:
Tafsiri ya Surat Ar-Rahman
Tafsiri ya Surat Ar-Rahman
Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
: 1 - 13 #
{الرَّحْمَنُ (1) عَلَّمَ الْقُرْآنَ (2) خَلَقَ الْإِنْسَانَ (3) عَلَّمَهُ الْبَيَانَ (4) الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ (5) وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ (6) وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ (7) أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ (8) وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ (9) وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ (10) فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ (11) وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ (12) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (13)}.
1. Arrah'man (Mwingi wa Rehema). 2. Amefundisha Qur-ani. 3. Amemuumba mwanadamu. 4. Akamfundisha kubaini. 5. Jua na mwezi huenda kwa hesabu. 6. Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea. 7. Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani. 8. Ili msidhulumu katika mizani. 9. Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani. 10. Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. 11. Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. 12. Na nafaka zenye makapi, na rehani. 13. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha.
#
{1} هذه السورة الكريمة الجليلةُ افتتحها باسمه الرحمن، الدالِّ على سعة رحمته وعموم إحسانه وجزيل برِّه وواسع فضله، ثم ذَكَرَ ما يدلُّ على رحمته وأثرها الذي أوصله الله إلى عباده من النعم الدينيَّة والدنيويَّة والأخرويَّة، وبعد كل جنس ونوع من نعمه ينبِّه الثقلين لشكره ويقول: {فبأيِّ آلاء ربِّكما تكذِّبان}.
{1} Sura hii tukufu na yenye kuheshimika ilifunguliwa kwa jina lake, Mwingi wa rehema, ambalo linaashiria upana wa rehema yake, ujumla wa hisani yake, wingi wa wema wake, na ukunjufu wa fadhila zake. Kisha akataja kile kinachoashiria rehema yake na athari zake ambazo Mwenyezi Mungu alizifikisha kwa waja wake kama vile neema za kidini, za kidunia na za kiakhera, na baada ya kutaja kila aina na sampuli ya neema zake, akawa anawatanabahisha viumbe viwili vikubwa (majini na wanadamu) kumshukuru na anasema: "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
#
{2} فذكر أنه: {علم القرآن}؛ أي: علَّم عباده ألفاظه ومعانيه ويسَّرها على عباده، وهذا أعظم منَّة ورحمة رحم بها العباد، حيث أنزل عليهم قرآناً عربياً بأحسن الألفاظ وأوضح المعاني ، مشتملٌ على كلِّ خير، زاجرٌ عن كلِّ شرٍّ.
{2} Basi akataja kuwa: "Alifundisha Qur-ani." Yaani, aliwafundisha waja wake maneno yake na maana zake na akaifanya kuwa nyepesi kwa waja wake, na hii ndiyo neema kubwa zaidi na rehema aliyowaneemesha kwayo waja wake. Kwani aliwateremshia Qur-ani ya Kiarabu kwa maneno bora zaidi na maana zilizo wazi zaidi, yenye kujumuisha heri zote, na kukataza maovu yote.
#
{3 - 4} {خلق الإنسان}: في أحسن تقويم، كامل الأعضاء، مستوفَى الأجزاء، محكم البناء، قد أتقن البارئ تعالى البديع خلقه أيَّ إتقان، وميَّزه على سائر الحيوانات بأن {علَّمه البيانَ}؛ أي: التبيين عمَّا في ضميره. وهذا شاملٌ للتعليم النُّطقيِّ والتعليم الخطِّيِّ؛ فالبيان الذي ميَّز الله به الآدميَّ على غيره من أجلِّ نعمه وأكبرها عليه.
{3 - 4} "Amemuumba mwanadamu" kwa umbo bora zaidi, na viungo kamili, sehemu zilizo sawasawa, na mwenye mjengo mzuri zaidi. Muumba Mtukufu mwenye ustadi wa kuumba alimumba kwa ukamilifu mkubwa, na akamtofautisha na wanyama wengine wote kwa "kumfundisha kubaini" yale yaliyo katika dhamiri yake. Hili linajumuisha kufunzwa kuandika. Kwa maana kubainisha ambako Mwenyezi Mungu alimtofautisha mwanadamu na wengineo wote ni katika neema kubwa zaidi na kubwa yake zaidi juu yake.
#
{5} {الشمسُ والقمرُ بحُسْبانٍ}؛ أي: خلق الله الشمس والقمر وسخَّرهما يجريان بحساب مقنَّن وتقدير مقدَّر رحمةً بالعباد وعنايةً بهم، وليقوم بذلك من مصالحهم ما يقوم، وليعرفوا عدد السنين والحساب.
{5} "Jua na mwezi huenda kwa hesabu." Yaani, Mwenyezi Mungu aliumba jua na mwezi na akavitiisha ili viende kwa hesabu iliyoratibiwa sawasawa na kipimo kilichopimwa sawasawa, kwa sababu ya kuwarehemu waja wake na kuwatunza, na ili awatimizie masilahi yao mbalimbali, na ili waweze kujua idadi ya miaka na hesabu.
#
{6} {والنجم والشجر يسجُدان}؛ أي: نجوم السماء وأشجار الأرض تعرِفُ ربَّها وتسجُد له وتطيع وتخضع وتنقاد لما سخَّرها له من مصالح عباده ومنافعهم.
{6} "Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea." Wanazuoni walisema kwamba maana yake pia inaweza kuwa nyota za mbingu na miti ya ardhini inamjua Mola wao Mlezi, inamsujudia, inamtii, inanyenyekea, na inatekeleza yale iliyotiishwa kufanya yenye masilahi na manufaa kwa waja wake.
#
{7 - 8} {والسماء رفعها}: سقفاً للمخلوقات الأرضيَّة، {ووضع} [اللَّه] {الميزان}؛ أي: العدل بين العبادِ في الأقوال والأفعال، وليس المراد به الميزان المعروف وحده، بل هو كما ذكرنا؛ يدخل فيه الميزان المعروف والمكيال الذي تُكال به الأشياء والمقادير والمساحات التي تُضْبَط بها المجهولات والحقائق التي يُفْصَل بها بين المخلوقات ويُقام بها العدل بينهم، ولهذا قال: {ألاَّ تَطْغَوْا في الميزان}؛ أي: أنزل الله الميزان لئلاَّ تتجاوزوا الحدَّ في الميزان؛ فإنَّ الأمر لو كان يرجع إلى عقولكم وآرائكم؛ لحصل من الخلل ما الله به عليم، ولفسدت السماواتُ والأرض ومن فيهنَّ.
{7 - 8} "Na mbingu ameziinua" ili ziwe paa la viumbe vya ardhini "na [Mwenyezi Mungu] ameweka mizani." Yaani, uadilifu baina ya waja katika kauli na vitendo, na maana yake si mizani inayojulikana peke yake, bali ni kama tulivyotaja. Inajumuisha mizani inayojulikana, kipimo cha ujazo kinachotumiwa kupimia vitu, vipimo vya urefu, umbali na ukubwa ambavyo vinatumika kujua vitu visivyojulikana kipimo chake, na mambo ya uhakika ambayo yanatumiwa kutenganisha kati ya viumbe na kufikia uadilifu kupitia hivyo, na ndiyo maana akasema: "Ili msidhulumu katika mizani." Kwani ikiwa jambo hilo mungeachiwa kutumia akili zenu na maoni yenu tu, basi zingetokea dosari mingi ambayo Mwenyezi Mungu tu ndiye anayezijua vyema, na mbingu na ardhi na kila kilichomo ndani yake vingeharibika.
#
{9} {وأقيموا الوزنَ بالقسطِ}؛ أي: اجعلوه قائماً بالعدل، الذي تصل إليه مقدرتكم وإمكانكم، {ولا تُخْسِروا الميزانَ}؛ أي: لا تنقصوه وتعملوا بضدِّه، وهو الجور والظلم والطغيان.
{9} "Na wekeni mizani kwa haki" kama muwezavyo, "wala msipunje katika mizani."
#
{10} {والأرضَ وضعها}: الله على ما كانت عليه من الكثافة والاستقرار واختلاف أوصافها وأحوالها {للأنام}؛ أي: للخلق؛ لكي يستقرُّوا عليها، وتكون لهم مهاداً وفراشاً، يبنون بها ويحرُثون ويغرِسون ويحفرون، ويسلكون سُبُلَها فجاجاً، وينتفعون بمعادنها، وجميع ما فيها مما تدعو إليه حاجتهم بل ضرورتهم.
{10} "Na ardhi ameiweka" Mwenyezi Mungu pamoja na ukubwa wake, na uthabiti wake, na tofauti zilizoko katika maelezo yake na hali zake "kwa ajili ya viumbe." Ili watulie juu yake, na ili iwe ni tandiko ambalo wataweza kujenga juu yake, kulima, kupanda mimea, kuichimba, kusafiri katika njia zake mbalimbali, na kufaidika kutokana na madini yake, na kila kitu kilichomo ndani yake ambacho wanakihitaji sana.
Kisha akataja riziki za lazima zilizo ndani yake, akasema:
#
{11} {فيها فاكهةٌ}: وهي جميع الأشجار التي تثمر الثمراتِ التي يتفكَّه بها العبادُ من العنب والتين والرمان والتُّفاح وغير ذلك، {والنَّخْلُ ذاتُ الأكمام}؛ أي: ذات الوعاء الذي ينفلق عن القِنْوان التي تَخْرُجُ شيئاً فشيئاً حتى تتمَّ فتكون قوتاً يدَّخر ويؤكل ويتزوَّد منه المقيم والمسافر وفاكهةً لذيذةً من أحسن الفواكه.
{11} "Humo yamo matunda" na miti yote yenye kuzaa matunda, ambayo waja huyala kama vile zabibu, tini, komamanga, tufaha na vitu mengineyo. "Na mitende yenye mafumba" ambayo yanapasuka kutoka katika mashada yanayochipuka kidogo kidogo mpaka yakamilike na yawe chakula kikuu kinachohifadhiwa na kuliwa na aliyeko nyumbani na msafiri, na pia matunda matamu zaidi miongoni mwa matunda.
#
{12} {والحبُّ ذو العصفِ}؛ أي: ذو الساق الذي يُداس فينتفع بتبنه للأنعام وغيرها، ويدخل في ذلك حبُّ البُرِّ والشعير والذُّرة والأرز والدخن وغير ذلك، {والريحانُ}: يُحتمل أنَّ المراد به جميع الأرزاق التي يأكلها الآدميُّون، فيكون هذا من باب عطف العامِّ على الخاصِّ، ويكون الله [تعالى] قد امتنَّ على عباده بالقوت والرزق عموماً وخصوصاً. ويُحتمل أنَّ المراد بالريحان الريحان المعروف، وأنَّ الله امتنَّ على عباده بما يسَّره في الأرض من أنواع الروائح الطيبة والمشامِّ الفاخرة التي تسرُّ الأرواح وتنشرح لها النفوس.
{12} "Na nafaka zenye makapi." Hili linajumuisha ngano, shayiri, mahindi, mchele, mtama na vitu vinginevyo, "na rehani." Inawezekana kwamba maana yake ni riziki zote wanazokula wanadamu, kwa hivyo hii inakuwa ni katika mbinu ya kuunganisha cha jumla juu ya kilicho mahususi. Na anakuwa Mwenyezi Mungu [Mtukufu] amewaneemesha waja wake kwa chakula kikuu na riziki kwa ujumla na kwa njia mahususi. Na pia inawezekana kwamba kinachomaanishwa hapa na rehani ni ule mti wa rehani unaojulikana, na kwamba Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja kwa yale aliyowapa ya aina mbalimbali za harufu nzuri ambazo zinazifurahisha roho na nafsi zinakunjuka kwa sababu yake.
#
{13} ولما ذَكَرَ جملةً كثيرةً من نعمه التي تشاهد بالأبصار والبصائر، وكان الخطابُ للثَّقلين الجن والإنس؛ قررهم تعالى بنعمه، فقال: {فبأيِّ آلاءِ ربِّكما تكذِّبانِ}؛ أي: فبأيِّ نعم الله الدينيَّة والدنيويَّة تكذِّبان؟ وما أحسن جواب الجن حين تلا عليهم النبيُّ - صلى الله عليه وسلم - هذه السورة؛ فكلَّما مرَّ بقوله: {فبأيِّ آلاءِ ربِّكما تكذِّبان}؛ قالوا: ولا بشيءٍ من آلائك ربنا نكذِّبُ؛ فلك الحمد. فهكذا ينبغي للعبد إذا تليت عليه نعم الله وآلاؤه أن يُقِرَّ بها ويشكر ويحمد الله عليها.
{13} Na alipotaja jumla ya neema zake nyingi zinazoonekana kwa macho na ufahamu, na ikawa kwamba maneno haya wanaambiwa viumbe viwili vikubwa: majini na watu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akawafanya kukiri neema zake, akasema: "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?" Yaani, ni neema gani za Mwenyezi Mungu za kidini na za kidunia mnazozikanusha? Na ni nzuri namna gani jibu la majini wakati Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – alipowasomea sura hii. Kila aliposema kauli yake: “Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnazozikanusha?" Wanasema: 'Hatukanushi hata chochote katika neema za Mola wetu Mlezi. Basi sifa njea zote ni zako.' Basi hivi ndivyo anavyofaa mja anaposomewa neema na baraka za Mwenyezi Mungu kwamba azikiri, amshukuru na amsifu Mwenyezi Mungu juu yake.
Kisha Mwenyezi Mungu akasema:
: 14 - 16 #
{خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ (14) وَخَلَقَ الْجَانَّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ (15) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (16)}.
14. Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo. 15. Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. 16. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha
#
{14} وهذا من نعمه تعالى على عباده؛ حيث أراهم من آثارِ قدرتِهِ وبديع صنعته أنْ {خَلَقَ} أبا {الإنسان}، وهو آدم عليه السلام، {من صلصالٍ كالفخَّارِ}؛ أي: من طينٍ مبلول، قد أحكم بلَّه وأتقن، حتى جفَّ فصار له صلصلةٌ وصوتٌ يشبه صوت الفخَّار، وهو الطين المشويُّ.
{14} Hii ni katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake. Ambapo aliwaonyesha katika athari za uwezo wake na kazi ya ajabu kwamba yeye "aliumba" baba "watu," ambaye ni Adam, amani iwe juu yake, "kwa udongo wa kinamo."
#
{15} {وخلق الجانَّ}؛ أي: أبا الجنِّ، وهو إبليس لعنه الله {من مارج من نارٍ}؛ أي: من لهب النار الصافي، أو الذي قد خالطه الدخان. وهذا يدلُّ على شرف عنصر الآدميِّ المخلوق من الطين والتراب، الذي هو محل الرزانة والثقل والمنافع؛ بخلاف عنصر الجانِّ، وهو النار، التي هي محلُّ الخفَّة والطيش والشرِّ والفساد.
{15} "Na akawaumba majini." Yaani, baba wa majini, naye ni Ibilisi, Mwenyezi Mungu amlaani "kwa ulimi wa moto." Yaani, kutoka kwa mwale wa moto safi, au ule uliochanganyika na moshi. Hili linaonyesha heshima ya aliyo nayo binadamu, ambaye aliumbwa kutokana na udongo, ambao ndio mahali pa utulivu, uzito na manufaa. Tofauti na majini ambao waliumbwa kwa moto, ambao ni mahali pa wepesi, kupitiliza mipaka, uovu na uharibifu.
#
{16} ولما بيَّن خَلْقَ الثَّقَلَين ومادة ذلك ، وكان ذلك مِنَّةً منه تعالى عليهم ؛ قال: {فبأيِّ آلاءِ ربِّكما تكذِّبانِ}؟!
{16} Na alipobainisha kuumbwa kwa vitu viwili vizito hivi na kiini chake, na hiyo ikawa ni neema aliyowapa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
: 17 - 18 #
{رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ (17) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (18)}.
17. Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili. 18. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{17 - 18} أي: هو تعالى ربُّ كلِّ ما أشرقت عليه الشمس والقمر والكواكب النيِّرة، وكلِّ ما غربت عليه، وكلِّ ما كانا فيه؛ فالجميع تحت تدبيره وربوبيته، وثنَّاهما هنا باعتبار مشارقها شتاءً وصيفاً. والله أعلم.
{17 - 18} Yaani, Yeye Mtukufu ndiye Mola Mlezi wa vyote ambavyo jua linavichomozea na mwezi na nyota kubwa kubwa angavu, na vyote ambavyo hivi vinakuchwa juu yake, na vyote vilivyomo. Kila vyote viko chini ya udhibiti wake na umola wake, na amevitaja hapa kwa uwili kwa kuzingatia kuchomozea kwake mashariki katika msimu wa baridi na wa kiangazi.
: 19 - 23 #
{مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ (19) بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَا يَبْغِيَانِ (20) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (21) يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ (22) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (23)}.
19. Anaziendesha bahari mbili zikutane. 20. Baina yake kipo kizuizi, zisiingiliane. 21. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 22. Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. 23. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{19 - 23} المراد بالبحرين: البحر العذب والبحر المالح؛ فهما يلتقيان [كلاهما]، فيصبُّ العذب في البحر المالح ويختلطان ويمتزجان، ولكنَّ الله تعالى جعل بينهما برزخاً من الأرض، حتى لا يبغي أحدهما على الآخر، ويحصُلَ النفع بكلٍّ منهما؛ فالعذب منه يشربون وتشرب أشجارهم وزروعهم وحروثهم، والملح به يطيبُ الهواء ويتولَّد الحوت والسمك واللؤلؤ والمرجان، ويكون مستقرًّا مسخراً للسفن والمراكب، ولهذا قال:
{19 - 23} Kinachomaanishwa na bahari mbili ni bahari ya maji matamu na bahari ya maji ya chumvi. Mbili hizo zinakutana, kisha hiyo ya maji matamu inamimina kwenye bahari ya maji ya chumvi, na yanachanganyika, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka kizuizi kati yake kwenye ardhi, ili moja yake isiingie katika nyingine, na ili yaweze kupatikana manufaa kutoka kwa kila moja yake. Kwani hiyo ya maji matamu watu, miti na mimea hunywa kutoka humo. Nayo hiyo ya maji ya chumvi husafisha hewa, huzalisha nyangumi, samaki, lulu na marijani, na kuzifanya safina na vipando vinginevyo vya majini kuwa imara juu ya maji. Ndiyo maana akasema:
: 24 - 25 #
{وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنْشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ (24) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (25)}.
24. Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyoundwa kama vilima. 25. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{24 - 25} أي: وسخَّر تعالى لعباده السفن الجواري التي تمخرُ البحر وتشقُّه بإذن الله، التي ينشئها الآدميون، فتكون من عِظَمِها وكبرها كالأعلام، وهي الجبال العظيمة، فيركبها الناس، ويحملون عليها أمتعتهم وأنواع تجاراتهم وغير ذلك ممّا تدعو إليه حاجتهم وضرورتهم، وقد حفظها حافظُ السماواتِ والأرض، وهذه من نعم الله الجليلة، ولهذا قال: {فبأيِّ آلاء ربِّكما تكذِّبان}؟!
{24 - 25} Yaani, na Mwenyezi aliwatiishia waja wake merikebu ziendazo baharini huku zikizipasua kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Nazo hutengenezwa na wanadamu, na kwa sababu ya upana na ukubwa wake zinakuwa ni kama vilima vikubwa. Wanaziabiri na wanabebea hapo mizigo yao, aina zao mbalimbali za biashara, na mambo mengineyo ambayo wanayahitaji kwa hali ya kawaida na ya lazima. Na amezihifadhi yule aliyezihifadhi mbingu na ardhi. Na hii ni katika neema kubwa za Mwenyezi Mungu, na ndiyo maana akasema: "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
: 26 - 28 #
{كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ (26) وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ (27) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (28)}.
26. Kila kilichoko juu yake kitatoweka. 27. Na utabakia uso wa Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. 28. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{26 - 28} أي: كلُّ مَن على الأرض من إنسٍ وجنٍّ ودوابٍّ وسائر المخلوقات يفنى [ويموت] ويبيد، ويبقى الحيُّ الذي لا يموت، {ذو الجلال والإكرام}؛ أي: ذو العظمة والكبرياء والمجد، الذي يعظَّم ويبجَّل ويجلُّ لأجله، والإكرام الذي هو سعة الفضل والجود، الذي يكرم أولياءه وخواصَّ خلقه بأنواع الإكرام، الذي يكرِمُه أولياؤه ويجلُّونه ويعظِّمونه ويحبُّونه وينيبون إليه ويعبدونه. {فبأيِّ آلاء ربِّكما تكذِّبانِ}؟!
{26 - 28} Yaani, kila mtu aliyeko katika ardhi, awe binadamu, jini, mnyama, au kiumbe chochote kile, ataangamia [kwa kufa], na kitakachobakia ni yule aliye hai daima ambaye hafi. "Mwenye Utukufu na Ukarimu." Ambaye kwa hayo vipenzi wake wanamheshimu, wanampa taadhima, wanampenda, wanamgeukia, na kumwabudu. "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
: 29 - 30 #
{يَسْأَلُهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ (29) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (30)}.
29. Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. 30. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{29 - 30} أي: هو الغنيُّ بذاته عن جميع مخلوقاته، وهو واسعُ الجود والكرم، فكلُّ الخلق مفتقرون إليه، يسألونه جميع حوائجهم بحالهم ومقالهم، ولا يستغنون عنه طرفةَ عينٍ ولا أقلَّ من ذلك، وهو تعالى {كلَّ يوم هو في شأنٍ}: يغني فقيراً ويجبرُ كسيراً ويعطي قوماً، ويمنع آخرينَ، ويميتُ، ويُحيي، ويخفض، ويرفع ، لا يشغلُه شأنٌ عن شأنٍ، ولا تغلِّطُه المسائل، ولا يبرِمُه إلحاح الملحين، ولا طول مسألةِ السائلين. فسبحان الكريم الوهَّاب، الذي عمَّت مواهبه أهل الأرض والسماواتِ، وعمَّ لطفه جميع الخلق في كلِّ الآنات واللحظات، وتعالى الذي لا يمنعه من الإعطاء معصيةُ العاصين ولا استغناءُ الفقراء الجاهلين به وبكرمِهِ. وهذه الشؤون التي أخبر أنَّه [تعالى] {كلَّ يوم هو في شأنٍ}: هي تقاديره وتدابيره التي قدَّرها في الأزل وقضاها، لا يزال تعالى يمضيها وينفذها في أوقاتها التي اقتضتها حكمته، وهي أحكامُه الدينيَّة التي هي الأمر والنهي، والقدريَّة التي يُجريها على عباده مدَّة مقامهم في هذه الدار، حتى إذا تمَّتْ هذه الخليقة، وأفناهم الله تعالى، وأراد أن ينفِّذَ فيهم أحكام الجزاء ويريهم من عدله وفضله وكثرة إحسانه ما به يعرِفونه ويوحِّدونه؛ نقل المكلَّفين من دار الابتلاء والامتحان إلى دار الحيوان، وفرغ حينئذٍ لتنفيذ هذه الأحكام التي جاء وقتُها، وهو المراد بقولِهِ:
{29 - 30} Yaani, Yeye mwenyewe anajitosheleza na wala hawahitaji viumbe vyake vyote. Naye ni mpana wa kupeana na ukarimu. Kwani viumbe vyote vinamhitaji Yeye, na vinamuomba mahitaji yao yote kwa hali zao na kwa maneno yao, na wala hawawezi kujitosheleza mbali naye kwa kiasi cha kupepesa jicho, wala kidogo zaidi yake, na Yeye Mtukufu: “Kila siku Yeye yumo katika mambo." Anawatosheleza masikini, na kuwafariji walio taabuni, na huwapa watu, na huwanyima wengine, hufisha, huhuisha, hushusha hadhi na hunyanyua, na hakuna jambo moja linalomshungulisha akaacha jambo jingine, na wala masuala mbalimbali hayamchanganyi, wala hakatishwi tamaa na msisitizo wa watu wanaoomba, wala urefu wa kuomba wa wale wanaoomba. Basi ametakasika Yeye mwenye ukarimu, Mpaji, ambaye upaji wake umewaenea wakazi wa ardhi na mbingu, na ambaye upole wake umeenea viumbe vyote katika kila dakika na muda. Na ametukuka Yule ambaye haumzuii kutoa uasi wa muasi wala kujitosheleza kwa masikini wasiomjua yeye na ukarimu wake. Na mambo haya aliyoyasema Yeye [Mwenyezi Mungu]: “Kila siku Yeye yumo katika mambo” ni mipango yake na uendeshaji mambo wake ambao aliupitisha zamani na akapanga hivyo. Yeye Mtukufu anaendelea kuyapitisha na kuyatekeleza katika nyakati zake zinazofaa kulingana na hekima yake. Na hizi ndizo hukumu zake za kidini, ambazo ni maamrisho na makatazo, na pia hukumu zake za mipango yake anazozitekeleza juu ya waja wake kwa muda wa maisha yao katika nyumba hii, mpaka pale uumbaji huu utakapokamilika, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akauangamiza, na akataka kuwatekelezea hukumu zake za malipo na kuwaonyesha uadilifu wake, fadhila zake, na wingi wa ihsani yake, ambazo kwazo watamtambua na kumpwekesha, atawahamisha wale wanaojukumishwa kisheria kutoka kwenye nyumba hii ya mtihani na kuwapeleka kwenye nyumba ya maisha ya milele, kisha akamaliza kutekeleza hukumu hizi ambazo wakati wake utakuwa umefika, nao ndio uliokusudiwa katika kauli yake:
: 31 - 32 #
{سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ (31) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (32)}.
31. Tutakufanyieni hesabuni enyi makundi mawili. 32. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{31 - 32} أي: سَنَفْرُغُ لحسابكم ومجازاتكم بأعمالكم التي عملتموها في دار الدُّنيا.
{31 - 32} Yaani, tutakukalieni kwa ajili ya kuwauliza juu ya matendo yenu ili tuwalipe kwa matendo yenu hayo ambayo mliyafanya katika nyumba ya dunia.
: 33 - 34 #
{يَامَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَنْ تَنْفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانْفُذُوا لَا تَنْفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ (33) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (34)}].
33. Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa mamlaka. 34. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{33 - 34} أي: إذا جمعهم الله في موقف القيامة؛ أخبرهم بعجزهم وضَعْفهم وكمال سلطانِهِ ونفوذ مشيئتِهِ وقدرتِهِ، فقال معجِّزاً لهم: {يا معشر الجنِّ والإنسِ إنِ اسْتَطَعْتُم أن تَنفُذوا من أقطارِ السمواتِ والأرضِ}؛ أي: تجدون مسلكاً ومنفذاً تخرجون به عن ملك الله وسلطانه، {فانفُذوا لا تَنفُذونَ إلاَّ بسلطانٍ}؛ أي: لا تخرجون منه إلاَّ بقوَّةٍ وتسلُّطٍ منكم وكمال قدرةٍ، وأنَّى لهم ذلك وهم لا يملكون لأنفسهم نفعاً ولا ضرًّا ولا موتاً ولا حياةً ولا نشوراً؛ ففي ذلك الموقف لا يتكلَّم أحدٌ إلاَّ بإذنه، ولا تسمعُ إلاَّ همساً، وفي ذلك الموقف يستوي الملوك والمماليك والرؤساء والمرؤوسون والأغنياء والفقراء.
{33 - 34} Yaani, Mwenyezi Mungu atakapowakusanya katika mahali pa Kiyama, atawajulisha juu ya kutoweza kwao na udhaifu wao na ukamilifu wa mamlaka yake na kutekelezeka kwa mapenzi yake na uwezo wake, atasema akiwapa changamoto: "Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi" mkatoka katika ufalme na mamlaka ya Mwenyezi Mungu "basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa mamlaka." Yaani, hamtaweza kutoka humo isipokuwa kwa nguvu na mamlaka makubwa, lakini watawezaje kufanya hivyo na hali wao wenyewe hawawezi kujimilikia manufaa yoyote, wala madhara, wala kifo, wala uhai wala ufufuo? Katika hali hiyo, hakuna atakayezungumza isipokuwa kwa idhini yake, na wala haitasikika isipokuwa mnong'ono tu, na katika mahali hapo watakuwa sawa wafalme na wale waliokuwa wakimilikiwa na wengine, maraisi na wale waliokuwa chini ya uongozi wao, matajiri na maskini.
Kisha akataja yaliyotayarishwa kwa ajili yao siku hiyo, na akasema:
: 35 - 36 #
{يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِنْ نَارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنْتَصِرَانِ (35) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (36)}.
35. Mtatumiwa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda. 36. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{35 - 36} أي: {يرسَل عليكما} لهبٌ صافٍ من النار {ونحاسٌ} وهو اللهب الذي قد خالَطَه الدخانُ. والمعنى: أنَّ هذين الأمرين الفظيعين يرسلانِ عليكما [يا معشر الجن والإنس] ويحيطانِ بكما فلا تنتصران؛ لا بناصرٍ من أنفسكم، ولا بأحدٍ ينصُرُكم من دون الله. ولما كان تخويفُهُ لعباده نعمةً منه عليهم وسوطاً يسوقهم به إلى أعلى المطالب وأشرف المواهب؛ ذكر منَّته بذلك فقال: {فبأيِّ آلاءِ ربِّكما تكذِّبانِ}؟!
{35 - 36} Yaani, "Mtatumiwa" mwali wa moto safi "na shaba." Maana yake ni kwamba haya mambo mawili ya kutisha mno yatatumwa juu yenu [Enyi makundi ya majini na watu] na yatawazingira, kwa hivyo hamtashinda. Hakuna atakayewasaidia miongoni mwenu wenyewe, wala hata yeyote yule kando na Mwenyezi Mungu. Na kwa vile kuwatisha kwake waja wake kulikuwa ni neema kutoka kwake juu yao na mjeledi ambao kwa huo anawaswaga kwenda kwenye matakwa ya juu zaidi na vipawa vya heshima, akataja neema hii aliyowapa, akasema: "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
: 37 - 42 #
[{فَإِذَا انْشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ (37) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (38) فَيَوْمَئِذٍ لَا يُسْأَلُ عَنْ ذَنْبِهِ إِنْسٌ وَلَا جَانٌّ (39) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (40) يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ (41) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (42)}].
37. Itakapopasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta. 38. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 39. Basi Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini. 40. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 41. Watajuulikana wahalifu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. 42. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{37 - 38} {فإذا انشقَّتِ السماءُ}؛ أي: يوم القيامة من الأهوال وكثرة البلبال وترادُف الأوجال، فانخسفتْ شمسُها وقمرُها، وانتثرتْ نجومُها؛ {فكانت}: من شدَّة الخوفِ والانزعاج {وردةً كالدِّهانِ}؛ أي: كانت كالمهل والرصاص المذابِ ونحوه. {فبأيِّ آلاء ربِّكما تكذِّبان}؟!
{37 - 38} "Itakapopasuka mbingu" Siku ya Kiyama kwa sababu ya balaa ya siku hiyo na wingi wa misukosuko yake, na jua na mwezi wake vikapatwa, na nyota zake zitawanyika, "na ikawa" kutokana na ukubwa wa hofu na kusumbukana kwake, "nyekundu kama mafuta" yaliyoyeyushwa. "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
#
{39 - 40} {فيومئذٍ لا يُسأل عن ذنبه إنسٌ ولا جانٌّ}؛ أي: سؤال استعلام بما وقع؛ لأنَّه تعالى عالم الغيب والشهادة والماضي والمستقبل، ويريد أن يجازي العباد بما علمه من أحوالهم، وقد جعل لأهل الخيرِ والشرِّ يوم القيامةِ علاماتٍ يُعرفون بها؛ كما قال تعالى: {يومَ تَبْيَضُّ وجوهٌ وتَسْوَدُّ وجوهٌ}.
{39 - 40} "Basi Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini." Yaani, suali la kutaka kujua yaliyotokea Kwani Yeye Mtukufu anayajua ya ghaibu na yanayoonekana, yaliyopita na yajayo, na anataka kuwalipa waja wake kwa aliyoyajua katika hali zao, na aliwawekea wana heri na wana uovu Siku ya Kiyama alama ambazo kwazo watajulikana. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: “Siku ambayo nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso zitakuwa nyeusi.”
#
{41 - 42} وقال هنا: {يُعْرَفُ المجرمون بسيماهم فيؤخَذُ بالنواصي والأقدام. فبأيِّ آلاءِ ربِّكما تكذِّبانِ}؛ أي: فيؤخذ بنواصي المجرمين وأقدامهم، فيُلْقَوْنَ في النار ويُسحبون إليها. وإنَّما يسألهم تعالى سؤال توبيخ وتقريرٍ بما وقع منهم، وهو أعلم به منهم، ولكنَّه تعالى يريد أن تَظْهَرَ للخلق حجَّته البالغة وحكمته الجليلة.
{41 - 42} Na akasema hapa: "Watajulikana wahalifu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?" Ila Mwenyezi Mungu atawauliza swali kwa njia ya kuwakemea na kuwafanya wakiri yale waliyoyafanya, na Yeye ndiye anayajua zaidi hata kuwaliko wao wenyewe, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba iwadhihirikie viumbe hoja yake ya uhakika na hekima yake kuu.
: 43 - 45 #
{هَذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ (43) يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ (44) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (45)}.
43. Hii ndiyo Jahannamu ambayo wahalifu walikuwa wakiikanusha. 44. Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayochemka. 45. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?
#
{43 - 45} أي: يقالُ للمكذِّبين بالوعد والوعيد حين تُسَعَّر الجحيم: {هذه جهنَّمُ التي يكذِّبُ بها المجرمون}: فلْيهنهم تكذيبُهم بها، ولْيذوقوا من عذابها ونَكالها وسعيرها وأغلالها ما هو جزاءٌ لهم على تكذيبهم ، يطوفون بين أطباق الجحيم ولهبها، {وبين حميم آنٍ}؛ أي: ماء حارٍّ جدًّا قد انتهى حرُّه، وزمهريرٍ قد اشتدَّ بردُه وقرُّه. {فبأيِّ آلاءِ ربِّكما تكذِّبانِ}؟!
{43 - 45} Yaani wataambiwa wale waliokadhibisha ahadi na tishio wakati Jahannamu itawashwa kwa mwako mkali: "Hii ndiyo Jahannamu ambayo wahalifu walikuwa wakiikanusha." Basi na wafedheheke kwa kuikanusha kwao huko, na waonje adhabu yake, mateso yake, na mwako wake mkali, na minyororo yake, mambo ambayo ni malipo yao kwa sababu ya kukanusha kwao. Watazunguka baina ya mapande ya Jahannam na mwako wake mkali na maji ya moto yanayochemka, na mengine baridi sana. "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
Alipotaja watakayofanyiwa wahalifu, akataja malipo ya wacha Mungu na wanaomwogopa, akasema:
: 46 - 78 #
{وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ (46) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (47) ذَوَاتَا أَفْنَانٍ (48) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (49) فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ (50) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (51) فِيهِمَا مِنْ كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ {(52) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (53) مُتَّكِئِينَ عَلَى فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ (54) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (55) فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ (56) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (57) كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ (58) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (59) هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ (60) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (61) وَمِنْ دُونِهِمَا جَنَّتَانِ (62) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (63) مُدْهَامَّتَانِ (64) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (65) فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ (66) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (67) فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ (68) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (69) فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ (70) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (71) حُورٌ مَقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ (72) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (73) لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ (74) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (75) مُتَّكِئِينَ عَلَى رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ (76) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (77) تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ (78)}.
46. Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili. 47. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 48. Bustani zenye matawi yaliyotanda. 49. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 50. Ndani yake zimo chemichemi mbili zinazopita. 51. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 52. Humo katika kila matunda zimo namna mbili. 53. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 54. Wawe wameegemea matandiko yenye bitana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. 55. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 56. Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini. 57. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 58. Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. 59. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha. 60. Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? 61. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 62. Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyingine mbili. 63. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 64. Za kijani kibivu. 65. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 66. Na chemichemi mbili zinazofurika. 67. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 68. Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga. 69. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 70. Humo wamo wanawake wema wazuri. 71. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 72. Wanawake wazuri wanaotawishwa katika mahema. 73. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 74. Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. 75. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 76. Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri. 77. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha? 78. Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
#
{46 - 47} أي: وللذي خاف ربَّه وقيامه عليه، فترك ما نهى عنه، وفعل ما أمره به؛ له {جنَّتانِ} من ذهبٍ آنيتهما وحليتهما وبنيانهما وما فيهما، إحدى الجنتين جزاءً على ترك المنهيَّات، والأخرى على فعل الطَّاعات.
{46 - 47} Yaani, kwa mwenye kumuogopa Mola wake Mlezi na kusimama mbele yake, basi akayaacha aliyoyakataza, na akafanya aliyomuamrisha, anazo "bustani mbili" za dhahabu, vyombo vyake, na mapambo yake, na mijengo yake, na vyote vilivyomo ndani yake. Moja ya mabustani hizo ni malipo ya kuacha mambo yaliyoharamishwa, na ya pili ni malipo kwa kutekeleza mambo ya utiifu.
#
{48 - 49} ومن أوصاف تلك الجنتين أنَّهما {ذواتا أفنانٍ}؛ أي: فيهما من ألوان النَّعيم المتنوِّعة؛ نعيم الظاهر والباطن؛ ما لا عينٌ رأتْ ولا أذنٌ سمعتْ ولا خطرَ على قلب بشرٍ؛ أي: فيهما الأشجار الكثيرة الزاهرة، ذوات الغصون الناعمة، التي فيها الثمار اليانعة الكثيرة اللَّذيذة.
{48 - 49} Na miongoni mwa sifa bustani hizo mbili ni kuwa "ni zenye matawi yaliyotanda" na kwamba zina aina mbalimbali za neema iliyo dhahiri na ya ndani, mambo ambayo hakuna jicho lililowahi kuona, wala hakuna sikio lililowahi kusikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote. Kwani ndani yake kuna miti mingi yenye maua, yenye matawi laini, yenye matunda mengi yaliyoiva na matamu.
#
{50 - 51} وفي تلك الجنتين {عينانِ تجريانِ}: يفجِّرونَهما على ما يريدون ويشتَهون.
{50 - 51} Na katika bustani hizo mbili ziko "chemichemi mbili zinazopita" wakizifanya zimiminike kwa wingi.
#
{52 - 53} {فيهما من كلِّ فاكهةٍ}: من جميع أصناف الفواكه {زوجان}؛ أي: صنفان؛ كلُّ صنف له لَذَّةٌ ولونٌ ليس للنوع الآخر.
{52 - 53} "Humo katika kila matunda zimo namna mbili." Kila aina ikiwa na ladha na rangi ambayo hiyo nyingine haina.
#
{54 - 55} {متكئين على فرشٍ بطائِنُها من إستبرقٍ}: هذه صفة فُرُشِ أهل الجنَّة وجلوسهم عليها، وأنَّهم متَّكئون عليها؛ أي: جلوسَ تمكُّن واستقرار وراحةٍ؛ كجلوس الملوك على الأسرَّة، وتلك الفُرُش لا يعلم وصفَها وحسنَها إلاَّ الله تعالى ، حتى إنَّ بطائنها التي تلي الأرض منها من إستبرقٍ وهو أحسن الحرير وأفخره؛ فكيف بظواهرها التي يباشرون ، {وجنى الجنَّتينِ دانٍ}: الجنى هو الثمر المستوي؛ أي: وثمر هاتين الجنتين قريبُ التناول، ينالُه القائم والقاعدُ والمضطجع.
{54 - 55} "Wawe wameegemea matandiko yenye bitana ya hariri nzito." Haya ndiyo maelezo ya matandiko ya watu wa Bustani za mbinguni na kuketi kwao juu yake, na kwamba wataegemea juu yake sawasawa kwa utulivu na raha. Kama vile wafalme wanavyokaa juu ya vitanda. Na hakuna anayejua maelezo hasa ya matandiko hayo na uzuri wake isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kiasi kwamba hata bitana zake zilizo karibu na ardhi ni za hariri nzito ya kifahari zaidi. Basi vipi kuhusu sura yake ya nje wanayoiona, "na matunda ya Bustani hizo yapo karibu" na yanaweza kuchunwa na aliyesimama, aliyekaa na aliyeegemea.
#
{56 - 59} {فيهنَّ قاصراتُ الطرفِ}؛ أي: قد قصرنَ طرفهنَّ على أزواجهنَّ من حسنهم وجمالهم وكمال محبتهنَّ لهم، وقصرنَ أيضاً طرفَ أزواجهنَّ عليهنَّ من حسنهنَّ وجمالهنَّ ولَذَّةِ وصالهنَّ وشدَّة محبَّتهنَّ، {لم يطمثهنَّ إنسٌ قبلَهم ولا جانٌّ}؛ أي: لم ينلهنَّ أحدٌ قبلهم من الإنس والجنِّ، بل هنَّ أبكارٌ عربٌ متحبِّباتٌ إلى أزواجهنَّ؛ بحسن التبعُّل والتغنُّج والملاحة والدَّلال، ولهذا قال: {كأنهنَّ الياقوت والمرجان}، وذلك لصفائهنَّ وجمال منظرهنَّ وبهائهنَّ.
{56 - 59} "Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao" kuwaangalia waume zao tu kwa sababu ya uzuri wao, urembo wao, na ukamilifu wa upendo wa wake hao kwao, na pia macho ya waume zao yanawaangalia wao tu kwa sababu ya uzuri wao, urembo wao, raha ya kuwa pamoja na ukubwa wa upendo wao. "Hajawagusa mtu kabla yao wala jini." Bali wao ni mabikira hirimu wanaofanya bidii kupendwa na waume zao. Kwa sababu ya kutunza ndoa vizuri, kujilegeza kwao sana, kuvalia kwao vizuri zaidi na kulainika mbele yao, na ndiyo maana akasema: "Kama kwamba wao ni yakuti na marijani," na hayo ni kwa sababu ya usafi wao, uzuri wa mwonekano wao na urembo wao.
#
{60 - 61} {هل جزاءُ الإحسان إلاَّ الإحسان}؛ أي: هل جزاء مَن أحسن في عبادة الخالق، ونفع عبيدَه إلاَّ أن يُحْسَنَ إليه بالثواب الجزيل والفوز الكبير والنعيم المقيم والعيش السليم؟ فهاتان الجنَّتان العاليتان للمقرَّبين.
{60 - 61} "Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?" Yaani je, kuna malipo kwa mwenye kufanya vizuri katika kumwabudu Muumba na kuwanufaisha waja wake isipokuwa kwa kumfanyia wema kwa malipo mengi, na kufuzu kukubwa, neema ya milele, na kuishi maisha yaliyo salama? Hizi ndizo bustani mbili za mbinguni zaa juu zilizoandaliwa wale walio karibu na Mwenyezi Mungu.
#
{62 - 69} {ومن دونِهما جنَّتانِ}: من فضَّة بنيانهما وحليتهما وآنيتهما وما فيهما لأصحاب اليمين، وتلك الجنتانِ {مدهامَّتان}؛ أي: سوداوان من شدَّة الخضرة والريِّ ، {فيهما عينان نَضَّاختانِ}؛ أي: فوَّارتان، {فيهما فاكهةٌ}: من جميع أصناف الفواكه، وأخصُّها النخل والرمان، اللذان فيهما من المنافع ما فيهما.
{62 - 69} "Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyingine mbili" za fedha kwenye mijengo yake, na mapambo yake, na vyombo vyake, na vilivyomo ndani yake, kwa watu wa kuliani, na bustani hizo mbili "ni za kijani kibivu." Pia ilisemekana kwamba ni nyeusi kutokana na ukubwa wa kijani kibichi chake na unyevu wake. "Na chemichemi mbili zinazofurika imo humo miti ya matunda" kutoka kwa kila aina ya matunda, hasa mitende na makomamanga, ambayo yana manufaa mengi sana.
#
{70 - 75} {فيهنَّ}؛ أي: في الجنات كلِّها {خيراتٌ حسانٌ}؛ أي: خيرات الأخلاق حسان الأوجه، فجمعنَ بين جمال الظاهر والباطن وحسن الخَلْق والخُلُق. {حورٌ مقصوراتٌ في الخيام}؛ أي: محبوسات في خيام اللؤلؤ، قد تهيأنَ وأعددنَ أنفسهنَّ لأزواجهنَّ، ولا ينفي ذلك خروجهنَّ في البساتين ورياض الجنة كما جرت العادةُ لبنات الملوك المخدَّرات الخَفِرات ، {لم يطمثهنَّ إنسٌ قبلهم ولا جانٌّ. فبأيِّ آلاء ربِّكما تكذِّبان}؟!
{70 - 75} "Humo wamo;" yaani, katika Pepo yote "wanawake wema wazuri." Yaani, wenye maadili bora ni nyuso nzuri. Kwa hivyo wakakusanya kati ya uzuri wa nje na wa ndani, na uzuri wa maumbile na tabia. "Wanawake wazuri wanaotawishwa katika mahema" ya lulu, wakiwa wamejitayarisha na kujiandaa kwa ajili ya waume zao, na hilo halipingani na kutoka kwenda katika makonde ya bustani za mbinguni kama ilivyo desturi ya mabinti wa wafalme waliolindwa na wenye staha. "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha?"
#
{76 - 77} {متَّكئين على رفرفٍ خضرٍ}؛ أي: أصحاب هاتين الجنتين متَّكأهم على الرفرف الأخضر، وهي الفرش التي تحت المجالس العالية، التي قد زادت على مجالسهم، فصار لها رفرفة من وراء مجالسهم؛ لزيادة البهاء وحسن المنظر، {وعبقريٍّ حسانٍ}: العبقريُّ نسبةً لكلِّ منسوج نسجاً حسناً فاخراً، ولهذا وصفها بالحسن الشامل لحسن الصفة و [حسن] المنظر ونعومة الملمس وهاتان الجنتان دون الجنتين الأولَيَيْن؛ كما نصَّ الله على ذلك بقوله: {ومن دونِهِما جنَّتانِ}، وكما وصف الأوليين بعدَّة أوصاف لم يصِفْ به الأخريين، فقال في الأوليين: {فيهما عينان تجريانِ}، وفي الأخريين: {عينان نضَّاختان}: ومن المعلوم الفرق بين الجارية والنضَّاخة، وقال في الأوليين: {ذواتا أفنانٍ}، ولم يقلْ ذلك في الأخريين، وقال في الأوليين: {فيهما من كلِّ فاكهةٍ زوجانِ}، وفي الأخريين: {فيهما فاكهةٌ ونخلٌ ورمانٌ}، وقد عُلِمَ ما بين الوصفين من التفاوت. وقال في الأوليين: {متَّكئين على فرشٍ بطائنها من إستبرقٍ وجنى الجنَّتين دانٍ}، ولم يقلْ ذلك في الأخريين، بل قال: {متكئينَ على رفرفٍ خضرٍ وعبقريٍّ حسانٍ}، وقال في الأوليين في وصف نسائهم وأزواجهم: {فيهن قاصراتُ الطرفِ [لم يطمثهن إنس قبلهم ولا جان]}، وفي الأخريين: {حور مقصوراتٌ في الخيام}، وقد عُلم التفاوت بين ذلك، وقال في الأوليين: {هل جزاءُ الإحسان إلاَّ الإحسانُ}، فدلَّ ذلك أنَّ الأوليين جزاء المحسنين، ولم يقل ذلك في الأخيرتين، ومجرَّد تقديم الأوليين على الأخريين يدلُّ على فضلهما. فبهذه الأوجه يُعْرَفُ فضلُ الأوليين على الأخريين، وأنهما معدَّتان للمقرَّبين من الأنبياء والصدِّيقين وخواصِّ عباد الله الصالحين، وأنَّ الأخريين معدَّتان لعموم المؤمنين. وفي كلٍّ من الجنات المذكورات ما لا عينٌ رأتْ ولا أذنٌ سمعتْ ولا خطر على قلب بشرٍ، وفيهنَّ ما تشتهيه الأنفسُ وتلذُّ الأعين، وأهلهنَّ في غاية الراحة والرضا والطمأنينة وحسن المأوى، حتى إنَّ كلَّ واحدٍ منهم لا يرى أحداً أحسن حالاً منه ولا أعلى من نعيمِهِ الذي هو فيه.
{76 - 77} "Wameegemea juu ya matakia ya kijani." Yaani, wenye bustani hizi mbili hizi wanaegemea kwenye matakia ya kijani "na mazulia mazuri." Hizi ni bustani mbili zilizo chini ya kiwango cha zile bustani mbili za mwanzo. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika kauli yake: "Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyingine mbili" na kama alivyozielezea zile mbili za mwanzo kwa maelezo kadhaa, ambayo hakuzielezea zile mbili za mwisho. "Ndani yake zimo chemichemi mbili zinazopita," na katika mbili za mwisho: "Na chemichemi mbili zinazofurika." Inajulikana vyema kwamba kuna tafauti baina ya kupita tu na kufurika. Na alisema kuhusu zile mbili za mwanzo: "Bustani zenye matawi yaliyotanda," na wala hakusema hayo kuhusu mbili za mwisho. Akasema katika mbili za mwanzo: "Humo katika kila matunda zimo namna mbili," na katika mbili za mwisho, "Imo humo miti ya matunda na mitende na mikomamanga," na inajulikana kuwa kuna tofauti baina ya maelezo mawili hayo. Akasema katika mbili za mwanzo: "Wawe wameegemea matandiko yenye bitana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu." Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri," wala hakusema hayo katika mbili za mwisho, bali alisema: "Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri," na akasema katika mbili za mwanzo katika kuwaelezea wake zao: "Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; [hawajagusa mtu wala jini kabla yao]." Na akasema kuhusu wale wengine "Wanawake wazuri wanaotawishwa katika mahema." Na hapa pia inajulikana kwamba kuna tofauti baina ya hayo. Na alisema katika mbili za mwanzo: "Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?" Kwa hivyo likaashiria hilo kwamba hayo ni malipo ya wema, na hakusema hivyo kuhusu zile mbili za mwisho, na kwa kutanguliza tu zile mbili za kwanza kabla ya zile mbili za mwisho ni jambo linaloashiria ubora wake. Kupitia mambo haya, unajulikana ubora wa zile bustani mbili za kwanza juu ya zile za mwisho, kwamba ziliandaliwa kwa ajili ya wale walio karibu na Mwenyezi Mungu kama vile Manabii, wakweli, na watu wema maalumu wa Mwenyezi Mungu, na kwamba zile mbili za mwisho zimetayarishwa kwa ajili ya waumini wote kwa ujumla. Na katika kila moja ya bustani hizo zilizotajwa kuna yale ambayo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia, na moyo wa mwanadamu haujapata kufikiria. Na ndani yake kuna yale yanayotamaniwa na macho, na watu wao wanastarehe vikubwa, kuridhika, kutulia na makazi mema, kiasi kwamba kila mmoja wao ataona kwamba hakuna mtu yeyote aliye katika hali bora kuliko yeye wala aliye juu zaidi ya neema yake aliyomo ndani yake.
#
{78} ولمَّا ذكر سعةَ فضله وإحسانه؛ قال: {تبارك اسمُ ربِّك ذي الجلال والإكرام}؛ أي: تعاظم وكثر خيره الذي له الجلال الباهر والمجدُ الكامل والإكرام لأوليائه.
{78} Na alipotaja upana wa fadhila zake na wema wake, akasema: "Limetukuka jina la Mola wako Mlezi, Mwenye utukufu na ukarimu." Yaani, wema wake na heri yake ni nyingi, na kwamba ana utukufu wa ajabu, heshima kamili, na kuwakirimu vipenzi wake.
Imekamilika tafsiri ya Surat Ar-Rahman, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na shukrani na kutajwa kwa uzuri.
******