Tafsiri ya Surat Al-Mursalat
Tafsiri ya Surat Al-Mursalat
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا (1) فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا (2) وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا (3) فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا (4) فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا (5 ضض) عُذْرًا أَوْ نُذْرًا (6) إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ (7) فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ (8) وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ (9) وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ (10) وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ (11) لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ (12) لِيَوْمِ الْفَصْلِ (13) وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ (14) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (15)}.
1. Ninaapa kwa zinazotumwa kwa upole! 2. Na zinazovuma kwa kasi! 3. Na zikaeneza maeneo yote! 4. Na zinazofarikisha zikatawanya! 5. Na zinazopeleka mawaidha! 6. Kuwa udhuru au kuonya. 7. Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka yatakuwa! 8. Wakati nyota zitakapofutwa. 9. Na mbingu zitakapopasuliwa. 10. Na milima itakapopeperushwa. 11. Na Mitume watakapo wekewa wakati wao. 12. Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? 13. Kwa siku ya kupambanua! 14. Na nini kitakachokujuulisha siku ya kupambanua ni nini? 15. Ole wao, siku hiyo hao wanaokanusha!
#
{1 - 6} أقسم تعالى على البعث والجزاء على الأعمال بـ {المُرْسَلات عُرْفاً}: وهي الملائكةُ التي يرسِلُها الله تعالى بشؤونه القدريَّة وتدبير العالم، وبشؤونه الشرعيَّة ووحيه إلى رسله، و {عُرْفاً}: حال من المرسلات؛ أي: أرسلت بالعُرْف والحكمة والمصلحة، لا بالنُّكر والعبث. {فالعاصفاتِ عصفاً}: وهي أيضاً الملائكة التي يرسِلُها الله تعالى، وَصَفَها بالمبادرة لأمره وسرعة تنفيذ أوامره كالريح العاصف أو أنَّ العاصفات الرياح الشديدة التي يُسْرِعُ هبوبها، {والناشرات نشراً}: يُحتمل أنَّ المراد بها الملائكة ؛ تنشر ما دُبِّرت على نشره، أو أنَّها السحاب التي يَنْشُرُ الله بها الأرض فيحييها بعد موتها. {فالمُلْقِياتِ ذِكْراً}: هي الملائكة تلقي أشرفَ الأوامر، وهو الذِّكْرُ الذي يرحم الله به عباده، ويذكِّرهم فيه منافعهم ومصالحهم؛ تلقيه إلى الرسل {عُذْراً أو نُذْراً}؛ أي: إعذاراً وإنذاراً للناس؛ تنذر الناس ما أمامهم من المخاوف وتقطَعُ أعذارهم ؛ فلا يكون لهم حُجَّةٌ على الله.
{1 - 6} Mwenyezi aliapa kwa kufufuliwa na malipo juu ya vitendo katika kauli yake. "Ninaapa kwa zinazotumwa kwa upole!" Nao ni Malaika ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu anawatuma kwa ajili ya mambo yake ya mipango yake iliyotangulia na kuendesha ulimwengu, na mambo yake ya kisheria na ufunuo wake kwa Mitume wake. Nao anawatuma kwa upole, hekima na masilahi, sio kwa ubaya na mchezo. "Na zinazovuma kwa kasi!" Nao pia ni Malaika anaowatuma Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawaelezea kwamba kuwa ni wenye kukimbilia na kutekeleza amri zake, kama vile upepo wa kimbunga, au kilichokusudiwa hapa ni tufani inayopunga vikali. "Na zikaeneza maeneo yote" inawezekana kwamba wanaokusudiwa hapa pia ni Malaika. Wao hueneza kile walichoamrishwa kukieneza, au ni mawingu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu huitandaza ardhi na kuihuisha baada ya kufa kwake. "Na zinazopeleka mawaidha!" Hawa pia ni Malaika watoao mambo matukufu zaidi, ambayo ni ukumbusho ambao Mwenyezi Mungu anawarehemu waja wake kwa huo, na kuwakumbusha kwa huo manufaa na maslahi yao. Wao huyapeleka mambo hayo kwa Mitume "kuwa udhuru au kuonya." Yaani, huwa udhuru na onyo kwa watu juu ya hofu iliyo mbele yao na kukata visingizio vyao. Kwa hivyo wanakuwa hawawezi kuwa na hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu.
#
{7} {إنَّما توعَدون}: من البعث والجزاء على الأعمال {لَواقِعٌ}؛ أي: متحتِّم وقوعه من غير شكٍّ ولا ارتياب.
{7} "Hakika mnayoahidiwa" ya ufufuo na kulipwa juu ya matendo "bila ya shaka yatakuwa!"
#
{8 - 14} فإذا وقع؛ حصل من التغيُّر للعالم والأهوال الشَّديدة ما يزعج القلوبَ وتشتدُّ له الكروب فتنطمس النُّجوم؛ أي: تتناثر وتزول عن أماكِنِها، وتُنْسَفُ الجبال، فتكون كالهباء المنثور، وتكون هي والأرض قاعاً صفصفاً، لا ترى فيها عوجاً ولا أمتاً، وذلك اليوم هو اليوم الذي {أُقِّتَتْ} فيه الرسل، وأجِّلَتْ للحكم بينها وبين أممها، ولهذا قال: {لأيِّ يوم أجِّلَتْ}: استفهامٌ للتعظيم والتفخيم والتهويل، ثم أجاب بقوله: {ليوم الفصل}؛ أي: بين الخلائق بعضهم من بعض، وحساب كلٍّ منهم منفرداً.
{8 - 14} Ikitokea, kutakuwa na mabadiliko katika dunia na mambo ya kutisha sana ambayo yatasumbua nyoyo na kufanya uchungu kuwa mkubwa kiasi kwamba nyota zitazimika, zianguke kutoka mahali pake, nayo milima itapasuka iwe kama mavumbi yaliyotawanywa, na hiyo hiyo milima pamoja na ardhi viwe tambarare uwanda, hutaona humo mdidimio wala muinuko. Na siku hiyo ndiyo siku ambayo Mitume "watakapowekewa wakati wao” na iliahirishwa kwa ajili ya kufanya hukumu baina yao na mataifa yao,
na ndiyo maana akasema: “Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?" Huku ni kuuliza kwa njia ya kuonyesha ukuu, ukubwa na uzito wa jambo hili.
Kisha akajibu kwa kauli yake: "Kwa siku ya kupambanua!" Yaani, baina ya viumbe wao kwa wao, na kumfanyia kila mmoja wao mahesabu yake juu ya matendo yake.
#
{15} ثم توعَّد المكذِّب بهذا اليوم، فقال: {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبينَ}؛ أي: يا حسرتهم وشدَّة عذابهم وسوءَ منقلبهم، أخبرهم الله وأقسم لهم فلم يصدقوه؛ فلذلك استحقُّوا العقوبة البليغةَ.
{15} Kisha akawaahidi adhabu wale wanaokadhibisha siku hii,
akasema: "Ole wao, siku hiyo hao wanaokanusha!" Yaani, Oh watakuwa na huzuni mkubwa namna gani, na adhabu kali namna gani, na mwisho mbaya namna gani. Kwani Mwenyezi Mungu aliwaambia haya na kuwaapia, lakini hawakumwamini, na ndiyo sababu wakastahili adhabu kali mno.
{أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ (16) ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ (17) كَذَلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ (18) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (19)}.
16. Kwani hatukuwaangamiza waliotangulia? 17. Kisha tukawafuatilizia waliofuatia? 18. Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! 19. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
#
{16 - 19} أي: أما أهلكنا المكذِّبين السابقين، ثم نتبعهم بإهلاك من كَذَّب من الآخرين، وهذه سنَّتُه السابقة واللاحقة في كلِّ مجرم، لا بدَّ من عقابه ، فلِمَ لا تعتبرون بما ترون وتسمعون؟! {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}: بعدما شاهدوا من الآيات البينات والعقوباتِ والمَثُلات.
{16 - 19} Yaani, kwani hatukuwaangamiza wale waliokanusha waliotangulia, kisha tukawafuatisha kwa kuwaangamiza wengine waliokadhibisha? Basi huu ndio mwendo wake uliotangulia na utajao kuhusiana na kila mhalifu, lazima apate kuadhibiwa. Kwa hivyo, kwa nini hamzingatii kutokana na yale mnayoyaona na kusikia? "Ole wao, siku hiyo hao wanaokanusha" baada ya kuona ishara zilizo wazi, na mateso na adhabu za mifano.
{أَلَمْ نَخْلُقْكُمْ مِنْ مَاءٍ مَهِينٍ (20) فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَكِينٍ (21) إِلَى قَدَرٍ مَعْلُومٍ (22) فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ (23) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (24)}.
20. Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? 21. Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? 22. Mpaka muda maalumu? 23. Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. 24. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
#
{20 - 24} أي: أما خلقناكم أيُّها الآدميُّون {من ماءٍ مَهينٍ}؛ أي: في غاية الحقارة، خرج من بين الصُّلب والتَّرائب، حتى جعله الله {في قرارٍ مَكينٍ}: وهو الرحم به يستقرُّ وينمو، {إلى قدرٍ معلومٍ}: ووقتٍ مقدَّرٍ. {فقَدَرْنا}؛ أي: قدَّرْنا ودَبَّرْنا ذلك الجنين في تلك الظُّلمات، ونقلناه من النُّطفة إلى العلقة إلى المضغة إلى أن جعله الله جسداً و نفخ فيه الروح، ومنهم من يموت قبل ذلك. {فنعم القادِرونَ}؛ يعني بذلك نفسه المقدَّسة؛ لأنَّ قَدَرَه تابعٌ لحكمته موافقٌ للحمد. {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبينَ}، [بعد ما بَيَّن اللهُ لهم الآياتِ وأراهم العبَر والبيِّناتِ].
{20 - 24} Yaani, je, hatukukuumbeni, enyi wanadamu, "kwa maji ya kudharauliwa" yaliyotoka baina ya mifupa ya mgongo na mbavu, kisha Mwenyezi Mungu akayaweka "mahali pa utulivu madhubuti" ambapo ni tumbo la uzazi ambalo humo hukaa na kukua "Mpaka muda maalumu" uliowekwa na Mwenyezi Mungu. "Tukakadiria" na kumpangia mambo kijusi huyo katika viza hivyo, na tukakihamisha kutoka kwenye tone la manii ya kiume hadi kwenye kipande cha damu iliyogandana hadi kwenye pande la nyama mpaka Mwenyezi Mungu akakifanya kuwa mwili na akakipulizia roho ndani yake. Basi baadhi yao huufa kabla ya hapo "na Sisi ni wabora wa kukadiria." Kwani kukadiria kwake kufuata hekima yake na kunaendana na sifa zake. "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha"
[baada ya Mwenyezi Mungu kuwabainishia Aya zake na kuwaonyesha mazingatio na hoja zilizo wazi].
{أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا (25) أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا (26) وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُمْ مَاءً فُرَاتًا (27) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (28)}.
25. Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya. 26. Walio hai na maiti? 27. Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? 28. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
#
{25 - 28} أي: أما مَنَنَّا عليكم وأنعمنا بتسخير الأرض لمصالحكم فجعلناها {كفاتاً}: لكم، {أحياءً}: في الدور، {وأمواتاً}: في القبور؛ فكما أنَّ الدور والقصور من نعم الله على عباده ومنَّته؛ فكذلك القبور رحمة في حقِّهم وسترٌ لهم عن كون أجسادهم باديةً للسِّباع وغيرها. {وجعلنا فيها رواسيَ}؛ أي: جبالاً ترسي الأرض لئلاَّ تميدَ بأهلها، فثبَّتها الله بالجبال الراسيات الشامخات؛ أي: الطوال العراض. {وأسْقَيْناكم ماءً فُراتاً}؛ أي: عذباً زلالاً؛ قال تعالى: {أفرأيْتُم الماءَ الذي تشربونَ. أأنتُم أنزَلْتُموه من المُزْنِ أمْ نحنُ المنزِلونَ. لو نشاءُ جعلناه أُجاجاً فلولا تَشْكُرونَ}. {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}: مع ما أراهم الله من النعم التي انفرد بها، واختصَّهم بها فقابلوها بالتكذيب.
{25 - 28} Yaani, kwani hakukuneemesheni kwa neema ya kuitiisha ardhi kwa masilahi yenu, tukaifanya "ardhi yenye kukusanya" nyinyi "Walio hai" majumbani "na maiti" makaburi. Kwa hivyo, kama vile majumba na makasri ni miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, vile vile makaburi ni rehema kwao na kuwafunika miili yao inapooza ili wanyama vitu vinginevyo visiikaribie. "Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti" ili ardhi isiwayumbishe wakazi wake,
basi Mwenyezi Mungu akaiweka imara kwa milima madhubuti na mirefu mipana "na tunakunywesheni maji matamu?" Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, mnayaona maji mnayoyanywa? Je, ni nyinyi mnayoyateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? Tungelipenda, tungeliyafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?" Na akasema "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha" pamoja na yote aliyowaonyesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa neema ambazo Yeye tu ndiye alizowaneemesha wao tu kwazo, lakini wakazikabili hizo kwa kukadhibisha.
{انْطَلِقُوا إِلَى مَا كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ (29) انْطَلِقُوا إِلَى ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ (30) لَا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ (31) إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ (32) كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ (33) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (34)}.
29. Nendeni kwenye adhabu mliyokuwa mkiikanusha! 30. Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! 31. Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. 32. Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! 33. Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! 34. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
#
{29 - 34} هذا من الويل الذي أُعِدَّ للمجرمين المكذِّبين أنْ يقال لهم يوم القيامةِ: {انطَلِقوا إلى ما كُنتُم به تكذِّبونَ}: ثم فسَّر ذلك بقوله: {انطَلِقوا إلى ظِلٍّ ذي ثلاثٍ شُعَبٍ}؛ أي: إلى ظلِّ نار جهنَّم التي تتمايز في خلاله ثلاث شعب؛ أي: قطع من النار تتعاوره وتتناوبه وتجتمع به. {لا ظليلٍ}: ذلك الظلُّ؛ أي: لا راحة فيه ولا طمأنينة، {ولا يُغْني}: من مَكَثَ فيه {من اللَّهب}: بل اللهب قد أحاط به يمنةً ويسرةً ومن كلِّ جانب؛ كما قال تعالى: {لهم من فوقهم ظُلَلٌ من النار ومن تحتِهِم ظُلَلٌ}، {لهم من جَهنَّمَ مهادٌ ومن فوقِهِم غواشٍ وكذلك نجزي الظَّالمينَ}.
ثم ذكر عِظَمَ شرر النار الدالِّ على عظمها وفظاعتها وسوء منظرها، فقال: {إنها تَرْمي بشررٍ كالقَصْر. كأنَّه جِمالةٌ صُفْرٌ}: وهي السود التي تضرِب إلى لونٍ فيه صفرة، وهذا يدلُّ على أن النار مظلمة لهبها وجمرها وشررها، وأنها سوداءُ كريهةُ المنظر شديدةُ الحرارة؛ نسأل الله العافية منها، ومن الأعمال المقرِّبة منها. {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}.
{29 - 34} Hii ni moja ya adhabu kali iliyotayarishwa kwa ajili ya wahalifu wanaokadhibisha kwamba wataambiwa Siku ya Kiyama: "Nendeni kwenye adhabu mliyokuwa mkiikanusha!" Kisha akaeleza hayo kwa kusema "Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!" Yaani, nendeni kwa kivuli cha moto wa Jahannamu, ambao umegawanyika matawi matatu. Kivuli hicho. "Hakikingi moto" kwani humo hamna faraja wala utulivu. "wala hakiwaepushi" mwenye kukaa humo "kutoka na mwako.
" Bali miali ya moto huo itamzunguka kulia na kushoto na pande zote; kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Yatawekwa juu yao mat'abaka ya moto, na chini yao matabaka." Na akasema "Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivi ndivyo tunavyowalipa madhalimu." Kisha akataja ukubwa wa cheche za moto huo, ambazo zinaonyesha ukuu wake, utisho wake, na mandhari yake mabaya. Akasema, "Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano." Hili linaashiria kuwa moto huo una giza katika miali yake, makaa yake na cheche zake, na kwamba ni mweusi, wa kuchukiza sana katika mandhari yake, wenye moto mkali sana. Tunamuomba Mwenyezu Mungu salama kutokana nao, na kutokana na matendo yanayomweka mtu karibu nao. "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!"
{هَذَا يَوْمُ لَا يَنْطِقُونَ (35) وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ (36) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (37) هَذَا يَوْمُ الْفَصْلِ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ (38) فَإِنْ كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ (39) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (40)}.
35. Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu. 36. Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. 37. Ole wao siku hiyo hao waliokanusha! 38. Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia. 39. Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! 40. Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!
#
{35 - 37} أي: هذا اليوم العظيم الشَّديد على المكذِّبين، لا ينطِقون فيه من الخوف والوَجَل الشديد، {ولا يُؤْذَنُ لهم فيعتَذِرون}؛ أي: لا تُقبل معذرتُهم ولو اعتذروا. {فيومئذٍ لا ينفع الذينَ ظَلَموا معذِرَتُهم ولا هم يُسْتَعْتَبونَ}.
{35 - 37} Maana yake ni kwamba hii ni siku kubwa na ngumu kwa makafiri, ambamo hawatasema chochote kwa sababu hofu kubwa, "Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru." Na hata kama wangeomba udhuru, hawatakubaliwa. "Basi Siku hiyo hautawafaa waliodhulumu udhuru wao, wala haitotakiwa toba yao."
#
{38 - 40} {هذا يومُ الفصل جَمَعْناكم والأوَّلينَ}: لنفصل بينَكم ونحكُمَ بين الخلائق. {فإن كانَ لكم كيدٌ}: تقدِرون على الخروج عن ملكي وتَنْجونَ به من عذابي، {فكيدونِ}؛ أي: ليس لكم قدرةٌ ولا سلطانٌ؛ كما قال تعالى: {يا معشرَ الجنِّ والإنسِ إنِ اسْتَطَعْتُم أن تنفُذوا من أقطارِ السمواتِ والأرضِ فانفُذوا، لا تَنفُذون إلاَّ بسلطانٍ}؛ ففي ذلك اليوم تبطُل حيل الظالمين، ويضمحلُّ مكرُهم وكيدُهم ويستسلمون لعذابِ الله، ويبين لهم كذِبُهم في تكذيبهم. {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}.
{38 - 40} "Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia" ili tupambanue baina yenu na tuhukumu baina ya viumbe. "Ikiwa mnayo hila" mnayoweza kufanya ili mtoke katika ufalme wangu na mkaepuka adhabu yangu kwa hayo, "basi nifanyieni hila Mimi!" Yaani, hamna uwezo wala mamlaka.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye pande za mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka." Basi Siku hiyo hila za madhalimu zitabatilika na vitatoweka, na watasalimu amri kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu, na uwongo wao utawabainikia katika kukadhibisha kwao. "Ole wao siku hiyo hao waliokanusha!"
{إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ (41) وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ (42) كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (43) إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (44) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (45)}.
41. Hakika wacha Mungu watakuwa katika vivuli na chemchemI. 42. Na matunda wanayoyapenda. 43. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. 44. Hakika ndio kama hivyo tunavyowalipa watendao mema. 45. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!
#
{41 - 45} لمَّا ذكر عقوبة المكذِّبين؛ ذكر مثوبة المحسنين، فقال: {إنَّ المتَّقين}؛ أي: للتكذيب، المتَّصفين بالتَّصديق في أقوالهم وأفعالهم وأعمالهم، ولا يكونون كذلك إلاَّ بأدائهم الواجبات وتركهم المحرَّمات، {في ظلالٍ}: من كثرة الأشجار المتنوِّعة الزاهرة البهيَّة، {وعيونٍ}: جاريةٍ من السلسبيل والرحيق وغيرهما، {وفواكهَ ممَّا يشتهونَ}؛ أي: من خيار الفواكه وأطيبها ، ويقال لهم: {كُلوا واشْرَبوا}: من المآكل الشهيَّة والأشربة اللَّذيذة، {هنيئاً}؛ أي: من غير منغِّص ولا مكدِّر، ولا يتمُّ هناؤه حتى يسلمَ الطعام والشرابُ من كلِّ آفةٍ ونقصٍ، وحتى يجزموا أنَّه غيرُ منقطع ولا زائل؛ {بما كنتُم تعملونَ}: فأعمالكم هي السبب الموصل لكم إلى جنَّات النعيم المقيم، وهكذا كلُّ من أحسن في عبادة الله وأحسن إلى عباد الله، ولهذا قال: {إنَّا كذلك نجزي المحسِنينَ. ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}: ولو لم يكن من هذا الويل إلاَّ فوات هذا النعيم؛ لكفى به حزناً وحرماناً.
{41 - 45} Alipotaja adhabu ya wale wanaokadhibisha; akataja malipo ya wale wafanyao wema,
akasema: "Hakika wacha Mungu" wakajiepusha kukadhibisha, wale wanaosifa na kusadiki katika kauli zao, vitendo vyao na matendo yao, na wao hawawi hivyo ila kwa kutekeleza wajibu na kuacha haramu, "watakuwa katika vivuli" vitokanavyo na wingi wa aina mbali mbali nzuri za miti inayochanua maua, "na chemichemi" itokayo katika salsabil, na kinywaji safi na vitu vinginevyo.
"Na matunda wanayoyapenda" na wataambiwa: "Kuleni na kunyweni" kutokana na vyakula vitamu na vinywaji vitamu, "kwa furaha" bila ya kumsumbuliwa wala kukerwa, na furaha yake haiwezi kukamilika mpaka chakula chake na kinywaji vyake visalimike viondolewe na kila balaa na upungufu, na mpaka wahakikishe kutokana na balaa na mapungufu. "Kwa yale mliyokuwa mkiyatenda" matendo yenu ndiyo sababu iliyokupelekeni kwenye Pepo zenye neema ya kudumu, na kadhalika kila anayefanya wema katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, na akawafanyia wema waja wa Mwenyezi Mungu,
na ndiyo maana akasema: "Hakika ndiyo kama hivyo tunavyowalipa watendao mema. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!" Na lau kuwa haikuwa kwamba adhabu hii haina chochote isipokuwa kukosa neema hii, basi hilo lingetosha kuwa huzuni na kunyimwa.
{كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُمْ مُجْرِمُونَ (46) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (47) وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ (48) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (49) فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ (50)}.
46. Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! 47. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha! 48.
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. 49. Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha! 50. Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
#
{46 - 50} هذا تهديدٌ ووعيدٌ للمكذِّبين أنَّهم وإن أكلوا في الدُّنيا وشربوا وتمتَّعوا باللَّذَّات وغفلوا عن القُرُبات؛ فإنَّهم مجرمون يستحقُّون ما يستحقُّه المجرمون، فتنقطع عنهم اللَّذَّات، وتبقى عليهم التَّبِعات. ومن إجرامهم أنَّهم إذا أمِروا بالصَّلاة التي هي أشرف العبادات، و {قيل لهم اركعوا}: امتنعوا من ذلك؛ فأيُّ إجرام فوق هذا؟ وأيُّ تكذيب يزيد على هذا؟ {ويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}: ومن الويل عليهم أنَّهم تنسدُّ عنهم أبواب التوفيق ويُحْرَمون كلَّ خيرٍ؛ فإنَّهم إذا كذَّبوا هذا القرآن الذي هو أعلى مراتب الصدق واليقين على الإطلاق؛ {فبأيِّ حديثٍ بعدَه يؤمنونَ}: أبالباطل الذي هو كاسمه لا يقوم عليه شبهةٌ فضلاً عن الدليل؟ أم بكلام مشركٍ كذَّابٍ أفَّاكٍ مبينٍ؟ فليس بعد النُّور المبين إلاَّ دياجي الظلمات، ولا بعد الصدق الذي قامت الأدلة والبراهين القاطعة إلاَّ الإفك الصراح والكذب المبينُ - الذي لا يَليقُ إلاَّ بمن يناسبه؛ فتبًّا لهم ما أعماهم! وويحاً لهم ما أخسرهم وأشقاهم! نسأل الله العفو والعافية؛ إنَّه جوادٌ كريمٌ.
{46 - 50} Hili ni tishio na ni onyo kwa wale wanaokadhibisha kwamba hata wakila na kunywa katika dunia na wakastarehe na wakapuuza kufanya ibada za kuwaweka karibu na Mwenyezi Mungu, hao hakika ni wahalifu wanaostahiki kile wanachostahiki wahalifu, kwa njia ya kwamba starehe hizo zitawaisha na watabaki wakilaumiwa. Na miongoni mwa uhalifu wao ni kwamba wanapoamrishwa kuswali swala ambayo ni ibada ya heshima kabisa,
na "wakiambiwa: Inameni! Hawainami" wanakataa kufanya hivyo. Basi ni uhalifu gani unaweza kuwa juu zaidi ya hili? Na ni ni kukadhibisha gani ambako ni zaidi ya huku? "Ole wao siku hiyo hao wanaokanusha!" Na katika adhabu yao ni kuwa watafungiwa milango ya kuwezeshwa na watanyimwa kila la heri. Kwani wakiikadhibisha Qur-ani hii, ambayo ni kiwango cha juu kabisa cha kusadiki na yakini, "Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?" Je, wataamini batili ambao ni kama jina lake ambalo hauwezi kuleta shaka potofu yoyote, achilia mbali kuleta ushahidi? Au kuamini maneno ya mshirikina, mwongo kabisa wa dhaahiri? Kwa hivyo, hakuna kitu baada ya nuru iliyo wazi isipokuwa viza totoro, wala baada ya ukweli ambao ushahidi na uthibitisho wa uhakika umeuthibitisha ila uzushi mkubwa wa moja kwa moja na uwongo wa wazi - ambao haumfailii isipokuwa ile anayeufailia. Mwenyezi Mungu awaangamize, ni vipofu namna gani! Na ole wao, ni hasara gani yao kubwa hii na upotofu mkubwa ulioje! Tunamwomba Mwenyezi Mungu msamaha na salama. Hakika Yeye ni Mpaji mno, Mkarimu zaidi.
Imekamilika tafsiri.
* * *