:
Tafsiri ya surat Taghabun
Tafsiri ya surat Taghabun
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 4 #
{يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ (1) هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنْكُمْ كَافِرٌ وَمِنْكُمْ مُؤْمِنٌ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (2) خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ (3) يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ (4)}.
1. Kinamtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo katika mbingu na katika ardhi. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. 2. Yeye ndiye aliyekuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mno mnayoyatenda. 3. Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake. 4. Anajua vilivyomo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayoyaficha na mnayoyaweka hadharani. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
#
{1} هذه الآيات الكريمات مشتملاتٌ على جملةٍ كثيرةٍ واسعة من أوصاف الباري العظيمة، فذَكَرَ كمال ألوهيَّته سبحانه [وتعالى]، وسعة غناه، وافتقارَ جميع الخلائق إليه، وتسبيح من في السماوات والأرض بحمد ربِّها، وأنَّ المُلْكَ كلَّه لله؛ فلا يخرج عن ملكه مخلوقٌ ، والحمد كله له؛ حمدٌ على ما له من صفات الكمال، وحمدٌ على ما أوجده من الأشياء، وحمدٌ على ما شرعه من الأحكام وأسداه من النِّعم، وقدرتُه شاملةٌ لا يخرج عنها موجودٌ؛ فلا يعجِزُهُ شيءٌ يريده.
{1} Aya hizi tukufu zina maelezo mengi makubwa ya Muumba. Alitaja ukamilifu wa uungu wake, Yeye aliyetakasika, Mtukufu, na upana wa utajiri wake, haja kubwa ya viumbe vyote kwake, na kutakaswa na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini kwa kumhimidi Mola wao Mlezi, na kwamba ufalme wote ni wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, hakuna kiumbe chenye kuondoka katika ufalme wake, na sifa njema zote ni zake. Kuhimidiwa kwote ni kwake kwa sababu ya sifa zake kamilifu, na anahimidiwa kwa sababu ya vitu alivyoviumba, na anahimidiwa kwa hukumu alizozitunga katika sheria na neema alizopeana. Na uwezo wake ni wa kujumuisha kila kitu ambao hakuna kitu kilichopo kinachoweza kutoka nje yake. Kwa hivyo hakuna anachotaka kinachoweza kumshinda.
#
{2} وذكر أنَّه خلق العباد، وجعل منهم المؤمن والكافر؛ فإيمانهم وكفرُهم كلُّه بقضاء الله وقدره، وهو الذي شاء ذلك منهم؛ بأنْ جعل لهم قدرةً وإرادةً بها يتمكَّنون من كلِّ ما يريدون من الأمر والنهي. {والله بما تعلمون بصيرٌ}.
{2} Alitaja kwamba Yeye ndiye aliyewaumba waja na akawafanya miongoni mwa Muumini na kafiri. Basi Imani yao na ukafiri wao vyote vinatokana na mipango ya Mwenyezi Mungu na mapitisho yake, na Yeye ndiye aliyetaka hayo hatokee kwao; kwa kuwapa uwezo na utashi, kwavyo wanaweza kufikia kila wanachotaka, kiwe ni maamrisho au makatazo. "Na Mwenyezi Mungu anayaona mno mnayoyatenda."
#
{3} فلمَّا ذكر خلق الإنسان المأمور المنهيِّ؛ ذكر خلق باقي المخلوقات، فقال: {خَلَقَ السمواتِ والأرض}؛ أي: أجرامهما وجميع ما فيهما فأحسنَ خَلْقَهما {بالحقِّ}؛ أي: بالحكمة والغاية المقصودة له تعالى، {وصَوَّرَكم فأحسن صُوَرَكم}؛ كما قال تعالى: {لقد خَلَقْنا الإنسان في أحسن تقويم}: فالإنسان أحسن المخلوقات صورةً، وأبهاها منظراً. {وإليه المصيرُ}؛ أي: المرجع يوم القيامةِ، فيجازيكم على إيمانكم وكفركم، ويسألكم عن النِّعم والنعيم الذي أولاكم؛ هل قمتُم بشكره أم لم تقوموا به ؟
{3} Alipotaja kuumbwa kwa mwanadamu, anayeamrishwa na kukatazwa, akataja kuumbwa kwa viumbe vilivyobakia, akasema: "Ameziumba mbingu na ardhi." Yaani, miili yake na vyote vilivyomo ndani yake, na akaviumba vyema sana "kwa haki." Yaani, kwa hekima na makusudio aliyoyakusudia "na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu." Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lililo bora kabisa," kwa hivyo, mwanaadamu ndiye kiumbe bora zaidi kuliko viumbe vyote kwa sura, na mwenye mwonekano mrembo zaidi. "Na marejeo ni kwake" siku ya Kiyama, kisha atakulipeni kwa imani yenu na ukafiri wenu, na atakuulizeni juu ya neema zake alizokujalieni. Je, mlimshukuru au la?
#
{4} ثم ذكر عموم علمه، فقال: {يعلم ما في السمواتِ والأرض}؛ أي: من السرائر والظواهر والغيب والشهادة، {ويعلمُ ما تُسِرُّون وما تُعْلِنونَ والله عليمٌ بذاتِ الصُّدور}؛ أي: بما فيها من الأسرار الطيِّبة والخبايا الخبيثة والنيَّات الصالحة والمقاصد الفاسدة؛ فإذا كان عليماً بذات الصُّدور؛ تعيَّن على العاقل البصير أن يحرص ويجتهد في حفظ باطِنِه من الأخلاق الرذيلة واتِّصافه بالأخلاق الجميلة.
{4} Kisha akataja ujumla ya elimu yake, na akasema: "Anajua vilivyomo katika mbingu na ardhi" Yaani, ya siri na dhahiri, ya ghaibu na yanayoonekana. "Na anajua mnayoyaficha na mnayoyaweka hadhanari. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani." Yaani, ikiwa ni pamoja na siri zake nzuri, na vitu vilivyofichika vibaya, nia njema na malengo mabovu. Na ikiwa anajua vyema yaliyomo vifuani, basi inamlazimu mtu mwenye akili timamu na mwenye msukumo wa kutenda mema ajitahidi kulinda ndani yake kutokana na tabia chafu na kusifika na tabia nzuri.
: 5 - 6 #
{أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ (5) ذَلِكَ بِأَنَّهُ كَانَتْ تَأْتِيهِمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوْا وَاسْتَغْنَى اللَّهُ وَاللَّهُ غَنِيٌّ حَمِيدٌ (6)}.
5. Kwani haikukujieni habari ya wale waliokufuru kabla, wakaonja matokeo mabaya ya mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu. 6. Hayo ni kwa kuwa Mitume wao walikuwa wakiwajia kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: 'Hivyo binadamu ndio atuongoe?' Basi wakakufuru, na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji, naye ni Msifiwa.
#
{5} لما ذكر تعالى من أوصافه الكاملة العظيمة ما به يُعرف، ويُعبد، ويُبذل الجهدُ في مرضاته، وتُجتنبُ مساخِطُه؛ أخبر بما فعل بالأمم السابقين والقرون الماضين، الذين لم تَزَلْ أنباؤهم يتحدَّثُ بها المتأخرون، ويُخْبِرُ بها الصادقون، وأنَّهم حين جاءتهم رسلُهم بالحقِّ؛ كذَّبوهم، وعاندوهم فأذاقهم الله وَبالَ أمرِهم في الدُّنيا، وأخزاهم فيها. {ولهم عذابٌ أليمٌ}: في الدار الآخرة.
{5} Mwenyezi Mungu alipotaja miongoni mwa sifa zake kubwa na kamilifu kile anachojulikana kwacho, na kuabudiwa, na kufanywa bidii katika yale yanayomridhisha, na kujiweka mbali na yenye kumkasirisha, akajulisha aliyowafanyia umma wa zamani na karne zilizopita, ambayo habari zao zinaendelea kusemwa na watu wa baadaye, na yasemwa na wakweli, na kwamba Mitume wao walipowajia kwa Haki, wakawakadhibisha na wakawafanyia ukaidi, basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha matokeo mabaya ya mambo yao katika dunia, na akawafedhehesha humo. "Na wao wana adhabu iliyo chungu" katika Akhera.
#
{6} ولهذا ذكر السبب في هذه العقوبة، فقال: {ذلك}: النكال والوبال الذي أحللناه بهم {بأنَّه كانت تأتيهم رُسُلُهم بالبيناتِ}؛ أي: بالآيات الواضحات الدالَّة على الحقِّ والباطل، فاشمأزُّوا واستكبروا على رسلهم، وقالوا: {أبشرٌ يهدونَنا}؛ أي: ليس لهم فضلٌ علينا؛ ولأيِّ شيءٍ خصَّهم الله دوننا؟! كما قال في الآية الأخرى: {قالتْ لهم رسُلُهم إن نحنُ إلاَّ بشرٌ مثلُكم ولكنَّ الله يمنُّ على مَن يشاءُ من عبادِه}: فهم حجروا فضل الله ومنَّته على أنبيائه أن يكونوا رسلاً للخلق، واستكبروا عن الانقياد لهم، فابْتُلوا بعبادة الأشجار والأحجار ونحوها، {فكفروا} بالله، {وتولَّوا} عن طاعته، {واستغنى الله} عنهم؛ فلا يبالي بهم ولا يضرُّه ضلالهم شيئاً. {والله غنيٌّ حميدٌ}؛ أي: هو الغنيُّ الذي له الغنى التامُّ المطلقُ من جميع الوجوه، الحميد في أقواله وأفعاله وأوصافه.
{6} Ndiyo maana akataja sababu ya adhabu hii, akasema: "Hayo" mateso na adhabu ambayo tuliwafikishia "kwa kuwa Mitume wao walikuwa wakiwajia kwa hoja zilizo wazi," zinazoashiria haki na batili, lakini wakazichukia mno na wakawatakabaria Mitume wao, na wakasema: "Hivyo binadamu ndio atuongoe?" Yaani, hawana ubora wowote juu yetu. Basi ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu akawachagua badala ya sisi? Kama alivyosema katika Aya nyengine: "Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote ila ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake." Basi wakataka kufungia fadhila na neema za Mwenyezi Mungu zisiwafikie Manabii wake kuwa ni Mitume kwa viumbe, na wakajivuna kuwafuata, basi wakapewa mtihani wa kuabudu miti na mawe na mengineyo, "basi wakamkufuru" Mwenyezi Mungu, "na wakageuka upande" wakaacha kumtii. "Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao." Hakuwajali na wala upotofu wao haumdhuru hata kidogo. "Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji, naye ni Msifiwa." Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha kikamilifu kabisa kwa namna zote. Naye ni msifiwa mno katika maneno yake, matendo yake na sifa zake.
: 7 #
{زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنْ لَنْ يُبْعَثُوا قُلْ بَلَى وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ وَذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ (7)}
7. Wale waliokufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyoyatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
#
{7} يخبر تعالى عن عناد الكافرين وزعمهم الباطل وتكذيبهم بالبعث بغير علمٍ ولا هدىً ولا كتابٍ منيرٍ، فأمر أشرف خلقِهِ أن يُقْسِمَ بربِّه على بعثهم وجزائهم بأعمالهم الخبيثة وتكذيبهم بالحقِّ. {وذلك على الله يسيرٌ}: فإنَّه وإن كان عسيراً، بل متعذِّراً بالنسبة إلى الخلق؛ فإنَّ قُواهم كلهم لو اجتمعت على إحياء ميتٍ واحدٍ؛ ما قدروا على ذلك، وأمَّا الله تعالى، فإنَّه إذا أراد شيئاً؛ قال له: كنْ فيكون؛ قال تعالى: {ونُفِخَ في الصُّورِ فَصَعِقَ مَن في السموات ومن في الأرض إلاَّ مَن شاء الله ثم نُفِخَ فيه أخرى فإذا هم قيامٌ ينظُرونَ}.
{7} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ukaidi wa makafiri, madai yao ya uwongo, na kukanusha kwao kufufuliwa bila ya elimu, wala mwongozo, wala Kitabu chenye nuru. Basi akamuamrisha kiumbe wake mtukufu zaidi kwamba aape kwa Mola wake Mlezi kuhusu kufufuliwa kwao, na malipo yao juu ya maovu yao na kukanusha kwao haki. "Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu." Kwani hata kama ni vigumu, au hata haiwezekani kulingana na viumbe, basi hakika ikiwa nguvu zao zote kama zingeunganishwa pamoja ili kumfufua mtu mmoja aliyekufa, hawangeweza kufanya hivyo. Ama Mwenyezi Mungu Mtukufu akitaka kitu, Yeye kwa hakika hukiambia: Kuwa na kinakuwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na itapulizwa katika barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipokuwa ambaye Mwenyezi Mungu alimtaka. Kisha itapulizwa ndani yake mara nyingine. Hapo, tazama, watainuka wawe wanangojea."
: 8 #
{فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنْزَلْنَا وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (8)}
8. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyoiteremsha. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
#
{8} لمَّا ذكر تعالى إنكارَ مَنْ أنكر البعث، وأنَّ ذلك منهم موجبٌ كفرَهم بالله وآياته؛ أمر بما يعصمُ من الهلكة والشقاء، وهو الإيمان به وبرسوله وبكتابه ، وسمَّاه الله نوراً؛ لأنَّ النور ضدُّ الظلمة؛ فما في الكتاب الذي أنزله الله من الأحكام والشرائع والأخبار أنوارٌ يُهتدى بها في ظُلمات الجهل المدلهمَّة، ويمشى بها في حِنْدِسِ الليل البهيم، وما سوى الاهتداء بكتاب الله؛ فهي علومٌ ضررها أكثر من نفعها، وشرُّها أكثر من خيرها، بل لا خير فيها ولا نفع؛ إلاَّ ما وافق ما جاءت به الرسل، والإيمانُ بالله ورسوله وكتابه يقتضي الجزم التامَّ واليقين الصادق بها والعمل بمقتضى ذاك التصديق من امتثال الأوامر واجتناب النواهي. {والله بما تعملونَ خبيرٌ}: فيجازيكم بأعمالكم الصالحة والسيِّئة.
{8} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja ukanushaji wa wale waliokanusha kufufuliwa, na kwamba hilo linawafanya kumkufuru Mwenyezi Mungu na Ishara zake, akaamrisha kinachotukinga mbali na maangamizo na mashaka, nacho ni kumwamini Yeye, Mtume wake, na Kitabu chake. Na Mwenyezi Mungu akakiita nuru kwa sababu nuru ni kinyume cha giza. Kwa hivyo, yaliyomo ndani ya Kitabu alichoteremsha Mwenyezi Mungu ya hukumu, sheria mbalimbali na habari mbalimbali ni nuru za kujiongoza kwazo katika viza vya ujinga ulioenea, na kutembea kwazo katika kina cha usiku mnene, na kingine kisichokuwa kukijali Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni elimu ambazo madhara yake ni zaidi kuliko manufaa yake, bali hata hazina heri wala manufaa, isipokuwa mambo yenye kuafikiana na yale waliyoyaleta Mitume. Na kumwamini Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Kitabu chake kunahitaji mtu kuwa na uhakika kamili na yakini ya ukweli juu yake na kutenda kwa mujibu wa kusadiki huko kwa kutekeleza maamrisho na kuepuka makatazo. "Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda." Kisha atakulipeni kwa matendo yenu mema na mabaya.
: 9 - 10 #
{يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ذَلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (9) وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ خَالِدِينَ فِيهَا وَبِئْسَ الْمَصِيرُ (10)}
9. Siku atakayokukusanyeni kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko. Hiyo ni siku ya kupunjana. Na anayemuamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yenye kupitiwa kati yake mito, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 10. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marejeo mabaya mno.
#
{9} يعني: اذكُروا يومَ الجمع الذي يجمع الله به الأوَّلين والآخرين، ويقفُهم موقفاً هائلا عظيماً، وينبِّئهم بما عملوا؛ فحينئذٍ يظهر الفرق والتغابن بين الخلائق، ويُرفع أقوامٌ إلى علِّيين في الغرف العاليات والمنازل المرتفعات المشتملة على جميع اللَّذَّات والشهوات، ويُخفض أقوامٌ إلى أسفل سافلين محلِّ الهمِّ والغمِّ والحزن والعذاب الشديد، وذلك نتيجة ما قدَّموه لأنفسهم وأسلفوه أيَّام حياتهم، ولهذا قال: {ذلك يومُ التغابنِ}؛ أي: يظهر فيه التغابن والتفاوت بين الخلائق، ويغبن المؤمنون الفاسقين، ويعرِفُ المجرمون أنَّهم على غير شيء، وأنَّهم هم الخاسرون. فكأنَّه قيل: بأيِّ شيءٍ يحصلُ الفلاحُ والشقاء والنعيم والعذاب؟ فذكر [تعالى] أسباب ذلك بقوله: {ومَن يؤمِن بالله}: إيماناً تامًّا شاملاً لجميع ما أمر الله بالإيمان به، {ويعملْ صالحاً}: من الفرائض والنوافل؛ من أداء حقوق الله وحقوق عباده، {يُدْخِلْه جناتٍ تجري من تحتها الأنهار}: فيها ما تشتهيه الأنفسُ، وتلذُّ الأعينُ، وتختارهُ الأرواح، وتحنُّ إليه القلوب، ويكون نهاية كلِّ مرغوب. {خالدين فيها أبداً ذلك الفوزُ العظيمُ}.
{9} Maana yake ni kwamba: Kumbukeni Siku ya mkusanyiko ambao Mwenyezi Mungu atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho, na atawasimamisha katika mahali pa kusimama makubwa mno, na atawaambia yale waliyoyatenda. Kisha itadhihiri tafauti na kupunjana baina ya viumbe, na baadhi ya watu watapandishwa daraja za juu katika vyumba vya juu na nyumba za juu zenye starehe na raha zote, na watu wengine watashushwa hadi ngazi za chini kabisa, mahali pa wasiwasi kubwa, masikitiko, huzuni na adhabu kali. Hayo ni kwa sababu ya yale waliyojitangulizia wenyewe katika siku za uhai wao, na ndiyo maana akasema: "Hiyo ni siku ya kupunjana." Waumini watawapunja waliovuka mipaka, na wahalifu watajua kwamba hawakuwa katika chochote chenye faida, na kwamba wao ndio wenye hasara. Ni kana kwamba ilisemwa: Mafanikio, mashaka, furaha na adhabu vitatokea kwa nini? Basi [Mwenyezi Mungu] akataja sababu za hayo kwa kusema: "Na anayemuamini Mwenyezi Mungu" kwa Imani kamili, yenye kujumlisha yale yote aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu kuyaamini, "na akatenda mema" miongoni mwa mambo ya faradhi na ya kujitolea, kama vile kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, "Atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yenye kupitiwa kati yake mito." Humo kuna yale yanayotamaniwa na nafsi, na macho yanapendezwa nayo, na roho zinayachagua, na nyoyo zinatamani sana, na utakuwa mwisho wa yote yanayotakiwa ni kwamba "watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa."
#
{10} {والذين كفروا وكذَّبوا بآياتنا}؛ أي: كفروا بها من غير مستندٍ شرعيٍّ ولا عقليٍّ، بل جاءتهم الأدلَّة والبيِّنات، فكذَّبوا بها وعاندوا ما دلَّت عليه، {أولئك أصحابُ النار خالدين فيها وبئسَ المصيرُ}: لأنَّها جمعت كلَّ بؤسٍ وشدةٍ وشقاءٍ وعذابٍ.
{10} "Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu" bila ya uthibitisho wa kisheria wala wa kiakili. Bali aliwajia na ushahidi ulio wazi, lakini wakaukadhibisha na wakayafanyia ukaidi yale ambayo uliashiria. "Hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele. Na hayo ndiyo marejeo mabaya mno" kwa sababu umejumuisha kila mabaya, ugumu, taabu na adhabu.
: 11 - 13 #
{مَا أَصَابَ مِنْ مُصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ (11) وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ فَإِنْ تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَى رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ (12) اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ (13)}.
11. Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu. 12. Na mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu. 13. Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipokuwa Yeye. Na juu ya Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini.
#
{11} يقول تعالى: {ما أصاب من مصيبةٍ إلاَّ بإذنِ الله}: وهذا عامٌّ لجميع المصائب في النفس والمال والولد والأحباب ونحوهم؛ فجميع ما أصاب العباد بقضاء الله وقدره؛ قد سبق بذلك علمُ الله وجرى به قلمُه ونفذت به مشيئتُه واقتضتْه حكمتُه، ولكنَّ الشأن كل الشأن: هل يقومُ العبد بالوظيفة التي عليه في هذا المقام أم لا يقوم بها؟ فإنْ قام بها؛ فله الثواب الجزيل والأجر الجميل في الدُّنيا والآخرة؛ فإذا آمن أنها من عند الله، فرضي بذلك وسلَّم لأمره؛ هدى الله قلبه، فاطمأنَّ ولم ينزعجْ عند المصائب؛ كما يجري ممَّن لم يهدِ الله قلبه، بل يرزقه الله الثبات عند ورودِها والقيام بموجب الصبر، فيحصل له بذلك ثوابٌ عاجلٌ مع ما يدَّخر اللهُ له يوم الجزاء من الأجر العظيم ؛ كما قال تعالى: {إنَّما يُوَفَّى الصابرون أجرهم بغير حساب}. وعُلِمَ من ذلك أنَّ من لم يؤمنْ بالله عند ورود المصائب؛ بأن لم يلحظْ قضاء الله وقدره بل وقف مع مجرَّد الأسباب؛ أنَّه يُخذل ويَكِلُه الله إلى نفسه، وإذا وُكِلَ العبد إلى نفسه؛ فالنفس ليس عندها إلاَّ الهلع والجزع الذي هو عقوبةٌ عاجلةٌ على العبد قبل عقوبة الآخرة على ما فرَّط في واجب الصبر، هذا ما يتعلَّق بقوله: {ومَن يؤمِنْ بالله يَهْدِ قلبَه} في مقام المصائب الخاصِّ، وأمَّا ما يتعلَّق بها من حيث العموم اللَّفظيُّ؛ فإنَّ الله أخبر أنَّ كلَّ مَنْ آمنَ؛ أي: الإيمان المأمور به، وهو الإيمان بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر والقدر خيره وشرِّه، وصدَّق إيمانه بما يقتضيه الإيمان من لوازمه وواجباته؛ أنَّ هذا السبب الذي قام به العبدُ أكبرُ سببٍ لهداية الله له في أقواله وأفعاله وجميع أحواله وفي علمه وعمله، وهذا أفضل جزاءٍ يعطيه الله لأهل الإيمان؛ كما قال تعالى مخبراً أنَّه يثبِّت المؤمنين في الحياة الدنيا وفي الآخرة، وأصل الثبات ثباتُ القلب وصبرُه ويقينُه عند ورود كلِّ فتنة، فقال: {يُثبِّتُ الله الذين آمنوا بالقول الثابتِ في الحياة الدُّنيا وفي الآخرة}؛ فأهلُ الإيمان أهدى الناس قلوباً وأثبتُهم عند المزعجات والمقلقات، وذلك لما معهم من الإيمان.
{11} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu." Hili linajumuisha misiba yote katika nafsi, mali, watoto, wapenzi na mengineyo. Kila linalowasibu waja wake ni kwa sababu ya mipango na mapitisho ya Mwenyezi Mungu. Tayari Mwenyezi Mungu alishayajua hayo, kalamu yake ikayaandika, mapenzi yake yakatekelezeka hivyo, na hekima yake ikahitaji yawe hivyo. Lakini suala zima ni: Je, mja atafanya kazi aliyo nayo katika nafasi hii au hataifanya? Akifanya hivyo, basi ana malipo mengi mazuri duniani na akhera. Ikiwa ataamini kuwa yametoka kwa Mwenyezi Mungu, akayakubali na akasalimu amri kwake, basi Mwenyezi Mungu atauongoza moyo wake. Kwa hivyo atatulia na wala hatasumbuka kwa sababu ya misiba, kama yatakavyomtokea yule ambaye moyo wake haujaongozwa na Mwenyezi Mungu. Bali Mwenyezi Mungu humjaalia uthabiti yanapotokea na kufanya kulingana na namna inavyotaka subira, kwa hivyo anapata malipo ya haraka zaidi ya malipo mengi ambayo Mwenyezi Mungu alimwekea Siku ya Kiyama. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hesabu." Na ikajulikana kutokana na hili kwamba yeyote asiyemwamini Mwenyezi Mungu wakati misiba inatokea, kwamba hakuona mipango na mapitisho ya Mwenyezi Mungu, bali alisimamia kwenye visababu vyake tu, basi ataachiliwa mbali na Mwenyezi Mungu atamkabidhi kwa nafsi yake. Na mja anapokabidhiwa nafsi yake, basi nafsi haina chochote isipokuwa hofu na wasiwasi kubwa, ambayo ni adhabu ya haraka kwa mja kabla ya adhabu ya Akhera kwa yale aliyoyapuuza katika wajibu wa kuwa na subira. Haya yanahusiana na kauli yake "Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, huuongoa moyo wake" katika hali ya misiba mahsusi. Na ama yale yanayohusiana nayo kwa ujumla wa maneno, basi Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba kila aaminiye, imani aliyoamrishwa ambayo ni kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na mipango yake ya heri yake na mibaya yake, basi ataisadikisha imani yake kwa yale yanayohitajiwa na imani hiyo miongoni mwa mambo yanayofungamana nayo na wajibu zake mbalimbali, na kwamba sababu hii aliyoifanya mja ndiyo kisababu kikubwa zaidi cha Mwenyezi Mungu kumwongoa katika maneno yake, vitendo, na hali zake zote, na katika elimu yake na matendo yake. Haya ndiyo malipo bora zaidi ambayo Mwenyezi Mungu huwapa wale walio na imani. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema akitujulisha kwamba Yeye huwaimarisha Waumini katika maisha ya dunia na ya Akhera. Na asili ya uthabiti ni uthabiti wa moyo, subira yake, na yakini yake yanapotokea kila majaribio, akasema, "Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera." Basi wale walio na imani ndio watu waongofu mno katika mioyo, na walio na uthabiti zaidi mbele ya hali za shida na wasiwasi, kwa sababu ya imani waliyo nayo.
#
{12} وقوله: {وأطيعوا الله وأطيعوا الرسولَ}؛ أي: في امتثال أمرهما واجتناب نهيهما؛ فإنَّ طاعة الله وطاعة رسولِهِ مدارُ السعادة وعنوانُ الفلاح، {فإن تولَّيْتُم}؛ أي: عن طاعة الله وطاعة رسوله، {فإنَّما على رسولنا البلاغُ المبينُ}؛ أي: يبلِّغُكم ما أرسل به إليكم بلاغاً بيِّناً واضحاً، فتقوم عليكم به الحجَّة، وليس بيده من هدايتكم ولا من حسابكم شيءٌ ، وإنَّما يحاسبكم على القيام بطاعة الله وطاعة رسوله أو عدم ذلك، عالمُ الغيب والشهادة.
{12} Na kauli yake, "Na mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume." Yaani, kwa kutekeleza amri yao na kujiepusha na makatazo yao. Kwani kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake ndio furaha inazungukia hao na ndiyo kichwa cha kufaulu. "Mkigeuka" mkaacha kumtii Mwenyezi Mungu na kumtii Mtume wake, "basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu." Yaani, anakufikishieni yale aliyokutuma nayo kwa njia iliyo bainifu na wazi, ndiyo hoja itathibitika juu yenu kwa hayo, wala hana chochote mikononi mwake kuhusiana na uongofu wenu wala kuhisabiwa kwenu matendo yenu. Ni Mwenyezi Mungu tu ndiye atakayekuhisabuni juu ya kumtii Mtume wake au la. Anajua ya siri na ya dhahiri.
#
{13} {الله} الذي {لا إله إلاَّ هو}؛ أي: هو المستحق للعبادة والألوهيَّة؛ فكل معبودٍ سواه فباطلٌ. {وعلى الله فليتوكَّل المؤمنون}؛ أي: فليعتمدوا عليه في كلِّ أمرٍ نابهم وفيما يريدون القيام به؛ فإنَّه لا يتيسَّر أمرٌ من الأمور إلاَّ بالله ولا سبيل إلى ذلك إلاَّ بالاعتماد على الله، ولا يتمُّ الاعتماد على الله حتى يُحْسِنَ العبدُ ظنَّه بربِّه ويثق به في كفايته الأمر الذي يعتمد عليه به، وبحسب إيمان العبد يكون توكُّله قوةً وضعفاً.
{13} "Mwenyezi Mungu" ambaye "hapana mungu isipokuwa Yeye." Yaani, yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa na kufanyiwa uungu. Kwa hivyo kila kinachoabudiwa kisichokuwa Yeye, hicho ni batili. "Na juu ya Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini." Yaani, wamtegemee Yeye tu katika kila jambo linalowapata na lolote wanalotaka kufanya. Kwa maana hakuna jambo linaloweza kuwa jepesi isipokuwa kwa uwezo Mwenyezi Mungu, na hakuna njia ya kufanya hivyo isipokuwa kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu. Na haiwezekani kumtegemea Mwenyezi Mungu mpaka mja awe na dhana nzuri juu ya Mola wake Mlezi na awe na imani naye katika kumtosheleza katika jambo ambalo anamtegemea juu yake. Na kutegemea kwa mja kunakuwa na kwa nguvu au dhaifu kulingana na imani ya mja.
: 14 - 15 #
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ وَإِنْ تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (14) إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَاللَّهُ عِنْدَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ (15)}
14. Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. 15. Hakika mali yenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa.
#
{14 - 15} هذا تحذيرٌ من الله للمؤمنين عن الاغترار بالأزواج والأولاد؛ فإنَّ بعضهم عدوٌّ لكم، والعدوُّ هو الذي يريد لك الشرَّ، فوظيفتُك الحذرُ ممَّن هذه صفته ، والنفس مجبولة على محبّة الأزواج والأولاد، فنصح تعالى عباده أن توجب لهم هذه المحبة الانقياد لمطالب الأزواج والأولاد، التي فيها محذورٌ شرعيٌّ ، ورغَّبهم في امتثال أوامره وتقديم مرضاته بما عنده من الأجر العظيم، المشتمل على المطالب العالية والمحابِّ الغالية، وأن يؤثِروا الآخرة على الدُّنيا الفانية المنقضية. ولما كان النهيُ عن طاعة الأزواج والأولاد فيما هو ضررٌ على العبد والتحذير من ذلك قد يوهِمُ الغِلْظَةَ عليهم وعقابهم؛ أمَرَ تعالى بالحذر منهم والصفح عنهم والعفو؛ فإنَّ في ذلك من المصالح ما لا يمكن حصرُه، فقال: {وإن تَعْفوا وتَصْفَحوا وتَغْفِروا فإنَّ الله غفورٌ رحيمٌ}؛ لأنَّ الجزاء من جنس العمل؛ فمن عفا؛ عفا الله عنه، ومن صَفَحَ؛ صفح [اللَّه] عنه، ومن عامَلَ الله [تعالى] فيما يحبُّ، وعامل عباده بما يحبُّون وينفعهم؛ نال محبَّة الله ومحبَّة عباده واستوسق له أمره.
{14 - 15} Hili ni onyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waumini kuhusu kudanganywa na wake wao na watoto wao. Kwani baadhi yao ni maadui zenu. Kwa sababu adui ni yule anayekutakia mabaya, basi jukumu lenu ni kujihadhari na wenye tabia hii, lakini nafsi zimefanywa kuwapenda wake na watoto, kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawausia waja wake ili upendo huu usiwasababishie kutii matakwa ya wake zao na watoto wao, ambayo yameharamishwa na sheria, na akawatia moyo wafuate amri zake na watangulize radhi zake kwa sababu ya malipo makubwa aliyo nayo, ambayo yanajumuisha mambo makubwa yanayotafutwa na mambo ghali yanayopendwa, na kwamba wapendelee akhera kuliko dunia inayopita na kuisha. Na kwa kuwa kukataza kuwatii wake na watoto katika mambo yenye madhara kwa mja na onyo dhidi ya hilo huenda kukaleta dhana ya kuwa mkali kwao na kuwaadhibu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamuru kuwatahadhari, kuachilia mbali na kuwasamehe. Kwani kuna manufaa katika haya ambayo hayahesabiki wala kufungika: "Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu." Kwa sababu malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa hivyo, mwenye kusamehe, Mwenyezi Mungu anamsamehe. Na anayeachilia mbali, Mwenyezi Mungu anaachilia mbali makosa yake. Na anayeamiliana na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale anayoyapenda na atamiliana na waja wake katika yale wanayoyapenda na kuwanufaisha, atapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi ya waja wake, na mambo yake yatanyooka sawa.
: 16 - 18 #
{فَاتَّقُوا اللَّهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنْفِقُوا خَيْرًا لِأَنْفُسِكُمْ وَمَنْ يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ (16) إِنْ تُقْرِضُوا اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَاللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ (17) عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (18)}.
16. Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na tiini, na toeni, itakuwa heri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio waliofanikiwa. 17. Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni maradufu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mstahamilivu. 18. Mwenye kujua siri na dhahiri, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{16} يأمر تعالى بتقواه التي هي امتثالُ أوامره واجتنابُ نواهيه، وقيَّد ذلك بالاستطاعة والقدرة. فهذه الآية تدلُّ على أنَّ كلَّ واجبٍ عجز عنه العبد يسقُطُ عنه، وأنَّه إذا قدر على بعض المأمور وعجز عن بعضه؛ فإنَّه يأتي بما يقدر عليه ويسقُطُ عنه ما يعجزُ عنه؛ كما قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -: «إذا أمرتُكم بأمرٍ؛ فأتوا منه ما استطعتُم ». ويدخل تحت هذه القاعدة الشرعيَّة من الفروع ما لا يدخُل تحت الحصر. وقوله: {واسمعوا}؛ أي: اسمعوا ما يعِظُكم الله به وما يَشْرَعُه لكم من الأحكام واعلموا ذلك وانقادوا له، {وأطيعوا}: الله ورسولَه في جميع أموركم، {وأنفِقوا}: من النفقات [الشرعية] الواجبة والمستحبَّة؛ يَكُنْ ذلك الفعل منكم خيراً لكم في الدُّنيا والآخرة؛ فإنَّ الخير كلَّه في امتثال أوامر الله [تعالى] وقَبول نصائحه والانقياد لشرعه، والشرَّ كلَّه في مخالفة ذلك، ولكن ثَمَّ آفةٌ تمنعُ كثيراً من الناس من النفقة المأمور بها، وهو الشحُّ المجبولة عليه أكثر النفوس؛ فإنَّها تشحُّ بالمال وتحبُّ وجوده وتكره خروجه من اليد غاية الكراهة، فمن وقاه اللَّهُ [تعالى] {شُحَّ نفسِه}: بأن سمحت نفسه بالإنفاق النافع لها، {فأولئك هم المفلحونَ}: لأنَّهم أدركوا المطلوب ونجوا من المرهوب، بل لعلَّ ذلك شاملٌّ لكلِّ ما أمر به العبدُ ونهي عنه؛ فإنَّه إن كانت نفسُه شحيحةً لا تنقاد لما أمرت به ولا تخرِج ما قِبَلَها؛ لم يفلح، بل خسر الدنيا والآخرة، وإن كانت نفسه نفساً سمحة مطمئنةً منشرحةً لشرع الله طالبةً لمرضاته ؛ فإنَّها ليس بينها وبين فعل ما كلِّفت به إلاَّ العلم به ووصول معرفته إليها والبصيرة بأنَّه مُرضٍ لله [تعالى]، وبذلك تفلح وتنجح وتفوز كلَّ الفوز.
{16} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha afanyiwe ucha Mungu, ambao ni kutii amri zake na kuepuka makatazo yake, na akafungia hilo kwamba mtu awe na uwezo. Basi aya hii inaashiria kwamba kila wajibu ambao mja hawezi kuufanya, anakuwa halazimiki kuufanya, na kwamba ikiwa ataweza kutekeleza baadhi ya maamrisho na akashindwa kutekeleza baadhi yake, anafanya kile anachoweza kufanya na kile ambacho hawezi kufanya kinakuwa si lazima juu yake. Kama alivyosema Nabii -rehema na amani na Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Nikikuamrisheni kufanya jambo, basi fanyeni kwacho kiasi muwezavyo.” Inaingia katika kanuni hii ya kisheria matawi madogo mengi sana. Na kauli yake: "Na sikilizeni." Yaani, sikilizeni anachokunasihini kwacho Mwenyezi Mungu na sheria ya hukumu mbalimbali anazokuwekeeni, na yajueni na muyafuate. "Na tiini" Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika mambo yenu yote, "na toeni" mali za kisheria za faradhi na za kupendekezwa. Kitendo chenu hicho kitakuwa heri kwenu duniani na akhera. Kwani heri yote iko katika kutii maamrisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kukubali nasaha zake, na kufuata sheria yake. Na ubaya wote upo katika kukiuka hilo. Lakini kuna ugonjwa ambao huzizuia nafsi nyingi kutoa mali iliyoamrishwa. Na ni ubahili ambao nafsi nyingi zimefanywa kuwa nao. Kwani hizo hufanyia mali ubahili, na zinapenda uwepo wake, na zinachukia sana kutoka kwake katika mkono. Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu atamkinga mbali na "uchoyo wa nafsi yake" kwa kuiruhusu nafsi yake kutoa mali za faida kwake, "basi hao ndio waliofanikiwa." Kwa sababu walifikia yale yaliyokuwa yakitamaniwa na wakaepukana na yale yaliyokuwa yakiogopewa. Bali huenda hili linajuuisha yote ambayo mja ameamrishwa na aliyokatazwa. Kwani ikiwa nafsi yake ni choyo, haiwezi kutekeleza yale iliyoamrishwa, wala haiwezi kutoa yaliyo mbele yake, basi tatafanikiwa. Bali atahasiri dunia na akhera, na ikiwa nafsi yake ni nafsi vumilivu na iliyotulia, yenye kuifungukia sheria ya Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, basi hakuna kitu baina yake na kufanya yale ambayo alijukumishwa kufanya isipokuwa kuyajua na kufahamu kwamba ni ya kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hiyo nafsi hiyo anafaulu na kushinda ushindi wote.
#
{17} ثم رغَّب تعالى في النفقة، فقال: {إن تقرِضوا الله قرضاً حسناً}: وهو كلُّ نفقة كانت من الحلال إذا قَصَدَ بها العبدُ وجه الله تعالى ووضعها موضعها، {يضاعِفْه لكم}: النفقة بعشر أمثالها إلى سبعمائة ضعفٍ إلى أضعافٍ كثيرة، {و} مع المضاعفة أيضاً {يَغْفِرْ} اللهُ {لكم}: بسبب الإنفاق والصدقة ذنوبَكم؛ فإنَّ الذُّنوبَ يكفرها [اللَّهُ] بالصدقات والحسنات؛ {إنَّ الحسنات يُذْهِبْنَ السيئات}. {والله شكورٌ حليمٌ}: لا يعاجِلُ من عصاه، بل يُمْهِلُه ولا يُهْمِلُه، {ولو يؤاخِذُ اللهُ الناس بما كَسَبوا ما ترك على ظهرها من دابَّةٍ ولكن يؤخِّرُهم إلى أجلٍ مسمًّى}، والله تعالى شكورٌ، يقبلُ من عباده اليسير من العمل، ويجازيهم عليه الكثير من الأجر، ويشكر تعالى لمن تحمَّل من أجله المشاقَّ والأثقال وأنواع التَّكاليف الثقال، ومن ترك شيئاً لله؛ عوَّضه الله خيراً منه.
{17} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatia moyo kuhusiana na suala la kutoa mali, akasema: "Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri" ambayo ni kila mali iliyotolewa kutokana na vilivyo halali ikiwa mja atataka kwayo uso wa Mwenyezi Mungu na akaiweka mahali pake. "Atakuzidishieni maradufu." Na kila alichotoa pia kitazidishwa mara kumi mfano wake, hadi mizidisho mara mia saba, hadi mizidisho mara nyingi zaidi. Na pamoja na mizidisho hiyo, Mwenyezi Mungu "atakusameheni" dhambi zenu kwa sababu ya mali mlizotoa na sadaka yenu. Kwani [Mwenyezi Mungu] hufuta dhambi kwa sadaka na matendo mema. "Hakika mema huondoa maovu" na akasema "Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukrani, Mstahamilivu." Haharakishi kumwadhibu yule anayemuasi, bali humpa muhula wala hampuuzi. "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa waliyoyachuma, basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu." Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kushukuru mno. Anapokea kutoka kwa waja wake matendo kidogo, na huwalipa juu yake ujira mwingi. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anashukuru wale wanaostahimili taabu, mambo mazito, na aina nzito nzito za majukumu kwa ajili yake. Na mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anamlipa mema zaidi yake.
#
{18} {عالمُ الغيبِ والشهادةِ}؛ أي: ما غاب من العباد من الجنود التي لا يعلمها إلاَّ هو وما يشاهدونه من المخلوقات. {العزيزُ}: الذي لا يغالَب ولا يمانَع، الذي قهر جميع الأشياء. {الحكيمُ}: في خلقه وأمره، الذي يضع الأشياء مواضعها.
{18} "Mwenye kujua siri na dhahiri." Yaani, yale ambayo hawayaoni wala hawayajui waja miongoni mwa askari ambao Yeye tu ndiye anayewajua, na wanayoyaona miongoni mwa viumbe. "Mwenye nguvu" ambaye hashindwi au kuzuiwa, ambaye alishinda kila kitu. "Mwenye hekima" katika uumbaji wake na amri zake, anayeweka vitu mahali pake sahihi.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
* * *