:
Tafsiri ya Surat Aal-'Imran
Tafsiri ya Surat Aal-'Imran
Nayo iliteremka Madina
: 1 - 6 #
{الم (1) اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ (2) نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنْزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ (3) مِنْ قَبْلُ هُدًى لِلنَّاسِ وَأَنْزَلَ الْفُرْقَانَ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَاللَّهُ عَزِيزٌ ذُو انْتِقَامٍ (4) إِنَّ اللَّهَ لَا يَخْفَى عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ (5) هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (6)}.
1. Alif Laam Miim. 2. Mwenyezi Mungu, hakuna mungu isipokuwa Yeye. Aliye hai, Msimamizi wa yote milele. 3. Amekiteremsha Kitabu juu yako kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili. 4. Kabla yake, viwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika, wale waliozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu wana adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye kulipiza. 5. Hakika, Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, katika dunia wala katika mbingu. 6. Yeye ndiye anayewaunda ndani ya matumbo ya uzazi kwa namna apendavyo. Hapana mungu isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{1} {الم}؛ من الحروف التي لا يعلم معناها إلا الله.
{1} Alif Laam Miim ni katika herufi ambazo hajui maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu.
#
{2} فأخبر تعالى أنه {الحي}؛ كامل الحياة {القيوم}؛ القائم بنفسه المقيم لأحوال خلقه، وقد أقام أحوالهم الدينية وأحوالهم الدنيوية والقدرية، فأنزل على رسوله محمد - صلى الله عليه وسلم - الكتاب بالحق الذي لا ريب فيه وهو مشتمل على الحق.
{2} Kisha Mola Mtukufu akajulisha kwamba Yeye ndiye "Aliye hai," uhai kamili. "Msimamizi wa yote milele." Anayejisimamia mwenyewe, mwenye kusimamia hali za viumbe wake. Na anasimamia hali zao za kidini na hali zao za kidunia na za kimajaaliwa. Kwa hivyo, akateremsha juu ya Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - Kitabu kwa haki, ambacho hakina shaka yoyote ndani yake, nacho kinajumuisha haki.
#
{3 - 4} {مصدقاً لما بين يديه}؛ من الكتب أي شهد بما شهدت به ووافقها وصدق من جاء بها من المرسلين. وكذلك {أنزل التوراة والإنجيل من قبل} هذا الكتاب، {هدى للناس}؛ وأكمل الرسالة وختمها بمحمد - صلى الله عليه وسلم - وكتابه العظيم الذي هدى الله به الخلق من الضلالات واستنقذهم به من الجهالات، وفرق به بين الحق والباطل والسعادة والشقاوة، والصراط المستقيم وطرق الجحيم، فالذين آمنوا به، واهتدوا حصل لهم به الخير الكثير والثواب العاجل والآجل و {الذين كفروا بآيات الله}؛ التي بينها في كتابه وعلى لسان رسوله {لهم عذاب شديد والله عزيز ذو انتقام}؛ ممن عصاه.
{3 - 4} "Kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake" katika Vitabu. Yani, kinashuhudia yale viliyoshuhudia, na kinakubaliana navyo, na kinasadikisha wale waliokuja navyo miongoni mwa Mitume. Na vile vile "aliteremsha Taurati na Injili kabla yake" Kitabu hiki. "Viwe uwongofu kwa watu." Na akakamilisha ujumbe na akauhitimisha kwa Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na Kitabu chake kitukufu. Ambacho kwacho Mwenyezi Mungu amewaongoa viumbe kutoka kwenye upotevu mbalimbali. Na akawaokoa kwacho kutoka kwa ujinga mbalimbali. Na akapambanua kwacho baina ya haki na batili, na furaha na taabu, na njia iliyonyooka na njia za Jahim. Basi wale waliomwamini na wakaongoka, walipata kwake heri nyingi na thawabu ya haraka na ya baadaye. Na "wale waliozikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu" ambazo alizibainisha katika Kitabu chake na kwa ulimi wa Mtume wake; "wana adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kulipiza," kwa mwenye kumuasi.
#
{5 - 6} ومن تمام قيوميته تعالى أن علمه محيط بالخلائق {لا يخفى عليه شيء في الأرض ولا في السماء}؛ حتى ما في بطون الحوامل فهو {الذي يصوركم في الأرحام كيف يشاء}؛ من ذكر وأنثى وكامل الخلق وناقصه متنقلين في أطوار خلقته وبديع حكمته، فمن هذا شأنه مع عباده واعتناؤه العظيم بأحوالهم من حين أنشأهم إلى منتهى أمورهم لا مشارك له في ذلك فيتعين أنه لا يستحق العبادة إلا هو {لا إله إلا هو العزيز}؛ الذي قهر الخلائق بقوته، واعتز عن أن يوصف بنقص، أو ينعت بذم. {الحكيم}؛ في خلقه وشرعه.
{5 - 6} Na katika ukamilifu wa usimamizi wake Yeye Mtukufu ni kwamba, elimu yake imevizunguka viumbe vyote. "Hakifichiki chochote kwake, katika dunia wala katika mbingu," hata yaliyomo ndani ya matumbo ya wajawazito. Yeye "ndiye anayewaunda ndani ya matumbo ya uzazi kwa namna apendavyo." Kama vile vya kiume na vya kike, na viumbe kamilifu na vipungufu vyake, wakipitia katika awamu za uumbaji wake na hekima yake kubwa. Basi yule ambaye jambo lake ni hili kwa waja wake, na kujali kwake kukubwa juu ya hali zao tangu wakati alipowaumba hadi mwisho wa mambo yao; hana mshirika katika hilo. Kwa hivyo, inabaki kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye tu. "Hapana mungu isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu" ambaye alivishinda viumbe kwa nguvu zake. Na akatukuka kusifiwa na upungufu wowote, au kuelezwa na kashfa. "Mwenye hekima" katika uumbaji wake na sheria yake.
: 7 - 8 #
{هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ (7) رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنْتَ الْوَهَّابُ (8)}.
7.Yeye ndiye aliyeteremsha juu yako Kitabu hiki. Ndani yake zimo Aya muhkam (zenye maana wazi). Hizo ndizo msingi wa Kitabu hiki. Na zimo nyingine Mutashabihat (zenye maana zisizo wazi). Ama wale ambao katika nyoyo zao umo upotovu, wao wanafuata zile zenye maana zisizo wazi kwa kutafuta fitina, na kutafuta maana yake. Na wala hapana ajuaye maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wale waliokita katika elimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki (hayo) isipokuwa wenye akili. 8. (Na wao husema) Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoa, na tutunuku rehema itokayo kwako. Hakika, Wewe ndiye Mwenye kutunuku.
#
{7} يخبر تعالى عن عظمته وكمال قيوميته أنه هو الذي تفرد بإنزال هذا الكتاب العظيم، الذي لم يوجد، ولن يوجد له نظير أو مقارب في هدايته وبلاغته وإعجازه وإصلاحه للخلق، وأن هذا الكتاب يحتوي على المحكم الواضح المعاني، البين الذي لا يشتبه بغيره، ومنه آيات متشابهات تحتمل بعض المعاني، ولا يتعين منها واحد من الاحتمالين بمجردها حتى تضم إلى المحكم، فالذين في قلوبهم مرض وزيغ وانحراف لسوء قصدهم يتبعون المتشابه منه؛ فيستدلون به على مقالاتهم الباطلة، وآرائهم الزائفة، طلباً للفتنة وتحريفاً لكتابه، وتأويلاً له على مشاربهم ومذاهبهم ليَضِلوا ويُضِلوا. وأما أهل العلم الراسخون فيه الذين وصل العلم واليقين إلى أفئدتهم، فأثمر لهم العمل والمعارف فيعلمون أن القرآن كله من عند الله وأنه كله حق محكمه ومتشابهه، وأن الحق لا يتناقض ولا يختلف، فلعلمهم أن المحكمات معناها في غاية الصراحة والبيان، يردون إليها المشتبه الذي تحصل فيه الحيرة لناقص العلم وناقص المعرفة، فيردون المتشابه إلى المحكم فيعود كله محكماً ويقولون: {آمنا به كل من عند ربنا وما يذكر}؛ للأمور النافعة والعلوم الصائبة {إلا أولو الألباب}؛ أي: أهل العقول الرزينة، ففي هذا دليل على أن هذا من علامة أولي الألباب وأن اتباع المتشابه من أوصاف أهل الآراء السقيمة والعقول الواهية والقصود السيئة. وقوله: {وما يعلم تأويله إلا الله}؛ إن أريد بالتأويل معرفة عاقبة الأمور وما تنتهي وتؤول إليه تعين الوقوف على {إلا الله} حيث هو تعالى المتفرد بالتأويل بهذا المعنى، وإن أريد بالتأويل معنى التفسير ومعرفة معنى الكلام كان العطف أولى؛ فيكون هذا مدحاً للراسخين في العلم، أنهم يعلمون كيف ينزلون نصوص الكتاب والسنة محكمها ومتشابهها. ولما كان المقام مقام انقسام إلى منحرفين ومستقيمين دعوا الله تعالى أن يثبتهم على الإيمان فقالوا:
{7} Mola Mtukufu anajulisha juu ya ukuu wake na ukamilifu wa usimamizi wake kwamba Yeye peke yake ndiye aliyekiteremsha kitabu hiki kitukufu, ambacho hakikuwepo. Na kamwe hakitakuwepo kilicho sawa nacho au chenye kukikaribia katika uwongofu wake, na ufasaha wake, na ushindi wake, na utengenezaji wake wa viumbe. Na kwamba Kitabu hiki kinajumuisha Aya zenye maana zilizo wazi, zilizo bainifu ambazo hazifanani ni nyinginezo. Na kina Aya zenye maana zisizo wazi, ambazo zina baadhi ya maana na wala moja ya maana zinazowezekana haiainiki kuwa ndiyo maana kivyake mpaka iunganishwe na zenye maana wazi. Kwa hivyo, wale ambao katika nyoyo zao kuna maradhi, na kuchepuka, na upotofu, kwa sababu ya nia yao mbaya, wanafuata zile zisizo na maana wazi katika Aya hizo. Kwa hivyo, wanazitumia kuwa ni ushahidi juu ya maneno yao ya batili, na maoni yao ya uwongo, kwa kutaka fitina na kupotosha kitabu chake, na kukifasiri kulingana na matamanio yao na madhehebu yao ili wapotee na wapoteze. Na ama wenye elimu, ambao wamekita mizizi ndani yake, ambao elimu na yakini imefika katika nyoyo zao, basi ikawaletea matunda ya kutenda matendo na maarifa. Kwa hivyo, wanajua kwamba Qur-ani yote imetoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba yote ni haki, ya wazi yake na isiyokuwa ya wazi yake, na kwamba haki haitenguani wala haihitalafiani. Na kwa sababu ya kujua kwao kwamba Aya zile zilizo wazi maana yake iko wazi mno na bainifu zaidi, wanazirudisha zile zisizo na maana wazi kwa zile zilizo wazi. Kwa hivyo zote zinakuwa na maana wazi, na wanasema, "sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi, lakini hawakumbuki" mambo ya manufaa na elimu sahihi. "Isipokuwa wenye akili" yani wenye akili timamu. Basi katika hili kuna ushahidi kwamba hii ni katika alama za wenye akili. Na kwamba kufuata Aya zisizo wazi ni katika sifa za wenye maoni magonjwa, na akili dhaifu, na makusudio mabaya. Na kauli yake, "na wala hapana anayejua maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu." Ikiwa makusudio ya 'Ta-awiil' hapa ni kujua mwisho wa mambo na namna yanavyomalizika, basi inalazimu kusimamia kwenye kauli yake, "isipokuwa Mwenyezi Mungu." Kwa vile Yeye Mtukufu ndiye tu anayejua Ta-awiil yake kwa maana hii. Na ikiwa makusudio ya 'Ta-awiil' hapa ina maana ya tafsiri na kujua maana ya usemi, basi kuunganisha kunakuwa ndio bora zaidi. Na hili linakuwa ni sifa kwa wale ambao wamekita katika elimu. Kwamba wao wanajua jinsi ya kuteremsha maandiko ya Kitabu na Sunna yenye maana wazi yake, na yasiyokuwa na maana wazi yake. Na pale muktadha ulikuwa ni muktadha wa kugawanyika watu katika wapotofu na wale walionyooka. Wakamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba awaimarishe juu ya Imani, wakasema:
#
{8} {ربنا لا تزغ قلوبنا}؛ أي: لا تملها عن الحق إلى الباطل {بعد إذ هديتنا وهب لنا من لدنك رحمة} تصلح بها أحوالنا؛ {إنك أنت الوهاب}؛ أي: كثير الفضل والهبات. وهذه الآية تصلح مثالاً للطريقة التي يتعين سلوكها في المتشابهات، وذلك أن الله تعالى ذكر عن الراسخين أنهم يسألونه أن لا يزيغ قلوبهم بعد إذ هداهم؛ وقد أخبر في آيات أخر الأسباب التي بها تزيغ قلوب أهل الانحراف وأن ذلك بسبب كسبهم كقوله: {فلما زاغوا أزاغ الله قلوبهم}؛ {ثم انصرفوا صرف الله قلوبهم}؛ {ونقلب أفئدتهم وأبصارهم كما لم يؤمنوا به أول مرة}؛ فالعبد إذا تولى عن ربه، ووالى عدوه، ورأى الحق فصدف عنه ورأى الباطل فاختاره ولاه الله ما تولى لنفسه، وأزاغ قلبه عقوبة له على زيغه، وما ظلمه الله ولكنه ظلم نفسه، فلا يلم إلا نفسه الأمارة بالسوء. والله أعلم.
{8} "Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu." Yani usizigeuze kutoka kwenye haki kwenda kwenye batili. "Baada ya kutuongoa, na tutunuku rehema itokayo kwako," ili kwazo uzirekebishe hali zetu. "Hakika, Wewe ndiye Mwenye kutunuku" yani Mwingi wa fadhila na vipawa. Na Aya hizi ni mfano mzuri wa njia ambayo ni lazima kuifuata katika mambo yasiyokuwa wazi. Na hilo ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja kuhusu wale waliokita (katika elimu) kwamba wanamuomba asizipotoe nyoyo zao baada ya kuwaongoa. Na alijulisha katika Aya nyingine sababu ambazo kwazo zinapotoka nyoyo za wenye upotovu, na kwamba hilo ni kwa sababu ya kuchuma kwao. Kama kauli yake, "walipopotoka, Mwenyezi Mungu, akazipotosha nyoyo zao." "Kisha wakageuka wakaenda, Mwenyezi Mungu akazigeuza nyoyo zao." "Nasi tunazigeuza nyoyo zao na macho yao, kama walivyokuwa hawakuyaamini mara ya kwanza." Basi mja anapogeuka akamwacha Mola wake Mlezi, na akamfanya adui wake kuwa ndiye rafiki, na akaiona haki na akaiacha, na akaiona batili na akaichagua, Mwenyezi Mungu anamuachia yale aliyojifanyia mwenyewe kuwa rafiki yake. Na anaupoteza moyo wake kama adhabu kwake kwa sababu ya upotovu wake. Basi, na asilaumu isipokuwa nafsi yake inayoamrisha mabaya. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua vyema.
: 9 #
{رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَا رَيْبَ فِيهِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ (9)}.
9. Mola wetu Mlezi! Hakika, Wewe ndiye utakayewakusanya watu kwa Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika, Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
#
{9} هذا من تتمة كلام الراسخين في العلم، وهو يتضمن الإقرار بالبعث والجزاء واليقين التام، وأن الله لا بد أن يوقع ما وعد به، وذلك يستلزم موجبه ومقتضاه من العمل والاستعداد لذلك اليوم، فإن الإيمان بالبعث والجزاء أصل صلاح القلوب، وأصل الرغبة في الخير والرهبة من الشر اللذين هما أساس الخيرات.
{9} Haya ni katika yale yanayokamilisha maneno ya wale waliokita katika elimu. Nayo yanajumuisha kukiri ufufuo, na malipo, na yakini kamili, na kwamba Mwenyezi Mungu lazima atatenda yale aliyoyaahidi. Na hilo linalazimu matokeo yake na matakwa yake kama vile kutenda matendo (mema) na kujitayarisha kwa ajili ya siku hiyo. Kwa sababu, kuamini katika ufufuo na malipo ndiyo chimbuko la nyoyo kuwa miema. Na chimbuko la kutaka kufanya mema, na kuyahofu maovu, ambayo mawili haya ndiyo msingi wa heri nyingi.
: 10 - 11 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَنْ تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا وَأُولَئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ (10) كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ وَاللَّهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ (11)}.
10. Kwa hakika, wale waliokufuru, hazitawafaa kitu mali zao wala watoto wao kutokana na Mwenyezi Mungu. Na hao ndio kuni za Moto. 11. Kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao. Walikadhibisha Ishara zetu, basi Mwenyezi Mungu akawachukua kwa dhambi zao; na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
#
{10 - 11} لما ذكر يوم القيامة، ذكر أن جميع من كفر بالله، وكذب رسل الله لا بد أن يدخلوا النار ويصلوها، وأن أموالهم وأولادهم لن تغني عنهم شيئاً من عذاب الله، وأنه سيجري عليهم في الدنيا من الأخْذات والعقوبات ما جرى على فرعون وسائر الأمم المكذبة بآيات الله، {أخذهم الله بذنوبهم}؛ وعجل لهم العقوبات الدنيوية متصلة بالعقوبات الأخروية {والله شديد العقاب}؛ فإياكم أن تَسْتَهْوِنوا بعقابه فيهون عليكم الإقامة على الكفر والتكذيب.
{10 - 11} Alipoitaja Siku ya Kiyama, akataja kuwa kila aliyemkufuru Mwenyezi Mungu na akawakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, lazima wataingia Motoni na watateketea humo. Na kwamba mali zao na watoto wao havitawafaa chochote kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na kwamba katika dunia watachukuliwa na wataadhibiwa. Kama ilivyowapata kaumu ya Firauni na umma zote zilizozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. "Mwenyezi Mungu aliwachukua kwa dhambi zao," na akawaharakishia adhabu za kidunia zilizoungana na adhabu za kiakhera. "Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu." Kwa hivyo, ole wenu kuidharau adhabu yake, hivyo ikawawia rahisi kuendelea juu ya ukafiri na kukadhibisha.
: 12 - 13 #
{قُلْ لِلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَى جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمِهَادُ (12) قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَأُخْرَى كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُمْ مِثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ وَاللَّهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَنْ يَشَاءُ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَعِبْرَةً لِأُولِي الْأَبْصَارِ (13)}.
12. Waambie wale waliokufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa mtiwe kwenye Jahannam; napo ndipo pahali paovu zaidi pa mapumziko. 13. Hakika, mlikuwa na Ishara katika yale makundi mawili yalipokutaka (katika vita). Kundi moja likipigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, nalo lingine kafiri likiwaona zaidi kuliko wao mara mbili, kwa kuona kwa macho. Na Mwenyezi Mungu humuunga mkono amtakaye kwa nusura yake. Hakika, katika hayo kuna mazingatio kwa wenye macho.
#
{12 - 13} وهذا خبر وبشرى للمؤمنين، وتخويف للكافرين أنهم لا بد أن يغلبوا في هذه الدنيا، وقد وقع كما أخبر الله فغلبوا غلبة لم يكن لها مثيل ولا نظير، وجعل الله تعالى ما وقع في بدر من آياته الدالة على صدق رسوله، وأنه هو على الحق وأعداؤه على الباطل حيث التقت فئتان فئة المؤمنين لا يبلغون إلا ثلاثمائة وبضعة عشر رجلاً مع قلة عُددهم، وفئة الكافرين يناهزون الألف مع استعدادهم التام في السلاح وغيره، فأيد الله المؤمنين بنصره فهزموهم بإذن الله. ففي هذا عبرة لأهل البصائر، فلولا أن هذا هو الحق الذي إذا قابل الباطل أزهقه، واضمحل الباطل لكان بحسب الأسباب الحسية الأمر بالعكس.
{12 - 13} Na hii ni habari na bishara njema kwa Waumini, na kuwahofisha makafiri ya kwamba lazima watashindwa katika dunia hii. Na tayari lilishatokea kama alivyojulisha Mwenyezi Mungu, wakashindwa kushindwa ambako hakukuwa na mfano wala kilicho sawa nako. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akayafanya yaliyotokea Badr katika ishara zake zinazoonyesha ukweli wa Mtume wake. Na kwamba Yeye yu juu ya haki, nao maadui zake wako juu ya batili. Ambapo makundi mawili yalikutana, kundi la Waumini wasiofikia isipokuwa wanaume mia tatu na kumi tu. Licha ya uchache wa maandalizi yao, na kundi la makafiri lililokaribia elfu moja pamoja na kujiandaa kwao kamili katika silaha na mengineyo. Basi Mwenyezi Mungu akawaunga mkono Waumini kwa nusura yake, hivyo wakawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na katika hili kuna mazingatio kwa wenye kuona. Na lau kuwa hii siyo haki ambayo ikikumbana na batili, inaiangamiza. Na batili hiyo inatoweka, basi kulingana na sababu za hisia, lingekuwa jambo hili ni kinyume chake.
: 14 - 15 #
{زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنْطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ذَلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاللَّهُ عِنْدَهُ حُسْنُ الْمَآبِ (14) قُلْ أَؤُنَبِّئُكُمْ بِخَيْرٍ مِنْ ذَلِكُمْ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِنْدَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِنَ اللَّهِ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ (15)}.
14. Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundo mingi ya dhahabu na fedha, na farasi wazuri zaidi, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani, na Mwenyezi Mungu ana marejeo mazuri. 15. Sema: Je, niwaambie yaliyo bora kuliko hayo? Kwa waliomcha Mungu kwa Mola wao Mlezi ziko Bustani zipitazo mito chini yake. Watadumu humo, na wake waliotakaswa, na radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
#
{14} أخبر تعالى في هاتين الآيتين عن حالة الناس في إيثار الدنيا على الآخرة، وبين التفاوت العظيم والفرق الجسيم بين الدارين، فأخبر أن الناس زينت لهم هذه الأمور فرمقوها بالأبصار، واستحلوها بالقلوب، وعكفت على لذاتها النفوس، كل طائفة من الناس تميل إلى نوع من هذه الأنواع، قد جعلوها هي أكبر همهم ومبلغ علمهم، وهي مع هذا متاع قليل مُنْقَضٍ في مدة يسيرة، فهذا {متاع الحياة الدنيا والله عنده حسن المآب}.
{14} Mola Mtukufu alijulisha katika Aya hizi mbili kuhusu hali ya watu katika kuipendelea dunia kuliko Akhera. Na akabainisha kuboresha kukubwa na tofauti kubwa iliyopo baina ya nyumba mbili hizi. Kwa hivyo, akajulisha kwamba watu wamepambiwa mambo haya, wakavitazama kwa macho yao na wakavihalalisha kwa nyoyo zao, na nafsi zikajishughulisha na ladha zavyo. Kila kundi katika watu linaegemea kwenye aina katika aina hizi. Na walivifanya kuwa ndivyo hamu yao kubwa zaidi, na kiwango cha elimu yao. Navyo pamoja na hayo ni starehe ndogo yenye kwisha katika muda mfupi. Na hii, "ni starehe ya maisha ya duniani, na Mwenyezi Mungu ana marejeo mazuri."
#
{15} ثم أخبر عن ذلك بأن المتقين لله القائمين بعبوديته لهم خير من هذه اللذات، فلهم أصناف الخيرات والنعيم المقيم مما لا عين رأت ولا أذن سمعت ولا خطر على قلب بشر، ولهم رضوان الله الذي هو أكبر من كل شيء، ولهم الأزواجُ المطهرةُ من كل آفة ونقص، جميلاتُ الأخلاق كاملاتُ الخلائق، لأن النفي يستلزم ضده، فتطهيرها من الآفات مستلزم لوصفها بالكمالات. {والله بصير بالعباد}؛ فييسر كلًّا منهم لما خلق له، أما أهل السعادة فييسرهم للعمل لهذه الدار الباقية ويأخذون من هذه الحياة الدنيا ما يعينهم على عبادة الله وطاعته، وأما أهل الشقاوة والإعراض فيقيضهم لعمل أهل الشقاوة، ويرضون بالحياة الدنيا، ويطمئنون بها، ويتخذونها قراراً.
{15} Kisha akajulisha kuhusu hilo kwamba wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, wanaomuabudu wana kilicho bora kuliko ladha hizi. Wana aina za neema za heri na neema ya kudumu ambazo jicho halijapata kuona, wala sikio halijapata kusikia, wala halijapata kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Na wana radhi za Mwenyezi Mungu ambazo ndio kubwa kuliko kila kitu. Na wana wake waliotakaswa kutokana na kila maradhi na upungufu, wenye maadili mazuri, wenye maumbile kamili, kwa sababu kukanusha kunalazimu kinyume chake. Kwa hivyo, kuwatakasa kutokana na maradhi kunalazimu kuwasifu kwa sifa kamilifu. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake" kwa hivyo anamrahishia kila mmoja wao kwa kile alichoumbiwa. Ama watu wa furaha, anawarahisishia kufanya matendo kwa ajili ya nyumba hii ya yenye kudumu. Na wanachukua katika maisha haya ya dunia yale yenye kuwasaidia kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumtii. Na ama watu wa upotovu na kupeana mgongo, anawafungamanisha na matendo ya watu wa upotovu. Na wanauridhia uhai wa dunia hii, na wanatulia nao, na wanauchukulia kuwa ndipo pahali pa kutua.
: 16 - 17 #
{الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ (16) الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنْفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ (17)}.
16. Wale wanaosema: Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumeamini. Basi tusamehe dhambi zetu, na tuepushe na adhabu ya Moto. 17. Wanaovumulia, na wakweli, na wanyenyekevu, na watoao, na wanao omba msamaha katika masaa ya mwisho ya usiku.
#
{16} أي: هؤلاء الراسخون في العلم أهل العلم والإيمان يتوسلون إلى ربهم بإيمانهم لمغفرة ذنوبهم ووقايتهم عذاب النار، وهذا من الوسائل التي يحبها الله أن يتوسل العبد إلى ربه بما منَّ به عليه من الإيمان والأعمال الصالحة إلى تكميل نعم الله عليه بحصول الثواب الكامل واندفاع العقاب.
{16} Yani hawa waliokita katika elimu, wenye elimu na Imani, wanatafuta njia ya kumwendea Mola wao Mlezi kwa imani yao ili awasamehe dhambi zao, na awakinge kutokana na adhabu ya Moto. Na hili ni katika njia ambazo Mwenyezi Mungu anapenda kwamba, mja atafute njia ya kumwendea Mola wake Mlezi kwa yale aliyomneemesha kwayo ya imani na matendo mema. Ili zitimie neema za Mwenyezi Mungu juu yake kwa kupata thawabu kamili na kuzuilika adhabu.
#
{17} ثم وصفهم بأجمل الصفات: بالصبر الذي هو حبس النفوس على ما يحبه الله طلباً لمرضاته، يصبرون على طاعة الله ويصبرون عن معاصيه ويصبرون على أقداره المؤلمة، وبالصدق بالأقوال والأحوال وهو استواء الظاهر والباطن وصدق العزيمة على سلوك الصراط المستقيم، وبالقنوت الذي هو دوام الطاعة مع مصاحبة الخشوع والخضوع، وبالنفقات في سبل الخيرات وعلى الفقراء وأهل الحاجات، وبالاستغفار خصوصاً وقت الأسحار، فإنهم مدوا الصلاة إلى وقت السحر؛ فجلسوا يستغفرون الله تعالى.
{17} Kisha akawasifu kwa sifa nzuri kabisa: Kwa subira ambayo ni kuzizuilia nafsi kwa yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu ili kutafuta radhi zake. Wao wanavumulia juu ya kumtii Mwenyezi Mungu. Na wanavumilia katika kutomuasi. Na wanavumilia juu ya maamuzi yake machungu. Na akawasifu kwa ukweli katika maneno na hali. Nao ni kusawazisha mambo ya dhahiri na ya ndani. Na kuwa na azimio la ukweli juu ya kufuata njia iliyonyooka. Na akawasifu kwa qunuut ambayo ni kudumu katika utiifu pamoja na kuwa na unyenyekevu na utiifu. Na akawasifu kwa kupeana katika njia za heri, na mafakiri na wenye mahitaji. Na akawasifu kwa kuomba msamaha hususan katika maasa ya mwisho ya usiku. Kwani, walirefusha Swala mpaka masaa ya mwisho ya usiku, kisha wakaketi wakimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha.
: 18 #
{شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (18)}.
18. Mwenyezi Mungu alishuhudia kuwa hakika hapana mungu isipokuwa Yeye, na pia (walishuhudia) Malaika, na wenye elimu akisimamisha uadilifu. Hapana mungu isipokuwa Yeye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{18} هذه أجل الشهادات الصادرة من الملك العظيم، ومن الملائكة، وأهل العلم على أجلِّ مشهود عليه وهو توحيد الله وقيامه بالقسط، وذلك يتضمن الشهادةَ على جميع الشرع وجميع أحكام الجزاء، فإن الشرع والدين أصله وقاعدته توحيد الله وإفراده بالعبودية والاعتراف بانفراده بصفات العظمة والكبرياء والمجد والعز والقدرة والجلال وبنعوت الجود والبر والرحمة والإحسان والجمال، وبكماله المطلق الذي لا يحصي أحد من الخلق أن يحيطوا بشيء منه أو يبلغوه أو يصلوا إلى الثناء عليه، والعبادات الشرعية والمعاملات وتوابعها والأمر والنهي كله عدل وقسط لا ظلمَ فيه ولا جورَ بوجه من الوجوه، بل هو في غاية الحكمة والإحكام، والجزاء على الأعمال الصالحة والسيئة كله قِسط وعدل، {قل أي شيء أكبر شهادة قل الله}؛ فتوحيد الله ودينه وجزاؤه قد ثبت ثبوتاً لا ريب فيه وهو أعظم الحقائق وأوضحها، وقد أقام الله على ذلك من البراهين والأدلة ما لا يمكن إحصاؤه وعده. وفي هذه الآية فضيلة العلم والعلماء لأن الله خصهم بالذكر من دون البشر، وقرن شهادتهم بشهادته وشهادة ملائكته وجعل شهادتهم من أكبر الأدلة والبراهين على توحيده ودينه وجزائه، وأنه يجب على المكلفين قبول هذه الشهادة العادلة الصادقة، وفي ضمن ذلك تعديلهم وأن الخلق تبع لهم وأنهم هم الأئمة والمتبوعون، وفي هذا من الفضل والشرف وعلو المكانة ما لا يقادر قدره.
{18} Huu ndio ushahidi mtukufu zaidi uliotoka kwake Mfalme Mkuu, na kutoka Malaika, na wenye elimu, juu ya kilicho kitukufu zaidi chenye kushuhudiliwa, ambacho ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kufanya kwake uadilifu. Na hilo linajumuisha kushuhudia juu ya sheria yote na hukumu zote za malipo. Kwani sheria na dini chimbuko lake na msingi wake ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Na kumpwekesha katika ibada na kuukiri upweke wake katika sifa ya ukuu na ukubwa na heshima, na nguvu, na uwezo, na utukufu. Na kwa sifa za ukarimu, na wema, na rehema, na hisani, na uzuri. Na kwa ukamilifu wake ambao hakuna yeyote katika viumbe anayeweza kuujua vyema na kuzunguka chochote chake, au waufikie, au wafikie kumsifu. Na ibada za kisheria na miamiliano na yale yanayofuatana nayo. Na maamrisho na makatazo, yote ni uadilifu na haki, hakuna dhuluma yoyote ndani yake kwa namna yoyote ile. Bali yeye ana hekima ya juu kabisa na kushikilia amri vilivyo. Na malipo juu ya matendo mema na mabaya yote ni haki na uadilifu. "Sema: Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi? Sema: Mwenyezi Mungu" Kwa hivyo, kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na dini yake, na malipo yake yamethibiti kuthibiti kusikokuwa na shaka yoyote. Nayo ndiyo uhakika mkubwa zaidi na ulio wazi kabisa. Na Mwenyezi Mungu amesimamisha juu ya hayo ushahidi na dalili zisizowezekana kudhibitiwa na kuhesabiwa. Na katika Aya hii, kuna fadhila ya elimu na wanachuoni, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewataja hususan kando na wanadamu wengine. Na akaufungamanisha ushahidi wao na ushuhuda wake na ushuhuda wa Malaika wake. Na akaufanya ushahidi wao kuwa miongoni mwa dalili na ushahidi mkubwa zaidi juu ya upweke wake, na dini yake, na malipo yake. Na kwamba inawalazimu mukallaf (watu wazima wanaoamrishwa na kukatazwa) kukubali ushahidi huu wa uadilifu (wa haki) na wa kweli. Na ndani ya hayo kuna kuwasifu kwa sifa njema, na kwamba viumbe vyote vinawafuata wao, na kwamba wao ndio viongozi wanaofuatwa. Na katika hili kuna fadhila na heshima na cheo cha juu ambacho haiwezekani kupima kiwango chake.
: 19 #
{إِنَّ الدِّينَ عِنْدَ اللَّهِ الْإِسْلَامُ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ وَمَنْ يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّهِ فَإِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ (19)}.
19. Hakika, Dini kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na hawakuhitalifiana wale waliopewa Kitabu isipokuwa baada ya kuwajia na elimu, kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Na mwenye kuzikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.
#
{19} يخبر تعالى {إن الدين عند الله}؛ أي الدين الذي لا دين لله سواه ولا مقبول غيره هو {الإسلام}؛ وهو الانقياد لله وحده ظاهراً وباطناً بما شرعه على ألسنة رسله، قال تعالى: {ومن يبتغ غير الإسلام ديناً فلن يقبل منه وهو في الآخرة من الخاسرين}؛ فمن دان بغير دين الإسلام فهو لم يدن لله حقيقة لأنه لم يسلك الطريق الذي شرعه على ألسنة رسله. ثم أخبر تعالى أن أهل الكتاب يعلمون ذلك وإنما اختلفوا فانحرفوا عنه عناداً وبغياً. وإلا فقد جاءهم العلم المقتضي لعدم الاختلاف الموجب للزوم الدين الحقيقي، ثم لما جاءهم محمد - صلى الله عليه وسلم - عرفوه حق المعرفة، ولكن الحسد والبغي والكفر بآيات الله هي التي صدتهم عن اتباع الحق {ومن يكفر بآيات الله فإن الله سريع الحساب}؛ أي: فلينتظروا ذلك فإنه آت وسيجزيهم الله بما كانوا يعملون.
{19} Mola Mtukufu anajulisha, "hakika, Dini kwa Mwenyezi Mungu." Yani dini ambayo Mwenyezi Mungu hana dini isiyokuwa hiyo, wala dini inayokubaliwa isiyokuwa hiyo ni "Uislamu." Nayo ni kumfuata Mwenyezi Mungu peke yake kwa dhahiri na ndani, kwa yale aliyoyaweka kuwa sheria kwa ndimi za Mitume wake. Yeye Mtukufu amesema: "Na mwenye kutafuta dini isiyokuwa Uislamu, haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa miongoni mwa waliohasiri." Kwa hivyo, mwenye kushika dini isiyokuwa dini ya Uislamu, basi hajashika dini ya Mwenyezi Mungu kwa uhakika. Kwa sababu, hakufuata njia aliyoiweka kuwa sheria juu ya ndimi za Mitume wake. Kisha Yeye Mtukufu akajulisha kwamba Watu wa Kitabu wanalijua hilo, lakini walihitalifiana na wakapotoka wakaiacha kwa ukaidi na uadui. Vinginevyo, walikwisha jiwa na elimu inayolazimu kutokuwepo na hitilafu, inayowalazimu kushikamana na dini ya uhakika. Kisha alipowajia Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - wakamjua kwa elimu ya kweli, lakini husuda, dhuluma na kukufuru Ishara za Mwenyezi Mungu ndivyo vilivyowazuia kufuata haki. "Na mwenye kuzikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu". Yani na wangoje hayo, kwani linakuja, na Mwenyezi Mungu atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
: 20 #
{فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ وَقُلْ لِلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوْا وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ (20)}.
20. Na wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na vile vile walionifuata. Na waambie wale waliopewa Kitabu na wale wasiojua kusoma: Je, mmesilimu? Wakisilimu, basi hakika wameongoka. Na wakikengeuka, basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
#
{20} لما بين أن الدين الحقيقي عنده الإسلام، وكان أهل الكتاب قد شافهوا النبي - صلى الله عليه وسلم - بالمجادلة وقامت عليهم الحجة فعاندوها، أمره الله تعالى عند ذلك أن يقول ويعلن أنه قد أسلم وجهه أي ظاهره وباطنه لله، وأن من اتبعه كذلك قد وافقوه على هذا الإذعان الخالص، وأن يقول للناس كلهم من أهل الكتاب والأميين أي الذين ليس لهم كتاب من العرب وغيرهم إن أسلمتم فأنتم على الطريق المستقيم والهدى والحق وإن توليتم فحسابكم على الله، وأنا ليس عليَّ إلا البلاغ، وقد أبلغتكم وأقمت عليكم الحجة.
{20} Alipobainisha kwamba Dini ya uhakika kwake ni Uislamu, na Watu wa Kitabu walikuwa wamemwongelesha Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa kuhojiana naye. Na hoja ikasimama juu yao, nao wakaipinga. Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwamrisha hapo kwamba aseme na atangaze kwamba ameusalimisha uso wake. Yani dhahiri yake na ndani yake kwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba wale waliomfuata pia walikubaliana naye katika kunyenyekea huku halisi. Na kwamba awaambie watu wote katika Watu wa Kitabu, na wale wasiojua kusoma na kuandika. Yani wale wasiokuwa na kitabu miongoni mwa Waarabu na wengineo: Mkisilimu, basi nyinyi mko kwenye njia iliyonyooka, na uwongofu, na haki. Na mkikengeuka, basi hesabu yenu iko kwa Mwenyezi Mungu. Na mimi si juu yangu isipokuwa kifikisha tu, na tayari nimeshawafikishia, na nimewasimamishia hoja juu yenu.
: 21 - 22 #
{إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُمْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (21) أُولَئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُمْ مِنْ نَاصِرِينَ (22)}.
21. Hakika, wale wanaozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawaua Manabii bila ya haki, na wakawaua wale wanaoamrisha haki katika watu, basi wabashirie adhabu kali. 22. Hao ndio ambao vitendo vyao viliharibika duniani na Akhera. Nao hawana wowote wa kuwanusuru.
#
{21 - 22} أي: الذين جمعوا بين هذه الشرور: الكفر بآيات الله، وتكذيب رسل الله، والجناية العظيمة على أعظم الخلق حقًّا على الخلق وهم الرسل وأئمة الهدى، الذين يأمرون الناس بالقسط الذي اتفقت عليه الأديان والعقول فهؤلاء قد {حبطت أعمالهم في الدنيا والآخرة}؛ واستحقوا العذاب الأليم، وليس لهم ناصر من عذاب الله ولا منقذ من عقوبته.
{21 - 22} Yani wale waliojumuisha kati ya maovu haya: Kukufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu. Na kosa kubwa dhidi ya wakubwa zaidi wa viumbe wote wenye haki kubwa zaidi juu ya viumbe. Nao ni Mitume na viongozi wa uongofu, ambao wanawaamrisha watu kuwa uadilifu, ambao dini zote na akili zilikubaliana juu yake. Basi hawa, "matendo yao yalikwisha haribika katika dunia na Akhera" na wakastahiki adhabu iumizayo. Nao hawana wa kuwanusuru yeyote kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala wa kuwaokoa kutokana na adhabu yake.
: 23 - 25 #
{أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَى كِتَابِ اللَّهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّى فَرِيقٌ مِنْهُمْ وَهُمْ مُعْرِضُونَ (23) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَنْ تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ (24) فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (25)}.
23. Je, huwaoni wale waliopewa fungu katika Kitabu? Wanaitwa kukiendea Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kihukumu baina yao; kisha kundi miongoni mwao wanageuka huku wamepeana mgongo. 24. Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipokuwa kwa siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe walikuwa wakiyazua. 25. Basi itakuwaje tutakapowakusanya kwa ajili ya Siku ambayo hakuna shaka nayo? Na kila nafsi italipwa ilichochuma, nao hawatadhulumiwa.
#
{23 - 25} أي: ألا تنظر وتعجب من هؤلاء {الذين أوتوا نصيباً من الكتاب} و {يدعون إلى كتاب الله}؛ الذي يصدق ما أنزله على رسله {ثم يتولى فريق منهم وهم معرضون}؛ عن اتباع الحق فكأنه قيل: لأي داعٍ دعاهم إلى هذا الإعراض وهم أحق بالاتباع وأعرفهم بحقيقة ما جاء به محمد - صلى الله عليه وسلم -؟ فذكر لذلك سببين: أمنهم وشهادتهم الباطلة لأنفسهم بالنجاة وأن النار لا تمسهم إلا أياماً معدودة حددوها بحسب أهوائهم الفاسدة، كأنَّ تدبير الملك راجع إليهم حيث قالوا: {لن يدخل الجنة إلا من كان هوداً أو نصارى}؛ ومن المعلوم أن هذه أمانيّ باطلة شرعاً وعقلاً. والسبب الثاني: أنهم لما كذبوا بآيات الله، وافتروا عليه زين لهم الشيطان سوء عملهم، واغتروا بذلك وتراءى لهم أنه الحق عقوبة لهم على إعراضهم عن الحق، فهؤلاء كيف يكون حالهم إذا جمعهم الله يوم القيامة، ووفّى العاملين ما عملوا وجرى عدل الله في عباده؟ فهنالك لا تسأل عما يصلون إليه من العقاب وما يفوتهم من الخير والثواب، وذلك بما كسبت أيديهم، وما ربك بظلام للعبيد.
{23 - 25} Yani kwani huwaoni na kustaajabishwa na hawa, "waliopewa fungu katika Kitabu?" Na "wanaitwa kukiendea Kitabu cha Mwenyezi Mungu" ambacho kinayasadikisha yale aliyoyateremsha juu ya Mitume wake. "Kisha kundi miongoni mwao wanageuka huku wamepeana mgongo" wakiacha kuifuata haki. Na ni kana kwamba ilisemwa: Ni sababu gani iliyowafanya kupeana mgongo huku, ilhali wao ndio wanaostahiki zaidi kufuata; na ninaofaa kujua zaidi uhakika wa yale aliyokuja nayo Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake? Kwa hivyo, akataja sababu mbili za hilo: Kuwa kwao na amani, na ushahidi wa batili juu ya nafsi zao kwamba wataokoka (na Moto). Na kwamba Moto hautawagusa isipokuwa kwa siku chache tu. Walizipima kulingana na matamanio yao maovu, kana kwamba uendeshaji wa ufalme unarudi kwao. Kama walivyosema, "hataingia Peponi isipokuwa aliyekuwa Muyahudi au Mkristo." Na inavyojulikana ni kwamba matarajio haya ni batili, kisheria na kiakili. Na sababu ya pili ni kwamba walipozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakumzulia uongo, Shetani akawapambia matendo yao maovu na wakadanganyika nayo. Na ikawafanya kuona kwamba hiyo ndiyo haki ili iwe adhabu kwao kwa sababu ya kuipa kwao mgongo haki. Basi, hawa hali yao itakuwaje wakati Mwenyezi Mungu atapowakusanya Siku ya Kiyama? Na awatimizie malipo wale wafanyao matendo yale waliyoyafanya; na uadilifu wa Mwenyezi Mungu ufanyie kwa waja wake? Basi, hapo hutauliza kiwango watakachofikia katika adhabu, na kile watakachokosa katika heri na thawabu. Na hayo ni kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono yao. Na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.
: 26 - 27 #
{قُلِ اللَّهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ بِيَدِكَ الْخَيْرُ إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (26) تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَتَرْزُقُ مَنْ تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ (27)}.
26. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye mmiliki wa ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye. Na humtukuza umtakaye, na humdhalilisha umtakaye. Heri yote iko mkononi mwako. Hakika, Wewe ni Muweza wa kila kitu. 27. Wewe huuingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku. Na humtoa hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Na unamruzuku umtakaye bila ya hesabu.
#
{26 - 27} يأمر تعالى نبيه - صلى الله عليه وسلم - أصلاً وغيره تبعاً أن يقول عن ربه معلناً بتفرده بتصريف الأمور، وتدبير العالم العلوي والسفلي، واستحقاقه باختصاصه بالملك المطلق والتصريف المحكم، وأنه يؤتي الملك من يشاء، وينزع الملك ممن يشاء، ويعز من يشاء ويذل من يشاء، فليس الأمر بأماني أهل الكتاب ولا غيرهم، بل الأمر أمر الله، والتدبير له، فليس له معارض في تدبيره، ولا معاون في تقديره وأنه كما أنه المتصرف بمداولة الأيام بين الناس فهو المتصرف بنفس الزمان: يولج النهار في الليل ويولج الليل في النهار؛ أي: يدخل هذا على هذا ويحل هذا محل هذا ويزيد في هذا ما ينقص من هذا ليقيم بذلك مصالح خلقه، ويخرج الحي من الميت كما يخرج الزروع والأشجار المتنوعة من بذورها والمؤمن من الكافر والميت من الحي، كما يخرج الحبوب والنوى والزروع والأشجار والبيضة من الطائر، فهو الذي يخرج المتضادات بعضها من بعض، وقد انقادت له جميع العناصر. وقوله: {بيدك الخير}؛ أي: الخير كله منك ولا يأتي بالحسنات والخيرات إلا الله، وأما الشر فإنه لا يضاف إلى الله تعالى لا وصفاً ولا اسماً ولا فعلاً، ولكنه يدخل في مفعولاته ويندرج في قضائه وقدره، فالخير والشر كله داخل في القضاء والقدر فلا يقع في ملكه إلا ما شاءه، ولكن الشرَّ لا يضاف إلى الله، فلا يقال بيدك الخير والشر، بل يقال بيدك الخير كما قاله الله وقاله رسوله، وأما استدراك بعض المفسرين حيث قال: وكذلك الشر بيد الله فإنه وهم محض، ملحظهم حيث ظنوا أن تخصيص الخير بالذكر ينافي قضاءه وقدره العام، وجوابه ما فصلناه. وقوله: {وترزق من تشاء بغير حساب}؛ وقد ذكر الله في غير هذه الآية الأسباب التي ينال بها رزقه كقوله: {ومن يتق الله يجعل له مخرجاً ويرزقه من حيث لا يحتسب}؛ {ومن يتوكل على الله فهو حسبه}؛ فعلى العباد أن لا يطلبوا الرزق إلا من الله، ويسعوا فيه بالأسباب التي يسرها الله وأباحها.
{26-27} Yeye Mtukufu anamwamrisha Nabii wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kimsingi, na wengineo kwa kumfuata yeye kwamba aseme kuhusu Mola wake Mlezi. Akitangaza upweke wake katika uendeshaji mambo, na upangiliaji wa ulimwengu wa juu na wa chini. Na kwamba anastahiki Yeye peke yake ufalme kamili, na uendeshaji mambo madhubuti. Na kwamba yeye humpa ufalme amtakaye, na humwondolea ufalme amtakaye. Na humtukuza amtakaye na humdhalilisha amtakaye. Na jambo hili si kwa matamanio ya Watu wa Kitabu wala wengineo. Bali jambo hili ni jambo la Mwenyezi Mungu, na upangiliaji wake. Yeye hana mpinzani katika upangiliaji wake, wala msaidizi katika makadirio yake. Naye kama vile yeye ndiye anayeendesha mzunguko wa siku kati ya watu, yeye ndiye anayeuendesha wakati wenyewe: Anaingiza mchana katika usiku, na anaingiza usiku katika mchana. Yani anaingiza hiki katika kile, na anakiweka hiki katika nafasi ya kile. Na anaongeza katika hili yale yanayopungukiwa katika lile ili asimamishe kwa hilo masilahi ya viumbe vyake. Na anatoa vilivyo hai kutokana na vilivyokufa, kama vile anavyoitoa mimea na miti mbalimbali kutoka katika mbegu zake. Na Muumini kutoka kwa kafiri, na maiti kutoka kwa aliye hai, kama vile inavyotoka nafaka, mbegu, mimea, miti, na yai kutoka kwa ndege.Yeye ndiye anayetoa vinyume vyenyewe kwa vyenyewe. Na vipengele vyote vya msingi vimemtii. Na kauli yake, "heri yote iko mkononi mwako". Yani, heri yote inatoka kwako, na wala haileti mema na heri isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na ama shari, hiyo haiunganishwi na Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kama sifa, wala jina, wala kitendo. Lakini, shari inaingia katika athari za vitendo vyake (yani viumbe vyake), na inaingia katika hukumu zake na makadirio yake. Kwa hivyo, heri na shari, vyote vinaingia katika hukumu yake na makadirio yake. Na hakifanyiki katika miliki yake isipokuwa akitakacho, lakini shari haiunganishwi Kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, haisemwi kuwa heri na shari vimo mkononi mwako, bali inasemwa kwamba heri iko mkononi mwako kama alivyosema Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ama kujazilia kwa baadhi ya wafasiri waliposema kwamba shari pia iko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, hilo ni dhana potovu tupu. Kwa sababu, walidhani kuwa kuitaja heri peke yake kunapingana na hukumu yake na makadirio yake ya jumla, lakini jawabu lake ni kama tulivyoeleza kwa kina. Na kauli yake, "na unamruzuku umtakaye bila ya hesabu." Mwenyezi Mungu alitaja katika zisizokuwa Aya hii sababu ambazo kwazo yeye hupata riziki yake, kama kauli yake: "Na mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, atamtengenezea njia ya kutokea, na atamruzuku kutoka ambapo hakutarajia." (Na) "Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi Yeye atamtosheleza." Basi ni juu ya waja wasitafute riziki isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu tu, na waitafute kwa njia ambazo Mwenyezi Mungu alizirahisisha na kuziruhusu.
: 28 #
{لَا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَنْ تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّهُ نَفْسَهُ وَإِلَى اللَّهِ الْمَصِيرُ (28)}.
28. Waumini wasiwafanye makafiri kuwa marafiki wa kuwasaidia badala ya Waumini. Na mwenye kufanya hilo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anawahadharisha naye mwenyewe. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
#
{28} هذا نهي من الله وتحذير للمؤمنين أن يتخذوا الكافرين أولياء من دون المؤمنين، فإن المؤمنين بعضهم أولياء بعض، والله وليهم {ومن يفعل ذلك}؛ التولي، {فليس من الله في شيء}؛ أي: فهو بريء من الله، والله بريء منه كقوله تعالى: {ومن يتولهم منكم فإنه منهم}؛ وقوله: {إلا أن تتقوا منهم تقاة}؛ أي: إلا أن تخافوا على أنفسكم في إبداء العداوة للكافرين فلكم في هذه الحال الرخصة في المسالمة والمهادنة لا في التولي الذي هو محبة القلب الذي تتبعه النصرة، {ويحذركم الله نفسه}؛ أي: فخافوه واخشوه وقدموا خشيته على خشية الناس فإنه هو الذي يتولى شؤون العباد، وقد أخذ بنواصيهم وإليه يرجعون وسيصيرون إليه، فيجازي من قدم خوفه ورجاءه على غيره بالثواب الجزيل، ويعاقب الكافرين ومن تولاهم بالعذاب الوبيل.
{28} Hili ni katazo litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni tahadharisho kwa Waumini kwamba, wasiwafanye makafiri kuwa ni marafiki wasaidizi wao badala ya Waumini. Kwani, Waumini ni marafiki wasaidizi wao kwa wao, na Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wao. "Na mwenye kufanya hilo," yani kuwafanya marafiki wasaidizi, "hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu." Yani yeye yuko mbali na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu yuko mbali naye. Kama kauli yake Mola Mtukufu, "na mwenye kuwafanya kuwa marafiki wasaidizi miongoni mwenu, basi huyo ni miongoni mwao." Na kauli yake, "isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao." Yani isipokuwa ikiwa mtazihofia nafsi zenu katika kuwaonyesha uadui makafiri, basi katika hali hii mna ruhusa ya kufanya amani na kusuluhisha. Lakini si katika urafiki wa kusaidiana ambao ni upendo wa moyo ambao unafuatwa na kunusuriana. "Na Mwenyezi Mungu anawahadharisha naye mwenyewe." Yani basi mhofuni na muogopeni, na tangulizeni kumuogopa yeye mbele ya kuwaogopa watu. Kwani, yeye ndiye anayesimamia mambo ya waja. Na alishachukua nywele zao za na, kwake watarejea, na wataishia kwake. Kisha, atamlipa yule aliyetanguliza kumhofu yeye na kumtumaini yeye juu ya mwengineye kwa thawabu nyingi. Na anawaadhibu makafiri na mwenye kuwafanya marafiki wasaidizi adhabu kali.
: 29 - 30 #
{قُلْ إِنْ تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّهُ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (29) يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِنْ سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّهُ نَفْسَهُ وَاللَّهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ (30)}.
( 29 ) Sema: Mkificha yaliyo katika vifua vyenu au mkiyaweka wazi, Mwenyezi Mungu anayajua. Na anayajua yaliyo katika mbingu na yaliyo katika dunia. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. 30. Siku ambayo kila nafsi itakuta iliyofanya katika mema yamehudhurishwa, na pia iliofanya katika ubaya. Itapenda lau baina ya hayo (mabaya) na yeye ungekuwepo umbali mrefu. Na Mwenyezi Mungu anawatadharisha na yeye mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
#
{29 - 30} يخبر تعالى بإحاطة علمه بما في الصدور سواء أخفاه العباد أو أبدوه، كما أن علمه محيط بكل شيء في السماء والأرض فلا تخفى عليه خافية، ومع إحاطة علمه فهو العظيم القدير على كل شيء الذي لا يمتنع عن إرادته موجود. ولما ذكر لهم من عظمته وسعة أوصافه ما يوجب للعباد أن يراقبوه في كل أحوالهم، ذكر لهم أيضاً داعياً آخر إلى مراقبته وتقواه وهو أنهم كلهم صائرون إليه وأعمالهم حينئذ من خير وشر محضرة، فحينئذ يغتبط أهل الخير بما قدموه لأنفسهم، ويتحسر أهل الشر إذا وجدوا ما عملوه محضراً، ويودون أن بينهم وبينه أمداً بعيداً. فإذا عرف العبد أنه ساعٍ إلى ربه وكادحٌ في هذه الحياة، وأنه لا بد أن يلاقي ربه ويلاقي سعيه أوجب له أخذ الحذر والتوقي من الأعمال التي توجب الفضيحة والعقوبة، والاستعداد بالأعمال الصالحة التي توجب السعادة والمثوبة، ولهذا قال تعالى: {ويحذركم الله نفسه}؛ وذلك بما يبدي لكم من أوصاف عظمته وكمال عدله وشدَّة نكاله، ومع شدَّة عقابه فإنه رءوف رحيم، ومن رأفته ورحمته أنه خوَّف العباد، وزجرهم عن الغيِّ والفساد، كما قال تعالى لما ذكر العقوبات: {ذلك يخوِّف الله به عباده، يا عباد فاتقون}؛ فرأفته ورحمته سهلت لهم الطرق التي ينالون بها الخيرات، ورأفته ورحمته حذرتهم من الطرق التي تفضي بهم إلى المكروهات. فنسأله تعالى أن يتمم علينا إحسانه بسلوك الصراط المستقيم والسلامة من الطرق التي تفضي بسالكها إلى الجحيم.
{29-30} Mola Mtukufu anajulisha kuhusu kuzunguka kwa elimu yake yale yaliyo katika vifua, sawa waja wayafiche au wayadhihirishe. Kama vile elimu yake pia imekizunguka kila kitu kilicho katika mbingu na ardhi. Hivyo hakuna siri yoyote inayofichika kwake. Na pamoja na kuzunguka kwa elimu yake, Yeye ndiye Mkuu, Mwenye uwezo juu ya kila kitu, ambaye hakuna chochote kipatikanacho kinaweza kukataa kutaka kwake. Na alipowatajia ukubwa wake na upana wa sifa zake chenye kuwafanya waja kumwangalia katika hali zao zote, akawatajia pia sababu nyingine ya kumwangalia na kumwogopa. Nayo ni kwamba wote watarudi kwake, na matendo yao wakati huo ya heri na ya shari yatahudhurishwa. Wakati huo, watu wa heri watahusudiwa kwa kile walichojitangulizia nafsi zao. Nao watu wa shari watasikitika watakapopata kile walichofanya kimehudhurishwa, na watapenda lau kuwa kati yao na hayo (matendo) kuna umbali mrefu. Kwa hivyo, mja anapojua kwamba anajitahidi kwenda kwa Mola wake Mlezi, na anataabika katika maisha haya; na kwamba ni lazima atakutana na Mola wake Mlezi. Basi itamlazimu kuchukua tahadhari na kujiepusha na matendo yenye kuleta fedheha na adhabu. Na kujiandaa na matendo mema ambayo huleta furaha na thawabu. Na kwa sababu hiyo, Mola Mtukufu alisema, "na Mwenyezi Mungu anawatadharisha na yeye mwenyewe." Na hilo ni kwa yale anayowaonyesha ya sifa za ukuu wake, na ukamilifu wa uadilifu wake, na ukali wa adhabu yake. Na pamoja na ukali wa adhabu yake, yeye kwa hakika ni Mpole, Mwenye kurehemu. Na katika Upole wake na rehema yake ni kwamba aliwahofisha waja, na akawakemea dhidi ya kupotea na ufisadi, kama alivyosema yeye mtukufu alipotaja adhabu. "Kwa hayo, Mwenyezi Mungu anawahofisha waja wake, enyi waja, basi nicheni Mimi." Na upole wake na rehema yake viliwarahisishia njia ambazo kwazo wanapata heri. Na Upole wake na rehema yake viliwatahadharisha dhidi ya njia zinazowapeleka kwenye machukizo. Tunamuomba Mola Mtukufu atutimizie ihsan yake kwa kufuata njia iliyonyooka na kusalimika kutokana na njia zinazopeleka Jahiim (Motoni).1
: 31 - 32 #
{قُلْ إِنْ كُنْتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (31) قُلْ أَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ (32)}.
31. Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atawapenda na atawafutia dhambi zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. 32. Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka, basi hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.
#
{31 - 32} هذه الآية هي الميزان التي يُعرَف بها من أحب الله حقيقة ومن ادعى ذلك دعوى مجردة؛ فعلامة محبة الله اتباع محمد - صلى الله عليه وسلم - الذي جعل متابعته وجميع ما يدعو إليه طريقاً إلى محبته ورضوانه فلا تُنال محبة الله ورضوانه وثوابه إلا بتصديق ما جاء به الرسول من الكتاب والسنة وامتثال أمرهما واجتناب نهيهما، فمن فعل ذلك أحبه الله وجازاه جزاء المحبين، وغفر له ذنوبه وستر عليه عيوبه، فكأنه قيل: ومع ذلك فما حقيقة اتباع الرسول وصفتها؟ فأجاب بقوله: {قل أطيعوا الله والرسول}؛ بامتثال الأمر واجتناب النهي وتصديق الخبر {فإن تولوا}؛ عن ذلك؛ فهذا هو الكفر والله {لا يحب الكافرين}.
{31 - 32} Aya hii ndiyo mizani ambayo kwayo anajulikana yule anayempenda Mwenyezi Mungu kikweli, na yule anayedai hilo kwa madai matupu tu. Hivyo, alama ya kumpenda Mwenyezi Mungu ni kumfuata Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. – Ambaye alifanywa kumfuata yeye na kila anacholingania ndiyo njia ya kumpenda na radhi zake. Kwa hivyo, hayafikiwi mapenzi ya Mwenyezi Mungu na radhi zake na thawabu zake, isipokuwa kwa kusadiki aliyokuja nayo Mtume katika Kitabu na Sunna. Na kutekeleza amri za viwili hivyo na kuepuka makatazo ya viwili hivyo. Kwa hivyo, mwenye kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu atampenda na kumlipa malipo ya wapenzi. Na atamfutia dhambi zake na atamsitiria aibu zake. Na ni kana kwamba ilisemwa: Pamoja na hayo, ni nini ukweli wa kumfuata Mtume na sifa yake? Akajibu kwa kauli yake: "Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume," kwa kutekeleza amri na kujiepusha na katazo na kusadiki habari zake. "Na wakigeuka" wakaliacha hilo, basi hii ndiyo kufuru, na Mwenyezi Mungu, "hawapendi makafiri".
: 33 - 55 #
{إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ (33) ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِنْ بَعْضٍ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (34) إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي إِنَّكَ أَنْتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (35) فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنْثَى وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنْثَى وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ {(36) فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنْبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِنْدَهَا رِزْقًا قَالَ يَامَرْيَمُ أَنَّى لَكِ هَذَا قَالَتْ هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ (37) هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِنْ لَدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ (38) فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَى مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِنَ الصَّالِحِينَ (39) قَالَ رَبِّ أَنَّى يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ قَالَ كَذَلِكَ اللَّهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ (40) قَالَ رَبِّ اجْعَلْ لِي آيَةً قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا وَاذْكُرْ رَبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ (41) وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَامَرْيَمُ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَى نِسَاءِ الْعَالَمِينَ (42) يَامَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ (43) ذَلِكَ مِنْ أَنْبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ وَمَا كُنْتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنْتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ (44) إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَامَرْيَمُ إِنَّ اللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ (45) وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ (46) قَالَتْ رَبِّ أَنَّى يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ قَالَ كَذَلِكِ اللَّهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ إِذَا قَضَى أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ (47) وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ (48) وَرَسُولًا إِلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُمْ بِآيَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُمْ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنْفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّهِ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِ الْمَوْتَى بِإِذْنِ اللَّهِ وَأُنَبِّئُكُمْ بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَةً لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (49) وَمُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُمْ بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ وَجِئْتُكُمْ بِآيَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ (50) إِنَّ اللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ هَذَا صِرَاطٌ مُسْتَقِيمٌ (51) فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَى مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنْصَارِي إِلَى اللَّهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنْصَارُ اللَّهِ آمَنَّا بِاللَّهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ (52) رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنْزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ (53) وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ (54) إِذْ قَالَ اللَّهُ يَاعِيسَى إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنْتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ (55)}.
33. Hakika, Mwenyezi Mungu alimteua Adam, na Nuhu, na ukoo wa Ibrahim, na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote. 34. Ni dhuria wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 35. Aliposema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, nimekuwekea nadhiri kilicho katika tumbo langu la uzazi awe mtumishi wako, basi nikubalie. Hakika, Wewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 36. Basi alipomzaa, akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, nimemzaa wa kike - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa. -Na wa kiume si sawa na wa kike. Na mimi kwa hakika nimemwita Mariam. Nami kwa hakika ninamkinga kwako, yeye na dhuria yake kutokana na Shetani aliyelaaniwa. 37. Basi Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipoingia chumbani kwake, alimkuta na vyakula. Basi alisema: Ewe Mariam! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hesabu. 38. Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nitunuku kutoka kwako dhuria njema. Hakika, Wewe ndiye unayesikia maombi. 39. Kwa hivyo, Malaika wakamwita hali ya kuwa amesimama katika chumba akisali kwamba: Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya Yahya, atakayesadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana, na mtawa, na ni Nabii miongoni mwa walio wema. 40. Zakariya akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana, ilhali tayari uzee umeshanifikia, na mke wangu ni tasa? Akasema: Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu, yeye hufanya apendalo. 41. Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama. Akasema: Alama yako ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipokuwa kwa kuashiria tu. Na mtaje Mola wako Mlezi kwa wingi, na mtakase jioni na asubuhi. 42. Na tazama, pale Malaika waliposema: Ewe Maryam! Kwa hakika, Mwenyezi Mungu amekuteua, na amekutakasa, na amekuteua juu ya wanawake wa walimwengu wote. 43. Ewe Maryam! Mnyenyekee Mola wako Mlezi, na usujudu, na urukuu pamoja na wanaorukuu. 44. Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Nawe hukuwa nao walipokuwa wakitupa kalamu zao ni nani wao atakayemlea Maryam? Na hukuwa nao walipokuwa wakizozana. 45. Pale Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika, Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya (mwana kwa) neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryam, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na ni miongoni mwa waliowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu). 46. Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utu uzima wake, na atakuwa katika walio wema. 47. Maryam akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana ilhali hajanigusa mwanaadamu? Akasema: Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu, yeye huumba apendacho. Anapohukumu jambo, yeye kwa hakika huliambia: Kuwa! Na linakuwa. 48. Na atamfundisha kuandika na hekima na Taurati na Injili. 49. Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi kwa hakika nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola wenu Mlezi, ya kwamba mimi kwa hakika ninawaundia kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha ninapuliza ndani yake na anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaambia mnachokila na mnachoweka akiba katika nyumba zenu. Hakika, katika haya ipo Ishara kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. 50. Na ninasadikisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na ili niwahalalishie baadhi ya yale mliyoharimishiwa. Na nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo, mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini mimi. 51. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia iliyonyooka. 52. Isa alipohisi ukafiri miongoni mwao, akasema: Ni nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. 53. Mola wetu Mlezi! Tuliyaamini uliyoyateremsha, na tulimfuata Mtume huyu, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia. 54. Na makafiri wakapanga vitimbi, na Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga vitimbi. 55. Pale Mwenyezi Mungu aliposema: Ewe Isa! Mimi nitakuchukua, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa kutokana na wale waliokufuru, na nitawaweka wale waliokufuata juu ya wale waliokufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha kwangu ndiko marejeo yenu, na nihukumu kati yenu katika yale mliyokuwa mkihitalifiana.
#
{33 - 55} لله تعالى من عباده أصفياء يصطفيهم ويختارهم ويمن عليهم بالفضائل العالية والنعوت السامية والعلوم النافعة والأعمال الصالحة والخصائص المتنوعة، فذكر هذه البيوت الكبار وما احتوت عليه من كُمَّل الرجال الذين حازوا أوصاف الكمال، وأن الفضل والخير تسلسل في ذراريهم، وشمل ذكورهم ونساءهم وهذا من أجل مننه وأفضل مواقع جوده وكرمه {والله سميع عليم}؛ يعلم من يستحق الفضل والتفضيل فيضع فضله حيث اقتضت حكمته. فلما قرر عظمة هذه البيوت ذكر قصة مريم وابنها عيسى - صلى الله عليه وسلم - وكيف تسلسلا من هذه البيوت الفاضلة، وكيف تنقلت بهما الأحوال من ابتداء أمرهما إلى آخره، وأن امرأة عمران قالت متضرعة إلى ربها متقربة إليه بهذه القربة التي يحبها، التي فيها تعظيم بيته وملازمة طاعته: {إني نذرت لك ما في بطني محرراً}؛ أي خادماً لبيت العبادة المشحون بالمتعبدين {فتقبل مني}؛ هذا العمل أي اجعله مؤسساً على الإيمان والإخلاص مثمراً للخير والثواب {إنك أنت السميع العليم. فلما وضعتها قالت رب إني وضعتها أنثى والله أعلم بما وضعت وليس الذكر كالأنثى}؛ كأن في هذا الكلام نوع تضرع منها وانكسار نفس حيث كان نذرها بناءً على أنه يكون ذكراً يحصل منه من القوة والخدمة والقيام بذلك ما يحصل من أهل القوة، والأنثى بخلاف ذلك، فجبر الله قلبها وتقبل الله نذرها، وصارت هذه الأنثى أكمل وأتم من كثير من الذكور، بل من أكثرهم، وحصل بها من المقاصد أعظم مما يحصل بالذكر، ولهذا قال: {فتقبلها ربها بقبول حسن وأنبتها نباتاً حسناً}؛ أي: ربيت تربية عجيبة دينية أخلاقية أدبية، كملت بها أحوالها، وصلحت بها أقوالها وأفعالها، ونما فيها كمالها، ويسر الله لها زكريا كافلاً، وهذا من مِنَّةِ الله على العبد أن يجعل من يتولى تربيته من الكاملين المصلحين. ثم إن الله تعالى أكرم مريم وزكريا حيث يسَّر لمريم من الرزق الحاصل بلا كدٍّ ولا تعب، وإنما هو كرامة أكرمها الله به، إذ {كلما دخل عليها زكريا المحراب}؛ وهو محل العبادة وفيه إشارة إلى كثرة صلاتها وملازمتها لمحرابها {وجد عندها رزقاً}؛ هنيئاً معدًّا قال: {أنى لك هذا قالت هو من عند الله إن الله يرزقُ من يشاء بغير حساب}؛ فلما رأى زكريا هذه الحال والبر واللطف من الله بها، ذكَّرَه أن يسأل الله تعالى حصول الولد على حين اليأس منه فقال: {رب هَب لي من لَدُنك ذرية طيبة إنك سميعُ الدُّعاء. فنادته الملائكة وهو قائم يصلي في المحراب أنَّ الله يبشرك بيحيى مصدقاً بكلمة من الله}؛ اسمه أي: الكلمة التي مِنَ الله عيسى بن مريم فكانت بشارته بهذا النبي الكريم تتضمن البشارة بعيسى بن مريم والتصديق له والشهادة له بالرسالة، فهذه الكلمة من الله كلمة شريفة اختص الله بها عيسى بن مريم، وإلا فهي من جملة كلماته التي أوجد بها المخلوقات، كما قال تعالى: {إن مثل عيسى عند الله كمثل آدم خلقه من تراب ثم قال له كن فيكون}. وقوله: {وسيداً وحصوراً}؛ أي: هذا المبَشَّر به وهو يحيى سيد من فضلاء الرسل وكرامهم، والحصور قيل هو الذي لا يولد له ولا شهوة له في النساء، وقيل هو الذي عصم وحفظ من الذنوب والشهوات الضارة، وهذا أليق المعنيين، {ونبياً من الصالحين}؛ الذين بلغوا في الصلاح ذروته العالية، {قال رب أنى يكون لي غلام وقد بلغني الكبر وامرأتي عاقر}؛ فهذان مانعان فمن أي طريق يا رب يحصل لي ذلك مع ما ينافي ذلك {قال كذلك الله يفعل ما يشاء}؛ فإنه كما اقتضت حكمته جريان الأمور بأسبابها المعروفة، فإنه قد يخرق ذلك لأنه الفعَّالُ لما يريد، الذي قد انقادت الأسباب لقدرته، ونفذت فيها مشيئته وإرادته فلا يتعاصى على قدرته شيء من الأسباب ولو بلغت في القوة ما بلغت {قال رب اجعل لي آية}؛ ليحصل السرور والاستبشار وإن كنت يا رب متيقناً ما أخبرتني به ولكن النفس تفرح، ويطمئن القلب إلى مقدمات الرحمة واللطف، {قال آيتك أن لا تكلم الناس ثلاثة أيام إلا رمزاً}؛ وفي هذه المدة {اذكر ربك كثيراً وسبح بالعشي والإبكار}؛ أول النهار وآخره، فمنع من الكلام في هذه المدة، فكان في هذا مناسبة لحصول الولد من بين الشيخ الكبير والمرأة العاقر، وكونه لا يقدر على مخاطبة الآدميين ولسانه منطلق بذكر الله وتسبيحه آية أخرى، فحينئذ حصل له الفرح والاستبشار، وشكر الله، وأكثر من الذكر والتسبيح بالعشايا والإبكار. وكان هذا المولود من بركات مريم بنت عمران على زكريا، فإن ما منَّ الله به عليها من ذلك الرزق الهني الذي يحصل بغير حساب ذكَّره وهيَّجه على التضرع والسؤال، والله تعالى هو المتفضل بالسبب والمسبب ولكنه يقدر أموراً محبوبة على يد من يحبه ليرفع الله قدره ويُعْظِمَ أجره، ثم عاد تعالى إلى ذكر مريم وأنها بلغت في العبادة والكمال مبلغاً عظيماً فقال تعالى: {وإذ قالت الملائكة يا مريم إن الله اصطفاك}؛ أي: اختارك ووهب لك من الصفات الجليلة والأخلاق الجميلة {وطهرك}؛ من الأخلاق الرذيلة {واصطفاك على نساء العالمين}؛ ولهذا قال - صلى الله عليه وسلم -: «كمل من الرجال كثير، ولم يكمل من النساء إلا مريم بنت عمران وآسية بنت مزاحم وخديجة بنت خويلد، وفضل عائشة على النساء كفضل الثريد على سائر الطعام» ، فنادتها الملائكة عن أمر الله لها بذلك لتغتبط بنعم الله وتشكر الله، وتقوم بحقوقه، وتشتغل بخدمته، ولهذا قال الملائكة: {يا مريم اقنتي لربك}؛ أي: أكثري من الطاعة والخضوع والخشوع لربك وأديمي ذلك {واركعي مع الراكعين}؛ أي: صلي مع المصلين فقامت بكل ما أمرت به وبرزت وفاقت في كمالها. ولما كانت هذه القصة وغيرها من أكبر الأدلة على رسالة محمد - صلى الله عليه وسلم - حيث أخبر بها مفصلة محققة لا زيادة فيها ولا نقص، وما ذاك إلا لأنه وحي من الله العزيز الحكيم لا بتعلم من الناس قال تعالى: {ذلك من أنباء الغيب نوحيه إليك، وما كنت لديهم إذ يلقون أقلامهم أيهم يكفل مريم}؛ حيث جاءت بها أمها فاختصموا أيهم يكفلها لأنها بنت إمامهم ومقدمهم، وكلهم يريد الخير والأجر من الله حتى وصلت بهم الخصومة إلى أن اقترعوا عليها فألقوا أقلامهم مقترعين، فأصابت القرعة زكريا رحمة من الله به وبها فأنت - يا أيها الرسول - لم تحضر تلك الحالة لتعرفها فتقصها على الناس، وإنما الله نبأك بها، وهذا هو المقصود الأعظم من سياق القصص أنه يحصل بها العبرة، وأعظم العبر والاستدلال بها على التوحيد والرسالة والبعث وغيرها من الأصول الكبار {إذ قالت الملائكة يا مريم إن الله يبشرك بكلمة منه اسمه المسيح عيسى ابن مريم وجيهاً في الدنيا والآخرة ومن المقربين}؛ أي: له الوجاهة والجاه العظيم في الدنيا والآخرة عند الخلق، ومع ذلك فهو عند الله من المقربين الذين هم أقرب الخلائق إلى الله وأعلاهم درجة، وهذه بشارة لا يشبهها شيء من البشارات، ومن تمام هذه البشارة أنه {يكلم الناس في المهد}؛ فيكون تكليمه آية من آيات الله ورحمة منه بأمه وبالخلق، وكذلك يكلمهم {كهلاً}؛ أي: في حال كهولته، وهذا تكليم النبوة والدعوة والإرشاد، فكلامه في المهد فيه آيات وبراهين على صدقه ونبوته وبراءة أمِّه مما يظن بها من الظنون السيئة، وكلامه في كهولته فيه نفعه العظيم للخلق وكونه واسطة بينهم وبين ربهم في وحيه وتبليغ دينه وشرعه، ومع ذلك فهو {من الصالحين}؛ الذين أصلح الله قلوبهم بمعرفته وحبه، وألسنتهم بالثناء عليه وذكره وجوارحهم بطاعته وخدمته {قالت رب أنى يكون لي ولد ولم يمسسني بشر}؛ وهذا هو من الأمور المستغربة {قال كذلك الله يخلق ما يشاء}؛ ليعلم العباد أنه على كل شيء قدير وأنه لا ممانع لإرادته {إذا قضى أمراً فإنما يقول له كن فيكون. ويعلمه الكتاب}؛ أي: جنس الكتب السابقة والحكم بين الناس ويعطيه النبوة ويجعله {رسولاً إلى بني إسرائيل}؛ ويؤيده بالآيات البينات والأدلة القاهرة حيث قال: {أني قد جئتكم بآية من ربكم}؛ تدلكم أني رسول الله حقاً، وذلك {أني أخلق لكم من الطين كهيئة الطير فأنفخ فيه فيكون طيراً بإذن الله وأبرئ الأكمه}؛ وهو ممسوح العينين الذي فقد بصره وعيناه {والأبرص وأحيي الموتى بإذن الله وأنبئكم بما تأكلون وما تدخرون في بيوتكم، إن في ذلك}؛ المذكور {لآية لكم إن كنتم مؤمنين. ومصدقاً لما بين يدي من التوراة}؛ فأيده الله بجنسين من الآيات والبراهين الخوارق المستغربة التي لا يمكن لغير الأنبياء الإتيان بها، والرسالة والدعوة والدين الذي جاء به وأنه دين التوراة ودين الأنبياء السابقين، وهذا أكبر الأدلة على صدق الصادقين، فإنه لو كان من الكاذبين لخالف ما جاءت به الرسل ولناقضهم في أصولهم وفروعهم، فعلم بذلك أنه رسول الله وأن ما جاء به حق لا ريب فيه، وأيضاً فقوله: {ولأحل لكم بعض الذي حرم عليكم}؛ أي: ولأخفف عنكم بعض الآصار والأغلال {فاتقوا الله وأطيعون. إن الله ربي وربكم فاعبدوه}؛ وهذا ما يدعو إليه جميع الرسل عبادة الله وحده لا شريك له وطاعتهم، وهذا هو الصراط المستقيم الذي من سلكه أوصله إلى جنات النعيم. فحينئذ اختلفت أحزاب بني إسرائيل في عيسى فمنهم من آمن به واتبعه ومنهم من كفر به وكذبه ورمى أمه بالفاحشة كاليهود {فلما أحس عيسى منهم الكفر}؛ والاتفاق على رد دعوته {قال}؛ نادباً لبني إسرائيل على مؤازرته: {من أنصاري إلى الله، قال الحواريون}؛ أي: الأنصار: {نحن أنصار الله آمنَّا بالله واشهد بأنا مسلمون}؛ وهذا من مِنَّةِ الله عليهم وعلى عيسى حيث ألهم هؤلاء الحواريين الإيمان به والانقياد لطاعته والنصرة لرسوله {ربنا آمنا بما أنزلت واتبعنا الرسول}؛ وهذا التزام تام للإيمان بكل ما أنزل الله ولطاعة رسوله {فاكتبنا مع الشاهدين}؛ لك بالوحدانية ولنبيك بالرسالة ولدينك بالحق والصدق. وأما من أحسَّ عيسى منهم الكفرَ وهم جمهور بني إسرائيل فإنهم {مكروا}؛ بعيسى {ومكر الله}؛ بهم {والله خير الماكرين}؛ فاتفقوا على قتله وصلبه، وشُبِّهَ لهم شَبَهُ عيسى فقبضوا على من شُبِّهَ لهم به وقال الله لعيسى: {إني متوفيك ورافعك إليَّ ومطهرك من الذين كفروا}؛ فرفعه الله إليه، وطهره من الذين كفروا، وصلبوا من قتلوه، ظانِّين أنه عيسى، وباؤوا بالإثم العظيم. وسينزل عيسى بن مريم في آخر هذه الأمة حكماً عدلاً يقتل الخنزير ويكسر الصليب ويتبع ما جاء به محمد - صلى الله عليه وسلم -، ويعلم الكاذبون غرورَهم وخداعَهم وأنهم مغرورون مخدوعون. وقوله: {وجاعل الذين اتبعوك فوق الذين كفروا إلى يوم القيامة}؛ المراد بمن اتبعه الطائفة التي آمنت به ونصرهم الله على من انحرف عن دينه، ثم لما جاءت أمة محمد - صلى الله عليه وسلم - كانوا هم أتباعه حقًّا فأيدهم ونصرهم على الكفار كلهم، وأظهرهم بالدين الذي جاءهم به محمد - صلى الله عليه وسلم - {وعد الله الذين آمنوا منكم وعملوا الصالحات ليستخلفنهم في الأرض}؛ الآية. ولكن حكمة الله عادلة فإنها اقتضت أن من تمسك بالدين نصره النصر المبين، وأن من ترك أمره ونهيه ونبذ شرعه وتجرأ على معاصيه أن يعاقبه ويسلط عليه الأعداء. والله عزيز حكيم. وقوله: {ثم إليَّ مرجعكم فأحكم بينكم فيما كنتم فيه تختلفون}.
{33 - 55} Mwenyezi Mungu Mtukufu anao wateule miongoni mwa waja wake. Anawateua na kuwachagua, na anawaneemesha kwa fadhila za hali ya juu, na sifa tukufu, na elimu zenye manufaa, na matendo mema, na sifa maalumu mbalimbali. Kwa hivyo, alitaja nyumba hizi kubwa, na yale zilizoyajumuisha ya wanaume wakamilifu ambao walipata sifa za ukamilifu. Na kwamba fadhila hii na heri ni mfululizo katika dhuria zao. Na hilo liliwajumuisha wa kiume wao na wanawake wao. Na haya ni katika neema zake kubwa, na maeneo bora zaidi ya ukarimu wake na utukufu wake. "Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, Mwenye kujua". Anajua anayestahiki fadhila na kuboreshwa, naye huiweka fadhila yake pale ambapo hekima yake inahitaji. Alipothibitisha ukuu wa nyumba hizi, akataja kisa cha Maryam na mwanawe, Isa - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na jinsi walivyofululiza kutoka katika nyumba hizi nzuri. Na jinsi hali zilivyowapeleka tangu mwanzo wa jambo lao hadi mwisho wake. Na kwamba mke wa 'Imran alisema akimnyenyekea Mola wake Mlezi, akijiweka karibu naye kwa kurubani hii ambayo anaipenda. Ambayo ndani yake kuna kuitukuza nyumba yake na kushikamana na utiifu kwake. "Hakika mimi, nimekuwekea nadhiri kilicho katika tumbo langu la uzazi awe mtumishi wako." Yani mtumishi wa nyumba ya ibada iliyojaa wenye kufanya ibada. "Basi nikubalie" tendo hili." Yani lifanye (tendo hili) lijiasisi juu ya imani na ikhlasi, yenye kuzaa matunda ya heri na thawabu. "Hakika, Wewe ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Basi alipomzaa, akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, nimemzaa wa kike - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa. -Na wa kiume si sawa na wa kike." Na ni kana kwamba katika maneno haya kuna aina ya kunyenyekea kutoka kwake na kuvunjika kwa nafsi, kwani nadhiri yake ilijengeka juu ya hali ya kwamba atakuwa ni wa kiume. Ambaye atapata nguvu kwa sababu ya hilo, na huduma na kufanya hivyo kama linavyotoka kwa watu wenye nguvu. Naye wa kike ni tofauti na hivyo. Basi Mwenyezi Mungu akauponya moyo wake na Mwenyezi Mungu akaikubali nadhiri yake. Na huyu wa kike akawa mkamilifu zaidi na mtimilifu zaidi kuliko wengi katika wa kiume. Bali kuliko wengi wao. Na kupitia kwake, yalipatikana malengo makubwa zaidi kuliko yale yanayopatikana kutoka kwa wa kiume. Ndio maana akasema: "Basi Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema." Yani alilelewa malezi ya ajabu, ya kidini, ya kimaadili na ya kiadabu. Ambayo kwayo alikamilika katika hali zake, na akatengenezeka kwayo maneno yake na matendo yake. Na ukakua ukamilifu wake ndani yake. Na Mwenyezi Mungu akamfanyia Zakariya kuwa mlezi wake. Na hii ni katika neema ya Mwenyezi Mungu juu ya mja wake kwamba, amfanye yule anayesimamia malezi yake kuwa miongoni mwa wakamilifu na watengenezaji. Kisha, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtukuza Maryamu na Zakariya. Kwani alimrahisishia Maryamu riziki iliyopatikana bila ya shida wala taabu. Na ulikuwa ukarimu tu ambao Mwenyezi Mungu alimpa. Kwa sababu:"Kila mara Zakariya alipoingia chumbani mwake mwa kuabudia." Na ndani yake kuna ishara juu ya wingi wa swala zake, na kushikamana kwake na pahali pake pa kuswalia. "Alimkuta na vyakula" chenye raha, kilichokwisha andaliwa. Akasema, “Basi alisema: Ewe Mariam! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hesabu." Na Zakariya alipoiona hali hii na wema na upole kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yake (Maryamu), ilimkumbusha kwamba amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu kupata mtoto alipokuwa amefikia wakati wa kukata tamaa. Akasema, "Mola wangu Mlezi! Nitunuku kutoka kwako dhuria njema. Hakika, Wewe ndiye unayesikia maombi. Kwa hivyo, Malaika wakamwita hali ya kuwa amesimama katika chumba akisali kwamba: Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya Yahya, atakayesadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu." Yani neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu ni Isa mwana wa Maryamu. Kwa hivyo, ikawa bishara yake juu ya Nabii huyu mtukufu inajumuisha bishara ya Isa mwana wa Maryamu, na kumsadikisha, na kuushuhudia ujumbe wake. Na neno hili litokalo kwa Mwenyezi Mungu ni neno tukufu. Mwenyezi Mungu aliliteua kwa ajili ya Isa mwana wa Maryamu. Vinginevyo, hilo ni miongoni mwa maneno yake ambayo aliumba kwalo viumbe, kama alivyosema Yeye Mtukufu. "Hakika, mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam. Alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa." Na kauli yake, "na ni bwana na mtawa." Yani huyu ni aliye bishara ambaye ni Yahya ni bwana miongoni mwa bora wa Mitume na watukufu wao. Na mtawa ilisemwa kuwa ni yule ambaye hawezi kupata watoto wala hana matamanio ya wanawake. Na ilisemwa kuwa ni yule ambaye aliyelindwa na kuhifadhiwa kutokana na dhambi na matamanio yenye madhara. Na hili ndiyo maana inayofaa zaidi kati ya maana mbili hizi. "Na ni Nabii miongoni mwa walio wema," ambao walifikia kilele cha juu katika wema. Akasema, "Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana, ilhali tayari uzee umeshanifikia, na mke wangu ni tasa?" Kwa maana viwili hivi ni vizuizi. Basi ni kwa njia gani, ewe Mola wangu Mlezi hili litaweza kunipata pamoja na kuwepo kwa yenye kupingana nalo? "Akasema: Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu, Yeye hufanya apendalo." Kwani kama vile hekima yake ilivyohitaji kutokea kwa mambo kupitia sababu zake zinazojulikana, basi Yeye kwa hakika anaweza kukiuka hilo kwa sababu yeye ni mtendaji wa anachotaka; ambaye sababu zote zimeutii uwezo wake. Na mapenzi yake na kutaka kwake kunatekelezeka ndani yake, na hakuna sababu yoyote inayoweza kuasi uwezo wake, hata kikifikia kwa nguvu kinavyofikia. "Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama." Ili nipate furaha na bishara njema, ingawa ewe Mola Mlezi nina yakini juu ya uliyoniambia, lakini nafsi inafurahi, na moyo unatulia kwa yale yanayotangulia rehema na upole. "Akasema: Alama yako ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipokuwa kwa kuashiria tu." Na katika kipindi hiki "mtaje Mola wako Mlezi kwa wingi, na mtakase jioni na asubuhi." Yani mwanzo wa siku na mwisho wake. Kwa hivyo akazuiliwa kuzungumza katika kipindi hiki. Na hili lilikuwa ndilo tukio la kuzaliwa kwa mtoto baina ya mzee na mwanamke tasa. Na hali ikiwa kwamba hana uwezo wa kuwaongelesha wanadamu ilhali ulimi wake unasonga kwa utajo wa Mwenyezi Mungu na kumtakasa ni alama nyingine. Hapo, akapata furaha na bishara njema. Na akamshukuru Mwenyezi Mungu, na akazidisha kufanya dhikri na tasbihi kwa wingi jioni na asubuhi. Na huyu mzaliwa alikuwa ni katika baraka za Maryam binti Imran juu ya Zakariya. Kwani, Mwenyezi Mungu alimneemesha kwa riziki hiyo yenye furaha, ambayo inapatikana bila hesabu. Hilo lilimkumbusha (Zakariya) na kumchochea kunyenyekea na kuomba. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayetoa fadhila ya sababu na matokeo yake. Naye hukadiria vitu vinavyopendeza kupitia mkono wa yule anayempenda ili Mwenyezi Mungu aiyanyue hadhi yake, na ampe malipo makubwa. Kisha Mola Mtukufu akarejea kwenye kumtaja Maryamu, na kwamba alifikia kiwango kikubwa katika ibada na ukamilifu. Mola Mtukufu akasema: "Na tazama, pale Malaika waliposema: Ewe Maryam! Kwa hakika, Mwenyezi Mungu amekuteua." Yani amekuchagua na akakutunuku sifa kubwa na maadili mazuri. "Na amekutakasa," kutokana na tabia mbovu. "Na amekuteua juu ya wanawake wa walimwengu wote." Ndio maana akasema – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake,– “Walikamilika wengi katika wanaume. Na hawakukamilika katika wanawake isipokuwa Maryamu binti Imran, Asiya binti Muzahim, na Khadija binti Khuwaylid. Na ubora wa Aisha juu ya wanawake wote ni kama ubora wa Tharid (mkate kwa supu yenye nyama) juu ya vyakula vingine vyote.” Basi Malaika wakamwita kwa amri hii ya Mwenyezi Mungu juu yake ili azifurahie neema za Mwenyezi Mungu, na amshukuru Mwenyezi Mungu, na atekeleze haki zake, na ashughulike na kumtumikia. Na ndio maana Malaika wakasema, "Ewe Maryamu, mnyenyekee Mola wako Mlezi." Yani fanya kwa wingi utiifu, kunyenyekea Mola wako Mlezi, na udumishe hilo {na urukuu pamoja na wanaorukuu." Yani swali pamoja na wanaoswali. Kwa hivyo, akafanya kila alichoamrishwa, na akajitokeza, na akainuka juu katika ukamilifu wake. Na kwa kuwa kisa hiki na vinginevyo ni miongoni mwa dalili kubwa kabisa juu ya ujumbe wa Muhammad, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake,- kwa maana alikieleza kwa kina na kusadikisha, bila ya kuongeza wala kupunguza. Na hilo siyo isipokuwa ni kwa sababu ulikuwa ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, na si kwa kusoma kutoka kwa watu. Mola Mtukufu akasema, "Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Nawe hukuwa nao walipokuwa wakitupa kalamu zao ni nani wao atamlea Maryam? Wakati mama yake alipomleta, nao wakazozana ni nani miongoni mwao atakayemlea, kwa sababu yeye ni binti wa imamu wao na wa mbele wao. Nao wote walitaka heri na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mpaka mzozo huo ukawafikisha kupigia kura juu yake. Basi wakazitupa kalamu zao wakipiga kura (kwazo). Basi kura hiyo ikamwangukia Zakariya, kwa rehema ya Mwenyezi Mungu juu yake na juu ya Maryamu. Basi wewe - ewe Mtume - hukuwepo katika hali hiyo ili uijue na uwasimulie watu. Lakini Mwenyezi Mungu tu ndiye aliyekuambia kuihusu. Na hili ndilo lengo kuu la kusimulia visa, kwamba mazingatio hupatikana ndani yake. Na mazingatio makubwa zaidi ni kuvitumia kama ushahidi juu ya Tauhidi, utume, ufufuo na mengineyo katika misingi mikubwa. "45. Pale Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika, Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema (ya mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryam, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na ni miongoni mwa waliowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu)." Yani ana heshima na hadhi kubwa katika dunia na Akhera mbele ya viumbe, na pamoja na hayo yeye kwa Mwenyezi Mungu ni katika wale waliowekwa karibu. Ambao ndio viumbe walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu na wa daraja la juu zaidi wao. Na bishara hii njema ambayo haifanani nayo chochote katika bishara zote. Na katika katika ukamilifu wa bishara hii ni kwamba, "atazungumza na watu katika utoto wake.” Basi kutakuwa kumzungumzisha kwake ni alama katika alama za Mwenyezi Mungu, na rehema itokayo kwake, kwa mama yake na juu ya viumbe. Na vile vile atawazungumzisha “katika utu uzima wake.” Yani katika hali ya uzee wake. Na huku ni kumzungumzisha kwa unabii, kulingania na kuongoza. Hivyo basi, kuzungumza kwake katika utoto wake kuna alama na ushahidi juu ya ukweli wake na unabii wake na kutokuwa na hatia kwa mama yake kutokana na yale wanayomdhania katika dhana mbaya. Na kuzungumza kwake katika uzee wake kuna manufaa yake makubwa kwa viumbe, na kwamba ni njia baina yao na Mola wao Mlezi katika wahyi wake na kuifikisha dini yake na sheria yake. Na pamoja na hayo, Yeye ni “katika walio wema” ambao Mwenyezi Mungu alizitengeneza nyoyo zao kwa kumjua na kumpenda. Na ndimi zao kwa kumsifu na kumtaja. Na viungo vyao kwa kumtii na kumtumikia. “Akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana ilhali hajanigusa mwanaadamu?” Na hili ni miongoni mwa mambo ya kushangaza. “Akasema: Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu, yeye huumba apendacho.” Ili waja wajue kwamba Yeye ni muweza wa kila kitu, na kwamba hakuna chenye kuzuia mapenzi yake. “Anapohukumu jambo, yeye kwa hakika huliambia: Kuwa! Na linakuwa. Na atamfundisha kuandika” Vitabu vilivyotangulia na kuhukumu baina ya watu, na atampa unabii, na atamfanya awe “Mtume kwa Wana wa Israili.” Na atamuunga mkono kwa Aya zilizo wazi, na hoja zenye ushindi, pale aliposema, “Mimi kwa hakika nimewajia na Ishara kutoka kwa Mola wenu Mlezi,” zinazowaonyesha kwamba mimi hakika ni Mtume wa Mwenyezi Mungu wa haki. Na hilo ni kwamba “mimi kwa hakika ninawaundia kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha ninapuliza ndani yake na anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa.” Naye ni aliyefunikwa macho mawili, ambaye alipoteza kuona kwake na macho yake. “Na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaambia mnachokila na mnachoweka akiba katika nyumba zenu. Hakika, katika hayo,” yaliyotajwa “ipo Ishara kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. Na ninasadikisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati.” Basi Mwenyezi Mungu akamuunga mkono kwa Aya za aina mbili na ushahidi wa usio wa kawaida na wa ajabu ambazo haziwezi kuletwa na wasiokuwa manabii. Na ujumbe, na wito na dini ambayo alikuja nayo, na kwamba ni dini ya Taurati, na dini ya Manabii waliotangulia. Na huu ndio ushahidi mkubwa zaidi wa ukweli wa wakweli. Kwani, lau kuwa angekuwa miongoni mwa waongo, angeyahalifu yale waliyokuja nayo Mitume, na angewatengua katika misingi yao na matawi yao. Basi ikajulikana kwa hayo kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwamba yale aliyokuja nayo ni haki, hayana shaka yoyote ndani yake. Na pia kauli yake, ”Na ili niwahalalishie baadhi ya yale mliyoharimishiwa.” Yani niwapunguzieni baadhi ya mizigo na minyororo yenu. “Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini mimi. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabudni Yeye.” Na hili ndilo wanalolingania Mitume wote; kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, ambaye hana mshirika yeyote, na kuwatii wao. Na hii ndiyo njia iliyonyooka ambayo mwenye kuishika, itamfikisha kwenye mabustani yenye neema. Hapo, makundi ya Wana wa Israili yakahitalifiana kuhusiana na Isa. Miongoni mwao kuna yule aliyemwamini na akamfuata. Na miongoni mwao kuna yule aliyekufuru na akamkadhibisha na akamtuhumu mama yake na uchafu, kama vile Mayahudi. “Basi, Isa alipohisi ukafiri miongoni mwao,” na makubaliano ya kuukataa ulunganizi wake. “Akasema," akiwaita Wana wa Israili ili wamsaidie, “Ni nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi wake.” Yani wale wanaomnusuru, “Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.” Na hii ni katika neema ya Mwenyezi Mungu juu yao, na juu ya Isa. Kwani wanafunzi hao walifunuliwa na Mwenyezi Mungu kumwamini na kufuata na kutii amri zake, na kumnusuru Mtume wake. “Mola wetu Mlezi! Tuliyaamini uliyoyateremsha, na tulimfuata Mtume huyu.” Na hii ni ahadi kamili ya kuamini kila alichoteremsha Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake. "Basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia,” kuwa wewe ni mpweke, na kwamba nabii wako ni Mtume, na kwamba dini yako ni ya haki na ukweli. Na ama wale ambao Isa alihisi kufuru miongoni mwao, nao ndio wengi katika Wana wa Israili, wao kwa hakika “wakapanga vitimbi” dhidi ya Isa. “Na Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi” dhidi yao, “na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga vitimbi.” Basi wakakubali kumwua na kumsulubisha. Naye wakafananishiwa anayefanana na Isa, kwa hivyo wakamkamata yule waliofananishiwa. Na Mwenyezi Mungu akamwambia Isa, “Mimi nitakuchukua, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa kutokana na wale waliokufuru.” Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamnyanyua kwenda kwake, na akamtakasa kutokana na wale waliokufuru. Na wakamsulubisha yule waliyemuua wakidhani kuwa yeye ndiye Isa, na wakarudi na dhambi kubwa. Isa bin Maryamu atashuka katika mwisho wa umma huu akihukumu kwa uadilifu, atawachinja nguruwe; na atavunja msalaba, na atafuata yale aliyokuja nayo Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - Na waongo watajua kudanganywa kwao na kuhadaiwa kwao, na kwamba wao walidanganywa na wakahadaiwa. Na kauli yake, “Na nitawaweka wale waliokufuata juu ya wale waliokufuru, mpaka Siku ya Kiyama.” Kinachokusudiwa na wale waliomfuata ni kundi lile lililomuamini, na Mwenyezi Mungu akawanusuru juu ya wale walioiacha dini yake. Kisha umma wa Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ulipokuja, walikuwa wao ndio wafuasi wake, kwa hivyo akawaunga mkono na akawanusuru dhidi ya makafiri wote. Na akawapa ushindi kwa dini aliyowajia nayo Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. – “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi,” hadi mwisho wa Aya. Hata hivyo, hekima ya Mwenyezi Mungu ni ya uadilifu. Kwani, ilipita kwamba mwenye kushikamana na dini, atamnusuru kumnusuru kuliko wazi. Na kwamba mwenye kuacha amri yake na makatazo yake, na akaitupa sheria yake, na akayafanyia ujasiri maasia yake kwamba atamwadhibu na atawapa maadui wake mdono juu yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. Na kauli yake, ” Kisha kwangu ndiko marejeo yenu, na nihukumu kati yenu katika yale mliyokuwa mkihitalifiana.”
Kisha akabainisha atakachowafanyia, akasema:
: 56 - 57 #
{فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُمْ مِنْ نَاصِرِينَ (56) وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ (57)}.
56. Ama wale waliokufuru, basi nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Akhera, na wala hawatapata wowote wa kuwanusuru. 57. Na ama wale walioamini na wakatenda mema, basi Mwenyezi Mungu atawalipa ujira wao kamili. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu.
#
{56 - 57} وهذا الجزاء عام لكل من اتصف بهذه الأوصاف من جميع أهل الأديان السابقة. ثم لما بعث سيد المرسلين وخاتم النبيين، ونسخت رسالته الرسالات كلها، ونسخ دينه جميع الأديان صار المتمسك بغير هذا الدين من الهالكين. وقوله تعالى:
{56 - 57} Na haya ni malipo ya jumla kwa kila mwenye kusifika kwa sifa hizi kutoka kwa watu wote wa dini zilizotangulia. Kisha alipotuma bwana wa Mitume, na wa mwisho wa Manabii, na ujumbe wake ukafuta jumbe zote, na dini yake ikafuta dini zote. Anakuwa mwenye kushikamana na dini isiyokuwa hii ni miongoni mwa walioangamia. Na kauli yake Mola Mtukufu:
: 58 #
{ذَلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ (58)}.
58. Haya tunayokusomea ni katika Aya na ukumbusho wenye hekima.
#
{58} أي: هذا القرآن العظيم الذي فيه نبأ الأولين والآخرين والأنبياء والمرسلين هو آيات الله البينات، وهو الذي يذكر العباد كل ما يحتاجونه، وهو الحكيم المحكم صادق الأخبار، حسن الأحكام.
{58} Yani, Qur-ani hii tukufu, ambayo ndani yake kuna habari za wa mwanzo na wa mwisho, na Manabii na Mitume, ni Ishara za Mwenyezi Mungu zilizo wazi. Nayo ndiyo ambayo inawakumbusha waja kila wanachohitaji. Nayo ni yenye hekima, iliyo madhubuti, ya habari za kweli, yenye hukumu nzuri.
: 59 - 63 #
{إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آدَمَ خَلَقَهُ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ (59) الْحَقُّ مِنْ رَبِّكَ فَلَا تَكُنْ مِنَ الْمُمْتَرِينَ (60) فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنْفُسَنَا وَأَنْفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَلْ لَعْنَتَ اللَّهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ (61) إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ وَمَا مِنْ إِلَهٍ إِلَّا اللَّهُ وَإِنَّ اللَّهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (62) [فَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ (63)] }.
59. Hakika, mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam. Alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. 60. Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka. 61. Basi mwenye kukuhoji katika haya baada ya yale yaliyokufikia katika elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo. 62. Hakika, haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna mungu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 63. Na wakigeuka, basi Mwenyezi Mungu anawajua waharibifu.
#
{59 - 62} لما ذكر قصة مريم وعيسى ونبأهما الحق، وأنه عبد أنعم الله عليه، وأن من زعم أن فيه شيئاً من الإلهية فقد كذب على الله، وكذب جميع أنبيائه وكذب عيسى - صلى الله عليه وسلم - فإن الشبهة التي عرضت لمن اتخذه إلهاً شبهة باطلة، فلو كان لها وجه صحيح لكان آدم أحق منه فإنه خلق من دون أم ولا أب، ومع ذلك فاتفق البشر كلُّهم على أنه عبد من عباد الله، فدعوى إلهية عيسى بكونه خلق من أم بلا أب دعوى من أبطل الدعاوي، وهذا هو الحق الذي لا ريب فيه أن عيسى كما قال عن نفسه: {ما قلت لهم إلا ما أمرتني به أن اعبدوا الله ربي وربكم}؛ وكان قد قدم على النبي - صلى الله عليه وسلم - وفد نصارى نجران ، وقد تصلبوا على باطلهم بعدما أقام عليهم النبي - صلى الله عليه وسلم - البراهين بأن عيسى عبد الله ورسوله حيث زعموا إلهيته، فوصلت به وبهم الحال إلى أن أمره الله تعالى أن يباهلهم فإنه قد اتضح لهم الحق ولكن العناد والتعصب منعاهم منه، فدعاهم رسول الله - صلى الله عليه وسلم - إلى المباهلة بأن يحضر هو وأهله وأبناؤه، وهم يحضرون بأهلهم وأبنائهم ثم يدعون الله تعالى أن ينزل عقوبته ولعنته على الكاذبين، فتشاوروا هل يجيبونه إلى ذلك، فاتفق رأيهم أن لا يجيبوه لأنهم عرفوا أنه نبي الله حقًّا، وأنهم إن باهلوه هلكوا هم وأولادهم وأهلوهم فصالحوه وبذلوا له الجزية، وطلبوا منه الموادعة والمهادنة فأجابهم - صلى الله عليه وسلم - ولم يحرجهم لأنه حصل المقصود من وضوح الحق، وتبين عنادهم حيث صمموا على الامتناع عن المباهلة، وذلك يبرهن على أنهم كانوا ظالمين. ولهذا قال تعالى: {إن هذا لهو القصص الحق}؛ أي: الذي لا ريب فيه، {وإن الله لهو العزيز} الذي قهر بقدرته وقوته جميع الموجودات وأذعنت له سكان الأرض والسماوات، ومع ذلك فهو {الحكيم}؛ الذي يضع الأشياء مواضعها وينزلها منازلها.
{59 - 62} Alipotaja kisa cha Maryamu na Isa, na akawaambia haki, na kwamba yeye ni mja ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha. Na kwamba mwenye kudai kuwa ndani yake kuna kitu cha uungu, basi hakika amesema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu. Na amesema uongo juu ya Manabii wake wote, na amesema uwongo juu ya Isa - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - basi fikira iliyomjia aliyemfanya yeye kuwa Mungu, ni fikira batili. Lau kuwa yalikuwa na sura sahihi, basi Adam angestahiki zaidi kuliko yeye. Kwa sababu, Yeye Mwenyezi Mungu aliumbwa bila ya mama wala baba. Na pamoja na hayo, wanadamu wote walikubaliana kuwa yeye ni mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, madai ya uungu wa Isa kwa sababu aliumbwa kutokana na mama bila ya baba ni madai miongoni mwa madai batili zaidi. Na hii ndiyo haki ambayo haina shaka yoyote ndani yake, kama alivyosema Isa juu ya nafsi yake. “Sikuwaambia lolote isipokuwa yale uliyoniamrisha, kwamba muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi.” Na ulikuja ujumbe wa Wakristo kutoka Najran kwa Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - hali ya kuwa wameshikilia vigumu batili yao baada ya Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – kuwasimamishia hoja kwamba Isa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake walipodai uungu wake. Basi hali ikamfikia yeye na wao kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwamrisha alaaniane nao. Kwani, haki ilikwisha wadhihirikia, lakini ukaidi na ushabiki mpofu vikawazuia na hilo. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akawaita kwenye kulaaniana, kwamba yeye aje mwenyewe na wake zake na watoto wake. Nao waje pamoja na wake zao na watoto wao, kisha wamwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba aiteremshe adhabu yake na laana yake juu ya waongo. Basi wakashauriana je wamwitikie katika hilo? Kwa hivyo, maoni yao yakakubaliana kwamba wasimwitikie, kwa sababu walijua kwamba hakika yeye ni Nabii wa Mwenyezi Mungu, na kwamba wakilaaniana, wataangamia wao na watoto wao na wake zao. Basi wakafanya suluhu na yeye, na wakamlipa kodi, na wakamwomba kwamba wafanye amani na makubaliano naye, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. – Na wala hakuwatia katika ugumu, kwa sababu lengo la kubainisha haki lilikwisha patikana, na kubainisha ukaidi wao walipoazimia kukataa kulaaniana. Na hilo linathibitisha kuwa walikuwa madhalimu. Ndiyo maana Mola Mtukufu akasema, "Hakika, hii ndiyo hadithi ya kweli" Yani ambayo haina shaka yoyote ndani yake. "Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu." Ambaye alikishinda nguvu kwa uwezo wake na nguvu zake kila kinachopatikana, wakazi wa ardhi na mbingu wakamnyenyekea. Na pamoja na hayo, yeye ni "Mwenye hekima" ambaye anaviweka vitu mahali pake, na anaviteremsha katika daraja zavyo.
: 64 #
{قُلْ يَاأَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ (64)}.
64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote. Wala tusifanyane waungu sisi kwa sisi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi kwa hakika ni Waislamu.
#
{64} هذه الآية الكريمة كان النبي - صلى الله عليه وسلم - يكتب بها إلى ملوك أهل الكتاب. وكان يقرأ أحياناً في الركعة الأولى من سنة الفجر {قولوا آمنا بالله}؛ الآية؛ ويقرأ بها في الركعة الآخرة من سنة الصبح لاشتمالها على الدعوة إلى دين واحد، قد اتفقت عليه الأنبياء والمرسلون، واحتوت على توحيد الإلهية المبني على عبادة الله وحده لا شريك له، وأن يعتقد أن البشر وجميع الخلق كلهم في طور البشرية لا يستحق منهم أحد شيئاً من خصائص الربوبية ولا من نعوت الإلهية، فإن انقاد أهل الكتاب وغيرهم إلى هذا فقد اهتدوا و {إن تولوا فقولوا اشهدوا بأنا مسلمون}؛ كقوله تعالى: {قل يا أيها الكافرون ... }؛ إلى آخرها.
{64} Aya hii tukufu alikuwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akiwaandikia wafalme wa Watu wa Kitabu. Na alikuwa akisoma saa zingine katika rakaa ya kwanza ya Sunna ya Alfajiri. “Semeni: Tumemuamini Mwenyezi Mungu” hadi mwisho wa Aya. Na anaisoma katika rakaa ya mwisho ya sunna ya asubuhi kwa sababu inajumuisha mwito katika dini moja waliyokubaliana juu yake Manabii na Mitume. Na imejumuisha Tauhidi ya uungu iliyojengwa juu ya kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika. Na kwamba aamini kuwa wanadamu na viumbe vyote viko katika daraja la ubinadamu, na hakuna hata mmoja wao anayestahiki chochote katika sifa maalumu za umola, wala katika sifa za kiungu. Na wakifuata Watu wa Kitabu na wengineo hayo, basi watakuwa wameongoka. Na “wakigeuka, basi semeni: Shuhudieni kwamba sisi kwa hakika ni Waislamu.” Kama kauli yake Mola Mtukufu, “Sema: enyi makafiri...” hadi mwisho wake.
: 65 - 68 #
{يَاأَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنْزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنْجِيلُ إِلَّا مِنْ بَعْدِهِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (65) هَاأَنْتُمْ هَؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُمْ بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُمْ بِهِ عِلْمٌ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ (66) مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَكِنْ كَانَ حَنِيفًا مُسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ (67) إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ (68)}.
65. Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili havikuteremshwa isipokuwa baada yake? Kwani hamtumii akili? 66. Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyoyajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyoyajua? Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui. 67. Ibrahim hakuwa Muyahudi wala Mkristo. Lakini alikuwa mnyoofu, Muislamu, na wala hakuwa katika washirikina. 68. Hakika, watu wanaomstahiki zaidi Ibrahim ni wale waliomfuata yeye, na Nabii huyu, na wale walioamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini.
#
{65 - 68} كانت الأديان كلها اليهود والنصارى والمشركون وكذلك المسلمون كلهم يدعون أنهم على ملة إبراهيم، فأخبر الله تعالى أن أولى الناس به محمد - صلى الله عليه وسلم - وأتباعه وأتباع الخليل قبل محمد - صلى الله عليه وسلم -، وأما اليهود والنصارى والمشركون فإبراهيم بريء منهم ومن ولايتهم لأن دينه الحنيفية السمحة التي فيها الإيمان بجميع الرسل وجميع الكتب، وهذه خصيصة المسلمين، وأما دعوى اليهود والنصارى أنهم على ملة إبراهيم فقد علم أن اليهودية والنصرانية التي هم يدعون أنهم عليها لم تؤسس إلا بعد الخليل، فكيف يحاجون في هذا الأمر الذي يعلم به كذبهم وافتراؤهم، فهب أنهم حاجوا فيما لهم به علم فكيف يحاجون في هذه الحالة، فهذا قبل أن ينظر ما احتوى عليه قولهم من البطلان يعلم فساد دعواهم، وفي هذه الآية دليل على أنه لا يحل للإنسان أن يقول أو يجادل فيما لا علم له به. وقوله: {والله ولي المؤمنين}؛ فكلما قوي إيمان العبد تولاه الله بلطفه، ويسره لليسرى وجنبه العسرى.
{65 - 68} Dini zote Mayahudi, Wakristo, na washirikina na vile vile Waislamu walikuwa wote wakidai kuwa wao wako katika mila ya Ibrahim. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba watu wanaomstahiki zaidi ni Muhammad, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na wafuasi wake, na wafuasi wake Al-Khalil kabla ya Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na ama Mayahudi, Wakristo na washirikina, yeye Ibrahim yuko mbali na wao, na yuko mbali na kuwafanya marafiki. Kwa sababu, dini yake ni ile iliyonyooka vyema, ambayo imo kuwaamini Mitume wote na vitabu vyote. Na hii ndiyo sifa ya kipekee kwa Waislamu. Na ama madai ya Mayahudi na Wakristo kwamba wanafuata mila ya Ibrahim, basi ilikwisha julikana kuwa Uyahudi na Ukristo ambao wanadai kuwa wao wako juu yake, haukuanzishwa isipokuwa baada ya Al-Khalil. Basi vipi wanabishana juu ya jambo hili ambalo kwalo unajulikana uongo wao na uzushi wao. Acha tuseme walibishana katika yale wanayoyajua, basi wanajadiliana vipi katika hali hii? Hili kabla ya kuangalia kile ambacho kauli yao inajumuisha, unajulikana ubatili wa madai yao. Na katika Aya hii kuna ushahidi kwamba hairuhusiwi kwa mtu kusema au kubishana katika yale asiyoyajua. Na kauli yake, “Na Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi wa Waumini” kila imani ya mja inapokuwa na nguvu. Mwenyezi Mungu anakuwa ndiye mlinzi wake kwa Upole wake, na anamrahisishia yawe mepesi, na anamwepusha magumu.
: 69 - 74 #
{وَدَّتْ طَائِفَةٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ (69) يَاأَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَأَنْتُمْ تَشْهَدُونَ (70) يَاأَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ (71) وَقَالَتْ طَائِفَةٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنْزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (72) وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَنْ تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَى هُدَى اللَّهِ أَنْ يُؤْتَى أَحَدٌ مِثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِنْدَ رَبِّكُمْ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ (73) يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ (74)}.
69. Kilipenda kikundi katika Watu wa Kitabu lau kuwa wangewapoteza. Lakini hawapotezi isipokuwa nafsi zao, nao wenyewe hawatambui. 70. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnazikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia? 71. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnaivisha haki uongo, na mnaificha haki ilhali mnajua? 72. Na kilisema kikundi kimoja katika Watu wa Kitabu: Yaaminini yale waliyoteremshiwa wale walioamini mwanzo wa mchana, na yakufuruni mwisho wake; huenda wakarejea. 73. Wala msimuamini isipokuwa yule anayeifuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa mliopewa nyinyi au wawahoji mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa hizo amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua. 74. Yeye humchagua kumpa rehema zake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.
#
{69 - 74} هذا من منة الله على هذه الأمة حيث أخبرهم بمكر أعدائهم من أهل الكتاب وأنهم من حرصهم على إضلال المؤمنين ينوعون المكرات الخبيثة فقالت طائفة منهم: {آمنوا بالذي أنزل على الذين آمنوا وجه النهار}؛ أي: أوله وارجعوا عن دينهم آخر النهار فإنهم إذا رأوكم راجعين وهم يعتقدون فيكم العلم استرابوا بدينهم وقالوا لولا أنهم رأوا فيه ما لا يعجبهم ولا يوافق الكتب السابقة لم يرجعوا، هذا مكرهم والله تعالى هو الذي يهدي من يشاء وهو الذي بيده الفضل يختص به من يشاء، فخصكم يا هذه الأمة بما لم يخص به غيركم، ولم يدر هؤلاء الماكرون أن دين الله حق إذا وصلت حقيقته إلى القلوب لم يزدد صاحبه على طول المدى إلا إيماناً ويقيناً، ولم تزده الشبه إلا تمسكاً بدينه وحمداً لله وثناء عليه حيث منَّ به عليه. وقولهم: {أن يؤتى أحد مثل ما أوتيتم أو يحاجوكم عند ربكم}؛ يعني أن الذي حملهم على هذه الأعمال المنكرة الحسد والبغي وخشية الاحتجاج عليهم، كما قال تعالى: {ود كثير من أهل الكتاب لو يردونكم من بعد إيمانكم كفاراً حسداً من عند أنفسهم من بعد ما تبين لهم الحق}؛ الآية.
{69 - 74} Haya ni katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya umma huu, kwa kuwa aliwajulisha vitimbi vya maadui zao katika Watu wa Kitabu. Na kwamba kwa sababu ya uchu wao wa kuwapoteza Waumini, wanatumia vitimbi mbalimbali viovu. Basi lilisema kundi moja miongoni mwao. “Yaaminini yale yaliyoteremshwa juu ya wale walioamini mwanzo wa mchana” na muiache dini yao mwisho wa siku. Kwa sababu, wakikuona mkiiacha na ilhali wanaitakidi kwamba nyinyi mna elimu, basi watakuwa na shaka na dini yao na watasema. “Lau kuwa si kwamba waliona ndani yake yale wasiyoyapenda na wala hayakukubaliani na vitabu vilivyotangulia, basi hawangeiacha. Hivi ndivyo vitimbi vyao. Na Mwenyezi Mungu ndiye ambaye mkononi mwake kuna fadhila, anampa hizo amtakaye. Naye amewateua enyi ummah huu kwa kile ambacho hakuwateua kwacho wengineo. Na watu hawa wenye vitimbi hawakutambua kuwa Dini ya Mwenyezi Mungu ni ya haki, uhakika wake ukifika katika nyoyo, mwenyewe hatazidi muda huo wote isipokuwa imani na yakini. Na fikira potovu hazitamzidishia isipokuwa kukamata kwa nguvu dini yake na kumhimidi na kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sababu alimneemesha. Na kauli yao, “kuwa apewe mtu mfano wa mliopewa nyinyi au wawahoji mbele ya Mola wenu Mlezi.” Inamaanisha kwamba kile kilichofanya kutenda matendo haya yaliyotajwa ni husuda, na udhalimu, na woga wa hoja kufanywa dhidi yao kwayo. Kama vile yeye Mtukufu alivyosema, “Wengi katika Watu wa Kitabu wanatamani lau kuwa wangewafanya kuwa makafiri baada ya kuamini kwenu. Kwa sababu ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya haki kuwapambanukia.” Hadi mwisho wa Aya.
: 75 - 76 #
{وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِنْ تَأْمَنْهُ بِقِنْطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُمْ مَنْ إِنْ تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ (75) بَلَى مَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ وَاتَّقَى فَإِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ (76)}.
75. Na miongoni mwa Watu wa Kitabu yupo ambaye ukimpa amana ya mrundo wa mali, atakurudishia. Na miongoni mwao yupo ambaye ukimpa amana ya dinari moja, hakurudishii isipokuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa walisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasiojua kusoma na kuandika. Na wanasema uongo juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua. 76. Sivyo hivyo! Bali mwenye kuitimiza ahadi yake na akawa mchamungu, basi hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamungu.
#
{75} يخبر تعالى عن أهل الكتاب أن منهم طائفة أمناء بحيث لو أمنته على قناطير من النقود وهي المال الكثير يؤده إليك، ومنهم طائفة خونة يخونك في أقل القليل، ومع هذه الخيانة الشنيعة فإنهم يتأولون بالأعذار الباطلة فيقولون: {ليس علينا في الأميين سبيل}؛ أي: ليس علينا جناح إذا خناهم واستبحنا أموالهم، لأنهم لا حرمة لهم، قال تعالى: {ويقولون على الله الكذب وهم يعلمون}؛ أن عليهم أشد الحرج، فجمعوا بين الخيانة وبين احتقار العرب وبين الكذب على الله، وهم يعلمون ذلك ليسوا كمن فعل ذلك جهلاً وضلالاً.
{75} Mwenyezi Mungu anajulisha kuhusu Watu wa Kitabu kwamba miongoni mwao lipo kundi la watu waaminifu kiasi kwamba, ukiwakabidhi amana ya Qintar, yani rundo la mali nyingi, atakurudisha kwako. Na miongoni mwao kuna kundi la wahaini wanaokufanyia hiana hata katika kitu kidogo sana. Na pamoja na hiana hii mbaya, wao wanatumia visingizio vya uongo na wanasema, “Hatuna ubaya wowote juu yetu kwa hawa wasiojua kusoma na kuandika.” Yani hakuna ubaya wowote juu yetu tukiwafanyia hiana na kuzihalalisha mali zao. Kwa kuwa wao hawana uharamu wowote. Mola Mtukufu akasema, “Na wanasema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua,” kwamba kuna ubaya mkubwa juu yao. Kwa hivyo, wakachanganya kati ya uhaini na kuwadharau Waarabu, na kati ya kusema uwongo kwa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua hilo kwamba, wao si kama mwenye kulifanya hilo kwa kutojua na upotovu.
#
{76} ثم قال تعالى: {بلى}؛ أي: ليس الأمر كما قالوا. {من أوفى بعهده واتقى}؛ أي: قام بحقوق الله وحقوق خلقه فإن هذا هو المتقي والله يحبه، أي: ومن كان بخلاف ذلك فلم يف بعهده وعقوده التي بينه وبين الخلق ولا قام بتقوى الله، فإن الله يمقته، وسيجازيه على ذلك أعظم النكال.
{76} Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Sivyo hivyo!” Yani jambo hili si kama walivyosema. “Mwenye kuitimiza ahadi yake na akawa mchamungu.” Yani alitimiza haki za Mwenyezi Mungu na haki za viumbe vyake, kwani huyu ndiye anayemcha Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anampenda. Yani na yule ambaye ni kinyume na hilo, na hakutimiza ahadi yake na mikataba yake ambayo iko baina yake na viumbe. Na wala hakumcha Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu anamchukia, na atamlipa kwa hayo adhabu kubwa kabisa.
: 77 #
{إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّهُ وَلَا يَنْظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (77)}.
77. Hakika, wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawatakuwa na fungu lolote katika Akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao, wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao wana adhabu chungu.
#
{77} أي: إن الذين يشترون الدنيا بالدين فيختارون الحطام القليل من الدنيا ويتوسلون إليها بالأيمان الكاذبة والعهود المنكوثة فهؤلاء {لا يكلمهم الله ولا ينظر إليهم يوم القيامة ولا يزكيهم ولهم عذاب أليم}؛ أي: قد حق عليهم سخط الله ووجب عليهم عقابه، وحرموا ثوابه، ومنعوا من التزكية، وهي التطهير. بل يردون القيامة متلوثون بالجرائم، متدنسون بالذنوب العظائم.
{77} Yani hakika wale wanaonunua dunia kwa Dini, kwa hivyo wakachagua uharibifu mdogo wa kidunia na wakaufikia kwa viapo vya uwongo na ahadi zenye kuvunjwa, basi hao, “Mwenyezi Mungu hatasema nao, wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao wana adhabu chungu”. Yani imewafikia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na ikawajibika adhabu yake juu yao, na wakanyimwa thawabu zake, na wakazuiliwa utakaso, yani kusafishwa. Bali watakuja kwenye Kiyama huku wamechafuliwa na makosa na madhambi makubwa.
: 78 #
{وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُمْ بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ (78)}.
78. Na hakika wapo miongoni mwao kundi lipindualo ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Nao husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wanasema uongo juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua.
#
{78} أي: وإن من أهل الكتاب فريقاً محرفون لكتاب الله {يلوون ألسنتهم بالكتاب لتحسبوه من الكتاب}؛ وهذا يشمل التحريف اللفظي والتحريف المعنوي، ثم هم مع هذا التحريف الشنيع، يوهمون أنه من الكتاب وهم كذبة في ذلك ويصرحون بالكذب على الله، وهم يعلمون حالهم وسوء مغبتهم.
{78} Yani, hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu lipo kundi linalokipotoa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, “linalopindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni.” Na hili linajumuisha upotoshaji wa matamshi, na upotoshaji wa maana. Kisha wao pamoja na upotoshaji huu mbaya, wanafanya idhaniwe kwamba hayo yametoka katika Kitabu ilhali wao ni waongo katika hilo. Na wanasema uongo waziwazi juu ya Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanajua hali zao na ubaya wa matokeo yao.
: 79 - 80 #
{مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَنْ يُؤْتِيَهُ اللَّهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِي مِنْ دُونِ اللَّهِ وَلَكِنْ كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنْتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنْتُمْ تَدْرُسُونَ (79) وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَنْ تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا أَيَأْمُرُكُمْ بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنْتُمْ مُسْلِمُونَ (80)}.
79. Haikumfailia mtu yeyote kwamba Mwenyezi Mungu ampe Kitabu na hekima na Unabii, kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma. 80. Wala hatawaamrisha kwamba muwafanye Malaika na Manabii kuwa ni miungu. Je, atawaamrisha ukafiri baada ya nyinyi kuwa Waislamu?
#
{79 - 80} أي: يمتنع ويستحيل كل الاستحالة لبشر منَّ الله عليه بالوحي والكتاب والنبوة وأعطاه الحكم الشرعي، أن يأمر الناس بعبادته ولا بعبادة النبيين والملائكة واتخاذهم أرباباً، لأن هذا هو الكفر، فكيف وقد بعث بالإسلام المنافي للكفر من كل وجه فكيف يأمر بضده، هذا من الممتنع لأن حاله وما هو عليه وما منَّ الله به عليه من الفضائل والخصائص تقتضي العبودية الكاملة والخضوع التام لله الواحد القهار، وهذا جواب لوفد نجران حين تمادى بهم الغرور ووصلت بهم الحال والكبر أن قالوا أتأمرنا يا محمد أن نعبدك حين أمرهم بعبادة الله وطاعته، فبين الباري انتفاء ما قالوا وأن كلامهم وكلام أمثالهم في هذا ظاهر البطلان.
{79 - 80} Yani, inakatalika na haiwezekani kabisa kwa mwanadamu ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha na Wahyi, na Kitabu, na Unabii. Na akampa hukumu ya kisheria, kwamba awaamrishe watu wamwabudu, wala kuwaabudu Manabii na Malaika na kuwafanya kuwa ni miungu. Kwa sababu huku ndiko kukufuru. Basi itakuwa vipi na hali ni kwamba alitumwa na Uislamu unaopingana na ukafiri katika kila namna? Basi vipi ataamrisha kinyume chake? Hili ni katika yasiyowezekana, kwa sababu hali yake, na namna alivyo, na yale ambayo Mwenyezi Mungu alimneemesha kwayo katika fadhila na sifa maalumu, yanahitaji utumwa kamili na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi. Na hili ni jibu kwa ujumbe wa Najran pale kudanganyika kwao kuliendelea na hali yao na kiburi vikawafikisha kusema: Je, unatuamrisha Ewe Muhammad kwamba tukuabudu? Wakati alipowaamrisha kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumtii. Basi Al-Bari (Muumba mwanzilishi) akabainisha yenye kukanusha yale waliyoyasema, na kwamba maneno yao na maneno ya mfano wao katika hili ni ya batili iliyo dhahiri.
: 81 - 82 #
{وَإِذْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُمْ مِنْ كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُصَدِّقٌ لِمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنْصُرُنَّهُ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَى ذَلِكُمْ إِصْرِي قَالُوا أَقْرَرْنَا قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُمْ مِنَ الشَّاهِدِينَ (81) فَمَنْ تَوَلَّى بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ (82)}.
81. Na pale Mwenyezi Mungu alipochukua ahadi za Manabii: Nikishawapa Kitabu na hekima, kisha akawajia Mtume mwenye kusadikisha yale mliyo nayo, basi hakika mtamuamini na mtamsaidia. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika wanaoshuhudia. 82. Kwa hivyo, mwenye kugeuka baada ya haya, basi hao ndio wapotovu.
#
{81 - 82} هذا إخبار منه تعالى أنه أخذ عهد النبيين وميثاقهم كلِّهم بسبب ما أعطاهم، ومنَّ به عليهم من الكتاب والحكمة المقتضي للقيام التام بحق الله وتوفيته، أنه إن جاءهم رسول مصدق لما معهم بُعِثَ بما بعثوا به من التوحيد والحق والقسط والأصول التي اتفقت عليها الشرائع أنهم يؤمنون به وينصرونه، فأقروا على ذلك، واعترفوا، والتزموا، وأشهدهم، وشهد عليهم، وتوعد من خالف هذا الميثاق. وهذا أمر عام بين الأنبياء أن جميعهم طريقهم واحد وأن دعوة كل واحد منهم قد اتفقوا وتعاقدوا عليها، وعموم ذلك أنه أخذ على جميعهم الميثاق بالإيمان والنصرة لمحمد - صلى الله عليه وسلم -، فمن ادعى أنه من أتباعهم فهذا دينهم الذي أخذه الله عليهم وأقروا به واعترفوا، فمن تولى عن اتباع محمد ممن يزعم أنه من أتباعهم فإنه فاسق خارج عن طاعة الله مكذب للرسول الذي يزعم أنه من أتباعه مخالف لطريقه، وفي هذا إقامة الحجة والبرهان على كل من لم يؤمن بمحمد - صلى الله عليه وسلم - من أهل الكتب والأديان، وأنه لا يمكنهم الإيمان برسلهم الذين يزعمون أنهم أتباعهم حتى يؤمنوا بإمامهم وخاتمهم - صلى الله عليه وسلم -.
{81 - 82} Huu ni ujumbe utokao kwake Yeye Mtukufu ya kwamba alichukua ahadi ya Manabii na maagano yao wote kwa sababu ya yale aliyowapa. Na akawaneemesha kwa Kitabu na hekima inayolazimu kutekeleza kitimilifu haki ya Mwenyezi Mungu na kuikamilisha; kwamba ikiwa watawajia na Mtume anayesadikisha yale yaliyo pamoja nao. Yani wakitumwa na yale waliyotumwa nayo ya Tauhidi, na haki, na uadilifu na misingi ambayo sheria zote zilikubaliana juu yake kwamba watamwamini na watamnusuru. Kwa hivyo, wakakiri hilo, na wakakubali, na wakaahidi, na akawashuhudisha, na akashuhudia hilo juu yao, na akamwahidi adhabu mwenye kuhalifu agano hili. Na hili ni jambo la jumla miongoni mwa Manabii, kwamba wote wana njia moja, na kwamba wito wa kila mmoja wao umeafikiana na wakaingia katika mkataba juu yake. Na jumla ya hayo ni kuwa alichukua juu yao wote ahadi ya kumwamini Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na kumnusuru. Kwa hivyo, mwenye kuadai kuwa yeye ni miongoni mwa wafuasi wao, basi hii ndiyo dini yao aliyoichukua Mwenyezi Mungu juu yao, na wakaikiri na wakaikubali. Hivyo basi, mwenye kugeuka na asimfuate Muhammad miongoni mwa wale wanaodai kuwa ni miongoni mwa wafuasi wao, basi yeye kwa hakika ni ameruka mipaka; aliyetoka katika utiifu wa Mwenyezi Mungu. Mwenye kumkadhibisha Mtume ambaye yeye anadai kuwa ni miongoni mwa wafuasi wake, naye anahalifu njia yake. Na katika hili kuna kusimamisha hoja na ushahidi dhidi ya kila asiyemwamini Muhammad, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - miongoni mwa Watu wa Vitabu na dini. Na kwamba hawawezi kuwaamini Mitume wao ambao wanadai kuwa ni wafuasi wao, mpaka wamuamini imamu wao na wa mwisho wao rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
: 83 - 85 #
{أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ (83) قُلْ آمَنَّا بِاللَّهِ وَمَا أُنْزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنْزِلَ عَلَى إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَى وَعِيسَى وَالنَّبِيُّونَ مِنْ رَبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ (84) وَمَنْ يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَنْ يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ (85)}.
83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, ilhali kila kilicho katika mbingu na katika ardhi kimejisalimisha kwake kwa kumtii Yeye kwa kupenda na kwa kutopenda, na kwake Yeye watarejeshwa? 84. Sema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu, na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wana wake, na yale aliyopewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatutofautishi yeyote baina yao, na sisi ni wenye kujisalimisha kwake. 85. Na mwenye kutafuta dini isiyokuwa Uislamu, basi haitakubaliwa kwake. Naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa waliohasirika.
#
{83 - 85} قد تقدم في سورة البقرة أن هذه الأصول التي هي أصول الإيمان التي أمر الله بها هذه الأمة قد اتفقت عليها الكتب والرسل، وأنها هي الغرض الموجه لكل أحد وأنها هي الدين والإسلام الحقيقي، وأن من ابتغى غيرها فعمله مردود وليس له دين يعول عليه، فمن زهد عنه ورغب عنه فأين يذهب؟ إلى عبادة الأشجار والأحجار والنيران، أو إلى اتخاذ الأحبار والرهبان والصلبان، أو إلى التعطيل لرب العالمين، أو إلى الأديان الباطلة التي هي من وحي الشياطين؟ وهؤلاء كلهم في الآخرة من الخاسرين.
{83 - 85} Imeshatangulia katika Surat Al-Baqara kwamba misingi hii ambayo ndiyo misingi ya imani ambayo Mwenyezi Mungu aliuamrisha umma huu. Vimeafikiana juu yake na Vitabu na Mitume, na kwamba hiyo ndiyo lengo linalomwongoza kila mtu. Na kwamba hiyo ndiyo Dini na Uislamu wa kihakika, na kwamba mwenye kutaka isiyokuwa hiyo, basi matendo yake yatakataliwa naye hana dini atakayoirudia. Kwa hivyo, mwenye kutokuwa na hamu nayo, na asiitake, basi atakwenda wapi? Atakwenda katika kuiabudu miti, na mawe, na mioto, au kujichukulia marabi, na watawa, na misalaba. Au katika kumpinga Mola Mlezi wa walimwengu wote, au katika dini za batili ambazo ni katika ufunuo wa mashetani? Na hao wote katika Akhera ni miongoni mwa waliohasirika.
: 86 - 91 #
{كَيْفَ يَهْدِي اللَّهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ (86) أُولَئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ (87) خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنْظَرُونَ (88) إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (89) إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَنْ تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ (90) إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَنْ يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِمْ مِلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَى بِهِ أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُمْ مِنْ نَاصِرِينَ (91)}.
86. Vipi Mwenyezi Mungu atawaongoa kaumu waliokufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawajia hoja zilizo wazi? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu ya madhaalimu. 87. Hao malipo yao ni kuwa ipo juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote. 88. Humo watadumu. Hawatapunguziwa adhabu, wala hawatapewa nafasi. 89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea. Basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 90. Hakika, wale waliokufuru baada ya kuamini kwao, kisha wakazidi kukufuru, haitakubaliwa toba yao, na hao ndio waliopotea. 91. Hakika, wale waliokufuru, na wakafa hali ya kuwa ni makafiri, haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeliitoa. Hao wana adhabu chungu, wala hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru.
#
{86 - 88} يعني أنه يبعد كل البعد أن يهدي الله قوماً عرفوا الإيمان، ودخلوا فيه وشهدوا أن الرسول حق ثم ارتدوا على أعقابهم ناكصين ناكثين، لأنهم عرفوا الحق فرفضوه، ولأن من هذه الحالة وصفه فإن الله يعاقبه بالانتكاس وانقلاب القلب جزاء له إذ عرف الحق فتركه، والباطل فآثره فولاه الله ما تولى لنفسه، فهؤلاء {عليهم لعنة الله والملائكة والناس أجمعين}؛ خالدين في اللعنة والعذاب {لا يخفف عنهم العذاب ولا هم ينظرون}؛ إذا جاءهم أمر الله، لأن الله عمرهم ما يتذكر فيه ما تذكر، وجاءهم النذير.
{86 - 88} Maana yake ni kuwa ni mbali sana kwamba Mwenyezi Mungu awaongoe kaumu walioijua imani, na wakaingia ndani yake. Na wakashuhudia kuwa Mtume ni wa haki, kisha wakarudi nyuma kwa visigino vyao, wakipinga na kuvunja ahadi. Kwa sababu, waliijua haki na wakaikataa. Na kwa sababu yule ambaye hii ndiyo hali yake na sifa yake, basi Mwenyezi Mungu humuadhibu kwa kumrudisha nyuma, na kuugeuza moyo wake kama malipo kwake alipoijua haki na akaiacha, na akaujua uongo na akaupendelea, basi Mwenyezi Mungu akamwacha atawaliwe na kile alichokifanya kuitawala nafsi yake. Na hao, “juu yao kuna laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.” Watadumu katika laana na adhabu, “hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa nafasi,” itakapowajia amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa, Mwenyezi Mungu ndiye aliyewapa umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka, na akawajia mwonyaji.
#
{89 - 91} ثم إنه تعالى استثنى من هذا الوعيد التائبين من كفرهم وذنوبهم المصلحين لعيوبهم فإن الله يغفر لهم ما قدموه ويعفو عنهم ما أسلفوه، ولكن من كفر وأصر على كفره، ولم يزدد إلا كفراً حتى مات على كفره، فهؤلاء هم الضالون عن طريق الهدى السالكون لطريق الشقاء، وقد استحقوا بهذا العذاب الأليم، فليس لهم ناصر من عذاب الله ولو بذلوا ملء الأرض ذهباً ليفتدوا به لم ينفعهم شيئاً. فعياذًا بالله من الكفر وفروعه.
{89 - 91} Kisha Yeye Mwenyezi Mungu akaondoa kutoka katika onyo hili wale wanaotubia ukafiri wao na dhambi zao, wanaosahihisha makosa yao. Kwani Mwenyezi Mungu atawafutia yale waliyotanguliza, na atawasamehe yale waliyoyatanguliza. Lakini mwenye kukufuru na akaendelea kuwa katika ukafiri wake, na hakuzidisha isipokuwa ukafiri mpaka akafia katika ukafiri wake. Basi hao ndio waliopotea njia ya uwongofu, walioshika njia ya upotovu. Na walistahiki adhabu chungu kwa hili. Kwa hivyo, hawana wa kuwanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, hata lau kuwa wangetoa dhahabu ya kujaza dunia nzima ili wajifidie kwayo, haingewafaa kitu. Basi tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ukafiri na matawi yake.
: 92 #
{لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ (92)}.
92. Kamwe hamtaufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachokitoa, basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.
#
{92} يعني {لن تنالوا} وتدركوا {البر}، الذي هو اسم جامع للخيرات وهو: الطريق الموصل إلى الجنة {حتى تنفقوا مما تحبون} من أطيب أموالكم وأزكاها، فإن النفقة من الطيب المحبوب للنفوس من أكبر الأدلة على سماحة النفس واتصافها بمكارم الأخلاق ورحمتها ورقتها، ومن أدل الدلائل على محبة الله وتقديم محبته على محبة الأموال التي جبلت النفوس على قوة التعلق بها، فمن آثر محبة الله على محبة نفسه فقد بلغ الذروة العليا من الكمال وكذلك من أنفق الطيبات وأحسن إلى عباد الله أحسن الله إليه ووفقه أعمالاً وأخلاقاً لا تحصل بدون هذه الحالة. وأيضاً فمن قام بهذه النفقة على هذا الوجه كان قيامه ببقية الأعمال الصالحة والأخلاق الفاضلة من طريق الأولى والأحرى، ومع أن النفقة من الطيبات هي أكمل الحالات فمهما أنفق العبد من نفقة قليلة أو كثيرة من طيب أو غيره {فإن الله به عليم}، وسيجزي كل منفق بحسب عمله، سيجزيه في الدنيا بالخلف العاجل وفي الآخرة بالنعيم الآجل.
{92} Maana yake ni “kamwe hamtaufikia” na kupata “wema” ambao ni jina linalokusanya heri mbalimbali. Nao ni njia inayofikisha katika Pepo “mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda,” kutoka katika vilivyo vizuri zaidi katika mali zenu na visafi vyake zaidi. Kwani, kutoa katika vile vilivyo vizuri, vinavyopendwa na nafsi ni katika dalili kubwa juu ya ukarimu wa nafsi na kusifika kwake kwa tabia za ukarimu na rehema yake na upole wake. Na ni katika dalili zinazoashiria zaidi mapenzi kwa Mwenyezi Mungu, na kutanguliza upendo wake juu ya upendo wa mali ambazo nafsi zimeumbiwa nguvu ya kufungamana nazo. Kwa hivyo, mwenye kuupendelea upendo wa Mwenyezi Mungu juu ya kujipenda mwenyewe, basi amefikia kilele cha juu kabisa katika ukamilifu. Na vile vile anayetoa vitu vizuri na akawatendea wema waja wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamtendea wema na atamwezesha kufanya matendo na maadili ambayo hayawezi kupatikana bila ya hali hii. Na vile vile, mwenye kutekeleza kutoa huku kwa njia hii, basi kutakuwa kutekeleza kwake matendo mengineyo mema na maadili bora ni katika njia ya uwezekano mkubwa na ifaayo zaidi. Na pamoja na kwamba kutoa katika vile vilivyo vizuri ndiyo hali iliyo kamili zaidi, basi chochote atakachotoa mja, sawa kiwe kichache au kingi, kutoka katika vilivyo vizuri au vinginevyo. "Basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua,” na atamlipa kila mtoaji kulingana na matendo yake. Atamlipa katika dunia kwa kumrudishia kwa haraka, na katika Akhera kwa neema ya baadaye.
: 93 - 94 #
{كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَى نَفْسِهِ مِنْ قَبْلِ أَنْ تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (93) فَمَنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ (94)}.
93. Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipokuwa kile alichojiharamishia Israili mwenyewe kabla ya kuteremshwa Taurati. Sema: Ileteni Taurati, na muisome ikiwa nyinyi ni wakweli. 94. Na mwenye kumzulia uongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao ndio madhalimu.
#
{93 - 94} من جملة الأمور التي قدح فيها اليهود بنبوة عيسى ومحمد - صلى الله عليه وسلم - أنهم زعموا أن النسخ باطل، وأنه لا يمكن أن يأتي نبي يخالف النبي الذي قبله. فكذبهم الله بأمر يعرفونه، فإنهم يعترفون بأن جميع الطعام قبل نزول التوراة كان حلالاً لبني إسرائيل إلا أشياء يسيرة، حرمها إسرائيل وهو يعقوب عليه السلام على نفسه ومنعها إياه لمرض أصابه، ثم إن التوراة فيها من التحريمات التي نسخت ما كان حلاًّ قبل ذلك شيء كثير. قل لهم إن أنكروا ذلك {فأتوا بالتوراة فاتلوها إن كنتم صادقين}؛ بزعمكم أنه لا نسخ ولا تحليل ولا تحريم. وهذا من أبلغ الحجج أن يحتج على الإنسان بأمر يقوله ويعترف به ولا ينكره، فإن انقاد للحق فهو الواجب، وإن أبى ولم ينقد بعد هذا البيان تبين كذبه وافتراؤه وظلمه وبطلان ما هو عليه، وهو الواقع من اليهود.
{93-94} Miongoni mwa mambo ambayo Mayahudi waliukashifu unabii wa Isa na Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – ni kwamba walidai kuwa kufuta (kitu katika sheria) ni batili. Na kwamba haiwezekani kwamba aje nabii akitofautiana na nabii aliyekuwa kabla yake. Basi Mwenyezi Mungu akawakadhibisha kwa jambo wanalolijua. Kwani, wanakiri kwamba chakula chote kabla ya kuteremka kwa Taurati kilikuwa halali kwa Wana wa Israili. Isipokuwa vitu vichache tu ambavyo Israili ambaye ni Yaqub amani iwe juu yake alijiharamishia mwenyewe, na akaizuia hivyo kwa sababu ya ugonjwa uliompata. Zaidi ya hayo ni kwamba Taurati ndani yake kuna maharamisho mengi ambayo yalifuta yale yaliyokuwa halali kabla ya hapo. Waambie ikiwa watakanusha hayo, “Basi ileteni Taurati na muisome ikiwa nyinyi ni wakweli,” katika madai yenu kuwa hakuna ufutaji, wala uhalalishaji, wala uharamishaji. Na hili ni katika hoja zenye nguvu sana kuwa itumiwe hoja dhidi ya mtu kwa jambo analolisema na kulikiri na wala halikanushi. Kwa hivyo, ikiwa ataifuata haki, basi hilo ndilo la wajibu. Na akikataa na asifuate baada ya kubainisha huku, utabainika uongo wake, na uzushi wake, na dhuluma yake, na ubatili wa yale aliyo juu yake, ni hii ndiyo hali ya hakika ya Mayahudi.
: 95 #
{قُلْ صَدَقَ اللَّهُ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ (95)}.
95. Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
#
{95} أي: قل صدق الله في كل ما قاله ومن أصدق من الله قيلاً وحديثاً؟ وقد بين في هذه الآيات من الأدلة على صحة رسالة محمد - صلى الله عليه وسلم - وبراهين دعوته وبطلان ما عليه المنحرفون من أهل الكتاب الذين كذبوا رسوله وردوا دعوته، فقد صدق الله في ذلك وأقنع عباده على ذلك ببراهين وحجج تتصدع لها الجبال وتخضع لها الرجال، فتعين عند ذلك على الناس كلهم اتباع ملة إبراهيم من توحيد الله وحده لا شريك له، وتصديق كل رسول أرسله الله، وكل كتاب أنزله والإعراض عن الأديان الباطلة المنحرفة، فإن إبراهيم كان معرضاً عن كل ما يخالف التوحيد متبرئاً من الشرك وأهله.
{95} Yani Sema: Mwenyezi Mungu ni Mkweli katika yote aliyoyasema. Na ni nani mkweli zaidi kumliko Mwenyezi Mungu kwa kauli na usemi? Katika aya hizi, alibainisha ushahidi wa usahihi wa ujumbe wa Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. – Na ushahidi wa wito wake na ubatili wa yale waliyoko wapotofu katika Watu wa Kitabu ambao walimkadhibisha Mtume wake, na wakaukataa wito wake. Na Mwenyezi Mungu alisema kweli katika hilo, na akawashawishi waja wake katika hilo kwa ushahidi na hoja ambazo milima inaweza kupasuka kwazo, na wanaume wananyenyekea kwazo. Kwa hivyo, ikabaki tu hapo juu ya watu wote kwamba wafuate mila ya Ibrahim ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu peke yake asiyekuwa na mshirika. Na kumsadiki kila Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu, na kila Kitabu alichokiteremsha. Na wazipe mgongo kila dini za batili, zilizo potofu. Kwa sababu, Ibrahim alikuwa amekipa mgongo kila kitu chenye kupingana na Tauhidi, akijieka mbali na ushirikina na watu wake.
: 96 - 97 #
{إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِلْعَالَمِينَ (96) فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَقَامُ إِبْرَاهِيمَ وَمَنْ دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا وَمَنْ كَفَرَ فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ (97)}.
96. Hakika, Nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ibada ni ile iliyo Bakka, iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu. 97. Ndani yake kuna Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim. Na mwenye kuingia humo, anakuwa na amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezaye njia ya kuiendea. Na atakayekufuru, basi hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.
#
{96 - 97} يخبر تعالى بعظمة بيته الحرام، وأنه أول البيوت التي وضعها الله في الأرض لعبادته وإقامة ذكره، وأن فيه من البركات وأنواع الهدايات وتنوع المصالح والمنافع للعالمين شيء كثير وفضل غزير، وأن فيه آيات بينات تُذَكِّر بمقامات إبراهيم الخليل وتنقلاته في الحج ومن بعده تذكر بمقامات سيد الرسل وإمامهم، وفيه الأمن الذي من دخله كان آمناً قدراً مؤمناً شرعاً وديناً. فلما احتوى على هذه الأمور التي هذه مجملاتها وتكثر تفصيلاتها، أوجب الله حجّه على المكلفين المستطيعين إليه سبيلاً، وهو الذي يقدر على الوصول إليه بأي مركوب يناسبه وزاد يتزوده، ولهذا أتى بهذا اللفظ الذي يمكنه تطبيقه على جميع المركوبات الحادثة والتي ستحدث، وهذا من آيات القرآن حيث كانت أحكامه صالحة لكل زمان وكل حال ولا يمكن الصلاح التام بدونها. فمن أذعن لذلك وقام به فهو من المهتدين المؤمنين، ومن كفر فلم يلتزم حج بيته فهو خارج عن الدين، {ومن كفر فإن الله غني عن العالمين}.
{96-97} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ukuu wa Nyumba yake Takatifu, na kwamba ndiyo ya kwanza katika nyumba zote ambazo, Mwenyezi Mungu aliziweka katika dunia kwa ajili ya kumuabudu Yeye na kusimamisha utajo wake. Na kwamba ndani yake kuna baraka nyingi na aina mbalimbali za uongofu, na aina mbalimbali za masilahi na manufaa mengi na fadhila tele kwa walimwengu. Na kwamba ndani yake kuna ishara zilizo wazi zinazokumbusha vituo alivyosimama Ibrahim Al-Khalil, na harakati zake katika Hija. Na baada yake zinakumbusha kuhusu vituo vya bwana wa Mitume na imamu wao. Na ndani yake kuna amani ambayo mwenye kuingia humo, anakuwa na amani kwa majaaliwa ya Mwenyezi Mungu na anapewa amani kisheria na kidini. Na ilipojumuisha mambo haya ambayo haya ndiyo jumla yake, na maelezo yake ya kina ni mengi, Mwenyezi Mungu akawajibisha kufanya Hija hapo juu ya wale wanaojukumika (Mukallafun), wenye uwezo wa kupata njia ya kuiendea. Naye (mwenye uwezo) ni yule anayeweza kuifikia kwa chombo chochote kinachomfaa na ana masurufu anayoyabeba. Na kwa sababu ya hili, alitumia neno hili ambalo linaweza kutumika kwa vipando vyote vilivyotokea na vitakavyotokea. Na hili ni katika ishara za Qur-ani, kwani hukumu zake ni nzuri kwa kila wakati na kila hali, na kutengenea kukamilifu hakuwezekani bila ya hukumu hizo. Kwa hivyo, mwenye kulitii hilo na akalitekeleza, basi huyo ni miongoni mwa Waumini walioongoka. Na mwenye kukufuru na asitekeleze kuihiji Nyumba yake, basi yeye yuko nje ya Dini. “Na mwenye kukufuru, basi hakika Mwenyezi Mungu hawahitaji walimwengu.”
: 98 - 99 #
{قُلْ يَاأَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَاللَّهُ شَهِيدٌ عَلَى مَا تَعْمَلُونَ (98) قُلْ يَاأَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنْتُمْ شُهَدَاءُ وَمَا اللَّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ (99)}.
98. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnazikufuru ishara za Mwenyezi Mungu, na ilhali Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayoyatenda? 99. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu aliyeamini mkiitakia ipotoke, ilhali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyatenda.
#
{98 - 99} لمّا أقام فيما تقدم الحجج على أهل الكتاب مع أنهم قبل ذلك يعرفون النبي - صلى الله عليه وسلم -، كما يعرفون أبناءهم، وَبَّخَ المعاندين منهم بكفرهم بآيات الله وصدهم الخلق عن سبيل الله لأن عوامهم تبع لعلمائهم، والله تعالى يعلم أحوالهم وسيجازيهم على ذلك أتمَّ الجزاء وأوفاه.
{98-99} Alipozisimamisha hoja katika yaliyotangulia juu ya Watu wa Kitabu, pamoja na kwamba kabla ya hapo walikuwa wanamjua Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kama wanavyowajua watoto wao. Aliwakemea wakaidi miongoni mwao kwa kukufuru kwao Ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwazuilia kwao viumbe Njia ya Mwenyezi Mungu; kwa sababu watu wao wa kawaida wanawafuata wanachuoni wao. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anazijua hali zao, na atawalipa kwa hayo, malipo kamili na timilifu zaidi.
: 100 - 101 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تُطِيعُوا فَرِيقًا مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ يَرُدُّوكُمْ بَعْدَ إِيمَانِكُمْ كَافِرِينَ (100) وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنْتُمْ تُتْلَى عَلَيْكُمْ آيَاتُ اللَّهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُ وَمَنْ يَعْتَصِمْ بِاللَّهِ فَقَدْ هُدِيَ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (101)}.
100. Enyi mlioamini! Mkilitii kundi katika wale waliopewa Kitabu, watawarudisha baada ya kuamini kwenu muwe makafiri. 101. Na vipi mkufuru hali ya kuwa nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu, na Mtume wake yuko miongoni mwenu? Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu, basi huyo hakika ameongolewa kwenye Njia iliyonyooka.
#
{100 - 101} لمّا أقام الحجج على أهل الكتاب ووبَّخهم بكفرهم وعنادهم، حذر عباده المؤمنين عن الاغترار بهم، وبين لهم أن هذا الفريق منهم حريصون على إضراركم وردكم إلى الكفر بعد الإيمان، ولكن ولله الحمد أنتم يا معشر المؤمنين، بعدما منَّ الله عليكم بالدين ورأيتم آياته ومحاسنه ومناقبه وفضائله، وفيكم رسول الله الذي أرشدكم إلى جميع مصالحكم، واعتصمتم بالله وبحبله الذي هو دينه يستحيل أن يردوكم عن دينكم، لأن الدين الذي بني على هذه الأصولِ والدعائمِ الثابتة الأساس، المشرقة الأنوار تنجذب إليه الأفئدة، ويأخذ بمجامع القلوب، ويوصل العباد إلى أجل غاية وأفضل مطلوب. {ومن يعتصم بالله}؛ أي: يتوكل عليه ويحتمي بحماه {فقد هدي إلى صراط مستقيم}؛ وهذا فيه الحث على الاعتصام به وأنه السبيل إلى السلامة والهداية.
{100-101} Aliposimamisha hoja juu ya Watu wa Kitabu, na akawakemea kwa kukufuru kwao na ukaidi wao, akawaonya waja wake Waumini dhidi ya kudanganywa nao. Na akawabainishia kuwa kundi hili miongoni mwao wana utu wa kuwadhuru nyinyi na kuwarudisha katika ukafiri baada ya imani. Lakini – na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu - enyi kundi la Waumini. Baada ya Mwenyezi Mungu kuwaneemesha kwa Dini, na mkaziona ishara zake, na mema yake, na sifa zake nzuri, na fadhila zake. Na miongoni mwenu yuko Mtume wa Mwenyezi Mungu ambaye aliwaongoza kwenye masilahi yenu yote. Na mkashikamana na Mwenyezi Mungu na kamba yake ambayo ni Dini yake, itakuwa haiwezekani kwamba wawarudishe muiache Dini yenu. Kwa sababu, dini ambayo imejengwa juu ya misingi hii na nguzo zenye msingi imara, zenye nuru zinazong’aa, ambayo nyoyo zinavutika kwayo. Na inakusanya pamoja pande zote za nyoyo, na inawafikisha waja kwenye lengo tukufu zaidi, na bora zaidi kinachotafutwa. “Na mwenye kushikamana na Mwenyezi Mungu,” yani mwenye kumtegemea na anajilinda kwa ulinzi wake. “Basi huyo hakika ameongolewa kwenye Njia iliyonyooka”. Na hili ndani yake kuna himizo juu ya kushikamana nayo, na kwamba ndiyo njia ya kufikisha kwenye usalama na uwongofu.
: 102 - 105 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ (102) وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَى شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ فَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ (103) وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (104) وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَأُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ (105)}.
102. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu haki ya kumcha, wala msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu. 103. Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msitengane. Na ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu: mlipokuwa maadui nyinyi kwa nyinyi, naye akaziunganisha nyoyo zenu; na kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa kwenye ukingo wa shimo la Moto, naye akawaokoa kutokana nalo. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Ishara zake ili mpate kuongoka. 104. Na uwepo umma miongoni mwenu wanaoilingania heri, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu. Na hao ndio waliofaulu. 105. Wala msiwe kama wale waliotengana na wakahitilafiana baada ya kufikiwa na hoja zilizo wazi. Na hao ndio wana adhabu kubwa.
#
{102 - 105} هذه الآيات فيها حث الله عباده المؤمنين أن يقوموا بشكر نعمه العظيمة بأن يتقوه حق تقواه، وأن يقوموا بطاعته وترك معصيته مخلصين له بذلك، وأن يقيموا دينهم ويستمسكوا بحبله الذي أوصله إليهم، وجعله السبب بينهم وبينه وهو دينه وكتابه، والاجتماع على ذلك وعدم التفرق، وأن يستديموا ذلك إلى الممات. وذكرهم ما هم عليه قبل هذه النعمة وهو أنهم كانوا أعداء متفرقين فجمعهم بهذا الدين وألّف بين قلوبهم وجعلهم إخواناً، وكانوا على شفا حفرة من النار فأنقذهم من الشقاء، ونهج بهم طريق السعادة؛ لذلك بين {الله لكم آياته لعلكم تهتدون}؛ إلى شكر الله والتمسك بحبله. وأمرهم بتتميم هذه الحالة، والسبب الأقوى الذي يتمكنون به من إقامة دينهم بأن يتصدى منهم طائفة يحصل فيها الكفاية {يدعون إلى الخير}؛ وهو الدين: أصوله وفروعه وشرائعه {ويأمرون بالمعروف}؛ وهو ما عرف حسنه شرعاً وعقلاً {وينهون عن المنكر}؛ وهو ما عرف قبحه شرعاً وعقلاً {وأولئك هم المفلحون}؛ المدركون لكل مطلوب الناجون من كل مرهوب، ويدخل في هذه الطائفة أهل العلم والتعليم والمتصدون للخطابة ووعظ الناس عموماً وخصوصاً والمحتسبون، الذين يقومون بإلزام الناس بإقامة الصلوات وإيتاء الزكاة والقيام بشرائع الدين، وينهونهم عن المنكرات. فكل من دعا الناس إلى خير على وجه العموم أو على وجه الخصوص، أو قام بنصيحة عامة أو خاصة فإنه داخل في هذه الآية الكريمة. ثم نهاهم عن سلوك مسلك المتفرقين الذين جاءهم الدين والبينات الموجب لقيامهم به واجتماعهم، فتفرقوا واختلفوا وصاروا شيعاً، ولم يصدر ذلك عن جهل وضلال وإنما صدر عن علم وقصد سيئ وبغي من بعضهم على بعض، ولهذا قال: {وأولئك لهم عذاب عظيم}؛ ثم بين متى يكون هذا العذاب العظيم ويمسهم هذا العذاب الأليم فقال:
{105-102} Katika aya hizi, kuna himizo la Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini kwamba washukuru neema zake kubwa kwa kumcha haki ya kumcha Na kwamba wamtii na waache kumuasi huku wakimfanyia Yeye tu hayo. Na kwamba waisimamishe Dini yao na washikamane kwa Kamba yake ambayo aliwafikishia, na akaifanya kuwa ndio njia baina yao na Yeye; nayo ni Dini yake na Kitabu chake. Na kuungana juu ya hilo, na kutotengana, na kwamba wadumishe hilo mpaka kufa. Na akawakumbusha yale waliyokuwa juu yake kabla ya neema hii. Nayo ni kwamba walikuwa maadui waliotengana, kwa hivyo akawaunganisha kwa hili. Dini. Na akaziunganisha nyoyo zao, na akawafanya kuwa ndugu. Na walikuwa kwenye ukingo wa shimo la Moto, na akawaokoa kutokana na taabu, na akawaongoza kwenye njia ya furaha. Ndiyo maana akabainisha, "Mwenyezi Mungu Aya zake kwenu ili mpate kuongoka" kwenye kumshukuru Mwenyezi Mungu na kushikamana kwa Kamba yake. Na akawaamrisha kuikamilisha hali hii. Na sababu yenye nguvu zaidi ambayo kwayo wanaweza kuisimamisha Dini yao ni kwamba kundi miongoni mwao lenye kutosheleza lisimamie, "kulingania kwenye heri". Nayo ni Dini: misingi yake, na matawi yake, na sheria zake, "na wanaamrisha mema". Nayo ni yale yanayojulikana uzuri wake kisheria na kiakili. "Na wanakataza maovu". Nayo ni yale yanyojulikana ubaya wake kisheria na kiakili. "Na hao ndio waliofaulu," waliopata kila linalotafutwa, waliookoka kutokana na kila lenye kuogopwa. Na wanaingia katika kundi hili wanachuoni, na waalimu, na wenye kusimamia kutoa khutba na kuwapa watu mawaidha kiujumla na hasa. Na wale wanaojitolea kulingania kwa Mwenyezi Mungu ambao wanawalazimisha watu kusimamisha swala, na kutoa Zaka, na kutekeleza sheria za dini, na wanawakataza maovu. Kwa hivyo, kila mwenye kuwalingania watu kwenye heri kwa namna ya ujumla au kwa namna maalumu, au kutoa nasiha ya ujumla au maalumu, basi yeye anaingia katika aya hii tukufu. Kisha akawakataza kufuata njia ya waliotengana ambao walijiwa na Dini na hoja zilizo wazi zenye kuwalazimu kusimama kwazo na kuungana kwao. Lakini wakatengana na wakahitalifiana na wakawa makundi makundi. Na hilo halikutokea kwa kutojua na upotovu. Bali lilitokea pamoja na kuwa na elimu, na nia mbaya, na dhuluma kutoka kwa baadhi yao dhidi ya wenzao. Na kwa sababu ya hayo, akasema, "Na hao wana adhabu kubwa." Kisha akabainisha ni lini itatokea adhabu hii kubwa, na lini itawagusa adhabu hii chungu, akasema:
: 106 - 107 #
{يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُمْ بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنْتُمْ تَكْفُرُونَ (106) وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (107)}.
106. Siku zitakapokuwa nyuso nyeupe, na nyuso nyingine zikawa nyeusi. Basi, ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi ionjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru. 107. Na ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watadumu.
#
{106 - 107} يخبر تعالى بتفاوت الخلق يوم القيامة في السعادة والشقاوة، وأنه تبيض وجوه أهل السعادة، الذين آمنوا بالله، وصدقوا رسله وامتثلوا أمره واجتنبوا نهيه، وأن الله تعالى يدخلهم الجنات ويفيض عليهم أنواع الكرامات وهم فيها خالدون، وتسود وجوه أهل الشقاوة الذين كذبوا رسله وعصوا أمره وفرقوا دينهم شيعاً وأنهم يوبخون فيقال: {أكفرتم بعد إيمانكم}؛ فكيف اخترتم الكفر على الإيمان {فذوقوا العذاب بما كنتم تكفرون}.
{106-107} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu kutofautiana kwa viumbe Siku ya Kiyama katika furaha na taabu (huzuni). Na kwamba nyuso za watu wa furaha zitakuwa nyeupe. Wale waliomwamini Mwenyezi Mungu, na wakawasadiki Mitume wake, na wakatekeleza amri yake, na wakaepukana na makatazo yake. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaingiza Peponi, na awamiminie aina mbalimbali za utukufu, nao watadumu humo. Na nyuso za watu wenye taabu zitakuwa nyeusi. Wale waliowakadhibisha Mitume wake, na wakaasi amri yake, na wakaigawanya dini yao makundi makundi. Na kwamba watakemewa wakiambiwa. "Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu." Basi vipi mliuchagua ukafiri badala ya Imani? "Basi ionjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru."
: 108 - 109 #
{تِلْكَ آيَاتُ اللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ وَمَا اللَّهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِلْعَالَمِينَ (108) وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ (109)}.
108. Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunazokusomea kwa haki. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu walimwengu. 109. Na ni cha Mwenyezi Mungu kilicho katika mbingu na kilicho katika ardhi, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko mambo yote yatarejeshwa.
#
{108} يثني تعالى على ما قصه على نبيه من آياته التي حصل بها الفرقان بين الحق والباطل وبين أولياء الله وأعدائه، وما أعده لهؤلاء من الثواب وللآخرين من العقاب، وأن ذلك مقتضى فضله وعدله وحكمته، وأنه لم يظلم عباده ولم ينقصهم من أعمالهم أو يعذب أحداً بغير ذنبه أو يحمل عليه وزر غيره. ولما ذكر أن له الأمر والشرع ذكر أن له تمام الملك والتصرف والسلطان فقال:
{108} Yeye Mtukufu anayasifu yale aliyomsimulia Nabii wake katika Ishara zake ambazo kwazo kilitokea kipambanuzi baina ya haki na batili, na baina ya marafiki wa Mwenyezi Mungu na maadui wake. Na yale aliyowaandalia hawa miongoni mwa thawabu, na wale wengine ya adhabu. Na kwamba hayo ndiyo matakwa ya fadhila yake, na uadilifu wake, na hekima yake. Na kwamba hakuwadhulumu waja wake. Na wala hakuwapunguzia katika matendo yao au kumuadhibu yeyote kwa dhambi isiyokuwa yake, au kumbebesha mzigo wa mwengineye. Na alipotaja kuwa ni yake amri na sheria, akataja kuwa ni wake ufalme kamili, na kuendesha mambo, na mamlaka. Kwa hivyo, akasema:
#
{109} {ولله ما في السموات وما في الأرض وإلى الله ترجع الأمور}؛ فيجازي المحسنين بإحسانهم والمسيئين بعصيانهم، وكثيراً ما يذكر الله أحكامه الثلاثة مجتمعة يبين لعباده أنه الحاكم المطلق فله الأحكام القدرية والأحكام الشرعية والأحكام الجزائية، فهو الحاكم بين عباده في الدنيا والآخرة، ومن سواه من المخلوقات محكوم عليها ليس لها من الأمر شيء.
{109} "Na ni vya Mwenyezi Mungu vile vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, na kwa Mwenyezi Mungu ndiko mambo yote yatarejeshwa." Kisha atawalipa watendao mema kwa wema wao, na watendao maovu kwa uasi wao. Na mara nyingi Mwenyezi Mungu huzitaja hukumu zake tatu pamoja, ili awabainishie waja wake kwamba Yeye ndiye Hakimu wa pekee. Ni zake hukumu za kimajaaliwa, na hukumu za kisheria, na hukumu za malipo. Yeye ndiye anayehukumu baina ya waja wake katika dunia na Akhera. Na asiyekuwa Yeye miongoni mwa viumbe vinavyohukumiwa, havina chochote katika jambo hili.
: 110 - 111 #
{كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَهُمْ مِنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ (110) لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ (111)}.
110. Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliotolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu waliamini, ingelikuwa bora kwao. Miongoni mwao wako Waumini, lakini wengi wao ni wapotovu. 111. Maadui hawatawadhuru isipokuwa kwa maudhi tu. Na wakipigana nanyi, watawapa migongo, kisha hawatanusuriwa.
#
{110 - 111} هذا تفضيل من الله لهذه الأمة بهذه الأسباب، التي تميزوا بها وفاقوا بها سائر الأمم، وأنهم خير الناس للناس نصحاً ومحبة للخير ودعوة وتعليماً وإرشاداً وأمراً بالمعروف ونهياً عن المنكر وجمعاً بين تكميل الخلق والسعي في منافعهم بحسب الإمكان، وبين تكميل النفس بالإيمان بالله والقيام بحقوق الإيمان، وأن أهل الكتاب لو آمنوا بمثل ما آمنتم به لاهتدوا وكان خيراً لهم ولكن لم يؤمن منهم إلا القليل، وأما الكثير فهم فاسقون خارجون عن طاعة الله وطاعة رسوله محاربون للمؤمنين ساعون في إضرارهم بكل مقدورهم، ومع ذلك فلن يضروا المؤمنين إلا أذى باللسان، وإلا فلو قاتلوهم لولوا الأدبار ثم لا ينصرون. وقد وقع ما أخبر الله به، فإنهم لما قاتلوا المسلمين ولوا الأدبار ونصر الله المسلمين عليهم.
{110-111} Huku ni kuboresha kutokako kwa Mwenyezi Mungu kwa umma huu kwa sababu hizi ambazo walipambanuka kwazo na wakazipita umma zingine zote. Na kwamba wao ndio watu bora zaidi kwa watu katika kushauri, na kupenda heri, na kulingania, na kufundisha, na kuongoza, na kuamrisha mema na kukataza maovu. Na kujumuisha baina ya kukamilika maumbile na kujitahidi katika manufaa yao kulingana na inavyowezekana. Na baina ya kukamilika nafsi kwa kumwamini Mwenyezi Mungu na kutekeleza haki za imani. Na kwamba ikiwa Watu wa Kitabu wangeliamini kama mlivyoamini, basi wangeliongoka na ingelikuwa bora kwao. Lakini hawakuamini miongoni mwao isipokuwa wachache tu. Na ama wengi, wao ni mafasiki waliotoka katika kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake, wanawapiga vita Waumini wakijitahidi kuwadhuru kwa uwezo wao wote. Na pamoja na hayo, hawatawadhuru Waumini isipokuwa maudhi kwa ulimi tu. Vinginevyo, lau kuwa wangepigana nao, basi wangeigeuza migongo yao kisha wasingenusuriwa. Na yale aliyosema Mwenyezi Mungu tayari yalikwisha tokea. Kwa sababu, walipopigana vita na Waislamu, waliigeuza migongo yao, na Mwenyezi Mungu akawanusuru Waislamu dhidi yao.
: 112 #
{ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللَّهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِنَ اللَّهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنْبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ذَلِكَ بِمَا عَصَوْا وَكَانُوا يَعْتَدُونَ (112)}.
112. Umepigwa udhalilifu juu yao popote wanapokutwa, isipokuwa kwa kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na walirudi na ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na unyonge umepigwa juu yao. Hayo ni kwa sababu walikuwa wakizikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakiwaua Manabii bila ya haki. Hayo ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka.
#
{112} هذا إخبار من الله تعالى أن اليهود ضربت عليهم الذلة فهم خائفون أينما ثقفوا، ولا يؤمنهم شيء إلا معاهدة وسبب يأمنون به يرضخون لأحكام الإسلام ويعترفون بالجزية أو بحبلٍ {من الناس}؛ أي: إذا كانوا تحت ولاية غيرهم ونظارتهم كما شوهد حالهم سابقاً ولاحقاً، فإنهم لم يتمكنوا في الوقت الأخير من الملك المؤقت في فلسطين إلا بنصر الدول الكبرى وتمهيدهم لهم كل سبب {وباؤوا بغضب من الله}؛ أي: قد غضب الله عليهم وعاقبهم بالذلة والمسكنة، والسبب في ذلك كفرهم بآيات الله وقتلهم الأنبياء {بغير حق}، أي: ليس ذلك عن جهل وإنما هو بغي وعناد، تلك العقوبات المتنوعة عليهم {بما عصوا وكانوا يعتدون}؛ فالله تعالى لم يظلمهم ويعاقبهم بغير ذنب، وإنما الذي أجراه عليهم بسبب بغيهم وعدوانهم وكفرهم وتكذيبهم للرسل وجناياتهم الفظيعة.
{112} Huku ni kujulisha kutokako kwa Yeye Mtukufu kwamba udhalilifu ulipigwa juu ya Mayahudi, kwa hivyo wao huwa na hofu popote wanapokutwa. Na wala hakuna chochote kinachowapa amani isipokuwa mkataba na sababu wanayopata amani kwayo. Wanazitii hukumu za Uislamu na wanakubali kulipa Jizya (Kodi), au kwa kamba "ya watu." Yani wanapokuwa chini ya ulinzi wa wengine na uangalizi wao, kama hali yao ilivyoonekana hapo awali na baadaye. Kwa maana, hawakuweza katika wakati wa mwisho kuwa na umiliki wa muda huko Palestina isipokuwa kwa usaidizi wa nchi kubwa kubwa na kuwaandalia kwao kila sababu (njia). "Na wakarudi na ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu." Yani Mwenyezi Mungu aliwakasirikia na akawaadhibu kwa udhalilifu na unyonge. Na sababu ya hayo ni kuzikufuru kwao Ishara za Mwenyezi Mungu na kuwaua kwao Manabii "bila ya haki." Yani, hilo si kwa kutojua, bali ni kwa ukaidi na dhuluma. Hizo adhabu mbalimbali kwao, "ni kwa sababu waliasi na walikuwa wakiruka mipaka." Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwadhulumu na kuwaadhibu bila ya dhambi. Bali yale aliyowapitishia ni kwa sababu ya dhuluma yao, na kuruka kwao mipaka, na ukafiri wao, na kukadhibisha kwao Mitume, na makosa yao mabaya mno.
: 113 - 115 #
{لَيْسُوا سَوَاءً مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ (113) يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ (114) وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَنْ يُكْفَرُوهُ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ (115)}.
113. Wote hao si wamoja. Miongoni mwa Watu wa Kitabu kuna watu waliosimama barabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, nao wanasujudu. 114. Wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu, na wanakimbilia katika mambo ya heri. Na hao wako miongoni mwa walio wema. 115. Na heri yoyote wanayoifanya, basi hawatanyimwa malipo yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamungu.
#
{113 - 114} لما ذكر الله المنحرفين من أهل الكتاب بيَّن حالة المستقيمين منهم وأن منهم أمة مقيمون لأصول الدين وفروعه {يؤمنون بالله واليوم الآخر ويأمرون بالمعروف}؛ وهو الخير كله، وينهون عن المنكر وهو جميع الشر، كما قال تعالى: {ومن قوم موسى أمة يهدون بالحق وبه يعدلون}؛ و {يسارعون في الخيرات}؛ والمسارعة إلى الخيرات قدر زائد على مجرد فعلها، فهو وصف لهم بفعل الخيرات والمبادرة إليها وتكميلها بكل ما تتم به من واجب ومستحب.
{113-114} Mwenyezi Mungu alipowataja waliopotoka miongoni mwa Watu wa Kitabu, akabainisha hali ya wale walionyooka miongoni mwao. Na kwamba miongoni mwao kuna umma wanaosimamisha misingi ya dini na matawi yake. "Wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema." Nayo ni heri yote. Na wanakataza maovu. Nayo ni shari zote, kama alivyosema Yeye Mtukufu: "Na katika kaumu ya Musa kuna kundi la watu wanaoongoa kwa haki, na kwayo wanafanya uadilifu." Na "wanakimbilia katika mambo ya heri." Na kukimbilia kutenda heri ni kiwango kilicho zaidi ya kuzifanya tu. Na huko ni kuwaeleza kwa kufanya matendo mema na kuharakisha kuyatenda na kuyakamilisha kwa yale yote yanayotimia kwayo ya wajibu na ya kupendekezwa.
#
{115} ثم بين تعالى أن كل ما فعلوه من خير قليل أو كثير فإن الله تعالى سيقبله حيث كان صادراً عن إيمان وإخلاص، {فلن يكفروه}؛ يعني لن ينكر ما عملوه ولن يهدر {والله عليم بالمتقين}؛ وهم الذين قاموا بالخيرات وتركوا المحرمات لقصد رضا الله وطلب ثوابه.
{115} Kisha Yeye Mtukufu akabainisha kwamba chochote wanachokifanya cha heri, kidogo au kingi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atakikubali. Kwa kuwa kilitokana na imani na ikhlasi, "hawatanyimwa malipo yake." Yani, hatakataa waliyoyafanya, wala hatayapoteza. "Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamungu." Nao ndio wale waliotenda mema na wakaacha yaliyoharamishwa kwa nia ya kumridhisha Mwenyezi Mungu na kutafuta thawabu zake.
: 116 - 117 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَنْ تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا وَأُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (116) مَثَلُ مَا يُنْفِقُونَ فِي هَذِهِ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّهُ وَلَكِنْ أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ (117)}.
116. Hakika, wale waliokufuru, hazitawafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenza wa Moto. Wao watadumu humo. 117. Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai wao wa duniani ni kama upepo ambao ndani yake ipo baridi ya barafu, ukalipiga shamba la kaumu waliozidhulumu nafsi zao, basi ukaliharibu. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali wao wenyewe wanazidhulumu nafsi zao.
#
{116 - 117} بين تعالى أن الكفار الذين كفروا بآيات الله وكذبوا رسله أنه لا ينقذهم من عذاب الله منقذ ولا ينفعهم نافع ولا يشفع لهم عند الله شافع، وأن أموالهم وأولادهم التي كانوا يعدونها للشدائد والمكاره لا تفيدهم شيئاً وأن نفقاتهم التي أنفقوها في الدنيا لنصر باطلهم ستضمحل، وأن مثلها {كمثل}؛ حرث أصابته {ريح}؛ شديدة {فيها صر}؛ أي: برد شديد أو نار محرقة فأهلكت ذلك الحرث وذلك بظلمهم فلم يظلمهم الله، ويعاقبهم بغير ذنب، وإنما ظلموا أنفسهم. وهذه كقوله تعالى: {إن الذين كفروا ينفقون أموالهم ليصدوا عن سبيل الله فسينفقونها ثم تكون عليهم حسرة ثم يغلبون}.
{116-117} Yeye Mtukufu alibainisha kuwa makafiri waliozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu na wakawakadhibisha Mitume wake, kwamba hakuna mwokozi yeyote atakayewaokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Wala hakuna mwenye kunufaisha atakayewanufaisha, wala hakuna mwombezi yeyote atakayewaombea mbele ya Mwenyezi Mungu. Na kwamba mali zao na watoto wao walivyokuwa wakiviandalia shida na machukizo, havitawanufaisha chochote. Na kwamba kutoa kwao walikotoa hapa duniani kwa ajili ya kunusuru batili yao, kutatoweka. Na mfano wao, "ni kama mfano" wa mazao yaliyopigwa na "upepo" mkali "wenye barafu ndani yake." Yani, barafu nyingi au moto uunguzao. Kwa hivyo, ukaharibu mazao hayo, na hayo ni kwa sababu ya dhuluma yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, na akawaadhibu bila ya dhambi. Bali walizidhulumu nafsi zao. Na haya ni kama kauli yake Mtukufu, "Hakika, wale waliokufuru wanatoa mali zao ili waizuilie Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto makubwa kwao, kisha watashindwa."
: 118 - 120 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِنْ دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَاعَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ (118) هَاأَنْتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (119) إِنْ تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِنْ تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا وَإِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا إِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ (120)}.
118. Enyi mlioamini! Msiwafanye wandani wenu kuwa watu wasiokuwa katika nyinyi. Hawataacha kuwafikishia lolote la kuwadhuru. Wanapenda mngepata taabu. Imekwisha dhihirika chuki yao kutoka katika midomo yao. Na yanayofichwa na vifua vyao ni makubwazaidi. Tumekwisha wabainishia Ishara ikiwa nyinyi mnatumia akili. 119. Nyinyi ndio hawa mnawapenda watu hao, wala wao hawawapendi. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapokutana nanyi husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wanawaumia vidole kwa chuki. Sema: Kufeni na chuki yenu! Hakika, Mwenyezi Mungu anayajua yale yaliyo katika vifua. 120. Ikiwagusa heri, inawawia vibaya. Na ikiwapata shari, wanaifurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkamcha Mwenyezi Mungu, havitawadhuru kitu vitimbi vyao. Hakika, Mwenyezi Mungu ameyazunguka yote wayatendayo.
#
{118 - 119} هذا تحذير من الله لعباده عن ولاية الكفار واتخاذهم بطانة أو خصيصة وأصدقاء، يسرون إليهم ويفضون لهم بأسرار المؤمنين، فوضح لعباده المؤمنين الأمور الموجبة للبراءة من اتخاذهم بطانة، بأنهم {لا يألونكم خبالاً} أي حريصون غير مقصرين في إيصال الضرر بكم، وقد بدت البغضاء من كلامهم وفلتات ألسنتهم وما تخفيه صدورهم من البغضاء والعداوة {أكبر} مما ظهر لكم من أقوالهم وأفعالهم، فإن كانت لكم فهوم وعقول فقد وضح الله لكم أمرهم، وأيضاً فما الموجب لمحبتهم واتخاذهم أولياء وبطانة، وقد تعلمون منهم الانحراف العظيم في الدين وفي مقابلة إحسانكم؟ فأنتم مستقيمون على أديان الرسل تؤمنون بكل رسول أرسله الله وبكل كتاب أنزله الله وهم يكفرون بأجلّ الكتب وأشرف الرسل، وأنتم تبذلون لهم من الشفقة والمحبة ما لا يكافئونكم على أقل القليل منه، فكيف تحبونهم وهم لا يحبونكم وهم يداهنونكم وينافقونكم، فإذا لقوكم {قالوا آمنا وإذا خلوا} مع بني جنسهم {عضوا عليكم الأنامل} من شدة الغيظ والبغض لكم ولدينكم، قال تعالى: {قل موتوا بغيظكم}؛ أي: سترون من عز الإسلام وذل الكفر ما يسوءكم، وتموتون بغيظكم فلن تدركوا شفاء ذلك بما تقصدون {إن الله عليم بذات الصدور}؛ فلذلك بين لعباده المؤمنين ما تنطوي عليه صدور أعداء الدين من الكفار والمنافقين.
{118-119} Hili ni tahadharisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake juu ya kuwafanya makafiri kuwa wandani, au kuwa watu maalumu na marafiki wanaowafichulia na kuwafikishia siri za Waumini. Kwa hivyo, aliwawekea wazi waja wake Waumini mambo ambayo yanalazimu kujitenga mbali na kuwachukua kama wandani, kwamba "hawataacha kuwafikishia lolote la kuwadhuru." Yani wanakakamia bila ya kuzembea katika kuwadhuru. Na chuki imeshadhihirika kutoka katika maneno yao, na kuteleza kwa ndimi zao. Na yale yanayofichwa na vifua vyao ya chuki na uadui "ni makubwa zaidi," kuliko yale yaliyowadhihirikia katika kauli zao na matendo yao. Basi ikiwa nyinyi mna ufahamu na akili, basi Mwenyezi Mungu ameshawabainishia jambo lao. Na pia nini sababu ya kuwapenda na kuwafanya wasaidizi na wandani, na mnajua vyema kutoka kwao upotofu mkubwa katika Dini na katika kukabiliana na wema wenu? Nyinyi ni wanyoofu kwenye Dini za Mitume. Mnamwamini kila Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu na kila kitabu alichokiteremsha Mwenyezi Mungu. Nao wanakikufuru kitukufu zaidi cha vitabu vyote, na mtukufu zaidi wa Mitume wote. Nanyi mnawafanyia huruma kubwa, na upendo kiwango wasichowalipa kwa kidogo ya vidogo vyote kwa hayo. Basi mnawapenda vipi ilhali wao hawawapendi? Nao wanajilainisha kwenu na wanawafanyia unafiki. Kwa hivyo, wakikutana nanyi, wanasema, "Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao" pamoja walio sawa nao, "wanawaumia vidole vyao;" kwa sababu ya ghadhabu kali juu yenu na kuwachukia nyinyi na dini yenu. Akasema Mtukufu, "Sema: Kufeni katika hasira zenu." Yani, mtaona katika utukufu wa Uislamu na udhalilifu wa ukafiri kitu ambacho kitawachukiza. Na mtakufa katika ghadhabu zenu, na humtafikia uponyaji wa hayo kutoka kwa yale mnayoyakusudia. "Hakika, Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo ndani ya vifua." Ndio maana akawabainishia waja wake Waumini yale yaliyofichwa na vifua vya maadui wa Dini miongoni mwa makafiri na wanafiki.
#
{120} {إن تمسسكم حسنة}؛ عز ونصر وعافية وخير {تسؤهم، وإن تصبكم سيئة}؛ من إدالة العدو أو حصول بعض المصائب الدنيوية {يفرحوا بها}؛ وهذا وصف العدو الشديدة عداوته. لما بين تعالى شدة عداوتهم، وشرح ما هم عليه من الصفات الخبيثة أمر عباده المؤمنين بالصبر ولزوم التقوى، وأنهم إذا قاموا بذلك فلن يضرهم كيد أعدائهم شيئاً، فإن الله محيط بهم وبأعمالهم وبمكائدهم التي يكيدونكم فيها، وقد وعدكم عند القيام بالتقوى أنهم لا يضرونكم شيئاً فلا تشكوا في حصول ذلك.
{120} "Yakiwagusa mazuri" yani, utukufu, na nusura, na usalama, na heri, "yanawawia mabaya. Na mkipatwa na ubaya", kama vile na kurejelewa na maadui au kupatwa na baadhi ya misiba ya kidunia, "wanaufurahia." Haya ni maelezo kuhusu adui mwenye uadui mkubwa. Mola alipobainisha ukali wa uadui wao, na akaeleza waliyo nayo miongoni mwa sifa mbaya, akawaamrisha waja wake Waumini wawe na subira na kushikamana na uchamungu. Na kwamba wakifanya hivyo, vitimbi vya maadui wao havitawadhuru kitu. Kwani, Mwenyezi Mungu amewazunguka wao, na vitendo vyao, na vitimbi vyao ambavyo wanawafanyia. Na aliwaahidi mtakapofanya uchamungu, kwamba hawatawadhuru kwa kitu. Basi msiwe na shaka katika kutokea kwa hilo.
: 121 - 127 #
{وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (121) إِذْ هَمَّتْ طَائِفَتَانِ مِنْكُمْ أَنْ تَفْشَلَا وَاللَّهُ وَلِيُّهُمَا وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ (122) وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّهُ بِبَدْرٍ وَأَنْتُمْ أَذِلَّةٌ فَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (123) إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَنْ يَكْفِيَكُمْ أَنْ يُمِدَّكُمْ رَبُّكُمْ بِثَلَاثَةِ آلَافٍ مِنَ الْمَلَائِكَةِ مُنْزَلِينَ (124) بَلَى إِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُمْ مِنْ فَوْرِهِمْ هَذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُمْ بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ (125) وَمَا جَعَلَهُ اللَّهُ إِلَّا بُشْرَى لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُمْ بِهِ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ (126) لِيَقْطَعَ طَرَفًا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنْقَلِبُوا خَائِبِينَ (127)}.
121. Na pale ulipotoka asubuhi, ukaacha ahali zako ili uwapange Waumini kwenye vituo kwa ajili ya vita. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, mwenye kujua. 122. Makundi mawili miongoni mwenu yalipoingiwa na woga kuwa watashindwa - na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao. Na kwa Mwenyezi Mungu tu, na wategemee Waumini. 123. Na Mwenyezi Mungu alishawanusuru huko Badri hali ya kuwa nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru. 124. Ulipowaambia Waumini: Je, haiwatoshi kwamba Mola wenu Mlezi awasaidie kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa? 125. Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamcha Mungu, na hata maadui wakiwajia mara hii, basi hapo Mola wenu Mlezi atawasaidia kwa Malaika elfu tano wenye alama maalumu. 126. Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya isipokuwa iwe ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua kwa hilo. Na nusura haitoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye hekima. 127. Ili akate sehemu katika wale waliokufuru, au awahizi; wapate kurejea nyuma hali ya kuwa wameambulia patupu.
#
{121} وذلك يوم أحد حين خرج - صلى الله عليه وسلم - بالمسلمين، حين وصل المشركون بجمعهم إلى قريب من أحد، فنزَّلهم - صلى الله عليه وسلم - منازلهم، ورتبهم في مقاعدهم، ونظمهم تنظيماً عجيباً، يدل على كمال رأيه وبراعته الكاملة في علوم السياسة، كما كان كاملاً في كل المقامات، {والله سميع عليم}؛ لا يخفى عليه شيء من أموركم.
{121} Na hilo lilikuwa siku ya Uhud alipotoka yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - pamoja na Waislamu, wakati walipofika washirikina katika mkusanyiko wao karibu na Uhud. Kwa hivyo, akawateremsha katika mashukio yao, na akawaweka taratibu katika vituo vyao. Na akawapanga mpangilio wa ajabu unaoonyesha ukamilifu wa rai yake na ustadi wake kamili katika elimu za kuongoza. Kama vile vile alivyokuwa mkamilifu katika nyadhifa zote. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua." Hakuna kinachofichikana kwake katika mambo yenu.
#
{122} {إذ همت طائفتان منكم أن تفشلا}؛ وهم بنو سلمة وبنو حارثة لكن تولاهما الباري بلطفه ورعايته وتوفيقه، {وعلى الله فليتوكل المؤمنون}؛ فإنهم إذا توكلوا عليه كفاهم وأعانهم وعصمهم من وقوع ما يضرهم في دينهم ودنياهم. وفي هذه الآية ونحوها وجوب التوكل وأنه على حسب إيمان العبد يكون توكله، والتوكل: هو اعتماد العبد على ربه في حصول منافعه ودفع مضاره.
{122} "Wakati makundi mawili miongoni mwenu yalipokaribia kuingiwa na woga wa kushindwa." Nao ni Banu Salama na Banu Haritha, lakini yeye Al-Bari (Muumba mwanzilishi) akawasimamia kwa upole wake, na ulezi wake, na mafanikio yake. "Na kwa Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini." Kwani wakimtegemea Yeye, atawatosheleza, na atawasaidia, na atawalinda kutokana na kutokea kwa yenye kuwadhuru katika mambo ya dini yao na dunia yao. Na katika Aya hii na mfano wake kuna ulazima wa kutegemea. Na kwamba kulingana na imani ya mja ndio kunakuwa kutegemea kwake. Na Tawakkul ni kutegemea mja kwa Mola wake Mlezi ili kupata yenye kumnufaisha na kuzuia yenye kumdhuru.
Na alipotaja hali yao katika Uhud, na msiba uliowapata, aliingiza humo kuwakumbusha nusura yake, na neema yake juu yao siku ya Badr; ili wapate kumshukuru Mola wao Mlezi, na ili hili lilipunguze lile. Akasema:
#
{123} وإذ {نصركم الله ببدر وأنتم أذلة}؛ في عَددكم وعِددكم، فكانوا ثلاثمائة وبضعة عشر في قلة ظهْرٍ ورثاثة سلاح، وأعداؤهم يناهزون الألف في كمال العدة والسلاح {فاتقوا الله لعلكم تشكرون}؛ الذي أنعم عليكم بنصره.
{123} Na "Mwenyezi Mungu alipowanusuru katika Badr, hali ya kuwa nyinyi ni wadhalilifu," katika idadi yenu na maandalizi yenu. Wao walikuwa mia tatu na kumi na, wakiwa na vipando vichache na silaha mbivu. Nao maadui zao walikaribia elfu moja wakiwa katika ukamilifu wa idadi na silaha. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru" yule aliyewaneemesha kwa nusura yake.
#
{124} {إذ تقول} مبشراً {للمؤمنين}؛ مثبتاً لجنانهم: {ألن يكفيكم أن يمدكم ربكم بثلاثة آلاف من الملائكة منزلين}.
{124} "Uliposema" ukiwabashiria Waumini, ukiwaimarisha nyoyo zao, "Je, haitawatosha ikiwa Mola wenu Mlezi awasaidie kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa?"
#
{125} {بلى إن تصبروا وتتقوا ويأتوكم من فورهم هذا}؛ أي: من حملتهم هذه بهذا الوجه. {يمددكم ربكم بخمسة آلاف من الملائكة مسومين}؛ أي: معلمين علامة الشجعان. واختلف الناس هل كان هذا الإمداد حصل فيه من الملائكة مباشرة للقتال، كما قاله بعضهم أو أن ذلك تثبيت من الله لعباده المؤمنين، وإلقاء الرعب في قلوب المشركين كما قاله كثير من المفسرين ويدل عليه قوله:
{125} "Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamcha Mwenyezi Mungu, na hata maadui wakiwajia kwa haraka yao hii" Yani, kwa mshamubulio wao wa namna hii, "basi hapo Mola wenu Mlezi atawasaidia kwa Malaika elfu tano waliotiwa alama maalumu." Yani, waliotiwa alama za ushujaa. Na watu walihitalifiana kuhusu kusaidiwa huku kulikotokea. Je, Malaika walihusika moja kwa moja katika kupigana vita kama walivyosema hivyo baadhi yao? Au hilo lilikuwa kuimarisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini, na kutia hofu katika nyoyo za washirikina kama walivyosema wengi miongoni mwa wafasiri? Na hilo linaashiriwa na kauli yake:
#
{126} {وما جعله الله إلا بشرى لكم ولتطمئن قلوبكم به وما النصر إلا من عند الله العزيز الحكيم}، وفي هذا أن الأسباب لا يعتمد عليها العبد بل يعتمد على الله، وإنما الأسباب وتوفرها فيها طمأنينة للقلوب وثبات على الخير.
{126} "Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya isipokuwa yawe ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua kwayo. Na nusura haitoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Na katika hili kuna kwamba mja asizitegemee sababu tu. Bali anamtegemea Mwenyezi Mungu. Lakini sababu na kupatikana kwake kuna utulivu wa nyoyo ndani yake na uthabiti juu ya heri.
#
{127} {ليقطع طرفا من الذين كفروا أو يكبتهم فينقلبوا خائبين}؛ أي: نصر الله لعباده المؤمنين لا يعدو أن يكون قطعاً لطرف من الكفار، أو ينقلبوا بغيظهم لم ينالوا خيراً كما أرجعهم يوم الخندق بعد ما كانوا قد أتوا على حرد قادرين أرجعهم الله بغيظهم خائبين.
{127} "Ili akate sehemu katika wale waliokufuru, au awahizi ndio wapate kurejea nyuma hali ya kuwa wameambulia patupu." Yani, nusura ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini haipiti kuwa kukata kundi miongoni mwa makafiri. Au warejee na ghadhabu zao bila kupata heri yoyote, kama alivyowarudisha Siku ya Handaki baada ya kwamba walikuwa wamekuja huku wameshikilia azimio hilo wakijiona wenye uwezo. Lakini Mwenyezi Mungu akawarudisha katika ghadhabu yao hali ya kuwa wameambulia patupu.
: 128 #
{لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ (128)}.
128. Wewe huna chochote katika jambo hili. Ama atawakubalia toba au atawaadhibu, kwani wao hakika ni madhaalim.
#
{128} لما أصيب - صلى الله عليه وسلم - يوم أحد وكسرت رباعيته وشج رأسه جعل يقول: «كيف يفلح قوم شجوا وجه نبيهم وكسروا رباعيته »؛ فأنزل الله تعالى هذه الآية، وبيَّن أن الأمر كله لله وأن الرسول - صلى الله عليه وسلم - ليس له من الأمر شيء، لأنه عبد من عبيد الله والجميع تحت عبودية ربهم مدبَّرون لا مدبِّرون، وهؤلاء الذين دعوت عليهم أيها الرسول أو تباعدت فلاحهم وهدايتهم إن شاء الله تاب عليهم ووفقهم للدخول في الإسلام، وقد فعل، فإن أكثر أولئك هداهم الله فأسلموا، وإن شاء الله عذبهم فإنهم ظالمون مستحقون لعقوبات الله وعذابه.
{128} (Mtume) - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipojeruhiwa Siku ya Uhud, na machonge yake manne yakavunjwa, na kichwa chake kikajeruhiwa, akawa anasema. “Vipi watafaulu kaumu waliojeruhi uso wa Nabii wao na wakayavunja machonge yake?” Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha Aya hii, na akabainisha kuwa jambo hili lote ni la Mwenyezi Mungu. Na kwamba Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - hana kitu chochote katika jambo hili. Kwa sababu, yeye ni mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu. Na wote wako chini ya uja wa Mola wao Mlezi, wanaendeshwa, siyo waendeshaji. Na hawa ambao uliwaapiza, ewe Mtume, au ulioona kwamba mafanikio yao na uwongofu wao yako mbali sana, akipenda Mwenyezi Mungu, atakawakubalia toba yao na awawezeshe kuingia katika Uislamu, na alikwisha fanya hivyo. Kwa sababu, wengi wa hao, Mwenyezi Mungu aliwaongoa na wakasilimu. Na Mwenyezi Mungu akipenda atawaadhibu, kwa kuwa wao ni madhalimu na wanastahiki mateso ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake.
: 129 #
{وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ يَغْفِرُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (129)}.
129. Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Yeye humfutia dhambi amtakaye na humwadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
#
{129} يخبر تعالى أنه هو المتصرف في العالم العلوي والسفلي وأنه يتوب على من يشاء فيغفر له ويخذل من يشاء فيعذبه، {والله غفور رحيم} فمن صفته اللازمة كمال المغفرة والرحمة ووجود مقتضياتها في الخلق والأمر يغفر للتائبين ويرحم من قام بالأسباب الموجبة للرحمة، قال تعالى: {وأطيعوا الله والرسول لعلكم تُرحمون}.
{129} Yeye Mtukufu anajulisha kuwa Yeye ndiye mwendeshaji mambo katika ulimwengu wa juu na wa chini. Na kwamba humkubalia toba amtakaye na anamfutia dhambi. Na anaacha kumsaidia amtakaye, na anamwadhibu. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Na katika sifa zake za kudumu ni ukamilifu wa kufuta dhambi na rehema. Na kupatikana kwa matakwa yake katika viumbe na amri. Anawafutia dhambi wanaotubia, na anamrehemu yule aliyefanya sababu za kuleta rehema. Yeye Mtukufu alisema, "Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mrehemewe."
* * *
Juzuu ya pili ya Taysir Al-Karim Al-Mannan fi Tafsiri Kalaam Ar-rahman kwa mkusanyiko wake masikini kwa Mwenyezi Mungu Abdur-Rahman bin Nasir bin Abdullah bin Saadi, Mwenyezi Mungu amfutie dhambi yeye na wazazi wake; na Waislamu wanaume na Waislamu wanawake walio hai miongoni mwao na wafu, kwa rehema zako. Ewe mbora zaidi wa wanaorehemu, Amin! Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Na kwake tunatafuta msaada, na kwake tunategemea. Mola Mlezi, fanya wepesi na usaidie, ewe mkarimu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, tunamhimidi, na tunamuomba msaada, na tunamwomba atufutie dhambi, na tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na maovu ya nafsi zetu na mabaya ya matendo yetu. Mwenye kuongozwa na Mwenyezi Mungu, basi hakuna wa kumpoteza. Na anayempoteza, basi hana wa kumwongoa. Na ninashuhudia ya kwamba hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye mmoja peke pake, hana mshirika. Na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na amani nyingi iwe juu yake. Mola Mtukufu alisema:
: 130 - 136 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُضَاعَفَةً وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (130) وَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ (131) وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (132) وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ (133) الَّذِينَ يُنْفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ (134) وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَنْ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَى مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ (135) أُولَئِكَ جَزَاؤُهُمْ مَغْفِرَةٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ (136)}.
130. Enyi mlioamini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu. 131. Na ucheni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri. 132. Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa. 133. Na kimbilieni kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi. Iliandaliwa kwa ajili ya wachamungu. 134. Wale ambao hutoa wanapokuwa katika nyakati nzuri na wanapokuwa katika dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema. 135. Na wale ambao wanapofanya uchafu au wakazidhulumu nafsi zao, humkumbuka Mwenyezi Mungu; basi wanamwomba kufutiwa dhambi zao. Na ni nani anayefuta dhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu? Na wala hawaendelei na waliyoyafanya na hali ya kuwa wanajua. 136. Hao malipo yao ni kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito chini yake. Humo watadumu, na bora zaidi ni ujira wa watendao (wema).
#
{130} تقدم في مقدمة هذا التفسير: أن العبدَ ينبغي له مراعاة الأوامر والنواهي في نفسه وفي غيره، وأن الله تعالى إذا أمره بأمر وجب عليه أولاً أن يعرف حدَّه وما هو الذي أُمِر به ليتمكن بذلك من امتثاله، فإذا عرف ذلك اجتهد واستعان بالله على امتثاله في نفسه وفي غيره بحسب قدرته وإمكانه. وكذلك إذا نُهِيَ عن أمر عرف حده وما يدخل فيه وما لا يدخل، ثم اجتهد واستعان بربه في تركه. وأن هذا ينبغي مراعاته في جميع الأوامر الإلهية والنواهي. وهذه الآيات الكريمات قد اشتملت على أوامر وخصال من خصال الخير، أمر الله بها وحثَّ على فعلها، وأخبر عن جزاء أهلها، وعلى نواهٍ حثَّ على تركها. ولعل الحكمةَ ـ والله أعلم ـ في إدخال هذه الآيات أثناء قصة أحد أنه قد تقدم أن اللهَ تعالى وعدَ عبادَه المؤمنين أنهم إذا صبروا واتقوا نصرهم على أعدائهم وخذلَ الأعداءَ عنهم، كما في قوله تعالى: {وإن تصبروا وتتقوا لا يضركم كيدهم شيئاً}، ثم قال: {وإن تصبروا وتتقوا ويأتوكم من فورهم هذا يمددكم ربكم ... } الآيات. فكأن النفوس اشتاقت إلى معرفة خصال التقوى التي يحصل بها النصر والفلاح والسعادة، فذكر الله في هذه الآيات أهم خصال التقوى التي إذا قام العبد بها، فقيامه بغيرها من باب أولى وأحرى. ويدل على ما قلنا أن الله ذكر لفظ التقوى في هذه الآيات ثلاث مرات، مرة مطلقة، وهي قول: {أعدت للمتقين}، ومرتين مقيدتين فقال: {واتقوا الله} {واتقوا النار}. فقوله تعالى: {يا أيها الذين آمنوا} كل ما في القرآن من قوله تعالى: يا أيها الذين آمنوا افعلوا كذا أو اتركوا كذا يدل على أن الإيمان هو السبب الداعي والموجب لامتثال ذلك الأمر واجتناب ذلك النهي، لأن الإيمان هو التصديق الكامل بما يجب التصديق به المستلزم لأعمال الجوارح، فنهاهم عن أكل الربا أضعافاً مضاعفة، وذلك هو ما اعتاده أهل الجاهلية ومن لا يبالي بالأوامر الشرعية، من أنه إذا حل الدَّين على المعسر ولم يحصل منه شيء، قالوا له إما أن تقضي ما عليك من الدين، وإما أن نزيد في المدة ونزيد ما في ذمتك فيضطر الفقير ويستدفع غريمه ويلتزم ذلك اغتناماً لراحته الحاضرة فيزداد بذلك ما في ذمته أضعافاً مضاعفة من غير نفع وانتفاع. ففي قوله: {أضعافاً مضاعفة}؛ تنبيه على شدة شناعته بكثرته وتنبيه لحكمة تحريمه، وأن تحريم الربا حكمته أن الله منع منه لما فيه من الظلم، وذلك أن الله أوجب إنظار المعسر وبقاء ما في ذمته من غير زيادة، فإلزامه بما فوق ذلك ظلم متضاعف، فيتعين على المؤمن المتقي تركه وعدم قربانه لأن تركه من موجبات التقوى، والفلاح متوقف على التقوى، فلهذا قال: {واتقوا الله لعلكم تفلحون}.
{130} Ilitangulia katika utangulizi wa tafsiri hii kwamba, inampasa mja kuzingatia maamrisho na makatazo katika nafsi yake mwenyewe na katika wengineye. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anapomwamrisha jambo fulani, inamlazimu kwanza ajue kikomo chake na kile alichoamrishwa; ili aweze kwa hilo kuitekeleza. Kwa hivyo, anapojua hilo, basi anajitahidi na kutafuta msaada wa Mwenyezi Mungu juu ya kuitekeleza yeye mwenyewe na kwa wengineye kulingana na uwezo wake na uwezekano wake. Na vile vile, anapokatazwa jambo, anajua mipaka yake na kinachoingia ndani yake na kisichoingia. Kisha anajitahidi na kutafuta msaada wa Mola wake Mlezi katika kuliacha. Na kwamba hili linapaswa kuzingatiwa katika maamrisho na makatazo yote ya Mwenyezi Mungu. Aya hizi tukufu zimejumuisha maamrisho na sifa miongoni mwa sifa za heri alizoamrisha Mwenyezi Mungu. Na akahimiza zifanywe, na akajulisha kuhusu malipo ya wanaozistahiki, na makatazo aliyohimiza kuyaacha. Na huenda, - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - hekima katika kuziingiza aya hizi wakati wa kisa cha Uhud ni kwamba, ilikwisha tangulia kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaahidi waja wake Waumini kwamba ikiwa watakuwa na subira na kumcha Yeye tu; basi atawanusuru juu ya maadui zao. Na ataacha kuwasaidia maadui zao dhidi yao, kama ilivyo katika kauli yake Mtukufu. "Na mkisubiri, na mkamcha Mwenyezi Mungu, basi havitawadhuru kitu vitimbi vyao." Kisha akasema, "Na mkisubiri na mkamcha Mwenyezi Mungu, na hata wakiwajia kwa haraka yao hii, hapo Mola wenu Mlezi atawasaidia," hadi mwisho wa Aya. Ni kana kwamba nafsi zilitamani kujua sifa za uchamungu ambazo kwazo unaweza kupata ushindi, kufaulu na furaha. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akataja katika aya hizi sifa muhimu zaidi za uchamungu ambazo ikiwa mja akizitekeleza, basi kutekeleza kwake mengineyo ni katika mlango wa yale yanayostahiki zaidi na yanayofaa zaidi. Na tuliyoyasema yanaashiriwa kwa kuwa Mwenyezi Mungu alitaja neno uchamungu katika Aya hizi mara tatu. Mara moja bila ya kulifungamanisha na Mwenyezi Mungu, nayo ni kauli yake, “Imeandaliwa kwa wachamungu.” Na mara mbili kwa kulifungamanisha na Mwenyezi Mungu, akasema: “Na mcheni Mwenyezi Mungu” (na) “Na ucheni Moto.” Basi kauli yake Mola Mtukufu, “Enyi mlioamini”, yote yaliyomo ndani ya Qur-ani ya kauli yake Mola Mtukufu: Enyi mlioamini, fanyeni hivi au liacheni hili, yanaashiria kwamba imani ndiyo sababu inayopelekea na yenye kusababisha kutekeleza amri hiyo na kujiepusha na makatazo. Kwa sababu, imani ni kusadiki kamili kwa yale yanayopasa kusadikiwa, yenye kulazimu kufanya matendo kwa viungo. Basi akawakataza kula riba kwa kuzidisha juu kwa juu. Na hilo ndilo walilokuwa wamelizoea watu wa Jahiliyya, na yule ambaye hayajali maamrisho ya kisheria. Kwamba deni likifikia muda wake juu ya mwenye ugumu na asilipe kwalo chochote, wanamwambia: Ima ulipe deni lililo juu yako, au tuongeze katika muda na pia tuongeze katika kile kilicho katika dhima yako (yani deni). Kwa hivyo, masikini analazimika, na anafanikiwa kumrudisha mdai wake nyuma, na anaahidi kutekeleza hilo ili apate fursa ya kutulia kwa sasa. Hivyo basi kinaongezeka kwa hilo kile ambacho kilicho katika dhima yake, mizidisho juu ya mizidisho bila manufaa na wala kunufaika. Basi katika kauli yake, “mkizidisha juu kwa juu,” kuna kujulisha juu ya ukali wa ubaya wake kwa sababu ya wingi wake. Na pia kujulisha hekima ya kuharamishwa kwake, na kwamba kukataza riba hekima yake ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameikataza kwa sababu ya dhuluma iliyo ndani yake. Na hilo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amewajibisha kumpa muda mwenye ugumu, na kuacha kile kilicho katika dhima yake kilivyo bila ya nyongeza yoyote. Hivyo basi, kumlazimisha kufanya kilicho zaidi ya hayo ni dhuluma maradufu. Kwa hivyo, inamlazimu Muumini mchamungu kuiacha na asiikaribie (riba) kwa sababu kuiacha ni miongoni mwa yenye kuleta uchamungu, nako kufaulu kunategemea uchamungu. Na kwa sababu ya hilo ndiyo akasema, “Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.”
#
{131} {واتقوا النار التي أُعدت للكافرين}، بترك ما يوجب دخولها من الكفر والمعاصي على اختلاف درجاتها، فإن المعاصي كلها وخصوصاً المعاصي الكبار تجر إلى الكفر، بل هي من خصال الكفر الذي أعد الله النار لأهله، فترك المعاصي ينجي من النار ويقي من سخط الجبار، وأفعال الخير والطاعة توجب رضا الرحمن ودخول الجنان وحصول الرحمة، ولهذا قال:
{131} “Na ucheni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri” kwa kuacha yale yanayosababisha kuingia humo kama vile, ukafiri na maasia kwa daraja zake tofauti tofauti. Kwani, maasia yote hasa maasia makubwa yanapelekea kwenye ukafiri. Bali ni katika sifa za ukafiri ambao Mwenyezi Mungu amewaandalia watu wake Moto. Kwa hivyo, kuacha maasia kunaokoa kutokana na Moto na kunakinga kutokana na ghadhabu ya Al-Jabbar (Afanyae atakalo). Nayo matendo ya heri na utiifu, husababisha radhi ya Mwingi wa Rehema, na kuingia Peponi, na kupata rehema. Na kwa sababu hii, akasema:
#
{132} {وأطيعوا الله والرسول}، بفعل الأوامر امتثالاً واجتناب النواهي {لعلكم تُرحمون}، فطاعة الله وطاعة رسوله من أسباب حصول الرحمة، كما قال تعالى: {ورحمتي وسعت كل شيء فسأكتبها للذين يتقون ويؤتون الزكاة ... } الآيات.
{132} “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume” kwa kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo “ili mpate kurehemewa”. Kwa hivyo, kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake ni miongoni mwa sababu za kupata rehema, kama alivyosema Yeye Mtukufu; “Na rehema yangu imeenea kila kitu. Lakini nitawaandikia wamchao Mwenyezi Mungu na wakatoa zaka,” hadi mwisho wa Aya.
#
{133} ثم أمرهم تعالى بالمسارعة إلى مغفرته وإدراك جنته التي عرضها السماوات والأرض، فكيف بطولها التي أعدها الله للمتقين؟! فهم أهلها وأعمال التقوى هي الموصلة إليها.
{133} Kisha Yeye Mtukufu akawaamrisha kukimbilia kufutiwa dhambi kwake na kupata Pepo yake ambayo upana wake ni mbingu na ardhi. Basi vipi urefu wake ambao Mwenyezi Mungu amewaandalia wenye wachamungu? Wao ndio wanaoistahiki, nayo matendo ya uchamungu ndiyo yenye kufikisha huko.
#
{134} ثم وصف المتقين وأعمالهم فقال: {الذين ينفقون في السراء والضراء}؛ أي: في حال عسرهم ويسرهم إن أيسروا أكثروا من النفقة وإن أعسروا لم يحتقروا من المعروف شيئاً ولو قل، {والكاظمين الغيظ}: أي: إذا حصل لهم من غيرهم أذية توجب غيظهم، وهو امتلاء قلوبهم من الحنق الموجب للانتقام بالقول والفعل. هؤلاء لا يعملون بمقتضى الطباع البشرية بل يكظمون ما في القلوب من الغيظ، ويصبرون عن مقابلة المسيء إليهم. {والعافين عن الناس}، يدخل في العفو عن الناس العفو عن كل من أساء إليك بقول أو فعل، والعفو أبلغ من الكظم، لأن العفو ترك المؤاخذة مع السماحة عن المسيء، وهذا إنما يكون ممن تحلى بالأخلاق الجميلة وتخلى من الأخلاق الرذيلة، وممن تاجر مع الله وعفا عن عباد الله رحمة بهم وإحساناً إليهم، وكراهة لحصول الشر عليهم، وليعفو الله عنه ويكون أجره على ربه الكريم لا على العبد الفقير، كما قال تعالى: {فمن عفا وأصلح فأجره على الله}. ثم ذكر حالة أعم من غيرها وأحسن وأعلى وأجل، وهي الإحسان، فقال تعالى: {والله يحب المحسنين}، والإحسان نوعان: الإحسان في عبادة الخالق والإحسان إلى المخلوق. فالإحسان في عبادة الخالق فسرها النبي - صلى الله عليه وسلم - بقوله: «أن تعبد الله كأنك تراه، فإن لم تكن تراه فإنه يراك». وأما الإحسان إلى المخلوق فهو إيصال النفع الديني والدنيوي إليهم ودفع الشر الديني والدنيوي عنهم، فيدخل في ذلك أمرهم بالمعروف ونهيهم عن المنكر وتعليم جاهلهم ووعظ غافلهم والنصيحة لعامتهم وخاصتهم، والسعي في جمع كلمتهم وإيصال الصدقات والنفقات الواجبة والمستحبة إليهم على اختلاف أحوالهم وتباين أوصافهم، فيدخل في ذلك بذل الندى وكف الأذى واحتمال الأذى، كما وصف الله به المتقين في هذه الآيات، فمن قام بهذه الأمور فقد قام بحق الله وحق عبيده.
{134} Kisha akatoa maelezo kuhusu wachamungu na matendo yao, akasema. “Wale ambao hutoa katika nyakati nzuri na nyakati mbaya.” Yani katika hali ya ugumu wao na wepesi wao. Wakiwa katika hali nzuri, hutoa kwa wingi, na wakiwa katika hali ngumu, hawadharau kitu katika mema, hata kama ni kidogo. “Na wanajizuia ghadhabu.” Yani, wanapoudhiwa na wengine maudhi yanayosababisha kuwa na ghadhabu kwao, ambayo ni kuzijaza nyoyo zao hasira zinazolazimu kulipiza kisasi kwa kauli na vitendo. Watu hawa hawatendi kulingana na maumbile ya kibinadamu. Lakini badala yake huzuilia yale yaliyo ndani ya mioyo ya hasira, na huvumilia kukabiliana na wale wanaowaudhi. “Na wanaowasamehe watu.” Na inaingia katika kuwasamehe watu kumsamehe kila aliyekufanyia ubaya kwa kauli au kitendo. Na kusamehe ni bora zaidi kuliko kujizuilia ghadhabu. Kwa sababu, kusamehe ni kuacha kuchukulia ubaya pamoja na kumwachilia mbali aliyefanya ubaya. “Na wanaowasamehe watu.” Na inaingia katika kuwasamehe watu kumsamehe kila aliyekufanyia ubaya kwa kauli au kitendo. Na kusamehe ni bora zaidi kuliko kujizuilia ghadhabu. Kwa sababu, kusamehe ni kuacha kuchukulia ubaya pamoja na kumwachilia mbali aliyefanya ubaya. Na hii huwa tu kwa yule ambaye amejipamba kwa tabia nzuri na akaziacha tabia mbovu, miongoni mwa wale wanaofanya biashara na Mwenyezi Mungu. Na wanawasamehe waja wa Mwenyezi Mungu ili kuwarehemu na kuwafanyia wema, na kuchukia wapatwe na mabaya. Na ili Mwenyezi Mungu amsamehe na malipo yake yawe kwa Mola wake Mlezi Mkarimu, na siyo kwa mja fakiri, kama alivyosema Yeye Mtukufu. “Na mwenye kusamehe na akatengenea, basi malipo yake ni kwa Mwenyezi Mungu.” Kisha akataja hali iliyo ya jumla zaidi kuliko nyingine, na bora zaidi, na ya juu zaidi, na tukufu zaidi, nayo ni ihsan (wema). Yeye Mtukufu alisema, “Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao ihsan (wema). Nayo ihsan ni aina mbili: Ihsan katika kumuabudu Muumba, na ihsan kwa viumbe. Na Ihsan katika kumuabudu Muumba iliielezwa na Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa kauli yake. “Ni kwamba umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona. Na ikiwa hamuoni, basi Yeye kwa hakika anakuona.” Na ama ihsan kwa kiumbe ni kuwafikishia manufaa ya kidini na kidunia na kuwaondolea maovu ya kidini na kidunia. Kwa hivyo inaingia katika hilo kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na kuwafunza wasiojua wao. Na kuwapa mawaidha walioghafilika wao, na kuwapa nasiha watu wao wa kawaida na wale wao walio mahususi. Na kujitahidi katika kuunganisha neno lao, na kuwafikishia sadaka na matumizi ya lazima na ya kupendekezwa kulingana na hali zao tofauti tofauti, na sifa zao mbalimbali. Kwa hivyo, inaingia ndani ya hilo kutoa kwa ukarimu, na kuzuia madhara, na kuvumilia madhara, kama vile Mwenyezi Mungu alivyowaeleza wachamungu katika aya hizi. Kwa hivyo, mwenye kufanya mambo haya, basi atakuwa ametekeleza haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya waja wake.
Kisha akataja udhuru wao kwa Mola wao Mlezi kwa makosa yao na dhambi zao, akasema:
#
{135} {والذين إذا فعلوا فاحشة أو ظلموا أنفسهم}؛ أي: صدر منهم أعمال سيئة كبيرة أو ما دون ذلك، بادروا إلى التوبة والاستغفار، وذكروا ربهم وما توعد به العاصين، ووعد به المتقين فسألوه المغفرة لذنوبهم، والستر لعيوبهم، مع إقلاعهم عنها وندمهم عليها، فلهذا قال: {ولم يصروا على ما فعلوا وهم يعلمون}.
{135} “Na wale ambao wanapofanya uchafu au wakazidhulumu nafsi zao.” Yani, yatokeapo kwao maovu makubwa au kitu kidogo kuliko hayo, wanakimbilia kutubia na kuomba kufutiwa dhambi. Wanamkumbuka Mola wao Mlezi na yale aliyowatishia kwayo waasi, na aliyowaahidi wachamungu. Kwa hivyo wanamwomba maghufira kwa dhambi zao, na kuzisitiri aibu zao, pamoja na kuyaacha na kuyajutia. Na ndiyo maana akasema, “na wala hawaendelei na waliyoyafanya hali ya kuwa wanajua.”
#
{136} {أولئك}؛ الموصوفون بتلك الصفات {جزاؤهم مغفرة من ربهم} تزيل عنهم كل محذور، {وجنات تجري من تحتها الأنهار} فيها من النعيم المقيم والبهجة والسرور والبهاء والخير والسرور والقصور والمنازل الأنيقة العاليات والأشجار المثمرة البهية والأنهار الجاريات في تلك المساكن الطيبات {خالدين فيها} لا يحولون عنها ولا يبغون بها بدلاً ولا يغير ما هم فيه من النعيم {ونعم أجر العاملين} عملوا لله قليلاً فأجروا كثيراً، فعند الصباح يحمَد القومُ السَّرى وعند الجزاء يجد العامل أجره كاملاً موفراً. وهذه الآيات الكريمات من أدلة أهل السنة والجماعة، على أن الأعمال تدخل في الإيمان خلافاً للمرجئة، ووجه الدلالة إنما يتم بذكر الآية التي في سورة الحديد نظير هذه الآيات وهي قوله: {سابقوا إلى مغفرة من ربكم وجنة عرضها كعرض السماء والأرض أعدت للذين آمنوا بالله ورسله}، فلم يذكر فيها إلا لفظ الإيمان به وبرسله، وهنا قال: {أُعدت للمتقين}، ثم وصف المتقين بهذه الأعمال المالية والبدنية، فدل على أن هؤلاء المتقين هم الموصوفين بهذه الصفات هم أولئك المؤمنون. ثم قال تعالى:
{136} “Hao” walioelezwa kwa sifa hizo, “malipo yao ni kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wao Mlezi” kwenye kuwaondolea kila kinachoepukwa. “Na Bustani zipitazo mito chini yake,” ambamo kuna neema ya kudumu, na ya pendezayo, na furaha, na uzuri, na heri, na makasri, na majumba mazuri ya juu, na miti mizuri yenye matunda, na mito ipitayo maji katika makazi hayo mazuri. “Humo watadumu” wala hawataondolewa humo, wala hawatatafuta badala ya hayo, wala hayabadilika yale waliyomo ya neema. “Na ni mwema mno ujira wa watendao.” Walitenda machache kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi wakalipwa malipo mengi. Kwa hivyo, asubuhi kaumu hao wanasifu yaliyo mazuri, na wakati wa malipo, mwenye kutenda atapata malipo yake kwa ukamilifu na wingi. Na Aya hizi tukufu ni miongoni mwa ushahidi wa Ahlul-Sunnah wal-Jama'ah kwamba matendo yanaingia katika imani, tofauti na Al-Murji-ah. Na namna ya ushahidi wenyewe inatimia kwa kuitaja ile Aya ambayo iko katika Surat Al-Hadid iliyo sawa na hizi. Nayo ni kauli yake, “Kimbilieni kwenye kutaka kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wenu Mlezi na Pepo ambayo, upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake.” Na hakutaja ndani yake isipokuwa neno kumwamini Yeye na Mitume wake. Na hapa akasema, “iliyoandaliwa kwa ajili ya wachamungu.” Kisha akawaeleza wachamungu kwa matendo haya ya kimali na kimwili. Kwa hivyo, ikaashiria kuwa wachamungu hawa ndio walioelezwa kwa sifa hizi ndio wale Waumini. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
: 137 - 138 #
{قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ (137) هَذَا بَيَانٌ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِلْمُتَّقِينَ (138)}.
137. Tayari zimepita kabla yenu nyendo nyingi. Basi tembeeni katika ulimwengu na muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanaokanusha. 138. Huu ni ubainisho kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamungu.
#
{137} وهذه الآيات الكريمات، وما بعدها في قصة أحد، يعزي تعالى عباده المؤمنين، ويسليهم ويخبرهم أنه مضى قبلهم أجيال وأمم كثيرة امتحنوا، وابتلي المؤمنون منهم بقتال الكافرين، فلم يزالوا في مداولة ومجاولة حتى جعل الله العاقبة للمتقين والنصر لعباده المؤمنين، وآخر الأمر حصلت الدولة على المكذبين وخذلهم الله بنصر رسله وأتباعهم، {فسيروا في الأرض} بأبدانكم وقلوبكم {فانظروا كيف كان عاقبة المكذبين}، فإنكم لا تجدونهم إلا معذبين بأنواع العقوبات الدنيوية، قد خوت ديارهم وتبين لكل أحد خسارهم، وذهب عزهم وملكهم وزال بذخهم وفخرهم، أفليس في هذا أعظم دليل وأكبر شاهد على صدق ما جاءت به الرسل، وحكمة الله التي يمتحن بها عباده ليبلوهم ويتبين صادقهم من كاذبهم؟ ولهذا قال تعالى:
{137} Na Aya hizi tukufu, na zile zilizo baada yake katika kisa cha Uhud, Mwenyezi Mungu Mtukufu anaomboleza waja wake Waumini. Na anawafariji, na anawajulisha ya kwamba kabla yao vilipita vizazi na umma nyingi waliopewa mtihani. Na Waumini miongoni mwao wakajaribiwa kwa kupigana na makafiri. Basi hawakuacha kurejea rejea na kuzunguka zunguka mpaka Mwenyezi Mungu alipoufanya mwisho mwema kuwa ni wachamungu, na ushindi kuwa wa waja wake Waumini. Na mwisho wa mambo ulikuwa kwamba kushindwa kuliwapata wakadhibishao, na Mwenyezi Mungu akaacha kuwasaidia na akawasaidia Mitume wake na wafuasi wao. “Basi tembeeni katika ulimwengu” kwa miili yenu na mioyo yenu. “Na muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanaokanusha.” Nyinyi hakika hamtawakuta ispokuwa hali ya kuwa wameadhibiwa kwa aina za adhabu za kidunia. Tayari makazi yao yalikwisha anguka, na ikambainikia kila mmoja hasara yao. Na ikaenda heshima yao na ufalme wao, ukaisha na ubadhirifu wao na kiburi chao. Kwani katika hayo hakuna dalili kubwa na ushuhuda mkubwa juu ya ukweli wa yale waliyokuja nayo Mitume? Na hekima ya Mwenyezi Mungu ambayo anawapa mtihani kwayo waja wake ili kuwajaribu; na abainike mkweli wao kutokana na mwongo wao? Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema:
#
{138} {هذا بيان للناس}؛ أي: دلالة ظاهرة تبين للناس الحق من الباطل، وأهل السعادة من أهل الشقاوة، وهو الإشارة إلى ما أوقع الله بالمكذبين، {وهدى وموعظة للمتقين}، لأنهم هم المنتفعون بالآيات، فتهديهم إلى سبيل الرشاد وتعظهم وتزجرهم عن طريق الغي، وأما باقي الناس فهي بيان لهم تقوم عليهم الحجة من الله ليهلك من هلك عن بينة، ويحتمل أن الإشارة في قوله: {هذا بيان للناس}، للقرآن العظيم والذكر الحكيم وأنه بيان للناس عموماً، وهدى وموعظة للمتقين خصوصاً، وكلا المعنيين حق.
{138} “Huu ni ubainisho kwa watu wote.” Yani dalili iliyo dhahiri yenye kuwabainishia watu haki kutokana na batili, na watu wa furaha kutokana na watu wa taabu. Nayo ni ishara kwa yale aliyowafanyia Mwenyezi Mungu wakadhibishaji. “Na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamungu.” Kwa sababu ndio wanaonufaika na Aya, basi zikawaongoza kwenye njia ya uwongofu, na zinawapa mawaidha, na zinawakemea kutokana na njia ya upotovu. Na ama watu waliobakia, hizo ni ubainisho kwao ambao kwa huo inasimama hoja juu yao kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ili aangamie mwenye kuangamia kwa dalili zilizo wazi. Na inawezekana kuwa ishara katika kauli yake, “Huu ni ubainisho kwa watu;” ni kwa Qur-ani Tukufu na Ukumbusho wenye hekima. Na kwamba ni ubainisho kwa watu kwa ujumla, na uwongofu na mawaidha kwa wachamungu hasa. Na maana mbili hizi zote ni za kweli.
: 139 - 143 #
{وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنْتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (139) إِنْ يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِثْلُهُ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنْكُمْ شُهَدَاءَ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ (140) وَلِيُمَحِّصَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ (141) أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنْكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ (142) وَلَقَدْ كُنْتُمْ تَمَنَّوْنَ الْمَوْتَ مِنْ قَبْلِ أَنْ تَلْقَوْهُ فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنْتُمْ تَنْظُرُونَ (143)}.
139. Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa nyinyi ni Waumini. 140. Ikiwa mtaguswa na majeraha, basi kwa hakika hao watu wengine walikwisha patwa na majeraha mfano wake. Na siku za namna hii tunawaletea watu kwa zamu, ili Mwenyezi Mungu awajue wale walioamini na awateue miongoni mwenu mashahidi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalim. 141. Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walioamini na awafutilie mbali makafiri. 142. Je, mnadhani kwamba mtaingia Peponi ilhali Mwenyezi Mungu hajawajua wale miongoni mwenu waliopigana Jihadi, na akawajua waliosubiri? 143. Na nyinyi mlikuwa mkiyatamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi sasa mmekwisha yaona na huku mnayatazama.
#
{139} يقول تعالى مشجعاً لعباده المؤمنين ومقوياً لعزائمهم ومنهضاً لهممهم: {ولا تهنوا ولا تحزنوا}؛ أي: ولا تهنوا وتضعفوا في أبدانكم، ولا تحزنوا في قلوبكم عندما أصابتكم المصيبة، وابتليتم بهذه البلوى، فإن الحزن في القلوب والوهن على الأبدان زيادة مصيبة عليكم، وعون لعدوكم عليكم بل شجعوا قلوبكم وصبروها وادفعوا عنها الحزن وتصلبوا على قتال عدوكم، وذكر تعالى أنه لا ينبغي ولا يليق بهم الوهن والحزن وهم الأعلون في الإيمان ورجاء نصر الله وثوابه، فالمؤمن المبتغي ما وعده الله من الثواب الدنيوي والأخروي لا ينبغي له ذلك، ولهذا قال تعالى: {وأنتم الأعلون إن كنتم مؤمنين}.
{139} Yeye Mtukufu anasema huku akiwatia moyo waja wake Waumini; akiimarisha maazimio yao, na akiziamsha hamasa zao. “Wala msilegee, wala msihuzunike.” Yani msiwe wanyonge na mkadhoofika katika miili yenu, wala msihuzunike katika nyoyo zenu pale msiba ulipowapata, na mkajaribiwa na msiba huu. Kwani huzuni katika nyoyo na udhaifu kwenye miili ni ongezeko la msiba juu yenu, na ni msaada kwa adui yenu dhidi yenu. Bali zitieni moyo nyoyo zenu, na zivumilisheni, zisukume huzuni mbali nazo, na kuweni imara juu ya kupigana na adui yenu. Na Yeye Mtukufu alitaja kuwa haifai wala haiendani nao kuwa dhaifu na kuhuzunika hali ya kuwa wao ndio wa juu katika imani; na kutumai nusura ya Mwenyezi Mungu na malipo yake. Basi Muumini anayetafuta yale aliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu ya malipo ya kidunia na ya kiakhera, halimfai hilo. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema; “kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.”
Kisha akawafariji juu ya yale yaliyowapata ya kushindwa, na akabainisha hekima kubwa zilizotokana na hayo, akasema:
#
{140} {إن يمسسكم قرح فقد مس القوم قرح مثله}، فأنتم وهم قد تساويتم في القرح، ولكنكم ترجون من الله ما لا يرجون كما قال تعالى: {إن تكونوا تألمون فإنهم يألمون كما تألمون وترجون من الله ما لا يرجون}. ومن الحكم في ذلك أن هذه الدار يعطي الله منها المؤمن والكافر والبر والفاجر فيداول الله الأيام بين الناس: يوم لهذه الطائفة ويوم للطائفة الأخرى، لأن هذه الدارَ الدنيا منقضية فانية، وهذا بخلاف الدار الآخرة فإنها خالصة للذين آمنوا. {وليعلم الله الذين آمنوا}، هذا أيضاً من الحكم أنه يبتلي الله عباده بالهزيمة والابتلاء ليتبين المؤمن من المنافق، لأنه لو استمر النصر للمؤمنين في جميع الوقائع لدخل في الإسلام من لا يريده، فإذا حصل في بعض الوقائع بعض أنواع الابتلاء تبين المؤمن حقيقة الذي يرغب في الإسلام في الضراء والسراء واليسر والعسر ممن ليس كذلك، {ويتخذ منكم شهداء}. وهذا أيضاً من بعض الحكم، لأن الشهادة عند الله من أرفع المنازل، ولا سبيل لنيلها إلا بما يحصل من وجود أسبابها، فهذا من رحمته بعباده المؤمنين، أن قيَّض لهم من الأسباب ما تكرهه النفوس، لينيلهم ما يحبون من المنازل العالية والنعيم المقيم. {والله لا يحب الظالمين}، الذين ظلموا أنفسهم وتقاعدوا عن القتال في سبيله، وكأن في هذا تعريضاً بذم المنافقين وأنهم مبغوضون لله، ولهذا ثبطهم عن القتال في سبيله، ولو أرادوا الخروج لأعدوا له عدة، ولكن كره الله انبعاثهم فثبطهم وقيل اقعدوا مع القاعدين.
{140} “Na mkiguswa na majeraha, basi na hao kaumu wengine yaliguswa na majeraha mfano wake.” Basi nyinyi na wao mmekuwa sawa katika kujeruhiwa, lakini nyinyi mnatarajia kwa Mwenyezi Mungu yale wasiyoyatarajia. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Ikiwa mnaumia, basi wao hakika pia wanaumia kama mnavyoumia nyinyi. Nanyi mnatarajia kwa Mwenyezi Mungu yale wasiyoyatarajia.” Na miongoni mwa hekima katika hilo ni kwamba katika Nyumba hii Mwenyezi Mungu humpa Muumini na kafiri, na mwema na mwovu. Kisha Mwenyezi Mungu hubadilisha siku kwa zamu baina ya watu: Siku kwa kundi hili na siku kwa lile kundi lingine. Kwa sababu Nyumba hii ya duniani ni yenye kupita na kwisha. Na hii ni tofauti na Nyumba ya Akhera, ambayo ni ya wale walioamini peke yao. "Na ili Mwenyezi Mungu awajue wale walioamini.” Hili pia ni katika hekima kwamba Mwenyezi Mungu huwajaribu waja wake kwa kushindwa na majaribio ili abainike Muumini kutokana na mnafiki. Kwa sababu lau kuwa ushindi utaendelea kwa Waumini katika matukio yote, basi angeingia katika Uislamu yule asiyeutaka. Basi iwapo katika baadhi ya matukio yatatokea aina fulani ya mitihani, anabainika Muumini wa kweli ambaye anautaka Uislamu katika dhiki na nyakati nzuri, na wepesi na ugumu, kutokana na yule asiyekuwa hivyo. “Na awateue miongoni mwenu mashahidi” Hii pia ni katika hekima, kwa sababu kufa kishahidi kwa Mwenyezi Mungu ni moja ya daraja za juu, na hakuna njia ya kuipata isipokuwa kwa yale yanayotokea kutokana na kuwepo kwa sababu zake. Basi hii ni katika rehema yake kwa waja wake Waumini. Kwamba aliwawekea katika sababu ambazo nafsi zinachukia, ili awape wanayoyapenda ya vyeo vya juu, na neema ya milele. “Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu.” Ambao walizidhulumu nafsi zao na wakakaa wakaacha kupigana vita katika Njia Yake. Na ni kana kwamba katika hili kuna kuwakashifu wanaafiki kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja, na kwamba wanachukiwa na Mwenyezi Mungu. Na ndio maana akawazuilia wasipigane katika njia yake. Na lau kuwa walitaka kutoka, basi wangeliandalia maandalizi, lakini Mwenyezi Mungu alichukia kutoka kwao, kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni nyuma pamoja na waliokaa nyuma.
#
{141} {وليمحص الله الذين آمنوا}، وهذا أيضاً من الحكم أن الله يمحص بذلك المؤمنين من ذنوبهم وعيوبهم، يدل ذلك على أن الشهادة والقتال في سبيل الله تكفر الذنوب وتزيل العيوب ، وليمحص الله أيضاً المؤمنين من غيرهم من المنافقين فيتخلصون منهم ويعرفون المؤمن من المنافق. ومن الحكم أيضاً أنه يقدر ذلك ليمحق الكافرين، أي: ليكون سبباً لمحقهم واستئصالهم بالعقوبة، فإنهم إذا انتصروا بغوا وازدادوا طغياناً إلى طغيانهم يستحقون به المعاجلة بالعقوبة رحمة بعباده المؤمنين. ثم قال تعالى:
{141} “Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walioamini.” Na hili pia ni katika hekima ya kwamba Mwenyezi Mungu anasafisha Waumini kwa hilo kutokana na dhambi zao na aibu zao. Hilo linaashiria kwamba kufa kishahidi na kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu vinafuta dhambi na vinaondoa aibu. Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe Waumini kutokana na wengineo miongoni mwa wanafiki. Kwa hivyo, wanaondolewa kutokana nao na wanajulikana; Muumini kutoka kwa mnafiki. Na pia katika hekima ni kwamba Yeye anajaalia hayo ili awafutilie mbali makafiri. Yani ili iwe sababu ya kuwafutilia mbali na kuwaangamiza kwa adhabu. Kwa sababu, wao wakishinda, wanavuka mipaka na wanazidisha uasi juu ya uasi wao, ambao wanastahili kwao adhabu ya haraka kama rehema kwa waja wake Waumini. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
#
{142} {أم حسبتم أن تدخلوا الجنة ولما يعلم الله الذين جاهدوا منكم ويعلم الصابرين}، هذا استفهام إنكاري، أي: لا تظنوا ولا يخطر ببالكم أن تدخلوا الجنة من دون مشقة واحتمال المكاره في سبيل الله، وابتغاء مرضاته، فإن الجنة أعلى المطالب وأفضل ما به يتنافس المتنافسون، وكلما عظم المطلوب عظمت وسيلته والعمل الموصل إليه، فلا يوصل إلى الراحة إلا بترك الراحة ولا يدرك النعيم إلا بترك النعيم، ولكن مكاره الدنيا التي تصيب العبد في سبيل الله، عند توطين النفس لها وتمرينها عليها ومعرفة ما تَؤول إليه تنقلب عند أرباب البصائر منحًا يسرون بها ولا يبالون بها، وذلك فضل الله يؤتيه من يشاء، ثم وبخهم تعالى على عدم صبرهم بأمر كانوا يتمنونه ويودون حصوله، فقال:
{142} "Je, mnadhani kwamba mtaingia Peponi ilhali Mwenyezi Mungu hajawajua wale miongoni mwenu waliopigana Jihadi, na akawajua waliosubiri?" Hili ni swali la kejeli lenye maana ya kuwa msidhanie wala isiwajie akilini mwenu kwamba, mtaingia Pepo bila ya dhiki na kustahimili yachukizayo katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kutafuta radhi zake. Kwani, Pepo ndiyo kitakwacho cha juu zaidi na kilicho bora zaidi wanachoshindania wenye kushindana. Na kila kinapokuwa kitakwacho kikubwa, basi njia yake na matendo yake yenye kukifikia yanakuwa makubwa. Kwa hivyo starehe haifikiwi isipokuwa kwa kuacha starehe. Na wala neema haipatikani isipokuwa kwa kuacha neema. Lakini machukizo ya kidunia ambayo yanamfika mja katika njia ya Mwenyezi Mungu, wakati nafsi inapoyavumilia na kuyazoea na kujua hali ambayo itaishia, (machukizo hayo) yanageukia kwa wababe wa busara yanakuwa tunu wanazofurahishwa nayo, wala hawayajali. Na hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakaye. Kisha Yeye Mtukufu akawakemea kwa kukosa kwao kusubiri juu ya jambo walilokuwa wakilitamani na wanapenda litokee. Akasema:
#
{143} {ولقد كنتم تمنون الموت من قبل أن تلقوه}، وذلك أن كثيراً من الصحابة رضي الله عنهم ممن فاته بدر، يتمنون أن يحضرهم الله مشهداً يبذلون فيه جهدهم، قال الله تعالى لهم: {فقد رأيتموه}؛ [أي: رأيتم] ما تمنيتم بأعينكم {وأنتم تنظرون}، فما بالكم وترك الصبر؟ هذه حالة لا تليق ولا تحسن، خصوصاً لمن تمنى ذلك وحصل له ما تمنى، فإن الواجب عليه بذل الجهد واستفراغ الوسع في ذلك. وفي هذه الآية دليل على أنه لا يكره تمني الشهادة. ووجه الدلالة أن الله تعالى أقرهم على أمنيتهم، ولم ينكر عليهم، وإنما أنكر عليهم عدم العمل بمقتضاها والله أعلم. ثم قال تعالى:
{143} “Na nyinyi mlikuwa mkitamani mauti kabla hamjakutana nayo ” Na hilo ni kwamba wengi katika maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, miongoni mwa wale waliokoswa na Badr, walitamani Mwenyezi Mungu awaletee tukio ambalo watalifanyia juhudi zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaambia, “Basi sasa mmekwisha yaona” [yani, mmeona] yale mliyoyatamani kwa macho yenu, “na huku mnayatazama.” Basi mna nini na kuacha subira? Hali hii haimfai wala siyo nzuri hasa kwa yule aliyelitamani hilo na akalipata alilotamani. Basi la wajibu juu yake ni kufanya juhudi na kufanya kila liwezekanalo katika hilo. Na katika aya hii, kuna ushahidi kwamba haichukizi kutamani kufa kishahidi. Na namna ya ushahidi wenyewe ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaridhia katika matamanio yao, na wala hakuwashutumu. Bali aliwashutumu kwa kutotenda kulingana na matakwa yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
: 144 - 145 #
{وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ أَفَإِنْ مَاتَ أَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ وَمَنْ يَنْقَلِبْ عَلَى عَقِبَيْهِ فَلَنْ يَضُرَّ اللَّهَ شَيْئًا وَسَيَجْزِي اللَّهُ الشَّاكِرِينَ (144) وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَنْ تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ كِتَابًا مُؤَجَّلًا وَمَنْ يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَنْ يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ (145)}.
144. Na Muhammad si isipokuwa Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa, mtageuka mrudi kwa visigino vyenu? Na atakayegeuka akarudi kwa visigino vyake, basi huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru. 145. Na haikuwa kwa nafsi kufa isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyoandikiwa muda wake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani, tutampa kwayo. Na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa kwayo. Na tutawalipa wenye kushukuru.
#
{144} يقول تعالى: {وما محمد إلا رسول قد خلت من قبله الرسل}؛ أي: ليس ببدع من الرسل، بل هو من جنس الرسل الذين قبله، وظيفتهم تبليغ رسالة ربهم وتنفيذ أوامره ليسوا بمخلدين، وليس بقاؤهم شرطاً في امتثال أوامر الله، بل الواجب على الأمم عبادة ربهم في كل وقت وبكل حال، ولهذا قال: {أفإن مات أو قُتل انقلبتم على أعقابكم}؛ بترك ما جاءكم به من إيمان أو جهاد أو غير ذلك، قال الله تعالى: {ومن ينقلب على عقبيه فلن يضر الله شيئاً}، إنما يضر نفسه، وإلا فالله تعالى غني عنه، وسيقيم دينه، ويعز عباده المؤمنين. فلما وبخ تعالى من انقلب على عقبيه، مدح من ثبت مع رسوله، وامتثل أمر ربه فقال: {وسيجزي الله الشاكرين}، والشكر لا يكون إلا بالقيام بعبودية الله تعالى في كل حال. وفي هذه الآية الكريمة إرشاد من الله تعالى لعباده أن يكونوا بحالة لا يزعزعهم عن إيمانهم أو عن بعض لوازمه فَقْدُ رئيس ولو عظم، وما ذاك إلا بالاستعداد في كل أمر من أمور الدين بعدة أناس من أهل الكفاءة فيه إذا فُقِدَ أحدُهم قام به غيره، وأن يكون عموم المؤمنين قصدهم إقامة دين الله والجهاد عنه بحسب الإمكان، لا يكون لهم قصد في رئيس دون رئيس، فبهذه الحال يستتب لهم أمرهم، وتستقيم أمورهم. وفي هذه الآية أيضاً أعظم دليل على فضيلة الصديق الأكبر أبي بكر وأصحابه الذين قاتلوا المرتدين بعد رسول الله - صلى الله عليه وسلم - لأنهم هم سادات الشاكرين.
{144} Yeye Mtukufu anasema, "Na Muhammad si isipokuwa Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume." Yani, Yeye si kitu kipya katika Mitume. Bali yeye ni katika jamii ya Mitume waliokuwa kabla yake. Kazi yao ni kufikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi na kutekeleza maamrisho yake. Wao si wa kuishi milele, na wala kubaki kwao si sharti la kutii amri za Mwenyezi Mungu. Bali, la wajibu kwa umma zote ni kumwabudu Mola wao Mlezi kila wakati na kwa kila hali. Na kwa sababu hiyo akasema, "Je, akifa au akiuawa, mtageuka mrudi kwa visigino vyenu?" Kwa kuacha yale aliyowajia nayo ya imani, au jihadi, au mengineyo. Yeye Mtukufu alisema, "Na atakayegeuka akarudi kwa visigino vyake, basi huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu." Yeye anajidhuru tu mwenyewe. La sivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu anajitosheleza, na atasimamisha Dini yake, na atawapa nguvu waja wake Waumini. Yeye Mtukufu alipomkemea yule aliyegeuka kwenye visigino vyake, akamsifu yule aliyesimama imara pamoja na Mtume wake na akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi. Akasema, “Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru.” Na kushukuru haiwi isipokuwa kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kila hali. Na katika Aya hii tukufu, kuna mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kwamba, wawe katika hali ambayo hakuwatikisi katika imani yao au katika baadhi ya matakwa yake kumpoteza kiongozi hata akiwa mkubwa vipi. Na hilo si isipokuwa kwa kujitayarisha katika kila jambo katika mambo ya Dini kwa idadi ya watu wenye uwezo katika hilo. Ikiwa mmoja wao atapotea, analifanya mtu mwingine. Na kwamba Waumini wote liwe na lengo lao ni kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu na kuifanyia Jihadi kulingana na inavyowezekana. Na wala wasiwe wana lengo kwa kiongozi mmoja na si kiongozi mwingine. Na kwa hali hii, mambo yao yatatulia, na mambo yao yatanyooka. Na vile vile katika Aya hii kuna ushahidi mkubwa zaidi juu ya fadhila za rafiki mkubwa Abu Bakr na maswahaba wake, ambao walipigana vita na walioritadi baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - Kwa sababu wao ndio mabwana wa wenye kushukuru.
#
{145} ثم أخبر تعالى أن النفوس جميعها معلقة بآجالها بإذن الله وقدره وقضائه، فمن حتم عليه بالقدر أن يموت مات ولو بغير سبب، ومن أراد بقاءه فلو وقع من الأسباب كل سبب لم يضره ذلك قبل بلوغ أجله، وذلك أن الله قضاه وقدره وكتبه إلى أجل مسمى إذا جاء أجلهم فلا يستأخرون عنه ساعة ولا يستقدمون. ثم أخبر تعالى أنه يعطي الناس من ثواب الدنيا والآخرة ما تعلقت به إرادتهم، فقال: {ومن يرد ثواب الدنيا نؤته منها ومن يرد ثواب الآخرة نؤته منها}، قال الله تعالى: {كلاًّ نمد هؤلاء وهؤلاء من عطاء ربك وما كان عطاء ربك محظوراً. انظر كيف فضلنا بعضهم على بعض وللآخرة أكبر درجات وأكبر تفضيلاً}. {وسنجزي الشاكرين}، ولم يذكر جزاءهم ليدل ذلك على كثرته وعظمته، وليعلم أن الجزاء على قدر الشكر قلة وكثرة وحسناً.
{145} Kisha Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba nafsi zote zimefungamanishwa na muda wake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na majaaliwa yake, na hukumu yake. Basi aliyewekewa majaaliwa kufa, basi atakufa hata bila ya sababu. Na aliyemtaka abaki, basi hata kama sababu zitatokea, kila sababu haitamdhuru kabla ya kufika kwa muda wake. Na hilo ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu alipitisha hilo na akalijaalia, na akaliandikia muda uliowekwa. Muda wao ukifika, basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia. Kisha Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba, Yeye huwapa watu katika thawabu za dunia na Akhera yale yaliyofungamana na mapenzi yao. Kwa hivyo, akasema, “Na mwenye kutaka malipo ya duniani, tutampa kwayo. Na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa kwayo.” Na alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Wote hao tunawapa - hawa na hao - katika neema za Mola wako Mlezi. Wala neema za Mola wako Mlezi hazikuwa ni zenye kuzuilika. Angalia vipi tulivyowaboresha baadhi yao kuliko wengine wao. Na hakika, Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na kuboresha kukubwa zaidi.” “Na tutawalipa wanaoshukuru.” Na wala hakutaja malipo yao; ili hilo liashirie wingi wake na ukubwa wake. Na ili ijulikane kwamba, malipo ni kwa kiwango cha shukrani, kwa uchache, na wingi uzuri.
: 146 - 148 #
{وَكَأَيِّنْ مِنْ نَبِيٍّ قَاتَلَ مَعَهُ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُوا لِمَا أَصَابَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَمَا ضَعُفُوا وَمَا {اسْتَكَانُوا وَاللَّهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ (146) وَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّا أَنْ قَالُوا رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (147) فَآتَاهُمُ اللَّهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الْآخِرَةِ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ (148)}.
146. Na ni Manabii wangapi waliopigana vita pamoja nao Waumini wenye ikhlasi wengi! Na hawakulegea kwa yaliyowapata katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakusalimu amri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanaosubiri. 147. Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: Mola wetu Mlezi! Tufutie dhambi zetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru dhidi ya kaumu ya makafiri. 148. Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na malipo bora ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.
#
{146} هذا تسلية للمؤمنين وحثٌّ على الاقتداء بهم والفعل كفعلهم، وأن هذا أمر قد كان متقدماً لم تزل سنة الله جارية بذلك، فقال: {وكأين من نبي}؛ أي: وكم من نبي {قاتل معه ربيون كثير}؛ أي: جماعات كثيرون من أتباعهم الذين قد ربتهم الأنبياء بالإيمان والأعمال الصالحة فأصابهم قتل وجراح وغير ذلك، {فما وهنوا لما أصابهم في سبيل الله وما ضعفوا وما استكانوا}؛ أي: ما ضعفت قلوبهم، ولا وهنت أبدانهم، ولا استكانوا؛ أي: ذلُّوا لعدوهم، بل صبروا وثبتوا وشجعوا أنفسهم، ولهذا قال: {والله يحب الصابرين}.
{146} Huku ni kuwafariji Waumini na kuwahimiza kufuata mfano wao na kufanya kama walivyofanya. Na kwamba jambo hili lilikuwa limeshatangulia na ni nyendo ya Mwenyezi Mungu ambayo bado inaendelea hivyo. Kwa hivyo, akasema, “Na ni Manabii wangapi.” Yani, ni wangapi katika Manabii? “Waliopigana vita pamoja nao Waumini wenye ikhlasi.” Yani, makundi mengi katika wafuasi wao ambao walilelewa na Manabii kwa imani na matendo mema, na wakafikwa na mauaji, na majeraha na yasiyokuwa hayo. “Na hawakulegea kwa yaliyowapata katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakusalimu amri.” Yani, mioyo yao haikudhoofika, wala miili yao haikulegea, wala hawakujidhalilisha mbele ya maadui zao kwa kusalimu amri. Bali, walisubiri, na wakawa madhubuti, na wakajipa moyo. Na kwa sababu hiyo ndio akasema, “Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanaosubiri.”
#
{147} ثم ذكر قولهم واستنصارهم لربهم فقال: {وما كان قولهم}؛ أي: في تلك المواطن الصعبة {إلا أن قالوا ربنا اغفر لنا ذنوبنا وإسرافنا في أمرنا}، والإسراف هو: مجاوزة الحد إلى ما حرم، علموا أن الذنوب والإسراف من أعظم أسباب الخذلان وأن التخلي منها من أسباب النصر، فسألوا ربهم مغفرتها. ثم إنهم لم يتكلوا على ما بذلوا جهدهم به من الصبر، بل اعتمدوا على الله، وسألوه أن يثبت أقدامهم عند ملاقاة الأعداء الكافرين، وأن ينصرهم عليهم، فجمعوا بين الصبر وترك ضده، والتوبة والاستغفار والاستنصار بربهم، لا جرم أن الله نصرهم، وجعل لهم العاقبة في الدنيا والآخرة ولهذا قال:
{147} Kisha akaitaja kauli yao na kutafuta kwao msaada kwa Mola wao Mlezi, akasema, “Na haikuwa kauli yao.” Yani, katika hali hizo ngumu, “isipokuwa walisema: Mola wetu Mlezi! Tufutie dhambi zetu, na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu.” Na Israaf ni kupindukia mipaka hadi katika kilicho haramishwa. Walijua kwamba madhambi na kupindukia mipaka ni miongoni mwa sababu kubwa za kutosaidiwa, na kwamba kuziacha ni katika sababu za ushindi. Kwa hivyo, wakamwomba Mola wao Mlezi awafutie dhambi. Kisha hawakuitegemea juhudi waliyoifanya katika kusubiri. Bali walimtegemea Mwenyezi Mungu, na wakamwomba kwamba aiimarishe miguu yao wakati wanapokutana na maadui makafiri, na kwamba awanusuru dhidi yao. Kwa hivyo, wakaunganisha baina ya subira na kuacha kinyume chake, na toba, na kuomba kufutiwa dhambi na kuomba msaada kwa Mola wao Mlezi. Hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu aliwanusuru, na akawafanyia mwisho mwema katika dunia na Akhera. Na ndiyo maana akasema:
#
{148} {فآتاهم الله ثواب الدنيا} من النصر والظفر والغنيمة {وحُسن ثواب الآخرة} وهو الفوز برضا ربهم والنعيم المقيم الذي قد سلم من جميع المنكدات، وما ذاك إلا أنهم أحسنوا له الأعمال فجازاهم بأحسن الجزاء، فلهذا قال: {والله يحب المحسنين} في عبادة الخالق ومعاملة الخلق، ومن الإحسان أن يفعل عند جهاد الأعداء كفعل هؤلاء المؤمنين. ثم قال تعالى:
{148} “Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani” ya msaada, na ushindi, na ngawira, “na malipo bora ya Akhera." Nayo ni kupata radhi za Mola wao Mlezi na neema ya kudumu ambayo imesalimika kutokana na misiba yote. Na hilo si isipokuwa kwamba wao walimfanyia matendo mema, kwa hivyo akawalipa malipo bora zaidi. Na ndiyo maana akasema, “Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.” katika kumuabudu Muumba na kuamiliana na viumbe. Na katika wema ni kufanya wakati wa kupigana jihadi dhidi ya maadui kama walivyofanya Waumini wale. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
: 149 - 151 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تُطِيعُوا الَّذِينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ فَتَنْقَلِبُوا خَاسِرِينَ (149) بَلِ اللَّهُ مَوْلَاكُمْ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ (150) سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا {الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ (151)}.
149. Enyi mlioamini! Ikiwa mtawatii wale waliokufuru, watawarudisha kwa visigino vyenu, na hapo mtageuka huku mmehasirika. 150. Bali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wenu. Naye ndiye mbora wa wanaonusuru. 151. Tutatia hofu katika nyoyo za wale waliokufuru kwa vile walivyomshirikisha Mwenyezi Mungu na yale ambayo hakuyateremshia hoja yoyote. Na makazi yao ni Motoni. Na maovu mno ni maskani ya wenye kudhulumu!
#
{149} وهذا نهي من اللَّهِ للمؤمنين، أن يطيعوا الكافرين من المنافقين والمشركين فإنهم إذا أطاعوهم لم يريدوا لهم إلا الشر، وهم قصدهم ردهم إلى الكفر الذي عاقبته الخيبة والخسران.
{149} Na hili ni katazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Waumini kuwatii makafiri kama vile wanafiki na washirikina. Kwa sababu, ikiwa watawatii, basi hawatawatakia isipokuwa shari. Nao makusudio yao ni kuwarudisha kwenye ukafiri ambao mwisho wake ni kuambulia patupu na kuhasirika.
#
{150} ثم أخبر أنه مولاهم وناصرهم، ففيه إخبار لهم بذلك وبشارة، بأنه يتولى أمورهم بلطفه ويعصمهم من أنواع الشرور، وفي ضمن ذلك الحث لهم على اتخاذه وحده وليًّا وناصراً من دون كل أحد.
{150} Kisha akajulisha kuwa Yeye ndiye mlinzi wao na msaidizi wao. Basi, ndani yake kuna kuwajulisha hilo na kuwabashiria kwamba Yeye ndiye anayesimamia mambo yao kwa upole wake, na anawalinda kutokana na kila aina ya shari. Na ndani ya hilo kuna kuwahimiza wamchukue Yeye peke yake kama mlinzi na msaidizi kando na kila yeyote.
#
{151} فمن ولايته ونصره لهم أنه وعدهم أنه سيلقي في قلوب أعدائهم من الكافرين الرعب، وهو الخوف العظيم الذي يمنعهم من كثير من مقاصدهم، وقد فعل تعالى، وذلك أن المشركين بعد ما انصرفوا من وقعة أُحد تشاوروا بينهم، وقالوا: كيف ننصرف بعد أن قتلنا منهم من قتلنا وهزمناهم ولما نستأصلهم؟ فهَمُّوا بذلك، فألقى اللَّهُ الرعبَ في قلوبهم فانصرفوا خائبين. ولا شكَّ أن هذا من أعظم النصر، لأنه قد تقدم أن نصر الله لعباده المؤمنين لا يخرج عن أحد أمرين: إما أن يقطعَ طرفاً ممن كفروا أو يكبتهم فينقلبوا خائبين. وهذا من الثاني. ثم ذكر السبب الموجب لإلقاء الرعب في قلوب الكافرين فقال: {بما أشركوا بالله ما لم ينزل به سلطاناً}؛ أي: ذلك بسبب ما اتخذوا من دونه من الأنداد والأصنام التي اتخذوها على حسب أهوائهم وإراداتهم الفاسدة من غير حجة ولا برهان، وانقطعوا من ولاية الواحد الرحمن، فمن ثَمَّ كان المشرك مرعوباً من المؤمنين لا يعتمد على ركن وثيق، وليس له ملجأ عند كل شدة وضيق، هذا حاله في الدنيا وأما في الآخرة فأشد وأعظم، ولهذا قال: {ومأواهم النار}؛ أي: مستقرهم الذي يأوون إليه وليس لهم عنها خروج {وبئس مثوى الظالمين}، بسبب ظلمهم وعدوانهم؛ صارت النارُ مثواهم.
{151} Basi katika ulinzi wake na usaidizi wake kwao ni kwamba aliwaahidi kwamba atatia hofu katika nyoyo za maadui zao miongoni mwa makafiri. Nayo ni hofu kubwa ambayo inawazuia na mengi ya malengo yao. Na tayari Yeye Mtukufu alikwisha fanya (hivyo). Na hilo ni kwamba washirikina baada ya kutoka katika vita vya Uhud, walishauriana wao kwa wao, na wakasema. “Vipi tunaondoka baada ya kuwa tumewaua miongoni mwao wale tuliowaua na kuwashinda, na bado hatujawaangamiza? kwa hivyo, wakaazimia kufanya hivyo. Basi Mwenyezi Mungu akatia hofu katika nyoyo zao, kwa hivyo wakaondoka hali ya kuwa wameambulia patupu. Na hakuna shaka kwamba huu ni katika ushindi mkubwa kabisa. Kwa sababu, ilikwisha tangulia nusura ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini haitoki nje ya moja ya mambo mawili: Ima akate sehemu katika wale waliokufuru, au awafutilie mbali na warudi hali ya kuwa wameambulia patupu. Na hili ni katika hili la pili. Kisha akataja sababu inayolazimu kutia hofu katika nyoyo za makafiri, akasema, “Kwa vile walivyomshirikisha Mwenyezi Mungu na wale ambao hakuwateremshia hoja yoyote.” Yani, hayo ni kwa sababu ya yale waliyoyachukua kando na Yeye kama vile washirika na masanamu ambayo walivichukua kulingana na matamanio yao na kutaka kwake kwao kubovu bila ya hoja yoyote wala ushahidi. Na wakakatika kutoka kwa ulinzi wa Mwingi wa Rehema. Basi kwa sababu ya hilo, ndio mshirikina akawa anawaogopa Waumini. Haitegemei nguzo yoyote imara, na hana kimbilio wakati wa kila ugumu na dhiki. Na hii ndiyo hali yake katika dunia. Na ama katika Akhera, basi ni kali zaidi na kubwa zaidi. Na kwa sababu hii, akasema, “Na makazi yao ni Motoni.” Yani, pahala pao pa kutulia ambapo watakimbilia, na hawataweza kutoka humo. “Na maovu mno ni maskani ya wenye kudhulumu!” Kwa sababu ya dhuluma yao na ukaidi wao, Moto ukawa ndio makazi yao.
: 152 #
{وَلَقَدْ صَدَقَكُمُ اللَّهُ وَعْدَهُ إِذْ تَحُسُّونَهُمْ بِإِذْنِهِ حَتَّى إِذَا فَشِلْتُمْ وَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَعَصَيْتُمْ مِنْ بَعْدِ مَا أَرَاكُمْ مَا تُحِبُّونَ مِنْكُمْ مَنْ يُرِيدُ الدُّنْيَا وَمِنْكُمْ مَنْ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ثُمَّ صَرَفَكُمْ عَنْهُمْ لِيَبْتَلِيَكُمْ وَلَقَدْ عَفَا عَنْكُمْ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ (152)}.
152. Na Mwenyezi Mungu aliwatimilizia ahadi yake, vile mlivyokuwa mnawaua kwa idhini yake, mpaka mlipolegea na mkazozana katika amri hii, na mkaasi baada ya Yeye kuwaonyesha yale mnayoyapenda. Wapo miongoni mwenu wanaotaka dunia, na wapo miongoni mwenu wanaotaka Akhera. Kisha akawatenga nao (maadui) ili awajaribu. Naye sasa amekwisha wasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.
#
{152} أي: {ولقد صدقكم الله وعده} بالنصر فنصركم عليهم حتى ولوكم أكتافهم، وطفقتم فيهم قتلاً حتى صرتم سبباً لأنفسكم وعوناً لأعدائكم عليكم، فلما حصل منكم الفشل وهو الضعف والخور {وتنازعتم في الأمر} الذي فيه ترك أمر الله بالائتلاف وعدم الاختلاف، فاختلفتم؛ فمن قائل نقيم في مركزنا الذي جعلنا فيه النبي - صلى الله عليه وسلم -، ومن قائل ما مقامنا فيه وقد انهزم العدو ولم يبق محذور، فعصيتم الرسول وتركتم أمره، من بعد ما أراكم الله ما تحبون، وهو انخذال أعدائكم، لأن الواجب على من أنعم الله عليه بما أحب أعظم من غيره، فالواجب في هذه الحال خصوصاً وفي غيرها عموماً امتثال أمر الله ورسوله، {منكم من يريد الدنيا}؛ وهم الذين أوجب لهم ذلك ما أوجب، {ومنكم من يريد الآخرة}؛ وهم الذين لزموا أمر رسول الله. وثبتوا حيث أُمروا، {ثم صرفكم عنهم}؛ أي: بعد ما وجدت هذه الأمور منكم، صرف الله وجوهكم عنهم، فصار الوجه لعدوكم ابتلاء من الله لكم وامتحاناً، ليتبين المؤمن من الكافر والطائع من العاصي، وليكفِّرَ الله عنكم بهذه المصيبة ما صدر منكم فلهذا قال: {ولقد عفا عنكم والله ذو فضل على المؤمنين}؛ أي: ذو فضل عظيم عليهم، حيث مَنَّ عليهم بالإسلام، وهداهم لشرائعه، وعفا عنهم سيئاتهم، وأثابهم على مصيباتهم، ومن فضله على المؤمنين أنه لا يُقَدِّرُ عليهم خيراً ولا مصيبةً إلا كان خيراً لهم، إن أصابتهم سرَّاء فشكروا، جازاهم جزاءَ الشاكرين، وإن أصابتهم ضرَّاء فصبروا، جازاهم جزاء الصابرين.
{152} Yani, “Na Mwenyezi Mungu aliwatimilizia ahadi yake” ya ushindi, basi akawapa ushindi juu yao mpaka wakawapa mabega yao. Na mkawa mnawaua mpaka mlipokuwa sababu ya nafsi zenu na msaada kwa maadui zenu dhidi yenu. Na kushindwa ambako ni udhaifu na kulegea kulipotokea kwenu, “na mkazozana katika amri hii” ambalo ndani yake kulikuwepo kuiacha amri ya Mwenyezi Mungu ya kuungana na kutohitalifiana, nanyi mkahitilafiana. Kukawa na mwenye kusema: Tukae katika mahali petu ambapo Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alituweka. Na kukawa na mwenye kusema: Hatutakaa hapa hali ya kuwa adui ameshindwa na hakuna chochote cha kuhofia kilichobakia. Kwa hivyo, mkamuasi Mtume na mkaiacha amri yake, baada ya Mwenyezi Mungu kuwaonyesha yale mnayoyapenda, ambacho ni kutosaidiwa kwa maadui zenu. Kwa sababu wajibu kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu alimneemesha kwa kile anachokipenda ni mkubwa kuliko asiyekuwa yeye. Kwa hivyo, wajibu katika hali hii hasa na katika zisizokuwa hii kwa ujumla ni kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. “Wapo miongoni mwenu wanaotaka dunia.” Nao ndio wale walioletewa na hilo yale lililoleta. “Na wapo miongoni mwenu wanaotaka Akhera.” Nao ndio wale walioshikamana na amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wakasimama imara pale walipoamrishwa, “kisha akawaepusha nao” Yani, baada ya kupatikana kwa mambo haya kutoka kwenu. Basi uso utukufu ni wa maadui zenu kama majaribio kwenu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mtihani, ili abainike Muumini kutoka kwa kafiri, na mtiifu kutoka kwa muasi, na ili Mwenyezi Mungu akufutie kwa msiba huu yale yaliyotokea kutoka kwenu. Na kwa sababu ya hayo, akasema, “Naye amekwisha wasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini.” Yani, Mwenye fadhila kubwa juu yao, kwa maana aliwaneemesha kwa Uislamu, akawaongoa kwenye sheria zake, akawasamehe makosa yao, na akawalipa kwa misiba yao. Na katika fadhila zake juu ya Waumini ni kwamba hawaandikii heri yoyote wala msiba isipokuwa vinakuwa heri kwao. Na wakipatwa na ya furaha na wakashukuru, anawalipa malipo ya wenye kushukuru. Na wakipatwa na mabaya na wakasubiri, anawalipa malipo ya wenye kusubiri.
: 153 - 154 #
{إِذْ تُصْعِدُونَ وَلَا تَلْوُونَ عَلَى أَحَدٍ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ فِي أُخْرَاكُمْ فَأَثَابَكُمْ غَمًّا بِغَمٍّ لِكَيْلَا تَحْزَنُوا عَلَى مَا فَاتَكُمْ وَلَا مَا أَصَابَكُمْ وَاللَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ (153) ثُمَّ أَنْزَلَ عَلَيْكُمْ مِنْ بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُعَاسًا يَغْشَى طَائِفَةً مِنْكُمْ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنْفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ يَقُولُونَ هَلْ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ مِنْ شَيْءٍ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّهِ يُخْفُونَ فِي أَنْفُسِهِمْ مَا لَا يُبْدُونَ لَكَ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَا قُتِلْنَا هَاهُنَا قُلْ لَوْ كُنْتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَى مَضَاجِعِهِمْ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (154)}.
153. Pale mlipokuwa mkikimbia mbio, wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anawaita, yuko nyuma yenu. Basi Mwenyezi Mungu akawapa dhiki juu ya dhiki, ili msisikitike kwa yale yaliyowakosa wala kwa yale yaliyowapata. Na Mwenyezi Mungu ana habari za yote mnayoyatenda. 154. Kisha baada ya dhiki aliwateremshia utulivu - usingizi ambao ulifunika kundi moja kati yenu. Na kundi jingine nafsi zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyokuwa ya haki, dhana ya kijinga. Wakisema: Je, sisi tuna lolote katika jambo hili? Sema: Jambo hili lote ni la Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyokudhihirishia. Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili, tusingeulia papa hapa. Sema: Hata mngelikuwa majumbani mwenu, basi wangelitoka wale walioandikiwa kufa, wakaenda mahali pao pa kuangukia wafe. (Haya ni hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyo katika vifua vyenu, na asafishe yaliyo katika nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.
#
{153} يذكرهم تعالى حالهم في وقت انهزامهم عن القتال، ويعاتبهم على ذلك فقال: {إذ تُصعدون}؛ أي: تَجِدُّون في الهرب {ولا تلوون على أحد}؛ أي: لا يلوي أحد منكم على أحد ولا ينظر إليه، بل ليس لكم هَمٌّ إلا الفرار والنجاء عن القتال، والحال أنه ليس عليكم خطر كبير، إذ لستم آخر الناس مما يلي الأعداء ويباشر الهيجاء، بل {الرسول يدعوكم في أخراكم}؛ أي: مما يلي القوم يقول: «إليَّ عباد الله» ، فلم تلتفتوا إليه ولا عرجتم عليه، فالفرار نفسه موجب للوم، ودعوة الرسول الموجبة لتقديمه على النفس أعظم لوماً بتخلفكم عنها {فأثابكم}؛ أي: جازاكم على فعلكم {غمًّا بغم}؛ أي: غمًّا يتبعه غمٌّ، غمٌّ بفوات النصر وفوات الغنيمة، وغمٌّ بانهزامكم، وغمٌّ أنساكم كل غمٍّ وهو سماعكم أن محمداً - صلى الله عليه وسلم - قد قتل. ولكن الله بلطفه وحسن نظره لعباده جعل اجتماع هذه الأمور لعباده المؤمنين خيراً لهم فقال: {لكيلا تحزنوا على ما فاتكم}؛ من النصر والظفر، {ولا ما أصابكم}؛ من الهزيمة والقتل والجراح إذا تحققتم أن الرسول - صلى الله عليه وسلم - لم يقتل، هانت عليكم تلك المصيبات، واغتبطتم بوجوده المسلي عن كل مصيبة ومحنة، فلله ما في ضمن البلايا والمحن من الأسرار والحكم، وكل هذا صادر عن علمه وكمال خبرته بأعمالكم وظواهركم وبواطنكم، ولهذا قال: {والله خبير بما تعملون}، ويحتمل أن معنى قوله: {لكيلا تحزنوا على ما فاتكم ولا ما أصابكم}؛ يعني: أنه قدَّر ذلك الغم والمصيبة عليكم، لكي تتوطن نفوسكم وتمَرَّنُوا على الصبر على المصيبات، ويخف عليكم تحمل المشقات.
{153} Yeye Mtukufu anawakumbusha hali yao katika wakati wa kushindwa kwao vitani, na anawalaumu juu ya hilo, akasema, “Mlipokuwa mnapanda” Yani, mlipojitahidi katika kutoroka, “wala msimgeukie yeyote” Yani, hakuna yeyote miongoni anayemgeukia mwingine wala kumtazama. Bali hamna hamu yoyote isipokuwa kukimbia tu na kuokoka kutokana na kupigana vita. Na hali ni kwamba hakuna hatari kubwa juu yenu, kwani nyinyi siyo wa mwisho katika watu wanaofuatana na maadui, na wanaokumbana na ghasia. Bali, “Mtume anawaita yuko nyuma yenu.” Yani, kutokea karibu na watu hao (maadui) akisema, “Njooni kwangu enyi waja wa Mwenyezi Mungu.” Lakini hamkugeuka kumwelekea wala hamkumwendea. Kwa hivyo, kukimbia kwenyewe kunasababisha kulaumiwa, na wito wa Mtume unaomlazimu kumtanguliza yeye juu ya nafsi ni kwenye lawama kubwa zaidi kwa kubakia nyuma yake. “Kwa hivyo akawapa,” Yani, akawalipa kwa kitendo chenu “dhiki kwa dhiki.” Yani, dhiki ikifuatwa na dhiki. Dhiki ya kupoteza ushindi na kupoteza ngawira, na dhiki ya kushindwa kwenu, na dhiki iliyowasahaulisha kila dhiki, nayo ni kusikia kwenu kwamba Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ameuawa. Lakini Mwenyezi Mungu kwa upole wake na kwa uangalizi wake mzuri kwa waja wake, akafanya kukusanyika kwa mambo haya kwa waja wake Waumini kuwa heri kwao. Akasema, “Ili msihuzunike kwa yaliyowakosa” ya nusura na ushindi, “wala yaliyowasibu” ya kushindwa, na kuuawa, na majeraha. Mtakapohakikisha kuwa Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - hakuuawa, basi misiba hiyo itakuwa nyepesi kwenu, na mtafurahia kwa uwepo wake unaofariji kila msiba na msukosuko. Basi ni za Mwenyezi Mungu siri na hekima za yaliyomo ndani ya misiba na misukosuko. Na yote haya yanatokana na elimu yake na ukamilifu wa uzoefu wake kwa matendo yenu, na dhahiri zenu, na ndani zenu. Na kwa sababu ya hayo, akasema, “Na Mwenyezi Mungu ana habari za yote mnayotenda.” Na inawezekana kuwa maana ya kauli yake, “Ili msihuzunike kwa yaliyowakosa wala yaliyowasibu.” Yani, Yeye aliyajaalia dhiki hiyo na msiba juu yenu ili nafsi zenu ziwe tayari, na zizoee kuwa na subira juu ya misiba, na iwe rahisi kwenu kuvumilia taabu.
#
{154} {ثم أنزل عليكم من بعد الغم}، الذي أصابكم، {أمنة نُعاساً يغشى طائفة منكم}، ولا شك أن هذا رحمة بهم وإحسان وتثبيت لقلوبهم وزيادة طمأنينة، لأن الخائف لا يأتيه النعاس، لما في قلبه من الخوف، فإذا زال الخوف عن القلب أمكن أن يأتيه النعاس، وهذه الطائفة التي أنعم الله عليها بالنعاس، هم المؤمنون الذين ليس لهم إلا إقامة دين الله ورضا الله ورسوله ومصلحة إخوانهم المسلمين، وأما الطائفة الأخرى الذين {قد أهمتهم أنفسهم}، فليس لهم هَمٌّ في غيرها لنفاقهم أو ضعف إيمانهم، فلهذا لم يصبهم من النعاس ما أصاب غيرهم، {يقولون هل لنا من الأمر من شيء}، وهذا استفهام إنكاري، أي: ما لنا من الأمر، أي: النصر والظهور شيء، فأساؤوا الظنَّ بربهم وبدينه وبنبيه، وظنوا أن الله لا يتم أمر رسوله، وأن هذه الهزيمة هي الفيصلة والقاضية على دين الله. قال الله في جوابهم: {قل إن الأمر كله لله}، الأمر يشمل الأمر القدري والأمر الشرعي، فجميع الأشياء بقضاء الله وقدره، وعاقبتها النصر والظفر لأوليائه وأهل طاعته وإن جرى عليهم ما جرى، {يخفون} يعني المنافقين {في أنفسهم ما لا يبدون لك}، ثم بيَّن الأمر الذي يخفونه فقال: {يقولون لو كان لنا من الأمر شيء}؛ أي: لو كان لنا في هذه الواقعة رأي ومشورة {ما قتلنا ههنا}، وهذا إنكار منهم، وتكذيب بقدر الله، وتسفيه منهم لرأي رسول الله ورأي أصحابه، وتزكية منهم لأنفسهم، فرد الله عليهم بقوله: {قل لو كنتم في بيوتكم} التي هي أبعد شيء عن مظان القتل {لبرز الذين كتب عليهم القتل إلى مضاجعهم}، فالأسباب وإن عظمت إنما تنفع إذا لم يعارضها القدر والقضاء، فإذا عارضها القدر لم تنفع شيئاً، بل لا بد أن يمضي الله ما كتب في اللوح المحفوظ من الموت والحياة {وليبتلي الله ما في صدوركم}؛ أي: يختبر ما فيها من نفاق وإيمان وضعف إيمان، {وليمحص ما في قلوبكم} من وساوس الشيطان وما تأثر عنها من الصفات غير الحميدة {والله عليم بذات الصدور}؛ أي: بما فيها وما أكنته، فاقتضى علمه وحكمته أن قدر من الأسباب ما به تظهر مخبآت الصدور وسرائر الأمور. ثم قال تعالى:
{154} “Kisha akawateremshia baada ya dhiki” iliyowasibu “utulivu – usingizi ambao ulifunika kundi miongoni mwenu.” Na hakuna shaka kuwa hili ni kwa ajili ya kuwarehemu, na wema, na kuimarisha nyoyo zao, na kuzidisha utulivu. Kwa sababu, mwenye hofu hajiwi na usingizi kwa sababu ya hofu iliyo ndani ya moyo wake. Na hofu inapoondoka kutoka katika moyo, inawezekana ajiwe na usingizi. Na kundi hili ambalo Mwenyezi Mungu alilineemesha kwa usingizi, ndio Waumini ambao hawana isipokuwa kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu na radhi za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na masilahi ya ndugu zao Waislamu. Na lile kundi jingine ambao, “nafsi zao ziliwashughulisha,” basi hawana hamu katika wasiokuwa wao, kwa sababu ya unafiki wao au udhaifu wa imani yao. Ndiyo maana hawakupatwa na usingizi kama uliowapata wasiokuwa wao. “Wanasema: Je, tuna lolote katika jambo hili?" Na hili ni swali la kejeli. Yani, sisi hatuna chochote katika jambo hili. Yani, nusura na ushindi ni jambo. Basi wakamdhania vibaya Mola wao Mlezi, na Dini yake, na Nabii wake. Na wakadhania kuwa Mwenyezi Mungu hatakamilisha amri ya Mtume wake. Na kwamba kushindwa huku ndiko hukumu ya mwisho na wenye kuimaliza Dini ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akasema katika kuwajibu, “Sema: Hakika, jambo hili lote ni la Mwenyezi Mungu.” Na jambo linajumuisha amri na kimajaaliwa, na amri ya kisheria. Basi vitu vyote ni kwa mapitisho ya Mwenyezi Mungu na majaaliwa yake. Na mwisho wake ni nusura na ushindi kwa marafiki zake na wale wanaomtii, hata yakiwafika yale yanayowafika, “wanaficha.” Yani wanafiki hao “katika nafsi zao yale wasiyokudhihirishia.” Kisha akabainisha jambo ambalo wanalificha. Akasema, “Wanasema: Lau tungekuwa kitu katika jambo hili.” Yani, lau tungelikuwa na rai na nasaha katika vita hivi, “hatungeuliwa papa hapa.” Na huku ndiko kukanusha kwao, na kukanusha hukumu ya Mwenyezi Mungu, na kuona kwao kwamba rai ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na rai ya maswahaba zake ni upumbavu, na kujitaka kwao nafsi zao. Basi Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake, “Sema: Hata mngelikuwa majumbani mwenu” ambayo ndiyo yako mbali mno na mahali penye uwezekano mkubwa wa kuuawa, “wangetoka wale walioandikiwa kuuawa hadi mahali pao pa kuangukia wake.” Kwa hivyo sababu, hata zikiwa kubwa vipi, zinafaa iwapo tu hazipingani na hukumu na majaaliwa. Lakini hukumu ikipingana nazo, basi hazinufaishi kitu. Bali Mwenyezi Mungu ni lazima apitishe yale aliyoandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa ya mauti na uhai. “Na ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyo katika vifua vyenu.” Yani, anayajaribu yaliyo ndani yake ya unafiki, na Imani, na udhaifu wa imani. “Na ili ayasafishe yaliyo katika nyoyo zenu” ya minong'ono ya Shetani na yanayotokana na hayo ya sifa zisizokuwa nzuri. “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye anayajua yaliyomo vifuani.” Yani, yaliyo ndani yake, na yale vinavyoficha. Kwa hivyo, elimu yake na hekima yake vikalazimu kwamba aliweka sababu ambazo kwazo zinadhihirika siri za vifua na siri za mambo. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
: 155 #
{إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْا مِنْكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا وَلَقَدْ عَفَا اللَّهُ عَنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ (155)}.
155. Hakika, wale waliogeuka wakakimbia miongoni mwenu siku yalipokutana makundi mawili, hakika Shetani tu ndiye aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyoyafanya. Na Mwenyezi Mungu amekwisha wasamehe. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole.
#
{155} يخبر تعالى عن حال الذين انهزموا يوم أُحد، وما الذي أوجب لهم الفرار وأنه من تسويل الشيطان، وأنه تسلط عليهم ببعض ذنوبهم، فهم الذين أدخلوه على أنفسهم ومكنوه بما فعلوا من المعاصي لأنها مركبة ومدخلة، فلو اعتصموا بطاعة ربهم لما كان له عليهم من سلطان، قال تعالى: {إن عبادي ليس لك عليهم سلطان}، ثم أخبر أنه عفا عنهم بعد ما فعلوا ما يوجب المؤاخذة، وإلا فلو آخذهم لاستأصلهم {إن الله غفور} للمذنبين الخطائين بما يوفقهم له من التوبة والاستغفار والمصائب المكفرة {حليم} لا يعاجل من عصاه بل يستأني به ويدعوه إلى الإنابة إليه والإقبال عليه، ثم إن تاب، وأناب قبل منه، وصيره كأنه لم يجر منه ذنب، ولم يصدر عنه عيب. فلله الحمد على إحسانه.
{155} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya wale walioshindwa Siku ya Uhud, na yale yaliyowaletea kukimbia. Na kwamba ni katika kushawishi kwa Shetani, na kwamba aliwatawala kwa sababu ya baadhi ya dhambi zao. Wao ndio waliomwingiza katika nafsi zao na wakamwezesha kwa sababu ya yale waliyoyafanya ya maasia, kwa hayo ndiyo pahali pa kupandia na pa kuingilia. Na lau wangeshikamana na utiifu kwa Mola wao Mlezi, asingekuwa na mamlaka juu yao. Yeye Mtukufu alisema, “Hakika waja wangu, wewe huna mamlaka yoyote juu yao.” Kisha akajulisha kuwa aliwasamehe baada ya wao kufanya yenye kusababisha kuadhibiwa. Vinginevyo, lau angewaadhibu, basi angewaangamiza. “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole;” kwa wafanyao dhambi, wakosefu kwa yale anayowawezesha ya kutubia na kuomba kufutiwa dhambi na misiba yenye kufuta dhambi. “Mpole” Yeye hamharakishii yule anayemuasi (kumwadhibu). Bali humpa muhula na kumuita arejee na aelekee kwake. Kisha akitubu na akarudi kwake, anamkubalia, na anamfanya kuwa kana kwamba dhambi yoyote haikutokea kwake, na wala kasoro yoyote hakutokea kwake. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa wema wake.
: 156 - 158 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَوْ كَانُوا عِنْدَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّهُ ذَلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ وَاللَّهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (156) وَلَئِنْ قُتِلْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِنَ اللَّهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ (157) وَلَئِنْ مُتُّمْ أَوْ قُتِلْتُمْ لَإِلَى اللَّهِ تُحْشَرُونَ (158)}.
156. Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakawaambia ndugu zao wanaposafiri katika nchi au wanapokuwa vitani: Lau wangelikuwa nasi, wasingelikufa na wasingeliuwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo kuwa ni majuto makubwa katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayoyatenda. 157. Na mkiuliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, au mkifa, hakika kufutiwa dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na rehema ni bora kuliko yale wanayoyakusanya. 158. Na mkifa au mkiuliwa, basi ni kwa Mwenyezi Mungu ndiko mtakakokusanywa.
#
{156} ينهى تعالى عباده المؤمنين أن يشابهوا الكافرين، الذين لا يؤمنون بربهم ولا بقضائه وقدره من المنافقين وغيرهم، ينهاهم عن مشابهتهم في كل شيء وفي هذا الأمر الخاص وهم أنهم يقولون لإخوانهم في الدين أو في النسب {إذا ضربوا في الأرض}؛ أي: سافروا للتجارة {أو كانوا غزًّى}؛ أي: غزاة ثم جرى عليهم قتل أو موت يعارضون القدر ويقولون: {لو كانوا عندنا ما ماتوا وما قُتلوا} وهذا كذب منهم، فقد قال تعالى: {قل لو كنتم في بيوتكم لبرز الذين كتب عليهم القتل إلى مضاجعهم}، ولكن هذا التكذيب لم يفدهم، إلا أن الله يجعل هذا القول وهذه العقيدة حسرة في قلوبهم، فتزداد مصيبتهم، وأما المؤمنون فإنهم يعلمون أن ذلك بقدر الله فيؤمنون ويسلمون فيهدي الله قلوبهم ويثبتها ويخفف بذلك عنهم المصيبة، قال الله ردًّا عليهم: {والله يحيي ويُميت}؛ أي: هو المتفرد بذلك فلا يغني حذر عن قدر، {والله بما تعملون بصير}؛ فيجازيكم بأعمالكم وتكذيبكم.
{156} Yeye Mtukufu anawakataza waja wake Waumini kujifananisha na makafiri, ambao hawamuamini Mola wao Mlezi wala hukumu yake na majaliwa yake miongoni mwa wanafiki na wengineo. Aliwakataza kujifananisha nao katika kila kitu, na katika jambo hili hasa. Nalo ni kwamba wao wanawaambia ndugu zao katika dini au katika nasaba. “Wanaposafiri katika nchi.” Yani, wanaposafiri kwa ajili ya biashara “au wanapokuwa vitani” kisha wakapatwa na mauaji au wakafa, wanayapinga majaliwa na wanasema. “Lau wangelikuwa nasi, wasingelikufa na wasingeliuawa.” Na huu ni uongo kutoka kwao. Yeye Mtukufu alikwisha sema, “Sema: Hata mngelikuwa majumbani mwenu, wangetoka wale walioandikiwa kuuawa hadi mahali pao pa kuangukia wafe.” Lakini kukanusha huku hakukuwafaa, isipokuwa tu Mwenyezi Mungu aliifanya kauli hii na itikadi hii kuwa majuto makubwa katika nyoyo zao, ndio msiba wao uongezeke. Na ama Waumini, wao wanajua ya kwamba hayo ni kwa majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, wanaamini na wanasalimu amri. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu huziongoza nyoyo zao na kuziimarisha, na anaepesishwa misiba kwa hayo. Mwenyezi Mungu alisema akiwajibu, “Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha.” Yani, Yeye peke yake ndiye anayeweza hayo. Kwa hivyo, tahadhari haifai kitu mbele ya majaliwa. “Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayoyafanya” na atawalipa kwa matendo yenu na kukadhibisha kwenu.
#
{157} ثم أخبر تعالى أن القتل في سبيله أو الموت فيه، ليس فيه نقص ولا محذور، وإنما هو مما ينبغي أن يتنافس فيه المتنافسون، لأنه سبب مفضٍ وموصل إلى مغفرة الله ورحمته، وذلك خير مما يجمع أهل الدنيا من دنياهم.
{157} Kisha Yeye Mtukufu akajulisha kwamba kuuawa katika njia yake au kufa ndani yake hakuna upungufu wala kinachokatazwa. Bali, ni katika yale ambayo inafaa washindane juu yake wale wanaoshindana. Kwa kuwa, hilo ni sababu inayopelekea na kufikisha kwenye kufutiwa dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na rehema zake. Na hilo ni bora zaidi kuliko kile ambacho watu wa dunia wanakikusanya kutoka katika dunia yao.
#
{158} وأن الخلق أيضاً إذا ماتوا، أو قتلوا بأي حالة كانت، فإنما مرجعهم إلى الله ومآلهم إليه، فيجازي كلاًّ بعمله، فأين الفرار إلا إلى الله، وما للخلق عاصم إلا الاعتصام بحبل الله.
{158} Na kwamba viumbe pia wanapokufa au wakiuliwa katika hali yoyote ile, basi marejeo yao na maishio yao ni kwa Mwenyezi Mungu tu, naye atamlipa kila mmoja kwa matendo yake. Basi ni wapi pa kukimbilia isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu? Na viumbe havina ulinzi isipokuwa kushikamana kwa kamba ya Mwenyezi Mungu.
: 159 #
{فَبِمَا رَحْمَةٍ مِنَ اللَّهِ لِنْتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنْتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانْفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ (159)}.
159. Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia. Basi wasamehe, na waombee kufutiwa dhambi, na shauriana nao katika mambo. Na ukishakata shauri, basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaomtegemea.
#
{159} أي: برحمة الله لك ولأصحابك، منَّ الله عليك أن ألنت لهم جانبك وخفضت لهم جناحك، وترققت عليهم، وحسنت لهم خلقك، فاجتمعوا عليك، وأحبوك وامتثلوا أمرك، {ولو كنت فظاً}؛ أي: سيئ الخلق {غليظ القلب}؛ أي: قاسيه، {لانفضوا من حولك} لأن هذا ينفرهم ويبغضهم لمن قام به هذا الخلق السيئ، فالأخلاق الحسنة من الرئيس في الدين تجذب الناس إلى دين الله وترغبهم فيه، مع ما لصاحبه من المدح والثواب الخاص، والأخلاق السيئة من الرئيس في الدين تنفر الناس عن الدين وتبغضهم إليه، مع ما لصاحبها من الذم والعقاب الخاص. فهذا الرسول المعصوم يقول الله له ما يقول، فكيف بغيره؟ أليس من أوجب الواجبات وأهم المهمات الاقتداء بأخلاقه الكريمة، ومعاملة الناس بما يعاملهم به - صلى الله عليه وسلم -، من اللين وحسن الخلق والتأليف؟ امتثالاً لأمر الله وجذباً لعباد الله لدين الله؟ ثم أمر الله تعالى بأن يعفو عنهم ما صدر منهم من التقصير في حقه - صلى الله عليه وسلم - ويستغفر لهم في التقصير في حق الله فيجمع بين العفو والإحسان، {وشاورهم في الأمر}؛ أي: الأمور التي تحتاج إلى استشارة ونظر وفكر، فإن في الاستشارة من الفوائد والمصالح الدينية والدنيوية ما لا يمكن حصره: منها: أن المشاورة من العبادات المتقرب بها إلى الله. ومنها: أن فيها تسميحاً لخواطرهم وإزالة لما يصير في القلوب عند الحوادث، فإنَّ مَنْ له الأمرُ على الناس إذا جمع أهل الرأي والفضل، وشاورهم في حادثة من الحوادث، اطمأنت نفوسهم وأحبوه وعلموا أنه ليس يستبد عليهم، وإنما ينظر إلى المصلحة الكلية العامة للجميع، فبذلوا جهدهم ومقدورهم في طاعته لعلمهم بسعيه في مصالح العموم، بخلاف من ليس كذلك فإنهم لا يكادون يحبونه محبة صادقة ولا يطيعونه، وإن أطاعوه فطاعة غير تامة. ومنها: أن في الاستشارة تنور الأفكار بسبب إعمالها فيما وضعت له، فصار في ذلك زيادة للعقول. ومنها: ما تنتجه الاستشارة من الرأي المصيب، فإن المشاور لا يكاد يخطئ في فعله، وإن أخطأ أو لم يتم له مطلوب فليس بملوم. فإذا كان الله يقول لرسوله - صلى الله عليه وسلم - ـ وهو أكمل الناس عقلاً وأغزرهم علماً وأفضلهم رأياً ـ: {وشاورهم في الأمر}، فكيف بغيره؟ ثم قال تعالى: {فإذا عزمت}؛ أي: على أمر من الأمور بعد الاستشارة فيه إن كان يحتاج إلى استشارة {فتوكل على الله}؛ أي: اعتمد على حول الله وقوته متبرئاً من حولك وقوتك، {إن الله يحب المتوكلين} عليه اللاجئين إليه.
{159} Yani, kwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwako na kwa masahaba wako, Mwenyezi Mungu alikuneemesha kuwa uliwalainishia upande wako, na ukawainamishia bawa lako, na ukawafanyia huruma, na ukawafanyia tabia yako kuwa nzuri. Kwa hivyo, wakakukusanyikia, na wakakupenda, na wakatekeleza amri yako. “Na lau ungelikuwa mkali” Yani, wa tabia mbaya “mwenye moyo mgumu” yani moyo sugu “bila ya shaka wangelikukimbia.” Kwa sababu, hilo linawafanya kujitenga na kumchukia anayefanya tabia hii mbaya. Kwani maadili mema kutoka kwa kiongozi katika dini yanawavuta watu kwenye dini ya Mwenyezi Mungu na kuwahimiza kwayo, pamoja na kile anachosifika mwenyewe cha sifa na malipo maalumu. Na maadili mabaya kutoka kwa kiongozi katika dini yanawaepusha watu na dini, na kuwafanya waichukie, pamoja na kile anachosifika mwenyewe kwacho cha kashfa na adhabu maalumu. Basi, huyu ndiye Mtume asiyekosea, Mwenyezi Mungu anamwambia anachomwambia, basi itakuwa vipi kuhusu asiyekuwa yeye? Je, si ni miongoni mwa wajibu za wajibu zote? Na majukumu muhimu ya majukumu yote kuyafuata maadili yake matukufu? Na kuamiliana na watu kwa namna anavyoamiliana nao yeye, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ya kuwa laini, na wa tabia njema, na kuunganisha? Kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na kuwavuta waja wa Mwenyezi Mungu kwenye dini ya Mwenyezi Mungu? Kisha Yeye Mtukufu akamwamrisha awasamehe yale yaliyotoka kwao ya uzembe wao katika haki yake yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – naye awaombee kufutiwa dhambi katika uzembe wao katika haki za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, awe amejumuisha kati ya kusamehe na kufanya wema. “Na shauriana nao katika mambo.” Yani, mambo ambayo yanahitaji mashauriano, na kuangaliwa vizuri, na kutafakari. Kwa maana, katika kushauriana kuna manufaa na masilahi mengi ya kidini na ya kidunia ambayo hayawezi kuwekewa mipaka. Miongoni mwake ni kwamba, kushauriana ni katika ibada za kujileta kwazo karibu na Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwake ni kwamba, ndani yake kuna kutuliza fikira zao na kuondoa yale yanaiyongia ndani ya nyoyo wakati matukio yanapotokea. Kwa sababu, mwenye mamlaka juu ya watu anapowakusanya watu wenye maono na fadhila, na akashauriana nao katika tukio miongoni mwa matukio, nafsi zao zinatua na wanampenda na wanajua kwamba yeye hawanyanyasi; bali anaangalia masilahi ya jumla ya wote. Kwa hivyo, wanafanya juhudi zao na uwezo wao katika kumtii, kwa sababu ya kujua kwao kwamba yeye anajitahidi katika masilahi ya umma; tofauti na yule ambaye si hivyo. Kwa sababu wao hawakaribii kumpenda upendo wa kweli, wala hawamtii. Na hata wakimtii, basi ni utii usio kamili. Na miongoni mwake ni kwamba, katika kushauriana mawazo hutiwa nuru kwa sababu ya kuyatumia katika yale yaliyowekwa kwa ajili yake. Kwa hivyo, ikawa katika hilo kuna kuongezeka kwa akili. Na miongoni mwake, ni yale yanayotokana na mashauriano kama vile maoni sahihi. Kwa sababu, mwenye kutafuta ushauri, hakaribii kufanya makosa katika matendo yake. Na hata akikosea au hayakutimia mahitaji yake, basi yeye halaumiwi. Basi ikiwa Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – hali ya kuwa yeye ndiye mkamilifu wa watu katika akili, na mwingi wao wa elimu, na mbora wao katika maoni. “Na shauriana nao katika mambo.” Basi itakuwa vipi asiyekuwa yeye? Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Na ukishaazimia,” yani, katika jambo miongoni mwa mambo baada ya kutafuta ushauri juu yake ikiwa linahitaji mashauriano; “basi mtegemee Mwenyezi Mungu.” Yani, kutegemea uwezo wa Mwenyezi Mungu na nguvu zake, ukijitenga na uwezo wako na zako. “Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaomtegemea” yeye; wanaokimbilia kwake.
: 160 #
{إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ (160)}.
160. Akiwanusuru (nyinyi) Mwenyezi Mungu, hapana wa kuwashinda. Na asipowasaidia, basi ni nani huyo baada yake atayewanusuru? Na kwa Mwenyezi Mungu tu, basi na wategemee Waumini.
#
{160} أي: إن يمددكم الله بنصره ومعونته {فلا غالب لكم}، فلو اجتمع عليكم مَنْ في أقطارها وما عندهم من العَدَد والعُدَد لأن الله لا مغالب له، وقد قهر العباد وأخذ بنواصيهم، فلا تتحرك دابة إلا بإذنه، ولا تسكن إلا بإذنه، {وإن يخذلكم} ويكلكم إلى أنفسكم {فمن ذا الذي ينصركم من بعده}، فلا بد أن تنخذلوا ولو أعانكم جميع الخلق، وفي ضمن ذلك الأمر بالاستنصار بالله والاعتماد عليه والبراءة من الحول والقوة، ولهذا قال: {وعلى الله فليتوكل المؤمنون}، تقدم المعمول يؤذن بالحصر، أي: على الله توكلوا لا على غيره، لأنه قد علم أنه هو الناصر وحده، فالاعتماد عليه توحيد محصل للمقصود، والاعتماد على غيره شرك غير نافع لصاحبه بل ضار، وفي هذه الآية الأمر بالتوكل على الله وحده، وأنه بحسب إيمان العبد يكون توكله.
{160} Yani, ikiwa Mwenyezi Mungu atawapa nusura yake na msaada wake, “basi hapana wa kuwashinda.” Hata wakiwakusanyikia wote walio katika maeneo yake na kile walicho nacho katika idadi na maandalizi. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hana wa kumshinda. Na aliwashinda waja na akawachukua kwa nywele zao za upande wa mbele ya kichwa, basi hasongi mnyama yeyote isipokuwa kwa idhini yake, wala hatulii isipokuwa kwa idhini yake. “Na asipowasaidia” na akawaachia nafsi zenu “basi ni nani huyo baada yake atakayewanusuru?” Basi hakuna budi kwamba mtashindwa hata kama viumbe vyote vitawasaidia. Na ndani ya hayo, kuna amri ya kuomba msaada kwa Mwenyezi Mungu na kumtegemea Yeye na kujitenga na kuwa na nguvu na uwezo. Na ndiyo maana akasema, “Na kwa Mwenyezi Mungu tu, basi na wategemee Waumini.” Na kutanguliza mtendwa, kunaidhinisha kumwekea mipaka. Yani, kwa Mwenyezi Mungu, tegemeeni, na si kwa asiyekuwa Yeye. Kwa sababu ilikwisha julikana kuwa Yeye pekee ndiye msaidizi. Kwa hivyo kumtegemea Yeye ni upwekeshaji unaoleta kile kilichokusudiwa. Na kumtegemea asiyekuwa Yeye ni shirki isiyo na manufaa kwa mwenyewe, bali ni yenye madhara. Na katika Aya hii kuna amri ya kumtegemea Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba kulingana na imani ya mja kunakuwa kutegemea kwake.
: 161 #
{وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَغُلَّ وَمَنْ يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (161)}.
161. Na haikuwa kwa Nabii yeyote kufanya hiyana. Na atakayefanya hiyana, atakuja Siku ya Kiyama na kile alichofanyia hiyana, kisha kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa.
#
{161} الغلول: هو الكتمان من الغنيمة والخيانة في كل مالٍ يتولاه الإنسان وهو محرَّم إجماعاً، بل هو من الكبائر كما تدل عليه هذه الآية الكريمة وغيرها من النصوص، فأخبر الله تعالى أنه ما ينبغي ولا يليق بنبي أن يغل، لأن الغلول ـ كما علمت ـ من أعظم الذنوب وشر العيوب. وقد صان الله تعالى أنبياءه عن كل ما يدنسهم ويقدح فيهم، وجعلهم أفضل العالمين أخلاقاً وأطهرهم نفوساً، وأزكاهم وأطيبهم ونزههم عن كل عيب، وجعلهم محل رسالته ومعدن حكمته، {الله أعلم حيث يجعل رسالته}، فبمجرد علم العبد بالواحد منهم يجزم بسلامتهم من كل أمر يقدح فيهم، ولا يحتاج إلى دليل على ما قيل فيهم من أعدائهم، لأن معرفته بنبوتهم مستلزم لدفع ذلك، ولذلك أتى بصيغة يمتنع معها وجود الفعل منهم فقال: {وما كان لنبي أن يغل}؛ أي: يمتنع ذلك ويستحيل على من اختارهم الله لنبوته. ثم ذكر الوعيد على من غل فقال: {ومن يغلل يأت بما غل يوم القيامة}؛ أي: يأت به حامله على ظهره حيواناً كان أو متاعاً أو غير ذلك يعذب به يوم القيامة {ثم توفى كل نفس ما كسبت}؛ الغالُّ وغيره كلٌّ يوفَّى أجره ووزره على مقدار كسبه {وهم لا يظلمون}؛ أي: لا يزداد في سيئاتهم ولا يهضمون شيئاً من حسناتهم. وتأمل حسن هذا الاحتراز في هذه الآية الكريمة لمَّا ذكر عقوبة الغالِّ وأنه يأتي يوم القيامة بما غله، ولمَّا أراد أن يذكر توفيته وجزاءه وكان اقتصاره على الغال يوهم بالمفهوم أن غيره من أنواع العاملين قد لا يوفون، أتى بلفظ عامٍّ جامع له ولغيره.
{161} Al-Ghulul ni kuficha katika ngawira na kufanya hiyana katika kila mali anayoisimamia mtu. Nayo imeharamishwa kwa kauli moja. Bali, ni katika dhambi kubwa, kama inavyoonyesha na aya hii tukufu na maandiko mengineyo. Kwa hivyo, Yeye Mtukufu akajulisha kwamba haifai wala haiendani na Nabii yeyote kufanya uhaini. Kwa sababu uhaini - kama ulivyojua - ni katika dhambi kubwa zaidi na kasoro mbaya zaidi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwalinda Manabii wake kutokana na kila kinachowachafua, na kuwatia dosari. Na akawafanya kuwa bora zaidi wa walimwengu katika maadili na wasafi wao zaidi wa nafsi, na waliotakasika wao zaidi, na wazuri wao zaidi. Na akawaepusha na kila dosari. Na akawafanya kuwa mahali pa ujumbe wake na johari za hekima yake. "Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anaweka ujumbe wake." Na mara tu mja anapojua kuhusu mmoja miongoni mwao, anakuwa na uhakika kwamba wamesalimika kutokana na kila jambo lenye kuwatia dosari. Na wala hahitaji ushahidi wowote kwa yale yaliyosemwa juu yao na maadui zao. Kwa sababu, kujua kwake unabii wao kunalazimu kuzuia hilo. Na ndiyo maana akaja na mbinu inayozuia kuwepo kwa kitendo kutoka kwao. Akasema, "Na haikuwa kwa Nabii yeyote kufanya hiyana." Yani, hilo haliwezekani na ni muhali kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwachagua kwa unabii wake. Kisha akataja ahadi ya adhabu kwa mwenye kufanya hiyana. Akasema, "Na atakayefanya hiyana, atakuja Siku ya Kiyama na kile alichofanyia hiyana." Yani atakuja nacho hali ya kuwa amekibeba juu ya ya mgongo wake, awe ni mnyama au bidhaa au kitu kingine chochote. Ataadhibiwa kwacho Siku ya Kiyama. "Kisha kila nafsi italipwa kwa iliyoyachuma kwa ukamilifu." Hiyana na mengineyo. Kila mmoja atalipwa kwa ukamilifu ujira wake na mzigo wake kwa kiwango cha kuchuma kwake. "Nao hawatadhulumiwa." Yani, hawatazidishiwa katika maovu yao, na wala hawatapunjwa kitu katika mema yao. Na tafakari kuondoa huku kuzuri katika Aya hii tukufu alipotaja adhabu ya mwenye kufanya hiyana, na kwamba atakuja Siku ya Kiyama na kile alichohaini. Na alipotaka kutaja kukamilisha kwake na malipo yake, na kukawa kusimamia kwake kwa mwenye kufanya hiyana, kunaweza kuleta dhana ya maana isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba, asiyekuwa yeye miongoni mwa watendao matendo huenda wasikamilishiwe. Akaja na neno la jumla lenye kumjumuisha yeye na asiyekuwa yeye.
: 162 - 163 #
{أَفَمَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَ اللَّهِ كَمَنْ بَاءَ بِسَخَطٍ مِنَ اللَّهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (162) هُمْ دَرَجَاتٌ عِنْدَ اللَّهِ وَاللَّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ (163)}.
162. Je, aliyeyafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule aliyerudi na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makazi yake yakawa Jahannamu? Napo ndipo pahali pabaya mno pa kurejea. 163. Hao wana vyeo mbalimbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo.
#
{162 - 163} يخبر تعالى أنه لا يستوي من كان قصده رضوان رَبِّه والعمل على ما يرضيه كمن ليس كذلك ممن هو مكب على المعاصي مسخط لربه، هذان لا يستويان في حكم الله وحكمة الله وفي فِطَر عباد الله {أفمن كان مؤمناً كمن كان فاسقاً لا يستوون}؛ لهذا قال هنا: {هم درجات عند الله}؛ أي: كل هؤلاء متفاوتون في درجاتهم ومنازلهم بحسب تفاوتهم في أعمالهم. فالمتبعون لرضوان الله يسعون في نيل الدرجات العاليات والمنازل والغرفات، فيعطيهم الله من فضله وجوده على قدر أعمالهم، والمتبعون لمساخط الله يسعون في النزول في الدركات إلى أسفل سافلين كل على حسب عمله، والله بصير بأعمالهم لا يخفى عليه منها شيء، بل قد علمها وأثبتها في اللوح المحفوظ ووكل ملائكته الأمناء الكرام أن يكتبوها ويحفظوها ويضبطوها.
{162 - 163} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba, hatoshani yule ambaye makusudio yake ni kumridhisha Mola wake Mlezi na kutenda yale yanayomridhisha; si sawa na yule ambaye si hivyo miongoni mwa wale ambao walijibwaga katika maasia, mwenye kumkasirikia Mola wake Mlezi. Wawili hawa hawatoshani katika hukumu ya Mwenyezi Mungu na hekima Mwenyezi Mungu na katika maumbile ya asili ya waja wa Mwenyezi Mungu. “Ati yule ambaye ni Muumini ni kama yule aliyepindukia mipaka? Hawawi sawa.” Ndiyo maana akasema hapa, “Hao wana vyeo mbalimbali kwa Mwenyezi Mungu.” Yani, wote hawa wanatofautiana katika daraja zao na vyeo vyao kulingana na tofauti zao katika matendo yao. Kwa hivyo, wale wanaofuata radhi za Mwenyezi Mungu, hujitahidi katika kuzifikia daraja za juu, na nyumba na vyumba. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu huwapa katika fadhila zake na ukarimu wake kwa kiwango cha matendo yao. Nao wale wanaofuata yenye kumghadhabisha Mwenyezi Mungu hutafuta kuteremka katika matabaka hadi wa chini wa walio chini kabisa, kila mmoja kulingana na matendo yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona matendo yao. Hayafichiki kwake kitu kwayo. Bali alikwisha yajua na akayaandika katika Ubao Uliohifadhiwa, na akawaweka Malaika wake waaminifu watukufu kwamba wayaandike na wayahifadhi, na wayadhibiti.
: 164 #
{لَقَدْ مَنَّ اللَّهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِنْ كَانُوا مِنْ قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (164)}.
164. Hakika, Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini alipowaletea Mtume kutoka miongoni mwao wenyewe, anayewasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi.
#
{164} هذه المنَّةُ التي امتنَّ الله بها على عباده أكبر النعم بل أصلها، وهي الامتنان عليهم بهذا الرسول الكريم الذي أنقذهم الله به من الضلالة، وعصمهم به من الهلكة فقال: {لقد منَّ الله على المؤمنين إذ بعث فيهم رسولاً من أنفسهم}؛ يعرفون نسبه وحاله ولسانه من قومهم وقبيلتهم ناصحاً لهم مشفقاً عليهم يتلو عليهم آيات الله؛ يعلمهم ألفاظها ومعانيها {ويزكيهم}؛ من الشرك والمعاصي والرذائل وسائر مساوئ الأخلاق {ويعلمهم الكتاب}؛ إما جنس الكتاب الذي هو القرآن فيكون قوله: {يتلو عليهم آياته}؛ المراد به الآيات الكونية، أو المراد بالكتاب هنا الكتابة فيكون قد امتنَّ عليهم بتعليم الكتاب والكتابة التي بها تدرك العلوم وتحفظ {والحكمة}؛ هي: السنة التي هي شقيقة القرآن، أو وضع الأشياء مواضعها ومعرفة أسرار الشريعة فجمع لهم بين تعليم الأحكام وما به تُنَفَّذ الأحكام وما به تدرك فوائدها وثمراتها ففاقوا بهذه الأمور العظيمة جميع المخلوقين، وكانوا من العلماء الربانيين {وإن كانوا من قبل}؛ بعثة هذا الرسول {لفي ضلال مبين}؛ لا يعرفون الطريق الموصل إلى ربهم، ولا ما يزكي النفوس، ويطهرها، بل ما يزين لهم جهلهم فعلوه، ولو ناقض ذلك عقول العالمين!
{164} Neema hii ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake ndiyo neema kubwa zaidi. Bali ndiyo asili yake. Nayo ni kuwaneemesha kwa Mtume huyu mtukufu ambaye kwaye Mwenyezi Mungu aliwaokoa kutokana na upotovu, na akawalinda kwaye na kutokana na kuangamia. Akasema, “Hakika, Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa Waumini alipowaletea Mtume kutoka miongoni mwao wenyewe.” Wanaijua nasaba yake, na hali yake, na lugha yake. Ni wa kutoka kwa watu wao, na kabila lao. Ni mwenye kuwanasihi, mwenye kuwahurumia. Anawasomea Aya za Mwenyezi Mungu. Anawafundisha matamshi yake na maana zake. “Anawatakasa” kutokana na ushirikina, na maasia, na machafu, tabia zote mabaya. “Na anawafundisha Kitabu.” Ima ni hiki kitabu ambacho ni Qur-ani, basi inakuwa kauli yake, “Anawasomea Aya zake.” Kinachokusudiwa nayo ni ishara za kiulimwengu, au kinachomaanishwa na kitabu hapa ni kuandika, basi anakuwa aliwaneemesha kwa kuwafundisha kitabu na kuandika ambako kwako elimu zinafahamika na kuhifadhiwa. “Na hekima.” Nayo ni Sunnah ambayo ni dada wa Qur-ani, au kuweka vitu pahali pake na kujua siri za Sharia. Basi akawakusanyia kuwafunza hukumu na kile ambacho kwacho hukumu zinatekelezwa, na kile ambacho kwacho yanapatikana manufaa yake na matunda yake. Basi wakawapita viumbe vyote kwa mambo haya makubwa, na wakawa miongoni mwa wanachuoni wanaomuabudu Mola wao Mlezi peke yake. “Ijapokuwa kabla ya hapo,” yani, kutumwa kwa Mtume huyu; “walikuwa katika upotovu ulio wazi.” Hawaijui njia yenye kufikisha kwa Mola wao Mlezi, wala yale yenye kutakasa nafsi na kuzitakasa. Lakini yale yenye kuwapambia ujinga wao, wanayafanya hata kama hayo yanapingana na mawazo ya walimwengu.
: 165 - 168 #
{أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُمْ مُصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُمْ مِثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّى هَذَا قُلْ هُوَ مِنْ عِنْدِ أَنْفُسِكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (165) وَمَا أَصَابَكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ فَبِإِذْنِ اللَّهِ وَلِيَعْلَمَ الْمُؤْمِنِينَ (166) وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ نَافَقُوا وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا قَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوِ ادْفَعُوا قَالُوا لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَاتَّبَعْنَاكُمْ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَانِ يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِمْ مَا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ (167) الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنْفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (168)}.
165. Nyinyi mlipopatwa na msiba ambao nyinyi mmekwisha watia mara mbili mfano wake, mkasema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo umetoka kwenu wenyewe. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu. 166. Na yale yaliyowapata siku yalipokutana makundi mawili, yalikuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awajue Waumini. 167. Na ili awajue wale waliofanya unafiki, walipoambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: Tungelijua kuna kupigana vita, bila ya shaka tungeliwafuata. Wao siku ile walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyaficha. 168. Wale waliowaambia ndugu zao, na wao wenyewe walikuwa wamekaa: Lau wangelitutii, wasingeliuliwa. Sema: Ziondoleeni nafsi zenu mauti kama nyinyi ni wakweli.
#
{165} هذا تسلية من الله تعالى لعباده المؤمنين حين أصابهم ما أصابهم يوم أحد وقتل منهم نحو سبعين، فقال الله: إنكم {قد أصبتم}؛ من المشركين {مثليها} [يوم بدر]؛ فقتلتم سبعين من كبارهم وأسرتم سبعين، فَلْيَهُنِ الأمرُ ولِتَخِفَّ المصيبةُ عليكم مع أنكم لا تستوون أنتم وهم، فإن قتلاكم في الجنة وقتلاهم في النار، {قلتم أنى هذا}؛ أي: من أين أصابنا ما أصابنا وهزمنا؟ {قل هو من عند أنفسكم}؛ حين تنازعتم وعصيتم من بعد ما أراكم ما تحبون، فعودوا على أنفسكم باللوم واحذروا من الأسباب المردية {إن الله على كل شيء قدير}؛ فإياكم وسوء الظن بالله، فإنه قادر على نصركم، ولكن له أتم الحكمة في ابتلائكم ومصيبتكم ذلك، ولو شاء الله لانتصر منهم، ولكن ليبلوَ بعضكم ببعض.
{165} Huku ni kufariji kutokako kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake Waumini wakati yalipowasibu yale yaliyowasibu siku ya Uhud, waliuawa miongoni mwao wapatao sabini, Mwenyezi Mungu akasema: Nyinyi kwa hakika, “nyinyi mmekwisha wasibu” miongoni mwa washirikina “mara mbili mfano wake” [siku ya Badr]. Basi mkawaua sabini katika wakuu wao, na mkawateka sabini. Basi na liwe jepesi jambo hili, na ukawe msiba mwepesi juu yenu, pamoja na kuwa nyinyi na wao hamko sawa. Kwa maana, wale wenu waliouawa wako Peponi, na wale wao waliouwawa wako Motoni. “Mkasema: Umetoka wapi huu?” Yani, yametusibu kutokea wapi yaliyotusibu na tukashindwa? “Sema: Huo umetoka kwenu wenyewe.” Wakati mlipozozana na mkaasi baada ya Yeye kuwaonyesha yale mnayoyapenda. Basi zirudishieni nafsi zenu lawama, na jihadharini kutokana na sababu za kupotoka. “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.” Kwa hivyo, jihadhari na kuwa na dhana mbaya na Mwenyezi Mungu. Kwani yeye ni muweza wa kuwanusuru, lakini ana hekima kamili zaidi katika majaribio yenu na misibu yenu hiyo. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, angeliwashinda. Lakini ni ili awajaribu nyinyi kwa nyinyi.
#
{166 - 167} ثم أخبر أن ما أصابهم يوم التقى الجمعان: جمعُ المسلمين وجمعُ المشركين في أحد من القتل والهزيمة، أنه بإذنه وقضائه وقدره، لا مرد له ولا بد من وقوعه، والأمر القدري إذا نفذ لم يبق إلا التسليم له وأنه قدَّره لحكم عظيمة وفوائد جسيمة، وأنه ليتبين بذلك المؤمن من المنافق الذين لما أمروا بالقتال {وقيل لهم تعالوا قاتلوا في سبيل الله}؛ أي: ذبًّا عن دين الله وحماية له وطلباً لمرضاة الله، {أو ادفعوا} عن محارمكم وبلدكم إن لم يكن لكم نية صالحة، فأبوا ذلك واعتذروا بأن: {قالوا لو نعلم قتالاً لاتبعناكم}؛ أي: لو نعلم أنكم يصير بينكم وبينهم قتال لاتبعناكم، وهم كذبة في هذا، قد علموا وتيقنوا، وعلم كل أحد أن هؤلاء المشركين قد مُلئوا من الحنق والغيظ على المؤمنين بما أصابوا منهم، وأنهم قد بذلوا أموالهم وجمعوا ما يقدرون عليه من الرجال والعدد، وأقبلوا في جيش عظيم قاصدين المؤمنين في بلدهم متحرقين على قتالهم، فمن كانت هذه حالهم كيف يتصور أنه لا يصير بينهم وبين المؤمنين قتال؟ خصوصاً وقد خرج المسلمون من المدينة وبرزوا لهم، هذا من المستحيل، ولكن المنافقين ظنوا أن هذا العذر يروج على المؤمنين، قال تعالى: {هم للكفر يومئذ}؛ أي: في تلك الحال التي تركوا فيها الخروج مع المؤمنين {أقرب منهم للإيمان، يقولون بأفواههم ما ليس في قلوبهم}، وهذه خاصة المنافقين يظهرون بكلامهم وفعالهم ما يبطنون ضده في قلوبهم وسرائرهم، ومنه قولهم: {لو نعلم قتالاً لاتبعناكم}، فإنهم قد علموا وقوع القتال. ويستدل بهذه الآية على قاعدة ارتكاب أخف المفسدتين، لدفع أعلاهما وفعل أدنى المصلحتين للعجز عن أعلاهما، لأن المنافقين أُمروا أن يقاتلوا للدين، فإن لم يفعلوا فللمدافعة عن العيال والأوطان {والله أعلم بما يكتمون}، فيبديه لعباده المؤمنين، ويعاقبهم عليه.
{166 - 167} Kisha akajulisha kwamba yale yaliyowasibu siku yalipokutana makundi yale mawili: Kundi la Waislamu na kundi la washirikina katika Uhud ya kuuwawa na kushindwa, kwamba ni kwa idhini yake, na hukumu yake, na majaliwa yake. Hakuna cha kuyazuia, na hakuna budi yatokee. Na jambo la kimajaliwa likitekelezeka, basi haibaki isipokuwa ni kujisalimisha kwalo, na kwamba alilijaalia kwa sababu ya hekima kubwa na manufaa makubwa, na ili abainike kwalo Muumini kutokana na mnafiki, ambao walipoamrishwa kupigana vita; “Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu.” Yani, kuiondoshea mabaya Dini ya Mwenyezi Mungu na kuilinda na kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, “au lindeni” vitakatifu vyenu na nchi yenu ikiwa hamna nia njema. Lakini walikataa hilo na wakaomba udhuru, “Wakasema: Tungelijua kuna kupigana vita, bila ya shaka tungeliwafuata.” Yani, lau tungelijua kuwa kutakuwa na vita baina yenu na wao, basi tungelikufuata. Nao ni waongo katika hili. Bila shaka walikwisha jua na wakawa na yakini, na kila mmoja alijua kwamba washirikina hawa walikuwa wamejawa na hasira na ghadhabu dhidi ya Waumini, kwa sababu ya yale yaliyokuwa wamewasibu. Na kwamba walitoa mali zao na wakakusanya wawezavyo miongoni mwa wanaume na matayarisho. Na wakaja katika jeshi kubwa, wakiwaendea Waumini katika nchi yao, likiwa na shauku ya kupigana vita nao. Basi yule ambaye hali yake ni hii, vipi itafikiriwa kwamba hakutakuwa na vita baina yao na Waumini? Hasa kwamba Waislamu walikuwa wameshatoka Madina na wakawatokea maadui zao. Hili ni katika yasiyowezekana. Lakini wanafiki walidhani kuwa udhuru huu utawaonekania Waumini kuwa mzuri. Mwenyezi Mungu akasema, “Wao siku ile na ukafiri.” Yani, katika hali ile ambayo waliacha kutoka ndani yake pamoja na Waumini, “walikuwa karibu zaidi kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa katika nyoyo zao.” Na hili ni jambo mahsusi kwa wanafiki. Wanadhihirisha kwa maneno yao na matendo yao yale wanayoficha kinyume chake katika nyoyo zao na siri zao. Na katika hayo ni kauli yao, “Lau tungelijua kuna kupigana vita, bila ya shaka tungeliwafuata.” Kwani wao kwa hakika walikwisha jua kutokea kwa vita. Na Aya hii inatumika kama ushahidi juu ya kanuni ya kufanya ovu dogo zaidi kati ya maovu mawili, ili kuzuia la juu zaidi kati ya mawili hayo. Na kufanya masilahi ya chini zaidi kati ya masilahi mawili kwa sababu ya kutoliweza liliko juu zaidi kati ya mawili hayo. Kwa sababu, wanafiki waliamrishwa kuipigania dini. Na ikiwa hawatafanya hivyo, basi kwa ajili ya kuwalinda familia na nchi. “Na Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyaficha.” Basi atayadhihirisha kwa waja wake Waumini na kuwaadhibu kwa hayo.
#
{168} ثم قال تعالى: {الذين قالوا لإخوانهم وقعدوا لو أطاعونا ما قتلوا}؛ أي: جمعوا بين التخلف عن الجهاد وبين الاعتراض والتكذيب بقضاء الله وقدره، قال الله ردًّا عليهم: {قل فادرأوا}؛ أي: ادفعوا {عن أنفسكم الموت إن كنتم صادقين}، أنهم لو أطاعوكم ما قتلوا لا تقدرون على ذلك ولا تستطيعونه. وفي هذه الآيات دليل على أن العبد قد يكون فيه خصلة كفر وخصلة إيمان، وقد يكون إلى إحداهما أقرب منه إلى الأخرى.
{168} Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Wale waliowaambia ndugu zao, na wao wenyewe walikuwa wamekaa: Lau wengelitutii, wasingeliuliwa.” Yani, walichanganya kati ya kubaki nyuma ya jihadi na kupinga na kukadhibisha hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaliwa yake. Mwenyezi Mungu akasema akiwajibu, “Sema: Ziondoleeni,” yani zizuieni “nafsi zenu mauti kama nyinyi ni wakweli.” Kwamba lau wangewatii nyinyi (wanafiki) wasingeliuawa. Hamna uwezo juu ya hilo wala hamliwezi. Na katika Aya hizi kuna ushahidi kwamba mja anaweza kuwa na sifa ya ukafiri ndani yake na sifa ya imani. Na anaweza kuwa karibu zaidi na mmoja ya mbili hizi kuliko ile nyingine.
: 169 - 171 #
{وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَمْوَاتًا بَلْ أَحْيَاءٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ (169) فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِمْ مِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (170) يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ (171)}.
169. Wala kabisa usiwadhanie wale waliouliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu. Bali hao wa hai kwa Mola wao Mlezi wanaruzukiwa. 170. Wanafurahia yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake, na wanawapa bishara wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. 171. Wanapata bishara ya neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.
#
{169} هذه الآيات الكريمات فيها فضل الشهداء وكرامتهم، وما منَّ الله عليهم به من فضله وإحسانه، وفي ضمنها تسلية الأحياء عن قتلاهم وتعزيتهم وتنشيطهم للقتال في سبيل الله والتعرض للشهادة فقال: {ولا تحسبن الذين قتلوا في سبيل الله}؛ أي: في جهاد أعداء الدين قاصدين بذلك إعلاء كلمة الله، {أمواتاً}؛ أي: لا يخطر ببالك وحسبانك أنهم ماتوا، وفقدوا، وذهبت عنهم لذة الحياة الدنيا والتمتع بزهرتها، الذي يحذر من فواته من جبن عن القتال وزهد في الشهادة، {بل} قد حصل لهم أعظم مما يتنافس فيه المتنافسون، فهم {أحياء عند ربهم} في دار كرامته، ولفظ: عند ربهم، يقتضي علو درجتهم وقربهم من ربهم، {يرزقون} من أنواع النعيم الذي لا يعلم وصفه إلا من أنعم به عليهم.
{169} Aya hizi tukufu zina fadhila za mashahidi na utukufu wao, na yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu katika fadhila zake na wema wake. Na ndani yake kuna kuwafariji walio hai kwa ajili ya wafu wao, ni kuwaomboleza na kuwatia moyo katika kupigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu na kutafuta kufa kishahidi. Akasema, “Wala kabisa usiwadhanie wale waliouliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu." Yani, katika jihadi dhidi ya maadui wa dini, wakikusudia kwa hilo kuliinua neno la Mwenyezi Mungu, “kuwa ni wafu.” Yani, isiingie katika mawazo yako na dhana yako kwamba walikufa, na wakapotea, na ikawatoka ladha ya maisha ya dunia na starehe ya mapambo yake, ambayo inajitahadharisha juu ya kuyapoteza yule mwenye woga wa kupigana vita na akakata tamaa kufa kishahidi. “Bali” limekwisha wafikia jambo kubwa zaidi kuliko yale wanayoyashindania ndani yake washindani. Kwani wao, “ni hai kwa Mola wao Mlezi” katika nyumba ya utukufu wake. Na maneno “kwa Mola wao Mlezi” yanalazimu kuinuka juu kwa daraja zao na ukarubu wao kwa Mola wao Mlezi. “Wanaruzukiwa” katika aina za neema ambazo hayajui maelezo yake isipokuwa yule aliyeneemeshwa kwazo.
#
{170} ومع هذا {فرحين بما آتاهم الله من فضله}؛ أي: مغتبطين بذلك وقد قرت به عيونهم وفرحت به نفوسهم، وذلك لحسنه وكثرته وعظمته وكمال اللذة في الوصول إليه وعدم المنغص، فجمع الله لهم بين نعيم البدن بالرزق ونعيم القلب والروح بالفرح بما آتاهم من فضله، فتم له النعيم والسرور وجعلوا {يستبشرون بالذين لم يلحقوا بهم من خلفهم}؛ أي: يبشر بعضهم بعضاً بوصول إخوانهم الذين لم يلحقوا بهم وأنهم سينالون ما نالوا {ألا خوف عليهم ولا هم يحزنون}؛ أي: يستبشرون بزوال المحذور عنهم وعن إخوانهم المستلزم كمال السرور.
{170} Na pamoja na haya, “wanafurahia yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake.” Yani, wanafurahishwa hayo, na macho yao yalikwisha farijika kwayo na nafsi zao zikayafurahia. Na hilo ni kwa sababu ya uzuri wake, na wingi wake, na ukubwa wake, na ukamilifu wa ladha katika kuyafikia na kutokuwepo na cha kukasirisha. Basi Mwenyezi Mungu akuwaunganisha baina ya raha ya mwili kwa riziki na raha ya moyo na roho kwa kufurahia yale aliyowapa katika fadhila yake. Kwa hivyo, neema na furaha zikatimia kwake, na wakawa, “wanawapa bishara wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao.” Yani, wanabashiriana wao kwa wao kufika kwa ndugu zao ambao hawajaungana nao, na kwamba watapata yale waliyoyapata. “Ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika”. Yani Wanafurahia kuondokewa wao na ndugu zao kile kinachohofiwa, ambako kunalazimu ukamilifu wa furaha.
#
{171} {يستبشرون بنعمة من الله وفضل} أي: يهنئ بعضهم بعضاً بأعظم مهنأ به وهو نعمة ربهم وفضله وإحسانه {وأن الله لا يضيع أجر المؤمنين}؛ بل ينميه ويشكره، ويزيده من فضله ما لا يصل إليه سعيهم. وفي هذه الآيات إثبات نعيم البرزخ، وأن الشهداء في أعلى مكان عند ربهم، وفيه تلاقي أرواح أهل الخير، وزيارة بعضهم بعضاً، وتبشير بعضهم بعضاً.
{171} “Wanapata bishara ya neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila.” Yani, wanapongezana wao kwa wao kwa kikubwa zaidi cha kupongezwa juu yake. Nayo ni neema ya Mola wao Mlezi, na fadhila zake, na wema wake. “Na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.” Bali yeye huukuza na kuushukuru, na anamzidishia katika fadhila zake kile ambacho juhudi zao hazikifikii. Na katika Aya hizi, kuna uthibitisho wa neema ya Barzakh (maisha ya kaburini), na kwamba Mashahidi wako katika pahali pa juu kabisa kwa Mola wao Mlezi. Na ndani yake kuna kukutana kwa roho za wafanyao wema, na kutembeleana wao kwa wao, na kupeana bishara wao kwa wao.
: 172 - 175 #
{الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّهِ وَالرَّسُولِ مِنْ بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ (172) الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ (173) فَانْقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّهِ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ (174) إِنَّمَا ذَلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (175)}.
172. Wale waliomwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kwisha patwa na majeraha. Kwa waliofanya wema miongoni mwao na wakamcha Mungu, utakuwa ujira mkubwa. 173. Wale walioambiwa na watu: Hakika, kuna watu wamewakusanyikia, hivyo waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora zaidi wa kutegemewa. 174. Basi wakarudi na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila. Hapana baya liliowagusa, na wakafuata yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa. 175. Hakika, huyo ni Shetani anawatia hofu marafiki zake. Basi msiwaogope. Bali niogopeni Mimi ikiwa nyinyi ni Waumini.
#
{172 - 173} لما رجع النبي - صلى الله عليه وسلم - من أحد إلى المدينة وسمع أن أبا سفيان ومن معه من المشركين قد هموا بالرجوع إلى المدينة ندب أصحابه إلى الخروج، فخرجوا على ما بهم من الجراح استجابة لله ولرسوله وطاعة لله ولرسوله، فوصلوا إلى حمراء الأسد ، وجاءهم من جاءهم وقال لهم: {إن الناس قد جمعوا لكم}؛ وهمُّوا باستئصالكم تخويفاً لهم وترهيباً، فلم يزدهم ذلك إلا إيماناً بالله واتكالاً عليه {وقالوا حسبنا الله}؛ أي: كافينا كل ما أهمنا {ونعم الوكيل}؛ المفوض إليه تدبير عباده والقائم بمصالحهم.
{172 - 173} Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliporejea kutoka Uhud kwenda Madina, na akasikia kwamba Abu Sufyan na wale waliokuwa pamoja naye miongoni mwa washirikina wameazimia kurejea Madina, aliwaita maswahaba zake watoke nje. Basi wakatoka pamoja na majeraha waliyokuwa nayo kwa kumwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa hivyo, wakafika Hamra Al-Asad, na wakajiwa na yule aliyewajia na akawaambia; “Hakika, kuna watu wamewakusanyikia” na wameazimia kuwaangamiza, ili kuwatisha na kuwatia hofu. Lakini hilo halikuwazidishia isipokuwa imani kwa Mwenyezi Mungu na kumtegemea Yeye. “Na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha.” Yani, anatutosheleza kila chenye kututia wasiwasi. “Naye ni mbora zaidi wa kutegemewa.” Anayeachiwa kuwaendesha waja wake, na mwenye kuyasimamia masilahi yao.
#
{174} {فانقلبوا}؛ أي: رجعوا {بنعمة من الله وفضل لم يمسسهم سوء}، وجاء الخبرُ المشركين: أن الرسول وأصحابه قد خرجوا إليكم وندم من تخلف منهم، فألقى الله الرعب في قلوبهم واستمروا راجعين إلى مكة، ورجع المؤمنون بنعمة من الله وفضل حيث منَّ عليهم بالتوفيق للخروج بهذه الحالة والاتكال على ربهم، ثم إنه قد كتب لهم أجر غزاة تامة، فبسبب إحسانهم بطاعة ربهم وتقواهم عن معصيتهم لهم أجر عظيم، وهذا فضل الله عليهم.
{174} “Basi wakarudi,” yani walirejea, “na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila. Hapana baya liliowagusa.” Na zikawafikia washirikina habari ya kwamba Mtume na maswahaba wake wamewatokea, na wakajuta yule aliyebaki nyuma miongoni mwao. Basi Mwenyezi Mungu akatia hofu katika nyoyo zao, wakaendelea kurejea Makka. Nao Waumini wakarejea na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila, ambapo aliwaneemesha na mafanikio ya kutoka katika hali hii, na kumtegemea Mola wao Mlezi. Kisha Yeye tena alikwisha waandikia ujira kamili wa wapiganaji. Na kwa sababu ya kumtii kwao Mola wao Mlezi kwa uzuri, na kujiepusha kwao na kumuasi, wana malipo makubwa. Na hii ni fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yao.
#
{175} ثم قال تعالى: {إنما ذلكم الشيطان يُخوف أولياءه}؛ أي: إن ترهيب من رهب من المشركين ـ وقال: إنهم {جمعوا لكم ... } ـ داعٍ من دعاة الشيطان يخوف بها أولياءه الذين عُدِم إيمانهم أو ضعف، {فلا تخافوهم وخافون إن كنتم مؤمنين}؛ أي: فلا تخافوا المشركين أولياء الشيطان فإن نواصيهم بيد الله لا يتصرفون إلا بقدره، بل خافوا الله الذين ينصر أولياءه الخائفين له، المستجيبين لدعوته. وفي هذه الآية وجوب الخوف من الله وحده وأنه من لوازم الإيمان، فعلى قدر إيمان العبد يكون خوفه من الله، والخوف المحمود ما حجز العبد عن محارم الله.
{175} Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Hakika, huyo ni Shetani anawatia hofu marafiki zake.” Yani, hofu aliyopata yule aliyehofishwa miongoni mwa washirikina - na akasema: Hakika wao, "Wamewakusanyikia..." - ni mlinganiaji katika walinganiaji wa Shetani anawahofisha kwa hayo washirika wake ambao haikupatikana imani yao au ilidhoofika. “Basi msiwaogope. Bali niogopeni Mimi ikiwa nyinyi ni Waumini.” Yani, msiwaogope washirikina, washirika wa Shetani. Kwa maana, nywele zao za upande wa mbele ya kichwa ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu. Hawatendi isipokuwa kwa majaliwa yake. Bali mwogopeni Mwenyezi Mungu ambaye anawanusuru marafiki zake wanaomwogopa, wanaoitikia wito wake. Na katika Aya hii kuna ulazima wa kumwogopa Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba ni katika matakwa ya imani. Kwa hivyo, kulingana na ukubwa wa imani ya mja, inakuwa hofu yake kwa Mwenyezi Mungu. Na hofu yenye kusifiwa ni ile inayomzuia mja kutokana na makatazo ya Mwenyezi Mungu.
: 176 - 177 #
{وَلَا يَحْزُنْكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ إِنَّهُمْ لَنْ يَضُرُّوا اللَّهَ شَيْئًا يُرِيدُ اللَّهُ أَلَّا يَجْعَلَ لَهُمْ حَظًّا فِي الْآخِرَةِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ (176) إِنَّ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ لَنْ يَضُرُّوا اللَّهَ شَيْئًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (177)}.
176. Wala wasikuhuzunishe wale wanaoukimbilia ukafiri. Hakika, hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee fungu lolote katika Akhera. Na wana adhabu kubwa. 177. Hakika, wale walioununua ukafiri kwa Imani, hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na wana adhabu chungu.
#
{176} كان النبي - صلى الله عليه وسلم - حريصاً على الخلق مجتهداً في هدايتهم، وكان يحزن إذا لم يهتدوا، قال الله تعالى: {ولا يحزنك الذين يسارعون في الكفر} من شدة رغبتهم فيه وحرصهم عليه {إنهم لن يضروا الله شيئاً} فالله ناصر دينه ومؤيد رسوله ومنفذ أمره من دونهم، فلا تبالهم ولا تحفل بهم، إنما يضرون ويسعون في ضرر أنفسهم بفوات الإيمان في الدنيا، وحصول العذاب الأليم في الأخرى، من هوانهم على الله وسقوطهم من عينه وإرادته أن لا يجعل لهم نصيباً في الآخرة من ثوابه؛ خذلهم فلم يوفقهم لما وفق إليه أولياءه، ومن أراد به خيراً عدلاً منه وحكمة، لعلمه بأنهم غير زاكين على الهدى ولا قابلين للرشاد لفساد أخلاقهم وسوء قصدهم.
{176} Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa akiwajali sana viumbe, na akijitahidi katika kuwaongoza. Na alikuwa akihuzunika ikiwa hawaongoki. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “Wala wasikuhuzunishe wale wanaoukimbilia ukafiri” kwa sababu ya kuutaka kwao kukubwa, na kufanya kwao bidii juu yake. “Hakika, hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu.” Kwa maana, Mwenyezi Mungu atainusuru dini yake, na atamsaidia Mtume wake, ataitekeleza amri yake pasipo wao. Basi usiwajali, wala usiwachukulie kuwa ni muhimu. Wao hakika wanajidhuru na wanajitahidi kudhuru nafsi zao kwa kukosa imani katika dunia, na kupata adhabu chungu katika Akhera, kama vile kuwadunisha kwa Mwenyezi Mungu, na kuanguka kwao machoni pake, na kutaka kwake kutowawekea fungu katika Akhera katika thawabu zake. Aliacha kuwasaidia, kwa hivyo hakuwafanikisha kwenye yale waliyoongoka kwayo marafiki zake, na yule aliyemtakia heri kama uadilifu kutoka kwake na hekima. Kwa sababu ya kujua kwake kwamba wao si safi juu ya uwongofu wala si wenye kuongoka kwa sababu ya tabia yao chafu, na nia yao mbaya.
#
{177} ثم أخبر أن الذين اختاروا الكفر على الإيمان ورغبوا فيه رَغْبَةَ مَنْ بذلَ ما يحب من المال في شراء ما يحب من السلع {لن يضروا الله شيئاً}، بل ضرر فعلهم يعود على أنفسهم، ولهذا قال: {ولهم عذاب أليم}، وكيف يضرون الله شيئاً؟! وهم قد زهدوا أشد الزهد في الإيمان ورغبوا كل الرغبة بالكفر بالرحمن فالله غني عنهم، وقد قيض لدينه من عباده الأبرار الأزكياء سواهم وأعد له ممن ارتضاه لنصرته أهل البصائر والعقول، وذوي الألباب من الرجال الفحول، قال الله تعالى: {قل آمنوا به أو لا تؤمنوا إن الذين أوتوا العلم من قبله إذا يتلى عليهم يخرون للأذقان سجداً ... } الآيات.
{177} Kisha akajulisha wale waliouchagua ukafiri badala ya Imani, na wakautaka kutaka kwa yule aliyetoa anachokipenda katika mali ili kununua kile anachokipenda katika bidhaa. “Hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu” bali madhara ya vitendo vyao yanarejea kwa nafsi zao. Na ndiyo maana akasema, “Na wana adhabu chungu.” Na vipi watamdhuru Mwenyezi Mungu kitu? Na ilhali walikata tamaa kukata kukubwa katika imani, na wakataka kutaka kwote kumkufuru Mwingi wa Rehema. Lakini Mwenyezi Mungu hawahitaji. Na aliiwekea Dini yake katika waje wake wema, watakatifu, aliowafanya sawasawa, na akaiandalia katika wale aliowaridhia kuinusuru, watu wenye maono, na akili, na wenye ufahamu miongoni mwa wanaume wenye nguvu. Akasema Yeye Mtukufu, “Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika, wale waliopewa elimu kabla yake, wanaposomewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu.”Hadi mwisho wa Aya.
: 178 #
{وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ خَيْرٌ لِأَنْفُسِهِمْ إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا وَلَهُمْ عَذَابٌ مُهِينٌ (178)}.
178. Wala wasidhani kabisa wale wanaokufuru kwamba muhula huu tunaowapa ni heri kwao. Hakika, tunawapa muhula ili wazidishe dhambi. Na wana adhabu ya kudunisha.
#
{178} أي: ولا يظن الذين كفروا بربهم، ونابذوا دينه، وحاربوا رسوله أنَّ تركنا إياهم في هذه الحياة الدنيا وعدم استئصالنا لهم وإملائنا لهم خير لأنفسهم ومحبة منا لهم، كلا ليس الأمر كما زعموا، وإنما ذلك لشر يريده الله بهم وزيادة عذاب وعقوبة إلى عذابهم، ولهذا قال: {إنما نملي لهم ليزدادوا إثماً ولهم عذاب مهين}، فالله تعالى يملي للظالم حتى يزداد طغيانه، ويترادف كفرانه حتى إذا أخذه أخذه أخذ عزيز مقتدر، فليحذر الظالمون من الإمهال، ولا يظنوا أن يفوتوا الكبير المتعال.
{178} Yani, wala wasidhani wale waliomkufuru Mola wao Mlezi, na wakaiacha Dini yake, na wakapigana na Mtume wake, kwamba kuwaacha kwetu katika maisha haya ya dunia, na kutowaangamiza kwetu, na kuwapa kwetu muda ni heri kwa nafsi zao na upendo wetu juu yao. Hapana, jambo hili si kama walivyodai. Bali hilo ni kwa sababu ya shari anayowatakia Mwenyezi Mungu, na kuzidishia (yani waliokufuru) adhabu juu ya adhabu yao. Na ndiyo maana akasema, “Hakika, tunawapa muhula ili wazidishe dhambi. Na wana adhabu ya kudunisha.” Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anampa muhula dhalimu ili azidishe upotovu wake, na ukafiri wake ufuatane mpaka anapomshika, anamshika mshiko wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo. Basi na wajihadhari madhalimu kutokana na kupewa muhula, na wala wasidhani kuwa watamwepuka Mkubwa, Mtukufu.
: 179 #
{مَا كَانَ اللَّهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى مَا أَنْتُمْ عَلَيْهِ حَتَّى يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَكِنَّ اللَّهَ يَجْتَبِي مِنْ رُسُلِهِ مَنْ يَشَاءُ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ وَإِنْ تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ (179)}.
179. Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue mbaya kutokana na mwema. Na wala hakuwa Mwenyezi Mungu mwenye kuwajulisha mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume wake amtakaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume yake. Na mkiamini, na mkamcha Mungu, basi mtakuwa na ujira mkubwa.
#
{179} أي: ما كان في حكمة الله أن يترك المؤمنين على ما أنتم عليه من الاختلاط وعدم التمييز ، حتى يميز الخبيث من الطيب والمؤمن من المنافق والصادق من الكاذب، ولم يكن في حكمته أيضاً أن يطلع عباده على الغيب الذي يعلمه من عباده، فاقتضت حكمته الباهرة أن يبتلي عباده، ويفتنهم بما به يتميز الخبيث من الطيب من أنواع الابتلاء والامتحان، فأرسل الله رسله وأمر بطاعتهم والانقياد لهم والإيمان بهم، ووعدهم على الإيمان والتقوى الأجر العظيم، فانقسم الناس بحسب اتباعهم للرسل قسمين: مطيعين وعاصين ومؤمنين ومنافقين ومسلمين وكافرين، ليرتب على ذلك الثواب والعقاب، وليظهر عدله وفضله وحكمته لخلقه.
{179} Yani, haikuwa katika hekima ya Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo ya kuchanganyika na kutotenganisha, mpaka apambanue mbaya kutokana na mwema, na Muumini kutokana na mnafiki, na mkweli kutokana na mwongo. Na haikuwa katika hekima yake pia kuwajulisha waja wake mambo ya ghaibu ambayo anaijua kuhusu waja wake. Kwa hivyo, hekima yake ya kustaajabisha ikalazimu awajaribu waja wake kwa kuwajaribu kwa yale yenye kuwapambanua waovu kutokana na wema kwa aina za majaribio na mitihani. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawatuma Mitume wake, na akaamrisha watiiwe, na kuwafuata, na kuwaamini, na akawaahidi kwa imani na uchamungu malipo makubwa. Basi watu wakagawanyika kulingana na kufuata kwao Mitume katika makundi mawili: Watiifu na waasi. Na Waumini na Wanafiki. Na Waislamu na Makafiri. Ili itokee kwa sababu ya hayo thawabu na adhabu. Na ili udhihirike uadilifu wake, na fadhila zake, na hekima yake kwa viumbe vyake.
: 180 #
{وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَهُمْ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَهُمْ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلِلَّهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (180)}.
180. Wala wasidhani kabisa wale ambao wanafanya ubahili katika aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni heri kwao. Bali hiyo ni shari kwao. Watafungwa shingoni yale waliyoyafanyia ubahili Siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ana habari za yote myatendayo.
#
{180} أي: ولا يظن الذين يبخلون؛ أي: يمنعون ما عندهم مما آتاهم الله من فضله من المال والجاه والعلم وغير ذلك، مما منحهم الله وأحسن إليهم به، وأمرهم ببذل ما لا يضرهم منه لعباده فبخلوا بذلك، وأمسكوه وضنوا به على عباد الله، وظنوا أنه خير لهم بل هو شر لهم في دينهم ودنياهم وعاجلهم وآجلهم، {سيطوقون ما بخلوا به يوم القيامة}؛ أي يجعل ما بخلوا به طوقاً في أعناقهم يعذبون به كما ورد في الحديث الصحيح: «إن البخيل يمثل له ماله يوم القيامة شجاعاً أقرع له زبيبتان يأخذ بلهزمته يقول: أنا مالك، أنا كنزك» ، وتلا رسول الله - صلى الله عليه وسلم - مصداق ذلك هذه الآية، فهؤلاء حسبوا أن بخلهم نافعهم ومجدٍ عليهم فانقلب عليهم الأمر، وصار من أعظم مضارهم وسبب عقابهم. {ولله ميراث السموات والأرض}؛ أي: هو تعالى مالك الملك وتردّ جميع الأملاك إلى مالكها وينقلب العباد من الدنيا ما معهم درهم ولا دينار ولا غير ذلك من المال. قال تعالى: {إنا نحن نرث الأرض ومن عليها وإلينا يرجعون}، وتأمل كيف ذكر السبب الابتدائي والسبب الغائي، الموجب كل واحد منهما أن لا يبخل العبد بما أعطاه الله. أخبر أولاً أن الذي عنده وفي يده فضل من الله ونعمة ليس ملكاً للعبد، بل لولا فضل الله عليه وإحسانه لم يصل إليه منه شيء. فمنْعُه ذلك منْعٌ لفضل الله وإحسانه، ولأن إحسانه موجب للإحسان إلى عبيده، كما قال تعالى: {وأحسن كما أحسن الله إليك}، فمن تحقق أن ما بيده فضل من الله لم يمنع الفضل الذي لا يضره بل ينفعه في قلبه وماله وزيادة إيمانه وحفظه من الآفات. ثم ذكر ثانياً أن هذا الذي بيد العباد، كلُّها ترجع إلى الله ويرثها تعالى وهو خير الوارثين، فلا معنى للبخل بشيء هو زائل عنك، منتقل إلى غيرك. ثم ذكر ثالثاً السبب الجزائي فقال: {والله بما تعملون خبير}، فإذا كان خبيراً بأعمالكم جميعها ويستلزم ذلك الجزاء الحسن على الخيرات والعقوبات على الشر لم يتخلف من في قلبه مثقال ذرة من إيمان عن الإنفاق الذي يجزي به الثواب ولا يرضى بالإمساك الذي به العقاب.
{180} Yani, wala wasidhani wale wanaofanya ubahili. Yani wanaozuia walichonacho katika kile alichowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kama mali, na hadhi, elimu, na mengineyo ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa na akawaneemesha kwayo. Na akawaamrisha watoe wawape waja wake kwayo kile kisichowadhuru wao, lakini wakafanya ubahili kwayo, na wakaishikilia na wakaifanyia ubahili waja wa Mwenyezi Mungu, na wakadhani kuwa ni heri kwao. Bali ni shari kwao katika Dini yao, na dunia yao, na maisha yao ya karibuni na yao ya mustakbali. “Watafungwa shingoni yale waliyoyafanyia ubahili Siku ya Kiyama.” Yani atayafanya yale waliyofanyia ubahili kuwa kongwa shingoni mwao, wakiadhibiwa kwayo, kama ilivyokuja katika Hadithi Sahihi. “Hakika, bahili atafanyiwa mfano wa mali yake Siku ya Kiyama kama nyoka wa kiume, mwenye sumu kali na kipara, mwenye madoa meusi juu ya macho yake (au mwenye tundu mbili za sumu mdomoni mwake). Atamshika kwenye upande wa mdomo wake, kisha atasema, 'Mimi ni mali yako. Mimi ni hazina yako.' Na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake– akakariri Aya hii yenye kuyasadikisha hayo. Kwa kuwa hawa walidhani kuwa ubakhili wao utawafaa, ni chanzo cha heshima kwao. Lakini jambo hilo likawawia kinyume, na likawa miongoni mwa yenye madhara makubwa zaidi juu yao na sababu ya kuadhabiwa kwao. “Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu.” Yani, Yeye Mtukufu ndiye mmiliki wa ufalme, na vyote vinavyomilikiwa vitarudishwa kwa mmiliki wake, na waja watatoka katika dunia pasi na dirhamu wala dinari pamoja nao, wala kisichokuwa hivyo katika mali. Yeye Mtukufu alisema, “Hakika Sisi, tutairithi ardhi na wale walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.” Na tafakari jinsi alivyoitaja sababu ya msingi na sababu ya mwisho, zenye kulazimu kila moja yake kwamba mja asifanye ubahili kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa. Alijulisha kwanza kwamba kile alicho nacho na mkononi mwake ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na neema ambayo si miliki ya mja. Bali kama si fadhila za Mwenyezi Mungu na wema wake, hakingemfikia kitu katika hayo. Kwa hivyo, kuzuia kwake huko, ni kuzuia fadhila za Mwenyezi Mungu na wema wake. Na kwa sababu wema wake juu yake unalazimu awafanyie wema waja wake, kama alivyosema Yeye Mtukufu. “Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia wema wewe.” Na mwenye kutambua kwamba kile kilicho mkononi mwake ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hawezi kuizuia fadhila ambayo haimdhuru. Bali inamnufaisha katika moyo wake na mali yake, na inamzidishia imani yake na inamhifadhi kutokana na balaa. Kisha akataja la pili kwamba vyote ambavyo vimo mikononi mwa waja, vitarejea kwa Mwenyezi Mungu, naye Mtukufu atavirithi, na Yeye ndiye mbora wa wanaorithi. Basi, hakuna maana ya kuwa bahili kwa kitu ambacho kitatoweka kutoka kwako na kuhamishiwa kwa mtu mwingine. Kisha, tatu, akataja sababu ya kuwaadhibu, akasema, “Na Mwenyezi Mungu ana habari za yote myatendayo.” Basi ikiwa Yeye ana habari za matendo yenu yote, na hilo linalazimu malipo mema kwa mambo ya heri, na adhabu kwa maovu, basi mwenye imani ya uzito wa chembe katika moyo wake hatabaki nyuma katika kutoa matumizi ambako analipwa kwako thawabu, na wala hataridhia kuzuia ambako kunasababisha adhabu.
: 181 - 182 #
{لَقَدْ سَمِعَ اللَّهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنْبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ (181) ذَلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِلْعَبِيدِ (182)}.
181. Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya wale waliosema: Hakika, Mwenyezi Mungu ni fakiri, na sisi ni matajiri. Tutayaandika yale waliyoyasema, na pia kuwaua kwao Manabii bila ya haki, na tutawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni adhabu ya kuunguza. 182. Hayo ni kwa sababu ya iliyotanguliza mikono yenu, na kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.
#
{181} يخبر تعالى عن قول هؤلاء المتمردين الذين قالوا أقبح المقالة وأشنعَها وأسمجَها، فأخبر أنه قد سمع ما قالوه، وأنه سيكتبه ويحفظه مع أفعالهم الشنيعة وهو قتلهم الأنبياء الناصحين، وأنه سيعاقبهم على ذلك أشد العقوبة وأنه يقال لهم بدل قولهم إن الله فقير ونحن أغنياء: {ذوقوا عذاب الحريق}؛ المحرق النافذ من البدن إلى الأفئدة، وأن عذابهم ليس ظلماً من الله لهم فإنه {ليس بظلام للعبيد}؛ فإنه منزه عن ذلك.
{181} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu kauli ya hawa wanaoasi, waliosema maneno mabaya zaidi, na maovu yake zaidi, na yenye kudharauliwa yake zaidi. Kwa hivyo akajulisha kwamba alisikia waliyoyasema, na kwamba atayaandika na kuyahifadhi pamoja na matendo yao maovu. Ambayo ni kuwauwa kwao Mitume wanaonasihi. Na kwamba atawaadhibu kwa hilo adhabu kali kabisa. Na kwamba wataambiwa badala ya kauli yao: Hakika Mwenyezi Mungu ni fakiri, na sisi ni matajiri: “Onjeni adhabu ya kuunguza.” Yenye kuunguza na kupenya kutoka kwenye mwili hadi kwenye nyoyo. Na kwamba adhabu yao si dhuluma kwao kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, “si mwenye kuwadhulumu waja.” Kwani, Yeye ametakasika na hilo.
#
{182} وإنما {ذلك بما قدمت} أيديهم من المخازي والقبائح التي أوجبت استحقاقهم العذاب وحرمانهم الثواب. وقد ذكر المفسرون أن هذه الآية نزلت في قوم من اليهود تكلموا بذلك، وذكروا منهم فنحاص بن عازوراء من رؤساء علماء اليهود في المدينة ، وأنه لما سمع قول الله تعالى: {من ذا الذي يُقرض اللهَ قرضاً حسناً}، {وأقرضوا الله قرضاً حسناً}، قال على وجه التكبر والتجرهم هذه المقالة قبحه الله، فذكرها الله عنهم، وأخبر أنه ليس ببدعٍ من شنائعهم، بل قد سبق لهم من الشنائع ما هو نظير ذلك وهو قتلهم الأنبياء بغير حقٍّ، هذا القيد يراد به أنهم تجرؤوا على قتلهم مع علمهم بشناعته لا جهلاً وضلالاً بل تمرداً وعناداً.
{182} Lakini “Hayo ni kwa sababu ya iliyotanguliza” mikono yao ya fedheha na mabaya ambayo yaliwafanya kustahiki adhabu na kunyimwa kwao thawabu. Na wafasiri walitaja kuwa Aya hii iliteremka kuhusu kundi la Mayahudi walioyazungumza hayo, na wakataja miongoni mwao Finhaas bin ‘Aazuuraa aliyekuwa miongoni mwa wanachuoni wakuu wa Mayahudi wa Madina; na kwamba aliposikia kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema?” “Na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema.” Akasema kwa njia ya kiburi na ujasiri maneno haya – na Mwenyezi Mungu amtweze. Basi Mwenyezi Mungu akayataja kutoka kwao, akajulisha kuwa si jambo geni katika maovu yao. Bali ilikwisha tangulia katika maovu yao yale ambayo yanafanana na hilo, nalo ni kuwaua kwao Mitume bila ya haki. Na huku kuzuia (yani bila ya haki) kumekusudiwa kwako kwamba walifanya ujasiri kuwaua pamoja na kujua kwao uovu wake, si kwa kutojua, na upotovu. Bali kwa uasi na ukaidi.
: 183 - 184 #
{الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ عَهِدَ إِلَيْنَا أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّى يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ النَّارُ قُلْ قَدْ جَاءَكُمْ رُسُلٌ مِنْ قَبْلِي بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالَّذِي قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (183) فَإِنْ كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِنْ قَبْلِكَ جَاءُوا بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَالْكِتَابِ الْمُنِيرِ (184)}.
183. Waliosema: Hakika, Mwenyezi Mungu alituusia kwamba tusimwamini Mtume yeyote mpaka atujie na kafara inayoliwa na moto. Waambie: Walikujieni Mitume kabla yangu kwa hoja zilizo wazi na kwa hayo mnayosema. Basi kwa nini mliwaua ikiwa nyinyi ni wakweli? 184. Na wakikukadhibisha, basi walikadhibishwa Mitume wengine kabla yako, waliokuja na hoja zilizo wazi, na Vitabu vyenye hekima, na Kitabu chenye nuru.
#
{183} يخبر تعالى عن حال هؤلاء المفترين القائلين {إن الله عهد إلينا}؛ أي: تقدم إلينا وأوصى أن لا نؤمن لرسول حتى يأتينا بقربان تأكله النار فجمعوا بين الكذب على الله وحصر آية الرسل بما قالوه من هذا الإفك المبين، وأنهم إن لم يؤمنوا برسول لم يأتهم بقربان تأكله النار فهم في ذلك مطيعون لربهم ملتزمون عهده، وقد علم أن كل رسول يرسله الله يؤيده من الآيات والبراهين ما على مثله آمن البشر، ولم يقصرها على ما قالوه، ومع هذا فقد قالوا إفكاً لم يلتزموه وباطلاً لم يعملوا به، ولهذا أمر الله رسوله أن يقول لهم: {قل قد جاءكم رسل من قبلي بالبينات} الدالات على صدقهم {وبالذي قلتم} بأن أتاكم بقربان تأكله النار {فلم قتلتموهم إن كنتم صادقين}؛ أي: في دعواكم الإيمان برسول يأتيكم بقربان تأكله النار، فقد تبين بهذا كذبهم وعنادهم وتناقضهم.
{183} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu hali ya hawa wazushi wanaosema, “Hakika, Mwenyezi Mungu alituusia.” Yani, alitupatia na akatuusia tusimwamini Mtume yeyote mpaka atujie na kafara inayoliwa na moto. Basi wakajumuisha kati ya kumzulia uongo Mwenyezi Mungu na kuzuilia ishara za Mitume katika yale waliyoyasema tu katika uongo huu ulio wazi. Na kwamba ikiwa hawatamwamini Mtume ambaye hakuwaletea kafara inayoliwa na moto, basi watakuwa katika hilo wamemtii Mola wao Mlezi na wameshikamana na ahadi yake. Na ilikwisha julikana kuwa kila Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu humsaidia kwa ishara na hoja ambazo mfano wake waliamini watu, na wala hakuzifungia katika yale wanayoyasema. Na pamoja na hayo, hakika walisema uongo ambao hawakushikamana nao, na batili ambayo hawakuifanyia kazi. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwaambia, “Sema: Walikujieni Mitume kabla yangu kwa hoja zilizo wazi” zinazoashiria ukweli wao, “kwa hayo mnayoyasema.” Kwamba aliwajia na kafara inayoliwa na moto. “Basi kwa nini mliwaua ikiwa nyinyi ni wakweli?” Yani, katika madai yenu ya kumwamini Mtume atakayewajia na kafara inayoliwa moto. Basi ulikwisha bainika kwa hili uongo wao, na ukaidi wao, na kugongana kwao.
#
{184} ثم سَلَّى رسولَه - صلى الله عليه وسلم - فقال: {فإن كذبوك فقد كُذِّبَ رسلٌ من قبلك}؛ أي: هذه عادة الظالمين ودأبهم الكفر بالله وتكذيب رسل الله، وليس تكذيبهم لرسل الله عن قصور بما أتوا به أو عدم تبين حجة، بل قد {جاءوا بالبينات}؛ أي: الحجج العقلية والبراهين النقلية {والزبر}؛ أي: الكتب المزبورة المنزلة من السماء التي لا يمكن أن يأتي بها غير الرسل، {والكتاب المنير} للأحكام الشرعية وبيان ما اشتملت عليه من المحاسن العقلية، ومنير أيضاً للأخبار الصادقة، فإذا كان هذا عادتهم في عدم الإيمان بالرسل الذين هذا وصفهم فلا يحزنك أمرهم ولا يهمنك شأنهم، ثم قال تعالى:
{184} Kisha akamfariji Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akasema: “Na wakikukadhibisha, basi walikadhibishwa Mitume wengine kabla yako.” Yani, hii ni ada ya madhalimu na tabia yao ya kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuwakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu. Na kuwakanusha kwao Mitume wa Mwenyezi Mungu si kwa sababu ya upungufu wa yale waliyowajia nayo au kutobainisha hoja. Bali tayari, "walikuja na hoja zilizo wazi.” Yani, hoja za kiakili na ushahidi wa kimaandiko, “na Vitabu;” yani, vitabu vilivyoandikwa, vilivyoteremshwa kutoka mbinguni, ambavyo hawawezi kuvileta wasiokuwa Mitume. “Na Kitabu chenye nuru” juu ya hukumu za kisheria, na ubainisho wa yale yaliyomo ndani yake ya mema ya kiakili, na pia yenye kutia nuru habari za kweli. Hivyo basi, ikiwa hii ndio ada yao ya kutowaamini Mitume ambao haya ndiyo maelezo yao, basi usihuzunishwe na mambo yao, na wala kabisa mambo yao yasikufanye kujali. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
: 185 #
{كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ (185)}.
185. Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Kiyama. Na atakayeepushwa na Moto, na akaingizwa Peponi, basi huyo hakika amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu isipokuwa starehe ya udanganyifu.
#
{185} هذه الآية الكريمة فيها التزهيد في الدنيا بفنائها وعدم بقائها وأنها متاع الغرور، تفتن بزخرفها وتخدع بغرورها وتغر بمحاسنها، ثم هي منتقلِة ومنتقَل عنها إلى دار القرار التي توفَّى فيها النفوس ما عملت في هذه الدار من خير وشر {فمن زحزح}؛ أي: أخرج {عن النار وأدخل الجنة فقد فاز}؛ أي: حصل له الفوز العظيم بالنجاة من العذاب الأليم والوصول إلى جنات النعيم التي فيها ما لا عين رأت ولا أذن سمعت ولا خطر على قلب بشر. ومفهوم الآية: أن من لم يزحزح عن النار، ويدخل الجنة فإنه لم يفز بل قد شقي الشقاء الأبدي، وابتلي بالعذاب السرمدي. وفي هذه الآية إشارة لطيفة إلى نعيم البرزخ وعذابه وأن العاملين يجزون فيه بعض الجزاء مما عملوه ويقدم لهم أنموذج مما أسلفوه، يفهم هذا من قوله: {وإنما توفون أجوركم يوم القيامة}؛ أي: توفية الأعمال التامة إنما يكون يوم القيامة، وأما ما دون ذلك فيكون في البرزخ، بل قد يكون قبل ذلك في الدنيا كقوله: {ولنذيقنهم من العذاب الأدنى دون العذاب الأكبر}.
{185} Katika Aya hii tukufu, kuna kukatisha tamaa juu ya dunia kwa sababu ya kuisha kwake na kutodumu kwake. Na kwamba starehe ya udanganyifu inafitinisha kwa mapambo yake, na inahadaa kwa udanganyifu wake, na inadanganya kwa mazuri yake. Kisha itahamishwa na itahamwa kwenda kwenye nyumba ya kudumu, ambako nafsi zitatimiziwa yale zilizofanya katika nyumba hii; ya heri na ya shari. "Na atakayeepushwa," yani atakayeondolewa, "na Moto, na akaingizwa Peponi, basi huyo hakika amefuzu." Yani, atakuwa amepata ushindi mkubwa kwa kuokoka na adhabu chungu na kufika kwenye Bustani za neema, ambazo ndani yake kuna kile ambacho jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi kusikia, na wala halijawahi kupita katika moyo wa mwanadamu. Na maana ya Aya isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba yule ambaye hataepushwa na Moto na akaingia Peponi, basi hatakuwa amefuzu. Bali atakuwa amepata taabu ya milele, na atapata adhabu ya milele. Na katika Aya hii, kuna ishara nzuri ya neema ya kaburini na adhabu yake. Na kwamba watendao matendo watalipwa humo baadhi ya malipo ya yale waliyoyafanya, na watapewa mfano wa yale waliyoyatanguliza. Na hilo linafahamika katika kauli yake, "Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Kiyama." Yani, malipo kamili kwa matendo yatakuwa Siku ya Kiyama tu. Na ama kilicho chini ya hayo, hicho kitakuwa kwenye kaburi. Bali huenda ikawa kabla ya hayo katika dunia kama kauli yake, "Na tutawaonjesha adhabu hafifu kabla ya adhabu kubwa."
: 186 #
{لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا وَإِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ (186)}.
186. Hapana shaka yoyote mtajaribiwa katika mali zenu, na nafsi zenu. Na bila ya shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na wale walioshirikisha. Na ikiwa mtasubiri na mkamcha Mungu, basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia.
#
{186} يخبر تعالى ويخاطب المؤمنين أنهم سيبتلون في أموالهم من النفقات الواجبة والمستحبة ومن التعريض لإتلافها في سبيل الله وفي أنفسهم من التكليف بأعباء التكاليف الثقيلة على كثير من الناس كالجهاد في سبيل الله والتعرض فيه للتعب والقتل والأسر والجراح وكالأمراض التي تصيبه في نفسه أو فيمن يحب، ولتسمعن من الذين أوتوا الكتاب والمشركين {أذى كثيراً} من الطعن فيكم وفي دينكم وكتابكم ورسولكم. وفي إخباره لعباده المؤمنين بذلك عدة فوائد: منها: أن حكمته تعالى تقتضي ذلك ليتميز المؤمن الصادق من غيره. ومنها: أنه تعالى يقدر عليهم هذه الأمور لما يريده بهم من الخير ليعلي درجاتهم ويكفر من سيئاتهم وليزداد بذلك إيمانهم ويتم به إيقانهم فإنه إذا أخبرهم بذلك ووقع كما أخبر، {قالوا هذا ما وعدنا الله ورسوله وصدق الله ورسوله وما زادهم إلا إيماناً وتسليماً}. ومنها: أنه أخبرهم بذلك لتتوطن نفوسهم على وقوع ذلك والصبر عليه إذا وقع لأنهم قد استعدوا لوقوعه فيهون عليهم حمله وتخف عليهم مؤنته ويلجؤون إلى الصبر والتقوى، ولهذا قال: {وإن تصبروا وتتقوا}؛ أي: إن تصبروا على ما نالكم في أموالكم وأنفسكم من الابتلاء والامتحان وعلى أذية الظالمين وتتقوا الله في ذلك الصبر بأن تنووا به وجه الله والتقرب إليه ولم تتعدوا في صبركم الحد الشرعي من الصبر في موضع لا يحل لكم فيه الاحتمال بل وظيفتكم فيه الانتقام من أعداء الله. {فإن ذلك من عزم الأمور}؛ أي: من الأمور التي يعزم عليها وينافس فيها ولا يوفق لها إلا أهل العزائم والهمم العالية، كما قال تعالى: {وما يلقاها إلا الذين صبروا وما يلقاها إلا ذو حظ عظيم}.
{186} Yeye Mtukufu anajulisha na anawaongelesha Waumini kwamba watajaribiwa katika mali zao kutokana na matumizi ya lazima na ya kupendekezwa. Na kutokana na kuyaharibia katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na katika nafsi zao kwa kuwaamrisha amri zenye mizigo mizito wengi wa watu, kama vile jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kukabiliana katika hilo na uchovu, na kuuawa, na kutekwa, na majeraha, na kama maradhi yanayomsibu katika nafsi yake au katika wale awapendao. Na bila ya shaka, mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu na washirikina "udhia mwingi" kama vile kukashifiwa nyinyi na Dini yenu, na Kitabu chenu, na Mtume wenu. Na katika kuwajulisha waja wake Waumini kuhusu hayo, kuna manufaa kadhaa: Miongoni mwake ni kwamba hekima yake, Yeye Mtukufu inataka hivyo ili apambanuke Muumini wa kweli kutokana na wengineo. Na miongoni mwake ni kwamba Yeye Mtukufu anawaandikia mambo haya kwa sababu ya yale anayowatakia ya heri ili awanyanyue daraja zao. Na awafutie mabaya yao, na azidishe kwa hayo imani yao na ikamilike kwayo yakini yao. Kwani ikiwa atawajulisha hayo, na yakatokea kama alivyojulisha; "Wakasema hivi ndivyo alivyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakasema kweli, na ikawazidishia imani na utiifu." Na miongoni mwake ni kwamba, aliwajulisha hayo ili nafsi zao zizoee kutokea kwa hayo ili wawe na subira juu yake yakitokea. Kwa sababu, walikuwa wamejitayarisha kwa ajili ya kutokea kwake, basi inakuwa rahisi juu yao kuyabeba, na mzigo wake utakuwa hafifu kwao, na watakimbilia kwenye subira na uchamungu. Na ndio maana akasema, "Na ikiwa mtasubiri na mkamcha Mungu," yani, mkisubiri kwa yale yaliyowasibu katika mali zenu, na nafsi zenu ya majaribio na mitihani, na juu ya udhia wa madhalimu, na mkamcha Mwenyezi Mungu katika subira hiyo kwa kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu na kujiweka karibu naye. Na hamkukiuka katika subira yenu mpaka wa kisheria wa subira katika hali ambayo hairuhusiwi kwenu kuvumilia, bali kazi yenu ndani yake ni kulipiza kisasi kwa maadui wa Mwenyezi Mungu. "Basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia." Yani ni miongoni mwa mambo ambayo yanaazimiwa na yanashindaniwa, wala hawezeshwi kuyafikia isipokuwa wale wenye azimio na hima kubwa, kama alivyosema Yeye Mtukufu." Lakini hawapewi wema huu isipokuwa wale wanaosubiri, na wala hawapewi isipokuwa wale wenye bahati kubwa.
: 187 - 188 #
{وَإِذْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ (187) لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوْا وَيُحِبُّونَ أَنْ يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُمْ بِمَفَازَةٍ مِنَ الْعَذَابِ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (188)}.
187. Na pale Mwenyezi Mungu alipochukua agano la wale waliopewa Kitabu kuwa: Bila shaka mtawabainishia watu, na wala hamtakificha. Lakini wakakitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani kidogo. Basi ni kiovu mno hicho wanachokinunua. 188. Kamwe usiwadhanie wale wanaofurahia yale waliyoyafanya, na wakapenda kwamba wasifiwe kwa yale ambayo hawakuyatenda. Basi kamwe usiwadhanie kuwa watasalimika na adhabu. Na wana adhabu chungu.
#
{187} الميثاق: هو العهد الثقيل المؤكد، وهذا الميثاق أخذه الله تعالى على كل من أعطاه الله الكتب، وعلَّمه العلمَ أن يبين للناس ما يحتاجون إليه مما علمه الله ولا يكتمهم ذلك ويبخل عليهم به، خصوصاً إذا سألوه أو وقع ما يوجب ذلك، فإنَّ كلَّ من عنده علم يجب عليه في تلك الحال أن يبينه ويوضح الحق من الباطل. فأما الموفقون فقاموا بهذا أتم القيام وعلَّموا الناس مما علَّمَهم الله ابتغاء مرضاة ربهم وشفقة على الخلق وخوفاً من إثم الكتمان. وأما الذين أوتوا الكتاب من اليهود والنصارى ومن شابههم فنبذوا هذه العهود والمواثيق وراء ظهورهم فلم يعبؤوا بها فكتموا الحق وأظهروا الباطل تجرؤاً على محارم الله وتهاوناً بحقوقه تعالى وحقوق الخلق واشتروا بذلك الكتمان {ثمناً قليلاً} وهو ما يحصل لهم إن حصل من بعض الرياسات والأموال الحقيرة من سفلتهم المتبعين أهواءهم المقدمين شهواتهم على الحق {فبئس ما يشترون} لأنه أخسّ العوض والذي رغبوا عنه وهو بيان الحق الذي فيه السعادة الأبدية والمصالح الدينية والدنيوية أعظمُ المطالب وأجلُّها، فَلَمْ يختاروا الدني الخسيس ويتركوا العالي النفيس إلا لسوء حظهم وهوانهم وكونهم لا يصلحون لغير ما خلقوا له. ثم قال تعالى:
{187} Agano ni ahadi nzito iliyosisitizwa. Na agano hili Mwenyezi Mungu Mtukufu alilichukuwa juu ya kila ambaye Mwenyezi Mungu alimpa Vitabu, na akamfundisha elimu kwamba awabainishie watu yale wanayohitaji katika yale aliyomfundisha Mwenyezi Mungu wala asiwafiche hayo na kufanya ubahili nayo. Hususan wanapomuuliza au likatokea lenye kulazimu hayo, basi kila mwenye elimu ni inamlazimu katika hali hiyo kuibainisha na kuiweka wazi haki kutokana na batili. Basi ama wale waliowezeshwa, hao walifanya hivyo kufanya kukamilifu. Na wakawafundisha watu katika yale aliyowafundisha Mwenyezi Mungu, kwa kutaka radhi za Mola wao Mlezi na huruma kwa viumbe, na kuogopa dhambi ya kuficha. Na ama wale waliopewa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Manasara na yeyote aliye mfano wao, walizitupa ahadi hizi na maagano haya nyuma ya migongo yao, wala hawakuzijali. Hivyo, wakaificha haki na wakaidhihirisha batili, wakajasiri kuvuka makatazo ya Mwenyezi Mungu, na wakazipuuza haki zake Yeye Mtukufu, na haki za viumbe. Na wakanunua kwa kuficha huko, "thamani ndogo." Nayo ni kile wanachokipata ikiwa kitapatikana miongoni mwa baadhi ya uongozi, na mali duni kutoka kwa wale wa chini wao, wanaofuata matamanio yao, wanaotanguliza matamanio yao mbele ya haki ya Mwenyezi Mungu. "Basi ni kiovu mno hicho wanachokinunua." Kwa sababu ni badala ya chini kabisa. Na yale waliyoyakataa ambayo ni kubainisha haki ambayo ndani yake kuna furaha ya milele, na masilahi ya kidini na ya kidunia ndiyo matakwa makubwa zaidi na matukufu zaidi. Kwa hivyo, hawakuyachagua yaliyo duni na ya kudharauliwa na wakayaacha yaliyo juu na ya thamani isipokuwa kwa bahati yao mbaya, na unyonge wao, na kwamba wao hawafailii kisichokuwa walichoumbiwa kwa ajili yake. Kisha Yeye Mtukufu akasema:
#
{188} {لا تحسبن الذين يفرحون بما أتوا}؛ أي: من القبائح والباطل القولي والفعلي {ويحبون أن يحمدوا بما لم يفعلوا}؛ أي: بالخير الذي لم يفعلوه والحق الذي لم يقولوه، فجمعوا بين فعل الشر وقوله والفرح بذلك ومحبة أن يحمدوا على فعل الخير الذي ما فعلوه، {فلا تحسبنهم بمفازة من العذاب}؛ أي: بمحلِّ نجوة منه وسلامة، بل قد استحقوه وسيصيرون إليه ولهذا قال: {ولهم عذاب أليم}. ويدخل في هذه الآية الكريمة أهل الكتاب الذين فرحوا بما عندهم من العلم ولم ينقادوا للرسول، وزعموا أنهم هم المحقون في حالهم ومقالهم، وكذلك كل من ابتدع بدعة قولية أو فعلية، وفرح بها، ودعا إليها، وزعم أنه محق وغيره مبطل كما هو الواقع من أهل البدع. ودلت الآية بمفهومها على أن من أحبَّ أن يحمدَ ويُثْنَى عليه بما فعله من الخير واتِّباع الحقِّ إذا لم يكن قصده بذلك الرياء والسمعة أنه غير مذموم، بل هذا من الأمور المطلوبة التي أخبر الله أنه يجزي بها المحسنين له الأعمال والأقوال، وأنه جازى بها خواص خلقه وسألوها منه كما قال إبراهيم عليه السلام: {واجعل لي لسان صدق في الآخرين}، وقال: {سلام على نوح في العالمين إنا كذلك نجزي المحسنين}، وقد قال عباد الرحمن: {واجعلنا للمتقين إماماً}، وهي من نعم الباري على عبده ومننه التي تحتاج إلى شكر.
{188} "Kamwe usiwadhanie wale wanaofurahia yale waliyoyafanya." Yani, katika mabaya na batili ya kikauli vitendo. "Na wakapenda kwamba wasifiwe kwa yale ambayo hawakuyatenda." Yani, kwa wema ambao hawakuufanya, na haki ambayo hawakuisema. Basi wakajumuisha baina ya kutenda maovu na kuyasema na kulifurahia hilo, na kupenda kwamba wasifiwe kwa kutenda mema ambayo hawakuyafanya. "Basi kamwe usiwadhanie kuwa watasalimika na adhabu." Yani, kwamba watapata pahali pa kukimbilia kutokana nao na kuwa salama. Bali waliistahiki na wataishia huko. Na kwa sababu ya hayo akasema, "Na wana adhabu chungu." Na wanaingia katika Aya hii tukufu Watu wa Kitabu ambao walifurahia kile walicho nacho cha elimu lakini hawakumfuata Mtume, na wakadai kuwa wao ndio walio kwenye haki katika hali yao na maneno yao. Na vile vile kila aliyezua uzushi wa kikauli au wa kimatendo, na akaufurahia, na akaulingania, na akadai kuwa yuko kwenye haki, na asiyekuwa yeye yuko kwenye batili, kama ilivyo hali ya wenye kuzua uzushi. Na Aya iliashiria kwa maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja kwamba anayependa kuhimidiwa na kusifiwa kwa mema aliyoyafanya na kufuata haki, ikiwa makusudio yake kwa hilo si kujionyesha na kusifiwa, kwamba yeye hakashifiwi. Bali haya ni miongoni mwa mambo yanayotakikana ambayo Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba Yeye hakika huwalipa kwayo wanaomfanyia wema katika matendo na maneno. Na kwamba huwalipa kwayo wale walio maalumu katika viumbe vyake, na wakayaomba kutoka kwake, kama alivyosema Ibrahimu. "Na unijaalie nitajwe kwa wema katika wale watakaokuja baadaye." Na akasema, "Iwe salama kwa Nuhu katika walimwengu wote! Kwa hakika, hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema." Na waja wa Mwingi wa Rehema wakasema, "Na utufanye mfano kwa wachamungu." Nayo ni miongoni mwa neema za Muumba mwanzilishi juu ya mja wake, na neema zake zinazihitaji kushukuriwa.
: 189 #
{وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (189)}.
189. Na ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.
#
{189} أي: هو المالك للسماوات والأرض وما فيهما من سائر أصناف الخلق المتصرف فيهم بكمال القدرة وبديع الصنعة، فلا يمتنع عليه منهم أحد، ولا يعجزه أحد.
{189} Yani, Yeye ndiye mmiliki wa mbingu na ardhi, na vilivyomo ndani ya viwili hivyo miongoni mwa aina zote za viumbe. Mwenye kuviendesha kwa nguvu kamili, Mwanzilishi wa uundaji. Kwa hivyo, hakuna hata mmoja miongoni mwao asiyewezekana kwake, wala hakuwa yeyote anayeweza kumshinda.
: 190 - 194 #
{إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِأُولِي الْأَلْبَابِ (190) الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَى جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ (191) رَبَّنَا إِنَّكَ مَنْ تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ (192) رَبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ (193) رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدْتَنَا عَلَى رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ (194)}.
190. Hakika, katika kuumbwa mbingu na ardhi na kuhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. 191. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wamesimama, na wakiketi, na ubavuni kwao. Na hutafakari katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka (umetakasika)! Basi tukinge kutokana na adhabu ya Moto. 192. Mola wetu Mlezi! Hakika, yule unayemwingiza Motoni, basi umemhizi. Na waliodhulumu hawana wasaidizi wowote. 193. Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumemsikia mwitaji akiita kwenye Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; kwa hivyo, tukaamini. Basi tufutie dhambi zetu, na utufunikie makosa yetu, na utufishe pamoja na walio wema. 194. Mola wetu Mlezi! Na utupe yule uliyotuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika, Wewe huvunji miadi.
#
{190} يخبر تعالى: {إن في خلق السموات والأرض واختلاف الليل والنهار لآيات لأولي الألباب}، وفي ضمن ذلك حث العباد على التفكر فيها والتبصر بآياتها وتدبر خلقها. وأبهم قوله: {آيات}، ولم يقل على المطلب الفلاني إشارة لكثرتها وعمومها، وذلك لأن فيها من الآيات العجيبة ما يُبِهر الناظرين ويقنع المتفكرين ويجذب أفئدة الصادقين وينبه العقول النيرة على جميع المطالب الإلهية، فأما تفصيل ما اشتملت عليه فلا يمكِّن مخلوقاً أن يحصره ويحيط ببعضه، وفي الجملة فما فيها من العظمة والسعة وانتظام السير والحركة يدل على عظمة خالقها وعظمة سلطانه وشمول قدرته، وما فيها من الإحكام والإتقان وبديع الصنع ولطائف الفعل يدل على حكمة الله ووضعه الأشياء مواضعها وسعة علمه، وما فيها من المنافع للخلق يدل على سعة رحمة الله وعموم فضله وشمول بره ووجوب شكره، وكل ذلك يدل على تعلق القلب بخالقها ومبدعها وبذل الجهد في مرضاته، وأن لا يشرك به سواه ممن لا يملك لنفسه ولا لغيره مثقال ذرة في الأرض ولا في السماء، وخص الله بالآيات أولي الألباب وهم أهل العقول لأنهم هم المنتفعون بها الناظرون إليها بعقولهم لا بأبصارهم.
{190} Yeye Mtukufu anajulisha, "Hakika, katika kuumbwa mbingu na ardhi na kuhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili." Na ndani ya hayo kuna kuwahimiza waja wayatafakari hayo, na wazitazame Aya zake, na wazingatie kuumbwa kwake. Na akasema bila kubainisha kauli yake, "ishara" na wala hakusema ni kwa matakwa fulani, ili liashirie wingi wake na ujumla wake. Na hilo ni kwa sababu ndani yake kuna ishara za ajabu zenye kuwashangaza watazamaji, na kumshawishi mwenye kutafakari, na zenye kuvutia nyoyo za wakweli, na zinazindua akili zenye nuru juu ya matakwa yote ya Mwenyezi Mungu. Na ama kubainisha kwa kina yale yaliyomo ndani yake, hakuna kiumbe anayeweza kuyadhibiti na kuyajua vyema ijapokuwa baadhi yake. Lakini kwa ujumla, yale yaliyomo ndani yake ya ukuu, na wasaa, na mpangilio mzuri wa mwendo na harakati vinaonyesha ukubwa wa Muumba wake, ukubwa wa mamlaka yake, na ujumlishaji wa uwezo wake. Na yaliyomo ndani yake ya udhibiti mambo, na utengenezaji vilivyo wa vitu, na ufundi wa hali ya juu, na uzuri wa vitendo vinaashiria hekima ya Mwenyezi Mungu na kuweka kwake vitu mahali pake, na upana wa elimu yake. Na yale yaliyomo ndani yake ya manufaa kwa viumbe yanaashiria wingi wa rehema za Mwenyezi Mungu na ujumla wa fadhila zake, ujumuishaji wema wake, na ulazima wa kumshukuru, na yote haya yanaashiria kufungamana kwa moyo na Muumba wake na Muumba mwanzilishi wake, na kufanya juhudi katika kumridhisha Yeye. Na kwamba asishirikishwe asiyekuwa yeye pamoja naye miongoni mwa wale wasiozimilikia nafsi zao uzito wa chembe katika ardhi na katika mbingu. Na Mwenyezi Mungu alizifanya ishara kuwa za wenye akili hususan kwa sababu wao ndio wenye kunufaika nazo, wanaozitazama kwa akili zao, na si kwa macho yao.
#
{191} ثم وصف أولي الألباب بأنهم: {يذكرون الله} في جميع أحوالهم {قياماً وقعوداً وعلى جنوبهم}، وهذا يشمل جميع أنواع الذكر بالقول والقلب، ويدخل في ذلك الصلاة قائماً، فإن لم يستطع فقاعداً، فإن لم يستطع فعلى جنب، وأنهم: {يتفكرون في خلق السموات والأرض}؛ أي: ليستدلوا بها على المقصود منها، ودل هذا على أن التفكر عبادة من صفات أولياء الله العارفين، فإذا تفكروا بها عرفوا أن الله لم يخلقها عبثاً فيقولون: {ربنا ما خلقت هذا باطلاً سبحانك} عن كل ما لا يليق بجلالك بالحق وللحق بل خلقتها مشتملة على الحق {فقنا عذاب النار}، بأن تعصمنا من السيئات وتوفقنا للأعمال الصالحات لننال بذلك النجاة من النار. ويتضمن ذلك سؤال الجنة لأنهم إذا وقاهم الله عذاب النار حصلت لهم الجنة، ولكن لما قام الخوف بقلوبهم، دعوا الله بأهم الأمور عندهم:
{191} Kisha akawaeleza wenye akili kwamba wao, "Wanamdhukuru Mwenyezi Mungu" katika hali zao zote. "Hali ya kuwa wamesimama, na wakiketi, na ubavuni kwao." Na hili linajumuisha kila aina ya utajo kwa maneno na kwa moyo. Na inaingia katika hilo kuswali kwa kusimama, na asipoweza, basi kwa kuketi, na asipoweza, basi kwenye ubavu wake. Na kwamba wao, "hutafakari katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi." Yani, ili watumie hayo kama ushahidi juu ya kilichokusudiwa nayo. Na hili linaashiria kuwa kutafakari ni ibada ambayo ni miongoni mwa sifa za marafiki wa Mwenyezi Mungu, wenye elimu. Basi wakizitafakari, wanajua kuwa Mwenyezi Mungu hakuziumba bure. Kwa hivyo, husema, "Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka (umetakasika!)" kutokana na kila kisicholingana na utukufu wako kwa haki na kwa ajili ya haki. Bali wewe uliziumba zikiwa zimejumuisha haki. "Basi tukinge kutokana na adhabu ya Moto." Kwa kutukinga kutokana na maovu, na utuwezeshe kutenda mema, ili tupate kwa hilo kuokoka kutokana na Moto. Na hilo linajumuisha kuomba Pepo. Kwa sababu, ikiwa Mwenyezi Mungu atawalinda kutokana na adhabu ya Moto, basi wanapata Pepo. Lakini, pindi hofu ilipotanda mioyoni mwao, walimwomba Mwenyezi Mungu kile cha muhimu zaidi kwao:
#
{192} {ربنا إنك من تدخل النار فقد أخزيته}؛ أي: لحصوله على السخط من الله ومن ملائكته وأوليائه ووقوع الفضيحة التي لا نجاة منها ولا منقذ منها، ولهذا قال: {وما للظالمين من أنصار} ينقذونهم من عذابه، وفيه دلالة على أنهم دخلوها بظلمهم.
{192} "Mola wetu Mlezi! Hakika, yule unayemwingiza Motoni, basi umemhizi." Yani, kwa sababu ya kupata kwake ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kutoka kwa Malaika wake na marafiki wake. Na kutokea kwa fedheha ambayo haina njia ya kuikimbia wala hakuna wa kuokoa kutokana nayo. Na ndiyo maana akasema, "Na waliodhulumu hawana wasaidizi wowote" wanaoweza kuwaokoa kutokana na adhabu yake. Na ndani yake kuna ushahidi kwamba waliingia humo kwa dhuluma yao.
#
{193} {ربنا إننا سمعنا منادياً ينادي للإيمان} وهو محمد - صلى الله عليه وسلم -؛ [أي]: يدعو الناس إليه ويرغبهم فيه في أصوله وفروعه {فآمنا}؛ أي: أجبناه مبادرة وسارعنا إليه. وفي هذا إخبار منهم بمنة الله عليهم وتبجح بنعمته وتوسل إليه بذلك أن يغفر ذنوبهم ويكفر سيئاتهم لأن الحسنات يذهبن السيئات. والذي مَنَّ عليهم بالإيمان سيمنُّ عليهم بالأمان التام، {وتوفنا مع الأبرار}، يتضمن هذا الدعاء التوفيق لفعل الخير وترك الشر الذي به يكون العبد من الأبرار والاستمرار عليه والثبات إلى الممات.
{193} "Mola wetu Mlezi! Hakika, sisi tumemsikia mwitaji akiita kwenye Imani." Naye ni Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - [yani]: Anawalingania watu kwayo, na anawahimiza kwayo katika misingi yake na matawi yake, "kwa hivyo tukaamini." Yani, tulimwitikia mara moja na tukaharakisha kumwendea. Na katika haya kuna kujulisha kwao kuhusu neema za Mwenyezi Mungu juu yao, na kujisifu kwa neema zake. Na kutafuta njia ya kumwendea kuzipitia hizo ili awafutie dhambi zao na awafunikie maovu yao. Kwa sababu, matendo mema huyaondoa maovu. Na yule aliyewaneemesha kwa imani, atawaneemesha kwa amani kamili. "Na utufishe pamoja na walio wema." Dua hii inajumuisha kuwezeshwa kufanya mema na kuacha maovu ambayo kwayo mja anakuwa miongoni mwa walio wema, na kuendelea nayo na kusimama imara mpaka kufa.
#
{194} ولما ذكروا توفيق الله إياهم للإيمان وتوسلهم به إلى تمام النعمة، سألوه الثواب على ذلك، وأن ينجز لهم ما وعدهم به على ألسنة رسله من النصر والظهور في الدنيا، ومن الفوز برضوان الله وجنته في الآخرة، فإنه تعالى لا يخلف الميعاد، فأجاب الله دعاءهم وقبل تضرعهم فلهذا قال:
{194} Na walipotaja kuwezeshwa kwao na Mwenyezi Mungu kuamini, na kutafuta kwao njia kwayo kufikia neema kamilifu, wakamwomba thawabu juu ya hayo. Na kwamba awatimizie yale aliyowaahidi kwa ndimi za Mitume wake ya nusura na ushindi katika dunia, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo yake huko Akhera. Kwani, Yeye Mtukufu havunji miadi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawajibu dua yao, na akakubali kunyenyekea kwao. Na kwa sababu ya hayo akasema:
: 195 #
{فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِنْكُمْ مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَى بَعْضُكُمْ مِنْ بَعْضٍ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ وَاللَّهُ عِنْدَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ (195)}.
195. Basi, Mola wao Mlezi akayakubali maombi yao akayajibu: Hakika Mimi, sipotezi matendo ya mfanya matendo yeyote miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi. Basi waliohama, na waliotolewa katika makazi yao, na wakaudhiwa katika Njia yangu, na wakapigana vita, na wakauliwa, kwa yakini Mimi nitawafunikia makosa yao; na kwa yakini nitawaingiza katika Mabustani yanayopita mito chini yake. Hizo ndizo thawabu zinazotoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu kwake zipo thawabu njema kabisa.
#
{195} أي: أجاب الله دعاءهم دعاء العبادة ودعاء الطلب وقال: {إني لا أُضيع عمل عامل منكم من ذكر أو أنثى} فالجميع سيلقون ثواب أعمالهم كاملاً موفراً، أي: كلكم على حد سواء في الثواب والعقاب، {فالذين هاجروا وأُخرجوا من ديارهم وأُوذوا في سبيلي وقاتلوا وقتلوا} فجمعوا بين الإيمان والهجرة ومفارقة المحبوبات من الأوطان والأموال طلباً لمرضاة ربهم وجاهدوا في سبيل الله {لأكفرنَّ عنهم سيئاتهم ولأدخلنهم جنات تجري من تحتها الأنهار ثواباً من عند الله} الذي يعطي عبده الثواب الجزيل على العمل القليل، {والله عنده حسن الثواب}، مما لا عين رأت ولا أُذن سمعت ولا خطر على قلب بشر، فمن أراد ذلك فليطلبه من الله بطاعته والتقرب إليه بما يقدر عليه العبد.
{195} Yani, Mwenyezi Mungu akajibu dua yao, dua ya ibada na dua kuomba, na akasema. "Hakika Mimi, sipotezi matendo ya mfanya matendo yeyote miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke." Wote watapata malipo ya matendo yake kwa ukamilifu na kwa wingi. Yani nyinyi nyote ni sawa katika thawabu na adhabu. "Basi waliohama, na waliotolewa katika makazi yao, na wakaudhiwa katika Njia yangu, na wakapigana vita, na wakauliwa." Basi wakajumuisha kati ya Imani, na kuhama, na kuachana na wavipendavyo miongoni mwa nchi na mali ili kutafuta kumridhisha Mola wao Mlezi, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu. "Kwa yakini Mimi nitawafunikia makosa yao, na kwa yakini nitawaingiza katika Mabustani yanayopita mito chini yake. Hizo ndizo thawabu zinazotoka kwa Mwenyezi Mungu" ambaye humpa mja wake thawabu nyingi kwa matendo machache. "Na Mwenyezi Mungu kwake zipo thawabu njema kabisa." Miongoni mwa yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa binadamu yeyote. Kwa hivyo, anayetaka hiyo, basi na ayaombe kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kujiweka karibu naye kwa kile ambacho mja anakiweza.
: 196 - 198 #
{لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ (196) مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمِهَادُ (197) لَكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نُزُلًا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ وَمَا عِنْدَ اللَّهِ خَيْرٌ لِلْأَبْرَارِ (198)}.
196. Kamwe kusiwadanganye kutangatanga kwa wale waliokufuru katika nchi. 197. Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makazi yao yatakuwa Jahannamu. Na ni pahali pabaya mno pa kupumzikia. 198. Lakini wale waliomcha Mola wao Mlezi wana Mabustani yanayopita mito chini yake. Watadumu humo. Hayo ni makaribisho yao yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa walio wema.
#
{196} وهذه الآية المقصود منها التسلية عما يحصل للذين كفروا من متاع الدنيا وتنعمهم فيها، وتقلبهم في البلاد بأنواع التجارات والمكاسب واللذات وأنواع العز والغلبة في بعض الأوقات، فإن هذا كله:
{196} Na Aya hii inakusudiwa kuwa maliwazo kwa yale wanayopata wale waliokufuru miongoni mwa starehe za dunia na kuneemeshwa kwao humo. Na kutangatanga kwao katika nchi kwa aina mbalimbali za biashara, na michumo, na starehe, na aina mbalimbali za utukufu, na ushindi katika baadhi ya nyakati. Kwa maana hivi vyote:
#
{197} {متاع قليل} ليس له ثبوت ولا بقاء، بل يتمتعون به قليلاً ويعذبون عليه طويلاً، هذه أعلى حالة تكون للكافر، وقد رأيت ما تؤول إليه.
{197} "Ni starehe ndogo" ambayo haina uimara au kubakia. Bali wanastarehe kwayo kidogo, na wataadhibiwa juu yake kwa muda mrefu. Hii ndiyo hali ya juu kabisa anayofikia kafiri. Na tayari umeshaona pale inapoishia.
#
{198} وأما المتقون لربهم المؤمنون به فمع ما يحصل لهم من عز الدنيا ونعيمها {لهم جنات تجري من تحتها الأنهار خالدين فيها}؛ فلو قدر أنهم في دار الدنيا قد حصل لهم كلُّ بؤسٍ وشدَّةٍ وعَناءٍ ومشقةٍ، لكان هذا بالنسبة إلى النعيم المقيم والعيش السليم والسرور والحبور والبهجة نزراً يسيراً ومنحة في صورة محنة، ولهذا قال تعالى: {وما عند الله خير للأبرار} وهم الذين برّت قلوبهم فبرّت أقوالهم وأفعالهم فأثابهم البَرُّ الرحيم من بِرِّه أجراً عظيماً وعطاءً جسيماً وفوزاً دائماً.
{198} Na ama wale wanaomcha Mola wao Mlezi, wanaomuamini, basi pamoja na yale yanayowafikia miongoni mwa utukufu wa dunia na neema zake, "wana Mabustani yanayopita mito chini yake. Watadumu humo." Na lau kuwa inachukuliwa kwamba wao katika nyumba ya dunia iliwapata kila shida, na ugumu, na taabu, na dhiki; basi kwa kulinganishwa haya na neema ya kudumu, na kuishi kwa usalama, na furaha, na raha, na uzuri yangekuwa kama jambo duni dogo, na zawadi katika mfano wa mtihani. Na kwa sababu ya hayo Yeye Mtukufu akasema, "Na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa walio wema." Nao ni wale ambao nyoyo zao ni njema, kwa hivyo maneno yao na matendo yao yakawa mema. Kwa hivyo, Yeye Mwema, Mwingi wa Rehema akawalipa katika wema wake malipo makubwa, na kipawa kikubwa, na kufaulu kwa daima.
: 199 - 200 #
{وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَنْ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ (199) يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (200)}.
199. Na hakika, miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanaomwamini Mwenyezi Mungu na yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwao, wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawanunui kwa Aya za Mwenyezi Mungu thamani ndogo. Hao wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. 200. Enyi mlioamini! Subirini, na vumilieni, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufaulu.
#
{199} أي: {وإن من أهل الكتاب} طائفة موفقة للخير يؤمنون بالله ويؤمنون بما {أُنزل إليكم وما أُنزل إليهم}، وهذا الإيمان النافع لا كمن يؤمن ببعض الرسل والكتب ويكفر ببعض، ولهذا لما كان إيمانهم عامًّا حقيقيًّا صار نافعاً فأحدث لهم خشية الله وخضوعهم لجلاله الموجب للانقياد لأوامره ونواهيه والوقوف عند حدوده وهؤلاء أهل الكتاب والعلم على الحقيقة، كما قال تعالى: {إنما يخشى اللهَ من عباده العلماءُ}، ومن تمام خشيتهم لله أنهم {لا يشترون بآيات الله ثمناً قليلاً}، فلا يقدمون الدنيا على الدين كما فعل أهل الانحراف الذين يكتمون ما أنزل الله ويشترون به ثمناً قليلاً، وأما هؤلاء فعرفوا الأمر على الحقيقة وعلموا أن من أعظم الخسران الرضا بالدون عن الدين، والوقوف مع بعض حظوظ النفس السفلية وترك الحق الذي هو أكبر حظ وفوز في الدنيا والآخرة، فآثروا الحق وبينوه ودعوا إليه، وحذروا عن الباطل، فأثابهم الله على ذلك بأن وعدهم الأجر الجزيل والثواب الجميل، وأخبرهم بقربه وأنه {سريع الحساب} فلا يستبطئون ما وعدهم الله، لأن ما هو آت محقق حصوله فهو قريب.
{199} Yani, "Na hakika, miongoni mwa Watu wa Kitabu" lipo kundi lililowezeshwa kufanya heri. Wanamwamini Mwenyezi Mungu, na wanayaamini "yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwao." Na hii ndiyo Imani yenye manufaa. Si kama mwenye kuwaamini baadhi ya Mitume na vitabu, na anawakufuru baadhi. Na kwa sababu hii, pindi imani yao ilipokuwa ya ujumla, ya uhakika, ikawa ni yenye manufaa. Kwa hivyo, ikawasababishia kumhofu Mwenyezi Mungu, na kuunyenyekea utukufu wake, yenye kulazimu kufuata amri zake na makatazo yake, na kusimamia katika mipaka yake. Na hawa ndio Watu wa Kitabu na elimu kwa uhakika, kama alivyosema Yeye Mtukufu. "Kwa hakika, wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanachuoni." Na katika kunyenyekea kwao kukamilifu kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba wao, "Hawanunui kwa Aya za Mwenyezi Mungu thamani ndogo". Kwa hivyo, hawaitangulizi dunia mbele ya dini, kama walivyofanya watu wapotovu; ambao wanaficha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na wananunua kwayo thamani ndogo. Na ama hawa, wao walilijua jambo hilo kwa uhalisia wake na wakajua kwamba katika hasara kubwa zaidi ni kutosheka na kilicho duni badala ya dini. Na kusimama na baadhi ya mafungu ya nafsi zilizo duni na kuiacha haki ambayo ndiyo fungu kubwa zaidi, na kufaulu katika dunia na Akhera. Basi wakaipendelea haki na wakaibainisha na wakailingania, na wakaonya dhidi ya batili. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawalipa kwa hayo kwamba aliwaahidi ujira mkubwa na thawabu nzuri, na akawajulisha ukaribu wake, na kwamba Yeye, "ni mwepesi wa kuhesabu.” Kwa hivyo, hawaoni kuwa yale aliyowaahidi Mwenyezi Mungu yaja polepole. Kwa sababu yale yanayokuja, ambayo hayana shaka kutokea kwake, basi hayo yako karibu.
#
{200} ثم حض المؤمنين على ما يوصلهم إلى الفلاح، وهو الفوز بالسعادة والنجاح، وأن الطريق الموصل إلى ذلك لزوم الصبر: الذي هو حبس النفس على ما تكرهه من ترك المعاصي ومن الصبر على المصائب وعلى الأوامر الثقيلة على النفوس، فأمرهم بالصبر على جميع ذلك. والمصابرة: هي الملازمة والاستمرار على ذلك على الدوام، ومقاومة الأعداء في جميع الأحوال. والمرابطة: وهو لزوم المحل الذي يُخاف من وصول العدو منه وأن يراقبوا أعداءهم ويمنعوهم من الوصول إلى مقاصدهم، لعلهم يفلحون: يفوزون بالمحبوب الديني والدنيوي والأخروي وينجون من المكروه كذلك. فعلم من هذا أنه لا سبيل إلى الفلاح بدون الصبر والمصابرة والمرابطة المذكورات، فلم يفلح مَنْ أفلح إلا بها ولم يفت أحداً الفلاحُ إلا بالإخلال بها أو ببعضها.
{200} Kisha akawahimiza Waumini kwa yale yanayowafikisha kwenye kufaulu. Nayo ni kupata furaha na kufaulu, na kwamba njia inayofikisha huko ni kushikamana na subira; ambayo ni kuizuia nafsi juu ya yale inayoyachukia ya kuacha dhambi na kuwa na subira juu ya misiba, na juu ya maamrisho mazito juu ya nafsi. Basi akawaamrisha wawe na subira juu ya hayo yote. Na uvumilivu ni kushikamana na kuendelea kufanya hivyo daima, na kupigana vita na maadui katika hali zote. Na Al-Murabata ni kushikamana na sehemu ambayo adui anahofiwa kufika kupitia hapo, na kwamba wawakalie macho maadui zao na wawazuie kuyafikia malengo yao, ili wapate kufaulu. Yani wafaulu kupata wanachokipenda cha kidini, na kidunia, na cha kiakhera. Na wapate kuokoka kutokana na wanachokichukia vile vile. Basi hajafaulu aliyefaulu isipokuwa kwa hayo. Na hakujamkosa mtu kufaulu isipokuwa kwa kuyakiuka hayo au baadhi yake.
Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwezesha, na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwake. Imetimia tafsiri ya Surat Al-Imran. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa neema zake. Na tunamuomba neema kamili.
* * *