Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ وَاتَّقُوا اللَّهَ رَبَّكُمْ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنْ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَنْ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ وَمَنْ يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَلِكَ أَمْرًا (1) فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِنْكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّهِ ذَلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا (2) وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا (3)}.
1. Ewe Nabii! Mtakapowapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi hakika amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jingine baada ya haya. 2.Basi wanapofikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hayo anaaidhiwa kwayo anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, humtengezea njia ya kutokea. 3. Na humruzuku kutokea asipotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu, Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.
#
{1} يقول تعالى مخاطباً لنبيِّه [محمد]- صلى الله عليه وسلم - وللمؤمنين: {يا أيُّها النبيُّ إذا طلَّقْتُم النساءَ}؛ أي: [إذا] أردتم طلاقهنَّ، {فـ}: التمسوا لطلاقهنَّ الأمر المشروع، ولا تبادروا بالطَّلاق من حين يوجد سببه من غير مراعاةٍ لأمر الله، بل {طلِّقوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ}؛ أي: لأجل عدَّتهن؛ بأن يطلِّقَها زوجها وهي طاهرٌ في طهرٍ لم يجامِعْها فيه؛ فهذا الطلاق هو الذي تكون العدَّة فيه واضحةً بيِّنة؛ بخلاف ما لو طلَّقَها وهي حائضٌ؛ فإنَّها لا تحتسب تلك الحيضة التي وقع فيها الطلاق، وتطول عليها العدَّة بسبب ذلك، وكذلك لو طلَّقَها في طهرٍ وطئ فيه؛ فإنَّه لا يؤمَن حملها، فلا يتبيَّن ولا يتَّضح بأيِّ عدَّةٍ تعتدُّ، وأمر تعالى بإحصاء العدَّة، أي: ضبطها بالحيض إن كانت تحيض، أو بالأشهر إن لم تكن تحيضُ وليست حاملاً؛ فإنَّ في إحصائها أداءً لحقِّ الله، وحق الزوج المطلِّق، وحقِّ من سيتزوجها بعد، وحقِّها في النفقة ونحوها؛ فإذا ضبطت عدَّتها؛ علمت حالها على بصيرةٍ، وعلم ما يترتّب عليها من الحقوق وما لها منها، وهذا الأمر بإحصاء العدَّة يتوجَّه للزوج وللمرأة إن كانت مكلَّفة، وإلاَّ؛ فلوليِّها. وقوله: {واتَّقوا الله ربَّكم}؛ أي: في جميع أموركم، وخافوه في حقِّ الزوجات المطلَّقات.
فـ {لا تخرجوهنَّ من بيوتهنَّ}: مدة العدَّة، بل تلزم بيتها الذي طلَّقها زوجها وهي فيه. {ولا يَخْرُجْنَ}؛ أي: لا يجوز لهنَّ الخروج منها، أما النَّهي عن إخراجها؛ فلأنَّ المسكن يجب على الزوج للزوجة لتستكمل فيه عدَّتها التي هي حقٌّ من حقوقه، وأما النهي عن خروجها؛ فلما في خروجها من إضاعة حقِّ الزوج وعدم صونه، ويستمرُّ هذا النهي عن الخروج من البيوت والإخراج إلى تمام العدَّة. {إلاَّ أن يأتينَ بفاحشةٍ مُبَيِّنَةٍ}؛ أي: بأمر قبيح واضح موجبٍ لإخراجها؛ بحيث يُدْخِلُ على أهل البيت الضَّرر من عدم إخراجها؛ كالأذى بالأقوال والأفعال الفاحشة؛ ففي هذه الحال يجوز لهم إخراجُها؛ لأنَّها هي التي تسبَّبت لإخراج نفسها، والإسكانُ فيه جبرٌ لخاطرها ورفقٌ بها؛ فهي التي أدخلت الضرر عليها. وهذا في المعتدَّة الرجعيَّة، وأمَّا البائن؛ فليس لها سكنى واجبةٌ؛ لأنَّ السكنى تبعٌ للنفقة، والنفقة تجب للرجعيَّة دون البائن.
{وتلك حدودُ الله}؛ أي: التي حدَّها لعباده وشرعها لهم وأمرهم بلزومها والوقوف معها، {ومن يتعدَّ حدودَ الله}: بأن لم يقف معها، بل تجاوَزها أو قصَّر عنها، {فقد ظلم نفسَه}؛ أي: بخسها حقَّها ، وأضاع نصيبه من اتِّباع حدود الله التي هي الصلاحُ في الدُّنيا والآخرة. {لاتَدْري لعلَّ الله يحدِثُ بعد ذلك أمراً}؛ أي: شرع الله العدَّة، وحدَّد الطلاق بها لحِكَم عظيمةٍ: فمنها: أنَّه لعلَّ الله يحدِثُ في قلب المطلِّق الرحمة والمودَّة، فيراجع من طلَّقها، ويستأنف عشرتها، فيتمكَّن من ذلك مدَّة العدة، أو لعلَّه يطلِّقها لسبب منها، فيزول ذلك السبب في مدَّة العدَّة، فيراجعها؛ لانتفاء سبب الطلاق.
ومن الحِكَم أنَّها مدة التربُّص يُعلم براءة رحمها من زوجها.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akimwambia Nabii wake
[Muhammad] - rehema na amani na Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -
na akiwaambia Waumini pia: "Ewe Nabii! Mtakapowapa talaka wanawake." Yaani, mnapotaka kuwapa talaka, basi itafuteni talaka hiyo jambo linalokubaliwa kisheria, wala msifanye haraka kutoa talaka wakati sababu yake inapatikana bila ya kuangalia amri ya Mwenyezi Mungu. Bali "wapeni talaka katika wakati wa eda zao." Yaani, ampe talaka hali ya kuwa mke huyo yu safi, na kwamba hakuwa ameingiliana naye katika hali yake ya usafi hiyo. Hii ndiyo talaka ambayo eda yake huwa wazi kabisa. Tofauti na ikiwa atamtaliki akiwa katika hedhi. Hedhi hiyo haitahesabiwa ambayo alimtaliki ndani yake, na hilo litamsababishia eda kuwa ndefu. Vile vile ikiwa atamlatiki hali ya kuwa yu safi lakini aliingiliana naye. Hapo hatakuwa salama kutokana na ujauzito, na wala haitakuwa wazi ni eda ipi atakaa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamrisha uhesabiwe muda wa eda; kwa kuhesabu hedhi ikiwa ni katika wale wanaopata hedhi, au kuhesabu miezi ikiwa si katika wale wanaopata hedhi na wala hana mimba. Kwa maana katika kuihesabu kuna kutimiza haki ya Mwenyezi Mungu, haki ya mume aliyepeana talaka, haki ya yule atakayemuoa baadaye, na haki yake mke huyu ya kupewa matunzo na mengineyo. Kwa hivyo, muda wake wa eda utadhibitiwa vyema, itajulikana hali yake vizuri zaidi, na zitajulikana haki zinazoambatana nayo na kile ambacho ni chake ndani yake. Amri hii ya kuhesabu eda anaambiwa mume na mke ikiwa ni katika wanawake wanaojukumishwa na sheria. Vinginevyo, basi anaambiwa mlezi wake.
Na kauli yake: "Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi." Yaani, katika mambo yenu yote, na mhofuni katika mambo ya wake waliopewa talaka. “Msiwatoe katika nyumba zao" katika muda wa eda. Bali anapaswa kukaa katika nyumba ambayo mume wake alimtaliki akiwa ndani yake. "Wala wasitoke wenyewe" ama katazo la kuwatoa, ni kwa sababu kuwapa nyumba ni wajibu wa mume kwa mke ili akamilishe eda yake, ambayo ni moja ya haki zake. Na ama katazo kutoka mwenyewe, ni kwa sababu katika kutoka kwake kuna kupoteza haki ya mume na kutoilinda, na katazo hili la kutomtoa na kutoka kwake katika nyumba litaendelea hadi kukamilika kwa muda wa eda. "Ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi" unaohitaji watolewe, kwa manaa unawasababishia watu wa nyumba hiyo madhara ikiwa hatatoka; kama vile madhara kwa maneno na vitendo vichafu. Basi katika hali hii, inaruhusiwa kwa waume kuwatoa. Kwa sababu yeye mwenyewe ndiye aliyejisababishia kutolewa. Na kukalishwa nyumbani alikokuwa amekalishwa kulikuwa kwa sababu ya kumfurahisha mawazo yake na kumfanyia upole. Haya ni kuhusiana na mwanamke aliyetalikiwa talaka ya kurudiana bila ya kufunga nikaa mpya. Ama yule aliyetalikiwa talaka ya kurudiana kwa nikaa mpya, huyo hailazimu kupewa mahali pa kukaa, kwa kwa sababu makazi yatafuatana na kupewa matumizi ya kila siku. Na matumizi ya kila siku ni lazima apewe mwanamke aliyetalikiwa talaka isiyohitaji nikaa mpya ili kurudiana si ile anayohitaji nikaa mpya. "Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu" ambayo aliwawekea waja wake na akawawekea hiyo kuwa sheria na akawaamrisha kushikamana nayo na kusimamia hapo, "Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu" kwa kutosimamia hapo, bali aliikiuka au aliipuuza sana, "basi hakika amejidhulumu nafsi yake" haki yake, na akapoteza fungu lake katika kufuata mipaka ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni ndiyo sababu ya kutengenea katika dunia na akhera. "Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya." Yaani, Mwenyezi Mungu ameweka sheria ya eda na akaiweka kuanza baada ya talaka kwa sababu ya hekima mbalimbali kubwa. Miongoni mwake ni kwamba huenda Mwenyezi Mungu akaleta rehema na mapenzi katika moyo wa aliyetoa talaka, kwa hivyo akamrudisha yule aliyempa talaka, kisha wakaendelea kuishi vyema. Na hilo linawezekana katika kipindi cha eda. Au huenda alimpa talaka kutokana na sababu aliyoisababisha mke huyo, kisha ikaisha katika muda wa eda, kwa hivyo, wakarudiana kwa sababu ya kutokuwepo sababu ya talaka ile. Na miongoni mwa hekima ni kwamba muda wa eda utupu wa tumbo lake kutokana na ujauzito wa mumewe.
#
{2} وقوله: {فإذا بَلَغْنَ أجَلَهُنَّ}؛ أي: [إذا] قاربن انقضاء العدَّة؛ لأنهنَّ لو خرجنَ من العدَّة؛ لم يكن الزوج مخيَّراً بين الإمساك والفراق، {فأمسكوهنَّ بمعروفٍ}؛ أي: على وجه المعاشرة الحسنة والصحبة الجميلة، لا على وجه الضِّرار وإرادة الشرِّ والحبس؛ فإنَّ إمساكها على هذا الوجه لا يجوز، {أو فارِقوهنَّ بمعروفٍ}؛ أي: فراقاً لا محذور فيه، من غير تشاتُم ولا تخاصُم ولا قهرٍ لها على أخذ شيءٍ من مالها، {وأشهدوا}: على طلاقها ورجعتها، {ذَوَيْ عدلٍ منكم}؛ أي: رجلين مسلميْنِ عَدْلَيْنِ؛ لأنَّ في الإشهاد المذكور سدًّا لباب المخاصمة وكتمان كلٍّ منهما ما يلزم بيانه، {وأقيموا}: أيُّها الشهداء {الشهادةَ لله}؛ أي: ائتوا بها على وجهها من غير زيادةٍ ولا نقصٍ، واقصدوا بإقامتها وجهَ الله تعالى ، ولا تُراعوا بها قريباً لقرابته ولا صاحباً لمحبَّته. {ذلكم}: الذي ذكَرنا لكم من الأحكام والحدود، {يوعَظُ به مَن كان يؤمنُ باللهِ واليوم الآخر}: فإنَّ الإيمان بالله واليوم الآخر يوجِبُ لصاحبه أن يتَّعِظَ بمواعظ الله وأن يقدِّم لآخرته من الأعمال الصالحة ما يتمكَّن منها ؛ بخلاف من ترحَّل الإيمان من قلبه؛ فإنَّه لا يبالي بما أقدم عليه من الشرِّ، ولا يعظِّم مواعظ الله؛ لعدم الموجب لذلك. ولما كان الطلاق قد يوقع في الضيق والكرب والغمِّ؛ أمر تعالى بتقواه، ووعد مَنْ اتَّقاه في الطلاق وغيره بأن يجعل له فرجاً ومخرجاً. فإذا أراد العبد الطلاق، ففعله على الوجه الشرعيِّ، بأن أوقعه طلقةً واحدةً في غير حيضٍ ولا طهرٍ أصابها فيه ؛ فإنه لا يضيق عليه الأمر، بل جعل الله له فرجاً وسعةً يتمكَّن بها من الرجوع إلى النّكاح إذا ندم على الطلاق.
والآية وإن كانت في سياق الطلاق والرجعة؛ فإنَّ العبرة بعموم اللفظ فكل من اتقى الله [تعالى] ولازم مرضاته في جميع أحواله؛ فإنَّ الله يثيبه في الدُّنيا والآخرة، ومن جملة ثوابه أن يجعل له فرجاً ومخرجاً من كلِّ شدَّة ومشقَّة، وكما أنَّ من اتَّقى الله؛ جعل له فرجاً ومخرجاً؛ فمن لم يتَّق الله؛ يقع في الآصار والأغلال التي لا يقدر على التخلُّص منها والخروج من تَبِعَتها، واعتبرْ ذلك في الطلاق ؛ فإنَّ العبد إذا لم يَتَّق الله فيه، بل أوقعه على الوجه المحرَّم؛ كالثلاث ونحوها؛ فإنَّه لا بدَّ أن يندم ندامةً لا يتمكَّن من استدراكها والخروج منها.
{2} Na kauli yake: "Basi wanapofikia muda wao." Yaani, watakapokaribia karibia kumaliza kipindi cha eda, kwani ikiwa watakuwa wameshatoka katika eda; mume hatakuwa na hiyari baina ya kumshikilia na kumwacha. "Ima warejeeni muwaweke kwa wema" si kwa namna ya kuwadhuru na kuwatakia maovu. Kwa sababu, hairuhusiki kuwashikilia kwa njia hii "au farikianeni nao kwa wema" isiyo na kudhuriana, bila ya kutukanana, kugombana, au kumshinda na kuchukua kitu katika mali yake. "Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu" wa kiume, Waislamu. Kwa sababu huo ushahidi huo kuna kufunga mlango wa mabishano na kila mmoja wao kuficha yale yanayopasa kuwekwa wazi. "Na simamisheni" enyi mashahidi "ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu" bila ya kuongeza wala kupunguza, na kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala kumwelekea na ushahidi huo jamaa wa karibu kwa sababu ya ujamaa wake wala sahibu kwa sababu ya kumpenda. "Hayo" tuliyokutajieni katika hukumu mbalimbali na mipaka, "anaaidhiwa kwayo anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho" Kwa maana, kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho inamlazimu mwenye imani hiyo kuaidhika mawaidha ya Mwenyezi Mungu, na kuitangulizia akhera yake matendo mema kiasi awezavyo. Tofauti na yule ambaye imani yake imetoka moyoni mwake. Yeye hajali maovu ambayo anafanya, na hayaheshimu mawaidha ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu ya kutokuwepo cha kumfanya afanya hayo. Na kwa kuwa talaka inaweza kusababisha dhiki, uchungu na huzuni, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamrisha afanyiwe ucha Mungu, na akawaahidi wale wanaomcha katika talaka na mambo mengine kwamba atampa faraja na njia ya kutokea. Kwa hivyo, mja anapotaka talaka, kisha akaifanya kwa mujibu wa Sheria, kwa kumpa talaka moja nje ya kipindi cha hedhi au hali anapokuwa safi bila ya kuingiliana naye, basi jambo lake halitamuwiya gumu, bali Mwenyezi Mungu atamfanyia faraja na wasaa ambayo kwayo ataweza kurejea kwenye ndoa ikiwa atajutia talaka yake. Na Aya hii, hata ikiwa ni katika muktadha wa talaka na kurejeana baada ya taaka, kitu kinachozingatiwa ni maana ya jumla ya maneno yaliyotumika. Kwa hivyo, kila mwenye kumcha Mwenyezi Mungu Mwenyezi na kushikamana na radhi zake katika hali zake zote, basi hakika Mwenyezi Mungu atamlipa mema duniani na Akhera. Na miongoni mwa thawabu zake ni kumpa faraja na njia ya kutokea katika dhiki na ugumu. Kama vile mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, anamfanyia faraja na njia ya kutokea, basi kile asiyemcha Mwenyezi Mungu, anaanguka kwenye minyororo na pingu ambazo hawezi kujiondoa humo na hata mambo yanayofungamana nayo. Tena zingatia hili katika talaka. Ikiwa mja hamchi Mwenyezi Mungu ndani yake, bali anaifanya kwa njia ya haramu, kama vile kutoa tatu na mfano wake, basi lazima atajuta majuto ambayo hataweza kuyarekebisha na kutoka nje yake.
#
{3} وقوله: {ويرزُقْه من حيث لا يحتسِبُ}؛ أي: يسوق الله الرزق للمتَّقي من وجه لا يحتسبه ولا يشعر به، {ومن يَتَوَكَّلْ على الله}: في أمر دينه ودنياه؛ بأن يعتمد على الله في جلب ما ينفعه ودفع ما يضرُّه ويثق به في تسهيل ذلك {فهو حسبُه}؛ أي: كافيه الأمر الذي توكَّل عليه فيه ، وإذا كان الأمرُ في كفالة الغنيِّ القويِّ العزيز الرحيم؛ فهو أقرب إلى العبد من كل شيء، ولكن ربَّما أن الحكمة الإلهيَّة اقتضت تأخيره إلى الوقت المناسب له؛ فلهذا قال تعالى: {إنَّ الله بالغُ أمرِه}؛ أي: لا بدَّ من نفوذ قضائه وقدره، ولكنه قد جعل {لكلِّ شيءٍ قَدْرَاً}؛ أي: وقتاً ومقداراً لا يتعدَّاه ولا يقصر عنه.
{3} Na kauli yake: "Na humruzuku kutokea asipotazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu" katika mambo ya dini yake na mambo yake ya kidunia, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kumletea yenye kumanufaisha na kumuepusha mbali na yenye kumdhuru, na akawa na imani naye katika kuyasahilisha hayo, basi "Yeye humtosha." Yaani, atamtosha katika jambo alilomtegemea ndani yake. Na ikiwa jambo liko chini ya Mkwasi, Mwenye nguvu, Mshindi, Mwingi wa kurehemu, basi Yeye yuko karibu na mja kuliko kitu kingine chochote. Lakini labda hekima ya kimungu ikahitaji kulichelewesha hadi wakati ufaao kwake. Kwa ajili hiyo,
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake." Yaani, mipango yake na hukumu zake zitekelezeke, lakini amekifanyia "kila kitu na kipimo chake" ambao hakiuvuki wala kukipunguza.
{وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِنْ نِسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَنْ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا (4) ذَلِكَ أَمْرُ اللَّهِ أَنْزَلَهُ إِلَيْكُمْ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُعْظِمْ لَهُ أَجْرًا (5)}.
4. Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba, eda yao mpaka watakapozaa. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi. 5. Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu amekuteremshieni. Na anayemcha Mwenyezi Mungu, atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa.
#
{4} لمَّا ذكر تعالى أن الطلاق المأمور به يكون لعدَّة النساء؛ ذكر العدَّة، فقال: {واللاَّئي يَئِسْنَ من المحيض من نسائِكُم}: بأن كنَّ يَحِضْنَ ثم ارتفع حيضُهُنَّ لكبرٍ أو غيره ولم يُرْجَ رجوعُه؛ فإنَّ عدَّتها ثلاثة أشهر، جعل كلَّ شهرٍ مقابلة حيضة. {واللاَّئي لم يَحِضْنَ}؛ أي: الصغار اللائي لم يأتهنَّ الحيضُ بعدُ أو البالغات اللاتي لم يأتهنَّ حيضٌ بالكلِّيَّة؛ فإنَّهنَّ كالآيسات، عدَّتهنَّ ثلاثة أشهر، وأمَّا اللائي يحِضْنَ؛ فذكر الله عدَّتهنَّ في قوله: {والمطلَّقاتُ يتربَّصْنَّ بأنفسهنَّ ثلاثةَ قروءٍ}. وقوله: {وأولاتُ الأحمال أجَلُهُنَّ}؛ أي: عدَّتُهنَّ {أن يَضَعْنَ حملَهُنَّ}؛ أي: جميع ما في بطونهنَّ من واحدٍ ومتعددٍ، ولا عبرة حينئدٍ بالأشهر ولا غيرها. {ومن يتَّقِ اللهَ يجعلْ له من أمره يُسراً}؛ أي: من اتَّقى الله يَسَّرَ له الأمور، وسهَّل عليه كلَّ عسير.
{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa talaka sahihi iliyoamrishwa ni ile ambayo wanawake wanaweza kuanza eda yao, akataja eda,
na akasema: "Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wanawake wenu." Yaani, wale waliokuwa wakipata hedhi, kisha hedhi yao ikakatika kwa sababu ya uzee au kitu kingine, na hakuna matumaini ya kurudi kwake. Basi eda yao ni miezi mitatu, kila mwezi inapaswa kuchukuliwa kuwa ni hedhi moja. "Pamoja na ambao hawapati hedhi." Yaani, wasichana wadogo ambao bado hawajapata hedhi, au wanawake watu wazima ambao hawajapata hedhi kabisa. Hao ni kama wanawake walioacha kupata hedhi, eda yao ni miezi mitatu. Ama wale wanaopata hedhi,
basi Mwenyezi Mungu akataja eda yao katika kauli yake: "Na wanawake walioachwa kwa talaka wangoje peke yao mpaka tahara
(au hedhi) tatu zipite.
" Na kauli yake: "Na wenye mimba, eda yao mpaka watakapozaa" vyote vilivyomo matumboni mwao, kiwe kimoja au vingi, na hapo haitazingatiwa miezi au kitu chochote kile. "Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi."
#
{5} {ذلك}؛ أي: الحكم الذي بيَّنه الله لكم {أمرُ الله أنزلَه إليكم}: لتمشوا عليه وتأتمُّوا به وتُعظموه. {ومَن يتَّقِ الله يُكَفِّرْ عنه سيئاتِهِ ويُعْظِمْ له أجراً}؛ أي: يندفع عنه المحذور ويحصل له المطلوب.
{5} "Hiyo" hukumu ambayo Mwenyezi Mungu amekubainishieni "ni amri ya Mwenyezi Mungu amekuteremshieni" ili muifuate, na kuitimiza na kuipa taadhima. "Na anayemcha Mwenyezi Mungu, atamfutia maovu yake, na atampa ujira mkubwa." Yaani, atazuiwa kutokana na yale yaliyoharamishwa na atapata anachotaka.
{أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنْتُمْ مِنْ وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ وَإِنْ كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنْفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّى يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَأْتَمِرُوا بَيْنَكُمْ بِمَعْرُوفٍ وَإِنْ تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُ أُخْرَى (6) لِيُنْفِقْ ذُو سَعَةٍ مِنْ سَعَتِهِ وَمَنْ قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنْفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّهُ لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا سَيَجْعَلُ اللَّهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا (7)}.
6. Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi kwa kiasi cha pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwapa dhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine. 7. Mwenye wasaa atoe kiasi ya wasaa wake, na mwenye dhiki, atoe katika kile ambacho Mwenyezi Mungu alimpa. Mwenyezi Mungu hamjukumishi mtu ila kwa kiasi cha alichompa. Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja.
#
{6} تقدَّم أنَّ الله نهى عن إخراج المطلَّقات عن البيوت، وهنا أمر بإسكانهنَّ وقدر إسكانهنَّ بالمعروف، وهو البيت الذي يسكنه مثلُه ومثلُها؛ بحسب وُجْد الزوج وعسره، {ولا تُضارُّوهنَّ لِتُضَيِّقوا عليهنَّ}؛ أي: لا تضاروهنَّ عند سكناهنَّ بالقول أو الفعل؛ لأجل أن يمللنَ فيخرجنَ من البيوت قبل تمام العدة، فتكونوا أنتم المخرِجين لهنَّ. وحاصل هذا أنَّه نهى عن إخراجهنَّ ونهاهنَّ عن الخروج، وأمر بسكناهنَّ على وجهٍ لا يحصلُ عليهن ضررٌ ولا مشقَّة، وذلك راجعٌ إلى العرف. {وإن كنَّ}؛ أي: المطلَّقات {أولاتِ حَمْلٍ فأنفقوا عليهنَّ حتى يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ}: وذلك لأجل الحمل الذي في بطنها إن كانت بائناً، ولها ولحملها إن كانت رجعيةً، ومنتهى النَّفقة إلى وضع الحمل ؛ فإذا وضَعْنَ حملَهُنَّ؛ فإمَّا أن يرضِعْن أولادهنَّ أو لا، {فإنْ أرْضَعْنَ لكم فآتوهنَّ أجورهنَّ}: المسمَّاة لهنَّ إن كان مسمًّى، وإلاَّ؛ فأجر المثل، {وائْتَمِروا بينكم بمعروفٍ}؛ أي: ليأمر كلُّ واحدٍ من الزوجين وغيرهما الآخر بالمعروف، وهو كلُّ ما فيه منفعةٌ ومصلحةٌ في الدُّنيا والآخرة؛ فإنَّ الغفلة عن الائتمار بالمعروف يحصُلُ فيها من الضَّرر والشرِّ ما لا يعلمه إلاَّ الله، وفي الائتمار تعاونٌ على البرِّ والتَّقوى. ومما يناسب هذا المقام أنَّ الزوجين عند الفراق وقت العدَّة، خصوصاً إذا ولد بينهما ولدٌ، في الغالب يحصُلُ من التنازع والتشاجر لأجل النفقة عليها وعلى الولد مع الفراق الذي لا يحصُلُ في الغالب إلاَّ مقروناً بالبغض، فيتأثَّر من ذلك شيءٌ كثيرٌ، فكلٌّ منهما يؤمر بالمعروف والمعاشرة الحسنة وعدم المشاقَّة والمنازعة وينصحُ على ذلك، {وإن تعاسَرْتُم}: بأن لم يتَّفق الزوجان على إرضاعها لولدها، {فسترضِعُ له أخرى}: غيرها، و {لا جُناح عليكم إذا سلَّمتم ما آتيتم بالمعروف}، وهذا حيثُ كان الولد يقبلُ ثدي غير أمِّه؛ فإنْ لم يقبلْ إلاَّ ثدي أمِّه؛ تعينتْ لإرضاعه، ووجب عليها، وأجْبِرَتْ إن امتنعتْ، وكان لها أجرة المثل إن لم يتَّفقا على مسمًّى. وهذا مأخوذ من الآية الكريمة من حيث المعنى؛ فإنَّ الولد لمَّا كان في بطن أمِّه مدةَ الحمل لا خروج له منه ؛ عيَّن تعالى على وليِّه النفقة، فلما ولد وكان يتمكَّن أن يتقوَّت من أمِّه ومن غيرها؛ أباح تعالى الأمرين؛ فإذا كان بحالة لا يمكن أن يتقوَّت إلاَّ من أمِّه؛ كان بمنزلة الحمل، وتعينت أمُّه طريقاً لِقُوتِه.
{6} Imetajwa hapo awali kuwa Mwenyezi Mungu amekataza kuwatoa wanawake waliopewa talaka majumbani, na hapa akaamrisha wawekwe nyumbani kwa wema. Nayo ni nyumba ambayo watu kama yeye na kama mkewe huishi. Kwa mujibu wa kiasi awezavyo mume. "Wala msiwaletee madhara kwa kuwapa dhiki" kwa kauli au vitendo. Ili wapate kuchoka na kuondoka nyumbani kabla ya kumaliza eda yao, na hapo mnakuwa ndio mumewatoa. Jumla ya hayo ni kwamba aliwakataza kuwatoa na akawakataza kutoka nje, na akawaamrisha kuwafanya waishi katika njia ambayo haitawaletea madhara wala taabu, na hilo ni kulingana na desturi. "Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue." Hilo ni kwa sababu ya mimba iliyomo tumboni mwake ikiwa ni mwanamke aliyetalikiwa talaka isiyo ya kurudiana, na kwa sababu yake mwenyewe na mimba yake ikiwa ni talaka ya kurudiana, na mwisho waa matunzo hayo ni mpaka ajifungue. Basi wakishajifungua, ima watawanyonyesha watoto wao au la. "Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao" kama walivyosikilizana ikiwa watasikilizana juu ya kiwango maalumu. Vinginevyo, basi atapewa ujira kama ule wanaopewa mfano wake. "Na shaurianeni kwa wema" wenye manufaa na masilahi katika dunia na akhera. Kwa maana kughafilika katika kushauriana yaliyo mema kunasababisha madhara na maovu anayojua Mwenyezi Mungu pekee. Na katika kushauriana kuna ushirikiano katika wema na ucha Mungu. Na katika kinachonasibiana na hali hii ni kwamba wanandoa wanapotengana wakati wa eda, hasa ikiwa mtoto amezaliwa kati yao, mara nyingi hutokea migogoro na ugomvi juu ya matunzo ya mke huyu na mtoto kwa sababu ya chuki iliyoko kati yao, kwa hivyo mambo mengi yanaathiriwa na hayo. Basi kila mmoja wao anafaa kushauri kwa wema na kuishi kwa uzuri, siyo kugombana kupingana au kugombana. "Na mkiona uzito kati yenu" ikiwa wanandoa hao hawatakubaliana juu ya kumnyonyesha mtoto wake, "basi amnyonyeshee mwanamke mwengine"
asiyekuwa yeye, "wala hapana ubaya kwenu mkitoa mlichoahidi kwa mujibu wa ada." Hili ni pale mtoto anakubali kunyonya mtu asiyekuwa mama yake. Lakini ikiwa hakubali isipokuwa titi la mama yake, basi mama yake tu ndiye atakayemnyonyesha, na itamlazimu kufanya hivyo ikiwa atakataa, na atastahiki ujira mfano wa ule wanaopewa mfano wake ikiwa hawakuwa hawatakubaliana juu ya ujira maalumu. Hili limechukuliwa kutoka katika Aya hii tukufu kulingana na maana yake. Kwa maana, mtoto alipokuwa tumboni mwa mama yake kwa kipindi chote cha ujauzito, hakukuwa na njia ya kutoka humo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamuamrisha mlinzi wake kumpa matumizi ya kila siku. Basi pale alipozaliwa na kukawa na uwezekano wa kunyonyeshwa na mama yake au na wengineo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaruhusu mambo yote hayo mawili. Basi ikiwa yuko katika hali ambayo hawezi kunyonyeshwa isipokuwa na mama yake tu, basi hilo linakuwa sawa na wakati alivyokuwa tumboni, na mama yake anakuwa ndiye peke yake anayeweza kumnyonyesha.
#
{7} ثم قدَّر تعالى النفقة بحسب حال الزوج، فقال: {لِيُنفِقْ ذو سَعةٍ من سعتِهِ}؛ أي: لينفق الغنيُّ من غناه؛ فلا ينفق نفقة الفقراء، {ومن قُدِرَ عليه رزقُه}؛ أي: ضيِّق عليه، {فلينفِقْ ممَّا آتاه الله}: من الرزق. {لا يكلِّفُ الله نفساً إلاَّ ما آتاها}: وهذا مناسبٌ للحكمة والرحمة الإلهية؛ حيث جعل كلاًّ بحسبه، وخفَّف عن المعسر، وأنَّه لا يكلِّفه إلاَّ ما آتاه؛ فلا يكلِّف الله نفساً إلا وسعها في باب النفقة وغيرها، {سيجعلُ الله بعد عسرٍ يُسْراً}: وهذه بشارةٌ للمعسرين أنَّ الله تعالى سيزيلُ عنهم الشدَّة ويرفع عنهم المشقَّة؛ فإنَّ مع العسر يسراً، إنَّ مع العسر يسراً.
{7} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaweka kipimo cha mali ya matumizi ya kila siku kulingana na hali ya mume,
akasema: "Mwenye wasaa atoe kiasi ya wasaa wake." Yaani, tajiri na atoe kutoka katika utajiri wake, wala asitoe matumizi kama ya masikini. "Na mwenye dhiki, atoe katika kile ambacho Mwenyezi Mungu alimpa. Mwenyezi Mungu hamjukumishi mtu ila kwa kiasi cha alichompa." Haya yanafailiana na hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema zake. Ambapo alimuamrisha kila mmoja kulingana na hali yake, na akamwepesishia mwenye uzito, na kwamba hamtwiki ila kile alichompa, sawa iwe ni katika mlango wa kutoa matumizi ya kila siku au mengineyo. "Mwenyezi Mungu atajaalia baada ya dhiki faraja." Hii ni bishara njema kwa wale walio katika matatizo kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaondolea dhiki na ugumu wake. Kwa maana pamoja na dhiki kuna wepesi. Hakika pamoja na dhiki kuna wepesi.
{وَكَأَيِّنْ مِنْ قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِ فَحَاسَبْنَاهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَاهَا عَذَابًا نُكْرًا (8) فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَاقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا (9) أَعَدَّ اللَّهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فَاتَّقُوا اللَّهَ يَاأُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ آمَنُوا قَدْ أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا (10) رَسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّهِ مُبَيِّنَاتٍ لِيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا قَدْ أَحْسَنَ اللَّهُ لَهُ رِزْقًا (11) اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا (12)}.
8. Na miji mingapi iliyovunja amri ya Mola wake Mlezi na Mitume wake, basi tuliihisabia hisabu ngumu na tukaiadhibu kwa adhabu kali. 9. Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ilikuwa hasara. 10. Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlioamini! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Ukumbusho. 11. Mtume anayekusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zinazobainisha, ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka vizani kuwapeleka kwenye nuru. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani za mbinguni zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwisha mpa riziki nzuri. 12. Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba mbingu saba, na ardhi kwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka baina yake, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza mno juu ya kila kitu, na kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa elimu yake.
#
{8 - 10} يخبر تعالى عن إهلاكه الأمم العاتية والقرونَ المكذِّبة للرُّسل، وأنَّ كثرتهم وقوَّتهم لم تُغْنِ عنهم شيئاً حين جاءهم الحساب الشديد والعذاب الأليم، وأنَّ الله أذاقَهم من العذاب ما هو موجبُ أعمالهم السيَّئة، ومع عذاب الدُّنيا؛ فإنَّ الله أعدَّ لهم في الآخرة عذاباً شديداً، {فاتَّقوا اللهَ يا أولي الألبابِ}؛ أي: يا ذوي العقول التي تفهم عن الله آياته وعبره، وأنَّ الذي أهلك القرون الماضية بتكذيبهم؛ أنَّ مَنْ بعدَهم مثلهم، لا فرق بين الطائفتين.
{8 - 10} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya maangamizo yake mataifa yenye nguvu na karne ambazo ziliwakadhibisha Mitume, na kwamba wingi wao na nguvu zao havikuwafaa kitu ilipowajia hesabu kali na adhabu chungu, na kwamba Mwenyezi Mungu akawaonjesha adhabu iliyotokana na matendo yao mabaya. Na pamoja na adhabu ya dunia, basi hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali katika Akhera. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili." Yaani, enyi watu wenye akili zinazozifahamu ishara na mazingatio ya Mwenyezi Mungu, na kwamba yule aliyeziangamiza karne zilizopita kwa sababu ya kukadhibisha kwao, basi wale wa baada yao watakuwa mfano wao, na hakuna tofauti baina ya makundi mawili haya.
#
{11} ثم ذكَّر عباده المؤمنين بما أنزل عليهم من كتابه الذي أنزله على رسوله محمدٍ - صلى الله عليه وسلم -؛ ليخرج الخلق من ظُلُمات الجهل والكفر والمعصية إلى نور العلم والإيمان والطاعة؛ فمن الناس من آمن به، ومنهم مَنْ لم يؤمنْ به، {ومَن يؤمِن بالله ويعملْ صالحاً}: من الواجبات والمستحبَّات، {يُدْخِلْهُ جناتٍ تجري من تحتِها الأنهارُ}: فيها من النعيم المقيم ما لا عينٌ رأتْ ولا أذنٌ سمعتْ ولا خطر على قلبِ بشرٍ. {خالدين فيها أبداً قد أحسنَ اللهُ له رِزْقاً}؛ أي: ومن لم يؤمن بالله ورسوله؛ فأولئك أصحابُ النار هم فيها خالدون.
{11} Kisha akawakumbusha waja wake yale walioteremshiwa ya Kitabu chake alichokiteremsha kwa Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ili kuwatoa watu katika viza vya ujinga, ukafiri na uasi na kuwaingiza kwenye nuru ya elimu, imani na utii. Kwa hivyo, miongoni mwa watu wapo wanaoiamini, na miongoni mwao wapo wasioiamini." Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema" miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yanayopendekezwa "atamwingiza katika Bustani za mbinguni zipitazo mito kati yake" ambayo ndani yake kuna raha ya milele ambayo jicho halijawahi kuona, wala sikio halijawahi kusikia, wala moyo wa mwanadamu haujapata kuyaona; "wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwishampa riziki nzuri." Yaani, na asiyemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hao ndio watu wa Motoni, na humo watakaa milele.
#
{12} ثم أخبر تعالى أنَّه خلق السماوات والأرض ومن فيهنَّ والأرضين السبع ومن فيهنَّ وما بينهنَّ، وأنزل الأمر، وهو الشرائع والأحكام الدينيَّة، التي أوحاها إلى رسله لتذكير العباد ووعظهم، وكذلك الأوامر الكونيَّة والقدريَّة التي يدبِّر بها الخلق؛ كلُّ ذلك لأجل أن يعرِفَه العباد ويعلموا إحاطةَ قدرته بالأشياء كلِّها وإحاطة علمِهِ بجميع الأشياء؛ فإذا عَرَفوه بأسمائه الحسنى وأوصافه المقدَّسة ؛ عبدوه وأحبُّوه وقاموا بحقِّه؛ فهذه الغاية المقصودة من الخلق والأمْر؛ معرفة الله وعبادته، فقام بذلك الموفَّقون من عباد الله الصالحين، وأعرض عن ذلك الظالمون المعرضون.
{12} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kwamba ameziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na ardhi saba na vilivyomo ndani yake na vilivyomo baina yake, na akateremsha amri ambayo ni sheria na hukumu za dini alizoziteremsha kwa Mitume wake ili kuwakumbusha na kuwaaidhi waja wake, pamoja na amri za kiulimwengu na zile za mipango ya Mwenyezi Mungu ambazo kwazo Yeye huwaendesha viumbe. Yote haya ni ili waja wamjue na wajue kwamba uweza wake umekizunguka kila kitu na elimu yake imekizingira kila kitu. Kwa hivyo, ikiwa watamjua kwa majina yake mazuri na sifa zake takatifu, watamwabudu, watampenda, na watatimiza haki zake,
na hayo ndiyo lengo lililokusudiwa katika uumbaji na amri: Kumjua Mwenyezi Mungu na kumuabudu. Basi wakafanya hayo wale waliowezeshwa miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, nao madhalimu wakayapa kisogo.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *