Tafsiri ya surat Al-Mumtahana
Tafsiri ya surat Al-Mumtahana
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُمْ مِنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ أَنْ تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ رَبِّكُمْ إِنْ كُنْتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي تُسِرُّونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنْتُمْ وَمَنْ يَفْعَلْهُ مِنْكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ (1) إِنْ يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُمْ بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ (2) لَنْ تَنْفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ (3) قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنْكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّى تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ شَيْءٍ رَبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ (4) رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا إِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (5) لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِمَنْ كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَمَنْ يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ (6) عَسَى اللَّهُ أَنْ يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ الَّذِينَ عَادَيْتُمْ مِنْهُمْ مَوَدَّةً وَاللَّهُ قَدِيرٌ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَحِيمٌ (7) لَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ أَنْ تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ (8) إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ (9)}.
1. Enyi mlioamini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyokujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu, basi ameipotea njia ya sawa. 2. Wakikuwezeni, wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri. 3. Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mno mnayoyatenda. 4. Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye,
walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomuamini Mwenyezi Mungu peke yake.
Isipokuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndiyo marejeo. 5. Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 6. Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao, kwa anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka, basi hakika Mwnyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa mno. 7. Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Mweza, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe zaidi, Mwenye kurehemu mno. 8. Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. 9. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki wa kusaidiana nao, na wale waliokupigeni vita kwa sababu ya dini, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki, basi hao ndio madhalimu.
Wafasiri wengi, Mwenyezi Mungu awarehemu, walitaja kuwa sababu ya kuteremshwa aya hizi tukufu ni kuhusiana na kisa cha Hatib bin Abi Balta’a, wakati Nabii – rehema na amani zimshukie – alipotaka kwenda vita vya utekaji Makka, Hatib aliwaandikia washirikina wa kutoka kwa watu wa Makka akiwajulisha kuhusu kundoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akiwajia; ili apate wa kumsaidia kwa hilo miongoni mwao, siyo kwa sababu ya kuwa na shaka wala unafiki. Aliituma pamoja na mwanamke fulani, lakini Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akajulishwa juu yake, kwa hivyo akatuma atafutwe mwanamke huyo kabla hajafika huko. Basi wakaichukua barua hiyo kutoka kwake, na akamlaumu Hatib, naye akaomba radhi kwa udhuru ambao Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – aliukubali. Aya hizi zina makatazo makali ya kuwaunga mkono makafiri, wawe ni washirikina au wengineo, na kuwapa mapenzi, na kwamba jambo hilo ni kinyume na imani na ni kinyume na dini ya Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na ni kinyume na akili, ambayo inahitaji kuchukua tahadhari kamili dhidi ya adui ambaye haachi chochote katika juhudi zake za kufanya uadui na kuchukua fursa ya kufikisha madhara kwa adui yake.
#
{1} فقال تعالى: {يا أيُّها الذين آمنوا}؛ أي: اعملوا بمقتضى إيمانكم من ولايةِ مَنْ قام بالإيمان ومعاداة من عاداه؛ فإنَّه عدوٌّ لله وعدوٌّ للمؤمنين، فـ {لا تتَّخذوا عدوِّي وعدوَّكم أولياءَ تُلْقون إليهم بالمودَّة}؛ أي: تسارعون في مودَّتهم والسعي في أسبابها؛ فإنَّ المودَّة إذا حصلت؛ تبعتْها النصرةُ والموالاةُ، فخرج العبد من الإيمان، وصار من جملة أهل الكفران [وانفصل عن أهل الإيمان]. وهذا المتَّخذُ للكافر وليًّا عادمُ المروءة أيضاً؛ فإنَّه كيف يوالي أعدى أعدائه، الذي لا يريد له إلاَّ الشرَّ، ويخالف ربَّه ووليَّه الذي يريد به الخير، ويأمره به ويحثُّه عليه. ومما يدعو المؤمن أيضاً إلى معاداة الكفار أنَّهم قد كفروا بما جاء المؤمنين من الحقِّ، ولا أعظم من هذه المخالفة والمشاقَّة؛ فإنَّهم قد كفروا بأصل دينكم، وزعموا أنَّكم ضلاَّلٌ على غير هدىً، والحالُ أنَّهم كفروا بالحقِّ الذي لا شكَّ فيه ولا مريةَ، ومن ردَّ الحقَّ؛ فمحالٌ أن يوجد له دليلٌ أو حجَّةٌ تدلُّ على صحة قوله. بل مجرَّد العلم بالحقِّ يدلُّ على بطلان قول من ردَّه وفساده.
ومن عداوتهم البليغة أنَّهم {يُخْرِجون الرسولَ وإيَّاكم}: أيُّها المؤمنون من دياركم ويشرِّدونكم من أوطانكم ولا ذنبَ لكم في ذلك عندهم إلاَّ أنكم تؤمنون {بالله ربِّكم}: الذي يتعيَّن على الخلق كلِّهم القيام بعبوديَّته؛ لأنَّه ربَّاهم، وأنعم عليهم بالنِّعم الظاهرة والباطنة [وهو اللَّه تعالى]، فلمَّا أعرضوا عن هذا الأمر الذي هو أوجبُ الواجبات وقمتُم به؛ عادَوْكم وأخرجوكم من أجله من دياركم، فأيُّ دين وأيُّ مروءة وعقل يبقى مع العبد إذا والى الكفار الذين هذا وصفُهم في كلِّ زمانٍ أو مكان، ولا يمنعهم منه إلاَّ خوفٌ أو مانعٌ قويٌّ. {إن كنتُم خرجتُم جهاداً في سبيلي وابتغاء مرضاتي}؛ أي: إن كان خروجُكم مقصودُكم به الجهادُ في سبيل الله لإعلاء كلمة الله وابتغاء رضاه؛ فاعملوا بمقتضى هذا من موالاة أولياء الله ومعاداة أعدائهِ؛ فإنَّ هذا من أعظم الجهاد في سبيله، ومن أعظم ما يتقرَّب به المتقرِّبون إلى الله ويبتغون به رضاه.
{تُسِرُّون إليهم بالمودَّةِ وأنا أعلمُ بما أخفيتُم وما أعلنتُم}؛ أي: كيف تسرُّون المودَّة للكافرين وتخفونها مع علمكم أنَّ الله عالمٌ بما تخفون وما تعلنون؛ فهو وإن خفي على المؤمنين؛ فلا يخفى على الله تعالى، وسيجازي العباد بما يعلمه منهم من الخير والشرِّ. {ومن يَفْعَلْه منكم}؛ أي: موالاة الكافرين بعدما حذَّركم الله منها، {فقد ضلَّ سواءَ السبيل}: لأنَّه سلك مسلكاً مخالفاً للشرع وللعقل والمروءة الإنسانيَّة.
{1} Akasema Mwenyezi Mungu:
“Enyi mlioamini;” yaani, tenda kwa mujibu wa imani yenu, ya kuwafanya vipenzi wale walioamini, na kuwafanyia uadui wale wanaoifanyia uadui. Kwani yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu na ni adui wa Waumini. Basi
“Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi.” Yaani, msikimbilie kuwapenda na kujitahidi kufanya visababu vyake. Kwani ikiwa mapenzi kama hayo yakitokea, basi yatafuatwa na usaidizi na kushirikiana mno, basi mja akawa ametoka katika Imani na akawa miongoni mwa watu makafiri
[na kujitenga na watu wa imani]. Mtu huyu anayemchukulia kafiri kuwa rafiki mlinzi msaidizi pia hana uungwana. Vipi anamfanya rafiki mlinzi msaidizi yule ambaye ndiye adui yake kuliko maadui wote, ambaye hamtakii isipokuwa uovu, na anakwenda kinyume na Mola wake Mlezi na rafiki mlinzi msaidizi wake huyu ambaye anamtakia heri, na anamwamrisha na kumhimiza juu yake? Na pia katika yale yanayomwita Muumini kuwafanyia uadui makafiri ni kwamba wamekufuru haki iliyowajia Waumini, na hakuna kubwa zaidi ya kuhalifu huku na upinzani huu. Kwani walikufuru msingi wa dini yenu, na wakadai kwamba nyinyi mmepotea na hamko kwenye uwongofu. Lakini hali halisi ni kwamba wao waliikufuru haki isiyo na shaka yoyote wala kusitasita. Na mwenye kuikataa haki, basi haiwezekani awe na ushahidi au hoja inayoonyesha usahihi wa kauli yake. Bali kujua tu haki, kunaonyesha ubatili na uharibifu wa kauli ya aliyeikataa. Miongoni mwa uadui wao mkubwa zaidi ni kwamba
“walimfukuza Mtume na nyinyi” enyi Waumini, na kukutoeni katika nyumba zenu, na kukufukuzeni kutoka katika nchi yenu hali ya kuwa hamkuwakosea lolote ndo wafanye hivyo, isipokuwa dhambi mnamwamini Mola wenu Mlezi,
“Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi.” Ambye ni lazima kwa viumbe vyote kumuabudu, Kwa sababu Yeye ndiye aliyewalea, na akawapa neema za dhahiri na zilizofichika
[naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu]. basi walipolipa mgongo jambo hili ambalo ndilo faradhi kubwa zaidi, nany mkalitekeleza, wakufanyieni uadui na kukutoeni majumbani mwenu. Basi ni dini gani, uungwana gani, na akili gani inabakiapamoja na mja ikiwa atawafanya makafiri kuwa vipenzi wasaidizi, wale ambao haya ndiyo maelezo yao katika kila wakati au mahali, na wala hakuna kinachowazuilia kufanya hivyo isipokuwa hofu tu au kizuizi chenye nguvu.
“Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu.“ Yaani: Ikiwa nia yenu ilikuwa kwenda kufanya hijadi katika njia ye Mwenyezi Mungu, ili kuinua juu neno la Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, basi tendeni kulingana na hili, kwa kufanya urafiki wendani na vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwa na kuwafanyia uadui adui zake. Hii hakika ni miongoni mwa jihadi kubwa zaidi katika njia yake, na ni katika mambo mkubwa zaidi ambayo kwayo wale wanaojiweka karibu wanajiweka karibu na Mwenyezi Mungu na kutafuta kwayo radhi zake. “Mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha.” Yaani, vipi mnafanya urafiki kwa siri ya makafiri na hali mnajua kwamba Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha? Hata ikiwa hilo likafichika kwa Waumini, halifichiki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atawalipa waja wake kwa yale anayoyajua kwao; mema na mabaya.
“Na mwenye kufanya hayo kati yenu.” Yaani, kufanya urafiki wandani na kuwaunga mkono makafiri baada ya Mwenyezi Mungu kuwahadharisha nalo
“basi ameipotea njia ya sawa;” kwa sababu yeye alishika njia iliyo kinyume na sheria, akili na uungwana.
#
{2} ثم بيَّن تعالى شدَّة عداوتهم تهييجاً للمؤمنين على عداوتهم: {إن يَثْقَفوكم}؛ أي: يجدوكم وتسنح لهم الفرصة في أذاكم، {يكونوا لكم أعداءً}: ظاهرين، {ويَبْسُطوا إليكم أيدِيَهم}: بالقتل والضَّرب ونحو ذلك، {وألسنَتَهم بالسوءِ}؛ أي: بالقول الذي يسوء من شَتْمٍ وغيره، {وودُّوا لو تكفُرون}: فإنَّ هذا غاية ما يريدون منكم.
{2} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akabainisha ukubwa wa uadui wao ili hilo liwachochee Waumini nao pia wawafanyie uadui:
“Wakikuwezeni” wanapopata fursa ya kuwadhuru
“wanakuwa maadui zenu” wa dhahiri,
“na wanakukunjulieni mikono yao” kwa kuwaua, kumpiga na mfano wa hayo,
“na ndimi zao kwa uovu” wenye kuwafanya msikie vibaya kama vile matusi na mambo mengine,
“na wanapenda muwe makafiri” kwani hili ndilo lengo lao la mwisho wanalolitaka kwenu.
#
{3} فإن احتجَجْتُم وقلتُم: نوالي الكفار لأجل القرابة والأموال؛ فلن تغنيَ عنكم أَموالُكم ولا أولادُكم من الله شيئاً {والله بما تعملون بصيرٌ} فلذلك حذَّركم من موالاة الكافرين الذين تضرُّكم موالاتهم.
{3} Mkibishana na mkasema: ‘Tunakuwa marafiki na kusaidiana na makafiri kwa ajili ya ujamaa uliopo kati yetu na mali.’ Lakini mali zenu wala watoto wenu havitakunufaisheni chochote mbele ya Mwenyezi Mungu,
“Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mno mnayoyatenda.” Ndiyo maana akakuonyeni kuwafanya makafiri kuwa warafiki wa kusaidiana nao, ambao urafiki wenu huo wa kusaidiana unakudhuruni.
#
{4} {قد} كان {لكم}: يا معشر المؤمنينَ، {أسوةٌ حسنةٌ}؛ أي: قدوةٌ صالحةٌ وائتمامٌ ينفعكم {في إبراهيم والذين معه}: من المؤمنين؛ لأنَّكم قد أمرتم أن تتَّبعوا ملَّة إبراهيم حنيفاً، {إذْ قالوا لقومهم إنا بُرءَاءُ منكم وممَّا تعبُدون من دونِ اللهِ}؛ أي: إذ تبرأ إبراهيم عليه السلام ومَنْ معه من المؤمنين من قومهم المشركين وممَّا يعبُدون من دون الله، ثم صرَّحوا بعداوتهم غاية التصريح، فقالوا: {كَفَرْنا بكم وبدا}؛ أي: ظهر وبان {بينَنا وبينَكم العداوةُ والبغضاءُ}؛ أي: البغض بالقلوب وزوال مودَّتها والعداوة بالأبدان. وليس لتلك العداوة والبغضاء وقتٌ ولا حدٌّ، بل ذلك {أبداً} ما دمتم مستمرِّين على كفركم، {حتى تؤمِنوا بالله وحدَه}؛ أي: فإذا آمنتم بالله وحده؛ زالت العداوةُ والبغضاءُ وانقلبتْ مودَّةً وولايةً؛ فلكم أيُّها المؤمنون أسوةٌ حسنةٌ في إبراهيم ومن معه في القيام بالإيمان والتوحيد ولوازم ذلك ومقتضياته وفي كلِّ شيءٍ تَعَبَّدُوا به لله وحده، {إلاَّ}: في خصلةٍ واحدةٍ، وهي: {قولَ إبراهيمَ لأبيه}: آزر المشرك الكافر المعاند حين دعاه إلى الإيمان والتوحيدِ، فامتنع، فقال إبراهيمُ له: {لأستغفرنَّ لك و}: الحال أني لا {أملِكُ لك من اللهِ من شيءٍ}: ولكنِّي أدعو ربِّي عسى أن لا أكونَ بدعاءِ ربِّي شقيًّا، فليس لكم أن تقتدوا بإبراهيم في هذه الحالة التي دعا بها للمشرك، فليس لكم أن تدعوا للمشركين وتقولوا: إنَّا في ذلك متَّبِعون لملَّة إبراهيم؛ فإنَّ الله ذَكَرَ عذرَ إبراهيم في ذلك بقوله: {وما كان استغفارُ إبراهيمَ لأبيهِ إلاَّ عن مَوْعِدَةٍ وَعَدَها إيَّاه فلمَّا تَبَيَّنَ له أنَّه عدوٌّ لله تبرَّأ منه ... } الآية، ولكم أسوةٌ حسنةٌ في إبراهيم ومن معه حين دَعَوُا الله وتوكَّلوا عليه وأنابوا إليه واعترفوا بالعجز والتقصير، فقالوا: {ربَّنا عليك توكَّلْنا}؛ أي: اعتمدنا عليك في جلب ما ينفعنا ودفع ما يضرُّنا ووثقنا بك يا ربَّنا في ذلك، {وإليك أنَبْنا}؛ أي: رجعنا إلى طاعتك ومرضاتك وجميع ما يقرِّبُ إليك؛ فنحن في ذلك ساعون، وبفعل الخيرات مجتهدون، ونعلم أنَّا إليك نصيرُ، فسنستعدُّ للقدوم عليك، ونعمل ما يزلفنا إليك.
{4} “Hakika” enyi kundi la waumini, “mna mfano mzuri“ na kigezo chema na kufuata kutakaokufaeni “katika Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye” miongoni mwa Waumini; kwa sababu mliamrishwa kufuata mila ya Ibrahim mwongofu,
“walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu.” Yaani, Ibrahim amani iwe juu yake na Waumini waliokuwa pamoja naye walipojitenga mbali watu wao washirikina na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi wakauweka wazi uadui wao,
na wakasema: “umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi” na Hakuna wakati maalumu wala kikomo kwa uadui huo na chuki hii, lakini hilo ni
“abadani” maadamu mnaendelea na ukafiri wenu, “mpaka mtakapomuamini Mwenyezi Mungu peke yake” Yaani: mkimwamini Mwenyezi Mungu peke yake, uadui na chuki vitatoweka na vitageuka kuwa mapenzi na kusaidiana. Basi nyinyi enyi Waumini mnao mfano mzuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye katika kusimamisha Imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu na mambo yanayofungamana na hayo, na matakwa yake, na katika kila jambo walilomuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwalo,
“isipokuwa” jambo moja, nalo ni: “kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake” Azar, mshirikina, kafiri, mkaidi alipomwita kwenye imani na kumpwekesha Mwenyezi Mungu lakini akakataa.
Ibrahim akamwambia: “Hakika nitakuombea msamaha” lakini mimi
“similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu” lakini mimi namuomba Mola wangu Mlezi, labda nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi. Kwa hivyo, nyinyi msimfuate Ibrahim katika hali hii aliyomlingania mshirikina,
kwani hamfai kuwaombea washirikina mkisema kwamba: ‘Hakika sisi ni wafuasi wa mila ya Ibrahim katika hilo.’ Kwa maana,
Mwenyezi Mungu alitaja udhuru wa Ibrahim katika hilo katika kauli yake: “Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu wa ahadi aliyofanya naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye...” hadi mwisho wa Aya hii. Basi nyinyi mnao mfano mzuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye walipomuomba Mwenyezi Mungu na wakamtegemea na wakarejea kwake na wakakiri kutoweza kwao na kutofanya kwao ibada zingine vyema,
waliposema: “Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea” katika kutuletea yale yenye manufaa kwetu na kutuepushe kutokana na yale yanayotudhuru, na tuna imani nawe katika hilo, ewe Mola wetu Mlezi,
“na kwako tumeelekea” kwa kutubu, na kurudi katika utii na yote yenye kukuridhisha na yote yenye kutuweka karibu nawe. Sisi utafanya bidii katika hayo, na pia tunajitahidi kufanya mema, na tunajua kwamba tutarudi kwako, kwa hivyo tunajitayarisha kuja kwako, na kufanya yenye kutuweka karibu mno nawe.
#
{5} {ربَّنا لا تجعَلْنا فتنةً للذين كفروا}؛ أي: لا تسلِّطْهم علينا بذنوبنا، فيفتنونا، ويمنعونا مما يقدرون عليه من أمور الإيمان، ويفتتنون أيضاً بأنفسهم؛ فإنَّهم إذا رأوا لهم الغلبة؛ ظنُّوا أنَّهم على الحقِّ وأنَّا على الباطل، فازدادوا كفراً وطغياناً، {واغفِرْ لنا}: ما اقترفنا من الذُّنوب والسيئات وما قصَّرْنا به من المأمورات. {ربَّنا إنَّك أنت العزيز}: القاهر لكلِّ شيءٍ. {الحكيمُ}: الذي يضع الأشياء مواضعها؛ فبعزَّتك وحكمتك انصُرْنا على أعدائنا، واغفر لنا ذنوبنا، وأصلِحْ عيوبنا.
{5} “Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru.” Yaani, usiwape mamlaka juu yetu kwa sababu ya madhambi yetu, wakatutia majaribuni na wakatuzuia kufanya yale wanayoweza kutuzuia miongoni mwa mambo ya imani, na wao pia wakajiingiza majaribuni. Kwa maana ikiwa wataona kwamba wana mkono wa juu, watadhani kwamba wako kwenye haki, nasi tuko katika batili, basi wakazidisha ukafiri na kuvuka mipaka.
“Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu,” Mshindi wa kila kitu.
“Mwenye hekima” anayeweka vitu mahali pake. Kwa nguvu zako na hekima yako, tupe ushindi dhidi ya maadui zetu, utusamehe madhambi yetu, na urekebishe kosoro zetu.
#
{6} ثم كرَّر الحثَّ لهم على الاقتداء بهم وقال: {لقد كان لكم فيهم أسوةٌ حسنةٌ}: وليس كلُّ أحدٍ تسهُلُ عليه هذه الأسوة، وإنما تسهل على من {كان يرجو اللهَ واليومَ الآخرَ}: فإنَّ الإيمان واحتساب الأجر والثواب يسهِّل على العبد كلَّ عسير، ويقلِّل لديه كلَّ كثير، ويوجِبُ له [الإكثار مِن] الاقتداء بعباد الله الصالحين والأنبياء والمرسلين؛ فإنَّه يرى نفسه مفتقراً [و] مضطرًّا إلى ذلك غاية الاضطرار، {ومن يتولَّ}: عن طاعة الله والتأسِّي برسل الله؛ فلن يضرَّ إلاَّ نفسه، ولا يضرُّ الله شيئاً، {فإنَّ الله هو الغنيُّ}: الذي له الغنى التامُّ المطلقُ من جميع الوجوه؛ فلا يحتاج إلى أحدٍ من خلقه بوجه. {الحميدُ}: في ذاته [وأسمائه] وصفاته وأفعاله؛ فإنَّه محمود على ذلك كله.
{6} Kisha akarudia kuwahimiza kuwaiga na akasema:
“Kwa yakini umekuwa mfano mzuri kwenu katika mwendo wao.” Lakini mfano huu si rahisi kwa kila mtu, bali ni rahisi kwa wale
“anayemtarajia Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho” kwani imani na kutaraji malipo mazuri humrahisishia mja kila lililo gumu, na linampunguzia kila kilicho kingi, na linamsababishia kuzidisha kuwaiga waja wema wa Mwenyezi Mungu, Manabii na Mitume. Kwani anajiona kuwa anahitaji na kulazimika sana kufanya hivyo,
“Na mwenye kugeuka” akaacha kumtii Mwenyezi Mungu na kuwafuata Mitume wa Mwenyezi Mungu, basi hatamdhuru yeyote ila nafsi yake mwenyewe, na wala hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu,
“Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha” mwenye kujitosheleza kikamilifu katika kila jambo, na wala hahitaji kiumbe chake chochote.
“Msifiwa mno” katika dhati yake,
[majina yake], sifa zake, na vitendo vyake. Yeye anasifiwa kwa yote hayo.
#
{7} ثم أخبر تعالى أنَّ هذه العداوة التي أمَرَ [اللَّهُ] بها المؤمنين للمشركين ووصفهم بالقيام بها؛ أنَّهم ما داموا على شركهم وكفرهم، وأنَّهم إن انتقلوا إلى الإيمان؛ فإنَّ الحكم يدور مع علته، والمودَّة الإيمانيَّة ترجع؛ فلا تيأسوا أيُّها المؤمنون من رجوعهم إلى الإيمان؛ {عسى اللهُ أن يجعلَ بينكم وبين الذين عادَيْتُم منهم مودةً}: سببها رجوعهم إلى الإيمان. {والله قديرٌ}: على كلِّ شيءٍ، ومن ذلك هداية القلوب وتقليبها من حال إلى حال. {والله غفورٌ رحيمٌ}: لا يتعاظمُهُ ذنبٌ أن يغفِرَه ولا [يكبر عليه] عيبٌ أن يستُرَه، {قلْ يا عبادي الذين أسْرَفوا على أنفسِهِم لا تَقْنَطوا من رحمةِ الله إنَّ اللهَ يغفرُ الذُّنوب جميعاً إنَّه هو الغفورُ الرحيمُ}. وفي هذه الآية إشارةٌ وبشارةٌ بإسلام بعض المشركين، الذين كانوا إذ ذاك أعداء للمؤمنين، وقد وقع ذلك، ولله الحمد والمنة.
{7} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba uadui huu ambao
[Mwenyezi Mungu] aliwaamrisha Waumini kwa washirikina na akawaelezea kuyafanya hivyo, kwamba hilo ni maadamu wanaendelea na ushirikina na ukafiri wao, na kwamba wakihamia imani, basi hakika hukumu inazunguka pamoja na sababu zake, na mapenzi ya kiimani yatarudi. Basi msikate tamaa, enyi waumini, ya kurudi kwao kwenye imani.
“Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu” kwa kurejea kwao katika Imani.
“na Mwenyezi Mungu ni Mweza” juu ya kila kitu. Na katika hilo ni kuziongoa nyoyo na kuzigeuza kutoka katika hali moja kwenda nyengine.
“na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe zaidi, Mwenye kurehemu mno.” Hakuna dhambi isiyoweza kusamehewa naye, na wala hakuna aibu asiyoweza kuisitiri.
“Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemuzaidi.” Katika Aya hii kuna ishara na habari njema ya kusilimu kwa baadhi ya washirikina, waliokuwa maadui wa waumini wakati huo. Na hayo yalikwisha tokea, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.
#
{8} ولمَّا نزلت هذه الآيات الكريمات المهيِّجةُ على عداوة الكافرين؛ وقعتْ من المؤمنين كلَّ موقع، وقاموا بها أتمَّ القيام، وتَأثَّموا من صِلَةِ بعض أقاربهم المشركين، وظنُّوا أنَّ ذلك داخل فيما نهى الله عنه، فأخبرهم الله أن ذلك لا يدخُلُ في المحرم، فقال: {لا ينهاكُمُ الله عن الذين لم يقاتِلوكم في الدِّينِ ولم يُخْرِجُوكم من دياركُم أن تَبَرُّوهم وتُقْسِطوا إليهم إنَّ الله يحبُّ المقسِطينَ}؛ أي: لا ينهاكم الله عن البرِّ والصِّلة والمكافأة بالمعروف والقسطِ للمشركين من أقاربكم وغيرهم؛ حيث كانوا بحالٍ لم ينتصبوا لقتالكم في الدين والإخراج من دياركم؛ فليس عليكم جناحٌ أن تَصِلوهم؛ فإنَّ صِلَتَهم في هذه الحالة لا محذورَ فيها ولا تَبِعَةَ ؛ كما قال تعالى في الأبوين الكافرين إذا كان ولدهما مسلماً: {وإن جاهَداك على أن تشرِكَ بي ما ليس لك به علمٌ فلا تُطِعْهما وصاحِبْهما في الدُّنيا معروفاً}.
{8} Na zilipoteremshwa Aya hizi tukufu zenye kuwashawishi kuwafanyia uadui makafiri, ziliwaathiri Waumini sana, nao wakafanya walivyoamrishwa kikamilifu zaidi, na hata wakaona kwamba ni dhambi kuwaunga baadhi ya jamaa zao washirikina, na wakadhania kuwa hilo linajumuishwa katika yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu akawaambia kuwa haya hayakujumuishwa katika yale aliyoyaharamisha,
akasema: “Mwenyezi Mungu hawakatazi kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakuwapiga vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” Yaani, Mwenyezi Mungu hakukatazeni kuwa wema, kuwaunga, na kuwalipa washirikina miongoni mwa jamaa zenu na wengineo kwa wema na uadilifu. Walikuwa katika hali ambayo hawawezi kusimama imara kupigana nanyi kwa ajili ya dini yenu na kuwatoa majumbani mwenu. Basi hakuna dhambi juu yenu mkiwaunga; kwa manaa kuwaunga katika hali hii hakujakatazwa wala hakuna lawama.
Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kuhusu wazazi makafiri ikiwa mtoto wao ni Mwislamu: “Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa wema duniani.”
#
{9} وقوله: {إنَّما ينهاكُم اللهُ عن الذين قاتَلوكم في الدِّين}؛ أي: لأجل دينكم؛ عداوةً لدين الله ولِمَنْ قام به، {وأخْرَجوكم من دِياركم وظاهَروا}؛ أي: عاونوا غيرهم {على إخراجِكم}: نهاكم الله {أن تَوَلَّوهم}: بالنصرة والموَّدة بالقول والفعل، وأما بِرُّكم وإحسانُكم الذي ليس بتولٍّ للمشركين؛ فلم ينهكم الله عنه، بل ذلك داخلٌ في عموم الأمر بالإحسان إلى الأقارب وغيرهم من الآدميين وغيرهم، {ومن يَتَوَلَّهم} منكم {فأولئك هم الظالمونَ}: وذلك الظلمُ يكون بحسب التولِّي؛ فإنْ كان تولياً تامًّا؛ كان ذلك كفراً مخرجاً عن دائرة الإسلام وتحت ذلك من المراتب ما هو غليظٌ وما هو دونه.
{9} Na kauli yake:
“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki wa kusaidiana nao, na wale waliokupigeni vita kwa sababu ya dini” na kwa sababu ya kuifanyia uadui Dini ya Mwenyezi Mungu na wale wanaoisimamisha,
“na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia” na watu wengine
“katika kufukuzwa kwenu.” Mwenyezi Mungu amekukatazeni kuwafanya marafiki wa kusaidiana nao na kwa mapenzi kwa kauli na vitendo. Ama kuwafanyia kwenu wema bila ya kuwafanya marafiki wendani washirikina, basi Mwenyezi Mungu hakukukatazeni hayo, bali hayo yamo katika amri ya jumla ya kuwafanyia wema jamaa na wanadamu wengineo,
“Na wanaowafanya hao marafiki wendani” miongoni mwenu
“basi hao ndio madhalimu.” Dhuluma hii inakuwa kulingana na kiasi cha kuwafanya marafiki. Na kama ni kuwafanya marafiki wendani kikamilifu, basi hilo linakuwa ukafiri unaotoa nje ya duara la Uislamu, na chini ya hapo kuna viwango vingine ambavyo ni vikubwa na vingine viko chini ya hapo.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ اللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ لَا هُنَّ حِلٌّ لَهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ وَآتُوهُمْ مَا أَنْفَقُوا وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَنْ تَنْكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنْفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنْفَقُوا ذَلِكُمْ حُكْمُ اللَّهِ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ (10) وَإِنْ فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ إِلَى الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ أَزْوَاجُهُمْ مِثْلَ مَا أَنْفَقُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي أَنْتُمْ بِهِ مُؤْمِنُونَ (11)}.
10. Enyi mlioamini! Wakikujilieni wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini, basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari waliotoa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takeni mlichokitoa, na wao watake walichokitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayokuhukumuni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima. 11. Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni waliokimbiwa na wake zao kiasi cha mahari waliyoyatoa. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini.
#
{10} لما كان صلح الحديبية؛ صالَحَ النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - المشركين على أنَّ مَن جاء منهم إلى المسلمين مسلماً؛ أنَّه يردُّ إلى المشركين، وكان هذا لفظاً عامًّا مطلقاً يدخل في عمومه النساء والرجال، فأمَّا الرجال؛ فإنَّ الله لم ينه رسولَه عن ردِّهم إلى الكفار وفاءً بالشرط وتتميماً للصلح الذي هو من أكبر المصالح، وأمَّا النساءُ؛ فلمَّا كان ردُّهنَّ فيه مفاسد كثيرةٌ؛ أمرَ المؤمنين إذا جاءهم {المؤمناتُ مهاجراتٍ}: وشَكُّوا في صدق إيمانهنَّ أن يمتحنوهنَّ ويختبروهنَّ بما يظهر به من صدقهنَّ من أيمانٍ مغلظةٍ وغيرها؛ فإنَّه يُحْتمل أن يكون إيمانُها غيرَ صادقٍ، بل رغبةً في زوج أو بلدٍ أو غير ذلك من المقاصد الدنيويِّة؛ فإنْ كُنَّ بهذا الوصف؛ تعيَّن ردُّهنَّ وفاءً بالشرط من غير حصول مفسدةٍ؛ وإن امتحنوهنَّ فوجدنَ صادقاتٍ، أو علموا ذلك منهنَّ من غير امتحانٍ؛ فلا يَرْجِعوهنَّ إلى الكفار. {لا هنَّ حلٌّ لهم ولا هم يَحِلُّون لهنَّ}: فهذه مفسدةٌ كبيرةٌ [في ردهنَّ] راعاها الشارع وراعى أيضاً الوفاء بالشرط؛ بأن يُعطوا الكفار أزواجهنَّ ما أنفقوا عليهنَّ من المهر وتوابعه عوضاً عنهنَّ، ولا جناح حينئذٍ على المسلمين أن ينكحوهنَّ، ولو كان لهنَّ أزواجٌ في دار الشرك، ولكن بشرطِ أن يؤتوهنَّ أجورهنَّ من المهر والنفقة، وكما أنَّ المسلمة لا تحلُّ للكافر؛ فكذلك الكافرة لا تحلُّ للمسلم [أن يمسكها] ما دامت على كفرها؛ غير أهل الكتاب، ولهذا قال تعالى: {ولا تُمسِكوا بعِصَم الكَوافِرِ}. وإذا نهي عن الإمساك بعصمتها؛ فالنهي عن ابتداء تزويجها أولى، {واسألوا ما أنفقتم}: أيُّها المؤمنون حين ترجِعُ زوجاتكم مرتداتٍ إلى الكفار؛ فإذا كان الكفار يأخذون من المسلمين نفقة من أسلمت من نسائهم؛ استحقَّ المسلمون أن يأخذوا مقابلة ما ذهب من زوجاتهم إلى الكفار.
وفي هذا دليلٌ على أنَّ خُروجَ البُضْع من الزوج متقوَّمٌ؛ فإذا أفسد مفسدٌ نكاح امرأة رجل برضاع أو غيره؛ كان عليه ضمانُ المهرِ.
وقوله: {ذلكم حكم الله}؛ أي: ذلكم الحكم الذي ذكره الله وبيَّنه لكم حكمُ الله؛ بيَّنه لكم ووضَّحه. {والله عليمٌ حكيمٌ}: فيعلم تعالى ما يصلح لكم من الأحكام، فيشرعه بحسب حكمته ورحمته.
{10} Ulipohitimishwa Mkataba wa Hudaybiyyah; Nabii– Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – alifanya suluhu na washirikina kwa sharti kwamba yeyote miongoni mwao atakayewajia Waislamu akiwa ni Muislamu, kwamba italazimu arudishwe kwa washirikina, na hili lilikuwa neno la jumla kabisa ambalo kwa ujumla wake linajumuisha wanawake na wanaume. Ama wanaume, Mwenyezi Mungu hakumkataza Mtume wake kuwarejesha kwa makafiri kwa kutimiza sharti hilo na kukamilisha suluhu ambayo ni miongoni mwa masilahi makubwa zaidi. Ama wanawake, pindi kuwarudisha kwao kulikuwa na maovu mengi, aliwaamrisha Waumini wakijiwa na
“wanawake Waumini waliohama” na wakawa na shaka kuhusu imani yao kwamba wawape mtihani kwa kitu cha kudhihirisha ukweli wao, kama vile viapo vikali na mambo mengineyo. Kwa maana, inawezekana kwamba imani yao hiyo si ya kweli, bali ni kwa kutaka tu mume, nchi, au malengo mengine ya kidunia. Kwa hivyo ikiwa wanasifika hivi, basi inalazimu warudishwe kwa washirikina katika kutimiza sharti walilowekeana na Waislamu bila ya kuleta madhara yoyote. Na ikiwa watawatia mtihanini na wakawaona kuwa ni wakweli, au wakajua hilo kwao bila ya kuwapa mtihani, basi hawakufaa kuwarudisha kwa makafiri.
“Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini.” Kwa maana, huu ni uharibifu mkubwa
[katika kuwarusha huko] ambao Mwenye sheria aliuzingatia na pia akazingatia utimizaji wa sharti; Kwamba wawape makafiri kile walichotumia kwa ajili ya wake zao kama vile mahari na gharama zinazohusiana nao kwa kubadilishana nao, na hapo hakuna ubaya kwa Waislamu kuwaoa, hata kama wana waume katika nchi za ushirikina lakini kwa sharti kwamba wawape ujira wao kama vile mahari na matunzo. Kama vile mwanamke wa Kiislamu si halali kwa kafiri, kadhalika, mwanamke kafiri haruhusiwi kwa mwanamume Mwislamu maadamu bado yuko katika ukafiri wake, isipokuwa Watu wa Kitabu.
Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu.” Na ikiwa ni haramu kushikilia kifungo chao cha ndoa, basi hata kukianzisha kwa kuwaoa kinafailia zaidi kukatazwa.
“Na takeni mlichokitoa” enyi Waumini, watakaporudi wake zenu kwa makafiri kwa kutoka kwa Uislamu. Na ikiwa makafiri wanachukua kutoka kwa Waislamu matunzo waliyoyatoa juu ya ya wake zao waliosilimu, basi Waislamu wanastahiki pia kupata fidia kwa kile walichotoa juu ya wake zao waliokwenda kwa makafiri. Katika hili kuna ushahidi kwamba kuondoka kwa tendo la ndoa kwa mume ni kitu kinachoweza kupimwa thamani yake. Kwa hivyo, ikiwa mharibifu ataharibu ndoa ya mke wa mwanamume fulani kwa njia ya kunyonyesha au vinginevyo, basi itamlazimu adhamini mahari aliyotoa.
Na kauli yake: “Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu” aliyoitaja, akaibainisha na akaiweka wazi, ni hukumu ya Mwenyezi Mungu.
“Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima.” Basi anazijua hukumu zinazokufaeni, kwa hivyo akaziweka katika sheria yenu kulingana na hekima yake na rehema zake.
#
{11} وقوله: {وإن فاتَكم شيءٌ من أزواجِكم إلى الكفَّار}: بأن ذهبنَ مرتدَّاتٍ، {فعاقبتُم فآتوا الذين ذهبتْ أزواجُهم مثل ما أنفقوا}: كما تقدَّم أنَّ الكفار إذا كانوا يأخذون بدل ما يفوت من أزواجهم إلى المسلمين؛ فمن ذهبت زوجتُه من المسلمين إلى الكفار، وفاتت عليه؛ فعلى المسلمين أن يعطوه من الغنيمة بدل ما أنفق. {واتَّقوا الله الذي أنتم به مؤمنونَ}: فإيمانكم بالله يقتضي منكم أن تكونوا ملازمين للتقوى على الدَّوام.
{11} Na kauli yake:
“Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri” ikiwa wataenda huku wamritadi,
“tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni waliokimbiwa na wake zao kiasi cha mahari waliyoyatoa” kama iliyotajwa hapo awali, kwamba ikiwa makafiri wanachukua fidia kwa yale wale waliowakosa miongoni mwa wake zao wakaenda kwa Waislamu, basi yule miongoni mwa wanaume waislamu ambaye mke wake atawaendea makafiri na akamkosa, basi ni juu ya Waislamu wampe baadhi ya ngawira badala ya kile alichotoa.
“Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini” kwa maana, imani yenu kwa Mwenyezi Mungu inakutakeni kushikamana na ucha Mungu kila wakati.
{يَاأَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَى أَنْ لَا يُشْرِكْنَ بِاللَّهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ (12)}.
12. Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu mno.
#
{12} هذه الشروط المذكورة في هذه الآية تسمَّى مبايعة النساء، اللاتي كنَّ يبايِعْنَّ على إقامة الواجبات المشتركة التي تجب على الذُّكور والنساء في جميع الأوقات، وأما الرجال؛ فيتفاوتُ ما يلزمُهم بحسب أحوالهم ومراتبهم وما يتعيَّن عليهم، فكان النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - يمتثل ما أمره الله [به]، فكان إذا جاءته النساءُ يبايِعْنَه والتزمن بهذه الشروط؛ بايَعَهُنَّ وجَبَرَ قلوبَهُنَّ، واستغفر لهنَّ الله فيما يحصل منهنَّ من التقصير وأدخلهنَّ في جملة المؤمنين، {على أن لا يُشْرِكنَ بالله شيئاً}: بل يفرِدْنَ الله وحده بالعبادة، {ولا يَقْتُلْنَ أولادهنَّ}: كما يجري لنساء الجاهليَّة الجهلاء، {ولا يَزْنينَ}: كما كان ذلك موجوداً كثيراً في البغايا وذوات الأخدان، {ولا يأتين ببُهتانٍ يفترينَه بين أيديهنَّ وأرجُلهنَّ}: والبهتان الافتراء على الغير؛ أي: لا يفترين بكلِّ حالة، سواءً أتعلَّقت بهنَّ مع أزواجهنَّ أو تعلَّق ذلك بغيرهم، {ولا يَعْصينَكَ في معروفٍ}؛ أي: لا يعصينك في كلِّ أمرٍ تأمرهنَّ به؛ لأنَّ أمرك لا يكون إلاَّ بمعروفٍ، ومن ذلك طاعتهنَّ لك في النهي عن النياحة وشقِّ الجيوب وخمش الوجوه والدُّعاء بدعوى الجاهلية، {فبايِعْهُنَّ}: إذا التزمنَ بجميع ما ذُكِر، {واستَغْفِرْ لهنَّ اللهَ}: عن تقصيرهنَّ وتطييباً لخواطرهنَّ. {إنَّ الله غفورٌ}؛ أي: كثير المغفرة للعاصين والإحسان إلى المذنبين التائبين. {رحيمٌ}: وسعت رحمتُه كلَّ شيءٍ وعمَّ إحسانُه البَرايا.
{12} Masharti haya yaliyotajwa katika Aya hii yanaitwa kiapo cha utii cha wanawake, ambao walikuwa wakipeana ahadi ya utii juu ya kutekeleza majukumu ya wajibu wanayoshiriki ndani yake wanaume na wanawake wakati wote. Ama wanaume, yale yanayowalazimu yanatofautiana kulingana na hali zao, daraja zao, na yale yanayowalazimu wao tu. Basi Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa akitekeleza yale aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, alikuwa wanawake wanapomjia, wakimpa kiapo chao cha utii na kushika sawasawa masharti haya, anawachukulia viapo hivyo vya na kuliwaza nyoyo zao, na kuwaombea Mwenyezi Mungu msamaha kwa mapungufu yao, na kuwajumuisha miongoni mwa Waumini,
“kwa sharti kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote,” bali watampwekesha Mwenyezi Mungu peke yake katika ibada.
“Wala hawatawauwa watoto wao” kama walivyokuwa wakifanya wanawake wajinga wa zama za kabla ya Uislamu.
“Wala hawatazini” ilivyokuwa ikifanywa sana na wazinzi wa kike na kufanya urafiki wa kimapenzi na wanaume wasiokuwa waume zao.
“Wala hawataleta uzushi wanaouzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao” katika kila hali, sawa uwe unahusiana na waume zao au unahusiana na mtu mwingine
“wala hawatakuasi katika jambo jema.” Yaani, hawatakuasi katika kila amri unayowaamrisha. Kwa sababu amri yako haiwezi kuwa ila kwa wema. Na katika hili ni utiifu wao kwako katika kukataza kwako kuomboleza kwa sauti kubwa, kurarua mifuko ya nguo zao
(katika kuomboleza), kujikwaruza uso, na kuomba dua za zama za kabla ya Uislamu.
“Basi peana nao ahadi” ikiwa watashikamana na yote yaliyotajwa,
“na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu” katika yale waliyozembea, na kwa ajili ya kuwafurahisha mawazo yao.
“Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi maghfira” kwa wanaoasi na ni mwenye kuwafanyia wema wafanyao dhambi na wakatubu.
“Mwenye kurehemu mno.” Ambaye rehema zake zimekienea kila kitu na wema wake umekijumuisha kila kiumbe.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ (13)}.
13. Enyi mlioamini! Msiwafanye marafiki wa kusaidiana nao katika watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini.
#
{13} أي: يا أيُّها المؤمنون إن كنتُم مؤمنين بربِّكم، ومتَّبعين لرضاه، ومجانبين لسخطه، {لا تَتَوَلَّوا قوماً غضب الله عليهم}: وإنَّما غضب عليهم لكفرهم، وهذا شاملٌ لجميع أصناف الكفار، {قد يَئِسوا من الآخرةِ}؛ أي: قد حُرِموا من خير الآخرة، فليس لهم منها نصيبٌ؛ فاحذروا أن تَتَوَلَّوهم فتوافقوهم على شرِّهم وشركهم ، فتُحرموا خير الآخرة كما حُرِمُوا. وقوله: {كما يئِس الكفَّار من أصحاب القبور}: حين أفضوا إلى الدار الآخرة، وشاهدوا حقيقة الأمر، وعلموا علم اليقين أنَّهم لا نصيب لهم منها.
ويُحتمل أنَّ المعنى: قد يئسوا من الآخرة؛ أي: قد أنكروها وكفروا بها؛ فلا يُسْتَغربُ حينئذٍ منهم الإقدام على مساخط الله وموجباتِ عذابِه، وإياسهم من الآخرة كما يئس الكفارُ المنكرون للبعث في الدُّنيا من رجوع أصحاب القبور إلى الله تعالى.
{13} Yaani, enyi Waumini, ikiwa mnamuamini Mola wenu Mlezi, na mnafuata radhi zake, na mnaepuka ghadhabu yake,
“Msiwafanye rafiki wa kusaidiana nao katika watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia.” Kwani, aliwakasirikia kwa sababu ya ukafiri wao, na hili linajumuisha kila aina ya makafiri,
“Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera.” Yaani, wamenyimwa heri ya Akhera, kwa hivyo huko hawana fungu lolote. Basi jihadharini msije mkawa marafiki wendani wao mkaja mkakubaliana nao katika uovu wao na ushirikina wao, kwa hivyo mkanyimwa heri ya Akhera kama walivyonyimwa wao.
Na kauli yake: “kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini” walipofika Akhera na wakaona ukweli wa jambo hilo, na wakajua kwa yakini kwamba wao hawana fungu huko. Inawezekana kwamba maana ya
“Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera” ni kuwa waliikataa na wakaikufuru. Kwa hivyo haliwi jambo la kushangaza kwamba wanakimbilia katika mambo anayoyachukia Mwenyezi Mungu na mambo yenye kusababisha adhabu yake, na kwamba walikata tamaa na maisha ya akhera kama vile makafiri hapa duniani wanaokanusha kufufuliwa walivyokata tamaa ya kurudi kwa watu wa makaburini kwa Mwenyezi Mungu.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.
* * *