Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (1) يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ (2) كَبُرَ مَقْتًا عِنْدَ اللَّهِ أَنْ تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ (3)}.
1. Vinamtakasa Mwenyezi Mungu vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 2. Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda? 3. Yanachukiza vikubwa mno kwa Mwenyezi Mungu kuwa mnasema msiyoyatenda.
#
{1} وهذا بيانٌ لعظمته تعالى وقهره وذلِّ جميع الأشياء له تبارك وتعالى وأنَّ جميع مَن في السماوات والأرض يسبِّحون بحمدِ ربِّهم ويعبُدونه ويسألونَه حوائجهم. {وهو العزيزُ}: الذي قهر الأشياء بعزَّته وسلطانِهِ. {الحكيمُ}: في خلقه وأمره.
{1} Huu ni ufafanuzi wa ukuu wake Mtukufu, ishindi wake mkubwa na kumnyenyekea kwa kila kitu Yeye aliyetakasika, Mtukufu, na kwamba vyote vilivyomo mbinguni na ardhini vinamtakasa kwa sifa zake njema, na vinamuabudu, na vinamwomba mahitaji yake.
“Na Yeye ni Mwenye nguvu” ambaye alishinda vitu vyote kwa nguvu zake na mamlaka yake.
“Mwenye hekima” katika uumbaji wake na amri zake.
#
{2 - 3} {يا أيُّها الذين آمنوا لم تقولونَ ما لا تفعلونَ}؛ أي: لم تقولونَ الخير وتحثُّون عليه، وربما تمدَّحتم به وأنتم لا تفعلونه، وتَنْهَوْنَ عن الشرِّ، وربَّما نزَّهتم أنفسكم عنه وأنتم متلوِّثون متَّصفون به؛ فهل تليقُ بالمؤمنين هذه الحالة الذَّميمة؟! أم من أكبر المقت عند الله أن يقولَ العبدُ ما لا يفعل؟! ولهذا ينبغي للآمر بالخير أن يكونَ أولَ الناس إليه مبادرةً، والناهي عن الشرِّ أن يكون أبعدَ الناس عنه ؛ قال تعالى: {أتأمرونَ الناس بالبِرِّ وتَنسَوْنَ أنفسَكم وأنتُم تتلونَ الكِتابَ أفَلا تَعْقِلونَ}، وقال شعيبٌ عليه السلام [لقومه]: {وما أريدُ أن أخالِفَكُم إلى ما أنهاكم عنه}.
{2 - 3} “Enyi mlioamini! Kwa nini mnasema msiyoyatenda?” Yaani, kwa nini mnasema ya heri na mkahimiza juu yake, na pengine mnasifu wengine kwa sababu yake ilhali nyinyi wenyewe hamuifanyi, na mnakataza maovu, na pengine mkajifanya kwamba mnajiweka mbali nayo ilhali mnasifika na kujichafua kwayo? Je, hali hii ya kukashifiwa inawafailia waumini? Au ni katika chukizo kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu mja kusema asichofanya? Kwa ajili hiyo, mwenye kuamrisha mema na awe mtu wa kwanza kuharakisha kuifanya. Na mwenye kukataza maovu na awe mbali zaidi nayo kuliko watu wote.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Je, mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamtumii akili?” Na Nabii Shuaib, amani iwe juu yake, alisema
[akiwaambia watu wake]:
“Wala mimi sipendi kukuhalifuni nikafanya yale ninayokukatazeni.”
{إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُمْ بُنْيَانٌ مَرْصُوصٌ (4)}.
4. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaopigana katika Njia yake kwa safu kama jengo liliokamatana.
#
{4} هذا حثٌّ من الله لعباده على الجهاد في سبيله، وتعليمٌ لهم كيف يصنعون، وأنهم ينبغي لهم أن يَصُفُّوا في الجهاد صفًّا متراصًّا متساوياً من غير خلل يحصُلُ في الصفوف، وتكون صفوفُهم على نظام وترتيبٍ به تحصُلُ المساواة بين المجاهدين والتعاضُد وإرهاب العدوِّ وتنشيط بعضهم بعضاً، ولهذا كان النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - إذا حضر القتال؛ صفّ أصحابه ورتَّبهم في مواقفهم بحيث لايحصُلُ اتِّكالُ بعضهم على بعض، بل تكون كلُّ طائفةٍ منهم مهتمةً بمركزها وقائمةً بوظيفتها، وبهذه الطريقة تتمُّ الأعمال ويحصُلُ الكمال.
{4} Huku ni kuhimiza kutoka kwa Mwenyezi Mungu waja wake kupigana jihadi katika njia yake, na ni kuwafundisha jinsi ya kufanya hivyo, na kwamba wanapaswa wajipange katika jihadi kwa safu zilizoshikamana, zilizo sawa bila ya kuwepo nafasi katika safu, na kwamba safu zao ziwe katika mfumo na mpangilio unaoleta usawa baina ya wanaopigana wanaoshikamana sawasawa ili kuwatishia adui, na kuamshana wao kwa wao, na ndio maana Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – alikuwa anapohudhuria katika vita, anawaweka masahaba zake katika safu na kuwapanga katika nafasi zao ili pasiwe na kutegemeana. Bali kila kundi miongoni mwao lilipaswa kujishughulisha na nafasi yake na kutekeleza kazi yake, na kwa njia hii matendo yanakamilika na ukamilifu unapatikana.
{وَإِذْ قَالَ مُوسَى لِقَوْمِهِ يَاقَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَدْ تَعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّهُ قُلُوبَهُمْ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ (5)}.
5.
Na Musa alipowaambia watu wake: 'Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliyetumwa kwenu?' Walipokengeuka, Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wavukao mipaka.
#
{5} أي: {وإذْ قال موسى لقومِهِ}: موبخاً لهم على صنيعهم، ومقرعاً لهم على أذيَّته، وهم يعلمون أنَّه رسول الله: {لم تُؤذونَني}: بالأقوال والأفعال، {وقد تعلمونَ أنِّي رسولُ الله إليكم}: والرسولُ من حقِّه الإكرام والإعظام والقيام بأوامره والابتدار لحكمِهِ، وأمَّا أذيَّة الرسول الذي إحسانُه إلى الخلق فوق كلِّ إحسان بعد إحسان الله؛ ففي غاية الوقاحة والجراءة والزيغ عن الصراط المستقيم، الذي قد عَلِموه وتَرَكوه، ولهذا قال: {فلمَّا زاغوا}؛ أي: انصرفوا عن الحقِّ بقصدهم، {أزاغَ الله قلوبَهم}: عقوبةً لهم على زيغهم الذي اختاروه لأنفسهم ورضوه لها، ولم يوفِّقْهم الله للهدى؛ لأنَّهم لا يَليقُ بهم الخير ولا يَصلُحون إلاَّ للشرِّ. {والله لا يهدي القومَ الفاسقينَ}؛ أي: الذينَ لم يزلِ الفسقُ وصفاً لهم، ليس لهم قصد في الهدى. وهذه الآية الكريمة تفيد أن إضلال الله لعبيده ليس ظلماً منه ولا حجَّة لهم عليه، وإنَّما ذلك بسببٍ منهم؛ فإنَّهم الذين أغلقوا على أنفسهم باب الهدى بعدما عرفوه، فيجازيهم بعد ذلك بالإضلال والزيغ وتقليب القلوب عقوبةً لهم وعدلاً منه بهم؛ كما قال تعالى: {ونقلِّبُ أفئِدَتَهم وأبصارَهم كما لم يؤمِنوا به أولَ مرةٍ ونَذَرُهُم في طغيانِهم يعمهونَ}.
{5} Yaani,
“Na Musa alipowaambia watu wake” akiwakemea kwa vitendo vyao na kuwakaripia kwa sababu ya kumudhi kwao ilhali wanajua kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
“Kwa nini mnaniudhi” kwa maneno na vitendo
“nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliyetumwa kwenu?” Na Mtume ana haki ya kuheshimiwa na kupewa taadhima, na kutekeleza amri zake na kuharakisha kushika hukumu zake. Na kumdhuru Mtume ambaye wema wake kwa viumbe uko juu ya wema wote baada ya wema wa Mwenyezi Mungu, hilo ni katika dhuluma kubwa zaidi, ujasiri dhidi yake, kukengeuka na kupotea mbali na njia iliyonyooka, ambayo waliijua na wakaiacha,
na ndiyo maana akasema: “Walipokengeuka” wakaiacha Haki makusudi,
“Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao” ili iwe ni adhabu ya kukengeuka kwao huko walikokuchagua wenyewe na wakakuridhia, na Mwenyezi Mungu hakuwawezesha kufikia uwongofu. Kwa sababu hawafailii wema na wala hawafailii isipokuwa uovu tu.
“Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wavukao mipaka” ambao hiyo ndiyo sifa yao na wala hawana nia ya kuongoka. Aya hii tukufu inaashiria kwamba Mwenyezi Mungu kuwapotoa waja wake si dhuluma kwa upande wake wala si udhuru kwao dhidi yake. Bali hilo ni wao waliojisababishia wenyewe. Kwani wao wenyewe ndio waliojifungia mlango wa uwongofu baada ya kuutambua, na baada ya hayo akawalipa kwa upotofu, kukengeuka, na kubadilisha nyoyo, ili iwe ni adhabu kwao na kuwafanyia uadilifu.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyokuwa hawakuiamini mara ya kwanza, kisha tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga.”
{وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَابَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِنْ بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ فَلَمَّا جَاءَهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَذَا سِحْرٌ مُبِينٌ (6) وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَى إِلَى الْإِسْلَامِ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ (7) يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ (8) هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ (9)}.
6.
Na Isa bin Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi,
walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri! 7. Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu. 8. Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia. 9. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.
#
{6} يقول تعالى مخبراً عن عناد بني إسرائيل المتقدِّمين الذين دعاهم عيسى بن مريم وقال لهم: {يا بني إسرائيلَ إنِّي رسولُ اللهِ إليكم}؛ أي: أرسلني الله لأدعوكم إلى الخير وأنهاكم عن الشرِّ، وأيَّدني بالبراهين الظاهرة، ومما يدلُّ على صدقي كوني {مصدِّقاً لما بين يديَّ من التَّوراة}؛ أي: جئت بما جاء به موسى من التوراة والشرائع السماويَّة، ولو كنت مدَّع للنبوَّةِ؛ لجئتُ بغير ما جاء به المرسلون، و {مصدِّقاً لما بين يديَّ من التَّوراة}: أيضاً أنها أخبرت بي وبشَّرت، فجئتُ وبعثتُ مصدقاً لها، {ومبشراً برسول يأتي من بعدي اسمُهُ أحمدُ}: وهو محمد بن عبد الله بن عبد المطلب النبيُّ الهاشميُّ؛ فعيسى عليه الصلاة والسلام كسائر الأنبياء ؛ يصدِّق بالنبيِّ السابق، ويبشِّر بالنبيِّ اللاحق؛ بخلاف الكذَّابين؛ فإنَّهم يناقضون الأنبياء أشدَّ مناقضة، ويخالِفونهم في الأوصاف والأخلاق والأمرِ والنهي، {فلمَّا جاءهم}: محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - الذي بَشَّرَ به عيسى {بالبيِّناتِ}؛ أي: الأدلَّة الواضحة الدالَّة على أنه هو، وأنَّه رسول الله حقًّا، {قالوا}: معاندين للحقِّ مكذِّبين له: {هذا سحرٌ مبينٌ}: وهذا من أعجب العجائب، الرسول الذي قد وضحت رسالتُه وصارتْ أبين من شمس النهار؛ يُجعل ساحراً بيِّناً سحره؛ فهل في الخذلان أعظم من هذا؟! وهل في الافتراء أبلغ من هذا الافتراء الذي نفى عنه ما كان معلوماً من رسالته وأثبتَ له ما كان أبعد الناس عنه ؟!
{6} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akieleza kuhusu ukaidi wa Wana wa Israili waliotangulia,
ambao Isa bin Maryamu aliwalingania na kuwaambia: “Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu.’” Yaani, Mwenyezi Mungu alinituma ili nikuiteni kwenye heri na kukukatazeni maovu, na akaniunga mkono kwa hoja zilizo wazi, na katika yale yanayoonyesha ukweli wangu ni kuwa
“ninayathibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati.” Yaani, Nimeleta yale aliyoyaleta Musa katika Taurati na sheria za mbinguni, kama mimi ningekuwa ninadai tu kwamba mimi ni Nabii, ilhali si Nabii, basi ningekuja na kisichokuwa kile walichokuja nacho Mitume waliotangulia, na
“ninayathibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati” pia ni kwamba kitabu hicho kilitoa habari na bishara njema ya kuja kwangu, nimi nimetumwa ili kusadikisha hilo,
“na kubashiria kuja Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad!” Naye ni Muhammad bin Abdullah bin Abdul Muttalib Nabii wa kabila la Hashim. Basi Isa, rehema na amani ziwe juu yake, ni kama manabii wengine wote. Anamsadiki nabii aliyetangulia, na anapeana bishara njema ya nabii atakayekuja baadaye. Tofauti na waongo; Kwani wao wanapingana na Manabii vikali zaidi, na wanahitalifiana nao kwa maelezo, maadili, maamrisho na makatazo.
“Lakini alipowajia;” yaani, Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ambaye Isa alipeana bishara njema ya kuja kwake
“na hoja zilizo wazi.” Yaani, ushahidi wa wazi wenye kuwaonyesha kwamba yeye ndiye, na kwamba hakika yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu,
“wakasema” wakiikaidi na kukadhibisha haki: “Huu ni uchawi ulio dhahiri!” Na hili ni katika maajabu makubwa zaidi. Mtume ambaye ujumbe wake umekwisha dhihirika zaidi kuliko jua la mchana, anafanywa kuwa mchawi ambaye uchawi wake uko wazi. Je, kuna kuachiliwa mbali kukubwa zaidi kuliko huku? Je, kuzulia uongo kukubwa zaidi kuliko kuzulia huku, ambako kunamkanushia yale yaliyokuwa yanajulikana kwake ya ujumbe wake na kumthibitishia yale ambayo yeye ndiye mtu wa mbali zaidi nayo kuliko watu wote?
#
{7} {ومن أظلمُ ممَّنِ افترى على الله الكذب}: بهذا أو غيره والحال أنه لا عذر له وقد انقطعت حجته لأنه {يدعى إلى الإسلام}: ويُبَيَّن له ببراهينه وبيناته، {واللهُ لا يهدي القوم الظالمينَ}: الذين لا يزالون على ظلمهم مستقيمين، لا تردُّهم عنه موعظةٌ ولا يزجُرُهُم بيانٌ ولا برهانٌ، خصوصاً هؤلاء الظَّلمة القائمين بمقابلة الحقِّ ليردُّوه، ولينصروا الباطل.
{7} “Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo” kama huu au mwingineo, ilhali hana udhuru wowote, na tayari hoja zake zilikwisha katika, kwa sababu
“anaitwa kwenye Uislamu” na anabainishiwa hoja zake na ushahidi wake ulio wazi.
“Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.” Wale wanaoendelea kung'ang'ania katika dhuluma yao, ambao hakuna mawaidha yanayoweza kuwarudisha wala hawakemewi na ubainisho wala hoja, hasa madhalimu hawa wanaosimama kidete kukabiliana na haki ili kuikataa na kuinusuru batili.
#
{8} ولهذا قال [اللَّه] عنهم: {يريدونَ لِيُطْفِئوا نورَ الله بأفواههم}؛ أي: بما يَصْدُرُ منهم من المقالات الفاسدة التي يردُّون بها الحقَّ، وهي لا حقيقة لها، بل تزيد البصير معرفةً بما هم عليه من الباطل، {والله متمُّ نورِهِ ولو كَرِهَ الكافرونَ}؛ أي: قد تكفَّل الله بنصر دينه وإتمام الحقِّ الذي أرسل به رسلَه وإظهار نورِهِ في سائر الأقطار، ولو كَرِهِ الكافرونَ، وبَذَلوا بسبب كراهته كلَّ ما قدروا عليه مما يتوصَّلون به إلى إطفاء نور الله؛ فإنَّهم مغلوبون، ومَثَلُهم كمثل مَن ينفخ عين الشمس بفيه ليطفِئَها؛ فلا على مرادهم حصلوا، ولا سلمتْ عقولهم من النقص والقدح فيها.
{8} Ndiyo maana
[Mwenyezi Mungu] akasema juu yao:
“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao” Yaani: kwa sababu ya kauli za upotovu wanazozitoa ambazo kwazo wanaikanusha haki, ilhali hazina uhakika wowote, bali zinamzidishia mwenye kuona elimu kuhusu uongo batili wanayoifanya.
“Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia.” Yaani, Mwenyezi Mungu ameshachukua dhamana kuinusuru dini yake, na kuitimiza haki aliyowatuma nayo Mitume wake, na kuifanya nuru yake ionekane katika nchi zote, hata kama makafiri watachukia, na kwa sababu ya kuichukia wakatoa kila wawezalo miongoni mwa yale wanayoyatumia kufikia kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana watashindwa, na mfano wao ni kama mtu anayepuliza jua kwa kinywa chake ili kulizima. Kwa hivyo, hawakufanikiwa kufikia kile walichotaka, wala akili zao hazikusalimika kutokana na upungufu na kashfa.
#
{9} ثم ذكر سبب الظُّهور والانتصار للدين الإسلاميِّ الحسِّي والمعنويِّ، فقال: {هو الذي أرسل رسولَه بالهُدى ودين الحقِّ}: أي: بالعلم النافع والعمل الصالح، بالعلم الذي يهدي إلى الله وإلى دار كرامته، ويهدي لأحسن الأعمال والأخلاق، ويهدي إلى مصالح الدُّنيا والآخرة، {ودين الحقِّ}؛ أي: الدين الذي يُدان به ويُتَعَبَّدُ لربِّ العالمين، الذي هو حقٌّ وصدقٌ لا نقص فيه ولا خلل يعتريه، بل أوامره غذاءُ القلوب والأرواح وراحةُ الأبدان، وترك نواهيه سلامةً من الشرِّ والفساد ، فما بُعِثَ به النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - من الهدي ودين الحقِّ أكبر دليل وبرهان على صدقِهِ، وهو برهانٌ باقٍ ما بقي الدهر، كلَّما ازداد به العاقل تفكُّراً؛ ازداد به فرحاً وتبصُّراً. {ليظهِرَه على الدِّين كلِّه}؛ أي: ليعليه على سائر الأديان بالحجَّة والبرهان، ويُظْهِرَ أهلَه القائمين به بالسيف والسّنان.
فأمَّا نفس الدين؛ فهذا الوصف ملازمٌ له في كلِّ وقت، فلا يمكن أن يُغَالِبَهُ مغالبٌ أو يخاصِمَهُ مخاصمٌ إلاَّ فَلَجَه وبلسه، وصار له الظهورُ والقهرُ، وأمَّا المنتسبون إليه؛ فإنَّهم إذا قاموا به واستناروا بنوره واهتدَوْا بهديه في مصالح دينهم ودُنياهم؛ فكذلك لا يقوم لهم أحدٌ، ولا بدَّ أن يظهروا على أهل الأديان، وإذا ضيَّعوا واكتفَوْا منه بمجرَّد الانتساب إليه؛ لم ينفعْهم ذلك، وصار إهمالهم له سببَ تسليطِ الأعداء عليهم، ويَعْرِفُ هذا من استقرأ الأحوال والنظر في أول المسلمين وآخرهم.
{9} Kisha akataja sababu ya kudhihiri na ushindi wa Dini ya Kiislamu, za kuonekana na zisizoonekana,
akasema: “Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya haki” yaani: kwa elimu yenye manufaa na matendo mema. Kwa elimu yenye kuongoa kwenda kwa Mwenyezi Mungu na kwenye maskani ya utukufu wake, yenye kuongoa kufikia matendo na maadili mema zaidi, na yenye kuongoa kufikia masilahi ya dunia na Akhera,
“na Dini ya haki” Yaani, Dini ambayo kwayo mtu humfuata na kumuabudu Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambayo ni ya haki na ya ukweli, isiyo na upungufu wowote wala dosari ndani yake. Bali amri zake ni lishe ya nyoyo na nafsi, na ni raha kwa miili. Na kuacha makatazo yake ni kusalimika kutoakana na maovu na uharibifu. Kwa hivyo yale aliyotumwa nayo Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ya uwongofu na dini ya haki ni ushahidi mkubwa zaidi juu ya ukweli wake. Nayo ni hoja yenye kusalia maadamu zama bado zimebakia. Kila mwenye akili anavyoitafakari, anazidi kwayo furaha na ufahamu wake,
“ili ipate kuzishinda dini zote” kwa hoja na ushahidi, na kuwapa ushindi watu wake wanaoisimamisha kwa upanga na mkuki. Ama dini yenyewe, haya ndiyo maelezo ambayo hayaachani nayo kila wakati, na haiwezekani kwa mshindi yeyote kuishinda au mpinzani yeyote kubishana nayo isipokuwa itampasua na kumkatisha tamaa kabisa, nayo anasalia iimedhihirika na kushinda. Na ama wanaohusiana nayo, wanapoitekeleza na wakaangaza kwa nuru yake na wakaongoka kwa uwongofu wake katika masilahi ya dini yao na maisha yao ya kidunia, hao pia hakuna atakayesimama dhidi yao, na lazima watapata ushindi dhidi ya watu wa dini zote. Lakini wakipoteza na wakaridhika na kujihusisha nayo tu, hilo haliwezi kuwanufaisha, na kuipuuza kwao huko kunakuwa sababu ya maadui kuwatawala, na hilo analijua vyema mwenye kuzichunguza hali na kuangalia katika Waislamu wa mwanzo na wa mwisho.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَى تِجَارَةٍ تُنْجِيكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ (10) تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (11) يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (12) وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ (13) يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنْصَارَ اللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنْصَارِي إِلَى اللَّهِ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنْصَارُ اللَّهِ فَآمَنَتْ طَائِفَةٌ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَتْ طَائِفَةٌ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَى عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ (14)}.
10. Enyi mlioamini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iliyo chungu? 11. Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua. 12. Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 13. Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini! 14. Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu,
kama alivyosema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: 'Ni nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu?' Wakasema wanafunzi: 'Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!' Basi kundi moja la Wana wa Israili liliamini, na kundi jingine lilikufuru. Basi tukawaunga mkono wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.
#
{10} هذه وصيةٌ ودلالةٌ وإرشادٌ من أرحم الراحمين لعباده المؤمنين لأعظم تجارةٍ وأجلِّ مطلوب وأعلى مرغوبٍ يحصل بها النجاة من العذاب الأليم والفوز بالنعيم المقيم، وأتى بأداة العرض الدالَّة على أنَّ هذا أمرٌ يرغب فيه كلُّ متصبِّر ويسمو إليه كل لبيبٍ.
{10} Huu ni wasia, kuelekeza na kuongoza kutoka kwa Mwenye kurehemu zaidi ya wote wenye kurehemu kwa waja wake waumini kwa ajili ya biashara kubwa zaidi na jambo kubwa zaidi litafutwalo, na jambo la juu zaidi litakwalo ambalo kwalo mtu anaepuka kutokana na adhabu chungu na kushinda neema ya kudumu. Na ilitumia neno la kuhimiza ili kuonyesha kwamba hili ni jambo ambalo analolitaka kila mwenye subira, na anapanda kuliendea kila wenye akili.
#
{11} فكأنَّه قيل: ما هذه التِّجارة التي هذا قدرها؟ فقال: {تؤمنون باللهِ ورسوله}: ومن المعلوم أنَّ الإيمان التامَّ هو التصديقُ الجازم بما أمر الله بالتصديق به، المستلزم لأعمال الجوارح، التي من أجَلِّها الجهاد في سبيله ؛ فلهذا قال: {وتجاهدون في سبيلِ اللهِ بأموالِكم وأنفسِكم}؛ بأن تبذلوا نفوسكم ومُهَجَكُم لمصادمة أعداء الإسلام، والقصدُ نصرُ دين الله وإعلاءُ كلمته، وتنفقون ما تيسَّر من أموالكم في ذلك المطلوب؛ فإنَّ ذلك وإنْ كان كريهاً للنفوس شاقًّا عليها؛ فإنَّه {خيرٌ لكم إن كنتُم تعلمون}: فإنَّ فيه الخير الدنيويَّ من النصر على الأعداء والعزَّ المنافي للذُّلِّ والرزق الواسع وسعة الصدر وانشراحه، والخير الأخروي بالفوز بثواب الله والنجاة من عقابه.
{11} Ni kana kwamba ilisemwa: ‘Ni biashara gani hii ambayo hiki ndicho kiwango chake?’ Akasema:
“Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Na inavyojulikana ni kwamba imani kamili ni kusadiki kikamilifu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliamuru kuyasadiki, na kushikamana na matendo ya viungo, ambayo kubwa yake zaidi ni kufanya Jihad katika njia yake.
Ndiyo maana akasema: “Na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu.” Kwa kutoa nafsi zenu na bidii zenu katika kupambana na maadui wa Uislamu, na kusudi la hayo liwe ni kuinusuru wa dini ya Mwenyezi Mungu na kuunga mkono neno lake, na mtoa kilicho rahisi katika mali zenu kwa ajili ya hicho kinachotafutwa. Kwani hayo, hata ikiwa yanachukiwa na nafsi na ni ngumu kwake,
“ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.” Kwani ndani yake kuna heri ya kidunia kama vile kuwashinda maadui na utukufu ambao ni kinyume na kudhalilika, na riziki pana, na kupanuka kifua na kukunjuka kwake, na pia lina heri ya kiakhera ya kupata malipo mazuri ya Mwenyezi Mungu na kuokoka mbali na adhabu yake.
#
{12} ولهذا ذَكَرَ الجزاء في الآخرة فقال: {يَغْفِرْ لكم ذُنوبَكم}: وهو شاملٌ للصغائر والكبائر؛ فإنَّ الإيمان بالله والجهاد في سبيله مكفِّرٌ للذُّنوب، ولو كانت كبائر، {ويدخِلْكم جناتٍ تجري من تحتها الأنهار}؛ أي: من تحت مساكنها وقصورها وغُرَفِها وأشجارها أنهارٌ من ماءٍ غير آسن وأنهارٌ من لبنٍ لم يتغيَّرْ طعمُه وأنهارٌ من خمر لذَّةٍ للشاربين وأنهارٌ من عسل مصفى ولهم فيها من كلِّ الثمرات، {ومساكنَ طيِّبةً في جناتِ عدنٍ}؛ أي: جمعت كلَّ طيبٍ من علوٍّ وارتفاع وحسن بناءٍ وزخرفةٍ، حتَّى إنَّ أهل الغرف من أهل علِّيين يتراءاهم أهلُ الجنَّة كما يُتراءى الكوكب الدُّرِّي في الأفق الشرقيِّ أو الغربيِّ، وحتَّى إنَّ بناء الجنَّة بعضُه من لَبِنِ ذهبٍ وبعضُه من لَبِنِ فضَّةٍ ، وخيامها من اللؤلؤ والمرجان، وبعض المنازل من الزُّمُرُّد والجواهر الملونة بأحسن الألوان، حتى إنَّها من صفائها يُرى ظاهرُها من باطنها وباطنُها من ظاهرها، وفيها من الطيبِ والحُسن ما لا يأتي عليه وصفُ الواصفين ولا خَطَرَ على قلب أحدٍ من العالمين، لا يمكن أن يدرِكوه حتى يَرَوْه ويتمتَّعوا بحسنه، وتقرَّ به أعينُهم.
ففي تلك الحالة لولا أنَّ الله خَلَقَ أهل الجنَّة وأنشأهم نشأةً كاملةً لا تقبلُ العدم؛ لأوشك أن يموتوا من الفرح؛ فسبحان من لا يحصي أحدٌ من خلقه ثناءً عليه، بل هو كما أثنى على نفسه، وفوق ما يُثْني عليه أحدٌ من خلقه، وتبارك الجليلُ الجميلُ، الذي أنشأ دار النعيم، وجعل فيها من الجلال والجمال ما يبهر عقولَ الخلق ويأخُذُ بأفئِدتهم، وتعالى من له الحكمةُ التامَّة، الذي من جملتها أنه لو أرى العباد الجنَّة ونظروا إلى ما فيها من النعيم؛ لما تخلَّف عنها أحدٌ، ولما هناهم العيش في هذه الدار المنغصة المَشوب نعيمها بألمها وفرحها بِتَرَحِها. وسُمِّيت [الجنة] جنَّة عدن؛ لأنَّ أهلها مقيمون فيها، لا يخرجون منها أبداً، ولا يبغون عنها حِوَلاً. ذلك الثواب الجزيل والأجر الجميل هو الفوزُ العظيم الذي لا فوزَ مثله؛ فهذا الثواب الأخرويُّ.
{12} Ndiyo sababu akataja malipo ya huko Akhera,
akasema: “Atakusameheni dhambi zenu.” Na hili linajumuisha madhambi madogo na makubwa. Kwa sababu kumuamini Mwenyezi Mungu na kufanya jihad katika njia yake ni mambo yanayofuta madhambi, hata kama ni makubwa,
“na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake” yaani, chini ya majengo yake, vyumba vyake, miti yake, mito yake ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda,
“na maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele.” Yaani, zilikusanya uzuri wote wa urefu, kuinuka juu, ujenzi mzuri na mapambo, kiasi kwamba wenye vyumba hivyo katika wale wa juu zaidi wataangaliwa na wakazi wa bustani za mbinguni na waonekane kama nyota inayomeremeta kwenye upeo wa macho wa mashariki au magharibi, na tena mijengo ya bustani za mbinguni baadhi ya matofali yake ni ya dhahabu na zingine ni za fedha, na mahema yake ni ya lulu na marijani, na nyumba zake ni za johari na vito vya thamani zenye rangi nzuri zaidi, kiasi kwamba kutokana na usafi wake inaonekana nje yake kutokea ndani yake, na ndani yake kutokea nje yake, na ndani yake kuna manukato na uzuri usioweza kusifiwa na wenye kusifu, wala hata haukuwahi kupita katika moyo yeyote miongoni mwa walimwengu, haiwezi kuufikia hadi wauone na kufurahia kwa uzuri wake, na macho yao yatue kwa ajili yake. Kwa hivyo katika wa hali hiyo, lau kuwa Mwenyezi Mungu hakuwaumba wakazi wa bustani za mbinguni na akawafanya kuwa katika umbo kamilifu lisilokubali kuisha, basi wangekaribia kufa kutokana na furaha basi ametakasika Yule ambaye hakuna anayeweza kudhibiti sifa zake miongoni mwa viumbe vyake, bali Yeye ni kama alivyojisifu mwenyewe, na yuko juu zaidi ya namna anavyomsifu yeyote katika viumbe vyake, na ni Mwenye baraka nyinyi, Mzuri. Ambaye aliumba nyumba ya neema, na akaweka humo utukufu na uzuri kiasi cha kushangaza akili za viumbe na kuzishika nyoyo zao. Na ametukuka Yule ambaye ana hekima kamilifu, ambayo ni kwamba kama angewaonyesha waja bustani ya mbinguni na wakayaona yaliyo ndani yake ya neema, basi hangebakia nyuma akashindwa kuingia humo yeyote, wala hawangepata raha yoyote ya kuishi katika nyumba hii yenye dhiki, ambayo neema yake imechanganyika na machungu, na furaha zake na taabu zake. Bustani hii iliitwa Edeni; kwa sababu wakazi wake watakaa humo milele na kamwe hawatatoka humo, na wala hawatatafuta pengine pasipo hapo pa kwenda. Malipo hayo makubwa na mazuri ndiyo ushindi mkubwa ambao hakuna ushindi mwingine mfano wake. Haya ndiyo malipo ya kiakhera.
#
{13} وأما الثواب الدنيويُّ لهذه التجارة؛ فذكره بقوله: {وأخرى تحبُّونها}؛ أي: ويحصُلُ لكم خَصْلَةٌ أخرى تحبُّونها، وهي: {نصرٌ من الله}: لكم على الأعداء، يحصُلُ به العزُّ والفرح، {وفتحٌ قريبٌ}: تتَّسع به دائرة الإسلام، ويحصُلُ به الرزق الواسع؛ فهذا جزاء المؤمنين المجاهدين، وأما المؤمنون من غير أهل الجهاد إذا قام غيرهم بالجهادِ؛ فلم يؤيِّسْهُمُ الله تعالى من فضله وإحسانه، بل قال: {وبشِّرِ المؤمنينَ}؛ أي: بالثواب العاجل والآجل؛ كلٌّ على حسب إيمانه، وإن كانوا لا يبلغون مبلغ المجاهدين في سبيل الله؛ كما قال النبيُّ - صلى الله عليه وسلم -: «مَنْ رَضِي بالله ربًّا، وبالإسلام ديناً، وبمحمدٍ رسولاً؛ وجبتْ له الجنةُ». فعجب لها أبو سعيد الخدريُّ راوي الحديث، فقال: أعدها عليَّ يا رسول الله! فأعادها عليه، ثم قال: «وأخرى يُرْفَعُ بها العبدُ مائة درجةٍ في الجنة، ما بين كلِّ درجتين كما بين السماء والأرض». فقال: وما هي يا رسولَ الله؟ قال: «الجهادُ في سبيل الله، الجهاد في سبيل الله». رواه مسلم.
{13} Ama malipo ya kidunia kwa biashara hii,
basi aliyataja katika kauli yake: “Na kinginecho mkipendacho” Yaani, na mtapata kitu kingine mnachokipenda,
nacho ni: “nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu” dhidi ya maadui zenu, ambayo kwayo mtapata utukufu na furaha,
“na ushindi ulio karibu” ambao kwao duara la Uislamu litapanuka, na ambao kwao mtapata riziki ya kunjufu. Haya ndiyo malipo ya waumini wanaopambana katika jihadi. Na ama waumini wasio watu wa kufanya jihadi, wenzao wanapofanya jihadi, Mwenyezi Mungu hakuwakunjulia katika fadhila zake na wema wake.
Bali alisema: “Na wabashirieni Waumini” kwa malipo ya haraka na ya baada ya muda mrefu. Kila mmoja kulingana na imani yake, hata wasipofikia daraja ya wale wanaopambana katika jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kama alivyosema Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: “Mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola Mlezi, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammad kuwa ndiye Mtume, atakuwa amestahiki kuingia katika bustani za mbinguni.” Abu Said Al-Khudri, msimuliaji wa Hadithi hii,
alistaajabishwa na hilo na akasema: ‘Irudie niisikie tena ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!’ Kwa hivyo akamrudilia tena,
kisha akasema: “Na nyingine ambayo kwayo mja atanyanyuliwa ngazi mia moja katika bustani za mbinguni, na umbali uliopo baina ya kila ngazi mbili ni kama umbali uliopo baina ya mbingu na ardhi.
’ Akasema: ‘Ni nini hilo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Akasema: Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu. Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.’ Imepokelewa na Muslim.
#
{14} ثم قال تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا كونوا أنصارَ اللهِ}؛ أي: بالأقوال والأفعال، وذلك بالقيام بدين الله، والحرص على تنفيذه على الغير وجهادِ مَنْ عانده ونابذه بالأبدان والأموال، ومَنْ نَصَرَ الباطلَ بما يزعمُه من العلم، وَرَدَّ الحقَّ بدحض حجَّته وإقامة الحجَّة عليه والتحذير منه، ومن نصرِ دين الله تعلُّم كتاب الله وسنَّة رسوله [وتعليمه] والحثُّ على ذلك والأمر بالمعروف والنهيُ عن المنكر.
ثم هيَّج الله المؤمنين بالاقتداء بمَنْ قبلَهم من الصالحين بقوله: {كما قال عيسى ابنُ مريم للحواريِّينَ مَنْ أنصاري إلى الله}؛ أي: قال لهم منبهاً: من يعاونني ويقوم معي في نصر دين الله ويَدْخُلُ مدخلي ويَخْرُجُ مخرجي؟ فابتدرَ الحواريُّون فقالوا: {نحنُ أنصارُ اللهِ}: فمضى [عيسى] عليه السلام على [أمر اللَّه و] نصرِ دين الله هو ومن معه من الحواريِّين، {فآمنتْ طائفةٌ من بني إسرائيلَ}: بسبب دعوة عيسى والحواريِّين، {وكفرت طائفةٌ}: منهم، فلم ينقادوا لدعوتهم، فجاهد المؤمنونَ الكافرين، {فأيَّدْنا الذين آمنوا على عَدُوِّهِم}؛ أي: قوَّيْناهم ونصرناهم عليهم، {فأصبحوا ظاهرينَ}: عليهم، قاهرين لهم. فأنتم يا أمَّة محمدٍ! كونوا أنصارَ الله ودعاةَ دينه؛ يَنْصُرْكُم الله كما نَصَرَ مَنْ قبلكم، ويُظْهِرْكم على عدوِّكم.
{14} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Enyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu." Yaani, kwa kauli na vitendo, kwa kushikamana na dini ya Mwenyezi Mungu, na kufanya bidii ya kuitekeleza kwa wengine, na kufanya jihadi kwa miili na mali dhidi ya mwenye kuikaidi na kuikataa. Na mwenye kuunga mkono batili kwa elimu anayodai kwamba anayo, na anaikanusha haki kwa kuiangusha hoja yake, na kusimamisha ushahidi dhidi yake, na kuonya dhidi yake, na mwenye kuunga mkono Dini ya Mwenyezi Mungu kwa kujifunza Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake na kuyahimiza hayo na kuamrisha mema na kukataza maovu.
Kisha Mwenyezi Mungu akawachochea Waumini wawaige watu wema waliokuwa kabla yao kwa kusema: "Kama alivyosema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: 'Ni nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu?'" Yaani,
aliwaambia kwa njia ya kuwatanabahisha: Ni nani atakayenisaidia na kusimama pamoja nami katika kuiunga mkono dini ya Mwenyezi Mungu na aingie kwenye maingilio yangu na kutoka kupitia pale ninapotokea? Kisha wanafunzi wake wakaharakisha kusema: "Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!" Basi
[Isa], amani iwe juu yake, akaendelea na
[maamrisho ya Mwenyezi Mungu na] kuunga mkono dini ya Mwenyezi Mungu, yeye na wale wanafunzi waliokuwa pamoja naye. "Basi kundi moja la Wana wa Israili liliamini" kwa sababu ya mwito wa Isa na wanafunzi wake, "na kundi jingine lilikufuru." Hawakukubali wito wao. Kwa hivyo, Waumini wakapigana dhidi ya makafiri. "Basi tukawaunga mkono wale walioamini dhidi ya maadui zao" kwa kuwatia nguvu na tukawanusuru dhidi yao, "wakawa wenye kushinda" dhidi yao. Basi enyi umma wa Muhammad! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu na watetezi wa dini yake. Mwenyezi Mungu atakusaidieni kama alivyowasaidia wale waliokuwa kabla yenu, na atakupeni ushindi juu ya adui yenu.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *