:
Tafsiri ya surat At-Tahrim
Tafsiri ya surat At-Tahrim
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 5 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّهُ لَكَ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (1) قَدْ فَرَضَ اللَّهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ وَاللَّهُ مَوْلَاكُمْ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ (2) وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَى بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَنْ بَعْضٍ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنْبَأَكَ هَذَا قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ (3) إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا وَإِنْ تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَلِكَ ظَهِيرٌ (4) عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا (5)}.
1. Ewe Nabii! Kwa nini unaharamisha alichokuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu. 2. Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sheria ya kufungua viapo vyenu, na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima. 3. Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipolitangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya sehemu na akaacha sehemu nyingine. Alipomwambia hayo, huyo mke akasema: 'Ni nani aliyekwambia haya?' Mtume akasema: 'Kaniambia Yule ajuaye zaidi, Mwenye habari zote!' 4. Kama nyinyi wawili hamtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume), basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia. 5. Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi, wanyenyekevu, Waumini, watawa, waliotubu, wenye kushika ibada, wafanyao heri, waliowahi kuoleka na wale ambao hawajawahi kuoleka.
#
{1} هذا عتابٌ من الله لنبيِّه محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - حين حرَّم على نفسه سُرِّيَّته مارية أو شُرْبَ العسل مراعاةً لخاطر بعض زوجاته في قصَّةٍ معروفة ، فأنزل الله [تعالى] هذه الآيات. {يا أيُّها النبيُّ}؛ أي: يا أيُّها الذي أنعم الله عليه بالنبوَّة والرسالة والوحي ، {لم تحرِّمُ ما أحلَّ الله لك}: من الطيِّبات التي أنعم الله بها عليك وعلى أمَّتك، {تبتغي}: بذلك التحريم {مرضاةَ أزواجِك واللهُ غفورٌ رحيمٌ}: هذا تصريحٌ بأنَّ الله قد غفر لرسوله ورفع عنه اللومَ ورحِمَه.
{1} Hii ni lawama ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipojiharamishia suria wake Maria au kunywa asali kwa sababu ya kutaka kuwafurahisha baadhi ya wake zake katika kisa kinachojulikana, basi Mwenyezi Mungu [Mtukufu] akateremsha Aya hizi. "Ewe Nabii;" yaani, ewe ambaye Mwenyezi Mungu amekupa neema ya unabii na utume na ufunuo, "kwa nini unaharamisha alichokuhalilishia Mwenyezi Mungu" katika vizuri alivyokuneemesha Mwenyezi Mungu kwayo na umma wako? "Unatafuta" kwa kujiharamishia huko "kuwaridhi wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu." Hii ni kauli ya wasi kwamba Mwenyezi Mungu alimsamehe Mtume wake, na akamuondolea lawama hiyo, na akamrehemu.
#
{2} وصار ذلك التحريمُ الصادرُ منه سبباً لشرع حكم عامٍّ لجميع الأمَّة، فقال تعالى: {قد فَرَضَ الله لكم تَحِلَّةَ أيمانِكم}: وهذا عامٌّ في جميع أيمان المؤمنين ؛ أي: قد شرع لكم وقدَّر ما به تَنْحَلُّ أيمانُكم قبل الحِنْثِ وما به تتكفَّر بعد الحنث، وذلك كما في قوله تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا لا تُحَرِّمُوا طيباتِ ما أحلَّ الله لكم ولا تَعْتَدَوا إنَّ الله لا يحبُّ المعتدين ... } إلى أن قال: {فكفَّارتُه إطعامُ عَشَرَةِ مساكين من أوسطِ ما تُطْعِمونَ أهليكم أو كِسْوَتُهم أو تحريرُ رقبةٍ فمن لم يَجِدْ فصيامُ ثلاثةِ أيَّام ذلك كفَّارةُ أيمانِكم إذا حَلَفْتُم}: فكلُّ مَنْ حرَّم حلالاً عليه من طعام أو شرابٍ أو سُرِّيَّة أو حلف يميناً بالله على فعلٍ أو ترك ثم حنثَ وأراد الحِنْثَ؛ فعليه هذه الكفارة المذكورة. وقوله: {واللهُ مولاكم}؛ أي: متولِّي أموركم ومربِّيكم أحسن تربيةٍ في أمر دينكم ودُنياكم وما به يندفعُ عنكم الشرُّ؛ فلذلك فرض لكم تَحِلَّةَ أيمانِكم لتبرأ ذِمَمُكم. {وهو العليم الحكيم}: الذي أحاط علمُه بظواهِرِكم وبواطِنِكم، وهو الحكيم في جميع ما خلقه وحكم به؛ فلذلك شرع لكم من الأحكام ما يعلم أنَّه موافقٌ لمصالحكم ومناسبٌ لأحوالكم.
{2} Na kujiharamishia huku alikojiharamishia kukawa ni sababu ya kuuwekea umma wote sheria ya jumla, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sheria ya kufungua viapo vyenu." Hili ni jambo la jumla katika viapo vyote vya Waumini. Yaani, amekuwekeeni sheria na akapitisha yale ambayo kwayo viapo vyenu vitafunguliwa kabla ya kuvivunja, na yale ambayo vitafutiliwa mbali baada ya kuvivunja. Hayo ni kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi mlioamini! Msiharamishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wakiukao mipaka." Mpaka akasema: "Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnachowalisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiyepata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa." Basi, kila anayeharamishia kilicho halali kama vile chakula, kinywaji, au suria, au kuapa kwa Mwenyezi Mungu kiapo kutenda kitendo au kuacha kutenda, kisha akavunja kiapo chake au akataka kuvunja kiapo chake, basi ni lazima afanye kafara hii iliyotajwa. Na kauli yake: "Na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu," yaani: anayesimamia mambo yenu na anayekuleeni malezi mazuri zaidi katika mambo ya dini yenu na dunia yenu, na yale ambayo kwayo maovu yataepukika kutoka kwenu. Ndiyo sababu akakuwekeeni sheria ya kufungua viapo vyenu ili mpate kufutiwa jambo hilo mlilojijukumisha. "Na Yeye ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima." Ambaye elimu yake imeenea vilivyo ndani yenu na nje yenu, naye ni Mwenye hekima katika kila alichoumba na akahukumu kwacho. Ndiyo maana, akakuwekeeni sheria za hukumu ambazo anajua kwamba zinaendana na masilahi yenu na zinafailiana na hali zenu.
#
{3} وقوله: {وإذْ أسرَّ النبيُّ إلى بعضِ أزواجِهِ حديثاً}: قال كثيرٌ من المفسرين: هي حفصة أم المؤمنين رضي الله عنها، أسرَّ لها النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - حديثاً، وأمر أن لا تُخْبِرَ به أحداً، فحدَّثت به عائشة رضي الله عنها، وأخبره الله بذلك الخبر الذي أذاعتْه، فَعرَّفها - صلى الله عليه وسلم - ببعض ما قالتْ وأعرضَ عن بعضِهِ كرماً منه - صلى الله عليه وسلم - وحِلْماً، فقالت له: {مَنْ أنبأكَ هذا}: الخبر الذي لم يَخْرُجْ منَّا، {قال نَبَّأَنِيَ العليمُ الخبيرُ}: الذي لا تخفى عليه خافية، يعلم السرَّ وأخفى.
{3} Na kauli yake: "Na Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri." Wafasiri wengi walisema: Huyu ni Hafsa, mama wa Waumini, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi. Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimwambia jambo la siri, na akaamuaru asimwambie mtu yeyote, lakini akamwambia Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamjulisha kuhusu hilo alilolitangaza. Kisha Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akamjulisha Hafsa baadhi ya yale aliyoyasema na akaacha mengine kwa sababu ya ukarimu wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na ustahimilivu wake. Basi akamwambia, "Ni nani aliyekwambia haya" ambayo hayakutoka kwetu? "Mtume akasema: 'Kaniambia Yule ajuaye zaidi, Mwenye habari zote!'" Ambaye hakifichiki chochote kwake, anayejua siri na kilichofichikana mno.
#
{4} وقوله: {إن تَتوبا إلى الله فَقَدْ صَغَتْ قلوبُكما}: الخطاب للزوجتين الكريمتين حفصة وعائشة رضي الله عنهما حين كانتا سبباً لتحريم النبيِّ - صلى الله عليه وسلم - على نفسه ما يحبُّه، فعرض الله عليهما التوبة، وعاتبهما على ذلك، وأخبرهما أنَّ قلوبكما قد صَغَتْ؛ أي: مالت وانحرفت عمَّا ينبغي لهنَّ من الورع والأدب مع الرسول - صلى الله عليه وسلم - واحترامه، وأن لا يَشْقُقْنَ عليه، {وإن تَظاهرا عليه}؛ أي: تعاونا على ما يشقُّ عليه ويستمرُّ هذا الأمر منكنَّ، {فإنَّ الله هو مولاهُ وجبريلُ وصالحُ المؤمنين والملائكةُ بعد ذلك ظهيرٌ}؛ أي: الجميع أعوانٌ للرسول مظاهرون. ومَنْ كان هؤلاء أنصاره ؛ فهو المنصور، وغيره إن يناوئه؛ فهو مخذولٌ ، وفي هذا أكبر فضيلة وشرفٍ لسيِّد المرسلين؛ حيث جعل الباري نفسه الكريمة وخواصَّ خلقه أعواناً لهذا الرسول الكريم. وفيه من التَّحذير للزوجتين الكريمتين ما لا يخفى.
{4} Na kauli yake: "Kama nyinyi wawili hamtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko." Maneno haya wanaambiwa hao wake zake wawili watukufu: Hafsa na Aisha, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, walipokuwa sababu ya Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kujiharamishia alichokipenda, basi Mwenyezi Mungu akawataka watubu, na akawalaumu juu ya hilo, na akawaambia kuwa nyoyo zenu zimeshakengeuka kutoka katika yale wanayopaswa kuwa nayo ya ucha Mungu na adabu nzuri kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – na kumheshimu, na kwamba wasimfanyie ugumu. "Na mkisaidiana dhidi yake (Mtume)" na mkaendelea kufanya jambo hilo, "basi hakika Mwenyezi Mungu ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia." Na yule ambaye hawa ndio wasaidizi wake, basi yeye ndiye atakayenusuriwa kweli, naye mwingine ikiwa atampinga, basi yeye ndiye atakayeachiliwa mbali bila msaada. Na katika hilo kuna utukufu na fadhila kubwa zaidi za Bwana wa Mitume. Ambapo Muumba Mwenyewe aliifanya nafsi yake tukufu na viumbe wake maalumu kuwa ndio wasaidizi wa Mtume huyu mtukufu. Pia kuna onyo la wazi kwa wake hawa wawili watukufu.
#
{5} ثم خوَّفهما أيضاً بحالةٍ تشقُّ على النساء غاية المشقَّة، وهو الطلاق، الذي هو أكبر شيءٍ عليهنَّ، فقال: {عسى ربُّه إن طَلَّقَكُنَّ أن يُبْدِلَه أزواجاً خيراً منكنَّ}؛ أي: فلا ترفعْنَ عليه؛ فإنَّه لو طلَّقكنَّ لا يضيق عليه الأمر، ولم يكن مضطراً إليكنَّ؛ فإنَّه سيجد ويبدله الله أزواجاً خيراً منكنَّ ديناً وجمالاً، وهذا من باب التعليق الذي لم يوجد ولا يلزمُ وجودُه؛ فإنَّه ما طلقهنَّ، ولو طلَّقهنَّ؛ لكان ما ذكره الله من هذه الأزواج الفاضلات، الجامعات بين الإسلام وهو القيام بالشرائع الظاهرة، والإيمان وهو القيام بالشرائع الباطنة من العقائد وأعمال القلوب، والقنوت وهو دوام الطاعة واستمرارها. {تائباتٍ}: عمَّا يكرهه الله، فوصفهنَّ بالقيام بما يحبُّه الله والتوبة عما يكرهه الله. {ثيباتٍ وأبكاراً} ؛ أي: بعضهنَّ ثَيِّبٌ وبعضهنَّ أبكارٌ؛ ليتنوَّع - صلى الله عليه وسلم - فيما يحبُّ. فلمَّا سمعن رضي الله عنهنَّ هذا التخويف والتأديب؛ بادرنَ إلى رضا رسول الله - صلى الله عليه وسلم -، فكان هذا الوصف منطبقاً عليهنَّ، فصرن أفضل نساء المؤمنين. [وفي هذا دليلٌ على أنّ اللهَ تعالى لا يختار لرسوله إلاَّ أكملَ الأحوال وأعلى الأمورِ، فلمّا اختار اللهُ لرسوله بقاء نسائه المذكورات معه دلَّ على أنهنَّ خيرُ النساء وأكملهن].
{5} Kisha akawatia hofu kwa hali ambayo ni ngumu sana kwa wanawake, nayo ni talaka, ambayo ndiyo jambo kubwa zaidi kwao. Akasema: “Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko nyinyi." kwa hivyo, msijiinue juu yake. Kwani kama atakupeni talaka, jambo hilo halitamuwiya gumu, na wala hatalazimika kuwashikilia. Kwa sababu atapata na Mwenyezi Mungu atambadilishia wake bora kuliko nyinyi kwa dini na uzuri. Na hili ni suala la kufungamanisha jambo na kitu ambacho hakijakuwepo na wala si lazima kwamba kitatokea. Kwani hakuwataliki, na kama ingekuwa kwamba aliwataliki, basi angepata wanawake hawa bora ambao Mwenyezi Mungu aliwataja, ambao wanajumuisha baina ya Uislamu, ambao ni kutekeleza sheria za dhahiri, na imani, ambayo ni kutekeleza sheria zilizofichika kama vile itikadi na matendo ya nyoyo, na kunyenyekea katika kutii daima. "waliotubu" na kuacha yale anayochukia Mwenyezi Mungu. Hapa, akawa amewasifu kwa tabia ya kufanya yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kutubu kutokana na yale anayochukia Mwenyezi Mungu. "waliowahi kuoleka na wale ambao hawajawahi kuoleka." Ili afurahie yeye - rehema na amani ziwe juu yake - katika yale anayoyapenda. Basi wakati wao - Mwenyezi Mungu awe radhi nao - waliposikia vitisho hivi na kutiwa adabu huku, wakaharakisha kumridhisha Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Basi maelezo haya yakaingiliana nao sawasawa, na wakawa ndio wanawake bora zaidi katika Waumini. [Katika haya kuna ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hamchagulii Mtume wake isipokuwa hali kamilifu zaidi na mambo ya juu kabisa. Mwenyezi Mungu alipomteua Mtume wake kusalia pamoja na wake hao waliotajwa, hilo liliashiria kwamba wao walikuwa ndio wanawake bora na wakamilifu zaidi].
: 6 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ (6)}.
6. Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu kutokana na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa.
#
{6} أي: يا مَن منَّ الله عليهم بالإيمان! قوموا بلوازمه وشروطه، فَـ {قُوا أنفسكم وأهليكم ناراً} موصوفةً بهذه الأوصاف الفظيعة، ووقاية الأنفس بإلزامها أمر الله امتثالاً ونهيه اجتناباً والتوبة عمَّا يُسْخِطُ الله ويوجب العذاب، ووقاية الأهل والأولاد بتأديبهم وتعليمهم وإجبارهم على أمر الله؛ فلا يسلم العبد إلاَّ إذا قام بما أمر الله به في نفسه وفيمن تحت ولايته من الزوجات والأولاد وغيرهم ممَّن هم تحت ولايته وتصرُّفه، ووصف الله النار بهذه الأوصاف؛ ليزجر عباده عن التَّهاون بأمره، فقال: {وَقودها الناسُ والحجارةُ}؛ كما قال تعالى: {إنَّكم وما تعبُدونَ مِن دونِ اللهِ حَصَبُ جهنَّم أنتم لها وارِدونَ}، {عليها ملائكةٌ غلاظٌ شدادٌ}؛ أي: غليظةٌ أخلاقُهم، شديدٌ انتهارُهم يفزعون بأصواتهم ويزعجون بمرآهم ويهينون أصحابَ النار بقوَّتهم، وينفِّذون فيهم أمرَ الله الذي حتم عليهم بالعذاب ، وأوجب عليهم شدَّة العقاب، {لا يعصونَ اللهَ ما أمَرَهم ويفعلون ما يُؤمرونَ}: وهذا فيه أيضاً مدحٌ للملائكة الكرام، وانقيادهم لأمر الله، وطاعتهم له في كلِّ ما أمرهم به.
{6} Yaani: Enyi ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa imani! Shikamaneni na matakwa yake na masharti yake. Kwa hivyo, "Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu kutokana na Moto" unaosifika kwa sifa hizi za kutisha. Na kuzilinda nafsi kunakuwa kwa kuzilazimisha kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake, na kutubia kutokana na yale yanayomchukiza Mwenyezi Mungu na kusababisha adhabu, na kuwalinda familia na watoto kwa kuwafunza adabu, kuwafundisha, na kuwalazimisha kufuata amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, mja hatasalimika isipokuwa afanye mwenyewe yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu na kwa kuwaamrisha wale walio chini ya ulezi wake kuyafanya pia, kama vile wake zake, watoto, na wengineo ambao wako chini ya ulinzi na udhibiti wake. Na Mwenyezi Mungu aliuelezea Moto wa Jahannam kwa maelezo haya; ili kuwakemea waja wake kutokana na kughafilika mbali na amri yake. Alisema: "kuni zake ni watu na mawe." Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu." Na akasema "Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu." Yaani: tabia zao ngumu, na makemeo yao ni makali, wanatisha mno kwa sauti zao, na mwonekano wake unasumbua, na wanawatweza watu wa Motoni kwa nguvu zao, na wanatekeleza juu yao amri ya adhabu aliyoipitisha Mwenyezi Mungu juu yao, na akawawekea adhabu kali mno, "hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa." Hili pia linawasifu Malaika watukufu, kufuata kwao amri ya Mwenyezi Mungu, na kumtii kwao katika kila alichowaamuru.
: 7 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَعْتَذِرُوا الْيَوْمَ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (7)}.
7. Enyi mliokufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyokuwa mkiyatenda.
#
{7} أي: يوبَّخ أهل النار يوم القيامة بهذا التوبيخ، فيقال لهم: {يا أيُّها الذين كفروا لا تعتذروا اليوم}؛ أي: فإنَّه ذهب وقت الاعتذار وزال نفعه، فلم يبقَ الآنَ إلاَّ الجزاء على الأعمال، وأنتم لم تقدِّموا إلاَّ الكفر بالله والتكذيب بآياته ومحاربة رسله وأوليائِهِ.
{7} Yaani watu wa Motoni watakemewa Siku ya Kiyama kwa karipio hili, na wataambiwa: "Enyi mliokufuru! Msilete udhuru leo." Kwa maana, wakati wa kuomba udhuru ulishapita na manufaa yake yakaisha, na sasa hakuna kilichobakia isipokuwa malipo ya matendo, lakini nyinyi hamkujitangulizia ila kumkufuru Mwenyezi Mungu, kukanusha Aya zake, na kumpiga vita Mitume wake na vipenzi wake.
: 8 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحًا عَسَى رَبُّكُمْ أَنْ يُكَفِّرَ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ نُورُهُمْ يَسْعَى بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (8)}.
8. Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: 'Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.'
#
{8} قد أمر الله بالتوبة النَّصوح في هذه الآية، ووعد عليها بتكفير السيئات ودخول الجنات والفوز والفلاح، حين يسعى المؤمنون يوم القيامةِ بنور إيمانهم، ويمشون بضيائِهِ، ويتمتَّعون بروحِهِ وراحته، ويشفِقون إذا طُفِئَتِ الأنوار التي تُعطى المنافقين، ويسألون الله أن يُتِمَّ لهم نورَهم، فيستجيب الله دعوتَهم، ويوصلهم بما معهم من النور واليقين إلى جناتِ النعيم وجوار الربِّ الكريم، وكلُّ هذا من آثار التوبة النَّصوح، والمراد بها التَّوبة العامَّة الشاملة لجميع الذُّنوب ، التي عقدها العبدُ لله، لا يريد بها إلاَّ وجه الله والقرب منه، ويستمرُّ عليها في جميع أحواله.
{8} Mwenyezi Mungu ameamrisha toba ya kweli katika Aya hii, na akaahidi kufuta kwayo madhambi na kuingia katika bustani za mbinguni na kupata kufaulu, wakati Waumini watakapokwenda Siku ya Kiyama kwa nuru ya imani yao, na kutembea kwa mwangaza wake kufurahia raha yake, na watahofu sana zitakapozimwa nuru walizopewa wanafiki, na kumuomba Mwenyezi Mungu awatimizie nuru yao. Basi atawakubalia dua yao na atawafikisha kwa nuru ya yakini waliyo nayo katika bustani za mbinguni za neema na ujirani wa Mola Mtukufu. Yote haya ni katika athari za toba ya kweli. Nayo ilikusudiwa toba ya jumla, inayojumuisha dhambi zote, ambayo mja aliifanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hakutaka kwayo isipokuwa uso wa Mwenyezi Mungu na kuwa karibu naye, na akaendelea kufanya hivyo katika hali zake zote.
: 9 #
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (9)}.
9. Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki, na kuwa mgumu kwao! Na makazi yao ni Jahannamu. Na hayo ni marejeo mabaya.
#
{9} يأمر اللهُ تعالى نبيَّه - صلى الله عليه وسلم - بجهاد الكفار والمنافقين والإغلاظ عليهم في ذلك، وهذا شاملٌ لجهادهم بإقامة الحجَّة عليهم ودعوتهم بالموعظة الحسنة وإبطال ما هم عليه من أنواع الضلال، وجهادهم بالسلاح والقتال لمن أبى أن يُجيبَ دعوةَ اللهِ وينقادَ لحكمه؛ فإنَّ هذا يجاهدُ ويغلظُ له، وأما المرتبة الأولى؛ فتكون بالتي هي أحسنُ؛ فالكفَّار والمنافقون لهم عذابٌ في الدُّنيا بتسليط الله لرسوله وحزبِهِ عليهم وعلى جهادهم، وعذاب النار في الآخرة {وبئس المصير}: الذي يصير إليها كل شقيٍّ خاسر.
{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwamrisha Nabii wake -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kufanya jihadi dhidi ya makafiri na wanafiki na kuwa mkali juu yao katika hilo, na hii linajumuisha kupambana nao kwa kusimamisha hoja dhidi yao na kuwalingania kwa mawaidha mazuri, na kubatilisha aina za upotofu wanazozifuata, na kupambana nao kwa silaha na kupigana vita na wale wanaokataa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu na kusalimu amri kwa hukumu yake. Huyu anfanyiwa jihadi na ugumu. Ama daraja la kwanza, hilo linakuwa kwa mawaidha yaliyo mazuri. Kwa maana makafiri na wanafiki watapata adhabu katika dunia kwa njia ya Mwenyezi Mungu kumpa mamlaka Mtume wake na kundi lake juu yao na kuwapa nguvu ya kufanya jihadi dhidi yao, na pia wana adhabu ya Moto huko Akhera. "Na hayo ni marejeo mabaya" ambayo ataishia kila mwenye mpotofu aliyehasirika.
: 10 - 12 #
{ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا لِلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ (10) وَضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا لِلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِنْدَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِنْ فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (11) وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِنْ رُوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ (12)}
10. Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale waliokufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawafanyia uhaini waume zao, nao wasiwafae kitu kutokana na Mwenyezi Mungu. Na ikasemwa: 'Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia!' 11. Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale walioamini - mkewe Firauni, aliposema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhalimu. 12. Na Mariamu binti wa Imrani, aliyelinda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu.
Hii ni mifano miwili ambayo Mwenyezi Mungu aliwapigia waumini na makafiri. Ili kuwabainishia kwamba mawasiliano ya kafiri na Muumini na ukaribu wake kwake hakumnufaishi hata kidogo, na kwamba muumini kuwasiliana na kafiri hakumdhuru hata kidogo wakati anatekeleza wajibu wake. Ni kama kwamba katika hili kuna ishara na maonyo kwa wake za Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – dhidi ya kufanya maasia, na kwamba kuwasiliana kwao naye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – si kitu cha kuwanufaisha kwa chochote ikiwa watafanya mabaya. Akasema:
#
{10} {ضَرَبَ الله مثلا للذين كَفَروا امرأة نوحٍ وامرأة لوطٍ كانتا}؛ أي: المرأتان {تحت عبدينِ من عبادِنا صالِحَيْنِ}: وهما نوحٌ ولوطٌ عليهما السلام، {فخانَتاهما}: في الدين؛ بأن كانتا على غير دين زوجيهما، وهذا المراد بالخيانة، لا خيانة النَّسب والفراش؛ فإنَّه ما بغت امرأةُ نبيِّ قطُّ، وما كان الله ليجعلَ امرأةَ أحدٍ من أنبيائه بَغِيًّا، {فلم يُغْنيا}؛ أي: نوحٌ ولوطٌ {عنهما}؛ أي: عن امرأتيها، {من اللهِ شيئاً وقيل} لهما {ادْخُلا النارَ مع الدَّاخِلين}.
{10} "Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale waliokufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu." Yaani Nuhu na Lut'i, amani iwe juu yao. "Lakini wakawafanyia uhaini waume zao" katika dini, ambapo walikuwa katika dini tofauti na ya waume zao. Huu ndio uhaini uliokusudiwa hapa. Siyo uhaini wa nasaba na kitanda. Kwa maana hakuna mwanamke yeyote wa Nabii aliyewahi kufanya ukahaba, kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kumfanya yeyote katika wake za Manabii wake kuwa kahaba. "Nao wasiwafae kitu." Yaani, Nuhu na Lut hawakuwafaa wake zao kitu "kutokana na Mwenyezi Mungu. Na ikasemwa: 'Ingieni Motoni pamoja na wanaoingia!."
#
{11} {وضرب الله مثلاً للذين آمنوا امرأةَ فرعونَ}: وهي آسيةُ بنتُ مزاحم رضي الله عنها، {إذ قالتْ ربِّ ابنِ لي عندك بيتاً في الجنَّة ونَجِّني من فرعونَ وعملِهِ ونجِّني من القوم الظَّالمين}: فوصفها الله بالإيمان والتضرُّع لربِّها وسؤالها أجلَّ المطالب، وهو دخول الجنَّة ومجاورة الربِّ الكريم، وسؤالها أن ينجِّيَها [اللَّهُ] من فتنة فرعون وأعماله الخبيثة ومن فتنة كلِّ ظالم، فاستجاب الله لها، فعاشتْ في إيمانٍ كامل وثباتٍ تامٍّ ونجاةٍ من الفتن، ولهذا قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -: «كَمُلَ من الرجال كثيرٌ، ولم يَكْمُلْ من النساء إلاَّ مريمُ بنتُ عمرانَ، وآسيةُ بنتُ مزاحم، وخديجةُ بنتُ خويلدٍ. وفضلُ عائشةَ على النساء كفضل الثريدِ على سائر الطعام ».
{11} "Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wale walioamini - mkewe Firauni" ambaye jina lake lilikuwa ni Asiya bint Muzahim, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi. "Aliposema: 'Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhalimu.'" Basi Mwenyezi Mungu akamuelezea kwamba alikuwa na imani na kuomba dua kwa unyenyekevu kwa Mola wake Mlezi, na kuomba kwake kitu kikubwa zaidi kinachotakiwa, ambacho ni kuingia katika bustani za mbinguni, na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mola Mlezi Mtukufu, na ombi lake kwamba [Mwenyezi Mungu] amwokoe kutokana na majaribu ya Firauni na matendo yake maovu na kutokana na majaribu ya kila dhalimu. Basi Mwenyezi Mungu akamwitikia, kwa hivyo akaishi katika imani kamili, na uthabiti timilifu, na kuepuka majaribio. Ndiyo maana Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akasema: 'Walikamilika wengi katika wanaume, lakini hakuna aliyekamilika katika wanawake isipokuwa Maryam bint Imran, Asiya bint Muzahim, na Khadija bint Khuwaylid. Na ubora wa Aisha juu ya wanawake wote ni kama ubora wa mkate kwa nyama juu ya vyakula vingine vyote.'
#
{12} وقوله: {ومريمَ ابنة عمرانَ التي أحصنتْ فَرْجَها}؛ أي: حفظته وصانته عن الفاحشة؛ لكمال ديانتها وعفَّتها ونزاهتها، {فنَفَخْنا فيه من رُوحنا}: بأن نَفَخَ جبريل عليه السلام في جيب دِرْعها، فوصلت نفخته إلى مريم، فجاء منها عيسى عليه السلام الرسول الكريم والسيد العظيم، {وصَدَّقَتْ بكلماتِ ربِّها وكتبِهِ}: وهذا وصفٌ لها بالعلم والمعرفة؛ فإنَّ التصديق بكلمات الله يشمل كلماتِهِ الدينيَّة والقدريَّة، والتصديق بكتبه يقتضي معرفة ما به يحصلُ التَّصديق، ولا يكون ذلك إلاَّ بالعلم والعمل، ولهذا قال: {وكانت من القانتينَ}؛ أي: المداومين على طاعة الله بخشيةٍ وخشوعٍ. وهذا وصفٌ لها بكمال العمل؛ فإنَّها رضي الله عنها صدِّيقةٌ. والصدِّيقيَّة هي كمال العلم والعمل.
{12} Na kauli yake: "Na Mariamu binti wa Imrani, aliyelinda ubikira wake" kutokana na uasherati. Kwa sababu ya utimilifu wa Dini yake na kuwa kwake mbali na matamani ya kimwili na usafi wake. "Basi tukampulizia humo kutoka roho yetu." Yaani, Jibril, amani iwe juu yake, akapuliza katika mfuko wa nguo yake, na pumzi yake hiyo ikamfikia Mariamu kwa hivyo akamzaa Isa, amani iwe juu yake, ambaye ni Mtume Mtukufu na bwana mkuu. "Na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake." Huku ni kumuelezea kwamba alikuwa na elimu na maarifa. Kwa maana kusadiki maneno ya Mwenyezi Mungu kunajumuisha maneno yake ya kidini na ya kimipango yake. Na kusadiki vitabu vyake kunahitaji kujua yale yanaymfanya mtu kusadiki. Na hilo haliwi isipokuwa kwa elimu na matendo, na ndiyo maana akasema, "na alikuwa miongoni mwa watiifu." Yaani, wale wanaodumu katika kumtii Mwenyezi Mungu kwa hofu na unyenyekevu. Haya ni kumuelezea kwamba alikuwa ni mwenye kutenda matendo makamilifu. Kwa kuwa yeye, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ni mkweli mno. Sifa ambayo inajumuisha ukamilifu wa elimu na matendo.
Imekamilika tafsiri ya sura hii [na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu].
* * *