:
Tafsiri ya Surat 'Abasa
Tafsiri ya Surat 'Abasa
Iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 10 #
{عَبَسَ وَتَوَلَّى (1) أَنْ جَاءَهُ الْأَعْمَى (2) وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّى (3) أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنْفَعَهُ الذِّكْرَى (4) أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَى (5) فَأَنْتَ لَهُ تَصَدَّى (6) وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّى (7) وَأَمَّا مَنْ جَاءَكَ يَسْعَى (8) وَهُوَ يَخْشَى (9) فَأَنْتَ عَنْهُ تَلَهَّى (10)}.
1. Alikunja kipaji na akageuka. 2. Kwa sababu alimjia kipofu! 3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? 4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? 5. Ama ajionaye hana haja, 6. Wewe ndiyo unamshughulikia? 7. Na si juu yako kama hakutakasika. 8. Ama anayekujia kwa juhudi. 9. Naye anaogopa, 10. Ndiyo wewe unampuuza?
Sababu ya kuteremshwa aya hizi tukufu ni kwamba alikuja kipofu mmoja miongoni mwa waumini kumwomba Mtume - rehema na amani zimshukie - na ajifunze kutoka kwake, kisha akaja tajiri mmoja, naye Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa na hamu kubwa ya kuwaongoza viumbe, kwa hivyo, yeye Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - akaegemea na kumsikiliza vyema yule tajiri na akakataa kumsikiliza huyo maskini kipofu; akiwa na matarajio ya kumwongoza tajiri huyo na akitumaini atakasike, lakini Mwenyezi Mungu akamlaumu kwa lawama hii ya upole, akisema:
#
{1 - 10} {عبس}؛ أي: في وجهه، {وتولَّى}: في بدنه لأجل مجيء الأعمى له. ثم ذكر الفائدة في الإقبال عليه، فقال: {وما يدريكَ لعلَّه}؛ أي: الأعمى، {يَزَّكَّى}؛ أي: يتطهر عن الأخلاق الرذيلة ويتصف بالأخلاق الجميلة، {أو يَذَّكَّرُ فَتَنفعهُ الذِّكرَى}؛ أي: يتذكَّر ما ينفعه فينتفع بتلك الذِّكرى، وهذه فائدةٌ كبيرةٌ، هي المقصودة من بعثة الرسل ووعظ الوعَّاظ وتذكير المذكِّرين؛ فإقبالُك على مَنْ جاء بنفسه مفتقراً لذلك مقبلاً هو الأليقُ الواجب، وأما تصدِّيك وتعرُّضِك للغنيِّ المستغني الذي لا يسأل ولا يستفتي لعدم رغبته في الخير مع تركك مَنْ - أهمُّ منه؛ فإنَّه لا ينبغي لك؛ فإنَّه ليس عليك أن لا يَزَّكَّى؛ فلو لم يَتَزَكَّ؛ فلست بمحاسبٍ على ما عمله من الشرِّ، فدلَّ هذا على القاعدة المشهورة؛ أنَّه لا يُترَك أمرٌ معلومٌ لأمرٍ موهومٍ، ولا مصلحة متحقِّقة لمصلحة متوهَّمة، وأنَّه ينبغي الإقبال على طالب العلم المفتقر إليه الحريص عليه أزيد من غيره.
{1 - 10} "Alikunja kipaji" cha uso wake "na akageuka" kwa mwili wake kwa sababu alijiwa na kipofu. Kisha akataja manufaa ya kumwelekea, akasema: "Na nini kitakujuulisha pengine yeye" yaani kipofu huyo, "atatakasika" kwa kujiepusha na tabia mbaya na akasifika kwa sifa nzuri. "Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?" Na hii ni faida kubwa, ambayo ndiyo lengo la kuwatuma Mitume, kuwaidhi kwa wale wanaowaidhi, na kukumbusha kwa wale wanaokumbusha. Kwa hivyo, wewe kumwelekea yule ambaye yeye mwenyewe alikuja akilitaka jambo hilo, basi yeye ndiye anayefailia zaidi na anayestahiki zaidi kuelekewa. Na ama kumshughulikia kwako na kumwelekea tajiri na mwenye kujiona kwamba kajitosheleza ambaye haulizi wala kutafuta ushauri wa kisheria (fatwa) kwa sababu hana haja na heri, huku ukimwacha yule aliye muhimu zaidi kuliko yeye, basi haupaswi kufanya hivyo. Kwani hutalaumiwa ikiwa hatatakasika. Kwa maana ikiwa hatatakasika, basi wewe hutaulizwa yale aliyofanya ya uovu. Kwa hivyo hili likaonyesha kanuni inayojulikana sana; kwamba jambo linalojulikana halipaswi kuachwa kwa ajili ya jambo la kufikirika tu, wala kuacha masilahi yenye uhakika kwa ajili ya masilahi ya kufikirika tu, na kwamba mtu anafaa kumshughulikia mtafutaji wa elimu ambaye anaihitaji, mwenye uchu nayo zaidi kuliko wengineye.
: 11 - 32 #
{كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ (11) فَمَنْ شَاءَ ذَكَرَهُ (12) فِي صُحُفٍ مُكَرَّمَةٍ (13) مَرْفُوعَةٍ مُطَهَّرَةٍ (14) بِأَيْدِي سَفَرَةٍ (15) كِرَامٍ بَرَرَةٍ (16) قُتِلَ الْإِنْسَانُ مَا أَكْفَرَهُ (17) مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ (18) مِنْ نُطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ (19) ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ (20) ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ (21) ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنْشَرَهُ (22) كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ (23) فَلْيَنْظُرِ الْإِنْسَانُ إِلَى طَعَامِهِ (24) أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا (25) ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا (26) فَأَنْبَتْنَا فِيهَا حَبًّا (27) وَعِنَبًا وَقَضْبًا (28) وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا (29) وَحَدَائِقَ غُلْبًا (30) وَفَاكِهَةً وَأَبًّا (31) مَتَاعًا لَكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ (32)}.
11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. 12. Basi anayependa akumbuke. 13. Yamo katika kurasa zilizoheshimiwa. 14. Zilizoinuliwa, zilizotakaswa. 15. Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, 16. Watukufu, wema. 17. Ameangamia mwanaadamu! Nini kinachomkufurisha? 18. Kwa kitu gani amemuumba? 19. Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. 20. Kisha akamsahilishia njia. 21. Kisha akamfisha, akamtia kaburini. 22. Kisha apendapo atamfufua. 23. La! Hajamaliza aliyomuamuru. 24. Hebu mtu na atazame chakula chake. 25. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu. 26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu. 27. Kisha tukaotesha humo nafaka. 28. Na zabibu, na mimea ya majani. 29. Na mizaituni, na mitende. 30. Na bustani zenye miti iliyosongana baraabara. 31. Na matunda, na malisho ya wanyama. 32. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
#
{11 - 16} يقول تعالى: {كلاَّ إنَّها تذكرةٌ}: أي: حقًّا إنَّ هذه الموعظة تذكرةٌ من الله يُذَكِّر بها عباده ويبيِّن لهم في كتابه ما يحتاجون إليه ويبيِّن الرُّشد من الغيِّ؛ فإذا تبيَّن ذلك؛ {فَمْن شاء ذَكَرَه}؛ أي: عمل به؛ كقوله تعالى: {وقلِ الحقُّ مِن ربِّكم فَمَن شاء فَلْيُؤْمِن ومَن شاءَ فَلْيَكْفُر}. ثم ذكر محلَّ هذه التذكرة وعظمها ورفع قدرها، فقال: {في صحفٍ مكرمةٍ. مرفوعةٍ}: القدر والرتبة، {مُطَهَّرَةٍ}: من الآفات وعن أن تنالها أيدي الشياطين أو يسترقوها، بل هي {بأيدي سفرةٍ}: وهم الملائكة الذين هم سفراء بين الله وبين عباده، {كرامٍ}؛ أي: كثيري الخير والبركة، {بَرَرةٍ}: قلوبهم وأعمالهم. وذلك كلُّه حفظٌ من الله لكتابه؛ أن جعل السفراء فيه إلى الرسل الملائكة الكرام الأقوياء الأتقياء، ولم يجعلْ للشياطين عليه سبيلاً، وهذا مما يوجب الإيمان به وتلقِّيه بالقَبول.
{11 - 16} Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: "Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana" kutoka kwa Mwenyezi Mungu, anawakumbusha kwa huo waja wake na anawabainishia katika Kitabu chake kile wanachokihitaji pamoja na kubainisha uwongofu mbali na upotofu. Kwa hivyo ikishakubainikia hivyo "basi anayependa akumbuke." Yaani, ayafanyie kazi; kama kauli yake Mola Mlezi: "Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae." Kisha akataja mahali pa ukumbusho huu, ukubwa wake, na thamani yake kubwa, akasema: "Yamo katika kurasa zilizoheshimiwa. Zilizoinuliwa" cheo na daraja, "zilizotakaswa" kutokana na maovu na kutokana na kufikiwa na mikono ya mashetani au hat kuzisikiliza kwa siri. Bali ziko "mikononi mwa Malaika waandishi" nao ni malaika ambao ni mabalozi kati ya Mwenyezi Mungu na waja wake. "Watukufu" yaani, wenye heri na baraka nyingi. "wema" katika nyoyo zao na vitendo vyao. Na haya yote ni kuhifadhi kwa Mwenyezi Mungu Kitabu chake; kwamba aliwafanya mabalozi wake kwa Mitume kuwa Malaika watukufu, wenye nguvu na wacha Mungu, tena hakuwaruhusu mashetani kuwa na njia yoyote kukifikia kitabu chake. Na haya ni katika yale yanayolazimu kukiamini na kukikubali.
#
{17 - 23} ولكنْ مع هذا أبى الإنسان إلاَّ كُفوراً، ولهذا قال تعالى: {قُتِلَ الإنسانُ ما أكفَرَه}: لنعمة الله، وما أشدَّ معاندته للحقِّ بعدما تبيَّن، وهو؛ ما هو؟ هو من أضعفِ الأشياء، خلقه الله من ماء مَهين، ثم قدَّر خلقه وسوَّاه بشراً سويًّا، وأتقن قواه الظاهرة والباطنة، {ثم السَّبيلَ يَسَّرَه}؛ أي: يسَّر له الأسباب الدينيَّة والدنيويَّة، وهداه السبيل، وبيَّنه، وامتحنه بالأمر والنهي، {ثم أماتَه فأقْبَرَهُ}؛ أي: أكرمه بالدفن، ولم يجعلْه كسائر الحيوانات التي تكون جِيَفُها على وجه الأرض، {ثم إذا شاءَ أنشَرَه}؛ أي: بعثه بعد موته للجزاء؛ فالله هو المنفرد بتدبير الإنسان وتصريفه بهذه التَّصاريف، لم يشارِكْه فيه مشاركٌ، وهو مع هذا لا يقوم بما أمره الله، ولم يقضِ ما فرضه عليه، بل لا يزال مقصِّراً تحت الطلب!
{17 - 23} Lakini pamoja na hayo, mwanadamu alikataa isipokuwa tu kuwa mtu asiye na shukrani, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: " Ameangamia mwanaadamu! Nini kinachomkufurisha" neema ya Mwenyezi Mungu, na ana upinzani mkubwa namna gani huu dhidi ya haki baada ya kuwa wazi. Naye pamoja na hayo yote ni nani? Yeye ndiye kitu dhaifu zaidi. Mwenyezi Mungu alimuumba kutokana na maji ya kudharauliwa, kisha akakadiria uumbaji wake na akamfanya kuwa mwanadamu mkamilifu sawasawa, na akakamilisha nguvu zake za dhahiri na zilizofichika. "Kisha akamsahilishia njia" za kidini na za kidunia, akamuongoza kwenye njia sahihi, akaibainishia, na akamtia katika mtihani kwa maamrisho na makatazo. "Kisha akamfisha, akamtia kaburini." Yaani, akamtukuza kwa kumfanya azikwe, na wala hakumfanya kama wanyama wengine wote ambao mizoga yao iko juu ya uso wa ardhi. "Kisha apendapo atamfufua" baada ya kufa kwake kwa ajili ya malipo. Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayesimamia uendeshaji wa mwanadamu na kumgeuza katika migeuzo hii. Hakuna mshirika anayeshiriki naye katika hilo, na licha ya hayo yeye hafanyi yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na hakutekeleza yale aliyomfaradhishia. Bali bado anazembea, huku akitakiwa kutekeleza aliyoamrishwa.
#
{24 - 32} ثم أرشده الله إلى النظر والتفكُّر في طعامه، وكيف وصل إليه بعدما تكرَّرت عليه طبقاتٌ عديدةٌ ويسَّره [اللَّهُ] له؛ فقال: {فلينظُرِ الإنسانُ إلى طعامه. أنَّا صَبَبْنا الماء صَبًّا}؛ أي: أنزلنا المطر على الأرض بكثرة {ثم شَقَقْنا الأرض} للنبات {شقًّا. فأنبَتْنا فيها}: أصنافاً مصنَّفة من أنواع الأطعمة اللذيذة والأقوات الشهيَّة، {حبًّا}: وهذا شاملٌ لسائر الحبوب على اختلاف أصنافها، {وعنباً وقضباً}: وهو القتُّ، {وزيتوناً ونخلاً}: وخصَّ هذه الأربعة لكثرة فوائدها ومنافعها، {وحدائق غُلْباً}؛ أي: بساتين فيها الأشجار الكثيرة الملتفَّة ، {وفاكهةً وأبًّا}: الفاكهة ما يتفكَّه فيه الإنسان من تينٍ وعنبٍ وخوخٍ ورمانٍ وغير ذلك. والأبُّ ما تأكله البهائم والأنعام، ولهذا قال: {متاعاً لكم ولأنعامكم}: التي خلقها الله وسخَّرَها لكم. فمن نظر في هذه النعم؛ أوجب له ذلك شكر ربِّه وبذلَ الجهد في الإنابة إليه والإقبال على طاعته والتَّصديق لأخباره.
{24 - 32} Kisha Mwenyezi Mungu akamwelekeza kutazama na kufikiria juu ya chakula chake, na jinsi kilivyomfikia baada ya kupitia hatua nyingi, na [Mwenyezi Mungu] akamfanyia wepesi. Akasema: "Hebu mtu na atazame chakula chake. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu" juu ya ardhi. "Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu. Kisha tukaotesha humo" aina mbalimbali za vyakula vitamu na vizuri, "nafaka" zinazojumuisha nafaka za kila namna, "na zabibu, na mimea ya majani. Na mizaituni, na mitende." Hapa ametaja hivi vinne kwa njia hii maalumu kwa sababu ya manufaa yake mengi. "Na bustani zenye miti iliyo songana barabara. Na matunda, na malisho ya wanyama." Ndiyo maana akasema: "Kwa manufaa yenu na mifugo yenu" ambayo Mwenyezi Mungu ameiumba na akaitiisha kwa ajili yenu. Kwa hivyo, mwenye kutazama katika neema hizi, hilo linamlazimu kumshukuru Mola wake Mlezi na kufanya juhudi kubwa ya kurejea kwake, kumtii na kusadiki habari zake.
: 33 - 42 #
{فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ (33) يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ (34) وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ (35) وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ (36) لِكُلِّ امْرِئٍ مِنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ (37) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُسْفِرَةٌ (38) ضَاحِكَةٌ مُسْتَبْشِرَةٌ (39) وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ (40) تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ (41) أُولَئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ (42)}.
33. Basi utakapokuja ukelele. 34. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye. 35. Na mamaye na babaye. 36. Na mkewe na wanawe. 37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. 38. Siku hiyo ziko nyuso zitakazonawiri. 39. Zitacheka, zitachangamka. 40. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi. 41. Giza totoro litazifunika. 42. Hao ndio makafiri watenda maovu.
#
{33 - 42} أي: إذا جاءت صيحة القيامةِ التي تُصَخُّ لهولها الأسماع وتنزعج لها الأفئدة يومئذٍ؛ ممَّا يرى الناس من الأهوال وشدَّة الحاجة لسالف الأعمال؛ يفرُّ المرء من أعزِّ الناس إليه وأشفقهم عليه ؛ من أخيه وأمِّه وأبيه وصاحبته؛ أي: زوجته وبنيه، وذلك لأنَّه {لكلِّ امرئٍ منهم يومئدٍ شأنٌ يُغنيه}؛ أي: قد أشغلته نفسُه، واهتمَّ لفكاكها، ولم يكنْ له التفاتٌ إلى غيرها. فحينئذٍ ينقسم الخلقُ إلى فريقين: سعداء وأشقياء: فأمَّا السعداءُ؛ فوجوههم {يومئذٍ مسفرةٌ}؛ أي: قد ظهر فيها السرور والبهجةُ مما عرفوا من نجاتهم وفوزهم بالنعيم، {ضاحكةٌ مستبشرةٌ. ووجوهٌ}: الأشقياء {يومئذٍ عليها غَبَرَةٌ. ترهقُها}؛ أي: تغشاها {قترةٌ}: فهي سوداء مظلمةٌ مدلهمةٌ، قد أيست من كلِّ خير، وعرفتْ شقاءها وهلاكها. {أولئك}: الذين بهذا الوصف، {هم الكفرةُ الفجرةُ}؛ أي: الذين كفروا بنعمة الله، وكذَّبوا بآياته، وتجرَّؤوا على محارمِهِ. نسأل الله العفوَ والعافيةَ؛ إنَّه جوادٌ كريمٌ.
{33 - 42} Yaani, utakapokuja ukelele wa Kiyama, ambao kwa sababu ya mahangaiko yake masikio yatapata shida kubwa, na nyoyo zitafadhaika siku hiyo; kutokana na yale watu wataona ya kutisha na haja kubwa ya kuwa matendo mazuri yaliyotangulia. Mtu atawakimbia watu ambao ni wapenzi zaidi kwake na wanaomhurumia zaidi. Atakimbia kutoka kwa kaka yake, mama yake, baba yake, mkewe na watoto wake, kwa sababu "Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha." Yaani, nafsi yake itakuwa imemshughulisha, na akajishughulisha na kuiokoa, na hatajali kitu kingine chochote. Hapo viumbe vitagawanyika katika makundi mawili: wenye furaha na wenye huzuni. Ama wenye furaha, nyuso zao "Siku hiyo zitanawiri" kwa furaha kutokana na yale waliyoyajua ya wokovu wao na kufuzu kwao kufikia neema. "Zitacheka, zitachangamka. Na nyuso" za wana mashakani "siku hiyo zitakuwa na mavumbi. Giza totoro litazifunika." Zitakuwa tayari zimekata tamaa kabisa ya kufikia heri yoyote, na zikajua mashaka yatakayozipata, na maangamio yake. "Hao" wenye maelezo haya, "ndio makafiri watenda maovu." Yaani, wale waliokufuru neema ya Mwenyezi Mungu, wakakadhibisha ishara zake, na wakathubutu kufanya aliyoyaharamisha. Tunamwomba Mwenyezi Mungu msamaha na salama. Hakika Yeye ndiye Mpaji, Mkarimu mno.
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
***