Tafsir ya Surat An-Naziat
Tafsir ya Surat An-Naziat
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا (1) وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا (2) وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا (3) فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا (4) فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا (5) يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ (6) تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ (7) قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ (8) أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ (9) يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ (10) أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَخِرَةً (11) قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ (12) فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ (13) فَإِذَا هُمْ بِالسَّاهِرَةِ (14)}.
1. Ninaapa kwa wanaokomoa kwa nguvu. 2. Na kwa wanaotoa kwa upole. 3. Na wanaoogelea sawasawa. 4. Wakishindana mbio kweli kweli. 5. Wakidabiri mambo. 6. Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka. 7. Kifuate cha kufuatia. 8. Siku hiyo nyoyo zitapigapiga. 9. Macho yatainama chini. 10.
Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? 11. Hata tukiwa mifupa iliyobunguliwa? 12.
Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye hasara! 13. Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu. 14. Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
#
{1 - 5} هذه الإقسامات بالملائكة الكرام وأفعالهم الدالَّة على كمال انقيادهم لأمر الله وإسراعهم في تنفيذه ؛ يُحتمل أنَّ المقسم عليه الجزاء والبعث؛ بدليل الإتيان بأحوال القيامة بعد ذلك، ويُحتمل أنَّ المقسَم عليه والمقسَم به متَّحِدان، وأنَّه أقسم على الملائكة؛ لأنَّ الإيمان بهم أحدُ أركان الإيمان الستَّة، ولأنَّ في ذكر أفعالهم هنا ما يتضمَّن الجزاء الذي تتولاَّه الملائكة عند الموت وقبله وبعده، فقال: {والنازعاتِ غَرْقاً}: وهم الملائكة التي تنزع الأرواح بقوَّة، وتغرق في نزعها حتى تخرج الرُّوح فتجازى بعملها. {والناشطاتِ نشطاً}: وهي الملائكة أيضاً تجتذبُ الأرواحَ بقوَّة ونشاطٍ، أو أنَّ النشطَ يكون لأرواح المؤمنين والنَّزْع لأرواح الكفَّار. {والسَّابحاتِ}؛ أي: المتردِّدات في الهواء صعوداً ونزولاً، {سبحاً. فالسَّابقاتِ}: لغيرها {سبقاً}: فتبادِرُ لأمر الله وتسبق الشياطين في إيصال الوحي إلى رسل الله؛ لئلاَّ تسترِقه ، {فالمدبِّراتِ أمراً}؛ [أي]: الملائكة الذين جعلهم الله يدبِّرون كثيراً من أمور العالم العلويِّ والسفليِّ من الأمطار والنَّبات [والأشجار] والرِّياح والبحار والأجنَّة والحيوانات والجنَّة والنار وغير ذلك.
{1 - 5} Hivi ni viapo kwa Malaika watukufu na vitendo vyao vinavyoashiria utiifu wao kamili kwa amri za Mwenyezi Mungu na uharaka wao katika kuzitekeleza. Inawezekana kwamba yule kinachokusudiwa na viapo hivi ni malipo na ufufuo; kwa ushahidi wa kutajwa hali za siku ya Kiyama baada ya hapo. Na inawezekana kwamba kinachoapiwa na kinachokusudiwa na viapo hivi ni kitu kimoja, nao ni Malaika. Kwa sababu kuwaamini ni miongoni mwa nguzo sita za imani, na kwa sababu kutajwa kwa vitendo vyao hapa kunajumuisha malipo ambayo Malaika husimamia wakati wa kufa kwa viumbe, na kabla yake, na baada yake. Akasema, "Ninaapa kwa wanaokomoa kwa nguvu." Hao ni Malaika wanaozitoa roho kwa nguvu, mpaka roho itoke na ilipwe kwa matendo yake. "Na kwa wanaotoa kwa upole." Nao pia ni Malaika wanaovuta roho kwa nguvu na ukakamavu, au ukakamavu huo huwa wanapotoa roho za Waumini, nayo nguvu huwa wanapotoa roho za makafiri. "Na wanaoogelea sawasawa" angani, wakipanda na kushuka. "Wakishindana mbio kweli kweli" wenzao huku wakiharakisha kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na kuwatangulia mashetani katika kufikisha ufunuo kwa Mitume wa Mwenyezi Mungu; ili wasiusikilize kwa siri. "Wakidabiri mambo" nao ni wale Malaika ambao Mwenyezi Mungu aliwaweka wasimamie mambo mengi ya ulimwengu wa juu na wa chini, kama vile mvua, mimea
[na miti], pepo, bahari, vijusi matumboni mwa mama, wanyama, bustani za mbinguni, Moto wa mbinguni na vitu vinginevyo.
#
{6 - 9} {يومَ ترجُفُ الرَّاجفةُ}: وهي قيام الساعة، {تتبعُها الرادفةُ}؛ أي: الرجفة الأخرى التي تَرْدُفُها وتأتي تلوَها. {قلوبٌ يومئذٍ واجفةٌ}؛ أي: منزعجةٌ من شدَّة ما ترى وتسمع، {أبصارُها خاشعةٌ}؛ أي: ذليلةٌ حقيرةٌ قد ملك قلوبهم الخوف وأذهل أفئدتهم الفزع وغلب عليهم التأسُّف، واستولت عليهم الحسرة.
{6 - 9} "Siku kitakapotetemeka cha kutetemeka" ambayo ni kuja kwa Saa
(ya Kiyama), "Kifuate cha kufuatia" Yaani, mtetemeko mwingine unaoifuata na kuja baada yake. "Siku hiyo nyoyo zitapigapiga" kwa sababu ya ukali wa yale ambayo zinayaona na kukisikia. "Macho yatainama chini" huku yamedhalilika, kutwezwa, kwa sababu nyoyo zao zitakuwa zimetawaliwa na hofu na majuto makubwa.
#
{10 - 14} {يقولونَ} ؛ أي: الكفار في الدُّنيا على وجه التكذيب: {أإذا كُنَّا عظاماً نخرةً}؛ أي: باليةً فتاتاً، {قالوا تلك إذاً كَرَّةٌ خاسرةٌ}؛ أي: استبعدوا أن يبعثهم الله ويعيدهم بعدما كانوا عظاماً نخرةً جهلاً منهم بقدرة الله وتجرياً عليه! قال الله في بيان سهولة هذا الأمر عليه: {فإنَّما هي زجرةٌ واحدةٌ}: يُنفخ في الصور؛ فإذا الخلائقُ كلُّهم {بالسَّاهرةِ}؛ أي: على وجه الأرض قيامٌ ينظرونَ، فيجمعهم الله، ويقضي بينهم بحكمه العدل، ويجازيهم.
{10 - 14} "Sasa wanasema" makafiri hapa duniani kwa njia ya kukadhibisha "Hata tukiwa mifupa iliyobunguliwa? Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye hasara!" Yaani, waliona kwamba haliwezekani kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua na kuwarudisha baada ya kuwa mifupa iliyooza,
kwa sababu ya ujinga wao kuhusiana na uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa kumdharau Yeye! Mwenyezi Mungu alisema katika kufafanua wepesi wa jambo hili: "Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu." Ambapo itapulizwa katika baragumu, na hapo viumbe vyote "watakuwa kwenye uwanda wa mkutano" wamesimama wakingoja. Kisha Mwenyezi Mungu atawakusanya pamoja, na kuhukumu kati yao kwa hukumu yake ya uadilifu, na awalipe.
{هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَى (15) إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى (16) اذْهَبْ إِلَى فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَى (17) فَقُلْ هَلْ لَكَ إِلَى أَنْ تَزَكَّى (18) وَأَهْدِيَكَ إِلَى رَبِّكَ فَتَخْشَى (19) فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَى (20) فَكَذَّبَ وَعَصَى (21) ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَى (22) فَحَشَرَ فَنَادَى (23) فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَى (24) فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَى (25) إِنَّ فِي ذَلِكَ لَعِبْرَةً لِمَنْ يَخْشَى (26)}.
15. Je! Imekufikia hadithi ya Musa? 16. Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la Tuwaa,
akamwambia: 17. Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. 18.
Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? 19. Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. 20. Basi alimwonyesha Ishara kubwa. 21.Lakini aliikadhibisha na akaasi. 22. Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. 23. Akakusanya watu akanadi. 24.
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. 25. Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. 26. Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa.
#
{15 - 25} يقول الله تعالى لنبيِّه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -: {هل أتاك حديثُ موسى}: وهذا الاستفهام عن أمرٍ عظيمٍ متحقِّق وقوعه؛ أي: هل أتاك حديثه. {إذ ناداه ربُّه بالوادِ المقدَّس طوىً}: وهو المحلُّ الذي كلَّمه الله فيه، وامتنَّ عليه بالرسالة، وابتعثه بالوحي، واجتباه ، فقال له: {اذهبْ إلى فرعونَ إنَّه طغى}؛ أي: فانهه عن طغيانه وشركه وعصيانه بقولٍ ليِّنٍ وخطابٍ لطيفٍ لعله يتذكر أو يخشى، {فَقُل له هل لك إلى أن تَزكَّى}؛ أي: هل لك في خصلةٍ حميدةٍ ومحمدةٍ جميلةٍ يتنافس فيها أولو الألباب؟ وهي أن تزكِّيَ نفسك وتطهِّرَها من دَنَس الكفر والطغيان إلى الإيمان والعمل الصالح. {وأهدِيَك إلى ربِّك}؛ أي: أدلُّك عليه، وأبيِّن لك مواقع رضاه من مواقع سخطه، {فتخشى}: الله إذا علمت الصراط المستقيم. فامتنع فرعون ممَّا دعاه إليه موسى، {فأراه الآيةَ الكبرى}؛ أي: جنس الآية الكبرى؛ فلا ينافي تعدُّدها، {فألقى عصاه فإذا هي ثعبانٌ مبينٌ. ونزعَ يدَه فإذا هي بيضاءُ للنَّاظرين}. {فكذَّب}: بالحقِّ، {وعصى}: الأمر، {ثم أدبر يسعى}؛ أي: يجتهد في مبارزة الحقِّ ومحاربته. {فحشر}: جنودَه؛ أي: جمعهم، {فنادى. فقال}: لهم: {أنا ربُّكم الأعلى}: فأذعنوا له وأقرُّوا بباطله حين استخفَّهم. {فأخذه اللهُ نَكالَ الآخرةِ والأولى}؛ أي: جعل الله عقوبته دليلاً وزاجراً ومبيِّنةً لعقوبة الدُّنيا والآخرة.
{15 - 25} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "Je! Imekufikia hadithi ya Musa?" Swali hili linahusu jambo kubwa ambalo ni la yakini kutokea kwake. Yaani, je, ilikufikia hadithi yake "Mola wake Mlezi alipomwita katika bonde takatifu la T'uwaa?" Napo ni pale mahali alipozungumza naye Mwenyezi Mungu, akamneemesha kwa utume, na akamtuma kwa ufunuo, na akamteua,
na akamwambia: "Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri." Yaani, basi mkamkataze uasi wake, na ushirikina, na uovu wake kwa maneno laini na ya upole, labda atakumbuka au akaogopa.
"Umwambie: Je, unapenda kujitakasa?" Yaani, je, hutaki jambo la kusifiwa lililo zuri ambalo watu wenye ufahamu mzuri hushindana ndani yake? Nalo ni kwamba ujitakase kutokana na uchafu wa ukafiri na kuvuka mipaka na kuelekea kwenye imani na matendo mema. "Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi" kwa kukubainishia pahala pa radhi zake na pahala pa ghadhabu yake "upate kumcha" Mwenyezi Mungu utakapojua njia iliyonyooka. Lakini Firauni akakataa yale ambayo Musa alimwitia, "Basi alimwonyesha Ishara kubwa." Nazo zilikuwa aina mbalimbali za ishara kubwa kubwa. "Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhahiri. Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao." Lakini Firauni "aliikadhibisha" haki "na akaasi" amri. "Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi" za kupinga na kupigana na haki. "Akakusanya" askari wake "akanadi.
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa." Kwa hivyo, wakamtii na kukiri batili yake hivyo wakati alipowachezea mchezo huo. "Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo." Yaani, Mwenyezi Mungu aliifanya adhabu yake kuwa ni mwongozo, karipio na ufafanuzi wa adhabu ya dunia na akhera.
#
{26} {إنَّ في ذلك لَعبرةً لمَن يَخْشى}: فإنَّ مَنْ يخشى الله هو الذي ينتفع بالآيات والعبر؛ فإذا رأى عقوبة فرعون؛ عرف أنَّ [كلَّ] من تكبَّر وعصى وبارز الملك الأعلى؛ يعاقِبه في الدُّنيا والآخرة، وأمَّا مَن ترحَّلت خشيةُ الله من قلبه؛ فلو جاءته كلُّ آيةٍ؛ لم يؤمنْ بها.
{26} "Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanaoogopa." Kwa maana anayemcha Mwenyezi Mungu ndiye anayefaidika na Ishara na mazingatio. Ikiwa ataona adhabu ya Firauni; atajua kwamba
[kila mtu] aliyekuwa na kiburi, akaasi, na akapigana na Mfalme Mkuu, atamuadhibu katika dunia na Akhera. Lakini yule ambaye hofu ya Mwenyezi Mungu iliondoka moyoni mwake, basi hata kama atajiwa na ishara zote, hataziamini.
{أَأَنْتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ بَنَاهَا (27) رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا (28) وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا (29) وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَلِكَ دَحَاهَا (30) أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا (31) وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا (32) مَتَاعًا لَكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ (33)}.
27. Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliyeijenga! 28. Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. 29. Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. 30. Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. 31. Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. 32. Na milima akaisimamisha imara. 33. Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
#
{27 - 33} يقول تعالى مبيناً دليلاً واضحاً لمنكري البعث ومستبعدي إعادة الله للأجساد: {أأنتُم}: أيُّها البشر، {أشدُّ خلقاً أم السماءُ}: ذات الجرم العظيم والخلق القويِّ والارتفاع الباهر، {بناها}: الله، {رفَعَ سَمْكَها}؛ أي: جرمها وصورتها. {فسوَّاها}: بإحكام وإتقانٍ يحيِّر العقول ويذهل الألباب، {وأغطشَ ليلَها}؛ أي: أظلمه، فعمَّت الظُّلمة جميع أرجاء السماء، فأظلم وجه الأرض، {وأخرج ضُحاها}؛ أي: أظهر فيه النُّور العظيم حين أتى بالشمس، فانتشر الناس في مصالح دينهم ودُنْياهم، {والأرضَ بعد ذلك}؛ أي: بعد خلق السماء {دحاها}؛ أي: أودع فيها منافعها، وفسر ذلك بقوله: {أخرج منها ماءها ومرعاها. والجبال أرساها}؛ أي: ثبَّتها بالأرض ، فدحى الأرض بعد خَلْق السماواتِ؛ كما هو نصُّ هذه الآيات الكريمة، وأمَّا خلق نفس الأرض؛ فمتقدِّم على خلق السماء؛ كما قال تعالى: {قل أإنَّكم لتكفرونَ بالذي خلق الأرضَ في يومين وتجعلون له أنداداً ذلك ربُّ العالمين ... } إلى أن قال: {ثمَّ استوى إلى السَّماء وهي دخان فقال لها وللأرض ائتيا طوعاً أو كرها قالتا أتينا طائعين. فقضاهنَّ سبع سمواتٍ ... }: فالذي خلق السماواتِ العظام وما فيها من الأنوار والأجرام والأرض الغبراء الكثيفة ، وما فيها من ضروريَّات الخلق ومنافعهم لا بدَّ أن يبعث الخلق المكلَّفين فيجازيهم بأعمالهم ؛ فمن أحسن؛ فله الحسنى، وَمن أساء؛ فلا يلومنَّ إلاَّ نفسه.
{27 - 33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema,
akiwabainishia ushahidi wazi wale wanaokanusha ufufuo na wanaokataa suala la Mwenyezi Mungu kurejesha miili: "Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi" watu "au mbingu" zenye maumbile makubwa, ya nguvu, zilizoinuka juu sana? "Yeye" Mwenyezi Mungu "ndiye aliyeijenga! Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri" na ukamilifu wa hali ya juu unaozichanganya akili na kuzishangaza nyoyo. "Na akautia giza usiku wake" nalo likatanda pande zote za mbingu, kwa hivyo uso wa ardhi ukawa giza. "Na akautokeza mchana wake" jua lilipochomoza, kwa hivyo watu wakaenea kwa ajili ya masilahi ya dini yao na dunia yao. "Na juu ya hivyo" baada ya kuumbwa mbingu "ameitandaza ardhi" na kutia humo manufaa yake,
kama alivyofasiri hilo kwa kauli yake: "Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. Na milima akaisimamisha imara." Na suala la kuitandaza ardhi kulikuwa baada ya kuumba mbingu. Kama ilivyo katika maandiko ya Aya hizi tukufu. Na ama kuumbwa kwa ardhi yenyewe, huko kulitangulia kuumbwa mbingu,
kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote...
" mpaka aliposema: "Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi,
akaziambia hizo na ardhi: Njooni,
kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu. Basi akazifanya mbingu saba..." Kwa hivyo, yule aliyeziumba mbingu kubwa na mianga na miili iliyomo ndani yake, na ardhi yenye mavumbi na nene, na mahitaji ya lazima na manufaa ya viumbe, ni lazima atawafufua viumbe waliojukumishwa kisheria ili awalipe kwa matendo yao. Kwa hivyo, aliyefanya wema, basi atalipwa na wema. Naye aliyefanya ubaya, basi kamwe asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe tu.
Ndiyo maana baada ya haya akataja kuja kwa Saa (ya Kiyama) kisha malipo, akasema:
{فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَى (34) يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنْسَانُ مَا سَعَى (35) وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَنْ يَرَى (36) فَأَمَّا مَنْ طَغَى (37) وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (38) فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَى (39) وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَى (40) فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَى (41)}.
34. Basi itakapofika hiyo balaa kubwa, 35. Siku ambayo mtu atakumbuka aliyoyafanya, 36. Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, 37. Basi ama yule aliyezidi ujeuri, 38. Na akakhiari maisha ya dunia, 39. Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! 40. Na ama yule anayeogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, 41. Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
#
{34 - 36} أي: إذا جاءت القيامةُ الكبرى والشدَّةُ العظمى، التي يَهون عندها كلُّ شدَّةٍ؛ فحينئذٍ يذهل الوالد عن ولده، والصاحب عن صاحبه، وكلُّ محبٍّ عن حبيبه، و {يتذكَّرُ الإنسانُ ما سعى}: في الدُّنيا من خير وشرٍّ، فيتمنَّى زيادة مثقال ذرَّةٍ في حسناته، ويغمُّه ويحزن لزيادة مثقال ذرَّةٍ في سيئاته، ويعلم إذ ذاك أنَّ مادة ربحه وخسرانه ما سعاه في الدُّنيا، وينقطع كلُّ سبب ووصلةٍ كانت في الدُّنيا سوى الأعمال، {وبُرِّزَت الجحيم لمن يرى}؛ أي: جُعِلَت في البراز ظاهرةً لكلِّ أحدٍ؛ قد هُيِّئت لأهلها، واستعدَّت لأخذهم منتظرةً لأمر ربِّها.
{34 - 36} Yaani, wakati Ufufuo Mkuu na Dhiki Kuu itakapokuja, wakati huo kila dhiki itakuwa rahisi. Kisha baba hatamjali mtoto wake, na rafiki hatamjali rafiki yake, na kila apendwaye hatampenda kipenzi chake, na "mtu atakumbuka aliyoyafanya" katika dunia ya heri na maovu, na atatamani kuongezewa uzito wa chembe katika matendo yake mema, na atahuzunika na kupata wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka uzito wa chembe katika matendo yake mabaya, na atajua wakati huo kuwa kiini cha faida yake na hasara yake ni yale aliyofanya katika dunia, na kila njia na mafungamano aliyokuwa nayo hapa duniani yatakatika isipokuwa matendo. "Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona" ili kila mmoja aione. Kwani itakuwa tayari imeandaliwa wakazi wake ili iwachukue, huku ikingojea amri ya Mola wake Mlezi.
#
{37 - 39} {فأمَّا مَن طغى}؛ أي: جاوز الحدَّ بأن تجرَّأ على المعاصي الكبار ولم يقتصرْ على ما حدَّه الله، {وآثرَ الحياة الدُّنيا}: على الآخرة، فصار سعيه لها ووقته مستغرقاً في حظوظها وشهواتها، ونسي الآخرة والعمل لها؛ {فإنَّ الجحيم هي المأوى}: له؛ أي: المقرُّ والمسكن لمن هذه حاله.
{37 - 39} "Basi ama yule aliye zidi ujeuri" kwa kuvuka mipaka kwa kuthubutu kufanya maasi makubwa na hakukomekea kwenye mipaka aliyowekewa na Mwenyezi Mungu, "na akakhiari maisha ya dunia" kuliko ya akhera, kwa hivyo akajitahidi kwa ajili yake, na akamaliza wakati wake katika kufuata mazuri yake na matamanio yake, na akaisahau Akhera na kuifanyia kazi, "kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!"
#
{40 - 41} {وأمَّا مَنْ خافَ مقامَ ربِّه}؛ أي: خاف القيام عليه ومجازاته بالعدل؛ فأثَّر هذا الخوف في قلبه، فنهى {النفس عن}: هواها الذي يصدُّها عن طاعة الله، وصار هواه تبعاً لما جاء به الرسول، وجاهد الهوى والشهوة الصادَّيْن عن الخير؛ {فإنَّ الجنَّة}: المشتملة على كلِّ خيرٍ وسرورٍ ونعيم، {هي المأوى}: لمن هذا وصفُه.
{40 - 41} "Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi" kwa hivyo, hofu hii akaathiri katika moyo wake, basi "na akajizuilia nafsi yake" na matamanio yake, ambayo yanaizuia kumtii Mwenyezi Mungu, kwa hivyo matamanio yake hayo yakawa yanafuata yale aliyoyaleta Mtume, na akapigana na matamanio na vivutio viovu vinavyozuia kufanya wema, "Basi huyo, Pepo" yenye kila heri, furaha na neema "itakuwa ndiyo makaazi yake!"
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا (42) فِيمَ أَنْتَ مِنْ ذِكْرَاهَا (43) إِلَى رَبِّكَ مُنْتَهَاهَا (44) إِنَّمَا أَنْتَ مُنْذِرُ مَنْ يَخْشَاهَا (45) كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا (46)}.
42. Wanakuuliza Saa
(ya Kiyama) itakuwa lini? 43. Una nini wewe hata uitaje? 44. Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. 45. Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu. 46. Ni kama kwamba wao siku watakapoiona
(hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.
#
{42 - 44} أي: يسألك المتعنِّتون المكذِّبون بالبعث {عن الساعة}: متى وقوعُها؟ و {أيَّان مُرْساها}؟! فأجابهم الله بقوله: {فيم أنت من ذكراها}؛ أي: ما الفائدة لك ولهم في ذكرها ومعرفة وقت مجيئها؛ فليس تحت ذلك نتيجةٌ، ولهذا لمَّا كان علم العباد للساعة ليس لهم فيه مصلحةٌ دينيةٌ ولا دنيويةٌ، بل المصلحة في إخفائه عليهم، طوى علم ذلك عن جميع الخلق واستأثر بعلمه فقال: {إلى ربك منتهاها}؛ أي: إليه ينتهي علمها؛ كما قال في الآية الأخرى: {يسألونَكَ عن الساعة أيَّانَ مُرْساها قل إنَّما علمُها عند ربِّي لا يُجَلِّيها لوقتها إلاَّ هو}.
{42 - 44} Maana yake ni kwamba wanakuuliza wenye ukaidi wanaokadhibisha ufufuo "Saa
(ya Kiyama)" na kwamba "itakuwa lini?" Kwa hivyo,
Mwenyezi Mungu akawajibu kwa kauli yake: "Una nini wewe hata uitaje?" Yaani, kuna faida gani kwako na kwao katika kuitaja na kujua muda wa kuja kwake? Hakuna natija katika hilo, na ndiyo sababu hii, kwa kuwa kujua kwa waja kuhusu Saa ya Kiyama hakuna masilahi yao ya kidini wala ya kidunia, bali masilahi yao ni katika kuwaficha wasiijue, basi akaficha elimu ya hilo mbali na viumbe vyote na akajiwekea Yeye tu elimu ya hilo,
akasema: "Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake." Yaani, kwake ndiyo ujua wake unaishia,
kama alivyosema katika Aya nyingine: “Wanakuuliza hiyo Saa
(ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye."
#
{45 - 46} {إنَّما أنت منذرُ مَنْ يَخْشاها}؛ أي: إنَّما نذارتك نفعها لمن يخشى مجيء الساعة ويخاف الوقوف بين يدي الله ؛ فهم الذين لا يُهِمُّهم إلاَّ الاستعداد لها والعمل لأجلها، وأما مَنْ لم - يؤمن بها؛ فلا يُبَالى به ولا بتعنُّته؛ لأنَّه تعنتٌ مبنيٌّ على التَّكذيب والعناد ، وإذا وصل إلى هذه الحال؛ كان الإجابة عنه عبثاً، ينزَّه أحكم الحاكمين عنه.
{45 - 46} "Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuihofu.
" Yaani: Kuonya kwako kutawanufaisha wale tu wanaoogopa kuja kwa Saa
(ya Kiyama) na wanaogopa kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio hawajishungulishi isipokuwa kujitayarisha kwa ajili yake na kuifanyia kazi. Ama wale wasioiamini, hao asiwajali wala usugu wao. Kwa maana ni usugu unaotokana na kukadhibisha na ukaidi. Na ikifikia hali hii, basi kumjibu ni bure tu, ambako ametakasika mbali nako mbora zaidi wa wanaohukumu.
Imekamilika, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *