Tafsiri ya Surat Al-Ghashiya
Tafsiri ya Surat Al-Ghashiya
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ (1) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ (2) عَامِلَةٌ نَاصِبَةٌ (3) تَصْلَى نَارًا حَامِيَةً (4) تُسْقَى مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ (5) لَيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِنْ ضَرِيعٍ (6) لَا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِنْ جُوعٍ (7) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَاعِمَةٌ (8) لِسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ (9) فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ (10) لَا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً (11) فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ (12) فِيهَا سُرُرٌ مَرْفُوعَةٌ (13) وَأَكْوَابٌ مَوْضُوعَةٌ (14) وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ (15) وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ (16)}.
1. Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? 2. Siku hiyo nyuso zitainama. 3. Zikifanya kazi, nazo taabani. 4. Ziingie katika Moto unaowaka. 5. Zikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka. 6. Hawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba. 7. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. 8. Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. 9. Zitakuwa radhi kwa juhudi yao. 10. Katika Bustani ya juu. 11. Hawatasikia humo upuuzi. 12. Humo imo chemchemi inayomiminika. 13. Humo vimo viti vilivyonyanyuliwa. 14. Na bilauri zilizopangwa. 15. Na matakia safu safu. 16. Na mazulia yaliyotandikwa.
#
{1} يذكر تعالى أحوال يوم القيامة وما فيها من الأهوال الطامَّة، وأنَّها تغشى الخلائق بشدائدها، فيجازَوْن بأعمالهم، ويتميَّزون إلى فريقين: فريق في الجنَّة، وفريق في السَّعير. فأخبر عن وصف كلا الفريقين:
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja hali za Siku ya Kiyama na mambo ya kutisha yaliyo ndani yake, na kwamba yatawafunika viumbe kwa shida zake, kisha watalipwa kwa vitendo vyao,
na watagawanyika makundi mawili: kundi la Peponi na kundi la Moto wa kuunguza.
Kwa hivyo akajulisha kuhusu sifa za vikundi vyote viwili:
#
{2 - 7} فقال في وصف أهل النار: {وجوهٌ يومئذٍ}؛ أي: يوم القيامة، {خاشعةٌ}: من الذُّلِّ والفضيحة والخزي، {عاملةٌ ناصبةٌ}؛ أي: تاعبة في العذاب، تجرُّ على وجوهها، {وتغشى وجوهَهم النارُ}؛ ويحتمل أن المراد بقوله: {وجوهٌ يومئذٍ خاشعةٌ. عاملةٌ نَّاصبةٌ}: في الدنيا لكونهم في الدُّنيا أهل عباداتٍ وعمل، ولكنَّه لما عدم شرطه، وهو الإيمان؛ صار يوم القيامة هباءً منثوراً.
وهذا الاحتمال وإن كان صحيحاً من حيث المعنى؛ فلا يدلُّ عليه سياق الكلام، بل الصواب المقطوع به هو الاحتمال الأول؛ لأنَّه قيَّده بالظرف، وهو يوم القيامةِ، ولأنَّ المقصود هنا بيان ذكر أهل النار عموماً، وذلك الاحتمال جزءٌ قليلٌ بالنسبة إلى أهل النار ، ولأنَّ الكلام في بيان حال الناس عند غشيان الغاشية؛ فليس فيه تعرُّضٌ لأحوالهم في الدُّنيا.
وقوله: {تَصْلى ناراً حاميةً}؛ أي: شديداً حرُّها تحيط بهم من كلِّ مكان، {تُسْقى من عينٍ آنيةٍ}؛ أي: شديدة الحرارة ، {وإن يَسْتَغيثوا يُغاثوا بماءٍ كالمهل يَشْوي الوجوهَ}؛ فهذا شرابهم، وأمَّا طعامُهم؛ فَـ {ليس لهم طعامٌ إلاَّ من ضريعٍ. لا يُسْمِنُ ولا يُغْني من جوع}: وذلك لأنَّ المقصود من الطعام أحد أمرين: إمَّا أن يسدَّ جوع صاحبه ويزيل عنه ألمه، وإمَّا أن يُسْمِنَ بدنَه من الهزال، وهذا الطعام ليس فيه شيءٌ من هذين الأمرين، بل هو طعامٌ في غاية المرارة والنَّتن والخسَّة، نسأل الله العافية.
{2 - 7} Basi akasema katika kuwaelezea watu wa Motoni: "Siku hiyo" ya Kiyama "nyuso zitainama" kutokana na fedheha na hizaya "Zikifanya kazi, nazo taabani" na zitahangaika katika adhabu, huku wakiburutwa "na Moto utazigubika nyuso zao.
" Na inawezekana kwamba kile kinachomaanishwa na kauli yake: “Siku hiyo nyuso zitainama. Zikifanya kazi, nazo taabani" kwa sababu walifanya ibada na matendo katika dunia hii, lakini hayakuwa yameambatana na masharti yake, ambayo ni imani; basi Siku ya Kiyama yakawa mavumbi yaliyotawanywa. Ingawa uwezekano huu ni sahihi katika maana yake, lakini muktadha wa mazungumzo hayaionyeshi. Bali maana sahihi ya uhakika ni ile maana ya kwanza. Kwa sababu aliiwekea mipaka ya wakati, yaani Siku ya Kiyama, na kwa sababu kinachokusudiwa hapa ni kueleza watu wa Motoni kwa ujumla, na uwezekano huo ni sehemu ndogo tu kuhusiana na watu wa Motoni, na kwa sababu mazungumzo haya yanaelezea hali ya watu watakapojiwa na msiba mkubwa, na hayaashirii hali zao katika dunia hii.
Na kauli yake: "Ziingie katika Moto unaowaka" utakaowazunguka kutokea kila mahali, "Zikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka" sana "Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyotibuka. Yatayo wababua nyuso zao." Hiki ndicho kinywaji chao, na ama chakula chao; “Hawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba.
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa" Haya ni kwa sababu makusudio ya chakula ni moja ya mambo mawili: ima kukidhi njaa ya mtu na kumpunguzia maumivu yake, au kuufanya mwili wake unenepe na kutodhoofika. Na chakula hiki hakina chochote katika vitu hivi viwili. Badala yake, ni chakula kichungu mno, kinachonuka na kibaya sana. Tunamuomba Mwenyezi Mungu salama.
#
{8 - 16} وأمَّا أهلُ الخير؛ فوجوههم يوم القيامةِ {ناعمةٌ}؛ أي: قد جرت عليهم نَضْرَةُ النعيم فَنَضَّرَتْ أبدانهم واستنارت وجوههم وسُرُّوا غاية السرور، {لسعيها}: الذي قدَّمته في الدُّنيا من الأعمال الصالحة والإحسان إلى عباد الله، {راضيةٌ}: إذْ وجدت ثوابه مدَّخراً مضاعفاً، فحمدت عقباه، وحصل لها كلُّ ما تتمنَّاه. وذلك أنَّها {في جنَّةٍ}: جامعةٍ لأنواع النَّعيم كلّها، {عاليةٍ}: في محلِّها ومنازلها؛ فمحلُّها في أعلى عِلِّيين، ومنازلها مساكنُ عاليةٌ، لها غرفٌ، ومن فوق الغرف غرفٌ مبنيَّةٌ يشرفون منها على ما أعدَّ الله لهم من الكرامة. ({قطوفُها دانيةٌ}؛ أي: كثيرة الفواكه اللذيذة المثمرة بالثمار الحسنة السهلة التناول؛ بحيث ينالونها على أيِّ حال كانوا، لا يحتاجون أن يَصْعَدوا شجرةً أو يستعصي عليهم منها ثمرةٌ). {لا تسمع فيها}؛ أي: الجنَّة {لاغيةً}؛ أي: كلمة لغوٍ وباطلٍ فضلاً عن الكلام المحرَّم، بل كلامُهم كلامٌ حسنٌ نافعٌ، مشتملٌ على ذكر الله وذكر نعمه المتواترة عليهم وعلى الآداب الحسنة بين المتعاشِرين الذي يسرُّ القلوب ويشرح الصدور. {فيها عينٌ جاريةٌ}: وهذا اسم جنس؛ أي: فيها العيون الجارية التي يفجِّرونها ويصرِّفونها كيف شاؤوا وأنَّى أرادوا. {فيها سررٌ مرفوعةٌ}: والسرر جمعُ سريرٍ، وهي المجالس المرتفعة في ذاتها وبما عليها من الفُرُش الليِّنة الوطيئة. {وأكوابٌ موضوعةٌ}؛ أي: أوانٍ ممتلئةٌ من أنواع الأشربة اللذيذة، قد وضعت بين أيديهم، وأعدَّت لهم، وصارت تحت طلبهم واختيارهم، يطوفُ بها عليهم الولدان المخلدون. {ونمارقُ مصفوفةٌ}؛ أي: وسائد من الحرير والإستبرق وغيرهما مما لا يعلمه إلاَّ الله، قد صُفَّتْ للجلوس والاتِّكاء عليها، وقد أريحوا عن أن يضعوها أو يصفوها بأنفسهم. {وزَرابِيُّ مبثوثةٌ}: والزرابِيُّ هي البسط الحسان، مبثوثةٌ؛ أي: مملوءةٌ بها مجالسهم من كلِّ جانب.
{8 - 16} Ama watu wema; Nyuso zao Siku ya Kiyama "zitakuwa kunjufu." Yaani, mng'aro wa neema utakuwa umewashukia, na kuifanya miili yao kuwa safi, nyuso zao zikawa na nuru, na wakawa na furaha tele. "Zitakuwa radhi kwa juhudi yao" ambazo walizitanguliza katika dunia hii miongoni mwa matendo mema na kuwafanyia hisani waja wa Mwenyezi Mungu. Kwani watapokuta malipo malipo yake yamewekwa na kuongezwa maradufu, basi watasifu mwisho wake na wakapata kila walichokuwa wakitaka. Haya ni kwa sababu watakuwa "Katika Bustani ya mbinguni" yenye kujumuisha kila namna ya neema "za juu" katika mahali na makao. Kwa sababu, mahali pake ni mahali pa juu zaidi na makao yake ni katika nyumba za juu, yenye vyumba, na juu ya vyumba hivyo kuna vimejengwa vyumba ambavyo kutokea hapo wataangalia mambo matukufu ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia. "Matunda yake yakaribu" ni mengi, matamu na ni rahisi kuyachuma, kiasi kwamba wataweza kuyachuma kwa hali yao yoyote ile, na hawatahitaji kupanda mti au wala hakuna tunda litakalokuwa gumu kulifikia humo. "Hawatasikia humo" Peponi "upuuzi" na maneno batili achilia mbali maneno ya haramu. Bali maneno yao ni maneno mazuri na yenye manufaa, ambayo yanajumuisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kukumbuka neema zake za mara kwa mara juu yao, na tabia njema baina ya wanaoishi pamoja, yanayopendeza nyoyo na kupanua vifua. "Humo imo chemchemi inayomiminika" wataifanya imiminike watakavyo na popote wapendapo. "Humo vimo viti vilivyonyanyuliwa." Navyo ni viti vya aina ya kitanda ambavyo ni viliinuliwa juu vyenyewe na pia kwa sababu ya magodoro laini na mazuri yaliyo juu yake. "Na bilauri zilizopangwa" huku zimejaa aina mbalimbali za vinywaji vya ladha, vilivyowekwa mbele yao, na zikatayarishwa kwa ajili yao, na zikawa zinapatikana kwa ombi lao na hiari yao, ambazo wataletewa mara kwa mara na watoto wa ujana wa milele. "Na matakia safu safu" yaliyotengenezwa kwa hariri laini na hariri nzito na vitu vinginevyo ambavyo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua. Hivyo vitakuwa vimeshapangwa kwa ajili yao kukalia na kuegemea, na watapumzishwa na suala la kuviweka hapo au kuvipanga wenyewe. "Na mazulia yaliyotandikwa" kila upande katika mahali pao pa kukaa.
{أَفَلَا يَنْظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ (17) وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ (18) وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ (19) وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ (20) فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنْتَ مُذَكِّرٌ (21) لَسْتَ عَلَيْهِمْ بِمُصَيْطِرٍ (22) إِلَّا مَنْ تَوَلَّى وَكَفَرَ (23) فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ (24) إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ (25) ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُمْ (26)}.
17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyoumbwa? 18. Na mbingu jinsi ilivyoinuliwa? 19. Na milima jinsi ilivyothibitishwa? 20. Na ardhi jinsi ilivyotandazwa? 21. Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. 22. Wewe si mwenye kuwatawalia. 23. Lakini anayerudi nyuma na kukataa. 24. Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa! 25. Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. 26. Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
#
{17 - 20} يقول تعالى حثًّا للذين لا يصدِّقون الرسول - صلى الله عليه وسلم - ولغيرهم من الناس أنْ يتفكَّروا في مخلوقات الله الدالَّة على توحيده. {أفلا ينظُرون إلى الإبل كيف خُلِقَتْ}؛ أي: ألا ينظُرون إلى خَلْقها البديع وكيف سخَّرها الله للعباد وذلَّلها لمنافعهم الكثيرة التي يضطَرُّون إليها؟ {وإلى الجبال كيف نُصِبَتْ}: بهيئةٍ باهرةٍ حصل بها الاستقرار للأرض وثباتُها من الاضطراب وأودع [الله] فيها من المنافع الجليلة ما أودع، {وإلى الأرض كيف سُطِحَتْ}؛ أي: مُدَّت مدًّا واسعاً، وسُهِّلت غاية التسهيل؛ ليستقرَّ العبادُ على ظهرها ويتمكَّنوا من حرثها وغراسها والبنيان فيها وسلوك طرقها.
واعلم أنَّ تسطيحها لا ينافي أنَّها كرةٌ مستديرةٌ قد أحاطتِ الأفلاك فيها من جميع جوانبها كما دلَّ على ذلك النقل والعقل والحسُّ والمشاهدة؛ كما هو مذكورٌ معروفٌ عند كثيرٍ من الناس ، خصوصاً في هذه الأزمنة، التي وقف الناس على أكثر أرجائها بما أعطاهم الله من الأسباب المقرِّبة للبعيد؛ فإنَّ التسطيح إنَّما ينافي كرويَّة الجسم الصغير جدًّا، الذي لو سطح؛ لم يبق له استدارةٌ تُذْكَر، وأمَّا جسم الأرض الذي هو كبيرٌ جدًّا واسعٌ ، فيكون كرويًّا مسطحاً، ولا يتنافى الأمران كما يعرف ذلك أرباب الخبرة.
{17-20} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akiwahimiza wale wasiomwamini Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikishie - na watu wengine kwamba wafikirie kuhusu viumbe vya Mwenyezi Mungu vinavyoashiria upweke wake. "Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyoumbwa" kwa uumbaji wa ajabu na jinsi Mwenyezi Mungu alivyomtiisha kwa ajili ya waja wake na kumfanya anyenyekee kwa sababu ya manufaa mengi wanayohitaji sana? "Na milima jinsi ilivyothibitishwa" kwa umbo la kung'aa ambalo kwalo ardhi ilipata utulivu na uthabiti ili isiyumbeyumbe, na akaweka humo manufaa makubwa. "Na ardhi jinsi ilivyotandazwa" na kufanywa rahisi sana. Ili waja wakae kwa utulivu juu ya mgongo wake na waweze kulima, kupanda, kujenga juu yake na kupitia katika njia zake. Na jua kuwa kutandazwa kwake hakupingani na suala la kwamba ni ya umbo la mpira wa duara ambamo sayari zinaizunguka pande zake zote, kama ilivyothibitishwa na mapokezi ya kimaandiko, akili, hisia na kuangalia kwa macho. Kama ilivyotajwa na inavyojulikana kwa watu wengi, hasa katika nyakati hizi, ambazo watu wameweza kufika katika sehemu nyingi za dunia kwa sababu ya kile ambacho Mwenyezi Mungu amewapa cha sababu zinazoweza kuleta karibu kilicho mbali. Kwa maana kutandazwa kunapingana tu na umbo la mwili mdogo sana, ambalo ikiwa litatandazwa, basi halitakuwa na mduara unaoonekana utakaobakia. Lakini mwili wa ardhi ambao ni mkubwa sana na wenye wasaa, basi huo unaweza kuwa wa duara na tambarare, na mambo hayo mawili hayapingani kama wale walio na uzoefu wanavyojua hilo.
#
{21 - 22} {فذكِّرْ إنَّما أنت مذكِّرٌ}؛ أي: ذكِّر الناس وعِظْهم وأنذِرْهم وبشِّرْهم؛ فإنَّك مبعوثٌ لدعوة الخلق إلى الله وتذكيرهم، ولم تُبْعَثْ عليهم مسيطراً عليهم مسلطاً موكلاً بأعمالهم؛ فإذا قمت بما عليك؛ فلا عليك بعد ذلك لومٌ؛ كقوله تعالى: {وما أنت عليهم بجبارٍ. فَذكِّرْ بالقرآنِ مَن يخافُ وعيدِ}.
{21 - 22} "Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji." Yaani, wakumbushe watu, na wape mawaidha, waonye na wabashirie. Kwa maana ulitumwa kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwakumbusha, na wala hukutumwa kuwatawala kwa nguvu na kukabidhiwa kusimamia matendo yao. Kwa hivyo, ukifanya kile unachopaswa kufanya, basi huna lawama baada ya hayo,
kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeliogopa onyo."
#
{23 - 24} وقوله: {إلاَّ مَن تولَّى وكَفَرَ}؛ أي: لكن مَن تولَّى عن الطاعة وكفر بالله، {فيعذِّبُه الله العذابَ الأكبرَ}؛ أي: الشديد الدائم.
{23 - 24} Na kauli yake: "Lakini anayerudi nyuma" akaacha kutii "na akakufuru" Mwenyezi Mungu. "Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa" ya kudumu.
#
{25 - 26} {إنَّ إلينا إيابَهم}؛ أي: رجوع الخلائق وجمعهم في يوم القيامةِ. {ثم إنَّ علينا حسابَهم}: على ما عملوا من خيرٍ وشرٍّ.
{25 - 26} "Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao." Yaani, marejeo ya viumbe vyote na kukusanywa kwao Siku ya Kiyama. "Kisha hakika ni juu yetu Sisi hesabu yao!"
Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *