Tafsiri ya Surat Iqtarabat As-Saa (Saa imekaribia)
Tafsiri ya Surat Iqtarabat As-Saa
(Saa imekaribia)
Ilishuka Makka.
{اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ (1) وَإِنْ يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُسْتَمِرٌّ (2) وَكَذَّبُوا وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ وَكُلُّ أَمْرٍ مُسْتَقِرٌّ (3) وَلَقَدْ جَاءَهُمْ مِنَ الْأَنْبَاءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ (4) حِكْمَةٌ بَالِغَةٌ فَمَا تُغْنِ النُّذُرُ (5)}.
1. Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! 2. Na wakiona Ishara,
hugeuka upande na husema: 'Huu uchawi tu unazidi kuendelea.' 3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti. 4. Na bila ya shaka zimewajia habari zenye makaripio. 5. Hekima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
#
{1} يخبر تعالى أنَّ الساعة ـ وهي القيامة ـ اقتربت، وآن أوانُها، وحان وقتُ مجيئها، ومع هذا ؛ فهؤلاء المكذِّبون لم يزالوا مكذِّبين بها غير مستعدين لنزولها، ويريهم الله من الآيات العظيمة الدالَّة على وقوعها ما يؤمنُ على مثله البشرُ؛ فمن أعظم الآياتِ الدالَّة على صحَّة ما جاء به محمد بن عبد الله - صلى الله عليه وسلم - أنَّه لما طلب منه المكذِّبون أن يُرِيَهم من خوارق العادات ما يدلُّ على صحَّة ما جاء به وصدقه ؛ أشار - صلى الله عليه وسلم - إلى القمر، فانشقَّ بإذن الله فلقتين؛ فلقةً على جبل أبي قُبيس، وفلقةً على جبل قعيقعان، والمشركون وغيرهم يشاهدون هذه الآية العظيمة الكائنة في العالم العلويِّ، التي لا يقدر الخلقُ على التمويه بها والتخييل، فشاهدوا أمراً ما رأوا مثلَه، بل ولم يسمعوا أنَّه جرى لأحدٍ من المرسلين قبلَه نظيره، فانبهروا لذلك، ولم يدخُل الإيمانُ في قلوبهم، ولم يردِ الله بهم خيراً، ففزعوا إلى بهتهم وطغيانهم، وقالوا: سحرنا محمدٌ! ولكنَّ علامة ذلك أنكم تسألون من وَرَدَ عليكم من السفر؛ فإنَّه إن قدر على سحركم؛ لم يقدِرْ أن يسحرَ مَن ليس مشاهداً مثلكم! فسألوا كلَّ من قدم، فأخبروهم بوقوع ذلك، فقالوا: {سحرٌ مستمرٌّ}! سحرنا محمدٌ وسحر غيرنا!! وهذا من البَهْتِ الذي لا يروج إلاَّ على أسفه الخلق وأضلِّهم عن الهدى والعقل.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kwamba Saa - ambayo ni Kiyama - imekaribia, na wakati wa kuja kwake umefika, lakini pamoja na haya, wale wanaokadhibisha wanaendelea tu kuikadhibisha na wala hawajiandai kwa ajili ya kuteremka kwake. Na Mwenyezi Mungu anawaonyesha miongoni mwa ishara kubwa zinazoonyesha kutokea kwake, ambazo mfano wake wameshaamini watu wengine. Basi katika ishara kubwa zaidi zinazoashiria usahihi wa yale aliyokuja nayo Muhammad bin Abdullah – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie ni pale wakadhibishaji walipomtaka awaonyeshe muujiza wa kuunga mkono usahihi na ukweli wa kile alichokileta, yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie - akauashiria mwezi, nao ukagawanyika sehemu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kipande kimoja kilikuwa juu ya mlima unaoitwa Abu Qubays, na kipande kingine kikawa juu ya mlima unaoitwa Qu’ayqa'an, ilhali washirikina na wengineo wanaitazama ishara hii kubwa iliyotokea katika ulimwengu wa juu, ambayo mtu hawezi kuficha uhalisia wake na kuchukulia kwamba ni mazingaumbwe. Basi wakaona jambo ambalo hawakuwahi kuona mfano wake, bali hata hawakuwahi kusikia kwamba kuna hata mmoja wa Mitume kabla yake aliyefanya mfano wake. Basi wakalistaajabia hilo, lakini Imani haikuingia nyoyoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwatakia heri, kwa hivyo wakaingiwa na hofu na kukimbilia jeuri yao na kupindukia kwao mipaka,
na wakasema: ‘Muhammad ameturoga!’ Lakini alama ya hilo ni kuwa mtamuuliza aliyekujieni kutoka safarini. Kwani hata kama ataweza kuwaroga nyinyi, basi hataweza kumroga yule ambaye yuko hapa akiangalia kama nyinyi. Basi wakawauliza kila aliyewajia, nao wakawaambia kwamba kweli hilo lilitokea,
lakini hawa wakasema: "Huu ni uchawi tu unazidi kuendelea!" Muhammad alituroga na akaroga watu wengine pia!! Hili ni katika uwongo ambao hauenei isipokuwa kwa watu wapumbavu zaidi na waliopotoka zaidi mbali na uwongofu na akili.
#
{2} وهذا ليس إنكاراً منهم لهذه الآية وحدَها، بل كلُّ آية تأتيهم؛ فإنَّهم مستعدُّون لمقابلتها بالتكذيب والردِّ لها، ولهذا قال: {وإن يَرَوا آيةً يعرِضوا}: فلم يعدْ الضمير على انشقاق القمر، [فلم يقل: وإن يروها]، بل قال: {وإن يَرَوا آيةً يعرضوا}؛ فليس قصدهم اتِّباع الحق والهدى، وإنَّما مقصودهم اتِّباع الهوى.
{2} Huku si kukataa kwao Aya hii peke yake, bali ni kila Aya inayowajia. Kwani wao wako tayari kuikabili kwa kuikataa na kuirudiq,
na ndio maana Akasema: "Na wakiona Ishara,
hugeuka upande": Kiwakilishi hakikurejelea juu ya kupasuka kwa mwezi,
wala hakusema: Na lau wakiiona],
bali Yeye alisema: "Na wakiona Ishara, hugeuka upande." Makusudio yao si kufuata haki na uongofu, bali ni kufuata matamanio yao.
#
{3} ولهذا قال: {وكذَّبوا واتَّبعوا أهواءهم}؛ كقوله تعالى: {فإن لم يستجيبوا لك فاعْلَمْ أنَّما يتَّبِعون أهواءَهم}؛ فإنَّه لو كان قصدُهم اتِّباعَ الهدى؛ لآمنوا قطعاً واتَّبعوا محمداً - صلى الله عليه وسلم -؛ لأنه أراهم الله على يديه من البينات والبراهين والحجج القواطع ما دلَّ على جميع المطالب الإلهيَّة والمقاصد الشرعيَّة، {وكلُّ أمرٍ مستقرٍّ}؛ أي: إلى الآن لم يبلغ الأمر غايته ومنتهاه، وسيصير الأمر إلى آخره؛ فالمصدِّق يتقلَّب في جنَّات النعيم ومغفرة الله ورضوانه، والمكذِّب يتقلَّب في سخط الله وعذابِهِ خالداً مخلداً أبداً.
{3} Ndiyo maana akasema: "Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao.
" Kama Asemavyo Mwenyezi Mungu: "Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu." Kwani ikiwa nia yao ingekuwa ni kufuata uwongofu, basi bila ya shaka wangeliamini kabisa na kumfuata Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungi ziwe juu yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaonyesha kupitia mikono yake Nabii ushahidi wa wazi, uthibitisho na hoja za uhakika zilizoonyesha matakwa yote ya kimungu na makusudio ya kisheria; "na kila jambo ni lenye kuthibiti." Yaani, mpaka sasa jambo hilo halijafikia mwisho wake, na jambo hilo litaendelea hadi mwisho wake. Hapo mkweli atakwenda huku na kule katika bustani za mbinguni za neema na msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi zake. Naye mwenye kukadhibisha atapendukapenduka katika ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake adumu humo milele na milele.
#
{4} وقال تعالى مبيِّناً أنَّهم ليس لهم قصدٌ صحيحٌ واتباعٌ للهدى: {ولقد جاءهم من الأنباءِ}؛ [أي: الأخبار السابقة واللاحقة والمعجزات الظاهرة] {ما فيه مُزْدَجَرٌ}؛ أي: زاجر يزجرهم عن غيِّهم وضلالهم.
{4} Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha kuwa hawana nia njema na kufuata uwongofu: "Na bila ya shaka zimewajia habari."
[Yaani, habari zilizotangulia, zitakazofuatia na miujiza iliyo dhahiri], "zenye makaripio" ya kuwakaripia dhidi ya ukengeufu wao na upotofu wao.
#
{5} وذلك {حكمةٌ}: منه تعالى {بالغةٌ}؛ أي: لتقوم حجَّته على العالمين ، ولا يبقى لأحدٍ على الله حجَّةٌ بعد الرسل، {فما تغني النُّذُر}؛ كقوله تعالى: {ولو جاءتهم كلُّ آيةٍ لا يؤمنوا حتى يَرَوُا العذابَ الأليم}.
{5} Na hiyo ni "hekima" kutoka kwake Mtukufu "kaamili." Yaani, ili hoja yake ithibitike juu ya walimwengu wote,
na asibakie mtu yeyote akiwa na hoja dhidi ya Mwenyezi Mungu baada ya Mitume; "lakini maonyo hayafai kitu!" Kama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hata kama itawajia kila Ishara” hawataamini
“mpaka waione adhabu iliyo chungu.”
{فَتَوَلَّ عَنْهُمْ يَوْمَ يَدْعُ الدَّاعِ إِلَى شَيْءٍ نُكُرٍ (6) خُشَّعًا أَبْصَارُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُنْتَشِرٌ (7) مُهْطِعِينَ إِلَى الدَّاعِ يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَذَا يَوْمٌ عَسِرٌ (8)}.
6. Basi jiepushe nao. Siku atakapoita mwitaji kuliendea jambo linalochusha. 7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige waliotawanyika. 8. Wanamkimbilia mwitaji,
na makafiri wanasema: 'Hii ni siku ngumu.'
#
{6} يقول تعالى لرسوله - صلى الله عليه وسلم -: قد بان أنَّ المكذِّبين لا حيلة في هداهم، فلم يبق إلاَّ الإعراضُ عنهم ، فقال: {فتولَّ عنهم}: وانتظرْ بهم يوماً عظيماً وهولاً جسيماً، وذلك حين {يَدعُ الداعِ}؛ وهو إسرافيلُ عليه السلام {إلى شيء نُكُرٍ}؛ أي: إلى أمر فظيع تنكره الخليقة، فلم تر منظراً أفظع ولا أوجع منه، فينفخُ إسرافيل نفخةً يخرج بها الأمواتُ من قبورهم لموقف القيامة.
{6} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – kwamba, imeshadhihirika ya kwamba hakuna njia ya wakadhibishaji kuongoka, basi hakuna kinachobakia ila kujiepusha nao.
Akasema: "Basi jiepushe nao" na wangojelee siku kuu na mahangaiko ya kutisha, na hapo ndipo "atakapoita mwitaji;" yaani Israfil, amani iwe juu yake "kuliendea jambo linalochusha." Kwani hawakuwahi kuona mandhari ya kutisha zaidi au machungu zaidi kuliko hayo. Kwa hivyo Israfil atapuliza mpulizo ambao kwa huo wafu watatoka makaburini mwao hadi mahali pa kisimamo cha Kiyama.
#
{7} {خُشَّعاً أبصارُهم}؛ أي: من الهول والفزع الذي وصل إلى قلوبهم، فخضعت وذلَّت، وخشعت لذلك أبصارهم {يخرجون من الأجْداثِ}: وهي القبورُ {كأنَّهم}: من كثرتهم ورَوَجان بعضهم ببعض {جرادٌ منتشرٌ}؛ أي: مبثوثٌ في الأرض متكاثرٌ جدًّا.
{7} "Macho yao yatainama" kutokana na mahangaiko na hofu kubwa iliyozifikia nyoyo zao, basi macho yao yakanyenyekea na kudhalilika kwa sababu ya hilo. "Watatoka makaburini kana kwamba" kutokana na wingi wao na kuchanganyikana kwao "kama nzige waliotawanyika" juu ya ardhi wakiwa katika idadi kubwa sana.
#
{8} {مهطعينَ إلى الدَّاعِ}؛ أي: مسرعين لإجابة نداء الدَّاعي، وهذا يدلُّ على أنَّ الدَّاعي يدعوهم ويأمرهم بالحضور لموقف القيامة، فيلبُّون دعوته ويسرعون إلى إجابته، {يقول الكافرون}: الذين قد حَضَرَ عذابُهم: {هذا يومٌ عَسِرٌ}؛ كما قال تعالى: {على الكافرين غيرُ يسيرٍ}: مفهوم ذلك أنَّه يسيرٌ سهلٌ على المؤمنين.
{8} "Wanakimbilia mwitaji." Hili linaashiria kuwa mwitaji atawaita na kuwaamrisha kufika mahala pa kisimamo cha Kiyama, kwa hivyo wanaitikia wito wake na kukimbilia kumuitikia. "Na makafiri” waliohudhuria hapo ili waadhibiwe
“watasema: Hii ni siku ngumu." Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.” Na maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba itakuwa nyepesi na rahisi kwa Waumini.
{كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ (9) فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانْتَصِرْ (10) فَفَتَحْنَا أَبْوَابَ السَّمَاءِ بِمَاءٍ مُنْهَمِرٍ (11) وَفَجَّرْنَا الْأَرْضَ عُيُونًا فَالْتَقَى الْمَاءُ عَلَى أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ (12) وَحَمَلْنَاهُ عَلَى ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ (13) تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا جَزَاءً لِمَنْ كَانَ كُفِرَ (14) وَلَقَدْ تَرَكْنَاهَا آيَةً فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ (15) فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ (16) وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ (17)}.
9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. 10.
Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: 'Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!' 11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayomiminika. 12. Na tukazipasua ardhi kwa chemichemi, yakakutana maji kwa jambo lililokwisha pangwa. 13. Na tukambeba kwenye safina ya mbao na kamba. 14. Ikawa inakwenda kwa macho yetu, kuwa ni malipo kwa alivyokuwa amekanushwa. 15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anayekumbuka? 16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu. 17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka?
#
{9} لما ذكر تبارك وتعالى حالَ المكذِّبين لرسوله وأنَّ الآياتِ لا تنفع فيهم ولا تُجدي عليهم شيئاً؛ أنذرهم وخوَّفهم بعقوبات الأمم الماضية المكذِّبة للرسل وكيف أهلهكم اللهُ وأحلَّ بهم عقابه، فذكر قومَ نوحٍ؛ أول رسول بعثه الله إلى قوم يعبُدون الأصنام، فدعاهم إلى توحيد الله وعبادته وحده لا شريك له، فامتنعوا من ترك الشرك، وقالوا: {لا تَذَرُنَّ آلهتكم ولا تَذَرُنَّ وَدًّا ولا سُواعاً ولا يَغوثَ ويَعوقَ ونَسْراً}، ولم يزل نوحٌ يدعوهم إلى الله ليلاً ونهاراً سرًّا وجهاراً، فلم يزدْهم ذلك إلاَّ عناداً وطغياناً وقدحاً في نبيِّهم، ولهذا قال هنا: {فكذَّبوا عبدَنا وقالوا مجنونٌ}: لزعمهم أنَّ ما هم عليه وآباؤهم من الشرك والضلال هو الذي يدلُّ عليه العقل، وأنَّ ما جاء به نوحٌ عليه السلام جهلٌ وضلالٌ لا يصدُر إلاَّ من المجانين، وكَذَبوا في ذلك، وقَلَبوا الحقائق الثابتة شرعاً وعقلاً ؛ فإنَّ ما جاء به هو الحقُّ الثابت الذي يرشد العقول النيِّرة المستقيمة إلى الهدى والنور والرُّشد، وما هم عليه جهلٌ وضلالٌ مبينٌ. وقوله: {وازْدُجِرَ}؛ أي: زجره قومه وعنَّفوه لما دعاهم إلى الله تعالى، فلم يكفِهِم قبَّحَهُمُ اللهُ عدمُ الإيمان به ولا تكذيبُهم إيَّاه، حتى أوصلوا إليه من أذيَّتهم ما قدروا عليه، وهكذا جميع أعداء الرسل هذه حالهم مع أنبيائهم.
{9} Alipotaja Mwenyezi Mungu Mwenye baraka nyingi, Mtukufu hali ya wale waliomkadhibisha Mtume wake, na kwamba ishara haziwaingii kitu wala haziwanufaishi chochote, akawaonya na kuwaogopesha kwa adhabu za umma wa zamani waliowakadhibisha Mitume, na jinsi Mwenyezi Mungu alivyowaangamiza na kuwaletea adhabu yake. Basi akawataja watu wa Nuhu, ambaye alikuwa Mtume wa kwanza ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwa watu wanaoabudu masanamu. Akawalingania kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumwabudu Yeye peke yake bila mshirika,
lakini wakasema: "Kamwe msiwaache miungu yenu, wala kamwe msimwache Wadda, wala Suwaa', wala Yaghutha, wala Yau'qa wala Nasra.” Naye Nuhu akaendelea kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa siri, mchana na usiku. Lakini, hilo halikuwazidishia isipokuwa kuwa na ukaidi, kupindukia mipaka na kumkashifu Nabii wao.
Ndiyo maana akasema hapa: "Wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu." Kwa sababu ya madai yao ya kwamba yale ambayo wao na baba zao wanayaamini ya ushirikina na upotofu ndiyo yanayoashiriwa na akili timamu, na kwamba yale ambayo Nuhu, amani iwe juu yake, alikuja nayo ni ujinga na upotofu ambao hauwezi kutokea isipokuwa kwa wendawazimu, lakini walidanganya katika hilo, na wakapindua mambo ya uhakika yaliyothibiti kisheria na kiakili. Kwani, aliyokuja nayo ndiyo haki iliyo dhabiti isiyobadilika inayoongoza akili angavu na nyoofu kwenye uwongofu, nuru na uwongofu. Ilhali hayo wanayoyafanya ni ujinga na upotofu ulio wazi.
Na kauli yake: "Na akakaripiwa." Yaani, watu wake walimkemea na kumkaripia pale alipowaita kwa Mwenyezi Mungu, na tena haikuwatosha - Mwenyezi Mungu awaangamize – kutomwamini kwao wala kumkadhibisha kwao. Bali pia walimfikishia udhia namna walivyoweza. Na hivyo ndivyo walivyo maadui wote wa Mitume. Walikuwa wakiwafanyia hivi tu Mitume wao.
#
{10} فعند ذلك دعا نوحٌ ربَّه، فقال: {إنِّي مغلوبٌ}: لا قدرةَ لي على الانتصار منهم؛ لأنه لم يؤمن من قومه إلاَّ القليل النادر، ولا قدرة لهم على مقاومة قومهم، {فانتَصِرْ}: اللهمَّ لي منهم، وقال في الآية الأخرى: {ربِّ لا تَذَرْ على الأرضِ من الكافرين دَيَّاراً ... } الآيات.
{10} Kisha Nuhu akamwomba Mola wake Mlezi,
na akasema: "Kwa hakika mimi nimeshindwa." Mimi siwezi kuwashinda. Kwa sababu hawakuamini katika kaumu yake isipokuwa wachache tu, na hawakuwa na uwezo wa kukabiliana watu wao.
“Basi ninusuru” ewe Mwenyezi Mungu dhidi yao.
Na alisema katika Aya nyingine: “Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkazi wake yeyote katika makafiri...” hadi mwisho wa Aya.
#
{11} فأجاب الله سؤاله، فانتصر له من قومه؛ قال تعالى: {ففَتَحْنا أبوابَ السماءِ بماءٍ منهمرٍ}؛ أي: كثير جدًّا متتابع.
{11} Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaitikia ombi lake, na akampa ushindi dhidi ya watu wake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayomiminika."
#
{12} {وفجَّرْنا الأرض عُيوناً}: فجعلتِ السماءُ ينزل منها من الماء شيءٌ خارقٌ للعادة، وتفجَّرت الأرضُ كلُّها، حتى التنُّور الذي لم تَجْرِ العادةُ بوجود الماء فيه، فضلاً عن كونِهِ منبعاً للماء؛ لأنَّه موضع النار، {فالتقى الماء}؛ أي: ماء السماء والأرض، {على أمرٍ}: من الله له بذلك، {قد قُدِرَ}؛ أي: قد كتبه الله في الأزل وقضاه عقوبةً لهؤلاء الظالمين الطاغين.
{12} "Na tukazipasua ardhi kwa chemichemi." Mbingu zilianza kuteremsha maji yasiyo ya kawaida, na ardhi yote ikapasukapasuka, mpaka tanuru ambayo katika hali ya kawaida huwa haina maji, mbali na kwamba inawezakuwa chanzo cha maji. Kwa sababu ni mahali pa moto. "Yakakutana maji;" yaani, maji ya mbingu na ya ardhi, "kwa jambo" lililotoka kwa Mwenyezi Mungu "lililokwisha pangwa." Yaani, Mwenyezi Mungu alikwisha liandika tangu mwanzo na akalipitisha ili liwe adhabu kwa madhalimu hawa waruka mipaka.
#
{13} {وحَمَلْناه على ذاتِ ألواح ودُسُرٍ}؛ أي: ونجَّينا عبدنا نوحاً على السفينة ذات الألواح والدُّسُر ؛ أي: المسامير التي قد سُمِرَتْ بها ألواحُها وشُدَّ بها أسرها.
{13} "Na tukambeba kwenye safina ya mbao na kamba." Yaani, na tukamwokoa mja wetu Nuhu kwenye jahazi lililoundwa kwa mbao na kamba. Pia ilisemekana kwamba maana ya ‘dusur’ hapa ni misumari iliyotumiwa kupigilia mbao zake.
#
{14} {تجري بأعْيُنِنا}؛ أي: تجري بنوح ومَنْ آمن معه ومَنْ حمله مِن أصناف المخلوقات برعايةٍ من الله وحفظٍ منه لها عن الغرق ونظرٍ وكلاءةٍ منه تعالى، وهو نعم الحافظُ الوكيلُ، {جزاءً لِمَنْ كان كُفِرَ}؛ أي: فعلنا بنوح ما فعلنا من النَّجاة من الغرق العامِّ جزاءً له؛ حيث كذَّبه قومُه وكفروا به، فصبر على دعوتِهِم، واستمرَّ على أمر الله، فلم يردَّه عنه رادٌّ ولا صدَّه عن ذلك صادٌّ؛ كما قال تعالى في الآية الأخرى: {قيل يا نوحُ اهبطْ بسلام مِنَّا وبَرَكاتٍ عليك وعلى أمم مِمَّن معك ... } الآية. ويُحتمل أنَّ المراد أنَّا أهلَكنا قومَ نوح وفعلنا بهم ما فَعَلنا مِن العذاب والخزي جزاءً لهم على كفرِهم وعنادهم. وهذا متوجِّهٌ على قراءة من قرأها بفتح الكاف.
{14} "Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu." Yaani, ilikuwa inakwenda na Nuhu pamoja na wale walioamini, na alivyovibeba miongoni mwa sampuli za viumbe, kwa utunzaji na ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kuzama majini. Naye ndiye Mlinzi na Mtegemewa bora. "Yawe ni malipo kwa anayekufuru." Yaani, tulimfanyia Nuhu yale tuliyofanya ya kumwokoa kutokana na kuzama majini kwa ujumla ili yawe ni malipo kwake. Kwa vile watu wake walivyomkadhibisha na kumkufuru, naye akawa na subira katika kuwalingania, na akaendelea kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, na hakuna cha kumrudisha nyuma kilichomrudisha nyuma, wala cha kumzuilia kilichomzuia kufanya hivyo,
kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya nyingine: "Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na juu ya watu walio pamoja nawe..." hadi mwisho wa Aya. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba tuliwaangamiza watu wa Nuhu na tukawafanyia yale tuliyowafanyia ya adhabu na fedheha ili yawe ni malipo ya ukafiri wao na ukaidi wao. Maana hii inakuwa wazi kwa yule anayesoma kwa kutia Fat-ha kwenye herufi Kaf.
#
{15} {ولقد تركناها آيةً فهل من مُدَّكِرٍ}؛ أي: ولقد تركنا قصة نوح مع قومه آيةً يتذكَّر بها المتذكِّرون على أنَّ من عصى الرُّسل وعاندهم أهْلَكَه الله بعقابٍ عامٍّ شديدٍ، أو أنَّ الضمير يعود إلى السفينة وجنسها، وأنَّ أصل صنعتها تعليمٌ من الله لرسوله نوح عليه السلام، ثم أبقى الله صنعتها وجنسها بين الناس؛ ليدلَّ ذلك على رحمته بخلقه وعنايته وكمال قدرته وبديع صنعته. {فهل من مُدَّكِرٍ}؛ أي: فهل متذكِّر للآيات ملقٍ ذهنَه وفكرته لما يأتيه منها؛ فإنَّها في غاية البيان واليُسر؟
{15} "Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anayekumbuka?" Yaani, tumeiacha hadithi ya Nuhu pamoja na watu wake kuwa ni ishara ambayo kwayo wanaokumbuka watakumbuka kwamba mwenye kuwaasi Mitume na kuwapinga, Mwenyezi Mungu atamwangamiza kwa adhabu kali ya jumla, au kwamba kinachozungumziwa katika neno ‘tuliiacha’ ni ile jahazi na mfano wake, na kwamba asili ya kuundwa kwake ni kitu ambacho Mwenyezi Mungu alimfundisha Mtume wake Nuhu, amani iwe juu yake, kisha Mwenyezi Mungu akaiacha kazi ya kuiunda na kuunda mfano wake imejulikana baina ya watu; ili hili liashirie rehema yake kwa viumbe wake, utunzaji wake, ukamilifu wa uwezo wake, na ufundi wake wa hali ya juu. "Lakini je, yupo anayekumbuka?” Kwani hayo kwa hakika yako wazi sana na mepesi mno?
#
{16} {فكيف كان عذابي ونُذُرِ}؛ أي: فكيف رأيتَ أيها المخاطَبُ عذابَ الله الأليم وإنذاره الذي لا يبقى لأحدٍ عليه حجة.
{16} "Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu?" Yaani, ewe unayeongeleshwa ulionaje adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo chungu na maonyo yake, ambayo hakuna yeyote anayeweza kubaki na hoja yoyote dhidi yake.
#
{17} {ولقد يَسَّرْنا القرآنَ للذِّكْرِ فهل من مُدَّكِرٍ}؛ أي: ولقد يسَّرْنا وسهَّلْنا هذا القرآن الكريم ألفاظه للحفظ والأداء ومعانيه للفهم والعلم؛ لأنَّه أحسن الكلام لفظاً، وأصدقُه معنىً، وأبينه تفسيراً؛ فكلُّ من أقبل عليه؛ يَسَّرَ الله عليه مطلوبه غاية التيسير، وسهَّله عليه، والذِّكر شاملٌ لكل ما يتذكَّر به العالمون من الحلال والحرام وأحكام الأمرِ والنَّهْي وأحكام الجزاء والمواعظ والعِبَرِ والعقائِد النَّافعة والأخبار الصادقة، ولهذا كان علم القرآن حفظاً وتفسيراً أسهل العلوم وأجلُّها على الإطلاق، وهو العلمُ النافعُ الذي إذا طلبه العبدُ؛ أُعِينَ عليه. قال بعضُ السَّلف عند هذه الآية: هل من طالب علم فيعان عليه. ولهذا يدعو الله عباده إلى الإقبال عليه والتذكُّر بقوله: {فهل من مُدَّكِرٍ}.
{17} "Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka?” Yaani, hakika tumeifanya Qur-ani hii Tukufu kuwa nyepesi na rahisi katika maneno yake kwa ajili ya kuihifadhi akilini, kuitekeleza, na kufanya maana zake rahisi kwa ajili ya kuzifahamu na kuzijua vyema. Kwa sababu ndiyo mazungumzo yenye matamshi bora zaidi, na yenye maana ya ukweli zaidi, na yenye maelezo yaliyo wazi zaidi. Kwa hivyo, kila mwenye kuichukua, Mwenyezi Mungu humfanyia wepesi mno katika matakwa yake, na huifanya kuwa rahisi kwake. Na ukumbusho unajumuisha kila wanachokikumbuka wanaojua kama vile halali, haramu, hukumu za maamrisho na makatazo, hukumu za kimalipo, mawaidha, mazingatio, itikadi zenye manufaa na habari za ukweli. Ndiyo maana ikawa elimu ya Qur-ani sawa iwe ni kuhifadhi moyoni na kuifasiri ndiyo elimu nyepesi zaidi na tukufu zaidi kuliko zote. Nayo ndiyo elimu yenye manufaa ambayo mtu akiitafuta mja akiitafuta, husaidiwa na Mwenyezi Mungu juu yake.
Baadhi ya wema waliotangulia walisema kuhusiana na Aya hii kwamba inamaanisha: ‘Je,
yuko yeyote anayetafuta elimu ili asaidiwe juu yake?’ Ndiyo maana Mwenyezi Mungu anawaita waja wake kuichukua na kuikumbuka katika kauli yake: "Lakini yupo anayekumbuka?"
{كَذَّبَتْ عَادٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ (18) إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي يَوْمِ نَحْسٍ مُسْتَمِرٍّ (19) تَنْزِعُ النَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ مُنْقَعِرٍ (20) فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ (21) وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ (22)}.
18. Kina 'Adi walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? 19. Hakika Sisi tuliwatumia upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo. 20. Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilivyong'olewa. 21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? 22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anayekumbuka?
#
{18 - 19} وعادٌ هي القبيلة المعروفة باليمن، أرسل الله إليهم هوداً عليه السلام يدعوهم إلى توحيد الله وعبادته، فكذَّبوه، فأرسل الله عليهم {ريحاً صرصراً}؛ أي: شديدة جدًّا. {في يوم نحسٍ}؛ أي: شديد العذاب والشقاء عليهم {مستمِّرٍ}: عليهم سبع ليال وثمانية أيام حسوماً.
{18 - 19} Adi ni kabila inayojulikana iliyokuwa ikiishi huko Yemen, kisha Mwenyezi Mungu akawatumia Nabii Hud, amani iwe juu yake, akiwalingania wampwekeshe Mwenyezi Mungu na wamuabudu, lakini wakamkadhibisha. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia "upepo wa kimbunga" mkali sana "katika siku korofi." Yaani, zenye adhabu kali na mbaya zaidi kwao "mfululizo" kwao kwa usiku saba na siku nane bila ya kusita.
#
{20} {تنزِعُ الناسَ}: من شدَّتها فترفعهم إلى جوِّ السماء، ثم تدمغهم بالأرض، فتهلكهم، فيصبحون {كأنَّهم أعجازُ نخل مُنقَعِرٍ}؛ أي: كأنَّ جثثهم بعد هلاكهم مثل جذوع النخل الخاوي الذي اقتلعتْه الريح فسقط على الأرض؛ فما أهون الخلق على الله إذا عَصَوْا أمرَه!
{20} "Ukiwang'oa watu" kwa sababu ya ukali wake, na ukiwanyanyua juu hadi angani, kisha unawapondaponda kwenye ardhi na kuwaangamiza, kisha wakaamka asubuhi "kama vigogo vya mitende vilivyong'olewa" na upepo kisha ikaanguka chini. Basi viumbe ni dhaifu zaidi vipi kwa Mwenyezi Mungu kuwaangamiza wanapoasi amri yake!
#
{21} {فكيف كان عذابي ونُذُرِ}: كان والله العذاب الأليم والنِّذارة التي ما أبقت لأحدٍ عليه حجة.
{21} "Basi ilikuwaje adhabu na maonyo yangu?" Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ilikuwa ni adhabu chungu na onyo ambalo halikumuachia yeyote hoja dhidi yake.
#
{22} {ولقد يَسَّرْنا القرآن للذِّكْر فهل من مُدَّكِرٍ}: كرَّر تعالى ذلك رحمة بعباده وعناية بهم؛ حيث دعاهم إلى ما يصلِحُ دنياهم وأخراهم.
{22} "Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anayekumbuka?" Mwenyezi Mungu Mtukufu alirudia hili kwa sababu ya rehema yake kwa waja wake na kuwajali sana; ambapo aliwaita kwa yale ambayo yanafanya dunia yao na dini yao kutengenea.
{كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ (23) فَقَالُوا أَبَشَرًا مِنَّا وَاحِدًا نَتَّبِعُهُ إِنَّا إِذًا لَفِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ (24) أَأُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِنْ بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ (25) سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَنِ الْكَذَّابُ الْأَشِرُ (26) إِنَّا مُرْسِلُو النَّاقَةِ فِتْنَةً لَهُمْ فَارْتَقِبْهُمْ وَاصْطَبِرْ (27) وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ الْمَاءَ قِسْمَةٌ بَيْنَهُمْ كُلُّ شِرْبٍ مُحْتَضَرٌ (28) فَنَادَوْا صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَى فَعَقَرَ (29) فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ (30) إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَاحِدَةً فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ (31) وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ (32)}.
23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji. 24.
Wakasema: 'Ati tumfuate binadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa! 25. Ni yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mno mwenye mshari mkubwa! 26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi. 27. Hakika Sisi tutawatumia ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame vyema tu na ustahamili. 28. Na waambie kwamba hakika maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliyehusika. 29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja. 30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu! 31. Hakika Sisi tuliwatumia ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea ua. 32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
#
{23} أي: {كذَّبت ثمودُ}: وهم القبيلة المعروفة المشهورة في أرض الحِجْر نبيَّهم صالحاً عليه السلام حين دعاهم إلى عبادة الله وحده لا شريك له، وأنذرهم العقاب إنْ هم خالفوه.
{23} Yaani, "Thamudi waliwakanusha" Mtume wao. Nao ni kaumu mashuhuri na wanaojulikana waliokuwa wakiishi katika ardhi ya Al-Hijr, na Nabii wao aliitwa Saleh, rehema na Amani zimshukie. Aliwalingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya washirika, na akawaonya kutokana na adhabu ikiwa watamuasi.
#
{24} فكذَّبوه واستكبروا عليه وقالوا كبراً وتيهاً: {أبشراً مِنَّا واحداً نَتَّبِعُهُ}؛ أي: كيف نتَّبع بشراً لا مَلَكاً، منَّا لا من غيرنا ممَّن هو أكبر عند الناس منَّا، ومع ذلك؛ فهو شخصٌ واحدٌ. {إنَّا إذاً}؛ أي: إن اتَّبعناه وهو في هذه الحالة {لفي ضلال وسُعُرٍ}؛ أي: [إنَّا] لضالُّون أشقياء. وهذا الكلام من ضلالهم وشقائهم؛ فإنهم أنِفوا أن يَتَّبِعوا رسولاً من البشر، ولم يأنفوا أن يكونوا عابدين للشجر والحجر والصُّوَر.
{24} Basi wakamkadhibisha, na wakamfanyia jeuri,
na wakasema kwa kiburi na majivuno: "Ati tumfuate binadamu mmoja katika sisi?" Yaani, vipi tutamfuata mwanadamu na si Malaika, kutoka miongoni mwetu na siyo kutoka kwa wasiokuwa sisi ambaye ni mkubwa zaidi machoni pa watu kuliko sisi, na pamoja na hayo, yeye ni mtu mmoja tu. "Basi hivyo sisi" tukimfuata hali yuko katika hali hii "tutakuwa katika upotofu na kichaa!" Maneno haya ni katika upotofu wao na usugu wao. Kwani walikataa kumfuata Mtume wa kibinadamu, na hawakukataa kuwa katika wale wanaoabudu miti, mawe na masanamu.
#
{25 - 26} {أألقي الذِّكر عليه من بيننا}؛ أي: كيف يخصُّه الله من بيننا وينزِّل عليه الذِّكر؛ فأيُّ مزيَّةٍ خصَّه من بيننا؟! وهذا اعتراضٌ من المكذِّبين على الله لم يزالوا يُدلون به ويصولون [ويحولون] ويردُّون به دعوة الرسل، وقد أجاب الله عن هذه الشبهة بقول الرسل لأممهم: {قالتْ رسُلُهم إن نحنُ إلاَّ بشرٌ مثلُكم ولكنَّ الله يَمُنُّ على مَنْ يشاءُ من عبادِه}: فالرسل مَنَّ الله عليهم بصفاتٍ وأخلاق وكمالاتٍ بها صلحوا لرسالات ربِّهم والاختصاص بوحيه، ومن رحمته وحكمته أن كانوا من البشر؛ فلو كانوا من الملائكة؛ لم يمكن البشر أن يتلقَّوا عنهم، ولو جعلَهم من الملائكة؛ لعاجل المكذِّبين لهم بالعقاب العاجل. والمقصود من هذا الكلام الصادر من ثمود لنبيِّهم صالح تكذيبه، ولهذا حكموا عليه بهذا الحكم الجائر، فقالوا: {بل هو كذَّابٌ أشِرٌ}؛ أي: كثير الكذب والشرِّ! فقبَّحهم الله ما أسفه أحلامهم وأظلمهم وأشدَّهم مقابلةً للصادقين الناصحين بالخطاب الشنيع.
{25 - 26} "Ni yeye tu aliyeteremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote?" Yaani, vipi Mwenyezi Mungu anamchangua yeye tu miongoni mwetu na kumteremshia ukumbusho? Ni sifa gani maalumu aliyo nayo inayomtofautisha na sisi? Na hili ni pingamizi kutoka kwa wale wanaomkadhibisha Mwenyezi Mungu ambalo wameendelea kulitumia na kulitetea na kukataa kwalo wito wa Mitume, lakini Mwenyezi Mungu alijibu fikira hii potofu kwa kauli ya Mitume kwa watu wao,
"Mitume wao wakawaambia: 'Sisi kweli si chochote ila ni wanadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake.'" Basi Mitume wamepewa neema na Mwenyezi Mungu za sifa, na maadili, na mambo ya ukamilifu ambayo kwayo waliufailia kufanywa kuwa mitume wa Mola wao Mlezi, na kupewa wao tu Ufunuo wake, na ni kutokana na rehema zake na hekima yake kwamba walikuwa ni wanadamu. Kama wangelikuwa katika malaika, isingekuwa rahisi kwa wanadamu kupokea kutoka kwao. Na kama angewafanya kuwa ni wa kutoka katika malaika, basi angewaharakishia wale wanaowakadhibisha adhabu. Na lengo la maneno haya yaliyotoka kwa Thamudi wakimwambia Nabii wao Saleh ni kumkadhibisha, na ndiyo maana wakamhukumu kwa hukumu hii isiyo ya haki,
wakasema: "Bali huyu ni mwongo mno mwenye mshari mkubwa!" Mwenyezi Mungu awaangamize! Ni wapumbavu namna gani hawa katika maono yao, na dhalimu wakubwa namna gani, na wabaya zaidi namna gani katika kupinga wakweli na wanyoofu kwa maneno mabaya zaidi.
#
{27} لا جرم عاقبهم الله حين اشتدَّ طغيانُهم، فأرسل الله الناقة التي هي من أكبر النعم عليهم آية من آيات الله ونعمة؛ يحلبونَ من دَرِّها ما يكفيهم أجمعين، {فتنةً لهم}؛ أي: اختباراً منه لهم وامتحاناً، {فارتَقِبْهم واصْطَبِر}؛ أي: اصبر على دعوتك إيَّاهم وارتقبْ ما يحلُّ بهم، أو ارتقبْ هل يؤمنون أو يكفُرون.
{27} Basi hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu akawaadhibu uasi wao ulipozidi kuwa mkubwa, basi Mwenyezi Mungu akawatumia ngamia jike, ambaye alikuwa neema kubwa zaidi juu yao, kuwa ni ishara ya Mwenyezi Mungu na neema; ili wakame katika maziwa yake mengi ya kuwatosha wote na ili uwe "ni mtihani kwao basi watazame vyema tu na ustahamili" katika kuwalingania kwako na ungoje yatakayowapata, au ngojea je wataamini au wataendelea kukufuru.
#
{28} {ونبِّئْهم أنَّ الماءَ قسمةٌ بينهم}؛ أي: وأخبرهم أنَّ الماء؛ أي: موردهم الذي يستعذبونه، قسمةٌ بينهم وبين الناقة، لها شِرْبُ يوم ولهم شِرْبُ يوم آخر معلوم. {كلُّ شِرْبٍ مُحْتَضَرٌ}؛ أي: يحضره من كان قسمته، ويُحْظَر على من ليس بقسمة له.
{28} "Na waambie kwamba hakika maji yatagawanywa baina yao" na ngamia jike huyo Anapata siku yake ya kunywa, nao watakunywa siku nyingine inayojulikana. "Kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliyehusika." Yaani, atayahudhuria yule ambaye ni siku yake ya kunywa, lakini atakatazwa kuyahudhuria yule ambaye si siku yake ya kunywa.
#
{29} {فنادوا صاحبَهم}: الذي باشر عقرها، الذي هو أشقى القبيلة، {فتعاطى}؛ أي: انقاد لما أمروه به من عقرها، {فعقر}.
{29} "Basi wakamwita mwenzao" yule aliyemuua, ambaye alikuwa ndiye mwovu zaidi katika kabila hilo, "basi akaja" kutekeleza yale waliyomwamrisha kwamba amchinje, naye "akamchinja."
#
{30 - 32} {فكيف كان عذابي ونُذُرِ}: كان أشدَّ عذاب، أرسل الله عليهم صيحةً ورجفةً أهلكتهم عن آخرهم، ونجَّى الله صالحاً ومَن آمن معه، {ولقد يَسَّرْنا القرآنَ للذِّكْر فهل من مُدَّكِرٍ}.
{30 - 32} "Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!" Ilikuwa ni adhabu kali kabisa, Mwenyezi Mungu akawatumia ukelele na tetemeko ambao uliwaangamiza mpaka mwisho wa wao, na Mwenyezi Mungu akamuokoa Saleh na wale walioamini. "Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye? "
{كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ بِالنُّذُرِ (33) إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبًا إِلَّا آلَ لُوطٍ نَجَّيْنَاهُمْ بِسَحَرٍ (34) نِعْمَةً مِنْ عِنْدِنَا كَذَلِكَ نَجْزِي مَنْ شَكَرَ (35) وَلَقَدْ أَنْذَرَهُمْ بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا بِالنُّذُرِ (36) وَلَقَدْ رَاوَدُوهُ عَنْ ضَيْفِهِ فَطَمَسْنَا أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ (37) وَلَقَدْ صَبَّحَهُمْ بُكْرَةً عَذَابٌ مُسْتَقِرٌّ (38) فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ (39) وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ (40)}.
33. Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji. 34. Hakika Sisi tukawatumia kimbunga cha vijiwe, isipokuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri. 35. Kwa neema inayotoka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anayeshukuru. 36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo. 37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao,
na tukawaambia: 'Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!' 38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea. 39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu! 40. Na hakika tumeisahilisha Qur-ani kuikumbuka. Lakini yupo anayekumbuka?
#
{33 - 40} أي: {كذَّبت قومُ لوط}: لوطاً عليه السلام حين دعاهم إلى عبادة الله وحده لا شريك له ونهاهم عن الشرك والفاحشة التي ما سبقهم بها أحدٌ من العالمين، فكذَّبوه واستمرُّوا على شركهم وقبائحهم، حتى إنَّ الملائكة الذين جاؤوه بصورة أضياف، حين سمع بهم قومُه؛ جاؤوا مسرعين يريدون إيقاع الفاحشة فيهم لعنهم الله وقبَّحهم وراودوه عنهم، فأمر الله جبريل عليه السلام، فطمس أعينهم بجناحه، وأنذرهم نبيُّهم بطشة الله وعقوبته، {فتمارَوْا بالنُّذُر}، {ولقد صبَّحهم بُكرةً عذابٌ مستقرٌّ}: قلب الله عليهم ديارهم، وجعل أسفلها أعلاها، وتتبَّعهم بحجارة من سِجِّيل منضودٍ مسوَّمة عند ربِّك للمسرفين، ونجَّى الله لوطاً وأهله من الكرب العظيم؛ جزاء لهم على شكرهم لربِّهم وعبادته وحدَه لا شريك له.
{33 - 40} Yaani, "Kaumu ya Lut'i nao waliwakadhibisha" Lut', amani iwe juu yake, alipowalingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika, na akawakataza shirki na uchafu ambao hapana hata mmoja katika walimwengu aliwatangulia katika hilo. Basi wakamkadhibisha na wakaendelea na ushirikina wao na maovu yao, mpaka Malaika wakamjia kwa sura ya wageni, na waliposikia watu wake kuwahusu, wakaja kwa haraka wakitaka kuwatia uchafu, Mwenyezi Mungu awalaani na awaangamize, na walimbembeleza sana ili awape wageni hao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwamuru Jibril, amani iwe juu yake, akafumba macho yao kwa bawa lake, naye Nabii wao akaendelea kuwaonya juu ya adhabu na mateso ya Mwenyezi Mungu, "lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea." Mwenyezi Mungu alipindua miji yao, akaifanya sehemu ya chini kuwa juu, na akawafuatishia mawe ya udongo mgumu uliokamatana wa Motoni, yaliyotiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanaopindukia mipaka. Na Mwenyezi Mungu akamwokoa Luti na watu wa familia yake kutokana na dhiki hiyo kubwa; ili yawe malipo kwao kwa kushukuru kwao Mola wao Mlezi na kumwabudu Yeye peke yake, bila ya mshirika.
{وَلَقَدْ جَاءَ آلَ فِرْعَوْنَ النُّذُرُ (41) كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَاهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُقْتَدِرٍ (42) أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِنْ أُولَئِكُمْ أَمْ لَكُمْ بَرَاءَةٌ فِي الزُّبُرِ (43) أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُنْتَصِرٌ (44) سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ (45) بَلِ السَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَالسَّاعَةُ أَدْهَى وَأَمَرُّ (46) إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ (47) يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَى وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ (48) إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ (49) وَمَا أَمْرُنَا إِلَّا وَاحِدَةٌ كَلَمْحٍ بِالْبَصَرِ (50) وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ (51) وَكُلُّ شَيْءٍ فَعَلُوهُ فِي الزُّبُرِ (52) وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُسْتَطَرٌ (53) إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ (54) فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيكٍ مُقْتَدِرٍ (55)}.
41. Na Waonyaji waliwajia watu wa Firauni. 42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika mshiko wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo. 43. Je, makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? 44.
Au ndiyo wanasema: 'Sisi ni wengi tutashinda tu.' 45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma. 46. Bali Saa ya Kiyama ndiyo miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi. 47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. 48.
Siku watakapokokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: 'Onjeni mguso wa Saqar!' 49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. 50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. 51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anayekumbuka? 52. Na kila jambo walilolifanya limo vitabuni. 53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa. 54. Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na mito. 55. Katika mahali pa kukalia pa haki kwa Mfalme Mwenye uweza.
#
{41 - 42} أي: {ولقد جاء آلَ فرعونَ}؛ أي: فرعون وقومه، {النُّذُرُ}: فأرسل الله إليهم موسى الكليم، وأيَّده بالآيات البيِّنات والمعجزات الباهرات، وأشهدهم من العبر ما لم يشهدْ غيرهم ، فكذَّبوا بآيات الله كلِّها، فأخذهم أخذَ عزيزٍ مقتدرٍ، فأغرقه وجنوده في اليمِّ.
{41 - 42} Yaani, "Na waliwajia watu wa Firauni waonyaji." Yaani, Mwenyezi Mungu aliwatumia Musa ambye Yeye mwenyewe alimwongelesha, na akamsaidia kwa Ishara zilizo wazi na miujiza ya kung'aa, na akawawekea ushahidi wenye mazingatio ambao hakuwawekea watu wengine wowote. Lakini wakazikanusha Ishara zote za Mwenyezi Mungu, basi akawashika kwa mshiko wa Mwenye nguvu, Mwenye uwezo, na akamzamisha yeye na askari wake baharini.
#
{43} والمراد من ذِكر هذه القصص تحذير الناس والمكذِّبين لمحمد - صلى الله عليه وسلم -، ولهذا قال: {أكفَّارُكم خيرٌ من أولئكم}؛ أي: أهؤلاء الذين كذَّبوا أفضل الرسل خيرٌ من أولئك المكذِّبين الذين ذكر الله هلاكَهم وما جرى عليهم؟ فإنْ كانوا خيراً منهم؛ أمكن أن يَنْجوا من العذاب ولم يصبهم ما أصاب أولئك الأشرار، وليس الأمر كذلك؛ فإنَّهم إن لم يكونوا شرًّا منهم؛ فليسوا بخير منهم. {أم لكم بَرَآءَةٌ في الزُّبُرِ}؛ أي: أم أعطاكم الله عهداً وميثاقاً في الكتب التي أنزلها على الأنبياء، فتعتقدون حينئذٍ أنَّكم الناجون بأخبار الله ووعده؟! وهذا غير واقع، بل غير ممكنٍ عقلاً وشرعاً أن تُكتب براءتهم في الكُتب الإلهية المتضمِّنة للعدل والحكمة؛ فليس من الحكمة نجاةُ أمثال هؤلاء المعاندين المكذِّبين لأفضل الرسل وأكرمهم على الله.
{43} Malengo ya kutaja hadithi hizi ni kuwaonya watu na wale waliomkadhibisha Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -
na ndiyo maana akasema: "Je, makafiri wenu ni bora kuliko hao?" Yaani, je, hawa waliomkanusha Mitume bora zaidi ni bora kuliko wale waliokanusha ambao Mwenyezi Mungu alitaja maangamizo yao na yaliyowasibu? Ikiwa hawa ni bora kuliko wale; basi wataweza kuokoka kutokana na adhabu na hawatakumbwa na yale yaliyowapata watu wale waovu. Lakini sivyo ilivyo. Kwani ikiwa hawa si wabaya kuliko wale, basi wao si bora kuliko wale. "au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?" Yaani, au je, Mwenyezi Mungu alikupeni ahadi na agano katika vitabu alivyoteremsha kwa Manabii, kwa hivyo mnaamini kwamba nyinyi ndio mtakaofaulu kutokana na habari alizowapa Mwenyezi Mungu na ahadi yake? Hili si jambo la kweli. Bali hata haliwezekani, kiakili na kisheria, kwamba waliandikiwa kutotiwa kwao makosani katika vitabu vya kimungu vinavyojumuisha uadilifu na hekima. Basi siyo katika hekima kuwaokoa watu kama hawa, wakaidi, wanaomkadhibisha Mitume bora zaidi na mtukufu zaidi wao kwa Mwenyezi Mungu.
#
{44} فلم يبق إلاَّ أن يكون بهم قوَّةٌ ينتصرون بها، فأخبر تعالى أنهم يقولون: {نحن جميعٌ منتصرٌ}.
{44} Basi hakikubakia isipokuwa kwamba wanao uwezo wa kushinda,
basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba watasema: "Sisi ni wengi tutashinda tu."
#
{45} قال تعالى مبيناً لضعفهم وأنهم مهزومون: {سيُهْزَمُ الجمعُ ويولُّون الدُّبُرَ}: فوقع كما أخبر؛ هزم الله جمعهم الأكبر يوم بدرٍ، وقُتلت صناديدُهم وكبراؤهم، فأذلُّوا ، ونصر الله دينه ونبيَّه وحزبه المؤمنين.
{45} Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibainisha udhaifu wao na kwamba watashindwa: "Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma." Basi ikawa kama alivyojulisha. Mwenyezi Mungu alilishinda kundi lao kubwa siku ya Badr, na vigogo wao na viongozi wao wakauawa, wakafedheheshwa, na Mwenyezi Mungu akaishinda dini yake, Nabii wake, na kundi lake la Waumini.
#
{46} ومع ذلك؛ فلهم موعدٌ يجمع به أولهم وآخرهم ومن أصيب في الدُّنيا منهم ومن متع بلذاته، ولهذا قال: {بل الساعةُ موعدُهم}: الذي يجازون به ويؤخذ منهم الحقُّ بالقسط، {والساعةُ أدهى وأمرُّ}؛ أي: أعظم وأشقُّ وأكبر من كلِّ ما يتوهَّم أو يدور في الخيال.
{46} Hata hivyo, wanayo miadi ambayo kwayo watakusanywa wa mwanzo wao na wa mwisho wao, na aliyefikwa na msiba miongoni mwao katika dunia na aliyestareheshwa kwa anasa zake,
na ndiyo maana akasema: "Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao" ambayo watalipwa wakati huo, na itachukuliwa haki kutoka kwao kwa uadilifu. "Na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi" kuliko kitu chochote kinachofikiriwa au kinachozunguka katika mawazo.
#
{47} {إنَّ المجرمينَ}؛ أي: الذين أكثروا من فعل الجرائم، وهي الذنوب العظيمة؛ من الشرك وغيره من المعاصي {في ضلال وسُعُرٍ}؛ أي: هم ضالُّون في الدُّنيا، ضُلاَّلٌ عن العلم وضُلاَّلٌ عن العمل الذي ينجِّيهم من العذاب، ويوم القيامةِ في العذاب الأليم والنار التي تستعر بهم وتشتعل في أجسامهم حتى تبلغ أفئدتهم.
{47} "Hakika wakosefu" waliofanya madhambi mengi makubwa ya ushirikina na madhambi mengineyo "wamo katika upotofu na wazimu." Yaani, wamepotea katika dunia hii, wamepotea mbali na elimu na kufanya matendo ya kuwaepusha na adhabu, na Siku ya Kiyama watakuwa katika adhabu chungu na Moto utakaowaka kwa ukali juu yao na kuwaunguza katika miili yao mpaka ufikie mioyo yao.
#
{48} {يوم يُسْحَبون في النار على وجوهِهِم}: التي هي أشرف ما بهم من الأعضاء، وألمها أشدُّ من [أَلَمِ] غيرها، فيُهانون بذلك ويُخْزَون، ويقال لهم: {ذوقوا مَسَّ سَقَرَ}؛ أي: ذوقوا ألم النار وأسفها وغيظها ولهبها.
{48} "Siku watakapokokotwa Motoni kifudifudi waambiwe." Yaani, kwa uso wao ambao ndiyo sehemu tukufu zaidi katika viungo vyao, na maumivu yake ni makali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote. Basi wakawa wanadhalilishwa na kutiwa hizaya kwa kufanyiwa hivyo,
na wataambiwa: "Onjeni mguso wa Saqar." Yaani, onja uchungu, huzuni, ghadhabu, na mwako mkali wa moto.
#
{49} {إنَّا كلَّ شيءٍ خَلَقْناه بقدرٍ}: وهذا شاملٌ للمخلوقات والعوالم العلويَّة والسفليَّة؛ إنَّ الله تعالى وحدَه خلَقَها، لا خالق لها سواه، ولا مشارك له في خلقه ، وخلقها بقضاءٍ سبق به علمُه وجرى به قلمُه بوقتها ومقدارها، وجميع ما اشتملت عليه من الأوصاف.
{49} "Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo." Hili linajumuisha viumbe vyote na walio katika ulimwengu wa juu na wa chini. Hakika Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliyeviumba, hakuna muumba mwingine isipokuwa Yeye, na hana mshirika katika uumbaji wake. Aliwaumba kwa mipango aliyoijua kabla na kalamu yake ikaiandika kwamba itatokea wakati gani na kwa kiasi gani, na maelezo yake yote.
#
{50} وذلك على الله يسيرٌ؛ فلهذا قال: {وما أمرُنا إلاَّ واحدةٌ كلمحٍ بالبصرِ}: فإذا أراد شيئاً؛ قال له: كن فيكونُ؛ كما أراد؛ كلمح البصر؛ من غير ممانعةٍ ولا صعوبةٍ.
{50} Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Ndiyo maana akasema: "Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho." Basi akitaka kitu,
anakiambia tu: 'Kuwa' na kinakuwa kama alivyotaka; kama vile kupepesa kwa jicho, bila kukataa wala shida yoyote.
#
{51} {ولقد أهْلَكْنا أشياعَكم}: من الأمم السابقين، الذين عملوا كما عملتُم وكذَّبوا كما كذَّبتم، {فهل من مُدَّكِرٍ}؛ أي: متذكِّر يعلم أن سنَّة الله في الأولين والآخرين واحدةٌ، وأن حكمتَه كما اقتضت إهلاك أولئك الأشرار فإنَّ هؤلاء مثلهم، ولا فرق بين الفريقين.
{51} "Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu" katika mataifa yaliyotangulia, waliofanya kama mlivyofanya, na wakakadhibisha kama mlivyokadhibisha, "lakini yupo anayekumbuka" na kujua kwamba desturi ya Mwenyezi Mungu katika wale wa kwanza na wa mwisho ni ile ile, na kwamba hekima yake kama ilivyohitaji kwamba waangamizwe watu wale waovu, basi hakika hawa ni sawa na wale, wala hakuna tofauti yoyote baina ya vikundi viwili hivi.
#
{52} {وكلُّ شيءٍ فعلوه في الزُّبر}؛ أي: كل ما فعلوه من خيرٍ وشرٍّ مكتوبٌ عليهم في الكتب القدريَّة.
{52} "Na kila jambo walilolifanya limo vitabuni." Yaani, kila walichofanya, kiwe chema au kibaya, waliandikiwa katika vitabu vya mipango ya Mwenyezi Mungu.
#
{53} {وكلُّ صغيرٍ وكبيرٍ مُسْتَطَرٌ}؛ أي: مسطَّرٌ مكتوبٌ، وهذه حقيقة القضاء والقدر، وأنَّ جميع الأشياء كلها قد علمها الله تعالى وسطرها عنده في اللوح المحفوظ؛ فما شاء الله كان، وما لم يشأ لم يكنْ؛ فما أصاب الإنسان لم يكن ليخطِئَه، وما أخطأه لم يكن ليصيبَه.
{53} "Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa." Huu ndio uhakika wa mipango na mapitisho ya Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu alikwisha jua vitu vyote na kuandikwa vyote kwake katika Ubao Uliohifadhiwa. Basi chochote ambacho Mwenyezi Mungu anataka, kinafanyika. Na kile ambacho hakitaki, hakifanyiki. Kwa hivyo, lolote linalompata mtu, halikuwa ni la kumkosa. Na lolote lililomkosa, halikuwa ni la kumpata.
#
{54 - 55} {إنَّ المتَّقين}: لله بفعل أوامره وترك نواهيه، الذين اتَّقوا الشرك والكبائر والصغائر {في جناتٍ ونَهَرٍ}؛ أي: في جنات النعيم، التي فيها ما لا عين رأت ولا أذن سمعت ولا خطر على قلب بشر؛ من الأشجار اليانعة، والأنهار الجارية، والقصور الرفيعة، والمنازل الأنيقة، والمآكل والمشارب اللذيذة، والحور الحسان، والروضات البهية في الجنان، ورضا الملك الدَّيَّان والفوز بقربه، ولهذا قال: {في مقعدِ صدقٍ عند مليكٍ مقتدرٍ}؛ فلا تسأل بعد هذا عما يعطيهم ربُّهم من كرامته وجوده ويمدُّهم به من إحسانه ومنَّته! جعلنا الله منهم، ولا حرمنا خير ما عنده بشرِّ ما عندنا.
{54 - 55} "Hakika wacha Mungu" waliokuwa wakifanya maamrisho yake na kuacha makatazo yake, wale waliojiepusha na ushirikina na madhambi makubwa na madogo "watakuwa katika Mabustani na mito" yenye neema. Ambazo ndani yake kuna yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala moyo wa mwanadamu yeyote haujawahi kuyafikiria. Na ndani yake pia kuna miti yenye majani mabichi na matunda, na mito inayotiririka, na makasri yaliyoinuka juu, na majumba mazuri mazuri, na vyakula na vinywaji vitamu, mahurulaini wazuri, na makonde yenye urembo Peponi, na radhi za Mfalme, Mlipaji, na kufaulu kuwa karibu naye,
na ndiyo maana akasema: "Katika mahali pa kukalia pa haki kwa Mfalme Mwenye uwezo." Basi hata usiulize baada ya haya yale atakayowapa Mola wao Mlezi katika utukufu wake na utoaji wake kwa wingi, na kuwazidishia wema wake na neema yake. Mwenyezi Mungu atufanye miongoni mwao, wala asitunyime heri aliyo nayo kwa ubaya wa yale tuliyo nayo.
Imekamilika tafsiri ya Sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
******