَهَوْا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (192) وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّهِ فَإِنِ انْتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ (193)}.
(190) Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaopigana nanyi, wala msianzishe uadui. Kwani Mwenyezi Mungu kwa hakika hawapendi waanzao uadui. (191) Na waueni popote muwakutapo, na watoeni popote walipowatoa; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wawapigie huko. Wakikupigeni huko, basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri. (192) Lakini wakiacha, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. (193) Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha, basi usiwepo uadui isipokuwa kwa madhulumu (waliodhulumiwa).
#
{190} هذه الآيات تتضمن الأمر بالقتال في سبيل الله، وهذا كان بعد الهجرة إلى المدينة، لَمَّا قَوِيَ المسلمون للقتال أمرهم الله به بعدما كانوا مأمورين بكفِّ أيديهم، وفي تخصيص القتال {في سبيل الله}؛ حث على الإخلاص ونهيٌ عن الاقتتال في الفتن بين المسلمين، {الذين يقاتلونكم}؛ أي: الذين هم مستعدون لقتالكم، وهم المكلفون الرجال غير الشيوخ الذين لا رأي لهم ولا قتال. والنهي عن الاعتداء يشمل أنواع الاعتداء كلها من قتل من لا يقاتل من النساء والمجانين والأطفال والرهبان ونحوهم، والتمثيل بالقتلى وقتل الحيوانات وقطع الأشجار ونحوها، لغير مصلحة تعود للمسلمين، ومن الاعتداء مقاتلة من تقبل منهم الجزية، إذا بذلوها فإن ذلك لا يجوز.
Aya hizi zinajumuisha amri ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na hili lilikuwa baada ya kuhamia Madina, wakati Waislamu walipokuwa na nguvu za kupigana, Mwenyezi Mungu akawaamrisha kufanya hivyo, baada ya kwamba walikuwa wameamrishwa waizuie mikono yao. Na katika kukuzuia kupigana “katika njia ya Mwenyezi Mungu” kuna kuhimiza watu kuwa na ikhlasi; na kukataza kupigana katika kufitinisha baina ya Waislamu. “Wale wanaopigana nanyi,” yani ambao wako tayari kupigana na nyinyi, nao ni wanaume wa umri wa kuamrishwa na kukatazwa na sio wazee ambao hawana maoni wala uwezo wa kupigana. Na kukataza kuanzisha uadui kunajumuisha aina zote za kuanzisha uchokozi, kama vile kuua asiyepigana kama vile wanawake, vichaa, watoto, watawa na wengineo. Na kukatakata wale waliouawa, kuua wanyama, kukata miti [na mengineyo], bila ya kuwepo masilahi yanayowarudia Waislamu. Na katika kuanzisha uadui ni kupigana na wale ambao jizya inakubaliwa kutoka kwao wanapoitoa, kwa sababu hilo haliruhusiki.
#
{191 - 192} {واقتلوهم حيث ثقفتموهم}؛ هذا أمر بقتالهم أينما وجدوا في كل وقت وفي كل زمان قتال مدافعة وقتال مهاجمة، ثم استثنى من هذا العموم قتالهم {عند المسجد الحرام}؛ وأنه لا يجوز إلا أن يَبْدَؤوا بالقتال فإنهم يُقَاتَلُون جزاء لهم على اعتدائهم، وهذا مستمر في كل وقت حتى ينتهوا عن كفرهم فيسلموا، فإن الله يتوب عليهم ولو حصل منهم ما حصل من الكفر بالله والشرك في المسجد الحرام وصد الرسول والمؤمنين عنه، وهذا من رحمته وكرمه بعباده. ولما كان القتال عند المسجد الحرام يتوهم أنه مفسدة في هذا البلد الحرام أخبر تعالى أن المفسدة بالفتنة عنده بالشرك والصد عن دينه أشد من مفسدة القتل، فليس عليكم أيها المسلمون حرج في قتالهم. ويستدل في هذه الآية على القاعدة المشهورة وهي أنه يرتكب أخف المفسدتين لدفع أعلاهما.
{191-192} “Na waueni popote muwakutapo.” Hii ni amri ya kupigana nao popote wanakopatikana kila wakati na kila zama kupigana kwa kujilinda, na kupigana kwa kushambulia. Kisha akatoa katika ujumla huo kupigana nao “kwenye Msikiti Mtakatifu.” Na kwamba hilo haliruhusiki mpaka isipokuwa wao tu waanzishe kupigana, kwa hivyo, watapigana ili kuwalipa kuanzisha kwao vita. Na hilo litaendelea katika kila wakati mpaka waache ukafiri wao na wasilimu. Kwa maana, Mwenyezi Mungu atawakubalia toba pamoja na yale yaliyotokea kutoka kwao ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na ushirikina katika Msikiti Mtakatifu, na kumzuia Mtume na Waumini kuufikia. Na hili ni katika rehema na ukarimu wake kwa waja wake. Na kwa vile kupigana vita katika Msikiti Mtukufu kunaweza fikiriwa kuwa ni uharibifu katika ardhi hii tukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa; uharibifu wa fitina hapo kwa ushirikina na kuizuia dini yake ni mbaya zaidi kuliko uharibifu wa kuua. Hivyo basi, hakuna ubaya wowote juu yenu - enyi Waislamu - katika kupigana nao. Aya hii inatumika juu ya msingi mashuhuri sana, ambao ni kufanya ovu dogo kati ya maovu mawili, ili kuzuia lililo juu zaidi ya mawili hayo.
#
{193} ثم ذكر تعالى المقصود من القتال في سبيله، وأنه ليس المقصود به سفك دماء الكفار وأخذ أموالهم، ولكن المقصود به أن {يكون الدين لله} تعالى، فيظهر دين الله تعالى على سائر الأديان، ويدفع كل ما يعارضه من الشرك وغيره وهو المراد بالفتنة، فإذا حصل هذا المقصود فلا قتل ولا قتال. {فإن انتهوا}؛ عن قتالكم عند المسجد الحرام، {فلا عدوان إلا على الظالمين}؛ أي: فليس عليهم منكم اعتداء إلا من ظلم منهم؛ فإنه يستحق المعاقبة بقدر ظلمه.
Kisha Yeye Mtukufu akataja lengo la kupigana katika njia yake. Na kwamba haikusudii kumwaga damu za makafiri na kuchukua mali zao. Bali kinachokusudiwa kwayo ni kuwa, “Dini iwe tu ya Mwenyezi Mungu” Mtukufu. Ili Dini ya Mwenyezi Mungu [Mtukufu] idhihiri dini nyingine zote, na kizuiwe kila kinachoipinga, kama vile ushirikina na mengineyo, ambayo ndiyo iliyokusudiwa na fitina. Na makusudio haya yanapopatikana, basi hakuna kuua wala kupigana, “wakiacha” kuwapiga katika Msikiti Mtakatifu. “Basi usiwepo uadui isipokuwa kwa madhulumu,” yani wasishambulie na yeyote katika nyinyi, isipokuwa mwenye kudhulumu miongoni mwao. Basi huyo anastahili kuadhibiwa, kwa kiwango cha dhuluma yake.
: 194 #
{الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ فَمَنِ اعْتَدَى عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَى عَلَيْكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ (194)}.
(194) Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Basi, anayewashambulia, nanyi mshambulieni kwa sawa na alivyowashambulia. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika yu pamoja na wachamungu.
#
{194} يقول تعالى: {الشهر الحرام بالشهر الحرام} يحتمل أن يكون المراد به ما وقع من صد المشركين للنبي - صلى الله عليه وسلم -، وأصحابه عام الحديبية عن الدخول لمكة وقاضوهم على دخولها من قابل، وكان الصد والقضاء في شهر حرام وهو ذو القعدة فيكون هذا بهذا، فيكون فيه تطييب لقلوب الصحابة بتمام نسكهم وكماله، ويحتمل أن يكون المعنى أنكم إن قاتلتموهم في الشهر الحرام، فقد قاتلوكم فيه وهم المعتدون، فليس عليكم في ذلك حرج، وعلى هذا فيكون قوله: {والحرمات قصاص}؛ من باب عطف العام على الخاص، أي كل شيء يحترم من شهر حرام أو بلد حرام أو إحرام، أو ما هو أعم من ذلك جميع ما أمر الشرع باحترامه، فمن تجرأ عليها فإنه يقتص منه: فمن قاتل في الشهر الحرام قوتل، ومن هتك البلد الحرام أخذ منه الحد ولم يكن له حرمة، ومن قتل مكافئاً له قتل به، ومن جرحه، أو قطع عضواً منه اقتص منه، ومن أخذ مال غيره المحترم؛ أخذ منه بدله، ولكن هل لصاحب الحق أن يأخذ من ماله بقدر حقه أم لا؟ خلاف بين العلماء، الراجح من ذلك أنه إن كان سبب الحق ظاهراً كالضيف إذا لم يقره غيره، والزوجة والقريب إذا امتنع من تجب عليه، النفقة من الإنفاق عليه، فإنه يجوز أخذه من ماله، وإن كان السبب خفيًّا كمن جحد دَيْن غيره أو خانه في وديعة أو سرق منه ونحو ذلك، فإنه لا يجوز له أن يأخذ من ماله مقابلة له جمعاً بين الأدلة، ولهذا قال تعالى توكيداً وتقوية لما تقدم: {فمن اعتدى عليكم فاعتدوا عليه بمثل ما اعتدى عليكم}؛ هذا تفسير لصفة المقاصة وأنها هي المماثلة في مقابلة المعتدي. ولما كانت النفوس ـ في الغالب ـ لا تقف على حدها إذا رخص لها في المعاقبة لطلبها التشفي أمر تعالى بلزوم تقواه التي هي الوقوف عند حدوده وعدم تجاوزها وأخبر تعالى أنه {مع المتقين}؛ أي: بالعون والنصر والتأييد والتوفيق، ومن كان الله معه حصل له السعادة الأبدية، ومن لم يلزم التقوى تخلى عنه وليه، وخذله فَوَكَلَه إلى نفسه، فصار هلاكه أقرب إليه من حبل الوريد.
{194} Yeye Mtukufu anasema: "Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu." inawezekana kwamba kinachokusudiwa kwayo ni kile kilichotokea pale washirikina walipomzuia Nabii, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – na maswahaba wake katika mwaka wa Hudaybiyah; ili wasiingie Makka. Na wakadanganya suluhu kwamba wataingia humo mwaka uliofuata. Na kulikuwa kuzuilia huko katika mwezi mtukufu ambao ni Dhul-Qa`dah, kwa hivyo linakuwa hili kwa lile. Na ndani yake kuna kufurahisha nyoyo za maswahaba kwa kutimiza ibada yao na kuikamilisha. Na yawezekana kwamba maana yake kuwa mkiwapiga vita katika mwezi mtukufu, basi wao walikwisha pigana nanyi humo, na wao ndio walioanzisha. Basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika hilo. Na kwa kuzingatia hilo, inakuwa kauli yake, “na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi.” Ni katika mlango wa kuunganisha lililo la ujumla kwa lililo mahususi. Yani kila chenye kuheshimiwa kama vile mwezi mtakatifu, au mji mtakatifu, au ihramu, au lililo la ujumla zaidi kuliko hayo. Kila ambayo Sheria iliamrisha yaheshimiwe, basi mwenye kujasiri kulivunja, basi atafanyiwa kisasi. Na mwenye kupigana katika mwezi mtakatifu, yeye pia atapigwa (humo). Na mwenye kuukiuka mji mtakatifu, atafanyiwa adhabu ya Hadd (adhabu maalumu), na hana ulinzi katika mahali patakatifu. Na mwenye kumuua (mtu) aliye sawa na yeye, atauawa kwa ajili yake. Na atakayemjeruhi au kumkata kiungo chake, basi atalipizwa kisasi kwa ajili yake. Na atakayechukua mali ya mtu mwingine ambayo ni haramu kwake, itachukuliwa badala yake kutoka kwake. Lakini je, mwenye haki ana haki ya kuchukua kutoka katika mali yake kwa kiwango cha haki yake au hapana? Hili lina ikhtilafu baina ya wanachuoni. Na lililo sahihi zaidi katika kauli hizo ni kwamba ikiwa sababu ya kustahiki ni dhahiri, kama vile mgeni. Ikiwa hakuna mtu mwingine atakayemkaribisha isipokuwa yeye, na mke na jamaa. Ikiwa yule anayelazimika kuwatunza atakataa kuwapa matumizi, basi inaruhusika kuichukua kutoka katika mali yake. Na ikiwa sababu yake imefichika, kama vile mtu anayekanusha kuwa na deni la mtu mwingine. Au alimfanyia hiyana katika amana yake, au aliiba kutoka kwake, na mfano wa hayo, basi hairuhusiki kwake kuchukua katika mali yake ili kujilipa. Hili ni kwa ajili ya kupatanisha kati ya dalili hizi, na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akisisitiza na kuimarisha hayo yaliyotangulia. “Basi, anayewashambulia, nanyi mshambulieni kwa sawa na alivyowashambulia.” Huu ndio ufafanuzi wa namna ya kulipiza kisasi, na kwamba hiyo (namna) ndiyo iliyo sawa katika kukabiliana na mwenye kuanzisha uadui. Na kwa vile nafsi - katika hali nyingi - hazisimami katika mipaka yake ikiwa zimeruhusiwa kuadhibu kwa sababu ya kutaka kwake kupona. Yeye Mtukufu akaamrisha kudumu katika kumcha, ambako ndiko kusimamia kwenye mipaka yake, bila ya kuivuka. Na Yeye Mtukufu akajulisha kwamba Yeye kwa hakika yu “pamoja na wachamungu”. Yani kwa msaada, na nusura, na kuunga mkono, na kuwezesha. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu yu pamoja naye, basi atapata furaha ya milele. Na yule asiyeshikamana na uchamungu, basi mlinzi wake atamwacha na asimsaidie, na amwachie nafsi yake. Basi maangamizo yake yatakuwa karibu zaidi naye kuliko mshipa wa shingo yake.
: 195 #
{وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ وَأَحْسِنُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ (195)}.
(195) Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitupe katika maangamivu kwa mikono yenu. Na fanyeni wema. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaofanya wema.
#
{195} يأمر تعالى عباده بالنفقة في سبيله، وهو إخراج الأموال في الطرق الموصلة إلى الله، وهي كل طرق الخير من صدقة على مسكين أو قريب أو إنفاق على من تجب مؤنته، وأعظم ذلك وأول ما دخل في ذلك الإنفاق في الجهاد في سبيل الله، فإن النفقة فيه جهاد بالمال وهو فرض كالجهاد بالبدن، وفيها من المصالح العظيمة الإعانة على تقوية المسلمين و [على] توهية الشرك وأهله وعلى إقامة دين الله وإعزازه، فالجهاد في سبيل الله، لا يقوم إلا على ساق النفقة، فالنفقة له كالروح لا يمكن وجوده بدونها، وفي ترك الإنفاق في سبيل الله إبطال للجهاد وتسليط للأعداء، وشدة تكالبهم، فيكون قوله تعالى: {ولا تلقوا بأيديكم إلى التهلكة}؛ كالتعليل لذلك. والإلقاء باليد إلى التهلكة يرجع إلى أمرين: ترك ما أمر به العبد إذا كان تركه موجباً أو مقارباً لهلاك البدن أو الروح، وفعل ما هو سبب موصل إلى تلف النفس أو الروح فيدخل تحت ذلك أمور كثيرة، فمن ذلك ترك الجهاد في سبيل الله، أو النفقة فيه الموجب لتسلط الأعداء، ومن ذلك تغرير الإنسان بنفسه في مقاتلة أو سفر مخوف أو محل مسبعة أو حيات، أو يصعد شجراً أو بنياناً خطراً، أو يدخل تحت شيء فيه خطر ونحو ذلك، فهذا ونحوه ممن ألقى بيده إلى التهلكة، ومن ذلك الإقامة على معاصي الله واليأس من التوبة، ومنها ترك ما أمر الله به من الفرائض التي تركها هلاك للروح والدين. ولما كانت النفقة في سبيل الله نوعاً من أنواع الإحسان أمر بالإحسان عموماً فقال: {وأحسنوا إن الله يحب المحسنين}؛ وهذا يشمل جميع أنواع الإحسان لأنه لم يقيده بشيء دون شيء، فيدخل فيه الإحسان بالمال كما تقدم، ويدخل فيه الإحسان بالجاه بالشفاعات ونحو ذلك، ويدخل في ذلك الإحسان بالأمر بالمعروف والنهي عن المنكر وتعليم العلم النافع، ويدخل في ذلك قضاء حوائج الناس من تفريج كرباتهم، وإزالة شداتهم وعيادة مرضاهم وتشييع جنائزهم وإرشاد ضالهم وإعانة من يعمل عملاً، والعمل لمن لا يحسن العمل، ونحو ذلك مما هو من الإحسان الذي أمر الله به، ويدخل في الإحسان أيضاً الإحسان في عبادة الله تعالى، وهو كما ذكر النبي - صلى الله عليه وسلم -: «أن تعبد الله كأنك تراه فإن لم تكن تراه فإنه يراك» ، فمن اتصف بهذه الصفات كان من الذين قال الله فيهم: {للذين أحسنوا الحسنى وزيادة}؛ وكان الله معه يسدده ويرشده ويعينه على كل أموره.
{195} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake watoe katika njia yake. Nako ni kutoa mali katika njia zinazofikisha kwa Mwenyezi Mungu. Nazo ni kila njia ya wema, kama vile kuwapa masikini sadaka, au jamaa, au kupeana matumizi kwa yule ambaye inalazimika kumpa matumizi. Na kubwa zaidi katika hilo, na la kwanza linaloingia katika hilo ni kutoa katika jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kupeana matumizi katika hilo ni kufanya jihadi kwa mali, na ni wajibu kama kufanya jihadi kwa mwili. Na ndani yake kuna manufaa makubwa, kama vile kusaidia kuwaimarisha Waislamu, na kudhoofisha ushirikina na watu wake, na kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu na kuipa nguvu. Kwa hivyo, jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu haisimami isipokuwa juu ya shina la kutoa (mali). Kwani, kutoa ni kama roho kwake, haiwezekani kuwepo kwake bila ya hiyo (roho). Na katika kuacha kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kubatilisha jihadi, kuwapa nguvu maadui, na kukithirisha mashambulizi yao. Kwa hivyo inakuwa kauli yake Mola Mtukufu, “wala msijitupe katika maangamivu kwa mikono yenu” ni kubainisha sababu ya hilo. Na kujitupa katika maangamivu kwa mkono kunarudi kwa mambo mawili: Mja kuacha yale aliyoamrishwa, ikiwa kuyaacha kunaleta au kunakaribia kuleta maangamivu kwa mwili au roho. Na (pili) kufanya lile ambalo ni sababu inayopelekea kuharibika kwa nafsi au roho. Kwa hivyo, mambo mengi sana yanaingia chini ya hayo .Na katika hayo ni kuacha jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, au kupeana matumizi juu yake ambako kunasababisha kuwapa nguvu maadui. Na katika hayo ni mtu hujidanganya kwenda katika vita au safari yenye kuhofisha, au mahali penye wanyama pori, au nyoka. Au kukwea miti au majengo hatari, au kuingia chini ya kitu ambacho ndani yake kuna hatari, na mfano wa hayo. Basi haya na mfano wake ni miongoni mwa wale waliojitupa katika maangamivu kwa mikono yao. Na katika kujitupa katika maangamivu kwa mkono ni kudumu katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa ya kutubu. Na katika hilo ni kuacha yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu ya faradhi, ambayo katika kuyaacha kuna kuangamiza roho na dini. Na kwa kuwa kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni aina katika aina za wema, akaamrisha kufanya wema kwa ujumla, akasema: “Na fanyeni wema. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaofanya wema.” Na hili linajumuisha kila aina ya wema, kwa sababu hakulifanya kuwa mahususi kwa kitu fulani kando na vitu vinginevyo. Kwa hivyo kunaingia humo kufanya wema kwa mali kama ilivyotangulia hapo awali. Na inaingia ndani yake kufanya wema kwa kupitia heshima ya mtu, kwa kufanya uombezi na mfano wa hilo. Na inaingia katika hilo kufanya wema kwa kuamrisha mema na kukataza maovu, na kufundisha elimu yenye manufaa. Na inaingia katika hilo kuwatimizia watu mahitaji yao kama vile kuwaondolea dhiki zao na kuwaondolea ugumu wao, kuwatembelea wagonjwa wao, kuhudhuria mazishi yao, kuwaongoza waliopotea wao, kuwasaidia wanaofanya kazi ambayo hawawezi kuifanya vizuri na mfano wa hayo, ambayo ni katika wema ambao Mwenyezi Mungu aliamrisha. Na inaingia katika wema pia kufanya wema (vizuri) katika kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nalo ni kama ilivyotaja Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Ihsan ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamwona. Na ikiwa humwoni, basi Yeye kwa hakika anakuona.” Basi mwenye kusifika kwa hizi sifa, atakuwa miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu alisema kuwahusu, “kwa wale wanaofanya wema ni wema na zaidi.” Na Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja naye, akimweka sawasawa, akimuongoa, na kumsaidia katika mambo yake yote.
Na Mola Mtukufu alipomaliza [kutaja] hukumu za Saumu na jihadi, akataja hukumu za Hijja, akasema:
: 196 #
{وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّهِ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّى يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِنْ رَأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِنْ صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ فَإِذَا أَمِنْتُمْ فَمَنْ تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ذَلِكَ لِمَنْ لَمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ (196)}.
{196} Na timizeni Hijja na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa mtazuiwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu au ana vya kumuudhi kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga saumu au kwa kutoa sadaka au kuchinja wanyama. Na mtakapokuwa na amani, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiyepata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakaporudi. Hizo ni kumi kamili. Hayo ni kwa yule ambaye jamaa zake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
#
{196} يستدل بقوله: {وأتموا الحج والعمرة}؛ على أمور: أحدها وجوب الحج والعمرة وفرضيتهما. الثاني وجوب إتمامهما بأركانهما وواجباتهما التي قد دل عليها فعل النبي - صلى الله عليه وسلم -، وقوله: «خذوا عني مناسككم». الثالث أن فيه حجة لمن قال بوجوب العمرة. الرابع أن الحج والعمرة يجب إتمامهما بالشروع فيهما ولو كانا نفلاً. الخامس الأمر بإتقانهما وإحسانهما، وهذا قدر زائد على فعل ما يلزم لهما. السادس فيه الأمر بإخلاصهما {لله} تعالى. السابع أنه لا يخرج المحرم بهما بشيء من الأشياء حتى يكملهما، إلا بما استثناه الله وهو الحصر، فلهذا قال: {فإن أحصرتم}؛ أي: منعتم من الوصول إلى البيت لتكميلهما بمرض أو ضلالة أو عدو، ونحو ذلك من أنواع الحصر الذي هو المنع {فما استيسر من الهدي}؛ أي: فاذبحوا ما استيسر من الهدي وهو سبع بدنة أو سبع بقرة أو شاة يذبحها المحصر، ويحلق، ويحل من إحرامه بسبب الحصر كما فعل النبي - صلى الله عليه وسلم -، وأصحابه لما صدهم المشركون عام الحديبية ، فإن لم يجد الهدي فليصم بدله عشرة أيام كما في المتمتع ثم يحل. ثم قال تعالى: {ولا تحلقوا رؤوسكم حتى يبلغ الهديُ محله}؛ وهذا من محظورات الإحرام إزالة الشعر بحلق أو غيره لأن المعنى واحد من الرأس أو من البدن، لأن المقصود من ذلك، حصول الشعث والمنع من الترفه بإزالته وهو موجود في بقية الشعر، وقاس كثير من العلماء على إزالة الشعر تقليم الأظفار بجامع الترفه، ويستمر المنع مما ذكر حتى يبلغ الهدي محله وهو يوم النحر، والأفضل أن يكون الحلق بعد النحر كما تدل عليه الآية. ويستدل بهذه الآية على أن المتمتع إذا ساق الهدي لم يتحلل من عمرته قبل يوم النحر، فإذا طاف وسعى للعمرة أحرم بالحج، ولم يكن له إحلال بسبب سوق الهدي، وإنما منع تبارك وتعالى من ذلك لما فيه من الذل والخضوع لله والانكسار له والتواضع الذي هو عين مصلحة العبد، وليس عليه في ذلك من ضرر؛ فإذا حصل الضرر بأن كان به أذى من مرض ينتفع بحلق رأسه له أو قروح أو قمل ونحو ذلك، فإنه يحل له أن يحلق رأسه، ولكن يكون عليه فدية من صيام ثلاثة أيام، أو إطعام ستة مساكين ، أو نسك ما يجزي في أضحية فهو مخير، والنسك أفضل فالصدقة فالصيام، ومثل هذا، كل ما كان في معنى ذلك من تقليم الأظفار أو تغطية الرأس أو لبس المخيط أو الطيب؛ فإنه يجوز عند الضرورة مع وجوب الفدية المذكورة، لأن القصد من الجميع إزالة ما به يترفه. ثم قال تعالى: {فإذا أمنتم}؛ أي: بأن قدرتم على البيت من غير مانع عدو وغيره {فمن تمتع بالعمرة إلى الحج}؛ بأن توصل بها إليه، وانتفع بتمتعه بعد الفراغ منها {فما استيسر من الهدي}؛ أي فعليه ما تيسر من الهدي، وهو ما يجزي في أضحية، وهذا دم نسك مقابلة لحصول النسكين له في سفرة واحدة، ولإنعام الله عليه بحصول الانتفاع بالمتعة بعد فراغ العمرة وقبل الشروع في الحج، ومثلها القِران لحصول النسكين له، ويدل مفهوم الآية على أن المفرد للحج ليس عليه هدي، ودلت الآية على جواز بل فضيلة المتعة وعلى جواز فعلها في أشهر الحج {فمن لم يجد}؛ أي الهدي أو ثمنه {فصيام ثلاثة أيام في الحج}؛ أول جوازها من حين الإحرام بالعمرة، وآخرها ثلاثة أيام بعد النحر، أيام رمي الجمار والمبيت بمنى، ولكن الأفضل منها أن يصوم السابع والثامن والتاسع {وسبعة إذا رجعتم}؛ أي: فرغتم من أعمال الحج، فيجوز فعلها في مكة، وفي الطريق، وعند وصوله إلى أهله. ذلك المذكور من وجوب الهدي على المتمتع {لمن لم يكن أهله حاضري المسجد الحرام}؛ بأن كان عنه مسافة قصر فأكثر أو بعيداً عنه عرفا، فهذا الذي يجب عليه الهدي لحصول النسكين له في سفر واحد، وأما من كان أهله من حاضري المسجد الحرام، فليس عليه هدي لعدم الموجب لذلك. {واتقوا الله}؛ أي: في جميع أموركم بامتثال أوامره واجتناب نواهيه، ومن ذلك امتثالكم لهذه المأمورات واجتناب هذه المحظورات المذكورة في هذه الآية {واعلموا أن الله شديد العقاب}؛ أي: لمن عصاه، وهذا هو الموجب للتقوى، فإن من خاف عقاب الله؛ انكف عما يوجب العقاب، كما أن من رجا ثواب الله؛ عمل لما يوصله إلى الثواب، وأما من لم يخف العقاب، ولم يرج الثواب؛ اقتحم المحارم، وتجرأ على ترك الواجبات.
{196} Aya hii inatumika kama ushahidi wa kwamba Kauli yake [Mola Mtukufu] “na timizeni Hijja na Umra” inatumika kama dalili ya mambo haya: La kwanza: Ulazima wa kufanya Hija na Umra na ufaradhi wake. La pili: Ulazima wa kuzikamilisha kwa nguzo zake na wajibu zake ambazo ziliashiriwa na kitendo cha Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na kauli yake. “Chukueni kutoka kwangu ibada zenu (za Hijja).” La tatu: Kwamba kuna hoja ndani yake kwa yule aliyesema kuwa Umra ni wajibu. La nne: Kwamba Hija na Umra ni lazima zikamilishwe baada ya kuzianza, hata kama ni za sunna. La tano: Amri ya kuzifanya kwa ukamilifu na kwa uzuri. Na hilo ni kiwango cha ziada juu ya kufanya yale yanayowapasa kufanya ndani yake. La sita: Ndani yake kuna amri ya kuzifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake. La saba: Kwamba mwenye kuingia katika ihraam ya hayo mawili hawezi kutoki kabisa katika ihraam mpaka atakapozikamilisha. Isipokuwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiondoa katika hiyo hukumu, nacho ni kuzuiwa, ndio maana akasema: “Na ikiwa mtazuiwa,” yani mmezuiwa kuifikia Nyumba ili kuzikamilisha, kwa sababu ya maradhi, au kupotea, au adui, na mfano wa hayo katika aina za kuzuiwa. “Basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana.” Basi chinjeni kilicho chepesi katika dhabihu, ambacho ni subui ya ngamia, au subui ya ng'ombe, au kondoo anayechinjwa na aliyezuiwa. Na anyoe nywele na atoke katika ihramu yake kwa sababu ya kuzuiwa, kama alivyofanya Nabii rehema na amani ziwe juu yake na maswahaba wake, pale washirikina walipowazuia (katika) mwaka wa Al-Hudaybiya. Na asipopata dhabihu, basi afunge badala yake siku kumi kama anavyofanya Al-Mutamatti’ (mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji), kisha atoke katika ihraam. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao.” Na hili ni katika makatazo ya (aliyepo katika) Ihram, yani kuondoa nywele kwa kunyoa au kinginecho kutoka kichwani, au kutoka kwenye mwili, kwa sababu lengo lake ni moja. Kwa sababu, madhumuni ya hilo ni kuwa na nywele timutimu na kuzuia kupata raha ya kuiondoa, na hilo linapatikana pia katika nywele nyinginezo. Na wanachuoni wengi walilinganisha kukata kucha na uondoaji wa nywele kwa sababu ya starehe inayopatikana ndani ya mawili hayo. Na katazo hilo la hayo yaliyotajwa linaendelea mpaka mnyama huyo afike machinjoni mwake. Nayo ni siku ya An-Nahr. Na ni bora zaidi kunyoa kuwe baada ya kuchinja, kama Aya inavyoashiria hilo. Aya hii inatumika kama dalili ya kwamba Al-Mutamatti’, (mtu anayejistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndiyo akahiji), anapomleta dhabihu haruhusiwi kutoka katika ihram ya Umra yake kabla ya siku ya An-Nahr (Siku ya kuchinja). Na anapoizunguka Al-Kaa’ba na akafanya Saa'yi ya Umra, anaingia katika Ihram ya Hija, na hawezi kutoka katika Ihram kwa sababu ya kumleta dhabihu huyo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikataza hilo kwa sababu ya yale yaliyomo katika hilo ya unyenyekevu na utiifu kwa sababu ya Mwenyezi Mungu. Na kuvunjika kwa sababu yake, na kujiweka chini sana kwa sababu yake, ambako ndiko masilahi ya mja yenyewe, ikiwa hakuna ubaya wowote juu yake katika hilo. Lakini yakitokea madhara yoyote kama vile akiwa na maudhi kutokana na maradhi ambayo kwa kunyoa kichwa chake atanufaika kwa hilo, au vidonda, au chawa na mfano wa hayo. Basi anaruhusiwa kunyoa kichwa chake, lakini inamlazimu atoe fidia ya kufunga saumu siku tatu, au kuwapa masikini sita sadaka, au kuchinja kile kinachotosheleza katika udh-hiya (dhabihu wanochinjwa siku ya Iddi). Naye amepewa chaguo, lakini kuchinja ni bora zaidi, kisha sadaka, kisha kufunga saumu. Na mfano wa hivyo ni kila kitu chenye maana hiyo kama vile kukata kucha, au kufunika kichwa, au kuvaa nguo zilizoshonwa, au manukato. Haya yote yanaruhusiwa wakati wa dharura, pamoja na ulazima wa kutoa fidia iliyotajwa hapo awali, kwa sababu makusudio ya hayo yote ni kuondoa kila ambacho anastareheka kwacho. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Na mtakapokuwa na amani,” yani mnaweza kuifikia Nyumba ya Al-Ka’ba bila ya kuzuiwa na adui na mfano wake. “Basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndiyo akahiji” kwa kuitumia kama njia ya kuifikia (Hijja) kwa kufaidika katika kustarehe baada ya kuikamilisha (yani Umra). "Basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata.” Yani inamlazimu chochote ambacho ni chepesi kwake katika dhabihu. Naye ni yule anayetosheleza katika Udh-hiya. Na hii ndiyo damu ya dhabihu ya ibada kwa sababu ya kuweza kufanya ibada hizo mbili katika safari moja. Na kwa sababu ya neema ambayo Mwenyezi Mungu amempa ya kujistarehesha baada ya kumaliza Umra, na kabla ya kuanza Hijja. Na mfano wa hilo ni Al-Qir-an (mtu anayefanya Umra kwa kuiingiza ndani ya Hija) kwa sababu ya kufanya ibada hizo mbili kwa pamoja. Na maana ya Aya hii isiyo ya moja kwa moja inaashiria kuwa mwenye kufanya Hijja peke yake halazimiki kutoa dhabihu. Na Aya hii pia inaashiria kuruhusiwa, bali ni fadhila ya kujistarehesha baada ya kumaliza Umra, na kuruhusika kuifanya (Umra) katika miezi ya Hijja. “Na asiyepata,” yani dhabihu au bei yake, “afunge siku tatu katika Hijja.” Ambayo inaruhusika kuanzia wakati wa kuingia katika Ihraam ya Umra, na mwisho wake ni siku tatu baada ya kuchinja, zile siku za kupiga vijiwe kwenye Al-Jamaraat, na kulala usiku huko Mina. Lakini lililo bora zaidi katika hizo ni kwamba afunge (siku) ya saba, na ya nane, na ya tisa. “Na siku saba mtakaporudi,” yani mtakapokuwa mmemaliza matendo ya Hijja. Kwa hivyo, inaruhusika kufanya hivyo huko Makka, na njiani, na baada ya kuwasili kwake kwa watu wake. “Hayo,” yaliyotajwa ya uwajibu wa kutoa dhabihu kwa Al-Mutamtti’ “ni kwa yule ambaye jamaa zake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu.” Ikiwa yuko kwenye umbali wa kufupisha swala au zaidi, au mbali zaidi kulingana na ada. Na huyu ndiye anayewajibika kutoa dhabihu, kwa sababu aliweza kufanya ibada hizo mbili katika safari moja. Na ama yule ambaye jamaa zake wako karibu na Msikiti Mtakatifu, basi halazimiki kutoa dhabihu kwa sababu ya kutokuwepo lenye kulazimisha hilo. “Na mcheni Mwenyezi Mungu.” Yani katika mambo yenu yote kwa kufuata maamrisho yake na kujiepusha makatazo yake. Na katika hayo ni kufuata kwenu maamrisho haya, na kujiepusha na makatazo haya yaliyotajwa katika Aya hii. “Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu,” yani mwenye kumuasi. Na hili ndilo lenye kuleta uchamungu. Kwa sababu, mwenye kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu, atajiepusha na yenye kusababisha adhabu. Kama vile mwenye kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu, atafanya yenye kumfikisha kwenye malipo. Na ama yule ambaye haogopi adhabu, wala hatarajii malipo, hujiingiza ndani ya yale yaliyoharamishwa na akajasiri kuwacha yale ya wajibu.
: 197 #
{الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَعْلُومَاتٌ فَمَنْ فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّهُ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى وَاتَّقُونِ يَاأُولِي الْأَلْبَابِ (197)}.
(197) Hijja ni miezi maalumu. Basi anayehirimia Hijja ndani yake (miezi hiyo), basi asijamiiane wala asipindukie mipaka wala asibishane katika Hijja. Na chochote mnachokifanya katika heri, Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu. Na hakika, masurufu (yaliyo) bora zaidi ni uchamungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili na busara!
#
{197} يخبر تعالى أن {الحج} واقع في {أشهر معلومات}؛ عند المخاطبين مشهورات بحيث لا تحتاج إلى تخصيص، كما احتاج الصيام إلى تعيين شهره، وكما بين تعالى أوقات الصلوات الخمس، وأما الحج فقد كان من ملة إبراهيم التي لم تزل مستمرة في ذريته معروفة بينهم. والمراد بالأشهر المعلومات عند الجمهور: شوال وذو القعدة وعشر من ذي الحجة، فهي التي يقع فيها الإحرام بالحج غالباً {فمن فرض فيهن الحج}؛ أي: أحرم به، لأن الشروع فيه يصيره فرضاً، ولو كان نفلاً. واستدل بهذه الآية الشافعي ومن تابعه على أنه لا يجوز الإحرام بالحج قبل أشهره، قلت: لو قيل [أنّ] فيها دلالة لقول الجمهور بصحة الإحرام بالحج قبل أشهره لكان قريباً، فإن قوله: {فمن فرض فيهن الحج}؛ دليل على أن الفرض قد يقع في الأشهر المذكورة، وقد لا يقع فيها وإلا لم يقيده، وقوله: {فلا رفث ولا فسوق ولا جدال في الحج}؛ أي: يجب أن تعظموا الإحرام بالحج وخصوصاً الواقع في أشهره، وتصونوه عن كل ما يفسده أو ينقصه من الرفث وهو الجماع، ومقدماته الفعلية والقولية، خصوصاً عند النساء بحضرتهن، والفسوق وهو جميع المعاصي، ومنها محظورات الإحرام، والجدال وهو المماراة والمنازعة والمخاصمة، لكونها تثير الشر وتوقع العداوة، والمقصود من الحج الذل والانكسار لله والتقرب إليه بما أمكن من القربات والتنزه عن مقارفة السيئات، فإنه بذلك يكون مبروراً، والمبرور ليس له جزاء إلا الجنة ، وهذه الأشياء وإن كانت ممنوعة في كل مكان وزمان، فإنه يتغلظ المنع عنها في الحج. واعلم أنه لا يتم التقرب إلى الله بترك المعاصي حتى يفعل الأوامر، ولهذا قال تعالى: {وما تفعلوا من خير يعلمه الله}؛ أتى بمن لتنصيص العموم فكل خير وقربة وعبادة داخل في ذلك، أي: فإن الله به عليم، وهذا يتضمن غاية الحث على أفعال الخير خصوصاً في تلك البقاع الشريفة والحرمات المنيفة، فإنه ينبغي تدارك ما أمكن تداركه فيها من صلاة وصيام وصدقة وطواف وإحسان قولي وفعلي، ثم أمر تعالى بالتزود لهذا السفر المبارك؛ فإن التزود فيه الاستغناء عن المخلوقين، والكف عن أموالهم سؤالاً واستشرافاً، وفي الإكثار منه نفع، وإعانة للمسافرين، وزيادة قربة لرب العالمين، وهذا الزاد الذي المراد منه إقامة البِنْية بُلْغَةٌ ومتاع، وأما الزاد الحقيقي المستمر نفعه لصاحبه في دنياه وأخراه فهو زاد التقوى؛ الذي هو زاد إلى دار القرار، وهو الموصل لأكمل لذة وأجل نعيم دائماً أبداً، ومن ترك هذا الزاد فهو المنقطع به، الذي هو عرضة لكل شر وممنوع من الوصول إلى دار المتقين، فهذا مدح للتقوى، ثم أمر بها أولي الألباب فقال: {واتقوني يا أولي الألباب}؛ أي: يا أهل العقول الرزينة، اتقوا ربكم، الذي تقواه أعظم ما تأمر به العقولُ، وتركها دليل على الجهل وفساد الرأي.
Mola Mtukufu anajulisha kwamba, "Hija" iko ndani ya "miezi maalumu.” Kwa wale walioongeleshwa kiasi kwamba haihitajiki kubainisha, kama vile Saumu ilivyohitajika kubainishwa mwezi wake, na kama vile Mwenyezi Mungu alivyobainisha nyakati za zile swala tano (za kila siku). Ama Hijja, hiyo ilikuwa katika mila ya Ibrahim, ambayo bado haikuacha kuendelea katika kizazi chake, na yenye kujulikana kati yao. Na kilichokusudiwa na miezi maalumu kwa wengi wa wanachuoni ni Shawwal, Dhul-Qa’da, na siku kumi (za mwanzo) katika Dhul-Hijja. Hiyo ndiyo ambayo Ihraam ya Hijja huwa mara nyingi. “Basi anayehirimia Hijja ndani yake (miezi hiyo)," yani alitia nia ya Hijja (Ihraam) ndani yake. Kwa sababu, kuianza tu, kunaifanya kuwa lazima, hata kama ni sunna. Shafii na wale waliomfuata waliitumia Aya hii kama dalili kwamba hairuhusiki kutia nia ya Hija (Ihraam) kabla ya miezi yake. Nikasema: Lau kuwa itasemwa: Ndani yake (aya hii) kuna dalili ya kauli ya wengi wa wanachuoni kwamba ni sahihi kuhirimia [Hijja] kabla ya miezi yake, basi ingekuwa karibu (na usawa). Kwa maana, kauli yake: “Basi anayehirimia Hijja ndani yake (miezi hiyo) ni dalili ya kwamba kuhirimia kunaweza kuwa au kunaweza kutokuwa ndani yake. Vinginevyo, hangezuilia hilo (la kuhirimia) ndani yake. Na kauli yake: “Basi asijamiiane wala asipindukie mipaka wala asibishane katika Hija.” Yani ni lazima muiheshimu nia ya kufanya Hija (Ihraam) hususan ile inayofanyika katika miezi yake. Na muilinde kutokana na kila chenye kuiharibu au kuipunguza, kama vile kujamiiana na vitangulizi vyake vya kimatendo na kimaneno; hususan mbele ya wanawake wanapokuwepo. Na Fusuuq ni kila maasia, ambayo ndani yake ni makatazo ya ihraam. Na Al-jidaal ni mabishano, mavutano, na mashindano kwa sababu yanasababisha shari (maovu) na huleta uadui. Na makusudio ya Hijja ni kudhalilika na kuvunjika mbele ya Mwenyezi Mungu, na kujikurubisha kwake iwezekanavyo kwa ibada mbalimbali, na kujiepusha na kufanya maovu. Kwa sababu kwa hayo, inakuwa (Hijja) iliyokubaliwa. Na Hija iliyokubaliwa haina malipo isipokuwa Pepo. Na mambo haya, hata ikiwa yameharamishwa katika kila sehemu na wakati, yameharamishwa vikali katika Hijja. Na jua ya kwamba haitimii kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuacha madhambi peke yake mpaka atekeleze maamrisho. Na kwa sababu hii, Mola Aliyetukuka akasema: “Na chochote mnachokifanya katika kheri, Mwenyezi Mungu anaijua.” Na alitumia ‘katika’ hapa ili kuonyesha ujumla wa hilo. Kwani, kila kheri, kujikurubisha, na ibada vinaingia katika hilo. Yani kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua hilo. Na hili linajumuisha kuwahimiza kukubwa mno juu ya matendo mema, hasa katika sehemu hii tukufu na matakatifu ya hali ya juu. Kwani inafaa kufanya kwa bidii yale anayoweza kufanya, kama vile swala, saumu, sadaka, kuizunguka Al-Ka’ba, kufanya wema kwa maneno na matendo. Kisha Mola Mtukufu akaamrisha kuchukua masurufu kwa ajili ya safari hii yenye baraka. Kwa maana, kuchukua masurufu ndani yake ni kujitosheleza na viumbe, na kuachana na mali zao, kwa kuziomba na kuzitaka kwa uchu. Na kuichukua kwa wingi kuna manufaa na kuna kuwasadia wasafiri, na kunaongeza kujikurubisha kwa Mola Mlezi wa walimwengu. Na masurufu haya ambayo yamekusudiwa kumpa nguvu katika mwili na kumsaidia kufika anakokwenda na kurejea. Na ama masurufu ya kweli yanayoendelea kumnufaisha mwenyewe katika dunia yake na akhera yake, basi ni masurufu ya uchamungu. Ambao (uchamungu huo) ni masurufu ya kwenda katika makazi ya daima. Nayo ndiyo yenye kufikisha kwenye ladha kamili zaidi; na neema nzuri zaidi yenye kudumu milele. Na mwenye kuyaacha masurufu haya, basi huyo ndiye aliyekatikiwa. Ambaye ana uwezekano mkubwa wa kupatwa na kila shari (maovu); na anayezuiliwa kufika kwenye nyumba ya wachamungu. Na huku ni ya uchamungu. Kisha akawaamrisha hilo wenye akili, akasema: “Na nicheni Mimi, enyi wenye akili na busara,” yani enyi watu wenye akili ya kina, mcheni Mola wenu Mlezi ambaye kumcha ndiko kikubwa mno ambacho akili zinaamrisha. Na kuiacha ni dalili ya ujinga na upotovu wa rai.
: 198 - 202 #
{لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلًا مِنْ رَبِّكُمْ فَإِذَا أَفَضْتُمْ مِنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّهَ عِنْدَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِنْ كُنْتُمْ مِنْ قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ (198) ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (199) فَإِذَا قَضَيْتُمْ مَنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا فَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ (200) وَمِنْهُمْ مَنْ يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ (201) أُولَئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِمَّا كَسَبُوا وَاللَّهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ (202)}
(198) Hakuna ubaya wowote juu yenu kutafuta fadhila kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu). Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapo kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea. (199) Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. (200) Na mkishatimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu au utajo mkubwa zaidi. Na katika watu kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani!” Naye katika Akhera hana fungu lolote. (201) Na miongoni mwao kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde kutokana na adhabu ya Moto!” (202) Hao ndio walio na fungu kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
#
{198} لما أمر تعالى بالتقوى أخبر تعالى أن ابتغاء فضل الله بالتكسب في مواسم الحج وغيره ليس فيه حرج إذا لم يشغل عما يحب إذا كان المقصود هو الحج، وكان الكسب حلالاً منسوباً إلى فضل الله؛ لا منسوباً إلى حذق العبد والوقوف مع السبب ونسيان المسبب، فإن هذا هو الحرج بعينه وفي قوله: {فإذا أفضتم من عرفات فاذكروا الله عند المشعر الحرام}؛ دلالة على أمور: أحدها: الوقوف بعرفة، وأنه كان معروفاً أنه ركن من أركان الحج، فالإفاضة من عرفات لا تكون إلا بعد الوقوف. الثاني: الأمر بذكر الله عند المشعر الحرام وهو المزدلفة، وذلك أيضاً معروف يكون ليلة النحر بائتاً بها، وبعد صلاة الفجر يقف في المزدلفة داعياً حتى يسفر جدًّا، ويدخل في ذكر الله عنده إيقاع الفرائض والنوافل فيه. الثالث: أن الوقوف بمزدلفة متأخر عن الوقوف بعرفة كما تدل عليه الفاء والترتيب. الرابع والخامس: أن عرفات ومزدلفة كلاهما من مشاعر الحج المقصود فعلها وإظهارها. السادس: أن مزدلفة في الحرم كما قيده بالحرام. السابع: أن عرفة في الحل كما هو مفهوم التقييد بمزدلفة. {واذكروه كما هداكم وإن كنتم من قبله لمن الضالين}؛ أي اذكروا الله تعالى كما منَّ عليكم بالهداية بعد الضلال، وكما علمكم ما لم تكونوا تعلمون. فهذه من أكبر النعم التي يجب شكرها ومقابلتها بذكر المنعم بالقلب واللسان.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamrisha uchamungu, alijulisha Yeye Mtukufu kwamba kutafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa kuchuma katika misimu ya Hija na mingineyo, hakuna ubaya wowote; ikiwa hakutashughulisha na yale ambayo ni ya lazima ikiwa lengo ni kuhiji. Na yakawa hayo mapato ni halali yanayohusishwa na fadhila ya Mwenyezi Mungu, siyo yenye kunasibishwa na ustadi wa mja, na kutegemea sababu tu na kumsahau mwenye kusababisha. Basi huo ndiyo ubaya wenyewe. Na katika kauli yake :“Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu).” Kuna dalili ya mambo: La kwanza: Kusimama ‘Arafa, na kwamba ilikuwa inajulikana kuwa ni nguzo katika nguzo za Hijja. Kwa maana, kumiminika kutoka ‘Arafa hakuwi isipokuwa baada ya kusimama ‘Arafa. La pili: Amri ya kumtaja Mwenyezi Mungu katika Mash’aril Haram, napo ni Muzdalifah. Na hili pia ni maarufu. Analala usiku wa kuamkia (siku ya) kuchinja hapo. Na baada ya swalah ya Alfajiri, atasimama Muzdalifah akiomba dua, mpaka kuangaze sana. Na anaingia katika kumtaja Mwenyezi Mungu hapo, akitekeleza sala za faradhi na za sunna hapo. La tatu: Kusimama Muzdalifah kuko nyuma ya kusimama ‘Arafah, kama inavyoonyeshwa na neno ‘kisha’ na utaratibu (uliopo katika vitendo vya aya). La nne na la tano: Kwamba ‘Arafa na Muzdalifah zote ni katika maeneo takatifu ya Hija yanayokusudiwa kufanywa na kudhihirishwa. La sita: Kwamba Muzdalifah iko katika Haram (eneo takatifu), kama alivyoifunganisha na neno ‘takatifu’. La saba: Kwamba ‘Arafa iko katika eneo lisilokuwa takatifu (Al-Hill), kama inavyofahamika katika maana isiyokuwa ya moja kwa moja katika kufunganisha Muzdalifah na neno ‘takatifu’. “Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapo kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea.” Yani mtajeni Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyowaneemesha kwa uwongofu baada ya upotovu, na kama alivyowafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. Na hii ni katika neema kubwa mno ambazo kuu ni lazima kuzishukuru na kuzikabili kwa kumtaja aliyeneemesha kwa moyo na ulimi.
#
{199} {ثم أفيضوا من حيث أفاض الناس}؛ أي: ثم أفيضوا من مزدلفة من حيث أفاض الناس من لدن إبراهيم عليه السلام إلى الآن، والمقصود من هذه الإفاضة كان معروفاً عندهم، وهو رمي الجمار، وذبح الهدايا، والطواف والسعي والمبيت بمنى ليالي التشريق، وتكميل باقي المناسك، ولما كانت هذه الإفاضة يقصد بها ما ذكر والمذكورات آخر المناسك، أمر تعالى عند الفراغ منها باستغفاره والإكثار من ذكره، فالاستغفار للخلل الواقع من العبد في أداء عبادته وتقصيره فيها، وذكر الله شكر الله على إنعامه عليه بالتوفيق لهذه العبادة العظيمة والمنة الجسيمة، وهكذا ينبغي للعبد كلما فرغ من عبادة أن يستغفر الله عن التقصير، ويشكره على التوفيق، لا كمن يرى أنه قد أكمل العبادة، ومنَّ بها على ربه، وجعلت له محلاًّ ومنزلة رفيعة، فهذا حقيق بالمقت ورد العمل، كما أن الأول حقيق بالقبول والتوفيق لأعمال أخر.
“Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu,” yani kisha miminikeni kutoka Muzdalifah kutoka pale ambapo watu wanamiminika tangu siku za Ibrahim, amani iwe juu yake, mpaka sasa. Na kilichokusudiwa na kuunganisha huku (yani kutoka pale wanapomiminika watu) kilikuwa kinajulikana kwao (yani Maqureshi). Ambayo ni kutupa vijiwe kwenye Al-Jamarat, kuchinja dhabihu, kuzunguka Al-Ka’aba, kufanya Sa’ayi, kulala Mina katika siku za At-Tashriq na kukamilisha ibada zinginezo za Hijja. Na kwa vile [huku] kumiminika kusudi lake ni hayo yaliyotajwa, na kwamba yaliyotajwa ndiyo mambo ya mwisho wa ibada za Hijja. Yeye Aliyetukuka aliamrisha baada ya kuikamilisha kumwomba msamaha na kumtaja kwa wingi. Na kuomba msamaha ni kwa sababu ya makosa yaliyotokea kutoka kwa mja katika kutekeleza ibada zake na mapungufu yake ndani yake. Na kumtaja Mwenyezi Mungu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema yake juu yake kwa kumwezesha kufanya hii ibada tukufu na neema kubwa mno. Hivyo basi, mja anafaa kila anapomaliza ibada, amuombe msamaha Mwenyezi Mungu kwa upungufu wake. Na amshukuru kwa kumwezesha, na siyo kama yule anayeona kwamba amekamilisha ibada. Hivyo akaona kuwa amemfanyia hisani Mola wake Mlezi kwa kuifanya na kwamba itampa cheo na hadhi ya juu. Basi huyu anastahiki kuchukiwa na kukataliwa matendo yake, kama vile yule wa kwanza anavyostahiki kukubaliwa matendo na kuwezeshwa kufanya matendo mengine.
#
{200 - 201 - 202} ثم أخبر تعالى عن أحوال الخلق، وأن الجميع يسألونه مطالبهم، ويستدفعونه ما يضرهم، ولكن مقاصدهم تختلف، فمنهم {من يقول ربنا آتنا في الدنيا}؛ أي: يسأله من مطالب الدنيا ما هو من شهواته، وليس له في الآخرة من نصيب لرغبته عنها، وقصر همته على الدنيا، ومنهم من يدعو الله لمصلحة الدارين، ويفتقر إليه في مهمات دينه ودنياه، وكل من هؤلاء وهؤلاء لهم نصيب من كسبهم وعملهم، وسيجازيهم تعالى على حسب أعمالهم وهماتهم ونياتهم جزاءً دائراً بين العدل والفضل، يحمد عليه أكمل حمد وأتمه. وفي هذه الآية دليل على أن الله يجيب دعوة كل داعٍ مسلماً أو كافراً أو فاسقاً، ولكن ليست إجابته دعاء من دعاه دليلاً على محبته له وقربه منه إلا في مطالب الآخرة ومهمات الدين، والحسنة المطلوبة في الدنيا، يدخل فيها كل ما يحسن وقعه عند العبد من رزق هني واسع حلال، وزوجة صالحة، وولد تقر به العين، وراحة، وعلم نافع، وعمل صالح، ونحو ذلك من المطالب المحبوبة والمباحة، وحسنة الآخرة هي السلامة من العقوبات في القبر والموقف والنار، وحصول رضا الله، والفوز بالنعيم المقيم، والقرب من الرب الرحيم، فصار هذا الدعاء أجمع دعاء وأكمله وأولاه بالإيثار، ولهذا كان النبي - صلى الله عليه وسلم -، يكثر من الدعاء به والحث عليه.
Kisha Mola Mtukufu akajulisha kuhusu hali za viumbe, na kwamba wote wanamuomba mahitaji yao, na wanamwomba awazuie yenye kuwadhuru, lakini makusudio yao yanatofautiana. Miongoni mwao “kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani” yani anamuomba katika matakwa ya kidunia. Na yale ambayo ni katika matamanio yake, ilhali hana fungu lolote katika Akhera, kwa sababu ya kutoitaka; na akaiweka hima yake katika dunia peke yake. Na miongoni mwao kuna wale wanaomuomba Mwenyezi Mungu kwa manufaa ya Nyumba hizi mbili, na anamhitaji katika mambo ya dini yake na dunia yake. Na kila mmoja kati ya hawa na hao ana fungu la walichochuma na matendo yao. Na Mola Mtukufu atawalipa kulingana na matendo yao, na hima zao, na nia zao malipo yanayozunguka kati ya uadilifu na fadhila, ambayo kwayo anasifiwa sifa kamilifu zaidi na timilifu zaidi. Na katika Aya hii kuna dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu anajibu dua ya kila mwombaji, awe Muislamu au kafiri, au mwenye kupindukia mipaka. Lakini jawabu lake kwa dua ya mwenye kumwomba siyo dalili ya mapenzi yake kwake na ukaribu wake kwake, isipokuwa katika matakwa ya Akhera na mambo ya dini. Na kheri inayotakiwa katika dunia hii inaingia ndani yake kila kinachopendwa na mja. Kama vile riziki nyingi, yenye baraka na halali, na mke mwema, na mtoto anayelipendeza jicho lake, na starehe, na elimu yenye manufaa, na matendo mema, na mfano wa hayo; miongoni mwa mahitaji yanayopendwa na yanayoruhusiwa. Na kheri ya Akhera, ambayo ni kusalimika kutokana na adhabu kaburini, na kisimamo, na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kupata neema ya kudumu, na kuwa karibu na Mola Mlezi. Kwa hivyo, dua hii ikawa ni ndio dua inayojumuisha zaidi na kamilika zaidi na inayofaa zaidi kupendelewa. Na ndio maana Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alikuwa akiiomba sana kwa dua hii, na akahimiza juu yake.
: 203 #
{وَاذْكُرُوا اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَعْدُودَاتٍ فَمَنْ تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَنْ تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ لِمَنِ اتَّقَى وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ (203)}
(203) Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazohisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka (akarejea) katika siku mbili, basi hakuna dhambi juu yake. Na mwenye kukawia, pia hakuna dhambi juu yake, kwa mwenye kumcha Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.
#
{203} يأمر تعالى بذكره في الأيام المعدودات وهي أيام التشريق الثلاثة بعد العيد لمزيتها وشرفها، وكون بقية المناسك تفعل بها، ولكون الناس أضيافاً لله فيها، ولهذا حرم صيامها، فللذكر فيها مزية ليست لغيرها، ولهذا قال النبي - صلى الله عليه وسلم -: «أيام التشريق أيام أكل وشرب وذكر الله» ، ويدخل في ذكر الله فيها؛ ذكره عند رمي الجمار، وعند الذبح، والذكر المقيد عقب الفرائض، بل قال بعض العلماء إنه يستحب فيها التكبير المطلق كالعشر وليس ببعيد {فمن تعجل في يومين}؛ أي: خرج من منى، ونفر منها قبل غروب شمس اليوم الثاني {فلا إثم عليه ومن تأخر}؛ بأن بات بها ليلة الثالث، ورمى من الغد {فلا إثم عليه}؛ وهذا تخفيف من الله تعالى على عباده في إباحة كلا الأمرين، ولكن من المعلوم أنه إذا أبيح كلا الأمرين، فالتأخُّر أفضل؛ لأنه أكثر عبادة. ولما كان نفي الحرج قد يفهم منه نفي الحرج في ذلك المذكور وفي غيره، والحاصل أن الحرج منفي عن المتقدم والمتأخر فقط، قيده بقوله: {لمن اتقى}؛ أي: اتقى الله في جميع أموره وأحوال الحج، فمن اتقى الله في كل شيء، حصل له نفي الحرج في كل شيء، ومن اتقاه في شيء دون شيء كان الجزاء من جنس العمل {واتقوا الله}؛ بامتثال أوامره، واجتناب معاصيه {واعلموا أنكم إليه تحشرون}؛ فمجازيكم بأعمالكم، فمن اتقاه وجد جزاء التقوى عنده، ومن لم يتقه عاقبه أشدَّ العقوبة، فالعلم بالجزاء من أعظم الدواعي لتقوى الله، فلهذا حثَّ تعالى على العلم بذلك.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kumtaja Yeye katika siku zinazohesabiwa, ambazo ni zile siku tatu za Tashriiq baada ya Idi. Kwa sababu ya umaalumu wake na utukufu wake, na kwa kuwa matendo yaliyobaki ya Hijja hufanyika ndani yake na kuwa watu ni wageni wa Mwenyezi Mungu ndani yake. Na kwa sababu hii, imeharamishwa kufunga Saumu ndani yake. Kwa hivyo kumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake kuna umaalumu ambao hauko katika siku zinginezo. Na ndiyo maana Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema. “Siku za tashriiq ni siku za kula, kunywa, na kumtaja Mwenyezi Mungu”. Na inaingia katika hilo kumtaja Mwenyezi Mungu katika hizo siku, kumtaja wakati wa kutupa vijiwe kwenye Jamaraat, na wakati wa kuchinja, na utajo unaofanya baada ya swala za faradhi tu. Bali baadhi ya wanachuoni walisema: “Inapendekezwa mtu kufanya takbira isiyo na mipaka, kama inavyokuwa katika zile siku kumi za kwanza za Dhul-Hijja”. Na hili haliko mbali (na usawa). “Lakini mwenye kufanya haraka (akarejea) katika siku mbili.” Yani alitoka Mina kabla ya kuzama kwa jua katika siku ya pili (baada ya siku ya Idi), “basi hakuna dhambi juu yake. Na mwenye kukawia” kwa kulala huko (Mina) usiku wa kuamkia siku ya tatu (baada ya Idi) na kesho yake akatupa vijiwe kwenye Jamaraat, “pia hakuna dhambi juu yake”. Na huku ni kupunguziwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu [Mtukufu] kwa waja wake katika kuruhusu mambo hayo mawili. Lakini inajulikana kwamba ikiwa mambo mawili yanaruhusiwa, basi (jambo) la nyuma ndilo bora zaidi, kwa sababu lina ibada nyingi zaidi. Na kwa kuwa huenda ikafahamika kutokana na kukanusha dhambi kuwa ni kukanusha dhambi katika hilo lililotajwa na mengineyo. Na ukweli ni kwamba dhambi imekanushwa kwa aliyetanguliza na aliyechelewesha peke yao. Akazuia hilo (la kukanusha dhambi) kwa kauli yake, “kwa mwenye kumcha Mungu”. Yani alimcha Mwenyezi Mungu katika mambo yake yote na hali za Hijja. Kwa hivyo, mwenye kumcha Mwenyezi Mungu katika kila kitu, basi akapata kukanushiwa dhambi katika kila kitu. Na mwenye kumcha katika kitu na siyo katika kitu kingine, malipo yake yanakuwa ya aina sawa na matendo yake. “Na mcheni Mwenyezi Mungu” kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na maasia yake. “Na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake,” na awalipe kwa matendo yenu. Kwa hivyo, mwenye kumcha, atapata malipo ya uchamungu kwake. Na yule asiyemcha, atamuadhibu adhabu kali kabisa. Hivyo basi, kujua malipo, ni miongoni mwa sababu kubwa zaidi zenye kusababisha kumcha Mwenyezi Mungu. Ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akahimiza kwamba hilo lijulikane.
: 204 - 206 #
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّهَ عَلَى مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ (204) وَإِذَا تَوَلَّى سَعَى فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ (205) وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ (206)}
(204) Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukupendeza; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo katika moyo wake, na hali yeye ndiye mgomvi mkubwa mno. (205) Na akishageuka akaenda, anazunguka katika ardhi ili afanye humo ufisadi na anaharibu mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi. (206) Na akiambiwa, “mche Mwenyezi Mungu,” hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo kinachomtosha ni Jahannam. Napo hakika ni pahali pabaya mno pa kupumzikia.
#
{204} لما أمر تعالى بالإكثار من ذكره، وخصوصاً في الأوقات الفاضلة الذي هو خيرٌ ومصلحة وبرٌّ أخبر تعالى بحال من يتكلم بلسانه، ويخالف فعلُه قولَه، فالكلام إما أن يرفع الإنسان أو يخفضه فقال: {ومن الناس من يعجبك قوله في الحياة الدنيا}؛ أي: إذا تكلم راق كلامُه السامعَ، وإذا نطق ظننته يتكلم بكلام نافع، ويؤكد ما يقول بأنه {يشهد الله على ما في قلبه}؛ بأن يخبر أن الله يعلم أن ما في قلبه موافق لما نطق به، وهو كاذب في ذلك لأنه يخالف قوله فعله، فلو كان صادقاً لتوافق القول والفعل كحال المؤمن غير المنافق، ولهذا قال: {وهو ألد الخصام}؛ أي: إذا خاصمته، وجدت فيه من اللدد والصعوبة والتعصب وما يترتب على ذلك ما هو من مقابح الصفات، ليس كأخلاق المؤمنين؛ الذين جعلوا السهولة مركبهم والانقياد للحق وظيفتهم والسماحة سجيتهم.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoamrisha kumtaja kwa wingi hasa katika nyakati bora, ambalo (yani kumtaja) ni heri na lenye masilahi na wema. Yeye Mtukufu akajulisha kuhusu hali ya yule anayezungumza kwa ulimi wake na kitendo chake kinapingana na kauli yake. Na mazungumzo ima humnyanyua mtu au humshusha. Akasema: “Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukupendeza.” Yani anapozungumza, maneno yake yanamvutia msikilizaji. Na anapotamka utamdhania anazungumza maneno yenye manufaa, na anayasisitiza anayoyasema kuwa: “Humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo katika moyo wake;” kwa kusema kuwa Mwenyezi Mungu anajua kwamba yale yaliyomo ndani ya moyo wake yanaafikiana na yale aliyotamka. Ilhali yeye ni mwongo katika hayo, kwa sababu kauli yake inapingana na kitendo chake. Na lau kuwa alikuwa mkweli, maneno yake na vitendo vyake vingeafikiana, kama ilivyo hali ya Muumini asiyekuwa mnafiki. Ndio maana akasema, “na hali yeye ndiye mgomvi mkubwa mno.” Yani unapogombana naye, utakuta ndani yake ugomvi mkubwa, na ugumu na kutetea batili. Na yale yanayotokana na hayo ambayo ni katika sifa mbaya. Si kama tabia za Waumini ambao walifanya wepesi ndiyo kipando chao, na kufuata haki ndiyo kazi yao, na uzuri katika kuamiliana ndiyo tabia yao.
#
{205} {وإذا تولى}؛ هذا الذي يعجبك قوله إذا حضر عندك {سعى في الأرض ليفسد فيها}؛ أي: يجتهد على أعمال المعاصي التي هي إفساد في الأرض فيهلك بسبب ذلك {الحرث والنسل}؛ فالزروع والثمار والمواشي تتلف، وتنقص، وتقل بركتها بسبب العمل في المعاصي، {والله لا يحب الفساد}؛ فإذا كان لا يحب الفساد فهو يبغض العبد المفسد في الأرض غاية البغض، وإن قال بلسانه قولاً حسناً. ففي هذه الآية دليل على أن الأقوال التي تصدر من الأشخاص ليست دليلاً على صدقٍ ولا كذبٍ ولا برٍّ ولا فجورٍ، حتى يوجد العمل المصدق لها، المزكي لها، وأنه ينبغي اختبار أحوال الشهود والمحق والمبطل من الناس ببرِّ أعمالهم، والنظر لقرائن أحوالهم، وأن لا يغتر بتمويههم وتزكيتهم أنفسهم، ثم ذكر أن هذا المفسد في الأرض بمعاصي الله إذا أمر بتقوى الله تكبر وأنف.
“Na akishageuka akaenda,” huyo ambaye kauli yake hukupendeza anapokuwa pamoja nawe; “anazunguka katika ardhi ili afanye humo ufisadi.” Yani anajitahidi kufanya maasia ambayo ni kufanya uharibifu katika ardhi, “na anaharibu” kwa sababu ya hilo “mimea na viumbe”. Kwa hivyo, mimea, matunda na mifugo vinaharibika na vinapunguka na baraka zake zinakuwa chache kwa sababu ya matenddo yake. “Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” Na kama hapendi ufisadi, basi yeye humchukia mja anayefanya ufisadi katika ardhi kuchukia kukubwa, hata akisema kwa ulimi wake maneno mema. Katika Aya hii, kuna dalili ya kwamba maneno yanayotoka kwa watu siyo ushahidi wa ukweli wala uwongo, wala wema wala upotovu; mpaka yapatikane matendo na yanayoyasadikisha, yenye kuyatakasa, na kwamba ni lazima kupima hali ya mashahidi. Na aliye katika haki na aliye katika batili miongoni mwa watu, kwa kuchunguza matendo yao yote, na kuangalia yale yanayofungamana na hizo hali zao. Na kwamba mtu asidanganyike na kujionyesha kwao na kujitakasa kwao nafsi zao. Kisha akataja kwamba mharibifu huyu katika ardhi kwa kumuasi Mwenyezi Mungu anapoamrishwa kumcha Mwenyezi Mungu, anafanya kiburi na ukaidi.
#
{206} {وأخذته العزة بالإثم}؛ فيجمع بين العمل بالمعاصي والتكبر على الناصحين {فحسبه جهنم}؛ التي هي دار العاصين والمتكبرين {وبئس المهاد}؛ أي المستقر والمسكن، عذاب دائم، وهمٌ لا ينقطع، ويأس مستمر، لا يخفف عنهم العذاب ولا يرجون الثواب، جزاءً لجنايتهم ومقابلة لأعمالهم، فعياذاً بالله من أحوالهم.
(206) Na “hupandwa na mori wa kutenda madhambi.” Kwa hivyo anajumuisha kati ya kufanya maasia na kiburi kwa wanaomshauri. “Basi huyo kinachomtosha ni Jahannam,” ambayo ndio makazi ya wafanyao maasia na wanaotakabari. “Napo hakika ni pahali pabaya mno pa kupumzikia.” Yani pahali pa kukaa na maskani, yenye adhabu ya daima, na huzuni isiyoisha, na kukata tamaa kwenye kuendelea. Hawatapunguziwa adhabu, wala hawatarajii malipo mazuri. Haya ni malipo ya makosa yao na matendo yao. Basi Mwenyezi Mungu atuepushe na hali zao.
: 207 #
{وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ وَاللَّهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ (207)}
(207) Na katika watu kuna yule anayeiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
#
{207} [هؤلاء هم الموفقون الذين باعوا أنفسهم، وأرخصوها، وبذلوها طلباً لمرضاة الله، ورجاءً لثوابه، فهم بذلوا الثمن للملي الوفي، الرءوف بالعباد، الذي من رأفته ورحمته أن وفقهم لذلك، وقد وَعَدَ الوفاء بذلك، فقال: {إن الله اشترى من المؤمنين أنفسهم وأموالهم بأنَّ لهم الجنة ... } إلى آخر الآية. وفي هذه الآية أخبر أنهم اشتروا أنفسهم وبذلوها، وأخبر برأفته الموجبة لتحصيل ما طلبوا، وبذل ما به رغبوا، فلا تسأل بعد هذا عمّا يحصل لهم من الكريم، وما ينالهم من الفوز والتكريم].
{207} Hawa ndio waliowezeshwa, ambao waliziuza nafsi zao kwa bei nafuu na wakazitoa kwa kutafuta kumridhisha Mwenyezi Mungu na kutarajia malipo yake. Basi wao walitoa thamani kumpa Mkwasi, Mwenye kulipa vikamilifu, Mpole kwa waja wake. Ambaye katika Upole wake na rehema zake ni kwamba aliwawezesha kufanya hayo, na akaahidi kulipa kwa ukamilifu, akasema: “Hakika, Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo.” Hadi mwisho wa Aya. Na katika Aya hii Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba waliziuza nafsi zao na wakazitoa. Na akajulisha kuhusu upole wake unaosababisha wao kupata walichoomba, na wakatoa walichokitaka. Basi usiulize baada ya haya yale yanayowapata kutoka kwa Mkarimu, na kile kinachowapata cha kufaulu na kuheshimiwa.
: 208 - 209 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ (208) فَإِنْ زَلَلْتُمْ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (209)}.
(208) Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika, yeye kwenu ni adui wa dhahiri. (209) Na mkiteleza baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi, basi jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{208} هذا أمر من الله تعالى للمؤمنين أن يدخلوا {في السلم كافة}؛ أي: في جميع شرائع الدين، ولا يتركوا منها شيئاً، وأن لا يكونوا ممن اتخذ إلهه هواه؛ إن وافق الأمر المشروع هواه فعله، وإن خالفه تركه، بل الواجب أن يكون الهوى تبعاً للدين، وأن يفعل كل ما يقدر عليه من أفعال الخير، وما يعجز عنه يلتزمه، وينويه فيدركه بنيته، ولما كان الدخول في السلم كافة لا يمكن ولا يتصور إلا بمخالفة طرق الشيطان قال: {ولا تتبعوا خطوات الشيطان}؛ أي: في العمل بمعاصي الله، {إنه لكم عدو مبين}؛ والعدو المبين لا يأمر إلا بالسوء والفحشاء وما به الضرر عليكم، ولما كان العبد لا بد أن يقع منه خللٌ وزللٌ قال تعالى:
{208} Hii ni amri kutoka kwa Mola Mtukufu kwa Waumini kwamba waingie, “Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu.” Yani katika sheria zote za dini, wala wasiache chochote chake, na kwamba wasiwe miongoni mwa wale walioyafanya matamanio yao kuwa ndiyo mungu wao. Ikiwa jambo lililo katika sheria litakubaliana na matamanio yao, analifanya. Na likitofautiana nayo, analiacha. Lakini, wajibu ni kwamba matamanio yafuate dini, na kwamba yote anayoweza katika matendo mema. Na yale asiyoyaweza, anayawekea azma, na anayatilia nia, kwa hayo anayapata kwa nia yake. Na kwa kuwa kuingia katika Uislamu kwa ukimilifu hakuwezekani kuingia akilini isipokuwa kwa kuhalifu njia za Shetani, akasema; “wala msifuate nyayo za Shetani.” Yani katika kumuasi Mwenyezi Mungu. “Hakika, yeye kwenu ni adui wa dhahiri.” Na adui wa dhahiri haamrishi isipokuwa uovu na machafu, na yale yenye kuwadhuru. Na kwa kuwa mja hana budi kufanya kosa na kuteleza, Mola Mtukufu akasema:
#
{209} {فإن زللتم من بعد ما جاءتكم البينات}؛ أي: على علم ويقين، {فاعلموا أن الله عزيز حكيم}، وفيه من الوعيد الشديد والتخويف ما يوجب ترك الزلل، فإن العزيز المقام الحكيم إذا عصاه العاصي، قهره بقوته، وعذبه بمقتضى حكمته، فإن من حكمته تعذيب العصاة والجناة.
(209) “Na mkiteleza baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi,” yani kwa kujua na kwa yakini; “basi jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” Na ndani yake kuna tishio kali na kuhofisha yanayolazimu kuacha kuteleza. Kwani Mwenye nguvu, Mshindi, Mwenye hekima anapofanyiwa maasia na muasi, anamshinda kwa nguvu zake. Na anamwadhibu kulingana na hekima yake. Kwa maana katika hekima yake ni kuwaadhibu waasi na wakosaji.
: 210 #
{هَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا أَنْ يَأْتِيَهُمُ اللَّهُ فِي ظُلَلٍ مِنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ (210)}
(210) Je, wanangoja mpaka Mwenyezi Mungu awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika, na hukumu iwe imekwisha tolewa? Na kwa Mwenyezi Mungu ndiyo hurejeshwa mambo yote.
#
{210} وهذا فيه من الوعيد الشديد والتهديد ما تنخلع له القلوب، يقول تعالى: هل ينتظر الساعون في الفساد في الأرض، المتبعون لخطوات الشيطان، النابذون لأمر الله إلا يوم الجزاء بالأعمال، الذي قد حُشِي من الأهوال والشدائد والفظائع ما يقلقل قلوب الظالمين، ويحق به الجزاء السَّيئ على المفسدين، وذلك أن الله تعالى يطوي السماواتِ والأرضَ، وتنتثر الكواكبُ، وتُكوَّر الشمس والقمر، وتنزل الملائكة الكرام فتحيط بالخلائق، وينزل الباري تبارك وتعالى {في ظلل من الغمام} ليفصل بين عباده بالقضاء العدل، فتوضع الموازين، وتنشر الدواوين، وتبيَّض وجوه أهل السعادة، وتسوَّد وجوه أهل الشقاوة، ويتميز أهل الخير من أهل الشرِّ، وكل يجازى بعمله، فهنالك يعضُّ الظالم على يديه إذا علم حقيقة ما هو عليه. وهذه الآية وما أشبهها دليل لمذهب أهل السنة والجماعة المثبتين للصفات الاختيارية؛ كالاستواء، والنزول، والمجيء، ونحو ذلك من الصفات التي أخبر بها تعالى عن نفسه، أو أخبر بها عنه رسوله - صلى الله عليه وسلم -، فيثبتونها على وجه يليق بجلال الله وعظمته من غير تشبيه ولا تحريف، خلافاً للمعطلة على اختلاف أنواعهم، من الجهمية والمعتزلة والأشعرية ونحوهم، ممن ينفي هذه الصفات، ويتأول لأجلها الآيات بتأويلات ما أنزل الله عليها من سلطان، بل حقيقتها القدح في بيان الله وبيان رسوله، والزعم بأن كلامهم هو الذي تحصل به الهداية في هذا الباب، فهؤلاء ليس معهم دليل نقلي؛ بل ولا دليل عقلي. أما النقلي فقد اعترفوا أن النصوص الواردة في الكتاب والسنة، ظاهرها بل صريحها دال على مذهب أهل السنة والجماعة، وأنها تحتاج لدلالتها على مذهبهم الباطل أن تخرج عن ظاهرها ويزاد فيها وينقص، وهذا كما ترى لا يرتضيه من في قلبه مثقال ذرة من إيمان. وأما العقل فليس في العقل ما يدل على نفي هذه الصفات، بل العقل دل على أن الفاعل أكمل من الذي لا يقدر على الفعل، وأن فعله تعالى المتعلق بنفسه والمتعلق بخلقه هو كمال، فإن زعموا أن إثباتها يدل على التشبيه بخلقه، قيل لهم الكلام على الصفات يتبع الكلام على الذات، فكما أن لله ذاتاً لا تشبهها الذوات فلله صفات لا تشبهها الصفات، فصفاته تبع لذاته وصفات خلقه تبع لذواتهم، فليس في إثباتها ما يقتضي التشبيه بوجه، ويقال أيضاً لمن أثبت بعض الصفات، ونفى بعضاً، أو أثبت الأسماء دون الصفات: إما أن تثبت الجميع كما أثبته الله لنفسه، وأثبته رسوله، وإما أن تنفي الجميع، وتكون منكراً لرب العالمين. وأما إثباتك بعض ذلك ونفيك لبعضه فهذا تناقض، فَفَرِّقْ بين ما أثبته وبين ما نفيته، ولن تجد إلى الفرق سبيلاً. فإن قلت ما أثبته لا يقتضي تشبيهاً، قال لك أهل السنة والإثبات لما نفيته لا يقتضي تشبيهاً، فإن قلت لا أعقل من الذي نفيته إلا التشبيه، قال لك النفاة ونحن لا نعقل من الذي أثبته إلا التشبيه، فما أجبت به النفاة أجابك به أهل السنة لما نفيته. والحاصل أن من نفى شيئاً، وأثبت شيئاً مما دل الكتاب والسنة على إثباته فهو متناقض؛ لا يثبت له دليل شرعي ولا عقلي، بل قد خالف المعقول والمنقول.
Na haya, ndani yake yamo onyo kali na tishio ambayo nyoyo hutetemeka kwa sababu yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Je, wanangoja hao wanaozunguka katika ardhi wakifanya ufisadi, wanaofuata nyayo za Shetani, wanaoitupilia mbali amri ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa Siku ya Malipo kwa matendo. Ambayo imejazwa mahangaiko, dhiki na mambo ya kutisha yenye kutia wasiwasi katika nyoyo za madhalimu ambayo kwayo yatawafika malipo mabaya wafanyao ufisadi? Na hayo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atazikunja mbingu na ardhi, na sayari zitatawanywa, jua na mwezi vitakunjwa, na malaika watukufu watateremka na wawazunguke viumbe. Na Al-Bari (Muumba mwanzilishi), [Mwenye baraka], Mtukufu atateremka “katika vivuli vya mawingu” ili apambanue kati ya waja wake kwa hukumu ya uadilifu. Kwa hivyo mizani itawekwa, na vitabu vitaenezwa. Na nyuso za watu wa furaha (waliofaulu) zikakuwa nyeupe, nazo nyuso za watu wa taabuni zitakuwa nyeusi. Na watu wa heri watatenganishwa na watu wa shari (uovu), na kila mmoja atalipwa kwa matendo yake. Basi hapo, dhalimu atajiuma mikono yake atakapojua uhakika wa hali yake. Na Aya hii na mfano wake ni dalili ya dhehebu la Ahlul-Sunnah wal-Jama`ah, ambao huthibitisha sifa za hiari (za Mwenyezi Mungu). Kama vile istiwaa (kuinuka juu), kushuka, kuja na mfano wa hizo miongoni mwa sifa ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kuhusu nafsi yake. Au Mtume wake rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ndiye aliyetoa habari juu yake. Wao huthibitisha kwa namna ambayo inalingana na utukufu wake na ukuu wake, bila ya kufananisha, wala kupotosha. Kinyume na Al-Mu’atila na mfano wao miongoni mwa wale wanaozipinga sifa hizi. Na wanazifasiri aya kwa sababu ya hilo tafsiri ambazo Mwenyezi Mungu hakuziteremshia hoja yoyote. Bali uhakika wake ni kukashifu katika ubainisho wa Mwenyezi Mungu, na ubainisho wa Mtume wake na kudai kuwa maneno yao ndiyo yanayotokana nayo uongofu katika mlango huu. Na hawa hawana daili yoyote ya kimaandiko bali hata hawana dalili ya kiakili. Ama dalili ya kimaandiko, wao kwa hakika walikiri kwamba maandiko yaliyokuja ndani ya Kitabu na Sunna, maana yake ya dhahiri bali ya moja kwa moja inaashiria kwenye dhehebu la Ahlul-Sunnah wal Jama`ah. Na kwamba inahitaji ili ziashirie kwenye dhehebu lao batili zinapaswa kuondolewa katika maana zake za dhahiri na ziongezewe ndani yake na zinapunguzwe. Na hili, kama unavyoona, haliridhii yule ambaye ndani ya moyo wake kuna uzito wa chembe moja ya imani. Ama dalili ya kiakili, basi hakuna kitu katika akili kinachoashiria kukanusha sifa hizi. Bali akili inaashiria kuwa mtendaji ni mkamilifu zaidi kuliko asiyeweza kutenda. Na kwamba kitendo chake Mtukufu kinachohusiana na nafsi yake na kuhusiana na viumbe wake ndiyo ukamilifu. Wakidai kuwa kuzithibitisha kunaashiria kufanana na viumbe wake, basi wataambiwa: Kuongea juu ya sifa zake kunafuata kuongea juu ya dhati yake. Kwa hivyo, kama vile Mwenyezi Mungu ana dhati ambayo dhati nyinginezo hazifanani nayo, basi Mwenyezi Mungu ana sifa ambazo sifa nyinginezo hazifanani nazo. Sifa zake zinafuata dhati yake, na sifa za viumbe wake zinafuata dhati zao. Kwa hivyo, hakuna chochote katika kuzithibitisha ambacho kinalazimu mfanano kwa namna yoyote. Na vile vile inasemwa kwa mwenye kuthibitisha baadhi ya sifa na kukanusha baadhi, au alithibitisha majina na sio sifa: Ima uvithibitishe vyote kama Mwenyezi Mungu alivyovithibitisha, na Mtume wake alivyovithibitisha, au uvikanushe vyote. Hivyo, utakuwa unamkanusha Mola Mlezi wa walimwengu. Ama kuthibitisha kwako baadhi ya hayo na kukanusha kwako baadhi yake, huko ni kujipinga mwenye, na hutapata njia ya kutofautisha. Ukisema: Alichokithibitisha hakilazimu mfanano, basi Ahlul-Sunnah watakwambia: Na kuthibitisha mnayoyakataa hakulazimu mfanano. Ukisema: Mimi sielewi katika yale niliyoyakanusha isipokuwa mfanano, basi wanaokanusha watakuambia: Na sisi hatuelewi katika yale uliyothibitisha isipokuwa mfanano. Basi uliyowajibu kwayo wakanushaji, Ahlul-Sunnah watakujibu kwa hayo hayo kwa yale uliyoyakanusha. Jambo la msingi ni kwamba mwenye kukanusha kitu na akathibitisha kitu katika yale ambayo Kitabu na Sunnah viliashiria kuthibitishwa kwake. Basi huyo anajipinga mwenyewe, na wala hana dalili yoyote imara ya kisheria wala ya kiakili bali amehalifu yale ya kiakili na yale ya kimaandiko.
: 211 #
{سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُمْ مِنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ وَمَنْ يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ (211)}
(211) Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi? Na anayezibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.
#
{211} يقول تعالى: {سل بني إسرائيل كم آتيناهم من آية بينة}، تدل على الحق وعلى صدق الرسل فتيقنوها، وعرفوها، فلم يقوموا بشكر هذه النعمة التي تقتضي القيام بها، بل كفروا بها، وبدلوا نعمة الله كفراً؛ فلهذا استحقوا أن ينزل الله عليهم عقابه، ويحرمهم من ثوابه، وسمى الله تعالى كفر النعمة تبديلاً لها؛ لأن من أنعم الله عليه نعمة دينية أو دنيوية فلم يشكرها، ولم يقم بواجبها اضمحلت عنه، وذهبت وتبدلت بالكفر والمعاصي، فصار الكفر بدل النعمة، وأما من شكر الله تعالى، وقام بحقها فإنها تثبت، وتستمر، ويزيده الله منها.
(211) Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu “Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi?” Zinazoashiria haki, na ukweli wa Mitume, na wakawa na yakini nazo na kuzijua, lakini hawakuzishukuru neema hizi ambazo zinahitaji kuzitekeleza. Bali walizikufuru na wakabadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na kwa sababu ya hilo wakastahiki Mwenyezi Mungu kuwateremshia adhabu yake na kuwanyima malipo yake mazuri. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekuita kukufuru neema kuwa ni kuzibadalisha. Kwa sababu yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha neema ya kidini au ya kidunia, naye hakuishukuru, na wala hakutimiza wajibu wake, itampungukia na kwenda zake. Na ikabadilishwa na kufuru na maasia, basi kufuru ikawa badala ya neema. Na ama mwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na akatekeleza haki yake, basi hiyo (neema) itakaa imara na kuendelea, na Mwenyezi Mungu atamzidishia katika hiyo.
: 212 #
{زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَاللَّهُ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ (212)}
(212) Waliokufuru wamepambiwa maisha ya duniani; na wanawafanyia masihara wale walioamini. Na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa juu yao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
#
{212} يخبر تعالى أن الذين كفروا بالله وبآياته ورسله، ولم ينقادوا لشرعه أنهم زينت لهم الحياة الدنيا، فزينت في أعينهم وقلوبهم، فرضوا بها، واطمأنوا بها، فصارت أهواؤهم وإراداتهم وأعمالهم كلها لها، فأقبلوا عليها، وأكبوا على تحصيلها، وعظموها، وعظموا من شاركهم في صنيعهم، واحتقروا المؤمنين، واستهزؤوا بهم، وقالوا: أهؤلاء منَّ الله عليهم من بيننا، وهذا من ضعف عقولهم ونظرهم القاصر، فإن الدنيا دار ابتلاء وامتحان، وسيحصل الشقاء فيها لأهل الإيمان والكفران، بل المؤمن في الدنيا وإن ناله مكروه فإنه يصبر ويحتسب، فيخفف الله عنه بإيمانه وصبره ما لا يكون لغيره، وإنما الشأن كلُّ الشأن والتفضيل الحقيقي في الدار الباقية، فلهذا قال تعالى: {والذين اتقوا فوقهم يوم القيامة}؛ فيكون المتقون في أعلى الدرجات متمتعين بأنواع النعيم والسرور والبهجة والحبور، والكفار تحتهم في أسفل الدركات، معذبين بأنواع العذاب والإهانة والشقاء السرمدي الذي لا منتهى له، ففي هذه الآية تسلية للمؤمنين، ونعي على الكافرين، ولما كانت الأرزاق الدنيوية والأخروية لا تحصل إلا بتقدير الله، ولن تنال إلا بمشيئة الله قال تعالى: {والله يرزق من يشاء بغير حساب}؛ فالرزق الدنيوي يحصل للمؤمن والكافر، وأما رزق القلوب من العلم والإيمان ومحبة الله وخشيته ورجائه ونحو ذلك فلا يعطيها إلا من يحبه.
Mola Mtukufu anajulisha kwamba wale wanaomkufuru Mwenyezi Mungu, na ishara zake na Mitume wake. Na wala hawakuifuata sheria yake, kwamba wamepambiwa maisha ya duniani. Imepambwa kwao katika macho yao na nyoyo zao, na wakayaridhia, na wakatulia nayo, na matamanio yao, mapenzi yao, na matendo yao vikawa vyote kwa ajili yake. Kwa hivyo, wakavielekea, na wakazama katika kuutafuta, na wakautukuza, na wakamtukuza mwenye kushirikiana nao katika hicho kitendo chao. Na wakawadharau Waumini na wakawafanyia masihara, na wakasema: Je, hawa ndio Mwenyezi Mungu aliwafadhilisha miongoni mwetu? Na hili ni kwa sababu ya udhaifu wa akili zao, na uoni wao mfupi. Kwani dunia ni nyumba ya majaribio na mitihani, na zitawapata humo taabu watu wa imani na wa ukafiri. Lakini Muumini hapa duniani hata kama atapatwa na jambo la kuchukiza, yeye atavumilia na kutarajia malipo kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anampunguzia kwa imani yake na subira yake jambo ambalo haliwi kwa asiyekuwa yeye. Bali jambo zima na mapendeleo ya kweli ni katika nyumba yenye kudumu. Ndio maana Yeye Mtukufu akasema “Na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa juu yao Siku ya Kiyama.” Basi wachamungu watakuwa katika daraja za juu, wakifurahia kila aina ya neema na furaha, shangwe na nderemo. Na makafiri watakuwa chini yao katika daraja za chini kabisa, wakiadhibiwa kwa kila aina ya adhabu, na kudunishwa, na taabu ya milele isiyo na mwisho. Hivyo basi, katika Aya hii kuna kuwafariji Waumini, na maombolezo kwa makafiri. Na kwa kuwa riziki ya kidunia na ya kiakhera haziwezi kupatikana isipokuwa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu, na hazipatikani isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, yeye Mtukufu akesema: “Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” Kwa hivyo, riziki ya kidunia humjia Muumini na Kafiri. Na ama riziki ya nyoyo kama vile elimu, imani, kumpenda Mwenyezi Mungu, kumnyenyekea, kumtumaini na mfano wa hayo, yeye hampi hayo isipokuwa yule ampendaye.
: 213 #
{كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ وَأَنْزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ فَهَدَى اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ وَاللَّهُ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (213)}.
(213) Watu wote walikuwa umma mmoja. Kisha Mwenyezi Mungu akawatuma Manabii wenye kupeana habari njema na waonyaji. Na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki, ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyohitilafiana. Na wala hawakuhitilafiana ndani yake isipokuwa wale waliopewa Kitabu hicho baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina yao. Ndipo Mwenyezi Mungu kwa idhini yake akawaongoa walioamini kwendea haki katika yale waliyohitilafiana ndani yake. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka.
#
{213}؛ [أي: كانوا مجتمعين على الهدى، وذلك عشرة قرون بعد نوح عليه السلام، فلما اختلفوا في الدِّين، فكفر فريقٌ منهم، وبقي الفريقُ الآخرُ على الهدى، وحصل النزاع، بعث اللهُ الرُّسل؛ ليفصلوا بين الخلائق، ويقيموا الحجة عليهم، وقيل: بل كانوا]؛ أي: كان الناس مجتمعين على الكفر والضلال والشقاء ليس لهم نور ولا إيمان، فرحمهم الله تعالى بإرسال الرسل إليهم {مبشرين}؛ من أطاع الله بثمرات الطاعات من الرزق والقوة في البدن والقلب والحياة الطيبة، وأعلى ذلك الفوز برضوان الله والجنة {ومنذرين}؛ من عصى الله بثمرات المعصية من حرمان الرزق والضعف والإهانة والحياة الضيقة، وأشد ذلك سخط الله والنار، وأنزل الكتب عليهم بالحق؛ وهو الإخبارات الصادقة والأوامر العادلة. فكل ما اشتملت عليه الكتب فهو حق يفصل بين المختلفين في الأصول والفروع، وهذا هو الواجب عند الاختلاف والتنازع أن يرد الاختلاف إلى الله وإلى رسوله، ولولا أن في كتابه وسنة رسوله فصلَ النزاع لما أمر بالرد إليهما، ولما ذكر نعمته العظيمة بإنزال الكتب على أهل الكتاب، وكان هذا يقتضي اتفاقهم عليها واجتماعهم فأخبر تعالى أنهم بغى بعضهم على بعض، وحصل النزاع والخصام وكثرة الاختلاف، فاختلفوا في الكتاب الذي ينبغي أن يكونوا أولى الناس بالاجتماع عليه وذلك من بعد ما علموه وتيقنوه بالآيات البينات والأدلة القاطعات، وضلوا بذلك ضلالاً بعيداً، وهدى الله {الذين آمنوا}؛ من هذه الأمة {لما اختلفوا فيه من الحق}؛ فكل ما اختلف فيه أهل الكتاب، وأخطَؤوا فيه الحق والصواب، هدى الله للحق فيه هذه الأمة {بإذنه}؛ تعالى وتيسيره لهم ورحمته. {والله يهدي من يشاء إلى صراط مستقيم}؛ فعم الخلق تعالى بالدعوة إلى الصراط المستقيم عدلاً منه تعالى وإقامة حجة على الخلق؛ لئلا يقولوا ما جاءنا من بشير ولا نذير، وهدى ـ بفضله ورحمته وإعانته ولطفه ـ مَنْ شاء مِنْ عباده، فهذا فضله وإحسانه، وذاك عدله وحكمته تبارك وتعالى.
{213} (Watu walikuwa) inamaanisha [walikuwa kitu kimoja kwenye uwongofu, na hilo lilikuwa kwa karne kumi baada ya Nuhu, amani iwe juu yake. Basi walipohitilafiana katika Dini, kwa hivyo kundi moja katika wao likakufuru na lile kundi lingine likabaki katika Dini, na mabishano yakatokea. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawatuma Mitume ili wahukumu kati ya viumbe na wasimamishe hoja juu yao. Na ilisemwa bali walikuwa kitu kimoja kwenye ukafiri, upotovu, na ukaidi. Hawakuwa na nuru wala imani. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawarehemu kwa kuwatumia Mitume “wenye kupeana habari njema.” Kwa wale wanaomtii Mwenyezi Mungu kwa matunda ya utiifu kama vile riziki, nguvu katika mwili na moyo, maisha mema, na juu zaidi ya hayo, kupata radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo. “Na waonyaji” kwa wanaomuasi Mwenyezi Mungu kwa matunda ya maasia kama vile kunyimwa riziki, udhaifu, kudunishwa, maisha finyu, na mbaya zaidi ya hayo ni ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Moto. “Na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki” ambayo ni habari za kweli, na maamrisho ya uadilifu. Hivyo basi, kila ambacho kitabu kimejumuisha ni haki yenye kupambanua baina ya wanaohitilafiana katika misingi na matawi. Na hili ndilo jambo la wajibu panapokuwa na hitilafu na mvutano kwamba hitilafu hiyo irejeshwe kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake. Na lau kuwa si kwamba katika Kitabu chake na Sunnah za Mtume wake kuna upambanuzi wa mvutano, basi hangeamrisha kuvirejelea viwili hivyo. Na alipotaja neema yake kubwa kwa kuteremsha vitabu kwa Watu wa Kitabu, na hili likawa linalazimu kuafikiana kwao juu yake na kuwa kwao kitu kimoja. Kwa hivyo Mola Mtukufu akajulisha kwamba walihusudiana wao kwa wao, na mizozo na ugomvi vikatokea, na kuhitilafiana kwa wingi. Basi wakahitilafiana katika Kitabu ambacho wanapaswa wawe wa kwanza wa watu wote kuungana juu yake. Na hilo lilikuwa baada ya wao kukijua na kuwa na yakini na Aya zake zilizo wazi, na hoja zisizo na shaka, kwa hivyo wakapotea kwa hilo kupotea kwa mbali. “Ndipo Mwenyezi Mungu akawaongoa walioamini” katika Umma huu “katika yale waliyohitilafiana ndani yake ya haki.” Basi kila walichohitilafiana ndani yake watu wa Kitabu, na wakakosea humo haki na yaliyo sahihi. Mwenyezi Mungu akauongoza huu umma kuiendea haki “kwa idhini yake” yeye Mtukufu, na kuwarahisishia kwake na rehema zake. “Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka.” Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawalingania viumbe wote kwenye njia iliyonyooka kwa sababu ya uadilifu wake, na kusimamisha hoja juu ya viumbe, wasije wakasema: “Hatukujiwa na mpeanaji wa habari njema yeyote wala waonyaji”. Na akaongoa - kwa fadhila zake, rehema zake, usaidizi wake, na upole wake - amtakaye katika waja wake. Na hii ndiyo fadhila yake na wema wake, na huo ndio uadilifu wake na hekima yake Mwenye baraka, Mtukufu.
: 214 #
{أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُمْ مَثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلِكُمْ مَسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيبٌ (214)}
(214) Ama mnadhani kuwa mtaingia Peponi, ilhali bado hamjajiwa na mfano wa (yaliyowajia) wale waliopita kabla yenu? Uliwapata ufukara (shida) na maradhi, na wakatikiswa mpaka Mtume na walioamini pamoja naye wakasema. “Ni lini nusura ya Mwenyezi Mungu (itakuja)?” Jueni kuwa hakika nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.
#
{214} يخبر تبارك وتعالى أنه لا بد أن يمتحن عباده بالسراء والضراء والمشقة كما فعل بمن قبلهم، فهي سنته الجارية التي لا تتغير ولا تتبدل، أن من قام بدينه وشرعه لا بد أن يبتليه، فإن صبر على أمر الله، ولم يبال بالمكاره الواقفة في سبيله، فهو الصادق الذي قد نال من السعادة كمالها ومن السيادة آلتها، ومن جعل فتنة الناس كعذاب الله، بأن صدته المكاره عما هو بصدده، وثنته المحن عن مقصده، فهو الكاذب في دعوى الإيمان، فإنه ليس الإيمان بالتحلي والتمني ومجرد الدعاوي؛ حتى تصدقه الأعمال أو تكذبه، فقد جرى على الأمم الأقدمين ما ذكر الله عنهم {مستهم البأساء والضراء}؛ أي: الفقر والأمراض في أبدانهم {وزلزلوا}؛ بأنواع المخاوف من التهديد بالقتل والنفي، وأخذ الأموال، وقتل الأحبة، وأنواع المضار، حتى وصلت بهم الحال، وآل بهم الزلزال إلى أن استبطؤوا نصر الله مع يقينهم به، ولكن لشدة الأمر وضيقه قال {الرسول والذين آمنوا معه متى نصر الله}؛ فلما كان الفرج عند الشدة، وكلما ضاق الأمر اتسع قال تعالى: {ألا إن نصر الله قريب}؛ فهكذا كل من قام بالحق فإنه يمتحن، فكلما اشتدت عليه وصعبت إذا صابر وثابر على ما هو عليه؛ انقلبت المحنة في حقه منحة، والمشقات راحات، وأعقبه ذلك الانتصار على الأعداء وشفاء ما في قلبه من الداء. وهذه الآية نظير قوله تعالى: {أم حسبتم أن تدخلوا الجنة ولما يعلم الله الذين جاهدوا منكم ويعلم الصابرين}؛ وقوله تعالى: {ألم. أحسب الناس أن يتركوا أن يقولوا آمنا وهم لا يفتنون، ولقد فتنا الذين من قبلهم فليعلمن الله الذين صدقوا وليعلمن الكاذبين}؛ فعند الامتحان يكرم المرء أو يهان.
Yeye Mwenye baraka na Mtukufu anajulisha kwamba ni lazima awajaribu waja wake kwa yenye wasaa na yenye dhiki na taabu, kama alivyowafanyia wale waliokuwa kabla yao. Kwani hii ndiyo ada yake inayoendelea ambayo haigeuki wala haibadiliki, kwamba mwenye kusimamisha dini yake na sheria yake lazima ajaribiwe. Akisubiri juu ya amri ya Mwenyezi Mungu na hayajali machukizo yanayotokea katika njia yake, basi yeye ndiye mkweli ambaye amepata katika furaha ukamilifu wake, na katika ukuu chombo chake. Na mwenye kufanya mateso ya watu kuwa kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba machukizo yakamzuia yale anayokaribia kuyafanya. Na majaribio yakamzuia lengo lake, basi yeye ndiye mwongo katika madai ya kuwa na imani. Kwani, imani sio kwa kujipamba na kutamani tu, na madai matupu, mpaka matendo yaisadikishe au yaikadhibishe. Na yaliwatokea mataifa ya kale yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu juu yao. “Uliwapata ufukara (shida) na maradhi” katika miili yao “na wakatikiswa” kwa aina mbalimbali za hofu kama vile vitisho vya kuuawa, kuhamishwa, kuchukuliwa mali, kuuawa kwa vipenzi, na aina mbalimbali za madhara mpaka hali ikawafikisha. Na mitetemeko ikawafikisha kuona kwamba nusura ya Mwenyezi Mungu imechelewa pamoja na kuwa na yakini nayo. Lakini kwa sababu ya ukali na jambo hilo, na dhiki yake, alisema: Mtume na walioamini pamoja naye wakasema: “Ni lini nusura ya Mwenyezi Mungu (itakuja?) Na kwa kuwa faraja huja wakati wa ugumu, na kila jambo linapokuwa finyu, linakunjuka, Mwenyezi Mungu akasema: “Jueni kuwa hakika nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” Na namna hiyo, kila mwenye kuisimamia haki, yeye kwa hakika atajaribiwa. Na kila inapokuwa hali ni kali na ngumu kwake, ikiwa atadumu na akavumilia katika yale aliyomo ndani yake, basi majaribio yanageuka katika haki yake na yanakuwa neema. Na dhiki zinakuwa raha mbalimbali, na hayo yakamfuatisha ushindi juu ya maadui na uponyaji wa maradhi yaliyomo ndani ya moyo wake. Na Aya hii ni sawa na kauli yake Mola Mtukufu. “Je, mnadhani kwamba mtaingia Peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawapambanua wale miongoni mwenu waliopigana Jihadi, na hajawapambanua waliosubiri?” Na kauli yake Mtukufu: “Je, wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.” Na wakati wa mtihani, mtu hupewa heshima au hudunishwa.
: 215 #
{يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنْفِقُونَ قُلْ مَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ (215)}
(215) Wanakuuliza watoe nini? Sema: Chochote mnachotoa katika heri ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na msafiri. Na chochote mnachofanya katika heri, basi Mwenyezi Mungu kwa hakika anaijua.
#
{215} أي: يسألونك عن النفقة وهذا يعم السؤال عن المنفَق والمنفَق عليه، فأجابهم عنها فقال: {قل ما أنفقتم من خير}؛ أي: مال قليل أو كثير فأولى الناس به وأحقهم بالتقديم أعظمهم حقًّا عليك، وهم الوالدان الواجب برهما والمحرم عقوقهما، ومن أعظم برهما، النفقة عليهما، ومن أعظم العقوق ترك الإنفاق عليهما، ولهذا كانت النفقة عليهما واجبة على الولد الموسر، ومن بعد الوالدين الأقربون على اختلاف طبقاتهم، الأقرب، فالأقرب، على حسب القرب والحاجة، فالإنفاق عليهم صدقة وصلة {واليتامى}؛ وهم الصغار الذين لا كاسب لهم فهم في مظنة الحاجة، لعدم قيامهم بمصالح أنفسهم وفقد الكاسب، فوصى الله بهم العباد رحمة منه بهم ولطفاً {والمساكين}؛ وهم أهل الحاجات وأرباب الضرورات الذين أسكنتهم الحاجة، فينفَق عليهم لدفع حاجاتهم وإغنائهم {وابن السبيل}؛ أي: الغريب المنقطع به في غير بلده، فيعان على سفره بالنفقة التي توصله إلى مقصده. ولما خصص الله تعالى هؤلاء الأصناف لشدة الحاجة، عمم تعالى فقال: {وما تفعلوا من خير}؛ من صدقة على هؤلاء وغيرهم بل ومن جميع أنواع الطاعات والقربات لأنها تدخل في اسم الخير {فإن الله به عليم}؛ فيجازيكم عليه، ويحفظه لكم كلٌّ على حسب نيته وإخلاصه، وكثرة نفقته وقلتها، وشدة الحاجة إليها، وعظم وقعها ونفعها.
{215} Yani wanakuuliza juu ya kutoa matumizi. Na hili linajumuisha kuuliza kuhusu mtoaji na anayepewa. Basi akawajibu hayo, akasema. “Sema: Chochote mnachotoa katika heri,” yani mali kidogo au nyingi, basi watu wanaoistahili zaidi, na wanaostahiki zaidi kutangulizwa, ni wale wenye haki kubwa zaidi juu yako. Nao ni wazazi wawili ambao ni wajibu kuwafanyia wema, ambao ni haramu kuwa na utovu na nidhamu kwao na kuacha kuwapa matumizi. Ndiyo maana kuwapa matumizi ni wajibu juu ya mtoto mwenye wasaa. Kisha baada ya wazazi ni jamaa wa karibu zaidi kulingana na tabaka zao tofauti, wa karibu zaidi, kisha wa karibu kulingana ukaribu wao na mahitaji. Kwa hivyo, kuwapa matumizi ni sadaka na kuunga ukoo “na mayatima”. Nao ni watoto wadogo ambao hawana wa kuwachumia. Basi, wao kwa kawaida huwa wahitaji kwa sababu ya kutoweza kujisimamia masilahi ya nafsi zao, na kumpoteza anayewachumia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawausia waja wake juu yao, kwa rehema yake na huruma yake juu yao. “Na masikini”. Nao ni watu wenye mahitaji ya lazima, na wenye mahitaji ya lazima ambao mahitaji yaliwanyamazisha. Basi wanapewa ili kuwatimizia mahitaji yao na kuwatosheleza. “Na msafiri” yani mgeni aliyekatikiwa katika nchi isiyokuwa yake. Basi atasaidiwa juu ya safari yake kwa matumizi ambayo yatamfikisha kwenye pahali anapokwenda. Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowachagua watu wa haya makundi kwa sababu ya ugumu wa mahitaji yao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajumlisha, akasema: “Na chochote mnachofanya katika heri” kama vile sadaka mnayowapa hawa na wengineo, bali katika kila aina ya utiifu na ibada, kwa sababu zinaingia katika jina ‘heri.’ “Basi Mwenyezi Mungu kwa hakika anaijua.” Atawalipa juu yake, na atawahifadhia hayo, kila mmoja kulingana na nia yake na ikhlasi yake, na wingi wa kutoa kwake na uchache wake, na ukali wa haja yake juu yake, na ukubwa wa athari yake na manufaa yake.
: 216 #
{كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَكُمْ وَعَسَى أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ وَعَسَى أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ (216)}
(216) Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinawachukiza. Lakini huenda mkachukia kitu, nacho ni heri kwenu. Na huenda mkapenda kitu, nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.
#
{216} هذه الآية فيها فرض القتال في سبيل الله بعد ما كان المؤمنون مأمورين بتركه لضعفهم وعدم احتمالهم لذلك، فلما هاجر النبي - صلى الله عليه وسلم - إلى المدينة، وكثر المسلمون، وقووا؛ أمرهم الله تعالى بالقتال، وأخبر أنه مكروه للنفوس، لما فيه من التعب والمشقة وحصول أنواع المخاوف والتعرض للمتالف، ومع هذا فهو خير محض لما فيه من الثواب العظيم والتحرز من العقاب الأليم والنصر على الأعداء والظفر بالغنائم، وغير ذلك مما هو مُربٍ على ما فيه من الكراهة {وعسى أن تحبوا شيئاً وهو شر لكم}؛ وذلك مثل القعود عن الجهاد لطلب الراحة فإنه شرٌّ؛ لأنه يعقب الخذلان، وتسلط الأعداء على الإسلام وأهله، وحصول الذلِّ والهوان، وفوات الأجر العظيم، وحصول العقاب. وهذه الآيات عامة مطردة في أن أفعال الخير التي تكرهها النفوس لما فيها من المشقة أنها خير بلا شك، وأن أفعال الشر التي تحبها النفوس لما تتوهمه فيها من الراحة واللذة فهي شرٌّ بلا شك، وأما أحوال الدنيا فليس الأمر مطرداً، ولكن الغالب على العبد المؤمن أنه إذا أحب أمراً من الأمور فقيض الله له من الأسباب ما يصرفه عنه أنه خير له، فالأوفق له في ذلك أن يشكر الله، ويعتقد الخير في الواقع، لأنه يعلم أن الله تعالى أرحم بالعبد من نفسه، وأقدر على مصلحة عبده منه، وأعلم بمصلحته منه كما قال تعالى: {والله يعلم وأنتم لا تعلمون}؛ فاللائق بكم أن تتمشوا مع أقداره سواء سرتكم أو ساءتكم.
{216} Aya hii ina kuwajibishwa kwa kupigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu baada ya kwamba Waumini walikuwa wameamrishwa kuviacha, kwa sababu ya udhaifu wao na kutoweza kwao kustahimili hilo. Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alipohamia Madina, na Waislamu wakawa wengi, wakapata nguvu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaamrisha kupigana vita. Na akajulisha kwamba hilo linachukiza nafsi. Kwa sababu ya uchovu na dhiki vilivyomo ndani yake na kutokea kwa aina mbalimbali za hofu na kujiweka mbele ya mambo yenye kuharibu. Pamoja na hayo, ni nzuri tupu, kwa sababu ya yale yaliyomo ndani yake kama vile thawabu kubwa, kujiepusha na adhabu chungu, kuwashinda maadui, kupata ngawira. Na mengineyo ambayo yanapendwa, pamoja na yaliyomo ndani yake yenye kuchukiza. “Na huenda mkapenda kitu, nacho ni shari kwenu.” Na hilo mfano kutoenda katika vita kwa sababu ya kutafuta starehe. Hilo ni shari (uovu), kwa sababu linasababisha kuachwa na Mwenyezi Mungu. Na kuwapa nguvu maadui juu ya Uislamu na watu wake, kutokea kwa udhalilifu na unyonge, na kupotea kwa malipo makubwa, na kupata adhabu. Aya hizi ni za jumla na zenye kuingia katika kila kitu kwamba matendo mema ambayo nafsi zinazichukia kwa sababu ya ugumu uliomo ndani yake ni heri bila shaka, na kwamba matendo maovu ambayo nafsi zinapenda kwa sababu ya starehe na ladha ambazo zinafikiria kwamba ziko ndani yake, basi hayo ni shari (maovu) bila shaka. Ama hali za dunia, basi hili jambo haliingii katika kila kitu kwa ujumla. Lakini ni aghalabu kwa mja Muumini kuwa akipenda kitu miongoni mwa vitu, kisha Mwenyezi Mungu atamwekea sababu zinazomtolea kitu hicho. Basi hilo ni kheri kwake, na lililo bora kwake katika hayo ni kwamba amshukuru Mwenyezi Mungu, na aweke heri katika hilo lililotokea. Kwa sababu, anajua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye rehema zaidi juu ya waja wake kuliko yeye mwenyewe. Na mwenye uwezo zaidi juu ya masilahi ya mja wake kuliko yeye mwenyewe, na mwenye elimu zaidi juu ya masilahi yake kuliko yeye mwenyewe, kama alivyosema [Mwenyezi Mungu Mtukufu]. “Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.” Basi linalofaa zaidi kwenu kwenda pamoja na majaaliwa yake, sawa yatawapendeza au yawawiye mabaya.
Na kwa vile amri ya kupigana vita lau kuwa haikuwekwa katika wakati maalumu, basi ingejumuisha miezi mitukufu na mingineyo, Mwenyezi Mungu akaondoa kupigana vita katika miezi mitukufu, akasema:
: 217 #
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ وَصَدٌّ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِنْدَ اللَّهِ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَنْ دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا وَمَنْ يَرْتَدِدْ مِنْكُمْ عَنْ دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (217)}.
(217) Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita ndani yake ni dhambi kubwa. Lakini kuzuia watu wasiende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkufuru Yeye, na kuzuilia watu wasiende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni jambo kubwa zaidi kuliko kuua. Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wawatoe katika Dini yenu kama wakiweza. Na yeyote katika nyinyi atakayeacha Dini yake, na akafa hali ya kuwa ni kafiri, basi hao ndio ambao matendo yao yameharibika katika dunia na Akhera. Na hao ndio wenza wa Moto. Wao humo watadumu.
#
{217} الجمهور على أن تحريم القتال في الأشهر الحرم منسوخ بالأمر بقتال المشركين حيثما وجدوا. وقال بعض المفسرين: إنه لم ينسخ لأن المطلق محمول على المقيد، وهذه الآية مقيدة لعموم الأمر بالقتال مطلقاً، ولأن من جملة مزية الأشهر الحرم بل أكبر مزاياها تحريم القتال فيها، وهذا إنما هو في قتال الابتداء وأما قتال الدفع فإنه يجوز في الأشهر الحرم كما يجوز في البلد الحرام. ولما كانت هذه الآية نازلة بسبب ما حصل لسرية عبد الله بن جحش وقتلهم عمرو بن الحضرمي وأخذهم أموالهم ـ وكان ذلك على ما قيل في شهر رجب ـ عيرهم المشركون بالقتال بالأشهر الحرم وكانوا في تعييرهم ظالمين إذ فيهم من القبائح ما بعضه أعظم مما عيروا به المسلمين، قال تعالى في بيان ما فيهم: {وصد عن سبيل الله}؛ أي: صد المشركين من يريد الإيمان بالله وبرسوله وفتنتهم من آمن به وسعيهم في ردهم عن دينهم وكفرهم الحاصل في الشهر الحرام والبلد الحرام الذي هو بمجرده كاف في الشرِّ، فكيف وقد كان في شهر حرام وبلد حرام {وإخراج أهله}؛ أي: أهل المسجد الحرام وهم النبي - صلى الله عليه وسلم -، وأصحابه لأنهم أحق به من المشركين وهم عُمَّاره على الحقيقة فأخرجوهم {منه}؛ ولم يمكنوهم من الوصول إليه مع أن هذا البيت سواء العاكف فيه والباد، فهذه الأمور كل واحد منها {أكبر من القتل}؛ في الشهر الحرام فكيف وقد اجتمعت فيهم فعلم أنهم فسقة ظلمة في تعييرهم المؤمنين. ثم أخبر تعالى أنهم لن يزالوا يقاتلون المؤمنين، وليس غرضهم في أموالهم وقتلهم وإنما غرضهم أن يرجعوهم عن دينهم ويكونوا كفاراً بعد إيمانهم حتى يكونوا من أصحاب السعير، فهم باذلون قدرتهم في ذلك ساعون بما أمكنهم ويأبى الله إلا أن يتم نوره ولو كره الكافرون. وهذا الوصف عامٌّ لكل الكفار لا يزالون يقاتلون غيرهم حتى يردوهم عن دينهم، وخصوصاً أهل الكتاب من اليهود والنصارى الذين بذلوا الجمعيات، ونشروا الدعاة، وبثوا الأطباء، وبنوا المدارس لجذب الأمم إلى دينهم، وتدخيلهم عليهم كل ما يمكنهم من الشبه التي تشككهم في دينهم، ولكن المرجو من الله تعالى الذي منَّ على المؤمنين بالإسلام، واختار لهم دينه القيم، وأكمل لهم دينه أن يتم عليهم نعمته بالقيام به أتم قيام، وأن يخذل كل من أراد أن يطفئ نوره، ويجعل كيدهم في نحورهم، وينصر دينه، ويعلي كلمته وتكون هذه الآية صادقة على هؤلاء الموجودين من الكفار كما صدقت على من قبلهم {إن الذين كفروا ينفقون أموالهم ليصدوا عن سبيل الله، فسينفقونها ثم تكون عليهم حسرة ثم يغلبون، والذين كفروا إلى جهنم يحشرون}؛ ثم أخبر تعالى أن من ارتد عن الإسلام بأن اختار عليه الكفر واستمر على ذلك حتى مات كافراً {فأولئك حبطت أعمالهم في الدنيا والآخرة}؛ لعدم وجود شرطها وهو الإسلام {وأولئك أصحاب النار هم فيها خالدون}. ودلت الآية بمفهومها أن من ارتد ثم عاد إلى الإسلام أنه يرجع إليه عمله [الذي قبل ردته]، وكذلك من تاب من المعاصي فإنها تعود إليه أعماله المتقدمة.
(217) Wengi wa wanachuoni wanaona kuwa uharamu wa kupigana vita katika miezi mitukufu ulibatilishwa kwa amri ya kupigana vita na washirikina popote wanapopatwa. Na baadhi ya wafasiri walisema: Haikubatilishwa. Kwa sababu Al-Mutlaq (andiko ambalo halikufungiwa) linapaswa kueleweka kwa mujibu wa Al-Muqayyad (andiko lililofungiwa). Na Aya hii inafunga ujumla wa amri ya kupigana bila mipaka. Na kwa sababu miongoni mwa sifa maalumu za miezi mitukufu, bali sifa kubwa mno yake ni kuharamisha kupigana vita ndani yake. Na hilo linakuwa tu katika kuanzisha kupigana vita. Ama kupigana vita kwa sababu ya kujikinga, huko kunaruhusika katika miezi mitukufu, kama vile kunavyoruhusika katika nchi tukufu. Na kwa kuwa Aya hii iliteremka kwa sababu ya yale yaliyotokea kwa kikosi cha kijeshi cha ‘Abdullah bin Jahsh, na kumuua kwao ‘Amr bin Al-Hadhrami, na kuchukua kwao mali zao, na hilo lilikuwa - kulingana na ilivyosemwa - katika mwezi wa Rajab. Washirikina wakawakosoa kwa kupigana vita katika miezi mitukufu. Nao walidhulumu katika kuwakosoa kwao. Kwani, walikuwa na baadhi ya mabaya ambayo baadhi yake yalikuwa makubwa zaidi kuliko yale waliyowakosoa kwayo Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kueleza yaliyomo ndani yao, "na kuzuia kuiendea Njia ya Mwenyezi Mungu." Yani washirikina kumzuia anayetaka kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kumtesa aliyemwamini, na juhudi zao za kuwageuza waiache dini yao. Na ukafiri wao unaotokea katika mwezi mtukufu na nchi takatifu ambao wenyewe tu unatosha kuwa shari kubwa mno. Basi itakuwaje na yalikuwa hayo katika mwezi mtakatifu na nchi takatifu? “Na kuwatoa watu wake.” Yani watu wa Msikiti Mtakatifu, ambao ni Nabii rehema na amani za, swala na salamu za Mwenyezi Mungu Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na maswahaba wake. Kwa sababu wao ndio wanaoustahiki zaidi kuliko washirikina. Nao ndio wanauimarisha kwa uhakika, basi wakatoa “humo” Na hawakuwawezesha kuufikia, pamoja na kwamba nyumba hii ni sawasawa kwa anayekaa ndani yake na wageni. Na mambo haya kila moja kati yake ni “jambo kubwa zaidi kuliko kuua,” katika mwezi mtukufu. Basi vipi na ilhali yote yamekujumuika ndani yao? Kwa hivyo, ikajulikana kwamba wao ni wapitao mipaka, madhalimu katika kuwakemea kwao Waumini. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa kamwe hawataacha kupigana vita na Waumini, na lengo lao si katika mali yao na kuwaua, bali lengo lao ni kuwarudisha kutoka katika Dini yao, na wawe makafiri baada ya Imani yao ili wawe miongoni mwa wenza Moto mkali. Kwa hivyo, wanatoa uwezo wao katika hilo, kwa kujitahidi namna wawezavyo. “Lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kutimiza nuru yake, hata kama makafiri watachukia.” Na sifa hii ni ya jumla kwa makafiri wote. Wao hawaachi kuwapiga vita wasiokuwa wao mpaka wawarudishe kutoka katika dini yao. Hususan Watu wa Kitabu kama vile Mayahudi na Wakristo, ambao walifanya juhudi za kuanzisha taasisi mbalimbali, na wakaeneza walinganizi, na wakaeneza madaktari, na wakajenga shule, ili kuwavutia mataifa kwenye dini yao. Na kuingiza ndani yao kila wawezalo katika fikira potofu ambazo zinawafanya kuwa na shaka juu ya dini yao. Lakini linalotarajiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaneemesha Waumini kwa Uislamu, na akawachagulia Dini yake iliyonyooka sawa. Na akawakamilishia Dini yake ni kwamba atawatimizia neema yake waweze kuisimamia kusimama kukamilifu. Na kwamba asimsaidie kila anayetaka kuizima nuru yake, na atie vitimbi vyao kwenye shingo zao, na ainurusu Dini yake; na aliinue juu neno lake. Na Aya hii inakuwa kweli kwa hawa walio miongoni mwa makafiri, kama ilivyokuwa ya kweli juu ya wale waliokuwa kabla yao. “Hakika, wale waliokufuru hutoa mali zao ili kuzuia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto juu yao, na kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” Kisha Mola Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuacha Uislamu kwa kuuchagua ukafiri badala yake. Na akaendelea na hilo mpaka akafa hali ya kuwa ni kafiri; “basi hao ndio ambao matendo yao yameharibika katika dunia na Akhera.” Kwa sababu kukosekana kwa sharti lake, ambalo ni Uislamu. “Na hao ndio wenza wa Moto. Wao humo watadumu”. Na Aya hii iliashiria kwa maana yake isiyo ya moja kwa moja kuwa, mwenye kuritadi kisha akarejea katika Uislamu, yanamrudia matendo yake yaliyokuwa kabla ya kuritadi kwake. Na vile vile mwenye kutubu akaacha dhambi, basi yeye pia matendo yake yaliyotangulia yatarudia.
: 218 #
{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّهِ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (218)}
(218) Hakika, wale walioamini, na wale waliohama na wakafanya juhudi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanaotarajia rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
#
{218} هذه الأعمال الثلاثة هي عنوان السعادة وقطب رَحَى العبودية، وبها يعرف ما مع الإنسان من الربح والخسران، فأما الإيمان فلا تسأل عن فضيلته وكيف تسأل عن شيء هو الفاصل بين أهل السعادة وأهل الشقاوة، وأهل الجنة من أهل النار، وهو الذي إذا كان مع العبد قبلت أعمال الخير منه، وإذا عدم منه لم يقبل له صرف ولا عدل ولا فرض ولا نفل، وأما الهجرة فهي مفارقة المحبوب المألوف لرضا الله تعالى فيترك المهاجر وطنه وأمواله وأهله وخلانه تقرباً إلى الله ونصرة لدينه، وأما الجهاد فهو بذل الجهد في مقارعة الأعداء، والسعي التام في نصرة دين الله وقمع دين الشيطان، وهو ذروة الأعمال الصالحة وجزاؤه أفضل الجزاء، وهو السبب الأكبر لتوسيع دائرة الإسلام، وخذلان عباد الأصنام وأمن المسلمين على أنفسهم وأموالهم وأولادهم، فمن قام بهذه الأعمال الثلاثة على لأوائها ومشقتها، كان لغيرها أشد قياماً به وتكميلاً، فحقيق بهؤلاء أن يكونوا هم الراجون رحمة الله لأنهم أتوا بالسبب الموجب للرحمة، وفي هذا دليل على أن الرجاء لا يكون إلا بعد القيام بأسباب السعادة، وأما الرجاء المقارن للكسل وعدم القيام بالأسباب فهذا عجز وتمنٍّ وغرور، وهو دالٌّ على ضعف همة صاحبه، ونقص عقله، بمنزلة من يرجو وجود الولد بلا نكاح، ووجود الغلة بلا بذر وسقي ونحو ذلك. وفي قوله: {أولئك يرجون رحمة الله}؛ إشارة إلى أن العبد ولو أتى من الأعمال بما أتى به لا ينبغي له أن يعتمد عليها ويعول عليها، بل يرجو رحمة ربه ويرجو قبول أعماله ومغفرة ذنوبه وستر عيوبه، ولهذا قال: {والله غفور}؛ أي: لمن تاب توبة نصوحاً، {رحيم}؛ وسعت رحمته كلَّ شيء وعمَّ جُودُه وإحسانُه كلَّ حيٍّ، وفي هذا دليل على أن من قام بهذه الأعمال المذكورة حصل له مغفرة الله، إذ الحسنات يذهبن السيئات، وحصلت له رحمة الله، وإذا حصلت له المغفرة اندفعت عنه عقوبات الدنيا والآخرة التي هي آثار الذنوب التي قد غفرت، واضمحلت آثارها، وإذا حصلت له الرحمة حصل على كل خير في الدنيا والآخرة، بل أعمالهم المذكورة من رحمة الله بهم، فلولا توفيقه إياهم لم يريدوها، ولولا إقدارهم عليها، لم يقدروا عليها ولولا إحسانه لم يتمها ويقبلها منهم، فله الفضل أولاً وآخراً وهو الذي مَنَّ بالسبب والمسبب، ثم قال تعالى:
{218} Matendo haya matatu ndiyo kichwa cha furaha na nguzo ya uja, na kwalo yanajulikana yale ambayo mtu anayo ya faida na hasara. Ama imani, basi usiulize juu ya fadhila zake. Na vipi utauliza kuhusu kitu ambacho ndicho kitenganishi cha watu wa furaha na watu wa taabuni, na watu wa Peponi na watu wa Motoni? Nayo ndiyo ambayo ikiwa pamoja na mja, matendo mema hukubaliwa kutoka kwake. Na isipokuwa naye, haitakubaliwa kwake kikomboleo wala toba, wala faradhi wala sunna. Na ama kuhama, huku ni kujitenga yale yanayopendwa na mtu na yaliyozoeleka, kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, mwenye kuhama anaiacha nchi yake, mali zake, familia yake na marafiki zake, ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kunusuru dini yake. Na ama jihadi, hii ni kufanya juhudi katika kupigana vita na maadui, na kujitahidi kikamilifu kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, na kukomesha dini ya Shetani. Kwa hivyo, atakayetelekeza matendo haya matatu licha ya dhiki zake na ugumu wake, basi atakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzifanya matendo mengineyo kwa ukamilifu. Basi, hawa wanafaa zaidi kwamba wao ndio wanaotarajia rehema ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, walileta sababu inayoleta rehema. Na katika hili kuna ushahidi kwamba matarajio hayawezi kuwepo isipokuwa baada ya kutimiza sababu za furaha. Na ama matarajio yanayofungamana na uvivu, na kutofanya sababu, hilo ni kutoweza, kutamani tu na kudanganyika. Na hilo linaashiria udhaifu wa hima ya mwenyewe, na upungufu wa akili yake, kama mtu anayetarajia kupata mtoto bila ya kuoa; na kupatikana kwa mavuno bila ya mbegu wala kumwagilia maji, na mfano wa hayo. Na katika kauli yake, “hao ndio wanaotarajia rehema za Mwenyezi Mungu;” kuna ishara ya kwamba mja hata akitenda atendayo katika matendo, hafai kuyategemea, na kutaka msaada wake. Bali anafaa kutarajia rehema za Mola wake Mlezi, na anatarajia kukubaliwa kwa matendo yake, na kusamehewa dhambi zake, na kufunikiwa kasoro zake. Ndiyo maana akasema: “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe.” Yani kwa anayetubia toba ya kweli, “Mwenye kurehemu” ambaye rehema zake zimeenea kila kitu, na ukarimu wake na hisani yake vimejumuisha kila kilicho hai. Na katika hili, kuna ushahidi kwamba yeyote anayefanya haya matendo yaliyotajwa, atapata msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa maana, mema huondoa maovu, na anapata rehema za Mwenyezi Mungu. Na ikipata msamaha, basi zinamwondokea adhabu za duniani na Akhera, ambazo ni athari za dhambi ambazo zimeshasamehewa na athari zake zikaondoka. Na akipata rehema, atapata kila heri duniani na Akhera. Bali matendo yao yaliyotajwa ni kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na lau kuwa sio kuwafanikisha kwake, wasingeyataka. Na lau kuwa si kuwapa kwake uwezo juu ya yake, basi wasingeweza kuyafanya. Na lau kuwa si hisani yake, basi wasingeyakamilisha na akayakubali kutoka kwao. Basi, fadhila zote ni zake mwanzoni na mwishoni. Naye ndiye aliyeweka bure sababu na matokeo yake. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 219 #
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِنْ نَفْعِهِمَا}
(219) Wanakuuliza juu ya mvinyo na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake ili mpate kutafakari.
#
{219} أي: يسألك يا أيها الرسولُ، المؤمنون عن أحكام الخمر والميسر، وقد كانا مستعمليْنِ في الجاهلية وأول الإسلام، فكأنه وقع فيهما إشكال، فلهذا سألوا عن حكمهما، فأمر الله تعالى نبيَّه أن يبين لهم منافعهما ومضارهما ليكون ذلك مقدمة لتحريمهما وتحتيم تركهما، فأخبر أن إثمهما ومضارهما وما يصدر عنهما من ذهاب العقل والمال والصد عن ذكر الله وعن الصلاة والعداوة والبغضاء أكبر مما يظنونه من نفعهما من كسب المال بالتجارة بالخمر وتحصيله بالقمار والطرب للنفوس عند تعاطيهما، وكان هذا البيان زاجراً للنفوس عنهما لأن العاقل يرجح ما ترجحت مصلحته، ويجتنب ما ترجحت مضرته، ولكن لما كانوا قد ألفوهما، وصعب التحتيم بتركهما أول وهلة؛ قدم هذه الآية مقدمة للتحريم الذي ذكره في قوله: {يا أيها الذين آمنوا إنما الخمر والميسر والأنصاب والأزلام رجس من عمل الشيطان} إلى قوله: {منتهون}، وهذا من لطفه ورحمته وحكمته، ولهذا لما نزلت قال عمر رضي الله عنه: انتهينا انتهينا. فأما الخمر فهو كل مسكر خامر العقل وغطاه من أي نوع كان، وأما الميسر فهو كل المغالبات التي يكون فيها عوض من الطرفين من النرد والشطرنج وكل مغالبة قولية أو فعلية بعوض، سوى مسابقة الخيل والإبل والسهام؛ فإنها مباحة لكونها معينة على الجهاد؛ [فلهذا] رخص فيها الشارع. {وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنْفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ (219) فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ} وهذا سؤال عن مقدار ما ينفقونه من أموالهم، فيسر الله لهم الأمر وأمرهم أن ينفقوا العفو، وهو المتيسر من أموالهم الذي لا تتعلق به حاجتهم وضرورتهم، وهذا يرجع إلى كل أحد بحسبه من غني وفقير ومتوسط، كل له قدرة على إنفاق ما عفا من ماله ولو شق تمرة، ولهذا أمر الله رسوله - صلى الله عليه وسلم -، أن يأخذ العفو من أخلاق الناس وصدقاتهم، ولا يكلفهم ما يشق عليهم؛ ذلك بأن الله تعالى لم يأمرنا بما أمرنا به حاجة منه لنا أو تكليفاً لنا بما يشق، بل أمرنا بما فيه سعادتنا وما يسهل علينا وما به النفع لنا ولإخواننا فيستحق على ذلك أتم الحمد. ولما بين تعالى هذا البيان الشافي وأطلع العباد على أسرار شرعه قال: {كذلك يبين الله لكم الآيات}؛ أي: الدالات على الحق المحصلات للعلم النافع والفرقان، {لعلكم تتفكرون في الدنيا والآخرة}؛ أي: لكي تستعملوا أفكاركم في أسرار شرعه، وتعرفوا أن أوامره فيها مصالح الدنيا والآخرة، وأيضاً لكي تتفكروا في الدنيا وسرعة انقضائها فترفضوها، وفي الآخرة وبقائها، وأنها دار الجزاء فتعمروها.
{219} Yani wanakuuliza – ewe mtume - Waumini juu ya hukumu za mvinyo na kamari. Na vilikuwa vikitumika katika zama za kabla ya Uislamu na mwanzoni mwa Uislamu. Na ni kana kwamba kulitokea tatizo katika mawili hayo, ndio maana wakauliza juu ya hukumu yake. Kwa hivyo, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwamrisha Nabii wake awabainishie manufaa yake na madhara yake, ili liwe hilo ni utangulizi wa kuviharamisha na kuviacha kabisa. Basi akajulisha kwamba dhambi zake na madhara yake, na yale yanayowatokea ya kupotea kwa akili na mali, na kuzuia kumtaja Mwenyezi Mungu, na swala, na uadui, na chuki, ni makubwa kuliko yale wanayofikiri katika manufaa yake. Kama vile kuchuma mali kwa kufanya biashara ya mvinyo, na kuipata kwa kucheza kamari na kufurahisha nafsi wakati wa kuvitumia. Basi ubainisho huu ukawa wa kuzikataza nafsi dhidi yake. Kwa sababu, mtu mwenye akili timamu hupitisha yale yenye uwezekano mkubwa wa manufaa, na hujiepusha na yale yenye uwezekano mkubwa wa kudhuru. Lakini pindi walipokuwa wamevizoea, na ikawa vigumu kukataza kuviwacha kabisa katika mara ya kwanza, akatanguliza Aya hii kama utangulizi wa kuviharamisha, ambavyo alivitaja katika kauli yake. “Enyi mlioamini, hakika mvinyo, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu tu katika kazi ya shetani.” Hadi kauli yake “mmeacha?” Na hili ni kutokana na upole wake, na rehema yake, na hekima yake. Na ndiyo maana ilipoteremka, Umar Mwenyezi Mungu amwiye radhi akasema, “Tumeacha, tumeacha”. Ama mvinyo, hiyo ni kila kileo chenye kuifunika akili cha aina yoyote ile. Na ama kamari, hiyo ni kila mashindano yote ambayo ndani yake kuna malipo kutoka pande zote mbili, kama vile kete, chesi. Na kila mashindano ya kikauli au ya kivitendo kwa malipo isipokuwa mashindano ya farasi, ngamia, na mishale. Hiyo inaruhusika, kwa sababu yanasaidia katika kufanya jihadi. Ndio maana Mweka sheria akayaruhusu. (219) Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilichozidi mahitaji. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya zake ili mpate kufikiri. Katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera. Na hili ni swali kuhusu kiasi wanachopaswa kutoa katika mali zao. Basi Mwenyezi Mungu akawafanyia wepesi katika jambo hilo. Na akawaamrisha kutoa cha ziada ambacho ni kile chepesi katika mali zao. Ambacho hakihusiani na mahitaji yao ya kawaida na mahitaji yao ya dharura. Na hili linarudi kwa kila mtu kulingana na yeye, kuanzia tajiri, fakiri, na wa wastani, kila mmoja ana uwezo wa kutoa kile kilichozidi mahitaji yake katika mali yake, hata kama ni kwa nusu ya tende. Ndio maana Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba achukue katika tabia nzuri watu. Na sadaka katika kilichozidi mahitaji, na wala asiwabebeshe kile ambacho ni kigumu kwao. Haya ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutuamrisha kile alichotuamrisha kwa sababu ya haja yake kutoka kwetu. Au kutuamrisha [yale ambayo ni magumu], bali alituamrisha yale ambayo yana furaha yetu. Ambayo ni mepesi kwetu, na yenye manufaa kwetu na kwa ndugu zetu, kwa hivyo anastahiki kusifiwa kikamilifu kwa hilo. Na pale Mwenyezi Mungu alipobainisha huku kubainisha kwenye kuponya, na akawaonyesha waja siri za sheria yake. Akasema, “hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake.” Yani zenye kuonyesha haki, zenye kuleta elimu yenye manufaa na upambanuzi, “ili mpate kutafakari. Katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera” yani ili mtumie fikira zenu katika siri za sheria yake, na ili mjue kuwa amri zake zina masilahi ya duniani na Akhera. Na pia ili muweze kufikiri juu ya dunia na uharaka wa kuisha kwake, ndio muikatae. Na juu ya Akhera na kubaki kwake, na kwamba ndiyo nyumba ya malipo, ndiyo muiimarishe.
: 220 #
{وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَى قُلْ إِصْلَاحٌ لَهُمْ خَيْرٌ وَإِنْ تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَأَعْنَتَكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (220)}.
(220) Katika dunia na Akhera na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio heri. Na mkichanganyika nao, basi ni ndugu zenu. Na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu, na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angelipenda, angeliwatia katika udhia. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{220} لما نزل قوله تعالى: {إن الذين يأكلون أموال اليتامى ظلماً إنما يأكلون في بطونهم ناراً وسيصلون سعيراً}؛ شق ذلك على المسلمين وعزلوا طعامهم عن طعام اليتامى خوفاً على أنفسهم من تناولها ولو في هذه الحالة التي جرت العادة بالمشاركة فيها، وسألوا النبي - صلى الله عليه وسلم -، عن ذلك ، فأخبرهم تعالى أن المقصود إصلاح أموال اليتامى بحفظها وصيانتها والاتجار فيها، وأن خلطتهم إياهم في طعام وغيره جائز على وجه لا يضر باليتامى لأنهم إخوانكم ومن شأن الأخ مخالطة أخيه، والمرجع في ذلك إلى النية والعمل، فمن علم [اللهُ] من نيته أنه مصلح لليتيم وليس له طمع في ماله فلو دخل عليه شيء من غير قصد لم يكن عليه بأس، ومن علم الله من نيته أن قصده بالمخالطة التوصل إلى أكلها [وتناولها] فذلك الذي حُرِّجَ وأُثِّم، والوسائل لها أحكام المقاصد. وفي هذه الآية دليل على جواز أنواع المخالطات في المآكل والمشارب والعقود وغيرها، وهذه الرخصة لطف من الله تعالى وإحسان وتوسعة على المؤمنين وإلا، فلو {شاء الله لأعنتكم}؛ أي: شق عليكم بعدم الرخصة بذلك فحُرِّجْتُم وشُقَّ عليكم وأثمتم {إن الله عزيز}؛ أي: له القوة الكاملة والقهر لكل شيء ولكنه مع ذلك {حكيم}؛ لا يفعل إلا ما هو مقتضى حكمته الكاملة وعنايته التامة فعزته لا تنافي حكمته فلا يقال إنه ما شاء فعل وافق الحكمة أو خالفها، بل يقال إن أفعاله وكذلك أحكامه تابعة لحكمته فلا يخلق شيئًا عبثًا بل لا بد له من حكمة عرفناها أم لم نعرفها، وكذلك لم يشرع لعباده شيئًا مجردًا عن الحكمة، فلا يأمر إلا بما فيه مصلحة خالصة أو راجحة ولا ينهى إلا عما فيه مفسدة خالصة أو راجحة لتمام حكمته ورحمته.
{220} Ilipoteremka kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika, wale wanaokula 0700205910mali za mayatima kwa dhulu, bila shaka wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni.” Hayo yaliwawia magumu Waislamu, basi wakakitenga na chakula chao kando na chakula cha mayatima wakiziogopea nafsi zao kwamba wasije wakazila; hata katika hali hii ambayo ni desturi kushirikiana ndani yake. Kwa hivyo, wakamuliza Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu kuhusu hilo. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia kwamba kinachokusudiwa ni kutengeneza mali za mayatima kwa kuzihifadhi na kuzitunza, na kuzifanyia biashara. Na kwamba kuchanganyika kwao nao katika chakula au vitu vinginevyo kunaruhusika kwa namna ambayo haiwadhuru mayatima. Kwa sababu wao ni ndugu yenu, na katika mambo ya ndugu ni kuchanganyika na nduguye. Na marejeo katika hayo ni nia na matendo. Kwa hivyo, yule ambaye Mwenyezi Mungu anajua nia yake kuwa yeye ni mtengenezaji wa yatima, wala hana tamaa na mali yake. Basi kama kitu kitamuingia bila ya kukusudia, basi hakutakuwa na ubaya juu yake. Naye yule ambaye Mwenyezi Mungu anajua katika nia yake kwamba makusudio yake katika kuchanganya ni kuzila na kuzitumia, basi huyo ndiye aliyefanya ubaya na akapata dhambi. Na njia zina hukumu sawa na makusudio yake. Na katika Aya hii, kuna ushahidi wa kuruhusiwa kwa kila aina ya kuchanganyika, katika vyakula na vinywaji na mikataba na kadhalika. Na ruhusa hii ni upole kutoka kwa Mwenyezi Mungu [Mtukufu] na hisani, na kuwakunjulia Waumini. Na sivyo basi, “na Mwenyezi Mungu angelipenda, angeliwatia katika udhia.” Yani angewafanyia ugumu kwa kutoruhusu hilo, hivyo basi ukawa ubaya juu yenu, na akawafanyia kuwa ugumu na mkapata dhambi. “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu.” Yani ana uwezo kamili, na kushinda kila kitu, lakini yeye pamoja na hayo, “ni Mwenye hekima”. Hafanyi isipokuwa kile kinachotakiwa na hekima yake kamilifu, na uangalizi wake timilifu. Kwa hivyo, nguvu zake hazipingani na hekima yake. Hivyo basi, haisemwi kwamba: Yeye atakalo, hulifanya, sawa linakubaliana na hekima yake au linapingana nayo. Bali inasemwa kwamba: Matendo yake na vile vile hukumu zake zinafuata hekima yake. Kwa hivyo, haumbi kitu bure tu. Lakini ni lazima kina hekima, tuijue au tusiijue. Kadhalika, hakuwawekea waja wake sheria yoyote isiyokuwa na hekima. Kwa hivyo, haamrishi chochote isipokuwa chenye masilahi tupu, au hayo ndiyo mengi zaidi. Na wala hakatazi isipokuwa chenye uharibifu mtupu, au huo ndio mwingi zaidi, kwa sababu ya ukamilifu wa hekima yake na rehema yake.
: 221 #
{وَلَا تَنْكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّى يُؤْمِنَّ وَلَأَمَةٌ مُؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ وَلَا تُنْكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّى يُؤْمِنُوا وَلَعَبْدٌ مُؤْمِنٌ خَيْرٌ مِنْ مُشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ أُولَئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَاللَّهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ (221)}
(221) Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mwanamke mshirikina hata akiwapendeza. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mwanamume mshirikina hata akiwapendeza. Hao wanaitia kwenye Moto, naye Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghfira kwa idhini yake. Naye huwabainishia Aya zake watu ili wapate kukumbuka.
#
{221} أي: {ولا تنكحوا}؛ النساء، {المشركات}؛ ما دمن على شركهن {حتى يؤمن}؛ لأن المؤمنة ولو بلغت من الدمامة ما بلغت خير من المشركة ولو بلغت من الحسن ما بلغت، وهذه عامة في جميع النساء المشركات، وخصصتها آية المائدة في إباحة نساء أهل الكتاب كما قال تعالى: {والمحصنات من الذين أوتوا الكتاب}؛ {ولا تنكحوا المشركين حتى يؤمنوا}؛ وهذا عام لا تخصيص فيه، ثم ذكر تعالى الحكمة في تحريم نكاح المسلم أو المسلمة لمن خالفهما في الدين فقال: {أولئك يدعون إلى النار}؛ أي: في أقوالهم وأفعالهم وأحوالهم، فمخالطتهم على خطر منهم، والخطر ليس من الأخطار الدنيوية إنما هو الشقاء الأبدي. ويستفاد من تعليل الآية النهي عن مخالطة كل مشرك ومبتدع؛ لأنه إذا لم يجز التزوج مع أن فيه مصالح كثيرة؛ فالخلطة المجردة من باب أولى وخصوصاً الخلطة التي فيها ارتفاع المشرك ونحوه على المسلم كالخدمة ونحوها. وفي قوله: {ولا تنكحوا المشركين}؛ دليل على اعتبار الولي في النكاح {والله يدعو إلى الجنة والمغفرة}؛ أي: يدعو عباده لتحصيل الجنة والمغفرة التي من آثارها دفع العقوبات؛ وذلك بالدعوة إلى أسبابها من الأعمال الصالحة والتوبة النصوح والعلم النافع والعمل الصالح، {ويبين آياته}؛ أي: أحكامه وحكمها {للناس لعلهم يتذكرون}؛ فيوجب لهم ذلك التذكر لما نسوه وعلم ما جهلوه والامتثال لما ضيَّعوه. ثم قال تعالى:
{221} Yani, “wala msiwaoe” wanawake, “washirikina”, maadamu wanaendelea juu ya shirki yao, “mpaka waamini.” Kwa maana Muumini mwanamke hata akifikia vipi katika mwonekano mbaya, yeye ni bora kuliko mwanamke mshirikina hata ikiwa atafikia vipi katika uzuri. Na hili ni jambo la jumla katika wanawake washirikina wote, na Aya ya Al-Maidah iliwaondoa wanawake wa Watu wa Kitabu katika aya hii, ikaruhusu kuwaoa, kama alivyosema Mtukufu. “Na wanawake wema miongoni mwa wale waliopewa Kitabu”. “Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini.” Na hii (Aya) ni ya jumla, haina chochote cha kuifanya kuwa maalumu. Kisha Mola Mtukufu akataja hekima ya kuharamisha ndoa ya Mwislamu mwanamume au mwanamke kwa mwenye kutofautiana nao katika dini, akasema: “Hao wanaitia kwenye Moto.” Yani katika kauli zao, na matendo yao, na hali zao, basi kuchanganyika nao ni hatari kwao. Nayo hii hatari si hatari ya kidunia, bali ni taabu ya milele. Na inafahamika kutokana na hoja ya Aya hii, katazo la kuchanganyika na kila mshirikina na mzushi. Kwa sababu ikiwa ndoa hairuhusiwi pamoja na kwamba ina masilahi mengi ndani yake, basi kuchanganyika kutupu (kusiko kuwa na faida), kunastahili zaidi. Hususan kuchanganyika ambako ndani yake mshirikina na mfano wake wanainuliwa juu ya Muislamu, kama vile kuwatumikia na mengineyo. Na katika kauli yake, “wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina.” Kuna ushahidi wa kuzingatiwa kwa walii (yani mlezi) [katika ndoa]. “Naye Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghfira.” Yani anawalingania waja wake kupata Pepo na maghfira, ambayo katika athari zake ni kuwaondolea adhabu, na hilo ni kwa kuwalingania kuendea sababu zake kama vile matendo mema, na toba ya kweli, na elimu yenye manufaa. “Naye huwabainishia Aya zake,” yani hukumu zake na hekima zake “kwa watu ili wapate kukumbuka.” Basi hilo linawafanya kukumbuka yale waliyoyasahau, na kujua yale ambayo hawakuyajua, na kuyafuata yale waliyoyapoteza. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 222 - 223 #
{وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّى يَطْهُرْنَ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ (222) نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُوا لِأَنْفُسِكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ مُلَاقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ (223)}
(222) Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie: hayo ni madhara. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka wawe safi. Na wakishajisafisha, basi waendeeni namna alivyowaamrisha Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu, na huwapenda wanaojisafisha. (223) Wake zenu ni konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini zitangulizieni heri nafsi zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana naye. Na wape habari njema Waumini.
#
{222} يخبر تعالى عن سؤالهم عن المحيض وهل تكون المرأة بحالها بعد الحيض كما كانت قبل ذلك أم تجتنب مطلقاً كما يفعله اليهود؟ فأخبر تعالى أن الحيض أذى وإذا كان أذى فمن الحكمة أن يمنع الله تعالى عباده عن الأذى وحده، ولهذا قال: {فاعتزلوا النساء في المحيض}؛ أي: مكان الحيض وهو الوطء في الفرج خاصة فهذا المحرم إجماعاً، وتخصيص الاعتزال في المحيض يدل على أن مباشرة الحائض وملامستها في غير الوطء في الفرج جائز، لكن قوله: {ولا تقربوهن حتى يطهرن}؛ يدل على ترك المباشرة فيما قرب من الفرج وذلك فيما بين السرة والركبة ينبغي تركه كما كان النبي - صلى الله عليه وسلم -، إذا أراد أن يباشر امرأته وهي حائض أمرها أن تتزر فيباشرها ، وحد هذا الاعتزال وعدم القربان للحيض {حتى يطهرن}؛ أي: ينقطع دمهن، فإذا انقطع الدم زال المنع الموجود وقت جريانه، الذي كان لحله شرطان: انقطاع الدم والاغتسال منه، فلما انقطع الدم زال الشرط الأول وبقي الثاني فلهذا قال: {فإذا تطهرن}؛ أي: اغتسلن، {فأتوهن من حيث أمركم الله}؛ أي: في القبل لا في الدبر لأنه محل الحرث، وفيه دليل على وجوب الاغتسال للحائض وإن انقطاع الدم شرط لصحته، ولما كان هذا المنع لطفاً منه تعالى بعباده وصيانة عن الأذى، قال تعالى: {إن الله يحب التوابين}؛ أي: من ذنوبهم على الدوام، {ويحب المتطهرين}؛ أي: المتنزهين عن الآثام، وهذا يشمل التطهر الحسي من الأنجاس والأحداث، ففيه مشروعية الطهارة مطلقاً؛ لأن الله تعالى يحب المتصف بها، ولهذا كانت الطهارة مطلقاً شرطاً لصحة الصلاة والطواف وجواز مس المصحف، ويشمل التطهر المعنوي عن الأخلاق الرذيلة والصفات القبيحة والأفعال الخسيسة.
{222} Mola Mtukufu anajulisha kuhusu swali lao kuhusu hedhi. Na je mwanamke hubaki katika hali yake baada ya hedhi, kama alivyokuwa kabla ya hilo, au anaepukwa kabisa, kama wanavyofanya Mayahudi? Basi Mola Mtukufu akajulisha kuwa hedhi ni madhara, na ikiwa ni madhara, basi katika hekima ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu awazuie waja wake kutokana na madhara peke yake. Na kwa sababu ya hili akasema: “Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi” yani sehemu ya hedhi, ambayo ni kujamiiana katika tupu ya uke hasa. Na hilo ndilo lililoharamishwa kwa Ijmaa (makubaliano ya wanachuoni). Na kufanya kujitenga nao kuhusiana na kujamiiana tu, kunaashiria kwamba inaruhusiwa kumwendea mwanamke aliye katika hedhi na kumpapasa bila ya kujamiiana naye katika uke. Lakini kauli yake, “wala msiwakaribie mpaka wawe safi.” Inaashiria kuwa kupapasa kilicho karibu na uke yani kilicho baina ya kitovu na goti kinapaswa kuachwa. Kama Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alivyokuwa akitaka kumpapasa mke wake hali ya kuwa yuko katika hedhi, alikuwa akimwamrisha afunge leso, kisha anampapasa. Na muda wa huku kujitenga na kuacha kuwa karibu na mke aliye katika hedhi ni, “mpaka asafike” yani damu yake ikatike. Na damu ikikatika, katazo lililokuwepo wakati wa kutoka kwake hukoma, ambalo lilikuwa na masharti mawili ya kulihahalisha: Kukatika kwa damu na kuoga kutokana nayo. Na pindi damu ilipokatika, sharti la kwanza likaondoka na likabaki la pili, ndiyo maana akasema. “Na wakishajisafisha” yani watakapooga, “basi waendeeni namna alivyowaamrisha Mwenyezi Mungu.” Yani katika uke, sio kwa tupu yao ya nyuma, kwa sababu hapo ndipo mahali pa kulima. Na kuna ushahidi juu ya uwajibu wa kuoga kwa mwanamke aliye katika hedhi, na kwamba kukatika kwa damu ndiko sharti la usahihi wake. Na kwa kuwa katazo hili lilikuwa ni upole wake Mola Mtukufu kwa waja wake, na kuwatunza dhidi ya madhara, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu. “Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu.” Yani kutokana na dhambi zao kwa daima, “na huwapenda wanaojisafisha.” Yani wale wanaojiepusha na dhambi. Na hilo linajumuisha kujisafisha kwa kihisia kutokana na najisi na hadathi. Basi ndani yake kuna sheria ya kujisafisha kwote. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda mwenye kusifika kwa hilo. Na ndiyo maana kujisafisha ni sharti la usahihi wa swala na kuizunguka Al-Ka’ba, na kuruhusika kuugusa Msahafu. Na kunajumuisha kujisafisha kwa kimaana kutokana na maadili maovu, na sifa mbaya, na matendo yenye kudharauliwa.
#
{223} {نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أَنى شئتم}؛ مقبلة ومدبرة غير أنه لا يكون إلا في القبل لكونه موضع الحرث وهو الموضع الذي يكون منه الولد، وفيه دليل على تحريم الوطء في الدبر؛ لأن الله لم يبح إتيان المرأة إلا في الموضع الذي منه الحرث. وقد تكاثرت الأحاديث عن النبي - صلى الله عليه وسلم -، في تحريم ذلك ولعن فاعله. {وقدموا لأنفسكم}؛ أي: من التقرب إلى الله بفعل الخيرات، ومن ذلك أن يباشر الرجل امرأته ويجامعها على وجه القربة والاحتساب وعلى رجاء تحصيل الذرية الذين ينفع الله بهم. {واتقوا الله}؛ أي: في جميع أحوالكم كونوا ملازمين لتقوى الله مستعينين على ذلك بعلمكم، {أنكم ملاقوه}؛ ومجازيكم على أعمالكم الصالحة وغيرها، [ثم قال]: {وبشر المؤمنين}؛ لم يذكر المبَشر به ليدل على العموم وأن لهم البشرى في الحياة الدنيا وفي الآخرة، وكل خير واندفاع كل ضير رُتِّب على الإيمان فهو داخل في هذه البشارة، وفيها محبة الله للمؤمنين ومحبة ما يسرهم واستحباب تنشيطهم وتشويقهم بما أعد الله لهم من الجزاء الدنيوي والأخروي.
(223) “Wake zenu ni konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo” kwa kutokea mbele na kwa kutokea nyuma. Lakini isiwe isipokuwa katika uke, kwa sababu ndipo pahali pa kulima, na ndipo pahali ambapo mtoto hutokana napo. Na kuna ushahidi wa kuharamishwa kujamiiana kwenye tupu ya nyuma. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hakuruhusu kumuingilia mwanamke isipokuwa katika mahali ambapo kuna kulima. Na kuna hadithi nyingi za Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika kuharamisha hilo, na kumlaani mwenye kulifanya. “Lakini zitangulizieni heri nafsi zenu.” Yani kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kutenda mema. Na katika hayo ni mtu kumpapasa mkewe na kumuingilia kwa namna ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kutaraji malipo, na kwa kutaraji kupata kizazi ambacho Mwenyezi Mungu atafaidisha kwao. “Na mcheni Mwenyezi Mungu” yani katika hali zenu zote. Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, mkitafuta msaada katika hilo, mkijua, “hakika nyinyi mtakutana naye.” Na atawalipa kwa matendo yenu mema na mengineyo. Kisha akasema: “Na wape habari njema Waumini,” lakini hakutaja ni bishara njema ya nini ili iashirie ujumla. Na kwamba wana bishara njema katika maisha ya duniani na katika Akhera. Na kila kheri, na kuepushwa na kila shari vinavyofungamanishwa na imani, basi inaingia katika bishara njema hii. Na ndani yake kuna mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa Waumini, na mapenzi ya yale yanayowafurahisha, na kupendekeza kuwasisimua na kuwatia shauku kwa yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu ya malipo ya kidunia na ya kiakhera.
: 224 #
{وَلَا تَجْعَلُوا اللَّهَ عُرْضَةً لِأَيْمَانِكُمْ أَنْ تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (224)}
(224) Wala msifanye Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa kisingizio cha kuacha kufanya wema, na kumcha Mungu, na kupatanisha baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
#
{224} المقصود من اليمين والقسم تعظيم المُقْسَمِ به وتأكيد المُقْسَم عليه. وكان الله تعالى قد أمر بحفظ الأيمان وكان مقتضى ذلك حفظها في كل شيء، ولكن الله تعالى استثنى من ذلك إذا كان البر باليمين يتضمن ترك ما هو أحب إليه فنهى عباده أن يجعلوا أيمانهم عرضة أي مانعة وحائلة عن أن يبروا أي يفعلوا خيراً ويتقوا شرًّا ويصلحوا بين الناس، فمن حلف على ترك واجب وجب حِنْثه وحرم إقامته على يمينه، ومن حلف على ترك مستحب استحب له الحِنْثُ، ومن حلف على فعل محرَّم وجب الحِنْثُ، أو على فعل مكروه استحب الحِنْث. وأما المباح فينبغي فيه حفظ اليمين عن الحِنْث. ويستدل بهذه الآية على القاعدة المشهورة أنه إذا تزاحمت المصالح قدم أهمها، فهنا تتميم اليمين مصلحة، وامتثال أوامر الله في هذه الأشياء مصلحة أكبر من ذلك، فقدمت لذلك. ثم ختم الآية بهذين الاسمين الكريمين فقال: {والله سميع}؛ أي: لجميع الأصوات، {عليم}؛ بالمقاصد والنيات، ومنه سماعه لأقوال الحالفين وعلمه بمقاصدهم هل هي خير أم شرٌّ، وفي ضمن ذلك التحذير من مجازاته، وأن أعمالكم ونياتكم قد استقر علمها عنده. ثم قال تعالى:
{224} Maana ya kiapo, ni kumtukuza yule ambaye imeapwa kwa jina lake, na kusisitiza kilichoapwa kutekelezwa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa ameamrisha kuhifadhi viapo. Na hilo lilikuwa linahitaji vihifadhiwe katika kila kitu. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alitoa katika hali hiyo inapokuwa kutekeleza kiapo kunajumuisha kuacha yale ambayo ni wajibu zaidi kwake. Kwa hivyo, akawakataza waja wake kuvifanya viapo vyao kuwa kisingizio, yani kipingamizi na kizuizi cha wao kufanya wema: Kama kufanya wema, au kuepuka shari (uovu), au kupatanisha baina ya watu. Basi anayeapa kuacha wajibu, italazimu ivunjwe, na ni haramu kuendelea kukishikilia kiapo chake hicho. Na mwenye kuapa kuacha kitu kinachopendekezwa, itapendekezwa kwamba aivunje. Na mwenye kuapa kufanya jambo la haramu, italazimu ivunjwe. Na ama jambo linaloruhusika, hilo inafaa kukihifadhi kiapo kisivunjwe. Aya hii inatumika kama ushahidi juu ya misingi maalumu wa kwamba, “ikiwa masilahi yataingiliana, basi litapewa kipaumbele lililo muhimu zaidi kati yake.” Na hapa, kutimiza kiapo ni masilahi, na kutii amri za Mwenyezi Mungu katika mambo haya ni masilahi makubwa kuliko hilo. Kwa hivyo, hili likapewa kipaumbele kwa sababu ya hilo. Kisha akahitimisha Aya hii kwa majina haya mawili matukufu, akasema, “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia” yani sauti zote “Mwenye kujua” wa makusudio na nia. Na katika hayo, ni kusikia kwake maneno ya wanaoapa, na kujua kwake, makusudio yao. Je, ni heri au shari (maovu)? Na ndani ya hilo kuna onyo dhidi ya malipo yake, na kwamba matendo yenu na nia zenu, tayari elimu ya hayo imeshatulia kwaye.
: 225 #
{لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَكِنْ يُؤَاخِذُكُمْ بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ (225)}
(225) Mwenyezi Mungu hawachukulii ubaya katika viapo vyenu ambavyo hamkuvikusudia. Lakini anawachukulia ubaya kwa yale ambayo nyoyo zenu zinachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.
#
{225} أي: لا يؤاخذكم بما يجري على ألسنتكم من الأيمان اللاغية التي يتكلم بها العبد، من غير قصد منه، ولا كسب قلب، ولكنها جرت على لسانه، كقول الرجل في عرض كلامه: لا والله وبلى والله، وكحلفه على أمر ماضٍ يظن صدق نفسه، وإنما المؤاخذة على ما قصده القلب، وفي هذا دليل على اعتبار المقاصد في الأقوال كما هي معتبرة في الأفعال، والله غفور لمن تاب إليه، حليم بمن عصاه حيث لم يعاجلْه بالعقوبة، بل حلم عنه، وستر، وصفح مع قدرته عليه وكونه بين يديه.
{225} Yani (Mwenyezi Mungu) hawachukulii ubaya katika viapo vinavyopita tu juu ya ndimi zenu bila ya kuvikusudia, ambavyo mja anavisema bila ya yeye kuvikusudia wala kuchuma kwa moyo. Lakini vinapita tu kwenye ulimi wake, kama vile mtu kusema katika kuwasilisha maneno yake. “Hapana, wallahi (Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu) na “Ndiyo, wallahi (Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu).” Na kama kiapo chake juu ya jambo lililopita analodhani kwama yeye ni mkweli. Na ama kuchukuliwa ubaya, huko kunakuwa kwa yale ambayo moyo umekusudia. Katika hili kuna ushahidi juu ya kuzingatia makusudio katika maneno, kama vile yanavyozingatiwa katika matendo. “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe.” Kwa anayetubia kwake “Mpole” kwa anayemuasi, kwa sababu hakumharakishia adhabu. Lakini alimfanyia upole na akasitiri, na akatupilia mbali pamoja na uwezo wake juu yake, kwamba yuko mbele yake.
: 226 - 227 #
{لِلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِنْ نِسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ فَإِنْ فَاءُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (226) وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (227)}
(226)Kwa wale wanaoapa kujitenga na wake zao, wangojee miezi minne. Na wakirejea, basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. (227) Na wakiazimia kuwapa talaka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mweye kujua.
#
{226} وهذا من الأيمان الخاصة بالزوجة في أمر خاص وهو حلف الرجل على ترك وطء زوجته مطلقاً أو مقيداً بأقل من أربعة أشهر أو أكثر، فمن آلى من زوجته خاصة فإن كان لدون أربعة أشهر فهذا مثل سائر الأيمان إن حنث كفَّر وإن أتم يمينه فلا شيء عليه، وليس لزوجته عليه سبيل لأنه مَلَّكَه أربعة أشهر، وإن كان أبداً أو مدة تزيد على أربعة أشهر ضربت له مدة أربعة أشهر من يمينه إذا طلبت زوجته ذلك لأنه حق لها، فإذا تمت أمر بالفيئة وهو الوطء، فإن وطئ فلا شيء عليه إلا كفارة اليمين، وإن امتنع أجبر على الطلاق، فإن امتنع طلق عليه الحاكم ولكن الفيئة والرجوع إلى زوجته أحب إلى الله تعالى، ولهذا قال: {فإن فاءوا}؛ أي: رجعوا إلى ما حلفوا على تركه وهو الوطء، {فإن الله غفور}؛ يغفر لهم ما حصل منهم من الحلف بسبب رجوعهم {رحيم}؛ حيث جعل لأيمانهم كفارة وتحلة ولم يجعلها لازمة لهم غير قابلة للانفكاك، ورحيم بهم أيضاً حيث فاءوا إلى زوجاتهم وحنوا عليهن ورحموهن.
{226} Na hivi ni katika viapo mahususi kwa mke, katika jambo maalum, ambalo ni kiapo mumewe kuapa kuacha kumjamii mkewe kabisa, au kwa kuweka muda wa chini ya miezi minne au zaidi. Kwa hivyo, anayeapa kuacha kumjamii mkewe hasa, basi ikiwa ni chini ya miezi minne, hicho kitakuwa mfano wa viapo vinginevyo tu. Akikivunja kiapo chake, atatoa fidia. Na akikitimiza kiapo chake, basi hakuna chochote juu yake, na mkewe hana njia juu yake, kwa sababu amejizuia kwa muda wa miezi minne. Na ikiwa ni cha kuendelea milele, au kwa muda wa zaidi ya miezi minne, basi atapewa muda wa miezi minne katika kiapo chake, ikiwa mke wake atataka hivyo. Kwa sababu hiyo ni haki yake. Na muda huo ukiisha, ataamrishwa kumrudia, yani kujamii. Na akimjamii, basi hakuna kitu juu yake isipokuwa fidia ya kiapo. Na akikataa, atalazimishwa kumtaliki. Na akikataa, hakimu atamtalikia. Hata hivyo, kumrudia mkewe ndiko kunakopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ndiyo maana akasema: “Na wakirejea”yani kuachana na yale waliyoapa kuyaacha, nako ni kujamii. “Basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe” Anawasamehe kwa yale yaliyotokea kwa kuapa kwa sababu ya kurudi kwao. “Mwenye kurehemu,” kwa maana aliviwekea fidia viapo vyao, na cha kuwaondoa katika hilo, wala hakuvilazimisha juu yao, ambavyo haviwezekani kuvunjika. Na pia ni mwenye rehema juu yao kwa maana waliwarudia wake zao, na wakawahurumia na wakawarehemu.
#
{227} {وإن عزموا الطلاق}؛ أي امتنعوا من الفيئة فكان ذلك دليلاً على رغبتهم عنهن وعدم إرادتهم لأزواجهم، وهذا لا يكون إلا عزماً على الطلاق فإن حصل هذا الحق الواجب منه مباشرة وإلا أجبره الحاكم عليه أو قام به {فإن الله سميع عليم}؛ فيه وعيد وتهديد لمن يحلف هذا الحلف ويقصد بذلك المضارة والمشاقة. ويستدل بهذه الآية على أن الإيلاء خاص بالزوجة لقوله من نسائهم، وعلى وجوب الوطء في كل أربعة أشهر مرة؛ لأنه بعد الأربعة يجبر إما على الوطء أو على الطلاق، ولا يكون ذلك إلا لتركه واجباً.
{227} “Na wakiazimia kuwapa talaka.” Yani wakikataa kuwarudia wake zao, hilo litakuwa dalili ya kutowapenda kwao na kutowataka wake zao. Na hili haliwi isipokuwa ni kuazimia kufanya talaka. Na hili likifanyika, basi atalazimika kumpa talaka mara moja, vinginevyo mtawala atamlazimisha kuifanya au yeye mwenyewe atafanya hivyo. “Basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” Ndani yake kuna onyo na tishio kwa mwenye kuapa kiapo hiki, na akakusudia kwacho kudhuru na kufanya ugumu. Na Aya hii inatumika kama dalili kwamba Al-iilaa ni mahususi tu kwa mke, kwa sababu ya kauli yake, “wake zao.” Na pia juu ya kwamba ni wajibu kujamiiana mara moja kila baada ya miezi minne. Kwa sababu, baada ya miezi minne, atalazimishwa ima kufanya jimai au talaka. Na hilo haliwi isipokuwa kwa sababu ameacha la wajibu.
: 228 #
{وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنْفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَنْ يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِنْ كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (228)}.
(228) Na wanawake waliopewa talaka, wazizuie nafsi zao tahara (au hedhi) tatu. Wala sio halali kwao kuficha alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao ya uzazi, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki zaidi ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu. Nao wanawake wanayo haki sawa na ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{228} أي: النساء [اللاتي] طلقهن أزواجهن {يتربصن بأنفسهن}؛ أي: ينتظرن ويعتددن مدة {ثلاثة قروء}؛ أي: حيض أو أطهار على اختلاف العلماء في المراد بذلك مع أن الصحيح أن القرء الحيض، ولهذه العدة عدة حكم منها العلم ببراءة الرحم إذا تكررت عليها ثلاثة الأقراء علم أنه ليس في رحمها حمل فلا يفضي إلى اختلاط الأنساب، ولهذا أوجب تعالى عليهن الإخبار عن، {ما خلق الله في أرحامهن}؛ وحرم عليهن كتمان ذلك من حمل أو حيض، لأن كتمان ذلك يفضي إلى مفاسد كثيرة فكتمان الحمل موجب أن تلحقه بغير من هو له رغبة فيه أو استعجالاً لانقضاء العدة فإذا ألحقته بغير أبيه حصل من قطع الرحم والإرث واحتجاب محارمه وأقاربه عنه، وربما تزوج ذوات محارمه وحصل في مقابلة ذلك إلحاقه بغير أبيه وثبوت توابع ذلك من الإرث منه وله، ومن جعل أقارب الملحق به أقارب له وفي ذلك من الشر والفساد ما لا يعلمه إلا رب العباد، ولو لم يكن في ذلك إلا إقامتها مع من نكاحها باطل في حقه، وفيه الإصرار على الكبيرة العظيمة وهي الزنا لكفى بذلك شرًّا. وأما كتمان الحيض فإن استعجلت فأخبرت به وهي كاذبة ففيه من انقطاع حق الزوج عنها وإباحتها لغيره وما يتفرع عن ذلك من الشرِّ كما ذكرنا، وإن كذبت وأخبرت بعدم وجود الحيض لتطول العدة فتأخذ منه نفقة غير واجبة عليه بل هي سحت عليها محرمة من جهتين: من كونها لا تستحقه، ومن كونها نسبته إلى حكم الشرع وهي كاذبة، وربما راجعها بعد انقضاء العدة فيكون ذلك سفاحاً لكونها أجنبية منه، فلهذا قال تعالى: {ولا يحل لهن أن يكتمن ما خلق الله في أرحامهن إن كن يؤمن بالله واليوم الآخر}. فصدور الكتمان منهن دليل على عدم إيمانهن بالله واليوم الآخر وإلا فلو آمنَّ بالله واليوم الآخر وعرفن أنهن مجزيات عن أعمالهن لم يصدر منهن شيء من ذلك، وفي ذلك دليل على قبول خبر المرأة عما تخبر بها عن نفسها من الأمر الذي لا يطلع عليه غيرها كالحمل والحيض ونحوهما. ثم قال تعالى: {وبعولتهن أحق بردهن في ذلك}؛ أي: لأزواجهن ما دامت متربصة في تلك العدة أن يردوهن إلى نكاحهن {إن أرادوا إصلاحاً}؛ أي: رغبة وألفة ومودة، ومفهوم الآية أنهم إن لم يريدوا الإصلاح فليسوا بأحق بردهن فلا يحل لهم أن يراجعوهن لقصد المضارة لها وتطويل العدة عليها، وهل يملك ذلك مع هذا القصد؟ فيه قولان: الجمهور على أنه يملك ذلك مع التحريم، والصحيح أنه إذا لم يرد الإصلاح لا يملك ذلك كما هو ظاهر الآية الكريمة، وهذه حكمة أخرى في هذا التربص، وهي أنه ربما أن زوجها ندم على فراقه لها فجعلت له هذه المدة ليتروى بها ويقطع نظره، وهذا يدل على محبته تعالى للألفة بين الزوجين وكراهته للفراق كما قال النبي - صلى الله عليه وسلم -: «أبغض الحلال إلى الله الطلاق» ، وهذا خاص في الطلاق الرجعي، وأما الطلاق البائن فليس البعل بأحق برجعتها، بل إن تراضيا على التراجع فلا بد من عقد جديد مجتمع الشروط. ثم قال تعالى: {ولهن مثل الذي عليهن بالمعروف}؛ أي: وللنساء على بعولتهن من الحقوق واللوازم مثل الذي عليهن لأزواجهن من الحقوق اللازمة والمستحبة، ومرجع الحقوق بين الزوجين إلى المعروف وهو العادة الجارية في ذلك البلد وذلك الزمان من مثلها لمثله، ويختلف ذلك باختلاف الأزمنة والأمكنة والأحوال والأشخاص والعوائد، وفي هذا دليل على أن النفقة والكسوة والمعاشرة والمسكن وكذلك الوطء الكل يرجع إلى المعروف، فهذا موجب العقد المطلق، وأما مع الشرط فعلى شرطهما، إلا شرطاً أحل حراماً أو حرم حلالاً. {وللرجال عليهن درجة}؛ أي: رفعة ورياسة وزيادة حق عليها كما قال تعالى: {الرجال قوامون على النساء بما فضل الله بعضهم على بعض وبما أنفقوا من أموالهم}؛ ومنصب النبوة والقضاء والإمامة الصغرى والكبرى وسائر الولايات [مختصٌّ] بالرجال، وله ضعفا ما لها في كثير من الأمور كالميراث ونحوه {والله عزيز حكيم}؛ أي: له العزة القاهرة والسلطان العظيم الذي دانت له جميع الأشياء، ولكنه مع عزته حكيم في تصرفه. ويخرج من عموم هذه الآية الحوامل فعدتهن وضع الحمل، واللاتي لم يدخل بهن فليس لهن عدة، والإماء فعدتهن حيضتان كما هو قول الصحابة رضي الله عنهم، وسياق الآية يدل على أن المراد بها الحرة.
{228} Yani wanawake ambao waume zao wamewapa talaka “wazizuie nafsi zao.” Yani wangoje na wakae eda kwa muda wa “Quruu tatu,” yani hedhi. Au tahara kulingana na tafauti ya wanazuoni juu ya kile kinachokusudiwa kwa hilo, ijapokuwa la sahihi ni kwamba Quruu ni hedhi. Na eda (muda wa kungojea) hii ina hukumu kadhaa, zikiwemo: Kuujua utupu wa tumbo la uzazi. Quruu tatu zikimrudia, basi itajulikana kuwa hakuna mimba katika tumbo lake la uzazi, kwa hivyo haitasababisha kuchanganyika kwa nasaba. Na kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewawajibishia kueleza “alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao ya uzazi.” Na akawaharamishia kuyaficha hayo, sawa iwe mimba au hedhi. Kwa sababu, kuficha hilo kunapelekea kwenye maovu mengi. Huko kuificha mimba kunalazimu kwamba atamnasibisha na asiyekuwa wake, kwa kumtaka na kuharakisha kuimaliza eda. Kwa hivyo, akimnasibisha na asiyekuwa baba yake, itatokea kukata ukoo na urithi, na kuwazuia naye maharimu na jamaa zake. Na huenda hata akawaoa maharimu wake, na ikatokea katika hilo kumnasibisha na asiyekuwa baba yake na kupatikana yanayofuatana na hilo kama vile kumrithi, na yeye kurithi, na kuwafanya jamaa za yule aliyenasibishwa nao kuwa jamaa zake. Na katika hilo kuna uovu na ufisadi ambao haujui isipokuwa Mola Mlezi wa waja. Na lau kuwa haingekuwa katika hilo isipokuwa kukaa kwake (mwanamke huyu mtalikiwa) pamoja na yule aliyemuoa kwa namna iliyo batili juu yake. Ambalo ndani yake kuna kusisitiza kuendelea kufanya dhambi kubwa, ambalo ni zinaa, basi hilo lingetosha kuwa uovu mkubwa. Na ama kuificha hedhi, kwa namna kwamba aliiharakisha na kusema kuwa ameipata hali ya kuwa yeye ni mwongo. Basi ndani yake kuna kuitatiza haki ya mume wake juu yake, na kuiruhusu kwa asiyekuwa mumewe, na shari inayotokana na hilo kama tulivyotaja. Na akidanganya na kusema kwamba hakuna hedhi, ili airefushe eda. Ili achukue kutoka kwake matumizi yasiyokuwa lazima juu yake. Bali hiyo ni mali haramu juu yake, iliyoharamishwa kwa njia mbili: Kwa sababu haistahiki, na kwa sababu aliyanasibisha na hukumu ya kisheria hali ya kuwa ni mwongo (katika hilo). Na huenda akamrudia mkewe baada ya kwisha kwa eda yake. Kwa hivyo unakuwa uhusianao usiokuwa wa maadili, kwa sababu yeye (mke) haruhusiwi kwake tena. Na ndio maana Mola Mtukufu akasema: “Wala sio halali kwao kuficha alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao ya uzazi, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho”. Na kutokea kwa tendo la kuficha kutoka kwao ni dalili ya kutomuamini kwao Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Sivyo, wangemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na wakajua kwamba watalipwa kwa matendo yao, basi kisingetokea kutoka kwao kitu katika hayo. Na katika hilo, kuna ushahidi wa kukubalika kwa habari za mwanamke, kuhusu yale anayoeleza juu ya nafsi yake; katika mambo ambayo hakuna mtu mwingine asiyekuwa yeye anayeyajua. Kama vile ujauzito, hedhi na mengineyo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na waume wao wana haki zaidi ya kuwarejesha katika muda huo." Yani madamu bado wamengojea katika eda hiyo au wawarudishe katika ndoa zao "kama wanataka kufanya suluhu." Yani kwa kuwataka, na kuwaweka karibu, na mapenzi. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya ni kwamba, ikiwa hawataki kufanya suluhu, basi hawastahiki kuwarejesha. Kwa hivyo, haiwawii halali kuwarejesha kwa lengo la kuwadhuru, na kurefusha (muda wa) eda. Na je, analimiliki hilo (la kustahiki kumrejesha) pamoja na nia hiyo? Kuna kauli mbili: Wengi wa wanachuoni wanaona kuwa analimiliki hilo pamoja na uharamu. Lakini mtazamo sahihi ni kwamba ikiwa hataki suluhu, basi halimiliki hilo, kama inavyodhihirika katika Aya tukufu. Na hii ni hekima nyingine katika kungojea huku, ambayo ni kwamba pengine mumewe huenda akajuta kutengana naye, basi akapewa muda huu ili afikiri juu ya jambo hilo na afanye uamuzi. Na hili linaashiria kupenda kwake Mola Mtukufu kuwepo kwa ukaribu baina ya wanandoa na kuchukia kwake kutengana. Kama Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alivyosema: "Halali inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni talaka." Na hili ni mahususi katika talaka anayoweza mume kumrejesha mkewe. Na ama talaka ambayo mke anaachika kabisa (yani mumewe hawezi kumrejesha isipokuwa kwa nikaa mpya), basi mume hana haki zaidi ya kumrejesha. Bali wakikubaliana kurudiana, basi ni lazima wafunge nikaa mpya yenye kujumuisha masharti yote. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Nao wanawake wanayo haki sawa na ile haki iliyo juu yao kwa wema." Yani wanawake wana haki na mahitaji juu ya waume zao, sawa na zile za waume zao zilizo juu yao miongoni mwa haki za lazima na zile zinazopendekezwa. Na marejeo ya haki kati ya wanandoa ni kulingana na ada iliyo katika nchi hiyo na katika wakati huo. Kwa mfano wake mke na kwa mfano wa mume. Na hili linatofautiana kulingana na nyakati, mahali, hali, watu, na ada. Na katika hili kuna dalili ya kwamba matumizi, mavazi, kuishi pamoja kwa uzuri, makazi, na vile vile kujamiiana, hayo yote yanarejelea ada. Na huu ndio msingi ambao mkataba wa ndoa wa kawaida umejengeka juu yake. Na ama ule ambao una masharti fulani, basi itakuwa kulingana na masharti hayo, isipokuwa sharti linalohalalisha kilchoharamishwa au kuharamisha kilichohalalishwa. "Na wanaume wana daraja zaidi juu yao." Yani katika kunyanyuliwa, uongozi, na kuongezwa (mume) haki juu yake (mke), kama alivyosema Mtukufu. "Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amefadhilisha baadhi yao juu ya baadhi, na kwa kile wanachotoa katika mali zao." Na nafasi ya unabii, uhakimu, uimamu mdogo na mkubwa, na vyeo vinginevyo ni [mahsusi] kwa wanaume. Naye ana mara mbili ya waliyo nayo katika mambo mengi, kama vile mirathi na mengineyo. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yani ana nguvu za ushindi na mamlaka makuu, ambaye vitu vyote vimeingia chini ya hukumu yake. Lakini yeye pamoja na nguvu zake ni mwenye hekima katika kuendesha kwake mambo. Na wanatokana na ujumla wa Aya hii wanawake wajawazito. Hao eda yao inaisha kwa kuzaa. Na wale ambao hawakuingiliwa na waume zao, kwani hawana eda. Na wajakazi, kwani eda yao ni hedhi mbili, kama ilivyo kauli ya Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi. Na muktadha wa Aya unaashiria kwamba anayekusudiwa nayo ni mwanamke huru.
: 229 #
{الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَنْ تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَنْ يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا وَمَنْ يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ (229)}
(229) Talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa uzuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika kile mlichowapa wake zenu, isipokuwa ikiwa wote wawili watahofia ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkihofia kuwa hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu, hapo hakuna ubaya juu yao katika kile ambacho mke atajikomboa kwacho. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi msiikiuke. Na mwenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.
#
{229} كان الطلاق في الجاهلية واستمر أول الإسلام يطلق الرجل زوجته بلا نهاية، فكان إذا أراد مضارتها طلقها فإذا شارفت انقضاء عدتها راجعها ثم طلقها وصنع بها مثل ذلك أبداً، فيحصل عليها من الضرر ما الله به عليم. فأخبر تعالى أن {الطلاق}؛ أي: الذي تحصل به الرجعة، {مرتان}؛ ليتمكن الزوج إن لم يرد المضارة من ارتجاعها ويراجع رأيه في هذه المدة، وأما ما فوقها فليس محلاًّ لذلك؛ لأن من زاد على الثنتين فإما متجرئ على المحرم أو ليس له رغبة في إمساكها بل قصده المضارة، فلهذا أمر تعالى الزوج أن يمسك زوجته {بمعروف}؛ أي: عشرة حسنة ويجري مجرى أمثاله مع زوجاتهم، وهذا هو الأرجح، وإلا يسرحها ويفارقها، {بإحسان}؛ ومن الإحسان أن لا يأخذ على فراقه لها شيئاً من مالها لأنه ظلم وأخذ للمال في غير مقابلة بشيء، فلهذا قال: {ولا يحل لكم أن تأخذوا مما آتيتموهن شيئاً إلا أن يخافا أن لا يقيما حدود الله}؛ وهي المخالعة بالمعروف بأن كرهت الزوجة زوجها لخُلُقِه أو خَلْقِه أو نقص دينه، وخافت أن لا تطيع الله فيه {فإن خفتم ألا يقيما حدود الله فلا جناح عليهما فيما افتدت به}؛ لأنه عوض لتحصيل مقصودها من الفرقة، وفي هذا مشروعية الخلع إذا وجدت هذه الحكمة {تلك}؛ أي: ما تقدم من الأحكام الشرعية، {حدود الله}؛ أي: أحكامه التي شرعها لكم وأمر بالوقوف معها {ومن يتعد حدود الله فأولئك هم الظالمون}، وأي ظلم أعظم ممن اقتحم الحلال وتعدى منه إلى الحرام فلم يسعه ما أحل الله؟ والظلم ثلاثة أقسام: ظلم العبد فيما بينه وبين الله، وظلم العبد الأكبر الذي هو الشرك، وظلم العبد فيما بينه وبين الخلق. فالشرك لا يغفره الله إلاَّ بالتوبة، وحقوق العباد لا يترك الله منها شيئاً، والظلم الذي بين العبد وربه فيما دون الشرك تحت المشيئة والحكمة.
{229} Talaka ilikuwa katika Jahiliyya, na ikaendelea hivyo mwanzo wa Uislamu. Mwanamume alikuwa akimtaliki mkewe bila ya kuwepo na kikomo (cha talaka hizo). Kwa hivyo, alikuwa anapotaka kumdhuru (mkewe), alimpa talaka, na anapokaribia kumaliza eda yake, anamrejesha. Kisha anamtaliki, na anamfanyia vivyo hivyo milele, kwa hivyo anapata kutokana na hilo madhara ambayo Mwenyezi Mungu ndiye anayeyajua tu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akasema kwamba, "talaka" ambayo mume anaweza kumrejesha mkewe, "ni mara mbili." Ili ikiwa mume hakukusudia kumdhuru, ataweza kumrejesha na kufikiria tena katika kipindi hiki. Lakini jambo lolote zaidi ya hilo, basi hilo halifai. Kwa sababu, mwenye kufanya hivyo zaidi ya mara mbili, ima anatafuta la haramu au hataki kuendelea kukaa naye. Bali lengo lake ni kumdhuru. Ndiyo maana Mola Mtukufu akamwamrisha mume akae na mkewe "kwa wema." Yani aishi naye kwa wema mfano wa wanavyowafanyia wenzake wake zao. Na hii ndiyo rai sahihi zaidi. La sivyo, amwachilie na aachane naye "kwa uzuri". Na katika uzuri, ni kwamba (mume) asichukue wakati wa kuachana naye chochote katika mali ya mkewe. Kwa sababu, hiyo ni dhuluma, na kachukua mali bila ya malipo yoyote. Na ndio maana akasema: "Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika kile mlichowapa wake zenu, isipokuwa ikiwa wote wawili watahofia kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu." Na hii ndiyo Mukhala' (yani mke kujinunua) kwa wema, ikiwa mke atamchukia mumewe kwa sababu ya maadili yake au maumbile yake au upungufu katika dini yake. Na akaogopa kwamba hatamtii Mwenyezi Mungu katika huyu mumuwe. "Basi mkihofia kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu, hapo hakuna ubaya juu yao katika kile ambacho mke atajikomboa kwacho." Kwa sababu ndicho kibadala cha yeye kufikia lengo lake la kuachana naye. Na katika hili kuna kuwekwa kwa sheria ya khulu ikiwa hekima hii itapatikana. "Hii," yani hukumu kisheria zilizotangulia "ni mipaka ya Mwenyezi Mungu." Yani hukumu zake ambazo aliziweka kama sheria kwenu, na akawaamrisha kusimama nazo. "Na mwenye kuruka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu." Na ni dhuluma gani iliyo kubwa zaidi kuliko yule aliyeingia ndani ya halali, kisha akaivuka na kuiendea haramu, na kutotosheka na kile ambacho Mungu amekihalalisha? Na dhuluma ni aina tatu: Dhuluma ya mja katika yale yaliyo kati yake na Mwenyezi Mungu. Na dhuluma kubwa ya mja, ambayo ni shirki. Na dhuluma ya mja katika yale yaliyo kati yake na viumbe. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu haisamehei shirki isipokuwa kwa toba. Na haki za waja, Mwenyezi Mungu haachi chochote katika hizo. Na dhuluma ambayo ipo baina ya mja na Mola wake katika yale yaliyo chini ya shirki yapo chini ya mapenzi na hekima ya Mwenyezi Mungu.
: 230 - 231 #
{فَإِنْ طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِنْ بَعْدُ حَتَّى تَنْكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ فَإِنْ طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَنْ يَتَرَاجَعَا إِنْ ظَنَّا أَنْ يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ (230) وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِتَعْتَدُوا وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّهِ هُزُوًا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنْزَلَ عَلَيْكُمْ مِنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُمْ بِهِ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (231)}
(230) Na akimtaliki (talaka ya tatu), basi yeye si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume asiyekuwa yeye. Na (huyo mwingine) akimtaliki, basi hakuna ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wanaojua. (231) Na mtakapowataliki wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakayefanya hivyo, ameidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa masikhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyowateremshia katika Kitabu na hekima anachowaonya kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
#
{230} يقول تعالى: {فإن طلقها}؛ أي: الطلقة الثالثة {فلا تحل له من بعد حتى تنكح زوجًا غيره}؛ أي: نكاحاً صحيحاً ويطأها، لأن النكاح الشرعي لا يكون إلا صحيحاً ويدخل فيه العقد والوطء وهذا بالاتفاق، ويتعين أن يكون نكاح الثاني نكاح رغبة، فإن قصد به تحليلها للأول فليس بنكاح ولا يفيد التحليل، ولا يفيد وطء السيد لأنه ليس بزوج، فإذا تزوجها الثاني راغباً، ووطأها، ثم فارقها وانقضت عدتها {فلا جناح عليهما}؛ أي: على الزوج الأول والزوجة {أن يتراجعا}؛ أي: يجددا عقداً جديداً بينهما لإضافته التراجع إليهما، فدل على اعتبار التراضي، ولكن يشترط في التراجع أن يظنا {أن يقيما حدود الله}؛ بأن يقوم كل منهما بحق صاحبه، وذلك إذا ندما على عشرتهما السابقة الموجبة للفراق، وعزما أن يبدلاها بعشرة حسنة، فهنا لا جناح عليهما في التراجع. ومفهوم الآية الكريمة أنهما إن لم يظنا أن يقيما حدود الله بأن غلب على ظنهما أن الحال السابقة باقية والعشرة السيئة غير زائلة أن عليهما في ذلك جناحاً، لأن جميع الأمور إن لم يقم فيها أمر الله ويسلك بها طاعته لم يحل الإقدام عليها، وفي هذا دلالة على أنه ينبغي للإنسان إذا أراد أن يدخل في أمر من الأمور، خصوصاً الولايات الصغار والكبار، أن ينظر في نفسه، فإن رأى من نفسه قوة على ذلك ووثق بها أقدم وإلا أحجم. ولما بيَّن تعالى هذه الأحكام العظيمة قال: {وتلك حدود الله}؛ أي: شرائعه التي حددها وبينها ووضحها، {يبينها لقوم يعلمون}؛ لأنهم هم المنتفعون بها النافعون لغيرهم، وفي هذا من فضيلة أهل العلم ما لا يخفى، لأن الله تعالى جعل تبيينه لحدوده خاصًّا بهم وأنهم المقصودون بذلك، وفيه أن الله تعالى يحب من عباده معرفة حدود ما أنزل على رسوله والتفقه بها.
{230} Mola Mtukufu anasema: "Na akimtaliki" yani talaka ya tatu, "basi yeye si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume asiyekuwa yeye." Yani nikaha sahihi, halali na amjamii. Kwa sababu, nikaha ya kisheria haiwi isipokuwa ile iliyo halali, na ambayo ina mkataba na kujamiiana. Na haya ndiyo makubaliano ya wanachuoni wote. Na nikaha ya pili ni lazima iwe nikaha ya kutaka kuoa. Na ikiwa itakusudiwa nayo kumhalalisha mwanamke huyo kwa ajili ya yule wa kwanza, basi hiyo sio ndoa wala haitasaidia katika kuhalalisha, wala kujaamii kwa bwana huyo, kwa sababu yeye si mume (wake). Na wa pili akimwoa kwa kutaka, na akamjaamii, kisha akamwacha, na eda yake ikamalizika; "basi hakuna ubaya juu yao." Yani juu ya yule mume na mkewe wa kwanza, "kurejeana" yani wafunge nikaha mpya kwa sababu amefungamanisha kurejea na wao tu. Kwa hivyo, ikaashiria kuwa kuridhiana kunazingatiwa, lakini kwa sharti katika kurejeana huko idhaniwe "kwamba watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu." Kwa namna ya kwamba kila mmoja wao ataitekeleza haki ya mwenzake. Na hilo ni ikiwa watajutia ule uhusiano wao uliopita uliosababisha kutengana, na waazimie kuubadilisha kwa uhusiano mwema. Basi hapa, hakuna ubaya wowote juu yao kurudiana. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya tukufu ni kwamba, ikiwa hawadhani kuwa watasimamisha mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu, kwa namna ya kwamba wanadhani kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba hali iliyopita itabaki. Na ule uhusiano mbaya hautaondoka, basi kuna ubaya juu yao katika hayo. Kwa sababu, mambo yote ikiwa amri ya Mwenyezi Mungu haitasimamishwa ndani yake, na utiifu kwake haukutekelezwa ndani yake; basi siyo halali kuyaendea. Na katika hili kuna dalili ya kuwa mtu anapaswa akitaka kuingia katika jambo miongoni mwa mambo, hasa uongozi mdogo na mkubwa, ajiangalie katika nafsi yake. Akiona katika nafsi yake nguvu juu yake, na akajiamini, basi na aliendee. Vinginevyo, arudi nyuma. Na Mwenyezi Mungu mtukufu alipozibainisha hukumu hizo kubwa, akasema: "Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu." Yani sheria zake ambazo aliipima, na akaibainisha, na akaiweka wazi, "anayoibainisha kwa watu wanaojua." Kwa sababu, wao ndio wanaonufaika kwayo, na wanaowanufaisha wengine. Na katika hili kuna katika fadhila za wenye elimu zisizofichika. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alikufanya kubainisha kwake kwa mipaka yake kuwa mahusisi tu kwao (wenye elimu). Na kwamba wao ndio waliokusudiwa na hilo. Na ndani yake kuna kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kwamba waja wake wajue mipaka ya yale aliyoyateremsha juu ya Mtume wake, na wayaelewe.
#
{231} ثم قال تعالى: {وإذا طلقتم النساء}؛ أي: طلاقاً رجعياً بواحدة أو اثنتين {فبلغن أجلهن}؛ أي: قاربن انقضاء عدتهن {فأمسكوهن بمعروف أو سرحوهن بمعروف}؛ أي: إما أن تراجعوهن ونيتكم القيام بحقوقهن، أو تتركوهن بلا رجعة ولا إضرار، ولهذا قال: {ولا تمسكوهن ضرارًا}؛ أي: مضارة بهن {لتعتدوا} في فعلكم هذا الحلال إلى الحرام، فالحلال الإمساك بالمعروف والحرام المضارة، {ومن يفعل ذلك فقد ظلم نفسه}، ولو كان الحق يعود للمخلوق فالضرر عائد إلى من أراد الضرار، {ولا تتخذوا آيات الله هزواً}، لما بين تعالى حدوده غاية التبيين وكان المقصود العلم بها والعمل والوقوف معها وعدم مجاوزتها، لأنه تعالى لم ينزلها عبثاً بل أنزلها بالحق والصدق والجد، نهى عن اتخاذها هزواً، أي: لعباً بها وهو التجري عليها وعدم الامتثال لواجبها، مثل: استعمال المضارة في الإمساك أو الفراق أو كثرة الطلاق أو جمع الثلاث، والله من رحمته جعل له واحدة بعد واحدة رفقاً به، وسعياً في مصلحته. {واذكروا نعمة الله عليكم}؛ عموماً باللسان حمداً وثناء وبالقلب اعترافاً وإقراراً وبالأركان بصرفها في طاعة الله {وما أنزل عليكم من الكتاب والحكمة}؛ أي: السنة، اللذين بَيَّن لكم بهما طرق الخير، ورغبكم فيها، وطرق الشر، وحذركم إياها، وعرفكم نفسه ووقائعه في أوليائه وأعدائه، وعلمكم ما لم تكونوا تعلمون، وقيل المراد بالحكمة أسرار الشريعة، فالكتاب فيه الحكم، والحكمة فيها بيان حكمة الله في أوامره ونواهيه، وكلا المعنيين صحيح، ولهذا قال: {يعظكم به}؛ أي: بما أنزل عليكم، وهذا مما يقوي أن المراد بالحكمة أسرارُ الشريعة لأن الموعظة ببيان الحكم والحكمة والترغيب أو الترهيب، فالحكم به يزول الجهل، والحكمة مع الترغيب يوجب الرغبة، والحكمة مع الترهيب يوجب الرهبة {واتقوا الله} في جميع أموركم {واعلموا أن الله بكل شيء عليم}؛ فلهذا بين لكم هذه الأحكام بغاية الإتقان والإحكام التي هي جارية مع المصالح في كل زمان ومكان، فله الحمد والمنة.
{231} Kisha Yeye Mtukufu akasema, "Na mtakapowataliki wanawake" yani talaka ya kurejeleana bila ya nikaha mpya, kama vile talaka moja au mbili. "Nao wakafikia kumaliza muda wao (wa eda)" yani muda wakakaribia kumaliza muda wao wa eda. "Basi washikilieni kwa wema au waachilieni kwa wema." Yani ima muwarudishe hali ya kuwa nia zenu ni kuwatimizia haki zao, au muwaache bila ya kuwarudisha wala kuwadhuru. Na ndio maana akasema, "wala msiwashikilie kwa kuwadhuru, ili mkiuke mipaka" katika kufanya kwenu halali kuwa haramu. Kwani halali ni kushikilia kwa wema, nayo haramu ni kuwadhuru. "Na mwenye kufanya hilo, basi kwa hakika ameidhulumu nafsi yake." Na hata kama haki ni ya kiumbe, lakini madhara yanamrudia yule aliyetaka kufanya madhara, "wala msizifanyie Aya za Mwenyezi Mungu mzaha". Mwenyezi Mungu alipoibainisha mipaka yake kwa uwazi kabisa, na yakawa makusudio ni kuijua, kuifanyia kazi, kusimama nayo, na kutoikiuka, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuibainisha bure. Bali aliiteremsha kwa haki, ukweli, na kuipa uzito mkubwa. Kwa hivyo, akakataza kuifanyia mzaha, yani kuifanyia mchezo kwa kuiasi na kutotekeleza wajibu wake, kama vile: Kukusudia madhara katika kumshikilia mke (aliyetalikiwa), au kuachana naye, au kutaliki kwa wingi, au kufanya talaka tatu kwa pamoja. Ilhali Mwenyezi Mungu katika rehema yake alimfanyia talaka mmoja baada ya nyingine kwa sababu ya kufanyia upole na kutaka kumtekelezea masilahi yake. "Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu" kwa ujumla, kwa kuhimidi na kusifu kwa ulimi. Na kwa kukubali na kukiri kwa moyo, na kwa viungo kwa kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu. "Na yale aliyowateremshia katika Kitabu na hekima," yani Sunna ambayo kwa mawili hayo aliwabainishia njia za heri; na akawahimiza juu yake. Na njia za shari, na akawatahadharisha dhidi yake. Na akajijulisha kwenu, na matukio yake katika marafiki wake na maadui zake, na akawafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. Na ilisemwa kuwa kinachokusudiwa ni hekima ni siri za Sheria. Kwa sababu, Kitabu kina hukumu, nayo hekima ina ufafanuzi wa hekima ya Mwenyezi Mungu katika maamrisho yake na makatazo yake. Na kila maana mbili hizi ni sahihi. Na ndio maana akasema, "anayowawaidhi kwayo." Yani kwa yale aliyoyateremsha juu yenu. Na hili ni katika yale yenye kutilia nguvu kuwa kilichokusudiwa na hekima ni siri za sheria. Kwa sababu, mawaidha ni kubainisha hukumu na hekima, na kutia moyo au kutishia. Kwa hivyo, kuhukumu kwayo kunaondoa ujinga. Nayo hekima pamoja na kutia moyo yanasababisha mtu kuwa na moyo katika jambo. Nayo hekima pamoja na kutishia yanasababisha hofu "na mcheni Mwenyezi Mungu" katika mambo yenu yote. "Na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu." Ndio maana akawabainishia hukumu hizi kwa ukamilifu wa hali ya juu na zaidi, na hukumu ambazo zinakwendana na masilahi (ya watu) katika kila wakati na mahali. Kwa hivyo, sifa njema zote na wema ni vyake.
: 232 #
{وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَنْ يَنْكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُمْ بِالْمَعْرُوفِ ذَلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَنْ كَانَ مِنْكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَلِكُمْ أَزْكَى لَكُمْ وَأَطْهَرُ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ (232)}
(232) Na mtakapowataliki wanawake, nao wakamaliza muda wao (wa eda), basi msiwazuie kuoleka kwa waume zao endapo baina yao wamekubaliana kwa wema. Hayo anawaidhiwa kwayo yule miongoni mwenu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ni bora zaidi kwenu na safi kabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua, lakini nyinyi hamjui.
#
{232} هذا خطاب لأولياء المرأة المطلقة دون الثلاث إذا خرجت من العدة وأراد زوجها أن ينكحها ورضيت بذلك فلا يجوز لوليها من أب وغيره أن يعضلها أي يمنعها من التزوج به حنقاً عليه وغضباً واشمئزازاً لما فعل من الطلاق الأول، وذكر أن من كان يؤمن بالله واليوم الآخر؛ فإيمانه يمنعه من العضل، ذلك {أزكى لكم وأطهر}؛ وأطيب مما يظن الولي أن عدم تزويجه هو الرأي واللائق وأنه يقابل بطلاقه الأول بعدم تزويجه كما هو عادة المترفعين المتكبرين، فإن كان يظن أن المصلحة في عدم تزويجه. فالله {يعلم وأنتم لا تعلمون}؛ فامتثلوا أمر من هو عالم بمصالحكم، مريد لها قادر عليها، ميسر لها من الوجه الذي تعرفون وغيره. وفي هذه الآية دليل على أنه لا بد من الولي في النكاح لأنه نهى الأولياء عن العضل، ولا ينهاهم إلا عن أمر هو تحت تدبيرهم ولهم فيه حق. ثم قال تعالى:
{232} Haya ni maneno kwa wasimamizi wa mwanamke aliyetalikiwa talaka chini ya tatu. Anapotoka katika eda na akataka kwamba mumewe amuoe, na (mwanamke) akaridhia hilo, basi hairuhusiwi kwa msimamizi wake kama vile baba na wengineo kumzuia kumuoa kwa sababu ya kuwa na hasira kubwa naye; na kuchukizwa na alichokifanya cha ile talaka ya kwanza. Na akataja kwamba anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, imani yake humzuia na hilo. Na hayo, "ni bora zaidi kwenu na safi kabisa" na nzuri zaidi kuliko vile anavyodhania msimamizi huyu. Kwamba kutomwozesha huyu mwanamume ndiyo rai iliyo sawa na inayofaa, na kwamba akabiliwe kwa ile talaka yake ya kwanza kwa kutomwozesha, kama ilivyo ada ya wenye starehe, wenye kutakabari. Na ikiwa anadhania kuwa masilahi yako katika kutomwozesha, basi Mwenyezi Mungu "anajua, na nyinyi hamjui". Kwa hivyo, fuateni amri ya yule anayeyajua masilahi yenu, anayeyataka, mwenye uwezo juu yake, na anayeyarahisisha kwa kwa njia ambazo mnazijua, na nyinginezo (msizojua). Katika Aya hii kuna dalili ya kuwa ni lazima kuwepo msimamizi katika nikaha. Kwa sababu aliwakataza wasimamizi kuzuia, na wala hawakatazi isipokuwa jambo ambalo lipo chini ya uendeshaji wao ambalo wana haki ndani yake. Kisha yeye Mtukufu akasema:
: 233 #
{وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ لِمَنْ أَرَادَ أَنْ يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَهُ بِوَلَدِهِ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَلِكَ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَنْ تَرَاضٍ مِنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا وَإِنْ أَرَدْتُمْ أَنْ تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُمْ مَا آتَيْتُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (233)}
(233) Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya aliyezaliwa mwana huyo chakula chao na kuwalisha mavazi yao kwa wema. Wala halazimishwi mtu isipokuwa kwa kiwango cha uwezo wake. Mama asitaabishwe kwa sababu ya mwanawe, wala yule aliyezaliwa mwana kwa sababu ya mwanawe. Na juu ya mrithi ni mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha kunyonya kwa kuridhiana na kushauriana, basi hakuna ubaya juu yao. Na mkitaka kuwapa watoto wenu mama wa kuwanyonyesha, basi hakuna ubaya juu yenu ikiwa mtapeana mlichoahidi kwa wema. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda.
#
{233} هذا خبر بمعنى الأمر تنزيلاً له منزلة المتقرر الذي لا يحتاج إلى أمر بأن {يرضعن أولادهن حولين}؛ ولما كان الحول يطلق على الكامل وعلى معظم الحول قال: {كاملين لمن أراد أن يتم الرضاعة}؛ فإذا تم للرضيع حولان فقد تم رضاعه وصار اللبن بعد ذلك بمنزلة سائر الأغذية، فلهذا كان الرضاع بعد الحولين غير معتبر لا يُحَرِّم. ويؤخذ من هذا النص ومن قوله تعالى: {وحمله وفصاله ثلاثون شهراً}؛ أن أقل مدة الحمل ستة أشهر وأنه يمكن وجود الولد بها {وعلى المولود له}؛ أي: الأب، {رزقهن وكسوتهن بالمعروف}؛ وهذا شامل لما إذا كانت في حباله أو مطلقة، فإن على الأب رزقها؛ أي: نفقتها وكسوتها وهي الأجرة للرضاع، ودل هذا على أنها إذا كانت في حباله لا يجب لها أجرة غير النفقة والكسوة وكل بحسب حاله، فلهذا قال: {لا تكلف نفس إلا وسعها}؛ فلا يكلف الفقير أن ينفق نفقة الغني ولا من لم يجد شيئاً بالنفقة حتى يجد {لا تضار والدة بولدها ولا مولود له بولده}؛ أي: لا يحل أن تضار الوالدة بسبب ولدها، إما أن تمنع من إرضاعه أو لا تعطى ما يجب لها من النفقة والكسوة أو الأجرة {ولا مولود له بولده}؛ بأن تمتنع من إرضاعه على وجه المضارة [له] أو تطلب زيادة عن الواجب ونحو ذلك من أنواع الضرر، ودل قوله: {مولود له}؛ أن الولد لأبيه لأنه موهوب له ولأنه من كسبه، فلذلك جاز له الأخذ من ماله رضيَ أو لم يرضَ، بخلاف الأم. وقوله: {وعلى الوارث مثل ذلك}؛ أي: على وارث الطفل إذا عدم الأب، وكان الطفل ليس له مال مثل ما على الأب من النفقة للمرضع والكسوة، فدل على وجوب نفقة الأقارب المعسرين على القريب الوارث الموسر، {فإن أرادا}؛ أي: الأبوان، {فصالاً}؛ أي: فطام الصبي قبل الحولين، {عن تراضٍ منهما}؛ بأن يكونا راضيين، {وتشاور}؛ فيما بينهما هل هو مصلحة للصبي أم لا؟ فإن كان مصلحة ورضيا {فلا جناح عليهما}؛ في فطامه قبل الحولين، فدلت الآية بمفهومها على أنه إن رضي أحدهما دون الآخر أو لم يكن مصلحة للطفل أنه لا يجوز فطامه. وقوله: {وإن أردتم أن تسترضعوا أولادكم}؛ أي: تطلبوا لهم المراضع غير أمهاتهم على غير وجه المضارة، {فلا جناح عليكم إذا سلمتم ما آتيتم بالمعروف}؛ أي: للمرضعات، {واعلموا أن الله بما تعملون بصير}؛ فمجازيكم على ذلك بالخير والشر.
{233} Hii ni habari yenye maana ya amri, kwa kuiteremsha katika hali ya kile ambacho kimeshathibiti, kisichohitaji kuamrishwa kwamba, "na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili". Na kwa kuwa mwaka huitwa hivyo ukiwa kamili, au sehemu ya kubwa ya mwaka. Akasema, "kamili kwa anayetaka kutimiza kunyonyesha." Kwa hivyo, mtoto anayenyonya anapokamilisha miaka miwili, basi kunyonya kwake kutakuwa kumekamilika. Na yanakuwa maziwa hayo baada ya hapo kama vyakula vinginevyo. Kwa hivyo, kunyonyesha baada ya miaka miwili hakuzingatiwi na wala hakuharamishwi. Na inachukuliwa kutoka katika andiko hili na katika kauli yake Mola Mtukufu. "Na mimba yake na kumwachisha kwake kunyonya ni miezi thelathini." Kwamba muda wa chini zaidi wa ujauzito ni miezi sita, na kwamba inawezekana mtoto kuwepo ndani yake. "Na ni juu ya aliyezaliwa mwana," yani baba yake, "chakula chao na kuwavalisha mavazi yao kwa wema". Na hili linajumuisha ikiwa yupo chini yake au ametalikiwa. Basi ni juu ya baba (ya mwana) ruzuku yao, yani kumpa matumizi na mavazi, na kila mmoja ni kulingana na hali yake. Ndiyo maana Mola Mtukufu akasema: "Wala halazimishwi mtu isipokuwa kwa kiwango cha uwezo wake". Hivyo basi, fakiri hatakiwi kutoa matumizi ya tajiri, wala yule ambaye hana chochote kwamba atoe, mpaka apate. "Mama asitaabishwe kwa sababu ya mwanawe, wala yule aliyezaliwa mwana kwa sababu ya mwanawe." Yani sio halali mama kudhuriwa kwa sababu ya mwanawe, ima kwa kumzuia kumnyonyesha au kutompa anachotakiwa cha matumizi, na mavazi, au kodi (ujira). "Wala yule aliyezaliwa mwana kwa sababu ya mwanawe." Kwa mama kukataa kumnyonyesha kwa kutaka kumdhuru [baba] au kumuomba (baba) zaidi ya kile kilicho wajibu, na mfano wa hayo miongoni mwa aina za madhara. Na iliashiria kauli yake, "yule aliyezaliwa mwana" kwamba mtoto ni wa baba yake; kwa sababu alipewa kama zawadi, na kwa sababu ni kutokana na alichochuma. Na ndiyo maana inaruhusika kwake kuchukua katika mali yake, aridhie au asiridhie, tofauti na mama. Na kauli yake, "na juu ya mrithi ni mfano wa hivyo." Yani ni juu ya anayemrithi mtoto huyo ikiwa baba hatakuwepo, na mtoto huyo hana mali, basi mrithi wake ni juu yake sawa kile ambacho kiko juu ya baba kama vile kumpa mnyonyeshaji matumizi na mavazi. Kwa hivyo, ikaonyesha ulazima wa jamaa wasio na mali kupewa matumizi na jamaa ambaye ni mrithi mwenye wasaa wa mali. "Na kama wote wawili wakitaka," yani baba na mama "kumwachisha kunyonya." Yani (kumwachisha kunyonya) mtoto huyo kabla ya miaka miwili, "kwa kuridhiana" kwa namna kwamba wote wawili wameridhia. "Na kushauriana," kati yao wawili, je ni kwa masilahi ya mtoto au hapana? Basi ikiwa ni kwa masilahi yake, "basi hakuna ubaya wowote juu yao" katika kumwachisha kunyonya kabla ya miaka miwili. Na Aya pia iliashiria kwa maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba ikiwa mmoja wao ataridhika bila ya mwingineye, au ikiwa siyo kwa masilahi ya mtoto, basi hairuhusiki kumwachisha kunyonya. Na kauli yake, "Na mkitaka kuwapa watoto wenu mama wa kuwanyonyesha." Yani kuwatafutia wanyonyeshaji wasiokuwa mama zao kwa njia isiyokuwa na madhara. "Basi hakuna ubaya juu yenu ikiwa mtapeana mlichoahidi kwa wema". Yani kuwapa hao wanawake wanyonyeshaji "Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda," na atawalipa juu ya hayo kwa mema na mabaya.
: 234 #
{وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنْكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنْفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنْفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (234)}
(234) Na wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanaacha wake, hawa wake wazizuie nafsi zao miezi minne na siku kumi. Na wanapotimiza muda wao (wa eda), basi hakuna ubaya wowote juu yao katika yale wanayojifanyia kwa wema. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.
#
{234} أي: إذا توفي الزوج مكثت زوجته متربصة أربعة أشهر وعشرة أيام وجوباً، والحكمة في ذلك ليتبين الحمل في مدة الأربعة ويتحرك في ابتدائه في الشهر الخامس، وهذا العام مخصوص بالحوامل، فإن عدتهن بوضع الحمل، وكذلك الأمة عدتها على النصف من عدة الحرة شهران وخمسة أيام. وقوله: {فإذا بلغن أجلهن}؛ أي: انقضت عدتهن، {فلا جناح عليكم فيما فعلن في أنفسهن}؛ أي: من مراجعتها للزينة والطيب، {بالمعروف}؛ أي: على وجه غير محرم ولا مكروه، وفي هذا وجوب الإحداد مدة العدة على المتوفى عنها زوجها دون غيرها من المطلقات والمفارقات وهو مجمع عليه بين العلماء، {والله بما تعملون خبير}؛ أي: عالم بأعمالكم ظاهرها وباطنها جليِّها وخفيها فمجازيكم عليها، وفي خطابه للأولياء بقوله: {فلا جناح عليكم فيما فعلن في أنفسهن}؛ دليل على أن الولي ينظر على المرأة ويمنعها مما لا يجوز فعله، ويجبرها على ما يجب وأنه مخاطب بذلك واجب عليه.
{234} Yani mume atakapokufa, mke wake atakaa akingoja kwa lazima miezi minne na siku kumi. Na hekima katika hilo ni kubainisha mimba katika muda huo wa miezi minne. Naye mtoto aliye ndani ya tumbo ataanza kusongasonga mwanzoni mwa mwezi wa tano. Na ujumla huu umefanywa kuwa mahususi katika hali ya wanawake wajawazito. Hao eda yao inaisha kwa kuzaa. Na vile vile mjakazi, muda wake ni nusu ya muda wa mwanamke huru; miezi miwili na siku tano. Na kauli yake "na wakimaliza muda wao (wa eda), basi hakuna ubaya wowote juu yao katika yale wanayozifanyia nafsi zao." Yani kuyarudia kwao mapambo na manukato "kwa wema" yani namna isiyokuwa haramu wala inayochukiza. Na katika hili kuna ulazima wa kuacha mapambo katika muda wa eda kwa mwanamke aliyefiwa mume peke yake. Siyo wale wanawake wengineo wanaoachwa kwa talaka na kuachana kwingineko. Na hili wamekubaliana juu yake wanachuoni. "Na Mwenyezi Mungu anazo habari zote za mnayoyatenda." Yani anayajua matendo yenu, ya dhahiri yake na ya ndani yake, ya waziwazi kabisa na yaliyofichika, kisha atawalipa juu yake. Na katika kuwaongelesha kwake wasimamizi (wa wanawake) katika kauli yake, "basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika yale wanayozifanyia nafsi zao." Kuna dalili ya kwamba msimamizi amtunze mwanamke na amzuie yale yasiyoruhusiwa kufanywa. Na amlazimishe kufanya yale ambayo ni ya lazima, na kwamba yeye ndiye anayeongeleshwa hayo, na ni wajibu juu yake.
: 235 #
{وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُمْ بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنْتُمْ فِي أَنْفُسِكُمْ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَكِنْ لَا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَنْ تَقُولُوا قَوْلًا مَعْرُوفًا وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّى يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنْفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ (235)}
(235) Wala hakuna ubaya juu yenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake walio katika eda au mkalificha ndani ya nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu alikwisha jua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, isipokuwa mseme maneno mema. Wala msiazimie kufunga mkataba wa ndoa mpaka andiko (la amri ya eda) lifike muda wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basi jitahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.
#
{235} هذا حكم المعتدة من وفاة أو المبانة في الحياة، فيحرم على غير مبينها أن يصرح لها في الخطبة وهو المراد بقوله: {ولكن لا تواعدوهن سرًّا}؛ وأما التعريض فقد أسقط تعالى فيه الجناح، والفرق بينهما أن التصريح لا يحتمل غير النكاح فلهذا حرم خوفاً من استعجالها وكذبها في انقضاء عدتها رغبة في النكاح، ففيه دلالة على منع وسائل المحرم وقضاء لحق زوجها الأول بعدم مواعدتها لغيره مدة عدتها، وأما التعريض وهو الذي يحتمل النكاح وغيره فهو جائز للبائن كأن يقول [لها]: إني أريد التزوج وإني أحب أن تشاوريني عند انقضاء عدتك ونحو ذلك، فهذا جائز لأنه ليس بمنزلة الصريح، وفي النفوس داعٍ قوي إليه، وكذا إضمار الإنسان في نفسه أن يتزوج من هي في عدتها إذا انقضت، ولهذا قال: {أو أكننتم في أنفسكم علم الله أنكم ستذكرونهن}؛ هذا التفصيل كله في مقدمات العقد، وأما عقد النكاح فلا يحل، {حتى يبلغ الكتاب أجله}؛ أي: تنقضي العدة. {واعلموا أن الله يعلم ما في أنفسكم}؛ أي: فانووا الخير ولا تنووا الشرَّ خوفاً من عقابه ورجاء لثوابه، {واعلموا أن الله غفور}؛ لمن صدرت منه الذنوب فتاب منها، ورجع إلى ربه، {حليم}؛ حيث لم يعاجل العاصينَ على معاصيهم مع قدرته عليهم.
{235} Hii ni hukumu ya mwanamke ambaye anakaa eda ya kufiwa mume. Au yule aliyeachana naye katika uhai kuachana ambako hawawezi kurudiana isipokuwa kwa nikaha mpya. Kwa hivyo, ni haramu kwa asiyekuwa aliyemwacha kumposa waziwazi. Na ndilo lililokusudiwa katika kauli yake, "lakini msiwaahidi kwa siri." Na ama kwa nanma ya kuficha, basi Mwenyezi Mungu amedondoa ubaya ndani yake. Na tafauti baina yake ni kuwa namna ya waziwazi haimaanishi chochote isipokuwa ndoa. Ndio maana ikaharamishwa kwa kuhofia (mwanamke) asije akaharakisha na akadanganya kuhusu kumalizika kwa eda yake kwa sababu ya kutaka kuoleka. Na ndani yake kuna dalili juu ya kuzuia njia za kufikia haramu, na kutimiza haki ya mume wake wa kwanza kwa kutoahidiana na asiyekuwa yeye katika muda wa eda yake. Na ama kwa namna ya kuficha, nayo ni (ile namna) yenye uwezekano wa ndoa na mengineyo. Basi hiyo (namna) inaruhusika kwa yule aliyeachana kuachana kunakolazimu nikaha mpya ili kurudiana, kama vile aseme [amwambie mke huyo]: 'Mimi kwa hakika ninataka kuoa' na 'mimi kwa hakika ningependa unishauri wakati eda yako inaisha,' na mfano wa hayo. Basi hili linaruhusika kwa sababu siyo kama kusema waziwazi. Na ni jambo ambalo huwa kuna msukumo mkubwa wa kulifanya katika nafsi. Na ndio maana alisema, "au mkalificha ndani ya nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu alikwisha jua kwamba nyinyi mtawakumbuka." Na haya maelezo yote ni kuhusiana na utangulizi wa mkataba wa nikaha. Na ama mkataba wa ndoa, huo hauruhusiki, "mpaka andiko (la amri ya eda) lifike muda wake," yani mpaka eda imalizike. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika anajua yaliyomo katika nafsi zenu." Yani kusudieni mema, wala msikusudie maovu; kwa kuhofia adhabu yake na kutarajia malipo yake mazuri. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe;" kwa anayefanya dhambi kisha akazitubia. Na akarejea kwa Mola wake Mlezi "Mpole" kwa kuwa hakuwaharakishia adhabu waasi juu ya dhambi zao, pamoja na uwezo wake juu yao.
: 236 #
{لَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِنْ طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ (236)}
(236) Hakuna ubaya wowote juu yenu mkiwataliki wanawake ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari yao. Lakini wapeni cha kuwaliwaza, mwenye wasaa kwa kiwango awezacho na mwenye dhiki kwa kiwango awezacho, maliwazo kwa wema, ni haki juu ya watendao mema.
#
{236} أي: ليس عليكم ـ يا معشر الأزواج ـ جناح وإثم بتطليق النساء قبل المسيس وفرض المهر وإن كان في ذلك كسر لها فإنه ينجبر بالمتعة فعليكم أن تمتعوهن؛ بأن تعطوهن شيئاً من المال جبراً لخواطرهن {على الموسع قدره وعلى المقتر}؛ أي: المعسر، {قدره}؛ وهذا يرجع إلى العرف وأنه يختلف باختلاف الأحوال ولهذا قال: {متاعاً بالمعروف}؛ فهذا حق واجب {على المحسنين}؛ ليس لهم أن يبخسوهن، فكما تسببوا لتشوفهن واشتياقهن وتعلق قلوبهن، ثم لم يعطوهن ما رغبن فيه فعليهم في مقابلة ذلك المتعة. فلله ما أحسن هذا الحكم الإلهي وأدله على حكمة شارعه ورحمته! ومن أحسن من الله حكماً لقوم يوقنون؟! فهذا حكم المطلقات قبل المسيس وقبل فرض المهر، ثم ذكر حكم المفروض لهن فقال:
{236} Yani hakuna juu yenu - enyi kundi la waume - ubaya na dhambi kuwataliki wanawake kabla ya kuwagusa, na kuwakatia mahari yao. Na ingawa katika hilo kuna kumvunja, lakini hilo linazibwa kwa kumpa cha kumliwaza. Kwa hivyo, ni juu yenu kuwapa kitu cha kuwaliwaza katika mali, ili kuwapoza fikira zao. "Mwenye wasaa kwa kiwango awezacho na mwenye dhiki kwa kiwango awezacho" na hilo ni linarudi kwa ada, na kwamba inatofautiana kulingana na hali. Na ndiyo maana akasema, "maliwazo kwa wema". Na hii ni haki ya wajibu "juu ya watendao mema". Hawana haki ya kuwapunja. Na kwa vile walivyowafanya watarajie ndoa, na mioyo yao ikafungamana nao, lakini hawakuwapa walichokuwa wakitaka. Basi ni lazima badala ya hayo wawape cha kuwaliwaza. Wallahi! Ni hukumu nzuri hii ya Mwenyezi Mungu, na yenye kuashiriaje hekima ya aliyeiweka kama sheria na rehema zake? Na ni nani aliye bora zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini? Na hii ni hukumu ya wanawake waliotalikiwa kabla ya kuguswa, na kabla ya kuwabainishia mahari yao. Kisha akataja hukumu ya wale waliobainishiwa mahari yao, akasema:
: 237 #
{وَإِنْ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِنْ قَبْلِ أَنْ تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَنْ يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ وَأَنْ تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى وَلَا تَنْسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ إِنَّ اللَّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (237)}
(237) Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa, na tayari mmeshawakatia mahari mahususi, basi wapeni nusu ya mahari mliyowakatia. Isipokuwa ikiwa wanawake wenyewe watasamehe, au amesamehe yule ambaye fundo la ndoa liko mkononi mwake. Na mkisamehe ndiyo kuwa karibu zaidi na uchamungu. Wala msisahau fadhila zilizo baina yenu. Hakika, Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda.
#
{237} أي: إذا طلقتم النساء قبل المسيس وبعد فرض المهر فللمطلقات من المهر المفروض نصفه ولكم نصفه، هذا هو الواجب ما لم يدخله عفو ومسامحة بأن تعفو عن نصفها لزوجها إذا كان يصح عفوها، {أو يعفو الذي بيده عقدة النكاح}؛ وهو الزوج على الصحيح لأنه الذي بيده حل عقدته، ولأن الولي لا يصح أن يعفو عن ما وجب للمرأة لكونه غير مالك ولا وكيل، وقيل: إنه الأب وهو الذي يدل عليه لفظ الآية الكريمة. ثم رغب في العفو وأن من عفا كان أقرب لتقواه لكونه إحساناً موجباً لشرح الصدر، ولكون الإنسان لا ينبغي أن يهمل نفسه من الإحسان والمعروف، وينسى الفضل الذي هو أعلى درجات المعاملة، لأن معاملة الناس فيما بينهم على درجتين: إما عدل وإنصاف واجب، وهو أخذ الواجب وإعطاء الواجب، وإما فضل وإحسان، وهو إعطاء ما ليس بواجب والتسامح في الحقوق والغض مما في النفس، فلا ينبغي للإنسان أن ينسى هذه الدرجة ولو في بعض الأوقات، وخصوصاً لمن بينك وبينه معاملة أو مخالطة، فإن اللهَ مجازٍ المحسنين بالفضل والكرم، ولهذا قال: {إن الله بما تعملون بصير}. ثم قال تعالى:
{237} Yani mkiwataliki wanawake kabla ya kuwagusa, na baada ya kuwakatia mahari maalumu, basi wanawake hao waliotalikiwa wana nusu ya mahari iliyokatwa, nanyi mna nusu yake. Hilo ndilo la wajibu, maadamu halijaingiliwa na kusamahe na kutupilia mbali, kwa namna kwamba mwanamke amsamehe mumewe nusu yake hiyo ikiwa msamaha wake ni sahihi. "Au amesamehe yule ambaye fundo la ndoa liko mkononi mwake" naye ni mume kulingana na rai iliyo sahihi. Kwa sababu, yeye ndiye ambaye mkononi mwake kuna kufungua fundo lake. Na kwa sababu msimamizi (wa mwanamke) si sahihi kwa kusamehe kile ambacho ni haki ya mwanamke, kwa sababu yeye si mmiliki (wa hilo) wala wakili (wa mwanamke). Na ilisemwa: Huyo ni baba, naye ndiye ambaye matamshi ya Aya hii tukufu yanaashiria. Kisha akahimiza kusamehe, na kwamba mwenye kusamehe, anakuwa karibu zaidi na kumcha Mungu. Kwa sababu ni wema unaolazimu kufunguka kwa kifua, na kwa sababu mtu hatakiwi kuipuuza nafsi yake katika suala la hisani na wema. Na anasahau fadhila ambazo ndizo daraja la juu zaidi za kuamiliana. Kwa sababu, kuamiliana na watu baina yao kwa wao kuna daraja mbili: Ima uadilifu ulio wajibu. Nao ni kuchukua kilicho wajibu na kupeana kilicho wajibu. Na ima fadhila na hisani. Nao ni kupeana kisicho wajibu, na kuwa rahisi wa kuamiliana katika haki zake, na kutoangalia yale yaliyomo ndani ya nafsi yake. Hivyo basi, mtu hafai kusahau daraja hii, angalau katika baadhi ya nyakati. Hasa kwa yule ambaye kati yako na yeye kuna kuamiliana au kuchanganyika. Kwani Mwenyezi Mungu huwalipa wafanyao wema kwa fadhila na ukarimu. Na ndiyo maana akasema, "hakika, Mwenyezi Mungu anayaona vyema mnayoyatenda." Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:
: 238 - 239 #
{حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَى وَقُومُوا لِلَّهِ قَانِتِينَ (238) فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا فَإِذَا أَمِنْتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُمْ مَا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ (239)}
(238) Zilindeni Swala, na hasa Swala ya katikati. Na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu. (239) Na mkiwa na hofu, basi (swalini) hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyowafunza yale ambayo hamkuwa mnayajua.
#
{238} يأمر تعالى بالمحافظة {على الصلوات}؛ عموماً وعلى، {الصلاة الوسطى}؛ وهي العصر خصوصاً، والمحافظة عليها أداؤها بوقتها وشروطها وأركانها وخشوعها وجميعِ ما لها من واجب ومستحب. وبالمحافظة على الصلوات تحصل المحافظة على سائر العبادات وتفيد النهيَ عن الفحشاء والمنكر، خصوصاً إذا أكملها كما أمر بقوله: {وقوموا لله قانتين}؛ أي: ذليلين مخلصين خاشعين، فإن القنوت دوام الطاعة مع الخشوع.
{238} Mwenyezi Mtukufu anaamrisha kuzihifadhi "swala" kwa ujumla, na na hususan "swala ya katikati" ambayo ni swala ya Alasiri. Na kuzihifadhi ni kuzitekeleza kwa wakati wake, na masharti yake, na nguzo zake, na kunyenyekea kwake, na kila faradhi zake na yale yanayopendekezwa. Na kwa kuzihifadhi swala, kunapatikana kuzihifadhi ibada zinginezo zote. Na pia kunaleta kumkataza mtu machafu na maovu. Hasa akizikamilisha kama alivyoamrishwa, kwa kauli yake: "Na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu." Yani kwa kudhalilika, na ikhlasi na kunyenyekea. Kwani maana, Qunuut ni kufanya utiifu kwa daima pamoja na kunyenyekea.
#
{239} وقوله: {فإن خفتم}؛ حذف المتعلق ليعم الخوف من العدو والسبع وفواتِ ما يتضرر العبد بفوته فصلوا {رجالاً}؛ ماشين على أرجلكم، {أو ركباناً}؛ على الخيل والإبل وسائر المركوبات، وفي هذه الحال لا يلزمه الاستقبال. فهذه صفة صلاة المعذور بالخوف فإذا حصل الأمن صلى صلاة كاملة ويدخل في قوله: {فإذا أمنتم فاذكروا الله}؛ تكميل الصلوات، ويدخل فيه أيضاً الإكثار من ذكر الله شكراً له على نعمة الأمن وعلى نعمة التعليم لما فيه سعادة العبد. وفي الآية الكريمة فضيلة العلم وأن على من علمه الله ما لم يكن يعلم الإكثارَ من ذكر الله، وفيه الإشعارُ أيضاً أن الإكثار من ذكره سبب لتعليم علوم أخر لأن الشكر مقرون بالمزيد. ثم قال تعالى:
{239} Na kauli yake, "na mkiwa na hofu" kimefutwa kinachohofiwa; ili (Aya) ienee hofu ya adui na mnyama mwitu na kupotea kwa yale ambayo mja atadhurika kwa kupotea kwake. Basi swalini, "hali ya kuwa mnakwenda kwa miguu au mmepanda" juu ya farasi, ngamia na vipando vinginevyo. Na katika hali hii haimlazimu (mtu) kuelekea kibla. Basi hii ndiyo namna (sifa) ya swala ya mwenye udhuru ya hofu. Na amani itakapotokea, ataswali swala kamili. Na inaingia katika kauli yake, "na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu," kuzikamilisha swala. Na inaingia humo pia kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa kumshukuru juu ya neema ya amani, na juu ya neema ya kufundisha (waja) yale ambayo yana furaha ya mja ndani yake. Na katika Aya hii tukufu, kuna fadhila ya elimu. Na kwamba yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfundisha yale ambayo hakuwa anayajua amkumbuke Mwenyezi Mungu kwa wingi. Na pia ndani yake kuna kujulisha ya kwamba kumkumbuka kwa wingi ni sababu ya kufundishwa elimu zingine. Kwa sababu, kushukuru kumefungamanishwa na kuzidishiwa. Kisha yeye Mtukufu akasema:
: 240 #
{وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنْكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِأَزْوَاجِهِمْ مَتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِي مَا فَعَلْنَ فِي أَنْفُسِهِنَّ مِنْ مَعْرُوفٍ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (240)}
(240) Na wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanawaacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumbani. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika yale waliyojifanyia wenyewe kwa wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{240} اشتهر عند كثير من المفسرين أن هذه الآية الكريمة نسختها الآية التي قبلها وهي قوله تعالى: {والذين يتوفون منكم ويذرون أزواجاً يتربصن بأنفسهن أربعة أشهر وعشراً}؛ وأن الأمر كان على الزوجة أن تتربص حولاً كاملاً ثم نسخ بأربعة أشهر وعشر، ويجيبون عن تقدم الآية الناسخة أن ذلك تقدم في الوضع لا في النزول لأن شرط الناسخ أن يتأخر عن المنسوخ، وهذا القول لا دليل عليه، ومن تأمل الآيتين اتضح له أن القول الآخر في الآية هو الصواب، وأن الآية الأولى في وجوب التربص أربعة أشهر وعشراً على وجه التحتيم على المرأة، وأما في هذه الآية فإنها وصية لأهل الميت أن يبقوا زوجة ميتهم عندهم حولاً كاملاً جبراً لخاطرها وبرًّا بميتهم، ولهذا قال: {وصية لأزواجهم}؛ أي: وصية من الله لأهل الميت أن يستوصوا بزوجته ويمتعوها ولا يخرجوها، فإن رغبت أقامت في وصيتها وإن أحبت الخروج فلا حرج عليها، ولهذا قال: {فإن خرجن فلا جناح عليكم فيما فعلن في أنفسهن}؛ أي: من التجمل واللباس، لكن الشرط أن يكون بالمعروف الذي لا يخرجها عن حدود الدين والاعتبار. وختم الآية بهذين الاسمين العظيمين الدالين على كمال العزة وكمال الحكمة، لأن هذه أحكام صدرت عن عزته، ودلت على كمال حكمته حيث وضعها في مواضعها اللائقة بها.
{240} Inajulikana kwa wafasiri wengi kwamba Aya hii tukufu ilifutwa na Aya ya kabla yake, ambayo ni kauli yake Mola Mtukufu. "Na wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanawaacha wake, basi wake hawa wazizuie nafsi zao miezi minne na siku kumi." Na kwamba jambo lilikuwa kwamba mke alilazimika kujizuia mwaka mzima, kisha likafutwa kwa miezi minne na usiku kumi. Na wanajibu kuhusu kutanguliza Aya iliyofuta (mbele ya Aya iliyofutwa) kuwa huko ni kutangulia tu katika mahali (pa Aya katika Qur-ani), na si katika kuteremka kwake. Kwa sababu, sharti la Aya yenye kufuta ni kwamba ije nyuma ya ile aliyofutwa. Na kauli hii haina ushahidi juu yake. Na mwenye kuzitafakari Aya mbili hizi, itamdhihirikia kuwa ile kauli nyingine kuhusu Aya hii ndiyo sahihi. Na kwamba Aya ya kwanza yenye uwajibu wa kujizuia miezi minne na usiku kumi ni jambo la lazima kwa mwanamke. Na ama katika Aya hii, ina wasia kwa jamaa za maiti kwamba, waendelee kubaki pamoja na mke wa maiti wao kwa muda wa mwaka mzima ili kupoza fikira zake na kumfanyia wema maiti wao. Na ndio maana akasema, "na wausie kwa ajili ya wake zao." Yani ni wasia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa jamaa za maiti kwamba, watafute ushauri kutoka kwa mkewe, na wampe cha kumliwaza, na wasimtoe nje. Na akitaka, basi ataendelea kukaa katika wasia wake, na akipenda kuondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yake. Na ndiyo maana akasema, "na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hakuna ubaya wowote juu yenu katika waliyojifanyia wenyewe kwa wema." Yani kama vile kujirembesha na (kuvalia) mavazi (mazuri), lakini sharti ni kwamba yawe hayo kwa wema ambao hauyatoi nje ya mipaka ya dini na kuzingatia. Na akahitimisha Aya kwa majina haya mawili makubwa yanayoashiria ukamilifu wa nguvu yake na ukamilifu wa hekima yake. Kwa sababu, hukumu hizi zilitokana na nguvu yake, na zinaashiria ukamilifu wa hekima yake, kwa kuwa iliziweka katika mahali pake panapozifaa.
: 241 - 242 #
{وَلِلْمُطَلَّقَاتِ مَتَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ (241) كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ (242)}
(241) Na wanawake waliotalikiwa wapewe cha kuwaliwaza kwa wema. Hii ni haki juu ya wachamungu. (242) Namna hivi ndivyo anavyowabainishia Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu.
#
{241 - 242} لما بين في الآية السابقة إمتاع المفارقة بالموت ذكر هنا أن كل مطلقة فلها على زوجها أن يمتعها ويعطيها ما يناسب حاله وحالها وأنه حق إنما يقوم به المتقون، فهو من خصال التقوى الواجبة أو المستحبة، فإن كانت المرأة لم يسم لها صداق وطلقها قبل الدخول فتقدم أنه يجب عليه بحسب يساره وإعساره، وإن كان مسمى لها فمتاعها نصف المسمى، وإن كانت مدخولاً بها صارت المتعة مستحبة في قول جمهور العلماء ومن العلماء من أوجب ذلك استدلالاً بقوله: {حقاً على المتقين}؛ والأصل في الحق أنه واجب خصوصاً وقد أضافه إلى المتقين، وأصل التقوى واجبة، فلما بين تعالى هذه الأحكام الجليلة بين الزوجين؛ أثنى على أحكامه، وعلى بيانه لها وتوضيحه، وموافقتها للعقول السليمة، وأن القصد من بيانه لعباده أن يعقلوا عنه ما بينه فيعقلونها حفظاً وفهماً وعملاً بها، فإن ذلك من تمام عقلها.
{241 - 242} Alipoeleza katika Aya iliyotangulia kuwaliwaza wanawake walioachwa kwa sababu ya mauti; akataja hapa kwamba, kila mwanamke aliyetalikiwa ana haki kwa mumewe kumpa cha kumliwaza. Na kumpa kinacholingana na hali yake na hali ya mkewe, na kwamba ni haki waifanyayo wachamungu peke yake. Kwa hivyo, ni miongoni mwa sifa za uchamungu za lazima au za kupendekezwa. Basi ikiwa mwanamke huyo hakubainishiwa mahari maalumu, na akamtaliki kabla ya kuingiliana naye, basi imeshatangulia kuwa inamlazimu mahari kulingana na uwezo wepesi wake na uzito wake. Na kama ameshabainishiwa, basi maliwazo yake yatakuwa nusu ya hicho kilichotajwa. Na akiwa aliingiliwa, basi inapendekezwa kumliwaza kulingana na kauli ya wanachuoni. Na miongoni mwa wanachuoni, kuna wale walioliwajibisha hilo kwa tumia ushahidi wa kauli yake; "ni haki juu ya wachamungu." Na hali ya asili ya haki ni kuwa ni wajibu, hasa na imeifungamanishwa na wachamungu. Na hali ya asili ya uchamungu ni uwajibu. Na Mola Mtukufu alipozibainisha hukumu hizi tukufu kati ya wanandoa wawili, akazisifu hukumu zake. Na kuzibainisha kwake, na kuziweka kwake waziwazi, na kukubaliana kwake na akili zilizo timamu. Na kwamba makusudio ya kuzibainisha kwa waja wake ni kwamba waelewe kutoka kwake yale aliyoyaeleza. Kwa hivyo, wanazielewa kwa kuzihifadhi, na kuzifahamu, na kuzitendea kazi. Kwani, hayo ndiyo katika ukamilifu wa kuzielewa.
: 243 #
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ (243)}
(243) Je, hukuwaona wale waliotoka katika maboma yao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Na Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akawahuisha. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.
#
{243} أي: ألم تسمع بهذه القصة العجيبة الجارية على من قبلكم من بني إسرائيل حيث حل الوباء بديارهم فخرجوا بهذه الكثرة فراراً من الموت فلم ينجِهِمُ الفرارُ ولا أغنى عنهم من وقوع ما كانوا يحذرون، فعاملهم بنقيض مقصودهم وأماتهم الله عن آخرهم، ثم تفضل عليهم فأحياهم إما بدعوة نبي كما قاله كثير من المفسرين وإما بغير ذلك، ولكن ذلك بفضله وإحسانه وهو لا يزال فضله على الناس وذلك موجب لشكرهم لنعم الله بالاعتراف بها وصرفها في مرضاة الله ومع ذلك فأكثر الناس قد قصروا بواجب الشكر. وفي هذه القصة عبرة بأنه على كل شيء قدير وذلك آية محسوسة على البعث؛ فإن هذه القصة معروفة منقولة نقلاً متواتراً عند بني إسرائيل ومن اتصل بهم، ولهذا أتى بها تعالى بأسلوب الأمر الذي قد تقرر عند المخاطبين، ويحتمل أن هؤلاء الذين خرجوا من ديارهم خوفاً من الأعداء وجبناً عن لقائهم، ويؤيد هذا أن الله ذكر بعدها الأمر بالقتال وأخبر عن بني إسرائيل أنهم كانوا مخرجين من ديارهم وأبنائهم، وعلى الاحتمالين فإن فيها ترغيباً في الجهاد وترهيباً من التقاعد عنه وأن ذلك لا يغني عن الموت شيئاً {قل لو كنتم في بيوتكم لبرز الذين كتب عليهم القتل إلى مضاجعهم}.
{243} Yani, je, haukukisikia kisa hiki cha ajabu kilichowatokea wale waliokuwa kabla yenu miongoni mwa Wana wa Israili. Wakati ugonjwa ulipofika katika makazi yao, kwa hivyo wakatoka kwa wingi huu wakiyakimbia mauti. Lakini kukumbia huko hakukuwaokoa, wala hakukuwasaidia kutokana na kuingia katika yale waliyokuwa wakiyatahadhari. Basi akawafanyia kinyume cha makusudio yao, na Mwenyezi Mungu akawafisha hadi mwisho wao. Kisha akawafanyia hisani. Na akawahuisha ima kwa dua ya Nabii kama walivyosema wengi wa wafasiri; na ima kwa lisilokuwa hilo. Lakini hilo ni kwa sababu ya fadhila zake na hisani yake. Naye haijaacha fadhila yake kuwa juu ya watu. Na hilo linawalazimu kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu kwa kuzikubali na kuzitumia katika radhi za Mwenyezi Mungu. Na pamoja na hayo, watu wengi wamepuuza katika wajibu wa kushukuru. Na katika kisa hiki kuna somo kwamba Yeye ana uwezo juu ya kila kitu. Na hiyo ni dalili inayoonekana ya ufufuo. Kwa maana kisa hiki kinajulikana, na kusimuliwa kusimuliwa kusikokuwa na shaka yoyote kwa Wana wa Israili na wale wanaohusiana nao. Na kwa sababu hii ndiyo Mola Mtukufu akakileta kwa mtindo wa amri ambayo inajulikana vizuri miongoni mwa wale walioongeleshwa. Na inawezekana kwamba ni wale waliotoka katika maboma yao kwa sababu ya kuhofia maadui na woga wa kukutana nao. Na hili linaungwa mkono na ukweli kwamba Mwenyezi Mungu alitaja baada ya hapo amri ya kupigana vita. Na akajulisha kuhusu Wana wa Israili kwamba walikuwa wametolewa katika maboma yao na watoto wao. Na kwa uwezekano huu muwili, ndani yake kuna himizo la kufanya jihadi na onyo dhidi ya kukaa na kuiacha. Na kwamba hayo hayafai kitu kutokana na mauti, "Sema: Hata mngelikuwa katika nyumba zenu, basi wangelitoka wale walioandikiwa kuuawa, wakaenda hadi mahali pao pa kufia."
: 244 - 245 #
{وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (244) مَنْ ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً وَاللَّهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ (245)}
(244) Na piganeni vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Msikizi, Mjuzi. (245) Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema; ili amzidishie mizidisho mingi. Na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na kwake Yeye mtarejeshwa.
#
{244 - 245} جمع الله بين الأمر بالقتال في سبيله بالمال والبدن؛ لأن الجهاد لا يقوم إلا بالأمرين، وحث على الإخلاص فيه بأن يقاتل العبد لتكون كلمة الله هي العليا فإن الله {سميع}؛ للأقوال وإن خفيت {عليم}؛ بما تحتوي عليه القلوب من النيات الصالحة وضدها. وأيضاً فإنه إذا علم المجاهد في سبيله أن الله سميع عليم، هان عليه ذلك وعلم أنه بعينه ما يتحمل المتحملون من أجله وأنه لا بد أن يمدهم بعونه ولطفه. وتأمل هذا الحث اللطيف على النفقة وإن المنفق قد أقرض الله الملي الكريم ووعده المضاعفة الكثيرة كما قال تعالى: {مثل الذين ينفقون أموالهم في سبيل الله كمثل حبة أنبتت سبع سنابل في كل سنبلة مائة حبة، والله يضاعف لمن يشاء والله واسع عليم}؛ ولما كان المانع الأكبر من الإنفاق خوفَ الإملاقِ أخبر تعالى أنَّ الغنى والفقرَ بيد الله، وأنه يقبض الرزق على من يشاء ويبسطه على من يشاء، فلا يتأخر من يريد الإنفاق خوفَ الفقر، ولا يظن أنه ضائع، بل مرجع العباد كلهم إلى الله فيجد المنفقون والعاملون أجرهم عنده مدخراً أحوج ما يكونون إليه، ويكون له من الوقع العظيم ما لا يمكن التعبير عنه. والمراد بالقرض الحسن هو ما جمع أوصاف الحسن من النية الصالحة وسماحة النفس بالنفقة ووقوعها في محلها وأن لا يتبعها المنفِقُ مَنًّا ولا أذىً ولا مبطلاً ومنقصاً.
{244 - 245} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiunganisha pamoja amri ya kupigana vita katika njia yake kwa mali na mwili. Kwa sababu, jihadi haisimami isipokuwa kwa mambo mawili haya. Na alihimiza juu ya kuwa na ikhlasi ndani yake kwamba mja apigane ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu. Kwa maana, kwa hakika Mwenyezi Mungu "ni Mwenye kusikia" maneno hata yakifichika. "Ni mwenye elimu" juu yale yaliyomo ndani ya nyoyo kama vile nia njema na kinyume chake. Pia yule anayefanya jihadi katika njia yake anapojua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye elimu, hilo linamuwiya rahisi. Na anajua kwamba hakika Yeye ni wale wanaovumilia kwa ajili Yake, na kwamba hakuna budi awape msaada na wema wake. Na tafakari kuhimiza huku kupole juu ya kutoa, na kwamba mtoaji huwa amemkopesha Mwenyezi Mungu, Tajiri, Mwingi wa ukarimu. Na akamuahidi mizidisho mingi, kama alivyosema Mola Mtukufu. "Mfano wa wale wanaotumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua." Na kwa vile kizuizi kikubwa kinachozuia kutoa ni kuhofia umasikini, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa utajiri na umasikini vimo mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba Yeye huikunja riziki kwa amtakaye, na huikunjua kwa amtakaye. Basi na asichelewe anayetaka kutoa kwa kuhofia umasikini. Na wala asifikirie kuwa amepoteza, bali marejeo ya waja wote ni kwa Mwenyezi Mungu. Kisha watoaji na watendaji kazi watapata malipo yao kwake; wameekewa akiba watakapokuwa wanayahitaji zaidi. Na hilo litawaathiri vikubwa kiasi ambacho haiwezekani kueleza. Na maana ya mkopo mzuri ni ule unaojumuisha sifa za wema kama vile nia njema na ukunjufu wa nafsi wakati wa kutoa. Na kuifikisha katika mahali pake, na kwamba mtoaji asiufuatishe kwa masimbulizi. Wala udhia, wala kubatilisha na kupunguza.
: 246 - 252 #
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الْمَلَإِ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى إِذْ قَالُوا لِنَبِيٍّ لَهُمُ ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ أَلَّا تُقَاتِلُوا قَالُوا وَمَا لَنَا أَلَّا نُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِنْ دِيَارِنَا وَأَبْنَائِنَا فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ تَوَلَّوْا إِلَّا قَلِيلًا مِنْهُمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ (246) وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا قَالُوا أَنَّى يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِنَ الْمَالِ قَالَ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ وَاللَّهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ (247) وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَنْ يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَى وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (248) فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللَّهَ مُبْتَلِيكُمْ بِنَهَرٍ فَمَنْ شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَنْ لَمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّي إِلَّا مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ فَشَرِبُوا مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِنْهُمْ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ قَالُوا لَا طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُمْ مُلَاقُو اللَّهِ كَمْ مِنْ فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّهِ وَاللَّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ (249) وَلَمَّا بَرَزُوا لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُوا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (250) فَهَزَمُوهُمْ بِإِذْنِ اللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُودُ جَالُوتَ وَآتَاهُ اللَّهُ الْمُلْكَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُ مِمَّا يَشَاءُ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّهِ النَّاسَ بَعْضَهُمْ بِبَعْضٍ لَفَسَدَتِ الْأَرْضُ وَلَكِنَّ اللَّهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْعَالَمِينَ (251) تِلْكَ آيَاتُ اللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ (252)}.
(246) Je, hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baada ya Musa, walipomwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Je, haielekei ikiwa mtaandikiwa vita kuwa msipigane? Wakasema: Itakuwaje tusipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ilhali tumeshatolewa katika maboma yetu na watoto wetu? Lakini walipoandikiwa kupigana vita, wakageuka, isipokuwa wachache miongoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema madhalimu. (247) Na Nabii wao akawaambia: Hakika, Mwenyezi Mungu ameshawateulia Taluti (Sauli) kuwa ndiye mfalme. Wakasema: Vipi atakuwa na ufalme juu yetu, ilhali sisi tuna haki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa mali? Akasema: Hakika, Mwenyezi Mungu amemteua yeye juu yenu na amemzidishia ukunjufu wa elimu na kiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. (248) Na Nabii wao akawaambia: Hakika, alama ya ufalme wake ni kwamba awaletee lile sanduku ambalo ndani yake mna kituliza nyoyo zenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na mabaki ya waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Harun, linalobebwa na Malaika. Bila shaka, katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. (249) Basi Taluti alipoondoka na majeshi, alisema: Hakika, Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa mto. Hivyo basi, atakayekunywa humo, si pamoja nami. Na yule asiyeyaonja, basi huyo atakuwa pamoja nami; ila atakayeteka humo kiasi ya kitanga cha mkono wake. Lakini walikunywa humo isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Na alipovuka mto yeye na wale walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Ni makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri. (250) Na walipotoka ili kupambana na Jaluti na majeshi yake, walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utunusuru juu ya watu hawa Makafiri. (251) Kwa hivyo, wakawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na Daudi akamuua Jaluti. Na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hekima, na akamfundisha katika aliyoyapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawazuii watu kwa watu, basi dunia ingeliharibika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote. (252) Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume.
#
{246 - 247} يقص الله تعالى هذه القصة على الأمة ليعتبروا وليرغبوا في الجهاد ولا ينكلوا عنه، فإن الصابرين صارت لهم العواقب الحميدة في الدنيا والآخرة والناكلين خسروا الأمرين، فأخبر تعالى أن أهل الرأي من بني إسرائيل وأصحاب الكلمة النافذة تراودوا في شأن الجهاد واتفقوا على أن يطلبوا من نبيهم أن يعين لهم ملكاً لينقطع النزاع بتعيينه وتحصلَ الطاعة التامة ولا يبقى لقائل مقال، وأن نبيهم خشي أن طلبهم هذا مجردُ كلام لا فعل معه، فأجابوا نبيهم بالعزم الجازم وأنهم التزموا ذلك التزاماً تامًّا، وأن القتال متعين عليهم حيث كان وسيلة لاسترجاع ديارهم ورجوعهم إلى مقرهم ووطنهم، وأنه عين لهم نبيهم طالوت ملكاً يقودهم في هذا الأمر الذي لا بد له من قائد يحسن القيادة، وأنهم استغربوا تعيينه لطالوت وثَمَّ من هو أحق منه بيتاً وأكثر مالاً، فأجابهم نبيهم: إن الله اختاره عليكم بما آتاه الله من قوة العلم بالسياسة وقوة الجسم، اللذين هما آلة الشجاعة والنجدة وحسن التدبير، وأن الملك ليس بكثرة المال، ولا بكون صاحبه ممن كان الملك والسيادة في بيوتهم، فالله يؤتي ملكه من يشاء. ثم لم يكتف ذلك النبي الكريم بتقنيعهم بما ذكره من كفاءة طالوت واجتماع الصفات المطلوبة فيه حتى قال لهم:
{246 - 247} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawasimulia watu kisa hiki ili wakizingatie na wapate moyo wa kufanya jihadi, na wasiwe na uoga juu yake. Kwa maana, wale wanaosubiri walipata matokeo ya kusifiwa katika dunia na Akhera, nao wenye uoga walipata hasara ya mawili hayo. Kwa hivyo, Mola Mtukufu akajulisha kwamba watu wenye maoni miongoni mwa Wana wa Israili na watu wa neno lenye taathira, walijadiliana kuhusu jambo la jihadi. Na wakaafikiana juu ya kwamba wamuombe Nabii wao awawekee mfalme, ili mzozo huo ukatike kwa yeye kumteua. Na upatikane utiifu kamili, na ili mwenye kusema asibaki na la kusema. Na kwamba Nabii wao huyo alichelea kwamba kuomba kwao huko ni mazungumzo matupu tu, yasiyokuwa na matendo pamoja nao. Basi wakamjibu Nabii wao kwa dhamira thabiti, na kwamba watashikamana na hilo kushikamana kukamilifu. Na kwamba kupigana vita kulikuwa ni lazima juu yao; kwani, ilikuwa ndiyo njia ya kuzirudisha maboma yao, na kurejea kwao katika makazi yao na nchi yao. Na kwamba Nabii wao aliwateulia Taluti kuwa mfalme wa kuwaongoza katika jambo hili, ambalo lazima liwe na kiongozi ambaye ni mzuri katika uongozi. Na kwamba walishangazwa na uteuzi wake wa Taluti licha ya kuwepo yule anayestahiki zaidi kwa sababu ya (heshima ya ki) nyumba na mwenye mali zaidi yake. Basi Nabii wao akawajibu: Hakika Mwenyezi Mungu amemteua juu yenu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa ya nguvu ya elimu ya kuongoza, na nguvu za mwili, ambazo mbili hizo ndizo zana za ujasiri, na kupeana msaada, na uedeshaji mambo vizuri, na kwamba ufalme si kwa wingi wa mali, wala kwa sababu tu kwamba mwenye ufalme ni miongoni mwa wale ambao ufalme na utukufu uko katika nyumba zao. Kwani, Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. Kisha Nabii huyo mtukufu hakutosheka na kuwashawishi na yale aliyoyataja kuhusu umahiri wa Taluti na kukutana kwa sifa zinazohitajika ndani yake mpaka alipowaambia:
#
{248} {إن آية ملكه أن يأتيكم التابوت فيه سكينة من ربكم وبقية مما ترك آل موسى وآل هارون}؛ وكان هذا التابوت قد استولت عليه الأعداء، فلم يكتفوا بالصفات المعنوية في طالوت ولا بتعيين الله له على لسان نبيهم حتى يؤيد ذلك هذه المعجزة ولهذا قال: {إن في ذلك لآية لكم إن كنتم مؤمنين}؛ فحينئذ سلموا وانقادوا. فلما ترأس فيهم طالوت وجندهم ورتبهم وفصل بهم إلى قتال عدوهم وكان قد رأى منهم من ضعف العزائم والهمم ما يحتاج إلى تمييز الصابر من الناكل فقال:
{248} "Hakika, alama ya ufalme wake ni kwamba awaletee lile sanduku ambalo ndani yake mna kituliza nyoyo zenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na mabaki ya waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Harun," na sanduku hilo lilikuwa limetwaliwa na maadui. Kwa hivyo, hawakutosheka na sifa za kimaadili katika Taluti, wala kwa Mwenyezi Mungu kumteua kwa ulimi wa Nabii wao mpaka muujiza huu uyatie hayo nguvu. Kwa hivyo, akasema, "bila shaka, katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini." Basi hapo wakajisalimisha na wakafuata. Na Taluti alipokwishakuwa kiongozi wao, na akawafanya kuwa majeshi, na akawapanga. Na akaondoka pamoja nao wakaenda kupigana na adui yao, na alikuwa ameona miongoni mwa udhaifu wa azimio na hima ambao ulihitaji kumtofautisha mwenye subira na mwoga, akasema:
#
{249 - 250} {إن الله مبتليكم بنهر}؛ تمرون عليه وقت حاجة إلى الماء، {فمن شرب منه فليس مني}؛ أي لا يتبعني؛ لأن ذلك برهان على قلة صبره ووفور جزعه {ومن لم يطعمه فإنه مني}؛ لصدقه وصبره، {إلا من اغترف غرفة بيده}؛ أي: فإنه مسامح فيها. فلما وصلوا إلى ذلك النهر وكانوا محتاجين إلى الماء شربوا كلهم منه {إلا قليلاً منهم}؛ فإنهم صبروا ولم يشربوا {فلما جاوزه هو والذين آمنوا معه قالوا}؛ أي: الناكلون أو الذين عبروا {لا طاقة لنا اليوم بجالوت وجنوده}؛ فإن كان القائلون هم الناكلين فهذا قول يبررون به نكولهم، وإن كان القائلون هم الذين عبروا مع طالوت فإنه حصل معهم نوع استضعاف لأنفسهم، ولكن شجعهم على الثبات والإقدام أهل الإيمان الكامل حيث قالوا: {كم من فئة قليلة غلبت فئة كثيرة بإذن الله والله مع الصابرين}؛ بعونه وتأييده ونصره فثبتوا وصبروا لقتال عدوهم جالوت وجنوده.
{249 - 250} "Hakika, Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa mto." Mtakaopita karibu nao wakati mtakapokuwa mnahitaji maji, "atakayekunywa humo, si pamoja nami" yani asinifuate. Kwa sababu, hiyo ni dalili ya uchache wa subira yake na wingi wa kutosubiri kwake. "Na yule asiyeyaonja, basi huyo atakuwa pamoja nami" kwa sababu ya ukweli wake na subira yake. "Isipokuwa yule atakayeteka humo kiasi ya kitanga cha mkono wake" yani huyo ameruhusiwa hilo. Na walipoufikia mto huo, nao walikuwa wanahitaji maji, wote wakanywa kutoka humo. "Wachache tu miongoni mwao" hao walisubiri na hawakunywa. "Na alipovuka mto yeye na wale walioamini pamoja naye, wakasema" yani waoga au wale waliovuka ng'ambo. "Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake." Ikiwa wanaosema ni wale waoga, basi hii ni kauli ambayo kwayo wanaifanya kuwa ndiyo sababu ya woga wao. Na ikiwa wanaosema ni wale waliovuka ng'ambo pamoja na Talut, basi ni kama walipatwa na namna fulani ya udhaifu katika nafsi zao. Lakini wenye imani kamili wakawatia moyo wawe imara na waende kupambana, waliposema: "Ni makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri" kwa msaada wake, na kutia kwake nguvu, na nusura yake. Kwa hivyo wakawa imara na wakasubiri ili kupigana vita na adui yao Jalut (Goliathi) na majeshi yake.
#
{251} {وقتل داود}؛ - صلى الله عليه وسلم -، {جالوت}؛ وحصل بذلك الفتح والنصر على عدوهم {وآتاه الله}؛ أي: داود {الملك والحكمة}؛ النبوة والعلوم النافعة وآتاه الله الحكمة وفصل الخطاب. ثم بين تعالى فائدة الجهاد فقال: {ولولا دفع الله الناس بعضهم ببعض لفسدت الأرض}؛ باستيلاء الكفرة والفجار وأهل الشر والفساد {ولكن الله ذو فضل على العالمين}؛ حيث لطف بالمؤمنين ودافع عنهم وعن دينهم بما شرعه وبما قدره. فلما بين هذه القصة قال لرسوله - صلى الله عليه وسلم -:
{251} "Na Daudi akamuua" rehema na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake "Jalut (Goliati)." Na kwa hilo wakapata ushindi na nusura juu ya adui yao. "Na Mwenyezi Mungu akampa." Yani Daudi, "ufalme na hekima" unabii na elimu zenye manufaa, na Mwenyezi Mungu akampa hekima na kukata hukumu. Kisha Mola Mtukufu akabainisha manufaa ya jihadi, akasema. "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawazuii watu wenyewe kwa wenyewe, basi dunia ingeliharibika." Kwa sababu ya kutawala kwa makafiri, na waovu, na watu wa shari na ufisadi. "Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote." Kwa kuwa aliwafanyia upole Waumini na akawatetea wao na dini yao kwa yale aliyoyaweka kama sheria na yale aliyokadiria. Na alipokibainisha kisa hiki, akamwambia Mtume wake rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
#
{252} {تلك آيات الله نتلوها عليك بالحق وإنك لمن المرسلين}؛ ومن جملة الأدلة على رسالته هذه القصة حيث أخبر بها وحياً من الله مطابقاً للواقع. وفي هذه القصة عِبَرٌ كثيرةٌ للأمة: منها: فضيلة الجهاد في سبيله وفوائده وثمراته وأنه السبب الوحيد في حفظ الدين وحفظ الأوطان وحفظ الأبدان والأموال، وأنَّ المجاهدين ولو شقت عليهم الأمور فإن عواقبهم حميدة، كما أن الناكلين ولو استراحوا قليلاً فإنهم سيتعبون طويلاً. ومنها: الانتداب لرياسة من فيه كفاءة وأن الكفاءة ترجع إلى أمرين: إلى العلم الذي هو علم السياسة والتدبير، وإلى القوة التي ينفذ بها الحق، وأن من اجتمع فيه الأمران فهو أحق من غيره. ومنها: الاستدلال بهذه القصة على ما قاله العلماء أنه ينبغي للأمير للجيوش أن يتفقدها عند فصولها؛ فيمنع من لا يصلح للقتال من رجال وخيل وركاب، لضعفه أو ضعف صبره أو لتخذيله أو خوف الضرر بصحبته، فإن هذا القسم ضرر محض على الناس. ومنها: أنه ينبغي عند حضور البأس تقوية المجاهدين وتشجيعهم وحثهم على القوة الإيمانية والاتِّكال الكامل على الله والاعتماد عليه، وسؤال الله التثبيت والإعانة على الصبر والنصر على الأعداء. ومنها: أن العزم على القتال والجهاد غير حقيقته، فقد يعزم الإنسان ولكن عند حضوره تنحل عزيمته، ولهذا من دعاء النبي - صلى الله عليه وسلم -: «أسألك الثبات في الأمر والعزيمة على الرشد» ، فهؤلاء الذين عزموا على القتال وأتوا بكلام يدل على العزم المصمم لما جاء الوقت نكص أكثرهم، ويشبه هذا قوله - صلى الله عليه وسلم -: «وأسألك الرضا بعد القضا» ؛ لأن الرضا بعد وقوع القضاء المكروه للنفوس هو الرضا الحقيقي.
{252} "Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume." Na miongoni mwa ushahidi wa ujumbe wake ni kisa hiki, ambapo alikisimulia kwa ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kikilingana na namna kilivyotokea. Na katika kisa hiki kuna masomo mengi kwa umma huu: Miongoni mwake ni fadhila za jihadi katika njia yake, manufaa yake na matunda yake. Na kwamba ndio sababu pekee ya kuihifadhi dini, kuihifadhi nchi, kuihifadhi miili na mali. Na kwamba wanaopigana jihadi hata kama mambo ni magumu kwao, mwisho wao ni wa kusifika. Kama vile wale wanaofanya woga hata wakipumzika kidogo, wao kwa hakika watachoka kwa muda mrefu. Na miongoni mwake ni kukasimisha uongozi kwa yule ambaye ana uwezo, na kwamba uwezo huo unarudi kwa mambo mawili: Kwa elimu ambayo ni elimu ya kuongoza na kuendesha mambo, na kwa nguvu ambayo anatekeleza kwayo haki. Na kwamba yeyote ambaye mawili haya yamekutana ndani yake, basi yeye ndiye anayestahiki zaidi kuliko mwingine. Na miongoni mwake ni kukitumia kisa hiki kama dalili juu ya yale waliyoyasema wanachuoni. Kwamba amiri jeshi anatakiwa kuwakagua majeshi wakati wa kutoka. Ili amzuie asiyefaa kupigana vita miongoni mwa wanajeshi wanaopigana kwa miguu, na wapanda farasi, na wapanda magari kwa sababu ya udhaifu wake, au udhaifu wa subira yake. Au kwa sababu ya udanganyifu wake, au hofu ya kupata madhara katika kuandamana naye. Kwa sababu, kundi hilo ni madhara matupu kwa watu. Na miongoni mwake ni kwamba vita vinapokuwepo, inafaa kuwatia nguvu wanaopigana jihadi, na kuwatia moyo. Na kuwahimiza kuwa na nguvu ya kiimani na kumwachia kabisa Mwenyezi Mungu mambo na kumtegemea Yeye. Na kumwomba Mwenyezi Mungu uimara na msaada katika subira na ushindi juu ya maadui. Na miongoni mwake ni kwamba kuazimia kupigana vita na kufanya jihadi siyo (vita wala jihadi) yenyewe. Kwa sababu, mtu anaweza kuazimia, lakini anapohudhuria, azimio lake hilo linakatika. Na ndiyo maana katika dua za Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ni: "Ninakuomba uimara katika jambo hili, na azimio juu ya uwongofu.” Ndiyo hawa walioazimia kupigana vita, na wakaja na maneno yanayoonyesha azimio kubwa. Na muda ulipofika, wengi wao walighairi. Na hili linafanana na kauli yake (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. “Na ninakuomba ridhaa baada ya kunikatia jambo." Kwa sababu, kuridhika baada ya kupitishwa kwa jambo linalochukiwa na nafsi ndiyo ridhaa ya kweli.
: 253 #
قوله تعالى: {تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ مِنْهُمْ مَنْ كَلَّمَ اللَّهُ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِنْ بَعْدِهِمْ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُمْ مَنْ آمَنَ وَمِنْهُمْ مَنْ كَفَرَ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَكِنَّ اللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ (253)}.
(253) Mitume hao tumewaboresha baadhi yao juu ya wengineo. Miongoni mwao kuna wale ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na akawapandisha vyeo baadhi yao. Na tukampa Isa mwana wa Maryam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho mtakatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelipigana wale waliokuwa baada yao, baada ya kujiwa na hoja zilizo wazi. Lakini walihitalifiana. Basi miongoni mwao kuna wale walioamini, na miongoni mwao kuna wale waliokufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelipigana. Lakini Mwenyezi Mungu hufanya kile akitakacho.
#
{253} يخبر الباري أنه فاوت بين الرسل في الفضائل الجليلة والتخصيصات الجميلة، بحسب ما منَّ الله به عليهم وقاموا به من الإيمان الكامل واليقين الراسخ والأخلاق العالية والآداب السامية والدعوة والتعليم والنفع العميم، فمنهم من اتخذه خليلاً، ومنهم من كلمه تكليماً، ومنهم من رفعه فوق الخلائق درجات، وجميعهم لا سبيل لأحد من البشر إلى الوصول إلى فضلهم الشامخ. وخص عيسى بن مريم أنه آتاه البينات الدالة على أنه رسول الله حقًّا وعبده صدقاً وأن ما جاء به من عند الله كله حق، فجعله يبرئ الأكمه والأبرص ويحيي الموتى بإذن الله وكلم الناس في المهد صبياً وأيده بروح القدس أي بروح الإيمان، فجعل روحانيتَهُ فائقةً روحانيةَ غيرِهِ، فحصل له بذلك القوة والتأييد، وإن كان أصل التأييد بهذه الروح عامًّا لكل مؤمن بحسب إيمانه كما قال: {وأيدهم بروح منه}؛ لكن ما لعيسى أعظم مما لغيره لهذا خصه الله بالذكر، وقيل: إن روح القدس هنا جبريل أيده الله بإعانته ومؤازرته لكن المعنى هو الأول. ولما أخبر عن كمال الرسل وما أعطاهم من الفضل والخصائص وأن دينهم واحد ودعوتهم إلى الخير واحدة، وكان موجب ذلك ومقتضاه أن تجتمع الأمم على تصديقهم والانقياد لهم لما آتاهم من البينات التي على مثلها يؤمن البشر، لكن أكثرهم انحرفوا عن الصراط المستقيم، ووقع الاختلاف بين الأمم فمنهم من آمن ومنهم من كفر ووقع لأجل ذلك الاقتتال، الذي هو موجب الاختلاف والتعادي، ولو شاء الله لجمعهم على الهدى فما اختلفوا، ولو شاء الله أيضاً بعدما وقع الاختلاف الموجب للاقتتال ما اقتتلوا، ولكن حكمته اقتضت جريان الأمور على هذا النظام بحسب الأسباب. ففي هذه الآية أكبر شاهد على أنه تعالى يتصرف في جميع الأسباب المقتضية لمسبباتها، وأنه إن شاء أبقاها وإن شاء منعها، وكل ذلك تبع لحكمته وحده فإنه فعال لما يريد، فليس لإرادته ومشيئته ممانع ولا معارض ولا معاون.
{253} Al-Bari (Muumba mwanzilishi) anajulisha kwamba Yeye alitofautisha kati ya Mitume katika fadhila kubwa na mateuzi mazuri. Kulingana na kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa na walichofanya wao kama vile imani kamili, yakini madhubuti, tabia na maadili ya juu, kulingania, kuelimisha na manufaa ya jumla. Miongoni mwao kuna yule aliyemfanya kuwa rafiki mwandani. Na miongoni mwao kuna yule aliyezungumza naye kwa maneno. Na miongoni mwao kuna yule aliyemnyanyua daraja juu ya viumbe. Na wote, hakuna njia kwa yeyote kati ya watu ya kufikia fadhila zao za juu mno. Na akamteua Isa bin Maryam kwa kumpa hoja zilizo wazi zenye kuoyesha kwamba yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa haki, na mja wake kwa ukweli. Na kwamba yale aliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni haki. Basi akamfanya kuwaponya vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma. Na akawafufuwa maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na aliwaongelesha watu katika malezi hali ya kuwa ni mtoto. Na akamtia nguvu kwa Roho mtakatifu. Yani kwa roho wa imani. Kwa hivyo, akaifanya hali yake ya kiroho kuwa bora zaidi ya hali za kiroho za wengine. Na akapata nguvu na kuungwa mkono kwa hilo. Hata ingawa asili ya kuungwa mkono na roho hii ni ya jumla kwa kila Muumini kulingana na imani yake, kama alivyosema. "Na akawaunga mkono kwa roho itokayo kwake". Lakini alicho nacho Isa ni kikubwa zaidi kuliko kile walicho nacho wengine. Na ndio maana Mwenyezi Mungu akamtaja hususan. Na ikasemwa: Roho Mtakatifu hapa ni Jibril, Mwenyezi Mungu alimuunga mkono kwa msaada na kumtia nguvu, lakini maana sawa ni ile ya kwanza. Na alipojulisha kuhusu ukamilifu wa Mitume na alichowapa katika fadhila na sifa maalumu. Na kwamba Dini yao ni moja, na wito wao kwa heri ni mmoja. Na ilikuwa inalazimu kwa sababu ya hilo kwamba umma zote zikusanyike juu ya kuwasadiki. Na kuwafuata kwa sababu ya yale aliyowapa miongoni mwa hoja zilizo wazi ambazo mfano wake watu waliamini. Lakini wengi wao walipotoka njia iliyonyooka, na hitilafu ikatokea kati ya umma. Basi miongoni mwao kuna wale walioamini na miongoni mwao kuna wale waliokufuru, kwa hivyo kwa sababu ya hilo vikatokea vita ambavyo ni matokeo ya hitilafu hiyo na uadui huo. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa, angeliwakusanya juu ya uwongofu, na wasingelihitalifiana. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa pia baada ya kutokea hitilafu hiyo iliyolazimu kupigana, hawangepigana. Lakini hekima yake ililazimu mambo yaende kulingana na mfumo huu kulingana na sababu. Basi katika aya hii kuna ushahidi mkubwa kabisa kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu anaziendesha sababu zote zinazolazimu matokeo yake, na kwamba akipenda, anazibakisha. Na akipenda, anazizuia. Na hayo yote yanafuata hekima yake peke yake. Kwani, yeye ndiye afanyaye atakalo. Kwa hivyo, mapenzi yake na kutaka kwake hakuna kizuizi chochote, wala mpinzani, wala msaidizi.
: 254 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنْفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُمْ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَ يَوْمٌ لَا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ (254)}
(254) Enyi mlioamini! Toeni katika tulivyowaruzuku kabla haijakuja Siku ambayo hapatakuwapo biashara yoyote, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio madhalimu.
#
{254} يحث الله المؤمنين على النفقات في جميع طرق الخير، لأن حذف المعمول يفيد التعميم، ويذكرهم نعمته عليهم بأنه هو الذي رزقهم ونوَّع عليهم النعم، وأنه لم يأمرهم بإخراج جميع ما في أيديهم بل أتى بِمِنْ الدالة على التبعيض، فهذا مما يدعوهم إلى الإنفاق، ومما يدعوهم أيضاً إخبارهم أن هذه النفقات مدخرة عند الله في يوم لا تفيد فيه المعاوضات بالبيع ونحوه ولا التبرعات ولا الشفاعات فكل أحد يقول ما قدمت لحياتي، فتنقطع الأسباب كلها إلا الأسباب المتعلقة بطاعة الله والإيمان به يوم لا ينفع مال ولا بنون إلا من أتى الله بقلب سليم. {وما أموالكم ولا أولادكم بالتي تقربكم عندنا زلفى إلا من آمن وعمل صالحاً فأولئك لهم جزاء الضعف بما عملوا وهم في الغرفات آمنون}، {وما تقدموا لأنفسكم من خير تجدوه عند الله هو خيراً وأعظم أجراً}. ثم قال تعالى: {والكافرون هم الظالمون}؛ وذلك لأن الله خلقهم لعبادته، ورزقهم، وعافاهم، ليستعينوا بذلك على طاعته، فخرجوا عما خلقهم الله له، وأشركوا بالله ما لم ينزل به سلطاناً، واستعانوا بنعمه على الكفر والفسوق والعصيان، فلم يبقوا للعدل موضعاً، فلهذا حصر الظلم المطلق فيهم.
{254} Mwenyezi Mungu anawahimiza Waumini watoe katika njia zote za heri. Kwa sababu, kufuta kwa njia zinazotolewa, kuna maana ya ujumla. Na anawakumbusha neema yake juu yao kwamba yeye ndiye aliyewaruzuku na akawapa aina mbalimbali za neema. Na kwamba hakuwaamrisha watoe chote kilichomo mikononi mwao. Bali alitumia "katika" linalomaanisha kutoa baadhi tu. Basi hili ndilo analowaita watoe. Na katika yale anayowaita kwayo pia, ni kuwaambia kuwa kutoa huku kunahifadhiwa kwa Mwenyezi Mungu katika siku ambayo mabadilishano hayatafaidi kitu kwa biashara na mfano wake. Na wala misaada, wala uombezi. Kwa hivyo, kila mtu atasema: Ni nini nilichotanguliza kwa ajili ya maisha yangu? Kwa hivyo, sababu zote zitakatika isipokuwa zile sababu zinazohusiana na utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na kumuamini siku ambayo mali haitafaidi kitu wala watoto. Isipokuwa yule atakayemjia Mwenyezi Mungu kwa moyo ulio sawa. "Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowaweka karibu nasi muwe karibu, isipokuwa aliyeamini na akatenda mema. Basi hao wana malipo maradufu kwa walioyafanya. Nao watakuwa na amani katika vyumba." "Na chochote mnachokitanguliza katika heri kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Mwenyezi Mungu, kimekuwa bora zaidi, na chenye malipo makubwa sana." Kisha Mola Mtukufu akasema: "Na makafiri ndio madhalimu." Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amewaumba kwa ajili ya kumuabudu, na akawaruzuku na akawaweka salama ili watafute msaada wa hayo katika kumtii. Lakini wakatoka katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumba kwa ajili yake, na wakamshirikisha Mwenyezi Mungu yale ambayo hajayateremshia mamlaka yoyote. Na wakatafuta msaada wa neema zake katika kumkufuru na kukiuka mipaka na kuasi. Kwa hivyo, hawakuuachia uadilifu mahali. Kwa sababu hiyo, ndiyo maana akaifanya dhuluma kubwa kabisa kuwa katika wao tu.
: 255 #
{اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مَنْ ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ (255)}
(255) Mwenyezi Mungu - hapana mungu isipokuwa Yeye, Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika elimu yake isipokuwa kwa kile akitakacho. Kursi yake imeenea mbingu na dunia, na wala halemewi na kuvilinda vyote viwili. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu.
#
{255} أخبر - صلى الله عليه وسلم - أن هذه الآية أعظم آيات القرآن لما احتوت عليه من معاني التوحيد والعظمة وسعة الصفات للباري تعالى، فأخبر أنه {الله}؛ الذي له جميع معاني الألوهية، وأنه لا يستحق الألوهية والعبودية إلا هو، فألوهية غيره وعبادة غيره باطلة، وأنه {الحي} الذي له جميع معاني الحياة الكاملة من السمع والبصر والقدرة والإرادة وغيرها من الصفات الذاتية، كما أن {القيوم}؛ تدخل فيه جميع صفات الأفعال لأنه القيوم الذي قام بنفسه واستغنى عن جميع مخلوقاته وقام بجميع الموجودات فأوجدها وأبقاها وأمدها بجميع ما تحتاج إليه في وجودها وبقائها. ومن كمال حياته وقيوميته أنه {لا تأخذه سنة}؛ أي: نعاس {ولا نوم}؛ لأن السنة والنوم إنما يعرضان للمخلوق الذي يعتريه الضعف والعجز والانحلال، ولا يعرضان لذي العظمة والكبرياء والجلال، وأخبر أنه مالك جميع ما في السماوات والأرض، فكلهم عبيد لله مماليك لا يخرج أحد منهم عن هذا الطور {إن كل من في السموات والأرض إلا آتي الرحمن عبداً}؛ فهو المالك لجميع الممالك وهو الذي له صفات الملك والتصرف والسلطان والكبرياء، ومن تمام ملكه أنه لا {يشفع عنده}؛ أحد {إلا بإذنه}؛ فكل الوجهاء والشفعاء عبيد له مماليك لا يَقْدِمُون على شفاعة حتى يأذن لهم {قل لله الشفاعة جميعاً له ملك السموات والأرض}؛ والله لا يأذن لأحد أن يشفع إلا فيمن ارتضى ولا يرتضي إلا توحيده واتباع رسله، فمن لم يتصف بهذا فليس له في الشفاعة نصيب. ثم أخبر عن علمه الواسع المحيط وأنه يعلم ما بين أيدي الخلائق من الأمور المستقبلة التي لا نهاية لها {وما خلفهم}؛ من الأمور الماضية التي لا حد لها، وأنه لا تخفى عليه خافية {يعلم خائنة الأعين وما تخفي الصدور}؛ وأن الخلق لا يحيط أحد بشيء من علم الله ومعلوماته {إلا بما شاء} منها وهو ما أطلعهم عليه من الأمور الشرعية والقدرية، وهو جزء يسير جدًّا مضمحل في علوم الباري ومعلوماته كما قال أعلم الخلق به وهم الرسل والملائكة: {سبحانك لا علم لنا إلا ما علمتنا}؛ ثم أخبر عن عظمته وجلاله وأن كرسيه وسع السماوات والأرض، وأنه قد حفظهما ومن فيهما من العوالم بالأسباب والنظامات التي جعلها الله في المخلوقات، ومع ذلك فلا يؤوده أي يثقله حفظهما لكمال عظمته واقتداره وسعة حكمته في أحكامه {وهو العلي}؛ بذاته على جميع مخلوقاته، وهو العلي بعظمة صفاته، وهو العلي الذي قهر المخلوقات، ودانت له الموجودات، وخضعت له الصعاب، وذلت له الرقاب {العظيم}؛ الجامع لجميع صفات العظمة والكبرياء والمجد والبهاء، الذي تحبه القلوب، وتعظمه الأرواح، ويعرف العارفون أن عظمة كل شيء وإن جلت عن الصفة فإنها مضمحلة في جانب عظمة العلي العظيم. فآية احتوت على هذه المعاني التي هي أجل المعاني يحق أن تكون أعظم آيات القرآن، ويحق لمن قرأها متدبراً متفهماً أن يمتلئ قلبه من اليقين والعرفان والإيمان، وأن يكون محفوظاً بذلك من شرور الشيطان.
{255} Alisema (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba, Aya hii ndiyo kubwa zaidi katika Aya za Qur-ani. Kwa sababu ya kile ilichojumuisha cha maana ya Tauhidi, ukubwa, na wingi wa sifa za Al-Bari (Muumba mwanzilishi) Mtukufu. Alisema kuwa yeye ni "Allah (Mwenyezi Mungu)" ambaye ana maana zote za uungu. Na kwamba hakuna anayestahiki uungu na ibada isipokuwa Yeye tu. Kwani, uungu wa asiyekuwa Yeye na ibada ya asiyekuwa Yeye ni batili, na kwamba yeye ndiye "Al-Hayyu (Aliye hai)." Ambaye ana maana zote za uhai mkamilifu kama vile kusikia, kuona, nguvu, kutaka (mapenzi), na sifa nyinginezo miongoni mwa sifa za kibinafsi. Kama vile "Al-Qayyum (Msimamia mambo yote)" ambayo zinaingia ndani yake Sifa zote za kimatendo. Kwa sababu Yeye ndiye Msimamizi ambaye anajisimamia mwenyewe bila ya kuvihitaji viumbe vyake vyote. Na alivisimamia vyote vinavyopatikana kwani aliviumba vyote, na akavifanya kuendelea kuwepo. Na akavipa kila vinachohitaji kwa ajili ya kuwepo kwake na kuendelea kwake kuishi. Na katika ukamilifu wa uhai wake na Usimamizi wake ni kwamba "hashikwi na kusinzia wala kulala". Kwa sababu, kusinzia na kulala huwa vinampata kiumbe ambaye amepatwa na udhaifu, kutoweza na kuharibika. Na wala havimpati yule mwenye Ukuu, Ukubwa, na Utukufu. Na katika ukamilifu wa ufalme wake ni kwamba "hafanyi uombezi mbele yake" yeyote "isipokuwa kwa idhini yake". Kila wenye heshima, na waombezi wote ni waja wake, na wanamilikiwa na wala hawajitokezi kufanya uombezi mpaka awape idhini. "Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi." Na Mwenyezi Mungu hamruhusu yeyote kufanya uombezi isipokuwa kwa anayemridhia. Na wala haridhii isipokuwa kumpwekesha na kuwafuata Mitume wake. Kwa hivyo, asiyesifika kwa haya, basi hana fungu lolote katika uombezi. Kisha akajulisha kuhusu elimu yake pana inayoenea, na kwamba anayajua yaliyo mbele ya viumbe ya mambo yajayo ambayo hayana mwisho. “Na yaliyo nyuma yao” katika mambo yaliyopita ambayo hayana mpaka, na kwamba haifichiki siri yoyote kwake. “Anajua hiyana ya macho na vinavyoficha vifua.” Na kwamba, yeyote katika viumbe hajui vyema chochote katika elimu ya Mwenyezi Mungu na habari zake. “Isipokuwa kwa kile atakacho” katika hayo. Nayo ni yale aliyowafahamisha katika mambo ya kisheria na ya majaaliwa. Nayo ni sehemu ndogo sana ya elimu yenye kuisha (kwa viumbe) katika elimu za Al-Bari (Muumba mwanzilishi) na habari zake. Na kama walivyosema wenye kumjua zaidi kati ya viumbe, ambao ni Mitume na Malaika; “Subhanaka (Wewe umetakasika)! Hatuna elimu isipokuwa kile ulichotufunza”. Kisha akajulisha kuhusu ukuu wake na utukufu wake, na kwamba Kursi yake imeenea mbingu na ardhi. Na kwamba amehifadhi vyote viwili na vilivyomo miongoni mwa walimwengu kwa njia (sababu) na mifumo ambayo Mwenyezi Mungu aliweka katika viumbe. Hata hivyo, halemewi, yani haimuwii vigumu kuvihifadhi vyote viwili kwa sababu ya ukamilifu wa ukuu wake, uwezo wake, na upana wa hekima yake katika hukumu zake. “Na Yeye ndiye aliye juu zaidi” kwa dhati yake juu ya viumbe vyake. Naye ndiye aliye juu zaidi kwa ukuu wa sifa zake. Naye ndiye aliye juu zaidi ambaye amevishinda nguvu viumbe, na vyote vilivyo chini ya hukumu yake, na magumu yote yamenyenyekea, na shingo zote zimemdhalilikia. “Mkuu” aliyekusanya sifa zote za ukuu, ukubwa, utukufu, uzuri ambaye anapendwa na nyoyo, na roho zinamtukuza. Na wale wanaojua wanajua kwamba ukuu wa kila kitu, hata ukiwa mkuu vipi kwa sababu ya sifa zake, basi huo hupunguka kwa kulinganisha na ukuu wa Al-‘Ali (Mtukufu), Al-‘Adhim (Mkuu). Ni Aya iliyojumuisha maana hizi ambazo ni katika maana tukufu zaidi ina haki ya kuwa kubwa zaidi katika Aya za Qur-ani. Na mwenye kuisoma kwa kutafakari na kuelewa anayo haki ya moyo wake kujaa yakini na shukran na imani, na kwamba ahifadhiwe kwa hayo kutokana na shari ya Shetani.
: 256 #
{لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ قَدْ تَبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ فَمَنْ يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِنْ بِاللَّهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَى لَا انْفِصَامَ لَهَا وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (256)}
(256) Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani uwongofu umekwisha pambanuka kutokana na upotovu. Basi anayemkufuru Taaghuut na akamwamini Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisichovunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua vyema.
#
{256} هذا بيان لكمال هذا الدين الإسلامي، وأنه لكمال براهينه، واتضاح آياته وكونه هو دين العقل والعلم ودين الفطرة والحكمة ودين الصلاح والإصلاح ودين الحق والرشد، فلكماله وقبول الفطر له لا يحتاج إلى الإكراه عليه، لأن الإكراه إنما يقع على ما تنفر عنه القلوب، ويتنافى مع الحقيقة والحق أو لما تخفى براهينه وآياته، وإلا فمن جاءه هذا الدين ورده ولم يقبله فإنه لعناده، فإنه {قد تبين الرشد من الغي} فلم يبق لأحد عذر ولا حجة إذا رده ولم يقبله. ولا منافاة بين هذا المعنى وبين الآيات الكثيرة الموجبة للجهاد، فإن الله أمر بالقتال ليكون الدين كله لله، ولدفع اعتداء المعتدين على الدين، وأجمع المسلمون على أن الجهاد ماضٍ مع البر والفاجر، وأنه من الفروض المستمرة الجهاد القولي والجهاد الفعلي، ومن ظن من المفسرين أن هذه الآية تنافي آيات الجهاد فجزم بأنها منسوخة فقوله ضعيف لفظاً ومعنى كما هو واضح بين لمن تدبر الآية الكريمة كما نبهنا عليه. ثم ذكر الله انقسام الناس إلى قسمين: قسم آمن بالله وحده لا شريك له وكفر بالطاغوت ـ وهو كل ما ينافي الإيمان بالله من الشرك وغيره ـ فهذا قد {استمسك بالعروة الوثقى} التي لا انفصام لها، بل هو مستقيم على الدين الصحيح حتى يصل به إلى الله وإلى دار كرامته. ويؤخذ القسم الثاني من مفهوم الآية أن من لم يؤمن بالله بل كفر به وآمن بالطاغوت فإنه هالك هلاكاً أبدياً ومعذب عذاباً سرمدياً. وقوله {والله سميع}؛ أي: لجميع الأصوات باختلاف اللغات على تفنن الحاجات، وسميع لدعاء الداعين وخضوع المتضرعين. {عليم}؛ بما أكنته الصدور، وما خفي من خفايا الأمور، فيجازي كل أحد بحسب ما يعلمه من نياته وعمله.
{256} Huku ni kubainisha ukamilifu wa dini hii ya Uislamu, na kwamba ni sababu ya ukamilifu wa dalili zake, na uwazi wa Aya zake. Na kwa kuwa ni Dini ya akili na elimu, na Dini ya fitra (umbile la asili), na hekima, Dini ya wema na urekebishaji, na Dini ya haki na uongofu. Na kwa ukamilifu wake na kukubaliwa na fitra (umbile la asili), haihitaji kulazimisha juu yake. Kwa sababu, kulazimisha kunakuwa tu kwa kile ambacho nyoyo zimejitenga nacho, na kinapingana na uhakika na haki. Au kile ambacho dalili zake na aya (ishara) zake zimefichika, na vinginevyo. Mwenye kujiwa na dini hii naye akaikataa na wala asiikubali, basi hilo ni kwa sababu ya ukaidi wake. Kwani, “uwongofu umekwisha pambanuka kutokana na upotovu;” na mtu yeyote hajabaki na kisingizio wala hoja yoyote ikiwa ataikataa na asiikubali. Na wala hakuna upinzani baina ya maana hii na Aya nyingi zinazolazimu kuwepo kwa Jihadi. Kwani, Mwenyezi Mungu ameamrisha kupigana vita ili Dini yote iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kuzuia uadui wa wenye kufanya uadui dhidi ya dini. Waislamu wamekubaliana kwamba jihadi itaendelea kuwepo pamoja na (kiongozi) mwema na muovu. Na kwamba miongoni mwa faradhi zinazoendelea ni Jihadi ya kimaneno na Jihadi ya kimatendo. Na mwenye kudhani kwamba Aya hii inapingana na Aya za Jihadi, kwa hivyo akawa na uhakika kuwa ilifutwa; basi kauli yake hiyo ni dhaifu kimaandiko na kimaana. Kama ilivyo dhahiri na bainifu kwa mwenye kuitafakari Aya hii tukufu, kama tulivyoashiria hilo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja kugawanyika kwa watu katika makundi mawili: Kundi lililomwamini Mwenyezi Mungu peke yake bila ya mshirika yeyote na likakufuru Taaghut. – Nayo ni kila lenye kupingana na imani juu ya Mwenyezi Mungu kama vile shirki na mengineyo. Basi huyo bila ya shaka, “amekamata kishikio madhubuti” ambacho hakiwezi kuvunjika. Bali yeye amenyooka kwenye Dini sahihi mpaka afike kwayo kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake. Na kundi la pili linachukuliwa kutoka katika maana isiyo ya moja kwa moja ya aya. Kwamba asiyemwamini Mwenyezi Mungu, bali alimkufuru na akamuamini Taaghut; basi yeye ataangamia milele na ataadhibiwa adhabu ya milele. Na kauli yake, “na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema” yani sauti zote katika lugha mbalimbali, kwa mahitaji mbalimbali. Na ni mwenye kusikia dua ya waombaji dua, na kunyenyekea kwa wanaonyenyekea. “Mwenye kujua vyema” yale yaliyofichwa na vifua, na yale yanayofichika katika mambo ya siri. Kisha anamlipa kila mtu kulingana na anayojua katika nia zake na matendo yake.
: 257 #
{اللَّهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُمْ مِنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (257)}
(257) Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa walioamini. Huwatoa hadi katika giza mbalimbali kwenda katika nuru. Lakini wale waliokufuru, walinzi wao ni Taaghut. Huwatoa katika nuru kwenda hadi katika giza mbalimbali. Hao ndio wenza wa Moto, humo watadumu.
#
{257} هذه الآية مترتبة على الآية التي قبلها، فالسابقة هي الأساس وهذه هي الثمرة. فأخبر تعالى أن الذين آمنوا بالله وصدقوا إيمانهم بالقيام بواجبات الإيمان وترك كل ما ينافيه أنه وليهم يتولاهم بولايته الخاصة، ويتولى تربيتهم، فيخرجهم من ظلمات الجهل والكفر والمعاصي والغفلة والإعراض، إلى نور العلم واليقين والإيمان والطاعة والإقبال الكامل على ربهم، وينور قلوبهم بما يقذفه فيها من نور الوحي والإيمان، وييسرهم لليسرى، ويجنبهم العسرى، وأما الذين كفروا فإنهم لما تولوا غير وليهم، ولاهم الله ما تولوا لأنفسهم، وخذلهم، ووكلهم إلى رعاية من تولاهم ممن ليس عنده نفع ولا ضر، فأضلوهم، وأشقوهم، وحرموهم هداية العلم النافع والعمل الصالح، وحرموهم السعادة، وصارت النار مثواهم خالدين فيها مخلدين. اللهم تولنا فيمن توليت.
{257} Aya hii inafuata Aya iliyotangulia, kwa hivyo iliyo tangulizi ndiyo msingi, na hii ndiyo matunda. Basi Mola Mtukufu akajulisha kwamba wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakasadikisha imani yao kwa kutekeleza wajibu wa imani na kuacha kila kinachopingana nayo. Kwamba Yeye ndiye Mlinzi wao anayewasimamia kusimamia kwake maalumu, na anayasimamia malezi yao. Kwa hivyo, huwatoa katika giza mbalimbali la ujinga na ukafiri na maasia na kughafilika na kupeana mgongo hadi katika nuru ya elimu, na yakini, na imani, na utiifu, na kumwelekea Mola wa Mlezi kikamilifu. Na anaziangaza nyoyo zao kwa yale anayoyatia ndani yake ya nuru ya Wahyi na imani. Na anawasahilishia yawe mepesi, na anawaepushia ugumu. Na ama wale waliokufuru, wao walipomfanya asiyekuwa mlinzi wao kuwa rafiki yao, Mwenyezi Mungu aliwaachia wale walichojifanyia wenyewe kuwa rafiki yao. Na akaacha kuwasaidia, na akawakabidhi katika uangalizi wa wale waliowafanya kuwa rafiki miongoni mwa wale wasiofaidi wala kudhuru. Wakawafanya kuwa wapotovu, na wakawanyima uongofu wa elimu yenye manufaa na matendo mema, na wakawanyima furaha, na Moto ukawa ndio makazi yao, watakaa humo milele. Ewe Mwenyezi Mungu, kuwa mlinzi wetu katika wale unaowalinda.
: 258 #
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ (258)}
(258) Kwani hukumuona yule aliyehojiana na Ibrahim kuhusu Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema: Mola wangu Mlezi ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia ninahuisha na ninafisha. Ibrahim akasema: Kwa hakika, Mwenyezi Mungu hulileta jua kutokea mashariki, basi wewe lilete kutokea magharibi. Kwa hivyo, akashindwa yule aliyekufuru.(1) Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu dhalimu.
#
{258} يقص الله علينا من أنباء الرسل والسالفين ما به تتبين الحقائق، وتقوم البراهين المتنوعة على التوحيد، فأخبر تعالى عن خليله إبراهيم - صلى الله عليه وسلم -، حيث حاج هذا الملك الجبار، وهو نمرود البابلي المعطل المنكر لرب العالمين، وانتدب لمقاومة إبراهيم الخليل ومحاجته في هذا الأمر الذي لا يقبل شكًّا ولا إشكالاً ولا ريباً وهو توحيد الله وربوبيته الذي هو أجلى الأمور وأوضحها. ولكن هذا الجبار غره ملكه وأطغاه حتى وصلت به الحال إلى أن نفاه، وحاج إبراهيمَ الرسولَ العظيمَ الذي أعطاه الله من العلم واليقين ما لم يعط أحداً من الرسل سوى محمد - صلى الله عليه وسلم -، فقال إبراهيم مناظراً له: {ربي الذي يحيي ويميت}؛ أي: هو المنفرد بالخلق والتدبير والإحياء والإماتة، فذكر من هذا الجنس أظهرها وهو الإحياء والإماتة، فقال ذلك الجبار مباهتاً: {أنا أحيي وأميت}؛ وعنى بذلك أني أقتل من أردت قتله وأستبقي من أردت استبقاءه، ومن المعلوم أن هذا تمويه وتزوير عن المقصود، وأن المقصود أن الله تعالى هو الذي تفرد بإيجاد الحياة في المعدومات وردها على الأموات، وأنه هو الذي يميت العباد والحيوانات بآجالها بأسباب ربطها وبغير أسباب. فلما رآه الخليل مموهاً تمويهاً ربما راج على الهمج الرَّعاع قال إبراهيم ملزماً له بتصديق قوله إن كان كما يزعم: {فإن الله يأتي بالشمس من المشرق فأت بها من المغرب، فبهت الذي كفر}؛ أي: وقف وانقطعت حجته، واضمحلت شبهته. وليس هذا من الخليل انتقالاً من دليل إلى آخر، وإنما هو إلزام لنمرود بطرد دليله إن كان صادقاً وأتى بهذا الذي لا يقبل الترويج والتزوير والتمويه، فجميع الأدلة السمعية والعقلية والفطرية قد قامت شاهدة بتوحيد الله معترفة بانفراده بالخلق والتدبير وأن من هذا شأنه لا يستحق العبادة إلا هو، وجميع الرسل متفقون على هذا الأصل العظيم، ولم ينكره إلا معاند مكابر مماثل لهذا الجبار العنيد، فهذا من أدلة التوحيد، ثم ذكر أدلة كمال القدرة والبعث والجزاء فقال:
{258} Mwenyezi Mungu anatuhadithia katika habari za Mitume na wale waliotangulia ambazo hakika zinabainika kwazo, na hoja mbalimbali zinasimama juu ya Tauhidi. Basi Mola Mtukufu akajulisha kuhusu rafiki mwandani wake Ibrahim – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake wakati alipomhoji mfalme huyu mkandamizaji. Ambaye ni Namrud wa Babeli, aliyemkanusha na kumkataa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na akajitoa kumpinga Ibrahim Al-Khalil na kuhojiana naye katika jambo hili ambalo halikubali shaka yoyote, wala tatizo, wala shaka. Na ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu na umola wake ambao ndiyo mambo yaliyo wazi kabisa na yaliyo dhahiri zaidi. Lakini mkandamizaji huyu alidanganywa na ufalme wake, na ukamfanya kupindukia mpaka hali ikamfikisha kwamba alimkataa (Mwenyezi Mungu). Na akahojiana na Ibrahim Mtume mtukufu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa elimu na yakini. Ambavyo hakumpa yeyote katika Mitume isipokuwa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Ibrahim akasema akihojiana naye, “Mola wangu Mlezi ndiye anayehuisha na anayefisha.” Yani Yeye ndiye pekee yake mwenye kuumba, kuendesha mambo, kuhuisha na kufisha. Kwa hivyo akataja katika aina hii kile cha dhahiri mno, ambacho kuhuisha na kufisha. Hivyo, mkandamizaji huyu akasema akijifahirisha, “mimi pia ninahuisha na ninafisha.” Na akamaanisha kwa hilo kuwa ninamuua nitakaye kumuua na ninamwacha hai ninayetaka kumuacha. Na Inavyojulikana ni kwamba huku ni kuficha na kupotosha kando na kilichokusudiwa. Na kwamba kilichokusudiwa ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye wa pekee katika kuleta uhai katika mambo yasiyokuwapo na kuurejesha kwa wafu. Na kwamba Yeye ndiye anayewafisha waja na wanyama kwa mida yao kwa sababu alizofungamanisha na hilo, na bila ya sababu. Basi Al-Khalil alipomwona akificha kuficha ambako huenda ukaenea miongoni mwa watu wa kawaida, Ibrahim akasema kwa kumlazimisha kusadikisha kauli yake ikiwa ni kama anavyodai. “Kwa hakika, Mwenyezi Mungu hulileta jua kutokea mashariki, basi wewe lilete kutokea magharibi. Kwa hivyo, akashindwa yule aliyekufuru.” Yani alisimama na hoja yake ikakatika, na fikira yake potofu ikatoweka. Na hili kutoka kwa Al-Khalil sio kuhama kutoka kwa ushahidi mmoja hadi ushahidi mwingine. Bali ni kumlazimu Namrud kuendelea kuthibitisha ushahidi wake ikiwa yeye ni mkweli. Na alitumia ushahidi huu ambao haukubali kuenezwa, wala kughushi, na wala kufichwa. Kwa hivyo ushahidi wote wa kusikia, wa kiakili na wa umbile la asili (wa kuzaliwa) wote ulikwisha simama kama shahidi juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu. Ukikubali upweke wake katika kuumba, kuendesha mambo, na kwamba yule ambaye jambo lake ni hili, basi haistahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu. Na Mitume wote wanaafikiana juu ya msingi huu mkubwa, na wala hakuwahi kuupinga isipokuwa mkaidi, mwenye kiburi mfano wa mkandamizaji huyu mkaidi. Basi hizi ni katika dalili za Tauhidi. Kisha akataja dalili za ukamilifu wa uwezo, na ufufuo, na malipo. Akasema:
: 259 - 260 #
{أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَى قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَى عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّى يُحْيِي هَذِهِ اللَّهُ بَعْدَ مَوْتِهَا فَأَمَاتَهُ اللَّهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ قَالَ بَلْ لَبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانْظُرْ إِلَى طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ وَانْظُرْ إِلَى حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِلنَّاسِ وَانْظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنْشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (259) وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِ الْمَوْتَى قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِنْ قَالَ بَلَى وَلَكِنْ لِيَطْمَئِنَّ قَلْبِي قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَى كُلِّ جَبَلٍ مِنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (260)}.
(259) Au kama yule aliyepita karibu na mji hali ya kuwa umekwisha kuwa magofu tu. Akasema: Vipi Mwenyezi Mungu ataufufua mji huu baada ya kufa kwake? Basi Mwenyezi Mungu akamfisha yeye (muda wa) miaka mia moja, kisha akamfufua. Akasema: Je umekaa muda gani? Akasema: (Labda) nimekaa siku moja au sehemu ya siku. Akasema: Bali umekaa miaka mia moja. Hebu angalia chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika. Na mwangalie punda wako. Na ili tukufanye uwe ni ishara kwa watu. Na iangalie mifupa yake hii jinsi tunavyoinyanyua kisha tuivishe nyama. Basi yalipombainikia, alinena: Ninajua kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu. (260) Na Ibrahim aliposema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyofufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue. Akasema: Basi wachukue wanne katika ndege na uwazoeshe kwako. Kisha weka juu ya kila kilima sehemu katika hao, kisha waite, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{259} هذان دليلان عظيمان محسوسان في الدنيا قبل الآخرة على البعث والجزاء، واحد أجراه الله على يد رجل شاك في البعث على الصحيح كما تدل عليه الآية الكريمة، والآخر على يد خليله إبراهيم، كما أجرى دليل التوحيد السابق على يده. فهذا الرجل مرَّ على قرية قد دمرت تدميراً وخوت على عروشها قد مات أهلها وخربت عمارتها، فقال على وجه الشك والاستبعاد: {أنى يحيي هذه الله بعد موتها}؟ أي: ذلك بعيد وهي في هذه الحال، يعني وغيرها مثلها بحسب ما قام بقلبه تلك الساعة، فأراد الله رحمته ورحمة الناس حيث أماته الله مئة عام، وكان معه حمار فأماته معه، ومعه طعام وشراب فأبقاهما الله بحالهما كل هذه المدد الطويلة. فلما مضت الأعوام المائة بعثه الله فقال: {كم لبثت قال: لبثت يوماً أو بعض يوم}؛ وذلك بحسب ما ظنه، فقال الله: {بل لبثت مائة عام}؛ والظاهر أن هذه المجاوبة على يد بعض الأنبياء الكرام. ومن تمام رحمة الله به وبالناس أنه أراه الآية عياناً ليقتنع بها، فبعد ما عرف أنه ميت قد أحياه الله قيل له: انظر {إلى طعامك وشرابك لم يتسنه}؛ أي: لم يتغير في هذه المُدَد الطويلة. وذلك من آيات قدرة الله فإن الطعام والشراب خصوصاً ما ذكره المفسرون أنه فاكهة وعصير لا يلبث أن يتغير وهذا قد حفظه الله مئة عام وقيل له: {انظر إلى حمارك}؛ فإذا هو قد تمزق وتفرق وصار عظاماً نخرة، {وانظر إلى العظام كيف ننشزها}؛ أي: نرفع بعضها إلى بعض ونصل بعضها ببعض بعدما تفرقت وتمزقت {ثم نكسوها}؛ بعد الالتئام {لحماً}؛ ثم نعيد فيه الحياة {فلما تبين له}؛ رأيَ عين لا يقبل الريب بوجه من الوجوه {قال أعلم أن الله على كل شيء قدير}؛ فاعترف بقدرة الله على كل شيء وصار آية للناس، لأنهم قد عرفوا موته وموت حماره وعرفوا قضيته ثم شاهدوا هذه الآية الكبرى. هذا هو الصواب في هذا الرجل. وأما قول كثير من المفسرين: أن هذا الرجل مؤمن أو نبي من الأنبياء إما عزير أو غيره وأن قوله: {أنى يحيي هذه الله بعد موتها}؛ يعني كيف تعمر هذه القرية بعد أن كانت خراباً، وأن الله أماته ليريه ما يعيد لهذه القرية من عمارتها بالخلق وأنها عمرت في هذه المدة وتراجع الناس إليها وصارت عامرة بعد أن كانت دامرة، فهذا لا يدل عليه اللفظ بل ينافيه، ولا يدل عليه المعنى، فأي آية وبرهان برجوع البلدان الدامرة إلى العمارة، وهذه لم تزل تشاهد تعمر قرى ومساكن، وتخرب أخرى، وإنما الآية العظيمة في إحيائه بعد موته وإحياء حماره وإبقاء طعامه وشرابه لم يتعفن ولم يتغير، ثم قوله: {فلما تبين له}؛ صريح في أنه لم يتبين له إلا بعدما شاهد هذه الحال الدالة على كمال قدرته عيانا.
{259} Hizi ni dalili mbili kubwa na zinazoonekana katika dunia hii kabla ya Akhera juu ya ufufuo na malipo. Moja, Mwenyezi Mungu aliifanya kwa mkono wa mwanamume aliyekuwa na shaka juu ya ufufuo, nayo ndiyo kauli sahihi kulingana na inavyoonyesha Aya tukufu juu yake. Nayo nyingine ilikuwa juu ya mkono wa rafiki mwandani wake Ibrahim, kama alivyoifanyisha dalili ya Tauhid iliyopita hapo awali juu ya mkono wake. Mtu mwanamume alipita karibu na kijiji kilichokuwa kimeharibiwa kuharibika kukubwa kikatokomea kabisa. Watu wake walikuwa wamekwisha kufa na mijengo yake ikawa imekwisha haribika. Kwa hivyo, akasema kwa namna ya shaka na kuona kwamba hilo haliwezekani. "Vipi Mwenyezi Mungu ataufufua mji huu baada ya kufa kwake?" Yani, hilo liko mbali hali ya kuwa uko (mji huu) katika hali hii, akimaanisha miji mingine mfano wake kulingana na kile kilichokuwa ndani ya moyo wake saa ile. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akataka kumrehemu na kuwarehemu watu. Kwani Mwenyezi Mungu alimfisha kwa miaka mia moja, na alikuwa na punda pamoja naye, kwa hivyo akamfisha pamoja naye. Na alikuwa na chakula na kinywaji pamoja naye. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaviacha vilivyokuwa kwa mida yote hii mirefu. Na miaka hiyo mia moja ilipopita, Mwenyezi Mungu akamhuisha na akasema: "Je umekaa muda gani? Akasema: (Labda) nimekaa siku moja au sehemu ya siku." Na hayo ni kulingana na vile alivyodhania. Basi Mwenyezi Mungu akasema, "Bali umekaa miaka mia moja." Na lililo dhahiri zaidi ni kwamba majibu haya yalikuwa kutoka kwa baadhi ya manabii watukufu. Na katika utimilifu wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwake na kwa watu ni kwamba alimwonyesha Aya kwa macho yake ili apate kuridhika nayo. Na baada ya kujua kuwa alikufa, kisha Mwenyezi Mungu akamfufua, akaambiwa: Angalia, "chakula chako na kinywaji chako, havikuharibika!" Yani havikubadilika katika mida hii mirefu. Na hayo ni katika dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu. Kwani chakula na kinywaji, hasa walichokitaja wafasiri kuwa matunda na juisi havikai muda isipokuwa vinakuwa vimeshabadilika. Na Mwenyezi Mungu huyu alivihifadhi kwa muda wa miaka mia moja. Na akaambiwa, "Mwangalie punda wako." Tazama! Alikuwa amekwisha katikakatika na akaachanika ameshakuwa mifupa iliyooza. "Na iangalie mifupa yake hii jinsi tunavyoinyanyua." Yani tunavyoiinua baadhi yake juu ya nyingine na kuunganisha baadhi yake juu ya nyingine baada ya kutawanyika na kuachanika. "Kisha tuivishe" baada ya kushikana "nyama." Kisha tunarudisha uhai ndani yake. "Basi yalipombainikia" kwa mtazamo wa macho usiokubali shaka yoyote kwa namna yoyote; "ninajua kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu." Kwa hivyo akakiri uwezo wa Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu, na akawa ishara kwa watu. Kwa sababu walijua kifo chake na kifo cha punda wake, na walikijua kisa chake, kisha wakashuhudia ishara hii kubwa. Na hayo ndiyo yaliyo sahihi kuhusu mwanamume huyu. Na ama kauli ya wengi miongoni mwa wafasiri kuwa, mwanamume huyu ni Muumini au Nabii miongoni mwa Manabii. Ima Ezra au mtu mwingine, na kwamba kauli yake: "Vipi Mwenyezi Mungu ataufufua mji huu baada ya kufa kwake?" Inamaanisha: Vipi kijiji hiki kitaimarishwa upya baada ya kuharibika. Na kwamba Mwenyezi Mungu alimfisha ili amwonyeshe kile atakachorudishia kijiji hiki cha kukiimarisha kwa viumbe. Na kwamba kiliimarishwa katika muda huu na watu wakakirudia, na kikawa kimeimarika baada ya kuwa kimeharibika. Hili haliashiriwi na matamshi ya aya, bali yanalipinga, na wala maana yake hayaliashirii. Ni ishara gani na uthibitisho gani uliopo katika miji iliyoharibika kurudi ikaimarika, ilhali hiki hakijaacha kushuhudia ujenzi wa vijiji na makazi; kisha kinaharibika mara ya pili? Lakini ishara kubwa ni katika ufufuo wake baada ya kufa kwake, na ufufuo wa punda wake. Na kukihifadhi chakula chake na kinywaji chake ambavyo havikuoza wala kubadilika. Kisha kauli yake: "Na ilipombainikia" ni wazi kwamba, haikumbainikia isipokuwa mpaka baada ya kuona hali hii inayoashiria ukamilifu wa uwezo wake kwa macho.
#
{260} وأما البرهان الآخر فإن إبراهيم قال طالباً من الله أن يريه كيف يحيي الموتى فقال الله له: {أو لم تؤمن}؛ ليزيل الشبهة عن خليله، {قال}؛ إبراهيم: {بلى}؛ يا رب قد آمنت أنك على كل شيء قدير وأنك تحيي الموتى وتجازي العباد، ولكن أريد أن يطمئن قلبي وأصل إلى درجة عين اليقين، فأجاب الله دعوته كرامة له ورحمة بالعباد، {قال فخذ أربعة من الطير}؛ ولم يبين أي الطيور هي فالآية حاصلة بأي نوع منها وهو المقصود، {فصرهن إليك}؛ أي: ضمهن واذبحهن ومزقهن {ثم اجعل على كل جبل منهن جزءاً ثم ادعهن يأتينك سعياً واعلم أن الله عزيز حكيم}؛ ففعل ذلك وفرق أجزاءهن على الجبال التي حوله ودعاهن بأسمائهن فأقبلن إليه أي سريعات، لأن السعي السرعة، وليس المراد أنهن جئن على قوائمهن، وإنما جئن طائرات على أكمل ما يكون من الحياة، وخص الطيور بذلك لأن إحياءهن أكمل وأوضح من غيرهن، وأيضاً أزال في هذا كل وهم ربما يعرض للنفوس المبطلة، فجعلهن متعددات أربعة، ومزقهن جميعاً، وجعلهن على رؤوس الجبال، ليكون ذلك ظاهراً علناً يشاهد من قرب ومن بعد، وأنه نحاهن عنه كثيراً لئلا يظن أن يكون عاملاً حيلة من الحيل، وأيضاً أمره أن يدعوهن فجئن مسرعات، فصارت هذه الآية أكبر برهان على كمال عزة الله وحكمته. وفيه تنبيه على أن البعث فيه يظهر للعباد كمال عزة الله وحكمته وعظمته وسعة سلطانه وتمام عدله وفضله.
{260} Na ama ule ushahidi mwingine, basi, Ibrahim alisema akimwomba Mwenyezi Mungu amwonyeshe jinsi anavyowafufua wafu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwambia, “kwani huamini?” Ili amuondolee mwandani wake fikira potofu. “Akasema” Ibrahim, “Hasha!” ewe Mola mlezi, nilikwisha amini kuwa wewe ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu, na kwamba unahuisha wafu na utawalipa waja. Lakini ninataka moyo wangu utulie na ufikie kiwango cha yakini. Basi Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake kwa ajili ya kumtukuza na kuwafanyia rehema waja wake. “Akasema: Basi wachukue wanne katika ndege” lakini hakubainisha ni ndege wagani hao, kwani ishara hiyo inaweza tokea kwa aina yoyote ile kati yake. Na hilo ndilo lililokusudiwa “Na uwazoeshe kwako” yani wawake karibu sana na wewe, kisha wachinje na uwakatekate. “Kisha weka juu ya kila kilima sehemu katika hao, kisha waite, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” Basi akafanya hivyo, na akatenganisha sehemu zao juu ya milima iliyomzunguka na akawaita kwa majina yao, nao wakamjia, yani mbio. Kwa sababu neno ‘assa’y’ linamaanisha kwenda mbio. Na haikukusudiwa kwamba walimjia kwa miguu yao. Bali walikuja kwa kupaa wakiwa katika hali ya ukamilifu zaidi ya uhai. Na aliwachagua ndege hususan kwa ajili ya hilo, kwa sababu kuhuishwa kwao ni kukamilifu zaidi kuko wazi zaidi kuliko wengineo. Na pia aliondoa katika hilo kila fikira mbovu ambayo huenda ikaingia ndani ya nafsi zinazofuata batili. Na aliwafanya kuwa wanne tofauti tofauti, na akawakatakata wote. Na akawaweka juu ya vilele vya milima, ili jambo hilo liwe dhahiri lenye kuonekana hadharani, anaweza kulitazama aliye karibu na wa mbali. Na kwamba aliwaweka mbali sana na yeye mwenyewe ili isifikiriwe kwamba alikuwa anafanya hila. Na pia alimwamrisha awaite, basi wakaja mbio. Kwa hivyo, ikawa ishara hii ndio ushahidi mkubwa mno juu ya ukamilifu wa Nguvu ya Mwenyezi Mungu na hekima yake. Na ndani yake kuna tanbihi kwamba ufufuo, ndani yake unawadhihirishia waja ukamilifu wa Nguvu za Mwenyezi Mungu, na hekima yake. Na ukuu wake, na upana wa mamlaka yake, na ukamilifu wa uadilifu wake na fadhila yake.
: 261 - 262 #
{مَثَلُ الَّذِينَ يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنْبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنْبُلَةٍ مِائَةُ حَبَّةٍ وَاللَّهُ يُضَاعِفُ لِمَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ (261) الَّذِينَ يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنْفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (262)}
(261) Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia moja. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. (262) Wale wanaotoa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishi kile walichotoa masimbulizi wala udhia, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.
#
{261} هذا حث عظيم من الله لعباده في إنفاق أموالهم في سبيله، وهو طريقه الموصل إليه، فيدخل في هذا إنفاقه في ترقية العلوم النافعة، وفي الاستعداد للجهاد في سبيله، وفي تجهز المجاهدين وتجهيزهم، وفي جميع المشاريع الخيرية النافعة للمسلمين، ويلي ذلك الإنفاق على المحتاجين والفقراء والمساكين، وقد يجتمع الأمران فيكون في النفقة دفع الحاجات والإعانة على الخير والطاعات، فهذه النفقات مضاعفة هذه المضاعفة بسبعمائة إلى أضعاف أكثر من ذلك، ولهذا قال: {والله يضاعف لمن يشاء}؛ وذلك بحسب ما يقوم بقلب المنفق من الإيمان والإخلاص التام وفي ثمرات نفقته ونفعها، فإن بعض طرق الخيرات يترتب على الإنفاق فيها منافع متسلسلة ومصالح متنوعة فكان الجزاء من جنس العمل.
{261} Huku ni kuhimiza kukubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake juu ya kutoa mali zao katika njia yake. Nayo ni njia yake inayofikisha kwake. Kwa hivyo, inaingia katika hili kutoa kwake kwa ajili ya kukuza elimu zenye manufaa. Na katika kutayarisha jihadi katika njia yake, na katika kujitayarisha na kuwaandaa wale wanaopigana katika Jihadi, na katika miradi yote ya heri yenye manufaa kwa Waislamu. Kisha hilo linafuatwa na kuwapa wenye mahitaji, na mafakiri, na masikini. Na inawezekana mambo mawili haya kukutana, basi ikawa katika kutoa kuna kuondoa mahitaji na kusaidia katika heri na utiifu. Kwa hivyo, kutoa huku kwa ajili ya matumizi kunazidishwa kuzidisha huku mara mia saba hadi zaidi ya hapo. Na ndio maana akasema, “na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye.” Na hilo ni kulingana na yale yaliyomo katika moyo wa mtoaji ya imani na ikhlasi kamili, na katika matunda ya aliyotoa kwa ajili ya matumizi na manufaa yake. Kwa maana, baadhi ya njia za heri, matokeo ya kutoa matumizi katika hizo huwa yenye manufaa ya kuendelea, na masilahi mbalimbali. Basi yakawa malipo ni ya aina sawa na matendo.
#
{262} ثم أيضاً ذكر ثواباً آخر للمنفقين أموالهم في سبيله نفقة صادرة مستوفية لشروطها منتفية موانعها، فلا يتبعون المنفق عليه، منًّا منهم عليه وتعداداً للنعم وأذية له قولية أو فعلية فهؤلاء {لهم أجرهم عند ربهم}؛ بحسب ما يعلمه منهم وبحسب نفقاتهم ونفعها وبفضله الذي لا تناله ولا تصل إليه صدقاتهم، {ولا خوف عليهم ولا هم يحزنون}؛ فنفى عنهم المكروه الماضي بنفي الحزن، والمستقبل بنفي الخوف عليهم فقد حصل لهم المحبوب واندفع عنهم المكروه.
{262} Kisha pia alitaja malipo mengine kwa wale wanaotoa mali zao kwa ajili ya matumizi katika njia yake. Kutoa ambako kunatoka huku kumetimiza masharti yake na ambako hakuna vizuizi vyake. Basi hawamfuati aliyepewa kwa masimbulizi juu yake na kuhesabu neema na kumuudhi kwa maneno au vitendo. Basi hao “wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi” kulingana na kile anachojua ndani yao. Na kulingana na kile walichotoa na manufaa yake, na kwa fadhila yake ambayo kutoa kwao hakuipati wala hakuifikii “na wala haitakuwa hofu juu yao wala hao hawatahuzunika”. Kwa hivyo, akakanusha juu yao machukizo yaliyopita kwa kukanusha huzuni (juu yao), na yajayo kwa kukanusha hofu (juu yao). Basi watakuwa wameshapata wakipendacho na kikazuilika wanachokichukia juu yao.
: 263 #
{قَوْلٌ مَعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِنْ صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى وَاللَّهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ (263)}
(263) Kauli njema na msamaha ni bora kuliko sadaka inayofuatwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosheleza, Mpole.
#
{263} ذكر الله أربع مراتب للإحسان: المرتبة العليا: النفقة الصادرة عن نية صالحة ولم يتبعها المنفق منًّا ولا أذى. ثم يليها قول المعروف وهو الإحسان القولي بجميع وجوهه الذي فيه سرور المسلم، والاعتذار من السائل إذا لم يوافق عنده شيئاً، وغير ذلك من أقوال المعروف. والثالثة الإحسان بالعفو والمغفرة عمن أساء إليك بقول أو فعل. وهذان أفضل من الرابعة وخير منها وهي: التي يتبعها المتصدق الأذى للمعطي لأنه كدر إحسانه وفعل خيراً وشرًّا. فالخير المحض وإن كان مفضولاً خير من الخير الذي يخالطه شرٌّ وإن كان فاضلاً، وفي هذا التحذير العظيم لمن يؤذي من تصدق عليه كما يفعله أهل اللؤم والحمق والجهل، {والله}؛ تعالى {غني}؛ عن صدقاتهم وعن جميع عباده {حليم}؛ مع كمال غناه وسعة عطاياه يحلم عن العاصين، ولا يعاجلهم بالعقوبة بل يعافيهم، ويرزقهم، ويدر عليهم خيره، وهم مبارزون له بالمعاصي. ثم نهى أشد النهي عن المنِّ والأذى وضرب لذلك مثلاً:
{263} Mwenyezi Mungu alitaja daraja nne za ihsaan: Daraja la juu zaidi: Kutoa kunakotokana na nia njema, na aliyetoa hakukufuatisha masimbulizi wala maudhi. Kisha linafuatwa na kusema mema. Nalo ni kufanya ihsani katika kuzungumza kwa aina zake zote, ambako ndani yake kuna kumfurahisha Muislamu. Na kutaka udhuru kutoka kwa mwombaji ikiwa hatapata kitu kutoka kwake, na yasiyokuwa hayo katika maneno mema. Na la tatu ni kufanya ihsani kwa kumsamehe na kutupilia mbali aliyekufanyia ubaya kwa kauli au kitendo. Na mawili haya ni bora kuliko la nne na la heri zaidi kuziliko. Nalo ni lile ambalo mwenye kutoa sadaka anafuatisha maudhi kwa aliyempa. Kwa sababu aliharibu wema wake na akafanya mema na mabaya. Basi heri tupu, hata kama ni chache, ni bora kuliko heri iliyochanganyika na shari hata kama ni nyingi. Na katika hili, kuna tahadharisho kubwa kwa anayemuudhi yule anayempa sadaka, kama wanavyofanya watu wachoyo, wapumbavu na wajinga. "Na Mwenyezi Mungu" Mtukufu "ndiye Mwenye kujitosheleza" kwa kutohitaji sadaka zao. Na pia hawahitaji waja wake wote "Mpole" pamoja na ukamilifu wa kujitosheleza kwake, na wasaa (wingi) wa vipawa vyake. Anawafanyia upole waasi, na wala hawaharakishii kuwaadhibu. Bali huwaweka salama, na kuwaruzuku, na kuwapa heri zake nyingi, na huku wao wanamkabili kwa maasia. Kisha akakataza vikali masimbulizi na maudhi, akayapigia mfano hayo:
: 264 - 266 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُمْ بِالْمَنِّ وَالْأَذَى كَالَّذِي يُنْفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا لَا يَقْدِرُونَ عَلَى شَيْءٍ مِمَّا كَسَبُوا وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ (264) وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّهِ وَتَثْبِيتًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِنْ لَمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (265) أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَنْ تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِنْ نَخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِنْ كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ (266)}
(264) Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na maudhi. Kama yule anayetoa mali yake ili kujionyesha kwa watu, wala hamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu yake kuna udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi hawatakuwa na uweza wowote kwa kile walichochuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu ya makafiri. (265) Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kwa kuitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu. Ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake maradufu. Na hata kama haifikiwi na mvua kubwa, basi manyunyu tu yanatosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda. (266) Je, angependa mmoja wenu kwamba awe na bustani ya mitende na mizabibu ipitayo mito chini yake. Naye humo hupata katika mazao ya kila namna, na uzee ukamfikia ilhali ana watoto dhuria nyonge. Kisha ikapigwa na kimbunga chenye moto, kwa hivyo ikaungua? Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia ishara ili mtafakari.
#
{264 - 266} ضرب الله في هذه الآيات ثلاثة أمثلة: للمنفق ابتغاء وجهه ولم يتبع نفقته منًّا ولا أذى، ولمن أتبعها منًّا وأذى، وللمرائي. فأما الأول فإنه لما كانت نفقته مقبولة مضاعفة لصدورها عن الإيمان والإخلاص التام {ابتغاء مرضاة الله وتثبيتاً من أنفسهم}؛ أي: ينفقون وهم ثابتون على وجه السماحة والصدق فمثل هذا العمل، {كمثل جنة بربوة}؛ وهو المكان المرتفع لأنه يتبين للرياح والشمس، والماء فيها غزير، فإن لم يصبها ذلك الوابل الغزير، حصل لها طلٌّ كافٍ لطيب منبتها وحسن أرضها وحصول جميع الأسباب الموفرة لنموها وازدهارها وإثمارها، ولهذا {آتت أكلها ضعفين}؛ أي: متضاعفاً، وهذه الجنة التي على هذا الوصف هي أعلى ما يطلبه الناس، فهذا العمل الفاضل بأعلى المنازل. وأما من أنفق لله ثم أتبع نفقته منًّا وأذى، أو عمل عملاً فأتى بمبطل لذلك العمل فهذا مثله مثال صاحب هذه الجنة، لكن سلط عليها {إعصار}؛ وهو الريح الشديدة {فيه نار فاحترقت}؛ وله ذرية ضعفاء وهو ضعيف قد أصابه الكبر، فهذه الحال من أفظع الأحوال، ولهذا صدَّر هذا المثل بقوله: {أيود أحدكم}؛ إلى آخرها بالاستفهام المتقرر عند المخاطبين فظاعته، فإن تَلَفَها دفعة واحدة بعد زهاء أشجارها وإيناع ثمارها مصيبة كبرى، ثم حصول هذه الفاجعة وصاحبها كبير قد ضعف عن العمل وله ذرية ضعفاء لا مساعدة منهم له ومؤنتهم عليه فاجعة أخرى، فصار صاحب هذا المثل الذي عمل لله ثم أبطل عمله بمنافٍ له يشبه حال صاحب الجنة التي جرى عليها ما جرى حين اشتدت ضرورته إليها. المثل الثالث الذي يرائي الناس وليس معه إيمان بالله ولا احتساب لثوابه حيث شبه قلبه بالصفوان وهو الحجر الأملس عليه تراب يظن الرائي أنه إذا أصابه المطر أنبت كما تنبت الأراضي الطيبة، ولكنه كالحجر الذي أصابه الوابل الشديد فأذهب ما عليه من التراب وتركه صلداً، وهذا مثل مطابق لقلب المرائي الذي ليس فيه إيمان بل هو قاسٍ لا يلين ولا يخشع، فهذا أعماله ونفقاته لا أصل لها تؤسس عليه ولا غاية لها تنتهي إليه، بل ما عمله فهو باطل لعدم شرطه. والذي قبله بطل بعد وجود الشرط لوجود المانع، والأول مقبول مضاعف لوجود شرطه الذي هو الإيمان والإخلاص والثبات وانتفاء الموانع المفسدة. وهذه الأمثال الثلاثة تنطبق على جميع العاملين، فليزن العبد نفسه وغيره بهذه الموازين العادلة والأمثال المطابقة {وتلك الأمثال نضربها للناس وما يعقلها إلا العالمون}.
{264 - 266} Katika Aya hizi, Mwenyezi Mungu alipiga mifano mitatu: Kwa yule anayetoa kwa ajili ya kutafuta uso wake, na hakukifuatisha alichokitoa masimbulizi wala maudhi. Na kwa yule aliyekifuatisha masimbulizi na maudhi, na kwa anayejionyesha (katika kutoa). Ama huyo wa kwanza, pale kutoa kwake kwa ajili ya matumizi kulipokubaliwa, kwenye kuzidishwa maradufu kwa sababu kulitoka kwa imani na ikhlasi kamili. "Kwa kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao." Yani wanatoa na hali wamesimama imara kwa namna ya kufanya ukarimu na ukweli, basi mfano wa matendo haya "ni kama mfano wa bustani iliyo mahali pa juu." Napo ni mahali palipoinuka juu kwa sababu huwa panaonekana wazi kwa upepo na jua, na maji ndani yake ni mengi. Na hata kama mvua hiyo kubwa isipoinyea, inakuwa na umande wa kutosha kwa sababu ya uzuri wa mimea yake, na uzuri wa ardhi yake, na kupatikana kwa sababu zote zinazoleta kukua kwake, na kustawi kwake na kuzaa kwake. Na kwa sababu hii "ikaleta mazao yake maradufu" yani ikawa imezidishwa mizidisho. Na pepo hii iliyo na sifa hizi ndiyo ya juu zaidi wanayoiomba watu, kwani matendo mema yanalipwa kwa daraja za juu kabisa. Na ama mwenye kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha akafuatisha kutoa kwake masimbulizi na maudhi, au alifanya kitendo kisha akafanya cha kukibatilisha kitendo hicho, basi huyu mfano wake ni mfano wa mwenye hii bustani. Lakini ilitumiwa "kimbunga chenye moto, kwa hivyo ikaungua" ilhali ana dhuria dhaifu, naye pia ni dhaifu amekwisha patwa na uzee. Basi hali hii ni miongoni mwa hali za kutisha sana, na ndio maana alianzisha huu mfano kwa kauli yake. "Je, angependa mmoja wenu" hadi mwisho wake kwa swali linalojulikana kwa anayeongeleshwa kutisha kwake. Kwa maana, kuharibika kwake mara moja baada ya miti yake kuchanua na matunda yake kuiva, ni msiba mkubwa. Kisha kupatikana kwa huu mpigo hali ya kuwa mwenyewe ni mzee ambaye ameshadhoofika kufanya kazi. Naye ana dhuria dhaifu ambao hawawezi kumsaidia na hata matumizi yao yako juu yake ni msiba mwingine. Basi akawa mwenye mfano huu, ambaye alifanya matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Kisha akayabatilisha matendo yake kwa chenye kuyapinga inafanana na hali ya yule mwenye bustani ambayo yaliifanyikia yale yaliyofanyika wakati alipokuwa anaihitaji sana. Mfano wa tatu ni yule anayejionyesha kwa watu na hana imani kwa Mwenyezi Mungu wala hatarajii malipo yake mazuri. Kwani moyo wake unafananishwa na jiwe linaloteleza lenye udongo juu yake. Mwenye kuangalia atadhani kwamba mvua ikilinyeshea litaotesha mimea kama zinazvyootesha mimea ardhi nzuri. Lakini hili ni kama jiwe lililonyeshewa na mvua kubwa na ikaondoa udongo uliokuwa juu yake na ikaliacha tupu. Na huu ni mfano unaolingana na moyo wa yule anayejionyesha kwa watu ambao hauna imani. Bali yeye ni mgumu na wala halainiki wala hanyenyekei. Basi haya ndiyo matendo yake na kutoa kwake, havina msingi wa kuvisimamisha juu yake wala mwisho ambao vinaishia. Bali alichokifanya ni batili kwa sababu hakikuwa na masharti yake. Na kilicho kabla yake kilibatilika baada ya kupatikana kwa sharti kwa sababu ya kuwepo kizuizi. Na la kwanza lilikubaliwa na linazidishwa maradufu kwa sababu ya kuwepo kwa sharti lake ambalo ni imani na ikhlasi na uimara, na kutokuwepo vizuizi vyenye kuharibu. Na mifano hii tatu inaingia vizuri juu ya watenda matendo wote. Basi mja aipime nafsi yake na wengine kwa mizani hizi ya uadilifu na mifano inayolingana. "Na hiyo mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu isipokuwa wenye elimu."
: 267 - 268 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنْفِقُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُمْ مِنَ الْأَرْضِ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنْفِقُونَ وَلَسْتُمْ بِآخِذِيهِ إِلَّا أَنْ تُغْمِضُوا فِيهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ (267) الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُمْ بِالْفَحْشَاءِ وَاللَّهُ يَعِدُكُمْ مَغْفِرَةً مِنْهُ وَفَضْلًا وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ (268)}
(267) Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyowatolea katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, ilhali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa. 268. Shetani anawatia hofu ya ufakiri, na anawaamrisha machafu. Na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha kutoka kwake na fadhila. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.
#
{267 - 268} يحث الباري عباده على الإنفاق مما كسبوا في التجارات، ومما أخرج لهم من الأرض من الحبوب والثمار، وهذا يشمل زكاة النقدين والعروض كلها المعدة للبيع والشراء والخارج من الأرض من الحبوب والثمار. ويدخل في عمومها الفرض والنفل، وأمر تعالى أن يقصدوا الطيب منها ولا يقصدوا الخبيث وهو الرديء الدون يجعلونه لله، ولو بذله لهم من لهم حق عليه لم يرتضوه، ولم يقبلوه إلا على وجه المغاضاة والإغماض، فالواجب إخراج الوسط من هذه الأشياء والكمال إخراج العالي، والممنوع إخراج الرديء فإن هذا لا يجزي عن الواجب، ولا يحصل فيه الثواب التام في المندوب. {واعلموا أن الله غني حميد}؛ فهو غني عن جميع المخلوقين، وهو الغني عن نفقات المنفقين وعن طاعات الطائعين، وإنما أمرهم بها وحثهم عليها لنفعهم ومحض فضله وكرمه عليهم، ومع كمال غناه وسعة عطاياه فهو الحميد فيما يشرعه لعباده من الأحكام الموصلة لهم إلى دار السلام، وحميد في أفعاله التي لا تخرج عن الفضل والعدل والحكمة، وحميد الأوصاف لأن أوصافه كلها محاسن وكمالات لا يبلغ العباد كنهها ولا يدركون وصفها. فلما حثهم على الإنفاق النافع نهاهم عن الإمساك الضار، وبين لهم أنهم بين داعيين: داعي الرحمن يدعوهم إلى الخير ويعدهم عليه الخير والفضل والثواب العاجل والآجل وإخلاف ما أنفقوا، وداعي الشيطان الذي يحثهم على الإمساك، ويخوفهم إن أنفقوا أن يفتقروا. فمن كان مجيباً لداعي الرحمن، وأنفق مما رزقه الله فليُبْشِر بمغفرة الذنوب وحصول كل مطلوب، ومن كان مجيباً لداعي الشيطان فإنه إنما يدعو حزبه ليكونوا من أصحاب السعير، فليختر العبد أي الأمرين أليق به. وختم الآية بأنه {واسع عليم}؛ أي واسع الصفات كثير الهبات عليم بمن يستحق المضاعفة من العاملين، وعليم بمن هو أهل فيوفقه لفعل الخيرات، وترك المنكرات.
{267 - 268} Al-Bari (Muumba mwanzilishi) anawahimiza waja wake watoe katika yale waliyoyachuma katika biashara, na katika yale aliyowatolea katika ardhi kama vile nafaka na matunda. Na hili linajumuisha Zaka ya dhahabu na fedha na vitu vilivyotayarishwa kwa ajili ya kuuza na kununua, na kinachotoka katika ardhi kama vile nafaka na matunda. Na linajumlisha katika ujumla wake (kutoa kwa) faradhi na sunna. Na Mola Mtukufu aliamrisha kwamba wayakusudie vilivyo vizuri vyake, wala wasikusudie vilivyo vibaya na vilivyo duni; ati ndivyo wanavyompa Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa wao wangepewa hivyo na wale ambao wao wana haki juu yao, basi hawangeviridhia, na wala hawangevikubali isipokuwa kwa njia ya kupepesa na kufumba macho. Basi, la wajibu ni kutoa cha wastani katika mambo haya. Na ukamilifu ni kutoa cha juu, na kilichokatazwa ni kutoa kibaya. Kwa sababu, hili halitoshelezi wajibu, na wala hazipatikani ndani yake thawabu kamili katika lile linalopendekezwa. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa." Yeye havihitaji viumbe vyote, na hakuhitaji kutoa kwa wanaotoa, na hauhitaji utiifu wa watiifu. Yeye aliwaamrisha hayo tu na akawahimiza juu yake kwa manufaa yao na fadhila yake tupu na ukarimu juu yao. Na pamoja na ukamilifu wa kujitegemea kwake na upana wa vipawa vyake, Yeye ndiye Msifiwa katika yale anayowawekea waja wake sheria kama vile hukumu zenye kuwafikisha kwenye nyumba ya amani. Naye ni Msifiwa katika vitendo vyake visivyotoka nje ya fadhila, na uadilifu, na hekima. Naye ni mwenye sifa nzuri zaidi kwa sababu sifa zake zote ni nzuri na kamilifu ambazo waja hawafikii dhati zake, na hawafikii maelezo yake. Na alipowahimiza juu ya kutoa kwenye kuwanufaisha, akawakataza kutotoa kwenye kuwadhuru. Na akawabainishia kuwa wao wako baina ya walinganiaji wawili: Mlinganiaji wa Mwingi wa Rehema anayewalingania kwenye heri; na anawaahidi heri kwa hayo na fadhila na thawabu ya haraka na ya baadaye, na kuwarudishia walichotoa. Na mlinganiaji wa Shetani, ambaye anawahimiza juu ya kutotoa, na anawahofisha kwamba wakitoa, watakuwa mafakiri. Hivyo basi, atakayekuwa mwenye kumuitikia mlinganiaji wa Mwingi wa Rehema, na akatoa katika yale aliyomruzuku Mwenyezi Mungu. Basi na awe na bishara njema ya msamaha wa dhambi na kupata kila anachotafuta. Na yeyote atakayemuitikia mlinganiaji wa Shetani, basi yeye kwa hakika analiita kundi lake ili wawe miongoni mwa wenza wa Moto wenye mwako mkali. Basi mja na achague lolote la mambo mawili haya; lile linalomfaa zaidi. Na alihitimisha Aya hiyo kwa kusema; "ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua." Yani mwenye sifa pana, mwingi wa vipawa, mwenye kujua ni nani anayestahiki kuzidishiwa miongoni mwa watendaji matendo. Na mwenye kujua wanaostahiki, kwa hivyo anamuwezesha kufanya mema, na kuacha maovu.
: 269 #
{يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَنْ يَشَاءُ وَمَنْ يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ (269)}
(269) Yeye humpa hekima amtakaye. Na mwenye kupewa hekima, basi bila ya shaka amepewa heri nyingi. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili.
#
{269} لما ذكر أحوال المنفقين للأموال، وأن الله أعطاهم، ومنَّ عليهم بالأموال التي يدركون بها النفقات في الطرق الخيرية، وينالون بها المقامات السنية، ذكر ما هو أفضل من ذلك وهو أنه يعطي الحكمة من يشاء من عباده، ومن أراد بهم خيراً من خلقه، والحكمة هي العلوم النافعة والمعارف الصائبة والعقول المسددة والألباب الرزينة وإصابة الصواب في الأقوال والأفعال، وهذا أفضل العطايا وأجل الهبات، ولهذا قال: {ومن يؤت الحكمة فقد أوتي خيراً كثيراً}؛ لأنه خرج من ظلمة الجهالات إلى نور الهدى، ومن حمق الانحراف في الأقوال والأفعال إلى إصابة الصواب فيها وحصول السداد، ولأنه كمل نفسه بهذا الخير العظيم واستعد لنفع الخلق أعظم نفع في دينهم ودنياهم، وجميع الأمور لا تصلح إلا بالحكمة التي هي وضع الأشياء مواضعها وتنزيل الأمور منازلها، والإقدام في محل الإقدام، والإحجام في موضع الإحجام. ولكن ما يتذكر هذا الأمر العظيم وما يعرف قدر هذا العطاء الجسيم، {إلا أولو الألباب}؛ وهم أهل العقول الوافية والأحلام الكاملة، فهم الذين يعرفون النافع فيعملونه والضار فيتركونه، وهذان الأمران وهما بذل النفقات المالية وبذل الحكمة العلمية أفضل ما تقرب به المتقربون إلى الله وأعلى ما وصلوا به إلى أجل الكرامات، وهما اللذان ذكرهما النبي - صلى الله عليه وسلم - بقوله: «لا حسد إلا في اثنتين: رجل آتاه الله مالاً فسلطه على هلكته في الحق، ورجل آتاه الله الحكمة فهو يعلمها الناس».
{269} Alipotaja hali za watoao mali, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwapa na akawaneemesha na mali ambazo wanazitoa katika njia za heri. Na wanapata kwazo daraja tukufu, akataja kilicho bora kuliko hayo. Nacho ni kwamba yeye humpa hekima amtakaye katika waja wake, na anayewatakia heri katika viumbe vyake. Na hekima ni elimu zenye manufaa, na maarifa sahihi, na akili zilizonyooka, na uelewa timamu, na kufikia usahihi wa maneno na vitendo. Na hiki ndicho kipawa bora zaidi na zawadi kubwa zaidi. Na ndiyo maana akasema: "Na mwenye kupewa hekima, basi bila ya shaka amepewa heri nyingi." Kwa sababu, alitoka kwenye giza la ujinga hadi kwenye nuru ya uwongofu. Na kutoka katika upumbavu wa kupotoka katika maneno na vitendo hadi kufikia usahihi katika hayo, na kupata kunyooka. Na kwa sababu aliikamilisha nafsi yake kwa heri hii kubwa, na akajitayarisha kuwanufaisha viumbe manufaa makubwa zaidi katika dini yao na dunia yao. Na mambo yote hayawi mazuri isipokuwa kwa hekima ambayo ni kuweka vitu mahali pake, na kuteremsha vitu katika daraja zake. Na kwenda mbele katika pahali pa kwenda mbele, na kurudi nyuma katika pahali pa kurudi nyuma. Lakini halikumbuki jambo hili kubwa, na hajui thamani ya kipawa hiki kikubwa, "isipokuwa wenye ufahamu." Na wao ni wale wenye akili ya kutosha na busara kamilifu. Hao ndio wanaojua chenye manufaa na kwa hivyo wanakifanya. Na chenye madhara, kwa hivyo wanakiacha. Na mambo haya mawili ambayo ni kutoa matumizi ya kimali kwa wingi, na kutoa hekima ya kielimu kwa wingi, ndiyo bora zaidi cha vile wanavyojikurubisha kwavyo wale wanaojikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Na ndiyo ya juu zaidi waliyoyafika kwayo utukufu mkubwa. Na ndiyo mawili aliyoyataja Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwa kauli yake. “Hapana husuda isipokuwa katika mambo mawili: Mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa mali, basi akampa mamlaka juu ya kuitumia katika haki. Na mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa hekima, kwa hivyo huifundisha kwa watu.
: 270 - 271 #
{وَمَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ نَفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُمْ مِنْ نَذْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُهُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ (270) إِنْ تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ وَإِنْ تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ وَيُكَفِّرُ عَنْكُمْ مِنْ سَيِّئَاتِكُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (271)}
(270) Na chochote mnachotoa au nadhiri mnazoweka, basi hakika Mwenyezi Mungu anajua hayo. Na madhalimu hawana wowote wa kuwanusuru. (271) Mkizidhihirisha sadaka, basi hilo ni vizuri. Na mkizificha na mkawapa mafakiri kwa siri, basi hilo ni heri kwenu, na yatawaondolea katika maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu ana habari ya mnayoyatenda.
#
{270 - 271} يخبر تعالى أنه مهما أنفق المنفقون أو تصدق المتصدقون أو نذر الناذرون فإن الله يعلم ذلك. ومضمون الإخبار بعلمه يدل على الجزاء وأن الله لا يضيع عنده مثقالُ ذرة، ويعلم ما صدرت عنه من نيات صالحة أو سيئة، وأن الظالمين الذين يمنعون ما أوجب الله عليهم، أو يقتحمون ما حرم عليهم، ليس لهم من دونه أنصار ينصرونهم ويمنعونهم. وأنه لا بد أن تقع بهم العقوبات، وأخبر أن الصدقة إن أبداها المتصدق فهي خير، وإن أخفاها وسلمها للفقير كان أفضل، لأن الإخفاء على الفقير إحسان آخر، وأيضاً فإنه يدل على قوة الإخلاص. وأحد السبعة الذين يظلهم الله في ظله من تصدق بصدقة فأخفاها حتى لا تعلم شماله ما تنفق يمينه، وفي قوله: {وإن تخفوها وتؤتوها الفقراء فهو خير لكم}؛ فائدة لطيفة، وهو أن إخفاءها خير من إظهارها إذا أعطيت الفقير. فأما إذا صرفت في مشروع خيري لم يكن في الآية ما يدل على فضيلة إخفائها، بل هنا قواعد الشرع تدل على مراعاة المصلحة، فربما كان الإظهار خيراً لحصول الأسوة والاقتداء وتنشيط النفوس على أعمال الخير. وقوله: {ويكفر عنكم من سيئاتكم}؛ في هذا أن الصدقات يجتمع فيها الأمران: حصول الخير وهو كثرة الحسنات والثواب والأجر، ودفع الشرِّ والبلاء الدنيوي والأخروي بتكفير السيئات {والله بما تعملون خبير}؛ فيجازي كلا بعمله بحسب حكمته.
{270 - 271} Mola Mtukufu anajulisha kwamba chochote watoacho cha matumizi wenye kutoa, au sadaka watoayo wenye kutoa sadaka, au nadhiri wawekayo wenye kuweka nadhiri; basi hakika Mwenyezi Mungu anajua hilo. Na maudhui ya kujulisha kuhusu elimu yake yanaashiria malipo. Na kwamba Mwenyezi Mungu haupotei uzito wa chembe kwake. Na anajua nia gani nzuri au mbaya iliyotoka kwake. Na kwamba madhalimu wanaozuia yale aliyowawajibishia Mwenyezi Mungu au wanaoingia katika yale aliyowaharamishia; wao hawana kando na Yeye wasaidizi wowote wa kuwasaidia na kuwazuia. Na kwamba ni lazima adhabu ziwashukie. Na alijulisha kwamba ikiwa mwenye kutoa sadaka akiidhihirisha, basi hiyo ni bora. Na akiificha na akaikabidhi kwa fakiri, basi linakuwa bora zadi. Kwa sababu, kumpa masikini kwa kuficha ni wema mwingine. Na pia inaonyesha nguvu ya ikhlasi. Na mmoja wa wale saba ambao Mwenyezi Mungu atawatia katika kivuli chake, ni yule anayetoa sadaka na akaificha; mpaka mkono wake wa kushoto hukujua kile ambacho mkono wake wa kulia ulitoa. Na katika kauli yake: "Na mkiificha na mkawapa mafakiri kwa siri, basi hivyo ni heri kwenu," kuna faida nzuri. Nayo ni kwamba ukimpa fakiri, kuificha (sadaka) ni bora kuliko kuidhihirisha . Lakini ikiwa itatumika katika mradi wa hisani, basi hakuna katika aya chenye kuonyesha ubora katika kukificha. Bali, hapa misingi ya sheria inaonyesha kuzingatia masilahi. Kwa maana, pengine kuidhihirisha kukawa bora ili kuwe kielelezo na kuhamasisha nafsi juu ya kufanya matendo mema. Na kauli yake: "Na atawafutia katika maovu yenu." Kuna kwamba katika sadaka yanajumuika mambo mawili ndani yake: Kupatikana kwa heri, ambayo ni wingi wa mema na thawabu na malipo. Na kuepusha shari na balaa ya kidunia na kiakhera kwa kufuta maovu. "Na Mwenyezi Mungu ana habari ya mnayoyatenda." Kwa hivyo atamlipa kila mmoja kulingana na hekima yake.
: 272 #
{لَيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنْفُسِكُمْ وَمَا تُنْفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّهِ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنْتُمْ لَا تُظْلَمُونَ (272)]}.
(272) Si juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na chochote mnachotoa katika heri, basi ni cha nafsi zenu. Wala hamtoi isipokuwa kwa kutafuta uso wa Mwenyezi Mungu. Na chochote mnachotoa katika heri, mtalipwa kwa ukamilifu, nanyi hamtadhulumiwa.
#
{272} أي: إنما عليك أيها الرسول البلاغ وحث الناس على الخير وزجرهم عن الشرِّ، وأما الهداية فبيد الله تعالى. ويخبر عن المؤمنين حقاً أنهم لا ينفقون إلا لطلب مرضاة ربهم واحتساب ثوابه لأن إيمانهم يدعوهم إلى ذلك، فهذا خير وتزكية للمؤمنين، ويتضمن التذكير لهم بالإخلاص، وكرَّر علمه تعالى بنفقاتهم لإعلامهم أنه لا يضيع عنده مثقال ذرة وإن تك حسنة يضاعفها، ويؤت من لدنه أجراً عظيماً.
{272} Yani, ewe Mtume kilicho juu yako ni kufikisha tu na kuwahimiza watu kutenda mema, na kuwakemea kutokana na maovu. Ama uwongofu, basi hilo limo mkononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na anajulisha kuhusu Waumini wa kweli kwamba wao hawatoi ispokuwa kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na kutarajia thawabu yake. Kwa sababu imani yao inawaita katika hayo. Na hili ndio utakaso bora wa Waumini. Na inajumuisha kuwakumbusha kuwa na ikhlasi. Na alirudia elimu yake yeye Mtukufu kuhusu kutoa kwa matumizi ili kuwajulisha kuwa Yeye haupotei kwake uzito wa chembe. Hata kama ni wema mmoja, yeye huuzidisha, na hupeana kutoka kwake malipo makubwa.
: 273 - 274 #
{لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُمْ بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ (273) الَّذِينَ يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (274)}
273. Na wapewe mafakiri waliozuilika katika njia za Mwenyezi Mungu, wasioweza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiyewajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama zao; hawawang'ang'anilii watu kwa kuwaomba. Na chochote mnachotoa katika heri, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua. (274) Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao, wala wao hawatahuzunika.
#
{273} يعني أنه ينبغي أن تتحروا بصدقاتكم الفقراء الذين حبسوا أنفسهم في سبيل الله وعلى طاعته، وليس لهم إرادة في الاكتساب أو ليس لهم قدرة عليه وهم يتعففون إذا رآهم الجاهل ظن أنهم أغنياء {لا يسألون النّاس إلحافاً}؛ فهم لا يسألون بالكلية وإن سألوا اضطراراً لم يلحفوا في السؤال، فهذا الصنف من الفقراء أفضل ما وضعت فيهم النفقات لدفع حاجتهم وإعانة لهم على مقصدهم وطريق الخير وشكراً لهم على ما اتصفوا به من الصبر والنظر إلى الخالق لا إلى الخلق، ومع ذلك فالإنفاق في طرق الإحسان وعلى المحاويج حيثما كانوا فإنه خير وأجر وثواب عند الله ولهذا قال:
{273} Anamaanisha kwamba, mfanye hima kuwajua mafakiri ili muwape sadaka zenu ambao walijizuilia nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na utiifu wake. Na hawana nia ya kuchuma (kutoka kwa sadaka) wala hawana uwezo wa kuchuma. Nao wanajizuia kiwango kwamba wasiowajua wakiwaona, wanafikiri kwamba wao ni matajiri. "Hawawang'ang'anilii watu kwa kuwaomba." Wao hawaombi kabisa, na hata wakiomba kwa sababu ya dharura hawang'ang'anilii katika kuomba. Na aina hii ya mafakiri ndiyo bora zaidi ya kuyaweka matumizi haya ndani yao ili kuzuia mahitaji yao na kuwasaidia katika makusudio yao. Na njia ya heri na kuwashukuru juu ya kile wanachosifika kwacho cha subira, na kumtazama Muumba na siyo viumbe. Na pamoja na hayo, kutoa kutumia katika njia za wema, na juu ya wenye mahitaji popote pale walipo, ni jambo la heri na lenye malipo na thawabu kwa Mwenyezi Mungu. Na kwa sababu ya hili akasema:
#
{274} {الذين ينفقون أموالهم بالليل والنهار سراً وعلانية فلهم أجرهم عند ربهم ولا خوف عليهم ولا هم يحزنون}؛ فإن الله يظلهم بظله يوم لا ظل إلا ظله، وإن الله ينيلهم الخيرات ويدفع عنهم الأحزان والمخاوف والكريهات. وقوله: {فلهم أجرهم عند ربهم}؛ أي: كل أحد منهم بحسب حاله، وتخصيص ذلك بأنه عند ربهم يدل على شرف هذه الحال ووقوعها في الموقع الأكبر كما في الحديث الصحيح «إن العبد ليتصدق بالتمرة من كسب طيب فيتقبلها الجبار بيده فيربيها لأحدكم كما يربي أحدكم فَلُوَّه حتى تكون مثل الجبل العظيم».
{274} "Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao, wala wao hawatahuzunika." Mwenyezi Mungu atawatia katika kivuli chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake. Na Mwenyezi Mungu atawapa mema na kuwazuia huzuni, hofu na machukizo. Na kauli yake, "wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi." Yani kila mmoja wao kulingana na hali yake. Na kusema kwamba hilo liko hususan kwa Mola wao Mlezi kunaashiria utukufu wa hali hii, na kufikia kwake katika nafasi kubwa zaidi, kama ilivyo katika hadithi sahihi: “Hakika, mja anaweza toa sadaka ya tende kutoka katika kuchuma kuzuri, kwa hivyo Al-Jabbar (Afanyaye atakalo) anaikubali kwa mkono wake. Kisha akaikuzia mmoja wenu, kama vile mmoja wenu anavyomkuza mwana farasi wake aliyemwachisha kunyonya mpaka awe mfano wa mlima mkubwa.”
: 275 - 281 #
{الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَنْ جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِنْ رَبِّهِ فَانْتَهَى فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّهِ وَمَنْ عَادَ فَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (275) يَمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ (276) إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (277) يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (278) فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَإِنْ تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ (279) وَإِنْ كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَى مَيْسَرَةٍ وَأَنْ تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (280) وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّهِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (281)}
(275) Wale wanaokula riba, hawasimami isipokuwa kama anavyosimama aliyezugwa na Shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa walisema: Hakika, biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi mwenye kujiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akakomeka, basi yake ni yaliyokwisha pita. Na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia, basi hao ndio wenza wa Moto, wao watadumu humo. (276) Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukufuru na afanyae dhambi nyingi. (277) Hakika, wale walioamini na wakatenda mema na wakashika Swala na wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Wala haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika. (278) Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobaki, ikiwa nyinyi ni Waumini. (279) Na msipofanya, basi jitangazieni vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe. (280) Na (mdaiwa) akiwa ana ugumu, basi (mdai) angoje mpaka awe katika wepesi. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua. (281) Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilichochuma. Nao hawatadhulumiwa.
#
{275} لما ذكر الله حالة المنفقين وما لهم من الله من الخيرات وما يكفر عنهم من الذنوب والخطيئات ذكر الظالمين أهل الربا والمعاملات الخبيثة، وأخبر أنهم يجازون بحسب أعمالهم، فكما كانوا في الدنيا في طلب المكاسب الخبيثة كالمجانين عوقبوا في البرزخ والقيامة أنهم لا يقومون من قبورهم إلى يوم بعثهم ونشورهم {إلا كما يقوم الذي يتخبطه الشيطان من المس}؛ أي: من الجنون والصرع وذلك عقوبة وخزي وفضيحة لهم وجزاء لهم على مراباتهم ومجاهرتهم بقولهم: {إنما البيع مثل الربا}؛ فجمعوا ـ بجراءتهم ـ بين ما أحل الله وبين ما حرم الله واستباحوا بذلك الربا. ثم عرض تعالى التوبة على المرابين وغيرهم فقال: {فمن جاءه موعظة من ربه}؛ بيان مقرون به الوعد والوعيد {فانتهى}؛ عما كان يتعاطاه من الربا {فله ما سلف}؛ مما تجرأ عليه وتاب منه {وأمره إلى الله}؛ فيما يستقبل من زمانه فإن استمر على توبته، فالله لا يضيع أجر المحسنين. {ومن عاد}؛ بعد بيان الله وتذكيره وتوعده لأكل الربا {فأولئك أصحاب النار هم فيها خالدون}؛ في هذا أن الربا موجب لدخول النار والخلود فيها، وذلك لشناعته ما لم يمنع من الخلود مانع الإيمان، وهذا من جملة الأحكام التي تتوقف على وجود شروطها وانتفاء موانعها؛ وليس فيها حجة للخوارج كغيرها من آيات الوعيد، فالواجب أن تصدق جميع نصوص الكتاب والسنة فيؤمن العبد بما تواترت به النصوص من خروج من في قلبه أدنى مثقالِ حبة خردل من الإيمان من النار، ومن استحقاق هذه الموبقات لدخول النار إن لم يتب منها.
{275} Mwenyezi Mungu alipoitaja hali ya watoao, na heri walizo nazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na namna anavyowafutia katika dhambi na makosa. Akawataja madhalimu, watu wa riba na biashara mbaya, na akajulisha kuwa watalipwa kulingana na matendo yao. Basi kama walivyokuwa katika dunia wakitafuta mapato mabaya kama wendawazimu, wakaadhibiwa katika makaburi na siku ya Kiyama. Kwamba hawatasimama kutoka makaburini mwao mpaka siku ya kufufuliwa kwao na kutawanyika kwao. "Isipokuwa kama anavyosimama aliyezugwa na Shetani kwa kumgusa," yani kutokana na uwendawazimu na kifafa. Na hiyo ni adhabu, na hizaya, na fedheha kwao, na kuwalipa juu ya riba yao na kudhihirisha kwao kwa kauli yao. "Hakika, biashara ni kama riba tu." Basi wakajumuisha - pamoja na ujasiri wao - baina ya aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu na aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, na wakaruhusu riba kwa hilo. Kisha Mola Mtukufu akawawekea toba wale wanaoamiliana na riba na wengineo, akasema: "Basi mwenye kujiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi," na huku ni kubainisha kulikoambatana na ahadi na tishio. "Kisha akakomeka" na yale aliyokuwa akichukua katika riba, "basi yake ni yaliyokwisha pita" katika yale aliyoyafanyia ujasiri. Kisha akatubia akayaacha "na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu" katika siku zake zijazo. Ikiwa ataendelea na toba yake hiyo, basi Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mema. "Na wenye kurudia" baada ya kubainisha kwa Mwenyezi Mungu, na kumkumbusha kwake, na kumuonya kwake mwenye kula riba; "basi hao ndio wenza wa Moto, wao watadumu humo." Katika hili kuna kwamba riba inalazimu (mtu) kuingia Motoni na kudumu humo. Na hilo ni kwa sababu ya ubaya wake maadamu hajazuiwa kudumu humo na kuzuizi cha imani. Na hii ni miongoni mwa hukumu zinazotegemea kuwepo kwa masharti yake na kutokuwepo kwa vizuizi vyake. Na hakuna hoja ndani yake ya Khawarij kama maandiko mengineyo ya vitishio. Kwa hivyo, la lazima ni kusadiki maandiko yote ya Kitabu na Sunna. Kwa hivyo, mja anaamini yale yaliyokuja katika maandishi yasiyo na shaka, kuhusu kutoka kwa Motoni kwa yule ambaye; ndani ya moyo wake kuna uzito mdogo zaidi wa chembe ya haradali wa imani. Na kuhusu kustahiki mwenye kuyafanya madhambi yaangamizayo haya yanayomlazimu kuingia Motoni ikiwa hatatubu kutokana nayo.
#
{276} ثم أخبر تعالى أنه يمحق مكاسب المرابين ويربي صدقات المنفقين، عكس ما يتبادر لأذهان كثير من الخلق أن الإنفاق ينقص المال وأن الربا يزيده، فإن مادة الرزق وحصول ثمراته من الله تعالى، وما عند الله لا ينال إلا بطاعته وامتثال أمره، فالمتجرئ على الربا يعاقبه بنقيض مقصوده، وهذا مشاهد بالتجربة ومن أصدق من الله قيلاً {والله لا يحب كل كفار أثيم}؛ وهو الذي كفر نعمة الله، وجحد منَّة ربه وأثم بإصراره على معاصيه. ومفهوم الآية أن الله يحب من كان شكوراً على النعماء تائباً من المآثم والذنوب. ثم أدخل هذه الآية بين آيات الربا وهي قوله:
{276} Kisha Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba Yeye huyaondolea baraka mapato ya wenye riba, na huzibariki sadaka za wenye kutoa. Kinyume na inavyotangulia kuwajia wengi wa viumbe kwamba kutoa matumizi kunapunguza mali, na kwamba riba inaizidisha. Lakini asili ya riziki na kupata matunda yake ni kutoka kwa Mola Mtukufu. Na kile kilicho kwa Mwenyezi Mungu hakipatikani isipokuwa kwa kumtii Yeye na kufuata amri yake. Kwa hivyo mwenye kujasiri kuingia katika riba, ataadhibiwa kwa kinyume cha makusudio yake. Na hili linashuhudiwa kwa tajiriba. Na ni nani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu. "Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukufuru, afanyae dhambi." Naye ni yule aliyekufuru neema ya Mwenyezi Mungu, na akaikanusha hisani ya Mola wake Mlezi, na akapata dhambi kwa kuendelea kwake kumuasi. Maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya hii ni kwamba Mwenyezi Mungu humpenda kila mwenye kushukuru kwa neema, mwenye kutubia maovu na dhambi. Kisha akaiingiza Aya hii kati ya Aya za riba, nayo ni kauli yake:
#
{277 - 279} {إن الذين آمنوا وعملوا الصالحات وأقاموا الصلاة وآتوا الزكاة}؛ الآية لبيان أن أكبر الأسباب لاجتناب ما حرم الله من المكاسب الربوية تكميل الإيمان وحقوقه، خصوصاً إقامة الصلاة وإيتاء الزكاة، فإن الصلاة تنهى عن الفحشاء والمنكر، والزكاة إحسان إلى الخلق ينافي تعاطي الربا الذي هو ظلم لهم وإساءة عليهم، ثم وجه الخطاب للمؤمنين وأمرهم أن يتقوه ويذروا ما بقي من معاملات الربا التي كانوا يتعاطونها قبل ذلك وأنهم إن لم يفعلوا ذلك فإنهم محارِبون لله ورسوله، وهذا من أعظم ما يدل على شناعة الربا حيث جعل المصرَّ عليه محارباً لله ورسوله، ثم قال: {وإن تبتم}؛ يعني من المعاملات الربوية {فلكم رؤوس أموالكم لا تظلمون}؛ الناس بأخذ الربا {ولا تظلمون}؛ ببخسكم رؤوس أموالكم، فكل من تاب من الربا فإن كانت معاملات سالفة فله ما سلف وأمره منظور فيه، وإن كانت معاملات موجودة وجب عليه أن يقتصر على رأس ماله، فإن أخذ زيادة فقد تجرأ على الربا. وفي هذه الآية بيان لحكمة الربا وأنه يتضمن الظلم للمحتاجين بأخذ الزيادة وتضاعف الربا عليهم وهو واجب إنظارهم، ولهذا قال:
{277 - 279} "Hakika, wale walioamini na wakatenda mema na wakashika Swala na wakatoa Zaka." Aya hii ni kwa ajili ya kubainisha kuwa kubwa zaidi ya sababu za kujiepusha na yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu katika mapato yenye riba ni kuikamilisha imani na haki zake, hasa kushika swala na kutoa zaka. Kwa sababu, swala inakataza machafu na maovu. Nayo Zaka ambayo ni kuwafanyia viumbe wema inapingana na riba ambayo ni kuwadhulumu na kuwafanyia ubaya. Kisha akaelekeza mazungumzo kwa Waumini, na akawaamrisha kuiogopa (riba), na waache yale yaliyobaki katika mapatano ya riba ambayo walikuwa wakiyafanya kabla ya hapo. Na kwamba wasipofanya hivyo, basi wao wanapigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hili ni katika makubwa mno yanayoonyesha ubaya wa riba, kwani alimfanya mwenye kuendelea kuifanya kuwa anapigana vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kisha akasema, "na mkitubu" yani kutokana na miamala ya riba "basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu" watu kwa kuchukua riba "wala msidhulumiwe" kwa kupunguziwa mtaji wenu. Kwa hivyo, kila mwenye kutubia kutokana na riba, ikiwa ni miamala iliyopita, basi ni chake kilichopita, na jambo lake litachunguzwa. Na ikiwa ni miamila iliyopo basi inamlazimu kuchukua mtaji wake peke yake. Na ikichukua ziada, basi atakuwa ameifanyia riba ujasiri. Na katika Aya hii, kuna ubainisho wa hekima ya riba, na kwamba ni inajumuisha kuwadhulumu wenye mahitaji kwa kuchukua ziada na kuwazidishia riba, ingawa ni wajibu kuwapa muda. Na kwa sababu hii, akasema:
#
{280 - 281} {وإن كان ذو عسرة فنظرة إلى ميسرة}؛ أي: وإن كان الذي عليه الدَّين معسراً لا يقدر على الوفاء وجب على غريمه أن يُنْظِره إلى ميسرة، وهو يجب عليه إذا حصل له وفاء بأي طريق مباح أن يوفي ما عليه، وإن تصدق عليه غريمه بإسقاط الدَّينِ كلِّه أو بعضه فهو خير له، ويهون على العبد التزام الأمور الشرعية واجتناب المعاملات الربوية والإحسان إلى المعسرين؛ عِلْمُه بأن له يوماً يرجع فيه إلى الله ويوفيه عمله ولا يظلمه مثقال ذرة. كما ختم هذه الآية بقوله: {واتقوا يوماً ترجعون فيه إلى الله ثم توفى كل نفس ما كسبت وهم لا يظلمون}؛ ثم قال تعالى:
{280-281} "Na (mdaiwa) akiwa ni mwenye ugumu, basi (mdai) ampe muhula mpaka awe katika wepesi." Yani ikiwa anayedaiwa deni yuko katika hali ngumu, na hawezi kulilipa, basi inamlazimu mdai wake kumpa muda hadi apate wepesi. Naye inamlazimu akipata njia yoyote ile ya kulipa inayoruhusika kwamba alipe anachodaiwa. Na ikiwa mdai wake atampa sadaka kwa kulitupilia mbali deni lote au sehemu yake, basi hilo ni heri kwake. Na inamrahisishia mja kushikamana na mambo ya kisheria, na kuepuka miamala ya riba. Na kuwafanyia wema wale wenye ugumu akijua kwamba atakuwa na siku ambayo ndani yake atarejea kwa Mwenyezi Mungu. Na atamlipa matendo yake, na hatamdhulumu uzito wa chembe, kama alivyohitimisha Aya hii kwa kauli yake. "Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilichochuma. Nao hawatadhulumiwa." Kisha Mola Mtukufu akasema:
: 282 - 283 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنْتُمْ بِدَيْنٍ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى فَاكْتُبُوهُ وَلْيَكْتُبْ بَيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَنْ يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّهُ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا فَإِنْ كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِنْ رِجَالِكُمْ فَإِنْ لَمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّنْ تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَنْ تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَى وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا وَلَا تَسْأَمُوا أَنْ تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَى أَجَلِهِ ذَلِكُمْ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَى أَلَّا تَرْتَابُوا إِلَّا أَنْ تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ وَإِنْ تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّهُ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (282) وَإِنْ كُنْتُمْ عَلَى سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَقْبُوضَةٌ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُمْ بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّهَ رَبَّهُ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ وَمَنْ يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ (283)}.
(282) Enyi mlioamini! Mnapodaiana deni hadi muda maalumu, basi liandikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika kama alivyomfunza Mwenyezi Mungu. Basi na aandike, na mwenye deni juu yake aandikishe; na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi, wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na washuhudisheni mashahidi wawili katika wanaume wenu. Na ikiwa wanaume wawili hawapo, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao atapotea, basi mmoja wao amkumbushe huyo mwengine. Na mashahidi wasikatae pindi wanapoitwa. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo ya uadilifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na ya chini zaidi ili msiwe na shaka. Isipokuwa ikiwa ni biashara ya mkono kwa mkono mnayoifanya baina yenu, basi hapo hakuna ubaya juu yenu msipoiandika. Lakini wekeni mashahidi mnapouziana. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo, basi hakika huko ni kupita mipaka mlio nako. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kila kitu. (283) Na mkiwa katika safari, na hamkupata mwandishi, basi yatosha kukabidhiwa rehani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe, basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakayeuficha, basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda
#
{282} احتوت هذه الآيات على إرشاد الباري عباده في معاملاتهم إلى حفظ حقوقهم بالطرق النافعة والإصلاحات التي لا يقترح العقلاء أعلى ولا أكمل منها فإن فيها فوائد كثيرة: منها: جواز المعاملات في الديون سواء كانت ديون سلم أو شراء مؤجلاً ثمنه فكله جائز، لأن الله أخبر به عن المؤمنين، وما أخبر به عن المؤمنين فإنه من مقتضيات الإيمان وقد أقرهم عليه الملك الديان. ومنها: وجوب تسمية الأجل في جميع المداينات وحلول الإجارات. ومنها: أنه إذا كان الأجل مجهولاً فإنه لا يحل لأنه غرر وخطر فيدخل في الميسر. ومنها: أمره تعالى بكتابة الديون، وهذا الأمر قد يجب إذا وجب حفظ الحق كالذي للعبد عليه ولاية، كأموال اليتامى والأوقاف والوكلاء والأمناء، وقد يقارب الوجوب كما إذا كان الحق متمحضاً للعبد فقد يقوى الوجوب وقد يقوى الاستحباب، بحسب الأحوال المقتضية لذلك، وعلى كل حال فالكتابة من أعظم ما تحفظ به هذه المعاملات المؤجلة لكثرة النسيان ولوقوع المغالطات، وللاحتراز من الخونة الذين لا يخشون الله تعالى. ومنها: أمره تعالى للكاتب أن يكتب بين المتعاملين بالعدل فلا يميل مع أحدهما لقرابة ولا غيرها ولا على أحدهما لعداوة ونحوها. ومنها: أن الكتابة بين المتعاملين من أفضل الأعمال ومن الإحسان إليهما، وفيها حفظ حقوقهما وبراءة ذممهما كما أمره الله بذلك فليحتسب الكاتب بين الناس هذه الأمور ليحظى بثوابها. ومنها: أن الكاتب لا بد أن يكون عارفاً بالعدل معروفاً بالعدل، لأنه إذا لم يكن عارفاً بالعدل لم يتمكن منه، وإذا لم يكن معتبراً، عدلاً عند الناس، رضياً، لم تكن كتابته معتبرة، ولا حاصلاً بها المقصود الذي هو حفظ الحقوق. ومنها: أن من تمام الكتابة والعدل فيها أن يحسن الكاتب الإنشاء والألفاظ المعتبرة في كل معاملة بحسبها، وللعرف في هذا المقام اعتبار عظيم. ومنها: أن الكتابة من نعم الله على العباد التي لا تستقيم أمورهم الدينية ولا الدنيوية إلا بها، وأن من علَّمه الله الكتابة فقد تفضل عليه بفضل عظيم، فمن تمام شكره لنعمة الله تعالى أن يقضي بكتابته حاجات العباد ولا يمتنع من الكتابة ولهذا قال: {ولا يأب كاتب أن يكتب كما علمه الله}. ومنها: أن الذي يكتبه الكاتب هو اعتراف من عليه الحق إذا كان يحسن التعبير عن الحق الذي عليه، فإن كان لا يحسن ذلك لصغره أو سفهه أو جنونه أو خرسه أو عدم استطاعته، أملى عنه وليه، وقام وليه في ذلك مقامه. ومنها: أن الاعتراف من أعظم الطرق التي تُثبَت بها الحقوق حيث أمر الله تعالى أن يكتب الكاتب ما أملى عليه من عليه الحق. ومنها: ثبوت الولاية على القاصرين من الصغار والمجانين والسفهاء ونحوهم. ومنها: أن الولي يقوم مقام موليه في جميع اعترافاته المتعلقة بحقوقه. ومنها: أن من أمنته في معاملة وفوضته فيها فقوله في ذلك مقبول وهو نائب منابك، لأنه إذا كان الولي على القاصرين ينوب منابهم، فالذي وليته باختيارك وفوضت إليه الأمر أولى بالقبول واعتبار قوله وتقديمه على قولك عند الاختلاف. ومنها: أنه يجب على الذي عليه الحق إذا أملى على الكاتب أن يتقي الله ولا يبخس الحق الذي عليه فلا ينقصه في قدره ولا في وصفه ولا في شرط من شروطه أو قيد من قيوده، بل عليه أن يعترف بكل ما عليه من متعلقات الحق كما يجب ذلك إذا كان الحق على غيره له، فمن لم يفعل ذلك فهو من المطففين الباخسين. ومنها: وجوب الاعتراف بالحقوق الجلية والحقوق الخفية وأن ذلك من أعظم خصال التقوى، كما أن ترك الاعتراف بها من نواقض التقوى ونواقصها. ومنها: الإرشاد إلى الإشهاد في البيع فإن كانت في المداينات فحكمها حكم الكتابة كما تقدم، لأن الكتابة هي كتابة الشهادة، وإن كان البيع بيعاً حاضراً فينبغي الإشهاد فيه ولا حرج فيه بترك الكتابة لكثرته وحصول المشقة فيه. ومنها: الإرشاد إلى إشهاد رجلين عدلين فإن لم يمكن أو تعذر أو تعسر فرجل وامرأتان، وذلك شامل لجميع المعاملات، بيوع الإدارة وبيوع الديون وتوابعها من الشروط والوثائق وغيرها. وإذا قيل قد ثبت أنه - صلى الله عليه وسلم - قضى بالشاهد الواحد مع اليمين ، والآية الكريمة ليس فيها إلا شهادة رجلين أو رجل وامرأتين، قيل: الآية الكريمة فيها إرشاد الباري عباده إلى حفظ حقوقهم ولهذا أتى فيها بأكمل الطرق وأقواها، وليس فيها ما ينافي ما ذكره النبي - صلى الله عليه وسلم - من الحكم بالشاهد واليمين، فباب حفظ الحقوق في ابتداء الأمر يرشد فيه العبد إلى الاحتراز والتحفظ التام، وباب الحكم بين المتنازعين ينظر فيه إلى المرجحات والبينات بحسب حالها. ومنها: أن شهادة المرأتين قائمة مقام الرجل الواحد في الحقوق الدنيوية وأما في الأمور الدينية كالرواية والفتوى فإن المرأة فيه تقوم مقام الرجل، والفرق ظاهر بين البابين. ومنها: الإرشاد إلى الحكمة في كون شهادة المرأتين عن شهادة الرجل وأنه لضعف ذاكرة المرأة غالباً وقوة حافظة الرجل. ومنها: أن الشاهد لو نسي شهادته فذكره الشاهد الآخر فذكر، أنه لا يضر ذلك النسيان إذا زال بالتذكير لقوله: {أن تضل إحداهما فتذكر إحداهما الأخرى}؛ ومن باب أولى إذا نسي الشاهد ثم ذكر من دون تذكير، فإن الشهادة مدارها على العلم واليقين. ومنها: أن الشهادة لا بد أن تكون عن علم ويقين لا عن شكِّ، فمتى صار عند الشاهد ريب في شهادته ولو غلب على ظنه لم يحل له أن يشهد إلا بما يعلم. ومنها: أن الشاهد ليس له أن يمتنع إذا دعي للشهادة سواء دعي للتحمل أو للأداء وأن القيام بالشهادة من أفضل الأعمال الصالحة كما أمر الله بها وأخبر عن نفعها ومصالحها. ومنها: أنه لا يحل الإضرار بالكاتب ولا بالشهيد بأن يدعيا في وقت أو حالة تضرهما. وكما أنه نهي لأهل الحقوق والمتعاملين أن يضاروا الشهود والكتاب فإنه أيضاً نهي للكاتب والشهيد أن يضار المتعامليْن أو أحدهما. وفي هذا أيضاً أن الشاهد والكاتب إذا حصل عليهما ضرر في الكتابة والشهادة أنه يسقط عنهما الوجوب. وفيها: التنبيه على أن جميع المحسنين الفاعلين للمعروف لا يحل إضرارهم وتحميلهم ما لا يطيقون، فهل جزاء الإحسان إلا الإحسان؟ وكذلك على من أحسن وفعل معروفاً أن يتمم إحسانه بترك الإضرار القولي والفعلي بمن أوقع به المعروف، فإن الإحسان لا يتم إلا بذلك. ومنها: أنه لا يجوز أخذ الأجرة على الكتابة والشهادة حيث وجبت لأنه حق أوجبه الله على الكاتب والشهيد، ولأنه من مضارة المتعاملين. ومنها: التنبيه على المصالح والفوائد المترتبة على العمل بهذه الإرشادات الجليلة وأن فيها حفظ الحقوق والعدل وقطع التنازع والسلامة من النسيان والذهول ولهذا قال: {ذلكم أقسط عند الله وأقوم للشهادة وأدنى ألا ترتابوا}؛ وهذه مصالح ضرورية للعباد. ومنها: أن تعلم الكتابة من الأمور الدينية، لأنها وسيلة إلى حفظ الدين والدنيا وسبب للإحسان. ومنها: أن من خصه الله بنعمة من النعم يحتاج الناس إليها فمن تمام شكر هذه النعمة أن يعود بها على عباد الله وأن يقضي بها حاجاتهم لتعليل الله النهي عن الامتناع عن الكتابة بتذكير الكاتب بقوله: {كما علمه الله}؛ ومع هذا فمن كان في حاجة أخيه كان الله في حاجته. ومنها: أن الإضرار بالشهود والكتاب فسوق بالإنسان، فإن الفسوق هو الخروج عن طاعة الله إلى معصيته، وهو يزيد وينقص ويتبعض، ولهذا لم يقل فأنتم فساق أو فاسقون بل قال: {فإنه فسوق بكم}؛ فبقدر خروج العبد عن طاعة ربه فإنه يحصل به من الفسوق بحسب ذلك، واستدل بقوله تعالى: {واتقوا الله ويعلمكم الله}؛ أن تقوى الله وسيلة إلى حصول العلم، وأوضح من هذا قوله تعالى: {يا أيها الذين آمنوا إن تتقوا الله يجعل لكم فرقاناً}؛ أي: علماً تفرقون به بين الحقائق والحق والباطل. ومنها: أنه كما أنه من العلم النافع تعليم الأمور الدينية المتعلقة بالعبادات فمنه أيضاً تعليم الأمور الدنيوية المتعلقة بالمعاملات، فإن الله تعالى حفظ على العباد أمور دينهم ودنياهم، وكتابه العظيم فيه تبيان كل شيء. ومنها: مشروعية الوثيقة بالحقوق وهي الرهون والضمانات التي تكفل للعبد حصول حقه سواء عامل برًّا أو فاجراً أميناً أو خائناً، فكم في الوثائق من حفظ حقوق وانقطاع منازعات. ومنها: أن تمام الوثيقة في الرهن أن يكون مقبوضاً، ولا يدل ذلك على أنه لا يصح الرهن إلا بالقبض بل التقييد بكون الرهن مقبوضاً يدل على أنه قد يكون مقبوضاً تحصل به الثقة التامة وقد لا يكون مقبوضاً فيكون ناقصاً. ومنها: أنه يستدل بقوله:
{282} Aya hizi zinajumuisha Al-Bari (Muumba mwanzilishi) kuwaelekeza waja wake katika kuamiliana kwao. Kwamba wahifadhi haki zao kwa njia zenye manufaa na marekebisho ambayo hawawezi watu wenye hekima kupendekeza kilicho juu zaidi wala kamili zaidi kuliko hili. Kwani ndani yake kuna manufaa mengi: Miongoni mwake ni kuruhusika kufanya miamala katika madeni, sawa yawe ni madeni ya Salam, au kununua ambako thamani italipwa baadaye. Yote hayo yanaruhusika, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliyajulisha kuhusu Waumini. Na lolote alilojulisha kuhusu Waumini, hilo ni miongoni mwa matakwa ya imani. Na aliwakubalia hilo yeye Mfalme, Atakayehesabu matendo yao. Na miongoni mwake ni ulazima wa kutaja muda maalumu katika madeni yote, na muda wa mwisho wa mikataba ya kukodisha. Na miongoni mwake ni kwamba, ikiwa muda haujulikani, basi hilo haliruhusiki. Kwa sababu ni udanganyifu na hatari, hivyo linaingia katika kamari. Na miongoni mwake, ni amri yake Mola Mtukufu ya kuyaandika madeni. Na amri hii inaweza kuwa wajibu inapokuwa ni wajibu kuihifadhi haki. Kama ile ambayo ni ya mja aliye katika ulinzi wake, kama vile mali za mayatima, na wakfu, na mawakala na wadhamini. Na inaweza kukaribia kuwa wajibu kama vile inapokuwa haki ni ya mtu mwenyewe peke yake. Basi ulazima unaweza kuwa na nguvu, na (kusamehe na) kutarajia malipo kwa Mwenyezi Mungu kulingana na hali zinazolazimu hilo. Na kwa vyovyote vile, kuandika ni katika mambo makubwa zaidi ambayo miamala hii ya baadaye huhifadhiwa kwayo. Kwa sababu ya wingi wa usahaulifu na kutokea kwa makosa, na kwa ajili ya kuilinda dhidi ya wasaliti ambao hawamchi Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na miongoni mwake, ni amri yake Mola Mtukufu kwamba mwandishi andike baina ya wawili wanaoamiliana kwa uadilifu. Wala asiegemee upande wa mmoja wao kwa sababu ya ujamaa kati yao au kitu kinginecho. Wala dhidi ya mmoja wao sababu ya uadui kati yao na mfano wake. Na miongoni mwake ni kwamba, kuandika baina ya wale wanaoamiliana ni miongoni mwa matendo bora kabisa zaidi, na ni miongoni mwa kuwatendea wema. Na ndani yake kuna kuhifadhi haki zao na kuwafanya kutokuwa na hatia, kama Mwenyezi Mungu alivyomwamrisha kufanya hivyo. Basi mwandishi kati ya watu na atarajie malipo kwa Mwenyezi mungu juu ya mambo haya ili apate thawabu zake. Na miongoni mwake ni kwamba, mwandishi ni lazima atambue uadilifu na ajulikane kwa uadilifu. Kwani asipoujua uadilifu, basi hataufikia. Na akiwa hazingatiwi kuwa mwadilifu kwa watu mwenye kuridhiwa, basi kuandika kwake huko hakutazingatiwa. Na wala makusudio ambayo ni kuhifadhi haki, hayatafikiwa kupitia kuandika huko. Na miongoni mwake ni kwamba, katika ukamilifu wa uandishi na uadilifu katika hilo ni kwamba mwandishi awe na utunzi mzuri. Na utumizi wa maneno yanayozingatiwa katika kila muamala kwa mujibu wake. Na desturi katika suala hili ina mazingatio makubwa. Na miongoni mwake ni kwamba, uandishi ni katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake; ambao mambo yao ya kidini wala ya kidunia hayanyooki isipokuwa kwayo. Na kwamba yule ambaye Mwenyezi Mungu alimfundisha kuandika, basi amempa fadhila kubwa. Basi katika ukamilifu wa shukrani yake juu ya neema hiyo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuwatimizia waja mahitaji yao kwa kuandika kwake huko, wala asikatae kuandika. Na kwa sababu, akasema, "wala mwandishi asikatae kuandika kama alivyomfunza Mwenyezi Mungu." Na miongoni mwake ni kile anachoandika mwandishi ni kukiri kwa yule ambaye haki iko juu yake ikiwa ana uwezo wa kuieleza haki ambayo iko juu yake. Na ikiwa hawezi kufanya hivyo vizuri kwa sababu ya umri wake mdogo, au upumbavu wake, au wazimu wake, au ububu wake au kutokuwa na uwezo kwake; basi mlinzi wake atamwandikishia, na mlinzi wake atachukua mahali pake. Na miongoni mwake ni kwamba, kukiri ni katika njia kubwa zaidi ambazo haki huthibitishwa. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyoamrisha kwamba, mwandishi aandike yale aliyoandikishwa na yule ambaye deni liko juu yake. Na miongoni mwake, ni kuwepo kwa ulinzi juu ya wale wasiojiweza kama vile watoto, wendawazimu, wapumbavu, na mfano wao. Na miongoni mwake ni kwamba, mlinzi anachukua nafasi ya mlezi wake katika kukiri kwake kwote kunakohusiana na haki zake. Na miongoni mwake ni kwamba, yule unayemkabidhi amana katika muamala na ukamkabidhi usimamizi katika hilo; basi kauli yake katika hilo inakubalika, naye ni mwakilishi wako. Kwa sababu ikiwa mlezi wa wasiojiweza anafanya kwa niaba yao, basi yule uliyempa mamlaka kwa uteuzi wako na ukamkabidhi jambo lako anastahiki zaidi kukubaliwa, na kuzingatiwa kauli yake na kuitanguliza mbele ya kauli yako iwapo kuna hitilafu. Na miongoni mwake ni kwamba, ni wajibu juu ya yule ambaye haki iko juu yake anapomwandikisha mwandishi amche Mwenyezi Mungu; na wala asipunguze haki ambayo iko juu yake. Basi na asipunguze katika kiwango chake wala maelezo yake, wala katika sharti miongoni mwa masharti yake wala kikwazo katika vikwazo vyake. Bali ni juu yake akiri kila anachodaiwa na vinavyoambatana na haki hiyo. Na hilo linavyokuwa wajibu ikiwa ni haki yake juu ya wengine. Kwa hivyo asiyefanya hivyo, basi yeye ni miongoni mwa wapunjao, wapunguzao. Na miongoni mwake ni ulazima wa kukiri haki zilizo dhahiri, na haki zilizofichika, na kwamba hilo ni katika kubwa zaidi ya sifa za uchamungu. Kama vile kuacha kuzikiri ni miongoni mwa yale yanayobatilisha uchamungu na yenye kuupunguza. Na miongoni mwake, ni kuelekeza kushuhudisha katika mauziano. Na ikiwa ni katika kudaiana, basi hukumu yake ni sawa na hukumu ya kuandika kama ilivyotangulia. Kwa sababu, kuandika ni kuandika ushahidi. Na ikiwa mauziano ni ya papo hapo, basi inapaswa kushuhudiwa hilo. Lakini hakuna ubaya kuacha kuandika kwa sababu ya wingi wake na kutokea kwa ugumu ndani yake. Na miongoni mwake, ni kuelekeza kuwashuhudisha wanaume wawili waadilifu. Na ikiwa hawapo, au haiwezekani, au ni vigumu, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili. Na hilo linajumuisha maamiliano yote. Mauziano ya papo hapo, na mauziano kwa mkopo, na yale yanayoambatana nayo kama vile masharti na hati na mengineyo. Na ikisemekana kwamba imethibiti kwamba yeye, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alihukumu kwa ushahidi wa mtu mmoja pamoja na kiapo. Ilhali Aya hii tukufu haina isipokuwa ushahidi wa wanaume wawili au mwanamume mmoja na wanawake wawili. Itasemwa: Aya hii tukufu ina mwongozo wa Al-Bari (Muumba mwanazilishi) kwa waja wake katika kuzihifadhi haki zao. Na kwa sababu hii ndiyo akaweka ndani yake njia kamili zaidi ya hilo na yenye nguvu zaidi. Na hakuna chochote ndani yake kinachopingana na alichotaja Nabii, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - cha kuhukumu kwa shahidi mmoja na kiapo. Kwa hivyo, mlango wa kuhifadhi haki mwanzo kwa jambo hilo, mja anaelekezwa katika hilo kutahadhari na kuhifadhi kikamilifu. Na mlango wa kuhukumu baina ya wanaogombana hapo inaangaliwa kilicho sahihi zaidi na maelezo kulingana na hali zake. Na miongoni mwake ni kwamba, ushahidi wa wanawake wawili unasimama katika nafasi ya mwanamume mmoja katika haki za kidunia. Ama katika mambo ya kidini, kama vile riwaya (ya Qurani na hadithi) na fatwa, basi mwanamke katika hayo anasimama katika nafasi ya mwanamume mmoja. Na tofauti iko wazi baina ya milango hii miwili. Na miongoni mwake, ni kuelekeza kwenye hekima katika ukweli kwamba, ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na ushahidi wa mwanamume mmoja. Na kwamba kwa sababu ya udhaifu wa kumbukumbu za mwanamke mara nyingi, na nguvu ya kumbukumbu ya mwanamume. Na miongoni mwake, ni ikiwa shahidi atasahau ushahidi wake, na shahidi mwingine akamkumbusha naye akakumbuka, kwamba hakudhuru kusahau huko kunapoisha. Kwa sababu ya kauli yake, "ili akisahau mmoja wao, basi mmoja wao atamkumbusha huyo mwingine". Na hata la aula zaidi ni kwamba shahidi akisahau, kisha akakumbuka bila ya kukumbushwa, basi ushahidi unazunguka kwenye elimu na yakini. Na miongoni mwake, ni ushahidi ni lazima uwe kutokana na elimu na yakini, na siyo kutokana na shaka. Na pindi shahidi atakuwa na shaka katika ushahidi wake, hata ikiwa ni uwezekano mkubwa tu wa shaka; basi haiwi halali kwake kushuhudia isipokuwa kwa anachokijua. Na miongoni mwake, ni kwamba shahidi hana haki ya kukataa akiitwa kutoa ushahidi, sawa aliitwa kusikiliza au kutoa ushahidi. Na kwamba kutoa ushahidi ni miongoni mwa matendo mema yaliyo bora zaidi. Kama alivyoamrisha kwalo Mwenyezi Mungu na akajulisha kuhusu manufaa yake na masilahi yake. Na miongoni mwake ni kwamba, siyo halali kumdhuru mwandishi au shahidi kwa kuwaita katika wakati au hali inayoweza kuwadhuru. Kama vile lilivyo katazo kwa wenye haki na wale wanaoamiliana kuwadhuru mashahidi na waandishi. Na vile vile ni katazo kwa mwandishi na shahidi kuwadhuru wale wanaoamiliana au mmoja wao. Na katika hili pia, ni kwamba ikiwa shahidi na mwandishi watapatwa na madhara katika kuandika na kushuhudia, basi ulazima unawaondokea. Na miongoni mwake, ni kupeana tanbihi kwamba wahisani wote wanaofanya wema siyo halali kuwadhuru na kuwabebesha wasiyoyaweza. Kwani malipo ya ihsani siyo (kingine) isipokuwa ihsani? Basi vile vile, mwenye kufanya hisani na akatenda wema ni juu yake kukamilisha ihsani yake hiyo, kwa kuacha kuwadhuru kimaneno na kikauli wale aliowafanyia wema; kwa sababu ihsani haikamiliki isipokuwa kwa hilo. Na miongoni mwake ni kuwa, hairuhusiki kuchukua malipo kwa ajili ya kuandika na kutoa ushahidi pale inapolazimu. Kwa sababu ni haki ambayo Mwenyezi Mungu ameilazimisha juu ya mwandishi na shahidi, na kwa sababu ni katika kuwadhuru wale wanaoamiliana. Na miongoni mwake ni tanbihi juu ya masilahi na manufaa yanayotokana na kutenda kulingana na maelekezo haya makubwa. Na kwamba yamo kuhifadhiwa kwa haki, na uadilifu, na kukata migogoro. Na kuwa usalama kutokana na kusahau na kupoteza mawazo. Na ndiyo maana akasema: "Hayo ndiyo uadilifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na ya chini zaidi kuwafanya msiwe na shaka". Haya ni masilahi ya lazima ya waja. Na miongoni mwake ni kwamba kujifunza kuandika ni miongoni mwa mambo ya kidini. Kwa sababu ni njia ya kuhifadhi dini na dunia, na ni sababu ya kufanya wema. Na miongoni mwake ni kwamba, mwenye kuteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa kumpa neema fulani miongoni mwa neema wanazozihitaji watu, basi katika ukamilifu wa kuzishukuru neema hizi ni kuzirudisha kwa waja wa Mwenyezi Mungu. Na kuwatimizia mahitaji yao kwazo, kwa sababu Mwenyezi Mungu alifanya sababu ya kumkataza kuandika, kwa kumkumbusha mwandishi juu ya kauli yake. "Kama Mwenyezi Mungu alivyomfundisha." Pamoja na hayo, yeyote anayemkidhia ndugu yake mahitaji, basi Mwenyezi Mungu atamkidhia mahitaji yake. Na miongoni mwake ni kwamba kuwadhuru mashahidi na mwandishi ni kuruka mipaka kwa mtu. Kwa sababu Al-Fusuuq ni kutoka katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kumuasi. Nayo huongezeka na hupungua na inagawanyia sehemu. Na ndiyo maana hakusema, "basi nyinyi ni mafasiki (yani mtu kutoka katika utiifu)." Bali alisema, "basi hakika huko ni kupita mipaka mliko nako." Na kwa kiwango cha mja kutoka katika utiifu wa Mola wake Mlezi, basi anatoka katika mipaka kulingana na hilo. Na kauli ya Mwenyezi Mungu, "na mcheni Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawafundisha," ilitumika kama ushahidi kwamba uchamungu ni njia ya kupata elimu. Na iliyo wazi zaidi kuliko hiyo ni kauli yake Mtukufu. "Enyi mlioamini, ikiwa mtamcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuzi." Yani elimu ambayo kwayo mnatofautisha baina ya uhakika, haki na batili. Na miongoni mwake ni kwamba, kama ilivyo elimu yenye manufaa kujifundisha mambo ya kidini yanayohusiana na ibada. Pia katika hilo ni kujifundisha mambo ya kidunia yanayohusiana na miamala. Kwa maana, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewahifadhia waja mambo ya dini yao na dunia yao, na kitabu chake kitukufu kimo ubainisho wa kila kitu. Na miongoni mwake ni uhalali wa kudhamini haki, ambako ni rehani na dhamana ambazo zinamhakikishia mja kwamba atapata haki yake. Sawa awe anaamiliana na mtu mwema au muovu, mkweli au msaliti. Na ni kwa dhamana ngapi ambazo zinazohifadhiwa haki na kukata migogoro. Na miongoni mwake ni kwamba ukamilifu wa dhamana katika rehani ni kwamba iwe imepokewa tayari. Na hilo halionyeshi kwamba rehani siyo halali isipokuwa kwa kuipokea. Bali kutaja hususan kuwa rahani iwe imepokewa kunaashiria kwamba, inaweza kuwa imepokewa kupokewa kunakoleta dhamana kamili. Na huenda ikawa haijapokewa, kwa hivyo ikawa pungufu. Na miongoni mwake ni kwamba ushahidi unachukuliwa katika kauli yake:
#
{283} {فرهان مقبوضة}؛ أنه إذا اختلف الراهن والمرتهن في مقدار الدين الذي به الرهن أن القول قول المرتهن صاحب الحق لأن الله جعل الرهن وثيقة به فلولا أنه يقبل قوله في ذلك لم تحصل به الوثيقة لعدم الكتابة والشهود. ومنها: أنه يجوز التعامل بغير وثيقة ولا شهود لقوله: {فإن أمن بعضكم بعضاً فليؤد الذي ائتمن أمانته}؛ ولكن في هذه الحال يحتاج إلى التقوى والخوف من الله وإلا فصاحب الحق مخاطر في حقه ولهذا أمر الله في هذه الحال من عليه الحق أن يتقي الله ويؤدي أمانته. ومنها: أن من ائتمنه معاملة فقد عمل معه معروفاً عظيماً ورضي بدينه وأمانته فيتأكد على من عليه الحق أداء الأمانة من الجهتين: أداء لحق الله وامتثالاً لأمره، ووفاء بحق صاحبه الذي رضي بأمانته ووثق به. ومنها: تحريم كتم الشهادة وأن كاتمها قد أثم قلبه الذي هو ملك الأعضاء، وذلك لأن كتمها كالشهادة بالباطل والزور فيها ضياع الحقوق وفساد المعاملات والإثم المتكرر في حقه وحق من عليه الحق. وأما تقييد الرهن بالسفر مع أنه يجوز حضراً وسفراً فللحاجة إليه لعدم الكاتب والشهيد. وختم الآية بأنه عليم بكل ما يعمله العباد كالترغيب لهم في المعاملات الحسنة والترهيب من المعاملات السيئة.
{283} "Basi yatosha kukabidhiwa rehani " Kwamba ikiwa aliyeweka rehani na aliyepewa rehani watatofautiana katika kiasi cha deni ambalo limewekewa rehani; kwamba kauli sahihi ni kauli ya aliyeweka rehani, mwenye haki. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliifanya rehani kuwa ni dhamana ya kulinda haki yake. Na lau kuwa isingekubaliwa kauli yake katika hilo, basi dhamana isingepatikana ndani yake kwa sababu ya ukosefu wa maandishi na mashahidi. Na miongoni mwake ni kwamba, inaruhusika kuamiliana bila ya dhamana wala mashahidi. Kwa kauli yake, "na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe, basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake." Lakini katika hali hii, anahitaji uchamungu na hofu kwa Mwenyezi Mungu, vinginevyo mwenye haki anahatarisha haki yake. Na kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu aliamrisha katika hali hii yule ambaye haki iko juu yake, kumcha Mwenyezi Mungu na kuirudisha amana yake. Na miongoni mwake ni kwamba, unayemkabidhi muamala, basi amemfanyia hisani kubwa na ameridhika na dini yake na uaminifu wake. Basi anamlazimu mno yule ambaye kuna haki juu yake kutekeleza amana yake kwa pande mbili: Kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu na kufuata amri yake. Na kutimiza haki ya mwenzake ambaye aliridhika na uaminifu wake na akamwamini. Na miongoni mwake ni, uharamu wa kuficha ushuhuda. Na kwamba mwenye kuificha moyo wake umetenda dhambi ambayo ndio mfalme wa viungo. Na hilo ni kwa sababu kuificha ni sawa na kutoa ushahidi wa batili na uwongo. Ambao ndani yake kuna kupoteza haki na kuharibika kwa miamala, na dhambi ya kujirudia katika dhima yake na dhima ya yule ambaye haki iko juu yake. Na ama kuifungamanisha rehani na safari pamoja na kwamba inaruhusika nyumbani na safarini, ni kwa sababu ya kulihitaji hilo kwa sababu ya kutokuwepo mwandishi na shahidi. Na alihitimisha Aya hii kwa kusema kuwa Yeye ni Mwenye kujua kila wanachofanya waja wake. (Ili) iwe kama himizo kwao kufanya maamiliano mazuri, na kuwatia hofu kutokana na maamiliano maovu.
: 284 #
{لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَإِنْ تُبْدُوا مَا فِي أَنْفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُمْ بِهِ اللَّهُ فَيَغْفِرُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (284)}.
284. Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo katika mbingu na viliomo katika dunia. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atawahesabu kwayo. Kisha atamsamehe amtakaye na amwadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.
#
{284} يخبر تعالى بعموم ملكه لأهل السماء والأرض وإحاطة علمه بما أبداه العباد وما أخفوه في أنفسهم، وأنه سيحاسبهم به {فيغفر لمن يشاء} وهو المنيب إلى ربه الأواب إليه، {إنه كان للأوابين غفوراً}؛ {ويعذب من يشاء} وهو المصر على المعاصي في باطنه وظاهره، وهذه الآية لا تنافي الأحاديث الواردة في العفو عما حدَّث به العبد نفسه ما لم يعمل أو يتكلم ، فتلك الخطرات التي تتحدث بها النفوس التي لا يتصف بها العبد ولا يصمم عليها، وأما هنا فهي العزائم المصممة والأوصاف الثابتة في النفوس، أوصاف الخير وأوصاف الشر، ولهذا قال: {ما في أنفسكم}؛ أي: استقر فيها وثبت من العزائم والأوصاف. وأخبر أنه {على كل شيء قدير}؛ فمن تمام قدرته محاسبة الخلائق وإيصال ما يستحقونه من الثواب والعقاب.
{284} Mola Mtukufu anajulisha ujumla wa ufalme wake juu ya wakazi wa mbinguni na ardhini. Na kuenea kwa elimu yake yale waliyoyaweka wazi waja wake na yale waliyoyaficha katika nafsi zao, na kwamba atawahesabu kwayo. "Kisha atamsamehe amtakaye." Naye ni yule anayerejea kwa Mola wake Mlezi na kutubia kwake. "Basi Yeye hakika, ni Mwenye kuwasamehe wanaotubia kwake." "Na amwadhibu amtakaye," naye ni yule anayeendelea kufanya maasia kwa ndani yake na nje yake. Na Aya hii haipingani na hadithi zilizokuja kuhusu kumsamehe alichojisemeza mja ndani ya nafsi yake, maadamu hakufanya wala kuzungumza. Hayo ni mawazo ambayo yanapita ndani ya nafsi, ambayo hasifiki mja kwayo wala hayaazimii. Ama hapa, ni maazimio aliyokwisha yaamulia na sifa zilizoimarika katika nafsi yake, na sifa nzuri na sifa mbaya. Na ndiyo maana akasema, "yaliyomo katika nafsi zenu" yani yaliyokwisha makinika ndani yake na yakaimarika miongoni mwa maazimio na sifa. kukaa ndani yake na kuimarika kutokana na maazimio na maelezo. Na akajulisha kuwa Yeye "ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu." Na katika ukamilifu wa uwezo wake, ni kuwahesabu viumbe na kufikisha wanachostahiki katika malipo na adhabu.
: 285 - 286 #
{آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ (285) لَا {يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنْتَ مَوْلَانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (286)}.
285. Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na Waumini vile vile. Wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumetii. Tunakutaka maghfira Mola wetu Mlezi! Na marejeo ni kwako. 286. Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kiwango cha iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia. (Semeni) Mola wetu Mlezi! Usituchukulie ubaya tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi! Usitutwike tusiyoyaweza, na uyatupilie mbali mabaya yetu, na utusamehe na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri.
#
{285 - 286} ثبت عنه - صلى الله عليه وسلم - أن من قرأ هاتين الآيتين في ليلة كفتاه ؛ أي: من جميع الشرور، وذلك لما احتوتا عليه من المعاني الجليلة، فإن الله أمر في أول هذه السورة الناس بالإيمان بجميع أصوله في قوله: {قولوا آمنا بالله وما أنزل إلينا}؛ الآية، وأخبر في هذه الآية أن الرسول - صلى الله عليه وسلم - ومن معه من المؤمنين آمنوا بهذه الأصول العظيمة وبجميع الرسل وجميع الكتب، ولم يصنعوا صنيع من آمن ببعض وكفر ببعض كحالة المنحرفين من أهل الأديان المنحرفة. وفي قرن المؤمنين بالرسول - صلى الله عليه وسلم - والإخبار عنهم جميعاً بخبر واحد شرف عظيم للمؤمنين، وفيه أنه - صلى الله عليه وسلم - مشارك للأمة في توجه الخطاب الشرعي له وقيامه التام به وأنه فاق المؤمنين بل فاق جميع المرسلين في القيام بالإيمان وحقوقه. وقوله: {وقالوا سمعنا وأطعنا}؛ هذا التزام من المؤمنين عام لجميع ما جاء به النبي - صلى الله عليه وسلم - من الكتاب والسنة، وأنهم سمعوه سماع قبول وإذعان وانقياد. ومضمون ذلك تضرعهم إلى الله في طلب الإعانة على القيام به وأن الله يغفر لهم ما قصروا فيه من الواجبات وما ارتكبوه من المحرمات، وكذلك تضرعوا إلى الله في هذه الأدعية النافعة، والله تعالى قد أجاب دعاءهم على لسان نبيه - صلى الله عليه وسلم - فقال: «قد فعلت». فهذه الدعوات مقبولة من مجموع المؤمنين قطعاً ومن أفرادهم إذا لم يمنع من ذلك مانع في الأفراد، وذلك أن الله رفع عنهم المؤاخذة في الخطأ والنسيان وأن الله سهل عليهم شرعه غاية التسهيل، ولم يحملهم من المشاق والآصار والأغلال ما حمله على من قبلهم، ولم يحملهم فوق طاقتهم، وقد غفر لهم ورحمهم ونصرهم على القوم الكافرين. فنسأل الله تعالى بأسمائه وصفاته وبما منَّ به علينا من التزام دينه أن يحقق لنا ذلك وأن ينجز لنا ما وعدنا على لسان نبيه، وأن يصلح أحوال المؤمنين. ويؤخذ من هذا قاعدة التيسير ونفي الحرج في أمور الدين كلها، وقاعدة العفو عن النسيان والخطأ في العبادات وفي حقوق الله تعالى، وكذلك في حقوق الخلق من جهة رفع المأثم وتوجيه الذم، وأما وجوب ضمان المتلفات خطأً أو نسياناً في النفوس والأموال فإنه مرتب على الإتلاف بغير حق، وذلك شامل لحالة الخطأ والنسيان والعمد. تم تفسير سورة البقرة. ولله الحمد والثناء. وصلى الله على محمد وسلم.
{285-286} Ilithibiti kutoka kwake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwamba, mwenye kuzisoma Aya mbili hizi usiku, zitamtosheleza. Yani kutokana na shari zote. Na hilo ni kwa sababu ya yale iliyojumuisha katika maana kubwa. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliwaamrisha watu mwanzoni mwa sura hii kumwamini Mwenyezi Mungu kwa misingi yake yote katika kauli yake. "Semeni: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale yaliyoteremshwa kwetu." Na akajulisha katika Aya hii kwamba Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na wale walio pamoja naye miongoni mwa Waumini waliiamini misingi hii mikubwa na Mitume wote na Vitabu vyote. Na hawakufanya kitendo cha wale walioamini baadhi na wakakufuru baadhi yake, kama hali ya wale wapotofu katika watu wa dini potofu. Na katika kuwaunganisha Waumini pamoja na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – na kujulisha kuwahusu wote kwa habari moja ni heshima kubwa kwa Waumini. Na ndani yake kuna kwamba, yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - anawashiriki umma huu katika kumlenga na mazungumzo ya kisheria, na kuitekeleza kwake kamili. Na kwamba yeye amewapita Waumini, bali amewapita Mitume wote kwa kuisimamia imani na haki zake. Na kauli yake, "na wakasema: Tumesikia na tumetii". Ahadi hii ya Waumini ni ya jumla kwa yale yote aliyoyaleta Nabii, -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika Kitabu na Sunna. Na kwamba waliisikia kusikia kwa kukubali, kusalimu amri na kufuata. Na madhumuni ya hayo ni kunyenyekea kwao kwa Mwenyezi Mungu katika kuomba msaada wa kufanya hivyo. Na kwamba Mwenyezi Mungu atawasamehe yale waliyopungukiwa katika majukumu, na waliyoyafanya ya haramu. Na vile walimnyenyekea Mwenyezi Mungu katika dua hizi zenye manufaa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikwisha jibu dua yao kwa ulimi wa Nabii wake, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema, “Nimeshafanya.” Kwa hivyo, dua hizi zinakubaliwa kutoka kwa Waumini wote bila ya shaka. Na kutoka kwa kila mmoja wao binafsi, ikiwa hakuna kizuizi kwa hilo kutoka kwa mtu binafsi. Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaondolea kuwachukulia ubaya katika kukosea na kusahau. Na kwamba Mwenyezi Mungu aliifanya sheria yake kuwa nyepesi sana kwao, na wala hakuwatwika katika uzito, dhiki, na minyororo aliyowatwika wale waliokuwa kabla yao. Na hakuwabebesha zaidi ya uwezo wao, na alikwisha wasamehe na akawarehemu na akawapa ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa majina yake na sifa zake. Na kwa yale aliyotuneemesha kwayo ya kushikamana na dini yake, kwamba atufanikishie hayo. Na atutimizie yale aliyotuahidi kwa ulimi wa Nabii wake, na kwamba atengeneze hali za Waumini. Na inachukuliwa kutokana na hili msingi wa kurahisisha, na kukanusha ugumu katika mambo yote ya dini. Na msingi wa kufutilia mbali mabaya yaliyotokana na kusahau na kukosea katika ibada na katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na vile vile katika haki za viumbe katika upande wa kuondoa dhambi na kukashifiwa. Na ama kuhusu wajibu wa kudhamini uharibifu uliotokea kimakosa au kwa kusahau katika nafsi na mali, hilo linaingia katika kuharibu bila ya haki. Na hilo linajumuisha hali ya kukosea, kusahau na kukusudia. Imetimia tafsiri ya Surat Al-Baqara, na kuhimidiwa na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad.