Ilishuka Makka
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
{وَالطُّورِ (1) وَكِتَابٍ مَسْطُورٍ (2) فِي رَقٍّ مَنْشُورٍ (3) وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ (4) وَالسَّقْفِ الْمَرْفُوعِ (5) وَالْبَحْرِ الْمَسْجُورِ (6) إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَاقِعٌ (7) مَا لَهُ مِنْ دَافِعٍ (8) يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا (9) وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا (10) فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِلْمُكَذِّبِينَ (11) الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ (12) يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَى نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا (13) هَذِهِ النَّارُ الَّتِي كُنْتُمْ بِهَا تُكَذِّبُونَ (14) أَفَسِحْرٌ هَذَا أَمْ أَنْتُمْ لَا تُبْصِرُونَ (15) اصْلَوْهَا فَاصْبِرُوا أَوْ لَا تَصْبِرُوا سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (16)}.
1. Ninaapa kwa mlima wa T'ur. 2. Na Kitabu kilichoandikwa. 3. Katika ngozi iliyokunjuliwa. 4. Na kwa Nyumba iliyojengwa. 5. Na kwa dari iliyonyanyuliwa. 6. Na kwa bahari iliyojazwa. 7. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea. 8. Hapana wa kuizuia. 9. Siku zitakapotikisika mbingu kwa mtikiso. 10. Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa. 11. Basi ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha. 12. Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi. 13. Siku watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu. 14.
(Waambiwe): Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukadhibisha! 15. Je, huu ni uchawi, au hamwoni tu? 16. Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyokuwa mkiyatenda.
#
{1} يقسم تعالى بهذه الأمور العظيمة المشتملة على الحِكَم الجليلة على البعث والجزاء للمتَّقين وللمكذِّبين ، فأقسم بالطور، وهو الجبلُ الذي كلَّم الله عليه موسى بن عمران عليه الصلاة والسلام، وأوحى إليه ما أوحى من الأحكام، وفي ذلك من المنَّة عليه وعلى أمَّته ما هو من آيات الله العظيمة ونعمه التي لا يَقْدِرُ العباد لها على عدٍّ ولا ثمن.
{1} Mwenyezi Mungu Mtukufu anaapa kwa mambo haya mkubwa ambayo yanajumuisha hekima tukufu katika suala la kufufuliwa na malipo kwa wacha Mungu na wakanushaji. Basi akaapa kwa At-Tur, ambao ni mlima ule ambapo Mwenyezi Mungu alizungumzisha Musa bin Imran, amani iwe juu yake, na akamteremshia yale aliyoyateremsha miongoni mwa hukumu. Na katika hilo kuna kujulisha juu ya neema ya Mwenyezi Mungu juu yake na juu ya umma wake, na ni katika ishara na neema kubwa za Mwenyezi Mungu ambazo waja wake hawawezi kuzihesabu wala kujua vyema thamani yake.
#
{2} {وكتابٍ مسطورٍ}: يُحتمل أنَّ المراد به اللوحُ المحفوظ، الذي كتب الله به كلَّ شيءٍ، ويُحتمل أنَّ المراد به القرآن الكريم، الذي هو أفضل الكتب ، أنزله الله محتوياً على نبأ الأوَّلين والآخرين وعلوم السَّابقين واللاحقين.
{2} "Na kitabu kilichoandikwa." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni Ubao Uliohifadhiwa ambao Mwenyezi Mungu aliandika kila kitu ndani yake, na inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni Qur-ani Tukufu ambayo ndiyo kitabu bora zaidi, ambacho Mwenyezi Mungu alikiteremsha huku kikijumuisha habari za wa mwanzo na wa mwisho, na elimu za waliotangulia na waliofuatia baadaye.
#
{3} وقوله: {في رَقٍّ}؛ أي: ورقٍ {منشورٍ}؛ أي: مكتوبٍ، مسطرٍ، ظاهرٍ غير خفيٍّ، لا تخفى حالُه على كلِّ عاقل بصيرٍ.
{3} Na kauli yake: "Katika ngozi iliyokunjuliwa." Yaani, iliyoandikwa na iliyo dhahiri, isiyofichika hali yake kwa kila mtu mwenye akili na utambuzi.
#
{4} {والبيت المعمورِ}: وهو البيتُ الذي فوق السماء السابعة، المعمور مدى الأوقات بالملائكة الكرام، [الذي] يدخُله كلُّ يوم سبعون ألف مَلَك، يتعبَّدون فيه لربِّهم، ثمَّ لا يعودون إليه إلى يوم القيامةِ، وقيل: إنَّ البيت المعمور هو بيت الله الحرام المعمور بالطائفين والمصلِّين والذَّاكرين كلَّ وقت وبالوفود إليه بالحجِّ والعمرة؛ كما أقسم الله به في قوله: {وهذا البلدِ الأمين}، وحقيقٌ ببيت هو أفضل بيوت الأرض، الذي يَقْصِدُه الناس بالحجِّ والعمرة، أحد أركان الإسلام ومبانيه العظام، التي لا يتمُّ إلاَّ بها، وهو الذي بناه إبراهيمُ وإسماعيلُ، وجعله الله مثابةً للناس وأمناً؛ أنْ يُقْسِمَ الله به، ويبيِّن من عظمته ما هو اللائقُ به وبحرمته.
{4} "Na kwa Nyumba iliyojengwa." Nayo ni Nyumba iliyo juu ya mbingu ya saba inayokaliwa daima na Malaika watukufu, ambayo huingiwa na Malaika elfu sabini kila siku, wakimuabudu humo Mola wa Mlezi, kisha hawarudi humo mpaka Siku ya Kiyama. Na imesemekana kwamba Al-Bayt Al-Ma'mur ni nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu
(ya Makka), ambayo hujawa na wanaozunguka Tawafu, wanaoswali , na wanaomtaja Mola kila wakati, na wanaomjia kwa ajili ya Hija na Umra.
Kama vile Mwenyezi Mungu alivyoapa kwayo katika kauli yake: "Na kwa mji huu wenye amani!" Basi inafilia zaidi kuapiwa na kubainishwa ukuu wake unaoifailia na utukufu wake nyumba iliyo bora kabisa miongoni mwa nyumba zilizo katika ardhi - ambayo wanaikusudia watu kwa ajili ya kufanya Hija na Umra, mojawapo ya nguzo za Uislamu na majengo yake makubwa, ambayo haukamiliki Uisilamu bila ya hiyo, na ndiyo iliyojengwa na Ibrahim na Ismail, na Mwenyezi Mungu akapafanya ni pahali pa kukusanyikia watu na pahala pa amani.
#
{5} {والسقفِ المرفوع}؛ أي: السماء التي جعلها الله سقفاً للمخلوقات وبناءً للأرض تستمدُّ منها أنوارها، ويُقتدى بعلاماتها ومنارها، ويُنْزِلُ اللهُ منها المطر والرحمة وأنواع الرزق.
{5} "Na kwa dari iliyonyanyuliwa." Yaani, mbingu ambayo Mwenyezi Mungu aliifanya kuwa paa kwa ajili ya viumbe na jengo kwa ajili ya ardhi ambayo inapata nuru kwayo, na watu wanaongoka kwa alama zake, na Mwenyezi Mungu huteremsha kutoka huko mvua, rehema, na aina mbalimbali za riziki.
#
{6} {والبحر المَسْجورِ}: أي: المملوء ماءً، قد سجره الله ومنعه من أن يَفيضَ على وجه الأرض، مع أنَّ مقتضى الطبيعة أن يغمرَ وجه الأرض، ولكنَّ حكمته اقتضت أن يمنعه عن الجريان والفيضان؛ ليعيش مَنْ على وجه الأرض من أنواع الحيوان. وقيل: إنَّ المراد بالمسجور: الموقَد، الذي يوقَدُ ناراً يوم القيامةِ، فيصير ناراً تَلَظَّى، ممتلئاً على سعته من أصناف العذاب.
{6} "Na kwa bahari iliyojazwa" maji, ambayo Mwenyezi Mungu ameijaza na akaizuia isifurike juu ya uso wa ardhi, ijapokuwa kulingana na maumbile ya asili hilo linahitaji kwamba yamiminike kwa wingi juu ya uso wa ardhi, lakini hekima yake ilihitaji kwamba ayazuie kutiririka na kufurika; ili kila aina ya mnyama waweze kuishi juu ya uso wa ardhi. Na ilisemekana kwamba maana ya “masjuur” ni iliyoashwa moto. Yaani, itawashwa moto Siku ya Kiyama, iwe moto wenye mwako mkali, ijae pamoja na upana wake kila aina ya adhabu.
#
{7} هذه الأشياء التي أقسم الله بها ممَّا يدلُّ على أنَّها من آيات الله وأدلَّة توحيده وبراهين قدرته وبعثه الأموات، ولهذا قال: {إنَّ عذابَ ربِّك لواقعٌ}؛ أي: لابدَّ أن يقع، ولا يخلفُ اللهُ وعده وقيله.
{7} Haya ni mambo aliyoapa kwayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa yale yanayoashiria ya kwamba ni miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu na ushahidi wa upweke wake na hoja za uwezo wake na kufufuwa kwake wafu,
basi ndiyo maana akasema: "Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea" na Mwenyezi Mungu huwa havunji ahadi yake na maneno yake.
#
{8} {ما له من دافع}: يدفعُه، ولا مانع يمنعُه، لأنَّ قدرة الله لا يغالبها مغالبٌ ولا يفوتها هاربٌ.
{8} "Hapana wa kuizuia" atakayeweza kuizuia, kwa sababu uwezo wa Mwenyezi Mungu hauwezi kushindwa na mshindi yeyote, wala hawezi kuukwepa mwenye kukimbia.
#
{9} ثم ذكر وصفَ ذلك اليوم الذي يقع فيه العذابُ، فقال: {يوم تمورُ السَّماء مَوْراً}؛ أي: تدور السماء وتضطرب وتدوم حركتها بانزعاج وعدم سكونٍ.
{9} Kisha akataja maelezo ya siku hiyo ambayo adhabu itatokea,
akasema: "Siku zitakapotikisika mbingu kwa mtikiso" pamoja na kuzunguka kwa harakati za usumbufu bila ya utulivu.
#
{10} {وتسير الجبالُ سيراً}؛ أي: تزولُ عن أماكنها، وتسير كسير السحاب، وتتلوَّن كالعهن المنفوش، وتبثُّ بعد ذلك حتى تصير مثل الهباء، وذلك كلُّه لعظم هول يوم القيامةِ؛ [وفظاعة ما فيه من الأمور المزعجة والزلازل المقلقة التي أزعجت هذه الأجرام العظيمة] فكيف بالآدميِّ الضعيف؟!
{10} "Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa." Yaani, itatoka mahali pake, na zitakwenda mwendo wa mawingu, na watakuwa na rangi kama ya sufu zilizochambuliwa, kisha baadaye zitatupwa na kusambaa hadi ziwe kama chembechembe ndogo za vumbi, na hayo yote ni kutokana na ukubwa wa balaa ya Siku ya Kiyama
[na ubaya mkubwa wa mambo yaliyo ndani yake ya kutisha na mitetemeko itakayosumbua miili hii mikubwa] basi itakuwaje kuhusu mwanadamu dhaifu?
#
{11} {فويلٌ يومئذٍ للمكذِّبين}: والويل كلمةٌ جامعةٌ لكلِّ عقوبةٍ وحزنٍ وعذابٍ وخوفٍ.
{11} "Basi ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha." Na hili neno linajumuisha kila mateso, huzuni, adhabu na hofu.
#
{12} ثم ذَكَرَ وصفَ المكذِّبين، الذين استحقُّوا به الويل، فقال: {الذين هم في خَوْضٍ يلعبون}؛ أي: خوض بالباطل ولعب به؛ فعلومُهم وبحوثهم بالعلوم الضارَّة المتضمِّنة للتكذيب بالحقِّ والتصديق بالباطل، وأعمالُهم أعمال أهل الجهل والسَّفَه واللعب؛ بخلاف ما عليه أهل التصديق والإيمان من العلوم النافعة والأعمال الصالحة.
{12} Kisha akataja maelezo ya wakanushaji ambayo kwayo walistahiki adhabu hiyo,
akasema: "Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi." Basi elimu zao na tafiti zao ni katika elimu zenye madhara ambazo zinajumuisha kukadhibisha haki na kusadiki batili, na matendo yao ni matendo ya watu wa ujinga, upumbavu na mchezo, kinyume na waliyo nayo watu wasadikishao na kuamini wenye elimu zenye manufaa na matendo mema.
#
{13 - 14} {يومَ يُدَعُّونَ إلى نار جهنَّم دعاً}؛ أي: [يوم] يُدفعون إليها دفعاً، ويساقون إليها سوقاً عنيفاً، ويجرون على وجوههم، ويُقال لهم توبيخاً ولوماً: {هذه النارُ التي كنتمُ بها تكذِّبون}: فاليوم ذوقوا عذابَ الخُلد الذي لا يُبْلَغُ قدرهُ ولا يوصَفُ أمره.
{13 - 14} "Siku watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu" na wataburutwa kifudifudi,
na wataambiwa kwa kemeo na lawama: "Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukadhibisha!" Basi leo onjeni adhabu ya milele ambayo hakiwezi kufikiwa kiasi chake wala kuelezewa jambo zake.
#
{15} {أفسحرٌ هذا أم أنتم لا تُبصرونَ}: يُحتمل أنَّ الإشارة إلى النار والعذاب؛ كما تدلُّ عليه سياق الآيات ؛ أي: لما رأوا النار والعذاب؛ قيل لهم من باب التقريع: أهذا سحرٌ لا حقيقة له؛ فقد رأيتموه؟! أم أنتم في الدُّنيا لا تبصرون؛ أي: لا بصيرة لكم ولا علم عندَكم، بل كنتُم جاهلين بهذا الأمر، لم تقمْ عليكم الحجَّة؟! والجواب انتفاء الأمرين: أمَّا كونُه سحراً؛ فقد ظهر لهم أنَّه أحقُّ الحقِّ وأصدق الصدق المنافي للسحر من جميع الوجوه. وأمَّا كونُهم لا يبصرون؛ فإنَّ الأمر بخلاف ذلك، بل حجَّة الله قد قامت عليهم، ودعتهُمُ الرُّسل إلى الإيمان بذلك، وأقامت من الأدلَّة والبراهين على ذلك ما يجعله من أعظم الأمور المبرهَنَة الواضحة الجليَّة.
ويُحتمل أنَّ الإشارة بقولِهِ: {أفسحرٌ هذا أم أنتُم لا تبصرونَ}: إلى ما جاء به محمدٌ - صلى الله عليه وسلم - من الحقِّ المبين والصراط المستقيم؛ أي: أفيتصوَّر مَن له عقلٌ أن يقولَ عنه: إنَّه سحرٌ، وهو أعظم الحقِّ وأجلُّه، ولكن لعدم بصيرتهم قالوا فيه ما قالوا.
{15} "Je, huu ni uchawi au hamuoni tu?" Inawezekana kwamba kilichoashiriwa hapa ni Moto na adhabu. Kama linavyoonyeshwa hilo na muktadha wa aya hii. Yaani,
walipouona moto na adhabu; waliambiwa haya kwa njia ya kuwafokea: Je, huu ni uchawi ambao hauna uhakika wowote? Basi tayari mmeshauona? Au mlikuwa hamuoni katika dunia? Wala hamkuwa na ufahamu wala elimu. Bali mlikuwa mkilifanyia ujinga jambo hili, na hakuna hoja iliyothibiti juu yenu?! Na jibu la hayo ni kwamba mambo hayo yote mawili hayapo. Ama kuwa kwake uchawi; Basi imeshawadhihirikia kwamba hilo ndiyo haki ya haki zote na ukweli wa ukweli wote unaopingana na uchawi kwa njia zote. Ama kuhusu kwamba hawaoni; basi hakika jambo hili ni kinyume na hivyo, bali hoja ya Mwenyezi Mungu ilithibiti dhidi yao, na Mitume wakawalingania kuamini jambo hilo, na wakasimamisha ushahidi mbalimbali na hoja juu ya hilo mambo yanayolifanya suala hili kuwa ndilo jambo lenye ushidi mkubwa zaidi, lililo wazi kabisa. Inawezekana kwamba yaliyoashiriwa kwa kauli yake Mwenyezi Mungu "Je, huu ni uchawi, au hamwoni tu?" Ni yale aliyokuja nayo Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – ya haki iliyo wazi na njia iliyonyooka. Yaani, je, inawezekana kwa mwenye akili timamu kusema juu yake kwamba hayo ni uchawi, ilhali hayo ndiyo kweli kubwa kabisa na uliotukuka zaidi, lakini kwa sababu ya kukosa kwao utambuzi, wakasema waliyoyasema juu yake?
#
{16} {اصْلَوْها}؛ أي: ادخلوا النار على وجهٍ تحيطُ بكم وتشملُ أبدانكم وتطَّلع على أفئدتكم، {فاصْبِروا أو لا تصبروا سواءٌ عليكم}؛ أي: لا يفيدكم الصبر على النار شيئاً، ولا يتأسَّى بعضُكم ببعض، ولا يخفَّف عنكم العذاب، وليست من الأمور التي إذا صبر العبدُ عليها هانت مشقَّتها وزالت شدَّتها، وإنَّما فُعِلَ بهم ذلك بسبب أعمالهم الخبيثة وكسبهم، ولهذا قال: {إنَّما تُجْزَوْن ما كنتم تعملونَ}.
{16} "Uingieni." Yaani, ingieni Motoni kwa namna itakayowazingira, na kugubika miili yenu, na kuzifikia nyoyo zenu "Mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu." Kwani kustahmili juu ya Moto huo hakutowafaa chochote, wala hamtaliwazana nyinyi kwa nyinyi, wala hamtahafifishiwa adhabu, na hata siyo katika mambo ambayo akistamihili mja juu yake, itapungua taabu yake na kuondoka ukali wake. Na kwa hakika walifanyiwa hivyo kwa sababu ya matendo yao maovu na yale waliyochuma, nasi ndiyo maana akasema, "Hakika mnalipwa kwa mliyokuwa mkiyatenda."
{إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَعِيمٍ (17) فَاكِهِينَ بِمَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَاهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ (18) كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ (19) مُتَّكِئِينَ عَلَى سُرُرٍ مَصْفُوفَةٍ وَزَوَّجْنَاهُمْ بِحُورٍ عِينٍ (20)}.
17. Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na neema. 18. Wakifurahi kwa yale aliyowapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni. 19. Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyokuwa mkiyatenda. 20. Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyopangwa kwa safu. Na tutawaoza mahurulaini.
#
{17} لمَّا ذكر تعالى عقوبة المكذِّبين؛ ذكر نعيم المتَّقين؛ ليجمع بين الترغيب والترهيب، فتكون القلوبُ بين الخوف والرجاء، فقال: {إنَّ المتَّقين}: لربِّهم، الذين اتَّقوا سخطه وعذابه بفعل أسبابه من امتثال الأوامر واجتناب النواهي، {في جنَّاتٍ}؛ أي: بساتين، قد اكتست رياضها من الأشجار الملتفَّة والأنهار المتدفِّقة والقصور المُحْدِقة والمنازل المُزَخْرَفة، {ونعِيمٍ}: وهذا شاملٌ لنعيم القلب والروح والبدن.
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoitaja adhabu ya wale wanaokanusha, akataja pia neema za wacha Mungu; Ili ajumuishe kati ya kutia moyo na kutishia, ili nyoyo ziwe baina ya hofu na matumaini,
akasema: "Hakika wacha Mungu" wanaomcha Mola wao Mlezi, wale wanaoiogopa ghadhabu yake na adhabu yake kwa kutekeleza visababu vyake kama vile kujiepusha na makatazo, "watakuwa katika Mabustani" yenye miti iliyoshikana, na mito ibubujikayo, na makasri na majumba yaliyopambwa "na neema." Hili linajumuisha ya moyo, nafsi na mwili.
#
{18} {فاكهين بما آتاهم ربُّهم}؛ أي: معجبين به، متمتِّعين على وجه الفرح والسرور بما أعطاهم الله من النعيم الذي لا يمكن وصفُه، و {لا تعلمُ نفسٌ ما أُخْفِيَ لهم من قرَّةِ أعينٍ}، {ووقاهم ربُّهم عذابَ الجحيم}: فرزقهم المحبوب، ونجَّاهم من المرهوب، لمَّا فعلوا ما أحبَّه [اللَّهُ] وجانبوا ما يسخطه.
{18} "Wakifurahi kwa yale aliyowapa Mola wao Mlezi" ya neema ambayo haiwezekani kuzielezea, na "Nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho." Kisha akasema, "Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni." Basi akawa amewaruzuku yale wanayoyapenda, na akawaokoa kutokana na yale wanayoyahofu, pindi walipofanya yale anayoyapenda "Mwenyezi Mungu" na wakajiepusha na yale yanayomghadhibisha.
#
{19} {كلوا واشربوا}؛ أي: مما تشتهيه أنفسكم من أصناف المآكل والمشارب اللذيذة {هنيئاً}؛ أي: متهنِّئين بذلك على وجه البهجة والفرح والسرور والحبور، {بما كنتُم تعملون}؛ أي: نلتم ما نلتم بسبب أعمالكم الحسنة وأقوالكم المستحسنة.
{19} "Kuleni na kunyweni." Yaani, chochote kinachotamaniwa na nafsi zenu katika vyakula na vinywaji vitamu "kwa raha kabisa." Yaani, wakijipongeza kwa hilo kwa njia ya bashasha, furaha, raha na shangwe, "kwa sababu ya mliyokuwa mkiyatenda." Yaani, mumepata hayo mliyoyapata kwa sababu ya matendo yenu mema na maneno yenu mazuri.
#
{20} {متَّكِئينَ على سررٍ مصفوفةٍ}: الاتِّكاء هو الجلوس على وجه التمكُّن والراحة والاستقرار، والسرر هي الأرائك المزيَّنة بأنواع الزينة من اللباس الفاخر والفرش الزاهية. ووصف الله السُّرر بأنها مصفوفةٌ؛ ليدلَّ ذلك على كثرتها وحسن تنظيمها واجتماع أهلها وسرورهم بحسن معاشرتهم وملاطفة بعضهم بعضاً. فلمَّا اجتمع لهم من نعيم القلب والرُّوح والبدن ما لا يخطُرُ بالبال ولا يدور في الخيال من المآكل والمشارب اللذيذة والمجالس الحسنة الأنيقة؛ لم يبق إلاَّ التمتُّع بالنساء اللاتي لا يتمُّ سرورٌ إلاَّ بهنَّ، فذكر تعالى أنَّ لهم من الأزواج أكمل النساء أوصافاً وخلقاً وأخلاقاً، ولهذا قال: {وزوَّجْناهم بحورٍ عينٍ}: وهنَّ النساء اللواتي قد جَمَعْنَ جمال الصورة الظاهرة وبهاءها ومن الأخلاق الفاضلة ما يوجب أن يحيِّرْنَ بحسنهنَّ الناظرين، ويسلبنَ عقول العالمين، وتكاد الأفئدة أن تطير شوقاً إليهن ورغبةً في وصالهنَّ، والعِيْن: حسان الأعين مليحاتها، التي صفا بياضها وسوادها.
{20} "Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyopangwa kwa safu." Na Mwenyezi Mungu amevielezea viti hivyo kwamba vilipangwa kwa safu ili hilo liashirie wingi wake, na uzuri wa mpangilio wake na mkusanyiko wa watu wake, na furaha yao kwa sababu ya kuishi kwao pamoja kwa uzuri, na kufanyiana kwao upole. Wakati furaha ya moyo, nafsi, na mwili ilipokusanyika kwa ajili yao, kutokana na yale yasiyofikirika akilini wala hata kuzunguka mawazani kama vile chakula kitamu na vinywaji, na mahali pa kukaa pazuri na ya kifahari, halikubakia lolote ila kustareheshwa kwa wanawake ambao kwamba haitimii furaha isipokuwa kwa hao. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja kwamba wana wake wakamilifu katika sifa zao, maumbile yao na maadili yao,
na ndiyo maana akasema: "Na tutawaoza mahurulaini." Nao ni wanawake ambao wamekusanya uzuri wa sura ya nje na pamoja uzuri wake mkubwa, na ni wenye tabia njema ambayo kwayo inasababisha kuwachanganya wenye kutazama kwa sababu ya uzuri wake, na kukanganya akili za walimwengu, na mioyo inakaribia kuruka kwa hamu kubwa ya kuwataka na kuwafikia. Nao ni wenye macho mazuri yenye weupe na weusi uliobanika wazi.
{وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُمْ بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُمْ مِنْ عَمَلِهِمْ مِنْ شَيْءٍ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ (21) وَأَمْدَدْنَاهُمْ بِفَاكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِمَّا يَشْتَهُونَ (22) يَتَنَازَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ (23) وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَكْنُونٌ (24) وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ (25) قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ (26) فَمَنَّ اللَّهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ (27) إِنَّا كُنَّا مِنْ قَبْلُ نَدْعُوهُ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ (28)}.
21. Na wale walioamini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani, tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alichokichuma. 22. Na tutawapa matunda, na nyama kama watakavyopenda. 23. Watapeana humo bilauri zisizo na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi. 24. Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza. 25. Wataelekeana wakiulizana. 26.
Waseme: Hakika tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa mno. 27. Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda mbali adhabu ya upepo wa Moto. 28. Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwingi wa kurehemu.
#
{21} وهذا من تمام نعيم [أهلِ] الجنَّة: أنْ ألحَقَ الله بهم ذُرِّيَّتهم الذين اتَّبعوهم بإيمان؛ أي: لحقوهم بالإيمان الصادر من آبائهم، فصارت الذُّرِّية تبعاً لهم بالإيمان، ومن باب أولى؛ إذا تبعتهم ذُرِّيَّتهم بإيمانهم الصادر من أنفسهم؛ فهولاء المذكورون يُلْحِقُهُمُ اللهُ بمنازل آبائهم في الجنة، وإن لم يبلغوها؛ جزاءً لآبائهم، وزيادةً في ثوابهم، ومع ذلك؛ لا يَنْقُصُ اللهُ الآباء من أعمالهم شيئاً. ولمَّا كان ربَّما توهَّم متوهِّم أن أهل النار كذلك يُلْحِقُ اللهُ بهم ذرِّيَّتهم ؛ أخبر أنه ليس حكم الدارين حكماً واحداً؛ فإنَّ النار دار العدل، ومن عدله تعالى أن لا يعذِّب أحداً إلاَّ بذنبٍ، ولهذا قال: {كلُّ امرئٍ بما كَسَبَ رهينٌ}؛ أي: مرتهنٌ بعمله؛ فلا تزر وازرةٌ وزرَ أخرى، ولا يُحْمَلُ على أحدٍ ذنبُ أحدٍ، فهذا اعتراضٌ من فوائده إزالة هذا الوهم المذكور.
{21} Na hii ni miongoni mwa mambo yanayokamilisha neema za wana Peponi: kwamba Mwenyezi Mungu atawakutanisha na dhuria zao waliowafuata kwa Imani. Yaani, waliwafuata katika imani iliyotoka kwa baba zao. Kwa hivyo kizazi kikawa wafuasi wao katika imani, na muhimu zaidi ni ikiwa vizazi vyao vitawafuata kwa imani yao inayotokana na wa wenyewe. Watu hawa waliotajwa Mwenyezi Mungu atawakutanisha na vyeo vya baba zao Peponi, hata kama hawakuvifikia; yawe kama malipo kwa baba zao, na nyongeza ya ujira wao. Na pamoja na hayo Mwenyezi Mungu hatawapunguzia akina baba zao chochote katika matendo yao. Na kwa vile mtu anaweza kufikiri kuwa wana Motoni wao pia ni hivyo, kwamba Mwenyezi Mungu atawakutanisha na dhuriya zao, akajulisha kwamba hukumu ya nyumba mbili hizi si hukumu moja. Kwani Moto ni nyumba ya uadilifu. Na katika uadilifu wake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hamuadhibu yeyote isipokuwa kwa dhambi,
na ndiyo maana akasema: "Kila mtu lazima atapata alichokichuma." Yaani, hakuna mbebaji hatambebea mwengine madhambi yake, na wala hakuna atakayebebeshwa mzigo wa mwingine. Hili limekusudiwa kuondoa dhana isiyokuwa ya kweli hiyo iliyotajwa.
#
{22} وقوله: {وأمددْناهم}؛ أي: أمددنا أهل الجنة من فضلنا الواسع ورزقنا العميم، {بفاكهةٍ}: من العنب والرُّمان والتُّفاح وأصناف الفواكه اللذيذة الزائدة على ما به يتقوَّتون، {ولحمٍ ممَّا يشتهونَ}: من كلِّ ما طلبوه واشتهته أنفسُهم من لحوم الطير وغيرها.
{22} Na kauli yake: "Na tutawapa" wana Peponi kutokana na fadhila zetu kubwa, na riziki zetu mingi kama vile "matunda" ya zabibu, makomanga, tufaha na aina mbalimbali za matunda matamu zaidi ambayo watafurahia. "Na nyama kama watavyopenda," kutokana na kila kitu watakachoomba na kutamaniwa na nafsi zao, kama vile nyama ya ndege na vitu vinginevyo.
#
{23} {يتنازَعون فيها كأساً}؛ أي: تدور كاسات الرحيق والخمر عليهم، ويتعاطَونها فيما بينهم، وتطوف عليهم الولدانُ المخلَّدون بأكواب وأباريق. {لا لغوٌ فيها ولا تأثيمٌ}؛ أي: ليس في الجنَّة كلامُ لغوٍ، وهو الذي لا فائدة فيه، ولا تأثيمٍ، وهو الذي فيه إثمٌ ومعصيةٌ. وإذا انتفى الأمران؛ ثبت الأمر الثالث، وهو أن كلامهم فيها سلامٌ طيبٌ طاهرٌ مسرٌّ للنفوس مفرحٌ للقلوب، يتعاشرون أحسن عشرة، ويتنادمون أطيب المنادمة، ولا يسمعون من ربِّهم إلاَّ ما يُقِرُّ أعينَهم ويدلُّ على رضاه عنهم ومحبَّته لهم.
{23} "Watapeana humo bilauri." Yaani, wataletewa mara kwa mara vikombe vyenye vinywaji safi na vyenye tembo, na watapeana wao kwa wao. Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wa ujana wa milele wakiwa na vikombe na birika "zisizo na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi." Yaani, hakuna mazungumzo ya upuuzi katika Pepo. Nao upuuzi ni maneno yasiyokuwa na faida, nayo dhambi ni yale ambayo ndani yake kuna dhambi na uasi. Na mambo mawili haya yasipokuwapo, basi jambo la tatu linathibiti, nalo ni kwamba maneno yao humo ni mazuri, yenye amani, ni safi na ya kufurahisha nafsi na nyoyo. Wanaishi kwa utangamano mzuri zaidi, na wanaingiliana kuingiliana kuzuri zaidi, na hawasikii kutoka kwa Mola wao Mlezi isipokuwa yanayofurahisha macho yao, na yanayoonyesha kwamba amewaridhia na anawapenda.
#
{24} {ويطوف عليهم غلمانٌ لهم}؛ أي: خدمٌ شبابٌ، {كأنَّهم لؤلؤٌ [مكنون] } من حسنهم وبهائهم، يدورون عليهم بالخدمة وقضاء أشغالهم ، وهذا يدلُّ على كثرة نعيمهم وسعته وكمال راحتهم.
{24} "Iwe wanawapitia watumishi wao" walio vijana, "kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza" kwa sababu ya uzuri na urembo wao. Wakiwajia mara kwa mara ili kuwatumikia na kuwakidhia mahitaji yao, na hili linaashiria wingi wa neema yao, upana wake na ukamilifu wa raha yao.
#
{25} {وأقبلَ بعضُهم على بعض يتساءلونَ}: عن أمور الدُّنيا وأحوالها.
{25} "Wataelekeana wakiulizana" kuhusu mambo ya dunia na hali zake.
#
{26} {قالوا}: في ذكر بيان الذي أوصَلَهم إلى ما هم فيه من الحبرة والسرور: {إنَّا كنَّا قبلُ}؛ أي: في دار الدُّنيا {في أهلِنا مشفقينَ}؛ أي: خائفين وجِلين، فتركْنَا من خوفه الذُّنوب، وأصلحنا لذلك العيوب.
{26} "Waseme" katika kubainisha yaliyowapelekea kwenye bashasha na furaha waliyomo. "Hakika tulikuwa zamani pamoja" Yaani, katika makazi ya dunia "na ahali zetu tukiogopa mno." Basi kwa sababu ya kumhofu ndiyo tukajiepusha na madhambi na kwa sababu ya hayo tukarekebisha makosa yetu.
#
{27} {فمنَّ اللهُ علينا}: بالهداية والتوفيق، {ووَقانا عذابَ السَّموم}؛ أي: العذاب الحار الشديد حرُّه.
{27} "Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani" kwa kutuongoa na kutuwezesha, "na akatulinda mbali adhabu ya upepo wa Moto."
#
{28} {إنَّا كنَّا من قبلُ ندعوه}: أن يَقِيَنا عذابَ السَّموم، ويوصِلَنا إلى النعيم، وهذا شاملٌ لدعاء العبادة ودعاء المسألة؛ أي: لم نزل نتقرَّب إليه بأنواع العبادات ، وندعوه في سائر الأوقات. {إنَّه هو البرُّ الرحيم}: فمن برِّه [بنا] ورحمته إيَّانا أنالَنا رضاه والجنة، ووقانا سخطه والنار.
{28} "Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu" atulinde mbali na adhabu ya upepo wa Moto, na atufikishe kwenye neema. Na hili linajumuisha dua ya ibada na dua ya kuomba kitu. Yaani, hatukuacha kujikurubisha kwake kwa njia mbalimbali za ibada, na tukimwomba Yeye kila wakati. "Hakika Yeye ndiye Mwema Mwingi wa kurehemu." Katika wema wake
[juu yetu] na rehema yake kwetu ni kwamba ameturidhia na akatuingiza katika bustani za mbinguni, na akatulinda mbali na ghadhabu yake na Moto.
{فَذَكِّرْ فَمَا أَنْتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ (29) أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَتَرَبَّصُ بِهِ رَيْبَ الْمَنُونِ (30) قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُمْ مِنَ الْمُتَرَبِّصِينَ (31) أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَامُهُمْ بِهَذَا أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ (32) أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُ بَلْ لَا يُؤْمِنُونَ (33) فَلْيَأْتُوا بِحَدِيثٍ مِثْلِهِ إِنْ كَانُوا صَادِقِينَ (34) أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ (35) أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بَلْ لَا يُوقِنُونَ (36) أَمْ عِنْدَهُمْ خَزَائِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ الْمُصَيْطِرُونَ (37) أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُمْ بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ (38) أَمْ لَهُ الْبَنَاتُ وَلَكُمُ الْبَنُونَ (39) أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُمْ مِنْ مَغْرَمٍ مُثْقَلُونَ (40) أَمْ عِنْدَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ (41) أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا فَالَّذِينَ كَفَرُوا هُمُ الْمَكِيدُونَ (42) أَمْ لَهُمْ إِلَهٌ غَيْرُ اللَّهِ سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ (43)}.
29. Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. 30.
Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari. 31.
Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. 32. Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? 33.
Au ndiyo wanasema: 'Ameitunga hii!' Bali basi tu hawaamini! 34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. 35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? 36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini. 37. Au wanazo hazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? 38. Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja iliyo wazi! 39. Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana? 40. Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama? 41. Au wanayo elimu ya ghaibu, nao wameandika? 42. Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao waliokufuru ndio watakaotegeka. 43. Au wanaye mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ametaksika Mwenyezi Mungu mbali na hao wanaowashirikisha naye.
#
{29} يأمر الله تعالى رسوله - صلى الله عليه وسلم - أن يُذَكِّرَ الناس مسلمهم وكافرهم؛ لتقوم حجَّة الله على الظَّالمين، ويهتدي بتذكيره الموفَّقون، وأن لا يبالي بقول المشركين المكذِّبين وأذيَّتهم وأقوالهم التي يَصدُّون بها الناس عن اتِّباعه، مع علمهم أنَّه أبعدُ الناس عنها، ولهذا نفى عنه كلَّ نقص رَمَوْه به، فقال: {فما أنتَ بنعمةِ ربِّكَ}؛ أي: منَّه ولطفه {بكاهنٍ}؛ أي: له رِئْيٌ من الجنِّ يأتيه بخبر بعض الغيوب التي يضمُّ إليها مئة كذبةٍ، {ولا مجنونٍ}: فاقد العقل ، بل أنت أكملُ الناس عقلاً، وأبعدهم عن الشياطين، وأعظمهم صدقاً، وأجلُّهم، وأكملهم.
{29} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwamrisha Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kuwakumbusha watu, wawe ni Waislamu au makafiri. Ili hoja ya Mwenyezi Mungu isimame juu ya madhalimu, na wale waliowezeshwa waongoke kwa ukumbusho wake, wala asijali maneno ya washirikina wanaokadhibisha, maudhi yao, na maneno yao wanayowazuilia watu kumfuata, ijapokuwa wanajua vyema kwamba yeye ndiye wa mbali zaidi na hayo kati ya watu wote, na ndiyo maana akamkanushia kila upungufu waliokuwa wakimtuhumu nao,
na akasema: "Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi si kuhani" ambaye huwa na mwenye kumwangalilia kutoka kwa majini anayemletea habari za ghaibu, kisha akazidisha humo uongo mia moja. "Wala mwendawazimu." Bali wewe ndiye mwenye akili zaidi ya watu wote, wa mbali zaidi na mashetani, mbora wao zaidi katika ukweli, mtukufu wao zaidi na mkamilifu wao zaidi.
#
{30} وتارةً {يقولون} فيه: إنَّه {شاعرٌ}: يقول الشعر، والذي جاء به شعرٌ، والله يقول: {وما علَّمناه الشعرَ وما ينبغي له}، {نتربَّصُ به ريبَ المَنونِ}؛ أي: ننتظر به الموتَ، فيبطُلُ أمرُه ونستريح منه.
{30} Na mara nyingine "wanasema" kwamba yeye ni "mtunga mashairi" na kwamba alicholeta ni mashairi.
Naye Mwenyezi Mungu anasema: "Wala hatukumfundisha
(Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo." Na akasema "tunamtarajia kupatilizwa na dahari." Yaani, tunamngoja afe, kisha jambo lake litabatilika na tutapumzika kutokana naye.
#
{31} {قل}: لهم جواباً لهذا الكلام السخيف: {تربَّصوا}؛ أي: انتظروا بي الموت، {فإنِّي معكم من المتربِّصين}: نتربَّص بكم أن يصيبكم الله بعذابٍ من عنده، أو بأيدينا.
{31} "Sema" ukiwajibu maneno haya ya kipuuzi: "Tarajieni" nife. "na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia" kwamba aje Mwenyezi Mungu kukusibuni na adhabu itokayo kwake au kwa mikono yetu.
#
{32} {أم تأمُرُهم أحلامُهم بهذا أم هم قومٌ طاغونَ}؛ أي: أهذا التكذيبُ لك والأقوال التي قالوها؛ هل صدرتْ عن عقولِهم وأحلامِهم؛ فبئس العقولُ والأحلامُ التي هذه نتائجها وهذه ثمراتها ؛ فإنَّ عقولاً جعلتْ أكملَ الخلق عقلاً مجنوناً، وجعلت أصدقَ الصِّدق وأحقَّ الحقِّ كذِباً وباطلاً؛ لهي العقول التي ينزَّه المجانين عنها؟ أم الذي حملهم على ذلك ظلمُهم وطغيانُهم؟ وهو الواقع؛ فالطغيانُ ليس له حدٌّ يقف عليه؛ فلا يُستغرب من الطاغي المتجاوزِ الحدَّ ، كلُّ قول وفعل صَدَرَ منه.
{32} "Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?" Yaani, je, huku kukanusha kwao na kauli zao hizo ambazo walizisema, je zilitokea katika akili na maoni yao? Basi ni mbaya mno akili na maoni ambazo haya ndiyo matokeo na matunda yake. Kwani akili zilizomfanya yule aliye mkamilifu zaidi wa akili katika viumbe wote kuwa ni wazimu, na zikafanya ukweli zaidi katika ukweli na haki iliyo haki zaidi ya zote kuwa uongo na batili, ndizo akili ambazo watu wazimu wanawekwa mbali nazo? Au kilichowapelekea wafanye hiyo ni dhuluma yao na kuruka kwao mipaka? Huu ndio ukweli hasa. Kwani jeuri haina kikomo ambacho hukomekea hapo. Basi haishangazi kwamba mwenye kuvuka mipaka mno anaweza kusema kila neno na kitendo.
#
{33} {أم يقولون تَقَوَّلَه}؛ أي: تقوَّل محمدٌ القرآن وقاله من تلقاء نفسه، {بل لا يؤمنونَ}؛ فلو آمنوا؛ لم يقولوا ما قالوا.
{33} "Au ndiyo wanasema: 'Ameitunga hii!'" Yaani, wanasema kwamba Muhammad alijitungia Qur-ani na akaisema mwenyewe tu. "Bali basi tu hawaamini!" Kwani Iau wangaliamini, basi wasingalisema waliyoyasema.
#
{34} {فَلْيَأتوا بحديثٍ مثلِهِ إنْ كانوا صادقينَ}: إنَّه تقوَّله؛ فإنَّكم العرب الفصحاء والفحول البلغاء، وقد تحدَّاكم أن تأتوا بمثلِهِ؛ فتصدق معارضتكم، أو تقرُّوا بصدقه، وإنكم لو اجتمعتم أنتم والإنس والجنُّ؛ لم تقدروا على معارضته والإتيان بمثله؛ فحينئذٍ أنتم بين أمرين: إمَّا مؤمنون به مقتدون بهديِهِ، وإمَّا معاندون متَّبعون لما علمتُم من الباطل.
{34} "Basi na walete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli." Kwani nyinyi ni Waarabu fasaha na mafahali walio bora wa usemi. Na amekupeni changamoto mlete kitu mfano wake, ili usadikike upinzani wenu au mkiri ukweli wake. Nanyi hakika hata kama mkijikusanya nyinyi wanadamu na majini; hamtaweza kuipinga na kuleta mfano wa Qur-ani hii.
Basi hapo mko baina ya mambo mawili: ima muiamini na mfwate uwongofu wake, au mkaidi na muwe mnafuata yale mliyokwisha jua kwamba ni batili.
#
{35} {أم خُلِقوا من غير شيءٍ أم هُمُ الخالقونَ}: وهذا استدلالٌ عليهم بأمرٍ لا يمكنهم فيه إلاَّ التسليمُ للحقِّ، أو الخروج عن موجب العقل والدين. وبيان ذلك أنهم منكرون لتوحيد الله، مكذِّبون لرسوله، وذلك مستلزمٌ لإنكار أنَّ الله خَلَقَهم، وقد تقرَّر في العقل مع الشرع أنَّ ذلك لا يخلو من أحد ثلاثة أمورٍ: إمَّا أنهم {خُلِقوا من غير شيءٍ}؛ أي: لا خالق خلقهم؛ بل وجدوا من غير إيجادٍ ولا موجدٍ؛ وهذا عينُ المحال. {أم هم الخالقونَ}: لأنفسِهم؛ وهذا أيضاً محالٌ؛ فإنَّه لا يتصوَّر أن يوجِدَ أحدٌ نفسَه. فإذا بطل هذان الأمران وبان استحالتُهما؛ تعيَّن القسم الثالثُ، وهو أنَّ الله هو الذي خلقهم. وإذا تعين ذلك؛ عُلِمَ أنَّ الله تعالى هو المعبودُ وحدَه، الذي لا تنبغي العبادة ولا تَصْلُح إلاَّ له تعالى.
{35} "Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?" Huku ni kuwasimamishia ushahidi kwa kitu ambacho hawawezi chochote isipokuwa kuisalimishia haki amri, au kukengeuka mbali na inavyohitaji akili na dini. Ufafanuzi wa hayo ni kuwa wao wanakanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, wanamkanusha Mtume wake. Na hilo linalazimu kukanusha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba. Lakini imeshathibiti katika akili pamoja na sheria kwamba jambo hili halitoki nje ya mambo matatu. Ima wao "wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote." Yaani, hakuna Muumba aliyewaumba. Hili haliwezekani kabisa. "Au ni wao ndio waumbaji" waliojiumba wenyewe? Hili pia haliwezekani. Kwa maana haiwezekani kuwa mtu yeyote anaweza kujiumba mwenyewe. Kwa hivyo, mambo haya mawili yakibatilika na kutowezekana kwake kukadhihirika, inabakia tu sehemu ya tatu. Ambayo ni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba. Na kama inasalia sehemu hii tu, inajulikana kwamba Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayepaswa kuabudiwa, ambaye haifai kufanya ibada kwa ajili ya chochote kile isipokuwa Yeye Mtukufu.
#
{36} وقوله: {أم خَلَقوا السمواتِ والأرضَ}: وهذا استفهامٌ يدلُّ على تقرير النفي؛ أي: ما خلقوا السماواتِ والأرضَ، فيكونوا شركاء لله، وهذا أمرٌ واضحٌ جدًّا. {بل} المكذبونَ {لا يوقنونَ}؛ أي: ليس عندهم [علم تامٌّ و] يقينٌ يوجب لهم الانتفاع بالأدلَّة الشرعيَّة والعقليَّة.
{36} Na kauli yake: "Au wameziumba mbingu na ardhi?" Huku ni kuuliza swali lenye maana ya kukanusha. Yaani, hawakuziumba mbingu na ardhi ili wawe washirika wa Mwenyezi Mungu. Na hili ni jambo lililo wazi kabisa. "Bali" wanaokadhibisha hao "hawana yakini." Yaani, hawana
[elimu kamili na] yakini inayoweza kuwafanya kunufaika na ushahidi wa kisheria na wa kiakili.
#
{37} {أمْ عندَهم خزائنُ ربِّك أم هم المُصَيْطِرونَ}؛ أي: أعند هؤلاء المكذِّبين خزائنُ رحمة ربِّك، فيعطوا من يشاؤون ويمنعوا من يشاؤون ؛ أي: فلذلك حجروا على الله أن يُعطي النبوَّة عبدَه ورسولَه محمداً - صلى الله عليه وسلم -، وكأنَّهم الوكلاء المفوَّضون على خزائن رحمة الله، وهم أحقرُ وأذلُّ من ذلك؛ فليس في أيديهم لأنفسهم نفعٌ ولا ضرٌّ ولا موتٌ ولا حياةٌ ولا نشورٌ؛ {أهم يقسِمونَ رحمةَ ربِّك نحنُ قَسَمْنا بينهم معيشَتَهم في الحياة الدُّنيا}؟ {أم هم المُصَيْطِرُونَ}؛ أي: المتسلِّطون على خلق الله وملكه بالقهر والغلبة؟! ليس الأمر كذلك، بل هم العاجزون الفقراء.
{37} "Au wanazo hazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?" Yaani, je, wanazo hawa wanaokanusha hazina za rehema za Mola wako Mlezi, basi wakawa wanampa wamtakaye na wanamnyima wamtakaye? Ndiyo maana wakamzuia Mwenyezi Mungu kumpa utume mja wake na Mtume wake Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kana kwamba wao ndio wasimamizi waliokabidhiwa usimamizi wa hazina za rehema za Mwenyezi Mungu, ilhali wao ni wenye kudharauliwa na madhalili zaidi kuwa hivyo. Kwani hakuna mikononi mwao uwezo wa kujinufaisha, wala madhara, wala mauti, wala uhai, wala kufufua. "Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani." Kisha akasema, "Au wao ndio wenye madaraka" juu ya viumbe wa Mwenyezi Mungu na ufalme wake kwa ushindi mkubwa na ukandamizaji! Sivyo hivyo jambo hilo. Bali wao wameshindwa na hata ni wahitaji zaidi.
#
{38} {أمْ لهم سُلَّمٌ يستمعون فيه}؛ أي: ألهم اطِّلاع على الغيب واستماعٌ له بين الملأ الأعلى، فيخبرون عن أمورٍ لا يعلمُها غيرُهم، {فليأتِ مستمِعُهم}: المدَّعي لذلك {بسلطانٍ مبينٍ}: وأنَّى له ذلك والله تعالى عالم الغيب والشهادة؛ فلا يُظْهِرُ على غيبه أحداً؛ إلاَّ من ارتضى من رسولٍ يخبره بما أراد من علمِهِ، وإذا كان محمدٌ - صلى الله عليه وسلم -، أفضل الرسل وأعلمهم وإمامهم، وهو المخبر بما أخبر به من توحيد الله ووعده ووعيده وغير ذلك من أخباره الصادقة، والمكذِّبون هم أهل الجهل والضَّلال والغيِّ والعناد؛ فأيُّ المخبرين أحقُّ بقَبول خبره، خصوصاً والرسول - صلى الله عليه وسلم - قد أقام من الأدلَّة والبراهين على ما أخبر به ما يوجِبُ أن يكون ذلك عين اليقين وأكمل الصدق، وهم لم يُقيموا على ما ادَّعَوْه شبهةً فضلاً عن إقامة حجَّة؟!
{38} "Au wanazo ngazi za kusikilizia?" Yaani, je, wanaweza kujua za ghaibu na kusisikiliza kutoka kwa viumbe watukufu wa juu kabisa, ndiyo wakawa wanawajulisha wengine mambo wasiyoyajua. "Basi huyo msikilizaji wao na alete" anayefikia kuyajua hayo "hoja iliyo wazi!" Lakini atawezaje kufanya hivyo na hali Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anyeajua ghaibu na mambo ya dhahiri? Na wala hamdhihirishii yeyote siri yake. Isipokuwa Mtume wake aliyemridhia, ambaye anamwambia anachotaka katika elimu yake. Na ikiwa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ndiye mbora wa Mitume wote, ajuaye zaidi yao wote, na imamu wao, na yeye ndiye aliyejulisha yale aliyoyajulisha kuhusu upweke wa Mwenyezi Mungu, ahadi yake nzuri, tishio lake la adhabu, na mengineyo miongoni mwa habari za ukweli, nao wakunashaji ndio watu wajinga, upotofu, ukengeufu na ukaidi. Basi ni yupi kati ya watoa habari wawili hawa ana haki zaidi ya kukubaliwa habari zake, hasa pale Mtume - rehema na amani zimshukie - alisimamisha ushahidi na hoja mbalimbali juu ya yale aliyoyajulisha, mambo ambayo yanalazimu anayoyasema kuwa ni jicho la yakini, na ukweli kamili zaidi, nao hawakusimamisha juu ya yale waliyodai si tuhuma ya kweli wala mbali na kusimamisha hoja juu yake?
#
{39} وقوله: {أم له البناتُ}: كما زعمتُم، {ولكم البنونَ}: فتجمعون بين المحذورَيْن: جَعْلُكُم له الولد، واختيارُكُم له أنقص الصنفين؛ فهل بعد هذا التنقُّص لربِّ العالمين غايةٌ أو دونه نهايةٌ؟!
{39} Na kauli yake: "Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana,
" kama mlivyodai: "na nyinyi ndio mna wavulana?" Basi kwa hilo mnakuwa mmejumuisha vitu viwili vilivyoharamishwa: Mlimfanyia mwana, na kumchagulia yule ambaye ndiye mpungufu zaidi katika aina mbili hizi. Basi je, kuna kiwango kingine baada ya kumpunguzia heshima Mola Mlezi wa walimwengu hivi au je kuna mwisho chini ya hilo?
#
{40} {أم تسألُهُم}: يا أيُّها الرسولُ، {أجراً}: على تبليغ الرسالة، {فهم من مَغْرَمٍ مُثْقَلونَ}: ليس الأمر كذلك، بل أنت الحريص على تعليمهم تبرُّعاً من غير شيء، بل تبذلُ لهم الأموالَ الجزيلة على قَبول رسالتك والاستجابة لأمرِك ودعوتك ، وتعطي المؤلَّفة قلوبهم؛ ليتمكَّن العلم والإيمان من قلوبهم.
{40} "Au wewe unawaomba" Ewe Mtume, "ujira" kwa ajili ya kufikisha ujumbe. "Kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?" Si hivyo, lakini wewe unajishughulisha sana na kuwafundisha bure bila ya kuwaomba chochote. Bali unawapa kiasi kikubwa cha mali kwa sababu ya kuukubali ujumbe wako na kuitikia amri na wito wako, na unawapa wale wanaohitaji kuzipa nyoyo zao nguvu. Ili elimu na imani vikae imara katika nyoyo zao.
#
{41} {أم عندَهم الغيبُ فهم يكتبونَ}: ما كانوا يعلمونَه من الغُيوب، فيكونون قد اطِّلعوا على ما لم يطَّلع عليه رسولُ الله، فعارضوه وعاندوه بما عندَهم من علم الغيب، وقد عُلِمَ أنَّهم الأمَّة الأميَّة الجهَّال الضَّالون، ورسول الله - صلى الله عليه وسلم - هو الذي عنده من العلم أعظم من غيره، وأنبأه الله من علم الغيب على ما لم يَطَّلِعْ عليه أحدٌ من الخلق، وهذا كلُّه إلزامٌ لهم بالطرق العقليَّة والنقليَّة على فساد قولهم وتصوير بطلانِهِ بأحسن الطُّرق وأوضحها وأسلمها من الاعتراض.
{41} "Au wanayo elimu ya ghaibu, nao wameandika" yale waliyoyajua ya ghaibu, kwa hivyo wakawa wamefikia kujua yale ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuyaona, basi ndiyo wakampinga na wakamfanyia ukaidi kwa yale waliyo nayo ya elimu ya ghaibu. Lakini ilishajulikana kwamba wao ni watu wasiojua kusoma na kuandika, wajinga na wapotevu, na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - ndiye mwenye elimu kubwa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, na Mwenyezi Mungu alimjulisha elimu ya ghaibu ambayo hakuna yeyote katika viumbe alikuwa kupewa. Haya yote ni kuwafanya waukubali ukweli kwa njia za kiakili na kimaandiko juu ya ubovu wa kauli yao na kuonyesha ubatili wake kwa njia bora zaidi, zilizo wazi zaidi na zilizo salama zaidi kutokana na upinzani.
#
{42} وقوله: {أم يريدون}: بقدحِهِم فيك وفيما جئتَ به {كيداً}: يُبْطلونَ به دينَك، ويفسدون به أمرَك. {فالذين كفروا هُمُ المَكيدونَ}؛ أي: كيدُهم في نحورهم، ومضرَّته عائدةٌ إليهم، وقد فعل الله ذلك، ولله الحمد، فلم يُبْقِ الكفارُ من مقدورهم من المكر شيئاً إلاَّ فعلوه، فنصر الله نبيَّه عليهم، وأظهر دينَه ، وخَذَلَهُم وانتصر منهم.
{42} Na kauli yake: "Au wanataka" katika kukukashifu wewe na yale uliyokuja nayo, "kufanya vitimbi tu" ili kuibatilisha dini yako kwa hayo na kuharibu mambo yako? "Lakini hao waliokufuru ndio watakaotegeka.
" Yaani: Vitimbi vyao vitawarudia wenyewe katika koo zao, na madhara yake yatawarudia, na tayari Mwenyezi Mungu alishafanya hayo, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu. Basi makafiri hawakubakishiwa na uwezo wa kufanya kitimbi chochote ila walikifanya, lakini Mwenyezi Mungu akamnusuru Mtume wake dhidi yao, na akadhihirisha dini yake, na akawaangusha na kuwashinda.
#
{43} {أم لهم إلهٌ غير اللهِ}؛ أي: ألهم إلهٌ يُدعى ويرجى نفعُه ويُخاف من ضرِّه غير الله تعالى؟ {سبحان اللهِ عمَّا يشرِكون}: فليس له شريكٌ في الملك، ولا شريكٌ في الوحدانيَّة والعبادة، وهذا هو المقصود من الكلام الذي سيق لأجله، وهو بطلانُ عبادة ما سوى الله، وبيانُ فسادها بتلك الأدلَّة القاطعة، وأنَّ ما عليه المشركون هو الباطل، وأنَّ الذي ينبغي أن يُعْبَدَ ويصلَّى له ويُسْجَدَ ويُخْلَصَ له دعاءُ العبادة ودعاءُ المسألة هو الله المألوهُ المعبود، كاملُ الأسماء والصفاتِ، كثيرُ النعوتِ الحسنة والأفعال الجميلة، ذو الجلال والإكرام والعزِّ الذي لا يُرام، الواحد الأحدُ، الفردُ الصمدُ، الكبيرُ الحميدُ المجيدُ.
{43} "Au wanaye mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu?" Yaani, je, wanaye mungu anayetarajiwa, ambaye yanatarajiwa manufaa yake na kuhofiwa madhara yake badala ya Mwenyezi Mungu? "Subhanallah
(Ametakasika Mwenyezi Mungu) mbali na hao wanaowashirikisha naye." Yeye hana mshirika katika ufalme, wala hana mshirika katika umoja wake wala ibada zake. Na haya ndiyo yaliyokusudiwa katika maneno haya, nayo ni ubatili wa kuabudu kitu kingine chochote mbali na Mwenyezi Mungu, na kueleza uharibifu wake kwa hoja hizi za kukata kabisa, na kwamba hayo wayafanyayo washirikina ni batili, na kwamba yule anayepaswa kuabudiwa, kuswalia, kusujudia, na kutakasia dua ya ibada na dua ya kutaka kitu ni Mwenyezi Mungu, afanyiwaye uungu wa kweli, muabudiwa wa kweli, mkamilifu wa majina na sifa, mwingi wa sifa nzuri nyingi na matendo mazuri, mwenye heshima, ukarimu, na nguvu isiyoshindika, Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, Mkubwa, Msifiwa mno, Mtukufu.
{وَإِنْ يَرَوْا كِسْفًا مِنَ السَّمَاءِ سَاقِطًا يَقُولُوا سَحَابٌ مَرْكُومٌ (44) فَذَرْهُمْ حَتَّى يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي فِيهِ يُصْعَقُونَ (45) يَوْمَ لَا يُغْنِي عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنْصَرُونَ (46)}.
44.
Na hata wangeona pande linatoka mbinguni linaanguka wangesema: Ni mawingu yaliyobebana. 45. Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapohilikishwa. 46. Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
#
{44} يقول تعالى في ذكر بيان أنَّ المشركين المكذِّبين بالحقِّ الواضح قد عَتَوا عن الحقِّ وعسوا على الباطل، وأنَّه لو قام على الحقِّ كلُّ دليل؛ لما اتَّبعوه، ولخالفوه وعاندوه: {وإنْ يروا كِسْفَاً من السماء ساقطاً}؛ أي: لو سقط عليهم من السماء من الآيات الباهرة كِسْفٌ ؛ أي: قطعٌ كبارٌ من العذاب، {يقولوا سحابٌ مركومٌ}؛ أي: هذا سحابٌ متراكمٌ على العادة؛ أي: فلا يبالون بما رأوا من الآيات، ولا يعتبرون بها!
{44} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akitaja na kubainisha kwamba washirikina wanaoukanusha ukweli ulio wazi wameasi haki na kushikilia batili sawasawa, na kwamba hata kama hoja zote zitasimama kwa ajili ya kudhibitisha haki, wasingeliifwata,
wangeliihalifu na kuipinga: "Na hata wangeona pande linatoka mbinguni linaanguka." Yaani, lau zingeliwashukia ishara zinazong'aa kutoka mbinguni kama wingu la adhabu,
"wangesema: Ni mawingu yaliyobebana" kama kawaida tu, kisha wakaendelea kutojali ishara walizoziona, wala hawazizingatii!
#
{45} وهؤلاء لا دواء لهم إلاَّ العذاب والنَّكال، ولهذا قال: {فَذَرْهُم حتى يُلاقوا يومَهم الذي فيه يُصْعَقون}: وهو يوم القيامةِ، الذي يصيبهم فيه من العذاب ما لا يقادَرُ قَدْرُه ولا يوصَف أمرُه.
{45} Hawa hawana dawa ila adhabu na mateso,
na ndiyo maana akasema: "Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapohilikishwa" nayo ni siku ya Kiyama, ambayo watapatwa ndani yake na adhabu isiyowezekana kukadiria kiasi chake, wala kulielezea jambo lake.
#
{46} {يوم لا يُغْني عنهم كيدُهم شيئاً}؛ أي: لا قليلاً ولا كثيراً، وإنْ كان في الدُّنيا قد يوجد منهم كيدٌ يعيشون به زمناً قليلاً؛ فيوم القيامةِ يضمحلُّ كيدُهم، وتبطلُ مساعيهم، ولا ينتصرون من عذاب الله، {ولا هم يُنصَرون}.
{46} "Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo." Si kidogo wala nyingi, hata kama katika dunia huenda wakawa na hila wanazoishi kwazo kwa muda mfupi; Lakini siku ya Kiyama hila zao hizo vitatoweka, juhudi zao zitabatilika, na hawataepukana na adhabu ya Mwenyezi Mungu,
“wala wao hawatanusuriwa.”
{وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا عَذَابًا دُونَ ذَلِكَ وَلَكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ (47) وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ (48) وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَارَ النُّجُومِ (49)}.
47. Na hakika wale waliodhulumu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hii, lakini wengi wao hawajui. 48. Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, 49. Na usiku pia mtakase, na zinapokuchwa nyota.
#
{47} لما ذَكَرَ اللهُ عذابَ الظالمين في الآخرة؛ أخبر أنَّ لهم عذاباً قبل عذاب يوم القيامةِ، وذلك شاملٌ لعذاب الدُّنيا بالقتل والسبي والإخراج من الديار، ولعذابِ البرزخ والقبر. {ولكنَّ أكثرهم لا يعلمونَ}؛ أي: فلذلك أقاموا على ما يوجب العذاب وشدة العقاب.
{47} Mwenyezi Mungu alipoitaja adhabu ya madhalimu katika Akhera, akajulisha kwamba watapata adhabu nyingine kabla ya adhabu ya Siku ya Kiyama, na hilo linajumuisha adhabu ya duniani kwa kuuawa, kutekwa, na kufukuzwa nyumbani kwao, na pia adhabu ya kaburini. "Lakini wengi wao hawajui." Basi ndiyo maana wakaendelea juu ya yale yaliyowasababishia kupata adhabu na mateso makali.
#
{48 - 49} ولمَّا بيَّن تعالى الحجج والبراهين على بطلان أقوال المكذِّبين؛ أمر رسوله - صلى الله عليه وسلم - أن لا يعبأ بهم شيئاً، وأنْ يصبِرَ لحكم ربِّه القدريِّ والشرعيِّ؛ بلزومه والاستقامة عليه، وَوَعَدَهُ الله الكفاية بقوله: {فإنَّك بأعيننا}؛ أي: بمرأى منَّا وحفظٍ واعتناءٍ بأمرك، وأمره أن يستعين على الصبر بالذكر والعبادة، فقال: {وسبِّح بحمد ربِّك حين تقومُ}؛ [أي]: من الليل؛ ففيه الأمر بقيام الليل، أو حين تقومُ إلى الصلوات الخمس؛ بدليل قوله: {ومن الليل فسبِّحْه وإدْبارَ النُّجومِ}؛ أي: آخر الليل، ويدخل فيه صلاة الفجر. والله أعلم.
{48 - 49} Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alipozifafanua hoja na ushahidi wa kubatilisha ubatili wa kauli za wanaokadhibisha, alimuamrisha Mtume wake – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – asiwajali hata kidogo, na kwamba asubiri hukumu ya Mola wake Mlezi ya kimipango ya azali ya Mwenyezi Mungu na ya kisheria, kwa kushikamana nazo na kuwa mnyoofu juu yake,
na Mwenyezi Mungu akamuahidi kumtosheleza kwa kauli yake: "Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu." Yaani, tunakutazama, na kukulinda na kujali mambo yako, na akamuamrisha kutafuta juu ya msaada kwa kumtaja na kufanya ibada,
na akasema: "Na mtakase Mola wako Mlezi unaposimama,"
[yaani] usiku. Na katika hili kuna amri ya kuswali Swala za usiku, au unaposimama kwenda katika Swala tano za kila siku.
Maana hizi zinaashiriwa na kauli yake: "Na usiku pia mtakase, na zinapokuchwa nyota." Yaani, mwisho wa usiku, ambao ni pamoja na sala ya alfajiri. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.
Imekamilika tafiri ya Surat At-Tur, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.
******