:
Tafsiri ya Surat Al-Insan
Tafsiri ya Surat Al-Insan
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
: 1 - 3 #
{هَلْ أَتَى عَلَى الْإِنْسَانِ حِينٌ مِنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُنْ شَيْئًا مَذْكُورًا (1) إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا (ضض 2) إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا (3)}.
1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinachotajwa. 2. Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona. 3. Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
#
{1} ذكر الله في هذه السورة أول حال الإنسان ومنتهاها ومتوسِّطها: فذكر أنَّه مرَّ عليه دهرٌ طويلٌ، وهو الذي قبل وجوده، وهو معدوم، بل ليس مذكوراً.
{1} Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu ametaja hali ya mwanzo, mwisho, na hali ya kati ya mwanadamu: Ametaja kwamba muda mrefu umepita juu yake, nao ni ule uliotangulia kabla ya kuwepo kwake, na hata hakuwa kitu cha kutajwa.
#
{2} ثمَّ لمَّا أراد خلقه؛ خلق أباه آدم من طين، ثم جعل نسله متسلسلاً {من نطفةٍ أمشاج}؛ أي: ماء مَهينٍ مستقذرٍ، {نبتليه}: بذلك؛ لنعلم هل يرى حاله الأولى ويتفطن لها أم ينساها وتغرُّه نفسه؟ فأنشأه الله وخَلَقَ له القُوى الظاهرة والباطنة ؛ كالسمع والبصر وسائر الأعضاء، فأتمَّها له وجعلها سالمةً يتمكَّن بها من تحصيل مقاصده.
{2} Kisha alipotaka kumuumba, alimuumba baba yake, Adam kwa udongo, kisha akawajaalia dhuriya zake "kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika" yanayoonwa kwamba ni machafu "ili tumfanyie mtihani" kwa hayo. Ili tujue iwapo ataiona hali yake ya mwanzo na kuitambua, au ataisahau na kudanganywa na nafsi yake? Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamuumba na kumpa nguvu za dhahiri na zilizofichika, kama vile kusikia, kuona, na viungo vingine, kwa hivyo alivikamilisha hivyo vote kwa ajili yake na akaviweka salama ili aweze kufikia malengo yake.
#
{3} ثم أرسل إليه الرُّسل، وأنزل عليه الكتب، وهداه الطريق الموصلة إليه ، وبيَّنها، ورغَّبه فيها، وأخبره بما له عند الوصول إليه ، ثم أخبره بالطريق الموصلة إلى الهلاك، ورهَّبه عنها ، وأخبره بما له إذا سلكها، وابتلاه بذلك، فانقسم الناس إلى شاكرٍ لنعمة الله عليه، قائم بما حمله الله من حقوقه. وإلى كفورٍ للنعم أنعم الله عليه بالنعم الدينيَّة والدنيويَّة، فردَّها وكفر بربه، وسلك الطريق الموصلة إلى الهلاك. [ثم ذكر تعالى الفريقين عند الجزاء، فقال]:
{3} Kisha akamtumia Mitume, na akamteremshia vitabu, na akamwongoza kwenye njia ya kumfikisha kwake, na akaifafanua, na akamtia moyo wa kuifuata, na akamwambia yale yatakayokuwa yake atakapoifikia. Kisha akamwambia njia itakayoelekea kwenye maangamizo, na akamtia woga wa kuifuata, na akamwambia yale ambayo yatakuwa yake iwapo ataishika, na akamtia mtihani kwa hayo. Basi watu wakagawanyika wenye kushukuru kwa ajili ya neema za Mwenyezi Mungu juu yake, na ambaye anashika sawasawa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimbebesha katika haki zake. Na pia wakawapo wasioshukuru neema ambazo Mwenyezi Mungu amemneemesha; za kidini na za kidunia, na pia anamkufuru Mola wake Mlezi, na anafuata njia ya kumfikisha katika maangamizo. [Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja makundi hayo mawili wakati wa malipo yao, akasema]:
: 4 - 31 #
{إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا (4) إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِنْ كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا (5) عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا (6) يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا (7) وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَى حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا (8) إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنْكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا (9) إِنَّا نَخَافُ مِنْ رَبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا (10) فَوَقَاهُمُ اللَّهُ شَرَّ ذَلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا (11) وَجَزَاهُمْ بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا (12) مُتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا (13) وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا (14) وَيُطَافُ عَلَيْهِمْ بِآنِيَةٍ مِنْ فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا (15) قَوَارِيرَ مِنْ فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا (16) وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنْجَبِيلًا (17) عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّى سَلْسَبِيلًا (18) وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَنْثُورًا (19) وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا (20) عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُنْدُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِنْ فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا (21) إِنَّ هَذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُمْ مَشْكُورًا (22) إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنْزِيلًا (23) فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا (24) وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا (25) وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا (26) إِنَّ هَؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا (27) نَحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا (28) إِنَّ هَذِهِ تَذْكِرَةٌ فَمَنْ شَاءَ اتَّخَذَ إِلَى رَبِّهِ سَبِيلًا (29) وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا (30) يُدْخِلُ مَنْ يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا (31)}.
4. Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali. 5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyochanganyika na kafuri 6. Ni chemchemi watakaoinywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. 7. Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana. 8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. 9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. 10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. 11. Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. 12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri. 13. Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. 14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. 15. Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae. 16. Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. 17. Na humo watanyweshwa kinywaji kilichochanganyika na tangawizi. 18. Hiyo ni chemchemi iliyo humo inaitwa Salsabil. 19. Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasiopevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa. 20. Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa. 21. Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya atilasi. Na watavishwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. 22. Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa. 23. Hakika Sisi tumekuteremshia Qur-ani kidogo kidogo. 24. Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. 25. Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni. 26. Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu. 27. Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku nzito. 28. Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao. 29. Hakika haya ni mawaidha; basi anayetaka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. 30. Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu, Mwenye hekima. 31. Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu.
#
{4} أي: إنَّا هيَّأنا وأرصدنا لمن كفر باللَّه وكذَّب رسله وتجرَّأ على معاصيه، {سلاسل}: في نار جهنَّم؛ كما قال تعالى: {ثمَّ في سلسلةٍ ذَرْعُها سبعونَ ذِراعاً فاسلكوه}، {وأغلالاً}: تُغَلُّ بها أيديهم إلى أعناقهم ويوثقون بها، {وسعيراً}؛ أي: ناراً تستعر بها أجسامُهم وتُحرق بها أبدانُهم، كلَّما نَضِجَتْ جلودُهم؛ بدَّلناهم جلوداً غيرها ليذوقوا العذاب، وهذا العذاب الدَّائم مؤبَّدٌ لهم ، مخلَّدون فيه سرمداً.
{4} Yaani, hakika Sisi tumewaandalia wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na wakakadhibisha Mitume wake, na wakathubutu kumuasi; "minyororo" katika Moto wa Jahannamu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!" Kisha hapa akasema "na pingu" ambazo mikono yao itafungwa kwazo hadi shingoni mwao, "na Moto mkali" utakachoma miili yao na miili yao. Kila zitakapoiva ngozi zao, tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje hiyo adhabu. Nayo adhabu hii ni ya milele kwao.
#
{5} وأمَّا {الأبرار}، وهم الذين بَرَّتْ قلوبُهم بما فيها من معرفة الله ومحبَّته والأخلاق الجميلة؛ فبرَّت أعمالُهم ، واستعملوها بأعمال البرِّ، فأخبر أنَّهم {يشربون من كأسٍ}؛ أي: شرابٍ لذيذٍ من خمرٍ [قد] مُزِجَ بكافورٍ؛ أي: خلط به ليبرِّده ويكسر حدَّته، وهذا الكافور في غاية اللَّذَّة، قد سلم من كلِّ مكدِّرٍ ومنغِّص موجودٍ في كافور الدُّنيا؛ فإنَّ الآفة الموجودة في الدُّنيا تعدم من الأسماء التي ذكرها الله في الجنة ؛ كما قال تعالى: {في سِدْرٍ مخضودٍ. وطلح منضودٍ}، {وأزواجٌ مطهرةٌ}، {لهم دارُ السلام عند ربِّهم}، {وفيها ما تشتهيهِ الأنفسُ وتَلَذُّ الأعينُ}.
{5} Ama "watu wema" ambao mioyo yao ni yenye njema kwa sababu ya yale yaliyo ndani yake ya kumjua Mwenyezi Mungu, kumpenda na maadili mema. Basi matendo yao yakawa mema, kwa hivyo ikawaambia kwamba “watakunywa katika kikombe vya vinywaji" vitamu vya mvinyo [ambao] umechanganywa na kafuri, ili ichanganyike nayo ili kuipoza na kuvunja ukali wake. Na kafuri hiyo itakuwa na ladha ya hali ya juu, ambayo atakuwa imesalimika mbali na machafu yanayopatikana katika kafuri ya duniani. Kwani kasoro zilizoko duniani haziko katika majina ambayo Mwenyezi Mungu alitaja katika bustani za mbinguni, kama Mwenyezi Mungu alivyosema: "Katika mikunazi isiyo na miba. Na migomba iliyopangiliwa" na akasema "na wake waliotakaswa," na akasema "Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao." Na akasema "na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia."
#
{6} {عيناً يشربُ بها عبادُ اللهِ}؛ أي: ذلك الكأس اللذيذ الذي يشربونه لا يخافون نفاذه، بل له مادَّة لا تنقطع، وهي عينٌ دائمةُ الفيضان والجريان، يفجِّرها عباد الله تفجيراً أنَّى شاؤوا وكيف أرادوا؛ فإن شاؤوا؛ صرفوها إلى البساتين الزاهرات أو إلى الرياض النضرات، أو بين جوانب القصور والمساكن المزخرفات، أو إلى أيِّ جهةٍ يَرَوْنَها من الجهات المؤنَّقات.
{6} "Ni chemchemi watakaoinywa waja wa Mwenyezi Mungu." Yaani, hicho kikombe chenye ladha nzuri watakachokunywa, hawataogopa kwamba kitakwisha, bali kina asili isiyokoma, nayo ni chemchemi inayofurika na kutiririka daima, na waja wa Mwenyezi Mungu wataifanya imiminike kwa wingi mahali watakapo na jinsi watakavyo. Wakitaka, wanaitumia kwenye bustani zenye miti mirefu au makonde mazuri, au kati ya pande za makasri yaliyopambwa kifahari na upande wowote wa kifahari wanaouona.
#
{7} ثم ذكر جملةً من أعمالهم ، فقال: {يوفون بالنَّذْرِ}؛ أي: بما ألزموا به أنفسهم للَّه من النذور والمعاهدات، وإذا كانوا يوفون بالنذر الذي هو غير واجبٍ في الأصل عليهم إلا بإيجابهم على أنفسهم؛ كان فعلُهم وقيامهم بالفروض الأصليَّة من باب أولى وأحرى، {ويخافون يوماً كان شَرُّه مستطيراً}؛ أي: فاشياً منتشراً، فخافوا أن ينالهم شرُّه، فتركوا كلَّ سببٍ موجبٍ لذلك.
{7} Kisha akataja baadhi ya vitendo vyao, akasema: "Wanatimiza nadhiri" waliyojiwekea wenyewe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na maagano mengineyo. Na ikiwa wanatimiza nadhiri ambayo si wajibu katika asili yake isipokuwa kama mtu mwenyewe atajiwajibishia, basi kutakuwa kufanya kwao mambo ya faradhi ya asili ni jambo la awali zaidi na linalostahiki zaidi. “Na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana." Kwa hivyo, wakahofu wasije patwa na uovu wake, basi wakaacha kila sababu ya kuwasababishia hilo.
#
{8 - 10} {ويطعِمونَ الطَّعامَ على حبِّه}؛ أي: وهم في حال يحبُّون فيها المال والطعام، لكنَّهم قدَّموا محبَّة الله على محبَّة نفوسهم، ويتحرَّوْن في إطعامهم أولى الناس وأحوجَهم، {مسكيناً ويتيماً وأسيراً}: ويقصدون بإنفاقهم وإطعامهم وجهَ الله تعالى، ويقولون بلسان الحال: {إنَّما نطعِمُكم لوجه الله لا نريدُ منكم جزاءً ولا شكوراً}؛ أي: لا جزاءً ماليًّا ولا ثناءً قوليًّا، {إنا نخاف من ربِّنا يوماً عبوساً}؛ أي: شديد الجهمة والشرِّ، {قمطريراً}؛ أي: ضنكاً ضيقاً.
{8 - 10} "Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake" kwa sababu wametanguliza mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuliko mapenzi ya nafsi zao wenyewe, na wako makini zaidi kuwalisha watu wanaostahiki zaidi na walio wahitaji zaidi miongoni mwao, ambao ni "masikini, na yatima, na wafungwa" na kwa utoaji wao huo na kuwalisha kwao huko wanakusudia uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wanasema kwa ulimi wa hali zao: "Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani." Yaani, hatutaki malipo ya kimali wala kusifiwa kwa maneno. "Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida" nyingi na maovu "na taabu."
#
{11} {فوقاهُمُ اللهُ شرَّ ذلك اليوم}: فلا يحزنهم الفزعُ الأكبر، وتتلقَّاهم الملائكة هذا يومكم الذي كنتُم توعدون، {ولَقَّاهُم}؛ أي: أكرمهم وأعطاهم {نضرةً}: في وجوههم، {وسروراً}: في قلوبهم، فجمع لهم بين نعيم الظَّاهر والباطن.
{11} "Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo" na hicho Kitisho Kikubwa hakitawahuzunisha. Na Malaika watawapokea kwa kuwaambia: 'Hii ndiyo Siku yenu mliyokuwa mkiahidiwa!' Na tena "atawakutanisha na raha" katika nyuso zao, "na furaha" katika nyoyo zao. Hapo atakuwa amewakusanyia neema ya nje na ya ndani.
#
{12} {وجزاهم بما صبروا}: على طاعته فعملوا ما أمكنهم منها، وعن معاصيه فتركوها، وعلى أقداره المؤلمة فلم يتسخَّطوها {جنَّةً}: جامعةً لكلِّ نعيمٍ سالمةً من كلِّ مكدِّرٍ ومنغِّص، {وحريراً}؛ كما قال تعالى: {ولباسُهم فيها حريرٌ}: ولعلَّ اللهَ إنَّما خصَّ الحريرَ لأنَّه لباسهم الظَّاهر الدالُّ على حال صاحبه.
{12} "Na atawajazi kwa sababu ya kuwa na subira" katika kumtii. Wakafanya yale aliyowawezesha, kuwaepusha na kumuasi, na wakaacha kuchukia mipango yake mikali. "Bustani za Peponi" zilizokusanya neema, zisizo na kila dhiki na taabu, "na maguo ya hariri." Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nguo zao humo ni za hariri." Labda Mwenyezi Mungu ameichagua hariri kwa sababu ni nguo zao za dhahiri zinazoonyesha hali ya mwenye kuzivalia.
#
{13} {متَّكئين فيها على الأرائكِ}: الاتِّكاء: التمكُّن من الجلوس في حال الطُّمأنينة والراحة والرَّفاهية ، والأرائك هي السُّرُر التي عليها اللباس المزيَّن، {لا يَرَوْن فيها}؛ أي: في الجنة {شمساً}: يضرُّهم حرُّها، {ولا زمهريراً}؛ أي: برداً شديداً، بل جميع أوقاتهم في ظلٍّ ظليلٍ، لا حرٌّ ولا بردٌ؛ بحيث تلتذُّ به الأجساد ولا تتألَّم من حرٍّ ولا بردٍ.
{13} "Humo wataegemea juu ya viti vya enzi" vya sampuli ya kitanda kilichovalishwa vitambaa maridadi. "Hawataona humo" Peponi "jua" la kuwadhuru kwa joto lake, "wala baridi kali." Badala yake, nyakati zao zote zitakuwa kwenye vivuli vizuri kweli. Si joto wala baridi, ambapo miili yao itafurahia na haitateseka kwa sababu ya joto au baridi.
#
{14} {ودانيةً عليهم ظِلالها وذُلِّلَتْ قطوفُها تذليلاً}؛ أي: قُرِّبَتْ ثمراتها من مريدها تقريباً، ينالها وهو قائمٌ أو قاعدٌ أو مضطجعٌ.
{14} "Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini" kiasi kwamba anayeyataka ataweza kuyapata akiwa amesimama, amekaa au amelala.
#
{15 - 16} {ويُطافُ عليهم}؛ أي: يدور الولدان والخدم على أهل الجنة ، {بآنيةٍ من فضَّةٍ وأكوابٍ كانت قواريرَ. قواريرَ من فضَّةٍ}؛ أي: مادتها فضَّةٌ، وهي على صفاء القوارير، وهذا من أعجب الأشياء؛ أن تكون الفضَّةُ الكثيفة من صفاء جوهرها وطيب معدنها على صفاء القوارير، {قدَّروها تَقْديراً}؛ أي: قدَّروا الأواني المذكورة على قدرِ رِيِّهم؛ لا تزيدُ ولا تنقصُ؛ لأنَّها لو زادت؛ نقصتْ لذَّتها، ولو نقصت؛ لم تكفِهِم لرِيِّهم. ويُحتمل أنَّ المراد: قدَّرها أهلُ الجنة - بمقدارٍ يوافقُ لذَّتَهم، فأتتْهم على ما قدَّروا في خواطرهم.
{15 - 16} "Na watapitishiwa." Yaani, watoto na watumishi watawajia mara kwa mara Peponi, "kwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae. Vya fedha safi kama kiyoo." Haya ni katika mambo ya ajabu sana, kwamba fedha ambayo huwa imesongana bila ya kuonekana ndani iwe safi mno kama kioo katika usafi wake na uzuri wake, "wamevipima kwa vipimo." Yaani, walivipima vyombo hivyo vilivyotajwa kulingana na kiwango cha kuwashibisha kiu chao, bila ya kuzidisha wala kupunguza. Kwa sababu ikiwa vingezidi, basi ladha yake ingepungua, na kama vikipungua, basi havingeweza kuwakatia kiu. Lakini inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni: wakazi wa Peponi walivipima kwa kipimo kinacholingana na ladha zao, kwa hivyo vikawajia kulingana na walivyokadiria katika fikira zao.
#
{17 - 18} {ويُسْقَوْنَ فيها}؛ أي: الجنة {كأساً}: وهو الإناء [المملوء] من خمرٍ ورحيقٍ. {كان مِزاجُها}؛ أي: خلطها {زنجبيلاً}: ليطيب طعمُه وريحُه. {عيناً فيها}؛ [أي: في الجنة] {تسمّى سَلْسَبيلاً}: سمِّيت بذلك لسلاستها ولذَّتها وحسنها.
{17 - 18} "Na humo watanyweshwa" katika "kikombe" [kilichojaa] mvinyo safi zaidi "kilicho changanyika na tangawizi" ili kuifanya ladha na harufu yake kuwa nzuri. "Hiyo ni chemchemi iliyo humo." [Yaani, Peponi] "inaitwa Salsabil," iliitwa hivyo kwa sababu ya ulaini wake, ladha yake na uzuri wake.
#
{19} {ويطوفُ}: على أهل الجنة في طعامهم وشرابهم وخدمتهم، {ولدانٌ مخلَّدون}؛ أي: خلقوا من الجنة للبقاء؛ لا يتغيَّرون ولا يكبرون، وهم في غاية الحسن، {إذا رأيتَهم}: منتشرين في خدمتهم، {حسبتَهم}: من حسنهم {لؤلؤاً منثوراً}: وهذا من تمام لذَّة أهل الجنة؛ أن يكون خُدَّامُهم الولدان المخلَّدون، الذين تَسُرُّ رؤيتُهم، ويدخُلون في مساكنهم آمنين من تَبِعَتِهِم، ويأتونَهم بما يدَّعون وتطلُبُه نفوسُهم.
{19} "Na watawazungukia" wakazi wa Peponi katika vyakula vyao, na vinywaji vyao, na utumishi wao "wavulana wasiopevuka" kwa maana waliumbwa huko Peponi waishi milele. Hawabadiliki wala hawakui wakubwa, na ni uzuri wa kiwango cha juu zaidi. "Ukiwaona" wakienea katika utumishi wao "utawafikiri" kwa sababu ya uzuri wao kwamba ni "lulu zilizo tawanywa." Na hili ni katika jambo la kutimiza starehe ya wakazi wa Peponi; kwamba watumishi wao wawe wavulana wanaoishi milele, ambao wanafurahisha kuwatazama, na wataingia majumbani mwao wakiwa salama kutokana na lawama yoyote, na watawaletea yale wanayoyaitisha na kutakiwa na nafsi zao.
#
{20} {وإذا رأيتَ ثَمَّ}؛ أي: رمقتَ ما أهل الجنة عليه من النعيم الكامل، {رأيتَ نعيماً وملكاً كبيراً}: فتجد الواحد منهم عنده من [القصور و] المساكن والغرف المزيَّنة المزخرفة ما لا يدرِكُه الوصفُ، ولديه من البساتين الزاهرة والثِّمار الدَّانية والفواكه اللَّذيذة والأنهار الجارية والرِّياض المعجِبَة والطُّيور المطربة المُشْجِيَة، ما يأخُذُ بالقلوب ويُفْرِحُ النفوس، وعنده من الزَّوْجاتِ اللاَّتي هنَّ في غاية الحسن والإحسان الجامعات لجمال الظاهر والباطن الخَيِّراتِ الحسانِ، ما يملأ القلبَ سروراً ولذَّةً وحبوراً، وحوله من الوِلْدان المخلَّدين والخدم المؤبَّدين ما به تحصل الراحة والطُّمأنينة، وتتمُّ لَذَّة العيش وتكمل الغِبطة، ثم علاوة ذلك ومعظمه الفوز برضا الربِّ الرحيم وسماع خطابه ولَذَّة قربه والابتهاج برضاه والخلود الدائم، وتزايد ما هم فيه من النعيم كلَّ وقتٍ وحينٍ؛ فسبحان المالك الملك الحقِّ المُبين، الذي لا تَنْفَدُ خزائنُه ولا يقلُّ خيرُه؛ كما لا نهاية لأوصافِهِ؛ فلا نهايةَ لبرِّه وإحسانه.
{20} "Na utakapoyaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa." Utakuta kwamba kila mmoja wao anayo [makasri na] maskani na vyumba vilivyopambwa na visivyoelezeka, na pia ana bustani nzuri matunda yanayoning'inia chini, matamu, mito itiririkayo, makonde ya ajabu, na ndege waimbao kwa uzuri mkubwa, yale yanayoteka nyoyo na kuzifurahisha nafsi, na pia atakuwa na wake walio wazuri mno na wema, wanaokusanya uzuri wa nje na wa ndani, yale yanayoujaza moyo furaha, raha na starehe kubwa, na kandoni mwake kutakuwa na watoto wasiokufa na watumishi wa kudumu milele, ambao kwao faraja na utulivu itapatikana, na raha na furaha kubwa ya maisha itakamilika. Kisha juu zaidi ya hayo, na kubwa yake zaidi ni kupata radhi za Mola Mwingi wa rehema, kusikia mazungumzo yake, raha ya kuwa karibu naye, kufurahia radhi zake na kuishi milele daima, na pia kuongezeka kwa neema waliyo ndani yake kila wakati. Basi ametakasika Mwenye kumiliki, Mfalme wa Haki, Aliye Wazi, ambaye hazina zake haziishi, na ambaye wema wake haupungui. Na kama vile hakuna mwisho wa sifa zake, hakuna mwisho wa wema na hisani yake.
#
{21} {عاليهم ثيابُ سندسٍ خضرٌ}؛ أي: قد جلَّلتهم ثياب السندس والإستبرق الأخضران اللَّذان هما أجلُّ أنواع الحرير، فالسُّندس ما غلظ من الحرير، والإستبرقُ ما رقَّ منه، {وحُلُّوا أساوِرَ من فضَّةٍ}؛ أي: حُلُّوا في أيديهم أساور الفضَّة؛ ذكورهم وإناثهم. وهذا وعدٌ وَعَدَهم الله، وكان وعدُه مفعولاً؛ لأنَّه لا أصدق منه قيلاً ولا حديثاً. وقوله: {وسقاهم ربُّهم شراباً طهوراً}؛ أي: لا كدر فيه بوجهٍ من الوجوه، مطهراً لما في بطونهم من كلِّ أذىً وقذىً.
{21} "Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi" na hariri nzito, ambazo ndizo aina bora zaidi za hariri. "Na watavishwa vikuku vya fedha" wanaume na wanawake. Hii ni ahadi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaahidi, na ahadi yake lazima itatekelezeka. Kwa sababu hakuna aliye mkweli zaidi yake katika usemi na mazungumzo. Na kauli yake: "Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa." Yaani, hakina uchafu ndani yake kwa namna yoyote ile, na kitawatakasa yaliyomo matumboni mwao kutokana na madhara na uchafu wote.
#
{22} {[إنَّ] هذا}: الجزاء الجزيل [والعطاء الجميل] {كان لكم جزاءً}: على ما أسلَفْتموه من الأعمال، {وكان سعيُكم مشكوراً}؛ أي: القليل [منه] يجعل الله لكم به من النعيم [المقيم] ما لا يمكن حصره.
{22} "Hakika haya" malipo makubwa [na kipawa kizuri] hiki "ni malipo yenu" kwa yale mliyoyafanya hapo awali. "Na juhudi zenu zimekubaliwa." Yaani, juhudi zenu kidogo Mwenyezi Mungu amekupeni kwazo neema [ya kudumu] isiyohesabika.
#
{23} وقوله تعالى لما ذكر نعيم الجنة: {إنَّا نحن نزَّلْنا عليك القرآن تنزيلاً}: فيه الوعد والوعيد وبيانُ كلِّ ما يحتاجه العباد، وفيه الأمر بالقيام بأوامره وشرائعه أتمَّ القيام والسعي في تنفيذها والصبر على ذلك.
{23} Na kauli yake Mwenyezi Mungu alipotaja neema ya Peponi: "Hakika Sisi tumekuteremshia Qur-ani kidogo kidogo," ina ahadi nzuri na ahadi ya adhabu, na kubainisha kila jambo ambalo waja wanahitaji, na ina amri ya kutekeleza amri na sheria zake kamilifu zaidi na kujitahidi sana katika kuzitekeleza na kuwa na subira kwa hilo.
#
{24} ولهذا قال: {فاصبر لحكم ربِّكَ ولا تُطِعْ منهم آثماً أو كفوراً}؛ أي: اصبر لحكمه القدريِّ؛ فلا تسخطه، ولحكمه الدينيِّ؛ فامض عليه، ولا يعوقَنَّك عنه عائقٌ، {ولا تطعْ}: من المعاندين الذين يريدونَ أن يَصُدُّوك {آثماً}؛ أي: فاعلاً إثماً ومعصيةً، {ولا كفوراً}: فإنَّ طاعة الكفَّار والفجَّار والفسَّاق لا بدَّ أن تكون معصيةً لله ؛ فإنَّهم لا يأمرون إلاَّ بما تهواه أنفسهم.
{24} Ndiyo maana akasema: "Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru." Yaani, kuwa msubirifu kwa hukumu za mipango yake, na usikasirishwe nazo, na hukumu zake za kidini; kwa kuzitekeleza, na kamwe kisikuzuie mbali nazo kizuizi chochote. "Wala usimtii" katika wakaidi wanaotaka kukuzuia. "Wala mwenye kufuru" kwa maana utii kwa mwenye kufuru, mwovu, mvuka mipaka lazima ni uasi kwa Mwenyezi Mungu. Kwani wao hawaamrishi isipokuwa yale yanayotamaniwa na nafsi zao tu.
#
{25} ولما كان الصبر يُسْتَمَدُّ من القيام بطاعة الله والإكثار من ذِكْرِه؛ أمر الله بذلك، فقال: {واذكُرِ اسمَ ربِّك بكرةً وأصيلاً}؛ أي: أول النهار وآخره، فدخل في ذلك الصلوات المكتوبات، وما يتبعها من النَّوافل والذِّكْر والتَّسبيح والتَّهليل والتَّكبير في هذه الأوقات.
{25} Na kwa kuwa subira inatokana na kumtii Mwenyezi Mungu na kumkumbuka mara kwa mara; Mwenyezi Mungu akaamrisha hilo, akasema: "Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni." Yaani, mwanzo wa siku na mwisho wake, kwa hivyo hilo likajumuisha swala za faradhi, na swala za hiari zinazozifuata, dhikri, kumtakasa, kusema hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kumtukuza katika nyakati hizi.
#
{26} {ومن الليل فاسْجُدْ له}؛ أي: أكثر له من السُّجود، وذلك متضمِّن لكثرة الصلاة ، {وسبِّحْه ليلاً طويلاً}: وقد تقدَّم تقييد هذا المطلق بقوله: {يا أيُّها المزَّمِّلُ. قم الليلَ إلاَّ قليلاً. نِصْفَهُ أو انقُصْ منه قليلاً. أو زِدْ عليه ... }.
{26} "Na usiku msujudie Yeye." Na hilo linajumuisha kuswali kwa wingi, "na umtakase usiku, wakati mrefu." Na tayari agizo hili lililo wazi limeshafungiwa na kauli Yake: "Ewe uliyejifunika! Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! Nusu yake, au ipunguze kidogo. Au izidishe..."
#
{27} وقوله: {إنَّ هؤلاء}؛ أي: المكَذِّبين لك أيها الرسول بعدما بُيِّنَتْ لهم الآيات ورُغِّبوا ورُهِّبوا، ومع ذلك لم يُفِدْ فيهم ذلك شيئاً، بل لا يزالون يُؤْثرون {العاجلةَ}: ويطمئنُّون إليها، {ويذرونَ}؛ أي: يتركون العمل ويهملون {وراءهم}؛ أي: أمامهم {يوماً ثقيلاً}: وهو يوم القيامةِ، الذي مقداره خمسون ألفَ سنةٍ ممَّا تعدُّون، وقال تعالى: {يقولُ الكافرون هذا يومٌ عَسِرٌ}؛ فكأنَّهم ما خُلِقوا إلاَّ للدُّنيا والإقامة فيها.
{27} Na kauli yake: "Kwa hakika watu hawa;" yaani, wale waliokukadhibisha ewe Mtume, baada ya kubainishiwa Aya, na wakati wa moyo na wakaogopeshwa, lakini pamoja na hayo, hayo hayakuwafaa kitu. Bali bado wanapendelea "maisha ya kidunia" na wanatulizana juu yake "na wanaiacha nyuma yao siku nzito." Yaani, kwa kuacha kutenda matendo na kuyapuuza kwa ajili ya Siku ya Kiyama, ambayo urefu wake ni miaka hamsini elfu kama mnavyohesabu nyinyi, na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu." Na tena ni kama kwamba hawakuumbwa isipokuwa kwa ajili ya dunia hii na kudumu humo.
#
{28} ثم استدلَّ عليهم وعلى بعثهم بدليل عقليٍّ، وهو دليلُ الابتداء، فقال: {نحن خَلَقْناهم}؛ أي: أوجدناهم من العدم، {وشَدَدْنا أسْرَهم}؛ أي: أحكمنا خِلْقَتَهم بالأعصاب والعروق والأوتار والقُوى الظاهرة والباطنة، حتى تمَّ الجسم واستكمل وتمكَّن من كلِّ ما يريده؛ فالذي أوجدهم على هذه الحالة قادرٌ على أن يعيدَهم بعد موتهم لجزائهم، والذي نقَّلهم في هذه الدار إلى هذه الأطوار لا يَليقُ به أن يَتْرُكَهم سدىً، لا يُؤْمَرون، ولا يُنْهَوْن، ولا يُثابون، ولا يُعاقبون، ولهذا قال: {وإذا شِئْنا بَدَّلْنا أمثالَهم تَبْديلاً}؛ أي: أنشأناكم للبعث نشأةً أخرى، وأعدْناكم بأعيانكم، وهم بأنفسهم أمثالهم.
{28} Kisha akatumia ushahidi wa kiakili dhidi yao na wa kuunga mkono kufufuliwa kwao, nao ni ushahidi wa mwanzo wao, akasema: "Sisi tumewaumba" baada ya kutokuwepo kwenu "na tukavitia nguvu viungo vyao" kama vile mishipa ya fahamu, mishipa ya damu na nguvu zinazoonekana na zisizoonekana, mpaka mwili ukakamilika sawasawa na akaweza kufanya kila alitakalo. Kwa hivyo, aliyewaumba katika hali hii ana uwezo wa kuwarudisha baada ya kufa kwao na kuwalipa. Na aliyewapitisha katika nyumba hii katika awamu hizi zote haimfailii kuwaacha bure bila ya kuamrishwa kukatazwa wala kulipwa mazuri wala kuadhibiwa. Ndiyo maana akasema: "Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao." Yaani, tutawafufua kwa kwa ajili ya ufufuo kwa namna nyingine, na tukurudisheni nyinyi wenyewe hasa, na wao pia wenyewe hasa.
#
{29} {إنَّ هذه تذكرةٌ}؛ أي: يتذكَّر بها المؤمن، فينتفع بما فيها من التخويف والترغيب، {فمَن شاءَ اتَّخَذَ إلى ربِّه سَبيلاً}؛ أي: طريقاً موصلاً إليه؛ فالله يبيِّن الحقَّ والهدى، ثم يخيِّر الناس بين الاهتداء بها أو النُّفور عنها؛ إقامةً للحُجَّة ؛ ليهلكَ من هَلَكَ عن بيِّنةٍ، ويحيا من حيَّ عن بينةٍ.
{29} "Hakika huu ni ukumbusho" ambao Muumini anakumbushwa kwa huo na kunufaika kwa yaliyo ndani yake ya kuhofisha na pia ya kutia moyo. "Basi anayetaka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi" na kumfikisha huko. Kwani Mwenyezi Mungu huweka wazi haki na uwongofu, kisha huwapa watu chaguo kati ya kuongoka kwa hayo au kuyaacha. Ili hilo liwe ni kusimamisha hoja; ili mwenye kuangamia aangamie kwa ushahidi wa wazi, na mwenye kusalia hai asalie hai kwa ushahidi wa wazi.
#
{30} {وما تشاؤون إلاَّ أن يشاءَ اللهُ}: فإنَّ مشيئة الله نافذةٌ. {إنَّ الله كان عليماً حكيماً}: فله الحكمةُ في هداية المهتدي وإضلال الضالِّ.
{30} "Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu" kwani utashi wa Mwenyezi Mungu ndio wa kutekelezeka. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu, Mwenye hekima." Kwa maana ana hekima katika kuwaongoa wale walioongoka na kuwapoteza waliopotea.
#
{31} {يُدْخِلُ مَن يشاءُ في رحمتِهِ}: فيختصُّه بعنايته، ويوفِّقه لأسباب السعادة، ويهديه لطُرُقِها، {والظَّالمين}: الذين اختاروا الشقاء على الهدى، {أعدَّ لهم عذاباً أليماً}: بظلمهم وعدوانهم.
{31} "Humuingiza amtakaye katika rehema yake" kwa kumtunza kwa njia mahususi, na humuwezesha kufikia visababu vya kupata furaha, na humuongoza kwenye njia zake. "Na wenye kudhulumu" ambao walichagua upotofu badala ya uwongofu, "amewawekea adhabu iliyo chungu" kwa sababu ya dhuluma ya na kuvuka kwao mipaka.
Imekamilika tafsiri yake, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *