Tafsiri ya surat Al-Jumua
Tafsiri ya surat Al-Jumua
Ilishuka Madina
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ (1)}.
1. Vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
#
{1} {الملكِ القدوسِ العزيزِ الحكيمِ}؛ أي: يسبح لله وينقاد لأمره ويتألَّهه ويعبده جميعُ ما في السموات والأرض؛ لأنَّه الكامل الملك، الذي له ملك العالم العلويِّ والسفليِّ؛ فالجميعُ مماليكه وتحت تدبيره. القُدُّوس المعظَّم المنزَّه عن كل آفة ونقص. العزيز القاهر للأشياء كلِّها. الحكيم في خلقه وأمره؛ فهذه الأوصاف العظيمة تدعو إلى عبادة الله وحدَه لا شريك له.
{1} "Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yaani, vinamtakasa Mwenyezi Mungu, na kusalimu amri yake, na kumfanyia uungu, na kumuabudu Yeye vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Kwa sababu Yeye ndiye Mfalme kamili, ambaye ana ufalme wa ulimwengu wa juu na wa chini. Kila mtu ni miliki yake na chini ya uendeshaji wake. Aliye Mtakatifu zaidi, aliyetukuka, aliyesafika kutokana na kila balaa na upungufu. Mwenye nguvu, Muweza wa kila kitu. Mwenye hekima katika kuumba kwake na kuamrisha kwake. Sifa hizi kuu zinaitia kuabudiwa Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika.
{هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِنْ كَانُوا مِنْ قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُبِينٍ (2) وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (3) ذَلِكَ فَضْلُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ (4)}.
2. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume kwenye watu wasiojua kusoma na kuandika, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhahiri. 3. Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima. 4. Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayompa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
#
{2} {هو الذي بَعَثَ في الأمِّيِّين رسولاً}: المراد بالأمِّيِّين الذين لا كتاب عندهم ولا أثر رسالة من العرب وغيرهم ممَّن ليسوا من أهل الكتاب، فامتنَّ الله تعالى عليهم منَّةً عظيمةً أعظم من منَّته على غيرهم؛ لأنهم عادمون للعلم والخير، وكانوا في {ضلال مبين}؛ يتعبدون للأصنام والأشجار والأحجار، ويتخلَّقون بأخلاق السباع الضارية، يأكل قويُّهم ضعيفَهم، وقد كانوا في غاية الجهل بعلوم الأنبياء، فبعث الله فيهم رسولاً منهم يعرِفون نسبه وأوصافه الجميلة وصدقه، وأنزل عليه كتابه، {يَتْلو عليهم آياتِهِ}: القاطعة الموجبة للإيمان واليقين، {ويزكِّيهم}: بأن يفصِّل لهم الأخلاق الفاضلة ويحثَّهم عليها ويزجرهم عن الأخلاق الرذيلة، {ويعلِّمُهم الكتاب والحكمة}؛ أي: علم الكتاب والسنة، المشتمل على علوم الأوَّلين والآخرين، فكانوا بعد هذا التعليم والتزكية من أعلم الخلق، بل كانوا أئمة أهل العلم والدين وأكمل الخلق أخلاقاً وأحسنهم هدياً وسمتاً، اهتدوا بأنفسهم، وهَدَوا غيرهم، فصاروا أئمة المهتدين وقادة المتقين ، فلله تعالى عليهم ببعثة هذا الرسول أكملُ نعمة وأجلُّ منحة.
{2} "Yeye ndiye aliyemtuma Mtume kwenye watu wasiojua kusoma na kuandika." Maana yake wasiojua kusoma na kuandika ni wale wasio na kitabu chochote wala alama ya utume miongoni mwa Waarabu na wengineo miongoni mwa Watu wa Kitabu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawapa neema kubwa kuliko neema aliyowapa wengineo. Kwa sababu wao hawakuwa na elimu na heri, na walikuwa katika "upotofu ulio dhahiri." Walikuwa wakiabudu masanamu, miti na mawe, na walikuwa na tabia za wanyama mwitu, ambapo wanyonge wao walikuwa wakiliwa na wenye nguvu wao. Na walikuwa katika ujinga mkubwa mno bila kujua elimu za Manabii. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia Mtume kutokana nao wenyewe, ambaye wanajua nasaba yake, sifa zake nzuri, na ukweli wake, na akamteremshia Kitabu chake, "ili awasomee Aya zake" zenye kukata, zenye kuwalazimu waamini na wawe na yakini. "Na awatakase" kwa kuwabainishia kwa kina maadili mema, na kuwahimiza kushikamana nao, na kuwakemea kutokana na tabia mbaya, "na awafunze Kitabu na hekima." Yaani, elimu ya Kitabu
(Qur-ani) na Sunna, ambayo inajumuisha elimu za watu wa kale na za wa mwisho. Kwa hivyo, wakawa baada ya kufundishwa huku na kutakaswa huku miongoni mwa viumbe wajuao zaidi. Bali walikuwa waongozi wa wenye elimu, dini na wenye maadili makamilifu zaidi katika viumbe vyote, na wabora wao zaidi katika uwongofu na heshima, wao wenyewe waliongoka na pia wakawaongoza wengine, basi wakawa ni maimamu wa waongofu na viongozi wa wacha Mungu. Basi Mwenyezi Mungu ni mwenye neema kamili zaidi na zawadi tukufu zaidi kwao kwa kuwatumia Mtume huyu.
#
{3} وقوله: {وآخرين منهم لَمَّا يَلْحَقوا بهم}؛ أي: وامتنَّ على آخرين من غيرهم، أي: من غير الأمِّيِّين ممَّن يأتي بعدهم ومن أهل الكتاب {لما يلحقوا بهم}؛ أي: فيمن باشر دعوة الرسول؛ يحتمل أنَّهم لَمَّا يلحقوا بهم في الفضل، ويحتمل أن يكونوا لمَّا يلحقوا بهم في الزمان، وعلى كلٍّ؛ فكلا المعنيين صحيحٌ؛ فإن الذين بعث الله فيهم رسوله وشاهدوه وباشروا دعوته حصل لهم من الخصائص والفضائل ما لا يمكن أحداً أن يلحقَهم فيها.
{3} Na kauli yake: "Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao." Yaani, aliwaneemesha wengineo wasiokuwa miongoni mwa wale wasiojua kusoma na kuandika miongoni mwa wale watakaokuja baada yao, na pia miongoni mwa Watu wa Kitabu "bado hawajaungana nao." Yaani, miongoni mwa waliousikia wito wa Mtume, inawezekana kwamba hawajawapata kwa fadhila, na pia inawezekana kwamba hawajawapata katika zama watakazoishi. Lakini maana hizi mbili ni sahihi. Kwa maana wale ambao Mwenyezi Mungu alituma kwao Mtume wake, wakamuona, na wakaishi katika siku za wito wake, walipata sifa maalumu na fadhila ambazo hakuna anayeweza kuwafikia katika hizo.
#
{4} وهذا من عزَّته وحكمته؛ حيث لم يترك عباده هَمَلاً ولا سُدىً، بل ابتعث فيهم الرسل وأمرهم ونهاهم، وذلك من [فضل اللَّه العظيم] الذي يؤتيه مَن يشاءُ من عباده، وهو أفضل من نعمته عليهم بعافية البدن وسعة الرزق وغير ذلك من النِّعم الدُّنيوية؛ فلا أفضل من نعمة الدين التي هي مادة الفوز والسعادة الأبديَّة.
{4} Haya ni katika nguvu zake na hekima yake. Kwa kuwa hakuwaacha waja wake wakiwa wamepuuzwa au bure tu. Bali aliwatuma Mitume miongoni mwao na akawaamrisha na akawakataza, na hayo ni katika
[fadhila kubwa za Mwenyezi Mungu] anazompa amtakaye katika waja wake, nazo ni bora kuliko fadhila zake juu yao kwa afya ya kimwili, riziki kunjufu, na neema nyinginezo za kidunia. Kwa hivyo, hakuna kitu bora kuliko neema ya dini, ambayo ndiyo kiini cha kufaulu na furaha ya milele.
{مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّهِ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ (5) قُلْ يَاأَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِنْ زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّهِ مِنْ دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (6) وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ (7) قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (8)}.
5. Mfano wa wale waliobebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu. 6.
Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipokuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema ukweli. 7. Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyokwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua mno madhalimu. 8.
Sema: Hayo mauti mnayoyakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye, mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana. Hapo atakwambieni mliyokuwa mkiyatenda.
#
{5} لمَّا ذكر تعالى منَّته على هذه الأمة الذين بَعَثَ فيهم النبيَّ الأميَّ وما خصَّهم الله [به] من المزايا والمناقب التي لا يلحقهم فيها أحدٌ، وهم الأمة الأميَّة، الذين فاقوا الأوَّلين والآخرين، حتى أهل الكتاب الذين يزعمون أنهم العلماء الربانيون والأحبار المتقدِّمون؛ ذكر أن الذين حمَّلهم الله التوراة من اليهود وكذا النصارى وأمرهم أن يتعلَّموها ويعملوا بها فلم يحملوها ولم يقوموا بما حُمِّلوا به؛ أنَّهم لا فضيلة لَهم، وأنَّ مَثَلَهم كمثل الحمار الذي يحمل فوق ظهره أسفاراً من كتب العلم؛ فهل يستفيد ذلك الحمار من تلك الكتب التي فوق ظهره؟! وهل تلحقه فضيلةٌ بسبب ذلك؟! أم حظُّه منها حملها فقط؟ فهذا مَثَلُ علماء أهل الكتاب ، الذين لم يعملوا بما في التوراة الذي من أجلِّه وأعظمه الأمر باتِّباع محمدٍ - صلى الله عليه وسلم - والبشارة به والإيمان بما جاء به من القرآن؛ فهل استفاد مَن هذا وصفه من التوراة إلاَّ الخيبة والخسران وإقامة الحجَّة عليه؛ فهذا المثل مطابقٌ لأحوالهم. {بئس مَثَلُ القوم الذين كذَّبوا} بآياتنا الدالَّة على صدق رسولنا وصحة ما جاء به {والله لا يَهْدي القوم الظالمين}؛ أي: لا يرشدهم إلى مصالحهم ما دام الظلم لهم وصفاً والعناد لهم نعتاً.
{5} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja neema yake juu ya umma huu ambao alituma miongoni mwao Nabii asiyejua kusoma na kuandika, na yale aliyowapa Mwenyezi Mungu wao tu ya sifa maalumu, ambayo hakuna anayeweza kuwafikia katika hayo, nao ni umma wasiojua kusoma na kuandika, waliopiku wa kale na wa mwisho, hata Watu wa Kitabu wanaojidai kuwa ni wanavyuoni wacha Mungu na makohani walio mbele sana, akataja wale ambao Mwenyezi Mungu aliwabebesha Taurat miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, na akawaamrisha waijifunze na kuifanyia kazi, lakini hawakuibeba na hawakufanya yale waliyobebeshwa, kwamba hawana ubora, na kwamba mfano wao ni kama punda anayebeba juu ya mgongo wake vitabu vya elimu; Je, punda huyo anafaidika na vitabu hivyo vilivyo juu ya mgongo wake? Je, ubora wowote utampata kwa sababu hilo? Au fungu lake katika hilo ni kuvibeba tu? Huu ndio mfano wa wanavyuoni wa Watu wa Kitabu ambao hawakutenda kulingana na yale yaliyomo ndani ya Taurati ambayo kubwa yake zaidi na tukufu yake zaidi ni ile amri ya kumfuata Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kupeana bishara ya kuja kwake na kuamini aliyoyaleta katika Qur-ani. Basi je, kuna yeyote ambaye hizi ndizo sifa zake kutoka katika Taurati isipokuwa kuambulia patupu, hasara, kusimamishiwa hoja dhidi yake? Mfano huu unaingiliana vyema na hali zao. "Mfano muovu mno wa watu waliokadhibisha" Aya zetu zinazoashiria ukweli wa Mtume wetu na usahihi wa yale aliyokuja nayo, "na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu" kufikia masilahi yao maadamu dhuluma na ukaidi bado ndizo sifa zao.
#
{6} ومن ظلم اليهود وعنادهم أنَّهم يعلمون أنَّهم على باطل ويزعمون أنَّهم على حقٍّ، وأنَّهم أولياء لله من دون الناس! ولهذا أمر الله رسوله أن يقولَ لهم: إن كنتُم صادقين في زعمِكُم أنَّكم على الحقِّ وأولياء الله؛ {فَتَمَنَّوُا الموتَ}: وهذا أمرٌ خفيفٌ؛ فإنَّهم لو علموا أنَّهم على حقٍّ؛ لما توقَّفوا عن هذا التحدِّي الذي جعله الله دليلاً على صدقهم إن تَمَنَّوْه و كَذِبِهم إن لم يَتَمَنَّوْه.
{6} Na katika dhuluma na ukaidi wa Mayahudi kwamba wanajua kuwa wako katika batili na wanadai kwamba wako katika haki,
na kwamba wao ni vipenzi wa Mwenyezi Mungu kuliko watu wote! Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kuwaambia: Ikiwa nyinyi ni wakweli katika madai yenu ya kwamba nyinyi mko katika Haki na ni vipenzi wa Mwenyezi Mungu; "basi yatamanini mauti" Hili ni jambo dogo. Kwani ikiwa walijua kwamba wako katika haki, basi wasingesika kufanya changamoto hii, ambayo Mwenyezi Mungu aliwafanyia kuwa uthibitisho wa ukweli wao ikiwa watayatamani, na uongo wao ikiwa hawatayatamani.
#
{7} ولمَّا لم يقعْ منهم مع الإعلانِ لهم بذلك؛ عُلِمَ أنَّهم عالمون ببطلان ما هم عليه وفساده، ولهذا قال: {ولا يَتَمَنَّوْنَه أبداً بما قدَّمت أيديهم}؛ أي: من الذنوب والمعاصي التي يستوحشون من الموت من أجلها، {واللهُ عليمٌ بالظالمين}: فلا يمكن أن يَخْفى عليه من ظلمهم شيءٌ.
{7} Na pindi hawakufanya hivyo, baada ya kuwatangazia hilo, basi ikajulikana kuwa wao wanatambua ubatili wa wanayoyafanya na uharibifu wake,
na ndiyo maana akasema: "Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyokwisha yatanguliza mikono yao" ya madhambi na maasia ambayo wanaogopa kufa kwa sababu yake. "Na Mwenyezi Mungu anawajua mno madhalimu." Hakuna chochote kinachoweza kufichikana kwake katika dhuluma zao.
#
{8} هذا؛ وإن كانوا لا يَتَمَنَّوْنَ الموت بما قدَّمت أيديهم، بل يفرُّون منه غايةَ الفرار؛ فإنَّ ذلك لا يُنجيهم، بل لابدَّ أن يُلاقيهم الموتُ الذي قد حَتَّمه الله على العباد [وكتبه عليهم]، ثم بعد الموت واستكمال الآجال يُرَدُّ الخَلْقُ كلُّهم يوم القيامةِ إلى عالم الغيب والشهادة، فينبِّئهم بما كانوا يعملون من خيرٍ وشرٍّ قليل وكثيرٍ.
{8} Ni hivyo, na ikiwa hawatamani kufa kwa sababu ya yale iliyoyatanguliza mikono yao, bali wanayakimbia kabisa. Lakini hilo halitawaokoa kutokana nayo, bali ni lazima watakutana na mauti, ambayo Mwenyezi Mungu ameshapitishia waja wake
[na akawaandikia]. Kisha, baada ya kufa na kukamilika kwa mida, viumbe vyote vitarudishwa Siku ya Kiyama kwa ajuaye zaidi ghaibu na mambo yanayoonekana, na atawaambia mema na mabaya, machache na mengi waliyokuwa wakiyafanya.
{يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ (9) فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانْتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِنْ فَضْلِ اللَّهِ وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيرًا لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ (10) وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انْفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا قُلْ مَا عِنْدَ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ اللَّهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ وَاللَّهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ (11)}.
9. Enyi mlioamini! Ikiadhiniwa kwa ajili ya Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye utajo wa Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua. 10. Na itakapokwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa. 11. Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama.
Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki.
#
{9} يأمر تعالى عباده المؤمنين بالحضور لصلاة الجمعة والمبادرة إليها من حين يُنادى لها والسعي إليها، والمراد بالسَّعْي هنا المبادرة [إليها] والاهتمام لها وجعلها أهمَّ الأشغال، لا العدو الذي قد نُهِيَ عنه عند المضيِّ إلى الصلاة. وقوله: {وذَروا البيعَ}؛ أي: اتركوا البيع إذا نودي للصلاة وامضوا إليها؛ فإنَّ {ذلكم خيرٌ لكم}: من اشتغالكم بالبيع، أو تفويتكم الصلاة الفريضة التي هي من آكدِ الفروض {إن كنتُم تعلمون}: أن ما عند الله خيرٌ وأبقى، وأنَّ مَنْ آثر الدُّنيا على الدين؛ فقد خسر الخسارة الحقيقيَّة؛ من حيث يظنُّ أنَّه يربح.
{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake waumini kuhudhuria Sala ya Ijumaa na kuifanyia hima kila iitwapo na kujitahidi kuifikia na kuipa muhimu mkubwa, wala haikumaanishwa kuikimbilia ambako kumekatazwa wakati wa kuiendea swala.
Na kauli yake: "Na wacheni biashara." Yaani, acheni kuuza na kununua inapoitwa kwa ajili ya swala na muiendee. Kwani "hayo ni bora kwenu" kuliko kujishughulisha kwenu na kuuza na kununua, au kukosa Swala ya faradhi, ambayo ni miongoni mwa faradhi ya lazima zaidi. "Lau kama mnajua" kwamba kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na ni cha kudumu zaidi, na kwamba anayeipendelea dunia hii kuliko akhera, basi hakika amehasiri hasara ya uhakika, ilhali yeye alifikiria kwamba amepata faida.
#
{10} وهذا الأمر بترك البيع موقَّت مدَّة الصلاة؛ {فإذا قُضِيَتِ الصلاةُ فانتشروا في الأرض}: لطلب المكاسب والتجارات، ولما كان الاشتغال بالتجارة مَظِنَّةُ الغفلة عن ذكر الله؛ أمر الله بالإكثار من ذكره؛ لينجبر بهذا، فقال: {واذكروا الله كثيراً}؛ أي: في حال قيامكم وقعودكم وعلى جنوبكم، {لعلَّكم تفلحون}: فإنَّ الإكثار من ذِكْر الله أكبر أسباب الفلاح.
{10} Hii ni amri ya kuacha kuuza wakati wa sala; "Na itakapokwisha Sala, tawanyikeni katika nchi" ili kutafuta machumo na biashara. Na kwa kuwa kujishughulisha na biashara ni jambo lenye uwezekano mkubwa wa kumfanya mtu kughafilika kumkumbuka Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu aliamuru atajwe kwa wingi; ili hilo litengenezwe na hili.
Akasema: "na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi." Yaani, mnapokuwa mmesimama, mmekaa, na mmelala kwa ubavu, "ili mpate kufanikiwa." Kwani kumkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi ndiyo sababu kuu ya kufaulu.
#
{11} {وإذا رَأوْا تجارةً أو لهواً انفضُّوا إليها}؛ أي: خرجوا من المسجد حرصاً على ذلك اللهو وتلك التجارة وتركوا الخير، {وتركوكَ قائماً}: تخطُبُ الناس، وذلك في يوم الجمعة، بينما النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - يخطب الناس؛ إذ قَدِمَ المدينةَ عيرٌ تحمل تجارةً، فلمَّا سمع الناس بها وهم في المسجد؛ انفضُّوا من المسجد ، وتركوا النبيَّ - صلى الله عليه وسلم - يخطبُ استعجالاً لما لا ينبغي أن يُستعجل له وترك أدب، {قل ما عندَ الله}: من الأجر والثواب لمن لازم الخير وصَبَّرَ نفسَه على عبادة الله ، {خيرٌ من اللهوِ ومن التجارةِ}: التي وإن حَصَلَ منها بعض المقاصد؛ فإنَّ ذلك قليلٌ منقضٍ ، مفوتٌ لخير الآخرة، وليس الصبر على طاعة الله مفوتاً للرزق؛ {فإنَّ الله خير الرازقين}؛ فمن اتَّقى الله؛ رزقه من حيث لا يحتسب.
{11} "Na wanapoiona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo." Yaani wanatoka msikitini kwa kutafuta kwa bidii pumbao hilo na biashara hiyo, na wakaacha heri, "na wakakuacha umesimama" ukihutubia watu. Hilo lilikuwa siku ya Ijumaa, wakati Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipokuwa anahutubia watu, tazama, ukaja msafara wa kibiashara Madina. Watu waliposikia juu yake ilhali wapo msikitini, wakatawanyika kutoka msikitini na wakamwacha Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akitoa khutba, wakiharakishia kile kisichofaa kuharakishiwa, na kuacha adabu nzuri.
"Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu" ya malipo mazuri kwa anayedumu katika heri na akajisubirisha katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, "ni bora kuliko pumbao na biashara" ambayo ingawa makusudio machache yanaweza kutokea humo, lakini hayo ni machache na ya kuisha, na ya kukosesha heri ya Akhera, nayo subira juu ya kumtii Mwenyezi Mungu haikoseshi riziki. "Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki." Kwa hivyo, mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, anamruzuku kutokea pale asipotarajia.
Kuna faida nyingi katika aya hizi: Miongoni mwake ni kwamba swala ya Siku ya Ijumaa ni wajibu kwa Waumini [wote] na wanalazimuka kuifanyia hima, kuiharakishia na kuijali sana. Miongoni mwake ni kwamba khutba mbili za siku ya Ijumaa ni wajibu na lazima zihudhuriwe. Kwa sababu alielezea ukumbusho hapa kwa hotuba hizo mbili, na Mwenyezi Mungu akaamuru kwamba kuziendea na kuzifanyia hima kwa haraka. Miongoni mwake ni kwamba ni katika sheria kuadhini kwa ajili ya Sala ya Ijumaa na kwamba hilo limeamrishwa. Miongoni mwake ni kukataza kununua na kuuza baada ya adhana ya Ijumaa na kuharamisha hayo. Na hilo si isipokuwa kwa sababu yanakosesha faradhi na kujishughulisha mbali nayo. Basi hilo likaashiria kwamba kila jambo hata kama linaruhusika katika asili yake, ikiwa linasababisha kupoteza jambo la wajibu, basi haliruhusiki katika hali hiyo. Miongoni mwake ni amri ya kuhudhuria khutba mbili za siku ya Ijumaa, na kumkashifu asiyezihudhuria, na inamlazimu mwenye kuzihudhuria kuzisikiliza kwa utulivu. Miongoni mwake ni kwamba mja ambaye anakaribia kumwabudu Mwenyezi Mungu wakati ambapo nafsi yake inamuita kwenye mambo ya pumbao, biashara na matamanio, anapaswa kuikumbusha mambo mema aliyo nayo Mwenyezi Mungu na kuipendelea radhi ya Mwenyezi Mungu kuliko matamanio yake.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Jumu'a kwa neema na msaada Mwenyezi Mungu. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
* * *