:
Tafsiri ya Surat Al-A'la
Tafsiri ya Surat Al-A'la
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 19 #
{سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى (1) الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّى (2) وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَى (3) وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَى (4) فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَى (5) سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنْسَى (6) إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَى (7) وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَى (8) فَذَكِّرْ إِنْ نَفَعَتِ الذِّكْرَى (9) سَيَذَّكَّرُ مَنْ يَخْشَى (10) وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى (11) الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَى (12) ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَى (13) قَدْ أَفْلَحَ مَنْ تَزَكَّى (14) وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّى (15) بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (16) وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَى (17) إِنَّ هَذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَى (18) صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى (19)}.
1. Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa. 2. Aliyeumba, na akaweka sawa. 3. Na ambaye amekadiria na akaongoa. 4. Na aliyeotesha malisho. 5. Kisha akayafanya makavu, meusi. 6. Tutakusomesha wala hutasahau. 7. Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhahiri na yaliyofichikana. 8. Na tutakusahilishia yawe mepesi. 9. Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. 10. Atakumbuka mwenye kuogopa. 11. Na atajitenga mbali nayo mpotovu. 12. Ambaye atauingia Moto mkubwa. 13. Tena humo hatakufa wala hawi hai. 14. Hakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa. 15. Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. 16. Lakini nyinyi mnahiari maisha ya dunia! 17. Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. 18. Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo. 19. Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
#
{1 - 3} يأمر تعالى بتسبيحه المتضمِّن لذكره وعبادته والخضوع لجلاله والاستكانة لعظمته، وأن يكون تسبيحاً يليق بعظمة الله تعالى؛ بأن تُذْكَرَ أسماؤه الحسنى العالية على كل اسم بمعناها العظيم الجليل ، وتذكر أفعاله التي منها أنَّه خلق المخلوقات فسواها؛ أي: أتقن وأحسن خلقها، {والذي قَدَّرَ}: تقديراً تتبعه جميع المقدَّرات، {فهدى}: إلى ذلك جميع المخلوقات، وهذه الهداية العامَّة التي مضمونها أنَّه هدى كلَّ مخلوق لمصلحته.
{1 - 3} Mwenyezi Mungu anaamuru atakaswe, jambo linalojumuisha kumkumbuka, kumuabudu, kunyenyekea kwa ajili ya utukufu wake na kujisalimisha kwa ukuu wake, na kwamba kuwe kumtakasa kunakoufailia ukuu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa kutaja majina yake mazuri, yaliyo juu ya kila jina kwa maana zake kuu na tukufu, na kutaja matendo yake ambayo miongoni mwake ni kwamba aliumba viumbe na akawafanya kuwa sawasawa. "Na ambaye amekadiria na akaongoa." Huku ni kuongoza kwa jumla ambako ni kwamba aliongoza kila kiumbe kufikia mambo yenye masilahi yake.
#
{4 - 5} وتُذكَر فيها نِعَمه الدنيويَّة، ولهذا قال: {والذي أخرج المرعى}؛ أي: أنزل من السماء ماءً، فأنبت به أصناف النبات والعشب الكثير، فرتع فيه الناسُ والبهائم وجميع الحيوانات. ثم بعد أن استكمل ما قَدَّرَ له من الشباب؛ ألوى نباته وصوَّح عشبه، {فجعله غثاءً أحوى}؛ أي: أسود؛ أي: جعله هشيماً رميماً.
{4 - 5} Na kwamba zitajwe neema zake za kidunia, na ndiyo sababu akasema: "Na aliyeotesha malisho" Yaani aliteremsha maji kutoka mbinguni, na kwa hayo akaotesha aina mbalimbali za mimea na nyasi nyingi. Kwa hivyo watu, mifugo na wanyama wote wakala kwa hayo. Halafu baada ya kuikamilishia hali ya mwonekano wake mzuri zaidi, alinyausha mimea yake na akakausha nyasi yake "Kisha akayafanya makavu, meusi."
#
{6 - 7} ويذكر فيها نعمه الدينيَّة، ولهذا امتنَّ الله بأصلها ومادَّتها، وهو القرآن، فقال: {سنقرِئُك فلا تَنسى}؛ أي: سنحفظ ما أوحيناه إليك من الكتاب ونوعيه قلبك؛ فلا تنسى منه شيئاً، وهذه بشارةٌ من الله كبيرةٌ لعبده ورسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -؛ أنَّ الله سيعلمه علماً لا ينساه، {إلاَّ ما شاء الله}: مما اقتضت حكمتُه أن ينسيكه لمصلحةٍ وحكمةٍ بالغةٍ. {إنَّه يعلم الجهر وما يَخْفى}: ومن ذلك أنَّه يعلم ما يُصْلِحُ عباده؛ أي: فلذلك يشرع ما أراد ويحكم بما يريد.
{6 - 7} Na kwamba zitajwe humo neema zake za kidini. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja asili na kiini cha neema hii ambayo ni Qurani, akasema: "Tutakusomesha wala hutasahau." Yaani, tutayahifadhi yale tuliyokuteremshia katika katika moyo wako, kwa hivyo hutasahau chochote humo. Na hii ni bishara kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mja wake na Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba Mwenyezi Mungu atamfundisha elimu ambayo hataisahau. "Ila akipenda Mwenyezi Mungu" katika yale yatakayotakiwa na hekima yake kwamba akusahaulishe hayo kwa ajili ya masilahi na hekima ya kubwa. "Hakika Yeye anayajua yaliyo dhahiri na yaliyofichikana." Na katika hayo ni kwamba anajua yale yanayowafanya waja kutengenea. Ndiyo maana akawawekea sheria ya yale ayatakayo na kuhukumu anachotaka.
#
{8} {ونيسِّرُك لليُسرى}: وهذه أيضاً بشارةٌ أخرى ؛ أنَّ الله ييسِّر رسولَه - صلى الله عليه وسلم - لليُسرى في جميع أموره، ويجعل شرعَه ودينَه يسيراً.
{8} "Na tutakusahilishia yawe mepesi." Hii pia ni bishara njema kwamba Mwenyezi Mungu atamfanyia Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - yawe mepesi katika mambo yake yote, na ataifanya sheria yake na dini yake kuwa nyepesi.
#
{9 - 13} {فذكِّر}: بشرع الله وآياته، {إن نفعتِ الذِّكْرى}؛ أي: ما دامت الذِّكرى مقبولةً والموعظة مسموعةً، سواء حصل من الذكرى جميع المقصود أو بعضه. ومفهوم الآية أنَّه إن لم تنفع الذِّكرى؛ بأنْ كان التَّذكير يزيد في الشرِّ أو يَنْقُصُ من الخير؛ لم تكن مأموراً بها، بل منهيًّا عنها؛ فالذِّكرى ينقسم الناس فيها قسمين: منتفعون، وغير منتفعين. فأمّا المنتفعون فقد ذكرهم بقوله: {سيذَّكَّر مَن يخشى}: الله؛ فإنَّ خشية الله تعالى والعلم بمجازاته على الأعمال توجب للعبد الانكفاف عمَّا يكرهه الله والسعي في الخيرات، وأمَّا غير المنتفعين؛ فذكرهم بقوله: {ويتجنَّبُها الأشقى. الذي يَصْلى النارَ الكُبرى}: وهي النار الموقدة، التي تطَّلِعُ على الأفئدة، {ثمَّ لا يموت فيها ولا يَحْيا}؛ أي: يعذَّب عذاباً أليماً من غير راحةٍ ولا استراحةٍ، حتَّى إنَّهم يتمنَّوْن الموت؛ فلا يحصُلُ لهم؛ كما قال تعالى: {لا يقضى عليهم فيموتوا ولا يخفَّفُ عنهم من عذابها}.
{9 - 13} "Basi kumbusha" kwa Sheria ya Mwenyezi Mungu na Aya zake, "kama kukumbusha kunafaa." Yaani, maadamu ukumbusho huo unakubaliwa na mawaidha hayo yanasikiwa, hata kama kutapatikana kwa hayo yote anayokusudiwa au baadhi yake. Na maana isiyo ya moja kwa moja ya Aya hii ni kwamba ikiwa ukumbusho haufai; kwa njia ya kwamba yanaongeza maovu au yanapunguza mema, basi haitaamrishwa kufanya hivyo. Bali yatakuwa yamekatazwa. Kwa hivyo, watu wamegawanyika katika makundi mawili wakati wa ukumbusho: wale wanaonufaika nao na wasionufaika nao. Ama wale wanaonufaika, hao aliwataja kwa kauli yake: “Atakumbuka mwenye kuogopa" Mwenyezi Mungu. Kwa maana kumcha Mwenyezi Mungu na kujua malipo yake juu ya matendo inamlazimu mja kujiepusha na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu na kujitahidi kufanya mema. Na ama wasionufaika, aliwataja katika kauli yake: "Na atajitenga mbali nayo mpotovu. Ambaye atauingia Moto mkubwa" uliowashwa. Ambao utapanda nyoyoni. "Tena humo hatakufa wala hawi hai." Ataadhibiwa adhabu chungu bila ya kupumzishwa kiasi kwamba watatamani kufa. Lakini hilo pia hawatalipata, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake."
#
{14 - 15} {قد أفلح من تَزَكَّى}؛ أي: قد فاز وربح من طهَّر نفسه ونقَّاها من الشرك والظلم ومساوئ الأخلاق، {وذَكَرَ اسمَ ربِّه فصلَّى}؛ أي: اتَّصف بذكر الله، وانصبغ به قلبُه، فأوجب له ذلك العمل بما يرضي الله، خصوصاً الصلاة، التي هي ميزانُ الإيمان. هذا معنى الآية [الكريمة]، وأمَّا من فسَّر قوله: {تزكى}؛ يعني: أخرج زكاة الفطر، و {ذكر اسم ربِّه فصلى}؛ أنَّه صلاة العيد؛ فإنَّه وإن كان داخلاً في اللفظ وبعض جزئيَّاته؛ فليس هو المعنى وحده.
{14 - 15} "Hakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa" kutokana na ushirikina, dhuluma na maadili mabaya. "Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali." Yaani, alisifika na sifa ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na moyo wake ukajaa hayo, kwa hivyo matendo hayo yakamsababishia kufanya anayoridhia Mwenyezi Mungu, hasa swala, ambayo ndiyo kipimo cha imani. Hii ndiyo maana ya Aya hii. Na ama aliyeifafanua kauli yake: "aliyejitakasa;" yaani, kutoa Zakaatul-Fitr. "Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akaswali" kwamba ni swala ya Idi, basi hata ikiwa maana hizi zimejumuishwa katika maneno ya aya hizi na ni baadhi yake, hiyo siyo maana yake ya pekee.
#
{16 - 17} {بل تؤثرون الحياة الدُّنيا}؛ أي: تقدِّمونها على الآخرة، وتختارون نعيمها المنغَّص المكدَّر الزائل على الآخرة، {والآخرةُ خيرٌ وأبقى}: خيرٌ من الدُّنيا في كلِّ وصفٍ مطلوبٍ، {وأبقى}؛ لكونها دار خلدٍ وبقاءٍ [وصفاء] والدنيا دار فناء. فالمؤمن العاقل لا يختار الأردأ على الأجود، ولا يبيع لذَّةَ ساعةٍ بترحة الأبد، فحبُّ الدُّنيا وإيثارها على الآخرة رأس كلِّ خطيئة.
{16 - 17} "Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia" kuliko ya Akhera, na kuchagua neema zake zenye dhiki na za kupita tu. "Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi" kwa maana ndiyo nyumba ya kudumu milele, nayo dunia ni makazi ya kwisha. Kwa hivyo Muumini mwenye akili timamu hachagui lililo baya zaidi kuliko lililo bora zaidi, na wala hauzi starehe ya saa moja na akaacha raha ya milele, kwani kuipenda dunia na kuipendelea kuliko akhera ndicho kichwa cha kila dhambi.
#
{18 - 19} {إنَّ هذا}: المذكور لكم في هذه السورة المباركة من الأوامر الحسنة والأخبار المستحسنة، {لفي الصُّحُفِ الأولى. صُحُفِ إبراهيم وموسى}: اللَّذيْنِ هما أشرف المرسلين بعد محمدٍ صلى الله عليه وعليهم أجمعين. فهذه أوامر في كلِّ شريعةٍ؛ لكونها عائدةٌ إلى مصالح الدارين، وهي مصالح في كلِّ زمانٍ ومكانٍ.
{18 - 19} "Hakika haya" mliyotajiwa katika Sura hii iliyobarikiwa ya maamrisho mema na habari nzuri "yamo katika Vitabu vya mwanzo. Vitabu vya Ibrahimu na Musa." Ambao ndio Mitume watukufu zaidi baada ya Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote. Kwa hivyo haya ni maamrisho yaliyo katika kila sheria; kwa sababu yanarudi katika masilahi ya nyumba zote mbili, na ni masilahi katika kila wakati na mahali.
Imekamilika, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *