Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{وَالْفَجْرِ (1) وَلَيَالٍ عَشْرٍ (2) وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ (3) وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ (4) هَلْ فِي ذَلِكَ قَسَمٌ لِذِي حِجْرٍ (5)}.
1. Ninaapa kwa alfajiri. 2. Na kwa masiku kumi. 3. Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja. 4. Na kwa usiku unapopita. 5. Je, hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
#
{1 - 5} الظاهر أن المقسم عليه هو المقسَم به ، وذلك جائزٌ مستعملٌ إذا كان أمراً ظاهراً مهمًّا، وهو كذلك في هذا الموضع. أقسم تعالى بالفجر، الذي هو آخرُ الليل ومقدِّمة النهار؛ لما في إدبار الليل وإقبال النهار من الآيات الدالَّة على كمال قدرة الله تعالى، وأنَّه تعالى هو المدبِّر لجميع الأمور، الذي لا تنبغي العبادة إلاَّ له. ويقع في الفجر صلاةٌ فاضلةٌ معظَّمة يَحْسُنُ أن يُقسم الله بها، ولهذا أقسم بعده بالليالي العشر، وهي على الصحيح ليالي عشر رمضان أو عشر ذي الحجَّة ؛ فإنَّها ليالٍ مشتملةٌ على أيَّام فاضلةٍ، ويقع فيها من العبادات والقُرُبات ما لا يقع بغيرها. وفي ليالي عشر رمضان ليلة القدر، التي هي خيرٌ من ألف شهر، وفي نهارها صيامُ آخر رمضان، الذي هو أحد أركان الإسلام العظام. وفي أيَّام عشر ذي الحجَّة الوقوف بعرفة، الذي يغفر الله فيه لعباده مغفرةً يحزن لها الشيطان؛ فإنَّه ما رُئي الشيطان أحقر ولا أدحر منه في يوم عرفة ؛ لما يرى من تنزُّل الأملاك والرحمة من الله على عباده ، ويقع فيها كثيرٌ من أفعال الحجِّ والعمرة، وهذه أشياء معظَّمة مستحقَّة أن يقسم الله بها، {والليل إذا يَسْرِ}؛ أي: وقت سريانه وإرخائه ظلامه على العباد، فيسكنون ويستريحون ويطمئنُّون رحمةً منه تعالى وحكمةً. {هل في ذلك}: المذكور، {قَسَمٌ لذي حِجْرٍ}؛ أي: لذي عقل؟ نعم بعضُ ذلك يكفي لمن كان له قلبٌ أو ألقى السمع وهو شهيدٌ.
{1 - 5} Hapa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliapa kwa alfajiri, kwa sababu katika kuondoka usiku na kuingia mchana kuna ishara zinazoashiria ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba Yeye Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuendesha kila jambo, ambaye hakuna anayepasa kuabudiwa isipokuwa Yeye tu. Pia wakati wa Alfajiri kuna swala bora na yenye heshima ambayo ni vizuri Mwenyezi Mungu kuapa kwa wakati huo. Na ndiyo maana akaapa baada yake kwa usiku kumi, ambayo kwa mtazamo sahihi ni usiku kumi za Ramadhani au usiku kumi za Dhul-Hijja. Kwani hizo ni usiku zinazojumuisha masiku adhimu, na ndani yake kuna ibada na vitendo vya kujiweka karibu na Mweneyezi Mungu ambavyo havitokei katika nyakati zinginezo. Katika usiku kumi za Ramadhani, kuna Laylatul-Qadr, ambayo ni bora kuliko miezi elfu moja, na katika mchana wake kuna kufunga saumu mwishoni mwa Ramadhani, ambayo ni moja katika nguzo kuu za Uislamu. Na katika siku kumi za Dhul-Hijja, kuna kusimama Arafa, ambapo Mwenyezi Mungu huwasamehe waja wake kwa msamaha unaomhuzunisha Shetani. Kwani Shetani hakuwahi kuonekana amedunika zaidi wala kushindwa zaidi kuliko Siku ya Arafa. Kwa sababu ya yale anayoona ya kuteremka kwa malaika na rehema za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na vitendo vingi vya Hija na Umra vinafanyika humo, na haya ni mambo makubwa yanayostahiki Mwenyezi Mungu kuapa kwayo. "Na kwa usiku unapopita;" yaani, wakati linapoanza giza lake na kuwafunika waja, kwa hivyo wakatulia, wakatulia na wakatua, jambo ambalo ni rehema kwao na hekima kutoka kwake. "Je, hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?" Ndiyo, baadhi ya hayo yanatosha kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.
{أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ (6) إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ (7) الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ (8) وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ (9) وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ (10) الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ (11) فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ (12) فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ (13) إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ (14)}.
6. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya kina A'di? 7. Wa Iram, wenye majumba marefu? 8. Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? 9. Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni? 10. Na Firauni mwenye vigingi? 11. Ambao walifanya jeuri katika nchi? 12. Wakakithirisha humo ufisadi? 13. Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. 14. Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
#
{6 - 14} يقول تعالى: {ألم تر}: بقلبك وبصيرتك، {كيف فَعَلَ}: بهذه الأمم الطاغية، عاد وهي {إرم}: القبيلة المعروفة في اليمن، {ذات العِماد}؛ أي: القوَّة الشديدة والعتوِّ والتجبُّر، {التي لم يُخْلَقْ مثلُها في البلاد} ؛ أي: في جميع البلدان في القوَّة والشدَّة؛ كما قال لهم نبيُّهم هودٌ عليه السلام: {واذكُروا إذْ جَعَلَكُم خُلَفاء من بعدِ قوم نوح وزادَكُم في الخَلْقِ بَسْطَةً فاذكُروا آلاء الله لعلَّكُم تفلِحونَ}. {وثمودَ الذين جابوا الصَّخْر بالواد}؛ أي: وادي القرى؛ نحتوا بقوَّتهم الصخور فاتَّخذوها مساكن، {وفرعونَ ذي الأوتادِ}؛ أي: ذي الجنود الذي ثبَّتوا ملكه كما تثبت الأوتاد [و] ما يراد إمساكه بها، {الذين طَغَوْا في البلاد}: هذا الوصف عائدٌ إلى عادٍ وثمودَ وفرعونَ ومن تَبِعَهم؛ فإنَّهم طَغَوْا في بلاد الله، وآذوا عباد الله في دينهم ودنياهم. ولهذا قال: {فأكثروا فيها الفسادَ}: وهو العمل بالكفر وشعبه من جميع أجناس المعاصي، وسعوا في محاربة الرُّسُل وصدِّ الناس عن سبيل الله، فلما بلغوا من العتوِّ ما هو موجبٌ لهلاكهم؛ أرسل الله عليهم من عذابه ذَنُوباً وسوطَ عذاب، {إنَّ ربَّك لبالمرصادِ}: لمن يعصيه ؛ يمهِلُه قليلاً ثم يأخُذُه أخذَ عزيزٍ مقتدرٍ.
{6 - 14} Mwenyezi Mungu anasema: "Kwani hukuona" kwa moyo wako na ufahamu wako, "jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya" mataifa haya dhalimu, ambayo ni 'Adi ambayo ndio "Iram" ambao ni kabila maarufu huko Yemeni "wenye majumba marefu" na nguvu iliyokithiri na kiburi. "Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?" Kwa sababu ya nguvu zao na ukali wao; kama alivyowaambia Nabii wao Hud - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "Na kumbukeni alivyokufanyeni mshike pahala pa kaumu ya Nuhu, na akakuzidisheni katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.
" Na akasema "Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?" Yaani: bonde la Al-Qura. Walikuwa wakichonga majabali kwa nguvu zao, na wakayafanya kuwa maskani yao. "Na Firauni mwenye vigingi?" Yaani, mwenye askari waliouimarisha ufalme wake kama vile vigingi vinavyoimarisha kile ambacho vinashikilia. "Ambao walifanya jeuri katika nchi?" Maelezo haya yanawahusu akina Adi, Thamudi, Firauni na wale waliowafuata. Hao walifanya jeuri katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na wakawadhuru waja wa Mwenyezi Mungu katika dini yao na dunia yao.
Ndiyo maana akasema: "Wakakithirisha humo uharibifu?" Nao ni ukafiri na matawi yake ya kila aina ya maasia, na wakajitahidi kupigana vita na Mitume na kuwazuilia watu njia ya Mwenyezi Mungu. Lakini walipofika kiwango cha uasi ambacho kililazimu waangamizwe, Mwenyezi Mungu akawaletea mjeledi wa adhabu. "Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia" kwa mwenye kumuasi. Yeye humpa muda kidogo, kisha mchukue amshike mshiko wa Mwenye nguvu Mwenye uwezo mno.
{فَأَمَّا الْإِنْسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ (15) وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ (16) كَلَّا بَلْ لَا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ (17) وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَى طَعَامِ الْمِسْكِينِ (18) وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَمًّا (19) وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا (20)}.
15. Ama mtu anapojaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha,
husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! 16. Na ama anapomjaribu akampunguzia riziki yake,
husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! 17. Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima. 18. Wala hamhimizani kulisha masikini. 19. Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa. 20. Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
#
{15 - 20} يخبر تعالى عن طبيعة الإنسان من حيث هو، وأنَّه جاهلٌ ظالمٌ لا علم له بالعواقب، يظنُّ الحالة التي تقع فيه تستمرُّ ولا تزول، ويظنُّ أنَّ إكرام الله في الدُّنيا وإنعامه عليه يدلُّ على كرامته [عنده] وقربِهِ منه، وأنَّه إذا {قَدَرَ عليه رِزْقَه}؛ أي: ضيَّقه، فصار بِقَدَرِ قوتِهِ لا يفضُلُ عنه؛ أنَّ هذا إهانةٌ من الله له، فردَّ الله عليه هذا الحسبان، فقال: {كلا}؛ أي: ليس كلُّ مَنْ نَعَّمْتُهُ في الدُّنيا فهو كريمٌ عليَّ، ولا كلُّ من قَدَرْتُ عليه رِزْقَه فهو مهانٌ لديَّ، وإنَّما الغِنى والفقر والسعة والضيق ابتلاءٌ من الله وامتحانٌ يمتحن به العباد؛ ليرى من يقوم له بالشكر والصبر، فيثيبه على ذلك الثواب الجزيل، ممَّن ليس كذلك، فينقله إلى العذاب الوبيل. وأيضاً؛ فإنَّ وقوف همَّة العبد عند مراد نفسه فقط من ضعف الهمَّة، ولهذا لامَهُمُ الله على عدم اهتمامهم بأحوال الخلق المحتاجين، فقال: {كلاَّ بل لا تكرِمون اليتيمَ}: الذي فقد أباه وكاسبه واحتاج إلى جبر خاطره والإحسان إليه؛ فأنتُم لا تكرِمونه بل تهينونه، وهذا يدلُّ على عدم الرحمة في قلوبكم وعدم الرغبة في الخير، {ولا تحاضُّون على طعام المسكين}؛ أي: لا يحضُّ بعضكم بعضاً على إطعام المحاويج من الفقراء والمساكين ، وذلك لأجل الشحِّ على الدنيا ومحبَّتها الشديدة المتمكَّنة من القلوب. ولهذا قال: {وتأكُلون التُّراثَ}؛ أي: المال المخلَّف، {أكلاً لَمًّا}؛ أي: ذريعاً، لا تبقون على شيء منه، {وتحبُّون المال حُبًّا جَمًّا}؛ أي: شديداً ، وهذا كقوله: {بل تؤثرون الحياةَ الدُّنيا والآخرةُ خيرٌ وأبقى}، {كلاَّ بل تحبُّونَ العاجِلَةَ وتَذَرون الآخرةَ}.
{15 - 20} Mwenyezi Mungu anatuambia kuhusu asili ya mwanadamu jinsi alivyo, na kwamba yeye ni mjinga na dhalimu na hana elimu ya matokeo ya mambo. Anadhani kwamba hali inayompata itaendelea na haitaondoka, na anadhani kuwa kumtukuza ambako Mwenyezi Mungu anamtukuza katika dunia na neema zake anazompa vinaashiria heshima yake
[kwake] na ukaribu wake kwake, na kwamba ikiwa "atampunguzia riziki yake" ikawa kiasi cha chakula kisichozidi mahitaji yake, kwamba hilo ni kumdunisha kutokako kwa Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akamjibu dhana yake hii,
akasema: "Sivyo hivyo!" Yaani, siyo kila niliyembariki katika dunia hii ni mtukufu kwangu, wala kila mtu ambaye nimempunguzia riziki yake ni duni mbele yangu. Bali utajiri na umasikini, wingi na dhiki ni majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mtihani ambao kwa huo huwajaribu waja wake; ili kumuona anayemshukuru na kuwa na subira, ndiyo amlipe malipo makubwa kwa hayo. Na yule asiyekuwa hivyo, basi amhamishe hadi kwenye adhabu kali. Na pia; hima ya mja kusimamia tu kwenye kile anachokitaka tu ni katika hima dhaifu, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawalaumu kwa kukosa kwao kujali masilahi ya wahitaji,
kwa hivyo akasema: “Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima" aliyefiwa na baba yake na yule aliyekuwa akimchumia, na akahitaji wa kumliwaza na kumfanyia wema. Nyinyi hamumkirimu, lakini badala yake mnamtweza, na hili linaashiria ukosefu wa huruma katika nyoyo zenu na kutotaka kwenu mema. "Wala hamhimizani kulisha masikini" Na hili ni kwa sababu ya ubahili wenu juu ya mambo ya dunia na kuipenda sana ambako kumeimarika katika nyoyo zenu.
Ndiyo maana akasema: "Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa" bila kubakisha kitu katika huo. "Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
" Na hili ni kama kauli yake: "Lakini nyinyi mnahiari maisha ya dunia! Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi." Na akasema "Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani. Na mnaacha maisha ya Akhera."
{كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا (21) وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا (22) وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنْسَانُ وَأَنَّى لَهُ الذِّكْرَى (23) يَقُولُ يَالَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي (24) فَيَوْمَئِذٍ لَا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ (25) وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ (26) يَاأَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ (27) ارْجِعِي إِلَى رَبِّكِ رَاضِيَةً مَرْضِيَّةً (28) فَادْخُلِي فِي عِبَادِي (29) وَادْخُلِي جَنَّتِي (30)}
21. Sivyo hivyo! Itakapovunjwa ardhi vipande vipande. 22. Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu. 23. Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? 24.
Atasema: Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu! 25. Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. 26 Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. 27. Ewe nafsi iliyotua! 28. Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umeridhiwa. 29. Basi ingia miongoni mwa waja wangu. 30. Na ingia katika Pepo yangu.
#
{21 - 24} {كلاَّ}؛ أي: ليس كلُّ ما أحببتم من الأموال وتنافستُم فيه من اللَّذَّات بباقٍ لكم، بل أمامكم يومٌ عظيمٌ وهولٌ جسيمٌ تُدَكُّ فيه الأرض والجبال وما عليها حتى تُجْعَلَ قاعاً صفصفاً لا عِوَجَ فيه ولا أمتا، ويجيء الله لفصل القضاء بين عباده في ظُلَلٍ من الغمام، ويجيء الملائكة الكرام أهل السماواتِ كلُّهم {صفًّا صفًّا}؛ أي: صفّاً بعد صفٍّ، كلُّ سماءٍ يجيء ملائكتها صفًّا، يحيطون بمن دونَهم من الخلق، وهذه الصفوف صفوفُ خضوع وذُلٍّ للملك الجبار، {وجيء يومئذٍ بجهنَّم}: تقودُها الملائكة بالسلاسل؛ فإذا وقعت هذه الأمور؛ فَـ {يومئذٍ يتذكَّرُ الإنسان}: ما قدَّمه من خيرٍ وشرٍّ، {وأنَّى له الذِّكرى}: فقد فات أوانُها وذهب زمانها، {يقول}: متحسِّراً على ما فرَّط في جنب الله: {يا ليتني قدَّمتُ لحياتي}: الباقية الدائمة - عملاً صالحاً؛ كما قال تعالى: {يقول يا ليتني اتَّخَذْتُ مع الرسولِ سبيلاً. يا ويلتى لَيْتَني لم أتَّخِذْ فلاناً خليلاً}، وفي هذا دليلٌ على أنَّ الحياة التي ينبغي السعي في كمالها وتحصيلها وكمالها وفي تتميم لَذَّاتها هي الحياة في دار القرار؛ فإنَّها دارُ الخُلد والبقاء.
{21 - 24} "Sivyo hivyo!" Yaani, si mali zote mlizozipenda na starehe mlizoshindania zitabaki pamoja nanyi. Bali mbele yenu iko siku kuu na ya kutisha ambayo ardhi na milima na vyote vilivyomo vitateketezwa mpaka vifanywe kuwa tambarare, uwanda, usiokwa na mdidimio wala mwinuko. Na Mwenyezi Mungu atakuja kuhukumu baina ya waja wake katika vivuli vya mawingu, na watakuja Malaika watukufu wakazi wa mbinguni wote "safu safu." Kila mbingu watawajia Malaika wake safu safu wakiwazunguka wasiokuwa wao chini miongoni mwa viumbe. Na safu hizi ni safu za kunyenyekea na kumdhalilikia Mfalme, afanyaye atakavyo. "Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo" malaika wakiivuruta kwa minyororo. Kwa hivyo, mambo haya yakishatokea, basi "siku hiyo mtu atakumbuka" mema na maovu aliyoyatanguliza. "Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?" Kwani wakati wake utakuwa umeshapita,
"atasema" akijuta kwa yale aliyoyapuuza upande wa Mwenyezi Mungu: "Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu" ya kubakia milele - matendo mema.
Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake,
na huku anasema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume! Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki!" Na katika hili kuna ushahidi kwamba maisha ambayo mtu anapaswa kujitahidi kuyakamilisha, kuyapata na kutimiza raha zake ni maisha ya nyumba ya kudumu milele.
#
{25 - 26} {فيومئذٍ لا يعذِّبُ عذابَه أحدٌ}: لمن أهمل ذلك اليوم ونسي العمل له، {ولا يوثِقُ وَثاقَه أحدٌ}؛ فإنَّهم يقرنون بسلاسل من نارٍ، ويسحَبون على وجوههم في الحميم، ثم في النار يُسْجَرون؛ فهذا جزاءُ المجرمين.
{25 - 26} "Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake" kwa yule aliyeipuuza siku hiyo na akasahau kuifanyia kazi. "Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake." Kwani watafungwa pamoja kwa minyororo ya moto, na wataburutwa juu ya nyuso zao kwenye maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni. Haya ndiyo malipo ya wahalifu.
#
{27 - 30} وأمَّا مَن آمن بالله واطمأنَّ به وصدَّق رسله؛ فيقال له: {يا أيَّتها النفسُ المطمئنَّةُ}: إلى ذِكْرِ الله، الساكنة إلى حبِّه ، التي قرَّتْ عينُها بالله، {ارجِعي إلى ربِّك}: الذي ربَّاك بنعمته، [وأسدى عليك من إحسانه ما صرت به من أوليائه وأحبابه] {راضيةً مَرْضِيَّةً}؛ أي: راضيةً عن الله وعن ما أكرمها به من الثواب، والله قد رضي عنها، {فادْخُلي في عبادي. وادْخُلي جنَّتي}: وهذا تخاطَبُ به الرُّوح يوم القيامةِ، وتخاطَبُ به وقتَ السياق والموت.
{27 - 30} Ama anayemuamini Mwenyezi Mungu, na akatulizana naye na akawasadiki Mitume wake,
basi ataambiwa: "Ewe nafsi iliyotua" kwa sababu ya ukumbusho wa Mwenyezi Mungu na ikatulia kwa sababu ya mapenzi yake, ambayo macho yake yalifurahia kwa sababu ya Mwenyezi Mungu. "Rejea kwa Mola wako Mlezi" ambaye alikulea kwa neema zake,
[na akafikishia wema wake ambavyo kwayo ukawa katika wendani wake na vipenzi vyake] "umeridhika, na umemridhiwa." Yaani, umeridhika na Mwenyezi Mungu na ujira aliokukirimu nao, naye Mwenyezi Mungu ameridhika nawe. "Basi ingia miongoni mwa waja wangu. Na ingia katika Pepo yangu." Haya ndiyo itakayoambiwa roho Siku ya Kiyama, na pia ataambiwa hayo wakati wa kufa kwake.
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.