Iliteremka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ (1) عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ (2) الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ (3) كَلَّا سَيَعْلَمُونَ (4) ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ (5)}.
1. Wanaulizana kuhusu nini? 2. Kuhusu Ile habari kuu. 3. Ambayo kwayo wanahitalifiana. 4. La! Karibu watakuja jua. 5. Tena la! Karibu watakuja jua.
#
{1 - 5} أي: عن أيِّ شيءٍ يتساءل المكذِّبون بآيات الله؟ ثم بيَّن ما يتساءلون عنه فقال: {عن النبإ العظيم. الذي هم فيه مختلفونَ}؛ أي: عن الخبر العظيم الذي طال فيه نزاعُهم وانتشر فيه خلافُهم على وجه التَّكذيب والاستبعاد، وهو النبأ الذي لا يقبل الشكَّ ولا يدخُلُه الريبُ، ولكن المكذِّبون بلقاء ربِّهم لا يؤمنون، ولو جاءتهم كلُّ آيةٍ، حتى يَرَوُا العذاب الأليم، ولهذا قال: {كلاَّ سيعلمونَ. ثم كلاَّ سيعلمونَ}؛ أي: سيعلمون إذا نزل بهم العذابُ ما كانوا به يكذبون حين {يُدَعُّون إلى نار جَهَنَّم دعًّا}. ويقال لهم: {هذه النَّار التي كنتُم بها تكذِّبونَ}.
{1 - 5} Yaani, je, wanauliza hao wanaokadhibisha ishara za Mwenyezi Mungu juu ya kitu gani? Kisha akaeleza waliyokuwa wakiulizana juu yake,
akasema: "Kuhusu ile habari kuu. Ambayo kwayo wanahitalifiana" kwa muda mrefu kwa namna ya kuikadhibisha na kuona kwamba ni jambo lisilowezekana. Lakini ni habari isiyokubali shaka yoyote, lakini wale wanaokadhibisha kukutana na Mola wao Mlezi hawaamini, hata ikiwafikia kila Ishara, mpaka waione adhabu chungu,
na ndiyo maana akasema: "La! Karibu watakuja jua. Tena la! Karibu watakuja jua" itakapowashukia adhabu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikadhibisha siku "watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu" na waambiwe, "Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukanusha!"
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja neema na ushahidi vinavyoonyesha yale waliyoyaleta Mitume, akasema:
{أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا (6) وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا (7) وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا (8) وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا (9) وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا (10) وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا (11) وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا (12) وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا (13) وَأَنْزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا (14) لِنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا (15) وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا (16)}.
6. Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? 7. Na milima kama vigingi? 8. Na tukakuumbeni kwa jozi? 9. Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? 10. Na tukaufanya usiku ni nguo? 11. Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? 12. Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? 13. Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto. 14. Na tukateremsha maji yanayoanguka kwa kasi kutoka mawinguni. 15. Ili tutoe kwayo nafaka na mimea. 16. Na mabustani yenye miti iliyokamatana.
#
{6 - 16}؛ أي: أما أنعمنا عليكم بنعمٍ جليلةٍ، فجعلنا لكم {الأرضَ مِهاداً}؛ أي: ممهَّدة مذلَّلة لكم ولمصالحكم من الحروث والمساكن والسُّبل، {والجبالَ أوتاداً}: تمسك الأرض لئلاَّ تضطرب بكم وتميدَ، {وخَلَقْناكم أزواجاً}؛ أي: ذكوراً وإناثاً من جنس واحدٍ؛ ليسكن كلٌّ منهما إلى الآخر، فتتكوَّن الموَّدة والرحمة، وتنشأ عنهما الذُّرِّيَّة. وفي ضمن هذا الامتنان بلذَّة المنكح. {وجَعَلْنا نومَكم سُباتاً}؛ أى: راحةً لكم وقطعاً لأشغالكم التي متى تمادت بكم؛ أضرَّت بأبدانكم، فجعل الله الليل والنوم يُغْشي الناس لتسكنَ - حركاتُهم الضارَّة وتحصل راحتُهم النافعةُ، {وبنينا فوقَكم سبعاً شِداداً}؛ أي: سبع سماواتٍ في غاية القوَّة والصَّلابة والشِّدَّة، وقد أمسكها الله بقدرته، وجعلها سقفاً للأرض، فيها عدَّة منافع لهم، ولهذا ذكر من منافعها الشمس، فقال: {وجَعَلْنا سراجاً وهَّاجاً}: نبَّه بالسِّراج على النِّعمة بنورها الذي صار ضرورةً للخلق، وبالوهَّاج - وهي حرارتها - على ما فيها من الإنضاج والمنافع ، {وأنزلنا من المعصِراتِ}؛ أي: السَّحاب {ماءً ثَجَّاجاً}؛ أي: كثيراً جدًّا؛ {لِنُخْرِجَ به حبًّا}: من برٍّ وشعيرٍ وذرةٍ وأرزٍّ وغير ذلك ممّا يأكله الآدميُّون، {ونباتاً}: يشملُ سائر النَّبات الذي جعله الله قوتاً لمواشيهم، {وجناتٍ ألفافاً}؛ أي: بساتين ملتفَّة فيها من جميع أصناف الفواكه اللَّذيذة؛ فالذي أنعم [عليكم] بهذه النِّعم الجليلة التي لا يقدر قدرها ولا يحصى عددها؛ كيف تكفُرون به وتكذِّبون ما أخبركم به من البعث والنُّشور؟! أم كيف تستعينون بنعمِهِ على معاصيه وتجحَدونها؟!
{6 - 16} Yaani, je, hatukuneemesheni kwa neema kubwa kubwa, na tukakufanyieni "ardhi kama tandiko" kwa ajili ya masilahi yenu kama vile kupanda mimea na kujenga majumba na kujifanyia njia za kupitia? "Na milima kama vigingi" vya kuishikilia ardhi isije ikavurugika na kuwayumbayumbisha. "Na tukakuumbeni kwa jozi?" Yaani, wanaume na wanawake wa jinsia moja; ili kila mmoja wao apate utulivu katika mwenziwe, na hapo yapatikane mapenzi na huruma, na uzao utokee kutoka kwa hayo. Basi katika hayo kuna ukumbusho juu ya neema ya kufurahia ngono. "Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?" Ili kumaliza shughuli zenu nyingi, ambazo ikiwa mtaendelea kuzifanya, zitawadhuru miili yenu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akaujaalieni usiku na usingizi kuwafunika watu ili harakati zenu zenye madhara zitulie na yapatikane mapumziko yao yenye manufaa kwao. "Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?" Yaani, mbingu saba zenye nguvu mno na uthabiti, na Mwenyezi Mungu akazishikilia kwa uweza wake, na akazifanya kuwa ni paa la ardhi, ndani yake yamo manufaa mengi kwao, na ndiyo maana akataja jua miongoni mwa manufaa yake,
akasema: "Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto." Kwa kutaja taa, akawa anaashiria manufaa yake ambayo ni mwangaza, ambao unahitajiwa mno na viumbe, na pia akataja joto lake ambalo linaivusha na pia lina manufaa mengine. "Na tukateremsha maji yanayoanguka kwa kasi kutoka mawinguni. Ili tutoe kwayo nafaka" kama vile ngano, shayiri, mahindi, mchele na vitu vinginevyo wanavyokula wanadamu. "Na mimea" yote ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni chakula cha mifugo yao. "Na mabustani yenye miti iliyokamatana" yenye kila aina ya matunda matamu. Kwa hivyo, Yule ambaye amekuneemesheni neema hizi kubwa ambazo thamani yake haina kikomo wala idadi yake haihesabiki, basi vipi mnamkufuru na kumkadhibisha katika yale aliyokuambieni kuhusu kufufuliwa na kutawanywa? Au mnatafutaje msaada kutoka kwa neema zake katika kumuasi na tena mnazikataa?
{إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا (17) يَوْمَ يُنْفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا (18) وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا (19) وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا (20) إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا (21) لِلطَّاغِينَ مَآبًا (22) لَابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا (23) لَا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا (24) إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا (25) جَزَاءً وِفَاقًا (26) إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا (27) وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا (28) وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا (29) فَذُوقُوا فَلَنْ نَزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا (30)}.
17. Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake. 18. Siku litakapopulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi. 19. Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango. 20. Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. 21. Hakika Jahannamu inangojea! 22. Kwa walioasi ndio makazi yao. 23. Wakae humo karne baada ya karne. 24. Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji. 25. Ila maji ya moto sana na usaha. 26. Ndio malipo mwafaka. 27. Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hesabu
(juu ya matendo yao). 28. Na wakakanusha Aya zetu kwa nguvu. 29. Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. 30. Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
#
{17 - 25} ذكر الله تعالى ما يكون في يوم القيامةِ الذي يتساءل عنه المكذِّبون ويجحده المعاندون؛ أنَّه يومٌ عظيمٌ، وأن الله جعله {ميقاتاً} للخلق، {يُنفَخُ في الصُّور} فيأتون {أفواجاً}: ويجري فيه من الزعازع والقلاقل ما يَشيبُ له المولودُ وتنزعجُ له القلوبُ، فتسير الجبال حتى تكون كالهباء المبثوثِ، وتنشقُّ السماء حتى تكون أبواباً، ويفصل الله بين الخلائق بحكمه الذي لا يجور، وتوقدُ نارُ جهنَّم التي أرصدها الله وأعدَّها للطَّاغين وجعلها مثوىً لهم ومآباً، وأنَّهم يلبَثون فيها أحقاباً كثيرةً، والحقبُ على ما قاله كثيرٌ من المفسِّرين ثمانون سنة؛ فإذا وردوها ؛ {لا يذوقون فيها برداً ولا شراباً}؛ أي: لا ما يبرِّدُ جلودَهم ولا ما يدفع ظمأهم؛ {إلاَّ حميماً}؛ أي: ماءً حارًّا يشوي وجوههم ويقطِّع أمعاءهم {وغَسَّاقاً}: وهو صديدُ أهل النار: الذي هو في غاية النتن وكراهة المذاق.
{17 - 25} Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja yatakayotokea Siku ya Kiyama, ambayo wale wanaokadhibisha wanaulizana juu yake, na wakaidi wanayakataa. Hakika ni siku kuu, na Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni yenye "wakati wake" maalumu kwa ajili ya viumbe; "litakapopulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi." Siku hiyo masumbufu na wasiwasi vipatatokea kiasi kwamba mtoto atazeeka, na mioyo itavurugika kwa sababu yake, nayo milima itakwenda mbio mpaka iwe kama mavumbi yaliyopeperushwa, na mbingu zitapasuka mpaka ziwe kama milango, na Mwenyezi Mungu atatoa uamuzi kati ya viumbe kwa uamuzi wake usio wa dhuluma. Nao moto wa Jahannam utawashwa, ambao Mwenyezi Mungu aliufanya kungojea na kuutayarisha kwa ajili ya madhalimu, na akaufanya kuwa makazi yao na mahali pao pa kurejea, na watakaa humo kwa karne na karne nyingi sana. Na muda wa huqba moja kama walivyosema wafasiri wengi ni miaka themanini. Kisha watakapoufikia, "Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji." Yaani, hawatapata cha kuwapa ubaridi kwenye ngozi zao, wala cha kukata kiu chao. "Ila maji yamoto sana" yenye kubabua nyuso zao na kuwakata matumbo yao. "Na usaha" wa watu wa Motoni, ambao ni wenye uvundo mkubwa mno na wenye ladha isiyopendeza.
#
{26 - 30} وإنَّما استحقُّوا هذه العقوبات الفظيعة جزاءً لهم وفاقاً على ما عملوا من الأعمال الموصلة إليها، لم يظلمهم الله ولكن ظلموا أنفسهم، ولهذا ذكر أعمالهم التي استحقُّوا بها هذا الجزاء، فقال: {إنَّهم كانوا لا يرجونَ حساباً}؛ أي: لا يؤمنون بالبعث، ولا أنَّ الله يجازي الخلق بالخير والشرِّ؛ فلذلك أهملوا العمل للآخرة، {وكذَّبوا بآياتِنا كِذَّاباً}؛ أي: كذَّبوا بها تكذيباً واضحاً صريحاً، وجاءتهم البيِّنات فعاندوها، {وكلَّ شيءٍ}: من قليلٍ وكثيرٍ وخيرٍ وشرٍّ، {أحصيناه كتاباً}؛ أي: أثبتناه في اللوح المحفوظ؛ فلا يحسب المجرمون أنَّا عذَّبناهم بذنوب لم يعملوها، ولا يحسبوا أنَّه يضيع من أعمالهم شيءٌ أو يُنسى منها مثقالُ ذرَّةٍ؛ كما قال تعالى: {ووُضِعَ الكتابُ فترى المجرمين مشفقين ممَّا فيه ويقولون يا ويلتنا مالِ هذا الكتاب لا يغادِرُ صغيرةً ولا كبيرةً إلاَّ أحصاها ووجدَوا ما عمِلوا حاضراً ولا يظلِمُ ربُّك أحداً}. {فذوقوا}: أيُّها المكذِّبون هذا العذاب الأليم والخزيَ الدائم، {فلن نزيدكم إلاَّ عذاباً}: فكلُّ وقتٍ وحينٍ يزدادُ عذابُهم. وهذه الآيةُ أشدُّ الآيات في شدَّة عذاب أهل النار، أجارنا الله منها.
{26 - 30} Na hakika walistahiki adhabu hizi mbaya ziwe ndiyo malipo yao mwafaka kwa mujibu wa matendo waliyoyafanya yaliyowapelekea huko. Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walijidhulumu nafsi zao wenyewe, na ndiyo maana akataja matendo yao yaliyowafanya kustahiki malipo haya,
akasema: "Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hesabu
(juu ya matendo yao)." Yaani, hawakuwa wakiamini kufufuliwa, wala kwamba Mwenyezi Mungu atawalipa viumbe kwa wema na uovu. Basi wakapuuza kuifanyia Akhera matendo, "Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu" wazi wazi, na zikawajia hoja zilizo wazi, lakini wakazipinga. "Na kila kitu" kichache, kingi, chema na kibaya "Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika" katika Ubao uliohifadhiwa. Kwa hivyo, wasidhanie wahalifu kuwa tumewaadhibu kwa madhambi ambayo hawakuyafanya, wala wasidhanie kuwa chochote katika vitendo vyao kitapotea au kusahauliwa uzito wa chembe.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kitawekwa kitabu. Basi utawaona wakosefu wanavyoogopa kwa yale yaliomo humo.
Na watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa ila huliandika? Na watayakuta yote waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote." Kisha akasema "Basi onjeni" enyi mnaokadhibisha adhabu hii chungu na hizaya ya daima. "Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!" Kwani adhabu yao hii itazidishwa kila wakati. Aya hii ndiyo aya kali zaidi miongoni mwa Aya zinazohusu ukali wa adhabu ya wakazi wa Motoni.
{إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا (31) حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا (32) وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا (33) وَكَأْسًا دِهَاقًا (34) لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا (35) جَزَاءً مِنْ رَبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا (36)}.
31. Hakika wacha Mungu wanastahiki kufuzu. 32. Mabustani na mizabibu. 33. Na wake wazuri waliolingana nao. 34. Na bilauri zilizojaa. 35. Hawatasikia humo upuuzi wala uongo. 36. Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
#
{31 - 36} لمَّا ذكر حال المجرمين؛ ذَكَرَ مآلَ المتَّقين، فقال: {إنَّ للمتَّقين مفازاً}؛ أي: الذين اتَّقوا سَخَطَ ربِّهم بالتَّمسُّك بطاعته والانكفاف عن معصيته ؛ فلهم مفازٌ ومنجىً وبعدٌ عن النار، وفي ذلك المفاز لهم {حدائق}: وهي البساتين الجامعة لأصناف الأشجار الزاهية بالثِّمار التي تتفجَّر بين خلالها الأنهار، وخصَّ العنب - لشرفه وكثرته في تلك الحدائق. ولهم فيها زوجاتٌ على مطالب النُّفوس {كواعبَ}: وهي النواهِدُ اللاَّتي لم تتكسَّر ثديُهُنَّ من شبابهنَّ وقوَّتهن ونضارتهنَّ. والأتراب اللاَّتي على سنٍّ واحدٍ متقاربٍ، ومن عادة الأتراب أن يكنَّ متآلفاتٍ متعاشراتٍ، وذلك السنُّ الذي هنَّ فيه ثلاثٌ وثلاثونَ سنةً أعدل ما يكون من الشباب ، {وكأساً دِهاقاً}؛ أي: مملوءة من رحيقٍ لَذَّةٍ للشاربين، {لا يسمعون فيها لغواً}؛ أي: كلاماً لا فائدة فيه، {ولا كِذَّاباً}؛ أي: إثماً؛ كما قال تعالى: {لا يسمعون فيها لغواً ولا تأثيماً. إلاَّ قِيلاً سلاماً سلاماً}، وإنَّما أعطاهم الله هذا الثَّواب الجزيل من فضله وإحسانه. {عطاءً حساباً}؛ أي: بسبب أعمالهم التي وفَّقهم الله لها، وجعلها سبباً للوصول إلى كرامته.
{31 - 36} Mwenyezi Mungu alipotaja hali ya wahalifu, akataja mwisho wa wachamungu,
akasema: "Hakika wacha Mungu." Yaani, wale waliojiepusha mbali na ghadhabu ya Mola wao Mlezi kwa kushikamana na kumtii na kujiepusha na kumuasi "wanastahiki kufuzu" kwa kupewa njia ya kutokea na kuokoka kutokana na kuwa mbali na Moto. Na katika kufuzu huko watakuwa na "Mabustani" yanayokusanya aina za miti inayong'aa kwa matunda, yapitayo mito kati yake, na hapa alizitaja zabibu hasa kwa sababu ya heshima yake na wingi wake katika bustani hizo. Na wana wake humo kulingana na zitakavyo nafsi zao nao ni "wake wazuri" barubaru ambao matiti yao hayajaanguka kutokana na ujana wao, nguvu zao na urembo wao, "waliolingana nao." Na wake wa rika moja na waume zao kwa kawaida huwa nahisi vizuri kuwa pamoja na waume zao na huwa wanaishi nao kwa uzuri. Na miaka hii ya rika moja ambayo ndio umri wao ni miaka thelathini na tatu ambayo ndiyo mzuri zaidi ya ujana. "Na bilauri zilizojaa" vinywaji vizuri, vyenye ladha nzuri zaidi kwa wanywao. "Hawatasikia humo upuuzi." Yaani, mazungumzo yasiyo na faida "wala uwongo" kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi. Isipokuwa maneno ya Salama, Salama." Na Mwenyezi Mungu aliwapa malipo haya makubwa kutokana na fadhila zake na ukarimu wake, "kipawa cha kutosha" kwa sababu ya matendo yao ambayo Mwenyezi Mungu aliwawezesha kuyafanya, na akawafanya hayo kuwa njia ya kufikia utukufu wake.
{رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَنِ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا (37) يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا لَا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَنُ وَقَالَ صَوَابًا (38) ذَلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَى رَبِّهِ مَآبًا (39) إِنَّا أَنْذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنْظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَالَيْتَنِي كُنْتُ تُرَابًا (40)}.
37. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Arrahman
(Mwingi wa rehema); hawamiliki usemi mbele yake! 38. Siku atakaposimama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila yule ambaye Mwingi wa rehema atamruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. 39. Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anayetaka, na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi. 40.
Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu ataona yale yaliyotangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa udongo!
#
{37 - 39} أي: الذي أعطاهم هذه العطايا هو ربُّهم، {ربُّ السمواتِ والأرضِ}: الذي خلقها ودبَّرها. {الرحمن}: الذي رحمته وسعتْ كلَّ شيءٍ، فربَّاهم ورحمهم ولطف بهم حتى أدركوا ما أدركوا. ثم ذكر عَظَمَتَه وملكَه العظيم يوم القيامةِ، وأنَّ جميع الخلق كلَّهم ساكتون ذلك اليوم لا يتكلَّمون و {لا يملِكونَ منه خطاباً}؛ {إلاَّ مَنْ أذِنَ له الرحمن وقال صواباً}: فلا يتكلَّم أحدٌ إلاَّ بهذين الشرطين: أن يأذنَ الله له في الكلام، وأنْ يكونَ ما تكلَّم به صواباً؛ لأنَّ {ذلك اليوم} [هو] {الحقُّ}: الذي لا يَروج فيه الباطلُ ولا ينفعُ فيه الكذب. وفي ذلك اليوم {يقومُ الرُّوح}: وهو جبريلُ عليه السلام، الذي هو أفضلُ الملائكة، {والملائكةُ}: أيضاً يقوم الجميع {صفًّا}: خاضعين لله، لا يتكلَّمون إلاَّ بإذنه. فلمَّا رَغَّب ورَهَّب وبشَّرَ وأنذر؛ قال: {فَمَن شاء اتَّخذ إلى ربِّه مآباً}؛ أي: عملاً وقَدَمَ صدقٍ يرجع إليه يوم القيامةِ.
{37 - 39} Yaani Yule aliyewapa vipawa hivi ndiye Mola wao Mlezi, "Mola Mlezi wa mbingu na ardhi" aliyeziumba na kuziendesha. "Arrahman
(Mwingi wa rehema)" ambaye rehema zake zimekienea kila kitu. Aliwalea, akawarehemu na akawafanyia upole mpaka wakapata yale waliyopata. Kisha akataja ukubwa wake na mamlaka yake makubwa Siku ya Kiyama, na kwamba viumbe vyote vitanyamaza siku hiyo na havitasema na "hawatamiliki usemi mbele yake. Ila yule ambaye Mwingi wa rehema atamruhusu, na atasema yaliyo sawa tu." Kwa hivyo,
hatasema yeyote ila kwa masharti haya mawili: ya kwamba Mwenyezi Mungu amemruhusu kusema, na kwamba anayosema yawe ni sawa. Kwa sababu "Hiyo ndiyo Siku ya haki" ambayo haitaenea batili ndani yake wala uwongo hautafaidisha kitu. Na katika siku hiyo "Roho atasimama" naye ni Jibril, amani imshukie, ambaye ndiye mbora zaidi wa Malaika wote. "Na Malaika" pia watasimama "kwa safu" huku wamemnyenyekea Mwenyezi Mungu, bila ya kusema lolote ila kwa idhini yake. Basi alipotia moyo na akaogopehsa, na akatoa bishara njema na akaonya.
Akasema: "Basi anayetaka, na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi." Yaani, matendo mema aliyotanguliza atakayoyarudia Siku ya Kiyama.
#
{40} {إنَّا أنذَرْناكم عذاباً قريباً}: لأنَّه قد أزِفَ مقبلاً، وكلُّ ما هو آتٍ [فهو] قريبٌ. {يوم ينظُرُ المرءُ ما قدَّمتْ يداه}؛ أي: هذا الذي يهمُّه ويفزع إليه، فلينظر في هذه الدار ما قدَّم لدار القرار ، {يا أيُّها الذين آمنوا اتَّقوا الله وَلْتَنظُرْ نفسٌ ما قدَّمت لغدٍ واتَّقوا اللهَ إنَّ الله خبيرٌ بما تعملونَ ... } الآيات؛ فإن وجد خيراً؛ فليحمدِ الله، وإن وجدَ غير ذلك؛ فلا يلومنَّ إلاَّ نفسه. ولهذا كان الكفار يتمنَّوْن الموت من شدَّة الحسرة والندم. نسأل الله أن يعافِيَنا من الكفر والشرِّ كلِّه إنَّه جوادٌ كريمٌ.
{40} "Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika" Na hakika kila kinachokuja, kiko karibu. "Siku ambayo mtu ataona yale yaliyotangulizwa na mikono yake." Yaani, hayo ndiyo yanafaa kumtia wasiwasi. Basi na azingatie katika nyumba hii yale aliyoyawasilishwa kwa ajili ya nyumba ya kusalia milele. "Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayoyatenda" hadi mwisho wa aya hizi. Kwa hivyo, akipata heri, basi na amsifu Mwenyezi Mungu. Na akipata yasiyokuwa hayo, basi kamwe asijilaumu isipokuwa yeye mwenyewe. Na ndiyo maana makafiri watatamani kifo kwa sababu ya huzuni na majuto makubwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe salama kutokana na ukafiri na maovu yote. Hakika Yeye ni Mpaji, Mkarimu zaidi.
Imekamilika tafsiri yake.
***