:
Tafsir ya Suratul-Anfaal
Tafsir ya Suratul-Anfaal
Nayo ilishukia Madina
: 1 - 4 #
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنْفَالِ قُلِ الْأَنْفَالُ لِلَّهِ وَالرَّسُولِ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ (1) إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ (2) الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ (3) أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَهُمْ دَرَجَاتٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ (4)}.
1. Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini. 2. Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao zinaingia hofu. Na wanaposomewa Aya zake, zinawazidishia Imani, na kwa Mola wao Mlezi wakamtegemea. 3. Wale wanaosimamisha Swala, na wanatoa katika yale tunayowaruzuku. 4. Hao ndio Waumini wa uhakika. Wana vyeo kwa Mola wao Mlezi, na kusitiriwa dhambi, na riziki tukufu.
#
{1} الأنفال: هي الغنائم التي يُنَفِّلُها اللهُ لهذه الأمة من أموال الكفار. وكانت هذه الآيات في هذه السورة قد نزلت في قصَّة بدرٍ، أول غنيمة كبيرة غنمها المسلمون من المشركين، فحصل بين بعض المسلمين فيها نزاعٌ، فسألوا رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم - عنها، فأنزل الله: {يسألونَكَ عن الأنفالِ}: كيف تُقْسَمُ؟ وعلى مَن تُقْسَمُ؟ {قل}: لهم الأنفال لله ورسولِهِ يضعانِها حيث شاءا؛ فلا اعتراض لكم على حكم الله ورسوله، بل عليكم إذا حكم الله ورسوله أن ترضوا بحكمهما وتسلِّموا الأمر لهما، وذلك داخلٌ في قوله: {فاتَّقوا الله}: بامتثال أوامره واجتناب نواهيه، {وأصلِحوا ذاتَ بينِكم}؛ أي: أصلِحوا ما بينكم من التشاحن والتقاطع والتدابر بالتوادد والتحاب والتواصل؛ فبذلك تجتمع كلمتُكم ويزولُ ما يحصُلُ بسبب التقاطع من التخاصُم والتشاجُر والتنازع. ويدخُلُ في إصلاح ذاتِ البين تحسينُ الخُلُق لهم والعفو عن المسيئين منهم؛ فإنه بذلك يزول كثير مما يكون في القلوب من البغضاء والتدابر، والأمر الجامع لذلك كله قوله: {وأطيعوا الله ورسولَه إن كنتم مؤمنين}: فإنَّ الإيمان يدعو إلى طاعة الله ورسوله؛ كما أنَّ من لم يطع الله ورسوله فليس بمؤمنٍ، ومن نقصت طاعتُهُ لله ورسوله؛ فذلك لنقص إيمانه.
{1} Al-Anfal ni ngawira ambazo Mwenyezi Mungu anawapa umma huu kutoka katika mali za makafiri. Na Aya hizi katika Sura hii zilikuwa zimeteremka kuhusiana na kisa cha Badr, ngawira kubwa ya kwanza waliyoiteka Waislamu kutoka kwa washirikina. Basi kukatokea mzozo baina ya baadhi ya Waislamu juu ya jambo hilo, kwa hivyo wakamwomba Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake; - juu yake. Basi Mwenyezi Mungu akateremsha: "Wanakuuliza juu ya Ngawira." inagawanywa vipi? Na inagawanyiwa nani? "Sema" uwaambie ngawira ni za Mwenyezi Mungu na mtume wake, wanaziweka pale wanapotaka. Basi nyinyi hamna kipingamizi juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Bali ni juu yenu anapohukumu Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwamba mridhike na hukumu yao na muwasalimishie jambo hilo. Na hayo yanaingia katika kauli yake: "Basi mcheni Mwenyezi Mungu" kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake; "Na suluhisheni mambo baina yenu." Yaani patanisheni ugomvi na kutengana kuliko kati yenu, na kupeana mgongo kwa kupendana, na kuungana. Na kwa hayo, neno lenu litakusanyika pamoja, na yataisha yale yanayotokea kwa sababu ya kutengana miongoni mwa ugomvi, na migogoro, na kuzozana. Na inaingia katika kusuluhisha kati ya watu kuwafanyia tabia kuwa nzuri, na kuwasamehe wanaowakosea miongoni mwao. Kwa maana kwa kufanya hivyo, yanaondoka mengi yanayokuwa katika moyo ya chuki na kupeana migongo. Na jambo linalojumlisha hayo yote ni kauli yake: "Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini." Kwa maana imani inaitia kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kama vile asiyemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake si Muumini; na mwenye utii mpungufu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hilo ni kutokana na upungufu wa imani yake.
#
{2} ولما كان الإيمانُ قسمين: إيماناً كاملاً يترتَّب عليه المدح والثناء والفوزُ التامُّ، وإيماناً دون ذلك؛ ذَكَرَ الإيمانَ الكامل، فقال: {إنما المؤمنون}: الألف واللام للاستغراق لشرائع الإيمان، {الذين إذا ذُكِرَ اللهُ وَجِلَتْ قلوبُهم}؛ أي: خافت ورهبت فأوجبت لهم خشية الله تعالى الانكفافَ عن المحارم؛ فإنَّ خوف الله تعالى أكبر علاماته أن يَحْجُزَ صاحبَه عن الذنوب. {وإذا تُلِيَتْ عليهم آياتُهُ زادتهم إيماناً}: ووجه ذلك أنَّهم يلقون له السمع ويحضِرون قلوبهم لتدبُّره؛ فعند ذلك يزيد إيمانهم؛ لأنَّ التدبُّر من أعمال القلوب، ولأنَّه لا بدَّ أنْ يبيِّن لهم معنىً كانوا يجهلونَه ويتذكَّرون ما كانوا نَسوه أو يُحْدِثَ في قلوبهم رغبةً في الخير واشتياقاً إلى كرامة ربِّهم أو وَجَلاً من العقوبات وازدجاراً عن المعاصي، وكلُّ هذا مما يزداد به الإيمان. {وعلى ربِّهم}: وحده لا شريك له {يتوكَّلون}؛ أي: يعتَمِدون في قلوبهم على ربِّهم في جلب مصالحهم ودفع مضارِّهم الدينيَّة والدنيويَّة، ويثقون بأنَّ الله تعالى سيفعلُ ذلك، والتوكُّل هو الحامل للأعمال كلِّها؛ فلا توجَدُ ولا تكْمُلُ إلا به.
{2} Na kwa kuwa imani ni aina mbili: imani kamili inayotokana nayo kusifiwa, na kufaulu kamili, na imani isiyokuwa hiyo. Akataja Imani kamili, akasema: "Hakika Waumini" Alif na laam katika neno hili ni za kujumuisha sheria zote za Imani, "ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao huhofu." Yaani, zinahofu na kuogopa, kwa hivyo kumnyenyekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kukawasababishia kujizuia na maharamisho. Kwa maana kumhofu Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiko alama kubwa zaidi ya kumzuia mwenyewe kutokana na dhambi. "Na wanaposomewa Aya zake, zinawazidishia Imani." Na hilo ni kwamba wanaisikiliza na kuzihudhurisha nyoyo zao ili kuitafakari, na hapo imani yao inaongezeka. Kwa sababu kutafakari ni miongoni mwa matendo ya nyoyo, na kwa sababu ni lazima iwabainishie maana waliyokuwa hawaijui, na wanakumbuka yale waliyokuwa wameyasahau, au ile katika nyoyo zao kutamani heri na kuwa na shauku juu ya utukufu wa Mola wao Mlezi, au hofu juu ya adhabu, na kukomeka na maasia, na hayo yote ni katika yake ambayo imani inaongezeka kwayo. “Na kwa Mola wao Mlezi” peke yake bila ya mshirika yeyote "wanamtegemea." Yaani, wanategemea katika nyoyo zao kwa Mola wao Mlezi katika kuwaletea masilahi yao na kuwazuia na madhara yao ya kidini na ya kidunia, na wana imani kuwa Mwenyezi Mungu mtukufu atafanya hivyo. Na kutegemea ndiko kunakosababisha matendo yote, kwa hivyo hayapatikani wala hayakamiliki isipokuwa kwayo.
#
{3} {الذين يقيمون الصلاة}: من فرائض ونوافل، بأعمالها الظاهرة والباطنة؛ كحضور القلب فيها، الذي هو رُوح الصلاة ولُبُّها، {ومما رزقْناهم ينفقونَ}: النفقاتِ الواجبةَ؛ كالزكوات والكفَّارات والنفقة على الزوجات والأقارب وما ملكت أيمانهم، والمستحبَّة؛ كالصدقة في جميع طرق الخير.
{3} "Wale wanaosimamisha Swala" miongoni mwa swala za faradhi na za sunna kwa matendo yake ya dhahiri na ya ndani, kama vile kuwepo kwa moyo ndani yake, ambako ndiko roho ya Swala na kiini chake, "na katika yale tunayowaruzuku wanatoa" matumizi ya lazima, kama vile zaka, na kafara, na kutoa matunzo kwa wake, na jamaa, na wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia, na yale yanayopendekezwa kama vile sadaka katika njia zote za wema.
#
{4} {أولئك}: الذين اتَّصفوا بتلك الصفات، {هم المؤمنون حقًّا}: لأنهم جمعوا بين الإسلام والإيمان، بين الأعمال الباطنة والأعمال الظاهرة، بين العلم والعمل، بين أداء حقوق الله وحقوق عباده. وقدَّم تعالى أعمال القلوب لأنَّها أصلٌ لأعمال الجوارح وأفضلُ منها. وفيها دليلٌ على أن الإيمان يزيدُ وينقُصُ؛ فيزيدُ بفعل الطاعة وينقُصُ بضدِّها. وأنه ينبغي للعبد أن يتعاهَدَ إيمانه ويُنْميه. وأنَّ أولى ما يحصُلُ به ذلك تدبُّر كتاب الله تعالى والتأمُّل لمعانيه. ثم ذكر ثواب المؤمنين حقًّا، فقال: {لهم درجاتٌ عند ربِّهم}؛ أي: عاليةٌ بحسب علوِّ أعمالهم. {ومغفرةٌ}: لذُنوبهم، {ورزقٌ كريمٌ}: وهو ما أعدَّ الله لهم في دار كرامته مما لا عين رأتْ ولا أذن سمعتْ ولا خطر على قلبِ بشرٍ. ودلَّ هذا على أنَّ مَن لم يصِلْ إلى درجتهم في الإيمان وإن دَخَلَ الجنة؛ فلن ينال ما نالوا من كرامةِ الله التامَّةِ.
{4} "Hao" waliosifika kwa sifa hizo, "ndio Waumini wa kweli" kwa sababu wao walikusanya kati ya Uislamu na Imani, baina ya matendo ya siri na matendo ya dhahiri, baina ya elimu na matendo, baina ya kutimiza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alitangulliza matendo ya nyoyo kwa sababu hayo ndiyo msingi wa matendo ya viungo na ndio bora zaidi kuyaliko. Na kuna ushahidi kwamba imani huongezeka na kupungua. Kwa hivyo huongezeka kwa kutenda utiifu, na hupungua kwa kinyume chake. Na kwamba mja anapaswa kuirudia imani yake mara kwa mara na kuikuza, na kwamba jambo la kwanza lenye kuyaleta hayo ni kukizingatia Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutafakari maana zake. Kisha akataja malipo ya Waumini wa kweli, akasema: "Wana vyeo kwa Mola wao Mlezi." Yaani, vya juu kulingana na ujuu wa matendo yao; "na kusitiriwa dhambi na riziki tukufu." Nayo ni yale aliyowaandalia Mwenyezi Mungu katika nyumba ya utukufu wake, katika yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Na hili liliashiria kwamba yule ambaye hakufikia katika daraja yao ya imani, hata akiingia Peponi, basi hawatapata katika utukufu kamili wa Mwenyezi Mungu.
: 5 - 8 #
{كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِنْ بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ (5) يُجَادِلُونَكَ فِي الْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى الْمَوْتِ وَهُمْ يَنْظُرُونَ (6) وَإِذْ يَعِدُكُمُ اللَّهُ إِحْدَى الطَّائِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ الشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ اللَّهُ أَنْ يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ (7) لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ (8)}.
5. Kama alivyokutoa Mola wako Mlezi katika nyumba yako kwa haki, na hakika kundi moja katika Waumini linachukia. 6. Wanakujadili kuhusu haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba wanasukumwa kwenye mauti hali ya kuwa wanatazama. 7. Na Mwenyezi Mungu alipowaahidi moja ya vikundi vile viwili kuwa ni chenu. Nanyi mkapenda kwamba kile kisichokuwa kikali ndicho kiwe chenu. Naye Mwenyezi Mungu anataka ahakikishe haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri. 8. Ili aihakikishe haki na aibatilishe batili hata kama watachukia wahalifu.
Yeye Mtukufu alitanguliza mbele ya vita hivi vikubwa vilivyobarikiwa sifa ambazo Waumini wanapaswa kuzitekeleza. Kwa sababu mwenye kuzifanya, hali zake zitanyooka, na matendo yake yatatengenea, ambayo katika kubwa zaidi yake ni jihadi katika njia yake.
#
{5 - 6} فكما أنَّ إيمانهم هو الإيمان الحقيقي وجزاءهم هو الحقُّ الذي وعدهم الله به؛ كذلك أخرج الله رسوله - صلى الله عليه وسلم - من بيته إلى لقاء المشركين في بدرٍ بالحقِّ الذي يحبُّه الله تعالى وقد قدَّره وقضاه، وإنْ كان المؤمنون لم يخطُرْ ببالهم في ذلك الخروج أنَّه يكون بينهم وبين عدوِّهم قتالٌ؛ فحين تبيَّن لهم أنَّ ذلك واقعٌ؛ جعل فريقٌ من المؤمنين يجادلون النبي - صلى الله عليه وسلم - في ذلك ويكرهون لقاء عدوِّهم كأنَّما يُساقونَ إلى الموت وهم ينظُرون! والحال أن هذا لا ينبغي منهم، خصوصاً بعدما تبيَّن لهم أن خروجهم بالحقِّ ومما أمر الله به ورضيه؛ فبهذه الحال ليس للجدال فيها محلٌّ؛ لأنَّ الجدال محلُّه وفائدته عند اشتباه الحقِّ والتباس الأمر، فأما إذا وَضَحَ وبان؛ فليس إلا الانقياد والإذعان. هذا؛ وكثير من المؤمنين لم يجرِ منهم من هذه المجادلة شيءٌ ولا كرهوا لقاء عدوِّهم، وكذلك الذين عاتبهم الله انقادوا للجهاد أشدَّ الانقياد، وثبَّتهم الله، وقيَّض لهم من الأسباب ما تطمئنُّ به قلوبهم كما سيأتي ذكرُ بعضها.
{5 - 6} Kwa hivyo kama vile imani yao ndiyo imani ya kweli, na malipo yao ndiyo haki ambayo Mwenyezi Mungu aliwaahidi, basi vile vile Mwenyezi Mungu alimtoa Mtume wake – rehema na amani ziwe juu yake – kutoka katika nyumba yake, kwenda kukutana na washirikina huko Badr kwa haki ambayo Mwenyezi Mungu anaipenda na alikwisha ijaalia na kuipitisha, ijapokuwa Waumini hawakudhani wakati wa kutoka huko kwamba kungekuwa na vita baina yao na adui yao. Kwa hivyo, ilipowabainikia kwamba jambo hili lilikuwa ni la kutokea, wakawa kundi katika Waumini wanamjadili Nabii– rehema na amani ziwe juu yake – katika hilo, na wakachukia kukutana na adui yao kana kwamba wanasukumwa kwenda kwenye mauti hali ya kuwa wanatazama! Na ukweli ni kwamba halikufaa kutoka kwao, hasa baada ya kuwabainikia kwamba kuondoka kwao ni kwa haki, na ni katika yale aliyoamarisha Mwenyezi Mungu na kuyaridhia. Basi katika hali hii, kujadili hakuna nafasi yoyote. Kwa sababu mjadala mahali pake na faida yake ni wakati kuna mchanganyiko kuhusiana na haki na kuwepo na kutatanisha katika jambo. Lakini linapokuwa wazi na likabainika, basi hakuna isipokuwa kufuata na kutii. Na Wengi miongoni mwa Waumini hakikutokea kwao kitu chochote katika mjadala huu, wala hawakuchukia kukutana na adui yao. Na kadhalika wale ambao Mwenyezi Mungu aliwalaumu walifuata amri ya jihadi kufuata kukubwa mno, na Mwenyezi Mungu akawaimarisha, na akawawekea katika sababu za kuzituliza nyoyo zao, kama itakavyokuja kutajwa baadhi yake.
#
{7} وكان أصلُ خروجهم يتعرَّضون لعير خرجت مع أبي سفيان بن حرب لقريش إلى الشام قافلة كبيرة، فلما سمعوا برجوعها من الشام؛ ندب النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - الناس، فخرج معه ثلاثمائة وبضعة عشر رجلاً معهم سبعون بعيراً يعتقبون عليها ويحملون عليها متاعَهم، فسمع بخبرهم قريشٌ، فخرجوا لمنع عيرهم في عَدَدٍ كثيرٍ وعُدَدٍ وافرة من السلاح والخيل والرجال، يبلغ عددهم قريباً من الألف، فوعد الله المؤمنين إحدى الطائفتين: إما أن يظفروا بالعير، أو بالنفير، فأحبوا العير لقلَّة ذات يد المسلمين ولأنَّها غير ذات الشوكة. ولكن الله تعالى أحبَّ لهم وأراد أمراً أعلى مما أحبُّوا، أراد أن يظفروا بالنَّفير الذي خرج فيه كبراء المشركين وصناديدُهم. فيريد اللهُ أن يُحِقَّ الحقَّ بكلماتِهِ فينصر أهله، {ويقطَعَ دابرَ الكافرين}؛ أي: يستأصل أهلَ الباطل ويُري عبادَهُ من نصرِهِ للحقِّ أمراً لم يكن يخطر ببالهم.
{7} Na nia kubwa ya kutoka kwao ilikuwa ni kwenda kuuteka msafara ule wa Maquraishi uliokuwa umetoka pamoja na Abu Sufyan bin Harb ukienda Shaam katika msafara mkubwa sana. Basi waliposikia kuhusu kutoka kwake huko Shaam, yeye Nabii rehema na amani zimshukie akawaita watu, na wakatoka pamoja naye wanaume mia tatu na kumi na tano hivi wakiwa pamoja na ngamia sabini waliokuwa wakiwapanda kwa zamu, na wanabebea juu yao mizigo yao. Maquraishi wakasikia kuhusu kutoka kwao, kwa hivyo wakatoka ili wakauzuie msafara wao katika idadi kubwa na maandalizi makubwa ya silaha, na farasi, na wanaume, ikifikia idadi yao karibu elfu moja. Basi Mwenyezi Mungu akaahidi Waumini moja ya makundi mawili: ima washinde katika kuuteka msafara huo au vita, lakini wao wakaupenda msafara kwa sababu ya uchache wa kilichokuwa katika mkono wa Waislamu na kwa kuwa hawakuwa na nguvu madhubuti. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akawapendea na akawatakia kitu cha juu zaidi kuliko kile walichokipenda. Alitaka kwamba washinde kwenye vita ambavyo walitoka ndani yake wakubwa wa washirikina na waheshimiwa wao. Basi Mwenyezi Mungu anataka aihakikishe haki kwa maneno yake na awanusuru watu wake, "na aikate mizizi ya makafiri.” Yaani, aung’oe msingi wa batili na awaonyeshe waja wake jambo ambalo halikuwahi kupita katika akili zao la kuinusuru haki.
#
{8} {لِيُحِقَّ الحقَّ}: بما يُظْهِرُ من الشواهد والبراهين على صحته وصدقه، {ويُبْطِل الباطل}: بما يقيم من الأدلة والشواهد على بطلانه، {ولو كره المجرمون}: فلا يبالي الله بهم.
{8} “Ili aihakikishe haki” kwa yale anayodhihirisha miongoni mwa ushahidi mbalimbali na uthibitisho wa usahihi wake na ukweli wake, "na aibatilishe batili” kwa yale anayosimamisha miongoni mwa hoja na ushahidi juu ya ubatili wake. “Hata kama watachukia wahalifu,” na Mwenyezi Mungu hajali nao.
: 9 - 14 #
{إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُمْ بِأَلْفٍ مِنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ (9) وَمَا جَعَلَهُ اللَّهُ إِلَّا بُشْرَى وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (10) إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُمْ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً لِيُطَهِّرَكُمْ بِهِ وَيُذْهِبَ عَنْكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَى قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ (11) إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ (12) ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَمَنْ يُشَاقِقِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ (13) ذَلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابَ النَّارِ (14)}.
9. Mlipokuwa mnamuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akawaitikia kuwa Mimi hakika nitawasaidia kwa elfu moja miongoni mwa Malaika wakifuatana mfululizo. 10. Na Mwenyezi Mungu hakufanya hayo isipokuwa yawe ni bishara na ili nyoyo zenu zitue kwayo. Na nusura haiwi isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 11. Alipowafunika kwa usingizi uwe ni amani kutoka kwake, na akawateremshia maji kutoka mbinguni ili awasafishe kwayo na awaondolee uchafu wa Shetani, na ili azifunge nyoyo zenu, na aimarishe kwayo miguu yenu. 12. Mola wako Mlezi alipowafunulia Malaika: Hakika Mimi niko pamoja nanyi, basi watieni nguvu wale walioamini. Nitatupa uoga katika nyoyo za wale waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole. 13. Hayo ni kwa sababu walimuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 14. Ndivyo hivyo! Basi ionjeni! Na bila ya shaka makafiri wana adhabu ya Moto.
#
{9} أي: اذكروا نعمة الله عليكم لمَّا قارب التقاؤكم بعدوِّكم؛ استغثتُم بربِّكم وطلبتُم منه أن يعينكم وينصركم، {فاستجاب لكم}: وأغاثكم بعدَّة أمور؛ منها: أنَّ الله أمدَّكم {بألفٍ من الملائكة مردفينَ}؛ أي: يَرْدُفُ بعضُهم بعضاً.
{9} Yaani, ikumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu wakati kulipokaribia kukutana kwenu na adui yenu, mkamuomba msaada Mola wenu Mlezi, na mkamtaka awasaidie na awanusuru; "naye akawaitikia” na akawasaidia kwa mambo kadhaa: Miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu aliwasaidia “kwa elfu moja miongoni mwa Malaika wakifuatana mfululizo.” Yaani, wanafuatana wao kwa wao.
#
{10} {وما جعله الله}؛ أي: إنزال الملائكة {إلا بشرى}؛ أي: لتستبشر بذلك نفوسكم، {ولتطمئنَّ به قلوبُكم}: وإلاَّ؛ فالنصر بيد الله، ليس بكثرة عَدَدٍ ولا عُدَدٍ. {إن الله عزيزٌ}: لا يغالبُه مغالبٌ، بل هو القهار الذي يخذل من بلغوا من الكثرة وقوة العدد والآلات ما بلغوا، {حكيمٌ}: حيث قدَّر الأمور بأسبابها ووضع الأشياء مواضعها.
{10} "Na Mwenyezi Mungu hakufanya hayo,” yaani kuwateremsha Malaika "isipokuwa yawe ni bishara." Yaani, ili nafsi zenu zifurahi kwa hayo, "na ili nyoyo zenu zitue kwayo;” vinginevyo, ushindi umo mkononi mwa Mwenyezi Mungu, na siyo kwa wingi wa idadi wala maandalizi. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu nyingi," hakuna yeyote wa kumshinda, bali Yeye ni Mshindi ambaye anawaangusha wenye kufikia katika wingi na idadi na nguvu na ala zozote wanazoofikia. “Mwenye hekima kubwa” kwa kuwa alijaalia mambo na sababu zake, na akaweka vitu pahali pake.
#
{11} ومن نصرِهِ واستجابته لدعائكم أن أنزل عليكم نعاساً {يُغَشِّيكم}؛ أي: فيُذْهِب ما في قلوبكم من الخوف والوجل، ويكون {أمَنَةً}: لكم وعلامةً على النصر والطمأنينة. ومن ذلك أنه أنزل عليكم من السماء مطراً ليطهِّركم به من الحَدَث والخَبَث، وليطهِّركم به من وساوس الشيطان ورجزه، {ولِيَرْبِطَ على قلوبكم}؛ أي: يثبِّتها؛ فإنَّ ثبات القلب أصلُ ثبات البدن، {ويُثَبِّتَ به الأقدام}: فإن الأرض كانت سهلةً دهسةً، فلما نزل عليها المطر؛ تلبَّدت، وثبتت به الأقدام.
{11} Na katika nusura yake na kuitikia kwake dua zenu ni kwamba aliwateremshia usingizi ambao "aliwafunika." Yaani, kisha yakaondoa yale yaliyo ndanu ya nyonyo zenu ya hofu na kicho katika nyoyo zenu, na inakuwa ni “amani” kwenu na alama ya ushindi na utulivu. Na katika hayo ni kwamba aliwateremshia mvua kutoka mbinguni ili awasafishe kwayo kutokana na hadathi na uchafu, na ili awasafishe kwayo kutokana na wasiwasi za Shetani uchafu wake, na ili azifunge nyoyo zenu, yaani aziimarishe. Kwa maana uimara wa moyo ndio msingi wa uimara wa mwili; “na aimarishe kwayo miguu yenu.” Kwa sababu ardhi ilikuwa rahisi kukanyagwa. Basi mvua iliponyesha juu yake, ukaimarika, na miguu ikawa thabitti juu yake.
#
{12} ومن ذلك أنَّ الله أوحى إلى الملائكة: {أنِّي معكم}: بالعون والنصر والتأييد، {فثبِّتوا الذين آمنوا}؛ أي: ألقوا في قلوبهم وألهموهم الجراءة على عدوِّهم ورغِّبوهم في الجهاد وفضله. {سألقي في قلوبِ الذين كَفَروا الرُّعْبَ}: الذي هو أعظم جندٍ لكم عليهم؛ فإنَّ الله إذا ثبَّت المؤمنين وألقى الرعب في قلوب الكافرين؛ لم يقدِرِ الكافرون على الثَّبات لهم، ومَنَحَهُمُ الله أكتافهم، {فاضربوا فوقَ الأعناق}؛ أي: على الرقاب، {واضرِبوا منهم كلَّ بنانٍ}؛ أي: مفصل. وهذا خطابٌ: إما للملائكة الذين أوحى [اللهُ] إليهم أن يثبِّتوا الذين آمنوا فيكون في ذلك دليلٌ أنَّهم باشروا القتال يوم بدر، أو للمؤمنين يشجِّعهم الله ويعلِّمهم كيف يقتلون المشركين وأنهم لا يرحمونهم.
{12} Na miongoni mwa hayo ni kwamba, Mwenyezi Mungu aliwafunulia Malaika kwamba, "Hakika Mimi niko pamoja nanyi” kwa msaada, na nusura, na kuunga mkono; "basi watieni nguvu wale walioamini.” Yaani, tupeni katika nyoyo zao na waingizeni ujasiri dhidi ya adui yao na wahimizeni kushiriki katika jihadi na fadhila zake. "Nitatupa kicho katika nyoyo za wale waliokufuru" ambayo ndilo jeshi lenu kubwa zaidi dhidi yao. Kwa maana Mwenyezi Mungu akiwaimarisha Waumini na akatupa hofu katika nyoyo za makafiri, basi makafiri hawawezi kusimama imara dhidi yao, na Mwenyezi Mungu atawapa mabega yao. “Basi wapigeni juu ya shingo," yaani kwenye shingo. "Na wapigeni kwenye kila ncha za vidole;” yaani, kiungo. Na maneno haya ima ni kwa Malaika ambao [Mwenyezi Mungu] aliwafunulia wahyi kwamba wawaimarishe wale walioamini, na huu unakuwa ushahidi kwamba walipigana hasa Siku ya Badr, au ni kwa Waumini ambao Mwenyezi Mungu anawahimiza na anawafundisha namna ya kuwaua washirikina na kwamba hawawahurumii.
#
{13} ذلك لأنَّهم شاقُّوا اللهَ ورسولَه؛ أي: حاربوهما وبارزوهما بالعداوة، {ومَن يشاقِقِ اللهَ ورسوله فإنَّ الله شديد العقاب}: ومن عقابه تسليطُ أوليائه على أعدائه وتقتيلهم.
{13} Hayo ni kwa sababu walimuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Yaani, walipigana nao, na wakawatokea vita vya uadui. "Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu." Na katika adhabu yake ni kuwapa mamlaka marafiki zake juu ya maadui zake na kuwaua.
#
{14} {ذلكم}: العذاب المذكور، {فَذوقوهُ}: أيُّها المشاققون لله ورسولِهِ عذاباً معجَّلاً. {وأنَّ للكافرين عذابَ النارِ}. وفي هذه القصة من آيات الله العظيمة ما يدلُّ على أن ما جاء به محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - رسول الله حقًّا: منها: أنَّ الله وعَدَهم وعداً فأنجزَهُموه. ومنها: ما قال الله تعالى: {قد كانَ لَكُمْ آيةٌ في فئتينِ التَقَتا فئةٌ تقاتِلُ في سبيل اللهِ وأخرى كافرةٌ يَرَوْنَهم مِثْلَيْهِم رَأيَ العين ... } الآية. ومنها: إجابة دعوة الله للمؤمنين لما استغاثوه بما ذَكَره من الأسباب. وفيها الاعتناءُ العظيم بحال عباده المؤمنين وتقييضُ الأسباب التي بها ثَبَتَ إيمانُهم، وثبتتْ أقدامُهم، وزال عنهم المكروه والوساوس الشيطانية. ومنها: أن من لطف الله بعبده أن يُسَهِّلَ عليه طاعته وييسِّرها بأسبابٍ داخليَّة وخارجيَّة.
{14} "Hiyo" adhabu iliyotajwa, "basi ionjeni" enyi mnaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni adhabu ya haraka. "Basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” Na katika kisa hiki kuna baadhi ya ishara kubwa za Mwenyezi Mungu zinazoashiria kuwa yale aliyokuja nayo Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake - Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kweli. Miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi, na akawatekelezea ahadi hiyo. Na miongoni mwake ni yale aliyoyasema Mwenyezi Mungu: "Hakika, mlikuwa na Ishara katika yale makundi mawili yalipokutaka (katika vita). Kundi moja likipigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, nalo lingine kafiri likiwaona zaidi kuliko wao mara mbili, kwa kuona kwa macho..." hadi mwisho wa Aya. Na miongoni mwake ni Mwenyezi Mungu kuwaitikia dua Waumini wanapomwomba msaada kwa sababu alizozitaja. Na ndani yake kuna kuijali sana hali ya waja wake Waumini, na kuwawekea sababu ambazo kwazo imani yao iliimarika, na miguu yao ikaimarika, na yakawaondokea machukizo, na wasiwasi za kishetani. Na miongoni mwake ni kwamba, katika upole wa Mwenyezi Mungu kwa mja wake ni kumsahilishia kumtii Yeye, na kumrahisishia hilo kwa sababu za kindani na za kinje.
: 15 - 16 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ (15) وَمَنْ يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَى فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِنَ اللَّهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (16)}.
15. Enyi Mlioamini! Mnapokutana na wale waliokufuru vitani, msiwageuzie migongo. 16. Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo, isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, basi hakika atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahali pake ni Jahannam, na huo ni mwisho muovu.
#
{15} يأمر تعالى عبادَهُ المؤمنين بالشجاعة الإيمانيَّة والقوَّة في أمره والسعي في جَلْب الأسباب المقويَّة للقلوب والأبدان، ونهاهم عن الفرار إذا التقى الزحفان، فقال: {يا أيُّها الذين آمنوا إذا لقيتُمُ الذين كَفَروا زحفاً}؛ أي: في صفِّ القتال وتزاحف الرجال واقتراب بعضهم من بعض، {فلا تولُّوهم الأدبارَ}: بل اثبُتوا لقتالِهِم واصبِروا على جِلادِهم؛ فإنَّ في ذلك نُصرةً لدين الله وقوَّةً لقلوب المؤمنين وإرهاباً للكافرين.
{15} Yeye Mtukufu anawaamrisha waja wake Waumini kuwa na ujasiri wa kiimani na nguvu katika jambo lake na kujitahidi kuleta sababu zinazotia nguvu nyoyo na miili, na akawakataza kukimbia pindi yanapokutana safu mbili za vita. Akasema: "Enyi Mlioamini! Mnapokutana na wale waliokufuru vitani;" yaani, katika safu ya vita, kukaribiana mno kwa wanaume wapiganaji pamoja na watu kusonga mbele na kukaribiana, "basi msiwageuzie migongo;" bali simameni imara kupigana nao na subirini katika kupambana nao; kwani katika hilo kuna kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, na nguvu kwa nyoyo za Waumini, na kuwahofisha makafiri.
#
{16} {ومَن يُوَلِّهِم يومئذٍ دُبُرَهُ إلا متحرِّفاً لقتال أو متحيِّزاً إلى فئةٍ فقد باء}؛ أي: رجع {بغضبٍ من الله ومأواه}؛ أي: مقره {جهنَّم وبئس المصير}. وهذا يدلُّ على أن الفرار من الزحف من غير عذرٍ من أكبر الكبائر؛ كما وردت بذلك الأحاديث الصحيحة ، وكما نصَّ هنا على وعيده بهذا الوعيد الشديد. ومفهوم الآية أن المتحرِّف للقتال ـ وهو الذي ينحرفُ من جهة إلى أخرى ليكون أمكن له في القتال وأنكى لعدوِّه ـ فإنه لا بأس بذلك؛ لأنه لم يولِّ دُبُرَهُ فارًّا، وإنما ولَّى دُبُره ليستعلي على عدوِّه أو يأتيه من محلٍّ يصيب فيه غِرَّته أو ليخدِعَه بذلك أو غير ذلك من مقاصد المحاربين. وأن المتحيِّز إلى فئةٍ تمنعه وتعينه على قتال الكفار؛ فإنَّ ذلك جائزٌ؛ فإن كانت الفئة في العسكر؛ فالأمر في هذا واضح، وإن كانت الفئة في غير محلِّ المعركة؛ كانهزام المسلمين بين يدي الكافرين والتجائهم إلى بلد من بلدان المسلمين أو إلى عسكرٍ آخر من عسكر المسلمين؛ فقد ورد من آثار الصحابة ما يدلُّ على أنَّ هذا جائزٌ، ولعلَّ هذا يقيَّدُ بما إذا ظنَّ المسلمون أنَّ الانهزام أحمدُ عاقبة وأبقى عليهم، أما إذا ظنُّوا غلبتهم للكفار في ثباتهم لقتالهم؛ فيبعد في هذه الحال أن تكون من الأحوال المرخَّص فيها؛ لأنه على هذا لا يتصوَّر الفرار المنهيُّ عنه. وهذه الآية مطلقةٌ، وسيأتي في آخر السورة تقييدها بالعدد.
{16} "Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo, isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, basi hakika atakuwa amekwisha rudi na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahali pake." Yaani, makazi yake ni "Jahannam, na ni pahali pabaya zaidi pa kuishia." Na hili linaashiria kwamba kukimbia kutoka safu za vita bila udhuru ni katika madhambi makubwa zaidi. Kama ilivyokuja hivyo katika hadithi mbalimbali sahihi, na kama alivyotaja hapa moja kwa moja ahadi ya adhabu kali juu yake. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya hii ni kwamba mwenye kupinduka kwa ajili ya mbinu za kupigana vita – naye ni yule anayepinduka kutoka upande mmoja kwenda mwingine ili aweze kupigana na kumteka zaidi adui yake, - basi huyo hana ubaya wowote juu yake katika hilo. Kwa sababu hakupeana mgongo wake ili kukimbia, bali aliupeana mgongo wake ili kupata nguvu juu ya adui yake, au kumjia kutokea mahali ambapo atamshambulia bila kujua au kumhadaa kwa hilo, au yasiyokuwa hayo miongoni mwa makusudio ya wapiganaji. Na kwamba mwenye kuungana na kikosi chenye kumzuia na kumsaidia kupigana na makafiri, basi hilo linaruhusiwa. Kwa hivyo ikiwa kikundi hicho kiko katika jeshi, basi jambo katika hili liko wazi. Na kama kikundi hicho kiko katika pahali ambapo si pa vita hivyo, kama vile kushindwa kwa Waislamu mikononi mwa makafiri na kukimbilia kwao katika mji miongoni mwa miji ya Waislamu au kwenye jeshi jingine la Waislamu, basi imekuwa katika simulizi kutoka katika riwaya za Maswahaba zinazoashiria kuwa jambo hilo linaruhusika. Na pengine hili limefungiwa tu katika hali ikiwa Waislamu watadhani kuwa kushindwa kutakuwa ndiyo natija bora zaidi na kwenye kuwadumisha zaidi. Lakini wakidhani kuwa watawashinda makafiri katika kukaa kwao imara katika vita, basi katika hali hii ni mbali zaidi kwa iwe moja ya hali ambayo inaruhusiwa. Kwa sababu kwa msingi wa hii, kutoroka kulikokatazwa hakuwezi kufikiriwa. Na Aya hii ni ya jumla, na itakuja katika mwisho wa sura hii kuifungia kwa idadi fulani.
: 17 - 19 #
{فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ قَتَلَهُمْ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَكِنَّ اللَّهَ رَمَى وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (17) ذَلِكُمْ وَأَنَّ اللَّهَ مُوهِنُ كَيْدِ الْكَافِرِينَ (18) إِنْ تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ وَإِنْ تَنْتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ وَإِنْ تَعُودُوا نَعُدْ وَلَنْ تُغْنِيَ عَنْكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْئًا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ (19)}.
17. Kwa hivyo, hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua. Nawe hukutupa ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa, na ili awajaribu Waumini majaribio mazuri kutoka kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote. 18. Hayo! Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri. 19. Mkiomba msaada wa ushindi, basi msaada wa ushindi ulikwisha wajia. Na mkikomeka, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkirejea, Sisi pia tutarejea. Na kundi lenu halitawanufaisha kitu hata kama yatakuwa mengi. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini.
#
{17} يقول تعالى لما انهزم المشركون يوم بدرٍ وقتلهم المسلمونَ: {فلم تقتُلوهم}: بحولِكم وقوَّتكم، {ولكنَّ الله قتلهم}: حيث أعانكم على ذلك بما تقدَّم ذكره، {وما رميتَ إذْ رميتَ ولكنَّ الله رمى}: وذلك أنَّ النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - وقتَ القتال دخل العريش، وجعل يدعو الله، ويناشده في نصرته ، ثم خرج منه، فأخذ حَفْنَةً من تراب، فرماها في وجوه المشركين، فأوصلها الله إلى وجوههم، فما بقي منهم واحدٌ إلاَّ وقد أصاب وجهَهُ وفمه وعينيه منها ؛ فحينئذ انكسر حدهم وفتر زَندُهم وبان فيهم الفشل والضعف فانهزموا. يقول تعالى لنبيِّه: لستَ بقوَّتك حين رميتَ الترابَ أوصلتَهُ إلى أعينهم، وإنَّما أوصلناه إليهم بقوَّتنا واقتدارنا. {وَلِيُبْلِيَ المؤمنينَ منه بلاءً حسناً}؛ أي: إن الله تعالى قادرٌ على انتصار المؤمنين من الكافرين من دون مباشرةِ قتال، ولكنَّ الله أراد أن يمتحنَ المؤمنين ويوصِلَهم بالجهاد إلى أعلى الدرجات وأرفع المقامات ويعطيهم أجراً حسناً وثواباً جزيلاً. {إنَّ الله سميعٌ عليمٌ}: يسمع تعالى ما أسرَّ به العبد وما أعلن، ويعلم ما في قلبه من النيات الصالحة وضدِّها، فيقدِّر على العباد أقداراً موافقةً لعلمه وحكمته ومصلحة عباده، ويجزي كلاًّ بحسب نيَّته وعمله.
{17} Yeye Mtukufu Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu waliposhindwa washirikina siku ya Badr na Waislamu wakawaua: "Hamkuwaua nyinyi" kwa uwezo wenu na nguvu zenu, "Lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua;" aliwasaidia juu ya hilo kwa yale yaliyotangulia kutajwa hapo awali. "Nawe hukutupa ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa." Na hiyo ni kwa sababu Nabii -Rehema na Amani zimshukie - wakati wa kupigana vita aliingia katika Al-Ariish (hema) na akaanza kumuomba Mwenyezi Mungu na kumsihi kwa ajili ya ushindi wake, kisha akatoka humo na akachukua mkono mzima wa udongo na akaurusha kwenye nyuso za washirikina, na Mwenyezi Mungu akaufikisha kwenye nyuso zao. Basi hakubaki hata mmoja miongoni mwao isipokuwa alisibu uso wake, na mdomo wake, na macho yake kwa huo. Na hapo ukali wao ukavunjika, na nguvu zao zikadhoofika, na kushindwa na udhaifu ukabainika ndani yao, kwa hivyo wakashindika. Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake, “Si kwa nguvu zako ulipotupa udongo uliufikisha katika macho pao, bali tuliufikisha kwao kwa nguvu zetu na uwezo wetu. "Na ili awajaribu Waumini majaribio mazuri kutoka kwake;" yaani, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweza kuwanusuru Waumini kutoka kwa makafiri bila ya kupigana vita moja kwa moja, lakini Mwenyezi Mungu alitaka kuwapa mtihani Waumini na kuwafikisha kwa jihadi katika daraja na vyeo vya juu zaidi, na awape malipo mazuri na thawabu nyingi. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote." Yeye Mtukufu anayasikia aliyofanya mja kwa siri na yale aliyofanya wazi wazi, na anayajua yale yaliyomo katika moyo wake miongoni mwa nia njema na kinyume chake, basi anawaandikia waja majaliwa yanayowiana na elimu yake, na hekima yake, na masilahi ya waja wake, na anamlipa kila mmoja kwa nia yake na matendo yake.
#
{18} {ذلكم}: النصر من الله لكم، {وأنَّ الله موهنُ كيدِ الكافرين}؛ أي: مُضْعِفُ كلَّ مكر وكيد يكيدون به الإسلام وأهله، وجاعلُ مكرهم محيقاً بهم.
{18} "Ndivyo hivyo!" Nusura kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenu. "Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri." Yaani, atadhoofisha kila vitimbi, na njama wanayoupangia Uislamu na watu wake, na atavifanya vitimbi vyao dhidi yao.
#
{19} {إن تستفتحوا}: أيُّها المشركون؛ أي: تطلبون من الله أن يوقع بأسه وعذابه على المعتدين الظالمين، {فقد جاءكم الفتحُ}: حين أوقع الله بكم من عقابِهِ ما كان نَكالاً لكم وعبرةً للمتقين. {وإن تنتهوا}: عن الاستفتاح {فهو خيرٌ لكم}: لأنَّه ربَّما أمهلكم ولم تُعَجَّلْ لكم النقمةُ. {وإن تعودوا}: إلى الاستفتاح وقتال حزب الله المؤمنين {نَعُدْ}: في نصرهم عليكم، {ولن تُغْنِيَ عنكم فئتُكم}؛ أي: أعوانكم وأنصاركم الذين تحاربون وتقاتلون معتمدين عليهم شيئاً. {وأنَّ الله مع المؤمنين}: ومن كان الله معه؛ فهو المنصور، وإن كان ضعيفاً قليلاً عدده. وهذه المعيَّة التي أخبر الله أنه يؤيِّد بها المؤمنين تكون بحسب ما قاموا به من أعمال الإيمان؛ فإذا أديل العدوُّ على المؤمنين في بعض الأوقات؛ فليس ذلك إلا تفريطاً من المؤمنين وعدم قيامٍ بواجب الإيمان ومقتضاه، وإلاَّ؛ فلو قاموا بما أمر الله به من كلِّ وجهٍ؛ لما انهزم لهم رايةٌ انهزاماً مستقرًّا ولا أدِيلَ عليهم عدوُّهم أبداً.
{19} "Mkiomba ushindi" enyi washirikina! Yaani, mkimuomba Mwenyezi Mungu awape mateso yake na adhabu yake wale waliovuka mipaka madhalimu, "basi msaada wa ushindi ulikwisha wajia" wakati Mwenyezi Mungu alipowatia mateso yake ambayo yalikuwa ni adhabu kwenu na mazingatio kwa wachamungu. "Na mkikomeka" kuomba ushindi, "basi hilo ndilo heri kwenu" kwa sababu huenda akawapa muhula, wala asiwaharakishie adhabu. "Na mkirejea;" katika kuomba ushindi na kupigana vita na kundi la Mwenyezi Mungu walio Waumini "sisi pia tutarejea" katika kuwanusuru wao dhidi yenu, "Na kundi lenu halitawanufaisha." Yaani, hawatawafaa kitu wasaidizi wenu, na wale wanaowanusuru ambao mnapigana mkiwategemea. "Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini." Na yule ambaye Mwenyezi Mungu yuko pamoja naye, basi yeye ndiye aliyenusuruwa, hata kama ni dhaifu, mwenye idadi chache. Ufuatano huu ambao Mungu alisema kuwa anawaunga mkono waumini utakuwa sawa na matendo ya imani waliyoyafanya. Adui akiwageukia Waumini nyakati fulani; haya si chochote ila ni uzembe wa waumini na kushindwa kutimiza wajibu na matakwa ya imani, vinginevyo; ikiwa walifanya yale ambayo Mungu aliwaamuru kwa kila njia; waliposhindwa, bendera yao ilishindwa kabisa, na adui yao hakuwahi kuwasaliti.
: 20 - 21 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَوَلَّوْا عَنْهُ وَأَنْتُمْ تَسْمَعُونَ (20) وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ (21)}.
20. Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msigeuke mkamuacha hali ya kuwa mnasikia. 21.Wala msiwe kama wale wanaosema, "Tumesikia" na hali hawasikii.
#
{20} لما أخبر تعالى أنه مع المؤمنين؛ أمرهم أن يقوموا بمقتضى الإيمان الذي يدركون معيَّتَه، فقال: {يا أيُّها الذين آمنوا أطيعوا اللهَ ورسولَه}: بامتثال أمرِهما واجتنابِ نهيِهما. {ولا تَوَلَّوْا عنه}؛ أي: عن هذا الأمر الذي هو طاعة الله وطاعة رسوله، {وأنتم تسمعونَ}: ما يُتلى عليكم من كتاب الله وأوامره ووصاياه ونصائحه؛ فتولِّيكم في هذه الحال من أقبح الأحوال.
{20} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipojulisha kwamba Yeye yu pamoja na Waumini, akawaamrisha kwamba wafanye kulingana na matakwa ya imani ambayo watafikia kuwa pamoja naye. Akasema: "Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake" kwa kufuata amri zao na kuepuka makatazo yao. "Wala msigeuke mkamwacha;" yaani, katika amri hii ambayo ni kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume Wake, "hali ya kuwa mnasikia" yale mnayosomewa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na amri zake, na wasia zake, na nasaha zake. Basi kugeuka kwenu kumuacha katika hali hii ni katika hali mbaya zaidi.
#
{21} {ولا تكونوا كالذين قالوا سمِعْنا وهم لا يسمعون}؛ أي: لا تكتفوا بمجرَّدِ الدعوى الخالية التي لا حقيقة لها؛ فإنها حالة لا يرضاها الله ولا رسوله، فليس الإيمانُ بالتمنِّي والتحلِّي، ولكنَّه ما وَقَرَ في القلوب، وصدَّقته الأعمال.
{21} "Wala msiwe kama wale wanaosema, "Tumesikia" na hali hawasikii." Yaani, msiachie kwa madai matupu tu ambayo hayana uhakika wowote. Kwani ni hali ambayo hairidhii Mwenyezi Mungu wala Mtume wake. Kwa maana, Imani si kwa kutamani tu na kuvaa, bali ni kile kilichoko mathubuti katika nyoyo na kikasadikishwa na matendo.
: 22 - 23 #
{إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِنْدَ اللَّهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ (22) وَلَوْ عَلِمَ اللَّهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَأَسْمَعَهُمْ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوْا وَهُمْ مُعْرِضُونَ (23)}.
22. Hakika waovu mno wa wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale viziwi, na mabubu wasiotumia akili zao. 23. Na Mwenyezi Mungu angelijua heri yoyote ndani yao, angewasikilizisha, na lau angewasikilizisha, wangeligeuka hali ya kuwa wamepuuza.
#
{22} يقول تعالى: {إنَّ شرَّ الدوابِّ عند الله}: مَنْ لم تُفِذْ فيهم الآيات والنذر، وهم {الصُّمُّ}: عن استماع الحق، {البكم}: عن النطق به، {الذين لا يعقلونَ}: ما ينفعهم ويؤثرونَه على ما يضرُّهم؛ فهؤلاء شرٌّ عند الله من شرار الدواب ؛ لأنَّ الله أعطاهم أسماعاً وأبصاراً وأفئدة ليستعملوها في طاعة الله، فاستعملوها في معاصيه، وعدموا بذلك الخير الكثير؛ فإنَّهم كانوا بصدد أن يكونوا من خيار البريَّة، فأبوا هذا الطريق، واختاروا لأنفسهم أن يكونوا من شرِّ البريَّة. والسمعُ الذين نفاه الله عنهم سمعُ المعنى المؤثِّر في القلب، وأما سمعُ الحجَّة؛ فقد قامت حجَّة الله تعالى عليهم بما سمعوه من آياته.
{22} Yeye Mtukufu Anasema: "Hakika waovu mno wa wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu" ni wale ambao hazikuathiri ndani yao ishara na maonyo, nao "ni viziwi" wa kusikia haki, "mabubu." Wa kuitamka haki, "wasiotumia akili zao" kwa yenye kuwanufaisha, na kuyapendelea kuliko yale yanayowadhuru. Basi hawa ndio waovu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wabaya zaidi wa wanyama wote. Kwa sababu mwenyezi Mungu aliwapa masikio, na macho, na mioyo ya kutumia katika kumtii Mwenyezi Mungu, lakini wakavitumia katika kumuasi, na wakapoteza kwa hilo heri nyingi. Kwa kuwa walikuwa karibu kuwa miongoni mwa walio bora zaidi wa viumbe, lakini wakaikataa njia hii na wakajichagulia kuwa miongoni mwa wabaya zaidi wa viumbe. Na kusikia ambako Mwenyezi Mungu alikukanusha kuhusiana nao ni kusikia maana inayoathiri katika moyo. Na ama kusikia hoja, basi hakika tayari hoja ya Mwenyezi Mungu imeshasimama juu yao, kwa yale walisikia katika ishara zake.
#
{23} وإنما لم يُسمعْهم السماعَ النافع؛ لأنَّه لم يعلم فيهم خيراً يَصْلُحون به لسماع آياته. {ولو علم الله فيهم خيراً لأسمَعَهم ولو أسمَعَهم}: على الفرض والتقدير، {لَتَوَلَّوا}: عن الطاعة {وهم معرضونَ}: لا التفات لهم إلى الحقِّ بوجه من الوجوه. وهذا دليلٌ على أن الله تعالى لا يمنع الإيمان والخير إلاَّ لمن لا خير فيه الذي لا يزكو لديه ولا يثمرُ عنده، وله الحمد تعالى والحكمة في هذا.
{23} Na hakuwasikizisha kusikia kwa manufaa, kwa sababu hakujua jema lolote ndani yao ambalo wangetengenea kwa kuzisikia Aya zake. "Na Mwenyezi Mungu angelijua wema wowote kwao, angewasikilizisha, na lau angewasikilizisha" kwa kuchukulia hivyo na kukadiria hivyo; "basi wangeligeuka" wakauacha utiifu "hali ya kuwa wamepeana mgongo " bila ya kugeuka kuitazama haki kwa njia yoyote ile. Na huu ni ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu haizuii imani na heri isipokuwa kwa yule asiyekuwa na heri yoyote ndani yake, ambaye haitakasiki kwake wala haizai kwake. Basi sifa njema zote ni zake Yeye Mtukufu, na hekima katika jambo hili.
: 24 - 25 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ (24) وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ (25)}.
24. Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaitia yale yenye kuwahuisha. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huizuia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye mtakusanywa. 25. Na jikingeni na mtihani ambao hautawasibu wale waliodhulumu pekee miongoni mwenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
#
{24} يأمر تعالى عباده المؤمنين بما يقتضيه الإيمان منهم، وهو الاستجابة لله وللرسول؛ أي: الانقياد لما أمرا به والمبادرة إلى ذلك والدعوة إليه، والاجتناب لما نهيا عنه والانكفاف عنه والنهي عنه. وقوله: {إذا دعاكم لما يُحييكم}: وصفٌ ملازمٌ لكل ما دعا الله ورسوله إليه وبيانٌ لفائدته وحكمته؛ فإن حياة القلب والروح بعبوديَّة الله تعالى ولزوم طاعته وطاعة رسوله على الدوام. ثم حذَّر عن عدم الاستجابة لله وللرسول، فقال: {واعلموا أنَّ الله يَحول بين المرء وقلبِهِ}: فإياكم أن تردُّوا أمر الله أول ما يأتيكم، فيُحال بينكم وبينه إذا أردتموه بعد ذلك، وتختلف قلوبكم؛ فإن الله يَحولُ بين المرء وقلبه؛ يقلِّب القلوب حيث شاء، ويصرِّفها أنَّى شاء، فليكثرِ العبد من قول: يا مقلِّب القلوب! ثبِّتْ قلبي على دينك. يا مصرِّف القلوب! اصرفْ قلبي إلى طاعتك. {وأنَّه إليه تُحشرون}؛ أي: تُجمعون ليوم لا ريبَ فيه، فيجازي المحسن بإحسانه والمسيء بعصيانه.
{24} Yeye Mtukufu anawaamrisha waja wake Waumini yale kile ambacho imani inahitaji kutoka kwao, nacho ni kumuitikia Mwenyezi Mungu na Mtume. Yaani, kufuata yale yale waliyoyaamrisha, na kuharakisha kuyafanya hivyo na kuyalingania, na kuyaepuka yale waliyoyakataza, na kukomeka nayo, na kuyakataza. Na kauli yake: "anapowaitia yenye kuwahuisha'" ni maelezo yaliyomo katika kila alichoitia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kubainisha faida yake na hekima yake. Kwa maana, uhai wa moyo na roho ni kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu na kushikamana na kumtii Yeye na kumtii Mtume Wake daima. Kisha akatahadharisha juu ya kutomwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume, akasema: "Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huzuia kati ya mtu na moyo wake.” Basi jihadharini na kuikataa amri ya Mwenyezi Mungu mara ya kwanza linapowajia, kwa hivyo ikazuilika baina yenu nayo, mtakapoitaka baada ya hayo, na nyoyo zenu zikabadilika. Kwa maana Mwenyezi Mungu huzuia kati ya mtu na moyo wake. Anazigeuza nyoyo popote anapotaka, na anazielekeza popote atakapo. Basi mja na aseme kwa wingi: Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo! Uimarishe moyo wangu juu ya dini yako. Ewe Mwenye kuelekeza mioyo! Uelekeze moyo wangu kukutii Wewe. "Na kwamba hakika kwake Yeye mtakusanywa.” Yaani, mtakusanywa kwa ajili ya siku isiyokuwa na shaka yoyote ndani yake, kisha amlipe mwema kwa wema wake, na mtenda mabaya kwa maasia yake.
#
{25} {واتَّقوا فتنةً لا تُصيبَنَّ الذين ظلموا منكم خاصةً}: بل تصيب فاعل الظُّلم وغيره، وذلك إذا ظهر الظلم فلم يغيَّر؛ فإنَّ عقوبته تعمُّ الفاعل وغيره. وتقوى هذه الفتنة بالنهي عن المنكر وقمع أهل الشرِّ والفساد وأن لا يُمَكَّنوا من المعاصي والظُّلم مهما أمكن. {واعلموا أنَّ الله شديدُ العقاب}: لمن تعرَّض لمساخطِهِ وجانبَ رضاه.
{25} "Na jikingeni na Fitna ambayo haitawasibu wale waliodhulumu pekee miongoni mwenu." Bali utampata mwenye kudhulumu na wengineo, na hilo ni ikiwa dhulma itadhihirika na isibadilishwe. Kwa maana, adhabu yake inamuenea aliyetenda na wengineo. Na kujiepusha na mtihani huu unakuwa kwa kukataza maovu na kuwakomesha watu maovu na uharibifu, na kwamba wasiwezeshwe kutenda maasia na dhulma kiasi iwezekanavyo. "Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu,” kwa mwenye kuyaendea yamkasirishayo na akajitenga na radhi yake.
: 26 #
{وَاذْكُرُوا إِذْ أَنْتُمْ قَلِيلٌ مُسْتَضْعَفُونَ فِي الْأَرْضِ تَخَافُونَ أَنْ يَتَخَطَّفَكُمُ النَّاسُ فَآوَاكُمْ وَأَيَّدَكُمْ بِنَصْرِهِ وَرَزَقَكُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ (26)}.
26. Na kumbukeni mlipokuwa wachache, mkidhoofishwa katika ardhi, mkiogopa kwamba watu watawanyakua, naye akawapa pahali pazuri pa kukaa, na akawaunga mkono kwa nusura yake, na akawaruzuku katika vilivyo vizuri ili mshukuru.
#
{26} يقول تعالى ممتنًّا على عباده في نصرهم بعد الذِّلَّة وتكثيرهم بعد القِلَّة وإغنائهم بعد العيلة: {واذكُروا إذ أنتم قليلٌ مستَضْعَفون في الأرض}؛ أي: مقهورون تحت حكم غيركم، {تخافون أن يَتَخَطَّفَكُم الناسُ}؛ أي: يأخذونكم، {فآواكم وأيَّدكم بنصرِهِ ورَزَقَكم من الطّيِّبات}: فجعل لكم بلداً تأوون إليه، وانتصر من أعدائكم على أيديكم، وغنمتم من أموالهم ما كنتم به أغنياء، {لعلَّكم تشكرونَ}: الله على مِنَّتِهِ العظيمة وإحسانه التامِّ بأن تعبدوه، ولا تشركوا به شيئاً.
{26} Yeye Mtukufu anasema akiwakumbusha waja wake neema yake ya kuwanusuru baada ya udhalilifu, na kuwafanya wawe wengi kwake baada ya uchache wao, na kuwatajirisha kwake baada ya umaskini wao. "Na kumbukeni mlipokuwa wachache, mkidhoofishwa katika ardhi,” yaani, mlipokuwa mnakandamizwa chini ya utawala wa wasiokuwa nyinyi, "mkiogopa kwamba watu watawanyakua.” Yaani, kuwachukua, "naye akawapa pahali pazuri pa kukaa, na akawaunga mkono kwa nusura yake, na akawaruzuku katika vilivyo vizuri." Basi akawafanyia nchi mnayoweza kukaa, na akawashindia maadui zenu mikononi mwenu, na mkachukua ngawira kutoka katika mali zao ambazo kwazo mlitajirika "ili mshukuru" Mwenyezi Mungu kwa neema yake kubwa na ihsan yake kamili kwa kumuabudu, wala msimshirikishe na chochote.
: 27 - 28 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ (27) وَاعْلَمُوا أَنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ (28)}.
27. Enyi mlioamini! Msimhini Mwenyezi Mungu na Mtume, na mkahini amana zenu, hali ya kuwa mnajua. 28. Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni mtihani, na kwamba Mwenyezi Mungu ana ujira mkubwa kwake.
#
{27} يأمر تعالى عباده المؤمنين أن يؤدُّوا ما ائتمنهم الله عليه من أوامره ونواهيه؛ فإنَّ الأمانة قد عرضها الله على السماوات والأرض والجبال فأبَيْنَ أن يَحْمِلْنها وأشفَقْنَ منها وحملها الإنسانُ إنَّه كان ظلوماً جهولاً؛ فمن أدَّى الأمانة؛ استحقَّ من الله الثواب الجزيل، ومن لم يؤدِّها، بل خانها؛ استحقَّ العقاب الوبيل، وصار خائناً لله وللرسول ولأمانته، منقصاً لنفسه بكونه اتَّصفت نفسه بأخس الصفات وأقبح الشيات، وهو الخيانة، مفوتاً لها أكمل الصفات وأتمها، وهي الأمانة.
{27} Yeye Mtukufu anawaamuru waja Wake Waumini kwamba watekeleze yale aliyowapa kama amani miongoni mwa maamrisho yake na makatazo yake. Kwani Mwenyezi Mungu aliiweka amana kwa mbingu zote, na ardhi, na milima, lakini vikakataa kuibeba, na vikaiogopa, lakini mwanadamu akaibeba, naye hakika alikuwa dhalimu na mjinga. Kwa hivyo, mwenye kutimiza amana, basi anastahiki thawabu nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na asiyeitekeleza, bali aliihini, basi anastahiki adhabu ya kutisha, na anakuwa haini kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume, na amana yake. Mwenye kuipunguza nafsi yake kwa kuwa nafsi yake ilisifika kwa sifa za chini kabisa na dhambi mbaya zaidi, nao ni uhaini, mwenye kuikosesha sifa kamilifu zaidi na tumilifu zaidi zake, nayo ni amana.
#
{28} ولما كان العبد ممْتَحَناً بأمواله وأولاده، فربما حمله محبَّتهُ ذلك على تقديم هوى نفسه على أداء أمانته؛ أخبر الله تعالى أنَّ الأموال والأولاد فتنةٌ يبتلي الله بهما عباده، وأنها عاريَّة ستؤدَّى لمن أعطاها وتردُّ لمن استَوْدَعَها. {وأنَّ الله عنده أجرٌ عظيمٌ}: فإن كان لكم عقلٌ ورأيٌ؛ فآثِروا فضله العظيم على لذَّة صغيرةٍ فانيةٍ مضمحلَّةٍ؛ فالعاقل يوازِنُ بين الأشياء، ويؤثِرُ أولاها بالإيثار وأحقَّها بالتقديم.
{28} Na kwa vile mja anajaribiwa kwa mali zake na watoto wake, basi pengine mapenzi yake kwa hayo yakampelekea kutanguliza matamanio ya nafsi yake mbele ya kutekeleza amana yake, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa mali na watoto ni mtihani ambayo Mwenyezi Mungu anawaribu kwayo waja wake. Na kwamba hayo ni cha kuazima kitakachorudishwa kwa yule aliyekitoa na kitarudishwa kwa aliyekiweka ili kihifadhiwe. “Na kwamba Mwenyezi Mungu ana ujira mkubwa kwake.” Kwa hivyo, ikiwa nyinyi mna akili na maoni, Basi ipendeleeni fadhila yake kubwa zaidi kuliko starehe ndogo, ya kwisha na kudhoofika. Basi Mwenye akili hulinganisha baina ya vitu, na anapendelea kinachostahili chake zaidi na kinachostahiki zaidi kutangulizwa.
: 29 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَتَّقُوا اللَّهَ يَجْعَلْ لَكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ (29)}.
29. Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuo, na atawasitiria mabaya yenu,na awafutie dhambi, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.
#
{29} امتثالُ العبد لتقوى ربه عنوان السعادة وعلامة الفلاح، وقد رتَّب اللَّه على التقوى من خير الدنيا والآخرة شيئاً كثيراً، فذكر هنا أنَّ مَن اتَّقى اللَّه؛ حصل له أربعةُ أشياء، كلُّ واحدٍ منها خيرٌ من الدنيا وما فيها: الأول: الفُرقان، وهو العلم والهدى الذي يفرِّق به صاحبه بين الهدى والضلال والحقِّ والباطل والحلال والحرام وأهل السعادة من أهل الشقاوة. الثاني والثالث: تكفير السيئات ومغفرة الذنوب، وكل واحد منهما داخلٌ في الآخر عند الإطلاق، وعند الاجتماع يفسَّر تكفير السيئات بالذُّنوب الصغائر، ومغفرة الذنوب بتكفير الكبائر. الرابع: الأجر العظيم والثوابُ الجزيل لمن اتَّقاه وآثر رضاه على هوى نفسه. {والله ذو الفضل العظيم}.
{29} Kutekeleza kwa mja uchaji wa Mola wake Mlezi ni anuani ya furaha na alama ya kufaulu. Na Mwenyezi Mungu ameuwekea uchamungu katika heri nyingi za duniani na akhera. Kwa hiyo akataja hapa kwamba anayemcha Mwenyezi Mungu, anapata mambo manne, kila moja yake ni bora zaidi kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. La kwanza ni kipambanuo, nacho ni elimu na uwongofu ambao kwayo mwenyewe hupambanua baina ya uwongofu na upotovu, na haki na batili, na halali na haramu, na watu wa furaha kutokana na watu wa taabu. Ya pili na ya tatu ni kufuta mabaya na kusitiri dhambi. Na kila moja miongoni mwa hayo linaingia katika linginelo likiwa halikufungiwa, lakini yanatajwa yote kwa pamoja, kufuta kunakuwa kwa dhambi ndogo, na kusitiri dhambi kunakuwa kwa kufuta madhambi makubwa. La nne ni malipo makubwa na thawabu nyingi kwa mwenye kumcha na akaipendelea ridha yake kuliko matamanio ya nafsi yake. “Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.”
: 30 #
{وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ (30)}.
30. Na walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe. Na wakapanga vitimbi vyao, naye Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi vyake. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa wapangao vitimbi.
#
{30} أي: {و} اذكر أيُّها الرسول ما مَنَّ الله بك عليك، {إذ يَمْكُرُ بك الذين كفروا}: حين تشاور المشركون في دار الندوة فيما يصنعون بالنبيِّ - صلى الله عليه وسلم -: إما أن يُثْبِتوه عندهم بالحبس ويوثِقوه، وإما أن يقتلوه فيستريحوا بزعمهم من شرِّه! وإما أن يخرِجوه ويُجْلوه من ديارهم؛ فكلٌّ أبدى من هذه الآراء رأياً رآه، فاتفق رأيُهم على رأي رآه شريرهم أبو جهل لعنه الله، وهو أن يأخذوا من كلِّ قبيلةٍ من قبائل قريش فتى، ويعطوه سيفاً صارماً، ويقتله الجميع قِتلةَ رجل واحدٍ؛ ليتفرَّق دمُهُ في القبائل، فيرضى بنو هاشم ثَمَّ بديتِهِ، فلا يقدرون على مقاومة جميع قريش ، فترصَّدوا للنبي - صلى الله عليه وسلم - في الليل ليوقعوا به إذا قام من فراشه، فجاءه الوحي من السماء، وخَرَجَ عليهم، فَذَرَّ على رؤوسهم التراب وخرج، وأعمى الله أبصارهم عنه، حتى إذا استبطؤوه؛ جاءهم آتٍ وقال: خيَّبكم الله! قد خرج محمدٌ وذَرَّ على رؤوسكم الترابَ! فنفض كلٌّ منهم التراب [عن] رأسه ، ومنع الله رسولَه منهم، وأذِنَ له في الهجرة إلى المدينة، فهاجر إليها، وأيَّده الله بأصحابه المهاجرين والأنصار، ولم يزل أمره يعلو حتى دخل مكة عنوةً وقَهَرَ أهلها فأذعنوا له وصاروا تحت حكمِهِ بعد أن خرج مستخفياً منهم خائفاً على نفسه؛ فسبحان اللطيف بعبده الذي لا يغالبه مغالبٌ. وقوله:
{30} Yaani, "Na" kumbuka, ewe Mtume, yale aliyokuneemesha kwayo Mwenyezi Mungu, "walipokufanyia vitimbi wale waliokufuru" wakati waliposhauriana washirikina katika Dar An-Nadwah kuhusu yale watakayomfanyia Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Ima wamweke chini ya ulinzi wao kwa kumzuia na kumfunga, au wamuue ili wapumzike kutokana na uovu wake kwa madai yao! Au wamtoe na wamfukuze kutoka katika nchi yao. Na kila mmoja alitoa katika rai hizi rai aliyoiona, na rai zao zikaafikiana juu ya rai ambayo aliyoiona muovu wao zaidi, Abu Jahl, Mwenyezi Mungu amlaani. Nayo ni kwamba, wachukue kutoka katika kila kabila la Kiquraishi mvulana, na wampe upanga mkali, kisha wamwue wote kuua kwa mwanamume mmoja, ili damu yake itawanyike kati ya makabila hayo, ndiyo Banu Hashim waridhike hapo tu na mali ya damu yake, na wasiweze kupambana na Maquraishi wote. Kwa hivyo wakamvizia Nabii - rehema na amani ziwe juu yake - usiku ili wamshambulie atakapoamka kutoka katika kitanda chake. Lakini ukamjia wahyi kutoka mbinguni, na akawatokea, kisha akawanyunyizia udongo juu ya vichwa vyao, na akaondoka. Na Mwenyezi Mungu akawapofusha macho yao wasimwone mpaka walipomuona amechelewa, mwenye kuwajia mmoja akawajia na kusema: Mwenyezi Mungu amewafanya kuambulia patupu! Hakika Muhammad ameshatoka na akanyunyizia vumbi juu ya vichwa vyenu! Basi kila mmoja wao akatikisa mavumbi kutoka kwenye kichwa chake, na Mwenyezi Mungu akamzuia Mtume wake, na akampa ruhusa ya kuhama kwenda Madina. Akahamia huko, na Mwenyezi Mungu akamuunga mkono kwa maswahaba wake, Wahajiri na Ansari. Na jambo lake halikuacha kuendelea kupanda juu mpaka alipoingia Makka kwa nguvu, na akawashinda watu wake, kwa hivyo wakajisalimisha kwake na kuwa chini ya hukumu yake baada ya kutoka kwa kujificha wasimuone. Basi ametakasika Yule ambaye ni Mpole kwa mja wake, ambaye hashindwi mwenye kushinda. Na kauli yake:
: 31 - 34 #
{وَإِذَا تُتْلَى عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا قَالُوا قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَاءُ لَقُلْنَا مِثْلَ هَذَا إِنْ هَذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (31) وَإِذْ قَالُوا اللَّهُمَّ إِنْ كَانَ هَذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِنْدِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (32) وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنْتَ فِيهِمْ وَمَا كَانَ اللَّهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ (33) وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (34)}.
31. Na wanaposomewa Aya zetu, wao husema: Hakika tumesikia. Lau tungetaka, tungesema mfano wa haya. Haya si chochote isipokuwa ngano za wa mwanzo. 32. Na waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu. 33. Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba kusitiriwa dhambi. 34. Lakini wana nini hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu, wala wao hawakuwa ndio walinzi wake? Bali walinzi wake si isipokuwa wachamungu tu, lakini wengi wao hawajui.
#
{31} يقول تعالى في بيان عناد المكذِّبين للرسول - صلى الله عليه وسلم -: {وإذا تُتْلى عليهم آياتُنا}: الدالَّة على صدق ما جاء به الرسول، {قالوا قد سَمِعْنا لو نشاء لَقُلْنا مثل هذا إن هذا إلا أساطيرُ الأوَّلين}: وهذا من عنادهم وظلمهم؛ وإلاَّ؛ فقد تحدَّاهم الله أن يأتوا بسورة من مثله، ويدعوا من استطاعوا من دون الله، فلم يقدروا على ذلك، وتبيَّن عجزهم؛ فهذا القول الصادر من هذا القائل مجرَّد دعوى كذَّبه الواقع، وقد علم أنه - صلى الله عليه وسلم - أميٌّ، لا يقرأ، ولا يكتب، ولا رحل ليدرس من أخبار الأولين، فأتى بهذا الكتاب الجليل الذي لا يأتيه الباطل من بين يديه ولا من خلفه تنزيلٌ من حكيم حميدٍ.
{31} Yeye Mtukufu anasema katika kubainisha ukaidi wa wale wanaomkadhibisha Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: - "Na wanaposomewa Aya zetu" zenye kuonyesha ukweli wa yale aliyosema Mtume, "wao husema: Hakika tumesikia. Lau tungetaka, tungesema mfano wa haya. Haya si chochote isipokuwa ngano za wa mwanzo.” Na hili ni kutokana na ukaidi wao na dhuluma yao. La sivyo, basi Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto kwamba waje na sura mfano wake, na wamuite wale wanaoweza kando na Mwenyezi Mungu, lakini hawakuweza kufanya hivyo, na kukadhihirika kutoweza kwao. Na kauli hii iliyotoka kwa msemaji huyu ni madai matupu ambayo yalikadhibishwa na uhakika wa mambo. Na tayari ilikwisha julikana kwamba yeye rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake hajui kusoma na kuandika, wala hakutoka kwenda kusoma katika habari za wa mwanzo, ndiyo akaja na kitabu hiki kitukufu ambacho hakijiwi na batili kwa mbele yake wala kwa nyuma yake, ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima kubwa, Msifiwa sana.
#
{32} {وإذْ قالوا اللهمَّ إن كان هذا}: الذي يدعو إليه محمدٌ، {هو الحقَّ من عندك فأمطِرْ علينا حجارةً من السماء أو ائتِنا بعذابٍ أليم}: قالوه على وجه الجزم منهم بباطلهم، والجهل بما ينبغي من الخطاب؛ فلو أنَّهم إذا قاموا على باطلهم من الشبه والتمويهات ما أوجب لهم أن يكونوا على بصيرةٍ ويقينٍ منه قالوا لمن ناظَرَهم وادَّعى أن الحقَّ معه: إنْ كان هذا هو الحقَّ من عندك؛ فاهِدنا له؛ لكان أولى لهم وأستر لظلمهم؛ فمذ قالوا: {اللهمَّ إن كان هذا هو الحقَّ من عندك ... } الآية؛ عُلم بمجرَّد قولهم أنهم السفهاء الأغبياء الجهلة الظالمون.
{32} "Na waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya" ambayo Muhammad anayaligania, "ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu." Waliyasema kwa njia ya kuwa na uhakika juu ya batili yao, na kutojua yale yanayopaswa kusemwa. Na lau kuwa wangesimamisha juu ya batili yao miongoni mwa fikira potofu na kuficha ukweli kile ambacho kingewafanya wawe na ufahamu na yakini juu yake, basi wangemwambia mwenye kuwajadili na akadai kwamba haki iko pamoja naye. “Ikiwa hii ndiyo haki kutoka kwako, basi tuongoze kuiendea;” ingefailia zaidi kwao na yenye kusitiri zaidi udhalimu wao. Na kwa kuwa walisema, "Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako..." hadi mwisho wa aya, ikajulikana mara tu kwa kauli yao hiyo kwamba wao ndio wapumbavu, na wajinga, wasiojua, madhalimu.
#
{33} فلو عاجلهم الله بالعقاب؛ لما أبقى منهم باقيةً، ولكنَّه تعالى دَفَعَ عنهم العذابَ بسبب وجود الرسول بين أظهرهم، فقال: {وما كان الله لِيُعَذِّبَهم وأنت فيهم}: فوجوده - صلى الله عليه وسلم -[بين أظهرهم] أمَنَةٌ لهم من العذاب، وكانوا مع قولهم هذه المقالة التي يظهِرونها على رؤوس الأشهاد يدرون بقُبحها، فكانوا يخافون من وقوعها فيهم، فيستغفرونَ الله تعالى؛ فلهذا قال: {وما كان الله ليُعَذِّبَهم وهم يستغفرونَ}: فهذا مانعٌ يمنع من وقوع العذاب بهم بعدما انعقدتْ أسبابُه.
{33} Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwaharakishia adhabu, basi asingebakisha miongoni mwa yeyote mwenye kubaki, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwazuilia adhabu kwa sababu ya kuwepo kwa Mtume miongoni mwao. Kwa hivyo akasema: "Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao" kwa hivyo uwepo wake yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - [miongoni mwao] ni amani kwao kutokana na adhabu. Na walikuwa pamoja na kusema kwao maneno haya ambayo wanayadhihirisha mbele ya kila wanaoshuhudia huku wakijua ubaya wake, basi wakawa wanahofu kuwatokea kwake, kwa hivyo wakamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwasitiria dhambi. Na ndiyo maana akasema: "Na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba kusitiriwa dhambi." Basi hiki ni kizuizi kinachozuia adhabu kutokea juu yao baada ya sababu zake kupatikana tayari.
#
{34} ثم قال: {وما لهم أن لا يعذِّبَهم الله}؛ أي: أيُّ شيء يمنعُهم من عذاب الله وقد فعلوا ما يوجِبُ ذلك؟ وهو صدُّ الناس عن المسجد الحرام، خصوصاً صدَّهم النبي - صلى الله عليه وسلم - وأصحابه الذين هم أولى به منهم، ولهذا قال: {وما كانوا}؛ أي: المشركون، {أولياءه}: يُحتمل أنَّ الضمير يعود إلى الله؛ أي: أولياء الله، ويحتمل أن يعود إلى المسجد الحرام؛ أي: وما كانوا أولى به من غيرهم. {إن أولياؤُهُ إلا المتَّقون}: وهم الذين آمنوا بالله ورسوله وأفردوا الله بالتوحيد والعبادة وأخلصوا له الدين. {ولكنَّ أكثرهم لا يعلمونَ}: فلذلك ادَّعوا لأنفسهم أمراً غيرُهم أولى به.
{34} Kisha akasema, "Lakini wana nini hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu?" Yaani, ni kitu gani kitakachowazuia kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu na tayari wameshafanya yenye kusababisha hilo? Nalo ni kuwazuia watu na Msikiti Mtakatifu, na hasa kumzuia kwao Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na maswahaba wake ambao ndio wanaustahili zaidi kuwaliko wao. Na ndiyo maana akasema: "Wala wao hawakuwa," yaani, washirikina hao, "walinzi wake." Inawezekana kwamba ‘wake’ inamrudia Mwenyezi Mungu, yaani, walinzi wa Mwenyezi Mungu. Na inawezekana kwamba anaurudia Msikiti Mtakatifu, yaani, hawakuwa wenye kuustahili zaidi kuliko wengineo. "Bali walinzi wake si isipokuwa wachamungu tu," nao ni wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamshirikisha Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uchamungu na ibada na wakamwokoa katika dini. Lakini wengi wao hawajui: Basi wakajidai wenyewe kitu ambacho wengine wanastahiki zaidi.
: 35 #
{وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِنْدَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنْتُمْ تَكْفُرُونَ (35)}.
35. Na hakukuwa kuswalia kwao kwenye hiyo Nyumba (Al-Kaaba) isipokuwa ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.
#
{35} يعني: أن الله تعالى إنما جعل بيته الحرام ليقامَ فيه دينُه وتُخْلَصَ له فيه العبادة؛ فالمؤمنون هم الذين قاموا بهذا الأمر، وأما هؤلاء المشركون الذين يصدُّون عنه؛ فما كان صلاتُهم فيه، التي هي أكبر أنواع العبادات {إلَّا مُكاءً وتصديةً}؛ أي: صفيراً وتصفيقاً؛ فعلَ الجهلة الأغبياء، الذين ليس في قلوبهم تعظيمٌ لربِّهم ولا معرفة بحقوقه ولا احترام لأفضل البقاع وأشرفها؛ فإذا كانت هذه صلاتهم فيه؛ فكيف ببقيَّة العبادات؟! فبأيِّ شيء كانوا أولى بهذا البيت من المؤمنين، الذين هم في صلاتهم خاشعون، والذين هم عن اللغو معرضون؟! ... إلى آخر ما وصفهم الله به من الصفات الحميدة والأفعال السديدة لا جرم أورثهم الله بيته الحرام ومكَّنهم منه، وقال [لهم] بعدما مكَّن لهم فيه: {يا أيُّها الذين آمنوا إنَّما المشركون نَجَسٌ فلا يَقْرَبوا المسجدَ الحرامَ بعد عامهم هذا}، وقال هنا: {فذوقوا العذابَ بما كنتُم تكفرون}.
{35} Inamaanisha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliifanya Nyumba yake Takatifu ili kuisimamisha ndani yake dini yake na kumwepekesha katika ibada humo. Basi Waumini ndio waliofanya jambo hili, na ama washirikina hawa ambao wanaizuilia, basi hakukuwa kuswali kwao ndani yake ambako ndiko aina kubwa zaidi ya ibada zote "isipokuwa ni kupiga miunzi na makofi;" ambayo ni matendo ya kijahiliya (zama za ujinga), ambao hawana katika mioyo yao kumtukuza Mola wao Mlezi, wala kujua haki zake, wala kupaheshimu mahali bora zaidi na patukufu pake zaidi. Kwa hivyo ikiwa hii ndiyo swala yao ndani yake, basi vipi ibada zinginezo? Basi ni kwa kitu gani walikuwa ndio wanaoistahiki zaidi nyumba hii kuliko Waumini, ambao wao hunyenyekea katika sala zao, na ambao huyapa mgongo mambo ya upuuzi?... hadi mwisho wa yale aliyowaelezea kwayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa sifa njema na matendo yaliyo sawa. Na hakuna shaka yoyote kwamba Mwenyezi Mungu aliwarithisha Nyumba Yake Tukufu na akawawezesha wao juu yake, na akawaambia baada ya kuwawezesha ndani yake: "Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu." Na hapa akasema: "Basi onjeni adhabu kwa yale mliyokuwa mkiyakufuru."
: 36 - 37 #
{إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنْفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنْفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ (36) لِيَمِيزَ اللَّهُ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ الْخَبِيثَ بَعْضَهُ عَلَى بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُ فِي جَهَنَّمَ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ (37)}.
36. Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili waizuilie Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam. 37. Ili Mwenyezi Mungu awapambanue waovu kutokana na wazuri, na awaweke waovu juu ya waovu wengine, na awarundike wote pamoja, na awatie katika Jahannam. Hao ndio waliohasirika.
#
{36} يقول تعالى مبيناً لعداوة المشركين وكيدهم ومكرهم ومبارزتهم لله ولرسوله وسعيهم في إطفاء نوره وإخماد كلمتِهِ، وأنَّ وبالَ مكرِهم سيعود عليهم، ولا يَحيقُ المكر السِّيئ إلاَّ بأهله، فقال: {إنَّ الذين كفروا ينفقون أموالَهم لِيَصُدُّوا عن سبيل الله}؛ أي: ليبطلوا الحقَّ، وينصروا الباطل، ويَبْطُلَ توحيدُ الرحمن، ويقومَ دينُ عبادة الأوثان. {فسينفقونها}؛ أي: فسيصدِرون هذه النفقة، وتَخِفُّ عليهم، لتمسُّكهم بالباطل، وشدة بغضهم للحق، ولكنها ستكون {عليهم حسرةً}؛ أي: ندامةً وخزياً وذلاًّ، {ثم يُغْلَبون}: فتذهب أموالهم وما أمَّلوا، ويعذَّبون في الآخرة أشدَّ العذاب، ولهذا قال: {والذين كفروا إلى جهنَّم يُحشرون}؛ أي: يجمعون إليها ليذوقوا عذابها، وذلك لأنَّها دار الخبث والخبثاء.
{36} Anasema Yeye Mtukufu akibainisha uadui wa washirikina, na njama zao, na vitimbi vyao, na kuwatokea vita kwao Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kuwania kwao katika kuzima nuru Yake na kuuzima neno Lake, na kwamba janga la hila zao litawarudia, na hila mbaya haisumbuliwi ila familia yake. Na akasema: "Hakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili waizuilie Njia ya Mwenyezi Mungu." Yaani, ili waibatilishe haki, na wainusuru batili, na wabatilishe kumpwekesha Mwingi wa rehema, na isimame dini ya kuabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu (masanamu). "Basi watazitoa;" yaani, watayatoa matumizi haya na itapunguzwa kwao, kwa sababu ya kufuata kwao uongo, na ukali wa chuki yao ya ukweli, lakini itakuwa juu yao kuvunja moyo. Yaani, majuto, aibu na fedheha, "basi watashinda." Kwa hivyo, fedha zao na yale waliyoyatarajia yatakwenda, na watateswa katika Akhera adhabu kali zaidi, na hii ndiyo sababu alisema: "Na wale waliokufuru Jahannamu watapigwa."
#
{37} والله تعالى يريد أن يَميز الخبيثَ من الطيب، ويجعلَ كلَّ واحدةٍ على حِدَةٍ وفي دار تخصُّه، فيجعل الخبيث بعضه على بعض من الأعمال والأموال والأشخاص، {فَيَرْكُمَهُ جميعا فيجعله في جهنم أولئك هم الخاسرون}: الذين خسروا أنفسهم وأهليهم يوم القيامة، ألا ذلك هو الخسران المبين.
{37} Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka kuwapambanua waovu na wazuri, na amfanye kila mmoja kuwa peke yake, na katika katika nyumba maalumu kwake. Kwa hivyo afanye viovu baadhi yake kwa baadhi yake miongoni mwa matendo, na mali, na watu, “kisha awarundike wote pamoja, na awatie katika Jahannam. Hao ndio waliohasirika.” Wale waliohasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Qiyama. Tazama, huku ndiko kuhasiri kwa wazi.
: 38 - 40 #
{قُلْ لِلَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ يَنْتَهُوا يُغْفَرْ لَهُمْ مَا قَدْ سَلَفَ وَإِنْ يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ (38) وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ فَإِنِ انْتَهَوْا فَإِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (39) وَإِنْ تَوَلَّوْا فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَوْلَاكُمْ نِعْمَ الْمَوْلَى وَنِعْمَ النَّصِيرُ (40)}.
38. Waambie wale waliokufuru ikiwa watakoma, watasitiriwa yale yaliyokwisha pita. Na wakiyarudia, basi hakika imekwisha pita mifano ya wa mwanzo. 39. Na piganeni nao mpaka kusiwepo majaribio na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayayatenda. 40. Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema.
#
{38} هذا من لطفه تعالى بعباده؛ لا يمنعُهُ كفرُ العباد ولا استمرارُهم في العناد من أن يدعُوهم إلى طريق الرشاد والهدى وينهاهم عما يُهْلِكُهم من أسباب الغيِّ والرَّدى، فقال: {قل للذين كفروا إن يَنتَهوا}: عن كفرهم، وذلك بالإسلام لله وحده لا شريك له، {يُغْفَرْ لهم ما قد سَلَفَ}: منهم من الجرائم. {وإن يعودوا}: إلى كفرِهم وعنادهم، {فقد مضتْ سُنَّةُ الأولين}: بإهلاك الأمم المكذِّبة؛ فلينتظروا ما حلَّ بالمعاندين؛ فسوف يأتيهم أنباءُ ما كانوا به يستهزئون. فهذا خطابُهُ للمكذِّبين.
{38} Hili ni kulutokana na wema wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, haimzuii kutoka kwa ukafiri wa watumishi wala kuendelea kwao kwa ukaidi kuwaita kwenye njia ya uwongofu na uwongofu, na kuwakataza na yale yanayowaangamiza kutokana na sababu za ubatili na uasi. Basi akasema "Waambie wale waliokufuru kwamba wanaishia," kuhusu kufuru yao, na kwamba Uislamu ni wa Mwenyezi Mungu pekee hauna mshirika, "wasamehe yale ambayo tayari yamekwisha fanyika;" baadhi yao ya uhalifu. "Na wakirudi;" kwa ukafiri wao na ukaidi wao, "basi hakika imekwisha pita mifano ya wa mwanzo;" kwa uharibifu wa mataifa ya uongo, na wasubiri kile kilichowapata wale walio na ukaidi. Hii ni kauli yake kwa waongo.
#
{39} وأمَّا خطابه للمؤمنين عندما أمرهم بمعاملة الكافرين؛ فقال: {وقاتلوهم حتى لا تكونَ فتنةٌ}؛ أي: شركٌ وصدٌّ عن سبيل الله، ويذعنوا لأحكام الإسلام. {ويكونَ الدِّينُ كلُّه لله}: فهذا المقصود من القتال والجهاد لأعداء الدين: أن يُدْفَعَ شرُّهم عن الدين، وأن يُذَبَّ عن دين الله الذي خَلقَ الخلق له، حتى يكون هو العالي على سائر الأديان. {فإن انتهوا}: عن ما هم عليه من الظلم، {فإنَّ الله بما يعملون بصير}: لا تخفى عليه منهم خافيةٌ.
{39} Na ama kuhusu kuwaongelesha kwake waumini alipowaamrisha kuamiliana na makafiri, akasema, "Na piganeni nao mpaka yasiwepo majaribio." Yaani, shirki na kuizuia Njia ya Mwenyezi Mungu, na kwamba watii hukumu za Uislamu. "Na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Basi hili ndilo linalokusudiwa katika kupigana vita na Jihadi dhidi ya maadui wa dini. Kwamba uzuie uovu wao kutoka kwa dini, na kwamba itetewe dini ya Mwenyezi Mungu ambayo waliumbwa viumbe kwa ajili yake, mpaka iwe hiyo ndiyo ya juu zaidi kuliko dini nyingine zote. "Wakikomeka" wakaacha yale wanayofanya ya udhalimu, "basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda" wala hayafichiki kwake chochote kutoka kwao.
#
{40} {وإن تولَّوا}: عن الطاعة، وأوضعوا في الإضاعة، {فاعلموا أنَّ الله مولاكم نعم المولى}: الذي يتولَّى عباده المؤمنين، ويوصِلُ إليهم مصالحهم وييسِّر لهم منافعهم الدينيَّة والدنيويَّة. {ونعم النصيرُ}: الذي ينصُرُهم فيدفع عنهم كيدَ الفجَّار وتكالب الأشرار، ومَن كان الله مولاه وناصره؛ فلا خوفٌ عليه، ومَنْ كان الله عليه؛ فلا عزَّ له ولا قائمة له.
{40} “Na wakigeuka” kutoka katika utiifu, na wakaanguka katika upotovu, "basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema sana" ambaye anawasimamia waja wake Waumini, na anawafikishia masilahi yao, na anawarahisishia manufaa yao ya kidini na ya kidunia. “Na ni Msaidizi Mwema mno” ambaye anawanusuru na anazuilia njama ya wakosefu, na vitimbi vya waovu. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wake na msaidizi wake, basi hapana hofu yoyote juu yake. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu yuko dhidi yake, basi hana utukufu wowote wala hana kisimamio chochote.
: 41 - 42 #
{وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُمْ مِنْ شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ إِنْ كُنْتُمْ آمَنْتُمْ بِاللَّهِ وَمَا أَنْزَلْنَا عَلَى عَبْدِنَا يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (41) إِذْ أَنْتُمْ بِالْعُدْوَةِ الدُّنْيَا وَهُمْ بِالْعُدْوَةِ الْقُصْوَى وَالرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنْكُمْ وَلَوْ تَوَاعَدْتُمْ لَاخْتَلَفْتُمْ فِي الْمِيعَادِ وَلَكِنْ لِيَقْضِيَ اللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَنْ بَيِّنَةٍ وَيَحْيَى مَنْ حَيَّ عَنْ بَيِّنَةٍ وَإِنَّ اللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ (42)}.
41. Na jueni ya kwamba ngawira yoyote mnayoipata, basi humusi yake ni ya Mwenyezi Mungu na ni ya Mtume, na ni ya jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mlimwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipokutana makundi yale mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. 42. Kumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa kwenye ng'ambo ya mbali, na msafara ulipokuwa chini yenu. Na ingelikuwa mliagana, basi mngelihitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe. Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio wazi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
#
{41} يقول تعالى: {واعلموا أنَّما غنمتُم من شيءٍ}؛ أي: أخذتم من مال الكفار قهراً بحقٍّ قليلاً كان أو كثيراً، {فأنَّ لله خُمُسَه}؛ أي: وباقيه لكم أيها الغانمون؛ لأنه أضاف الغنيمة إليهم، وأخرج منها خمسها، فدلَّ على أن الباقي لهم، يُقسم على ما قسمه رسول الله - صلى الله عليه وسلم -: للراجل سهمٌ، وللفارس سهمان لفرسه وسهم له، وأما هذا الخمس؛ فيقسم خمسة أسهم: سهمٌ لله ولرسوله يُصْرَف في مصالح المسلمين العامة من غير تعيين لمصلحة؛ لأنَّ الله جعله له ولرسوله، والله ورسوله غنيَّان عنه، فعُلِمَ أنه لعباد الله؛ فإذا لم يعيِّن الله له مصرفاً؛ دلَّ على أن مَصْرِفَه للمصالح العامة. والخمس الثاني: لذي القربى، وهم قرابة النبي - صلى الله عليه وسلم - من بني هاشم وبني المطلب، وأضافه الله إلى القرابة دليلاً على أنَّ العلة فيه مجرَّد القرابة، فيستوي فيه غنيُّهم وفقيرهم ذكرهم وأنثاهم. والخمس الثالث: لليتامى، وهم الذين فقدت آباؤهم وهم صغارٌ، جعل الله لهم خُمُسَ الخمس رحمةً بهم، حيث كانوا عاجزين عن القيام بمصالحهم، وقد فُقِدَ من يقوم بمصالحهم. والخمس الرابع: للمساكين؛ أي: المحتاجين الفقراء من صغار وكبار ذكور وإناث. والخمس الخامس: لابن السبيل، و [هو] الغريب المنقطَعُ به في غير بلده، وبعض المفسرين يقول: إن خمس الغنيمة لا يخرُجُ عن هذه الأصناف، ولا يلزم أن يكونوا فيه على السواء، بل ذلك تَبَعٌ للمصلحة، وهذا هو الأولى. وجعل الله أداء الخُمُس على وجهه شرطاً للإيمان، فقال: {إن كُنتم آمنتُم بالله وما أنزلْنا على عبدِنا يوم الفرقان}: وهو يوم بدرٍ، الذي فرَّق الله به بين الحقِّ والباطل، وأظهر الحقَّ وأبطل الباطل. {يوم التقى الجمعانِ}: جمع المسلمين وجمع الكافرين؛ أي: إن كان إيمانُكم بالله وبالحقِّ الذي أنزله الله على رسوله يوم الفرقان الذي حصل فيه من الآيات والبراهين ما دلَّ على أن ما جاء به هو الحقُّ. {والله على كلِّ شيء قدير}: لا يغالبه أحدٌ إلا غلبه.
{41} Yeye Mtukufu anasema, "Na jueni ya kwamba ngawira yoyote mnayoipata;” yaani, mliyochukua katika mali ya makafiri kwa nguvu, kwa hakika, iwe kidogo au nyingi, "basi humusi yake ni ya Mwenyezi Mungu." Yaani, na kilichobaki ni chenu, enyi mlioipata ngawira hiyo. Kwa sababu aliifungamanisha ngawira na wao, kisha akatoa humo humusi moja yake, kwa hivyo hilo likaonyesha kwamba kilichobaki ni chao, kitagawanywa kulingana na alivyoigawanya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake aligawanya: Fungu moja kwa mpiganaji apiganaye kwa miguu, na mafungu mawili kwa mpiganaji apiganaye kwa kupanda farasi, fungu moja kwa ajili yake, na fungu moja kwa ajili yake. Na ama humusi hii hiyo inagawanywa mafungu matano. Fungu moja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, linatumika kwa masilahi ya jumla ya Waislamu bila ya kuteua masilahi fulani, kwa sababu Mwenyezi Mungu alilifanya kuwa ni lake na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawalihitaji, kwa hivyo ikajulikana kuwa ni kwa ajili ya waja wa Mwenyezi Mungu. Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu hakuliweka kwa ajili ya masilahi fulani maalumu, basi ikajulikana kwamba hilo ni kwa ajili ya masilahi ya jumla. Nayo humusi ya pili ni kwa jamaa, ambao ni jamaa za Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kama vile Banu Hashim, na Bani Al-Muttalib. Na Mwenyezi Mungu alilifungamanisha na jamaa ili uwe ushahidi kwamba sababu ya hilo ni jamaa tu. Kwa hivyo wako sawa katika hilo, matajiri wao na masikini wao, wa kiume wao na wa kike wao. Nayo humusi ya tatu ni ya mayatima. Nao ni wale waliopoteza baba zao hali ya kuwa wao ni wadogo. Mwenyezi Mungu aliwapa humusi moja ili kuwarehemu, kwani walikuwa hawawezi kutekeleza masilahi yao, na tayari walishapoteza anayeyasimamia masilahi yao. Nayo humusi ya nne ni ya maskini. Yaani wale wanaohitaji, mafukara wadogo kwa wakubwa, wa kiume na wa kike. Nayo humusi ya tano ni ya mwana njia. Na [yeye] ni mgeni ambaye amekatikiwa katika mji usiokuwa wake. Na baadhi ya wafasiri wanasema kuwa humusi ya ngawira haitoki nje ya makundi haya, na hawahitaji kuwa sawa wote katika hilo, lakini hilo linafuatana na masilahi. Na hii ndiyo kauli ifaayo zaidi. Na Mwenyezi Mungu alifanya kuitekeleza humusi moja hiyo namna ipasavyo kuwa ni sharti ya kuwa na imani. Akasema: " ikiwa nyinyi mlimwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo." Nayo ni siku ya Badr, ambayo kwayo Mwenyezi Mungu alipambanua baina ya haki na batili, na akaidhihirisha haki, na akaibaitilisha batili. "Siku yalipokutana makundi yale mawili," kundi la Waislamu na kundi la makafiri. Yaani, ikiwa imani yenu kwa Mwenyezi Mungu na kwa haki ambayo Mwenyezi Mungu aliiteremsha kwa Mtume wake siku ya Al-Furqan, ambayo ndani yake kulitokea ishara mbalimbali na ushahidi mbalimbali yaliyoonyesha kwamba kile alichokuja nacho ndiyo haki. "Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu" hawezi yeyote kushindana naye isipokuwa Yeye atamshinda.
#
{42} {إذ أنتم بالعُدْوَةِ الدُّنيا}؛ أي: بعُدْوَة الوادي القريبة من المدينة. وهم بعدوته؛ أي: جانبه البعيدة من المدينة؛ فقد جمعكم وادٍ واحدٌ. {والركب}: الذي خرجتُم لطلبه، وأراد الله غيره {أسفلَ منكم}: مما يلي ساحل البحر. {ولو تواعدتُم}: أنتم وإيَّاهم على هذا الوصف وبهذه الحال، {لاختلفتُم في الميعادِ}؛ أي: لا بدَّ من تقدُّم أو تأخُّر أو اختيار منزل أو غير ذلك مما يعرض لكم أو لهم يصدُفُكم عن ميعادهم. ولكنَّ: اللهَ جمعكم على هذه الحال، {لِيَقْضِيَ الله أمرا كان مفعولا}؛ أي: مقدراً في الأزل لا بدَّ من وقوعه. {لِيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عن بيِّنة}؛ أي: ليكون حجَّة وبيَّنة للمعاند، فيختار الكفر على بصيرة وجزم ببطلانه، فلا يبقى له عذرٌ عند الله. {ويحيا مَنْ حَيَّ عن بيِّنةٍ}؛ أي: يزداد المؤمن بصيرةً ويقيناً بما أرى الله الطائفتين من أدلَّة الحقِّ وبراهينه ما هو تذكرة لأولي الألباب. {وإن الله لسميعٌ عليمٌ}: سميعٌ لجميع الأصوات باختلاف اللُّغات على تفنُّن الحاجات، عليمٌ بالظواهر والضمائر والسرائر والغيب والشهادة.
{42} "Kumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde;" yaani, kwenye ng’ambo ya bonde iliyo karibu na Madina. Nao walikuwa upande wake wa mbali kutoka Madina, kwa maana mlikusanywa na bonde moja. "Na msafara" mliotoka kwenda kuutafuta, na Mwenyezi Mungu akataka kinginecho "ulipokuwa chini yenu" karibu na pwani ya bahari. "Na ingelikuwa mliagana" nyinyi na wao kwa maelezo haya na katika hali hii, "basi mngelihitalifiana katika miadi." Yaani, hakungekuwa na budi kutangulia, au kuchelewesha, au kuchagua mahali pa kushukia, au mambo mengineyo ambayo yangewatokea nyinyi au wao ambayo yangewazuia na miadi yenu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwakusanya pamoja katika hali hii, "ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe." Yaani, kilipitishwa katika kitambo sana kwamba ni lazima kitokee. "Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi" yaani, ili iwe hoja iliyo wazi dhidi ya mkaidi, kwa hivyo anauchagua ukafiri kwa ufahamu, na kwa kuwa na uhakika na ubatili wake, kwa hivyo habakishi udhuru wowote kwa Mwenyezi Mungu. "Na aishi mwenye kuishi kwa ushahidi ulio wazi;" yaani, Muumini aongeze ufahamu na yakini kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwaonyesha makundi hayo mawili katika hoja juu ya haki na ushahidi wake, ambayo ni ukumbusho kwa wenye akili. "Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote." Anasikia sauti zote pamoja na kutofautiana kwa lugha zote, pamoja na kutofautiana kwa mahitaji. Ni mwenye kujua vyema ya dhahiri, na ya ndani, na yaliyofichikana, na siri, na ghaibu, na yaliyo wazi.
: 43 - 44 #
{إِذْ يُرِيكَهُمُ اللَّهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلًا وَلَوْ أَرَاكَهُمْ كَثِيرًا لَفَشِلْتُمْ وَلَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَلَكِنَّ اللَّهَ سَلَّمَ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (43) وَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ الْتَقَيْتُمْ فِي أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا وَيُقَلِّلُكُمْ فِي أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِيَ اللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ (44)}.
43. Kumbuka Mwenyezi Mungu alipokuonyesha wao katika usingizi wako kwamba wao ni wachache, na lau angelikuonyesha kuwa ni wengi, basi mngeliingiwa na woga, na mngelizozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu akawapa salama. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyo vifuani. 44. Na alipowaonyesha mlipokutana, katika macho yenu kuwa wao ni wachache, na akawafanya nyinyi ni wachache katika macho yao, ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lililokuwa lifanywe. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.
#
{43 - 44} وكان الله قد أرى رسولَه المشركين في الرؤيا العدو قليلاً، فبشَّر بذلك أصحابه، فاطمأنَّت قلوبُهم وثبتت أفئدتهم. {ولو أراكَهم اللهُ كثيراً}: فأخبرتَ بذلك أصحابك، {لَفَشِلْتُم ولَتَنازَعْتُم في الأمر}: فمنكم من يرى الإقدامَ على قتالهم ومنكم من لا يرى ذلك، والتنازع مما يوجب الفشل ، {ولكنَّ الله سلَّم}؛ أي: لطف بكم. {إنَّه عليمٌ بذات الصُّدور}؛ أي: بما فيها من ثبات وجَزَع وصدق وكذب، فعلم الله من قلوبكم ما صار سبباً للطفه وإحسانِهِ بكم وصدق رؤيا رسوله، فأرى الله المؤمنين عدوَّهم قليلاً في أعينهم، ويقلِّلكم يا معشر المؤمنين في أعينهم؛ فكلٌّ من الطائفتين ترى الأخرى قليلة؛ لِتُقْدِمَ كلٌّ منهما على الأخرى. {ليقضيَ اللهُ أمراً كان مفعولاً}: من نصر المؤمنين، وخذلان الكافرين، وقتل قادتهم ورؤساء الضلال منهم، ولم يَبْقَ منهم أحدٌ له اسم يذكر، فيتيسَّر بعد ذلك انقيادُهم إذا دُعوا إلى الإسلام، فصار أيضاً لطفاً بالباقين، الذين مَنَّ الله عليهم بالإسلام. {وإلى الله تُرْجَعُ الأمور}؛ أي: جميع أمور الخلائق تَرْجِعُ إلى الله، فَيميزُ الخبيثَ من الطيب، ويحكمُ في الخلائق بحكمه العادل الذي لا جَوْر فيه ولا ظلم.
{43-44} Na Mwenyezi Mungu alikuwa amemwonyesha Mtume wake washirikina katika ndoto kwamba maadui ni wachache, kwa hivyo akawapa masahaba wake habari hiyo njema, kwa hivyo nyoyo zao zikatulia na zikaimarika. "Na lau angelikuonyesha kuwa ni wengi" na ukawaambia hilo maswahaba wako, "basi mngeliingiwa na woga, na mngelizozana katika jambo hilo.” Baadhi yenu wangeona kwenda kupigana, na baadhi yenu wasingeona hilo. Na kuzozana ni katika yale yanayosababisha kushindwa. "Lakini Mwenyezi Mungu akawapa salama;" yaani, aliwaonea huruma. "Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyo vifuani;" yaani, yale yaliyomo ya uimara, na kutoridhika, na ukweli, na uongo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu alijua kutoka katika nyoyo zenu kile kilichokuja kuwa sababu ya huruma yake na ihsani yake kwenu, na akaisadikisha ndoto ya Mtume wake, kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawaonyesha waumini kuwa maadui zao ni wachache katika macho yao, na akawafanya kuwa wachahe, enyi Waumini katika macho yao. Kwa hivyo kila moja ya makundi haya mawili yanawaona wenziwe kuwa ni wachache, ili kila moja yake liliendee lingine kwa ajili ya vita. "Ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lililokuwa lifanywe;" la kuwanusuru Waumini, na kuwaangusha makafiri, na kuwaua viongozi wao, vichwa vya upotovu miongoni mwao, na hakuna yeyote aliyebaki miongoni mwao ambaye ana jina la kutajwa. Kwa hivyo ikawa rahisi baada ya hayo kufuata kwao wanapolinganiwa kwenye Uislamu. "Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote." Yaani, mambo yote ya viumbe yatarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo apambanue kiovu kutokana na kizuri, na awahukumu viumbe kwa hukumu yake ya uadilifu ambayo hakandamizi ndani yake wala hadhulumu.
: 45 - 49 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيرًا لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (45) وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ وَاصْبِرُوا إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ (46) وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ خَرَجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ بَطَرًا وَرِئَاءَ النَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَاللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ (47) وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ الْيَوْمَ مِنَ النَّاسِ وَإِنِّي جَارٌ لَكُمْ فَلَمَّا تَرَاءَتِ الْفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَى عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِنْكُمْ إِنِّي أَرَى مَا لَا تَرَوْنَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ وَاللَّهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ (48) إِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَإِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (49)}.
45. Enyi mlioamini! Mkikutana na kikundi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mfaulu. 46. Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri. 47. Wala msiwe kama wale waliotoka katika majumba yao kwa fahari na kujionyesha kwa watu, na wakiwazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka yote wanayoyafanya. 48. Na wakati Shetani alipowapambia vitendo vyao, na akasema, "Hakuna yeyote wa kuwashinda leo hii katika watu, nami hakika ni mlinzi wenu." Basi yalipoonana makundi mawili hayo, akarudi nyuma juu ya visigino vyake, na akasema, "Hakika mimi niko mbali sana nanyi. Hakika mimi naona msiyoyaona. Hakika mimi ninamhofu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu." 49. Waliposema wanafiki, na wale wenye ugonjwa katika nyoyo zao, "Watu hawa dini yao imewadanganya." Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{45} يقول تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا إذا لَقيتُم فئةً}؛ أي: طائفة من الكفار تقاتلكم، {فاثبُتوا}: لقتالها، واستعمِلوا الصبر وحبس النفس على هذه الطاعة الكبيرة، التي عاقبتُها العزُّ والنصر، واستعينوا على ذلك بالإكثار من ذكر اللَّه. {لعلَّكم تفلحون}؛ أي: تدركون ما تطلبون من الانتصار على أعدائكم؛ فالصبرُ والثبات والإكثار من ذِكْر الله من أكبر الأسباب للنصر.
{45} Yeye Mtukufu anasema: "Enyi mlioamini! Mkikutana na kikundi;" yaani, kundi la makafiri wanaopigana nanyi, "basi kueni imara" kwa ajili ya kupigana nacho, na itumieni subira, na kuizuilia nafsi juu ya utiifu huu mkubwa, ambao mwisho wake ni utukufu na ushindi. Na tafuteni msaada juu ya hilo katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi; "ili mfaulu." Yaani, myafikie yale mnayotafuta miongoni mwa ushindi juu ya maadui zenu. Kwa hivyo, subira, na kuimarika, na kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi ni miongoni mwa sababu kubwa zaidi za ushindi.
#
{46} {وأطيعوا الله ورسوله}: في استعمال ما أمرا به والمشي خلف ذلك في جميع الأحوال، {ولا تنازعوا}: تنازعاً يوجِبُ تشتُت القلوب وتفرقها، {فتفشلوا}؛ أي: تجبُنوا، {وتذهبَ ريحُكم}؛ أي: تنحلُّ عزائمكم وتُفرَّقُ قوتكم ويُرْفَعُ ما وُعِدتم به من النصر على طاعة الله ورسوله، {واصبروا}: نفوسَكم على طاعة الله. {إنَّ الله مع الصابرين}: بالعون والنصر والتأييد.
{46} "Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake" katika kutumia yale aliyoamrisha, na kutembea nyuma ya hayo katika hali zote, "wala msizozane" kuzozana kunakolazimu kugawanyika kwa mioyo na kutengana kwake; "mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu;" yaani, maazimio yenu yakavunjika, zikagawanyishwa nguvu zenu, na yakaondolewa yale mliyoahidiwa ya ushindi juu ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. "Na subirini" nafsi zenu katika kumtii Mwenyezi Mungu. "Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri" kwa msaada, na nusura, na kuunga mkono.
#
{47} واخشعوا لربكم واخضعوا له، {ولا تكونوا كالذين خَرَجوا من ديارهم بطراً ورِئاءَ الناس ويصدُّون عن سبيل الله}؛ أي: هذا مقصدهم الذي خرجوا إليه، وهذا الذي أبرزهم من ديارِهم؛ لقصدِ الأشَرِ والبطر في الأرض، وليراهم الناس ويفخروا لديهم، والمقصود الأعظم أنهم خرجوا ليصدُّوا عن سبيل الله من أراد سلوكه. {والله بما يعملون محيطٌ}: فلذلك أخبركم بمقاصدهم، وحذَّركم أن تشبَّهوا بهم؛ فإنه سيعاقبهم على ذلك أشدَّ العقوبة، فليكنْ قصدُكم في خروجكم وجهَ الله تعالى، وإعلاء دين الله، والصدَّ عن الطرق الموصلة إلى سَخَطِ الله وعقابِهِ، وجَذْبَ الناس إلى سبيل الله القويم الموصل لجنات النعيم.
{47} Na mumnyenyekee Mola wenu Mlezi, na mumdhalilikie, "Wala msiwe kama wale waliotoka katika majumba yao kwa fahari na kujionyesha kwa watu, na wakiwazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu.” Yaani, haya ndiyo makusudio yao ambayo walitoka kwa ajili yake, na hayo ndiyo yaliyowatoa nje ya maskani yao wakikusudia uovu na ufahari katika ardhi, na ili watu wawaone na kujivuna mbele yao. Na makusudio makubwa ni kwamba walitoka ili wamzuie njia ya Mwenyezi Mungu yule anayetaka kuifuata. “Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka yote wanayoyafanya.” Na kwa sababu ya hilo akawajulisha makusudio yao na akatahadharisha kuwaiga wao, kwa maana atawaadhibu kwa hilo adhabu kali zaidi. Basi na yawe makusudio yenu katika kutoka kwenu ni uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuiinua Dini ya Mwenyezi Mungu, na kuzuia njia zinazofikisha kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake, na kuwavutia watu kwenye njia nyoofu ya Mwenyezi Mungu inayofikisha katika mabustani ya neema.
#
{48} {وإذ زيَّنَ لهم الشيطان أعمالهم}: حسَّنها في قلوبهم [وخدعهم]، {وقال لا غالبَ لكمُ اليومَ من الناس}: فإنكم في عَدَدٍ وعُدَدٍ وهيئةٍ لا يقاومكم فيها محمدٌ ومن معه. {وإني جارٌ لكم}: من أن يأتيكم أحدٌ ممَّن تخشون غائلته؛ لأنَّ إبليس قد تبدَّى لقريش في صورة سراقة بن مالك بن جُعْشُم المدلجي، وكانوا يخافون من بني مدلج لعداوةٍ كانت بينهم، فقال لهم الشيطان: أنا جارٌ لكم! فاطمأنت نفوسُهم وأتوا على حَرْدٍ قادرينَ. فلما {تراءتِ الفئتان}: المسلمون والكافرون، فرأى الشيطان جبريلَ عليه السلام يَزَع الملائكة؛ خاف خوفاً شديداً، {ونكص على عقبيه}؛ أي: ولى مدبراً، {وقال}: لمن خدعهم وغرهم: {إني بريء منكم إني أرى ما لا ترون}؛ أي: أرى الملائكة الذين لا يدان لأحد بقتالهم؛ {إني أخاف الله}؛ أي: أخاف أن يعاجِلَني بالعقوبة في الدنيا، {والله شديد العقاب}. ومن المحتمل أن يكون الشيطان [قد] سوَّلَ لهم، ووسوس في صدورهم أنَّه لا غالبَ لهم اليوم من الناس وأنَّه جار لهم، فلما أوردهم موارِدَهم؛ نكص عنهم، وتبرَّأ منهم؛ كما قال تعالى: {كَمَثَل الشيطان إذْ قال للإنسانِ اكفُرْ فلمَّا كَفَرَ قال إنِّي بريءٌ منك إني أخافُ اللهَ ربَّ العالمين فكانَ عاقِبَتَهُما أنَّهما في النارِ خالِدَيْن فيها وذلك جزاء الظالمين}.
{48} “Na wakati Shetani alipowapambia vitendo vyao;” yaani, alivifanya kuonekana kuwa vizuri katika nyoyo zao, na akawahadaa “na akasema, "Hakuna yeyote wa kuwashinda leo hii katika watu” kwa maana, mna idadi kubwa, na maandalizi imara, na haiba ambayo Muhammad na wale walio pamoja naye hawataweza kuwapinga. "Nami hakika ni mlinzi wenu," asije akawajia yeyote miongoni mwa wale mnaohofia mashambulizi yake. Kwa sababu Iblis aliwatokea Maquraishi kwa mfano wa Suraqa bin Malik bin Jash’am Al-Mudliji, na walikuwa wakiwahofu Banu Mudlij kwa sababu ya uadui uliokuwa baina yao. Kwa hivyo Shetani akawaambia, “Mimi ni mlinzi wenu!” Kwa hivyo nafsi zao zikatulia, kwa hivyo wakaja makusudi wakidhani wana uwezo. Basi "yalipoonana makundi mawili hayo," waislamu na makafiri, na Shetani akamuona Jibril amani iwe juu yake akiwahamisha Malaika, akahofu hofu kubwa, na "akarudi nyuma juu ya visigino vyake," yaani akageuka akenda zake. "Na akasema" akiwaambia wale aliowadanganya na kuwahadaa: "Hakika mimi niko mbali sana nanyi. Hakika mimi naona msiyoyaona;" yaani, ninawaona Malaika ambao hakuna yeyote anayeweza kupigana nao. "Hakika mimi ninamhofu Mwenyezi Mungu;" yaani, ninahofu kwamba ataniadhibu kwa haraka katika dunia, “na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.” Na inawezekana kwamba Shetani aliwashawishi, na kuwatia wasiwasi katika vifua vyao kwamba hakuna yeyote wa kuwashinda leo katika watu, kwamba yeye ni mlinzi wao. Kwa hivyo alipowafikisha walipokuwa wanakwenda, akageuka akawaacha, akajitenga nao. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Ni kama mfano wa Shetani anapomwambia mtu, “Kufuru.” Na anapokufuru, humwambia: Hakika mimi niko mbali sana nawe. Hakika mimi namhofu Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao ni kwamba wako katika Moto, wadumu humo, na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.”
#
{49} {إذ يقول المنافقون والذين في قلوبهم مرضٌ}؛ أي: شكٌّ وشبهةٌ من ضعفاء الإيمان للمؤمنين حين أقدموا مع قلَّتهم على قتال المشركين مع كثرتهم: {غرَّ هؤلاء دينُهم}؛ أي: أوردهم الدينُ الذي هم عليه هذه الموارد التي لا يدان لهم بها ولا استطاعةَ لهم بها، يقولونه احتقاراً لهم واستخفافاً لعقولهم، وهم والله الأخفاءُ عقولاً الضعفاءُ أحلاماً؛ فإنَّ الإيمان يوجبُ لصاحبه الإقدام على الأمور الهائلةِ التي لا يقدِمُ عليها الجيوش العظام؛ فإنَّ المؤمن المتوكِّل على الله الذي يعلم أنه ما من حولٍ ولا قوةٍ ولا استطاعةٍ لأحدٍ إلا بالله تعالى، وأنَّ الخلق لو اجتمعوا كلُّهم على نفع شخص بمثقال ذرَّةٍ؛ لم ينفعوه، ولو اجتمعوا على أن يضرُّوه؛ لم يضرُّوه؛ إلا بشيءٍ قد كتبه الله عليه، وعلم أنَّه على الحقِّ، وأن الله تعالى حكيمٌ رحيمٌ في كلِّ ما قدَّره وقضاه؛ فإنَّه لا يبالي بما أقدم عليه من قوَّةٍ وكثرةٍ، وكان واثقاً بربِّه مطمئن القلب لا فزعاً ولا جباناً، ولهذا قال: {ومن يتوكَّلْ على الله فإنَّ الله عزيزٌ}: لا يغالِبُ قوتَه قوةٌ. {حكيمٌ}: فيما قضاه وأجراه.
{49} "Waliposema wanafiki, na wale wenye ugonjwa katika nyoyo zao;" yaani, shaka na fikira potofu miongoni mwa wenye imani dhaifu wakiwaambia Waumini wakati walipokwenda pamoja na uchache wao kupigana na washirikina pamoja na wingi wao. “Watu hawa dini yao imewadanganya." Yaani, dini ambayo wako juu yake imewafikisha mahali hapa ambapo hawawezi kufanya kitu chochote wala hawana uwezo wowote kwayo. Waliyasema kwa kuwadharau na kupuuza akili zao, ilhali wao - ninaapa kwa Mwenyezi Mungu - ndio wenye akili hafifu zaidi, wadhaifu wa akili. Kwani Imani inamlazimu mwenyewe kuyaendea mambo makubwa ambayo majeshi makubwa hayayaendei. Kwa maana, Muumini anayemtegemea Mwenyezi Mungu ambaye anajua kuwa hakuna hila, wala nguvu, wala uwezo kwa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba viumbe vyote lau kuwa vitakusanyika ili kumnufaisha mtu kwa uzito wa chembe, basi hawatamnufaisha. Na lau kuwa watakusanyika kumdhuru, basi hawatamdhuru, isipokuwa kwa kitu ambacho Mwenyezi Mungu alikwisha mwandikia na akajua kwamba hiyo ndiyo haki, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kurehemu sana katika yote aliyopitisha na akayatendesha. Basi yeye hajali yale anayoyaendea hata yakiwa ni ya nguvu na mengi, na anakuwa mwenye kumuamini Mola wake Mlezi, mwenye moyo uliotulizana, sio mwenye hofu wala mwoga. Na ndiyo maana akasema, "Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu.” Nguvu zake hazishindwi na nguvu zozote zile. "Mwenye hekima kubwa" katika yale aliyoyapitisha na kuyatendesha.
: 50 - 52 #
{وَلَوْ تَرَى إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ (50) ذَلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِلْعَبِيدِ (51) كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّهِ فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ (52)}.
50. Na laiti ungeliona Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, (na kuwaambia), "Ionjeni adhabu iunguzayo!" 51. Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyotangulizwa na mikono yenu, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja. 52. Kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawachukua kwa madhambi yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.
#
{50} يقول تعالى: {ولو ترى}: الذين كفروا بآيات الله حين توفَّاهم الملائكةُ الموكلون بقبض أرواحهم وقد اشتد بهم القلق وعظم كربهم والملائكة {يضرِبون وجوهَهم وأدبارَهم}: يقولون لهم: أخرجوا أنفسكم! ونفوسُهم متمنِّعة متعصِّية على الخروج؛ لعلمها ما أمامها من العذاب الأليم. ولهذا قال: {وذوقوا عذابَ الحريق}؛ أي: العذاب الشديد المحرق.
{50} Yeye Mtukufu anasema, "Na laiti ungeliwaona" wale waliozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu wakati wanapofishwa na Malaika waliopewa jukumu la kuchukua roho zao, na huku wasiwasi umewazidi sana, na taabu zao zikawa kubwa sana. Na huku Malaika "wakiwapiga nyuso zao na migongo yao" wakiwaambia, “Zitoeni nafsi zenu” na huku nafsi zao hizo zimekataa na kuasi kutoka nje, kwa sababu ya kujua kwake adhabu chungu iliyo mbele yake. Na ndiyo maana akasema, "Ionjeni adhabu iunguzayo!" yaani, adhabu kali iunguzayo.
#
{51} ذلك العذاب حصل لكم غير ظلم ولا جور من ربكم، وإنما هو بما قدَّمت أيديكم من المعاصي التي أثرت لكم ما أثرت.
{51} Adhabu hiyo iliwapata siyo dhuluma wala ukandamizaji kutoka kwa Mola wenu Mlezi, lakini ni kwa yale iliyotanguliza mikono yenu ya maasia ambayo yaliwafikishia yale yaliyofikisha.
#
{52} وهذه سنة الله في الأولين والآخرين؛ فإنَّ دأب هؤلاء المكذِّبين؛ أي: سنتهم وما أجرى اللَّه عليهم من الهلاك بذنوبهم، {كدأب آل فرعون والذين من قبلهم}: من الأمم المكذبة، {كفروا بآياتِ الله فأخَذَهم الله}: بالعقاب {بذنوبهم إنَّ الله قويٌّ شديد العقاب}: لا يعجِزُه أحدٌ يريد أخذه. {ما من دابَّةٍ إلا هو آخذٌ بناصيتها}.
{52} Na hii ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu katika wa mwanzo na wa mwisho. Kwa maana ada ya hawa wanaokadhibisha, yaani, mwendo wao na kile Mwenyezi Mungu alichowafanyia cha kuwaangamiza kwa dhambi zao. "Kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao" miongoni mwa umma zilizokadhibisha "walizikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawachukua" kwa adhabu "kwa madhambi yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu." Hakuna anayetaka kumchukua anayeweza kumshinda. "Na wala hakuna mnyama yeyote isipokuwa Yeye amemchukua kwa nywele za upande wa mbele wa kichwa chake."
: 53 - 54 #
{ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ لَمْ يَكُ مُغَيِّرًا نِعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَى قَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ وَأَنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (53) كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُمْ بِذُنُوبِهِمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَكُلٌّ كَانُوا ظَالِمِينَ (54)}.
53. Hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuibadilisha neema aliyowaneemesha kwayo kaumu, mpaka wao wabadilishe yale yaliyoko katika nafsi zao, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote. 54. Ni kama ada ya watu wa Firauni na wale walio kabla yao, walizikadhibisha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawaangamiza kwa madhambi yao, na tukawazamisha watu wa Firauni. Na kila mmoja wao walikuwa madhalimu.
#
{53} {ذلك}: العذاب الذي أوقعه الله بالأمم المكذِّبة وأزال عنهم ما هم فيه من النِّعم والنعيم بسبب ذنوبهم وتغييرهم ما بأنفسهم، فإنَّ {الله لم يكن مغيِّراً نعمةً أنعمها على قوم}: من نعم الدِّين والدُّنيا، بل يبقيها ويزيدُهم منها إن ازدادوا له شكراً، {حتى يغيِّروا ما بأنفسهم}: من الطاعة إلى المعصية، فيكفروا نعمة الله، ويبدِّلوا بها كفراً، فيسلُبُهم إيَّاها ويغيِّرها عليهم كما غيروا ما بأنفسهم، ولله الحكمة في ذلك والعدل والإحسان إلى عباده ؛ حيث لم يعاقبهم إلاَّ بظُلمهم، وحيث جَذَبَ قلوب أوليائه إليه بما يذيقُ العباد من النَّكال إذا خالفوا أمره. {وأنَّ الله سميعٌ عليمٌ}: يسمع جميعَ ما نطق به الناطقون، سواءٌ من أسرَّ القول ومن جهر به. ويعلم ما تنطوي عليه الضمائرُ وتخفيه السرائرُ، فيُجري على عباده من الأقدار ما اقتضاه علمُهُ، وجرت به مشيئتُهُ.
{53} "Hiyo" adhabu ambayo Mwenyezi Mungu aliwafikishia umma zilizokadhibisha, na akawaondolea yale waliyokuwa nayo ya neema na starehe ni kwa sababu ya dhambi zao na kubadilisha kwao yale yaliyo katika nafsi zao. Kwa maana "Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuibadilisha neema aliyowaneemesha kwayo kaumu" miongoni mwa neema za dini na dunia. Bali Yeye huzibakisha na kuwaongeza kwazo ikiwa watazidisha kumshukuru Yeye, “mpaka wabadilishe yale yaliyo katika nafsi zao” kutoka kwa utiifu hadi kwa maasia. Wakawa wameikufuru neema ya Mwenyezi Mungu, na wakaibadilisha na kufuru, kwa hivyo akawanyang’anya neema hiyo na akawabadilishia neema hiyo kama walivyobadilisha yale yaliyo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ana hekima katika hilo na uadilifu na ihsani kwa waja wake. Kwa maana hakuwaadhibu isipokuwa kwa udhalimu wao, na kwa maana alizivutia nyoyo ya marafiki wake kwake kwa sababu ya yale anayowaonjesha waja ya mateso wanapohalifu amri yake. “Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote” Yeye huyasikia yote waliyoyasema wasemao, ni sawa anayeificha kauli yake na anayeidhihirisha. Na anajua yale yaliyo ndani ya dhamiri, yaliyofichika katika siri. Kwa hivyo, anawapitishia majaaliwa waja wake kulingana na kile ambacho elimu yake inahitaji, na yakafanyika hivyo mapenzi yake.
#
{54} {كدأب آل فرعون}؛ أي: فرعون وقومه، {والذين من قبلهم كذَّبوا بآيات ربِّهم}: حين جاءتهم، {فأهْلَكْناهم بذُنوبهم}: كل بحسب جرمه، {وأغْرَقنا آلَ فرعون وكلٌّ}: من المهلَكين المعذَّبين {كانوا ظالمين}: لأنفسهم ساعين في هلاكها، لم يظلمْهُمُ الله ولا أخَذَهم بغير جُرم اقترفوه؛ فليحذرِ المخاطَبون أن يشابهوهم في الظلم، فيُحِلَّ الله بهم من عقابه ما أحلَّ بأولئك الفاسقين.
{54} “Ni kama ada ya watu wa Firauni;” yaani, Firauni na kaumu yake, “na wale walio kabla yao, walizikadhibisha Ishara za Mola wao Mlezi” wakati zilipowajia, "basi tukawaangamiza kwa madhambi yao" kila mmoja kulingana na kosa lake. "Na tukawazamisha watu wa Firauni, na kila mmoja wao" katika wale walioangamizwa, walioadhibiwa "walikuwa madhalimu" juu ya nafsi zao, wakiwania katika kuziangamiza. Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, wala hakuwachukua bila kosa walilolifanya. Kwa hivyo na watahadhari wale wanaoongeleshwa kufanana nao katika udhalimu, Mwenyezi Mungu atawatia katika adhabu Yake namna alivyowatia wale walivuka mipaka.
: 55 - 57 #
{إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِنْدَ اللَّهِ الَّذِينَ كَفَرُوا فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (55) الَّذِينَ عَاهَدْتَ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنْقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِي كُلِّ مَرَّةٍ وَهُمْ لَا يَتَّقُونَ (56) فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ [يَذَّكَّرُونَ] (57)}.
55. Hakika waovu zaidi ya wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale waliokufuru, basi hao hawaamini. 56. Wale ambao miongoni mwao ulifanya agano nao, kisha wanavunja agano lao katika kila mara, wala wao hawamchi Mungu. 57. Kwa hivyo, ukiwakuta katika vita, basi wakimbize kwa hawa wale walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.
#
{55 - 56} هؤلاء الذين جمعوا هذه الخصالَ الثلاث - الكفر وعدم الإيمان والخيانة - بحيث لا يثبُتون على عهدٍ عاهدوه ولا قول قالوه هم {شرُّ الدوابِّ عند الله}: فهم شرٌّ من الحمير والكلاب وغيرها؛ لأنَّ الخير معدوم منهم، والشرَّ متوقَّع فيهم.
{55-56} Hawa ambao walijumuisha sifa hizi tatu – ukafiri, na kutoamini, na uhaini – kwa namna kwamba hawawi thabiti juu ya agano waliloagana, wala kauli waliyoisema, wao ndio “waovu zaidi ya wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu." Basi wao ni waovu zaidi kutoka punda, na mbwa na wengineo. Kwa sababu heri haipatikani ndani yao, na uovu unatarajiwa ndani yao.
#
{57} فإذْهابُ هؤلاء ومحقُهم هو المتعيِّن؛ لئلاَّ يسري داؤهم لغيرهم، ولهذا قال: {فإمَّا تَثْقَفَنَّهُم في الحربِ}؛ أي: تجدنَّهم في حال المحاربة؛ بحيث لا يكون لهم عهدٌ وميثاقٌ. {فشَرِّدْ بهم مَنْ خلفَهم}؛ أي: نكِّل بهم غيرهم، وأوقِعْ بهم من العقوبة ما يصيرون عبرةً لمن بعدهم، {لعلَّهم}؛ أي: من خلفهم [يتقون] صنيعهم؛ لئلاَّ يصيبهم ما أصابهم. وهذه من فوائد العقوبات والحدود المرتَّبة على المعاصي أنها سببٌ لازدجار من لم يعمل المعاصي بل وزجراً لمن عملها أن لا يعاوِدَها. ودل تقييدُ هذه العقوبة في الحرب أنَّ الكافر ولو كان كثير الخيانة سريع الغدر؛ أنه إذا أُعْطِيَ عهداً؛ لا يجوز خيانته وعقوبته.
{57} Kwa hivyo kuwaondoa hawa na kuwafutilia mbali ndilo la wajibu tu, ili usije ukaenea ugonjwa wao kwa wengineo. Na ndiyo maana akasema, " Kwa hivyo, ukiwakuta katika vita;” yaani, ukikutana nao katika hali ya vita, katika hali ambayo hawana ahadi na agano, “basi wakimbize kwa hawa wale walio nyuma yao.” Yaani, watie mateso wengineo kwa hawa, waadhibu hawa namna ambayo watakuwa mazingatio kwa wale watakaokuja baada yao; "ili" hao wa nyuma yao [wapate kukumbuka] kitendo chao, ili yasiwapate yale yaliyowapata hawa. Na hii ni katika faida za adhabu zozote zile na adhabu maalumu za kisheria zilizowekwa juu ya dhambi kwamba ni sababu ya kukomeka kwa yule ambaye hajatenda dhambi, bali ni karipio kwa yule aliyefanya ili asiyarudie. Na kuliashiria kuizuia adhabu hii katika vita tu kwamba hata kama kafiri ni mwenye wingi wa hiana, na ni mwepesi wa kusaliti, kwamba ikiwa atapewa agano, basi hairuhusiki kumfanyia hiana, wala kumuadhibu.
: 58 #
{وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِنْ قَوْمٍ خِيَانَةً فَانْبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَى سَوَاءٍ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ (58)}.
58. Na ukichelea hiana kwa kaumu fulani, basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wahaini.
#
{58} أي: وإذا كان بينك وبين قوم عهدٌ وميثاقٌ على ترك القتال، فخفتَ منهم خيانةً؛ بأن ظهر من قرائن أحوالهم ما يدلُّ على خيانتهم من غير تصريح منهم بالخيانة. {فانبِذْ إليهم}: عهدَهم؛ أي: ارمه عليهم، وأخبرهم أنَّه لا عهدَ بينك وبينهم {على سواءٍ}؛ أي: حتى يستوي علمُك وعلمُهم بذلك، ولا يحلُّ لك أن تغدرهم أو تسعى في شيء مما مَنَعَهُ موجبُ العهدِ حتى تخبرهم بذلك. {إنَّ الله لا يُحِبُّ الخائنين}: بل يُبْغِضُهم أشدَّ البغض؛ فلا بدَّ من أمرٍ بيِّنٍ يبرئكم من الخيانة. ودلَّت الآية على أنه إذا وجدت الخيانة [المحققة] منهم؛ لم يحتج أن ينبذ إليهم عهدَهم؛ لأنَّه لم يخفَ منهم، بل عُلِمَ ذلك، ولعدم الفائدة، ولقوله: {على سواءٍ}، وهنا قد كان معلوماً عند الجميع غدرُكم. ودلَّ مفهومُها أيضاً أنه إذا لم يخفْ منهم خيانةً؛ بأنْ لم يوجدْ منهم ما يدلُّ على ذلك؛ أنَّه لا يجوز نبذ العهد إليهم، بل يجب الوفاء [به] إلى أن تتمَّ مدتُه.
{58} Yaani, kama kati yako na kaumu fulani kuna ahadi na agano la kuacha kupigana vita, lakini ukahofia usaliti kutoka kwao, kwa sababu ulidhihirika ushahidi wa hali zao unaoonyesha usaliti wao bila ya wao kusema hilo waziwazi, "basi watupilie" ahadi yao. Yaani, watupie na uwaambie kwamba hakuna agano lolote baina yako na wao. "Kwa usawa;" yaani, mpaka elimu yako na yao iwe sawa juu ya hilo, wala hairuhusiwi kwako kuwafanyia usaliti, au kuwania katika kitu chochote miongoni mwa yale yaliyokatazwa na matakwa ya agano hilo mpaka uwaambie hilo. "Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wahaini" bali anawachukia kuchukia kukubwa zaidi. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na jambo lililo wazi ambalo litawaondoa katika uhaini. Na Aya hii inaonyesha kwamba kama utapatikana uhaini [wa kweli] kutoka kwao, basi haihitaji kuwatupia agano lao hilo, kwa sababu hakuna hofu juu yao, bali hilo lilijulikana, na kwa sababu hakuna faida yoyote. Na kwa sababu ya kauli yake "kwa usawa," na hapa tayari ulikwisha julikana uhaini wao kwa wote. Na maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja ilionyesha pia kwamba ikiwa haitahofia hiana kutoka kwao, kwa namna kwamba hakuna chochote cha kuonyesha hilo kutoka kwao, kwamba hairuhusiki kuwatupia agano lao hilo, bali ni lazima kulitimiza hadi ukamilike muda wake.
: 59 #
{وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَبَقُوا إِنَّهُمْ لَا يُعْجِزُونَ (59)}.
59. Wala kamwe wasidhanie wale waliokufuru kwamba wao wametangulia mbele. Hakika, wao hawatashinda.
#
{59} أي: لا يحسب الكافرون بربِّهم المكذِّبون بآياته أنهم سبقوا الله وفاتوه؛ فإنهم لا يعجزونه، والله لهم بالمرصاد، وله تعالى الحكمة البالغة في إمهالهم وعدم معاجلتهم بالعقوبة، التي من جملتها ابتلاء عباده المؤمنين وامتحانُهم وتزوُّدهم من طاعته ومراضيه ما يصلون به إلى المنازل العالية واتصافُهم بأخلاق وصفات لم يكونوا بغيره بالغيها؛ فلهذا قال لعباده المؤمنين:
{59} Yaani, wasidhani wale wanaomkufuru Mola wao Mlezi, wale wanaozikadhibisha Ishara zake kwamba walimtangulia Mwenyezi Mungu na walimpotea. Wao hakika hawamshindi. Na Mwenyezi Mungu anawaangalia vyema, na Yeye Mtukufu ana hekima kubwa katika kuwapa muda na kutowaharakishia adhabu, ambayo inajumuisha kuwajaribu waja Wake Waumini, na kuwapa mtihani, na kuwazidishia katika utiifu wake na ridhaa zake yale watakayofika kwayo kwenye vyeo vya juu, na kusifika kwao kwa maadili na sifa ambazo hawakuwa ni wenye kuzifikia kwa yasiyokuwa hayo. Na ndiyo maana akawaambia waja wake Waumini:
: 60 #
{وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِنْ دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنْتُمْ لَا تُظْلَمُونَ (60)}.
60. Na waandalieni muwezavyo katika nguvu, na kwa farasi waliofungwa tayari tayari, ili muwatie hofu kwavyo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo kando na hao ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mnachotoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mtarudishiwa kikamilifu, nanyi hamtadhulumiwa.
#
{60} أي: {وأعدُّوا}: لأعدائكم الكفار الساعين في هلاككم وإبطال دينكم، {ما استطعتُم من قوَّةٍ}؛ أي: كل ما تقدرون عليه من القوَّة العقليَّة والبدنيَّة وأنواع الأسلحة ونحو ذلك مما يعين على قتالهم، فدخل في ذلك أنواع الصناعات التي تُعمل فيها أصنافُ الأسلحة والآلات من المدافع والرشاشات والبنادق والطيارات الجويَّة والمراكب البريَّة والبحريَّة [والحصون] والقلاع والخنادق وآلات الدفاع والرأي والسياسة التي بها يتقدَّم المسلمون ويندفعُ عنهم به شرُّ أعدائهم وتعلُّم الرمي والشجاعة والتدبير، ولهذا قال النبي - صلى الله عليه وسلم -: «ألا إنَّ القوَّة الرمي». ومن ذلك الاستعداد بالمراكب المحتاج إليها عند القتال، ولهذا قال تعالى: {ومِن رِباط الخيل تُرهِبونَ به عدوَّ الله وعدوَّكم}: وهذه العلة موجودةٌ فيها في ذلك الزمان، وهي إرهاب الأعداء. والحكمُ يدور مع علَّته؛ فإذا كان موجوداً شيء أكثر إرهاباً منها ـ كالسيارات البريَّة والهوائيَّة المعدَّة للقتال التي تكون النكاية فيها أشد؛ كانت مأموراً بالاستعداد بها والسعي لتحصيلها، حتى إنها إذا لم توجد إلا بتعلُّم الصناعة؛ وجب ذلك؛ لأنَّ ما لا يتمُّ الواجب إلا به فهو واجب. وقوله: {تُرْهِبونَ به عدوَّ اللهِ وعدوَّكم}: ممن تعلمون أنهم أعداؤكم، {وآخرين مِن دونهم لا تعلمونَهم}: ممَّن سيقاتلونكم بعد هذا الوقت الذي يخاطبهم الله به، {الله يعلمُهم}: فلذلك أمرهم بالاستعداد لهم. ومن أعظم ما يُعين على قتالهم بذلُ النفقات المالية في جهاد الكفار، ولهذا قال تعالى مرغباً في ذلك: {وما تنفقوا من شيءٍ في سبيل الله}: قليلاً كان أو كثيراً، {يوفَّ إليكم}: أجره يوم القيامة مضاعفاً أضعافاً كثيرة، حتى إن النفقة في سبيل الله تضاعف إلى سبعمائة ضعف إلى أضعاف كثيرة، {وأنتم لا تُظلمون}؛ أي: لا تُنْقَصون من أجرها وثوابها شيئاً.
{60} Yaani, "Na waandalieni" maadui zenu makafiri wanaowania katika kuwaangamiza na kuibatilisha dini yenu, "muwezavyo katika nguvu." Yaani, kila mnachoweza kama vile nguvu za kiakili na kimwili, na aina mbalimbali za silaha na mfano wa hayo miongoni mwa yenye kusaidia katika kupigana nao vita. Basi ikaingia katika hilo aina mbalimbali za viwanda ambazo ndani yake hutengenezwa aina mbalimbali za silaha na ala mbalimbali kama vile mizinga, na bunduki kubwa na bunduki ndogo, na ndege, na vipando vya nchi kavu na baharini [na ngome], na majumba, na mitaro, na ala za ulinzi, na maoni. Na siasa ambazo Waislamu wanaenedelea mbele na unazuilika kwa hayo uovu wa maadui zao; na kujifunza kupiga risasi au mishale, na ujasiri, na uendeshaji mambo. Na ndiyo maana Nabii akasema: Tazameni! Hakika Nguvu ni kutupa. Na katika hilo ni kujitayarisha na vipando vinavyohitajika wakati wa kupigana vita, na ndiyo maana yeye Mtukufu akasema: "Na kwa farasi waliofungwa tayari tayari, ili muwatishe kwavyo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu." Na sababu hii ilipatikana ndani yake katika wakati huo. Nayo ni kuwahofisha maadui. Na hukumu huzunguka pamoja na sababu yake. Kwa hivyo, kitu kingine kitakuwepo chenye kuhofisha zaidi, kama vile magari ya kwenye nchi kavu, na ya kwenye hewa yaliyoandaliwa kwa ajili ya kupigana vita, ambayo ushindi kwacho utakuwa mkubwa zaidi, basi kinakuwa kimeamrishwa. Kwamba wajiandae kwacho, na kuwania kukipata, kiasi kwamba ikiwa hakiwezi kupatikana isipokuwa kwa kujifunza kukitengeneza, basi inakuwa lazima kufanya hivyo. Kwa sababu kile ambacho wajibu haitimii isipokuwa kwacho, basi hilo ni wajibu. Na kauli yake, "ili muwatie hofu kwavyo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu” ni katika wale mnaowajua kuwa ni maadui zenu. “Na wengineo kando na hao ambao hamuwajui” miongoni mwa wale ambao watapigana nanyi baada ya wakati huu ambao Mwenyezi Mungu anawaongelesha ndani yake. “Lakini Mwenyezi Mungu anawajua.” Na ndiyo maana akawaamuru wajitayarishe kwa ajili yao. Na katika makubwa zaidi yanayosaidia kupigana nao vita ni kutoa mali kwa wingi katika kupambana na makafiri. Na ndiyo maana yeye Mtukufu akasema akihimiza katika hilo: "Na mnachotoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu” kiwe kichache au kingi, "mtarudishiwa kikamilifu" malipo yake Siku ya Qiyama yakiwa yameongezwa mara nyingi hadi mizidisho mia saba hadi mizidisho mingi. "Nanyi hamtadhulumiwa ." Yaani, hamtapunguziwa kitu katika malipo yake na thawabu zake.
: 61 - 64 #
{وَإِنْ جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (61) وَإِنْ يُرِيدُوا أَنْ يَخْدَعُوكَ فَإِنَّ حَسْبَكَ اللَّهُ هُوَ الَّذِي أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ (62) وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ لَوْ أَنْفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (63) يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (64)}.
61. Na wakiielekea amani, basi nawe pia ielekee, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote. 62. Na wakitaka kukufanyia hiana, basi hakika Mwenyezi Mungu atakutoshelezea. Yeye ndiye aliyekuunga mkono kwa nusura yake, na kwa Waumini. 63. Na akaziunga pamoja nyoyo zao. Lau wewe ungelitoa vyote vilivyo katika dunia, usingeliweza kuziunga pamoja nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima kubwa. 64. Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutosha wewe na mwenye kukufuata miongoni mwa Waumini.
#
{61} يقول تعالى {وإن جنحوا}؛ أي: الكفار المحاربون؛ أي: مالوا إلى السَّلْم؛ أي: الصلح وترك القتال، {فاجنحْ لها وتوكَّلْ على الله}؛ أي: أجبهم إلى ما طلبوا متوكلاً على ربِّك؛ فإنَّ في ذلك فوائد كثيرةً: منها: أن طلب العافية مطلوبٌ كلَّ وقت؛ فإذا كانوا هم المبتدئين في ذلك؛ كان أولى لإجابتهم. ومنها: أن في ذلك إجماماً لِقُواكم واستعداداً منكم لقتالهم في وقت آخر إن احتيج إلى ذلك. ومنها: أنَّكم إذا أصلحتُم وأمن بعضكم بعضاً وتمكَّن كلٌّ من معرفة ما عليه الآخر؛ فإن الإسلام يعلو ولا يُعلى عليه؛ فكلُّ مَن له عقلٌ وبصيرة إذا كان معه إنصافٌ؛ فلا بدَّ أن يؤثره على غيره من الأديان؛ لحسنه في أوامره ونواهيه، وحسنه في معاملته للخلق والعدل فيهم. وأنه لا جور فيه ولا ظلم بوجه؛ فحينئذ يكثر الراغبون فيه والمتَّبعون له، فصار هذا السلم عوناً للمسلمين على الكافرين.
{61} Yeye Mtukufu anasema "Na wakiielekea amani;” yaani, makafiri wanaopigana vita nawe. Yaani, wakielekea kwenye amani, yaani, suluhu na kuacha kupigana vita, "basi nawe pia ielekee na mtegemee Mwenyezi Mungu.” Yaani, waitikie yale waliyoomba ukimtegemea Mola wako Mlezi. kwani katika hilo kuna faida nyingi. Mongoni mwake ni kwamba, kuomba kuwa salama, kunahitajika kila wakati. Na ikiwa wao ndio walioanza katika hilo, basi inakuwa ni bora zaidi kuwaitikia. Na miongoni mwake ni kwamba, katika hilo kuna kuzidisha nguvu zenu na kujiandaa kwenu kwa ajili ya kupigana nao katika wakati mwingine ikiwa hilo litahitajika. Na miongoni mwake ni kwamba, mtasuluhisha na kila mmoja wenu akawa na amani kutoka kwa mwenzake, na akaweza kila mmoja wenu kujua kile anachofanya mwenzake, basi Uislamu unakuwa juu na wala hakiwi juu yake chochote. Kwa hivyo kila mwenye akili na ufahamu, kama ni mwadilifu, basi ni lazima ataupendelea juu ya dini nyingineyo miongoni mwa dini mbalimbali, kwa sababu ya uzuri wake katika amri zake na makatazo yake. Na uzuri wake katika kuamiliana kwake na viumbe, na kufanya uadilifu kwao. Na kwamba hakuna ukandamizaji ndani yake wala dhuluma kwa namna yoyote ile. Basi hapo wanakuwa wengi wanaoitaka na waifuatao, kwa hivyo amani hii ikawa ni msaada kwa Waislamu dhidi ya makafiri.
#
{62 - 63} ولا يُخاف من السلم إلا خَصْلة واحدة، وهي أن يكون الكفار قصدهم بذلك خَدْع المسلمين وانتهاز الفرصة فيهم، فأخبرهم الله أنَّه حسبُهم وكافيهم خداعهم، وأنَّ ذلك يعود عليهم ضرره، فقال: {وإن يريدوا أن يَخْدَعوك فإنَّ حسبَك الله}؛ أي: كافيك ما يؤذيك، وهو القائم بمصالحك ومهمَّاتك؛ فقد سبق لك من كفايته لك ونصره ما يطمئنُّ به قلبك، فَلَهُوَ {الذي أيَّدك بنصره وبالمؤمنين}؛ أي: أعانك بمعونة سماويَّة، وهو النصر منه الذي لا يقاومه شيء، ومعونة بالمؤمنين بأن قيَّضهم لنصرك، {وألَّف بين قلوبهم}: فاجتمعوا، وائتلفوا، وازدادت قوَّتهم بسبب اجتماعهم، ولم يكن هذا بسعي أحدٍ، ولا بقوَّة غير قوَّة الله، فلو {أنفقت ما في الأرض جميعاً}: من ذهبٍ وفضة وغيرهما لتأليفهم بعد تلك النفرة والفرقة الشديدة، {ما ألَّفْتَ بين قلوبهم}: لأنه لا يقدر على تقليب القلوب إلا الله تعالى. {ولكنَّ الله ألَّف بينهم إنَّه عزيزٌ حكيمٌ}: ومن عزَّته أن ألَّف بين قلوبهم وجمعها بعد الفرقة؛ كما قال تعالى: {واذكُروا نعمة الله عليكم إذ كنتُم أعداءً فألَّفَ بين قلوبِكُم فأصبحتُم بنعمتِهِ إخواناً وكنتُم على شفا حُفْرَةٍ من النار فأنقذكم منها}.
Na haihofiwi katika amani isipokuwa sifa moja, nayo ni kwamba wawe makafiri makusudio yao katika hilo ni kuwahadaa Waislamu na kuchukua fursa dhidi yao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawaambia kwamba atawatoshelezea hadaa yao, na kwamba hilo litawarudia wao madhara yake. Kwa hivyo, akasema: "Na wakitaka kukufanyia hiana, basi hakika Mwenyezi Mungu atakutoshelezea.” Yaani, atakutosheleza yenye kukudhuru, naye ndiye anayeyasimamia masilahi yako na mambo yako. Kwani tayari ilikwisha tangulia katika kukutosheleza kwake na kukunusuru kwake ambayo kwayo moyo wako utatulia. Kwa maana Yeye “ndiye aliyekuunga mkono kwa nusura yake, na kwa Waumini;” yaani, aliwasaidia kwa msaada wa kimbinguni. Nao ni nusura kutoka kwake ambayo haipingwi na chochote, na msaada wa Waumini kwamba aliwaweka ili wakunusuru; “Na akaziunga pamoja nyoyo zao.” Basi wakakusanyika, na wakaungana, na nguvu zao zikaongezeka kwa sababu ya kukusanyika kwao. Na hili halikuwa kwa juhudi ya yeyote, wala kwa nguvu nyingine isiyokuwa nguvu ya Mwenyezi Mungu. Na lau “wewe ungelitoa vyote vilivyo katika dunia” vya dhahabu, na fedha na vinginevyo ili kuwaunganisha pamoja baada ya kujitenga mbali huko, na kugawanyika kukubwa huko, "usingeliweza kuziunga pamoja nyoyo zao;” kwa sababu hawezi kuzigeuza nyoyo isipokuwa mwenyezi Mungu Mtukufu. "Lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima kubwa.” Na katika nguvu zake ni kwamba aliziunga pamoja nyoyo zao, na akawakusanya baada ya mgawanyiko, kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, wakati mlipokuwa maadui nyinyi kwa nyinyi, naye akaziunganisha pamoja nyoyo zenu, basi kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akawaokoa kutokana nalo.”
#
{64} ثم قال تعالى: {يا أيها النبيُّ حسبك الله}؛ أي: كافيك، {ومن اتَّبعك من المؤمنين}؛ أي: وكافي أتباعك من المؤمنين. وهذا وعدٌ من الله لعباده المؤمنين المتَّبعين لرسوله بالكفاية والنصرة على الأعداء؛ فإذا أتوا بالسبب الذي هو الإيمان والاتباع؛ فلا بدَّ أن يكفِيَهم ما أهمَّهم من أمور الدين والدنيا، وإنما تتخلَّف الكفاية بتخلُّف شرطها.
{64} Kisha Yeye Mtukufu akasema, " Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutosha wewe na mwenye kukufuata miongoni mwa Waumini.” Yaani, anawatosha wafuasi wako miongoni mwa Waumini. Na hii ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini, wamfuatao Mtume wake kwamba atawatosha na kuwanusuru dhidi ya maadui. Kwa hivyo, wakifanya sababu ambayo ni imani na kufuata, basi hakuna budi kwamba atawatosha yenye kuwatia wasiwasi katika mambo ya dini na dunia. Lakini kutosha huku kunakosa kuwepo ikiwa sharti lake litakosa kuwepo.
: 65 - 66 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ إِنْ يَكُنْ مِنْكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ وَإِنْ يَكُنْ مِنْكُمْ مِائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَا يَفْقَهُونَ (65) الْآنَ خَفَّفَ اللَّهُ عَنْكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا فَإِنْ يَكُنْ مِنْكُمْ مِائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ وَإِنْ يَكُنْ مِنْكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّهِ وَاللَّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ (66)}.
65. Ewe Nabii! Wahimize Waumini juu ya kupigana vita. Wakiwapo miongoni mwenu ishirini wanaosubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo miongoni mwenu mia, watawashinda elfu moja katika wale waliokufuru, kwa sababu wao ni kaumu wasiofahamu. 66. Sasa Mwenyezi Mungu amewapunguzia, na alijua kuwa ndani yenu upo udhaifu. Kwa hivyo, wakiwapo watu mia moja miongoni mwenu wenye kusubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja, watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
#
{65} يقول تعالى لنبيه - صلى الله عليه وسلم -: {يا أيُّها النبيُّ حرِّض المؤمنين على القتال}؛ أي: حُثَّهم ونهِّضْهم إليه بكل ما يقوِّي عزائمهم وينشط هممهم؛ من الترغيب في الجهاد ومقارعة الأعداء، والترهيب من ضدِّ ذلك، وذكر فضائل الشجاعة والصبر، وما يترتَّب على ذلك من خير الدنيا والآخرة، وذكر مضارِّ الجبن، وأنه من الأخلاق الرذيلة المنقصة للدين والمروءة، وأن الشجاعة بالمؤمنين أولى من غيرهم، {إن تكونوا تألَمونَ فإنَّهم يألَمونَ كما تألَمونَ وترجونَ من الله ما لا يرجون}. {إن يكن منكم}: أيها المؤمنون، {عشرون صابرون يغلبوا مائتين وإن يكن منكُم مائةٌ يغلبوا ألفاً من الذين كفروا}: يكون الواحد بنسبة عشرة من الكفار، وذلك بأنَّ الكفار {قومٌ لا يفقهون}؛ أي: لا علم عندهم بما أعدَّ الله للمجاهدين في سبيله؛ فهم يقاتلون لأجل العلوِّ في الأرض والفساد فيها، وأنتم تفقهون المقصود من القتال أنَّه لإعلاء كلمة الله، وإظهار دينه، والذبِّ عن كتاب الله وحصول الفوز الأكبر عند الله، وهذه كلُّها دواعٍ للشجاعة والصبر والإقدام على القتال.
{65} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: - "Ewe Nabii! Wahimize Waumini juu ya kupigana vita.” Yaani, wahimize na wafanye wanyanyuke kuviendea kwa kila chenye kutia nguvu azimio lao na kukakamsha hamasa zao, miongoni mwa kutia moyo wa kufanya jihadi na kupigana na maadui, na kutishia dhidi ya hilo, na kutaja fadhila za ujasiri na subira, na yale yanayoambatana na hayo ya manufaa ya dunia hii na ya Akhera; na kutaja madhara ya uwoga, na kwamba ni katika tabia duni ambazo hupunguza dini na maadili, na kwamba Waumini wanafaa zaidi kuwa na ujasiri kuliko wengineo. “Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyoumia. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu yale wasiyoyataraji.” “Wakiwapo miongoni mwenu” enyi Waumini, “ishirini wanaosubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo miongoni mwenu mia, watawashinda elfu moja katika wale waliokufuru.” Atakuwa mmoja sawa na kumi katika makafiri, na hilo ni kwamba makafiri ni “kaumu wasiofahamu.” Yaani, hawana elimu ya yale Mwenyezi Mungu aliwaandalia wanaopambana katika njia yake. Kwani wao wanapigana vita kwa ajili ya kuinuka katika dunia na kufanya uharibifu humo, nanyi mnafahamu makusudio katika kupigana vita kwamba ni kwa ajili ya kuliinua neno la Mwenyezi Mungu, na kuidhihirisha dini yake, na kukitetea Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kupata ushindi mkubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu, na hizi zote ni sababu za kumfanya mtu awe na ujasiri, na subira, na kuviendea vita.
#
{66} ثُمَّ إن هذا الحكم خففه الله على العباد، فقال: {الآن خفَّف الله عنكم وعلم أن فيكم ضعفاً}: فلذلك اقتضت رحمته وحكمته التخفيف. {فإن يكن منكم مائةٌ صابرةٌ يغلبوا مائتين وإن يكن منكم ألفٌ يغلبوا ألفين بإذن الله والله مع الصابرين}: بعونه وتأييده. وهذه الآيات صورتها صورة الإخبار عن المؤمنين بأنهم إذا بلغوا هذا المقدار المعيَّن يغلبون ذلك المقدار المعيَّن، في مقابلته من الكفار، وأن الله يمتنُّ عليهم بما جعل فيهم من الشجاعة الإيمانية، ولكنَّ معناها وحقيقتها الأمر، وأنَّ الله أمر المؤمنين في أول الأمر أن الواحد لا يجوز له أن يفرَّ من العشرة والعشرة من المائة والمائة من الألف، ثم إنَّ الله خفَّف ذلك، فصار لا يجوز فرار المسلمين من مثليهم من الكفار؛ فإن زادوا على مثليهم؛ جاز لهم الفرار. ولكن يرِدُ على هذا أمران: أحدهما: أنها بصورة الخبر، والأصل في الخبر أن يكون على بابه، وأنَّ المقصود بذلك الامتنان والإخبار بالواقع. والثاني: تقييدُ ذلك العدد أن يكونوا صابرين؛ بأن يكونوا متدرِّبين على الصبر، ومفهوم هذا أنَّهم إذا لم يكونوا صابرين؛ فإنه يجوز لهم الفرار، ولو أقل من مثليهم، إذا غَلَبَ على ظنِّهم الضرر؛ كما تقتضيه الحكمة الإلهية. ويجاب عن الأول بأنَّ قوله: {الآن خفَّف الله عنكم ... } إلى آخرها: دليلٌ على أن هذا الأمر لازمٌ وأمر محتَّم، ثم إن الله خفَّفه إلى ذلك العدد؛ فهذا ظاهرٌ في أنه أمر، وإن كان في صيغة الخبر، وقد يقال: إن في إتيانه بلفظ الخبر نكتةٌ بديعة لا توجد فيه إذا كان بلفظ الأمر، وهي تقوية قلوب المؤمنين، والبشارة بأنهم سيغلبون الكافرين. ويجاب عن الثاني: أن المقصود بتقييد ذلك بالصابرين أنه حثٌّ على الصبر، وأنه ينبغي منكم أن تفعلوا الأسباب الموجبة لذلك؛ فإذا فعلوها؛ صارت الأسباب الإيمانيَّة والأسباب الماديَّة مبشِّرة بحصول ما أخبر الله به من النصر لهذا العدد القليل.
{66} Kisha hukumu hii ilipunguzwa na Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, kwa hivyo akasema: "Sasa Mwenyezi Mungu amewapunguzia, na alijua kuwa ndani yenu upo udhaifu.” Kwa hivyo, ikahitaji rehema yake na hekima yake kupunguziwa. “Kwa hivyo, wakiwapo watu mia moja miongoni mwenu wenye kusubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja, watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri;" kwa msaada wake na kuunga kwake mkono. Na Aya hizi mwonekano wake ni mwonekano wa kujulisha kuhusu Waumini kwamba wakifikia kiwango hiki maalumu, watafikia kiwango kile maalumu inayokabiliana nayo katika makafiri. Na kwamba Mwenyezi Mungu atawaneemesha kwa kile alichowatia cha ujasiri wa kiimani, lakini maana yake na uhakika wake ni amri, na kwamba Mwenyezi Mungu aliwaamuru Waumini katika mwanzo wa amri hii kwamba haruhusiwi mtu mmoja kuwakimbia watu kumi, na watu kumi kutoka kwa watu mia moja, na watu mia moja kutoka kwa watu elfu moja, kisha Mwenyezi Mungu akapunguza hilo, kwa hivyo ikawa hairuhusiwi kwa Waislamu kuwakimbia wale walio mfano wao katika makafiri. Lakini wakiwazidi walio mfano wao mara mbili, basi wanaweza kukimbia. Lakini kuna mambo mawili kwa hili ambayo yanajitokeza: La kwanza yake ni kwamba aya hizi ni za muundo wa kupeana habari tu, na jambo la msingi katika kupeana habari ni kuwa ieleweke kwamba ni habari tu, na kwamba kilichokusudiwa katika hilo ni kukumbusha juu ya neema na kujulisha juu ya hali halisi. Ya pili ni kuifungia idadi hiyo na sifa kwamba wawe ni wenye subira, kwa hali ya kwamba wamefundishwa kuwa na subira. Na maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba ikiwa hawana subira, basi wanaweza kukimbia, hata kama adui ni wachache kuliko mfano wao mara mbili, ikiwa watakuwa na dhana kubwa kwamba watadhurika, kama inavyotakiwa na hekima ya kimungu. Na la kwanza linajibiwa kwa kusema, "Sasa mwenyezi Mungu amewapunguzia ... " hadi mwisho wake ni ushahidi kwamba jambo hili ni lazima na lisiloepukika, kisha Mwenyezi Mungu alilipunguza hadi idadi hiyo. Basi hili ni dhahiri kwamba hiyo ni amri, hata kama ni katika muundo wa habari. Na inaweza kusemwa kwamba kuja kwake kwa muundo wa kupeana habari ni mbinu ya ufasaha mkubwa ambayo haipo ndani yake ikiwa itakuwa kwa neno la amri, nalo ni kuziimarisha nyoyo za Waumini, na kupeana habari njema kwamba watawashinda makafiri. Na la pili linajibiwa kwamba kile kinachokusudiwa kwa kuzuia hilo kwa wenye subira ni kwamba ni himizo juu ya kuwa na subira, na kwamba mnapaswa kufanya sababu ziletazo hilo. Kwa hivyo, wanapozifanya, zinakuwa sababu za kiimani na sababu za kimwili ni zenye kuleta habari njema ya kupatikana kwa kile Mwenyezi Mungu alijulisha cha ushindi wa idadi hii chache.
: 67 - 69 #
{مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَكُونَ لَهُ أَسْرَى حَتَّى يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (67) لَوْلَا كِتَابٌ مِنَ اللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ (68) فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (69)}.
67. Haikuwa kwa Nabii yeyote kwamba awe na mateka, mpaka awe ameshinda sawasawa katika ardhi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima kubwa. 68. Lau lisingelikuwa andiko lililokwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ingewagusa adhabu kubwa kwa vile mlivyochukua. 69. Basi kuleni katika mlivyoteka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu.
#
{67} هذه معاتبة من الله لرسوله وللمؤمنين يوم بدر إذ أسروا المشركين وأبقوهم لأجل الفداء، وكان رأي أمير المؤمنين عمر بن الخطاب في هذه الحال قتلَهم واستئصالهم، فقال تعالى: {ما كان لنبيٍّ أن يكونَ له أسرى حتَّى يُثْخِنَ في الأرض}؛ أي: ما ينبغي ولا يليق به إذا قاتل الكفار الذين يريدون أن يطفئوا نور الله، ويسعَوْن لإخماد دينه وأن لا يبقى على وجه الأرض مَن يعبدُ الله أن يتسرَّع إلى أسرهم وإبقائهم لأجل الفداء الذي يحصُلُ منهم، وهو عَرَضٌ قليلٌ بالنسبة إلى المصلحة المقتضية لإبادتهم وإبطال شرِّهم؛ فما دام لهم شرٌّ وصولةٌ؛ فالأوفق أن لا يؤسروا؛ فإذا أُثخنوا، وبَطَلَ شرُّهم، واضمحلَّ أمرُهم؛ فحينئذٍ لا بأس بأخذ الأسرى منهم وإبقائهم. يقول تعالى: {تريدون}: بأخذكم الفداء وإبقائهم {عَرَضَ الحياة الدُّنيا}؛ أي: لا لمصلحة تعودُ إلى دينكم. {والله يريدُ الآخرة}: بإعزاز دينه ونصر أوليائه وجعل كلمتهم عاليةً فوق غيرهم، فيأمركم بما يوصل إلى ذلك. {والله عزيزٌ حكيمٌ}؛ أي: كامل العزة، لو شاء أن ينتصر من الكفار من دون قتال؛ لفعلَ، ولكنه حكيمٌ يبتلي بعضكم ببعض.
{67} Huku ni kulaumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake na Waumini siku ya Badr walipowakamata washirikina kama mateka na kuwabakisha kwa ajili ya ukombozi, na yalikuwa maoni ya amiri wa Waumini, Umar Ibn Al-Khattab katika hali hii ni kuwaua na kuwaangamiza. Kwa hivyo, Yeye Mtukufu akasema: "Haikuwa kwa Nabii yeyote kwamba awe na mateka, mpaka awe ameshinda sawasawa katika ardhi." Yaani, haifai wala haiendani naye anapopigana na makafiri ambao wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu, na wanawania kuizima Dini Yake, na kwamba asibaki kwenye uso wa ardhi anayemwabudu Mwenyezi Mungu akimbilie kuwateka na kuwabakisha kwa ajili ya ukombozi ambao utapatikana kutoka kwao, nao ni kitu kidogo kwa kulinganisha na masilahi yanayohitaji kuwaangamiza na kubatilisha uovu wao. Kwa hivyo, mradi bado wana uovu na nguvu, basi la sahihi zaidi ni kwamba wasikamatwe mateka. Kwa hivyo, wakishakamatwa barabara na uovu wao ukabatilika, na amri yao ikapungua, basi hapo hakuna ubaya kuwachukua mateka miongoni mwao na kuwabakisha. Yeye Mtukufu anasema: "Mnataka" kwa kuchukua kwenu ukombozi na kuwabakishia "vitu vya maisha ya kidunia." Yaani, si kwa masilahi yenye kuirudia dini yenu. "Na Mwenyezi Mungu anataka Akhera," kwa kuitia nguvu Dini Yake na kuwanusuru marafiki wake, na kulifanya neno lao kuwa juu zaidi kuliko wengineo, basi anawaamrisha yenye kufikisha katika hilo. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima kubwa." Yaani, Mwenye nguvu kamili, kama angetaka kuwashinda makafiri bila kupigana vita vyovyote, angefanya. Lakini yeye ni Mwenye hekima kubwa, anawajaribu nyinyi kwa nyinyi wenyewe.
#
{68} {لولا كتابٌ من الله سَبَقَ}: به القضاء والقدر؛ أنَّه قد أحلَّ لكم الغنائم، وأنَّ الله رفع عنكم أيُّها الأمة العذاب، {لمسَّكم فيما أخذتم عذابٌ عظيمٌ}. وفي الحديث: «لو نزل عذابٌ يوم بدر؛ ما نجا منه إلا عمر».
{68} "Lau lisingelikuwa andiko lililokwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu" kupitia majaliwa na hukumu yake kwamba aliwahalalishia nyara, na kwamba Mwenyezi Mungu amewaondolea enyi umma adhabu "ingewagusa adhabu kubwa kwa vile mlivyochukua." Na katika hadithi, "Kama adhabu ingeteremka siku ya Badr, hangepona yeyote kutokana nayo isipokuwa Umar."
#
{69} {فكلوا مما غنمتُم حلالاً طيِّباً}: وهذا من لطفه تعالى بهذه الأمة أن أحلَّ لها الغنائم ولم تحلَّ لأمة قبلها، {واتَّقوا الله}: في جميع أموركم، ولازموها شكراً لنعم الله عليكم. {إنَّ الله غفورٌ}: يغفر لمن تاب إليه جميع الذنوب، ويغفر لمن لم يشركْ به شيئاً جميع المعاصي، {رحيمٌ}: بكم حيث أباح لكم الغنائم وجعلها حلالاً طيباً.
{69} "Basi kuleni katika mlivyoteka, ni halali na vizuri" na huu ni katika upole wake Yeye Mtukufu kwa umma huu kwamba aliwahalalishia nyara na wala haikuhalalishwa kwa umma wowote kabla yake. "Na mcheni Mwenyezi Mungu" katika mambo yenu yote, na shikamaneni nao ili kushukuru neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi;" anamsitri dhambi mwenye kutubia kwake dhambi zote, na anamsitiri dhambi yule ambaye hakumshirikisha na chochote. "Mwenye kurehemu," juu yenu kwa kuwa aliwaruhusu kutumia nyara, na akaifanya kuwa halali na nzuri.
: 70 - 71 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ قُلْ لِمَنْ فِي أَيْدِيكُمْ مِنَ الْأَسْرَى إِنْ يَعْلَمِ اللَّهُ فِي قُلُوبِكُمْ خَيْرًا يُؤْتِكُمْ خَيْرًا مِمَّا أُخِذَ مِنْكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (70) وَإِنْ يُرِيدُوا خِيَانَتَكَ فَقَدْ خَانُوا اللَّهَ مِنْ قَبْلُ فَأَمْكَنَ مِنْهُمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ (71)}.
70. Ewe Nabii! Waambie wale walio katika mikono yenu miongoni mwa mateka: Kama Mwenyezi akijua heri yoyote katika nyoyo zenu, atawapa bora kuliko vilivyochukuliwa kutoka kwenu, na atawasitiria dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu. 71. Na ikiwa wanataka kukufanyia hiana, basi hakika walikwisha mfanyia hiana Mwenyezi Mungu kabla, naye akawawezesha nyinyi kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.
#
{70} وهذه نزلت في أسارى يوم بدر ، وكان من جملتهم العباس عمُّ رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، فلما طلب منه الفداء؛ ادَّعى أنه مسلم قبل ذلك، فلم يسقِطوا عنه الفداء، فأنزل الله تعالى جبراً لخاطره ومَنْ كان على مثل حالِهِ: {يا أيُّها النبيُّ قلْ لِمَن في أيديكم من الأسرى إن يعلم اللهُ في قلوبكم خيراً يؤتِكُم خيراً ممَّا أُخِذَ منكم}؛ أي: من المال، بأن ييسِّر لكم من فضله خيراً كثيراً مما أخذ منكم، {ويَغْفِرْ لكم}: ذنوبكم ويدخلكم الجنة. {والله غفورٌ رحيمٌ}: وقد أنجز الله وعده للعباس وغيره، فحصل له بعد ذلك من المال شيءٌ كثيرٌ، حتى إنه مرَّة لما قدم على النبي - صلى الله عليه وسلم - مال كثير؛ أتاه العباس، فأمره أن يأخذ منه بثوبه ما يطيق حملَه، فأخذ منه ما كاد أن يعجزَ عن حمله.
{70} Na hii iliteremka kuhusiana na mateka wa siku ya Badr, na miongoni mwao alikuwemo Al-Abbas, ami ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na alipoitishwa ukombozi, akadai kuwa alikuwa Muislamu kabla ya hapo, lakini hawakumuachia kutolipa ukombozi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha chenye kuunga moyo wake na wale wote waliokuwa katika hali kama yake: "Ewe Nabii! Wale walio katika mikono yenu miongoni mwa mateka: Kama Mwenyezi akijua heri yoyote katika nyoyo zenu, atawapa bora kuliko vilivyochukuliwa kutoka kwenu." Yaani, kama vile mali, kwamba atawarahisishia katika fadhila zake heri nyingi kuliko yale yaliyochukuliwa kutoka kwenu; "na atawasitiria" dhambi zenu na kuwaingiza Peponi. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri dhambi, Mwenye kurehemu;" na Mwenyezi Mungu alitimiza ahadi yake kwa Al-Abbas na wengineo, na baada ya hapo akapata mali nyingi, mpaka mara moja zilipomjia Nabii rehema na amani za Allah zimshukie mali nyingi, Al-Abbas akamjia, naye akamuamuru achukue kwayo kwa nguo yake kile anachoweza kubeba, kwa hivyo akachukua kwayo kile kilichokaribia kumshinda kubeba.
#
{71} {وإن يريدوا خيانَتَكَ}: في السعي لحربك ومنابذتك، {فقد خانوا الله من قبلُ فأمْكَنَ منهم}: فليحذَروا خيانتك؛ فإنه تعالى قادرٌ عليهم، وهم تحت قبضته. {والله عليمٌ حكيمٌ}؛ أي: عليم بكل شيء، حكيم يضع الأشياء مواضعها، ومن علمه وحكمته أن شَرَعَ لكم هذه الأحكام الجليلة الجميلة، وقد تكفَّل بكفايتكم شأنَ الأسرى وشرَّهم إن أرادوا خيانةً.
{71} "Na ikiwa wanataka kukufanyia hiana" katika kuwania kupigana vita nawe, na kukutupia agano lako nao; "basi hakika walikwisha mfanyia hiana Mwenyezi Mungu kabla, naye akawawezesha nyinyi kuwashinda." Basi na watahadhari kukufanyia hiana. Kwani Yeye Mtukufu ana uwezo juu yao, nao wako chini ya mshiko wake. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima." Yaani, anajua vyema kila kitu, na ni mwenye hekima, anayeweka vitu katika pahali pake. Na katika elimu yake na hekima yake ni kwamba aliwawekea sheria ya hukumu hizi tukufu, na nzuri. Naye alikwisha chukua jukumu la kukutoshelezea jambo la mateka na uovu wao ikiwa watataka kukufanyia hiana.
: 72 #
{إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ آوَوْا {وَنَصَرُوا أُولَئِكَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يُهَاجِرُوا مَا لَكُمْ مِنْ وَلَايَتِهِمْ مِنْ شَيْءٍ حَتَّى يُهَاجِرُوا وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ إِلَّا عَلَى قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ مِيثَاقٌ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (72)}.
72. Hakika wale walioamini na wakahama na wakaipigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, na wale waliotoa pahali pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walioamini lakini hawakuhama, nyinyi hamna wajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipokuwa juu ya kaumu ambao lipo agano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona vyema yale mnayoyatenda.
#
{72} هذا عقدُ موالاة ومحبَّة عقدها الله بين المهاجرين الذين آمنوا وهاجروا في سبيل الله وتركوا أوطانهم لله لأجل الجهاد في سبيل الله وبين الأنصار الذين آوَوْا رسولَ الله - صلى الله عليه وسلم - وأصحابه وأعانوهم في ديارهم وأموالهم وأنفسهم؛ فهؤلاء بعضُهم أولياءُ بعض؛ لكمال إيمانهم وتمام اتِّصال بعضهم ببعض. {والذين آمنوا ولم يهاجروا ما لكم من ولايتهم من شيء حتى يهاجروا} فإنَّهم قطعوا ولايتكم بانفصالهم عنكم في وقت شدَّة الحاجة إلى الرجال، فلمَّا لم يهاجروا؛ لم يكن لهم من ولاية المؤمنين شيءٌ، لكنَّهم {إن استنصروكم في الدين}؛ أي: لأجل قتال من قاتلهم؛ [لأجل دينهم] {فعليكُمُ النصرُ}: والقتال معهم، وأما من قاتلوهم لغير ذلك من المقاصد؛ فليس عليكم نصرهم. وقوله تعالى: {إلَّا على قوم بينكم وبينَهم ميثاقٌ}؛ أي: عهدٌ بترك القتال؛ فإنهم إذا أراد المؤمنون المتميِّزون الذين لم يهاجروا قتالهم؛ فلا تعينوهم عليهم؛ لأجل ما بينَكم وبينَهم من الميثاق. {والله بما تعملونَ بصيرٌ}: يعلمُ ما أنتم عليه من الأحوال، فيشرعُ لكم من الأحكام ما يَليقُ بكم.
{72} Huu ni mkataba wa urafiki wa ulinzi na upendo aliouhitimisha Mwenyezi Mungu kati ya Muhajirina (wahamiaji) ambao waliamini na kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakaacha miji yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kati ya Ansari ambao walimhifadhi Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na masahaba zake, na wakawasaidia katika makazi yao, na mali zao, na nafsi zao. Basi hawa wenyewe kwa wenyewe ni marafiki na walinzi, kwa sababu ya ukamilifu wa imani yao, na utimilifu wa muungano kati yao wenyewe kwa wenyewe. "Na wale walioamini lakini hawakuhama, nyinyi hamna wajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame." Kwa maana walikata urafiki na ulinzi kwenu kwa kujitenga kwao nanyi katika wakati wa haja kubwa ya wanaume. Basi pindi hawakuhama, hawakuwa na kitu chochote katika urafiki na ulinzi wa Waumini. Lakini "wakiomba msaada kwenu katika Dini;" yaani kwa ajili ya kupigana vita na wale waliopigana nao [kwa ajili ya dini yao]; "basi ni juu yenu kuwasaidia" na kupigana vita pamoja nao. Na ama wale waliopigana nao kwa madhumuni mengineyo yasiyokuwa hilo, basi si juu yenu kuwasaidia. Na kauli yake Yeye Mtukufu, "isipokuwa juu ya kaumu ambao lipo agano baina yenu na wao" yaani, agano la kuacha vita. Basi hao ikiwa Waumini wanaotambulika ambao hawakuhama watataka kupigana nao, basi msiwasaidie dhidi yao, kwa sababu ya kile kilicho kati yenu na wao cha agano. "Na Mwenyezi Mungu anayaona vyema yale mnayoyatenda." Anajua hali mlizo nazo, ndiyo maana anawawekea sheria ya hukumu mbalimbali zinazowafailia nyinyi.
: 73 #
{وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُنْ فِتْنَةٌ فِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ (73)}.
73. Na wale waliokufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipofanya hivi, itakuwepo fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa.
#
{73} لما عقد الولاية بين المؤمنين؛ أخبر أن الكفار حيث جمعهم الكفر فبعضُهم أولياء بعض ؛ فلا يواليهم إلاَّ كافر مثلهم، وقوله: {إلَّا تفعلوه}؛ أي: موالاة المؤمنين ومعاداة الكافرين؛ بأن والَيْتموهم كلَّهم أو عاديتموهم كلَّهم أو واليتم الكافرين وعاديتم المؤمنين، {تكن فتنةٌ في الأرض وفسادٌ كبيرٌ}: فإنه يحصُلُ بذلك من الشرِّ ما لا ينحصر من اختلاط الحقِّ بالباطل والمؤمن بالكافر وعدم كثير من العبادات الكبار كالجهاد والهجرة وغير ذلك من مقاصد الشرع والدين التي تفوت إذا لم يُتَّخذ المؤمنون وحدهم أولياء بعضهم لبعض.
{73} Alipofunga urafiki wa ulinzi kati ya Waumini, akajulisha kuwa makafiri kwa kuwa wanakusanywa na ukafiri, baadhi yao kwa baadhi ni marafiki walinzi, kwa hivyo hafanyi kuwa urafiki mlinzi isipokuwa kafiri mfano wao. Na kauli yake, "Msipolifanya," yaani, Waumini kufanyiana urafiki wa ulinzi, na kufanya uadui na makafiri, yani kwa kuwafanya makafiri wote kuwa marafiki walinzi au kuwafanya makafiri wote kuwa maadui, au kuwafanya makafiri kuwa marafiki walinzi na kuwafanya Waumini kuwa maadui, "kutakuwa na fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa." Kwa maana, kutapatikana kwa sababu ya hilo uovu ambao hauwezi kufungika, kama vile kuchanganya haki na batili, na Muumini na kafiri, na kutokuwepo kwa ibada nyingi kama vile jihadi, na kuhama, na yasiyokuwa hayo miongoni mwa makusudio ya Sheria na Dini, ambayo yatapotea ikiwa Waumini hawatakuwa marafiki walinzi wao kwa wao peke yao.
: 74 - 75 #
{وَالَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ آوَوْا وَنَصَرُوا أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ {حَقًّا لَهُمْ مَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ (74) وَالَّذِينَ آمَنُوا مِنْ بَعْدُ وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا مَعَكُمْ فَأُولَئِكَ مِنْكُمْ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَى بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (75)}.
74. Na wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wale waliotoa pahali pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Wana kusitiriwa dhambi na riziki njema. 75. Na wale walioamini baadaye, na wakahama, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni miongoni mwenu. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana zaidi wenyewe kwa wenyewe katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Na Aya zilizotangulia zinahusiana na kutaja mkataba wa urafiki wa ulinzi kati ya Waumini miongoni mwa Muhajirina na Ansari, nazo Aya hizi zinahusiana na kubainisha kuwasifu na thawabu zao:
#
{74} فقال: {والذين آمنوا وهاجروا وجاهدوا في سبيل الله والذين آوَوْا ونصروا أولئك هم المؤمنون }: من المهاجرين والأنصار؛ هم: المؤمنون {حقًّا}؛ لأنهم صدَّقوا إيمانهم بما قاموا به من الهجرة والنصرة والموالاة بعضهم لبعض وجهادهم لأعدائهم من الكفار والمنافقين. {لهم مغفرة}: من الله تُمحى بها سيئاتهم وتضمحلُّ بها زلاَّتُهم. {و} لهم {رزقٌ كريمٌ}؛ أي: خير كثير من الربِّ الكريم في جنات النعيم، وربما حصل لهم من الثواب المعجَّل ما تَقَرُّ به أعينهم، وتطمئنُّ به قلوبهم.
{74} Kwa hivyo, Akasema: "Na wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wale waliotoa pahali pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini" miongoni mwa Muhajirina na Ansari, ndio Waumini "wa kweli." Kwa sababu waliisadikisha imani yao kwa yale waliyoyafanya ya kuhama, na nusura, na urafiki wa ulinzi wenyewe kwa wenyewe, na kufanya kwa jihadi dhidi ya maadui zao miongoni mwa makafiri na wanafiki. "Wana kusitiriwa dhambi" kutoka kwa Mwenyezi Mungu, atafuta kwayo mabaya yao, na yatapunguka kwayo makosa yao. "Na" wana "riziki njema;" yaani, heri nyingi kutoka kwa Mola Mlezi katika mabustani ya neema, na huenda wakapata thawabu ya haraka haraka yenye kuwafurahisha macho yao, na nyoyo zao kutulizwa kwayo.
#
{75} وكذلك مَن جاء بعد هؤلاء المهاجرين والأنصار ممَّن اتَّبعهم بإحسان فآمن وهاجر وجاهد في سبيل الله. {فأولئك منكم}: لهم ما لكم وعليهم ما عليكم؛ فهذه الموالاة الإيمانية، وقد كانت في أول الإسلام لها وقع كبيرٌ وشأنٌ عظيم، حتى إنَّ النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - آخى بين المهاجرين والأنصار أخوَّة خاصَّة غير الأخوة الإيمانية العامة، وحتى كانوا يتوارثون بها، فأنزل الله: {وأولو الأرحام بعضُهم أولى ببعض في كتاب الله} فلا يرثه إلا أقاربه من العصبات وأصحاب الفروض فإن لم يكونوا؛ فأقرب قراباته من ذوي الأرحام كما دلَّ عليه عموم الآية الكريمة، وقوله: {في كتاب الله}؛ أي: في حكمه وشرعه. {إنَّ الله بكلِّ شيء عليمٌ}: ومنه ما يعلمه من أحوالكم التي يجري من شرائعه الدينية عليكم ما يناسبها.
{75} Na vivyo hivyo, wale waliokuja baada ya hawa Muhajirina na Ansari miongoni mwa wale waliowafuata kwa wema, na wakaamini, na wakahama, na wakafanya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, "basi hao ni miongoni mwenu." Wana yale mliyo nayo, na ni juu yao yale yaliyo juu yenu. Basi huu ndio urafiki wa ulinzi wa kiimani. Na ulikuwa katika mwanzo mwa Uislamu una athari kubwa na jambo kubwa, mpaka Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alifanya kati ya Muhajirina na Ansari udugu maalumu usiokuwa udugu wa kiimani wa jumla, na mpaka walikuwa wakirithiana kwa huo. Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha, "Na jamaa wa nasaba wanastahikiana zaidi wenyewe kwa wenyewe katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo hamrithi isipokuwa jamaa zake tu miongoni mwa wale wanaochukua mali yote iliyosalia, na wale wenye mafungu maalumu. Na kama hawako, basi ni jamaa zake wa karibu zaidi miongoni mwa jamaa wengineo, kama ulivyoashiria hilo ujumla wa aya hii tukufu. Na kauli yake, "Katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu" yaani, katika hukumu yake na sheria Yake. "Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu." Na katika hilo ni yale anayoyajua kuhusu hali zenu, ambazo anawawekea sheria za kidini ambazo zinawafailia.
Imetimia Tafsir ya Surat Al-Anfaal, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.
***