:
Tafsir ya Suratul-An'aam
Tafsir ya Suratul-An'aam
Nayo iliteremka Makkah
: 1 - 2 #
{الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ (1) هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ طِينٍ ثُمَّ قَضَى أَجَلًا وَأَجَلٌ مُسَمًّى عِنْدَهُ ثُمَّ أَنْتُمْ تَمْتَرُونَ (2)}.
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye aliumba mbingu na ardhi, na akafanya giza mbalimbali na nuru. Kisha wale waliokufuru wanawafanya wengine kuwa sawa na Mola wao Mlezi. 2. Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na udongo, kisha akawahukumia muda, na muda maalumu uko kwake tu. Kisha nyinyi mnatia shaka.
#
{1} هذا إخبارٌ عن حمدِهِ والثناء عليه بصفات الكمال ونعوت العظمة والجلال عموماً وعلى هذه المذكورات خصوصاً؛ فحمد نفسه على خلقه السماوات والأرض الدالَّةِ على كمال قدرته وسعة علمه ورحمته وعموم حكمته وانفراده بالخلق والتدبير، وعلى جَعْلِهِ الظلماتِ والنور، وذلك شاملٌ للحسيِّ من ذلك؛ كالليل والنهار والشمس والقمر، والمعنوي؛ كظلمات الجهل والشَّكِّ والشِّرك والمعصية والغفلة ونور العلم والإيمان واليقين والطاعة، وهذا كلُّه يدلُّ دلالة قاطعة أنه تعالى هو المستحقُّ للعبادة وإخلاص الدين له، ومع هذا الدليل ووضوح البرهان: {ثم الذين كَفَروا بربِّهم يعدِلون}؛ [أي: يعدلون] به سواه؛ يسوُّونهم به في العبادة والتعظيم، مع أنَّهم لم يساووا الله في شيء من الكمال، وهم فقراء عاجزون ناقصون من كل وجه.
{1} Huku ni kujulisha kuhusu kuhimidiwa kwake na kusifiwa kwake kwa sifa za ukamilifu, na sifa za ukuu na utukufu kwa ujumla, na kwa mambo haya yaliyotajwa hasa. Basi akajisifu kwa kuumba Yeye mbingu na ardhi, yenye kuashiria ukamilifu wa uwezo wake, na upana wa elimu yake, na rehema yake, na ujumla wa hekima yake, na upekee wake katika kuumba na kuendesha mambo. Na katika kufanya kwake giza mbalimbali na nuru, na hilo linajumuisha yanayohisiwa katika hayo kama vile usiku na mchana, jua na mwezi, na yasiyohisiwa kama vile giza mbalimbali za ujinga, na shaka, na ushirikina, na uasi, na kughafilika, na nuru ya elimu, na imani, na yakini, na utiifu. Na yote haya yanaashiria ishara ya uhakika kwamba Yeye Mtukufu ndiye anayestahiki kuabudiwa na kumfanyia dini Yeye tu; na pamoja na ushahidi huu na hoja iliyo wazi. "Kisha wale waliokufuru wanawafanya wengine kuwa sawa na Mola wao Mlezi." Wanawafanya kuwa sawa na Yeye katika ibada na utukufu, ijapokuwa hawakumsawazisha Mwenyezi Mungu (na wao) katika chochote cha ukamilifu. Na wao ni masikini, wasiojiweza, na wenye upungufu wa kila namna.
#
{2} {هو الذي خَلَقَكُم من طينٍ}: وذلك بخَلْقِ مادَّتكم وأبيكم آدم عليه السلام. {ثم قضى أجلاً}؛ أي: ضرب لمدَّة إقامتكم في هذه الدار أجلاً تتمَتَّعون به، وتُمْتَحنون، وتُبْتَلَون بما يرسل إليهم به رسله؛ ليبلُوَكُم أيُّكم أحسنُ عملاً، ويعمِّرَكُم، ما يتذكَّر فيه من تذكَّر. {وأجلٌ مسمًّى عنده}: وهي الدار الآخرةُ التي ينتقل العباد إليها من هذه الدار، فيجازيهم بأعمالهم من خير وشر، {ثمَّ}: مع هذا البيان التامِّ وقطع الحجة {أنتم تَمْتَرون}؛ أي: تشكُّون في وعد الله ووعيدِهِ ووقوع الجزاء يوم القيامة. وذكر الله الظُّلمات بالجمع لكثرة موادِّها وتنوُّع طرقها، ووحَّد النور لكون الصراط الموصلة إلى الله واحدةً لا تعدُّد فيها، وهي الصراط المتضمِّنة للعلم بالحق والعمل به؛ كما قال تعالى: {وأنَّ هذا صراطي مستقيماً فاتَّبِعوه ولا تَتَّبعوا السُّبُلَ فَتَفَرَّق بكم عن سبيلِهِ}.
"Yeye ndiye aliyewaumba kutokana na udongo;" na hayo ni kwa asili yenu na baba yenu Adam, amani iwe juu yake. "Kisha akawahukumia muda;" yaani, aliweka kipimo kwa muda wa kukaa kwenu katika Nyumba hii mkistareheshwa, na kupewa mtihani, na kujaribiwa kwa yale Anayowatuma nayo Mitume Wake; ili awajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri zaidi, na awape umri wa kutosha mwenye ndani yake mwenye kukumbuka? "Na muda maalum uko kwake tu" nayo ni nyumba ya Akhera ambayo ataihamia mja kutoka katika Nyumba hii, na awalipe kwa matendo yao ya heri na maovu. "Kisha" baada ya ubainisho huu mkamilifu na kukata hoja; "Kisha nyinyi mnatia shaka," yaani, mnashuku katika ahadi ya Mwenyezi Mungu ya mema na ahadi yake ya adhabu, na kutokea kwa malipo Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu alitaja giza kwa wingi kwa sababu ya wingi wa nyenzo zake na utofauti wa njia zake, na akaitaja nuru kwa umoja kwa sababu njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu ni moja, na isiyo nyingi, nayo ni njia ile inayojumuisha kujua haki na kuifanyia kazi. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na kwamba, kwa hakika hii ndiyo Njia yangu iliyoyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyinginezo, zikawatengenisha na Njia yake."
: 3 #
{وَهُوَ اللَّهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ (3)}.
3. Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na katika ardhi. Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu. Na anajua mnayoyachuma.
#
{3} أي: وهو المألوهُ المعبودُ، {في السموات وفي الأرض}: فأهلُ السماء والأرض متعبِّدون لربِّهم خاضعون لعظمتِهِ مستكينون لعزِّه وجلاله؛ الملائكةُ المقرَّبون والأنبياءُ والمرسلون والصِّدِّيقون والشهداء والصالحون. وهو تعالى {يَعْلَمُ سِرَّكم وجَهْرَكم ويعلمُ ما تكسِبون}: فاحذروا معاصيه وارغبوا في الأعمال التي تقرِّبكم منه، وتُدْنيكم من رحمتِهِ، واحذروا من كلِّ عمل يبعدكم منه ومن رحمته.
{3} Yani Yeye ndiye anayefanyiwa uungu, anayeabudiwa "katika mbingu na katika ardhi." Basi wakazi wa mbinguni na ardhi wanamwabudu Mola wao Mlezi wakimnyenyekea kwa ukuu wake na wakimdhalilikia kwa nguvu yake na utukufu wake. Nao ni Malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu, na Manabii, na Mitume, na wakweli, na Mashahidi, na wale walio wema. Naye Mtukufu "Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu. Na anajua mnayoyachuma." Basi jihadharini na kumuasi na myatake zaidi matendo ambayo yatakayowaweka karibu naye, na yawatie karibu na rehema zake, na jihadharini na kila kitendo kitakachowaweka mbali naye, na mbali na rehema zake.
: 4 - 6 #
{وَمَا تَأْتِيهِمْ مِنْ آيَةٍ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ (4) فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنْبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (5) أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِنْ قَبْلِهِمْ مِنْ قَرْنٍ مَكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّنْ لَكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِمْ مِدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُمْ بِذُنُوبِهِمْ وَأَنْشَأْنَا مِنْ بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ (6)}.
4. Na haiwajii ishara miongoni mwa ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa walikuwa wakiipa mgongo. 5. Basi hakika walikwisha ikadhibisha haki ilipowajia. Kwa hivyo, zitawajia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha. 6. Je, hawakuona ni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao? Tuliwaimarisha katika dunia namna ambavyo hatukuwaimarisha nyinyi; na tukawatumia mvua nyingi na tukaifanya mito inapita kwa chini yao. Mwishowe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yao kizazi kingine.
#
{4} هذا إخبارٌ منه تعالى عن إعراض المشركين وشدَّة تكذيبهم وعداوتهم، وأنهم لا تنفع فيهم الآيات حتى تَحِلَّ بهم المَثُلات، فقال: {وما تأتيهم من آيةٍ من آيات ربِّهم}: الدالَّة على الحقِّ دلالة قاطعة، الداعية لهم إلى اتِّباعه وقبوله، {إلَّا كانوا عنها معرِضين}: لا يُلقون لها بالاً ولا يُصْغونَ لها سمعاً، قد انصرفت قلوبُهم إلى غيرها، وولَّوْها أدبارَهم.
{4} Hizi ni habari kutoka kwake Yeye Mtukufu kuhusu kupeana mgongo kwa washirikina na ukali wa kukadhibisha kwao na uadui wao, na kwamba haziwafai Aya zozote mpaka ziwafikie dhabu kali za kupigiwa mifano. Kwa hivyo Akasema, "Na haiwajii ishara miongoni mwa ishara za Mola wao Mlezi" zenye kuonyesha haki, kuonyesha kwa uhakika, zenye kuwafanya kuzifuata na kuzikubali, "isipokuwa walikuwa wakiipa mgongo." Wala hawazijali, wala hawazipi sikio, na nyoyo zao zilikwisha kwenda kwa yasiyokuwa hizo, na wakazipa migongo yao.
#
{5} {فقد كذَّبوا بالحقِّ لما جاءهم}: والحقُّ حقُّه أن يُتَّبع ويُشكر الله على تيسيره لهم وإتيانهم به، فقابلوه بضدِّ ما يجب مقابلته به، فاستحقوا العقاب الشديد. {فسوف يأتيهم أنباء ما كانوا به يستهزِئون}؛ أي: فسوف يَرَوْن ما استهزؤوا به أنَّه الحقُّ والصدق، ويُبَيِّنُ الله للمكذِّبين كذبهم وافتراءهم، وكانوا يستهزئون بالبعث والجنة والنار؛ فإذا كان يوم القيامة؛ قيل للمكذبين: هذه النارُ التي كنتم بها تكذِّبون، وقال تعالى: {وأقْسَموا باللهِ جَهْدَ أيْمانِهِمْ لا يَبْعَثُ اللهُ مَنْ يَموتُ بَلى وَعْداً عليهِ حقًّا ولكنَّ أكْثَرَ الناس لا يعلمونَ. لِيُبَيِّنَ لهم الذي يختلفونَ فيه ولِيَعْلَمَ الذين كفروا أنَّهم كانوا كاذبين}.
{5} "Basi hakika walikwisha ikadhibisha haki ilipowajia." Na haki ni haki yake kwamba, ifuatwe na ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia wepesi na kuileta kwao. Lakini wao wakaikabili kwa kinyume cha anavyopasa kuikabili, kwa hivyo wakastahiki adhabu kali. "Kwa hivyo, zitawajia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha." Yaani, wataona yale waliyoyafanyia mzaha kwamba ndiyo haki na ukweli, na Mwenyezi Mungu atawabainishia waliokadhibisha kukadhibisha kwao, na kuzua kwao, na walikuwa wakiufanyia mzaha Ufufuo, na Pepo, na Moto. Basi itakapokuwa ni Siku ya Kiyama, wale waliokadhibisha Wataambiwa. Huu ndio Moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha. Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatomfufua aliyekufa. Sivyo hivyo! Ni ahadi ya haki iliyo juu yake; lakini wengi wa watu hawajui. Ili awabainishie yale wanayohitalifiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao hakika walikuwa ni waongo}.
#
{6} ثم أمرهم أن يعتبروا بالأمم السابقة، فقال: {ألَم يَرَوْا كم أهلكنا من قبلهم من قرنٍ}؛ أي: كم تتابع إهلاكنا للأمم المكذِّبين وأمهلناهم قبل ذلك الإهلاك بأن {مَكَّنَّاهم في الأرض ما لم نمكِّنْ}: لهؤلاء من الأموال والبنين والرفاهية، {وأرْسَلْنا السماءَ عليهم مِدراراً وجعلنا الأنهار تجري من تحتهم}: تُنْبِتُ لهم بذلك ما شاء الله من زروع وثمار يتمتَّعون بها ويتناولون منها ما يشتهون، فلم يشكروا الله على نِعَمِهِ، بل أقبلوا على الشهوات، وألهتهم [أنواع] اللَّذَّات، فجاءتهم رسلهم بالبينات، فلم يصدِّقوها، بل ردُّوها وكذَّبوها، فأهلكهم الله بذُنوبهم، وأنشأ من بعدهم قَرْناً آخرين؛ فهذه سُنَّةُ الله ودأبه في الأمم السابقين واللاحقين؛ فاعتبروا بمن قَصَّ الله عليكم نبأهم.
{6} Kisha akawaamrisha wazingatie kwa umma waliotangulia, kwa hivyo akasema, "Je, hawakuona ni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao?" Yaani, ni mara ngapi kumefuatana kuangamiza kwetu umma zinazokadhibisha na tukawapa muhula kabla ya maangamizo hayo, kwamba, "Tuliwaimarisha katika dunia namna ambavyo hatukuwaimarisha" hawa kwa mali, na watoto, na starehe. “Na tukawatumia mvua nyingi na tukaifanya mito inapita kwa chini yao.” Ikawa inawaoteshea mazao na matunda alivyotaka Mwenyezi Mungu wakawa wanastareheka kwayo na walikula kwayo wanavyotamani, lakini hawakumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake. Bali waliyageukia matamanio na wakapumbazwa na [aina mbalimbali za] ladha, kisha wakawajia Mitume wao na hoja zilizo wazi, lakini hawakuzisadiki, bali walizikataa na wakazikadhibisha. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa dhambi zao, na akaanzisha kizazi kingine baada yao. Basi huu ndio mwenendo wa Mwenyezi Mungu na ada yake katika umma zilizotangulia na zilizofuata. Basi zingatieni kutoka kwa wale ambao Mwenyezi Mungu aliwasimulia habari zao.
: 7 - 9 #
{وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَذَا إِلَّا سِحْرٌ مُبِينٌ (7) وَقَالُوا لَوْلَا أُنْزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ وَلَوْ أَنْزَلْنَا مَلَكًا لَقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنْظَرُونَ (8) وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِمْ مَا يَلْبِسُونَ (9)}
7. Na lau tungelikuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangelisema wale waliokufuru: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio wazi. 8. Na walisema, "Mbona hakuteremshiwa Malaika?" Na kama tungelimteremsha Malaika, basi bila ya shaka ingeshahukumiwa amri, kisha wasingelipewa muhula. 9. Na kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume, na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao.
#
{7} هذا إخبارٌ من الله لرسوله عن شدَّة عناد الكافرين، وأنَّه ليس تكذيبهم لقصورٍ فيما جئتهم به ولا لجهل منهم بذلك، وإنما ذلك ظلمٌ وبغيٌ لا حيلة لكم فيه، فقال: {ولو نزَّلْنا عليك كتاباً في قِرْطاس فلَمَسوه بأيديهم}: وتيقَّنوه، {لقال الذين كفروا}: ظلماً وعلواً: {إن هذا إلا سحرٌ مبينٌ}؛ فأيُّ بينةٍ أعظم من هذه البينة، وهذا قولهم الشنيع فيها، حيث كابروا المحسوس الذي لا يمكن من له أدنى مُسْكَةٍ من عقله دفعه؟!
{7} Huku ni kumjulisha Mtume kunatoka kwa Mwenyezi Mungu kuhusu ukali wa ukaidi wa makafiri. Na kwamba, kukadhibisha kwao si kwa sababu ya upungufu ulio katika yale uliyowajia nayo, wala kutojua kwao hayo. Bali hilo ni dhuluma na kupita mipaka ambayo hamna hila yoyote katika hayo.” Kwa hivyo Akasema, "Na lau tungelikuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao" na wakawa na yakini nacho, "basi wangelisema wale waliokufuru" kwa dhuluma na kiburi. "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio wazi" basi ni ushahidi gani ulio mkubwa zaidi kuliko ushahidi huu. Na hii ndiyo kauli yao mbaya juu yake, ambapo walilifanyia kiburi linalohisiwa ambalo hawezi mwenye akili hata kidogo kulikataa?
#
{8} {وقالوا} أيضاً تعنُّتاً مبنيًّا على الجهل وعدم العلم بالمعقول: {لولا أُنزِلَ عليه مَلَكٌ}؛ أي: هلاَّ أُنْزِل مع محمدٍ مَلَك يعاوِنُه ويساعده على ما هو عليه؛ بزعمهم أنَّه بشرٌ وأنَّ رسالة الله لا تكون إلا على أيدي الملائكة. قال الله في بيان رحمته ولطفه بعباده حيث أرسل إليهم بشراً منهم يكون الإيمان بما جاء به عن علم وبصيرةٍ وغيبٍ: {ولو أنزَلْنا مَلَكاً}: برسالتنا؛ لكان الإيمانُ لا يصدُرُ عن معرفةٍ بالحقِّ، ولكان إيماناً بالشهادة الذي لا ينفع شيئاً وحده، هذا إن آمنوا، والغالب أنهم لا يؤمنون بهذه الحالة، فإذا لم يؤمنوا؛ {لَقُضِيَ الأمرُ}: بتعجيل الهلاك عليهم وعدم إنظارِهم؛ لأنَّ هذه سنة الله فيمن طَلَبَ الآيات المقترحة فلم يؤمن بها؛ فإرسال الرسول البشريِّ إليهم بالآيات البيِّنات التي يعلمُ الله أنها أصلحُ للعباد وأرفق بهم مع إمهال الله للكافرين والمكذِّبين خيرٌ لهم وأنفعُ، فطلبُهم لإنزال المَلَكِ شرٌّ لهم لو كانوا يعلمون.
{8} "Na walisema," pia kwa kuuegemea ujinga na kutokuwa na elimu mambo ya busara. "Mbona hakuteremshiwa Malaika?" Yaani, mbona hakuteremshwa Malaika pamoja na Muhammad ili amsaidie katika jambo lake? Kwa kudai kwao kwamba yeye ni mwanadamu na kwamba ujumbe wa Mwenyezi Mungu hauwi isipokuwa katika mikono ya malaika. Mwenyezi Mungu akasema katika kubainisha rehema yake na upole wake kwa waja wake kwa kuwa aliwatumia mwanadamu kutoka miongoni mwao, ili kuamini katika aliyoyaleta iwe juu ya elimu, na ufahamu na mambo ya ghaibu: "Na kama tungelimteremsha Malaika," kwa ujumbe wetu, basi Imani ingekuwa si kwa kutokana na kujua haki, lakini ingekuwa imani kwa ushahidi ambayo peke yake hainufaishi kitu. Hii ni ikiwa wataamini. Lakini uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba hawataamini katika hali hii. Basi ikiwa hawaamini, "basi bila ya shaka ingeshahukumiwa amri;" kwa kuwaharakishia maangamizo juu yao na wala wasingengojewa. Kwa sababu hii ndiyo ada ya Mwenyezi Mungu katika wale wanaoomba aya wanazozipendekeza wao, kisha wasiziamini. Basi kuwatumia Mtume wa kibinadamu na Aya zilizo wazi ambazo Mwenyezi Mungu anajua kuwa, hizo ndizo bora zaidi kwa waja wake na nyepesi zaidi kwao, pamoja na Mwenyezi Mungu kuwapa muhula makafiri na wale wanaokadhibisha ni bora kwao na ni lenye manufaa zaidi. Basi maombi yao kwamba ateremshwe Malaika ni ubaya kwao, laiti wangelikuwa wanajua.
#
{9} ومع ذلك؛ فالمَلَك لو أُنزِل عليهم وأُرْسِل؛ لم يطيقوا التلقِّي عنه ولا احتملوا ذلك ولا أطاقته قُواهم الفانية، فلو {جَعَلْناه ملكاً لجعلناه رجلاً}: لأنَّ الحكمة لا تقتضي سوى ذلك، {ولَلَبَسْنا عليهم ما يَلْبِسونَ}؛ أي: ولكان الأمر مختلطاً عليهم وملبوساً، وذلك بسبب ما لَبَّسوه على أنفسهم؛ فإنهم بَنَوا أمرهم على هذه القاعدة التي فيها اللَّبْس وعدم بيان الحق، فلما جاءهم الحقُّ بطرقه الصحيحة وقواعده التي هي قواعدُه؛ لم يكنْ ذلك هدايةً لهم إذا اهتدى بذلك غيرهم، والذنب ذنبهم؛ حيث أغلقوا على أنفسهم باب الهدى، وفتحوا أبواب الضلال.
{9} Na pamoja na hayo, ikiwa Malaika angeteremshwa kwao, hawangeweza kupokea kutoka kwake, wala hawangeweza kustahimili hilo, wala uwezo wao unaoisha haungeweza hilo. "Na kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume" kwa sababu hekima haitaki isipokuwa hilo; "na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao." Yaani, jambo hilo lingeliwachanganya, na hilo ni kwa sababu walivyojichanganya wenyewe. Kwa maana Walijenga mambo yao juu ya kanuni hii ambayo ina mkanganyiko na kutobainisha haki. Na haki ilipowajia kwa njia zake sahihi na kanuni zake, ambazo ndizo kanuni zake halisi, hilo halikuweza kuwaongoa huku wengine wakiongoka kwalo. Na dhambi ni yao wenyewe kwa sababu walijifungia wenyewe milango ya uwongofu na wakajifungulia milango ya upotovu.
: 10 - 11 #
{وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِنْ قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُمْ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (10) قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ (11)}
10. Na hakika walifanyiwa mzaha Mitume waliokuwa kabla yako, lakini wale waliowafanyia mzaha yakawafika yale yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha. 11. Sema: Tembeeni katika dunia, kisha mtazame vipi ulikuwa mwisho wa wanaokadhibisha.
#
{10} يقول تعالى مسلياً لرسوله ومصبِّراً ومتهدداً أعداءه ومتوعداً: {ولقد استُهْزِئ برسل من قبلِكَ}: لما جاؤوا أممهم بالبينات؛ كذَّبوهم واستهزؤوا بهم وبما جاؤوا به، فأهلكهم الله بذلك الكفر والتكذيب، ووفَّى لهم من العذاب أكمل نصيب، {فحاق بالذين سَخِروا منهم ما كانوا به يستهزِئونَ}: فاحذروا أيُّها المكذبون أن تستمِرُّوا على تكذيبكم، فيصيبكم ما أصابهم.
{10} Yeye Mtukufu anasema akimfariji Mtume wake, na akimhimiza kuwa na subira, na akiwatishia maadui zake, na akiwaahidi adhabu; "Na hakika walifanyiwa mzaha Mitume waliokuwa kabla yako." Walipowajia umma wao na hoja zilizo wazi, wakawakadhibisha na wakawafanyia mzaha, na yale waliyokuja nayo, basi Mwenyezi Mungu akawaangamiza kwa sababu ya ukafiri huo na kukadhibisha, na akawatimizia sehemu yao kamili ya adhabu. "Lakini wale waliowafanyia mzaha yakawafika yale yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha. Basi jihadharini enyi mnaokadhibisha na kuendelea na kukadhibisha kwenu, mkaja kupatwa na yale yaliyowapata.
#
{11} فإن شككتُم في ذلك أو ارتَبْتم؛ {فسيروا في الأرض ثم انظُروا كيف كان عاقبةُ المكذِّبين}؛ فلن تجدوا إلا قوماً مُهْلَكين، وأمماً في المَثُلات تالفين، قد أوحشت منهم المنازل، وعَدِمَ من تلك الرُّبوع كلُّ متمتِّع بالسرور نازل، أبادهم الملك الجبار، وكان نبؤهم عِبرةً لأولي الأبصار. وهذا السير المأمور به سير القلوب والأبدان الذي يتولَّد منه الاعتبار، وأما مجرَّد النظر من غير اعتبار؛ فإن ذلك لا يفيد شيئاً.
{11} Basi ikiwa una shaka au mnasitasita; "Tembeeni katika dunia, kisha mtazame vipi ulikuwa mwisho wa wanaokadhibisha." Hamtapata isipokuwa kaumu walioangamizwa, na umma walioadhibiwa vikali wakawa magofu, ambao maskani yao yamekuwa ukiwa, na makazi hayo yakakosa kila mwenye kushukia hapo kwa ajili ya starehe. Aliwaangamiza Mfalme, Mwenye kufanya atakalo, na habari yao ikawa mazingatio kwa wenye kuona. Na kutembea huku ambako kuliamrishwa ni kutembea kwa nyoyo na miili ambako yanatokana nako mazingatio. Na ama kuangalia tu bila ya kuzingatia, basi hilo halifaidi kitu.
: 12 #
{قُلْ لِمَنْ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلْ لِلَّهِ كَتَبَ عَلَى نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (12)}.
12. Sema: Ni vya nani vilivyo katika mbingu na katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ameiandika rehemu juu ya nafsi yake. Hakika atawakusanya hadi Siku ya Qiyama isiyokuwa na shaka. Wale waliojihasiri nafsi zao, wao hawaamini.
#
{12} يقول تعالى لنبيه - صلى الله عليه وسلم -: {قُلْ} لهؤلاء المشركين [باللهِ] مقرِّراً لهم وملزماً بالتوحيد: {لِمَن ما في السموات والأرض}؛ أي: من الخالق لذلك المالك له المتصرِّف فيه؟ {قُلْ} لهم: {لله}، وهم مقرُّون بذلك لا ينكرونه، أفلا حين اعترفوا بانفرادِ الله بالملك والتدبير أن يعترِفوا له بالإخلاص والتوحيد؟ وقوله: {كَتَبَ على نفسه الرحمةَ}؛ أي: العالم العلويُّ والسفليُّ تحت ملكه وتدبيرِهِ، وهو تعالى قد بَسَطَ عليهم رحمته وإحسانه، وتغمَّدهم برحمته وامتنانه، وكتب على نفسه كتاباً: أنَّ رحمته تغلب غضبه، وأن العطاء أحبُّ إليه من المنع، وأن الله قد فتح لجميع العباد أبواب الرحمة إن لم يغلقوا عليهم أبوابها بذُنوبهم، ودعاهم إليها إن لم تمنعهم من طلبها معاصيهم وعيوبهم. وقوله: {لَيَجْمَعَنَّكم إلى يوم القيامة لا ريبَ فيه}: وهذا قَسَمٌ منه، وهو أصدق المخبرين، وقد أقام على ذلك من الحجج والبراهين ما يجعله حقَّ اليقين، ولكن أبى الظالمون إلا جحوداً، وأنكروا قدرة الله على بعث الخلائِق، فأوضعوا في معاصيه، وتجرَّؤوا على الكفر به، فخسروا دنياهم وأخراهم، ولهذا قال: {الذين خَسِروا أنفسَهم فهم لا يؤمنونَ}.
{12} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake - rehema na amani zimshukie - "Sema" washirikina hawa [kwa Mwenyezi Mungu] ukiwafanya kukukiri, na ukiwafanya wailazimu Tauhidi: Ni vya nani vilivyo katika mbingu na katika ardhi?" Yaani, ni nani Muumba wa hivyo, Mmiliki wake, Mwenye kuviendesha? "Sema," ukiwaambia, "Ni vya Mwenyezi Mungu," nao wanakiri hilo wala hawalikanushi. Je, kwa nini wanapomkiria Mwenyezi Mungu upweke katika ufalme na kuendesha mambo, hawakumkiria pia kumfanyia mambo kwa ikhlas na kumuabudu Yeye tu. "Yeye ameiandika rehemu juu ya nafsi yake;" Yaani, ulimwengu wa juu na wa chini uko chini ya ufalme wake na uendeshaji Wake. Naye Mtukufu amewakunjulia rehema zake na ihsan yake, na akawafunika kwa rehema zake na neema zake; na akajiandikia andiko kwamba rehema yake inashinda ghadhabu yake. Na kwamba, kutoa ni kupendeza zaidi Kwake kuliko kuzuilia, na kwamba Mwenyezi Mungu amewafungulia waja wake wote milango ya rehema ikiwa hawataifunga wenyewe milango yake kwa dhambi zao, na akawaita kwayo ikiwa dhambi zao na makosa hayatawazuia kuitafuta. Na kauli yake, "Hakika atawakusanya hadi Siku ya Qiyama isiyokuwa na shaka."Na hiki ni kiapo kutoka kwake, na Yeye ndiye Mkweli zaidi wa watoa habari. Na amesimamisha juu ya hayo hoja na ushahidi yenye kuyafanya kuwa yakini ya uhakika, lakini madhalimu walikataa isipokuwa kukanusha tu. Na wakakanusha uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kufufuliwa kwa viumbe, kwa hivyo wakaanguka katika kumuasi, wakafanya ujasiri juu ya kumkufuru Yeye. Kwa hivyo wanahasiri dunia yao na akhera yao, na ndiyo maana akasema; "Wale waliojihasiri nafsi zao, wao hawaamini."
: 13 - 20 #
{وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (13) قُلْ أَغَيْرَ اللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ (14) قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ (15) مَنْ يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ وَذَلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ (16) وَإِنْ يَمْسَسْكَ اللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ وَإِنْ يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (17) وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ (18) قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً قُلِ اللَّهُ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَذَا الْقُرْآنُ لِأُنْذِرَكُمْ بِهِ وَمَنْ بَلَغَ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّهِ آلِهَةً أُخْرَى قُلْ لَا أَشْهَدُ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِمَّا تُشْرِكُونَ (19) الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنْفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (20)}.
13. Na ni vyake vilivyotulia katika usiku na mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 14. Sema: Je, nimfanye rafiki mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mwanzilishi wa mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Hakika Mimi nimeamrishwa kwamba niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 15. Sema: Hakika Mimi ninahofu nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku kubwa. 16. Mwenye kuepushwa nayo Siku hiyo, basi hakika atakuwa amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kuliko wazi. 17. Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara, basi hapana wa kuyaondoa isipokuwa Yeye. Na ikiwa akikugusa kwa heri, basi Yeye ndiye Muweza wa kila kitu. 18. Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake, naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye habari zote. 19. Sema: Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na imefunuliwa kwangu Qur-ani hii ili kwayo niwaonye nyinyi na kila inayemfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami hakika niko mbali na mnaowashirikisha. 20. Wale tuliowapa Kitabu wanakijua kama wanavyowajua watoto wao. Wale waliozihasiri nafsi zao, basi wao hawaamini.
Jua kwamba Sura hii tukufu ilijumuisha kuisimamisha tauhidi kwa kila ushahidi wa kiakili na kimaandiko. Bali ilikuwa karibu yote kuhusiana na tauhidi tu na kuwajadili wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaomkadhibisha Mtume wake. Na katika aya hizi, Mwenyezi Mungu alitaja chenye kubainisha kwazo uongofu, na kuangamiza kwazo shirki.
#
{13} فذكر أن {له} تعالى {ما سَكَنَ في الليل والنهار}، وذلك هو المخلوقاتُ كلُّها من آدميِّها وجنِّها وملائكتها وحيواناتها وجماداتها؛ فالكلُّ خَلْقٌ مدبَّرون وعبيدٌ مسخَّرون لربِّهم العظيم القاهر المالك؛ فهل يصحُّ في عقل ونقل أن يُعْبَدَ من هؤلاء المماليك الذي لا نفع عنده ولا ضُرَّ ويُتْرَكَ الإخلاصُ للخالق المدبِّر المالك الضارِّ النافع؟! أم العقول السليمة والفطر المستقيمة تدعو إلى إخلاص العبادة والحبِّ والخوف والرجاء لله ربِّ العالمين؟ {السميع}: لجميع الأصوات على اختلاف اللُّغات بتفنُّن الحاجات. {العليم}: بما كان وما يكونُ وما لم يكنْ لو كان كيف كان يكونُ، المطَّلع على الظواهر والبواطن.
{13} Basi ikataja kwamba "ni vyake" Yeye Mtukufu "vilivyotulia katika usiku na mchana" na hivyo ni viumbe vyote, kuanzia wanadamu wake, na majini yake, na Malaika wake, na wanyama wake, na visivyo na uhai vyake. Vyote hivyo ni viumbe vinavyoendeshwa, na ni waja waliotiishwa kwa Mola wao Mlezi, Mkuu, Mshindi, Mmiliki. Basi Je, ni sahihi katika akili na maandiko kwamba aabudiwe yeyote katika hao wanaomilikiwa ambao hawana manufaa kwake, wala madhara, na aachwe kufanyiwa ikhlasi Muumba, na Mwendesha mambo, Mmiliki, Mwenye madhara, na Mwenye manufaa? Au je, akili timamu na nyoofu zinaita kwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote ibada, na mapenzi, na hofu na matumaini? "Mwenye kusikia;" sauti zote pamoja na kutofautiana kwa lugha na mahitaji mbalimbali. "Mwenye kujua vyema," yale yaliyokuwa, na yale yatakayokuwa, na yale ambayo hayakuwa lau yangekuwa, yangekuwaje, Mwenye kuyajua yaliyo dhahiri na yaliyofichika.
#
{14} {قل} لهؤلاء المشركين بالله: {أغيرَ الله أتَّخِذُ وليًّا}: من هؤلاء المخلوقات العاجزة يتولاَّني وينصُرُني؛ فلا أتَّخذ من دونه تعالى وليًّا؛ لأنَّه {فاطر السموات والأرض}؛ أي: خالقهما ومدبِّرهما، {وهو يُطْعِمُ ولا يُطْعَمُ}؛ أي: وهو الرازق لجميع الخلق من غير حاجةٍ منه تعالى إليهم؛ فكيف يَليقُ أن أتَّخِذَ وليًّا غير الخالق الرازق الغني الحميد. {قل إنِّي أمِرْتُ أن أكونَ أولَ من أسلم}: لله بالتوحيدِ وأنقاد له بالطاعةِ؛ لأنِّي أولى من غيري بامتثال أوامر ربِّي، {ولا تكوننَّ من المشركين}؛ أي: ونُهيت أيضاً عن أن أكون من المشركين؛ لا في اعتقادِهِم، ولا في مجالستهم، ولا في الاجتماع بهم؛ فهذا أفرضُ الفروض عليَّ وأوجب الواجبات.
{14} "Sema," uwaambie hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, "nimfanye rafiki mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu," katika viumbe hawa wasiojiweza ili wanipe ulinzi na kunisaidia? Basi simchukui asiyekuwa Yeye, Mtukufu kuwa rafiki mwandani. Kwa sababu Yeye "ndiye Muumba mwanzilishi wa mbingu na ardhi;" yaani, Muumba wake na Mwendeshaji wake, "naye ndiye anayelisha wala halishwi?" Yaani, Yeye ndiye Mwenye kuwaruzuku viumbe vyote bila ya Yeye kuwa na haja yoyote kutoka kwao. Basi vipi inafaa kwangu kumchukua rafiki mlinzi asiyekuwa Yeye Muumba, mwenye kuruzuku, mwenye kujitosheleza, Msifiwa? "Sema: Hakika Mimi nimeamrishwa kwamba niwe wa kwanza wa wenye kusilimu;" kwa Mwenyezi Mungu kwa tauhidi na kumfuata kwa utiifu. Kwa sababu mimi ninastahiki zaidi kuliko wengine yeyote kufuata amri za Mola wangu Mlezi, "Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina." Yaani, pia nimekatazwa kuwa miongoni mwa washirikina. Si katika itikadi yao, wala katika kukaa nao, wala katika kukusanyika nao. Na hili ndiyo faradhi ya lazima kwangu, na wajibu wa lazima kwangu.
#
{15} {قل إنِّي أخافُ إن عصيتُ ربِّي عذابَ يوم عظيم}: فإنَّ المعصية في الشرك توجِبُ الخلود في النار وسَخَطَ الجبار.
{15} "Sema: Hakika Mimi ninahofu nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku kubwa;" kwa maana, maasia katika ushirikina yanalazimu kudumu katika Moto na ghadhabu ya Mola Afanyaye atakalo.
#
{16} وذلك اليوم هو اليوم الذي يُخاف عذابُه ويُحذر عقابُه؛ لأنه من صُرِفَ عنه العذابُ يومئذٍ فهو المرحومُ، ومن نجا فيه فهو الفائز حَقًّا؛ كما أنَّ من لم ينجُ منه؛ فهو الهالك الشقيُّ.
{16} Na siku hiyo ndiyo siku ambayo inahofiwa adhabu yake, na yanatahadhariwa mateso yake. Kwa sababu atakayeepushwa na adhabu siku hiyo, basi yeye ndiye aliyerehemewa. Na atakayeokoka ndani yake, basi yeye ndiye aliyefuzu kiuhakika. Kama vile ambaye hataokoka kutokana nayo, basi yeye ndiye aliyeangamia, muovu.
#
{17} ومن أدلة توحيده أنه تعالى المنفرد بكشف الضَّرَّاء وجلب الخير والسَّرَّاء، ولهذا قال: {وإن يَمسَسْكَ الله بضُرٍّ}: من فقرٍ أو مرضٍ أو عسرٍ أو غمٍّ أو همٍّ أو نحوه، {فلا كاشفَ له إلَّا هو وإن يَمْسَسْكَ بخيرٍ فهو على كل شيء قديرٌ}: فإذا كان وحدَه النافعَ الضارَّ؛ فهو الذي يستحقُّ أن يُفْرَدَ بالعبوديَّة والإلهيَّة.
{17} Na miongoni mwa ushahidi upweke ni kwamba Yeye Mtukufu ndiye pekee anayeondoa madhara, na kuleta heri na yale yafurahishayo. Na ndiyo maana akasema, "Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara;" kama vile ufukara, au maradhi, au dhiki, au huzuni, au wasiwasi au mfano wake, "basi hapana wa kuyaondoa isipokuwa Yeye. Na ikiwa akikugusa kwa heri, basi Yeye ndiye Muweza wa kila kitu." Basi ikiwa Yeye peke yake ndiye mwenye kunufaisha na mwenye kudhuru, basi Yeye ndiye anayestahiki peke yake kufanyiwa ibada na kufanyiwa uungu.
#
{18} {وهو القاهرُ فوق عبادِهِ}: فلا يتصرَّفُ منهم متصرِّف ولا يتحرَّك متحرِّك ولا يسكن ساكنٌ إلا بمشيئتِهِ، وليس للملوك وغيرهم الخروجُ عن ملكه وسلطانِهِ، بل هم مدبَّرون مقهورون؛ فإذا كان هو القاهرَ وغيرُه مقهوراً؛ كان هو المستحقَّ للعبادة. {وهو الحكيم}: فيما أمَرَ به ونهى، وأثابَ وعاقبَ، وفيما خَلَقَ وقدَّر، {الخبير}: المطَّلع على السرائر والضمائر وخفايا الأمور، وهذا كلُّه من أدلة التوحيد.
{18} "Na Yeye ndiye Mwenye nguvu za ushindi juu ya waja wake," basi hakuna hata mmoja katika wao awezaye kufanya kitu, hakuna mwenye kusonga awezaye kusonga, wala hatulii mwenye kutulia isipokuwa kwa kutaka kwake, na wafalme na wengineo hawawezi kutoka katika ufalme wake wala mamlaka yake. Bali wao huendeshwa, wametiwa katika nguvu zake za ushindi. Basi ikiwa yeye ndiye Mwenye nguvu za ushindi, na wengineo wametiwa chini ya nguvu zake za ushindi, basi yeye ndiye Anayestahiki kuabudiwa. "Na Yeye ndiye Mwenye hekima" katika yale Aliyoyaamrisha na kuyakataza, na akalipa thawabu na akaadhibu, na katika aliyoyaumba na kuyakadiria "Mwenye habari zote;" Mwenye kujua siri na dhamiri na yaliyofichika ya mambo yote. Na yote haya ni katika ushahidi wa upweke wake.
#
{19} {قل} لهم لمَّا بيَّنَّا لهم الهدى وأوضحنا لهم المسالك: {أيُّ شيء أكبرُ شهادةً}: على هذا الأصل العظيم، {قل اللهُ} أكبرُ شهادةً؛ فهو {شهيدٌ بيني وبينَكم}؛ فلا أعظمَ منه شهادةً ولا أكبرَ، وهو يشهدُ لي بإقراره وفعلِهِ، فَيُقِرُّني على ما قلتُ لكم؛ كما قال تعالى: {ولو تَقَوَّلَ عَلَيْنا بَعْضَ الأقاويل لأخَذْنا منه باليمين ثم لَقَطَعْنا منه الوتينَ}؛ فالله حكيمٌ قديرٌ، فلا يليق بحكمتِهِ وقدرتِهِ أن يقرَّ كاذباً عليه، زاعماً أنَّ الله أرسلَه ولم يرسِلْه، وأن الله أمره بدعوة الخلق ولم يأمره، وأن الله أباح له دماء من خالفَه وأموالهم ونساءهم وهو مع ذلك يصدِّقه بإقرارِهِ وبفعلِهِ، فيؤيِّده على ما قال بالمعجزاتِ الباهرةِ والآياتِ الظاهرة، وينصرُهُ ويخذِلُ مَن خالفه وعاداه؛ فأيُّ شهادةٍ أكبرُ من هذه الشهادة. وقوله: {وأُوْحيَ إليَّ هذا القرآن لأنذِرَكُم به ومَن بَلَغَ}؛ أي: وأوحى الله إليَّ هذا القرآن الكريم لمنفعتِكم ومصلحتِكم؛ لأنْذِرَكُم به من العقاب الأليم، والنّذارة إنما تكون بذكر ما ينذِرُهم به من الترغيب والترهيب وببيان الأعمال والأقوال الظاهرة والباطنة التي مَن قام بها فقد قَبِلَ النذارة؛ فهذا القرآن فيه النذارةُ لكم أيُّها المخاطَبون وكل مَن بَلَغَهُ القرآن إلى يوم القيامة؛ فإن فيه بيان كلِّ ما يُحتاج إليه من المطالب الإلهية. لما بيَّن تعالى شهادَته التي هي أكبر الشهادات على توحيدِهِ؛ قال: قلْ لهؤلاء المعارضين لخبر الله والمكذِّبين لرسله: {أئنَّكم لَتشهدونَ أنَّ مع الله آلهةً أخرى قل لا أشهدُ}؛ أي: إن شهدوا؛ فلا تشهدْ معهم، فوازنْ بين شهادةِ أصدق القائلين وربِّ العالمين، وشهادة أزكى الخلق المؤيَّدة بالبراهين القاطعة والحجج الساطعة على توحيد الله وحدَه لا شريك له، وشهادةِ أهل الشِّرك الذين مَرَجَتْ عقولُهم وأديانُهم وفَسَدَتْ آراؤهم وأخلاقهم وأضحكوا على أنفسهم العقلاءَ، بل خالفتْ شهادتُهم فِطَرَهم وتناقضتْ أقوالُهم على إثبات أنَّ مع الله آلهةً أخرى مع أنه لا يقومُ على ما خالفوه أدنى شُبهة فضلاً عن الحُجج، واختر لنفسك أيَّ الشهادتين إن كنت تعقلُ، ونحن نختارُ لأنفسنا ما اختارَه الله لنبيِّه الذي أمرنا الله بالاقتداء به فقال: {قلْ إنَّما هو إله واحدٌ}؛ أي: منفرد لا يستحقُّ العبوديَّة والإلهية سواه كما أنه المنفرد بالخلق والتدبير. {وإنني بريءٌ مما تشرِكون} به من الأوثان والأنداد وكل ما أُشْرِكَ به مع الله. فهذا حقيقة التوحيد: إثبات الإلهية لله، ونفيها عما عداه.
{19} "Sema," uwaambie tunapowabainishia uwongofu na tukawawekea wazi njia; "Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa kabisa?" Juu ya kanuni hii kuu "Sema: Mwenyezi Mungu," ndiye shahidi mkubwa zaidi. Yeye ndiye "shahidi baina yangu na nyinyi;" kwa hivyo hakuna aliye mkuu zaidi yake wala mkubwa zaidi yake katika ushahidi. Naye ananishuhudia mimi kwa kukiri kwake na kitendo chake. Hivyo basi ananikiria kwa niliyowaambia, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno, basi bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo!" Basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima, Mwenye uwezo, na wala haifai kwa hekima yake na uwezo wake kumkiria mwenye kumzulia uongo, akidai kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyemtuma na ilhali hakumtuma. Na kwamba, Mwenyezi Mungu alimwamrisha kuwalingania viumbe ilhali hakumwamrisha, na kwamba Mwenyezi Mungu alimruhusu kumwaga damu ya wale wanaomhalifu, na mali zao, na wanawake wao, naye pamoja na hayo anamsadiki kwa kumkiria kwake na kitendo chake. Kwa hivyo anamuunga mkono kwa aliyoyasema kwa miujiza ya kushangaza, na Aya zilizo dhahiri, na amnusuru , na awaangushe anayemhalifu na kumfanyia uadui. Basi Je, ni ushahidi gani mkubwa zaidi kuliko ushahidi huu? Na kauli yake, "Na imefunuliwa kwangu Qur-ani hii ili kwayo niwaonye nyinyi na kila inayemfikia;" yaani, Mwenyezi Mungu aliniteremshia hii Qur-ani Tukufu kwa manufaa yenu na masilahi yenu. Kwamba niwaonye kwayo kutokana na adhabu chungu, na maonyo huwa kwa kutaja yale anayowaonya nayo kama vile kutia moyo, na vitisho, na kwa kubainisha vitendo na maneno ya nje na yaliyofichika ambayo mwenye kuyafanya, basi hakika atakuwa ameyakubali maonyo hayo. Basi Qur-ani hii ina maonyo kwenu, enyi mnaoongeleshwa, na kwa kila mwenye kufikiwa na Qur’ani hadi Siku ya Kiyama. Kwa maana, ndani yake kuna ubainisho wa kila matakwa ya kimungu yanayohitajiwa. Wakati Yeye Mtukufu alipobainisha ushahidi Wake, ambao ndio ushahidi mkubwa zaidi wa upweke wake, Akasema: Waambie hawa wanaopinga habari za Mwenyezi Mungu na kuwakadhibisha Mitume wake; "Je kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo." Yaani, wakishuhudia; basi usishuhudie wewe pamoja nao. Linganisha baina ya ushahidi wa msema kweli zaidi kati ya wasemao, na Mola Mlezi wa walimwengu wote, na ushahidi wa aliye safi zaidi katika viumbe vyote unaoungwa mkono na ushahidi wa uhakika, na hoja za wazi juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu peke yake asiyekuwa na mshirika. Na ushahidi wa wenye ushirikina ambao akili zao na dini zao zimepotoshwa, na maoni yao na maadili yao yameharibika; na ambao wamezicheka nafsi zao zenye akili, bali ushahidi wao umehalifu maumbile yao. Na kauli zao zilipingana katika kuthibitisha kwamba kuna miungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu, pamoja na kwamba hata fikira ndogo potofu haitokei kwa yale waliyoyahalifu; achilia mbali hoja mbalimbali. Na jichagulie mwenyewe ni upi kati ya huo ushahidi mbili ikiwa unatumia akili, na sisi tunajichagulia kile alichomchagulia Mwenyezi Mungu Nabii wake ambaye Mwenyezi Mungu alituamrisha tumwige. Kwa hivyo akasema, "Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu;" yaani, Yuko peke yake tu, na hakuna anayestahiki kuabudiwa wala uungu isipokuwa Yeye tu, kama vile Yeye yu peke yake katika uumbaji na uendeshaji. "Nami hakika niko mbali na mnaowashirikisha" naye miongoni mwa viabudiwavyo, na wenza, na kila kinachoshirikishwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi huu ndio uhakika wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu; kuthibitisha uungu kwa Mwenyezi Mungu na kuukanusha kwa asiyekuwa Yeye.
#
{20} لما بيَّن شهادته وشهادة رسوله على التوحيد وشهادة المشركين الذين لا علمَ لديهم على ضدِّه؛ ذكر أنَّ أهل الكتاب من اليهود والنصارى {يعرِفونَه}؛ أي: يعرفون صحة التوحيد، {كما يعرِفون أبناءَهم}؛ أي: لا شكَّ عندهم فيه بوجهٍ؛ كما أنهم لا يشتَبِهون بأولادهم، خصوصاً البنين الملازمين في الغالب لآبائهم، ويُحتمل أن الضمير عائد إلى الرسول محمد - صلى الله عليه وسلم -، وأن أهل الكتاب لا يشتبِهون بصحَّة رسالته ولا يمترون بها لما عندهم من البشارات به ونعوتِهِ التي تنطبق عليه ولا تَصْلُحُ لغيره، والمعنيان متلازمان. قوله: {الذين خَسِروا أنفُسَهم}؛ أي: فَوَّتوها ما خُلِقَتْ له من الإيمان والتوحيد وحَرَموها الفضل من الملك المجيد، {فهم لا يؤمنون}: فإذا لم يوجدِ الإيمان منهم؛ فلا تسألْ عن الخسارِ والشرِّ الذي يحصل لهم.
{20} Alipofafanua ushahidi wake na ushahidi wa Mtume wake juu ya upweke wake, na ushahidi wa washirikina ambao hawana elimu juu ya kinyume chake, akataja kuwa Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, "wanalijua hilo." Yaani, wanajua usahihi wa upweke wake, "kama wanavyowajua watoto wao;" yaani, hawana shaka yoyote katika hilo kwa namna yoyote, kama vile hawachanganyiki kuhusu watoto wao, hasa watoto wao wa kiume ambao wanaandamana aghalabu na baba zao. Na inawezekana kwamba kivumishi (katika wanamjua) kunamrejelea Mtume Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake - na kwamba, Watu wa Kitabu hawachanganyiki kuhusu usahihi wa ujumbe wake wala hawautilii shaka kwa sababu ya bishara njema walizo nazo juu yake na sifa zake ambazo zinamwingia yeye tu, na wala hazimfailii asiyekuwa yeye. Na maana hizo mbili zinaambatana. Kauli yake, "Wale waliozihasiri nafsi zao;" yaani, walizikosesha kile zilizoumbiwa, miongoni mwa imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na wakaziharamishia fadhila ya ufalme wenye heshima, "basi wao hawaamini." Kwa hivyo, ikiwa haikupatikana imani kutoka kwao, basi usiulize juu ya hasara na uovu ambao unawapata.
: 21 #
{وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ (21)}.
21. Na nani dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu, au akazikadhibisha Ishara zake? Hakika madhalimu hawafaulu.
#
{21} أي: لا أعظم ظلماً وعناداً ممَّن كان فيه أحد الوصفين؛ فكيف لو اجتمعا: افتراء الكذب على الله، أو التكذيب بآياته التي جاءت بها المرسلون؟! فإنَّ هذا أظلم الناس، والظالم لا يفلِحُ أبداً، ويدخل في هذا كلُّ من كذب على الله بادِّعاء الشريك له والعوين، أو زعم أنه ينبغي أن يُعْبَدَ غيره، أو اتَّخذ له صاحبةً أو ولداً، وكلُّ من ردَّ الحقَّ الذي جاءت به الرسل أو من قام مقامهم.
{21} Yaani, hakuna kubwa zaidi katika dhuluma na ukaidi kuliko yule ambaye ana sifa moja kati ya mbili hizi. Basi itakuwaje zikijumuika, kumsingizia Mwenyezi Mungu uwongo, au kuzikadhibisha Ishara zake ambazo walikuja nazo Mitume? Basi huyu hakika ndiye dhalimu zaidi miongoni mwa watu. Na dhalimu hafaulu kamwe. Na anaingia katika hili kila mwenye kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu kwa kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika na msaidizi; au anayedai kwamba anafaa kuabudiwa asiyekuwa Yeye; au alimfanya kuwa na mke; au mtoto, na kila mwenye kuikataa haki ambayo walikuja nayo Mitume au mwenye kusimama mahali pao.
: 22 - 24 #
{وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنْتُمْ تَزْعُمُونَ (22) ثُمَّ لَمْ تَكُنْ فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَنْ قَالُوا وَاللَّهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ (23) انْظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ وَضَلَّ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَفْتَرُونَ (24)}
22. Siku tutakapowakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie wale walioshirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mliokuwa mkidai? 23. Kisha hautakuwa udhuru wao isipokuwa ni kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina. 24. Tazama jinsi wanavyosema uongo juu ya nafsi zao wenyewe. Na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua.
#
{22} يخبر تعالى عن مآل أهل الشرك يوم القيامة، وأنهم يُسْألون ويُوَبَّخُونَ فيُقال لهم: أين شركائي الذين كُنْتُم تزعمونَ؛ أي: إن الله ليس له شريك، وإنَّما ذلك على وجه الزعم منهم والافتراء.
{22} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu hatima ya wenye ushirikina Siku ya Kiyama, na kwamba wataulizwa na kukemewa, na wataambiwa: Wako wapi washirika wangu ambao mlikuwa mkidai? Yaani, hakika Mwenyezi Mungu hana mshirika, bali hayo yanatokana na yale waliyodai na kuzua.
#
{23} {ثم لم تكن فتنتُهم}؛ أي: لم يكن جوابُهم حين يُفتنون ويُختبرون بذلك السؤال إلاَّ إنكارَهم لشِرْكهم وحَلِفَهم أنهم ما كانوا مشركين.
{23} "Kisha hautakuwa udhuru wao;" yaani, halitakuwa jawabu lao wakati watakapojaribiwa na kupewa mtihani kwa swali hilo, isipokuwa kukataa kwao ushirikina wao na kuapa kwao kwamba hawakuwa washirikina.
#
{24} {انظر}: متعجباً منهم ومن أحوالهم، {كيف كَذَبوا على أنفسهم}؛ أي: كذبوا كذباً عاد بالخَسارِ على أنفسهم وضَرَّهُم ـ واللهِ ـ غايةَ الضَّرر، {وَضَلَّ عنهم ما كانوا يفترونَ}: من الشُّركاء الذين زعَموهم مع الله، تعالى الله عن ذلك علوًّا كبيراً.
{24} "Tazama," ukiwastaajabu wao na hali zao, "jinsi wanavyosema uongo juu ya nafsi zao wenyewe." Yaani, walisema uongo uliowarudia wenyewe na hasara na ukawadhuru – ninaapa kwa Mwenyezi Mungu – kudhuru kukubwa sana. "Na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua" miongoni mwa washirika ambao walidai kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametukuka kutukuka kukubwa sana juu ya hayo.
: 25 #
{وَمِنْهُمْ مَنْ يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ وَجَعَلْنَا عَلَى قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَنْ يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِنْ يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَا يُؤْمِنُوا بِهَا حَتَّى إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (25)}.
25. Na miongoni mwao wapo wanaokusikiliza; na tumezitia pazia kwenye nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi katika masikio yao, na wakiona kila Ishara, hawaiamini. Mpaka wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema wale waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa hadithi za watu wa kale.
#
{25} أي: ومن هؤلاء المشركين قومٌ يحمِلُهم بعض الأوقات بعض الدواعي إلى الاستماع [لما تقول]، ولكنه استماعٌ خالٍ من قصد الحقِّ واتباعِهِ، ولهذا لا ينتفعونَ بذلك الاستماع لعدم إرادتِهِم للخير. {وجَعَلْنا على قلوبهم أكِنَّةً}؛ أي: أغطيةً وأغشيةً لئلاَّ يَفْقَهوا كلام الله، فصان كلامَه عن أمثال هؤلاء. {وفي آذانِهِم}: جعلنا {وَقْراً}؛ أي: صمماً، فلا يستمِعون ما ينفعهم، {وإن يَرَوْا كلَّ آيةٍ لا يؤمنوا بها}: وهذا غاية الظُّلم والعناد: أنَّ الآيات البيِّنات الدالَّة على الحقِّ لا ينقادون لها ولا يصدِّقون بها، بل يجادِلون الحق بالباطل لِيُدْحِضوه، ولهذا قال: {حتَّى إذا جاؤوك يجادِلونك يقولُ الذين كفروا إنْ هذا إلَّا أساطيرُ الأوَّلين}؛ أي: مأخوذ من صحف الأولين المسطورة التي ليست عن الله ولا عن رسله، وهذا من كفرِهم، وإلاَّ؛ فكيف يكون هذا الكتاب الحاوي لأنباء السابقين واللاحقين والحقائق التي جاءت بها الأنبياء والمرسلون والحق والقسط والعدل التام من كل وجهٍ أساطير الأولين؟!
{25} Yaani, miongoni mwa washirikina hawa wamo kaumu ambao nyakati fulani wanafanywa na mambo fulani kusikiliza [unayoyasema], lakini huko ni kusikiliza bila kukusudia haki na kuifuata. Na ndiyo maana hawanufaiki na kusikiliza huko kwa sababu ya kutotaka kwao heri. "Na tumezitia pazia kwenye nyoyo." Yaani, vya kuifunika na vigubiko ili wasielewe maneno ya Mwenyezi Mungu, hivyo basi akayalinda maneno Yake dhidi ya mfano wa hawa. "Na masikioni mwao" tukatia "uziwi." Basi hawasikii cha kuwanufaisha "na wakiona kila Ishara, hawaiamini." Na huu ndio udhalimu wa mwisho na ukaidi, kwamba Aya zilizo wazi zenye kuonyesha kwenye haki hawazifuati wala hawazisadiki, bali wao wanaijadili haki kwa batili ili waikanushe. Na kwa sababu ya hayo akasema, "Mpaka wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema wale waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa hadithi za watu wa kale. Yaani, yamechukuliwa kutoka katika maandishi ya watu wa kale ambayo hayatokani na Mwenyezi Mungu wala Mitume wake. Na huu ni katika kufuru yao, vinginevyo, basi vipi kitabu hiki chenye habari za waliokuja kabla na baada yao, na mambo ya uhakika ambayo walikuja nayo Manabii na Mitume, na haki, na uadilifu kamili katika kila namna yanaweza kuwa ngano za watu wa kale?
: 26 #
{وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ وَإِنْ يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ (26)}.
26. Nao huwazuia watu hayo, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi isipokuwa nafsi zao tu, wala wao hawatambui.
#
{26} {وهم}؛ أي: المشركون بالله المكذِّبون لرسوله يجمعون بين الضَّلال والإضلال؛ ينهون الناس عن اتباع الحقِّ، ويحذِّرونهم منه، ويبعدون بأنفسهم عنه، ولن يضرُّوا الله ولا عباده المؤمنين بفعلهم هذا شيئاً. {إن يُهلكون إلا أنفُسَهم وما يشعرونَ}: بذلك.
{26} "Nao;" yaani wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaomkadhibisha Mtume wake wanajumuisha kati ya upotovu na kupotosha. Wanawakataza watu kufuata haki, wanawatahadharisha dhidi yake, na wanajiweka wao wenyewe mbali nayo, na hawatamdhuru Mwenyezi Mungu wala waja Wake Waumini kwa kitendo chao hiki hata kidogo. "Nao hawaangamizi isipokuwa nafsi zao tu, wala wao hawalitambui" hilo.
: 27 - 29 #
{وَلَوْ تَرَى إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَالَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (27) بَلْ بَدَا لَهُمْ مَا كَانُوا يُخْفُونَ مِنْ قَبْلُ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ (28) وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ (29)}
27. Na lau ungeona waliposimamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungelirudishwa, wala tusizikadhibishe tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tuwe miongoni wa Waumini. 28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha zamani. Na lau wangelirudishwa, bila ya shaka wangeliyarejea yale yale waliyokatazwa. Na hakika wao ni waongo. 29. Na walisema: Hakuna mengine isipokuwa maisha yetu haya ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa.
#
{27} يقول تعالى مخبراً عن حال المشركين يوم القيامة وإحضارهم النار: {ولو ترى إذْ وُقِفوا على النار}: ليوبَّخوا ويُقَرَّعوا؛ لرأيت أمراً هائلاً وحالاً مفظعة، ولرأيتهم كيف أقرُّوا على أنفسهم بالكفر والفسوق، وتمنَّوا أنْ لو يُرَدُّوا إلى الدُّنيا، {فقالوا يا لَيْتَنا نُرَدُّ ولا نكذِّبَ بآيات ربِّنا ونكونَ من المؤمنين}.
{27} Yeye Mtukufu Anasema akijulisha kuhusu hali ya washirikina Siku ya Kiyama na kuletwa kwao kwenye Moto. "Na lau ungeona waliposimamishwa kwenye Moto," ili wakemewe na kukaripiwa, ungeliona jambo kubwa na hali ya kutisha, na ungewaona namna walivyojikiria nafsi zao ukafiri na kupita mipaka, na wakatamani kwamba lau warejeshwe katika dunia. "Wanasema: Laiti tungelirudishwa, wala asizikadhibishe tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tuwe miongoni wa Waumini."
#
{28} {بل بدا لهم ما كانوا يُخفون من قبلُ}: فإنهم كانوا يُخفون في أنفسهم أنَّهم كانوا كاذبين، ويبدو في قلوبهم في كثير من الأوقات، ولكن الأغراض الفاسدة صدَّتهم عن ذلك وصَدَفَتْ قلوبَهم عن الخير، وهم كَذَبَةٌ في هذه الأمنية، وإنما قصدهم أن يدفعوا بها عن أنفسهم العذاب. فلو {رُدُّوا لعادوا لما نُهوا عنه وإنَّهم لكاذبون}.
{28} "Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha zamani." Wao kwa hakika walikuwa wakijificha katika nafsi zao kwamba wao walikuwa ni waongo, na ikadhihirika katika nyoyo zao mara nyingi. Lakini makusudio maovu yaliwazuia na hayo, na yakazigeuza nyoyo zao kutoka katika heri, nao ni waongo katika matamanio haya, bali nia yao katika ni kuziepusha nafsi zao na adhabu. Na lau "wangelirudishwa, bila ya shaka wangeliyarejea yale yale waliyokatazwa. Na hakika wao ni waongo."
#
{29} {وقالوا} منكرين للبعثِ: {إن هي إلَّا حياتُنا الدُّنيا}؛ أي: ما حقيقة الحال والأمر وما المقصودُ من إيجادِنا إلاَّ الحياة الدُّنيا وحدها، {وما نحن بمبعوثينَ}.
{29} "Na walisema" huku wakikadhibisha ufufuo, "Hakuna mengine isipokuwa maisha yetu haya ya duniani." Yaani, uhakika wa hali na jambo hili, na makusudio ya kuumbwa kwetu si isipokuwa maisha ya dunia pekee, "wala sisi hatutafufuliwa."
: 30 #
{وَلَوْ تَرَى إِذْ وُقِفُوا عَلَى رَبِّهِمْ قَالَ أَلَيْسَ هَذَا بِالْحَقِّ قَالُوا بَلَى وَرَبِّنَا قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنْتُمْ تَكْفُرُونَ (30)}.
30. Na lau utaona walivyosimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akasema, "Je, huu si uhakika?" Na wao wakasema, "Ndiyo? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu (ni uhakika)." Yeye akasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mnakufuru.
#
{30} أي: {ولو ترى} الكافرينَ {إذ وُقِفوا على ربِّهم}؛ لرأيت أمراً عظيماً وهولاً جسيماً، {قال} لهم موبخاً ومقرعاً: {أليس هذا} الذي تَرَوْنَ من العذاب {بالحقِّ قالوا بلى وربِّنا}: فأقرُّوا واعترفوا حيث لا ينفعُهم ذلك، {قال فذوقوا العذابَ بما كنتُم تكفُرون}.
{30} Yaani, "Na lau utawaona" makafiri, "waliposimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi," ungeliona jambo kubwa na la mahangaiko makubwa. "Akasema," akiwaambia kwa kuwakemea na kuwakaripia. "Je, huu" mnaoona katika adhabu? "Si uhakika?" Na wao wakasema, "Ndiyo? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu (ni uhakika)." Kwa hivyo wakakiri na kukubali pale ambapo hilo haliwafai. "Akasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mnakufuru."
: 31 #
{قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّهِ حَتَّى إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَاحَسْرَتَنَا عَلَى مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَى ظُهُورِهِمْ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ (31)}.
31. Hakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipowajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ee majuto yetu kwa yale tuliyoyapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Tazama! Ni maovu mno hayo wanayoyabeba.
#
{31} أي: قد خاب وخَسِرَ وحُرِمَ الخيرُ كلُّه من كذَّب بلقاء الله، فأوجب له هذا التكذيبُ الاجتراء على المحرَّمات واقتراف الموبقات، {حتى إذا جاءتْهم الساعةُ}: وهم على أقبح حال وأسوئهِ، فأظهروا غايةَ الندم، {وقالوا يا حسرتنا على ما فرطنا فيها}: ولكن هذا تحسر ذهب وقته، {وهم يحملون أوزارهم على ظهورهم ألا ساء ما يزِرونَ}: فإنَّ وِزْرَهُم وزرٌ يُثْقِلُهم ولا يقدرون على التخلُّص منه، ولهذا خُلِّدوا في النار، واستحقوا التأبيد في غضب الجبار.
{31} Yaani ameambulia patupu, na amehasirika, na amenyimwa heri mwenye kukanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, na kukamsababishia kukadhibisha huku kuyafanyia ujasiri mambo yaliyoharamishwa, na kufanya madhambi yaangamizayo," "mpaka ilipowajia Saa" hali ya kuwa wamo katika hali mbaya zaidi na mbovu zaidi. Kwa hivyo wakadhihirisha majuto makubwa kabisa, "Ee majuto yetu kwa yale tuliyoyapuuza!" Lakini haya ni majuto ambayo wakati wake ulikwishapita. "Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Tazama! Ni maovu mno hayo wanayoyabeba." Kwani mzigo wao ni mzigo unaowaelemea na wala hawawezi kuuondoa. Na ndiyo maana wakadumishwa milele ndani ya Moto, wakastahiki kudumu milele katika ghadhabu ya Yule Afanyaye atakalo.
: 32 #
{وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (32)}.
32. Na maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao tu. Na hakika Nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wale wanaomcha Mwenyezi Mungu. Basi, je, hamtumii akili?
#
{32} هذه حقيقة الدُّنيا وحقيقة الآخرة: أما حقيقة الدنيا؛ فإنها لعب ولهو، لعب في الأبدان، ولهو في القلوب؛ فالقلوب لها والهةٌ، والنفوس لها عاشقةٌ، والهموم فيها متعلقةٌ، والاشتغال بها كلعب الصبيان. وأما الآخرة؛ فإنَّها {خيرٌ للذين يتَّقون}؛ في ذاتها وصفاتها، وبقائها ودوامها، وفيها ما تشتهيه الأنفُسُ وتَلَذُّ الأعينُ؛ من نعيم القلوب والأرواح، وكثرة السرور والأفراح، ولكنها ليست لكلِّ أحدٍ، وإنما هي للمتَّقين، الذين يفعلون أوامر الله، ويتركون نواهِيَهُ وزواجِرَه، {أفلا تعقِلون}؛ أي: أفلا يكون لكم عقولٌ بها تدرِكون أيَّ الدارين أحق بالإيثارِ؟!
{32} Huu ndio uhakika wa dunia na uhakika wa akhera. Ama uhakika wa dunia, hiyo ni mchezo na pumbao. Ni mchezo katika miili, na pumbao katika nyoyo. Mioyo inauchezea, nafsi inaupenda sana, wasiwasi zimeshikamana nao, na kujishughulisha nao ni kama mchezo wa mtoto. Na ama akhera; hiyo ni "bora zaidi kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu, ni bora hiyo yenyewe na katika sifa zake, na kubaki kwake, na kudumu kwake. Na ndani yake kuna yale yanayotamaniwa na nafsi na macho yanayafurahia; katika neema za nyoyo na roho, na wingi wa furaha, lakini si kwa kila mtu, bali ni kwa wachamungu, wanaotekeleza amri za Mwenyezi Mungu, na wanaacha makatazo yake na makemeo Yake. "Basi je! Hamtumii akili?" Yaani; je, hamna akili ambayo kwayo mnaweza kutambua ni gani kati ya hizi nyumba mbili ndiyo inayostahiki zaidi kupendelewa?
: 33 - 35 #
{قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّهِ يَجْحَدُونَ (33) وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِنْ قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَى مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّى أَتَاهُمْ نَصْرُنَا وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّهِ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِنْ نَبَإِ الْمُرْسَلِينَ (34) وَإِنْ كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُمْ بِآيَةٍ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَى فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ (35)}.
33. Hakika tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu. 34. Na hakika walikadhibiwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipowafikia nusura yetu. Na hapana wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na hakika imekwisha kujia katika habari za Mitume hao. 35. Na ikiwa ni makubwa kwako huku kupeana kwao mgongo, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, angeliwakusanya kwenye uwongofu. Basi kamwe usiwe miongoni mwa wajinga.
#
{33} أي: قد نعلم أنَّ الذي يقول المكذِّبون فيك يَحْزُنُك ويسوؤك، ولم نأمُرْك بما أمَرْناك به من الصبر إلاَّ لِتَحْصَلَ لك المنازلُ العالية، والأحوال الغاليةُ؛ فلا تظنَّ أنَّ قولَهم صادرٌ عن اشتباهٍ في أمرك وشكٍّ فيك؛ {فإنَّهم لا يكذِّبونَك}: لأنهم يعرفون صِدْقَكَ ومَدْخَلَك ومَخْرَجَك وجميع أحوالك، حتى إنَّهم كانوا يسمُّونه قبل بعثتِهِ الأمين، {ولكنَّ الظالمينَ بآياتِ الله يَجْحَدونَ}؛ أي: فإنَّ تكذيبهم لآيات الله التي جعلها الله على يديك.
{33} Yaani, hakika tunajua ya kwamba hayo wanayoyasema wale wanaokadhibisha kukuhusu yanakuhuzunisha na yanakuwiya mabaya. Na hatukukuamrisha yale tuliyokuamrisha ya kuwa na subira isipokuwa tu ili upate vyeo vya juu na hali za thamani. Kwa hivyo usifikiri kwamba kauli yao hiyo inatokana na kuwepo mchanganyiko katika jambo lako na hata kukuhusu wewe mwenyewe. "Hakika wao hawakukadhibishi wewe" kwa sababu wao hakika wanajua ukweli wako, na kuingia kwako na kutoka kwako, na hali zako zote; kiasi kwamba kabla ya utume wake walikuwa wakimuita Al-Amin. "Lakini hao madhalimu wanazikataa ishara za Mwenyezi Mungu," yaani, kukadhibisha kwao huko ni kukadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu alizoweka Mwenyezi Mungu juu ya mikono yako.
#
{34} {ولقد كُذِّبَتْ رسلٌ من قبلك فصبروا على ما كُذِّبوا وأوذوا حتى أتاهم نصرُنا}: فاصبرْ كما صبروا؛ تظفرْ كما ظفروا، {ولقد جاءك من نبإِ المرسلين}؛ ما به يَثْبُتُ فؤادُك، ويطمئنُّ به قلبك.
{34} "Na hakika walikadhibiwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipowajia nusura yetu." Basi wewe subiri kama walivyosubiri, utashinda kama walivyoshinda. "Na hakika imekwisha kujia katika habari za Mitume hao;" yale ambayo yataufanya moyo wako kuwa thabiti na mtulivu.
#
{35} {وإن كان كَبُرَ عليك إعراضُهم}؛ أي: شقَّ عليك من حرصِك عليهم ومحبَّتِك لإيمانهم؛ فابذلْ وسعكَ في ذلك؛ فليس في مقدورك أن تهدي من لم يُرِدِ الله هدايَتَه. {فإنِ استطعتَ أن تبتغيَ نفقاً في الأرض أو سُلَّماً في السماء فتأتيهم بآية}؛ أي: فافعل ذلك؛ فإنه لا يفيدُهم شيئاً، وهذا قطعٌ لطمعه في هدايته أشباه هؤلاء المعاندين، {ولو شاء الله لَجَمعهم على الهُدى}: ولكنَّ حكمته تعالى اقتضت أنَّهم يَبْقَوْن على الضلال، {فلا تكوننَّ من الجاهلينَ}: الذين لا يعرِفون حقائق الأمور ولا ينزِلونها على منازلها.
{35} "Na ikiwa ni makubwa kwako huku kupeana kwao mgongo." Yaani, ikiwa ni vigumu kwako kwa sababu ya hima yako kubwa juu yao, na upendo wako kuona wakiamini, basi jitahidi katika hilo. Lakini si katika uwezo wako kumwongoa yule ambaye Mwenyezi Mungu hakutaka kumwongoa. "Basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara." Yaani, fanya hivyo; kwani haitawanufaisha chochote. Na katika hili kuna kukata matumaini yake katika kuongoa mfano wa hawa wakaidi. "Na lau Mwenyezi Mungu angelitaka, angeliwakusanya juu ya uwongofu." Lakini hekima yake Yeye Mtukufu ilitaka kwamba wabaki katika upotofu. "Basi kamwe usiwe miongoni mwa wajinga;" wale wasiojua uhakika wa mambo na wala hawayaingizi katika nafasi zake.
: 36 - 37 #
{إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ وَالْمَوْتَى يَبْعَثُهُمُ اللَّهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ (36) وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِنْ رَبِّهِ قُلْ إِنَّ اللَّهَ قَادِرٌ عَلَى أَنْ يُنَزِّلَ آيَةً وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (37)}
36. Hakika wanaoitikia ni wale wanaosikia. Na ama wafu, Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake Yeye ndiko watakakorejeshwa. 37. Na walisema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza. Lakini wengi wao hawajui.
#
{36} يقول تعالى لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم -: {إنَّما يستجيب} لدعوتك ويلبِّي رسالتك وينقادُ لأمرك ونهيك، {الذين يسمعونَ}: بقلوبهم ما ينفعُهم، وهم أولو الألباب والأسماع، والمراد بالسماع هنا سماعُ القلب والاستجابة، وإلا فمجرَّد سماع الأذن يشترك فيه البَرُّ والفاجر، فكل المكلَّفين قد قامت عليهم حجة الله تعالى باستماع آياته، فلم يبق لهم عذرٌ في عدم القبول. {والموتى يبعثُهُم اللهُ ثم إليه يُرْجَعون}: يُحتمل أنَّ المعنى مقابل للمعنى المذكور؛ أي: إنما يستجيب لك أحياءُ القلوب، وأما أموات القلوب الذين لا يشعرون بسعادتهم ولا يُحِسُّون بما ينجيهم؛ فإنهم لا يستجيبون لك ولا ينقادون، وموعدهم القيامة، يبعثهم الله ثم إليه يُرْجَعون. ويحتمل أنَّ المراد بالآية على ظاهرِها، وأنَّ الله تعالى يقرِّر المعادَ، وأنه سيبعث الأموات يوم القيامة، ثم ينبِّئهم بما كانوا يعملون، ويكون هذا متضمِّنا للترغيب في الاستجابة لله ورسوله، والترهيب من عدم ذلك.
Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake - "hakika wanoitikia" kulingania kwako, na kuukubali ujumbe wako, na wanafuata amri yako na makatazo yao ni "wale wanaosikia" kwa nyoyo zao yale ya kuwanufaisha, nao ni wale wenye akili na masikio. Na kinachokusudiwa na kusikia hapa ni kusikia kwa moyo na kuitikia; vinginevyo, kusikia kwa masikio tu wanashirikiana katika hilo mwema na muovu. Basi kila anayejukumishwa na sheria tayari hoja ya Mwenyezi Mungu Mtukufu imeshasimama juu yake kwa kusikia Aya zake, na hawakubaki na udhuru wowote wa kutokubali. "Na ama wafu, Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake Yeye ndiko watakakorejeshwa." Inawezekana kwamba maana yake ni kinyume cha maana iliyotajwa hapo juu; yaani, walio hai moyoni tu ndio wanaokuitikia. Ama wale waliokufa mioyoni mwao ambao hawaisikii furaha yao na wala hawahisi kitakachowaokoa; wao hawatakuitikia, wala hawatakufuata, na miadi yao ni siku ya Qiyama. Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake ndiko watakakorejeshwa. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa na Aya hii ni maana yake ya dhahiri, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasimulia uhakika wa kuwepo kwa Qiyama. Na kwamba atawafufua wafu Siku ya Kiyama, kisha atawapa habari juu ya yale waliyokuwa wakiyafanya. Na inakuwa katika hilo, kuhimiza kumuitikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na vitishio dhidi ya kutofanya hivyo.
#
{37} {وقالوا}؛ أي: المكذبون بالرسول تعنُّتاً وعناداً: {لولا نُزِّلَ عليه آيةٌ من ربِّه}؛ يعنون بذلك آيات الاقتراح التي يقترِحونها بعقولهم الفاسدة وآرائهم الكاسدة؛ كقولهم: {وقالوا لن نؤمنَ لك حتى تَفْجُرَ لنا من الأرض يَنبوعاً. أو تكون لك جنَّةٌ من نخيل وعنبٍ فتفجِّرَ الأنهار خلالها تفجيراً. أو تُسْقِطَ السماءَ كما زعمتَ علينا كِسَفاً أو تأتي بالله والملائكة قبيلاً ... } الآيات. {قل}: مجيباً لقولهم: {إن الله قادرٌ على أن ينزِّل آيةً}: فليس في قدرته قصور عن ذلك، كيف وجميع الأشياء منقادةٌ لعزَّته مذعنة لسلطانه. ولكنَّ أكثر الناس لا يعلمونَ، فهم لجهلهم وعدم علمهم يطلبون ما هو شرٌّ لهم من الآيات، التي لو جاءتهم فلم يؤمنوا بها؛ لَعوجِل {وَمَا مِنْ دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُمْ مَا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِنْ شَيْءٍ ثُمَّ إِلَى رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ (38)} وا بالعقاب؛ كما هي سنة الله التي لا تبديل لها، ومع هذا؛ فإنْ كان قصدُهم الآيات التي تبيِّن لهم الحقَّ وتوضِّح السبيل؛ فقد أتى محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - بكلِّ آية قاطعةٍ، وحُجَّةٍ ساطعةٍ، دالَّةٍ على ما جاء به من الحق، بحيث يتمكَّن العبدُ في كل مسألة من مسائل الدين أن يَجِدَ فيما جاء به عدَّة أدلَّة عقليَّة ونقليَّة؛ بحيث لا تبقي في القلوب أدنى شكٍّ وارتياب، فتبارك الذي أرسل رسوله بالهدى ودين الحقِّ وأيَّده بالآيات البيِّنات لِيَهْلِكَ من هَلَكَ عن بينة ويحيا من حَيَّ عن بينةٍ، وإن الله لسميعٌ عليمٌ.
{37} "Na walisema;" yaani, wale waliomkadhibisha Mtume kwa usugu na ukaidi, "kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Wakimaanisha kwa hilo Aya za mapendekezo wanazozipendekeza wao kwa akili zao mbovu na maoni potovu. Kama kauli yao, "Na walisema; Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii. Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, na utupasulie mito kati yake ikimiminika. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso..." hadi mwisho wa Aya. "Sema" ukiwajibu kauli yao: "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza." Kwani hakuna upungufu wa kufanya hivyo katika uwezo Wake, vipi na ilhali vitu vyote vinafuata kwa sababu ya nguvu zake, na vinanyenyekea kwa sababu ya mamlaka yake. Lakini wengi wa watu hawajui, na hivyo wao kwa sababu ya ujinga wao na kutojua kwao, wanataka kile ambacho ni shari kwao miongoni mwa ishara ambazo lau zitawajia na wasiziamini, basi wangeharakishiwa adhabu. "Na hapana mnyama yeyote katika ardhi, wala ndege anayepaa kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza chochote katika Kitabu. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa." Na kwa adhabu kama ilivyo ni Sunna ya mwenyezi Mungu ambayo haiwezi kubadilishwa. Na pamoja na hili, ikiwa makusudio yao ni Aya zinazowabainishia Haki na zinazowawekea njia wazi, basi hakika Muhammad - Swalah na salamu zimshukie - alikwisha kuja na kila Aya ya mkato, na hoja iliyo wazi inayoonyesha yale aliyokuja nayo ya haki; kiasi kwamba mja anaweza katika kila suala la dini kupata katika yale aliyoleta ushahidi kadhaa wa kiakili na wa kimaandiko, kiasi kwamba haibaki katika mioyo shaka hata kidogo na kusitasita. Basi ni mwingi wa baraka yule aliyemtuma Mtume wake na uwongofu na dini ya haki, na akaiunga mkono kwa Aya zilizo wazi. Ili mwenye kuangamia aangamie kwa hoja iliyo wazi, na mwenye kubaki hai abaki hai kwa hoja iliyo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye elimu ya yote.
: 38 #
{وَمَا مِنْ دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُمْ مَا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِنْ شَيْءٍ ثُمَّ إِلَى رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ (38)}
38. Na hakuna mnyama yeyote katika ardhi, wala ndege anayepaa kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza kitu chochote katika Kitabu. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.
#
{38} أي: جميع الحيوانات الأرضية والهوائية من البهائم والوحوش والطيور كلُّها أممٌ أمثالُكم، خلَقْناها كما خلَقْناكم، ورزقْناها كما رزقناكم، ونفذتْ فيها مشيئتُنا وقدرتُنا كما كانت نافذة فيكم. {ما فرَّطْنا في الكتاب من شيء}؛ أي: ما أهملنا ولا أغفلنا في اللوح المحفوظ شيئاً من الأشياء، بل جميعُ الأشياء ـ صغيرها وكبيرها ـ مثبتةٌ في اللوح المحفوظ على ما هي عليه، فتقع جميع الحوادث طِبْقَ ما جرى به القلم. وفي هذه الآية دليلٌ على أن الكتاب الأول قد حوى جميع الكائنات، وهذا أحدُ مراتب القضاء والقدر؛ فإنها أربعُ مراتب: علمُ الله الشامل لجميع الأشياء، وكتابُهُ المحيط بجميع الموجودات، ومشيئتُهُ وقدرتُهُ النافذة العامَّة لكلِّ شيءٍ، وخَلْقُه لجميع المخلوقات حتى أفعال العباد. ويُحتمل أنَّ المراد بالكتاب هذا القرآن، وأنَّ المعنى كالمعنى في قوله تعالى: {ونَزَّلْنا عَلَيْكَ الكِتابَ تِبيْاناً لِكُلِّ شيءٍ}. وقوله: {ثمَّ إلى رَبِّهِمْ يُحْشَرونَ}؛ أي: جميع الأمم تُحشر وتُجمع إلى الله في موقف القيامة، في ذلك الموقف العظيم الهائل، فيجازيهم بعدلِهِ وإحسانِهِ، ويُمضي عليهم حُكمَهُ الذي يَحْمَدُه عليه الأولون والآخرون؛ أهل السماء وأهل الأرض.
{38} Yaani, Wanyama wote wa ardhini na wa angani, miongoni mwa wanyama wa mifugo, na wanyama mwitu, na ndege, wote ni umma mfano wenu. Tuliwaumba kama tulivyowaumba nyinyi, na tukawaruzuku kama tulivyowaruzuku nyinyi, na mapenzi yetu na uwezo wetu yanatekelezeka kwao kama vile yanavyotekelezeka kwenu. "Hatukupuuza chochote katika Kitabu." Yaani, hatukupuuza wala kughafilika tukaacha kitu katika Ubao uliohofadhiwa. Bali vitu vyote - vidogo vyake na vikubwa vyake - vimenakiliwa katika Ubao Uliohifadhiwa jinsi vilivyo. Basi matukio yote yanatokea kama yalivyoandikwa na Kalamu. Na katika Aya hii kuna ushahidi kwamba lile andiko la kwanza lilijumuisha viumbe vyote. Na hili ni moja ya daraja za hukumu na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kwani ni daraja nne: Elimu ya Mwenyezi Mungu inayojumuisha kila kitu, na kuandika kwake kunakojumuisha vitu vyote vilivyopo, na mapenzi Yake na uwezo wake unaotekelezeka kiujumla juu ya kila kitu, na kuumba Kwake viumbe vyote, hata vitendo vya waja Wake. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa na Kitabu ni Qur’ani hii, na kwamba maana yake ni kama maana ya kauli yake Mola Mtukufu; "Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu." Na kauli yake, "Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa;" yaani, umma zote watakusanywa na kujumuishwa kwa Mwenyezi Mungu katika mahali pa Qiyama. Na katika mahali hapo pakubwa na pazito, atawalipa kwa uadilifu wake na ihsani yake, na atawapitishia hukumu yake ambayo kwayo atahimidiwa na wa mwanzo na wa mwisho. Wakazi wa mbinguni na wakazi wa duniani.
: 39 #
{وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ مَنْ يَشَإِ اللَّهُ يُضْلِلْهُ وَمَنْ يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (39)}.
39. Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu ni viziwi na mabubu wamo katika giza mbalimbali. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka, anampoteza, na yule ambaye anataka, anamuweka katika Njia iliyonyooka.
#
{39} هذا بيانٌ لحال المكذِّبين بآيات الله المكذِّبين لرسله: أنَّهم قد سدُّوا على أنفسهم باب الهُدى، وفتحوا باب الرَّدى، وأنهم {صُمٌّ} عن سماع الحقِّ، {بُكْمٌ} عن النُّطق به؛ فلا ينطِقون إلا بالباطل ، {في الظُّلمات}؛ أي: منغمِسون في ظلمات الجهل والكفر والظُّلم والعناد والمعاصي، وهذا من إضلال اللهِ إيَّاهم؛ فمن {يَشَإِ اللهُ يُضْلِلْهُ ومن يَشَأ يَجْعَلْهُ على صراطٍ مستقيم}؛ لأنَّه المنفرد بالهداية والإضلال بحسبِ ما اقتضاه فضله وحكمته.
{39} Haya ni kubainisha hali ya wale waliokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na waliowakadhibisha Mitume wake, kwamba wao wenyewe walijifungia mlango wa uwongofu, na wakajifungulia mlango wa maangamivu; na kwamba wao ni "viziwi" wasioisikia haki, "mabubu" wasioweza kuizungumza. Basi hawazungumzi isipokuwa batili "wamo katika giza mbalimbali". Yaani, walitumbukia katika giza mbalimbali la ujinga, na ukafiri, na dhulma, na ukaidi, na maasia; na haya ni katika Mwenyezi Mungu kuwapoteza. Basi yule ambaye "Mwenyezi Mungu anataka, anampoteza, na yule ambaye anataka, anamuweka katika Njia iliyonyooka." Kwa sababu ni Yeye pekee wa kuongoza na kupotosha kulingana na inavyotaka neema yake na hekima yake.
: 40 - 41 #
{قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّهِ تَدْعُونَ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (40) بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِنْ شَاءَ وَتَنْسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ (41)}
40. Sema: Mwaonaje ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikawajia hiyo Saa, asiyekuwa Mwenyezi Mungu ndiye mtakayemuomba, ikiwa nyinyi ni wakweli? 41. Bali Yeye ndiye mtakayemuomba, naye atawaondolea mnachomwombea akipenda. Na mtasahau hao mnaowafanya washirika wake.
#
{40} يقول تعالى لرسوله: {قُلْ} للمشركين بالله العادلينَ به غيره: {أرأيْتَكُم إن أتاكم عذابُ اللهِ أو أتَتْكُمُ الساعةُ أغير الله تدعونَ إن كنتم صادقين}؛ أي: إذا حَصَلَتْ هذه المشقات وهذه الكروب التي يُضْطَرُّ إلى دفعِها؛ هل تدعونَ آلهتكم وأصنامكم أم تدعونَ ربَّكم المَلِكَ الحقَّ المبين؟
{40} Yeye Mtukufu anamwambia Mtume wake, "Sema" uwaambie wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaolinganisha na asiyekuwa yeye. "Mwaonaje ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikawajia hiyo Saa, asiyekuwa Mwenyezi Mungu ndiye mtakayemuomba, ikiwa nyinyi ni wakweli?" Yaani, ikiwa taabu hizi zitatokea na dhiki hizi ambazo analazimika kuzizuia. Je, mtawaomba miungu wenu na masanamu yenu au mtamuomba Mola wenu Mlezi, Mfalme wa Haki na aliye wazi?
#
{41} {بل إيَّاه تدعونَ فيكشِفُ ما تدعونَ إليه إن شاءَ وَتَنْسَوْنَ ما تُشْرِكون}: فإذا كانت هذه حالُكم مع أندادِكُم عند الشدائد؛ تَنْسَوْنَهم لعلمِكُم أنهم لا يملِكون لكم ضَرًّا ولا نفعاً ولا موتاً ولا حياة ولا نشوراً، وتخلِصونَ لله الدعاءَ؛ لِعلْمِكُم أنَّه هو الضارُّ النافعُ المجيبُ لدعوةِ المضطرِّ؛ فما بالُكم في الرخاء تُشْرِكونَ به وتجعلونَ له شركاء؟! هل دلَّكم على ذلك عقلٌ أو نقلٌ؟ أم عندَكم من سلطان بهذا؟ أم تفترونَ على الله الكذب؟
{41} "Bali Yeye ndiye mtakayemuomba, naye atawaondolea mnachomwombea akipenda. Na mtasahau hao mnaowafanya washirika wake." Basi ikiwa hii ndiyo hali yenu pamoja na wenza wenu hawa katika nyakati za shida, mnawasahau kwa sababu mnajua kwamba wao hawawamilikii kudhuru, wala kunufaisha, wala mauti, wala uhai, wala kufufua, na mnamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake dua Kwa sababu mnajua kwamba Yeye tu ndiye mwenye kudhuru, mwenye kunufaisha, mwenye kuitikia maombi ya mwenye haja kubwa. Basi mna nini katika hali nzuri mnamshirikisha na mnamfanyia washirika? Je, iliwaonyesha hilo akili au andiko? Au mna mamlaka yoyote juu ya hili? Au mnamzulia Mwenyezi Mungu uongo?
: 42 - 45 #
{وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَى أُمَمٍ مِنْ قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُمْ بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ (42) فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُمْ بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَكِنْ قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (43) فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّى إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُمْ بَغْتَةً فَإِذَا هُمْ مُبْلِسُونَ (44) فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ (45)}.
42. Na kwa yakini tuliwatuma Mitume kwa kaumu zilizokuwa kabla yako, kisha tukawatia katika dhiki na mashaka ili wanyenyekee. 43. Kwa nini wasinyenyekee ilipowafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu, na Shetani akawapambia waliyokuwa wakiyafanya. 44. Basi waliposahau yale waliyokumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipofurahia yale waliyopewa, tukawashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa. 45. Ikakatwa mizizi ya kaumu waliodhulumu, na kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
#
{42} يقول تعالى: {ولقد أرْسَلْنا إلى أمم من قبلِكَ}: من الأمم السالفينَ، والقرونِ المتقدِّمينَ، فكذَّبوا رُسَلنا، وجحدوا بآياتنا، {فأخذْناهم بالبأساءِ والضَّرَّاء}؛ أي: بالفقر والمرض والآفات والمصائب رحمةً منَّا بهم، {لعلَّهم يَتَضَرَّعونَ} إلينا، ويلجؤون عند الشدةِ إلينا.
{42} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kwa yakini tuliwatuma Mitume kwa kaumu zilizokuwa kabla yako," katika umma zilizotangulia, na vizazi vya mbeleni, lakini wakawakadhibisha Mitume wetu na wakazikataa Ishara zetu. "Kisha tukawatia katika dhiki na mashaka;" yaani, umaskini, na maradhi, na dhiki, na misiba kwa sababu ya rehema yetu juu yao; "ili wanyenyekee" na wakimbilie kwetu wakati wa ugumu.
#
{43} {فلولا إذ جاءهم بأسنا تضرعوا ولكن قست قلوبهم}؛ أي: استحجرت فلا تلين للحقِّ، {وزيَّن لهم الشيطانُ ما كانوا يعملونَ}: فظنُّوا أنَّ ما هم عليه دينُ الحق، فتمتَّعوا في باطلهم برهةً من الزمان، ولعب بعقولهم الشيطان.
{43} "Kwa nini wasinyenyekee ilipowafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu." Yaani, zilikuwa mawe na hazikulainikia haki, “na Shetani akawapambia waliyokuwa wakiyafanya.” Kwa hivyo wakadhani kwamba yale wanayoyafuata ndiyo dini ya haki, kwa hivyo wakafurahia katika batili yao kiasi fulani katika muda, na Shetani akazichezea akili zao.
#
{44} {فلمَّا نَسُوا ما ذُكِّروا به فَتَحْنا عليهم أبوابَ كلِّ شيءٍ}: من الدنيا ولذَّاتها وغفلاتها، {حتى إذا فرحوا بما أوتوا أخَذْناهم بغتةً فإذا هم مُبْلِسونَ}؛ أي: آيسون من كل خيرٍ، وهذا أشدُّ ما يكون من العذاب: أن يُؤْخَذوا على غِرَّةٍ وغفلةٍ وطمأنينةٍ؛ ليكون أشد لعقوبتهم، وأعظم لمصيبتهم.
{44} "Basi waliposahau yale waliyokumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu," katika dunia na starehe zake na yale yake ya kusahaulisha. "Mpaka walipofurahia yale waliyopewa, tukawashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa." Yaani, walikata tamaa ya kufikia kila heri. Na hii ndiyo adhabu kali zaidi kwamba washikwe kwa ghafla huku wameghafilika, na wametulia, ili liwe kali zaidi katika kuwaadhibu, na kubwa zaidi kwa msiba wao.
#
{45} {فقُطِعَ دابرُ القوم الذين ظلموا}؛ أي: اصطلموا العذاب، وتقطَّعت بهم الأسباب {والحمدُ لله ربِّ العالمين}: على ما قضاه وقدَّره من هلاك المكذِّبين؛ فإنَّ بذلك تتبيَّن آياتُهُ وإكرامُهُ لأوليائِهِ، وإهانتُهُ لأعدائِهِ، وصدقُ ما جاءت به المرسلون.
{45} "Ikakatwa mizizi ya kaumu waliodhulumu," yaani, walipitiwa na adhabu, na njia zao zikakatizwa baina yao. "Na kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote," kwa yale aliyoyahukumu na kujalia ya kuwaangamiza wanaokadhibisha. Kwani kwa hilo zinabainika Aya zake, na heshima yake, na marafiki wake, na kuwadunisha kwake maadui zake, na ukweli wa yale waliyokuja nayo Mitume.
: 46 - 47 #
{قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَى قُلُوبِكُمْ مَنْ إِلَهٌ غَيْرُ اللَّهِ يَأْتِيكُمْ بِهِ انْظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ (46) قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ (47)}.
46. Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea hayo tena? Angalia vipi tunavyozieleza Ishara, kisha wao wanapuuza. 47. Sema: Mwaonaje, ikiwafikia adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhahiri, je wataangamizwa isipokuwa kaumu waliodhulumu?
#
{46} يخبر تعالى أنَّه كما هو المتفرِّد بخَلْق الأشياء وتدبيرها؛ فإنَّه المنفرد بالوحدانيَّةِ والإلهية، فقال: قل: {أرأيتُم إن أخذ الله سمعكم وأبصاركم وخَتَمَ على قلوبكم}: فبقيتُم بلا سمع ولا بصر ولا عقل. {من إلهٌ غيرُ الله يأتيكم به}: فإذا لم يكن غير الله يأتي بذلك؛ فلم عبدتُم معه من لا قدرةَ له على شيءٍ إلاَّ إذا شاءه الله؟ وهذا من أدلة التوحيد وبطلان الشرك، ولهذا قال: {انظرْ كيف نصرِّفُ الآياتِ}؛ أي: ننوِّعها، ونأتي بها في كلِّ فنٍّ، ولتنير الحقَّ، وتتبيَّن سبيل المجرمين. {ثم هم}: مع هذا البيان التامِّ، {يصدِفونَ}: عن آيات الله، ويعرِضون عنها.
{46} Yeye mtukufu anajulisha kwamba, kama vile Yeye peke yake katika kuumba na kusimamia vitu; kwani Yeye pekee ndiye mwenye upweke na Uungu. Na akasema, Sema: "Je Mwaonaje Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu?" Basi mkabaki bila kusikia, kuona, wala akili. "Ni mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea hayo tena?" Ikiwa hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu awezaye kukuletea; kwa nini uliabudu pamoja naye mtu ambaye hana uwezo wa kufanya chochote isipokuwa Mungu akitaka? Huu ni ushahidi wa tauhidi na ubatili wa ushirikina, na ndiyo maana akasema, "Angalia vipi tunavyozieleza Ishar." Yaani, tunaigawanya, na tunaileta katika kila sanaa, ili iangazie haki na kudhihirisha njia ya wahalifu. "Kisha wao," pamoja na kubainisha huku kamili "wanazipuuza" Ishara za Mwenyezi Mungu, na wanazipa mgongo.
#
{47} {قل أرأيْتَكُم}؛ أي: أخبروني {إن أتاكم عذابُ الله بغتةً أو جهرةً}؛ أي: مفاجأةً أو قد تقدَّم أمامه مقدماتٌ تعلمون بها وقوعَه، {هل يُهْلَكُ إلَّا القومُ الظالمون}: الذين صاروا سبباً لوقوع العذابِ بهم بظلمِهم وعنادِهم؛ فاحذروا أن تقيموا على الظُّلم؛ فإنه الهلاك الأبدي، والشقاءُ السرمديُّ.
{47} "Sema: Mwaonaje;" yaani, niambieni, “ikiwafikia adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhahiri.” Yaani, kwa ghafla au baada ya kutangulia vile vitangulizi mnavyojua kwavyo kutokea kwake; "je wataangamizwa isipokuwa kaumu waliodhulumu?" Wale ambao wamekuwa ni sababu ya kuwapata adhabu kwa dhulma yao na ukaidi. Kwa hivyo jihadhari na kuendelea juu ya dhuluma. Kwani huo ni uangamivu wa milele na mashaka ya milele.
: 48 - 49 #
{وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ (48) وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ (49)}.
48. Na hatuwatumi Mitume isipokuwa huwa ni wabashiri na waonyaji. Basi mwenye kuamini na akatengenea, haitakuwa hofu yoyote juu yao, wala hawatahuzunika. 49. Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka.
#
{48} يذكر تعالى زبدةَ ما أرسل به المرسلين أنَّه البِشارة والنِّذارة، وذلك مستلزمٌ لبيان: المبشِّر والمبَشَّر به والأعمال التي إذا عملها العبدُ حصلت له البشارة، والمنْذِر والمنذَر والمنْذَر به والأعمال التي من عَمِلَها حقَّت عليه النِّذارة، ولكن الناس انقَسموا بحسب إجابتهم لدعوتهم وعدمها إلى قسمين: {فَمنْ آمنَ وأصلحَ}؛ أي: آمن باللهِ وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر، وأصلح إيمانه وأعماله ونيَّته، {فلا خوفٌ عليهم}: فيما يُستقبل، {ولا هم يحزنونَ}: على ما مضى.
{48} Yeye Mtukufu anataja kiini alichowatuma nacho Mitume, kuwa ni bishara na maonyo, na hilo linalazimu kufafanuliwa: mwenye bishara, na bishara yeyewe, na vitendo ambavyo mja akivifanya, anaipata bishara hii, na mwonyaji, na anayeonywa, na kinachoonywa dhidi yake, na matendo ambayo mwenye kuyafanya, atastahiki maonyo. Lakini watu waligawanyika kulingana na kuwalingania kwao na kutoitikia katika sehemu mbili: "Basi mwenye kuamini na akatengenea;" yaani, alimwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho. Na akaifanya Imani yake kuwa nzuri, na vitendo vyake, na makusudio yake, "haitakuwa hofu yoyote juu yao," kuhusu yale yajayo; "wala hawatahuzunika" juu ya yale yaliyopita.
#
{49} {والذين كذَّبوا بآياتِنا يَمَسُّهُم العذابُ}؛ أي: ينالُهم ويذوقونه، {بما كانوا يفسقون}.
{49} "Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu itawagusa adhabu." Yaani itawafikia na wataionja, "kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka."
: 50 #
{قُلْ لَا أَقُولُ لَكُمْ عِنْدِي خَزَائِنُ اللَّهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَى إِلَيَّ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَى وَالْبَصِيرُ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ (50)}.
50. Sema: Mimi siwaambii kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyofichikana. Wala siwaambii kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?
#
{50} يقول تعالى لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم - المقترِحين عليه الآياتِ، أو القائلينَ له إنَّما تدعونا لنتَّخِذَك إلهاً مع الله: {لا أقولُ لكم عندي خزائنُ الله}؛ أي: مفاتيح رزقِهِ ورحمتِهِ، {ولا أعلم الغيبَ}: وإنَّما ذلك كلُّه عند الله؛ فهو الذي ما يفتحُ للناس من رحمةٍ فلا ممسك لها وما يمسكُ فلا مرسلَ له من بعدِهِ، وهو وحده عالمُ الغيب والشهادة فلا يُظْهِرُ على غيبِهِ أحداً إلا من ارتضى من رسول. {ولا أقولُ لكم إني مَلَكٌ}: فأكون نافذَ التصرُّف قويًّا، فلست أدَّعي فوق منزلتي التي أنزلني الله بها، {إن أتَّبِعُ إلَّا ما يُوحى إليَّ}؛ أي: هذا غايتي ومنتهى أمري وأعلاه، إنْ أتَّبِع إلاَّ ما يوحى إليَّ، فأعمل به في نفسي، وأدعو الخلق كلَّهم إلى ذلك؛ فإذا عُرِفت منزلتي؛ فلأي شيء يبحثُ الباحث معي أو يطلب مني أمراً لست أدَّعيه؟! وهل يُلْزَمُ الإنسان بغير ما هو بصددِهِ؟! ولأي شيء إذا دعوتكم بما يوحى إليَّ أن تلزموني أني أدَّعي لنفسي غير مرتبتي؟! وهل هذا إلا ظلمٌ منكم وعنادٌ وتمرُّدٌ؟! قل لهم في بيان الفرق بينَ مَنْ قَبِلَ دعوتي وانقاد لما أوحي إليَّ وبين من لم يكن كذلك: {قُلْ هل يَسْتوي الأعمى والبصيرُ أفلا تتفكَّرونَ}: فتنزِلون الأشياءَ منازلَها وتختارون ما هو أولى بالاختيار والإيثار.
{50} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake – rehema na amani ziwe juu yake – juu ya wale waliompendekezea Aya mbalimbali, au wale wanaomwambia: Wewe hakika unatuita tu ili tukufanye wewe kuwa mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. "Mimi siwaambii kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu;" yaani, funguo za riziki yake na rehema yake, "Wala sijui ghaibu." Lakini hayo yote yako kwa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye rehema ambayo anawafungulia watu, hapana wa kuizuia. Na kile anachokizuia, hapana wa kukiachilia isipokuwa Yeye tu. Na Yeye peke yake ndiye anayejua ghaibu na yanayoshuhudiwa. Kwa hivyo, hamdhihirishii yeyote ghaibu yake isipokuwa yule anayemridhia miongoni mwa Mitume. "Wala siwaambii kuwa mimi ni Malaika" ili niwe mwenye kutekeleza amri yangu, mwenye nguvu, wala sidai kuwa juu ya daraja yangu ambayo Mwenyezi Mungu ameniteremsha kwayo. "Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu;" yaani, hiki ndicho kikomo changu na mwisho wa jambo langu, na la juu lake zaidi. Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu, kwa hivyo ninayafanyia kazi mimi mwenyewe, na ninawalingania viumbe vyote kufanya hivyo. Kwa hivyo ikiwa daraja yangu inajulikana; basi ni kwa kitu gani mtafutaji anatafuta kwangu, au anataka kutoka kwangu jambo ambalo silidai? Na je ,mtu anapaswa kulazimishwa kitu kingine zaidi ya yale aliyoyakusudia? Na ni kwa kitu gani nikiwalingania kwa yale niliyoteremshiwa, mnanilazimisha kwamba mimi ninajidaisha mwenyewe isiyokuwa daraja yangu? Na je, hii si isipokuwa dhuluma kutoka kwenu, na ukaidi na uasi? Waambie katika kubainisha tafauti baina ya mwenye kukubali wito wangu na akafuata yale niliyoteremshiwa, na yule asiyekuwa hivyo. "Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?" Kwa hivyo mkaviteremsha vitu katika daraja zake, na mchague kile kinachostahili zaidi kuchaguliwa na kupendelewa.
: 51 - 55 #
{وَأَنْذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْ يُحْشَرُوا إِلَى رَبِّهِمْ لَيْسَ لَهُمْ مِنْ دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ (51) وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِمْ مِنْ شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِمْ مِنْ شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ (52) وَكَذَلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُمْ بِبَعْضٍ لِيَقُولُوا أَهَؤُلَاءِ مَنَّ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنْ بَيْنِنَا أَلَيْسَ اللَّهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ (53) وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَى نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنْكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِنْ بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (54) وَكَذَلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ (55)}.
51. Na waonye kwayo wale wanaohofu kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali ya kuwa hawana kando naye mlinzi wala mwombezi, ili wamche Mwenyezi Mungu. 52. Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu. 53. Na hivi ndivyo tunavyowajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanaoshukuru? 54. Na wanapokujia wanaoziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! (Amani iwe juu yenu!) Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakayefanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. 55. Na ndivyo hivyo tunavyozieleza Ishara, na ili ibainike njia ya wahalifu.
#
{51} هذا القرآن نذارةٌ للخلق كلِّهم، ولكن إنَّما ينتفع به {الذين يخافون أن يُحْشَروا إلى ربِّهم}؛ فهم متيقِّنون للانتقال من هذه الدار إلى دار القرار؛ فلذلك يستصحِبون ما ينفعهم ويَدَعون ما يضرُّهم. {ليس لهم من دونه}؛ أي: من دون الله {وليٌّ ولا شفيعٌ}؛ أي: لا من يتولى أمرهم فيحصِّلُ لهم المطلوب، ويدفعُ عنهم المحذور، ولا من يشفعُ لهم؛ لأن الخلق كلَّهم ليس لهم من الأمر شيء. {لعلهم يتَّقون}: الله بامتثال أوامرِهِ واجتنابِ نواهيه؛ فإنَّ الإنذار موجب لذلك وسبب من أسبابه.
{51} Qur’ani hii ni onyo kwa viumbe wote, lakini wanafaidika nayo tu; "wale wanaohofu kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi." Basi wao wana yakini ya kuondoka kutoka kwenye Nyumba hii hadi kwenye nyumba ya kudumu. Ndiyo maana wanachukua pamoja nao yale yatakayowanufaisha na wanayaacha yale ambayo yatawadhuru. "Hawana kando naye"; yaani, kando na Mwenyezi Mungu, "msimamizi wala mwombezi." Yaani, hakuna wa kuwasimamia mambo yao ili wapate wanayoyataka, na kuwazuia kutokana na yale wanayoyatahadhari, wala hakuna wa kuwaombea. Kwa sababu viumbe wote hawana kitu chochote katika jambo hilo. "Ili wamche Mwenyezi Mungu" kwa kutekeleza amri zake na kuepuka makatazo yake. Kwa maana onyo linasababisha hayo, na ni sababu miongoni mwa sababu zake.
#
{52} {ولا تطردِ الذين يدعون ربَّهم بالغداة والعشي يريدون وجهه}؛ أي: لا تطرد عنك وعن مجالستك أهل العبادة والإخلاص رغبةً في مجالسة غيرهم، من الملازمين لدعاءِ ربِّهم دعاء العبادة بالذِّكر والصلاة ونحوها ودعاء المسألة في أول النهار وآخره، وهم قاصدون بذلك وجه الله، ليس لهم من الأغراض سوى ذلك الغرض الجليل؛ فهؤلاء ليسوا مستحقين للطرد والإعراض عنهم، بل هم مستحقُّون لموالاتهم ومحبتهم وإدنائهم وتقريبهم؛ لأنهم الصفوة من الخلق ـ وإن كانوا فقراء ـ الأعزاء في الحقيقة، وإن كانوا عند الناس أذلاء. {ما عليك من حسابِهِم من شيءٍ وما من حسابِكَ عليهم من شيءٍ}؛ أي: كلٌّ له حسابُهُ وله عملُهُ الحسنُ وعملُهُ القبيحُ، {فتطرُدَهم فتكونَ من الظالمين}: وقد امتثلَ - صلى الله عليه وسلم - هذا الأمر أشدَّ امتثال، فكان إذا جلس الفقراء من المؤمنين؛ صبَّر نفسه معهم، وأحسن معاملتهم، وألان لهم جانبه، وحسَّن خلقه، وقرَّبهم منه، بل كانوا هم أكثر أهل مجلسِهِ رضي الله عنهم. وكان سبب نزول هذه الآيات أن أناساً من قريش أو من أجلاف العرب قالوا للنبيِّ - صلى الله عليه وسلم -: إن أردتَ أن نؤمنَ لك ونتَّبِعَكَ؛ فاطردْ فلاناً وفلاناً ـ أناساً من فقراء الصحابة ـ؛ فإنا نستحي أن ترانا العرب جالسين مع هؤلاء الفقراء. فحَمَلَهُ حبُّه لإسلامهم واتِّباعهم له فحدَّثته نفسُه بذلك، فعاتبه الله بهذه الآيات ونحوها.
{52} "Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka uso wake." Yaani, usiwafukuze wakuondokee na kutoka katika kukaa pamoja nawe wale wafanyao ibaada, na wenye ikhlasi kwa kutaka kukaa pamoja na wasiokuwa wao, miongoni mwa wale wanaoshikamana na kumuomba Mola wao Mlezi kwa maombi ya ibada kwa dhikri , na Swala, na mfano wake; na dua ya kutaka kitu katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, hali ya kuwa wanakusudia kwa hayo uso wa mwenyezi Mungu; na hawana makusudio mengine isipokuwa kusudi hilo tukufu. Basi hawa hawastahiki kufukuzwa na kupewa mgongo. Bali wanastahiki kuwafanya marafiki wandani, na kuwapenda, na kuwasongea, na kuwaleta karibu zaidi. Kwa sababu, wao ndio wateule miongoni mwa viumbe - hata kama ni masikini – wao ni watukufu katika hali halisi, hata kama wao wanadhalilishwa na watu. "Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo." Yaani, kila mmoja ana hisabu yake, na ana matendo yake mema na matendo yake mabaya, "hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu." Na hakika yeye Nabii - swalah ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie - alitekeleza amri hii vikubwa kabisa. Basi akawa wanapoketi masikini miongoni mwa Waumini, anajisubirisha pamoja nao, na anaamiliana nao kwa uzuri, na anawawia laini, na anawaonyesha tabia nzuri, na akawasogeza karibu naye, bali wao walikuwa ndio wengi wa wale waliokuwa katika mkusanyiko wake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Na ilikuwa Sababu ya kuteremka kwa Aya hizi ni kwamba watu miongoni mwa Maquraishi au miongoni mwa Waarabu walimwambia Nabii - rehema na amani zimshukie:- ikiwa unataka tukuamini wewe na tukufuate, basi mfukuze fulani na fulani – watu miongoni mwa Maswahaba masikini; - kwani sisi hakika tunaona aibu Waarabu kutuona hali ya kuwa tumekaa pamoja na hawa watu masikini. Kwa hivyo, akabebwa na kupenda kwake kuwaona wakisilimu na kumfuata kwao, basi nafsi yake ikamwambia kuhusu hilo, lakini mwenyezi Mungu akamlaumu kwa aya hizi na mfano wake.
#
{53} {وكذلك فَتَنَّا بعضَهم ببعضٍ ليقولوا أهؤلاءِ مَنَّ الله عليهم من بيننا}؛ أي: هذا من ابتلاء الله لعبادِهِ حيث جعل بعضَهم غنيًّا وبعضهم فقيراً وبعضهم شريفاً وبعضهم وضيعاً؛ فإذا مَنَّ الله بالإيمان على الفقير أو الوضيع، كان ذلك محلَّ محنةٍ للغني والشريف؛ فإنْ كان قصدُهُ الحقَّ واتباعه؛ آمن وأسلم ولم يمنعْه من ذلك مشاركة الذي يراه دونه بالغنى أو الشرف، وإن لم يكن صادقاً في طلب الحقِّ؛ كانت هذه عقبةً تردُّه عن اتِّباع الحق، وقالوا محتقرين لمن يَرَوْنَهم دونهم: {أهؤلاءِ مَنَّ الله عليهم من بيننا}: فمنعهم هذا من اتباع الحق لعدم زكائهم. قال الله مجيباً لكلامهم المتضمِّن الاعتراض على الله في هداية هؤلاء وعدم هدايتهم هم: {أليس اللهُ بأعلمَ بالشاكرينَ} الذين يعرِفون النعمةَ ويُقِرُّون بها ويقومون بما تقتضيه من العمل الصالح، فيضع فضلَه ومنَّته عليهم دون من ليس بشاكرٍ؛ فإنَّ الله تعالى حكيمٌ لا يضع فضله عند من ليس له بأهل، وهؤلاء المعترضون بهذا الوصف بخلاف مَنْ مَنَّ الله عليهم بالإيمان من الفقراء وغيرهم؛ فإنهم هم الشاكرون.
{53} "Na hivi ndivyo tunavyowajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu?" Yaani, haya ni majaribio ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, alivyowafanya baadhi yao kuwa matajiri, na wengine wao kuwa maskini, na wengine wao kuwa waheshimiwa, na wengine wao kuwa wanyonge. Basi Mwenyezi Mungu akimpa imani masikini au mnyonge, hilo linakuwa jambo la majaribio kwa tajiri na mheshimiwa. Basi ikiwa makusudio yake ni haki na kuifuata, ataamini na kusilimu, na haitamzuia na hilo kushiriki pamoja na yule anayemuona kuwa chini yake kwa mali au heshima.Na ikiwa yeye si mkweli katika kutafuta haki, basi hili linakuwa ni kizuizi kinachomzuia kufuata haki, na wakasema wakiwadharau wale wanaowaona kuwa ni duni kuwaliko wao: "Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu?" Kwa hivyo, hili likawazuia kufuata haki kwa sababu ya kukosa kwao kuwa safi. Mwenyezi Mungu akasema katika kujibu maneno yao ambayo yanajumuisha kumpinga Mwenyezi Mungu kuhusiana na kuwaongoa watu hawa na kutowaongoa wao wenyewe: "Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanaoshukuru?" Ambao wanaijua neema na kuikiri na wanatekeleza yale inayoyataka miongoni mwa matendo mema. Basi Yeye Anawapa fadhila zake na neema zake juu yao kando na yule ambaye siyo mwenye kushukuru. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye hekima, na haweki fadhila zake kwa yule ambaye hazistahili, na hawa wanaopinga wana sifa hii. kinyume na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwa imani miongoni mwa masikini na wengineo. Wao kwa hakika ndio wenye kushukuru.
#
{54} ولما نهى الله رسوله عن طردِ المؤمنين القانتين؛ أمره بمقابلتِهِم بالإكرام والإعظام والتبجيل والاحترام، فقال: {وإذا جاءَكَ الذين يؤمنونَ بآياتِنا فَقُلْ سلامٌ عليكم}؛ أي: وإذا جاءك المؤمنون؛ فحيِّهم، ورحِّبْ بهم، ولقِّهم منك تحيةً وسلاماً، وبشِّرهم بما ينشِّط عزائمهم وهممهم من رحمة الله وسعة جوده وإحسانه، وحُثَّهم على كل سبب وطريق يوصِلُ لذلك، ورهِّبْهم من الإقامة على الذُّنوب، وأمُرْهم بالتوبة من المعاصي لينالوا مغفرةَ ربِّهم وجوده، ولهذا قال: {كَتَبَ ربُّكم على نفسِهِ الرحمةَ أنَّه من عَمِلَ منكم سوءاً بجهالةٍ ثمَّ تاب من بعدِهِ وأصلحَ}؛ أي: فلا بدَّ مع ترك الذُّنوب والإقلاع والندم عليها من إصلاح العمل وأداء ما أوجبَ الله وإصلاح ما فَسَدَ من الأعمال الظاهرة والباطنة؛ فإذا وُجِدَ ذلك كله؛ {فإنَّه غفورٌ رحيمٌ}؛ أي: صبَّ عليهم من مغفرتِهِ ورحمتِهِ بحسب ما قاموا به مما أمرهم به.
{54} Na Mwenyezi Mungu alipomkataza Mtume wake kuwafukuza Waumini watiifu, Akamuamrisha kuamiliana nao kwa ukarimu, na taadhima, na utukufu, na heshima. Kwa hivyo akasema: "Na wanapokujia wanaoziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! (Amani iwe juu yenu!)" Yaani, na Waumini wanapokujia, basi wasalimie, na wapokee, na wape maakizi kutoka kwako na amani, na wape bishara ya yale yatakayoamsha azima yao na hima zao miongoni mwa rehema ya Mwenyezi Mungu na ukarimu wake mwingi na ihsani yake. Na wahimize juu ya kufuata kila sababu na njia inayofikisha katika hayo, na wahofishe dhidi ya kudumu katika madhambi. Na waamrishe watubie madhambi ili wapate kufutiwa dhambi na Mola wao Mlezi na ukarimu wake mwingi. Na ndiyo maana akasema, "Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakayefanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea. Yaani, hapana budi pamoja na kuacha madhambi, na kujiepusha nayo na kuyajutia, kurekebisha matendo na kutekeleza yale ambayo mwenyezi Mungu aliyowajibisha, na kurekebisha yale ambayo yaliharibika katika matendo ya dhahiri na yale yaliyofichika. Na ikiwa yote haya yatapatikana, basi "hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu"; Yaani, Atawamiminia katika kufuta dhambi kwake, na rehema yake kulingana na yale waliyoyatenda miongoni mwa yale aliyowaamrisha.
#
{55} {وكذلك نفصِّلُ الآياتِ}؛ أي: نوضِّحها ونبيِّنها ونميِّز بين طريق الهدى من الضلال والغي والرشاد؛ ليهتديَ بذلك المهتدون ويتبيَّن الحقُّ الذي ينبغي سلوكه. {ولتستبينَ سبيلُ المجرمين}: الموصلةُ إلى سَخَطِ الله وعذابه؛ فإنَّ سبيل المجرمين إذا استبانت واتَّضحت؛ أمكنَ اجتنابُها والبعدُ منها؛ بخلاف ما لو كانت مشتبهةً ملتبسةً؛ فإنه لا يحصُلُ هذا المقصود الجليل.
{55} "Na hivyo ndivyo tunavyozieleza Aya;" yaani, tunavyoziweka wazi, na kuzibainisha na kupambanua baina ya njia ya makosa, na ile iliyo sawa, Ili wanongoke kwa hilo waongofu, na ibainike haki ambayo inapaswa kufuatwa. "Na ili ibainike njia ya wahalifu" inayofikisha katika ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana ikiwa njia ya wahalifu itakuwa bainifu na wazi, itawezekana kuiepuka na kukaa mbali nayo. Tofauti na kama itakuwa imefanana na kuchanganyika, basi kusudi hili kubwa halitafikiwa.
: 56 - 58 #
{قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ قُلْ لَا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ (56) قُلْ إِنِّي عَلَى بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّي وَكَذَّبْتُمْ بِهِ مَا عِنْدِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ يَقُصُّ الْحَقَّ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ (57) قُلْ لَوْ أَنَّ عِنْدِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ (58)}
56. Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu. Sema: mimi sifuati matamanio yenu. Hivyo nitakuwa nimepotea, na sitakuwa miongoni mwa walioongoka. 57. Sema: Mimi nipo kwenye sheria iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, nanyi mnaikanusha. Mimi sina hicho mnachokihimiza. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote. 58. Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnachokihimiza, ingelikwisha katwa shauri baina yangu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayewajua zaidi madhalimu.
#
{56} يقول تعالى لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم -: {قُلْ} لهؤلاء المشركين الذين يَدْعون مع الله آلهةً أخرى: {إني نُهيت أن أعبدَ الذين تدعون من دونِ الله}: من الأنداد والأوثان التي لا تملك نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً؛ فإن هذا باطلٌ، وليس لكم فيه حجةٌ ولا شبهةٌ إلاَّ اتباع الهوى الذي اتِّباعه أعظم الضلال. ولهذا قال: {قل لا أتَّبِعُ أهواءَكم قد ضللتُ إذاً}؛ أي: إن اتَّبعت أهواءكم، {وما أنا من المهتدينَ}: بوجهٍ من الوجوه.
{56} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake - rehema na amani zimshukie - "Sema" uwaambie washirikina hawa wanaowaabudu miungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu: "Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu;" miongoni mwa wenza na vyote viabudiwavyo ambavyo havimiliki manufaa wala madhara, wala mauti, wala uhai. Kwani hii ni batili, na wala hamna hoja katika hilo wala shaka juu yake isipokuwa kufuata matamanio yenu, ambayo kuyafuata ndiyo upotofu mkubwa zaidi. Ndiyo maana akasema, "Sema: mimi sifuati matamanio yenu. Hivyo nitakuwa nimepotea;" yaani, nikifuata matamanio yenu, "na sitakuwa miongoni mwa walioongoka" kwa vyovyote vile.
#
{57} وأما ما أنا عليه من توحيد الله وإخلاص العمل له؛ فإنه هو الحقُّ الذي تقوم عليه البراهين والأدلة القاطعة، وأنا {على بيِّنة من ربي}؛ أي: على يقين مبينٍ بصحته وبطلان ما عداه. وهذه شهادةٌ من الرسول جازمةٌ لا تقبل التردُّد، وهو أعدل الشهود [من الخلق] على الإطلاق، فصدَّق بها المؤمنون، وتبيَّن لهم من صحَّتها وصدقها بحسب ما مَنَّ الله به عليهم، ولكنكم أيها المشركون {كذبتم به}، وهو لا يستحقُّ هذا منكم، ولا يَليقُ به إلاَّ التصديق، وإذا استمررتُم على تكذيبكم؛ فاعلموا أنَّ العذابَ واقعٌ بكم لا محالةَ، وهو عند الله، هو الذي ينزله عليكم إذا شاء وكيف شاء، وإن استعجلتم به؛ فليس بيدي من الأمر شيء، {إن الحُكْمُ إلا للهِ}؛ فكما أنه هو الذي حكم بالحكم الشرعيِّ فأمر ونهى؛ فإنه سيحكم بالحكم الجزائيِّ فيثيب ويعاقب بحسب ما تقتضيه حكمته؛ فالاعتراض على حكمه مطلقاً مدفوع، وقد أوضح السبيل وقصَّ على عباده الحقَّ قصًّا قَطَعَ به معاذيرَهم وانقطعتْ له حُجَّتُهم؛ ليهلِك مَن هَلَكَ عن بيِّنة ويحيا من حيَّ عن بيِّنة. {وهو خيرُ الفاصلينَ}: بين عبادِهِ في الدُّنيا والآخرة، فيفصل بينهم فصلاً يحمدُه عليه حتى من قضى عليه ووجَّه الحق نحوه.
{57} Na ama yale niliyo juu yake ya kumpwekesha mwenyezi Mungu na kumfanyia yeye tu matendo, basi hiyo hakika ndio haki ambayo ina ushahidi na hoja za mkato juu yake. Na "mimi nipo kwenye ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi; yaani, niko katika yakini iliyo wazi juu ya uhalali wake na ubatili wa kitu kingine chochote. Na huu ni ushahidi madhubuti kutoka kwa Mtume usiokubali kusitasita, naye ndiye shahidi mwadilifu zaidi kuliko [viumbe] wote. Basi Waumini wakauamini, na ikawabainikia katika usahihi wake na ukweli wake kulingana na yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu. Lakini nyinyi, enyi washirikina, “mnamkanusha,” na yeye hastahiki haya kutoka kwenu, wala haifailii ila kumsadiki. Na mkiendelea kukadhibisha kwenu huku, basi jueni ya kwamba adhabu itawafikia, hakuna kizuizi, nayo iko kwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye atakayeiteremsha juu yenu akitaka na apendavyo. Na mkiiharakisha, basi sina kitu mkononi mwangu katika jambo hili. "Hukumu si isipokuwa ya Mwenyezi Mungu tu." Basi Kama vile Yeye ndiye aliyehukumu kwa hukumu ya kisheria, akaamrisha na akakataza, basi Yeye hakika Atahukumu kwa hukumu ya malipo; basi atalipa mazuri na aadhibu kulingana na kile hekima yake inavyotaka. Kwa hivyo kuipinga hukumu yake kwa ujumla kunatupiliwa mbali. Kwa kuwa alikwisha iweka wazi njia na akawaambia waja wake haki ya kuwaambia ambako alimaliza kwa huko udhuru zao, na zikakatika hoja zao kwa hilo. Ili mwenye kuangamia na aangamie kwa hoja iliyo wazi, na anayeishi na aishi kwa hoja iliyo wazi. "Naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote," baina ya waja wake katika dunia na Akhera. Basi Atahukumu kati yao kwa hukumu ambayo hata yule aliyehukumiwa dhidi yake atamhimidi kwayo, na haki ikaelekezwa kwake.
#
{58} {قل} للمستعجلين بالعذاب جهلاً وعناداً وظلماً: {لو أنَّ عندي ما تستعجلونَ به لَقُضِيَ الأمرُ بيني وبينكم}: فأوقعتُه بكم، ولا خير لكم في ذلك، ولكنَّ الأمر عند الحليم الصبور الذي يعصيه العاصون ويتجرَّأ عليه المتجرِّئون وهو يعافيهم ويرزقُهم ويسدي عليهم نعمه الظاهرة والباطنة. {والله أعلم بالظالمين}: لا يخفى عليه من أحوالهم شيءٌ فيمهِلُهم ولا يهمِلُهم.
{58} "Waambie" wale wanaoiharakisha adhabu kwa ujinga, na ukaidi na dhuluma. "Au kuwa ninacho hicho mnachokihimiza, ingelikwisha katwa shauri baina yangu na nyinyi.” Na nikaifikisha kwenu, na wala hakuna heri yoyote kwenu katika hilo. Lakini jambo hili liko kwa Mpole wa wote, Mwenye subira kubwa ambaye waasi humuasi, na wanamfanyia ujasiri wanaofanya ujasiri ilhali anawapa salama, na anawaruzuku na anawapa neema zake zilizo dhahiri na zilizofichika. "Na Mwenyezi Mungu ndiye anayewajua zaidi madhaalimu." Hakifichiki kwake kitu katika hali zao, lakini Yeye huwapa muhula na wala hawapuuzi wao.
: 59 #
{وَعِنْدَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَا تَسْقُطُ مِنْ وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُبِينٍ (59)}.
59. Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilicho katika nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.
#
{59} هذه الآية العظيمة من أعظم الآيات تفصيلاً لعلمه المحيط، وأنَّه شامل للغيوب كلِّها، التي يُطْلِعُ منها ما شاء من خلقه، وكثير منها طوى علمَهُ عن الملائكة المقرَّبين والأنبياء المرسلين فضلاً عن غيرهم من العالمين، وأنَّه يعلم ما في البراري والقفار من الحيوانات والأشجار والرمال والحصى والتراب، وما في البحار من حيواناتها ومعادنها وصيدها وغير ذلك مما تحتويه أرجاؤها ويشتمل عليه ماؤها. {وما تسقُطُ من ورقةٍ}: من أشجار البر والبحر والبلدان والقفر والدنيا والآخرة إلاَّ يعلمها، {ولا حبةٍ في ظلمات الأرض}: من حبوب الثمار والزُّروع وحبوب البذور التي يبذرها الخلقُ وبذور النوابت البريَّة التي ينشأ منها أصناف النباتات، {ولا رطبٍ ولا يابس}: هذا عموم بعد خصوص {إلَّا في كتابٍ مبينٍ}: وهو اللوحُ المحفوظُ؛ قد حواها واشتمل عليها، وبعضُ هذا المذكور يبهر عقول العقلاء، ويذهِلُ أفئدة النبلاء، فدلَّ هذا على عظمة الربِّ العظيم وسعته في أوصافه كلِّها، وأنَّ الخلق من أولهم إلى آخرهم لو اجتمعوا على أن يحيطوا ببعض صفاته؛ لم يكنْ لهم قدرةٌ ولا وسعٌ في ذلك، فتبارك الربُّ العظيم الواسع العليم الحميد المجيد الشهيد المحيط، وجلَّ مِن إلهٍ لا يُحْصي أحدٌ ثناءً عليه، بل هو كما أثنى على نفسِهِ وفوق ما يثني عليه عباده. فهذه الآية دلَّت على علمه المحيط بجميع الأشياء وكتابه المحيط بجميع الحوادث.
{59} Aya hii kubwa ni miongoni mwa Aya kubwa kabisa katika kubainisha elimu Yake iliyoenea kila kitu. Na kwamba Yeye imeizunguka ghaibu yote, ambayo Anaonyesha kwayo atakavyo kwa viumbe Vyake, na nyingi katika hiyo Ameificha elimu yake kutoka kwa Malaika wa karibu zaidi na Manabii waliotumwa; achilia mbali wasiokuwa wao miongoni mwa walimwengu wengine. Na kwamba, Yeye anayajua yaliyomo katika majangwa, na nyika miongoni mwa wanyama, na miti, na mchanga, na changarawe, na udongo, na vilivyomo ndani ya bahari miongoni mwa wanyama wake, madini yake, na mawindo yake, na vitu vinginevyo vilivyomo katika sehemu pande zake, na vinajumuishwa na maji yake. "Na halidondoki jani lolote," kutoka katika miti ya nchi kavu, na bahari, na miji mbalimbali, na nyika, na dunia, na Akhera, isipokuwa Analijua."Wala punje katika giza mbalimbali ya ardhi" miongoni mwa punje za matunda na mimea, na punje za mbegu ambazo viumbe wanazipanda, na mbegu za mimea ya porini ambazo kwazo zinatoka aina mbalimbali za mimea. "Wala kinyevu, wala kikavu. Huu ni jumla baada ya umaalumu "isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha;" ambacho ni Ubao uliohifadhiwa. Ambao Alivibeba na kuvijumuisha; na baadhi ya haya yaliyotajwa yanashangaza akili za watu wenye akili timamu, na yanashangaza nyoyo za watu watukufu. Kwa hivyo hili likaashiria ukubwa wa Mola Mlezi Mkuu na ukunjufu wake katika sifa zake zote, na kwamba viumbe tokea wa mwanzo wake hadi wa mwisho wake, lau watakusanyika ili wazunguke vyema baadhi ya sifa zake; hawangekuwa na nguvu zozote wala uwezo wa kufanya hivyo. Basi ni mwingi wa baraka Mola Mlezi Mkuu, Mwenye wasaa, Mwenye kujua yote, Msifiwa, Mheshimiwa, Mwenye kushuhudia yote, Mwenye kuzunguka vyote, na ametukuka Mungu hakuna anayeweza vyema kumsifu. Bali Yeye yuko vile alivyojisifu Mwenyewe, na juu ya vile waja Wake wanavyomsifu. Basi Aya hii iliashiria elimu Yake iliyokizunguka kila kitu na andiko lake lililoyazunguka matukio yote.
: 60 - 62 #
{وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُمْ بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَى أَجَلٌ مُسَمًّى ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (60) وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّى إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ (61) ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ (62)}
60. Naye ndiye anayewafisha usiku, na anakijua mlichokifanya mchana. Kisha Yeye huwafufua humo mchana ili muda uliowekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu, kisha atawaambia yale mliyokuwa mkiyafanya. 61. Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na huwapelekea (nyinyi) waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri. 62. Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Hakika, hukumu ni yake. Naye ni Mwepesi kuliko wote wanaohisabu.
Yote haya ni uthibitisho wa uungu Wake, na ni hoja dhidi ya wale wanaomshirikisha Yeye, na ni ubainisho kwamba Yeye, Mtukufu ndiye anastahiki kupendwa, na ukuu, na heshima, na utukufu.
#
{60} فأخبر أنه وحده المتفرِّدُ بتدبير عباده في يقظتهم ومنامهم، وأنه يتوفَّاهم بالليل وفاة النوم، فتهدأ حركاتهم وتستريح أبدانهم، ويبعثهم في اليقظة من نومهم؛ ليتصرَّفوا في مصالحهم الدينيَّة والدنيويَّة، وهو تعالى يعلم ما جَرَحوا وما كَسَبوا من تلك الأعمال، ثم لا يزال تعالى هكذا يتصرَّف فيهم حتى يستوفوا آجالهم، فيَقضي بهذا التدبير أجلٌ مسمّى، وهو أجل الحياة، وأجل آخر فيما بعد ذلك، وهو البعث بعد الموت، ولهذا قال: {ثم إليه مرجِعُكم}: لا إلى غيره، {ثم ينبِّئكُم بما كنتم تعملون}: من خير وشر.
{60} Akajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye Mwenye mwenye kuwaendesha waja wake katika hali yao ya kuwa macho, na katika kulala kwao, na kwamba Yeye huwafisha usiku kufisha kwa kulala. Kwa hivyo harakati zao zinatulia, na miili yao inastareheka, na huwaamsha katika usingizi wao. Ili watekeleze maslahi yao ya kidini na ya kidunia, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua waliyofanya na kuchuma katika vitendo hivyo. Kisha yeye Mtukufu haachi kuwaendesha hivi mpaka watimize mida yao. Kwa hivyo anamaliza kwa kuendesha huku muda maalumu, nao ni muda wa maisha, na muda mwingine baada ya hapo, nao ni kufufuliwa baada ya kufa. Na ndiyo maana akasema, "kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu;" si kwa mwingineye. "Kisha atawaambia yale mliyokuwa mkiyafanya;" ya heri na maovu.
#
{61} {وهو} تعالى {القاهرُ فوقَ عبادِهِ}: يُنَفِّذُ فيهم إرادته الشاملةَ ومشيئته العامة، فليسوا يملكون من الأمر شيئاً، ولا يتحرَّكون ولا يسكنون إلاَّ بإذنه، ومع ذلك؛ فقد وَكَّلَ بالعباد حفظةً من الملائكة يحفظون العبدَ ويحفظون عليه ما عَمِلَ؛ كما قال تعالى: {وإنَّ عليكم لَحافظينَ. كراماً كاتبينَ. يعلمونَ ما تفعلونَ}، {عن اليمينِ وعن الشمال قعيدٌ. ما يَلْفِظُ من قول إلا لَدَيْهِ رقيبٌ عتيدٌ}: فهذا حفظه لهم في حال الحياة. {حتى إذا جاء أحَدَكُمُ الموتُ توفَّتْه رُسُلُنا}؛ أي: الملائكة الموكلون بقبض الأرواح، {وهم لا يُفَرِّطون} في ذلك؛ فلا يزيدون ساعةً مما قَدَّرَ اللهُ، وقضاه، ولا يُنْقِصون، ولا ينفِّذون من ذلك إلا بحسب المراسيم الإلهيَّة والتقادير الربانيَّة.
{61} "Na Yeye" mtukufu ni "Mwenye nguvu za kushinda juu ya waja wake." Kunatekelezeka kwao kutaka kwake kwa ujumla, na mapenzi yake ya ujumla, kwa hivyo wao hawana mamlaka yoyote juu ya jambo hili, na wala hawasongi wala hawatulii isipokuwa kwa idhini yake. Na licha ya haya, Amewawekea waja walinzi miongoni mwa Malaika wanaomlinda mja na wanamhifadhia yale aliyoyafanya. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu. Waandishi wenye heshima. Wanayajua yale mnayoyatenda." "Wanaokaa kuliani na kushotoni. Hatamki neno lolote, isipokuwa karibu yake yupo mwangalizi aliye tayari;" basi huu ndio ulinzi wake kwao katika hali ya uhai; "mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha." Yaani, Malaika waliopewa jukumu ya kuchukua roho, "nao hawafanyi upungufu wowote" katika hilo. Basi hawaongezi hata saa moja katika yale aliyohukumu Mwenyezi Mungu na akajalia, wala hawapunguzi, wala hawatekelezi katika hilo isipokuwa kwa amri za Mwenyezi Mungu na mapitisho ya Mwenyezi Mungu.
#
{62} {ثم}: بعد الموت والحياة البرزخيَّة وما فيها من الخير والشر، {رُدُّوا إلى الله مولاهم الحقِّ}؛ أي: الذي تولاَّهم بحكمه القدري فنفذ فيهم ما شاء من أنواع التدبير، ثم تولاَّهم بأمره ونهيه وأرسل إليهم الرسل وأنزل عليهم الكتب، ثم رُدُّوا إليه ليتولَّى الحكم فيهم بالجزاء. ويثيبَهم على ما عملوا من الخيرات ويعاقِبَهم على الشرور والسيئات، ولهذا قال: {ألا له الحكمُ}: وحدَه لا شريك له، {وهو أسرعُ الحاسبينَ}: لكمال علمِهِ وحفظِهِ لأعمالهم بما أثبته في اللوح المحفوظ ثم أثبتته ملائكته في الكتاب الذي بأيديهم. فإذا كان تعالى هو المنفرد بالخلق والتدبير، وهو القاهر فوق عباده، وقد اعتنى بهم كل الاعتناء في جميع أحوالهم، وهو الذي له الحكم القدري والحكم الشرعي والحكم الجزائي؛ فأين للمشركين العدول عن مَن هذا وصفه ونعته إلى عبادة من ليس له من الأمر شيء ولا عنده مثقال ذرةٍ من النفع ولا له قدرة وإرادة، أما والله؛ لو علموا حلم الله عليهم، وعفوه ورحمته بهم، وهم يبارزونه بالشرك والكفران، ويتجرؤون على عظمته بالإفك والبهتان، وهو يعافيهم ويرزقهم؛ لانجذبت دواعيهم إلى معرفته، وذهلت عقولهم في حبِّه، ولمقتوا أنفسهم أشدَّ المقت حيث انقادوا لداعي الشيطان، الموجب للخزي والخسران، ولكنهم قومٌ لا يعقلون.
{62} "Kisha," baada ya kufa, na uhai wa Barzakh (kaburini) na yaliyomo ya kheri na shari, "watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki ." Yaani, ambaye aliwasimamia kwa hukumu yake ya kimajaliwa, na akawatekelezea aina zote za uendeshaji Aliotaka. Kisha akawasimamia kwa maamrisho yake na makatazo yake, na akawatumia Mitume na akawateremshia Vitabu; kisha wakarudishwa Kwake ili awasimamie katika kuwahukumu kwa malipo. Na Awalipe juu ya yale waliyoyafanya miongoni mwa mema na awaadhibu kwa maovu na mabaya. Na ndiyo maana Akasema, "Hakika, hukumu ni yake," peke yake bila ya mshirika; "Naye ni Mwepesi kuliko wote wanaohesabu." Kwa sababu ya ukamilifu wa elimu yake na kuhifadhi kwake matendo yao, kulingana na Aliyoyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa; kisha Malaika Wake wakayaandika katika Kitabu ambacho kiko katika mikono yao. basi ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye wa peke Yake katika kuumba na kuenda kwa mambo, na Yeye ndiye Mwenye nguvu ya ushindi juu ya waja Wake, na Amewachunga sana katika hali zao zote. Na Yeye ndiye Mwenye hukumu ya kimajaliwa, na hukumu ya kisheria, na hukumu ya kimalipo. Basi ni vipi washirikina wanaweza kumwacha yule ambaye hizi ndizo sifa zake na maelezo yake na wakamuabudu yule asiyekuwa na chochote katika mambo haya, wala hana uzito wa chembe ya manufaa, wala hana uwezo na utashi. Basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu; lau wangejua upole wa Mwenyezi Mungu juu yao, na usamehevu wake na rehema yake kwao; ilhali wao wanapigana naye kwa ushirikina na ukafiri, na wanafanya ujasiri katika kuukana ukuu wake kwa uwongo na uzushi, na hali Yeye anawapa salama, na anawaruzuku. Basi misukumo yao ingevutika katika kumjua Yeye, na akili zao zingestaajabishwa na kumpenda yeye, na wangejichukia wenyewe kwa chuki kubwa zaidi kwa kuwa waliufuata msukumo wa Shetani; ambao unaleta hizaya na hasara; lakini wao ni kaumu wasiotumia akili.
: 63 - 64 #
{قُلْ مَنْ يُنَجِّيكُمْ مِنْ ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَئِنْ أَنْجَانَا مِنْ هَذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ (63) قُلِ اللَّهُ يُنَجِّيكُمْ مِنْهَا وَمِنْ كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنْتُمْ تُشْرِكُونَ (64)}.
63. Sema: Ni nani anayewaokoa kutoka katika giza la nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru. 64. Sema: Mwenyezi Mungu hukuwaokoa kutoka katika hayo, na kutoka kila mashaka, na kisha nyinyi mnamshirikisha!
#
{63} أي: {قل}: للمشركين بالله الداعين معه آلهةً أخرى ملزماً لهم بما أثبتوه من توحيد الربوبية على ما أنكروه من توحيد الإلهية، {مَنْ يُنَجِّيكم من ظلماتِ البرِّ والبحر}؛ أي: شدائدهما ومشقاتهما وحين يتعذَّر أو يتعسَّر عليكم وجه الحيلة، فتدعون ربكم تضرُّعاً بقلبٍ خاضع ولسان لا يزال يَلْهَجُ بحاجته في الدُّعاء وتقولون وأنتم في تلك الحال: {لَئِنْ أنجانا من هذه}: الشدة التي وقعنا فيها، {لَنَكونَنَّ من الشاكرينَ}: لله؛ أي: المعترفين بنعمتِهِ، الواضعينَ لها في طاعة ربِّهم، الذين حفظوها عن أن يبذلوها في معصيته.
{63} Yaani: "Sema," uwaambie wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, wanaoomba pamoja naye miungu mingine, ukiwalazimisha kwa yale waliyoyathibitisha ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Umola wake kwa yale waliyoyakanusha ya kumpwekesha katika Uungu. "Ni nani huwaokoa kutoka katika giza mbalimbali la nchi kavu na baharini?" Yaani, shida zake na ugumu wake, na wakati inaposhindikana au inakuwa vigumu njia ya kufanya hila. Basi mkawa mnamwomba Mola wenu Mlezi kwa moyo ulionyenyekea na ulimi ambao hauachi kusema haja yake katika dua, na mnasema huku mkiwa katika hali hiyo: "Akituokoa tu kutoka katika hili," la ugumu ambao tuko ndani yake, "bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye shukrani" kwa Mwenyezi Mungu. Yaani, wale wanaoikubali neema yake, na wanaoiweka kumtii Mola wao Mlezi, wale walioihifadhi ili wasiitumie katika kumuasi.
#
{64} {قل الله ينجيكم منها ومن كل كربٍ}؛ أي: من هذه الشدة الخاصة، ومن جميع الكروب العامة، {ثم أنتم تشركونَ}: لا تفون لله بما قلتُم، وتنسَوْن نعمه عليكم؛ فأي برهان أوضح من هذا على بطلان الشرك وصحة التوحيد.
{64} "Sema: Mwenyezi Mungu ndiye atakayewaokoa kutoka humo na kutoka katika kila dhiki." Yaani, kutoka katika dhiki hii mahsusi, na dhiki zote kwa ujumla, "kisha mnamshirikisha na wengine" hamumtimizii Mwenyezi Mungu yale mliyosema, na mnasahau neema zake juu yenu. Basi je, ni uthibitisho gani ulio wazi zaidi kuliko huu juu ya ubatili wa ushirikina na usahihi wa tauhidi?
: 65 - 67 #
{قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَى أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِنْ فَوْقِكُمْ أَوْ مِنْ تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُمْ بَأْسَ بَعْضٍ انْظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ (65) وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ قُلْ لَسْتُ عَلَيْكُمْ بِوَكِيلٍ (66) لِكُلِّ نَبَإٍ مُسْتَقَرٌّ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ (67)}
65. Sema: Yeye ndiye Muweza wa kuwatumia adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au awavishe fujo la mfarakano, na awaonjeshe baadhi yenu jeuri ya wenzi wenu. Tazama vipi tunavyozieleza Aya ili wafahamu. 66. Na kaumu yako waliikadhibisha, nayo ndiyo Haki. Sema: Mimi si wakili juu yenu. 67. Kila habari ina kipindi chake. Nanyi mtakuja jua.
#
{65} أي: هو تعالى قادرٌ على إرسال العذاب إليكم من كل جهة، {من فوقِكم أو من تحتِ أرجُلِكم أو يَلْبِسَكُم}؛ أي: يَخْلُطَكم {شيعاً ويذيقَ بعضَكم بأسَ بعض}؛ أي: في الفتنة وقتل بعضكم بعضاً؛ فهو قادر على ذلك كله؛ فاحذروا من الإقامة على معاصيه فيصيبكم من العذاب ما يتلفكم ويمحقكم، ومع هذا؛ فقد أخبر أنه قادر على ذلك، ولكن من رحمته أن رفع عن هذه الأمة العذاب من فوقهم بالرجم والحصب ونحوه ومن تحت أرجلهم بالخسف، ولكن عاقَبَ من عاقَبَ منهم بأن أذاق بعضهم بأس بعض وسلَّط بعضهم على بعض بهذه العقوبات المذكورة عقوبةً عاجلةً يراها المعتبرون ويشعر بها العاملون. {انظر كيف نصرِّفُ الآياتِ}؛ أي: ننوِّعُها ونأتي بها على أوجهٍ كثيرةٍ، وكلُّها دالةٌ على الحق، {لعلَّهم يفقهون}؛ أي: يفهمون ما خُلقوا من أجله ويفقهون الحقائق الشرعية والمطالب الإلهية.
{65} Yaani, Yeye Mwenyezi ni Muweza wa kuwatumia adhabu kutokea kila upande, "kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au awavishe fujo." Yaani, Awachanganye "fujo la mfarakano, na awaonjeshe baadhi yenu jeuri ya wenzi wenu." Yaani, katika majaribio na kuuana wenyewe kwa wenyewe. Basi yeye ni muweza wa yote hayo. Basi jihadhari na kudumu katika kumuasi, ikaja kuwapata adhabu itakayowangamiza na kuwafutilia mbali. Na pamoja na hili, akasema kwamba Yeye ni Muweza wa hayo, lakini katika rehema Zake ni kwamba Aliwaondolea Ummah huu adhabu kutokea juu yao kwa kupigwa kwa mawe, na changarawe, na mfano wake, na kutokea chini ya miguu yao kwa kudidimizwa. Lakini aliwaadhibu baadhi ya wale aliowaadhibu miongoni mwao kwa kuwaonjesha baadhi yao jeuri ya baadhi yao, na akawapa baadhi yao mamlaka juu ya wenzi wao kwa adhabu hizi zilizotajwa, kama adhabu ya haraka ambayo wataiona wenye kuzingatia na wanaoifanyia kazi wataihisi. "Tazama vipi tunavyozieleza Aya;" yaani, tunavyozitofautisha na kuzileta kwa namna nyingi, na zote zinaonyesha haki, "ili wafahamu." Yaani, wafahamu kile walichoumbwa kwa ajili yake na waelewe uhakika wa kisheria na matakwa ya kimungu.
#
{66} {وكذَّب به}؛ أي: بالقرآن {قومُك وهو الحقُّ}: الذي لا مِرْيَةَ فيه ولا شك يعتريه. {قل لستُ عليكم بوكيل}: أحفظُ أعمالَكم وأجازيكم عليها، وإنَّما أنا منذرٌ ومبلِّغ.
{66} "Na waliikadhibisha," yaani, Qur-ani hii "kaumu yako, nayo ndiyo haki" ambayo shaka yoyote wala kusitasita haviijii. "Mimi si wakili juu yenu" ambaye ninahifadhi vitendo vyenu na kuwalipa juu yake. Lakini mimi ni mwonyaji tu na mfikishaji.
#
{67} {لكلِّ نبإٍ مستقرٌّ}؛ أي: وقتٌ يستقرُّ فيه وزمانٌ لا يتقدَّم عنه ولا يتأخر، {وسوف تعلمونَ}: ما توعدون به من العذاب.
{67} "Kila habari ina kipindi chake;" yaani, wakati itakapotulia ndani yake, na muda ambao hautatangulia wala hautachelewa zaidi yake, "nanyi mtakuja yajua" yale mnayoahidiwa ya adhabu.
: 68 - 69 #
{وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّى يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ وَإِمَّا يُنْسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَى مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (68) وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِمْ مِنْ شَيْءٍ وَلَكِنْ ذِكْرَى لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ (69)}
68. Na unapowaona wanaoziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shet'ani akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhalimu. 69. Wala hakuna jukumu lolote kwa wale wamchao Mungu, lakini ni kukumbusha tu, asaa wapate kumcha Mwenyezi Mungu.
#
{68} المراد بالخوض في آيات الله التكلُّم بما يخالف الحقَّ من تحسين المقالات الباطلة والدعوة إليها ومدح أهلها والإعراض عن الحقِّ والقدح فيه وفي أهله؛ فأمر الله رسوله أصلاً وأمته تبعاً إذا رأوا من يخوض بآياتِ الله بشيء مما ذُكِرَ بالإعراض عنهم وعدم حضور مجالس الخائضين بالباطل والاستمرار على ذلك حتى يكونَ البحثُ والخوضُ في كلام غيره؛ فإذا كان في كلام غيره؛ زال النهي المذكور؛ فإن كان مصلحةً؛ كان مأموراً به، وإن كان غير ذلك؛ كان غير مفيد ولا مأمور به، وفي ذمِّ الخوض بالباطل حثٌّ على البحث والنظر والمناظرة بالحق. ثم قال: {وإما ينسينَّك الشيطانُ}؛ أي: بأن جلستَ معهم على وجه النسيان والغفلة، {فلا تقعُدْ بعد الذِّكرى مع القوم الظالمين}: يشملُ الخائضين بالباطل وكلَّ متكلِّم بمحرَّم أو فاعل لمحرم؛ فإنه يحرم الجلوس والحضور عند حضور المنكر الذي لا يقدِرُ على إزالته، هذا النهي والتحريم لمن جلس معهم، ولم يستعمل تقوى الله بأن كان يشارِكُهم في القول والعمل المحرم أو يسكت عنهم وعن الإنكار؛ فإن استعمل تقوى الله تعالى بأن كان يأمرهم بالخير وينهاهم عن الشرِّ والكلام الذي يصدُرُ منهم؛ فيترتَّب على ذلك زوال الشر أو تخفيفه؛ فهذا ليس عليه حرجٌ ولا إثم، ولهذا قال:
{68} Kinachomaanishwa na kuingilia Aya za Mwenyezi Mungu ni kusema yale yanayopingana na haki, kama vile kuboresha maneno batili, na kuyalingania, na kuwasifu watu wake, na kuipa mgongo haki, na kuikashifu na watu wake. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kwanza, na umma wake kwa kumfuata, wanapomwona mwenye kuziingilia Aya za Mwenyezi Mungu kwa kitu miongini mwa yale yaliyotajwa. Kwamba wajitenge nao, na wala wasihudhurie mikusanyiko ya hao wanaoziingia kwa batili, na wakaendelee katika hayo, mpaka watafute na kuingia katika maneno yasiyokuwa hayo. Na ikiwa ni katika maneno yasiyokuwa hayo, basi Katazo lililotajwa hapo juu linaondoka. Na ikiwa ni masilahi, basi hilo limeamrishwa. Na kama ni kisichokuwa hilo, basi halitakuwa na manufaa na wala halikuamrishwa. Na katika kushutumu kujiingiza kwa batili katika Aya za Mwenyezi Mungu kuna himizo la kutafiti, na kuzingatia, na kujadiliana kwa haki. Kisha akasema, “Na kama Shetani atakusahaulisha.” Yaani ikiwa utakaa pamoja nao kwa kusahau na kughafilika, "basi baada ya kutanabahi, usikae pamoja na kaumu madhalimu."Hili linajumuisha wale wanaojiingiza humo kwa batili, na kila mwenye kuzungumza jambo lililoharamishwa au mwenye kufanya kitendo kilichoharamishwa. Basi ni haramu kukaa na kuhudhuria wakati wa kuwepo kwa maovu ambayo mtu hawezi kuyaondoa. Katazo hili na kuharamisha ni kwa mwenye kukaa pamoja nao na hatumii kumcha Mwenyezi Mungu kwa namna kwamba, anashiriki nao katika kuzungumza maneno na vitendo vilivyoharamishwa au kuwanyamazia, na akaacha kuwakataza. Na akitumia kumcha Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kuwaamrisha kutenda mema na kuwakataza maovu na maneno ambayo yanatoka kwao, kwa hivyo hili linasababisha kuondoka kwa uovu huu au kuupunguza, basi huyu hapana ubaya juu yake wala dhambi, na ndiyo maana akasema:
#
{69} {وما على الذين يتَّقون من حسابِهم من شيءٍ ولكن ذِكْرى لعلَّهم يتَّقون}؛ أي: ولكن لِيذكِّرَهم ويَعِظَهم لعلَّهم يتَّقون الله تعالى. وفي هذا دليلٌ على أنه ينبغي أن يستعملَ المذكِّر من الكلام ما يكون أقربَ إلى حصول مقصود التقوى، وفيه دليلٌ على أنه إذا كان التذكير والوعظ مما يزيد الموعوظَ شرًّا إلى شرِّه؛ كان تركُهُ هو الواجب ؛ لأنَّه إذا ناقض المقصود؛ كان تركُهُ مقصوداً.
{69} "Wala hakuna jukumu lolote kwa wale wamchao Mungu, lakini ni kukumbusha tu, asaa wapate kumcha Mwenyezi Mungu." Yaani, lakini awakumbushe na awaaidhi ili wamche Mwenyezi Mungu mtukufu. Na katika hili kuna ushahidi kwamba, mwenye kukumbusha anafaa kutumia maneno ambayo yanakaribia zaidi kufikia lengo la uchamungu. Na ndani yake kuna ushahidi kwamba ikiwa kukumbusha na kuaidhi ndiyo yataongeza uovu juu ya uovu wake, basi kutakuwa kuliacha hilo ndiyo wajibu. Kwa sababu, ikiwa kutapingana na kile kilichokusudiwa, basi kuliwacha kunakuwa ndio makusudio.
: 70 #
{وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَذَكِّرْ بِهِ أَنْ تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِنْ دُونِ اللَّهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِنْ تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَا يُؤْخَذْ مِنْهَا أُولَئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ (70)}
70. Waachilie mbali walioifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyoyachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingetoa kila fidia haitokubaliwa. Hao ndio walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu.
#
{70} المقصود من العباد أن يُخْلِصوا لله الدين بأن يعبُدوه وحدَه لا شريك له ويبذُلوا مقدورَهم في مرضاتِهِ ومَحَابِّه، وذلك متضمِّن لإقبال القلب على الله وتوجُّهه إليه وكون سعي العبد نافعاً، وجِدًّا لا هزلاً، وإخلاصاً لوجه الله لا رياء وسمعة، هذا هو الدين الحقيقي الذي يُقالُ له: دينٌ، فأما من زعم أنه على الحقِّ، وأنه صاحب دين وتقوى، وقد اتَّخذ دينه لعباً ولهواً؛ بأنْ لَهَا قلبُهُ عن محبة الله ومعرفته، وأقبل على كلِّ ما يضرُّه، ولَهَا في باطله، ولعب فيه ببدنِهِ؛ لأن العمل والسعي إذا كان لغير الله؛ فهو لعبٌ؛ فهذا أمر الله تعالى أن يُتْرَكَ ويحذرَ ولا يغترَّ به، وتنظر حاله، ويحذر من أفعاله ، ولا يغتر بتعويقه عما يقرب إلى الله. {وذكِّر به}؛ أي: ذكِّر بالقرآن ما ينفع العباد أمراً وتفصيلاً وتحسيناً له بذكر ما فيه من أوصاف الحسن، وما يضرُّ العباد نهياً عنه وتفصيلاً لأنواعه وبيان ما فيه من الأوصاف القبيحة الشنيعة الداعية لتركِهِ، وكلُّ هذا لئلا تُبْسَلَ نفسٌ بما كَسَبَتْ؛ أي: قبل اقتحام العبد للذنوب وتجرُّئِهِ على علاَّم الغيوب واستمراره على ذلك المرهوب؛ فذكِّرْها وَعِظْهَا لترتدعَ وتنزجرَ وتكفَّ عن فعلها. وقوله: {ليس لها من دونِ الله وليٌّ ولا شفيعٌ}؛ أي: قبل أن تحيطَ بها ذنوبُها ثم لا ينفعُها أحدٌ من الخلق لا قريبٌ ولا صديقٌ ولا يتولاَّها من دون الله أحدٌ ولا يشفع لها شافعٌ. {وإن تَعْدِلْ كلَّ عَدْل}؛ أي: تفتدي بكل فداءٍ ولو بملء الأرض ذهباً {لا يُؤْخَذْ منها}؛ أي: لا يُقبل ولا يُفيد. {أولئك}: الموصوفون بما ذُكِرَ {الذين أُبْسِلوا}؛ أي: أهلِكوا وأيسوا من الخير، وذلك {بما كَسَبوا لهم شرابٌ من حميم}؛ أي: ماء حارٌّ قد انتهى حرُّه يَشْوي وجوههم ويقطع أمعاءهم {وعذابٌ أليمٌ بما كانوا يكفرون}.
{70} Kinachokusudiwa kwa waja ni kuwa na ikhlasi kwa mwenyezi Mungu katika dini kwa kumwabudu Yeye pekee, bila mshirika yeyote, na wafanye wawezalo ili kumridhisha Yeye na kumpenda. Na hilo linajumuisha moyo kuja kwa Mwenyezi Mungu na kumuelekea, na kwamba juhudi ya mja iwe yenye manufaa, na yenye bidii na si ya mzaha, na ikhlasi kwa uso wa Mwenyezi Mungu na siyo kwa kujionyesha wala kusifiwa. Na hii ndiyo Dini ya hakika ambayo inasemwa; Dini. Ama mwenye kudai kuwa yuko katika haki, na kwamba yeye ni mwenye dini na uchamungu, na ilhali aliifanya dini yake kuwa ni mchezo na pumbao, kwa kuwa moyo wake ulifanya pumbao ukaacha kumpenda mwenyezi mungu na kumjua. Na akayajia kila yenye kumdhuru, na akafanya pumbao katika batili yake, na akacheza ndani yake kwa mwili wake. Kwa sababu matendo na juhudi ikiwa ni kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi hayo ni mchezo. Na kwa sababu hii Mwenyezi Mungu mtukufu akaamrisha ya kwamba aachwe, na atahadhariwe, na wala mtu asidanganywe naye; na iangaliwe hali yake, na mtu ajitahadhari na matendo yake; na wala asidanganywe na kuzuia kwake yale yenye kumuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu. "Nawe kumbusha kwayo;" yaani, kumbusha kwa Qur-aani yale yenye kuwanufaisha waja kwa amri na kwa undani, na kwa kuiboresha kwa kutaja yale yaliyomo ya sifa nzuri nzuri, na yale yanayowadhuru waja kwa kuyakataza, na kubainisha kwa undani aina zake, na kubainisha yale yaliyomo ya sifa mbaya, mbovu zenye kuitia kuyaacha. Na yote haya ni ili nafsi yoyote ile isiangamizwe kwa yale iliyoyachuma. Yaani, kabla mja hajaingia katika madhambi na kumfanyia ujasiri Mwenye kuyajua vyema ya ghaibu na kuendelea kwake kufanya hayo yanayohofisha. Kwa hivyo ikumbushe na ipe mawaidha ili ijizuie, na ikomeke, na iache kuyafanya. Na kauli yake, "hali ya kuwa haina kando na Mwenyezi Mungu, mlinzi yeyote wala mwombezi." Yaani kabla ya kumzunguka madhambi yake, kisha hakuna hata mmoja katika viumbe atakayeinufaisha, si jamaa wala rafiki, na wala hakuna wa kuisimamia kando na Mwenyezi Mungu yeyote wala mwombezi wa kuiombea. "Na hata ikitoa kila fidia;" yaani, ikitoa kila fidia, hata kama ni kwa dhahabu ya ujazo wa ardhi, "haitakubaliwa kutoka kwake." Yaani, haitakubalika wala haitafaa. "Hao," walioelezwa kuwa yale yaliyotajwa, "ndio walioangamizwa;" na wakakata tamaa ya heri yoyote. Na hayo ni "kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao wana kinywaji cha maji ya moto kabisa." Yaani, maji ya moto ambayo joto lake linafikia kubambua nyuso zao na kuyakata matumbo yao; "na adhabu chungu kwa yale waliyokuwa wakikufuru."
: 71 - 73 #
{قُلْ أَنَدْعُو مِنْ دُونِ اللَّهِ مَا لَا يَنْفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَى أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَى وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ (71) وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ (72) وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَيَوْمَ يَقُولُ كُنْ فَيَكُونُ قَوْلُهُ الْحَقُّ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنْفَخُ فِي الصُّورِ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ (73)}
71. Sema: Je, tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa? Tuwe kama ambao mashetani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanaomwita aende kwenye uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. 72. Na mshike Sala, na mcheni Yeye, na kwake Yeye ndiko mtakakokusanywa 73. Naye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litakapopulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana. Naye ndiye Mwenye hekima na Mwenye habari.
#
{71} {قل} يا أيها الرسولُ للمشركين بالله، الداعين معه غيرَه، الذين يدعونكم إلى دينهم؛ مبيناً وشارحاً لوصف آلهتهم التي يكتفي العاقل بذِكْرِ وصفها عن النهي عنها؛ فإنَّ كلَّ عاقل إذا تصوَّر مذهب المشركين؛ جزم ببطلانِهِ قبل أن تُقام البراهين على ذلك، فقال: {أنَدْعو من دونِ الله ما لا يَنفَعُنا ولا يضرُّنا}؟ وهذا وصفٌ يدخل فيه كلُّ من عُبِدَ من دون الله؛ فإنه لا ينفع ولا يضرُّ، وليس له من الأمر شيء، إن الأمر إلا لله. {ونُرَدُّ على أعقابنا بعد إذ هدانا الله}؛ أي: وننقلب بعد هداية الله لنا إلى الضلال، ومن الرشد إلى الغيِّ، ومن الصراط الموصل إلى جنات النعيم إلى الطرق التي تُفْضي بسالِكِها إلى العذاب الأليم!! فهذه حالٌ لا يرتضيها ذو رشدٍ، وصاحبها {كالذي استهوتْه الشياطينُ في الأرض}؛ أي: أضلَّته وتيَّهته عن طريقه ومنهجه الموصل إلى مقصده، فبقي {حيرانَ له أصحابٌ يدعونَه إلى الهدى}، والشياطين يدعونه إلى الردى، فبقي بين الداعيين حائراً، وهذه حال الناس كلِّهم؛ إلا من عصمه الله تعالى؛ فإنهم يجدون فيهم جواذب ودواعي متعارضة؛ داعي الرسالة والعقل الصحيح والفطرة المستقيمة يدعونَه إلى الهدى والصعود إلى أعلى عليين، ودواعي الشيطان ومن سَلَكَ مسلَكَه والنفس الأمارة بالسوء يدعونه إلى الضلال والنزول إلى أسفل سافلين؛ فمن الناس من يكونُ مع دواعي الهدى في أمورِهِ كلِّها أو أغلبها، ومنهم من بالعكس من ذلك، ومنهم من يتساوى لديه الداعيانِ ويتعارضُ عندَهُ الجاذبانِ، وفي هذا الموضع تعرف أهل السعادة من أهل الشقاوة. وقوله: {قل إن هدى الله هو الهدى}؛ أي: ليس الهدى إلا الطريق التي شرعها الله على لسان رسوله، وما عداه فهو ضلالٌ وردىً وهلاكٌ. {وأُمِرْنا لِنُسْلِمَ لربِّ العالمينَ}: بأنْ ننقادَ لتوحيدِهِ ونستسلمَ لأوامرِهِ ونواهيهِ وندخلَ تحت [رِقٍّ] عبوديَّته؛ فإنَّ هذا أفضل نعمة أنعم الله بها على العباد، وأكمل تربية أوصلها إليهم.
{71} "Sema" ewe Mtume, kuwaambia wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, ambao wanawaomba wengine pamoja naye, wale wanaowalinginia nyinyi katika Dini yao, ukiwabainishia na kufafanua sifa za miungu yao, ambayo anazuilika mwenye akili timamu kwa kuitaja tu badala ya kumkataza juu yao. Kwa maana, kila mwenye akili timamu anapolitafakari dhehebu la washirikina, anakuwa na uhakika juu ya ubatili wake kabla kusimamishwa hoja dhidi yake. Kwa hivyo akasema, "Je, tumwombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru?" Na ni maelezo yanayojumuisha kila anayeabudiwa badala ya mwenyezi Mungu. Hanufaishi wala hadhuru, na wala hana kitu chochote katika jambo hilo. Jambo hilo ni la Mwenyezi Mungu tu. "Na turejeshwe nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa?" Yaani, tugeuke baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoa, tukaenda katika upotovu, na kutoka kwenye njia iliyonyooka kwenda kwenye upotofu, na kutoka kwenye njia inayofikisha kwenye mabustani ya neema na kuelekea kwenye njia ziendazo kwenye adhabu chungu! Basi hii ni hali ambayo hakuna mtu mwenye akili timamu anayeiridhia, na mwenye hali hii ni “kama yule ambaye mashetani wamempumbaza katika ardhi?” Yaani, walimpotoa na wakampoteza kutoka kwenye njia yake na mwongozo wake unaomfikisha kwenye makusudio yake, kwa hivyo akabaki “amechanganyikiwa? Anao wenza wanaomwita aende kwenye uwongofu” nao mashetani wanamwita kwenye maangamio, kwa hivyo akabakia amechanganyikiwa kati ya wawili hao wanaomwita. Na hii ndiyo hali ya watu wote, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu amemlinda. Wao kwa hakika wanapata ndani yao vivutio na sababu zinazopingana. Mwenye kuitaka kwenye Ujumbe na, akili sahihi, timamu, na umbile la asili lililonyooka anamwita kwenye uwongofu na kupanda hadi daraja za juu zaidi, na waitaji wa Shetani na mwenye kufuatao njia yake, na nafsi iamrishayo maovu wanamwita kwenye upotevu na kuteremka hadi kiwango cha chini kuliko walio chini. Basi Miongoni mwa watu kuna yule ambaye anakuwa pamoja na walinganizi wa uwongofu katika mambo yake yote au mengi yake. Na miongoni mwao kuna yule ambaye ni kinyume cha huyu. na miongoni mwao kuna yule ambaye miito hii miwili ni sawa kwake, na mivuto hii miwili inapingana kwake; na katika maudhui haya kuna kuwajua watu wa furaha, na watu wa mashaka. Na kauli yake, "Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu;" yaani, uwongofu si chochote isipokuwa ile njia ambayo Mwenyezi Mungu ameiwekea sheria kwenye ulimi wa Mtume wake, na kisichokuwa hicho ni upotovu na maangamizo. "Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote;" kwa kufuata kumpwekesha yeye na tusalimu amri yake na makatazo yake na tuingie katika [kundi la] uja wake. Kwa maana hii ndiyo neema bora zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwayo waja wake, na malezi kamili zaidi aliyowafikishia.
#
{72} {وأن أقيموا الصلاة}؛ أي: وأُمِرْنا أن نقيمَ الصلاة بأركانها وشروطها وسننها ومكمِّلاتها، {واتَّقوه}: بفعل ما أمر به واجتناب ما عنه نهى. {وهو الذي إليه تُحشرون}؛ أي: تجمعون ليوم القيامة، فيجازيكم بأعمالكم خيرها وشرها.
{72} "Na simamisheni Swala;" yaani, tumeamrishwa tusimamishe Swalah pamoja na nguzo zake, na masharti yake, na Sunna zake na yale yanayoikamilisha. "Na mcheni Yeye," kwa kufanya yale Aliyoyaamrisha na kuyaepuka yale Aliyoyakataza; "na kwake Yeye ndiko mtakakokusanywa." Yaani, mtakusanywa kwa ajili ya Siku ya Kiyama, na Atawalipa kwa matendo yenu, mema yake na maovu yake.
#
{73} {وهو الذي خلق السموات والأرض بالحقِّ}: ليأمرَ العباد وينهاهم ويثيبَهم ويعاقِبَهم، {ويومَ يقولُ كُن فيكونُ قولُهُ الحقُّ}: الذي لا مِرْيَةَ فيه ولا مثنوية ولا يقولُ شيئاً عبثاً. {وله الملك يوم يُنفخ في الصور}؛ أي: يوم القيامة خصَّه بالذِّكر مع أنه مالك كل شيء؛ لأنه تنقطع فيه الأملاك، فلا يبقى مَلِكٌ إلا الله الواحد القهار. {عالم الغيب والشهادة وهو الحكيم الخبير}: الذي له الحكمة التامة، والنعمة السابغة، والإحسان العظيم، والعلم المحيط بالسرائر والبواطن والخفايا، لا إله إلا هو، ولا ربَّ سواه.
{73} "Naye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi kwa Haki," ili awaamrishe waja wake na awakataze, na awalipe mazuri na awaadhibu, "Na siku atakaposema: Kuwa! Basi likawa. Kauli yake ni Haki." Ambayo haina shaka yoyote juu yake wala uwili, na wala hasemi kitu bure. "Na wake ufalme wote Siku litapopulizwa katika barugumu." Yaani, Siku ya Qiyaama Atampwekesha kwa ukumbusho ingawa Yeye ndiye Mwenye kila kitu. Kwa sababu mali zimekatiliwa mbali ndani yake, basi hakuna mfalme aliyesalia isipokuwa Mungu Mmoja, Mwenye Nguvu Zote. "Mwenye kuyajua vyema ya ghaibu na yanayoonekana. Naye ndiye Mwenye hekima kubwa, Mwenye habari zote." Yeye ndiye Mwenye hekima kamili, na neema nyingi, na fadhila kubwa, na elimu inayojumuisha siri, na mambo ya ndani na yaliyofichika. Hakuna mungu isipokuwa Yeye, na hakuna Mola Mlezi mwingine isipokuwa Yeye.
: 74 - 83 #
{وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (74) وَكَذَلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ (75) [فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَى كَوْكَبًا قَالَ هَذَا رَبِّي فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ (76) فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَذَا رَبِّي فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِنْ لَمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ (77) فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَذَا رَبِّي هَذَا أَكْبَرُ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَاقَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِمَّا تُشْرِكُونَ (78) إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ (79) وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّهِ وَقَدْ هَدَانِ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ (80) وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُمْ بِاللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (81) الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُمْ بِظُلْمٍ أُولَئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُمْ مُهْتَدُونَ (82) وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَى قَوْمِهِ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَنْ نَشَاءُ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ] (83)}
74. Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mmo katika upotovu ulio wazi. 75. Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini. 76. Na ulipomwingilia usiku aliona nyota, akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Na ilipotua, akasema: Siwapendi wanaotua. 77. Alipouona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Na ulipotua, akasema: Kama Mola Mlezi wangu hataniongoa, basi hakika nitakuwa miongoni mwa kaumu waliopotea. 78. Na alipoliona jua linachomoza, akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Huyu ni mkubwa zaidi. Na lilipotua, akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi niko mbali na hayo mnayoshirikisha. 79. Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, kwa unyoofu, wala mimi si miongoni mwa washirikina. 80. Na kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye hakika amekwisha niongoa? Wala siogopi hao mnaowashirikisha naye, isipokuwa ikiwa Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya elimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki? 81. Na vipi nivihofu hivyo mlivyovishirikisha, ilhali nyinyi hamhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakuwateremshia uthibitisho juu yake. Basi ni kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, ikiwa nyinyi mnajua? 82. Wale ambao waliamini, na hawakuchanganya imani yao na dhuluma, hao ndio wana amani, na wao ndio walioongoka. 83. Na hizo ndizo hoja zetu tulizompa Ibrahim dhidi ya kaumu yake. Tunamnyanyua tumtakaye daraja mbalimbali. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua yote.
#
{74} يقول تعالى: واذكُرْ قصة إبراهيم عليه الصلاة والسلام مثنياً عليه ومعظماً في حال دعوته إلى التوحيد ونهيه عن الشرك. {إذ قال إبراهيمُ لأبيه آزَرَ أتتَّخِذُ أصناماً آلهةً}؛ أي: لا تنفع ولا تضرُّ، وليس لها من الأمر شيء، {إني أراك وقومَكَ في ضلال مبينٍ}: حيث عبدتُم مَن لا يستحقُّ من العبادة شيئاً، وتركتُم عبادةَ خاِلقِكُم ورازِقِكم ومدبِّرِكم.
{74} Yeye Mtukufu Anasema, Kikumbuke kisa cha Ibrahim, amani iwe juu yake, ukimsifu na kumtukuza katika hali alipolingania tauhidi na kukataza kwake ushirikina. "Pale Ibrahim alipomwambia baba yake, Azar: Je, unayafanya masanamu kuwa ni miungu?" Yaani, hayanufaishi wala hayadhuru, na wala hayana kitu katika jambo hilo. "Hakika mimi nakuona wewe na kaumu yako mmo katika opotofu ulio wazi," pale mlipowaabudu kile kisichostahiki chochote katika ibada, na kumuacha kwenu kumwabudu Muumba wenu, na Mwenye kuwaruzuku, na Mwenye kuwaendesha.
#
{75} {وكذلك}: حين وفَّقناه للتوحيد والدعوة إليه، {نُري إبراهيمَ ملكوتَ السمواتِ والأرضِ}؛ أي: ليرى ببصيرتِهِ ما اشتملتْ عليه من الأدلة القاطعة والبراهين الساطعة، {وَلِيَكونَ من الموقنينَ}: فإنه بحسب قيام الأدلَّة يحصُلُ له الإيقان والعلم التامُّ بجميع المطالب.
{75} "Na vivyo hivyo" tulipomuwezesha kusimamisha Tauhidi na kuilingania, "ndivyo tulivyomwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi." Yaani, ili aone kwa ufahamu wake yale yaliyomo miongoni mwa ushahidi wa mkato na hoja zilizo wazi. "Na ili awe miongoni mwa wenye yakini" kwani kulingana na kusimama kwa ushahidi, ndiyo anapata yakini na elimu kamili ya mahitaji yote.
#
{76} {فلما جَنَّ عليه الليلُ}؛ أي: أظلم، {رأى كوكباً}: لعله من الكواكب المضيئة؛ لأنَّ تخصيصَه بالذكر يدلُّ على زيادتِهِ عن غيره، ولهذا ـ والله أعلم ـ قال من قال: إنه الزُّهرة، {قال هذا ربي}؛ أي: على وجه التنزُّل مع الخصم؛ أي: هذا ربي؛ فهلمَّ ننظرْ: هل يستحقُّ الربوبيَّة؟ وهل يقوم لنا دليلٌ على ذلك؟ فإنه لا ينبغي لعاقل أن يتَّخذ إلهه هواه بغير حُجَّة ولا برهان، {فلمَّا أفَلَ}؛ أي: غاب ذلك الكوكب، {قال لا أحبُّ الآفلينَ}؛ أي: الذي يغيبُ ويختفي عمَّن عبده؛ فإنَّ المعبود لا بدَّ أن يكون قائماً بمصالح مَن عَبَدَهُ ومدبِّراً له في جميع شؤونه، فأما الذي يَمضي وقتٌ كثيرٌ وهو غائبٌ؛ فمن أين يستحقُّ العبادة، وهل اتِّخاذُهُ إلهاَ إلاَّ من أسفه السَّفه وأبطل الباطل؟!
{76} "Na ulipomuingilia usiku;" yaani, giza lilipoingia, "akaiona nyota," labda ni ilikuwa ni katika nyota angavu. Kwa sababu kuitaja kwa njia maalumu kunaashiria kuwa ni bora kuliko nyinginezo. Na ndiyo maana - na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye zaidi – akasema aliyesema kwamba ni Zuhura "Huyu ndiye Mola Mlezi wangu;" yaani, kwa namna ya kujishusha kwa daraja la mpinzani. Yaani, huyu ndiye Mola wangu Mlezi; basi njooni tuangalie: Je, anastahiki Umola? Na je, utasimama ushahidi wowote wetu kwa hilo? Kwani haimfailii mwenye akili timamu kuyachukua matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake bila ya uthibitisho wala hoja. "Na ilipotua;" yaani, nyota hiyo ilipotoweka; "Akasema: Siwapendi wanaotua.” Yaani, mwenye kutoweka na kufichikana kwa yule anayemwabudu. Kwa maana, muabudiwa ni lazima ayasimamie masilahi ya mwenye kumuabudu na kumuendeshea mambo yake yote. Ama yule ambaye unapita muda mwingi hali ya kuwa hayupo, basi ni vipi atastahiki kuabudiwa? Na je, kumchukua yeye kuwa mungu si isipokuwa upumbavu wa upumbavu wote, na batili ya batili zote?
#
{77} {فلما رأى القمر بازغاً}؛ أي: طالعاً، ورأى زيادَتَه على نور الكواكب ومخالفته لها، {قال هذا ربِّي}: تنزُّلاً، {فلمَّا أفَلَ قال لَئِن لَمْ يَهْدِني ربِّي لأكوننَّ من القوم الضالين}: فافتقر غاية الافتقار إلى هداية ربِّه، وعلم أنه إن لم يهدِهِ الله؛ فلا هاديَ له، وإن لم يُعِنْه على طاعته؛ فلا معين له.
{77} "Alipouona mwezi unachomoza, yaani, ukichomoza na akaona umeongezeka juu ya nuru ya nyota ile, na kuhalifiana nayo. "Akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi," kwa namna ya kujishusha katika daraja la mpinzani. "Na ulipotua akasema: Kama hataniongoa Mola Mlezi wangu, basi hakika nitakuwa miongoni mwa kaumu waliopotea." Kwa hivyo, akahitaji ukomo wa kuhitaji kuongolewa na Mola wake Mlezi, na ikajulikana kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu hatamuongoa; basi hakuna wa kumuongoa. Na kama hatamsaidia juu ya kumtii Yeye, basi hakuna wa kumsaidia.
#
{78} {فلما رأى الشمس بازغةً قال هذا ربِّي هذا أكبرُ}: من الكوكب ومن القمر، {فلما أفلتْ}: تقرَّر حينئذٍ الهُدى، واضمحل الرَّدى فـ {قال يا قوم إني بريءٌ مما تشركونَ}: حيث قام البرهانُ الصادق الواضح على بطلانِهِ.
{78} "Na alipoliona jua linachomoza, akasema: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Huyu ni mkubwa zaidi" kuliko nyota ile na ule mwezi. "Na lilipotua" ndipo uwongofu ukasimama imara, na upotofu ukatoweka. Kwa hivyo "Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi niko mbali na hayo mnayoshirikisha." Ambapo hoja ya ukweli, iliyo wazi imesimama juu ya ubatili wake.
#
{79} {إني وجهتُ وجهيَ للذي فطر السمواتِ والأرضَ حنيفاً}؛ أي: لله وحده، مقبلاً عليه، معرضاً عن من سواه، {وما أَنَا من المشركين}: فتبرَّأ من الشرك، وأذعن بالتوحيد، وأقام على ذلك البرهان. وهذا الذي ذكرنا في تفسير هذه الآيات هو الصواب، وهو أنَّ المقامَ مقامُ مناظرةٍ من إبراهيم لقومِهِ وبيانُ بطلان إلهيَّة هذه الأجرام العلويَّة وغيرها، وأما من قال: إنه مقامُ نظرٍ في حال طفوليَّته؛ فليس عليه دليلٌ.
{79} "Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, kwa unyoofu." Yaani, kwa Mwenyezi Mungu peke yake, kwa kumuelekea, na kuvipa mgongo visivyokuwa Yeye, "wala mimi si miongoni mwa washirikina." Basi akajiweka mbali na ushirikina, akasalimu amri kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na akasimamisha hoja juu ya hayo. Na hili ambayo tumeyataja katika tafsiri ya Aya hizi ndiyo sahihi. Nao ni kuwa muktadha huu ni wa mahali pa Ibrahim kujadiliana na kaumu yake, na kubainisha ubatili wa uungu hivi vyombo vya mbinguni na vinginevyo. Na ama aliyesema: ni katika muktadha wa kutafakari katika hali ya utoto wake; basi hilo hakuna ushahidi wowote juu yake.
#
{80} {وحاجَّه قومُه قال أتُحاجُّونِّي في الله وقد هدانِ}: أيُّ فائدةٍ لمحاجَّة من لم يتبيَّنْ له الهدى؟ فأما من هداه الله ووصلَ إلى أعلى درجات اليقين؛ فإنه هو بنفسه يدعو الناس إلى ما هو عليه. {ولا أخافُ ما تشرِكونَ به}: فإنَّها لن تضرَّني ولن تمنعَ عني من النفع شيئاً، {إلَّا أن يشاء ربِّي شيئاً وَسِعَ ربِّي كلَّ شيءٍ علماً أفلا تتذكَّرونَ}: فتعلمون أنه وحدَه المعبودُ المستحقُّ للعبودية.
{80} "Na kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye hakika amekwisha niongoa?” Kuna faida gani katika kuhojiana na yule ambaye haujambainikia uwongofu? Na ama yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, na akafikia katika daraja za juu zaidi za yakini. Basi yeye mwenyewe anawalingania tu watu kwenda katika yale aliyo juu yake. "Wala siogopi hao mnaowashirikisha naye." Kwani hawatanidhuru, wala hawatanizuilia chochote katika manufaa, "Isipokuwa ikiwa Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya elimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?" Mkajua kwamba, Yeye peke yake ndiye muabudiwa anayestahiki kuabudiwa.
#
{81} {وكيف أخاف ما أشركتم}: وحالُها حالُ العجز وعدم النفع، {ولا تخافونَ أنَّكم أشركتُم بالله ما لم ينزِّلْ به عليكم سلطاناً}؛ أي: إلا بمجرَّد اتِّباع الهوى؟! {فأيُّ الفريقين أحقُّ بالأمن إن كنتُم تعلمونَ}؟!
{81} "Na vipi nivihofu hivyo mlivyovishirikisha," na ilhali hali yavyo ni hali ya kutokuwa na uwezo na kutonufaisha, "ilhali nyinyi hamhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakuwateremshia uthibitisho juu yake;" yaani, isipokuwa kufuata tu matamanio? "Basi ni kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, ikiwa nyinyi mnajua?"
#
{82} قال الله تعالى فاصلاً بين الفريقين: {الذين آمنوا ولم يلبِسوا}؛ أي: يخلُطوا {إيمانَهم بظُلْم أولئك لهمُ الأمنُ وهم مهتدونَ}: الأمنُ من المخاوف والعذاب والشقاء، والهداية إلى الصراط المستقيم؛ فإن كانوا لم يلبِسوا إيمانَهم بظلم مطلقاً لا بشركٍ ولا بمعاصٍ؛ حصل لهم الأمنُ التامُّ والهداية التامَّة، وإن كانوا لم يلبِسوا إيمانَهم بالشرك وحده، ولكنَّهم يعملون السيئاتِ؛ حصل لهم أصلُ الهداية وأصل الأمنِ، وإن لم يحصل لهم كمالها. ومفهوم الآية الكريمة: أنَّ الذين لم يحصُل لهم الأمران؛ لم يحصُل لهم هدايةٌ ولا أمنٌ، بل حظُّهم الضلالُ والشقاءُ.
{82} Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema kwa kutoa hukumu kati ya makundi haya mawili: "Wale ambao waliamini, na hawakuchanganya imani yao na dhuluma, hao ndio wana amani, na wao ndio walioongoka." Amani kutokana na yenye kuhofisha, na adhabu, na mashaka, na uwongofu kwenda katika njia iliyonyooka. Na ikiwa hawakuichanganya imani yao na dhuluma hata kidogo, si kwa ushirikina wala kwa maasia, basi wangepata amani kamili na uwongofu kamili. Na ikiwa hawakuichanganya imani yao na ushirikina peke yake, lakini wanafanya mabaya, basi wanapata msingi wa uwongofu na msingi wa amani, hata kama hawakufikia ukamilifu wake. Maana ya Aya tukufu isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba wale ambao hawakupata mambo yote mawili, ni kwamba hawakupata uongofu wala amani, bali fungu lao ni upotofu na mashaka.
#
{83} ولما حكم لإبراهيم عليه السلام بما بيَّن به من البراهين القاطعة قال: {وتلكَ حُجَّتُنا آتَيْناها إبراهيمَ على قومِهِ}؛ أي: علا بها عليهم وفلجهم بها. {نرفعُ درجاتٍ من نشاءُ}: كما رفعنا درجاتِ إبراهيم عليه السلام في الدنيا والآخرة؛ فإنَّ العلم يرفعُ اللهُ به صاحِبَه فوق العباد درجاتٍ، خصوصاً العالم العامل المعلِّم؛ فإنه يجعلُه الله إماماً للناس بحسب حاله، تُرمق أفعالُهُ، وتُقتفى آثارُه، ويُستضاء بنوره، ويُمشى بعلمه في ظلمة ديجوره؛ قال تعالى: {يرفع اللهُ الذين آمنوا منكم والذين أوتوا العلم درجات}. {إنَّ ربَّك حكيمٌ عليمٌ}: فلا يضعُ العلم والحكمةَ إلاَّ في المحلِّ اللائق بها، وهو أعلم بذلك المحلِّ، وبما ينبغي له.
{83} Na alipohukumu kwa ajili ya Ibrahim, amani iwe juu yake, kwa yale aliyobainisha kwayo miongoni mwa hoja za mkato. Akasema, "Na hizo ndizo hoja zetu tulizompa Ibrahim dhidi ya kaumu yake; yaani, aliinuka kwazo juu yao, na akawashinda kwazo. "Tunamnyanyua tumtakaye daraja mbalimbali" kama tulivyonyanyua daraja za Ibrahim, amani iwe juu yake katika dunia na Akhera. Kwa maana, kwa elimu, mwenyezi Mungu humpandisha daraja mbalimbali mwenyewe juu ya waja wake, hasa mwenye elimu anayeifanyia kazi, anayeifunza wengine. Yeye Mwenyezi Mungu humfanya kuwa imamu kwa watu kulingana na hali yake. Matendo yake yanatukuzwa, na nyayo zake zinafuatwa, na nuru yake inatumika kuangazia, na inatembewa kwa elimu yake katika giza la mazingira yake. Yeye Mtukufu amesema, "Mwenyezi Mungu huwainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja mbalimbali." "Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua yote," kwa hivyo, haiweki elimu na hekima isipokuwa katika mahali pake vinapostahiki, naye ndiye Anayepajua zaidi pahali hapa, na panavyopaswa kuwa.
: 84 - 90 #
{وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ كُلًّا هَدَيْنَا وَنُوحًا هَدَيْنَا مِنْ قَبْلُ وَمِنْ ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَى وَهَارُونَ وَكَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (84) وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَى وَعِيسَى وَإِلْيَاسَ كُلٌّ مِنَ الصَّالِحِينَ (85) وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ (86) وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ (87) ذَلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِي بِهِ مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (88) أُولَئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ فَإِنْ يَكْفُرْ بِهَا هَؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ (89) أُولَئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّهُ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ قُلْ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَى لِلْعَالَمِينَ (90)}.
84. Na tukamtunuku (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wafanyao mazuri. 85. Na Zakaria, na Yahya, na Isa, na Ilyas. Kila mmoja wao ni miongoni mwa walio wema. 86. Na Ismail, na Al-Yasaa, na Yunus, na Lut'. Na kila mmoja wao tulimfadhilisha juu ya walimwengu wote. 87. Na katika baba zao, na vizazi vyao, na ndugu zao. Na tukawateua na tukawaongoa kwenye njia iliyonyooka. 88. Huo ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu, anaongoa kwao amtakaye katika waja wake. Na lau wangelimshirikisha, basi yangeliwaharibikia yale waliyokuwa wakiyatenda. 89. Hao ndio tuliowapa Kitabu, na hukumu, na Unabii. Kwa hivyo, ikiwa hawa watayakufuru, basi hakika tumekwisha yawakilisha kwa kaumu wasioyakufuru. 90. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa. Basi fuata uwongofu wao. Sema: Mimi siwaombi ujira wowote juu yake. Haya si isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtaja mja wake na rafiki mwandani wake Ibrahim, amani iwe juu yake, na akataja yale aliyomneemesha kwayo ya elimu, na kulingania, na subira. Akataja yale ambayo Mwenyezi Mungu alimtukuza kwayo miongoni mwa dhuria njema, na kizazi kizuri, na kwamba Mwenyezi Mungu alimweka aliye bora zaidi wa viumbe vyote kutoka katika kizazi chake. Basi ni kukubwa kulioje hadhi hii, heshima kubwa ambayo haina mfano wake! Kwa hivyo, Akasema:
#
{84} {ووهبنا له إسحاقَ ويعقوبَ}: ابنه الذي هو إسرائيلُ أبو الشعب الذي فضَّله الله على العالمين، {كُلًّا} منهما هَدَيْناهُ الصراطَ المستقيم في علمه وعمله، و {نوحاً} هديناهُ {من قبلُ}، وهدايته من أعلى أنواع الهدايات الخاصة التي لم تحصَلْ إلا لأفرادٍ من العالم، وهم أولو العزم من الرسل، الذي هو أحدهم، {ومن ذُرِّيَّتِهِ} ـ: يُحتمل أنَّ الضمير عائدٌ إلى نوح؛ لأنه أقرب مذكور، ولأن الله ذكر مع مَن ذَكَرَ لوطاً، وهو من ذُرِّيَّةِ نوح لا من ذُرِّيَّة إبراهيم؛ لأنه ابن أخيه، ويحتمل أن الضمير يعود إلى إبراهيم؛ لأنَّ السياق في مدحه والثناء عليه، ولوطٌ وإن لم يكن من ذُرِّيَّتِهِ؛ فإنه ممَّن آمن على يده، فكان منقبةُ الخليل وفضيلتُه بذلك أبلغَ من كونه مجردَ ابن له. ـ {داودَ وسليمانَ} ابنَ داود {وأيوبَ ويوسفَ} ابن يعقوبَ {وموسى وهارون} ابني عِمْران. {وكذلك}: كما أصلحنا ذُرِّيَّة إبراهيم الخليل لأنَّه أحسن في عبادة ربِّه وأحسن في نفع الخلق، كذلك {نَجْزي المحسنين}: بأن نجعلَ لهم من الثناء الصدق والذُّرِّيَّة الصالحة بحسب إحسانهم.
{84} "Na tukamtunuku (Ibrahim) Is-haq na Yaakub," mwanawe ambaye ndiye Israili, baba wa mataifa ambaye Mwenyezi Mungu alimfadhilisha juu ya walimwengu wote. "Kila mmoja wao" katika wawili hao tulimuongoa kwenye njia iliyonyooka katika elimu yake na vitendo vyake. Na "Nuhu" tulimuongoa "kabla," na uwongofu wake ni miongoni mwa uwongofu wa juu zaidi maalumu ambao haukuwahi kufanyika isipokuwa tu kwa watu fulani tu miongoni mwa walimwengu. Nao ni wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume ambao yeye ni miongoni mwao. "Na katika dhuria zake," inawezekana kwamba neno hili (yake) linamrejea Nuhu. Kwa sababu yeye ndiye aliyetajwa mwisho, na kwa sababu Mwenyezi Mungu alimtaja Lut’ pamoja na wale aliowataja, naye ni katika dhuria ya Nuhu, na si katika dhuria ya Ibrahim. Kwa sababu yeye ni kijana wa kaka yake (Nuhu). Na inawezekana kwamba neno hilo (yake) linamrudia Ibrahim. Kwa sababu muktadha huu ni katika kumsifu. Na Lut, ijapokuwa si katika kizazi chake, lakini alikuwa miongoni mwa wale walioamini kupitia mkononi mwake, kwa hivyo hadhi yake na fadhila yake Al-Khalil ikawa kubwa zaidi kuliko ile ya kuwa kwake mwanawe tu. "Na Daudi na Suleman" mwana wa Daud, "na Ayyub na Yusuf" mwana wa Yaakub, "na Musa na Harun" wana wa ‘Imran. "Na hivi ndivyo" kama tulivyowafanya dhuria ya Ibrahim Al-Khalil kuwa wema. Kwa sababu alimuabudu Mola wake Mlezi kwa uzuri, na akafanya uzuri katika kuwanufaisha viumbe, basi vivyo hivyo ndivyo "tunavyowalipa wafanyao mazuri" kwa kuwapa sifa njema ya ukweli, na dhuria njema kulingana na kufanya kwao mazuri.
#
{85} {وزكريا ويحيى}: ابنه، {وعيسى} ابن مريم، {وإلياس كلٌّ}: من هؤلاء {من الصالحين}: في أخلاقهم وأعمالهم وعلومهم، بل هم سادةُ الصالحين وقادتِهم وأئمتهم.
{85} "Na Zakaria na Yahya" mwanawe "na Isa" bin Maryam "na Al-Yasaa, na kila mmoja wao" katika hawa "ni miongoni mwa walio wema" katika tabia zao, na matendo yao, na elimu zao, bali wao ndio mabwana wa wale walio wema, na viongozi wao, na maimamu wao.
#
{86} {وإسماعيل} ابن إبراهيم، أبو الشعب الذي هو أفضل الشعوب، وهو الشعب العربي، ووالد سيد ولد آدم محمد - صلى الله عليه وسلم -، {ويونُس} ابن متى، {ولوطاً} ابن هارون أخي إبراهيم، {وكلًّا}: من هؤلاء الأنبياء والمرسلين {فضَّلْنا على العالمين}: لأن درجات الفضائل أربع، وهي التي ذكرها الله بقوله: {ومَن يُطِع اللهَ والرَّسولَ فأولئكَ مع الذين أنعمَ اللهُ عليهم من النبيِّين والصدِّيقين والشهداء والصالحين}: فهؤلاء من الدرجة العليا، بل هم أفضل الرسل على الإطلاق، فالرسل الذين قصَّهم الله في كتابه أفضلُ ممَّن لم يَقْصُصْ علينا نبأهم بلا شك.
{86} "Na Ismail" mwana wa Ibrahim, baba wa taifa ambalo ndilo taifa bora zaidi, nalo ni taifa la Kiarabu, na baba wa bwana wa mwana wa Adam Muhammad - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani. "Na Yunus" bin Mata, "na Lut’" bin Harun, kaka yake Ibrahim, "na kila mmoja wao" katika hawa Manabii na Mitume; "tulimfadhilisha juu ya walimwengu wote." Kwa sababu daraja za fadhila ni nne. Nazo ni zile alizotaja Mwenyezi Mungu kwa kauli yake, "Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao wako pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema." Basi hawa wako katika daraja la juu, bali wao ndio Mitume bora zaidi kuliko wote. Kwa maana Mitume ambao Mwenyezi Mungu alitusimulia katika Kitabu chake bila ya shaka ndio bora zaidi kuwaliko wale ambao hakutusimulia habari yao.
#
{87} {ومن آبائهم}؛ أي: آباء هؤلاء المذكورين، {وذُرِّيَّاتهم وإخوانهم}؛ أي: وهدينا من آباء هؤلاء وذُرِّيَّاتهم وإخوانهم، {واجتبيناهم}؛ أي: اخترناهم، {وهديناهُم إلى صراط مستقيم}.
{87} "Na katika baba zao; yaani, baba za hawa waliotajwa, "na dhuria zao na ndugu zao." Yaani, tuliongoa katika baba zao hawa na dhuria zao na ndugu zao, "na tukawateua." Yaani, tuliwachagua, "na tukawaongoa kwenye njia iliyonyooka."
#
{88 - 89} {ذلك}: الهدى المذكور {هُدى الله}: الذي لا هدى إلا هداه. {يهدي به من يشاءُ من عبادِهِ}: فاطلبوا منه الهُدى؛ فإنّه إنْ لم يهدِكُم؛ فلا هادي لكم غيره، وممن شاء هدايته هؤلاء المذكورين. {ولو أشركوا}: على الفَرَض والتقدير، {لَحَبِطَ عنهم ما كانوا يعملون}: فإن الشرك محبطٌ للعمل موجبٌ للخلودِ في النار؛ فإذا كان هؤلاء الصفوة الأخيار لو أشركوا - وحاشاهم - لحبطتْ أعمالُهم؛ فغيرُهم أولى.
{88 - 89} "Huo," uwongofu uliotajwa "ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu," ambaye hakuna uwongofu isipokuwa uwongofu wake. "Anaongoa kwao amtakaye katika waja wake." Basi tafuteni uwongofu kutoka Kwake; kwani ikiwa hatawaongoa, basi hakuna wa kuwaongoa isipokuwa Yeye. Na miongoni mwa wale aliotaka kuwaongoa, ni hawa waliotajwa. "Na lau wangelimshirikisha," kama ingechukuliwa hivyo na kukadiriwa hivyo, "basi yangeliwaharibikia yale waliyokuwa wakiyatenda." Kwani ushirikina unabatilisha matendo, na unasababisha kudumu katika Moto. Basi ikiwa hawa wa hali ya juu sana, walio bora zaidi lau kuwa wangelimshirikisha, na haiwezekani hilo kwao –matendo yao yangeliharibika, basi wengine wanastahili hilo zaidi.
#
{90} {أولئك}: المذكورون {الذين هدى الله فبهداهُمُ اقْتَدِهْ}؛ أي: امش أيها الرسول، الكريمُ خلفَ هؤلاءِ الأنبياءِ الأخيارِ واتَّبعْ ملتَهم. وقد امتثل - صلى الله عليه وسلم - فاهتدى بهدي الرسل قبله، وجمع كلَّ كمال فيهم، فاجتمعت لديه فضائل وخصائص فاق بها جميع العالمين، وكان سيد المرسلين وإمام المتقين صلوات الله وسلامه عليه وعليهم أجمعين. وبهذا الملحظ استدلَّ بهذه من استدلَّ من الصحابة أن رسول الله - صلى الله عليه وسلم - أفضل الرسل كلهم، {قل} للذين أعرضوا عن دعوتك: {لا أسألكم عليه أجراً}؛ أي: لا أطلبُ منكم مغرماً ومالاً جزاء عن إبلاغي إياكم ودعوتي لكم، فيكون من أسباب امتناعكم، إنْ أجري إلاَّ على الله. {إنْ هو إلا ذِكرى للعالمين}: يتذكَّرون به ما ينفعُهم فيفعلونَه وما يضُرُّهم فيذرونَه، ويتذكَّرون به معرفةَ ربِّهم بأسمائه وأوصافه، ويتذكَّرون به الأخلاق الحميدةَ والطُّرق الموصلة إليها، والأخلاق الرذيلة والطرق المفضية إليها؛ فإذا كان ذكرى للعالمين؛ كان أعظم نعمة أنعم الله بها عليهم، فعليهم قبولها، والشكر عليها.
{90} "Hao" waliotajwa "ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa. Basi fuata uongofu wao." Yaani, tembea, ewe Mtume mtukufu, nyuma ya Manabii hawa walio bora zaidi, na ufuate mila yao. Naye Nabii - swalah na salamu za Mwenyezi Mungu zimshukie – alitekeleza, na akafuata uwongofu wa Mitume wa kabla yake, na akajumuisha kila ukamilifu ulio ndani yao. Kwa hivyo, zikakusanyika ndani yake fadhila na sifa maalum alizopita kwazo walimwengu wote, na akawa bwana wa Mitume, na imamu wa wachamungu swalah na salamu zimshukie yeye na wote. Kwa kuzingatia mazingatio haya, aliyachukuwa kuwa ushahidi yule aliyeyachukua miongoni mwa Maswahabah juu ya kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – ndiye mbora wa Mitume wote. "Sema," uwaambie wale walioupa mgongo ulinganizi wako, "Mimi siwaombi ujira wowote juu yake;" yaani, siwaombi gharama, wala mali kama malipo juu ya kuwafikishia kwangu nyinyi na kuwalingania kwangu nyingi, ndiyo iwe katika sababu za kukataa kwenu. Malipo yangu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. "Haya si isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote." Wanakumbuka kwayo yale yanayowanufaisha, basi wanayatenda, na yale yanayowadhuru, basi wanayaacha. Na kwayo wanakumbuka kumjua Mola wao Mlezi kwa majina yake na sifa zake. Na wanakumbuka kwayo maadili mema na njia zinazofikisha kwayo, na maadili mabaya na njia zinazofikisha kwayo. Basi kama ukumbusho ni kwa walimwengu wote, unakuwa ndio neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo; kwa hivyo ni juu yao kuikubali na kushukuru juu yake.
: 91 #
{وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى بَشَرٍ مِنْ شَيْءٍ قُلْ مَنْ أَنْزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَى نُورًا وَهُدًى لِلنَّاسِ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا وَعُلِّمْتُمْ مَا لَمْ تَعْلَمُوا أَنْتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ قُلِ اللَّهُ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ (91)}.
91. Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, waliposema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyekiteremsha Kitabu alichokuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlichokifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha? Na mkafunzwa mliyokuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache wacheze katika porojo lao.
#
{91} هذا تشنيعٌ على من نفى الرسالة من اليهود والمشركين وزَعَمَ أنَّ الله ما أنزل على بشر من شيء؛ فمن قال هذا؛ فما قَدَرَ الله حقَّ قدرِهِ ولا عظَّمه حقَّ عظمته؛ إذ هذا قدحٌ في حكمته، وزعمٌ أنه يترك عباده هملاً لا يأمرهم ولا ينهاهم، ونفيٌ لأعظم مِنَّةٍ امْتَنَّ الله بها على عباده، وهي الرسالة التي لا طريق للعباد إلى نيل السعادة والكرامة والفلاح إلا بها؛ فأيُّ قدح في الله أعظم من هذا؟! {قل} لهم ملزماً بفساد قولهم وقَرِّرْهم بما به يُقِرُّون: {من أنزل الكتابَ الذي جاء به موسى}: وهو التوراة العظيمة {نوراً}: في ظلمات الجهل، {وهدىً}: من الضلالة، وهادياً إلى الصراط المستقيم علماً وعملاً، وهو الكتاب الذي شاع وذاع وملأ ذكرُهُ القلوب والأسماع، حتى إنهم جعلوا يتناسَخونه في القراطيس ويتصرَّفون فيه بما شاؤوا؛ فما وافق أهواءهم منه؛ أبدَوْه وأظهروه، وما خالف ذلك؛ أخفَوْه وكتموه، وذلك كثير. {وعُلِّمْتُم}: من العلوم التي بسبب ذلك الكتاب الجليل {ما لم تعلموا أنتم ولا آباؤكم}. فإذا سألتهم عن من أنزل هذا الكتاب الموصوف بتلك الصفات؛ فأجب عن هذا السؤال و {قلِ اللهُ}: الذي أنزله، فحينئذٍ يتضح الحق، وينجلي مثل الشمس؛ وتقوم عليهم الحجة. {ثم} إذا ألزمتهم بهذا الإلزام {ذَرْهم في خوضِهِم يلعبونَ}؛ أي: اتركهم يخوضوا في الباطل ويلعبوا بما لا فائدةَ فيه حتى يُلاقوا يومَهم الذي يوعدون.
{91} Haya ni kuonyesha ubaya wa yule ambaye aliukataa jumbe miongoni wa Mayahudi na washirikina, na akadai kuwa Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote kwa mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, mwenye kusema haya, basi hajamheshimu mwenyezi Mungu haki ya kumheshimu, wala hakumtukuza haki ya kumtukuza. Kwa maana, haya ni kuitusi hekima yake, na ni madai kwamba anawaacha waja wake bila ya kuwajali. Wala hawaamrishi wala hawakatazi, na ni kuikanusha neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha kwayo waja wake, ambayo ni ujumbe ambao hakuna njia kwa waja ya kupata furaha, na utukufu, na kufaulu isipokuwa kwa njia hiyo. Basi ni tusi gani kwa Mwenyezi Mungu lililo kubwa zaidi ya hili? "Sema," uwaambie huku ukiwalazimu kukubali ubovu wa maneno yao, na wafanye kukiri kwa yale wanayoyakiri. "Ni nani aliyekiteremsha Kitabu alichokuja nacho Musa?" Nacho ni Taurati tukufu, "huku ikiwa nuru" katika giza mbalimbali ya ujinga, "na uwongofu;" kutoka katika upotovu, na chenye kuongoa kwenye njia iliyonyooka kwa elimu na vitendo, nacho ni Kitabu ambacho kilienea na kutangazika na utajo wake ukajaa nyoyoni na masikioni, mpaka wakawa wanakiandika katika nyaraka, na kukifanyia kama wanavyotaka. Basi Chochote kinachoafikiana na matamanio yao kwacho, wanakionyesha na kukidhihirisha. Na chochote chenye kuhalifu hilo, wanakificha, na hayo ni mengi. "Na mkafundishwa" katika elimu mbalimbali ambazo ni kutokana na Kitabu hicho kitukufu "yale mliyokuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu?" Basi ukiwauliza kuhusu ni nani aliyekiteremsha Kitabu hiki kilichoelezwa kwa sifa hizi; basi jibu swali hili na "Sema: Mwenyezi Mungu" ndiye aliyekiteremsha. Na hapo ukweli utakuwa wazi, na kudhihirika kama jua, na hoja itasimama juu yao. "Kisha" ukishawalazimisha kulazimisha huku, "waache wacheze katika porojo lao;" Yaani, waache waingie kwenye batili na wacheze na yale yasiyokuwa na faida mpaka wakutane na siku yao ambayo wanaahidiwa.
: 92 #
{وَهَذَا كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنْذِرَ أُمَّ الْقُرَى وَمَنْ حَوْلَهَا وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ وَهُمْ عَلَى صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ (92)}.
92.Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kusadikisha yale yaliyokitangulia, na ili uuonye Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake. Na wale wanaoiamini Akhera wanakiamini, nao wanazihifadhi Swala zao.
#
{92} أي: {وهذا}: القرآن الذي {أنزلناه} إليك {مباركٌ}؛ أي: وصفه البركة، وذلك لكثرة خيراتِهِ وسعة مَبَرَّاتِهِ {مصدقُ الذي بين يديه}؛ أي: موافقٌ للكتب السابقة وشاهدٌ لها بالصدق، {ولِتُنذِرَ أمَّ القُرى ومن حولَها}؛ أي: وأنزلناه أيضاً لتنذرَ أمَّ القرى ـ وهي مكة المكرمة ـ ومن حولها من ديار العرب، بل ومن سائر البلدان، فتحذِّر الناس عقوبة الله وأخذه الأمم، وتحذِّرهم مما يوجب ذلك. {والذين يؤمنون بالآخرة يؤمنون به}: لأنَّ الخوف إذا كان في القلب؛ عمرتْ أركانُهُ وانقادَ لمراضي الله، {وهم على صلاتهم يحافظونَ}؛ أي: يداومون عليها ويحفظون أركانها وحدودَها وشروطها وآدابها ومكمِّلاتها. جعلنا الله منهم.
{92} Yaani, "na hiki" (kitabu cha) Qur-aani ambacho "tulikiteremsha" kwako "kilichobarikiwa;" yaani sifa yake ni kwamba kimebarikiwa. Na hilo ni kwa sababu ya wingi wa heri zake, na wingi wa wema wake { chenye kusadikisha yale yaliyokitangulia. Yaani, chenye kuafikiana na Vitabu vilivyotangulia, na chenye kushuhudia ukweli wake, "na ili uuonye Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake." Yaani, pia tulikiteremsha ili uuonye Mama wa Miji - nayo ni Makka Al-Mukarramah - na wale walio pembezoni mwake miongoni mwa nchi za Waarabu, na hata katika nchi nyingine zote; ili uwaonye watu adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kuchukua kwake umma mbalimbali, na uwaonye dhidi ya yale yanayosababisha hayo. "Na wale wanaoiamini Akhera wanakiamini." Kwa sababu hofu inapokuwa katika moyo, nguzo zake zinaimarika na kufuata yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu; "nao wanazihifadhi Swala zao." Yaani, wanadumu juu yake na wanazihifadhi nguzo zake, na mipaka yake, na masharti yake, na adabu zake, na yale yote yenye kuikamilisha. Mwenyezi Mungu atufanye tuwe miongoni mwao.
: 93 - 94 #
{وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَنْ قَالَ سَأُنْزِلُ مِثْلَ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَوْ تَرَى إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنْفُسَكُمُ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنْتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنْتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ (93) وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَى كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُمْ مَا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ وَمَا نَرَى مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ لَقَدْ تَقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنْكُمْ مَا كُنْتُمْ تَزْعُمُونَ (94)}.
93. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au anayesema: Mimi nimeletewa wahyi; na ilhali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anayesema: Nitateremsha kama alivyoteremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeliwaona madhalimu wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya kudunisha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake. 94. Nanyi mlitujia wapweke kama tulivywaumba mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyowapa, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika mahusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyokuwa mkiyadai.
#
{93} يقول تعالى: لا أحد أعظم ظلماً ولا أكبر جُرماً ممَّن كَذَبَ على الله بأن نسب إلى الله قولاً أو حكماً وهو تعالى بريء منه، وإنما كان هذا أظلم الخلق؛ لأن فيه من الكذب وتغيير الأديان أصولها وفروعها ونسبة ذلك إلى الله ما هو من أكبر المفاسد، ويدخل في ذلك ادِّعاء النبوة، وأنَّ الله يوحي إليه، وهو كاذب في ذلك؛ فإنَّه مع كذبه على الله وجرأته على عظمته وسلطانه يوجب على الخلق أن يتَّبِعوه ويجاهِدَهم على ذلك ويستحلَّ دماء مَن خالفه وأموالهم. ويدخل في هذه الآية كلُّ من ادَّعى النبوة كمسيلمة الكذاب والأسود العنسي والمختار وغيرهم ممن اتصف بهذا الوصف. {ومن قال سأنزِلُ مثلَ ما أنزلَ الله}؛ أي: ومن أظلم ممَّن زعم أنه يقدر على ما يقدر الله عليه ويجاري الله في أحكامه ويشرعُ من الشرائع كما يشرعه الله. ويدخل في هذا كل من يزعم أنه يقدِرُ على معارضة القرآن، وأنَّه في إمكانه أن يأتي بمثله! وأي ظلم أعظمُ من دعوى الفقير العاجز بالذات الناقص من كل وجه، مشاركةَ القوي الغني الذي له الكمال المطلق من جميع الوجوه في ذاته وأسمائه وصفاته؟! ولما ذمَّ الظالمين؛ ذَكَرَ ما أعدَّ لهم من العقوبة في حال الاحتضار ويوم القيامة، فقال: {وَلَوْ تَرى إذ الظالمونَ في غَمَراتِ الموتِ}؛ أي: شدائدِهِ وأهواله الفظيعة وكُرَبه الشنيعة؛ لرأيت أمراً هائلاً وحالةً لا يقدر الواصف أن يصفها. {والملائكة باسطو أيديهم}: إلى أولئك الظالمين المحتضرينَ بالضَّرب والعذاب؛ يقولون لهم عند منازعة أرواحهم وقلقها وتعصِّيها عن الخروج من الأبدان: {أخْرِجوا أنفُسَكُم اليومَ تُجْزَوْنَ عذاب الهُونِ}؛ أي: العذاب الشديد الذي يُهينكم ويُذِلُّكم، والجزاء من جنس العمل؛ فإنَّ هذا العذاب {بما كُنتم تقولونَ على الله غير الحقِّ}: من كذبِكم عليه وردِّكم للحقِّ الذي جاءت به الرسل، {وكنتُم عن آياتِهِ تستكبرونَ}؛ أي: تَرَفَّعُون عن الانقياد لها والاستسلام لأحكامها. وفي هذا دليل على عذاب البرزخ ونعيمه؛ فإنَّ هذا الخطاب والعذاب الموجه إليهم إنما هو عند الاحتضار وقُبيل الموت وبعده. وفيه دليل على أن الرُّوح جسم يدخُلُ، ويخرُجُ، ويخاطَب، ويساكِن الجسد، ويفارقه.
{93} Yeye Mtukufu Anasema, hakuna aliye dhalimu mkubwa zaidi wala mhalifu mkubwa zaidi kuliko yule anayemsingizia uongo Mwenyezi Mungu, kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu neno au hukumu ilhali Yeye mtukufu yuko mbali nayo. Na huyu ndiye dhalimu zaidi katika viumbe kwa sababu, ndani ya hilo kuna uongo na kubadili dini mbalimbali, na misingi yake, na matawi yake; na kunasibisha hayo na Mwenyezi Mungu, ambayo ni miongoni mwa maharibifu makubwa zaidi. Na inaingia katika hili kudai unabii, na kwamba Mwenyezi Mungu humteremshia wahyi, ilhali yeye ni mwongo katika hilo. Kwani, pamoja na uongo wake juu ya Mwenyezi Mungu na ujasiri wake juu ya ukuu wake na mamlaka yake, yeye anawawajibishia watu kumfuata, na anapigane nao vita juu ya hilo, na anahalalisha damu ya mwenye kumhalifu, na mali zao. Na anaingia katika Aya hii kila aliyedai unabii, kama vile Musaylimah Mwongo mkubwa, na Al-Aswad Al-‘Ansi, na Al-Mukhtar, na wengineo ambao miongoni mwa wale walioelezewa kwa maelezo haya. "Na yule anayesema: Nitateremsha mfano wa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu." Yaani, ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayedai kuwa yeye ni muweza wa kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu anayaweza, na anafanya pamoja na Mwenyezi Mungu katika hukumu zake, na anaweka sheria miongoni mwa sheria mbalimbali kama vile Mwenyezi Mungu anavyoweka sheria? Na anaingia katika hili kila anayedai kwamba ana uwezo wa kuipinga Qur-aani, na kwamba anaweza kuleta mfano wake! Na je, ni dhuluma gani kubwa zaidi kuliko kudai kwamba fakiri, asiyejiweza yeye mwenyewe, mpungufu katika kila njia, kushirikiana Mwenye nguvu, anayejitosheleza ambaye ana ukamilifu wote katika kila njia, katika dhati yake, na majina yake, na sifa zake? Na alipotaja shutuma juu ya madhalimu, Akataja adhabu aliyowaandalia katika hali ya kufa na Siku ya Qiyama. Kwa hivyo akasema, "Na lau ungeliwaona madhalimu wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti; yaani, taabu zake, na ugumu wake wa kutisha, na dhiki yake mbaya, basi ungeliona jambo kubwa na hali ambayo hawezi mwenye kueleza kuieleza. "Malaika wamewanyooshea mikono yao" madhalimu hao wanaokufa kwa kupiga na kuadhibu, na wanawaambia wakati wa kutoa roho zao, na wasiwasi wake, na kukataa kwake kutoka katika miili yao: "Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya kudunisha." Yaani, adhabu kali ambayo itawadunisha na kuwadhalilisha. Na malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwani adhabu hii ni "kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki;" miongoni mwa kumsingizia kwenu uwongo na kuikataa kwenu haki ambayo walikuja nayo Mitume. "Na mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake," yaani mnajiinua juu kwa kukataa kuzifuata na kujisalimisha kwa hukumu zake. Na katika hili kuna ushahidi juu ya adhabu ya Barzakh (kaburini). Kwa maana, maneno haya na adhabu yanayoelekezwa kwao ni wakati wa kufa tu, kabla ya kufa na baada yake. Na ndani yake kuna ushahidi kwamba roho ni mwili unaoingia, na unatoka, na unaongeleshwa, na unakaa ndani ya mwili, na kuuacha.
#
{94} فهذه حالهم في البرزخ، وأما يوم القيامة؛ فإنهم إذا وردوها؛ وردوها مفلسين فرادى بلا أهل ولا مال ولا أولاد ولا جنودٍ ولا أنصارٍ؛ كما خلقهم الله أول مرة، عارين من كل شيء؛ فإن الأشياء إنما تُتَمَوَّلُ وتحصُل بعد ذلك بأسبابها التي هي أسبابها، وفي ذلك اليوم تنقطع جميع الأمور التي كانت مع العبد في الدنيا سوى العمل الصالح والعمل السيئ الذي هو مادة الدار الآخرة الذي تنشأ عنه ويكون حسنها وقبحها وسرورها وغمومها وعذابها ونعيمها بحسب الأعمال؛ فهي التي تنفع أو تضرُّ وتسوء أو تسرُّ، وما سواها من الأهل والولد والمال والأنصار فعواري خارجية وأوصاف زائلة وأحوال حائلة، ولهذا قال تعالى: {ولقد جئتُمونا فُرادى كما خلقْناكم أولَ مرةٍ وتركتُم ما خوَّلْناكم}؛ أي: أعطيناكُم وأنعمنا به عليكم {وراءَ ظهورِكم}: لا يُغنون عنكم شيئاً، {وما نرى معكم شُفعاءَكُم الذين زعمتُم أنهم فيكم شركاءُ}: فإن المشركين يشركون بالله ويعبُدون معه الملائكة والأنبياء والصالحين وغيرهم، وهم كلُّهم لله، ولكنهم يجعلون لهذه المخلوقات نصيباً من أنفسهم وشركة في عبادتهم، وهذا زعمٌ منهم وظلمٌ؛ فإن الجميع عبيد لله، والله مالكهم والمستحقُّ لعبادتهم؛ فشركُهم في العبادة وصرفها لبعض العبيد تنزيلٌ لهم منزلة الخالق المالك، فيوبَّخون يوم القيامة، ويُقال لهم هذه المقالة {ما نرى معكم شفعاءَكم الذين زعمتُم أنهم فيكم شركاء لقد تقطَّع بينَكم}؛ أي: تقطَّعت الوصل والأسباب بينكم وبين شركائكم من الشفاعة وغيرها، فلم تنفعْ ولم تُجْدِ شيئاً. {وضلَّ عنكم ما كنتُم تزعُمون}: من الرِّبح والأمن والسعادة والنجاة التي زيَّنها لكم الشيطانُ وحسَّنها في قلوبكم، فنطقتْ بها ألسنتكُم، واغتررتُم بهذا الزعم الباطل الذي لا حقيقةَ له حين تبيَّن لكم نقيضُ ما كنتم تزعُمون، وظهر أنَّكم الخاسرون لأنفسكم وأهليكم وأموالكم.
94. Basi hii ndiyo hali yao katika Barzakh (kaburini). Na ama siku ya Qiyama, wao kwa hakika watakapoifikia hali ya kuwa ni wafilisi, wakiwa mmoja mmoja, bila ya familia, wala mali, wala wana, wala askari, wala wasaidizi. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyowaumba mara ya kwanza huku wakiwa hawana kila kitu. Kwani vitu huchukuliwa kama mali, na vinakuja baada ya hayo kupitia sababu zake ambazo ni sababu zake. Na katika siku hiyo yatakatika mambo yote ambayo yalikuwa pamoja na mja katika dunia isipokuwa matendo mema na matendo mabaya ambayo ndiyo uhakika wa Nyumba ya Akhera, ambayo yanatoka humo, na unakuwa uzuri wake, na ubaya wake, na furaha yake, na huzuni yake, na wasiwasi yake kubwa, na adhabu yake, na neema yake kulingana na matendo. Hayo ndiyo yenye kunufaisha au kudhuru, na kuwa mabaya au kufurahisha. na ama yasiykuwa hayo miongoni mwa familia, na wana, na mali, na wasaidizi, ni msaada tu wa kutoka nje, na sifa zenye kuondoka, na hali zenye kuzuia. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Nanyi hakika mmetujia mmoja mmoja kama tulivyowaumba mara ya kwanza. Na mkayaacha yote yale tuliyowapa." Yaani, tuliwapa na tukawaneemesha kwavyo "nyuma ya migongo yenu." Hayawafai kitu, "na wala hatuwaoni pamoja nanyi hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu." Kwa maana, washirikina wanamshirikisha Mwenyezi Mungu na wanaabudu pamoja naye Malaika, na Manabii, na wale walio wema na wasiokuwa hao. Nao hao wote ni wa Mwenyezi Mungu, lakini wanawafanyia viumbe hawa sehemu katika nafsi zao, na ushirika katika ibada zao. Na haya ni madai tu kutoka kwao na ni dhuluma. Kwa maana wote ni waja wa mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mmiliki wao na anayestahiki kuabudiwa. Basi ushirikina wao katika ibada, na kuwafanyia kwao baadhi ya waja ni kuwafanya hao kuwa katika daraja la Muumba, Mmiliki. Kwa hivyo watakemewa Siku ya Qiyama, na waambiwe maneno haya; "na wala hatuwaoni pamoja nanyi hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Hakika, yamekatika mahusiano baina yenu." Yaani, yalikatika mafungamano na njia zilizo baina yenu na washirika wenu, kama vile uombezi na mambo mengine, kwa hivyo hayakuwa na manufaa yoyote na hayakufanikisha chochote. "Na yamewapotea yale mliyokuwa mkidai" miongoni mwa faida, na amani, na furaha, na wokovu ambayo Shetani aliwapambia, na akayafanya kuwa mazuri katika nyoyo zenu; basi ndimi zenu zikayatamka, na mkadanganyika na madai haya batili, ambayo hayana uhakika wowote, wakati kilipowabainikia kinyume cha yale mliyokuwa mkidai. Na ikadhihirika kuwa nyinyi ndio wenye hasara kubwa kwa nafsi zenu, na ahali zenu, na mali zenu.
: 95 - 98 #
{إِنَّ اللَّهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَى يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ذَلِكُمُ اللَّهُ فَأَنَّى تُؤْفَكُونَ (95) فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ (96) وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ (97) وَهُوَ الَّذِي أَنْشَأَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ (98)}.
95. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka na mbegu za tende, zikachipua. Humtoa aliye hai kutokana na maiti, na mwenye kumtoa maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnadanganywa? 96. Ndiye anayepambaza mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Hayo ndiyo makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote. 97. Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali ya bara na bahari. Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaojua. 98. Na Yeye ndiye aliyewazalishia kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanaofahamu.
#
{95} يخبر تعالى عن كماله وعظمةِ سلطانه وقوة اقتداره وسعة رحمته وعموم كرمه وشدة عنايته بخلقه، فقال: {إنَّ الله فالقُ الحبِّ} شاملٌ لسائر الحبوب التي يباشر الناس زرعَها، والتي لا يباشِرونها منها؛ كالحبوب التي يبثها الله في البراري والقفار، فيفلق الحبوب عن الزروع والنوابت على اختلاف أنواعها وأشكالها ومنافعها، ويفلق النوى عن الأشجار من النخيل والفواكه وغير ذلك، فينتفع الخلقُ من الآدميين والأنعام والدواب، ويرتعون فيما فَلَقَ الله من الحبِّ والنوى، ويقتاتون وينتفعون بجميع أنواع المنافع التي جعلها الله في ذلك، ويريهم الله من برِّه وإحسانه ما يبهر العقول ويُذْهِلُ الفحول، ويريهم من بدائع صنعته وكمال حكمته ما به يعرفونه ويوحِّدونه ويعلمون أنه هو الحقُّ وأن عبادة ما سواه باطلة. {يُخْرِجُ الحيَّ من الميِّت}: كما يخرِجُ من المنيِّ حيواناً ومن البيضة فرخاً ومن الحبِّ والنوى زرعاً وشجراً، {ومُخْرِجُ الميِّتِ}: وهو الذي لا نموَّ فيه أو لا روح {من الحيِّ}: كما يخرِجُ من الأشجار والزُّروع النوى والحب، ويخرِجُ من الطائر بيضاً ونحو ذلك. {ذلكم} الذي فعل ما فعل وانفردَ بخلقِ هذه الأشياء وتدبيرِها {اللهُ ربُّكم}؛ أي: الذي له الألوهيَّة والعبادة على خلقه أجمعينَ، وهو الذي ربَّى جميع العالَمين بنعمِهِ وغذَّاهم بكرمه، {فأنَّى تؤفَكونَ}؛ أي: فأنَّى تصرَفون وتَصُدُّون عن عبادة من هذا شأنه إلى عبادة من لا يملك لنفسه نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً؟
{95} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu Wake, na ukubwa wa mamlaka Yake, na nguvu ya uwezo Wake, na upana wa rehema Yake, na ujumla wa ukarimu Wake, na ukubwa wa utunzaji Wake kwa viumbe Vyake. Akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka," hili linajumuisha nafaka zote ambazo watu huzipanda, na zile ambazo hawazipandi. Kama vile zile nafaka ambazo Mwenyezi Mungu huzitawanya katika nyika na porini, kisha anapasua nafaka kutokana na mazao na mimea ya kila aina zake, sura zake, na manufaa yake. Na hupasua mbegu kutoka katika miti kame vile mitende, na matunda na isiyokuwa hiyo. Kwa hivyo, wananufaika wanadamu, na mifugo, na wanyama, na wanakula katika vile alivyovipasua Mwenyezi Mungu miongoni mwa nafaka na mbegu, na wanavila na wananufaika na kila aina ya manufaa aliyoyaweka Mwenyezi Mungu katika hivyo. Na Mwenyezi Mungu anawonyesha katika wema wake na ihsani yake yale ambayo huangaza akili na kuzishangaza wanaume wenye nguvu, na huwaonyesha katika ufundi wake wa ajabu na ukamilifu wa hekima yake ambayo kwayo wanamjua na wanampwekesha, na wanajua kuwa Yeye ndiye Haki, na kwamba kumuabudu asiyekuwa Yeye ni batili. "Humtoa aliye hai kutokana na maiti," kama vile anavyotoa mnyama kutoka katika manii, na kifaranga kutoka katika yai, na nafaka na kokwa kutoka katika mimea na miti. "Mwenye kumtoa maiti," naye ni yule ambaye hamei wala hana roho "kutokana na aliye hai;" kama vile anavyotoa kokwa na nafaka kutoka katika miti na mazao. Na anatoa mayai kutoka katika ndege na kadhalika. "Huyo" ambaye alifanya aliyoyafanya, na akawa peke yake katika kuumba vitu hivi, na kuviendesha ndiye "Mwenyezi Mungu" Mola wenu Mlezi. Yaani, Yeye ndiye mwenye uungu na ibada juu ya viumbe vyake vyote. Na ndiye aliyewalea walimwengu wote kwa neema zake, na akawalisha kwa ukarimu wake. "Basi vipi mnadanganywa?" Yaani, vipi mnageuzwa, na mnakataa kumwabudu Yule ambaye mambo yake ni hivi, na mkamuabudu yule asiyeimilikia nafsi yake manufaa yoyote, wala madhara, wala kifo, wala uhai, wala ufufuo?
#
{96} ولما ذكر تعالى مادة خلق الأقواتِ؛ ذكر مِنَّته بتهيئة المساكن وخلقه كلَّ ما يحتاجُ إليه العباد من الضياء والظلمة وما يترتَّب على ذلك من أنواع المنافع والمصالح، فقال: {فالقُ الإصباح}؛ أي: كما أنه فالق الحبِّ والنَّوى، كذلك هو فالقُ ظلمةِ الليل الداجي الشامل لما على وجه الأرض بضياء الصُّبح الذي يفلقه شيئاً فشيئاً، حتى تذهبَ ظلمةُ الليل كلُّها ويخلُفُها الضياءُ والنورُ العامُّ الذي يتصرَّف به الخلقُ في مصالحهم ومعايشهم ومنافع دينهم ودنياهم. ولما كان الخلقُ محتاجين إلى السكون والاستقرار والراحة التي لا تتمُّ إلا بوجود النهار والنور؛ {جعل}: الله الليلَ سَكَناً يسكن فيه الآدميُّون إلى دورهم ومنامهم والأنعامُ إلى مأواها والطيورُ إلى أوكارها فتأخذ نصيبها من الراحة، ثم يزيل الله ذلك بالضياء، وهكذا أبداً إلى يوم القيامة. {و} جعل تعالى {الشمسَ والقمرَ حُسْباناً}: بهما تُعرف الأزمنة والأوقات؛ فتنضبِطُ بذلك أوقات العبادات وآجال المعاملات، ويُعْرَفُ بها مدة ما مضى من الأوقات التي لولا وجودُ الشمس والقمر وتناوُبُهما واختلافُهما لما عَرَفَ ذلك عامة الناس واشتركوا في علمه، بل كان لا يعرفه إلا أفرادٌ من الناس بعد الاجتهاد، وبذلك يفوت من المصالح الضرورية ما يفوت. {ذلك}: التقدير المذكور، {تقديرُ العزيز العليم}: الذي من عزَّته انقادت له هذه المخلوقاتُ العظيمة فَجَرَتْ مذلَّلة مسخَّرة بأمره، بحيثُ لا تتعدَّى ما حدَّه الله لها ولا تتقدَّم عنه ولا تتأخَّر، العليم الذي أحاط علمُهُ بالظواهر والبواطن والأوائل والأواخر. ومن الأدلة العقلية على إحاطة علمِهِ تسخيرُ هذه المخلوقات العظيمة على تقديرٍ ونظام بديع تَحير العقول في حسنِهِ وكماله وموافقته للمصالح والحكم.
{96} Na Yeye Mtukufu alipotaja asili ya kuumbwa kwa vyakula, Akataja neema yake ya kutayarisha makazi, na kuumba kwake kila wanachokihitaji waja wake miongoni mwa mwangaza na giza; na yanayotokana na hayo miongoni mwa aina mbalimbali za manufaa na maslahi. Kwa hivyo Akasema, "Ndiye anayepambazua mwangaza wa asubuhi;" yaani, kama vile anavyopasua nafaka na kokwa. Vile vile Yeye ndiye mpasuaji wa giza la usiku totoro linaloenea kila kitu kilicho juu ya uso wa ardhi, kwa mwangaza wa asubuhi, ambao huipambazua kidogo kidogo, mpaka litoweke giza lote la usiku, na uje nyuma yake mwangaza na nuru ya jumla ambayo viumbe wanavitumia katika maslahi yao, na maisha yao, na manufaa yao ya kidini yao na dunia. Na kwa kuwa viumbe wanahitaji utulivu, na uthabiti, na mapumziko, ambavyo haviwezi kupatikana isipokuwa kwa kuwepo kwa mchana na mwangaza, mwenyezi Mungu "akaufanya" usiku kuwa mahali pa kupumzika, ambapo wandamu wanapumzikia katika nyumba zao, na katika kulala kwao. Nao mifugo katika mazizi yao, na ndege katika viota vyao, ili wapate fungu lao katika mapumziko. Kisha mwenyezi Mungu anaondoa hilo kwa mwangaza, na vivyo hivyo milele mpaka Siku ya Qiyama. "Na" Yeye mtukufu akalifanya "jua na mwezi kwenda kwa hesabu," ambapo kwa viwili hivyo zinajulikana zama na nyakati. Kwa hivyo, zinakuwa sawaswa nyakati za ibada kwa hilo, na tarehe za mwisho za miamala; inajulikana kwa hilo muda wa zama zilizopita. Na lau si kwa sababu ya kuwepo kwa jua na mwezi, na kupishana kwake, na kutofautiana kwake, basi watu wote hawangejua hayo, na wakawa sawa katika kuyajua. Bali hangeyajua isipokuwa watu fulani tu miongoni mwa watu, tena baada ya kujitahidi. Na kwa sababu ya hilo, yanapotea yale yangepotea miongoni mwa maslahi muhimu. "Hayo" makadirio yaliyotajwa ni "makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote." Ambaye katika nguvu yake, vilifuata amri yake vitu hivi vikubwa, kwa hivyo vikakwenda kwa kunyenyekea, na kutiishwa kwa amri yake, kwa kiasi kwamba havipiti kile alichovipimia Mwenyezi Mungu, wala havitangulii kabla yake, wala havichelewi. Yeye ni Mwenye kujua ambaye kujua kwake kumeenea yote ya dhahiri na ya ndani, na ya mwanzo na ya mwisho. Na katika ushahidi wa kiakili juu ya kuenea kwa elimu ni kutiishwa kwa viumbe hivi vikubwa kwa makadirio na mpangilio wa ajabu unaoshangaza akili katika uzuri wake, na ukamilifu wake, na kuwiana kwake na masilahi na hekima.
#
{97} {وهو الذي جعل لكم النُّجومَ لِتَهْتَدوا بها في ظلمات البرِّ والبحر}: حين تشتبه عليكم المسالك، ويتحيَّر في سيره السالك، فجعل الله النجوم هدايةً للخلق إلى السبيل التي يحتاجون إلى سلوكها لمصالحهم وتجاراتهم وأسفارهم، منها نجومٌ لا تزال تُرى ولا تسيرُ عن محلِّها، ومنها ما هو مستمرُّ السير يعرِفُ سيرَه أهلُ المعرفة بذلك، ويعرفون به الجهاتِ والأوقاتِ. ودلَّت هذه الآيةُ ونحوها على مشروعيَّة تعلُّم سير الكواكب ومحالِّها الذي يسمَّى علم التسيير؛ فإنه لا تتمُّ الهداية ولا تُمْكِنُ إلاَّ بذلك. {قد فصَّلْنا الآياتِ}؛ أي: بيَّناها ووضَّحناها وميَّزنا كل جنس ونوع منها عن الآخر بحيث صارت آياتُ الله باديةً ظاهرة، {لقوم يعلمونَ}؛ أي: لأهل العلم والمعرفة؛ فإنَّهم الذين يوجَّه إليهم الخطاب، ويُطلب منهم الجواب؛ بخلاف أهل الجهل والجفاء المعرضين عن آيات الله وعن العلم الذي جاءت به الرسل؛ فإن البيان لا يفيدُهم شيئاً، والتفصيل لا يزيل عنهم ملتبساً، والإيضاح لا يكشف لهم مشكلاً.
{97} "Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali ya bara na bahari} wakati njia zinapowachanganya, na anapochanganyikiwa mwenye kupitia hapo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akazifanya nyota kuwa mwongozo kwa viumbe kuiendea njia wanayoihitaji kuifuata kwa sababu ya maslahi yao, na biashara zao, na safari zao. Miongoni mwake kuna nyota ambazo haziachi kuonekana, wala hazisongi kutoka pahali pake. Na kuna zile zinazoendelea kusonga, ambazo wanajua kusonga kwake watu wa elimu ya hayo, na wanajua kwazo mielekeo na nyakati. Na Aya hii na nyinginezo mfano wake zilionyesha kuruhusiwa kujifunza mwendo wa sayari na masimamo yake, ambayo inaitwa sayansi ya miendo. Kwa maana mwongozo hauwezi kutimia wala hauwezekani isipokuwa kwa njia hii. "Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi," yaani,tumezibainisha, na kuziweka wazi, na kuzipambanua kila sampuli na aina katika hizo kutoka kwa nyingine, kwa kiasi kwamba zikawa Aya za Mwenyezi Mungu ni wazi na dhahiri "kwa kaumu wanaojua;" yaani, kwa watu wa elimu na maarifa. Kwa maana hao ndio ambao wanaoongeleshwa, na wanaotakiwa kuitikia. Tofauti na watu wa ujinga na ugumu wanaozipa mgongo Aya za Mwenyezi Mungu, na elimu ambayo walikuja nayo Mitume. Basi ubainisho huu hauwanufaishi kitu, na kueleza kwa kina hakuwaondolei chenye kuwachanganya, na kuweka wazi hakuwaondolei tatizo lolote.
#
{98} {وهو الذي أنشأكم من نفس واحدة}: وهو آدمُ عليه السلام، أنشأ الله منه هذا العنصر الآدميَّ الذي قد ملأ الأرض، ولم يزل في زيادة ونموٍّ، الذي قد تفاوت في أخلاقه وخلقه وأوصافه تفاوتاً لا يمكن ضبطه، ولا يُدْرَكُ وصفُه، وجعل الله لهم مستقرًّا؛ أي: منتهى ينتهون إليه وغاية يُساقون إليها، وهي دار القرار التي لا مستقرَّ وراءها ولا نهايةَ فوقَها؛ فهذه الدار هي التي خلق الخلق لسكناها، وأوجدوا في الدنيا ليسعوا في أسبابها التي تنشأ عليها وتعمر بها، وأودعهم الله في أصلاب آبائهم وأرحام أمهاتهم، ثم في دار الدنيا، ثم في البرزخ؛ كلُّ ذلك على وجه الوديعة التي لا تستقرُّ ولا تثبت، بل ينتقل منها، حتى يوصل إلى الدار التي هي المستقر، وأما هذه الدار؛ فإنَّها مستودعٌ وممرٌّ. {قد فصَّلْنا الآيات لقوم يفقهون}: عن الله آياتِهِ، ويفهمون عنه حججَهُ وبيِّناتِهِ.
{98} "Na Yeye ndiye aliyewaanzisha kutokana na nafsi moja;" naye ni Adam, amani iwe juu yake. Mwenyezi Mungu alianzisha kutoka kwake kitu hii sampuli ya kibinadamu ambayo iliijaza ardhi, na haijaacha kuzidi na kukua. Ambayo ametofautiana katika maadili yake, maumbile yake, na sifa zake kutofautiana ambako haiwezekani kuudhibiti, wala haifikiwi kuueleza.Na mwenyezi Mungu akawafanyia pahali pa kutulia. Yaani, mwisho wanaoufikia na marejeo wanayopelekwa kwayo. Nayo ni Nyumba ya kudumu ambayo hakuna pahali pengine pa kutulia pasipokuwa hapo, wala hakuna utulivu mwisho juu yake. Basi Nyumba hii ndiyo Nyumba ambayo viumbe viliumbwa ili vikae hapo, na wakawekwa katika dunia hii ili wajitahidi katika sababu zake ambazo inaanzishwa juu yake na inaimarishwa kwayo. Na Mwenyezi Mungu aliwaweka katika migongo ya baba zao na matumbo ya uzazi ya mama zao, kisha katika nyumba ya dunia, kisha katika Barzakh; yote hayo ni kwa jina la amana ambayo haitulii wala kukaa imara. Lakini inahamishwa kutoka humo, mpaka ifikishwe kwenye nyumba ambayo ndiyo pahali pa kutulia. Na ama nyumba hii; hiyo ni mahali pa kuhifadhi tu, na njia ya kupita. "Hakika, tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaofahamu" kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aya zake, na wanafahamu kutoka kwake hoja zake na ushahidi wake ulio wazi.
: 99 #
{وَهُوَ الَّذِي أَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِنْ طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ انْظُرُوا إِلَى ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ إِنَّ فِي ذَلِكُمْ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ (99)}
99. Na Yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tukatoa mimea ya kila kitu. Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani, tukatoa ndani yake punje zilizopandana; na kutokana na mitende katika makole yake yakatoka mashada yaliyo karibu; na mabustani ya mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na yakaiva. Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini.
#
{99} وهذا من أعظم مننه العظيمة التي يضطرُّ إليها الخلق من الآدميين، وغيرهم، وهو أنه أنزل من السماء ماء متتابعاً وقت حاجة الناس إليه، فأنبت الله به كل شيء مما يأكل الناس والأنعام، فرتع الخلق بفضل الله وانبسطوا برزقِهِ وفرحوا بإحسانه وزال عنهم الجدب واليأس والقحط، ففرحتِ القلوبُ وأسفرتِ الوجوه وحصل للعباد من رحمة الرحمن الرحيم ما به يتمتَّعون وبه يرتعون، مما يوجِبُ لهم أن يبذُلوا جهدهم في شكر من أسدى النعم وعبادته والإنابة إليه والمحبة له. ولما ذكر عموم ما ينبت بالماء من أنواع الأشجار والنبات؛ ذَكَرَ الزرع والنخل لكثرة نفعهما وكونهما قوتاً لأكثر الناس، فقال: {فأخرجنا منه خَضِراً نخرِجُ منه}؛ أي: من ذلك النبات الخضر {حبًّا متراكباً}: بعضُه فوق بعض من بُرٍّ وشعير وذرة وأرز وغير ذلك من أصناف الزروع، وفي وصفه بأنه متراكبٌ إشارة إلى أنَّ حبوبه متعددة، وجميعها تستمدُّ من مادةٍ واحدةٍ، وهي لا تختلط، بل هي متفرِّقة الحبوب مجتمعة الأصول، وإشارة أيضاً إلى كثرتها وشمول ريعها وغلتها؛ ليبقى أصل البذر، ويبقى بقية كثيرةٌ للأكل والادِّخار. {ومن النخل}: أخرج اللهُ {من طَلْعِها}: وهو الكُفُرَّى والوعاء قبل ظهور القنو منه، فيخرج من ذلك الوعاء {قِنْوانٌ دانيةٌ}؛ أي: قريبة سهلة التناول متدلية على من أرادها؛ بحيث لا يعسُرُ التناول من النخل، وإن طالت؛ فإنه يوجد فيها كَرَبٌ ومراقي يَسْهُلُ صعودها. {و}: أخرج تعالى بالماء {جناتٍ من أعناب والزيتون والرمان}: فهذه من الأشجار الكثيرة النفع العظيمة الوقع؛ فلذلك خصَّصها الله بالذِّكر بعد أن عمَّ جميع الأشجار والنوابت. وقوله: {مشتبهاً وغير متشابهٍ}: يحتملُ أن يرجعَ إلى الرُّمَّانِ والزيتون؛ أي: مشتبهاً في شجره وورقه غير متشابه في ثمره، ويحتمل أن يرجع ذلك إلى سائر الأشجار والفواكه، وأن بعضها مشتبه؛ يشبه بعضه بعضاً، ويتقارب في بعض أوصافه، وبعضها لا مشابهة بينه وبين غيره، والكل ينتفع به العباد ويتفكَّهون، ويقتاتون ويعتبرون، ولهذا أمر تعالى بالاعتبار به، فقال: {انظروا}: نظر فكرٍ واعتبار {إلى ثمره}؛ أي: الأشجار كلها، خصوصاً النخل، {إذا أثْمَرَ وينعِهِ}؛ أي: انظروا إليه وقت إطلاعه ووقت نضجه وإيناعه؛ فإن في ذلك عبراً وآياتٍ يُستدلُّ بها على رحمة الله وسَعَة إحسانِهِ وجودِهِ وكمال اقتداره وعنايته بعباده، ولكن ليس كل أحدٍ يَعْتَبِرُ ويتفكَّر، وليس كلُّ من تفكَّر؛ أدرك المعنى المقصود، ولهذا قَيَّدَ تعالى الانتفاع بالآيات بالمؤمنين، فقال: {إنَّ في ذلكم لآياتٍ لقوم يؤمنونَ}: فإن المؤمنين يحمِلُهم ما معهم من الإيمان على العمل بمقتضياته ولوازمه التي منها التفكر في آيات الله والاستنتاج منها ما يراد منها وما تدلُّ عليه عقلاً وفطرةً وشرعاً.
{99} Na hii ni miongoni mwa neema zake kubwa zaidi ambazo viumbe vyote wanazihitaji sana miongoni mwa wanadamu na wengineo. Nayo ni kwamba aliteremsha maji kutoka mbinguni kwa mfululizo wakati watu wanapoyahitaji. Kisha Mwenyezi Mungu akaoteshea kwayo kila kitu miongoni mwa vile wanavyovila watu na mifugo. Kwa hivyo viumbe vikalia kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, na wakawa na wasaa kwa riziki yake, na wakafurahia kwa sababu ya ihsani yake, na wakaondokewa na kiangazi, na kukata tamaa, na ukame. Kwa hivyo nyoyo zao zikafurahi, na nyuso zikang’aa, na waja wakapata katika rehema ya Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu, yale ambayo wanafurahi kwayo na wanakula, jambo ambalo linawasababishia kufanya juhudi zao katika kumshukuru Yule aliyewapa neema hizo, na kumuabudu Yeye, na kurudi kwake, na kumpenda. Na Alipotaja ujumla wa aina za vile vinavyomea kwa maji miongoni mwa aina mbalimbali za miti na mimea, Akataja mazao na mitende kwa sababu ya wingi wa manufaa yake na kuwa ni chakula kikuu cha wengi wa watu. Kwa hivyo akasema, "Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani;" yaani, kutokana na mimea hiyo ya kijani tunatoa "nafaka zilizopandana," baadhi yake zikiwa juu ya nyingine zake, kama vile ngano, na shayiri, na mahindi, na mchele na aina nyinginezo za mazao. Na katika kueleza kwake kuwa zinapandana kuna ishara kwamba nafaka zake ni nyingi, na zote zimetokana na kitu kimoja, wala hazichanganyikani, bali ni nafaka zilizo mbalimbali lakini zenye asili moja. Na kuna ishara ya wingi wake, na wingi wa kubaki kwake na mapato yake, ili msingi wa mbegu hii ubaki, na mengi yabaki ya kula na kuhifadhi. "Na kutokana na mitende" Mwenyezi Mungu alitoa "katika makole yake;" nayo ganda la mtende kabla ya shada kutoka humo. Kisha yanatoka kutoka katika ganda hilo "mashada yaliyo karibu" yani, yaliyokaribu ambayo ni rahisi kuyachuma, yanayoinama karibu sana na mwenye kuyataka kiasi kwamba siyo vigumu kuyachuma kutoka kwenye mitende, hata kama ni mirefu. Kwa maana yana karab (yani sehemu ya mwanzo kabisa katika tawi la mtende) na vipandio ambavyo vinafanya kuwa rahisi kuipanda. "Na" Yeye Mtukufu Akatoa kwa maji haya "mabustani ya mizabibu, na mizaituni, na mikomamanga." Basi hii ni miongoni mwa miti yenye manufaa mengi, na thamani kubwa. Na ndiyo maana mwenyezi Mungu akayataja kwa njia maalumu baada ya kuitaja miti yote na mimea kwa ujumla. Na kauli yake. " yanayofanana na yasiyofanana;" inawezekana kuwa inarudi kwa makomamanga na mazaituni, yaani inayofanana katika mti wake na majani yake, lakini matunda yake hayafanani. Na inawezekana kwamba hilo linarudi kwa miti yote na matunda, na kwamba baadhi yake inafanana yenyewe kwa yenyewe, na inakaribiana katika baadhi ya sifa zake. Na baadhi yake haifanani na mingineyo. Na yote wananufaika kwayo waja, na wanayala matunda yake, na wanayala kama chakula kikuu, na wanapata mazingatio. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akaamrisha kuzingatia katika hayo, kwa hivyo akasema: "Angalieni," kuangalia kwa kutafakari na kuzingatia "matunda yake." Yaani, ya miti yote, hasa mitende, "yanapozaa na yakaiva;" yaani yatazameni wakati wa kuchipuka kwake, na wakati wa kukomaa kwake, na kuiva kwake. Kwani katika hayo kuna mazingatio, na Aya mbalimbali zinazotumiwa kuwa ushahidi juu ya rehema ya Mwenyezi Mungu, na upana wa ihsani yake, na kuwepo Kwake, na ukamilifu wa uwezo Wake, na uangalizi Wake mzuri kwa waja Wake. Hata hivyo, si kila mmoja anayezingatia na anatafakari; na si kila mwenye kutafakari akaitambua maana iliyokusudiwa. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akafungia kunufaika kwa Aya hizi kwa Waumini tu, kwa hivyo akasema, "Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini." Kwa sababu Waumini wanabebwa na imani waliyo nayo kufanya kulingana na matakwa yake, na mahitaji yake ambayo miongoni mwake ni kutafakari katika Aya za mwenyezi Mungu na kutoa kutoka kwayo yale yanayokusudiwa kwayo, na yale ambayo hayo yanayaashiria kiakili, na kiamaumbile ya asili, na kisheria.
: 100 - 104 #
{وَجَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يَصِفُونَ (100) بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنَّى يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُنْ لَهُ صَاحِبَةٌ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (101) ذَلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ (102) لَا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ (103) قَدْ جَاءَكُمْ بَصَائِرُ مِنْ رَبِّكُمْ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا وَمَا أَنَا عَلَيْكُمْ بِحَفِيظٍ (104)}.
100. Lakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu ya hayo wanayomsifu kwayo! 101. Yeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke? Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu. 102. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi, hapana mungu isipokuwa Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu. 103. Hazungukwi na macho, naye anayazunguka macho. Naye ni Mjua siri, Mwenye habari zote. 104. Hakika zimekwishawajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, mwenye kuona, basi ni kwa faida yake mwenyewe. Na mwenye kupofuka, basi ni hasara yake. Wala mimi si mtunzaji wenu.
#
{100} يخبر تعالى أنه مع إحسانه لعباده وتعرفه إليهم بآياته البينات وحججه الواضحات؛ أن المشركين به من قريش وغيرهم جعلوا له شركاء يدعونهم ويعبُدونهم من الجنِّ والملائكة، الذين هم خَلْقٌ مِن خَلْق الله، ليس فيهم من خصائص الربوبيَّة والألوهيَّة شيء، فجعلوها شركاء لمن له الخلقُ والأمرُ، وهو المنعم بسائر أصناف النعم، الدافع لجميع النقم، وكذلك خَرَقَ المشركون؛ أي: ائتفكوا وافتروا من تلقاء أنفسهم لله بنينَ وبناتٍ بغير علم منهم، ومن أظلم ممن قال على الله بلا علم، وافترى عليه أشنعَ النَّقص الذي يجب تنزيهُ الله عنه، ولهذا نزَّه نفسه عما افتراه عليه المشركون، فقال: {سبحانَه وتعالى عمَّا يَصِفونَ}؛ فإنه تعالى الموصوف بكل كمالٍ، المنزَّه عن كل نقصٍ وآفةٍ وعَيْبٍ.
{100} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba pamoja na ihsani yake kwa waja Wake, na kuwajulisha kwake Ishara Zake zilizo wazi na hoja zake zilizo wazi, kwamba wale wanaoshirikisha katika Maquraishi na wengineo walimfanyia Yeye washirika wanaowaomba na kuwaabudu miongoni mwa majini na Malaika, ambao ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu, na ambao hawana sifa yoyote ya umola wala uungu. Lakini wao wakawafanya kuwa washirika kwa Yule aliye na uumbaji na amri, na Yeye ndiye anayeneemesha kwa kila aina ya neema, Mwenye kuzuia adhabu zote. Na tena washirikina walisingizia uongo na wakazua wao wenyewe kuwa Mwenyezi Mungu ana wana wa kiume na wana wa kike bila ya wao kuwa na elimu juu ya hilo. Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemsingizia Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na elimu, na akamzulia upungufu mbaya zaidi ambao ni lazima Mwenyezi Mungu atakaswe kutokana nao? Na kwa sababu hii, akajitakasa Mwenyewe kutokana na yale waliyomzulia washirikina, kwa hivyo akasema; "Yeye Ametakasika, na ametukuka juu ya hayo wanayomsifu kwayo!" Kwa maana Yeye Ametukuka huyo anayesifiwa kwa kila ukamilifu, na ametakasika kutokana na kila upungufu, na kasoro, na dosari.
#
{101} {بديع السموات والأرض}؛ أي: خالقهما ومتقن صنعتهما على غير مثال سبق بأحسن خلق ونظام وبهاء لا تقترحُ عقول أولي الألباب مثله، وليس له في خلقهما مشارك. {أنَّى يكونُ له ولدٌ ولم تكن له صاحبةٌ}؛ أي: كيف يكون لله الولد وهو الإله السيد الصمد الذي لا صاحبةَ له؛ أي: لا زوجة، وهو الغني عن مخلوقاته، وكلها فقيرةٌ إليه مضطرةٌ في جميع أحوالها إليه، والولد لا بدَّ أن يكون من جنس والده، والله خالق كل شيء، وليس شيءٌ من المخلوقات مشابهاً لله بوجه من الوجوه. ولما ذكر عمومَ خَلْقِهِ للأشياء؛ ذكر إحاطة علمه بها، فقال: {وهو بكلِّ شيءٍ عليمٌ}، وفي ذكر العلم بعد الخلق إشارة إلى الدليل العقلي إلى ثبوت علمه، وهو هذه المخلوقات وما اشتملت عليه من النظام التامِّ والخلق الباهر؛ فإنَّ في ذلك دلالة على سَعَة علم الخالق وكمال حكمته؛ كما قال تعالى: {ألا يعلمُ مَنْ خَلَقَ وهو اللطيف الخبير}، وكما قال تعالى: {وهو الخلاَّقُ العليم}.
{101} "Yeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi;" yaani, Muumba wa viwili hivyo, aliyeviunda vyema bila ya mfano wa kabla, kwa uumbaji mzuri zaidi na mpangilio, na uzuri, ambao akili za watu wenye akili timamu haziwezi kupendekeza chochote mfano wake, na wala hana mshirika yeyote katika kuumba kwa viwili hivyo. "Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke?" Yaani, vipi Mwenyezi Mungu atakuwa na mwana na ilhali Yeye ndiye Mungu, bwana mkusudiwa na wote ambaye hana mke? Naye hawahitaji viumbe wake, nao wote wanamhitaji Yeye, wanalazimika kutafuta msaada wake katika hali zao zote. Na mwana ni lazima awe kutoka katika aina moja na baba yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na hakuna chochote katika kiumbe kinachofanana na mwenyezi Mungu kwa njia yoyote ile. Na alipotaja ujumla wa kuumba kwake vitu, Akataja elimu yake kuvienea. Kwa hivyo akasema, "Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu." Na katika kuitaja elimu baada ya kuumba kuna ishara kwa ushahidi wa kiakili juu ya kuthibiti kwa elimu yake, nayo ni viumbe hivi na yale vinavyojumuisha ya mpangilio kamili, na uumbaji wa kimaajabu. Kwani katika hilo kuna ushahidi juu ya upana wa elimu ya Muumba wake, na ukamilifu wa hekima Yake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Kwa hajui yule aliyeumba, ilhali Yeye ndiye Mjua siri, Mwenye habari zote?" Na kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mwenye kujua yote."
#
{102} ذلكم الذي خلق ما خلق وقدَّر ما قدَّر؛ {اللهُ ربُّكم}؛ أي: المألوهُ المعبودُ الذي يستحقُّ نهاية الذُّلِّ ونهاية الحبِّ، الربُّ الذي ربَّى جميع الخلق بالنعم، وصرف عنهم صنوف النقم، خالق كل شيءٍ لا إله إلا هو {فاعبدوه}؛ أي: إذا استقرَّ وثبت أنه الله الذي لا إله إلاَّ هو؛ فاصرِفوا له جميع أنواع العبادة، وأخلصوها لله، واقصدوا بها وجهه؛ فإنَّ هذا هو المقصود من الخلق الذي خُلِقوا لأجله، {وما خَلَقْتُ الجنَّ والإنسَ إلا لِيَعبُدُونِ}. {وهو على كل شيء وكيل}، أي: جميع الأشياء تحت وكالة الله وتدبيره خلقاً وتدبيراً وتصريفاً. ومن المعلوم أن الأمر المتصرَّف فيه يكون استقامته وتمامه وكمال انتظامه بحسب حال الوكيل عليه، ووكالته تعالى على الأشياء ليست من جنس وكالة الخلق؛ فإن وكالتهم وكالة نيابة، والوكيل فيها تابع لموكله، وأما الباري تبارك وتعالى؛ فوكالته من نفسه لنفسه، متضمنة لكمال العلم وحسن التدبير والإحسان فيه والعدل، فلا يمكن أحداً أن يستدرك على الله، ولا يرى في خلقه خللاً ولا فطوراً، ولا في تدبيره نقصاً وعيباً، ومن وكالته أنه تعالى توكَّل ببيان دينه وحفظه عن المزيلات والمغيِّرات، وأنه تولَّى حفظ المؤمنين وعصمتهم عما يزيل إيمانهم ودينهم.
{102} Huyo ambaye aliumba alichokiumba, na akakadiria aliyoyakadiria ndiye "Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi;" yaani, mwenye kufanyiwa Uungu, mwenye kuabudiwa, ambaye anastahiki kufanyiwa udhalilifu wa mwisho na mapenzi ya mwisho. Mola Mlezi ambaye alivilea viumbe vyote kwa neema na akaviepushia kila aina ya adhabu, Muumba wa kila kitu, hapana mungu ila Yeye. "Basi muabuduni Yeye," yaani, itakaposimama imara na kuthubiti kuwa Yeye ndiye Mungu, ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye; basi mfayieni aina zote za ibada, na mfanyieni ikhlasi katika hilo, na ukusudieni uso wake katika hayo. Kwa maana Haya ndiyo makusudio ya kuumbwa ambako waliumbwa wa ajili yake. "Sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu Mimi tu." "Na Yeye ni Msimamizi wa kila kitu;" maana yake, vitu vyote viko chini ya usimamizi wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji, na uendeshaji, na usimamizi. Na inavyojulikana ni kuwa jambo linaloendeshwa unakuwa unyoofu wake, na utimilifu wake, na ukamilifu wa mpangilio wake kulingana na hali ya mwenye kulisimamia. Na usimamizi wake yeye Mtukufu juu ya mambo si wa aina ya usimamizi wa viumbe. Kwa maana, usimamizi wao ni usimamizi wa uwakilishi, na wakili katika hayo yuko chini ya yule anayemwakilisha. Ama Uwakili wake Yeye Muumba mwanzilishi, mwingi wa baraka, Mtukufu ni uwakili wake kutoka kwake mwenyewe, unaojumuisha ukamilifu wa elimu, na usimamizi mzuri, na kuufanya kwa uzuri zaidi, na uadilifu. Na haiwezekani kwa yeyote yule kumdiriki Mwenyezi Mungu alichokifanya, wala kuona dosari au kasoro katika uumbaji wake, wala upungufu au dosari katika uendeshaji wake mambo. Na katika usimamizi wake ni kuwa Yeye, Mwenyezi, Alijiwekea usimamizi katika kubainisha dini yake na kuihifadhi kutokana na mambo ya kuiondosha na kuibadilisha. Na kwamba yeye Mtukufu alisimamia Kuwahifadhi Waumini na kuwalinda kutokana na yale yanayowaondolea imani na dini yao.
#
{103} {لا تدركه الأبصار}: لعظمته وجلالِهِ وكماله، أي: لا تحيط به الأبصار وإن كانت تراه وتفرح بالنظر إلى وجهه الكريم، فنَفْيُ الإدراك لا يَنْفي الرؤية، بل يثبتها بالمفهوم؛ فإنه إذا نفى الإدراك الذي هو أخص أوصاف الرؤية؛ دلَّ على أن الرؤية ثابتة؛ فإنه لو أراد نفي الرؤية؛ لقال: لا تراه الأبصارُ ... ونحو ذلك، فعلم أنه ليس في الآية حجة لمذهب المعطلة الذين ينفون رؤية ربِّهم في الآخرة، بل فيها ما يدل على نقيض قولهم. {وهو يدرِكُ الأبصار}؛ أي: هو الذي أحاط علمُهُ بالظواهر والبواطن، وسمعُهُ بجميع الأصوات الظاهرة والخفية، وبصرُهُ بجميع المبصرات صغارها وكبارها، ولهذا قال: {وهو اللطيف الخبير}؛ أي: الذي لَطُفَ علمه وخبرته ودقَّ حتى أدرك السرائر والخفايا والخبايا والبواطن، ومن لطفه أنه يسوقُ عبدَه إلى مصالح دينه، ويوصلها إليه بالطرق التي لا يشعر بها العبد ولا يسعى فيها، ويوصله إلى السعادة الأبدية والفلاح السرمديِّ من حيث لا يحتسب، حتى إنه يقدِّرُ عليه الأمورَ التي يكرهها العبدُ ويتألَّمُ منها ويدعو اللهَ أن يزيلَها؛ لعلمه أن دينَهُ أصلح؛ وأن كمالَه متوقِّفٌ عليها؛ فسبحان اللطيفِ لما يشاء الرحيم بالمؤمنين.
{103} "Hazungukwi na macho," kwa sababu ya ukuu wake, na taadhima yake, na ukamilifu wake; yaani, macho hayamzunguki, hata ingawa yanamwona na kufurahi kwa kuutazama uso wake mtukufu. Kwa hivyo kukanusha kuzunguka hakukanushi kuona; bali kunauthibitisha kuona kulingana na maana isiyokuwa ya moja kwa moja. Kwani ikiwa anakanusha kuzunguka ambako ni maalumu zaidi katika sifa za kuona, hilo linaonyesha kwamba kuona kumethibiti. Kwa maana ikiwa angetaka kukanusha kuona Angesema: ‘Macho hayamuoni ...’ na mfano wa hilo. Basi ikajulikana kwamba hakuna hoja katika Aya ya dhehebu la Mu’atwila, ambao wanakanusha kumuona Mola wao Mlezi katika Akhera. Bali ndani yake kuna ushahidi kinyume cha kauli yao. "Naye anayazunguka macho," yaani, Yeye ndiye ambaye elimu yake imekizunguka kilicho dhahiri na kilichofichika, na kusikia kwake kumezunguka sauti zote za dhahiri na zilizofichika, na kuona kwake yamekizunguka kila kinachoonekana, kidogo chake na kikubwa chake. Na ndiyo maana akasema, "Naye ni Mjua siri, Mwenye habari zote." Yaani, Yule ambaye elimu yake na kuwa kwake na habari ni kubwa sana na kwa makini kiasi kwamba anazizunguka siri, na yaliyofichika, na ya ndani. Na katika kujua kwake siri, ni kwamba ampeleka mja wake kwenye masilahi ya dini yake, na anayafikisha kwake kwa njia ambazo mja hazihisi wala hazifanyii bidii, na anamfikisha kwenye furaha ya milele na kufaulu kwa milele kutokea mahali asipotarajia, kiasi kwamba Yeye anamkadiria Mambo ambayo mja anayachukia na anapata uchungu kwa sababu yake, na anamuomba mwenyezi Mungu ayaondoe. Kwa sababu anajua kwamba dini yake ni yenye kutengenea zaidi, na kwamba ukamilifu wake unategemea juu yake. Basi Ametakasika yule ambaye ni Mjua siri wa atakalo, Mwenye kuwarehemu Waumini.
#
{104} {قد جاءكم بصائرُ من ربِّكم فمن أبصر فلنفسِهِ ومن عَمِيَ فعليها وما أنا عليكم بحفيظٍ}: لما بيَّن تعالى من الآيات البينات والأدلة الواضحات الدالة على الحقِّ في جميع المطالب والمقاصد؛ نبَّه العباد عليها، وأخبر أن هدايتهم وضدها لأنفسهم، فقال: {قد جاءَكُم بصائِرُ من ربِّكُم}؛ أي: آيات تبيِّن الحقَّ وتجعله للقلب بمنزلة الشمس للأبصار؛ لما اشتملت عليه من فصاحة اللفظ وبيانه ووضوحه ومطابقته للمعاني الجليلة والحقائق الجميلة؛ لأنَّها صادرةٌ من الربِّ الذي ربَّى خلقه بصنوف نعمه الظاهرة والباطنة، التي من أفضلها وأجلها تبيين الآيات وتوضيح المشكلات. {فمن أبصر}: بتلك الآياتِ مواقعَ العبرة وعمل بمقتضاها {فلنفسه}: فإنَّ الله هو الغنيُّ الحميد، ومن عَمِيَ بأن بُصِّرَ فلم يَتَبَصَّر، وزُجِرَ فلم ينزجِرْ، وبُيِّن له الحقُّ فما انقاد له ولا تواضع؛ فإنما عماه مضرَّتُه عليه. {وما أنا}: أيها الرسول، {عليكم بحفيظٍ}: أحفظ أعمالَكم وأراقِبُها على الدوام، إنما عليَّ البلاغُ المبين، وقد أدَّيته وبلَّغت ما أنزل الله إليَّ؛ فهذه وظيفتي، وما عدا ذلك فلست موظفاً فيه.
{104} "Hakika zimekwisha wajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, mwenye kuziona, basi ni kwa faida yake mwenyewe. Na mwenye kupofuka, basi ni hasara yake. Nami si mtunzaji wenu." Kwa sababu ya yale aliyoyabainisha Yeye Mtukufu miongoni mwa Aya mbalimbali zilizo wazi, na ushahidi ulio wazi, unaoashiria kwenye haki katika matakwa yote na makusudio yote. Akawatanabahisha waja juu yake, na akajulisha kuwa uwongofu wao na kinyume chake ni juu yao wenyewe, kwa hivyo akasema; "Hakika zimekwisha wajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, Aya mbalimbali zinazobainisha haki na kuuwekea moyo iwe wazi kama jua linavyokuwa kwa macho. Kwa sababu yaliyo ndani yake ya ufasaha wa matamshi, na ubainifu wake, na uwazi wake, na kulingana kwake na maana tukufu na hakika nzuri nzuri. Kwa sababu zinatoka kwa Mola Mlezi, ambaye aliwalea viumbe wake kwa kila aina ya neema zake za dhahiri na zilizofichika, ambazo katika bora zake zaidi na tukufu zaidi ni ubainifu wa Aya mbalimbali na kuweka wazi wa matatizo. "Kwa hivyo, mwenye kuona," kwa Aya hizo sehemu za mazingatio na anafanya matendo kulingana na matakwa yake, "basi ni kwa faida yake mwenyewe" kwa maana Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitegemea, Msifiwa. Na mwenye kupofuka kwa kuonyeshwa, naye akaacha kuona, na akakemewa, lakini hakukemeka, na akabainishiwa haki, lakini hakuifuata wala kuinyenyekea. Basi upofu wake madhara yake ni juu yake. "Wala mimi" Ewe Mtume "si mtunzaji wenu wenu." Nikihifadhi vitendo vyenu na kuviangalia kila wakati. Lakini lililo juu yangu ni kufikisha kuliko wazi, na tayari nilikwisha tekeleza hilo, na nikafikisha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwangu. Basi hii ndiyo kazi yangu, na zaidi ya hilo, mimi sikupewa kazi hiyo.
: 105 - 108 #
{[وَكَذَلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ (105) اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنْ رَبِّكَ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ (106) وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا أَشْرَكُوا وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا وَمَا أَنْتَ عَلَيْهِمْ بِوَكِيلٍ (107)] وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ فَيَسُبُّوا اللَّهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ كَذَلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَى رَبِّهِمْ مَرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (108)}.
105. Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanaojua. 106. Fuata yale yaliyofunuliwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Na jitenge na washirikina. 107. Na lau Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelimshirikisha. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao. 108. Wala msiwatukane hao ambao wao wanawaomba badala ya Mwenyezi Mungu, nao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao ni kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{108} ينهى الله المؤمنين عن أمر كان جائزاً بل مشروعاً في الأصل، وهو سبُّ آلهة المشركين التي اتُّخذت أوثاناً وآلهة مع الله، التي يُتَقَرَّب إلى الله بإهانتها وسبها، ولكن لمَّا كان هذا السبُّ طريقاً إلى سبِّ المشركين لربِّ العالمين، الذي يجب تنزيه جنابه العظيم عن كل عيبٍ وآفةٍ وسبٍّ وقدح؛ نهى الله عن سبِّ آلهة المشركين؛ لأنهم يحمون لدينهم ويتعصَّبون له؛ لأن كلَّ أمة زين الله لهم عملهم فرأوه حسناً وذبوا عنه ودافعوا بكل طريق، حتى إنهم يسبُّون الله ربَّ العالمين الذي رسخت عظمتُهُ في قلوب الأبرار والفجار إذا سبَّ المسلمون آلهتهم، ولكن الخلقَ كلَّهم مرجعُهم ومآلُهم إلى الله يوم القيامة، يعرَضون عليه وتعرَضُ أعمالهم، فينبِّئهم بما كانوا يعملون من خيرٍ وشرٍّ. وفي هذه الآية الكريمة دليلٌ للقاعدة الشرعيَّة، وهو أن الوسائل تُعتبر بالأمور التي توصِلُ إليها، وأن وسائل المحرم ـ ولو كانت جائزة ـ تكون محرمةً إذا كانت تفضي إلى الشرِّ.
{108} Mwenyezi Mungu anawakataza Waumini kufanya jambo ambalo lilikuwa linaruhusiwa, bali mwanzoni lilikuwa katika sheria. Nalo ni kuwatukana miungu wa washirikina ambao walichukuliwa kuwa viabudiwa, na miungu pamoja na Mwenyezi Mungu, ambao wanamuweka karibu na Mwenyezi Mungu kwa kuidunisha na kuilaani. Lakini pindi kutukana huku kulipokuwa ni njia ya washirikina kufikia kumtukana Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye heshima yake kubwa ni lazima itakaswe kutokana na kila kasoro, na maradhi, na matusi, na kashfa; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akakataza kuwatukana miungu ya washirikina. Kwa sababu wao wanailinda dini yao na wanaitetea. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameupambia kila umma vitendo vyao ,kwa hivyo wakaviona kuwa ni vizuri, na wakavilinda na kuvizuilia kwa kila njia, mpaka wanamtukana Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye ukuu wake umethibiti katika nyoyo za walio wema na waovu, Waislamu wanaitukana miungu yao. Lakini viumbe wote marejeo yao na mwisho wao ni kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama. Watahudhurishwa kwake, na yatahudhurishwa matendo yao, kisha atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda, ya heri na maovu. Na katika Aya hii tukufu kuna ushahidi wa kanuni ya kisheria, ambayo ni kwamba njia zinazingatiwa kulingana na mambo zinayoyafikia, na kwamba njia za kilichoharamishwa - hata zikiwa zinaruhusika - zinakuwa haramu ikiwa zitafikisha katika maovu.
: 109 - 111 #
{وَأَقْسَمُوا بِاللَّهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِنْ جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَيُؤْمِنُنَّ بِهَا قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِنْدَ اللَّهِ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ (109) وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ (110) وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَى وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اللَّهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ (111)}.
109. Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vyao vikali zaidi, kuwa ikiwajia Ishara, bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Ishara hizo ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na ni nini kitawajulisha kuwa zikija, hawataamini? 110. Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza. Kisha tutawaacha katika upotovu wao wakitangatanga kwa upofu. 111. Na lau kuwa tungeliwateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado hawakuwa ni wa kuamini, isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wanafanya ujinga.
#
{109} أي: وأقسم المشركون المكذِّبون للرسول محمد - صلى الله عليه وسلم - {بالله جَهْدَ أيمانِهِم}؛ أي: قسماً اجتهدوا فيه وأكَّدوه، {لئن جاءتْهم آيةٌ}: تدلُّ على صدق محمد - صلى الله عليه وسلم -، {ليؤمنُنَّ بها}: وهذا الكلام الذي صدر منهم لم يكن قصدُهم فيه الرشاد، وإنما قصدُهم دفع الاعتراض عليهم وردُّ ما جاء به الرسول قطعاً؛ فإنَّ الله أيَّد رسوله - صلى الله عليه وسلم - بالآيات البينات والأدلة الواضحات التي عند الالتفات لها لا تَبْقَى أدنى شُبهة ولا إشكال في صحَّة ما جاء به؛ فطلبهم بعد ذلك للآيات من باب التعنُّت الذي لا يلزم إجابته، بل قد يكون المنع من إجابتهم أصلح لهم؛ فإنَّ الله جرت سنَّتُهُ في عباده أن المقترحين للآيات على رسلهم إذا جاءتهم فلم يؤمنوا بها أنه يعاجلهم بالعقوبة، ولهذا قال: {قل إنَّما الآياتُ عند الله}؛ أي: هو الذي يرسلها إذا شاء، ويمنعها إذا شاء، ليس لي من الأمر شيء، فطلبُكم مني الآيات ظلمٌ وطلبٌ لما لا أملك، وإنما توجَّهون إلى توضيح ما جئتكم به وتصديقه، وقد حصل، ومع ذلك؛ فليس معلوماً أنَّهم إذا جاءتهم الآيات يؤمنون ويصدِّقون، بل الغالب ممن هذه حاله [أنه] لا يؤمن، ولهذا قال: {وما يشعِرُكم أنها إذا جاءتْ لا يؤمنونَ}.
{109} Yaani, na waliapa washirikina waliomkadhibisha Mtume Muhammad -rehema na amani zimshukie - kwa Mwenyezi Mungu "viapo vyao vikali zaidi." Yani viapo walivyojitahiji ndani yake, na wakavisisitiza, "kwamba ikiwajia Ishara" yenye kuonyesha ukweli wa Muhammad -rehema na amani zimshukie - "bila ya shaka wataiamini." Na maneno haya ambayo yalitoka kwao, makusudio yao hayakuwa na uwongofu ndani yake bali makusudio yao yalikuwa ni kujiondolea upinzani, na kukataa yale aliyokuja nayo Mtume bila ya shaka yoyote. Kwa maana Mwenyezi Mungu alimuunga mkono Mtume wake – rehema na amani ziwe juu yake – kwa Aya zilizo wazi, na ushahidi ulio wazi, ambazo pindi tu zinapozingatiwa, haibaki tuhuma yoyote ya chini kabisa, wala tatizo hata kidogo katika usahihi wa yale aliyokuja nayo. Basi ombi lao la Aya, baada ya hayo ni katika mlango wa ukaidi ambao hauhitaji jawabu; bali huenda kuacha kuwajibu ndiyo bora zaidi kwao. Kwani Mwenyezi Mungu ilikwisha pita Sunna yake katika waja wake kwamba wale wanaowapendekezea Mitume wao Aya, ikiwajia na wasiziamini, basi Yeye kwa hakika huwaharakishia adhabu. Na ndiyo maana akasema, "Sema: Hakika, Ishara hizo ziko kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, Yeye ndiye anayezituma akitaka, na anazizuia akitaka. Mimi sina chochote katika jambo hilo basi kuniomba kwenu mimi Aya ni dhuluma na ombi la kile nisichokimiliki. Lakini mnapaswa kunielekezea kufafanua yale niliyowajia nayo, na kuyasadiki, na tayari yameshafanyika. Lakini pamoja na hayo, haijulikani ikiwa zitakapowajia Ishara hizo wataziamini na kuzisadiki. Bali uwezekano mkubwa kwa yule ambaye hii ndiyo hali yake [ni kwamba], hataamini. Ndiyo maana akasema, "Na ni nini kitawajulisha kuwa zikija, hawataamini?"
#
{110} {ونُقَلِّبُ أفئدتَهم وأبصارَهم كما لم يؤمِنوا به أولَ مرةٍ ونذرُهم في طُغيانهم يعمَهونَ}؛ أي: ونعاقبهم إذا لم يؤمنوا أول مرة يأتيهم فيه الداعي وتقوم عليهم الحجَّة بتقليب القلوب والحيلولة بينهم وبين الإيمان وعدم التوفيق لسلوك الصراط المستقيم، وهذا من عدل الله وحكمته بعباده؛ فإنهم الذين جَنَوْا على أنفسهم، وفُتح لهم الباب فلم يدخلوا، وبُيِّن لهم الطريق فلم يسلكوا؛ فبعد ذلك إذا حُرِموا التوفيق؛ كان مناسباً لأحوالهم.
{110} "Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza. Kisha tutawaacha katika upotovu wao wakitangatanga kwa upofu." Yaani, tutawaadhibu ikiwa hawataamini mara ya kwanza atakapowajia mwitaji, na ikasimama hoja juu yao, kwa kuzigeuza nyoyo na kuzuia kati yao na kuamini, na kutowawezesha kuifuata njia iliyonyooka. Na hii ni katika uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na hekima yake kwa waja wake; kwa maana, hao ndio kwa hakika waliojifanyia uhalifu nafsi zao, na mlango ulifunguliwa kwa ajili yao, lakini hawakuingia, na walibainishiwa njia, lakini hawakuifuata. Kwa hivyo baada ya haya, ikiwa watanyimwa kuwezeshwa, basi hilo litakuwa linafaana na hali zao.
#
{111} وكذلك تعليقهم الإيمان بإرادتهم ومشيئتهم وحدهم وعدم الاعتماد على الله من أكبر الغلط؛ فإنهم لو جاءتهم الآياتُ العظيمة من تنزيل الملائكة إليهم يشهدون للرسول بالرسالة وتكليم الموتى وبعثهم بعد موتهم، وحشرنا عليهم كلَّ شيءٍ حتى يكلِّمهم قبلاً ومشاهدةً ومباشرة بصدق ما جاء به الرسول؛ ما حَصَلَ لهم الإيمان إذا لم يشأ الله إيمانهم، ولكن أكثرهم يجهلون؛ فلذلك رتَّبوا إيمانهم على مجرد إتيان الآيات، وإنما العقل والعلم أن يكون العبد مقصوده اتِّباع الحق، ويطلبه بالطرق التي بيَّنها الله، ويعمل بذلك، ويستعين ربَّه في اتباعه، ولا يتَّكل على نفسه وحوله وقوته، ولا يطلب من الآيات الاقتراحية ما لا فائدة فيه.
{111} Na vivyo hivyo, kuifungamanisha imani na kutaka kwao na mapenzi yao peke yao, na kutomtegemea mwenyezi Mungu, ni miongoni mwa makosa makubwa zaidi. Kwa maana, lau zingewajia Ishara kubwa kama vile kuwateremshia Malaika wakimshuhudia Mtume ujumbe, na kuwaongelesha wafu, na kuwafufua baada ya kufa kwao. Na tukawakusanyia kila kitu ili kiwaongeleshe mbele yao, kwa kuviona, na kwa moja kwa moja vikishuhudia ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume; basi hawangepata imani kama mwenyezi Mungu hangetaka waamini, lakini wengi wao wanafanya ujinga. Ndiyo maana wakafungamanisha kuamini kwao na kuja kwa Aya tu. lakini akili na elimu ni kwamba mja awe lengo lake ni kufuata haki, na aitafute kwa njia ambazo Mwenyezi Mungu alizibainisha, na azitendee kazi, amuombe msaada Mola wake Mlezi katika kuifuata, na wala asijitegemee nafsi yake na uwezo wake na nguvu zake, na wala asitafute katika Aya anazopendekeza yeye, zisizokuwa na faida yoyote.
: 112 - 113 #
{وَكَذَلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنْسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ (112) وَلِتَصْغَى إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُمْ مُقْتَرِفُونَ (113)}.
112. Na kadhalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashetani wa kiwatu, na kijini, wanafundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba, kwa udanganyifu. Na angelipenda Mola wako Mlezi, wasingelifanya hayo. Basi waache na hayo wanayoyazua. 113. Na ili ziyaelekee hayo nyoyo za wale wasioiamini Akhera, nao wayaridhie, na wayachume yale wanayoyachuma.
#
{112} يقول تعالى مسلياً لرسولِه [محمدٍ]- صلى الله عليه وسلم -: وكما جعلنا لك أعداء يردُّون دعوتك ويحاربونك ويحسدونك؛ فهذه سنتنا أن نجعل لكلِّ نبي نرسله إلى الخلق أعداءً من شياطين الإنس والجن يقومون بضد ما جاءت به الرسل، {يوحي بعضُهم إلى بعض زُخْرُفَ القول غروراً}؛ أي: يزين بعضُهم لبعض الأمر الذي يدعون إليه من الباطل ويزخرفونَ له العبارات حتى يجعلوه في أحسن صورة ليغترَّ به السفهاءُ وينقادَ له الأغبياءُ الذين لا يفهمون الحقائق ولا يفقهون المعاني، بل تعجبهم الألفاظ المزخرفة والعبارات المموِّهة، فيعتقدون الحقَّ باطلاً والباطل حقًّا.
{112} Yeye Mtukufu anasema, akimfariji Mtume Wake [Muhammad] - Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani. - Na kama vile tulivyokufanyia maadui wanaoukataa wito wako, na wanakupiga vita, na wanakuhusudu, basi hii ndiyo sunnah yetu, kwamba tunamfanyia maadui kila Nabii tunayemtuma kwa viumbe, miongoni mwa mashetani wa watu, na majini, wanaopinga yale waliyoyaleta Mitume. "Wanafundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba, kwa udanganyifu." Yaani, baadhi yao wanawapambia wenzi wao jambo ambalo wanalingania la batili, na wanalipambia misemo mpaka walifanye katika umbo nzuri zaidi ili wapumbavu wadanganywe nalo, na walifuate wajinga ambao hawafahamu uhakika wala hawaelewi maana zake. Bali wanavutiwa tu na maneno yaliyopambwa, na misemo iliyofichwa, kwa hivyo wanaitakidi haki kwamba ni batili, na batili kwamba ni haki.
#
{113} ولهذا قال تعالى: {ولِتَصْغَى إليه}؛ أي: ولتميلَ إلى ذلك الكلام المزخرف {أفئدةُ الذين لا يؤمنون بالآخرة}: لأن عدم إيمانهم باليوم الآخر وعدم عقولهم النافعة يحمِلُهم على ذلك، {ولِيَرْضَوْه}: بعد أن يَصْغَوا إليه، فيصغَوْن إليه أولاً، فإذا مالوا إليه ورأوا تلك العبارات المستحسنة؛ رضوه وزُيِّن في قلوبهم وصار عقيدةً راسخةً وصفة لازمة، ثم ينتجُ من ذلك أن يقترفوا من الأعمال والأقوال ما هم مقترفون؛ أي: يأتون من الكذب بالقول والفعل ما هو من لوازم تلك العقائد القبيحة؛ فهذه حال المفترين شياطين الإنس والجن المستجيبين لدعوتهم، وأما أهل الإيمان بالآخرة وأولو العقول الوافية والألباب الرزينة؛ فإنهم لا يغترُّون بتلك العبارات، ولا تخلبهم تلك التمويهات، بل همَّتهم مصروفةٌ إلى معرفة الحقائق، فينظرون إلى المعاني التي يدعو إليها الدعاة؛ فإن كانت حقًّا؛ قبلوها وانقادوا لها، ولو كُسِيَتْ عباراتٍ رديةً وألفاظاً غير وافية، وإن كانت باطلاً؛ ردُّوها على من قالها، كائناً مَن كان، ولو ألبست من العبارات المستحسنة ما هو أرقُّ من الحرير. ومن حكمةِ اللهِ تعالى في جعله للأنبياء أعداءً وللباطل أنصاراً قائمين بالدعوة إليه: أن يحصُلَ لعبادِهِ الابتلاءُ والامتحانُ؛ ليتميَّز الصادقُ من الكاذب، والعاقل من الجاهل، والبصير من الأعمى. ومن حكمتِهِ: أنَّ في ذلك بياناً للحقِّ وتوضيحاً له؛ فإنَّ الحقَّ يستنير ويتَّضح إذا قام الباطل يصارعه ويقاومه؛ فإنه حينئذ يتبيَّن من أدلة الحقِّ وشواهده الدالة على صدقه وحقيقته ومن فساد الباطل وبطلانه ما هو من أكبر المطالب التي يتنافس فيها المتنافسون.
{113} Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, "Na ili ziyaelekee." Yaani, ili ziyaelekee katika maneno hayo yaliyopambwa "nyoyo za wale wasioiamini Akhera" sababu kutoiamini kwao Siku ya Mwisho na kutokuwa kwao na akili zenye kunufaisha vinawabeba kufanya hivyo; "nao wayaridhie" baada ya kuyaelekea. Kwa hivyo wanayaelekea kwanza, na wanapoyaelekea na wakaiona misemo hiyo ya iliyofanywa kuwa nzuri, Wanairidhia, na ikapambwa katika nyoyo zao, na ikawa ni itikadi thabiti na sifa isiyowaacha, kisha inatokana na hayo kwamba wafanye matendo na maneno wanayoyafanya. Yaani, wanafanya uongo kwa maneno na vitendo, ambayo ni katika yale yasiyoachana na itikadi hizo mbaya. Basi hii ndiyo hali ya wanaotenda maovu, mashetani wa watu na majini, wanaouitikia wito wao. Na ama watu wanaoiamini Akhera na wenye akili kamili na akili zilizo sawa, wao hawadanganywi na misemo hiyo, wala hawapotoshwi na ufichaji huo. Bali, hima yao inaelekezwa katika kujua mambo ya uhakika, kwa hivyo wanaangalia maana ambazo walinganizi wanayalingania. Basi kama ni haki, wanayakubali na kuyafuata, hata ikiwa yatavalishwa misemo mibaya na maneno yasiyotosha. Na ikiwa ni ya batili, wanayarudisha kwa yule aliyeyasema, yeyote yule, hata kama yatavalishwa misemo iliyofanywa kuwa mizuri iliyo laini zaidi kuliko hariri. Na Miongoni mwa hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwafanyia Mitume maadui, na batili kuwa na watetezi wanaoilingania ni ili waja Wake wapate majaribio, na mtihani. Ili apambanuke mkweli na mwongo, na mwenye akili timamu na mjinga, na mwenye kuona na kipofu. Na katika hekima yake ni kuwa hatika haya kuna ubainisho wa haki, na kuuweka wazi. Kwa maana, unaangazika, na inakuwa wazi pale batili inapoisimama hupambana nayo na kuipinga. Basi hapo inabainika katika hoja za haki na ushahidi wake yenye kuashiria ukweli wake, na uhakika wake, na ubaya wa batili na ubatili wake ambayo ni katika mahitaji makubwa zaidi ambayo washindani ndani yake wale wanaoshindana.
: 114 - 115 #
{أَفَغَيْرَ اللَّهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنْزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِنْ رَبِّكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ (114) وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (115)}.
114. Je, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliyewateremshia Kitabu hiki kilichoelezwa kwa kina? Na wale tuliowapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi kamwe usiwe katika wale wanaotia shaka. 115. Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa ukweli na uadilifu. Hakuna yeyote wa kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
#
{114} أي: قلْ يا أيُّها الرسولُ: {أفغير الله أبتغي حَكَماً}: أحاكم إليه وأتقيَّد بأوامره ونواهيه؛ فإن غير الله محكومٌ عليه لا حاكم، وكلُّ تدبير وحكم للمخلوق؛ فإنه مشتمل على النقص والعيب والجور، وإنما الذي يجب أن يُتَّخذ حاكماً؛ فهو الله وحده لا شريك له، الذي له الخلق والأمر {الذي أنزل إليكم الكتاب مفصَّلاً}؛ أي: موضحاً فيه الحلال والحرام والأحكام الشرعية وأصول الدين وفروعه، الذي لا بيان فوقَ بيانِهِ، ولا برهانَ أجلى من برهانه، ولا أحسن منه حكماً، ولا أقوم قيلاً؛ لأنَّ أحكامه مشتملة على الحكمة والرحمة، وأهل الكتب السابقة من اليهود والنصارى يعترفون بذلك و {يعلمونَ أنَّه منزَّلٌ من ربِّك بالحقِّ}: ولهذا تواطأت الإخبارات، {فلا} تَشُكَّنَّ في ذلك ولا {تكوننَّ من الممترين}.
{114} Yani, sema, ewe Mtume, "Je, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu?" Nitafute hukumu kutoka Kwake, na ninashikamana na amri zake na makatazo yake. Kwani asiyekuwa mwenyezi Mungu anahukumiwa yeye mwenyewe, si hakimu. Na kila uendeshaji mambo na hukumu ya viumbe vyote hivyo vinajumuisha upungufu, na kasoro, na dhuluma. Na hakika yule anayepasa kufanywa hakimu ni Yeye mwenyezi Mungu peke yake, asiyekuwa na mshirika yeyote, ambaye ana uumbaji na amri "ndiye aliyewateremshia Kitabu hiki kilichoelezwa kwa kina?" Yaani, ambacho ndani yake imewekwa wazi halali na haramu, na hukumu za kisharia, na misingi ya dini na matawi yake, ambayo hakuna ubainifu mkubwa zaidi kuliko ubainifu wake, na hakuna uthibitisho ulio bora zaidi kuliko uthibitisho wake, wala hakuna kilicho kizuri zaidi yake katika hukumu, wala hakuna kauli madhubuti zaidi kuiliko. Kwa sababu hukumu zake zinajumuisha hekima na rehema. na watu wa Vitabu vilivyotangulia, miongoni mwa Mayahudi na Manaswara wanakiri hilo, na "wanajua ya kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa Haki." Na ndiyo maana habari zote zilikubaliana juu ya hilo "basi" kamwe usisitesite katika hayo wala "usiwe katika wale wanaotia shaka."
#
{115} ثم وصف تفصيلها فقال: {وتمَّتْ كلمةُ ربِّك صدقاً وعدلاً}؛ أي: صدقاً في الإخبار وعدلاً في الأمر والنهي؛ فلا أصدق من أخبار الله التي أودعها هذا الكتاب العزيز، ولا أعدل من أوامره ونواهيه، {لا مبدِّلَ لكلماتِهِ}؛ حيثُ حفظها وأحكمها بأعلى أنواع الصدق وبغاية الحقِّ؛ فلا يمكن تغييرها ولا اقتراح أحسن منها. {وهو السميع}: لسائر الأصوات، باختلاف اللغات، على تفنن الحاجات، {العليم}: الذي أحاط علمُهُ بالظواهر والبواطن والماضي والمستقبل.
{115} Kisha akaeleza kwa kina, akasema, "Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa ukweli na uadilifu;" yaani, ni ukweli katika kutoa habari, na uadilifu katika kuamirisha na kukataza. Kwa hivyo hakuna ya ukweli zaidi kuliko habari za Mwenyezi Mungu ambazo aliziweka katika Kitabu hiki kitukufu, wala hakuna la uadilifu zaidi ya maamrisho yake na makatazo yake. "Hakuna yeyote wa kuyabadilisha maneno yake." Kwa maana aliyahifadhi, na akayaweka sawasawa kwa aina ya juu zaidi ya ukweli, na ukomo wa haki. Bali haiwezekani kuyabadilisha wala kupendekeza kilicho bora zaidi yake. "Na Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema" sauti zote kwa lugha mbali mbali, kwa aina zote za mahitaji. "Mwenye kujua yote" ambaye elimu yake imeyazunguka yote ya dhahiri na ya ndani, na yaliyopita na yajayo.
: 116 - 117 #
{وَإِنْ تُطِعْ أَكْثَرَ مَنْ فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ إِنْ يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ (116) إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَنْ يَضِلُّ عَنْ سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ (117)}.
116. Na ukiwatii wengi wa hawa waliomo katika dunia, watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa isipokuwa ni wenye kusema uwongo tu. 117. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Anayejua vyema yule aliyepotea Njia yake, naye ndiye Anayejua vyema wale walioongoka.
#
{116} يقول تعالى لنبيِّه محمد - صلى الله عليه وسلم - محذراً عن طاعة أكثر الناس: {وإن تُطِعْ أكثرَ مَنْ في الأرض يضلُّوكَ عن سبيل الله}: فإنَّ أكثرهم قدِ انحرفوا في أديانهم وأعمالهم وعلومهم؛ فأديانُهم فاسدةٌ، وأعمالُهم تبعٌ لأهوائِهِم، وعلومُهم ليس فيها تحقيقٌ ولا إيصالٌ لسواء الطريق، بل غايتُهم أنَّهم يتَّبعون الظنَّ الذي لا يغني من الحقِّ شيئاً، ويتخرَّصون في القول على الله ما لا يعلمون.
{116} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad-rehema na Amani zimshukie – akimtahadharisha juu ya kuwatii wengi wa watu: "Na ukiwatii wengi wa hawa waliomo katika dunia, watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu." Kwa maana wengi wao, walikwisha potoka katika dini zao, na matendo yao, na elimu zao. Hivyo basi dini zao ni mbovu, na matendo yao yanafuata matamanio yao, na elimu zao hazina uhakika wala kufikisha katika njia iliyo sawa. Bali ukomo wao ni kwamba wanafuata dhana ambayo haifai kitu mbele ya haki, na wanadanganya katika kusema juu ya Mwenyezi Mungu kwa yale wasiyoyajua.
#
{117} ومَن كان بهذه المثابة؛ فحريٌّ أن يحذِّر اللهُ منه عبادَه ويصفُ لهم أحواله؛ لأنَّ هذا وإن كان خطاباً للنبي - صلى الله عليه وسلم -؛ فإنَّ أمتَه أسوةٌ له في سائر الأحكام التي ليست من خصائصه، والله تعالى أصدقُ قيلاً وأصدقُ حديثاً، و {هو أعلم بمن يَضِلُّ عن سبيله}، وأعلم بمن يهتدي ويهدي، فيجب عليكم أيُّها المؤمنون أن تتَّبعوا نصائحه وأوامره ونواهيه؛ لأنه أعلم بمصالحكم، وأرحم بكم من أنفسكم. ودلت هذه الآية على أنه لا يستدل على الحقِّ بكثرة أهله، ولا يدلُّ قلةُ السالكين لأمرٍ من الأمور أن يكون غير حقٍّ، بل الواقع بخلاف ذلك؛ فإنَّ أهل الحقِّ هم الأقلون عدداً الأعظمون عند الله قدراً وأجراً، بل الواجب أن يستدلَّ على الحق والباطل بالطرق الموصلة إليه.
{117} Na yule ambaye ni namna hii, basi mwenyezi Mungu anafaa zaidi kuwaonya waja wake kuhusiana naye, na awaeleze hali zake. Kwa sababu hata kama haya anaambiwa Nabii -rehema na amani ziwe juu yake, - Ummah wake wanachukua kiigizo kwake katika hukumu zote ambazo si maalumu kwake tu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mkweli zaidi wa usemi, na mkweli zaidi wa maneno. Na "ndiye Anayejua vyema yule aliyepotea Njia yake," naye ndiye anayejua vyema anayeongoka, na wa kumuongoa. Kwa hivyo, enyi Waumini, ni lazima mfuate nasaha zake, na amri zake, na makatazo yake. Kwa sababu Yeye ndiye anayejua zaidi masilahi yenu, na mwenye rehema zaidi kwenu kuliko nyinyi wenyewe kwa nafsi zenu. Na Aya hii iliashiria kwamba idadi kubwa ya watu wanaofuata jambo haionyeshi kuwa ndiyo haki, wala idadi ndogo ya watu wanaofuata jambo haionyeshi kuwa si haki. Bali uhakika wa mambo uko kinyume cha hayo. Kwa kuwa Watu wa haki ndio wachache zaidi kwa idadi, na ndio wakubwa wa cheo na malipo kwa Mwenyezi Mungu. Bali, kinachotakiwa ni kutumia njia zinazofikisha kwa haki au batili kuwa ndizo ushahidi wake.
: 118 - 119 #
{فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ إِنْ كُنْتُمْ بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ (118) وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُمْ مَا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ وَإِنَّ كَثِيرًا لَيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِمْ بِغَيْرِ عِلْمٍ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ (119)}
118. Basi kuleni katika yale yaliyotajiwa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake. 119. Na mna nini msile katika yale yaliyotajiwa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha wabainishia kwa kina vile alivyowaharimishia, isipokuwa vile mnavyolazimishwa? Na hakika wengi wanapotea kwa matamanio yao bila ya kuwa na elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua vyema wale wanaopindukia mipaka.
#
{118 - 119} يأمر تعالى عباده المؤمنين بمقتضى الإيمان، وأنهم إن كانوا مؤمنين؛ فليأكلوا مما ذُكِرَ اسم الله عليه من بهيمة الأنعام وغيرها من الحيوانات المحلَّلة، ويعتقدوا حلَّها، ولا يفعلوا كما يفعله أهل الجاهلية من تحريم كثير من الحلال ابتداعاً من عند أنفسهم وإضلالاً من شياطينهم؛ فذكر الله أنَّ علامة المؤمن مخالفةُ أهل الجاهلية في هذه العادة الذميمة المتضمِّنة لتغيير شرع الله، وأنَّه أي شيء يمنعُهم من أكل ما ذُكِر اسم الله عليه؛ وقد فصَّل الله لعباده ما حرَّم عليهم وبيَّنه ووضَّحه، فلم يبق فيه إشكالٌ ولا شبهةٌ توجِبُ أن يمتنعَ من أكل بعض الحلال خوفاً من الوقوع في الحرام. ودلت الآية الكريمة على أن الأصل في الأشياء والأطعمة الإباحة، وأنه إذا لم يرد الشرعُ بتحريم شيءٍ منها؛ فإنَّه باق على الإباحة؛ فما سكتَ الله عنه؛ فهو حلالٌ؛ لأنَّ الحرام قد فصَّله الله؛ فما لم يفصِّله الله؛ فليس بحرام. ومع ذلك؛ فالحرام الذي قد فصَّله الله وأوضحه قد أباحه عند الضرورة والمخمصة؛ كما قال تعالى: {حُرِّمَتْ عليكمُ الميتةُ والدمُ ولحمُ الخنزيرِ ... } إلى أن قال: {فمنِ اضْطُرَّ في مخمصةٍ غير متجانفٍ لإثم فإنَّ الله غفورٌ رحيمٌ}. ثم حذر عن كثير من الناس، فقال: {وإنَّ كثيراً لَيُضِلُّونَ بأهوائهم}؛ أي: بمجرَّد ما تهوى أنفسهم {بغيرِ علم}: ولا حجَّة؛ فليحذرِ العبد من أمثال هؤلاء، وعلامتُهم كما وصَفَهم الله لعبادِهِ أنَّ دعوتَهم غير مبنيَّة على برهانٍ ولا لهم حجَّة شرعيَّة، وإنما يوجد لهم شبهٌ بحسب أهوائهم الفاسدة، وآرائهم القاصرة؛ فهؤلاء معتدونَ على شرع الله وعلى عبادِ الله، والله لا يحبُّ المعتدين؛ بخلاف الهادين المهتدين؛ فإنهم يدعون إلى الحقِّ والهدى، ويؤيِّدون دعوتهم بالحجج العقليَّة والنقليَّة، ولا يتَّبعون في دعوتهم إلا رضا ربِّهم والقرب منه.
{118 - 119} Yeye Mtukufu anawaamrisha waja wake Waumini kulingana na matakwa ya imani, na kwamba ikiwa ni Waumini, Basi na wale waliotajiwa jina la Mwenyezi Mungu miongoni mwa mifugo na wanyama wengineo walio halali, na waitakidi uhalali wake, na wala wasifanye kama wanavyofanya watu wa zama za Ujinga kwa kuharamisha mengi ya halali kwa kuzua hilo wao wenyewe, na kwa sababu ya kupotoshwa na mashetani wao. Kwa hivyo mwenyezi Mungu akataja kuwa alama ya Muumini ni kuwahalifu watu wa zama za Ujinga katika ada hii inayoshutumiwa, inayojumuisha kubadilisha sheria ya Mwenyezi Mungu, na kwamba ni kitu gani kinachowazuia kula katika kile kilichotajiwa jina la mwenyezi Mungu, na tayari Mwenyezi Mungu alikwisha waelezea kwa kina waja wake vile alivyowaharimishia, na akavibainisha, na akaviweka wazi. Kwa hivyo hakuna tatizo lolote wala shaka yoyote iliyobaki ndani yake inayomtaka mtu ajizuie kula baadhi ya vilivyo halali kwa kuhofia kuingia katika haramu. Na Aya hii tukufu iliashiria kwamba kanuni ya msingi katika vitu na vyakula ni kwamba vinaruhusiwa, na kwamba ikiwa sheria haijaleta uharamisho wa kitu katika hivyo, basi vinabakia kuwa vinaruhusiwa. Kwa hivyo vile ambavyo Mwenyezi Mungu alivinyamazia, basi hivyo vinaruhusiwa. Kwa sababu haramu Mwenyezi Mungu amekwisha ieleza kwa kina, na kile ambacho hakunieleza kwa kina, basi hicho si haramu. Lakini pamoja na hayo, haramu ambayo Mwenyezi Mungu aliieleza kwa kina na akaiweka wazi, aliiruhusu katika hali ya dharura, na shida kubwa, Kama alivyosema Yeye Mtukufu: "Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe..." mpaka aliposema; "Lakini aliyefikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Kisha akaonya juu ya wengi katika watu, akasema: "Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao." Yaani, kwa yale tu ambayo nafsi zao zinayatamani "bila ya kuwa na elimu," wala hoja. Basi mja ajihadhari na mfano wa hawa, , na alama zao ni kama Mwenyezi Mungu alivyowaelezea waja wake kuwahusu, kwamba wito wao haujengeki juu ya ushahidi wowote wala hawana hoja yoyote ya kisheria. Lakini wana fikira potofu kulingana na matamanio yao maovu, na maoni yao yenye upungufu. Basi hawa wameivuka sheria ya Mwenyezi Mungu na dhidi ya waja wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipaka. Tofauti na waongoao, waongofu. Wao wanalingania kwenye haki na uwongofu, na wanauunga mkono wito wao kwa hoja za kiakili na za kimaandiko, na wala hawafuati katika wito wao isipokuwa ridhaa ya Mola wao Mlezi na kujiweka karibu naye.
: 120 #
{وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ (120)}
120. Na acheni dhambi iliyo dhahiri na iliyofichikana yake. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
#
{120} المراد بالإثم: جميع المعاصي التي تؤثم العبدَ؛ أي: توقعه في الإثم والحَرَج من الأشياء المتعلِّقة بحقوق الله وحقوق عباده، فنهى الله عبادَهُ عن اقتراف الإثم الظاهر والباطن؛ أي: السر والعلانية المتعلِّقة بالبدن والجوارح والمتعلقة بالقلب، ولا يتمُّ للعبد ترك المعاصي الظاهرة والباطنة إلا بعد معرفتها والبحث عنها، فيكون البحث عنها ومعرفة معاصي القلب والبدن والعلم بذلك واجباً متعيناً على المكلَّف، وكثيرٌ من الناس تخفى عليه كثيرٌ من المعاصي، خصوصاً معاصي القلب؛ كالكبر والعجب والرياء ... ونحو ذلك حتى إنّه يكون به كثيرٌ منها وهو لا يحسُّ به ولا يشعر، وهذا من الإعراض عن العلم وعدم البصيرة. ثم أخبر تعالى أن الذين يكسبون الإثم الظاهر والباطن سيُجْزَون على حسب كسبهم وعلى قدر ذنوبهم قلَّت أو كثرت، وهذا الجزاء يكون في الآخرة، وقد يكون في الدُّنيا؛ يعاقَب العبد فيخفَّف عنه بذلك من سيئاته.
{120} Kinachomaanishwa na dhambi ni maasia yote ambayo yanamfanya mja kuwa na dhambi. Yaani, kuingia kwake katika dhambi na ubaya ni katika mambo yanayohusiana na haki za Mwenyezi Mungu, na haki za waja wake, basi Mwenyezi Mungu akawakataza waja wake kufanya dhambi ya dhahiri, na ile iliyofichika. Yaani, ya siri na ya wazi, zinazohusiana na mwili na viungo, na kuhusiana na moyo. Na wala mja hawezi kuacha kabisa maasia ya dhahiri na yaliyofichika isipokuwa baada ya kuyajua na kutafuta kuyajua. Kwa hivyo kunakuwa kutafuta kuyajua na kuyajua maasia ya moyo, na mwili, na kuyajua hayo ni wajibu kwa yule anayewajibishwa na sheria. Na wengi katika watu dhambi nyingi zimefichwa kwake, hasa dhambi za moyo, Kama vile kiburi, kujifahiri, na riyaa ... na mfano wa hayo, mpaka akawa na mengi katika hayo hali ya kuwa hahisi wala hatambui. Na hilo ni katika kuipa mgongo elimu na kutokuwa na utambuzi. Kisha Yeye Mtukufu akajulisha kwamba wale wanaochuma madhambi yaliyo dhahiri na yaliyofichika, watalipwa kulingana na kuchuma kwao, na kwa kiasi cha madhambi yao, yawe machache au mengi. Na malipo haya yatakuwa katika Akhera, na huenda yakawa katika dunia hii. Mja anaadhibiwa, kwa hivyo anahafifishiwa hilo katika mabaya yake.
: 121 #
{وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَى أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ (121)}
121. Wala msile katika vile ambavyo halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu juu yake. Kwani huko hakika ni kuvuka mipaka. Na kwa yakini mashetani wanawaletea wahyi marafiki zao ili wabishane nanyi. Na mkiwatii, basi nyinyi kwa hakika mtakuwa washirikina.
#
{121} ويدخل تحت هذا المنهي عنه ما ذُكِرَ عليه اسم غير الله؛ كالذي يُذبح للأصنام وآلهة المشركين ؛ فإنَّ هذا مما أُهلَّ لغير الله به المحرَّم بالنصِّ عليه خصوصاً. ويدخل في ذلك متروك التسمية مما ذبح لله كالضحايا والهدايا، أو للحم والأكل، إذا كان الذابح متعمِّداً ترك التسمية عند كثير من العلماء، ويخرج من هذا العموم الناسي بالنصوص الأخر الدالة على رفع الحرج عنه. ويدخل في هذه الآية ما مات بغير ذكاة من الميتات؛ فإنها مما لم يذكر اسم الله عليه، ونص الله عليها بخصوصها في قوله: {حُرِّمَتْ عليكم الميتةُ}، ولعلها سبب نزول الآية؛ لقوله: {وإنَّ الشياطينَ لَيوحون إلى أوليائهم ليجادِلوكم} بغير علم؛ فإن المشركين حين سمعوا تحريم الله ورسوله للميتة وتحليله للمذكاة، وكانوا يستحلون أكل الميتة قالوا معاندة لله ورسوله ومجادلة بغير حجة ولا برهان: أتأكلونَ ما قتلتُم ولا تأكلون ما قَتَلَ الله يعنون بذلك الميتة؟! وهذا رأي فاسدٌ لا يستند على حجة ولا دليل، بل يستند إلى آرائهم الفاسدة التي لو كان الحق تبعاً لها لفسدت السماوات والأرض ومن فيهن؛ فتبًّا لمن قدَّم هذه العقول على شرع الله وأحكامه الموافقة للمصالح العامة والمنافع الخاصة. ولا يُستغرب هذا منهم؛ فإن هذه الآراء وأشباهها صادرة عن وحي أوليائهم من الشياطين الذين يريدون أن يُضِلُّوا الخلق عن دينهم ويدعوهم ليكونوا من أصحاب السعير. {وإنْ أطعتُموهم}: في شركهم وتحليلهم الحرام وتحريمهم الحلال، {إنَّكم لمشركونَ}؛ لأنكم اتَّخذتموهم أولياء من دون الله، ووافقتموهم على ما به فارقوا المسلمين؛ فلذلك كان طريقكم طريقهم. ودلت هذه الآية الكريمة على أن ما يقع في القلوب من الإلهامات والكشوف التي يكثر وقوعها عند الصوفية ونحوهم لا تدلُّ بمجرَّدها على أنها حقٌّ ولا تصدَّق حتى تعرض على كتاب الله وسنة رسوله؛ فإن شهدا لها بالقبول؛ قبلت، وإن ناقضتْهما؛ رُدَّتْ، وإن لم يعلم شيء من ذلك؛ توقف فيها ولم تصدَّق ولم تكذَّب؛ لأن الوحي والإلهام يكون من الرحمن ويكون من الشيطان؛ فلا بد من التمييز بينهما والفرقان، وبعدم التفريق بين الأمرين حصل من الغلط والضلال ما لا يحصيه إلا الله.
{121} Na inaingia katika katazo hili vile vilivyotajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kama vile kile kinachochinjwa kwa ajili ya masanamu, na miungu ya washirikina. Basi hayo ni katika vile vilivyochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, vilivyoharamishwa hasa kwa andiko la moja kwa moja. Na inaingia katika hilo vile ambavyo havikutajiwa Bismillah miongoni mwa vile vilivyochinjwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kama vile wanyama wa dhabihu na wale wanaopelekwa kama zawadi Makka, au kwa ajili ya nyama na chakula, ikiwa mchinjaji alikusudia kuacha kusema Bismillah kulingana na wengi wa wanachuoni. Na inatoka katika huu ujumla, aliyesahau kulingana na maandiko mengine yanayoonyesha kuondolewa kwa ugumu juu ya yake. Na inaingia katika Aya hii wale waliokufa bila kuchinjwa kisheria miongoni mwa wanyamafu. Hao ni miongoni mwa vile ambavyo jina la Mwenyezi Mungu halikutajwa juu yake. Na Mwenyezi Mungu aliwataja hawa hasa katika kauli yake: "Mmeharamishiwa mnyamafu," na huenda ikawa hii ndiyo sababu ya kuteremshwa kwa Aya hii. Kwa sababu ya kauli yake: "Na kwa yakini mashetani wanawaletea wahyi marafiki zao ili wabishane nanyi" bila ya elimu. Kwa maana, Washirikina walipomsikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakiharamisha wanyamafu, na kuhalalisha kwake wanyama waliochinjwa kisheria, na walikuwa wakihalalisha kula nyamafu, wakasema kwa kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kubishana bila ya hoja wala ushahidi: “Je, mnakula wale mliowaua nyinyi, wala hamli wale aliowaua Mwenyezi Mungu?” Wakimaanisha kwa hilo nyamafu! Na haya ni maoni potovu ambayo hayaegemei juu ya hoja yoyote wala ushahidi, bali yanaegemea juu ya rai zao potovu, ambazo lau kuwa haki ingekuwa inaegemea juu yake, basi zingeharibika mbingu na ardhi na kila kilichomo ndani yake. Basi ameangamia mwenye kutanguliza akili hizi mbele ya sheria ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake zinazoafikiana na masilahi ya ujumla na manufaa mahususi. Lakini hili halishangazi kutoka kwao. Kwa maana Maoni haya na yanayofanana na hayo yanatokana na wahyi wa marafiki walinzi wao miongoni mwa mashetani ambao wanataka kuwapoteza viumbe kutoka katika dini yao, na kuwaita ili wawe miongoni mwa watu wa Motoni. "Na mkiwatii" katika ushirikina wao na kuhalalisha kwao haramu na kuharamisha kwao halali, "basi nyinyi kwa hakika ni washirikina." Kwa sababu nyinyi mliwafanya wao kuwa marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na mkaafikiana nao katika yale waliyojitenga na Waislamu kwayo. Na kwa sababu hiyo ikawa njia yenu ndiyo njia yao. Na Aya hii tukufu iliashiria kwamba yale yanayoingia katika nyoyo miongoni mwa wahyi na kuona mambo ambayo hutokea mara kwa mara miongoni mwa Masufi na mfano wao, hayaonyeshi yenyewe tu kuwa hayo ndiyo haki wala hayasadikiwi mpaka yaletwe mbele ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake. Na ikiwa vitayashuhudia kuwa yanakubaliwa, yanakubalika. Na ikiwa vitapingana nayo, basi yatakataliwa. Na kama hakuna chochote kinachojulikana kuhusiana nayo, basi itasimamwa katika hayo, kwa hivyo hayataaminiwa wala kukadhibishwa. Kwa sababu wahyi na kuonyeshwa mambo yanakuwa kutoka kwa Mwingi wa Rehema na vinatoka kwa Shetani. Basi Ni lazima kutofautisha baina yao na kupambanua. Na kwa sababu ya kutotofautisha kati ya mambo mawili haya kulitokea mchanganyiko na upotovu ambayo hawezi kuyahesabu isipokuwa Mwenyezi Mungu.
: 122 - 124 #
{أَوَمَنْ كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَنْ مَثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِنْهَا كَذَلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (122) وَكَذَلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنْفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ (123) وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَنْ نُؤْمِنَ حَتَّى نُؤْتَى مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّهِ اللَّهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ (124)}
122. Je, yule aliyekuwa maiti, kisha tukamhuisha, na tukamfanyia nuru akatembea kwayo katika watu, ni kama yule ambaye mfano wake yuko katika giza mbalimbali, sio wa kutoka humo? Kama hivyo ndivyo makafiri walivyopambiwa yale waliyokuwa wakiyafanya. 123. Na namna hivi tumeweka katika kila mji wakubwa wa wahalifu ili wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipokuwa nafsi zao ilhali hawatambui. 124. Na inapowajia Ishara, wao husema: Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia wale waliofanya uhalifu udhalili kwa Mwenyezi Mungu, na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.
#
{122} يقول تعالى: {أوَمَن كان}: من قبل هداية الله له {مَيْتاً}: في ظلمات الكفر والجهل والمعاصي، {فأحييناهُ}: بنور العلم والإيمان والطاعة، فصار يمشي بين الناس في النور، متبصراً في أموره، مهتدياً لسبيله، عارفاً للخير، مؤثراً له، مجتهداً في تنفيذه في نفسه وغيره، عارفاً بالشر، مبغضاً له، مجتهداً في تركه وإزالته عن نفسه وعن غيره، أفيستوي هذا بمن هو في الظلمات؟ ظلمات الجهل والغي والكفر والمعاصي، {ليس بخارج منها}، قد التبستْ عليه الطرق، وأظلمت عليه المسالكُ، فحضره الهمُّ والغمُّ والحزن والشقاء، فنبه تعالى العقولَ بما تدركه وتعرفه أنه لا يستوي هذا ولا هذا كما لا يستوي الليل والنهار والضياء والظلمة والأحياء والأموات، فكأنه قيل: فكيف يؤثِرُ مَن له أدنى مُسْكةٍ من عقل أن يكون بهذه الحالة وأن يبقى في الظلمات متحيراً؟! فأجاب بأنه {زُيِّنَ للكافرين ما كانوا يعملونَ}، فلم يزل الشيطانُ يحسِّنُ لهم أعمالهم ويزيِّنُها في قلوبهم حتى استحسنوها ورأوها حقًّا وصار ذلك عقيدةً في قلوبهم وصفةً راسخةً ملازمةً لهم؛ فلذلك رضوا بما هم عليه من الشرِّ والقبائح.
{122} Yeye Mtukufu Anasema: "Je, yule aliyekuwa" kabla ya Mwenyezi Mungu kumuongoa "maiti" katika giza mbalimbali ya ukafiri, na ujinga, na maasia, "kisha tukamhuisha" kwa nuru ya elimu, na imani, na utiifu. Kwa hivyo akawa anatembea miongoni mwa watu katika nuru, akiwa na utambuzi katika mambo yake, akiwa ameongoka kwenye njia yake, akiwa anajua heri, huku akiipendelea, akijitahidi katika kuitekeleza yeye mwenyewe na kwa wengine, huku akiujua uovu, akawa anauchukia, na anajitahidi katika kuuacha, na kuuondoa kutoka kwa nafsi yake mwenyewe na kutoka kwa wengine. Je, huyu ni sawa na yule aliye katika giza mbalimbali? Giza la ujinga, na upotovu, na ukafiri, na maasia, "sio wa kutoka humo," tayari njia zimemchanganyikia, na mahali pa kupitia pamemuwiya giza. Kwa hivyo akapatwa na wasiwasi mkubwa, na masikitiko, na huzuni na mashaka. Basi Yeye Mtukufu akazitanabahisha akili kwa yale zinayoyatambua, na kuyajua kwamba haya na haya hayawi sawa. Kama vile usiku na mchana haviwi sawa, na mwangaza na giza, na walio hai na wafu hawawi sawa. Na ni kama ilisemwa: Vipi atapendelea yule ambaye ana akili kidogo tu katika hali hii na kwamba abaki katika giza mbalimbali akiwa amechanganyikiwa? Kwa hivyo Akajibu: “makafiri wamepambiwa yale waliyokuwa wakiyafanya” kwa hivyo Shetani hakuacha kuwafanyia matendo yao kuonekena kuwa mazuri na kuwapambia hayo katika nyoyo zao mpaka wakayaona kuwa ni mazuri na wakayaona kuwa ndiyo haki. Na hayo yakawa ndiyo itikadi katika mioyo yao, na sifa madhubuti, yenye kutoachana nao. Kwa hivyo, waliridhika na yale waliyo juu yake ya uovu na mabaya.
#
{123} وهؤلاء الذين في الظلمات يعمهون وفي باطلهم يتردَّدون غير متساوين؛ فمنهم القادةُ والرؤساء والمتبوعون، ومنهم التابعون المرؤوسون، والأولون منهم الذين فازوا بأشقى الأحوال، ولهذا قال: {وكذلك جَعَلْنا في كلِّ قريةٍ أكابرَ مجرِميها}؛ أي: الرؤساء الذين قد كبر جرمهم واشتدَّ طغيانهم؛ {ليمكُروا فيها}: بالخديعة والدعوة إلى سبيل الشيطان ومحاربة الرسل وأتباعهم بالقول والفعل، وإنما مكرهم وكيدهم يعود على أنفسهم؛ لأنهم يمكُرون ويمكُر الله والله خير الماكرين. وكذلك يجعل الله كبار أئمة الهدى وأفاضلهم يناضلون هؤلاء المجرمين ويردُّون عليهم أقوالهم، ويجاهدونهم في سبيل الله، ويسلكون بذلك السُّبُل الموصلة إلى ذلك، ويعينهم الله، ويسدِّد رأيهم، ويثبِّت أقدامهم، ويداوِلُ الأيام بينَهم وبين أعدائهم حتى يَدولَ الأمر في عاقبته بنصرِهِم وظهورِهم. والعاقبة للمتقين.
{123} Na hawa ndio ambao wanatangantanga katika giza mbalimbali, na katika batili yao wanasitasita, na wala hawatoshani wote. Miongoni mwao wamo viongozi, na maraisi na wale wanaofuatwa, na miongoni mwao wapo wafuasi walio chini ya uongozi wao. Na wale wa kwanza miongoni mwao ndio wale walijishindia hali mbaya sana. Na kwa sababu hiyo akasema: "Na namna hivi tumeweka katika kila mji wakubwa wa wahalifu wake;" yaani viongozi ambao uhalifu wao umeshakuwa mkubwa, na upotofu wao ukawa mkali, "ili wafanye vitimbi ndani yake," kwa hadaa na kulingania kwenye njia ya Shetani na kupigana na Mitume na wafuasi wao kwa kauli na vitendo. Lakini vitimbi vyao na hila zao zinawarudia wao wenyewe, kwa sababu wanafanya vitimbi na Mwenyezi Mungu anafanya vitimbi, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora zaidi wa wapangao vitimbi. Na kadhalika Mwenyezi Mungu huwafanya maimamu wakubwa wa uongofu na walio bora wao wapigane na wahalifu hawa na kuyakanusha maneno yao. Na wanapigana vita dhidi yao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wafuata kwa sababu ya hilo njia zinazowafikisha katika hilo, na Mwenyezi Mungu anawasaidia; na anaweka sawasawa rai yao, na anaiimarisha miguu yao, na anabadilisha siku baina za ushindi kati yao na maadui zao mpaka ilibadilishe jambo hili katika mwisho wake kwa kuwapa ushindi na kuwa kwao juu. Na mwisho mwema ni wa wachamungu.
#
{124} وإنما ثبتَ أكابر المجرمين على باطلهم، وقاموا بردِّ الحقِّ الذي جاءت به الرسل، حسداً منهم وبغياً، فقالوا: {لن نؤمنَ حتَّى نُؤتى مثلَ ما أوتي رسلُ الله}: من النبوة والرسالة، وفي هذا اعتراض منهم على الله، وعجبٌ بأنفسهم، وتكبُّرٌ على الحقِّ الذي أنزله على أيدي رسله، وتحجُّرٌ على فضل الله وإحسانه، فردَّ الله عليهم اعتراضهم الفاسد، وأخبر أنهم لا يصلحون للخير، ولا فيهم ما يوجِبُ أن يكونوا من عبادِ الله الصالحين، فضلاً أن يكونوا من النبيين والمرسلين، فقال: {الله أعلم حيثُ يجعلُ رسالَتَه}؛ فمَنْ عَلِمَهُ يَصْلُحُ لها ويقوم بأعبائها وهو متَّصفٌ بكلِّ خلق جميل ومتبرئ من كل خلق دنيء، أعطاه الله ما تقتضيه حكمتُه أصلاً وتبعاً، ومَن لم يكن كذلك؛ لم يضع أفضل مواهبه عند من لا يستأهله ولا يزكو عنده. وفي هذه الآية دليل على كمال حكمة الله تعالى: لأنَّه وإن كان تعالى رحيماً واسع الجود كثير الإحسان؛ فإنه حكيمٌ لا يضع جوده إلا عند أهله. ثم توعَّد المجرمين، فقال: {سيصيبُ الذين أجرموا صَغارٌ عند الله}؛ أي: إهانةٌ وذُلٌّ؛ كما تكبَّروا على الحقِّ؛ أذلَّهم الله، {وعذابٌ شديدٌ بما كانوا يمكُرون}؛ أي: بسبب مكرِهم لا ظلماً منه تعالى.
{124} Lakini wahalifu wakubwa walibakia katika batili yao, na wakaikanusha haki ambayo walikuja nayo Mitume kwa ajili ya husuda yao na uadui. Kwa hivyo wakasema: "Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu" miongoni mwa unabii na utume. Na katika hayo kuna upinzani wao dhidi ya Mwenyezi Mungu, na kujiona, na kuifanyia kiburi haki ambayo aliiteremsha juu ya mikono ya mitume wake, na kujizuia fadhila ya Mwenyezi Mungu na ukarimu wake. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawajibu pingamizi lao potovu, na akajulisha kuwa hawaifailii heri, wala hawana ndani yao chenye kufanya wawe miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, achilia mbali kwamba wawe miongoni mwa Manabii na Mitume. Ndiyo akasema: "Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anauweka ujumbe wake." Kwa hivyo Yeyote yule anayemjua kuwa anafaa kwa hilo, na atatekeleza majukumu yake, huku akiwa anasifika na kila tabia nzuri, anayejiweka mbali na kila tabia mbaya, basi Mwenyezi Mungu atampa kile ambacho hekima yake inakihitaji katika asili na matokeo yake. Na asiyekuwa hivyo, hataweka tunu zake bora zaidi kwa yule ambaye hazistahili na si mtakatifu kwake. Na katika Aya hii kuna ushahidi wa ukamilifu wa hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa sababu, hata ikiwa Yeye Mtukufu ni Mwenye kurehemu, na Mwenye kupeana kwa wingi, mwingi wa ihsani, basi yeye hakika ni mwenye hekima kubwa, na haweki ukarimu wake isipokuwa kwa anayeustahili. Kisha akaahidi wahalifu adhabu, akisema: “Itawafikia wale waliofanya uhalifu udhalili kwa Mwenyezi Mungu.” Yaani, kudunishwa na udhalilifu. Kama vile walivyoifanyia haki kiburi, basi Mwenyezi Mungu aliwadhalilisha "na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya." Yaani, kwa sababu vitimbi vyao, si kwa sababu ya Yeye Mtukufu kuwadhulumu.
: 125 #
{فَمَنْ يُرِدِ اللَّهُ أَنْ يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ وَمَنْ يُرِدْ أَنْ يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ كَذَلِكَ يَجْعَلُ اللَّهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ (125)}
125. Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumuongoa, humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule anayetaka kumpoteza, hukifanya kifua chake kuwa kifinyu, kimebana, kama kwamba anapanda katika mbingu. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anaweka uchafu juu ya wale wasioamini.
#
{125} يقول تعالى مبيِّناً لعبادِهِ علامة سعادة العبد وهدايته وعلامة شقاوته وضلاله: إنَّ مَن انشرح صدره للإسلام؛ أي: اتسع وانفسح فاستنار بنور الإيمان وحيي بضوء اليقين فاطمأنت بذلك نفسه وأحبَّ الخير وطوَّعت له نفسُهُ فعلَه متلذذاً به غير مستثقل؛ فإن هذا علامة على أن اللهَ قد هداه ومنَّ عليه بالتوفيق وسلوك أقوم الطريق، وأنَّ علامة من يُرِدِ اللهُ {أن يُضِلَّه}: أنه {يجعلْ صدرَه ضيِّقاً حَرَجاً}؛ أي: في غاية الضيق عن الإيمان والعلم واليقين، قد انغمس قلبُهُ في الشبهات والشهوات، فلا يصل إليه خير، لا ينشرحُ قلبه لفعل الخير. كأنه من ضيقه وشدَّته يكاد {يَصَّعَّدُ في السماء}؛ أي: كأنه يكلَّف الصعود إلى السماء الذي لا حيلة فيه، وهذا سببه عدم إيمانهم؛ هو الذي أوجب أن يجعل الله الرجس عليهم؛ لأنهم سدُّوا على أنفسهم باب الرحمة والإحسان، وهذا ميزان لا يعول وطريق لا يتغير؛ فإنَّ مَن أعطى واتَّقى وصدَّق بالحسنى؛ ييسِّره الله لليسرى، ومن بخل واستغنى وكذب بالحسنى؛ فسيُيَسِّره للعسرى.
{125} Yeye Mtukufu anasema akiwabainishia waja wake alama ya furaha ya mja, na uongofu wake; na alama ya mshaka yake, na upotevu wake: Hakika yule ambaye kifua chake kuliufungukia Uislamu. Yaani, kunapanuka na kuwa na nafasi, kwa hivyo kikaangazwa na nuru ya imani, na kikahuishwa na mwangaza wa yakini. Kwa hivyo nafsi yake ikatulia kwa hilo, na akapenda heri, na nafsi yake ikatii ili afanye mema, akawa anapata ladha katika hilo, bila ya kuona uzito ndani yake. Basi hii ni alama ishara Mwenyezi Mungu amemuongoa na akamneemesha kwa kumwezesha kutenda mema, na kufuata njia iliyonyooka kabisa. Na kwamba alama ya yule ambaye mwenyezi Mungu anataka “kumpotosha” ni kwamba “hukifanya kifua chake kuwa kifinyu, kimebana.” Yaani, kinakuwa kifinyu mno katika kuwa na imani na elimu na yakini. Tayari moyo wake umezama ndani ya fikira potofu, na matamanio, basi hakuna kheri inayoufikia, wala haufunguki moyo wake kufanya heri. Kana kwamba kutokana na ufinyu wake na ugumu wake, unakaribia " anapanda katika mbingu." Yaani, ni kana kwamba ameelemewa na kupanda mbinguni ambako hakuna msaada wowote. Na hili ni kwa sababu ya kutoamini kwao;na hilo ndilo lililomfanya Mwenyezi Mungu kuwawekea uchafu juu yao. Kwa sababu walijifungia wenyewe mlango wa rehema na ihsani, na hii ndiyo mizani isiyopunja na njia isiyobadilika. Kwani mwenye kutoa, na akamcha Mwenyezi Mungu, na akasadiki yaliyo mema zaidi, Mwenyezi Mungu atamsahilishia yawe mepesi. Na ama mwenye kufanya ubahili na mwenye kujiona anajitosheleza, na akayakadhibisha yaliyo mema zaidi, basi atamrahisishia yawe magumu.
: 126 - 127 #
{وَهَذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ (126) لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَهُوَ وَلِيُّهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (127)}.
126. Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi iliyonyooka. Tumeshazieleza Aya kwa kina kwa kaumu wanaokumbuka. 127. Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
#
{126} أي: معتدلاً موصلاً إلى الله وإلى دار كرامتِهِ، قد بُيِّنَتْ أحكامُه، وفصِّلت شرائعه، وميز الخير من الشر. ولكن هذا التفصيل والبيان ليس لكل أحد، إنما هو {لقومٍ يَذَّكَّرونَ}؛ فإنهم الذين علموا فانتفعوا بعلمهم، وأعد الله لهم الجزاء الجزيل والأجر الجميل.
{126} Yaani, ya wastani inayofikisha kwa mwenyezi Mungu, na kwa Nyumba Yake ya utukufu; kwani hukumu zake zimeshabainishwa, sheria zake zimeshaelezwa kwa kina, na heri ikatofautishwa na uovu. Lakini kueleza huku kwa kina na kubainisha huku si wa kila mmoja, bali ni kwa "kaumu wanaokumbuka." Kwa maana, wao ndio waliojua na wakafaidika na elimu yao, na Mwenyezi Mungu amewaandalia malipo makubwa na ujira mazuri.
#
{127} فلهذا قال: {لهم دارُ السلام عند ربِّهم}، وسميت الجنة دار السلام لسلامتها من كل عيب وآفة وكَدَرٍ وهمٍّ وغمٍّ وغير ذلك من المنغِّصات، ويلزم من ذلك أن يكون نعيمُها في غاية الكمال ونهاية التمام؛ بحيث لا يقدر على وصفه الواصفون، ولا يتمنَّى فوقه المتمنون؛ من نعيم الروح والقلب والبدن، ولهم فيها ما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعين وهم فيها خالدون. {وهو وَليُّهم}: الذي تولَّى تدبيرهم وتربيتهم، ولطفَ بهم في جميع أمورهم، وأعانهم على طاعتِهِ، ويسَّر لهم كل سبب موصل إلى محبَّته، وإنما تولاَّهم بسبب أعمالهم الصالحة ومقدِّماتهم التي قصدوا بها رضا مولاهم؛ بخلاف مَن أعرض عن مولاه، واتَّبع هواه؛ فإنه سلَّطَ عليه الشيطان، فتولاَّه، فأفسد عليه دينَه ودُنياه.
127. Na ndiyo maana akasema, "Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao." Na Pepo iliitwa nyumba ya amani kwa sababu ya usalama wake kutokana na kila dosari, na maradhi, na machafu, na wasiwasi, dhiki na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale yanayokera. Na inalazimu kutokana na hilo kwamba furaha yake ni kamilifu sana na timilifu zaidi, kiasi kwamba hawawezi kuieleza wenye kueleza, na wala wenye kutamani hawatamani zaidi yake, miongoni mwa raha ya nafsi, na moyo na mwili. Na watakuwa ndani yake na yale yanayotamaniwa na nafsi na yale yanayopendeza macho, nao watadumu humo. "Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao" ambaye amesimamia kuwaendesha, na kuwalea, na akawafanyia upole katika mambo yao yote, na akawasaidia katika kumtii Yeye, na akawasahilishia kila sababu inayofikisha kwenye mapenzi yake. Na aliwasimamia kwa sababu ya matendo yao mema na yale waliyotanguliza walikusudia kwayo ridhaa ya Mola wao Mlezi. Tofauti na yule aliyempa mgongo Mola wake Mlezi na akafuata matamanio yake, basi huyo alipewa Shetani mamlaka juu yake, kwa hivyo akamsimamia, na akamharibia dini yake na dunia yake.
: 128 - 135 #
{وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَامَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُمْ مِنَ الْإِنْسِ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُمْ مِنَ الْإِنْسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ (128) وَكَذَلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ (129) يَامَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِنْكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنْذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَذَا قَالُوا شَهِدْنَا عَلَى أَنْفُسِنَا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ (130) ذَلِكَ أَنْ لَمْ يَكُنْ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَى بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ (131) وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِمَّا عَمِلُوا وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ (132) وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ إِنْ يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِنْ بَعْدِكُمْ مَا يَشَاءُ كَمَا أَنْشَأَكُمْ مِنْ ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ (133) إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ وَمَا أَنْتُمْ بِمُعْجِزِينَ (134) قُلْ يَاقَوْمِ اعْمَلُوا عَلَى مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَنْ تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ (135)}.
128. Na ile Siku atakapowakusanya wote, “Enyi kundi la majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu.” Na marafiki zao katika wanadamu watasema: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana baadhi yetu kwa wenzi wetu, na tumefikia muda wetu uliotuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndiyo makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua zaidi. 129. Na namna hivi ndivyo tunavyowafanya baadhi ya madhalimu wapendane wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma. 130. Enyi kundi la majini na watu! Je, hawakuwajia Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakiwabainishia Aya zangu, na wakiwasimulia kukutana na Siku yenu hii? Nao watasema, “Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu.” Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri. 131. Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa ni wa kuiangamiza miji kwa dhuluma, hali ya kuwa wenyewe wameghafilika. 132. Na kila mmoja ana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda. 133. Na Mola wako Mlezi ndiye Asiyemhitaji yeyote, Mwenye rehema. Akitaka, atawaondoa na awaweke nyuma yenu wengine awatakao, kama vile alivyowatoa kutokana na dhuria ya kaumu wengine. 134. Hakika, yale mnayoahidiwa yatafika, wala nyinyi hamtaweza kushinda. 135. Sema: Enyi kaumu yangu! Fanyeni pahali penu mlipo, na hakika mimi ninafanya. Mtakuja jua ni ya nani yatakuwa makaazi mema mwishoni. Hakika, madhalimu hawafaulu.
#
{128} يقول تعالى: {ويوم يحشُرُهم جميعاً}؛ أي: جميع الثقلين من الإنس والجن، مَنْ ضلَّ منهم ومَنْ أضلَّ غيره، فيقول موبخاً للجنِّ الذين أضلُّوا الإنس وزيَّنوا لهم الشرَّ وأزُّوهم إلى المعاصي: {يا معشر الجنِّ قد استكثرتُم من الإنس}؛ أي: من إضلالهم وصدِّهم عن سبيل الله؛ فكيف أقدمتم على محارمي، وتجرَّأتم على معاندة رسلي، وقمتم محاربين لله، ساعين في صدِّ عباد الله عن سبيله إلى سبيل الجحيم؟! فاليوم حقَّت عليكم لعنتي، ووجبت لكم نقمتي، وسنزيدكم من العذاب بحسب كفرِكُم وإضلالكم لغيرِكم، وليس لكم عذرٌ به تعتذِرون، ولا ملجأ إليه تلجؤون، ولا شافع يشفع، ولا دعاء يُسمع! فلا تسأل حينئذٍ عما يحل بهم من النَّكال والخِزْي والوَبال، ولهذا لم يذكِر الله لهم اعتذاراً، وأما أولياؤهم من الإنس؛ فأبدوا عذراً غير مقبول، فقالوا: {ربَّنا استمتعَ بعضُنا ببعض}؛ أي: تمتَّع كلٌّ من الجني والإنسي بصاحبه وانتفع به؛ فالجنيُّ يستمتع بطاعة الإنسيِّ له وعبادته وتعظيمه واستعاذته به، والإنسيُّ يستمتع بنيل أغراضه وبلوغه بحسب خدمة الجنيِّ له بعض شهواته؛ فإن الإنسيَّ يعبُدُ الجنيَّ فيخدمُهُ الجنيُّ ويحصِّلُ له بعض الحوائج الدنيويَّة؛ أي: حصل منا من الذنوب ما حصل، ولا يمكن ردُّ ذلك. {وبَلَغْنا أجَلَنا الذي أجَّلْتَ لنا}؛ أي: وقد وصلنا المحل الذي تُجازي فيه بالأعمال؛ فافعل بنا الآن ما تشاء، واحكم فينا بما تريدُ، قد انقطعت حُجَّتُنا، ولم يبق لنا عذرٌ، والأمر أمرُك والحكم حكمُك، وكأَن في هذا الكلام منهم نوع تضرُّع وترقُّق، ولكن في غير أوانه، ولهذا حكم فيهم بحكمه العادل، الذي لا جَوْر فيه، فقال: {النارُ مَثْواكم خالدين فيها}، ولما كان هذا الحكم من مقتضى حكمتِهِ وعلمِهِ؛ ختم الآية بقوله: {إنَّ ربَّك حكيمٌ عليمٌ}؛ فكما أن علمه وسع الأشياء كلَّها وعمَّها؛ فحكمتُهُ الغائيةُ شملت الأشياء، وعمَّتها، ووسعتها.
{128} Yeye Mtukufu Anasema, "Na ile Siku atakapowakusanya wote;" yaani, wazito wawili wote miongoni mwa wanadamu na majini, aliyepotea miongoni mwao na aliyempoteza mwingineye. Basi anasema akiwakemea majini waliowapoteza watu na wakawapambia uovu, na wakawaingiza katika maasia: "Enyi kundi la majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu." Yaani, katika kuwapoteza na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Basi vipi mliyajia maharamisho yangu, mkafanya ujasiri katika kuwapinga mitume wangu, na mkasimama kumpiga vita Mwenyezi Mungu, mkifanya juhudi katika kuwazuia waja wa Mwenyezi Mungu kutoka kwenye njia yake hadi kwenye njia ya Jahiim? Basi leo hii laana yangu imewekwa juu yenu, na adhabu yangu imekuwa wajibu juu yenu, na tutawazidishia adhabu kulingana na kiasi cha ukafiri wenu na kupoteza kwenu wengine. Na hamna udhuru wowote kuuwasilisha, wala kimbilio mtakalokimbilia huko, wala mwombezi wa kuwaombea, wala dua itakayosikilizwa! Basi hapo usiulize juu ya yale yatakayowapata miongoni mwa adhabu na hizaya na mateso. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu hakutaja udhuru wowote kuwahusu. Na marafiki wasaidizi wao miongoni mwa watu, wao walitoa udhuru usiokubalika, na wakasema: "Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana baadhi yetu kwa wenzi wetu." Yaani, kila mmoja katika Majini na wanadamu alimfurahisha mwenzake na akanufaika naye. Jini alifurahia utiifu wa mwanadamu kwake, kwa kumwabudu, na kumtukuza, na kutafuta hifadhi kwake. Naye mwanadamu alifurahia kwa kupata malengo yake na kuyafikia kulingana na jini kumtumikia katika baadhi ya matamanio yake. Mwanadamu anaabudu jini, basi jini humtumikia na kumtimizia baadhi ya mahitaji ya kidunia. Yaani, tulifanya dhambi zilizotokea, na wala haziwezekani kuzitendua. "Na tumefikia muda wetu uliotuwekea;" yaani, tumefika mahali ambapo unalipia kwa matendo. Basi tufanyie sasa unavyotaka, na utuhukumu kwa utakalo, tayari hoja zetu zimekwisha katika, na hatuna udhuru wowote, na jambo ni jambo lako, na hukumu ni hukumu yako. Na ni kana kwamba katika maneno haya kuna aina fulani ya kunyenyekea upole, lakini kwa wakati usiokuwa wakati wake, na ndiyo maana akawahukumu kwa hukumu yake ya uadilifu isiyokuwa na dhulma. Akasema, "Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo." Na kwa kuwa hukumu hii ilitokana na matakwa ya hekima yake na elimu yake, Akahitimisha Aya hii kwa kauli yake: "Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua zaidi." Basi kama vile elimu yake ilienea kila kitu na kuvijumuisha, hekima yake isiyokuwa na kikomo imejumuisha mambo yote, na kuyaenea.
#
{129} {وكذلك نُوَلِّي بعضَ الظالمين بعضاً بما كانوا يكسِبون}؛ أي: وكما ولَّيْنا الجنَّ المردة وسلَّطْناهم على إضلال أوليائهم من الإنس وعقَدْنا بينهم عقد الموالاة والموافقة بسبب كسبِهم وسعيهم بذلك؛ كذلك من سنَّتنا أن نولِّي كلَّ ظالم ظالماً مثلَه يؤزُّه إلى الشرِّ ويحثُّه عليه ويزهِّده في الخير وينفِّره عنه، وذلك من عقوبات الله العظيمة الشنيع أثرها البليغ خطرها، والذنب ذنبُ الظالم؛ فهو الذي أدخل الضرر على نفسه وعلى نفسه جنى، وما ربك بظلاَّم للعبيد. ومن ذلك أنَّ العباد إذا كَثُرَ ظلمُهم وفسادُهم ومنعُهم الحقوق الواجبة؛ وُلِّي عليهم ظلمةٌ يسومونهم سوء العذاب، ويأخذون منهم بالظُّلم والجَوْر أضعاف ما منعوا من حقوق الله وحقوق عباده على وجه غير مأجورين فيه ولا محتسبين؛ كما أن العباد إذا صلحوا واستقاموا؛ أصلح الله رعاتهم، وجعلهم أئمة عدل وإنصاف، لا ولاة ظلم واعتساف.
{129} "Na namna hivi ndivyo tunavyowafanya baadhi ya madhalimu wapendane wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma." Yaani, kama vile tulivyofanya urafiki katika majini waasi na tukawapa mamlaka juu ya kuwapoteza marafiki zao miongoni mwa wanadamu, na tukafunga baina yao mkataba wa mapatano na kuafikiana kwa sababu ya kuchuma kwao na juhudi zao kufanya hivyo. Na vile vile katika Sunnah zetu ni kufanya urafiki kati ya kila dhalimu na dhalimu mwingine mfano wake anayemsukuma kufanya maovu, na anamhimiza kufanya hivyo, na kumkatisha tamaa ya kujiepusha na kheri, na kumtengenisha nayo. Na hii ni miongoni mwa adhabu za Mwenyezi Mungu zenye athari mbaya, zenye hatari kubwa. Na dhambi hizi ni dhambi za dhalimu huyo kwa maana Yeye ndiye aliyejiingizia madhara katika nafsi yake na akajifanyia makosa, na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake. Na katika hayo ni kwamba waja ikiwa dhuluma yao itakithiri, na uharibifu wao, na kuzuia kwao haki za wajibu, wanawekwa chini ya madhalimu wanaowatia adhabu kali, na wanachukua kutoka kwao kwa dhuluma na ukandamizaji mara nyingi zaidi ya mali walizozuia katika haki za Mwenyezi Mungu na waja wake kwa njia ambayo hawalipwi wala hawatafuti malipo kwa Mwenyezi Mungu. Vivyo hivyo ikiwa waja watatengenea na wakanyooka, basi Mwenyezi Mungu atawafanya viongozi wao kutengenea, na atawafanya kuwa maimamu waadilifu na wasiodhulumu, sio watawala madhalimu na wanyanyasaji.
#
{130} ثم وبَّخ الله جميع من أعرض عن الحق وردَّه من الجنِّ والإنس، وبيَّن خطأهم، فاعترفوا بذلك، فقال: {يا مَعْشَرَ الجنِّ والإنسِ ألم يأتِكُم رسلٌ منكم يقصُّونَ عليكُم آياتي}: الواضحات البيِّنات التي فيها تفاصيل الأمر والنهي والخير والشرِّ والوعد والوعيد، {وينذِرونَكم لقاءَ يومِكم هذا}: ويعلِّمونكم أنَّ النجاةَ فيه والفوزَ إنَّما هو بامتثال أوامر الله واجتناب نواهيه، وأنَّ الشقاء والخسران في تضييع ذلك، فأقروا بذلك واعترفوا، فقالوا: بلى، {شَهِدْنا على أنفُسِنا وغرَّتْهُمُ الحياةُ الدُّنيا}: بزينتها وزُخرفها ونعيمها، فاطمأنوا بها ورضوا وألهتْهم عن الآخرةِ، {وشهِدوا على أنفسهم أنَّهم كانوا كافرين}: فقامت عليهم حجةُ الله، وعَلِمَ حينئذٍ كلُّ أحدٍ حتى هم بأنفسهم عدلَ الله فيهم، [فقال لهم حاكماً عليهم بالعذاب الأليم: ادخُلوا في جملة أمم قد خلت من قبلكم من الجنِّ والإنس؛ صنعوا كصنيعكم، واستمتعوا بخلاقهم كما استمتعتم، وخاضوا بالباطل كما خضتم؛ إنهم كانوا خاسرين؛ أي: الأولون من هؤلاء والآخرون، وأيُّ خسرانٍ أعظم من خسران جنات النعيم وحرمان جوار أكرم الأكرمين] ؟!
{130} Kisha Mwenyezi Mungu akawakemea wote wale walioipa mgongo haki na wakaikataa miongoni mwa majini na watu, na akabainisha makaosa yao, kwa hivyo wakakiri hilo. Akasema, "Enyi kundi la majini na watu! Je, hawakuwajia Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakiwabainishia Aya zangu," zilizo wazi na bainifu, ambazo ndani yake kuna maelezo ya kina ya maamrisho na makatazo, na heri na shari, na ahadi nzuri na ahadi ya adhabu; "Na wakiwasimulia kukutana na Siku yenu hii?" Na wanawafunza kuwa kunusurika ndani yake na kufuzu ni kwa kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake, na kwamba mashaka na hasara ni katika kuyapoteza hayo. Kwa hivyo, wakakiri hilo na wakakubali, na wakasema, "Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia;" kwa mapambo yake, na merembesho yake, na neema yake; kwa hivyo, wakatulia na kuridhika navyo, lakini vikawashughulisha na maisha ya akhera. "Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri." Basi hoja ya Mwenyezi Mungu ikasimama juu yao, na wakati huo kila mmoja wao akajua kwamba hata wao wenyewe uadilifu wa Mwenyezi Mungu juu yao. [Basi akawaambia kwa kuwahukumu kwa adhabu chungu: Ingieni katika kundi la umma uliopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu. Walifanya kama mliyoyafanya, na wakafurahia kwa fungu lao kama mlivyofurahia, na wakazama katika batili kama mlivyozama. Wao kwa hakika walikuwa wenye hasara. Yaani, wa mwanzo katika hawa na wa mwisho. Na ni hasara gani iliyo kubwa zaidi kuliko kuzipoteza bustani za neema na kunyimwa kuwa karibu na Mkarimu zaidi wa wakarimu?]
#
{132} ولكنَّهم وإن اشتركوا في الخسران؛ فإنهم يتفاوتون في مقداره تفاوتاً عظيماً، {ولكلٍّ}: منهم {درجات مما عملوا}: بحسب أعمالهم، لا يُجعل قليل الشرِّ منهم ككثيره، ولا التابع كالمتبوع، ولا المرؤوس كالرئيس؛ كما أن أهل الثواب والجنة وإن اشتركوا في الربح والفلاح ودخول الجنة؛ فإن بينهم من الفرق ما لا يعلمه إلا الله، مع أنهم كلهم [قد] رضوا بما آتاهم مولاهم وقنعوا بما حباهم، فنسأله تعالى أن يجعلَنا من أهل الفردوس الأعلى التي أعدَّها الله للمقربين من عباده والمصطَفَيْن من خلقه وأهل الصفوة من أهل وداده. {وما ربُّك بغافل عما يعملونَ} فيجازي كلًّا بحسب عمله، وبما يعلمه من مقصده.
{132} Lakini hata kama wanashiriki katika hasara, Wao hakika wanatofautiana katika kiasi chake kutofautiana kukubwa. "Na kila mmoja" wao "ana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda" kulingana na vitendo vyao, hachukuliwi wa ubaya mdogo miongoni mwao kama wa ubaya mwingi wao, wala mfuasi kama aliyefuatwa, wala anayeongozwa kama kiongozi. Kama vile wale wa thawabu na Pepo hata wakishirikiana katika faida, na kufaulu, na kuingia Peponi, lakini kati yao kuna tofauti ambayo haijui isipokuwa Mwenyezi Mungu tu, pamoja na kwamba wote walikwisha ridhia yale aliyowapa Mola wao na wakatosheka na yale aliyowapa bila ya malipo. Basi tunamuomba Mola Mtukufu atujaalie kuwa miongoni mwa wale watakaokuwa katika Firdaws ya juu kabisa, ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia wale walio karibu miongoni mwa waja Wake, na wale walioteuliwa miongoni mwa viumbe Wake, na wale wa juu zaidi miongoni mwa wale anaowapenda. "Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda." Basi atamlipa kila mmoja kulingana na matendo yake, na kwa yale anayoyajua katika makusudio yake.
#
{133} وإنما أمر الله العباد بالأعمال الصالحة ونهاهم عن الأعمال السيئة رحمةً بهم وقصداً لمصالحهم، وإلاَّ؛ فهو الغني بذاته عن جميع مخلوقاته؛ فلا تنفعه طاعة الطائعين؛ كما لا تضره معصية العاصين. {إن يشأ يُذْهِبْكم}: بالإهلاك، {ويستخلِفْ من بعدِكم ما يشاء كما أنشأكم من ذُرِّيَّة قوم آخرين}: فإذا عرفتم بأنكم لا بدَّ أن تنتقلوا من هذه الدار كما انتقل غيركم، وترحلون منها وتخلونها لمن بعدكم كما رَحَلَ عنها مَنْ قبلكم وخلَّوها لكم؛ فَلِمَ اتَّخذتموها قراراً، وتوطنتم بها، ونسيتم أنها دار ممرٍّ، لا دار مقرٍّ وأن أمامكم داراً هي الدار التي جمعتْ كلَّ نعيم وسلمتْ من كلِّ آفة ونقص؟ وهي الدار التي يسعى إليها الأوَّلون والآخرون، ويرتحل نحوها السابقون واللاحقون، التي إذا وصلوها؛ فثم الخلودُ الدائم والإقامة اللازمة والغاية التي لا غاية وراءها والمطلوب الذي ينتهي إليه كل مطلوب والمرغوب الذي يضمحلُّ دونه كل مرغوب، هنالك والله ما تشتهيه الأنفس وتلذُّ الأعين ويتنافس فيه المتنافسون من لذَّة الأرواح وكثرة الأفراح ونعيم الأبدان والقلوب والقرب من علام الغيوب؛ فلله همةٌ تعلَّقت بتلك الكرامات، وإرادة سَمَتْ إلى أعلى الدرجات، وما أبخس حظَّ من رضي بالدُّون، وأدنى همة من اختار صفقة المغبون!
{133} Na Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waja wake kutenda matendo mema, na akawakataza matendo mabaya kwa kuwahurumia na kuwatakia masilahi yao. Na vinginevyo, Yeye ndiye anayejitosheleza kwa dhati yake asiyewahitaji viumbe vyake vyote. Kwa hivyo, utiifu wa mtiifu haumnufaishi, kama vile maasi ya waasi hayamdhuru. "Akitaka, atawaondoa" kwa kuwaangamiza, "na awaweke nyuma yenu wengine awatakao, kama vile alivyowatoa kutokana na dhuria ya kaumu wengine." Basi ikiwa mnajua kwamba nyinyi ni lazima mtatoka katika nyumba hii kama walivyotoka wasiokuwa nyinyi, nanyi mtaondoka humo na muiachie wale walio baada yenu kama walivyoondoka wale wa kabla yenu na wakaicha kwa ajili yenu. Basi kwa nini mliichukua kuwa mahali pa kukaa, na mkaifanya kuwa makazi, na mkasahau kuwa ni nyumba ya mapito, si nyumba ya kukaa; na kwamba mbele yenu kuna nyumba ambayo ndiyo nyumba iliyokusanya kila neema na imesalimika na kila balaa na upungufu? Nayo ndiyo nyumba wanayoifanyia juhudi wale wa mwanzo na wa mwisho, na wanaielekea wale waliotangulia na waliofuatia ambako wakipafikia, basi hapo ndipo pana kudumu na makazi ya lazima, na lengo ambalo hakuna lengo lingine zaidi yake, na lile linalotafutwa ambalo kila linalotafutwa linaishia hapo, na yale yanayohofiwa ambayo kinatoweka kila kitu kinachohofiwa isipokuwa hayo. Hapo, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuna yale yanayotamaniwa na nafsi na yale yanayopendeza macho, na wanashindana kwa ajili yake wale wanaoshindana miongoni mwa ladha za nafsi, na wingi wa furaha, furaha ya miili na mioyo, na kuwa karibu na Mwenye kuijua zaidi ghaibu. Basi na kwa jina la Mwenyezi Mungu mtu na afanye hima inayohusiana na matukufu haya, na nia inayokwenda juu hadi katika viwango vya juu zaidi. Na ni kupunjwa kupi huku kwa fungu la mwenye kuridhia yaliyo duni, na ni ya chini mno vipi hima ya mwenye kuchagua mapatano ya waliopunjwa.
#
{134} ولا يستبعد المعرض الغافل سرعة الوصول إلى هذه الدار؛ فإنَّ {ما توعدونَ لآتٍ وما أنتُم بمعجزينَ}: لله، فارِّين من عقابه؛ فإنَّ نواصِيَكم تحت قبضته، وأنتم تحت تدبيره وتصرفه.
{134} Na wala mwenywe kupeana mgongo aliye na akili timamu hawezi kukataa kuwasili kwa haraka kwa nyumba hii. Kwa maana, hakika "yale mnayoahidiwa yatafika, wala nyinyi hamtaweza kumshinda" Mwenyezi Mungu, na kuikimbia adhabu yake. Kwa sababu, nywele zenu za mbele ya kichwa ziko chini ya mshiko Wake, na nyinyi mko chini ya uendeshaji wake na udhibiti Wake.
#
{135} {قل}: يا أيها الرسولُ لقومك إذا دعوتَهم إلى الله وبينت لهم مآلهم وما عليهم من حقوقه فامتنعوا من الانقياد لأمرِهِ واتَّبعوا أهواءهم واستمروا على شركهم: {يا قومِ اعملوا على مكانتِكُم}؛ أي: على حالتكم التي أنتم عليها ورضيتموها لأنفسكم، {إني عاملٌ}: على أمر الله ومتبعٌ لمراضي الله: {فسوف تعلمونَ من تكونُ له عاقبةُ الدار}: أنا أو أنتم، وهذا من الإنصاف بموضع عظيم؛ حيث بيَّن الأعمال وعامليها، وجعل الجزاء مقروناً بنظر البصير، ضارباً فيه صفحاً عن التصريح الذي يغني عنه التلويح، وقد علم أن العاقبة الحسنة في الدنيا والآخرة للمتقين، وأن المؤمنين لهم عُقبى الدار، وأنَّ كلَّ معرض عن ما جاءت به الرسل عاقبته عاقبة سوء وشر، ولهذا قال: {إنه لا يفلحُ الظالمونَ}: فكلُّ ظالم وإن تمتَّع في الدُّنيا بما تمتع به؛ فنهايته فيه الاضمحلال والتلف؛ إن الله ليملي للظالم حتى إذا أخذه لم يُفْلِتْه.
{135} "Sema:" Ewe Mtume kwa kaumu yako, unapowalingania kwa Mwenyezi Mungu na ukawabainishia hatima yao na haki zake zilizo juu yao, lakini wakakataa kufuata amri yake, na wakafuata matamanio yao, na wakaendelea juu ya Ushirikina wao: "Enyi kaumu yangu! Fanyeni mahali penu mlipo." Yaani, katika hali yenu ambayo mmo, na mkairidhia nafsi zenu, "na hakika mimi ninafanya" kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na ninafuata anayoridhia Mwenyezi Mungu. "Mtakuja jua ni ya nani yatakuwa makaazi mema mwishoni;" mimi au nyinyi. Na huu ni miongoni mwa uadilifu katika mahali pakubwa. Ambapo alibainisha matendo na wanaoyafanya, na akafanya malipo kuwa yanafungamana na utambuzi wa Mwenye kuona, na akaacha kuisema kwa kauli ya waziwazi ambayo inatoshelezwa na kudokezwa tu. Na tayari ilikwisha julikana kwamba mwisho mzuri katika dunia na Akhera ni wa wachamungu, na kwamba Waumini ndio wenye nyumba ya mwisho iliyo bora, na kwamba kila mwenye kupeana mgongo kwa yale yaliyoletwa na Mitume mwisho wake ni mwisho mbaya na muovu. Na ndiyo maana akasema, "Hakika, madhalimu hawafaulu." Basi kila dhalimu, hata akistareheka katika dunia kwa yale anayostareheka kwayo, mwisho wake ni kupotea na kuharibika. Hakika Mwenyezi Mungu humpa muhula dhalimu, mpaka anapomkamata, hawezi kumkwepa.
: 136 - 140 #
{وَجَعَلُوا لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَذَا لِلَّهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَذَا لِشُرَكَائِنَا فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّهِ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَى شُرَكَائِهِمْ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ (136) وَكَذَلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ (137) وَقَالُوا هَذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَنْ نَشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ سَيَجْزِيهِمْ بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ (138) وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَى أَزْوَاجِنَا وَإِنْ يَكُنْ مَيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ (139) قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّهِ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ (140)}
136. Na walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu. Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu, vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu, huwafikia washirikishwa wao. Ni uovu mno hayo wanayoyahukumu. 137. Na kadhalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwaua watoto wao ili kuwaangamiza na kuwachanganyia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelifanya hayo. Basi waache na hayo wanayozua ya uongo. 138. Nao walisema: "Mifugo hawa na mimea ni miiko. Hawavili isipokuwa tumtakaye" - kwa madai yao tu. Na mifugo wengine imeharimishwa migongo. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, kwa kumzulia uongo tu. Atawalipa kwa hayo ya uongo waliyokuwa wakiyazua. 139. Na walisema: Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni ya wanaume wetu tu, na vimeharimishwa kwa wake zetu. Lakini wakiwa nyamafu, basi wanashirikiana ndani yake. Atawalipa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua vyema. 140. Hakika walipata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya elimu, na wakaharimisha vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu uongo. Hakika walipotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.
#
{136} يخبر تعالى عما عليه المشركون المكذِّبون للنبي - صلى الله عليه وسلم - من سفاهة العقل وخفة الأحلام والجهل البليغ، وعدَّد تبارك وتعالى شيئاً من خرافاتهم؛ لينبِّه بذلك على ضلالهم والحذر منهم، وأن معارضة أمثال هؤلاء السفهاء للحقِّ الذي جاء به الرسول لا تقدح فيه أصلاً؛ فإنَّهم لا أهليَّة لهم في مقابلة الحق، فذكر من ذلك أنهم: {جعلوا للهِ} نصيباً {مما ذَرَأ من الحَرْثِ والأنعام}: ولشركائهم من ذلك نصيباً، والحال أنَّ الله تعالى هو الذي ذرأه للعباد وأوجده رزقاً، فجمعوا بين محذورين محظورين، بل ثلاثة محاذير: منَّتهم على الله في جعلهم له نصيباً مع اعتقادهم أنَّ ذلك منهم تبرُّع. وإشراك الشركاء الذين لم يرزُقوهم ولم يوجدوا لهم شيئاً في ذلك. وحكمهم الجائر في أنَّ ما كان للهِ لم يبالوا به ولم يهتمُّوا، ولو كان واصلاً إلى الشركاء وما كان لشركائهم؛ اعتنوا به واحتفظوا به ولم يصلْ إلى الله منه شيءٌ، وذلك أنهم إذا حصل لهم من زروعهم وثمارهم وأنعامهم التي أوجدها الله لهم شيء؛ جعلوه قسمينِ: قسماً قالوا: هذا لله بقولهم وزعمهم، وإلاَّ؛ فالله لا يقبلُ إلا ما كان خالصاً لوجهه ولا يقبلُ عمل مَن أشرك به، وقسماً جعلوه حصة شركائِهِم من الأوثان والأنداد؛ فإن وصل شيء مما جعلوه لله واختلط بما جعلوه لغيره؛ لم يبالوا بذلك، وقالوا: الله غنيٌّ عنه فلا يردُّونه، وإن وصل شيءٌ مما جعلوه لآلهتهم إلى ما جعلوه لله؛ ردُّوه إلى محلِّه، وقالوا: إنها فقراء، لا بدَّ من ردِّ نصيبها؛ فهل أسوأ من هذا الحكم وأظلم حيث جعلوا ما للمخلوق يجتهد فيه وينصح ويحفظ أكثر مما يفعل بحقِّ الله. ويحتمل أن تأويل الآية الكريمة ما ثبت في «الصحيح» عن النبي - صلى الله عليه وسلم -: أنَّه قال عن الله تعالى: أنّه قال: «أنا أغنى الشُّركاءِ عن الشرك، مَنْ أشرك معي شيئاً؛ تركتُه وشِرْكَه» ، وأنَّ معنى الآية أنَّ ما جعلوه وتقربوا به لأوثانهم فهو تقرُّبٌ خالصٌ لغير الله، ليس لله منه شيءٌ، وما جعلوه لله على زعمهم؛ فإنه لا يصل إليه؛ لكونِهِ شركاً، بل يكون حظَّ الشركاء والأنداد؛ لأن الله غنيٌّ عنه، لا يقبل العمل الذي أشرك به معه أحدٌ من الخلق.
{136} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu yale wanayoyafanya washirikina wanaomkadhibisha Nabii -rehema na amani zimshukie – ya upumbavu wa akili, na uhafifu wa maoni, na ujinga mkubwa; na Yeye Mwingi wa baraka, Mtukufu akahesabu baadhi ya itikadi zao potofu. Ili atanabahishe kwa hilo upotovu wao na kutahadharisha nao, na kwamba upinzani wa mfano wa wapumbavu hao kwa haki ambayo ililetwa na Mtume (s.a.w) haiitii dosari hata kidogo. Kwani wao hawana sifa za kuwawezesha kukabiliana na haki, kwa hivyo ikataja katika hayo kuwa, "walimwekea Mwenyezi Mungu" fungu "katika mimea na wanyama aliowaumba," na washirikishwa wao pia wana fungu katika hayo. Na hali ni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyeviumba kwa ajili ya waja wake na akavifanya kuwapo ili iwe riziki kwao. Lakini hao wakajumuisha haramu mbili, na hata haramu tatu. Wao kumtajia Mwenyezi Mungu kwamba walimneemesha kwa kumuwekea fungu pamoja na wao kuitakidi kwamba hilo ni sadaka kutoka kwao. Na kuwashirikisha washirikishwa ambao hawakuwaruzuku wao wala hawakuwapa chochote katika hayo. Na hukumu yao ya dhuluma ambayo ni kwamba vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu hawakuvitia maanani wala hawakuvijali, hata ikiwa vitawafikia washirikishwa wao ingawa havikuwa vya washirikishwa wao hao, wanavitunza na kuvihifadhi, na hakuna chochote kwavyo chenye kumfikia Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa sababu ikiwa wangepata chochote katika mazao yao, na matunda, na mifugo yao ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia, wangekifanya sehemu mbili. Sehemu moja wakasema: Hiki ni cha Mwenyezi Mungu - kwa mujibu wa maneno yao na madai yao. - Vinginevyo; hakika Mwenyezi Mungu hakubali isipokuwa kile kilichokusudiwa kwacho uso wake peke yake, na wala hayakubali matendo ya mwenye kumshirikisha na wengine. Na sehemu nyingine wakaifanya kuwa fungu la washirikishwa wao miongoni mwa vyote viabudiwavyo visivyo Mwenyezi Mungu, na wenza. Basi ikiwa kitu katika vile walivyovifanya kuwa ni vya Mwenyezi Mungu kitafika na kikachanganyika na vile walivyovifanya kuwa ni vya asiyekuwa yeye, hawayajali hayo, na wanasema, “Mwenyezi Mungu hayahitaji;” kwa hivyo, hawaviregeshi. Na kikifika chochote katika vile walivyowawekea miungu wao katika vile walivyomwekea mwenyezi mungu, Wanavirudisha mahali pake, na wanasema: hawa miungu ni wahitaji (masikini), lazima fungu lao lirudishwe. Je, kuna baya zaidi kuliko hukumu hii na yenye dhulma zaidi, kwa vile wanavyoyafanya yale ya kiumbe wanajitahidi ndani yake, na kushauri juu yake, na kuhifadhi zaidi ya yale yanayofanywa katika haki ya Mwenyezi Mungu? Na inawezekana kwamba tafsiri ya Aya hii tukufu kuwa yale yaliyothibiti katika “Sahihi” kutoka kwa Nabii – Rehema na Amani zimshukie – kwamba alisema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa alisema: “Mimi ndiye nisiyehitaji zaidi kuwa na mshirika kati ya washirika. Mwenye kunishirikisha na chochote, ninamuacha yeye na hicho alichoshirikisha ndani yake.” Na kwamba, maana ya Aya ni kuwa yale waliyofanya na wakajikurubisha kwacho kwa viabudiwa vyao, basi huko ni kujikurubisha kutupu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, na walichokifanya kuwa ni cha Mwenyezi Mungu kulingana na madai yao, hicho hakimfikii. Kwa sababu ni shirki, bali ni fungu la washirika na wenza hao. Kwa sababu mwenyezi Mungu hakihitaji, na hakubali matendo ambayo alishirikishwa pamoja naye chochote katika viumbe vyake.
#
{137} ومن سَفَه المشركين وضلالهم أنه {زَيَّنَ لكثيرٍ من المشركين} شركاؤهم ـ أي: رؤساؤهم وشياطينهم ـ قتلَ أولادهم، وهو الوأد الذين يدفنون أولادهم خشية الافتقار والإناث خشية العار، وكل هذا من خدع الشياطين الذين يريدون أن يُرْدوهم بالهلاك ويَلْبِسوا عليهم دينهم فيفعلون الأفعال التي في غاية القبح، ولا يزال شركاؤهم يزيِّنونها لهم حتى تكونَ عندهم من الأمور الحسنة والخصال المستحسنة، ولو شاء الله أن يمنَعَهم ويحَولَ بينهم وبين هذه الأفعال ويمنعَ أولادَهم عن قتل الأبوين لهم؛ ما فعلوه، ولكنِ اقتضتْ حكمتُهُ التخليةَ بينهم وبين أفعالهم؛ استدراجاً منه لهم وإمهالاً لهم وعدم مبالاة بما هم عليه، ولهذا قال: {فذَرْهُم وما يفترونَ}؛ أي: دعهم مع كذِبِهم وافترائهم، ولا تحزن عليهم؛ فإنَّهم لن يضرُّوا الله شيئاً.
{137} Na miongoni mwa upumbavu wa washirikina na upotovu wao ni kwamba "Na kadhalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina." - Yaani, viongozi wao na mashetani wao – kuwaua watoto wao. Nao ndio wale wanaowazika watoto wao kwa kuogopa umasikini, na wanawake kwa kuogopa fedheha. Na yote haya ni mbaya mno, na washirika wao hao hawajaacha kuwapambia hayo ili yawe kwao katika mambo mazuri na sifa zenye kutamanika. Na kama Mwenyezi Mungu angetaka kuwazuia na kuweka kuzuizi kati yao na vitendo vyao hivi, na kuwazuia watoto wao kuuawa na wazazi wao; basi hawangefanya hivyo. Lakini hekima yake ilihitaji kuwaacha na matendo yao, ili awazidishe kuzama katika dhambi, na kuwapa muhula, na wao kutojali hali yao. Na ndiyo maana akasema, "Basi waache na hayo wanayozua ya uwongo." Yaani, waache na uongo wao na kuzua kwao uongo, na wala usihuzunike juu yao. Kwa maana, wao kwa hakika hawatamdhuru Mwenyzi Mungu kitu.
#
{138} ومن أنواع سفاهتهم أن الأنعام التي أحلَّها الله لهم عموماً وجعلها رزقاً ورحمة يتمتَّعون بها وينتفعون قد اخترعوا فيها بدعاً وأقوالاً من تلقاء أنفسهم؛ فعندهم اصطلاح في بعض الأنعام والحرث أنهم يقولون فيها: {هذه أنعامٌ وحَرْثٌ حِجْرٌ}؛ أي: محرم. لا يطعمه {إلا من نشاء}؛ أي: لا يجوز أن يَطْعَمُه أحدٌ إلاَّ مَن أردنا أن يُطعمه أو وصفناه بوصفٍ من عندنا، وكلُّ هذا بزعمهم لا مستندَ لهم ولا حجة إلا أهويتهم وآراؤهم الفاسدة. وأنعام ليست محرمةً من كل وجه، بل يحرِّمون ظهورها؛ أي: بالركوب والحمل عليها، ويحمون ظهرها، ويسمونها الحام. وأنعام لا يذكرون اسم الله عليها، بل يذكرون اسم أصنامهم وما كانوا يعبدون من دون الله عليها، وينسبون تلك الأفعال إلى الله، وهم كَذَبَةٌ فُجَّارٌ في ذلك. {سيجزيهم بما كانوا يفترونَ}: على الله من إحلال الشرك وتحريم الحلال من الأكل والمنافع.
{138} Na katika aina za upumbavu wao ni kuwa mifugo ambao Mwenyezi Mungu aliwahalalishia kwa ujumla na akawafanya kuwa riziki na rehema ili wafurahie kwayo na kunufaika nao, walizua ndani yake uzushi na maneno yao wenyewe. Wana maneno waliyokubaliana juu yake katika baadhi ya mifugo na mimea kwamba wanasema kuyahusu kuwa: "Mifugo hawa na mimea ni miiko." Yaani, vimeharamishwa, hawavili "isipokuwa tumtakaye;" yaani, hairuhusiki kwa yeyote kuvila isipokuwa yule tunayemtaka avile au tunayemueleza kwa maelezo yetu wenyewe. Na yote haya ni kwa madai yao tu, hayana msingi wowote wala hoja isipokuwa matamanio yao na maoni yao wenyewe mapotofu. Na mifugo wengine ambao si haramu kwa njia zote, bali wanaharamisha migongo yao tu. Yaani, kwa kuwapanda na kubeba juu yao, na wanailinda migongo yao, na wanawaita Al-Ham. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, bali wanayataja juu yao majina ya masanamu yao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na wanayanasibisha matendo hayo kwa Mwenyezi Mungu, lakini wao ni waongo, waovu katika hayo. "Atawalipa kwa hayo ya uwongo waliyokuwa wakiyazua" dhidi ya Mwenyezi Mungu, kama vile kuhalalisha ushirikina na kuharamisha yaliyo halali miongoni mwa vyakula na manufaa mbalimbali.
#
{139} ومن آرائهم السخيفة أنهم يجعلون بعض الأنعام ويعيِّنونها محرماً ما في بطنها على الإناث دون الذكور، فيقولون: {ما في بطونِ هذه الأنعام خالصةٌ لذكورنا}؛ أي: حلال لهم لا يشاركهم فيها النساء. {ومحرَّمٌ على أزواجنا}؛ أي: نسائنا، هذا إذا وُلِدَ حيًّا، وإن يكن ما في بطنها يولد ميتاً؛ فهم فيه شركاء؛ أي: فهو حلال للذكور والإناث. {سيَجْزيهم}: الله {وَصْفَهُمْ}: حيث وصفوا ما أحلَّه الله بأنه حرام، ووصفوا الحرام بالحلال، فناقضوا شرع الله وخالفوه ونسبوا ذلك إلى الله. {إنَّه حكيمٌ}؛ حيث أمهل لهم ومكَّنهم مما هم فيه من الضلال، {عليمٌ}: بهم لا تخفى عليه خافيةٌ، وهو تعالى يعلم بهم، وبما قالوه عليه، وافتَرَوْه وهو يعافيهم، ويرزقهم جل جلاله.
{139} Na miongoni mwa maoni yao ya kipuuzi ni kwamba wanawafanya baadhi ya mifugo na wanawatenga wakiharamisha vilivyomo matumboni mwao juu ya wanawake na si wanaume. Na wanasema: "Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni ya wanaume wetu tu." Yaani, ni halali kwao, na wala wanawake hawashiriki ndani yake. "Na vimeharimishwa kwa wake zetu;" yaani, wanawake wetu. Na hili ni ikiwa atazaliwa hai. Na ikiwa kilicho ndani ya tumbo lake ni mfu, basi wao ni washirika ndani yake. Yaani, ni halali kwa wanaume na wanawake. "Atawalipa," yaani, Mwenyezi Mungu "maelezo yao hayo" ambapo waliyaeleza yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu kuwa ni haramu, na wakaieleza hatamu kuwa ni halali; basi wakaipinga sheria ya Mwenyezi Mungu, na wakaihalifu, na wakalinasibisha hilo kwa Mwenyezi Mungu. "Hakika Yeye ni Mwenye hekima kubwa." Ambapo aliwapa muhula, na akawawezesha kuwa katika hali yao hiyo ya upotevu. "Mwenye kujua vyema" hali yao, na hakifichikani kwake chenye kufichikana. Naye Mtukufu anawajua, na yale waliyoyasema juu Yake, na wakazua ya uongo; naye anawapa salama, na Anawaruzuku Yeye Utukufu mkubwa.
#
{140} ثم بيَّن خُسرانهم وسفاهةَ عقولهم، فقال: {قد خَسِرَ الذين قتلوا أولادَهم سفهاً بغير علم}؛ أي: خسروا دينهم وأولادهم وعقولهم، وصار وصفهم بعد العقول الرزينة السَّفَه المردي والضلال، {وحرَّموا ما رزقهم الله}؛ أي: ما جعله رحمة لهم وساقه رزقاً لهم، فردُّوا كرامة ربِّهم، ولم يكتفوا بذلك، بل وصفوها بأنها حرام وهي من أحلِّ الحلال، وكل هذا {افتراءٌ على الله}؛ أي: كذب يَكْذِب به كلُّ معاندٍ كفارٍ، {قد ضَلُّوا وما كانوا مهتدينَ}؛ أي: قد ضلُّوا ضلالاً بعيداً ولم يكونوا مهتدينَ في شيءٍ من أمورِهم.
{140} Kisha akaeleza hasara yao na upumbavu wa akili zao, kwa hivyo akasema: "Hakika walipata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya elimu." Yaani, waliihasiri dini yao, na watoto wao, na akili zao, na baada ya kuwa na akili timamu, wakawa sasa wanasifiwa kwa upumbavu mbaya na upotovu, "na wakaharimisha vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu." Yaani, yale Aliyoyafanya kwa kuwa rehemu, akawapa kama riziki kwao, lakini wakaukataa ukarimu wa Mola wao Mlezi, na hawakutosheka na hilo, bali wakausifu kuwa ni haramu ilhali ni miongoni mwa yale yaliyo halali zaidi. Na yote haya ni "kumzulia Mwenyezi Mungu uongo;" yaani uwongo anaodanganya kwa huo kila mkaidi, kafiri mkubwa. "Hakika walipotea, wala hawakuwa wenye kuongoka," yaani walikwisha potea upotovu wa mbali, na wala hawakuwa waongofu katika chochote miongoni mwa mambo yao.
: 141 #
{وَهُوَ الَّذِي أَنْشَأَ جَنَّاتٍ مَعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ كُلُوا مِنْ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ وَلَا تُسْرِفُوا إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ (141)}
141. Na Yeye ndiye aliyeziumba mabustani yenye kutambaa kwenye fito, na yasiyotambaa kwenye fito, na mitende, na mimea yenye vyakula mbali mbali, na mizaituni na mikomanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni katika matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa kupitiliza. Hakika Yeye hawapendi watumiao kwa kupitiliza.
#
{141} لما ذكر تعالى تصرُّفَ المشركين في كثير مما أحلَّه الله لهم من الحروث والأنعام؛ ذكر تبارك وتعالى نعمتَه عليهم بذلك ووظيفَتَهم اللازمة عليهم في الحروثِ والأنعام، فقال: {وهو الذي أنشأ جناتٍ}؛ أي: بساتين فيها أنواع الأشجار المتنوعة والنباتات المختلفة، {معروشاتٍ وغير معروشاتٍ}؛ أي: بعض تلك الجنات مجعولٌ لها عريشٌ تنتشر عليه الأشجار ويعاونها في النهوض عن الأرض، وبعضها خالٍ من العروش تنبُتُ على ساقٍ أو تنفرش في الأرض. وفي هذا تنبيهٌ على كَثرة منافعها وخيراتها، وأنه تعالى علَّم العباد كيف يعرشونها وينمونها. {و}: أنشأ تعالى {النخل والزرع مختلفاً أُكُلُه}؛ أي: كله في محل واحد، ويشرب من ماء واحد، ويفضل الله بعضه على بعض في الأكل، وخص تعالى النخل والزرع على اختلاف أنواعه لكثرة منافعها ولكونها هي القوتُ لأكثر الخلق. {و} أنشأ تعالى {الزيتونَ والرُّمانَ متشابهاً}: في شجره، {وغير متشابهٍ}: في ثمره وطعمه، كأنه قيل: لأي شيء أنشأ الله هذه الجنات؟ وما عطف عليها؟ فأخبر أنه أنشأها لمنافع العباد، فقال: {كلوا من ثمرِهِ}؛ أي: النخل والزرع، {إذا أثمر وآتوا حَقَّه يومَ حصادِهِ}؛ أي: أعطوا حقَّ الزرع، وهو الزكاة ذات الأنصباء المقدَّرة في الشرع؛ أمرهم أن يعطوها يوم حصادها، وذلك لأنَّ حصادَ الزرع بمنزلة حَوَلان الحول؛ لأنه الوقت الذي تتشوَّف إليه نفوس الفقراء، ويسهُلُ حينئذٍ إخراجُه على أهل الزرع، ويكون الأمر فيها ظاهراً لمن أخرجها حتى يتميَّز المخرِج ممَّن لا يخرج. وقوله: {ولا تسرفوا}؛ يعمُّ النهي عن الإسراف في الأكل، وهو مجاوزة الحدِّ والعادة. وأن يأكلَ صاحبُ الزرعِ أكلاً يضرُّ بالزكاة، والإسراف في إخراج حقِّ الزرع بحيث يخرِجُ فوقَ الواجبِ عليه أو يضرُّ نفسه أو عائلتَه أو غرماءَه؛ فكلُّ هذا من الإسراف الذي نهى الله عنه الذي لا يحبُّه الله بل يبغِضُه، ويمقتُ عليه. وفي هذه الآية دليلٌ على وجوب الزكاة في الثمار، وأنه لا حَوْلَ لها، بل حولُها حصادُها في الزروع وجذاذ النخيل، وأنه لا تتكرَّر فيها الزكاة لو مكثت عند العبد أحوالاً كثيرةً إذا كانت لغير التجارة؛ لأنَّ الله لم يأمر بالإخراج منه إلاَّ وقتَ حصادِهِ، وأنَّه لو أصابها آفةٌ قبل ذلك بغير تفريط من صاحب الزرع والثمر؛ أنه لا يضمنها، وأنه يجوز الأكل من النخل والزرع قبل إخراج الزكاة منه، وأنه لا يُحْسَبُ ذلك من الزكاة، بل يزكِّي المال الذي يبقى بعده، وقد كان النبي - صلى الله عليه وسلم - يَبْعَثُ خارصاً يخرُصُ للناس ثمارَهم ويأمرُهُ أن يَدَعَ لأهلها الثلث أو الربع بحسب ما يعتريها من الأكل وغيره من أهلها وغيرهم.
{141} Yeye Mungu Mtukufu alipotaja matendo ya washirikina katika mengi ya yale aliyowahalalishia Mwenyezi Mungu miongoni mwa mimea na mifugo, yeye Mwingi wa baraka, Mtukufu akataja neema yake juu yao katika kwa hayo na majukumu yao ya wajibu juu yao katika mimea na mifugo hao, kwa hivyo akasema: "Na Yeye ndiye aliyeziumba mabustani." Yaani, mabustani yenye aina mbalimbali za miti na mimea tofautitofauti, "yenye kutambaa kwenye fito." Yaani, baadhi ya mabustani hayo yamefanyiwa fito ambazo juu yake inatambaa miti na kuisaidia kuinuka juu kutoka juu ya ardhini, na baadhi yake haina fito inayomea juu yake, lakini ina mashina au inajitandaza kwenye ardhi. Na katika hii kuna tanabahisho juu ya wingi wa manufaa zake na heri zake, na kwamba yeye Mtukufu aliwafundisha waja wake jinsi ya kuitia kwenye fito na kuikuza. "Na" yeye Mtukufu alianzisha "mitende na mimea yenye vyakula mbalimbali." Yaani, yote iko mahali pamoja, na inakunywa katika maji moja, na Mwenyezi Mungu hupendelea baadhi yake kuliko mingine katika vyakula. Na yeye Mtukufu aliufanya mtende kuwa maalumu na mimea kwa aina zake tofautitofauti kwa sababu ya wingi wa manufaa yake na kwa kuwa hiyo ndicho chakula kikuu cha wengi wa viumbe. "Na" yeye akaanzisha "mizaituni na mikomamanga inayofanana" katika miti yake, "na isiyofanana" katika matunda yake na ladha yake. Na ni kana kwamba ilisemwa: kwa nini yeye Mtukufu alianzisha mabustani haya? Na ni nini alichofungamanisha nayo? Basi akajulisha kwamba aliyaanzisha kwa sababu ya manufaa ya waja wake, na akasema: "Kuleni katika matunda yake;" yaani, mitende na mimea, "inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake." Yaani, toeni haki ya mazao hayo, ambayo ni Zaka yenye mafungu yaliyopimwa katika sheria. Aliwaamuru waitoe siku ya kuvunwa kwake. Na hilo ni kwa sababu mavuno ya mazao ni sawa na kupita kwa mwaka. Kwa sababu ndio wakati ambao nafsi za masikini huyatazamia, na ni rahisi kwa wenye mazao kuyatoa, na jambo hili wakati huo linakuwa dhahiri kwa mwenye kuitoa, ili apambauke mwenye kuitoa na yule asiyeitoa. Na kauli yake: "Wala msitumie kwa kupitiliza" inajumuisha katazo la kupitiliza katika kula. Nako ni kupitiliza kiwango. Na amekataza kwamba mwenye mazao hayo ale kula kwenye kuidhuru Zaka. Na kupitiliza katika kutoa haki ya mazao ni kwamba atoe zaidi ya kile wajibu ulioko juu yake, au ajidhuru mwenyewe, au familia yake, au wadai wake. Yote haya ni katika kupitiliza ambako Mwenyezi Mungu alikataza, ambako Mwenyezi Mungu hakupendi, bali anakuchukia, na anachukia sana. Na katika Aya hii kuna ushahidi wa ulazima wa Zaka katika matunda, na kwamba hakuna ulazima wa kupita mwaka mmoja, bali muda wake ni kwa kuvunwa kwake katika mazao na kuichuma mitende, na kwamba Zaka haitajirudia katika hayo ikiwa yatabaki kwa mja kwa miaka mingi ikiwa si kwa ajili ya biashara. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hakuamrisha itolewe humo ila wakati wa mavuno yake. Na ikiwa janga liliyapata kabla ya hapo bila ya kupuuza kwa mwenye mazao hayo na matunda, ni kwamba hayadhamini, na kwamba inaruhusika kula katika mitende na mazao kabla ya kutoa humo Zaka, na kwamba hilo halihesabiwi katika Zaka, bali atatoa Zaka katika mali iliyobaki baada yake. Na Nabii - sala za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie – alikuwa akimtuma mwenye kukadiria ili awakadirie watu matunda yao, na anamwamuru awaachie wenyewe theluthi moja au robo kulingana na yanayokuwa humo ya kula na mengineyo, wenyewe na wengineo.
: 142 - 144 #
{وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ (142) ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ مِنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنْثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنْثَيَيْنِ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (143) وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنْثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنْثَيَيْنِ أَمْ كُنْتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّهُ بِهَذَا فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ كَذِبًا لِيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ (144)}.
142. Na katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi. 143. (Amewaumbia) majozi manane: katika kondoo ni wawili, na katika mbuzi ni wawili. Sema: je, ameharimisha madume wawili hawa au majike wawili hawa, au wale waliomo matumboni mwa majike yote mawili haya? Niambieni kwa elimu ikiwa nyinyi ni wakweli. 144. Na katika ngamia ni wawili, na katika ng'ombe ni wawili. Sema: Je, ameharamisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlishuhudia Mwenyezi Mungu alipowausia haya? Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu uoongo, ili awapoteze watu bila ya elimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.
#
{142} أي: {و} خلق وأنشأ {من الأنعام حَمُولةً وفَرْشاً}؛ أي: بعضها تحملون عليه وتركبونه، وبعضها لا تصلح للحمل والركوب عليها لِصغَرِها كالفُصلان ونحوها، وهي الفرش؛ فهي من جهة الحمل والركوب تنقسم إلى هذين القسمين. وأما من جهة الأكل وأنواع الانتفاع؛ فإنها كلها تؤكل وينتفع بها، ولهذا قال: {كُلوا ممَّا رَزَقَكُمُ الله ولا تتَّبِعوا خطواتِ الشيطانِ}؛ أي: طرقه وأعماله التي من جملتها أن تُحَرِّموا بعض ما رزقكم الله. {إنَّه لكم عدوٌّ مبينٌ}: فلا يأمركم إلا بما فيه مضرتكم وشقاؤكم الأبدي.
{142} Yaani, "Na" amewaanzishia "katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na kutoa matandiko" yaani, baadhi yao mnabebea juu yao na mnawapanda, na mengine hawafai kubebeshwa na kupanda juu yao kwa sababu ya udogo wao, kama vile ngamia wadogo na mfano wake, na ambao ndio Al-Farsh. Kwa hivyo, kwa mtazamo wa kubeba na kupanda, wanagawanyika katika sehemu hizi mbili. Na ama kwa mtazamo wa kula na aina nyinginezo za kufaidika, hao wote wanaliwa na kunufaika nao. Na ndiyo maana akasema: "Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani;" yaani, Njia zake na matendo yake ambayo miongoni mwayo ni nyinyi kuharamisha baadhi ya yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu. "Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi." Kwa hivyo, hawaamrishi isipokuwa yale yenye kuwadhuru na mashaka yenu ya milele.
#
{143} وهذه الأنعام التي امتنَّ الله بها على عباده، وجعلها كلَّها حلالاً طيباً، فصَّلها بأنها: {ثمانيةُ أزواجٍ من الضأن اثنين}: ذكر وأنثى، {ومن المعز اثنين}: كذلك؛ فهذه أربعةٌ، كلُّها داخلةٌ فيما أحلَّ الله، لا فرق بين شيءٍ منها؛ فقلْ لهؤلاء المتكلِّفين الذين يحرمون منها شيئاً دون شيء أو يحرمون بعضها على الإناث دون الذكور ملزماً لهم بعدم وجود الفرق بين ما أباحوا منها وحرموا: {آلذَّكَرَيْنِ}: من الضأن والمعز {حرَّمَ}: الله فلستم تقولون بذلك وتطردونه، {أم الأُنثيين}: حرم الله من الضأن والمعز؛ فليس هذا قولكم؛ لا تحريم الذكور الخُلَّص، ولا الإناث الخُلَّص من الصنفين، بقي إذا كان الرحم مشتملاً على ذكر وأنثى أو على مجهول، فقال: {أم}: تحرمون {ما اشتملت عليه أرحام الأنثيين}؛ أي: أنثى الضأن وأنثى المعز من غير فرق بين ذكر وأنثى؛ فلستُم تقولون أيضاً بهذا القول؛ فإذا كنتم لا تقولون بأحدِ هذه الأقوال الثلاثة التي حصرت الأقسام الممكنة في ذلك؛ فإلى أي شيء تذهبون؟ {نبِّئوني بعلم إن كنتُم صادقينَ}: في قولِكم ودعواكم. ومن المعلوم أنهم لا يمكنهم أن يقولوا قولاً سائغاً في العقل إلا واحداً من هذه الثلاثة، وهم لا يقولون بشيء منها، إنما يقولون: إن بعضَ الأنعام التي يصطَلِحون عليها اصطلاحاتٍ من عند أنفسهم حرامٌ على الإناثِ دون الذكور، أو محرَّمة في وقت من الأوقات، أو نحو ذلك من الأقوال التي يعلم علماً لا شكَّ فيه أنَّ مصدرها من الجهل المركب والعقول المختلة المنحرفة والآراء الفاسدة، وأنَّ الله ما أنزل بما قالوه من سلطان، ولا لهم عليه حجة ولا برهان.
{143} Na hawa mifugo ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwao juu ya waja wake, na akawafanya wote kuwa halali na wazuri, aliwaeleza kwa kina kwamba ni: "majozi manane: katika kondoo ni wawili", dume na jike, "na katika mbuzi ni wawili" vile vile. Basi hawa ni wanne, wote wanaingia katika yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu, na hakuna tofauti baina yeyote katika hao. Basi waambie hawa wanaojitia katika ugumu, ambao wanaharamisha katika hao baadhi yao na kuacha baadhi yao, au wanawaharamisha baadhi yao kwa wanawake na sio kwa wanaume, ukiwalazimisha kuwa hakuna tafauti baina ya wale waliowaruhusu katika hao na wale waliowaharamisha: "Je, madume wawili hawa" katika kondoo na mbuzi ndiyo "ameharamisha" Mwenyezi Mungu? Lakini nyinyi hamsemi hivyo katika hali zote. "Majike wawili hawa," Mwenyezi Mungu aliharamisha katika kondoo na mbuzi. Lakini kauli yenu si hii. Si kuharamisha madume wote wawili, wala majike wote wawili katika aina mbili hizi. Na inabaki ikiwa tumbo lunajumuisha dume na jike au kisichojulikana. Basi akasema, "au" mnaharamisha "wale waliomo matumboni mwa majike yote mawili haya?" Yaani, kondoo jike na mbuzi jike, bila ya tofauti yoyote kati ya dume na jike. Lakini nyinyi pia hamsemi kauli hii. Kwa hivyo ikiwa hamsemi kwa mojawapo ya kauli hizi tatu ambazo zimefungia kategoria zinazowezekana katika hao, basi mnaenda kwa kitu gani? "Niambieni kwa elimu ikiwa nyinyi ni wakweli" katika kauli yenu hiyo na madai yenu. Na inajulikana kuwa hawawezi kusema kauli yenye kuingia katika akili isipokuwa moja katika hizi tatu, lakini wao hawasemi hata mmoja katika hizi. Bali wanasema, hakika baadhi ya mifugo ambao wanakubaliana juu yake kukubaliana kwao wenyewe tu ni haramu kwa wanawake na si kwa wanaume, au ni haramu katika wakati fulani miongoni mwa nyakati. Au mfano wa hayo miongoni mwa kauli ambazo anajulikana kwa elimu isiyokuwa na shaka ndani yake kwamba chanzo chake ni kwa sababu ya ujinga uliopandana, na akili mbaya, potofu, na maoni mabovu, na kwamba Mwenyezi Mungu hakuyateremshia yale waliyoyasema mamlaka yoyote, wala hawana hoja yoyote juu yake wala ushahidi.
#
{144} ثم ذكر في الإبل والبقر مثل ذلك، فلما بيَّن بطلان قولهم وفساده؛ قال لهم قولاً لا حيلة لهم في الخروج من تَبِعَتِهِ إلا في اتباع شرع الله، {أم كنتُم شهداءَ إذ وصَّاكم اللهُ}؛ أي: لم يبق عليكم إلا دعوى لا سبيل لكم إلى صدقها وصحتها، وهي أن تقولوا: إن الله وصَّانا بذلك وأوحى إلينا كما أوحى إلى رسله، بل أوحى إلينا وحياً مخالفاً لما دعت إليه الرسل ونزلت به الكتب، وهذا افتراءٌ لا يجهلُه أحدٌ، ولهذا قال: {فمن أظلم ممَّنِ افترى على الله كذباً ليضلَّ الناس بغير علم}؛ أي: مع كذبه وافترائه على الله قصدُهُ بذلك [إضلال] عباد الله عن سبيل الله بغير بيِّنةٍ منه ولا برهانٍ ولا عقلٍ ولا نقلٍ. {إنَّ الله لا يهدي القوم الظالمين}: الذين لا إرادةَ لهم في غير الظلم والجور والافتراء على الله.
{144} Kisha akataja mfano wa hayo kuhusu ngamia na ng'ombe. Na alipobainisha ubatili wa kauli yao na ubovu wake, akawaambia jambo kauli ambayo hawana hila yoyote ya kutoka katika matokeo yake isipokuwa katika kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu. “Nyinyi mlishuhudia Mwenyezi Mungu alipowausia?” Yaani, hamjabaki na isipokuwa madai ambayo hamna njia ya kuisadikisha na kuifanya kuwa sahihi. Nayo ni kusema kuwa: Mwenyezi Mungu alituusia hilo, na akatuteremshia ufunuo katika alivyowateremshia Mitume wake. Bali alituteremshia ufunuo ulio kinyume na yale waliyolingania Mitume na yale vitabu viliteremka nayo. Na huku ni kuzua uongo ambako hakuna yeyote asiyekujua. Na ndiyo maana akasema: “Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu uongo, ili awapoteze watu bila ya elimu?" Yaani, pamoja na uongo wake na kuzua kwake uongo dhidi ya Mwenyezi Mungu, makusudio yake kwa hilo yakiwa ni [kuwapoteza] waja wa Mwenyezi Mungu kutoka kwenye njia ya Mwenyezi Mungu bila ya ushahidi wa wazi kutoka Kwake, wala uthibitisho, wala hoja ya kiakili, wala andiko. "Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu" ambao hawataki chochote isipokuwa dhuluma, na ukandamizaji, na kumzulia Mwenyezi Mungu uongo.
: 145 - 146 #
{قُلْ لَا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَنْ يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنْزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (145) وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ذَلِكَ جَزَيْنَاهُمْ بِبَغْيِهِمْ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ (146)}
145. Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharimishwa kwa mlaji kukila isipokuwa ikiwa ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani huo ni uchafu; au kilichovukiwa mipaka kilichochinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. 146. Na wale waliotubu (yani Mayahudi) tuliwaharamishia kila mwenye kwato au mguu usio na mgawanyiko. Na katika ng'ombe, na kondoo, na mbuzi tuliwaharamishia shahamu yao, isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao, au iliyochanganyika na mifupa. Hayo tuliwalipa kwa sababu ya uasi wao. Nasi bila ya shaka ni wakweli.
#
{145} لما ذكر تعالى ذمَّ المشركين على ما حرَّموا من الحلال ونسبوه إلى الله وأبطل قولهم؛ أمر تعالى رسولَه أن يبيِّن للناس ما حرَّمه الله عليهم؛ ليعلموا أنَّ ما عدا ذلك حلالٌ؛ مَنْ نسب تحريمه إلى الله فهو كاذب مبطل؛ لأنَّ التحريم لا يكون إلا من عند الله على لسان رسوله، وقد قال لرسوله: {قل لا أجِدُ فيما أوحي إليَّ محرَّماً على طاعم}؛ أي: محرَّماً أكله؛ بقطع النظر عن تحريم الانتفاع بغير الأكل وعدمه، {إلاَّ أن يكون ميتةً}: والميتة ما مات بغير ذكاةٍ شرعيةٍ؛ فإنَّ ذلك لا يحلُّ؛ كما قال تعالى: {حُرِّمَتْ عليكمُ الميتةُ والدَّمُ ولحمُ الخنزيرِ}، {أو دماً مَسْفوحاً}: وهو الدمُ الذي يخرج من الذبيحة عند ذكاتها؛ فإنه الدَّمُ الذي يضرُّ احتباسه في البدن؛ فإذا خرج من البدن؛ زال الضرر بأكل اللحم. ومفهوم هذا اللفظ أنَّ الدَّمَ الذي يبقى في اللحم والعروق بعد الذبح أنه حلالٌ طاهرٌ، {أو لحم خنزيرٍ فإنه رجسٌ}؛ أي: فإن هذه الأشياء الثلاثة رجسٌ؛ أي: خبث نجس مضرٌّ حرمه الله لطفاً بكم ونزاهة لكم عن مقاربة الخبائث {أو}: إلا أن يكونَ {فسقاً أهِلَّ لغيرِ الله به}؛ أي: إلا أن تكون الذبيحةُ مذبوحةً لغير الله من الأوثان والآلهة التي يعبُدها المشركون؛ فإن هذا من الفسق الذي هو الخروج عن طاعة الله إلى معصيته. ومع هذا؛ فهذه الأشياء المحرَّمات؛ مَن اضْطُرَّ إليها؛ أي: حملته الحاجة والضرورة إلى أكل شيء منها بأن لم يكن عنده شيء وخاف على نفسه التلف، {غيرَ باغٍ ولا عادٍ}؛ أي: {غير باغٍ}؛ أي: مريد لأكلها من غير اضطرار، ولا متعدًّ؛ أي: متجاوز للحدِّ؛ بأن يأكل زيادة عن حاجته، {فمَنِ اضطُرَّ غير باغٍ ولا عادٍ فإنَّ ربَّك غفور رحيم}؛ أي: فالله قد سامح من كان بهذه الحال. واختلف العلماء رحمهم الله في هذا الحصر المذكور في هذه الآية مع أن ثَمَّ محرماتٌ لم تُذْكَر فيها كالسباع وكل ذي مخلب من الطير ونحو ذلك: فقال بعضهم: إن هذه الآية نازلة قبل تحريم ما زاد على ما ذُكِرَ فيها؛ فلا ينافي هذا الحصر المذكور فيها التحريمَ المتأخِّرَ بعد ذلك؛ لأنه لم يجده فيما أوحي إليه في ذلك الوقت. وقال بعضهم: إن هذه الآية مشتملة على سائرِ المحرَّمات، بعضها صريحاً وبعضها يُؤْخَذ من المعنى وعموم العلة؛ فإنَّ قوله تعالى في تعليل الميتة والدم ولحم الخنزير أو الأخير منها فقط: {فإنَّه رِجْسٌ}: وصفٌ شاملٌ لكلِّ محرَّم؛ فإنَّ المحرمات كلَّها رجسٌ وخبثٌ، وهي من الخبائث المستقذرة التي حرَّمها الله على عبادِهِ صيانةً لهم وتكرمةً عن مباشرة الخبيث الرجس، ويؤخذ تفاصيل الرجس المحرَّم من السُّنَّةِ؛ فإنها تفسِّرُ القرآنَ وتبيِّنُ المقصودَ منه. فإذا كان الله تعالى لم يحرِّم من المطاعم إلا ما ذُكِرَ، والتحريمُ لا يكونُ مصدرُهُ إلا شرعَ الله؛ دلَّ ذلك على أن المشركين الذين حَرَّموا ما رزقهم اللهُ مفترون على الله، متقوِّلون عليه ما لم يقلْ. وفي هذه الآية احتمالٌ قويٌّ لولا أن الله ذكر فيها الخنزير، وهو أن السياق في نقض أقوال المشركين المتقدِّمة في تحريمهم لما أحلَّه الله وخوضهم بذلك بحسب ما سوَّلت لهم أنفسهم، وذلك في بهيمة الأنعام خاصة، وليس منها محرم إلاَّ ما ذكر في الآية؛ الميتة منها وما أهِلَّ لغير الله به، وما سوى ذلك؛ فحلال. ولعل مناسبة ذكر الخنزير هنا على هذا الاحتمال أنَّ بعض الجهَّال قد يُدْخِلُهُ في بهيمة الأنعام، وأنه نوعٌ من أنواع الغنم؛ كما قد يتوهَّمه جهلة النصارى وأشباههم، فينمونها كما ينمون المواشي، ويستحلُّونها، ولا يفرِّقون بينها وبين الأنعام.
{145} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwashutumu washirikina kwa yale waliyoyaharamisha ya halali na wakayanasibisha kwa Mwenyezi Mungu, na akaibatilisha kauli yao hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwaamrisha Mtume wake kwamba awabainishie watu yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaharamishia; ili wajue kuwa chochote kisichokuwa hayo ni halali; na mwenye kunasibisha kuharamishwa kwake kwa Mwenyezi Mungu, ni mwongo mwenye batili. Kwa sababu, kuharamisha hakutoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu juu ya ulimi wa Mtume wake, na tayari alikwisha mwambia Mtume wake: "Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji." Yaani, kilichoharamishwa kukila bila ya kuangalia uharamu wa kunufaika kwa kutokila na kutofanya hivyo, "isipokuwa ikiwa ni nyamafu." Na nyamafu ni yule aliyekufa bila kuchinjwa kisheria, kwa sababu huyo si halali. Kama yeye Mtukufu alivyosema: "Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe," "au damu inayomwagika." Nayo ni damu inayotoka katika mnyama aliyechinjwa anapochinjwa kisheria. Na hiyo ni damu ambayo inadhuru kuizuilia katika mwili. Na inapotoka nje ya mwili, basi madhara ya kuila nyama hiyo yanaondoka. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya aya hii ni kuwa damu inayobakia katika nyama na mishipa baada ya kuchinja ni halali na safi, "au nyama ya nguruwe, kwani huo ni uchafu;" yaani, vitu hivi vitatu ni uchafu, vyenye kudhuru, ambavyo Mwenyezi Mungu aliwaharamishia hivyo kwa sababu ya kuwafanyia upole kuwasafisha kutokana na kukaribia vichafu. "Au" isipokuwa ikiwa ni "kilichovukiwa mipaka katika kilichochinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu." Yaani, isipokuwa ikiwa mnyama huyo aliyechinjwa alichinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, miongoni mwa viabudiwa vyote na miungu ambao wanaiabudu washirikina. Basi hivi ni katika Fusuuq, ambayo ni kutoka katika utii kwa Mwenyezi Mungu hadi kwenye kumuasi. Na pamoja na haya, vitu hivi viliharamishwa, mwenye kulazimishwa kuvitumia. Yaani, haja na ulazima vilimpelekea kula kitu katika hivyo kama hakuwa na kitu, na akahofia nafsi yake kuharibika, "bila ya kutamani wala kupita mipaka." Na maana ya "bila ya kutamani" ni bila ya kutaka kukila bila ya kuwepo dharura, wala kuvuka mipaka, yaani kuvuka kikomo, kwa kula zaidi ya haja yake. "Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Yaani, Mwenyezi Mungu amemsamehe yule aliyekuwa katika hali hii. Na Wanachuoni, Mwenyezi Mungu awarehemu, wamehitalifiana kuhusu kufungia huku kulikotajwa katika Aya hii, pamoja na kwamba kuna vilivyoharamishwa ambavyo havikutajwa ndani yake. Kama vile wanyama wa porini wanaowinda, na kila ndege mwenye kucha za kuwindia na mfano wa hao. Basi baadhi yao walisema: Hakika Aya hii iliteremka kabla ya kuharamishwa kwa yale yaliyo zaidi ya yale yaliyotajwa ndani yake. Kwa hivyo, kufungia huku kulikotajwa ndani yake hakupingani na uharamu uliokuja baadaye baada ya hapo. Kwa sababu hakukupata katika yale yaliyoteremshwa kwake wakati huo. Na baadhi yao walisema: Hakika Aya hii inajumuisha vitu vyote vilivyoharamishwa, ambavyo baadhi yake viko waziwazi, na baadhi yake vinachukuliwa kutoka katika maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja na kutoka katika ujumla wa sababu. Kwa maana Kauli yake yeye Mtukufu katika kubainisha sababu ya maiti, na damu, na nyama ya nguruwe, au ya mwisho yake tu "kwani huo ni uchafu" ni maelezo yanayojumuisha kila kilichoharamishwa. Kwa sababu yale yote yaliyoharamishwa ni machafu na mabaya, nayo ni miongoni mwa mambo mabaya na machafu ambayo Mwenyezi Mungu amewaharamishia waja wake ili kuwalinda na kuwatukuza ili wasiguse mabaya na machafu. Na yanachukuliwa maelezo ya kina ya uchafu ulioharamishwa kutoka katika Sunnah. Kwa maana hiyo inaifafanua Qur-aani na inaeleza makusudio yake. Kwa hivyo ikiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuharamisha katika vyakula isipokuwa yale yaliyotajwa, na kuharamisha chanzo chake hakiwi isipokuwa sheria ya Mwenyezi Mungu. Hilo linaashiria kuwa washirikina ambao waliharamisha yale aliyowaruzuku Mwenyezi Mungu wanamzulia Mwenyezi Mungu uongo, wanasema kumhusu kwa yale ambayo hakuyasema. Na katika aya hii Kuna uwezekano mkubwa, lau Mwenyezi Mungu asingemtaja nguruwe ndani yake. Nao ni kuwa muktadha ni katika kukanusha kauli za washirikina zilizotangulia kuhusu kuharamisha kwao yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu na kuingia kwao katika hilo kulingana na yale ambayo nafsi zao zinawaambia; na hayo ni katika mifugo hasa. Na hakuna kilichoharamishwa katika hao isipokuwa wale waliotajwa katika aya hii, nyamafu wake na wale waliochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa mwenyezi Mungu, na wasiokuwa hao, basi hao ni halali. Na pengine sababu ya kumtaja nguruwe hapa kwa uwezekano huu ni kwamba baadhi ya watu wasiojua wanaweza kumuingiza katika mifugo, na kwamba yeye ni aina katika aina za kondoo. Kama walivyofikiri hivyo wajinga katika Wakristo na mfano wao, wakawa wanamkuza kama wanavyowakuza mifugo, na hawatofautishi baina yake na mifugo walio halali.
#
{146} فهذا المحرَّم على هذه الأمة كلِّها من باب التنزيه لهم والصيانة، وأما ما حُرِّم على أهل الكتاب؛ فبعضه طيب، ولكنه حُرِّم عليهم عقوبةً لهم، ولهذا قال: {وعلى الذين هادوا حَرَّمْنا كلَّ ذي ظُفُرٍ}: وذلك كالإبل وما أشبهها. وحرمنا عليهم من البقر والغنم بعضَ أجزائها، وهو شحومها وليس المحرَّم جميع الشحوم منها، بل شحم الإلية والثرب، ولهذا استثنى الشحم الحلال من ذلك، فقال: {إلَّا ما حَمَلَتْ ظهورُهُما أو الحوايا}؛ أي: الشحم المخالط للأمعاء، {أو ما اختلط بعظم ذلك} ـ: التحريم على اليهود ـ {جَزَيْناهم بِبَغْيهم}؛ أي: ظلمهم وتعدِّيهم في حقوق الله وحقوق عباده، فحرَّم الله عليهم هذه الأشياء عقوبةً لهم ونكالاً. {وإنا لصادقون}: في كلِّ ما نقول ونفعل ونحكم به، ومَن أصدقُ من الله حديثاً؟ ومن أحسنُ من الله حكماً لقوم يوقنون؟
{146} Basi haya yaliyoharimishwa kwa Ummah huu yote ni kwa njia ya kuwasafisha na kuwalinda. Na ama yale aliyowaharamishia Watu wa Kitabu, baadhi yake ni mazuri, lakini yaliharamishwa kwao kuwa ni adhabu kwao. Na ndiyo maana akasema, "Na wale waliotubu (yani Mayahudi) tuliwaharimishia kila mwenye kwato au mguu usio na mgawanyiko." Na hao ni kama vile ngamia na mfano wake. Na tuliwaharimishia baadhi ya sehemu za ng'ombe na kondoo, ambayo ni shahamu yao. Lakini kilichoharamishwa si shahamu yao yote, bali ni shahamu ya kwenye makalio na ile inayofunika rumeni na matumbo, na kwa sababu hiyo akatoa katika hilo shahamu iliyo halali. Akasema, "isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao." Yaani, shahamu iliyochanganyika na matumbo, "au iliyochanganyika na mifupa. Hayo" maharamisho kwa Mayahudi - "tuliwalipa kwa sababu ya uasi wao." Yaani, dhuluma yao na kuvuka kwao mipaka katika haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaharimishia vitu hivi kuwa ni mateso na adhabu kwao. "Nasi bila ya shaka ni wakweli" katika kila tunalolisema, na tunalolifanya, na tunalolihukumu kwalo. Na ni nani mkweli zaidi katika usemi kuliko Mwenyezi Mungu? Na ni nani mzuri zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa kaumu wenye yakini?
: 147 #
{فَإِنْ كَذَّبُوكَ فَقُلْ رَبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ (147)}
147. Na wakikukadhibisha, basi wewe sema: Mola wenu Mlezi ni Mwenye rehema iliyoenea. Wala haizuiwi adhabu yake kwa kaumu wahalifu.
#
{147} أي: فإن كذَّبك هؤلاء المشركون؛ فاسْتَمِرَّ على دعوتهم بالترغيب والترهيب، وأخبرْهم بأن الله {ذو رحمةٍ واسعةٍ}؛ أي: عامة شاملة لجميع المخلوقات كلِّها؛ فسارِعوا إلى رحمته بأسبابها التي رأسُها وأُسُّها ومادتها تصديق محمد - صلى الله عليه وسلم - فيما جاء به. {ولا يُرَدُّ بأسُهُ عن القوم المجرمين}؛ أي: الذين كَثُرَ إجرامهم وذنوبهم؛ فاحذَروا الجرائم الموصلة لبأس الله التي أعظمها ورأسها تكذيب محمد - صلى الله عليه وسلم -.
{147} Yaani, ikiwa washirikina hawa watakukadhibisha, basi endelea kuwalingania kwa kuwatia moyo na kuwatishia, na waambie kwamba Mwenyezi Mungu ni "Mwenye rehema iliyoenea." Yaani, ya jumla na yenye kuingia ndani yake viumbe vyote. Basi ikimbilieni rehema yake kwa sababu zake, ambazo kichwa chake, na msingi wake, na kiini chake ni kumsadiki Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – katika yale aliyokuja nayo. "Wala haizuiwi adhabu yake kwa kaumu wahalifu." Yaani, wale ambao uhalifu wao ni mwingi, na dhambi zao. Basi jihadharini na uhalifu mbalimbali unaofikisha kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu, ambayo kubwa zaidi yake na kichwa chake ni kumkadhibisha Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake.
: 148 - 149 #
{سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِنْ شَيْءٍ كَذَلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ حَتَّى ذَاقُوا بَأْسَنَا قُلْ هَلْ عِنْدَكُمْ مِنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا إِنْ تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنْتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ (148) قُلْ فَلِلَّهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ (149)}.
148. Watasema wale walioshirikisha, "Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, tusingelishirikisha, wala baba zetu, wala tusingeliharamisha kitu chochote." Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao mpaka walipoionja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo? Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu. 149. Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Na kama angelitaka, angeliwaongoa nyote.
#
{148} هذا إخبار من الله أن المشركين سيحتجُّون على شركهم وتحريمهم ما أحل الله بالقضاء والقدر، ويجعلون مشيئة الله الشاملة لكلِّ شيءٍ من الخير والشرِّ حجةً لهم في دفع اللوم عنهم، وقد قالوا ما أخبر الله أنهم سيقولونه؛ كما قال في الآية الأخرى: {وقال الذين أشْرَكوا لو شاءَ اللهُ ما عَبَدْنا من دونِهِ من شيءٍ ... } الآية فأخبر تعالى أنَّ هذه الحجة لم تزل الأممُ المكذِّبة تدفعُ بها عنهم دعوةَ الرسل ويحتجُّون بها، فلم تُجْدِ فيهم شيئاً ولم تنفعْهم، فلم يزلْ هذا دأبَهم حتى أهلكهم الله وأذاقهم بأسه؛ فلو كانت حجةً صحيحةً؛ لدفعتْ عنهم العقابَ، ولَمَا أحلَّ الله بهم العذاب؛ لأنَّه لا يحلُّ بأسه إلا بمن استحقه فعلم أنها حجة فاسدة وشبهة كاسدة من عدة أوجه: منها: ما ذكر الله من أنها لو كانت صحيحةً لم تحلَّ بهم العقوبة. ومنها: أن الحجة لا بدَّ أن تكون حجةً مستندةً إلى العلم والبرهان، فأما إذا كانت مستندةً إلى مجرَّد الظنِّ والخرص الذي لا يغني من الحقِّ شيئاً؛ فإنها باطلة، ولهذا قال: {قل هل عندَكم من علم فتخرِجوه لنا}؛ فلو كان لهم علمٌ ـ وهم خصومٌ ألدَّاء ـ لأخرجوه، فلما لم يخرِجوه؛ عُلِمَ أنه لا علم عندهم. {إن تتَّبعون إلَّا الظَّنَّ وإنْ أنتم إلَّا تَخْرُصُونَ}: ومن بنى حُججه على الخرص والظنِّ؛ فهو مبطل خاسر؛ فكيف إذا بناها على البغي والعناد والشرِّ والفساد.
{148} Huku ni kujulisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba washirikina watasimamisha hoja juu ya ushirikina wao na kuharamisha kwa yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu kwa Qadha (majaliwa) na Qadar (kutokea kwake). Na wanakufanya kutaka kwa Mwenyezi Mungu kunakojumuisha kila kitu miongoni mwa heri na mabaya kuwa ni hoja ya kuwazuia wao kulaumiwa. Na walisema yale aliyojulisha Mwenyezi Mungu kwamba watayasema; kama alivyosema katika Aya nyingine: "Na walisema wale walioshirikisha: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake" hadi mwisho wa Aya. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa hoja hii hawajaacha Umma mbalimbali wanaokadhibisha kuitumia kujizuia dhidi ya kulingania kwa Mitume na wanaitumia kama hoja yao, lakini haikuleta chochote ndani yao na wala haikuwanufaisha. Na haijaacha hii kuwa ndiyo tabia yao mpaka Mwenyezi Mungu akawaangamiza na akawaonjesha adhabu yake. Na ikiwa ingekuwa hoja sahihi, basi ingeliwazuia adhabu hiyo. Na Mwenyezi Mungu alipowafikishia adhabu, kwa sababu adhabu yake haimfikii isipokuwa mwenye kuistahiki, basi inajulikana kuwa ni hoja mbovu na dhana potofu katika njia nyingi: Miongoni mwake ni yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu kuwa lau ingekuwa ya kweli, basi adhabu haingewapata. Na miongoni mwake ni kwamba, Hoja ni lazima iwe ni hoja yenye msingi wa elimu na ushahidi. Na ama ikiwa imeegemezwa juu ya dhana tu na kukisia, ambako hakunufaishi chochote mbele ya haki, basi hiyo ni batili. Na ndiyo maana akasema, "Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo?" Na lau wangekuwa na elimu - na wao ni wapinzani wakubwa mno- wangeitoa. Na pindi hawakuitoa, ilijulikana kuwa hawana elimu yoyote. "Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu." Na mwenye kuijenga hoja zake juu ya makisio na dhana, basi yeye yuko katika batili na mwenye hasara. Basi itakuwaje ikiwa ataijenga juu ya uasi, na ukaidi, na uovu, uharibifu?
#
{149} ومنها: أن الحجة لله، البالغة، التي لم تبقِ لأحدٍ عذراً، التي اتَّفقت عليها الأنبياء والمرسلون والكتب الإلهية والآثار النبوية والعقول الصحيحة والفطر المستقيمة والأخلاق القويمة، فعلم بذلك أن كلَّ ما خالف هذه الآية القاطعة باطلٌ؛ لأن نقيض الحقِّ لا يكون إلاَّ باطلاً. ومنها: أن الله تعالى أعطى كلَّ مخلوق قدرةً وإرادةً يتمكَّن بها من فعل ما كُلِّفَ به؛ فلا أوجب الله على أحدٍ ما لا يقدر على فعله، ولا حرَّم على أحدٍ ما لا يتمكَّن على تركه؛ فالاحتجاج بعد هذا بالقضاء والقدر ظلمٌ محضٌ وعنادٌ صرفٌ. ومنها: أن الله تعالى لم يجبر العباد على أفعالهم، بل جعل أفعالهم تبعاً لاختيارهم؛ فإن شاؤوا فعلوا وإن شاؤوا كَفُّوا، وهذا أمر مشاهدٌ لا ينكره إلا مَن كابر وأنكر المحسوسات؛ فإنَّ كلَّ أحد يفرق بين الحركة الاختياريَّة والحركة القسريَّة، وإن كان الجميع داخلاً في مشيئة الله ومندرجاً تحت إرادته. ومنها: أن المحتجِّين على المعاصي بالقضاء والقدر يتناقضون في ذلك؛ فإنهم لا يمكنهم أن يطردوا ذلك؛ بل لو أساء إليهم مسيء بضرب أو أخذ مال أو نحو ذلك، واحتج بالقضاء والقدر لما قبلوا منه هذا الاحتجاج ولغضبوا من ذلك أشد الغضب. فيا عجباً كيف يحتجون به على معاصي الله ومساخطه ولا يرضون من أحد أن يحتج به في مقابلة مساخطهم. ومنها: أن احتجاجهم بالقضاء والقدر ليس مقصوداً، ويعلمون أنَّه ليس بحجةٍ، وإنما المقصود منه دفع الحقِّ ويرون أن الحقَّ بمنزلة الصائل؛ فهم يدفعونه بكلِّ ما يخطر ببالهم من الكلام، [ولو كانوا يعتقدونه خطأً].
{149} Na miongoni mwake ni kuwa, hoja ni ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni ya kukata, ambayo hakubaki yeyote na udhuru wowote, na ambayo walikubaliana juu yake Manabii na Mitume, na Vitabu vya Mwenyezi Mungu, na hadithi za unabii, na akili timamu, na umbile la asili lilionyooka, na maadili mema. Kwa hivyo, ikajulikana kwa hilo kuwa kila kitu kinachopingana na aya hii ya mkato ni batili. Kwa sababu kinyume cha haki hakiwi isipokuwa batili. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa kila kiumbe uwezo na utashi anayoweza kwayo kufanya kile alichoamrishwa kufanya. Na Mwenyezi Mungu hakumlazimisha yeyote kufanya kile asichoweza, kufanya, wala hakumharamishia yeyote kile asichoweza kukiacha. Basi kutumia majaliwa na matokea yake kama hoja baada ya hayo, ni dhuluma tupu na ukaidi mtupu. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwalazimisha waja wake kufanya vitendo vyao. Bali aliyafanya matendo yao kufuatana na chaguo lao. Wakitaka, wanafanya, na wakitaka wanaacha. Na hili ni jambo linaloshuhudiwa na halikatai isipokuwa mwenye kiburi na akayakataa mambo ya hisia. Kwa maana kila mwenye kutofautisha kati ya harakati za hiari na harakati za kulazimishwa, ingawa zote hizo zinaingia katika mapenzi ya mwenyezi Mungu na yako chini ya kutaka kwake. Na miongoni mwake ni kwamba, wale wanaotumia majaliwa na matokeo yake juu ya kufanya maasia wanapingana katika hilo. Kwani hawawezi kuitumia katika kila hali. Bali lau kama mkosaji angewafanyia kosa kwa kuwapiga au kuchukua mali yao au mfano wa hayo, na akatumia majaliwa ya Mwenyezi Mungu na matokeo yake kuwa hoja yake, hawangekubali hoja hii kutoka kwake, na wangekasirika sana juu ya hilo. Basi ee maajabu haya! Vipi wanaitumia kama hoja juu ya kumuasi mwenyezi Mungu, na machukizo yake, wala hawakubali kwa yeyote kuitumia kama hoja yake dhidi ya yale yenye kuwakasirisha? Na miongoni mwake ni kwamba, kutumia majaliwa na matokeo yake kama hoja siyo makusudio yao, na wanajua vyema kuwa si hoja. Bali makusudio katika hilo ni kuipinga haki, na wanaona kuwa haki iko sawa na kitu kipya kilichowaingilia. Kwa hivyo wanaizuia kwa kila kitu kinachokuja akilini mwao miongoni mwa maneno [hata kama wanaitakidi kuwa ni kosa].
: 150 #
{قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّهَ حَرَّمَ هَذَا فَإِنْ شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُمْ بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ (150)}.
150. Sema: Waleteni mashahidi wenu ambao wanashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu amewaharamisha hawa. Kwa hivyo, wakishuhudia, basi wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya wale waliozikadhibisha Ishara zetu, na ambao hawaamini katika Akhera, nao wanamlinganisha Mola wao Mlezi na wengine.
#
{150} أي: قل لمن حرَّم ما أحل الله ونسب ذلك إلى الله: أحضِروا شهداءكم الذين يشهدون أن الله حرَّم هذا! فإذا قيل لهم هذا الكلام؛ فهم بين أمرين: إما أن لا يحضروا أحداً يشهدُ بهذا، فتكون دعواهم إذاً باطلةً خليةً من الشهود والبرهان. وإما أن يحضِروا أحداً يشهد لهم بذلك، ولا يمكن أن يشهد بهذا إلا كلُّ أفاكٍ أثيم غير مقبول الشهادة، وليس هذا من الأمور التي يصحُّ أن يشهد بها العدولُ، ولهذا قال تعالى ناهياً نبيَّه وأتباعه عن هذه الشهادة: {فإن شهدوا فلا تَشْهَدْ معهم ولا تتَّبِعْ أهواء الذين كذَّبوا بآياتنا والذين لا يؤمنون بالآخرة وهم بربِّهم يعدِلون}؛ أي: يسوون به غيره من الأنداد والأوثان؛ فإذا كانوا كافرين باليوم الآخر غير موحدين لله؛ كانت أهويتهم مناسبة لعقيدتهم، وكانت دائرة بين الشرك والتكذيب بالحق، فحريٌّ بهوىً هذا شأنه أن ينهى الله خيارَ خلقه عن اتِّباعه، وعن الشهادة مع أربابه، وعُلِمَ حينئذٍ أن تحريمهم لما أحلَّ اللهُ صادرٌ عن تلك الأهواء المضلَّة.
{150} Yaani, mwambie yule aliyeyaharamisha yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu na akayanasibisha hayo kwa Mwenyezi Mungu: Waleteni mashahidi wenu ambao wanashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ameyaharamisha haya! Na wakiambiwa maneno haya, basi wako baina ya mambo mawili: Ima wasimlete yeyote kushuhudia haya, basi madai yao yakawa ni batili, yasiyokuwa na mashahidi na ushahidi. Na ima wamlete yeyote anayewashuhudia hilo. Na hakuna anayaweza kushuhudia hayo isipokuwa kila mwongo mkubwa mwenye dhambi asiyekubaliwa ushahidi wake. Na hili si katika mambo ambayo inaruhusika kwa waadilifu kuyashuhudia. Na ndiyo maana Akasema yeye Mtukufu, akimkataza Nabii wake na wafuasi wake ushahidi huu: "Kwa hivyo, wakishuhudia, basi wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya wale waliozikadhibisha Ishara zetu, na ambao hawaamini katika Akhera, nao wanamlinganisha Mola wao Mlezi na wengine." Yaani, wanawafanya wengine kuwa sawa na Yeye miongoni mwa wenza, na viabudiwavyo vyote. Na ikiwa waliikufuru Siku ya Mwisho na hawampwekeshi Mwenyezi Mungu, matamanio yao yanakuwa yenye kuafikiana na itikadi zao, na yanakuwa yenye kuzunguka baina ya ushirikina na ukadhibishaji wa haki. Kwa hivyo ikafaa zaidi kwa matamanio ambayo hii ndiyo hali yake kwamba Mwenyezi Mungu awakataze walio bora zaidi wa viumbe vyake kuyafuata, na kushuhudia pamoja na mabwana wake, na ikajulikana hapo kwamba kuharamisha kwao yale ambayo Mwenyezi Mungu alihalalisha kulitokana na matamanio hayo potofu.
: 151 - 153 #
{قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ مِنْ إِمْلَاقٍ نَحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ (151) وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّى يَبْلُغَ أَشُدَّهُ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَى وَبِعَهْدِ اللَّهِ أَوْفُوا ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ (152) وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ (153)}.
151. Sema: Njooni niwasomee yale aliyowaharimishia Mola wenu Mlezi. Kwamba msimshirikishe Yeye na chochote, na wazazi wawili wafanyieni uzuri, wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunawaruzuku nyinyi na wao. Wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri yake, na yaliyofichikana yake. Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu aliiharimisha isipokuwa kwa haki. Hayo aliwausia ili myatie akilini. 152. Wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kile kilicho kizuri kabisa mpaka afike utu uzima wake. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatuibebeshi nafsi isipokuwa kwa uwezo wake. Na mnaposema, basi fanyeni uadilifu hata kama ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu,itimizeni. Hayo amewausia ili mkumbuke. 153. Na kwamba hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Wala msifuate njia nyinginezo, zikawatengeni na Njia yake. Haya amewausia ili mmche (Mwenyezi Mungu).
#
{151} يقول تعالى لنبيِّه - صلى الله عليه وسلم -: {قل}: لهؤلاء الذين حرَّموا ما أحلَّ الله: {تعالَوْا أتلُ ما حرَّمَ ربُّكم عليكم}: تحريماً عامًّا شاملاً لكل أحد، محتوياً على سائر المحرَّمات من المآكل والمشارب والأقوال والأفعال، {أن لا تشركوا به شيئاً}؛ أي: لا قليلاً ولا كثيراً. وحقيقة الشرك بالله أن يُعْبَدَ المخلوق كما يُعْبَدُ الله أو يعظَّمَ كما يعظَّمُ الله أو يصرفَ له نوعٌ من خصائص الربوبيَّة والإلهيَّة، وإذا تَرَكَ العبدُ الشرك كلَّه؛ صار موحِّداً مخلصاً لله في جميع أحواله؛ فهذا حقُّ الله على عباده: أن يعبُدوه ولا يشرِكوا به شيئاً. ثم بدأ بآكد الحقوق بعد حقه، فقال: {وبالوالدينِ إحساناً}: من الأقوال الكريمة الحسنة والأفعال الجميلة المستحسنة؛ فكلُّ قول وفعل يحصُلُ به منفعة للوالدين أو سرور لهما؛ فإنَّ ذلك من الإحسان، وإذا وُجِدَ الإحسان؛ انتفى العقوق، {ولا تقتلوا أولادكم}: من ذكور وإناث {من إملاق}؛ أي: بسبب الفقر وضيقكم من رزقهم؛ كما كان ذلك موجوداً في الجاهلية القاسية الظالمة، وإذا كانوا منهيِّين عن قتلهم في هذه الحال وهم أولادهم؛ فنهيهم عن قتلهم لغير موجب أو قتل أولاد غيرهم من باب أولى وأحرى. {نحن نرزُقُكم وإياهم}؛ أي: قد تكفَّلنا برزق الجميع، فلستم الذين ترزقون أولادكم، بل ولا أنفسكم، فليس عليكم منهم ضيق. {ولا تقرَبوا الفواحش}: وهي الذنوب العظام المستفحشة {ما ظهر منها وما بطن}؛ أي: لا تقربوا الظاهر منها والخفي أو المتعلق منها بالظاهر والمتعلق بالقلب والباطن، والنهي عن قربان الفواحش أبلغ من النهي عن مجرَّد فعلها؛ فإنه يتناول النهي عن مقدِّماتها ووسائلها الموصلة إليها. {ولا تقتُلوا النفس التي حرَّم الله}: وهي النفس المسلمة من ذكر وأنثى صغير وكبير بَرٍّ وفاجر: والكافرة التي قد عُصِمَتْ بالعهد والميثاق، {إلَّا بالحقِّ}: كالزاني المحصن والنفس بالنفس والتارك لدينه المفارق للجماعة. {ذلكم}: المذكور، {وصَّاكم} [الله] {به لعلَّكم تعقِلون}: عن الله وصيَّته ثم تحفظونها ثم تراعونها وتقومونَ بها. ودلَّت الآية على أنه بحسب عقل العبد يكون قيامه بما أمر الله به.
{151} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake-rehema na amani zimshukie-: "Sema" uwaambie hawa walioharamisha yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu: "Njooni niwasomee yale aliyowaharamishia Mola wenu Mlezi," kuharamisha kwa jumla kwenye kumuingiza ndani yake kila mmoja, kwenye kujumuisha maharamisho yote miongoni mwa vyakula, na vinywaji, na maneno, na vitendo. "Kwamba msimshirikishe Yeye na chochote;" yaani, si kidogo wala si kingi. Na uhakika wa kumshirikisha Mwenyezi Mungu ni kwamba kiumbe aabudiwe kama Mwenyezi Mungu anavyoabudiwa, au kutukuzwa kama anavyotukuzwa Mwenyezi Mungu, au kufanyiwa jambo ambalo ni katika mambo maalumu ya Umola na Uungu. Na ikiwa mja ataiacha shirki yote, anakuwa mpwekeshaji, mwenye kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika hali zake zote. Na kwa sababu ya hili ikawa haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake kwamba wamuabudu wala wasimshirikishe na chochote. Kisha akaanza na haki kubwa zaidi baada ya haki, akasema: "Na wazazi wawili wafanyieni uzuri," miongoni mwa maneno mema, mazuri, na matendo mazuri yapendezayo. Kwa hivyo kila neno na tendo lenye kuleta manufaa kwa wazazi wawili au furaha kwao, basi hilo ni katika uzuri. Na ikiwa uzuri utapatikana, basi uasi kwao unakosa kuwepo. "Wala msiwauwe watoto wenu" wa kiume na wa kike; "kwa sababbu ya umasikini." Yaani, kwa sababu ya umasikini na dhiki yenu kwa sababu ya kuwapa riziki, kama hilo lilivyokuwepo katika zama za ujinga mkubwa wenye dhaluma. Na ikiwa walikatazwa kuwaua katika hali hii ilhali ni watoto wao, basi kuwakataza kuwaua bila ya sababu au kuwaua watoto wa watu wengine ni jambo linalostahili na kufaa zaidi. "Sisi tunawaruzuku nyinyi na wao;" yaani, tumekwisha chukua dhamana ya kuwaruzuku wote. Basi si nyinyi mnaowaruzuku watoto wenu, na hata kujiruzuku nyinyi wenyewe, kwa hivyo hamna dhiki ya kuwafanyia hilo. "Wala msikaribie machafu," nayo ni madhambi makubwa na machafu "yaliyo dhahiri yake, na yaliyofichikana yake." Yaani, msiyakaribie yaliyo dhahiri yake na yaliyofichikana, au yanayohusiana na dhahiri na yanayohusiana na moyo na ndani. Na katazo la kuyakaribia machafu ni kubwa zaidi kuliko kukataza tu kuyafanya. Kwa maana hili linajumuisha kukataza vitangulizi vyake na njia zake zinazoyafikia. "Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu aliiharamisha;" nayo ni nafsi ya Kiislamu, ya kiume na ya kike, changa na nzee, njema na ovu, na ya kikafiri ambayo amekingwa kwa ahadi na agano; "isipokuwa kwa haki." Kama vile mzinifu aliyeoleka, na nafsi kwa nafsi, na mwenye kuacha dini yake na kujitenga na umma. "Hayo" yaliyotajwa "aliwausia" [Mwenyezi Mungu] "ili myatie akilini" kutoka kwa Mwenyezi Mungu wasia wake, kisha muihifadhi, kisha muizingatie, na muitekeleze. Na Aya hii iliashiria kwamba kulingana na akili ya mja, kunakuwa kusimamisha kwake kile ambacho mwenyezi Mungu alimuamrisha.
#
{152} {ولا تقربوا مال اليتيم}: بأكل أو معاوضة على وجه المحاباة لأنفسكم أو أخذ من غير سبب، {إلا بالتي هي أحسنُ}؛ أي: إلاَّ بالحال التي تصلُحُ بها أموالهم وينتفعون بها، فدل هذا على أنه لا يجوز قربانها والتصرُّف بها على وجه يضرُّ اليتامى أو على وجه لا مضرَّة فيه ولا مصلحة. {حتى يبلغَ}: اليتيم {أشدَّه}؛ أي: حتى يبلغ ويرشد ويعرف التصرف؛ فإذا بلغ أشُدَّه؛ أعطي حينئذ ماله، وتصرف فيه على نظره. وفي هذا دلالة على أن اليتيم قبل بلوغ الأشدِّ محجورٌ عليه، وأن وليَّه يتصرَّف في ماله بالأحظ، وأنَّ هذا الحجر ينتهي ببلوغ الأشدِّ. {وأوفوا الكيلَ والميزان بالقسْط}؛ أي: بالعدل والوفاء التامِّ؛ فإذا اجتهدتم في ذلك؛ فلا {نُكَلِّفُ نفساً إلَّا وُسْعَها}؛ أي بقدر ما تسعه ولا تضيق عنه؛ فمن حرص على الإيفاء في الكيل والوزن، ثم حصل منه تقصيرٌ؛ لم يفرِّط فيه ولم يعلَمْه؛ فإن الله غفور رحيم. وبهذه الآية [ونحوها] استدل الأصوليون بأن الله لا يكلِّف أحداً ما لا يطيق، وعلى أنَّ من اتَّقى الله فيما أمر وفَعَلَ ما يمكِنُهُ من ذلك؛ فلا حرج عليه فيما سوى ذلك. {وإذا قلتُم}: قولاً تحكمون به بين الناس، وتفصلون بينهم الخطاب، وتتكلَّمون به على المقالات والأحوال، {فاعدِلوا}: في قولكم بمراعاة الصدق فيمن تحبُّون ومَنْ تكرهون والإنصافِ وعدم كتمان ما يلزمُ بيانُهُ؛ فإنَّ الميل على من تكره بالكلام فيه أو في مقالته من الظلم المحرم، بل إذا تكلَّم العالم على مقالات أهل البدع؛ فالواجبُ عليه أن يعطي كلَّ ذي حقٍّ حقَّه وأن يبيِّن ما فيها من الحقِّ والباطل، ويعتبرَ قربَها من الحقِّ وبعدها منه، وذكر الفقهاء أنَّ القاضي يجب عليه العدلُ بين الخصمين في لحظِهِ ولفظِهِ. {وبعهد الله أوفوا}: وهذا يشملُ العهد الذي عاهده عليه العباد؛ من القيام بحقوقه والوفاء بها، ومن العهد الذي يقع التعاهد به بين الخلق؛ فالجميع يجب الوفاءُ به، ويحرُم نقضُه والإخلال به. {ذلكم}: الأحكام المذكورة، {وصَّاكُم} [الله] {به لعلَّكم تَذَكَّرونَ}: ما بيَّنه لكم من الأحكام، وتقومون بوصية الله لكم حقَّ القيام، وتعرفون ما فيها من الحِكم والأحكام.
{152} "Wala msiikaribie mali ya yatima" kwa kula au kuibadilishana kwa namna ya kujipa bure, au kuichukua bila ya sababu yoyote, "isipokuwa kile kilicho kizuri kabisa;" yaani, isipokuwa katika hali ambayo mali yao inabaki kuwa nzuri na wananufaika kwayo. Kwa hivyo, hili likaashiria kuwa hairuhusiwi kuikaribia kuitumia kwa njia inayowadhuru mayatima au kwa njia isiyokuwa na madhara wala manufaa; "mpaka afike" yatima huyo "utuuzima wake." Yaani, mpaka abaleghe na aweze kuwa wa kufanya uamuzi mzuri, na ajue namna ya kutenda mambo vyema. Kwa hivyo, anapofikia utuuzima wake, anapewa wakati huo mali yake, na inatumiwa chini ya uangalizi wake. Na katika hili kuna ishara ya kwamba yatima kabla ya kufikia utuuzima anazuiwa kusimamia mali yake, na kwamba mlezi wake anaendesha mali yake kwa kilicho bora zaidi kwake, na kwamba kuzuia huku kunaisha kwa kufikia utuuzima. "Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu;" yaani, kwa uadilifu na kutimika kukamilifu. Na mkifanya juhudi katika hayo, kwa bidii; basi "hatuibebeshi nafsi isipokuwa kwa uwezo wake." Yaani, kwa kiwango inavyoweza, wala hatuifanyii ugumu. Kwa hivyo, mwenye kufanya juhudi katika kutimiza kipimo cha wingi na cha uzito, kisha upungufu fulani ukapatikana kutoka kwake, lakini yeye hakupuuza katika hilo wala hakujua hilo, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. Na kwa Aya hii [na mfano wake], wanazuoni wa Misingi ya Fiqh waliitumia kama ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu hamtwiki yeyote asichokiweza, na kwamba mwenye kumcha Mwenyezi Mungu katika yale aliyoyaamrisha na akafanya yale anayoweza katika hayo, basi hakuna ubaya juu yake katika yasiyokuwa hayo. "Na mnaposema" neno ambalo kwalo mnahukumu baina ya watu, na mnatenganisha mazungumzo baina yao, na mkazungumza kwalo kwa maneno na hali mbalimbali, "basi fanyeni uadilifu" katika kauli yenu kwa kuzingatia ukweli kwa yule mnayempenda na yule mnayemchukia, na uadilifu, na kutoficha kile kinachohitaji kubainishwa. Kwa maana, kuegemea dhidi ya yule unayemchukia kwa kusema juu yake au katika mazungumzo yake kuna dhuluma iliyoharamishwa. Bali mwanachuoni akizungumzia maneno ya watu wa uzushi katika dini, basi la wajibu kwake ni kumpa kila mwenye haki haki yake na kwamba kueleza yale yaliyo ndani yake ya haki na batili, na azingatie ukaribu wake na haki, na umbali wake kutoka kwayo. Na wanachuoni wa Fiqh walitaja kwamba kadhi inamlazimu awe mwadilifu baina ya wapinzani wawili katika mtazamo wake na kauli yake. "Na ahadi ya Mwenyezi Mungu,itimizeni." Na hili linajumuisha ahadi aliyowafungia waja wake kama vile kuzitekeleza haki zake na kuzitimiza, na pia ahadi wanayofunga viumbe baina yao. Basi hizo zote ni lazima kizitimiza, na ni haramu kuzibatilisha na kuzikiuka. "Hayo" yaliyotajwa miongoni mwa hukumu mbalimbali, "amewausia" [Mwenyezi Mungu] "kwayo ili mkumbuke" yale Aliyowabainishia miongoni mwa hukumu mbalimbali, na mtekeleze wasia wa Mwenyezi Mungu kwenu kama inavyostahiki, na mjue yale yaliyomo ya hekima na hukumu mbalimbali.
#
{153} ولما بيَّن كثيراً من الأوامر الكبار والشرائع المهمَّة؛ أشار إليها وإلى ما هو أعمُّ منها، فقال: {وأنَّ هذا صراطي مستقيماً}؛ أي: هذه الأحكام وما أشبهها مما بيَّنه الله في كتابه ووضَّحه لعباده صراطُ الله الموصل إليه وإلى دار كرامته المعتدل السهل المختصر. {فاتَّبِعوه}: لتنالوا الفوزَ والفلاح، وتدركوا الآمالَ والأفراح، {ولا تتَّبِعوا السُّبُلَ}؛ أي: الطرق المخالفة لهذا الطريق، {فتفرَّقَ بكم عن سبيلِهِ}؛ أي: تضلُّكم عنه وتفرِّقكم يميناً وشمالاً؛ فإذا ضللتُم عن الصراط المستقيم؛ فليس ثمَّ إلا طرق توصِلُ إلى الجحيم. {ذلكم وصَّاكم به لعلَّكم تتَّقون}: فإنكم إذا قمتُم بما بيَّنه الله لكم علماً وعملاً؛ صرتُم من المتَّقين وعباد الله المفلحين. ووحَّد الصراطَ وأضافه إليه؛ لأنَّه سبيلٌ واحدٌ موصلٌ إليه، والله هو المعين للسالكين على سلوكِهِ.
{153} Na alipobainisha nyingi katika amri kubwa na sheria muhimu, Akayaashiria na kwa kile kilicho cha jumla zaidi yake, kwa hivyo akasema: "Na kwamba hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka." Yaani, hukumu hizi na mfano wake miongoni mwa yale aliyoyabainisha Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake na akayaweka wazi kwa waja wake ndio Njia ya Mwenyezi Mungu inayofikisha Kwake na kwenye nyumba ya utukufu wake, ambayo ni ya wastani, nyepesi, na fupi. "Basi ifuateni" ili mpate kufuzu na kufaulu, na mfikie matumaini na furaha mbalimbali, "Wala msifuate njia nyinginezo." Yaani, njia zinazohalifiana na Njia hii, "zikawafarikisha na Njia Yake;" yaani, zikawapoteza Njia hiyo, na zikawatawanya kulia na kushoto. Na mkipotea Njia hiyo iliyonyooka, basi hapo hakuna isipokuwa njia nyinginezo zinazofikisha katika Jahiim. "Haya amewausia ili mmche (Mwenyezi Mungu)." Kwani ikiwa mtafanya yale aliyowabainishia Mwenyezi Mungu kwa elimu na matendo, mtakuwa miongoni mwa Wachamungu, na waja wa Mwenyezi Mungu waliofaulu. Na Aliifanya Njia yake kuwa moja na akainasibisha naye Mwenyewe, kwa sababu ni njia moja tu inayofikisha Kwake, na Mwenyezi Mungu ndiye anayewasaidia wanafuata katika kuifuata.
: 154 - 157 #
{ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَعَلَّهُمْ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ (154) وَهَذَا كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ (155) أَنْ تَقُولُوا إِنَّمَا أُنْزِلَ الْكِتَابُ عَلَى طَائِفَتَيْنِ مِنْ قَبْلِنَا وَإِنْ كُنَّا عَنْ دِرَاسَتِهِمْ لَغَافِلِينَ (156) أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنْزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَى مِنْهُمْ فَقَدْ جَاءَكُمْ بَيِّنَةٌ مِنْ رَبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنْ كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَصَدَفَ عَنْهَا سَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ (157)}.
154. Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) yule aliyefanya uzuri, na kuwa ni maelezo kina ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili waamini katika kukutana na Mola wao Mlezi. 155. Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa. Basi kifuateni, na mcheni, ili mrehemewe. 156. Mkaja kusema, “Hakika waliteremshiwa Kitabu makundi mawili tu kabla yetu, na sisi tulikuwa hatuna habari ya waliyokuwa wakiyasoma.” 157. Au mkasema: "Lau hakika sisi tungeteremshiwa Kitabu hicho, basi tungelikuwa waongofu zaidi kuwaliko wao." Basi hakika imekwisha wajia hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Kwa hivyo, ni nani aliye dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Ishara zetu adhabu mbaya kabisa kwa sababu ya walivyokuwa wakijitenga.
#
{154} {ثم} في هذا الموضع ليس المراد منها الترتيب الزماني؛ فإن زمن موسى عليه السلام متقدِّم على تلاوة الرسول محمد - صلى الله عليه وسلم - هذا الكتاب، وإنما المراد الترتيب الإخباري،. فأخبر أنه آتى {موسى الكتاب}: وهو التوراة {تماماً}: لنعمته وكمالاً لإحسانه، {على الذي أحسن}: من أمة موسى؛ فإنَّ الله أنعم على المحسِنين منهم بنعم لا تُحصى من جُملتها وتمامها إنزال التوراة عليهم، فتمت عليهم نعمةُ الله ووَجَبَ عليهم القيام بشكرها، {وتفصيلاً لكلِّ شيء}: يحتاجون إلى تفصيله من الحلال والحرام والأمر والنهي والعقائد ونحوها، {وهدىً ورحمةً}؛ أي: يهديهم إلى الخير ويعرِّفهم بالشرِّ في الأصول والفروع، {ورحمة}: يحصُلُ به لهم السعادة والرحمة والخير الكثير، {لعلَّهم}: بسبب إنزالنا الكتاب والبيِّنات عليهم {بلقاءِ ربِّهم يؤمنونَ}؛ فإنه اشتمل من الأدلَّة القاطعة على البعث والجزاء بالأعمال، [ما] يوجب لهم الإيمان بلقاء ربِّهم والاستعداد له.
{154} Neno "Tena" katika nafasi hii, halikukusudiwa mpangilio wa matukio. Kwa maana zama za Musa, amani zimshukie, zilitangulia kusoma kwa Mtume Muhammad - rehema na amani ziwe juu yake - kitabu hiki. Na kilichokusudiwa ni mpangilio wa kutoa habari. Kwa hivyo, akajulisha kwamba alimpa "Musa Kitabu" ambacho ni Taurati "kwa kumtimizia" neema yake na ukamilifu wa ihsani yake, kwa "yule aliyefanya uzuri" katika umma wa Musa. Kwa maana, Mwenyezi Mungu aliwaneemesha wale wafanyao mazuri miongoni mwao kwa neema zisizodhibitika, ambazo miongoni mwake na utimilifu wake ni kuteremsha Taurati kwao. Basi ikatimia neema ya Mwenyezi Mungu juu yao, na ikawalazimu kuishukuru. "Na kuwa ni maelezo kina ya kila kitu" wanachohitaji kibainishwe, cha halali na haramu, na amri na makatazo, na itikadi na mfano wake, "na uwongofu na rehema." Yaani, inawaongoa kwenye heri, na inawajulisha shari katika misingi ya dini na matawi yake, "na rehema" ambayo kwayo wanapata furaha, na rehema, na heri nyingi; "ili" kwa sababu ya kukiteremsha kwetu Kitabu na hoja zilizo wazi kwao "waamini katika kukutana na Mola wao Mlezi." Kwani inajumuisha ushahidi mbalimbali wa uhakika juu ya kufufuliwa na malipo kwa matendo, [ambayo] yanawafanya kuamini katika kukutana na Mola wao Mlezi na kujiandaa kwa ajili ya hilo.
#
{155} {وهذا}: القرآن العظيم والذِّكْر الحكيم، {كتابٌ أنزلْناه مبارَكٌ}؛ أي: فيه الخير الكثير والعلم الغزير، وهو الذي تستمدُّ منه سائر العلوم وتستخرجُ منه البركاتُ؛ فما من خيرٍ إلاَّ وقد دعا إليه ورغَّب فيه وذكر الحِكَمَ والمصالح التي تحثُّ عليه، وما من شرٍّ إلا وقد نهى عنه وحذَّر منه وذكر الأسباب المنفِّرة عن فعله وعواقبها الوخيمة. {فاتَّبعوه}: فيما يأمر به وينهى، وابنوا أصولَ دينِكُم وفروعه عليه. {واتَّقوا}: الله تعالى أن تخالفوا له أمراً {لعلَّكم}: إن اتَّبعتموه {تُرْحَمونَ}: فأكبر سبب لنيل رحمة الله اتِّباعُ هذا الكتاب علماً وعملاً.
{155} "Na hiki" yaani Qur-aani hii Tukufu, na ukumbusho wenye hekima "ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa." Yaani, ndani yake kuna kheri nyingi na elimu tele, nayo ndiyo ambayo zinatolewa elimu nyinginezo zote, zinatolewa humo baraka. Basi hakuna kheri yoyote isipokuwa iliita kwayo na ilitia moyo wa kuiendea, na ikataja hekima mbalimbali na maslahi ambayo yanahimiza juu yake. Na hakuna uovu wowote isipokuwa iliukataza na kuonya dhidi yake, na ikataja sababu za kujitenga na kuufanya na matokeo yake mabaya. "Basi kifuateni" katika yale inayoyaamrisha na kuyakataza. Na jengeni misingi ya dini yenu na matawi yake juu yake. "Na mcheni" Mwenyezi Mungu Mtukufu mkaja mkahalifu amri yake yoyote "ili" mkiifuata "mrehemewe." Basi sababu kubwa zaidi ya kupata rehema ya Mwenyezi Mungu ni kukifuata kitabu hiki kwa elimu na vitendo.
#
{156} {أن تقولوا إنَّما أنزِلَ الكتاب على طائفتين من قبلنا وإن كنَّا عن دراستِهِم لغافلينَ}؛ أي: أنزلنا إليكم هذا الكتاب المبارك قطعاً لحجَّتكم وخشيةَ أن تقولوا إنما أنزل الكتابُ على طائفتين من قبلنا؛ أي اليهود والنصارى. {وإن كنَّا عن دراستِهِم لغافلينَ}؛ أي: تقولون: لم تنزِلْ علينا كتاباً، والكتب التي أنزلتها على الطائفتين ليس لنا بها علمٌ ولا معرفةٌ، فأنزلنا إليكم كتاباً لم ينزل من السماء كتابٌ أجمع ولا أوضح ولا أبين منه.
{156} “Mkaja kusema: Hakika waliteremshiwa Kitabu makundi mawili tu kabla yetu, na sisi tulikuwa hatuna habari ya waliyokuwa wakiyasoma.” Yaani, tuliwateremshia Kitabu hiki kilichobarikiwa kabisa ili kiwe hoja yenu, na kwa kuchelea mje kusema: Hakika waliteremshiwa Kitabu makundi mawili tu kabla yetu;” yaani, Mayahudi na Wakristo. "Na sisi tulikuwa hatuna habari ya waliyokuwa wakiyasoma;" yaani, waje kusema: Hukututeremshia kitabu chochote. Na vitabu ulivyoviteremsha kwa makundi mawili yale sisi hatuna elimu yoyote kuvihusu, wala maarifa yoyote. Kwa hivyo tukawateremshia kitabu ambacho hakikuteremka kitabu kutoka mbinguni chenye kujumuisha zaidi, wala kilicho wazi zaidi, wala kibainifu zaidi kukiliko.
#
{157} {أو تقولوا لو أنَّا أنزِلَ علينا الكتابُ لَكُنَّا أهدى منهم}؛ أي: إما أن تعتذروا بعدم وصول أصل الهداية إليكم، وإما أن تعتذِروا بعدم كمالها وتمامها، فحصل لكم بكتابكم أصل الهداية وكمالها، ولهذا قال: {فقد جاءكم بينة من ربكم}: وهذا اسم جنسٍ يدخل فيه كل ما يبين الحق، {وهدىً}: من الضلالة، {ورحمةٌ}؛ أي: سعادة لكم في دينكم ودنياكم؛ فهذا يوجِبُ لكم الانقياد لأحكامه والإيمان بأخباره وأنَّ مَنْ لم يرفعْ به رأساً وكذَّب به؛ فإنه أظلم الظالمين. ولهذا قال: {فمَنْ أظلمُ ممَّن كذَّبَ بآيات الله وصَدَفَ عنها}؛ أي: أعرض ونأى بجانبه، {سنجزي الذين يصدِفونَ عن آياتنا سوءَ العذاب}؛ [أي: العذاب] الذي يَسوءُ صاحبه ويشقُّ عليه، {بما كانوا يصدِفونَ}: لأنفسهم ولغيرهم جزاءً لهم على عملهم السيئ، وما ربُّك بظلام للعبيد. وفي هذه الآيات دليلٌ على أنَّ علم القرآن أجلُّ العلوم وأبركُها وأوسعُها، وأنه به تحصُل الهداية إلى الصراط المستقيم هدايةً تامةً لا يحتاج معها إلى تخرُّص المتكلمين ولا إلى أفكار المتفلسفين ولا لغير ذلك من علوم الأوَّلين والآخرين. وأنَّ المعروف أنَّه لم ينزل جنسُ الكتاب إلا على الطائفتين؛ من اليهود والنصارى؛ فهم أهل الكتاب عند الإطلاق، لا يدخل فيهم سائر الطوائف؛ لا المجوس ولا غيرهم. وفيه ما كان عليه الجاهلية قبل نزول القرآن من الجهل العظيم وعدم العلم بما عند أهل الكتاب الذين عندهم، مادةُ العلم، وغفلتُهم عن دراسة كتبهم.
{157} "Au mkasema: Lau hakika sisi tungeteremshiwa Kitabu hicho, basi tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao." Yaani, ima muweke udhuru kwamba hamkufikiwa na msingi wa uwongofu, au ima muweke udhuru wa kutokamilika kwake na kutokuwa kwake timilifu. Lakini mlipata kupitia kitabu chenu msingi wa uwongofu na ukamilifu wake, na ndiyo maana akasema: "Basi hakika imekwisha wajia hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Na hili ni jina lenye kujumuisha vitu vya aina moja ambalo kinaingia ndani yake kila chenye kubainisha haki, "na uwongofu" kutokana na upotofu, "na rehema." Yaani, furaha kwenu katika dini yenu na dunia yenu. Basi hili linawalazimu kufuata hukumu zake na kuziamini habari zake, na kwamba asiyechukulia hayo kwa uzito na akayakadhibisha, basi hakika yeye ndiye dhalimu zaidi wa madhalimu wote. Na ndiyo maana akasema, "Kwa hivyo, ni nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo?" Yaani, alipeana mgongo na kujitenga upande. "Tutawalipa wale wanaojitenga na Ishara zetu adhabu mbaya kabisa." [Yaani, adhabu] ambayo ni mbaya kwa mwenyewe na ni ngumu kwake, "kwa sababu ya walivyokuwa wakijitenga" wao wenyewe na wengineo kama malipo kwao kwa matendo yao mabaya, na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake kamwe. Na katika aya hizi kuna ushahidi kwamba, elimu ya Qur-aani ndiyo elimu tukufu zaidi, iliyobarikiwa yake zaidi, na ni pana yake zaidi, na kwamba kupitia kwayo unapatikana kuongoka kwenye njia iliyonyooka uwongofu timilifu usiohitaji pamoja nao kukisia kwa wanatheolojia, wala fikira za wanafalsafa, wala zisizokuwa hiyo miongoni mwa elimu za wa mwanzo na wa mwisho. Na kwamba inajulikana kuwa aina ya kitabu hicho haikuteremka isipokuwa kwa makundi mawili tu; ya Mayahudi na Wakristo. Basi Hao ndio watu wa Kitabu kwa jumla, na wala hayaingii ndani yao makundi mengine yote, si Mamajusi wala wasiokuwa wao. Na ndani yake ni kuwa hali waliyokuwamo watu wa zama za ujinga kabla ya kuteremka kwa Qur-aani miongoni mwa ujinga mkubwa na kutokuwa na elimu ya yale waliyokuwa nayo Watu wa Kitabu ambao wana kiini cha elimu, na kughafilika kwao kusoma vitabu vyao.
: 158 #
{هَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا أَنْ تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا قُلِ انْتَظِرُوا إِنَّا مُنْتَظِرُونَ (158)}
158. Je, wanangoja isipokuwa kwamba wajiwe na Malaika, au awajie Mola wako Mlezi, au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake. Sema, "Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja."
#
{158} يقول تعالى: هل ينظر هؤلاء الذين استمر ظلمُهُم وعنادهم، {إلَّا أن يأتِيَهم}؛ مقدمات العذاب ومقدمات الآخرة؛ بأن تأتيهم {الملائكة} لقبض أرواحهم؛ فإنهم إذا وصلوا إلى تلك الحال؛ لم ينفعهم الإيمان ولا صالح الأعمال، {أو يأتي ربُّك}: لفصل القضاء بين العباد ومجازاة المحسنين والمسيئين {أو يأتي بعض آيات ربك}: الدالَّة على قرب الساعة. {يوم يأتي بعضُ آيات ربِّك}: الخارقة للعادة، التي يعلم بها أن الساعة قد دنت وأن القيامة قد اقتربت. {لا ينفعُ نفساً إيمانُها لم تكنْ آمنتْ من قبلُ أو كسبتْ في إيمانها خيراً}؛ أي: إذا وجد بعض آيات الله؛ لم ينفع الكافرَ إيمانُه إنْ آمنَ ولا المؤمنَ المقصرَ أن يزدادَ خيرُهُ بعد ذلك، بل ينفعه ما كان معه من الإيمان قبل ذلك، وما كان له من الخير الموجود قبل أن يأتي بعضُ الآيات. والحكمة في هذا ظاهرة؛ فإنه إنَّما كان الإيمان ينفع إذا كان إيماناً بالغيب وكان اختياراً من العبد. فأما إذا وجدت الآيات؛ صار الأمر شهادةً، ولم يبق للإيمان فائدةٌ؛ لأنه يشبه الإيمان الضروري؛ كإيمان الغريق والحريق ونحوهما ممَّن إذا رأى الموت أقلع عمَّا هو فيه؛ كما قال تعالى: {فلمَّا رأوا بأسنا قالوا آمنَّا بالله وحدَه وكَفَرْنا بما كنا به مشركينَ. فلم يَكُ ينفعُهم إيمانُهم لما رأوا بأسنا سُنَّةَ اللَّهِ التي قد خلتْ في عبادِهِ} وقد تكاثرت الأحاديث الصحيحة عن النبي - صلى الله عليه وسلم - أنَّ المرادَ ببعض آيات الله طلوعُ الشمس من مغربها، وأنَّ الناس إذا رأوْها؛ آمنوا، فلم ينفعْهم إيمانُهم، ويغلقُ حينئذٍ باب التوبة. ولمَّا كان هذا وعيداً للمكذِّبين بالرسول - صلى الله عليه وسلم - مُنْتَظَراً وهم ينتظرون بالنبي - صلى الله عليه وسلم - وأتباعه قوارعَ الدهر ومصائب الأمور؛ قال: {قل انتَظِروا إنَّا منتَظِرون}: فستعلمون أيُّنا أحقُّ بالأمن. وفي هذه الآية دليل لمذهب أهل السنة والجماعة في إثبات الأفعال الاختيارية لله تعالى؛ كالاستواء والنزول والإتيان لله تبارك وتعالى من غير تشبيه له بصفات المخلوقين، وفي الكتاب والسنة من هذا شيءٌ كثير. وفيه أن من جملة أشراط الساعة طلوعَ الشمس من مغربها. وأنَّ الله تعالى حكيمٌ قد جرت عادته وسنَّته أن الإيمان إنما ينفع إذا كان اختياريًّا لا اضطراريًّا كما تقدَّم، وأن الإنسان يكتسب الخير بإيمانه؛ فالطاعة والبرُّ والتقوى إنما تنفع وتنمو إذا كان مع العبد إيمانٌ، فإذا خلا القلب من الإيمان؛ لم ينفعْه شيءٌ من ذلك.
{158} Yeye Mtukufu Anasema: Je, wanangoja hawa ambao imeendelea dhulma yao na ukaidi wao "isipokuwa kwamba wajiwe" na utangulizi wa adhabu, na utangulizi wa Akhera; ya kwamba wajiwe na "Malaika" ili kuchukua roho zao? Lakini wao wakifikia hali hiyo, haitawafaa kitu Imani yao wala mema ya matendo "au awajie Mola wako Mlezi" ili kupitisha hukumu baina ya waja na kuwalipa wafanyao mazuri na wafanyao mabaya "au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi?" Zinazoashiria ukaribu wa Saa (ya Qiyama). "Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi" ambazo si za kawaida, ambazo itajulikana kwazo kwamba Saa (ya Qiyama) imekwisha karibia na kwamba Qiyama kimeshakaribia; "kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake." Yaani, zikipatikana baadhi ya Ishara za Mwenyezi Mungu, basi kuamini kwa kafiri hakutamfaa ikiwa ataamini, wala Muumini anayepuuza kuzidishia heri baada ya hilo. Bali imani aliyokuwa nayo tu kabla ya hapo ndiyo itakayomnufaisha, na kheri aliyokuwa nayo kabla ya kuja kwa baadhi ya ishara hizo. Na hekima katika hili iko dhahiri. Nayo ni kwamba, imani ilikuwa yenye kunufaisha ikiwa ni kuamini ya ghaibu, na ikiwa ni kwa hiari ya mja. Ama zikipatikana Aya, basi jambo hilo linakuwa la wazi wazi, na imani haibaki kuwa na faida yoyote tena. Kwa sababu inafanana na imani ya lazima, kama vile imani ya mtu anayezama, na anayechomwa kwa moto, na mfano wake miongoni mwa yule ambaye akiona kifo, anaacha kile alichomo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na walipoiona adhabu yetu, walisema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tumevikufuru vile tulivyokuwa tukimshirikisha navyo. Lakini imani yao hiyo haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati walipoiona adhabu yetu. Hii ndiyo ada ya Mwenyezi Mungu ambayo ilikwisha pita kwa waja wake." Na hadithi nyingi sahihi zilikuja kutoka kwa Nabii - rehema na amani zimshukie - kwamba kinachomaanishwa na baadhi ya Aya za Mwenyezi Mungu ni kuchomoza kwa jua kutokea magharibi yake, na kwamba watu watakapoliona; wataamini, lakini imani yao hiyo haitawafaa, kisha hapo mlango wa toba utafungwa. Na kwa kuwa hii ni ahadi ya adhabu kwa wanaomkadhibisha Mtume – rehema na amani zimshukie – anayoingoja, nao pia wanamngojelea Nabii – Rehema na Amani zimshukie – na wafuasi wake kuja kwa shida za wakati, na masaibu ya mambo. Akasema, “Sema: Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja." Kisha mtakuja jua ni nani wetu anayestahiki zaidi amani. Na katika Aya hii kuna ushahidi wa dhehebu la Ahlus-Sunna Wal-Jamaa katika kuthibitisha matendo ya hiari ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama vile Al-Istiwaa (kukaa sawasawa), kushuka, na kuja kwa mwenyezi Mungu, mwingi wa baraka, Mtukufu bila ya kumfananisha na sifa za viumbe. Na katika Kitabu (yani Qur-aani) na Sunnah yako mengi katika haya. Na ndani yake pia ni kwamba miongoni mwa alama za Saa ni kuchomoza jua kutokea magharibi yake. Na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye hekima kubwa, na ni desturi yake na ada yake kwamba imani ina faida tu ikiwa ni ya hiari na si ya lazima, kama ilivyotangulia hapo awali. Na kwamba mtu anachuma heri kwa imani yake. Kwa hivyo Utii, na wema, na uchamungu hunufaisha na kukua iwapo mja ana imani. Lakini Ikiwa moyo wake hautakuwa na imani, basi Hatanufaishwa na chochote katika hayo.
: 159 - 160 #
{إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُمْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ (159) مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا وَمَنْ جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (160)}
159. Hakika wale waliofarakisha Dini yao na wakawa makundi makundi, wewe si miongoni mwao katika chochote. Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda. 160. Mwenye kuja na jema, basi ana mara kumi mfano wake. Na mwenye kuja na baya, basi hatalipwa isipokuwa mfano wake. Na wao hawatadhulumiwa.
#
{159} يتوعَّد تعالى الذين فرَّقوا دينهم؛ أي: شتَّتوه وتفرَّقوا فيه، وكلٌّ أخذ لنفسه نصيباً من الأسماء التي لا تفيد الإنسان في دينه شيئاً؛ كاليهودية والنصرانية والمجوسية، أو لا يكمل بها إيمانه؛ بأن يأخذ من الشريعة شيئاً ويجعله دينه ويدع مثله أو ما هو أولى منه؛ كما هو حال أهل الفرقة من أهل البدع والضلال والمفرقين للأمة. ودلَّت الآية الكريمة أن الدين يأمر بالاجتماع والائتلاف وينهى عن التفرق والاختلاف في أهل الدين وفي سائر مسائله الأصوليَّة والفروعيَّة، وأمره أن يتبرأ ممَّن فرَّقوا دينهم، فقال: {لستَ منهم في شيءٍ}؛ أي: لست منهم وليسوا منك؛ لأنهم خالفوك وعاندوك. {إنَّما أمرُهم إلى الله}: يردُّون إليه فيجازيهم بأعمالهم، {ثم ينبِّئهم بما كانوا يفعلونَ}.
{159} Yeye Mtukufu anawatishia wale walioigawanya dini yao; Yaani, waliitawanya na wakatawanyika ndani yake, na kila mmoja akajitwalia fungu katika majina ambayo hayamnufaishi mtu katika dini yake chochote. Kama vile Uyahudi, na Ukristo, na Umajusi, au haikamiliki kwayo imani yake; kwa kuchukua kitu katika Sharia na kukifanya kuwa ndiyo dini yake na kuacha mfano wake au kilicho bora zaidi yake. Kama ilivyo hali ya watu wa makundi miongoni mwa wana uzushi na upotovu, wanaougawanya umma. Na Aya hii tukufu iliashiria kuwa dini inaamrisha umoja na mfungamano, na inakataza mifarakano na kuhitilafiana baina ya watu wa dini na katika masuala yake yote ya msingi na tanzu, na kuamrisha kwake kujitenga na wale walioigawanya dini yao. Kwa hivyo akasema, "Wewe si miongoni mwao katika chochote;" yaani, wewe si katika wao na wao si katika wewe. Kwa sababu walikuhalifu na wakakupinga. "Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu," watarudishwa kwake, na atawalipa kwa vitendo vyao; "kisha atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda."
#
{160} ثم ذكر صفة الجزاء فقال: {من جاء بالحسنة}: القوليَّة والفعليَّة، الظاهرة والباطنة، المتعلقة بحقِّ الله أو حقِّ خلقه، {فله عشرُ أمثالها}: هذا أقل ما يكون من التضعيف، {ومن جاء بالسيئةِ فلا يُجْزى إلَّا مثلَها}: وهذا من تمام عدله تعالى وإحسانه، وأنه لا يظلم مثقال ذرَّة، ولهذا قال: {وهم لا يُظْلَمون}.
{160} Kisha akataja maelezo ya malipo, akasema, "Mwenye kuja na jema" la kimaneno au kimatendo, lililo dhahiri na lililofichikana, linalohusiana na haki ya Mwenyezi Mungu au haki ya viumbe vyake, {b"asi ana mara kumi mfano wake." Huku ndiko kuzidisha kwa chini zaidi. "Na mwenye kuja na baya, basi hatalipwa isipokuwa mfano wake." Na hili ni katika ukamilifu wa uadilifu Wake yeye Mtukufu na ihsani Yake, na kwamba hadhulumu hata uzito wa chembe; na ndiyo maana Akasema, “Na wao hawatadhulumiwa.”
: 161 - 165 #
{قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ (161) قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ (162) لَا شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ (163) قُلْ أَغَيْرَ اللَّهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى ثُمَّ إِلَى رَبِّكُمْ مَرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ (164) وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَحِيمٌ (165)}
161. Sema: Hakika mimi, Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye njia iliyonyooka, dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahim aliyekuwa mnyoofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. 162. Sema: Hakika Swala yangu, na kuchinja kwangu , na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu." 163. Hana mshirika yeyote. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. 164. Sema: Je nimtafute Mola Mlezi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na wala haichumi kila nafsi isipokuwa ni juu yake. Na wala hatabeba mbeba mzigo, mzigo wa mwingine. Kisha kwa Mola wenu Mlezi ndiyo marejeo yenu, kisha atawajulisha yale mliyokuwa mkihitalifiana ndani yake. 165. Naye ndiye aliyewafanya kuwa mahalifa katika dunia, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbalimbali ili awajaribu katika hayo aliyowapa. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi zaidi, Mwenye kurehemu sana.
#
{161} يأمر تعالى نبيَّه - صلى الله عليه وسلم - أنْ يقول ويعلن بما هو عليه من الهداية إلى الصراط المستقيم، الدِّين المعتدل، المتضمِّن للعقائد النافعة والأعمال الصالحة والأمر بكل حسن والنهي عن كل قبيح، الذي عليه الأنبياء والمرسلون، خصوصاً إمام الحنفاء ووالد من بُعِثَ من بعد موته من الأنبياء خليل الرحمن إبراهيم عليه الصلاة والسلام، وهو الدين الحنيف، المائل عن كل دين غير مستقيم من أديان أهل الانحراف كاليهود والنصارى والمشركين. وهذا عمومٌ.
{161} Yeye Mtukufu anamwamrisha Nabii wake – rehema na amani zimshukie – kwamba aseme na atangaze yale aliyo juu yake ya kuongoka kwenye Njia iliyonyooka; Dini ya wastani, inayojumuisha itikadi zenye kunufaisha na matendo mema, na inayoamrisha kila zuri; na inakataza kila baya ambayo wamo ndani yake Manabii na Mitume hasa imamu wa wale walionyooka; na baba wa wale waliotumwa baada ya kifo chake miongoni mwa Manabii, rafiki mwandani wa Ar-Rahman, Ibrahim - rehema na amani zimshukie. - Nayo ndiyo Dini iliyonyooka sawa, inayoegemea mbali na kila dini isiyokuwa nyoofu miongoni mwa dini za wana upotofu, kama vile Mayahudi, na Wakristo, na washirikina. Na huu ni ujumla.
#
{162} ثم خصَّص من ذلك أشرف العبادات، فقال: {قلْ إنَّ صلاتي ونسكي}؛ أي: ذبحي، وذلك لشرف هاتين العبادتين وفضلهما ودلالتهما على محبَّة الله تعالى وإخلاص الدين له والتقرُّب إليه بالقلب واللسان والجوارح وبالذبح الذي هو بذل ما تحبُّه النفس من المال لما هو أحبُّ إليها وهو الله تعالى، ومن أخلص في صلاته ونُسُكه؛ استلزم ذلك إخلاصه لله في سائر أعماله. وقوله: {ومحيايَ ومماتي}؛ أي: ما آتيه في حياتي وما يجريه الله عليَّ وما يقدِّر عليَّ في مماتي؛ الجميعُ {للهِ ربِّ العالمين}.
{162} Kisha akateua kutoka katika hayo ibada tukufu zaidi, akasema, "Sema: Hakika Swala yangu, na kuchinja kwangu." Na hiyo ni kutokana na utukufu wa ibada hizi mbili na fadhila zake, na kuonyesha kwake ya kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumfanyia yeye tu dini, na kujikurubisha Kwake kwa moyo, na ulimi na viungo, na kwa kuchinja, ambako ni kutoa kile ambacho nafsi inakipenda kutoka katika mali kwa ajili ya yule aliye mpendwa zaidi kwake, ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu na mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu peke yake swala yake na kuchinja kwake, hayo yatamlazimu kumfanyia yeye tu katika matendo yake mengineyo yote. Na kauli yake, "Na uhai wangu, na kufa kwangu;" yaani, ninayoyafanya katika uhai wangu, na yale anayonipitishia Mwenyezi Mungu, na yale anayoniandikia katika kufa kwangu; yote hayo “ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.”
#
{163} {لا شريكَ له}: في العبادة؛ كما أنه ليس له شريكٌ في الملك والتدبير، وليس هذا الإخلاص لله ابتداعاً مني وبدعاً أتيته من تلقاء نفسي، بل {بذلك أمِرْتُ}: أمراً حتماً لا أخرج من التبعة إلا بامتثاله، {وأنا أول المسلمين}: من هذه الأمة.
{163} "Hana mshirika yeyote" katika ibada, kama vile hana mshirika yeyote katika umiliki na kuendesha mambo. Na kumkusudia yeye peke yake huku si uzushi kutoka kwangu na uzushi niliojifanyia mwenyewe. Bali "hayo ndiyo niliyoamrishwa" kwa amri ya uhakika, na sitaachiliwa mbali na jukumu isipokuwa kwa kuyatekeleza. "Na mimi ni wa kwanza wa Waislamu" katika umma huu.
#
{164} {قل أغير الله}: من المخلوقين {أبغي ربًّا}؛ أي: يحسن ذلك، ويليق بي أن أتَّخذ غيره مربياً ومدبراً، والله ربُّ كلِّ شيءٍ؛ فالخلق كلهم داخلون تحت ربوبيته، منقادون لأمره، فتعيَّن عليَّ وعلى غيري أن يَتَّخِذَ اللهَ رَبًّا ويرضى به وأن لا يتعلَّق بأحد من المربوبين الفقراء العاجزين. ثم رغَّب ورهَّب بذلك الجزاء، فقال: {ولا تكسِبُ كلُّ نفس}: ـ من خير وشر.- {إلَّا عليها}؛ كما قال تعالى: {من عمل صالحاً فلنفسِهِ ومن أساءَ فعَلَيْها}، {ولا تزِرُ وازرةٌ وزرَ أخرى}: بل كلٌّ عليه وزرُ نفسِهِ، وإن كان أحد قد تسبَّب في ضلال غيره ووزره؛ فإن عليه وزر التسبب من غير أن ينقص من وِزْرِ المباشر شيء، {ثم إلى ربِّكم مرجِعُكم}: يوم القيامة، {فينبِّئُكم بما كنتُم فيه تختلفونَ }: من خير وشرٍّ، ويجازيكم على ذلك أوفى الجزاء.
{164} "Sema: "Je nimtafute Mola Mlezi asiyekuwa Mwenyezi Mungu" miongoni mwa viumbe. Yaani, je ni zuri hilo, na inanifailia kwamba nimchukue asiyekuwa Yeye kuwa ndiye Mlezi na Mwendesha mambo, na Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Basi viumbe vyote viko chini ya Umola Wake, na vinaifuata amri Yake. Kwa hivyo ikawa ni wajibu kwangu na wengineo kumchukua Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola Mlezi na amridhie, na kwamba asifungamane na yeyote miongoni mwa wanaolelewa, wenye mahitaji, wasio na uwezo. Kisha akatia moyo, na akahofisha kwa malipo hayo, akasema, "Na wala haichumi kila nafsi" katika heri na uovu "isipokuwa ni juu yake." Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Mwenye kutenda mema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, ni juu yake mwenyewe." "Na wala hatabeba mbeba mzigo, mzigo wa mwingine." Bali kila mmoja ni juu yake mzigo wa nafsi yake. Na ikiwa yeyote alisababisha kupotea kwa wengine na mzigo wake, basi ni juu yake mzigo wa kusababisha, bila ya kupunguza katika mzigo wa aliyetenda hasa. "Kisha kwa Mola wenu Mlezi ndiyo marejeo yenu" Siku ya Qiyama. "Kisha atawajulisha yale mliyokuwa mkihitalifiana ndani yake;" ya heri na maovu. Na Atawalipa kwa hayo malipo kamili zaidi.
#
{165} {وهو الذي جعلكم خلائفَ الأرض}؛ أي: يخلُفُ بعضُكم بعضاً، واستخلفكم الله في الأرض، وسخَّر لكم جميع ما فيها، وابتلاكم لينظر كيف تعملونَ، {ورَفَعَ بعضَكم فوق بعضٍ درجات}: في القوة والعافية والرزق والخَلْق والخُلُق؛ {ليبلُوَكُم فيما آتاكم}: فتفاوتت أعمالُكم. {إنَّ ربَّك سريعُ العقاب}: لمن عصاه وكذَّب بآياتِهِ، {وإنَّه لغفورٌ رحيمٌ}: لمن آمن به وعمل صالحاً، وتاب من الموبقات.
{165} "Naye ndiye aliyewafanya kuwa mahalifa katika dunia." Yaani, baadhi yenu wanakuja baada ya wenzao. Na Mwenyezi Mungu aliwafanya mahalifa katika ardhi, na akawatiishieni kila kilichomo ndani yake, na akawajaribu ili aone jinsi mnavyotenda. "Na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbalimbali" katika nguvu, na usalama, na riziki, na umbile, na tabia; "ili awajaribu katika hayo aliyowapa." Basi matendo yenu yakatofautiana. "Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu" kwa mwenye kumuasi, na akakadhibisha Aya zake, {na hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi zaidi, Mwenye kurehemu sana." Kwa mwenye kumuamini Yeye na akatenda mema, na akatubia dhambi ziangamizazo.
Mwisho wa tafsiri ya Surat Al-An'am. Basi kuhimidiwa kwote ni kwake mwenyezi Mungu na sifa. Na rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Muhammad na aali zake na maswahaba zake mpaka siku ya Qiyama.
***