:
Tafsiri ya surat Al-Ma'arij
Tafsiri ya surat Al-Ma'arij
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 7 #
{سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ (1) لِلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ (2) مِنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ (3) تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ (4) فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا (5) إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا (6) وَنَرَاهُ قَرِيبًا (7)}.
1. Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. 2. Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia. 3. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. 4. Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka hamsini elfu! 5. Basi subiri kwa subira njema. 6. Hakika wao wanaiona iko mbali. 7. Na Sisi tunaiona iko karibu.
#
{1 - 4} يقول تعالى مبيِّناً لجهل المعاندين واستعجالهم لعذاب الله استهزاءً وتعنُّتاً وتعجيزاً: {سأل سائلٌ} أي: دعا داعٍ واستفتح مستفتح، {بعذابٍ واقعٍ للكافرينَ}: لاستحقاقهم له بكفرِهم وعنادِهم. {ليس له دافع من الله}؛ أي: ليس لهذا العذاب الذي استعجلَ به مَنِ استعجلَ من متمرِّدي المشركين أحدٌ يدفعه قبل نزوله أو يرفعه بعد نزوله، وهذا حين دعا النَّضْر بن الحارث القرشيُّ أو غيره من المكذِّبين ، فقال: {اللهمَّ إنْ كان هذا هو الحقَّ من عندِكَ فأمطِرْ علينا حجارةً من السماء أو ائتنا بعذابٍ أليم ... } [إلى آخر الآيات]؛ فالعذابُ لا بدَّ أن يقع عليهم من الله؛ فإمَّا أن يُعَجَّلَ لهم في الدُّنيا، وإمَّا أن يُدَّخَرَ لهم في الآخرة؛ فلو عرفوا الله وعرفوا عظمته وسعة سلطانه وكمال أسمائِهِ وصفاتِهِ؛ لما استعجلوا، ولاستسلموا وتأدَّبوا، ولهذا ذكر تعالى من عظمته ما يضادُّ أقوالهم القبيحة، فقال: {ذي المعارج. تَعْرُجُ الملائكةُ والرُّوح إليه}؛ أي: ذي العلوِّ والجلال والعظمة والتَّدبير لسائر الخلق، الذي تَعْرُجُ إليه الملائكة بما جعلها على تدبيره، وتَعْرُجُ إليه الرُّوح، وهذا اسم جنس يشمل الأرواح كلَّها؛ بَرَّها وفاجِرَها، وهذا عند الوفاة، فأمَّا الأبرار؛ فتعرج أرواحُهم إلى الله، فيؤذن لهم من سماءٍ إلى سماءٍ، حتى تنتهي إلى السماء التي فيها اللهُ عزَّ وجلَّ، فتحيي ربَّها وتسلِّم عليه وتحظى بقربه، وتبتهج بالدنوِّ منه، ويحصُلُ لها منه الثناء والإكرام والبرُّ والإعظام، وأمَّا أرواحُ الفجَّار؛ فتعرج، فإذا وصلت إلى السماء؛ استأذنتْ، فلا يؤذَنُ لها، وأعيدت إلى الأرض. ثم ذكر المسافةَ التي تَعْرُجُ فيها الملائكةُ والرُّوح إلى الله، وأنَّها تعرج في يوم بما يَسِّر لها من الأسباب وأعانها عليه من اللَّطافة والخفَّة وسرعة السير، مع أنَّ تلك المسافة على السير المعتاد مقدار خمسين ألف سنةٍ، من ابتداء العروج إلى وصولها ما حُدَّ لها، وما تنتهي إليه من الملأ الأعلى؛ فهذا المُلْك العظيم والعالم الكبير علويُّه وسفليُّه جميعه قد تولَّى خلقه وتدبيره العليُّ الأعلى، فعلم أحوالهم الظاهرة والباطنة، [وَعَلِمَ] مستقرَّهم ومستودَعَهم، وأوصلهم من رحمته وبرِّه وإحسانه ما عمَّهم وشَمَلَهم، وأجرى عليهم حكمه القدريَّ وحكمه الشرعيَّ وحكمه الجزائيَّ؛ فبؤساً لأقوام جهلوا عظمته ولم يقدروه حقَّ قدره، فاستعجلوا بالعذاب على وجه التعجيز والامتحان. وسبحان الحليم الذي أمهلهم وما أهملهم، وآذَوْه فصبر عليهم وعافاهم ورَزَقَهم! هذا أحدُ الاحتمالات في تفسير هذه الآية الكريمة، فيكون هذا العروجُ والصعودُ في الدنيا؛ لأنَّ السِّياق الأول يدلُّ عليه. ويُحتمل أنَّ هذا في يوم القيامةِ، وأنَّ الله [تبارك و] تعالى يظهِرُ لعباده في يوم القيامةِ من عظمته وجلاله وكبريائه، ما هو أكبر دليل على معرفتِهِ مما يشاهدونه من عروج الأملاك والأرواح، صاعدةً ونازلةً بالتدابير الإلهيّة والشؤون الربَّانيَّة في ذلك اليوم الذي مقداره خمسين ألف سنة من طوله وشدَّته، لكنَّ الله تعالى يخفِّفه على المؤمن.
{1 - 4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akielezea ujinga wa watu wenye ukaidi na kuharakisha kwao adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuifanyia kejeli, usugu, na kuona kwamba wanaweza kumshinda Mwenyezi Mungu: "Muulizaji aliuliz juu ya adhabu itakayotokea. Kwa makafiri " kwa sababu walistahiki kuipata kwa ukafiri wao na ukaidi wao. "ambayo hapana awezaye kuizuia" kabla ya kuteremka kwake au hata kuiondoa baada ya kushuka kwake. Haya yalikuwa wakati An-Nadhr bin Al-Harith Al-Qurashi au mwengineye miongoni mwa wakaidi alipoomba: "Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo kwako basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu..." hadi mwisho wa aya hizi. Lakini adhabu hii ni lazima itawapata kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ima wataharakishiwa katika dunia hii, au wataekewa waipate huko Akhera. Na lau wangemjua Mwenyezi Mungu na kujua ukuu wake, upana wa mamlaka yake, na ukamilifu wa majina na sifa zake, basi hawangeharakisha, na wangejisalimisha kwake na wakawa na adabu ipasayo, ndiyo maana Mola Mtukufu akataja katika utukufu wake yale yanayopingana na hayo maneno yao machafu, akasema: "Mwenye mbingu za daraja. Malaika na Roho hupanda kwenda kwake." Yaani: Mwenye ujuu, utukufu, ukuu, na uendeshaji wa viumbe vyote, ambaye Malaika hupanda kwake kutokana na yale aliyoyawekea kusimamia, na pia Roho hupanda kwake. Na jina hili ni jina jumuishi linalojumuisha roho zote; njema na ovu, na hili huwa wakati wa kufa. Ama walio wema, roho zao hupanda kwa Mwenyezi Mungu, na huwapa idhini ya kupita kutoka mbingu kwenda mbingu nyingine, mpaka zifike katika mbingu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu yuko huko, kisha zinamsalimu Mola wao Mlezi na ninapata fursa ya kuwa karibu naye na kufurahia hilo, kisha zinasifiwa, kutukuzwa, kuwanyiwa wema na kuheshimiwa. Na ama zilizo ovu, hizo hupanda, na zinapofika katika mbingu ya kwanza, zinaomba idhini ya kuingia, lakini haziruhusiwi, kisha zinarudishwa katika ardhi. Kisha akataja umbali ambao Malaika na Roho hupanda ndani yake wakienda kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba wao hupanda katika siku moja kwa sababu ya jinsi alivyowarahisishia na kuwasaidia kuwa wepesi na wa mwendo wa kasi kubwa sana, pamoja na kwamba umbali huu katika safari ya kawaida ni sawa na miaka elfu hamsini, tangu mwanzo wa kupaa hadi kufika kwao pale kwenye kiwango walichowekewa, na pale wanapofikia katika viumbe watukufu wa juu zaidi. Basi ufalme huu mkuu na ulimwengu mkubwa, wa juu wake wote na wa chini wake wote anausimamia Mtukufu aliye juu zaidi. Anazijua hali zao za dhahiri na zilizofichikana, [na anajua] pahali pa kutulia na pa kupita njia, na anawafikishia rehema zake, wema wake na ihsani yake, ambavyo vinawajumuisha wote, na akatekeleza juu yao hukumu yake kulingana na mipango yake, hukumu yake ya kisheria na hukumu yake ya kimalipo. Basi wana taabu wale ambao hawakujua ukuu wake na hawakumheshimu kama alivyostahili, kwa hivyo wakaharakisha adhabu kwa njia ambayo walimfanya Mwenyezi Mungu kwamba hana uwezo na kumjaribu tu. Na ametakasika, Mwingi wa ustahamilivu, ambaye aliwapa muhula na hakuwapuuza, na wakamuudhi, lakini akawafanyia subira, akawapa salama na akawaruzuku! Huu ni uwezekano mmojawapo katika kufasiri Aya hii tukufu. Kwa hivyo kupanda huku kunakuwa ni duniani, kwa sababu muktadha wa kwanza unalionyesha hilo. Na inawezekana kwamba hii ni Siku ya Kiyama, na kwamba Mwenyezi Mungu [Mwenye baraka nyingi] Mtukufu atawadhihirishia waja wake Siku ya Kiyama ukuu wake, utukufu wake na ukubwa wake, ambavyo vitakuwa ni ushahidi mkubwa zaidi juu ya kujua kwake kutokana na watakayoyaona miongoni mwa kupanda kwa Malaika na roho, kupanda na kushuka kulingana na mipango ya Mwenyezi Mungu siku hiyo, ambayo kipimo chake ni miaka elfu hamsini kwa sababu ya urefu wake na ukali wake, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ataihafifisha kwa Muumini.
#
{5 - 7} وقوله: {فاصْبِرْ صبراً جميلاً}؛ أي: اصبر على دعوتك لقومك صبراً جميلاً، لا تَضَجُّرَ فيه ولا ملل، بل استمرَّ على أمر الله، وادعُ عباده إلى توحيده، ولا يمنعْك عنهم ما ترى من عدم انقيادهم وعدم رغبتهم؛ فإنَّ في الصَّبر على ذلك خيراً كثيراً. {إنَّهم يرونَه بعيداً ونراه قريباً}: الضمير يعود إلى البعث الذي فيه عذابُ السائلين بالعذاب؛ أي: إنَّ حالهم حال المنكر له، والذي غلبت عليه الشِّقْوة والسكرة، حتى تباعد جميع ما أمامه من البعث والنشور، والله يراه قريباً؛ لأنَّه رفيقٌ حليمٌ لا يَعْجَلُ، ويعلم أنَّه لا بدَّ أن يكون، و [كلُّ] ما هو آتٍ فهو قريبٌ.
{5 - 7} Na kauli yake: "Basi subiri kwa subira njema" juu ya wito wako kwa watu wako bila ya kulalamika wala kuchoka. Bali endelea na amri ya Mwenyezi Mungu, na waite waja wake kumpwekesha, wala kisikuzuie kile unachokiona cha kukosa kwao utii na kutotaka kwao. Kwani kuna mazuri mengi katika kuwa na subira juu ya hilo. "Hakika wao wanaiona iko mbali. Na Sisi tunaiona iko karibu." Hapa kinachokusudiwa ni ufufuo ambamo ndani yake kuna adhabu ya hao wanaoomba adhabu. Yaani, hali yao ni hali ya mwenye kukanusha hilo, na ni hali ya yule aliyeshindwa na upotofu na ulevi, mpaka yaliyo mbele yake ya kufufuliwa na kutawanyika yakamuwiya mbali mno, ilhali Mwenyezi Mungu anayaona kuwa yako karibu mno. Kwa sababu Yeye ni Mpole, Mstahamilivu, na anajua kwamba ni lazima yatatokea, na [kila] kinachokuja, kiko karibu.
Kisha akataja mahangaiko ya siku hiyo na yale yatakayotokea ndani yake, akasema:
: 8 - 18 #
{يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ (8) وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ (9) وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا (10) يُبَصَّرُونَهُمْ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ (11) وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ (12) وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ (13) وَمَنْ فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنْجِيهِ (14) كَلَّا إِنَّهَا لَظَى (15) نَزَّاعَةً لِلشَّوَى (16) تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّى (17) وَجَمَعَ فَأَوْعَى (18)}.
8. Siku ambayo mbingu zitakapokuwa kama maadeni iliyoyayushwa. 9. Na milima itakuwa kama sufi. 10. Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. 11. Ijapokuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe. 12. Na mkewe, na nduguye. 13. Na jamaa zake waliokuwa wakimkimu, 14. Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. 15. La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, 16. Unaobambua ngozi ya kichwa! 17. Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka. 18. Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
#
{8 - 9} أي: {يوم} القيامة تقع فيه هذه الأمور العظيمة {تكونُ السماءُ كالمُهْل}: وهو الرصاص المذاب من تشقُّقها وبلوغ الهول منها كلَّ مبلغ، {وتكونُ الجبالُ كالعِهْن}: وهو الصوف المنفوش، ثم تكون بعد ذلك هباءً منثوراً فتضمحلُّ.
{8 - 9} "Siku" yaani siku ya Kiyama ambayo yatatokea mambo makubwa haya, "mbingu zitakapokuwa kama maadeni iliyoyayushwa" kutokana na kupasuka kwake na kufikiwa na balaa kubwa zaidi. "Na milima itakuwa kama sufi." Kisha baada ya hilo vitakuwa kama mavumbi yaliyotawanywa na kupotelea mbali.
#
{10 - 14} فإذا كان هذا الانزعاج والقلق لهذه الأجرام الكبيرة الشديدة؛ فما ظنُّك بالعبد الضعيف الذي قد أثقل ظهره بالذنوب والأوزار؟! أليس حقيقياً أن ينخلِعَ قلبُه و [ينزعجَ] لبُّه ويذهلَ عن كلِّ أحدٍ؟! ولهذا قال: {ولا يسألُ حميمٌ حميماً يُبَصِّرونَهم}؛ أي: يشاهدُ الحميمُ - وهو القريب - حميمَه؛ فلا يبقى في قلبه متَّسع لسؤاله عن حاله ولا فيما يتعلَّق بعشرتهم ومودَّتهم ولا يهمُّه إلاَّ نفسُه. {يودُّ المجرِمُ}: الذي حقَّ عليه العذاب {لو يفتدي من عذاب يومِئِذٍ ببنيهِ. وصاحبتِهِ}؛ أي: زوجته، {وأخيه. وفصيلته}؛ أي: قرابته، {التي تُؤْويه}؛ أي: التي جرت عادتها في الدنيا أن تتناصَرَ ويعينَ بعضها بعضاً؛ ففي [يوم] القيامةِ لا ينفع أحدٌ أحداً، ولا يشفع أحدٌ إلاَّ بإذن الله، بل لو يفتدي المجرمُ المستحقُّ للعذاب بجميع ما في الأرض ثم ينجيه ذلك؛ لم ينفعه.
{10 - 14} Ikiwa usumbufu na wasiwasi huu utaipata miili hii mikubwa, migumu, basi je, unamwonaje mja dhaifu ambaye ameuelemesha mgongo wake kwa madhambi na mizigo? Je, si kweli kwamba unafailia zaidi moyo wake kukatikakatika [kusumbukana mno], na kujitenga mbali na kila mtu? Ndiyo maana akasema: "Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. Ijapokuwa wataonyeshwa waonane." Lakini hakutakuwa na nafasi iliyobaki moyoni mwake kumuuliza kuhusu hali yake au ni nini kinachohusiana na usuhuba wao na mapenzi yao, na hatajali isipokuwa yeye mwenyewe tu. "Atatamani mkosefu" ambaye alistahiki kuadhibiwa angependa "lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe. Na mkewe, na nduguye. Na jamaa zake waliokuwa wakimhifadhi" na kusaidiana wao kwa wao. Lakini siku ya Kiyama, hakuna atakayemnufaisha mwingine, na hakuna atakaemfayia uombezi mwingine isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Bali hata kama mhalifu anayestahili adhabu angejifidia kwa mali zote za duniani ili ajikomboe kutokana na adhabu kisha aokoke yeye, hilo halitamnufaisha kitu.
#
{15 - 18} {كلاَّ}؛ أي: لا حيلة ولا مناص لهم، قد حقَّت عليهم كلمةُ ربِّك ، وذهب نفعُ الأقارب والأصدقاء، {إنَّها لظى. نزاعةً للشَّوى}؛ أي: النار التي تتلظَّى تنزِعُ من شدَّتها للأعضاء الظاهرة والباطنة ، {تَدْعو}: إلى نفسها - {مَنْ أدْبَرَ وتَوَلَّى. وجَمَعَ فأوْعى}؛ أي: أدبر عن اتِّباع الحقِّ، وأعرض عنه؛ فلا غرض له فيه ، وجمع الأموال بعضها فوق بعض، وأوعاها فلم ينفِقْ منها ما ينفعه ويدفع عنه النار؛ فالنار تدعو هؤلاء إلى نفسها ، وتستعدُّ للالتهاب بهم.
{15 - 18} "La!" Yaani, hakuna hila wala pahali pa kukimbilia, kwani neno la Mola wako Mlezi limeshawafikia, na manufaa ya jamaa na marafiki yametoweka pia. "Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa. Unaombabua ngozi ya kichwa" na viungo vinginevyo vinavyoonekana na vilivyofichikana. "Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka" na akaacha haki. "Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi" bila ya kutoa chochote kwayo kile ambacho kingemfaa au kumkinga kutokana na Moto. Basi Moto huo unawaita watu hawa kuuendea, na unajitayarisha kuwaunguza.
: 19 - 35 #
{إِنَّ الْإِنْسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا (19) إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا (20) وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا (21) إِلَّا الْمُصَلِّينَ (22) الَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ (23) وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَعْلُومٌ (24) لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ (25) وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ (26) وَالَّذِينَ هُمْ مِنْ عَذَابِ رَبِّهِمْ مُشْفِقُونَ (27) إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ (28) وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ (29) إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ (30) فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاءَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ (31) وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ (32) وَالَّذِينَ هُمْ بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ (33) وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ (34) أُولَئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُكْرَمُونَ (35)}.
19. Hakika mtu ameumbwa na papara. 20. Inapomgusa shari hupapatika. 21. Na inapomgusa kheri huizuilia. 22. Isipokuwa wanaosali, 23. Ambao wanadumisha Sala zao, 24. Na ambao katika mali yao iko haki maalumu. 25. Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba; 26. Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo. 27. Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. 28. Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. 29. Na ambao wanahifadhi tupu zao. 30. Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi. 31. Lakini wanaotaka kinyume cha haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka. 32. Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, 33. Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, 34. Na ambao wanazihifadhi Sala zao. 35. Hao ndio watakaoheshimiwa Peponi.
#
{19 - 21} وهذا الوصف للإنسان من حيث هو؛ ووَصَفَ طبيعتَه [الأصليةَ] أنَّه هلوعٌ، وفسَّر الهَلوعَ بقوله: {إذا مسَّه الشَّرُّ جزوعاً}: فيجزع إن أصابه فقرٌ أو مرضٌ أو ذهابُ محبوبٍ له من مال أو أهل أو ولدٍ، ولا يستعمل في ذلك الصبر والرِّضا بما قضى الله، {وإذا مسَّه الخير منوعاً}: فلا يُنْفِقُ مما آتاه الله، ولا يشكر الله على نعمه وبرِّه فيجزع في الضَّراء ويمنع في السَّراء.
{19 - 21} Haya ni maelezo ya mwanadamu jinsi alivyo; ameielezea hali yake [ya asili] kuwa ni mwenye papara, na akaeleza papara hiyo kwa kusema: "Inapomgusa shari hupapatika." Huingiwa na papara iwapo utampata umasikini au maradhi, au kutoweka kwa mpendwa kama vile mali zake, familia, au mtoto, na wala hafanyi subira na kutosheka kwa yale aliyoyaandikia Mwenyezi Mungu katika hayo. "Na inapomgusa kheri huizuilia." Hatoi katika alichompa Mwenyezi Mungu, wala hamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na wema wake. Yeye hufanya papara wakati wa shida na hunyimana katika nyakati nzuri.
#
{22 - 23} {إلاَّ المصلِّين}: الموصوفين بتلك الأوصاف؛ فإنَّهم إذا مسَّهم الخير؛ شكروا الله وأنفقوا مما خوَّلهم [الله]، وإذا مسَّهم الشرُّ؛ صبروا واحتسبوا. وقوله في وصفهم: {الذين هم على صلاتهم دائمونَ}؛ أي: مداومون عليها في أوقاتها بشروطها ومكمِّلاتها، وليسوا كمن لا يفعلها، أو يفعلها وقتاً دون وقتٍ، أو يفعلها على وجهٍ ناقص.
{22 - 23} "Isipokuwa wanaosali" wale walioelezwa kwa maelezo hayo; ikiwa wema utawagusa; wanamshukuru Mwenyezi Mungu na wakatoa katika yale aliyowaruzuku. Na unapowafikia ubaya, wao huwa na subira na kutarajia malipo. Na kauli yake katika kuwaeleza: "Ambao wanadumisha Sala zao" kwa wakati wake uliowekwa, pamoja na masharti yake na vyote vya kuikamilisha, na si kama mtu asiyeifanya, au anayeifanya kwa wakati fulani tu, au kuifanya kwa njia pungufu.
#
{24 - 25} {والذين في أموالهم حقٌّ معلومٌ}: من زكاة وصدقة، {للسائل}: الذي يتعرَّض للسؤال، {والمحروم}: وهو المسكين الذي لا يسألُ الناس فيعطوه ولا يفطنُ له فيتصدَّق عليه.
{24 - 25} "Na ambao katika mali yao iko haki maalumu" kama vile Zaka na sadaka. Kwa mwenye kuomba na anayejizuilia kuomba" ambaye hata hapewi sadaka.
#
{26} {والذين يصدِّقون بيوم الدين}؛ أي: يؤمنون بما أخبر به وأخبرت به الرسلُ من الجزاء والبعث، ويتيقَّنون ذلك، فيستعدُّون للآخرة، ويَسْعَوْن لها سعيها. والتصديق بيوم الدين يلزم منه التصديق بالرسل وبما جاؤوا به من الكتب.
{26} "Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo." Yaani, wanaamini yale waliyoambiwa na Mitume ya malipo na ufufuo, na wana yakini nayo, kwa hivyo wanajitayarisha kwa ajili ya Akhera, na wanaifanyia bidii ipasavyo. Na kusadiki Siku ya Kiyama kunahitaji kuwasadiki Mitume na vitabu walivyokuja navyo.
#
{27 - 28} {والذين هم من عذاب ربِّهم مشفِقون}؛ أي: خائفون وجِلون، فيتركون لذلك كلَّ ما يقرِّبهم من عذاب الله. {إنَّ عذاب ربِّهم غيرُ مأمونٍ}؛ أي: هو العذاب الذي يُخشى ويُحذر.
{27 - 28} "Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi." Kwa hivyo wanaacha kwa sababu ya hilo kila kitu ambacho kitawaleta karibu na adhabu ya Mwenyezi Mungu. "Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo." Kwa hivyo inapasa kuogopewa na kujitahadharisha nayo.
#
{29 - 31} {والذين هم لفروجهم حافظون}: فلا يطؤون بها وطئاً محرماً من زنا أو لواطٍ أو وطءٍ في دُبُرٍ أو حيضٍ ونحو ذلك، ويحفظونها أيضاً من النظر إليها ومسِّها ممَّن لا يجوز له ذلك، ويتركون أيضاً وسائل المحرَّمات الداعية لفعل الفاحشة، {إلا على أزواجهم أو ما ملكتْ أيمانُهم}؛ أي: سُرِّيَّاتهم، {فإنَّهم غير ملومين}: في وطئهنَّ في المحلِّ الذي هو محلُّ الحرثِ. {فمنِ ابتغى وراء ذلك}؛ أي: غير الزوجة وملك اليمين، {فأولئك هم العادون}؛ أي: المتجاوزون ما أحل الله إلى ما حرم الله. ودلَّت هذه الآية على تحريم نكاح المتعة؛ لكونها غير زوجةٍ مقصودةٍ ولا ملك يمينٍ.
{29 - 31} "Na ambao wanahifadhi tupu zao." Kwa hivyo, hawaziingizi katika tendo la ndoa la haramu, kama vile zinaa, kulawiti, kujamiiana katika njia ya haja kubwa, au katika hedhi na mfano wake, na pia wanazilinda asimwangalie au kumgusa yule ambaye hairuhusiwi kwake kufanya hivyo, na pia wanaziacha njia zilizoharamishwa zinazoitia kufanya uchafu, "isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume" yaani masuria wao. "Basi hao hawalaumiwi" kwa kujamiiana nao katika mahali panaporuhusiwa. "Lakini wanaotaka kinyume cha haya;" yaani, mwenye kutafuta asiyekuwa mkewe au masuria wake, "basi hao ndio wanaoruka mipaka" ya yale aliyoyaruhusu Mwenyezi Mungu na wakaingia katika yale aliyoharamisha. Aya hii inaashiria kuharamishwa kwa ndoa ya muda (Mut'a). Kwa sababu yeye hakukusudiwa kuoelewa na kukaa naye kama mke wala si suria aliyemilikiwa na mkono wake wa kulia.
#
{32} {والذين هم لأماناتهم وعهدِهِم راعونَ}؛ أي: مراعون لها حافظون مجتهدون على أدائها والوفاء بها، وهذا شاملٌ لجميع الأمانات التي بين العبد وبين ربِّه؛ كالتكاليف السِّرِّيَّة التي لا يطَّلع عليها إلاَّ اللهُ، والأمانات التي بيْن العبد وبيْن الخلق في الأموال والأسرار، وكذلك العهد شاملٌ للعهد الذي عاهد عليه الله، والعهد الذي عاهد الخلق عليه ؛ فإنَّ العهد يُسأل عنه العبد؛ هل قام به ووفَّاه أم رفضه وخانه فلم يقم به.
{32} "Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao" na wana bidii katika kuzitekeleza kikamilifu. Hili linajumuisha amana zote zilizo baina ya mja na Mola wake Mlezi, kama vile majukumu ya kisiri ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeyajua tu, na amana zilizoko baina ya mja na viumbe kuhusiana na mali na siri mbalimbali. Na agano linajumuisha agano ambalo alimpa Mweyezi Mungu na agano alilowapa viumbe. Kwa maana, mja ataulizwa juu ya agano, je alilitimiza kikamilifu au alilikataa na akalifanyia uhaini na akaacha kulitekeleza?
#
{33} {والذين هم بشهادتهم قائمونَ}؛ أي: لا يشهدون إلاَّ بما يعلمونه من غير زيادةٍ ولا نقصٍ ولا كتمانٍ، ولا يحابي فيها قريباً ولا صديقاً ونحوه، ويكون القصد بإقامتها وجه الله؛ قال تعالى: {وأقيموا الشهادةَ لله}، {يا أيُّها الذين آمنوا كونوا قوَّامينَ بالقِسطِ شهداءَ لله ولو على أنفسِكُم أوِ الوالِدَيْن والأقربين}.
{33} "Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao." Yaani, wanashuhudia tu yale wanayoyajua, bila ya kuongeza, kupunguza, wala kuficha, na wala hawampendelei katika hilo jamaa, rafiki wala mfano wa hao, na makusudio yao katika kuufanya ni kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Na akasema "Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha mno uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu."
#
{34} {والذين هم على صلاتهم يحافظون}: بالمداومة عليها على أكمل الوجوه.
{34} "Na ambao wanazihifadhi Sala zao" kwa kudumu katika hilo kwa njia kamilifu zaidi.
#
{35} {أولئك}؛ أي: الموصفون بتلك الصفات، {في جناتٍ مُكْرَمون}؛ أي: قد أوصل الله لهم من الكرامة والنعيم المقيم، ما تشتهيه الأنفس، وتلذُّ الأعين، وهم فيها خالدون. وحاصل هذا أنَّ الله وصف أهل السعادة والخير بهذه الأوصاف الكاملة والأخلاق المرضيَّة الفاضلة من العبادات البدنيَّة؛ كالصلاة والمداومة عليها، والأعمال القلبيَّة؛ كخشية الله الداعية لكلِّ خير، والعبادات الماليَّة، والعقائد النافعة، والأخلاق الفاضلة؛ ومعاملة الله ومعاملة خلقِهِ أحسن معاملةٍ؛ من إنصافهم وحفظ حقوقهم وأماناتهم والعفَّة التامَّة بحفظ الفروج عمَّا يكرهه الله تعالى.
{35} "Hao" walioelezewa kwa sifa hizo, "ndio watakaoheshimiwa Peponi." Yaani, Mwenyezi Mungu ameshawafikishia utukufu na neema ya milele, miongoni mwa yale ambayo nafsi zinayapenda na macho yanayafurahia, na wao watakaa humo milele. Jumla ya haya ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwaeleza watu wa furaha na wema kwa maelezo haya kamili na maadili ya kuridhisha na yaliyo bora kama vile ibada za kimwili, kama vile sala, kudumu katika kuitekeleza, na matendo ya kimoyo, kama vile kumcha Mwenyezi Mungu, ambako kunaitia katika wema wote, ibada za kimali, itikadi zenye manufaa, na kuamiliana na Mwenyezi Mungu na viumbe vyake kwa njia bora zaidi, kama vile kuwafanyia uadilifu, kuhifadhi haki zao na amana zao, na usafi kamili kwa kulinda sehemu za siri kutokana na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu Mtukufu.
: 36 - 39 #
{فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ (36) عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ (37) أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِنْهُمْ أَنْ يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ (38) كَلَّا إِنَّا خَلَقْنَاهُمْ مِمَّا يَعْلَمُونَ (39)}.
36. Wana nini wale waliokufuru wanakutumbulia macho tu? 37. Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! 38. Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? 39. La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua.
#
{36 - 39} يقول تعالى مبيناً اغترار الكافرين: {فمال الذين كَفَروا قِبَلَكَ مُهْطِعينَ}؛ أي: مسرعين، {عن اليمين وعن الشمال عِزينَ}؛ أي: قطعاً متفرِّقة وجماعاتٍ متنوِّعة ، كلٌّ منهم بما لديه فرحٌ. {أيطمعُ كلُّ امرئٍ منهم أن يُدْخَلَ جنَّةَ نعيم}؛ أيُّ سببٍ أطمعهم وهم لم يقدِّموا سوى الكفر والجحود لربِّ - العالمين؟! ولهذا قال: {كلاَّ}: أي: ليس الأمر بأمانيهم ولا إدراك ما يشتهون بقوَّتهم، {إنَّا خلَقْناهم ممَّا يعلمونَ}؛ أي: من ماء دافقٍ يخرج من بين الصُّلب والترائب؛ فهم ضعفاء لا يملكون لأنفسهم نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً.
{36 - 39} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akieleza kudanganyika kwa makafiri: "Wana nini wale waliokufuru wanakutumbulia macho tu?" Na pia ilisemwa kwamba maana yake ni wanakukimbilia. "Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!" Kila mmoja na furahia yale aliyo nayo. "Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema?" Ni sababu gani iliwapa matumaini hayo ilhali hawakutanguliza ila ukafiri na kukataa Mola Mlezi wa walimwengu wote? Ndiyo maana akasema: "La, hasha!" Mambo si hivyo tu kwa matamanio yao, wala hawawezi kupata wanayoyatamani kwa uwezo wao. "Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanachokijua." Yaani, kutokana na maji yatokayo kwa kuchupa. Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu." Kwa hivyo, wao ni dhaifu ambao hawawezi kujimilikia manufaa wala madhara, wala kifo, wala uzima, wala ufufuo.
: 40 - 44 #
{فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ (40) عَلَى أَنْ نُبَدِّلَ خَيْرًا مِنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ (41) فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّى يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ (42) يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَى نُصُبٍ يُوفِضُونَ (43) خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ذَلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ (44)}.
40. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza. 41. Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. 42. Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayoahidiwa, 43. Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, 44. Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyokuwa wakiahidiwa.
#
{40 - 41} هذا إقسامٌ منه تعالى بالمشارق والمغارب للشمس والقمر والكواكب؛ لما فيها من الآيات الباهرات على البعث وقدرته على تبديل أمثالهم وهم بأعيانهم؛ كما قال تعالى: {وننشِئُكم فيما لا تعلمونَ}. {وما نحنُ بمسبوقينَ}؛ أي: ما أحدٌ يسبقنا ويفوتنا ويعجِزُنا إذا أردنا أن نعيدَه.
{40 - 41} Huku ni kuapa kwake Yeye Mtukufu kwa mashariki na magharibi za jua, mwezi na nyota; kwa sababu ya ishara zenye kung'aa zilizo ndani yake kuhusiana na ufufuo na uwezo wake wa kuwabadili kwa mfano wao wenyewe, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilolijua." Na akasema "na Sisi hatushindwi" tukitaka kumrudisha.
#
{42} فإذا تقرَّر البعث والجزاء، واستمرُّوا على تكذيبهم وعدم انقيادهم لآيات الله؛ {فذَرْهم يخوضوا ويلعبوا}؛ أي: يخوضوا بالأقوال الباطلة والعقائد الفاسدة، ويلعبوا بدينهم، ويأكلوا ويشربوا ويتمتَّعوا، {حتَّى يلاقوا يومَهُمُ الذي يوعدونَ}: فإنَّ الله قد أعدَّ لهم فيه من النَّكال والوبال ما هو عاقبةُ خوضهم ولعبهم.
{42} Basi likishakuwa wazi suala la kufufuliwa na kulipwa, na wakaendelea katika kukanusha na kutotii kwao ishara za Mwenyezi Mungu. "Basi waache wapige porojo na wacheze" kwa maneno batili na itikadi potofu, na waichezee dini yao, na wale, na wanywe na wastarehe, "mpaka wakutane na siku yao wanayoahidiwa." Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia humo adhabu na balaa kubwa itakayokuwa matokeo ya kuzama kwao katika porojo na kucheza kwao.
#
{43 - 44} ثم ذكر حال الخلق حين يلاقون اليوم الذي يوعدون، فقال: {يوم يَخْرُجونَ من الأجداثِ}؛ أي: القبور {سراعاً}: مجيبين لدعوة الداعي مهطِعين إليها، {كأنَّهم إلى نُصُبٍ يوفِضونَ}؛ أي: كأنَّهم إلى علم يَؤُمُّون ويقصدون؛ فلا يتمكَّنون من الاستعصاء على الدَّاعي ولا الالتواء عن نداء المنادي ، بل يأتون أذلاَّء مقهورين للقيام بين يدي ربِّ العالمين، {خاشعةً أبصارُهم ترهَقُهم ذِلَّةٌ}: وذلك أنَّ الذِّلَّة والقلق قد ملك قلوبهم، واستولى على أفئدتهم، فخشعتْ منهم الأبصار، وسكنتِ [منهم] الحركاتُ، وانقطعت الأصوات. فهذه الحال والمآل هو يومهم {الذي كانوا يوعدون}: ولا بدَّ من الوفاء بوعد الله.
{43 - 44} Kisha akataja hali ya viumbe wanapokutana na siku waliyoahidiwa, akasema: "Siku watakapotoka makaburini kwa upesi" kwa kuitikia mwito wa mwitaji, kuyakimbilia, "kama kwamba wanakimbilia mfundo." Hawataweza kukataa kumwendea mwitaji huyo wala hata kukengeuka mbali naye. Bali wanakuja huku wamedhalilika na wametiishwa ili wasimame mbele ya Mola Mlezi wa walimwengu wote. "Macho yao yatainama, fedheha itawafunika." Haya ni kwa sababu ya unyonge na wasiwasi kubwa itakayokuwa imezitawala nyoyo zao na kuzitawala fahamu za nyoyo zao, kwa hivyo macho yao yakanyenyekea, harakati zao zikatulia, na sauti zao zikakatika. Hali hii na mwisho huu ndio siku yao "waliyokuwa wakiahidiwa." na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni lazima itimie.
Imekamilika na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.