:
Juzuu ya tatu ya Taysir Ar-Rahman fi Tafsir al-Qur-an, ya mkusanyaji wake, mhitaji kwa Mwenyezi Mungu, Abdur-Rahman bin Nassir bin Sa'adi, Mwenyezi Mungu amsamehe yeye na wazazi wake na Waislamu wote, na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Nabii wetu Muhammad na aali zake na maswahaba zake wote mpaka siku ya Qiyama.
Tafsiri ya Suratul-A'raaf
Tafsiri ya Suratul-A'raaf
Nayo iliteremka Makka
: 1 - 7 #
{المص (1) كِتَابٌ أُنْزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُنْ فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِنْهُ لِتُنْذِرَ بِهِ وَذِكْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ (2) اتَّبِعُوا مَا أُنْزِلَ إِلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ قَلِيلًا مَا تَذَكَّرُونَ (3) وَكَمْ مِنْ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ قَائِلُونَ (4) فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُمْ بَأْسُنَا إِلَّا أَنْ قَالُوا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ (5) فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ (6) فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِمْ بِعِلْمٍ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ (7)}.
1. Alif Laam Miim Swaad 2. Kitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake, ili uonye kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini. 3. Yafuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, wala msifuate marafiki wasaidizi wowote badala yake. Ni machache mnayoyakumbuka. 4. Na ni miji mingapi tuliyoiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipokuwa wamelala adhuhuri. 5. Basi haukuwa mwito wao wakati ilipowajia adhabu yetu, isipokuwa walisema, "Hakika sisi tulikuwa madhalimu." 6. Na hakika tutawauliza wale waliotumiwa Ujumbe, na pia hakika tutawauliza hao Wajumbe. 7. Tena hakika tutawasimulia kwa elimu. Wala Sisi si kwamba hatukuwepo.
#
{1 - 2} يقول تعالى لرسوله محمد - صلى الله عليه وسلم - مبيناً له عظمة القران: {كتابٌ أنْزِلَ إليك}؛ أي: كتابٌ جليلٌ حوى كلَّ ما يحتاج إليه العباد وجميع المطالب الإلهيَّة والمقاصد الشرعيَّة محكماً مفصلاً. فلا يكنْ في صدرِكَ منه {حَرَجٌ}؛ أي: ضيقٌ وشكٌّ واشتباهٌ، بل لتعلمْ أنه تنزيلٌ من حكيم حميد، لا يأتيه الباطل من بين يديه ولا من خلفه ، فلينشرِحْ له صدرُك، ولتطمئنَّ به نفسُك، ولْتصدعْ بأوامره ونواهيه، ولا تخش لائماً ومعارضاً؛ {لتنذرَ به}: الخلق وتَعِظهم وتذكِّرهم فتقوم الحجة على المعاندين، {و} ليكنْ {ذكرى للمؤمنينَ}؛ كما قال تعالى: {وذكِّرْ فإنَّ الذِّكرى تنفعُ المؤمنينَ}: يتذكَّرون به الصراط المستقيم، وأعماله الظاهرة والباطنة، وما يحول بين العبد وبين سلوكه.
{1 - 2} Yeye Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad-rehema na amani zimshukie- akimueleza utukufu wa Qur-ani: "Kitabu kilichoteremshwa kwako." Yaani, Kitabu kitukufu kilichokusanya kila kitu wanachohitaji waja, na matakwa yote ya Mwenyezi Mungu na malengo ya kisheria kwa njia sahihi na ya kina. Basi isiwe katika kifua chako kwa sababu yake "dhiki yoyote" yaani dhiki, na shaka na mchanganyiko. Bali ili ujue kuwa ni Ufunuo kutoka kwa Mwenye hekima kubwa, Msifiwa sana, hakijiwi na batili kwa mbele yake wala kwa nyuma yake. Basi na kikifungukie kifua chako, na nafsi yako itulizane kwacho, na yatangaze maamrisho yake na makatazo yake, wala usihofu lawama ya mwenye kulaumu na mpinzani. "Ili uonye kwacho" viumbe, na uwaaidhi, na uwakumbushe ili hoja isimame juu ya wakaidi, "na" ili iwe "ukumbusho kwa Waumini." Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na kumbusha. Kwani ukumbusho unawafaa Waumini." Wanaikumbuka kwa huo Njia iliyonyooka, na matendo yake yaliyo dhahiri na yaliyofichika, na yale yanayozuia kati ya mja na kuifuata.
#
{3} ثم خاطب الله العباد، ولفتهم إلى الكتاب، فقال: {اتَّبِعوا ما أنزِلَ إليكم من ربِّكم}؛ أي: الكتاب الذي أريد إنزاله لأجلكم، وهو {من ربِّكم}، الذي يريد أن يُتِمَّ تربيتَه لكم، فأنزل عليكم هذا الكتاب الذي إن اتبعتموه كملتْ تربيتُكم وتمَّتْ عليكم النعمةُ وهُديتم لأحسن الأعمال والأخلاق ومعاليها، {ولا تتَّبِعوا من دونِهِ أولياءَ}؛ أي: تتولَّونهم، وتتَّبعون أهواءهم، وتتركون لأجلها الحقَّ، {قليلاً ما تَذَكَّرونَ}: فلو تذكَّرتم وعرفتم المصلحة؛ لما آثرتُم الضارَّ على النافع والعدوَّ على الولي.
{3} Kisha Mwenyezi Mungu akawaongelesha waja, na akawaelekeza kwenye Kitabu, akasema, "Yafuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi;" yaani, Kitabu ambacho ninachotaka kukiteremsha kwa ajili yenu, nacho ni "kutoka kwa Mola wenu Mlezi" ambaye anataka kukamilisha malezi yake kwenu. Kwa hivyo akawateremshia kitabu hiki ambacho mkikifuata, basi malezi yenu yatakamilika malezi yenu na neema itatimia juu yenu, nanyi mtaongolewa kwenye matendo mazuri zaidi na maadili, na ya juu yake zaidi. "Wala msifuate marafiki wasaidizi wowote badala yake;" yaani, kwamba kuwafanya kuwa marafiki wasaidizi, na mkafuata matamanio yao, na mkaiacha haki kwa ajili yao. "Ni machache mnayoyakumbuka," kwa maana, lau mngelikumbuka na kujua manufaa, basi hamngeliyapendelea madhara kuliko manufaa, na adui kuliko rafiki msaidizi.
#
{4} ثم حذرهم عقوباته للأمم الذين كذبوا ما جاءتهم به رسلهم فلا يشابهوهم، فقال: {وكم من قريةٍ أهلكْناها فجاءها بأسُنا}؛ أي: عذابُنا الشديد، {بياتاً أو هم قائلونَ}؛ أي: في حين غفلتهم وعلى غِرَّتهم غافلون، لم يخطر الهلاكُ على قلوبهم، فحين جاءهم العذاب؛ لم يدفعوه عن أنفسهم، ولا أغنت عنهم آلهتهم التي كانوا يرجونهم، ولا أنكروا ما كانوا يفعلونه من الظلم والمعاصي.
{4} Kisha akawatahadharisha na adhabu zake kwa umma waliokadhibisha yale yaliyowajia nayo Mitume wao, ili wasifanane nao. Kwa hivyo Akasema, "Na ni miji mingapi tuliyoiangamiza, ikaifikia adhabu yetu." Yaani, adhabu yetu kali, "usiku au walipokuwa wamelala adhuhuri" Yaani wakati walipokuwa wameghafilika, na ya wao kujua huku wameghafilika, na wala maangamizo hayakuwa yamepitia katika nyoyo zao, basi ilipowajia adhabu. Hawakujikinga nayo. Basi adhabu ilipowajia, hawakuweza kuzizuia nafsi zao kutokana nayo, wala miungu yao waliyokuwa wakiitarajia haikuwafaa, wala hawakukataza yale waliyokuwa wakifanya miongoni mwa dhuluma na maasia.
#
{5} {فما كان دَعْواهم إذ جاءَهُم بأسُنا إلَّا أن قالوا إنا كنَّا ظالمينَ}؛ كما قال تعالى: {وكم قَصَمْنا من قريةٍ كانت ظالمةً وأنشأنا بعدَها قوماً آخرينَ. فلما أحسُّوا بأسَنا إذا هُم منها يركُضونَ. لا تركُضوا وارجِعوا إلى ما أُتْرِفْتُم فيه ومساكِنِكُم لعلَّكم تُسْألونَ. قالوا يا وَيْلنا إنَّا كنَّا ظالمينَ. فما زالتْ تلك دعواهُم حتَّى جَعَلْناهم حصيداً خامدينَ}.
{5} “Basi haukuwa mwito wao wakati ilipowajia adhabu yetu, isipokuwa walisema: Hakika sisi tulikuwa madhalimu.” Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na ni mingapi tumeiteketeza miongoni mwa miji iliyokuwa dhalimu, na tukawasimamisha baada yake kaumu wengine. Basi walipoihisi adhabu yetu, mara wakaanza kuikimbia. Msikimbie! Na rejeeni kwenye yale mliyostareheshwa ndani yake, na maskani yenu, ili mpate kuulizwa! Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu. Basi haukuacha huo ndio mwito wao mpaka tulipowafanya kama waliofyekwa wakazimika."
#
{6} وقوله: {فَلَنَسْأَلَنَّ الذين أرسِل إليهم}؛ أي: لنسألن الأمم الذين أرسل الله إليهم المرسلين عما أجابوا [به] رسلهم، {وَيَوْمَ يُناديهم فَيَقولُ ماذا أجبتُمُ المرسلينَ ... } الآيات، {وَلَنَسْأَلَنَّ المرسلينَ}: عن تبليغهم لرسالات ربِّهم وعما أجابتهم به أممهم.
{6} Na kauli yake, "Na hakika tutawauliza wale waliotumiwa Ujumbe, yaani, hakika tutawauliza umma wale aliowatumia Mwenyezi Mungu Mitume kuhusu yale waliyowajibu [kwayo] Mitume wao. "Na siku atakapowaita na aseme: Mliwajibu nini Mitume?...”} hadi mwisho wa Aya hizi. "Na pia hakika tutawauliza hao Wajumbe" kuhusu kufikisha kwao jumbe za Mola wao Mlezi, na kuhusu yale waliyowajibu kwayo Umma zao.
#
{7} {فَلَنَقُصَّنَّ عليهم}؛ أي: على الخلق كلهم ما عملوا، {بعلم}: منه تعالى لأعمالهم، {وما كُنا غائبينَ}: في وقت من الأوقات؛ كما قال تعالى: {أحصاه الله وَنَسُوه}، وقال تعالى: {ولقد خَلَقْنا فوقَكم سبعَ طرائقَ وما كُنَّا عن الخلق غافلين}.
{7} "Tena hakika tutawasimulia;" yaani, tutawasimulia viumbe wote yale waliyotenda "kwa elimu" kutoka kwake Yeye Mtukufu juu ya matendo yao. "Nasi hatukukosa kuwepo" katika wakati wowote miongoni mwa nyakati, kama alivyosema Yeye Mtukufu "Mwenyezi Mungu alimhisabu, lakini wao wakamsahau." Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kwa yakini tuliumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe."
Kisha akataja malipo ya matendo, akasema:
: 8 - 9 #
{وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (8) وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ (9)}
8. Na kipimo Siku hiyo kitakuwa kwa haki. Kwa hivyo yule ambaye vipimo vyake vitakuwa vizito, basi hao ndio waliofaulu. 9. Na yule ambaye vipimo vyake vitakuwa hafifu, basi hao ndio waliozihasirisha nafsi zao kwa sababu ya vile walivyokuwa wakizifanyia Ishara zetu udhalimu.
#
{8} أي: والوزن يوم القيامة يكون بالعدل والقسط الذي لا جَوْر فيه ولا ظلم بوجه. {فمن ثَقُلَتْ موازينُه}: بأن رَجَحَتْ كفةُ حسناته على سيئاته، {فأولئك هم المفلحونَ}؛ أي: الناجون من المكروه، المدركون للمحبوب، الذين حصل لهم الربح العظيم والسعادة الدائمة.
{8} Yaani, kipimo Siku ya Qiyama kitakuwa kwa usawa na uadilifu, ambao ndani yake hakuna dhuluma yoyote wala ukandamizaji. "Kwa hivyo yule ambaye vipimo vyake vitakuwa vizito" ya kwamba mizani ya mema yake iwe nzito kuliko mabaya yake, "basi hao ndio waliofaulu." Yaani, wale waliopita kutokana na machukizo, wale waliopata yapendwayo, wale waliopata faida kubwa na furaha ya kudumu.
#
{9} {ومن خفَّتْ موازينُه}: بأن رجحتْ سيئاتُه وصار الحكم لها، {فأولئك الذين خسروا أنفسهم}: إذ فاتهم النعيمُ المقيمُ وحصل لهم العذابُ الأليم، {بما كانوا بآياتِنا يَظْلِمونَ}: فلم ينقادوا لها كما يجبُ عليهم ذلك.
{9} "Na yule ambaye vipimo vyake vitakuwa hafifu" ya kwamba mabaya yake yalizidi katika uzito (mazuri yake), basi yakapewa hukumu, "basi hao ndio waliozihasirisha nafsi zao," kwa kuwa walikosa raha ya milele na wakapata adhabu chungu; "kwa sababu ya vile walivyokuwa wakizifanyia Ishara zetu udhalimu; kwani hawakuzinyenyekea kama inavyowalazimu kufanya hivyo.
: 10 #
{وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ قَلِيلًا مَا تَشْكُرُونَ (10)}
10. Na hakika tumewaimarisha katika dunia, na tukawajalia humo njia za kupatia maisha. Ni kidogo tu mnavyoshukuru.
#
{10} يقول تعالى ممتنًّا على عباده بذكر المسكن والمعيشة: {ولقد مكَّنَّاكم في الأرض}؛ أي: هيأناها لكم بحيث تتمكَّنون من البناء عليها وحرثها ووجوه الانتفاع بها، {وجَعَلْنا لكم فيها معايشَ}: مما يخرج من الأشجار والنبات ومعادن الأرض وأنواع الصنائع والتجارات؛ فإنه هو الذي هيَّأها وسخَّر أسبابها، {قليلاً ما تشكُرون}: الله الذي أنعم عليكم بأصناف النعم، وصَرَفَ عنكم النقم.
{10} Yeye Mtukufu anasema kwa kuwaambia waja wake neema zake juu yake kwa kutaja makazi na maisha: "Na hakika tumewaimarisha katika dunia." Yaani, tuliiandaa kwa ajili yenu kwa namna ambayo mnaweza kujenga juu yake, na kuilima, na njia zingenezo za kunufaika kwayo "na tukawajalia humo njia za kupatia maisha;" miongoni mwa vinavyotoka katika miti, na mimea, na madini ya ardhi, na aina mbalimbali za ufundi na biashara mbalimbali. Hakika Yeye ndiye aliyevitayarisha na akatiisha njia zake. "Ni kidogo tu mnavyoshukuru" Mwenyezi Mungu ambaye ndiye anayewaneemesha kwa neema mbalimbali, na akawaepushia adhabu mbalimbali.
: 11 - 15 #
{وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُنْ مِنَ السَّاجِدِينَ (11) قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِنْهُ خَلَقْتَنِي مِنْ نَارٍ وَخَلَقْتَهُ مِنْ طِينٍ (12) قَالَ فَاهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَنْ تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَاخْرُجْ إِنَّكَ مِنَ الصَّاغِرِينَ (13) قَالَ أَنْظِرْنِي إِلَى يَوْمِ يُبْعَثُونَ (14) قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنْظَرِينَ (15)}.
11. Na hakika tuliwaumba, kisha tukawatia sura, kisha tukawaambia Malaika, "Msujudieni Adam." Basi wakasujudu isipokuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa waliosujudu. 12. (Mwenyezi Mungu) akasema, "Ni nini kilichokuzuia kusujudu nilipokuamrisha?" Akasema, "Mimi ni bora zaidi kumliko yeye. Uliniumba kwa moto, naye ulimuumba kwa udongo." 13. Akasema, "Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni." 14. Akasema, "Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa." 15. Akasema, "Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula."
#
{11} يقول تعالى مخاطباً لبني آدم: {ولقد خَلَقْناكم}: بخلق أصلِكم ومادَّتكم التي منها خرجتُم؛ أبيكم آدم عليه السلام، {ثم صوَّرْناكم}: في أحسن صورة وأحسن تقويم، وعلَّمه [اللهُ] تعالى ما به تكمُلُ صورتُه الباطنةُ؛ أسماءَ كل شيء، ثم أمر الملائكة الكرام أن يسجُدوا لآدم إكراماً واحتراماً وإظهاراً لفضلِهِ، فامتثلوا أمر ربهم، {فَسَجدوا} كلُّهم أجمعون {إلا إبليس}: أبى أن يسجدَ له تكبُّراً عليه وإعجاباً بنفسه.
{11} Yeye Mtukufu Anasema akiwaongelesha wanadamu: "Na hakika tuliwaumba" kwa kuumba asili yenu na kiini chenu ambacho mlitoka kwacho; Baba yenu Adam, amani iwe juu yake. "Kisha tukawatia sura" kwa sura nzuri zaidi, na umbo bora zaidi. Na [Mwenyezi Mungu] Mtukufu akamfundisha yale ambayo kwayo umbo lake la ndani linakamilika; majina ya kila kitu. Kisha akawaamrisha Malaika watukufu kwamba wamsujudie Adam kwa kumuonyesha utukufu, na heshima, na kudhihirisha fadhila yake. Kwa hivyo wakaitekeleza amri ya Mola wao Mlezi, "Basi wakasujudu" wote pamoja "isipokuwa Iblisi" alikataa kumsujudia kwa kimfanyia kiburi na kwa kujiona bora.
#
{12} فوبَّخه الله على ذلك، وقال ما منعك أن تسجد لما خلقت بيديَّ أي شرفته وفضلته بهذه الفضيلة التي لم تكن لغيرِهِ، فعصيتَ أمري وتهاونت بي. {قال} إبليسُ معارضاً لربِّه: {أنا خيرٌ منه}، ثم برهن على هذه الدعوى الباطلة بقوله له: {خلَقْتَني من نارٍ وخلقتَهُ من طينٍ}: وموجب هذا أن المخلوق من نار أفضل من المخلوق من طين لعلوِّ النار على الطين وصعودها. وهذا القياس من أفسد الأقيسة؛ فإنه باطلٌ من عدة أوجه: منها: أنه في مقابلة أمر الله له بالسجود، والقياس إذا عارض النصَّ فإنه قياسٌ باطل؛ لأنَّ المقصود بالقياس أن يكون الحكم الذي لم يأت فيه نصٌّ يقارب الأمور المنصوص عليها ويكون تابعاً لها، فأما قياس يعارضها ويلزم من اعتباره إلغاء النصوص؛ فهذا القياس من أشنع الأقيسة. ومنها: أنَّ قولَه: {أنا خيرٌ منه}؛ بمجرَّدها كافية لنقص إبليس الخبيث؛ فإنَّه برهن على نقصه بإعجابه بنفسه وتكبُّره والقول على الله بلا علم، وأيُّ نقص أعظم من هذا؟! ومنها: أنه كَذَبَ في تفضيل مادة النار على مادة الطين والتراب؛ فإنَّ مادة الطين فيها الخشوعُ والسكونُ والرزانةُ، ومنها تظهر بركات الأرض من الأشجار وأنواع النبات على اختلاف أجناسه وأنواعه، وأما النار؛ ففيها الخفة والطيش والإحراق.
{12} Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamkemea kwa hilo, na akasema: “Ni nini kilichokuzuia kumsujudia yule niliyemuumba kwa mikono yangu?" Yaani, nilimtukuza na nikamfadhilisha kwa wema huu ambao hakuna yeyote mwingine aliwahi kuwa nao, basi ukaasi amri yangu, na ukanidharau Mimi. Iblis "akasema" akimpinga Mola wake Mlezi, "Mimi ni mbora zaidi kumliko yeye." Kisha akaweka ushahidi juu ya madai hayo batili kwa kumwambia: "Uliniumba kwa moto, naye ulimuumba kwa udongo." Na kinacholazimu kutokana na haya ni kuwa aliyeumbwa kwa moto ni bora zaidi kuliko aliyeumbwa kwa udongo kwa sababu ya ujuu wa moto kwa udongo na kunapanda kwake juu. Na Ulinganisho huu ni katika ulinganisho mbovu zaidi kwa sababu ni batili kwa njia kadhaa: Miongoni mwake ni kwamba, ni kwa njia ya kukabiliana na amri ya Mwenyezi Mungu alipomuamrisha kusujudu na ulinganisho unapopingana na andiko, basi ulinganisho huo ni batili. Kwa sababu kinachokusudiwa katika ulinganisho ni kwamba, hukumu ambayo halikuja andiko kuhusiana nayo ikaribiane na mambo yaliyokuja maandiko kuhusiana nayo, na yawe yanayafuata hayo. Ama ulinganisho unapingana nayo na kulazimu kwamba yakizingatiwa, maandiko yanafutiliwa mbali, basi ulinganisho huo ni katika ulinganisho mbaya zaidi. Na miongoni mwake ni kwamba, Kauli yake, "Mimi ni bora zaidi kumliko yeye" peke yake tu inatosha kupunguza Iblisi muovu. Kwa maana, ni ushahidi juu ya upungufu wake kwa sababu ya kujiona yeye mwenyewe kwake, na majivuno yake, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu bila elimu. Na ni upungufu gani ulio mkuu zaidi kuliko huu? Na miongoni mwake ni kwamba, alidanganya katika kuboresha kitu cha moto juu ya kitu cha udongo na mchanga. Kwa maana, udongo una unyenyekevu ndani yake, na utulivu, na unyoofu, na kutokana nao zinadhihirika baraka za ardhi miongoni mwa miti na aina za mimea ya kila namna na aina. Na ama moto, huo una wepesi ndani yake, na kupindukia mipaka, na kuchoma.
#
{13} ولهذا؛ لما جرى من إبليس ما جرى؛ انحطَّ من مرتبته العالية إلى أسفل السافلين، فقال الله له: اهبطْ {منها} أي: من الجنة، {فما يكونُ لك أن تتكبَّرَ فيها}: لأنها دار الطيبين الطاهرين، فلا تَليقُ بأخبث خَلْق الله وأشرهم، {فاخرُجْ إنَّك من الصاغرين}؛ أي: المهانين الأذلين؛ جزاء على كبره وعجبه بالإهانة والذل.
{13} Na kwa sababu hii, pindi yalipotokea kutoka kwa Iblisi yale yaliyotokea, akateremka kutoka katika cheo chake cha juu hadi chini kabisa ya walio chini. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwambia: Teremka "kutoka humo," yaani kutoka Peponi; "Haikufalii kufanya kiburi humo." Kwa sababu hiyo ni nyumba ya wazuri, wasafi. basi haimfailii muovu zaidi wa viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, na mbaya zaidi wao, "humo. Basi toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni." Yaani, waliofedheheshwa na waliodhalilishwa kama malipo kwa kiburi chake na majivuno yake kwa kudunishwa na kudhalilishwa.
#
{14 - 15} فلما أعلن عدوُّ الله بعداوة الله وعداوة آدم وذريَّته؛ سأل الله النَّظِرة والإمهال إلى يوم البعث؛ ليتمكَّنَ من إغواءِ ما يقدِرُ عليه من بني آدم، ولما كانت حكمة الله مقتضيةً لابتلاء العباد واختبارهم ليتبيَّنَ الصادق من الكاذب ومَن يطيعه ومن يطيع عدوَّه؛ أجابه لما سأل، فقال: {إنَّك من المُنظَرينَ}.
{14 - 15} Basi Adui wa mwenyezi Mungu alipotangaza uadui wake kwa mwenyezi Mungu na uadui wake kwa Adamu na uzao wake, akamwomba Mwenyezi Mungu muda na muhula mpaka Siku ya Qiyama, Ili aweze kuwapotosha wale atakaoweza katika wanadamu. Na kwa kuwa hekima ya Mwenyezi Mungu inataka kuwajaribu waja Wake, na kuwapa mtihani ili ibainike mkweli na mwongo, na mwenye kumtii na mwenye kumtii adui yake, Akamuitikia kile alichouliza. Akasema, "Hakika Wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula."
: 16 - 17 #
{قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ (16) ثُمَّ لَآتِيَنَّهُمْ مِنْ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَنْ شَمَائِلِهِمْ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ (17)}
16. Akasema: Kwa kuwa umenipotosha, basi hakika nitawakalia katika Njia yako iliyonyooka. 17. Kisha nitawajia kwa mbele yao na kwa nyuma yao na kuliani kwao kwote na kushotoni kwao kwote. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani.
#
{16} أي: قال إبليس لَمَّا أُبْلِسَ وأَيِسَ من رحمة الله: {فبما أغْوَيْتَني لأقعدنَّ لهم}؛ أي: للخلق {صراطك المستقيم}؛ أي: لألزمنَّ الصِّراط، ولأسعى غاية جهدي على صدِّ الناس عنه وعدم سلوكهم إياه.
{16} Yaani, Iblisi alisema pindi alipokosa tumaini na akakata tamaa ya rehema ya Mwenyezi Mungu: "Kwa kuwa umenipotosha, basi hakika nitawakalia." Yaani, nitawakalia viumbe kwenye "Njia yako iliyonyooka;" Yaani, hakika nitaandamana nao kwenye njia yako, na nitajitahidi jitihada yangu yote katika kuwazuia nayo, ili wasiifuate.
#
{17} {ثمَّ لآتِيَنَّهُم مِنْ بينِ أيديهم ومن خلفِهم وعن أيمانِهِم وعن شمائِلِهم}؛ أي: من جميع الجهات والجوانب، ومن كل طريق يتمكن فيه من إدراك بعض مقصوده فيهم، ولما علم الخبيثُ أنهم ضعفاء قد تغلب الغفلةُ على كثير منهم، وكان جازماً ببذل مجهوده على إغوائهم؛ ظنَّ ـ وصدق ظنُّه ـ فقال: {ولا تجدُ أكثرَهُم شاكرينَ}: فإنَّ القيام بالشكر من سلوك الصراط المستقيم، وهو يريدُ صدَّهم عنه وعدم قيامهم به؛ قال تعالى: {إنَّما يَدْعو حِزْبَه ليكونوا من أصحابِ السَّعير}، وإنما نَبَّهَنا الله على ما قال، وعزم على فعله، لنأخذَ منه حِذْرَنا، ونستعدَّ لعدوِّنا، ونحترزَ منه بعلْمِنا بالطُرُق التي يأتي منها ومداخله التي ينفذ منها؛ فله تعالى علينا بذلك أكمل نعمة.
{17} "Kisha nitawajia kwa mbele yao na kwa nyuma yao na kuliani kwao kwote na kushotoni kwao kwote." Yaani, kutokea mielekeo yote na pande zote, na kutokea katika kila njia ambayo ataweza kwayo kupata baadhi ya makusudio yake ndani yao. Na pindi muovu huyu alipotambua kuwa wao ni dhaifu, ambao kughafilika kunaweza kuwashinda wengi miongoni mwao, na akawa na uhakika wa kufanya jitihada zake katika kuwapoteza, akadhani - na dhana yake ikawa kweli. - Na akasema: "Wala hutawakuta wengi wao ni wenye shukrani;" kwani kushukuru ni katika kutembea kwenye njia iliyonyooka. Naye anataka kuwazuia nayo, na kwamba wasifanye hilo. Yeye Mtukufu akasema, "Kwani yeye hakika analiita kundi lake ili liwe katika wenza wa Moto wenye mwako mkali." Lakini Mwenyezi Mungu alitutanabahisha na hayo aliyoyasema, na akaazimia kuyafanya, ili tuchukue tahadhari yetu dhidi yake, na tujiandae dhidi ya adui yetu, na tujilinde dhidi yake kwa kujua kwetu njia ambazo yeye huja kupitia hizo, na miingilio yake ambayo anapitia humo. Basi Yeye Mtukufu ana neema kamili zaidi juu yetu kwa hilo.
: 18 #
{قَالَ اخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَدْحُورًا لَمَنْ تَبِعَكَ مِنْهُمْ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنْكُمْ أَجْمَعِينَ (18)}.
18. Akasema: Toka humo ilhali umeshutumiwa, umefukuzwa. Hapana shaka atakayekufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.
#
{18} أي: قال الله لإبليس لما قال ما قال: {اخرُجْ منها}: خروج صَغار واحتقار، لا خروج إكرام، بل {مذؤوماً}؛ أي: مذموماً، {مدحوراً}: مبعداً عن الله وعن رحمته وعن كل خير. {لأملأنَّ جهنَّم}: منك وممَّن تَبِعَكَ منهم {أجمعين}: وهذا قَسَمٌ من الله تعالى أن النار دار العصاة، لا بد أن يملأها من إبليس وأتباعه من الجن والإنس.
{18} Yaani Mwenyezi Mungu alimwambia Ibilisi aliposema yale aliyosema: "Toka humo" kutoka kwa namna ya uduni na dharau, si kutoka kwa utukufu. Bali "ilhali umeshutumiwa, umefukuzwa," yaani, kuwekwa mbali na Mwenyezi Mungu, na rehema zake, na heri zote. "Basi hakika nitaijaza Jahannamu" kwako na kwa wale wanaokufuata miongoni mwao "nyote." Na hiki ni kiapo kitokacho kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kwamba Moto ni makazi ya waasi, na ni lazima aujaze kwa Iblisi na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu.
Kisha akamtahadharisha Adam kutokana na uovu wake na majaribio yake, akisema:
: 19 - 23 #
{وَيَاآدَمُ اسْكُنْ أَنْتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ (19) فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِنْ سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَنْ تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ (20) وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ (21) فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِنْ وَرَقِ الْجَنَّةِ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَنْ تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُلْ لَكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُبِينٌ (22) قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنْفُسَنَا وَإِنْ لَمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ (23)}
19. Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo Bustanini humo, na kuleni kwayo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, basi mkawa katika madhalimu. 20. Basi Shetani akawatia wasiwasi ili awafichulie tupu zao walizofichwa, na akasema: hakuwakataza Mola wenu Mlezi mti huu isipokuwa mkaja kuwa Malaika, au mkawa katika wanaoishi milele. 21. Naye akawaapia: Hakika mimi ni miongoni wa wanaowanasihi. 22. Basi akawatumbukiza kwa hadaa. Na walipouonja ule mti, tupu zao zikawafichukia na wakaanza kujibandikia katika majani ya Bustani hiyo. Na Mola wao Mlezi akawaita, "Je, sikuwakataza mti huo, na kuwaambia ya kwamba hakika Shetani kwenu ni adui wa dhahiri?" 23. Wakasema: Mola wetu Mlezi! Tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutatufutia dhambi na ukaturehemu, hakika tutakuwa katika waliohasirika.
#
{19} أي: أمر الله تعالى آدم وزوجته حواء التي أنعم الله بها عليه ليسكن إليها أن يأكلا من الجنة حيث شاءا ويتمتعا فيها بما أرادا؛ إلا أنه عيَّن لهما شجرةً ونهاهما عن أكلها، والله أعلم ما هي، وليس في تعيينها فائدةٌ لنا، وحرَّم عليهما أكلها؛ بدليل قوله: {فتكونا من الظالمين}.
{19} Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwamrisha Adam na mkewe Hawa, ambaye Mwenyezi Mungu alimneemesha kwaye ili akae naye kwa utulivu, kwamba wale katika Bustani hiyo popote wapendapo na wastarehe humo kwa chochote watakacho. Isipokuwa Yeye aliwatengea kando mti fulani na akawakataza kuula, Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni upi. Na hakuna faida yoyote kwetu katika kuubainisha. Na akawaharamishia kuula, kwa ushahidi wa kauli yake: "Basi mkawa katika madhalimu."
#
{20} فلم يزالا ممتثلينِ لأمر الله حتى تغلغل إليهما عدوُّهما إبليس بمكره، فوسوس لهما وسوسةً خدَعَهما بها وموَّه عليهما وقال: {ما نهكُما ربُّكما عن هذه الشجرة إلَّا أن تكونا مَلَكَيْن}؛ أي: من جنس الملائكة، {أو تكونا مِنَ الخالدينَ}: كما قال في الآية الأخرى: {هل أدُلُّكَ على شجرةِ الخُلْدِ وملكٍ لا يَبْلى}.
{20} Kwa hivyo hawakuacha kuitekeleza amri hiyo ya Mwenyezi Mungu mpaka adui yao Shetani alipowapenya kwa hila yake, na akawatia wasiwasi aliyowahadaa kwayo, na akawaficha ukweli. Akasema: "Mola wenu Mlezi mti huu isipokuwa mkaja kuwa Malaika." Yaani, wakawa katika aina ya Malaika, "au mkawa katika wanaoishi milele" kama alivyosema katika Aya nyingine: "Je, nikuelekeze kwenye mti wa kuishi milele na ufalme usioharibika."
#
{21} ومع قوله هذا أقسم لهما بالله: {إني لكما لمن الناصحين}؛ أي: من جملة الناصحين؛ حيث قلت لكما ما قلتُ.
{21} Na pamoja na kauli yake hii, akawaapia kwa Mwenyezi Mungu: "Hakika mimi ni miongoni wa wanaowanasihi." Yaani, miongoni mwa washauri, ambapo niliwaambia yale niliyoyasema.
#
{22} فاغترَّا بذلك، وغلبت الشهوة في تلك الحال على العقل، {فدلاَّهما}؛ أي: أنزلهما عن رتبتهما العالية التي هي البعدُ عن الذنوب والمعاصي إلى التلوُّث بأوضارِها، فأقدما على أكلها، {فلمَّا ذاقا الشجرةَ بَدَتْ لهما سوآتُهما}؛ أي: ظهرت عورة كل منهما بعدما كانت مستورةً، فصار للعري الباطن من التقوى في هذه الحال أثرٌ في اللباس الظاهر حتى انخلع، فظهرت عوراتُهما، ولما ظهرتْ عوراتُهما؛ خَجِلا وجَعَلا يخصِفان على عوراتهما من أوراق شجر الجنة ليستترا بذلك، {وناداهما ربهما}: وهما بتلك الحال ـ موبِّخاً ومعاتباً ـ: {ألم أنْهَكُما عن تلكما الشجرةِ وأقل لكما إنَّ الشيطان لكما عدوٌّ مبينٌ}: فَلِمَ اقترفتُما المنهيَّ وأطعتما عدوَّكما؟!
22. Basi wakadanganyika na hayo, na katika hali hiyo tamaa ikashinda akili. "Basi akawatumbukiza," Yaani, akawashusha kutoka katika daraja lao la juu ambalo ni kuwa mbali na madhambi na maasia hadi kuchafuka kwa uchafu wake, kwa hivyo wakaujia kuula. "Na walipouonja ule mti, tupu zao zikawafichukia."Yaani, uchi wa kila mmoja wao ukadhihirika baada ya kwamba ulikuwa umesitiriwa. Basi uchi wa ndani wa uchamungu katika hali hii ukawa na taathira kwenye vazi la nje mpaka ulipovulika, basi uchi wao ukadhihirika. Na uchi wao ukadhihirika, wakaona aibu, na wakaanza kujibandikia kwenye uchi wao majani ya miti ya Bustani hiyo, ili wajisitiri kwa hilo. "Na Mola wao Mlezi akawaita" hali ya kuwa wako katika hali hiyo akiwakemea na kuwalaumu, "Je, sikuwakataza mti huo, na kuwaambia ya kwamba hakika Shetani kwenu ni adui wa dhahiri?" Basi kwa nini mlilikaribia lililokatazwa, na mkamtii adui yenu?
#
{23} فحينئذٍ مَنَّ الله عليهما بالتوبة وقَبولها، فاعترفا بالذنب، وسألا من الله مغفرتَه، فقالا: {ربَّنا ظَلمْنا أنفُسَنا وإن لم تغفرْ لنا وترحَمْنا لَنَكونَنَّ من الخاسرينَ}؛ أي: قد فعلنا الذنب الذي نبَّهتنا عنه وأضررنا بأنفسنا باقتراف الذنب، وقد فعلنا سببَ الخسار إن لم تغفرْ لنا بمحو أثر الذنب وعقوبته وترحَمْنا بقَبول التوبة والمعافاة من أمثال هذه الخطايا، فغفر الله لهما ذلك، وعصى آدمُ ربَّه فغوى. ثم اجتباه ربُّه فتاب عليه وهَدَى. هذا وإبليس مستمرٌّ على طغيانِهِ، غير مقلع من عصيانه؛ فمن أشبه آدم بالاعتراف وسؤال المغفرة والندم والإقلاع إذا صدرت منه الذُّنوب؛ اجتباهُ ربُّه وهداه، ومن أشبهَ إبليس إذا صدر منه الذنبُ لا يزالُ يزدادُ من المعاصي؛ فإنه لا يزداد من الله إلا بعداً.
{23} Basi hapo, Mwenyezi Mungu akawaneemesha kwa toba na kuikubali nao wakakiri dhambi zao, na wakamwomba Mwenyezi Mungu kuwafutia dhambi, wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutatufutia dhambi na ukaturehemu, hakika tutakuwa katika waliohasirika." Yaani, tumeshatenda dhambi ambayo ulituhadharisha nayo na tumejidhuru nafsi zetu kwa kufanya dhambi hiyo, na tumeshafanya sababu ya hasara ikiwa hutatufutia dhambi kwa kufuta athari ya dhambi hii na adhabu yake na kuturehemu kwa kukubali toba na kutuepusha na mfano wa dhambi hizi. Basi Mwenyezi Mungu akawafutia dhambi hilo, na Adam akawa amemuasi Mola wake Mlezi na akapotea njia. Kisha Mola wake Mlezi akamteua, na akamkubalia toba, na akamuongoa. Haya, na wakati Shetani anaendelea kuvuka kwake mipaka, bila ya kuacha uasi wake. Kwa hivyo, mwenye kujifananisha na Adam katika kukiri, na kuomba kufutiwa dhambi, na kujuta, na kuacha na dhambi anapofanya, Mola wake Mlezi atamteua na kumuongoa. Na mwenye kujifananisha na Iblisi anapotenda dhambi, bila ya kuacha kuzidisha madhambi, basi yeye haongezi isipokuwa kuwa mbali na Mwenyezi Mungu.
: 24 - 26 #
{[قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَى حِينٍ] (24) قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ (25) يَابَنِي آدَمَ قَدْ أَنْزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا وَلِبَاسُ التَّقْوَى ذَلِكَ خَيْرٌ ذَلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ (26)}.
24. Akasema: Teremkeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Nanyi katika ardhi mtakuwa na makao na starehe mpaka ufike muda. 25. Akasema: Humo mtakuwa hai, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa. 26. Enyi wanadamu! Hakika tumewateremshia vazi la kuficha tupu zenu, na vazi la pambo. Na vazi la uchamungu, hilo ndilo bora zaidi. Hilo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili mpate kukumbuka.
#
{24 - 25} أي: لما أهبط الله آدم وزوجته وذريتهما إلى الأرض؛ أخبرهما بحال إقامتهم فيها، وأنه جعل لهم فيها حياةً، يتلوها الموتُ مشحونةً بالامتحان والابتلاء، وأنهم لا يزالون فيها، يرسِلُ إليهم رسلَه، ويُنْزِلُ عليهم كتبه، حتى يأتِيَهُمُ الموت فيدفَنون فيها، ثم إذا استكملوا بَعَثَهم اللهُ، وأخرجهم منها إلى الدارِ التي هي الدار حقيقة، التي هي دار المقامة.
{24 - 25} Yaani, Mwenyezi Mungu alipomteremsha Adam na mkewe na kizazi chao duniani, akawajulisha kuhusu hali ya kukaa kwao humo, na ya kwamba amewafanyia uhai humo ambao utafuatwa na mauti, wenye mitihani na majaribio. Na kwamba hawataacha kuwa humo akiwatuma Mitume wake, na akiwateremshia Vitabu vyake mpaka mauti yawajie na wazikwe humo. Kisha watakapokamilika, Mwenyezi Mungu atawafufua na kuwatoa humo kwenda katika nyumba ambayo ndiyo nyumba ya uhakika ambayo ndiyo nyumba ya makazi ya milele.
#
{26} ثم امتنَّ عليهم بما يسَّر لهم من اللباس الضروري واللباس الذي المقصود منه الجمال، وهكذا سائر الأشياء كالطعام والشراب والمراكب والمناكح، ونحوها قد يسر الله للعباد ضروريَّها ومكمِّل ذلك، وبيَّن لهم أن هذا ليس مقصوداً بالذات، وإنَّما أنزله الله ليكون معونةً لهم على عبادته وطاعته، ولهذا قال: {ولباسُ التَّقوى ذلك خيرٌ}: من اللباس الحسيِّ؛ فإن لباس التقوى يستمرُّ مع العبد ولا يبلى ولا يبيد، وهو جمال القلب والروح، وأما اللباس الظاهريُّ؛ فغايتُه أن يستُر العورة الظاهرة في وقت من الأوقات، أو يكون جمالاً للإنسان، وليس وراء ذلك منه نفع. وأيضاً؛ فبتقدير عدم هذا اللباس تنكشف عورتُهُ الظاهرةُ التي لا يضرُّه كشفُها مع الضرورة، وأما بتقدير عدم لباس التقوى؛ فإنها تنكشف عورته الباطنة، وينال الخزيَ والفضيحة. وقوله: {ذلك من آيات الله لعلَّهم يذَّكَّرونَ}؛ أي: ذلك المذكور لكم من اللباس مما تذكرون به ما ينفعُكم، ويضرُّكم، وتستعينون باللباس الظاهر على الباطن.
{26} Kisha akawakumbusha yale aliyowaneemesha kwayo ya kuwafanyia wepesi katika mavazi ya lazima na mavazi yanayokusudiwa kwayo kujipamba tu. Na vile vile vitu vingine vyote kama vile vyakula, na vinywaji, na vipando, na ndoa, na mfano wa hayo. Hakika Mwenyezi mungu amewarahisishia waja wake yale ya lazima yao na yale yanayoyakamilisha hayo, na akawabainishia kuwa haya hayakukusudiwa yenyewe, bali Mwenyezi Mungu aliyateremsha hayo ili yawe ni msaada kwao katika kumwabudu na kumtii. Na ndiyo maana akasema, "Na vazi la uchamungu, hilo ndilo bora zaidi" kuliko mavazi ya kihisia. Kwani vazi la uchamungu huendelea pamoja na mja na wala halichakai wala halipotei; nalo ndilo uzuri wa nafsi na roho. Na ama vazi la nje, hilo kilele chake ni kusitiri uchi wa dhahiri tu katika wakati fulani miongoni mwa nyakati, au kuwa pambo kwa mtu, lakini hakuna faida yoyote zaidi ya hayo. Na pia kwa kuchukulia kutokuwepo kwa vazi hili, unadhihirika uchi wake wa dhahiri ambao haumdhuru kuufichua ikibidi. Na ama kwa kuchukulia kutokuwepo kwa vazi la uchamungu, basi unafichuka Uchi wake wa ndani, na anapata hizaya na fedheha. Na kauli yake, "Hilo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili mpate kukumbuka." Yaani, hilo lililotajwa kwa ajili yenu miongoni mwa mavazi ni katika yale ambayo kwayo mnakumbuka yale yanayowafaa na yanayowadhuru, na mnatafuta msaada kutoka kwa vazi la nje juu ya la ndani.
: 27 #
{يَابَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ يَنْزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ (27)}
27. Enyi wanadamu! Kamwe Shetani asiwafitini kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani lile, akawavua vazi lao ili awaonyeshe tupu zao. Hakika yeye anawaona yeye na kabila yake kwa namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wasaidizi wa wale wasioamini.
#
{27} يقول تعالى محذِّراً لبني آدم أن يفعل بهم الشيطان كما فعل بأبيهم: {يا بني آدم لا يَفْتِنَنَّكُمُ الشيطانُ}: بأن يزيِّن لكم العصيانَ ويدعوكم إليه ويرغِّبكم فيه فتنقادون له، {كما أخرجَ أبَوَيْكم من الجنة}: وأنزلهما من المحلِّ العالي إلى أنزل منه؛ فأنتم يريد أن يفعل بكم كذلك ولا يألو جهده عنكم حتى يفتِنَكم إن استطاع؛ فعليكم أن تجعلوا الحَذَرَ منه في بالكم، وأن تَلْبَسوا لامةَ الحرب بينَكم وبينه، وأن لا تغفلوا عن المواضع التي يدخل منها إليكم. فإنَّه يراقِبُكم على الدوام، و {يراكم هو وقَبيلُهُ}: من شياطين الجن {من حيث لا تَرَوْنَهم إنا جعلنا الشياطينَ أولياءَ للذين لا يؤمنونَ}: فعدمُ الإيمان هو الموجبُ لعقد الولاية بين الإنسان والشيطان. {إنَّه ليسَ له سلطانٌ على الذين آمنوا وَعلى ربِّهِمْ يَتَوَكَّلونَ. إنَّما سلطانُهُ على الذين يَتَوَلَّوْنَهُ والذين هم بِهِ مشركونَ}.
{27} Yeye Mtukufu Anasema akiwatahadharisha wanadamu aje Shetani akawafanyia yale aliyomfanyia baba yao: "Enyi wanadamu! Kamwe Shetani asiwafitini" kwa kuwapambia uasi, na kuwaita kwake, na kuwatia moyo kumpenda ili mumfuate "kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani lile" na akawateremsha kutoka mahali pa juu mpaka pa chini zaidi kuliko hapo. Basi nyinyi pia anataka kuwafanyia vivyo hivyo, na wala hataacha jitihada zake zozote mpaka awafitini ikiwa ataweza. Basi ni lazima mutie akilini kujihadhari naye, na kwamba mvae nguo za vita kati yenu na yeye, na kwamba msighafilike na maeneo ambayo yeye huwaingilia kupitia hayo. Kwani Yeye anawaangalia daima, na "anawaona yeye na kabila yake" miongoni mwa mashetani wa majini "kwa namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wasaidizi wa wale wasioamini." Basi kutoamini ndiyo sababu ya kufunga mkataba wa urafiki wa ulinzi kati ya mwanadamu na Shetani. "Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wanamtegemea Mola wao Mlezi. Hakika Mamlaka yake tu ni juu ya wale wanaomfanya rafiki msaidizi na wale wanaomshirikisha yeye (na Mwenyezi Mungu).
: 28 - 30 #
{وَإِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً قَالُوا وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءَنَا وَاللَّهُ أَمَرَنَا بِهَا قُلْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ (28) قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ (29) فَرِيقًا هَدَى وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ الضَّلَالَةُ إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ مُهْتَدُونَ (30)}.
28. Na wanapofanya uchafu, husema: Tuliwakuta baba zetu juu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uchafu. Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua? 29. Sema: Mola wangu Mlezi ameamrisha uadilifu, na zielekezeni nyuso zenu kila mnaposujudu, na muombeni Yeye kwa kumfanyia yeye tu Dini. Kama alivyowaanzisha, ndivyo mtakavyorudi. 30. Kundi moja ameliongoa, na kundi jingine limethibitikiwa na upotovu. Kwa hakika hao waliwafanya mashetani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka.
#
{28} يقول تعالى مبيِّناً لقبح حال المشركين الذين يفعلون الذنوب وينسبون أن اللهَ أمرهم بها: {وإذا فعلوا فاحشةً}: وهي كل ما يُستفحش ويُستقبح، ومن ذلك طوافهم بالبيت عراة، {قالوا وَجَدْنا عليها آباءَنا}: وصَدَقوا في هذا، {واللهُ أمَرَنا بها}: وكذبوا في هذا، ولهذا ردَّ الله عليهم هذه النسبة، فقال: {قل إنَّ الله لا يأمرُ بالفحشاء}؛ أي: لا يليق بكماله وحكمته أن يأمر عبادَه بتعاطي الفواحش، لا هذا الذي يفعله المشركون ولا غيره، {أتقولونَ على الله ما لا تَعْلَمونَ}: وأيُّ افتراء أعظم من هذا؟
{28} Yeye Mtukufu anasema akieleza ubaya wa hali ya washirikina ambao wanafanya madhambi na wanayanasibisha kuwa Mwenyezi Mungu aliwaamrisha kuyafanya: "Na wanapofanya uchafu;" nayo ni kila lililo chafu na baya. Na miongoni mwa hayo ni kuzunguka kwao Al-Kaaba uchi, "husema: Tuliwakuta baba zetu juu yake." Nao ni wakweli katika haya, "na Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuamrisha hayo;" nao walidanganya katika hili. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawakanusha katika kunasibisha huku, akasema: "Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uchafu." Yaani, haiufailii ukamilifu wake na hekima yake kwamba awaamrishe waja wake kufanya machafu, si haya wanayoyafanya washirikina na wala yasiyokuwa hayo. "Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua?" Na ni uzushi gani wa uongo ulio mkubwa zaidi kuliko huu?
#
{29} ثم ذكر ما يأمر به، فقال: {قل أمَرَ ربِّي بالقِسْط}؛ أي: بالعدل في العبادات والمعاملات، لا بالظلم والجور، {وأقيموا وجوهَكم عند كلِّ مسجدٍ}؛ أي: توجَّهوا لله، واجتهدوا في تكميل العبادات، خصوصاً الصلاة، أقيموها ظاهراً وباطناً، ونقُّوها من كل مُنَقِّص ومفسد. {وادعوه مخلصين له الدينَ}؛ أي: قاصدين بذلك وجهه وحدَه لا شريك له، والدعاء يشمل دعاء المسألة ودعاء العبادة؛ أي: لا تريدُون ولا تقصدون من الأغراض في دعائكم سوى عبودية الله ورضاه، {كما بدأكم}: أول مرة {تعودونَ}: للبعث؛ فالقادر على بدء خلقكم قادرٌ على إعادته، بل الإعادةُ أهون من البداءَة.
{29} Kisha akataja yale aliyoyaamrisha, akasema: "Sema: Mola wangu Mlezi ameamrisha uadilifu;" yaani, kufanya uadilifu katika ibada na kuamiliana, si kwa dhuluma na ukandamizaji, "na mnyoosheeni nyuso zenu kwenye kila msikiti." Yaani elekeeni kwa Mwenyezi Mungu, na jitahidini katika kukamilisha ibada, hususan Sala, zisimamisheni kwa nje na ndani, na zisafisheni kutokana na kila chenye kuzipunguza na kuziharibu. "Na muombeni Yeye kwa kumfanyia yeye tu Dini;" yaani, kukusudia kwa hayo uso wake peke yake, bila ya mshirika yeyote. Na Dua inajumuisha dua ya kuomba na dua ya ibada. Yaani, hamtaki wala hamkusudii malengo yoyote katika dua yenu isipokuwa kumuabudu Mwenyezi Mungu na radhi yake; "kama alivyowaanzisha" mara ya kwanza "ndivyo mtakavyorudi" kwa ajili ya kufufuliwa. Kwa hivyo Mwenye uwezo wa kuanzisha uumbaji wenu ni muweza wa kuurudia, bali kurudia ni rahisi zaidi kuliko kuanza.
#
{30} {فريقاً}: منكم، {هَدَى}: اللهُ؛ أي: وفَّقهم للهداية ويسَّر لهم أسبابها وصرف عنهم موانعها، {وفريقاً حقَّ عليهم الضَّلالة}؛ أي: وجبت عليهم الضَّلالة بما تسبَّبوا لأنفسهم وعملوا بأسباب الغواية. فإنَّهم {اتَّخذوا الشياطينَ أولياء من دون اللهِ}؛ ومن يتَّخذ الشيطان وليًّا من دون الله؛ فقد خسر خسراناً مُبِيناً؛ فحين انسلخوا من ولاية الرحمن واستحبوا ولاية الشيطان؛ حصل لهم النصيبُ الوافر من الخذلان، ووُكِلوا إلى أنفسهم فخسروا أشد الخسران. وهم يحسبونَ {أنَّهم مهتدونَ}: لأنهم انقلبت عليهم الحقائقُ، فظنُّوا الباطل حقًّا والحقَّ باطلاً. وفي هذه الآيات دليلٌ على أن الأوامر والنواهي تابعة للحكمة والمصلحة؛ حيث ذكر تعالى أنه لا يُتَصَوَّر أن يأمر بما تستفحشه وتنكره العقول، وأنه لا يأمر إلا بالعدل والإخلاص. وفيه دليلٌ على أن الهداية بفضل الله ومَنِّه، وأن الضلالة بخذلانه للعبد إذ تولى ـ بجهله وظلمه ـ الشيطانَ، وتسبَّب لنفسه بالضلال، وأن من حسب أنه مهتدٍ وهو ضالٌّ فإنه لا عذر له؛ لأنه متمكِّن من الهدى، وإنما أتاه حسبانه من ظلمه بترك الطريق الموصل إلى الهدى.
{30} "Kundi moja" miongoni mwenu "ameliongoa" Mwenyezi Mungu. Yaani, aliwawezesha kwenye uwongofu, na akawarahisishia sababu zake, na akawaondolea vizuizi vyake, "na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu." Yaani, walithibitishiwa na kupotea kwa sababu ya yale waliyojisababishia nafsi zao na kufanya sababu za upotevu. Kwani wao kwa hakika "waliwafuata mashetani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu." Na mwenye kumfanya Shetani kuwa rafiki mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu, basi hakika amehasiri hasara ya wazi. Kwa hivyo walipotoka katika urafiki na ulinzi wa Mwingi wa Rehema, na wakapendelea urafiki na ulinzi wa Shetani, wakapata fungu jingi la kuangushwa, na wakaachiwa nafsi zao wenyewe, kwa hivyo wakahasiri hasara kubwa zaidi. Nao wanadhani "kuwa wameongoka," kwa sababu hakika ziliwageukia, basi wakadhani kwamba batili ni haki, na haki ni batili. Na aya hizi zina ushahidi kwamba maamrisho na makatazo yanafuata hekima na masilahi, kwa kuwa yeye Mtukufu alitaja kwamba, haiwezi kufikiriwa kwamba Yeye anaamrisha yale ambayo akili zinajua kwamba ni machafu na zinayakataa. Na kwamba haamrishi isipokuwa uadilifu na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake. Na ndani yake kuna ushahidi ya kwamba, uwongofu ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na neema yake, na kwamba upotovu ni kutokana na kumwacha kwake mja pale alipofanya Shetani rafiki mlinzi - kwa ujinga wake na dhuluma yake - na akajisababishia kupotea mwenyewe; na kwamba anayedhani kuwa ameongoka ilhali amepotea, basi yeye hana udhuru. Kwa sababu anaweza kuongoka, lakini dhana yake hiyo ilimjia kwa sababu ya dhuluma yake kwa kuacha njia inayofikisha kwenye uwongofu.
: 31 #
{يَابَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ (31)}
31. Enyi wanadamu! Chukueni pambo lenu kwenye msikiti, na kuleni, na kunyweni, wala msipitilize. Kwa hakika Yeye hapendi wanaopitiliza.
#
{31} يقول تعالى بعدما أنزل على بني آدم لباساً يواري سوآتهم وريشاً: {يا بني آدم خُذوا زينتكم عند كل مسجدٍ}؛ أي: استروا عوراتكم عند الصلاة كلِّها فرضها ونفلها؛ فإن سترها زينة للبدن؛ كما أن كشفها يدع البدن قبيحاً مشوهاً، ويحتمل أنَّ المراد بالزينة هنا ما فوق ذلك من اللباس النظيف الحسن. ففي هذا الأمر بستر العورة في الصلاة وباستعمال التجمل فيها ونظافة السترة من الأدناس والأنجاس. ثم قال: {وكلوا واشربوا}؛ أي: مما رزقكم الله من الطيبات، {ولا تسرِفوا}: في ذلك، والإسراف إما أن يكون بالزيادة على القدر الكافي والشره في المأكولات التي تضر بالجسم، وإما أن يكون بزيادة الترفُّه والتنوُّق في المآكل والمشارب واللباس، وإما بتجاوز الحلال إلى الحرام. {إنَّه لا يحبُّ المسرفين}: فإن السرف يبغضه الله، ويضرُّ بدن الإنسان ومعيشته، حتى إنه ربما أدَّت به الحالُ إلى أن يعجز عما يجب عليه من النفقات. ففي هذه الآية الكريمة الأمر بتناول الأكل والشرب والنهي عن تركهما وعن الإسراف فيهما.
{31} Yeye Mtukufu anasema baada ya kuwateremshia wanadamu vazi la kufunika uchi wao na pambo: "Enyi wanadamu! Chukueni pambo lenu kwenye msikiti." Yaani, funikeni uchi wenu wakati wa kuswali swala zote, za faradhi zake na za Sunnah zake. Kwa maana, kuufunika ni pambo la mwili, kama vile kuudhihirisha pia kunauacha mwili ukiwa mbaya na ukiwa umeharibika. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa na kujipamba hapa ni chochote zaidi ya hapo, kama vile mavazi safi na mazuri. Kwa hivyo, katika hili kuna amri ya kufunika uchi wakati wa sala, na kutumia mapambo mazuri ndani yake, na kusafika kwa kinachositiri kutokana na uchafu na najisi. Kisha akasema, "Na kuleni na kunyweni;" yaani, katika yale mazuri aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu, "wala msipitilize" katika hayo. Na israfu ima ni kwa kuzidi kiasi kinachotosha na ulafi katika vyakula kwa namna inayodhuru mwili, au kwa kuzidisha anasa na ubadhirifu katika vyakula, na vinywaji, na mavazi, au kwa kupindukia ya halali hadi kwenye haramu. "Hakika Yeye hawapendi wapitilizao;" kwa maana, Mwenyezi Mungu anachukia upitilizaji, na unadhuru mwili wa mtu, na maisha yake, kiasi kwamba hali hiyo inaweza kumpelekea kushindwa kufanya yale yanachowajibika juu yake ya matumizi. Kwa hivyo, katika Aya hii tukufu, kuna amri ya kula na kunywa, na katazo la kuyaacha hayo na kutopitiliza ndani yake.
: 32 - 33 #
{قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ كَذَلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ (32) قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَنْ تُشْرِكُوا بِاللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَنْ تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ (33)}.
32. Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilowatolea waja wake, na vile vilivyo vizuri katika riziki? Sema: hivyo ni kwa wale walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Qiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivyo ndivyo tunavyoeleza Ishara kwa kaumu wanaojua. 33. Sema: Hakika Mola wangu Mlezi ameharimisha machafu, yaliyodhihiri yake na ya siri, na dhambi, na kuvuka mipaka bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia uthibitisho wowote, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua.
#
{32} يقول تعالى منكراً على من تعنَّت وحرَّم ما أحلَّ الله من الطيبات: {قل مَنْ حَرَّمَ زينةَ الله التي أخرج لعباده}: من أنواع اللباس على اختلاف أصنافه والطيبات من الرزق من مأكل ومشرب بجميع أنواعه؛ أي: من هذا الذي يقدم على تحريم ما أنعم الله بها على العباد؟ ومن ذا الذي يضيِّق عليهم ما وسعه الله؟ وهذا التوسيع من الله لعباده بالطيبات جعله لهم ليستعينوا به على عبادته فلم يُبِحْه إلا لعباده المؤمنين، ولهذا قال: {قل هي للذين آمنوا في الحياة الدُّنيا خالصةً يوم القيامة}؛ أي: لا تبعة عليهم فيها. ومفهوم الآية أن من لم يؤمن بالله بل استعان بها على معاصيه؛ فإنها غير خالصة له ولا مباحة، بل يعاقب عليها وعلى التنعُّم بها، ويسأل عن النعيم يوم القيامة. {كذلك نفصِّل الآيات}؛ أي: نوضحها ونبيِّنها، {لقوم يعلمون}: لأنهم الذين ينتفعون بما فصَّله الله من الآيات، ويعلمون أنها من عند الله، فيعقلونها ويفهمونها.
{32} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuwakemea wale wanaofanya ukaidi na kuharamisha mema aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu: "Sema: Ni nani aliyeharimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilowatolea waja wake" miongoni mwa aina za mavazi kwa sampuli zake tofautitofauti, na vitu vizuri katika riziki, kama vile vyakula na vinywaji vya kila aina. Yaani, ni nani huyo anayependekeza kuharamisha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake? Na ni nani huyo anayefanyia ufingu katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwakunjulia? Na kukunjua huku kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa mambo mazuri aliwafanyia hayo ili wapate msaada kwayo katika kumuabudu, wala hakuyaruhusu isipokuwa kwa waja wake Waumini. Na ndiyo maana akasema, "Sema: hivyo ni kwa wale walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Qiyama vitakuwa vyao wao tu." Yaani, hakuna lawama juu yao katika hayo. Na maana ya Aya isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba asiyemwamini Mwenyezi Mungu, bali alitafuta msaada kwayo katika kumuasi; basi hayo si kwa ajili yake tu wala hayaruhusiki, bali ataadhibiwa kwa sababu yake na kwa kuyafurahia, na ataulizwa kuhusu neema hizo Siku ya Qiyama. "Namna hivyo ndivyo tunavyoeleza Ishara;" yaani, tunaziweka wazi na tunazibainisha, "kwa kaumu wanaojua;" kwa sababu wao ndio wanaonufaika na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameeyaeleza kwa kina miongoni mwa Aya mbalimbali, na wanajua kwamba hizo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanazielewa na kuzifahamu.
#
{33} ثم ذكر المحرمات التي حرَّمها الله في كلِّ شريعة من الشرائع، فقال: {قلْ إنَّما حرَّم ربِّي الفواحش}؛ أي: الذنوب الكبار التي تُستفحش، وتستقبح لشناعتها وقبحها، وذلك كالزِّنا واللواط ونحوهما. وقوله: {ما ظهر منها وما بطن}؛ أي: الفواحش التي تتعلَّق بحركات البدن والتي تتعلَّق بحركات القلوب؛ كالكبر والعُجْب والرياء والنفاق ونحو ذلك، {والإثم والبغي بغير الحقِّ}؛ أي: الذنوب التي تؤثم وتوجب العقوبة في حقوق الله، والبغي على الناس في دمائهم وأموالهم وأعراضهم. فدخل في هذا الذنوب المتعلقة بحق الله والمتعلقة بحق العباد، {وأن تشرِكوا بالله ما لم ينزِّلْ به سلطاناً}؛ أي: حجة، بل أنزل الحجة والبرهان على التوحيد. والشرك هو أن يُشْرَكَ مع الله في عبادته أحدٌ من الخلق، وربما دخل في هذا الشرك الأصغر؛ كالرياء والحلف بغير الله ونحو ذلك، {وأن تقولوا على الله ما لا تعلمونَ}: في أسمائِهِ وصفاتِهِ وأفعالِهِ وشرعِهِ؛ فكل هذه قد حرمها الله ونهى العباد عن تعاطيها؛ لما فيها من المفاسد الخاصة والعامة، ولما فيها من الظلم والتجري على الله والاستطالة على عباد الله وتغيير دين الله وشرعه.
{33} Kisha akataja yaliyoharamishwa ambayo Aliyaharamisha Mwenyezi Mungu katika kila sheria miongoni mwa sheria. Akasema, "Sema: Hakika Mola wangu Mlezi ameharimisha machafu; yaani; madhambi makubwa ambayo yanajulikana kwamba ni machafu na yanachukiza kwa sababu ya uchafu wake na ubaya wake; nayo ni kama vile uzinzi, na ulawiti na mengineyo. Na kauli yake, "yaliyodhihiri yake na ya siri;" yaani, machafu ambayo yanahusiana na harakati za mwili na yale yanayohusiana na harakati za mioyo, kama vile kiburi, na majivuno, na kujionyesha, na unafiki, na mengineyo, "na dhambi, na kuvuka mipaka bila ya haki." Yaani, dhambi ambazo zinatoa mtu makosani na zinalazimu adhabu katika haki za Mwenyezi Mungu, na kupitiliza kiasi dhidi ya watu katika damu zao, na mali zao, na heshima zao. Basi yakaingia katika hilo madhambi yanayohusiana na haki za Mwenyezi Mungu na yale yanayohusiana na haki za waja wake, "na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia uthibitisho wowote;" yaani, hoja. Bali aliteremsha hoja na uthibitisho wa tauhidi. Na Ushirikina ni kwamba amshirikishe yeyote miongoni mwa katika kumuabudu Mwenyezi Mungu; na pengine inaingia katika hili ushirikina mdogo, kama vile kujionyesha na kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na mfano wa hayo; "na kusema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua," katika majina yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na sheria zake. Yote hayo yameharamishwa na Mwenyezi Mungu na akawakataza waja wake kuyafanya, kwa sababu ya uharibifu wa kibinafsi na wa umma uliomo ndani yake, na kwa sababu ya yale yaliyomo ndani yake ya dhuluma na kufanya ujasiri dhidi ya Mwenyezi Mungu, na kuwanyanyasa waja wa mwenyezi Mungu, na kubadilisha dini ya Mwenyezi Mungu na sheria yake.
: 34 #
{وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ (34)}.
34. Na kila umma una muda wake. Na unapokuja muda wao, basi hawakawii hata saa moja, wala hawatangulii.
#
{34} أي: وقد أخرج الله بني آدم إلى الأرض، وأسكنهم فيها، وجعل لهم أجلاً مسمًّى، لا تتقدَّم أمة من الأمم على وقتها المسمَّى ولا تتأخَّر، لا الأمم المجتمعة ولا أفرادها.
{34} Yani Mwenyezi Mungu aliwatoa wanadamu hadi kwenye ardhi, na akawafanya kuishi humo, na akawawekea muda maalum. Hakuna umma wowote miongoni mwa umma unaoweza kutangulia wakati wake uliowekwa wala kuchelewa, si umma wote kwa pamoja wala watu wake binafsi.
: 35 - 36 #
{يَابَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِنْكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي فَمَنِ اتَّقَى وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (35) وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (36)}.
35. Enyi wanadamu! Watakapowajia Mitume miongoni mwenu wakiwasimulia Ishara zangu, basi mwenye kumcha Mungu na akatengenea, haitakuwa hofu kwao, wala wao hawatahuzunika. 36. Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ndio wenza wa Moto, wao humo watadumu.
#
{35} لما أخرج الله بني آدم من الجنة؛ ابتلاهم بإرسال الرسل وإنزال الكتب عليهم يقصُّون عليهم آيات الله ويبيِّنون لهم أحكامه. ثم ذكر فضلَ من استجاب لهم وخسارَ من لم يستجبْ لهم، فقال: {فمنِ اتَّقى}: ما حرم الله من الشرك والكبائر والصغائر، {وأصلح}: أعماله الظاهرة والباطنة، {فلا خوفٌ عليهم}: من الشرِّ الذي قد يخافه غيرهم، {ولا هم يحزنونَ}: على ما مضى. وإذا انتفى الخوفُ والحزنُ؛ حصل الأمنُ التامُّ والسعادة والفلاح الأبدي.
{35} Mwenyezi Mungu alipowatoa wanadamu katika Bustani ile, akawajaribu kwa kuwatumia Mitume na kuwateremshia vitabu, wakiwasimulia Aya za Mwenyezi Mungu na kuwabainishia hukumu zake. Kisha akataja fadhila za yule aliyewaitikia, na hasara ya yule ambaye hakuwaitikia, akasema: "Basi mwenye kumcha Mungu" katika yale Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu miongoni mwa ushirikina, na madhambi makubwa na madogo, "na akatengenea" katika matendo yake ya nje na yaliyofichika, "haitakuwa hofu juu yao" miongoni mwa maovu ambayo wengineo wanaweza kuhofu; "wala wao hawatahuzunika" kwa yale yaliyopita. Na ikiwa hofu na huzuni havitakuwepo, basi amani kamili, inapatikana, na furaha, na kufaulu kwa milele vitapatikana.
#
{36} {والذين كذَّبوا بآياتنا واستكبروا عنها}؛ أي: لا آمنت بها قلوبهم ولا انقادت لها جوارحهم، {أولئك أصحابُ النار هم فيها خالدون}: كما استهانوا بآياته، ولازموا التكذيب بها؛ أهينوا بالعذابِ الدائم الملازم.
{36} "Na wale waliokadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi;" yaani, nyoyo zao hazikuziamini, wala viungo vyao havikuzifuata; "hao ndio wenza wa Moto, wao humo watadumu." Kama walivyozifanyia stihizai Aya zake, na wakaendelea kuzikanusha, wakadunishwa kwa adhabu ya daima, ya milele.
: 37 - 39 #
{فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ أُولَئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُمْ مِنَ الْكِتَابِ حَتَّى إِذَا جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنْتُمْ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ (37) [قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِكُمْ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ فِي النَّارِ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَعَنَتْ أُخْتَهَا حَتَّى إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِنَ النَّارِ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَكِنْ لَا تَعْلَمُونَ (38) وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِنْ فَضْلٍ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنْتُمْ تَكْسِبُونَ (39)]}.
37. Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au akazikadhibisha Ishara zake? Hao litawafikia fungu lao waliloandikiwa, mpaka watakapowajia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea! Na watajishuhudia dhidi yao wenyewe kwamba walikuwa makafiri. 38. Mwenyezi Mungu atasema: Ingieni (Motoni) pamoja na umma zilizopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu. Kila utakapoingia umma, utalaani dada yake. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa mwisho wao atasema juu ya wa mwanzo wao: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni marudufu. Atasema: Kila mmoja ana marudufu, lakini nyinyi hamjui tu. 39. Na wa mwanzo wao atamwambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora wowote kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.
#
{37} أي: لا أحد أظلم {ممَّنِ افترى على الله كذباً}: بنسبة الشريك له والنقص له والتقوُّل عليه ما لم يقل، {أو كذَّب بآياته}: الواضحة المبينة للحقِّ المبين الهادية إلى الصراط المستقيم؛ فهؤلاء وإن تمتعوا بالدنيا ونالهم نصيبهم مما كان مكتوباً لهم في اللوح المحفوظ؛ فليس ذلك بمغنٍ عنهم شيئاً، يتمتَّعون قليلاً ثم يعذَّبون طويلاً. {حتى إذا جاءتهم رسُلُنا يتوفَّوْنهم}؛ أي: الملائكة الموكلون بقبض أرواحهم واستيفاء آجالهم، {قالوا}: لهم في تلك الحالة توبيخاً وعتاباً: {أين ما كنتم تَدْعون من دونِ الله}: من الأصنام والأوثان؛ فقد جاء وقت الحاجة إن كان فيها منفعةٌ لكم أو دفع مضرة، {قالوا ضَلُّوا عنا}؛ أي: اضمحلوا وبطلوا، وليسوا مغنين عنَّا من عذاب الله من شيء، {وشهدوا على أنفسِهم أنهم كانوا كافرين}: مستحقين للعذاب المهين الدائم.
{37} Yaani, hakuna yeyote dhalimu zaidi "kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uoongo" kwa kumnasibishia mshirika, na kumpunguzia hadhi, na kusema juu yake yale ambayo hakuyasema, "au akazikadhibisha Ishara zake?" Zilizo wazi, zibainishazo haki iliyo wazi, zenye kuongoa kwenye njia iliyonyooka. Basi hawa ijapokuwa waliifurahia dunia hii, na wakapata fungu lao miongoni mwa yale waliyoandikiwa katika Ubao Uliohifadhiwa, lakini hayo hayatawafaa chochote. Watafurahia kidogo na kisha wataadhibiwa kwa muda mrefu, "mpaka watakapowajia wajumbe wetu kuwafisha;" yaani, Malaika waliopewa usimamizi wa kuchukua roho zao na kutimiza miida yao. "Watasema" kuwaambia katika hali hiyo kwa kuwakaripia na kuwalaumu: "Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu?" Miongoni mwa masanamu, na viabudiwavyo vyote, na tayari wakati wa haja umefika ikiwa kuna manufaa yoyote yenu katika hao au kuzuia madhara. "Watasema: Wametupotea!" Yaani, wamedidimia, na wakabatilika, wala hawatatufaa kitu katika adhabu ya Mwenyezi Mungu. "Na watajishuhudia dhidi yao wenyewe kwamba walikuwa makafiri" wanaostahiki adhabu ya kuwadunisha, ya daima.
#
{38 - 39} فقالت لهم الملائكة: {ادخُلوا في أمم}؛ أي: في جملة أمم {قد خلت من قبلكم من الجنِّ والإنس}؛ أي: مضوا على ما مضيتم عليه من الكفر والاستكبار، فاستحق الجميعُ الخزيَ والبوارَ. {كلَّما دخلتْ أمةٌ}: من الأمم العاتية النار، {لعنتْ أختَها}؛ كما قال تعالى: {ويومَ القيامةِ يكفُرُ بعضُكم ببعضٍ ويلعنُ بعضكم بعضاً}، {حتَّى إذا ادَّاركوا فيها جميعاً}؛ أي: اجتمع في النار جميع أهلها من الأولين والآخرين والقادة والرؤساء والمقلِّدين الأتباع، {قالت أخراهم}؛ أي: متأخروهم المتبعون للرؤساء، {لأولاهم}: أي: لرؤسائهم شاكين إلى الله إضلالهم إياهم: {ربَّنا هؤلاء أضلُّونا فآتهم عذاباً ضعفاً من النار}؛ أي: عذِّبْهم عذاباً مضاعفاً لأنَّهم أضلُّونا وزينوا لنا الأعمال الخبيثة. فقالت {أولاهم لأخراهم}؛ أي: الرؤساء قالوا لأتباعهم: {فما كان لكم علينا من فضل}؛ أي: قد اشتركنا جميعاً في الغيِّ والضلال، وفي فعل أسباب العذاب؛ فأيُّ فضلٍ لكم علينا؟ {قال} اللَّه: {لكلٍّ} منكم {ضعفٌ}: ونصيب من العذاب، {فذوقوا العذاب بما كنتم تكسِبونَ}: ولكنه من المعلوم أن عذاب الرؤساء وأئمة الضلال أبلغُ وأشنعُ من عذاب الأتباع؛ كما أنَّ نعيم أئمة الهدى ورؤسائه أعظم من ثواب الأتباع؛ قال تعالى: {الذين كَفَروا وصدُّوا عن سبيل اللهِ زِدْناهم عذاباً فوق العذابِ بما كانوا يُفْسِدون}. فهذه الآيات ونحوها دلَّت على أن سائر أنواع المكذبين بآيات الله مخلَّدون في العذاب مشتركون فيه وفي أصله، وإن كانوا متفاوتين في مقداره بحسب أعمالهم وعنادهم وظلمهم وافترائهم وأن مودتهم التي كانت بينَهم في الدُّنيا تنقلب يوم القيامة عداوةً وملاعنةً.
{38-39} Basi Malaika wakawaambia: "Ingieni (Motoni) pamoja na umma zilizopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu." Yaani, walikwenda zao katika hali ambayo nyinyi pia mmekwenda zenu juu yake miongoni mwa ukafiri na kiburi, basi wote hao wakastahiki hizaya na kuangamia. "Kila utakapoingia umma" miongoni mwa umma ulioasi, Motoni "utalaani dada yake;" kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Siku ya Qiyama nyninyi kwa nyinyi mtakufuriana na mtalaaniana nyninyi kwa nyinyi;" "Mpaka watakapokusanyika wote humo." Yaani, watakapokusanyika wakazi wa Motoni wote, miongoni mwa wa mwanzo na wa mwisho, na viongozi, na wakuu, na waigaji, na wafuasi, "wa mwisho wao atamwambia." Yaani, wa baada yao, wale waliowafuata viongozi, "wa mwanzo wao" yaani, viongozi wao wakimlalamikia kwa Mwenyezi Mungu kwamba waliwapoteza: "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni marudufu." Yaani, waadhibu adhabu iliyozidishwa kwa sababu walitupoteza na wakatupambia matendo maovu. Basi, “wa mwanzo wao atamwambia wa mwisho wao." Yaani viongozi watawaambia wafuasi wao, "Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora wowote kuliko sisi." Yaani, sisi sote tumeshiriki katika upotovu, na katika kufanya sababu za adhabu; basi mna ubora gani kutuliko sisi? Mwenyezi Mungu "akasema": "Kila mmoja" wenu "ana marudufu" na fungu katika adhabu. "Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkiyachuma." Lakini inajulikana kuwa adhabu ya viongozi na maimamu wa upotovu ni kubwa zaidi na mbaya zaidi kuliko adhabu ya wafuasi. Kama vile neema ya maimamu na uwongofu na viongozi wake ni kubwa zaidi kuliko malipo ya wafuasi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wale waliokufuru na wakaizuilia njia ya Mwenyezi Mungu, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu yao kwa sababu yale walikuwa wakifanya uharibifu." Basi Aya hizi na mfano wake ziliashiria kuwa kila aina ya wakadhibishao Aya za Mwenyezi Mungu wataishi milele katika adhabu, wakishirikiana humo na katika asili yake; hata kama watatofautiana katika kiwango chake kulingana na matendo yao, na ukaidi wao, na dhuluma yao, kuzua kwao uongo. Na kwamba mapenzi yao ambayo yalikuwa baina yao hapa duniani yatageuka siku ya Qiyama kuwa uadui na laana.
: 40 - 41 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّى يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ (40) لَهُمْ مِنْ جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِنْ فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ وَكَذَلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ (41)}.
40. Hakika wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Bustanini mle mpaka aingie ngamia katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wahalifu. 41. Wana kitanda chao katika Jahannamu, na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.
#
{40} يخبر تعالى عن عقاب من كذَّب بآياته فلم يؤمنْ بها مع أنها آيات بيناتٌ واستكبر عنها فلم ينقدْ لأحكامها بل كذَّب، وتولى أنهم آيسون من كلِّ خير؛ فلا تفتَّحُ أبوابُ السماء لأرواحهم إذا ماتوا، وصعدت تريد العروجَ إلى الله، فتستأذنُ، فلا يؤذَنُ لها؛ كما لم تصعدْ في الدنيا إلى الإيمان بالله ومعرفته ومحبته، كذلك لا تصعد بعد الموت؛ فإن الجزاء من جنس العمل. ومفهوم الآية أنَّ أرواح المؤمنين المنقادين لأمرِ الله المصدِّقين بآياته تفتَّح لها أبواب السماء حتى تعرج إلى الله، وتصل إلى حيث أراد الله من العالم العلويِّ، وتبتهجَ بالقرب من ربِّها والحظُوةِ برضوانه. وقوله عن أهل النار: {ولا يدخُلونَ الجنَّة حتى يلجَ الجملُ}: وهو البعير المعروف {في سَمِّ الخِياطِ}؛ أي: حتى يدخُلَ البعير الذي هو من أكبر الحيوانات جسماً في خرق الإبرة الذي هو من أضيق الأشياء. وهذا من باب تعليق الشيء بالمحال؛ أي: فكما أنه محالٌ دخول الجمل في سَمِّ الخياطِ؛ فكذلك المكذِّبون بآيات الله محالٌ دخولهم الجنة؛ قال تعالى: {إنَّه من يُشْرِكْ بالله فقد حرَّم اللهُ عليه الجنةَ ومأواه النارُ}؛ وقال هنا: {وكذلك نَجْزي المجرمينَ}؛ أي: الذين كَثُرَ إجرامُهم، واشتدَّ طغيانُهم.
{40} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya adhabu ya yule aliyezikadhibisha Aya zake, wala haziamini pamoja na kwamba ni Ishara zilizo wazi, na akazifanyia kiburi, na wala hakufuata hukumu zake, bali alikadhibisha, na akageuka, kwamba watakata tamaa ya kupata heri yoyote. Basi milango ya mbingu haitafunguliwa kwa ajili ya roho zao wanapokufa, na zikapanda zikitaka kupaa kwenda kwa Mwenyezi Mungu. Basi zitaomba ruhusa ya kuingia, lakini hazitapewa ruhusa. Kama vile hazikupanda katika dunia hii kwenda katika kumwamini Mwenyezi Mungu, na kumjua Yeye, na kumpenda Yeye, vivyo hivyo huzitapanda baada ya kifo. Kwa maana malipo ni ya aina sawa na matendo. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya hii ni kwamba roho za Waumini wafuatao amri ya Mwenyezi Mungu na wasadikishao Ishara zake zitafunguliwa milango ya mbingu ili zipande hadi kwa Mwenyezi Mungu, na zifike pale anapotaka Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wa juu, na zitafurahi kwa kuwa karibu na Mola wao Mlezi, na kufikia radhi zake. Na kauli yake kuhusu waliomo Motoni: "Wala hawataingia Bustanini mle mpaka aingie ngamia" naye ni yule yule ngamia anayejulikana vyema "katika tundu ya sindano." Yaani, mpaka aingie ngamia ambaye ni miongoni wa wanyama wakubwa zaidi kimwili katika tundu ya sindano, ambayo ni miongoni mwa vitu vyembamba zaidi. Na hili ni katika mbinu za kufungamanisha kitu na kile kisichowezekana. Yaani, kama vile haiwezekani kwa ngamia kuingia kwenye tundu ya sindano, basi vile vile wale wanaokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu haiwezekani kwao kuingia Bustanini mle. Amesema Yeye Mtukufu, "Hakika, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia Bustani ile, na makazi yake ni Jahannamu." Na akasema hapa, "Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wahalifu." Yaani wale uliokithiri uhalifu wao, na dhuluma yao ikawa kubwa.
#
{41} {لهم من جهنَّمَ مِهادٌ}؛ أي: فراش من تحتهم، {ومن فوقِهِم غَواشٍ}؛ أي: ظلل من العذاب تغشاهم، {وكذلك نَجْزي الظالمين}: لأنفسهم جزاءً وفاقاً، وما ربُّك بظلام للعبيد.
{41} "Wana kitanda chao katika Jahannamu;" yaani, wana malazi chini yao, "na juu yao nguo za moto za kujifunika." Yaani, vivuli vya adhabu vinavyowafunika, "na hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu." Waliozidhulumu nafsi zao kama malipo yanayolingana sawa, na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake.
: 42 - 43 #
{وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ (42) وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِمْ مِنْ غِلٍّ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّهُ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ وَنُودُوا أَنْ تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (43)}
42. Na wale walioamini na wakatenda mema, hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Hao ndio wenza wa Bustani ile. Wao watadumu humo. 43. Na tutaondoa kilicho katika vifua vyao ya chuki, na chini yao itapita mito. Na watasema: Alhamdulillah (kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu), ambaye alituongoa kuyafikia haya. Wala hatukuwa wenye kuongoka wenyewe lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutuongoa. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walikuja na haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Bustani mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya.
#
{42} لما ذكر تعالى عقاب العاصين الظالمين؛ ذَكَرَ ثواب المطيعين، فقال: {والذين آمنوا}: بقلوبهم، {وعملوا الصالحات}: بجوارحهم؛ فجمعوا بين الإيمان والعمل، بين الأعمال الظاهرة والأعمال الباطنة، بين فعل الواجبات وترك المحرمات، ولما كان قوله: {وعَمِلوا الصالحاتِ} لفظاً عامًّا يشمل جميع الصالحات الواجبة والمستحبة، وقد يكون بعضها غير مقدور للعبد؛ قال تعالى: {لا نُكَلِّفُ نفساً إلَّا وُسْعَها}؛ أي: بمقدار ما تسعه طاقتها ولا يعسر على قدرتها؛ فعليها في هذه الحال أن تتقي الله بحسب استطاعتها، وإذا عجزت عن بعض الواجبات التي يقدر عليها غيرها؛ سقطت عنها؛ كما قال تعالى: {لا يُكَلِّفُ اللهُ نفساً إلاَّ وُسْعَها}، {لا يُكَلِّفُ الله نفساً إلاَّ ما آتاها}، {ما جَعَلَ عليكم في الدِّينِ مِنْ حَرَج}، {فاتَّقوا الله ما استطعتُم}؛ فلا واجب مع العجز، ولا محرَّم مع الضرورة. {أولئك}؛ أي: المتصفون بالإيمان والعمل الصالح، {أصحابُ الجنة هم فيها خالدون}؛ أي: لا يحولون عنها ولا يبغون بها بدلاً؛ لأنهم يَرَوْن فيها من أنواع اللَّذَّات وأصناف المشتهيات ما تقفُ عنده الغايات، ولا يطلب أعلى منه.
{42} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoitaja adhabu ya madhalimu waasi, Akataja malipo ya watiifu. Akasema, "Na wale walioamini" kwa nyoyo zao "na wakatenda mema" kwa viungo vyao. Basi wakajumuisha kati ya imani na matendo, baina ya matendo ya dhahiri na matendo yaliyofichikana, baina ya kufanya mambo ya wajibu na kuacha mambo yaliyoharamishwa. Na pindi ilipokuwa kauli yake: "Na wakatenda mema" ni neno la jumla linalojumuisha matendo yote mema ya wajibu na yanayopendekezwa, basi na baadhi yake huenda asiyaweze mja. Yeye Mtukufu amesema, "Hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake." Yaani, kwa kiwango cha ziwezavyo nguvu zake, wala siyo vigumu kwa uwezo wake. Basi ni juu yake katika hali hii imche Mwenyezi Mungu kulingana na uwezo wake. Na ikiwa haiwezi baadhi ya majukumu wajibu ambazo wengine wanaziweza; basi hizo haziilazimu. Kama alivyosema Yeye Mtukufu akasema, "Hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake;" "Hatuitwiki nafsi isipokuwa kwa kiasi cha yale aliyoipa;" "hakuwafanyia mazito yoyote katika dini;" "Basi mcheni mwenyezi Mungu kama muwezavyo." Kwa hivyo hakuwa wajibu wowote ikiwa kuna kutoweza, na hakuna haramu yoyote ikiwa kuna dhahrura. "Hao;" yaani, wale wanaosifika kwa sifa ya Imani na matendo mema, " ni wenza wa Bustani ile. Wao watadumu humo." Yaani, hawatatoka humo wala hawatatafuta chochote badala yake. Kwa sababu wanaona ndani yake aina mbalimbali za starehe, na aina mbalimbali za yatamaniwayo ambayo malengo yanasimamia hapo, wala hakitafutwi kilicho zaidi yake.
#
{43} {ونزعنا ما في صُدورهم من غِلٍّ}: وهذا من كرمه وإحسانِهِ على أهل الجنة؛ أنَّ الغلَّ الذي كان موجوداً في قلوبهم والتنافس الذي بينهم أن الله يقلعه ويزيله حتى يكونوا إخواناً متحابِّين وأخلاَّء متصافين؛ قال تعالى: {ونزعنا ما في صدورهم من غلٍّ إخواناً على سُرُرٍ متقابلينَ}، ويخلُقُ الله لهم من الكرامة ما به يحصُلُ لكلِّ واحد منهم الغِبْطَةَ والسرور، ويرى أنه لا فوق ما هو فيه من النعيم نعيمٌ؛ فبهذا يأمنون من التحاسد والتباغض؛ لأنه قد فقدت أسبابه. [و] قوله: {تجري من تحتهم الأنهار}؛ أي: يفجِّرونها تفجيراً حيث شاؤوا وأين أرادوا، إن شاؤوا في خلال القصور أو في تلك الغرف العاليات أو في رياض الجنات من تحت تلك الحدائق الزاهرات، أنهار تجري في غير أخدود، وخيراتٌ ليس لها حدٌّ محدودٌ. {و} لهذا لما رأوا ما أنعم الله عليهم وأكرمهم به؛ {قالوا الحمدُ لله الذي هدانا لهذا}: بأن منَّ علينا وأوحى إلى قلوبنا فآمنت به وانقادتْ للأعمال الموصلةِ إلى هذه الدار، وحفظ الله علينا إيماننا وأعمالَنا حتى أوصَلَنا بها إلى هذه الدار، فنعم الربُّ الكريم الذي ابتدأنا بالنعم، وأسدى من النعم الظاهرة والباطنة ما لا يحصيه المحصون ولا يعدُّه العادُّون. {وما كنَّا لنهتديَ لولا أن هدانا الله}؛ أي: ليس في نفوسنا قابليةٌ للهدى، لولا أنَّه تعالى منَّ بهدايته واتِّباع رسله، {لقد جاءت رسُلُ ربِّنا بالحق}؛ أي: حين كانوا يتمتَّعون بالنعيم الذي أخبرت به الرسل وصار حقَّ يقينٍ لهم بعد أن كان علم يقينٍ لهم قالوا: لقد تحقَّقنا ورأينا ما وعدتنا به الرسلُ وأنَّ جميع ما جاؤوا به حقُّ اليقين لامِرْيَةَ فيه ولا إشكال. {ونودوا}: تهنئةً لهم وإكراماً وتحية واحتراماً {أن تِلْكُمُ الجنة أورثتموها}؛ أي: كنتم الوارثين لها، وصارت إقطاعاً لكم إذ كان إقطاع الكفار النار، أورثتموها {بما كنتم تعملونَ}: قال بعضُ السلف: أهل الجنة نَجَوْا من النار بعفو الله، وأدخلوا الجنة برحمة الله، واقتسموا المنازل، وورثوها بالأعمال الصالحة، وهي من رحمته، بل من أعلى أنواع رحمته.
{43} "Na tutaondoa kilicho katika vifua vyao ya chuki;" na haya ni katika ukarimu wake na ihsani yake juu ya wale waliomo Bustanini humo; kwamba chuki ambayo ilikuwepo ndani ya nyoyo zao na ushindani ambao ulikuwepo baina yao ni kwamba, Mwenyezi Mungu ataing'oa na kuiondosha ili wawe ndugu wanaopendana na kuwa marafiki wandani walio safi. Amesema yeye Mtukufu, "Na tutayaondoa yale yaliyo katika vifua vyao ya chuki wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana." Na Mwenyezi Mungu atawaumbia utukufu kiasi kwamba kila mmoja wao atapata ghera na furaha, na ataona kuwa hakuna neema iliyo juu ziaidi ya neema aliyo ndani yake. Na kwa hayo wanakuwa salama kutokana na kuhusudiana na kuchukiana, kwa sababu zilikwisha potea sababu zake. [Na] kauli yake, "chini yao itapita mito;" yaani, wanaimimina kwa wingi popote wapendapo, wakitaka ndani ya majumba ya kifahari au katika vyumba hivyo vya juu au katika bustani mbalimbali za Bustanini humo chini ya hizo bustani zilizochanua kuna mito inayopita si katika kingo, na heri mbalimbali zisizokuwa na kikomo. "Na" ndiyo maana walipoyaona yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu kwayo na akawakirimu kwayo, "Wakasema: Alhamdulillah (kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu), ambaye alituongoa kuyafikia haya." Kwa kuwa ametuneemesha na akaziteremshia nyoyo zetu ufunuo, kwa hivyo zikamuamini na zikafuata matendo yafikishayo kwenye makao haya. Na Mwenyezi Mungu alituhifadhia Imani yetu na matendo yetu mpaka akatufikisha kwayo kwenye makazi haya. Basi ni mzuri zaidi Mola Mkarimu zaidi aliyetuanzisha kwa neema, na akatupa neema zilizo dhahiri na zilizofichika wasizoweza kuzidhibiti wenye kudhibiti, wala kuzihesabu wenye kuhesabu, {Wala hatukuwa wenye kuongoka wenyewe lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutuongoa." Yaani, nafsi zetu hazina uwezo wa kupata uwongofu, lau si kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alituneemesha kwa kuongoa kwake na kuwafuata Mitume wake. "Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walikuja na haki." Yaani, walipokuwa wanafurahia neema ambazo Mitume waliwajulisha juu yake na zikawa yakini ya haki kwao baada ya kuwa ilikuwa ni elimu ya yakini. Wakasema: Hakika tumeshayathibitisha na tumeshayaona yale waliyotuahidi Mitume na kwamba kila walichokuja nacho ni haki ya yakini isiyokuwa na shaka yoyote ndani yake wala shida yoyote. "Na wakanadiwa" kwa kuwapongeza, na kuwatukuza, na kuwasalimu, na kuwaheshimu "kwamba hiyo ndiyo Bustani mliyorithishwa." Yaani, mlikuwa warithi wake, na ikawa ndilo fungu lenu, wakati fungu la makafiri ni Moto. Mmeirithishwa "kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya." Baadhi ya watangulizi wema walisema: Watu wa Bustani ile waliokoka kutokana na Moto kwa msamaha wa Mwenyezi Mungu, na wakaingizwa Bustanini humo kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, na wakagawana nyumba, na wakazirithi kwa matendo mema; nanyi ni katika rehema yake, bali ni katika aina ya juu zaidi ya rehema.
: 44 - 45 #
{وَنَادَى أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَنْ قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدْتُمْ مَا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا قَالُوا نَعَمْ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَنْ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ (44) الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُمْ بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ (45)}.
44. Na wenza wa Bustani ile watawanadi wenza Moto kwamba, "Sisi tumeshakuta yale aliyotuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli. Na je, nyinyi pia mmekuta yale aliyowaahidi Mola wenu Mlezi kuwa ni kweli?" Watasema: "Ndiyo!" Basi mtangazaji atatangaza kati yao kwamba, "Laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu." 45. Wale wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka ipotoke, nao wanaikufuru Akhera.
#
{44 - 45} يقول تعالى بعد ما ذكر استقرار كلٍّ من الفريقين في الدارين ووجدا ما أخبرت به الرُّسل ونطقتْ به الكتبُ من الثواب والعقاب: إن أهل الجنة نادوا أصحاب النار بأن قالوا: {أن قد وَجَدْنا ما وَعَدَنا ربُّنا حقًّا}: حين وعدنا على الإيمان والعمل الصالح الجنة، فأدخلناها وأرانا ما وصفه لنا، {فهل وجدتُم ما وعدكم ربكم}: على الكفر والمعاصي {حقًّا قالوا نعم}: قد وجدناه حقًّا، فتبين للخلق كلِّهم بياناً لا شكَّ فيه صدق وعد الله، ومن أصدق من الله قيلاً، وذهبت عنهم الشكوك والشبه، وصار الأمر حقَّ اليقين، وفرح المؤمنون بوعد الله واغتبطوا، وأيس الكفار من الخير، وأقروا على أنفسهم بأنهم مستحقون للعذاب. {فأذَّن مؤذنٌ بينهم}؛ أي: بين أهل النار وأهل الجنة بأن قال: {أن لعنةُ الله}؛ أي: بعده وإقصاؤه عن كل خير {على الظالمين}: إذ فتح الله لهم أبوابَ رحمتِهِ، فصدَفوا أنفسهم عنها ظلماً وصدُّوا عن سبيل الله بأنفسهم وصدُّوا غيرهم فضلُّوا وأضلُّوا. والله تعالى يريد أن تكون مستقيمةً ويعتدل سير السالكين إليه، وهؤلاء يريدونها {عِوَجاً}: منحرفةً صادةً عن سواء السبيل. {وهم بالآخرة كافرونَ}: وهذا الذي أوجب لهم الانحرافَ عن الصراط والإقبالَ على شهوات النفوس المحرَّمة عدمُ إيمانهم بالبعث، وعدم خوفهم من العقاب ورجائهم للثواب. ومفهوم هذا [النداء] أن رحمة الله على المؤمنين، وبرَّه شاملٌ لهم، وإحسانه متواترٌ عليهم.
{44 - 45} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema baada ya kutaja kukaa sawasawa kila ya makundi mawili haya katika nyumba mbili hizi, na wakapata yale waliyoyajulisha Mitume na Vitabu vikayatamka miongoni mwa malipo na adhabu kwamba watu wa Peponi waliwaita watu wa Motoni wakisema: "Sisi tumeshakuta yale aliyotuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli." Alipotuahidi Pepo juu ya Imani na matendo mema, basi ametuingiza humo na akatuonyesha yale aliyotueleza. "Na je, nyinyi pia mmekuta yale aliyowaahidi Mola wenu Mlezi" juu ya ukafiri na maasia "kuwa ni kweli? Wakasema: Ndiyo" hakika tumeyakuta kuwa ni kweli. Basi ikawabainikia viumbe wote kubainika ambako hakuna shaka yoyote ndani yake juu ya ukweli wa ahadi ya Mwenyezi Mungu. Na ni nani mkweli zaidi katika kauli kuliko Mwenyezi Mungu? Sasa wameondokewa na shaka na fikira potovu, na jambo hilo likawa haki ya yakini, na Waumini wakaifurahia ahadi ya Mwenyezi Mungu na wakawa na ghera juu yake. Na makafiri wakakata tamaa na heri, na wakakiri juu ya nafsi zao kwamba wanastahiki adhabu. "Basi mtangazaji atatangaza kati yao;" yaani, baina ya watu wa Motoni na watu wa Peponi kwa kusema: "Laana ya Mwenyezi Mungu." Yaani, umbali wake na kutengwa kwake mbali na heri yote "iko juu ya madhalimu;" kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwafungulia milango ya rehema yake, lakini wakajitenga wenyewe nayo kwa dhuluma, na wakajizuia na njia ya Mwenyezi Mungu wao wenyewe, na wakawazuilia wengine, kwa hivyo wakapotea na wakapoteza. Na Mwenyezi Mungu anataka iwe sawa na kunyooke kwenda kwa wale wanaoifuata kwenda kwake, ilhali hawa wanataka “ipotoke” na kuzuilia njia iliyonyooka sawasawa. "Nao wanaikufuru Akhera" na haya yaliyowasababishia kupotea njia, na kuyaendea matamanio ya nafsi yaliyoharamishwa ni kutoamini kwao kufufuliwa, na kutohofu kwao adhabu na kutaraji kwao malipo. Na maana ya [mwito] huu ni kwamba rehema ya Mwenyezi Mungu iko juu ya Waumini, na wema wake unawajumuisha wote, na ihsan yake iko juu yao mara kwa mara.
: 46 - 49 #
{وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ (46) وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (47) وَنَادَى أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُمْ بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَى عَنْكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ (48) أَهَؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّهُ بِرَحْمَةٍ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنْتُمْ تَحْزَنُونَ (49)}
46. Na baina yao (makundi mawili hayo) patakuwapo pazia. Na juu ya Minyanyuko patakuwa watu watakaomjua kila mmoja kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Salamu Alaykum (amani iwe juu yenu)! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai. 47. Na yanapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa Motoni, watasema: Mola wetu Mlezi! Usitujaalie kuwa pamoja na kaaumu madhalimu. 48. Na watu hao wa Minyanyukoni watawaita watu wanaowajua kwa alama zao. Watasema: Kujumuika kwenu hakukuwafaa kitu, wala hicho mlichokuwa mnakifanyia kiburi. 49. Je, hawa ndio wale mliokuwa mkiwaapia kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema? Ingieni Peponi, hapana hofu kwenu, wala hamtahuzunika!
#
{46} أي: وبين أصحاب الجنة وأصحاب النار حجابٌ يُقال له: الأعراف، لا من الجنة ولا من النار، يشرف على الدارين، وينظُر من عليه حال الفريقين، وعلى هذا الحجاب رجالٌ يعرفونَ كلًّا من أهل الجنة والنار بسيماهم؛ أي: علاماتهم التي بها يُعْرَفون ويُمَيَّزون؛ فإذا نظروا إلى أهل الجنة؛ نادَوْهم: {أن سلامٌ عليكم}؛ أي: يحيُّونهم ويسلِّمون عليهم، وهم إلى الآن لم يدخلوا الجنة، ولكنهم يطمعون في دخولها، ولم يجعل الله الطمع في قلوبهم إلا لما يُريد بهم من كرامته.
{46} Yaani baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni kuna pazia liitwalo Al-A`raaf, si la Peponi wala si la Motoni, iko juu ya nyumba mbili hizi na inaangalia kutokea juu yake hali ya makundi mawili haya. Na juu ya pazia hili wako wanaume wanaowajua watu wa Peponi na Motoni kwa alama zao ambazo kwazo wanajulikana na kupambanuliwa. Kwa hivyo, wanapowatazama watu wa Peponi, wanawaita: "Amani iwe juu yenu." Yaani, wanawaamkua na kuwapa salamu, nao kufikia wakati huo bado hawajaingia Peponi, lakini wanataumai kuingia humo. Na Mwenyezi Mungu hakuweka tumaini katika nyoyo zao isipokuwa kwa kile anachokikusudia cha kuwatukuza.
#
{47} {وإذا صُرِفَتْ أبصارُهم تِلْقاءَ أصحابِ النَّارِ}: ورأوا منظراً شنيعاً وهولاً فظيعاً، {قالوا ربَّنا لا تَجْعَلْنا مع القوم الظالمين}: فأهل الجنة إذا رآهم أهلُ الأعراف يطمعون أن يكونوا معهم في الجنة ويحيُّونهم ويسلِّمون عليهم، وعند انصراف أبصارهم بغير اختيارهم لأهل النار يستجيرون [بالله] من حالهم هذا على وجه العموم.
{47} "Na yanapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa Motoni," na wakaona mwono mbaya na hali ya kutisha, "wanasema: Mola wetu Mlezi! Usitujaalie kuwa pamoja na kaaumu madhalimu." Basi watu wa Peponi wanapoonwa na watu wa Al-A’raf, wanatumaini kuwa pamoja nao Peponi, na wanawaamkua na kuwasalimia. Na wakati macho yao yanapogeuka bila ya kutaka kwao kuelekea watu wa Motoni, wanajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hali yao. Na hii ni kwa namna ya ujumla.
#
{48} ثم ذكر الخصوص بعد العموم، فقال: {ونادى أصحابُ الأعراف رجالاً يعرفونهم بسيماهُم}: وهم من أهل النار، وقد كانوا في الدنيا لهم أبهة وشرفٌ وأموالٌ وأولادٌ، فقال لهم أصحاب الأعراف حين رأوهم منفردين في العذاب بلا ناصرٍ ولا مغيث: {ما أغنى عنكُم جمعُكم}: في الدُّنيا الذي تستدفِعون به المكاره، وتوسلون به إلى مطالبكم في الدُّنيا؛ فاليوم اضمحل ولا أغنى عنكم شيئاً، وكذلك أيُّ شيءٍ نفعكم استكباركم على الحقِّ وعلى ما جاء به وعلى مَن اتبعه؟!
{48} Kisha akataja la mahususi baada ya la jumla, akasema: "Na watu hao wa Minyanyukoni watawaita watu wanaowajua kwa alama zao." Nao ni miongoni mwa watu wa Motoni, na katika dunia hii walikuwa na fahari, na heshima, na mali, na watoto. Kwa hivyo watu wa Minyanyukoni wakawaambia walipowaona wako peke yao katika adhabu, bila ya msaidizi wala mwokozi "hakukuwafaa kitu kujumuika kwenu" katika dunia ambako mlijizuia kwako machukizo, na kufikia kwako katika kutimiza matakwa yenu katika dunia. Lakini leo kumepotea na wala hakutawafaa kitu. Na vile vile kiliwafaa nini kiburi chenu dhidi ya haki na yale iliyokuja nayo na dhidi ya yule aliyeifuata?
#
{49} ثم أشاروا لهم إلى أناس من أهل الجنة كانوا في الدنيا فقراء ضعفاء يستهزئ بهم أهل النار، فقالوا لأهل النار: {أهؤلاء}: الذين أدخلهم الله الجنة، {الذين أقسمتُم لا ينالُهُم الله برحمةٍ}: احتقاراً لهم وازدراءً وإعجاباً بأنفسكم، قد حنثتم في أيمانكم، وبدا لكم من الله ما لم يكن لكم في حساب. {ادخلوا الجنة}: بما كنتم تعملونَ؛ أي: قيل لهؤلاء الضعفاء إكراماً واحتراماً: ادخلوا الجنة بأعمالكم الصالحة، {لا خوفٌ عليكم}: فيما يُستقبل من المكاره، {ولا أنتم تحزنونَ}: على ما مضى، بل آمنون مطمئنُّون فرحون بكل خير. وهذا كقولِهِ تعالى: {إنَّ الذين أجرموا كانوا من الذين آمنوا يضحكونَ. وإذا مَرُّوا بهم يتغامَزون ... } إلى أن قال: {فاليومَ الذين آمنوا مِنَ الكُفَّارِ يضحكون. على الأرائكِ ينظُرونَ}. واختلف أهل العلم والمفسِّرون من هم أصحاب الأعراف وما أعمالهم، والصحيح من ذلك أنهم قوم تساوت حسناتهم وسيئاتهم؛ فلا رجحتْ سيئاتهم فدخلوا النار، ولا رجحت حسناتهم فدخلوا الجنة، فصاروا في الأعراف ما شاء الله، ثم إن الله تعالى يدخِلُهم برحمته الجنة؛ فإن رحمته تسبق وتغلب غضبه، ورحمته وسعت كلَّ شيءٍ.
49. Kisha wakawaashiria kuelekea kwa watu miongoni mwa wakazi wa Peponi waliokuwa masikini na wanyonge katika dunia hii, ambao watu wa Motoni walikuwa wakiwafanyia kejeli. Basi wakawaambia watu wa Motoni, "Je, hawa" ambao Mwenyezi Mungu amewaingiza Peponi, "ndio wale mlioapa kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema yoyote," kwa kuwadharau, na kuwadunisha, na kujiona kwenu. Hakika mmevunja viapo vyenu, na ikawadhihirikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale ambayo hamkuwa mmeyazingatia. "Ingieni Peponi" kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda. Yaani, waliambiwa hawa madhaifu kwa kuwatukuza na kuwaheshimu: Ingieni Peponi kwa matendo yenu wema, "hapana hofu juu yenu" kuhusu yale machukizo yatakayokuja, "wala hamtahuzunika!" Juu ya yale yaliyopita. Bali mna amani, na utulivu, na furaha juu ya kila heri. Na hayo ni kama kauli yake Mtukufu: "Hakika wale waliofanya uhalifu, walikuwa wakiwacheka wale walioamini. Na wanapopita karibu yao, wanawakonyezea macho;" mpaka akasema: "Basi leo wale walioamini ndio wanawacheka makafiri. Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia." Na wanazuoni na wafasiri walihitilafiana kuhusu ni nani watu wa Al-A`raf na matendo yao ni yapi? Na lililo sahihi katika hayo ni kuwa wao ni kaumu ambao matendo yao mema na mabaya yalilingana. Basi matendo yao mabaya hayakuzidi, ili waingie Motoni, wala mazuri yao hayakuwazidi, ili waingie Peponi. Kwa hivyo, wakawa katika Minyanyuko atakavyo Mwenyezi Mungu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa rehema zake atawaingiza Peponi. Kwa maana rehema yake ilitangulia na kushinda ghadhabu yake, na rehema yake imekienea kila kitu.
: 50 - 53 #
{وَنَادَى أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ قَالُوا إِنَّ اللَّهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ (50) الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فَالْيَوْمَ نَنْسَاهُمْ كَمَا نَسُوا لِقَاءَ يَوْمِهِمْ هَذَا وَمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ (51) وَلَقَدْ جِئْنَاهُمْ بِكِتَابٍ فَصَّلْنَاهُ عَلَى عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ (52) هَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ الَّذِينَ نَسُوهُ مِنْ قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَلْ لَنَا مِنْ شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ قَدْ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ (53)}
50. Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi: Tumiminieni maji, au chochote alichowaruzuku Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharimisha hivyo kwa makafiri. 51. Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo sisi tunawasahau kama walivyousahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu. 52. Na hakika tumewaletea Kitabu tulichokipambanua kwa elimu, uwongofu na rehema kwa watu wenye kuamini. 53. Je, lipo wanalolingojea isipokuwa matokeo yake? Siku yatatapofika matokeo yake watasema wale waliokisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe ili tufanye yasiyokuwa yale tuliyokuwa tukiyafanya? Bila ya shaka wamejihasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua.
#
{50 - 52} أي: ينادي أصحاب النار أصحاب الجنة حين يبلغُ منهم العذابُ كلَّ مبلغ وحين يمسُّهم الجوع المفرط والظمأ الموجع؛ يستغيثون بهم فيقولون: {أفيضوا علينا من الماءِ أو ممَّا رزقكم الله}: من الطعام، فأجابهم أهل الجنة بقولهم: {إنَّ الله حرَّمَهما}؛ أي: ماء الجنة وطعامها {على الكافرين}: وذلك جزاء لهم على كفرهم بآيات الله واتخاذهم دينهم الذي أُمروا أن يستقيموا عليه ووُعدوا بالجزاء الجزيل عليه {لهواً ولعباً}؛ أي: لهت قلوبهم وأعرضت عنه ولعبوا واتَّخذوه سخريًّا، أو أنهم جعلوا بدل دينهم اللهو واللعب، واستعاضوا بذلك عن الدين القيم، {وغرَّتْهم الحياة الدنيا}: بزينتها وزخرفها وكثرة دعاتِها، فاطمأنوا إليها ورضوا بها وفرحوا وأعرضوا عن الآخرة ونسوها. {فاليوم ننساهم}؛ أي: نتركهم في العذاب، {كما نسوا لقاء يومهم هذا}: فكأنهم لم يُخْلقوا إلا للدُّنيا، وليس أمامهم عرض ولا جزاء، {وما كانوا بآياتنا يجحدون}: والحال أن جحودهم هذا لا عن قصور في آيات الله وبيِّناته، بل قد {جئناهم بكتابٍ فصَّلْناه}؛ أي: بينا فيه جميع المطالب التي يحتاج إليها الخلق {على علم}؛ من الله بأحوال العباد في كل زمان ومكان، وما يصلُحُ لهم وما لا يصلُحُ ليس تفصيله تفصيل غير عالم بالأمور، فتجهله بعض الأحوال فيحكم حكماً غير مناسب، بل تفصيل من أحاط علمه بكل شيء ووسعتْ رحمتُهُ كلَّ شيء. {هدىً ورحمةً لقوم يؤمنون}؛ أي: تحصل للمؤمنين بهذا الكتاب الهداية من الضلال وبيان الحق والباطل والغي والرشد، ويحصُل أيضاً لهم به الرحمة، وهي الخير والسعادة في الدنيا والآخرة، فينتفي عنهم بذلك الضلال والشقاء.
{50 - 52} Yaani, watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi wakati adhabu itakapowafikia vikamilifu na wakati watakapoguswa na njaa nyingi na kiu kikali, wakiwaomba msaada wakisema: "Tumimieni katika maji, au katika chochote alichowaruzuku Mwenyezi Mungu," kama vile chakula. Basi watu wa Peponi wakawajibu kwa kauli yao: "Hakika Mwenyezi Mungu ameviharamisha hivyo;" yaani, maji ya Peponi na chakula chake "kwa makafiri." Na hayo ni malipo yao kwa kuzikufuru kwao Aya za Mwenyezi Mungu na kuifanyia dini yao ambayo waliamrishwa na wakaahidiwa ujira mkubwa kwa hiyo kuwa "pumbao na mchezo." Yaani, nyoyo zao zilighafilika na zikajiepusha nazo, na wakaichezea na kuichukulia kuwa ni masihara, au walifanya pumbao na kucheza badala ya dini yao, na wakaibadilisha dini iliyonyooka sawa kwa hayo, "na maisha ya dunia yakawadanganya" kwa pambo lake na marembesho yake na wingi wa walinganizi . Kwa hivyo wakatulizwa nayo, wakaridhika nayo, na wakafurahi, na wakaipa Akhera mgongo na wakaisahau. "Basi leo Sisi tunawasahau;" yaani, tunawaacha katika adhabu, "kama walivyousahau mkutano wa Siku yao hii." Basi ni kama kwamba hawakuumbwa isipokuwa kwa ajili ya dunia, na wala mbele yao hakuna kuonyeshwa matendo wala malipo. "Na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu," na hali ni kwamba kukanusha kwao huku hakutokani na upungufu wowote katika Ishara za Mwenyezi Mungu na hoja zake zilizo wazi, bali hakika "tuliwajia na Kitabu tulichokieleza kwa kina." Yaani, tulibainisha ndani yake mahitaji yote ambayo viumbe wanahitaji "kwa elimu" Kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuhusu hali za waja wake katika kila wakati na mahali, na lipi linalowafaa na lisilowafaa, kufafanua kwake si kama yule asiyejua mambo; kwa hivyo, anakosa kujua baadhi ya hali basi anafanya hukumu isiyofaa. Bali ni maelezo ya yule ambaye elimu yake imezunguka kila kitu na ambaye rehema yake inaenea kwa kila kitu. "Uwongofu na rehema kwa kaumu wanaoamini;" yaani, wale wanaokiamini kitabu hiki wanapata uwongofu kutokana na upotofu na ubainisho wa haki na batili, upotofu na uwongofu. Na pia kwacho wanapata rehema, ambayo ndiyo heri na furaha katika dunia na akhera, kwa hivyo wanaondokewa kwa hayo upotovu na mashaka.
#
{53} وهؤلاء الذين حقَّ عليهم العذاب لم يؤمنوا بهذا الكتاب العظيم ولا انقادوا لأوامره ونواهيه، فلم يبق فيهم حيلة إلاَّ استحقاقُهم أن يحلَّ بهم ما أخبر به القرآن، ولهذا قال: {هل ينظُرون إلا تأويلَه}؛ أي: وقوع ما أخبر به؛ كما قال يوسف عليه السلام حين وقعت رؤياه: {هذا تأويلُ رؤيايَ مِن قَبْلُ}. {يومَ يأتي تأويلُهُ يقول الذين نسوه من قبل}: متندِّمين متأسِّفين على ما مضى متشفِّعين في مغفرة ذنوبهم مقرِّين بما أخبرت به الرسل: {قد جاءت رُسُلُ ربِّنا بالحقِّ فهل لنا من شفعاءَ فيشفعوا لنا أو نُردُّ}: إلى الدنيا؛ {فنعملَ غير الذي كُنَّا نعملُ}: وقد فات الوقتُ عن الرُّجوع إلى الدنيا؛ فما تنفعُهم شفاعة الشافعين. وسؤالهم الرجوع إلى الدنيا ليعملوا غيرَ عملهم كذبٌ منهم، مقصودُهم به دفعُ ما حلَّ بهم؛ قال تعالى: {ولو رُدُّوا لَعادوا لِما نُهوا عنه وإنَّهم لَكاذبونَ}. {قد خسروا أنفسَهم}: حين فوَّتوها الأرباحَ وسَلَكوا بها سبيل الهلاك، وليس ذلك كخسران الأموال والأثاث أو الأولاد، إنما هذا خسرانٌ لا جُبْرانَ لمصابِهِ. {وضلَّ عنهم ما كانوا يفترونَ}: في الدُّنيا مما تُمَنِّيهم أنفسُهم به، ويعدُهم به الشيطان، قدموا على ما لم يكن لهم في حساب، وتبيَّن لهم باطلهم وضلالهم، وصدق ما جاءتهم به الرسل.
{53} Na hawa ambao walithibitikia na adhabu, hawakukiamini Kitabu hiki kitukufu, wala hawakufuata amri zake na makatazo yake, kwa hivyo hawakusalia hila yoyote isipokuwa kustahiki kwao kupatwa na yale ambayo Qur-ani ilijulisha juu yake. Na ndiyo maana akasema, "Je, lipo wanalolingojea isipokuwa matokeo yake?" Yaani, kutokea kwa yale aliyojulisha juu yake, kama vile Yusuf, amani iwe juu yake, alivyosema ilipotokea ndoto yake: "Haya ndiyo matokeo ya ndoto yangu ya kabla." "Siku yatakapofika matokeo yake watasema wale waliokisahau hapo kabla," wakijuta na kusononeka juu ya yale yaliyopita, na wakiomba uombezi katika kufutiwa dhambi zao, wakikiri yale waliyojulisha juu yake Mitume: "Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe" katika dunia; "ili tufanye yasiyokuwa yale tuliyokuwa tukiyafanya?" Lakini wakati ulipita wa sisi kurejea duniani; basi Uombezi wa waombezi hautawafaa. Na kuomba kwao warejee katika dunia ili wafanye matendo ambayo si yale waliyokuwa wakifanya ni uongo wao tu. Nia yao kwa hilo ni kuyazuia yale yaliyowafika. Amesema yeye Mtukufu: "Na lau wangerudishwa, basi bila ya shaka wangerejea katika yale waliyokatazwa, nao hakika wao ni waongo." "Bila ya shaka wamejikhasiri nafsi zao;" wakati walipozipotezea faida na wakazipitisha katika njia ya maangamio. Na hilo si sawa na kuhasiri mali na vyombo, au watoto; bali hii ni hasara isiyokuwa na malipo kwa aliyesibiwa. "Na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua" katika dunia hii, kutokana na yale ambayo nafsi zao ziliwadanganya nayo, na Shetani akawaahidi hayo. Kwa hivyo, wakayaendea yale ambayo hawakuwa wakiyatarajia, na ikawabainikia batili yao na upotovu wao, na yakawa kweli yale waliyowajia nayo Mitume.
: 54 #
{إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ تَبَارَكَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ (54)}.
54. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu ambaye aliziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazotumika kwa amri yake. Fahamuni! Ni kwake kuumba na amri. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
#
{54} يقول تعالى مبيناً أنه الربُّ المعبود وحده لا شريك له: {إنَّ ربَّكم اللهُ الذي خَلَقَ السمواتِ والأرضَ}: وما فيهما على عظمهما وسعتهما وإحكامهما وإتقانهما وبديع خلقهما {في ستة أيام}: أولها يوم الأحد، وآخرها يوم الجمعة. فلما قضاهما وأودع فيهما من أمره ما أودع؛ {استوى}: تبارك وتعالى {على العرش}: العظيم الذي يسع السماوات والأرض وما فيهما وما بينهما؛ استوى استواءً يليق بجلاله وعظمته وسلطانه، فاستوى على العرش، واحتوى على الملك، ودبر الممالك، وأجرى عليهم أحكامه الكونيّة وأحكامه الدينيّة، ولهذا قال: {يُغْشي الليلَ}: المظلم {النهارَ}؛ المضيء، فيظلم ما على وجه الأرض، ويسكُن الآدميون، وتأوي المخلوقات إلى مساكنها، ويستريحون من التعب والذهاب والإياب الذي حصل لهم في النهار. {يطلُبُه حثيثاً}: كلَّما جاء الليل؛ ذهب النهار، وكلَّما جاء النهار؛ ذهب الليل ... وهكذا أبداً على الدوام حتى يطوي الله هذا العالم، وينتقل العباد إلى دار غير هذه الدار. {والشمس والقمر والنجوم مسخرات بأمره}؛ أي: بتسخيره وتدبيره الدالِّ على ما له من أوصاف الكمال، فخلقها وعظمها دالٌّ على كمال قدرته، وما فيها من الإحكام والانتظام والإتقان دالٌّ على كمال حكمته، وما فيها من المنافع والمصالح الضروريَّة وما دونها دالٌّ على سعة رحمته، وذلك دال على سعة علمه، وأنه الإله الحقُّ الذي لا تنبغي العبادة إلا له. {ألا له الخَلْق والأمر}؛ أي: له الخلق الذي صدرت عنه جميع المخلوقات علويّها وسفليّها أعيانها وأوصافها وأفعالها والأمر المتضمن للشرائع والنبوات؛ فالخلق يتضمَّن أحكامه الكونيَّة القدريَّة، والأمر يتضمَّن أحكامه الدينيَّة الشرعيَّة، وثم أحكام الجزاء، وذلك يكون في دار البقاء. {تبارك الله}؛ أي: عَظُم وتعالى وكثر خيره وإحسانه، فتبارك في نفسه لعظمة أوصافه وكمالها، وبارك في غيره بإحلال الخير الجزيل والبر الكثير؛ فكل بركة في الكون فمن آثار رحمته، ولهذا قال: {تبارك الله ربُّ العالمين}.
{54} Anasema Yeye Mtukufu akieleza kuwa Yeye ndiye Mola Mlezi anayeabudiwa peke yake, hana mshirika yeyote: "Hakika Mola wenu Mlezi ni mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi," na vilivyomo ndani yake, pamoja na ukubwa wake, na upana wake, usawa wake, uimara wake, na uumbaji wake wa ajabu "katika siku sita" ya kwanza yake ni Jumapili, na ya mwisho yake ni Ijumaa. Na alipoyatimiza na akatia ndani yake aliyoyatia, "alitawala" Yeye Mwingi wa baraka, Mtukufu "juu ya Kiti cha Enzi;" kikuu ambacho kinaenea mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake na vilivyomo baina yake. Alikaa juu kukaa kunakolingana na Utukufu wake, na Ukuu wake, na Mamlaka Yake. kwa hivyo alikaa juu kwenye Kiti cha Enzi, na akamiliki ufalme, na akaendesha wamilikiwa, na akatekeleza juu yao kanuni Zake za kiulimwengu na hukumu zake za kidini. Na ndiyo maana akasema, "Huufunika usiku" wenye giza “mchana” wenye mwangaza, kwa hivyo vilivyo juu ya uso wa ardhi vinakuwa katika giza, na wanadamu wanatulia, na viumbe vinaenda katika makazi yao, na wanapumzika kutokana na uchovu na kwenda na kurudi vilivyowatokea wakati wa mchana. "Unaoufuata upesi upesi" kila unapokuja usiku, mchana unakwenda. Na kila mchana unapokuja, usiku unakwenda... na kuendelea hivi milele mpaka Mwenyezi Mungu atakapoukunja ulimwengu huu, na waja wahamie kwenye nyumba nyingine isiyokuwa nyumba hii. "Na jua, na mwezi, na nyota vilivyotiishwa kwa amri yake;" yaani, kwa kuvitiisha kwake na uendeshaji wake, ambao unaashiria sifa za ukamilifu alizo nazo. Kwa hivyo uumbaji wake na ukuu wake unaonyesha ukamilifu wa uwezo wake, na usawa ulioko ndani yake, na mpangilio mzuri, na ustadi mkubwa vinaonyesha ukamilifu wa hekima yake. Na muhimu manufaa yaliyomo ndani yake na masilahi ya lazima na yaliyo chini yake yanaonyesha upana wa rehema yake. Na hilo linaonyesha upana wa elimu yake, na kwamba Yeye ndiye Mungu wa haki, ambaye haifai kufanywa ibada isipokuwa kwa ajili yake. "Fahamuni! Ni kwake kuumba na amri;" yaani, ni wake uumbaji ambao viumbe vyote vilitokana nao, vya juu vyake na vya chini vyake, hivyo vyenyewe, na sifa zake, na matendo yake, na amri inayojumuisha sheria mbalimbali na bishara mbalimbali. Basi Uumbaji unajumuisha hukumu zake za kiulimwengu za kimajaaliwa, na amri pia inajumuisha hukumu zake za kisheria za kidini. Na kisha kuna hukumu zake za malipo, na hilo litakuwa katika nyumba ile ya kudumu. "Mwenyezi Mungu ni mwingi wa baraka." Yaani, ni mkuu na Mtukufu, na ni nyingi heri zake na ihsani zake, basi yeye Mwenyewe ni Mwingi wa baraka kwa sababu ya ukubwa wa sifa zake na ukamilifu wake, na akawabariki asiyekuwa Yeye kwa kuwapa heri kubwa na wema mwingi. Kwa hivyo, kila baraka katika ulimwengu ni katika athari za rehema yake; na ndiyo maana akasema: "Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mola Mlezi wa viumbe vyote."
Na alipotaja katika ukuu wake na utukufu wake, vinavyoashiria wenye akili kwamba Yeye pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa, anayekusudiwa katika haja zote, akaamuru yanayotokana na hayo, akasema:
: 55 - 56 #
{ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ (55) وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا إِنَّ رَحْمَتَ اللَّهِ قَرِيبٌ مِنَ الْمُحْسِنِينَ (56)}.
55. Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi wavukao mipaka. 56. Wala msifanye uharibifu katika dunia baada ya kutengenea kwake. Na mwombeni kwa hofu na kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wafanyao uzuri.
#
{55} الدعاء يدخل فيه دعاء المسألة ودعاء العبادة، فأمر بدعائه {تضرعاً}؛ أي: إلحاحاً في المسألة ودؤوباً في العبادة، {وخُفية}؛ أي: لا جهراً وعلانيةً يُخاف منه الرياء، بل خفية وإخلاصاً لله تعالى. {إنه لا يحبُّ المعتدين}؛ أي: المتجاوزين للحدِّ في كل الأمور، ومن الاعتداء كون العبد يسأل الله مسائل لا تصلح له، أو يتنطع في السؤال، أو يبالغ في رفع صوته بالدعاء؛ فكلُّ هذا داخل في الاعتداء المنهيِّ عنه.
{55} Dua inajumuisha dua ya kuomba kitu na dua ya ́ibada. Basi akaamrisha kufanyiwa dua "kwa kunyenyekea." Yaani, kung'ang'ana katika kuomba na kufanya ́ibaada kuwa ada, "na kwa siri." Yaani, si kwa sauti kubwa na uwazi kwa kuhofia kujionyesha, bali kwa siri na kumkusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake. "Hakika Yeye hawapendi wavukao mipaka;" yaani, wale wanaovuka mipaka katika mambo yote. Na katika kuvuka mipaka ni mja kumuomba Mwenyezi Mungu maombi yasiyomfaa, au kujitwika ufasaha usiolazimu, au azidishe katika kuinua sauti yake katika kuomba. Basi yote haya yanajumuishwa katika kuvuka kulikokatazwa.
#
{56} {ولا تفسدوا في الأرض}: بعمل المعاصي {بعد إصلاحها}: بالطاعات؛ فإن المعاصي تفسد الأخلاق والأعمال والأرزاق؛ كما قال تعالى: {ظهر الفسادُ في البرِّ والبحر بما كسبتْ أيدي الناس}: كما أنَّ الطاعات تصلُحُ بها الأخلاق والأعمال والأرزاق وأحوال الدُّنيا والآخرة. {وادعوه خوفاً وطمعاً}؛ أي: خوفاً من عقابه، وطمعاً في ثوابه، طمعاً في قبولها وخوفاً من ردِّها، لا دعاء عبد مدلٍّ على ربه، قد أعجبته نفسه، ونزَّل نفسه فوق منزلته، أو دعاء من هو غافل لاهٍ. وحاصل ما ذكر الله من آداب الدعاء: الإخلاصُ فيه لله وحده؛ لأنَّ ذلك يتضمَّنه الخفية، وإخفاءه وإسراره، وأن يكون القلبُ خائفاً طامعاً لا غافلاً ولا آمناً ولا غير مبالٍ بالإجابة، وهذا من إحسان الدعاء؛ فإن الإحسان في كل عبادة بَذْلُ الجهد فيها وأداؤها كاملةً لا نقصَ فيها بوجه من الوجوه. ولهذا قال: {إنَّ رحمةَ الله قريبٌ من المحسنين}: في عبادة الله، المحسنين إلى عباد الله، فكلَّما كان العبد أكثر إحساناً؛ كان أقرب إلى رحمة ربِّه، وكان ربُّه قريباً منه برحمته. وفي هذا من الحثِّ على الإحسان ما لا يخفى.
{56} "Wala msifanye uharibifu katika dunia} kwa kufanya maasia "baada ya kutengenea kwake" kwa mambo ya utii. Kwa maana maasia huharibu maadili, na matendo, na riziki. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "umedhihiri uharibifu katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu." Kama vile utiifu yanatengenea kwayo maadili, na matendo, na riziki, na hali za dunia na akhera. "Na muombeni kwa hofu na kutumai." Yaani, kwa kuhofu adhabu yake, na kwa kutumai malipo yake, na kwa kutumai kukubaliwa kwake na kwa kuhofu kukataliwa kwake, na siyo dua ya mja mwenye kiburi kwa Mola wake Mlezi, ambaye anajiona na nafsi yake, na ameiweka nafsi yake zaidi ya daraja lake, au dua ya alighafilika, aliyejisahau. Na jumla ya yale aliyoyataja mwenyezi Mungu miongoni mwa adabu za dua ni: kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake ndani yake; kwa sababu hilo linaingia ndani ya kufanya kwa siri, na kuificha na kuifanya iwe ya siri kabisa, na kwamba moyo uwe na hofu na tumaini, sio kughafilika, wala kuwa na amani, wala kutojali kujibiwa. Na hili ni katika kufanya dua kwa wema, kwa maana, kufanya wema katika kila aina ya ibada ni kufanya juhudi ndani yake na kuifanya kikamilifu, bila ya upungufu wowote ndani yake kwa njia yoyote ile. Na ndiyo maana akasema, "Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wafanyao uzuri," katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, wale wanaowafanyia uzuri waja wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo kila mja anavyokuwa mfanya uzuri, anakuwa karibu zaidi na rehema za Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi anakuwa karibu zaidi naye kwa rehema yake. Na katika hili kuna himizo lisilofichika juu ya kufanya uzuri.
: 57 - 58 #
{وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ حَتَّى إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَيِّتٍ فَأَنْزَلْنَا بِهِ الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِنْ كُلِّ الثَّمَرَاتِ كَذَلِكَ نُخْرِجُ الْمَوْتَى لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ (57) وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا كَذَلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ (58)}.
57. Na Yeye ndiye anayetuma pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapobeba mawingu mazito, tunayapeleka kwenye nchi iliyokufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, na tukatoa kwayo kila aina ya matunda. Basi namna hiyo ndivyo tunavyowafufua wafu, ili mkumbuke. 58. Na ardhi nzuri hutoka mimea yake kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Nayo ardhi ambayo ni mbaya haitoki isipokuwa mimea michache, isiyokuwa na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara (Aya) kwa kaumu wanaoshukuru.
#
{57} بين تعالى أثراً من آثار قدرته ونفحة من نفحات رحمته، فقال: {وهو الذي يرسل الرياح بشراً بين يدي رحمته}؛ أي: الرياح المبشرات بالغيث، التي تثيره بإذن الله من الأرض، فيستبشر الخلق برحمة الله، وترتاح لها قلوبهم قبل نزوله. {حتى إذا أقلَّت}: الرياح {سحاباً ثقالاً}: قد أثاره بعضها، وألفه ريحٌ أخرى وألقحه ريح أخرى، {سُقْناه لبلدٍ ميِّتٍ}: قد كادت تهلك حيواناتُهُ وكاد أهله أن ييأسوا من رحمة الله. {فأنزلنا به}؛ أي: بذلك البلد الميت {الماء}: الغزير من ذلك السحاب، وسخَّر الله له ريحاً تدره وريحاً تفرِّقه بإذن الله. فأنبتنا به من كلِّ الثمرات: فأصبحوا مستبشرين برحمة الله، راتعين بخير الله. وقوله: {كذلك نخرِجُ الموتى لعلَّكم تَذَكَّرون}؛ أي: كما أحيينا الأرض بعد موتها بالنبات كذلك نخرج الموتى من قبورهم بعدما كانوا رفاتاً متمزِّقين. وهذا استدلال واضح؛ فإنه لا فرق بين الأمرين؛ فمنكِرُ البعثِ استبعاداً له مع أنه يرى ما هو نظيره من باب العناد وإنكار المحسوسات. وفي هذا الحثُّ على التذكُّر والتفكُّر في آلاء الله والنظر إليها بعين الاعتبار والاستدلال لا بعين الغفلة والإهمال.
{57} Mwenyezi Mungu Mtukufu alibainisha athari katika athari za uweza wake, na upepo katika pepo za rehema yake, akasema: "na Yeye ndiye anayezituma pepo ziletazo bishara mbele ya rehema yake," Yaani, pepo ziletazo bishara ya mvua, ambazo, Mwenyezi Mungu akipenda huinyanyua kutoka ardhini, kwa hivyo viumbe wanafurahia kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, na nyoyo zao zinatulia kwa sababu yake kabla ya kuteremka kwake. "Mpaka zinapobeba" pepo hizo "mawingu mazito" baadhi yake ilitimuliwa nazo na upepo mwingine ukaziunganisha, na upepo mwingine ukayapandishana, "tunayapeleka kwenye nchi iliyokufa." Wanyama wake walikuwa karibu kuangamia, na wakazi wake walikuwa karibu kukata tamaa na rehema ya mwenyezi Mungu. "Kisha tunateremsha huko;" yaani, katika ardhi hiyo iliyokufa "maji" mengi kutoka katika mawingu hayo. Na Mwenyezi Mungu aliyatiishia upepo unaoyapeperusha na upepo unaoyatengenisha kwa adhini ya Mwenyezi Mungu. Basi tukaotesha kwayo kila aina ya matunda; kwa hivyo, wakawa wanafurahi kwa rehema ya Mwenyezi Mungu na wanafurahia heri ya Mwenyezi Mungu. Na kauli yake: "Hivyo ndivyo tunavyowatoa wafu ili mkumbuke," yaani, kama vile tulivyoifufua ardhi baada ya kufa kwake kwa mimea, basi hivyo ndivyo tutakavyowatoa wafu kutoka katika makaburi yao baada ya kuwa kwoa mabaki yaliyochanika. Na huku ni kutumia ushahidi ulioo wazi kwa maana, hakuna tofauti yoyote kati ya mambo hayo mawili haya. Basi mkanusha ufufuo kwa kuona kuwa hauwezekani pamoja na kwamba anaona yale yaliyo mfano wake basi ni kwa njia ya ukaidi tu na kukanusha mambo ya hisia. Na katika hili kuna himizo juu ya kukumbuka na kutafakari juu ya neema za Mwenyezi Mungu, na kuzitazama kwa jicho la mazingatio na kuzitumia kama hoja, si kwa jicho la kughafilika na kupuuza.
#
{58} ثم ذكر تفاوت الأراضي التي ينزل عليها المطر، فقال: {والبلدُ الطيِّب}؛ أي: طيب التربة والمادة، إذا نزل عليه المطر؛ {يخرج نباتُهُ}: الذي هو مستعدٌّ له {بإذن ربِّه}؛ أي: بإرادة الله ومشيئته، فليست الأسباب مستقلَّةً بوجود الأشياء حتى يأذن الله بذلك. {والذي خَبُثَ}: من الأراضي {لا يخرُجُ إلَّا نَكِداً}؛ أي: إلا نباتاً خاسًّا لا نفع فيه ولا بركة. {كذلك نصرِّف الآيات لقوم يشكرونَ}؛ أي: ننوِّعها، ونبيِّنها، ونضرب فيها الأمثال، ونسوقها لقوم يشكرون الله بالاعتراف بنعمه والإقرار بها وصرفها في مرضاة الله؛ فهم الذين ينتفعون بما فصل الله في كتابه من الأحكام والمطالب الإلهية؛ لأنَّهم يرونها من أكبر النعم الواصلة إليهم من ربهم، فيتلقونها مفتقرين إليها فرحين بها، فيتدبَّرونها ويتأمَّلونها، فيبين لهم من معانيها بحسب استعدادهم. وهذا مثالٌ للقلوب حين ينزل عليها الوحي الذي هو مادةُ الحياة كما أن الغيث مادة الحيا؛ فإن القلوب الطيبة حين يجيئها الوحي تقبله وتعلمه وتنبُتُ بحسب طيب أصلها وحسن عنصرها، وأما القلوب الخبيثة التي لا خير فيها؛ فإذا جاءها الوحي؛ لم يجد محلاًّ قابلاً، بل يجدها غافلة معرضة أو معارضة، فيكون كالمطر الذي يمرُّ على السباخ والرمال والصخور فلا يؤثِّر فيها شيئاً، وهذا كقوله تعالى: {أنزل من السماءِ ماءً فسالتْ أوديةٌ بِقَدَرِها فاحتملَ السيلُ زبداً رابياً ... } الآيات.
58. Kisha akataja kutofautiana kwa ardhi mbalimbali zinazonyeshewa na mvua. Akasema: "Na ardhi nzuri;" yaani, yenye udongo mzuri, mvua inaponyesha juu yake; "hutoka Mmea yake" iliyo tayari kwa ajili yake "kwa idhini ya Mola wake Mlezi." Yaani, kwa kutaka kwa Mwenyezi Mungu na mapenzi yake, na sababu hazijitegemei peke yake tu kwa kuwepo kwa vitu mpaka Mwenyezi Mungu aruhusu hilo. "Nayo ile ambayo ni mbaya" miongoni mwa ardhi "haitoki isipokuwa mibovu." Yaani, isipokuwa mimea mibaya isiyokuwa na manufaa wala baraka. "Na hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara (Aya) kwa kaumu wanaoshukuru." Yaani, tunazitofautisha, na tunazifafanua, na tunazitolea mifano, na tunazipeleka kwa kaumu wanaomshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuzikubali neema zake, na kuzikiri, na kuzitumia katika radhi za Mwenyezi Mungu. Basi hao ndio wanaonufaika na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaeleza kwa kina katika Kitabu chake miongoni mwa hukumu mbalimbali na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu wanaziona kuwa ni miongoni mwa neema kubwa zaidi zilizowafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi wanazipokea kwa kuzihitaji na wanazifurahia; kwa hivyo, wanazizingatia na kuzitafakari. Kwa hivyo, inawabainikia katika maana zake kulingana na utayari wao. Na huu ni mfano wa nyoyo wakati unapoziteremkia wahyi, ambao ndio kiini cha uhai, kama vile mvua ilivyo kiini cha uhai. Kwani, nyoyo nzuri wakati zinapojiwa na wahyi, zinaukubali, na kuufunza, na kuota kulingana na uzuri wa chembe zake. Na ama nyoyo mbovu ambazo hazina heri yoyote ndani yake, unapozijia wahyi, haupati pahala panapofaa, bali unazikuta zimeghafilika, zimepena mgongo au zinapingana. Kwa hivyo, ikawa ni kama mvua ambayo inapita juu ya ardhi ya chumvi, na ya mchanga na ya mawe, hivyo basi haiathiri ndani yake hata kidogo. Na hili ni kama kauli yake Mtukufu: "Aliteremsha maji kutoka mbinguni, na mabonde yakamiminika kwa kiasi chake, na mafuriko yakabeba mapovu yaliyokusanyika juu yake..." hadi mwisho wa Aya hizi.
: 59 - 64 #
{لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَقَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ (59) قَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (60) قَالَ يَاقَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَكِنِّي رَسُولٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ (61) أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنْصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ (62) أَوَعَجِبْتُمْ أَنْ جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِنْ رَبِّكُمْ عَلَى رَجُلٍ مِنْكُمْ لِيُنْذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (63) فَكَذَّبُوهُ فَأَنْجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ (64)}.
59. Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninawahofia adhabu ya Siku iliyo kuu. 60. Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotofu ulio dhahiri. 61. Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 62. Nawafikishia Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na ninawanasihi; na ninayajua kwa Mwenyezi Mungu msiyoyajua nyinyi. 63. Je, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya mtu aliye ni mmoja katika nyinyi, ili akuonyeni na ili mumche Mungu, na ili mpate kurehemewa? 64. Basi walimkanusha. Nasi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye katika jahazi. Na tukawazamisha wale waliozikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu vipofu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja ushahidi wa tauhidi yake katika sentensi halali; Aliunga mkono hilo kwa kutaja yaliyowapata Mitume waliolingania tauhidi pamoja na mataifa yao waliokadhibisha hilo; na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaunga mkono watu wa tauhidi na kuwaangamiza wale waliokuwa wagumu na hawakunyenyekea kwao, na jinsi wito wa Mitume ulivyokubalika juu ya dini moja na imani moja.
#
{59} فقال عن نوح أول المرسلين: {لقد أرسلنا نوحاً إلى قومه}: يدعوهم إلى عبادة الله وحده حين كانوا يعبدُون الأوثان، {فقال}: لهم: {يا قوم اعبُدوا الله}؛ أي: وحدوه، {ما لكم من إلهٍ غيرُهُ}: لأنه الخالق الرازق المدبِّر لجميع الأمور، وما سواه مخلوقٌ مدبَّر ليس له من الأمر شيء. ثم خوَّفهم إن لم يطيعوه عذابَ الله، فقال: {إنِّي أخافُ عليكم عذابَ يوم عظيم}: وهذا من نصحه عليه الصلاة والسلام وشفقته عليهم؛ حيث خاف عليهم العذاب الأبديَّ والشقاء السرمديَّ؛ كإخوانه من المرسلين، الذين يشفِقون على الخَلْق أعظم من شفقة آبائهم وأمهاتهم.
{59} Amesema Nuhu wa kwanza katika Mitume: "Tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake" akiwalingania wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake walipokuwa wakiabudu masanamu. Akawaambia: Enyi watu wangu! kumwabudu Mungu;" yaani, muunganisheni, "Nyinyi hamna mungu isipokuwa Yeye." Kwa sababu, Yeye ndiye Muumbaji, Mlinzi, Mtawala wa kila kitu, na kila kitu kisichokuwa Yeye ni kiumbe kilichoumbwa na hakina uwezo juu Yake wala hakimiliki juu ya kitu chochote. Kisha akawatia hofu adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa hawakumtii, na akasema: "Mimi nawahofia adhabu ya Siku kubwa." Hii ni sehemu ya nasaha zake, rehema na amani ziwe juu yao. Ambapo waliogopa mateso ya milele na taabu ya milele. Kama ndugu zake katika Mitume ambao huruma yao kwa viumbe ni kubwa kuliko huruma ya baba zao na mama zao.
#
{60} فلما قال لهم هذه المقالة؛ ردُّوا عليه أقبح ردٍّ، فقال {الملأ من قومِهِ}؛ أي: الرؤساء الأغنياء المتبوعون، الذين قد جرت العادة باستكبارهم على الحقِّ وعدم انقيادهم للرسل: {إنا لنراك في ضلال مبين}: فلم يكفِهِم قبَّحَهُمُ اللهُ أنهم لم ينقادوا له، بل استكبروا عن الانقياد له، وقدحوا فيه أعظم قدح، ونسبوه إلى الضلال، ولم يكتفوا بمجرَّد الضلال، حتَّى جعلوه ضلالاً مبيناً واضحاً لكلِّ أحدٍ!! وهذا من أعظم أنواع المكابرة، التي لا تروج على أضعف الناس عقلاً، وإنَّما هذا الوصف منطبقٌ على قوم نوح، الذين جاؤوا إلى أصنام قد صوَّروها ونحتوها بأيديهم من الجمادات التي لا تسمع ولا تبصِرُ ولا تغني عنهم شيئاً، فنزَّلوها منزلة فاطر السماوات، وصرفوا لها ما أمكنهم من أنواع القُرُبات، فلولا أنَّ لهم أذهاناً تقوم بها حُجَّة الله عليهم؛ لَحُكِمَ عليهم بأن المجانين أهدى منهم، بل هم أهدى منهم وأعقل.
{60} Alipowaambia maneno haya, wakamjibu kwa jibu baya zaidi, na wakasema: “Waheshimiwa katika kaumu yake”; yaani, viongozi matajiri wanaofuatwa, ambao wamezoea kutakabari kwa haki na kutowanyenyekea Mitume: "Hakika sisi tunakuona uko katika upotovu ulio wazi," na fedheha ya Mwenyezi Mungu juu yao haikuwatosheleza. Wamenyenyekea Kwake, bali walikuwa wakitakabari na wakamtupia tuhuma kubwa, na wakamtia upotevu, wala hawakuridhika na upotovu tu, mpaka waufanye kuwa ni upotovu ulio wazi kwa kila mtu! Hii ni moja ya aina kubwa kabisa ya kiburi, ambayo haitumiki kwa watu dhaifu wa akili. Bali, maelezo haya yanawahusu watu wa Nuh, ambao walikuja kwenye masanamu waliyokuwa wakiyatengeneza na kuyachonga kwa mikono yao wenyewe kutoka kwa vitu visivyo na uhai. Msikie, wala msione, na wala haziwafai kitu, basi wakawaweka katika cheo cha Muumba wa mbingu, na wakawafanyia wanayostahiki, wao ni wenye uwezo wa kila aina ya ukaribu. Walikuwa na akili ambazo kwazo uthibitisho wa Mungu ungeweza kuthibitishwa dhidi yao; wangehukumiwa kuwa wendawazimu wameongoka zaidi kuliko wao, na hakika wao walikuwa waongofu na wenye akili zaidi kuliko wao.
#
{61 - 62} فرد نوح عليهم رَدًّا لطيفاً وترقَّق لهم لعلهم ينقادون له، فقال: {يا قوم ليس بي ضلالةٌ}؛ أي: لست ضالاًّ في مسألة من المسائل من جميع الوجوه، وإنما أنا هادٍ مهتدٍ، بل هدايتُهُ عليه الصلاة والسلام من جنس هداية إخوانِهِ أولي العزم من المرسلين، أعلى أنواع الهدايات وأكملها وأتمها، وهي هداية الرسالة التامَّة الكاملة، ولهذا قال: {ولكنِّي رسولٌ من ربِّ العالمينَ}؛ أي: ربي وربكم ورب جميع الخلق، الذي ربَّى جميع الخلق بأنواع التربية، الذي من أعظم تربيته أن أرسل إلى عباده رسلاً تأمرهم بالأعمال الصالحة والأخلاق الفاضلة والعقائد الحسنة، وتنهاهم عن أضدادها، ولهذا قال: {أبلِّغُكم رسالاتِ ربِّي وأنصحُ لكم}؛ أي: وظيفتي تبليغكم ببيان توحيده وأوامره ونواهيه على وجه النصيحة لكم والشفقة عليكم، {وأعلمُ من اللهِ مالا تعلمونَ}: فالذي يتعيَّن أن تطيعوني وتنقادوا لأمري إن كنتم تعلمونَ.
{61 - 62} Nuh akawajibu kwa wema na akawaonea huruma ili wapate kunyenyekea kwake, na akasema, "Enyi watu wangu! Yaani mimi sijapotea katika jambo lolote katika nyanja zote, bali mimi ni mwongozo, bali uwongofu wake, rehema na amani ziwe juu yake, ni kama uwongofu wa ndugu zake, Mwenye nguvu miongoni mwa Mitume. Aina ya uwongofu wa juu kabisa, uliokamilika na uliokamilika, nao ni uwongofu wa ujumbe uliokamilika na uliokamilika. Na ndiyo maana akasema, "Lakini mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote." Yaani, Mola wangu, Mola wenu Mlezi, na Mola wa viumbe vyote, ambaye ameviinua viumbe vyote kwa aina mbalimbali za elimu, na malezi yake makubwa zaidi ni kuwatuma kwa waja wake Mitume wenye kuwaamrisha kutenda mema, maadili mema, na wema, na Imani, na kuwakataza kinyume chake. Na ndiyo maana akasema, "Nawafikishia Aya za Mola wangu Mlezi na nawanasihi." Yaani, kazi yangu ni kuwafikishia ufafanuzi wa tauhidi yake na maamrisho yake na makatazo yake kwa namna ya kukunasihi na kukuhurumia. "Na ninayajua kwa Mwenyezi Mungu msiyoyajua." Ni wajibu kwamba mnitii mimi na mtiini amri yangu ikiwa mnajua.
#
{63} {أوَعَجِبْتُم أن جاءكم ذِكْرٌ من ربِّكم على رجل منكم}؛ أي: كيف تعجبون من حالة لا ينبغي العجب منها، وهو أن جاءكم التذكير والموعظة والنصيحة على يد رجل منكم، تعرفون حقيقتَه وصدقَه وحالَه؛ فهذه الحال من عناية الله بكم وبرِّه وإحسانه الذي يُتَلَقَّى بالقبول والشكر. وقوله: {لِيُنذِرَكُم ولتتَّقوا ولعلَّكم تُرحمون}؛ أي: لينذركم العذاب الأليم، وتفعلوا الأسباب المنجية من استعمال تقوى الله ظاهراً وباطناً، وبذلك تحصُلُ عليهم، وتنزل رحمة الله الواسعة.
{63} "Je, mnastaajabu kukufikieni ukumbusho kutoka kwa Mola wenu Mlezi juu ya mtu miongoni mwenu?" Yaani, vipi mnastaajabishwa na hali ambayo haifai kustaajabishwa nayo?Na ni kwamba mmwejiwa na ukumbusho, na mawaidha, na nasaha zilizokuja kutoka kwa mtu miongoni mwenu, ambaye ukweli, uaminifu, na hali yake mnaijua? Hali hii ya mambo ni matokeo ya utunzaji wa Mungu kwako, haki Yake, na ukarimu Wake, ambao unapokelewa kwa kukubalika na shukrani. Na kauli yake: {Ili akuonyeni, na mpate kuogopa, na mrehemewe}. Yaani: kukuonyasheni adhabu iumizayo, na kufanya sababu za kuokoa kwa kumcha Mwenyezi Mungu kwa nje na kwa ndani, na hivyo mtazipata, na rehema kubwa ya Mwenyezi Mungu itashuka.
#
{64} فلم يفد فيهم ولا نَجَحَ، {فكذَّبوه فأنجَيْناه والذين معه في الفُلْك}؛ أي: السفينة التي أمر الله نوحاً عليه السلام بصنعها، وأوحى إليه أن يحمِلَ من كلِّ صنف من الحيوانات زوجين اثنين وأهله ومَنْ آمن معه، فحملهم فيها، ونجَّاهم الله بها. {وأغرقنا الذين كذَّبوا بآياتنا إنَّهم كانوا قوماً عَمِينَ}: عن الهدى، أبصروا الحقَّ، وأراهم الله على يد نوح من الآيات البيناتِ ما به يؤمِنُ أولو الألباب، فسخروا منه، واستهزؤوا به، وكفروا.
{64} Lakini haikiwafaidi kitu wala kufaulu "Basi wakamkadhibisha, kwa hivyo tukamwokoa yeye na wale waliokuwa pamoja naye katika safina." Yaani, safina ile ambayo Mwenyezi Mungu alimwamuru Nuhu, amani iwe juu yake, kuitengeneza, na akamfunulia wahyi kuwa abebe jozi katika kila aina ya mnyama, na jamaa zake, na wale walioamini pamoja naye. Basi akawabeba ndani yake, na Mwenyezi Mungu akawaokoa kwa hiyo. "Na tuliwazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu, hakika wao walikuwa ni kaumu vipofu" wa uwongofu. Waliiona haki, na Mwenyezi Mungu akawaonyesha kwa mkono wa Nuhu katika Ishara zilizo wazi ambazo wenye akili wanaziamini, lakini wakamdhihaki, wakamfanyia stihizai, na wakakufuru.
: 65 - 72 #
{وَإِلَى عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا قَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ أَفَلَا تَتَّقُونَ (65) قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ (66) قَالَ يَاقَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَكِنِّي رَسُولٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ (67) أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ (68) أَوَعَجِبْتُمْ أَنْ جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِنْ رَبِّكُمْ عَلَى رَجُلٍ مِنْكُمْ لِيُنْذِرَكُمْ وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِنْ بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ وَزَادَكُمْ فِي الْخَلْقِ بَسْطَةً فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (69) قَالُوا أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللَّهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ (70) قَالَ قَدْ وَقَعَ عَلَيْكُمْ مِنْ رَبِّكُمْ رِجْسٌ وَغَضَبٌ أَتُجَادِلُونَنِي فِي أَسْمَاءٍ سَمَّيْتُمُوهَا أَنْتُمْ وَآبَاؤُكُمْ مَا نَزَّلَ اللَّهُ بِهَا مِنْ سُلْطَانٍ فَانْتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُمْ مِنَ الْمُنْتَظِرِينَ (71) فَأَنْجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ (72)}.
65. Na kwa 'Aadi tulimpeleka ndugu yao, Huud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi? 66. Wakasema watukufu wa wale waliokufuru katika kaumu yake: Sisi tunakuona umo katika upumbavu, na hakika sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo. 67. Akasema: Enyi watu wangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 68. Nawafikishia ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kuwanasihi, mwaminifu 69. Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayo toka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili awaonye? Na kumbukeni alivyo kufanyeni mshike pahala pa kaumu ya Nuhu, na akawazidishia katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. 70. Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli. 71. Akasema: Bila ya shaka adhabu na ghadhabu zimekwisha kuwaangukia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Mnabishana nami kwa ajili ya majina tu mliyoyaita nyinyi na baba zenu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho? Basi ngojeni, mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongoja 72. Basi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukaikata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.
#
{65} أي: {و}: أرسلنا {إلى عادٍ}: ـ الأولى، الذين كانوا في أرض اليمن ـ {أخاهم}: في النسب {هوداً}: عليه السلام، يدعوهم إلى التوحيد، وينهاهم عن الشرك، والطغيان في الأرض، فقال لهم: {يا قوم اعبُدوا اللهَ ما لكم من إلهٍ غيره أفلا تتقون}: سَخَطَهُ وعذابَهُ إن أقمتم على ما أنتم عليه.
{65} Yaani, "na", tulituma "kwa 'Aadi;" - wa kwanza waliokuwa katika ardhi ya Yemen - "ndugu yao" kwa nasaba ya "Hud," amani iwe juu yake, akiwalingania kwenye tauhidi, na akiwakataza ushirikina na kuvuka mipaka katika ardhi. Basi akawaambia, "Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?"
#
{66} فلم يستجيبوا ولا انقادوا، فقال {الملأُ الذين كفروا من قومِهِ}: رادِّين لدعوته قادحين في رأيه: {إنا لنراك في سَفاهةٍ وإنا لنظنُّك من الكاذبين}؛ أي: ما نراك إلاَّ سفيهاً غير رشيد، ويغلب على ظنِّنا أنك من جملة الكاذبين. وقد انقلبت عليهم الحقيقةُ واستحكم عماهم حيث رموا نبيَّهم عليه السلام بما هم متَّصفون به، وهو أبعدُ الناس عنه؛ فإنهم السفهاء حقًّا الكاذبون، وأيُّ سفهٍ أعظم ممَّن قابل أحقَّ الحقِّ بالردِّ والإنكار، وتكبَّر عن الانقياد للمرشدين والنصحاء، وانقاد قلبُهُ وقالبه لكلِّ شيطان مريدٍ، ووضع العبادة في غير موضعها، فعَبَدَ من لا يغني عنه شيئاً من الأشجار والأحجار؟! وأيُّ كذب أبلغ من كذب من نسب هذه الأمور إلى الله تعالى؟!
{66} Lakini hawakuitikia wala hawakufuta, na wakasema "watukufu wa wale waliokufuru katika kaumu yake;" wakiukataa wito wake na wakiishutumu kauli yake: "Hakika sisi tunakuona umo katika upumbavu, na hakika sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo." Yaani, sisi tunakuona wewe si chochote isipokuwa ni mpumbavu na mtu asiye na akili, na tunakudhania sana kuwa wewe ni miongoni mwa waongo. Lakini haki iliwageukia na upofu wao ukamakinika kwa vile walivyomtuhumu nabii wao - amani iwe juu yake- kwa yale wanayosifika kwayo, na yeye ndiye aliye mbali zaidi nayo. Kwani hakika wao ndio wapumbavu na waongo, na ni upumbavu gani mkubwa zaidi kuliko yule aliyeikabili haki ya haki zote kwa kuikataa na kuikanusha, na anajivuna akaacha kufuata waelekezaji na washauri, na moyo wake na ndani yake ikamfuata kila shetani muasi, akaiweka ibada mahali pasipokuwa pake, basi akamwabudu asiyekuwa na manufaa yoyote kwake miongoni mwa miti na mawe? Na je, ni uongo gani mkubwa zaidi kuliko uongo wa yule aliyeyanasibisha mambo haya kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu?
#
{67} {قال يا قوم ليس بي سفاهةٌ}: بوجهٍ من الوجوه، بل هو الرسول المرشدُ الرشيدُ، {ولكنِّي رسولٌ من ربِّ العالمين}.
{67} "Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi sina upumbavu," kwa vyovyote vile, bali yeye ni Mtume, mwenye kuongoza, Mwongofu. "Lakini mimi ni Mtume niliye toka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote."
#
{68} {أبلِّغُكم رسالاتِ ربِّي وأنا لكم ناصحٌ أمين}: فالواجب عليكم أن تتلقَّوا ذلك بالقبول والانقياد وطاعة رب العباد.
{68} "Nawafikishia jumbe za Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kuwanasihini, mwaminifu" basi la wajibu juu yenu ni kuyapokea haya kwa kuyakubali, na kufuata, na kumtii Mola Mlezi wa waja.
#
{69} {أوَعَجِبْتُم أن جاءكم ذِكْرٌ من ربِّكم على رجل منكُم لِيُنذِرَكُم}؛ أي: كيف تعجبون من أمر لا يُتَعَجَّبُ منه، وهو أن الله أرسل إليكم رجلاً منكم، تعرفون أمره، يذكِّركم بما فيه مصالحكم، ويحثُّكم على ما فيه النفع لكم، فتعجَّبتم من ذلك تعجُّب المنكرين. {واذْكُروا إذْ جَعَلَكم خلفاء من بعد قوم نوح}؛ أي: واحمدوا ربَّكم، واشكُروه إذ مَكَّنَ لكم في الأرض، وجعلكم تخلُفون الأمم الهالكة الذين كذَّبوا الرسل، فأهلكهم الله، وأبقاكم لينظر كيف تعملون، واحذروا أن تقيموا على التكذيب كما أقاموا، فيصيبكم ما أصابهم، {و} اذكروا نعمة الله عليكم التي خصَّكم بها، وهي أن {زادكم في الخلق بَسْطَةً}: في القوة وكبر الأجسام وشدَّة البطش، {فاذكُروا آلاءَ اللهِ}؛ أي: نعمه الواسعة وأياديه المتكررة، {لعلَّكُم}: إذا ذَكَرْتُموها بشكرها وأداء حقِّها، {تفلحونَ}؛ أي: تفوزون بالمطلوب، وتنجون من المرهوب.
{69} "Mnaona ajabu kuwafikia mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili awaonye?" Yaani, vipi mnastaajabishwa na jambo lisilo la kushangaza, ambalo ni kwamba Mwenyezi Mungu ametuma kwenu mtu kutoka miongoni mwenu, ambaye mnayajua mambo yake, akiwakumbusha yaliyo kwa maslahi yenu, na kuwahimiza kufanya yale yenye manufaa kwako; na ukastaajabishwa na hayo kama wanavyoyastaajabia wanaokadhibisha. "Na kumbukeni alipowafanyia makhalifa baada ya kaumu ya Nuhu." Yaani, Msifuni Mola wenu Mlezi, na mshukuruni alipowawekea ufalme katika ardhi na akawafanyia nyinyi baada ya mataifa yaliyoangamizwa yaliyowakadhibisha Mitume; basi Mwenyezi Mungu akawaangamiza na akawaacha muone jinsi mtakavyofanya. Nyinyi mnaendelea kukufuru kama walivyothibiti, yasije yakawasibu; "na" kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu aliyowapa. Na ni kuwa "Amewazidishia kwa wingi wa viumbe;" katika ukubwa wa miili, na katika ukali wa dhulma. "Basi kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu;" yaani, baraka zake nyingi na mikono yake ya mara kwa mara, "labda," ikiwa mtawakumbuka kwa kuwashukuru na kuwatimizia haki zao "mtafaulu." Yaani, utafikia kile unachotaka na kuokolewa na kile kinachoogopewa.
#
{70} فوعظهم وذكَّرهم وأمرهم بالتوحيد وذكر لهم وصف نفسه وأنه ناصح أمين، وحذَّرهم أن يأخذهم اللهُ كما أخذ من قبلهم، وذكَّرهم نعم الله عليهم وإدرار الأرزاق إليهم، فلم ينقادوا ولا استجابوا، فقالوا متعجِّبين من دعوته ومخبرين له أنهم من المحال أن يطيعوه: {أجئتَنا لنعبدَ اللهَ وحدَهُ ونَذَرَ ما كان يعبدُ آباؤنا}: قبَّحهم الله، جعلوا الأمر الذي هو أوجبُ الواجبات وأكملُ الأمور من الأمور التي لا يعارضون بها ما وجدوا عليه آباءهم، فقدَّموا ما عليه الآباء الضالون من الشرك وعبادة الأصنام على ما دعت إليه الرسل من توحيد الله وحده لا شريك له وكذبوا نبيهم وقالوا: {ائتنا بما تعِدُنا إن كنتَ من الصادقين}: وهذا الاستفتاحُ منهم على أنفسهم.
{70} Basi akawaidhi, na akawakumbusha, na akawaamrisha kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na akawatajia jinsi alivyojieleza kuwa ni mshauri mwaminifu, na akawaonya kwamba Mwenyezi Mungu atawachukua kama alivyowachukua wale wa kabla yao, na akawakumbusha neema za Mwenyezi Mungu juu yao na riziki yake nyingi kwao. Lakini hawakufuata, wala hawakuitikiwa, wakasema, wakishangazwa na wito wake na kumwambia kuwa haiwezekani kwao kumtii: "Je! Umetujia ili tumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu?" Mwenyezi mungu awalaani! Walilifanya jambo ambalo ni wajibu wa wajibu zote na ukamilifu na kamilifu zaidi ya mambo yote miongoni mwa mambo ambayo hawayapingi kwayo yale waliyowakuta nayo baba zao. Basi wakatanguliza yale waliyokuwa nayo baba zao wapotovu miongoni mwa ushirikina na kuabudu masanamu juu ya yale waliyoyalingania Mitume, ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu bila ya mshirika yeyote, na wakamkadhibisha Nabii wao na wakasema: “Basi tuletee hayo unayotuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli." Na huku ni kujiombea dhidi ya nafsi zao wenyewe.
#
{71} فقال لهم هودٌ عليه السلام: {قد وَقَعَ عليكم من ربِّكم رجْسٌ وغضبٌ}؛ أي: لا بدَّ من وقوعه؛ فإنه قد انعقدت أسبابه وحان وقتُ الهلاك. {أتجادِلونَني في أسماءٍ سمَّيْتموها أنتم وآباؤكم}؛ أي: كيف تجادلون على أمور لا حقائق لها وعلى أصنام سمَّيْتُموها آلهة وهي لا شيء من الإلهية فيها ولا مثقال ذرَّة و {ما أنزل الله بها من سلطانٍ}؛ فإنها لو كانت صحيحةً؛ لأنزل الله بها سلطانًا، فعدم إنزاله له دليلٌ على بطلانها؛ فإنه ما من مطلوب ومقصود ـ وخصوصاً الأمورَ الكبارَ ـ إلا وقد بيَّن الله فيها من الحجج ما يدلُّ عليها ومن السلطان ما لا تخفى معه، {فانتظروا}: ما يقعُ بكم من العقاب الذي وَعَدْتكم به. {إنِّي معكم من المنتظرين}: وفرق بين الانتظارَيْن؛ انتظارِ مَنْ يخشى وقوع العقاب ومَنْ يرجو من الله النصر والثواب.
71. Kisha Hud, amani imshukie, akawaambia: "Bila ya shaka adhabu na ghadhabu zimekwisha waangukia kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, ni lazima yatokee kwa kuwa sababu zake zimeshafanyika na wakati umefika wa maangamio. "Mnabishana nami kwa ajili ya majina tu mliyoyaita nyinyi na baba zenu." Yaani, vipi mnabishana juu ya mambo ambayo hayana ukweli, na masanamu mnayoyaita miungu, na hali hayana uungu ndani yake, wala uzito wa chembe, na "ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho wowote"; kwani kama yangekuwa sahihi, Mwenyezi Mungu angeyateremshia mamlaka. Kwa hivyo, kutokuwepo kuteremshwa kwake ni ushahidi juu ya ubatili wake. Kwani hakuna kitu kinachotakikana wala kilichokusudiwa - hasa mambo makubwa - isipokuwa Mwenyezi Mungu amebainisha kuhusiana nayo hoja mbalimbali zinazoyaashiria na mamlaka yasiyofichikana pamoja nayo. "Basi ngojeni" adhabu itakayowapata ambayo niliwaahidi. "Hakika mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongoja." Na kuna tafauti baina ya kungoja huko kuwili: kungoja kwa yule anayehofia kutokea adhabu, na anayetarajia ushindi na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
#
{72} ولهذا فتح الله بين الفريقين فقال: {فأنجَيْناه}؛ أي: هوداً، {والذين} آمنوا معه {برحمةٍ منا}: فإنه الذي هداهم للإيمان، وجعل إيمانهم سبباً ينالون به رحمته، فأنجاهم برحمته، {وقطَعْنا دابر الذين كذَّبوا بآياتنا}؛ أي: استأصلناهم بالعذاب الشديد الذي لم يُبْق منهم أحداً، وسَلَّطَ الله عليهم {الريح العقيم. ما تَذَرُ من شيءٍ أتت عليه إلا جعلته كالرَّميم}، {فأهْلِكوا فأصبحوا لا يُرى إلاَّ مساكِنُهم فانْظُرْ كيف كان عاقبةُ المنذَرين}، الذين أقيمت عليهم الحُجج فلم ينقادوا لها، وأمِروا بالإيمان فلم يؤمنوا، فكان عاقِبَتُهم الهلاك والخزي والفضيحة، {وأُتْبِعوا في هذه الدُّنيا لعنةً ويومَ القيامةِ. ألا إنَّ عاداً كَفَروا ربَّهم ألا بُعْداً لعادٍ قوم هود}. وقال هنا: {وقَطَعْنا دابرَ الذين كذَّبوا بآياتنا وما كانوا مؤمنينَ}: بوجهٍ من الوجوه، بل وَصْفُهمُ التكذيب والعناد، ونعتُهُم الكِبْر والفساد.
{72} Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akahukumu baina ya makundi mawili haya na akasema: "Basi tukamwokoa yeye." Yaani, Hud "na wale" walioamini pamoja naye "kwa rehema kutoka kwetu," kwani yeye ndiye aliyewaongoa kwenye Imani, na akaifanya imani yao kuwa ni njia ya kupata rehema yake, na akawaokoa; kwa rehema yake. "Na tukakata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu." Yaani, tuliwaangamiza kwa adhabu kali ambayo haikumwacha yeyote miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu akaupa mamlaka juu yao "upepo tasa. Haukuacha chochote ulichokijia isipokuwa ulikifanya kuwa kama kifusi." "Basi wakaangamizwa na wakawa haionekani isipokwa majumba yao tu, basi tazama vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa." Wale ambao hoja zilithibitishwa juu yao lakini hawakuzifuata, na wakaamrishwa kuamini lakini hawakuamini, basi ukawa mwisho wao ni maangamivu, na hizaya, na fedheha. "Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyama. Basi tambueni mtanabahi! Hakika kina 'Aadi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi kuwa hakika kina 'Aadi kaumu ya Hud waliangamizwa." Na Akasema hapa, "Na tukaikata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini" kwa namna yoyote ile. Bali maelezo yao yalikuwa ni kukadhibisha na kufanya ukaidi, na sifa yao ilikuwa ni kiburi na uharibifu.
: 73 - 79 #
{وَإِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا قَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءَتْكُمْ بَيِّنَةٌ مِنْ رَبِّكُمْ هَذِهِ نَاقَةُ اللَّهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (73) وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِنْ بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِنْ سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ (74) قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِنْ قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُرْسَلٌ مِنْ رَبِّهِ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ (75) قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنْتُمْ بِهِ كَافِرُونَ (76) فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَاصَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِنْ كُنْتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ (77) فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ (78) فَتَوَلَّى عَنْهُمْ وَقَالَ يَاقَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَكِنْ لَا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ (79)}.
73. Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Swaleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha wafikia Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu. 74. Na kumbukeni alivyowafanya wa Makhalifa wa A'adi na akawaweka vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi. 75. Waheshimiwa wa kaumu yake wanaojivuna waliwaambia wanaoonewa wenye kuamini miongoni mwao: Je, mnaitakidi ya kwamba Swaleh ametumwa na Mola wake Mlezi? Wakasema: Hakika sisi tunayaamini yale aliyotumwa nayo. 76. Wakasema wale wanaojivuna: Sisi tunayakataa hayo mnayoyaamini. 77. Na wakamuua yule ngamia, na wakaiasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume. 78. Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na kulipokucha wakawa majumbani mwao kifudifudi wamekwisha kufa. 79. Basi Swaleh akawaacha na akasema: Enyi watu wangu! Niliwafikishia Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikawanasihi, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha.
#
{73} أي: {و} أرسلنا {إلى ثمود}: القبيلة المعروفة الذين كانوا يسكُنون الحِجْر وما حوله من أرض الحجاز وجزيرة العرب، أرسل الله إليهم {أخاهم صالحاً}: نبيًّا يدعوهم إلى الإيمان والتوحيد وينهاهم عن الشرك والتنديد، فقال: {يا قوم اعبدوا الله مالَكُم من إلهٍ غيره}: دعوتُهُ عليه الصلاة والسلام من جنس دعوة إخوانه من المرسلين: الأمر بعبادةِ الله وبيان أنه ليس للعباد إله غير الله. {قد جاءتْكم بينةٌ من ربِّكم}؛ أي: خارق من خوارق العادات التي لا تكون إلا آية سماويَّة لا يقدر الناس عليها، ثم فسَّرها بقوله: {هذه ناقةُ الله لكم آية}؛ أي: هذه ناقةٌ شريفةٌ فاضلةٌ لإضافتها إلى الله تعالى إضافة تشريف، لكم فيها آية عظيمة، وقد ذكر وجه الآية في قوله: {لها شِرْبٌ ولكم شِرْبُ يوم معلوم}، وكان عندهم بئر كبيرةٌ، وهي المعروفة ببئر الناقة، يتناوبونها هم والناقة، للناقة يوم تشربها ويشربون اللبن من ضرعها، ولهم يوم يردونها وتصدر الناقة عنهم. وقال لهم نبيُّهم صالح عليه السلام: {فذَروها تأكلْ في أرض الله}: فلا عليكم من مؤونتها شيء، {ولا تَمَسُّوها بسوءٍ}؛ أي: بعقر أو غيره، {فيأخذَكُم عذابٌ أليم}.
{73} Yaani "Na" tuliwatuma "kwa Thamud;" Kaumu mashuhuri iliyokuwa inakaa Al-Hijr na ardhi ya Hijaz iliyoizunguka Bara la Arabu, Mwenyezi Mungu akawatuma kwao "ndugu yao Saleh;" Nabii anayewaita wao kwenye Imani na Tauhidi na kuwakataza ushirikina na ukafiri. Basi akasema, "Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, hamna mungu ila Yeye." "Imekufikieni hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi;" yaani, muujiza usio wa kawaida wa desturi ambazo si chochote ila ni dalili ya mbinguni ambayo watu hawawezi kuifahamu. Kisha akaifafanua kwa kusema: "Huyu ni ngamia jike wa Mungu kuwa ni Ishara kwenu." Yaani, huyu ni ngamia jike mtukufu na mwema kwa sababu ya kuwa ni nyongeza ya utukufu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuna Aya kubwa kwenu juu yake, na maana ya Aya ilitajwa katika kauli yake: "Ana kinywaji. Na mtakunywa katika siku maalumu." Na walikuwa na kisima kikubwa kinachojulikana kama kisima cha ngamia jike, wakabadilishana ndani yake na ngamia jike, kwa ajili ya ngamia siku anayokunywa. Na wanakunywa maziwa katika kiwele chake, na wapo siku watamrudisha na ngamia atawaacha. Na Nabii wao Saleh (amani iwe juu yake) akawaambia: "Basi waacheni mle katika ardhi ya Mwenyezi Mungu." Hamfai kufanya chochote kwa riziki zake, "Wala msiiguse kwa madhara;" yaani, pamoja na mtumwa au kitu kingine, "kisha itawashika adhabu chungu."
#
{74} {واذْكُروا إذ جَعَلَكُم خلفاءَ}: في الأرض تتمتَّعون بها وتدركون مطالبكم، {من بعد عادٍ}: الذين أهلكهم الله وجعَلَكم خلفاء من بعدهم، {وبوَّأكم في الأرض}؛ أي: مكَّن لكم فيها وسهَّل لكم الأسباب الموصلة إلى ما تريدون وتبتغون، {تتَّخذونَ من سهولها قصوراً}؛ أي: الأراضي السهلة التي ليست بجبال بيوتاً، ومن الجبال بيوتاً ينحتونها كما هو مشاهدٌ إلى الآن أعمالهم التي في الجبال من المساكن والحِجْر ونحوها، وهي باقية ما بقيت الجبال. {فاذكروا آلاء الله}؛ أي: نعمه وما خوَّلكم من الفضل والرزق والقوة، {ولا تعثَوا في الأرض مفسدين}؛ أي: لا تُخَرِّبوا في الأرض بالفساد والمعاصي؛ فإن المعاصي تدع الديارَ العامرةَ بلاقِعَ، وقد أخلتْ ديارَهُم منهم، وأبقتْ مساكِنَهم موحشةً بعدَهم.
{74} "Na kumbukeni Alipowafanya makhalifa" katika ardhi ili mpate kustarehesha na kuyatimiza matakwa yenu, "baada ya Aadi} wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaangamiza na akakufanyeni makhalifa wao, na akawaweka katika ardhi. Yaani, Amewafanyia humo na akawafanyia wepesi njia zinazoongoza kwenye mnayoyataka na kuyatafuta. "Mnachukua majumba katika tambarare zake;" yaani nchi tambarare zisizo na milima zina nyumba, na kutoka milimani kuna nyumba wanazozichonga, kama inavyoonekana hadi sasa, kazi zao milimani, kama makao, mawe na mengineyo, na kadhalika; yatabaki maadamu milima itabaki. "Basi kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu;" yaani, baraka zake, na fadhila, na riziki, na uwezo aliowapa. "Wala msieneze ufisadi katika ardhi kwa kueneza ufisadi;" yaani, msiharibu ardhi kwa ufisadi na uadui. Uhalifu umeziacha nyumba zinazokaliwa zikiwa zimeachwa, na kuzifanya nyumba zao kuwa tupu, na kuyaacha makazi yao kuwa ukiwa baada yao.
#
{75} {قال الملأُ الذين استكبروا من قومِهِ}؛ أي: الرؤساء والأشراف الذين تكبروا عن الحق، {للذين استضعفوا}: ولما كان المستضعَفون ليسوا كلُّهم مؤمنين؛ قالوا: {لِمَنْ آمن منهم أتعلَمون أنَّ صالحاً مرسلٌ من ربِّه}؛ أي: أهو صادقٌ أم كاذب؟ فقال المستضعفون: إنَّا بالذي {أرسِلَ به مؤمنونَ} من توحيد الله والخبر عنه وأمره ونهيه.
{75} "Wakasema watu mashuhuri waliojivuna katika kaumu yake;" yaani, viongozi na watukufu waliojivuna kwa ajili ya haki, "kwa wale waliodhulumiwa." Wakasema: "Kwa walioamini mnajua kwamba Saleh ametumwa kutoka kwa Mola wake Mlezi." Yaani, ni mkweli au mwongo? Wale waliodhulumiwa wakasema: Sisi ni kwa yale "tumetuma nayo waumini" katika upweke wa Mwenyezi Mungu na habari zake na maamrisho yake na makatazo yake.
#
{76} {قال الذين استكبَروا إنَّا بالذي آمنتُم به كافرونَ}: حَمَلَهُمُ الكِبْرُ أن لا ينقادوا للحقِّ الذي انقاد له الضعفاء.
{76} "Wakasema wale waliotakabari: Hakika sisi tunamkufuru yule ambaye nyinyi mmemuamini.” Kiburi hakikuwafanya waitii haki ambayo wanyonge wanainyenyekea.
#
{77} {فعقروا الناقة}: التي توعَّدهم إن مسوها بسوء أن يصيبَهم عذابٌ أليم. {وعَتَوا عن أمر ربِّهم}؛ أي: قسوا عنه واستكبروا عن أمره الذي مَنْ عتا عنه أذاقه العذاب الشديد، لا جرم أحلَّ الله بهم من النَّكال ما لم يُحِلَّ بغيرِهم. {وقالوا}: مع هذه الأفعال متجرِّئين على الله معجِزين له غير مبالين بما فعلوا بل مفتخرين بها: {يا صالحُ ائتِنا بما تعِدُنا}: - إن كنت من الصادقين - من العذاب، فقال: {تمتَّعوا في دارِكم ثلاثةَ أيَّام ذلك وعدٌ غيرُ مكذوبٍ}.
{77} "Basi wakamchinja ngamia jike," naye akawatishia ya kwamba wakimdhuru, itawafikia adhabu chungu. "Na wakaasi amri ya Mola wao Mlezi." Yaani, walikuwa wakimfanyia ukatili na wakamfanyia jeuri. Mwenye kumuasi ataonjeshwa adhabu kali, bila kosa lolote, Mwenyezi Mungu amewawekea adhabu ambayo hakuiwezesha kwa wengine. "Na wakasema" kwa vitendo hivyo walikuwa wakithubutu mbele ya Mwenyezi Mungu, wakimtukuza, bila kujali wanayoyafanya, bali wanajivuna nayo. Ewe Saleh! tuletee unayotuahidi - ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli - miongoni mwa adhabu." Kisha akasema: "Furahini majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo."
#
{78} {فأخذتهم الرجفةُ فأصبحوا في دارِهِم جاثمين}: على ركبهم قد أبادهم الله وقطع دابرهم.
{78} "Basi tetemeko la ardhi likawachukua, na wakawa majumbani mwao wako kifudifudi wamekwisha kufa," juu ya magoto yao, tayari Mwenyezi Mungu ameshawaangamiza na akaikata mizizi yao.
#
{79} {فتولَّى عنهم}: صالحٌ عليه السلام حين أحلَّ الله بهم العذاب، {وقال}: مخاطباً لهم توبيخاً وعتاباً بعدما أهلكهم الله: {يا قوم لقد أبلغتُكُم رسالةَ ربِّي ونصحتُ لكم}؛ أي: جميع ما أرسلني الله به إليكم قد أبلغتُكم به وحرصت على هدايتكم واجتهدتُ في سلوككم الصراط المستقيم والدين القويم، {ولكن لا تحبُّونَ الناصحين}: بل رددتُم قول النُّصحاء، وأطعتم كلَّ شيطان رجيم. واعلم أن كثيراً من المفسِّرين يذكرون في هذه القصة أنَّ الناقة خرجت من صخرةٍ صماء ملساء اقترحوها على صالح، وأنها تمخَّضت تمخُّض الحامل، فخرجت الناقة وهم ينظرون، وأن لها فصيلاً حين عقروها رغى ثلاث رغيات وانفلق له الجبل ودخل فيه، وأن صالحاً عليه السلام قال لهم: آية نزول العذاب بكم أن تصبحوا في اليوم الأول من الأيام الثلاثة ووجوهكم مصفرَّة، واليوم الثاني محمرَّة، والثالث مسودَّة، فكان كما قال. وهذا من الإسرائيليات التي لا ينبغي نقلها في تفسير كتاب الله، وليس في القرآن ما يدلُّ على شيء منها بوجه من الوجوه، بل لو كانت صحيحةً لَذَكَرها الله تعالى؛ لأن فيها من العجائب والعبر والآيات ما لا يهمله تعالى ويدع ذِكْرَهُ حتى يأتي من طريق مَنْ لا يوثَق بنقله، بل القرآن يكذِّب بعض هذه المذكورات؛ فإنَّ صالحاً قال لهم: {تمتَّعوا في دارِكُم ثلاثة [أيام]}؛ أي: تنعَّموا وتلذَّذوا بهذا الوقت القصير جدًّا؛ فإنه ليس لكم من المتاع واللَّذَّة سوى هذا، وأيُّ لذَّة وتمتُّع لمن وعدهم نبيُّهم وقوع العذاب وذكر لهم وقوع مقدِّماته فوقعت يوماً فيوماً على وجهٍ يعمُّهم ويشمُلهم؛ لأن احمرار وجوههم واصفرارها واسودادها من العذاب؟! هل هذا إلا مناقض للقرآن ومضادٌّ له؟! فالقرآن فيه الكفاية والهداية عن ما سواه. نعم؛ لو صحَّ شيء عن رسول الله - صلى الله عليه وسلم - مما لا يناقض كتاب الله؛ فعلى الرأس والعين، وهو مما أمر القرآن باتباعه: {وما آتاكُمُ الرسولُ فُخذوه وما نهاكم عنه فانتَهوا}. وقد تقدَّم أنه لا يجوز تفسير كتاب الله بالأخبار الإسرائيليَّة، ولو على تجويز الرواية عنهم بالأمور التي لا يُجْزَمُ بكذِبِها؛ فإنَّ معاني كتاب الله يقينيَّة، وتلك أمور لا تصدَّق ولا تكذَّب؛ فلا يمكن اتفاقهما.
{79} "Basi akawaacha" Swaleh, amani iwe juu yake, wakati Mwenyezi Mungu alipofikishia adhibu, "na akasema" akiwaambia kwa kuwakaripia, na kuwalaumu baada ya Mwenyezi Mungu kuwaangamiza. "Enyi kaumu yangu! Hakika, niliwafikishia ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikawanasihi." Yaani, yote aliyonituma nayo kwenu Mwenyezi Mungu nimekwisha wafikishia, na nimefanya hima kuwaongoa, na nimejitahidi kuwafanya mfuate Njia iliyonyooka na Dini iliyonyooka sawa; "lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi." Bali mliyakataa maneno ya wenye kunasihi, na mkamtii kila shetani aliyefukuziliwa mbali. Na jua kwamba wengi wa wafasiri wanataja katika kisa hiki kwamba ngamia jike yule alitoka kwenye jiwe imara, laini walilompendekezea Swaleh, na kwamba lilipata machungu kama machungu ya mwanamke mjamzito; basi ngamia jike huyo akatoka hali ya kuwa wanatazama. Na kwamba alikuwa na mwana ngamia mdogo wakati walipomchinja, aliyelia milio tatu na mlima ukampasukia na akaingia humo. Na kwamba Swaleh, amani iwe juu yake, aliwaambia: "Ishara ya kuwateremkia adhabu ni kwamba mtaamka katika siku ya kwanza miongoni mwa zile siku tatu hali ya kuwa nyuso zenu ni za njano, na siku ya pili ni nyekundu, na siku ya tatu ni nyeusi.” Basi ikawa kama alivyosema. Na hayo ni miongoni mwa hadithi za Banu Israili ambazo haifai kuzinukuu katika kukitafasiri Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na hakuna katika Qur-ani kinachoashiria chochote katika hayo kwa njia yoyote ile. Bali lau kuwa zingekuwa sahihi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu angezitaja, kwa sababu ndani yake kuna maajabu, na mazingatio, na Ishara mbalimbali Mwenyezi Mungu hawezi kuzipuuza, na kuacha kuzitaja mpaka zije kutokea kwa njia ya yule asiyeaminika katika kunukuu kwake. Bali Qur-aani inakadhibisha baadhi ya haya yaliyotajwa. Kwani Swaleh aliwaambia, “Jifurahisheni katika nyumba zenu siku tatu.” Yaani, furahieni na stareheni kwa wakati huu mfupi sana. Kwani, nyinyi hamna starehe wala kujifurahisha isipokuwa haya. Na ni furaha gani na starehe kwa wale ambao Nabii wao aliwaahidi kutokea kwa adhabu na akawatajia kutokea kwa vitangulizi vyake, kwa hivyo vikatokea siku baada ya siku kwa namna inayowajumlisha na kuwaenea; kwa sababu, wekundu wa nyuso zao, na umanjano wake, na weusi wake ni katika adhabu? Je, hili si isipokuwa lipinganalo na Qur-aani na kinyume chake? Kwani Qur-ani ina utoshelevu na mwongozo juu ya kila kitu kinginecho. Ndiyo, lau kuwa kulikuwepo na jambo lililo sahihi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – ambalo halipingani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi kwa kichwa na jicho tunalikubali. Nayo ni katika yale ambayo Qur-ani ilituamrisha kufuata, “Na anachowapa Mtume, basi kichukueni. Na anachowakataza, basi komekeni." Na tayari imeshatangulia kwamba hairuhusiki kukitafsiri Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa kutegemea habari za Banu Israili, hata kama ni kwa rai inayoruhusu kusimulia kutoka kwao mambo ambayo hayajathibitishwa kuwa ni ya uongo. Kwa sababu, maana za Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni ya hakika, na hayo ni mambo ambayo hayawezi kusadikiwa wala kukadhibishwa. Basi viwili hivyo haviwezi kufikiana.
: 80 - 84 #
{وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُمْ بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِنَ الْعَالَمِينَ (80) إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِنْ دُونِ النِّسَاءِ بَلْ أَنْتُمْ قَوْمٌ مُسْرِفُونَ (81) وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَنْ قَالُوا أَخْرِجُوهُمْ مِنْ قَرْيَتِكُمْ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ (82) فَأَنْجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ (83) وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ مَطَرًا فَانْظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ (84)}.
80. Na Lut alipowaambia kaumu yake, "Je, mnafanya uchafu ambao hajawatangulia kwa huo yeyote katika walimwengu?" 81. Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa shahawa na mnawaacha wanawake? Bali nyinyi ni watu wapitilizao! 82. Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema, "Watoeni kutoka katika mji wenu. Maana wao hakika ni watu wanaojitakasa." 83. Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe, alikuwa miongoni mwa walioangamia. 84. Na tukawanyeshea mvua. Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa wahalifu.
#
{80} أي: {و} اذكر عبدنا {لوطاً}: عليه الصلاة والسلام؛ إذ أرسلناه إلى قومه؛ يأمُرُهم بعبادة الله وحدَه، وينهاهم عن الفاحشة التي ما سبقَهم بها أحدٌ من العالمين؛ فقال: {أتأتونَ الفاحشةَ}؛ أي: الخصلة التي بلغت في العِظَم والشَّناعة إلى أن استغرقتْ أنواعَ الفحش، {ما سَبَقَكم بها من أحدٍ من العالمين}: فكونُها فاحشةً من أشنع الأشياء، وكونُهم ابتدعوها، وابتَكَروها، وسَنُّوها لمن بعدَهم من أشنع ما يكونُ أيضاً.
{80} Yani "na" mtaje mja wetu "Lut" amani iwe juu yake, tulipomtuma kwa kaumu yake, Awaamrishe kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na awakataze machafu ambayo hakuna yeyote aliyewatangulia kwayo katika walimwengu. Kwa hivyo Akasema, "Je, mnafanya uchafu." Yaani, jambo ambalo lilifikia ukubwa na ubaya kiasi kwamba umechukua aina za uchafu wote, "hakuwatangulia kwa huo yeyote katika walimwengu." Na kuwa kwake uchafu ni miongoni mwa mambo mabaya sana; na kuwa kwao wa kwanza katika hilo, na kulizua, na kuliweka kama ada kwa wale walio baada yao pia ni miongoni mwa mambo mabaya sana.
#
{81} ثم بيَّنها بقوله: {إنَّكم لَتأتونَ الرجال شهوةً من دون النساء}؛ أي: كيف تَذَرون النساء التي خلقهنَّ الله لكم، وفيهنَّ المستمتَعُ الموافق للشهوة والفطرة، وتقبِلون على أدبار الرجال، التي هي غايةُ ما يكون في الشناعة والخبث، محلٌّ تخرج منه الأنتان والأخباث التي يُسْتَحى من ذكرِها فضلاً عن ملامستها وقربها. {بل أنتم قومٌ مسرفونَ}؛ أي: متجاوِزون لما حدَّه الله، متجرِّئون على محارمه.
{81} Kisha akaubainisha kwa kauli yake, "Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa shahawa na mnawaacha wanawake?" Yaani, vipi mnawaacha wanawake ambao aliwaumbia Mwenyezi Mungu, na ndani yao ndiyo kuna starehe inayokubaliana na shahawa na maumbile. Na mnazijia tupu za nyuma za wanaume ambazo ndizo pahali pabaya zaidi na paovu zaidi, na mahali patokeapo uvundo na machafu, ambapo ni aibu kupataja tu achilia mbali kupagusa na kupakaribia. "Bali nyinyi ni kaumu wapitilizao." Yaani wanaovuka mipaka aliyoweka Mwenyezi Mungu, wanaoyafanyia ujasiri maharamisho yake.
#
{82} {وما كانَ جوابَ قومِهِ إلَّا أن قالوا أخرِجوهِم من قريتِكُم إنَّهم أناسٌ يتطهَّرونَ}؛ أي: يتنزَّهون عن فعل الفاحشة، {وما نَقَموا منهم إلاَّ أن يؤمنوا باللهِ العزيز الحميد}.
{82} "Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema, "Watoeni kutoka katika mji wenu. Maana wao hakika ni watu wanaojitakasa." Yaani wanajiepusha na kufanya machafu, "nao hawakuona baya lolote kwao isipokuwa kuwa walimwamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu kuu, Msifiwa zaidi."
#
{83} {فأنجيناه وأهلَهُ إلَّا امرأتَهُ كانت من الغابرينَ}؛ أي: الباقين المعذَّبين؛ أمره الله أن يسري بأهله ليلاً؛ فإنَّ العذابَ مصبِّحٌ قومَه، فسرى بهم إلاَّ امرأته أصابها ما أصابهم.
{83} "Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe, alikuwa miongoni mwa walioachwa nyuma." Yaani, waliobaki nyuma, walioadhibiwa; Mwenyezi Mungu alimwamrisha aende pamoja na ahali zake usiku. Kwani adhabu hiyo ilikuwa ya kuwafikia kaumu yake asubuhi. Basi akaondoka pamoja nao isipokuwa mkewe, yeye alipatwa na yale yaliyowapata.
#
{84} {وأمطَرْنا عليهم مطراً}؛ أي: حجارة حارَّة شديدةً من سِجِّيل، وجعل الله عالِيَها سافِلَها، {فانظرْ كيف كان عاقبةُ المجرِمين}: الهلاك والخزي الدائم.
{84} "Na tukawanyeshea mvua." Yaani, vijiwe vya moto kabisa kutoka Motoni, na Mwenyezi Mungu akamfanya juu yake kuwa chini yake. "Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa wahalifu." Maangamio na hizaya ya daima.
: 85 - 93 #
{وَإِلَى مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا قَالَ يَاقَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُمْ مِنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ قَدْ جَاءَتْكُمْ بَيِّنَةٌ مِنْ رَبِّكُمْ فَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (85) وَلَا تَقْعُدُوا بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجًا وَاذْكُرُوا إِذْ كُنْتُمْ قَلِيلًا فَكَثَّرَكُمْ وَانْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ (86) وَإِنْ كَانَ طَائِفَةٌ مِنْكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ لَمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّى يَحْكُمَ اللَّهُ بَيْنَنَا وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ (87) قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِنْ قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَاشُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِنْ قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ (88) قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُمْ بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّهُ مِنْهَا وَمَا يَكُونُ لَنَا أَنْ نَعُودَ فِيهَا إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّنَا وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا عَلَى اللَّهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنْتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ (89) وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَخَاسِرُونَ (90) فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ (91) الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَنْ لَمْ يَغْنَوْا فِيهَا الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ (92) فَتَوَلَّى عَنْهُمْ وَقَالَ يَاقَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ فَكَيْفَ آسَى عَلَى قَوْمٍ كَافِرِينَ (93)}.
85. Na kwa (watu wa) Madyana tulimtuma ndugu yao Shu'aib. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu yeyote isipokuwa Yeye. Hakika imekwisha wajia hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika ardhi baada ya kutengenea kwake. Hayo ndiyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.” 86. Wala msikae katika kila njia mkitishia, na mkiizuia njia ya Mwenyezi Mungu wale waliomuamini, na mkiitaka ipotoke. Na kumbukeni mlipokuwa wachache, naye akawafanya kuwa wengi. Na tazameni jinsi ulivyokuwa mwisho wa waharibifu. 87. Na kama liko kundi miongoni mwenu lililoamini haya niliyotumwa nayo, na kundi jingine halikuamini, basi subirini mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yetu. Naye ndiye Mbora zaidi wa wenye kuhukumu. 88. Wakasema waheshimiwa waliotakabari katika kaumu yake, "Lazima tutakutoa ewe Shu'aib na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au lazima mtarejea katika mila yetu." Akasema, "Je, hata kama tunachukia?" 89. "Bila ya shaka tutakuwa tumemzulia uwongo Mwenyezi Mungu ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuokoa kutokana nayo. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, isipokuwa akitaka Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi. Mola wetu Mlezi umekienea kila kitu kwa elimu. Kwa Mwenyezi Mungu tumetegemea. Mola wetu Mlezi, hukumu baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiwe Mbora zaidi wa wanaohukumu." 90. Na wakasema waheshimiwa waliokufuru katika kaumu yake, "Mkimfuata Shu'aib, basi hakika nyinyi mtahasiri." 91. Basi tetemeko la ardhi likawachukua, kwa hivyo wakawa katika makazi yao wameanguka kifudifudi. 92. Wale waliomkadhibisha Shu'aib ni kama kwamba hawakuishi humo. Wale waliomkadhibisha Shu'aib walikuwa ndio waliohasiri. 93. Basi akawaachilia mbali na akasema, "Enyi kaumu yangu! Hakika nimewafikishia jumbe za Mola wangu Mlezi, na nimewanasihi. Basi vipi niwahuzunikie kaumu makafiri?"
#
{85} أي: {و} أرسلنا إلى القبيلة المعروفة بمدين {أخاهم}: في النسب، {شُعَيْباً}: يدعوهم إلى عبادة الله وحده لا شريك له، ويأمرهم بإيفاء المكيال والميزان، وأن لا يبخسوا الناس أشياءهم، وأن لا يعثَوْا في الأرض مفسدين بالإكثار من عمل المعاصي، ولهذا قال: {ولا تفسدوا في الأرض بعد إصلاحها ذلكم خير لكم إن كنتم مؤمنين}: فإنَّ ترك المعاصي امتثالاً لأمر الله وتقرُّباً إليه خيرٌ وأنفع للعبد من ارتكابها الموجب لسخط الجبار وعذاب النار.
85. Yani "Na" tulituma kwa kabila la Madyana ambalo ni mashuhuri "ndugu yao" katika nasaba "Shu’aib" akiwaita wamwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya mshirika yeyote, na awaamrishe kutimiza vipimo na mizani, na kwamba wasiwapunje watu vitu vyao, na kwamba wasizidishe kufanya uharibifu katika ardhi, kwa kukithirisha maasia. Na ndiyo maana akasema, “wala msifanye uharibifu katika ardhi baada ya kutengenea kwake. Hayo ndiyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.” Kwani kuacha maasia kwa kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kujiweka karibu naye ni bora na ni yenye manufaa zaidi kwa mja kuliko kuyafanya ambako kunapelekea kwenye ghadhabu ya Yeye Afanyaye Atakalo, na adhabu ya Moto.
#
{86} {ولا تقعُدوا}: للناس {بكلِّ صراطٍ}؛ أي: طريق من الطرق التي يكثُرُ سلوكها؛ تحذِّرون الناس منها، و {توعِدونَ}: من سلكها، {وتَصُدُّون عن سبيل الله}: من أراد الاهتداء به، {وتبغونَها عِوَجاً}؛ أي: تبغون سبيل الله تكون معوجَّة، وتميلونها اتِّباعاً لأهوائكم، وقد كان الواجب عليكم وعلى غيركم الاحترام والتعظيم للسبيل التي نصبها الله لعباده، ليسلكوها إلى مرضاته ودار كرامته ورحمهم بها أعظمَ رحمةٍ، وتَصَدَّون لنصرتها والدعوة إليها والذبِّ عنها، لا أن تكونوا أنتم قطاع طريقها الصّادِّين الناس عنها؛ فإنَّ هذا كفرٌ لنعمة الله ومحادَّة لله وجعل أقوم الطرق وأعدلها مائلةً، وتشنِّعون على من سلكها، {واذكُروا}: نعمة الله عليكم {إذ كُنتُم قليلاً فكثَّرَكم}؛ أي: نمَّاكم بما أنعم عليكم من الزوجات والنسل والصحة، وأنه ما ابتلاكم بوباء أو أمراض من الأمراض المقلِّلة لكم، ولا سلَّط عليكم عدوًّا يجتاحُكم، ولا فرَّقكم في الأرض، بل أنعم عليكم باجتماعكم وإدرار الأرزاق وكثرة النسل. {وانظروا كيف كان عاقبةُ المفسدين}: فإنكم لا تجدون في جموعهم إلاَّ الشتات، ولا في ربوعهم إلاَّ الوَحْشة والانبتات، ولم يورثوا ذِكْراً حسناً، بل أُتْبِعوا في هذه الدُّنيا لعنةً ويوم القيامة [أشد] خزياً وفضيحة.
{86} "Wala msikae" kwa ajili ya watu "katika kila njia;" yaani, barabara miongoni mwa barabara ambayo inapitwa kwa wingi mkiwatahadharisha watu nayo, na "mkitishia" mwenye kuifuata, "na mkiizuilia njia ya Mwenyezi Mungu" yule anayetaka kuongoka kwayo, "Na mkiitaka ipotoke." Yaani, mkitaka njia ya Mwenyezi Mungu iwe potofu, na mnaigeuza kwa kufuata matamanio yenu. Na lililokuwa la wajibu kwenu na kwa wengine ni kuiheshimu na kuitukuza njia ambayo Mwenyezi Mungu amewawekea waja wake, ili waifuate hadi katika radhi zake na nyumba ya utukufu wake, na aliwarehemu kwayo rehema kubwa zaidi. Na mjibidiishe kuinusuru, na kuilingania, na kuitetea, na wala msiwe wakataao njia yake, wawazuiliao watu nayo. Kwani hilo ni kukufuru neema ya Mwenyezi Mungu na kupingana na Mwenyezi Mungu, na kuigeuza njia iliyonyooka zaidi na ya wastani zaidi, na mnamchukia mwenye kuifuata. "Na kumbukeni," neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu "mlipokuwa wachache, naye akawafanya kuwa wengi." Yaani, aliwakuza kwa yale aliyowaruzuku miongoni mwa wake, na uzao, na afya, na kwamba hakuwajaribu kwa maradhi ya mlipuko au maradhi yoyote miongoni mwa maradhi yenye kuwapunguza, wala hakumpa mamlaka adui yoyote ili awaangamize, wala hakuwagawanya katika ardhi. bali aliwabariki kwa umoja wenu, na kuwapa riziki kwa wingi, na wingi wa uzao. "Na tazameni jinsi ulivyokuwa mwisho wa waharibifu. Kwani hamtapata chochote katika mkusanyiko wao isipokuwa mtawanyiko, wala katika maboma yao isipokuwa ukiwa na uharibifu, na wala hawakurithisha utajo mzuri; bali walifuatishwa katika dunia hii laana, na Siku ya Qiyama ni hizaya "kubwa zaidi" na fedheha.
#
{87} {وإن كان طائفةٌ منكُم آمنوا بالذي أرْسِلْتُ به وطائفةٌ لم يؤمنوا}: وهم الجمهور منهم، {فاصبِروا حتى يحكُمَ اللهُ بيننا وهو خيرُ الحاكمينَ}: فينصر المحقَّ، ويوقع العقوبة على المبطل.
{87} "Na kama liko kundi miongoni mwenu lililoamini haya niliyotumwa nayo, na kundi jingine halikuamini," nao ndio wengi wao; basi subirini mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yetu. Naye ndiye Mbora zaidi wa wenye kuhukumu," basi atamnusuru aliye katika haki, na amwadhibu aliye katika batili.
#
{88} {قال الملأُ الذين استَكْبَروا من قومِهِ}: وهم الأشرافُ والكبراءُ منهم، الذين اتَّبعوا أهواءهم ولهوا بلذاتهم، فلما أتاهم الحقُّ ورأوه غير موافق لأهوائهم الرديئة؛ ردُّوه، واستكبروا عنه، فقالوا لنبيِّهم شعيب ومن معه من المؤمنين المستضعفين: {لنخرجَنَّكَ يا شعيبُ والذين آمنوا معك من قريتِنا أو لتعودُنَّ في مِلَّتنا}: استعملوا قوَّتهم السَّبُعية في مقابلة الحقِّ، ولم يراعوا ديناً ولا ذمَّةً ولا حقًّا، وإنما راعوا واتبعوا أهواءهم وعقولهم السفيهة، التي دلَّتهم على هذا القول الفاسد، فقالوا إمَّا أن ترجع أنت ومن معك إلى ديننا أو لنخرجنَّكم من قريتنا؛ فشعيبٌ عليه الصلاة والسلام كان يدعوهم طامعاً في إيمانهم، والآن لم يَسْلَم [من شرهم] حتى توعَّدوه إن لم يتابعهم بالجلاء عن وطنه الذي هو ومن معه أحقُّ به منهم. فقال لهم شعيبٌ عليه الصلاة والسلام متعجباً من قولهم: {أوَلَوْ كنَّا كارهينَ}؛ أي: أنتابعكم على دينكم وملَّتكم الباطلة ولو كُنَّا كارهين لها لعلمنا ببطلانها؛ فإنما يدعَى إليها من له نوعُ رغبة فيها، أما من يعلن بالنهي عنها والتشنيع على من اتَّبعها؛ فكيف يُدعى إليها.
{88} “Wakasema waheshimiwa waliotakabari katika kaumu yake,” nao ndio wale waheshimiwa na wakuu miongoni mwao, ambao walifuata matamanio yao, na wakacheza kwa anasa zao. Lakini ilipowajia haki na wakaiona haikubaliani na matamanio yao mabaya, wakaikataa na wakamfanyia jeuri. Kwa hivyo wakamwambia Nabii wao Shu’aib na wale waliokuwa pamoja naye miongoni mwa Waumini dhaifu: "Lazima tutakutoa ewe Shu'aib na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au lazima mrejee katika mila yetu." Walitumia nguvu zao za kinyama katika kukabiliana na haki, na hawakuzingatia dini, wala dhima, wala haki. Bali walizingatia na wakafuata matamanio yao, na akili zao za kipumbavu ambazo ziliwaashiria kuisema kauli hii ya upotovu. Wakasema, "Ima urudi wewe na wale walio pamoja nawe katika dini yetu, au lazima tutawatoa katika mji wetu." Naye Shu’aib, Rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akiwalingania kwa kuwataraji waamini, na sasa hakusalimika [kutokana na maovu yao] mpaka walipomtishia ikiwa hatawafuata watamhamisha kutoka tika nchi yake ambayo yeye na wale walio pamoja naye wanaistahiki zaidi kuliko wao. Shu’aib, rehema na amani ziwe juu yake, akawaambia huku akishangaa kwa kauli yao: "Je, hata ingawa tunaichukia?" Yaani, je, tuwafuate katika dini yenu na mila yenu batili hata ingawa tunaichukia, kwa sababu tunaujua ubatili wake? Na hakika analingania kwayo yule ambaye ana aina fulani ya kuitaka. Ama yule anayetangaza kuikataza na kumshutumu mwenye kuifuata, basi vipi analinganiwa kwayo?
#
{89} {قدِ افتَرَيْنا على الله كذباً إن عُدْنا في ملَّتكم بعد إذ نجَّانا الله منها}؛ أي: اشهدوا علينا أننا إن عُدنا [فيها] بعد ما نجَّانا الله منها وأنقذنا من شرِّها أننا كاذبون مفترون على الله الكذب؛ فإننا نعلمُ أنه لا أعظم افتراء ممَّن جعل لله شريكاً وهو الواحد الأحد الفرد الصمد الذي لم يتَّخذ صاحبة ولا ولداً ولا شريكاً في الملك. {وما يكونُ لنا أن نعودَ فيها}؛ أي: يمتنع على مثلنا أن نعودَ فيها؛ فإنَّ هذا من المحال، فآيَسَهم عليه الصلاة والسلام من كونه يوافقهم من وجوهٍ متعددةٍ. من جهة أنهم كارهون لها مبغضون لما هم عليه من الشرك. ومن جهة أنه جعل ما هم عليه كذباً وأشهدهم أنه إنِ اتَّبَعَهم ومن معه فإنَّهم كاذبون. ومنها اعترافُهم بمنَّة الله عليهم إذ أنقذهم الله منها، ومنها أنَّ عودَهم فيها بعدما هداهم الله من المحالات بالنظر إلى حالتهم الراهنة وما في قلوبهم من تعظيم الله تعالى والاعتراف له بالعبوديَّة وأنه الإله وحده الذي لا تنبغي العبادة إلاَّ له وحده لا شريك له، وأنَّ آلهة المشركين أبطل الباطل وأمحل المحال، وحيث إنَّ اللهَ منَّ عليهم بعقول يعرفون بها الحقَّ والباطل والهدى والضلال، وأما من حيث النظر إلى مشيئة الله وإرادته النافذة في خلقه التي لا خروجَ لأحدٍ عنها ولو تواترتِ الأسبابُ وتوافقت القوى؛ فإنَّهم لا يحكمون على أنفسهم أنهم سيفعلون شيئاً أو يتركونه، ولهذا استثنى: {وما يكونُ لنا أن نعودَ فيها إلا أن يشاء اللهُ ربُّنا}؛ أي: فلا يمكننا ولا غيرنا الخروج عن مشيئته التابعة لعلمه وحكمته، وقد {وَسِعَ ربُّنا كلَّ شيءٍ علماً}: فيعلم ما يصلُح للعباد، وما يدبِّرُهم عليه. {على الله توكَّلْنا}؛ أي: اعتمدنا أنه سيثبِّتنا على الصراط المستقيم، وأن يعصِمَنا من جميع طرق الجحيم؛ فإن من توكَّل على الله كفاه ويسَّر له أمر دينه ودنياه. {ربَّنا افتحْ بينَنا وبين قومِنا بالحقِّ}؛ أي: انصر المظلوم وصاحب الحق على الظالم المعاند للحق، {وأنت خيرُ الفاتحين}: وفتحُهُ تعالى لعباده نوعان: فتحُ العلم بتبيين الحقِّ من الباطل والهدى من الضلال ومَنْ هو المستقيمُ على الصراط ممَّن هو منحرفٌ عنه. والنوع الثاني: فتحُهُ بالجزاء وإيقاع العقوبة على الظالمين، والنجاة والإكرام للصالحين. فسألوا الله أن يفتحَ بينَهم وبين قومهم بالحقِّ والعدل، وأن يريَهم من آياتِهِ وعِبَرِهِ ما يكون فاصلاً بين الفريقين.
{89} "Bila ya shaka tutakuwa tumemzulia uongo Mwenyezi Mungu ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuokoa kutokana nayo." Yaani, shuhudieni juu yetu kwamba sisi hakika tukirejea [ndani yake] baada ya Mwenyezi Mungu kutuokoa kutokana nayo na akatuokoa kutokana na shari yake, kwamba sisi hakika ni waongo, tunamzulia Mwenyezi Mungu uongo. Kwa maana sisi hakika tunajua kwamba hakuna kuzua uongo mkubwa zaidi kuliko yule anayemfanyia Mwenyezi Mungu mshirika, ilhali Yeye ni Mmoja tu, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakujichukulia mke wala mwana, wala mshirika katika ufalme. "Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo; yaani, haiwezekani kwa mfano wetu kurejea humo. Kwa maana, haya katika yasiyowezekana, kwa hivyo Yeye amani iwe juu yake akawakatisha tamaa ya yeye kuafikiana nao kwa njia nyingi. Kwa upande wa kwamba wanaichukia huo ushirikina waliomo. Na Kwa upande kwamba aliyafanya yale waliyo juu yake kuwa ni uongo, na akawashuhudisha kwamba ikiwa atawafuata yeye na wale walio pamoja naye, basi hakika watakuwa waongo. Na miongoni mwake ni kukiri kwao neema ya Mwenyezi Mungu juu yao pale Mwenyezi Mungu alipowaokoa kutokana nayo. Na miongoni mwake ni kwamba, kurudi kwao humo baada ya Mwenyezi Mungu kuwaongoa ni katika yasiyowezekana kwa kuangalia hali yao ya sasa na yale yaliyo katika nyoyo zao ya kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumkiria umola, na kwamba Yeye ndiye Mungu peke yake ambaye haifai ibada yoyote isipokuwa kwa ajili yake tu, asiye na mshirika; na kwamba miungu ya washirikina ni batili zaidi ya batili zote, na kisichowezekana zaidi cha visiyowezekana vyote. Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwaneemesha akili wanazojua kwazo haki na batili, na uwongofu na upotofu. Na ama kwa kuangalia mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na kutaka kwake kutekelezekako katika viumbe vyake, ambako hakuna awezaye kutoka kwa huko, hata kama sababu zitakuwepo kwa wingi, na nguvu zote zikakubaliana. Kwani wao wenyewe hawajihukumu kuwa watafanya kitu au kukiacha, na ndiyo maana akatoa katika hayo, “Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, isipokuwa akitaka Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu.” Yaani, sisi wala yeyote yule hatuwezi kutoka katika mapenzi Yake ambayo yanafuatana na elimu yake na hekima yake, na “Mola wetu Mlezi umekienea kila kitu kwa elimu,” basi anajua kinachowafaa waja wake, na anachowaendesha kwacho. "Kwa Mwenyezi Mungu tumetegemea;" yaani, tumetegemea kuwa atatuweka imara kwenye Njia iliyonyooka na atatulinda kutokana na njia zote za Jahiim. Kwa maana mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, Yeye humtosheleza na humrahisishia mambo ya dini yake na dunia yake. “Mola wetu Mlezi! Hukumu baina yetu na kaumu yetu kwa haki.” Yaani, mnusuru aliyedhulumiwa na mwenye haki juu ya dhalimu, anayeipinga haki. “Nawe ndiye mbora zaidi wa wanaohukumu.” Na hukumu yake Yeye Mtukufu kwa waja wake ni ya aina mbili: Hukumu ya elimu kwa kubainisha haki kutokana na batili, na uwongofu kutokana na upotofu, na ni nani aliyenyooka kwenye njia kutokana na yule aliyepotoka mbali nayo. Na aina ya pili ni kuhukumu kwa malipo na kuwaadhibu madhalimu, na kuokoka, na utukufu kwa walio wema. Kwa hivyo, wakamwomba Mwenyezi Mungu kuhukumu baina yao na kaumu yao kwa haki na uadilifu, na kwamba awaonyeshe katika ishara zake na mazingatia yake yatakayokuwa kitenganishi kati ya makundi mawili haya.
#
{90} {وقال الملأُ الذين كفروا من قومه}: محذِّرين عن اتِّباع شعيب: {لئن اتَّبعتم شعيباً إنَّكم إذاً لخاسرونَ}: هذا ما سوَّلت لهم أنفسهم؛ أن الخسارة والشقاء في اتباع الرشد والهدى، ولم يدروا أن الخسارة كلَّ الخسارة في لزوم ما هم عليه من الضلال والإضلال، وقد علموا ذلك حين وقع بهم النَّكال.
{90} “Na wakasema waheshimiwa waliokufuru katika kaumu yake” wakionya juu ya kumfuata Shu’aib, “Mkimfuata Shu'aib, basi hakika nyinyi mtahasiri." Haya ndiyo yale nafsi zao ziliwashawishi kuyafanya. Kwamba hasara na mashaka ni katika kufuata unyoofu na uwongofu, na hawakujua kwamba hasara yote ni katika kushikamana na upotofu na upotoshaji walio ndani yake, na hakika walijua hilo ilipowafikia adhabu.
#
{91} {فأخذتْهُمُ الرجفةُ}؛ أي: الزلزلة الشديدة، {فأصبحوا في دارهم جاثمينَ}؛ أي: صرعى ميِّتين هامدين.
{91} “Basi tetemeko la ardhi likawachukua.” Yaani, tetemeko kubwa la ardhi, “kwa hivyo wakawa katika makazi yao wameanguka kifudifudi " Yaani, walianguka huku wamekufa, wametulia.
#
{92} قال تعالى ناعياً حالَهم: {الذين كذَّبوا شعيباً كأن لم يَغْنَوْا فيها}؛ أي: كأنهم ما أقاموا في ديارهم، وكأنهم ما تمتَّعوا في عَرَصاتهم، ولا تفيَّئوا في ظلالها، ولا غنوا في مسارح أنهارها، ولا أكلوا من ثمار أشجارها، فأخذهم العذاب فنقلهم من مورد اللهو واللعب واللَّذَّات إلى مستقرِّ الحزن والشقاء والعقاب والدرَكات، ولهذا قال: {الذين كذَّبوا شُعيباً كانوا هم الخاسرينَ}؛ أي: الخسار محصورٌ فيهم؛ لأنهم خسروا أنفسهم وأهليهم يوم القيامة، ألا ذلك هو الخسران المبين، لا مَنْ قالوا لهم: {لئنِ اتَّبعتُم شعيباً إنَّكم إذاً لخاسرونَ}.
{92} Amesema Yeye Mtukufu akijulisha kuhusu hali ya kufa kwao, “Wale waliomkadhibisha Shu'aib wakawa kama kwamba hawakuishi humo.” Yaani, ni kama kwamba hawakukaa katika makazi yao, na ni kana kwamba hawakustarehekea katika pahali pao hapo, wala hawakukaa chini ya vivuli vyake, wala hawakukaa katika mahali pake pa kupumzikia mchana, wala hawakula katika matunda ya miti yao, lakini adhabu ikawachukua na ikawahamisha kutoka katika sehemu ya pumbao, na michezo na starehe na kuwapeleka kwenye kamazi ya huzuni, na mashaka, na adhabu, na matabaka ya chini. Na ndiyo maana akasema, “Wale waliomkadhibisha Shu'aib ndio waliohasiri.” Yaani, hasara inawahusu wao tu, kwa sababu walizihasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Qiyama. Tazama! Hiyo ndiyo hasara iliyo wazi kabisa, si wale waliowaambia, “Mkimfuata Shu'aib, basi hakika nyinyi mtahasiri.”
#
{93} فحين هلكوا تولَّى عنهم نبيُّهم عليه الصلاة والسلام، {وقال} معاتباً وموبِّخاً ومخاطباً لهم بعد موتهم: {يا قوم لقد أبلغتُكم رسالاتِ ربِّي}؛ أي: أوصلتها إليكم وبيَّنتها حتَّى بلغت منكم أقصى ما يمكن أن تصل إليه وخالطت أفئدتكم، {ونصحتُ لكم}: فلم تقَبلوا نُصحي ولا انقدتم لإرشادي، بل فسقتُم وطغيتم؛ {فكيف آسى على قوم كافرينَ}؛ أي: فكيف أحزن على قوم لا خيرَ فيهم، أتاهم الخيرُ فردُّوه ولم يقبلوه، ولا يَليقُ بهم إلا الشرُّ؛ فهؤلاء غير حقيقين أن يُحْزَنَ عليهم، بل يُفْرَحُ بإهلاكهم ومَحْقِهم؛ فعياذاً بك اللهمَّ من الخزي والفضيحة! وأيُّ شقاء وعقوبة أبلغ من أن يصلوا إلى حالة يتبرأ منهم أنصح الخلق لهم؟!
{93} Basi wakati walipoangamia, Nabii wao rehema na amani zimshukie akawaachilia mbali "na akasema" akiwalaumu, na kuwakaripia akiwaongelesha baada ya kufa kwao, “Enyi kaumu yangu! Hakika nimewafikishia jumbe za Mola wangu Mlezi” Yaani, na nilizifikishia kwenu na nikazibainisha mpaka zikawafikia kwa kiwango kikubwa zaidi iwezekanavyo kufikia na zikachanganyika na nyoyo zenu, "na nikawanasihi." Lakini hamkukubali nasaha yangu wala hamkufuata maelekezo yangu, bali mlikuwa wagumu na wajeuri. "Basi vipi niwahuzunikie kaumu makafiri?" Yaani, vipi niwahuzunikie kaumu ambao hamna heri ndani yao. Heri iliwajia nao wakaikataa lakini hawakuikubali, na haiwafai isipokuwa uovu tu. Basi hawa si sawa hawastahiki kuhuzuninikiwa, bali inafurahiwa kuangamia kwao na kufutiliwa mbali kwao. Basi tunajilinda naye ewe Mwenyezi Mungu kutokana na huzuni na fedheha! Na je, ni mashaka gani na adhabu gani iliyo kubwa zaidi kuliko wafikie kiwango kwamba anajitenga nao yule ambaye ni Mwenye kunasihi zaidi wa viumbe vote?
: 94 - 95 #
{وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِنْ نَبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ (94) ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّى عَفَوْا وَقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُمْ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ (95)}
94. Na hatukumtuma katika mji wowote Nabii yeyote isipokuwa tuliwachukua wakazi wake kwa umaskini na maradhi ili wanyenyekee. 95. Kisha tukabadilisha pahali pa ubaya kwa wema, mpaka wakazidi, na wakasema, "Hakika ziliwafikia baba zetu taabu na raha." Basi tukawachukua kwa ghafla hali ya kuwa hawatambui.
#
{94} يقول تعالى: {وما أرسلنا في قرية من نبيٍّ}: يدعوهم إلى عبادة الله، وينهاهم عن ما هم فيه من الشرِّ، فلم ينقادوا له؛ إلاَّ ابتلاهم الله {بالبأساءِ والضرَّاءِ}؛ أي: بالفقر والمرض وأنواع البلايا، {لعلهم}: إذا أصابتهم؛ خضعتْ نفوسُهم؛ فتضرعوا إلى الله، واستكانوا للحق.
{94} Yeye Mtukufu anasema, “Na hatukumtuma katika mji wowote Nabii yeyote” akiwalingania katika kumwabudu Mwenyezi Mungu na kuwakataza maovu waliyomo, na hawakumfuata isipokuwa Mwenyezi Mungu aliwajaribu "kwa umaskini na maradhi." Yaani, kwa umaskini, na maradhi, na aina mbalimbali za misiba, "ili" zikiwakumba, nafsi zao zitatii, kwa hivyo wakamnyenyekea Mwenyezi Mungu, na wakaridhika na haki.
#
{95} {ثم}: إذا لم يُفِدْ فيهم واستمرَّ استكبارُهم وازداد طغيانُهم، {بدَّلْنا مكانَ السيئةِ الحسنةَ}: فأَدَرَّ عليهم الأرزاق، وعافى أبدانهم، ورفع عنهم البلايا، {حتى عَفَوْا}؛ أي: كثروا وكثرتْ أرزاقُهم وانبسطوا في نعمة الله وفضله ونسوا ما مرَّ عليهم من البلايا ، {وقالوا قد مسَّ آباءنا الضَّرَّاءُ والسَّرَّاءُ}؛ أي: هذه عادة جارية لم تزل موجودة في الأولين واللاحقين؛ تارة يكونون في سرَّاء، وتارة في ضرَّاء، وتارة في فرح، ومرة في ترح؛ على حسب تقلُّبات الزمان وتداول الأيام، وحسبوا أنها ليست للموعظة والتذكير ولا للاستدراج والنكير، حتى إذا اغتبطوا وفرحوا بما أوتوا، وكانت الدُّنيا أسرَّ ما كانت إليهم. أخذْناهم بالعذاب {بغتةً وهم لا يشعُرون}؛ أي: لا يخطُرُ لهم الهلاك على بالٍ، وظنُّوا أنهم قادرون على ما آتاهم الله، وأنهم غير زائلين ولا منتقلين عنه.
{95} "Kisha" ikiwa haiwanufaishi, na kikaendelea kiburi chao, na kukazidi kupindukia kwao mipaka, “tukabadilisha pahali pa ubaya kwa wema” kwa hivyo akawaruzuku kwa wingi, na akawapa afya katika miili yao, na akawaondolea balaa. "Mpaka wakazidi;" yaani, walikithiri, na riziki zao zikakithiri, na wakafurahia neema ya Mwenyezi Mungu na fadhila yake, na wakasahau yale yaliyowapitikia ya balaa mbalimbali. “Na wakasema, "Hakika ziliwafikia baba zetu taabu na raha." Yaani, hii ni desturi inayoendelea ambayo haijaacha kuwepo katika wale wa mwanzo na waliofuata. Mara wanakuwa katika nyakati nzuri, na mara katika nyakati mbaya, na mara katika furaha na mara katika huzuni kulingana na kubadilikabadilika kwa nyakati na kupita kwa masiku, na wakadhania kuwa si kwa sababu ya mawaidha na ukumbusho, wala si kwa kuwafitini na kuwakemea, mpaka walipofurahia yale waliyopewa, na dunia ikawa ndiyo ya kupendeza zaidi kwao, tukawachukua kwa adhabu “kwa ghafla hali ya kuwa hawatambui.” Yaani, maangamio hayakuwatokea katika fikira zao, na wakadhani kwamba wana uwezo wa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu, na kwamba hawataisha wala hawataondoka humo.
: 96 - 99 #
{وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (96) أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَى أَنْ يَأْتِيَهُمْ بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ (97) أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَى أَنْ يَأْتِيَهُمْ بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ (98) أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّهِ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ (99)}
96. Na lau kuwa watu wa miji wangeliamini na wakamcha Mungu, basi hakika tungeliwafungulia baraka za kutoka mbinguni na ardhi. Lakini walikadhibisha, basi tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma. 97. Je, wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu usiku hali ya kuwa wamelala? 98. Au wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu mchana hali ya kuwa wanacheza? 99. Je, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri.
#
{96} لما ذكر تعالى أنَّ المكذِّبين للرسل يُبتلون بالضراء موعظةً وإنذاراً، وبالسراء استدراجاً ومكراً؛ ذكر أنَّ أهل القُرى لو آمنوا بقلوبهم إيماناً صادقاً صدقتْه الأعمالُ، واستعملوا تقوى الله تعالى ظاهراً وباطناً بترك جميع ما حرَّم الله [تعالى]؛ لفتحَ عليهم بركاتِ السَّماء والأرض، فأرسل السماء عليهم مدراراً، وأنبتَ لهم من الأرض ما به يعيشون وتعيشُ بهائمهُم في أخصب عيش وأغزر رزق من غير عناء ولا تعبٍ ولا كدٍّ ولا نصبٍ، ولكنهم لم يؤمنوا ويتَّقوا، {فأخذناهم بما كانوا يكسِبون}: بالعقوبات والبلايا ونزع البركات وكثرة الآفات، وهي بعض جزاء أعمالهم، وإلاَّ؛ فلو آخذهم بجميع ما كسبوا؛ ما ترك على ظهرها من دابَّةٍ، {ظَهَرَ الفسادُ في البرِّ والبحر بما كَسَبَتْ أيدي الناس لِيُذيقَهم بعضَ الذي عملوا لعلَّهم يرجِعون}.
{96} Yeye Mtukufu alipotaja kwamba wale waliowakadhibisha Mitume hujaribiwa kwa dhiki ili iwe mawaidha na maonyo, na kwa mazuri ili kuwaachilia waendelee na hali yao, na kuwapangia mipango kabambe dhidi yao, akataja kwamba lau watu wa vijiji wangeamini kwa nyoyo zao imani ya ukweli, basi vitendo vyao vingeithibitisha, na wakamcha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dhahiri na ndani kwa kuacha kila alichoharamisha Mwenyezi Mungu [Mtukufu], basi angewafungulia baraka za mbingu na ardhi. Akawatumia (mvua kutoka katika) mbingu kwa mfululizo, na akawaoteshea kutoka katika ardhi yale watakayoishi kwayo, na waishi mifugo yao katika maisha yenye rutuba na riziki nyingi bila ya shida, wala uchovu, wala ugumu, wala taabu. Lakini wao hawakuamini na kumcha Mungu, “basi tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma” kwa adhabu mbalimbali, na balaa, na kuondoa baraka zile, na kuwepo kwa wingi wa majanga. Na hayo ni baadhi ya malipo ya matendo yao. Na vinginevyo, lau kuwa angewachukua kwa yote waliyochuma, basi hangeacha juu ya mgongo wake mnyama yeyote. “Umedhihiri uharibifu katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu, ili awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyafanya huenda wakarejea.”
#
{97} {أفأمِنَ أهلُ القرى}؛ أي: المكذبة بقرينة السياق، {أن يأتِيَهُم بأسُنا}؛ أي: عذابنا الشديد، {بَياتاً وهم نائمون}؛ أي: في غفلتهم وغرتهم وراحتهم.
{97} “Je, wakazi wa vijijini wana amani?”Yaani, wale wanaokadhibisha kulingana na ushahidi wa muktadha, “ya kuwa iwajie adhabu yetu.” Yaani, adhabu yetu kali, “usiku hali ya kuwa wamelala?” Yaani, katika kughafilika kwao, na kutojua kwao, na raha yao.
#
{98} {أوَ أمِنَ أهلُ القرى أن يأتِيَهم بأسُنا ضحىً وهم يلعبونَ}: أيُّ شيءٍ يؤمِّنُهم من ذلك وهم قد فعلوا أسبابه وارتكبوا من الجرائم العظيمة ما يوجب بعضُه الهلاك.
{98} “Au wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu mchana hali ya kuwa wanacheza?” Ni kitu gani kinawapa amani kutokana na hayo hali ya kuwa wamefanya sababu zake, na wakafanya mambo makubwa ya uhalifu ambayo baadhi yake yanalazimu kuangamia.
#
{99} {أفأمنوا مَكْرَ الله}: حيث يستدرِجُهم من حيث لا يعلمونَ، ويُملي لهم إنَّ كيده متين. {فلا يأمنُ مكرَ اللهِ إلا القومُ الخاسرون}: فإنَّ من أمِنَ من عذاب الله؛ فإنه لم يصدِّق بالجزاء على الأعمال ولا آمن بالرسل حقيقة الإيمان. وهذه الآية الكريمة فيها من التخويف البليغ على أنَّ العبد لا ينبغي له أن يكون آمناً على ما معه من الإيمان، بل لا يزالُ خائفاً وَجِلاً أن يُبتلى ببليَّةٍ تسلب ما معه من الإيمان، وأن لا يزال داعياً بقوله: يا مقلب القلوب! ثبِّتْ قلبي على دينك، وأن يعمل ويسعى في كلِّ سبب يخلِّصه من الشرِّ عند وقوع الفتن؛ فإنَّ العبد ولو بلغت به الحال ما بلغتْ؛ فليس على يقين من السلامة.
{99} "Je, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu?” Ambapo Yeye anawaachilia tu kutoka mahali wasipopajua, na anawapa muhula, hakika njama yake ni madhubuti. “Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri.” Kwa maana, mwenye kuwa na amani dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu, basi yeye hakusadiki malipo juu ya matendo, wala hakuwaamini Mitume imani ya uhakika. Na Aya hii tukufu ina kuhofisha kukubwa sana kwamba mja hafai kuwa na amani kwa yale aliyo nayo ya imani, bali haachi huwa na hofu na kuogopa kwamba huenda akajaribiwa kwa balaa yenye kile alicho nacho cha imani, na kwamba haachi kuendelea kuomba kwa kusema: Ewe mwenye kugeuza nyoyo! Uimarishe moyo wangu juu ya dini yako. Na kwamba ifanye matendo na kujitahidi kwa kila sababu yenye kumtoa katika maovu wakati wa kutokea kwa majaribio. Kwa maana, mja lau kuwa hali atamfikisha pale itakapofika, basi hawi na yakini kuwa yu salama.
: 100 - 102 #
{أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِنْ بَعْدِ أَهْلِهَا أَنْ لَوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُمْ بِذُنُوبِهِمْ وَنَطْبَعُ عَلَى قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ (100) تِلْكَ الْقُرَى نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَائِهَا وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِنْ قَبْلُ كَذَلِكَ يَطْبَعُ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِ الْكَافِرِينَ (101) وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِمْ مِنْ عَهْدٍ وَإِنْ وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ لَفَاسِقِينَ (102)}.
100. Kwani haijawabainikia wale wanaoirithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tunawasibu kwa madhambi yao, na tukaziba nyoyo zao, kwa hivyo hawatasikia? 101. Vijiji hivyo, tunakusimulia katika habari zake. Na hakika waliwajia Mitume wao na hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za makafiri. 102. Wala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye ahadi yoyote, bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka.
#
{100} يقول تعالى منبهاً للأمم الغابرين بعد هلاك الأمم الغابرين: {أوَلَمْ يَهْدِ للذين يرِثون الأرض من بعدِ أهلها أن لو نشاءُ أصبْناهم بذُنوبهم}؛ أي: أوَلم يتبيَّن ويتَّضح للأمم الذين ورثوا الأرض بعد إهلاك من قبلَهم بذنوبهم ثم عملوا كأعمال أولئك المهلَكين، أوَلم يهتدوا أنَّ الله لو شاء لأصابَهم بذُنوبهم؛ فإنَّ هذه سنته في الأولين والآخرين. وقوله: {ونطبَعُ على قلوبهم فهم لا يسمعونَ}؛ أي: إذا نبَّههم الله فلم ينتبهوا، وذكَّرهم فلم يتذكَّروا، وهداهم بالآيات والعِبَر فلم يهتَدوا؛ فإنَّ الله تعالى يعاقِبُهم ويطبعُ على قلوبهم فيعلوها الرَّانُ والدَّنَسُ حتى يُخْتَمَ عليها فلا يدخُلها حقٌّ ولا يصلُ إليها خيرٌ ولا يسمعون ما ينفعهم، وإنَّما يسمعون ما به تقوم الحجَّةُ عليهم.
{100} Anasema Yeye Mtukufu akitanabahisha juu ya umma ilizopita baada ya kuangamia kwa umma zilizopita, "kwani haijawabainikia wale wanaoirithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tunawasibu kwa madhambi yao." Yaani, je, haikuwabainikia na kuwawia wazi umma wale walioirithi ardhi baada ya kuangamizwa kwa wale waliokuwa kabla yao kwa sababu ya dhambi zao, kisha wakafanya kama matendo ya wale walioangamizwa. Kwani hawakuongoka kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka, angeliwasibu kwa sababu ya dhambi zao? Kwa maana, Hii ndiyo ada yake katika wa mwanzo na wa mwisho. Na kauli yake: “Na tukaziba nyoyo zao, kwa hivyo hawatasikia?” Yaani, ikiwa Mwenyezi Mungu atawatanabahisha, lakini wasitanabahi, na akawakumbusha, lakini wasikumbuke, na akawaongoa kwa Aya mbalimbali na mazingatia, lakini wasiongoke, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaadhibu na kuziba kwenye nyoyo zao, na ikafunikwa kwa kizibo na uchafu mpaka izibwe kabisa, kwani haiwezi kuingiwa na haki wala heri haiifikii, wala hawasikii yanayowafaa, bali wanayasikia yale inayosimama kwayo hoja dhidi yao.
#
{101} {تلك القرى}: الذين تقدَّم ذِكْرُهم، {نَقُصُّ عليك من أنبائها}: ما يحصُلُ به عبرة للمعتبرين، وازدجارٌ للظالمين، وموعظة للمتقين، {ولقد جاءتْهم رسُلُهم بالبيناتِ}؛ أي: [ولقد] جاءت هؤلاء المكذبين رسُلُهم تدعوهم إلى ما فيه سعادتهم، وأيَّدهم الله بالمعجزات الظاهرة والبيِّنات المبيِّنات للحقِّ بياناً كاملاً، ولكنهم لم يُفِدْهم هذا ولا أغنى عنهم شيئاً؛ {فما كانوا ليؤمِنوا بما كذَّبوا من قبلُ}؛ أي: بسبب تكذيبهم وردِّهم الحقّ أول مرة ما كان يهديهم للإيمان جزاءً لهم على ردِّهم الحق؛ كما قال تعالى: {ونقلِّبُ أفْئِدَتَهم وأبصارَهم كما لم يؤمنوا به أولَ مرَّةٍ ونَذَرُهم في طغيانِهِم يعمَهونَ}، {كذلك يطبعُ الله على قلوب الكافرين}: عقوبةً منه، وما ظلمهم الله، ولكنهم ظلموا أنفسهم.
{101} "Vijiji hivyo" ambavyo vimetangulia kuwatajwa, "tunakusimulia katika habari zake," yale yanayotokana nayo mazingatio kwa wanaozingatia, na kemeo kwa madhalimu, na mawaidha kwa wacha Mungu. "Na hakika waliwajia Mitume wao na hoja zilizo waziwazi." Yaani, [na hakika] waliwajia wanaokadhibisha hawa Mitume wao wakiwalingania yale yenye furaha yao, na Mwenyezi Mungu akawaunga mkono kwa miujiza iliyo dhahiri na hoja yenye kubainisha haki kubainisha kukamilifu, lakini wao haya hayakuwafaidi wala hayakuwafaa kitu. "Lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha zamani." Yaani, kwa sababu ya kukadhibisha na kuikataa kwao haki mara ya kwanza ilipokuwa inawaongoa kwenye Imani; kama malipo kwao kwa kuikataa kwao haki. Kama alivyosema Yeye Mtukufu: "Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama walivyokuwa hawakuiamini mara ya kwanza, na tutawaacha wakitangatanga kwa upofu katika uasi wao;" "Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za makafiri." Kama adhabu kutoka kwake, na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu nafsi zao wenyewe.
#
{102} {وما وَجَدْنا لأكثرِهم من عهدٍ}؛ أي: وما وجدنا لأكثر الأمم الذين أرسل الله إليهم الرسل من عهد؛ أي: من ثبات والتزام لوصية الله التي أوصى بها جميع العالمين، ولا انقادوا لأوامره التي ساقها إليهم على ألسنة رسله. {وإن وَجَدْنا أكْثَرَهُم لفاسقينَ}؛ أي: خارجين عن طاعة الله، متَّبعين لأهوائهم بغير هدىً من الله؛ فالله تعالى امتحن العباد بإرسال الرسل وإنزال الكتب، وأمرهم باتِّباع عهده وهداه، فلم يمتثلْ لأمره إلا القليل من الناس، الذين سبقتْ لهم من الله سابقةُ السعادة، وأما أكثر الخلق؛ فأعرضوا عن الهدى، واستكبروا عما جاءت به الرسل، فأحلَّ الله بهم من عقوباتِهِ المتنوِّعة ما أحلَّ.
{102} { Wala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye ahadi yoyote.” Yaani, hatukuwapata wengi wa umma ambao Mwenyezi Mungu aliwatumia Mitume wakiwa wenye ahadi yoyote. Yaani, miongoni mwa uthabiti na kudumu katika wasia wa Mwenyezi Mungu ambao aliwausia walimwengu wote, wala hawakufuata amri zake ambazo aliwafikishia kwa ndimi za Mitume wake. "Bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka." Yaani, watokao nje ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu, wafuatao matamanio yao bila ya uwongofu wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwajaribu waja wake kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu, na akawaamrisha kufuata agano lake na uwongofu wake. Lakini hawakuitekeleza amri yake hiyo isipokuwa wachache tu katika watu, ambao walikwisha andikiwa furaha kwa Mwenyezi Mungu. Na ama wengi wa viumbe, hao waliupa mgongo uwongofu na wakajivuna dhidi yale waliyokuja nayo Mitume; basi Mwenyezi Mungu akawashushia katika adhabu zake mbalimbali alizozishusha.
: 103 - 171 #
{ثُمَّ بَعَثْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ مُوسَى بِآيَاتِنَا إِلَى فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَظَلَمُوا بِهَا فَانْظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ (103) وَقَالَ مُوسَى يَافِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ (104) حَقِيقٌ عَلَى أَنْ لَا أَقُولَ عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ قَدْ جِئْتُكُمْ بِبَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ (105) قَالَ إِنْ كُنْتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ (106) فَأَلْقَى عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُبِينٌ (107) وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ (108) قَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ (109) يُرِيدُ أَنْ يُخْرِجَكُمْ مِنْ أَرْضِكُمْ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ (110) قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ (111) يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ (112) وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِنْ كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ (113) قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ (114) قَالُوا يَامُوسَى إِمَّا أَنْ تُلْقِيَ وَإِمَّا أَنْ نَكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ (115) قَالَ أَلْقُوا فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ (116) وَأَوْحَيْنَا إِلَى مُوسَى أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ (117) فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (118) فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانْقَلَبُوا صَاغِرِينَ (119) وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ (120) قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ (121) رَبِّ مُوسَى وَهَارُونَ (122) قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنْتُمْ بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ إِنَّ هَذَا لَمَكْرٌ مَكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ (123) لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ مِنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ (124) قَالُوا إِنَّا إِلَى رَبِّنَا مُنْقَلِبُونَ (125) وَمَا تَنْقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ (126) وَقَالَ الْمَلَأُ مِنْ قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَى وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ (127) قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّهِ وَاصْبِرُوا إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ (128) قَالُوا أُوذِينَا مِنْ قَبْلِ أَنْ تَأْتِيَنَا وَمِنْ بَعْدِ مَا جِئْتَنَا قَالَ عَسَى رَبُّكُمْ أَنْ يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ (129) وَلَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ (130) فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَذِهِ وَإِنْ تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَى وَمَنْ مَعَهُ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِنْدَ اللَّهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (131) وَقَالُوا مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِ مِنْ آيَةٍ لِتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ (132) فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُجْرِمِينَ (133) وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ الرِّجْزُ قَالُوا يَامُوسَى ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِنْدَكَ لَئِنْ كَشَفْتَ عَنَّا الرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِي إِسْرَائِيلَ (134) فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الرِّجْزَ إِلَى أَجَلٍ هُمْ بَالِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنْكُثُونَ (135) فَانْتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ (136) وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ الْحُسْنَى عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ (137) وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَى قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَى أَصْنَامٍ لَهُمْ قَالُوا يَامُوسَى اجْعَلْ لَنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ (138) إِنَّ هَؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (139) قَالَ أَغَيْرَ اللَّهِ أَبْغِيكُمْ إِلَهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ (140) وَإِذْ أَنْجَيْنَاكُمْ مِنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ وَفِي ذَلِكُمْ بَلَاءٌ مِنْ رَبِّكُمْ عَظِيمٌ (141) وَوَاعَدْنَا مُوسَى ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً وَقَالَ مُوسَى لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ (142) وَلَمَّا جَاءَ مُوسَى لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنْظُرْ إِلَيْكَ قَالَ لَنْ تَرَانِي وَلَكِنِ انْظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي فَلَمَّا تَجَلَّى رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَى صَعِقًا فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ (143) قَالَ يَامُوسَى إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاس بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُنْ مِنَ الشَّاكِرِينَ (144) وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ مَوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ (145) سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِنْ يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِنْ يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِنْ يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ (146) وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (147) وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَى مِنْ بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَهُ خُوَارٌ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ (148) وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِنْ لَمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ (149) وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَى إِلَى قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِي مِنْ بَعْدِي أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ وَأَلْقَى الْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُ إِلَيْهِ قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي فَلَا تُشْمِتْ بِيَ الْأَعْدَاءَ وَلَا تَجْعَلْنِي مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (150) قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ وَأَنْتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ (151) إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ (152) وَالَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ ثُمَّ تَابُوا مِنْ بَعْدِهَا وَآمَنُوا إِنَّ رَبَّكَ مِنْ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَحِيمٌ (153) وَلَمَّا سَكَتَ عَنْ مُوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ (154) وَاخْتَارَ مُوسَى قَوْمَهُ سَبْعِينَ رَجُلًا لِمِيقَاتِنَا فَلَمَّا أَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُمْ مِنْ قَبْلُ وَإِيَّايَ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا إِنْ هِيَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَنْ تَشَاءُ وَتَهْدِي مَنْ تَشَاءُ أَنْتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنْتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ (155) وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُمْ بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ (156) الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِنْدَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ يَأْمُرُهُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنْكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنْزِلَ مَعَهُ أُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (157) قُلْ يَاأَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ (158) وَمِنْ قَوْمِ مُوسَى أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ (159) وَقَطَّعْنَاهُمُ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أَسْبَاطًا أُمَمًا وَأَوْحَيْنَا إِلَى مُوسَى إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْحَجَرَ فَانْبَجَسَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَشْرَبَهُمْ وَظَلَّلْنَا عَلَيْهِمُ الْغَمَامَ وَأَنْزَلْنَا عَلَيْهِمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَى كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَكِنْ كَانُوا أَنْفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ (160) وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ اسْكُنُوا هَذِهِ الْقَرْيَةَ وَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا حِطَّةٌ وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا نَغْفِرْ لَكُمْ خَطِيئَاتِكُمْ سَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ (161) فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَظْلِمُونَ (162) وَاسْأَلْهُمْ عَنِ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ حَاضِرَةَ الْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِي السَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ لَا تَأْتِيهِمْ كَذَلِكَ نَبْلُوهُمْ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ (163) وَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا اللَّهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَى رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ (164) فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنْجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ (165) فَلَمَّا عَتَوْا عَنْ مَا نُهُوا عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ (166) وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبْعَثَنَّ عَلَيْهِمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ يَسُومُهُمْ سُوءَ الْعَذَابِ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَحِيمٌ (167) وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا مِنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَلِكَ وَبَلَوْنَاهُمْ بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (168) فَخَلَفَ مِنْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَذَا الْأَدْنَى وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِنْ يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِثْلُهُ يَأْخُذُوهُ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِمْ مِيثَاقُ الْكِتَابِ أَنْ لَا يَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (169) وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ (170) وَإِذْ نَتَقْنَا الْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُ ظُلَّةٌ وَظَنُّوا أَنَّهُ وَاقِعٌ بِهِمْ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُمْ بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ (171)}.
103. Kisha tukamtuma baada yao Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazifanyia dhuluma. Basi tazama namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu. 104. Na Musa akasema, "Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote " 105. Inastahiki zaidi juu yangu kwamba nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu. Hakika nimewajia na Ishara za waziwazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi waachilie pamoja nami Wana wa Israili. 106. Akasema (Firauni), "Ikiwa umekuja na ishara yoyote, basi ilete ikiwa wewe ni katika wakweli." 107. Basi akaitupa fimbo yake, na tazama, ikawa joka lililo dhahiri. 108. Na akautoa nje mkono wake, na tazama ulikuwa mweupe kwa watazamao. 109. Wakasema waheshimiwa kutoka katika kaumu ya Firauni, "Hakika huyo ni mchawi ajuaye vyema." 110. Anataka kuwatoa katika nchi yenu. Basi mnaamrisha nini? 111. Wakasema: Mwache kidogo yeye na kaka yake, na watume mijini wakusanyaji. 112. Wakujie na kila mchawi ajuaye vyema. 113. Na wakamjia wachawi Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutakuwa sisi ndio washindi. 114 . Akasema: Ndiyo! Nanyi bila ya shaka ni katika waliotiwa karibu nami. 115. Wakasema: Ewe Musa! Ima utupe wewe, au tuwe sisi ndio watupao? 116. Akasema: Tupeni! Basi walipotupa, waliyafanyia uchawi macho ya watu na wakawatia hofu, na wakaleta uchawi mkubwa. 117. Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Itupe fimbo yako, na tazama, ikawa inavimeza vyote vile walivyovizulia uwongo. 118. Basi haki ikathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda. 119. Kwa hivyo wakashindwa huko, na wakageuka kuwa wadogo. 120. Na wachawi wakatupwa chini wakisujudu 121. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa walimwengu vyote. 122. Mola Mlezi wa Musa na Haarun. 123. Akasema Firauni: Mmemuamini kabla mimi kuwapa idhini? Hakika, hii ni njama mliyoipangia huko mjini ili muwatoae humo wenyewe. Basi karibu mtajua! 124. Lazima nitaikata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Kisha lazima nitawasulubisha nyote. 125. Wakasema: Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. 126. Nawe hutushutumu kwa chuki isipokuwa kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola wetu Mlezi pindi zilipotujia. Ewe Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira na utufishe hali ya kuwa ni Waislamu. 127. Na wakasema waheshimiwa kutoka kwa kaumu ya Firauni: Je, unamuacha Musa na kaumu yake ili wafanye uharibifu katika ardhi na akuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauaua wavulana wao, na tuwaache hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao. 128. Musa akawaambia kaumu yake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu, anairithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu. 129. Wakasema: Tumeudhiwa kabla wewe kutujia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui wenu, na akawafanya nyinyi ndio wa kufuatia kushika ardhi, ili atazame mtakavyokuja tenda nyinyi. 130. Na hakika tuliwachukua watu wa Firauni kwa miaka (ya ukame), na kwa upungufu katika mazao, huenda wakakumbuka. 131. Basi wakijiwa na zuri, wanasema, "Ni haki yetu hii." Na likiwasibu ovu, wanaona mkosi kwa Musa na wale walio pamoja naye. Tazama! Hakika mkosi huo unatoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui. 132. Na walisema, "Hata ukitujia na Ishara yoyote ile kutufanyia uchawi kwazo, basi sisi hatutakuamini." 133. Basi tukawatumia tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, ziwe ni Ishara za kina. Lakini wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu. 134. Na ilipowaangukia adhabu, wakasema, "Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa yale aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu hii, hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili waende pamoja nawe." 135. Basi tulipowaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, tazama! Wakavunja ahadi yao. 136. Basi tukawapatiliza, tukawazamisha katika bahari kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na wakawa wanazighafilikia. 137. Na tukawarithisha kaumu wale waliokuwa wakidhoofishwa, mashariki ya ardhi na magharibi yake ambayo tulibariki ndani yake. Na likatimia neno jema la Mola wako Mlezi juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyosubiri. Na tukayaangamiza yale aliyokuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na yale waliyokuwa wakiyajenga. 138. Na tukawavusha bahari Wana wa Israili, kisha wakajia kaumu waliokuwa wanayaabudu masanamu yao. Wakasema, "Ewe Musa! Tufanyie mungu kama hawa walivyo na miungu." Musa akasema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojua kitu. 139. Hakika hawa, haya waliyomo yatakuja angamia, na ni batili hayo waliyokuwa wakiyafanya. 140. Akasema, "Je, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye aliyewafadhilisha juu ya walimwengu wote?" 141. Na pale tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowatia adhabu mbaya zaidi. Wakiwaua wavulana wenu, na wakawaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi. 142. Na tulimuahidi Musa masiku thelathini na tukayatimiza kwa kumi; basi ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi masiku arabaini. Na Musa akamwambia kaka yake, Haarun: Shika pahali pangu katika kaumu yangu na utengeneze, wala usifuate njia ya waharibifu. 143. Na alipokuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamuongelesha, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutaniona. Lakini utazame huo mlima. Ikiwa utabaki mahali pake, basi utaniona. Basi alipojionyesha Mola wake Mlezi kwa mlima huo, akaufanya upasukepasuke, na Musa akaanguka chini akazimia. Basi alipozindukana, akasema: Subhanaka (Umetakasika)! Nimetubia kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini. 144. (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Hakika Mimi nilikuteua uende kwa watu na jumbe zangu na maneno yangu. Basi chukua hayo niliyokupa na kuwa katika wanaoshukuru. 145. Na tukamuandikia kwenye mbao zile katika kila kitu, mawaidha na maelezo ya kina ya kila kitu. (Tukamwambia): Basi yachukue kwa nguvu na uwaamrishe kaumu yako wayachukue kwa ubora wake. Nami nitawaonyesha makazi ya wale waliovuka mipaka. 146. Nitawaepusha na Ishara zangu wale wanaotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara, hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu, hawaichukui kuwa ndiyo njia. Lakini wakiiona njia ya ukengeufu, wanaichukua kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na walikuwa wakizighafilikia. 147. Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu na kukutana na Akhera, matendo yao yameharibika. Kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda? 148. Na kaumu ya Musa wakamfanya baada yake kutoka katika mapambo yao ndama mwenye kiwiliwili, mwenye kutoa mlio wa ng'ombe. Kwani hawakuona kuwa hawasemeshi wala hawaongoi njia yoyote? Walimchukua (kamuabudu), na wakawa madhalimu. 149. Na wakati mambo yalipoangushwa katika mikono yao, na wakaona ya kwamba wamekwisha potea, wakasema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hataturehemu na akatufutia dhambi, basi bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa waliohasiri. 150. Na wakati aliporudi Musa kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kuhuzunika, akasema: Ni mabaya mno mliyonifanyia nyuma yangu! Je, mmeiharakisha amri ya Mola wenu Mlezi? Na akazitupa chini mbao zile, na akamkamata kaka yake kichwa akimvuta kwake. (Haarun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika kaumu hawa waliniona kuwa mimi ni dhaifu, na walikaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui zangu, wala usinifanye pamoja na kaumu madhalimu. 151. (Musa) akasema: Mola wangu Mlezi! Nifutie dhambi mimi na kaka yangu, na utuingize katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wenye kurehemu. 152. Hakika wale waliojifanyia (na kumuabudu) ndama, itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao Mlezi, na udhalilifu katika maisha ya dunia. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wazuao uongo. 153. Na wale waliotenda mabaya, kisha wakatubia baada yake na wakaamini, hakika Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. 154. Na wakati ghadhabu ilipomtulia Musa, akazichukua mbao zile. Na katika maandiko yake kuna uwongofu na rehema kwa wale ambao wao wanaomhofu Mola wao Mlezi. 155. Na Musa akawateua kaumu wake wanaume sabiini kwa ajili ya miadi yetu. Na ulipowachukua mtetemeko mkubwa, akasema: Mola wangu Mlezi! Ungelitaka, ungeliwaangamiza wao hapo kabla na hata mimi. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wapumbavu katika sisi? Haya si chochote isipokuwa ni majaribio yako, unampoteza kwayo umtakaye, na umuongoa umtakaye. Wewe ndiye rafiki mlinzi wetu. Basi tusitiri dhambi na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora zaidi wa wasitirio dhambi. 156. Na tuandikie mazuri katika dunia hii na katika Akhera. Hakika sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu kwayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Basi nitaiandika hii hasa kwa wale wanaomcha Mungu, na wanaotoa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu. 157. Wale ambao wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiyesoma wala kuandika, ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, anayewaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vizuri, na anawaharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo ambayo ilikuwa juu yao. Basi wale waliomwamini yeye, na wakampa taadhima, na wakamnusuru, na wakaifuata nuru ambayo iliteremshwa pamoja naye, hao ndio waliofaulu. 158. Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote, Yeye ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu isipokuwa Yeye. anahuisha na anafisha. Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Nabii asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili muongoke. 159. Na katika kaumu ya Musa upo umma unaowaongoa watu kwa haki, na kwayo wanafanya uadilifu. 160. Na tukawakatakata makabila kumi na mawili, mataifa mbali mbali. Na tulimfunulia Musa wakati kaumu yake walipomwomba maji kwamba: Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako. Mara zikabubujika kutoka humo chemchemi kumi na mbili, na kila watu wakajua pahali pao pa kunywea. Na tukawafunika kivuli kwa mawingu, na tukawateremshia Manna na Salwa. Kuleni katika vizuri hivi tulivyowaruzuku. Na hawakutudhulumu Sisi, bali walikuwa wakijidhulumu wenyewe. 161. Na pale walipoambiwa: Ukaeni mji huu, na mle humo popote mpendapo, na semeni: Tufutie dhambi zetu. Na uingieni mlango wake kwa kusujudu, tutawasitiria makosa yenu. Walio wema tutawazidishia. 162. Lakini wakabadilisha wale waliodhulumu miongoni mwao kauli isiyo ile waliyoambiwa. Basi tukawatumia adhabu kutoka mbinguni kwa vile walivyokuwa wakidhulumu. 163. Na waulize kuhusu kijiji kilichokuwa kando ya bahari, walipokuwa wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Walipokuwa samaki wakiwajia juu juu siku ya Sabato, na siku isiyokuwa ya Sabato hawawajii. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakivuka mipaka. 164. Na kikundi miongoni mwao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola wenu Mlezi, na huenda nao wakamcha Mungu. 165. Basi walipoyasahau yale waliyokumbushwa kwayo, tukawaokoa wale waliokuwa wakikataza mabaya, na tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya mno kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka. 166. Walipotakabari na kuasi yale waliyokatazwa, tukawaambia, "Kuweni manyani, mliodharauliwa." 167. Na wakati alipotangaza Mola wako Mlezi kwamba hakika atawatumia dhiki yao hadi Siku ya Qiyama mwenye kuwaadhibu kwa adhabu mbaya sana. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu sana. 168. Na tukawagawanya katika ardhi umma umma. Miongoni mwao kuna wale walio wema, na miongoni mwao kuna walio kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mazuri na mabaya huenda wakarejea. 169. Basi wakafuatia baada yao wafuatizi waliokirithi Kitabu. Wanachukua anasa za haya maisha duni, na wanasema, "Tutasitiriwa dhambi!" Na ikiwajia tena anasa mfano wake, wanaichukua pia. Je, halikuchukuliwa juu yao agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu? Nao wamekwishasoma yale yaliyomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wachao. Basi je, hamtii akilini? 170. Na wale wanaokikamata sawasawa Kitabu, na wakasimamisha Swala, hakika Sisi hatupotezi ujira wa watengenezao. 171. Na pale tulipounyanyua mlima juu yao ukawa kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika, na wakadhani kuwa utawaangukia, (tukawaambia): Chukueni yale tuliyowapa kwa nguvu, na yakumbukeni yaliyomo ndani yake ili mche.
#
{103} أي: ثم بعثنا من بعد أولئك الرسل موسى الكليم الإمام العظيم والرسول الكريم إلى قوم عتاةٍ جبابرةٍ ـ وهم فرعون وملؤه من أشرافهم وكبرائهم ـ فأراهم من آيات الله العظيمة ما لم يشاهَدْ له نظيرٌ. {فظلموا بها}: بأن لم ينقادوا لحقِّها الذي مَن لم ينقدْ له فهو ظالمٌ، بل استكبروا عنها، {فانظرْ كيفَ كان عاقبةُ المفسدينَ}: كيف أهلَكَهُمُ الله وأتْبَعَهم الذمَّ واللعنة في الدنيا، ويوم القيامة بئس الرِّفْدُ المرفود.
{103} Yaani, kisha tukamtuma baada ya Mitume hao Musa, aliyeongea moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, Imamu Mkuu na Mtume Mtukufu kwa kaumu madhalimu na majabar. Nao ni Firauni na waheshimiwa wake miongoni mwa watukufu wao na wakubwa wao. Basi akawaonyesha katika ishara kuu za Mwenyezi Mungu ambazo haijapata kuonekana mfano wake. "Nao wakazifanyia dhuluma" kwa kutoifuata haki yake ambayo asiyeifuata, basi yeye ni dhalimu. Bali wao wazifanyia kiburi. "Basi tazama namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu” jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaangamiza wao na akawafuatisha shutuma, na laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyama ni maovu mno watakayopewa.
#
{104} وهذا مجمل فصَّله بقوله: {وقال موسى}: حين جاء إلى فرعون يدعوه إلى الإيمان: {يا فرعونُ إنِّي رسولٌ من ربِّ العالَمين}؛ أي: إني رسولٌ من مُرسِل عظيم، وهو ربُّ العالَمين، الشامل للعالم العلويِّ والسفليِّ، مربِّي جميع خلقِهِ بأنواع التدابير الإلهيَّة، التي من جملتها أنه لا يترُكُهم سدىً، بل يرسل إليهم الرسل مبشِّرين ومنذرين، وهو الذي لا يقدر أحدٌ أن يتجرَّأ عليه ويدَّعي أنه أرسله ولم يرسله.
{104} Na huu ni ujumla alioueleza kwa kina kwa kauli yake, “Na Musa akasema” wakati alipomjia Firauni akimlingania kwenye Imani: “Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote." Yaani, hakika mimi ni mtume kutoka kwa Aliyetuma, Mkubwa, naye ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliyezunguka ulimwengu wa juu na wa chini, anayevilea viumbe vyake vyote kwa aina mbalimbali za mipangilio ya kiungu, ambayo miongoni mwake ni kwamba Yeye hawaachi wao bila ya kuamrishwa na kukatazwa. Bali huwatumia Mitume wabashiri na waonyaji, naye ndiye ambaye hakuna awezaye kufanya ujasiri na kudai kuwa Yeye amemtuma, ilhali hakumtuma.
#
{105} فإذا كان هذا شأنه، وأنا قد اختارني واصطفاني لرسالته؛ فحقيقٌ عليَّ أن لا أكذب عليه ولا أقول عليه إلا الحقَّ؛ فإني لو قلتُ غير ذلك؛ لعاجلني بالعقوبة، وأخذني أخذ عزيز مقتدر؛ فهذا موجبٌ لأن ينقادوا له ويتَبعوه، خصوصاً وقد جاءهم ببيِّنة من الله واضحةٍ على صحَّة ما جاء به من الحقِّ، فوجب عليهم أن يعملوا بمقصود رسالته، ولها مقصودان عظيمان: إيمانُهم به واتِّباعُهم له، وإرسالُ بني إسرائيل الشعب الذي فضَّله الله على العالمين أولاد الأنبياء وسلسلة يعقوب عليه السلام الذي موسى عليه الصلاة والسلام واحدٌ منهم.
{105} Kwa hivyo, ikiwa hili ndilo jambo lake, nami hakika amenichagua na kuniteua kwa ajili ya ujumbe wake, basi inastahiki zaidi juu yangu kwamba nisiseme uongo juu yake, wala nisiseme juu yake isipokuwa haki tu. Kwani mimi kama hakika ningesema yasiyokuwa hayo, basi angeniharakishia adhabu, na angenichukua kwa mchukuo wa Mwenye nguvu na Mwenye uwezo. Basi hili linawalazimu wamtii na wamfuate hasa kwa vile aliwajia na ushahidi wa wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya usahihi wa haki aliyokuja nayo. Kwa hivyo ikawa ni wajibu kwao kutenda kwa mujibu wa makusudio ya ujumbe wake. Nao una makusudio mawili: kumwamini kwao na kumfuata kwao, na kuwatuma wana wa Israili taifa ambalo Mwenyezi Mungu aliwaboresha juu ya walimwengu wote, wana wa Manabii na msururu wa Yaaqub, amani iwe juu yake, ambaye Musa, amani iwe juu yake, ni mmoja kutokana nao.
#
{106} فقال له فرعون: {إن كنتَ جئتَ بآيةٍ فأت بها إن كنتَ من الصادقين}.
{106} Kisha Firauni akamwambia, “"Ikiwa umekuja na ishara yoyote, basi ilete ikiwa wewe ni katika wakweli."
#
{107} {فألقى} موسى {عصاه}: في الأرض، {فإذا هي ثعبانٌ مبينٌ}؛ أي: حية ظاهرةٌ تسعى وهم يشاهدونها.
{107} "Basi" Musa "akaitupa fimbo yake" kwenye ardhi, “na tazama, ikawa joka lililo dhahiri.” Yaani, nyoka aliye dhahiri anayekwenda hali ya kuwa wanamtazama.
#
{108} {ونزع يده}: من جيبه، {فإذا هي بيضاء للناظرين}: من غير سوءٍ؛ فهاتان آيتان كبيرتان دالَّتان على صحة ما جاء به موسى وصدقِهِ، وأنَّه رسولُ ربِّ العالمين.
{108} “Na akautoa nje mkono wake” kutoka mfukoni mwake, “na tazama ulikuwa mweupe kwa watazamao” pasipo na maradhi. Basi Hizi ni Aya mbili kubwa zinazoashiria usahihi wa yale aliyokuja nayo Musa na ukweli wake, na kwamba yeye ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
#
{109} ولكن الذين لا يؤمنون لو جاءتهم كلُّ آيةٍ لا يؤمنون حتى يروا العذاب الأليم؛ فلهذا {قال الملأ من قوم فرعون} حين بهرهم ما رأوا من الآيات ولم يؤمنوا وطلبوا لها التأويلات الفاسدة: {إنَّ هذا لساحرٌ عليمٌ}؛ أي: ماهرٌ في سحره.
{109} Lakini wale wasioamini lau kuwa watajiwa na kila Ishara, hawaamini mpaka waione adhabu chungu. Na ndiyo maana "Wakasema waheshimiwa kutoka katika kaumu ya Firauni" wakati walipostaajabishwa na yale waliyoyaona miongoni mwa Aya mbalimbali na hawakuamini, na wakazitafutia tafsiri potovu: "Hakika huyo ni mchawi majuaye vyema;" yaani, mjuzi katika uchawi wake.
#
{110} ثم خوَّفوا ضعفاءَ الأحلام وسفهاء العقول بأنه {يريدُ} موسى بفعلِهِ هذا {أن يخرِجَكم من أرضكم}؛ أي: يريد أن يجليكم من أوطانكم، {فماذا تأمرونَ}؟ أي: إنهم تشاوروا فيما بينهم ما يفعلون بموسى، وما يندفع به ضررهم بزعمهم عنهم؛ فإنَّ ما جاء به إن لم يقابَلْ بما يبطِلُه ويدحضه، وإلا؛ دخل في عقول أكثر الناس.
{110} Kisha wakawahofisha wale wenye maono dhaifu na wapumbavu wa akili kwamba Musa "anataka" kwa kitendo chake hiki, “kuwatoa katika nchi yenu.” Yaani, anataka kuwatoa katika nchi zenu, "basi mnaamrisha nini?" Yaani, walishauriana kati yao kile watakachomfanyia Musa, na kile kitakachowaepushia madhara yao kulingana na madai yao. Kwani yale aliyokuja nayo ikiwa hayatakabiliwa na yenye kuyabatilisha na kuyakataa, na vinginevyo; yanaingia katika akili za wengi wa watu.
#
{111 - 112} فحينئذ انعقد رأيهم إلى أن قالوا لفرعون: {أرْجِهِ وأخاه}؛ أي: احبسهما وأمهلهما، وابعثْ في المدائن أناساً يحشُرون أهل المملكة ويأتون بكل سَحَّارٍ عليم؛ أي: يجيئون بالسحرة المهرة؛ ليقابلوا ما جاء به موسى، فقالوا: يا موسى {اجعلْ بيننا وبينَكَ موعداً لا نُخْلِفُهُ نحن ولا أنت مكاناً سُوىً. قال موعِدْكم يومُ الزينةِ وأن يُحْشَرَ الناس ضحىً. فتولَّى فرعونُ فجمَعَ كيدَه ثم أتى}.
{111 - 112} Basi hapo rai zao zikafungika mpaka wakamwambia Firauni: "Wakasema: Mwache kidogo yeye na kaka yake;” yaani, wazuie na wape muda, na tuma watu mijini wawakusanye wakazi wa ufalme huu na waje na kila mchawi ajuaye vyema. Yaani, waje na wachawi wenye ujuzi mkubwa, Ili wakabiliane na yale aliyokuja nayo Musa. Wakasema: Ewe Musa, “Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe, mahali palipo sawa. Akasema: Miadi yenu ni siku ya Sikukuu; na kwamba watu wakusanywe kabla ya adhuhuri. Basi Firauni akageuka akarudi, kisha akakusanya njama yake, kisha akaja.”
#
{113} وقال هنا: {وجاء السحرةُ فرعونَ}: طالبين منه الجزاء إن غلبوا، فقالوا: {إنَّ لنا لأجراً إن كُنَّا نحنُ الغالبينَ}.
{113} Na akasema hapa: "Na wakamjia wachawi Firauni" wakimwomba malipo ikiwa watashinda, na wakasema: "Hakika tutapata ujira ikiwa tutakuwa sisi ndio washindi."
#
{114} فقالَ فرعونُ: {نعم}: لكم أجر، {وإنَّكم لمن المقرَّبين}: فوعَدَهم الأجر والتقريب وعلو المنزلة عنده؛ ليجتهدوا ويبذُلوا، وسعهم وطاقتهم في مغالبة موسى.
{114} Firauni akasema: "Ndiyo!" Mna malipo, "Nanyi bila ya shaka ni katika waliotiwa karibu nami." Basi akawaahidi malipo, na kuwaweka karibu, na ujuu wa cheo kwake, ili wajitahidi na wafanye bidii, na uwezo na nguvu zao katika kumshinda Musa.
#
{115} فلما حضروا مع موسى بحضرة الخلق العظيم، {قالوا}: على وجه التألِّي وعدم المبالاة بما جاء به موسى، {يا موسى إما أن تُلْقِيَ}: ما معك، {وإما أن نكونَ نحنُ الملقينَ}.
{115} Basi walipohudhuria pamoja na Musa mbele ya viumbe vikubwa, "wakasema" kwa njia ya kujiinua juu na bila ya kujali yale aliyokuja nayo Musa, "Ewe Musa! Ima utupe wewe" hicho ulicho nacho "au tuwe sisi ndio watupao."
#
{116} فقالَ موسى: {ألقوا}: لأجل أن يرى الناسُ ما معهم وما مع موسى، {فلما ألقَوْا}: حبالَهم وعصيَّهم إذا هي من سحرهم كأنها حياتٌ تسعى، فسحروا {أعين الناس واسترهبوهم وجاؤوا بسحرٍ عظيم}: لم يوجدْ له نظيرٌ من السحر.
{116} Kwa hivo Musa akasema, “Tupeni!” ili watu waone yale waliyomo nayo na yale aliyo nayo Musa. "Basi walipotupa" kamba zao, na fimbo zao, basi tazama kutokana na uchawi ni kama kwamba ni nyoka wanaokwenda. Basi wakayaroga "macho ya watu na wakawatia hofu, na wakaleta uchawi mkubwa," ambao haukuwa na mfano wake katika uchawi.
#
{117} {وأوحَيْنا إلى موسى أن ألقِ عصاك}: فألقاها، {فإذا هي}: حيَّةٌ تسعى فتلقفت جميعَ ما يأفِكونَ؛ أي: يكذِّبون به ويموِّهون.
{117} "Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Itupe fimbo yako." Basi akaitupa, "Na tazama, ikawa" ni nyoka anayekwenda, na akavimeza vyote walivyovizulia uongo. Yaani, walivyokuwa wakidanganya kwavyo na kuficha ukweli.
#
{118} {فوقع الحقُّ}؛ أي: تبين، وظهر، واستعلن في ذلك المجمع، {وبَطَلَ ما كانوا يعملون}.
{118} "Basi haki ikathibiti;" yaani, ukabainika na kudhihirika, na ukawa wazi mkusanyiko huo "na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda."
#
{119} {فغُلِبوا هنالك}؛ أي: في ذلك المقام، {وانقلبوا صاغرينَ}؛ أي: حقيرين قد اضمحلَّ باطلُهم وتلاشى سحرهم ولم يحصُل لهم المقصود الذي ظنوا حصوله.
{119} "Kwa hivyo wakashindwa huko;" yaani, katika mahali pale, "na wakageuka kuwa wadogo." Yaani, hali ya kuwa wamedhalilika, tayari batili yao imekwisha isha, na uchawi wao umeshakatika, na wala hawakupata malengo ambayo walidhania kuwa watapata.
#
{120 - 122} وأعظم من تبيَّن له الحقُّ العظيم أهل الصنف والسحر [الذين] يعرفون من أنواع السحر وجزئياتِهِ ما لا يعرفه غيرُهم، فعرفوا أن هذه آية عظيمة من آيات الله، لا يدان لأحد بها، فألقي {السحرةُ ساجدينَ. قالوا آمنا بربِّ العالمين. ربِّ موسى وهارون}؛ أي: وصدَّقنا بما بُعِثَ به موسى من الآيات البينات.
{120 - 122} Na wakubwa zaidi waliobainikiwa na haki kubwa ni watu wa nyanja na uchawi ambao wanajua katika aina mbalimbali za uchawi na vipengele vyake kile ambacho hakijui asiyekuwa wao. Basi wakajua kwamba hii ni ishara kubwa katika ishara za Mwenyezi Mungu, na hakuna mtu ana uwezo dhidi yake. Kwa hivyo, "wachawi wakatupwa chini wakisujudu. Wakasema: Tumemwamini Mola Mlezi wa walimwengu wote. Mola Mlezi wa Musa na Haarun.” Yaani, na tumeyasadiki yale aliyotumwa nayo Musa katika Ishara zilizo wazi.
#
{123} فقال لهم {فرعونُ} متهدِّداً لهم على الإيمان: {آمنتُم به قبل أن آذنَ لكم}: كان الخبيث حاكماً مستبداً على الأبدان والأقوال، قد تقرَّر عنده وعندهم أن قوله هو المطاع وأمره نافذٌ فيهم ولا خروج لأحدٍ عن قوله وحكمه، وبهذه الحالة تنحطُّ الأمم وتضعف عقولها ونفوذها وتعجز عن المدافعة عن حقوقها، ولهذا قال الله عنه: {فاستخفَّ قومَه فأطاعوه}، وقال هنا: {آمنتُم به قبلَ أن آذنَ لكم}؛ أي: فهذا سوءُ أدبٍ منكم وتجرُّؤ عليَّ، ثم موَّه على قومه وقال: {إنَّ هذا لَمَكرٌ مكرتُموه في المدينة لتُخْرِجوا منها أهلها}؛ أي: إن موسى كبيركم الذي علَّمكم السحر، فتواطأتم أنتم وهو على أن تنغلِبوا له فيظهرَ فتتَّبعونه ثم يتَّبعكم الناس أو جمهورهم، فتُخْرِجوا منها أهلها، وهذا كذب يعلم هو ومن سبر الأحوال أن موسى عليه الصلاة والسلام لم يجتمع بأحدٍ منهم، وأنهم جُمِعوا على نظر فرعون ورسله، وأن ما جاء به موسى آية إلهيَّة، وأن السحرة قد بذلوا مجهودهم في مغالبة موسى حتى عجزوا وتبيَّن لهم الحق فاتبعوه. ثم توعَّدهم فرعون بقوله: فلسوف {تعلمونَ}: ما أحِلُّ بكم من العقوبة.
{123} "Firauni" akawaambia akiwatishia juu ya kuamini: " Mmemwamini kabla mimi kuwapa idhini" Mwovu huyu alikuwa mtawala dhalimu juu ya miili na maneno. Ilikwisha thibitika kwake na kwao kuwa kauli yake ndiyo yenye kutiiwa, na amri yake inatekelezeka juu yao na hakuna awezaye kutoka katika kauli yake na hukumu yake. Na katika hali hii umma zinaanguka, na akili zao zinadhoofika athari yake, na wanashindwa kutetea haki zao. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akasema juu yake: "Basi aliwachezea watu wake, na wakamtii;" na akasema hapa: "Mmemwamini kabla mimi kuwapa idhini?" Yaani, hii ni tabia mbaya kutoka kwenu na kufanya ujasiri wa kwenda kinyume nami, kisha akayabadilisha mambo kwa watu wake na akasema: "Hakika, hii ni njama mliyoipangia huko mjini ili muwatoae humo wenyewe." Yaani, Musa ni mkubwa wenu ambaye aliwafunza uchawi huu, basi mkakubaliana nyinyi na yeye kwamba wajishinde mbele yake, kwa hivyo awe mshindi na mumfuate, kisha watu wawafuate au wengi wao, na mkawatoe wenyewe humo. Na huu ni uongo ambao anajua yeye na mwenye kuchunguza hali kwamba Musa, rehema na amani ziwe juu yake, hakukutana na yeyote katika wao, na kwamba walikusanywa chini ya uangalizi wa Firauni na wajumbe wake, na kwamba yale aliyokuja nayo Musa ni Ishara ya kimungu, na kwamba wachawi walijitahidi uwezo wao kumshinda Musa mpaka wakashindwa na haki ikawabainikia, kwa hivyo wakamfuata. Kisha Firauni akawatishia kwa kauli yake: basi karibu “mtajua” adhabu itakayowapata.
#
{124} {لأقطِّعنَّ أيديَكم وأرجلَكم من خلافٍ}: زعم الخبيثُ أنَّهم مفسدون في الأرض، وسيصنع بهم ما يُصنع بالمفسدين من تقطيع الأيدي والأرجل من خلافٍ؛ أي: اليد اليمنى والرجل اليسرى، {ثم لأصَلِّبَنَّكُم}: في جذوع النخل؛ لتختَزوا بزعمه {أجمعينَ}؛ أي: لا أفعل هذا الفعل بأحدٍ دون أحدٍ، بل كلُّكم سيذوق هذا العذاب.
{124} "Lazima nitaikata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha." Mwovu huyu alidai kuwa wao ni waharibifu katika ardhi, na atawafanyia yale wanayofanyiwa waharibifu kwa kuikata mikono yao na miguu ya kwa kinyume. Yaani, mkono wa kulia na mguu wa kushoto, "Kisha lazima nitawasulubisha," kwenye mashina ya mitende, ili mfedheheke – kulingana na madai yake "nyote." Yaani, sitamfanyia kitendo hiki mtu mmoja bila ya mwingine. Bali nyinyi nyote mtaionja adhabu hii.
#
{125} فقال السحرة الذين آمنوا لفرعون حين تهدَّدهم: {إنَّا إلى ربِّنا منقلبونَ}؛ أي: فلا نبالي بعقوبتك؛ فالله خيرٌ وأبقى؛ فاقضِ ما أنت قاضٍ.
{125} Basi wachawi hao walioamini wakamwambia Firauni alipowatishia, “Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.” Yaani, sisi hatujali adhabu yako hiyo. Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mbora zaidi na wa kudumu zaidi. Kwa hivyo hukumu utakavyohukumu.
#
{126} {وما تَنقِمُ منَّا}؛ أي: وما تعيب منَّا على إنكارك علينا وتوعُّدك لنا؛ فليس لنا ذنبٌ {إلَّا أنْ آمنَّا بآيات ربِّنا لما جاءتْنا} ؛ فإنْ كان هذا ذنباً يُعاب عليه ويستحقُّ صاحبه العقوبة؛ فهو ذنبُنا. ثم دعوا الله أن يثبِّتهم ويصبِّرهم، فقالوا: {ربَّنا أفرغْ}؛ أي: أفض {عليْنا صبراً}؛ أي: عظيماً كما يدلُّ عليه التنكير؛ لأنَّ هذه محنة عظيمة تؤدي إلى ذهاب النفس، فيحتاج فيها من الصبر إلى شيء كثير؛ ليثبت الفؤاد ويطمئن المؤمن على إيمانِهِ ويزول عنه الانزعاج الكثير. {وتوفَّنا مسلمينَ}؛ أي: منقادين لأمرك متَّبعين لرسولك. والظاهر أنه أوقع بهم ما توعَّدهم عليه، وأنَّ الله تعالى ثبَّتهم على الإيمان.
{126} "Nawe hutushutumu kwa chuki;" yaani, mnaona kosa gani kwetu ndiyo unatupinga na kututishia? Sisi hatuna dhambi "isipokuwa kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola wetu Mlezi pindi zilipotujia." Kwa hivyo, ikiwa hii ndiyo dhambi ya kulaumiwa juu yake na mwenyewe astahiki adhabu, basi hii ni dhambi yetu. Kisha wakamwomba Mwenyezi Mungu awaweke imara na awafanye kuwa na subira, wakasema: "Ewe Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira;" yaani, kubwa kama linavyoonyeshwa hilo na ukawaida wa neno lililotumika ‘subira.’ Kwa sababu hili ni jaribio kubwa linalopelekea kupoteza nafsi. Kwa hivyo inahitajika subira kubwa katika hilo, ili kuuimarisha moyo, na kumtuliza Muumini juu ya imani yake, na aondokewe na masumbufu mengi; "utufishe hali ya kuwa ni Waislamu." Yaani, hali ya kuwa tunaifuata amri yako, na kumfuata Mtume wako. Na lililo dhahiri ni kwamba aliwafanyia yale aliyowatishia kwayo, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaweka imara juu ya imani.
#
{127} هذا وفرعون وملؤه وعامتهم المتبعون للملأ قد استكبروا عن آيات الله وجحدوا بها ظلماً وعلوًّا وقالوا لفرعون مهيجين له على الإيقاع بموسى وزاعمين أن ما جاء باطل وفساد: {أتذرُ موسى وقومَه ليفسِدوا في الأرض}: بالدعوة إلى الله وإلى مكارم الأخلاق ومحاسن الأعمال التي هي الصلاح في الأرض وما هم عليه هو الفساد، ولكنَّ الظالمين لا يبالون بما يقولون، {وَيَذَرَكَ وآلهتَكَ}؛ أي: يدعك أنت وآلهتك، وينهى عنك، ويصد الناس عن اتباعك، فقال فرعونُ مجيباً لهم بأنه سيدع بني إسرائيل مع موسى بحالةٍ لا ينمون فيها ويأمنُ فرعونُ وقومُه بزعمه من ضررهم: {سَنُقَتِّلُ أبناءَهم ونستحيي نساءَهم}؛ أي: نستبقيهنَّ فلا نقتلهنَّ؛ فإذا فعلْنا ذلك؛ أمنَّا مِن كثرتِهِم، وكنَّا مستخدمين لباقيهم ومسخِّرين لهم على ما نشاء من الأعمال، {وإنَّا فوقَهم قاهرونَ}: لا خروج لهم عن حكمنا ولا قدرة. وهذا نهاية الجَبَروت من فرعون والعتوِّ والقسوة.
127. Hayo, na Firauni na waheshimiwa wake na watu wao wa kawaida waliowafuata waheshimiwa hao, walizifanyia kiburi Aya za Mwenyezi Mungu, na wakazikataa kwa dhuluma na kiburi, na wakamwambia Firauni wakimshawishi achukue hatua kali dhidi ya Musa na kudai ya kwamba yale aliyokuja nayo ni batili na uharibifu, "unamuacha Musa na kaumu yake ili wafanye uharibifu katika ardhi;" kwa kulingania kwa Mwenyezi Mungu na kwa maadili mema na matendo mazuri ambayo ni kufanya mambo kutengenea katika ardhi, na ilhali wao wanayoyafanya ni uharibifu, lakini madhalimu hawajali yale wanayoyasema, "na akuache wewe na miungu yako?" Yaani, akuache wewe na miungu yako, na akataze dhidi yako, na kuwazuia watu kukufuata. Firauni akasema katika kuwajibu kuwa atawaacha wana wa Israili pamoja na Musa katika hali ambayo hawatakuwa, naye Firauni na kaumu yake kwa madai yake watasalimika kutokana na madhara yao. "Tutawauwauwa wavulana wao, na tuwaache hai wanawake wao;" yaani, tutawaacha wanawake na hatutawaua. Kwa hivyo, Tutakapofanya hivyo, Tukasalimika kutokana na wingi wao, na tutawatumia waliobakia wao na tutawatiisha katika kazi zozote zile tuzitakazo. "Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao," hawana pa kutokea nje ya utawala wetu wala uwezo wowote. Na huu ndio mwisho wa ukandamizaji wa Firauni na kiburi chake na ugumu wake.
#
{128} فقال {موسى لقومه}: موصياً لهم ـ في هذه الحالة التي لا يقدرون معها على شيء ولا مقاومة ـ بالمقاومة الإلهية والاستعانة الربانيَّة: {استعينوا بالله}؛ أي: اعتمدوا عليه في جلب ما ينفعكم ودفع ما يضرُّكم، وثِقوا بالله أنه سيتمُّ أمركم، {واصبروا}؛ أي: الزموا الصبر على ما يحلُّ بكم منتظرين للفرج. {إنَّ الأرض لله}: ليست لفرعون ولا لقومه حتى يتحكَّموا فيها، {يورِثُها مَن يشاءُ من عبادِهِ}؛ أي: يداولها بين الناس على حسب مشيئته وحكمته، ولكن العاقبة للمتَّقين؛ فإنهم وإن امتُحِنوا مدة ابتلاء من الله وحكمة؛ فإنَّ النصر لهم، {والعاقبةُ}: الحميدة لهم على قومهم. وهذه وظيفة العبد؛ أنَّه عند القدرة أن يفعل من الأسباب الدافعة عنه أذى الغير ما يقدر عليه وعند العجز أن يصبر ويستعين الله وينتظر الفرج.
{128} Kisha "Musa akawaambia kaumu yake" akiwausia - katika hali hii ambayo hawakuweza kufanya chochote au kupinga – kupinga kwa kiungu na usaidizi wa kiungu: "Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, mtegemeeni Yeye katika kuleta yenye kuwanufaisha na kuwaepushia yenye kuwadhuru, na kuweni na imani na Mwenyezi Mungu kwamba ataikamilisha amri yenu, "na subirini." Yaani, dumisheni subira kwa yale yanayowasibu mkiingojea faraja. "Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu" si ya Firauni wala kaumu yake ili wawe na mamlaka juu yake wao tu "anairithisha amtakaye katika waja wake." Yaani, anaizungusha baina ya watu kulingana na mapenzi yake na hekima yake, lakini mwisho mwema ni wa wale walio wema. Kwani wao hata kama watapewa mitihani kwa muda kama mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hekima, basi hakika ushindi ni wao, "mwisho" wa kusifiwa ni wao dhidi ya kaumu yao. Na hii ndiyo kazi ya mja, kwamba anapokuwa na uwezo, afanye sababu zozote awezazo kujizuia madhara ya wengine, na anaposhindwa, basi awe na subira, na atafute msaada wa Mwenyezi Mungu, na angojee faraja.
#
{129} {قالوا}: لموسى متضجِّرين من طول ما مكثوا في عذاب فرعون وأذيَّته: {أوذينا من قبل أن تأتِيَنا}: فإنهم يسوموننا سوء العذاب يذبِّحون أبناءنا ويستحيون نساءنا، {ومن بعدِ ما جئتنا}: كذلك، فقال لهم موسى مرجياً لهم بالفرج والخلاص من شرِّهم: {عسى ربُّكم أن يُهْلِكَ عدوَّكم ويستخلِفَكم في الأرض}؛ أي: يمكِّنكم فيها ويجعل لكم التدبير فيها، {فينظرَ كيف تعملونَ}: هل تشكُرون أم تكفُرون؟ وهذا وعدٌ أنجزه الله لمَّا جاء الوقت الذي أراده الله.
{129} "Wakasema" kumwambia Musa huku wakilalamika juu ya kukaa kwao muda mrefu katika adhabu ya Firauni na maudhi yake: "Tumeudhiwa kabla wewe kutujia" kwa maana wanatupa adhabu mbaya, wakiwachinja wana wetu wa kiume na wanawaacha hai wanawake wetu; "Na baada ya wewe kutujia! Vile vile. Basi Musa akawaambia akitaraji watapata faraja, na kuokoka kutokana na uovu wao: "Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui wenu, na akawafanya nyinyi ndio wa kufuatia kushika ardhi." Yaani, awape uthabiti ndani yake na awafanye nyinyi ndio wenye kuiendesha, "ili atazame mtakavyokuja tenda nyinyi." Je, mtashukuru au mtakufuru? Na hii ni ahadi ambayo Mwenyezi Mungu aliitimiza wakati ulipokuja muda ambao mwenyezi Mungu aliutaka.
#
{130} قال الله تعالى في بيان ما عامل به آلَ فرعون في هذه المدة الأخيرة ـ إنها على عادته وسنته في الأمم أن يأخُذَهم {بالبأساء والضرَّاء لعلهم يضَّرَّعون} الآيات ـ: {ولقد أخذنا آل فرعون بالسنين}؛ أي: بالدُّهور والجدب، {ونقص من الثمرات لعلهم يذَّكَّرون}؛ أي: يتَّعظون أنَّ ما حلَّ بهم وأصابهم معاتبة من الله لهم لعلَّهم يرجِعون عن كفرهم، فلم ينجعْ فيهم ولا أفاد، بل استمرُّوا على الظُّلم والفساد.
{130} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema katika kueleza yale aliyoyawafanyia watu wa Firauni katika kipindi hiki cha mwisho – Nacho ni kama desturi yake na sunna yake kwa umma mbalimbali kwamba huwachukua "kwa balaa na dhiki ili huenda wakanyenyekea" hadi mwisho wa Aya hizi. "Na hakika tuliwachukua watu wa Firauni kwa miaka" yaani, kwa misiba na ukame, “na kwa upungufu katika mazao, huenda wakakumbuka.” Yaani, wakaidhika kwamba yale yaliyowapata na kuwasibu ni lawama kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yao, huenda wakaiacha kufuru yao. Lakini hayakuawaathiri wala hayakuwafaa. Bali waliendelea na dhuluma na uharibifu.
#
{131} {فإذا جاءتهم الحسنةُ}؛ أي: الخصب وإدرار الرزق، {قالوا لنا هذه}؛ أي: نحن مستحقُّون لها، فلم يشكروا الله عليها، {وإن تصِبْهم سيئةٌ}؛ أي: قحط وجدب، {يطَّيَّروا بموسى ومن معه}؛ أي: يقولوا: إنما جاءنا بسبب مجيء موسى واتباع بني إسرائيل له. قال الله تعالى: {ألا إنَّما طائِرُهم عند الله}؛ أي: بقضائه وقدرته، ليس كما قالوا، بل إن ذنوبهم وكفرهم هو السبب في ذلك، بل أكثرهم لا يعلمونَ؛ أي: فلذلك قالوا ما قالوا.
{131} "Basi wakijiwa na zuri," yaani, rutuba na riziki nyingi, "wanasema: "Ni haki yetu hii." Yaani, sisi tunaustahiki (uzuri huu), basi hawakumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake. "Na likiwasibu ovu;" yaani, ukame na utasa, "wanaona mkosi kwa Musa na wale walio pamoja naye." Yaani wanasema: yametujia haya tu kwa sababu ya kuja kwa Musa na wana wa Israili kumfuata. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Tazama! Hakika mkosi huo unatoka kwa Mwenyezi Mungu.” Yaani, kwa majaliwa yake na uwezo wake, na si kama walivyosema. Bali dhambi zao na ukafiri wao ndiyo sababu ya hayo, lakini wengi wao hawajui. Yaani, ndiyo maana wakasema yale waliyoyasema.
#
{132} {وقالوا}: مبيِّنين لموسى أنهم لا يزالون ولا يزولون عن باطلهم: {مهما تأتِنا به من آيةٍ لِتَسْحَرَنا بها فما نحن لك بمؤمنين}؛ أي: قد تقرَّر عندنا أنك ساحرٌ؛ فمهما جئت بآية؛ جزمنا أنها سحرٌ؛ فلا نؤمن لك ولا نصدِّق. وهذا غاية ما يكون من العناد أن يبلغ بالكافرين إلى أن تستوي عندهم الحالات سواء نزلت عليهم الآيات أم لم تنزل.
{132} "Na walisema" wakimbainishia Musa kwamba hawataacha wala hawatatoka katika batili yao. "Hata ukitujia na Ishara yoyote ile kutufanyia uchawi kwazo, basi sisi hatutakuamini." Yaani, tayari imeshatuthibitikia kwamba wewe ni mchawi. Basi hata ukija na ishara ipi, tutakuwa na uhakika kwamba ni uchawi, kwa hivyo hatutakuamini, wala hatutakusadiki. Na hiki ndicho kiwango cha mwisho unachofikia ukaidi. Kwamba makafiri wafikie kiwango kwamba hali zao ziwe sawa. Sawa iwateremkie ishara mbalimbali au zisiteremke.
#
{133} {فأرسلنا عليهم الطوفان}؛ أي: الماء الكثير الذي أغرق أشجارهم وزروعهم وأضرَّهم ضرراً كثيراً، {والجراد}: فأكل ثمارَهم وزروعَهم ونباتهم، {والقُمَّلَ}: قيل: إنه الدُّباء؛ أي: صغار الجراد، والظاهر أنه القمل المعروف، {والضفادع}: فملأت أوعيتهم وأقلقتهم وآذتهم أذيَّة شديدةً، {والدم}: إما أن يكونَ الرعاف، أو كما قال كثير من المفسرين: إنَّ ماءهم الذي يشربون انقلب دماً، فكانوا لا يشربون إلاَّ دماً ولا يطبخون [إلاّ بدم]. {آياتٍ مفصَّلاتٍ}؛ أي: أدلَّة وبيِّنات على أنَّهم كانوا كاذبين ظالمين، وعلى أن ما جاء به موسى حقٌّ وصدقٌ. {فاستكبروا}: لما رأوا الآيات، {وكانوا}: في سابق أمرهم {قوماً مجرمين}: فلذلك عاقبهم الله تعالى بأن أبقاهم على الغيِّ والضلال.
{133} “Basi tukawatumia tufani;" yaani, maji mengi ambayo yaliizamisha miti yao na mimea yao, na ikawadhuru madhara mengi, "na nzige" wakala matunda yao na mazao yao na mimea yao, "na chawa." Ilisemwa ni nzige wachanga, lakini inavyojulikana ni kwamba walikuwa wale chawa wanaojulikana, "na vyura." Basi wakajaza vyombo vyao, na wakawatia wasiwasi na wakawaudhi udhia mkubwa, "na damu." Ima damu ya puani, au kama walivyosema wengi wa wafasiri kuwa maji yao ambayo walikuwa wakinywa yaligeuka yakawa damu. Kwa hivyo hawakuwa wakinywa isipokuwa damu, na wala hawapiki [isipokuwa damu]; "ili ziwe ishara za kina." Yaani, ishara na hoja za waziwazi juu ya kwamba wao walikuwa waongo na madhalimu, na juu ya kwamba aliyokuja nayo Musa ni ya haki na ukweli. "Lakini wakatakabari" walipoziona Ishara hizo, "na wakawa" katika mambo yao yaliyotangulia "kaumu wahalifu." Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaadhibu kwa kuwaacha katika ukengeufu na upotofu.
#
{134} {ولما وقع عليهم الرِّجْزُ}؛ أي: العذاب؛ يحتمل أنَّ المراد به الطاعون كما قاله كثيرٌ من المفسِّرين، ويحتمل أن يُراد به ما تقدَّم من الآيات الطوفان والجراد والقمَّل والضفادع والدَّم؛ فإنها رجزٌ وعذابٌ، وإنهم كلَّما أصابهم واحد منها؛ {قالوا يا موسى ادعُ لنا ربك بما عَهدَ عندك}؛ أي: تشفَّعوا بموسى بما عَهدَ الله عنده من الوحي والشرع. {لئن كشفتَ عنَّا الرِّجْزَ لنؤمننَّ لك ولنرسلنَّ معك بني إسرائيل}: وهم في ذلك كذبةٌ لا قصدَ لهم إلا زوالُ ما حلَّ بهم من العذاب، وظنُّوا إذا رفع لا يصيبهم غيره.
{134} “Na ilipowaangukia adhabu." Inawezekana kwamba kinachomaanishwa na hilo ni tauni kama walivyosema wengi wa wafasiri, na inawezekana kwamba kinachomaanishwa ni ishara zile zilizotangulia miongoni mwa tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu. Kwani hizo ni mateso na adhabu, na kwamba kila waliposibiwa na moja yake; "Wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa yale aliyokuahidi." Yaani, walitafuta uombezi kwa Musa kwa sababu ya yale aliyomuahidi Mwenyezi Mungu ya ufunuo na sheria. "Ukituondolea adhabu hii, hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili waende pamoja nawe." Lakini walikuwa waongo katika hilo, hawakuwa na lengo lolote isipokuwa kuisha kwa adhabu waliyomo, na wakadhani kwamba ikiondoka, haiwapati nyingineyo.
#
{135} {فلما كشَفْنا عنهم الرِّجْزَ إلى أجل هم بالغوهُ}؛ أي: إلى مدة قدر الله بقاءهم إليها، وليس كشفاً مؤبَّداً، وإنما هو موقت، {إذا هم ينكُثون}: العهد الذي عاهدوا عليه موسى ووعدوه بالإيمان به وإرسال بني إسرائيل؛ فلا آمنوا به ولا أرسلوا معه بني إسرائيل، بل استمرُّوا على كفرهم يعمهون وعلى تعذيب بني إسرائيل دائبين.
{135} "Basi tulipowaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie;" yaani, muda aliouandika Mwenyezi Mungu kwamba watabaki waufikie, wala si kuondoa kwa kudumu, bali ni kwa muda tu. "Tazama! wakavunja ahadi yao;" ambayo walimuahidi Musa, na walimuahidi kumuamini na kuwaachilia wana wa Israeli. Lakini hawakumuamini, wala hawakuwaachilia Wana wa Israili pamoja naye, bali waliendelea na ukafiri wao kipofu, na wakawatesa Wana wa Israili kama ada yao.
#
{136} {فانتقمنا منهم}؛ أي: حين جاء الوقت الموقَّت لهلاكهم؛ أمر الله موسى أن يسري ببني إسرائيل ليلاً، وأخبره أن فرعون سيتبعُهم هو وجنوده. {فأرسلَ فرعونُ في المدائن حاشرين} يجمعونَ الناس لِيَتْبَعوا بني إسرائيل، وقالوا لهم: {إنَّ هؤلاء لَشِرْذمةٌ قليلون. وإنَّهم لنا لغائظونَ. وإنَّا لجميعٌ حاذرون. فأخْرَجْناهم من جناتٍ وعيون. وكنوزٍ ومقام كريم. كذلك وأورَثْناها بني إسرائيل. فأتْبعوهم مشرقينَ. فلما تراءى الجمعانِ قال أصحابُ موسى إنا لَمُدْرَكونَ. قال كلاَّ إن معي ربي سيهدين. فأوحَيْنا إلى موسى أنِ اضرِبْ بعصاك البحرَ فانفلق فكان كلُّ فرقٍ كالطودِ العظيم. وأزلفنا ثَمَّ الآخرين. وأنجينا موسى ومن معه أجمعين. ثم أغرقنا الآخرين}. وقال هنا: {فأغرَقْناهم في اليمِّ بأنَّهم كذَّبوا بآياتنا وكانوا عنها غافلين}؛ أي: بسبب تكذيبهم بآيات الله، وإعراضهم عمَّا دلَّت عليه من الحقِّ.
{136} “Basi tukawapatiliza;” yaani, wakati uliowekwa wa kuangamizwa kwao ulipofika, Mwenyezi Mungu alimuamuru Musa akwende na Wana wa Israili usiku, na akamjulisha kuwa Firauni atamfuata pamoja na majeshi wake. "Kwa hivyo Firauni akawatuma mijini wakusanyaji," ili wawakusanye watu ili kuwafuata Wana wa Israili, na wakawaambia: "Hakika hawa ni kikundi kidogo. Nao wametuudhi. Nasi hakika ni wengi, wenye kuchukua hadhari. Basi tukawatoa katika mabustani na chemchemi. Na mahazina, na vyeo vya heshima. Kadhalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili. Basi wakawafuata lilipochomoza jua. Na ilipoonana mikusanyiko mawili hiyo, wenza wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumefikiwa! (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! Basi tukamfunulia wahyi Musa kwamba: Ipige bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. Na tukawajongeza hapo wale wengine. Na tukamuokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote. Kisha tukawazamisha hao wengine." Na akasema hapa: "Tukawazamisha katika bahari kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na wakawa wanazighafiliki." Yaani, kwa sababu ya kukadhibisha kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuyapa mgongo yale zilizoyaashiria ya haki.
#
{137} {وأورثنا القوم الذين كانوا يُسْتَضْعَفونَ}: في الأرض؛ أي: بني إسرائيل الذين كانوا خدمة لآل فرعون يسومونهم سوء العذاب، أورثهم الله {مشارقَ الأرض ومغاربها}: والمراد بالأرض ها هنا أرض مصر التي كانوا فيها مستضعفين أذلين؛ أي: ملَّكهم الله جميعها ومكَّنهم فيها، {التي باركنا فيها وتمَّتْ كلمةُ ربك الحسنى على بني إسرائيل بما صبروا}: حين قال لهم موسى: {استعينوا باللَّهِ واصبِروا إنَّ الأرضَ للَّه يورِثها من يشاءُ من عباده والعاقبةُ للمتَّقين}، {ودمَّرْنا ما كان يصنعُ فرعونُ وقومُهُ}: من الأبنية الهائلة والمساكن المزخرفة، {وما كانوا يعرِشون}: فتلك بيوتهم [خاوية] بما ظلموا إن في ذلك لآية لقوم يعلمون.
{137} “Na tukawarithisha kaumu wale waliokuwa wakidhoofishwa.” Yaani, Wana wa Israili ambao walikuwa wakiwatumikia watu wa Firauni, wakiwatia mateso makali sana. Mwenyezi Mungu akawarithisha "mashariki ya ardhi na magharibi yake." Na kinachomaanishwa na ardhi hapa ni nchi ya Misri ambayo walikuwa wakidhoofishwa humo, wakidhalilishwa. Yaani, Mwenyezi Mungu aliwamilikisha yote na akawatia nguvu humo, "ambayo tulibariki ndani yake. Na likatimia neno jema la Mola wako Mlezi juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyosubiri." Wakati Musa alipowaambia: "Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu, huirithisha amtakaye katika waja wake, na mwisho mwema ni wa wacha Mungu;" "Na tukayaangamiza yale aliyokuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake" miongoni mwa majumba makubwa na makazi ya yaliyopambwa, "na yale waliyokuwa wakiyajenga." Basi hizo ndizo nyumba zao "zilizo tupu" kwa sababu ya walivyodhulumu. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu wanaojua.
#
{138} {وجاوزنا ببني إسرائيل البحر}: بعدما أنجاهم الله من عدوِّهم فرعون وقومه وأهلكهم الله، وبنو إسرائيل ينظرون، {فأتَوْا}؛ أي: مرُّوا {على قوم يعكُفون على أصنامٍ لهم}؛ أي: يقيمون عندها ويتبرَّكون بها ويعبُدونها، فقالوا من جهلهم وسَفَهِهم لنبيِّهم موسى بعدما أراهم الله من الآيات ما أراهم: {يا موسى اجعلْ لنا إلهاً كما لهم آلهةٌ}؛ أي: اشرع لنا أن نتَّخذ أصناماً آلهة كما اتَّخذها هؤلاء، فقال لهم موسى: {إنَّكم قومٌ تجهلونَ}: وأيُّ جهل أعظم من جَهِل ربَّه وخالقَه، وأراد أن يسوِّيَ به غيره ممَّن لا يملِكُ نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً؟!
{138} "Na tukawavusha bahari Wana wa Israili" baada ya Mwenyezi Mungu kuwaokoa kutoka kwa adui yao Firauni na kaumu yake, na Mwenyezi Mungu akawaangamiza hali ya kuwa Wana wa Israili wanawatazama. "Kisha wakajia," yaani, walipita karibu na "kaumu waliokuwa wanaabudu masanamu yao." Yaani, wanakaa hapo na kutafuta baraka kutoka kwayo na kuyaabudu. Kwa hivyo kutokana na ujinga wao na upumbavu wao wakamwambia Nabii wao Musa baada ya Mwenyezi Mungu kuwaonyesha ishara mbalimbali alizowaonyesha:"Ewe Musa! Tufanyie mungu kama hawa walivyo na miungu." Yaani, tufanyie sheria inayoturuhusu kuyafanya masanamu kuwa miungu kama walivyoyafanya hawa, lakini Musa akawaambia: "Hakika nyinyi ni kaumu msiojua kitu." Na ni ujinga upi ulio mkubwa zaidi kuliko ujinga wa yule asiyemjua Mola wake Mlezi na Muumba wake, na akataka kumtoshanisha na asiyekuwa Yeye miongoni mwa wale wasiomiliki manufaa wala madhara, wala kifo, wala uhai, wala ufufuo?
#
{139} ولهذا قال لهم موسى: {إنَّ هؤلاء مُتَبَّرٌ ما هم فيه وباطلٌ ما كانوا يعملونَ}: لأن دعاءهم إياها باطلٌ وهي باطلة بنفسها؛ فالعمل باطلٌ وغايته باطلةٌ.
{139} Na ndiyo maana Musa akawaambia: "Hakika hawa, haya waliyomo yatakuja angamia, na ni batili hayo waliyokuwa wakiyafanya." Kwa sababu kuwaomba kwao ni batili, nao yenyewe ni batili. Kwa hivyo matendo hayo ni batili na makusudio yake ni batili.
#
{140} {قال أغيرَ الله أبغيكم إلهاً}؛ أي: أطلب لكم إلهاً غير الله المألوه الكامل في ذاته وصفاته وأفعاله. {وهو فضَّلكم على العالمين}: فيقتضي أن تقابلوا فضله وتفضيله بالشكرِ، وذلك بإفراد الله وحدَه بالعبادة والكفرِ بما يُدعى من دونه.
{140} "Akasema, "Je, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu." Yaani, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, anayefanyiwa uungu, Mkamilifu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake. "Ilhali Yeye ndiye aliyewafadhilisha juu ya walimwengu wote?" Basi inatakiwa muikabili adhila yake na kuwaboresha kwake kwa kushukuru, na hilo ni kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu peke yake kwa ibada, na kukufuru wanaoabudiwa kando na Yeye.
#
{141} ثم ذكَّرهم ما امتنَّ الله به عليهم فقال: {وإذ أنجيناكم من آل فرعونَ}؛ أي: من فرعون وآله، {يسومونكم سوءَ العذابِ}؛ أي: يوجِّهون إليكم من العذاب أسوأه، وهو أنهم كانوا يذبحون {أبناءكم ويَسْتَحيون نساءَكم وفي ذلِكم}؛ أي: النجاة من عذابهم، {بلاءٌ من ربِّكم عظيمٌ}؛ أي: نعمةٌ جليلةٌ ومنحةٌ جزيلةٌ، أو وفي ذلك العذاب الصادر منهم لكم بلاءٌ من ربِّكم عليكم عظيم.
{141} Kisha akawakumbusha yale aliyowaneemesha kwayo Mwenyezi Mungu, akasema: "Na pale tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni;" yaani, kutoka kwa Firauni na watu wake "waliowatia adhabu mbaya zaidi." Yaani, waliowaelekezea adhabu mbaya kabisa. Nayo ni kwamba walikuwa wakiwachinja "wavulana wenu, na wakawaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo." Yaani, kuokoka na adhabu yao, "yalikuwa majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, neema kubwa na kipawa kikubwa au katika adhabu hiyo iliyotoka kwao kulikuwa na majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi.
#
{142} فلما ذكَّرهم موسى ووعظهم؛ انتَهَوْا عن ذلك، ولما أتمَّ الله نعمته عليهم بالنجاة من عدوهم وتمكينهم في الأرض؛ أرادَ تبارك وتعالى أن يُتِمَّ نعمته عليهم بإنزال الكتاب الذي فيه الأحكام الشرعيَّة والعقائد المرضيَّة، فواعد موسى ثلاثين ليلة، وأتمَّها بعشر، فصارت أربعين ليلة؛ ليستعدَّ موسى ويتهيَّأ لوعد الله ويكون لنزولها موقع كبير لديهم وتشوق إلى إنزالها، ولما ذهب موسى إلى ميقات ربِّه، قال لهارون موصياً له على بني إسرائيل من حرصه عليهم وشفقته: {اخْلُفْني في قَوْمي}؛ أي: كنْ خليفتي فيهم، واعمل فيهم بما كنت أعمل، {وأصلِحْ}؛ أي: اتَّبع طريق الصلاح، {ولا تتَّبِعْ سبيلَ المفسدين}: وهم الذين يعملون بالمعاصي.
{142} Musa alipowakumbusha na akawapa mawaidha, wakakomeka na hilo. Na Mwenyezi Mungu alipokamilisha neema zake juu yao kwa kuwaokoa kutoka kwa adui yao na kuwatia nguvu katika ardhi, Yeye Mwingi wa baraka alitaka kuwatimizia neema yake juu yao kwa kuteremsha Kitabu ambacho kina hukumu za kisheria na itikadi zilizoridhiwa, basi akamuahidi Musa usiku thelathini, na akaikamilisha kwa (usiku) kumi, basi zikawa usiku arobaini. Ili Musa ajiandae na kujitayarisha kwa ajili ya ahadi ya Mwenyezi Mungu, na ili kushuka kwake kuwe na pahali pakubwa kwao, na wawe na hamu ya kushuka kwake. Na Musa alipokwenda kwenye miadi ya Mola wake Mlezi, akamwambia Haarun akimuusia kuhusu Wana wa Israili kwa sababu ya kuwajali kwake na huruma yake: "Shika pahali pangu katika kaumu yangu." Yaani, kuwa mfuatilizi wangu miongoni mwao, na fanya miongoni mwao kama nilivyokuwa nikitenda, "na utengeneze." Yaani, fuata njia ya utengenezaji mambo, "wala usifuate njia ya waharibifu." Nao ndio wale wafanyao maasia.
#
{143} {ولمَّا جاء موسى لميقاتنا}: الذي وقَّتْناه له لإنزال الكتاب، {وكلَّمَه ربُّه}: بما كلَّمه من وحيه وأمره ونهيه؛ تشوَّق إلى رؤية الله، ونَزَعَتْ نفسُه لذلك حبًّا لربِّه ومودَّة لرؤيته، فـ {قال ربِّ أرني أنظرْ إليك}، فقال الله: {لن تَراني}؛ أي: لن تقدِرَ الآن على رؤيتي؛ فإنَّ الله تبارك وتعالى أنشأ الخلق في هذه الدار على نشأة لا يقدرون بها ولا يثبتون لرؤية الله، وليس في هذا دليلٌ على أنَّهم لا يرونه في الجنة؛ فإنه قد دلَّت النصوص القرآنيَّة والأحاديث النبويَّة على أن أهل الجنة يرون ربَّهم تبارك وتعالى ويتمتَّعون بالنظر إلى وجهه الكريم. وأنه يُنْشِئُهم نشأةً كاملةً يقدرون معها على رؤية الله تعالى، ولهذا رتَّب الله الرؤية في هذه الآية على ثبوت الجبل، فقال مقنعاً لموسى في عدم إجابتِهِ للرؤية: {ولكِنِ انظرْ إلى الجبل فإنِ استقرَّ مكانَه}: إذا تجلَّى اللهُ له، {فسوف تراني فلمَّا تجلَّى ربُّه للجبل}: الأصمِّ الغليظ، {جعله دكًّا}؛ أي: انهال مثل الرمل انزعاجاً من رؤية الله وعدم ثبوتٍ لها، {وخرَّ موسى}: حين رأى ما رأى، صَعِقاً فتبيَّن له حينئذٍ أنه إذا لم يثبت الجبلُ لرؤية الله؛ فموسى أولى أن لا يثبتَ لذلك، واستغفر ربَّه لما صدر منه من السؤال الذي لم يوافقْ موضعاً، و {قالَ سبحانك}؛ أي: تنزيهاً لك وتعظيماً عما لا يليق بجلالك، {تبتُ إليك}: من جميع الذنوب وسوء الأدب معك، {وأنا أول المؤمنين}؛ أي: جدَّد عليه الصلاة والسلام إيمانه بما كمَّل اللهُ له مما كان يجهله قبل ذلك.
{143} "Na alipokuja Musa kwenye miadi yetu" ambao tulimuwekea kwa sababu ya kuteremsha Kitabu, "na Mola wake Mlezi akamuongelesha" kwa yale aliyomwongelesha katika wahyi wake na maamrisho yake na makatazo yake, akawa na hamu ya kumuona Mwenyezi Mungu, na nafsi yake ikaelekea kufanya hivyo kwa sababu ya kumpenda Mola wake Mlezi na kupenda kumuona. Kwa hivyo "alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame.” Basi Mwenyezi Mungu akasema: "Hutaniona." Yaani, Hutaweza kuniona sasa. Kwani Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka, Mtukufu aliwaanzisha viumbe katika nyumba hii kwa mwanzisho ambao hawawezi kwa huo wala hawawezi kuwa thabiti katika kumwona Mwenyezi Mungu. na hakuna ushahidi wowote katika hili kwamba hawatamwona katika Pepo. Kwa maana Maandiko ya Qur-ani Tukufu na Hadithi za Mtume zimeashiria kwamba wakazi wa Peponi watamuona Mola wao Mlezi, Mwingi wa baraka, Mtukufu, na watafurahia kwa kuutazama uso wake mtukufu. Na kwamba atawaanzisha mwanzisho kamilifu watakaoweza pamoja nao kumwona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akafungamanisha kuona katika Aya hii na uthabiti wa mlima ule. Kwa hivyo akasema akimfanya Musa kukubali kwamba hatamwezesha kumuona; "Lakini utazame huo mlima ikiwa utabaki pahali pake" wakati Mwenyezi Mungu atakapoudhihirikia "basi utaniona. Basi alipojionyesha Mola wake Mlezi kwa mlima huo" usiosikia, mkubwa mno, "akaufanya upasukepasuke." Yaani, ukabadilika kuwa kama mchanga kwa sababu ya kusumbuka kutokana na kumwona Mwenyezi Mungu na kukosa kwake utulivu. "Na Musa akaanguka chini akazimia" wakati alipoona yale aliyoyaona huku amezimia. Kwa hivyo ikambainikia wakati huo kwamba ikiwa mlima haukusimama imara kwa sababu ya kumwona Mwenyezi Mungu, basi Musa alistahiki zaidi kutosimama imara kwa sababu ya hilo. Basi akamwomba Mola wake Mlezi kumfutia dhambi kwa kile alichofanya cha kuomba ombi ambalo haliendani na mada. Na "akasema: Subhanaka (Umetakasika)!” Yaani, kwa kukutakasa na kukutukuza kutokana na yale yasiyoufailia utukufu wako. "Ninatubia kwako" kutokana na madhambi yote na kuwa na adabu mbaya mbele yako "na mimi ni wa kwanza wa Waumini." Yaani, yeye, rehema na amani ziwe juu yake, aliifanya upya imani yake kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimkamilishia miongoni mwa yale aliyokuwa hayajui kabla ya hilo.
#
{144} فلما منعه الله من رؤيته بعدما كان متشوقاً إليها؛ أعطاه خيراً كثيراً، فقال: {يا موسى إنِّي اصطفيتُك على الناس}؛ أي: اخترتك واجتبيتك وفضَّلتك وخصصتك بفضائل عظيمة ومناقب جليلة، {برسالاتي}: التي لا أجعلها ولا أخصُّ بها إلا أفضل الخلق، {وبكلامي}: إيَّاك من غير واسطة، وهذه فضيلة اختُصَّ بها موسى الكليم، وعُرِف بها من بين إخوانه من المرسلين، {فخُذْ ما آتيتُك}: من النعم، وخذ ما آتيتُك من الأمر والنهي بانشراح صدرٍ، وتلقَّه بالقَبول والانقياد، {وكن من الشاكرين}: لله على ما خصَّك وفضَّلك.
{144} Basi Mwenyezi Mungu alipomzuia kumwona baada ya kwamba alikuwa na hamu kubwa ya hilo, akampa heri nyingi. Kwa hivyo akasema: "Ewe Musa! Hakika Mimi nilikuteua wende kwa watu." Yaani, nimekuchagua, na nimekuteua, na nimekufadhilisha, na nimekupa wewe tu fadhila mbalimbali kubwa na sifa kubwa, "kwa jumbe zangu," ambazo siwapi wala kuwateua kwazo isipokuwa mbora zaidi wa viumbe, "na kwa maneno yangu;" kwako bila ya kupitia kwa yeyote. Na hii ni fadhila aliyofanyiwa Musa al-Kalim peke yake, na ambayo alijulikana kwayo katika ndugu zake miongoni mwa Mitume. "Basi chukua hayo niliyokupa" miongoni mwa neema, na chukua nilichokupa miongoni mwa maamrisho na makatazo kwa kifua kikunjufu, na yapokee kwa kuyakubali na kuyafuata, “na kuwa katika wanaomshukuru” Mwenyezi Mungu kwa yale aliyokuteua kwayo na kukufadhilisha
#
{145} {وكتبنا له في الألواح من كلِّ شيء}: يحتاج إليه العباد {موعظة}: ترغِّب النفوس في أفعال الخير وترهِّبهم من أفعال الشر، {وتفصيلاً لكلِّ شيء}: من الأحكام الشرعيَّة والعقائد والأخلاق والآداب، {فخذْها بقوَّةٍ}؛ أي: بجدٍّ واجتهاد على إقامتها، {وأمُرْ قومَك يأخذوا بأحسنها}: وهي الأوامر الواجبة والمستحبَّة؛ فإنها أحسنها. وفي هذا دليلٌ على أن أوامر الله في كل شريعة كاملة عادلة حسنة. {سأريكم دارَ الفاسقينَ}: بعدما أهلكهم الله وأبقى ديارهم عبرةً بعدهم يعتبر بها المؤمنون الموفَّقون المتواضعون.
{145} "Na tukamwandikia kwenye mbao zile katika kila kitu” wanachokihitaji waja "mawaidha" yenye kuzipa nafsi moyo wa kutenda matendo ya heri, na kuzihofisha dhidi ya matendo maovu, "na maelezo ya kina ya kila kitu" miongoni mwa hukumu mbalimbali za kisheria, na itikadi mbalimbali, na tabia mbalimbali, na adabu mbalimbali. "Basi yachukue kwa nguvu." Yaani, kwa bidii na jitihada juu ya kuyasimamisha, "na uwaamrishe kaumu yako wayachukue kwa ubora wake" nayo ni maamrisho ya wajibu na yanayopendekezwa. Kwani hizo ndizo bora yake zaidi. Na katika hili kuna ushahidi kwamba maamrisho ya Mwenyezi Mungu katika kila sheria ni kamilifu, maadilifu, mazuri. "Nami nitawaonyesha makazi ya wale waliovuka mipaka" baada ya Mwenyezi Mungu kuwaangamiza, na kuyabakisha makazi yao kuwa ni mazingatio baada yao wanayozingatiwa kwayo Waumini waliowezeshwa, wanyenyekevu.
#
{146} وأما غيرهم؛ فقال عنهم: {سأصرِفُ عن آياتي}؛ أي: عن الاعتبار في الآيات الأفقية والنفسيَّة والفهم لآيات الكتاب، {الذين يتكبَّرون في الأرض بغير الحقِّ}؛ أي: يتكبَّرون على عباد الله وعلى الحقِّ وعلى من جاء به؛ فمن كان بهذه الصفة؛ حَرَمَهُ الله خيراً كثيراً، وخَذَلَه، ولم يَفْقَهْ من آيات الله ما ينتفع به، بل ربَّما انقلبت عليه الحقائقُ واستحسن القبيحَ، {وإن يَرَوْا كلَّ آيةٍ لا يؤمنوا بها}: لإعراضهم واعتراضهم ومحادَّتهم لله ورسوله، {وإن يَرَوْا سبيلَ الرُّشد}؛ أي: الهدى والاستقامة، وهو الصراط الموصل إلى الله وإلى دار كرامته، {لا يتَّخذوه [سبيلاً]}؛ أي: لا يسلكوه ولا يرغبوا فيه، {وإن يَرَوْا سبيلَ الغَيِّ}؛ أي: الغواية الموصل لصاحبه إلى دار الشقاء، {يتَّخذوه سبيلاً}. والسبب في انحرافهم هذا الانحراف، {ذلك بأنَّهم كذَّبوا بآياتنا وكانوا عنها غافلين}: فردُّهم لآيات الله وغفلتُهم عمَّا يُراد بها واحتقارهم لها هو الذي أوجب لهم من سلوك طريق الغي وترك طريق الرُّشْدِ ما أوجب.
{146} Na ama wasiokuwa wao, akasema juu yao: "Nitawaepuka na Aya zangu." Yaani, nitawaepusha na kuzizingatia ishara za kipeo za mbali, na za kinafsi na kuzifahamu ishara za Kitabu; "wale wanaotakabari katika ardhi bila ya haki." Yaani, wanatakabari dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu, na dhidi ya haki, na dhidi ya yale aliyokuja nayo. Kwa hivyo yule ambaye ana sifa hii, Mwenyezi Mungu atamnyima heri nyingi, na atamwangusha, wala hatafahamu katika Ishara za Mwenyezi Mungu anachoweza kunufaika kwacho. Bali huenda hakika zikamgeukia na akayaona maovu kuwa ni mazuri. “Na wao wakiona kila Ishara, hawaiamini;” kwa sababu, kupeana kwao mgongo na kukanusha kwao na upinzani wao dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. “Wakiiona njia ya uwongofu” Yaani, uwongofu na unyoofu, nayo ndiyo njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake. "Hawaichukui [kuwa ndiyo njia]." Yaani, hawaifuati wala hawaitaki "Lakini wakiiona njia ya ukengeufu;" yaani, ya ukengeufu yenye kumfikisha mwenyewe kwenye nyumba ya taabu, "wanaichukulia kuwa ndiyo njia." Na sababu ya kupotoka kwao kupotoka huku, "Hayo ni kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na walikuwa wakizighafilikia." Basi kuzikataa kwao Ishara za Mwenyezi Mungu, na kuyaghafilikia kwao yale yanayokusudiwa kwazo, na kuzidharau kwao ndiko kulikowasababishia kile kilichosababisha kwa kufuata njia ya ukengeufu na kuacha njia ya uwongofu kile.
#
{147} {والذين كذبوا بآياتنا}: العظيمة الدالَّة على صحَّة ما أرسلنا به رسلنا، {ولقاء الآخرة حَبِطَتْ أعمالُهم}: لأنَّها على غير أساس، وقد فقد شرطها، وهو الإيمان بآيات الله والتصديق بجزائه. {هل يُجْزَوْنَ}: في بطلان أعمالهم وحصول ضدِّ مقصودهم {إلَّا ما كانوا يعملونَ}: فإن أعمال مَنْ لا يؤمن باليومِ الآخر لا يرجو فيها ثواباً، وليس لها غايةٌ تنتهي إليه؛ فلذلك اضمحلَّت وبطلت.
{147} "Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu" kubwa, zinazoashiria usahihi wa yale tuliyowatuma nayo Mitume wetu, "na kukutana na Akhera, matendo yao yameharibika" kwa sababu yako kwa usiokuwa msingi (wa sawa), na tayari yalipoteza sharti lake, ambalo ni kuziamini Ishara za Mwenyezi Mungu na kusadiki malipo yake. "Kwani watalipwa" katika ubatilifu wa matendo yao na kutokea kwa kinyume cha makusudio yao "isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda.” Kwa maana, matendo ya yule asiyeiamini Siku ya Mwisho, hatarajii malipo ndani yake, wala hayana lengo yanalolifikia. Basi ndiyo maana yakapotelea mbali na yakabatilika.
#
{148} {واتَّخذ قوم موسى مِن بعدِهِ من حُلِيِّهم عجلاً جسداً}: صاغه السامِرِيُّ وألقى عليه قبضةً من أثر الرسول فصار {له خُوارٌ} وصوتٌ، فعبدوه واتَّخذوه إلهاً، وقال: هذا إلهكم وإله موسى، فنسي موسى، وذهب يطلبه، وهذا من سفههم وقلة بصيرتهم؛ كيف اشتبه عليهم ربُّ الأرض والسماوات بعجل من أنقص المخلوقات؟! ولهذا قال مبيناً أنه ليس فيه من الصفات الذاتيَّة ولا الفعليَّة ما يوجِب أن يكون إلهاً: {ألم يَرَوْا أنَّه لا يكلِّمهم}؛ أي: وعدم الكلام نقصٌ عظيمٌ؛ فهم أكمل حالة من هذا الحيوان أو الجماد الذي لا يتكلَّم، {ولا يهديهم سبيلاً}؛ أي: لا يدلُّهم طريقاً دينيًّا ولا يحصِّل لهم مصلحةً دنيويَّةً؛ لأن من المتقرِّر في العقول والفطر أنَّ اتِّخاذَ إلهٍ لا يتكلم ولا ينفع ولا يضرُّ من أبطل الباطل وأسمج السفه، ولهذا قال: {اتَّخذوه وكانوا ظالمينَ}: حيث وضعوا العبادة في غير موضعها، وأشركوا بالله ما لم ينزِّل به سلطاناً. وفيها دليلٌ على أنَّ من أنكر كلام الله؛ فقد أنكر خصائص إلهيَّة الله تعالى؛ لأن الله ذكر أن عدم الكلام دليلٌ على عدم صلاحيَّة الذي لا يتكلَّم للإلهيَّة.
{148} "Na kaumu ya Musa wakamfanya baada yake kutoka katika mapambo yao ndama mwenye kiwiliwili" aliwafinyangia yule Msamaria, na akamtupia mshiko kutokana na unyayo wa Mtume yule, kwa hivyo akawa "mwenye kutoa mlio wa ng’ombe," na sauti. Kwa hivyo wakamwabudu na wakamchukua kuwa mungu, na akasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau, na akaenda kumtafuta. Lakini hili ni katika upumbavu wao na uchache wa ufahamu wao. Vipi walichanganyikiwa katika Mola Mlezi wa ardhi na mbingu zote na ndama miongoni mwa viumbe wenye upungufu mkubwa zaidi? Na ndiyo maana akasema akibainisha kwamba yeye hana sifa za kidhati wala za kimatendo zenye kusababisha awe mungu: “Kwani hawakuona kuwa hawasemeshi.” Yaani, kutoweza kuzungumza ni upungufu mkubwa. Kwa hivyo wao wako katika hali kamilifu zaidi kuliko mnyama huyu au kitu kisicho na uhai ambacho hakizungumzi, "wala hawaongoi njia yoyote?" Yaani, hawaelekezi kwenye njia yoyote ya kidini na wala hawafikishii manufaa yoyote ya kidunia. Kwa sababu yaliyokwisha thibiti katika akili na maumbile asili ni kwamba kumchukua mungu asiyesema, wala hanufaishi kitu, wala hadhuru, ni katika batili za batili zote, na ujinga wa upumbavu wote. Na ndiyo maana akasema: "Walimchukua (kamuabudu), na wakawa madhalimu." Kwa vile walivyoiweka ibada katika mahali pasipokuwa pake, na wakamshirikisha Mwenyezi Mungu na yale ambayo hakuyateremshia uthibitisho wowote. Na ndani yake kuna ushahidi kwamba yeyote yule mwenye kukataa maneno la Mwenyezi Mungu, basi hakika atakuwa amekataa sifa maalumu za kimungu za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alitaja kwamba kutoweza kuzungumza ni uthibitisho wa kutofaa kwa huyo ambaye hawezi kuongea kuwa mungu.
#
{149} {ولمَّا}: رجع موسى إلى قومه، فوجدهم على هذه الحال، وأخبرهم بضلالهم؛ ندموا، و {سُقِطَ في أيديهم}؛ أي: من الهمِّ والندم على فعلهم، {ورأوا أنَّهم قد ضلُّوا}: فتنصَّلوا إلى الله وتضرَّعوا، {وقالوا لئن لم يرحَمْنا ربُّنا}: فيدُّلنا عليه، ويرزقنا عبادته، ويوفِّقُنا لصالح الأعمال، {ويغفِرْ لنا}: ما صدر منا من عبادة العجل؛ {لَنَكونَنَّ من الخاسرينَ}: الذين خسروا الدنيا والآخرة.
{149} "Na wakati" aliporejea Musa kwa kaumu yake, na akawakuta katika hali hii, na akawajulisha kuhusu kupotea kwao, wakajuta, na “mambo yalipoangushwa katika mikono yao.” Yaani, kama vile wasiwasi kubwa na majuto kwa kitendo chao, "na wakaona ya kwamba wamekwishapotea," basi wakatubia kwa Mwenyezi Mungu na wakanyenyekea. "Wakasema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hataturehemu" na akatuelekeza kwake, na akaturuzuku kumuabudu Yeye, na akatuwezesha kufanya matendo kutengenea, "na akatufutia dhambi" yale yuliyoyafanya ya kumuabudu ndama; "basi bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa waliohasiri" ambao walihasiri dunia na Akhera.
#
{150} {ولما رجع موسى إلى قومِهِ غضبان أسِفاً}؛ أي: ممتلئاً غضباً وغيظاً عليهم لتمام غيرته عليه [الصلاة و] السلام وكمال نصحه وشفقته، {قال بئسَما خَلَفْتُموني من بعدي}؛ أي: بئس الحالة التي خلفتموني بها من بعد ذهابي عنكم؛ فإنها حالةٌ تفضي إلى الهلاك الأبدي والشقاء السرمديِّ. {أعَجِلْتُم أمرَ ربِّكُم}: حيث وَعَدَكم بإنزال الكتاب فبادرتُم برأيكم الفاسد إلى هذه الخصلة القبيحة، {وألقى الألواحَ}؛ أي: رماها من الغضب، {وأخذ برأس أخيه}: هارونَ ولحيتِهِ، {يجرُّه إليه}: وقال له: {ما منعك إذ رأيتَهم ضلُّوا. أن لا تتَّبِعَني أفعصيتَ أمري}: لك بقولي: {اخلُفْني في قومي وأصْلِحْ ولا تتَّبِعْ سبيل المفسدين}؟! فقال: {يا ابنَ أمَّ لا تأخُذْ بلحيتي ولا برأسي إني خشيتُ أن تقولَ فرَّقْتَ بين بني إسرائيل ولم ترقُبْ قولي} و {قال} هنا: {ابنَ أمَّ}: هذا ترقيقٌ لأخيه بذكر الأمِّ وحدها، وإلاَّ فهو شقيقه لأمِّه وأبيه. {إنَّ القوم استضعفوني}؛ أي: احتقروني حين قلتُ لهم: يا قوم! إنما فُتِنْتُم به، وإنَّ ربَّكم الرحمن؛ فاتَّبِعوني وأطيعوا أمري، {وكادوا يَقْتُلونَني}؛ أي: فلا تظنَّ بي تقصيراً، {فلا تُشْمِتْ بيَ الأعداء}: بنهرِك لي ومسِّك إيَّايَ بسوءٍ فإنَّ الأعداء حريصون على أن يجدوا عليَّ عثرةً أو يطَّلعوا لي على زَلَّة، {ولا تجعلني مع القوم الظالمين}: فتعامِلُني معاملتهم.
{150} “Na wakati aliporudi Musa kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kuhuzunika;" yaani, huku amejaa ghadhabu, na hasira kubwa dhidi yao kwa sababu ya utimilifu wa ghera yake, yeye swala na amani ziwe juu yake, na ukamilifu wa nasaha yake, na huruma yake. Yaani, “Ni mabaya mno mliyonifanyia nyuma yangu!” Yaani, ni hali mbaya zaidi ambayo mliyonifanyia nyuma yangu baada ya kwenda kwangu nikawaacha. Kwani ni hali inayolazimu maangamio ya milele na taabu ya milele. "Je, mmeiharakishia amri ya Mola wenu Mlezi?" Kwa kuwa Yeye aliwaahidi kuteremsha Kitabu, lakini mkaharakisha kwa maoni yenu maovu kuiendea tabia hii mbaya, "Na akazitupa chini mbao zile." Yaani, akazitupa kwa sababu ya hasira, “na akamkamata kaka yake kichwa” Haaruni na ndevu zake "akimvuta kwake" na akamwambia: "Ni nini kilichokuzuia, ulipowaona wamepotea? Kwamba usinifuate? Je, umeasi amri yangu?" Juu yako nilipokuambia, “Shika pahali pangu katika kaumu yangu na utengeneze, wala usifuate njia ya waharibifu.” Kwa hivyo, akasema, “Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike kwa ndevu zangu, wala kwa kichwa changu. Hakika mimi, nilihofia useme: Umewagawanya Wana wa Israili, na wala hukungojea kauli yangu.” Na "Akasema" hapa "ewe mwana wa mama yangu." Huku ni kumlainisha kaka yake kwa kumtaja mama yao peke yake. Vinginevyo, yeye ni ndugu yake wa kwa mama na baba. "Hakika kaumu hawa waliniona kuwa mimi ni dhaifu." Yaani, walinidharau wakati nilipowaambia: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmejaribiwa tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani, (Mwingi wa Rehema). Basi nifuateni mimi, na tiini amri yangu! “Na walikaribia kuniuwa;” yaani, usidhani kuwa nilizembee. "Basi usiwafurahishe maadui zangu," kwa kunikaripia na kunifikishia mabaya. Kwa maana maadui wananafanya juhudi kubwa ya kunitafutia kikwazo au kuona kosa ndani yangu. "Wala usinifanye pamoja na kaumu madhalimu," kwa hivyo ukaamiliana nami kama unavyoamiliana nao.
#
{151} فندم موسى عليه السلام على ما استعجل من صنعِهِ بأخيه قبل أن يعلم براءتَهُ مما ظنَّه فيه من التقصير، و {قال ربِّ اغفِرْ لي ولأخي}: هارون، {وأدخِلْنا في رحمتِكَ}؛ أي: في وسطها، واجعل رحمتك تحيطُ بنا من كل جانب؛ فإنها حصنٌ حصينٌ من جميع الشرور وثَمَّ كلُّ خير وسرور. {وأنت أرحمُ الراحمين}؛ أي: أرحم بنا من كلِّ راحم، أرحم بنا من آبائنا وأمَّهاتنا وأولادنا وأنفسنا.
{151} Kwa hivyo Musa, amani iwe juu yake, akajutia aliyomfanyia nduguye kwa haraka haraka kabla ya kujua kutokuwa kwake na hatia katika yale aliyomdhania kuwa alizembea ndani yake. Na "akasema: Mola wangu Mlezi! Nifutie dhambi mimi na kaka yangu" Haaruni, "na utuingize katika rehema yako." Yaani, katikati yake, na uifanye rehema yako ituzunguke katika kila upande. Kwa maana, hizo ni ngome mathubuti kutokana na maovu yote, na humo kuna kila heri na furaha. "Nawe ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wenye kurehemu;" yaani, unaturehemu zaidi kuliko yeyote yule mwenye kurehemu. Unaturehenu zaidi kuliko baba zetu, na mama zetu, na watoto wetu, na sisi wenyewe.
#
{152} قال الله تعالى مبيناً حال أهل العجل الذين عبدوه: {إنَّ الذين اتَّخذوا العجل}؛ أي: إلهاً، {سينالُهم غضبٌ من ربِّهم وذلَّةٌ في الحياة الدُّنيا}: كما أغضبوا ربَّهم واستهانوا بأمره. {وكذلك نجزي المفترين}: فكلُّ مفترٍ على الله كاذب على شرعه متقوِّل عليه ما لم يقلْ؛ فإنَّ له نصيباً من الغضب من الله والذُّلِّ في الحياة الدنيا.
{152} Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akibainisha hali ya wale watu wa ndama ambao walimwabudu: "Hakika wale waliojifanyia ndama;" yaani, kuwa ni mungu "itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao Mlezi, na udhalilifu katika maisha ya dunia" kama walivyomghadhibisha Mola wao Mlezi na wakaidharau amri yake. "Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wazuao uongo." Kwa hivyo, kila mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu ni mwenye kuidanganyia Sheria yake, mwenye kusema juu yake yale ambayo hakuyasema, basi yeye kwa hakika ana fungu katika ghadhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na udhalilifu katika maisha ya dunia.
#
{153} وقد نالهم غضبُ الله حيث أمرهم أن يقتُلوا أنفسهم، وأنَّه لا يرضى الله عنهم إلاَّ بذلك، فقتل بعضُهم بعضاً، وانجلت المعركة على قتلى كثيرةٍ، ثم تاب الله عليهم بعد ذلك، ولهذا ذكر حكماً عامًّا يدخُلون فيه هم وغيرهم، فقال: {والذين عمِلوا السيئاتِ}: من شرك وكبائر وصغائر، {ثم تابوا من بعدها}: بأن ندموا على ما مضى وأقلعوا عنها وعزموا على أن لا يعودوا، {وآمنوا}: بالله وبما أوجبَ الله الإيمان به، ولا يتمُّ الإيمان إلا بأعمال القلوب وأعمال الجوارح المترتِّبة على الإيمان. {إنَّ ربَّك من بعدها}؛ أي: بعد هذه الحالة ـ حالة التوبة من السيئات والرجوع إلى الطاعات ـ {لغفورٌ}: يغفر السيئات ويمحوها، ولو كانت قُراب الأرض. {رحيمٌ}: بقبول التوبة والتوفيق لأفعال الخير وقبولها.
153. Na hakika ilikwisha wapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kuwa aliwaamuru wajiue wenyewe, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hawi radhi nao isipokuwa kwa hayo. Basi baadhi yao wakawaua baadhi yao, na vita hivyo vikaisha baada ya mauaji mengi. Kisha Mwenyezi Mungu akawakubalia toba baada ya hayo, na ndiyo maana akataja hukumu ya jumla wanayoingia wao na wengineo. Akasema: "Na wale waliotenda mabaya" miongoni mwa ushirikina na madhambi makubwa na madhambi madogo, "kisha wakatubia baada yake" kwa kujutia yale yaliyopita, na wakayaacha, na wakaazimia kutoyarudia; "na wakaamini" Mwenyezi Mungu na yale aliyowajibisha Mwenyezi Mungu kuyaamini, na wala imani haitimii isipokuwa kwa matendo ya nyoyo, na matendo ya viungo yanayotokana na imani. "Hakika Mola wako Mlezi baada ya hayo;" yaani, baada ya hali hii - hali ya kutubia maovu na kurejea katika utiifu - "ni Mwenye kufuta dhambi" anasitiri maovu na anayafuta, hata yakiwa yanajaza ardhi. "Mwenye kurehemu" kwa kukubali toba na kuwezesha matendo mema na kuyakubali.
#
{154} {ولما سَكَتَ عن موسى الغضبُ}؛ أي: سكن غضبه وتراجعت نفسُهُ، وعَرَفَ ما هو فيه؛ اشتغل بأهمِّ الأشياء عنده، فَأَخَذَ {الألواحَ}: التي ألقاها، وهي ألواحٌ عظيمة المقدار جليلةٌ {في نُسْخَتِها}؛ أي: مشتملة ومتضمِّنة {هدىً ورحمةٌ}؛ أي: فيها الهدى من الضَّلالة، وبيان الحقِّ من الباطل، وأعمال الخير وأعمال الشر، والهدى لأحسن الأعمال والأخلاق والآداب، ورحمة وسعادة لمن عمل بها وعلم أحكامها ومعانيها، ولكن؛ ليس كل أحدٍ يقبل هدى الله ورحمته، وإنما يقبلُ ذلك، وينقاد له، ويتلقَّاه بالقَبول، {الذين هُم لربِّهم يرهَبونَ}؛ أي: يخافون منه ويخشونه، وأما مَنْ لم يخفِ الله ولا المقام بين يديه؛ فإنه لا يزداد بها إلا عتوًّا ونفوراً، وتقوم عليه حجة الله فيها.
{154} "Na wakati ghadhabu ilipomtulia Musa," yaani, ghadhabu yake ilitulia, na nafsi yake ikarudiana, na akajua kile alicho ndani yake, akajishughulisha na kitu muhimu zaidi kwake. Kwa hivyo, akachukua "mbao zile;" ambazo alizitupa chini, ambazo ni mbao zenye cheo kikubwa, tukufu. "Na katika maandiko yake," yaani, zilijumuisha na kukusanya "uwongofu na rehema." Yaani, ndani yake kuna uwongofu kutokana na upotovu, na kuibainisha haki kutokana na batili, na matendo ya heri na matendo maovu, na uwongofu kwenye matendo mazuri zaidi, na maadili, na adabu, na rehema, na furaha kwa mwenye kuyatenda na akajua hukumu zake na maana zake. Lakini siyo kila mmoja anakubali uwongofu wa Mwenyezi Mungu na rehema Yake. Lakini anaukubali huo, na kuufuata, na kuupokea kwa kuubali, "wale ambao wao wanamhofu Mola wao Mlezi." Yaani, wanaomhofu na wanamnyenyekea. Na ama mwenye kutomhofu Mwenyezi Mungu wala kusimama mbele yake, basi yeye hakika hazidi kwa hayo isipokuwa kuasi na kujiweka mbali, kwa hivyo hoja ya Mwenyezi Mungu inakuwa imesimama juu yake katika hayo.
#
{155} {و} لما تاب بنو إسرائيل، وتراجعوا إلى رُشْدِهم، {اختار موسى} منهم {سبعين رجلاً}: من خيارهم ليعتذروا لقومهم عند ربِّهم، ووعدهم الله ميقاتاً يحضُرون فيه، فلما حضروا؛ قالوا: يا موسى! أرِنا الله جهرةً! فتجرؤوا على الله جراءة كبيرة، وأساؤوا الأدب معه، فأخذتهم الرجفةُ، فصعقوا وهلكوا، فلم يزل موسى عليه الصلاة والسلام يتضرَّع إلى الله ويتبتَّل ويقول: {ربِّ لو شئتَ أهلكتَهم من قبلُ}: أن يحضُروا، ويكونون في حالة يعتذرون فيها لقومهم فصاروا هم الظالمين. {أتُهْلِكُنا بما فعل السفهاءُ منَّا}؛ أي: ضعفاء العقول سفهاء الأحلام، فتضرَّع إلى الله، واعتذر بأنَّ المتجرِّئين على الله ليس لهم عقولٌ كاملةٌ تردعُهم عما قالوا وفعلوا، وبأنهم حصل لهم فتنةٌ يخطر بها الإنسان ويخاف من ذهاب دينه، فقال: {إنْ هي إلَّا فتنتُك تُضِلُّ بها من تشاءُ وتهدي من تشاءُ أنت وَلِيُّنا فاغْفِرْ لنا وارْحَمْنا وأنت خير الغافرين}؛ أي: أنت خير من غفر، وأولى من رحم، وأكرم من أعطى وتفضَّل، فكأنَّ موسى عليه الصلاة والسلام قال: المقصود يا ربِّ بالقصد الأول لنا كلّنا، هو التزام طاعتك والإيمان بك، وأن من حَضَرَه عقله ورشده وتمَّ على ما وهبته من التوفيق؛ فإنه لم يزل مستقيماً، وأما من ضَعُفَ عقلُه وسَفِه رأيُهُ وصرفته الفتنة؛ فهو الذي فعل ما فعل لذينك السببين، ومع هذا؛ فأنت أرحم الراحمين وخير الغافرين؛ فاغفر لنا وارحمنا! فأجاب الله سؤاله، وأحياهم من بعد موتهم، وغفر لهم ذنوبهم.
{155} “Na” Wana wa Israili walipotubu na wakarejea kwenye fahamu zao, "Musa akawateuwa" miongoni mwao "wanaume sabiini" kutoka kwa walio bora zaidi wao ili wakaombe udhuru kwa ajili ya kaumu yao mbele ya Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu aliwaahidi miadi watakaohudhuria ndani yake. Na wakati walipohudhuria, wakasema, “Ewe Musa! Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi!” Kwa hivyo, wakafanya ujasiri mkubwa dhidi ya Mwenyezi Mungu, na wakawa na adabu mbaya mbele yake, kwa hivyo tetemeko kubwa likawachukua, hivyo basi wakapigwa wakazimika na wakaangamia. Basi Musa, rehema na amani ziwe juu yake, hakuacha kuendelea kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kuomba sana na akisema: "Mola wangu Mlezi! Ungelitaka, ungeliwaangamiza wao hapo kabla" ya wao kuhudhuria, na wakawa katika hali ya kuwaombea msamaha kaumu yao, na wakawa wao ndio madhalimu. "Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wapumbavu katika sisi?" Yaani, wenye akili dhaifu, na wapumbavu wa maono. Basi akamwomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu na akaomba udhuru kwamba wale waliofanya ujasiri dhidi ya Mwenyezi Mungu hawana akili kamilifu ambazo zinaweza kuwazuia kutoka kwa yale waliyoyasema na kuyatenda, na kwamba walipatwa na majaribio ambayo anahatarisha kwayo mja na kuhofu kuipoteza Dini yake. Akasema: "Haya si chochote isipokuwa ni majaribio yako, unampoteza kwayo umtakaye, na unamuongoa umtakaye. Wewe ndiye rafiki mlinzi wetu. Basi tusitiri dhambi na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora zaidi wa wasitirio dhambi.” Yaani, wewe ndiwe Mbora zaidi wa kusitiri dhambi, na mstahiki zaidi wa kurehemu, na mkarimu zaidi wa kupeana na kufadhilisha. Na ni kama kwamba Musa, rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Makusudio ewe Mola Mlezi kwa kusudio la kwanza kwetu sote, ni kushikamana na utiifu kwako na kukuamini Wewe, na kwamba yeyote yule mwenye akili zake, na uwongofu wake, na akawezeshwa kwa yale uliyomtunuku, basi yeye hukuacha kuwa mnyoofu. Na ama yule ambaye akili yake ilidhoofika na maoni yake yakawa ya upumbavu, na majaribio yakamtoa njiani, basi yeye ndiye aliyefanya aliyoyafanya kwa sababu hizi mbili. Na pamoja na haya , Wewe ndiwe mwenye kurehemu zaidi kuliko wanaorehemu, na ndiye Mbora zaidi wa wasitirio dhambi. Basi tusitirie dhambi, na uturehemu!” Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwitikia ombi lake, na akawahuisha baada ya kufa kwao, na akawasamehe dhambi zao.
#
{156} وقال موسى في تمام دعائه: {واكتبْ لنا في هذه الدنيا حسنةً}: من علم نافع ورزق واسع وعمل صالح، {وفي الآخرة}: حسنة، وهي ما أعد الله لأوليائه الصالحين من الثواب. {إنَّا هُدْنا إليك}؛ أي: رجعنا مقرِّين بتقصيرنا منيبين في جميع أمورنا، {قال} الله تعالى: {عذابي أصيبُ به من أشاءُ}: ممَّن كان شقيًّا متعرضاً لأسبابه، {ورحمتي وسعتْ كلَّ شيء}: من العالم العلويِّ والسفليِّ؛ البر والفاجر، المؤمن والكافر؛ فلا مخلوق إلا وقد وصلت إليه رحمة الله وغمره فضله وإحسانه، ولكن الرحمة الخاصة المقتضية لسعادة الدنيا والآخرة ليست لكل أحد، ولهذا قال عنها: {فسأكتُبها للذين يتَّقون}: المعاصي صغارها وكبارها، {ويؤتون الزَّكاة}: الواجبة مستحقيها، {والذين هم بآياتنا يؤمنون}.
{156} Na Musa akasema katika kukamilisha dua yake: "Na tuandikie mazuri katika dunia hii" miongoni mwa elimu yenye manufaa, na riziki kunjufu, na matendo mema, "na katika Akhera" utupe heri. Nayo ni yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwatayarishia marafiki wake wandani walio wema miongoni mwa thawabu. "Hakika sisi tumerejea kwako;" yaani, tumerudi huku tumekiri kufanya kwetu upungufu, na wenye kutubia kwako katika mambo yetu yote. "Akasema" Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Adhabu yangu nitamsibu kwayo nimtakaye" miongoni mwa wale waliokuwa waasi, wenye kuzifanya sababu zake. "Na rehema yangu imeenea kila kitu," katika ulimwengu wa juu na wa chini, mwema na muovu, Muumini na kafiri, basi hakuna kiumbe chochote isipokuwa kilikwishafikiwa na rehema ya Mwenyezi Mungu, na kikafunikwa na fadhila yake na wema wake. Lakini rehema maalum inayosababisha furaha ya dunia na Akhera si ya kila mmoja. Na ndiyo maana akasema kuihusu: "Basi nitaiandika hii hasa kwa wale wanaomcha Mungu" kutokana na maasia madogo yake na mkubwa yake. "Na wanaotoa Zaka” kuwapa wastahiki wake, "na wale ambao wanaziamini Ishara zetu.”
#
{157} ومن تمام الإيمان بآيات الله معرفة معناها والعمل بمقتضاها، ومن ذلك اتباع النبي - صلى الله عليه وسلم - ظاهراً وباطناً في أصول الدين وفروعه: {الذين يتَّبِعون الرسول النبيَّ الأميَّ}: احترازٌ عن سائر الأنبياء؛ فإن المقصود بهذا محمد بن عبد الله بن عبد المطلب والسياق في أحوال بني إسرائيل، وأن الإيمان بالنبيِّ محمد - صلى الله عليه وسلم - شرطٌ في دخولهم في الإيمان، وأن المؤمنين به المتَّبعين هم أهل الرحمة المطلقة التي كتبها الله لهم، ووصفه بالأمي لأنَّه من العرب الأمة الأميَّة التي لا تقرأ ولا تكتب وليس عندها قبل القرآن كتاب. {الذي يجِدونَهُ مكتوباً عندَهم في التوراة والإنجيل}: باسمه وصفته التي من أعظمها وأجلِّها ما يدعو إليه وينهى عنه، وأنه {يأمُرُهم بالمعروف}: وهو كل ما عُرِفَ حسنُهُ وصلاحه ونفعه. {وينهاهم عن المنكر}: وهو كلُّ ما عرف قبحه في العقول والفطر، فيأمرهم بالصلاة والزكاة والصوم والحج وصلة الأرحام وبر الوالدين والإحسان إلى الجار والمملوك وبذل النفع لسائر الخلق والصدق والعفاف والبر والنصيحة وما أشبه ذلك، وينهى عن الشرك بالله وقتل النفوس بغير حق والزِّنا وشرب ما يسكر العقل والظلم لسائر الخلق والكذب والفجور ونحو ذلك؛ فأعظم دليل يدلُّ على أنه رسول الله ما دعا إليه وأمر به ونهى عنه وأحلَّه وحرَّمه؛ فإنه يُحِلُّ الطيبات: من المطاعم والمشارب والمناكح. {ويحرِّمُ عليهم الخبائث}: من المطاعم والمشارب والمناكح والأقوال والأفعال. {ويَضَعُ عنهم إصْرَهُم والأغلال التي كانت عليهم}؛ أي: ومِنْ وَصْفِهِ أنَّ دينه سهلٌ سَمْحٌ ميسَّر لا إصر فيه ولا أغلال ولا مشقات ولا تكاليف ثقال. {فالذين آمنوا به وعزَّروه}؛ أي: عظَّموه وبجَّلوه، {ونصروه واتَّبعوا النور الذي أنزلَ معه}: وهو القرآن الذي يُستضاء به في ظلمات الشَّكِّ والجهالات، ويقتدى به إذا تعارضت المقالات. {أولئك هم المفلحون}: الظافرون بخير الدُّنيا والآخرة، والناجون من شرِّهما؛ لأنَّهم أتوا بأكبر أسباب الفلاح، وأما مَن لم يؤمنْ بهذا النبيِّ الأميِّ، ويعزِّره، وينصره، ولم يتَّبع النور الذي أنزل معه؛ فأولئك هم الخاسرون.
{157} Na katika utimilifu wa kuamini katika ishara za Mwenyezi Mungu ni kuzijua maana zake na kutenda kulingana na matakwa yake. Na katika hayo ni kumfuata Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – kwa dhahiri na ndani katika misingi ya dini na matawi yake. "Wale ambao wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiyesoma wala kuandika" hili linawaondoa Manabii wengineo wote. Kwa maana anayekusudiwa kwa haya ni Muhammad bin Abdullah bin Abdul-Muttalib, na muktadha ni katika hali za Bani Israili, na kwamba kumwamini Nabii Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - ni sharti la kuingia kwao katika Imani. Na kwamba wale wanaomwamini, wanaomfuata ndio watu wa rehema kamili ambazo Mwenyezi Mungu aliwaandikia. Na alimweleza kuwa yeye hajui kusoma na kuandika kwa sababu yeye ni kutoka kwa Warabu, umma usiojua kusoma wala kuandika, na wala hauna kitabu chochote kabla ya Qur-ani. "Ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili" kwa jina lake na sifa yake ambayo katika sifa kuu zake zaidi na tukufu zaidi ni yale anayolingania na anayokataza, na kwamba "anawaamrisha mema." Nayo ni kila kitu kinachojulikana uzuri wake na kutengenea kwake, na manufaa yake. "Na anawakataza maovu," nayo ni kila kinachojulikana ubaya wake katika akili na maumbile asili. Kwa hivyo anawaamrisha kuswali, na Zaka, na kufunga Saumu, na Hijja, na kufunga jamaa, na kuwafanyia wema wazazi, na kufanyia jirani ihsani na watumwa, na kufanya yenye kunufaisha viumbe vyote, na ukweli, na usafi wa tabia, na wema, na nasiha, na mfano wa hayo. Na anakataza kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuua nafsi bila ya haki, na uzinzi, na unywaji chenye kulewesha akili, na dhuluma dhidi ya viumbe wengineo wote, na uongo, na kufanya maovu na mfano wa hayo. Basi ushahidi mkubwa zaidi unaoonyesha kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kile anachokilingania, na alichoamrisha, na alichokataza, na alichohalalisha, na alichoharamisha. Yeye kwa hakika anahalalisha vitu vizuri miongoni mwa vyakula, na vinywaji, na mambo ya ndoa. “Na anawakataza maovu” miongoni mwa vyakula, na vinywaji, mambo ya ndoa, maneno, na vitendo. "Na anawaondolea mizigo yao na minyororo ambayo ilikuwa juu yao." Yaani, katika sifa zake ni kwamba dini yake ni rahisi, na ya uvumilivu, na nyepesi, haina mizigo ndani yake, wala minyororo, wala dhiki, wala majukumu mazito. "Basi wale waliomwamini yeye, na wakampa taadhima;" yaani, walimpa taadhima, na kumheshimu, "na wakamnusuru, na wakaifuata nuru ambayo iliteremshwa pamoja naye." Nayo ni Qur-ani ambayo kwayo mtu hupata mwangaza katika giza la shaka na ujinga mbalimbali, na ni kielelezo kwake wakati maneno yanapopingana. "Hao ndio waliofaulu"waliopata heri ya dunia na Akhera, waliofaulu kutokana na shari zake. Kwa sababu walifanya sababu kubwa zaidi ya kufaulu. Na ama asiyemwamini Nabii huyu asiyejua kusoma na kuandika, na akamheshimu, na kumnusuru, na wala hakuifuata nuru ambayo iliteremshwa pamoja naye, basi hao ndio waliohasiri.
#
{158} ولما دعا أهل التوراة من بني إسرائيل إلى اتباعه، وكان ربما توهَّم متوهِّم أن الحكم مقصورٌ عليهم، أتى بما يدلُّ على العموم، فقال: {قلْ يا أيُّها الناس إني رسولُ الله إليكم جميعاً}؛ أي: عربيّكم وعجميّكم، أهل الكتاب منكم وغيرهم، {الذي له ملكُ السموات والأرض}: يتصرَّف فيهما بأحكامه الكونيَّة والتدابير السلطانيَّة وبأحكامه الشرعيَّة الدينيَّة، التي من جملتها أن أرسل إليكم رسولاً عظيماً يدعوكم إلى الله وإلى دار كرامته، ويحذِّركم من كلِّ ما يباعدكم منه ومن دار كرامته. {لا إله إلاَّ هو}؛ أي: لا معبود بحقٍّ إلا الله وحده لا شريك له، ولا تُعْرَفُ عبادته إلا من طريق رسله. {يحيي ويميتُ}؛ أي: من جملة تدابيره الإحياء والإماتة، التي لا يشاركه فيها أحدٌ، التي جعل الله الموت جسراً ومعبراً، يُعبَرُ منه إلى دار البقاء التي من آمن بها صدَّق الرسول محمداً - صلى الله عليه وسلم - قطعاً. {فآمنوا بالله ورسولِهِ النبيِّ الأميِّ}: إيماناً في القلب متضمناً لأعمال القلوب والجوارح، {الذي يؤمِنُ بالله وكلماته}؛ أي: آمنوا بهذا الرسول المستقيم في عقائده وأعماله، {واتَّبِعوه لعلكم تهتدونَ}: في مصالِحِكم الدينيَّة والدنيويَّة؛ فإنكم إذا لم تتَّبعوه؛ ضللتم ضلالاً بعيداً.
{158} Na alipowaita watu wa Taurati kutoka kwa Wana wa Israili wamfuate, na pengine mwenye dhana isiyo sahihi akadhani kuwa hukumu hii inawahusu wao tu, akaja na kitu kinachoashiria ujumla, akasema: "Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi mungu kwenu nyinyi nyote." Yaani, Waarabu wenu na wasiokuwa Waarabu wenu, Watu wa Kitabu miongoni mwenu na wasiokuwa wao. "Yeye ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi" anafanya humo kwa hukumu zake za kiulimwengu na za uendeshaji wa kimamlaka, na hukumu za kisheria, za kidini ambazo miongoni mwake ni kuwatumia Mtume mtukufu anayewalingania kwa Mwenyezi Mungu na kwenye nyumba ya utukufu wake. Na anawatahadharisha kutokana na kila kitakachowaweka mbali na Yeye na mbali na nyumba ya utukufu wake. "Hapana mungu isipokuwa Yeye;” yaani, hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, hana mshirika, na ibada yake haijulikani isipokuwa kwa njia ya Mitume wake. “Anahuisha na anafisha;” yaani, miongoni mwa kuendesha kwake ni kuhuisha na kufisha, ambayo hakuna hata mmoja anayeshiriki naye katika hayo, ambayo Mwenyezi Mungu aliyafanya mauti kuwa daraja na mapitio yapitiwayo kwenda kwenda kwenye nyumba ya kudumu, ambayo mwenye kuiamini, anamsadiki Mtume Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake bila ya shaka yoyote. "Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Nabii asiyejua kusoma na kuandika" imani katika moyo inayojumuisha matendo ya nyoyo na viungo, "ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu na maneno yake." Yaani, mwaminini Mtume huyu mnyoofu katika itikadi zake na matendo yake, "Na mfuateni yeye ili muongoke;" katika masilahi yenu ya kidini na ya kidunia. Kwa maana, ikiwa nyinyi hamtamfuata, mtapotea kupotea kwa mbali.
#
{159} {ومن قوم موسى أمَّةٌ}؛ أي: جماعة، {يهدون بالحقِّ وبه يعدِلونَ}؛ أي: يهدون [به] الناس في تعليمهم إياهم وفتواهم لهم، ويعدِلون به بينهم في الحكم بينهم قضاياهم؛ كما قال تعالى: {وَجَعَلْناهم أئمةً يهدون بأمرِنا لما صبروا وكانوا بآياتنا يوقنون}. وفي هذا فضيلةٌ لأمة موسى عليه الصلاة والسلام، وأنَّ الله تعالى جعل منهم هُداةً يهدون بأمره. وكأنَّ الإتيان بهذه الآية الكريمة فيه نوعُ احتراز مما تقدَّم؛ فإنه تعالى ذكر فيما تقدَّم جملةً من معايب بني إسرائيل المنافية للكمال المناقضة للهداية، فربما توهَّم متوهِّم أن هذا يعمُّ جميعهم، فذكر تعالى أن منهم طائفة مستقيمة هادية مهدية.
{159} "Na katika kaumu ya Musa upo umma." Yaani, kundi, "unaowaongoa watu kwa haki, na kwayo wanafanya uadilifu." Yaani, wanawaongoa [kwayo] watu katika kuwafunza kwayo na kuwatolea fatwa, na wanafanyiana usawa katika kuhukumu masuala yao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na tukawafanya miongoni mwao viongozi wanaowaongoa watu kwa amri yetu, waliposubiri na wakawa na yakini na Ishara zetu." Na katika hili kuna fadhila kwa umma wa Musa, rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alifanya miongoni mwao viongozi wa kuongoa kwa amri yake. Na ni kana kwamba kuleta Aya hii tukufu kuna aina fulani ya kuondoa yale yaliyotangulia. Kwani yeye Mtukufu alitaja katika yale yaliyotangulia kasoro kadhaa za Wana wa Israili katika zinazopingana na ukamilifu, zinazotengua uwongofu. Na huenda mwenye dhana mbaya akadhani kwamba hili linawahusu wote. Kwa hivyo yeye Mtukufu akataja kwamba kundi miongoni mwao limenyooka, linaongoa, limeongolewa.
#
{160} {وقطَّعناهم}؛ أي: قسَّمناهم {اثنتي عشرة أسباطاً أمماً}؛ أي: اثنتي عشرة قبيلةً متعارفةً متوالفةً، كل بني رجل من أولاد يعقوب قبيلة، {وأوحينا إلى موسى إذِ استسقاه قومُهُ}؛ أي: طلبوا منه أن يدعو الله تعالى أن يسقيهم ماء يشربون منه وتشرب منه مواشيهم، وذلك لأنَّهم ـ والله أعلم ـ في محلٍّ قليل الماء، فأوحى الله لموسى إجابة لِطلبَتِهِم: {أنِ اضربْ بعصاك الحجرَ}: يُحتمل أنه حجرٌ معيَّن، ويُحتمل أنه اسم جنس يشمل أي حجر كان، فضربه، {فانبَجَستْ}؛ أي: انفجرت من ذلك الحجر {اثنتا عشرة عيناً}: جارية سارحة، {قد علم كلُّ أناس مشرَبَهم}؛ أي: قد قسم على كل قبيلة من تلك القبائل الاثنتي عشرة، وجعل لكلٍّ منهم عيناً، فعلموها، واطمأنُّوا واستراحوا من التعب والمزاحمة، وهذا من تمام نعمة الله عليهم، {وظلَّلْنا عليهم الغمام}: فكان يستُرهم من حرِّ الشمس، {وأنزلنا عليهم المنَّ}: وهو الحلوى، {والسَّلوى}: وهو لحم طير من أحسن أنواع الطيور وألذِّها، فجمع الله لهم بين الظلال والشراب والطعام الطيب من الحلوى واللحوم على وجه الراحة والطمأنينة، وقيل لهم: {كلوا من طيِّبات ما رَزَقْناكم وما ظلمونا}: حين لم يشكُروا الله ولم يقوموا بما أوجب الله عليهم. {ولكن كانوا أنفسَهم يظلمونَ}: حيث فوَّتوها كلَّ خير وعرَّضوها للشرِّ والنقمة، وهذا كان مدة لبثهم في التيه.
{160} “Na tukawakatakata.” Yaani, tuliwagawanya “makabila kumi na mawili, mataifa mbalimbali.” Yaani, makabila kumi na mawili yanayojuana, yanayoingiliana, kila wana wa mwanamume miongoni mwa wana wa Yaaqub ni kabila. "Na tulimfunulia Musa wakati kaumu yake walipomuomba maji;" Yaani, walimwomba kwamba amwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu awape maji ya kunywa kwayo na ya mifugo yao kunywa kwayo. Na hili ni kwa sababu wao - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - walikuwa mahali penye maji kidogo, basi mwenyezi Mungu alimfunulia Musa akiitikia ombi lao "kwamba: Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako." Inawezekana kwamba lilikuwa jiwe mahsusi, na inawezekana kwamba likawa ni jina la jumla, linalojumuisha jiwe lolote lile. Basi akalipiga, "mara zikabubujika;" yaani, zikatoka kwa msukumo mkubwa kutoka katika jiwe hilo "chemchemi kumi na mbili." Yaani, zenye kupita na kwenda "na kila watu wakajua mahali pao pa kunywea." Yaani, aliwagawia kila kabila katika yale makabila kumi na mawili, na akaliwekea kila mmoja yao chemchemi, nao wakaijua, na wakatulia, na wakastarehe kutokana na uchovu na msongamano. Na hii katika ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu juu yao. "Na tukawafunika kivuli kwa mawingu" basi kikawa kinawasitiri kutokana na joto la jua. "Na tukawateremshia Manna" nacho ni kitu kitamu "na Salwa" nayo ni nyama ya ndege, miongoni mwa ndege wazuri zaidi na wenye ladha zaidi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawajumuishia kati ya vivuli, na kinywaji, na chakula kizuri miongoni mwa vitu vitamu na nyama kwa namna ya starehe na utulivu. Na wakaambiwa: "Kuleni katika vizuri hivi tulivyowaruzuku. Na hawakutudhulumu Sisi" wakati hawakumshukuru Mwenyezi Mungu, na hawakufanya yale aliyowawajibishia; "bali walikuwa wakijidhulumu wenyewe." Kwa vile walivyozinyima kila heri, na wakaziweka mbele ya kila uovu na adhabu. Na haya yalikuwa katika muda ule wa kukaa kwao katika jangwa.
#
{161} {وإذ قيلَ لهم اسكنوا هذه القريةَ}؛ أي: ادخلوها لتكون وطناً لكم ومسكناً، وهي إيلياء، {وكلوا منها حيث شئتُم}؛ أي: قرية كانت كثيرة الأشجار غزيرة الثمار رغيدة العيش؛ فلذلك أمرهم الله أن يأكلوا منها حيث شاؤوا، {وقولوا}: حين تدخلون الباب: {حِطَّةٌ}؛ أي: احطُطْ عنَّا خطايانا واعفُ عنا، {وادخُلوا الباب سجَّداً}؛ أي خاضعين لربكم مستكينين لعزَّته شاكرين لنعمته؛ فأمرهم بالخضوع وسؤال المغفرة، ووعدهم على ذلك مغفرة ذنوبهم والثواب العاجل والآجل، فقال: {نغفر لكم خطيئاتِكُم سنزيدُ المحسنينَ}: من خير الدنيا والآخرة.
{161} "Na pale walipoambiwa: Ukaeni mji huu." Yaani, uingieni ili uwe nchi yenu na makazi, nayo ni Ilyaa. "Na mle humo popote mpendapo," yaani, kijiji ambacho kilikuwa na miti mingi, na matunda tele, na maisha ya starehe. Basi ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawaamrisha kwamba wale humo popote wapendapo. "Na semeni" wakati wanapoingia mlangoni, "Tufutie dhambi zetu;" yaani, tuondolee dhambi zetu na utusamehe, "Na uingieni mlango wake kwa kusujudu." Yaani, hali ya kuwa mmemnyenyekea Mola wenu Mlezi, mmejisalimisha kwa utukufu wake, mkishukuru neema yake. Basi akawaamrisha kunyenyekea na kuomba kusitiriwa dhambi, na akawaahidi juu ya hilo kuwasitiria dhambi zao, na kuwapa thawabu za sasa na za baadaye. Kwa hivyo akasema: "Tutawasitiria makosa yenu. Walio wema tutawazidishia" katika heri ya dunia na Akhera.
#
{162} فلم يمتثلوا هذا الأمر الإلهيَّ، بل بدَّل الذين ظلموا منهم؛ أي: عصوا الله واستهانوا بأمره {قولاً غير الذي قيل لهم}: فقالوا بدل طلب المغفرة وقولهم حطة: حبَّة في شعيرة، وإذا بدلوا القول مع يسره وسهولته؛ فتبديلهم للفعل من باب أولى، ولهذا دخلوا يزحفون على أَسْتَاهِهم، {فأرسلنا عليهم}: حين خالفوا أمر الله وعَصَوْه {رِجزاً من السماء}؛ أي: عذاباً شديداً إما الطاعون وإما غيره من العقوبات السماويَّة، وما ظلمهم الله بعقابه، وإنَّما كان ذلك {بما كانوا يظلمونَ}.
{162} Lakini hawakufuata amri hii ya kimungu, bali walibadilisha wale waliodhulumu miongoni mwao. Yaani, walimuasi Mwenyezi Mungu na wakaidharau amri yake, "kauli isiyo ile waliyoambiwa" na wakasema badala ya kuomba kusitiriwa dhambi na kusema kwao kusamehe, wao wakasema "punje katika shayiri.” Na wakati wanapobadilisha kauli pamoja na wepesi wake na usahali wake, basi kubadilisha kwao kitendo ni katika jambo linalowezekana zaidi. Na ndiyo maana wakaingia humo wakijikokota kwa makalio yao, "Basi tukawatumia" wakati walipohalifu amri ya Mwenyezi Mungu na wakamuasi "adhabu kutoka mbinguni." Yaani, adhabu kali, ima tauni au adhabu nyingineyo miongoni mwa adhabu mbalimbali za mbinguni. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu kwa adhabu yake, bali hayo yalikuwa "kwa vile walivyokuwa wakidhulumu."
#
{163} {واسْألْهُم}؛ أي: اسأل بني إسرائيل {عن القرية التي كانت حاضرةَ البحر}؛ أي: على ساحله في حال تعدِّيهم وعقاب الله إيَّاهم، {إذ يَعْدونَ في السبتِ}: وكان الله تعالى قد أمرهم أن يعظِّموه ويحترموه ولا يصيدوا فيه صيداً، فابتلاهُم الله وامتحنهم، فكانت الحيتان تأتيهم يومَ سبتهم شُرَّعاً؛ أي: كثيرة طافية على وجه البحر. {ويوم لا يَسْبِتونَ}؛ أي: إذا ذهب يوم السبت {لا تأتيهم}؛ أي: تذهب في البحر فلا يرون منها شيئاً. {كذلك نبلوهُم بما كانوا يفسُقون}: ففسقُهم هو الذي أوجب أن يبتلِيَهم الله وأن تكون لهم هذه المحنة، وإلاَّ؛ فلو لم يفسُقوا؛ لعافاهم الله، ولما عرَّضهم للبلاء والشرِّ.
{163} "Na waulize;" yaani, waulize wana wa Israili "kuhusu kijiji kilichokuwa kando ya bahari." Yaani, katika mwambao wake katika hali ya uasi wao na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwao, "walipokuwa wakiivunja Sabato." Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa amewaamrisha kuitukuza na kuiheshimu, wala wasiwinde windo lolote ndani yake. Basi Mwenyezi Mungu akawajaribu, na akawapa mtihani, basi zikawa samaki zinawajia siku ya Sabato yao juu juu. Yaani, nyingi zikielea juu ya uso wa bahari; "na siku isiyokuwa ya Sabato." Yaani, inapoisha siku ya Sabato, “hawawajii.” Yaani, zinakwenda katika bahari na hawaoni kwazo kitu, "kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakivuka mipaka." Basi kuvuka kwao mipaka ndiko kulikowasababishia kupewa majaribio na Mwenyezi Mungu, na wawe na mtihani huu. Vinginevyo, lau kuwa hawakuvuka mipaka, mwenyezi Mungu angewapa salama, na asingewaweka kwenye balaa na maovu.
#
{164} فتحيلوا على الصيد، فكانوا يحفرون لها حفراً، وينصبون لها الشباك؛ فإذا جاءت يوم السبت ووقعت في تلك الحفر والشِّباك؛ لم يأخذوها في ذلك اليوم؛ فإذا جاء يوم الأحد؛ أخذوها، وكثر فيهم ذلك، وانقسموا ثلاث فرق: معظمهم اعتَدَوا وتجرَّؤوا وأعلنوا بذلك. وفرقةٌ أعلنت بنهيهم والإنكار عليهم. وفرقةٌ اكتفتْ بإنكار أولئك عليهم ونهيهم لهم وقالوا: {لم تَعِظونَ قوماً اللهُ مهلِكُهم أو معذِّبهم عذاباً شديداً}: كأنَّهم يقولون: لا فائدة في وعظ مَن اقتحم محارم الله ولم يُصْغِ للنصيح بل استمرَّ على اعتدائه وطغيانه؛ فإنه لا بد أن يعاقبهم الله إما بهلاك أو عذاب شديد. فقال الواعظون: نعظهم وننهاهم {معذرةً إلى ربِّكم}؛ أي: لنُعْذَرَ فيهم، {ولعلَّهم يتَّقون}؛ أي: يتركون ما هم فيه من المعصية؛ فلا نيأس من هدايتهم؛ فربَّما نجع فيهم الوعظ وأثر فيهم اللوم، وهذا المقصود الأعظم من إنكار المنكر؛ ليكون معذرة وإقامة حجةٍ على المأمور المنهي، ولعل الله أن يهديه فيعمل بمقتضى ذلك الأمر والنهي.
{164} Basi wakafanya hila ya kuwinda, na wakawa wanazichimbia mashimo na wanawawekea nyavu. Kwa hivyo, inapokuja siku ya Jumamosi na wakatumbukia katika mashimo hayo na nyavu hizo, hawazichukui katika siku hiyo. Basi inapokuja siku ya Jumapili, wakazichukua, na hilo likawa jingi miongoni mwao, na wakagawanyika makundi matatu: wengi wao wakaasi, na wakafanya ujasiri juu yake, na wakayafanya hayo wazi. Na kundi lingine likawakataza waziwazi na kuwapinga kwa hilo. Na kundi lingine likatosheka na kupinga kwa hao dhidi yao na kuwakataza kwao, na wakasema: "Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu adhabu kali?" Ni kana kwamba wanasema: Hakuna faida ya kumuwaidhi yule ambaye aliingia katika maharamisho ya Mwenyezi Mungu na hakuisikia nasiha, bali aliendelea na uasi wake na kuvuka kwake mipaka. Basi huo ni lazima mwenyezi Mungu atawaadhibu ima kwa kuwaangamiza au adhabu kali. Basi wale waliokuwa wakiwawaidhi wakasema: tunawawaidhi na kuwakataza, "Ili uwe ni udhuru kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, ili tuwe na udhuru kuhusiana nao, "na huenda nao wakamcha Mungu." Yaani, wakaacha maasia waliyomo ndani yake. Kwa hivyo hatukati tamaa na uwongofu wao. Pengine mawaidha yakawaingia, na lawama ikawaathiri, na hili ndilo lengo kubwa la kukemea maovu, ili yawe ni udhuru na ili kusimamisha hoja juu ya yaliyoamrishwa na yaliyokatazwa, na pengine Mwenyezi Mungu akamwongoa na akatenda kwa mujibu wa amri hiyo na katazo hilo.
#
{165} {فلما نسوا ما ذُكِّروا به}؛ أي: تركوا ما ذُكِّروا به واستمروا على غَيِّهم واعتدائهم، {أنْجَيْنا الذين ينهون عن السوء}: وهكذا سنة الله في عباده أن العقوبة إذا نزلت نجا منها الآمرون بالمعروف والناهون عن المنكر، {وأخذنا الذين ظلموا}: وهم الذين اعتدَوْا في السبت {بعذابٍ بئيس}؛ أي: شديد {بما كانوا يفسُقون}. وأما الفرقة الأخرى التي قالت للناهين: لم تعِظون قوماً الله مهلكهم؛ فاختلف المفسرون في نجاتِهِم وهلاكهم، والظاهرُ أنهم كانوا من الناجين؛ لأنَّ الله خصَّ الهلاك بالظالمين، وهو لم يذكر أنهم ظالمون، فدلَّ على أن العقوبة خاصَّة بالمعتدين في السبت، ولأنَّ الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر فرضُ كفاية إذا قام به البعض سقط عن الآخرين؛ فاكتفوا بإنكار أولئك، ولأنهم أنكروا عليهم بقولهم: {لم تَعِظونَ قوماً الله مهلِكُهم أو معذِّبهم عذاباً شديداً}: فأبدَوْا من غضبهم عليهم ما يقتضي أنَّهم كارهون أشدَّ الكراهة لفعلهم، وأنَّ الله سيعاقبهم أشدَّ العقوبة.
{165} "Basi walipoyasahau yale waliyokumbushwa kwayo;" yaani, waliyaacha yale waliyokumbushwa kwayo na wakaendelea katika kukengeuka kwao na kuvuka kwao mipaka. "Tukawaokoa wale waliokuwa wakikataza mabaya." Na hivyo ndivyo ilivyo ada ya Mwenyezi Mungu katika waja wake kwamba inapoteremka adhabu, anawaokoa kutokana nayo wale wanaoamrisha mema na kukataza maovu. "Na tukawachukua wale waliodhulumu" nao ndio wale waliovuka mipaka katika Sabato kwa "adhabu mbaya mno kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka." Na ama lile kundi jingine ambalo liliwaambia wale waliokuwa wakikataza: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza, basi wafasiri walitofautiana kuhusu kunusurika kwao na kuangamizwa kwao, lakini la dhahiri ni kwamba walikuwa miongoni mwa waliosalimika. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alifungamanisha kuangamia na madhalimu tu, naye hakutaja kuwa wao ni madhalimu. Basi hili likaashiria kuwa adhabu ile ilikuwa mahsusi kwa wale waliovuka mipaka ya Sabato, na kwa sababu kuamrisha mema na kukataza maovu ni ya faradhi kutosheleza, ikiwa wengine wataitekeleza, basi itawaondokeaa wengineo. Kwa hivyo hawa walitosheka na kukataza kwa wale. Na kwa sababu waliwashutumu kwa kauli yao, “Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu adhabu kali?" Kwa hivyo, wakadhihirisha ghadhabu yao juu yao kwamba walichukia kuchukia kukubwa matendo yao hayo, na kwamba Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu kali kabisa.
#
{166} {فلما عَتَوْا عما نُهوا عنه}؛ أي: قسوا فلم يلينوا ولا اتَّعظوا، {قلنا لهم} قولاً قدريًّا: {كونوا قردةً خاسئين}: فانقلبوا بإذن الله قردةً وأبعدهم الله من رحمته.
{166} "Walipotakabari na kuasi yale waliyokatazwa." Yaani, walikuwa wagumu, wala hawakulainika wala hawakuwaidhika. "Tukawaambia" neno la kimajaliwa; "Kuweni manyani, mliodharauliwa." Basi wakageuka kuwa manyani, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu akawaweka mbali na rehema yake.
#
{167} ثم ذكر ضَرْبَ الذلة والصغار على من بقي منهم، فقال: {وإذ تأذَّنَ ربُّك}؛ أي: أعلم إعلاماً صريحاً، {ليبعثنَّ عليهم إلى يوم القيامة من يسومُهم سوء العذاب}؛ أي: يهينُهم ويذلُّهم، {إنَّ ربَّك لسريع العقاب}: لمن عصاه، حتى إنه يعجِّل له العقوبة في الدنيا. {وإنَّه لغفورٌ رحيم}: لمن تاب إليه وأناب؛ يغفر له الذُّنوب، ويستُر عليه العيوب، ويرحمه بأن يتقبَّل منه الطاعات ويثيبه عليها بأنواع المثوبات، وقد فعل الله بهم ما وعدهم به؛ فلا يزالون في ذلٍّ وإهانة، تحت حكم غيرهم، لا تقوم لهم رايةٌ ولا ينصر لهم عَلَمٌ.
{167} Kisha akataja kupigwa kwa udhalili na uduni juu ya wale waliobakia miongoni mwao. Kwa hivyo, akasema: "Na wakati alipotangaza Mola wako Mlezi;" yaani, alijulisha kujulisha kwa wazi wazi, "kwamba hakika atawatumia dhiki yao hadi Siku ya Qiyama mwenye kuwaadhibu kwa adhabu mbaya sana." Yaani, atawadunisha na kuwadhalilisha, "Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu" kwa mwenye kumuasi, kiasi kwamba Yeye humharakishia adhabu katika dunia hii. "Na hakika Yeye ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu sana" kwa mwenye kutubia kwake na kurejea. Anamsitiria dhambi, na anasitiri makosa yake, na anamrehemu kwa kumkubalia mambo ya utii na anamlipa juu yake kwa thawabu mbalimbali. Na Mwenyezi Mungu aliwafanyia yale aliyowaahidi. Basi hawataacha kuwa katika udhalili na uduni, chini ya utawala wa wasiokuwa wao. Haitawasimamia bendera yoyote, wala hakuna bendera yoyote itakayowaunga mkono.
#
{168} {وقطَّعناهم في الأرض أمماً}؛ أي: فرَّقناهم ومزَّقناهم في الأرض بعدما كانوا مجتمعين، {منهم الصالحون}: القائمون بحقوق الله وحقوق عباده، {ومنهم دون ذلك}؛ أي: دون الصلاح: إما مقتصدون، وإما الظالمون لأنفسهم. {وبَلَوْناهم}: على عادتنا وسنَّتنا {بالحسنات والسيئات}؛ أي: باليُسْر والعُسْر، {لعلَّهم يرجِعون}: عما هم عليه مقيمون من الرَّدى، ويراجعون ما خُلقوا له من الهدى، فلم يزالوا بين صالح وطالح ومقتصدٍ.
{168} "Na tukawagawanya katika ardhi umma umma;" yaani, tuliwafarikisha na tukawatenganisha katika ardhi baada ya kwamba walikuwa pamoja. "Miongoni mwao kuna wale walio wema" wanasimamisha haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, "na miongoni mwao kuna walio kinyume cha hivyo." Yaani, kinyume na wema: ima walio wastani, na ima wanaozidhulumu nafsi zao. "Na tukawajaribu" kama desturi yetu na Sunnah zetu "kwa mazuri na mabaya." Yaani, kwa wepesi na ugumu, "huenda wakarejea" wakaacha yale wanayodumisha kutenda miongoni mwa maovu, na wayarejee yale waliyoumbwa kwa ajili yake miongoni mwa uwongofu. Basi hawakuacha kuwa kati ya wema, na muovu, wale wa wastani.
#
{169} حتى خلف {من بعدِهم خَلْفٌ}: زاد شرُّهم {ورثوا}: بعدهم {الكتابَ}: وصار المرجع فيه إليهم، وصاروا يتصرَّفون فيه بأهوائهم، وتُبْذَلُ لهم الأموال ليفْتُوا ويحكموا بغير الحقِّ، وفشت فيهم الرشوة. {يأخُذون عَرَضَ هذا الأدنى ويقولونَ}: مقرِّين بأنه ذنب وأنهم ظلمة: {سَيُغْفَرُ لنا}: وهذا قول خالٍ من الحقيقة؛ فإنه ليس استغفاراً وطلباً للمغفرة على الحقيقة؛ فلو كان ذلك؛ لندموا على ما فعلوا، وعزموا على أن لا يعودوا، ولكنهم إذا أتاهم عرضٌ آخر ورشوةٌ أخرى؛ يأخذوه، فاشتروا بآيات الله ثمناً قليلاً، واستبدلوا الذي هو أدنى بالذي هو خير! قال الله تعالى في الإنكار عليهم وبيان جراءتهم: {ألم يؤخَذْ عليهم ميثاقُ الكتاب أن لا يقولوا على الله إلا الحقَّ}: فما بالُهم يقولون عليه غير الحقِّ اتِّباعاً لأهوائهم وميلاً مع مطامعهم؟! {و} الحالُ أنهم قد {دَرَسوا ما فيه}: فليس عليهم فيه إشكالٌ، بل قد أتوا أمرهم متعمِّدين، وكانوا في أمرهم مستبصرين، وهذا أعظمُ للذنب وأشدُّ للَّوم وأشنع للعقوبة، وهذا من نقص عقولهم وسفاهة رأيهم بإيثار الحياة الدُّنيا على الآخرة، ولهذا قال: {والدارُ الآخرة خيرٌ للذين يتَّقون}: ما حرَّم الله عليهم من المآكل التي تُصاب وتؤكل رشوة على الحكم بغير ما أنزل الله وغير ذلك من أنواع المحرمات. {أفلا تعقلون}؛ أي: أفلا يكون لكم عقولٌ توازن بين ما ينبغي إيثاره وما ينبغي الإيثار عليه، وما هو أولى بالسعي إليه والتقديم له على غيره؟! فخاصيَّة العقل النظر للعواقب، وأما من نَظَرَ إلى عاجل طفيف منقطع يفوِّت نعيماً عظيماً باقياً؛ فأنَّى له العقل والرأي؟!
{169} Mpaka wakafuatia "baada yao wafuatizi" waliozidi uovu wao "waliokirithi" baada yao "Kitabu," na yakawa marejeo katika hilo ni kwao, na wakaanza kukifanyia kulingana na matamanio yao. Na wanapewa mali ili watoe fatwa na wahukumu bila ya haki, na rushwa ikaenea miongoni mwao. "Wanachukua anasa za haya maisha duni, na wanasema" wakikiri kwamba ni dhambi na kwamba wao ni madhalimu: "Tutasitiriwa dhambi!" Na hii ni kauli isiyokuwa na uhakika. Kwani ingekuwa hivyo, basi wangejutia yale waliyoyafanya, na wangeazimia kwamba hawatarejea, lakini wao ikiwa wanajiwa na anasa nyingine na rushwa nyingine, wanaichukua. Kwa hivyo, wakanunua Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani chache, na wakabadilisha kile kilicho duni kwa kile kilicho bora zaidi! Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika kuwakadhibisha na kubainisha ujasiri wao dhidi yake, "Je, halikuchukuliwa juu yao agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu?" Basi wana nini hata wanasema juu Yake yasiyokuwa ya haki kwa kufuata matamanio yao na kuelekea kwenye tamaa zao? "Na" hali ni kuwa "Nao wamekwisha yasoma yale yaliyomo humo." Kwa hivyo, hawana shida yoyote nayo, bali walifanya mambo yao hayo kwa makusudi, na walikuwa wakijua vyema mambo yao hayo. Na hii ndiyo dhambi kubwa zaidi na yenye kulaumiwa zaidi, na baya zaidi la kuadhibiwa juu yake. Na hili ni kutokana na upungufu wa akili zao na upumbavu wa maoni yao kwa kuupendelea uhai wa dunia hii kuliko akhera. Na ndiyo maana akasema: "Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wachao" yale aliyowaharamishia Mwenyezi Mungu katika vyakula ambavyo vinachukuliwa na kuliwa kama rushwa, kwa ajili ya kuhukumu kwa yasiyokuwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu na yasiyokuwa hayo miongoni mwa haramu mbalimbali. "Basi je, hamtii akilini?" Yaani, je, hamna akili zenye kupima kati ya kile kinachopaswa kupendelewa na kile kinachopaswa kutopendelewa, na kile kinachostahiki zaidi kujitahidi kukielekea na kukitanguliza mbele ya vinginevyo? Kwani sifa maalum ya akili ni kuangalia katika matokeo. Na ama mwenye kutazama jambo la sasa tu, dogo, lenye kukatika, anakosa neema kubwa yenye kudumu, basi ana akili na maoni gani?
#
{170} وإنما العقلاءُ حقيقة من وصفهم الله بقوله: {والذين يمسِّكونَ بالكتاب}؛ أي: يتمسَّكون به علماً وعملاً، فيعلمون ما فيه من الأحكام والأخبار التي علمها أشرف العلوم، ويعملون بما فيها من الأوامر التي هي قرة العيون وسرور القلوب وأفراح الأرواح وصلاح الدنيا والآخرة. ومن أعظم ما يجب التمسُّك به من المأمورات إقامة الصلاة ظاهراً وباطناً، ولهذا خصها بالذِّكر لفضلها وشرفها وكونها ميزان الإيمان وإقامتها داعيةٌ لإقامة غيرها من العبادات. ولما كان عملهم كلُّه إصلاحاً؛ قال تعالى: {إنَّا لا نُضيعَ أجر المصلحين}: في أقوالهم وأعمالهم ونيَّاتهم، مصلحين لأنفسهم ولغيرهم. وهذه الآية وما أشبهها دلَّت على أنَّ الله بعث رسله عليهم الصلاة والسلام بالصلاح لا بالفساد، وبالمنافع لا بالمضار، وأنَّهم بُعِثوا بصلاح الدارين؛ فكلُّ مَن كان أصلح؛ كان أقرب إلى اتِّباعهم.
{170} Lakini wenye akili kiuhakika ni wale aliowaeleza Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: "Na wale wanaokikamata sawasawa Kitabu;" yaani, wanashikamana sawasawa nacho kielimu na kivitendo. Kwa hivyo wanajua yale yaliyomo ndani yake ya hukumu mbalimbali na habari ambazo zilifundishwa elimu yake ndiyo elimu tukufu zaidi, na wanatenda kulingana na yale yaliyomo ndani yake ya maamrisho ambayo ndiyo furaha ya macho, furaha ya nyoyo, furaha za roho, na kutengenea katika dunia na akhera. Na katika makubwa zaidi ambayo ni lazima kushikamana nayo vyema miongoni mwa maamrisho, ni kusimamisha Swala kwa dhahiri na kwa ndani. Na ndiyo maana akaitaja hasa kwa sababu ya fadhila yake na heshima yake na kwa kuwa ndiyo kipimo cha imani, na kuisimamaisha kwake kunaitia kusimamisha matendo yasiyokuwa hiyo miongoni mwa ibada. Na pindi matendo yao yote yalipokuwa ni ya kutengenea, Yeye Mtukufu akasema: "hakika Sisi hatupotezi ujira wa watengeneao;" katika kauli zao na matendo yao, na nia zao, wakijitengenea nafsi zao na wasiokuwa wao. Na Aya hii na mfano wake ziliashiria kwamba Mwenyezi Mungu aliwatuma Mitume wake, rehema na amani ziwe juu yao, ili kufanya mambo kutengenea, na si kuharibu, na kwa manufaa, si kwa madhara, na kwamba walitumwa kwa yanayotengenea nyumba hizi mbili. Kwa hivyo, Kila mtu aliyekuwa mwenye kutengenea, alikuwa ni karibu zaidi na kuwafuata.
#
{171} ثم قال تعالى: {وإذ نَتَقْنا الجبل فوقَهم}: حين امتنعوا من قَبول ما في التوراة، فألزمهم الله العمل، وَنَتقَ فوق رؤوسهم الجبل، فصار فوقهم: {كأنه ظُلَّة وظنُّوا أنه واقعٌ بهم}، وقيل لهم: {خذوا ما آتيناكم بقوَّةٍ}؛ أي: بجدٍّ واجتهاد. {واذكُروا ما فيه}: دراسة ومباحثة واتصافاً بالعمل به، {لعلَّكم تتَّقون}: إذا فعلتُم ذلك.
{171} Kisha Yeye Mtukufu akasema: "Na pale tulipounyanyua mlima juu yao" wakati walipokataa kuyakubali yale yaliyomo katika Taurati, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawalazimisha kufanya matendo, na akauinua mlima juu ya vichwa vyao, kwa hivyo ukawa juu yao. "Ukawa kama kwamba ni kiwingu kilicho wafunika} na wakaambiwa: "Chukueni yale tuliyowapa kwa nguvu" yaani, bidii na jitihada; "na yakumbukeni yaliyomo ndani yake" kwa kujifunza, na kutafiti na kusifika kwa kuyatendea matendo "ili muche" mtakapofanya hivyo.
: 172 - 174 #
{وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنْ بَنِي آدَمَ مِنْ ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنْفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ قَالُوا بَلَى شَهِدْنَا أَنْ تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ (172) أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِنْ قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِنْ بَعْدِهِمْ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ (173) وَكَذَلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ (174)}
172. Na pale Mola wako Mlezi alipochukua kutoka kwa wanadamu kutoka katika migongo yao dhuria zao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao (na kuwaambia), "Je, mimi si Mola wenu Mlezi?" Wakasema, "Ndiyo, tumeshuhudia." Mje mkasema Siku ya Qiyama, "Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika na haya." 173. Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao. Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyoyafanya wapotovu? 174. Na ndiyo kama hivyo tunavyozieleza Ishara kwa kina, ili huenda wakarejea.
#
{172 - 173} يقول تعالى: {وإذْ أخَذَ ربُّك من بني آدمَ من ظهورهم ذُرِّيَّتهم}؛ أي: أخرج من أصلابهم ذريتهم، وجعلهم يتناسلون ويتوالدون قرناً بعد قرنٍ. {و}: حين أخرجهم من بطون أمَّهاتهم وأصلاب آبائهم، {أشهدهم على أنفسِهِم ألستُ بربِّكم}؛ أي: قرَّرهم بإثبات ربوبيَّته بما أودعه في فطرهم من الإقرار بأنه ربُّهم وخالقهم ومليكهم. قالوا: بلى؛ قد أقررنا بذلك؛ فإنَّ الله تعالى فطر عباده على الدين الحنيف القيم، فكلُّ أحدٍ فهو مفطورٌ على ذلك، ولكن الفطرة قد تُغيَّر وتُبدَّل بما يطرأ على العقول والعقائد الفاسدة ، ولهذا {قالوا بلى شَهِدْنا أن تَقولوا يوم القيامةِ إنَّا كنَّا عن هذا غافلين}؛ أي: إنما امتحنَّاكم حتى أقررتم بما تقرَّر عندكم من أنَّ الله تعالى ربُّكم؛ خشية أن تنكِروا يوم القيامة فلا تقرُّوا بشيء من ذلك، وتزعمون أن حجَّة الله ما قامت عليكم، ولا عندكم بها علم، بل أنتم غافلون عنها لاهون؛ فاليوم قد انقطعت حجَّتكم، وثبتت الحجة البالغة لله عليكم. أو تحتجون أيضاً بحجَّة أخرى، فتقولون: {إنَّما أشركَ آباؤنا من قَبْلُ وكُنَّا ذُرِّيَّةً من بعدِهم}: فحذونا حَذْوَهم، وتبعناهم في باطلهم. {أفتهلِكُنا بما فعل المبطلون}؟ فقد أودع الله في فطركم ما يدلُّكم على أن ما مع آبائكم باطلٌ، وأنَّ الحقَّ ما جاءت به الرسل، وهذا يقاوم ما وجدتم عليه آباءكم ويعلو عليه. نعم؛ قد يعرض للعبد من أقوال آبائه الضالِّين ومذاهبهم الفاسدة ما يظنُّه هو الحقَّ، وما ذاك إلا لإعراضه عن حجج الله وبيِّناته وآياته الأفقيَّة والنفسيَّة؛ فإعراضه عن ذلك وإقباله على ما قاله المبطلون، ربَّما صيَّره بحالة يُفضِّل بها الباطل على الحق. هذا هو الصواب في تفسير هذه الآيات، وقد قيل: إن هذا يوم أخذ الله الميثاق على ذريَّة آدم حين استخرجهم من ظهره وأشهدهم على أنفسهم فشهدوا بذلك فاحتجَّ عليهم بما أمرهم به في ذلك الوقت على ظلمهم في كفرهم وعنادهم في الدنيا والآخرة! ولكن ليس في الآية ما يدلُّ على هذا، ولا له مناسبة، ولا تقتضيه حكمة الله تعالى، والواقع شاهدٌ بذلك؛ فإنَّ هذا العهد والميثاق الذي ذَكَروا أنه حين أخْرَجَ اللهُ ذُرِّيَّةَ آدم من ظهره حين كانوا في عالم كالذَّرِّ لا يذكُرُه أحدٌ ولا يخطُرُ ببال آدميٍّ؛ فكيف يحتجُّ الله عليهم بأمرٍ ليس عندهم به خبرٌ ولا له عينٌ ولا أثرٌ؟!
{172 - 173} Yeye Mtukufu anasema, “Na pale Mola wako Mlezi alipochukua kutoka kwa wanadamu kutoka katika viuno vyao dhuria zao.” Yaani, alitoa katika migongo yao dhuriya zao na akawafanya wazaane karne baada ya karne. "Na" wakati alipowatoa katika matumbo ya mama zao na migongo ya baba zao, "akawashuhudisha juu ya nafsi zao (na kuwaambia), "Je, mimi si Mola wenu Mlezi?" Yaani aliwafanya wakiri kuuthibitisha umola wake kwa yale aliyoyaweka katika maumbile yao ya asili kukiri kuwa Yeye ndiye Mola wao mlezi, na Muumba wao, na Mmiliki wao. Wakasema: Ndiyo; tumekiri hilo. Kwa maana Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa waje wake umbile asili la kuwa juu ya Dini iliyonyooka na iliyo sawasawa; basi kila mmoja ameumbwa juu ya hilo. Lakini maumbile ya asili huenda yakageuzwa na kubadilishwa kwa yale yanayoyatokea katika akili na itikadi mbovu. Na ndio maana "Wakasema: Ndiyo, tumeshuhudia." Mje mkasema Siku ya Qiyama, "Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika na haya." Yaani, hakika Sisi tuliwapa mtihani mpaka mkakiri yale yaliyothibiti kwenu kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mola wenu Mlezi, kwa kuchelea kwamba mtakataa Siku ya Kiyama na msikiri chochote katika hayo, na mkadai kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu haikusimama juu yenu, na kwamba hamna elimu kuhusiana nayo; bali mlighafilika nayo na mkapumbaa. Basi leo, hoja zenu zimekatika, na ikathibitika hoja ya kukata wa Mungu dhidi yenu, au pia mkatumia hoja nyengine, mkasema, “Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao." Basi tukafuata mfano wao, na tukawafuata katika batili yao. "Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyoyafanya wapotovu?" Kwani Mwenyezi Mungu aliweka katika maumbile yenu yale yanayowaonyesha ya kwamba yale waliyo nayo baba zenu ni batili, na kwamba haki ni yale waliyokuja nayo Mitume. Na hili linapingana na yale mliyowakuta nayo baba zenu na liko juu yake. Ndiyo; inaweza kufikiwa mja katika na maneno ya baba zake wapotofu na madhehebu yao potovu yale ambayo anayadhania kuwa ndiyo haki. Na hilo si isipokuwa kwa sababu ya kujiepusha kwake na hoja za mwenyezi Mungu, ushahidi wake wa waziwazi, na aya Zake za kiupeo wa macho na za kinafsi. Basi kupeana kwake mgongo hayo na kuelekea kwake kwa yale waliyoyasema wana batili huenda yakamfanya awe katika hali ambayo atapendelea ndani yake batili kuliko haki. Hii ndiyo tafsiri sahihi ya Aya hizi na ilisemwa: hii ni siku ile Mwenyezi Mungu alipochukua agano juu ya dhuria wa Adam wakati alipowatoa katika mgongo wake na akawashuhudishia juu ya nafsi zao, nao wakashuhudia hayo. Kwa hivyo akatumia kama ushahidi dhidi yao yale aliyowaamrisha kuyafanya wakati huo dhidi ya dhuluma yao katika ukafiri wao na ukaidi wao katika dunia na Akhera! Lakini hakuna chochote katika Aya hii kinachoonyesha hili, wala hali kinacholifaa hapa, wala si katika matakwa ya hekima ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na hali ya hakika ya mambo unalishahidia hilo. Kwa maana, ahadi hili na agano hili ambalo walilitaja kwamba wakati Mwenyezi Mungu alipowatoa dhuria ya Adamu kutoka katika mgongo wake walipokuwa katika ulimwengu kama chembe, ambao hakuna anayeukumbuka na wala haupiti katika akili ya mwanadamu. Basi vipi Mwenyezi Mungu atatumia dhidi ya hoja ya jambo ambalo hawana habari nalo wala hawana jicho wala alama?
#
{174} ولهذا؛ لما كان هذا أمراً واضحاً جليًّا؛ قال تعالى: {وكذلك نفصِّل الآيات}؛ أي: نبيِّنها ونوضِّحها، {ولعلَّهم يرجعون}: إلى ما أودع الله في فِطَرِهم وإلى ما عاهدوا الله عليه فيرتدعوا عن القبائح.
{174} Na ndiyo maana, kwa kuwa hili lilikuwa jambo lililo wazi, la peupe, Mwenyezi Mungu akasema: "Na ndiyo kama hivyo tunavyozieleza Ishara kwa kina." Yaani, tunazibainisha, na kuziweka wazi "ili huenda wakarejea" katika yale Mwenyezi Mungu aliyaweka katika maumbile yao ya asili, na katika kile walichomwahidi Mwenyezi Mungu juu yake; kwa hivyo wakakomeka kutokana na mabaya.
: 175 - 178 #
{وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانْسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ (175) وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِنْ تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَثْ ذَلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ (176) سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنْفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ (177) مَنْ يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِي وَمَنْ يُضْلِلْ فَأُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ (178)}.
175. Na wasomee habari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua kutoka kwazo, basi Shetani akamfuata. Kwa hivyo, akawa miongoni mwa waliopotea. 176. Na lau kuwa tungelitaka, tungelimwinua kwazo, lakini yeye alizama katika ulimwengu na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi nje, na ukimwacha, pia hupumua na kutoa ulimi nje. Huo ni mfano wa kaumu ambao walizikadhibisha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari. 177. Mfano mbaya zaidi ni wa kaumu waliozikadhibisha Ishara zetu na walikuwa wakizidhulumu nafsi zao. 178. Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi huyo ndiye mwongofu. Na yule aliyempoteza, basi hao ndio waliohasiri.
#
{175} يقول تعالى لنبيه - صلى الله عليه وسلم -: {واتلُ عليهم نبأ الذي آتَيْناه آياتِنا}؛ أي: علمناه [علم] كتاب الله فصار العالم الكبير والحبر النحرير فانسلخ منها فأتبعه الشيطان؛ أي: انسلخ من الاتِّصاف الحقيقيِّ بالعلم بآيات الله؛ فإنَّ العلم بذلك يصيِّر صاحبه متصفاً بمكارم الأخلاق ومحاسن الأعمال ويرقى إلى أعلى الدرجات وأرفع المقامات؛ فترك هذا كتاب الله وراء ظهره، ونبذ الأخلاق التي يأمر بها الكتاب، وخلعها كما يُخْلَعُ اللباس، فلما انسلخ منها؛ أتْبَعَهُ الشيطانُ؛ أي: تسلَّط عليه حين خرج من الحصن الحصين وصار إلى أسفل سافلين، فأزَّه إلى المعاصي أزًّا، {فكان من الغاوين}: بعد أن كان من الراشدين المرشدين.
{175} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: - "Na wasomee habari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu." Yaani, tuliyemfunza [elimu ya] Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa hivyo akawa yeye ndiye mwanachuoni mkubwa na wino wa kuandikia kwenye hariri, lakini akajivua kutoka humo, na Shetani akamfuata. Yaani, alijivua kutoka katika kusifika kwa hakika kwa elimu ya ishara za Mwenyezi Mungu. Kwani kuwa na elimu ya hayo kunamfanya mwenyewe asifike kwa tabia njema na matendo mazuri, na anapanda hadi katika viwango vya juu na vyeo vya juu zaidi. Kwa hivyo, kuacha kwa huyu Kitabu cha Mwenyezi Mungu nyuma ya mgongo wake, na kuyatupa maadili ambayo kitabu kinayaamrisha, na kuyavua kama yanavyovuliwa mavazi, na wakati ilipojivua kutoka kwayo, Shetani akamfuata. Yaani, akawa na mamlaka juu yake wakati alipotoka kwenye ngome madhubuti, na akaishia chini zaidi ya walio chini, kwa hivyo akamchochoa kwa uchochezi mkubwa. "Kwa hivyo, akawa miongoni waliopotea," baada ya kwamba alikuwa miongoni mwa walioongoka, walioongolewa.
#
{176} وهذا لأنَّ الله تعالى خَذَلَه ووَكَلَه إلى نفسه؛ فلهذا قال تعالى: {ولو شِئْنا لرَفَعْناه بها}: بأن نوفِّقه للعمل بها، فيرتفع في الدنيا والآخرة، فيتحصَّن من أعدائه، {ولكنَّه}: فعل ما يقتضي الخذلان؛ فأخلدَ إلى الأرضِ؛ أي: إلى الشهوات السفليَّة والمقاصد الدنيويَّة، {واتَّبع هواه}: وترك طاعة مولاه. {فَمَثله}: في شدة حرصه على الدنيا وانقطاع قلبه إليها {كمثل الكلب إن تَحْمِلْ عليه يَلْهَثْ أو تترُكْهُ يلهثْ}؛ أي: لا يزال لاهثاً في كل حال، وهذا لا يزال حريصاً حرصاً قاطعاً قلبه لا يسدُّ فاقتَهُ شيءٌ من الدُّنيا. {ذلك مَثَلُ القوم الذين كذَّبوا بآياتنا}: بعد أن ساقها الله إليهم، فلم ينقادوا لها، بل كذَّبوا بها وردُّوها لهوانهم على الله واتِّباعهم لأهوائهم بغير هدى من الله. {فاقصُص القَصَص لعلَّهم يتفكَّرون}: في ضرب الأمثال وفي العبر والآيات؛ فإذا تفكَّروا؛ علموا، وإذا علموا؛ عملوا.
{176} Na haya ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwacha na akamwachia nafsi yake. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na lau kuwa tungelitaka, tungelimuinua kwazo" kwa kumwezesha kuzitendea matendo, kwa hivyo akainuka katika dunia na Akhera, kwa hivyo akajilinda kutokana na adui zake; "Lakini yeye" aliyafanya yale yanayolazimu kuachwa, basi alizama katika dunia. Yaani, alizama katika matamanio ya chini na malengo ya kidunia, "na akafuata matamanio yake" na akaacha kumtii Mola wake. "Basi mfano wake" katika kuwania kwake dunia hii na moyo wake kuikatikia "ni kama mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi nje, na ukimwacha, pia hupumua na kutoa ulimi nje." Yaani, hataacha kuendelea kuhema katika kila hali. Na huyu hataacha kuwania kuwania kwa kukata moyo wake, na hakuna kitu chochote duaniani kinachoweza kujaza mahitaji yake. "Huo ni mfano wa kaumu ambao walizikadhibisha Ishara zetu" baada ya Mwenyezi Mungu kuwafikishia, lakini hawakuzifuata, bali walizikakadhibisha na wakazikataa kwa matamanio yao bila uwongofu wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kufuata matamanio yao bila ya uwongofu. kutoka kwa Mungu. "Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari" katika kupiga mifano na katika mazingatio na Aya mbalimbali. Kwa hivyo, wanafikiri; watajua, na wakijua, watafanya matendo.
#
{177} {ساء مَثَلاً القومُ الذين كذَّبوا بآياتِنا وأنفسَهم كانوا يظلمونَ}؛ أي: ساء وقَبُح مَثَلُ مَن كذب بآيات الله، وظلم نفسه بأنواع المعاصي؛ فإنَّ مَثَلَهم مَثَلُ السَّوْء. وهذا الذي آتاه الله آياته يُحتمل أنَّ المرادَ به شخصٌ معيَّن قد كان منه ما ذكره اللهُ فقص اللهُ قصَّته تنبيهاً للعباد، ويُحتمل أنَّ المراد بذلك أنه اسم جنس، وأنَّه شاملٌ لكلِّ من آتاه اللهُ آياته فانسلخ منها. وفي هذه الآيات الترغيب في العمل بالعلم، وأنَّ ذلك رفعة من الله لصاحبه وعصمة من الشيطان، والترهيب من عدم العمل به، وأنه نزولٌ إلى أسفل سافلين وتسليط للشيطان عليه. وفيه أنَّ اتِّباع الهوى وإخلادَ العبد إلى الشهوات يكون سبباً للخذلان.
{177} "Mfano mbaya zaidi ni wa kaumu waliozikadhibisha Ishara zetu na walikuwa wakijidhulumu nafsi zao." Yaani, ni mfano mbaya zaidi wa yule anayezikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu na akaidhulumu nafsi yake kwa kila aina za maasia. Basi mfano wao ni ule ulio mbaya zaidi. Na huyu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa ishara zake, inawezekana kinachomaanishwa kwa hilo ni mtu maalum, ambaye alifanya hayo ambayo Mwenyezi Mungu aliyataja. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akakisimulia kisa chake ili kuwatanabahisha waja wake. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa kwa hilo ni kwamba ni jina la ujumla, na kwamba linajumuisha kila mtu ambaye Mwenyezi Mungu alimpa ishara zake kisha akajivua kutoka kwazo. Na katika aya hizi kuna kuhimiza kufanya matendo kwa elimu, na kwamba hilo ni kuinuliwa juu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mwenyewe, na ni kinga dhidi ya Shetani. Na zina kuhofisha kutofanya matendo kwayo, na kwamba ni kushuka hadi chini zaidi ya walio chini, na kumpa Shetani mamlaka juu yake. Na ndani yake kuna kwamba kufuata matamanio ya mtu na mja kuzama katika matamanio yanakuwa sababu ya kuachiliwa mbali.
#
{178} ثم قال تعالى مبيناً أنه المنفرد بالهداية والإضلال: {مَن يهدِ الله}: بأن يوفِّقه للخيرات ويعصمه من المكروهات ويعلِّمه ما لم يكن يعلم، {فهو المهتدي}: حقًّا؛ لأنه آثر هدايته تعالى، {ومن يُضْلِلْ}: فيخذله ولا يوفِّقه للخير، {فأولئك هم الخاسرون}: لأنفسهم وأهليهم يوم القيامة، ألا ذلك هو الخسران المبين.
{178} Kisha Yeye Mtukufu akasema, akibainisha kuwa ni Yeye peke yake mwenye kuongoza na kupoteza: "Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa" kwa kumwezesha kwa matendo mema na kumlinda kutokana na machukizo, na kumfundisha yale ambacho hakuwa anayajua, "basi huyo ndiye mwongofu" kiuhakika. Kwa sababu, alipendelea uwongofu wake Yeye Mtukufu "Na yule aliyempoteza" kwa kumwachilia mbali na asimwezeshe kwa heri. "Basi hao ndio waliohasiri" nafsi zao na ahali zao Siku ya Qiyama. Tazama, huko ndiko kuhasiri kwa wazi.
: 179 #
{وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ لَهُمْ قُلُوبٌ لَا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَا يَسْمَعُونَ بِهَا أُولَئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ أُولَئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ (179)}.
179. Na hakika tumeiumbia Jahannamu wengi katika majini na watu. Wana nyoyo wasizofahamu kwazo. Na wana macho wasiyoona kwayo. Na wana masikio wasiyosikia kwayo. Hao ni kama wanyama wa mifugo, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika.
#
{179} يقول تعالى مبيناً كثرة الغاوين الضالِّين المتَّبعين إبليس اللعين: {ولقد ذَرَأنا}؛ أي: أنشأنا، وبثثنا {لجهنَّم كثيراً من الجنِّ والإنس}: صارت البهائم أحسن حالة منهم. {لهم قلوبٌ لا يفقهون بها}؛ أي: لا يصلُ إليها فقهٌ ولا علمٌ إلاَّ مجرَّد قيام الحجة، {ولهم أعينٌ لا يبصرون بها}: ما ينفعُهم، بل فقدوا منفعتها وفائدتها، {ولهم آذانٌ لا يسمعون بها}: سماعاً يصل معناه إلى قلوبهم. {أولئك}: الذين بهذه الأوصاف القبيحة {كالأنعام}؛ أي: البهائم التي فقدت العقول، وهؤلاء آثروا ما يفنى على ما يبقى فسُلِبوا خاصية العقل. {بل هم أضلُّ}: من البهائم؛ فإنَّ الأنعام مستعملة فيما خُلِقت له، ولها أذهانٌ تدرك بها مضرَّتها من منفعتها؛ فلذلك كانت أحسن حالاً منهم. و {أولئك هم الغافلون}: الذين غفلوا عن أنفع الأشياء؛ غفلوا عن الإيمان بالله وطاعته وذِكْره، خُلِقَتْ لهم الأفئدة والأسماع والأبصار لتكونَ عوناً لهم على القيام بأوامر الله وحقوقه، فاستعانوا بها على ضدِّ هذا المقصود؛ فهؤلاء حقيقون بأن يكونوا ممَّن ذرأ الله لجهنَّم وخلقهم لها؛ فخلقهم للنار وبأعمال أهلها يعملون، وأما مَن استعمل هذه الجوارح في عبادة الله وانصبغ قلبُهُ بالإيمان بالله ومحبَّته ولم يغفل عن الله؛ فهؤلاء أهل الجنة وبأعمال أهل الجنة يعملون.
{179} Yeye Mtukufu anasema, akibainisha wingi wale waliokengeuka, waliopotea, waliomfuata Shetani aliyelaaniwa: "Na hakika tumeiumbia" tulianzisha, na kueneza "Jahannamu wengi katika majini na watu" ambao wanyama wa mifugo wamekuwa katika hali bora zaidi kuwaliko wao. "Wana nyoyo wasizofahamu kwazo;" yaani, hazifikiwi na ufahamu wala elimu isipokuwa kwa kuwasimamishia hoja tu. "Na wana macho wasiyoona kwayo" yenye kuwanufaisha. Bali wamepoteza manufaa yake na faida yake, "Na wana masikio wasiyosikia kwayo" kusikia kunakoifikia maana yake mioyo yao. "Hao" wenye sifa hizi mbaya "ni kama wanyama wa mifugo." Yaani, wanyama ambao walipoteza akili. Na hawa walipendelea yenye kuisha badala ya yenye kubaki, kwa hivyo wakawa wamenyang’anywa sifa ya kuwa na akili. "Bali wao ni wapotofu zaidi" kuliko wanyama. Kwa sababu, wanyama wa mifugo wanatumiwa katika yale waliyoumbwa kwa ajili yake; nao wana bongo wanazotambua kwazo yenye kuwadhuru kando na yenye kuwanufaisha. Na ndiyo maana wakawa katika hali bora zaidi kuliko wao. Na "hao ndio walioghafilika'" ambao walivighafilikia vitu vyenye faida zaidi. Walighafilikia kumwamini Mwenyezi Mungu, na kumtii, na kumkumbuka. Waliumbiwa mioyo, na kusikia, na kuona ili viwe msaada kwao katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu na haki zake. Lakini wakazitumia kama msaada katika kinyume cha makusudio haya. Basi hawa wanastahiki zaidi kwamba wawe miongoni mwa wale aliowaandalia Mwenyezi mungu Jahannam na akawaumba kwa ajili yake. Kwa hivyo, aliwaumba kwa ajili ya Moto na kwa matendo ya watu wake wanaoyafanya. Na ama mwenye kuvitumia viungo hivi katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, na moyo wake ukajipaka rangi ya kumwamini Mwenyezi Mungu na kumpenda na wala hakumghafilikia Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watu wa Pepo, na kwa vitendo vya watu wa Pepo wanavifanya.
: 180 #
{وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَى فَادْعُوهُ بِهَا وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (180)}.
180. Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopindukia mipaka katika majina yake. Watakuja lipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{180} هذا بيانٌ لعظيم جلاله وسعة أوصافه بأن له الأسماء الحسنى؛ أي: له كل اسم حسن، وضابطه أنه كل اسم دال على صفة كمال عظيمة، وبذلك كانت حسنى؛ فإنها لو دلَّت على غير صفة، بل كانت علماً محضاً؛ لم تكن حسنى، وكذلك لو دلَّت على صفة ليست بصفة كمال، بل إما صفة نقص أو صفة منقسمة إلى المدح والقدح؛ لم تكن حسنى؛ فكلُّ اسم من أسمائه دال على جميع الصفة التي اشتُقَّ منها، مستغرقٌ لجميع معناها، وذلك نحو: {العليم} الدال على أنَّ له علماً محيطاً عامًّا لجميع الأشياء فلا يخرج عن علمه مثقال ذرةٍ في الأرض ولا في السماء، و {الرحيم} الدال على أن له رحمة عظيمة واسعة لكلِّ شيء، و {القدير} الدال على أن له قدرة عامَّة لا يُعْجِزُها شيء ... ونحو ذلك. ومن تمام كونها حسنى أنَّه لا يُدعى إلا بها، ولذلك قال: {فادعوه بها}: وهذا شاملٌ لدعاء العبادة ودعاء المسألة، فيُدعى في كل مطلوب بما يناسب ذلك المطلوب، فيقول الداعي مثلاً: اللهمَّ! اغفر لي، وارحمني؛ إنك أنت الغفور الرحيم. وتب عليَّ يا توَّاب! وارزقني يا رزاق! والطفْ بي يا لطيف! ونحو ذلك. وقوله: {وَذَروا الذين يُلحِدون في أسمائِهِ سيُجْزَوْن ما كانوا يعملون}؛ أي: عقوبة وعذاباً على إلحادهم في أسمائه. وحقيقة الإلحاد: الميلُ بها عما جُعِلَتْ له، إمَّا بأن يسمَّى بها من لا يستحقُّها؛ كتسمية المشركين بها لآلهتهم، وإما بنفي معانيها وتحريفها وأن يجعل لها معنى ما أراده الله ولا رسوله، وإما أن يشبِّه بها غيرها؛ فالواجب أن يُحذر الإلحاد فيها ويُحذر الملحدون فيها. وقد ثبت في الصحيح عن النبيِّ - صلى الله عليه وسلم -: «إنَّ لله تسعةً وتسعين اسماً من أحصاها دخل الجنة».
{180} Huku ni kubainisha ukubwa wa utukufu wake na upana wa sifa zake, kwamba ana majina mazuri sana. Yaani, ni lake kila jina jema na kanuni yake ni kila jina linaonyesha sifa ya ukamilifu mkubwa; na kwa hivyo yakawa ni mazuri. Kwani ikiwa yangeonyesha kitu kisichokuwa sifa, bali yangekuwa jina la kipekee tu, basi hayangekuwa mazuri. Na vile vile ikiwa yangeonyesha sifa ambayo si sifa ya ukamilifu, bali ima sifa ya upungufu au sifa inayogawanyika katika sifa na shutuma, basi hayangekuwa mazuri. Kwa hivyo, kila jina katika majina yake linaonyesha sifa nzima ambayo inatokana nayo, na kujumuisha maana yake yote, na hilo ni kama vile: "Mwenye kujua vyema" linaashiria kwamba Yeye ana elimu inayozunguka, yenye kujumuisha kila kitu, kwa hiyo haitoki katika elimu yake hata uzito wa chembe katika ardhi wala katika mbingu. Na "Mwenye kurehemu" ambayo inaashiria kwamba Yeye ana rehema kubwa, kunjufu juu ya kila kitu. Na "Mwenye uwezo" linaashiria kwamba Ana uwezo wa jumla ambao hakuna kinachoushinda... na mfano wa hayo. Na katika utimilifu wa kuwa ni mazuri ni kwamba mtu haombwi isipokuwa kwayo, na ndiyo maana akasema: "Basi muombeni kwayo." Na hili linajumuisha dua ya ibada na dua ya kuomba kupewa kitu. Kwa hivyo, anaombwa katika kila ombi kwa kile kinacholifaa ombi hilo. Kwa hivyo mwombaji atasema, kwa mfano, “Ee mwenyezi Mungu! Nisitirie dhambi, na unirehemu. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu. Na unikubalie toba, ewe Mwenye kukubali toba! Na uniruzuku, ewe Mwenye kuruzuku. Na unifanyie upole, ewe Mpole!” Na mfano wa hayo. Na kauli yake: "Na waacheni wale wanaopindukia mipaka katika majina yake. Watakuja lipwa yale waliyokuwa wakiyatenda." Yaani, adhabu na mateso kwa sababu ya kupindukia kwao mipaka katika majina yake. Na uhakika wa kupindukia mipaka ni kuyaondoa kutoka kwa kile yaliyokusudiwa, ima kwa kumwita kwao yule asiyeyastahiki, kama vile washirikina walivyowaita miungu yao kwayo, au kwa kuzikanusha maana zake na kuzipotosha, na kuyapa maana ambazo Mwenyezi Mungu hakuzikusudia wala Mtume wake, au kwa kuzifananisha na kitu kingine. Kwa hivyo la wajibu ni kutahadhari kupindukia mipaka ndani yake, na kutahadhari wale wapindukiao mipaka ndani yake. Na imethibiti katika hadithi Swahih kutoka kwa Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, “Hakika Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa. Mwenye kuyadhibiti, ataingia Peponi.”
: 181 #
{وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ (181)}.
181. Na katika wale tuliowaumba wako umma wanaoongoza kwa haki, na kwayo wanafanya uadilifu.
#
{181} أي: ومن جملة من خلقنا أمة فاضلة كاملة في نفسها مكمِّلة لغيرها يهدون أنفسهم وغيرهم بالحقِّ فيعلمون الحقَّ ويعملون به ويعلِّمونه ويدعون إليه وإلى العمل به. {وبه يعدلون}: بين الناس في أحكامهم إذا حكموا في الأموال والدماء والحقوق والمقالات وغير ذلك. وهؤلاء أئمة الهدى ومصابيح الدُّجى، وهم الذين أنعم الله عليهم بالإيمان والعمل الصالح والتواصي بالحقِّ والتواصي بالصبر، وهم الصدِّيقون الذين مرتبتهم تلي مرتبة الرسالة، وهم في أنفسهم مراتب متفاوتة؛ كل بحسب حاله وعلوِّ منزلته؛ فسبحان من يختصُّ برحمته من يشاء والله ذو الفضل العظيم.
{181} Yaani, na katika jumla ya wale tuliowaumba kuna umma wema, wakamilifu wao wenyewe, wenye kuwakamilisha wengineo, wanajiongoza wao wenyewe kwa haki na wengineo. Kwa hivyo wanaijua haki, na wanaifanyia matendo, na wanaifundisha, na wanailingania na katika kuitendea matendo, "na kwayo wanafanya uadilifu;" baina ya watu katika hukumu zao wanapohukumu katika mali, na damu, na haki mbalimbali, na maneno na yasiyokuwa hayo. Na hao ndio maimamu wa uwongofu na taa za giza, nao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwa Imani, na matendo mema, na kuusiana haki, na kuusiana subira, nao ndio wakweli ambao vyeo vyao vinafuata cheo cha utume, nao katika nafsi zao wana vyeo tofauti tofauti, kila mmoja kulingana na hali yake na cheo chake. Basi utukufu ni wa yule anayemteua amtakaye kwa rehema zake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
: 182 - 186 #
{وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُمْ مِنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ (182) وَأُمْلِي لَهُمْ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ (183) أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا مَا بِصَاحِبِهِمْ مِنْ جِنَّةٍ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُبِينٌ (184) أَوَلَمْ يَنْظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّهُ مِنْ شَيْءٍ وَأَنْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ (185) مَنْ يُضْلِلِ اللَّهُ فَلَا هَادِيَ لَهُ وَيَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ (186)}.
182. Na wale waliokadhibisha Ishara zetu, tutawapeleka katika maangamio pole pole kutokea pale wasipojua. 183. Nami nitawapa muda. Hakika njama yangu ni madhubuti. 184. Je, hawafikirii? Huyu mwenzao hana wazimu. Yeye siyo isipokuwa ni mwonyaji aliye dhahiri. 185. Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vile vyote alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na kwamba huenda muda wao umekwisha karibia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? 186. Yule Mwenyezi Mungu alimpoteza, basi hana wa kumwongoa. Atawaacha hao katika upotovu wao wakitangatanga.
#
{182} أي: والذين كذَّبوا بآيات الله الدالَّة على صحة ما جاء به محمد - صلى الله عليه وسلم - من الهدى فردُّوها ولم يقبلوها، {سنستدرِجُهم من حيث لا يعلمون}: بأن يدر لهم الأرزاق.
{182} Yaani, na wale waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu zinazoonyesha usahihi wa yale aliyokuja navyo Muhammad-rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - miongoni mwa uwongofu nao wakaukataa na hawakuukubali, "tutawapeleka katika maangamio pole pole kutokea pale wasipojua," kwa kuwaruzuku kwa wingi.
#
{183} {وأملي لهم}؛ أي: أمهلهم حتى يظنُّوا أنهم لا يؤخَذون ولا يعاقَبون، فيزدادون كفراً وطغياناً وشرًّا إلى شرِّهم، وبذلك تزيد عقوبتهم ويتضاعف عذابهم، فيضرُّون أنفسهم من حيث لا يعلمون. ولهذا قال: {إن كيدي متينٌ}؛ أي: قويٌّ بليغٌ.
{183} "{183} "Nami nitawapa muda;" yaani, nitawapa muhula mpaka wadhani kuwa hawatachukuliwa wala hawataadhibiwa, basi wakazidisha ukafiri, na kupindukia mipaka, na uovu juu ya uovu wao. Na kwa hivyo, adhabu yao inazidi, na mateso yao yanaongezeka maradufu, kwa hivyo wanakuwa wamejidhuru wenyewe kutokea pale ambapo hawajui. Na ndiyo maana akasema: "Hakika njama yangu ni madhubuti;" yaani, ni ya nguvu na kubwa mno.
#
{184} {أوَ لَمْ يتفكَّروا ما بصاحبهم}: [محمدٍ]- صلى الله عليه وسلم - {من جِنَّةٍ}؛ أي: أولم يُعْمِلوا أفكارهم وينظروا هل في صاحبهم الذي يعرفونه ولا يخفى عليهم من حاله شيءٌ؛ هل هو مجنونٌ؟! فلينظروا في أخلاقه وهديه ودلِّه وصفاته، وينظروا فيما دعا إليه؛ فلا يجدون فيه من الصفات إلا أكملها، ولا من الأخلاق إلا أتمَّها، ولا من العقل والرأي إلا ما فاق به العالمين، ولا يدعو إلا لكلِّ خير، ولا ينهى إلا عن كلِّ شرٍّ! أفبهذا يا أولي الألباب جِنَّة ؟! أم هو الإمام العظيم والناصح المبين والماجد الكريم والرءوف الرحيم؟! ولهذا قال: {إن هو إلا نذيرٌ مبينٌ}؛ أي: يدعو الخلق إلى ما يُنجيهم من العذاب، ويحصِّل لهم الثواب.
{184} "Je, hawafikirii? Huyu mwenzao" [Muhammad] - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani - "hana wazimu." Yaani, je, hawakutumia fikira zao na kuona ikiwa je ndani ya mwenzao huyu ambaye wanamjua wala hakifichiki kwao kitu chochote katika hali yake. Je yeye ni wazimu? Basi na watazame katika maadili yake, na mwongozo wake, na mwelekeo wake, na sifa zake, na watazame katika yale anayoyalingania, basi hawatapata ndani yake katika sifa isipokuwa za kamili zake, na rai isipokuwa ile aliyopiku kwayo walimwengu wote, na wala halinganii isipokuwa kwa kila heri, na wala hakatazi isipokuwa kila ovu! Je, huyu enyi wenye akili ndiye ana wazimu? Au yeye ndiye imamu mkuu, na mwenye nasaha wa wazi, na Mheshimiwa Mtukufu, na mpole, mwenye kurehemu? Na ndiyo maana akasema: "Yeye siyo isipokuwa ni mwonyaji aliye dhahiri." Yaani, anawalingania viumbe kwa yale yatakayowaepusha na adhabu, na yanawapatia thawabu.
#
{185} {أولم ينظروا في مَلَكوت السموات والأرض}: فإنهم إذا نظروا إليها؛ وجدوها أدلة دالة على توحيد ربِّها وعلى ما لَه من صفات الكمال. {و}: كذلك لينظروا إلى جميع {ما خَلَقَ الله من شيء}: فإن جميع أجزاء العالم يدلُّ أعظم دِلالة على علم الله وقدرته وحكمته وسَعَةِ رحمته وإحسانه ونفوذ مشيئته وغير ذلك من صفاته العظيمة الدالَّة على تفرُّده بالخلق والتدبير الموجبة لأن يكون هو المعبودَ المحمودَ المسبَّح الموحَّد المحبوب. وقوله: {وأنْ عسى أن يكونَ قد اقترب أجَلُهم}؛ أي: لينظروا في خصوص حالهم، وينظروا لأنفسهم قبل أن يقتربَ أجلُهم ويفجأهم الموتُ وهم في غفلةٍ معرضونَ؛ فلا يتمكَّنون حينئذٍ من استدراك الفارط. {فبأيِّ حديثٍ بعدَه يؤمنون}؛ أي: إذا لم يؤمنوا بهذا الكتاب الجليل؛ فبأيِّ حديث يؤمنون به؟! أبكتب الكذب والضلال؟! أم بحديث كل مفترٍ دجَّال؟!
{185} “Je, hawakutazama katika ufalme wa mbingu na ardhi.” Kwani wakiutazama, wataupata ni ushahidi juu ya upweke wa Mola wake Mlezi na juu ya yale aliyo nayo ya sifa kamilifu. "Na" vivyo hivyo, watazame vyote "alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika vitu." Kwa maana sehemu zote za ulimwengu zinaashiria kuashiria kukubwa zaidi juu ya elimu ya Mwenyezi Mungu, na uwezo wake, na hekima yake, na upana wa rehema Zake, na ihsani yake, na kutekelezeka kwa mapenzi yake, na yasiyokuwa hayo miongoni mwa sifa zake kubwa zinazoashiria upekee wake katika kuumba na kuendesha mambo, ambazo zinalazimu kwamba awe Yeye ndiye muabudiwa, Msifiwa, Mtakasiwa, apwekeshwaye, Mpendwa. Na kauli yake: "Na kwamba huenda muda wao umekwisha karibia?" Yaani, waangalie katika hali yao mahsusi, na wajitazame kabla ya kukaribia muda wao na mauti kuwapata ghafla hali ya kuwa wako katika kughafilika huku wamepeana mgongo. Basi wakawa wakati huo hawawezi kurekebisha walichokifanya kwa upungufu. "Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?" Yaani, ikiwa hawakiamini kitabu hiki kitukufu, basi ni hadithi gani wataimini? Je, wataviamini vitabu vya uongo na upotovu? Au maneno ya kila mzua uongo, mdanganyifu mkubwa?
#
{186} ولكن الضالَّ لا حيلة فيه ولا سبيل إلى هدايته، ولهذا قال تعالى: {مَن يُضْلِلِ الله فلا هاديَ له وَيَذَرُهم في طغيانِهِم يعمهونَ}؛ أي: متحيَّرون ، يتردَّدون لا يخرجون منه، ولا يهتدون إلى حقٍّ.
{186} Lakini mpotevu hakuna hila wala njia ya kumuongoa, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Yule Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana wa kumwongoa. Atawaacha hao katika upotofu wao wakitangatanga." Yaani, anabaki anachanganyikiwa, wakisitasita, hawatoki humo, wala hawaongoki kwenye haki.
: 187 - 188 #
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ رَبِّي لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ (187) قُلْ لَا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ وَلَوْ كُنْتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ (188)}.
187. Wanakuuliza kuhusu hiyo Saa (ya Qiyama) kusimama kwake ni lini? Sema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitawajia isipokuwa kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Elimu yake iko tu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wa watu hawajui. 188. Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu, ningalitenda mema sana, wala ubaya usingenigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa kaumu wanaoamini.
#
{187} يقول تعالى لرسوله محمد - صلى الله عليه وسلم -: {يسألونَك}؛ أي: المكذبون لك المتعنِّتون {عن الساعة أيان مُرْساها}؛ أي: متى وقتها التي تجيء به؟ ومتى تحِلُّ بالخلق؟ {قل إنَّما علمُها عند ربي}؛ أي: إنه تعالى المختصُّ بعلمها، {لا يجلِّيها لوقتها إلا هو}؛ أي: لا يظهرها لوقتها الذي قُدِّر أن تقوم فيه إلا هو. {ثَقُلَتْ في السموات والأرض}؛ أي: خفي علمها على أهل السماوات والأرض واشتدَّ أمرُها أيضاً عليهم فهم من الساعة مشفقون. {لا تأتيكم إلَّا بغتةً}؛ أي: فجأة من حيث لا يشعرون لم يستعدُّوا لها ولم يتهيؤوا لها. {يسألونك كأنَّك حَفِيٌّ عنها}؛ أي: هم حريصون على سؤالك عن الساعة كأنك مستحفٍ عن السؤال عنها، ولم يعلموا أنك لكمال علمك بربِّك وما ينفعُ السؤال عنه غير مبال بالسؤال [عنها، ولا حريص على ذلك، فَلِمَ لا يقتدون بك؟ ويكفون عن الاستحفاء عن هذا السؤال] الخالي من المصلحة المتعذِّر علمه؛ فإنَّه لا يعلمها نبيٌّ مرسلٌ ولا مَلَكٌ مقرَّب، وهي من الأمور التي أخفاها عن الخلق لكمال حكمته وسعة علمه. {قل إنَّما علمُها عند الله ولكنَّ أكثر الناس لا يعلمون}: فلذلك حرصوا على ما لا ينبغي الحرص عليه، وخصوصاً مثل حال هؤلاء الذين يتركون السؤال عن الأهمِّ ويَدَعون ما يجبُ عليهم من العلم، ثم يذهبون إلى ما لا سبيل لأحدٍ أن يدركه ولا هُم مطالبون بعلمه.
{187} Yeye Mtukufu anamwambia Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Wanakuuliza;" yaani, wale wanaokukadhibisha na wanaofanya ukaidi "kuhusu hiyo Saa (ya Qiyama) kusimama kwake ni lini?" Yaani, wakati wa kuja kwake ni lini? Na ni lini itawajia viumbe? "Sema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi." Yaani, Yeye Mtukufu ndiye peke yake ana elimu yake. "Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake isipokuwa Yeye;" yaani, hakuna atakayeidhihirisha kwa wakati wake ambao iliwekewa kusimama ndani yake isipokuwa Yeye. “Ni nzito katika mbingu na ardhi;” yaani, elimu yake imefichika kwa wakazi wa mbingu zote na ardhi, na pia jambo lake ni gumu sana kwao, basi wao wana wasiwasi kutokana na Saa. "Haitawajia isipokuwa kwa ghafla tu;" yaani, ghafla kutokea kule wasikojua, hawakujiandaa kwa ajili yake na hawakujitayarisha kwa ajili yake. "Wanakuuliza kama kwamba unaijua vyema;" yaani, wanawania kukuuliza juu ya Saa (ya Qiyama) kana kwamba wewe unawania sana kuuliza juu yake. Na hawakujua kwamba wewe kwa sababu ya elimu yako kamili ya Mola wako Mlezi na yanayonufaisha kuuliza juu yake, nawe hujali kuuliza [ juu yake, wala huna pupa juu ya hilo, basi kwa nini hawafuati mfano wako, na wakomeke kuwa na pupa ya kuuliza swali hili] ambalo halina masilahi, lisilowezekana kulijua? Kwani halijui Nabii yeyote aliyetumwa wala Malaika aliyekurubishwa. Nayo ni miongoni mwa mambo ambayo aliwaficha viumbe kwa sababu ya ukamilifu wa hekima yake na upana wa elimu yake. "Sema: Elimu yake iko tu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wa watu hawajui." Ndiyo maana wakawa na pupa sana na kile kisichofaa kuwa na pupa nacho, tena hasa mfano wa hali ya hawa ambao wanaacha kuuliza jambo muhimu zaidi, na wanaacha yale yanayowajibika juu yao miongoni mwa elimu, kisha wanayaendea yale ambayo hakuna njia kwa yeyote ya kuyafahamu wala hata hawakutakiwa kuyajua.
#
{188} {قل لا أملِكُ لنفسي نفعاً ولا ضرًّا}: فإني فقير مدبَّر، لا يأتيني خيرٌ إلا من الله، ولا يَدْفَعُ عني الشرَّ إلا هو، وليس لي من العلم إلا ما علمني الله تعالى. {ولو كنتُ أعلم الغيبَ لاستكثرتُ من الخير وما مسَّني السوءُ}؛ أي: لفعلت الأسباب التي أعلم أنها تنتج لي المصالح والمنافع، ولحذرتُ من كلِّ ما يفضي إلى سوءٍ ومكروهٍ؛ لعلمي بالأشياء قبل كونها، وعلمي بما تفضي إليه، ولكني لعدم علمي قد ينالني ما ينالني من السوء وقد يفوتني ما يفوتني من مصالح الدُّنيا ومنافعها؛ فهذا أدلُّ دليل على أني لا علم لي بالغيب. {إن أنا إلا نذيرٌ}: أنذر العقوبات الدينيَّة والدنيويَّة والأخرويَّة، وأبيِّن الأعمال المفضية إلى ذلك وأحذِّر منها. وبشير بالثواب العاجل والآجل، ببيان الأعمال الموصلة إليه والترغيب فيها، ولكن ليس كلُّ أحدٍ يقبل هذه البشارة والنذارة، وإنما ينتفع بذلك ويقبله المؤمنون. وهذه الآيات الكريمات مبيِّنة جهل من يقصد النبي - صلى الله عليه وسلم - ويدعوه لحصول نفع أو دفع ضرٍّ؛ فإنَّه ليس بيده شيء من الأمر، ولا ينفع مَنْ لم ينفعْه الله، ولا يدفعُ الضرَّ عمَّن لم يدفعْه الله عنه، ولا له من العلم إلاَّ ما علَّمه الله [تعالى]، وإنما ينفع مَنْ قَبِلَ ما أرسل به من البشارة والنذارة وعمل بذلك؛ فهذا نفعه عليه السلام الذي فاق نفع الآباء والأمهات والأخلاَّء والإخوان، بما حثَّ العباد على كلِّ خير، وحذَّرهم عن كلِّ شرٍّ، وبينه لهم غاية البيان والإيضاح.
{188} "Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara;" kwa hakika mimi ni mhitaji anayeendeshwa. Hainijii kheri isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, wala hapana anayenizuia uovu isipokuwa Yeye, nami sina katika elimu isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amenifundisha. "Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu, ningalitenda mema sana, wala ubaya usingenigusa. Yaani, ningefanya sababu ambazo ninajua kwamba zitanizalishia masilahi na manufaa na ningetahadhari kila kitu kinachofikisha kwenye ubaya na machukizo, kwa sababu ya kujua kwangu mambo kabla hayajakuwa, na kujua kwangu yale yanayoishia. Lakini kwa sababu ya kutokuwa kwangu na elimu, huenda mabaya yakanifika, na huenda yakanikosa yale yenye kunikosa miongoni mwa masilahi ya kidunia na manufaa yake, na hayo ni ushahidi wa kuashiria zaidi juu ya kwamba mimi sina elimu ya ghaibu. "Mimi si chochote ila ni mwonyaji" ninayeonya juu ya adhabu za kidini, na za kidunia na za kiakhera; na ninabainisha matendo yanayopelekea katika hayo na ninaonya dhidi yake. Na ni mbashiri wa malipo ya haraka na ya baadaye kwa kubainisha matendo yenye kufikisha huko, na kutia moyo katika hayo. Lakini si kila mmoja anayekubali bishara hii na maonyo haya, bali wananufaika nayo na wanayakubali Waumini tu. Na aya hizi tukufu zinabainisha ujinga wa wale wanaomkusudia Nabii - rehema na amani zimshukie - na kumwomba ili kupata manufaa au kuzuia madhara. Kwani yeye hakika hana katika mikono yake kitu katika jambo hilo, wala hamnufaishi ambaye Mwenyezi Mungu hakumnufaisha, wala hamzuii madhara ambaye Mwenyezi Mungu hakumzuia, wala hana katika elimu isipokuwa yale aliyomfunza Mwenyezi Mungu [Mtukufu]. Na badala yake, anamnufaisha yeyote aliyeyakubali yale aliyotumwa nayo miongoni mwa bishara na maonyo na akatenda kwayo. Basi haya ndiyo manufaa yake Yeye amani iwe juu yake ambayo yanazidi manufaa ya kina baba, na kina mama, na marafiki, na ndugu, kwa kuwa aliwahimiza waja kufanya heri yote, na akawaonya dhidi ya maovu yote, na akawabainishia hayo yote kubainisha na kuweka wazi kwa hali ya juu zaidi.
: 189 - 193 #
{هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ فَلَمَّا أَثْقَلَتْ دَعَوَا اللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ (189) فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا فَتَعَالَى اللَّهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ (190) أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ (191) وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَا أَنْفُسَهُمْ يَنْصُرُونَ (192) وَإِنْ تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَى لَا يَتَّبِعُوكُمْ سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ أَدَعَوْتُمُوهُمْ أَمْ أَنْتُمْ صَامِتُونَ (193)}.
189. Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili ajitulize kwake. Na alipomuingilia, akabeba mimba nyepesi, akitembea nao. Anapokuwa mjamzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Kama ukitupa mwana mwema hakika tutakuwa katika wanaoshukuru. 190. Basi alipowapa mwana mwema, wakamfanyia washirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa. Basi Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao. 191. Ati wanashirikisha kisichoumba kitu, hali ya kuwa wao wanaumbwa? 192. Wala hawawezi kuwanusuru wala wao wenyewe hawajinusuru. 193. Na mkiwaita kwenye uwongofu, hawawafuati. Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mkae kimya.
#
{189} أي: {هو الذي خلقكم}: أيها الرجال والنساء المنتشرون في الأرض على كثرتكم وتفرُّقكم، {من نفس واحدةٍ}: وهو آدمُ أبو البشر - صلى الله عليه وسلم -، {وجعل منها زوجَها}؛ أي: خلق من آدم زوجته حواء. لأجل أن يسكن إليها، لأنها إذا كانت منه؛ حصل بينهما من المناسبة والموافقة ما يقتضي سكونَ أحدهما إلى الآخر، فانقاد كلٌّ منهما إلى صاحبه بزمام الشهوة. {فلما تغشَّاها}؛ أي: تجلَّلها مجامعاً لها؛ قدَّر الباري أن يوجد من تلك الشهوة ـ وذلك الجماع ـ النسل، فحملتْ {حملاً خفيفاً}، وذلك في ابتداء الحمل لا تحس به الأنثى ولا يثقلها. {فلما} استمرَّت [به] و {أثقلت} به حين كبر في بطنها؛ فحينئذٍ صار في قلوبهما الشفقة على الولد وعلى خروجه حيًّا صحيحاً سالماً لا آفة فيه، فدَعَوَا {الله ربَّهما لئن آتَيْتنَا}: ولداً: {صالحاً}؛ أي: صالح الخلقة تامّها لا نقص فيه، {لنكوننَّ من الشاكرين}.
{189} Yaani, "Yeye ndiye aliyewaumba” enyi wanaume na wanawake mliotawanyika katika ardhi pamoja na wingi wenu na kutawanyika kwenu, "kutoka katika nafsi moja" naye ni Adam, baba wa watu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “na akafanya kutoka kwayo mwenzi wake.” Yaani, alimuumba kutoka kwa Adam mke wake, Hawa, ili atulie kwake kwa sababu kama Yeye (Hawa) ametokana naye, basi yatapatikana kati yao kufailiana, na mapatano ambayo yanalazimu mmoja wao kutulia kwa mwenzake, kwa hivyo kila mmoja wao akawa anawiana na mwenzake kwa mkanda wa matamanio. "Na alipomuingilia," yaani alipoingiana naye akimjaamii, Yeye Muumba akapitisha kwamba ipatikane kwa shahawa hiyo - na kujaamiiana huko – kizazi, kwa hivyo akabeba “mimba nyepesi.” Na hilo ni kwamba mwanzoni mwa ujauzito, mwanamke haihisi wala haimlemei. "Basi wakati" alipoendelea [nayo] na "ikamwiya nzito" wakati ilipokuwa kubwa katika tumbo lake, basi hapo ikaingia huruma katika nyoyo zao juu ya mtoto huyo, na juu ya kutoka kwake hai, sahihi, salama, asiyekuwa na balaa yoyote. Kwa hivyo wakamuomba "Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi, ukitupa:" Mwana: "mwema." Yaani, mwema wa maumbile, mkamilifu asiyekuwa na mapungufu ndani yake; "hakika tutakuwa katika wanaoshukuru."
#
{190} {فلما آتاهما صالحاً}: على وَفْق ما طَلَبَا وتمَّت عليهما النعمة فيه، {جعلا له شركاء فيما آتاهما}؛ أي: جعلا لله شركاء في ذلك الولد الذي انفرد الله بإيجاده والنعمة به وأقرَّ به أعين والديه، فعبَّداه لغير الله: إمّا أن يسمياه بعبد غير الله؛ كعبد الحارث وعبد العزَّى وعبد الكعبة ونحو ذلك، أو يشركا في الله في العبادة بعدما منَّ الله عليهما بما منَّ من النعم التي لا يحصيها أحدٌ من العباد، وهذا انتقالٌ من النوع إلى الجنس؛ فإنَّ أول الكلام في آدم وحواء، ثم انتقل [إلى] الكلام في الجنس، ولا شكَّ أنَّ هذا موجود في الذُّرية كثيراً؛ فلذلك قرَّرهم الله على بطلان الشرك، وأنهم في ذلك ظالمون أشدَّ الظلم، سواء كان الشرك في الأقوال أم في الأفعال؛ فإنَّ الخالق لهم من نفس واحدة، الذي خلق منها زوجها، وجعل لهم من أنفسهم أزواجاً، ثم جعل بينهم من المودَّة والرحمة ما يسكُنُ بعضُهم إلى بعض ويألفه ويلتذُّ به، ثم هداهم إلى ما به تحصل الشهوة واللَّذة والأولاد والنسل، ثم أوجد الذُّرية في بطون الأمهات وقتاً موقَّتاً تتشوَّف إليه نفوسهم ويدعون الله أن يخرِجَه سويًّا صحيحاً، فأتمَّ الله عليهم النعمة، وأنالهم مطلوبهم، أفلا يستحقُّ أن يعبدوه ولا يشركوا به في عبادته أحداً ويخلصوا له الدين؟!
{190} "Basi alipowapa mwana mwema" kulingana na yale waliyoyaomba, na ikawatimia neema katika huyo, "wakamfanyia washirika Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa.” Yaani, walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika katika mtoto huyo ambaye Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliyemuumba na kumfanya kuwa ni neema, na akayafurahisha kwaye macho ya wazazi wake, lakini wao wakamfanya kuwa mja wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Ima kwa kumwita kwa asiyekuwa mja wa Mwenyezi Mungu, kama vile Abdul-Harith, na Abdul-Uzza, Abdul-Kaaba, na kadhalika, au kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada baada ya kwamba Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa yale aliyowaneemesha, miongoni mwa neema mbalimbali ambazo hawezi kuzidhibiti hata mmoja katika waja. Na huku ni kusonga kutoka katika aina hadi kwa jinsi. Kwa maana, mwanzo wa mazungumzo unahusiana na Adamu na Hawa, kisha akahamia [kwenye] mazungumzo kuhusu jinsi, na hakuna shaka kwamba hili linapatikana katika dhuria kwa wingi. Na kwa sababu ya hilo, Mwenyezi Mungu akawafanya kukiri ubatili wa ushirikina, na kwamba wao katika hilo ni madhalimu dhuluma kubwa mno, sawa uwe ushirikina huo ni katika maneno au katika vitendo. Kwa maana yule aliyewaumba kutokana na nafsi moja, ambaye alimuumbia mwenza wake kutokana nayo, na akawafanyia wenzi kutokana na nafsi zao wenyewe, kisha akaweka baina yao mapenzi na rehema ambayo wanapata kutulia wenyewe katika wenyewe, na anamzoea, na kustareheka naye. Kisha akawaongoa kwenye yale ambayo kwayo hupatikana matamanio, na starehe, na dhuria, na kizazi. Kisha akakiumba kizazi katika matumbo ya akina mama, kwa muda maalumu ambao nafsi zao zinakuwa na uchu nacho, na wanamwomba Mwenyezi Mungu kwamba akitoe hali ya kuwa kiko sawasawa, sahihi. Basi Mwenyezi Mungu anawatimizia neema hiyo, na akawapa walichokitaka. Basi je, yeye hastahiki kwamba wamuabudu wala wasimshirikishe na yeyote katika ibada yake, na wamfanyie Yeye tu Dini yao?
#
{191 - 192} ولكنَّ الأمر جاء على العكس، فأشركوا بالله {مالا يَخْلُقُ شيئاً وهم يُخْلَقونَ. ولا يستطيعون لهم}؛ أي: لعابديها {نصراً ولا أنفسَهم ينصرونَ}: فإذا كانت لا تخلق شيئاً ولا مثقال ذرَّة، بل هي مخلوقة، ولا تستطيع أن تدفع المكروه عن من يعبُدُها ولا عن أنفسها؛ فكيف تُتَّخذ مع الله آلهة؟! إنْ هذا إلا أظلم الظلم وأسفه السفه.
{191 - 192} Lakini jambo likawa kinyume, kwa hivyo wakamshirikisha Mwenyezi Mungu "kisichoumba kitu, hali ya kuwa wao wanaoumbwa. Wala hawawezi kuwanusuru;" yaani, wale wanaowaabudu "wala wao wenyewe hawajinusuru." Basi ikiwa haviumbi kitu hata uzito wa chembe, bali hivyo vimeumbwa, wala haviwezi kuzuia machukizo dhidi ya yule anayeviabudu, wala hata hivyo vyenyewe, basi vipi vinafanywa miungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Haya si chochote isipokuwa ni dhuluma kubwa zaidi ya dhuluma zote, na upumbavu mkubwa zaidi ya upumbavu wote.
#
{193} وإن تدعوا أيُّها المشركون، هذه الأصنام التي عبدتم من دون الله {إلى الهدى لا يتَّبعوكم سواءٌ عليكم أدعوتُموهم أم أنتم صامتونَ}: فصار الإنسانُ أحسنَ حالةً منها؛ لأنَّها لا تسمع ولا تبصِرُ ولا تَهْدي ولا تُهْدَى، وكل هذا إذا تصوَّره اللبيب العاقل تصوراً مجرداً؛ جزم ببطلان إلهيتها وسفاهة مَنْ عبدها.
{193} Na mkiwaomba enyi washirikina masanamu haya ambayo mliyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu "kwenye uwongofu hawawafuati. Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mkae kimya." Basi mwanadamu akawa kwenye hali bora zaidi kuwaliko wao. Kwa sababu hayasikii, wala hayaoni, wala hayaongoi, wala hayaongolewi; na yote haya ikiwa mwerevu, mwenye akili atayawaza kwa njia ya kufikirika tu, basi atakuwa na uhakika juu ya ubatili wa uungu wake na upumbavu wa mwenye kuyaabudu.
: 194 - 196 #
{إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (194) أَلَهُمْ أَرْجُلٌ يَمْشُونَ بِهَا أَمْ لَهُمْ أَيْدٍ يَبْطِشُونَ بِهَا أَمْ لَهُمْ أَعْيُنٌ يُبْصِرُونَ بِهَا أَمْ لَهُمْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا قُلِ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنْظِرُونِ (195) إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتَابَ وَهُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ (196)}.
194. Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi. Basi waombeni, nao wawaitikie ikiwa nyinyi ni wakweli. 195. Je, wao wanayo miguu wanayotembea kwayo? Au wanayo mikono wanayokamata kwa nguvu kwayo? Au wanayo macho wanayoona kwayo? Au wanayo wanayosikia kwayo? Sema: Waiteni washirika wenu hao, kisha nifanyieni mimi njama, na wala msinipe muhula. 196. Hakika Mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu ambaye aliteremsha Kitabu. Naye ndiye anayewalinda walio wema.
#
{194} وهذا من نوع التحدي للمشركين العابدين للأوثان؛ يقول تعالى: {إنَّ الذين تَدْعون من دونِ الله عبادٌ أمثالكم}؛ أي: لا فرق بينكم وبينهم؛ فكلُّكم عبيدٌ لله مملوكون؛ فإن كنتم كما تزعمون صادقين في أنها تستحقُّ من العبادة شيئاً؛ {فادْعوهم فليستجيبوا لكم}: فإن استجابوا لكم وحصَّلوا مطلوبكم، وإلاَّ؛ تبيَّن أنكم كاذبون في هذه الدعوى مفترون على الله أعظم الفرية.
{194} Na hii ni aina ya changamoto kwa washirikina wanaowaabudu masanamu, Yeye Mtukufu anasema: "Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi." Yaani, hakuna tofauti baina yenu na wao. Nyinyi nyote ni waja wa Mwenyezi Mungu mnaomilikiwa. Kwa hivyo ikiwa nyinyi ni wakweli kama mnavyodai kwamba hao wanastahiki kitu katika ibada, "Basi waombeni, nao wawaitikie ikiwa nyinyi." Na wakiwaitikia na wakawatelekelezea mahitaji yenu, na kama sivyo, itabainika kwamba nyinyi ni waongo katika dai hili, mnamzulia Mwenyezi Mungu uongo mkubwa zaidi.
#
{195} وهذا لا يحتاج إلى تبيين فيه ؛ فإنَّكم إذا نظرتُم إليها؛ وجدتُم صورتها دالةً على أنه ليس لديها من النفع شيء، فليس لها أرجلٌ تمشي بها، ولا أيدٍ تبطش بها، ولا أعينٌ تبصر بها، ولا آذان تسمع بها؛ فهي عادمةٌ لجميع الآلات والقوى الموجودة في الإنسان؛ فإذا كانت لا تجيبكم إذا دعوتموها؛ فهي عبادٌ أمثالكم، بل أنتم أكمل منها وأقوى على كثير من الأشياء؛ فلأيِّ شيء عبدتموها؟! {قل ادعوا شركاءكم ثم كيدونِ فلا تُنظِرونِ}؛ أي: اجتمعوا أنتم وشركاؤكم على إيقاع السوء والمكروه بي من غير إمهال ولا إنظار فإنكم غير بالغين لشيء من المكروه بي.
{195} Na hili halihitaji kufafanuliwa. Kwani mkilitazama, mtaikuta sura yake ikionyesha kuwa haina manufaa yoyote. Kwa maana, haina miguu ya kutembea kwayo, wala haina mikono ya kukamata kwa nguvu kwayo, wala macho ya kuona kwayo, wala masikio ya kusikia kwayo. Basi haina kila ala na uwezo vinavyopatikana katika mwanadamu. Kwa hivyo ikiwa haiwajibu mnapoiomba, basi hayo ni waja mfano wenu. Bali nyinyi ni wakamilifu zaidi kuliko wao na wenye nguvu zaidi katika mengi ya mambo. Basi ni kwa nini mliiabudu? "Sema: Waiteni washirika wenu, kisha nifanyieni mimi njama, na wala msinipe muhula." Yaani, kusanyikeni nyinyi na washirika wenu juu ya kunifikishia mabaya na machukizo bila ya kupeana muhula wowote wala kuchelewesha, kwani hamwezi kunifikishia ubaya wowote.
#
{196} لأنَّ وَلِيِّيَ اللهُ الذي يتولاَّني فيجلب لي المنافع ويدفع عني المضار. {الذي نزَّل الكتابَ}: الذي فيه الهدى والشفاء والنور، وهو من تولِّيه وتربيته لعباده الخاصة الدينيَّة. {وهو يتولَّى الصالحين}: الذين صلحت نيَّاتهم وأعمالهم وأقوالهم؛ كما قال تعالى: {اللهُ وليُّ الذين آمنوا يخرِجُهم من الظُّلمات إلى النور}؛ فالمؤمنون الصالحون لمَّا تولَّوا ربَّهم بالإيمان والتقوى ولم يتولَّوا غيره ممَّن لا ينفع ولا يضرُّ؛ تولاَّهم الله ولطف بهم وأعانهم على ما فيه الخير والمصلحة لهم في دينهم ودنياهم ودفع عنهم بإيمانهم كلَّ مكروه؛ كما قال تعالى: {إنَّ الله يدافِعُ عن الذين آمنوا}.
{196} Kwa sababu mlinzi wangu ni Mwenyezi Mungu, ambaye ananilinda, kwa hivyo ananiletea manufaa na kunilinda kutokana na madhara; "ambaye aliteremsha Kitabu" ambacho ndani yake kuna uwongofu, na uponyaji, na nuru, nalo ni katika ulinzi wake na ulezi wake maalum wa kidini kwa waja wake. “Naye ndiye anayewalinda walio wema;” ambao nia zao ni njema, na vitendo vyao, na maneno yao. Kama alivyosema Yeye Mtukufu "Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa walioamini. Huwatoa katika giza mbalimbali hadi katika nuru.” Kwa hivyo, Waumini wema walipomfanya Mola wao Mlezi kuwa mlinzi kwa Imani na uchamungu, na wala hawakumfanya mlinzi yeyote asiyekuwa yeye miongoni mwa wale wasiofaa wala kudhuru, Mwenyezi Mungu akawa mlinzi wao na akawafanyia upole, na akawasaidia katika yale yaliyo na heri na masilahi yao katika dini yao na dunia yao, na akawazuia kwa imani yao machukizo yote. Kama alivyosema yeye Mtukufu "Hakika Mwenyezi Mungu huwatetea wale walioamini."
: 197 - 198 #
{وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنْفُسَهُمْ يَنْصُرُونَ (197) وَإِنْ تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَى لَا يَسْمَعُوا وَتَرَاهُمْ يَنْظُرُونَ إِلَيْكَ وَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ (198)}.
197. Na wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi hawawezi kuwanusuru, wala hawajinusuru wao wenyewe. 198. Na mkiwaita kwenye uwongofu, hawasikii. Na utawaona wanakutazama hali ya kuwa hawaoni.
#
{197 - 198} وهذا أيضاً في بيان عدم استحقاق هذه الأصنام التي يعبُدونها من دون الله شيئاً من العبادة؛ لأنها ليس لها استطاعةٌ ولا اقتدارٌ في نصر أنفسهم ولا في نصر عابديها، وليس لها قوة العقل والاستجابة؛ فلو دعوتَها إلى الهدى؛ لم تهتدِ، وهي صورٌ لا حياة فيها، فتراهم ينظرون إليك وهم لا يبصرونَ حقيقةً؛ لأنهم صوَّروها على صور الحيوانات من الآدميين أو غيرهم، وجعلوا لها أبصاراً وأعضاءً؛ فإذا رأيتها؛ قلت: هذه حيَّة؛ فإذا تأملتها؛ عرفت أنها جمادات لا حراك بها ولا حياة؛ فبأيِّ رأي اتَّخذها المشركون آلهةً مع الله؟! ولأيِّ مصلحة أو نفع عكفوا عندها وتقرَّبوا لها بأنواع العبادات؟! فإذا عُرِفَ هذا؛ عُرِفَ أن المشركين وآلهتهم التي عبدوها ولو اجتمعوا وأرادوا أن يكيدوا من تولاَّه فاطر السماوات والأرض متولِّي أحوال عباده الصالحين؛ لم يقدروا على كيده بمثقال ذرَّةٍ من الشرِّ؛ لكمال عجزهم وعجزها وكمال قوَّة الله واقتداره وقوَّة من احتمى بجلاله وتوكَّل عليه، وقيل: إنَّ معنى قوله: {وتَراهُم ينظُرونَ إليكَ وهم لا يبصِرونَ}: إنَّ الضمير يعود إلى المشركين المكذِّبين لرسول الله - صلى الله عليه وسلم -، فتحسبهم ينظُرون إليك يا رسول الله نظر اعتبارٍ يتبيَّن به الصادق من الكاذب، ولكنهم لا يبصرون حقيقتك وما يتوسَّمه المتوسِّمون فيك من الجمال والكمال والصدق.
{197 - 198} Na hii pia katika kubainisha kutostahiki kuabudiwa kwa masanamu haya ambayo yanaabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu chochote katika ibada. Kwa sababu hayana uwezo wala nguvu za kujinusuru yenyewe wala kuwanusuru wale wanaoyaabudu; wala hayana nguvu wa kufikiri na kuitikia. Kwa hivyo ukiyaita kwenye uwongofu, hayaongoki. Nayo ni sura tu zisizokuwa na uhai ndani yake. Kwa hivyo utawaona wakikutazama hali ya kuwa hawaoni kiuhakika. Kwa sababu waliyapa sura kama sura za wanyama miongoni mwa wanadamu au vinginevyo, na wakayapa macho na viungo. Kwa hivyo ukiyaona, utasema: Hili liko hao. Lakini ukilitafakari, utajua kuwa ni vitu visivyokuwa na uhai, visivyo na harakati yoyote wala uhai. Basi ni kwa rai gani washirikina waliyafanya kuwa miungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Na je, ni kwa masilahi gani au manufaa gani waliyodumu hapo kwayo na wakajikurubisha kwayo kwa aina mbalimbali za ibada? Kwa hivyo likijulikana hili, inajulikana kuwa washirikina na miungu yao ambayo waliiabudu, hata ikiwa watakusanyika na wakataka kumfanyia njama yule ambaye amelindwa na Muumba wa mbingu na ardhi anayesimamia hali za waja wake wema; basi hawawezi kumfanyia njama hiyo hata uzito wa chembe ya uovu, kwa sababu ya ukamilifu wa kutoweza kwao na kutoweza kwa masanamu hayo, na ukamilifu wa nguvu za Mwenyezi Mungu na uwezo wake, na uwezo wa mwenye kutafuta hifadhi ya utukufu Wake na akamtegemea Yeye. Na ilisemwa kuwa maana ya kauli yake: "Na utawaona wanakutazama hali ya kuwa hawaoni" ni kuwa inamaanisha washirikina hao wanaomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, – basi utadhani wanakutazama ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kutazama kwa mazingatio kinachobainika kwa huko cha kweli na cha uongo, lakini wao hawauoni uhakika wako, na ule uzuri, na ukamilifu, na ukweli ambao wale wanaokutafakari wanatafakari ndani yako.
: 199 #
{خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ (199)}.
199. Chukua yaliyo mepesi (katika matendo yao), na amrisha mema, na jitenge na majahili.
#
{199} هذه الآية جامعة لِحُسْنِ الخلق مع الناس وما ينبغي في معاملتهم: فالذي ينبغي أن يعامَلَ به الناس: أن يأخذَ العفوَ؛ أي: ما سمحتْ به أنفسُهم وما سَهُلَ عليهم من الأعمال والأخلاق؛ فلا يكلِّفهم ما لا تسمح به طبائعهم، بل يشكُر من كلِّ أحدٍ ما قابله به من قول وفعل جميل أو ما هو دونَ ذلك، ويتجاوزُ عن تقصيرِهم ويغضُّ طرفه عن نقصهم ولا يتكبَّر على الصغير لصغره ولا ناقص العقل لنقصه ولا الفقير لفقره، بل يعامل الجميع باللُّطف والمقابلة بما تقتضيه الحال وتنشرح له صدورهم. {وأمُرْ بالعُرْفِ}؛ أي: بكل قول حسن وفعل جميل وخلق كامل للقريب والبعيد؛ فاجعل ما يأتي إلى الناس منك إما تعليم علم أو حث على خير من صلة رحم أو برِّ والدين أو إصلاح بين الناس أو نصيحة نافعة أو رأي مصيب أو معاونة على برٍّ وتقوى أو زجر عن قبيح أو إرشاد إلى تحصيل مصلحة دينيَّة أو دنيويَّة. ولما كان لا بدَّ من أذيَّة الجاهل؛ أمر الله تعالى أن يقابَلَ الجاهل بالإعراض عنه وعدم مقابلته بجهله؛ فمن آذاك بقوله أو فعله؛ لا تؤذه، ومن حَرَمَكَ لا تحرِمْه، ومن قطعك فَصِلْه، ومن ظلمك فاعدل فيه.
{199} Aya hii inajumuisha tabia nzuri na watu na yale ambayo mtu anapaswa kuwatendea. Kwa kuwa kile ambacho mtu anapaswa kuwatendea watu ni kuchukua chepesi, yaani yale nafsi zao zinaruhusu kuyafanya na yale yaliyo rahisi kwao miongoni mwa matendo na maadili. Basi asiwatwike yale ambayo maumbile yao hayaruhusu. Bali amshukuru kila mtu kwa yale wanayowakabili nayo miongoni mwa maneno na matendo mazuri au yaliyo chini ya hayo. Na aachilie mbali kuzembea kwao na ayafumbie macho mapungufu yao, wala asimfanyie kiburi mdogo kwa sababu ya udogo wake, wala mwenye upungufu wa akili kwa sababu ya upungufu wake, wala masikini kwa sababu ya umasikini wake. Bali aamiliane nao wote kwa upole na kuwakabili na yale yanayohitajiwa na hali zao na wamkunjulie vifua vyao. "Na amrisha mema," yaani, kwa kila neno jema, na tendo zuri, na tabia kamilifu kwa walio karibu na walio mbali. Basi yafanye yale yanayowajia watu kutoka kwako yawe ima ni kufundisha elimu, au kuhimiza juu ya heri kama vile kuunga ukoo, au kuwatii wazazi, au kusuluhisha baina ya watu, au ushauri wenye manufaa, au maoni sahihi, au usaidizi katika wema na uchamungu, au kukemea maovu, au kuelekeza katika kuyafikia masilahi ya kidini au ya kidunia. Kwa kuwa ni lazima kuwepo udhia kutoka kwa asiyejua, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamuru kwamba asiyejua akabiliwe na kujitenga naye na kutomkabili kwa kutojua kwake. Kwa hivyo atakayekuudhi kwa kauli yake au kitendo chake, usimuudhi; na mwenye kukunyima, usimnyime. Na mwenye kukukata, basi muunge. Na mwenye kukudhulumu, basi mtendee uadilifu.
Na ama kile anachopaswa mja kuamiliana na mashetani wa kijini; basi Yeye Mtukufu akasema:
: 200 - 202 #
{وَإِمَّا يَنْزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (200) إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُمْ مُبْصِرُونَ (201) وَإِخْوَانُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِي الْغَيِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ (202)}.
200. Na kama uchochezi kutoka kwa Shetani utakuchochea, basi tafuta ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi mzuri, Mwenye kujua vyema. 201. Hakika wale wamchao Mungu, zinapowagusa pepesi kutoka kwa Shetani, mara huzindukana na hapo huwa wenye kuiona haki. 202. Na ndugu zao wanawavuta kwenye upotovu, kisha wao hawaachi.
#
{200} أي: أيَّ وقت وفي أيِّ حال، {ينزغنَّك من الشيطان نزغٌ}؛ أي: تحس منه بوسوسةٍ وتثبيطٍ عن الخير أو حثٍّ على الشرِّ وإيعازٍ إليه، {فاستعذْ بالله}؛ أي: التجئ واعتصم بالله واحتم بحماه. فإنَّه سميعٌ لما تقول، {عليمٌ}: بنيَّتك وضعفك وقوة التجائك له فسيحميك من فتنته ويقيك من وسوسته؛ كما قال تعالى: {قل أعوذُ بربِّ الناس ... } إلى آخر السورة.
{200} Yaani, wakati wowote na katika hali yoyote ile, "kama uchochezi kutoka kwa Shetani utakuchochea." Yaani, utahisi wasiwasi kutoka kwake, kuna kukuzembesha dhidi ya heri au kukuhimiza juu ya uovu na kuelekea huko, “basi tafuta ulinzi wa Mwenyezi Mungu.” Yaani, mkimbilie na ushikamane na Mwenyezi Mungu, na utafute ulinzi katika hifadhi yake. Kwani Yeye hakika ni Mwenye kuyasikia vyema yale unayoyasema, "ni Mwenye kujua vyema" makusudio yako, na udhaifu wako, na nguvu ya kukimbilia kwako kwake. Basi atakulinda kutokaka na fitina yake Shetani, na atakukinga na wasiwasi wake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu: "Sema, ninajikinga kwa Mola Mlezi wa watu..." mpaka mwisho wa sura hii.
#
{201} ولما كان العبدُ لا بدَّ أن يغفل وينال منه الشيطان الذي لا يزال مرابطاً ينتظر غرَّته وغفلته؛ ذكر تعالى علامة المتَّقين من الغاوين، وأن المتَّقي إذا أحسَّ بذنب ومسَّه طائفٌ من الشيطان فأذنب بفعل محرَّم أو ترك واجبٍ؛ تذكَّر من أي باب أُتِيَ ومن أيِّ مدخل دخل الشيطان عليه، وتذكَّر ما أوجب الله عليه وما عليه من لوازم الإيمان، فأبصر، واستغفر الله تعالى، واستدرك ما فرط منه بالتوبة النصوح والحسنات الكثيرة، فرد شيطانه خاسئاً حسيراً؛ قد أفسد عليه كلَّ ما أدركه منه.
{201} Na kwa vile mja hana budi kughafilika na kushawishiwa na Shetani, ambaye hajaacha kuvizia na kusubiri kughafilika kwake, Yeye Mtukufu akataja alama ya wachamungu kutokana na wale waliopotea, na kwamba mchamungu anapoihisi dhambi na akaguswa na pepesi kutoka kwa Shetani. Basi akafanya dhambi kwa kufanya kitendo kilichoharamishwa au kuacha wajibu, anakumbuka ni kutokea mlango gani alijiwa, na ni kutokea kiingilio gani alimwingilia Shetani; na anakumbuka yale ambayo Mwenyezi Mungu amemwajibishia na yale yaliyo juu yake yanayotakiwa na imani. Kwa hivyo akapata kuona, na akamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kumsitiria dhambi, na akalipa yale aliyozembea ndani yake kwa toba ya kweli na matendo mazuri mengi. Kwa hivyo akamrudhisha Shetani wake huku ameambulia patupu amechoka, na huku ameshamharibia kila kitu alichofanya ndani yake.
#
{202} وأما إخوان الشياطين وأولياؤهم؛ فإنهم إذا وقعوا في الذُّنوب لا يزالون يمدُّونهم في الغيِّ ذنباً بعد ذنبٍ، ولا يقصرون عن ذلك؛ فالشياطين لا تقصر عنهم بالإغواء؛ لأنها طمعت فيهم حين رأتهم سلسي القياد لها وهم لا يقصرون عن فعل الشرِّ.
{202} Na ama ndugu za mashetani na marafiki zao, wao wakianguka katika madhambi, hawaachi kuendelea kuwavuta katika ukengeufu kwa madhambi baada ya madhambi, na hawaachi kufanya hivyo. Kwa hivyo mashetani hawazembei katika kuwapoteza. Kwa sababu waliwatamani wakati walipowaona wakijinyenyekeza kwao kwa urahisi na hali hawazembei katika kufanya uovu.
: 203 #
{وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِمْ بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَى إِلَيَّ مِنْ رَبِّي هَذَا بَصَائِرُ مِنْ رَبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ (203)}.
203. Na usipowajia na Ishara, wanasema: Kwa nini hukuibuni? Sema: hakika mimi ninafuata tu yale yanayofunuliwa kwangu kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Hii (Qur'ani) ni hoja zinazotoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema kwa kaumu wanaoamini.
#
{203} أي: لا يزال هؤلاء المكذِّبون لك في تعنُّت وعناد، ولو جاءتهم الآيات الدالَّة على الهدى والرشاد؛ فإذا جئتهم بشيء من الآيات الدالَّة على صدقك؛ لم ينقادوا. {وإذا لم تأتهم بآيةٍ}: من آيات الاقتراح التي يعيِّنونها، {قالوا لولا اجتبيتها}؛ أي: هلاَّ اخترت الآية فصارت الآية الفلانية أو المعجزة الفلانية، كأنك أنت المنزِّل للآيات المدبِّر لجميع المخلوقات، ولم يعلموا أنه ليس لك من الأمر شيء، أو [أنّ المعنى]: لولا اخترعتها من نفسك، {قل إنَّما أتَّبع ما يوحى إليَّ من ربي}: فأنا عبدٌ مُتَّبِعٌ مدبَّر، والله تعالى هو الذي ينزل الآيات ويرسلها على حسب ما اقتضاه حمده، وَطَلبَتْهُ حكمته البالغة؛ فإن أردتم آية لا تضمحلُّ على تعاقب الأوقات وحجة لا تبطل في جميع الآنات؛ فهذا: القرآن العظيم والذكر الحكيم. {بصائرُ من ربِّكم}: يستبصر به في جميع المطالب الإلهيَّة والمقاصد الإنسانيَّة، وهو الدليل والمدلول؛ فمن تفكَّر فيه وتدبَّره؛ علم أنه تنزيلٌ من حكيم حميدٍ، لا يأتيه الباطل من بين يديه ولا من خلفه، وبه قامت الحجَّة على كلِّ من بلغه، ولكن أكثر الناس لا يؤمنون، وإلاَّ؛ فمن آمن؛ فهو {هدىً} له من الضلال {ورحمةٌ} له من الشقاء؛ فالمؤمن مهتدٍ بالقرآن، متَّبع له، سعيدٌ في دنياه وأخراه، وأما من لم يؤمنْ به؛ فإنه ضالٌّ شقيٌّ في الدنيا والآخرة.
{203} Yaani, hawaachi hawa wanaokukadhibisha kuwa katika ukaidi, hata wakijiwa ishara zinazoonyesha kwenye uwongofu na unyoofu. Kwa hivyo ukiwajia na kitu miongoni mwa ishara zinazoashiria kwenye ukweli wako, hawafuati. "Na usipowajia na Ishara" miongoni mwa ishara za kupendekezwa kwao ambazo wanazitaka wao, "wanasema: Kwa nini hukuileta?" Yaani, kwa nini hukuichagua ishara basi ikawa ishara fulani au muujiza fulani ni kana kwamba wewe ndiwe uteremshaye ishara, muendeshaji wa viumbe vyote, na hawakujua kuwa hauna chochote katika jambo hilo, au [maana yake ni] lau ungeibuni wewe mwenyewe tu. "Sema: hakika mimi ninafuata tu yale yanayofunuliwa kwangu kutoka kwa Mola wangu Mlezi." Mimi ni mja ninayefuata, ninayeendeshwa, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ambaye anaziteremsha ishara na anazituma kulingana na inavyohitaji sifa yake na ikataka hekima yake kubwa mno. Na kama mnataka ishara isiyofifia kwa kufuatana kwa nyakati, na hoja isiyobatilika katika nyakati zote, basi Qur-ani hii Tukufu na ukumbusho wenye hekima kubwa ni "hoja zinazotoka kwa Mola wenu Mlezi" inakuwa hoja katika kila matakwa ya kimungu na malengo ya kibinadamu. Nayo ni ushahidi na yenyewe inaeleza inachothibitisha. Kwa hivyo, anayeitafakari , na akizingatia, atajua kuwa uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima kubwa, Msifiwa zaidi, haijiwi na batili kwa mbele yake wala kwa nyuma yake, na kwayo hoja ilisimama juu ya kila mwenye kumfikia, lakini wengi wa watu hawaamini. Na vinginevyo, mwenye kuamini, basi hiyo ni "uwongofu" kwake kutokana na upotofu, na ni “rehema” kwake kutokana na taabu. Kwa hivyo Muumini anaongoka kwa Qur-ani, anaifuata, ana furaha katika dunia yake na Akhera yake. Na Ama asiyeiamini, yeye ni mpotevu, mwenye taabu katika dunia na akhera.
: 204 #
{وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنْصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (204)}.
204. Na inaposomwa Qur-ani, basi isikilizeni na mnyamaze ili mrehemewe.
#
{204} هذا الأمر عامٌّ في كلِّ من سمع كتاب الله يتلى؛ فإنه مأمور بالاستماع له والإنصات، والفرق بين الاستماع والإنصات أن الإنصات في الظاهر بترك التحدُّث أو الاشتغال بما يشغل عن استماعه، وأما الاستماع له؛ فهو أن يُلْقِيَ سَمْعَه ويحضِرَ قلبَه ويتدبَّر ما يستمع؛ فإنَّ من لازم على هذين الأمرين حين يُتلى كتاب الله؛ فإنه ينال خيراً كثيراً وعلماً غزيراً وإيماناً مستمرًّا متجدداً وهدىً متزايداً وبصيرةً في دينه، ولهذا رتَّب الله حصول الرحمة عليهما، فدلَّ ذلك على أن مَنْ تُلي عليه الكتاب فلم يستمع له وينصت أنه محروم الحظ من الرحمة، قد فاته خيرٌ كثير. ومن أوكدِ ما يؤمر [به] مستمع القرآن أن يستمعَ له وينصتَ في الصلاة الجهرية إذا قرأ إمامُهُ؛ فإنَّه مأمورٌ بالإنصات حتى إنَّ أكثر العلماء يقولون: إنَّ اشتغاله بالإنصات أولى من قراءته الفاتحة وغيرها.
{204} Jambo hili ni la jumla kwa kila anayekisikia Kitabu cha Mwenyezi Mungu kikisomwa. Ameamrishwa kukisikiliza na kunyamaza. Na tofauti kati ya kusikiliza na kunyamaza ni kwamba kunyamaza kunakuwa katika dhahiri kwa kuacha kuzungumza au kujishughulisha na yale yanayomshughulisha dhidi ya kuisikiliza. Na ama kuisikiliza, hilo linamaanisha kuipa kusikiliza kwake, na kuuweka hapo moyo wake, na kuzingatia yale anayosikiliza. Kwani mwenye kudumu katika mambo haya mawili kinaposomwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, yeye hakika atapata heri nyingi, na elimu nyingi, na imani yenye kuendelea mpya, na uwongofu wenye kuongezeka, na utambuzi katika dini yake, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu ameweka kupata rehema juu ya mawili hayo, basi hilo likaashiria kwamba mwenye kusomewa Kitabu hiki lakini hakukisikiliza na kunyamaza basi yeye hakika amenyimwa fungu katika rehema, na amekosa heri nyingi. Na katika mambo yenye msisitizo mkubwa anayoamrishwa [hayo] msikilizaji wa Qur-ani ni kwamba akisikilize na kunyamaza katika swala za kusoma kwa sauti kubwa imamu wake anaposoma. Kwa kuwa ameamrishwa kunyamaza, mpaka wengi wa wanachuoni wanasema kuwa kushughulika kwake na kunyamaza ni bora zaidi kuliko kusoma kwake Al-Fatiha na sura zingine zisizokuwa hiyo.
: 205 - 206 #
{وَاذْكُرْ رَبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُنْ مِنَ الْغَافِلِينَ (205) إِنَّ الَّذِينَ عِنْدَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ (206)}.
205. Na mkumbuke Mola wako Mlezi katika nafsi yako kwa unyenyekevu na hofu, na bila ya kuinua sauti juu kwa kauli, asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni wa walioghafilika. 206. Hakika wale walio kwa Mola wako Mlezi hawajivuni wakaacha kumuabdu, na wanamtakasa, na wanamsujudia Yeye.
#
{205} الذكر لله تعالى يكون بالقلب ويكون باللسان ويكون بهما وهو أكمل أنواع الذكر وأحواله، فأمر الله عبده ورسوله محمداً أصلاً وغيره تبعاً بذكر ربِّه في نفسه؛ أي: مخلصاً خالياً، {تضرُّعاً}؛ أي: متضرعاً بلسانك مكرِّراً لأنواع الذكر، {وخِيفةً}: في قلبك؛ بأن تكون خائفاً من الله، وَجِلَ القلب منه خوفاً أن يكون عملك غير مقبول، وعلامة الخوف أن يسعى ويجتهد في تكميل العمل وإصلاحه والنصح به. {ودون الجهر من القول} ـ؛ أي: كن متوسطاً، لا تجهرْ بصلاتك ولا تخافِتْ بها وابتغ بين ذلك سبيلاً ـ {بالغدو}: أول النهار، {والآصال}: آخره، وهذان الوقتان [لذكرِ اللهِ] فيهما مزيَّةٌ وفضيلةٌ على غيرهما. {ولا تكن من الغافلينَ}: الذين نَسُوا الله فأنساهم أنفُسَهم؛ فإنَّهم حُرِموا خير الدنيا والآخرة، وأعرضوا عمَّن كلُّ السعادة والفوز في ذكره وعبوديَّته، وأقبلوا على مَن كلُّ الشقاوة والخيبة في الاشتغال به. وهذه من الآداب التي ينبغي للعبد أن يراعِيَها حقَّ رعايتها، وهي الإكثار من ذكر الله آناء الليل والنهار، خصوصاً طرفي النهار، مخلصاً خاشعاً متضرِّعاً متذللاً ساكناً متواطئاً عليه قلبه ولسانه بأدبٍ ووَقارٍ وإقبال على الدُّعاء والذِّكر وإحضارٍ له بقلبه وعدم غفلة؛ فإنَّ الله لا يستجيبُ دعاءً من قلبٍ غافلٍ لاهٍ.
{205} Kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kunakuwa kwa moyo, na kunakuwa kwa ulimi, na kunakuwa kwa vyote viwili, na huku ndiko aina kamili zaidi ya kukumbuka na hali zake. Basi Mwenyezi Mungu akamwamrisha mja wake na Mtume wake Muhammad mwanzo na wengineo kwa kumfuata kumkumbuka Mola wake Mlezi katika nafsi yake. Yaani, kwa ikhlasi na akiwa peke yake, "kwa unyenyekevu;" yaani, kwa kunyenyekea kwa ulimi wako, na kwa kurudia aina za kukumbuka, "na hofu" katika moyo wako, kwa kuwa na hofu juu ya Mwenyezi Mungu, mwenye moyo wa hofu juu yake, akihofu kwamba matendo yake yanaweza kuwa hayakukubaliwa. Na alama ya hofu ni kwamba afanye bidii na kujitahidi katika kukamilisha matendo, na kuyafanya yatengenee, na kushauri juu yake. "Na bila ya kuinua sauti juu kwa kauli," yaani, kuwa wastani, usiswali kwa sauti kubwa wala usinyamaze katika swala zako, na tafuta njia baina ya hayo "asubuhi," mwanzo wa mchana, "na jioni" mwisho wake. Na nyakati hizi mbili [katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu] ndani yake zina ubora na fadhila juu ya zinginezo. "Wala usiwe miongoni wa walioghafilika," wale ambao walimsahau Mwenyezi Mungu, naye akawasahaulisha nafsi zao. Kwani walinyimwa heri ya dunia na akhera, na wakampa mgongo yule ambaye kila furaha na kufaulu kuko katika kumkumbuka na kumuabudu. Na wakamgeukia yule ambaye kila taabu na kuambulia patupu viko katika kujishughulisha naye. Na hizi ni katika adabu ambazo mja anapaswa kuzizingatia kwa haki ya kuzizingatia. Nazo ni kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi nyakati za usiku na mchana, hasa pande mbili za mchana, kwa ikhlasi, na khushuu, na unyenyekevu, na kujidhalilisha, kwa utulivu, huku moyo wake na ulimi wake vikiingiana, kwa adabu njema, na adhama, na kuielekea dua na ukumbusho, na kumhudhria kwa moyo wake na kutoghafilika. Kwani, Mwenyzi Mungu haitikii dua kutoka katika moyo ulioghafilika au uliopumbaa.
#
{206} ثم ذكر تعالى أن له عباداً مستديمين لعبادته، ملازمين لخدمته، وهم الملائكة. فلتعلموا أن الله لا يريدُ أن يتكثَّر بعبادتكم من قلَّة، ولا ليتعزَّز بها من ذِلَّة، وإنما يريدُ نفع أنفسكم، وأن تربحوا عليه أضعاف أضعاف ما عملتم، فقال: {إنَّ الذين عند ربِّك}: من الملائكة المقرَّبين وحملة العرش والكروبيين، {لا يستكبِرون عن عبادته}: بل يُذْعِنون لها وينقادون لأوامر ربِّهم، {ويسبِّحونه}: الليل والنهار لا يفترون. {وله} وحده لا شريك له {يسجُدون}: فليقتَدِ العبادُ بهؤلاء الملائكة الكرام، وليداوِموا على عبادة الملك العلاَّم.
{206} Kisha Yeye Mtukufu akataja kwamba Yeye anao waja ambao daima wanamuabudu na wanaodumu katika kumtumikia Yeye, na hao ni Malaika. Kwa hivyo mjue kuwa Mwenyezi Mungu hataki ibada yenu izidishe kwa sababu ya upungufu wake, wala apate nguvu kwayo kwa sababu ya unyonge wake. Bali anataka kuzinufaisha nafsi zenu, na kwamba mpate faida kutoka kwake mara nyingi zaidi sana kuliko mlivyotenda. Akasema: "Hakika wale walio kwa Mola wako Mlezi" miongoni mwa Malaika waliokurubishwa, na wanaobeba ‘Arshi na Malaika watukufu zaidi; "hawajivuni wakaacha kumuabdu," bali wanazinyenyekea na wanafuata maamrisho ya Mola wao Mlezi, "na wanamtakasa" usiku na mchana wala hawachoki "na Yeye" peke yake asiyekuwa na mshirika "wanamsujudia." Basi na waige waja Malaika hawa watukufu, na wadumu katika kumwabudu Mfalme, Mwenye kujua vyema.
Imetimia tafsir ya Suratul-A'raaf. Na kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, na shukrani, na sifa. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad na familia yake na maswahaba wake.
***