Tafsiri ya Surat Al-Waqi'ah
Tafsiri ya Surat Al-Waqi'ah
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu
{إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ (1) لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ (2) خَافِضَةٌ رَافِعَةٌ (3) إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا (4) وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا (5) فَكَانَتْ هَبَاءً مُنْبَثًّا (6) وَكُنْتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً (7) فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ (8) وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ (9) وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ (10) أُولَئِكَ الْمُقَرَّبُونَ (11) فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ (12) ثُلَّةٌ مِنَ الْأَوَّلِينَ (13) وَقَلِيلٌ مِنَ الْآخِرِينَ (14) عَلَى سُرُرٍ مَوْضُونَةٍ (15) مُتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ (16) يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُخَلَّدُونَ (17) بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِنْ مَعِينٍ (18) لَا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنْزِفُونَ (19) وَفَاكِهَةٍ مِمَّا يَتَخَيَّرُونَ (20) وَلَحْمِ طَيْرٍ مِمَّا يَشْتَهُونَ (21) وَحُورٌ عِينٌ (22) كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ (23) جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (24) لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا (25) إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا (26)}].
1. Litakapotokea hilo Tukio. 2. Hapana cha kukanusha kutokea kwake. 3. Literemshalo linyanyualo. 4. Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso. 5. Na milima itakaposagwasagwa. 6. Basi iwe mavumbi yanayopeperushwa. 7. Na nyinyi mtakuwa namna tatu. 8. Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? 9. Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? 10. Na wa mbele watakuwa mbele. 11. Hao ndio watakaowekwa karibu
(na Mwenyezi Mungu). 12. Katika Bustani zenye neema. 13. Fungu kubwa katika wa mwanzo. 14. Na wachache katika wa mwisho. 15. Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa. 16. Wakiviegemea wakielekeana. 17. Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele. 18. Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemichemi safi. 19. Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. 20. Na matunda wayapendayo. 21. Na nyama za ndege kama wanavyotamani. 22. Na Mahurulaini. 23. Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa. 24. Ni malipo kwa waliyokuwa wakiyatenda. 25. Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi. 26. Isipokuwa maneno ya Salama, Salama.
#
{1 - 3} يخبر تعالى بحال الواقعة التي لا بدَّ من وقوعها، وهي القيامة، التي {ليس لوقعتها كاذِبةٌ}؛ أي: لا شكَّ فيها؛ لأنَّها قد تظاهرت عليها الأدلَّة العقليَّة والسمعيَّة، ودلَّت عليها حكمته تعالى {خافضةٌ رافعةٌ}؛ أي: خافضةٌ لأناس في أسفل سافلين، رافعةٌ لأناس في أعلى عليين، أو: خفضت بصوتها فأسمعت القريب، ورفعتْ فأسمعتِ البعيد.
{1 - 3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatujulisha kuhusu hali ya tukio ambalo lazima litokee, ambalo ni Ufufuo, tukio ambalo
“hapana cha kukanusha kutokea kwake;” Yaani, hakuna shaka juu yake; kwa sababu zimedhihirika kwa ushahidi wa kiakili na wa kusikia juu ya hilo, na hekima yake Mtukufu pia ikaliashiria hilo. "Literemshalo linyanyualo." Yaani, literemshalo watu chini kuliko walio chini, na kuwanyanyua watu juu ya walio juu wa daraja la juu, au lilishusha sauti yake chini ili walio karibu wasikike, na likainyanyua ili wasikie walio mbali.
#
{4 - 6} {إذا رُجَّتِ الأرضُ رجًّا}؛ أي: حُركت واضطربتْ، {وبُسَّتِ الجبالُ بَسًّا}؛ أي: فتت، {فكانت هباءً منبثًّا}: فأصبحت ليس عليها جبلٌ ولا مَعْلمٌ، قاعاً صفصفاً، لا ترى فيها عوجاً ولا أمتاً.
{4 - 6} "Itakapotikiswa ardhi kwa mtikiso. Na milima itakaposagwasagwa. Basi iwe mavumbi yanayopeperushwa. Ikawa bure bila milima wala alama yoyote juu yake, ikawa mahali tambarare, na hutaona hapo mdidimio wala mwinuko.
#
{7 - 9} {وكنتم}: أيُّها الخلق، {أزواجاً ثلاثةً}؛ أي: انقسمتم ثلاث فرق بحسب أعمالكم الحسنة والسيئة. ثم فصَّل أحوال الأزواج الثلاثة، فقال: {فأصحابُ الميمنةِ ما أصحابُ الميمنةِ}: تعظيمٌ لشأنهم وتفخيمٌ لأحوالهم، {وأصحابُ المشأمة}؛ أي: الشمال، {ما أصحابُ المشأمة}: تهويلٌ لحالهم.
{7 - 9} "Na nyinyi" enyi viumbe! "mtakuwa namna tatu." Yaani, mtagawanyika katika makundi matatu kulingana na matendo yenu mema na mabaya. Kisha akabainisha kwa undani hali za namna tatu hizo,
akasema: "Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?" Hii ni kuonyesha hadhi yao kubwa na kuonyesha ukubwa wa hali yao. "Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?" Na hili ni la kuonyesha hali yao ya kutisha mno.
#
{10 - 14} {والسابقون السابقون. أولئك المقرَّبون}؛ أي: السابقون في الدنيا إلى الخيرات هم السابقون في الآخرة لدخول الجنات، أولئك الذين هذا وصفهم المقرَّبون عند الله {في جنات النعيم}: في أعلى علِّيين، في المنازل العاليات التي لا منزلة فوقها، وهؤلاء المذكورون {ثُلَّةٌ من الأوَّلين}؛ أي: جماعة كثيرون من المتقدِّمين من هذه الأمة وغيرهم. {وقليلٌ من الآخِرينَ}: وهذا يدلُّ على فضل صدر هذه الأمَّة في الجملة على متأخِّريها ؛ لكون المقرَّبين من الأولين أكثر من المتأخرين، والمقرَّبون هم خواصُّ الخلق.
{10 - 14} "Na wa mbele watakuwa mbele. Hao ndio watakaowekwa karibu
(na Mwenyezi Mungu)." Yaani, wa kwanza katika dunia kufanya wema ndio watakaokuwa wa kwanza Akhera kuingia katika bustani za mbinguni, wale wambao hizi ndizo sifa zao ndio watu wa karibu na Mwenyezi Mungu "katika Bustani zenye neema" katika walio juu kabisa, katika nyumba za juu kabisa ambazo hakuna daraja nyingine juu yake, na hao waliotajwa ndio "fungu kubwa katika wa mwanzo" kutoka katika umma huu na wengineo. "Na wachache katika wa mwisho." Na hili linaashiria ubora wa kizazi cha mwanzo cha umma huu kwa ujumla juu ya vizazi vyake vya baadaye. Kwa sababu walio karibu na Mwenyezi Mungu katika wale wa mwanzo ndio wengi zaidi kuliko wale wa baadaye, na walio karibu na Mwenyezi Mungu ndio viumbe maalumu.
#
{15 - 16} {على سررٍ موضونةٍ}؛ أي: مرمولةٍ بالذهب والفضة واللؤلؤ والجوهر وغير ذلك من الحليِّ والزينة التي لا يعلمها إلاَّ الله تعالى، {متكئين عليها}؛ أي: على تلك السرر، جلوس تمكُّن وطمأنينةٍ وراحةٍ واستقرارٍ، {متقابلين}: وجه كلٍّ منهم إلى وجه صاحبه؛ من صفاء قلوبهم وتقابلها بالمحبة وحسن أدبهم.
{15 - 16} "Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa" kwa dhahabu, fedha, lulu, na vito, na mapambo na marembesho mengineyo ambayo hayajui isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake. "Wakiviegemea" sawasawa kwa utulivu na raha "wakielekeana" uso kwa uso, kutokana na usafi wa nyoyo zao, upendo wao na tabia zao njema.
#
{17 - 19} {يطوفُ عليهم ولدانٌ مخلَّدونَ}؛ أي: يدور على أهل الجنة لخدمتهم وقضاء حوائجهم ولدانٌ صغارُ الأسنانِ في غاية الحسن والبهاء. {كأنَّهم لؤلؤٌ مكنونٌ}؛ أي: مستورٌ لا يناله ما يغيِّره، مخلوقون للبقاء والخلد؛ لا يهرمون ولا يتغيَّرون ولا يزيدون على أسنانهم، ويدورون عليهم بآنية شرابهم؛ {بأكوابٍ}: وهي التي لا عُرى لها، {وأباريقَ}: الأواني التي لها عرى، {وكأسٍ من مَعينٍ}؛ أي: من خمرٍ لذيذِ المشربِ لا آفة فيه، {لا يُصَدَّعونَ عنها}؛ أي: لا تصدِّعهم رؤوسُهم كما تصدِّعُ خمرة الدُّنيا رأس شاربها، ولا هم عنها {يُنزِفونَ}؛ أي: لا تُنْزَفُ عقولهم ولا تذهب أحلامُهم منها كما يكون لخمر الدنيا. والحاصلُ أنَّ كلَّ ما في الجنة من [أنواع] النعيم الموجود جنسه في الدُّنيا لا يوجد في الجنة فيه آفةٌ؛ كما قال تعالى: {فيها أنهارٌ من ماءٍ غير آسنٍ وأنهارٌ من لبنٍ لم يتغيَّرْ طعمُه وأنهارٌ من خمرٍ لَذَّةٍ للشاربين وأنهارٌ من عسل مُصَفًّى}، وذكر هنا خمر الجنَّة، ونفى عنه كلَّ آفة توجد في الدُّنيا.
{17 - 19} "Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele." Yaani, vijana wawili wadogo wa umri kiume, wazuri sana watawajia mara kwa mara wana Peponi ili kuwahudumia na kukidhi haja zao. "Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa" ambayo haipatwi na chochote kinachoweza kuibadilisha. Nao waliumbwa kwa ajili ya kukaa milele. Hawatazeeka, hawatabadilika wala hata umri wao hautazidi. Nao watawajia mara kwa mara wakiwaletea vyombo vya kinywaji chao. "Kwa vikombe" visivyo na kishikio "na mabirika" zenye kishikio "na bilauri za vinywaji kutoka katika chemichemi safi" vya mvinyo wenye ladha katika kuvinywa na visivyo na madhara. "Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo" baada ya kuvinywa, wala
“hawataloweshwa” na kuondolewa akili zao na uelewa wao kwa sababu yake kama ilivyo katika mvinyo wa duniani. Jambo la msingi ni kwamba aina zote za neema zote zilikozo Peponi ambazo mfano wake uko hapa duniani, hazina madhara yoyote huko.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Humo iko mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa mno." Na hapa, akataja pombe ya Peponi, na akasema kwamba haina madhara yoyote kama yale ya duniani.
#
{20} {وفاكهةٍ مما يتخيَّرون}؛ أي: مهما تخيَّروا وراق في أعينهم واشتهته نفوسُهم من أنواع الفواكه الشهيَّة والجنى اللذيذة؛ حَصَلَ لهم على أكمل وجهٍ وأحسنه.
{20} "Na matunda wayapendayo." Yaani, chochote watakachokichagua, na kikawapendeza machoni mwao, na nafsi zao zikayatamani sana katika kila aina ya matunda matamu, hayo watayapata kwa ukamilifu na kwa hali yake nzuri zaidi.
#
{21} {ولحم طيرٍ ممَّا يشتهون}؛ أي: من كلِّ صنف من الطيور يشتهونه، ومن أيِّ جنس من لحمه أرادوا؛ إن شاؤوا مشويًّا أو طبيخاً أو غير ذلك.
{21} "Na nyama za ndege kama wanavyotamani," sawa watake iliyomwa, iliyopikwa, au aina nyinginezo.
#
{22 - 23} {وحورٌ عينٌ كأمثال اللؤلؤ المكنون}؛ أي: ولهم حور عين، والحوراء: التي في عينها كحلٌ وملاحةٌ وحسنٌ وبهاءٌ، والعِينُ حسانُ الأعين ضخامها ، وحسنُ عين الأنثى ، من أعظم الأدلَّة على حسنها وجمالها. {كأمثال اللُّؤلؤ المكنونِ}؛ أي: كأنَّهن اللؤلؤ [الأبيض] الرطبُ الصافي البهيُّ المستور عن الأعين والريح والشمس، الذي يكون لونُه من أحسن الألوان، الذي لا عيب فيه بوجهٍ من الوجوه؛ فكذلك الحور العين، لا عيبَ فيهنَّ بوجهٍ، بل هنَّ كاملاتُ الأوصاف جميلاتُ النُّعوت؛ فكلُّ ما تأمَّلته منها؛ لم تجدْ فيه إلاَّ ما يسرُّ القلب ويروق الناظر.
{22 - 23} "Na Mahurulaini. Walio kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa." Hawa ni wanawake wenye kope zilizopakwa kuhl, ambazo ni nzuri, kubwa na rembo sana. Na uzuri wa macho ya mwanamke ni ishara ya uzuri wake na urembo wake. "Mfano wa lulu zilizohifadhiwa" mbali na macho, upepo, na jua, ambayo rangi yake huwa ndiyo mojawapo ya rangi bora kabisa, na isiyokuwa na kasoro yoyote. Basi vile vile mahurulaini hawa hawana kasoro yoyote kwa njia yoyote ile. Bali wao ni wenye sifa kamilifu na nzuri zaidi. Kwa hivyo, kila kitu unachofikiria kuhusiana nao, hutakipata ndani yake isipokuwa kwa njia inayopendeza moyo na kumfurahisha mtazamaji.
#
{24} وذلك النعيم المعدُّ لهم {جزاءً بما كانوا يعملون}؛ فكما حَسُنَتْ منهم الأعمال؛ أحسن الله لهم الجزاء، ووفَّر لهم الفوز والنعيم.
{24} Na hiyo neema waliyotayarishiwa "ni malipo kwa waliyokuwa wakiyatenda." Kama vile matendo yao yalikuwa mazuri, Mwenyezi Mungu akawalipa malipo mazuri, na akawapa ushindi na neema kwa wingi.
#
{25 - 26} {لا يسمعون فيها لغواً ولا تأثيماً}؛ أي: لا يسمعون في جنَّاتِ النعيم كلاماً يُلغي، ولا يكون فيه فائدةً ولا كلاماً يؤثم صاحبه {إلاَّ قيلاً سلاماً سلاماً}؛ أي: إلاَّ كلاماً طيباً، وذلك لأنَّها دار الطيبين، ولا يكون فيها إلاَّ كلُّ طيبٍ، وهذا دليلٌ على حسن أدب أهل الجنَّة في خطابهم فيما بينهم، وأنه أطيبُ كلام وأسرُّه للقلوب وأسلمه من كلِّ لغوٍ وإثم، نسأل الله من فضله.
{25-26} "Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi" kwa mwenye kuyazungumza. "Isipokuwa maneno ya Salama, Salama." Hii ni kwa sababu hiyo ni nyumba ya walio wazuri, na wala hakiwi humo isipokuwa kila kilicho kizuri tu, na huu ni ushahidi wa tabia njema za wakazi wa Peponi katika mazungumzo yao baina yao, na kwamba ni maneno yaliyo bora zaidi, ya kufurahisha zaidi mioyo, na yaliyo salama kabisa kutokana na maneno ya upuuzi na dhambi.
[{وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ (27) فِي سِدْرٍ مَخْضُودٍ (28) وَطَلْحٍ مَنْضُودٍ (29) وَظِلٍّ مَمْدُودٍ (30) وَمَاءٍ مَسْكُوبٍ (31) وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ (32) لَا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ (33) وَفُرُشٍ مَرْفُوعَةٍ (34) إِنَّا أَنْشَأْنَاهُنَّ إِنْشَاءً (35) فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا (36) عُرُبًا أَتْرَابًا (37) لِأَصْحَابِ الْيَمِينِ (38) ثُلَّةٌ مِنَ الْأَوَّلِينَ (39) وَثُلَّةٌ مِنَ الْآخِرِينَ (40)}].
27. Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? 28. Katika mikunazi isiyo na miba. 29. Na migomba iliyopangiliwa. 30. Na kivuli kilichotanda. 31. Na maji yanayomiminika. 32. Na matunda mengi. 33. Hayatindikii wala hayakatazwi. 34. Na matandiko yaliyonyanyuliwa. 35. Hakika Sisi tutawaumba
(Mahurulaini) upya. 36. Na tutawafanya vijana. 37. Wanapendana na waume zao, hirimu moja. 38. Kwa ajili ya watu wa kuliani. 39. Fungu kubwa katika wa mwanzo. 40. Na fungu kubwa katika wa mwisho.
#
{27 - 34} ثم ذَكَرَ ما أعدَّ لأصحاب اليمين ، فقال: {وأصحابُ اليمين ما أصحابُ اليمين}؛ أي: شأنُهم عظيمٌ وحالهم جسيمٌ، {في سدرٍ مخضودٍ}؛ أي: مقطوع ما فيه من الشوك والأغصان الرَّديئة المضرَّة، مجعول مكان ذلك الثمر الطيب. وللسِّدْرِ من الخواصِّ الظلُّ الظَّليل وراحة الجسم فيه، {وطلحٍ منضودٍ}: والطَّلْح معروفٌ، وهو شجرٌ كبارٌ يكون بالبادية تُنَضَّدُ أغصانه من الثمر اللذيذ الشهي، {وماءٍ مسكوبٍ}؛ أي: كثير من العيون والأنهار السارحة والمياه المتدفِّقة، {وفاكهةٍ كثيرةٍ. لا مقطوعةٍ ولا ممنوعةٍ}؛ أي: ليست بمنزلة فاكهة الدُّنيا؛ تنقطعُ في وقتٍ من الأوقات وتكون ممتنعةً؛ أي: متعسِّرة على مبتغيها، بل هي على الدوام موجودةٌ، وجناها قريبٌ يتناوله العبد على أيِّ حال يكون، {وفُرُشٍ مرفوعةٍ}؛ أي: مرفوعة فوق الأسرَّة ارتفاعاً عظيماً، وتلك الفرش من الحرير والذهب واللؤلؤ وما لا يعلمه إلاَّ الله.
{27 - 34} Kisha akataja aliyowaandalia watu wa kuliani,
akasema: "Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?" Yaani, jambo lao ni kuu na hali yao kubwa. "Katika mikunazi isiyo na miba" wala matawi mabaya, yenye madhara ndani yake, na matunda mazuri yameekwa mahali pa matawi hayo. Mti huu wa mkunazi ni katika miti maalumu yenye kivuli cha kufunika mno na pia mwili hupata raha ndani yake. "Na migomba iliyopangiliwa" Mti huu mkubwa unapatikana jangwani ambao matawi yake hujipanga kwa matunda matamu ya kuvutia. "Na maji yanayomiminika" kwa wingi kutoka katika chemichemi na mito ipitayo "na matunda mengi. Hayatindikii wala hayakatazwi." Yaani, si katika cheo kimoja na matunda ya duniani; ambayo hayapatikani katika wakati fulani na inakuwa haiwezekani na ni vigumu kwa mwenye kuyatafuta. Bali hayo yanapatikana siku zote, na matunda yake yako karibu na mja, anaweza kuyachukua hata awe katika hali gani. "Na matandiko yaliyonyanyuliwa" juu ya vitanda kwa urefu mkubwa, na magodoro hayo yametengenezwa kwa hariri, dhahabu, lulu, na yale ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anajua.
#
{35 - 38} {إنَّا أنشأناهنَّ إنشاءً}؛ أي: إنَّا أنشأنا نساءَ أهل الجنة نشأةً غير النشأة التي كانت في الدنيا، نشأةً كاملةً، لا تقبل الفناء، {فَجَعَلْناهنَّ أبكاراً}: صغارهنَّ وكبارهنَّ، وعموم ذلك يشمل الحور العين ونساء أهل الدنيا، وأنَّ هذا الوصف - وهو البكارةُ - ملازم لهنَّ في جميع الأحوال؛ كما أنَّ كونهنَّ {عُرُباً أتراباً}: ملازمٌ لهنَّ في كلِّ حال، والعَروبُ هي المرأة المتحبِّبة إلى بعلها بحسن لفظها وحسن هيئتها ودلالها وجمالها ومحبَّتها؛ فهي التي إن تكلَّمت سبتِ العقول، وودَّ السامعُ أنَّ كلامها لا ينقضي، خصوصاً عند غنائهنَّ بتلك الأصوات الرخيمة والنَّغَمات المطربة، وإنْ نَظَرَ إلى أدبها وسمتها ودَلِّها؛ ملأت قلبَ بعلها فرحاً وسروراً، وإن انتقلتْ من محلٍّ إلى آخر؛ امتلأ ذلك الموضع منها ريحاً طيباً ونوراً، ويدخُلُ في ذلك الغنجة عند الجماع، والأتراب: اللاتي على سنٍّ واحدةٍ ثلاث وثلاثين سنة، التي هي غايةُ ما يتمنَّى ونهاية سنِّ الشباب؛ فنساؤهم عربٌ أترابٌ متفقاتٌ مؤتلفاتٌ راضياتٌ مرضياتٌ لا يَحْزَنَّ ولا يُحْزِنَّ، بل هنَّ أفراح النفوس وقُرَّة العيون وجلاء الأبصار، {لأصحاب اليمين}؛ أي: معدات لهم مهيَّآت.
{35 - 38} "Hakika Sisi tutawaumba upya" wanawake wa wakazi wa bustani za mbinguni kwa namna tofauti na walivyokuwa katika dunia, uumbaji kamili usiokubali kuisha. "Na tutawafanya vijana" sawa wawe wadogo wao au wakubwa wao, na ujumla wa hilo unawajumuisha mahurulaini pia na wanawake wa watu wa duniani, na kwamba sifa hii ya ujana wataendelea kuwa yao katika hali zote, na pia watakuwa "Wanapendana na waume zao, hirimu moja." Hawa ni wale wanawake wanaofanya bidii ya kuwa wenye kupendeza kwa waume zao kwa kauli zao nzuri, mwonekano wao mzuri, kujilegeza kwao, urembo wao na mapenzi yao. Ni katika wale ambao akiongea, huvutia mno akili, na msikilizaji anatamani kwamba maneno yake yasiishe, hasa wakati wanapoimba kwa sauti hizo nzuri na midundo mizuri mizuri, na akitazama adabu yake, tabia yake na kujilegeza kwake, anaujaza moyo wa mume wake furaha na bashasha, hata akitoka mahali kwenda sehemu nyingine, anaijaza sehemu hiyo inajazwa na harufu nzuri na nuru, na hili pia linajumuisha kujimwaya kwake wakati wa kujamiiana. Nao watakuwa hirimu moja wa miaka thelathini na tatu, ambayo ndio upeo wa kile mtu anachotamani na mwisho wa ujana. Basi wataandaliwa ili wawe wenye kufurahisha nafsi na kipendezacho macho "kwa ajili ya watu wa kuliani."
#
{39 - 40} {ثلَّةٌ من الأوَّلين. وثُلَّةٌ من الآخرين}؛ أي: هذا القسم، وهم أصحاب اليمين، عددٌ كثيرٌ من الأوَّلين وعدد كثيرٌ من الآخرينِ.
{39 - 40} "Fungu kubwa katika wa mwanzo. Na fungu kubwa katika wa mwisho." Na hawa ndio watu wa kuliani, ambao ni idadi kubwa ya wale wa kwanza na idadi kubwa ya wa baadaye.
{وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ (41) فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ (42) وَظِلٍّ مِنْ يَحْمُومٍ (43) لَا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ (44) إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَلِكَ مُتْرَفِينَ (45) وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنْثِ الْعَظِيمِ (46) وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ (47) أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ (48)}
41. Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? 42. Katika upepo wa moto, na maji yanayochemka. 43. Na kivuli cha moshi mweusi. 44. Si baridi wala cha kustarehesha. 45. Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. 46. Na walikuwa wakiendelea tu kufanya madhambi makubwa. 47.
Na walikuwa wakisema: 'Tutakapokufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndiyo tutafufuliwa? 48. Au baba zetu wa zamani?'
#
{41 - 44} المرادُ بأصحاب الشمال هم أصحابُ النارِ والأعمال المشؤومة، فذكر الله لهم من العقاب ما هم حقيقون به، فأخبر أنَّهم {في سَموم}؛ أي: ريح حارَّة من حرِّ نار جهنَّم؛ تأخذ بأنفاسهم، وتقلِقُهم أشدَّ القلق، {وحميم}؛ أي: ماءٍ حارٍّ يقطِّع أمعاءهم، {وظِلٍّ من يَحْموم}؛ أي: لهب نارٍ يختلط - بدخان، {لا باردٍ ولا كريم}؛ أي: لا بردَ فيه ولا كرم. والمقصودُ أنَّ هناك الهمَّ والغمَّ والحزنَ والشرَّ الذي لا خير فيه؛ لأنَّ نفي الضدِّ إثباتٌ لضدِّه.
{41 - 44} Wanachokusudiwa watu wa kushoto ni watu wa Motoni na vitendo viovu. Basi Mwenyezi Mungu akawatajia adhabu wanayostahiki, na akajulisha kwamba wao watakuwa "katika upepo wa moto" wa wa Jahannam, utakaochukua pumzi zao na kuwafanya kuwa na wasiwasi kubwa mno, "na maji yanayochemka" yatakayokata matumbo yao. "Na kivuli cha moshi mweusi. Si baridi wala cha kustarehesha." Kinachokusudiwa hapa ni kwamba humo kuna wasiwasi kubwa, huzuni kubwa na uovu ambao hakuna heri yoyote ndani yake. Kwa sababu kutaja kitu pia ni kuthibitisha kinyume chake.
#
{45 - 48} ثم ذكر أعمالهم التي أوصلتهم إلى هذا الجزاء، فقال: {إنَّهم كانوا قبل ذلك مُتْرَفينَ}؛ أي: قد ألهتْهم دنياهم وعمِلوا لها وتنعَّموا وتمتَّعوا بها، فألهاهم الأملُ عن إحسان العمل؛ فهذا الترفُ الذي ذمَّهم الله عليه، {وكانوا يُصِرُّونَ على الحِنثِ العظيم}؛ أي: وكانوا يفعلون الذُّنوب الكبار ولا يتوبون منها ولا يندمون عليها، بل يصرُّون على ما يُسْخِطُ مولاهم، فقَدِموا عليه بأوزارٍ كثيرةٍ غير مغفورةٍ، وكانوا يُنْكِرونَ البعث، فيقولون استبعاداً لوقوعه: {أإذا مِتْنا وكُنَّا تراباً وعظاماً أإنا لمبعوثونَ. أوَ آباؤنا الأوَّلونَ}؛ أي: كيف نُبْعَثُ بعد موتنا وقد بلينا فكُنَّا تراباً وعظاماً! هذا من المحال.
{45 - 48} Kisha akataja vitendo vyao vilivyowapelekea kwenye malipo hayo,
akasema: "Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa." Yaani, walidanganywa na dunia yao na wakaifanyia matendo, na wakaifurahia, kwa hivyo matumaini yakawashughulisha mbali na kutenda mema. Hii ndiyo anasa aliyoikashifu Mwenyezi Mungu. "Na walikuwa wakiendelea tu kufanya madhambi makubwa" na wala hawatubii wala kujutia. Bali walikuwa waking'ang'ania kufanya yale yanayomchukiza Mola wao, kwa hiyo wakamjia wakiwa na madhambi mengi yasiyosamehewa. Na pia walikuwa wakipinga suala la kufufuliwa wafu, wakawa wanasema wakilikatalia mbali hilo, "Tutakapokufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? Au baba zetu wa zamani?" Yaani, vipi tutafufuliwa baada ya kufa na kupotelea mbali tukawa udongo na mifupa? Hilo haliwezekani.
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akiwajibu:
{قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ (49) لَمَجْمُوعُونَ إِلَى مِيقَاتِ يَوْمٍ مَعْلُومٍ (50) ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ (51) لَآكِلُونَ مِنْ شَجَرٍ مِنْ زَقُّومٍ (52) فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ (53) فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ (54) فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ (55) هَذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ (56) نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ (57)}].
49.
Sema: 'Hakika wa zamani na wa mwisho.' 50. Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. 51. Kisha nyinyi, mliopotea, mnaokanusha. 52. Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. 53. Na kwa mti huo mtajaza matumbo. 54. Na juu yake mtakunywa maji yanayochemka. 55. Tena mtakunywa kama wanavyokunywa ngamia wenye kiu. 56. Hiyo ndiyo karamu yao ya kuwakaribisha Siku ya Malipo. 57. Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
#
{49 - 50} أي: قل: إنَّ متقدِّم الخلق ومتأخِّرهم؛ الجميع سيبعثهم الله ويجمعهم لميقات يوم معلوم قدَّره الله لعباده حين تنقضي الخليقة، ويريد الله [تعالى] جزاءهم على أعمالهم التي عملوها في دار التكليف.
{49 - 50} Yaani,
sema: Hakika wa mwanzo katika viumbe na wa mwisho wao, wote hao watafufuliwa na Mwenyezi Mungu na watakusanywa pamoja kwa wakati uliowekwa wa siku maalumu ambao Mwenyezi Mungu aliwaandikia waja wake, wakati watakapomalizika viumbe, na Mwenyezi Mungu akataka kuwalipa kwa matendo yao waliyoyafanya katika Nyumba kujukumishwa.
#
{51 - 53} {ثم إنَّكم أيُّها الضالُّون}: عن طريق الهدى، التابعون لطريق الرَّدى، {المكذِّبون}: بالرسول - صلى الله عليه وسلم - وما جاء به من الحقِّ والوعد والوعيد، {لآكلون من شجرٍ من زَقومٍ}: وهو أقبح الأشجار وأخسُّها وأنتنُها ريحاً وأبشعها منظراً، {فمالِئونَ منها البطونَ}: والذي أوجب لهم أكلها مع ما هي عليه من الشناعة، الجوعُ المفرِطُ الذي يلتهبُ في أكبادِهم وتكادُ تنقطعُ منه أفئدتهم، هذا الطعام الذي يدفعون به الجوع، وهو الذي لا يسمِنُ ولا يُغْني من جوع.
{51 - 53} "Kisha nyinyi, mliopotea" kutoka kwenye njia ya uwongofu, mnaofuata njia ya maangamizo, "mnaokanusha" Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - na haki, ahadi, na tishio la adhabu aliyokuja nayo. "Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu." Nao ndio mti huu mbaya zaidi, duni zaidi, wenye harufu mbaya zaidi, na wenye mwonekano wa kutisha zaidi. "Na kwa mti huo mtajaza matumbo." Na kilichowasababishia kuula pamoja na ubaya wake mkubwa huu ni njaa kali zaidi inayowaka mno katika maini yao na nyoyo zao zinakaribia kukatika kwa sababu yake. Hiki ndicho chakula watakachozuilia njaa yao kwacho, nacho ndicho kile kisichonenepesha wala kuondoa njaa.
#
{54 - 56} وأما شرابهم؛ فهو بئس الشرابُ، وهو أنهم يشربون على هذا الطعام من الماء الحميم الذي يغلي في البطون {شُرْبَ الهيم}: وهي الإبل العطاش ، التي قد اشتدَّ عَطَشها، أو أنَّ الهَيَم داءٌ يصيب الإبل لا تَرْوَى معه من شرب الماء. {هذا}: الطعام والشراب {نُزُلُهم}؛ أي: ضيافتهم {يومَ الدِّين}: وهي الضيافة التي قدَّموها لأنفسهم وآثروها على ضيافةِ الله لأوليائه؛ قال تعالى: {إنَّ الذين آمنوا وعَمِلوا الصالحاتِ كانتْ لهم جنَّاتُ الفِرْدَوْسِ نُزُلاً. خالدين فيها لا يَبْغونَ عنها حِوَلاً}.
{54 - 56} Ama kinywaji chao, hicho kitakuwa ndicho kinywaji kibaya zaidi, nacho ni kwamba watakunywa pamoja na chakula hiki maji ya moto yanayochemka matumboni "kama wanavyokunywa ngamia wenye kiu." Na pia ilisemekana kwamba ni ngamia waliosibiwa na ugonjwa ambao unawafanya kutokata kiu chao hata wakinywa maji. "Hiyo ndiyo karamu yao ya kuwakaribisha Siku ya Malipo" ambayo wao wenyewe ndio waliojisababishia na kuipenedelea na wakakataa karamu ya makaribisho mazuri ya Mwenyezi Mungu kwa vipenzi wake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale walioamini na wakatenda mema, mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi. Watadumu humo; hawatataka kuondoka."
#
{57} ثم ذكر الدليل العقليَّ على البعث، فقال: {نحن خَلَقْناكم فلولا تصدِّقونَ}؛ أي: نحن الذين أوجَدْناكم بعد أن لم تكونوا شيئاً مذكوراً من غير عجزٍ ولا تعبٍ، أفليس القادر على ذلك بقادرٍ على أن يُحيي الموتى؟ بلى إنَّه على كلِّ شيءٍ قديرٌ، ولهذا وبَّخهم على عدم تصديقهم بالبعث وهم يشاهدون ما هو أعظم منه وأبلغ.
{57} Kisha akataja ushahidi wa kiakili juu ya suala la kufufuliwa wafu,
akasema: "Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?" Yaani, Sisi ndio tuliokuumbeni baada ya kutokuwa kitu cha kutajwa, bila ya kutoshindwa wala uchovu. Basi je, mwenye uwezo wa kufanya hivi hawezi kufufua wafu. La hasha! Anaweza. Hakika Yeye ni muweza mno wa kila kitu. Basi ndiyo maana akawakemea kwa kutosadiki ufufuo ilhali wanaona yale ambayo ni makubwa zaidi ya hilo.
{أَفَرَأَيْتُمْ مَا تُمْنُونَ (58) أَأَنْتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ (59) نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ (60) عَلَى أَنْ نُبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنْشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ (61) وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَى فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ (62)}.
58. Je, mnaiona mbegu ya uzazi mnayoidondokesha? 59. Je, mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? 60. Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi. 61. Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilolijua. 62. Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
#
{58 - 62} أي: {أفرأيتم} ابتداء خَلْقِكُم من المنيِّ الذي {تُمنون} فهل أنتم خالقون ذلك المنيَّ، وما ينشأ منه أم الله تعالى الخالق؟ الذي خَلَقَ فيكم من الشهوة وآلتها في الذكر والأنثى، وهدى كلاًّ منهما لما هنالك، وحبَّب بين الزوجين، وجعل بينهما من المودَّة والرَّحمة ما هو سبب التناسل ، ولهذا أحالهم اللهُ تعالى بالاستدلال - بالنَّشأة الأولى على النشأة الأخرى، فقال: {ولقد علمتُمُ النَّشْأةَ الأولى فلولا تَذَكَّرونَ}: أنَّ القادر على ابتداء خلقكم قادرٌ على إعادتكم.
{58 - 62} Yaani, "je, mnaiona" mwanzo wa kuumbwa kwenu kutokana na manii ambayo ni "mbegu ya uzazi mnayoidondokesha?" Je, nyinyi ndio waumbaji wa manii hayo, na yanayotoka humo, au Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Muumba? Ambaye ameumba ndani yenu matamanio na katika mwanamume na mwanamke, na akamuongoza kila mmoja katika yale yaliyomo, na akaweka mapenzi, rehema baina ya wanandoa, mambo ambayo ndiyo sababu ya kuzaana, basi ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwarejeza kuangalia ushahidi wa uumbaji wa kwanza juu ya uumbaji wa akhera,
akasema: "Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki" kwamba anayeweza kuwaumba mwanzoni ni muweza wa kuwarudisha.
{أَفَرَأَيْتُمْ مَا تَحْرُثُونَ (63) أَأَنْتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ (64) لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ (65) إِنَّا لَمُغْرَمُونَ (66) بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ (67)}.
63. Je, mnaona hivyo mnavyovipanda? 64. Je, ni nyinyi mnayoyaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? 65. Tungelitaka, tungeliyafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu. 66.
Mkisema: 'Hakika sisi tumegharimika.' 67. Bali sisi tumenyimwa.
#
{63 - 67} وهذا امتنانٌ منه على عباده؛ يدعوهم به إلى توحيدِهِ وعبادتِهِ والإنابةِ إليه؛ حيث أنعم عليهم بما يسَّره لهم من الحرث للزُّروع والثمار، فيخرجُ من ذلك من الأقوات والأرزاق والفواكه ما هو من ضروراتهم وحاجاتهم ومصالحهم التي لا يقدِرون أن يُحصوها، فضلاً عن شكرها وأداء حقِّها، فقرَّرهم بمنَّته، فقال: {أأنتُم تَزْرَعونَه أم نحنُ الزَّارِعونَ}؛ أي: أنتم أخرجْتُموه نباتاً من الأرض؟ أم أنتُم الذي نمَّيتموه؟ أم أنتم الذين أخرجتم سُنْبله وثمرَه حتى صار حبًّا حصيداً وثمراً نضيجاً؟ أم الله الذي انفرد بذلك وحدَه وأنعم به عليكم، وأنتم غايةُ ما تفعلون أن تحرُثوا الأرض، وتشقُّوها، وتُلْقوا فيها البذرَ، ثم لا علم عِندكم بما يكون بعد ذلك ولا قدرةَ لكم على أكثر من ذلك؟ ومع ذلك؛ فنبَّههم على أنَّ ذلك الحرثَ معرضٌ للأخطار لولا حفظُ الله وإبقاؤه بُلغةً لكم ومتاعاً إلى حين. فقال: {لو نشاء لجعلناه}؛ أي: الزرع المحروث وما فيه من الثمار {حُطاماً}؛ أي: فتاتاً متحطِّماً لا نفع فيه ولا رزق، {فظَلْتُمْ}؛ أي: فصرتُم بسبب جعله حطاماً بعد أن تعبتم فيه، وأنفقتم النفقات الكثيرة، {تَفَكَّهونَ}؛ أي: تندمون وتحسرون على ما أصابكم، ويزول بذلك فرحُكم وسرورُكم وتفكُّهكم، فتقولون: {إنَّا لَمُغْرَمونَ}؛ أي: إنَّا قد نقصنا وأصابتنا مصيبةٌ اجتاحَتْنا. ثم تعرفون بعد ذلك من أين أتيتُم، وبأيِّ سبب دُهيتم؟ فتقولون: {بل نحنُ محرومونَ}! فاحْمَدوا الله تعالى حيث زَرَعَه [اللَّهُ] لكم، ثم أبقاه وكمَّله لكم، ولم يرسلْ عليه من الآفات ما به تُحرمون من نفعِهِ وخيرِهِ.
{63 - 67} Hii ni neema itokayo kwake juu ya waja wake, ambayo kwayo anawaita wampwekeshe, wamwabudu, na wamgeukie yeye. Ambapo aliwaneemesha kwa yale aliyowarahisishia katika suala la kulima mazao na matunda, kisha vinatoka humo chakula, riziki, na matunda ambayo ni miongoni mwa mahitaji yao ya lazima, na masilahi ambayo hawawezi kuyahesabu wakayadhibiti, pamoja na kwamba hawawezi kushukuru hayo na kutimizia haki yake ya sawasawa,
basi akawafanya kukiri neema yake hii akasema: "Je, ni nyinyi mnayoyaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?" Yaani, je, nyinyi ndio mliiotesha mmea hii kutoka ardhini? Au nyinyi ndio mlioikuza? Au nyinyi ndio mliotoa masuke yake na matunda yake mpaka yakavunwa kama nafaka na matunda yaliyoiva? Au ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliyefanya haya na akawapa hivyo kama neema, nami kikubwa mnachofanya tu ni kulima ardhi, kuipasua, na kupanda humo mbegu, kisha huwa hamjui ni kinachotokea baada ya hayo, wala hata hamna uwezo wa kufanya zaidi ya hayo? Hata hivyo; akawatanabahisha kwamba shamba hilo liko kwenye hatari, lau si kutokana na ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kuliweka liwe ni lenye kusalia ili liwe ni la usaidizi kwenu na starehe kwa muda.
Akasema: " Tungelitaka, tungeliyafanya." Yaani, mazao yaliyolimwa humo na matunda yaliyo ndani yake "yakawa mapepe" yasiyokuwa na manufaa wala riziki, "mkabaki" kwa sababu ya kuyafanywa kuwa mapepe baada ya kutaabika kwenu ndani yake, na kutumia gharama nyingi humo, "mnastaajabu" na kujutia sana yaliyokusibuni, kwa hivyo hilo likaondoa furaha yenu,
mkawa mnasema: "Hakika sisi tumegharimika" kwa balaa hii iliyotupata ikatuangamiza. Kisha baada ya hayo ndiyo mtajua mlikotoka wapi,
na kwa sababu gani mliteswa? Basi mkasema: "Bali sisi tumenyimwa!" Basi msifuni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwa aliwapandia hayo, kisha akayahifadhi na kuyakamilisha kwa ajili yenu, na wala hakuyatumia balaa ambayo kwayo mngenyimwa manufaa na heri yake.
{أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ (68) أَأَنْتُمْ أَنْزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنْزِلُونَ (69) لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ (70)}
68. Je, mnayaona maji mnayoyanywa? 69. Je, ni nyinyi mnaoyateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? 70. Tungelipenda, tungeliyafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
#
{68 - 70} لما ذكر تعالى نعمته على عباده بالطعام؛ ذَكَرَ نعمته عليهم بالشراب العذب الذي منه يشربون، وأنَّه لولا أنَّ الله يسَّره وسهَّله؛ لما كان لكم إليه سبيلٌ ، وأنَّه الذي أنزله {من المزنِ}: وهو السحابُ والمطرُ الذي يُنْزِلُه الله تعالى، فيكون منه الأنهار الجارية على وجه الأرض وفي بطنها، ويكون منه الغدرانُ المتدفِّقة، ومن نعمته تعالى أن جعله عذباً فراتاً تُسيغُه النفوس، ولو شاء؛ لَجَعَلَهُ ملحاً {أجاجاً}: لا يُنتفع به ، {فلولا تشكرون}: الله تعالى على ما أنعم به عليكم.
{68 - 70} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja neema zake juu ya waja wake kwa chakula, akataja neema yake juu yao kwa kinywaji kitamu watakachokunywa, na kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu hakufanya hayo kuwa mepesi kwao, basi hamngeweza kupata njia ya kuyafikia, na kwamba Yeye ndiye aliyeyateremsha "kutoka mawinguni" kisha yakawa mito inayopita juu ya uso wa ardhi na ndani ya ardhi, na pia vidimbwi vinajitokeza kwa hayo. Na katika neema zake Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwamba ameyafanya kuwa matamu yenye ladha, mazuri kunywa, na kama angependa, angeyafanya kuwa ya chumvi "machungu" ambayo hayafaidishi kitu. "Basi kwa nini hamushukuru" Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyokuneemesheni kwayo.
{أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ (71) أَأَنْتُمْ أَنْشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنْشِئُونَ (72) نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِلْمُقْوِينَ (73) فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ (74)}.
71. Je, mnauona moto mnaouwasha? 72. Ni nyinyi mliouumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? 73. Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. 74. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
#
{71 - 73} وهذه نعمةٌ تدخل في الضروريَّات التي لا غنى للخلق عنها؛ فإنَّ الناس محتاجون إليها في كثيرٍ من أمورهم وحوائجهم، فقرَّرهم تعالى بالنار التي أوجدها في الأشجار، وأنَّ الخلق لا يقدرون أن ينشئوا شجرها، وإنَّما الله تعالى قد أنشأها من الشجر الأخضر؛ فإذا هي نارٌ توقد بقدر حاجة العباد؛ فإذا فرغوا من حاجتهم؛ أطفؤوها وأخمدوها. {نحن جَعَلْناها تذكرةً}: للعباد بنعمة ربِّهم، وتذكرةً بنار جهنَّم التي أعدَّها الله للعاصين، وجعلها سوطاً يسوقُ به عبادَه إلى دار النعيم، {ومتاعاً للمُقْوينِ}؛ أي المنتفعين أو المسافرين، وخصَّ الله المسافرين؛ لأنَّ نفع المسافر بها أعظم من غيره، ولعلَّ السبب في ذلك لأنَّ الدُّنيا كلَّها دارُ سفرٍ، والعبدُ من حين ولد فهو مسافرٌ إلى ربِّه؛ فهذه النار جعلها الله متاعاً للمسافرين في هذه الدار وتذكرةً لهم بدار القرار.
{71 - 73} Hii ni neema ambayo inaingia katika mahitaji ambayo ni ya lazima kwa viumbe, ambayo haviwezi kuishi bila hiyo. Kwani watu wanayahitaji katika mambo yao na mahitaji yao mengi. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafanya kukiri suala la moto aliouumba katika miti, na kwamba viumbe havina uwezo wa kuotesha miti yake, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliuumba moto huo kutoka kwa miti ya kijani kibichi, kisha ukawa moto unaowashwa kulingana na mahitaji ya waja. Wakimaliza haja zao, wanauzima. "Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho" kwa waja wa neema za Mola wao Mlezi, na ukumbusho wa Moto wa Jahannamu ambao Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri, na akaufanya kuwa ni mjeledi wa kuwapeleka kwa huo waja wake kwenda kwenye nyumba ya neema. "Na manufaa kwa walioko nyikani." Na Mwenyezi Mungu aliwataja hao kwa njia hii mahususi kwa sababu kufaidika ambako msafiri anafaidika nao ni kukubwa zaidi kuliko wengineo, na pengine sababu ya hilo ni kwamba dunia nzima ni nyumba ya kusafiria, na mja tangu kuzaliwa kwake ni msafiri kwenda kwa Mola wake Mlezi. Basi moto huu Mwenyezi Mungu aliufanya kuwa ni starehe kwa wasafiri katika nyumba hii na ukumbusho kwao wa nyumba ya kutulia milele.
#
{74} فلما بيَّن من نعمه ما يوجب الثناء عليه من عباده وشكره وعبادته؛ أمر بتسبيحه وتعظيمه ، فقال: {فسبِّحْ باسم ربِّك العظيم}؛ أي: نزِّهْ ربَّك العظيم كامل الأسماء والصفات، كثير الإحسان والخيرات، واحْمَدْه بقلبك ولسانك وجوارِحكَ؛ لأنَّه أهلٌ لذلك، وهو المستحقُّ لأن يُشْكَرَ فلا يُكْفَرَ ويُذْكَرَ فلا ينسى ويُطاعَ فلا يُعْصَى.
{74} Alipobainisha katika neema zake kile kilichohitaji asifiwe na ashukuriwe na aabudiwe na waja wake, akaamrisha atakaswe na atukuzwe,
akasema: "Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu" ambaye ni Mwenye majina na sifa kamilifu, mwingi wa ihsani na heri, na msifu kwa moyo wako, ulimi wako na viungo vyako. Kwa sababu Yeye ndiye anayestahiki hilo. Kwani anastahiki kushukuriwa wala asikufuriwe, na akumbukwe wala asisahauliwe, na atiiwe wala asiasiwe.
{فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ (75) وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ (76) إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ (77) فِي كِتَابٍ مَكْنُونٍ (78) لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ (79) تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ (80) أَفَبِهَذَا الْحَدِيثِ أَنْتُمْ مُدْهِنُونَ (81) وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ (82) فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ (83) وَأَنْتُمْ حِينَئِذٍ تَنْظُرُونَ (84) وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْكُمْ وَلَكِنْ لَا تُبْصِرُونَ (85) فَلَوْلَا إِنْ كُنْتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ (86) تَرْجِعُونَهَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ (87)}.
75. Basi ninaapa kwa maanguko ya nyota. 76. Na hakika bila ya shaka hiki ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua! 77. Hakika hii bila ya shaka ni Qur-ani Tukufu. 78. Katika Kitabu kilichohifadhiwa. 79. Hapana akigusaye ila waliotakaswa. 80. Ni uteremsho unaotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 81. Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? 82. Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? 83. Yawaje basi itakapofika roho kwenye koo. 84. Na nyinyi wakati huo mnatazama! 85. Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi, lakini hamuoni. 86. Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu. 87. Kwa nini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
#
{75 - 76} أقسم تعالى بالنُّجوم ومواقعها، أي: مساقطها في مغاربها وما يُحْدِثُ الله في تلك الأوقات من الحوادث الدالَّة على عظمته وكبريائه وتوحيده، ثم عظَّم هذا المقسم به، فقال: {وإنَّه لقسمٌ لو تعلمون عظيمٌ}، وإنَّما كان القسم عظيماً؛ لأنَّ في النجوم وجريانها وسقوطها عند مغاربها آياتٍ وعبراً لا يمكن حصرها.
{75 - 76} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliapa kwa nyota na maangukio yake, katika magharibi yake, na matukio ambayo Mwenyezi Mungu huyaleta katika nyakati hizo ambayo yanaashiria ukuu wake, ukubwa wake, na upweke wake. Kisha akakitukuza hicho kinachoapiwa,
akasema: "Na hakika bila ya shaka hiki ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua!" Na kiapo hicho kilikuwa kikubwa kwa sababu katika nyota, kuzunguka kwake na kuanguka kwake katika magharibi yake zimo ishara na mafunzo yasiyoweza kuhesabika yakadhibitiwa.
#
{77} وأمَّا المقسَمُ عليه؛ فهو إثبات القرآن، وأنَّه حقٌّ لا ريب فيه ولا شكَّ يعتريه، وأنَّه {كريمٌ}؛ أي: كثير الخير غزير العلم، فكلُّ خيرٍ وعلم؛ فإنَّما يُستفادُ من كتاب الله ويُسْتَنْبَطُ منه.
{77} Ama kile kilichoapiwa ambacho ni kuthibitisha Qur-ani, na kwamba ni haki isiyo na shaka wala kusitasita, na kwamba ni "Tukufu." Yaani, ni yenye heri nyingi na elimu tele. Kwa maana kila heri na elimu inapatikana na kutolewa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
#
{78} {في كتابٍ مكنونٍ}؛ أي: مستورٍ عن أعين الخلق، وهذا الكتاب المكنون هو اللوحُ المحفوظُ؛ أي: أنَّ هذا القرآن مكتوبٌ في اللوح المحفوظ، معظَّم عند الله وعند ملائكته في الملأ الأعلى.
ويُحتمل أنَّ المراد بالكتاب المكنون هو الكتاب الذي بأيدي الملائكة الذين يُنْزِلُهُمُ الله لوحيه ورسالته ، وأنَّ المرادَ بذلك أنَّه مستورٌ عن الشياطين، لا قدرةَ لهم على تغييره ولا الزيادة والنقص منه واستراقه.
{78} "Katika Kitabu kilichohifadhiwa." Yaani, kilichosiriwa mbali na macho ya viumbe, nacho ni Ubao uliohifadhiwa. Yaani, Qur-ani hii imeandikwa katika Ubao uliohifadhiwa, unaoheshimiwa sana kwa Mwenyezi Mungu na Malaika wake katika viumbe watukufu wa juu kabisa. Na inawezekana kwamba kinachomaanishwa na kitabu kilichohifadhiwa ni kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika ambao Mwenyezi Mungu huwateremshia wahyi na ujumbe wake, na kwamba kinachokusudiwa hapo ni kwamba kimefichika mbali na mashetani, na hawana uwezo wa kukibadilisha, kukiongezea, kukipunguzia chochote na kukisikiliza kwa siri.
#
{79} {لا يَمَسُّهُ إلاَّ المُطَهَّرونَ}؛ أي: لا يَمَسُّ القرآن إلاَّ الملائكةُ الكرام، الذينَ طهَّرهم الله تعالى من الآفات والذنوب والعيوب، وإذا كان لا يمسُّه إلاَّ المطهَّرون، وأنَّ أهل الخبث والشياطين لا استطاعة لهم ولا يدان إلى مسِّه؛ دلَّت الآية تنبيهاً على أنَّه لا يجوز أن يَمَسَّ القرآن إلاَّ طاهرٌ [كما ورد بذلك الحديثُ، ولهذا قيل: إنّ الآية خبرٌ بمعنى النهي؛ أي: لا يمسَّ القرآن إلاَّ طاهر].
{79} "Hapana akigusaye ila waliotakaswa." Yaani, Malaika watukufu, ambao Mwenyezi Mungu Amewatakasa kutokana na uchafu, dhambi na kasoro na kama hakiguswi isipokuwa na waliosafishwa, na kwamba wale wenye uchafu na mashetani hawana uwezo wala hawafailii kukiguza, basi aya hii inaashiria tanabahisho kwamba hairuhusiki kuigusa Qur-ani isipokuwa aliye safi [kama ilivyoelezwa hivyo katika Hadithi za Mtume, na ndiyo maana ikasemwa Aya hii inatoa habari yenye maana ya kukataza. Yaani, asiiguse Qur-ani isipokuwa aliyetakasika.
#
{80} {تنزيلٌ من ربِّ العالمين}؛ أي: إنَّ هذا القرآن الموصوف بتلك الصفات الجليلة هو تنزيلُ ربِّ العالمين، الذي يربِّي عباده بنعمه الدينيَّة والدنيويَّة، وأجلُّ تربيةٍ ربَّى بها عباده إنزالُه هذا القرآن، الذي قد اشتمل على مصالح الدَّارين، ورحم الله به العباد رحمةً لا يقدرون لها شكوراً، ومما يجب عليهم أن يقوموا به، ويعلنوه، ويدعوا إليه، ويصدعوا به.
{80} "Ni uteremsho unaotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote." Yaani, Qur-ani hii iliyoelezewa kwa sifa hizi tukufu ni uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote, ambaye anawalea waja wake kwa neema zake za kidini na za kidunia, na malezi bora zaidi aliyowalea kwayo waja wake ni kuwateremshia Qur-ani hii, ambayo ilijumuisha masilahi ya nyumba hizi mbili, na kwayo Mwenyezi Mungu akawarehemu waja wake rehema ambayo hawakuweza kuishukuru, na miongoni mwa yale yaliyo wajibu juu yao ni kusimama sawasawa nayo, kuitangaza na kuilingania.
#
{81} ولهذا قال: {أفبهذا الحديث أنتم مُدْهِنونَ}؛ أي: أفبهذا الكتاب العظيم والذِّكْرِ الحكيم {أنتم مُدْهِنون }؛ أي: تختفون وتدلِّسون خوفاً من الخلق وعارهم وألسنتهم! هذا لا ينبغي ولا يَليقُ! إنَّما يليق أن يُداهَنَ بالحديث الذي لا يثقُ صاحبه منه، وأمَّا القرآن الكريم؛ فهو الحقُّ الذي لا يغالِبُ به مغالِبٌ إلاَّ غَلَبَ، ولا يصول به صائلٌ إلاَّ كان العالي على غيره، وهو الذي لا يُداهَنُ به ويُختفى ، بل يُصْدَعُ به ويُعْلَن.
{81} Ndiyo maana akasema: "Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?" Yaani, je, ni kwa Kitabu hiki kitukufu na ukumbusho wenye hekima ndiyo "nyinyi mnayapuuza?" Kwa kukificha, kukifanyia uongo kwa sababu ya kuwaogopa watu, kukutieni kwao kasoro na ndimi zao! Hili halifai wala haliendani nayo! Kinachofailiana na hayo ni kulegeza kamba kuhusiana na hadithi ambayo mwenye hadithi hiyo hana uhakika nayo. Ama Qur-ani tukufu, hiyo ni haki ambayo hakuna mshindi anayeweza kuitumia kuishindana isipokuwa atashinda, na hakuna mwenye kushambulia kwayo isipokuwa atakuwa yeye ndiye mbora kuliko wengineo, nayo ni ile isiyofaa kulegeza kamba yake, na kufichwa, bali ni lazima kuitangaza na kuiweka wazi.
#
{82} وقوله: {وتجعلون رِزْقَكم أنَّكم تكذِّبون}؛ أي: تجعلون مقابلة منَّة الله عليكم بالرزق التكذيبَ والكفرَ لنعمة الله، فتقولون: مُطِرْنا بِنَوْء كذا وكذا! وتضيفون النعمة لغير مُسديها ومُوليها؛ فهلاَّ شكرتُم الله على إحسانه إذْ أنزله إليكم ليزيدَكم من فضله؛ فإنَّ التكذيب والكفر داعٍ لرفع النِّعم وحلول النِّقم.
{82} Na kauli yake: "Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?" Yaani, nyinyi mnazikabili neema za Mwenyezi Mungu juu yenu za kuwapa riziki, kwa kuzikadhibisha na kukufuru neema zake,
mkawa mnasema: Tumenyeshewa mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani! Na mnazifungamanisha neema kwa yule ambaye siye aliyewapa na kuwafikishia hizo. Kwa hivyo, kwa nini hamkumshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake alipokuteremshieni ili akuzidishieni katika fadhila zake. Kwani kukadhibisha na kukufuru ni visababu vya kuondolewa neema na kufikiwa na adhabu.
#
{83 - 85} {فلولا إذا بلغتِ الحلقوم. وأنتُم حينئذٍ تنظرونَ. ونحنُ أقربُ إليه منكُم ولكن لا تُبْصِرونَ}؛ أي: فهلاَّ إذا بلغت الروحُ الحلقومَ، وأنتم تنظُرون المحتضر في هذه الحالة، والحال أنَّا نحن أقربُ إليه منكم بعلمنا وملائكتنا، ولكن لا تبصرون.
{83 - 85} "Yawaje basi itakapofika roho kwenye koo. Na nyinyi wakati huo mnatazama! Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi" kwa elimu yetu na Malaika wetu, "lakini hamuoni."
#
{86 - 87} {فلولا إن كنتُم غير مَدينينَ}؛ أي: فهلاَّ إذ كنتُم تزعمون أنكم غير مبعوثين ولا محاسبين ومجازين، ترجعون الروح إلى بدنها {إن كنتُم صادقين}: وأنتم تقرُّون أنكم عاجزون عن ردِّها إلى موضعها؛ فحينئذٍ إمَّا أن تقرُّوا بالحقِّ الذي جاء به محمدٌ - صلى الله عليه وسلم -، وإمَّا أن تعانِدوا فتعلم حالكم وسوء مآلكم.
{86 - 87} "Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu" na kwamba mnadai kuwa hamtafufuliwa, wala hamtaulizwa juu ya matendo yenu na kulipwa kwayo, basi irejesheni roho ya anayekuwa katika kiwiliwili chake "ikiwa nyinyi mnasema kweli?" Lakini mnakiri kwamba hamwezi kuirudisha mahali pake. Basi hapo, ima mkiri haki aliyokuja nayo Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - au mumukaidi, kwa hivyo ijulikane vyema hali yenu na hatima yenu mbaya.
{فَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ (88) فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ (89) وَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ (90) فَسَلَامٌ لَكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ (91) وَأَمَّا إِنْ كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ (92) فَنُزُلٌ مِنْ حَمِيمٍ (93) وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ (94) إِنَّ هَذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ (95) فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ (96)}
88. Kwa hivyo, akiwa miongoni mwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu. 89. Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. 90. Na akiwa katika wale wa upande wa kulia. 91. Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa wale wa upande wa kulia. 92. Na ama akiwa katika wale waliokadhibisha, wapotovu. 93. Basi karamu ya makaribisho yake ni maji yanayochemka. 93. Na kutiwa Motoni. 94. Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. 96. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
#
{88 - 89} ذكر الله تعالى أحوال الطوائف الثلاث: المقرَّبين، وأصحاب اليمين، والمكذِّبين الضالِّين في أول السورةِ في دارِ القرارِ، ثم ذكر أحوالَهم في آخرها عند الاحتضارِ والموتِ، فقال: {فأمَّا إن كان من المقرَّبين}؛ أي: إن كان الميِّت من المقرَّبين إلى الله، المتقرِّبين إليه بأداء الواجبات والمستحبَّات وترك المحرَّمات والمكروهات وفضول المباحات، {فـ} لهم {روحٌ}؛ أي: راحةٌ وطمأنينةٌ وسرورٌ وبهجةٌ ونعيمُ القلب والروح، {ورَيْحانٌ}: وهو اسم جامعٌ لكل لذَّةٍ بدنيَّةٍ من أنواع المآكل والمشارب وغيرها، وقيل: الريحانُ هو الطيبُ المعروف، فيكون من باب التعبير بنوع الشيء عن جنسه العام، {وجنَّةُ نعيم}: جامعةٌ للأمرين كليهما، فيها ما لا عينٌ رأت ولا أذنٌ سمعت ولا خطر على قلب بشر، فيبشَّر المقرَّبون عند الاحتضار بهذه البشارة، التي تكاد تطير منها الأرواح فرحاً وسروراً ؛ كما قال تعالى: {إنَّ الذين قالوا ربُّنا الله ثم استقَاموا تَتَنَزَّلُ عليهم الملائكةُ أن لا تخافوا ولا تحزنوا وأبْشِروا بالجنَّةِ التي كُنتُمْ توعَدونَ. نحنُ أولياؤكم في الحياةِ الدُّنيا وفي الآخرةِ ولكم فيها ما تَشْتَهي أنفسُكم ولكم فيها ما تدَّعونَ. نُزُلاً من غفورٍ رحيم}، وقد فُسِّرَ قولُه [تبارك و] تعالى: {لهم البُشرى في الحياة الدُّنيا وفي الآخرة}: أنَّ هذه البشارة المذكورة هي البُشرى في الحياة الدنيا.
{88 - 89} Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaja hali za makundi haya matatu: walio karibu na Mwenyezi Mungu, wale wa mkono wa kulia, na wale wanaokadhibisha, wapotofu, pale mwanzoni mwa sura hii watakapokuwa katika nyumba ya kukaa milele, kisha akataja hali zao mwishoni mwake wakati wa kufa kwao,
akasema: "Kwa hivyo, akiwa miongoni mwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu." Anayejiweka karibu naye kwa kutekeleza faradhi na mambo yasiyo ya faradhi, na kuacha maharamisho na mambo yanayochukiza na mambo madogo madogo yanayoruhusiwa, "Basi" kwao itakuwa "ni raha" utulivu, furaha na bashasha za moyo na roho "na manukato." Pia ilisemekana kwamba maana ya 'rayhan' hapa ni jina linalojumuisha kila aina ya starehe za kimwili kwa aina zote za vyakula, vinywaji na mengineyo. Na pia ilisemekana kwamba 'rayhan' ni manukato yale yale yanayojulikana, na hii inakuwa ni katika mbinu za kutumia kitu fulani kuwakilisha aina zake zote, "na Bustani zenye neema" ambazo ndani yake yamo yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia na wala hayajawahi kupitia katika moyo wa mwanadamu yeyeote. Basi wale walio karibu na Mwenyezi Mungu hupewa habari njema wakati wa kifo, ambazo kwa sababu yake roho zinakaribia mno kuruka nje kwa furaha na bashasha.
Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika wale waliosema: 'Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu!' Kisha wakanyooka sawa,
hao huwateremkia Malaika wakawaambia: 'Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa bustani ya mbinguni mliyokuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka. Ni karamu ya kuwakaribisha itokayo kwa Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu zaidi." Na kauli yake
[Mwenye baraka tele] aliyetukuka: "Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera" ilifasiriwa kwamba bishara hii iliyotajwa ndiyo bishara watakayopewa katika maisha ya dunia hii.
#
{90 - 91} وقوله: {وأمَّا إن كان من أصحابِ اليمين}؛ وهم الذين أدَّوا الواجبات وتركوا المحرَّمات، وإن حَصَلَ منهم بعضُ التقصير في بعض الحقوق التي لا تُخِلُّ بإيمانهم وتوحيدهم، فيقالُ لأحدهم: {سلامٌ لك من أصحابِ اليمين}؛ أي: سلامٌ حاصلٌ لك من إخوانك أصحاب اليمين؛ أي: يسلِّمون عليه، ويحيُّونه عند وصوله إليهم ولقائهم له، أو يقال له: سلامٌ لك من الآفات والبليَّات والعذاب؛ لأنَّك من أصحاب اليمين، الذين سَلِموا من الموبقات.
{90 - 91} Na kauli yake: "Na akiwa katika wale wa upande wa kulia." Hao ndio wale waliotekeleza wajibu na wakaacha yale yaliyoharamishwa, hata kama watafanya upungufu fulani katika baadhi ya haki ambazo hazipunguzi imani yao na kumpwekesha kwao Mwenyezi Mungu,
basi mmoja wao ataambiwa: "Salamu kwako uliye miongoni mwa wale wa upande wa kulia" kutoka kwa ndugu zako wa kuliani. Yaani, watamsalimu na kumuamkuwa atapowafikia na kukutana naye,
au ataambiwa: Na usalimike kutokana na mapungufu, misiba na adhabu. Kwa sababu wewe ni miongoni mwa wana kuliani, ambao wamesalimika kutokana na misiba ya kuangamiza.
#
{92 - 94} {وأمَّا إن كان من المكذِّبين الضَّالِّين} أي: الذين كذَّبوا بالحقِّ وضلُّوا عن الهدى، {فنُزُلٌ من حميمٍ. وتصليةُ جَحيم}؛ أي: ضيافتهم يومَ قدومهم على ربِّهم تصليةُ الجحيم التي تحيط بهم وتصِلُ إلى أفئدتهم، وإذا استغاثوا من شدَّة العطش والظمأ؛ {يغاثوا بماءٍ كالمهل يَشْوي الوجوهَ بئس الشرابُ وساءتْ مُرْتَفَقاً}.
{92 - 94} "Na ama akiwa katika wale waliokadhibisha, wapotovu," waliokanusha haki na wakapotea mbali na uwongofu, "basi karamu ya makaribisho yake ni maji yanayochemka. Na kutiwa Motoni." Nao utawazunguka na kuzifikia nyoyo zao. Na wanapotafuta msaada kutokana na kiu chao kikali, "watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyotibuka. Yatakayowabambua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!"
#
{95} {إنَّ هذا}: الذي ذكره الله تعالى من جزاء العباد بأعمالهم خيرها وشرِّها وتفاصيل ذلك {لَهُوَ حقُّ اليقينِ}؛ أي: الذي لا شكَّ فيه ولا مريةَ، بل هو الحقُّ الثابتُ الذي لا بدَّ من وقوعه، وقد أشهد اللهُ عبادَه الأدلَّة القواطع على ذلك، حتى صار عند أولي الألباب كأنَّهم ذائقون له مشاهدونَ لحقيقتِهِ ، فحمدوا الله تعالى على ما خصَّهم من هذه النعمة العظيمة والمنحة الجسيمة.
{95} "Hakika haya" aliyoyataja Mwenyezi Mungu kuhusu malipo ya waja wake kwa matendo yao mema na maovu, na maelezo yake ya kina "ndiyo haki yenye yakini" ambayo haina shaka wala kusitasita. Bali ndiyo haki iliyothibitika ambayo lazima itatokea. Na Mwenyezi Mungu aliwapa waja wake ushahidi mbalimbali wa uhakika juu ya hilo, kiasi kwamba likawa kwa wale wenye akili ni kana wanalionja na kuuona uhalisia wake. Basi sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyowapa wao tu katika neema hizi kuu na ukarimu mkubwa.
#
{96} ولهذا قال تعالى: {فسبِّحْ باسم ربِّك العظيم}؛ فسبحان ربِّنا العظيم، وتعالى وتنزَّه عما يقول الظالمون والجاحدون علوًّا كبيراً، والحمدُ لله ربِّ العالمين حمداً كثيراً طيباً مباركاً فيه.
{96} Ndiyo maana akasema Mwenyezi Mungu: "Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu." Basi ametakasika Mola wetu Mkuu, Mtukufu, na ako mbali mno na juu zaidi ya yale wanayoyasema madhalimu wanaokataa. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote, sifa njema nyingi, nzuri zenye baraka.
Imekamilika tafsiri ya Surat Al-Waqi ́ah.
******